Simulizi : The Football (2)
Sehemu Ya Tano (5)
atumie busara katika suala la
Korea kaskazini.Kwa sasa amebaki
na watu wanaomsikiliza kwa kila
jambo anaweza akaingia katika
vita na Korea Kaskazini.Wakati
mwingine ninahisi yawezekana
labda ametaka niuawe kwa kuwa
nilikuwa nampinga sana katika
suala la kutaka kuanzisha vita na Korea kaskazini.Sasa anayo nafasi
kubwa ya kufanya kila
anachokitaka bila kupata upinzani
mkubwa” akasema Helmet .Dr
Vivian akamtazama na kusema
“Helmet mimi na wewe
tunaweza kufanya jambo kumzuia
Mike straw asifikie malengo yake
ya kutaka kuanzisha vita”
“Kwa sasa sina nguvu ya
kufanya jambo lolote na..”
akasema Hemet lakini Dr Vivian
akamkatisha
“Bado unayo nguvu Helmet”
akasema Dr Vivian na kumtazama
Helmet
“Tunao watu walioletwa
kufanya kazi moja tu ya
kukuua.Tutawahoji watu hao na tutapata ukweli wa jambo hili.Ni
vipi endapo tutapata ushahidi usio
na chembe ya shaka kwamba
Marekani wamesuka mpango wa
kukuua,halafu ukaanzisha
mchakato wa kumuondoa Mike
straw madarakani? Helmet
wamarekani wanakupenda sana
na endapo usingejitoa katika mbio
za urais hivi sasa ungekalia kiti cha
urais.Ninataka uanzishe vugu vugu
la kumtoa madarakani rais Mike
straw na serikali yake na kwa
kuwa unao uungwaji mkono
mkubwa utachaguliwa kuwa rais
wa Marekani na kwa pamoja
tutafanya mambo ambayo
yataishangaza dunia.Ninakuahidi
Helmet kuumaliza mgogoro huu unaofukuta hivi sasa.Sitaki unijibu
kwa sasa.Nenda kalifikirie hili
jambo na baadae tutazungumza”
akasema Dr Vivian
“Mheshimiwa rais
umezungumza suala zito sana ila
nashukru kwa busara zako kwa
kunipa nafasi ya kulitafakari suala
hili kwa kina na kisha kukupa
jibu.Ila ninapenda kukuhakikishia
kwamba hili ni jambo
linalowezekana kabisa.Ninao
ushawishi mkubwa sana ndani ya
serikali ya Marekani na ninaweza
kuendesha kampeni hiyo ya
kumuondoa madarakani rais Mike
straw lakini suala la mimi
kuchukua nafasi yake ya urais
ninahitaji muda wa kutafakari.Nimefurahiswa sana na
kauli yako kuhusiana na
kuumaliza mgogoro mkubwa
unaofukuta hivi sasa duniani
ambao kwa kiasi kikubwa ni Mike
straw ndiye aliyeuanzisha.Nina
tamani kuona mambo haya
yanamalizika na dunia inakuwa
kitu kimoja na mahala salama pa
kuishi.Ninatamani kuona nchi zote
zinazomiliki silaha kali za
maangamizi zinaingia
makubaliano ya kuteketeza silaha
zao na kuifanya dunia iwe sehemu
salama ya kuishi”
Mlinzi wa rais akaingia pale
sebuleni. “Mheshimiwa rais,Mathew
tayari amefika ” akasema na Dr
Vivian akavuta pumzi ndefu.
“Aruhusiwe aingie ndani”
akasema Dr Vivian halafu
akamtaka radhi Helmet akatoka na
kukutana na Meshack Jumbo.
“You were right Meshack,I
need him.We need him” akasema
Dr Vivian
“Unamzungumzia nani
mheshimiwa rais?
“Mathew.Ulikuwa sahihi
nilikosea sana kwa nilichotaka
kumfanyia.Mathew ni muhimu
kwetu.Bado tunamuhitaji sana”
akasema Dr Vivian na tabasamu
likaonekana usoni pa Meshack
Jumbo. “Nilikwambia mheshimiwa
rais ,bado tutamuhitaji sana
Mathew” akasema Meshack Jumbo
“Kuna mambo nimezungumza
na Helmet Brian na nimejikuta
nikimuhitaji tena Mathew katika
kuyatekeleza” akasema Dr Vivian
“Vipi kuhusu suala lake kule
polisi?
“Nitalimaliza” akajibu Dr
Vivian na Mathew akajitokeza
akiwa ameongozana na walinzi
wawili
“Madam president” akasema
Mathew
“Mathew karibu sana.Pole
kwa matatizo yote yaliyotokea”
akasema Dr Vivian “Ahsante sana mheshimiwa
rais” akasema Mathew na
kumtazama Meshack Jumbo
“Mzee nimekuja kuifanya ile
kazi uliyonieleza”
“Mathew kabla hujaifanya kazi
hiyo nina mazungumzo nawe
mafupi” akasema Dr Vivian na
kusogea pembeni
“Nadhani Meshack Jumbo
amekwisha kueleza kuhusiana na
Helmet.Amegoma kuondoka hapa
bila kukuona.Ametokea kukuamini
sana hivyo nataka umpeleka
mahala alipoandaliwa kisha urejee
hapa ikulu nina mazungumzo
nawe muhimu” akasema Dr Vivian “Sawa mheshimiwa rais”
akajibu Mathew na wakabaki
wanatazamana
“Kuna taarifa zozote
kuhusiana na maendeleo ya
Theresa?
“Taarifa ya mwisho niliyoipata
alikuwa hajazinduka bado lakini
madaktari wamenihakikishia
kwamba anaendelea vizuri na
atazinduka.Tuendelee
kumuombea” akasema Dr Vivian
kwa sauti ya upole.
“Mathew ni hilo tu nililotaka
kuzungumza nawe.Sasa ni wakati
wa kumuondoa Helmet brian na
kumpeleka kupumzika” akasema
Dr Vivian akaongozana na Mathew
hadi sebuleni kwake “Helmet ,rafiki yako Mathew
tayari amefika” akasema Dr Vivian
huku akitabasamu.Helmet Brian
akatabasamu pia baada ya
kumuona Mathew
“Simfahamu Mathew lakini
nimetokea kumuamini
mno.Ahsante sana Mathew kwa
kuja.Niliomba uwepo karibu yangu
wakati ninapelekwa mahala
nitakapokuwa ninaishi” akasema
Helmet
“Usijali mheshimiwa
waziri.Uko salama” akasema
Mathew na kutaka apewe
utaratibu wa namna ya
kumuondoa Helmet pale
ikulu.Meshack Jumbo akamueleza
kila kitu namna walivyojipanga na Mathew akatoa maelekezo yake
halafu wakamchukua Helmet na
kuondoka naye kumpeleka
sehemu ya siri.
WASHINGTON DC - MAREKANI
Kikao alichokiitisha rais wa
Marekani Mike Straw kwa ajili ya
kuwasilisha pendekezo lake la
kwenda Tanzania kilimalizika bila
kupata muafaka.Wajumbe wa
kikao kile hawakuridhia wazo la
Mike la kwenda Tanzania kuonana
ana kwa ana na rais Dr Vivian na
kuumaliza mzozo uliopo.Badala
yake wajumbe walitaka kwanza
kikosi ambacho tayari kimetumwa
kwenda Tanzania kuchunguza kuhusu shambulio lile lililotokea
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere kiachwe kifanye
uchunguzi wake na kama
kutaonekana ulazima wa Mike
kwenda Tanzania basi wataamua
lakini kwa muda huo hali ya
usalama ya Tanzania ilitia shaka
kwa rais wa Marekani kufanya
ziara
Pamoja na mvutano mkali
uliojitokeza katika kikao hicho
bado Mike straw alishikilia
msimamo wake wa kwenda
Tanzania kuzungumza ana kwa
ana na rais Dr Vivian.Kikao
kilimazika bila muafaka na Mike
straw kwa kutumia nguvu yake
kama rais akaagiza ndege yake iandaliwe kwa ajili ya safari ya
kwenda Tanzania ambayo alipanga
kuianza saa nne za usiku.Baada ya
kikao kile kumalizika akampigia
simu Willy Gadner
“Willy nimefanya
maamuzi.Ninakwenda Tanzania”
“Mheshimiwa rais !! Gadner
akashangaa
“Usiseme chochote
Willy,nimeamua kwenda Tanzania
kulimaliza hili suala.Ninataka
kuonana ana kwa ana na Dr Vivian
na kulifikisha mwisho hili
jambo.Ni mimi ndiye niliyeanzisha
hili suala na kama nisipochukua
juhudi za kulimaliza basi
litaniletea matatizo makubwa
hivyo basi nataka nipate taarifa zote za kuhusiana na yule mtoto
wa Dr Vivian ambazo naamini
zitanisaidia sana kuweza
kumshawishi akubaliane na
matakwa yangu” akasema Mike
“Lakini mheshimiwa rais hali
ya usalama kwa sasa nchini
Tanzania si nzuri na sikushauri
ufanye hivyo unavyotaka kufanya”
“Willy hakuna anayeweza
kunizuia kufanya jambo
lolote.Ninao ulinzi wa kutosha wa
hiyo siwezi kuogopa kwenda
katika nchi ndogo kama
Tanzania.Ninaomba faili lenye
taarifa zote za kumuhusu mtoto wa
Dr Vivian linifikie hapa kabla ya
saa tatu za usiku kwani ninaondoka saa nne usiku wa leo”
akasema Mike na kukata simu
“Lazima nifanye juhudi za
kulimaliza suala hili kwa njia
yoyote na njia pekee ninayoiona
kwa sasa ni kwenda Tanzania
mimi mwenyewe na kuzungumza
na Dr Vivian.Sitaki Helmet
afahamu kuhusiana na mpango
huu wa kumuua” akawaza Mike
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Baada ya kumfikisha Helmet
Brian mahala ambako iliaminiwa
ni salama zaidi kwa yeye kuwepo,
Mathew na Meshack Jumbo
walirejea ikulu kama alivyokuwa ameelekeza rais Dr Vivian.Moja
kwa moja wakaelekea katika
sehemu ya kupumzikia
“Mathew” rais akaanzisha
maongezi
“Awali ya yote naomba
nikushukuru sana kwa yote
uliyoyafanya leo hii na vile vile
kukupa pole kwa matatizo
yaliyokupata usiku wa leo”
“Ahsante sana mheshimiwa
rais .Yote yaliyotokea ni sehemu ya
kazi.Ninamshukuru sana mzee
Meshack kwa kuniondoa mikononi
mwa polisi lakini naomba
nikuweke wazi mheshimiwa rais
kwamba si mimi niliyemuua Dr
Robert Mwainamela.Kuna watu
waliomuua na mimi nikaangushiwa mzigo ule mzito wa
mauaji.Naomba uniamini na
unisaidie mheshimiwa rais katika
hilo kwani jeshi la polisi ninaamini
hivi sasa wananitafuta kila kona
hadi wahakikishe wamenipata na
kunifikisha mahakamani kwa kosa
la mauaji” akasema Mathew
“Usihofu Mathew.Suala lako
limekwisha malizika.Tayari
nimekwisha toa maelekezo
watafutwe wauaji halisi na wewe
uachwe huru kwani hauhusiki kwa
namna yoyote ile licha ya mauaji
hayo kufanyika nyumbani kwako”
akasema Dr Vivian
“Ahsante sana mheshimiwa
rais.Ahsante sana kwa kuniokoa”akasema Mathew kwa
furaha kubwa
“Mathew nilikueleza kwamba
kuna mambo muhimu ambayo
nataka tuzungumze.Nimeamua
kufunguka kwako na kukueleza
baadhi ya mambo ambayo nadhani
unapaswa
kuyafahamu.Nimechagua
kuwaamini wewe na mzee
Meshack na kuamua kuwaeleza
baadhi ya mambo yangu ya siri na
ninaamini mnavyo vifua vya
kuweza kuyahifadhi haya mambo
kwani sitaki kusikia mambo haya
yametoka vinywani mwenu na
kuwafikia watu wengine ambao
hawatakiwi kuyafahamu” Akasema Dr Vivian na kunyamaza kisha
akaendelea
“Mathew nilikuondoa katika
shughuli zako za biashara na
kukuomba unisaidie kuchunguza
nani waliomuua baba
yangu.Wakati ukiendelea na
uchunguzi wako nimekuzuia mara
mbili usiendelee na
uchunguzi.Nilifanya vile kwa
sababu kuna mambo ambayo
sikutaka uyafahamu kwani endapo
ungeendelea zaidi na uchunguzi
basi ungeweza kuyafahamu.Hata
hivyo nilikuwa najidanganya
kwani kila nilivyokuwa najaribu
kukuzuia ndivyo ulivyokuwa
unakaribia kuyafakia mambo hayo
ambayo sikutaka uyafikie.Baada ya kutafakari nimegundua kwamba
kuna ulazima wa kukueleza ukweli
na nimekuita hapa kukueleza
ukweli mtupu na nina hakika
baada ya kumaliza mazungumzo
haya tutakwenda sawa”
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Ulinifuata ukanieleza
kwamba una mashaka na Dr
Robert na ukaniomba ruhusa
umchunguze nikakataa.Nilikataa
kwa sababu Dr Robert ni mtu
ambaye anayafahamu mambo
yangu kadhaa ambayo wengine
hawayafahamu na kwa ufupi
naweza kusema kwamba ni mtu
niliyemuamini sana.Nilijua
kwamba kama utamchunguza Dr Robert lazima kuna mambo
utayafahamu kuhusu mimi ambayo
sikutaka wewe au mtu mwingine
ayafahamu kwani yangeweza
kuniletea matatizo kama rais
endapo yangefika kwa mahasimu
zangu wa kisiasa.Pamoja na
kujitahidi kuzuia usimfanyie
uchunguzi lakini bado ulijikuta
ukilazimika kufanya hivyo
kutokana na umuhimu wake
katika uchunguzi wake.Sikujua
kama Dr robert alitumia ukaribu
wangu kufanya mambo mengine
kama ulivyogundua kwamba
alikwa anashirkiana na
Marekani.Sikulifahamu hilo na
kama ningelifahamu hilo mapema
ningekwisha muondoa katika serikali yangu zamani.Niliamini Dr
Robert ni mtu safi na uadilifu wake
si wa kutiliwa shaka.Uliponieleza
kwamba Dr Robert ni mmoja wa
watu walioshiriki katika mpango
wa kumuua waziri Helmet Brian na
kwamba amekuwa akitumiwa na
Marekani katika mambo yao mbali
mbali hapa nchini nilistuka
sana.Nilikuwa naishi na nyoka
mwenye sumu kali.Uliponieleza
kuwa yuko nyumbani kwako
nikamtuma Meshack Jumbo atume
watu wake wakamuue.Niliamini
endapo ungemuhoji basi
angekueleza mambo mengi kuhusu
mimi kitu ambacho sikuwa tayari
kitokee.” Sura ya Mathew ikabadilika
baada ya maneno yale ya Dr Vivian
“You?! Akauliza kwa
hasira.Meshack na Dr Vivian
wakatazamana
“Mathew kaa chini endelea
kumsikiliza rais kwani ana mambo
mengi ya kukueleza” akasema
Meshack Jumbo
“Siamini kabisa.Kumbe na
wewe mzee umeshiriki katika
jambo hili?Ninakuamini sana mzee
wangu na siamini kama leo
umenitenda hivi!! Akasema
Mathew
“Mathew tafadhali kaa chini
bado kuna mengi nataka
nikueleze.Yale yote uliyotaka
kuyafahamu kutoka kwa Dr Robert utayapata hapa.Nitakueleza kila
kitu”akasema Dr Vivian na Mathew
akakaa chini lakini alikuwa
amekasirika mno
“Mathew naomba uelewe
kwamba si jambo jepesi kuamua
kufunguka mambo haya
kwako,mambo ambayo sikutaka
uyafahamu kabisa lakini kutokana
na umuhimu wako nimeamua
kufunguka kwako kila kitu na
ninakuomba hata kama utaumia
kiasi gani basi uvumilie hadi hapo
nitakapomaliza.” Akasema Dr
Vivian
“Sawa mheshimiwa rais”
akasema Mathew huku akitikisa
kichwa kuonyesha kushangazwa
kwake na maelezo yale ya rais “Baada ya kumuua Dr Robert
niliwasiliana na polisi na wakafika
nyumbani kwako mara moja na
ulipoofika tu ukatiwa
nguvuni.Lengo lilikuwa ni
kukuondoa katika uchunguzi
uliokuwa unaufanya ili usifike
mahala ambako sikutaka ufike”
“You wanted me to go to jail?!!
Akauliza Mathew kwa ukali
“Nilitaka kukuondoa
usiendelee na uchunguzi” akasema
Dr Vivian na Mathew akamtazama
kwa hasira
“Kwa haya yote
niliyokufanyia kwa nini
ukanifanyia haya mheshimiwa
rais? Jambo gani baya nilikufanyia
mheshimiwa rais hadi ukafikia hatua ya kufanya maamuzi
haya?Niliifanya kazi yako kwa
moyo na kwa kujituma lakini
kumbe nyuma yangu unapanga
kuniangamiza”akasema Mathew
“Mathew kama nilivyokueleza
kwamba jambo hili si rahisi
kwangu.Unadhani ni jambo rahisi
kukuita hapa na kukueleza haya
yote? Lakini nimeamua kuweka
kila kitu wazi kwako ili baada ya
kutoka hapa tuwe wote katika
ukurasa mmoja.Naomba uendelee
kuwa mvumilivu na usubiri hadi
nitakapomaliza kile nilichopanga
kukueleza.Tunaelewana Mathew?
“Ndiyo mheshimiwa rais”
akajibu Mathew. “Mzee Meshack
hakukubaliana na kile nilichotaka
kukifanya na akatumia akili yake
kuweza kukuondoa katika mikono
ya polisi.Aliponieleza kwamba
amekuchukua toka mikononi mwa
polisi tulishindwa kuelewana na
japo nilikuwa naongea kwa ukali
lakini kwa ndani nilikuwa na hofu
kubwa kwani tayari nimekwisha
kuogopa kwamba utafahamu
mambo yangu jambo ambalo
linaweza kuniweka katika
matatizo makubwa.Baadae
nikatafakari na kugundua kwamba
bado ninakuhitaji sana na ndiyo
maana nimekuita hapa na kuamua
kukueleza mambo haya yote” akanyamaza na kumtazama
Mathew halafu akaendelea
“Kubwa ambalo sikutaka
ulifahamu na ambalo niliamini
endapo ungemuhoji Dr Robert
angekueleza ni kuhusiana na
mahusiano yangu na kampuni ya
Tanbest Gemstone ltd.Tayari
unazo taarifa za mimi kuwa na
mahusiano na kampuni hii ya
Tanbest na nimejilaumu sana
kwani kitu ambacho nilikuwa
najitahidi kukizuia lakini hatimaye
umekifahamu hata hivyo nimeona
nikueleze kwa kina ili uweze
kuelewa kwani naamini taarifa
hiyo uliyoipata haijakamilika”
akanyamaza tena kwa muda wa
sekunde kadhaa halafu akaendelea “Ni kweli kampuni ya Tanbest
ni kampuni yangu”akanyamaza na
kumtazama Mathew,akaendelea
“Hii kampuni awali ilikuwa ya
rais Anorld Mubara ambayo
aliianzisha kabla hata ya kuwa rais
na baada ya kupata urais
alishindwa kuiendesha kutokana
na kutingwa na majukumu mengi
hivyo ikaanza kusua sua na kwa
kuwa alikuwa na mahusiano
mazuri na baba akamtaka
amuuzie.Baba hakuwa na fedha za
kuinunua kampuni hii hivyo
akawatafuta wenzake
wakaunganana ambao ni
marehemu George Mzabwa na
mwingine ni marehemu pia
anaitwa Isdory mteka.Walifanikiwa kuinunua
kampuni hii na kuanza kuiendesha
kwa pamoja lakini baadae
kukatokea mvurugano na chanzo
cha mvurugano huo ni George
Mzabwa.Baba hakuwahi kunieleza
chanzo cha mvurugano huo ila
anieleza kwamba kutokana na
ukorofi wake George Mzabwa
alipewa mgao wake na kuachana
na kampuni hiyo wakabaki baba
na Isdory wakiendeleza kampuni
hiyo.Kutokana na baba kutingwa
na shughuli nyingi alimuachia
Isdory aiongoze kampuni hiyo hadi
pale alipofariki kwa ajali ya gari na
baba akabaki mmiliki pekee.Kwa
mujibu wa baba,Isdory hakuwahi
kuwa na mtoto na mke wake alitangulia kufariki na kutokana
na urafiki mkubwa uliokuwepo
baina yao,kwa hiari yake aliamua
kuniandika mimi kama mrithi
wake.Baada ya kufariki
nikarithishwa hisa zote za Isdory
lakini kwa wakati huo bado
nilikuwa ninasoma hivyo baba
hakutaka kunishirikisha katika
biashara ila alinieleza kila kitu na
pale nilipomaliza masomo
alinitaka nirejee nyumbani
niendeshe kampuni yetu kwani
yeye alikuwa ametingwa na
majukumu mengi ya kikazi lakini
kwa wakati huo nilikuwa tayari na
kazi nyingine nje ya nchi hivyo
nikachagua kubaki
huko.Aliponusurika katika ajali ya ndege alinipigia simu na
kunifahamisha kwamba anataka
nirejee nyumbani kwani alikwisha
anza kuona hali ya usalama wake
si nzuri lakini nilipuuza hadi pale
alipofariki.Nilirejea nyumbani na
kuamua kubaki hapa ndipo
nilipoingia rasmi katika
kuiendesha kampuni hiyo”
akanyamaza kidogo akawatazama
Mathew na Meshack halafu
akaendelea
“Nilipoingia katika harakati za
kuwania urais ikanilazimu
kutafuta mtu ambaye
nitamkabidhi kampuni ile aweze
kuiendesha kwani kama mtumishi
wa umma sikutakiwa kuchanganya
biashara na kazi ndipo nilipoikabidhi kampuni kwa mtu
anaitwa Ranbir Kumar aweze
kuiendesha.Kuna kitu kimoja
katika kampuni hii ambacho
nilikikuta na ambacho hata mimi
niliendelea nacho.Ni kwamba
kampuni hii inachuma fedha
nyingi lakini hailipi kodi
serikalini” akatulia kidogo na
kuwatazama Mathew na Meshack
halafu akaendelea
“Kampuni hii ilikuwa ni ya
watu wakubwa kwa hiyo walifanya
mambo yao bila kulipa kodi
serikalini na mfumo huo hata mimi
nimeukuta na nikaurithi kwani
kiwango chakodi ambacho
wanapaswa kukilipa ni kikubwa
mno.Sikutaka jambo hili lifahamike kwani tuliokua
tunalifahamu ni watu watatu
tu.Mimi ,Dr Robert na Ranbir
Kumar.Ulifanikiwa kufahamu
kuhusu Ranbir Kumar na ukaanza
kumfuatilia ili kumuhoji
kuhusiana na kampuni ile na
aliogopa sana akanipigia simu
akanieleza kwamba unamfuatilia
na kama utakumbuka nilikupigia
simu na kukutaka uachane na kila
unachokifanya uje ikulu lakini
hukufanya hivyo na kwa kuwa
sikutaka umpate Ranbir nikatuma
vijana waliomuua Ranbir pamoja
na mke wa George Mzabwa
aliyekuwa anafanya kazi katika
kampuni hii.Usiku huo huo
nikaagiza ofisi za kampuni ya Tanbest zichomwe moto na
zikateketezwa.Sikutaka ufahamu
chochote.Nilikua na hofu kwamba
endapo ungefahamu siri hizi basi
ungeweza kuzianika kwa watu
wakazifahamu .Baada ya hapo
niliamini nimemaliza kazi na
sikuwa na wasiwasi kama
ungeweza kupata
chochote”Akanyamaza
akamtazama Mathew aliyekuwa
ameuma meno kwa hasira huku
sura yake ameikunja.
“Just relax Mathew.Nimeamua
kukueleza ukweli na siku zote
ukweli si mtamu.Vumilia kidogo
nimalizie” akasema Dr
Vivian.Meshack Jumbo alikuwa
kimya kabisa akisikiliza na mara kadhaa alionekana akifuta jasho
katika kipara chake
“Mahusiano ya kampuni hii na
Dr Robert yalianza pale
aliponifuata na kunieleza kwamba
kuna kampuni inaitwa Flamingo
na ambayo wanataka kufanya
biashara na kampuni
yangu.Nilimuachia Dr Robert na
Ranbir walishughulikie jambo hilo
kwa kuwa tayari mimi nilikuwa
rais na shughuli zote za uendeshaji
wa kampni ile nilimuachia Ranbir
Kumar.Walishughulikia suala hilo
na baadae wakanijulisha kwamba
wamekwisha malizana na kampuni
hiyo ya Flamingo na Dr Robert
akanieleza kwamba
nimefunguliwa akaunti maalum katika benki ya Escom ambayo
Flamingo watakuwa wananiwekea
fedha ambazo zitanisaidia katika
mamboyangu mbali mbali.Benki
hii ya Escom ina sifa ya kuficha
fedha chafu zisizolipiwa kodi na ni
kimbilio la matajiri na viongozi
mbalimbali ambao hawataki
utajiri wao ujulikane hivyo benki
hii ni kimbilio lao.Nilihakikishiwa
kwamba akaunti hiyo ni ya siri na
hakuna anayeweza
kuifahamu.Sijawahi kuchukua hata
senti moja katika akaunti hiyo na
sifahamu mpaka sasa kuna kiasi
lakini naamini kuna fedha nyingi
sana.” akanyamaza kidogo
akamtazama Mathew “Mathew naomba ufahamu
kwamba tunaokalia kiti hiki cha
urais si malaika ni wanadamu na
kila mwanadamu hakosi
mapungufu.Pamoja na mengi
mazuri ambayo nimeyafanya na
ninaendelea kuyafanya lakini hata
mimi si mkamilifu ninayo
mapungufu yangu na moja kati ya
mambo mabaya ambayo nakiri
nimeyafanya katika uongozi
wangu ni hili la kuwa na kampuni
isiyolipa kodi na kuwa na akaunti
ya siri yenye fedha nyingi
zisizotozwa kodi.Madini haya ni ya
watanzania na sikupaswa kufanya
hivi nilivyofanya” akanyamaza na
kumtazama Mathew “Mathew hayo ndiyo mambo
niliyotaka nikueleze”
Mathew akashusha pumzi na
baada ya muda akauliza
“Why are you telling me all
these madam president?
“Kwa sababu nataka twende
sawa.Katika uchunguzi wako
lazima ungekutana na haya
mambo kwa hiyo ni vyema endapo
nikakueleza mapema na kwa
mdomo wangu ili uyafahamu na
twende pamoja.Hii ni siri yangu
kubwa na ambayo ili kuificha
imegharimu uhai wa watu kadhaa
lakini nimeamua kukueleza kwani
naamini yote mliyoyasikia hapa
yatabaki katika vifua vyenu”
akasema Dr Vivian.Ukimya ukapita “Mathew say something !!
akasema Dr Vivian
“Sina cha kusema
mheshimiwa rais.Mambo haya
uliyonieleza ni makubwa lakini
mimi hayanihusu.Haya mambo
ulipaswa kuwaeleza watanzania na
si mimi.Kodi iliyokwepwa ni ya
watanzania kwa hiyo kama ni
kuwaomba msamaha unapaswa
kujitokeza mbele yao na
kuwaeleza kisha kuwaomba
msamaha.Lakini mheshimiwa rais
kwa nini ufanye hivi ulivyofanya?
Umekuwa kinara wa kupambana
na ukwepaji kodi na ufisadi lakini
kumbe na wewe pia ni mmoja wa
wakwepaji kodi wakubwa.Hii ni
kashfa kubwa sana kuwahi kutokea katika nchi yetu na
endapo wananchi watalifahamu
jambo hili sijui nini yatakuwa
maamuzi yao lakini tuachane na
hayo kwanza ninashukuru sana
kwa kuamua kuwa muwazi kwetu
na kutueleza mambo haya
mazito.Hayo mengine ya kodi na
nini mimi hayanihusu utajua
mwenyewe namna
utakavyoyamaliza.Hata hivyo kuna
mambo kadhaa nataka
kuyafahamu toka kwako na kwa
kuwa umeamua kunieleza ukweli
basi naamini utanieleza ukweli
wote” akasema Mathew na
kunyamaza akamtazama Dr Vivian
“Umeniambia kwamba George
Mzabwa aliwahi kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hii
akishirikiana na baba yako na
mzee Isdory na baadae
akatimuliwa lakini uchunguzi wetu
umegundua kwamba George
Mzabwa bado ana mashirikiano na
kampuni hii ya Tanbest.Kuna
fedha amekuwa anapokea kutoka
kampuni ya Flamingo na kiasi cha
mwisho kilichoingizwa katika
akaunti yake iliyopo katika benki
ya Escom ni shilingi milioni mia
saba na sabini.George alitoa fedha
hizo na kuziingiza katika akaunti
tatu tofauti katika benki hiyo hiyo
ya Escom.Akaunti hizo zote ni za
kampuni ya Tanbest gemstone
ltd.Akunti ya kwanza aliweka kiasi
cha shilingi milioni sabini na hizi zikatolewa na Ranbir
Kumar.Akaunti ya pili akaweka
kiasi cha shilingi milioni mia sita
na hamsini.Hizi zilitolewa na Dr
Robert na akaunti ya tatu aliweka
kiasi cha shilingi milioni hamsini
na hizi zikatolewa na Ranbir
Kumar.Kampuni hii ya Flamingo
na kampuni ya A.D Electronics
ambayo alikuwa anafanya kazi
Nathan zote ni kampuni zilizo chini
ya serikali ya Marekani kupitia
shirika lake la ujasusi CIA.George
alikuwa na mawasiliano na Nathan
na alikuwa katika mtandao wa CIA
na hii ni sababu kubwa
iliyomfanya ajiue,Dr Robert pia
alikuwemo katika mtandao wa CIA
kwani alishiriki katika mpango wa kumuua waziri Helmet
Brian.Flamingo ambayo ni
kampuni ya CIA wanapitishia fedha
katika benki ya Escom kupitia
kampuni yako ya Tanbest
Gemstone kwa ajili ya kufadhili
operesheni zao mbalimbali hapa
nchini Tanzania.Haya yote
hukuyafahamu? Akauliza Mathew
na sura ya Dr Vivian ilionyesha
mshangao mkubwa
Haya yote
hukuyafahamu? Akauliza Mathew
na sura ya Dr Vivian ilionyesha
mshangao mkubwa
“Mathew hayo mambo
unayonieleza ni mageni
kabisa.Kama nilivyokueleza
kwamba shughuli zote za
uendeshaji wa kampuni ya Tanbest
niliziacha kwa Ranbir Kumar
ambaye ndiye aliyekuwa
akiniletea taarifa za maendeleo ya kampuni na baadae Dr Robert
naye akaingia baada ya kuwaleta
Flamingo.Kuna kiasi fulani cha
fedha Dr Robert alikuwa anakipata
kila mauzo yanapofanyika lakini
hakuwa anahusika na chochote
katika mambo ya kifedha na
uendeshaji mzima wa
kampuni.George Mzabwa ni mtu
ambaye alikwisha ondolewa
zamani katika kampuni toka
wakati wa baba na hakuwa
anahusika na chochote, Nimestuka
sana kusikia kwamba watu hawa
wawili wanajihusisha na masuala
ya fedha za kampuni
yangu.Kwanza kampuni ina
akaunti moja tu na si tatu kama
unavyodai.Nitakupa namba za akaunti hiyo ya kampuni
uichunguze ili uamini
ninachokwambia.Kama kuna
akaunti nyingine zimefunguliwa
basi zimefunguliwa bila ya mimi
kufahamu.Inawezekana
walinizunguka wakaamua
kufungua akaunti hizo kwa jina la
kampuni ya Tanbest kwa ajili ya
mambo yao wenyewe” akasema Dr
Vivian
“Maelezo yako mheshimiw
arais yananifanya niamini kwamba
kulikuwa na mashirikiano baina ya
George Mzabwa ,Dr Robert na
Flamingo na walitumia kampuni
yako kwa ajili ya kupitishia fedha
zao chafu.Kingine ambacho
unapaswa ukifahamu ni kwamba benki hii ya Escom inamilikiwa na
Anderw Pillar au Edwin
Washington ambaye ndiye mmiliki
wa kampuni za Flamingo na A.D
Electronics.Huyu amewekwa kama
mmiliki wa kampuni hizi lakini
ukweli ni kwamba ziko chini ya
CIA na walimtumia Dr Robert
ambaye ni mtu wao
wakakufunguliwa akaunti katika
benki yao na kukuwekea fedha
ambazo hazikatwi kodi na huu
unaonekana ulikuwa ni mtego wa
CIA na wewe ukaingia kichwa
kichwa bila kujua na sasa wanazo
taarifa zako na wanaweza
wakazitumia katika mapambano
haya yanayoendelea hivi sasa
kukuchafua kwamba nawe ni mmoja wa marais wakwepa kodi
duniani” akasema Mathew
“Oh my God !! akasema Dr
Vivian na kushika kichwa chake
“How could I be so stupid ?!!
Huu ulikuwa ni mtego na
nikaingia bila kujua.Dr Robert set
me up.Nilimuamini sana Dr Robert
kwa nini akanitenda hivi?Kwa nini
sikuliona hili hapo kabla?
“Watu hawa” akasema
Meshack Jumbo ambaye muda
mwingi alikuwa kimya akisikiliza
“ Walifahamu kwamba siku
moja watamuhitaji Dr Vivian
kuwafanyia jambo fulani,hivyo
wakatafuta kitu ambacho
wanaweza wakakitumia kumfanya
Dr Vivian akubali kufanya kile watakachomtaka awafanyie kwa
kutishia kuvujisha taarifa zake za
kumiliki akaunti ya siri yenye
fedha zisizokatwa.Lakini na wewe
mheshmiwa rais kwa nini
ukakubali kwanza kuendesha
kampuni isiyolipa kodi na pili
kufunguliwa akaunti ya siri na
kuwekewa fedha nyingi ambazo
hazilipiwi kodi?.Hukujua kama
hawa jamaa siku moja wanaweza
wakatumia jambo hili kama fimbo
ya kukuchapia? Unadhani ni kitu
gani kitatokea endapo watanzania
wanaokuamini watagundua
kwamba rais wao wanayempenda
ni mmoja wa mafisadi na wakwepa
kodi? Huu utakua ni mwisho wako
Dr Vivian na hawa maadui zako hawatakuacha
salama.Watakuchapa kwa kila
fimbo waliyonayo hadi
wahakikishe hauwi kikwazo
kwao.Watakupeleka wanavyotaka
wao.Hautakuwa na kauli tena
kwao.Haya yote hukuyafahamu
Madam President? Akauliza
Meshack Jumbo
“Niliambiwa kwamba marais
wengi wanahifadhi fedha zao kwa
siri katika benki ya Escom na
ambazo zimekuwa zinawasaidia
kuishi maisha mazuri pale
wanapokuwa wamemaliza kipindi
chao cha uongozi.Niliona ni wazo
zuri nikakubali niwe na akaunti ya
siri.Sikufanya uchunguzi kubaini
kama siku moja suala hili
lingeweza kunigeukia.Sikuwahi
kusikia hata siku moja taarifa za
rais kuficha fedha katika benki ya
Escom zimevuja.Niliamini hata
mimi siri hii haiwezi kuvuja na
ndiyo maana nikatumia nguvu
yangu kulinda siri hii
isijulikane.Ninajiamini katika
maamuzi yangu mbali mbali
ninayoyafanya na mara nyingi
nimekuwa sahihi lakini katika hili
nakiri nilikosea.I was so
stupid.Sikupaswa kufanya hivi
nilivyofanya”akasema Dr Vivian na
kuinamisha kichwa.
“Hii ni kashfa kubwa kuwahi
kumpata rais wetu.Toka enzi za
baba wa taifa kumepita marais
kadhaa lakini hawajawahi kukumbwa na kashfa kubwa kama
hii”akasema Mathew.Ukimya
mfupi ukapita na Meshack Jumbo
akakuna kipara chake na kusema
“Dr Vivina naomba utuambie
ukweli,hujawahi kuchukua hata
senti moja katika fedha hizo
ambazo unawekewa katika akauni
ya siri?
“Hapana Meshack sijawahi
kugusa fedha hizo na wala sijui
ziko kiasi gani na wala sijawahi
kuweka fedhayangu huko bali
fedha zote ninawekewa na
kampuni ya Flamingo wakidai ni
ahsante yao kwangu kwa kufanya
nao biashara kwani madini yote
yanayochakatwa katika kampuni
ya Tanbest wanauziwa wao” akajibu Dr Vivian na Meshack
akamtazama kwa makini kwa
muda na kusema
“Sijafanya nawe kazi kwa
muda mrefu,lakini kwa muda huu
mfupi niliokuwa karibu nawe
nimegundua wewe ni mtu mkweli
japo katika hili jambo uliteleza
lakini hatuwezi kukuacha hivi
hivi.Mimi kama mkuu wako wa
idara ya usalama wa taifa siwezi
kukubali kuona kashfa hii
inaibuliwa na kukushusha
chini.Mathew rais wetu
amekwama na ni wajibu wetu
kumkwamua.Hii ni kashfa kubwa
sana endapo Marekani wataamua
kuitumia dhidi ya rais wetu.We
need to do something to get her out of this.Hili si suala lake tena.Ni
suala letu sote.Huyu ni kiongozi
wetu katika mapambano haya
yanayoendelea kwa hiyo haijalishi
amekosea au hajakosea lakini
lazima tupambane tuhakikishe
kwamba tunamtoa katika hili
suala” akasema Meshack Jumbo na
Mathew akawa kimya
“C’mon Mathew think fast.You
need to come up with something !!
akasema Meshack Jumbo
“Ndugu zangu kama kuna
namna yoyote ile mnayoweza
kunisaidia kunitoa katika janga
hili ninaomba mnisaidie kwani
sijui nitafanya nini endapo
Marekani wataamua kutumia
jambo hili kama fimbo ya
kunichapia.Sikujua kama benki ile
nayo ina mahusiano na CIA.Please
help me.Mathew najua
nimekukosea sana lakini naomba
kwa sasa tuyaweke hayo yote
pembeni na unisaidie katika
hili.Kama kuna namna yoyote
unaweza kufanya tafadhali
nisaidie.Ninaamini uwezo wako na
ninaamini unaweza kabisa
kunisadia kulimaliza hili
jambo.Please help me” akasema Dr
Vivian na Mathew akainama
akafikiri kwa muda na kusema
“Ok.Niachie suala hili nitaona
namna ya kufanya.Nitajitahidi
kadiri ya uwezo wangu lakini
siwezi kukupa uhakika wa moja
kwa moja kwamba ninaweza kulimaliza ila nitajitahidi”
akasema Mathew
“Mathew ahsante sana.Laiti
ungeuona moyo wangu namna
unavyoshukuru….”
“Pamoja na hayo” akaendelea
Mathew
“ Bado kuna mambo ambayo
nahitaji kuyafahamu kutoka
kwako “
“Kabla ya hapo kuna jambo
ambalo ninataka niwafahamishe.”
Akasema Dr Vivian
“Nilizungumza na Helmet
Brian.Huyu ni mtu mwenye nguvu
sana ndani ya chama chake na
alipaswa kuwa rais wa Marekani
lakini kwa urafiki mkubwa uliopo
kati yake na Mike Straw aliamua kujitoa katika harakati za kuwania
urais akamuachia Mike.Helmet
amechukizwa mno na kitendo cha
Mike straw kuandaa mpango wa
kumuua na yuko tayari kuanzisha
vuguvugu la kumuondoa
madarakani Mike straw lakini ni
pale tu ambapo ushahidi wa
kutosha utapatikana
ukimuhusisha Mike straw katika
mpango wa kumuua Helmet.Kwa
kuwa Helmet ana nguvu sana
katika chama chake akifanikiwa
kumuondoa Mike straw na
makamu wake wa rais madarakani
atapendekezwa yeye kushika
nafasi hiyo ya urais kwa muda na
kwa kushirikiana naye tutaweza
kuuzima mgogoro mkubwa unaofukuta hivi sasa baina ya
mataifa yenye kumiliki silaha
nzito.Kwa hiyo basi ninataka
Mathew uwahoji wale watu ambao
walitumwa kuja kumuua
Helmet.Jitahidi kwa kila uwezavyo
kuweza kupata taarifa muhimu
kutoka kwao.Meshack Jumbo
atakuwezesha kwa kila kitu katika
kufanikisha hili jambo”akasema Dr
Vivian
“Ahsante mheshimiwa rais
kwa kunikabidhi jukumu hilo na
ninakuahidi nitafanya kila
linalowezekana hadi nipate
ushahidi huo usiona hata chembe
ya shaka” akasema Mathew
“Ahsante sana.Meshack mpe
Mathew msaada wowote
atakouhitaji katika kulifanikisha
hilo jambo muhimu”akasema rais
“Sawa mheshimiwa
rais.Atapata kila aina ya
ushirikiano anaohitaji”
“Good”akasema Dr Vivian
“Mathew nilikukatisha kuna
jambo ulitaka kuuliza”
“Mheshimiwa rais bado kuna
jambo moja ambalo nahitaji
kulifahamu toka kwako kabla
sijaondoka hapa usiku huu”
akasema Mathew
“Jambo gani Mathew?
“CIA wamekuwa
wanakufuatilia kwa muda
mrefu.Toka angali unasoma chuo
kikuu nchini Marekani
walimpandikiza Nathan ambaye alikuwa na kazi ya kukuchunguza
na ambaye baadae mkawa wapenzi
na mlikaribia hata kufunga
ndoa.Baada ya Nathan wakamtuma
tena Tausi ambaye jina lake halisi
ni Olivia Howard.Wote hawa
walikuwa na kazi moja tu ya
kukuchunguza na kuhakikisha
wanapata taarifa zako
mbalimbali.Nimejiuliza maswali
mengi kuhusiana na CIA kutumia
muda mrefu kukufuatilia.Kuna
jambo lolote ambalo
wanalichunguza toka kwako?Kuna
siri yoyote ambayo unayo na
wanataka kuifahamu? Kama kuna
chochote unakifahamu kuhusiana
na hili mheshimiwa rais ni bora
ukaweka wazi kwetu ili kwa pamoja tuweze kujua namna ya
kukusaidia kwani hatujui mpaka
sasa CIA ni taarifa gani
wamekwisha zipata kwani
wamekuchunguza kwa muda
mrefu sana” akasema Mathew
“Anachokisema Mathew ni
sahihi mheshimiwa rais kama
kuna jambo ambalo unadhani
tunapaswa kulifahamu tafadhali
tueleze angali bado mapema.Sisi ni
washirika wako na
tutakulinda.Tutaichukua siri yako
katika vifua vyetu kwa maisha yetu
yote” akasema Meshack
Jumbo.Baada ya tafakari fupi Dr
Vivian akasema
“Naomba jambo hili
tulizungumze siku nyingine.Kwa usiku huu haya tuliyoyazungumza
yanatosha.Tushughulikieni
kwanza haya mambo
tuliyoyaongea usiku wa leo”
akasema Dr Vivian
“Sawa mheshimiwa
rais,tunakwenda kuanza kazi hiyo
sasa hivi” akasema Meshack
Jumbo.Wakainuka na kuagana na
kuanza kuondoka.Baada ya kama
hatua tano hivi Dr Vivian akamuita
Mathew
“Naam mheshimiwa rais”
akaitika Mathew kwa adabu na
kurejea mahala alipokuwa amekaa
rais
“Thank you so much for
today.Umefanya kazi kubwa sana
na unastahili pongezi.Sahau yale yote yaliyopita na tuanze ukurasa
mpya.Wewe ni mtu muhimu sana
kwangu.Nipigie simu muda
wowote ule uutakao” akasema Dr
Vivian.Mathew akatabasamu na
kusema
“Ahsante sana mheshimiwa
rais kwa heshima hii kubwa”
akasema Mathew na
kuondoka.Wakaingia katika gari la
Mathew na kuondoka.Safari
haikuwa na maongezi.Meshack
Jumbo akagundua kitu
“Mathew I’m sorry.” Akasema
“Umenisikitisha sana mzee
Jumbo.How can you do this to me?
Kwa nini hukunieleza kama
ulituma watu wakamuue Dr Robert mpaka ukaniacha nikaingia katika
matatizo?
“Mathew I’m sorry.I was just
following orders” akajibu mzee
Meshack
“Hata kama ulitumwa kufanya
hivyo ulipaswa kuniambia mzee
Jumbo.Wewe ni mtu ambae
ninakuamini sana na sikutegemea
kama unaweza kunificha jambo
kubwa kama hili na kuniacha
nikaingia katik amikono ya
polisi.Tulianza pamoja operesheni
hii lakini umeanza
kunigeuka.Yawezekana hata kama
kungekuwa na mpango wa kuniua
ungenificha!!
“Kwa nini unadiriki kusema
hivyo Mathew wakati unafahamu kabisa kwamba siwezi kufanya
hivyo?Mathew wewe ni kama
mwanangu.Jambo hili lilikuwa nje
ya uwezo wangu.Ilikuwa ni amri ya
rais ambayo nisingeweza
kuipinga.Unafahamu ni mambo
gani niliyokumbana nayo katika
suala hili hadi ukawa
huru?Nimepata misuko suko
mikubwa toka kwa rais kwa
sababu sikumuunga mkono katika
kitendo chake cha kutaka
kukuangushia mzigo ule mkubwa
wa kesi ya mauaji lakini
nimesimama imara na
kuhakikisha unakuwa
huru.Mambo haya yanatokea sana
katika hizi kazi na hata wewe
unafahamu Mathew.Nakubali nilifanya kosa na ninaomba
samahani”
“Jambo gani lingine
unalifahamu ulilotumwa na rais
ulifanye ambalo
hujanieleza?akauliza Mathew
“Hakuna jambo lingine”
“Are you sure?
“Yes I’m sure”
“Good.If we want to suceed in
this mission we need to trust each
other”
“You have to trust me
Mathew” akasema Meshack na
safari ikaendelea
“ Tunaanzia wapi? Akauliza
Meshack Jumbo
“Tunaanza kwanza
kulishughulikia suala la ile akaunti ya Dr Vivian.” Akasema Mathew na
kunyamaza kwa muda na kusema.
“Kwa nini lakini akafanya
vile? Hakujua kama siku moja
jambo hili lingefahamika?
“CIA walitumia mbinu kubwa
ya kumtumia mtu wa karibu na Dr
Vivian ili kulifanikisha
hilo.Tunapaswa kulishughulikia
suala hili kwa haraka zaidi ili
wasije wakalitumia kutaka
kumshinikiza aweze kufanya
wanavyotaka wao”akasema
Meshack
“Suala hili litamalizika
usihofu.Hata hivyo ninashukuru
kwa Dr Vivian kuamua kuwa
muwazi kuhusiana na mambo
yake.Kama angefunguka kuanzia mapema tayari tungekwisha
maliza haya mambo muda mrefu”
akasema Mathew
Walifika nyumbani kwa
Austin na kukuta shughuli ya
udukuzi inaendelea
“Kuna chochote mmekipata
hadi sasa? Akauliza
“Kuna jambo
tumeligundua.Pesa ambazo Dr
Robert alizitoa katika akaunti ya
kampuni ya Tanbest aliweka kiasi
cha shilingi milioni mia moja na
ishirini katika akaunti nyingine ya
siri iliyopo kwenye benki ya
Escom na baada ya kuichunguza
akaunti hiyo tumegundua kwamba
akaunti hiyo ni ya John Aminiel Mkoka mkuu wa jeshi la polisi
nchini.”
“IGP? Akauliza Mathew
“Ndiyo Mathew.”akajibu
Austin
“Hii ni hatari.Hata mkuu wa
jeshi la polisi naye yumo katika
mtandao huu?akasema Mathew na
kunyamaza kidogo halafu akasema
“Sasa nimepata jibu
kuhusiana na wale watu
waliokuwa wanavamia wakiwa na
sare na magari ya polisi.Huyu
mkuu wa jeshi la polisi anayo
majibu.Good job guys” akasema na
kuchukua simu yake akampigia
rais
“Hallow Mathew” akasema Dr
Vivian “Mheshimiwa rais kuna jambo
tumeligundua katika uchunguzi
wetu.Tumegundua kwamba mkuu
wa jeshi la polisi nchini Inspekta
jenerali John Aminiel Mkoka naye
ni mmoja wa watu waliomo katika
mtandao wa CIA.Ninaomba haraka
sana atiwe nguvuni ili tumfanyie
mahojiano” akasema Mathew na
Dr Vivian akavuta pumzi ndefu
“Mathew hili si suala
jepesi.Una uhakika nalo ?
“Yes I’m sure madam
president” akasema Mathew
“Ok sawa.Nitamuweka katika
kizuizi cha nyumbani kwake hadi
hapo mtakapomfanyia
mahojiano.Huyu ni mtu mkubwa
na hatuwezi kumuweka nguvuni bila kuwa na uhakika wa kutosha
wa tuhuma zinazomkabili.”
“Ahsante mheshimiwa rais”
“Mathew” akaita Dr Vivian
“Umeanza kulishughulikia lile
suala? Akauliza
“Ninalishughulikia
mheshimiwa rais”
“It is getting ugly please do it
fast”
“I’m on it madam
president”akajibu Mathew
“Thank you” akasema Dr
Vivian na kukata simu
“Jamani usiku wa leo hakuna
kufumba ukope kwani kuna
mambo makubwa ambayo
tunapaswa kuyakamilisha kabla hakujapambazuka” akasema
Mathew
“Mimi na Mzee Jumbo
tumetoka ikulu tulikuwa na
mazungumzo mazito na
mheshimiwa rais”
Mathew akawaeleza
kuhusiana na mazungumzo yao na
rais,kila mmoja akabaki na
mshangao
“Mshangao huo mlioupata
ndio huo hata mimi na mzee
Meshack tuliupata alipotueleza
mambo haya.Hata hivyo hatupaswi
kuendelea kushangaa.Tunapaswa
kumuondoa rais katika hili janga
kwani aliwekewa mtego na
akaingia kichwa kichwa bila
kupima athari zake” “Do you trust her? Akauliza
Peniela
“Yes I do” akajibu Mathew
“Mathew hili ni suala
kubwa.Ukwepaji wa kodi ni jambo
ambalo Dr Vivian amekuwa
akipambana nalo toka ameingia
madarakani lakini kumbe na yeye
mwenyewe ni mkwepaji mkubwa
wa kodi.Mathew hili suala
linapaswa kwenda kwa wananchi
walifahamu,wamfahamu rais wao
ni mtu wa namna gani.Mimi siwezi
kuwa sehemu ya kumsafisha mtu
kama huyu.Huu ni uhalifu mkubwa
na anapaswa awajibike kwa
uhalifu wake huu mkubwa!!
Akasema Austin kwa hasira “Austin naomba unielewe.Ni
kweli rais alikosea na amekiri
kwamba alikosea lakini ufahamu
kwamba hii ni vita na hawa jamaa
walifahamu kwamba itafika siku
ambayo watamtaka Dr Vivian
afanye watakavyo kwa kuwa
wanazifahamu siri zake na Dr
Vivian kwa kuogopa siri zake
kuvuja na hata kushtakiwa
angefanya kama ambavyo
wangemtaka afanye.Hajawahi
kugusa hata senti moja katika
akaunti hiyo na wala hajui kuna
shilingi ngapi mpaka sasa.Pamoja
na hayo yote aliyoyafanya lakini
tunapaswa tumsaidie.Hii si vita
yake sasa ni vita yetu
sote.Hatuwezi kuwaaacha Marekani wakashinda vita hii
kwani rais wetu akiwa mtumwa
wao na kufanya kila wakitakacho
watakaoumia si Dr Vivian bali ni
wananchi ambao rasilimali zao
zinanyonywa.Hivyo basi kumsaidia
Dr Vivian ni kuisaidia nchi
pia.Hakuna kati yetu aliye
mkamilifu kwa hiyo hata Dr Vivian
naye si mkamilifu,ana mapungufu
pia hivyo kama amekosea
tumrekebishe na makosa
aliyoyatenda yasijirudie tena
lakini kwa sasa mategemeo yake
yote yako kwetu.We have to help
her” akasema Mathew
“Mathew kama nilivyosema
kwamba siwezi kuwa sehemu ya
ujinga huu wa kumsafisha rais anayekwepa kodi.Unafahamu ni
kiasi gani cha kodi ninalipa kila
mwaka serikalini halafu mtu
mkubwa kama rais anakwepa
kodi?Hili halivumiliki lazima
afikishwe katika vyombo husika na
hatua stahiki zichukuliwe dhidi
yake.Amarachi twende tuondoke
zetu hatuwezi kuwa sehemu ya
ujinga huu unaotaka
kufanywa.Huu ni uhalifu
mkubwa.Let’s go!! Akasema Austin
kwa hasira huku akimshika mkono
mke wake Amarachi na kumvuta
waondoke
“No Austin! Akasema
Amarachi na kumfanya Austin
amtazame kwa hasira. “Siendi kokote.Mathew
ameeleza wazi kuhusu suala hili ni
suala letu pia.Tunatakaiwa
tupambane tuhakikishe
tunamuondoa rais katika janga
hili.I’m staying with them”
akasema Amarachi na kwa hasira
Austin akataka kumnasa kibao
lakini ghafla Camilla akageuka na
kumpa Austin pigo moja kali
lililompeleka chini.Wakati
akishangaa nini kilichotokea
akapewa tena pigo lingine na
Camilla akamfuata pale chini
akiwa na waya mkononi
akamfunga mikono.
“Samahani” akasema na
kwenda kukaa.Wote mle ndani wakabaki wameduwaa kwa wepesi
ule wa Camilla
“Peniela tupe chumba
tafadhali.We need to lock him
up.Hatuwezi kushindwa kufanya
kazi zetu kwa sababu yake”
akasema Mathew na kuchukua
waya mwingine akamfunga miguu
na kisha akamvuta na kwenda
kumfungia katika chumba
alichoelekeza Peniela
“I’m sorry Austin.Haya yote
umeyataka mwenyewe” akasema
Mathew na kutoka akaufunga
mlango akimuacha Austin akipiga
kelele
“Naomba niweke wazi ndugu
zangu kwamba jambo hili si jepesi
hata kidogo lakini lazima tulifanye ili kumlinda rais wetu kwani
aliingia katika mtego bila ya yeye
kufahamu.Marekani watalitumia
jambo hili ili kumlizimisha Dr
Vivian afanye watakavyo wao na
tukiruhusu hilo litokee ni jambo
baya sana kwa nchi
yetu.Watachota rasilimali zetu
watakavyo kwani Dr Vivian
hataweza kuwazuia kwa kuogopa
siri yake hii isijulikane.We have to
take her out of this in anyway we
can.It’s not right but we have to do
it.Kama kuna yeyote ambaye
hajisikii kuendelea na sisi aweke
wazi msimamo wake” akasema
Mathew na wote wakawa kimya.
“Good.Wote tuko pamoja”
akasema “Mathew tumekwishakuelewa
hivyo tupe kazi yakufanya kwani
muda unakwenda kwa kasi”
akasema Peniela
“Peniela wewe utatusaidia
sana kuhusu suala hili.Wewe ni
mmoja wa wamiliki wa benki hii ya
Escom tafadhali tupe namna bora
ya kufanya.Tutawezaje kuzitoa zile
fedha zote zilizomo katika akaunti
ya Dr Vivian? Tutawezaje kuifunga
hiyo akaunti? Akauliza Mathew
Peniela akafikiri kidogo na
kusema
“Akaunti hii ni ya siri kwa hiyo
taratibu zake huwa ngumu vile
vile.Hata hivyo bado tunaweza
kufanya hivyo ulivyoshauri yaani
kuhamisha fedha kutoka katika akaunti hiyo na kuifunga
kabisa.Tunachoweza kukifanya ni
kuzihamishia fedha hizo katika
akaunti yangu na halafu tutaifuta
kabisa hiyo akaunti ya Dr Vivian”
“Thank you so much
Peniela.Utasaidiana na Camilla
yeye ni mtaalamu sana wa
kompyuta na ni mbobezi katika
masuala ya udukuzi kwa hiyo
utakuwa naye mkisaidiana.Mimi
na Meshack Jumbo tuna kazi
kubwa ya kwenda kuwafanyia
mahojiano wale watu waliotumwa
kuja kumuua Helmet
Brian.Mtakapomaliza
tutawasiliana tuwajulishe na sisi
kitu tutakachokuwa tumefanikiwa
kukipata”akasema Mathew “Mathew I’m coming with you”
akasema Amarachi
“Amarachi utabaki hapa na
akina Peniela”
“Hapana Mathew ninakwenda
nanyi.Huwezi kwenda huko peke
yako” akasema Amarachi na
Mathew hakutaka kumkatalia
wakaongozana hadi garini
wakaondoka
“’I’m sorry about your
husband” akasema Mathew
wakiwa garini
“You don’t have
to.Alichokifaya ni kitu cha kijinga
sana na anastahili adhabu ile.Hili
ni suala la kitaifa na kama
tusipounganisha nguvu
tutashindwa hii vita” akasema Amarachi.Baada ya muda Mathew
akauliza
“Amarachi unajua kutumia
silaha? Akauliza Mathew
“Austin hajawahi kukueleza
chochote kuhusu mimi? Akauliza
Amarachi
“Hapana hajawahi kunieleza
chochote. Ni muda mrefu umepita
hatujaonana hadi leo hii”
“Ninajua kutumia silaha”
akasema Amarachi na kuwaeleza
Mathew na Meshack Jumbo kwa
ufupi kuhusu maisha yake namna
alivyotekwa na kuishi msituni na
kikundi cha kigaidi cha Boko
Haram.Mathew alishangaa sana
kusikia historia ile ya maisha ya
Amarachi “Pole sana Amarachi kwa
maisha haya uliyopitia” akasema
Mathew
“Imebaki ni historia.Nina
furaha na maisha yangu ya
sasa”akasema Amarachi.Wakiwa
njiani Mathew akapigiwa simu na
Dr Vivian
“Mheshimiwa rais” akasema
Mathew baada ya kupokea simu
“How is it going?akauliza Dr
Vivian
“Tayari tumeanza
kulishughulikia lile suala na hivi
sasa tunaelekea katika mahojiano
na wale wauaji”
“Mathew nimekupigia
kukujulisha kwamba tayari mkuu
wa jeshi la polisi nchini Inspekta jenerali John Aminiel Mkoka
amewekwa kizuizini nyumbani
kwake hadi hapo mtakapomfanyia
mahojiano.Jitahidi kila kitu
kimalizike usiku wa leo” akasema
Dr Vivian
“Nitajitahidi mheshimiwa
rais” akasema Mathew na kukata
simu
“Tayari Inspekta jenerali John
Mkoka amewekwa katika kizuizi
cha nyumbani” Mathew
akamwambia Meshack Jumbo
“ Good.Mtandao wote wa
Marekani hapa nchini lazima
ujulikane leo” akasema Meshack.
Mathew,Meshack Jumbo na
Amarachi waliwasili katika
nyumba ambayo watu watatu
walioletwa nchini kwa kazi moja tu
ya kumuua Helmet Brian walikuwa
wamehifadhiwa.Hii ilikua ni
nyumba maalum ambayo idara ya
usalam wa taifa walikuwa
wakiitumia kuwafanyia watu
mahojiano.Kulikuwa na sehemu
zaidi ya nane za mahojiano
kutegemea na aina ya mtu na
taarifa ambayo wanaihitaji.
Kutokana na umuhimu
wao,Meshack Jumbo alielekeza
watu wale wafanyiwe mahojiano katika chumba kilichopo chini ya
ardhi.
“Watahojiwa mmoja mmoja”
akasema Mathew na bila kupoteza
muda mtu wa kwanza akaingizwa
ndaniya kile chumba.Alikuwa
amefunikwa mfuko kichwani
akaketishwa katika kiti maalum
kilichombana miguu na mikono
halafu mfuko ule ukatolewa
kichwani.Mathew aliyekuwa
amesimama nje ya kile chumba
akamtazama kupitia kioo kikubwa
kilichowawezesha waliokuwa nje
kuona ndani halafu akachukua
karatasi iliyokuwa na picha za
wale jamaa akaitazama kwa muda
na kusema. “It’s time” akasema na
kuufungua mlango akaingia ndani.
WASHINGTON DC- MAREKANI
Willy Gadner mkurugenzi wa
shirika la ujasusi la Marekani
aliwasili katika ikulu ya
Marekani.Tayari ni saa mbili za
usiku kwa saa za Marekani.Rais
Mike straw akataarifiwa kuwa
Willy gadner amefika na wakaenda
katika chumba cha mazungumzo.
“Natumai umekuja na taarifa
zote kuhusiana na mtoto wa Dr
Vivian” akasema Mike straw
“Ndiyo mheshimiwa
rais.Taarifa zote ziko humu”
akasema Willy na kumkabidhi rais Mike straw faili lenye taarifa zote
za Florentina mtoto wa Dr
Vivian.Mike akalifungua na kuanza
kupitia nyaraka zilizokuwemo
ndani yake.
“Ni mrembo sana huyu binti”
akasema Mike na kulifunga lile
faili
“Ahsante sana Willy.Saa nne
kamili nitaanza safari ya kuelekea
Tanzania.Ni safari
itakayonichukua saa kumi na mbili
hadi kumi na tatu na ninategemea
kesho jioni niwe nchini
Tanzania.Ninataka nikalimalize
suala hili mimi mwenyewe”
akasema Mike
“Mheshimiwa rais una hakika
unataka kufanya hivi? “Ndiyo Willy.Ninataka kwenda
kuweka mambo sawa.Ninafahamu
athari za Helmet kuendelea kukaa
Tanzania na ndiyo maana ninataka
kufanya kila niwezalo kuhakikisha
ninamrejesha nyumbani”
“Mheshimiwa rais kitendo cha
kumfuata rais Dr Vivian nchini
kwake ni wazi kitaonyesha
kwamba tayari umeshindwa na
ndiyo maana ukaamua kwenda
mwenyewe kumshawishi.Huu ni
udhaifu mkubwa sana
mheshimiwa rais.Kwa mtazamo
wangu ninaona kama vile tunampa
ushindi Dr Vivian katika hii vita”
“Wengi watafikiri hivyo
kwamba niko dhaifu na hadi
nikaamua kumfuata Dr Vivian Tanzania lakini ukweli ni kwamba
baada ya mpango ule wa kumuua
Helmet kushindwa kufanikiwa
tumeharibu kila kitu na hakuna
mwingine anayeweza kuliweka
sawa hili jambo zaidi yangu.Ni
ziara itakayowastua wengi na
wengi watajiuliza kwa nini
nimeamua kwenda mwenyewe
Tanzania ila ukweli wote
ninaufahamu mimi.Bila kufanya
hivyo sote tutakwenda na
maji.Ninamfahamu vyema Helmet
ni mtu mwenye nguvu hapa
Marekani kwa hiyo lazima niende
Tanzania kusawazisha mambo”
Akasema Mike
“Sawa mheshimiwa
rais.Tayari umekwisha mtaarifu rais wa Tanzania kwamba
unakwenda?
“Sina mpango wa
kumjulisha.Nataka nimjulishe
wakati niko juu ya anga la
Tanzania”
“Hapana mheshimiwa rais hilo
si wazo zuri.Ni vyema endapo
utamjulisha kuwa unakwenda
kuonana naye ili taratibu zianze
kuchukuliwa”
“Wasiwasi wangu ni kwamba
anaweza akagoma nisiende nchini
kwake na ndiyo maana ninataka
nimfahamishe wakati tayari niko
juu ya anga la Tanzania.”
Willy Gadner akatoa faili
katika mkoba wake na kumpatia
Mike straw “Hiki nini Mike?
“Hiyo ni taarifa nyingine
inayomuhusu Dr Vivian ambayo
inaweza kutusaidia katikampango
wako.Dr Vivian ana akaunti ya siri
katika benki ya Escom yenye fedha
nyingi ambazo hazilipiwi
kodi.Hatakubali taarifa hii
ikawafikia wananchi wake kuwa
naye ni mkwepaji wa kodi hivyo
naamini akiliona faili hili atakubali
kufanya kila utakachomuelekeza
bila hata kumtumia mtoto wake”
akasema Willy Gadner.Mike
akalipitia lile faili na kutabasamu
“Ahsnate sana Willy.Hili ni
jambo kubwa sana
mmelifanya.Nina uhakika wa
kurejea hapa Marekani na Helmet Brian na wale watu wetu
waliopotea”akasema Mike straw
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Ni saa kumi na moja za alfajiri
Mathew akishirikiana na Meshack
Jumbo na Amarachi
walipokamilisha zoezi la kuwahoji
watu waliotumwa kuja nchini
kumuua waziri wa mambo ya nje
wa Marekani Helmet
Brian.Haikuwa kazi rahisi lakini
walifanikiwa kupata taarifa
muhimu walizokuwa
wakizihitaji.Wakati wa kuitekeleza
kazi ile ilimlazimu Mathew kuzima
simu yake na baada ya kumaliza
zoezi akaiwasha na kukutana na taarifa ya namba kadhaa
zilizomtafuta.Miongoni mwa
namna hizo ilikuwa namba ya simu
ya rais pia namba ya simu ya
Peniela.Simu ya kwanza kupiga
ilikuwa ni simu ya Peniela
“Hallow Peniela” akasema
Mathew baada ya Peniela kupokea
simu
“Mathew ! Umetupa wasiwasi
mkubwa sana kila mara tulipopiga
simu yako haikuwa
ikipatikana.Uko salama?
“Samahani sana kwa
kuwaweka roho juu lakini niko
salama kabisa.Nililazimika
kuizima simu kutokana na
shughuli nzito iliyokuwepo hapa
lakini nashukuru tumemaliza na tumefanikiwa kupata taarifa
muhimu tulizokuwa
tunazihitaji.Vipi kwa upande wenu
mmefikia wapi kuhusu lile zoezi?
“Sisi pia tumelimaliza.Haikua
kazi nyepesi lakini namshukuru
Camilla ana utalaamu wa ajabu
sana wa kompyuta na ndiye
aliyesaidia kwa kiasi kikubwa
tukafanikisha lile zoezi.Ilinilazimu
kumshirikisha pia mtu wangu kule
Ufaransa anaitwa Lydie ambaye
naye kuna watu aliwashirikisha
katika hii kazi lakini
tumefanikiwa.Akaunti ilikuwa na
fedha jumla ya shilingi trilioni tatu
na bilioni mia sita.Fedha hizi zote
zimeingizwa katika akaunti zangu
na akaunti ile ya Dr Vivian imefungwa kabisa.Rais yuko
salama” akasema Peniela.Mathew
akashusha pumzi na kusema
“Ahsante sana Peniela kwa
jambo hili kubwa ulilolifanya.Hivi
sasa bado kuna shughuli
ninakwenda kuifanya sehemu
fulani na baadae asubuhi nitakuja
hapo” akasema Mathew na kukata
simu kisha akampigia rais
“Habari yako
Mathew.Nimekutafuteni sana
wewe na Meshack Jumbo lakini
nyote hamkuwa mkipatikana
simuni nikapata wasiwasi kuhusu
usalama wenu.Vipi maendelo
yenu?
“Tunaendelea vyema
mheshimiwa rais.Ilitulazimu kuzima simu zetu kutokana na kazi
kubwa iliyokuwa inandelea lakini
nashukuru tumefanikiwa kumaliza
salama.Kwanza tumefanikiwa
kuwahoji wale watu na tayari
tumekwisha pata taarifa muhimu
tulizokuwa tunazihitaji” akasema
Mathew
“Really ? akauliza Dr Vivian
“Ndiyo mheshimiwa rais.Kuna
mambo ya msingi tumeyapata
kutoka kwa wale jamaa na
nitakueleza tutakapoonana
asubuhi” akasema Mathew
“Vipi kuhusu ile akaunti?
Akauliza Dr Vivian
“Kuhusu ile akaunti tayari
suala hilo nalo limemalizika” “Mathew ni Alfajiri sasa
naomba kusiwe na masihara
katika hili”
“Hakuna masihara
mheshimiwa rais.Jambo hili
limemalizika tayari .Nitakupa
maelezo kamili hapo baadae
tutakapoonana.Kwa sasa naelekea
nyumbani kwa mkuu wa jeshi la
polisi nchini Inspekta jenerali John
Mkoka kumfanyia mahojiano kisha
nitakuja ikulu” akasema Mathew
“Poleni sana Mathew kwa kazi
kubwa mliyoifanya katika usiku
wa leo.Nilipewa taarifa mida ya saa
tisa hivi kwamba kuna ndege
imetoka Marekani imebeba watu
waliotumwa kuja kuchunguza
kuhusiana na tukio la jana lililotokea pale uwanja wa ndege
na ufahamu alipo Helmet.Kama
ulivyosema kwamba baada ya
kufanya mauaji wangetuma kikosi
chao kuja Tanzania na
kuwakamata wale watu
waliowatuma na kama mpango
wao ulivyokuwa watu wale
wangekiri kutumwa na serikali ya
Korea Kaskazini na mpango wa
kuishambulia Korea Kaskazini
ungefanikiwa.Nimewazuia watu
hao kuingia nchini wala kutua
katika uwanja wa ndege wowote
hapa nchini na kwa taarifa
niliyopewa waligeuza na kwenda
kutua Nairobi kenya.Mathew
ahsante sana kwa kuung’amua ule
mpango wao” akasema Dr Vivian “Umefanya jambo zuri
mheshimiwa rais la kuwazuia
kuingia nchini kwani lengo lao
lilikuwa hilo kuja kuwakamata
wale jamaa ambao tayari
tumekwisha watia mikononi na
wameeleza kila kitu” akasema
Mathew
“Ahsante Mathew.Endelea na
kazi tutaonana baadae.Kama kuna
jambo lolote mnalihitaji tafadhali
naomba unijulishe” akasema Dr
Vivian na kukata simu.
“Marekani tayari wametuma
watu wao kuja nchini kwa ajili ya
kufanya uchunguzi wa tukio la
kushambuliwa Helmet.Kama
walivyokuwa wamepanga walitaka
kuja kuwakamata hawa jamaa ambao wangekiri kutumwa na
Korea kaskazini lakini
tumewawahi na kwa bahati nzuri
rais hajawaruhusu waingie
nchini”Mathew akamwambia
Meshack Jumbo
“Amefanya vizuri sana
kuwazuia kutokuingia nchini.Vipi
kuhusu akina Peniela
umewasiliana nao?
“Tayari nimewasiliana nao na
wamefanikiwa lile zoezi”
“Thank you Lord ! akasema
Meshack Jumbo
“Tusipoteze muda twendeni
nyumbani kwa mkuu wa jeshi la
polisi” akasema Mathew wakaingia
ndani ya gari na kuondoka
kuelekea nyumbani kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta
jenerali John Mkoka
“Amarachi nakupongeza sana
kwa kazi kubwa uliyoifanya usiku
wa leo.Nimefurahi sana kufanya
kazi nawe.Umeonyesha kiwango
kikubwa sana ambacho sikuwa
nimekitarajia.Umesaidia mno
katika kuwafanya wale jamaa
wafunguke.Ahsante sana” akasema
Mathew
“Kama nilivyowaeleza
kwamba niliishi na Boko Haram
kwa muda wamiaka kadhaa na
walinifunza mbinu nyingi za
kuweza kumfungua mtu mgumu ili
kupata taarifa muhimu” akasema
Amarachi “Vijana mmefanya kazi kubwa
na nzuri sana usiku wa
leo.Sikuamini kama tungeweza
kuwafungua wale jamaa kwani ni
majasusi wenye kuelewa mbinu
zote za kuhoji mateka lakini
mlifanikiwa kuwafungua” akasema
Meshack Jumbo
Walifika nyumbani kwa mkuu
wa jeshi la polisi nchini Inspekta
jenerali John Mkoka ambako
kulikuwa na watu kama kumi
kutoka idara ya usalama wa taifa
wameizunguka nyumba
yake.Tayari kulikwisha anza
kupambazuka.Sebuleni kulikuwa
na watu sita na wote walikuwa na
silaha na mkuu wa jeshi la polisi
nchini Inspekta jenerali John Aminiel Mkoka alikuwa amejilaza
sofani akiwa chini ya ulinzi na
hakuruhusiwa kuondoka pale
kwani hata alipokwenda chooni
alikuwa chini ya
ulinzi.Hakuruhusiwa kushika
chochote wala kuzungumza na
yeyote kwani hata simu yake
ilikuwa imechukuliwa.Meshack
Jumbo akawataka wale jamaa
watoke nje na wawape nafasi ya
kuweza kumuhoji mkuu yule wa
jeshi la polisi.
“Meshack Jumbo nini maana
ya hiki mlichonifanyia? Akauliza
John Mkoma kwa hasira
“John,haya ni mambo ya
kazi.Kuna mambo muhimu
tunataka kuyaweka sawa halafu tutaona nini kitafuata.Vijana
wangu wana mazungumzo nawe
naomba uwape ushirikiano”
akasema Meshack Jumbo
“Mathew he’s all yours.Make
sure he talks” Meshack
akamwambia Mathew halafu
akatoka nje wakabaki sebuleni
Mathew,Amarachi na John Mkoka
“Kama alivyosema mzee
Meshack huu ni muda wa kazi na
tutakuwa na maneno machache
sana ya kuzungumza nawe na
tunakuomba utupe
ushirikiano”akasema Mathew
“Nini hasa mnachokihitaji
kwangu? Akauliza
“Taratibu utafahamu mzee
wangu” akasema Mathew na kuchukua kiti akamsoglea
karibu.Amarachi akiwa na bastora
alikuwa makini sana kujihami
endapo hatari yoyote ingetokea
“George Mzabwa aliyekuwa
mkuu wa idara ya usalama wa taifa
unafahamiana naye?
“George nafahamiana naye
ndiyo,japo hatukuwa na ukaribu
sana.Mara nyingi tulikuwa
tunakutana katika vikao vya
kiserikali”
“Vipi kuhusu Dr Robert
Mwainamela unafahamiana naye?
“Dr Robert ninafahamiana
naye sana na kifo chake
kimenistua mno”
“Unafahamu chochote
kuhusiana na Escom bank? “Escom bank?!
“Ndiyo.Unaifahamu ?
“Huwa naisikia sikia tu lakini
siifahamu kiundani”
“Hujawahi kufungua akaunti
Escom Bank?
“Hapana sina akaunti Escom
bank na wala sifahamu mahala
ilipo”akasema John Mkoka na uso
wake ulionyesha wasi wasi
“Kama alivyosema
mkurugenzi wa idara ya usalama
wa taifa hatuna muda wa kutosha
kwa hiyo nataka nikueleze
kwamba nimechukizwa na kitendo
chako cha kutokutupa
ushirikiano.Umetudanganya.Taarif
a zako zote tunazo”akasema Mathew na kuzidi kumchanganya
yule mzee
“Sjawadangana vijana wangu
siifahamu hiyo benki kabisa”
“Ngoja nikueleze ukweli mzee
wangu.George Mzabwa alikuwa
akipokea fedha kutoka kampuni
ya Flamingo ambayo iko nchini
Marekani na mara ya mwisho
alipokea kiasi cha shilingi milioni
mia saba na sabini akaziweka
fedha hizo katika akaunti tatu za
kampuni ya kuchonga madini ya
Tanbest Gemstone.Katika moja ya
akaunti,fedha zilichukuliwa na Dr
Robert na akaweka katika akaunti
yako iliyopo benki ya Escom kiasi
cha shilingi milioni mia moja na
ishirini” “No ! No No ! that’s a
mistake.Mmekosea hiyo akaunti si
yangu!akasema John Mkoka huku
akitaka kuinuka
“Sit down !! akasema Mathew
kwa ukali
“George Mzabwa alikuwa
katika mtandao wa CIA hapa nchini
na alikuwa akisaidia kufanikisha
baadhi ya operesheni zao na
alikuwa akilipwa pesa nyingi
zilizopitia benki ya Escom.George
ndiye aliyekuwa akipokea fedha
halafu huzitawanya kwa watu
wengine walio katika mtandao
huo.Mtu mwingine ambaye
alikuwa katika mtandao huo ni Dr
Robert Mwainamela na sasa
tumegundua kwamba wewe nawe ni mmoja wa watu waliomo katika
mtandao huo na umekuwa
ukipokea fedha kutoka CIA.Nataka
kujua ni nani wengine walioko
katika mtandao huu? Nani
kiongozi wenu hapa nchini? Nini
mipango yenu hapa nchini? Ukijibu
maswali hayo mzee wangu nitaona
namna ya kukusaidia lakini kama
utaonyesha ukaidi nakuhakikishia
huu utakuwa ndio mwisho
wako.Maisha yako yote yaliyobaki
yatakuwa gerezani” akasema
Mathew
“Vijana wangu kama
nilivyowaeleza kwamba sina
ukaribu wowote na watu hao
wawili uliowataja ila
tunafahamiana kwa kuwa wote walikuwa watumishi wa umma na
tulikuwa tunakutana mara kadhaa
sehemu mbali mbali.Kuhusu kuwa
na akaunti katika benki ya Escom
hilo ni jambo ninalolisikia kwa
mara ya kwanza toka kwenu kwani
sijui hata ilipo hiyo benki.Hizo
fedha unazodai zimetumwa
kwangu ni kichekesho
kikubwa.Fedha zote hizo kwa kazi
gani ? Mmi ninaishi kwa mshahara
wangu na sina biashara yoyote ya
kuweza kuniingizia kiasi hicho
kikubwa cha fedha.Naomba
mniamini vijana wangu” akasema
Mkuu yule wa jeshi la polisi
“Mzee hivi utuonavyo
hatujafunga hata ukope,kwa usiku
mzima tumekuwa tunapambana kwa maslahi ya taifa letu kwa hiyo
hatutapenda kupoteza muda na
wewe wakati kila kitu kuhusu
wewe tunakifahamu.Inuka twende
chumbani kwako” akasema
Mathew na wakaongozana
kuelekea katika chumba cha kulala
akaufungua mlango wakaingia
ndani.
“Adabu gani hiyo mnaingia
chumbani kwangu bila hodi?
Akauliza kwa ukali mke John
Mkoka
“Samahani mama” akasema
Mathew
“Kitu gani hasa
mnachokitafuta toka kwetu?Mume
wangu halali usiku akifanya kazi ya kuhakikisha nchi iko salama
kwa nini leo mnamfanyia hivi?
“Mama,tunakubali kazi kubwa
anayoifanya mumeo katika
kuhakikisha raia wa nchi hii na
mali zao wanakuwa salama lakini
mumeo si malaika.Anajihusisha na
mtandao ambao umekuwa
ukifanya mambo mbali mbali
maovu hapa nchini mtandao
ambao unaundwa na shirika la
ujasusi la Marekani CIA.Mtandao
huo ndio unahusika katika kifo cha
rais Anorld Mubara na matukio
mengine mengi.Tunachotaka
kutoka kwa mumeo ni kuufahamu
mtandao wake wote na mambo
gani waliyopanga kuyafanya halafu tutamsaidia lakini hataki
kuonyesha ushir…”
“Mathew” akaita Amarachi na
Mathew akageuka
“Kuna kasiki hapa pembeni ya
kabati” akasema na Mathew
akamgeukia mke wa IGP
“Fungua lile kasiki”
“Siwezi kulifungua sina namba
za siri za kufungulia lile
kasiki.Huwa analifungua yeye
mwenyewe.Huhifadhi mamboyake
ya siri” akasema
“Fungua hilo kasiki” Mathew
akamwambia John Mkoka lakini
hakuonyesha kutaka kulifungua
“Baba Judy ni kweli haya
wanayoyasema hawa vijana? Akauliza mke wake lakini hakujibu
kitu akabaki kimya
“Nakuuliza baba Judy haya ni
ya kweli? Akauliza mke wake.
“Mbona hujibu unaninangalia
kama bubu?Nataka unijibu haya
wanayosema vijana ni ya kweli?!
Akauliza mke wake kwa ukali
lakini bado John hakujibu kitu
chochote.
“Fungua lile kasik..”
Mlango ukagongwa na
akaingia Meshack Jumbo akiwa na
simu mkononi.
Mlango ukagongwa na
akaingia Meshack Jumbo akiwa na
simu mkononi.
“Mathew nimepewa simu ya
John kuna hii namba imekuwa
inampigia kwa karibu usiku
mzima.” Akasema Meshack na kumpa Mathew ile simu.Jina
lililoandikwa lilikuwa ni 110C
“Huyu 110C ni nani? Akauliza
Mathew lakini John hakujibu kitu
Mathew akaipokea simu ile na
kuiweka katika sauti kubwa ili kila
mtu aliyemo mle ndani aweze
kusikia.
“Hallow” akasema na mtu
aliyepiga ile simu aliyeonekana
kuwa na haraka alidhani
aliyepokea simu ile ni John Mkoka
“John nimekutafuta kwa usiku
mzima haukupokea simu
yangu.Kwa nini ? Kuna tatizo
lilikupata? Anyway tutazungumza
baadae lakini kuna jambo la
dharura ambalo ninataka
kukujulisha na
kufanyiwa kazi haraka sana”
akasema yule mpigaji ambaye jina
lake lilionyesha ni 110C
“Hey John are you listening to
me? Akauliza 110C na kwa haraka
Mathew akatoa bastora na
kumnyooshea
“I’m listening” akajibu John
“Good.Nimepokea taarifa jana
kwamba kuna mwanamke mmoja
anaitwa Peniela amekuja hapa
nchini.Huyu anazo taarifa muhimu
sana ambazo zinaweza kuharibu
mipango yetu yote.Anatakiwa
ashughulikie haraka sana.Tayari
amekwisha fahamika mahala alipo
na unachopaswa kufanya kwa
haraka andaa kikosi kiweze
kumshughulikia haraka sana kabla hajakutana na watu wake akawapa
taarifa muhimu.Ukisha andaa
kikosi nijulishe mara moja ili
niweze kukujulisha mahala
alipo.Fanya hima hili jambo
lilitakiwa liwe limemalizika toka
usiku wa jana” akasema 110C.John
akavuta pumzi ndefu na kusema
kwa haraka
“Niko mikononi mwa
polisi.Please run they’re coming
for y..”kabla hajamaliza sentensi
yake Mathew akampiga ngumi
nzito iliyompeleka chini na
kuinyakua simu tayari
ilikwishakatwa.
“Mzee kwa haraka sana
hakikisha unafuatilia hizi namba
tujue ni namba za nani? Huyu mtu ambaye amempigia simu
anaonekana ndiye kiongozi wa
mtandao huu hapa nchini na
anaokana ndiye anayepokea
maelekezo kutoka makao makuu
CIA na kisha kuyagawa majukumu
kwa watu wa hapa Tanzania.We
need to find her as quick as
possible! Mathew akamwambia
Meshack Jumbo na Meshack
akatoka.Mathew akachukua simu
na kumpigia Peniela akamtaka
ampe simu Austin azungumze naye
“Nakusikiliza Mathew”
“Austin naomba
unisikilize.Peniela amekwisha
julikana kuwa you hapa nchini na
kuna watu wanaweza wakatumwa
sasa hivi kufika hapo kuwadhuru.Naomba uwatoe hapo
nyumbani watu wote wapeleke
sehemu salama.Nakuomba sana
ndugu yangu”
“Sawa Mathew nitafanya
hivyo”
“Ahsante Austin” akasema
Mathew na kukata simu
“Do you trust him? Amarachi
akauliza baada ya Mathew
kumaliza kuongea na Austin
simuni
“I trust him” akajibu Mathew
na kumgeukia John
“Nani aliyekupigia simu?
Mathew akamuuliza lakini
aliendelea kubaki kimya hakujibu
chochote “Hata usipojibu kitu,muda si
mrefu tutamfahamu mtu
aliyekupigia simu na kwa kitendo
ulichokifanya kimedhihirisha wazi
kwamba wewe ni mmoja watu mlio
katika mtandao wa Marekani hapa
nchini” akasema Mathew na
kumgeukia mke wa John
“Mama nadhani umeshuhudia
mwenyewe.Mumeo amekuwa
anajihusisha na mtandao
ulioundwa na shirika la ujasusi la
Marekani hapa nchini,mtandao
ambao umekuwa ukijihusisha na
mambo kadhaa maovu.Mtandao
huu umekuwa ukihusika na kuua
watu, viongozi na ndio waliomuua
rais Anorld Mubara na kwa sasa
wanamuwinda rais Vivian.Mumeo amekuwa akipokea kiasi kikubwa
cha fedha kutoka kwa CIA na mara
ya mwisho amepokea kiasi cha
shilingi milioni mia moja na
ishirini zilizowekwa katika
akaunti yake ya siri katika benki
ya Escom” akasema Mathew na
sura ya mke wa John ikabadilika
“Baba Judy kwa nini
umejiingiza katika hayo mambo?
Shetani gani amekuingia na
kukufanya ujiingize katika mambo
hayo maovu? Hukujua kama siku
moja unaweza kugundulika kama
ulivyogundulika leo na kutuletea
matatizo makubwa?!! Mama yule
aliongea kwa hisia kubwa huku
machozi yakimtoka “Mama,mumeo amejihusisha
katika jambo kubwa na la hatari
kwa usalama wa nchi na endapo
atafikishwa mbele ya vyombo vya
sheria basi maisha yake yote
yanaweza yakamalizikia gerezani
lakini endapo akionyesha
ushirikiano kwetu tunaweza
kumsaidia.Zungumza nay…..”
Akasema Mathew lakini
akakatishwa na Meshack Jumbo
aliyeingia mle ndani na kumuita
Mathew pembeni
“Namba ile tayari
imechunguzwa na imegundulika ni
namba ya April Mubara mke wa
marehemu rais Anorld Mubara”
akasema Meshack Jumbo.Kwa
takribani sekunde thelathini Mathew alishindwa kuzungumza
akabaki anamtazama Meshack
Jumbo.Taarifa ile ilimstua sana
“Nimestuka sana.Sikutegemea
kabisa kitu kama hiki.April
Mubara?!! Akasema Mathew kwa
mshangao
“Tuma watu haraka sana
wamuwahi wakamdhibiti kwani
tayari amekwisha pewa angalizo
kwamba tunamtafuta” akasema
Mathew.
“Mimi pia ninakwenda huko
kuhakikisha kwamba kila kitu
kinakwenda vyema.Hatupaswi
kufanya kosa” akasema Meshack
Jumbo
Mathew aliamuru mkuu wa
jeshi la polisi nchini Inspekta jenerali John Aminiel Mkoka na
mke wake wachukuliwe kwa ajili
ya kufanyiwa mahojiano kwani
kwa wakati ule hakuonekana
kutaka kusema chochote.Mathew
na Amarachi wakapekua chumbani
na kupata nyaraka mbali mbali
ambazo waliona zingeweza
kuwasaidia katika uchunguzi
wao.Iliwalazimu pia kuling’oa
kasiki lile na kuondoka nalo ili
kwenda kulifungua na kujua
kilichomo ndani yake.
Kutoka nyumbani kwa
Inspekta jenerali John Mkoka
Mathew na Amarachi wakaelekea
ikulu kuonana na rais.Walifika
ikulu wakakaribishwa na rais akajulishwa kuhusu ujio wao na
akaenda kuonana nao haraka
“Mathew poleni sana”
akasema Dr Vivian
“Ahsante mheshimiwa
rais”akasemaMathew na rais
akaketi
“ Mheshimiwa rais huyu
anaitwa Amarachi january ni mke
wa mwenzangu anayeitwa Austin
ambao wanashirikiana nasi pia
katika kazi tunayoendelea nayo”
Mathew akafanya utambulisho
“Karibu sana
Amarachi.Nimefurahi kukuona”
akasema rais na kusalimiana na
Amarachi
“Nipe habari Mathew”
akasema rais “Mheshimiwa rais kama
nilivyokueleza kwamba usiku wa
leo ulikuwa ni usiku wa
kazi.Tumepata mafanikio
makubwa.kwanza tumefanikiwa
kulimaliza lile suala la ile akanti ya
siri na fedha zote ziko salama na
akaunti ile imefungwa” akasema
Mathew na Dr Vivian akashindwa
kuyazuia machozi ya furaha
kumtoka
“I’m sorry nimeshindwa
kujizuia kutoa machozi kwa furaha
niliyonayo kwa jambo hili
kumalizika kwani nijambo
lililonifanya nikapungua uzito
ghafla.Ni kashfa kubwa sana
ambayo ingeweza kuniharibia
kabisa taswira yangu katika jamii.Hata hivyo ninawahakikishia
ndugu zangu kwamba fedha hizo
ambazo zilikuwemo katika hiyo
akaunti zitakwenda katika miradi
ya maendeleo.Zote zitakwenda
katika miradi ya elimu”
“Mheshimiwa rais sisi kazi
yetu ilikuwa ni kuhakikisha
tunakusaidia kulimaliza hilo suala
na namna utakavyozitumia fedha
hizo ni juu yako.Tuachane na
hilo.Tumewafanyia mahojiano
wale watu watatu waliotumwa
kuja kumuua Helmet
Brian.Haikuwa rahisi lakini
tumefanikiwa kupata taarifa
muhimu tulizokuwa tunazihitaji.”
“Oh thank you Lord! Akasema
DrVivian “Watu wale wamekiri
kutumwa na CIA kuifanya kazi ile
ya kumuua waziri Helmet Brian na
wamenieleza kila kitu ila kwa
masharti kwamba tutahakikisha
hawashtakiwi na hawarejeshwi
Marekani bali wanapelekwa katika
nchi wanazozitaka wao.”
“Hilo halina shaka
tutawatekelezea.Tunachohitaji sisi
ni taaarifa hizo
muhimu.Nitamtaarifu
mwanasheria mkuu wa serikali
alishughulikie hilo haraka
sana”akasema rais
“Ahsante mheshimiwa
rais.Tukiachana na hilo turejee
katika lile suala la mkuu wa
polisi.Tuligundua kwamba mkuu huyu wa polisi alipokea kiasi
kikubwa cha fedha kutoka kwa Dr
Robert na ahsante kwa
kunikubalia kumuweka
kizuizini.Tumemfanyia mahojiano
lakini amekuwa mgumu
kufunguka hivyo tumempeleka
sehemu maalum kwa ajili ya
kuendelea kumuhoji.Wakati
tukiwa nyumbani kwake alipigiwa
simu na mtu ambaye jina lake
liliandikwa 110C na
tulipozichunguza hizo namba
tukagundua kwamba ni namba za
April Mubara mjane wa rais Anorld
Mubara”
“April Mubara?!! Dr Vivian
akashangaa “Ndiyo mheshimiwa rais.April
Mubara alimtaarifu John Mkoka
kwamba Peniela yuko hapa nchini
na kwamba amekuja na taarifa
muhimu hivyo wanapaswa
wamshughulikie haraka lakini
mkuu wa polisi akamjulisha April
kwamba akimbie kwani
tunamfuatilia”
“I cant believe this.Madam
April?! Dr Vivian akazidi
kushangaa
“Ni kweli inashangaza sana
mheshimiwa rais”
“Kama ni hivyo basi sina wa
kumuamuni tena kwani
nimezungukwa na nyoka
watupu.Huyu bi April ni mtu
niliyemuheshimu kama mama yangu.Sasa nimepata picha
kwamba anahusika na mtandao
huu kwanindiye aliyemleta yule
msichana Tausi akaniomba nimpe
kazi ikulu na mimi kwa kuwa
ninamheshimu sana nikampa kazi
bila wasiwasi kumbe nilikuwa
najipeleka mwenyewe katika
mdomo wa Mamba.Mathew
ahsante sana kwa kunifumbua
macho.Mmechukua hatua gani za
kumkamata huyu April?
“Meshack Jumbo na vijana wa
usalama wa taifa wako njiani hivi
sasa wanaelekaa huko nyumbani
kwa April Mubara kwenda
kumkamata” “Good job Mathew” akasema
Dr Vivian na kuinamisha kichwa
akazama mawazoni
“Madam president sisi
tumepita mara moja
kukufahamisha mahali tulikofikia
katika kazi uliyotupa.Kwa sasa
tunakwenda kuendelea kumfanyia
mahojiano John Mkoka na baadae
April Mubara mara tu
atakapofanikiwa
kukamatwa.Tutakujulisha kila
kitakachojiri ila naomba suala la
wale jamaa lifanyiwe kazi haraka
kwani tayari nimekwisha waahidi
kuwa tutawatekelezea kile
wanachokihitaji” akasema Mathew
na kuagana na rais wakaondoka
moja kwamoja wakaeleka nyumbani kwa Austin ambako
walikuwepo akina Peniela.Mara tu
baada ya kufika mtu wa kwanza
aliyetaka kuonana naye ni mwanae
AnnaMaria lakini bado alikuwa
amelala na hivyo wakaendelea na
majadiliano ya kazi
“Austin ahsante sana kwa
msaada huu mkubwa kwa familia
yangu” Mathew akamwambia
Austin
“Mathew naomba samahani
sana kwa ujinga nilioufanya jana
usiku.Nimejifikiria na nimeumia
mno moyoni kwa mambo
niliyoyafanya. Naomba unisamehe
sana ndugu yangu na unishirikishe
tena katika operesheni hii.”
Akasema Austin “It’s ok Austin forget what
happened last night .What we did
wasn’t right lakini ilitulazimu
kufanya vile kwa ajili ya manufaa
ya nchi kwani watu wale walikuwa
wamemuingiza Dr Vivian katika
mtego naye akaingia bila kujua na
wangetumia kigezo kile
kumlazimisha afanye kila
wakitakacho na nchi yetu
ingeyumba sana kwani rais wetu
angefuata kila amacho
angeelekezwa na
marekani.Rasilimali zetu
zingeendelea kuchotwa kila uchao
kwa sababu rais wetu anaogopa
siri yake kujulikana.Tumelimaliza
suala hilo na kwa sasa rais yuko
salama.Hawataweza kutumia tena kigezo cha ile akaunti
kumlazimisha rais wetu afanye
mambo wanayoyataka wao hata
hivyo rais ameliona kosa lake
analijutia na ameahidi kutumia
kiasi chote cha fedha
kilichokuwemo katika akaunti ile
kwa ajili ya miradi ya
elimu.Tuachane na hayo usiku wa
leo tumepiga hatua kubwa sana”
Mathew akamueleza kila kitu
walichokifanya usiku na Austin
akajilaumu sana kwa kutokuwa
sehemu yao kwa usiku ule.
Wakiwa pale kwa Austin
walifanikiwa kulifungua lile kasiki
na ndani yake walikuta mabunda
ya fedha yakiwa yamepangwa na
vile vile wakakuta kuna nyaraka mbali mbali za muhimu ambazo
zilionyesha kwamba John Mkoka
alikuwa anapeleka kiasi kikubwa
cha fedha kwa miezi minne
mfululizo kwa kampuni ya ulinzi
ya Chemi Security company
“Sasa nimepata picha kwamba
wale watu waliokuwa wakitumia
sare na magari ya askari polisi
wakifanya kazi ya kuvamia
sehemu mbalimbali wanatoka
katika kampuni hii ya
ulinzi.Nilikuwa najiuliza namna
wale jamaa wanavyopata vifaa vya
jeshi la polisi wanavyotumia
katika shughuli zao za
uvamizi.Walikuwa wanapata
ufadhili kutoka kwa huyu mkuu wa
jeshi la polisi nchini Inspekta jenerali John Aminiel
Mkoka.Kampuni hii napaswa
kuwekwa chini ya ulinzi na
kuchunguzwa kwa kina.Lazima
wamilki wake wapatikane haraka
sana na tufahamu ni matukio
mangapi wamekuwa wakishiriki
na wanatumwa na nani” akasema
Mathew halafu wakaondoka
kuelekea mahala walikopelekwa
mkuu wa polisi John Mkoka na
mke wake kwa ajili ya kuwafanyia
mahojiano.Wakiwa njiani
akapigiwa simu na Meshack jumbo
ambaye alimjulisha kwamba
wamefanikiwa kumpata April
Mubara akiwa njiani kuelekea
Zanzibar na boti na kulitokea
mapigano na mmoja wa vijana wa Meshack alipigwa risasi na walinzi
wa April akafariki dunia.
******************
Saa tano za asubuhi rais wa
Tanzania Dr Vivian alijulishwa
kuhusu kuwepo angani kwa ndege
ya rais wa Marekani.Taarifa hiyo
ilimstua Dr Vivian kwani
hakukuwa na taarifa zozote rasmi
za ujio huo wa rais wa
Marekani.Dege hilo liliruhusiwa
kutua na Dr Vivian akamtuma
makamu wa rais aende uwanja wa
ndege akampokee rais huyo wa
taifa lenye nguvu kubwa duniani. Dr Vivian alijiuliza maswali
mengi kuhusiana na ujio ule wa
kimya kimya wa Mike straw.
“Anakuja kutafuta nini na kwa
nini anakuja kimya kimya ? Hii
inashangaza sana” akawaza Dr
Vivian na kumpigia simu Mathew
“Madam president” akasema
Mathew baada ya kupokea simu
“Mathew vipi maendeleo
yenu?
“Tunaendelea vyema
mheshimiwa rais.Tumekwisha
maliza kumfanyia mahojiano John
Mkoka na sasa tunamfanyia
mahojiano April Mubara ambaye
ameletwa hapa muda si mrefu”
“Good.Kuna jambo limetokea
ambalo nimeona ni vyema nikakujulisha.Rais wa Marekani
Mike straw yuko hapa nchini”
“Yuko nchini? How?
“Amekuja ghafla na mimi
nimepata taarifa muda mfupi
uliopita kwamba yuko katika anga
ya Tanzania”
“Anakuja kutafuta nini ?Kwa
nini aje kimya kimya?
“Hata mimi nimejiuliza
maswali hayo lakini sijapata
jibu.Nahisi kilichomleta ni hili
suala la Helmet Brian.Kwa sababu
hiyo kuna mambo nataka tufanye”
akasema Dr Vivian na kuwapa
maelekezo Mathew na Meshack
Jumbo ya kuwapeleka ikulu
Helmet Brian na wale wadunguaji
watatu waliotumwa na Marekani kuja kumuua Helmet Brian jambo
ambalo iliwalazimu Mathew na
Meshack wawaache Austin na
Camilla wakiendelea kumuhoji
April Mubara na wao
wakalishughulikia kwa haraka
agizo la rais
Helmet Brian alifikishwa ikulu
haraka sana kama alivyoelekeza
rais
“Helmet natumai unaendelea
vyema.Nimekuleta hapa kwa
haraka kutokana na dharura
iliyojitokeza.Hivi tuongeavyo rais
Mike straw yupo hapa nchini na
muda si mrefu atafika hapa ikulu”
“Mike yupo hapa nchini?
Helmet Brian naye akashangaa “Ndiyo.Amekuja kimya kimya
na mimi nimejulishwa wakati
tayari amekwisha ingia katika
anga ya Tanzania”
“Nini kimemleta ?
“Nina hakika lazima litakuwa
ni lile suala linalokuhusu wewe na
ndiyo maana nikakuita uje hapa ili
mpango wetu uweze kukamilika
leo”
“Imekuwa vizuri sana
ameamua kuja yeye
mwenyewe.Mungu ana makusudi
yake kumleta mtu huyu na kazi
yetu inakwenda kuwa
rahisi”akasema Helmet na
kuendelea na maongezi yao juu ya
jambo alilomuitia pale Katika uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere Mike straw
akapokewa na makamu wa rais na
kupelekwa moja kwa moja
ikulu.Hakukuwa na maandalizi
makubwa yaliyofanywa kutokana
na ujio ule wa ghafla lakini ulinzi
aliokuja nao Mike ulikuwa mkali
sana
Mike straw aliwasili ikulu na
kupokewa na Dr Vivian
“Karibu sana
Mike,nimeshangazwa sana na ujio
wako wa ghafla”
“Utanisamehe kwa kuja
namna hii bila taarifa lakini
sikutaka kuwapa wakati mgumu
wa kufanya maandalizi hata hivyo
safari yenyewe ilikuwa ya ghafla sana sikuwa nimepanga kuja
Tanzania.Pole sana kwa yale yote
yaliyotokea jana” akasema Mike
“Ahsante sana Mike” akasema
Dr Vivian
“Dr Vivian kwakuwa ziara hii
haitambuliki rasmi kiserikali
sitaki nichukue muda wako
mwingi hivyo ninaomba nimalize
kile kilichonileta kwako.Tunaweza
kupata faragha kwa mazungumzo?
Akauliza Mike na Dr Vivian
akampeleka katika chumba cha
mazungumzo ya faragha
“Dr Vivian narudia tena
kukuomba samahani kwa kuja bila
taarifa na kukuvurugia ratiba zako
hata hivyo nitaenda moja kwa
moja katika kitu cha msingi kilichonileta” akasema Mike na Dr
Vivian hakujibu kitu akawa kimya
akimsikiliza
“Kikubwa kilichonileta hapa
ni mazungumzo nawe.Nataka
tuyamalize mambo yaliyojitokeza
baina ya nchi zetu na ambayo
yanaendelea kujitokeza.Tanzania
na Marekani ni marafiki kwa
miaka mingi na Marekani
tumekuwa tukifadhili miradi mingi
ya maendeleo hapa Tanzania,vile
vile tumekuwa ni wachangiaji
wakubwa wa bajeti kuu ya serikali
kwa miaka mingi.Tanzania na
Marekani hazipaswi kuingia katika
msuguano kama huu unaoendelea
hivi sasa na ndiyo maana
nimeamua kuja mimi mwenyewe kulimaliza hili suala” akanyamaza
kidogo na kuendelea
“Nilimtuma waziri wangu wa
mambo ya nje aje kuzungumza
nawe kuhusiana na ule mpango
wako wa mashirikiano na Korea
kaskazini lakini likatokea
shambulio ambao tunaamini
lilimlenga yeye na mpaka sasa
hajulikani alipo na hatujapokea
taarifa yoyote rasmi kutoka
serikali ya Tanzania kuhusiana na
nani aliyefanya shambulio lile na
waziri wetu yuko wapi hadi hivi
sasa”
akanyamaza tena na kuendelea
“Tukiweka pembeni
hayo,mimi na wewe tunafahamu
fika nini hasa kilichotokea na unafahamu ni wapi alipo Helmet
Brian.Tunazo taarifa zote za
kilichotokea na sitaki kupoteza
muda hapa kuzungumzia hayo
mambo kwani unayafahamu na
ndiyo maana nimekuja mwenyewe
ili tulimalize hili suala kimya
kimya” Akanyamaza akamtazama
Dr Vivian na kuendelea
“Vijana wako tayari
wamekupa taarifa zote kuhusiana
na nini ulikuwa mpango wa
Marekani.Kwa bahati mbaya
mpango wetu haukwenda kama
tulivyokuwa tumeupanga na
ninafahamu kwamba kutokana na
msuguano kati yetu unaweza
ukautangazia ulimwengu nini
tulitaka kukifanya kwa waziri Helmet Brian jambo ambalo
linaweza kutushushia heshima
yetu duniani.Nimekuja kufanya
makubaliano nawe ili jambo hilo
libaki siri kati yetu” akasema Mike
straw na Dr Vivian akatoa kicheko
kidogo
“Makubaliano? Hicho ndicho
kilichokutoa Marekani hadi
Tanzania kufanya makubaliano
nami? Akauliza Dr Vivian
Makubaliano? Hicho ndicho
kilichokutoa Marekani hadi
Tanzania kufanya makubaliano
nami? Akauliza Dr Vivian
“Ndiyo Dr Vivian.Mimi na
wewe tayari tunafahamiana vyema
na kila mmoja ana mambo yake ya
siri ambayo hataki yajulikane
hivyo basi tutafanya makubaliano
ambayo yatafanya midomo yetu
ifungwe na kila mmoja apate
anachokihitaji na siri zetu ziendelee kuwa salama”akaema
Mike na Dr Vivian akatoa tena
kicheko
“Mike umenifurahisha
sana.Hukupaswa kupoteza mafuta
yako ya ndege kutoka Marekani
kuja hadi Tanzania wakati
ukifahamu fika kwamba mimi
nawe hatuwezi kufanya
makubaliano yoyote.Hakuna
chochote tunachoweza kukiongea
kwa sasa au kuweka makubaliano
yoyote.”akasema Dr Vivian na sauti
yake ilianza kuonyesha kukasirika
“Dr Vivian naomba
usikasirike.Maongezi haya ni ya
amani tupu.Twende taratibu
tutafikia makubaliano” akasema
Mike na kufungua mkoba wake akatoa faili na kumkabidhi Dr
Vivian.
“Tuanze kwanza na hili.Faili
hilo lina maelezo yote ya
kuhusiana na akaunti yako ya siri
ambayo iko katika benki ya Escom
ambako umekuwa ukificha fedha
nyingi ambazo hazilipiwi kodi.Dr
Vivian wewe ni mmoja kati ya
marais waliotajwa kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa katika mapambano
dhidi ya rushwa na ukwepaji kodi
barani Afrika na kuwa rais wa
mfano.Unadhani itakuaje
wananchi wako,bara la afrika na
dunia nzima watakapofahamu
kwamba umekuwa ni mkwepaji
kodi mkubwa na unaficha fedha
zako katika akaunti ya siri? Hii ni kashfa kubwa sana ambayo
haijawahi kutokea katika nchi ya
Tanzania na hili litakuwa ni
anguko lako kubwa kwani
utashtakiwa kwa uhujumu
uchumi.Kwa nini basi jambo hili
lisiendelee kuwa siri na wewe
ukaendelea kumiliki fedha zako
zote na utakapomaliza muda wako
wa uongozi uishi maisha mazuri
kama malaika? Hili litaendelea
kuwa siri endapo tu utakubaliana
na masharti yangu” akanyamaza
na kumpa nafasi DrVivian alipitie
lile faili.Alipomaliza akamtazama
Mike
“Nini hasa unachokihtaji
kwangu Mike? Akauliza.Mike akatabasamu na kwa haraka
akasema
“Kwanza nataka umrejeshe
Helmet Brian kwani najua kuna
mahala umemficha,nataka vile vile
uwarejeshe watu wetu wawili
waliopotelea hapa nchini kwako
ambao naamini unafahamu mahala
walipo,tatu nataka uufunge
mdomo wako kuhusiana na
mpango wa Marekani kutaka
kumuua Helmet Brian na nne
nataka mpango wa mashirikiano
baina ya Tanzania na Korea
kaskazini usitishwe haraka sana
na uitangazie dunia kwamba
Tanzania imewakamata watu
watatu waliotumwa na Korea
Kaskazini kumuua Helmet Brian.Ukifanya hayo hili suala
litabaki kuwa siri” akasema Mike
na Dr Vivian akamtazama kwa
dharau na kutoa kicheko kidogo
halafu akamrushia Mike lile faili
“Mike kwa nini unaidhalilisha
Marekani kiasi hiki? Kwa nini
umechoma mafuta
yanayonunuliwa kwa kodi za
wananchi wako kwa ajili ya kuja
kunieleza upuuzi huu? Una
uhakika na hiki
ulichokisema?Mimi siwezi kufanya
ujinga wa namna hiyo Mike.Mimi
ni rais ninayetembea katika
maneno yangu na siku zote
ninakuwa ni mfano wa
kuigwa.Siwezi kamwe kupambana
na wakwepaji kodi na wakati huohuo mimi nikawa mkwepaji
kodi wa kiwango hiki.Ninaomba
uwasiliane na watu wako
waliokupa taarifa hii na
wathibitishe kuhusu mimi kuwa na
akaunti hii na kama ni kweli nina
akaunti hii basi nitafanya kama
unavyotaka.Nakupa dakika tano
kunithibitishia hilo unalolisema na
kisha tutaendelea na
mazungumzo” akasema Dr Vivian
kwa kujiamini.Mike akaomba
mmoja wa walinzi wake aitwe
akamuelekeza jambo fulani
akatoka na baada ya dakika
kadhaa akaingia mle ndani mtu
mmoja akiwa na kompyuta ndogo
Mike akamtaka amthibitishie
kuhusu wepo wa akaunti ile ya Dr Vivian katika benki ya Escom.Yule
jamaa kwa haraka akaanza
kubonyesa bonyeza kompyuta
yake hukuMIke
akitabasamu.Mapigo ya moyo ya
Dr Vivian yalikuwa yanakwenda
kwa kasi kubwa
“Please help me Lord”
akaomba kimya kimya
Yule jamaa aliendelea
kubonyeza kompyuta yake na sura
yake ikaanza kubadilika
“Vipi bado? Mike akamuuliza
“Mheshimiwa rais kuna
tatizo.Ile akaunti haionekani
tena”akasema yule jamaa na
kumstua Mike
“Haionekani? Akauliza Mike
kwa ukali “Inawezekanaje?
“Mheshimiwa rais nipe dakika
chache niwasiliane na wataalamu
wa benki hii wanieleze kwa nini
akaunti hii haionekani tena”
akasema yule jamaa na
kutoka.Mike Straw akaonekana
kuchanganyikiwa
“Mike kwa nini umeamua
kunikashifu kiasi hiki?akauliza Dr
Vivian na Mike hakujibu kitu
akabaki akizunguka zuguka mle
chumbani baada ya dakika tatu
yule jamaa akarejea na kumpa jibu
ambalo lilimfanya akae
chini.Akaunti ile haikuwepo
ilikwisha fungwa na fedha zote
kuondolewa “Mike nadhani hatuna tena
kitu cha kuzungumza.Mipango
yako imeshindikana” akasema Dr
Vivian huku akitoa kicheko cha
dharau
“Bado kuna jambo moja la
kuzungumza.Wewe unajifanya ni
mtu mwenye akili nyingi siyo?
Akauliza Mike na kufungua tena
mkoba wake na kutoa faili lingine
na kumpa Dr Vivian akalifungua na
kustuka sana Mike akatabasamu
“Anaitwa Florentina
Paul.Mbona umestuka
ulipomuona? Akasema Mike lakini
Dr Vivian hakujibu kitu akabaki
anatazama picha zilizokuwemo
ndani ya lile faili “Naomba nikusaidie ili
kuokoa muda.Huyo binti anaitwa
Florentina Paul.Hilo ni jina lake la
sasa lakini jina lake halisi ni Nasrat
Said.Huyu ndiye mtoto ambaye
uliwahi kumzaa na Said Bazharan
kiongozi wa kikundi cha kigaidi
kinachopambana na serikali ya
Syria na kuua watu wengi wasio na
hatia.Nasrat alitelekezwa na baba
yake na akachukuliwa na watawa
wakambatiza na kumpa jina la
Florentina Paul na sasa yuko
Marekani anasoma.Ni binti
mrembo na mwenye akili nyingi
lakini hafahamu chochote
kuhusiana na wazazi
wake.Anachokijua ni kwamba yeye
kwa sasa ni yatima”akanyamza baada ya kumuona Dr Vivian
akifuta machozi
“Dr Vivian naamini hapo
umeguswa.Hakuna anayefahamu
kama uliwahi kuzaa mtoto na
ukamtelekeza.Hii ni siri yako
kubwa na itaendelea kubaki siri
endapo utakubaliana na mambo
niliyokueleza na ninakuahidi
kukuunganisha tena na mwanao
na dunia haitajua kama uliwahi
kuwa na mahusiano na Said
Bazharan.Naomba ufikirie na
unipe jibu mheshimiwa rais”
akasema Mike na Dr Vivian akafuta
machozi na kulifunika lile faili
akaenda mezani akainua mkono
wa simu na kuzungumza na mtu na
baada ya dakika mbili mlango ukafunguliwa wakingia mle ndani
watu wanne na mmoja wa watu
walioingia mle ndani.Sura ya Mike
straw ikabadilika baada ya
kumuona Helmet
Brian.Wakatazamana kwa muda
wa sekunde kadhaa na Dr Vivian
akamuelekeza Helmet aketi
“Hallow Helmet” akasema
Mike kwa sauti ambayo ilionyesha
woga ndani yake lakini Helmet
hakujibu kitu.Dr Vivian
akamtazama Mike straw na
kusema
“Mike mbele yako ni waziri
wako wako wa mambo ya nje wa
Marekani na rafiki yako
mkubwa.Mimi sitaki kuwa msemaji.Helmet atazungumza
badala yangu” akasema Dr Vivian
“Imekuwa vyema umekuja
mheshimiwa rais na nimefurahi
kukuona.Nitakuwa na machache
sana ya kuzungumza nawe.Hawa
watu watatu uwaonao ni watu
waliotumwa kuja Tanzania
kufanya kazi moja tu ya kunitoa
roho yangu mpango ambao
uliubariki. Tayari
wamekwishajieleza na kila kitu
kiko wazi hivi sasa.Mpango wenu
wote umejulikana.Ushahidi wote
upo na wako tayari kusimama
mbele ya runinga na kuieleza
dunia unyama wako na serikali
yako.Kwa nini ukafanya haya Mike? Akauliza Helmet na Mike
bado alikuwa kimya
“Helmet …”Mike akataka
kusema kitu akazuiwa
“Mike hupaswi kusema
chochote.Kila kitu kinajulikana na
kwa sababu hiyo nitakuwa na
maneno machache sana ya
kusema”akasema Helmet Brian na
Mike akakaa kimya
“Nitakwambia maneno
machache tu.Ndani ya dakika kumi
kutokea sasa utaondoka kuelekea
uwanja wa ndege na utaondoka
Tanzania kurejea Marekani na
kesho asubuhi nataka kitu cha
kwanza cha kufanya wewe na
makamu wako wa rais
muwasilishe barua zenu za kujiuzulu nafasi zenu.Nataka
mfanye hivyo kimya kimya na
mchague sababu yoyote ile
ambayo itawafanya watu waamini
na endapo mkifanya hivyo mambo
haya yote mliyoyafanya wewe na
serikali yako yatazikwa kimya
kimya na mtaondoka na heshima
zenu lakini endapo mtashindwa
kufanya hivyo dunia nzima
itafahamu mambo yote maovu
unayoyafanya wewe na serikali
yako na nitaanzisha kampeni
kubwa ya kuwaondoa Marekani na
mtaondolewa madarakani kwa
aibu.Nadhani unaifahamu nguvu
yangu ilivyo kwani kampeni yangu
itachukua muda mfupi sana
kuwaondoa katika nyadhifa zenu kwa aibu hivyo nakuomba
uzingatie hayo
niliyokueleza.Nitayaelekeza
masikio yangu katika vyombo vya
habari vya Marekani kusikia
kesho asubuhi nini kitatokea
Marekani na endapo sintasikia
chochote basi utaiona nguvu
yangu” akasema Helmet Brian na
kumgeukia rais
“Dr Vivian ni wakati sasa wa
kumpeleka Mike straw uwanja wa
ndege na arejee Marekani.Hii
itakuwa ni mara yake ya mwisho
kupanda airfoce one.Kwa heri
mheshimiwa rais” akasema Helmet
“Mheshimiwa Mike,nadhani
umemsikia vyema Helmet na
ninakutakia utekelezaji mwema wa maagizo yote aliyokupa”
akasema Dr Vivian na kumpigia
simu makamu wa rais afanye
maandalizi kwa ajili ya Mike Straw
kuondoka kuelekea uwanja wa
ndege
“Mungu ni mkubwa sana na
siku zote ana mipango
yake.Sikujua kama Mike straw
angekuja mwenyewe
Tanzania.Nini hasa kilichomleta?
Akauliza Helmet
“Suala lako ndilo lililomleta
hapa.Alitaka tulimalize suala hili
kimya kimya hakujua kama
tumekwisha fahamu kila kitu
kuhusu mpango wako”akasema Dr
Vivian na kulificha lile faili la
Florentina “Usijali Dr Vivian
nakushukuru sana kwa kazi kubwa
uliyoifanya na baada ya kufikiri
sana nimeamua kufanya kampeni
ili niweze kuchukua nafasi ya Mike
baada ya kuachia ngazi” akasema
Helmet na furaha ya Dr Vivian
haikuweza kuzuilika akaenda
kumpa mkono Helmet
“Helmet uamuzi huu
ulioufanya ni uamuzi wa busara
sana.Naamini ukichukua nafasi
hiyo mimi na wewe tutafanya
mambo makubwa”akasema Dr
Vivian
Helmet Brian alirudishwa
mahala salama anakoishi na akina
Mathew wakaenda kuendelea na
kazi ya kumfanyia mahojiano April Mubara ili kufahamu kwa undani
kuhusiana na mtandao wa CIA
hapa nchini
******************
“Nilikutana na rais Anorld
Mubara wakati anasoma nchini
Marekani.Tulifanya ziara chuoni
kwao na tulipokutana urafiki wetu
ukaanzia hapo.Tuliwasiliana na
kutembeleana mara kwa mara na
baadae urafiki wetu ukakua na
tukawa wapenzi.Hata baada ya
kumaliza chuo mapenzi yetu
yaliendea na baadae tukafunga
ndoa na wakati huo alikuwa
anafanya kazi katika wizara ya
mambo ya nje.Anorld alifanya kazi zake kwa bidii kubwa na baadae
akateuliwa kuwa naibu waziri na
baadae akawa waziri kamili wa
wizara ya mambo ya nje na hapo
ndipo safari yake ya kuelekea
ikulu ilipoanzia” April Mubara
alianza kutoa maelezo yake mbele
ya akina Mathew baada ya
kufikishwa katika chumba cha
kufanyia mahojiano
“Anorld alipopata urais
nilifuatwa na watu wawili
wakitokea Marekani na kunieleza
kwamba Anorld anashirikiana na
mataifa mengine kadhaa hasimu
wa Marekani kuihujumu
Marekani.Kuna jambo wanapanga
kulifanya kwa hiyo wakanitaka
nianze kumchunguza Anorld.Mimi ni mmarekani,wazazi
wangu,ndugu zangu wote wako
Marekani kwa hiyo sikutaka nchi
yangu ifanyiwe jambo lolote baya
hivyo nikakubali kumchunguza
mume wangu bila yeye kujua.Na
hapo ndipo nikaanza uwakala wa
CIA.Nilichunguza kila kitu
alichokifanya Anorld na kuwapa
taarifa na nililipwa fedha kila
mwezi kupitia kwa marehemu
George Mzabwa.” Akanyamaza na
kutazama chini kwa muda halafu
akaendelea
“Nilielekezwa kuuchunguza
mkoba wa Anorld aliokuwa
anatembea nao kila mahala
ulioitwa Football lakini
sikufanikiwa kujua chochote kilichokuwamo ndani ya mkoba
ule na ndipo CIA walipopanga
mpango wa kuteka ndege yake na
kuichukua hiyo football ambayo
walidai ina siri kubwa ndani yake
kuhusiana na mpango mbaya dhidi
ya Marekani.Utekaji huo
haukufanikiwa na Anorld na watu
wengine wote wakafariki
isipokuwa Seba”
“Ulijisikiaje uliposikia mumeo
amefariki dunia katika ajali ya
ndege? Akauliza Amarachi
“ Niliumia moyoni lakini
sikuwa na namna nyingine ya
kufanya kwani Anorld alikuwa
katika mpango mbaya dhidi ya
Marekani.” Akajibu April “Nini kilifuata baada ya
Anorld kufariki?
“Sebastian ambaye ndiye
alikuwa mbebaji mkuu wa football
alinusurika na hivyo kutuaminisha
kwamba anafahamu mahala
football ilipo hivyo bado
tuliendelea kumchunguza kwa
miezi kadhaa bila kupata chochote
na tuligundua kwamba alifahamu
kila kitu kilichotokea ndani ya
ndege ile na alikuwa tayari kuanza
kufunguka kilichotokea hivyo
ikalazimu auawe.”
“Nani walimuua Sebastian
Matope? Akauliza Mathew
“Kuna kampuni moja ya ulinzi
inaitwa Chemi security hii ni
kampuni ya John Mkoka ambaye ni mkuu wa jeshi la polisi nchini na
shughuli zetu zote zinafanywa na
watu kutoka kampuni hii ambao
hupewa mafunzo ya hali ya juu na
katika operesheni za siri hutumia
sare na vifaa vya jeshi la
polisi.Sebastian Matope aliuawa na
watu kutoka kampuni hii lakini
ikasemwa kwamba aliuawa na
majambazi.Aliuawa wakati akija
nyumbani kwangu.Hili ilikuwa ni
agizo kutoka kwa CIA makao
makuu” April akaeleza kila kitu
kuhusiana na mtandao wao na
kuwataja watu wengine waliomo
katika mtandao ule ulioundwa na
CIA hapa nchini.Yalikuwa ni
maelezo ya kushangaza sana. Baada ya kumaliza mahojiano
na April Mubara wakaondoka
kuelekea ikulu kuonana na na rais
ambaye walimueleza kila kitu
walichokipata.Dr Vivian
aliwashukuru sana kwa kazi ile
kubwa na kwa msaada wote
waliomsaidia.
“Mheshimiwa rais nadhani
sasa ninaweza kusema kwamba
lile fumbo gumu lililoshindwa
kufumbuliwa limefumbuka na kila
kitu kiko wazi.Kazi uliyonituma
nimeikamilisha na watu
waliomuua kanali Sebastian
Matope wamejulikana.” akasema
Mathew na kumkabidhi Dr Vivian
karatasi yenye majina ya watu
wote walio katika mtandao wa CIA.Dr Vivian akaisoma karatasi ile
na kufuta machozi
“Sina cha kusema Mathew kwa
kazi hii kubwa
uliyoifanya.Ahsan….” akashindwa
kujizuia na kumwaga
machozi.Mathew akamfuata na
kumsihi asiendelee kulia kwani
kazi bado inaendelea
“Kazi ya kwanza imemalizika
kwa mafanikio.Bado kuna swali
linahitaji majibu.Begi la football
liko wapi? Akauliza Mathew
“Kabla ya kuanza
kulishughulikia hilo Mathew kuna
mambo ambayo nahitaji
kuzungumza nanyi” akasema Dr
Vivian “Jana usiku uliniuliza swali
kwanini CIA wamekuwa
wananifuatilia kwa muda
mrefu?Kuna sababu ya CIA
kunifuatilia kwa muda mrefu na
bado wanaendelea kunifuatilia na
mimi ninafahamu kwamba
ninachunguzwa japo sikujua kama
Nathan ni mtu ambaye alitumwa
kuja kunichunguza.Niliumia sana
niliposikia kwamba ndiye
aliyetumwa kunichunguza” Dr
Vivian akawaeleza kila kitu
kuhusiana na maisha yake na kwa
nini CIA wanamfuatilia.Aliwaeleza
kila kitu kuhusiana na Said
Bazharan na pia kuhusiana na yeye
kuandaliwa kuja kuwa rais wa
Tanzania.Yalikuwa ni maelezo yaliyowaacha midomo wazi akina
Mathew
“Kwa hiyo jamani hayo ndiyo
mambo yanayonifanya
nichunguzwe na CIA” akasema Dr
Vivian
“Ahsante Dr Vivian kutuweka
wazi kuhusiana na maisha
yako.Vipi kuhusiana na huyu
mwanao Florentina una mpango
gani naye? Mathw akauliza na
kabla Dr Vivian hajajibu kitu
akapigiwa simu akazungumza na
alipomaliza akasema
“ Kwa sasa siwezi kulijibu
swali lako Mathew kwani
nimetaarifiwa kwamba Theresa
amekwisha zinduka na anahitaji
kuniona.Ninakwenda hospitali.Mtapenda kuongozana
nami? Akauliza Dr Vivian
akaongozana na akina Mathew
kuelekea hospitali kumuona
Theresa ambaye alikwisha zinduka
na alikuwa anaendelea
vyema.Alitaka kufahamu kuhusu
maendeleo ya uchuguzi na ndipo
walipomfahamisha kila kitu
kilichotokea.
“Dada Vivian nimefurahi
kusikia yote yaliyotokea.Baada ya
kunusurika kifo kuna jambo
muhimu nataka kuwaelezeni”
akasema Theresa na kuwaeleza
kila kitu kuhusiana na
kilichotokea ndani ya ndege na
hadi walivyofanikiwa kutoka
salama yeye na baba yake na hadi baba yake alivyouawa.Ilikuwa ni
simulizi iliyomfanya Dr Vivian atoe
machozi mengi.Ilimuumiza
sana.Mwisho aliweka wazi
kuhusiana na ule mkufu wa
dhahabu aliopewa na baba yake na
ndipo Mathew alipokumbuka
kwamba alipewa vifaa vya Theresa
na kwenda moja kwa moja garini
akafungua buti ya gari na kukuta
ule mkufu upo pamoja na nguo za
Theresa.Akauchukua ule mkufu na
kwenda nao ndani.Theresa akatoa
machozi alipuona ule mkufu na
kumkabidhi Mathew aufanyie kazi
ili wajue kuna nini.Mathew
akauchunguza ule mkufu na
akagundua kwamba ule msalaba
ulikuwa ni kifaa cha kuhifadhi kumbu kumbu.Akampigia simu
Austin na kumuomba ampeleke
Camilla haraka sana pale hospitali
na baada ya dakika ishirini Camilla
akafika akapewa ule msalaba
akauchomeka katika kompyuta
yake na kukatokea kitu mfano wa
ramani ambayo walipoichunguza
iliwaelekeza kwamba kuna kitu
kimefichwa ardhini sehemu fulani
katika nyumba ya kanali Sebastian
Matope.
Walitoka pale hospitali na
kuelekea moja kwa moja
nyumbani kwa Theresa na Dr
Vivian akawaelekeza ilipokuwa
nyumba ya baba yake iliyoungua
moto na kwa kufuata maelekezo
yaliyokuwamo katika msalaba ule wakafanikiwa kuipata sehemu
ambayo ilielekeza mahala
kulikofichwa kitu alichoelekeza
Sebastian.Walichimba mahala pale
na kulikuta begi lililofichwa
kiustadi mno.
“Madam president we have
the football !! akasema Mathew
kwa furaha na kumkabidhi rais lile
begi ambaye alimwaga machozi.
“Hatimaye football begi
lililochukua uhai wa baba yangu
limepatikana” akasema kwa sauti
ndogo
Kwa pamoja walichunguza
kilichokuwamo ndani ya lile begi
na wakagundua kwamba zilikuwa
ni nyaraka zinazohusiana na
utengenezaji wa gezi ya sumu katika ambacho kilikuwa chini ya
hospitali kuu ya Msindima
“Jambo hili limekuwa siri kwa
miaka mingi na walioificha siri hii
walitegemea sisi tuje kufanya
maamuzi kuhusiana na kiwanda
hiki.Binafsi siafikiani na
utengenezwaji wa gesi ya sumu
uliokuwa unafanyika katika
kiwanda hiki hivyo kiwanda hii
kitaharibiwa na badala yake
tutatengeneza kiwanda cha
kutengeneza dawa za
binadamu.Gesi hii ya sumu ni
silaha ya maangamizi na sisi tuko
mstari wa mbele katika kupinga
silaha za maangamizi hivyo
tunatakiw akuanza kuonyesha
mfano sisi wenyewe.Nyaraka zote zilizomo katika mkoba huu wa
football zinazohusiana na
kutengeneza gesi ya sumu
zitachomwa moto ili kuuzika
kabisa mradi huu.Huu utakuwa ni
mwisho wa the football begi
ambalo lilibeba siri kubwa na
maisha ya watu wengi yamepotea
kwa sababu ya begi hili.” Hayo
yalikuwa ni maamuzi ya rais Dr
Vivian kuhusiana na kiwanda kile
cha kutengeneza gesi ya sumu
“Mathew siwezi kuchoka
kukushukuru wewe na wenzako
kwa kazi kubwa
mliyoifanya.Nisamehe sana pia
kwa sintofahamu zilizojitokeza
baina yetu wakati ukitekeleza
jukumu hili.Wewe ni mtu ambaye sina namna ya kukushukuru kwani
umeniokoa kutoka katika janga
zito.Kama si wewe sijui hivi sasa
ningekuwa katika hali gani.Pamoja
na kunisaidia kuniondoa katika
kashfa ile napenda
kuwahakikishia kwamba zile fedha
zote nitazipeleka katika miradi ya
elimu.Kampuni ile ya Tanbest
ambayo iliharibiwa kwa moto
haitakuwepo tena na ninafunga
kila kitu na sitaki tena kujihusisha
na masuala ya biashara.Nataka
niwe mtumishi mwaminifu wa
waTanzania.”
“Hayo ni maamuzi yenye
busara sana mheshimiwa
rais.Jambo hili litabaki katika vifua
vyetu tutalibeba hadi siku
tunaingia kaburini.Hatafahamu
mtu mwingine yeyote” akasema
Meshack Jumbo.
“Jambo lingine ambalo
naliomba kutoka kwenu ni
ushirikiano wenu wa karibu
sana.Tumeumaliza mtandao wa
Marekani hapa nchini na wale
wote walioshiriki katika mtandao
huo lazima wafikishwe mbele ya
sheria na kupata adhabu kali
kulingana na makosa mbali mbali
waliyoyafanya.Nawaomba muwe
karibu sana nami.Kila pale
ninapowahitaji ninawaomba
msinikimbie.Mathew ikulu ni
kama nyumbani kwako
unakaribishwa kufika muda
wowote.Time to time let’s us have drinks and exchange ideas.Ushauri
wako nitauhitaji sana.Camilla
utapewa uraia wa Tanzania na
utaishi hapa kama
ukipenda.Nimefurahishwa sana na
kazi yako kubwa
uliyoifanya.Pamoja na hayo
nitaandaa chakula maalum na
kuwaita wote ikulu ili niweze
kuwashukuru kwa kazi kubwa
mliyoifanya.Mwisho kabisa
Mathew nitahitaji kufahamu
mahala alikozikwa
Nathan.Nitahitaji pia mwili wa
Tausi upatikane ili tuweze
kuikabidhi kwa familia zao na
kuzikwa kwa heshima ”
“Ahsante sana mheshimiwa
rais.Ni heshima kubwa umenipa na nitakuja kukutembelea mara kwa
mara.Kuhusu miili ninakuahidi
yote itapatikana na nitakukabidhi”
akasema Mathew kisha wakaagana
wakaondoa pale nyumbani na
kuwaacha rais na Meshack Jumbo
OHaikua kazi nyepesi ila
tumeimaliza.Ni kazi iliyochukua
miaka zaidi ya kumi bila
kukamilika lakini sisi
tumeikamilisa ndani ya kipindi
kifupi tu.Ahsanteni sana ndugu
zangu kwani bila ninyi kujitoa kwa
hali na mali tusingeweza
kuikamilisha ile kazi ngumu na
iliyojaa hatari” akasema Mathew
na safari ikaelekea nyumbani kwa
Austin walikokuwapo akina
Peniela. Mathew alimkumbatia kwa
furaha mwanae Anna Maria
ambaye alifurahi mno kumuona
tena baba yake
“Nimefurahi sana kukuona
baba” akasema Anna
“It’s over.Kila kitu
kimekwisha.Peniela ahsante sana
kwa msaada wako mkubwa bila
wewe kuja Tanzania sijui
tungemsaidiaje Dr Vivian”
akasema Mathew
“Mathew umejitoa sana
kumsaidia Dr Vivian inaonyesha ni
rafiki yako mkubwa.Is she single?
Akauliza Peniela
“yes she’s single” akajibu
Mathew
“Mathew” akaita Peniela “Sifahamu nianzie wapi
kukueleza kuhusiana na jambo
hili”
“Jambo gani Peniela?akauliza
Mathew na Peniela akafikiri
kidogo kisha akasema
“Mathew nilikukosea sana
wakati ule.Nilifanya kosa kubwa
sana kuachana nawe kwani
nilirubuniwa na Anderson.Katika
kipindi nilichokaa na Anderson
nimegundua kwamba hakuna
mwanaume ambaye anaweza
akanifaa zaidi yako.Mathew wewe
ni wa kipekee kabisa na kwa muda
ambao nilikuwa mbali nawe
nimeona umuhimu wako.Tafadhali
Mathew nakuomba urudishe moyo
na unisamehe kwa yale yote niliyokukosea.Bado nakuhitaji
sana Mathew.Nataka mapenzi yetu
yarejee” akasema Peniela huku
machozi yakimtoka akapiga
magoti kumuomba Mathew
msamaha.
“Inuka Peniela.” Akasema
Mathew
“Mimi na wewe tulikula kiapo
mbele ya madhabahu ya Mungu
kwamba hautatengana lakini
ulipita upepo ukatutikisa na
yakatoke ayale yaliyotokea.Pamoja
na kutengana lakini sikuwahi
kuwa na mpenzi yeyote kwani
ninaamini mwanamke pekee
ambaye Mungu alinipa niwe naye
ni wewe pekee.Bado ninakupenda
sana na nio tayari kukupokea tena na kuendelea na maisha yetu kama
tulivyoapa mbele za madhabahu”
akasema Mathew na Peniela
akamkumbatia kwa nguvu huku
akimwagia mabusu mengi.Huo
ukawa ni mwanzo mpya wa
wapenzi hawa ambao meli yao
ilikumbwa na dhoruba kali kiasi
cha kuwafanya watengane
MIEZI MINNE BAADAE
Viongozi zaidi ya ishirini wa
mataifa mbalimbali duniani
walikusanyika katika ukumbi wa
kimataifa wa mikutano wa
mwalimu Nyerere kushuhudia
kutiwa saini kwa makubaliano ya
kwanza ya kudhibiti silaha kali kati ya vongozi wa mataifa ya
Marekani na Korea Kaskazini.Hii
iliwezekana baada ya rais Mike
straw na makamu wake kuachia
madaraka na kuchaguliwa rais wa
mpito Helmet Brian ambaye kwa
kusaidiana na rais wa Tanzania Dr
Vivian Matope walifanikiwa
kuumaliza mgogoro wa miaka
mingi wa Korea Kaskazini na
Marekani baada ya viongozi wa
mataifa haya mawili kukubali
kukaa meza moja na kuzungumza
na hatimaye wakakubali kuweka
kando tofauti zao na hatimaye
kusaini mkataba wa amani baina
ya nchi hizi mbili na huu ukawa ni
mwanzo mpya wa mashirikiano
kati ya Marekani na Korea Kaskazini jambo ambalo hakuna
aliyewahi kuota kama
lingewezekana
Kwa mara nyingine tena
Tanzania ikangia katika historia ya
dunia kwa kuumaliza mgogoro huu
uliotishia amani ya dunia.Amani
kwa dunia ikarejea kwani
hakukuwa tena na kitisho cha
kuibuka vita ya tatu ya dunia
Ilikuwa ni siku ya furaha
kubwa kwa Mathew kuonana tena
na Camilla ambaye kwa sasa ni
mmoja kati ya walinzi wa rais
Helmet Brian.Camilla alifurahi
sana kumuona Theresa akiwa
tayari amepona na anaendelea
vyema. “Nimepitia operesheni nyingi
ngumu lakini sikuwahi kupitia
operesheni ngumu kama hii ya
kulifumbua fumbo la THE
FOOTBALL” akasema Mathew na
wote wakakumbatiana kwa furaha
wakipongezana kwa kuifanikisha
operesheni ile ngumu.
TAMATI