Simulizi : The Football
Sehemu Ya Tano (5)
alikuwa ni mtu muhimu katik
auchunguzi wetu na nilitarajia
sana kupata habari nyingi kutoka
kwake lakini naomba maumivu
haya yote yabaki ndani mwetu na
jambo hili libaki siri yetu io ili
uchunguzi endelee.Nathan
amekuja Tanzania kimya kimya na
apotee kimya kimya”akasema
Mathew “Mathew umeongea mambo
mengi lakini hakuna hata moja
lililoingia kichwani
mwangu.Nataka kusikia kitu
kimoja tu.Wapi ulipo mwili wa
Nathan?
“Mheshimiwa rais mwili wa
Nathan hautaweza kupatikana kwa
sababu tayari umekwisha pelekwa
mafichoni kwa hiyo hautaweza
kuonekana.Suala hili litabaki kama
lilivyo na hakuna atakayegundua
kama Nathan amefariki.”
“Umefanya nini Mathew?
Akauliza Dr.Vivian
“Mwili wa Nathan tayari
umepelekwa kwenda kuzikwa
mahala ambako hakuna atakayeweza kupafahamu”
akasema mathew
“Mathew nitakufunga miaka
isiyo na idadi gerezani kama hili
unalonieleza ni la kweli.Tafadhali
naomba uni…………….” Mara simu
ya Mathew ikaita ,akaitoa mfukoni
na kutazama mpigaji alikuwa ni
Meshack Jumbo.Haraka haraka
akaipokea
“Hallo mzee Meshack”
akasema Mathew
“Mathew I’m in trouble !!
akasema Meshack Jumbo huku
akihema kwa kasi
“What trouble?!
‘Mathew fanya haraka
nitafutie msaada kama uko karibu
na rais” “Mzee Meshack hebu tulia na
unieleze nini kimetokea?
“Nimevamiwa nyumbani
kwangu na askari ambao wameua
walinzi wangu na sasa wamevamia
ndani wanapekua kila mahali”
“Wewe uko wapi mzee Jumbo?
“Nimewahi kutoka na mke
wangu na msichana wetu wa kazi
tumekuja kujificha huku
shambani.Tulisikia milio ya risasi
hivyo nikawahi kuitoa familia
yangu haraka.Tafadhali naomba
msaada wako.Niombee msaada
kwa rais kwani watuhawa
wnaonekana hawana nia njema”
akasema Meshack Jumbo
“Sawa Mzee.Endelea kujificha
hapo hapo wakati naangalia kitu cha kufanya ,rais niko naye hapa
karibu nitamueleza na msaada
unakuja muda si mrefu” akasema
Mathew na kukata simu
akamgeukia Dr.Vivian
“Meshack Jumbo yuko katika
matatizo makubwa na anahitaji
msaada wa haraka sana” akasema
Mathew
“Kuna nini kimetokea?
Dr.Vivian akauliza
“Meshack anasema kwamba
amevamiwa na watu wenye mavazi
ya askari polisi wameua walinzi
wake na wameingia nyumbani
kwake wanapekua kila kona ya
nyumba yake.Anahitaji msaada wa
haraka sana” akasema Mathew
“Oh my God ! is he ok? “Yeye na familia yake
wamefanikiwa kutoka kabla
wavamizi hao hawajaingia ndani
na wamejificha shambani.Msaada
wa haraka unatakiwa ili kumsaidia
kwani hatujui watu hao wana
lengo gani na kuna uwezekano
kama wakikosa wanachokitafuta
watakwenda kuwatafuta shambani
mahala walikojificha”
“Jamani ! Mambo gani haya
yanatokea? Akasema Dr.Vivian
“Madam president msaada wa
haraka mno unahitajika” akasema
Mathew.Dr.Vivian akachukua simu
na kumpigia mkuu wa jeshi la
polisi na kumtaarifu kuhusiana na
tukio lile la kuvamiwa nyumba ya
Meshack Jumbo akamtaka atume askari waelekee hapo haraka sana
kumuokoa Meshack na familia
yake.
“Mathew hao watu
wanaotumia mavazi na sare za
askari wetu ni akina nani?akauliza
Dr.Vivian
“Mheshimiwa rais hao watu
lazima watafutwe haraka sana
kwani hata sisi tulivamiwa na watu
kama hao waliokuwa na sare na
magari ya polisi.Naomba kwa sasa
nielekee kwa Meshack Jumbo
kutoa msaada.Nitakuja baada ya
kutoka kwa Meshack Jumbo ili
tuendelee na mjadala wetu”
akasema Mathew na kutoka
haraka akaingia katika gari na kuondoka ikulu kuelekea kwa
Meshack Jumbo
“Hawa watu wanaotumia
mavazi ya askari ni akina nani?
Kwanza walituvamia sisi na
baadae wakatoweka baada ya
askari wenzao kutokea.Meshack
Jumbo anadai kwamba naye
amevamiwa na watu wale wale
wenye sare za askari polisi.Ni
akina nani hawa? Wanatafuta
nini?akajiuliza Mathew akiwa
katika mwendo mkali kuelekea
kwa Meshack Jumbo
“Taratibu ninaanza
kuwahusisha hawa watu hawa
wanaotumia mavazi ya askari na
mtandao wa siri ambao sifahamu
lengo lake ni nini.Kama wangekuwa ni askari polisi wa
kweli basi wasingekimbia baada
ya wenzao kutokea.Halafu
inaonekana walipewa taarifa ya
ujio wa wale askari kwani niliona
wanahimizana kuingia katika
magari yao na kuondoka kwa kasi
kubwa.Hili suala lazima
nilifukuliwe na niufahamu huu
mtandao wa askari wanaotumia
sare na vifaa vya jeshi la polisi
.Wanatafuta nini kwa Meshack
Jumbo? Kwa nini wakamvamia
usiku huu? Akajiuliza Mathew
“Hili suala litafukua vitu vingi
sana vilivyojificha kwani kila
ninavyozidi kuchimbua ndivyo
mambo mengi zaidi
yanavyoendelea kuibuka.Alianza Fakrim,akaja Nathan na sasa
limeibuka kundi la askari
wanaovamia na kutoweka ambao
nina uhakika mkubwa kwamba
wanatumiwa kwa ajili ya kazi
fulani.Nani anawatuma na kwa
nini?Nikiweza kupata fununu
kuhusiana na haa askari polisi
hawa basi nitaweza kugundua
jambo kubwa “ akawaza Mathew
Alikaribia kufika nyumbani
kwa Meshack Jumbo na kukuta
mtaa ukiwa katika heka heka
kubwa na watu walikuwa
wameamka .Magari ya poilisi
yaliwasha vimuli muli.
“Mtaa umejaa
watu,inaonekana kulitokea
mtafaruku mkubwa nyumbani kwa Meshack.Nadhani askari polisi
walifika kwa wakati kama
walivyotakiwa na rais” akawaza
Mathew akiendesha gari kwa
tahadhari kuelekea nyumbani kwa
Meshack Jumbo.Mita kadhaa
akakuta kuna uzio wa askari
akashuka garini na kujitambulisha
kuwa anatoka ikulu na
akaruhusiwa kupita .Kulikuwa na
gari nne za zimamoto na
wafanyakazi wa zimamoto
walikuwa wanamalizia kuuzima
moto uliokuwa unawaka.Jumba la
Meshack Jumbo lilikuwa
limeteketea kwa moto.Mathew
akahisi kuchanganyikiwa
“Oh my God ! akasimama nje
ya gari akishuhudia shughuli iliyokuwa inafanywa na askari wa
kikosi cha zimamoto.Eneo lote la
kuzunguka nyumba ya Meshack
Jumbo lilikuwa limezingirwa na
askari polisi wenye silaha.Mathew
akampigia simu Meshack Jumbo na
kumjulisha kwamba tayari
amekwisha fika na Meshack
akamuelekeza mahala
alipo,akamfuata
“Pole sana mzee Jumbo.Wote
wazima ?
“Sote wazima Mathew.Ahsante
sana kwa msaada wa haraka.Mara
tu baada ya kukupigia simu
hazikupita hata dakika kumi polisi
wakafika hapa kwa bahati mbaya
walikuta tayari nyumba imeanza
kuwaka moto lakini nawashukuru pia kikosi cha zimamoto kwani nao
walifika kwa wakati na kama
unavyoona wanamalizia kuuzima
moto” akasema Meshack
“Pole sana mzee
wangu.Kikubwa nashukuru wewe
na familia yako mko salama.Mzee
Meshack naomba tusogee kidogo
pembeni tuzungumze” akasema
Mathew
“Mathew naomba unisubiri
kama dakika kumi hivi nimalizane
kwanza na kamanda wa polisi
halafu tutazungumza” akasema
Meshack Jumbo na kumuacha
Mathew, akaenda kuzungumza na
kamanda wa polisi aliyeongozana
na kikosi kile cha askari waliofika
pale nyumbani kwake. “Huu ni ukatili mkubwa
sana.Ni akina nani hawa
wanafanya mambo haya? Hawa si
askari polisi.Hili ni genge la
wahalifu ambao wanatumia sare
na vifaa vya polisi na kujifanya
askari ili kuweza kufanikisha
mambo yao ya kihalifu.Ninaapa
lazim….” Mathew akatolewa
mawazoni na simu yake iliyoita
alikuwa ni rais akaipokea haraka
“Hallow mheshimiwa rais”
“Umekwisha fika nyumbani
kwa Meshack?
“Ndiyo mheshimiwa rais
nimekwisha fika hapa nyumbani
kwa Meshack Jumbo.Yuko salama
yeye na familia yake lakini nyumba
yake imeteketezwa kwa moto na kikosi cha zimamoto wamejitahidi
sana kufika kwa wakati na hivi
sasa wanamalizia kuuzima moto
huo.”
“Dah ! akasema rais na kuvuta
pumzi ndefu
“Umefanikiwa kuonana na
kuzungumza na Meshack Jumbo?
Askari polisi walifika kwa wakati
na kuwazuia hao askari wavamizi?
Wamefanikiwa kumpata hata
mmoja ili tuwafahamu ni akina
nani?akauliza rais
“Mheshimiwa rais
nimefanikiwa kuonana na
Meshack Jumbo lakini kwa hivi
sasa bado anatoa maelezo kwa
polisi na atakapomaliza nitapata
nafasi nzuri ya kuweza kuzungumza naye kwa upana
namna jambo hili lilivyotokea .Kwa
ufupi tu aliniambia kwamba askari
wale walifika kwa wakati sana ila
bado hajaweka wazi kama
walifanikiwa kuwapata wale
askari
wavamizi.Nitakapozungumza naye
muda mfupi ujao nitalifahamu
hilo.Mheshimwa rais ninakusihi
usihofu hawa watu watafahamika
tu.Mpaka hapa tunauhakika hawa
si askari wetu bali watakuwa
wanatumia sare na vifaa vya jeshi
letu.Nakuahidi kuwasaka hadi
kuwapata hawa watu”
“Mathew hawa watu
wanapaswa kutafutwa kwa udi na
uvumba hadi wapatikane kwani wameanza kuleta hofu
kubwa.Wanaonekana ni watu
wenye kufahamu mambo
mengi.Baada ya kutoka hapo
nakuhitaji uje hapa ikulu pamoja
na Meshack na familia
yake.Nitawatafutia sehemu ya
muda ya kuishi wakati
tunashughulikia kuyajenga upya
makazi yao.Halafu mimi na wewe
bado tuna mazungumzo” akasema
Dr.Vivian
“Mheshimiwa rais kuna jambo
nataka nikuombe”
“Unataka nini Mathew?
“Mapema uliniambia kwamba
nisiendelee na uchunguzi wangu
lakini nakuomba mheshimiwa rais
niendelee na uchunguzi wangu kwani mambo mengi yameanza
kuibuka likiwamo na hili kundi la
askari polisi wavamizi.Niachie
nimalizie uchunguzi wangu kwani
nikiachia hapa utakua ni ushindi
kwao mheshimiwa rais.Hatupaswi
tuwape ushindi”
“Mathew tutalizungumza hilo
utakapokuja huku ikulu. Lakini
naomba nikuweke wazi kwamba
nimekwisha kifunga kitabu hicho
kwa hiyo usitegemee nikifungue
tena” akasema Dr.Vivian na kukata
simu
“Theresa alikosea sana
kumuua Nathan.Nilifahamu
mambo kama haya yangeweza
kutokea na ndiyo maana nikataka
kufanya uchunguzi wangu kwa siri bila Dr.Vivian kufahamu
chochote.Sasa Dr.Vivian
amefahamu na kila kitu
kimesimama.Hataki niendelee
tena na uchunguzi wangu .Huu si
utani ni kweli hataki niendelee na
uchunguzi kwani ni kawaida yake
kutokurudi nyuma akishafanya
maamuzi yake.Atakuwa amefanya
kosa kubwa sana kuliacha suala
hili kati kati.Nilikaribia sana
kuanza kuupata mwanga “
akawaza
“Lakini hapana siwezi kufanya
anavyotaka rais.Siwezi kuachana
na hili suala.Hata kama yeye
hataki niendelee na uchunguzi
wangu mimi nitaendelea
kimyakimya bila ya kumshirikisha yeye na hadi niufahamu
ukweli.Sijawahi hata mara moja
kufanya uchunguzi na kuishia
njiani.Ninapoanza uchunguzi
wangu lazima nihakikishe
nimefika mwisho na majibu
yakapatikana na kama kuna
wahalifu basi wanafikishwa mbele
ya sheria.Lazima Tanzania
tufahamu wanachokitafuta
Marekani katika nchiyetu kwani
suala hili limekwisha onyesha
dalili kwamba limevuka mipaka ya
nchi kwa hiyo siwezi kuliacha hivi
hivi.Lazima nifahamu sababu ya
Dr.Vivian kuchunguzwa na
Marekani .Lazima ipo sababu ya
kumchunguza.Hawawezi kupoteza
muda wao kumchunguza kama hakuna jambo la msingi
wanalolitaka” akawaza Mathew na
Mzee Meshack akatokea
“Samahani kwa kukuacha
peke yako .Pilikapilika nyingi
sana.Nakuomba tusogee huku
pembeni” akasema Meshack
Jumbo wakasogea pembeni
“Siamini kilichotokea mzee
Jumbo.Pole sana mzee
wangu.Dakika chache zilizopita
hapa palisimama jumba la kifahari
lakini sasa limebaki gofu.Huu ni
ukatili mkubwa.Pokea salamu
nyingi za pole toka kwa rais na
amenitaka tukitoka hapa
tuongozane kuelekea ikulu wewe
na familia yako” “Ahsante sana
Mathew.Kikubwa
ninachomshukuru Mungu ni
kwamba mimi na familia yangu
wote tuko salama
kabisa.Nasikitika nimewapoteza
walinzi wangu wote wawili
.Imeniuma sana” akasema
Meshack Jumbo na kuinamisha
kichwa
“Hebu nipe picha halisi ya
kilichotokea mzee Jumbo lakini
kabla hujanieleza chochote nataka
kufahamu je lile begi nililoliacha
hapa liko salama nalo ni mojawapo
ya vitu vilivyoteketea? Akauliza
Mathew
“Lile begi liko salama.Ni kitu
pekee nilichofanikiwa kuokoa kwani naamini lina umuhimu
mkubwa sana”
Mathew akashusha pumzi kwa
jibu lile la Meshack Jumbo.Tayali
aliamini lile begi lenye vifaa
alivyotoa kwa Nathan liliteketea.
“ Nikiwa maktaba nikiendelea
na kazi zangu kwani niliamini
baada ya kutoka kwa rais lazima
ungerudi hapa hivyo sikutaka
kulala mapema,nilisikia mbwa
wangu wakibweka sana na mara
nikasikia milio ya risasi.Nikazima
taa zote ndani na kwenda
kuangalia runinga
iliyounganishwa na kamera za
ulinzi na hakukuwa na picha
zozote .Nikajua tayari kulikuwa na
tatizo.Nikawaamsha haraka mke wangu na binti yetu wa kazi
nikachukua kompyuta yangu
ndogo na lilebegi ulilolileta
tukaenda mafichoni.Hapa kwangu
nina sehemu ya siri ya
kujificha.Kuna njia ya chini kwa
chini ya kwenda kutokea
shambani.Niliitengeneza maalum
kwa ajili ya nyakati kama
hizi.Tulitoka mle ndani
kimyakimya na kwenda kujificha
shambani ndipo nikapata nafasi
ya kukupigia simu kuomba
msaada.Tukiwa tumejificha
shambani nilifanikiwa kuwaona
wale wavamizi wakiwa wamevaa
sare za polisi wakiwa na silaha kali
wakiwa wameizunguka nyumba
yangu wakipekua kila sehemu Wakifunua kila mfuniko
waliouona.Baada ya muda
nikawaona askari wanne
wakielekea mahala tulipokuwa
tumejificha mmoja wao akiwa na
kitu kama simu kubwa ambacho
nahisi kilikuwa kinampa
maelekezo.Alipofika karibu na
pale tulipokuwa tumejificha
wakasimama na nikaona
wanaelekezana jambo.Mimi tayari
nilikuwa na bastora nimejiandaa
kwa lolote.Mara ghafa yule jamaa
aliyekuwa na ile simu kubwa
mithili ya tablet akapigiwa simu na
kwa haraka sana wakaondoka
huku wakikimbia na hazikupita
dakika tatu jumba langu likaanza
kuwaka moto. Niliwapigia simu jeshi la zimamoto na wakafika kwa
haraka sana na hata polisi nao
walifika kwa wakati kabisa lakini
hakuna hata mmoja wao
aliyekamatwa “ akasema Meshack
Jumbo
“Who are they? Akauliza
Mathew
“Swali hilo ni dogo lenye
maneno matatu lakini majibu yake
ni magumu kupatikana kwa
haraka.Mathew wale watu siwezi
kusema kwamba si askari
polisi.Ninawafahamu askari na
wale jamaa walisogea karibu
kabisa na mahala nilipokuwa na
nikawatazama japokuwa wao
hawakuwa wananiona wale ni
askari kabisa tena wenye mafunzo ya hali ya juu kwani utaona kabla
ya kuingia ndani waliharibu
kamera zote ili kusiweze kuwa na
picha yoyote ya kuwafanya
watambulike hii inaonyesha hawa
si watu wa kawaida.Hata wewe
ulisema kwamba ulizingirwa na
askari waliokuwa wamejihami
vilivyo na walipotea mara tu askari
wenzao walipotokea .Hicho ndicho
kilichotokea hapa.Inaonekana
kuna watu ndani ya jeshi la polisi
wanawajiulisha kwamba kuna
askari wanakuja nao huondoka
haraka” akasema Meshack
“Ninaamini wale wale
waliotuvamia usiku huu kule
Uwazi Roadi ni hawa hawa
waliokuja hapa kwako.Je walikuwa wananifuatilia mimi? Walijuaje
kama niko hapa? Mathew akauliza
“Sina hakika kama walikuwa
wanakufuatilia wewe.Hawa kuna
kitu walikuwa wanakitafuta kwani
walikuwa na ile tablet iliyokuwa
inawapa maelekezo na wao
walikuwa wanaifuata hiyo ndiyo
maana walikaribia sana kufika
mahala nilipokuwa
nimejificha.Kama si kupigiwa simu
basi tungekuwa tunazunguma
mambo mengine” akasema
Meshack Jumbo.Mathew
akainamisha kichwa akatafakari
kidogo na kusema
“Mzee Jumbo inabidi
tuwaachie askari polisi suala hli
walishughulikie na watatupa majibu ni nani hawa askari
wanaotuvamia.Nadhani sasa
tuondoke twende ikulu na askari
polisi wataendelea kuwepo hapa
hadi kesho utakapofanyika
uchunguzi.” Akasema Mathew na
mzee Jumbo akaenda kuzungumza
na kamanda wa polisi aliyeongoza
kikosi cha askari waliofika pale
kwake na kumjulisha kwamba
ameitwa na rais ikulu hivyo yeye
na familia yake wanaondoka na
watawaachia askari polisi
waendelee na shughuli zao za
uchunguzi.Mzee Jumbo akarejea
akiwa ameongozana na mke wake
pamoja na mtumishi wao wa ndani
akamkabidhi Mathew mkoba wake
wenye zile simu tatu pamoja na saa alivyovitoa kwa Nathan kisha
wakoandoka kuelekea ikulu.
Mzee Jumbo sipati neno zuri
la kusema ila naomba wewe na
familia yako mfahamu kwamba
nimeguswa sana na hiki
kilichotokea na kwa niaba yangu
mwenyewe na watanzania wote
itoshe kusema pole
sana.Ninawaahidi kwamba hawa
wote waliofanya kitendo hiki cha
kikatili watatafutwa kokote waliko
na watapatikana.Hakuna
atakayesalia.”akasema Dr.Vivian
baada ya Meshack Jumbo na
familia yake kuwasili ikulu kuonana na rais kama alivyokuwa
ameelekeza
“Nashukuru sana rais na
kikubwa tunachoshukuru kwamba
sote ni wazima isipokuwa
tumewapoteza walinzi wetu
wawili.”akasema Meshack Jumbo
“Poleni sana.” Akasema rais na
kumuita mmoja wa walinzi wake
akamuelekeza jambo halafu
akawaelekea akina Meshack
“Mzee Meshack ,mama na
binti watakwenda kupumzika
mahala nilikoandaa kwa ajili yenu
kupumzika wakati tunawaandalia
sehemu nzuri ya kuishi ili nyumba
yenu iweze kufanyiwa ukarabati
mkubwa.Meshack Jumbo wewe
bado nahitaji uwepo hapa kuna mambo ya kujadili usiku huu”
akasema rais na mke wa Meshack
Jumbo na mtumihsi wao wa ndani
wakachukuliwa wakapelekwa
mahala alikoagiza rais paandaliwe
kwa ajili yao.Sebuleni walibaki
rais,Mathew,Meshack Jumbo na
Theresa.
“Mzee Jumbo narudia tena
kwa mara nyingine kukupa pole
kwa hili lililoikumba familia
yako.Kwa kuwa wote tuko hapa
nadhani ni wakati mzuri wa
kuweza kulijadili hili jambo.Hawa
watu ni akina nani ?Kweli ni askari
wetu? Wanatumwa na nani?
Akauliza Dr.Vivian “Mheshimiwa rais hawa watu
ni askari wa jeshi letu la polisi”
akasema Meshack Jumbo
“Mheshimiwa rais,ili
kuwafahamu watu hawa ni akina
nani inabidi tuunganishe tukio
lililotokea kwa Meshack Jumbo na
lile lililotupata mimi na Theresa
ambapo tulivamiwa na watu hao
ambao walikuwa na sare na vifaa
vya jeshi la polisi.Walikuwa na
magari na silaha za kivita.Baada ya
kukuomba msaada na ukatuma
askari kutusaidia wale wavamizi
wakakimbia.Kabla ya kuja hapa
nilikwenda kwanza kwa Meshack
Jumbo nikachukua gari lake na
kuja hapa na muda mfupi baada ya
mimi kuondoka nyumba yake imevamiwa na watu wale wale
wenye sare za polisi na kama
ilivyotokea kwetu watu wale
waliondoka haraka kabla polisi
hawajafika.Wale waliotuvamia
mimi na Theresa ni hawa hawa
waliomvamia Meshack Jumbo na
ninahisi hawa jama walikuwa
wananifuatilia mimi na
walifahamu kwamba niko pale
kwa Meshack Jumbo na ndiyo
maana wakavamia na kufanya
uharibifu ule mkubwa.Hawa kama
alivyosema Meshack ni askari
polisi lakini wanafanya matukio
haya kwa siri na ndiyo maana
hutoweka haraka baada ya
kupewa taarifa kwamba askari wenzao wanakuja” akasema
Mathew
“Una maanisha kwamba kuna
kikundi ndani ya jeshi la polisi
wanaofanya maovu haya? Rais
akauliza
“Kwa namna inavyoonekana
iko hivyo mheshimiwa rais”
akasema Mathew
“Kama ni hivyo lengo lao ni
nini? Nani anawatuma? Akauliza
rais
“Hatuwezi kupata majibu ya
maswali hayo mheshimiwa rais
bila kufanya uchunguzi ndiyo
maana ninakuomba uniruhusu
niendelee kufanya uchunguzi wa
suala hili.Kuna mambo mengi
yamejificha katika jambo hili na kadiri tunavyoendelea kulichimba
yazidi kuibuka na usiku wa leo
tumegundua uwepo wa kikundi
hiki cha askari polisi ambao
hatujui nani anawatuma
kutufuatilia na wanaonekana wana
lengo baya na sisi” akasema
Mathew
“Mathew unachosema ni kweli
kabisa kwamba tunahitaji sana
kufahamu kuhusu hawa askari
lakini utanisamehe kwani
nimekwisha sema sitaki uendelee
tena na uchunguzi wa suala
hili”akasema rais
“Madam preside…”
“I’m sorry Mathew tayari
nimekwisha fanya maamuzi”
akasema rais “Mheshimiwa rais..” Mathew
akataka kusema kitu lakini rais
akamzuia
“Mathew kama unataka
kuliongelea suala hili tafadhali
naomba usijisumbue kwani siwezi
kubadilisha msimamo wangu.It’s
over !!
“Whats going on here?
Akauliza Meshack Jumbo
Dr.Vivian akawatazama
Mathew na Theresa halafu
akasema
“Mzee Meshack nimeamua
kusitisha ule uchunguzi aliokuwa
anaufanya Mathew”
“Umesitisha?!! Kwa nini
mheshimiwa rais? Akauliza
Meshack Jumbo “Nimeamua hivyo mzee wangu
na atakueleza Mathew mwenyewe
kwa nini nimeamua hivyo”
akasema Dr.Vivian huku
akimtazama Mathew kwa hasira
“Madam president hili si suala
jepesi na haliwezi kuachwa hivi
hivi.Kuna tatizo lolote limetokea
na kukufanya usitishe uchunguzi
huu ambao tayari Mathew
amekwisha piga hatua na sasa
anaelekea kuzuri? Akauliza
Meshack
“Nimeamua hivyo mzee wangu
kwa sababu toka nilipompa
Meshack kazi hii hakuna kitu
chochote cha maana ambacho
amekifanya zaidi ya kuniongezea
matatizo kila uchao.Nimeamua kuachana na kazi hii.Sitaki tena
kutaka kuwajua watu waliomuua
baba yangu”
“Mheshimiwa rais tafadhali
mwanangu naomba kama kuna
tatizo limetokea litafutiwe
ufumbuzi lakini si kusitisha
uchunguzi huu ambao ni wa
muhimu sana sana.Kwa zaidi ya
miaka kumi sasa toka lilipotokea
tukio hakuna hatua yoyote
iliyowahi kupigwa katika
kufahamu ni akina nani walifanya
tukio lile lakini kwa siku hizi mbili
Mathew amefanya uchunguzi wake
na tayari kuna mwanga umeanza
kuonekana.Haya yote yaliyotokea
usiku wa leo ni matokea ya kazi
nzuri anayoifanya Mathew.Tafadhali mheshimiwa
rais usiliache suala hili njiani “
akasema Meshack Jumbo
“Mzee Jumbo nakuheshimu
mno lakini tayari nimekwisha
fanya maamuzi yangu na siwezi
kubadili nilichokiamua.Uchunguzi
huu hautaendelea.Ninashukuru
kwa namna Mathew alivyojitolea
na kuifanya kazi hii na kwa kipindi
kifupi imeweza kuleta mwanga
lakini sihitaji aendelee zaidi ya
hapa.Imetosha mzee Jumbo.”
“Kuna nini madam president
hadi ukaamua kusitisha uchunguzi
huu muhimu? Akauliza Meshack
“Meshack naomba
tusiliongelee hilo kwani hakuna
kauli inayoweza kubadilisha msimamo wangu.Nimeamua hivyo
na itabaki hivyo.Naomba
tusipoteze muda kulizungumzia
hilo.Tuendelee na masuala
mengine”
“Madam president No !
Hatuwezi kuachana na suala hili
kubwa ambalo linauweka hadi
usalama wa taifa
mashakani.Usalama wako uko
mashakani pia.Hili ni suala nyeti
sana hatuwezi kuliacha likaenda
hivi hivi.Rais Anorld aliuawa ,baba
yako aliuawa na hatua zimeanza
kupigwa kuupata ukweli wa nani
waliowaua kwa hiyo hatuwezi
kuliacha jambo hili hewani kama
lilivyoachwa miaka kumi
iliyopita.Binafsi siko tayari kuliona jambo hili likiishia hapa.Nataka
liendelee hadi lifike mwisho
wake.Madam president nakuomba
sana nafahamu wewe ni rais
mwenye msimamo mkali na ni
kawaida yako kusimama katika
maamuzi yako lakini nakuomba
kwa mara ya kwanza uende
kinyume na maamuzi yako na
uruhusu suala hili liendelee.”
Akasema Meshack Jumbo na
Dr.Vivian akasimama akiwa
amefura hasira
“Naomba tuelewane
jamani.Mimi ndire rais wa
jamhuroi ya muungano wa
Tanzania.Mimi ndiye mwenye
kuamua nini kifanyike na nani
afanye.Kauli yangu ni ya mwisho.Nimekwisha amua
kwamba suala hili halitaendelea
tena na huo ndio msimamo wangu
kwa nini mnakuwa wagumu
kunielewa? Akauliza Dr.Vivian kwa
hasira.Meshack Jumbo naye
akasimama na kumtazama rais
“ Is this because of Nathan’s
death? Akauliza.Dr.Vivian
hakujibu kitu alikuwa
ameinamisha kichwa
“Answer me madam president
is it because of Nathan’s death?
Akauliza tena Meshack
Jumbo.Dr.Vivian akainua uso wake
ulikuwa umeloa
machozi.Alishindwa kujiuzia
akaangusha kilio.Mathew akamfuata akamshika mkono na
kumketisha sofani.
“I’m sorry madam president”
akasema huku akimpiga piga
mgongoni.
“Let’s leave her alone for a
while” akasema Mathew na wote
wakatoka nje wakamuacha
Dr.Vivian peke yake akilia.
“Kwa namna yoyote ile zoezi
hili la uchunguzi haliwezi kuishia
hapa.Lazima uchunguzi
uendelee.Hatua kubwa imekwisha
pigwa kwa hiyo hatuwezi kuishia
njiani.Lazima tutumie kila namna
ya ushawishi kumfanya rais
akubali uchunguzi huu uendelee.”
Akasema Meshack Jumbo “Nilijua haya yote yatatokea
na ndiyo maana nikawa sitaki
uchunguzi huu ufanyike kwani
ungeibua mambo mengi ya
hatari.Hata hivyo kuna kitu
nimekigundua hapa.Baba aliuawa
na kikundi cha askari polisi ambao
niliwashuhudia mwenyewe kwa
macho yangu.Mambo yaliyotokea
usiku wa leo yamenifanya niamini
kwamba kuna mtandao mkubwa
ndani ya serikali ambao unatumia
kikundi cha askari polisi kwa ajili
ya shughuli zao.Nina hakika kabisa
wale askari waliotuvamia mimi na
Mathew na hawa waliokwenda
kuvamia na kuichoma nyumba ya
Meshack Jumbo ni kitu kimoja na
wale walimuua baba.Natamani nimueleze Mathew lakini naogopa
nisije nikaongeza matatizo
zaidi.Ngoja niliache suala hili kama
lilivyo.” Akawaza Theresa
“Nini hasa lengo la hawa
jamaa? Akauliza Meshack Jumbo
“Mzee Jumbo kama
nilivyosema awali kwamba hawa
jamaa lazima watakuwa
wananifuatilia mimi kwani
walituvamia njiani wakashindwa
kunipata na baadae wakanifuata
nyumbani kwako na waliamini
lazima nitakuwa pale”akasema
Mathew.Kukawa na ukimya kila
mmoja akiwaza lake na mara Mzee
Jumbo akasema
“Wale watu walikuwa na kifaa
walichokuwa wanakifuata kilichowaongoza hadi mahala
nilipokuwa.Hili limenifanya
nijiulize maswali mengi yasiyo na
majibu kwamba waliwe…..”
“Mr Jumbo wait” akasema
Mathew
“Kuna kitu nimekifikiria
kutokana na hayo maelezo yako.”
“Kitu gani Mathew? Akauliza
Meshack
“Unasema hao jamaa
walikuwa na kifaa kilichokuwa
kinawaelekeza na wakafika hadi
eneo ulilokuwa umejificha na kwa
bahati nzuri hawakuweza
kuendelea baada ya kutaarifiwa
kwamba kuna askari wanakuja
kwako hivyo wakaondoka haraka
sana.Hii inanifanya niamini kwamba kuna kitu walikuwa
wanakitafuta.Katika mkoba ule
niliouleta kwako kuna simu tatu za
Nathan pamoja na saa ya
mkononi.Ninahisi yawezekana
kifaa hicho unachokisema
walikuwa wanakifuatilia kilikuwa
kinanasa mawimbi ya mojawapo
ya kifaa na ndiyo maana waliweza
kufika hadi nyumbani kwako na
kama haitoshi wakakaribia hadi
eneo ulilokuwa umejificha kwa
msaada wa hicho kifaa
chao.Ninahisi hivyo kwa sababu
sioni sababu ya kuja kuvamiwa
nyumbani kwako na kufanya
uharibifu ule mkubwa.Kwa nini
iwe leo usiku tena baada ya mimi
kuuleta mkoba ule na kuondoka?Lazima walikuwa
wanaufuatilia ule mkoba na kifaa
hicho walichokuwa nacho kilikuwa
kinanasa mawimbi ya mojawapo
ya vitu vilivyokuwamo ndani ya
mkoba” akasema Mathew
“Mathew hiki unachokisema
kinaweza kuwa na mashiko na
hata mimi naweza kuamini
hivyo.Nimejiuliza sana sababu ya
kuvamiwa na sijaona kwa nini
nivamiwe.Watu wale hawakuwa
majambazi bali walivamia
wakitafuta kitu fulani mahususi
ambacho walikuwa na uhakika
kitakuwemo mle ndani.Sasa
nimepata picha kwamba
yawezekana walikuwa
wanalitafuta lile begi.Kile kifaa walichokuwa nacho kilikuwa
kinawaelekeza mahala begi lile
lilipo.Mwanga unaanza
kupatikana” akasema Meshack
Jumbo
“Mwanga unaanza kupatikana
lakini je hawa watu wana
mahusiano gani na vifaa vya
Nathan? Kwa nini wavitafute?
Mathew akauliza
“Hapo ndipo swali linapokuwa
gumu na linahitaji majibu”
akasema Meshack
“Ninahisi yawezekana wale si
askari bali ni kikundi cha watu
wanaotumia sare na vifaa vya
askari polisi kufanikisha mambo
yao. Kama ni hivyo basi lazima
kikundi hicho kina mashirikiano na Nathan na kama jibu ni ndiyo
basi kuna mtandao mrefu tayari
hapa nchini unaotumiwa na akina
Nathan na kwa kuwa Nathan ni CIA
basi lazima mtandao huo pia
utakuwa chini ya CIA na kama jibu
ni ndiyo basi lazima kuna jambo
kubwa wanalolitafuta hapa
Tanzania” akasema Mathew
“Mathew mtiririko huu
uliouelezea umenifanya niipate
picha kamili ya hili
jambo.Tukifahamu kuhusu
kikundi hicho cha askari polisi hao
wavamizi tutaweza kufahamu
mambo mengi yaliyojificha”
“Hilo litawezekana endapo tu
rais atakuwa tayari uchunguzi
uendelee.Kama ataendelea kuushikilia msimamo wake
kwamba uchunguzi huu ufikie
mwisho basi hakuna
kitakachoweza kujulikana na
atakuwa amefanya kosa kubwa
sana kwani hatujui nini lengo la
hawa jamaa.Wametengeneza
mtandao ndani ya
serikali,wanakusanya taarifa
mbali mbali za rais na hatujui
wana malengo gani” akasema
Mathew
“Mathew kwa namna yoyote
ile hatuwezi kuliacha suala hili
liishie hapa.Lazima tuhakikishe
limefika mwisho.Lazima ukweli
ujulikane.Lazima tuhakikishe
tunamshawishi rais kwa namna
yoyote ile akubali suala hili liendelee.Mathew tafadhali kijana
wangu nakusihi usikatishwe tamaa
na rais.Hata kama hataki suala hili
liendelee sisi lazima tuliendeleze
hata kwa siri bila ya yeye
kufahamu.Lazima tukubaliane sote
kwa pamoja kwamba suala hili
litaendelea.Theresa are you with
us?Mathew anakuhitaji sana kwa
ajili ya kupata nyaraka mbali
mbali muhimu” Akauliza Meshack
Jumbo na Theresa hakujibu kitu
akainamisha kichwa
“C’mon Theresa .Don’t shut us
down .We need you.Dada yako ana
hasira kutokana na kile
kilichotokea kwa Nathan lakini
ukweli ni kwamba yuko katika
hatari kubwa.Hatujui hawa watu ambao wamekuwa wakifuatilia
taarifa zake wana lengo
gani?Maamuzi tutakayoyachukua
vijana wangu yatakuwa na msaada
mkubwa kwa dada yako na kwa
taifa.Tuwe kitu kimoja sote.Are
you with us? Akauliza Meshack
Jumbo na Theresa akabaki kimya
“Kabla ya kufanya maamuzi
yoyote Theresa” akasema Mathew
“Lazima ufahamu kwamba hii
ni operesheni hatari sana na wewe
mwenyewe umeshuhudia hatari
inayojitokeza kwa hiyo
utakapoamua kuwa pamoja na sisi
katika operesheni hii ujue kwamba
tunapambana na watu hatari hivyo
unatakiwa ukubali kutoka moyoni ” akasema Mathew na Theresa
akafikiri kidogo na kusema
“I’m with you” akasema
Theresa.
“Good.Sasa tunaingia tena
ndani kumuona rais na
tutamueleza kwamba sote
tumekubaliana kwamba uchunguzi
huu uendelee.” Akasema Meshack
Jumbo na kuwaongoza akina
Mathew wakaingia sebuleni kwa
Dr.Vivian na wote wakasimama
wakimtazama Dr Vivan,
“What? Akauliza Dr.Vivian
akishangaa namna walivyokuwa
wamesimama wanamtazama
“Mbona wote mnanitazama
kama mmeona mzimu?akauliza
Dr.Vivian “Madam president
tunafahamu kwamba uko katika
wakati mgumu kutokana na hiki
kilichotokea leo.Umeumia na sote
tumeumia vile vile.Hatukutegemea
kama jambo hili litafika hapa
lilipofika lakini kwa kuwa
limetokea hatuna budi kulikabili
na kuendelea mbele.Kutokana na
hiki kilichotokea umezuia
uchunguzi
usiendelee.Tunaiheshimu sana
kauli yako kama mkuu wetu wa
nchi na hatuwezi kuipuuza lakini
kutokana na uzito wa jambo hili
mimi na wenzangu tumeamua
kuendelea na uchunguzi hadi
mwisho na tutakapomaliza
operesheni hii mimi na Theresa tutajisalimisha mbele ya vyombo
vya usalama kwa mauaji ya
Nathan.Tunakuomba mheshimiwa
rais uridhie ombi letu hili la
kuendelea na uchunguzi wetu
kwani hata ukikataa sisi
tutaendelea na uchunguzi wetu
hadi mwisho” akasema Mathew
“Madam president
tumejadiliana na vijana
wangu,tumeona ni vyema
uchunguzi uendelee.Madam
president kuna jambo ambalo
tumeligundua na unapaswa
kulifahamu kuhusiana na hiki
kinachoendelea.Mathew tell her”
akasema Meshack Jumbo
“Nilipokwenda katika chumba
cha Nathan usiku wa leo nimechukua simu tatu ambazo
niliziweka katika mkoba wangu
pamoja na saa yake ya
mkononi.Tulivamiwa na wale
askari na wakafanikiwa kuondoka
baada ya askari wenzao kutokea
na baada ya kuondoka pale
nilikwenda moja kwa moja kwa
Meshack Jumbo nikamuachia begi
lile lililokuwa na zile simu na ile
saa ndipo nikaja hapa.Baada tu ya
kuondoka nyumba ya Meshack
ikavamiwa na kwa mujibu wa
Meshack Jumbo baada ya nyumba
yake kuvamiwa alitoka ndani kwa
kutumia mlango wa siri na kwenda
kujificha nje ya nyumba lakini
mara wale wavamizi wakafika
mpaka eneo alikuwa amejificha.Hawakuweza kumuona
ila yeye aliweza kuwaona
vyema.Walikuwa na kifaa fulani
ambacho walikuwa wanakifuata
kilichokuwa kinawaelekeza kitu
fulani.Hii inatupa picha kwamba
kifaa kile walichokuwa nacho
kilikuwa kinanasa mawimbi ya
moja wapo ya kifaa kilichokuwamo
ndani ya lile begi.Kwa hiyo basi
tunaamini Nathan alikuwa na
mashirikiano na watu huku
Tanzania na kama ndiyo basi
lazima kuna mtandao mrefu wa
watu ambao unaweza hata
kutumia polisi wetu katika
kufanikisha mambo yao. Na
mtandao huu utakuwa umeundwa
kwa kazi maalum hivyo tumeamua kuendelea na uchunguzi kufahamu
nani walio katika huu mtandao na
lengo lao nini” akasema Mathew na
bada ya muda Dr.Vivian akasema
“Mmetumia kila aina ya
ushawishi hadi mmefanikiwa
kunishawishi nikubaliane nanyi
japokuwa bado moyo wangu
unaumia sana kwa hiki
mlichokifanya lakini kwa upande
wa pili baada ya maelezo yako
kuna kitu nimeanza kukiona
hapa.Kuna uwezekano Nathan
akawa anatumiwa kwa kazi
maalum.Yawezekana nilikua
kipofu wa mapenzi na sikuweza
kugundua chochote na wala
sikuwa na wasi wasi naye hata
kidogo.Nadhani inabidi kwa mara ya kwanza katika maisha yangu
nitengue msimamo wangu na
kuruhusu uchunguzi
uendelee.Mathew endelea
kuchunguza jambo hili na
tuufahamu mtandao huu
unaoweza hata kutumia askari
polisi au sare na vifaa vya jeshi letu
kwa ajili ya kufanyia
uhalifu.Chunguza ufahamu kama
mtandao huo una mahusiano
yoyote na CIA au serikaliya
Marekani na chochote
utakachohitaji nitakuwezesha
lakini bado ninataka kujua kitu
kimoja,mwili wa Nathan uko wapi?
“Mheshimiwa rais mwili wa
Nathan kwa sasa hautaweza
kuonekana mheshimiwa rais utanisamehe kwa hilo.Mwili huu
ukionekana ni hatari kubwa
sana.Kwa kuwa alikuja Tanzania
kwa siri hata kifo chake kinapaswa
kuwa cha siri vile vile.” akasema
Mathew
“Hapo ndipo ninapotofautiana
nawe Mathew.Kwa nini kifo chake
kiwe siri?kwa nini isitafutwe
namna ya kueleza labda alikufa
kwa ajali au kitu kingine na halafu
mwili wake ukabidhiwe kwao
wauzike kwa heshima zote za
familia?
Madam president
anachokisema Mathew ni sahihi
kabisa.Katika mambo kama haya
ya uchunguzi kuna nyakati
inawalazimu mfanye maamuzi magumu kama haa aliyoyafanya ya
kuuficha mwiliwa Nathan
usijulikane ili kumuwezesha yeye
kuendelea na uchunguzi
wake.Nathan alikuja Tanzania
kimya kimya na hata kupotea
kwake kunapaswa kuwa kimya
kimya.Marekani wakigundua
jambo hili utaibuka mzozo
mwingine mkubwa kwa hiyo ili
kuepusha hilo tunapaswa
kuendelea na mambo yetu kimya
kimya kama vile hakuna
kilichotokea.Najua ni mtu wako wa
muhimu japokuwa ulikuwa
umekorofishana naye lakini
hatujui moyoni mwako ulikuwa
unampenda kiasi gani kwa hiyo
itakulazimu ulie kimya kimya mheshimiwa rais kwani lazima
ifanyike hivi.Tumeamua
kulichuguza hili jambo ni gumu na
mambo kama haya tutakutana
nayo hivyo lazima tukubaliane
nayo” akasema Meshack Jumbo
“Mnajaribu sana kunishawishi
nikubaliane nanyi lakini moyo
wangu umeumia mno.Kutokana na
hoja mlizozijenga sina budi
kukubaliana nanyi uchunguzi
uendelee ila naomba tafadhali
kama huko mbeleni kutatokea
jambo lenye kunihusu moja kwa
moja mimi tafadhali naomba
msilitolee maamuzi ya haraka bila
ya kunishirikisha kwanza
mimi.Sitaki mambo yaliyotokea
kwa Nathan yajirudie tena.Tayari mmekwisha uumiza moyo wangu
mno” akasema Dr.Vivian
“Tumekuelewa madam
president.Ila kuna jambo nataka
nikuombe”
“Jambo gani Mathew?
“Naomba Theresa abaki na
wewe hapa ikulu.Au kama
hatapata nafasi ya kukaa nawe
hapa basi ulinzi uimarishwe
nyumbani kwake.Watu hawa kama
wameweza kunifahamu mimi basi
yawezekana kabisa kwamba hata
Theresa tayari wamekwisha
mfahamu kwani hatujui mtandao
huu umesambaa kiasi gani ndani
ya serikali.”akasema Mathew
“Nafasi ipo kubwa sana hapa
ikulu ila Theresa mwenyewe ndiye hataki kuishi hapa lakini kutokana
na hali ya usalama kuwa tete kwa
sasa atalazimika kuishi hapa hadi
hapo nitakapokuwa na uhakika
kwamba hali ya usalama huko nje
ni shwari.Vipi kuhusu wewe
Mathew unahitaji ulinzi nyumbani
kwako?Hawa jamaa watakuwa
wanakufuatilia kila mahala kwa
hiyo nyumbani kwako kunatakiwa
kuwa na ulinzi imara.Nitaagiza
wapelekwe askari nyumbani
kwako”
“Ahsante mheshimiwa rais
lakini sihitaji ulinzi wowote kwa
sasa.Ninaweza kujilinda mimi
mwenyewe lakini pale
nitakapohitaji ulinzi nitakujulisha”
akasema Mathew “Are you sure?
“Ndiyo mheshimiwa rais”
akasema Mathew
“Meshack Jumbo wewe na
familia yako yote mtaishi katika
nyumba moja ya serikali wakati
nyumba yako ikijengwa
upya.Mtapata ulinzi mkali na wa
kutosha kwa hiyo naomba ufanye
kazi zako kwa uhuru kabisa bila
hofu” akasema Dr.Vivian
“Ahsante sana mheshimiwa
rais” akasema Meshack
“Muda umekwenda sana
tayari ni usiku mwingi hivyo
nahitaji kupumzika.Naomba na
ninyi mkapumzike ili tuweze
kuikabili kesho”akasema Dr.Vivian “Theresa wewe utabaki hapa
ikulu hadi hapo tutakapokuwa na
usalama kuhusu maisha yako”
akasema Mathew
“Hapana Mathew.Tutaondoka
wote kama ni kufa niko tayari”
akasema Theresa akionekana bado
kuwa na hasira
“Kama yeye mwenyewe
anataka hivyo basi vizuri.Meshack
Jumbo vijana wangu
watakuchukua kukupeleka mahala
utakapoishi na familia yako kwa
muda.Nawatakia nyote usiku
mwema” akasema Dr.Vivian na
akina Mathew wakaondoka.
“Mzee Jumbo usiku wa leo
sintalala hadi nihakikishe
nimeufahamau ule mtandao wa wale askari” akasema Mathew
baada ya kutoka ofisini kwa
Dr.Vivian
“Huwezi kwenda peke yako
huko tutakwenda sote.Sijazeeka
kiasi ambacho siwezi
kupambana.Kwa hiyo umepanga
kufanya nini? Kuna sehemu yoyote
ya kuanzia?
“ Kama walikuwa wanafuatilia
mojawapo ya vifaa vya Nathan basi
itakuwa ni hii saa ambayo
nilimvua mkononi ambayo ndiyo
inafanya kazi lakini simu zake zote
zimezimwa kwa hiyo hakuna
mawimbi yanayosafiri.Hivyo
naamini bado watakuwa
wanaendelea kufuatilia kwa hiyo
lazima tufanye mtego mdogo.Tunakwenda katika
makaburi ya mkwajuni pale
tutaifukia saa ya Nathan chini
halafu tutasubiri pale kama
watatokea ila naamini lazima
watakuja.Kama wanacho kifaa
wanachokitumia kufuatilia hii saa
basi wataifuata” akasema Mathew.
Walifika mkwajuni na
kuegesha gari katika klabu moja
ambako kulikuwa na onyesho la
bendi ya muziki wa dansi
“Ninyi mtabaki hapa mimi
nitatembea kwa miguu.Kutoka
hapa hadi makaburini si mbali.Kila
kitakachojiri huko nitawajulisha”
“Mathew huwezi kwenda huko
peke yako .Nitaongozana nawe
kwenda huko makaburini na Theresa atabaki hapa.” Akasema
Meshack Jumbo
“Theresa utabaki hapa mimi
na Meshack Jumbo tunakwenda
makaburini.Kitakachojiri huko
tutakujulisha” akasema Mathew
“Mathew I’m so
scared.Tafadhali naomba niende
nanyi.naogopa kubaki hapa peke
yangu” akasema Theresa
“Huko tuendako ni hatari
Theresa na kunaweza kutokea
hata mapigano .Si sehemu salama
kwa wewe kuwepo”
“Ni afadhali nikiwa karibu
nanyi mtanilinda kuliko nivamiwe
hapa nikiwa peke yangu na mimi
sifahamu namna ya kujilinda”
akasema Theresa “Ok twende wote” akasema
Mathew wakashuka garini
akaubeba ule mkoba wake wenye
simu pamoja na ile saa ya Nathan
wakaondoka kuelekea makaburi
ya mkwajuni.Walitembea kwa
miguu umbali wa kilometa tatu
wakakunja kulia wakafuata njia
inayoelekea makaburini.Kulikuwa
kimya na sauti za ndege bundi
zilikuwa zinasikika.Theresa
aliogopa sana hakuwahi kufika
maeneo kama yale usiku.Kadiri
walivyozidi kwenda ndivyo giza
lilivyozidi kuongezeka na
wakajikuta wakaiingia katika
vichaka na miti miti.Kulitisha sana
“Tutafute sehemu nzuri
ambayo tutaweza kuifukia hii saa na halafu tupate sehemu nzuri ya
kujificha na kuwaona wale
watakaokuja” akasema
Mathew.Walichimba shimo katika
kaburi ambalo lilizikwa karibuni
wakaifukia ile saa ya Nathan halafu
wakaenda kujificha mbali
kidogo.Wakiwa wamejificha mara
ghafla majani yakasikika
yakitikisika.Mathew ambaye
alikuwa anaangaza kama bundi
akajiweka tayari .
“Kuna mtu atakuwa anakuja
nasikia majani yanatikisika”
akasema Meshack Jumbo.
“Jiweke tayari yawezekana ni
wale jamaa wanakuja” akasema
Mathew na kutokea pale mahala
walipokuwa wamekaa waliweza kuwaona watu watatu wakiwa
wamebeba mfuko mkubwa
wakauweka juu ya moja la kaburi
wakamwaga vitu vilivyokuwamo
ndani na kuanza kugawana
“Hawa ni wezi wametoka
kuiba na huku ndiko sehemu
wanayotumia kugawana mali
walizoiba.Tuwaache wafanye
shughuli zao na wakimaliza
wataondoka wenyewe ” akasema
Mathew wakiendelea kuwatazama
wezi wale wakigawana na kutaka
kupigana wenyewe kwa wenyewe
baada ya mmoja wao kuonekana
kutaka kuchukua mali nyingi zaidi
ya wenzake.Mara ghafla wote
wakatulia. “Nasikia kuna nyayo za mtu”
akasema moja wao
“Hao wanga tu.Nani anaweza
kuja huku usiku huu? Akasema
moja wao
“Hebu tulieni.Kuna watu
wanakuja huku” akasema na wote
wakakaa katika tahadhari kubwa
na mara wakatimua mbio
wakaacha kila kitu walichoiba juu
ya kaburi.Kitendo kile
kiliwashangaza kidogo akina
Mathew
“Mbona wanakimbia kuna
nini? Akauliza Meshack Jumbo na
kabla Mathew hajajibu kitu mara
wakaonekana watu wanne wakiwa
na mavazi ya polisi na bunduki wakielekea mahala ambako
Mathew alifukia ile saa ya Nathan
“Meshack it’s
them.Wamekuja.”akasema Mathew
kwa kunong’ona
“Kwa hiyo tunafanya nini?
Akauliza
“Jiweke tayari.Nikitoa
maelekezo tutaanza
mashambulizi.Lazima tuwafahamu
ni akina nani hawa” akasema
Mathew.
“Lakini tutawaweza hawa
wako wanne na hatujui kama kuna
wengine wako nao na halafu wana
silaha kali sisi tuna bastora mbili
tu” akasema Meshack Jumbo. “Usiogope Meshack lazima
tupambane nao.Get ready”
akasema Mathew .
Wale askari polisi wakiwa na
kifaa fulani mithili ya simu
walifika hadi katika lile kaburi
Mathew alikofukia saa ya
Nathan.Wakaanza kufukua mahala
pale huku wale wawili wenye
bunduki wakiwa katika tahadhari
kubwa wakitazama huku na huko
“Umewaona wale wawili
wenye bunduki ,tutaanza
nao.Mchukue wa kushoto mimi
nitamchukua wa kulia.Make sure
you don’t miss.Hakikisha
umemlenga kichwani kwani
mwilini wamejikinga kwa fulana za
kuzuia risasi.” Akasema Mathew “Usihofu Mathew.Let’ do this”
akasema Meshack Jumbo
“On my count ,three ,two,one”
Wale jamaa wawili waliokuwa
wanachimba wakashangaa baada
ya wenzao kuanguka ghafla.Wote
wakaacha kazi waliyokuwa
wanaifanya na kusimama
kushuhudia kile
kilichotokea.Kufumba na
kufumbua wakajikuta wakichezea
risasi zilizotoka katika bastora
zenye viwambo vya sauti kutoka
kwa akina Mathew.
“Good Job.I hope they’re all
dead.Mimi ninakwenda kuwaona
,cover me” akasema Mathew na
kutoka kwa tahadhari akaelekea
mahala walipokuwa wale
askari.Wote walikuwa
wameanguka chini na hawakuwa
na uhai kwani risasi zile zililengwa
katika vichwa vyao.Haraka haraka
akitoa ile saa ya Nathan akaiweka
mfukoni halafu akaanza
kuwapekua wale
jamaa.Hakuwakuta na kitu kingine
zaidi ya kile kifaa mithili ya simu
walichokuwa wanakitumia
kufuatilia ilipo saa ya Nathan.
Wakati anakitazama kifaa kile
mara akasikia vishindo vya watu
wakielekea mahala pale.Haraka
haraka akalala chini na mara
wakatokea watu watano wote
wakiwa na mavazi ya askari na
wakiwa na silaha. “Tonny” akaita mmoja
wao.Mathew akaishika bunduki
moja ya wale jamaa waliowaua
aina ya SMG na kujiweka
tayari.Wale jamaa walikuwa
wamesimama wakiangaza kila
kona
“Tonny”akaita tena mmoja
wao.Mathew akapiga mluzi wale
jamaa wakaanza kuelekea kule
mahala ilikotokea sauti ile ya
mluzi.Ghafla Mathew akasimama
na wale jamaa wakakutana na
mvua ya risasi kutoka katika
bunduki ile aliyokuwa ameishika
Mathew.Wale jamaa hawakuwa
wamejiandaa kwa shambulio
lolote kutokea hivyo hawakuweza
kupata muda wa kuachia risasi hata moja na wote wakafa.Mathew
akaitupa ile bunduki akachukua
nyingine mbili toka kwa wale
jamaa na kumfuata Meshack
Jumbo.Alimkuta akiwa ameloa
jasho.Theresa alikuwa
anatetemeka kwa woga
“Mzee Jumbo nakuomba
mchukue Theresa muondoke eneo
hili mshuke bondeni kwani
naamini hawa jamaa bado wako
wengi na milio ile ya risasi
imewastua na watakuja hapa muda
si mrefu kwa hiyo ni hatari sana
kwenu kuwepo eneo hili.Wasiliana
na rais mueleze kwamba tunahitaji
msaada wa polisi haraka sana
wafike hapa ili kuwadhibiti hawa
jamaa” akasema Mathew na bila ubishi Meshack Jumbo akamshika
mkono Theresa wakaanza
kuondoka kwa tahadhari kubwa
wakimuacha Mathew peke yake.
Kabla Mathew hajaamua nini
cha kufanya likatokea kundi
lingine la watu saba wote wakiwa
na silaha wakiwa katika tahadhari
kubwa.Mathew akiwa katika kile
kichaka walichokitumia kujificha
aliweza kuwaona vyema lakini wao
hawakuweza kumuona.Hakutaka
kuwapa nafasi akaanza
kuvurumisha risasi.Kwa bahati
mbaya ile bunduki aliyokuwa nayo
haikuwa na risasi za kutosha
akaitupa haraka ili achukue
nyingine lakini wale jamaa ambao
mara tu risasi zilipoanza kuvuma walilala chini, walikwisha fahamu
mahala risasi zilikokuwa
zinatokea hivyo wote wakasimama
kwa haraka na kuanza
kuvurumisha risasi kuelekea
upande ule aliokuwako Mathew
ambaye tayari alikwisha wasoma
na aliwahi kuondoka eneo lile
kabla ya wao hawajaanza
kushambulia.Ghafla wakajikuta
wakimiminiwa risasi kutokea kwa
nyuma yao.Mathew alikuwa
amejilaza juu ya kaburi moja
aliwaona vizuri na kuwaondoa
mmoja baada ya
mwingine.Kilichokuwa kinatokea
hapa usiku huu pale makaburini ni
kama katika filamu.Mathew
aliendelea kubana pale pale juu ya kaburi akisubiri kama kuna
wengine watajitokeza.Kwa dakika
tatu hakukuwa na mtu yeyote
aliyejitokeza.Mathew akawafuata
wale jamaa aliowaua mwanzo
akawapiga picha kwa kutumia
simu yake.
“Hawako peke yao.Lazima
kuna wengine bado wapo.Hawa
jamaa wamejiandaa vilivyo.”
Akawaza mathew na mara kwa
mbali akasikia ving’ora vya magari
ya polisi akajua tayari msaada
umefika,akaenda kujificha katika
kichaka kimoja kwani hakuwa na
imani kama yupi ni askari wa
kweli na yupi siye.Kundi la askari
polisi zaidi ya kumi na tano
wakatokea wakiwa na tochi kubwa wakimulika kila sehemu na
wakafanikiwa kuiona ile miili ya
askari waliouawa na Mathew.
“Haraka ipakieni garini kabla
hawajafika hapa kwani watafika
hapa muda wowote toka sasa”
akasema mmoja wao aliyeonekana
kiongozi
“Beka,Stanley na Jacob
imarisheni ulinzi mahala hapa
kwani hatujui hao jamaa wako
wangapi na wamejificha
wapi.Yeyote atakayejitokeza
mkate pumzi haraka sana”
akasema yule jamaa kiongozi
wao.Mathew akastuka
“Hawa ni askari polisi wa
kweli au nao ni kundi moja na
hawa jamaa?akajiuliza “Ngoja niendelee kujificha
nisijitokeze hadi hapo
nitakapokuwa na uhakika kama
hawa kweli ni askari au ni
mtandao wa wale wavamizi.”
Akawaza Mathew
Wale askari walimaliza
kuibeba ile miili haraka haraka na
kuondoka.Mathew akasikia
muungurumo wa magari
yakiondoka.Aliendelea kujificha
pale kwa muda akisubiri kuona
kama kuna chochote kitakachojiri
lakini kuliendelea kuwa kimya
kabisa.Akachukua simu na
kumpigia Meshack Jumbo
“Mzee mko wapi? “Tumeshuka huku chini
tumejificha .Tumesikia milio mingi
ya risasi uko salama?
“Niko salama mzee. Twendeni
tuondoke eneo hili.Kuna mambo
yametokea hapa ambayo si ya
kawaida lakini nimekwisha pata
picha halisi” akasema Mathew na
kuwasubiri akina Meshack na
Theresa
“Hawa waliochukua miili ya
wale jamaa niliowamaliza ni
wenzao.Hawa jamaa ni askari na
wanafahamu mbinu zote za
kupambana.Kwa bahati nzuri mimi
ni mjuzi zaidi yao ndiyo maana
nimefanikiwa kuwaondoa
vinginevyo si rahisi kuwaondoa
wale jamaa waliokuwa wamejihami vilivyo” akawaza
Mathew
“Nilifanya jambo zuri
kuwapiga picha kabla
hawajachukuliwa.Kupitia picha
hizo tutaweza kuwafahamu ni
akina nani.Swali
ninalojiul………………” Mathew
akatoka mawazoni baada ya
kusikia majani yakitikisika na
vishindo vya nyayo za mtu
zikisikika.Akajiweka sawa na mara
simu yake ikaita alikuwa ni
Meshack Jumbo.Mathew akaipokea
na kuongea kwa sauti ya chini
Meshack akamtaarifu kwamba
tayari amekwisha fika mahala
walipokuwa wamejificha mwanzo
na Mathew akawafuata. “Pole sana Mathew.Haikuwa
kazi nyepesi kupambana na hawa
jamaa” akasema Meshack Jumbo
“Mzee hatuna muda wa
kuendelea kukaa hapa
tumekwisha pata uhakika sasa wa
kile tulichokuwa
tunakitafuta.Tuondokeni haraka
eneo hili” akasema Mathew
akitangulia mbele na akina
Meshack wakimfuata
nyuma.Walipoondoka maeneo yale
ya makaburi Mathew akaitupa
kichakani silaha ile aliyokuwa
ameibeba aliyoichukua kutoka
kwa wale askari
waliokufa.walitembea kimya
kimya hadi katika gari lao
wakaondoka.Dakika chache baada ya kuondoka wakakutana na
msafara wa magari ya polisi
ukielekea kule makaburini
“Hawa wanakwenda wapi?
Muda wote hawakuwa wamepewa
taarifa hadi wavamizi
wakaondoka? Akauliza Meshack
Jumbo
“Mzee Jumbo nimegundua
kuna watu ndani ya jeshi la polisi
wanashirikiana au wanatumiwa na
watu wanaoshirikiana na akina
Nathan.Ulipopiga simu kwa rais
kuomba msaada kilikuja haraka
kikosi cha askari polisi ambao
waliichukua ile miili ya wale jamaa
waliouawa na kuondoka
haraka.Hawakuwa mbali nami na
niliwachunguza vizuri ni askari polisi waliokuwa na mafunzo yote
ya kipolisi.Hiki kinachokwenda
huko sasa hivi ni kikosi cha pili”
akasema Mathew na kumshangaza
Meshack Jumbo
“Kuna kikosi cha kwanza
kimekuja tayari na kuiondosha ile
miili ya wale askari waliouawa?
Akauliza Meshack kwa mshangao
“Ndiyo mzee .Ile miili yote
iliondolewa na kikosi kilichofika
mwanzo.Nilifanikiwa kupata picha
za wale jamaa niliowamaliza kabla
wenzao hawajafika halafu ninacho
kifaa kile ambacho wamekuwa
wanakitumia katika uchunguzi”
“Ulifanya jambo zuri sana
kuwapiga picha .Akili yako inafanya kazi haraka haraka”
akasema Meshack.
“Kitu kikubwa cha kufahamu
ni mahusiano yaliyopo kati yao na
Nathan. Kipaumbele kwa sasa ni
kuwasaka na kuwafahamu
viongozi wa huu mtandao ni akina
nani.Inaonekana ni watu waliomo
ndani ya serikali.Mpigie tena simu
rais mwambie tunakwenda
kumuona sasa hivi” Akasema
Mathew
“Ni saa kumi alfajiri sasa
atakubali kuonana nasi muda
huu?akauliza Meshack Jumbo
baada ya kutazama saa yake
“Lazima akubali kuonana
nasi.Jambo hili ni la muhimu
sana.Call her” akasema Mathew na Meshack Jumbo akampigia simu
rais akamjulisha kwamba
wanakwenda kwake kuonana
naye.
“Natamani nikimbie
nikajifiche mbali na hapa ambako
hakuna kashikashi kama hizi
zinazoendelea hapa
nyumbani.Nimeogopeshwa sana na
haya mambo yanayoendelea.Kwa
haya mambo ninayoyaona
simuamini mtu yeyote zaidi ya
Mathew.Huu mtandao wa hawa
askari polisi umenitisha sana .Ni
hawa ndio waliomuua baba.Ni
watu hatari na hawana
huruma.Sitaki kukaa mbali na
Mathew hata kidogo.Ni yeye pekee
ninayeamini anaweza akanilinda kwa wakati huu” akaendelea
kuwaza Theresa huku safari
ikiendelea kimya kimya
Waliwasili ikulu na rais
akawapokea wakaelekea katika
chumba cha mazungumzo
Mheshimiwa rais samahani
sana kwa kukusumbua alfajiri
namna hii” akasema Mathew
“Bila samahani karibuni
sana.Nafahamu msingeweza kuja
alfajiri yote hii kama kusingekuwa
na kitu cha maana cha kunijulisha”
akasema Dr.Vivian
“Ni kweli mheshimiwa rais
kuna jambo ambalo tunataka
kukujulisha” Akasema Mathew
“Karibuni” akasema Dr.Vivian “Mheshimiwa rais baada ya
kuondoka hapa hatukwenda kulala
bali tuliendelea na kazi.Tulitaka
kufahamu hawa askari
waliotuvamia mimi na Theresa na
baadae kuvamia nyumbani kwa
Meshack Jumbo ni akina nani?
Tukaamua kuweka mtego kwa
kwenda kuificha mahala saa ile ya
Nathan ambayo ndiyo tuliyokuwa
na uhakika kwamba walikuwa
wanaifuatilia.Tuliweka mtego
wetu katika makaburi ya
Mkwajuni na kama tulivyokuwa
tumetegemea wale jamaa walifika
hadi pale makaburini.Ni wale wale
jamaa waliokuwa wamevaa mavazi
ya jeshi la polisi na walijihami kwa
silaha za kivita.Wote walikuwa na SMG.Tulipambana nao na
kufanikiwa kuwaua wapatao tisa
ingawa haikuwa rahisi kwani ni
watu wenye mafunzo na uzoefu
namna ya kupambana na
kujihami.Baada ya hapo mzee
Meshack alikupigia simu na
kukuomba msaada”
“Ndiyo alinipigia simu na
kunijulisha kwamba mko katika
makaburi ya mkwajuni na
mnahitaji msaada ingawa
hakunieleza nini kilichokuwa
kinaendelea huko.Nilimpigia simu
Inspekta jenerali wa polisi mara
moja na kumtaka atoe maelekezo
kiende kikosi cha askari polisi
waliojihami kwa silaha kali haraka
sana katika makaburi ya
Mkwajuni.Poleni sana kwa
kilichotokea huko”
“Ahsante sana mheshimiwa
rais kwa msaada wako mkubwa
lakini kitu cha kushangaza kikosi
cha kwanza cha askari waliofika
pale hakikuwa kikosi cha kuja
kutoa msaada kwetu bali walikuja
kuondoa miili ya wale askari
waliokufa”
“What ?! Dr.Vivian akashangaa
“Walifika askari kwa haraka
sana lakini walichokuja kukifanya
ni kuchukua miili ya wale askari
waliokufa na kuondoka haraka na
niliwasikiwa kwa masikio yangu
kiongozi wao akiwaharakisha
kuipakia miili katika magari kabla
askari hawajafika.Dakika zaidi ya kumi na tano baadae wakati na sisi
tukiondoka tukakutana na kikosi
cha askari wakielekea huko.Kwa
hiyo mheshmiwa rais unaweza
kuona ni kitu gani kinachoendelea
hapa.Kuna watu wako ndani ya
jeshi la polisi au wana mawasiliano
na watu wakubwa waliomo ndani
ya jeshi la polisi ambao
wanashirikiana na hawa jamaa
ambao hatujui kama ni askari
polisi au ni akina nani.Tunahitaji
kuufahamu ni akina nani
wanaoendesha mtandao huu na
watu wale kama ni askari au
siyo.Nilifanikiwa kupiga picha
miili ya baadhi ya wale niliokuwa
nimewaua pamoja na silaha
zao.Nitakuachia picha hizo ili viongozi wa polisi waweze
kuwatambua kama ni askari
wao.Tukiwafahamu ni akina nani
na wanatoka kituo gani cha polisi
tutaweza kuwafahamu viongozi
wao.Hao viongozi wao lazima wana
mahusiano na akina Nathan na
ndio wanaotekeleza mipango
miovu ya Marekani kwa nchio
yetu.Tukiwapata hao viongozi wao
tutafahamu mambo mengi toka
kwao.Mheshimiwa rais hicho
ndicho kilichotokea usiku wa leo”
akasema Mathew
“Nimekosa neno la kusema ila
poleni sana na hongereni kwa kazi
nzuri mliyoifanya.Sasa naamini
kweli kutakuwa na mtandao wa
watu ndani ya serikali yangu ambao wanashirikiana na
Marekani.Nathan anafanya kazi
kwa niaba ya serikali ya Marekani
na kama kuna mtu ndani ya
serikali yangu anashirikiana na
Nathan basi anashirikiana moja
kwa moja na serikali ya
Marekani.Lazima tuwatafute hawa
wote tuwapate na wapate stahili
yao.Wakati huu ambao tuko vitani
tunapigania uchumi wetu
hatupaswi kuwa na watu kama
hawa.Inawezekana hata katika
watu wanaonizunguka kuna watu
wanaoshirikiana na Marekani
kunihujumu.Kuna kitu kilitokea
Marekani ambacho mpaka sasa
najiuliza kilitokeaje lakini
sijaweza kupata jibu.Nilikutana na wale wawakilishi wa wafanya
biashara wa China na yule mjumbe
wa rais wa Korea Kaskazini kwa
siri lakini kesho yake rais wa
Marekani alikuwa na taarifa zote
za yale yote tuliyoongea na
wajumbe wale na hapo ndipo
mgogoro kati yangu na Marekani
ulipoanzia.Mathew unadhani
Nathan anaweza akahusika
chochote na jambo hili? Unadhani
hii ni mojawapo ya kazi
anazozifanya Nathan za kupata
taarifa zangu?Akauliza Dr.Vivian
“ Kuna uwezekano mkubwa
wa hilo jambo mheshimiwa
rais.Naomba kwanza kuuliza je
Nathan kuna kitu chochote aliwahi
kukupa unakivaa aidha mkufu,bangili au saa? Akauliza
Mathew
“Mathew alinipa mkufu wa
thamani kubwa sana wenye kidani
chenye madini ya Tanzanite ambao
huwa ninauvaa mara chache
ingawa Nathan amekuwa
ananisisitiza kwamba niuvae mara
nyingi.Hupenda kuniona nikiwa
nimeuvaa” akasema Dr.Vivian
“Uliuvaa ulipokwenda
Marekani?Wakati unazungumza na
hao jamaa ulikuwa umeuvaa?
“Ndiyo nilikuwa
nimeuvaa.Nathan alikwisha
nitaarifu kwamba tutaonana New
york na kila mara anionapo
hupenda kuniona nikiwa
nimeuvaa mkufu huu alionipatia wenye kidani cha thamani kubwa
chenye alama ya V alama ya jina
langu.”
“Unaweza ukanipa huo mkufu
kama hutajali? Akasema Mathew
na Dr.Vivian akaenda chumbani
kwake akarejea na kiboksi kidogo
chenye nakshi za kupendeza na
toka ndani ya kiboksi kile akatoa
mkufu mzuri wa gharama kubwa
sana akampatia Mathew.
“Dah ! mkufu wa gharama
kubwa sana huu.Gharama yake ni
kiasi gani?
“Milioni mia moja na hamsini”
akasema Dr.Vivian na wote
wakatazamana.Mathew
akauchukua mkufu ule
akautazama kwa makini sana na kutoa kitu fulani katika mkoba
wake na kuchomoa kitu fulani
kama msumeno mdogo akaikata
sehemu ya nyuma ya kile kidani na
kisha akatoa kitu fulani ndani yake
akakitazama na kumuonyesha
Dr.Vivian.
“Kama nilivyokueleza awali
kwamba Nathan hakuwa na
mapenzi yoyote kwako bali
alikuwa karibu yako akikuonyesha
mapenzi makubwa ili kukupofusha
bali alikuwa na kazi maalum na
hiki ndicho alichokuwa
anakifanya.Alikuwa na kazi ya
kukusanya taarifa zako.Ndani ya
mkufu huu wa thamani kubwa
kumewekwa kifaa hiki kidogo
ambacho hukusanya taarifa zako zote.Kila unapouvaa mkufu huu
kuna kitu cha kuweza kuhisi joto la
mwili na hivyo vifaa vilivyofungwa
humu huanza kufanya kazi na
hurekodi kila kitu unachokiongea
wakati umeuvaa huu mkufu ndiyo
maana Nathan alikuomba uuvae
mara kwa mara ili waweze
kuyafahamu mambo yako
mengi.Kama ulikuwa umeuvaa
mkufu huu wakati ukizungumza na
hao jamaa basi waliweza kunasa
maongezi yako yote na ndiyo
sababu ya rais wa Marekani
kufahamu kuhusu mazungumzo
yako na mjumbe maalum wa rais
wa Korea Kaskazini.”
Dr.Vivian alitaka kusema kitu
midomo ikabaki inamtetemeka. “I hope he’s in hell right
now.Kumbe amekuwa
ananidanganya kwa muda mrefu
bila ya mimi kufahamu.Nilikuwa
mjinga sana kwa kukubali
kupofushwa na penzi lake la
bandia.Kama ni hivi kuna mambo
mengi sana watakuwa
wameyapata kutoka kwangu
kwani nimekuwa na mkufu huu
kwa muda mrefu.Kuna kitu gani
hasa wanakitafuta kutoka
kwangu?!! Akauliza Dr.Vivian
“Hilo ndilo jambo
tunalopaswa kulichunguza
mheshimiwa rais.Lazima kuna
jambo ambalo wanalichunguza
kwako” akasema Mathew “Mathew tafadhali naomba
ufanye kila uwezalo kuhakikisha
suala hili linafika
mwisho.Samahani kuhusu maneno
niliyoyazungumza
awali.Nakuomba hakikisha
unachunguza na kuwafahamu wote
waliomo katika mtandao huu wa
hapa Tanzania ambao
wanashirikiana na serikali ya
marekani”
“Nitajitahidi mheshimiwa rais
lakini kwa kuanzia kuufahamu
mtandao huu tunaomba utusaide
tuweze kuwafahamu hawa askari
waliouawa usiku wa leo kule
mkwajuni kama ni askari wa jeshi
letu na tutawafahamu watu
waliowatuma.Picha zao utabaki nazo na utazikabidhi kwa mkuu wa
jeshi la polisi ili ziweze kufanyiwa
kazi haraka sana na kuwafahamu
watu wale kama ni askari wetu”
akasema Mathew
“Kesho asubuhi kitu cha
kwanza kitakuwa hicho,nitakutana
na wakuu wa jeshi la polisi na
nitatoa maelekezo ya kuwatafuta
hawa jamaa na kufahamu ni akina
nani na kama ni askari wetu na
kama siyo wanatoa wapi sare na
vifaa vya jeshi la polisi” akasema
Dr.Vivian
“Ahsante Dr.Vivian,hiyo
itakuwa ni sehemu nzuri ya
kuanzia kuufahamu mtandao
huu.Vile vile naomba
nikukumbushe kwamba Camilla Snow anawasili asubuhi ya leo
akitokea Havana kwa hiyo kama
nilivyokuomba kwamba apate
kuruhusiwa kuingia nchini kwani
atanisaidia sana katika uchunguzi
wangu” akasema Mathew
“Nitalifanyia kazi hilo usijali”
akasema Dr.Vivian
“Ahsante Dr.Vivian .Sisi ngoja
tukapumzike walau kidogo kwani
usiku mzima tumekesha macho”
akasema Mathew na kumrushia
Dr.Vivian picha zile za wale watu
waliouawa makaburini katika
simu yake halafu akaiacha pia ile
saa ya Nathan ili rais
aitunze,wakaagana na Meshack
Jumbo akachukuliwa na walinzi wa
rais akapelekwa mahala walikoandaliwa nyumba,Mathew
na Theresa wao wakatumia gari la
Meshack Jumbo wakaondoka.
“Mathew sitaki unipeleke
nyumbani kwangu.Ninaogopa sana
wale jamaa wanaweza wakanifuata
nyumbani.Nataka twende wote
nyumbani kwako kama hutajali”
akasema Theresa
“Hakuna tatizo kuhusu hilo”
akasema Mathew kwa ufupi
“Nimesikia unamwambia dada
kuhusiana na huyo mtu anaitwa
Camilla Snow.Ni nani huyo?
“Camilla anatoka Marekani na
anakuja kwa lengo la kusaidiana
nami katika shughuli hii kama
ujuavyo kwamba suala hili tayari limekwisha vuka mipaka ya
nchi.”akasema Mathew.
“Mathew ahsante sana kwa
kile ulichokifanya leo.Nimeamini
wewe ni maalum kabisa na
unaweza ukalifumbua fumbo
hili.Sikutegemea kama kwa muda
mfupi namna hii ungeweza kupiga
hatua kubwa namna hii” akasema
Theresa
“Ahsante lakini haya yote
yasingewezakana bila ya
ushirikiano wako.Umefanya kazi
kubwa sana.Endapo
usingemmaliza Nathan haya yote
tusingeyafahamu.Tusingejua kama
kuna mtandao wenye mahusiano
naye” akasema Mathew na safari
ikaendelea
WASHINGTON DC - MAREKANI
Saa tatu za usiku jijini
Washington DC kikao cha siri
kinafanyika katika ikulu ya
Marekani ambacho
kiliwakutanisha wakuu wa shirika
la kijasusi la Marekani CIA na rais
Mike straw.
“Karibuni sana.Willy
uliponiambia kwamba unahitaji
kuja kuniona jioni ya leo
nimelazimika kuahirisha shughuli
zangu nyingine ili
tukutane.Naamini kuna jambo la
msingi sana unalokuja kunieleza”
akasema rais Mike straw
“Mheshimiwa
rais,nimelazimika kuja kukuona ili kukupa taarifa za muhimu.Kuna
matatizo yametokea Tanzania.”
Akasema Willy Gadner
mkurugenzi wa CIA
“Nini kimetokea
Tanzania?Kwa wakati huu hii ni
taarifa ambayo sitaki kuisikia
kabisa.Macho yetu yote
tumeyaelekeza
Tanzania.Tukiruhusu kosa lolote
hata dogo tutatoa mwanya kwa
Korea Kaskazini
kujimarisha.Tunapaswa kufanya
kila tuwezalo kuhakikisha
kwamba Korea Kaskazini na
Tanzania hazianzishi mashirikiano
ya kibiashara.Hebu nieleze kitu
gani kimetokea?akauliza Mike
Straw rais wa Marekani.“Kuna tatizo limetokea
Tanzania ambalo ni muhimu
ukajulishwa mapema ili ufahamu
kinachoendelea huko hasa
kutokana na umuhimu wa
Tanzania kwa sasa.Asubuhi ya leo
kituo 1212 ambacho ni rais wa
Tanzania na 1214 ambacho ni
mdogo wake vilika mawasiliano
ghafla na mpaka sasa bado
hatujafahamu nini kimetokea na
wala hatujafanikiwa kurejesha
mawasiliano na kompyuta
zetu.Hawa watu wawili ni muhimu
sana hivyo kupotea kwao ghafla
kumetustua lakini tayari
nimekwisha toa maelekezo kwa
110C alishughulikie jambo hili na
ahakikishe anafanya kila awezalo ili mawasiliano kati ya vituo hivyo
viwili muhimu na Washington
yarejee”
“Mawasiliano hayo
yamekatikaje? Mike straw akauliza
“Bado hatufahamu nini
sababu ya mawasiliano
kukatika.Inawezekana labda vifaa
vile vimeharibika kwani
mawasilino yetu yanapitia katika
simu za kampuni ambazo zina
programu maalum ambazo
huiwezesha ofisi yetu ya
Washington kuweza kunasa
mawasiliano yote.Kuanzia asubuhi
ya leo kompyuta zetuzinaonyesha
kwamba rais wa Tanzania
hajatumia simu yake wala
kompyuta na hata mdogo wake naye ni hivyo hivyo.Kukatika kwa
mawasiliano kwa pamoja
kunatufanya tuamini kwamba lipo
tatizo Tanzania na tumemuachia
110C afuatiie kuna tatizo gani na
alitatue haraka sana” akasema
Willy Gadner
“Gadner tafadhali sana
naomba wekeza nguvu kubwa sana
Tanzania.Usikubali hata kidogo
kumpoteza Dr.Vivian.Ni mtu
muhimu sana kwetu kwa
sasa.Lazima tufahamu kila kitu
anachokifanya .Lazima tunase
mawasiliano yake yote ili
tufahamu mipango yake na Korea
Kaskazini.Tanzania hawawezi
kutuzidi sisi maarifa .Lile ni taifa
dogo masikini na sisi ni taifa kubwa na tajiri duniani.Uwezo
wetu kiteknolojia ni mkubwa sana
na tunaweza kupata taarifa yoyote
toka kwa mtu yeyote duniani hivyo
lazima tuhakikishe kwamba vitaifa
vidogo kama Tanzania
havituyumbishi.Wekeza nguvu
kubwa na teknolojia ya kutosha ili
tupate kila tunachokihitaji.CIA
tunao watu wenye ujuzi mkubwa
,watume waende Tanzania
wakafanye kazi kwa ajili ya taifa
lao la marekani.Tusiweke mzaha
katika suala hili ambalo ni la
muhimu mno kwa sasa” akasema
Mike straw
“Mheshimiwa rais,kuhusu
rasilimali watu tunao wa kutosha
na tayari kuna mtandao mrefu umekwisha tengenezwa ambao
unatusaidia sana katika
kufanikisha mambo yetu mengi
nchini Tanzania.Tuna watu wetu
kule na wamejipanga vizuri.Karibu
katika kila idara nyeti ya serikali
kuna watu wetu hata ikulu.Itoshe
kusema tu kwamba hiki
kilichotokea hatukuwa
tumekitegemea na tunakifanyia
kazi kujua kimetokeaje na tutafute
namna ya kulimaliza.Kama
nilivyosema kwamba mtandao
wetu ni mpana na tunaweza
kufanya jambo lolote kwa muda
wowote na ninakuhakikishia
mheshimiwa rais kwamba suala
hilo la kukatika kwa mawasiliano
tunalifanyia kazi na litapatiwa fumbuzi muda si mrefu” akasema
Willy akanyamaza kidogo halafu
akasema
“Kuna tatizo lingine
mheshimiwa rais.Kuna mtu wetu
ambaye ni seli 12A.Huyu
tumemuweka karibu na Dr.Vivian
na wana mahusiano ya
kimapenzi.Anaitwa Nathan.Kama
hukuwa ukijua mheshimwa rais ni
kwamba tumeanza kumfuatilia
Vivian toka angali anasoma hapa
marekani.Kuna sababu
zilizopelekea tukaanza kumfuatilia
ila nitakueleza siku nyingine
.Tulimtumia huyu Nathan
kuanzisha urafiki na baadae
mahusiano ya kimapenzi .Taarifa
hizi zote tunazozipata sasa kutoka kwa Dr.Vivian ni kwa sababu ya
Nathan.Amefanya kazi kubwa sana
lakini kwa siku za karibuni
ameanza kujisahau na kuzama
mapenzini baada ya kutanganza
kutaka kumuoa
Dr.Vivian.Tulimuonya kuhusiana
na suala hili na kumkumbusha
kwamba hatakiwi kuzama
mapenzini.Pamoja na
kumkumbusha majukumu yake
Nathan aliendelea na mipango
yake ya kumuoa Dr.Vivian na juzi
ameondoka marekani baada ya
kuitelekeza kazi aliyokuwa
amepewa na akaenda
Tanzania.Leo kompyuta yetu
ilionyeha kuna tatizo kwa
Nathan.Labda kwa kukufahamisha mheshimiwa rais,Nathan ni mmoja
wa maajenti wetu ambaye alikuwa
katika mfumo wa majaribio wa
kuwatambua na kuwafuatilia
maajenti wote duniani.Huu ni
mfumo mpya na bado uko katika
majaribio japokuwa umeonyesha
matunda japokuwa kuna
changamoto chache ambazo
yatupasa kuzifanyia kazi.Kuna
kifaa kidogo hufungwa katika
mwili ambacho hurekodi
mwenendo wa mapigo ya moyo na
taarifa hizo huweza kusomwa kwa
kutumia saa ambayo huivaa
mkononi.Saa hiyo ambayo
imetengenezwa maalum huweza
kusomwa na kompyuta zetu na
kupata taarifa zote za ajenti na kujua maendeleo yake.Hapo awali
maajenti wetu walikuwa
wanapotea sana lakini kwa sasa
baada ya kuanza kwa mfumo huu
tumekuwa tunawafuatilia maajenti
wetu kote duniani na kujua kama
wako salama.Umetuwezesha
kufahamu kama ajenti ametekwa
au amekufa” akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Mapigo ya moyo yalianza
kupunguza kasi yake na baadae
kompyuta ikaonyesha mstari
mnyoofu hii ni ishara kwamba
hakuna mapigo ya moyo na ajenti
amekufa au ameivua ile saa ambao
hatakiwi kuivua hadi siku ya kufa
kwake.Saa yake ya mkononi bado
inaendelea kusomwa na kompyuta zetu na tumewaagiza watu wetu
walioko Tanzania wafuatilie
kufahamu kama Nathan ni mzima
au amekufa.Tumewatuma wafanye
kila juhudi kuweza kuipata saa
hiyo ambayo ni muhimu sana
kwetu kwani si saa kama saa za
kawaida tunazovaa kutazama
wakati.Ni saa iliyotengenezwa
maalum kabisa kwa kazi
maalum.Juhudi za watu wetu
kuifuatilia na kuipata hiyo saa
zinaendelea lakini mpaka sasa
bado hakuna mafanikio na saa
haijapatikana.Saa hiyo inaweza
kutujulisha kama Nathan amekufa
au bado.Ina kumbu kumbu
zote.Hiyo saa pia ina programu
maalum ya kuweza kuwasiliana na maajenti wengine walioko sehemu
mbali mbali duniani na kama kuna
tatizo basi hujulishwa kwa
kuwashwa taa nyekundu na hapo
ajenti huweza kujua kuna hatari na
akawasiliana na ofisi kuu au ajenti
aliyepo karibu.Endapo akiipata
mtu ambaye ana ufahamu na
mambo ya kielektroniki anaweza
akaitumia saa hiyo kufahamu
walipo maajenti wa Marekani
sehemu mbali mbali za dunia na
akawafanyia kitu kibaya.Taarifa
iliyonifikia wakati tunakuja hapa
ni kwamba kompyuta zetu
zinaonyesha kwamba saa hiyo iko
ikulu ya Tanzania na hiyo
inatuthbitishia kwamba Dr.Vivian
anayo.Tumeanza mikakati ya namna ya kuipata saa hiyo ili
tuweze kuwa na uhakika kama
Nathan amekufa au bado mzima”
akasema Willy na kumtazama rais
“Gadner hizo ni taarifa za
kustusha sana.Ninachotaka kujua
mna uhakika kwamba huyo
Nathan amekufa? Isije kuwa
ametekwa nyara” akasema Rais
“Uhakika wa kwamba
amekufa ni mkubwa kwani kama
ametekwa kuna namna ya
kutambua mapigo yake ya moyo
yanavyokwenda.Lakini haya ya
Nathan yalipanda ghafla kupita
kawaida halafu yakaanza kushuka
.Hii inatupa uhakika asilimia 99
kwamba atakuwa amekufa lakini
ni muhimu kuipata saa hiyo ili tuweze kuwa na uhakika kama
kweli amekufa”
“Kama amekufa hamjaweza
kugundua nini kinaweza
kusababisha kifo
chake.Yawezekana akatekwa na
kuteswa sana hadi
akauliwa.Mnahisi kuna uwezekano
akawa amefahamika nini
anafanya?akauliza Mike straw
“Kuna uwezekano mkubwa
serikali ya Tanzania wakawa
wamemfahamu ni nani na
wakaamuua au akajiua kabla ya
kutoa siri.Nikiliunganisha tukio
hili la Nathan na lile la kupotea
ghafla kwa mawasiliano ya Rais
ninapata wasiwasi kwamba kama
amekufa serikali ya Tanzania itakuwa inahusika katika kifo
chake.Saa yake kuendelea
kuonekana ikulu ni ishara tosha
kwamba kuna mkono wa serikali
katika masahibu yaliyomkuta
Nathan.Kupotea kwa Nathan
naweza kusema ni pigo kwetu
kwani alikuwa ni muhimu sana
hasa katika jitihada za muda mrefu
za kuitafuta football” akasema
Willy na Mike straw akastuka
“Football? Akauliza kwa
mshangao
“Ndiyo mheshimiwa
rais.Kumekuwa na juhudi za
kuitafuta football.Rais Anorld
Mubara wa Tanzania aliwahi
kuanzisha utaratibu wa kutembea
na begi alilolipa jina la footbal.Begi hilo linabeba siri kubwa ambayo
raisi alikuwa anatembea nayo na
ilitulazimu kufanya operesheni
maalum ya kulipata begi hilo lakini
hatukufanikiwa na badala yake
ndege ya rais ikaanguka na rais
Anold Mubara akafariki dunia na
Sebastian Matope ambaye alikuwa
mbebaji wa Football akitoka
salama ndani ya ndege akiwa na
begi hilo.Baadae Sebastian aliuawa
lakini football haijawahi
kuonekana.Dr.Vivian ni mtoto wa
Sebastian na ameanzisha
uchunguzi wa kutaka kujua nani
waliomuua baba yake na vile vile
kutafuta begi hilo la
football.Wapelelezi anaowatumia
katika uchunguzi huo tayari wamekwisha piga hatua kubwa na
tuna uhakika watafanikiwa
kugundua mahala lilipo football
kwani Sebastian matope alitoka
ndegeni akiwa na begi hilo na tuna
uhakika kuna mahala
alilificha.Ingekuwa rahisi sana
kwetu kufahamu kila kitu kama
Nathan angeendelea kuwa karibu
na rais kwani wachunguzi hao
wanaripoti kwa rais.”
“Mna hakika hao wachunguzi
hawataweza kugundua ushiriki wa
Marekani katika ajali ya ndege ya
rais wa Tanzania?akauliza Mike
kwa wasi wasi
“Hapana mheshimiwa rais
hawataweza kugundua
chochote.Hakuna chochote cha kutuunganisha na ajali ile kwani
watu wote waliokuwemo ndani ya
ile ndege walifariki dunia.Usiwe na
wasi wasi kabisa na hilo” akasema
Willy
“Kwa hiyo mheshimiw arais”
Will akaendelea.
“Tumekuja kukufahamisha
matatizo hayo tuliyonayo nchini
Tanzania lakini tunajitahidi
kuhakikisha kila kitu kinakwenda
vizuri.” Akasema Will Gadner na
ukimya ukatanda.Baada ya muda
Mike straw akasema
“Gadner kuna mzaha
ninauona unafanyika kuhusu suala
la Tanzania.Suala la Tanzania
naona halipewi kipaumbele stahiki
hadi mambo haya yakatokea.Sitaki kusikia tena mambo kama haya
yakiendelea kutokea
Tanzania.Kwa hivi sasa Tanzania
ni nchi ambayo tunaitolea macho
sana kutokana na ukaribu wake na
Korea kaskazini.Tukiweka mzaha
na mashirikiano kati ya tanzania
na Korea Kaskazini yakafanikiwa
na ikapata madini ya Urani na
kuongeza idadi ya silaha zake za
nyuklia,Usalama wa Marekani
utakuwa shakani.Uchumi wa Korea
Kaskazini unakua kwa kasi kubwa
na hatupaswi kuiacha nchi ile
ikajiimarisha zaidi kijeshi kwani
litakuwa ni taifa hatari sana kwa
usalama wa dunia.Katika suala hili
tunawategemea sana CIA ili
kuweza kupata taarifa mbali mbali za kila kinachoendelea katika
mchakato wa mashirikiano baina
ya mataifa haya mawili.Mnapaswa
kuifanya kazi yenu kwa umahiri
mkubwa sana.CIA ni shirika kubwa
la ujasusi duniani na hatuwezi
kusumbuliwa na kitaifa kidogo
kama Tanzania.Narudia tena
Gadner fanyeni kazi yenu
inavyotakiwa .Sitaki kuletewa
taarifa za operesheni
kushindikana.Nataka safari
nyingine ukija hapa uwe na taarifa
zitakazonipa tabasamu na si
taarifa za kunifanya nikune
kichwa.Mna watu wenye viwango
vya juu mno kuliko nchi nyingine
yoyote chini ya jua,wapelekeni
wakafanye kazi Tanzania .Kama rais wa Tanzania ndiye kikwazo
nileteeni mapendekezo ya
kumuondoa na mimi nitasaini
haraka sana.Hawezi mtu mmoja
akatuumiza vichwa
vyetu.Tunaumiza akili zetu kwa
nchi korofi kama Korea Kaskazini
na si nchi ndogo kama
Tanzania.Nileteeni pendekezo hilo
mkiona linafaa nami mimi
sintasita kuidhinisha aondolewe
mara moja.Tunazo mbinu nyingi za
kuweza kumuondoa ili asiweze
kuwa kikwazo kwetu.Nataka
mpaka kesho mchana muwe
mmeniletea mpango mkakati
namna mtakavyoweza kukabiliana
na hali iliyokoTanzania.Nataka
suala la Tanzania lipewe kipaumbele kikubwa sana katika
mipango yenu yote.Mkishindwa
katika jambo hili mtakuwa
mmeliangusha taifa la
Marekani.Msiwe sababu ya wa
marekani kuishi kwa hofu
kutokana na vitisho vya Korea
Kaskazini.Tukishindwa kumdhibiti
sasa na kumuacha akayapata
madini ya Urani toka Tanzania
watu wetu wataishi kwa hofu
kubwa kwani ataongeza uwezo
wake wa kuishambulia
Marekani.Kama zoezi hili litakuwa
gumu niambieni ili niweze
kutafuta watu wengine wenye
kuweza kuifanya kazi hiyo.Narudia
tena kwamba kama Dr Vivian ni
kikwazo kwenu nielezeni ili niwape ruhusa ya
kumuondoa.Tunao uwezo wa
kumuondoa rais yoyote wa nchi
yoyote duniani.” Akasema Mike
straw kwa ukali
“Tumekuelewa mheshimiwa
rais lakini suala kama hili
linahitaji umakini mkubwa sana
katika utekelezaji wake na hasa
kwa wakati huu ambao kuna
mvutano mkali.Tunao uwezo wa
kumuondoa rais wa Tanzania
lakini dunia nzima itafahamu
kwamba ni sisi na haitaleta picha
nzuri kwa washirika
wetu.Kikubwa tunachoshughulikia
kwa sasa ni kurejesha mawasiliano
kati ya Dr.Vivian na ofisi yetu hapa
Washington ambayo yatatuwezesha kufahamu kuhusu
mipango yote anayoipanga kuhusu
mashirikiano yake na Korea
kaskazini” akasema Willy Gadner
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Ndege ya shirika la ndege ya
Penny air ilitua katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam.Hii ni
ndege iliyomchukua Camilla Snow
kutoka Havana Cuba kumleta Dar
es salaam.Walinzi waliotumwa na
rais wakiwa wameambatana na
Mathew na Theresa walikuwepo
uwanjani pale kumlaki
Camilla.Ndege ikasimama mlango
ukafunguliwa na mwanamke mmoja mwenye umri kati ya miaka
ishirini na tano au na sita
akashuka ndegeni.Alikuwa amevaa
gauni fupi jeusi,viatu virefu vyeusi
na mkononi alikuwa ameshika
mkoba mweusi.Nywele zake ndefu
zenye weusi wa kung’aa zilipepea
kwa sababu ya upepo mkali
ikamlazimu kuutumia mkono
wake mmoja kuziweka sawa
Alishuka ngazi taratibu na
nyuma yake wakafuata watu
wanne wakiwa wamebeba
masanduku makubwa
matatu.Mathew na wale
alioongozana nao walikuwa chini
ya ngazi wakimsubiri Camilla.Mara
tu alipogusa ardhi ya Tanzania Mathew akamsogelea na kumpa
mkono
“Karibu Tanzania Camilla
Snow” akasema Mathew .Camila
hakujibu kitu akatabasamu na
kutikisa kichwa ishara ya
kushukuru.Mathew
akamtambulisha kwa Theresa na
wale walinzi wa rais halafu
wakaelekea katika gari.Mathew
akawashukuru wale jamaa
waliomsaidia Camilla kubeba
mabegi yake.Mizigo ya Camilla
ikapakiwa garini ,Mathew
akawaelekeza wale walinzi
wakaendelee na shughuli zao
halafu yeye,Theresa na Camilla
wakaingia katika gari wakaondoka.Tayari ilipata saa
moja za asubuhi
“Mathew mimi naomba
unipitishe nyumbani kwangu
nikapumzike kama utanihitaji
utanijulisha” akasema Theresa
“Sawa Theresa wewe pumzika
ila muda wowote nitakapokuhitaji
nitakujulisha .Pole sana kwa
kukesha macho usiku wa jana”
akasema Mathew.Camilla akatoa
kifaa cha kuhifadhia miziki mithili
ya simu akachomeka spika za
masikioni na kuvaa akaanza
kusikiliza muziki.Theresa
aliyekuwa amekaa kiti cha mbele
pembeni ya Mathew akasema
“Huyu mgeni wako mbona ana
nyodo namna hii? Kwa nini hataki kusalimia? Anadhani hatufahamu
kiingereza?akasema Theresa
“Theresa ni mapema sana
kutamka chochote kuhusu huyu
mgeni wetu.Inatakiwa kwanza
tumsome tabia zake.Tumsome
taratibu na tutamuelewa” akasema
Mathew na Theresa akabetua
midomo
“Wanawake !! akawaza
mathew na kutabasamu
akachukua simu na kumpigia
Hamis Chuma
“Mathew habari za asubuhi?
“Habari nzuri kabisa
Chuma.Sijapata mrejesho wowote
toka kwako kama kazi ilikwenda
vizuri.” “Nilikuwa mbioni kukupigia
simu kukupa taarifa .Tumerejea
dakika kama kumi zilizopita .Usiku
mzima tumefanya ile kazi na
tumeikamilisha .Mahala
tulikouficha ule mwili hakuna
atakayeweza kugundua
chochote.Tumeufukia mwili
katikati ya makaburi ya kwa
sadala”
“Mna hakika hakuna yeyote
anayeweza kutia shaka mahala
hapo?
“Hakuna Mathew.Tunafanya
hii kazi kwa utaalamu mkubwa
sana”
“Ok Ahsante .Kuna jambo
nataka unisaidie .Nisaidie gari
langu kuvutwa hadi gereji kwa Somji Kipara libadilishwe matairi
yote.Nitalipitiai hapo baadae”
“Sawa Mathew nitakusaidia”
akasema Hamis Chuma na kukata
simu.Mathew akamgeukia Theresa
“Wale jamaa tayari
wamekamilisha kazi.Hakuna
atakayeuona tena mwili wa
Nathan” akasema Mathew
“Sikufikiria kama siku moja
ningeweza kuingia katika orodha
ya wauaji.Nimetoa roho ya mtu
lakini ni kwa ajili ya kujilinda
mimi na dada yangu.Watu hawa
waliua familia yetu na sasa bado
wanaendelea kutuifuatilia mimi na
dada.Angeendelea kuwa hai
tugekuwa hatarini na sisi
kuuawa”akasema Theresa “Usijilaumu sana Theresa
kwani jambo ulilolifanya lina
manufaa makubwa.Bila kufanya
vile tusingefahamu kuhusu kile
kikundi cha askari ambao
wametuvamia jana.Kikundi kile
kimeibuka baada ya Nathan
kufariki.Pamoja na hayo jambo hili
limesababisha doa kati yako na
Vivian.Japokuwa walikuwa
wamekorofishana lakini Vivian
bado alikuwa anampenda Nathan
kwa hiyo ana kidonda kikubwa
moyoni mwake na kitachukua
muda kupona.Ninakushauri mpe
muda kidonda chake kipone.Kwa
sasa mahusiano yenu hayatakuwa
kama zamani ila nakuomba
usivunjike moyo ,endeleakumpenda na kumuheshjimu.Iko
siku naamini mambo yatakaa
sawa” akasema Mathew
“nalifahamu hilo Mathew na
ndiyo maana nataka nijiweke
mbali naye kwa muda huu ili
asinione mara kwa mara karibu
yake na kupata
hasira.Nilichokifanya si kitu kizuri
na hata kama ningekuwa mimi
mahala pake
ningekasirika.Naamini iko siku
yatakwisha” akasema Theresa
Mathew alimpitisha Theresa
nyumbani halafu yeyena Camilla
wakaendelea na safari .Hadi
walipofika katika makazi ya
Mathew, Camilla hakuwa
ameongea hata neno moja “Safari hii nimekutana na mtu
wa aina yake.Hataki kuongea.Ni
mgeni hapa Dar es salaam lakini
hageuzi hata shingo kutazama nje
kama wafanyavyo wageni
wengine.Inawezekana labda ni
kwa sababu ya ugeni.Hata hivyo
lazima nitafute namna ya
kuendana naye.Ninamshukuru
Mungu amenijalia uwezo wa
kuweza kuishi na mtu yeyote.Hata
shetani ninaweza kuishi naye”
akawaza na kutabasamu wakati
akimtazama Camilla kwa wizi
kupitia kioo kidogo cha
kumuwezesha dereva kutazama
nyuma
“Hata hivyo mhh ! Hiki kweli
kipusa.Mtoto amekamilika kila idara.Hakuna sehemu unayoweza
kutoa kasoro.Yawezekana
anajifahamu namna alivyo mzuri
ndiyo maana ana nyodo namna hii”
akawaza Mathew
Walifika katika makazi ya
Mathew ,akamkaribisha Camilla
ndani
“Hapa ni wapi? Kwa mara ya
kwanza Camilla akaongea na
Mathew akatabasamu
“Hapa ni nyumbani
kwangu.Ndipo utakapoishi kwa
sasa.Jisikie nyumbani ila endapo
hautajisikia huru hapa
nitakutafutia makazi mengine
lakini hapa ni sehemu salama”
“Unaishi na nani hapa? “Ninaishi mwenyewe hapa ila
nina wafanyakazi wawili ambao
huja asubuhi na kufanya kazi kisha
huondoka saa kumi na nusu jioni”
“Huna mke?
“Sina”
“Vizuri.Sipendi sehemu yenye
watu wengi .Nionyeshe chumba
changu nikapumzike” akasema
Camilla.Mmoja wa watumishi wa
Mathew ambaye hushughulika na
usafi akakokota mizigo ya Camilla
hadi katika chumba cha wageni
“Hiki ndicho chumba
utakacholala .Kuna wahudumu
wako hapa na chochote
utakachokihitaji utawaeleza
watakusaidia.Pumzika tutaonana
baadae” akasema Mathew “Ahsante sana Mathew”
akasema Camilla na kukaa
kitandani Mathew akafungua
mlango ili atoke Camilla akamuita.
“Mathew naweza kupata
kahawa tafadhali?
“Bila wasi wasi unaweza pata.”
Akasema Mathew na kutoka
akamuelekeza mpishi wake
kwamba amuandalie Camilla
kahawa.
“Taratibu ninaanza kumsoma
Camilla.Nitamzoea tu na nitafanya
naye kazi vizuri” akawaza Mathew
baada ya kuingia chumbani kwake
akajimwagia maji baridi na
kujilaza kitandani.Akachukua
simu na kumpigia Peniela
akamjulisha kwamba Camilla amefika salama na kumshukuru
kwa msaada ule mkubwa.Kwa
mbali kengele za kanisani
zikasikika zikilia na
kuwakumbusha watu kwamba
siku ile ni jumapili siku ya
bwana.Mathew akajilaza kwani
alihisi macho mazito sana hakuwa
amelala usiku mzima.
****************
Ni jumapili,siku ya
mapumziko lakini kwa rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania
alikuwa anaendelea na majukumu
yake ya kuwatumikia
wananchi.Saa mbili na nusu za
asubuhi tayari alikuwa katika kikao na viongozi wa juu wa jeshi
la polisi .Katika kikao hicho
alihudhuria waziri wa mambo ya
ndani ya nchi,mkuu wa jeshi la
polisi Tanzania na maafisa
wengine wa ngazi za juu waliofika
kwa wakati kufuatia wito wa rais
aliyewataka wafike asubuhi na
mapema
Rais alipoingia katika chumba
cha mkutano wote wakasimama
wakatoa heshima na rais akaketi
na ndipo wote wakaketi.Bila
kupoteza wakati Dr.Vivian
akafungua kikao
“Habari za asubuhi
waheshimiwa.Nawashukuru sana
kwa kufika kwenu kwa
wakati.Najua leo ni jumapili siku ya mapumziko lakini sisi tulio
katika kazi hizi za kuwatumikia
watu hatuna mapumziko.Muda
wote tuko kazini.Nawashukuru
kwa kuwa mnalifahamu hilo na
mmefika wote” akasema rais na
kuwatazama maafisa wale
akaendelea
“Kikao hiki hakitakuwa kirefu
na nimewaiteni hapa niwaeleze
jambo moja muhimu sana kwa
usalama wa nchi yetu.Naamini
tayari nyote mmekwisha pata
taarifa ya mambo yaliyotokea
usiku wa kuamkia leo.Kuna
matukio mawili yametokea usiku
wa kuamkia leo.Kwanza ni tukio la
kuvamiwa watumishi wawili wa
ofisi yangu akiwemo mdogowangu Theresa.Wakiwa katika barabara
ya uwazi walivamiwa na kikosi cha
askari.Nasema walivamiwa kwa
sababu taratibu za kawaida za
jeshi la polisi kumsimamisha mtu
wanayemtilia shaka
hazikufuatwa.Walichokifanya
askari hao walipiga risasi tairi
moja na gari likapoteza uelekeo
lakini wakajitahidi kulidhibiti
likasimama.Askari hao baada ya
kuona gari limesimama wakaanza
kulimiminia risasi kwa bahati
nzuri gari hilo halipenyi
risasi.Kama isingekuwa hivyo
nadhani lengo lao lilikuwa ni
kuwadhuru.Kuona hivyo ikawabidi
wanipigie mimi kuniomba msaada
na mimi nikawasiliana na IGP nikamuomba atume askari haraka
sana.Kitu cha kushangaza ni
kwamba askari wale wavamizi
walipewa taarifa ya kikosi cha
askari kilichokuwa kinakwenda
eneo lile wakaingia katika magari
yao na kuondoka haraka.Hii inatoa
picha ya wazi kwamba askari wale
ambao nawaita wavamizi
walikuwa na lengo baya na wale
wafanyakazi wangu na
inawezekana walikuwa na watu
wao ndani ya jeshi la polisi ambao
waliwapa taarifa za kuhusiana na
kikosi cha askari kilichokuwa
kinakwenda pale.” Akanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Haikuishia hapo.Askari hao
hao walikwenda kuvamia tena nyumbani kwa mkuu wa idara ya
ujasusi mstaafu Meshack Jumbo na
kufanya uharibifu mkubwa na
halafu wakaichoma nyumba
yake.Kwa bahati nzuri yeye na
familia yake hawakupata madhara
yoyote.Kufuatia matukio hayo
mawili vijana wangu walifanya
operesheni ya usiku mzima
kuwabaini watu hawa ni akina
nani na wakafanikiwa kuwapata
ila katika mapambano askari hao
wavamizi wapatao tisa walifariki
dunia” Akanyamaza tena
akawatazama maafisa wale halafu
akaendelea
“Ninazo hapa picha za askari
hao waliopoteza maisha kufuatia
mtego uliowekwa na vijana wangu jana usiku.Mheshimiwa waziri
nitakukabidhi picha hizo na
ninataka zifanyiwe kazi haraka
sana kuwabaini hawa watu ni
akina nani na ninataka mpaka saa
saba mchana wa leo wawe
wametambuliwa ni akina nani.Je ni
askari wetu ndani ya jeshi la
polisi? Kama ndiyo walitumwa na
nani kufanya matukio yale
ambayo naweza kuyaita ni ya
kihalifu?Nataka niufahamu
mtandao wao wote.Lakini kama
siyo nataka nifahamu wametoa
wapi sare na vifaa vya jeshi letu?
Nataka silaha hizi zichunguzwe je
ni za jeshi letu la polisi? Tatu watu
hawa wanaonekana kuwa na
mashirikiano na watu toka ndani ya jeshi la polisi nataka
muwatafute watu hao na
wapatikane.Mheshimiwa waziri
fuatilia suala hili nataka mpaka
saa saba mchana wa leo niwe
nimepata majina ya watu hawa ni
akina nani.” Akasema rais na
kumkabidhi waziri wa mambo ya
ndani ya nchi bahasha yenye picha
za wale jamaa waliouliwa na akina
Mathew .Kikao kikafungwa
akaagana na maafisa wale
wakaondoka
Alipomaliza kikao na maafisa
wale wa polisi akakutana na waziri
wa mambo ya nje ofisini kwake
wakawa na mazungumzo
mafupi.Katika mazungumzo hayo
waziri wa mambo ya nje alimjulisha rais kuhusu ujio wa
waziri wa mambo ya nje wa
Marekani.
“Mbona imekuwa ghafla sana?
Akauliza Dr.Vivian
“Hata mimi nimemuuliza
hivyo akadai ni safari ya dharura”
“Amekueleza sababu ya ziara
yake hiyo?
“Mheshimiwa rais hajanieleza
lakini amesema ni kwa ajili ya
kuzungumzia masuala muhimu
sana.Mheshimiwa rais serikali ya
Marekani kwa sasa wanajitahidi
kufanya kila njia ili kukushawishi
uweze kuachana na mpango wako
wa kuanzisha mashirikiano na
Korea Kaskazini.Nadhani hilo ndilo kubwa linalomleta Tanzania
kwa dharura”
Dr.Vivian akafikiri kidogo na
kusema
“Marekani wanajisumbua
sana.Msimamo wangu
hautabadilika kamwe.Nimekwisha
amua kusonga mbele na hakuna
kurudi nyuma.Watapoteza muda
wao bure” akasema Dr Vivian na
kutoa maelekezo kadhaa kwa
waziri yule wakaagana akarejea
kwake kupumzika
“Mike Straw bado hajaamini
kama kweli nimedhamiria
kuanzisha mashirikiano na Korea
Kaskazini.Muda si mrefu sana
atalishuhudia jambo hili likiwa
kweli na atazidi kuchanganyikiwa.Nimechoshwa
kwa nchi zetu kupangiwa mambo
ya kufanya kwa vile tu ni
masikini.Tanzania inahitaji
maendeleo ya haraka na
maendeleo hayo yatapatikana kwa
kufanya maamuzi
magumu.Naamini hiki
nilichokifanya ni sahihi kwa nchi”
akawaza Dr.Vivian akiwa sebuleni
kwake anapumzika
WASHINGTON DC – MAREKANI
Ni saa nane za usiku kwa saa
za Marekani,Willy Gadner mkuu
wa shirika la ujasuri la Marekani
CIA alipowasili ikulu ya Marekani kufuatia wito wa dharura wa rais
Mike straw.
“Ahsante sana Gadner kwa
kufika kwa wakati.Nimelazimika
kukuita ili tuzungumzie suala la
muhimu sana ila lenye usiri
mkubwa ndiyo maana sikutaka
kuzungumza wakati uko na wale
wenzako” akasema Mike straw na
kunyamaza kidogo
“Gadner tulipopewa dhamana
hii ya kuwaongoza wamarekani
tuliapa na kuwaahidi utumishi
uliotukuka na zaidi sana
tuliwahakikishia usalama
wao.Wamarekani wana imani
kubwa na serikali yao kwamba
itawalinda na sisi kama serikali
tuna imani kubwa sana na vyombo vyetu vya ulinzi na hasa shirika
letu la ujasusi CIA.Dhamana
uliyonayo Gadner ni kubwa sana
hivyo wewe na watu wako
hampaswi mlale usingizi ili
wamarekani waweze kupata
usingizi na wawe
salama.Wamarekani hawapaswi
kuishi kwa hofu hata
kidogo.Ukiondoa vitisho vya ugaidi
ambavyo tumekuwa tunapambana
kuwadhibiti, kuna taifa moja
ambalo limekuwa linawapa sana
hofu wamarekani nalo ni Korea
Kaskazini” akanyamza kwa muda
kisha akaendelea
“Hili ni taifa ambalo uchumi
wake kwa hivi sasa unakua kwa
kasi kubwa na wachumi wanatabiri kwamba kama uchumi
wa Korea Kaskazini utaendelea
kukua kwa kasi hii baada ya miaka
mitano unaweza kuwa umefikia
robo tatu ya uchumi wa China.Huu
utakuwa ni uchumi mkubwa na
taifa hili litazidi kuwa imara sana
kiuchumi na kijeshi pia.Hofu yetu
ni kwamba kadiri taifa hili
linavyozidi kujiimarisha kiuchumi
ndivyo linavyozidi kujiimarisha
pia kijeshi.Wanawekeza sana
katika teknolojia mpya za
kutengeneza silaha na hasa
makombora ya masafa marefu na
hivi karibuni wamefanya
majaribio ya kombora ambalo
linatajwa kuwa linaweza kufika
katika moja ya majiji makubwa ya Marekani.Haya ni mafanikio
makubwa kwa Korea Kaskazini na
hivyo kuzidisha hofu kwa
wamarekani.Kama haitoshi
wanataka pia kununua madini ya
Urani kutoka Tanzania na na lengo
kubwa ni kuongeza idadi ya silaha
zao za nyuklia.Hatuwezi kuiacha
Korea kaskazini ikaendelea na
harakati zake na kuwatishia kwa
Marekani.Lazima tufanye kila
tunaloweza kulifanya kuhakikisha
kwamba hawafanikiwi malengo
yao.Tumejitahidi kwa upande wa
vikwazo lakini mpaka leo
inaonekanaa vikwazo hivyo havina
nguvu yoyote na sasa kinachofuata
ni sisi kutafuta sababu ya
kuiadhibu vikali sana nchi hii na kufifisha juhudi zote za
kutengeneza makombora na silaha
kali za maangamizi.Umoja wa
mataifa hauwezi kuidhinisha
matumizi ya nguvu kwa Korea
Kaskazini kwa kuogopa kuzuka
kwa vita kubwa kwa hiyo sisi
lazima tutafute njia zetu wenyewe
za kutufanya tuingie vitani na
Korea kaskazini.Kuna mpango
nimeubuni ambao unaweza
ukalifanikisha hilo” akasema Mike
straw.
“Kwa ajili ya manufaa
makubwa kwa nchi,kuna nyakati
inatulazimu kufanya jambo gumu
ili watu wetu waendelee kuwa
salama.Kwa kuwa Korea Kaskazini
anaonekana kuwa hatari kwa usalama wetu hivyo basi
tunalazimika kumchapa.Dunia
mzima hivi sasa inafahamu kuhusu
mashirikiano yanayotaka
kuanzishwa kati ya Korea
kaskazini na Tanzania na
wanafahamu kwamba Marekani
tunalipinga hili suala kwa nguvu
zote.Kwa hiyo basi ninamtuma
waziri wa mambo ya nje wa
Marekani aende Tanzania kwa
lengo la kutaka kumshawishi rais
wa Tanzania asitishe mpango wa
kushirikiana na Korea Kaskazini
kibiashara.Nataka CIA mumuue
waziri wetu wa mambo ya nje
Helmet Brian akiwa katika ardhi
ya Tanzania” akanyamaza baada ya kuuona mstuko mkubwa usoni
kwa Willy Gadner
“Tumuue waziri wetu wa
mambo ya nje? Akauliza Willy
“Ndiyo Gadner.Tunatakiwa
kumuua Helmet Brian .Jambo hii
linapaswa kufanywa kwa ufundi
mkubwa ili ionekane ni Korea
Kaskazini ndio waliomuua waziri
wetu na baada ya hapo
tutalazimika kuchukua hatua
kufuatia mauaji hayo na tutapata
sababu ya kuiadhibu Korea
kijeshi.CIA mnao uwezo mkubwa
wa kuifanya dunia nzima iamini
kwamba Korea Kaskazini ndio
waliomuua waziri wetu na nchi
zote watasimama upande wetu na
tutahakikisha tunaiharibu vibaya sana Pyongyang na kuyateketeza
kabisa makombora yake
yote.Hatutaweza kupata sababu
nyingine ya kumpiga Korea
Kaskazini zaidi ya
hii.Ninakukabidhi jukumu hilo
Gadner hakikisha unakaa na
maafisa wako mlipange vizuri sana
namna ya kulitekeleza ila
kumbukeni sitaki kusikia
kumetokeauzembe au makosa
yoyote.Suala hili ni nyeti na
muhimu mno kwa nchi yetu”
Willy Gadner akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Mheshimiwa rais
nimekusikia na kukuelewa
vizuri,pia sababu ulizotoa
nimezielewa lakini naingiwa na hofu kwa maamuzi hayo ya
kumuua waziri wetu wa mambo ya
nje.Hauwezi kutafuta namna
nyingine ya kutimiza lengo letu hili
bila kumuua Helmet”
“Zipo njia nyingine lakini
nimechagua hii kwani ni muafaka
kwa wakati huu.Dunia nzima
watajua kwamba Korea Kaskazini
ndio waliomuua waziri wetu.Hivyo
italeta mzozo mkubwa na itakuwa
ni sababu nzuri kwetu kuichapa
Korea Kaskazini.Hiyo ndiyo njia
pekee ninayoitaka kwa sasa na
ninaomba ujipange vizuri na
maofisa wako mlitekeleze suala
hili.Narudia tena suala hili ni la siri
na la muhimu sana hivyo sitaki
kusikia kuna makosa au uzembe wowote umefanyika.Tumieni
mbinu na maarifa yote kufanikisha
jambo hii” akasema Mike straw na
kuendelea na mjadala kuhusiana
na suala lile
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Mlio wa simu ulimuondoa
Mathew usingizini akatazama
mpigaji na jina lilionekana ni
Somji.Akapokea haraka
“Hallow Somji”
“Mathew gari lako lililetwa
hapa gereji na Hamis Chuma tayari
tumebadili matairi na kuweka tairi
zile uzipendazo.Unaweza kuja
muda wowote kulichukua.”
“Ahsante sana Somji.Nitumie
gharama nikutumie sasa hivi”
akasema Mathew na Somji
akamtumia gharama za jumla
akamlipa kwa kumtumia simu.
“Kama si simu hii toka kwa
Somji ningeendelea kulala.Nahisi usingizi sana” akawaza Mathew na
kuingia bafuni kujimwagia maji
baridi halafu akaelekea jikoni na
kujimiminia Whiski katika glasi
akagugumia yote
“Hapa sasa najisikia vizuri.Ni
wakati wa kumuamsha Camilla ili
kazi iendelee” akawaza na kwenda
chumbani kwa Camilla akagonga
mlango mara tatu bila
majibu.Akagonga tena
hakujibiwa.Akaingiwa na wasi
wasi akakinyonga kitasa mlango
haukuwa
umefungwa,akachungulia ndani
chumba kilikuwa kitupu.Camilla
hakuwepo.Mathew akahisi mapigo
ya moyo wake
yanabadilika.Haraka akaenda kumuuliza mmoja wa watumishi
wake alipo Camilla,akamueleza
kwamba amekwenda kukaa katika
bwawa la kuogelea.Mathew
akashusha pumzi akatoka haraka
akaelekea katika bwawa la
kuogelea akamuona Camilla akiwa
amekaa ametulia akisoma kitabu
huku akiwa amevaa spika za
masikioni akisikiliza
muziki.Alikuwa amevaa fulana
ndogo nyeupe iliyofunika kifua
chake na kuliacha wazi tumbo
lake.Alivaa pia kaptura fupi
nyeupe na sehemu kubwa ya
mapaja yake ilikuwa
wazi.Alionekana kuifurahia sana
mandhari ile ya kupendeza pale
nyumbani .Mathew akaenda kukaa katika kiti cha pembeni.Camilla
akavua spika za masikioni
“Nimegonga chumbani kwako
nikastuka baada ya kukuta
chumba kitupu” akasema Mathew
“Sikuwa na usingizi nikaamua
kuja kupumzika hapa.Ninapenda
sana maji na hupenda kupumzika
kandoni mwa bahari hata nyumba
yangu iko karibu na bahari.”
Akasema Camilla na
alipotabasamu vishimo vikatokea
mashavuni pake.Mathew akaishika
chupa ya mvinyo aliokuwa
anakunywa Camilla
“Mvinyo huu unatengenezwa
na zabibu ya
Tanzania,umeupenda? “Nilimtuma yule mtumishi
wako Za..Zan..”
“Zamda.Anaitwa Zamda”
akasema Mathew
“Ndiyo Zamda.Nilimtuma
akaninunulie mvinyo wa Tanzania
akaniletea huu.Nimeupenda ni
mzuri sana.Sijawahi kutumia
bidhaa za kutoka Tanzania
nimeshangaa kwa mvinyo huu safi
ambao unaweza hata kuuzwa
katika masoko ya
kimataifa”akasema Camilla
“Tunazalisha bidhaa nyingi
nzuri ila changamoto inakuwa ni
ushindani mkubwa uliopo katika
soko la kimataifa.Ni mara yako ya
kwanza kufika Tanzania?“Ni mara yangu ya
kwanza.Baba aliponiambia
kwamba ninakuja Tanzania
nilistuka sana kwani ni nchi
ambayo haikuwemo katika akili
yangu kuitembelea.Nimewahi
kuisikia hapo kabla lakini hivi
majuzi Tanzania imekuwa
inatajwa sana duniani kote
kutokana na mambo yaliyotokea
ambayo naamini
unayafahamu.Sijawahi kufika bara
la Afrika ila kuna nchi ninasizikia
kama vile Afrika
kusini,Nigeria,Somalia na
Ethiopia.Ilinilazimu kutenga muda
kuisoma Tanzania ili niweze
kuifahamu vyema.Hata hivyo
nimesoma mambo mazuri sana kuhusu Tanzania.Ni nchi
iliyojaliwa utajiri mkubwa wa
madini ,ardhi nzuri,mbuga za
wanyama ,mlima mrefu sana
Kilimanjaro na zaidi sana watu
wenye upendo mkubwa.Ni nchi
nzuri kuishi ningependa
kuzunguka nchi yote na
kuushuhudia uzuri huu mkubwa
iliyojaliwa nchi hii.Kwa ufupi
nimeipenda sana” akasema
Camilla na kutabasamu
“Unaonekana unapenda sana
utalii” akasema Mathew
“Ni kweli ninapenda sana
utalii.Kila nipatapo nafasi huwa
ninakwenda sehemu mbali mbali
kutalii na kupumzika.Napenda
kujifunza mambo mapya,kujua mila na tamaduni za watu mbali
mbali duniani.” Akasema Camilla
na kunywa mvinyo
“Nisaidie kuhusu bonde la
Ngorongoro .Natamani nipate
picha namna kulivyo kabla
sijatembelea huko” akasema
Camilla.Mathew akatabasamu
“Sijawahi kufika bonde la
Ngorongoro kwa hiyo siwezi
kuelezea uzuri uliopo huko”
Camilla akatoa miwani na
kumtazama Mathew kwa
mshangao mkubwa
“Hujawahi kutembelea bonde
la ngorongoro?kwa nini?
“Sijawahi kwenda huko
japokuwa natamani siku moja
niende” “Umenishangaza sana.Kwa
nini msipende vya kwenu kwanza
kabla ya wageni kutoka nje ?Ninyi
kama watanzania mlipaswa kuwa
mstari wa mbele kutembelea
vivutio vilivyomo nchini kwenu na
kuipatia serikali
mapato.Nimesoma takwimu,idadi
ya watu ni zaidi ya milioni hamsini
na endapo nusu yao wangekuwa
wanatembelea hifadhi za taifa kila
mwaka serikali yenu ingepata
mapato mengi sana.Jifunzeni
kupenda vya kwenu na ndiyo
maana nilimtuma Zamda
akanitafutie mvinyo
uliotengenezwa
Tanzania.Nitakuwa mtu wa ajabu
nikija hapa na kutumia bidhaa za Marekani.Inaonyesha somo la
uzalendo bado linahitajika sana
hapa Tanzania.Mimi ni mmarekani
na ninaitanguliza Marekani kwa
kila ninachokifanya.Tunaipenda
nchi yetu na tunaipigania.Ninyi
vile vile mnapaswa kuwa
hivyo.Mnapaswa kuweka nchi
yenu mbele msisubiri watu wa nje
waje kuwajengea nchi.Tanzania
itajengwa na watanzania
wenyewe” akasema Camilla
“Dah ! Unafaa sana kuwa
mwanasiasa.” Akasema Mathew na
kwa mara ya kwanza akakisikia
kicheko cha Camilla
“Tunapokutana vijana kama
hivi tunabadilishana mawazo na
kupanuana akili.Tunajifunza mambo mapya.Kuhusu siasa
sipendi sana kuwa
mwanasiasa.Baba yangu alipenda
sana siku moja niwe mwanasiasa
kwani aliona chembe chembe za
siaza ndani mwangu lakini badala
yake nimeshia kuwa FBI kazi
ninayoipenda sana.Nilipenda kazi
hii toka nikiwa mdogo na hadi sasa
ndiyo kazi pekee ninayoipenda
.Napenda sana kufanya
uchunguzi,kufichua uovu
japokuwa watu wanasema
kwamba sifanani na hii kazi”
akasema Camilla na wote
wakacheka
“Nilipokuona wakati tunatoka
uwanja wa ndege nilipata wasiwasi
namna ya kuweza kuwa karibu nawe ulionekana ni mtu
usiyependa maongezi lakini
kumbe uko tofauti na vile
nilivyofikiria” akasema Mathew na
Camilla akatabasamu
“Ninaitwa kinyonga kwa jina
la utani kwa sababu ninabadilika
marakwa mara.Naweza kuwa mtu
nisiyependa maongezi,naweza
kuwa mtu wa watu,na nikawa
mkatili zaidi ya Hitler.Unatakiwa
unizoee.halafu …” Camilla akasita
“Niliambiwa kwamba
nitapokewa na mtu anaitwa
Meshack Jumbo lakini nikapokewa
na mtu anaitwa Mathew .Je jina
lako lingine ni Meshack Jumbo?
“Hapana mimi si Meshack
Jumbo.Huyo ni mstaafu aliwahi kuiongoza idara ya ujasusi ya taifa
.Baba yako Jimmy Snow na
Meshack Jumbo ni marafiki
wakubwa sana.Mimi niliwahi
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi lakini kwa sasa
nimekwisha achana na shughuli
hizo,ninafanya shughuli zangu za
biashara.Niliombwa na rais
nimfanyie kazi yake sikuweza
kukataa na nilipokwama
nikamshirikisha Mzee Jumbo naye
akaomba msaada kwa Jimmy Snow
na hapo ndipo ulipotokea na
yakatokea haya yote
yaliokupata.Kwa namna ya pekee
naomba nikushukuru sana kwa
msaada mkubwa uliotusaidia
ambao hatuwezi kuulipa.Vile vile pole sana kwa matatizo yote
yaliyokupata wakati ukiwa katika
harakati za kutusaidia kuupata
ukweli wa jambo tunalolichunguza
.Pamoja na yote yaliyokupata
nakuahidi kwamba utaishi
Tanzania kwa raha na
amani.Meshack Jumbo
nitakupeleka kwake atafurahi
sana kukuona vile vie kesho
nitakutambulisha kwa rais pia”
akasema Mathew
“Niliposoma kwamba
watanzania ni watu wakarimu
sana nilidhani labda ni maneno ya
kutuga lakini pale nilipoambiwa
kwamba kuna ndege maalum
inakuja kunichukua kunileta
Tanzania niliyaamii maneno hayo.Sikutegemea kabisa kama
ndege ile kubwa ingekuja Havana
kwa ajili ya kunichukua mimi
pekee.Ahsanteni sana nyote kwa
msaada huu mkubwa” akasema
Camilla
“Camilla wewe ni mtu muhimu
sana kwetu hivyo kila juhudi ilibidi
ifanyike kuhakikisha unafika
salama Tanzania”
Camilla akanywa mvinyo na
kusema
“Baada ya mambo kuharibika
kule Marekani nilitaka kwenda
Urusi kujificha huko aliko baba
lakini akaniomba kwamba nije
Tanzania kusaidia katika
uchunguzi.Nilikubali kwa kuwa
aliniomba sana hivyo nimekuja.Nataka nifahamu ni
uchunguzi gani ambao nimekuja
kusaidia? Akauliza Camilla
Mathew akamueleza Camilla
kila kitu kuhusiana na suala lile la
kuanguka kwa ndege ya
rais,mauaji ya kanali Sebastian na
kupotea kwa begi la siri lililopewa
jina la football.Camila alisikiliza
kwa makini sana halafu akanywa
mvinyo wake na kusema
“Ushiriki wa Fakrim Alnasor
ambaye ni CIA katika suala hili
unaweka picha ya wazi kwamba
alitumwa kufanya kazi hiyo na
shirika lake la CIA kwa hiyo
serikali ya Marekani inahusika
katika sakata hili.Hii ni aibu kwa
Marekani kwa kitendo kibaya kama hiki.Nakuahidi Mathew
kukusaidia katika jambo hili hadi
tuufahamu ukweli” akatulia kidogo
kisha akasema
“Ninaamini kabisa kwamba
Fakrim aliuawa na CIA na
inaonyesha kwamba walifahamu
kwamba tayari amekwisha
gundulika kuwa anahusika katika
sakata lile na anafuatiliwa.Ili
kuendelea kuificha siri yao
ikawalazimu wamuue.Hii ni mbinu
inayotumiwa sana na CIA endapo
watagundua kwamba kuna mmoja
wa watu wao amekuwa hatari
kwao.Kwa hiyo basi taarifa za
Fakrim kujulikana na kufuatiliwa
zilitoka hapa Tanzania.Tunapaswa
kuchunguza na kufahamu ni nani aliyetuma taarifa hizo.CIA lazima
wana watu wao hapa Tanzania .Pili
baada ya kupekua simu ya Fakrim
tuligundua kwamba mtu wa
mwisho kuwasiliana naye alikuwa
ni Nathan ambaye niliambiwa ni
mpenzi wa rais wa Tanzania”
“Ndiyo Nathan na Dr.Vivian ni
wapenzi.Ahsante kwa taarifa yako
hii imetusaidia sana.Tumefanikiwa
kugundua kwamba Nathan
alipandikizwa kumchunguza rais
ila bado hatujafamu nini hasa
wanachokitafuta .Tumegundua
kwamba Nathan ana mahusiano na
kikundi fulani cha watu hapa
Tanzania,bado tunaendelea
kuwafuatilia na pengine baadae leo tunaweza kupata jibu watu hao
ni akina nani”akasema Mathew
“Kama ni hivyo Nathan ni mtu
muhimu sana.Kwa kuwa ni mtu wa
karibu na rais,inapaswa kufanywa
mipango ili aweze kuja Tanzania
mara moja ili tuanze
kumchunguza” akasema Camilla
“Nathan amekwisha fariki”
akasema Mathew na kumstua
Camilla
“Nathan naye kafariki lini?
Umepata wapi taarifa hizo?
Akauliza Camilla
“Nathan kafariki jana
usiku.Amefia hapa Tanzania
“Amekufaje?Nini kimemuua?
Mathew akamueleza kila kitu
kilichotokea kuhusiana na Nathan.Camilla akabaki na
mshangao.
“Mpaka hapa ulipofika tayari
umepiga hatua kubwa
sana.Mwanga tayari umepatikana
.Nathan ni njia nzuri ya kuelekea
kuupata ukweli.Kilichotokea usiku
wa jana kinaonyesha dhahiri kuna
mtandao hapa Tanzania ambao
unatumiwa na CIA.Ili kuufahamu
vizuri tuchunguze vifaa vile vya
mawasiliano ulivyotoa kwa Nathan
tufahamu kama kuna mtu yeyote
hapa Tanzania aliyekuwa
anawasiliana naye” akasema
Camilla wakaelekea ndani.Mathew
akaleta zile simu alizotoa kwa
Nathan na kumpa Camilla “Hii ni simu maalum ambayo
hutumiwa na watuw a CIA kwa
shughuli za kiofisi pekee.Nina
rafiki zangu wako CIA na wana
simu kama hizi.Tunaweza
kufahamu mambo mengi kupitia
simu hi.Hii simu nyingine ni simu
yake ya matumizi ya kawaida .Hii
nyingine ya tatu ni simu
inayotumia mtandao wa intaneti
na hutumiwa mahala kusiko na
mtandao wa simu” akasema
Camilla na kuifungua kompyuta ya
Nathan
“Hii kompyuta ina namba za
siri ambazo ukifanikiwa kuzipata
basi unaingia moja kwa moja
katika mtandao wa CIA lakini
endapo ajenti akigundulika kupotea basi namba za siri
hubadilishwa haraka haraka sana
kuhofia labda ametekwa
nyara.Tuiweke kwanza pembeni
na tuyachunguze kwanza
mawasiliano yake ya simu.”
Akasema Camila akaenda
kuchukua moja wapo ya sanduku
lake kubwa akaja nalo sebuleni
akalifungua na kutoa kompyuta na
vifaa vingine vingi akaanza
kuviunganisha na alipomaliza
akaichukua ile simu ya Nathan
akaiunganisha na kompyuta yake
akaiwasha.
“Camilla,hawawezi
wakagundua kwamba uko
Tanzania baada ya kuiwasha simu
ya Nathan? Akauliza Mathew “Hawawezi kugundua
chochote kwani tayari nimekwisha
iingiza katika programu maalum
.Usihofu Mathew ninao utaalamu
mkubwa sana katika haya mambo”
akasema Camilla na sura yake
ilionyesha muda huo alikuwa
kazini.Alibonyeza bonyeza
kompyuta yake kwa muda halafu
akasubiri kidogo na mafaili mengi
yakaanza kufunguka .Baada ya
dakika tano likatokea faili
lililokuwa na kumbu kumbu za
mawasiliano ya Nathan
“Haya ndiyo mawasiliano yote
ya Nathan katika simu hii toka
alipoanza kuitumia.Ni orodha
ndefu sana lakini tuangalie
mawasilino ya hivi karibuni hasa kwa mwezi huu” akasema Camilla
na kuanza kubonyeza tena lakini
mara akaguna
“Mathew kuna tatizo.Mfumo
wao wa mawasiliano ni kwa
kutumia namba maalum.Kila ajenti
wa CIA ana namba yake na hakuna
jina la mtu wala namba yake ya
simu inayoonekana bali
kinachoonekana ni namba ya
ajenti.Ni vigumu kutambua nani
yuko wapi”
“Hakuna namna yoyote ya
kuweza kuzitambua namba hizo ili
tuwafahamu watu wake walioko
Tanzania? Au kama kuna ugumu
tuichunguze hii simu yake
anayotumia kwa mawasiliano ya
kawaida “Hatuwezi pata chochote cha
kutusaidia katika simu hiyo kwani
mambo yote ya muhimu yako
katika simu hii anayotumiwa kwa
shughuli za kiofisi” akasema
Camilla na kutafakari kwa muda
halafu akasema
“Itanilazimu kuomba msaada
Marekani ili tuweze kupata
tunachokihitaji.Kuna rafiki yangu
anafanya kazi CIA nitamuomba
anisaidie kuzitambua namba hizi”
“Camilla hilo ni jambo la
hatari sana.Unatafutwa na CIA
halafu unataka kuwasiliana nao?
Ni vipi kama wakifahamu kuwa
upo Tanzania?Sikushauri ufanye
hivyo Camilla.Tutafute namna
nyingine ya kufanya” “Hakuna namna nyingine ya
kufanya Mathew zaidi ya kuomba
msaada.Mtu ninayetaka
kumuomba msaada ninamuamini
niliwahi kuwa katika mahusiano
naye ya kimapenzi na amekuwa
ananisaidia mara kwa
mara.Usiogope hatari Mathew
kwani maisha yetu yamezungukwa
na hatari kila kona.Naomba simu
yako” akasema Camilla na Mathew
akampa simu yake.Akaandika
namba na kupiga simu ikaita
“Hallow” ikasema sauti ya
upande wa pili
“Jack,tafadhali naomba
usistuke wala usitamke jina langu
kama uko na watu karibu.Ni
mim….” “Catherine nimekuelewa
nitakujulisha baadae” akasema
yule jamaa wa upande wa pili na
kukata simu.
“Amekata simu ! akasema
Camilla
“Lazima atakuwa karibu na
watu ila atapiga tena”akasema
Camilla
“Camilla una hakika
hakutakuwa na tatizo lolote kwa
kuwasil……………………..” Mathew
hakumaliza sentensi yake simu
ikaita
“Amepiga” akasema Camilla
na kuipokea
“Hallo Jack”
“Camilla mambo gani hayo
unafanya? Kwa nini unanipigia wakati unafahamu kabisa kwamba
unatafutwa?Huogopi? Kuna msako
mkali sana unaendelea hivi sasa
kukutafuta”
“Usihofu Jack.Nafahamu kama
ninatafutwa lakini hawatoweza
kunipata kama hutawaambia
nilipo” akasema Camilla na ukimya
ukapita
“Nafahamu huwezi kufanya
hivyo Jack na ndiyo maana
nimekupigia.Nahitaji msaada
wako”
“Unahitaji nini Camilla?
“Ninakutumia namba ya simu
ya mmoja wa watu wenu,nataka
uingie katika kumbu kumbu zenu
uangalie kwa mwezi huu
amewasiliana na mtu yeyote wa Tanzania ? Kama yupo naomba
nipate namba zake za simu”
“Camilla hilo
haliwezekani.Nitajiingiza kwenye
matatizo makubwa .Hicho
unachotaka nikifanye ni kitu cha
hatari sana halafu sina uwezo wa
kuingia mahala zinakohifadhiwa
kumbukumbu hizo.Watu wa daraja
la juu zaidi yangu ndio wenye
kuruhusiwa kuingia katika
kompyuta za kuhifadhi
kumbukumbu hizo.Samahani
sintaweza kukusaidia
Camilla.Naomba huko ulikochukua
tahadhari sana kwani unatafutwa
mno.Mimi sintamueleza mtu
yeyote,itabaki siri yangu kwamba
uko Tanzania ila nakuomba usinipigie simu tena utaniweka
katika matatizo makubwa”
“Jack tafadhali usikate simu”
akasema Camilla
“Nafahamu kitu
ninachokuomba unisaidie ni
kigumu sana na cha hatari lakini
tafuta namna ya kufanya uweze
kunisaidia .Ni muhimu mno
kwangu.Ukishindwa wewe
kunisaidia hakuna mwingine
atakayenisaidia.Nakuomba sana
Jack unisaidie.Siku zote umekuwa
unaniomba turudiane ukidai
kwamba unanipenda kuliko kitu
chochote ,huu ni wakati wa
kuthibitisha maneno yako.Kama
kweli unanipenda,unanijali na
kunithamini hutaogopa kuingia katika hatari kwa ajili yangu,kama
ambavyo mimi sikuogopa kuingia
katika hatari wakati ule kwa ajili
yako” akasema Camila.Jack
akafikiri kwa muda na kusema
“Naomba unipe kama dakika
kumi halafu nitakupigia”
“Ahsante Jack” akasema
Camilla na kukata simu
Jack ameniomba nimpe muda
alifanyie kazi hilo suala na
atanipigia simu baada ya dakika
kumi.Si suala rahisi na ni kitu cha
hatari sana lakini sina mtu
mwingine anayeweza
kunisaidia.Tunahitaji taarifa na
mtu pekee anayeweza kutusaidia
kwa sasa ni Jack ambaye yuko
katika ofisi za CIA. Hawezi kukataa kunisaidia kwa sababu kwanza
ananipenda sana,pili hata mimi
nimewahi kumsaidia sana wakati
fulani na niliyaweka maisha yangu
hatarini kwa ajili yake.Tatu
ninayafahamu mambo yake mengi
kwa hiyo hawezi kukataa
kunisaidia wakati nina
shida.Usihofu Mathew tutapata
jibu ndani ya muda mfupi ujao”
akasema Camilla.Aliendelea
kubonyeza kompyuta yake na
mafaili mbali mbali yakaendelea
kufunguka
“Camilla amenikumbusha
niliwahi kuwa na rafiki yangu
anaitwa Anitha alikuwa ni
mtaalamu sana wa kompyuta na
alinisaidia mno katika shughuli zangu nyingi.Katu siwezi
kumsahau Anitha” akawaza
Mathew
Zilipita dakika ishirini,simu ya
Mathew ikapigwa alikuwa ni
Jack,Camilla akapokea
“hallow Jack”
“Nisikilize Camilla.Nimefanya
jambo ambalo sikuwa
nimetegemea kulifanya na tayari
nimeingia katika matatizo
makubwa.Hapa niongeapo tayari
ninafuatwa kwa hiyo nitakueleza
haraka haraka nilichokipata.Kuna
Seli mbili ambazo Nathan alikuwa
na mawasiliano nazo
nchiniTanzania ambazo ni 214A na
110C.Nimefanikiwa kupata namba
za simu za 214A naomba uchukue kalamu na karatasi nikutajie.”
Akasema Jack na haraka haraka
Camilla akachukua kalamu na
karatasi akaandika namba
alizotajiwa na Jack.
“Hiyo seli nyingine hujapata
namba zake? Camilla akauliza
“Hapana sikufanikiwa kupata
namba zake.Wakati nakaribia
kuzipata nilikutwa katika chumba
hicho na kulazimika kuua mtu ili
niweze kutoka salama na kukupa
taarifa hizi hivyo sikufanikiwa
kuzipata namba za seli
110C.Camilla nimeifanya kazi yako
na nimekuthibitishia kwamba nina
kupenda na niko tayari kufanya
chochote kwa ajili yako.Ninataka
ufahamu jambo moja ,hapa nilipo ninafuatwa na muda wowote
wanaweza wakanikamata,sitaki
wanikamate wanitese ili niwaeleze
kwa nini nimefanya vile
nilivyofanya kwani lazima
niwaeleze mahala
ulipo.Nimalizapo kuzungumza
nawe hapa ninaichoma moto hii
laini ya siku halafu na mimi …”
akasita kidogo kisha akasema
“Nitajiua”
“Jack !!..akaita Camilla kwa
sauti kubwa ya mstuko
“Nakupenda sana
Camilla.Nakupenda sana na
ninayafanya haya yote kwa sababu
ya upendo wangu mkubwa
kwako.Jitahidi sana kujiweka
salama kwani unatafutwa mno.Kwa heri Camilla” akasema
Jack na kukata simu.Camilla
akajaribu kupiga lakini
haikupatikana tena.Sura yake
ilibadilika na kuonyesha woga
mkubwa
“Kuna nini Camilla?
“Ile kazi niliyomuomba Jack
anisaidie imemletea matatizo,
amegundulika na anasakwa.Ili
kuepuka kuteswa na kutoa siri
kwamba ni mimi niliyemtuma
aifanye kazi ile hivyo ameamua
kujiua.” Akasema Camilla na
macho yake yakalengwa machozi
“Jikaze Camilla.Jack ni shujaa
na ana upendo wa dhati kwani na
ndiyo maana ameamua hata
kuyatoa maisha yake kwa ajili ya kukulinda wewe” akasema Mathew
na Camilla akafuta machozi
“Tuendelee” akasema
‘Jack ameniambia kwamba
katika seli hizi zote,ni seli mbili tu
ambazo Nathan amekuwa
akiwasiliana nazo nchini
Tanzania.Amezitaja seli hizo ni
214A na 110C.Amefanikiwa kupata
namba za simu za seli 214A
ambazo ni hizi hapa” akasema
Camilla na kumpa Mathew ile
karatasi aliyoandika namba zile za
simu.
“Hakufanikiwa kupata namba
za seli nyingine” Camilla
akashindwa kuyazuia machozi
kumtoka “Pole sana
Camilla.Tumuombee Jack ili
Mungu aweze kumsamehe makosa
yake na kumuweka mahala pazuri
ikiwezekana abadilishe nia yake ya
kutaka kujiua” akasema Mathew
“Alikuwa ni mtu mwema na
alinipenda sana.Mathew naomba
dakika chache nitarejea” akasema
Camilla na kuondoka akaelekea
chumbani kwake machozi mengi
yakimtoka
“Camilla ameumizwa sana
lakini haya ndiyo mambo ya
kuumiza tunayokutana nayo
wakati tunafanya hizi
kazi.Nakumbuka hata mimi
niliwahi kuumia sana
nilipowapoteza watu wangu wawili wa karibu sana Noah na
Anitha.Siwezi kuwasahau wale
marafiki zangu.Niliumia sana
wakati ule kwa hiyo ninaufahamu
uchugu alionao Camilla wa
kumpoteza Jack” akawaza Mathew
na kuishika ile karatasi yenye zile
namba za simu ambazo Camilla
alipewa na Jack akazitazama
“Jack anasema hizi ni namba
za simu za Tanzania lakini mbona
haziko kama namba za simu
tulizozizoea?Huu ni mtandao gani
wa simu?akajiuliza baada ya
namba zile kuonekana ziko tofauti
na zile za mitandao mbalimbali ya
simu iliyoipo Tanzania
“Sipaswi kuumiza kichwa
wakati msaada ninao” akawaza Mathew na kuchukua simu yake
akazitafuta namba za rais
akampigia
“Mathew habari za muda huu?
“Nzuri kabisa mheshimiwa
rais.Samahani kwa usumbufu”
“Hakuna usumbufu wowote
Mathew.Nilikuomba mwenyewe
kwamba unipigie muda wowote
utakaohitaji kuzungumza nami
jambo lolote.”
“Ahsante mheshimiwa
rais,nimekupigia kuna msaada
mdogo ninahitaji lakini kabla ya
kuomba msaada napenda kwanza
nishukuru kwa msaada wako yule
mtu wangu niliyekuomba
amewasili nchini salama.Ahsante
sana kwa hilo” akasema Mathew “Usijali Mathew ni furaha
yangu kama amefika salama.Kama
kuna kingine chochote unahitaji
usisite kunijulisha.Nimekwisha
kuahidi kitu chochote kilicho
ndani ya uwezo wangu
nitakusaidia”
“Nashukuru mheshimiwa
rais.Nina suala dogo nahitaji
msaada wako.Kuna namba fulani
za simu lakini zinaonekana ni
namba maalum haziko kama
namba za simu
tulizozizoea.Nahitaji kufahamu
namba hizi ni za nani” akasema
Mathew
“Namba hizo za simu
zinahusiana chochote na
uchunguzi wako? “Ndiyo mheshimiwa rais
nikimfahamu huyo mtu mwenye
hizi namba nitashukuru sana”
akasema Mathew na kumtajia rais
zile namba
“Sawa Mathew nitakupa jibu
muda si mrefu baada ya kupewa
jibu namba hizi ni za nani”
akasema Dr.Vivian na kuagana na
Mathew akakata simu.
“Camilla amenisaidia sana
kwani nisingeweza kupata mtu
ndani ya CIA wa kuweza kunisaidia
kuzifahamu namba hizi.Suala hili
sasa limeanza kuwa na
mwangaza.Nikifanikiwa kumpata
huyu mmoja basi nitafanikiwa
kumpata yule mwingine ambaye
Jack ameshindwa kumpata.Kama Nathan amekuwa na mawasiliano
nao basi watakuwa na mahusiano
na CIA na yawezekana wakawa
ndio viongozi wa mtandao
uliotengenezwa na CIA.Swali
ninalojiuliza ni kwa nini Marekani
wafanye jambo hili?Wamemuua
rais Anorld Mubara,wakamuua
kanali Sebastian lakini bado
hawajakata tamaa wanaendelea na
harakati zao na sasa
wanamchunguza rais
Dr.Vivian.Wanatafuta kitu gani?
Wanataka kumuua naye? Hapana
sina hakika kama wanataka
kumuua bali kuna kitu
wanakitafuta hapa Tanzania
ambacho lazima
nikifahamu.Wamewekeza sana katika jambo hilo wanalolitafuta
na lazima ni jambo lenye maslahi
makubwa kwao” akaendelea
kuwaza Mathew halafu akatoka
pale sebuleni akaenda chumbani
kwa Camilla akagonga
mlango.Camilla akamruhusu
mgongaji aingie ndani
“Mathew samahani kwa hili
lililotokea nimeshindwa
kujizuia.Jack ni mtu wangu wa
karibu sana na ndiyo maana
kitendo hiki kilichotokea
kimeniumiza mno.Mimi na Jack
tumewahi kuwa na nyakati za
furaha sana.Tulikuwa
tunapendana mno hata baada ya
kutengana lakini bado tuliendelea
kuonyeshana upendo.Sikutegemea kama mwisho wa Jack utakuwa
namna hii” akasema Camilla
“Pole sana Camilla.Nafahamu
uchungu ulio nao.Hata mimi
nimewahi kuwapoteza watu wangu
wawili wa karibu sana ambao ni
zaidi ya ndugu zangu.Walifariki
katika mazingira ya kikazi kama
haya yaliyomkuta Jack.Haya ndiyo
madhira tunayokutana nayo katika
kazi hizi.Jipe muda wa kutosha wa
kupumzika.Tutaendelea na kazi
zetu baadae”
“Mathew hata kama nikilala
hapa kitandani kwa mwezi mzima
siwezi kubadili kilichotokea.Kama
Jack amekufa sintaweza
kumrudisha.Twende tukaendelee
na kazi.Tayari nimekwisha poteza kazi yangu na nimeikimbia nchi
yangu kwa sababu ya hii kazi na
zaidi ya yote nimempoteza mtu
muhimu sana katika maisha
yangu.Tunachotakiwa kufanya ni
kuhakikisha haya yote hayaendi
bure bali yanakuwa na matunda”
akasema Camilla
“Nimemtumia rais zile namba
za simu tulizozipata toka kwa Jack
ili atusaidie tuweze kufahamu
namba zile ni za nani.Yeye ana
mkono mrefu kwa hiyo ni rahisi
sana kufahamu kuliko tukianza
kulichunguza suala hilo
sisi.Analifanyia kazi jambo hilo na
baada ya kupata nani mwenye hizo
namba ataujulisha” akasema Mathew na ukapita ukimya huku
Camilla akiwa amejiinamia
“Camilla ndani tunaweza
kuutumia muda huu kufahamiana
zaidi kama hutajali”akasema
Mathew na Camilla akainuka.
“Naomba tukaketi katika
bwawa la kuogelea.Nikikaa karibu
na maji mara nyingi huwa
inanisaidia sana kupunguza
mawazo niliyo nayo” akasema
Camilla wakatoka wakaenda
katika bwawa la kuogelea.
“Historia yangu si nzuri sana
na mara nyingi huwa sipendi
kuongelea kuhusu maisha yangu
binafsi kwani huamsha donge
kubwa lililonikaba kooni lakini
nadhani huu ni muda muafaka wa kuliondoa donge hilo” akasema
Camilla
“Kuwa huru nieleze kama
utaona inafaa” akasema
Mathew.Camilla akafikiri kwa
muda na kusema
“Nitakueleza kwa kifupi”
“Nimechanganya damu.Baba
yangu ni mzungu na mama ni
mwafrika.Historia ya mapenzi yao
baba aliniambia kwamba
walikutana katika tamasha la
muziki wakawa marafiki.Mama
alitokea katika familia masikini
sana wakati familia ya baba ilikua
na uwezo makubwa
kifedha.Walipendana na wakawa
wapenzi na baadae wakafunga
ndoa na wakanizaa mimi lakini kitendo cha baba kufunga ndoa na
mwanamke mweusi
hakikuwapendeza ndugu na
marafiki zake na kukawa na chuki
kubwa.Siku moja mama yangu
alitekwa akitokea kufanya
manunuzi tukamtafuta na kesho
yake akaokotwa akiwa amekufa
kwa kupigwa risasi.Hadi leo hii
hatufahamu ni nani waliomuua
lakini naamini ni mipango ya
ndugu za baba ambao walichukia
sana baba alipoamua kumuoa
mwanamke mweusi.Kitu hicho
kimenikaa kooni na kila
nikikumbuka huwa naumia
sana.Mama yangu alifariki nikiwa
mdogo na sikupata nafasi ya kukaa
naye kwa muda mrefu.Inaniumiza sana Mathew” akanyamaza na
kuinamisha kichwa
“Pole sana” akasema Mathew
“Ahsante”
“Niliamua kujiunga na FBI ili
niweze kufanya uchunguzi nani
alimuua mama yangu.Japo
sijafanikiwa bado kulifanya hilo
lakini ninaamini siku moja
nitafanya na nitawafahamu wale
waliomuua mama yangu na
watafikishwa mbele za
sheria.Kitendo cha kumpoteza Jack
leo kimekwangua tena kidonda
cha mama yangu.Naomba
nikwambie kitu kimoja Mathew
ambacho sijawahi kumwambia
mtu mwingine yeyote”
“Niambie tafadhali” “Naichukia Marekani sana.Ni
nchi yangu lakini naichukia mno.Ni
ngumu sana kuwa mweusi nchini
Marekani ingawa ni nchi yenye
kujipambanua kwamba ina
demokrasia ya kiwango cha juu
lakini sisi watu wenye asili ya
Afrika tunabaguliwa mno.Uwepo
wangu hapa Tanzania ndani ya
bara la Afrika najiona huru,nina
furaha na amani.Sina mpango wa
kurejea Marekani tena.Ila kuna
jambo moja nataka nilifanye na
nitahitaji msaada wako”
“Sema unahitaji nini Camilla?
Camilla akatafakari kidogo na
kusema
“Nataka tuhakikishe tunapata
ushahidi wa kutosha wa Marekani kujihusisha katika jambo hili
unalolichunguza na kisha
nitaianika nchi hii kwa dunia
nzima ifahamu namna taifa hili
kubwa linavyotumia nguvu zake
kukandamiza nchi ndogo.Mimi
nitakusaidia kwa kila namna
nitakavyoweza ili jambo hili liweze
kukamilika na tuufahamu
ukweli.Nataka nilipize kisasi kwa
kumuua mama yangu” akasema
Camilla.
“Camilla ahsante sana kwa
kuniamini na kunieleza historia
yako.Inaumiza na ninakupa pole
sana kwa kumpoteza mama yako.
Pili nakuahidi kwamba endapo
utapendezwa kuishi hapa
Tanzania mimi binafsi nitajitahidi kufanya kila linalowezekana ili
uweze kuyafurahia maisha ya hapa
ya amani na tatu suala hili
litafanikiwa kama tutashirikiana
kwa pamoja.Nakuahidi
litamalizika na ukweli utaujua
kwani hadi hapa lilipofika tayari
kuna mwanga umejitokeza.Kitu
muhimu ni kushirikiana na kwa
pamoja tutaweza kulifumbua
fumbo hili gumu”
“Mimi niko tayari kukupatia
kila aina ya ushirikiano Mathew ili
kufanikisha jambo hili na ndiyo
maana nilikubali kuja huku baada
ya kunusa harufu ya ushiriki wa
Marekani katika suala hili.Nina
ujuzi mwingi nina utaalamu
mkubwa katika teknolojia,nina uwezo wa kucheza na silaha kama
nimezaliwa nazo nina weza
kupigana kwa ujumla ninaweza
mambo mengi kwa hiyo ukiwa na
mimi jisikie amani jihesabu kama
uko na askari mia moja.” Akasema
Camila na Mathew akatabasamu
“Ahsante sana na karibu
katika operesheni hii” akasema
Mathew
“Vipi kuhusu wewe? Unaweza
ukanieleza japo kwa ufupi historia
yako?Camilla akauliza
“Historia yangu kama ilivyo
yako si nzuri sana na
nimekumbana na mambo mengi ya
kusikitisha pia na mimi pia wapo
wapendwa wangu nimewahi
kuwapoteza lakini nitakueleza kwa ufupi pia” akasema Mathew na
kumsimulia Camilla historia ya
maisha yake na mambo magumu
aliyopitia hadi alivyopoteza familia
yake na hadi alivyokutana na
Peniela wakaoana na mwisho
wakaachana
“Umepitia mambo mengi sana
Mathew pole” akasema Camilla
“Ahsante.Wengi tulio katika
kazi hizi tumepitia mambo mengi
ya kusikitisha lakini imekuwa ni
sehemu ya maisha yetu na ndiyo
maana ninajitahidi sana kuwekeza
katika biashara ili niweze kusahau
kabisa maisha haya.Nataka kuishi
maisha ya kawaida.Nataka nikae
mbali kabisa na hizi kazi lakini
kadiri ninavyojitahidi kukaa mbali nazo inaonekana zinanitafuata
zenyewe.Kwa mfano kazi hii
sikuwa nimefikiria kama
ningeweza kuifanya.Toka
nilipokutana na Peniela sikuwahi
kufanya kazi yoyote ile na
niliamini nimekwisha achana na
kazi hizi na nikaanza kuyafurahia
maisha lakini baada ya kuachana
na Peniela nikarudi nyumbani
nimekutana tena na hii kazi
nikashindwa kukataa ila naamini
sintafanya tena kazi nyingine
baada ya hii.Kwa wale wapenzi wa
mchezo wa mpira kuna lugha huwa
inatumika kwa wachezaji
wanaostaafu kwamba
wanatundika daruga.Na mimi nitatundika daruga endapo kazi hii
itakamilika na kuniacha salama.”
“Usihofu Mathew utakuwa
salama.Mungu ana makusudi yake
na siku zote atasimama upande
wetu kwani tunajitolea nafsi zetu
kwa ajili ya nchi zetu,kwa ajili ya
usalama wa watu wake” akasema
Camilla
“Vipi kuhusu huyu mwanamke
uliyeachana naye?Bado
mnawasiliana?Camilla akauliza
“Tunawasiliana .Tuna mtoto
mmoja mrembo anaitwa Anna
Maria hivyo mawasiliano yetu ni
mazuri,hatuna sababu ya kuwa na
ugomvi”
“Nini sababu ya kuachana
kwenu? “Ni migogoro tu inayotokea
katika ndoa”
“Nafahamu kuna migogoro
mingi ndani ya ndoa japokuwa
bado sijawahi kupitia huko ila
nafahamu kuna migogoro.Kwako
wewe na Peniela nini kilivunja
ndoa yenu?
“Ni usaliti.”
“Nani alimsaliti mwenzake?
“Peniela alianzisha mahusiano
ya kimapenzi na bilionea mmoja
wa kifaransa hivyo sikuona sababu
ya mimi kuendelea kung’ang’ania
mapenzi ambayo yamegeuka
mchezo wa kuigiza.Ni mimi ndiye
niliyeomba tuachane na kila
mmoja akaendelee na maisha
yake” “Bado anakupenda?Na wewe
bado unampenda?
“Masuala ya mapenzi hayo
yamekwisha kwani
kinachotuunganisha hivi sasa ni
mtoto wetu Ana Maria pekee.”
akasema Mathew na Camilla
akatabasamu
“Ukiona mtu anakwepa
kulijibu Swali kama hilo ujue bado
wanapendana” akasema Camilla
na wote wakacheka
“Kuachana si uadui na siwezi
kuwa na uadui na mama wa mtoto
wangu na isitoshe bado tuna
miradi kadhaa tunashirikiana kwa
hiyo lazima tuwasiliane”
“Nimekuelewa
Mathew.Mwenzako ameolewa vipi kuhusu wewe? Unasubiri nini
kuoa?
“Kwa sasa jambo hilo
nimeliweka pembeni na
ninawekeza katika biashara zangu
labda hapo baadae ninaweza
kulifikiria hilo suala.”
“Wengi baada ya kuachana na
wapenzi wao huwa wanasema
hivyo kwamba hawafikirii mapenzi
tena lakini kumbe ana wapenzi wa
siri zaidi ya wawili wa
kumfariji.Nakushauri Mathew
kama utampata mwanamke
ambaye unaona anakufaa na
anaweza kuendana nawe basi
usimuache.Maisha ni mafupi sana”
“Ahsante kwa ushauri huo
Camilla” “Unawekeza katika biashara
gani ?
Kabla Mathew hajajibu simu
yake ikaita alikuwa ni
rais,akaipokea
“Hallo mheshimiwa rais”
“Mathew lile suala
limekwisha fanyiwa kazi na watu
wangu na nimeletewa
majibu.Namba Ile kweli ni ya
Tanzania na namba kama zile
huwa zinatolewa kwa watu
maalum.Nimestuka kidogo baada
ya kumfahamu mwenye ile namba
kwamba ni George Mzabwa mkuu
wa idara ya usalama wa taifa
aliyejiua”
“George Mzabwa?! Mathew
akashangaa “Ndiyo Mathew” akasema rais
na ukimya ukatanda
“Mathew ! akaita rais baada ya
kuona kumekuwa kimya
“Mheshimiwa rais ahsante
sana nitawasiliana nawe baadae”
“Mathew kabla hujakata simu
naomba kuuliza.Ulisema kwamba
namba hizi zinahusiana na kile
unachokichunguza je huyu George
alikuwa anahusika pia katika
jambo hili? Akauliza
“Mheshimiwa rais
nitawasiliana nawe baadae na
tutazungumza zaidi.Vipi kuhusu
zile picha kuna taarifa yoyote
tayari umeipata?
“Mpaka sasa bado ila
nimewapa wakuu wa jeshi la polisi hadi saa saba mchana wa leo niwe
nimepata majibu watu wale ni
akina nani.Nitakapoletewa majibu
nitakujulisha mara moja”
“Ahsante mheshimiwa
rais,uwe na siku njema” akasema
Mathew na kukata simu
“Vipi Mathew mbona
umestuka ?akauliza Camilla
“Kuna kitu kimenistua
kidogo.Siku chache zilizopita
mkuu wa idara ya suala wa Taifa
alijiua kwa kujipiga risasi ofisini
kwake na chanzo cha kujiua kwake
hakikufahamika japo bado
uchunguzi unaendelea.Namba hizi
ambazo ametupa Jack zilizotoka
katika simu ya Nathan ni za huyo
George Mzabwa” akasema Mathew “Mambo yameanza kuiva.Ni
wazi huyo mkuu wa idara ya
usalama wa taifa alikuwa na
mawasiliano na Nathan hivyo naye
anahusika katika jambo
hili”akasema Camilla
“Kama ni hivyo basi mtandao
huu ni hatari sana na
unawahusisha watu wazito.Mkuu
wa usalama wa taifa ni mtu mzito
na ndiyo maana sishangazwi na
mambo haya yaliyotokea kumbe
kuna mikono ya watu wazito kama
huyu.George alijipiga risasi ofisini
kwake na kuacha ujumbe kwa rais
na katika ujumbe huo alimweleza
rais kwamba ameshindwa kupata
majibu ya suala hili na akataka rais
pia kuachana nalo kwani hataweza kupata majibu.George alikuwa
mshirika wa Nathan na nina
hakika alifahamu kila kitu kuhusu
sakata hili ila swali ni kwa nini
alijiua?Hapa lazima kuna sababu
iliyopelekea akachukua maamuzi
haya .Itabidi twende nyumbani
kwake tukazungumze na mke
wake na pengine tunaweza
kubahatika kupata kitu chochote
cha kuweza kutusaidia.George
ndiye atakayeweza kutuunganisha
na mtandao wote wa Nathan”
akasema Mathew na kuchukua
simu akampigia Theresa
“Unaendelea na huyo
mmarekani wako? Akauliza
Theresa na kumfanya Mathew
atabasamu “Hana tatizo huyu mtoto
ametulia hapa karibu yangu”
akasema Mathew
“Mhhn !! Theresa akaguna
“Mbona unaguna Theresa?
Akauliza Mathew
“Kwa nini hukunieleza kama
una mpenzi mwingine baada ya
kuachana na Peniela?
“Huyu si mpenzi wangu bali ni
rafiki yangu na amekuja kunisaidia
katika kazi hii” akasema Mathew
“Hongera”
“Tuachane na hayo
Theresa.Nimekupigia kukupa
taarifa za jambo moja la
muhimu.Nilichukua simu tatu kwa
Nathan.Camilla amezitambua na
katika simu hizo kuna moja ambayo huitumia kwa masuala
yake ya kikazi na katika simu hiyo
kwa msaada wa Camilla tumeweza
kugundua kwamba alikuwa na
mawasiliano na watu wawili hapa
Tanzania.Mtu ambaye tumeweza
kufahamu kwamba alikuwa
anawasiliana na Nathan ni George
Mzabwa”
“George Mzabwa? Akauliza
Theresa kwa mshangao mkubwa
“Ndiyo Theresa.Nathan
alikuwa anawasiliana na
George.Kuna mtu mwingine pia
alikuwa anawasiliana naye lakini
hatukuweza kupata namba
zake.George alikuwa na
mawasiliano na Nathan na hii
inatudhihirishia kwamba alikuwa anafahamu kinachoendelea na
inawezekana akawa alishiriki kwa
namna moja au nyingine katika
matukio yale mawili” akasema
Mathew
“Nimestuka sana.Kumbe
George naye alikuwa ana
mahusiano na Nathan! Mathew
nimezidi kuogopa kama watu
wakubwa kama George wanakuwa
wasaliti kwa taifa lao”
“Nguvu kubwa kwa sasa
inaelekezwa kwa George ili
kufahamu watu wengine
anaoshirikiana nao.Naomba
unielekeze nyumbani kwake ili
nikazungumze na mke wake”
akasema Mathew na Theresa akamuelekeza nyumbani kwa
George mzabwa
“Nitakutaarifu baadae
nikitoka nyumbani kwa
George.Wewe endelea kupumzika”
akasema Mathew na kukata simu
“Tunaweza kuondoka sasa
kwenda nyumbani kwa George”
Mathew akamwambia Camilla
wakajiandaa na kuondoka
kuelekea nyumbani kwa
George.Walipita gereji ambako
gari la Mathew lilipelekwa
akachukua gari lake na kuliacha
lile la Meshack Jumbo wakaelekea
nyumbani kwa George
Waliwasili nyumbani kwa
George Mzabwa kama
alivyoelekezwa na Theresa na kukuta watu wengi wakiendelea
na matanga.Mathew na Camilla
wakatoa pole kwa wafiwa halafu
wakataka kuonana na mke wa
marehemu.Jibu walilopewa
likamstua kidogo Mathew
“Amekuja kuchukuliwa hapa
muda si mrefu na mtu
fulani.Walitoka nje wakazungumza
na baada ya muda mama Mzabwa
akaja akatuaga kwamba kuna
mahala anakwenda atarejea muda
si mrefu,wakaingia katika gari na
kuondoka” akasema mama mmoja.
“Hakuwaeleza anakwenda
wapi?
“Hapana hakueleza chochote
na hakuna anayefahamu
anakwenda wapi.” Akasema mama yule na mara uso wake
ukaonekana kubadilika.Mathew
akagundua kitu usoni pa yule
mama akageuka nyuma na
kukutana na wanawake watatu
waliovaa mavazi marefu na
kujifunika nyuso zao wakabaki
wanaonekana macho pekee.
“Mbona huyu mama
ameogopa baada ya kuwaona hawa
wanawake wakiingia hapa?
Akajiuliza Mathew na ghafla
kukatokea jambo ambalo hakuna
aliyelitegemea.Wale wanawake
watatu waliokuwa wamevaa
magauni marefu kila mmoja
akatoa bunduki ndogo aliyokuwa
ameificha ndani ya gauni lile na
kuanza kuachia risasi na kuwataka watu wote walale chini .Watu wale
walitawanyika haraka sana na
kumbe hawakuwa peke yao
walikuwepo wengine nje na idadi
yao ikaongezeka mle ndani.Ndani
ya sekunde chache watu wote
waliokuwepo eneo lile wakalala
chini wakiwamo Mathew na
Camilla
NINI KITATOKEA HAPO
MSIBANI? NANI KAMCHUKUA MKE
WA GEORGE MZABWA? USIKOSE
SEASON 2
MWISHO WA SEASON 1
0 comments:
Post a Comment