Simulizi : Scandle (Kashfa) (3)
Sehemu Ya Tatu (3)
“Mchungaji unaweza
ukajitetea kwa kila namna uwezavyo lakini bado swali hili linahitaji majibu kwa nini wale jamaa wanawafuatilia wewe na wenzako?Kuna kitu gani wanakichunguza kwenu?Mathew akauliza
“Hapo hata mimi ninakosa majibu.Ninaomba ndugu zangu tusaidiane katika hilo tuweze kupata majibu kwani jambo hili hata mimi binafsi limenistua sana.Niko tayari kutoa kila aina ya ushirikiano ili majibu yaweze kupatikana kwa nini wanatufuatilia mimi na wenzangu hao watu ambao unadai ni wafanya biashara wa dawa za kulevya” akasema mchungaji Zabron.Mathew akamtazama kwa muda halafu akasema
“Mchungaji Zabron watu kadhaa wamekwisha poteza maisha hadi sasa na bado wanaendelea kupoteza maisha kama hatutawadhibiti watu hao.Tunahitaji sana msaada wako.Kama kuna kitu chochote ambacho unakifahamu ambacho unadhani kinaweza kutusaidia kujua sababu ya watu hawa kuwafuatilieni basi tueleze.Hata kama ni kitu kidogo sana kinaweza
kutusaidia” akasema Mathew
“Ndugu zangu
nimetafakari sana lakini bado sijaona kama kuna kitu chochote ambacho kinaweza kuwafanya hao jamaa wakatufuatilia mimi na wenzangu.Kwa nini jambo hili tusilifikishe kwa uongozi wa kanisa letu ili wafahamu kinachoendelea na uchunguzi ufanyike? akasema mchungaji Zabron
“Umezungumza kuhusu
uongozi wa kanisa lenu kuna kitu nimekumbuka.Kuna kitu ambacho binafsi bado kinanipa ukakasi kuhusu uongozi wa kanisa lenu” akasema Mathew na kumtaka Ruby kumsaidia kupandisha kitanda halafu akaendelea “Tulitaka kufahamu sababu iliyomfanya mchungaji Adam aache kumfuatilia mwanae aliyepotea na badala yake akaenda Morogoro tena yeye na mke wake.Katika hali ya kawaida hiki kitu hakiwezekani.Mchungaji Zabron wewe ni mzazi hebu jaribukuvaa viatu vya mchungaji Adam Watwila je ungefanya nini?Ungeweza kuacha kumtafuta mwanao
ambaye umeambiwa mambo ya kushangaza aliyoyafanya shuleni na badala yake ukaenda safari tena na mke wako?
“Hilo haliwezekani kabisa” akasema mchungaji Zabron
“Hivyo ndivyo ilivyotokea.Mchungaji Adam
aliacha zoezi la kumtafuta mwanae na akaenda Morogoro.Mimi na wenzangu tunajiuliza kwa nini aliamua kuacha zoezi hilo la kumsaka mwanae na akaenda Morogoro?Hapo bado tumekwama.Hatujapata jibu la kuturidhisha.Tulionana na mkuu wa kanisa lenu Nabii mkuu Kasiano tukamuuliza jambo hilo na akatueleza kwamba yeye ndiye aliyemtuma mchungaji Adam kwenda Morogoro kwa shughuli za kikanisa.Tuliendelea kujiuliza kanisa lina wachungaji zaidi ya nane ambao wako makao makuu peke yake kwa nini basi asitumwe mchungaji mwingine kwenda Morogoro na Adam akabaki kushughulikia suala la mwanae aliyetoweka? Akauliza
Mathew
“Mchungaji Lucas kidogo ametufumbua macho kidogo” Mathew akaendelea
“Kabla ya kuuawa Lucas alitueleza mambo kadhaa yaliyotokea siku ile alipofariki
Adam” akasema Mathew na kumuelezea Zabron kile alichoelezwa na mchungaji
Lucas
“Mimi pia nilikuwa mmoja wa walioitwa siku hiyo kwenda kushiriki maombi ya kumuombea binti wa mchungaji Adam aliyepotea.Mambo hayo aliyokueleza Lucas ni ya kweli kabisa” akasema Zabron
“Swali la mwisho ambalo nilimuuliza Lucas ni kama kulikuwa na shughuli yoyote ya kikanisa ambayo ingemlazimu Adam kwenda huko lakini nakumbuka Lucas alinijibu kwamba hakumbuki kama kulikuwa na sababu yoyote ya msingi iliyomfanya Adam aende
Morogoro.Aliuawa wakati akinijibu swali hilo” akasema
Mathew na kunyamaza
“Kwa upande wako una majibu gani?Unadhani kulikuwa na ulazima wa mchungaji Adam kwenda Morogoro na kuacha kumsaka mwanae?
“Jibu alilokupa Lucas ndilo hata mimi ninaweza kujibu kwamba sote tulishangaa kusikia Adam
amepata ajali akielekea Morogoro.Kama alivyokwambia Lucas kwamba baada ya maombi tuliachana na Adam akaelekea ofisini kwa nabii mkuu na ninaamini safari ya kwenda Morogoro ilianzia hapo kwani aliondoka akiwa na gari la nabii mkuu na hakuaga mtu yeyote hadi tulipopata taarifa amefariki dunia
“Hapo ndipo panaposhangaza mchungaji Zabron,kama nabii alifahamu kile kilichokuwa kinaendelea kwa Adam kwa nini akamtuma Morogoro tena yeye na mke wake? Kwa nini asingemtuma mchungaji mwingine na Adam akabaki kushughulikia suala la mwanae?Mathew akauliza “Kweli hapo kuna ukakasi.Kama kulikuwa na
suala lolote la kikanisa wachungaji wengine tulikuwepo pale tungeweza kutumwa lakini pamoja na mzigo mzito aliokuwa nao Adam bado alitumwa Morogoro.Inashangaza sana” akasema mchungaji Zabron
“Nadhani umeuona
ukakasi uliopo katika suala hili.Mimi na wenzangu tunaamini kwamba Adam aliuawa baada ya kufahamu kile alichokuwa anakifanya mwanae akiwa shuleni.Tunaamini mwanae Zowe alikuwa na mahusiano na mtu ambaye aidha ni mfanya biashara au ana mahusiano na wafanya biashara wa dawa za kulevya.Tunazo sababu za kuamini hivyo kutokana na maisha ya anasa kubwa aliyokuwa akiishi Zowe shuleni.Ukisikia maisha
aliyokuwa akiishi utahisi mwili unakutetemeka.Zowe aligharamiwa kwa kiasi kilichopitiliza.Hakuna mzazi anayeweza akamgharamia mwanae kama alivyokuwa anagharamiwa Zowe hivyo tunaamini mtu aliyekuwa anafanya hivyo ana pesa chafu na hakuona ugumu kuzitapanya na baada ya kitendo cha kuyafahamu haya kilisababisha kifo cha Adam.Ninajiuliza je safari ya
Adam na mkewe kwenda Morogoro ilipangwa makusudi ili Adam auawe? Ukitazama
kwa kina safari hiyo utagundua kwamba Adam hakuwa ameipanga bali ilitokea ghafla tena baada ya kuibuka suala la mwanae hivyo ni wazi safari ile ilipangwa makusudi ili aweze kuuawa na kuondolewa kwani tayari alikwisha onekana ni hatari kwao.Baada ya hapo linaibuka swali gumu kujibu je nabii Kasiano anahusika katika jambo hilo la kupanga mauaji ya Adam? Akauliza Mathew na wote wakabaki kimya wakitazamana
“Nimetafakari sana juu ya hili suala nikachambua nukta moja hadi nyingine nikabaki na hilo swali ambalo ninalileta
kwenu tulitafutie majibu” akasema Mathew “Nimekusikiliza maelezo yako kwa makini lakini swali lako ndilo ambalo nimeshindwa kulielewa.Una maanisha kwamba nabii Kasiano anajihusisha na dawa za kulevya? Akauliza mchungaji Zabron
“Sijasema anajihusisha kwani sina ushahidi wa kutosha.Kama umenisikia vizuri nimetoa maelezo ya namna suala hili linavyokwenda na mwisho nikauliza swali kama mkuu wa kanisa lako nabii Kasiano anahusika katika kupaga mauaji ya Adam?” akasema Mathew
“Kasiano hawezi kuwa na mahusiano kwa namna yoyote ile na wafanya biashara wa dawa za kulevya,Yule ni mtumishi nabii wa Mungu.Ni mpakwa mafuta wa bwana na
hawezi katu kujihusisha katika mambo machafu kama hayo.Nashauri ingekuwa vyema angeelezwa jambo hili angeweza kulipatia ufumbuzi wa kinabii.Kasiano ni nabii mwenye uwezo mkubwa na wa kushangaza kabisa ndiyo maana ana maelfu ya waumini wanaomkubali” akasema Zabron.Mathew akamtazama kisha akamtaka Ruby amtoe Zabron mle chumbani
“Ruby na Nawal naamini mmenielewa nilipouliza lile swali kama Kasiano nahusika katika kifo cha Adam na mke wake.Mchungaji Zabron hawezi akakubali hata kidogo hata kama ingekuwa ni kweli mkuu wake anahusika katika jambo hilo kutokana na utii mkubwa walio nao kwa viongozi wao.Hata pale wanapokuwa na uhakika mkubwa kwamba viongozi wao wamekosea hata kama upo ushahidi lakini huthubutu kusimama nao na kuwatetea.Tuachane na hilo turejee katika msingi wa swali langu.Nabii Kasiano alidai yeye ndiye aliyemtuma Adam Morogoro na ukifuatilia maelezo niliyoyatoa utaona kabisa kwamba kuuawa Adam ulikuwa ni mpango maalum
umepangwa na swali
linalokuja ndilo hilo nililouliza kama je Kasiano anahusika na mauaji yale?Kama si yeye je alitumiwa na watu kumtuma Adam Morogoro ili waweze kupata nafasi ya kumuua? Akauliza Mathew
“Nadhani tufungue tena
jalada jipya la Nabii
Kasiano.Tumchunguze tujue kama ana mahusiano na hawa watu wa Black
Mafia.Ninasema hivyo kwa sababu mkikumbuka hata
tukio la siku ile shuleni alikosoma Zowe ilikuwa ni baada ya kutoka kanisani kwake kumuhoji kuhusu Adam Watwila.Watu wale waliotuvamia ambao tunaamini ni Black Mafia walifahamuje kama tuko pale shuleni?Ukiacha hilo,lingine ni hili la wachungaji wa kanisa lake kufuatiliwa kila wakifanyacho.Ni kitu cha ajabu sana ambacho kinaleta maswali mengi na kuwasha taa nyekundu kuashiria kuna kitu
hapa katika kanisa la injili ya wokovu.Mtanisamehe kwa kumhisi vibaya mtumishi wa Mungu lakini mambo yamebadilika sana zama hizi ndugu zangu.Kumekuwa na wimbi la makanisa yanayoibuka kila uchao yakiongozwa na watu wajiitao manabii,wengine manabii wakuu kama Kasiano,wengine wanajiita mitume na nimewahi kusikia hata kiongozi wa kanisa akijiita kuhani mkuu.Sina maana mbaya msinielewe vibaya lakini nyuma ya haya makanisa yanayoibuka kila uchao kuna siri nyingi.Kuna baadhi ya makanisa ambayo yanatumika kama mwavuli wa kufunika mambo Fulani.Kuna makanisa ambayo yanaanzishwa lakini dhumuni lake ni kufanya ujasusi,wapo viongozi wa dini wanatumika katika ujasusi lakini pia yapo makanisa yanatumika kutakatisha fedha,wapo pia viongozi wa haya makanisa ambao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.Kuna mambo mengi nyuma ya haya makanisa ya kisasa sitaki kuingia ndani zaidi ila
ninataka tufungue uchunguzi wa hili kanisa la injili ya
wokovu.Tumchunguze
Kasiano tujue siri ya utajiri wake,tufahamu nyendo zake” akasema Mathew
“Tunasubiri mfumo wa
SNSA urejee kwani ndiyo tunaoutumia katika uchunguzi wetu” akasema Ruby
“Ngoja tumsubiri Zari arejee tujue kuna nini kimeendelea huko alikoenda” akasema Mathew akaendelea na mazungumzo mengine na
Nawal
**************
Rais Festus alikaa chumbani kwake akitafakari yale mambo yaliyokuwa yametokea usiku ule.Kulikuwa na mambo mawili yaliyokuwa yanamsumbua kichwa chake
kubwa likiwa ni lile aliloelezwa na Zari kwamba limepigwa bomu la kielektroniki na kuzima kila kifaa cha elektroniki katika eneo la kuzunguka SNSA.Kabla ya
kupata taarifa hizo za bomu,alikuwa amepewa taarifa nyingine kwamba mfungwa Frank Kang0le aliyekuwa anatumikia kifungo katika gereza la siri,alifariki dunia ghafla katika chumba chake.Ilikuwa ni taarifa iliyomstua sana Rais na akaelekeza mwili wake upelekwe hospitali kuu ya Mtodora kwa ajili ya uchunguzi.Alimtuma daktari wake akasimamie uchunguzi kujua kile kilichomuua Frank.
“Hawa jamaa kama wanamiliki hadi mabomu hatari namna hii basi si kundi dogo.Ni watu hatari mno ambao kuna ulazima wa kuongeza nguvu katika kuwashughulikia.Kama wana bomu hilo la kuzima vifaa vyote vya kielektroniki ni vipi kama wakipiga bomu hilo karibu na ikulu na kila kitu kikasimama? Hawa si watu wa kufanyia mzaha hata kidogo” akawaza Rais Festus akajaribu kumpigia simu Ruby lakini simu yake haikupatikana.
Wakati akiendelea kutafakari mara mlango wake ukagongwa akaenda kuufungua alikuwa ni mlinzi wake akamjulisha kwamba daktari wake alikuwa amefika,akatoka mara moja kwenda kuonana naye
“Dr Laurian karibu” akasema Rais Festus
“Ahsante mheshimiwa Rais samahani kwa usumbufu muda huu wa mapumziko” “Usijali.Karibu” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
kilichonileta hapa ni kuleta majibu ya uchunguzi uliofanywa kuhusu kilichosababisha kifo cha Yule mtu.Taarifa kamili hii hapa” akasema na kumkabidhi Rais bahasha
“Kwa ufupi imebainika kilichomuua Yule mtu ni sumu kali aliyochomwa ambayo inaweza kuua kwa muda mfupi sana” akasema Dr Laurian
“Sumu?
“Ndiyo mheshimiwa Rais” akajibu Dr Laurian
“Ahsante sana Dr Laurian kwa majibu haya” akasema Rais Festus na kuagana na Dr Laurian akaondoka
“Nilihisi kifo cha Frank kina walakin.Nani kamuua na kwa nini?Kwa nini auawe sasa? Akajiuliza Rais Festus
“Frank aliwahi kufanya kazi SNSA na nilielekeza afungwe gereza la siri kutokana na kile alichokifanya kushirikiana na majambazi kuiba kiasi kikubwa cha fedha benki.Kifo hiki cha Frank kina mahusiano yoyote na hiki kilichotokea leo SNSA? Akajiuliza Rais Festus.
“Nani kamuua
Frank?Gereza lina ulinzi mkali sana huyo muuaji amewezaje kuingia humo ndani na kumchoma sindano Frank bila walinzi kufahamu wakati kila chumba kina kamera ndani yake? Hapa kuna kitu ambacho lazima kichunguzwe” akawaza Rais Festus na kumpigia simu Zari lakini bado simu yake haikuwa inapatikana
“Zari aliniambia nisiende katika makazi yao kwa hofu ya usalama wao lakini lazima nikawafikishie jambo hili linaweza kuwa na msaada katika uchunguzi wao” akawaza na kumuita Godfrey Lamuli mkuu wa kikosi cha walinzi wa Rais ambaye alifika mara moja katika sebule ya Rais
“Godfrey kuna jambo nataka nikuombe unisaidie” “Ndiyo mheshimiwa Rais”
“Ninataka kwenda katika ile nyumba yangu ambayo hukutana na Zandile.Nataka niende kwa siri bila mtu yeyote kufahamu”akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais” akasema Godfrey
“Godfrey ninafahamu unachotaka kukisema ila ninaomba msaada wako tafadhali ni muhimu sana.Ninataka kwenda huko peke yangu bila mlinzi yeyote ninataka unipeleke kwa kutumia gari lako” akasema Rais Festus.Godfrey akafikiri kidogo halafu akasema “Sawa mheshimiwa
Rais.Tutaondoka na gari langu ngoja nikafanye maandalizi halafu nitakujulisha” akasema Godfrey na kutoka
“Lazima nikaonane na akina Mathew haya mapambano yanazidi kuwa makubwa.Vile vile ninataka kujua maendeleo ya Mathew Mulumbi” akawaza Rais Festus na mlango wake ukagongwa alikuwa ni Godfrey akampa maelekezo Rais namna watakavyoweza kuondoka **************
Gari la Godfrey lilifika katika nyumba ya Rais waliko
akina Mathew.Makomando
walilizuia gari lile na mara kioo cha nyuma ya gari kikashushwa na taa ya ndani ya gari ikawashwa komando Yule akastuka baada ya kumuona Rais Festus.Akasimama kwa ukakamavu mkubwa na kumsalimu Rais.Haraka haraka geti likafunguliwa na
gari lile likaingia ndani Rais akashuka akasalimiana na wale makomando waliokuwa wanalinda jengo lile kisha wakamuongoza kuelekea ndani.
Akina Ruby wakiwa katika chumba alimo Mathew wakipata chakula mara mlango ukafunguliwa na wote wakastuka baada ya kumuona Rais.Hawakuwa wametegemea kabisa kumuona Rais mahala pale.Ruby na Nawal wakasimama wakasalimiana na rais halafu akamfuata Mathew wakasalimiana
“Karibu sana mheshimiwa
Rais,sikutegemea kabisa kama ningekuona hapa muda huu” akasema Mathew
“Pole sana Mathew nimefuahi kukuona ukiendelea vyema” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais ninaendelea vyema ninakushukuru sana kwa kuwa pamoja nasi ninakushukuru pia sana kwa msaada wa damu”
“Mathew kama
nilivyowaambia kwamba ninyi ni jeshi langu ambalo nitalitumia katika mapambano yangu hivyo lazima
nihakikishe ninawaunga mkono na kuwa pamoja nanyi katika kila hali ndiyo maana nilipopata taarifa za lile tukio nilistuka sana nikaamua kuja kuungana nanyi” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
tumepata mgeni jioni ya leo anaitwa Nawal” akasema Mathew.Rais Festus na Nawal wakasalimiana
“Nawal ni mwenzetu na alipewa uraia wa Tanzania na Rais mstaafu Dr Fabian
Kelelo.Amewahi kufanya kazi CIA na kwa sasa anaishi
Riyadh Saudi Arabia” akasema Mathew
“Karibu sana Tanzania
Nawal” akasema Rais Festus
“Ahsante”
“Zari hajarejea? Akauliza Rais
“Hapana
bado.Umewasiliana naye? Akauliza Ruby
“Ndiyo alinipigia simu kuna mahala alikwama na alihitaji msaada wangu” “Alikwama? Akauliza Mathew
“Ndiyo alikwama.Kuna jambo limetokea usiku huu ndilo ambalo limenifanya nije hapa kuonana nanyi” akasema Rais Festus
“Kuna jambo limetokea katika maeneo ya kuzunguka ofisi za SNSA.Tukio lenyewe ni kwamba kila kitu cha kielektroniki kimesimama na hakifanyi kazi.Umeme umekatika eneo hilo,simu zote hazifanyi kazi,magari yamesimama,mifumo yote ya kompyuta haifanyi kazi lakini ni katika eneo la kilometa moja”
“EMP” akasema Mathew
“Hata Zari ameniambia hivyo kwamba hilo ni bomu la kielektroniki ambalo kazi yake ni kuzima vifaa vyote vya kielektroniki katika eneo litakapigwa”akasema Rais Festus
“Kama limepigwa karibu na SNSA basi walilenga jengo
hilo kwa kuwa tayari walifahamu Mathew Mulumbi yuko pale”akasema Ruby “Walifahamukama
Mathew yuko SNSA? Akauliza Rais Festus
“Ndiyo mheshimiwa Rais walifahamu Mathew yuko pale ndiyo maana tukamuhamisha” akasema Ruby
“Inashangaza sana.walifahamuje?Wana watu wao ndani ya SNSA? Akauliza Rais
“Bado hatujui kama wana watu wao ndani ya SNSA ndiyo maana tulikuwa na wasiwasi na wale walinzi wako uliokuja nao jana pale SNSA”
“Mhh ! Mlifahamuje kama wanazo taarifa za Mathew kuwepo pale SNSA? Akauliza Rais Festus
“Mheshimiwa Rais kuna jambo ambalo hatujakueleza bado ni kwamba kuna mtu ambaye amekuwa akinitumia ujumbe mara kadhaa akinipa maonyo mbali mbali.Tunaamini mtu huyo yuko pamoja na hao jamaa na anatusaidia kutupa taarifa”
“Hamjaweza kumfahamu mtu huyo ni nani?
“Hapana bado.Hawa
jamaa wanatumia teknolojia kubwa katika kujificha.Hawataki kuacha hata nafasi ndogo ambayo inaweza ikasababisha wakajulikana ndiyo maana wako makini sana katika kila wanachokifanya.Tunahisi vile vile kwamba huyo mtu atakuwa anatufahamu ndiyo maana anatusaidia kutupa taarifa.Usiku wa jana alinitumia ujumbe akanionya kwamba tumuhamishe Mathew kwani tayari wamekwisha jua mahala alipo” “Hiki kikundi ni hatari sana.Nashindwa kuelewa hawa wametumwa kuja kufanya ujasusi hapa nchini au ni watu wa namna gani?Ni kweli wanajihusisha na dawa za kulevya pekee au kuna kitu kingine? Akauliza Rais
“Mheshimiwa Rais kama tulivyowahi kukueleza kwamba hili ni kundi la Black Mafia na kazi yao ni kuwalinda miungu wa dawa za kulevya na kuhakikisha biashara hiyo inakwenda bila vikwazo vyovyote” akasema Mathew na kumueleza Rais kuhusiana na kundi hilo la Black Mafia
“Yote haya nisingeweza kuyafahamu kama si ninyi ndiyo maana niko tayari kufanya kila linalowezekana kuhakikisha vita hii tunaishinda”
“Tunashukuru sana mheshimiwa Rais
“Kwa hiyo ndugu zangu fahamuni SNSA kwa sasa hakuna kinachoendelea,kila kitu kimesimam.Lakini kuna kitu ambacho ninakihusisha na tukio hili” akasema Rais na kunyamaza kidogo
“Kuna mtu anaitwa Frank
Kangole aliwahi kufanya kazi SNSA.Aliwahi kuwasaidia majambazi kuiba fedha katika benki kwa kutumia mfumo wa SNSA na alipogundulika nikaelekeza afungwe katika gereza la siri.Kila siku jioni huwa ninapata taarifa ya
maendeleo ya wafungwa katika gereza hilo la siri lakini jioni ya leo nimepokea taarifa kwamba Frank amefariki nikashangaa na kuelekeza uchunguzi ufanyike kujua chanzo cha kifo chake nikamtuma daktari wangu akasimamie zoezi hilo na ameniletea majibu kwamba Frank aliuawa kwa sumu kali.Nimelazimika kuliunganisha tukio hilo la kuuawa Frank na hiki kilichotokea leo SNSA na nimeona niwaletee jambo hili mlitazame pengine linaweza kuwasaidia katika uchunguzi” akasema Rais Festus
“Tunashukuru mheshimiwa Rais kwa kutuletea jambo hili.Kama majibu ya uchunguzi yanaonyesha alikufa kwa sumu ni wazi kuna mtu alimlisha au kumchoma sindano ya sumu hiyo.Tunatakiwa kufanya uchunguzi wa haraka katika suala hili”akasema Mathew
“Jambo la kushangaza ni kwamba kila chumba katika gereza hilo kina kamera na kila mfungwa anafuatiliwa kwa saa ishirini na nne na kila anayeingia katika vyumba vyao anaonekana.Kama ni mtu alimchoma basi ni mpango ulikuwa umesukwa na unawahusisha pia waangalizi wa gereza” akasema Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais jambo hilo linatakiwa kuchunguzwa usiku huu huu.Tukifahamu namna Frank alivyouawa basi itaturahishia kujua kama tukio hilo lina mahusiano yoyote na
kilichotokea leo SNSA” akasema Mathew
“Mathew uwepo wako kitandani unakwamisha mambo mengi sana,nani atakwenda kuifanya kazi hiyo?akauliza Rais
“Bado hakijaharibika kitu mheshimiwa Rais.Japokuwa nipo kitandani lakini ninaendelea kufanya kazi nikiwa hapa kitandani na katika mapambano ataendelea Nawal”
“Nawal?! Rais akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Yeye ndiye anayechukua nafasi yangu na ndiyo maana yuko hapa” akasema Mathew
“Sawa hakuna tatizo kama unamuamini.Ni namna gani mtaufanya uchunguzi huo?akauliza Rais
“Kwa hapo tutahitaji msaada wako ili tuweze kuingia gerezani na kufuatilia kumbu kumbu za kamera na
kuwahoji wahusika wa gereza” akasema Ruby
“Basi nitawapeleka mimi mwenyewe mahala hapo”
“Mheshimiwa Rais ni hatari sana kwako usiku huu”akasema Mathew
“Usijali
Mathew.Nimeamua
kushirikiana nanyi katika hii vita hivyo na mimi lazima nitoe mchango wangu” akasema Rais Festus “Tunashukuru kwa hilo” akasema Mathew.
Rais Festus,Ruby na Nawal wakaingia katika gari la makomando ambalo halipenyi risasi wakaondoka kuelekea katika gereza la siri.
**************
Kasiano alilazimika kuacha mkesha wa sala ukiendelea akaondoka zake akarejea nyumbani.Alikuwa amechoka sana kwani kutwa nzima aliendesha ibada na kuwa na vikao mbali mbali.Mara tu alipoingia chumbani kwake akavua tai yake na kuitupa chini kwa hasira
“Hakuna siku ambayo
Black Mafia wameniudhi kama siku ya leo.Kwa nini wameshindwa kumpata Mathew Mulumbi? Halafu kibaya zaidi Paul amefanya maamuzi ya kijinga sana ambayo yametia doa kanisa baada ya mauaji kutokea pale kanisani.Paul hakupaswa kufanya maamuzi yale bila kunishirikisha kwanza.Hata kama hakunipata katika simu lakini anajua mahala nilipo kwa nini hakunifuata akaniomba ushauri?Imekuwa bahati naibu waziri Keofas amewahi kulimaliza lile suala kwa kudai wale ni majambazi waliokuja kupora kanisani wakauawa na walinzi wangu vinginevyo suala lile lingeweza kutuletea matatizo makubwa” akawaza Kasiano na mara mke wake akaingia
“Pole sana mpenzi” akasema Rita huku akimsaidia
kuvua shati
“Nimechukia sana leo ! Kwa nini kila kitu hakiendi kama ninavyotaka? Akauliza
“Hapa nilipo nina hasira sana na Black Mafia ! Wanalipwa fedha nyingi,millions of money lakini wanashindwa kufanya kazi yao ipasavyo.Wamewezaje kumkosa tena Mathew Mulumbi? Haikuwa rahisi kuipata taarifa ile ya mahala
alipo Mathew lakini wameshindwa kumpata.Wametumia hadi bomu ghali kabisa ambalo tulilinunua kwa mamilioni ya fedha lakini halijaleta manufaa yoyote nimechukia mno! akasema Kasiano
“Darling kuna kitu kimoja ambacho ninataka nikushauri.Kuwa na imani na Black Mafia.Siku zote wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana na hawajawahi kutuangusha hata mara moja.Ni wao wanaosababisha biashara zetu zinakwenda vyema.Wanahakikisha mzigo unaingia salama,wanauhifadhi na kuhakikisha unakuwa salama na ule wa kusafirisha nje ya nchi basi unakwenda.Waamini hata
katika hili watafanikiwa ila wanachopaswa kufahamu ni kwamba sasa hivi mtu wanayeshughulika naye si wa kawaida.Mathew Mulumbi ni mtu hatari ni jasusi nguli ana mbinu nyingi anazitumia anajua kujificha na anaweza kung’amua mahala pa hatari na akaondoka kabla hajafikiwa.Unachopaswa kukifanya ni kuwapa moyo ili waongeze bidii na maarifa” akasema Rita huku akimsugua mume wake mgongoni
“Kuna jambo lingine ambalo bado linaumiza kichwa changu.Mchungaji Zabron mpaka sasa hajapatikana na hajulikani alipo.Alitekwa na wale jamaa na hatujui wamempeleka wapi.Anatakiwa hadi kesho asubuhi awe amepatikana vinginevyo suala lake litachukua sura mpya.Yote haya ameyasababisha Paul kwa maamuzi ya kijinga aliyoyafanya ! Kasiano akanyamaza baada ya simu yake kuita
“Sijui anataka kuniambia nini tena huyu Paul ! akasema Kasiano na kuipokea simu “Paul unasemaje?
“Mkuu tumeendelea kuwahoji hawa mateka tuliowachukua kule SNSA na wamekiri kwamba Mathew Mulumbi alikuwa anapatiwa matibabu katika hospitali pale SNSA toka jana usiku lakini leo hii mchana amehamishwa na hajulikani amepelekwa wapi.Wanadai kwamba kuna watu wawili ambao wako na Mathew hivi sasa ambao ni mkurugenzi wa idara hiyo ya SNSA anaitwa Zarina Faheem na Ruby mke wa Rais mstaafu.Tukifanikiwa kuwapata hao basi tutakuwa tumempata Mathew Mulumbi.Nimekupigia kukupa taarifa hizo mkuu lakini bado tunaendelea kuwahoji hawa watu kujua zaidi namna tunavyoweza kuwapata hao akina Zari na Ruby”akasema Paul
“Ahsante kwa taarifa hiyo Paul japo sijafurahishwa na mambo yaliyofanyika leo hasa kile kilichotokea kanisani.Naomba siku nyingine usifanye maamuzi makubwa namna ile bila kunishirikisha kwanza mimi.Tazama sasa hatujui Zabron yuko wapi na asipopatikana hadi asubuhi ya kesho utakuwa ni mgogoro mwingine”
“Mkuu tunajitahidi sana kwa kila tuwezavyo kuhakikisha kwamba hadi kufika asubuhi ya kesho tuwe tayari tunafahamu mahala alipo Mathew Mulumbi.Tunaamini tukifanikiwa kujua mahala alipo tutakuwa tumempata pia Zabron” akasema Paul
“Nataka mjitahidi
Paul.Sitaki kusikia kuna jambo lingine limetokea” akasema Kasiano na kukata simu
“Walau kuna matumaini yameanza kuonekana.Kuna watu wawili ambao wako na Mathew na mmoja wao ni mke wa Rais mstaafu Fabian Kelelo.Akina Paul wanaendelea kuwasaka na wakifankiwa kujua mahala walipo basi watakuwa wamempata pia na Zabron” “Nini hasa sababu ya kumchukua Zabron?Kuna kitu chochote wanadhani anakifahamu kuhusu sisi? Rita akauliza
“Hapo ndipo
walipojidanganya kwani Zabron hajui chochote kinachoendelea na hata kama angekuwa anafahamu
chochote
asingewaeleza.Nimewajengea wachungaji wote utii mkubwa hata hivyo siwaamini kwa asilimia mia moja ndiyo maana nimeweka watu wa kuwafuatilia kila wakifanyacho na maisha yao kwa ujumla.Binadamu hawaaminiki kabisa anaweza akanasa siri Fulani na akaamua kuitoa lakini mpaka sasa hakuna mchungaji hata mmoja anayefahamu kitu chochote kuhusu mimi na hawajui kama wanafuatiliwa maisha yao kwa saa ishirini na nne” akasema Kasiano
“Natakiwa kuwasiliana na mama Bella kumpa taarifa za kile kinachoendelea” akasema Kasiano na kuchukua simu akampigia Bela
“Kasiano tayari nimeandaa shampeni na mvinyo safi kabisa nikitegemea taarifa njema kutoka kwako.Simu yako hii naamini ina taarifa zile nzuri zitakazonifanya niifungue shampeni yangu kwa madoido! akasema Bella huku akitabasamu.Kasiano akavuta pumzi ndefu na kusema
“Mama Bella utanisamehe lakini usiifungue shampeni yako kwanza” akasema Kasiano na ukimya mfupi ukapita
“We missed him again” akasema Kasiano “Again?!
“Ndiyo mama.Tumemkosa
tena” akasema Kasiano na kumueleza Bella kile kilichotokea usiku ule.
“Huyu Mathew ni mtu wa aina gani?Huyu lazima atakuwa anatumia nguvu za kichawi.Jana tuliambiwa yuko hoi anafanyiwa upasuaji halafu leo hii tunaambiwa amehamishwa.Kasiano wasukume vijana wafanye kazi usiku kucha na wahakikishe hadi kufika asubuhi kesho wawe wanafahamu aliko Mathew Mulumbi.Kuhusu huyu Ruby nitajaribu na mimi kutafuta namna ya kutafuta mahala alipo.Naamini lazima atakuwa na mawasiliano na Rais.Siwezi kuahidi chochote kwa sasa lakini nitajitahidi kufanya kitu ili nifahamu mahala alipo.Nitaendelea kumfuatilia Festus kwa karibu zaidi kwani yeye pia anaweza akatusaidia kufika mahala walipo hao watu kwani wanashirikiana” akasema Bella na kuagana na Kasiano **************
Gari la makomando wa
SNSA liliwasili katika gereza la siri likasimamishwa getini na walinzi.Rais Festus hakutaka kupoteza muda akafungua mlango akashuka na kuwastua sana wale walinzi akawataka wafungue geti gari likaingia ndani wakashuka na moja kwa moja wakaelekea katika jengo lililojengwa mfano wa bohari akausukuma mlango wakaingia ndani na kuelekea moja moja katika ofisi akawakuta watu wawili waliokuwa zamu ya usiku wakiwa wamelala katka sofa wakitazama mziki.Walistuka kama wameona mzimu walipomuona Rais amesimama mbele yao.Wakasimama na kumsalimu kwa adabu
“Vijana kamera zote za vyumbani zinafanya kazi? Akauliza
“Ndiyo zinafanya kazi”
“Nataka muende katika kumbu kumbu za kuanzia asubuhi ya leo katika chumba cha mfungwa namba 72 aliyefariki leo.Nataka kujua nini kilitokea” akasema Rais na mmoja kati ya wale jamaa akakaa katika kompyuta yake akafungua kumbu kumbu za siku ile wakaanza kuzipitia.Mara kukatokea kiza
“Nini kimetokea? Akauliza Rais.Ruby akamtaka Yule jamaa kutoka katika kompyuta akakaa na kuanza kubonyeza haraka haraka kisha akasema
“Hapa kamera ilizimwa na baada ya dakika chache ikawaka tena na cha kushangaza baada ya kamera kuwaka chumba kitupu mfungwa hayupo” akasema Ruby na kupeleka mbele kumbu kumbu ile na kukutana na kiza kingine tena halafu mbele kidogo akaonekana Frank akiwa amelala kitandani
“Kwa huu muda wote ambao mfungwa hakuonekana chumbani kwake alikuwa wapi? Akauliza Rais
“Mheshimiwa Rais sisi tumeingia zamu ya usiku hatujui kilichokuwa kimetokea asubuhi” akasema Yule jamaa “Nani walikuwa hapa asubuhi? Akauliza Rais na Yule jamaa akawataja.Rais akamgeukia komando mmoja aliyeongozana naye akamtaka aongozane na Yule jamaa waende wakawachukue wale jamaa waliokuwa zamu ya asubuhi ambao walikuwa wanaishi katika jengo moja la pembeni na ile bohari
Baada ya dakika chache wakarejea wakiwa na watu wawili waliokuwa wanatetemeka kwa woga baada ya kumuona Rais. “Nataka mniambie nini kilitokea katika chumba namba 72? Akauliza Rais
“Mfungwa namba 72 amekutwa jioni hii akiwa amefariki chumbani kwake nasi tukatuma taarifa kwa mkuu ambaye naamini amekujulisha” akajibu mmoja wao na Ruby akawarejesha katika kumbukumbu za kamera kuanzia asubuhi hadi pale zilipozimwa.
“Baada ya kamera kuwashwa mfungwa hakuwemo katika chumba chake” akasema Ruby na kupeleka mbele hadi pale kamera zilipozimwa tena
“Baada ya kamera kuwashwa Frank akaonekana akiwa kitandani na baadae akakutwa amefariki” akasema Ruby
“Nataka kufahamu muda huu wote ambao Frank haonekani chumbani kwake alikuwa wapi?akauliza Rais na wale jamaa wakabaki kimya
“Nawauliza ninyi ambao mlikuwa zamu ya asubuhi.Kwa nini kamera zikazimwa?Na baada ya kamera kuzimwa Frank alitolewa akapelekwa wapi?Nataka mnipe majibu ama sivyo mtaingia katika tanuru la moto.Mtafia gerezani kwa hiki mlichokifanya ! akasema Rais kwa hasira
“Mheshimiwa Rais
naomba nikueleze ukweli kilichotokea” akasema mmoja wao
“Eleza haraka sana!
“Alikuja asubuhi mkuu Asajile na kutupa maelekezo kwamba anamtaka mfungwa namba 72 na akaelekeza kamera zizimwe akamchukua akaondoka naye.Baadae alasiri akamrejesha akiwa hana fahamu akatutaka kumrejesha chumbani kwake tukafanya hivyo lakini kwa namna alivyokuwa tulibaini alikuwa amefariki dunia akatuambia tukae kimya na kesho kuna mzigo utakuja kwa ajili yetu”
“Mna uhakika Asajile ndiye aliyefanya haya?
“Ndiyo mheshimiwa Rais!
Akajibu mmoja wa wale jamaa “Mungu wangu ! akasema
Rais na kuwaza kidogo halafu akasema
“Ruby tunakwenda nyumbani kwa Asajile”
“Mheshimiwa Rais ! akasema Geodfrey
“It’s okay Godfrey” akasema Rais kisha wakawachukua wale jamaa wawili wakaingia nao garini wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Asajile
“Asajile ni mtu ninayemuamini sana kwa nini akafanya mambo kama haya? Alimpeleka wapi Frank ? Hii inazidi kunipa picha kwamba sina mtu wa kumuamini hata wale watu wangu wa karibu kabisa ambao niliwaamini nikawapa madaraka wamegeuka wasaliti.Asajile lazima ataeleza kila kitu leo ! akawaza Rais
“Ninawashukuru sana akina Mathew kwani bila wao haya yote yasingejulikana.Nisingeweza kufahamu kama kuna kikundi cha wauza dawa za kulevya wameotesha mizizi na wameunda hadi jeshi lao dogo la kuwalinda.Lazima nishirikiane nao kuhakikisha hawa watu wote wanafutiliwa mbali ! akaendelea kuwaza Rais Festus.
Walifika nyumbani kwa Asajile na Rais akashuka pamoja na wale makomando wawili pamoja na Godfrey wakafunguliwa mlango na kuingia ndani moja kwa moja Rais akagonga mlango wa sebuleni.Aliyefungua alikuwa ni mke wa Asajile ambaye nusura aanguke kwa mstuko mara alipomuona Rais .
Rais Festus na watu wake hawakusubri kukaribishwa moja kwa moja wakaingia ndani na kumkuta Asajile akiwa amekaa sofani akitazama luninga naye alistuka sana hadi kitanza mbali alichokuwa amekishika mkononi kikamponyoka na kuanguka.
“Mheshimiwa Rais! Akasema Asajile
“Asajile come with me ! Akasema Rais Festus na kutoka nje Asajile aliyekuwa anatetemeka kwa hofu naye akatoka akiwa amevaa kaptura akamfuata Rais hadi nje
“Get in the car” akasema Rais na Asajile akaingia garini.Alipowakuta wale jamaa wawili nao wako garini akatamani ageuke upepo apotee kwani tayari alikwisha jua mambo yameharibika.Gari likaondoka na kuiacha familia ya Asajile wakishangaa kwa ujio ule wa ghafla wa Rais **************
Rais Festus alirejea katika makazi ya akina Mathew akiwa amefura kwa hasira.
“Mheshimiwa Rais
nadhani ni wakati wa kurejea ikulu” akasema Godfrey
“Godfrey bado nina kazi ya kufanya hapa.Usihofu I’m safe.Hawa jamaa tulionao ni makomando hivyo ulinzi hapa ni wa uhakika ! akasema Rais wakati wakielekea ndani.
“Wasi wasi wangu mheshimiwa Rais ni pale watakapokutafuta wakakukosa” akasema Godfrey
“Usihofu Godfrey.Bado tuna kazi ya kufanya hapa tukimaliza tutaondoka” akasema Rais wakaelekea katika chumba alimo Mathew Mulumbi
“Mathew nimerejea.Zari bado hajarudi?
“Hapana bado
hajarudi”akajibu Mathew
“Asajile na wale jamaa wengine wawili wakaingizwa ndani ya kile chumba “Mathew huyu Anaitwa Asajile Mlabwa.Ni mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi hapa nchini.Hawa wengine wawili ni wafanyakazi wa gereza la siri alikokuwa amefungwa Frank Kangole.Ruby mueleze Mathew kile tulichokipata huko tulikotoka” akasema Rais na Ruby akamueleza Mathew kile walichokipata
“Asajile nadhani umesikia kile alichokisema Ruby.Nataka kufahamu ulimpeleka wapi Frank baada ya kumtoa gerezani?Hakuna haja ya kubishana kwani tunafahamu kila kitu na hawa jamaa wawili wamekiri kila kitu kilichotokea.Naomba uwe mkweli ama sivyo this will be the end of you.Hii ni kesi ya mauaji na nitahakikisha unanyongwa Asajile.Ninaapa nikiletewa hukumu yako ya kunyongwa naapa nitaweka sahihi unyongwe.Nataka unieleze ukweli wote labda ninaweza nikakusamehe” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais haya
yote yaliyotokea leo ni kwa ajili ya kukulinda wewe” akasema Asajile
“Kunilinda mimi? Akauliza Rais Festus
“Ndiyo mheshimiwa Rais” “Kunilinda kwa kuua?
“Huwezi ukaelewa mheshimiwa Rais !
“Nataka unieleweshe
Asajile ama sivyo huu utakuwa mwisho wako ! akafoka Rais Festus
“Mheshimiwa Rais hicho nilichokueleza kinatosha siwezi kueleza zaidi !
“Oh my God ! akasema Rais akimtazama Asajile kwa hasira
“Kwa nini unataka kuyaharibu maisha yako Asajile?Kwa nini unataka kuiacha familia yako inateseka?Wanakulipa kiasi gani hao wanaokutumia kwa manufaa yao? Akauliza Rais
“Mheshimiwa Rais
narudia tena nimeyafanya haya yote kwa ajili yako wewe !
“Simuelewi huyu mtu kitu gani anakizugumza ! akasema Rais Festus kwa hasira
“Mathew mimi ninarejea ikulu,nawaachia huyu mtu tafadhali hakikisheni hadi kufika asubuhi tayari awe amesema alishirikiana na akina nani kumuua Frank.Nataka washirika wake wote wafahamike ! akasema Rais Festus kwa hasira na kuagana na akina Ruby akaongozana na Godfrey huku akitanguliwa na gari la
makomando wakaondoka
kuelekea ikulu.Akiwa garini akampigia simu IGP Yeremia Mwaipopo
“IGP ninataka ufanyike utaratibu usiku huu huu watumwe askari nyumbani kwa mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi Asajile Mlabwa wakapekue nyumba yote waondoke na vifaa vyake vyote vya kutunzia kumbu kumbu,kompyuta,simu nk.Baada ya kuvipata vifaa hivyo nijulishe nitakupa maelekezo navihitaji ikulu usiku huu”akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais samahani kwa kuuliza.Kuna tatizo lolote kwa Asajile?
“Ndiyo.Kuna jambo kubwa amelifanya nitakueleza tutakapoonana” akasema Rais na kukata simu.
Mara tu Rais alipokata
simu IGP akampigia mama
Bella
“Yeremia”
“Bella mambo yameharibika”
“Kuna nini? Akauliza Bella kwa wasiwasi
“Asajile tayari ameingia matatani” akasema Yeremia na kumueleza Bella maagizo aliyopewa na Rais
“Nina uhakika tayari Rais amekwisha jua alichokifanya Asajile na sasa anatafuta kuwafahamu anaoshirikiana nao.Bella mambo yameharibika na tusipoangalia tunaweza kujikuta na sisi tunaharibikiwa.Kwanza hata Asajile mwenyewe anaweza akatutaja kuwa tumeshirikiana naye.Nimechanganyikiwa hapa nilipo.Nimebakiza miaka miwili ya kustaafu sitaki mambo yaniharibikie sasa.Please do something”akasema Yeremia
“Ahsante Yeremia kwa
taarifa hizi.Ngoja nilishughulikie hili jambo” akasema Bella na kukata simu,akatafakari kwa muda halafu akampigia Kasiano
“Mama Bella”
“Kasiano please release the photos ! akasema Bella
“Sijakuelewa mama Bella”
“Nimekwambia sambaza
zile picha za Rais usiku huu.Nataka kesho asubuhi gumzo liwe ni picha hizo !
akasema Bella na kukata simu
Saa kumi na moja
alfajiri,Bella aliamshwa na simu kutoka kwa mmoja wa marafiki zake wa karibu akamjulisha kuhusu kuvuja kwa picha za faragha za Rais.Bella akajifanya kustuka sana baada ya kupewa taarifa
ile
“Eh ! jamani aibu gani hii
huyu mzee amenipa? Akasema
Bella
“Bella usianze kuhukumu kwanza yawezekana picha zile si za kweli na zimetengenezwa kwa ajili ya kumchafua Rais.Fanyeni uchunguzi na mtajua tu ni akina nani wamefanya kitendo hicho na kwa malengo gani” akashauri Yule rafiki wa Bella wakaagana.Baada ya simu kukatwa uso wa Bella ukachanua tabasamu. “Mambo sasa yanakwenda
vizuri.Kuvuja kwa picha hizi kutamfanya asahau kila kitu kinachoendelea hivi sasa na atajikuta akishughulikia suala hili huku sisi tukiendelea kuwasaka akina Mathew Mulumbi.Natakiwa vile vile kufahamu mahala alipo
Asajile.Yule naye tayari ni mtu hatari sana kwetu na lazima tumuondoe” akawaza Bella na kufungua mtandaoni akazitazama picha zile
“Ni aibu kubwa kwa
familia kwa picha hizi lakini hii ni vita na kila silaha lazima itumike bila kujali madhara yake,ninachohitaji mimi ni kushinda hii vita” akawaza Bella halafu akampigia simu Kasiano
“Mama Bella shikamoo”
“Marahaba.Nimeziona
picha tayari.Asubuhi hii nchi itatikisika.Ninachohitaji asubuhi hii ni kuendelea na lile zoezi la kujua mahala alipo Asajile.Fanyeni kama nilivyowaelekeza kwani leo naamini Rais hatajishughulisha na kitu chochote zaidi ya hizi picha hivyo tutumie dirisha hilo kufanikisha mipango yetu yote” akasema Bella
“Ndiyo mama Bella tayari nimekwisha toa maelekezo kwa vijana wanalifanyia kazi suala hilo la kumtafuta Asajile
na asubuhi hii tayari vijana wamekwisha fika kwa Godfrey” akasema Kasiano na Bella akakata simu
“Kinachofuata sasa ni kumfuata Festus.Natakiwa kuwa naye karibu katika
wakati huu ili niweze kufahamu mambo mengi kutoka kwake” akawaza Bella na kuufunga mkanda wa nguo yake ya kulalia akaichukua kompyuta yake na kuelekea katika chumba cha Rais.Akagonga mlango na baada ya sekunde kadhaa Rais akaufungua akakutana na mke wake wakatazamana
“Can I come in? akauliza Bella.Rais Festus akamfanyia ishara aingie ndani
Bella akasimama akamtazama Rais Festus kwa sekunde kadhaa
“Sema kilichokuleta utoke” akasema Rais Festus ambaye hakuonekana kufurahishwa na ujio wa Bella mle chumbani kwake.Bella akatumia sekunde kadhaa kumtazama mume wake
“Mbona unanitazama kama hunijui?
“Festus nimechukua muda kukutazama vizuri kamani wewe kweli niliyekufahamu au ni Festus mwingine ! akasema Bella
“Bella nina mambo mengi
siku ya leo nahitaji kuanza kujiandaa hivyo kama kuna kitu umekuja kunieleza sema mara moja na utoke ! akasema Rais Festus
“Unaweza ukaniambia nini maana ya hiki ulichokifanya? Akauliza Bella na kuiweka kompyuta kitandani.Rais Festus alihisi moyo wake unataka kupasuka baada ya kuziona picha zake za faragha zikiwa tayari mtandaoni.Alizitazama picha zile halafu akainama akashika
kichwa
“Festus hii imevuka mipaka.Ninafahamu udhaifu wako wa kupenda wanawake lakini sikutegemea ungeweza kufika hatua hii ya kujipiga hadi picha kama hizi hatimaye zikanaswa na kusambazwa.Hawa makahaba wako ……”
“Bella stop ! Festus akamkatisha mke wake.
“Kwanza iwe mwanzo na mwisho kumuita huyu m wanamke kahaba.You don’t know her.Huyu ni mwanamke anayejitambua tofauti na wewe ambaye …!
“Festus ! Bella akasema
kwa sauti Kali na Rais festus akanyamaza
“Nimekuja hapa kujadili
suala hili la hizi picha na si
mambo mengine.Samahani kama nimemkosea heshima mwanamke wako lakini mimi bado ni mke wako na aibu hii inanihusu pia mimi kama mke wa rais.Ni aibu ya familia nzima.Watoto wetu watazificha wapi sura zao kwa aibu hii kubwa? Ulifikiria nini Festus kukubali kupiga picha kama hizi? Wewe ni kiongozi,Rais wa nchi oh my God ! akasema Bella na kuweka mikono kichwani
“Sijawahi kupiga hizi picha na siwezi kufanya kitu cha kijinga kama hiki ! akasema Festus
“Hizi picha ni za kutengeneza? I need to know” akasema Bella
“Sifahamu zimepigwaje au nani kapiga.Lazima nihakikishe nimempata mtu aliyepiga picha hizi na huyu aliy……….” Akanyamaza baada ya simu yake kuita alikuwa ni makamu wa Rais.
“Dr Haji habari za asubuhi”
“Nzuri sana mheshimiwa Rais.Mheshimiwa Rais nimepigiwa simu asubuhi hii na mmoja wa watumishi wangu akanieleza kuna kitu kimetokea huko mtandaoni sifahamu kama tayari una taarifa”
“Kama ni kuhusu picha
zangu tayari ninazo taarifa ! “Mhesh…….”
“Dr Haji naomba tuonane baadae tuzungumze” akasema Rais na kukata simu muda huo huo zikaanza kuingia simu mfululizo.
“Kazi imeanza ! akawaza Rais Festus na kuizima kabisa simu yake
“Festus hili ni tukio kubwa kuwahi kutokea katika nchi yetu,ni kashfa kubwa sana hii.Sina hakika kama imewahi kutokea hata sehemu nyingine huko duniani picha za faragha za Rais wa nchi zikavuja namna hii” Akasema Bella
“Bella ninaapa sikupiga hizi picha na wala sijui nani amepiga lakini ninachokifahamu haya ni matokeo ya vita niliyoitangaza dhidi ya biashara ya dawa ya kulevya.Wamenifuatilia hadi wakanipiga picha hizi faraghani wakiwa na malengo yao.Walitaka kutumia picha hizi ili kunilazimisha nifuate
matakwa yao lakini mimi msimamo wangu hauyumbi.Nimekwisha tangaza vita kupambana na biashara ya dawa za kulevya na sintainua mikono kusalimu amri.Walinitishia kuwa watazisambaza picha hizi endapo sintatekeleza matakwa yao lakini pamoja na vitisho hivyo sikuwa tayari kuwapa kile walichokuwa wanakihitaji na ndiyo maana wameamua kuzisambaza hizi picha ili kuniabisha na kunichafua ila mapambano yataendelea sintakata tamaa hata kidogo” akasema Rais Festus na sura
ya Bella ikaonyesha mshangao
mkubwa
“So you knew about this? Akauliza Bella
“Ndiyo nilifahamu jambo
hili litatokea”akajibu Festus
“Ooh Festus ! Festus ! kwa nini ukakubali basi jambo kama hili likatokea wakati ulikuwa na uwezo wa kulizuia? Kitu gani kikubwa walichokitaka hao watu ambacho ulishindwa kuwapa hadi ukatuingiza katika aibu hii? Hukuwafikiria wanao watakuwa katika hali gani baada ya picha hizi kusambazwa? Akauliza Bella “This will pass! Akasema Festus
“No ! this will stay ! Picha hizi zitadumu mtandaoni milele.Hakuna namna ya kuweza kuziondoa tena.Hili ni doa kama la Kaini na utatembea nalo hadi siku unaingia kaburini.Teknolojia haina huruma Festus na hiki kilichotokea hadi wajukuu wa wajukuu zako watakikuta.Dah ! sikutegemea kitu kama hiki kutokea katika maisha yangu.Nitapita wapi mimi ! akasema Bella na kubaki akimtazama Festus
“Watu hao walitaka nini?Fedha? akauliza Bella
“Hawakutaka
fedha.Something else !
“Hicho kitu walichokitaka hakikuwezekana kuwapatia hadi ukakubali aibu hii kubwa itokee Festus? Bella akauliza
“Nimekwisha kwambia
siko tayari kuwapa kile wanachokitaka na kama wana siri zangu nyingine waendelee kuzitoa,lakini siko tayari kusalimu amri kwao”
“Oh my God ! akasema Bella akimtazama mume wake kwa macho ya mshangao
“Arlight Festus jambo hili limekwisha tokea.What’s next? Akauliza Bella
“Hakuna cha kufanya,wamekwisha sambaza picha hizi tayari ni aibu imenipata lakini hakuna kingine cha kufanya” akasema Festus
“Hapana Festus.We need to do something.Huwezi ukaliacha jambo hili likapita hivi hivi”
“Hakuna kitu cha kufanya Bella ! akasema Festus
“Festus more than 50 million Tanzanians wanakutazama wewe kama kiongozi wao.Huwezi ukakaa kimya kwa jambo kama hili la aibu”akasema Bella
“Unataka nifanye nini? Nijitokeze na kudai kwamba picha hizi si zangu? Huyu mtu katika picha si mimi? Hilo haliwezekani.Haya ni malipo ambayo nayapata kwa kujitoa kupambana na biashara ya dawa za kulevya”
“Festus you need me in this ! akasema Bella
“Bella I don’t need anyone to back me up especially you.Nilikufuata nikakupigia magoti kukuomba usimame nami wakati ninakwenda kutangaza nina mtoto wa nje lakini ulikataa.Kwa nini sasa unataka kusimama nami?
“Festus weka pembeni
yaliyopita lakini katika hili we need to fight together.Najua tuna tofauti zetu,kwa sasa tuziweke pembeni na tuwe kitu kimoja.Unadhani ni rahisi kwangu kusimama nawe katika jambo hili? Wanawake wenzang watanichukuliaje mimi wakiona picha hizi? Wengi watatamani kuniona nikienda mahakamani kudai talaka yangu lakini siwezi kufanya hivyo ninataka kusimama nawe ili kupunguza makali ya hili jambo.Mara tu jua litakapochomoza na watu wakaipata habari hii,macho ya wengi yataelekezwa kwangu.Wengi watataka kufahamu ninazungumza nini kuhusu jambo hili.Japo jambo hili umelitenda wewe lakini kamera za waandishi wa habari na macho ya watanzania vyote vinanielekea mimi” akasema Bella
“Unataka kufanya nini? Akauliza Festus baada ya kutafakari
“Hili ni suala la kifamilia zaidi na si suala la kisiasa.I need to get out there and talk to the world.Nataka niwahakikishie watanzania kwamba kila kitu kiko sawa.Nataka niwaambie watu kwamba jambo hili ni la muda mrefu tunalifahamu ndani ya familia na picha hizi zimesambazwa na watu ambao walitaka kuivuruga familia yetu kwa chuki zao za kisiasa” akasema Bella
“That’s not convincing! akasema Rais Festus
“You need to come out with something very convincing.Kama utatokea mbele ya vyombo vya habari lazima uwe na kitu ambacho kitaweza kulipunguza makali hili jambo” akasema Rais
Festus
“Ahsante Festus kwa kunipa nafasi hii.Nipe muda nikatafakari nini cha kufanya.I’ll get you out of this” akasema Bella
“Thank you ! akasema Festus
“Kwa sasa pumzika niachie jambo hili nitalimaliza” akasema Bella na kumsogelea Festus akakaa pembeni yake.Wote wakawa kimya kwa muda mfupi halafu Bella akasema
“Kabla hatujaingia katika mafarakano tulikuwa ni watu wenye furaha sana.Tulikuwa tunaishi kwa amani na upendo mkubwa .Nini kilitokea Festus na kutufikisha hapa? Akauliza Bella
“Unataka kujua tumefikaje hapa? Yote haya ni kwa sababu ya baba yako ! akasema Festus
“Hapana Festus baba
hahusiki na chochote kwa sisi
kufikia hatua hii.Yote haya ni wewe umeyasababisha.Tulianza kuyumba pale ulipozaa na mdogo wangu ! Festus sintakusamehe kamwe kwa kile
ulichokifanya.Nilikusamehe ulipozaa na katibu wako lakini kuzaa na mdogo wangu toka nitoke hilo siwezi kulisamehe! Ni uchafu uliopitiliza Festus.Huwa nafikiria sana kukusamehe lakini nikiliwaza hilo huwa napatwa na hasira nyingi.Tamaa zako ona zilikotufikisha sasa tumepata
aibu ya karne”akasema Bella
“Hupaswi kunilaumu hata kidogo kwani yote umeyasababisha wewe mwenyewe ! akasema Festus “Mimi?! Bella akauliza
“Unadhani sikufahamu kuhusu mahusiano yako na Yule mwandishi wa vitabu ambaye ulimchukua awe mwandishi wa hotuba zako na baadae akawa mpenzi wako?
Ninafahamu kila kitu Bella.Najua mmekuwa mnakutana Dubai,Afrika kusini na hata Ulaya nakufanya mambo yenu.Nilipatwa na hasira ndiyo maana nikaamua kutembea na mdogo wako kulipiza kisasi kwa mambo uliyokuwa unanifanyia.Bella usitake tufukue makaburi tumekwisha kubaliana kuendelea kuigiza maisha ya furaha hadi pale nitakapokuwa nimemaliza kipindi changu cha urais halafu kila mmoja akaendelee na maisha yake kwani hakuna
mapenzi tena kati yetu.Kilichobaki kinatuunganisha ni watoto hakuna kingine.Tafadhali
nenda kafikirie kitu utakachokizungumza na waandishi wa habari na mimi nataka nianza kujiandaa kuikabili siku hii ngumu sana” akasema Rais Festus na kushusha pumzi.
“Don’t worry Festus I’ll handle this! akasema Bella na kuinuka akatoka
“Siku imeanza vibaya sana.Sifahamu ni namna gani nitaikabili dunia kutokana na zile picha za aibu.Bado najiuliza sana namna hawa watu walivyoweza kuzipiga picha zile bila mimi kufahamu.Waliwezaje kuingia mle ndani?Ama kweli hawa watu ni hatari sana” akawaza
Festus
“Lakini sipaswi kuogopa kwani nilifahamu jambo hili linakwenda kutokea na nilikubali litokee hivyo lazima nilikabili japo najua ni jambo litakalonitikisa ! akaendelea kuwaza
Bella alirejea chumbani kwake akiwa mwingi wa furaha na kitu cha kwanza alichokifanya ni kuchukua simu na kumpigia katibu mkuu wa chama profesa Simon
“Mama Bella” akasema profesa Simon
“Mzee Simba shikamoo baba”
“Marahaba mama
Bella.Unandeleaje?
“Huku mambo
yameharibika mzee Simba.Wale jamaa wamezisambaza zile picha”
“Wamesambaza zile picha? Akauliza Mzee Simba
“Ndiyo mzee
Simba”akajibu Bella na mzee Simba akabaki kimya
“Mzee Simba ilishindikana kumpata Mathew Mulumbi kwa wakati ndiyo maana mpango wetu ukashindwa
kufanikiwa na picha zile zikasambazwa.Ninachokuimba mzee wangu ibaki siri yetu na Festus asijue kama tulikuwa na mpango wa kuzuia picha zile zisisambae”
“Nimekuelewa Bella jambo
hilo litabaki siri
“Ahsante sana mzee Simba.Nataka kufahamu ndani ya chama kuna hatua zozote mtazichukua kwa Rais kutokana na picha hizi? Akauliza Bella
“Ni mapema sana kusema chochote lakini naamini kamati ya maadili itakaa na kumuita kuzungumza naye kuhusu jambo hilo kwani yeye ni mtu mkubwa katika chama na kuvuja kwa picha zile kunamshusha thamani yake na kukiabisha pia chama anachokiongoza.Tusubiri kwanza maamuzi ya kamati ya maadili halafu tutajua nini kinaendelea” akasema mzee Simba
“Nashukuru mzee Simba
naomba ulizingatie hilo nililokuomba la usiri” akasema Bella na kukata simu.
“Nimekipata nilichokuwa nakitaka ambacho ni ukaribu na Festus.Najua nikiwa karibu yake nitafahamu mambo yake mengi hususan mipango yake ya mapambano na hao anaowaita wafanya biashara wa dawa za kulevya.Nitaitumia nafasi hii kujua mahala alipo Mathew Mulumbi.Naamini bila Mulumbi hakuna tena vita itakayoendelea” akawaza Bella na kumpigia simu katibu wake akamtaka aandae mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za taasisi yake
***************
Vifo vya watu saba wanaodaiwa kuwa majambazi waliouawa wakiwa katika jaribio la kuvamia kanisa la injili ya wokovu pamoja na tukio la kuzimika kwa vifaa vyote vya kielektroniki katika eneo dogo karibu na ikulu ni habari ambazo zilitawala vichwa vya habari vya magazeti karibu yote.Wakati magazeti yakitawaliwa na habari hizo kubwa,mtandaoni kulichafuka kutokana na kusambaa kwa picha za faragha za Rais Festus
Mayungulu akiwa na mrembo ambaye amekuwa akitawala vyombo mbali mbali vya habari Afrika na duniani Zandile Wepener.Kulikuwa na picha kumi na moja zikiwaonyesha Rais Festus na Zandile wakiwa katika matukio tofauti ya kimahaba.Tatu kati ya picha hizo ziliwaonyesha wakiwa watupu kabisa kitandani.Ukuaji wa kasi wa teknolojia uliwezesha picha zile kusambaa kwa kasi kubwa.
Wakiwa katika makazi yao ya muda,Mathew Mulumbi na wenzake walizipata taarifa za kusamaba kwa picha zile za Rais na Zandile
“Jamaa wameamua
kusambaza picha baada ya Rais kukataa kuwapa kile walichokuwa wanakihitaji.Hawa watu ni wanyama sana unawezaje kusambaza picha kama hizi na kumdhalilisha Rais kiasi hiki? Akauliza Zari
“Rais alifahamu kitu ambacho kinakwenda kutokea baada ya kukataa kuwatimizia kile walichokitaka na ninaamini alikwisha jiandaa kwa jambo hili.Pamoja na kukubali jambo hili litokee lakini nawahakikishia si jambo jepesi hata kidogo kwake na kwa familia yake.Litampa wakati mgumu sana.Kwa kuwa Rais amekubali kuibeba aibu hii kwa ajili ya kutuwezesha sisi kuendelea na mapambano hivyo nawaomba sana ndugu zangu kwa namna yoyote ile tusikubali aibu hii ya Rais ipotee bure.Lazima tuhakikishe tunawapata hawa watu na kuufumua mtandao wao.Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Rais wao yuko katika vita kali na mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya hapa nchini hivyo hawapaswi kumbeza bali wanapaswa kusimama naye.Let’s get to work ladies ! akasema Mathew ambaye tayari alikwisha anza kunyanyuka kutoka kitandani na kukaa pia kutembea kidogo
“Ndugu zangu
mtanisamehe kwa siku ya leo nitawaacha peke yenu ninahitajika sana SNSA.Ofisi inatakiwa kurejea tena hivyo natakiwa niwepo pale kuhakikisha kila kitu kinarejea kama kilivyokuwa ila ninawaomba ndugu zangu mnisaidie kuwatafuta wale mateka.Timu ya makomando sita watakuwepo hapa kwa ulinzi na kazi yoyote ambayo itajitokeza na kama kuna kitu chochote mtakihitaji basi mtanijulisha.Mara tu mambo yatakapokuwa yamekaa sawa nitakuja hapa kuungana nanyi tena” akasema Zari
“Zari ninakuhakikishia watu wote waliotekwa nyara tutawapata” akasema Mathew na Zari akaondoka kuelekea SNSA
“Ruby kuna mambo matatu ambayo nilikupa maelekezo uyachunguze nataka uyafanyie kazi leo lakini kabla ya yote nataka uwasiliane na Rais mueleze kwamba tunahitaji kuipata
simu ya Asajile ili tufahamu ni akina nani ambao amekuwa akiwasiliana nao” akasema Mathew na Ruby akampigia simu Rais kwa kutumia simu ile maalum akamuomba awasaidie kupata simu ya Asajile
“Jana usiku nilituma watu kwenda nyumbani kwa Asajile kuchukua vifaa vyake vyote vya mawasiliano lakini hawakuipata simu yake.Kilichofanikiwa kupatikana ni kompyuta mpakato ambayo nitamtuma Godfrey ailete hapo kwenu muichunguze” akasema Rais Festus na kumtaka Ruby ampe Mathew simu ili wazungumze
“Mheshimiwa Rais” “Mathew unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri mheshimiwa Rais”
“Nafurahi kusikia hivyo.Mathew yawezekana tayari mmekwisha fahamu,wale jamaa wamesambaza zile picha mtandaoni” akasema Rais Festus
“Tayari tumekwisha lifahamu hilo mheshimiwa Rais.Pole sana”
“Hakuna sababu ya kunipa pole kwani tulilitegemea
jambo hili litokee lakini ni jambo zito.Hata hivyo pamoja na uzito wake nitalikabili.Ninataka wakati nikiendelea kulikabili hili jambo na ninyi kwa upande wenu mjitahidi sana kuendelea kuwasaka hawa jamaa kama tulivyokubaliana.Kama kuna kitu chochote mnakihitaji tafadhali mnijulishe mara moja nami naahidi kuwasaidia”akasema Rais Festus
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais,ninakuahidi hatutalala katika kuwasaka hawa jamaa hadi pale tutakapohakikisha tumewapata wote.Narudia tena kukuhakikishia mheshimiwa Rais kwamba hakuna atakayesalia katika mtandao huo” akasema Mathew
“Ahsante sana
Mathew.Nawatakia kazi njema” akasema Rais na kukata simu
“Wakati tunaendelea
kuisubiri kompyuta ya Asajile iletwe hapa Ruby endelea na kazi ya kuchunguza zile sehemu tatu nilizokueleza” akasema Mathew
Rais Festus baada ya kupata kifungua kinywa akaelekea katika ukumbi wa mikutano wa ikulu ambako tayari wafanyakazi wa ofisi yake walikuwa wamekusanyika kufuatia maelekezo yake ya kuwataka wakusanyike hapo .
“Habari za asubuhi ndugu zangu” akaanza kwa kuwasalimu mara tu alipoingia ukumbini
“Ndugu zangu nawashukuru kwa kuja.Ninataka kutumia dakika chache kuzungumza nanyi ili tukaendelee na majukumu yetu” akasema na kuvuta pumzi ndefu
“Naamini nyote tayari mmekwisha fahamu kile kilichotokea.Kuna picha Fulani za faragha za kwangu zimesambazwa mtandaoni.Hakuna kati yenu aliyetegemea siku moja kuona picha kama zile za Rais mtandaoni.Kwa leo sitaki kulizungumzia jambo hilo ila naamini ninyi kama watu wangu na wasaidizi wangu wa karibu mmefadhaishwa sana na jambo hili.Ninachowaomba tuendelee na majukumu yetu ya kazi kama kawaida na suala hili lisiweze kusababisha mabadiliko yoyote katika utendaji kazi wetu.Siku nyingine nitawaiteni na kuwaelezeni kuhusiana na hiki kilichotokea ila kwa sasa nawaombeni tukaendelee na kazi zetu kama vile hakuna kilichotokea.Ahsanteni sana” akasema Rais Festus na kuelekea ofisini kwake akampigia simu Godfrey akamtaka aipeleke komputa ya Asajile kwa akina Mathew
“Jtahidi kuwa makini sana Godfrey asifahamu mtu yeyote kama unakwenda mahala hapo” akasema Rais halafu akatoka akaelekea SNSA kujua kilichokuwa kimetokea usiku na jitihada zinazoendelea kuhakikisha SNSA inarejea katikahali yake ya kawaida ***************
Doroth Kimaro mke wa Godfrey aliwasha indiketa ya kulia akakata kona akashika barabara inayoelekea katika shule ya msingi ya Amazon wanakosoma wanae wawili.
“Mom please send us pizza today.I’m tired of s……………..” Janet mtoto wa Doroth anayesoma darasa la tano katika shule hiyo aliyekuwa amekaa pembeni ya mama yake hakumaliza sentensi yake mara gari moja likawapita kwa kasi kubwa na kwenda kufunga breki mbele yao hivyo kumlazimu Doroth naye kufunga breki za ghafla.Milango wa lile gari aina ya Landcruiser V8 lenye rangi nyeusi lililosimama mbele ya gari la Doroth ikafunguliwa na kwa kasi ya ajabu wakashuka watu wanne wakiwa na bastola wakakimbia
katika gari la Doroth wakamshusha yeye na wanae wakawaingiza katika gari lao kisha wakaondoka kwa kasi kubwa.Lilikuwa ni tukio la
ghafla sana lililowaacha watu wakishangaa namna lilivyotokea.Halikuchukua hata dakika tano.
Watu walikusanyika
mahala lilipotokea tukio lile na kuwataarifu polisi ambao walifika mara moja na kuanza uchunguzi.
***************
Godfrey alifikisha kompyuta kwa akina Mathew kama alivyokuwa ameelekezwa na Rais akakutana na Ruby.
“Tunashukuru sana
Godfrey kwa kutufikishia kompyuta hii.Nataka kufahamu kuna mtu yeyote ukiacha Rais anayefahamu kama umekuja hapa?akauliza Ruby aliyekuwa katika chumba walichokiteua kama ofisi yao wakati Mathew akiwa chumbani kwake na daktari
“Nimekuja kwa tahadhari kubwa kwani hata Rais alinitaka nichukue tahadhari wakati nikija huku hivyo nina
uhakika mkubwa kwamba hakuna aliyenifuatilia” akasema Godfrey “Hutajali nikiuliza kuna kitu gani kinachoendelea hivi sasa? Jana Rais ametoka usiku akaenda kumchukua mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi akamleta hapa.Nini kinaendelea? Akauliza Godfrey
“Kuna jambo linaendelea Godfrey ndiyo maana unatuona hapa.Kuna kikundi Fulani cha watu ambao tunawatafuta ni watu hatari”akasema Ruby
“Hiki kilichotokea leo cha picha za faragha za Rais kusambazwa kina mahusiano na hao jamaa mnaowatafuta? Akauliza Godfrey
“Ndiyo.Watu hao ambao tunawatafuta wanahusika na kusambaza picha za Rais” akajibu Ruby
“Ni akina nani hao watu”
“Bado hatujawafahamu
lakini tunaendelea kuwafuatilia”
“Inashangaza sana namna walivyoweza kuzipata zile picha za faragha za Rais” akasema Godfrey
“Kuna watu wa karibu na Rais ambao wanashirikiana na hawa jamaa ndiyo maana tumejaribu kumshauri Rais kuchukua tahadhari kubwa kwa mambo yake anayoyafanya” akasema Ruby kisha akaagana na Godfrey akaondoka zake
Akiwa njiani kuelekea ikulu baada ya kutoka kwa akina Mathew alikotumwa na Rais,Godfrey akapigiwa simu.Zilikuwa ni namba ngeni katika simu yake akabonyeza sehemu katika gari lake na kuipoke ile simu
“Hallow ! akasema Godfrey
“Hallow Godfrey uko wapi mida hii?
“Niko barabarani naendesha gari.Wewe ni nani?
Akauliza Godfrey
“Nataka unisikilize vizuri sana na ufuate kila nitakachokuelekeza”ikasema
sauti ile nzito ya kiume ya mtu aliyempigia simu
“Wewe ni nani? Akauliza
Godfrey
“Tunawashikilia mke na watoto wako wawili”akasema Yule jamaa
“What?! Akauliza Godfrey
“Tunawashikilia mkeo na watoto wako wawili na hatuna nia ya kuwadhuru kama
utafuata kile nitakachokuelekeza kukifanya
!
“Sijakuelewa wewe ! akasema kwa ukali Godfrey
“Nimekwambia
tunawashikilia mke wako na watoto wako wawili .Ukitaka kuwapata hai tafadhali fuata maelekezo nitakayokupa” akasema Yule jamaa
“Simaini hicho unachokisema ! akasema Godfrey na baada ya sekunde chache akasikia sauti ya yule jamaa akimuamuru mke wake
“Zungumza na mumeo!
Akasema Yule jamaa kwa ukali
“Mume wangu tuokoe tumetekwa ! akasema Doroth mke wa Godfrey
“Doroth ! Doroth ! akaita
Godfrey
“Nadhani umethibitisha ninachokwambia, sasa ukitaka kuwaokoa familia yako fuata maelekezo nitakayokupa”
“Naapa mkiwafanya chochote mke wangu na watoto nitawafanyia kitu kibaya sana mashetani wakubwa nyie ! akafoka Godfrey na Yule jamaa akacheka kidogo
“Sikiliza kwa makini Godfrey kwanza kabisa unatakiwa ukae kimya usimweleze mtu yeyote jambo hili wala usitoe taarifa polisi,ukithubutu kufanya hivyo nitakupigia simu ukachukue miili ya watoto wako na mkeo” akasema Yule jamaa na Godfrey akahisi mwili ukimtetemeka kwa ndani akalazimika kutoka nje ya barabara akazima gari halafu akavuta pumzi ndefu
“Godfrey unanisikia? Akauliza Yule jamaa
“Nini unakitaka? Akauliza
Godfrey
“Nenda hadi kwa
Mtuka,mtaa wa Mpenda mbele ya duka la vifaa vya umeme utakuta kuna gari lina rangi nyeupe imeegeshwa hapo.Fungua mlango wa nyuma ingia ndani
yake.Nakukumbusha kwamba
ukijaribu kupiga simu polisi au kumjulisha mtu yeyote tutajua kwani tunafuatilia simu yako.Ndani ya nusu saa uwe umefika mahala nilipokuelekeza! akasema Yule jamaa na kukata simu.Godfrey akapiga usukani kwa hasira
“Akina nani hawa wananifanyia hivi?Kwa nini wamewateka mke wangu na watoto wangu? Akajiuliza Godfrey
“Nifanye nini? Godfrey akahisi kuchanganyikiwa
“Natamani nimjulishe Rais lakini hawa jamaa wamenitahadharisha kwamba wanafuatilia simu yangu na siwezi kuwapuuza.Yawezekana kweli wananifuatilia na nikifanya kinyume na wanavyotaka ninaweza kuwaweka hatarini familia
yangu” akawaza na kuegemea kiti
“Ee Mungu nisaidie katika hili.Naomba usimame nami na kuiokoa familia yangu ! akaomba Godfrey
“Lazima niachane na kila kitu nishughulikie suala la kuiokoa familia yangu” akawaza Godfrey na kuwasha gari akaliingiza barabarani na kuanza safari ya kuelekea mahala alikoelekezwa.
“Nimekuwa nikitazama katika filamu mbali mbali kuhusu watu kutekwa na sikuwahi kuhisi kama siku moja na mimi nitakutwa na jambo hili.Kitu gani wanakitaka hawa jamaa kutoka kwangu hadi wakaiteka familia yangu? Lazima kitu wanachokitaka ni kikubwa sana.Ngoja nikawasikilize nijue kitu gani wanakitaka lakini leo lazima niikomboe familia yangu” akawaza Godfrey.
Godfrey alifika kwa Mtuka kama alivyokuwa ameelekezwa na Yule jamaa akautafuta mtaa wa Mpenda akaupata na taratibu akaanza kuendesha
gari akilitafuta duka la vifaa vya umeme akaliona na moyo ukampasuka baada ya kuliona gari moja likiwa limeegeshwa hatua chache baada ya duka lile akasimamisha gari na kuvuta pumzi ndefu
“I have to do this ! akawaza na kurudi nyuma hadi katika baa moja ambayo haikuwa mbali na lile duka akaegesha gari halafu akashuka akatembea kwa miguu kulifuata lile gari aliloelekezwa akaufungua mlango akaingia kama alivyoelekezwa.
Mara tu alipoingia ndani ya lile gari akakuta kuna watu watatu.
“Your gun ! akasema jamaa mmoja akiwa amefunika macho kwa miwani myeusi.Godfrey akatoa bastola yake akampatia.
“Your phone! Akasema tena Yule jamaa na Godfrey akatoa simu yake akampa jamaa akaizima kabisa halafu akachukua kifaa Fulani akakiwasha na kukipitisha mwilini mwa Godfrey kumchunguza kama ana kifaa chochote mwilini mwake cha mawasiliano akakutwa na akachukua vifaa vyote alivyokuwa navyo akampa mwenzake ambaye alishuka na kwenda kuvitupa katika pipa la takataka gari likawashwa wakaondoka.
Hali ya Mathew Mulumbi
iliendelea vizuri na alianza kufanya mazoezi mepesi.Akatoka chumbani kwake na kumfuata Ruby katika chumba walichokiteua kama ofisi
“Mathew ! akasema Ruby baada ya Mathew kuingia mle ndani
“Unatakiwa upumzike” akasema Ruby
“Sijazoea maisha ya kulala kitandani kutwa nzima,mimi ni mpiganaji kila wakati niko katika mapambano.Nataka nipone haraka.Kuna chochote umekipata mpaka sasa? Akauliza Mathew “Ninaendelea na
kukusanya taarifa na pale nitakapomaliza nitakupa taarifa” akasema Ruby
“Good keep working” akasema Mathew akatoka na kuelekea sebuleni akamtaka Nawal amuite tena Asajile.
“Habari za asubuhi Asajile”akasema Mathew lakini Asajile hakujibu kitu.Alikuwa amefungwa mkono mahala alipokuwa amevunjwa vidole na Nawal
“Asajile nimekuita tena nataka tuzungumze.Kwanza kabisa nataka kukufahamisha kwamba usiku wa kuamkia leo Rais Festus ametengua uteuzi wako na wewe si mkurugenzi tena wa idara ya kupambana na ugaidi” akasema Mathew na Asajile akastuka.Hakutegemea kusikia taarifa ile
“Rais hana imani nawe tena kutokana na kile ulichokifanya ndiyo maana ameamua kukuondoa katika nafasi yako na haya ni maandalizi ya kupelekwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya mauaji.Asajile ninataka nikusaidie na ninao uwezo wa kukusaidia kukutoa
katika hiki kitanzi ulichojivisha wewe mwenyewe.Ninao uwezo wa kumshawishi Rais akakusamehe lakini nitaweza kufanya hivyo kama utakuwa
tayari kushirikiana nasi” akasema Mathew na kunyamaza akamtazama Asajile ambaye alionekana kuchanganyikiwa
“Asajile nahitaji kuwafahamu watu
ulioshirikiana nao katika mauaji ya Frank.Labda nikuweke wazi Asajile kwamba hawa watu tunaowatafuta ni mtandao wa wafanya biashara wa dawa za kulevya.Wana kundi lao linaitwa Black Mafia ambalo wanalitumia katika kufanikisha biashara zao.Wamekuwa wakifanya mauaji ya watu hapa nchini,wanatengenezea watu kesi kama
walivyonitengenezea mimi kesi ya dawa za kulevya na mauaji.Ni kundi hatari sana.Jana usiku walifanya tukio baya kabisa walivamia ofisi za SNSA wakaua watu na kuwachukua wengine mateka.Tunaamini waliweza kuingia SNSA kwa msaada wa Frank ambaye wewe ndiye uliyefanikisha kumtoa gerezani.Kingine kibaya zaidi jamaa hao usiku wa kuamkia leo wamesambaza picha za faragha za Rais na kila kona leo hii gumzo ni picha hizo.Asajile wewe unawafahamu watu hao hivyo nataka unisaidie namna ya
kuweza kuwapata.Kama ukinisaidia katika hilo ninakuahidi Asajile nitakutoa
katika hili tatizo ulilokuwa nalo”akasema Mathew na Asajile akainama akazama mawazoni
“Asajile kwa hatua hii uliyofikia hutakiwi kujishauri mara mbili.Hakuna ubishi hapa umefika mwisho hakuna atakayekusaidia tena.Kwa sasa ni mimi pekee ambaye ni msaada wako.Nieleze ukweli na nitakusaidia.Rais ananisikiliza ninaweza kuzungumza naye na akanielewa akakupangia hata kazi nyingine” akasema
Mathew
“Anayosema Mathew
Mulumbi ni ya kweli.Nimefika mwisho.Kama Rais ameniondoa katika kazi hii ni dalili mbaya.Natamani nimweleze huyu jamaa kilichotokea lakini naogopa kuwaingiza matatani pia wenzangu ambao ni mke wa Rais na mkuu wa jeshi la polisi.Nina imani nikiendelea kukaa kimya na nisiwataje hawatakubali nikapotelea gerezani lazima watanisaidia.Ngoja niendelee kukaa kimya” akawaza Asajile “Asajile nadhani umenisikia.Uko tayari kutoa ushirikiano? Mathew akauliza
“Sina chochote cha kueleza.Naomba unirejeshe katika chumba mlichonifungia! Akasema Asajile.Mathew akamtazama halafu akamtaka Nawal amrejeshe Asajile katika chumba chake.
“Nawal nataka kwenda kuonana na mke wa Asajile nizungumze naye” akasema
Mathew
“Hapana Mathew wewe bado mgonjwa unatakiwa upumzike” akasema Nawal
“Nawal huu si wakati wa
kulala.Mimi sina tatizo lolote usihofu.Ninataka kuzungumza na huyo mwanamke ni muhimu sana” akasema Mathew
“Kwa nini usitupe nafasi sisi tukaenda kuzungumza naye nawe ukabaki hapa ukipumzika? Akasema Nawal
“Nawal nataka niende huko kuonana na huyo mwanamke mimi mwenyewe! Akasisitiza Mathew
“Mathew naomba
utuamini kamba hata sisi tunaweza tukaifanya kazi hiyo.Tuachie tuende tukaonane na huyo mwanamke au tumlete hapa uje uzungumze naye ! akasema Nawal
“Nawal ninawaamini sana lakini ninataka kuonana na huyo mwanamke.Fanyeni maandalizi mara moja nielekee huko” akasema Mathew Mulumbi.Nawal hakutaka kubishana naye akamfuata Ruby akamweleza kile anachokitaka Mathew,Ruby naye akashangaa akaacha kazi aliyokuwa anaifanya akaamfuata Mathew
“Nawal amenieleza kuhusu hicho unachotaka kukifanya.Mathew sikushauri uende huko kwa mke wa Asajile.Wewe bado mgonjwa endelea kupumzika tuachie sisi
kila kitu tutakifanya” akasema Ruby
“Ruby nataka nikaonane na mke wa Asajile.Fanyeni maandalizi mara moja” akasema Mathew na Ruby akabaini Mathew alikuwa anamaanisha kile alichokisema,akajadiliana na Nawal kisha wakaelekeza makomando wawili wajiandae wakaingia katika gari na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Asajile
***************
Rais Festus alirejea ikulu akitokea SNSA kushuhudia kile kilichokuwa kimetokea usiku.Moja kwa moja akaelekea ofisini kwake.Akajiegeneza kitini akiwa na mawazo mengi sana.
“Nimedhalilika mno.Kila ninakopita kila mmoja ananiangalia mimi.Naamini aibu hii ni ya muda tu na wale wote wanaohusika katika suala hili watakiona.Sintakuwa na huruma nao hata kidogo.Nitakuwa na roho mbaya sana kwa watu hawa na Mungu atanisamehe” akawaza Rais Festus akiwa amejaa hasira.Wakati Rais Festus akiendelea kuwaza mkurugenzi wake wa habari Gidion Benson akaingia ofisini akamsalimu na kuketi
“Unasemaje Gidion?
Akauliza Rais Festus
“Mheshimiwa Rais nimekuja kuzungumza nawe kuhusiana na hiki kilichotokea”
“Kuhusu picha zangu?
Akauliza Rais Festus
“Ndiyo mheshimiwa Rais” akajibu Gidion
“Nini unataka tukizungumze Gidion? Akauliza Rais Festus “Mheshimiwa Rais
nilikuwa nafikiria baada ya tukio lile tungeweza labda kutoa taarifa Fulani hata ya kukanusha kwamba picha zile ni za kutengeneza” akasema Gidion
“Gidion kwa sasa liache suala hili kama lilivyo na kama kutakuwa na maelekezo yoyote basi nitakuelekeza hapo baadaye” akasema Raus Festus
“Mheshimiwa Rais,huko mtandaoni kumechafuka na kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo picha hizo zinavyozidi kusambaa na …”
“Ninafahamu Gidion lakini kama nilivyokwambia kwamba kwa sasa hakuna chochote cha kusema hadi hapo baadaye kama kuna lolote la kusema nitakuelekeza” akasema Rais Festus na simu yake ikaita alikuwa ni mkuu wa jeshi la polisi.Gidion akaondoka ili kumpa nafasi Rais ya kupokea ile simu
“IGP habari yako”
“Shikamoo mheshimiwa
Rais”
“Marahaba.Jana
nilikuelekeza kuwatuma vijana kwenda kuitafuta simu ya Asajile je ilipatikana?
“Hapana mheshimiwa
Rais.Nimekupigia kukujulisha kwamba vijana walifanya upekuzi jana usiku nyumbani kwa Asajile kuitafuta simu hiyo lakini hawakuipata na leo hii wamerejea tena asubuhi kufanya upekuzi wa kina lakini hawajaipata na mke wake hajui chochote kuhusu mahala iliko simu ya mumewe” akasema IGP Yeremia
“Hii inashangaza sana.Lakini naamini huyo mke wa Asajile lazima atakuwa anafahamu mahala iliko simu ya mumewe”
“Mheshimiwa Rais inaonekana Yule mama hafahamu chochote kwani polisi wamejaribu kumuhoji kwa kina na hafahamu chochote.Kuna mahala Asajile ameificha simu hiyo.Anatakiwa ahojiwe yeye mwenyewe aeleze simu yake iko wapi” akasema Yeremia “Sawa Yeremia ahsante kwa ushauri huo.Kuna lingine unataka kuniambia?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Kuna hizi picha ambazo zimeanza kusambaa usiku wa leo mtandaoni na zinaendelea kusambaa kwa kasi kubwa.Jeshi la polisi tunajiandaa kutoa tamko la kuzuia usambazaji wa picha hizo na kwa yeyote atakayethubutu kusambaza picha hizo basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.Tayari kitengo cha uhalifu wa mtandao kiko kazini tangu usiku wa leo na tayari wamekwisha gundua kwamba mtumaji wa picha hizo alitumia kompyuta iliyokuwa katika mgahawa wa intaneti ndani ya kasino moja hapa jijini.Mmiliki wa kasino hilo tayari amekwisha kamatwa na jeshi la polisi na anaendelea kuhojiwa ili tuweze kumpata mtu ambaye aliweza kusambaza picha hizo”akasema IGP Yeremia
“Yeremia ninakushukuru sana kwa jitihada hizo endeleeni kuwaska watu hao na utanijulisha kila hatua mtakazozichukua” akasema Rais na kuagana na Yeremia
“Kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo uzito wa hili jambo unavyozidi kuwa mkubwa.Nilidhani ni suala dogo ambalo ningeweza kulibeba bila taabu lakini kumbe ni jambo zito” akatolewa mwazoni baada ya simu yake kuita alikuwa ni Zandile mapigo ya moyo yakabadilika akaitazama simu ile ikiita akaogopa kuipokea.
“Lazima Zandile
amekwisha ziona zile picha” akawaza na kuichukua simu akaipokea.
“Hallow Zandi” akasema
Rais festus
“Festus mpenzi habari za Tanzania?
“Kiafya niko mzima kabisa vipi wewe unaendeleaje?
“Vibaya.Niko vibaya sana Festus,nadhani umekwisha elewa ninachokimaanisha” akasema Zandile
“Kama ni kuhusu zile picha zetu zilizosambazwa mtandaoni nimekuelewa” akasema Festus
“Festus nataka maelezo ya kuniridhisha ni namna gani picha zile zimepigwa na kwa nini zikasambazwa? Akauliza Zandile na Festus akavuta pumzi
“Zandile kwanza kabisa naomba samahani sana kwa hiki kilichotokea naamini umekwazika mno”
“Si kukwazika tu ni aibu nzito hii.Ni kashfa kubwa sana hii Festus.Tayari picha hizi zimekwisha sambaa sehemu mbali mbali duniani nimepigiwa simu na watu kutoka Ulaya na hadi Marekani wakiniuliza ninafanya mambo gani.Nimekosa jibu la kuwapa.Ninao watu wasionipenda pia ambao wanatumia jambo hili kunichafua mtandaoni.Tukio hili linaunganishwa na lile la kuachana na mfalme na sasa ninaitwa kahaba.Nimelia sana Festus”
“Zandile pole sana mpenzi wangu.Hayo unayopitia hata mimi ninayapitia huku.Kwa ufupi tu ni kwamba sifahamu jambo hili limetokeaje.Sifahamu picha zile zimepigwaje na wala sifahamu nani aliyezisambaza”
“Festus watu wanawezaje kuingia ndani na kupiga picha zile wakati kuna ulinzi wa kutosha katika ile nyumba?
“Bado ninafuatilia kujua jambo ili limefanyikaje lakini ninachofahamu lazima kuna watu wangu wa karibu wanahusika kwani suala la mahusiano yetu ni la siri sana na wanaolifahamu ni watu wangu wa karibu.Ninaendelea na uchunguzi hivi sasa na nina uhakika mkubwa lazima nitawapata waliofanya haya mambo” akasema Festus
“Festus nina wasi wasi sana na mke wako anaweza kuwa anahusika katika hili jambo kwa lengo la kutukomoa” akasema Zandile
“Bella hawezi kuhusika na jambo hili kwani hata yeye mwenyewe litamuathiri pia na isitoshe hata yeye hafahamu kama mimi nawe tuna mahusiano.Zandile kwa sasa naomba utulie nipe nafasi ya kulichunguza hili jambo kuufahamu undani wake halafu nitakujulisha kila kinachoendelea.Tayari kuna watu kadhaa wanashikiliwa na
jeshi la polisi hivi sasa na uchunguzi unaendelea” akasema Festus
“Festus jambo hili limenifanya niingiwe na woga.Kama watu wameweza
kuingilia hadi faragha za Rais mtu ambaye anaaminika kuwa na ulinzi mkali kuliko mtu yeyote katika nchi basi siko katika mikono salama.Ninaweza hata kuuawa nikiwa mikononi mwako” akasema Zandile
“Zandile tafadhali naomba usifike huko.Wewe mwenyewe unafahamu namna ulinzi ulivyo imara.Naomba uwe mtulivu kwa sasa wakati ninalifuatilia jambo hili kujua ni kwa namna gani hawa jamaa wameweza kupiga zile picha.Ninaamini si muda mrefu sana nitakuwa na majibu”
“Festus kwa hili lililotokea nimeanza kufikiria mara mbili kama ninaweza kuendelea kuwa na mahusiano nawe.Aibu hii niliyoipata ni kubwa mno na isiyovumilika.Utupu wangu umeanikwa hadharani.Festus nadhani upo ulazima wa kusimamisha kwanza mahusiano yetu na kila mmoja akatumia muda huu kujitafakari” akasema Zandile na Festus akastuka
“Zandile unataka kusema nini?akauliza kwa wasiwasi
“Naomba mahusiano yetu yasimame Festus hadi pale jambo hili itakapokuwa limepatiwa ufumbuzi.Samahani sana kwa hilo Festus ! akasema Zandile na kukata simu
“Zandile ! ..Zandi….!
akaita Festus lakini tayari simu ilikwisha katwa.Festus akagonga meza kwa hasira
“Hapana! Mahusiano
yangu na Zandile hayawezi yakafika mwisho namna hii ! akawaza na kumpigia simu Zandile lakini simu yake haikuwa ikipatikana tayari ilikwisha zimwa
“Zandile hawezi akaniponyoka hivi hivi lazima nimrejeshe katika himaya yangu.Ni mwanamke ambaye sitakiwi kumkosa katika maisha yangu ! akawaza Festus akiwa amejaa hasira na mara simu yake ya mezani ikaita akaipokea na kujulishwa kuwa katika laini namba tatu kuna simu kutoka kwa katibu mkuu wa chama Profesa Simon.
“Mambo yameanza !
akasema Festus na kuipokea simu ile
Godfrey hakujua anapelekwa wapi kwani alikuwa amefunikwa mfuko kichwani na kulazwa chini ili asiweze kuona anakoelekea.Baada ya mwendo wa takribani dakika arobaini gari likapunguza mwendo na akasikia geti likifunguliwa halafu gari likangia ndani.Mlango ukafunguliwa akashushwa garini na kuingizwa ndani.Baada ya muda mfupi akatolewa ule mfuko kichwani akajikuta akitazamana na watu watatu “Habari yako Godfrey ! akasema mmoja wa wale jamaa waliokuwa wamesimama ambao hakuwafahamu .
“Nataka kuiona familia yangu kabla ya yote ! akasema Godfrey
“Usihofu utawaona familia yako wote wako salama kabisa” akasema Yule jamaa aliyeonekana kama kiongozi wao
“Siwezi kuzungumza chochote na ninyi kabla sijaiona familia yangu” akasema Godfrey na Yule jamaa akawaelekeza jamaa wengine wanne waliokuwa wamesimama katika pembe za kile chumba,waende wakawalete familia ya Godfrey
Baada ya sekunde chache mke wa Godfrey na watoto wake wakaletwa wote wakaangua kilio baada ya kumuona baba yao.Watoto wakalia wakataka wakamkumbatie baba yao,Yule jamaa kiongozi akawaruhusu wale jamaa wawaachie watoto waende kwa baba yao
“Baba tafadhali naomba utuokoe.Hawa watu wametuteka! Akasema mmoja wa watoto wake
“Msijali wanangu nitawaokoa.Kuweni majasiri !
Hawa jamaa wamewapiga? Wamewaumiza sehemu
yoyote? Akauliza Godfrey
“Hapana hawajatupiga wala kutuumiza”
“Good.Endeleeni kuvumilia ndani ya mua mfupi nitakuja kuwachukua” akasema Godfrey kisha watoto wake wakachukuliwa huku wakilia
“Umewaona familia yako wako salama kabisa.Sasa tunaweza kuzungumza” akasema Yule jamaa kiongozi
“Nawapa angalizo endapo mmoja wa wanafamilia yangu akipatwa na hata mkwaruzo nitawafanya kitu kibaya sana !
Hamnijui mimi ni nani ! akasema Godfrey
“Godfrey hapa si sehemu ya vitisho.Naomba utulize jazba na tuzungumze”
“Nini mnakitaka?
“Tunachokihitaji ni kitu rahisi sana.Jana usiku ulimpeleka Rais nyumbani kwa mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi Asajile Mlabwa na mkaondoka naye.Tunataka utueleze mahala mlikompeleka”
“Sifahamu mahala aliko huyo Asajile! Akasema Godfrey
“Godfrey hatuna muda wa kupoteza hapa.Tunataka kufahamu mahala aliko Asajile! Ulikuwa na Rais jana usiku mlimpeleka wapi Asajile?
“Sifahamu alipo” Godfrey akajibu
“Godfrey usisahau tunayo familia yako na tunaweza kuiteketeza yote mbele yako! akasema Yule jamaa akiwa ameanza kubadilika sura
“Sikiliza Godfrey hatuna haja ya kuidhuru familia yako.Tuonyeshe mahala alipo Asajile kisha familia yako itabaki huru” akasema Yule jamaa
“Mahala aliko Asajile hamuwezi kuingia hata kama nikiwaelekeza” akasema Godfrey
“Tuonyeshe yuko wapi na
sisi tutaingia”
“Amehifadhiwa katika kambi moja ya jeshi” akasema Godfrey
“Kambi ya jeshi? Yule jamaa akauliza na kuwatazama wenzake
“Ndiyo.Rais alielekeza awekwe huko katika kambi ya jeshi.Ninyi shida yenu ni kujua mahala alipo au mnamtaka Asajile?
“Tunamtaka Asajile”
“Basi kama mnamtaka Asajile hamuwezi kuingia ndani ya kambi ya jeshi lakini ninaweza kumleta kwenu endapo tutakubaliana familia yangu iachwe huru kwanza! Can you do that? Godfrey akauliza
“I don’t trust you !
“Kwa nini msiniamini wakati mmeishika mateka familia yangu?akauliza Godfrey kwa ukali
“Sawa utakwenda na mmoja wa watu wetu na pale
tutakapokuwa tumempata
Asajile ndipo tutaiachia familia yako”
“Ninakwenda peke yangu ! Kama hamtaki hilo basi hamtaweza kumpata Asajile ! akasema Godfrey wale jamaa wakajadiliana na kukubaliana na kile alichokisema Godfrey na kumpa maelekezo halafu Godfrey akavishwa mfuko kichwani akatolewa ndani na kuingizwa katika gari akarudishwa mahala alikokuwa ameliacha gari lake. **************
Mathew akiwa ameongozana na Nawal,Ruby na makomando wawili walifika nyumbani kwa Asajile Mlabwa,Taratibu Mathew akashuka garini wakajitambulisha kwa mlinzi kuwa wamekwenda kuonana na mke wa Asajile.Mlinzi akawasiliana na mke wa Asajile aliyekuwa ndani na akawaruhusu akina Mathew waingie ndani.
“Karibuni sana” akasema mke wa Asajile
“Tunashukuru
sana.Habari za hapa”akasema Mathew
“Nzuri kabisa.Karibuni”
“Ahsante sana.Tunatumai wewe ndiye mke wa Asajile
Mlabwa”
‘Ndiye mimi ninaitwa mama Isaya”
“Tunashukuru kukufahamu mama Isaya.Mimi naitwa Mathew Mulumbi,mwenzangu huyu anaitwa Nawal na Yule pale anaitwa Rubby”
“Ruby ninamfahamu ni mke wa Rais mstaafu Dr Fabian”
“Ndiyo”
“Karibuni sana.Umesema unaitwa Mathew Mulumbi?
“Ndiyo”
“Kuna mtu anaitwa Mathew Mulumbi ambaye siku chache zilizopita alikamatwa na dawa za kulevya na akawatoroka polisi”
“Ni mimi”akajibu Mathew na Yule mama akastuka sana
“Mama Isaya tumekuja hapa kuna jambo tunataka kuzungumza nawe.Jana usiku Rais alifika hapa na kumchukua mumeo Asajile”
“Ndiyo alikuja hapa na mpaka sasa hajarejea.Mnafahamu mahala aliko?
“Mama Isaya kuna kitu ambacho tunatataka kukufahamisha.Jana usiku kuna tukio lilitokea karibu na ikulu,bomu lilipigwa ambalo lilizima kila kifaa cha kielektroniki”
“Bomu? Mungu wangu ! Mama Isaya akastuka
“Ni bomu ambalo halina madhara kwa binadamu bali linaathiri kila kifaa cha kielektroniki mahala litakakopigwa.Waliopiga bomu hilo waliilenga idara moja
nyeti sana ya serikali na ili waweze kuvamia idara hiyo walihitaji taarifa kutoka kwa mtu ambaye analifahamu vyema jengo hilo.Kuna mtu anaitwa Frank ambaye alikuwa amefungwa katika gereza la siri ambalo liko chini ya idara
anayoiongoza mume wako Asajile na ili kumpata, watu hao waliwasiliana na Asajile na hatujui walikubaliana nini lakini Asajile alikwenda gerezani akamtoa mfungwa huyo na baadaye jioni mfungwa huyo akakutwa amefariki dunia.Mume wako anashikiliwa hivi sasa ili aweze kutoa maelezo ya namna mfugwa huyo alivyoweza kupoteza maisha lakini amekuwa mgumu kufunguka na hataki kusema chochote.Nataka kufahamu mama Isaya kuna kitu chochote unakifahamu kuhusiana na jambo hilo?Hakuna kitu amekueleza? Mathew akauliza
“Mume wangu huwa
hanishirikishi kabisa masuala yake yoyote ya kikazi.Tangu aliporudi nyumbani jana jioni hakunieleza kitu chochote tulikaa hapa sebuleni tukitazama muziki hadi alipofika Rais kumchukua.Sikujua kama anakabiliwa na tuhuma kubwa namna hiyo” akasema mama Isaya
“Mama Isaya kama unafuatilia vyombo vya habari,tayari Rais ametengua nafasi yake na haya ni maandalizi ya kufikishwa mahakamani.Kwa sasa ni sisi pekee ambao tunaweza kumsaidia.Tunachokihitaji kutoka kwake ni kuwafahamu watu alioshirikiana nao katika mauaji ya huyo mfungwa ni akina nani.Mama Isaya unaweza ukatupatia simu ya mumeo tuifanyie uchunguzi tujue ni watu gani alikuwa
anawasiliana nao? Akauliza Mathew
“Simu? Mama Isaya akastuka kidogo
“Ndiyo mama.Kama
tukiipata simu yake tutaweza kujua watu aliokuwa anawasiliana nao.Lengo letu ni kutaka kumsaidia mumeo” akasema Mathew
“Simu yake haipo na
haijulikani iko wapi.Jana usiku walikuja askari polisi wakaitafuta wakaikosa na leo tena asubuhi wamekuja na kupekua nyumba nzima tena wakiwa na kifaa cha kuwawezesha kuipata simu hiyo wakidhani imefichwa ndani lakini
hawakuipata”akasema mama
Isaya
“Mama Isaya mumeo
tuhuma zinazomkabili ni za mauaji na ushahidi upo wa kutosha.Kwa sasa kitu pekee kinachoweza kumuokoa ni msamaha wa Rais na msamaha huo hakuna anayeweza kumshawishi Rais amsamehe zaidi yetu sisi hapa.Nakushauri kubali kushirikiana nasi ili kumuokoa
mumeo.Kama unafahamu mahala iliko simu yake
tuonyeshe tafadhali” akasema Mathew
“Sifahamu mahala iliko simu yake”
“Ulituambia kwamba Rais alifika hapa akamchukua jana usiku.Unaweza ukatueleza kwamba Asajile aliondoka katika mazingira gani? Mathew akauliza
“Tulikuwa hapa tunatazama muziki na mlango ukagongwa nikainuka kwenda kufungua nikakutana na Rais.Nilistuka sana na Rais akaingia ndani bila hata salamu akamtaka Asajile amfuate nikajua labda kuna mambo wanakwenda kuzungumza mara nikasikia milango ya gari inafungwa wakaondoka na mpaka sasa sijamuona mume wangu” akasema mama Isaya
“Asajile ni mkuu wa idara
nyeti kabisa ya serikali na kama mkuu wa idara
anatakiwa kuwa hewani muda wote ili kujua kila kinachoendelea katika idara yake.Mahala aliko hana simu na hii inatupa picha kwamba simu yake aliiacha hapa nyumbani baada ya kuchukuliwa na Rais.Umetupa maelezo kwamba Rais aliingia akamtaka Asajile amfuate na hii inaonyesha kwamba Asajile hakutegemea kama Rais angeweza kuja hapa na alivyoitwa na Rais aliinuka akamfuata bila kuchukua kitu chochote,simu yake ilibaki hapa hivyo mama nakushauri itakuwa vyema kama ukituonyesha mahala iliko simu hiyo ya mumeo.Hii ni kwa faida ya mumeo.Tuna uhakika mumeo alirubuniwa na hao jamaa kwa fedha au kitu kingine hivyo tunayo
nafasi ya kumsaidia lakini pale wewe na yeye mtakapoamua kutoa ushirikiano katika suala hili.Jambo lingine endapo na wewe utakataa kutoa ushrikiano nawe pia utahesabika umeshiriki katika uhalifu huo na tutamshauri Rais nawe pia uweze kuchukuliwa kuunganishwa na mumeo katika tuhuma hizo.Hebu wafikirie watoto wako watabaki na nani kama nawe ukichukuliwa na kuunganishwa na mumeo? Mama Isaya sikulazimishi lakini nataka kukuhakikishia kwamba tuna lengo zuri la kumsaidia mume wako ambaye ni kwa bahati mbaya tu alipotoka lakini bado tunaweza kumsaidia”akasema Mathew na mke wa Asajile akaonyesha woga
“Mama Isaya tunaomba ufanye maamuzi tafadhali kama utakuwa tayari kushirikiana nasi kumsaidia mumeo au tuchukue hatua nyinginezo”akasema Mathew
“Ningefahamu mahala
iliko simu ninaapa ningewaeleza” akasema mama Isaya
“Ruby mpigie simu Rais” akasema Mathew na Ruby akachukua ile simu yake maalum akampigia Rais akataja namba zake za siri na baada ya muda sauti ya Rais ikasikika.Ruby akamsogezea Mathew simu na kuweka sauti kubwa ili mke wa Asajile aweze kusikia
“Mheshimia Rais,Mathew hapa ninaongea”
“Mathew vipi maendeleo yako?
“Ninaendelea vyema mheshimiwa Rais.Samahani kwa usumbufu mzee,nimekuja hapa nyumbani kwa Asajile kuzungumza na mke wake”
“Umekwenda nyumbani
kwa Asajile? Akauliza Rais Festus
“Ndiyo mheshimiwa Rais” “Mathew kwa hali yako
ilivyo unatakiwa upate mapumziko”
“Usijali mheshimiwa Rais hii ni moja ya mazoezi”
“Mmefanikiwa kuzungumza na mke wa Asajile?Rais akauliza
“Mheshimiwa Rais
kilichotuleta hapa ni kufahamu mahala ilipo simu ya Asajile ambayo tunaamini jana alipoondoka aliiacha hapa nyumbani kwake.Mke wake amekataa kutoa ushirikiano kuonyessha mahala iliko hiyo simu.Nina ushauri mheshimiwa Rais ! “Nakusikiliza Mathew”
“Mheshimiwa Rais ninashauri huyu mama naye achukuliwe aunganishwe na mume wake kwani wanaonekana wanashirikiana.Kuna kitu anakifahamu lakini anajitahidi kukificha.Ushauri wangu ni huo mheshimiwa Rais” akasema Mathew na sura ya mama Isaya ikazidi kuonyesha
woga
“Mathew nakubaliana na ushauri wako.Hatuna muda wa kubembeleza kama amekataa kutoa ushirikiano kwa hiyari yake basi atatoa ushirikiano kwa kutumia nguvu.Ninatoa maelekezo mchukueni na mkamuunganishe na mume wake”akasema Rais Festus
“Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Mathew na kukata simu akamtazama mama Isaya
“Mama Isaya naamini
umesikia vizuri alichokisema Rais.Ametup amaelekezo ya kukuchukua na kukuunganisha na mumeo katika tuhuma hizi za mauaji zinazomkabili.Bado muda unao wa kutueleza ukweli na
tukasitisha zoezi hilo” akasema Mathew na mama Isaya machozi yalikuwa yanamtoka
“Nitawaeleza tafadhali lakini naomba msinichukue tafadhali” akasema mama Isaya na kufuta machozi.
“Tueleze tafadhali mahala ilipo simu ya mumeo” akasema
Mathew na mama Isaya akafuta machozi halafu akasema
“Simu anayo mkuu wa
jeshi la polisi”
“IGP? Mathew akauliza kwa mshangao
“Ndiyo”akajibu mama
Isaya
“IGP ameipataje simu ya Asajile? Akauliza Mathew
“Alikuja hapa jana usiku akaniomba nimpatie simu hiyo pamoja na kompyuta akaondoka navyo”
“Una uhakika ulimpatia mkuu wa jeshi la polisi hiyo simu? Akauliza Mathew
“Ndiyo.Nilimpa yeye hiyo simu jana usiku” akasema mama Isaya
“Mama Isaya nataka unitazame usoni na uniambie tena hicho unachokisema” akasema Mathew
“Jana usiku alikuja hapa IGP nikampatia simu na kompyuta mpakato akaondoka navyo” akasema mama Isaya.Mathew na akina Ruby wakatazamana
“Mama Isaya
tunakushukuru sana kwa hili ulilotueleza.Tunakwenda kulifanyia kazi suala hilo kuufahamu ukweli na kama unatudanganya tutarudi tena hapa” akasema Mathew kisha wakasimama kwa ajili ya kuondoka
“Nataka kufahamu hatima ya mume wangu.Mliniambia kama nikitoa ushirikiano mtamsaidia”
“Mama Isaya ahsante sana kwa ushirikiano huu mkubwa uliotusaidia ninakuahidi kufanya kila linalowezekana kumsaidia mumeo” akasema Mathew kisha wakaondoka wakarejea garini
“Nimepatwa na mstuko sana kwa hiki nilichokisikia kutoka kwa mama Isaya” akasema Mathew mara tu walipoingia garini
“Unamuamini Yule mama?
Nawal akauliza
“Ndiyo ninamuamini anasema kweli.Kinachonishangaza ni kitendo cha IGP kufika yeye mwenyewe jana usiku na kuchukua simu na kompyuta halafu Rais akajulishwa kwamba simu haijulikani ilipo.Hamuoni kuna mchezo unachezwa hapa? Mathew akauliza
“Kwanza kwa nini IGP alikuja mwenyewe kufuatilia vifaa hivyo badala ya kutuma askari wadogo?akauliza Ruby
“Kuna harufu imejitokeza hapa ambayo si nzuri hata kidogo.Ruby mpigie simu Rais mara moja,anatakiwa alifahamu jambo hili” akasema Mathew na Ruby akampigia simu Rais
“Ruby” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais ni mimi Mathew ninaongea.Kuna kitu tumekipata kutoka kwa mke wa Asajile ambacho tunadhani unahitaji kukifahamu.Tumeambiwa kwamba simu ya Asajile anayo mkuu wa jeshi la polisi nchini”
“Yeremia? Akauliza Rais
Festus naye akishangaa
“Ndiyo mheshimiwa Rais.Tumeambiwa kwamba
alifika jana usiku hapa nyumbani kwa Asajile na akapewa kompyuta mpakato na simu”akasema Mathew ukapita muda kidogo halafu Rais akasema
“Mathew mna uhakika huyo mama anasema kweli?
“Ndiyo mheshimiwa Rais”
“Nimeuliza kama mna
uhakika kwa sababu taarifa hii imenistua sana” akasema Rais
Festus
“Hata sisi tumeshangaa sana mheshimiwa Rais kwanza kwa IGP mwenyewe kufika hapa kwa Asajile badala ya kutuma askari wadogo na halafu kukupa taarifa kwamba
simu haijulikani ilipo” akasema Mathew
“Jana usiku wakati ninarejea ikulu nilimpigia simu mkuu wa jeshi la polisi na kumtaka atoe maelekezo kwa kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam ili ufanyike utaratibu usiku ule watumwe askari nyumbani kwa Asajile wakachukue vifaa vyake vya mawasiliano ili vifanyiwe uchunguzi.Baadaye akanijulisha kwamba vijana waliotumwa wamefanikiwa kupata komputa peke yake lakini simu haikupatikana.Nilishangazwa na majibu yale nikamtuma tena atume vijana wake wakapekue nyumba yote usiku ule lakini jibu likawa lile lile kwamba simu ya Asajile haionekani .Nimeshangaa kusikia kwamba ni yeye mwenyewe aliyekwenda huko akaichukua kompyuta ya Asajile pamoja na simu. Swali tunalopaswa kujiuliza kwa nini alikwenda yeye mwenyewe wakati askari wadogo wapo? Kwa nini ameificha simu hiyo? Mathew hapa kuna jambo limejificha.Nawashukuruni sana kwa hiki mlichokigundua.Mmezidi kunifumbua macho yangu na sasa nimeanza kuwafahamu nyoka walionizunguka. Yeremia ni mmoja wa watu ambao ninawaamini sana na sikutegemea kabisa kama angeweza kufanya kitu kama hiki” akasema Rais Festus “Mheshimiwa Rais
tunahitaji kumpata Yeremia kwa mahojiano.Tunatakiwa kufahamu kwa nini aliichukua simu hiyo akaificha.Unaweza
ukatusaidia kwa hilo tafadhali” akasema Mathew
“Mathew hata mimi ninataka kujua kwa nini amefanya hivi,kwa nini amenidanganya.Fanyeni hivi,sasa hivi nendeni moja kwa moja katika lile shamba la mazoezi la makomando wa SNSA.Mimi nitamuita Yeremia aje hapa ikulu mara moja kisha nitakuja naye katika shamba hilo kwa kutumia helkopta” Akasema Rais Festus
“Tumekuelewa
mheshimiwa Rais tunaelekea huko” akasema Mathew na kukata simu akatoa maelekezo waelekee katika shamba la makomando wa SNSA kama
Rais alivyoelekeza
Ilikuwa ni ahueni kwa
Godfrey ambaye alifika katika makazi ya akina Mathew na kuwakosa.Makomando waliokuwepo pale wakilinda walimfahamu hivyo hakuwa na haja ya kujitambulisha akawaeleza kile kilichompeleka pale
“Nimekuja kumchukua
Asajile Yule mkurugenzi wa idara ya kupambana na ujasusi tuliyemleta hapa jana usiku.Rais anahitaji kuzungumza naye kisha nitamrejesha” akasema Godfrey na hakuna aliyemtilia shaka hata kidogo.Asajile akafungwa pingu na kuingizwa katika gari la Godfrey akaondoka.
“Unanipeleka wapi?
Akauliza Asajile
“Shut up ! akasema Godfrey
“Dah ! Inaniuma sana kwa hiki ninachokifanya lakini sina namna nyingine ya kuweza kuiokomboa familia yangu zaidi ya kufanya wanavyotaka wale jamaa.Nafahamu kwa hiki ninachokifaniya nimejitafutia matatizo makubwa kwani wale jamaa wanaweza wakamuua
Asajile.Sina namna nyingine nitajitahidi kukabiliana na kile nitakachokutana nacho kwa maamuzi haya niliyoyafanya lakini lazima niikomboe familia yangu” akawaza Godfrey
Alifuata maelekezo aliyopewa na wale jamaa na alipofika sehemu Fulani alipoelekezwa akakuta kuna gari limeegeshwa akapiga honi mara nne na jamaa wawili wakashuka katika gari
wakamfuata.Mmoja akamtaka atoke katika usukani arudi kiti cha nyuma akafanya hivyo kisha yeye na Asajile wakafunikwa mifuko vichwani ili wasijue wanakoelekea na jamaa mmoja akakaa kiti cha nyuma akiwa na bastola akiwalinda.
Mzunguko ulikuwa mrefu kidogo na gari liliposimama milango ya gari ikafunguliwa Asajile na Godfrey wakashushwa na kuingizwa ndani ya nyumba kisha wakavuliwa mifuko waliyofunikwa vichwani.Ndani ya chumba walichoingizwa kulikuwa na watu watatu. Mmoja wa watu wale akamtazama Asajile kwa makini halafu akaitazama na picha aliyokuwa nayo mkononi
“Ni mwenyewe? Akauliza mwingine.
“Ni mwenyewe” akasema Yule jamaa
“Nimefanikisha
mlichokitaka.Naitaka familia yangu” akasema Godfrey
“Not so fast Godfrey.Kazi bado hujaikamilisha” akasema kiongozi wa wale jamaa
“Makubaliano yalikuwa nimlete Asajile hapa kisha niichukue familia yangu ! akasema Asajile.Yule jamaa akampatia bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti
“Maliza kazi.Muue kwa mkono wako ! akasema Yule jamaa.Godfrey alitetemeka mwili
“Maliza kabisa kazi ili kuikomboa familia yako” akasema Yule jamaa na Godfrey akaishika ile bastola akamtazama Asajile kwa huruma ambaye macho yake yalijaa machozi
“Jamani msiniue ! akalia
Asajile
“Kill him ! akafoka Yule jamaa.
“Naomba
msiniue.Nitawasaidia kumpata Mathew Mulumbi nafahamu mahala alipo” akasema Asajile
“Wait don’t kil….akasema kiongozi wa wale jamaa lakini kwa kasi ya aina yake Godfrey akaizinga bastola yake na kutawanya risasi ndani ya kile chumba na wale jamaa watatu wote wakalamba sakafu hawakuwa na uhai tena.Asajile aliyekuwa amefumba macho hakuamini pale alipofunguliwa pingu na kupewa bastola na Godfrey
“Nisikilize Asajile tunatakiwa kujiokoa wenyewe.Hawa jamaa hawako peke yao kuna wenzao wako nao hapa ndani hivyo tunatakiwa kuhakikisha tunawamaliza wote ii tuweze kutoka hapa” akasema Godfrey
“Umenielewa Asajile? Akauliza Godfrey
“Nimekuelewa”
“Good” akasema Godfrey huku Asajile akiishika vyema bastola aliyopewa kwa mkono wa kulia kwani mkono wa kushoto ulikuwa umefugwa kufuatia kuvunjwa vidole na Nawal.
“Are you ready? Akauliza Gofrey na Asajile akatikisa kichwa kukubali kisha wakanyata taratibu kuelekea mlangoni.Kabla hajakishika kitasa cha mlango akasikia hatua za watu wakielekea katika chumba kile akamfanyia ishara Asajile ajiweke tayari.Mara mlango ukafunguliwa wakatokea watu watatu.Godfrey na Asajile walikuwa wamejiandaa vyema wakanyesha mvua ya risasi wale jamaa wote watatu wakaanguka na kufariki dunia.Bastola aliyoishika Asajile haikuwa imefungwa kiwambo cha kuzuia sauti hivyo ulisikika mlio wa risasi na nje ya kile chumba vikasikika vishindo vya watu wakikimbia.Godfrey na Asajile wakatoka haraka ndani ya kile chumba na mara kwa nje wakasikia muungurumo wa gari.Godfrey akachungulia katika dirisha na kuliona gari moja likiondoka huku gari lake likiteketea kwa moto
“Familia yangu ! akasema Godfrey na kuutafuta mlango wa kutokea nje lakini ulikuwa umefungwa.Akaitumia bstola aliyonayo kukisambaratisha kitasa halafu wakatoka nje hakukuwa na mtu yeyote.
“Familia yangu ! akasema Godfrey na kurudi tena ndani akaanza kupita chumba kimoja baada ya kingine lakini vyumba vyote vilikuwa vitupu na familia yake haikuwepo akahisi kuchanganyikiwa “Tunatakiwa kuondoka haraka mahala hapa hawa jamaa wamekwisha ondoka na watu wanaweza wakaanza kujaa eneo hili” akasema Asajile kisha wakatoka na kuchungulia nje halafu wakaanza kutembea haraka haraka na kuliacha gari la Godfrey likiteketea kwa moto.Walipotokanje wakajikuta kati kati ya shamba kubwa la mihogo
“Huku tuko wapi?
Akauliza Asajile
“Sifahamu tuko
wapi.Tufuate hii njia hadi tutakapoikuta barabara na tutauliza” akasema Godfrey wakaanza kutembea kwa tahadhari.Baada ya mwendo wa dakika kumi na tano wakatokea barabarani ambako walikutana na mzee mmoja aliyewaeleza kuwa walikuwa eneo la Kisiwa Mbega nje
kabisa ya jiji la Dar es salaam.Godfrey akamuuliza Yule mzee kuhusu nyumba ile walikotoka
“Lile lilkuwa shamba la marehemu mzee Idrisa lakini baada ya kufariki wanae waliuza mali hovyo na hatujui shamba lile kwa sasa analimiliki nani ila tumekuwa tukiwaona watu tofauti tofauti wakija na kuondoka” akawajibu Yule mzee na kuwaelekeza kituo cha basi kilichokuwa kilometa mbili kutoka pale mahala walipokuwa
“Nimechungulia kaburi leo ! akasema Asajile wakati wakitembea kuelekea katika kituo cha basi
“Ahsante kwa kile ulichokifanya kuyaokoa maisha yangu.Watu wale ni akina nani? Akauliza Asajile
“Hata mimi siwafahamu
lakini wameiteka familia yangu asubuhi ya leo na kunipigia simu wakanitaka nifuate maelekezo yao nikafuata nikapelekwa mahala nisikokufahamu kuonana nao na wakanitaka ili kuikomboa familia yangu niwaonyeshe mahala ulipo.Wanafahamu kila kitu kwamba nilikuwa na Rais jana usiku alipokuja kukuchukua nyumbani kwako.Sikutaka kuwaonyesha mahala ulipo kwa sababu
nilijua ni watu wale wale ambao akina Mathew wanawatafuta hivyo nikakubaliana nao kwamba nitakwenda kukuleta na kukukabidhi kwao ili nao wanikabidhi familia yangu.Utanisamehe sikuwa na namna nyingine ya kuweza kuiokoa familia yangu zaidi ya kufanya kile walichokitaka”
“Walipokupa ile bastora uniue ulikuwa tayari kuniua? Akauliza Asajile.Godfrey akamtazama halafu akasema “Jibu unalo mwenyewe.Sikuweza kukuua kama walivyonitaka.Asajile hiki nilichokifanya kitaigharimu familia yangu kwani wale jamaa waliokimbia watapeleka taarifa kwa wenzao na hii itazidi kuwaweka familia yangu katika hatari kubwa sana na yawezekana nisiwaone tena” akasema Godfrey
“Pole sana” akasema
Asajile
“I don’t know what to do.Sijui mahala pa kuanzia kuwatafuta familia yangu ! akasema Godfrey.Baada ya
kufikiri kidogo Asajile akasema
“Ninataka kuongea na Mathew Mulumbi naomba
unipeleke kwake tafadhali!
“Nini unataka kumweleza Mathew Mulumbi? Godfrey akauliza
“Nataka kumweleza ukweli wote ili anisaidie.Nimegundua kwamba nimejiingiza katika jambo la hatari kubwa na sasa maisha yangu tayari yako hatarini.Kuna mambo muhimu sana ambayo nataka kumweleza lakini kabla ya kunipeleka huko kwa Mathew nataka tupite nyumbani kwangu nikaichukue familia yangu” akasema Asajile huku wakitembea kwa tahadhari kubwa kuelekea katika kituo cha basi
Walikodisha piki piki mbili na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Godfrey ambako walichukua gari lingine na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Asajile wakaichukue familia yake na kuelekea katika nyumba waliko akina Mathew *****************
Waandishi wa habari walikusanyika kwa wingi katika ukumbi wa mikutano katika ofisi za taasisi ya mama Bella.Kufika kwa wingi katika ukumbi ule kulichangiwa na tukio la kuvuja kwa picha za faragha za Rais hivyo wengi walitaka kusikia kauli ya mke
wa Rais baada ya picha za mumewe akiwa na mwanamke mwingine kuvuja.
Mama Bella aliwasili
katika ofisi za taasisi yake na tangu gari lake likiingia getini waandishiwa habari walikuwa wanalipiga picha.Kama kawaida yake alishuka garini uso wake ukiwa na tabasamu angavu akasalimiana na wasaidizi wake na wafanyakazi wengine wa taasisi yake halafu akaelekea ofisini kwake.Wengi walitegemea kumuona akiwa amenyong’onyea kufuatia tukio lile la picha za mumewe kuvuja lakini alionekana kawaida kama vile hakukuwa na kitu chochote kibaya kilichotokea ndani ya familia yake.
Aliingia ofisini kwake na baada ya dakika kumi na tano akatoka akaelekea katika ukumbi wa mikutano kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.Huku akimulikwa na mianga ya kamera za waandishi wa habari akachukua nafasi na katibu wake akasimama na kutoa utangulizi halafu akamkaribisha mama Bella aweze kuzungumza na wanahabari
“Habari zenu wana habari” akasema huku akitabasamu “Ninataka nianze kwa kuwashukuru kwa kufika kwenu kwa wingi sana.Sikutegemea kama mngefika kwa wingi huu.Karibuni sana” akasema na kunyamaza kidogo
“Ndugu wanahabari nimewaiteni hapa kuna mambo mawili makubwa ambayo nataka kuwaeleza ili muweze kuwafikishia watanzania”
Bella akatumia zaidi ya dakika thelathini kuwaelezea wanahabari kuhusiana na mambo mawili makubwa ambayo yalikusudiwa kufanywa na taasisi yake siku chache zijazo na baada ya kumaliza akawatazama wanahabari halafu akatabasamu
“Nimemaliza” akasema na kutoa kicheko kidogo akawafanya waandishi wa habari nao waangue kicheko
“Ndugu wanahabari
niliyowaitia hapa siku ya leo ni hayo mawili,naombeni mkayafikishe kwa wananchi” akasema Bella akiendelea kutabasamu halafu akakusanya karatasi zake akampa katibu wake
“Ninafahamu kile mnachotaka kukisikia kutoka kwangu lakini nawaomba radhi kwamba sintaweza kuzungumzia suala hilo kwa leo kwa sababu ni suala la ndani la kifamilia.Pale familia watakapokuwa na kitu chochote cha kuwaeleza basi watawaeleza” akasema Bella na kunyanyuka akataka kuondoka halafu akakaa “Labda niongelee suala hili kwa ufupi sana maana naona wengi mna hamu ya kusikia nikiongea chochote kuhusu tukio hili” akasema na kuendelea kutabasamu
“Kama nilivyowaambia kwamba jambo hili ni la kifamilia zaidi lakini nitawapa picha ndogo tu ili jambo hili lisiwe kubwa kiasi cha kuathiri
utendaji kazi mzuri wa Rais wetu mpendwa.Ni kwamba Rais Festus aliwahi kuwa katika mahusiano na mwanamke Yule ambaye ameonekana katika zile picha ambaye wengi mnamfahamu tayari.Ni mahusiano ambayo niliyafahamu na kuyaridhia ndiyo maana nikasema hili ni suala la ndani sana la kifamilia.Ninasema niliyafahamu mahusiao hayo kwani ni mimi niliyemtaka mume wangu kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye angeweza kumtimizia baadhi ya mambo ambayo mimi nisingeweza kutokana na sababu za kiafya hivyo ninafahamu kila kinachoendelea kati ya mume wangu na mwanamke Yule katika picha.Kuna watu wachache ambao naweza kusema ni maadui zetu ambao baada ya kuligundua suala hilo wameamua kutafuta picha hizo na kuzivujisha kwa lengo la kumchafua Rais wetu.Kama familia tumeshangazwa sana na hawa waliovujisha picha hizo na tunaendelea na msako kwa wale wote walioingilia maisha binafsi ya Rais na familia yake.Najua swali mnalosubiri kuniuliza ni maradhi gani yanayonisumbua
hadi kunipelekea niridhie mume wangu awe na mahusiano na mwanamke mwingine lakini mtanisamehe hilo siwezi nikalisema leo.Swali lingine ambalo najua mnataka kuniuliza ni kama ninajisikiaje pale mume wangu anapokutana na mwanamke mwingine,jibu ni kwamba ninajisikia vibaya kwa kuwa mimi ndiye ambaye nilipaswa kutimiza majukumu hayo lakini siwezi kwa sababu za
kiafya.Swali lingine ni kama mwanamke huyo anafahamu kinachoendelea kuhusu mimi kuridhia awe na mahusiano na mume wangu jibu ni ndiyo anafahamu.Swali la mwisho ambalo ninaamini mngetaka kuniuliza ni vipi kama Rais akinogewa na penzi analopewa na huyo mwanamke?Jibu ni kwamba mimi na Festus
kilichopo kati yetu ni zaidi ya mapenzi ndiyo maana jambo kama hili likatokea.Ni jambo la kushangaza ambalo katika maisha ya kawaida haliwezekani lakini kutokana na upendo mkubwa uliopo kati yetu hata kama akinogewa lakini mimi nitabaki wa pekee ndani ya moyo wake na nafasi yangu haiwezi kuchukuliwa na mtu yeyote.Ndugu wanahabari maswali yamekwisha ninawashukuru sana kwa kuja” akasema Bella na kuinuka akaacha gumzo kwa waandishi wa habari
“Haikuwa rahisi lakini naamini nimejitahidi kwa kadiri niwezavyo kuweza kuligeuza jambo hili kuwa la kwangu.Mzigo nimeugeuza na kuubeba mimi na sasa nchi nzima watajua kwamba kile kilichotokea sababu ni mimi.Ninaamini kwa maneno yale machache niliyoyazungumza yataweza kupunguza ukali wa hili jambo.Nimeamua na mimi kujivua nguo ili kutafuta ukaribu na Festus nataka aniamini tena na nitaitumia nafasi hii kuweza kufahamu mahala alipo Mathew Mulumbi na wenzake !
akawaza Bella wakati akielekea ofisini kwake baada ya kutoka kuzungumza na wanahabari ***************
Helkopta ya Rais ilikaribia kutua katika shamba la mazoezi la makomando wa SNSA.Ruby na Nawal walikuwa nje wakimsubiri Rais wakati Mathew alikuwa ndani akipumzika.Taratibu helkopta ikatua mlango ukafunguliwa na walinzi wawili wa Rais wakashuka halafu akashuka IGP Yeremia Mwaipopo na wa mwisho alikuwa ni Rais Festus.
“Karibu sana mheshimiwa
Rais” akasema Ruby
“Ahsante sana Ruby” akasema Rais Festus na kumfuata Nawal
“Nawal nimefurahi tena kukutana nawe”akasema na kumpa mkono
“Nashukuru mheshimiwa
Rais karibu sana”akasema Nawal na kisha wakamuongoza Rais kuelekea ndani
“What is this place? Akauliza IGP Yeremia lakini hakuna aliyemjibu kwani hata Rais hakumwambiwa mahala walikokuwa wanaelekea Walielekea chini ya Ardhi na Yeremia akashangaa baada ya kukutana na nyumba nzuri yenye kupendeza.Moja kwa moja wakaelekea sebuleni na Yeremia akajikuta akipatwa na mstuko wa mwaka baada ya kumkuta Mathew Mulumbi akiwa amekaa sofani
“Tobaa ! Huyu si Mathew Mulumbi? Huku ndiko alikojificha?Akajiuliza
“Karibu sana
Yeremia.Hapa ni sehemu ya mazoezi ya makomando wa SNSA” akasema Rais Festus huku Yeremia akijitahidi kutabasamu lakini ni wazi alikuwa na mstuko mkubwa kwa ndani.
“Yeremia kutana na
Mathew Mulumbi”akasema Rais
“Nimestuka nilipomuna Mathew Mulumbi,sikutegemea kabisa kama ningeweza kumkuta mahala hapa” akasema Yeremia
“Usishangae Yeremia kwani Mathew Mulumbi yuko hapa.Nimekuwa na mashirikiano naye.Kuna mambo muhimu sana ambayo anayafanya yeye na wenzake kwa ajili ya nchi hii.Hapo alipo ana siku moja tangu afanyiwe upasuaji mkubwa baada ya kupigwa risasi tatu lakini hajalala kitandani anaendelea na majukumu na yote haya anayafanya kwa ajili ya taifa hili” akasema Rais Festus.
“Pole sana Mathew ! akasema Yeremia
“Yule pale anaitwa Ruby ni mke wa Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo na Yule pale anaitwa Nawal” Festus akaendelea na utambulisho.
“Yeremia nimekuleta hapa kuna jambo ambalo mimi na vijana wangu tunataka tuzungumze nawe” akasema Rais na kunyamaza
“Jana usiku nilikupigia simu na kukupa maelekezo ya kutuma watu kwenda nyumbani kwa Asajile Mlabwa kuchukua vifaa vyake vya mawasiliano”
“Ndiyo mheshimiwa Rais
ulinituma na nikafanya hivyo” akajibu Yeremia
“Nataka kuwafahamu vijana uliowatuma kwenda kuchukua vifaa hivyo”akauliza Rais na Yeremia akastuka
“Mheshimiwa Rais nilimpa maelekezo kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam yeye ndiye anayewafahamu” akasema Yeremia
“Una hakika?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Kuna nini mzee? Akauliza
Yeremia
“Ninahitaji kuwafahamu askari hao.Ngoja nimpigie simu kamanda wa polisi kanda maalum” akasema Rais Festus na kutoa simu yake
“Mheshimiwa Rais” akaita Yeremia ambaye macho yake yalionyesha woga mkubwa
“Unasemaje Yeremia?
Akauliza Rais Festus wakati akizitafuta namba za simu za kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam
“Kuna kitu ambacho nataka nikufafanulie” “Endelea”
“Uliponipa maelekezo ya kwenda kuchukua vifaa hivyo sikuona sababu ya kutuma askari wadogo hivyo nikaenda mwenyewe kuvichukua” akasema Yeremia na Rais Festus akamtazama kwa macho makali
“Kwa nini hukunieleza ukweli na ukaendelea kudai kwamba uliwatuma vijana?
“Nisamehe mheshimiwa
Rais lakini sikutaka ufahamu kuwa nilifanya kazi ile mimi mwenyewe badala ya kuwatuma askari wadogo lakini nilifanya hivyo ili kuwa na uhakika kwamba ……”
“Nataka unijibu Yeremia kwa nini hukunieleza ukweli kama ni wewe uliyekwenda kuchukua ile kompyuta?! Akauliza Festus kwa ukali
“Nisamehe mheshimiwa
Rais kwa hilo” akasema Yeremia.
“Dah ! akasema Rais Festus huku akitingisha kichwa kwa masikitiko “Mathew endelea” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa IGP jana ulipokwenda nyumbani kwa Asajile ulipewa simu na kompyuta lakini uliiwasilisha kompyua pekee kwa Rais.Tunataka kufahamu simu iko wapi? Akauliza Mathew
“Simu? Yeremia akashangaa
“Ndiyo.Iko wapi simu ya Asajile? Akauliza Mathew
“Sifahamu ilipo.Simu hiyo ilitafutwa sana lakini haikupatikana.Wametumwa askari mara mbili kwenda kuitafuta lakini haijapatikana”
“Mheshimiwa IGP
tumehakikishiwa na mke wa Asajile mama Isaya kwamba alikukabidhi wewe simu hiyo pamoja na kompyuta.Tunahitaji kufahamu mahala ilipo hiyo simu” akasema Mathew
“Sifahamu ilipo simu.Mheshimiwa Rais sifahamu simu hiyo ilipo.Kama nilivyokueleza simu hiyo imetafutwa sana
haijapatikana” akasema Yeremia
“Mheshimiwa IGP
tumetoka hivi sasa kuzungumza na mke wa Asajile na ametueleza kwamba alikupa wewe simu ya mume wake.Tunahitaji kujua mahala ilipo” akasema Mathew
“Yeremia sitaki hadithi ninataka kujua mahala iliko simu.Usitake kunipandisha hasira nikakuharibu sasa hivi.Wewe ni mmoja wa watu ninaowaamini sana Yeremia na nimekuwa nikikushirikisha katika mambo mengi muhimu kwa nini umefanya kitendo kama hiki?Tafadhali naomba uonyeshe mahala iliko simu ya
Asajile ! akasema kwa ukali Rais Festus
“Mheshimiwa Rais !
“Yeremia sitaki hadithi ninajua unayo simu nataka unipatie hiyo simu haraka sana” akasema Rais Festus
“Sifahamu iliko simu mheshimiwa Rais taarifa mliyopewa si taarifa ya kweli” akasema Yeremia
“Yeremia unazidi kuniudhi na kunilazimisha nichukue maamuzi magumu dhidi yako.Bado una nafasi nionyeshe simu iliko na nitakusamehe ! akasema Rais
“Sifahamu mheshimiwa
Rais iliko simu” akasema Yeremia na Rais akamtazama kwa macho yaliyojaa hasira kali
“Yeremia kwa nini unataka nikuharibu? Akauliza Rais
“Mheshimiwa IGP kwa kuendelea kukana kwamba hufahamu mahala iliko simu unatulazimisha tuamini kwamba ulishirikiana na Asajile katika mauaji ya Frank tambua hapo unakabiliwa na tuhuma za mauaji na pili unashirikiana na watu waliovamia na kuua katika ofisi za SNSA ambao ni wafanya biashara wa dawa za kulevya” akasema Mathew na sura ya Yeremia ikaendelea kubadilika
“Anachokisema Mathew ni kitu cha kweli kabisa Yeremia lakini wewe ni mtu wangu wa karibu sana kwa nini tufike huko.Tuonyeshe iliko simu na mambo haya yataishia huku porini na hakuna atakayefahamu chochote lakini ukiendelea kukana kuwa hauna simu unazidi kunipa hasira” akasema Rais Festus.Jasho lilimtoka
Yeremia usoni
“Yeremia nakupa nafasi ya mwisho kama ukishindwa kuitumia usinilaumu kwa hatua nitakazochukua dhidi yako” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais unanifahamu vizuri kama ningekuwa nafahamu kitu chochote kuhusiana na hiyo simu ningekwisha kueleza lakini sifahamu chochote ! Ukichukua hatua zozote juu yangu utakuwa unanionea mheshimiwa rais” akasema Yeremia.Rais Festus akamtazama kwa hasira kwa muda wa dakika mbili halafu akachukua simu akampigia katibu mkuu kiongozi
“Katibu mkuu kiongozi” akasema Rais na Yeremia akamtazama Rais kwa macho ya huruma
“Naam mheshimiwa Rais” akasema katibu mkuu kiongozi
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment