Search This Blog

Friday 7 April 2023

SCANDLE (KASHFA) (2) - 3

   

Simulizi : Scandle (Kashfa) (2)

Sehemu Ya Tatu (3)


“No I’m not ! akajibu Zari

“Wameniudhi sana wale watu wetu kwa nini wameshindwa kung’amua kama kuna watu wanatufuatilia hadi tukataka kuuawa? Akauliza Zari

“Zari hatupaswi kuwalaumu wale makomando.Hawa watu tunaowatafuta wana uwezo mkubwa na wana mbinu nyingi ndiyo maana wameweza kutufuatilia bila makomando wetu kuwabaini hata hivyo unapaswa kuwashukuru kwani wao ndio waliotuokoa.Hali ilikuwa mbaya sana kwa upande wetu” akasema Mathew na kumtazama Zari ambaye bado kichwa chake

alikiinamisha chini halafu akasema

“Zari naomba unisikilize vizuri.Hadi sasa ninatafutwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa na dawa kulevya vile vile mauaji.Ninatafutwa pia na hawa jamaa tusiowafahamu kwani tayari ni mtu hatari kwao.Papi Gosu Gosu anateseka gerezani na maisha yake yako katika hatari kubwa.Dr Fabian Kelelo anashikiliwa hivi sasa na jeshi la polisi na salama yao wat hawa wawili ni sisi pale tutakapofanikiwa kulinasa hili genge la wahalifu.Bila sisi kujitoa kuwatafuta hawa jamaa hatutaweza kuwakomboa hawa wenzetu hivyo basi nahitaji mtu ambaye atakuwa tayari kujitoa kikamilifu.Sipendi kufanya kazi na mtu mwoga mwenye kukata tamaa baada

ya kukoswa na risasi moja.Nataka mtu mwenye moyo mgumu kama jiwe ambaye haogopi kutoa uhai wake kwa ajili ya kuhakikisha misheni

inafanikiwa.Nakushukuru Zari umetukaribisha hapa kwako lakini sina hakika kama unafaa kuendelea na misheni hii ! akasema Mathew na Zari akainua kichwa

“Kwa nini Mathew?

Akauliza Zari

“Ni mwoga,huna

uvumilivu,unakata tamaa haraka.Matukio mawili tu umeyapitia lakini tayari unatetemeka.Siwezi kufanya kazi na mtu kama wewe ! akasema Mathew

“Mathew I’m sorry ! Please I’m very sorry ! akasema Zari

“Mathew we need her ! akasema Ruby

“Ruby nahitaji kufanya kazi na watu majasiri na huyu rafiki yako hana sifa hizo ! akasema Mathew na kutoka mle ndani akaenda sebuleni

“Sina hakika kama Zari anafaa kuendelea naye.Ni mwoga sana na mimi sipendi watu waoga.I miss Gosu Gosu.Kile chuma hakiogopi

kitu,haogopi risasi na ndiyo maana ninapenda kumshirikisha katika kila misheni.Ninaapa lazima nihakikishe ninamuondoa gerezani kwa namna yoyote ile” akawaza Mathew na kugeuka baada ya kuitwa na Ruby aliyemfuata sebuleni

“Mathew samahani sana kwa kilichotokea huko mlikokwenda lakini bado tunamuhitaji Zari” akasema Ruby

“No ! siwezi kufanya kazi na mtu anayeogopa risasi !

“Mathew Zari hajazoea kukutana na mambo kama haya.Nimezungumza naye na amenihakikishia kwamba amejifunza na atabadilika.Anaomba tuendelee kumshirikisha katika misheni hii ! akasema Ruby na kunyamaza baada ya Zari kutokea

“Mathew naomba

nisamehe kwa kilichotokea.Ni kweli nilipatwa na mstuko mkubwa kwa tukio lile lakini nakuahidi kwamba haitatokea tena.Tafadhali naomba niendelee na misheni hii.Ninakiri sijakutana na mikiki mikiki ya namna hii toka nimeanza kazi yangu lakini kadiri ninavyoendelea kukutana na mambo kama haya ndivyo ninaendelea kujengeka.Tafadhali Mathew naomba uniruhusu niendelee nawe katika hii misheni,naomba univmilie pale nitakapoonyesha udhaifu na unielekeze.Nahitaji kuwa bora zaidi,nahitaji kuwa kama Ruby na wengine na hilo litafanikiwa kama nitakuwa karibu yako.Naomba sana Mathew” akasema Zari.Mathew akamtazama halafu akasema

“Fine.Last chance.Misheni hii ni muhimu sana kwangu hivyo sitaki uzembe wa aina yoyote.Watu wengi wamekwisha poteza maisha hadi sasa na wengine bado wanaendelea kuuawa na hili

genge la wahalifu hivyo ni sisi ambao tunapaswa kufichua uovu wao,ni sisi ambao tunapaswa kuwasaidia ndugu zetu,Gosu Gosu na Dr

Fabian.Jina langu limekwisha chafuliwa na ninasakwa kama mhalifu hivyo nataka kulisafisha jina langu na njia pekee ya kujisafisha ni kulipata genge hili la wahalifu walionichafua.Ladies hii si kazi nyepesi hata kidogo.Hawa watu tunaowatafuta ni watu makini wenye mtandao mpana na wana uweo mkubwa na wao pia wako vitani hivi sasa wakiendelea kutusaka kama sisi tunavyowasaka wao hivyo tunahitaji kuwawahi kabla hawajatuwahi.Nina uhakika

mkubwa kama tukisimama

imara tutashinda vita hii lakini natoa angalizo angali mapema kwamba kwa yeyote ambaye anaona hataweza kuendelea na hii misheni basi aweke wazi angali mapema sitaki kukwamishwa huko mbeleni mambo yatakapokuwa magumu zaidi” akasema

Mathew

“Mathew mimi niko tayari kwa lolote sintakata tamaa nitapambana kwa kadiri niwezavyo kuhakikisha tunaifanikisha misheni hii” akasema Zari

“Good.Nenda kawaombe msamaha makomando wale kwa maneno uliyowatamkia.Wale ni watu muhimu sana kwetu” akasema Mathew na Zaria akaenda katika chumba cha mapumziko kuwaomba msamaha makomando kama alivyoelekezwa na Mathew. “Ahsante Mathew kwa

kumpa Zari nafasi nyingine.Hii ni nafasi ambayo anaihitaji sana ili kupata uzoefu ! akasema Ruby

“Anatakiwa kuwa

jasiri,sipendi mtu

mwoga”akasema Mathew na Ruby akarejea wakaelekea katika chumba chao cha mikakati.




“Jamani kama mnavyojua hatuna muda wa mapumziko.Hatuna hata sekunde moja ya kupoteza hivyo tunaendelea na mikakati” akasema Mathew na kuelekea ubaoni

“Siku ya leo japo tumekutana na mikiki mikiki lakini kuna mafanikio tumeyapata.Kwanza tumefahamu sababu ya kifo cha Adam Watwila baba mzazi wa Naomi.Pili tukafanikiwa kumuhoji nabii Kasiano naye akatupa ushirikiano kwa namna alivyoweza na picha kubwa tukaenda kuipata shuleni alikosoma Naomi.Tuanze kwanza na maelezo ya mdogo wake Adam.Alitueleza kuwa Adam alimpigia simu wakati akielekea Morogoro akamwambia kwamba kuna jambo zito atakuja kumueleza atakaporejea lakini papo hapo tukapata taarifa shuleni kwamba siku hiyo hiyo Adam aliitwa shuleni kuelezwa taarifa za mwanae na ni siku hiyo hiyo Naomi alipotoweka .Katika maelezo yake nabii mkuu Kasiano alisema kwamba safari ya Adam kwenda Morogoro ni yeye alimtuma kwa ajili ya shughuli za kanisa.Ninapata kigugumizi kidogo hapa.Tazameni jambo hili,Adam anaitwa shuleni na anapokea taarifa nzito za kuhusu mwanae na ghafla mwanae anatoweka katika mazingira kama yale tuliyoelezwa na wanaanza kumsaka.Kama haitoshi anaachana na zoezi kumtafuta mwanae halafu anaondoka yeye na mkewe kwenda Morogoro katika shughuli za kichungaji.Hili jambo mnalionaje? Akauliza Mathew

“Kweli kabisa jambo hili linashangaza kwa nini wakaondoka wazazi wote wawili? Kama Adam alitumwa kwa kazi za kanisa kwa nini hakwenda mwenyewe na kumuacha mke wake aendelee kumtafuta binti yao? Akauliza Zari

“Hili suala linawezekana katika filamu tu lakini katika uhalisia haliwezekani.Mimi ni mzazi na hata hapa nilipo

sipati usingizi nikiwafikiria wanangu japo naamini wako sehemu salama iweje Adam asionyeshe kuguswa na kupotea kwa mwanae tena wa pekee na halafu yeye na mke wake waache zoezi la kumsaka mtoto wao na waondoke kwenda Morogoro kwa kazi za kichungaji? Akauliza Ruby

“Na kama aliondoka hapa

Dar es salaam alasiri au jioni hii ina maana ni baada ya kutoka shuleni je hakumueleza mchungaji Kasiano kama mwanae amepotea ili aahirishe safari ya Morogoro hadi mwanae atakapopatikana? Kuna wachungaji wengine katika lile kanisa kwa nini hakutumwa mchungaji mwingine kwenda Morogoro na Adam akaachwa aendelee kufuatilia suala la

mwanae?Kingine cha kushangaza ni kama alivyosema Ruby kwamba walifahamu kuwa mtoto wao amepotea kwa nini wakaondoka wote wawili je

ilikuwa ni safari yenye ulazima mkubwa hadi wote waende?Hayo ni maswali ambayo yanahitaji majibu.Lakini wakati tukitafuta majibu tunakutana na mzizi wa suala hili ambao ni

Zoe au Naomi” akasema Mathew na kunyamaza kidogo.

“Kuna mambo ya

kushangaza sana yametokea katika suala hili la Naomi.Kwanza kabisa ni kitendo cha taarifa zake zote kuondolewa kila sehemu na hakuna mahala kwenye kumbu kumbu zake.Watu wale walihakikisha hakuna mahala ambako jina Zoe Watwila au Naomi Bambi linasalia.Wameliondoa kila sehemu ii kuhakikisha yeyote Yule ambaye atadiriki kufanya uchunguzi basi ashindwe kupata taarifa zozote.Ninawasifu hawa jamaa

they’re very smart” akasema

Mathew

“Kitendo kama hiki cha kuondoa kumbu kumbu za mtu ili kifanikiwe lazima uwe na mtandao mpana”akasema

Zari

“Exactly ! hawa jamaa ni mtandao mpana na ndiyo maana mambo yao mengi yanafanikiwa” akasema Ruby

“Tumesikia wote kwamba maisha ya Zoe au Naomi namna yalivyokuwa shuleni.Aliishi kama mtoto wa malkia.Aliishi kifahari kuliko hata watoto wa mabilionea wanaosoma shuleni hapo kwani shule ile ni shule wanakosoma watoto wa watu matajiri.Wazazi wa Naomi hawakuwa na kipato kikubwa cha kumsomesha mtoto wao katika shule kama ile bali alifadhiliwa na kanisa la Injili ya wokovu lakini maisha yake yaliwapita hata wale waliokuwa wanasomeshwa na wazazi wao.Lazima tujiulize aliwezaje kuishi maisha ya kifahari kama tulivyoelezwa kama wazazi wake hawakuwa na uwezo na alikuwa anasoma pale shuleni kwa ufadhili?Tumeambiwa toka alipofika pale shuleni Naomi hajawahi kula chakula cha shule bali alikuwa akiletewa chakula maalum kutoka hotelini kila siku asubuhi mchana na jioni.Hii ni kinyume cha taratibu za shule lakini kwake iliwezekana kutokana na nguvu ya pesa.Tumeelezwa pia kwamba alipofika kidato cha tatu alibadili jina bila wazazi wake kufahamu na kujiita Naomi Bambi.Tumesikia wote kwamba Naomi alikuwa na uwezo wa kuondoka shuleni muda wowote autakao bila kikwazo chochote.Tumesikia pia walimu walikuwa wakilipwa fedha kila mwisho wa mwezi ukiitwa mshahara wa Naomi ili kumtunza kama binti mfalme.Haya yote yanatupa picha pana kwamba kuna mtu nyuma yake aliyekuwa anamgharamia na huyo ndiye ambaye tunatakiwa kumtafuta” akasema Mathew

“Huyo si mtu mdogo.Lazima atakuwa ni mmoja wa matajiri wakubwa hapa Afrika na dunia kwani gharama kama zile alizokuwa anagharamiwa Naomi huyo mtu lazima ana pesa kama mchanga.Mwanafunzi wa kidato cha tatu unakutwa na milioni kumi na moja sandukuni hii imevuka viwango” akasema Ruby

“Swali ninalojiuliza je gharama hizi zote ambazo huyu mtu alikuwa anagharamia ni kwa ajili ya nini? Je alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Naomi? Akauliza Zari

“Swali zuri.Ni gharama kubwa mno hadi kufikia hatua ya kuwalipa mishahara walimu wote kwa ajili tuya kuhakikisha Naomi anatoka muda wowote autakao bila vikwazo.NI gharama kubwa mno” akasema Ruby

“Wengine tulikuwa tunaahidiwa chipsi kuku tunaruka ukuta wa shule kama ninja” akasema Zari na wote wakaangua kicheko

“Tumshukuru mwalimu

mkuu aliyelivumbua jambo hili na kulivalia njuga japo amefariki tayari,lakini ni yeye ambaye ametusababisha leo hii tunajiuliza maswali haya magumu.Huko aliko Mungu amrehemu kwa jambo hili alilolifanya.Mwalimu huyu ndiye aliyemuita Adam shuleni na kumueleza ukweli kuhusu mwanae na mchana huo huo Naomi akatoweka.Inaonyesha kwamba Naomi alifahamu ujio wa baba yake pale shuleni ndiyomaana akatoweka.Suala la pili ni kwamba baada ya kutoweka ndipo matatizo ya akili yalipomtokea na baadaye kuokotwa kituo cha basi akiwa hajitambui.Hapa tunarudi kwa Zawadi Mlola ambaye alichukuliwa na kwenda kumchoma Naomi sindano iliyomuharibu akili.Picha inayokuja hapa yawezekana Yule mtu aliyekuwa anamgharamia Naomi alipata taarifa kuwa Adam baba yake Naomi amekwisha fahamu kila kitu na mambo yangeharibika hivyo wakamtorosha Naomi shuleni na kumuharibu akili ili asiweze kukumbuka chochote na baadae wakamuua.Nina uhakika mkubwa Naomi hakujirusha ghorofani kama inavyodaiwa bali alisukumwa akafariki ili kuondoa kabisa ushahidi wote.Picha nyingine inayokuja ni kwamba hata wazazi wa Naomi watakuwa waliuawa baada ya kuufahamu ukweli jambo ambalo hawakupaswa kulifahamu.Baada ya hapo kila aliyejaribu kuendelea kulichunguza suala hili la Naomi aliuawa na kulifanya liwe ni suala hatari kabisa kulichunguza.Swali linaloibuka kwa nini baada ya

kutumia gharama hizo zote kwa Naomi wakamuua?Kwa pesa alizokuwa nazo huyo mtu angeweza kuzungumza na Adam na kumjengea hata kanisa kubwa ili kulimaliza jambo hili lakini wakaamua kumuua Naomi.Je kuna kitu alikifahamu ambacho hakutakiwa kujifahamu kilichosababisha auawe? Akauliza Mathew

“Kuna siri kubwa sana

imejificha hapa na hata sisi tunapaswa tujipongeze kwa hatua hii kubwa tuliyoipiga.Naamini wengine wote waliowahi kulifuatilia suala hili hawakuwahi kufika

hapa tulipofika sisi na ndiyo maana jamaa wanatumia nguvu kubwa kuhakikisha kwamba wanatuondoa ili tusiendelee kulichunguza jambo hili” akasema Mathew.

“Nini kinafuata baada ya haya yote tuliyoyagundua? Akauliza Ruby

“We need to dig deeper.Tulielezwa kule shuleni kwamba Naomi alikuwa na rafiki mkubwa ambaye ni mtoto wa gavana wa benki kuu na alihamishwa siku chache baada ya Naomi kufariki dunia.Kama tukimpata huyo binti anaweza akatusaidia sana kufahamu mambo mengi ya Naomi”akasema Zari

“She’s dead ! akasema Ruby

“Dead too? Mathew akashangaa

“Yes she’s dead.Nilitafuta taarifa zake tayari amekwisha

fariki dunia kwa ajali ya gari” akasema Ruby

“Dah ! Naomi ameondoka na watu wengi.Kila aliyekuwa karibu yake hayuko salama.!akasema Zari kwa masikitiko

“Baada ya shambulio lile pale shuleni nilimpekua mmoja wa wale jamaa nikachukua simu na pochi yake ndogo” akasema Mathew na kuitoa simu akampatia Ruby halafu akaifungua ile pochi akatoa vitu vilivyokuwemo ndani.Kulikuwa na leseni ya udereva,kadi mbili za benki na kitambulisho cha taifa chenye jina la Joseph Mgagala.

“Imekuwa bahati tumekipata kitambulisho chake cha taifa na kulifahamu jina lake.Nilikuja na kidole chake gumba ili tuweze kufuatilia kumfahamu lakini kwa vile tayari tunavyo vitambulisho basi kazi yetu imekuwa rahisi.Tuanze kumchimba huyu kupata taarifa zake.Ruby uwanja ni wako sasa” akasema Mathew na Ruby akaiwasha ile simu ya Joseph na kuiunganisha na kompyuta yake akaanza kuipekua kutafuta mawasiliano ya Joseph.Zari na Mathew walikaa nyuma yake wakimuangalia alivyokuwa akicheza na kompyuta kama alikuwa na vidole sita katika kila mkono.Mara Ruby akapiga meza kwa hasira “Aaagh !

“Nini Ruby? Akauliza Mathew

“Hakuna kitu.Wamefuta kila kitu.Hakuna mawasiliano yake yoyote”

“Ingia katika kumbu kumbu za SNSA.Tunahifadhi kumbu kumbu za kila simu” akasema Zari

“SNSA wanahifadhi kumbukumbu ya namba za

simu zilizosajiliwa pekee lakini hawa jamaa wanatumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa hivyo inakuwa vigumu kuwatambua na wako makini sana katika kuficha mawasiliano yao”akasema Ruby

“Wanawezaje kufanya

hivyo? Akauliza Zari

“Hata mimi

sifahamu.Laini za simu ambazo hazijasajiliwa hapa Tanzania haziruhusiwi lakini wenyewe wanaweza kuzitumia.Ukitazama watu wao ambao tumewafahamu wote wanatumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa” akasema Ruby na kuifungua ile simu akaitoa laini akaitazama kwa makini

“Wanawezaje watu hawa kutumia laini hizi ambazo hazijasajiliwa? Akauliza

“Jibu tutalipata katika mitandao ya simu.Lazima kuna mashirikiano kati ya hawa jamaa na mitandao ya simu ” akasema Mathew na mara ukasikika mlio Fulani uliomfanya Ruby ageuze shingo na kuitazama ile simu.Ujumbe mfupi uliingia katika simu ya Joseph akaichukua na kuufungua ujumbe ule uliosomeka

“Honey tayari nimefika hapa dukani nimeambiwa hujafika uko wapi?

“Ujumbe huo umetoka wapi? Akauliza Mathew

“Umetoka kwa mtu anaitwa Monica.Naombeni dakika moja kuna kitu kinanichanganya hapa” akasema Ruby na kuifungua ile simu akaanza kuichunguza.Akamuomba Ruby kifaa kidogo cha kufungulia akaletewa na kuifungua na mara sehemu Fulani ndani ya ile simu akakuta kuna laini ndogo ya simu.

“Tumempata.Huyu jamaa kumbe ana laini mbili.Moja ni ile ambayo haijasajiliwa na nyingine ni hii ambayo imefichwa ndani kabisa kiasi kwamba si rahisi kuonekana.Inaonekana hii laini iliyojificha ndani ndiyo huitumia kwa mawasiliano na watu wake wa kawaida na ile nyingine isiyosajiliwa hutumia kwa kazi zao”akasema Ruby

“Ahsante Ruby kwa kuligundua hilo”

“Huyu Monica

aliyemtumia ujumbe anaonekana ana miadi ya kukutana na huyu jamaa na tayari amekwisha fika eneo la kukutana.Tufanyaje? akauliza Ruby

“Inaonekana huyu Monica bado hajapata taarifa kama Joseph ameuawa.Mtumie ujumbe usomeke Nitachelewa

nifuate Sangara Plaza.Nitakwenda hapo kumsubiri halafu nitamchukua na kumuhoji kuhusu Joseph.Zari utabaki na Ruby nitaondoka na komando mmoja tutatumia gari lao.Endeleeni kufuatilia taarifa za huyu Joseph” akasema Mathew

“Sawa Mathew” akasema Ruby na Mathew akamfuata mmoja wa makomando akamtaka waongozane halafu akachukua ile simu ya Joseph wakaondoka

“Jina lako nani? Mathew akamuuliza Yule jamaa aliyeongozana naye

“Naitwa Nelson Lambada.Niite Lambada inatosha watu wengi huniita hivyo”

“Mimi naitwa Mathew Mulumbi”

“I know who you are

sir.Nimeanza kusikia taarifa zako tangu nikiwa mafunzoni na ninafurahi kufanikiwa kuonana nawe ana kwa ana” akasema Nelson “Tunakwenda kumchukua mwanamke mmoja ambaye ana ukaribu na mmoja wa wale jamaa tuliowaua pale shuleni mchana wa leo,atatusaidia kufahamu mambo mengi kuhusiana na jamaa anayeitwa Joseph”Mathew akasema

“Watu hawa ni akina nani? Akauliza Nelson

“Bado hatujawafahamu ni akina nani lakini ni watu hatari na kuna jambo wanalificha lisijulikane hata hivyo tunaelekea kuzuri” akasema Mathew

“Napenda sana kadhia kama hizi”akasema Nelson

“Kwa nini? Mathew

akauliza

“I like guns so much ndiyo maana nikachagua kwenda jeshini ambako nilifanya vizuri na kupelekwa katika kozi ya komando na baadae nikaletwa hapa SNSA” akasema Nelson

“Huyu anaonekana ana tabia kama za Gosu Gosu” akawaza Mathew

“Sijui Gosu Gosu anaendeleaje kule gerezani.Naomba Mungu aendelee kumsaidia naamini ndani ya siku chache kutoka sasa anaweza akawa huru kwani tunakoelekea ni kuzuri japo bado kuna kiza lakini nitafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha Gosu Gosu anatoka gerezani.” akawaza Mathew na kutabasamu





Msafara wa mke wa Rais uliwasili nyumbani kwa nabii mkuu Kasiano.Mama Bella akashuka garini na kupokewa na Kasiano na mke wake wakamkaribisha ndani

“Nimerejea tena” akasema Bella

“Karibu tena mama” akasema Kasiano

“Rita do you have anything strong to drink? Akauliza Bella

“Yes mam” akajibu Rita na kwenda kuleta chupa kadhaa za pombe kali na Bella akatabasamu

“This is what I like” akasema na Rita akammiminia katika glasi akanywa halafu akakohoa kidogo

“Hakuna waumini

wanaoingia huku? Akauliza Bella

“Hapana mama.Huku ni

maalum kwa ajili ya watu kama ninyi lakini wengine wote wanafikia kule chini”

“Good .Nilidhani kuna waumini huwa wanafika hadi huku wasije wakamkuta nabii wao anakunywa pombe kali

wakaanza maneno” akasema

Bella

“Ninajitahidi sana mama kuhakikisha ninavaa sura tofauti tofauti japo si kazi nyepesi kuishi katika sura tofauti lakini ninashukuru mpaka sasa ninaendelea vizuri na hakuna tatizo lolote hadi alipotokea huyu Mathew ambaye ameanza kuleta wasiwasi kidogo..”

“Usiwaze kuhusu huyo takataka Mathew Mulumbi.He’s nobody.Hawezi akafanya kitu chochote na hawezi akafika kokote.Amejiingiza mwenyewe katika tanuru la moto.Hata hivyo nakulaumu sana Kasiano kwa kuliacha suala hili hadi likafika hapa.Ilitakiwa pale ulipoona kuna viashiria vya hatari ungenijulisha ili haraka sana tuweze kumfinyanga

huyo mtu.Naomba jambo hili lisijirudie tena”

“Hata mimi mama

sikutegemea kama hili suala lingewezakufika hatua hii ya kumuhusisha hadi Rais na ndiyo maana lilipofika hatua hio nikakujulisha mara moja ili uweze kunisaidia” akasema Kasiano

“Lisijirudie tena jambo hili.Japo una kila kitu una kikundi chenye nguvu Black Mafia,una mtandao mpana lakini pale unapoona kuna kitisho chochote cha usalama unijulishe mara moja.Nimekuachia wewe kila kitu ukiongoze kwa sababu ninakuamini lakini si kila kitu utakiweza.Unapoona suala huliwezi toa taarifa haraka sana.Mimi ndiye Malkia,mimi ndiye mtawala eneo hili hivyo sitaki himaya yangu iingiliwe na mdudu wa aina yoyote ile.Nguvu yangu ni kubwa sana kwa taarifa yako.I can do anything in this country.Ninyi nyote mko huru kufanya biashara bila bughudha kwa sababu yangu.Nadhani umenielewa Kasiano”

“Nimekuelewa

mama”akajibu Kasiano

“Good.Tuyaweke kando mambo hayo .Nataka kwanza kufahamu mmefikia wapi katika kumsaka huyu Mathew Mulumbi ?

“Mama mpaka sasa bado

hatujui mahala alipo lakini vijana wako kazini wanaendelea kumsaka na tunapata pia taarifa kutoka jeshi la polisi ambao nao pia wanaendelea kumsaka” akasemaKasiano na kumeleza Bella kuhusiana na tukio lililotokea mchana ule katika shule ya kimataifa ya wasichana alikokuwa akisoma

Zoe

“Kasiano kwa mbinu hizo hamuwezi kumpata Mathew Mulumbi.Huyu mtu ni jasusi na si mtu wa mchezo kama mnavyodhani.Hadi wamefika hapo shuleni inaonekana tayari wamekwishapiga hatua kubwa.Hata hivyo……” Bella akanyamaza akachukua glasi akanywa kinywaji na kusema

“Nimezungumza na mkuu

wa jeshi la polisi Yeremia

Mwaipopo” akanyamaza tena kidogo

“Alifika ofisini kwangu kama nilivyomuelekeza nikiwa hapa..Mimi na Yeremia ni marafiki.Tumesoma pamoja sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na hata wazazi wetu

wanafahamiana.Baada ya Festus kuwa rais nilimpendekeza Yeremia awe mkuu wa jeshi la polisi wakati huo alikuwa ni kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam hivyo mimi na Yeremia ni watu wa karibu sana.Msishangae kwa nini ameweza kuacha shughuli zake na kufika ofisini kwangu mara moja nilipomuita” akasema Bella na kunyamaza kidogo

“Yeremia amenieleza ukweli kwamba maagizo ya Mathew Mulumbi kuhamishwa yalitoka kwa Rais.Nilimbana akanieleza ukweli kwamba tayari Rais anafahamu kuwa tuhuma zile zinazomkabili Mathew Mulumbi si za kweli na kwamba ni mchezo umechezwa ili kumuondoa katika ramani.Rais anafahamu tayari kwamba kuna kikundi cha watu wanafanya mambo ya kihalifu hapa nchini na ndiyo maana ukaandaliwa mpango ule wa kumteka Mathew Mulumbi ili aweze kuendelea kuwatafuta watu hao.Hivyo basi naomba mfahamu kwamba mpango ule uliandaliwa kwa siri na Rais anafahamu kila kitu” akasema Bella

“Hapa ndipo ngoma inapokuwa nzito ndiyo maana nikakushirikisha mama ” akasema Kasiano

“Msihofu ngoma

imempata mpigaji nah ii vita

ni nyepesi sana” akasema Bella na kunyamaza tena kidogo

“Festus anafahamu mahala alipo Mathew Mulumbi lakini ugumu ni namna ya kuweza kumshawishi anieleze kwani kama nilivyowaeleza muda ule kwamba mimi na Festus hatuna maelewano mazuri kwa sasa.Kwa maelezo ya Yeremia,katika mpango huu wa kumteka Mathew Rais anashirikiana na SNSA”

“SNSA? Kasiano na Rita wakauliza

“Ni kitu gani hicho?

“Hata mimi nilishangaa kama ninyi nilipoambiwa kuhusu SNSA.Kwa mujibu wa Yeremia SNSA ni idara ya siri ya usalama wa ndani wa

nchi.Idara hii iko chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kama lilivyo jina lake idara hii inafanya shughuli zake kwa siri kubwa na hata Yeremia mwenyewe hafahamu mahala zilipo ofisi zao.Ruby mke wa Dr Fabian amekuwa mkurugenzi wa idara hiyo kabla hajaolewa na Dr Fabian hivyo siri nyingi za nchi anazifahamu”

“SNSA wanafahamu

kuhusu sisi? Akauliza Kasiano

“Sifahamu bado lakini kuna kila dalili kwamba kuna kitu wanakifahamu kuhusu sisi kwani kama Ruby aliwahi kuwa mkurugenzi wa SNSA na ni mtu wa karibu sana wa Mathew Mulumbi basi lazima watakuwa wanafahamu kuhusu sisi na ni Ruby aliyemjulisha Rais kwamba tuhuma zile kuwahusu Mathew na mumewe DrFabian ni za kutengenezwa” akasema Bella na kunywa kinywaji chake halafu akaendelea

“Festus ni Rais na ana nguvu kubwa vyombo vyoe vya ulinzi na usalama viko chini yake hivyo kupambana naye ni sawa na kupigana na ukuta tutaumia sisi hivyo tutatumia njia nyingine. Festus ni Rais anayependa kusifiwa na hapendi kusemwa vibaya.Anaogopa kukosea na anajitahidi sana kuwa msafi katika kazi yake lakini yeye si malaika,anayo mapungufu na madhaifu pia hivyo basi tutatumia madhaifu yake kumpiga na kumlazimisha afuate tunavyotaka na hiyo ndiyo njia pekee itakayotufanya tushinde vita hii”

“Huo unaonekana ni mpango mzuri sana mama Bella” akasema Kasiano

“Niliwaambia mimi naye hatuna mahusiano mazuri siku

hizi na hili watu

hawalifahamu.Wananchi wanatuona tuko pamoja wakiamini tuna furaha ndani lakini humo ndani ni mgogoro mkubwa.Tuyaache hayo ninachotaka kuwaambia ni kwamba licha ya Festus kujitahidi sana kuwa msafi kwa nje lakini kwa ndani ni mtu mchafu mno.Kwanza amekuwa na matumizi makubwa sana ya fedha kitu ambacho wengi hawakifahamu.Kwa sasa ana mahusiano ya siri na mwanamke mmoja anaishi Afrika kusini anaitwa Zandile Wepener mwanamitindo na…..”

“Hakuna asiyemfahamu mwanamitindo Zandile Wepener.Aliviteka vyombo vya habari ulimwenguni pale alipoachwa na mfalme wa

Eswatini kwa usaliti katika ndoa yao” akasema Kasiano “That’s her ! akasema Bella

“Oh my Gosh ! Festus ana mahusiano na Zandile? Akauliza Rita

“Ndiyo.Mahusiano yao ni ya siri sana na ni moja ya sababu iliyopelekea mimi na Festus tuwe katika mgogoro mkubwa.Ninadhani umefika wakati wa kumuadhibu Festus ! akasema Bella na kuikunja sura yake




“Zandile anaishi kifahari jijini Pretoria lakini amekuwa akija Dar es salaam kila mwisho wa wiki na kufikia katika jumba kubwa la kifahari ambalo Festus amemnunulia kandoni mwa bahari.Huja ijumaa jioni na jumatatu asubuhi huondoka kurejea Afrika kusini.Festus amechanganyikiwa na penzi la Yule kahaba na ndiyo maana yuko tayari kutumia gharama kubwa kumsafirisha Zandile kila wiki kwa ndege tena daraja la kwanza”

“Dah ! akasema Kasiano

“Hilo ni moja ya jambo ambalo analificha sana lakini nina ushahidi wa kutosha ninazo picha zao wakiwa chumbani,ninayo hadi video zao wakifanya mambo yao ya hovyo ! akasema Bella na kuuma meno kwa hasira

“Mtu mzima kama Yule eti anaogeshwa kama mtoto mdogo ! stupid ! akasema Bella akionekana kukasirika.Kasiano na mke wake wakatazamana “Mama Bella umesema unazo picha zao wakiwa faragha? Akauliza Kasiano

“Hujanisikia Kasiano.Nimekwambia kwamba ninazo video na picha wakiwa faragha ! akasema Bella

“Good”

“Hiyo ni moja.Nataka niwape kombora la pili.Wakati akiwa wizara ya maji Festus aliwahi kuwa na mahusiano na katibu muhtasi wake na kuzaa naye mtoto mmoja halafu akamuachisha kazi kwa kuepuka aibu.Kwa sasa mtoto huyo amekwisha athirika na dawa za kulevya na anatunzwa katika nyumba moja ya kutunzia waathirika wa dawa za kulevya.Festus amelificha jambo hili lisijulikane akiogopa aibu.Haya ni makombora mawili ambayo tutaanza nayo na nina uhakika mkubwa kwamba Festus

hatakubali siri zake zijulikane na atakubali kufuata matakwa yetu”

“Mama Bella

umenisisimua sana kwa haya uliyotueleza.Kweli haya ni makombora mazito ambayo naamini tukiyatumia yatatupa ushindi” akasema Kasiano

“Nimewapa silaha hizo sasa siwezi kuwafundisha na namna ya kuzitumia.Nataka mzitumie vizuri na zilete manufaa.Pangeni mikakati yenu namna ya kuzitumia kisha mtanijulisha nione kama inafaa.Baadae jioni nitakutumia picha hizo na video chafu za Festus” akasema Bella

“Mama Bella

tunakushukuru sana kwa haya uliyotueleza sasa uhakika wa kumpata Mathew Mulumbi ni mkubwa.Ninakuahidi mama kwamba tutajipanga vyema mimi na timu yangu kuhakikisha kwamba tunakuja na mpango mzito ambao utatuwezesha kumpata Mathew Mulumbi bila kutumia nguvu kubwa” akasema Kasiano

“Mimi nimemaliza

ninawaachia ninyi mjipange na jioni ya leo mnijulishe namna mlivyojipanga.Nataka kusikia kishindo kikubwa.Nataka nchi itikisike kwa kashfa hizi mbili” akasema Bella na kunyanyuka,Kasiano na mke wake wakamsindikiza hadi katika gari lake akaondoka

“I made Festus president lakini baadae akajaa dharau na kuniona kama takataka.Aliwahi kusimama na kuniambia kwamba sijawahi kuwa na msaada wowote kwake.Pamoja na dharau hizo zote sikuwahi kufikiria kumfanya chochote lakini kwa hili lililotokea sina budi kumtumia kwa ajili ya kuhakikisha himaya yangu inakuwa salama.Najua mambo haya yakifika kwa wananchi itakuwa ni kashfa kubwa si kwa Festus peke yake bali hata familia nzima lakini ninachokiangalia ni maslahi mapana kwangu.Maneno ya watu yatakwisha lakini himaya angu itabaki salama” akawaza Bella akiwa garini

“Kweli haya ni makombora ya maangamizi.Kwa makombora haya lazima Festus apige magoti.Lazima tumpate Mathew Mulumbi na wale wote ambao wanakosa usingizi wanakesha wakitusaka” akasema Kasiano baada ya Bella kuondoka

“Nimeshangaa sana

kusikia eti Rais Festus ana mahusiano na Zandile Wepener.Mfalme wa Eswatini alimshindwa na sasa ameingia katika himaya ya Festus.Dah ! kweli hili ni kombora” akasema Rita na bila kupoteza muda Kasiano akawapigia simu washirika wake muhimu na kuwataka wakutane nyumbani kwake **************

Shughuli katika jengo la ghorofa saba la kampuni ya filamu ya African pictures ziliendelea kama kawaida.Katika ghorofa ya saba kulikuwa na ofisi za kundi la Black Mafia na hakuruhusiwa mtu yeyote asiyehusika kufika katika ghorofa hiyo.Paul Lewis kiongozi wa Black Mafia alikuwa katika ofisi yake akifuatilia namna shughuli zinavyokwenda.

Katika meza moja

iliyokuwa na luninga tatu ulisikika mlio katika moja ya luninga na jamaa aliyekuwa akifanya kazi katika meza ile akastuka na kuangalia sababu ya kutokea kwa mlio ule mara sura yake ikapatwa na mshangao halafu haraka haraka akaichukua simu na kumpigia Paul Lewis aliyekuwa ofisini kwake akamtaka aende katika meza yake.Haraka haraka Paul akashuka akaenda katika meza ya Yule jamaa aliyemuita. “Kuna nini Jeff? Akauliza

Paul

“Simu ya Jospeh imewashwa” akasema Jeff

“Waliichukua simu yake na kwenda kuichunguza.Hawa watu lazima kwa namna yoyote wana mahusiano na Mathew Muumbi.Unaweza ukafuatilia kujua mahala iliko hiyo simu ili tuwafuate? Akauliza paul na Jeff akaanza kucheza na kompyuta yake akafanikiwa kujua mahala ilipo ile simu ya Joseph.

“Good job Jeff” akasema Paul na kugeuka akaanza kupiga hatua Jeff akamuita

“Kuna mawasiliano

yanafanyika kupitia simu hii ya Joseph” akasema Jeff na kuanza kubonyeza tena kompyuta yake halafu akasema

“Kuna mwanamke

amemtumia Joseph ujumbe

kupitia laini yake ya siri na wale jamaa wanawasiliana naye.Mwanamke huyo anadhani anawasiliana na Joseph kumbe ni hao jamaa.Anaonekana hana habari kama Joseph

amekwisha fariki” akasema

Jeff

“Hawa jamaa wanakwenda kukutana na mwanamke huyo na lengo lao ni kumchunguza Joseph.Yawezekana mwanamke huyo kuna mambo anayafahamu kuhusu Joseph na anaweza akawaeleza hawa jamaa.Tunatakiwa kumuondoa mwanamke huyo haraka sana na kuwapata hao jamaa ambao naamini wanashirikiana na Mulumbi. Hii ni nafasi ya pekee kabisa ambayo hatuwezi kuichezea ! akasema Paul Lewis na kutaka watu wote waache kazi zao wamsikilize

“Mapema leo nilipokea taarifa kutoka kwa mkuu kwamba mwanamke mmoja mwandishi wa habari alimfuata ofisini kwake akamuhoji mambo kadhaa kuhusiana na mchungaji Adam Watwila na kama haitoshi mwanamke huyo akaenda katika shule alikosoma Naomi Bambi kwa ajili ya kutafuta taarifa zake.Nilipokea maelekezo kutoka kwa mkuu kwamba tumteke mwanamke huyo ili tumuhoji na tumfahamu ni nani ,nikatuma vijana wanne wakaenda kuungana na Josep aliyekuwa akimfuatilia huyo mwanamke lakini kwa namna ambayo mpaka sasa hatujafahamu watu wetu wote watano wamepoteza maisha.Ni moja ya tukio baya kabisa.Muda mfupi uliopita Jeff ameweza kugundua simu ya Joseph imewashwa na watu hao wanaitumia kuwasiliana na mwanamke mmoja ambaye tunaamini ana mahusiano na

Joseph na hivi tunavyozungumza tayari wamepanga wakutane Sangara plaza.Huyo mwanamke hana taarifa kama Jospeh ameuawa na anadhani anawasiliana naye kumbe ni watu wengine wanatumia simu yake.Hii ni nafasi kubwa ambayo hatupaswi kuipoteza kwani tuna uhakika mkubwa mwanamke huyo lazima anashirikiana na Mathew Mulumbi hivyo kuna mambo mawili ambayo tutayafanya.Kwanza ni kuhakikisha huyo mwanamke hakutani na hao jamaa wanaokwenda kukutana naye Sangara Plaza,pili tayari tunafahamu mahala aliko Yule mwandishi wa habari tunakwenda kuvamia mahala hapo na kumchukua na atatueleza mahala alipo

Mathew Mulumbi.Tutajipanga katika makundi mawili,kundi la kwanza wataelekea Sangara Plaza kuhakikisha mwanamke huyo hakutani na hao jamaa na kundi la pili watakwenda kuvamia mahala alipo mwandishi wa habari na kuondoka naye.Tunamuhitaji akiwa mzima yeye na wote watakaokutwa humo ndani ili watueleze alipo Mathew” akasema Paul kisha akawapanga watu wake katika timu mbili na baada ya maandalizi kukamilika wakashuka kwa kutumia lifti iliyo nyuma ya jengo lile ambayo ni maalum kwa ajili yao pekee wakatokea katika maegesho yao na kuinga katika magari wakaondoka.Paul alipohakikisha vijana wake wameondoka akarejea ofisini kwake akampigia simu nabii

Kasiano

“Unasemaje Paul?akauliza Kasiano

“Mkuu kuna taarifa nzuri.Tumefanikiwa kugundua mahala alipo Yule mwanamke mwandishi wa habari” “Kweli? Akauliza Kasiano

“Ndiyo mkuu” akajibu Paul

“Mmewezaje kuligundua hilo?

“Wale jamaa waliondoka na simu ya Joseph na kwa bahati nzuri wameiwasha na kuanza kutumia bila kufahamu kuwa imeunganishwa na mfumo wetu na kwa sasa tayari nimekwisha tuma vijana kwenda kuvamia mahala hapo na kumchukua huyo mwanamke na yeyote watakayemkuta”

“That’s good Paul.Nimefurahi sana.Mlifanikiwa kufuta kila kitu katika mawasiliano yote ya Joseph? Akauliza Kasiano “Tayari tumefuta kila kitu” “Good keep me posted ! akasema Kasiano

“Bado sijamaliza mkuu” akasema Paul

“Endelea” akasema Kasiano

“Kwa kutumia simu ya Joseph wamewasiliana na mwanamke ambaye tunaamini ana mahusiano na Josephn na wamepanga wakutane Sangara Plaza.Huyo mwanamke hana habari kama Joseph tayari amefariki dunia.Tayari nimetuma huko vijana wengine kuhakikisha huyo mwanamke haonani na hao jamaa”

“Very good Paul.Umefanya vizuri sana.wakumbushe vijana wako kwamba hii ni nafasi ya dhahabu hivyo tuitumie vyema.Nina uhakika mkubwa Yule mwanamke lazima ana mahusiano na Mathew Mulumbi.Paul nilimtuma John aende eneo la tukio afuatilie kujua watu wetu wameuawa vipi.Tayari amerejesha majibu?

“Hapana bado”

“Ok sawa.Shughulikia

suala hilo halafu utanijulisha kitakachoendelea.Paul msiwe na hofu muda si mrefu sana tutampata Mathew Mulumbi na maisha yatarejea kuwa ya kawaida” akasema Kasiano na kuagana na Paul





Mathew na Nelson

Lambada waliwasili katika jengo refu la kibiashara linalojulikana kama Sangara Plaza.Ni jengo lenye maduka mengi na ofisi mbali mbali hivyo muda mwingi huwa limefurika watu.

“Honey uko wapi mbona hufiki?” Mathew akamuandikia Monica ujumbe kisha akamtumia.Baada ya sekunde chache ukaingia ujumbe katika simu ile ya Joseph

“Nimekaribia kufika.Uko sehemu gani hapo Sangara?

“Ukifika nistue nitakulekeza” Mathew akajibu “K” akajibu Monica na Mathew akakunja uso

“Sipendi sana watu wenye majibu ya mkato namna hii.Ana maanisha nini akijibu K” akauliza Mathew

“Ana maanisha Okay ! akajibu Nelson

“Get ready Nelson,Monica anakaribia kufika.Akisha ingia tu garini nitamdhibiti na utaondoa gari haraka” akasema Mathew .

Baada ya dakika mbili ukaingia ujumbe katika simu ya Joseph

“Nimefika.Uko kwa wapi?

“Njoo hapa karibu na huu mwavuli wa kampuni ya simu kuna gari liko hapa rangi nyeusi mlango uko wazi ingia moja kwa moja”

“Kuna mtu niko naye siwezi kumuacha.Tuna haraka kidogo njoo mara moja huku nje mbele kidogo ya geti utamuona jamaa anayeuza madafu nimeegesha mbele yake” akajibu Monica “Change of plan.Monica anataka tumfuate” akasema Mathew na kumpa Nelson maelekezo,akawasha gari na kutoka wakafuata maelekezo ya Monica na kusimamisha gari mbele ya gari aina ya Rav 4 lenye rangi ya fedha.Kama walivyokuwa wamepanga,Nelson akafungua mlango akashuka na kuelekea katika gari alimo Monica akagonga kioo kikashushwa

“Hello Monica” akasema

Nelson huku akitabasamu “Hello.Wewe ni nani? Akauliza Monica

“Joseph anakuita katika lile gari pale mbele” akasema Nelson

Mara ghafla kikatokea kitu ambacho Mathew hakuwa amekitarajia,Nelson alianguka chini baada ya kupigwa risasi.Hakukuwa na mlio wowote wa risasi uliosikika hivyo risasi ilitoka katika bunduki au bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti.Monica akastuka sana baada ya kumuona Nelson ameanguka chini akaufungua mlango ili ashuke amsaidie lakini mara tu mlango ulipofunguliwa akapigwa risasi ya kichwa akaanguka kitini.Mwenzake aliyekuwa naye garini akachanganyikiwa na kabla hajafanya chochote naye pia akapigwa risasi

Kwa kasi Mathew akaufungua mlango akashuka huku akiwa na bastola mkononi akakimbilia katika gari la Monica na kukuta ubongo ukiwa umesambaa garini.

“Mathew get down ! Nelson akapiga ukelele na Mathew akajirusha pembeni huku vioo vya gari vikisambaratishwa na risasi.Nelson akaiokota bastola yake na kuachia risasi kadhaa kuelekea katika jengo la Sangara Plaza halafu Mathew akamfuata akamvuta na kumzungusha nyuma ya gari haraka haraka akamsaidia kuvua fulana ile ya kuzuia risasi. Pamoja na kusaidiwa na

fulana lakini alipata jeraha mgongoni

“Mathew I saw a Sniper !

akasema Nelson

“Hatuna muda wa

kumfuatilia tayari wanafahamu tuko hapa.We need to get out of here now ! akasema Mathew na kumsaidia Nelson kuinuka wakaelekea katika gari lao na kuondoka

“Damn these people ! akasema Mathew kwa hasira.


“Kama isingekuwa fulana hivi sasa tayari ningekwisha kufa.Wamejuaje kama tunakuja hapa hadi wakajiandaa na kumuweka mdunguaji? Akauliza Nelson na mara Mathew akakumbuka kitu.

“Ni kwa sababu ya hii simu.Hii ni simu ya mwenzao hivyo wanafuatilia mawasiliano yote na ndiyo maana ikawa rahisi kwao kumgundua Monica na kumuua” akasema Mathew na kufungua kioo cha dirisha akairusha ile simu barabarani.Akajipapasa sikioni hakuwa na kile kifaa cha mawasiliano kinachowawezesha uwasiliana na akina Ruby

“Damn ! akasema kwa hasira huku akiupiga usukani.


*************

Muda mfupi baada ya Mathew naNelson kuondoka kuelekea Sangara Plaza kuonana na Monica,simu ya Ruby aliyokuwa ameizima ikawaka,akastuka

“Nilikuwa nimeizima hii simu,mbona imewaka? Akaujiuliza Ruby na mara ukaingia ujumbe haraka haraka akaufungua na kuusoma

“They’re coming for you,Run !

“Kuna nini Ruby mbona

sura imebadilika ghafla? Zari akauliza

“It’s Zero again”akajibu

Ruby

“Zero? Anataka nini? Akauliza Zari na Ruby akamuonyesha ule ujumbe

“Ana maanisha nini kwa ujumbe huu? Zari akauliza “Tayari wanafahamu tuko hapa and they’re coming” akasema Ruby

“Oh my God ! Wamefahamuje kama tuko hapa? Zari akauliza

“Yawezekana walikuwa

wanaifuatilia simu ya Joseph na wakagundua tulikuwa tunaitumia hapa” akasema Ruby

“Do you trust that Zero? Akauliza Zari

“Simfahamu ni nani huyu mtu na ninashindwa nimuamini au vipi” akasema Ruby na kutazama juu akitafakari halafu akasema

“Nahitaji kujua kama huyu mtu ni mkweli au ni mtu ambaye anatumiwa ili kunivuruga.Hatukimbii tutajificha mahala na tutawaachia makomando kazi

ya kukabiliana na hao watakaokuwa wametumwa kwangu.Huu si muda wa kuogopa tena”akasema Ruby “Ruby are you sure?

“Hawajui kama wanakuja

katika shimo la moto.Let’s surprise them ! akasema Ruby kisha wakaitwa makomando waliokuwa wanapumzika pale nyumbani na Ruby akatoa maelekezo ya kitu wanachotakiwa kukifanya na maandalizi yakaanza haraka.

“Natakiwa kumjulisha Mathew ili wachukue tahadhari huko waliko. Kama hawa jamaa wameweza kufuatilia na kujua mahala tulipo basi lazima watakuwa wanafahamu pia kwamba akina Mathew wanakwenda kuonana na Monica” akasema Ruby na kujaribu kuwatafuta akina Mathew kupitia vifaa vyao vya mawasiliano lakini hawakuwa wakipatikana

“Siwapati akina Mathew,what’s wrong? Akauliza Ruby

“Jaribu kupiga katika ile simu waliyoondoka nayo” akasema Zari na Ruby akajaribu kupiga simu ile ya Joseph lakini haikuwa ikipatikana

“Haipatikani pia.Kuna kitu hakiko sawa” akasema Ruby “Don’t worry.Mathew’ll be fine ! akasema Zari

“Kwa nini unasema hivyo?Ni vipi kama kuna jambo litakuwa limewatokea baya?

“He knows how to take care of himself.Nimekuwa naye kwa muda mfupi tu na nimegundua Yule mtu ni wa ajabu sana.Anaweza akafanya mambo anbayo wengi hatuwezi na kubwa zaidi haogopi kufa ! akasema Zari

Walipakia vitu muhimu katika gari wakaondoka eneo lile na kwenda kujificha si mbali sana na pale nyumbani wakiwaacha makomando wakiwa wamejificha mle ndani wakiwasubiri jamaa watakaokuja


*************

Katika mojawapo ya chumba ndani ya jengo la Sangara Plaza jamaa mmoja alimalizia kuifungua bunduki yake kubwa na kuipanga vizuri katika sanduku huku mwingine akiiweka kompyuta yake katika mkoba halafu wakatoka ndani ya kile chumba na kuanza kushuka

taratibu bila mtu yeyote kufahamu kama wanahusika na mauaji yale ya wanawake wawili yaliyotokea muda mfupi uliopita .Tayari polisi walikwisha fika eneo lile na kuzungusha utepe wa njano mahala walikouawa Monica na mwenzake.Wale jamaa wakaelekea barabarani wakatembea kama hatua kumi

hivi likatokea gari moja na kusimama mbele yao wakapanda na kuondoka ************

Mathew na Nelson

walirejea katika makazi ya Zari na geti likafunguliwa wakaingia ndani.Wakashuka garini na Mathew akastuka kidogo baada ya kutoliona gari la Zari.Akatoa bastola yake kisha wakatembea kwa tahadhari kuelekea ndani.Akausukuma mlango wa

sebuleni na kukuta kumevurugwa sana

“Nini kimetokea humu? Akauliza Nelson

“Ruby ? akaita Mathew lakini kukawa na ukimya mkubwa.

“Nelson something is wrong here ! akasema Mathew na kutembea kwa tahadhari kuelekea katika chumba cha kulala na mara akasikia kama mlango ukifunguliwa

“Please don’t shoot it’s me Kendrick ! ikasema sauti ambayo mara moja Nelson akaitambua

“Mtu wetu” akasema

Nelson na Mathew akashusha mkono wake uliokuwa na bastola na mara akajitokeza Kendrick

“Nini kimetokea hapa?Wengine wote wako wapi? Akauliza Mathew

“Wameondoka na

kuniacha hapa niwasubiri kwani mawasiliano nanyi yalikatika”

“Nini kimetokea hapa? Akauliza Mathew na Kendrik akamsimulia kile kilichokuwa kimetokea

“Wameelekea wapi akina Zari kwa sasa?

“Kuna shamba letu huwa tunalitumia kwa mazoezi huko ndiko wameelekea.Nitawapeleka” akasema Kendrick kisha wakafunga nyumba na kuingia garini wakaondoka

“Una hakika watu wote wako salama? Mathew akauliza

“Wote wako salama.Wakati mapambano yanatokea Zari na Ruby hawakuwepo.Baada ya kuimaliza kazi ndipo tukawasiliana wakafika na kuondoka na wale jamaa tuliowakamata na maiti moja ya Yule jamaa aliyeuawa baada ya kukataa kutii amri” akasema Kendrick

“Jamaa wanaonekana wamewekeza pia katika teknolojia ndiyo maana wameweza kugundua kama tunakwenda kuonana na Monica na vile vile wakagundua makazi yetu.Mapambano na watuwa namna hii ni magumu” akawaza Mathew **************





Katika ofisi za black Mafia kulikuwa na sintofahamu kubwa baada ya mawasiliano


kati ya ofisi hiyo na watu waliotumwa kuvamia nyumba ya mwanamke mwandishi wa habai kukatika ghafla.


“Jeff nini kimetokea?


Akauliza Paul


“Tulikuwa tunawasiliana nao hadi walipofika eneo la tukio na kufanikiwa kuingia ndani ya hiyo nyumba lakini ghafla mawasiliano yalikatika na mpaka sasa hatujafanikiwa kuwapata”


“Endeleeni kuwatafuta


tafadhali.Sitaki kusikia tumewapoteza watu wengine.Tumia kila njia kuhakikisha umewapata watu hao ! akaelekeza Paul na kuelekea ofisini kwake alihisi kuchanganyikiwa akazivuruga rasta zake na kuegemea kitini


“Nini kimewapata watu wangu? Ni wazima au tayari wamepoteza maisha? Akajiuliza


“Sitaki tena kuwapoteza watu wengine.Kasiano hatanielewa” akawaza na mara simu yake ikaita akastuka sana baada ya kutazama mpigaji alikuwa ni nabii Kasiano


“Ninamuwaza halafu naye anapiga simu” akawaza Paul na kuipokea


“Paul nataka taarifa misheni imefikia wapi?


“Misheni imekwenda vizuri mkuu.Tumefanikiwa kumuondoa Yule mwanamke kabla hajakutana na wale jamaa”


“Jamaa? Kasiano akauliza


“Ndiyo mkuu.Watu


waliomfuata Monica pale Sangara Plaza walikuwa ni wanaume wawili hakukuwa na mwanamke” “Are you sure?


“Ndiyo mkuu”


“Mlifanikiwa kuwaondoa na hao jamaa pia?


“Hapana ilishindikana ila mmoja wao alijeruhiwa”


“Kwa nini mkawaacha


Paul? Akauliza kwa ukali Kasiano


“Ni kutokana na mazingira ya eneo lenyewe kuwa na msongamano mkubwa wa watu”


“Paul umeharibu kila kitu.Hujui kama wale jamaa mliowaacha watapeleka taarifa kwa wenzao kwamba wameshambuliwa?


“Wakati haya yanatokea pale Sangara Plaza tayari timu yetu nyingine ilikuwa imefika katika ile nyumba aliko Yule mwandishi wa habari”


“Wamefanikiwa kumpata?


“Mawasiliano yamekatika lakini tunajitahidi kuwatafuta ili kujua kama wamefanikiwa kumpata yule mwanamke na wenzake !


“Paul una hakika watu wetu bado wako hai?


“Nina uhakika mkuu.Nilituma watu wenye utaalamu


mkubwa.Nitakujulisha pale tutakapokuwa tumepata mrejesho kutoka kwao”


“Umepata mrejesho kutoka kwa John ni namna gani vijana wetu waliuawa pale shuleni? Akauliza Kasiano


“Mpaka sasa sijapata mrejesho wowoe kutoka kwake”


“Paul nataka watu uliowatuma kumfuata Yule mwandishi watafutwe na wapatikane.Sitaki kusikia tumepoteza tena watu wengine” akasema Kasiano “Nitakujulisha mkuu” akasema Paul na Kasiano akakata simu


Baada ya kuzungumza na


Kasiano,Paul akampigia simu John ili kupata mrejesho


“Paul nimetoka eneo la tukio pale shuleni walikouawa wenzetu nimejaribu kuzungumza na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanadai kwamba wakati majambazi yaani watu wetu wakifyatua risasi huku


wakielekea getini, lilitokea gari ambalo walishuka watu wenye bunduki nzito na kuanza kuwashambulia majambazi hao na kuwaua halafu gari mbili zikaondoka kwa haraka.Hii inaonyesha kwamba watu tuliokuwa tunawafuatilia alikuwa na ulinzi wa ziada.Kuna watu walikuwa nyuma yao na pale watu wetu walipovamia basi walinzi wao wakajitokeza bila watu wetu kujua na ndiyo sababu wote wakapoteza maisha.Paul kwa picha ninayoipata haraka haraka ni kwamba hawa jamaa lazima wana mahusiano na Mathew Mulumbi na vile vile ni watu hatari na waliojiandaa kikamilifu.Tunapowatuma watu wetu kuwafuatilia lazima tuwe tumewaanda kikamilifu na tuhakikishe wana ulinzi wa ziada vinginevyo tutaendelea kuwapoteza watu wetu kila wakati”


“Ahsante sana John kwa


taarifa hiyo itatusaidia sana.Tafadhali rejea ofisini kuna mambo mengi ya kufanya huku” akasema Paul


na kukata simu


“Picha ninayoanza kuipata hapa ni kwamba tunakabiliana na Mathew Mulumbi ambaye hayuko peke yake.Anashirikiana na watu wenye uwezo mkubwa pengine kuliko sisi.Tuna watu wenye uwezo mkubwa pia lakini inaonekana hawa wenzetu wametuzidi mbinu na maarifa.Ili kukabiliana nao itatulazimu kuruka hatua nne mbele yao” akawaza Paul na kuwasha sigara


“Kwa maelezo haya ya John nina wasiwasi kama watu wetu tuliowatuma kuvamia ile nyumba tunayoamini yuko yule mwandishi bado wako hai” akawaza Paul




*************


Akina Mathew waliwasili katika shamba linalomilikiwa na SNSA ambako makomando


hulitumia kwa ajili ya mazoezi.Ni shamba lililozungushiwa uzio mkubwa na ndani yake kulikuwa na msitu wa kupandwa pamoja na mazingira mbali mbali kwa ajili ya kuwawezesha makomando kufanya mazoezi. “Karibu Mathew Mulumbi huku ndiko mahala tunakofanyia mazoezi yetu” akasema Kendrick


“Sijawahi kufika mahala hapa” akasema Mathew na geti likafunguka wakaingia ndani


“Gari zetu zote zina sensa maalum ambayo inaonwa na


kifaa kilicho katika geti na kisha geti hujifungua” akasema Kendrick baada ya kuingia ndani huku wakipita kati kati ya miti iliyobanana wakatokea katika nyumba ndogo milango ikafunguka gari likaingia ndani.Baada ya sekunde chache gari lile likaanza kushuka chini na kukuta sehemu kubwa ya maegesho na magari mawili yakiwa yameegeshwa na lango likajifunga


“Nimeipenda sana


teknolojia ya mahala hapa” akasema Mathew


“Karibu Mathew


Mulumbi” akasema Kendrick na kumuongoza Mathew kuelekea katika vyumba.Ilikuwa ni sehemu ya kupendeza sana.


Waliingia katika chumba kikubwa kilichokuwa na luninga moja kubwa na kompyuta kadhaa.Ruby na Zari walikuwamo ndani ya chumba kile wakibadilishana mawazo.Mara tu Mathew alipoingia Ruby akamfuata akamkumbatia.


“Ahsante Mungu


amekurejesha salama” akasema Ruby


“Mko salama wote? Poleni


na misuko suko mliyoipata.Kendrick amenieleza kila kitu” “Haikuwa kazi kubwa sana kwani makomando waliweza kuwadhibiti wale jamaa mara tu walipoingia ndani.Tuliwawekea mtego bila wao kufahamu” akasema Ruby


“Mlifahamuje kama wanakuja kuwavamia? Akauliza Mathew


“Zero”


“Zero? Akauliza Mathew


“Ndiyo alinitumia ujumbe na kunijulisha nikimbie wananifuata.Huyu Zero amekuwa akinitumia ujumbe bila ya mimi kumfahamu hivyo nilitaka niyathibitishe maneno yake kama ni ya kweli ndiyo maana tukaweka ule mtego kumbe ni kweli kuna watu waliokuwa wananifuata.Nawashukuru Makomando waliumaliza mchezo na ndipo tulipoamua kuhamisha makazi na kuja hapa kwani wale jamaa tayari walikwisha fahamu makazi yetu na wangeweza kurejea tena”


“Mlifanya vizuri sana Ruby.Kwa hiyo kwa sasa tuna uhakika kwamba huo mtu uliyempa jina la Zero yuko ndani ya mtandao wa hao jamaa anaifahamu mipango yao yote.Swali linalokuja ni nani huyo mtu na kwa nini anakutahadharisha kila pale unapokuwa katika hatari?


“Naamini utafika wakati tutamfahamu ni nani.Vipi huko mlikoenda nini kimetokea?Mawasiliano yalikatika na tulipatwa na wasi wasi mkubwa.Monica mlifanikiwa kuonana naye? Akauliza Zari Mathew akawaeleza kila kitu kilichotokea


“Hawa jamaa


wanaonekana nao wako vizuri katika teknolojia ndiyo maana wameifuatilia simu ya mwenzao na kujua mahala ilipo.Watu wenye kutumia teknolojia kama hawa mara nyingi huwa ni watu hatari sana na waliojipanga vyema hivyo kamwe tusitegemee urahisi wakati tukiwasaka.Wako wapi hao jamaa mliowateka?


“Mmoja amefariki dunia wawili tumewahifadhi katika vyumba” akasema Zari “Good.Hawa watatusaidia sana kuufahamu mtandao wao.Mmewachunguza na kuhakikisha hawana vifaa vya kuwawezesha wenzao kuwafuatilia na kujua mahala walipo?


“Tumewakagua hawana


kifaa chochote”


“Good.Nataka waandaliwe


kwa ajili ya mahojiano.Naomba nitoe tahadhari kwamba hawa jamaa hawatafunguka kirahisi na nitalazimika kutumika nguvu hivyo basi nawaomba muwe wavumilivu” akasema Mathew


“Usijali Mathew ! akasema Zari halafu Mathew akawafuata makomando waliokuwa nje wakipumzika akawauliza kama wana vifaa vyovyote vya kutesea lakini hakukuwa na vifaa vyovote mahala pale kwa ajili ya kutesea watu kwani mahala pale ni maalum kwa mazoezi.Mathew akawataka akina Zari wamuonyeshe kilipo chumba walimowekwa wale jamaa.


Watu wawili walikuwa wamefungiwa katika chumba kinachotumika kama stoo ,Mathew akaagiza mmoja wao atolewe abaki mmoja.Ikaletwa meza na viti viwili Yule jamaa


akakalishwa kitini na bila kupoteza muda Mathew naye akaketi halafu mahojiano yakaanza


“Jina lako nani? Mathew akauliza Yule jamaa akabaki kimya


“Nakuuliza jina lako nani? Huna jina? Akauliza Mathew bado Yule jamaa alikuwa kimya.Mathew akavua ndevu na nywele bandia alivyokuwa amevaa na sura yake halisi ikaonekana


“Umeitambua hii sura?


Akauliza Mathew lakini bado Yule jamaa aliendelea kuwa kimya


“Naitwa Mathew


Mulumbi” akasema Mathew na sura ya Yule jamaa ikaonyesha mstuko


“Umestuka kuniona? Mimi ndiye Yule ambaye mmekuwa mkinisaka usiku na mchana.Mimi ndiye Yule mliyeniwekea mtego na nikakamatwa na dawa za kulevya” akasema Mathew na usoni kwa Yule jamaa kukaonekana matone ya jasho


“Naamini tayari mmekwisha elezwa na viongozi wenu kuhusu mimi ni nani.Naomba nikuweke wazi angali mapema kwamba mimi ni mtu mbaya sana hasa ninapokutana na watu kama wewe hivyo nakutahadharisha uwe makini unapohojiwa na mimi.Salama yako ni kunijibu kwa ufasaha kile nitakachokuuliza.Endapo utajifanya bubu na kushindwa kunipa majibu kwa yale nitakayokuuliza nakuhakikishia kwamba utajiweka katika wakati mgumu sana na ninao uwezo wa kukuharibu vibaya.Umenisikia? akauliza Mathew na kumtazama Yule jamaa


“Jina lako nani? Akauliza tena lakini Yule jamaa bado aliendelea kuwa kimya


“Narudia tena jina lako nani? Akauliza Mathew jamaa akaendelea kuwa kimya “Sipendi kuuliza mtu halafu akajifanya bubu ! akasema Mathew na kusimama


“Jina lako nani? Akauliza akiwa amekunja sura.Jamaa akamtazama hakuonyesha


dalili za kujibu.Kwa kasi ya aina yake Mathew akakigongesha kichwa chake mara mbili katika meza na Yule jamaa akaanza kutoka damu katika paji la uso.


“Ninapokuuliza sitaki ukae kimya kama bubu nitakuharibu vibaya


sana.Mimi nina roho mbaya kwa watu kama ninyi zaidi ya shetani hivyo kwa makini ! akasema kwa hasira Mathew huku akigonga meza.Yule jamaa akatema mate yenye damu pembeni halafu akasema


“You are just a bit*h ! akasema Yule jamaa kwa kiingereza


“Unasemaje? Akauliza Mathew kwa hasira


“You think I’m scared of you? Akauliza Yule jamaa ambaye alionekana kupandwa na hasira


“I’m not scared of you motherf** ker ! Just do what you gonna do ! akasema kwa ukali Yule jamaa


Mathew akamtazama


halafu akatoka


“Mbona mapema


sana?Tayari amefunguka? Akauliza Ruby


“Hapana bado.Yule jamaa anaongea kiingereza chenye lafudhi ya Marekani.Ninahisi si mtanzania.Tunatakiwa kumchunguza tufahamu kama ni mtanzania au ni raia wa Marekani.Nahitaji kupata alama za vidole za huyu jamaa ili tuweze kumchunguza tumfahamu vyema” akasema Mathew


“Simu yangu ina scanner tuitumie kupata alama za vidole halafu tutatumia mfumo wa SNSA kumchunguza na


kumfahamu ni nani” akasema Zari


“Good.Twende ndani” akasema Mathew na kuongozana na Zari hadi katika kile chumba alimo Yule jamaa akamkata pingu za plastiki alizokuwa amefungwa halafu akakishika kiganja cha mkono na kutaka kukiweka kidole gumba katika simu ya Zari kwa ajili ya kupata alama ya kidole gumba lakini ghafla Yule jamaa akaurusha mkono na kumtandika Zari ngumi iliyompeleka ukutani,Mathew akamuwahi na kumtandika vichwa viwili mfululizo jamaa akaanguka chini na kupoteza fahamu.Mathew akaichukua simu akakiweka kidole gumba cha Yule jamaa na kuchukua alama halafu akamfunga tena na pingu za plastiki.


“Pole Zari hajakuumiza huyu jamaa?


“Ana mkono mgumu sana shetani huyu.Ngoja niweke barafu” akasema Zari wakatoka ndani ya kile chumba na kumuacha Yule jamaa hana fahamu.Mathew akampa Ruby simu ili aweze kumchunguza Yule jamaa. Wakati Ruby akiendelea Mathew akamfuata jamaa aliyekuwa amewekwa katika chumba kingine.Hakukuwa na meza ndani ya chumba kile na Yule jamaa alikuwa amekaa sakafuni.Mathew akamsogelea akachuchumaa karibu yake


“Naamini tayari umekwisha ifahamu sura hii.Mimi ndiye Yule Mathew Mulumbi ambaye mmekuwa mkimsaka usiku na mchana.Nitakuuliza maswali kadhaa nataka unijibu kwa usahihi kabisa vinginevyo utakuwa umejiweka katika wakati mgumu sana.Umenielewa? akauliza Mathew


“Jina lako nani? Akauliza


Mathew


“I don’t have a name ! akasema Yule jamaa


“Tafadhali sitaki unifanyie mzaha.Jina lako nani? Akauliza Mathew


“I’ve told you I don’t have a name! don’t you understand? Akasema Yule jamaa kwa ukali.Mathew akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema


“Nawapenda sana watu


kama ninyi” akasema na bila kutarajia Yule jamaa ambaye mikono yake ilikuwa imefungwa kwa nyuma akajikuta ameinuliwa akakabwa kabali na Mathew akaweka kisu chini ya jicho


“Kwa mara ya mwisho


ninakuuliza jina lako nani? Jibu haraka kabla sijakuondoa macho yako ! akasema Mathew huku Yule jamaa akifurukuta kujinasua katika kabali ile.


“Nilikwambia sitaki mchezo na ninyi ! akasema Mathew na kisu kile kikali kikaanza kukata ngozi ya Yule jamaa akahisi maumivu


“Hey stop ! stop ! akapiga ukelele Yule jamaa.Mathew akamsukuma akaanguka chini.Akamtazama kwa macho makali halafu akamfuata pale chini


“JIna lako nani? Hujui


Kiswahili? Akauliza Mathew.Mara Yule jamaa akamtemea Mathew mate usoni


“Vete al infierno hijo de puta ! akasema Yule jamaa kwa lugha ya kihispaniola.Kitendo kile kilimuudhi Mathew na kuanza kumvurumishia makonde mazito .Ndani ya sekunde chache uso wa Yule jamaa haukuwa ukitazamika ulikuwa umechafuka damu.




“Nilikuonya tangu awali kwamba sihitaji mchezo” akasema Mathew na kusimamisha zoezi baada ya mlango kugongwa


“It’s not over I’ll be back ! akasema Mathew na kwenda kuufungua mlango akakutanana Zari ambaye alistuka baada ya kumuona amechafuka damu


“Hawa jamaa si wa kuwahoji huku unatabasamu.Inahitajika kazi ya ziada.Unasemaje Zari? Akauliza Mathew


“Tunakuhitaji kuna jambo tujadiliane” akasema Zari na Mathew akatoka ndani ya kile chumba akimuacha Yule jamaa akigugumia kwa maumivu makali


“Kuna nini Ruby? Akauliza Mathew


“Huyu jamaa hakuna


taarifa zake zozote hapa nchini.Nimetumia mfumo wa SNSA lakini tumeshindwa kuzipata alama za huyu jamaa” akasema Ruby


“Kama kawaida ya huu mtandao,hawataki watu wao wajulikane ndiyo maana inakuwa vigumu kupata taarifa zao.Hata hivyo hawa jamaa wawili wanaonekana si watanzania.Mmoja anazugumza kiingereza chenye lafudhi ya Marekani na mwingine anazungumza kihispaniola.Tunahitaji kupata msaada kutoka Marekani ili kuwatambua hawa jamaa.Kama tungeweza kumpata Nawal angetusaidia sana kwani ana watu wake ndani ya CIA” akasema Mathew


“Nina mtu ndani ya FBI anayeweza kunisaidia kuwatambua hawa jamaa ni akina nani” akasema Zari


“That’s good.Wasiliana naye mara moja ili tuweze kupata taarifa za hawa jamaa.Itakuwa vyema kama tukipata na alama za vidole za Yule jamaa mwingine” akasema Mathew akaichukua ile simu ya Zari akarejea katika chumba alimo Yule jamaa mwingine akamkata pingu za mikono na kuweka kidole gumba katika simu akachukua alama halafu akamfunga tena pingu.


Zari aliwasiliana na rafiki yake anayefanya kazi shirika la


ujasusi la shirikisho la Marekani (FBI) wakazungumza halafu akamtumia alama za vidole za


wale watu wawili ili amsaidie kuwachunguza na kuwafahamu watu wale ni akina nani.


“Nina uhakika mkubwa


hawa jamaa si watanzania hasa


kutoka na lafudhi zao” akasema Mathew


“Hapa Tanzania wamekuja kutafuta nini?


“Hilo ndilo tunalotaka kulifahamu ngoja tupate majibu kutoka Marekani tuwajue watu hawa ni akina nani” akasema Mathew


Zilipita dakika chache simu ya Zari ikapigwa alikuwa


ni rafiki yake kutoka FBI akamjulisha kwamba amemtumia taarifa katika barua pepe yake.Zari akamshukuru na kwa haraka akafungua barua pepe yake akakuta kuna ujumbe umetumwa.Kulikuwa na taarifa mbili tofauti.Wa kwanza aliitwa Thomas Calabrese.Ni raia wa Marekani ana umri wa miaka


31.Amewahi kufanya kazi idara ya secret service kabla ya kufungwa gerezani kwa kujihusisha na magenge ya biashara ya dawa za kulevya.Ni mtu anayetajwa kuwa hatari kwa jamii kutokana na uwezo mkubwa wa kutumia silaha alionao.Mtu wa pili anajulikana kama Alvaro Perez raia wa Colombia ambaye aliwahi kufungwa nchini marekani kwa kujihusisha na magenge ya wahalifu wa dawa za kulevya .Baada ya kuzipitia


taarifa zile wakabaki wanatazamana halafu Mathew akasema


“Kama taarifa inavyojieleza hawa watu wawili si raia wa Tanzania.Wote wawili wana sifa zinzaofanana kwamba wamewahi kufungwa kutokana na kujihusisha na magenge ya biashara ya dawa za kulevya.Wote wawili wanatajwa kuwa na uwezo wa kutumia silaha na huyu Thomas amewahi kufanya kazi idara ya secret service ambao ni watu wanaolinda viongozi


na familia zao hivyo ni mtu mwenye mafunzo makubwa.Picha ambayo ninaanza kuipata kutokana na


taarifa hii tuliyoipata ni kwamba hawa jamaa yawezekana wamekodishwa kuja hapa nchini kwa shughuli maalum.Tunachotakiwa kufahamu kwa sasa hawa jamaa wamekuja kufanya nini hapa nchini na vile vile tujue wameingiaje,nani kawaleta


,wanaishi wapi


n.k.Nitakwenda tena kuwahoji kupata taarifa zaidi na wakati huo Ruby endelea kuchimba zaidi katika taarifa zote za viwanja vya ndege tufahamu wako hapa nchini kwa muda gani na kwa shughuli gani” akasema Mathew na kurejea katika chumba alimo Thomas Calabrese ambaye tayari alikwisha rejewa na fahamu.Mathew akampiga piga shavuni akamuinua akamkalisha kitini “Tunaendelea pale tulipoishia” akasema Mathew na kumtazama


“Thomas Calabrese ndilo jina lako” akasema Mathew na Yule jamaa akaonekana kustuka akainua kichwa na kumtazama Mathew


“Wewe ni raia wa


Marekani na umewahi kufanya kazi idara ya sercret service kabla ya kufungwa kwa kushirikiana na magenge ya dawa za kulevya” akasema Mathew na kunyamaza tena “Ninataka kujua hapa nchini unafanya nini? Akauliza lakini Thoma akainamisha kichwa


“Thomas labda nikuweke wazi kwamba hakuna mtu anayefahamu uko hapa na hata wenzako hawataweza kuja kukuokoa hivyo nakushauri chukua hatua za kujiokoa wewe mwenyewe.Bila kufanya hivyo mambo yatakuwa mabaya sana kwa upande wako na ninakuhakikishia endapo utaendelea kuwa


kiburi hautaliona tena jua.Utawekwa mahala ambako utakufa taratibu na kwa mateso makali” akasema Mathew


“Fu** you ! akasema Thomas


“Thomas najitahidi


kukueleza kwa upole zaidi ili uweze kufahamu hali halisi inayokukabili.Hautakabidhiwa katika mikono ya vyombo vya usalama ambako watu wako wanaweza wakafanya namna ukatoka na ukaendelea na mambo yako.Sisi tunakumaliza taratibu,wenzako,ndugu zako,familia yako hakuna atakayefahamu mahala ulipo,hakuna atakayeiona maiti yako.Tutakuingiza katika pipa lenye asidi kali na utayeyuka kiungo kimoja kimoja,utakufa kifo cha kinyama sana.Sitaki tufike huko.Nieleze unafanya shughuli gani hapa Tanzania? Akasema Mathew


“I’m not scared of dying.You can kill me now


mothe**f***er ! akasema


Thomas


“Thomas ninataka kukusaidia.Ni vipi kama mimi na wewe tutaingia makubaliano? Nieleze kile ninachokitaka na mimi nitakusaidia uweze kuondoka hapa nchini kwenda sehemu yoyote ile unayoitaka” akasema Mathew


“I’m not gonna cut any deal with you.I want to die.You hear me you mothe*f***er ? Kill me now ! akasema kwa ukali Thomas


“Thomas umeipata nafasi kama hii umeichezea nakuonea huruma


sana.Utaijutia nafasi hii” akasema Mathew na kutoka mle ndani akarejea ofisini ambako Ruby na Zari walikuwa wanaendelea na kutafuta taarifa za wale jamaa


“Hakuna taarifa zozote katika viwanja vya ndege kuonyesha hawa jamaa waliingia lini hapa nchini”akasema Ruby


“Keep digging.Thomas amekuwa mgumu kufunguka, ninamfuata Alvaro” akasema Mathew na kuelekea katika chumba alimo Alvaro Perez aliyekuwa amelala kiubavu.Mathew akamshika shati na kumuinua


“Alvaro Perez ndilo jina lako? Akauliza Mathew na Yule jamaa akababaika kujibu


“Nakuuliza Alvaro Perez ndilo jina lako? akauliza na Alvaro akatingisha kichwa kukataa kwamba lile si jina lake.


“Wewe ni raia wa Colombia umewahi kufungwa nchini Marekani kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya” akasema Mathew na Alvaro akatikisa kichwa kukataa


“Alvaro nilikueleza asubuhi kwamba mimi ni mtu mbaya sana hasa kwa watu kama ninyi.Kwa kuwa unataka nitumie nguvu nitafanya hivyo” akasema Mathew na kutoka akamfuata Nelson akamtaka akamuonyeshe sehemu wanakofanyia mazoezi.Akampa maelekezo Fulani halafu akaenda kumchukua Alvaro na kumpeleka mahala kulikokuwa na chuma mithili ya kile kinachofungwa bembea.Alvaro akafungwa mikono na kuning’inizwa juu ya kile chuma halafu zikawekwa kuni chini yake


“Alvaro nitawasha moto ambao utakuunguza taratibu kuanzia miguuni na utapata maumivu makali sana lakini pale utakapoamua kunieleza ukweli ndiyo itakuwa salama yako.Ninakupa sekunde kumi za kuamua kunieleza ukweli na kama ukiendelea kuwa kiburi nitawasha moto” akasema Mathew na kumtaka Nelson ahesabu sekunde kumi zilipokamilika akawasha kiberiti


“Sekunde kumi tayari kazi inaanza” akasema Mathew na kuwasha moto ambao ulianza kuwaka taratibu na baada ya muda ukashika kasi na Alvaro akaanza kuhisi maumivu katika miguu yake.Moto ukawa mkubwa na kuanza kuifikia miguu ya Alvaro ambaye awali alivumilia lakini maumvu yalipokuwa makali zaidi akapiga ukelele akiwataka wamtoe katika kile chuma atasema ukweli.Moto ukamwagiwa maji halafu Alvaro akashushwa chini.Miguu yake tayari ilianza kubabuka na alikuwa analia kama mtoto mdogo.Mathew akachukua dawa Fulani na kumpaka miguuni mahala alikoungua na akahisi ganzi katika miguu yale maumivu yakatoweka.


“Haya nieleze ukweli ama


zoezi litaanza upya na safari hii


nakuhakikishia kwamba sintakusikiliza hata ulie machozi ya damu ! akasema


Mathew


“Alvaro Perez ni jina langu


! Mimi ni raia wa


Colombia”akasema Alvaro huku akitetemeka.


“Umekuja kufanya hapa Tanzania? Akauliza Mathew


“Baadaya kutoka gerezani nilijiunga na Black Mafia nikaletwa huku Tanzania” akasema Alvaro


“Black Mafia ni nini? Akauliza Mathew


“Tafadhali naomba mnifungue mikono yangu ninaumia.Nitawaeleza kila kitu” akasema Alvaro.Mathew akamuelekeza Nelson kukata kamba za mikono alizokuwa amefungwa Alvaro na mara akafanya kitu ambacho Mathew hakuwa amekitegemea.Mara tu Nelson alipomaliza kukata kamba zile kwa kasi ya ajabu Alvaro akamchoma Nelson kidole jichoni na Nelson akaachia kile kisu alichokuwa amekitumia kukatia kamba Alvaro akakikadaka na kwa haraka akakipitisha shingoni akajikata.Kitendo hicho kilifanyika kwa haraka sana kwa kasi ya kufumba na kufumbua.


“Oh noooo ! akapiga ukelele Mathew baada ya kuona damu zikianza kumwagika


“You cant die Alvaro ! akasema Mathew lakini alikwisha chelewa kwani tayari sekunde chache baadae akafariki dunia


“I can’t believe this !


akasema Mathew na kumfuata Nelson aliyekuwa amepiga magoti huku mkono mmoja


ukiwa jichoni


“Nelson nini kimetokea? Akauliza Mathew


“Mwanaharamu Yule


amenitoboa jicho kwa kidole ! akasema Nelson


“Lengo lake lilikuwa kukipata kisu ambacho amekitumia kujiua”


“Amekufa? Akauliza Nelson


“Ndiyo amejiua”


“Oh no ! akasema Nelson


“It’s okay”


“Mathew I’m


sorry.Sikutegemea kama yangetokea haya ! Kitendo kile kilitokea ghafla mno !akasema Nelson


“Usijali Nelson.Hawa watu wana mafunzo makubwa.Ameamua kujitoa


uhai ili asiweze kutoa siri lakini nashukuru tumefahamu kuna kikundi kinaitwa Black Mafia.Hapa ni sehemu nzuri ya kuanzia” akasema Mathew na kuongozana na Nelson wakaelekea ndani


“Nini kimetokea? Akauliza


Zari


“Nelson ameumia


anatakiwa kupelekwa hospitali mara moja” akasema Mathew na maandalizi ya kumpeleka Nelson hospitali yakaanza


“Nini kimetokea huko mlikokuwa Mathew? Ruby akauliza na Mathew akamuelezea kila kitu kilichotokea


“Dah ! hawa jamaa


wanaogopesha sana” akasema


Zari


“Ametamka kuwa alijiunga na Black Mafia na akaletwa Tanzania.Hii ina maanisha kwamba alijiunga na hilo kundi huko alikokuwa halafu akaletwa Tanzania.Tufanye uchunguzi wa kundi hili liko wapi na kazi zake ni nini halafu tutajua kinachoendelea” akasema Mathew na Ruby akaanza kulitafuta kundi hilo na kupata taarifa zake mbali mbali.


“Kuna taarifa nyingi za kuhusiana na Black Mafia


lakini hili linaonekana ni kundi ambalo limekuwa likijihusisha na dawa za


kulevya na liko Marekani.” Akasema Ruby





“Good.Picha inaendelea kujitengeneza.Zari wasiliana tena na Yule rafiki yako wa FBI muulize kuhusiana na kundi hili la Black Mafia kama wanalifahamu yawezekana tukapata taarifa za ndani zaidi kuliko hizi za mitandaoni ambazo zinaonyesha matukio pekee ambayo yamefanywa na Black Mafia” akasema Mathew na Zari akachukua simu yake akampigia tena rafiki yake aliyeko Marekani


akamshukuru kwa kumpa


taarifa zile za akina Alvaro lakini akataka kufahamu kuhusiana na kundi linaitwa Black Mafia


“Black Mafia? Akauliza rafiki yake na Zari


“Ndiyo.Unalifahamu hilo kundi?


“Umelifahamuje kundi hili na wewe uko Afrika? Akaliza


“Naomba unipe taarifa zake tafadhali kama unalifahamu kundi hilo” akasema Zari


“Black Mafia ni kundi mfano wa jeshi linalomilikiwa na wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya.Wanamiliki silaha nzito na wanaua watu kila uchao.Ni kundi ambalo kazi yake kubwa ni kuwalinda hao miungu wa dawa za kulevya na pili ni kuhakikisha hakuna


kikwazo kinaingilia biashara yao.Watu hao hupambana


vikali na polisi na kuna nyakati polisi wanashindwa kutokana na silaha nzito wanazozimiliki.Wengi wa watu


waliomo katika kundi hilo ni watu ambao wamewahi au wanafanya kazi katika vyombo mbali mbali vya ulinzi na usalama na wanajua kutumia silaha na mbinu mbali mbali za mapambano.Kundi hili lilianzia nchini Mexico na limezidi kusambaa sehemu mbali mbali kama Colombia,Ecuador nk” akasema Maria aliyekuwa akizungumza na Zari


“Muulize nani kiongozi wa kundi hilo? Mathew akaandika katika karatasi na kumpa Zari akamuuliza Maria


“Mpaka sasa bado


haifahamiki Black Mafia ni kundi lililoanzishwa na nani” akajibu Maria na Zaria akamshukuru kwa maelezo yale na kuagana


“Nyote mmesikia ni kundi linalojihusisha na dawa za kulevya”akasema Zari


“Kama wanajihusisha na dawa za kulevya hii ina maana kwamba hata huku Tanzania kundi hilo linajishughulisha na hiyo biashara.Watu hawa tunaowatafuta ni mtandao wa dawa za kulevya.Toka awali nilikwisha hisi watu hawa wanaweza kuwa ni wauzaji dawa za kulevya kutokana na namna wanavyoendesha mambo yao.Kwa maelezo aliyotoa Maria ni kwamba kundi hili la Black Mafia ni kwa ajili ya kuwalinda miungu wa dawa za kulevya na kuhakikisha biashara zao zinakwenda vizuri.Lazima yupo mfanya biashara mkubwa wa dawa za kulevya hapa Tanzania ambaye ana mashirikiano na wafanya biashara wakubwa wa nchi za Amerika ndiyo maana kundi la Black Mafia likaletwa huku kwa ajili ya kumlinda na kuhakikisha biashara yao haikutani na vikwazo.Siwafichi Ruby na Zari kwamba watu wanaofanya biashara hii wamejizatiti kweli kweli kuhakikisha kwamba biashara yao inafanyika bila vikwazo hivyo ni watu hatari sana.Kikwazo chochote kile kinachojitokeza mbele yao wanahakikisha wanakiondoa.Ni watu wenye nguvu kubwa kifedha na ndiyo maana kwa kutumia uwezo wao huo wa fedha wanapenyeza mizizi hadi katika serikali na hivyo kufanya biashara zao ziende vizuri bila bughudha.Naamini sasa mmekwisha pata picha kwa nini hawa jamaa wanao uwezo wa kutumia hata laini za simu ambazo hazijasajiliwa hapa nchini,kwa nini hawa jamaa wanao uwezo wa kufuta kumbu kumbu zozote za mtu yeyote wamtakaye ni kwa sababu tayari wana mizizi mikubwa ndani ya serikali.Si watu wa kufanyia mzaha hata kidogo ni watu hatari.Baada ya kuligundua hili sasa turejee katika msingi wa jambo hili ambao ni Naomi Bambi” Mathew akanyamaza kdogo halafu akaendelea


“Kuna maswali yanayoibuka hapa kwamba je Naomi Bambi alikuwa na mahusiano gani na hawa jamaa?Ninauliza swali hilo kwa sababu mpaka hatua hii nina uhakika mkubwa kwamba haya yote yaliyotokea kuanzia mauaji ya Lidya na Gosu Gosu kuangushiwa mzigo yote yamefanywa na Black Mafia sasa je wana mahusiano gani na Naomi Bambi?


“Tukirejea historia ya Naomi Bambi ambayo tumeipata shuleni leo mtaona lazima yupo mtu ambaye alikuwa anamgharamia maisha yake na mtuhuyo lazima atakuwa anajihusisha na dawa za kulevya kwani wao ndiyo wenye uwezo wa kuchezea hela namna ile.Yawezekana pia mtu huyo ndiye mkubwa wa Black Mafia hapa nchini na ndiyo maana amekuwa akiwatumia katika kuhakikissha wale wote wanaolichunguza suala la Naomi Bambi hawabaki salama” akasema Zari


“Ahsante sana Zari kwa ufafanuzi huo.Linaibuka swali lingine kwamba nini sababu ya mtu huyo kumgharamia Naomi Bambi kiasi kikubwa namna hii? Kuna faida yoyote alikuwa anaipata kwa kutumia gharama hizi kubwa? Akauliza Mathew


“Tunaye mmoja wa Black Mafia hapa ndani.Huyu atatusaidia kufahamu mahala walipo wenzake,ilipo ofisi yao na mkubwa wao ni nani?


Tukiyapata hayo basi suala hili litakuwa limekwisha.Ruby endelea kuchimba zaidi kundi hili la Black Mafia,Zari twende tukatafute majibu” akasema Mathew akaongozana na Zari wakaenda katika chumba alimo Thomas wakamtoa na kumpeleka mahala alikofia Alvaro Perez.Bado mwili wake ulikuwa mahala pale.


“Thomas mwenzako


Alvaro amefariki dunia kwa sababu ya kuwa na kiburi na kutotaka kujibu maswali yangu lakini kabla ya kumuua nimemuunguza kwanza na moto kama unavyoona miguu yake na hivi ndivyo ninavyokwenda kukufanya na wewe pia.Nitakuunguza kwa moto taratibu sana,utahisi maumivu makali na utakufa taratibu.Unayo nafasi ya kuepuka mateso hayo kwa kujibu maswali yangu nitakayokuuliza” akasema Mathew na kumtazama Thomas aliyekuwa amepiga magoti


“Mwenzako Alvaro kabla ya kumuua aliniambai kuhusu Black Mafia.Nataka kufahamu nani kiongozi wenu hapa nchini? Akauliza Mathew na Thomas akamtazama kwa dharau halafu akasema


“Amestahili kufa namna


hii na maiti yake inastahili kuliwa na fisi.Ni mtu mwoga na hafai kuwa Black Mafia.Nimekula kiapo cha damu na sintasema chochote hata kama mtanitesa vipi. ! akasema Thomas


“Hujakutana na mateso bado.Utasema tu” akasemaMathew na kumfunga kamba halafu wakamuinua na kumfunga juu ya chuma akaning’inia ,Mathew akapanga kuni chini na kabla hajawasha moto akasema


“Thomas nakupa nafasi nyingine ya kueleza ukweli kabla sijauwasha moto huu ambao utaanza kukuunguza miguu na utakufa ukijiona tena kwa maumivu makali sana” akasema Mathew lakini Thomas hakujibu kitu Mathew akawasha moto


“Mathew are you sure you want to burn him alive? Akauliza Zari


“Zari stay out of this! Akasema Mathew na Zari akaogopa na kumtazama Thomas kwa huruma alivyoanza kuhangaika pale moto ulivyoanza kuifikia miguu yake


“Thomas uko tayari kuongea? Akauliza Mathew na mara Thomas akaanza kupiga kelele za uchungu baada ya suruali yake iliyokuwa imekunjwa hadi magotini kushika moto.


“Mathew ! akasema Zari “Zari please ! akasema Mathew


“Thomas uko tayari kuzungumza? Akauliza Mathew lakini Thomas aliyekuwa ameikunja miguu yake aliendelea kulia kwa maumivu.Mathew akaongeza kuni na moto ukawa mkali zaidi.Zari alihisi mwili unamtetemeka.Ngozi nyeusi katika miguu ya Thomas iliungua yote na ikabaki ikionekana nyama nyeupe. “Thomas ! akaita Mathew “Nitasema ! Nitasema ! akapiga kelele Thomas.Haraka haraka moto ukazimwa na Thomas akashushwa chini akapakwa dawa miguuni alikoungua.


“What kind of a man is he? Hana huruma hata kidogo.Anathubutu kumchoma mwanadamu mwenzake kwa moto na anamuona akiungua.Huyu si mtu wa kawaida” akawaza Zari huku akimtazama Mathew kwa uoga


“Ruby anawezaje kuzama mapenzi na mtu mkatili kama huyu? Ndiyo maana hata mke wake wa kwanza wameachana hakuna mwanamke anayeweza akavumilia kuishi na mtu mkatili kama huyu ambaye alichobakisha ni kula tu nyama ya mtu.Zipo njia nyingi za mateso ambazo angeweza kuzitumia kuliko hii ya kumning’iniza mtu kisha kumchoma moto.Huu ni


ukatili uliopitiliza” akaendelea kuwaza Zari


Mathew alimaliza kumpaka Thomas dawa miguuni ili kumpunguzia maumivu


“Tayari nimekupata dawa hautasikia maumivu kwa sasa.Niele….” akanyamaza baada ya kugundua Thomas hakuwa na fahamu akavua fulana na kuanza kumpepea


“Ni vipi kama asingesema chochote angeunguzwa na moto hadi afe? Akauliza Zari


“Zari ninapokuwa kazini nikitafuta taarifa nyeti kama wakati huu,ubinadamu hunitoka hivyo niko tayari kufanya kitu chochote kile kwa ajili ya kuhakikisha ninapata taarifa niitakayo hivyo kama angeendelea kuwa kiburi angeteketea kwa moto huku akijiona.Please sihitaji maswali zaidi katika jambo hilo” akasema Mathew




Waumini wa kanisa la


injili ya wokovu huliita jumba la kiongozi wao mkuu kama jumba la kifalme la nabii mkuu Kasiano.Ni jumba lililostahili hadhi ya kifalme kwa namna lilivyojengwa.


Akiwa ndani ya jumba lake,nabii mkuu Kasiano


aliketi katika kiti chake maalum kabisa ndani ya chumba chake cha tafakari ambacho hukitumia yeye peke yake kwa ajili ya tafakari zake.Siku hii hakuwa peke yake alikuwa na mke wake Rita ambaye macho yake aliyaelekeza katika picha iliyokuwa ukutani mwa kile chumba.Ni picha iliyomuonyesha kijana mmoja akiwa amechoka amekaa juu ya jiwe akiwa na sura yenye kukata tamaa.Alionekana ni mtu asiyeifahamu kesho yake wala hatima ya maisha yake.


“Nimeiweka picha hii makusudi katika chumba hiki cha tafakari ili kila mara niwe nikitakafakari nilikotoka.Hii ilikuwa ni siku ya kwanza nilipokanyaga Italy baada ya kuokolewa baharini.Watu wananiona nimefanikiwa lakini hawajui mahala nilikotoka hadi nimefika hapa nilipo sasa” akasema Kasiano


“Ninatamani sana Kasiano kufahamu kuhusu historia yako hii ambayo hata mimi siifahamu.Nimekutana nawe ukiwa tayari tajiri na umekuwa mzito sana kunieleza historia yako.Kama hutajali unaweza ukanieleza tafadhali” akasema Rita


“Ni historia ambayo huwa sipendi kumuelezea mtu kwani nlipitia masahibu makubwa sana hadi kufika hapa nilipofika”


“Please darling ! akasema Rita na Kasiano akafumba macho kwa muda akikumbuka halafu akafumbua na kumtazama mkewe


“Sawa nitakueleza japo kwa ufupi” akasema Kasiano




MIAKA 7 ILIYOPITA


“Nilipata ushawishi wa kwenda ng’ambo nikiamini nitafanikiwa kimaisha baada ya baadhi ya marafiki zangu waliowahi kwenda ng’ambo kufanikiwa. Nililazimika kuuza ardhi na mali zote nilizoachiwa na wazazi wangu nikapata nauli na ndipo nilipounganishwa na mawakala wa kusafirisha watu kuelekea Libya .Safari ya kutoka hapa Tanzania kuelekea Tripoli Libya haikuwa safari nyepesi.Ni moja ya safari ngumu mno na hadi tunafika Libya nililia machozi kwani sikuamini kama kweli tumefika Tripoli.Tulisafirishwa kama mizigo ndani ya gari na hadi tunafika Libya wenzetu kumi na mbili walikuwa wamepoteza maisha.Nilikuwa na raia wengine kutoka


Elitrea,Ethiopia na


Somalia.Kutokana na ugumu


wa safari hiyo nilisali kila aina ya sala niliyoifahamu,niliimba kila wimbo nilioufahamu kumuomba Mungu anifikishe salama.It was hard! Akasema Kasiano na kunyamaza kidogo


“Nilikaa Tripoli wiki mbili nikijiandaa kwa safari ya kuelekea Italia.Tulikuwa tunafichwa ndani ya nyumba na hatukuruhusiwa kutoka.Siku ambayo niliingiza mguu katika boti ya kutupeleka Italia nilimkabidhi Mungu maisha yangu kwani sikutegemea kama nitafika salama.Nililipa kiasi cha shilingi milioni moja na zaidi kwa safari ile.Boti tuliyotumia kusafiria ilikuwa ni boti ya uvuvi kuu kuu ambayo haikuwa ikitumika tena katika shughuli za uvuvi.Ilifungwa injini mpya ili iweze kutumika kusafirisha watu kwenda Italia.Safari ilikuwa ngumu sana.Wenzetu wengi walipoteza maisha kwani tulikuwa tumejaa sana.Nilifumba macho sikutaka kuona kilichokuwa kinaendelea baharini.Nilikuwa nasubiri muda wa kufa


ufike.Boti yetu ilipoteza


mwelekeo nahodha hakuwa anafahamu hata tunakoelekea.Sikuamini pale ilipojitokeza helkopta ya uokoaji ya Italia na matumaini yakarejea.Tuliokolewa na kupelekwa katika kisiwa cha Lampedusa Italia.Picha hii niliyopiga ilikuwa ni siku ya pili baada ya kuwasili kisiwani hapo.Nilikata tamaa sikujua hatima ya maisha yangu ya mbele.” Akanyamaza tena na kuyaelekeza macho yake katika ile picha akaitazama.


“Siku tatu baadae tulihamishwa kutoka Lampedusa na kupelekwa katika kambi nyingine.Niliishiwa fedha zangu zote nilizokuwa nazo na nikalazimika kutafuta kibarua cha kufanya na kupata kazi ya kufanya usafi katika baa moja ambayo wateja wake wengi ni wale wanaojihusisha na dawa za kulevya na uhalifu.Ilikuwa ni kazi ya hatari sana lakini niliifanya kwa moyo na kulipwa ujira mdogo.Maisha yana maajabu sana na yanaweza kubadilika ndani ya sekunde chache kama maisha yangu yalivyobadilika ghafla ndani ya usiku mmoja.Ulitokea ugomvi kati ya wateja waliokuwa wanakunywa katika baa hiyo na kupelekea mmoja wa watu waliokuwa wanagombana kutoa bastola na kutishia kuua.Nilifanya kitu cha ujasiri mkubwa ambacho wengine hawakuwa wamekitarajia. Kwa ujasiri mkubwa niliweza kukabiliana na kumdhibiti mtu huyo mwenye silaha.Kitendo cha kumdhibiti Yule jamaa kilimfurahisha sana mmiliki wa baa ile akaniajiri kuwa mlinzi.Sifahamu ilikuaje hadi nikaamua kukabiliana na Yule jamaa mwenye silaha nadhani ni kutokana na kukata tamaa ya maisha ndiyo maana nikaamua kukabiliana naye na maisha yangu yalibadilika kuanzia usiku huo” akasema Kasiano na kumtazama mke wake aliyekuwa akimsikiliza kwa makini


“Kazi ya ulinzi nayo haikuwa nyepesi pia lakini niliifanya kwa kujiamini sana hadi siku moja nilipoitwa na meneja wa baa akaniambia kuna mtu anataka kuonana nami.Nilikwenda kuonana na mtu huyo ambaye alijitambulisha kwangu anaitwa Roberto Zullo na akanitambulisha kwa mke wake aliyeitwa Martina Durante.Roberto aliniambia kwamba amekuwa akifika pale baa na kufuatilia utendaji wangu wa kazi na amefurahishwa na kazi yangu hivyo anataka kunichukua na kwenda kunipa kazi kama nitakuwa tayari.Nilihitaji kazi hivyo sikusita kusema ndiyo japo sikujua ni kazi gani ninakwenda kuifanya.Roberto alinichukua na kunipeleka Afrika kusini ambako yeye na mke wake walikuwa na shamba kubwa la Zabibu na kiwanda kikubwa cha kutengeneza mvinyo utokanao na Zabibu.Nikiwa Afrika Kusini ndipo Roberto akaniambia kwamba kazi ninayotakiwa kuifanya inanihitaji kwanza niifahamu vya kutosha biblia.Nilianza


masomo ya biblia na baada ya mwaka mmoja


nikahitimu.Biblia ilinikaa kichwani lakini sikujua ni kazi gani ambayo ninakwenda kuifanya.Baada ya kumaliza mafunzo yangu ya biblia nikapelekwa nchini Nigeria ambako ndiko nilipewa nguvu ya unabii.Baada ya kupata unabii nilifanyiwa sherehe kubwa na Roberto akiwa amewaalika marafiki zake mbali mbali.Baada ya sherehe


ile kumalizika alinitambulisha kwa watu muhimu ambao ni Juan Castillo na Mama Bella.Usiku huo ndipo nilipofahamu kuwa Roberto anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya na wale watu wawili tuliokuwa nao mle ndani ni miungu wa dawa za kulevya.Nilihisi mwili wangu unanitetemeka baada ya utambulisho ule na hapo ndipo nilipojulishwa majukumu yangu na kwa nini nimesomeshwa biblia na baadae nikapewa unabii.Nilitakiwa kuja kufungua kanisa nchini Tanzania ambalo litakuwa ni mwavuli wa kujificha na biashara ya dawa za kulevya.Hiyo ndiyo historia yangu kwa ufupi na picha ile ni moja ya picha inayonikumbusha mbali sana katika safari yangu ya maisha hadi nilipofika hapa” akanyamaza baada ya simu ya Rita kuita akazungumza na mtu aliyempigia halafu akasema


“Nimetaarifiwa na walinzi kwamba Apollo amewasili” akasema Rita na Kasiano akanyanyuka wakatoka kwenda kumkaribisha mgeni.Dakika ishirini baadaye naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Keofas Mabula naye akawasili.


“Ndugu zangu karibuni sana katika kikao hiki cha dharura lakini muhimu sana kwa ajili ya mustakabali wetu.Katika kikao kilichopita tulizungumza kwa kirefu kuhusiana na suala la Mathew Mulumbi na taarifa ambayo tunayo mpaka jioni hii ni kwamba huyu jamaa amezidi kushika kasi” Kasiano akawaeleza kuhusiana na mwanamke aliyefika kanisani kwake akijifanya ni mwandishi wa habari na kumuhhoji kuhusiana na Adam Watwila akawaeleza vile vile kuhusu kile kilichotokea katika shule alikosoma Naomi Bambi na namna Black Mafia wanavyoendelea na jitihada za kumsaka Mathew.


“Hivi sasa ninasubiri kupata taarifa kuhusiana na wale jamaa waliotumwa kuvamia nyumba ambayo tunaamini ndiko aliko Yule mwanamke.Kwa ujumla tumepiga hatua kubwa na tunamkaribia sana Mathew Mulumbi na washirika wake” akasema Kasiano


“Lakini huo ni upande mmoja.Upande wa pili nako kuna mafanikio makubwa sana.Jana katika kikao chetu tulikubaliana kumchunguza mkuu wa jeshi la polisi na leo kazi hiyo imefanyika na kwa kinywa chake amekiri kwamba maagizo ya kumuhamisha Mathew Mulumbi kwenda gereza la Uwangwa yalitoka kwa Rais mwenyewe”


“Oh my God ! akasema Apollo


“Haikuishia hapo.Yeremia alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa kutekwa kwa Mathew ni mpango wa siri ulioandaliwa na rais mwenyewe kwani tayari anafahamu kuwa tuhuma zile zinazowakabili Mathew na Rais mstaafu Dr Fabian si za kweli bali ni mchezo umefanyika ili kuwachafua na hatimaye wafungwe gerezani.Kwa sasa Rais anashirikiana na akina Mathew kuwatafuta wahalifu hao ambao ni sisi hivyo tumeingia katika vita nyingine.Hii ni vita mbaya kwa kuwa inamshirikisha pia mkuu wa nchi ambaye ana nguvu kubwa kuliko sisi na kama tukipigana bila maarifa tutapigwa vibaya sana na utakuwa ni mwisho wetu.Hii si vita ya kutumia maguvu ni vita ya kutumia akili zaidi kwa upande wetu ndiyo maana baada ya kupata uhakika huo tumekuja na mpango ambao tuna uhakika mkubwa kwamba utamfanya Rais aweke chini silaha zake na kutusikiliza kile tukitakacho” akanyamaza tena kidogo kwa muda halafu akaendelea


“Silaha yetu ya kwanza ni kujua udhaifu wa Rais.Hiyo ni silaha kubwa sana.Nawakumbusha kwamba hapa tunapambana na Festus Mayungulu kama yeye ndiyo maana tunayaelekeza mashambulizi zaidi kwake.Hatutaki vita na polisi au na mtu yeyote kwani wote hawa wako chini ya Festus hivyo tukifanikiwa kumdhibiti huyu basi wote hao watarudi nyuma.Katika uchunguzi wetu tumefahamu kuwa Rais wetu anapenda mno kusifiwa.Hapendi kashfa au kitu chochote kile kitakachomuwekea doa.Siku zote amekuwa akijipambanua kwamba yeye ni mmoja wa marais wasafi kabisa katika uongozi wake.Ni rais anayependwa na watu kwa sababu ya usafi wake si wa mwili bali wa kiuongozi.Pamoja na usafi huo Festus si malaika naye ana udhaifu mkubwa ambao ni wanawake” akanyamaza baada ya Keofas kutabasamu


“Festus ana mambo kadhaa ambayo kama tukiyaanika kwa jamii basi heshima yake itashuka kwa kiwango kikubwa sana jambo ambalo halitaki.Kuna mambo mawili ambayo tumeyapata hadi sasa kuhusu yeye.Kwanza kabisa aliwahi kuzaa na katibu muhtasi wake wakati akiwa waziri wa maji.Kwa bahati mbaya mtoto huyo hivi sasa amejitumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya.Tutalifuatilia jambo hilo na kulianika kwa jamii.Hilo ni kombora la kwanza ambalo litamtikisa sana Rais Festus.Jambo la pili ni kwamba kwa hivi sasa ana


mahusiano ya siri na mwanamke mmoja anaitwa Zandile Wepener anaishi Afrika kusini”


“Zandile? Keofas akauliza “Ndiyo”


“Dah ! Festus kumbe ni hatari.Amevuka mipaka hadi kwa Zandile ! akasema Keo


“Huyu mwanamke amewahi kuwa mke wa mfalme wa Eswatini lakini alimuacha kwa kutokuwa mwaminifu katika ndoa yao.Zandile ni mwanamke ambaye anafahamika sana Afrika na duniani kwa mavazi yake ya gharama kubwa na kupenda maisha ya kifahari.Zandile amekuwa akija Dar es salaam kila mwisho wa wiki tena anasafiri katika daraja la kwanza.Inadaiwa kwamba kwa hivi sasa baada ya kumpata Festus Zandile anaishi kama malkia.Anaishi maisha ya kifahari mno.Hili ni kombora la pili ambalo litamfanya Festus apige magoti na kuomba msamaha.Kwa makombora hayo mawili Festus hatabaki salama” akasema Kasiano.


“Haya ni makombora mazito mno na maangamizi yake ni makubwa” akasema Apollo.


“Umeyapataje makombora


haya Kasiano ambayo hata sisi tulio ndani ya serikali hatuyafahamu? Akauliza Keo


“Nina vyanzo vingi vya taarifa na haya ninayowaeleza si mambo ya kubuni ni ukweli mtupu.Kuhusu hili la Zandile nitapata hadi picha zao wakiwa


faragha na hii itaongeza ukubwa wa kombora.Baada ya kuwafahamisheni hayo basi nataka tujadiliane namna ya kuyatumia makombora hayo mawili ili kushinda vita hii” akasema Kasiano.Kilipita kipindi cha ukimya halafu Apollo akasema


“Tutayatumia makombora


yote mawili lakini tutaanza kwanza na hili la kuzaa na katibu wake muhtasi na mtoto kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya.Hii itakuwa ni kashfa kubwa sana ambayo itamchafua mno Festus.Tunatakiwa kwanza kumpata mwanamke aliyezaa naye tumuhoji na kujiridhisha kweli amezaa na Festus na atueleze kama Festus amekuwa akimtunza mwanae.Kigezo cha mtoto huyo kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya ni aibu kubwa kwa Festus kwani ataonekana amemtelekeza na umaarufu wake utapungua.Black Mafia wafuatilie mawasiliano ya huyo mwanamke na kujua kama anawasiliana na Rais na baada ya kukusanya ushahidi tutaitoa taarifa hii katika gazeti moja linaloaminika sana hapa nchini kwa kuandika habari za kweli.Naamini utazuka mjadala mkubwa sana na kabla kombora hilo halijapoa tutatumia kombola la pili ambalo sishauri tulijadili sasa hadi pale tutakapata matokeo ya kombora la kwanza kama litakuwa na mafanikio au la.Huo ni ushauri wangu” akasema Apollo


“Binafsi sijawahi kuwa na dukuduku lolote na mipango yote anayoipanga Apollo ndiyo maana ni mtu pekee ambaye huwa ninamtumia katika kupanga mikakati mbali mbali.Hata katika hili ninakubaliana na mawazo yake kama hakuna mwenye wazo mbadala” akasema Kasiano na hakukuwa na mtu mwingine mwenye wazo la tofauti.


“Nawashukuru kwa


kulikubali wazo hili la Apollo.Tayari ninayo anuani ya mahala anakoishi huyo mwanamke anayeitwa Martha Mwailule.Jioni ya leo atatembelewa na vijana wetu ambao watajifanya ni waandishi wa habari na kumuhoji kuhusiana na mahusiano yake na Rais na kuhusu mtoto wake ambaye ameathirika na madawa ya kulevya” akasema Kasiano Majadiliano yaliendelea na baada ya makubaliano Kasiano akamuita Paul Lewis nyumbani kwake kwa ajili ya kumpa maelekezo



Paul Lewis aliwasili katika 

makazi ya nabii Kasiano kwa 

haraka baada ya kuitwa. 

 “Paul ahsante kwa kufika 

kwa haraka baada ya 

kuitwa.Kabla ya yote nataka 

tupate taarifa kuhusiana na 

kile kilichotokea leo.John amekupa mrejesho wa namna 

gani watu wetu walivyouawa 

kule shuleni? Akauliza Kasiano 

na Paul akawaeleza kila kitu 

alichoelezwa na John 

 “Ndugu zangu nadhani 

mnaweza kuona namna hawa 

jamaa 

walivyojiandaa.Nilikuwa 

sahihi kuhusu Yule mwanamke 

kwamba ana mahusiano na 

Mathew Mulumbi.Mathew 

anashirikiana na watu wenye 

nguvu na ninashawishika 

kuamini kwamba 

anashirikiana na SNSA.Hii ni 

idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi ambako Ruby 

mke wa Dr Fabian na ambaye 

ni rafiki mkubwa wa Mathew 

Mulumbi aliwahi kuwa 

mkurugenzi wake” akasema 

Kasiano 

 “Vipi kuhusu wale vijana 

uliowatuma kwenda 

kumfuatilia Yule 

mwanamke?Kuna mrejesho 

wowote kutoka kwao? 

 “Mkuu mpaka sasa hakuna 

mawasiliano yoyote kutoka 

kwa wale wenzetu na hii haitoi 

picha nzuri” akasema Paul  “Una maanisha nini 

Paul?Wameuawa? akauliza 

Kasiano akionekana kuwa na 

wasiwasi 

 “Kwa muda ambao 

walikwenda hadi sasa bila 

kupata mrejesho wowote 

kutoka kwao kuna mambo 

mawili ambayo ninahisi 

yanaweza kuwa yametokea 

aidha wameuawa au 

wametekwa.Ninashauri mkuu 

pale tunapotuma vijana 

kuanzia sasa kuwe na timu ya 

ziada ya kuwafuatilia kwani 

hawa jamaa ambao tulidhani 

ni watu wa kawaida wanaonekana ni watu hatari 

sana hivyo hatupaswi 

kuwadharau kwa namna 

yoyote” akasema Paul 

 “Ni bora kama watakuwa 

wmaeuawa lakini kama 

wametekwa itakuwa mbaya 

zaidi kwa upande wetu kwani 

wanaweza wakateswa na 

wakaeleza kila kitu” 

 “Watu niliowatuma huko 

ninawaamini hata kama 

wakiteswa hawataweza kutoa 

siri yoyote” akasema Paul 

 “Mathew Mulumbi ni 

jasusi nguli anazo mbinu nyingi za kuweza kumfanya 

mtu yeyote akatoa siri.Nataka 

baada ya kutoka hapa utume 

tena timu ya kwenda 

kuchunguza kuhusiana na 

watu wetu kama wameuawa au 

wametekwa vile vile katika 

sehemu zetu zote lazima kuwe 

na tahadhari kubwa 

sana.Ulinzi uimarishwe mara 

dufu kwani mwenendo wa 

huyu jamaa umeanza kuleta 

hofu ! akasema Kasiano 

 “Sawa mkuu nitafanya 

hivyo”  “Paul tumekuita hapa 

kuna kazi muhimu ya kufanya 

jioni ya leo” akasema Kasiano 

na kumpa maelekezo ya 

kufanya kuhusiana na Martha 

Mwailule. 

 “Hii ni njia mpya ambayo 

tunataka kuitumia kupambana 

na Rais.Tukifanikiwa 

kumuingiza katika kumi na 

nane zetu basi vita itakuwa 

imekwisha kwani 

anashirikiana na Mathew 

Mulumbi na kitu cha kwanza 

ambacho tutamtaka akifanye 

ni kumsalimisha kwetu na bila Mathew Mulumbi vita hakuna 

tena” akasema Kasiano. 

************* 

 Thomas Calabrese 

alizinduka na kuhisi mamivu 

makali miguuni. 

 “Nipelekeni hospitali 

tafadhali mmeniumiza mno ! 

akalalama Thomas huku sura 

yake ikionyesha alikuwa katika 

maumivu makali 

 “Hautakwenda hospitali 

hadi pale utakapotueleza kila 

kitu tunachotaka.Thomas tafadhali nieleze kila kitu bila 

kunificha ninakuahidi 

kukupeleka hospitali 

ukapatiwe matibabu ama sivyo 

nitakuacha ukiteseka na 

utakufa taratibu tena kwa 

maumivu makali 

sana.Umenielewa Thomas? 

Akauliza Mathew 

 “Nini mnakitaka? Akauliza 

Thomas 

 “Ninataka kufahamu 

kuhusu Black Mafia” 

 “Sifahamu chochote 

kuhusu Black Mafia.Nililetwa 

hapa kufanya kazi maalum hivyo sifahamu chochote 

kuhusu Black Mafia! 

 “Kazi gani ulikuja 

kuifanya? 

 “Kuua ! akajibu Thomas 

 “Kumuua nani? 

 “Sifahamu Alvalo ambaye 

mmemuua ndiye anayefahamu 

kila kitu kwani yeye ndiye 

aliyenileta huku” 

 “Mnaishi wapi hapa Dar es 

salaam? 

 “Sifahamu chochote 

Alvaro ndiye anayeniongoza 

kwa kila kitu”akasema Thomas.Mathew akamtazama 


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog