Search This Blog

Friday 7 April 2023

I WAS WRONG | NILIKOSEA - 4

  


Simulizi : I Was Wrong | Nilikosea 

Sehemu Ya Nne (4)


akafungue geti wakaingai ndani.hakuna 

mtu aliyekuwa akiishi katika jumba hili 

kubwa ambalo lilikwisha kamilika kila 

kitu .David akaliingza garindani hadi 

katika chumba cha garihalafu Vicky 

akashuka.  “ David holdmy hand 

please.Mwenzio nina hali mbaya sana” 

akasema Vicky na david akamshika 

mkono wakaelekea moja kwa moja hadi 

katika chumba kikubwa cha kulala.Vcky 

hakutaka kupoteza muda akavua nguo na 

kuzitupa chinihalafu akajitupakitandani. 

 “ Vicky ngoja kwanza nikajimwagie 

maji ninahisi joto” akasema David 

 “ David tafadhali usichelewe 

mwenzako nina hali mbaya sana” akasema 

Vicky madhahabu.David akaingia bafuni 

na kujimwagia maji haraka haraka halafu 

akarejea chumbani.sVicky alikuwa mtupu 

kama alivyozaliwa.David akasisimka sana. 

 “ David tafadhali usiendelee kunitesa 

kiasi hiki.Njoo mpenziwangu”akasema 

Vicky kwa sauti ndogo.Davidi 

katafakarikidogona kumpanda 

kitandani.Vicky akamrukia na 

kumkumbatia kwa nguvu. 

 “ Vicky ngoja kwanza” akasewma 

david 

 “ David kuna nini? Mbona unanitesa 

hivyo? Akauliza Vicky 

 “ SikutesiVicky.hata mimi 

mwenyewe hali yangu ni mbaya na 

ninakuhitaji sana.Lakinikabla hatujafanya lolote kunamamboambayo nataka 

tuyaongee.” 

 “ Ni mambo gani David?kwa nini 

tussongee wakati mwingine? David 

tufanye kwanza halafu tutaongea baadae” 

 “ Hatutakuwa teanna muda mzuri wa 

kuweza kuongea Vicky.Huu ni muda mzuri 

tumepata tuongee halafu tufanye yetu.” 

 “ haya sema unataka tongee kitu 

gani? Akauliza Vicky 

 “ Ni kuhusu ule mpango wetu” 

 “ kwani kuna tatizo lolote David/ 

Kial kitu kkinakwenda vzuri na siku 

yoyote ndaniya wiki hii basi pesa ile 

tutaipata.” 

 “ hakuna tatizo Vicky ila kuna jambo 

fulano dogo ambalo ninataka kukuomba.” 

 “ Omba chochote David” akasema 

Vicky 

 “ Kama unavyofahamu mimi 

niliokotwa tu mtaanina Pauline kwa hiyo 

nina wasiwasi mzee Zkaria anaweza 

akastushwa sana na mafaniko yangu ya 

ghafla kwa hiyo ninaomba kituimoja.Pesa 

ile yote ukae nayo wewe katika akaunti 

yako na mimiutanipa akaunyti namba 

yako na nambaza siri ili nikihitaji pesa 

basi iwe rahsi kutoa lakinisitaki kuweka 

katika akaunti yangu ya binafsi kuogopa kustukiwa na mzee Zakaria.” Akasema 

david 

 “ David sidhani kama hiloni wazo 

zuri.kama una wasi wasi ninaweza hata 

kukufunghulia akaunti ya siri ili ukaweke 

pesa zako lakini si wote wawili kutumia 

akaunti moja” akasem,a Vicky 

 “ Vicky naomba usinielewe vibaya na 

wala sina lengo baya kwa kukuomba hivi 

lakini ukae ukijua kwamba ni wewe ndiye 

uoyeniingiza katiak suala hili kwa 

iyosikuwa nimejiadaa kwa lolote.Kupata 

kiasi cha shilingi milioni miambili kwa 

mara moja si jambo dogo kwa maana hiyo 

basi zinaweza zikanipa kiwewew na 

nikajikuta nikianza kuzitumia hovyo na 

kumfanya mzee zakaria astuke na papo 

hapo ukubuke kwamba kwa hivi 

sasapauline atakuw amacho sana katika 

kutuchunguz ana hasa mimi kwa hiyo 

akina kitu chochote ambacho si cha 

kawaida basi lazima atamwambia baba 

yake kwa hiyo nakuomba ukubali pesa 

zote zikae kwako na miminiwe nikichukua 

kidogokidogo u paleambapo nitakuwa 

ikihitaji .Niyakapokuwa nimejipanga 

vozuri zaidi basi nitazichukua pesa zote” 

akasema David.Vicky akainamaakafikri 

kwa muda na kusema  “ David nihatari kubwa kutumia 

akauntimoja watu wawili labda tufanye 

hivi,kila ukitaka pesa uwe ukinitaarifu na 

mimi ninakuchukulia a kukupatia” 

Unaonaje kuhusu hilo? 

 “ Vicky unaoghopa nini? Don’t tou 

trusts me?akaulzia David 

 “ Id o trust you david” 

 “ Vizuri sana.Kama unaniamini na 

umediriki hata kunivulia nguo leo hii basi 

usisite kuniaminihata katika hili 

ninalokwambia.Siwezi kufanya chochote 

na hela yako na zaidi ya yote 

badonakutegemea sana katka 

mambomengi hukombeleni nataka 

unionyeshe njia namna tutakavyoweza 

kumchuna Zakaria na kujitengenezea 

maisha mazuri kwa hiyo kuna hela nyingi 

tu bado inatusubiri” akasema david na 

kumfanya Vicky atabasamu 

 “haya leta simu yako” akasemaVicky 

na david akampatia simyake 

akamuandikia kila kitukuhusianana 

akauntiyake . 

 “ Tayari kuhusu hilo.Kuna lingine? 

Akaulzia david. 

 “ hakuna “ akajibu David 

 “ kamahakuna kilichopo ohivi sasa ni 

kitu kimoja tu”akasema Vicvky na kumrukia David akaanza kumpiga 

mabusu.David alishindwa kuendelea na 

msimamo wake akajikuta kaitoa 

ushirikiano mkubwa na kumpagawiosha 

vilivyo Vicky madhahab ambaye alikuwa 

akitoa vilio kana kwamba anaadhibiwa 

.Walizamakatikaulimwengu wa huba.



Jumapili hii Ilikuwa ni nzuri sana kwa 

Robin na mwalimu Lucy. Ilikuwa ni siku ya 

kwanza toka walipoufungua ukurasa 

mpya katika maisha yao kwa kuwa 

wapenzi.Toka asubuhi nyumba ya 

mwalimu Lucy ilitawaliwa na maongezi ya 

furaha na vicheko tofauti na siku nyingine 

ambapo huwa kimya sana.Mchana Robin 

na mwalimu Lucy walisaidiana kuandaa 

chakula wakati Penina na dada yake wa 

kazi wakiendelea kufurahi 

bustanini.Chakula kilipokuwa tayari wote 

wakajumuika mezani na baadae Lucy na 

Robin wakaelekea chumbani 

kupumzika.Katika kipindi hiki kifupi 

ambacho wamekitumia toka 

walipoanzisha mahusiano yao,Lucy 

alikuwa na furaha 

isiyoelezeka.Alimshukuru Mungu kwa kumpatia mtu ambaye aliamini ndiye 

atakayeyafuta makovu yote ya vidonda 

alivyowahi kuumizwa huko 

nyuma.Aliamini Robin alikuwa ni chaguo 

sahihi kwake.Kitandai walikuwa 

wamemekumbatiana kwa mahaba mazito 

 “ Robin kuna jambo moja ambalo 

ninataka kukuuliza” akasema Lucy 

 “ Uliza Lucy wala usihofu kitu” 

akasema Robin.Lucy akamuangalia na 

kutabasamu kisha akasema 

 “ Mmi binafsi ninapenda nikiri 

kwako kwamba sijawahi kuhisi furaha 

kama niliyonayo sasa.Katika muda huu 

mchache tuliokuwa pamoja nimejihisi ni 

mwenye furaha pengine kuliko wanawake 

wote wa dunia hii.Sipingani na nfasi yangu 

kwamba wewe ndiye ambaye Mungu 

alikuweka kwa ajili yangu.Siwezi 

kuusemea moyo wako kwa sababu 

sifahamu unanipenda kiasi gani na nini 

unawaza juu yangu lakini kuna kitu 

ninataka kukisikia toka 

kwako.Mahusianoyetu haya yatakuwa ni 

mahusiano ya namna gani ? Tutakuwa ni 

wapenzi tu ambao tutakuwa tunakutana 

tunatimiziana haja zetu za mwili au 

tutakwedna zaidi ya hapo?  Robin akamtazama Lucy na 

kutabasamu halafu akamsogeza karibu 

akambusu 

 “ Kuna jambo moja kubwa 

umeliongea.Mimi na wewe tulipangwa 

tuwe pamoja toka tukiwa tumboni mwa 

mama zetu kwa hiyo kukutana kwetu si 

kwa bahati mbaya na urafiki tuliouanzisha 

jana ni mwanzo wa kuelekea katika jambo 

kubwa kabisa katika maisha yetu 

ambalokila mmojawetu analiot na 

kulitamani.Lucy umenifanya niwahi 

kukutamkia jambo hili ingawa sikuwa 

nimepanga kukueleza kwa wakati huu 

lakini ukweli wa moyo wangu ni kwamba 

dhamira yangu ni kuupeleka uhusiano huu 

mbali zaidi . Lucy nataka mimina wewe 

tufunge ndoa na tuishi kama mume na 

mke “ akasema Robin.Mwalimu Lucy 

alibaki anamuangalia kwa mshangao kana 

kwamba nim ara ya kwanza anaonana na 

Robin .Maneno yale ya Robin yalimtoa 

machozi .Robin akachukua kitambaa na 

kumfuta machozi 

 “ Usilie Lucy.” Akasema Robin na 

mwalimu Lucy akamkumbatia kwa nguvu 

 “ Robin kwa miaka mingi nimekuwa 

nikisubiri siku moja mtu atakayenitamia 

maneno haya mazito toka ndani kabisa mwa moyo wake na siku ya leo maneno 

haya umeyatamka wewe .Nmekosa neno la 

kusema Robin.Ahsante sana kwa uamuzi 

wako huu na mimi sina kipingamizi 

chochote .Niko tayari kuolewa na wewe 

hata sasa hivi.” Akasema Lucy. 

 “ Nitakuoa Lucy.Utakuwa mke wangu 

wa ndoa.Nitakuwamume wako na tutaishi 

kwa furaha katika siku zote za maisha 

yetu yaliyobaki hapa duniani” akasema 

Robin na kuzidi kumliza Lucy 

 “ Ahsante sana Robin.nakuahidi 

nitakuwa mke bora kuliko wote 

duniani.pamoja na hayo bado kuna jambo 

ninataka kukuuliza” akasema Lucy 

 “ Uliza Lucy usihofu” 

 “ ni kuhusu wewe na mkeo 

Vivian.Kisheria wewe na Vivian bado ni 

wanandoa kwa maana hiyo basi lazima 

tutakutana na kikwazo katika dhamira 

yetu hii ya kutaka kufunga ndoa na kuishi 

pamoja.” Akasema mwalimu Lucy.Robin 

akainama na kuzama ghafla katika 

mawazo. 

 “ Unalolisema Lucy ni la kweli 

kabisa.Mimi na Vivian bado 

tunatambuliwa kama wanandoa kwa 

sababu bado ndoa yetu haijatenguliwa .”  “ kwa hiyo tutafanya nini Robin? 

Ninavyofahamu mimi ni kwamba ndoa 

zetu sisi wakristu ikishafungwa 

imefungwa .Hiki ni kikwazo kikubwa sana 

kwetu ” akasema Lucy 

 “ Usijali Lucy.Nitalishughulikia suala 

hili na nitaliweka sawa.Hakuna 

kitakachoshindikana.Mimi na wewe 

lazima tufunge ndoa na kuishi pamoja” 

Akasema Robin 

 “ Utafanya nini Robin? Hili si suala 

rahisi kama unavyolichukulia” 

 “ Sijajua bado nini nitafanya lakini 

siwezi kukaa hivi hivi nitahakikisha 

ninalifanyia kazi na ninakusihi usihofu 

Mungu aliyetukutanisha ndiye 

atakayetuonyesha nini cha kufanya ili 

tuweze kuitimiza dhamira yetu hii njema “ 

akasema Robin. 

 Waliendelea na maongezi mengne ya 

kuhusiana namaisha yao ya siku za usoni 

na ilipotimu saa kumi na mbili za jioni 

Robin Penian na mtumishi wao wa ndani 

wakaondoka kurejea nyumbani kwao na 

kumuacha Lucy akiwa mkiwa 

sana.Hakutaka kuachana na Robin.  “ Ahsante sana David.leo umenikuna 

kisawa sawa.Ninakiri sijawahi kukutana 

na kijana aliyenipeleka mchaka mchaka 

kama wewe.Baada ya miaka mingi 

hatimaye leo hii nimesikia raha ya 

kufanya mapenzi.Mzee Zakaria alikuwa 

akinipapasa tu na hata vijana wengine 

wote ambao nimewahi kutembea nao 

hakuna kati yao ambaye amewahi 

kunifikisha pale ambapo wewe 

umenifikisha leo.David sikuachi 

ninaapa.Wewe ndiye haswa ambaye 

ninakutafuta.” Akasema Vicky madhahabu 

akiwa hoi kitandani kutokana na gwaride 

alilochezeshwa na David 

 “ Usiseme hivyo Vicky.Wewe ni mke 

wa mtu na hata hivi tunavyofanya ni kosa 

kubwa sana.Mzee Zakaria akigundua 

anaweza hata akaniua.Isitoshe tayari mimi 

nina mpenzi wangu ninayempenda .Jambo 

hili limetokea leo tu na halitajirudia tena” 

akasema David 

 “ David huu ni mwanzo tu wa mimi 

na wewe.Umenionjesha asali na ninataka 

kuchonga mzinga.Niko tayari kwa lolote 

lile ili mradi niwe na wewe.Simuogopi 

mtu yeyote yule awe Zakaria au nani.Mimi 

nimekupenda na nitafanya kila 

ninaloweza niwe na wewe.Tulichokifanya leo kitaendelea tena na tena .Hakitaishia 

leo hii pekee.David tafadhali nakuomba 

usiseme hapana.Tayari nimempata 

daktari wa kunitibu maradhi yangu 

ambaye ni wewe kwa hiyo basi nakuomba 

uendelee kunitibu.Nitakufanyia kila 

unachokitaka ili mradi tu niendelee kuwa 

na wewe,niendelee kuipata huduma yako.” 

Akasema Vicky. 

 “ Vicky hapana.Hatutaweza 

kuendelea na mchezo huu bila ya mzee 

Zakaria kustuka.Halafu mimi nina mpenzi 

wangu anayenipenda na mimi 

ninampenda sana kwa hiyo nakuomba 

Vicky tuishie hapa leo na tusiendelee na 

mchezo huu” akasema David 

 “ David hakuna mtu wa 

kumuhofia.Usimuogope kabisa mzee 

Zakaria.Yule ni mfu tarajiwa kwa hiyo 

yule niache mimi nitamshughulikia.Halafu 

sikukatazi kuwa na mpenzi wako Tamia 

lakini naomba na mimi uwe ukinihudumia 

.Ninakuhitaji sana David na sioni 

mwingine zaidi yako.Niambie unahitaji 

nikufanyie kitu gani David chochote 

nitakufanyia ili mradi tu uwe na mimi” 

akasema Vicky 

 “ Vicky tutaliongelea jambo hili siku 

nyingine .Tujiandae tuondoke kwani tukichelewa sana mzee Zakaria anaweza 

kuwa na wasi wasi.” Akasema David 

 “ sawa nimekuelewa david lakini 

naomba unihakikishie kwamba utakuwa 

tayari kila pale nitakapokuhitaji” 

 “ sawa usijali kuhusu hilo” akajibu 

David na Vicky akaelekea bafuni akaoga 

na kisha wakaondoka kurejea 

nyumbani.Wakati wa kurudi Vicky 

alikuwa amejilaza katika kiti alikuwa 

amechoka sana.shughuli aliyopewa na 

David haikuwa ndogo. 

 “ dah ! bado namuangalia David na 

kushindwa kummaliza.Sikujua kama ni 

kijana mjuzi wa mambo kiasi 

hiki.Hataniponyoka mikononi 

tena.Nitafanya kila linalowezekana hadi 

atakuwa wangu tu na tena wangu peke 

yangu.sitaki kuchanganywa na 

mwanamke mwingine .” akawaza Vicky 

**************** 

 Pauline alimaliza kupakia vitu 

vyake vichache katika sanduku lake dogo 

tayari kwa kuondoka.Akakitazama 

chumba chake na machoziyakamtoka. 

 “Nimekizoea sana chumba changu 

lakini hakuna namna nyingine zaidi ya kuondoka.” Akawaza Pauline na kulifunga 

kabati lake akatoka.Moja kwa moja 

akaelekea chumbani kwa baba yake 

akagonga mlango na mzee zakaria 

akamruhusu aingie ndani 

 “ Baba nimekuja kukuaga.”akasema 

pauline 

 “ Ina maana ndiyo unaondoka hivyo 

? akauliza mzee zakaria kwa mshangao 

 “ Ndiyo baba ninaondoka jioni ya 

leo.” 

 “ kwa nini usisubiri ukaondoka 

kesho? 

 “ Kuna gari ya rafiki yangu 

ninaondoka nayo kwa hiyo siwezi kusubiri 

hadi kesho” akasema Pauline 

Kimya kikatanda mle chumbani mzee 

Zakaria na mwanae wakaangaliana. 

 “ Pauline mimi siwezi kukuzuia 

usiende huko unakotaka kwenda lakini 

ninachokuomba ni mawasiliano ya karibu 

sana .Tufahamishe kila mara kuhusu 

maendeleo yako na kama una tatizo lolote 

usisite kunieleza.” 

 “ Nitafanya hivyo baba usijali” 

akasema Pauline halafu akamfuata baba 

yake kitandani akamkumbatia  “ baba ubaki salama.Nitakuwa 

nikikujulia hali kila mara ili kuhakikisha 

kama uko salama” akasema Pauline 

 “ Nitakuwa salama Pauline.Usihofu 

chochote kuhusu mimi.Nina hakika 

utakaporejea utanikuta nikiwa nimepona 

kabisa” akasema mzee zakaria na bila 

kupoteza muda Pauline akatoka huku 

machozi yakimtoka.Akalichukua begi lake 

akalikokota na kutoka .Akiwa nje ya 

nyumba yao akasimama akiwa na mawazo 

mengi.Akampigia simu dereva taksi ili aje 

amchukue pale nyumbani kwao.Wakati 

amesimama akisubiri taksi ije kumchukua 

ikaingia gari ya David .Pauline 

akaliangalia kwa hasira kali.Mlango 

ukafunguliwa akashuka David. 

 “ Nitajitahidi kumsahau 

David.Nitajitahidi kwa kila nitakavyoweza 

nim…” Mara mlango mwingine 

ukafunguliwa akashuka Vicky madhahabu 

 “ David na mama mdogo wametoka 

wapi? Akawaza Pauline akimkodolea 

macho Vicky 

 “ mama mdogo anaonekana 

amechoka sana.wametoka wapi? 

Akajiuliza Pauline na mara dereva taksi 

akampigia simu kwamba tayari 

amekwisha fika.Pauline akalikokota sanduku lake akatoka huku David akabaki 

amesimama anamuangalia 

 “ Kuna kitu nakihisi kinaendelea 

kati ya David na mama mdogo .kwa muda 

mrefu sasa nimekuwa nikihisi kuna kitu 

kinachoendelea kati ya David na mama 

mdogo .Itanilazimu kufanya uchunguzi wa 

kina kuhusiana na mahusiano yao “ 

akawaza Pauline na kumuelekeza dereva 

wa ile taksi ampeleke sehemu Fulani kuna 

mtu anahitaji kuonana naye. 

 Walifika hadi katika baa Fulani 

ambako pauline alikutana na mtu mmoja 

ambaye kazi yake ni kupiga picha 

 “ Davis mimi nina safiri kidogo lakini 

kuna kazi nataka kukupa uifanye katika 

kipindi hiki ambacho sintakuwepo.” 

 “ Kazi gani unataka nikufanyie 

Pauline? Akauliza Davis 

 “ Unamfahamu mama mdogo Vicky? 

Akauliza Pauline 

 “ Ndiyo ninamfahamu “ 

 “ Basi nataka ufanye kazi ya 

kumfuatilia kwa karibu kila anapokuwa 

na kijana mmoja anayeishi pale kwetu 

anaitwa david .Ninahisi mama mdogo ana 

mzunguka baba kwa hiyo nataka 

umfuatilie na kila unapomuona akiwa na 

yule kijana basi chukua picha zao za kila wanachokifanya.Ninaomba uwe 

unanitumia picha hizo katika email 

yangu.” Akasema Pauline 

 “ kama niyule kijana mgeni anayeishi 

pale kwenu ninamfahamu ,nimewahi 

kumkuta palwe nilipokuja kumpiga picha 

mzee zakaria.Mimi nitaifanya hii kazi 

kwani ndiyo fani yangu na wewe 

mwenyewe utafurahi.kama ni kweli hayo 

unayoyasema basi nitawaumbua.Mzee 

Zakaria ninamuheshimu sana na siwezi 

kukubali afanyiwe hivi na yule kijana.” 

Akasema Davis 

 “ Nitashukuru sana Davis kama 

utanifanyia kazi hii .” akasema pauline na 

kufungua pochi yake akatoa bunda la noti 

akamuhesabia Davis na kumpa. 

 “ Kila uaapokuwa unanitumia picha 

nitakulipa kila picha shilingi elfu hamsini” 

akasema Pauline na kuzidi kumpagawisha 

Davis.pauline akaachana naye akaingia 

garini na kuondoka kuelekea katika kituo 

cha mabasi ambako alipanda basi la 

kuelekea mjini Moshi 

 “ safari yangu imeanza.Nina hakika 

huku niendako nitayasahau yote 

yaliyonipata huku Arusha”akawaza 

Pauline akachomeka spika za masikioni katika simu yake na kuendelea kusikiliza 

mziki taratibu . 

Taratibu basi alilopanda Pauline likaanza 

kuliacha jiji la Arusha.Tayari kiza 

kimekwisha tanda angani.Pauline alikuwa 

amevaa spika za masikioni lakini machoni 

michirizi ya machozi ilionekana machoni 

mwake.Hakuna aliyeweza kuligundua hilo 

kutokana na kuwa na kiza ndani ya gari. 

 “ Ni vigumu kuamini kama leo hii 

ninalazimika kuiacha Arusha 

niliyopapenda sana. Ni jambo gumu 

kulifanya lakini sina namna nyingine ya 

kufanya zaidi ya kuondoka Arusha.Kwa 

upande Fulani ninashukuru kwa kufanya 

maamuzi haya kwani yawezekana 

nimeianza safari ya kuelekea katika 

furaha ya kudumu ya maisha yangu 

.Nimeishi maisha mazuri ya kuogelea 

katika utajiri mkubwa wa familia yangu na 

hata sifahamu neno shida maana yake nini 

lakini pamoja na hayo yote I’m not 

happy.Sielewi ni kwa nini sina furaha hata 

chembe katika maisha yangu japo 

ninapata kila kitu ninachokihitaji katika 

maisha . Nadhani kukaa mbali na 

nyumbani kunaweza kunisaidia nikaweza 

kuwa angalau na furaha.” Akawaza 

Pauline  “ Kitu kingine ambacho kinanifanya 

nizidi kukonda kila siku ni kuhusiana na 

hii tarehe 11 september ya kila 

mwaka.Kuna nini katika tarehe hii kiasi 

kwamba kila mwaka lazima kuna jambo 

baya linatokea? There is must be 

something.Lazima kuna kitu ambacho 

baba hataki kukiweka wazi kwa sababu 

haiwezekani kila ifikapo tarehe hii tu 

ndipo jambo baya hutokea katika familia 

yetu.Mama yangu alifariki tarehe kama 

hii,mdogo wangu,mchumba wangu pia na 

mwaka huu baba alinusurika kifo kama 

ingekuwa ni kwa msaada wa David..” Jina 

la David lilipomjia kichwani akajikuta 

akisisimkwa mwili na picha ya David 

ikamjia kichwani akauma meno kwa 

hasira 

 “ Nilimpenda David mara tu 

nilipomuona.Hakuwa katika hali ya 

kutazamika kiasi cha kuweza kupendwa 

na mtu kama mimi lakini kama 

wanavyosema kwamba mapenzi ni upofu 

nilijikuta nikimpenda na bila kujali 

uchakavu aliokuwa nao wala historia yake 

nikajitoa kwake.Nilifanya kila 

lililowezekana kuhakikisha kwamba 

anakuwa kijana wa kisasa ambaye 

anaweza akatazamika na kila mtu.Nilimfanya awe ni kijana wa hadhi 

yangu lakini kwa kumbe nilikosea sana.Ni 

heri ningefuga mbwa angenilinda na wezi 

kuliko namna alivyonifanyia 

David.Nilimpenda kwa moyo wangu wote 

na nilikuwa tayari kwa lolote lile ili mradi 

niwe naye lakini pamoja na upendo huo 

wote niliomuonyesha bado hakuridhika 

na mimi na akaamua kunisaliti kwa 

kuanzisha mahusiano na Yule kahaba 

Tamia.Moyo unaniuma sana kwa kitendo 

alichonifanyia mtu ambaye kwa miaka 

mingi nimemchukulia kama ndugu 

yangu.Tamia sikuwa namchukulia kama 

rafiki yangu bali ndugu kabisa kwani 

urafiki wetu ulianza muda mrefu sana 

lakini leo hii amenigeuzia kibao na 

kunichukulia mwanaume niliyempenda na 

ambaye niliamini ndiye atakayenirejeshea 

furaha yangu maishani.” Akawaza Pauline 

na kujifuta machozi 

 “ Nimefanya uamuzi wa busara sana 

kuondoka nyumbani na kuwaacha 

wakiendelea na mapenzi yao.Nawaombea 

kwa Mungu awabariki mapenzi yao 

yadumu lakini kwa namna 

ninavyomfahamu Tamia David amepotea 

njia sana.Siku moja atajuta na atanitafuta 

asinipate tena.Ninamfahamu vizuri Tamia ni mwanamke mwenye ugonjwa wa 

kupenda wanaume na huwa hatulii na 

mwanaume mmoja kwa miezi 

mitatu.Mpaka sasa tayari amekwisha 

kuwa na wanaume wengi ambao hata 

wengine siwakumbuki na tayari 

amekwisha vunja ndoa nyingi .Mwanamke 

kama Yule hatakiwi kuwa na mwanaume 

kama David.Lakini kwa kuwa yeye 

mwenyewe amekubali kushawishika na 

akakiri kumpenda Tamia ninamtakia kila 

la heri .Ninaamini Mungu atanijaalia 

furaha na siku moja nina hakika 

nitampata mwanaume Yule ambaye 

Mungu amemuweka kwa ajili 

yangu.Naamini mwanaume yupo ila 

sifahamu nitakutana naye lini na wapi ila 

ninachokiamini ni kwamba siku moja 

nitakutana naye and I’ll be happy forever.” 

Akaendelea kuwaza Pauline. 

 “ Baba naye ametokea kumuamini 

sana mama mdogo ambaye kwa sasa 

ameanzisha ukaribu na David.Sikujua 

kama David ni mdhaifu kiasi hiki.Yaani 

amekubali kurubuniwa na mama mdogo 

na nina hakika kabisa lazima wana 

mipango ya kumuibia baba.Nasikitika 

sana kwa baba kushindwa kuniamini mimi 

mwanae na kumuamini mama mdogo kwa kiasi kile huku mali zake zikiendelea 

kuteketea.Yule mama anaingiza mamilioni 

ya hasara kila mwaka lakini baba halioni 

hilo na bado anaendelea 

kuniamini.Anyway ni bora nikae pembeni 

na kuendelea na biashara zangu 

nimuache yeye aendeshe biashara zake 

akishirikiana na mama mdogo na Yule 

mwanaume dhaifu David” akawaza 

Pauline. 

 Basi liliwasili mjini Moshi akashuka 

na kuchukua taksi iliyompeleka hadi 

katika hoteli moja kubwa iliyo nje kidogo 

ya mji huu wa Moshi.Aliufahamu mji huu 

vizuri kwani amekuwa akija hapa mara 

kwa mara.Pale hotelini alipewa chumba 

kizuri chenye kujitosheleza kila kitu ndani 

akaoga na kisha akajitupa kitandani.Bado 

mawazo mengi yaliendelea kukisonga 

kichwa chake na hivyo kumlazimu kuagiza 

mvinyo mwepesi ili umsaidie kuondoa 

mawazo na kumpatia usingizi. 

********************* 

 Wakati Pauline akiteseka kwa 

mawazo akiwa mjini Moshi,David alikuwa amejilaza kitandani akiwa mwingi wa 

mawazo. 

 “ Sijui Pauline atakuwa wapi mida 

hii.Ninasikia uchungu mwingi sana kwa 

kumuumiza msichana mzuri kama Yule.Ni 

msichana ambaye ana roho nzuri sana ya 

huruma ambaye sijawahi kukutana 

naye.Sikuwahi kuwa na dada na 

nilipokutana na Pauline nilimchukulia 

kama dada yangu.Pauline aliniokota 

wakati ndio kwanza nimetoka gerezani 

nikiwa nimechakaa na wala sitamaniki 

lakini hakujali uchakavu wangu 

akanipokea na kunifanya mmoja wa 

wanafamilia.Pauline alikuwa ananipenda 

kwa dhati ya moyo wake na hili 

nililigundua toka mara ya kwanza 

tulipokutana.Japokuwa nilifahamu 

kwamba yeye alinipenda sana lakini kwa 

upande wangu niliogopa kujihusisha 

katika mahusiano naye kwa kwani 

nilikuwa namchukulia kama dada 

yangu.Ni madam Vick ndiye 

aliyenishawishi hadi nikakubali kujiingiza 

katika mahusiano na Pauline na 

kumuumiza kiasi hiki.Sijui nifaye nini ili 

niweze kumtuliza Pauline lakini 

nimekwisha chelewa.Kwa sasa hakuna 

ninaloweza kufanya kwani tayari Pauline amekwisha ondoka lakini ninachoweza 

kukifanya hapa ni kuhakikisha 

aliyesababisha haya yote analipa uovu 

wake.Mwisho wa madam Vicky 

umewadia.Nitamfanyia kitu ambacho 

hatakitegemea kabisa.Nitahakikisha kila 

alichokiiba kwa mzee Zakaria 

kikarejea.Mwanamke shetani Yule 

amekuwa anapatiwa kila kitu na mzee 

Zakaria lakini haridhiki na bado kila 

uchao amekuwa akimuibia.Amesababisha 

nikamuuza Pauline na mimi siwezi 

kumsamehe.Lazima nimuumize.Siku si 

nyingi toka sasa atalia na kusaga meno.” 

Akawaza David na kumbu kumbu za 

walichokifanya kule usa river katika 

nyumba ya Vicky zikamjia kichwani 

 “ Nimemkosea sana mzee Zakaria na 

sijui nitamweleza nini ili anielewe endapo 

atagundua kitendo nilichokifanya leo cha 

kutembea na mke wake .Mzee huyu kama 

alivyo mwanae amekuwa mwema sana 

kwangu.Ananilea kama mwanae wa damu 

na sikupaswa kabisa kumfanyia vile,lakini 

ili mipango yangu ifanikiwe ilinilazimu 

kufanya vile ili kuzidi kuujenga ukaribu na 

Vicky ukaribu ambao nina hakika 

utanisaidia mimi kumfahamu vyema 

kwani ni mwanamke ambaye amekuwa akifanya mambo yake kwa uficho sana” 

akaendelea kuwaza David na mara 

ujumbe wa simu ukaingia 

 “ David kwa namna ulivyonikuna leo 

natamani hata sasa hivi nikufuate 

chumbani kwako kwani kila nikikumbuka 

mambo uliyonifanyia leo najikuta 

nikiwashwa na wewe pekee ndiye 

unayeweza kunikuna.David 

ninachokiomba kwako ni kwamba walau 

kila wiki uwe ukitenga muda kwa ajili 

yangu.Nimekupata mwanaume niliyekuwa 

ninakuhitaji kwa miaka mingi kwa hiyo 

naomba usinifanyie ukatili.” 

 David akausoma ujumbe ule na 

kuufuta kabisa halafu akaitupa simu 

pembeni. 

 “ Dah ama kweli mwanamke si mtu 

wa kumuamini.Endapo ikitokea mzee 

Zakaria akausoma ujumbe kama huu ni 

wazi anaweza hata akadondoka na 

kufariki dunia.Anampenda sana mke wake 

na hajui mambo ambayo mke wake 

anayafanya pindi anapompa 

mgongo.Nitalimaliza suala hili na 

nitaondoka hapa kwa mzee Zakaria kwani 

japokuwa nitakuwa nimemsaidia kubaini 

ubazazi anaoufanya mke wake lakini nina 

hakika hatakuwa na imani tena kwangu kwa kitendo cha kukubali kutembea na 

mke wake.Potelea mbali silijali hilo lakini 

ninachotaka hata kama nikiondoka hapa 

mali za mzee Zakaria ziwe katika mikono 

salama” akaendelea kuwaza 

David.Akaichukua tena simu yake na 

kufungua sehemu ambako huwa 

anahifadhi picha na kuanza kuzipitia picha 

mbali mbali ambazo alipiga na Pauline 

 “ I’m so sorry Pauline.Najua 

nimekuumiza kwa kiwango cha juu 

mno.Haikuwa dhamira yangu kukuumiza 

kiasi hiki lakini ni mtu mmoja tu ambaye 

amesababisha haya yote kutokea.Bila 

mama yako mdogo katu nisingeingia 

katika mahusiano na wewe na 

kukusabishia mateso haya ya moyo.Sijui 

nitaongea lugha gani ili uweze kukubali 

kunisamehe lakini nina tumai iko siku 

moja utakubali kunisamehe” akawaza 

David huku akilengwa na machozi kwa 

kuziona picha zile walizopiga kipindi cha 

furaha sana akiwa na Pauline.Akiwa bado 

katika tafakari mara ukaingia ujumbe 

mwingine katika simu.Nao ulitoka kwa 

Vicky 

 “ Mbona hujanijibu David kipenzi 

changu? Unaogopa nini ? Nijibu mpenzi 

wangu huyu mzee amelala hapa kama chatu na wala hatikisiki.Nijibu basi ili 

kama vipi nikufuate huko chumbani 

kwako kwani leo Yule mtoto Mwanga 

hayupo.” 

 David kwa hasira akaufuta ujumbe 

ule na kuizima kabisa simu yake halafu 

akafunga mlango wake kwa funguo na 

kujitupa kitandani 

********************* 

 “ Mungu awatume malaika wake 

wakulinde usiku wa leo dhidi ya kila baya 

la usiku huu na kesho uamke salama ee 

kipenzi changu.Nakupenda sana Robin” 

 Huu ulikuwa ni ujumbe ulioingia 

katika simu ya Robin ukitoka kwa 

mwalimu Lucy.Robin ambaye kwa muda 

mrefu alikuwa amejilaza kitandani huku 

sura yake ikiwa na tabasamu lisilokauka 

akacheka kidogo na kisha akaandika 

ujumbe kumjibu mwalimu Lucy 

 “ Nashindwa kupata usingizi.Kila 

nifumbapo macho ninahisi miiko yako 

laini yenye joto inanipapasa kifua changu 

na nifumbuapo macho hujikuta mimi na 

mito yangu.Lucy ninamshukuru sana 

Mungu kwa kunikutanisha nawe na kama 

nilivyokuahidi nitafanya kila niwezalo ili kuharakisha zoezi la kubatilisha ndoa 

yangu na Vivian ili mimi na wewe tuweze 

kufunga ndoa.Malaika wakulinde pia 

usiku huu wa leo na kesho uamke salama 

pia.Nakupenda zaidi ya ninavyoweza 

kukueleza” 

 Robin akausoma tena ujumbe ule 

akaridhika nao kisha akautuma .Bado sura 

yake iliendelea kuwa katika tabasamu 

pana sana. 

 “ Sijui nimshukuruje Mungu kwa 

zawadi hii kubwa aliyonipatia ya 

mwanamke huyu ambaye ninaamini ndiye 

hasa aliyeumbwa kwa ajili 

yangu.Hatimaye baada ya miaka mingi ya 

kuishi katika kiapo changu nilichojiapiza 

cha kutojiingiza tena katika mahusiano ya 

kimapenzi kutokana na vitendo 

alivyonifanyia Vivian hatimaye 

nimekivunja kiapo hicho baada ya 

kukutana na Lucy and I’m in love 

again.Nimependa tena na nina furaha 

kubwa mno.Moyo wangu una amani na 

laiti kama isingekuwa ni kufuata sheria za 

kanisa basi kesho asubuhi na mapema 

ningekwenda kuandikisha ndoa yangu na 

Lucy lakini sheria bado zinatutambua 

mimi na Lucy kama wanandoa kwa hiyo ili 

niweze kufunga ndoa na Lucy yanibidi kwanza ndoa yangu na Vivian itenguliwe 

na suala hili ninaanza kulifuatilia kuanzia 

kesho asubuhi.Sitaki kabisa kupoteza 

muda kwani tayari nina hakika 

nimempata mwanamke wa maisha yangu.” 

Akawaza Robin 

 “ Vivian alinitesa sana na kunifanya 

niwachukie wanawake wote.Hakuwa na 

mapenzi na mimi hata kidogo bali 

alichonipendea ili pesa zangu na baada ya 

mambo yangu kuanza kwenda vibaya basi 

aliamua kuniacha na 

kuondoka.Nimekwisha msamehe na 

nimekwisha mtoa kabisa katika kichwa 

change .Lucy ni mwanamke ambaye ana 

upendo wa dhati na amepitia mambo 

mengi katika maisha yake.Ameteseka sana 

.Historia yake inasikitisha mno.Ni wakati 

wake na yeye wa kutabasamu.Ni wakati 

wake wa kuwa na furaha.Nitampenda Lucy 

kwa namna ya pekee na hata siku moja 

nitahakikisha hatoi tena chozi.Nitamfuta 

machozi yote aliyolia toka 

mwanzo.Nitahakikisha anakuwa ni 

mwanamke mwenye furaha kupita wote 

hapa duniani na kamwe hataulaumu moyo 

wake kwa kunipenda.” Akaendelea 

kuwaza Robin na kuzidi kutabasamu 

baada ya kumkumbuka mwanae Penina  “ Sipati picha ni furaha kiasi gani 

atakuwa nayo Penina atakaposikia 

kwamba mimi na mwalimu Lucy tuko 

katika mahusiano na tunatarajia kufunga 

ndoa.Penina na Lucy wamekuwa na 

mahusiano mazuri kwa muda mrefu na 

Lucy anampenda sana Penny na amekuwa 

akimchukulia kama mwanae.Penina 

halikadhalika anampenda sana Lucy na 

ndoto yake siku zote ni kumpata mama 

kama Lucy.Atafurahi sana kama akisikia 

kuhusiana na jambo hili kwani amekuwa 

akiomba kwa siku nyingi ndoto hii iwe 

kweli na kwa sasa inakwenda kuwa 

kweli.Suala hili tutamtaarifu tukiwa sote 

mimi na Lucy.” Akawaza Robin na mara 

akakumbuka kitu ambacho kikamfanya 

ainuke na kukaa 

 “ Kuna kitu ambacho kinamtesa sana 

Lucy.Ni kuhusu mwanae aliyekwenda 

kumtelekeza katika kituo cha kulelea 

watoto kule usa river.Jambo hili 

linamnyima amani sana na anatamani 

kuufahamu ukweli lakini anaogopa 

.Nitamsaidia kuutafuta ukweli ili awe na 

amani .Ninafahamu katika vituo vile huwa 

kuna kumbu kumbu za watoto wote 

wanaolelewa na nina hakika hata kumbu 

kumbu za Angela zitakuwepo.Ninaamini atakuwa na furaha sana endapo 

atagundua kama mwanae bado yuko 

hai.Hata mimi ninaomba Mungu atusaidie 

ili mtoto huyu awe hai na aweze kuungana 

tena na mama yake .Kama atakuwa hai 

nitafanya kila niwezalo kuwaunganisha 

tena na mama yake na huyu atakuwa ni 

dada yake Penina.” Akawaza Robin na 

taratibu kijiusingizi kikaanza kumpitia 

******************* 

 Kumekucha tena, siku nyingine 

imeanza.Mchaka mchaka wa maisha 

unaendelea kama kawaida.Tayari watu 

wamekwisha jihimu katika shughuli zao 

za kujitafutia kipato.Siku hii Robin 

alikuwa ni mwenye furaha kupita 

kiasi.Uso wake haukukaukiwa tabasamu. 

 Baada ya kumpeleka Penina shule 

,alikwenda ofisini kwake lakini hakukaa 

sana akatoka na hakuaga anaelekea 

wapi.Safari yake ikamfikisha moja kwa 

moja katika duka moja kubwa lenye kibao 

Vivy supermarket.Kwa takribani dakika 

mbili akabaki ndani ya gari akionekana 

kujishauri kama ashuke au la.Hatimaye 

akafungua mlango na kushuka kisha 

akaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya supermarket ile.Mara tu alipoingia ndani 

ya supermarket ile upande wa kushoto 

akamuona mwanamke mmoja mrefu 

mwembamba mwenye nywele fupi na 

ngozi nyororo.Alikuwa ni mwanamke 

mrembo sana.Mwanamke Yule alikuwa 

anaendelea na harakati zake na 

kuhudumia wateja kwani yeye ndiye 

aliyekuwa akipokea fedha kutoka kwa 

wateja.Robin akamtazama kwa sekunde 

kadhaa 

 “ She still as beautifull as she was 

before but she’s a snake” akawaza Robin 

na mara wateja waliokuwa 

wakihudumiwa na Yule mwanamke 

wakaondoka na Robin akabaki 

amesimama peke yake pale kaunta 

akimtazama Yule mwanamke 

 “ Karibu ka…” akasema Yule 

mwanamke na kustuka.Robin akavua 

miwani myeusi aliyokuwa amevaa na 

wakatazamana.. 

 “ Hallo Vivian” akasema Robin 

 “ Rob…Robin !!.akasema Vivian kwa 

mshangao.Hakuwa ametegemea kuonana 

na Robin muda ule. 

 “ Robin karibu..” akasema Vivian 

lakini sauti yake ilionyesha alikuwa katika 

mstuko mkubwa  “ Ahsante Vivian.” Akajibu Robin 

 “ Karibu hili ni duka langu jipya 

nimelifungua miezi miwili 

iliyopita.Umejuaje kama niko hapa? 

Akauliza Vivian 

 “ Vivian nimekuja hapa nina 

maongezi na wewe..” akasema Robin . 

 “ Imekuwa vizuri sana umewahi 

kunitafuta kwani hata mimi nilikuwa 

nataka nikutafute nina maongezi ya 

muhimu nawe” akasema Vivian huku 

akiinuka na kumuita mmoja wa 

wafanyakazi wake pale kaunta halafu 

akamuongoza Robin hadi katika mwavuli 

uliokuwa katika baa iliyokuwa pembeni 

ya supermarket ile kwa ajili ya 

maongezi.Vivian alikuwa ni mwanamke 

mrembo sana na kwa siku hii ya leo 

alikuwa amependeza mno.Alikuwa 

anatembea kwa madaha kama kawaida 

yake na kumfanya Robin atabasamu. 

Kwa takribani dakika mbili Robin na 

Vivian walikuwa kimya kila mmoja 

akimtazama mwenzake.Walionekana 

kama vile wanategenea kuanzisha 

maongezi lakini mwishowe Robin akaamu 

kuuvunja ukimya. 

 “ Naona maisha yako mazuri siku 

hizi” Vivian akanywa juice kidogo akatabasamu 

na kusema 

 “ Namshukuru mungu maisha 

yanakwenda vizuri.Naona hata wewe 

mambo yako si mabaya” 

 “ Hata mimi namshukuru Mungu 

sana,tunaendelea vizuri mimi na 

mwanangu.” Akasema Robin.Kimya 

kikatanda kidogo na baada ya sekunde 

kadhaa Vivian akasema 

 “ Anaendeleaje Penina? 

Robin akamtazama usoni halafu 

akatabasamu na kusema 

 “ Hatimaye leo umemkumbuka” 

 “ Nitashindwaje kumkumbuka 

mwanangu niliyemzaa mwenyewe? 

Akasema Vivian 

Robin akamuangalia bila kusema kitu 

.Vivian akaendelea 

 “ Penina amekuwa msichana 

mkubwa siku hizi.Nilikwenda 

kumtembelea shuleni kwao lakini 

hakutaka hata kuongea 

nami.Umempandikiza chuki kiasi kwamba 

hataki hata kuniona” akasema Vivian 

.Robin akamtazama na kupandwa na 

hasira lakini akajitahidi 

kujizuia.Akakohoa kidogo na kusema  “ Hata baada ya miaka mingi kupita 

bado haujabadilika.Macho yako bado 

hayana aibu hata kidogo.Ulimi wako bado 

hauchagui hata neno la kutamka.You are 

still the same Vivian I knew many years 

ago.The same devil ” akasema Robin na 

maneno yale yakaonekana kumkera sana 

Vivian akakunja uso 

 “ Robin tafadhali naomba usije hapa 

na kuanza kunitusi.Iwe ni mwanzo na 

mwisho kuniita mimi shetani.!!.akasema 

Vivian kwa ukali 

 “ Anyway sijaja hapa kugombana 

nawe.Nimekuja hapa kwa mambo ya 

msingi sana” akasema Robin 

 “ Sema kilichokuleta na si kuanza 

kunitusi” akasema Vivian. 

 Robin akatulia akamtazama Vivy 

kwa muda kisha akasema 

 “ Vivy kutokana na kilichotokea kati 

yangu nawe ni ukweli ulio wazi kwamba 

mimi na wewe hatuwezi kuwa pamoja 

tena.Kila mmoja kwa sasa ana maisha 

yake na hakuna mwenye mpango wa 

kuendelea na mwenzake.Wewe tayari una 

maisha yako mazuri na yenye furaha 

halikadhalika mimi pia nina maisha yangu 

kwa hiyo hakuna anayemuhitaji mwenzake tena.” Akanyamza kidogo na 

kuendelea 

 “ Baada ya mimi nawe kuachana 

nilijiapiza kwamba sintajiiingiza katika 

masuala ya kimahusiano tena na nimeishi 

kiapo change hicho na toka wakati ule 

sijawahi kujiingiza katika masuala ya 

mahusiano.Niliwaogopa sana wanawake 

.Hata hivyo bado Mungu ana mipango 

mizuri na mimi kwani baada ya kukaa 

kipindi hicho chote kirefu bila ya kuwa na 

mahusiano nimefanikiwa kukutana na 

mtu ambaye amenifanya nivunje kiapo 

changu na kwa sasa nimeingia tena katika 

mahusiano.Its a very serious relationship” 

akasema Robin .Vivian alikuwa kimya 

akimsikiliza.Robin akaendelea 

 “ Kwa hiyo basi nimekuja hapa 

kukiupa tarifa hizo na kukufahamisha 

kwamba ninatazamia kufunga ndoa na 

huyo mtu wangu mpya lakini kuna jambo 

linanikwamisha.Japokuwa hatuishi 

pamoja lakini mimi na wewe 

tunatambuliwa bado kama wanandoa kwa 

hiyo kwa sheria za kanisa hakuna 

anayeruhusiwa kuoa ama kuolewa kabla 

ya ndoa yetu hii haijatenguliwa.Kwa hiyo 

basi nimekuja hapa kukwambia kwamba 

nataka tuanze taratibu za kuitengua ndoa yetu ili kila mmoja wetu awe huru 

kuendelea na maisha yake bila kufungwa 

na kitu chochote kile” akasema 

Robin.Vivian akatabasamu baada ya 

kuisikia kauli ile ya Robin.Ni wazi 

ilionekana kumgusa sana. 

 “ Nimefurahi kusikia hivyo.Hata 

mimi nilikuwa katika mipango ya 

kukutafuta kwa ajili ya jambo hilo 

hilo.Hata mimi ninatazamia kufunga ndoa 

na mume wangu kwa hiyo kama hata 

wewe mwenyewe unawazo kama hilo basi 

hakuna haja ya kupoteza muda.Tuanze 

kulishughulikia suala hilo haraka “ 

akasema Vivian 

 “ Sawa kama umeridhika basi 

nitakwenda kuonana na viongozi wa dini 

kwanza ili kutafuta ushauri wao na 

taratibu zipi tunatakiwa kuzifuata ili 

kulikamilisha suala hili.Nitakachokipata 

nitakuja kukutaarifu” akasema Robin 

huku akiinuka na kutaka kuondoka 

 “ Ngoja kwanza Robin.” Akasema 

Vivian na Robin akamtazama kwa macho 

makali 

 “ Mbona unanitazama kwa ukali 

namna hiyo? Mimi na wewe hatuna 

ugomvi na wala si maadui kwa hiyo naomba ukae kuna jambo nataka 

kukuuliza.” Akasema Vivian.Robin akaketi 

 “ Niambie basi unachotaka 

kunieleza,nina shughuli nyngi za kufanya” 

akasema Robin 

 “How’s she doing? Akauliza Vivy 

 “ Nani? 

 “ Our daughter.Penina” 

 “ Vivian tafadhali naomba kabisa 

usitake kunichafua sasa hivi na kunifanya 

niongee mambo ambayo sikutaka 

kuongea.” Akasema Robin 

 “ kwani kuna ubaya gani Robin 

kuongelea suala la mtoto wetu? 

Robin akainuka 

 “ Stay far away from my 

daughter.Nilisikia ulikwenda 

kumtembelea shuleni anakosoma.Naomba 

usithubutu tena kwenda kumtembelea 

wala kutafuta ukaribu naye.Mwanamke 

katili wewe na haufai kabisa kuitwa 

mama.Leo hii baada ya mtoto kukua ndiop 

unadiriki kusimama na kusema una 

mtoto? I warn you once again ,stay far 

away from my child.Nikikuona au kusikia 

una mazoea na mwanangu nitakuvunja 

shingo yako. I hate you devil ” akasema 

Robin kwa hasira na kuanza kutembea 

kwa kasi kueleka katika gari lake.  “ Mwanamke mshenzi sana 

Yule.Nilikosea sana kujiingiza katika 

mahusiano na mwanamke mwenye roho 

mbaya kama shetani.Baada ya kumuacha 

mtoto kwa miaka mingi leo ndio 

anakumbuka ana mtoto.Ngoja ninyooshe 

moja kwa moja katika ofisi za kanisa 

nikapate ushauri toka kwa viongozi wa 

dini kuhusu taratibu za kufuata kuitengua 

ndoa yangu” akawaza Robin 

 Vivian bado aliendelea kukaa pale 

chini ya mwavuli hata baada ya Robin 

kuondoka.Alionekana kujawa na mawazo 

mengi sana 

 “ Maneno aliyoniambia Robin 

yanaumiza lakini yana ukweli ndani 

yake.Kwa kweli sistahili kabisa hata 

kuitwa mama.Nilimtelekeza mwanangu 

Vivian akiwa bado mdogo sana na toka 

wakati huo sijawahi hata kwenda 

kumuona hadi hivi majuzi nilipokwenda 

kumtembelea shuleni.Ninajilaumu sana 

kwa kosa hili nililolifanya na sina hakika 

kama Robin na Vivian wanaweza 

wakanisamehe.Woga wa kuishi katika 

Umasikni ndio ulionisababisha nikafanya 

vile lakini kwa sasa nimekuwa tajiri na 

nina mali za kutosha nahitaji sana ukaribu 

na mwanangu.Natamani sana kama ningeweza kupata nafasi ya kumuonyesha 

upendo mwanangu lakini sijui nifanye nini 

.Anyway bado sijachelewa.I’ll keep trying” 

akawaza Vivy na kuinuka akaingia ndani 

ya duka lake. 




Kengele ya mlangoni ikamstua 

Pauline toka usingizini.Akatazama saa 

ukutani ilionyesha ni saa nne na dakika 

nane 

 “ Nimelala mpaka 

nimepitiliza.Nadhani kwa sababu ya 

mvinyo niliokunywa jana” akawaza na 

kuinuka akaelekea mlangoni.Aliyegonga 

alikuwa ni mtumishi wa hoteli ile ambaye 

alihitaji kufanya usafi wa chumba.Wakati 

mtumishi wa hoteli akiendelea na 

shughuli zake za usafi,Pauline akaingia 

bafuni kuoga.Kisha oga akajilaza 

kitandani. 

 “ Sijisikii kwenda sehemu yoyote 

siku ya leo.Natamani nilale tu humu 

chumbani bila kuonana na mtu 

yeyote.Nahisi kama vile ninaanza 

kuwaogopa watu ” akawaza na kuwapigia 

simu hotelini akaagiza aletewe mlo wa asubuhi.Haukupita muda mrefu mlo wa 

asubuhi ukaletwa 

 “ Sikuzoea maisha haya ya kuwa 

mbali na nyumbani lakini afadhali kidogo 

ninajisikia amani.Niko mbali na wale 

ambao wamekuwa wakisababisha nikose 

furaha.Ninamkosa sana baba yangu lakini 

sina namna nyingine lazima nikubali kuwa 

mbali naye kwa sasa.Ninawakumbuka 

sana marafiki zangu wapenzi ingawa 

wengine wamegeuka wasaliti.Mungu 

atanijaalia marafiki wengine wazuri na 

safari hii nitakuwa makini sana katika 

kuchagua marafiki .Sitaki kuwa na 

marafiki kama Tamia wenye kubadilika 

rangi kama kinyonga.” Akawaza wakati 

akiendelea kupata kifungua kinywa. 

 Hali ya hewa siku hii haikuwa ni 

yenye baridi kama ilivyozoeleka kwa mji 

huu wa moshi.Angani kulikuwa na jua na 

hali ilikuwa ya joto.Pauline alichoka 

kukaa ndani na akaamua kutoka nje na 

kukaa kibarazani .Aliifurahia sana 

mandhari nzuri ya hoteli hii. 

 “ Ouh kumbe kuna bwawa zuri sana 

la kuogelea kule chini.Ngoja nikakae pale.” 

Akawaza Pauline na kuingia chumbani 

akachukua kitabu chake cha hadithi 

ambacho hupenda sana kukisoma bila kuchoka kiitwacho Moyo wa Ambola na 

kushuka ngazi akaelekea katika bwawa la 

kuogelea.Hakukuwa na watu wengi eneo 

hili..Alikaa katika moja wapo ya viti 

vilivyolizunguka bwawa lile na kuendelea 

kukisoma kitabu chake.Si mbali sana na 

mahala pale alikuwa amekaa mama 

mmoja akiwa na binti yake ambaye umri 

wake ulikaribia miaka mitano au sita hivi 

wakiwa katika mojawapo ya viti 

vilivyolizungukabwawa lile. 

 Akiwa amezama katika hadithi tamu 

aliyokuwa akiisoma mara akasikia 

kishindo kama cha mtu kurukia katika 

maji.Mwanzoni alihisi labda kuna mtu 

aliyerukia ndani ya bwawa kuogelea lakini 

baada ya muda akalazimika kuweka 

kitabu pembeni baada ya kusikia ukulele 

wa mtu akiomba msaada.Mama mmoja 

alikuwa akipiga kelele kuomba msaada 

akitaka wajitokeze watu kumuokoa 

mwanae aliyekuwa ndani ya bwawa 

akitapa tapa.Ghafla Pauline akapatwa na 

ujasiri wa aina yake na kujikuta amerukia 

majini na kumtoa mtoto Yule akamkabidhi 

kwa mama yake aliyekuwa akitetemeka 

huku machozi yakimtoka.Akamkumbatia 

binti yake sana huku akilia.Pauline 

alipongezwa na watu waliofika pale bwawani kwa kitendio chake cha kishujaa 

cha kumuokoa binti Yule toka katika maji. 

 “ Dada nakushukuru sana kwa 

kuniokolea mwanangu.Nilikuwa nimekaa 

naye pale katika kiti nikaondoka kwenda 

kununua juice na kumuacha akiwa 

amekaa pale.Nyumbani tuna bwawa lakini 

si kubwa kama hili na ambalo huwa 

anaogelea mara kwa mara.Nadhani 

aliamua kuingia ndani ya bwawa hili 

akidhani ni sawa na lile la 

nyumbani.Ahsante sana dada yangu kwa 

sababu sijui ningefanya nini leo” akasema 

Yule mama huku machozi yakiendelea 

kumtoka. 

 “ Watoto wamekuwa watundu sana 

hawa.Kitu cha msingi ni kuwa makini sana 

nao na kama anapenda kuogelea basi 

afundishwe ” akasema Pauline. 

 “ Dah ! mwili wote unanitetemeka na 

sina nguvu hata kidogo “ akasema Yule 

mwanadada .Pauline akamshika mkono 

Yule binti na huku akitabasamu akasema 

 “ Jina lako nani ? 

 “ Naitwa Macline” 

 “ Ouh Macline.Una jina zuri sana.Sasa 

Macline siku nyingine usirudie tena 

kuingia katika bwawa kubwa kama hili 

.Hili ni maalum kwa ajili ya watu wazima.Kama unataka kuogelea muulize 

kwanza mama kama bwawa hilo linafaa 

kuogelea kwa watoto.” Pauline 

akamwambia Yule binti. 

 “ Sawa aunt” akajibu Macline 

 “ She’s a good girl” Pauline 

akamwambia mama yake Macline ambaye 

alionekana bado kuchanganyikiwa sana 

na tukio lile la binti yake kutaka kuzama 

katika bwawa la kuogelea. 

 “ Yaani mwili wote hauna nguvu na 

sijui hata kama nitaweza kuendesha gari” 

akasema Yule mwanadada 

 “ Kwani unaishi wapi mbali sana na 

hapa ? 

 “ Hapana si mbali sana” 

 “ I will take you home” akasema 

Pauline 

 “ Hapana ntampigia simu mume 

wangu aje atuchukue.” 

 “ Usijali dada yangu.Nitawapeleka 

nyumbani.NI kweli huwezi kuendesha gari 

ukiwa katika mstuko kama huo.Nisubiri 

dakika mbili nikabadilishe nguo nakuja” 

akasema Pauline na kupanda chumbani 

kwake akaenda kubadili nguo na kurejea 

wakaongozana hadi katika gari la Yule 

mwanadada na Pauline akawaendesha 

kuwarejesha  nyuambani 

  “ Yaani nimechanganyikiwa hadi 

nimesahau hata kukuuliza jina lako.Kwani 

unaitwa nani dada? Akauliza Yule mama 

 “ Mimi naitwa Pauline” 

 “ Nafurahi sana kukufahamu 

Pauline.Wewe ni mwenyeji wa wapi? 

 “ Mimi ni mwenyeji wa Arusha lakini 

nimekuja hapa Moshi kwa ajili ya 

mapumziko” 

 “ Karibu sana Moshi Pauline.Mimi 

naitwa Zita au mama Macline na huyu 

ndiye mwanangu wa pekee na nimempata 

kwa shida sana ndiyo maana unaniona 

nimechanganyikiwa namna hii kwa tukio 

lile.” Akasema mama Macline 

 Pauline akawaendesha hadi 

nyumbani kwao.Wakamkaribisha ndani 

ya jumba kubwa la kifahari.Tayari urafiki 

mkubwa ukaanza kujengeka kati 

yao.Wakati maongezi yamekolea mara 

akaingia kijana mmoja nadhifu sana 

aliyevaa suti nzuri nyeusi iliyomkaa 

vyema.Mara tu alipomuona Pauline 

akastuka sana na kumtazama kwa 

sekunde kadhaa. 

 “ Dady !! ” akasema Macline na 

kumkimbilia akamkumbatia 

 “ Wow Macline..Pole sana 

mwanangu” akasema Yule jamaa na kuinama akambusu binti yake halafu 

akamfuata mama Macline na 

kumbusu.Kisha akageuka na kumtazama 

Pauline 

 “ Habari yako dada” 

 “ Habari yangu nzuri” akajibu 

Pauline 

 “ Karibu sana” 

 “ ahsante sana” akajibu Pauline 

 “ Nimestuka sana uliponiambia 

Macline amepatwa na tatizo.Nini hasa 

kimetokea? Akauliza 

 “ Macline alitaka kuzama katika 

bwawa la kuogelea.Bahati nzuri Pauline 

alikuwepo karibu na ndiye aliyemuokoa” 

akasema mama Macline.Yule jamaa 

akamgeukia Pauline na kwenda kumpa 

mkono 

 “ Nashukuru sana kwa kuokoa uhai 

wa mwanangu” 

 “ Usijali kaka yangu.Ni Mungu alitaka 

niwe karibu na eneo lile ili nimsaidie 

Macline” akasema Pauline huku 

akitabasamu na vishimo vikaonekana 

katika mashavu yake. 

 “ By the way naitwa Alfred.Ni baba 

yake na Macline na huyu hapa ni mke 

wangu.Kwa niaba ya familia yangu 

ninapenda sana kukushukuru kwa jambo 

hili kubwa ulilotusaidia.Huyu ni binti yetu 

wa pekee na jicho letu sote liko 

hapa.Tunashukuru sana” akasema 

Alfred.Pauline hakujibu kitu akabaki 

anatabasamu. 

 Maongezi yaliendelea kidogo na 

kisha Pauline akaaga ili aondoke 

 “ Ouh mbona mapema sana.Hutaki 

kuendelea kukaa nasi ? 

 “ Nimekwisha kaa vya kutosha .Kuna 

sehemu ninataka kwenda” akasema 

Pauline 

 “ Ok basi usijali hata mimi nilirejea 

mara moja kuja kumuona Macline na kwa 

sasa ninarejea tena kazini.Kama hutojali 

ninaomba nikusaidie usafiri” 

 “ Ahsante nitashukuru sana” 

akasema Pauline na kuagana na mama 

Macline kisha akaongozana na Alfred hadi 

katika gari akamfungulia mlango 

wakaondoka. 

 “ Unaishi wapi Pauline? Akauliza 

Alfred.Pauline akatabasamu kidogo na 

kusema 

 “ Mimi ninaishi hotelini kwa sasa.” 

 “ Hotelini? Alfred akashangaa 

 “ Ndiyo ninaishi hotelini” 

 “ Kwani wewe si mwenyeji wa hapa? 

Akauliza Alfred  “ Hapana mimi si mwenyeji wa hapa 

.Nimekuja hapa Moshi kwa mapumziko” 

akajibu Pauline 

 “ Ouh karibu sana Moshi.Mji huu ni 

mzuri sana na nina imani utakuwa na 

mapumziko mazuri” 

 “ Ahsante sana” akajibu Pauline na 

safari ikendelea. 

 “ Pauline narudia tena kukushukuru 

kwa kuniokolea mwanangu leo.Ninakuona 

kama malika ambaye Mungu alikutuma 

uje ulinde uhai wa mwanangu.Bila wewe 

sasa hivi tungekuwa katika vilio.Sijui 

nitumie neno gani kukushukuru zaidi ya 

ahsante sana.Pamoja na shukrani zangu 

hizi kubwa nina ombi moja 

kwako.Ninaomba mimi na familia yangu 

tuwe wenyeji wako katika kipindi chote 

utakachokuwa hapa Moshi.Tafadhali 

Pauline usiseme hapana.Tuna deni kubwa 

kwako na itakuwa ni furaha yetu kuwa 

wenyeji wako.” akasema Alfred.Pauline 

akacheka kidogo na kusema 

 “ Sina hakika kama nitahitaji 

mwenyeji.Ninaufahamu vizuri mji wa 

Moshi kwa hiyo hautanipa shida 

yoyote.Nashukuru hata hivyo kwa 

kujitolea kuwa mwenyeji wangu.”  “ Tafadhali usiseme hivyo 

Pauline.Itakuwa ni furaha yetu sisi kuwa 

wenyeji wako.Tafadhali naomba ulifikirie 

suala hili” akasema Alfred.Pauline 

akatabasamu na vishimo vikaonekana 

katika mashavu yake 

 “ Gosh ! She’s very beautifull.” 

Akawaza Alfred huku akimuangalia 

Pauline kwa jicho la wizi. 

“ Pauline unasemaje kuhusu ombi langu? 

Akasema Alfred baada ya Pauline kutojibu 

chochote .Pauline akatabasamu na 

kusema 

 “ Kama sintakuwa mzigo kwenu basi 

nitafurahi sana” 

Jibu lile la Pauline likamfurahisha sana 

Alfred na kumfanya aachie tabasamu pana 

 “ Nashukuru sana Pauline kwa jibu 

lako zuri.Ni heshima kwetu kuwa na 

mgeni kama wewe” akasema 

Alfred.Pauline hakujibu kitu akatabasamu 

na kuendelea kutazama pembeni. 

 “ Dah ! mtoto huyu ni mzuri sijapata 

kuona.Ninaogopa hata kumtazama 

machoni kwa namna 

anavyonisisimua.Mwili wake mzuri kama 

umechongwa vile.Sauti yake laini kama 

kinanda na inayopenya masikioni mpaka moyoni.Tabasamu lake linaweza likakupa 

kiwewe.Kila anatapotabasamu 

anaonekana ni kama malaika.Hata 

anavyotembea ni kama vile hataki 

kukanyaga chini.Kwa hapa mwenyezi 

Mungu anapaswa kusifiwa sana kwa 

kumpendelea kimwana huyu uzuri wa 

kipekee kabisa.Dah ! mbona ninaanza 

kuwekwa majaribuni? Akawaza Alfred 

 “ No ! Alfred usiruhusu mawazo haya 

mabaya ndani ya kichwa chako.Usiruhusu 

tamaa ikutawale” Alfred akasikia kama 

sauti ikimwambia.Akageuka na 

kugonganisha macho na Pauline wote 

wakajikuta wakitabasamu 

 Walifika katika hoteli aliyofikia 

Pauline na mara tu baada ya kuegesha gari 

katika maegesho Alfred akafungua mlango 

na kushuka haraka akaenda kumfungulia 

Pauline mlango. 

 “ Ahsante sana Alfred “ akajibu 

Pauline huku akitabasamu 

 “ Ahsante pia Pauline.Nategemea 

kuanzia sasa tutakuwa tukionana mara 

kwa mara.” Akasema Alfred 

 “ Usijali Alfred.Nitakuwa nikija mara 

kwa mara kuwatembelea” akasema 

Pauline  “ By the way can I get your phone 

number ? Akasema Alfred.Pauline 

akatabasamu tena kama kawaida yake na 

kusema 

 “ Kwa sasa niko mapumzikoni na 

nimeamua kutotumia simu kabisa.Kama 

mkinihitaji basi mtapiga simu ya hapa 

hotelini na wataniunganisha chumbani 

kwangu” akasema Pauline 

 “ Sawa.Ahsante sana Pauline na 

ninakutakia mchana mwema” akasema 

Alfred na Pauline akaanza kupiga hatua 

kuelekea ndani ya jengo la hoteli.Alfred 

alikaa ndani ya gari akimtazama Pauline 

anavyotembea kwa madaha akiingia ndani 

ya jengo la hoteli .Kama vile alijua 

anaangaliwa Pauline alitembea mwendo 

wa madaha sana . 

 “ Dah ama kweli duniani humu kuna 

wanawake wamependelewa uzuri.Huu wa 

Pauline ni zaidi ya uzuri.Najuta sijui kitu 

gani kilinirudisha nyumbani na 

kunikutanisha na jaribu hili kubwa.” 

Akawaza Alfred na kuwasha gari lake 

akaondoka 

 “ Nina hamu sana ya kutaka kumjua 

kwa undani Pauline.Ni mischana mwenye 

haiba ya aina yake na kwa hili siwezi 

kupingana na nafsi yangu kwamba amenisisimua sana.Nina mke na mtoto na 

siku zote nimekuwa nikijitahidi sana 

kupambana na vishawishi mbali mbali 

vinavyoweza kunifanya nikatenda dhambi 

ya usaliti kwa mke wangu lakini jaribu hili 

la leo naona limekuwa kubwa na kali sana 

kushinda yote na nakuna uwezekano 

ninaweza nikaanguka dhambini.” 

Akawaza Alfred akiwa njiani kuelekea 

katika shughuli zake.Toka alipoonana na 

Pauline kwa mara ya kwanza amekuwa 

katika hali ya tofauti . 

 Kwa upande wa Pauline baada ya 

kuagana na Alfred alipanda hadi 

chumbani kwake na kujitupa sofani. 

 “Siku yangu ilianza vibaya lakini 

kidogo imebadilika na nimekuwa na 

furaha kwa kitendo 

nilichokifanya.Nimeokoa maisha ya 

Macline.Hili ni jambo kubwa.Binafsi nina 

furaha sana kwa jambo lile nililolifanya na 

hasa baada ya kuwaona wazazi wake 

namna walivyokuwa na nyuso za 

tabasamu baada ya kumuokoa mtoto wao” 

akawaza Pauline na mara sura ya Alfred 

ikamjia 

 “ Alfred!!..akasema kwa sauti ndogo 

 “ He’s such a gentleman and a loving 

husband.Anaonekana kuijali sana familia yake.Natamani siku moja na mimi niwe na 

mume kama Alfred mwenye kujali na si 

hawa wadanganyifu ambao wana tamaa 

kama ya fisi.” Akawaza Pauline na mara 

akakumbuka namna wote walivyojikuta 

wakitabasamu ndani ya gari pale 

walipokutanisha macho. 

 “ He is handsome too.Ouh No ! 

sitakiwi kuanza kuwa na mawazo hayo 

kwa sasa.Ninachotakiwa kukifanya kwa 

sasa ni kujitahidi kupanga mipango mizuri 

ya maisha yangu ya mbeleni” akawaza 

huku akitabasamu na kupiga simu hotelini 

akaagiza apelekewe matunda. 

************************ 

 David aliwahi sana kufika ofisini 

kuliko kawaida yake.Pamoja na kuwahi 

kufika ofisini lakini bado alishindwa 

kufanya kitu chochote.Aliegemea kiti 

chake na alionekana kuwa na mawazo 

mengi sana 

 “ Usiku wa leo ulikuwa mrefu mno 

kwangu.Sikuweza kabisa kupata 

usingizi.Kitendo nilichokifanya na madam 

Vicky jana kimeninyima amani sana kiasi 

kwamba ninaogopa hata kuonana na mzee Zakaria.NImefanya usaliti mkubwa sana 

ambao sijui nitaificha wapi sura yangu 

pindi mzee Zakaria akigundua jambo 

nililomfanyia.Ninaumia sana moyoni.” 

Akawaza David 

 “ Yule mwanamke bila hata haya 

bado ananitumia ujumbe na eti anataka 

kuja chumbani kwangu.Hamuheshimu 

mume wake hata kidogo.Kitendo cha mimi 

kufanya naye mapenzi jana 

kimemuaminisha kwamba anaweza 

akanitumia kila pale anapotaka.Hapana 

sitaki jambo hili liendelee lazima lifike 

mwisho.Ni bora nikaishi maisha ya 

kawaida kuliko kuendelea kuishi maisha 

ya kitajiri lakini ndani yake yakiwa 

yamejaa usaliti mkubwa sana.I must end 

this” akawaza Alfred na mara akiwa katika 

mawazo simu yake ikaita akatazama 

mpigaji alikuwa ni Vicky madhahabu 

 “ Tayari ameanza mambo 

yake.Atakuwa amenitafuta akanikosa na 

ndiyo maana ameamua kunipigia 

simu.Dah ama kweli nimejiingiza mahala 

kusiko.Huyu mwanamke hajali kitu na 

anaweza akanisababishia matatizo 

makubwa.Lazima nimzuie haraka 

iwezekanavyo.” Akawaza David na simu ikaendelea kuita bila kupokelewa.Baada 

ya muda ukaingia ujumbe mfupi 

 “ Halow sweetie.Mbona hutaki 

kupokea simu yangu? Au kuna kitu 

nimekuudhi baby? Tafadhali usinifanyie 

hivyo.Nimekukosa asubuhi hii na nilitaka 

tu niisike sauti yako.I love you” 

 Ndiyo ulivyosomeka ujumbe 

ule.David akasonya na kuufuta ujumbe ule 

na kuendelea na kazi zake 

 “ Sijui Pauline atakuwa wapi mida hii 

.Nasikitika sana kwani mimi ndiye 

niliyesababisha hadi akaondoka 

nyumbani kwao.Yote hii ni kwa sababu ya 

Vicky” akawaza na mara akamkumbuka 

Tamia. 

 “ Ngoja niwasiliane na Tamia kwani 

toka jana sijawasiliana naye .” 

 Baada ya kuwasiliana na Tamia 

,David aliendelea na kazi zake kama 

kawaida na ilipotimu saa tano mlango wa 

ofisi yake ukafunguliwa bila ya hodi na 

Vicky madhahabu akaingia.Siku hii 

alikuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu 

na fulana nyeupe iliyombana na kama 

kawaida yake alikuwa anang’aa kwa vito 

vya dhahabu alivyojipamba kila kona ya mwili wake.Moja kwa moja akamfuata 

David na kumbusu 

 “ Vicky unafanya nini? Hii si sehemu 

sahihi ya kufanya kitu kama hiki? Humu 

ofisini wanaingia watu wengi na 

wanaweza wakatuona wakapeleka taarifa 

kwa mzee.” Akasema David akionyesha 

kutokifurahia kitendo kile cha kupigwa 

busu na Vicky 

 “ Usiogope chochote David.Hakuna 

chochote kinachoweza kutokea na wala 

usimuogope Zakaria.Yule mimi ndiye 

kiboko yake na kwangu mimi hana kauli 

yoyote.Muda mrefu sana nilikwisha 

mfunga ulimi.Hata akisikia kwamba 

ninatembea na wewe hatakuwa na lolote 

la kusema.Aseme nini wakati anajua fika 

kwamba hawezi kunitimizia mahitaji 

yangu? Anyway tuachane na hayo,habari 

za toka jana? Uliwahi sana kulala jana na 

hata nilipokutumia ujumbe hukujibu.” 

 “ Nilichoka sana jana na ndiyo maana 

nikawahi kulala,na hata hivyo kichwa 

changu hakikuwa vizuri jana” 

 “ Pole sana my love.Ulichoka 

kutokana na shughuli nzito ya 

jana.Nisikufiche David jana ulifanya kazi 

kubwa sana.Jana ulinifikisha mahala 

ambako hakuna mwanamume amewahi kunifikisha.Niliishiwa hata hamu lakini 

nilipopanda kitandani nikajikuta 

nikiwashwa tena na ndiyo maana 

nikakutumia ule ujumbe.Niliteseka sana 

usiku na nilitamani nikufuate usiku ule 

walau unikate kiu.David wewe ni wa 

pekee sana.Hakuna wa mfano 

wako.Asubuhi nilipoamka kitu cha 

kwanza ni kuja kukutafuta lakini 

hukuwepo ,nikakupigia simu hukupokea” 

akasema Vicky 

 “ Niliamka mapema sana leo kuna 

kazi ambazo sikuwa nimezimaliza siku ya 

jumamosi na ndiyo maana nikaona ni bora 

endapo nikawahi asubuhi nimalizie.Si 

unajua tena siku ya jumatatu inakuwa na 

mambo mengi.Uliponipigia simu nilikuwa 

nimeshuka kule chini.” 

 “ Basi usijali honey.Mimi nimepita tu 

mara moja kuja kukuona na kuhakikisha 

uko salama na hakuna 

kinachokusumbua.Nimefurahi uko mzima 

lakini mchana wa leo nitakuomba tutoke 

wote kwa ajili ya chakula cha mchana 

maalum kabisa kwa ajili yetu.” Akasema 

Vicky.David akataka kusema kitu lakini 

Vicky akamzuia 

 “ Please David don’t say no” 

David akatabasamu kidogo na kusema  “ Ok sawa tutaonana hiyo mchana” 

akajibu David na Vicky akamsogelea 

karibu akambusu na kuondoka.David 

akabaki ameduwaa akimtazama 

 “ Sifahamu ni kwa nini mzee Zakaria 

aliamua kuoa mwanamke kama huyu 

ambaye hana mapenzi yoyote kwake zaidi 

ya kuhitaji fedha zake.Mwanamke hatari 

sana huyu.Anadiriki kutamba kabisa 

kwamba mzee Zakaria hana kauli yoyote 

kwake kwani tayari amekwisha mfunga 

mdomo.Nina wasi wasi huyu mwanamke 

atakuwa akitumia uchawi pia kuweza 

kumpumbaza mzee Yule na ndiyo maana 

ana uwezo wa kufanya lolote lile bila ya 

kuulizwa.Ni kweli mzee Zakaria 

anasumbuliwa na maradhi na kutokana na 

maradhi aliyonayo anaweza akawa na 

tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume 

lakini hii si sababu ya kumfanyia 

hivi.Kama mke alitakiwa ashikamane na 

mume wake hadi mwisho.Hili ni tatizo la 

kudanganywa na sura na kusahau 

kwamba uzuri wa mwanamke si sura bali 

ni tabia alizonazo.Nadhani hapa mzee 

Zakaria alidanganywa na uzuri wa sura . 

Kwa sura mtu yeyote Yule anaweza 

akadanganyika na uzuri wa Vicky.Kwa 

uzuri wa sura na umbo mwanamke huyu amebarikiwa na kila mwanaume rijali 

lazima atetemeke lakini kwa ndani 

mwanamke huyu ni nyoka mwenye sumu 

kali sana na hafai hata kidogo kuwa 

mke.Kwake yeye pesa ni kitu cha muhimu 

kuliko vyote.Lakini siku zake zinakaribia 

.Mwisho wa uovu wake uko karibu sana” 

akawaza David. 

 Alipoondoka ofisini kwa David ,Vicky 

akaelekea moja kwa moja kwa Safia 

ambaye ni rafiki na mshauri wake 

mkubwa . 

 “ Wow ! Mtoto wa dhahabu.Karibu” 

Safia akamkaribisha Vicky ,akamchukua 

hadi katika chumba kidogo cha pembeni 

 “ Karibu sana Vicky” akasema Safia 

 “ Ahsante sana Safia.” 

 “ Mambo yanakwendaje Vicky? 

Naona leo uso wako haukaukiwi 

tabasamu.Hebu nijuze kulikoni? Akasema 

Safia 

 “ Shoga yangu nimekupitia hapa 

twende mahala kuna jambo kubwa nataka 

tuongee” 

 Safia akamtazama Vicky kwa makini 

na kusema 

 “ Vicky kwema huko lakini? 

 “ Kwema Safia wala usijali.”  “ Haya kama hakuna tatizo twende 

tuondoke nikasikie hilo jambo kubwa” 

akasema Safia wakaingia garini na 

kuondoka.Moja kwa moja wakaelekea 

katika hoteli moja ambayo iko eneo la 

Ngaramtoni. 

 “ Enhee niambie Vicky .Mpaka 

umenileta huku lazima kuna jambo 

kubwa”Safia akaanzisha mazungumzo 

 “ Ni kweli Safia.Nimekuleta huku 

mahala ambako hakuna watu na kutokana 

na unyeti wa suala nnalotaka kukueleza 

huku kunafaa sana” akasema Vicky na 

kunywa mvinyo kidogo akaendelea 

 “ Safia wewe ndiye mshauri wangu 

mkubwa na ninaweza kusema kwamba 

wewe umechangia sana katika mafanikio 

yangu.Umekuwa unanishauri mambo 

yangu mengi na yote uliyonishauri 

yamefanikiwa na yanakwenda vizuri 

sana.Kwa hilo ninapenda sana 

kukushukuru .” Akanyamaza akanywa 

funda moja la mvinyo akaendelea 

 “ Mara ya mwisho umenishauri 

kuhusiana na David na kwa kweli baada ya 

kuufuata ushauri wako mambo 

yamekwenda vizuri sana.Hii ni sababu 

ambayo inanifanya niwe na tabasamu kila 

dakika.Pamoja na mambo yangu kwenda vizuri sana kwa kumtumia David lakini 

kuna suala limejitokeza.” Akasema Vicky 

akanywa tena funda moja la mvinyo halafu 

akaendelea 

 “ Kama unakumbuka ulinishauri 

nijenge ukaribu na David na hili nililifanya 

na nikafanikiwa kumuweka 

karibu.Ukaribu huo umekwenda mbali 

zaidi.Jana nimejivinjari naye” 

 “ What ?!..Safia akashangaa 

 “ Usishangae Safia.Huu ulikuwa ni 

ushauri wako.Jana nimeshindwa 

kuvumilia na nikalazimika kumvulia nguo 

David.Safia najua utanishangaa sana na 

sijui hata nikueleze vipi lakini nilikuwa 

nimezidiwa na sikuwa na namna nyingine 

ya kufanya zaidi ya kumpa mwili wangu 

David anikate kiu.Kitu cha ajabu David 

Yule ambaye nilikuwa nikimdharau awali 

alinilionyesha mambo 

makubwa.Amenichanganya akili yangu 

mno.David ni kijana ambaye ndiye Yule 

niliyekuwa namtafuta kwa muda 

mrefu.Ninakuapia katika kuzunguka 

kwangu na wanaume mbali mbali sijawahi 

kukutana na mwanaume kama David.Ni 

mwanaume wa kipekee kabisa.Alinikuna 

ipasavyo.Alinifikisha mahala ambako 

sijawahi kufikishwa na mwanaume yeyote Yule katika maisha yangu.Yeye ni 

mwanaume wa kwanza kunifanya 

nikayafurahia mapenzi.Hawa wengine 

walikuwa wananipapasa tu lakini David 

alinikuna pale panapotakiwa” Akasema 

Vicky.Safia akatabasamu akanywa funda 

kubwa la mvinyo akasema 

 “ Dah ! katika kipindi chote ambacho 

nimekufahamu sijawahi kukusikia hata 

siku moja ukimsifia mtu yeyote ambaye 

umewahi kutembea naye.Hii ni mara 

yangu ya kwanza kukusikia ukimsifia 

mwanaume tena kwa kumwagia sifa kede 

kede.” 

 “ Umesema kweli Safia.Huwa sina 

tabia hiyo lakini kwa mambo ambayo 

alinifanyia David jana sina budi kumsifu.” 

 “ Vipi kuhusu Pauline? Hawezi 

kugundua lolote? 

 “ Pauline hayupo na hata kama 

angekuwepo asingefanya lolote kwani 

tayari walikwisha korofishana na hakuna 

kinachoendelea kati yao.” 

 “ Sikulifahamu hilo .Nini kilitokea na 

kusababisha wakakorofishana ndani ya 

kipindi kifupi namna hii? 

 “ Pauline aligundua kwamba David 

anatembea na rafiki yake Tamia kwa hiyo wakafarakana na ameamua kuondoka 

nyumbani.” 

 “ Ouh kumbe amekimbia na 

kukuachia uwanja ujinafasi 

mwenyewe.Sasa una mpango gani shoga 

yangu?Nini umepanga kukifanya kuhusu 

huyu David? 

 “ Nina mpango mkubwa sana na 

ambao nataka unishauri vizuri.” 

 “ Niambie tu Vicky niusikie huo 

mpango nitakushauri” akasema 

Safia.Vicky akanywa mvinyo kidogo na 

kuendelea 

 “ Safia pamoja na maisha mazuri 

ninayoishi lakini kwa kipindi kirefu 

nimekosa furaha kabisa katika maisha 

yangu.Nimechoshwa na Yule mzee.Najua 

ananipenda na ananijali sana,ananipatia 

kila kitu lakini kuna mambo mengine 

hawezi kunitimizia.Kwa sasa kutokana na 

matatizo yake ya kisukari na magonjwa 

mengine amepungukiwa kabisa nguvu za 

kiume.Mimi bado kijana na ninahitaji 

kutimiziwa mahitaji yangu yakiwemo ya 

tendo la ndoa.Ninateseka sana na ndiyo 

maana nimekuwa nikiruka ruka huko na 

huko kwa wanaume mbali mbali kutaka 

kutimiziwa haja zangu lakini kutokana na 

hali ya sasa ninaogopa kupata magonjwa kutokana na kutembea na wanaume 

mbalimbali tofauti tofauti kwa hiyo basi 

nimeamua kufanya maamuzi.” 

Akanyamaza akanywa funda la mvinyo 

 “ Kwa sasa ninaamini tayari 

nimekwisha mpata Yule ambaye 

nimekuwa nikimtafuta kwa miaka 

mingi,mwanaume wa ndoto zangu na huyu 

ni David kwa hiyo basi nimeamua 

sintokubali aondoke katika mikono 

yangu.Ninataka niwe naye katika maisha 

yangu.Ninaamini nitakuwa na furaha sana 

kama nitakuwa naye maishani.” 

 “ Mhh ! Hilo litawezekana vipi Vicky? 

Kwa sasa wewe bado ni mke wa 

mtu.Hutakiwi kuwaza kitu kama 

hicho.Unachotakiwa kufanya ni kujenga 

mazingira mazuri ambayo yatakuwezesha 

uwe unamtumia David kukata kiu yako na 

si kufikiria kuishi naye.Hilo haliwezekani 

kwa sasa labda uamue kuachana na mzee 

Zakaria” akasema Safia 

 “ Ni kama ulikuwa katika mawazo 

yangu Safia.Nitaachana na mzee Zakaria” 

 “ Kama utaachana naye sawa lakini 

utaachane naye vipi? Utafunga tu mizigo 

na kuondoka zako? Ukumbuke Yule ni 

mumeo wa ndoa na zaidi ya yote ana 

utajiri mkubwa ambao unaweza ukaukosa pindi ukiamua kufunga mizigo yako na 

kuondoka” akasema Safia 

 “ Ndiyo maana nakupenda shoga 

yangu.Huwa unanishauri mambo mazuri 

sana.Kwa kweli siko tayari kuondoka na 

kuuacha utajiri ule mkubwa.Kwa sasa 

mzee Zakaria ni mgonjwa na ombi langu 

kila siku ni mzee Yule afariki ili niweze 

kurithi mali zote lakini kadiri siku 

zinavyokwenda anazidi kupata nafuu na 

anazidi kukwamisha mipango yangu ya 

mimi kuishi maisha ya furaha.Kwa hiyo 

basi nilichofikiria ni kumuua mzee 

Zakaria” 

 “ What ?!..Safia akastuka sana na 

kuweka mikono kichwani 

“ Mbona umestuka sana Safia ? akauliza 

Vicky 

 “ Shoga kwa hili nililolisikia 

unadhani nitashindwa kustuka? 

Sikutegemea kama siku moja unaweza 

ukawaza jambo kubwa kama hili.Tafadhali 

Vicky naomba uachane kabisa na mpango 

huo unaotaka kuufanya.Ni kitu hatari 

sana” akasema Safia akiwa bado 

amemtumbulia macho Vicky ambaye 

alitabasamu na kusema 

 “ Relax Safia.Hata mimi nilipoanza 

kulifikiria suala hili nilipatwa na wasi wasi sana kama ulioupata wewe lakini 

baadae nikapata ujasiri.Kwa hiyo 

usiogope sana hili ni suala ambalo 

nimelifikiria na kulipanga kwa umakini 

mkubwa.” Akasema Vicky 

 “ Pamoja na hayo Vicky mimi kama 

rafiki yako sikushauri hata kidogo wewe 

ufanye hivyo unavyotaka kufanya.Ni 

dhambi kubwa.Ni heri ukachukua begi 

lako ukaondoka zako kuliko kutaka 

kumuua mzee wa watu.” 

 “ Safia hebu tuliza akili yako na 

uelewe kile ninachokueleza.Kuendelea 

kukaa na mzee Yule ni kuendelea kujitesa 

tu na kujinyima fursa nyingi za 

kuyafurahia maisha yangu .Ukiwema 

nifunge mizigo yangu na kuondoka 

nitamuachia nani mali zile zote? Hapana 

siwezi kukubali kuziacha zile mali .Nataka 

niachane na mzee Zakaria na papo hapo 

niupate utajiri ule mkubwa.Sikufichi Safia 

mzee Zakari ana utajiri mkubwa sana na 

sipati picha siku akifa na mimi kuumiliki 

utajiri ule mkubwa.Unadhani nikifanikiwa 

kuupata utajiri ule mkubwa nitaweza 

kukusahau wewe rafiki yangu? Lazima 

nikuondoe hapa ulipo na wewe uishi 

maisha ya kitajiri.Nitakapofanikiwa mimi 

basi tumefanikiwa sote Safia.Tafadhali naomba usinivunje moyo katika suala 

hili.” Akasema Vicky 

 “ Vicky amevuka mipaka.Yaani 

kumuibia kote anakomuibia Yule mzee 

hakujatosha na sasa anataka hata amuue 

kabisa ili arithi mali.Hii ni tamaa 

iliyopitliza.Hapana siwezi kuwa sehemu ya 

mpango wake huu muovu .lakini hata 

kama nikimkatalia mimi, tayari roho ya 

uuaji imemuingia na lazima atautekeleza 

tu mpango wake.Hakuna ninaloweza 

kumweleza likambadili mawazo.Ngoja 

nijifanye nimekubaliana na mpango wake 

kwa sasa lakini lazima nitafute namna ya 

kuweza kumzuai asifanye ujinga huu 

anaotaka kuufanya” akawaza Safia 

 “ Safia say something!! Akasema 

Vicky.Safia akatabasamu na kusema 

 “ Nilikuwa nakutania Vicky 

kukupima kama kweli umedhamiria 

kufanya hicho ulichokisema” 

 “ Ni kweli nimedhamiria 

Safia.Mateso ninayoyapata kwa kuishi na 

mzee Yule hakuna awezaye kuyafahamu 

kwa hiyo hili pekee ndilo litakuwa 

suluhisho la matatizo yangu na matatizo 

yetu kwa ujumla.Kama jambo hili 

litafanikiwa basi mimi na wewe tutaogelea 

katika bahari ya utajiri mkubwa.Sintakuacha shoga yangu 

nitakufanyia mambo makubwa 

sana.Ninachokuomba toka kwako ni 

kuniunga mkono tu katika suala hili na 

kunishauri vizuri” 

 “ Siwezi kukupinga hata siku moja 

Vicky katika jambo lolote ambalo linaweza 

kuwa la manufaa kwako kwani 

ninafahamu ukipata wewe na mimi 

nimepata pia.Kwa hiyo usijali mimi niko 

bega kwa bega nawe katika suala hili.Kwa 

hiyo umepanga kuufanyaje mpango huu 

kwani huu si mpango mdogo.Hili ni suala 

zito na linalohitaji umakini na unyeti wa 

hali ya juu sana” akasema Safia 

 “ Ahsante sana Safia kwa kukubali 

kuniunga mkono.Ni kweli suala hili ni zito 

na linalohitaji unyeti na umakini na ndiyo 

maana sijamweleza mtu yeyote Yule zaidi 

yako kwani wewe ndiye msiri wangu 

mkubwa.Kuhusu namna 

nitakavyoutekeleza mpango huu 

nimefikiria mambo mengi sana lakini 

nimekosa jibu.NImefikiria kumkaba usiku 

Yule mzee na kumuua kabisa lakini 

nimeogopa kwani unaweza ukafanyika 

uchunguzi na ikabainika kwamba 

amekabwa na mimi nitakuwa matatani na 

nitakosa kila kitu.Nimefikiria kumuwekea pia sumu lakini hata hii njia bado si 

nzuri.Nimefikiria mambo mengi lakini 

kuna jambo moja ambalo ninaona 

linaweza likafaa.Nimefikiria kutumia 

majambazi” akanyamaza akanywa mvinyo 

kidogo na kusema 

 “ Nimefikiria kukodisha kikundi cha 

majambazi ambao nitawalipa hela na 

watakachokifanya ni kuvamia nyumba na 

kisha watamuua Zakaria kwa risasi na 

mimi nitapigwa na kuumizwa vibaya na 

wataondoka na kiasi kikubwa cha 

pesa.Mpango huu hautakuwa na mashaka 

hata kidogo kwani itaonekana ulikuwa ni 

uvamizi wa kawaida .Unaonaje kuhusu 

mpango huu? Akauliza Vicky.Safia 

akafikiri na kusema 

 “ Sawa ni mpango mzuri na unaweza 

usilete shaka endapo utampata mtu sahihi 

anayeweza akautekeleza mpango huo.Mtu 

ambaye unatakiwa umpatie kazi hiyo 

anatakiwa awe ni mtu makini sana na 

ambaye hataacha watu wakiwa na alama 

za viulizo.” 

 “ Hapo ndipo ninapotaka 

unisaidie.Kama unakubaliana na njia hii 

basi nitaomba unisaidie kumtafuta mtu 

ambaye nitaweza kumkabidhi hii 

kazi.Wewe unafahamiana na watu wengi.” Akasema Vicky.Baada ya sekunde kadhaa 

za tafakari,Safia akasema 

 “ Kuna mtu ninamfahamu ingawa 

mimi na yeye hatuna mahusiano yoyote 

lakini nimemfahamu kupitia rafiki yangu 

Fulani ambaye aliwahi kuwa na 

mahusiano na mtu huyo ingawa kwa sasa 

wamekwisha achana na sababu kubwa 

iliyowatenganisha ni kwamba aligundua 

huyo jamaa ni jambazi mkubwa sana na 

ana mtandao mkubwa.Kazi zake ni 

kuvamia na kupora mabenki na wafanya 

biashara wakubwa wakubwa .Ninadhani 

mtu huyo kama ukionana naye anaweza 

akakufaa sana” akasema safia 

 “ Niambie ni nani huyo jamaa na 

nitamfuata mimi mwenyewe” akasema 

Vicky 

 “ Ninadhani utakuwa 

ukimfahamu.Anaitwa Chino Yule mmiliki 

wa vituo vya mafuta vya Chino Oil.” 

 “ Chino?!...Vicky akashangaa 

 “ Ndiyo .” 

 “ Ouh my Gosh ! kama ni Chino 

mbona ninamfahamu sana Yule kaka? Ni 

rafiki yangu wa muda mrefu ila sikuwa 

nikifahamu kama anashughulika na kazi 

hizi”  “ Kwa kumtazama huwezi kabisa 

kuhisi kama anaweza kuwa ni mtu 

anayeweza kujishughulisha na mambo 

kama haya kwanza kwa namna alivyo na 

pili kwa utajiri alionao.Lakini nasikia ni 

mtu hatari sana Yule kwa wanaomfahamu” 

 “ Basi nitamfuata .Nitaongea naye na 

nina imani tutaelewana tu” akasema Vicky 

 “ Vipi kuhusu David yeye 

utamfahamisha kuhusu jambo hili? 

Akauliza Safia 

 “ Hapana Safia.Sintomfahamisha 

David chochote kuhusu suala hili.Hii 

itakuwa ni siri yangu mimi na na wewe 

tu.Wa tatu atakuwa ni mtu atakayeifanya 

hiyo kazi.Zaidi ya hapo hakuna mwingine 

atakayefahamu chochote.” 

 “ Vizuri sana,Usimweleze chochote 

kile.Hawa vijana si wa kuamini kabisa” 

akasema Safia na halafu wakaendelea na 

maongezi mengine kuhusiana na mpango 

ule



Saa sita na nusu za mchana,mlango 

wa ofisi ya David ukagongwa na 

akamruhusu mgongaji aingie ndani.David akajikuta akitabasamu baada ya kuiona 

sura ya binti mwenye uzuri wa kipekee 

Tamia akiwa amesimama mbele yake.Siku 

hii alivaa mavazi meupe 

yaliyompendezesha sana 

 “ Hallow sweetie !! akasema Tamia 

huku akiitanua mikono yake akamfuata 

David na kumkumbatia kisha 

wakabusiana 

 “ Hallow Tamia..Karibu sana” 

 “ Ahsante sana David..Mzima lakini? 

 “ Mimi mzima kabisa,hofu kwako.” 

 “ Hata mimi mzima kabisa” 

 “ Samahani kwa kukuvamia bila 

taarifa lakini nimeshindwa kukaa ofisini 

kwa kutoiona sura yako toka 

jana.Nimekuja nikuone roho yangu itulie 

lakini vile vile kukuchukua kwenda 

lunch..” akasema Tamia.David 

akatabasamu 

 “ Hata mimi nimekuwa nakuwaza 

sana Tamia.Nilitamani sana kama 

ningekuona leo na ninashukuru umekuja.” 

Akasema David huku akivaa koti lake na 

kufunga ofisi wakaondoka kwenda kupata 

chakula cha mchana. 

 Dakika kumi tu baada ya David na 

Tamia kuondoka kwenda kupata chakula 

cha mchana Vicky madhahabu akawasili 

Moja kwa moja akaelekea katika ofisi ya 

David lakini ilikuwa 

imefungwa.Akashangaa sana 

 “ David kaenda wapi wakati 

nilimwambia kwamba mchana nitakuja 

kumchukua tukapate chakula ? akajiuliza 

Vicky na kuchukua simu yake akampigia 

David lakini haikuwa ikipatikana. 

 “ Mbona hata simu yake haipatikani? 

Akajiuliza na kisha akamfuata Agripina 

msichana ambaye naye anafanya kazi 

katika mojawapo ya miradi ya mzee 

Zakaria na kumuuliza kama amemuona 

David 

 “ Wakati nikipanda huku ofisini 

David nimekutana naye akishuka alikuwa 

na msichana mmoja rafiki wa Pauline” 

akasema Agripina.Vicky hakutaka 

maelezo zaidi kwani tayari alikwisha 

mfahamu alikuwa nani 

 “ Lazima atakuwa ni Tamia.” 

Akawaza huku akishuka ngazi kuelekea 

katika gari lake 

 “ Dah ! Huyu Tamia sasa ameanza 

kunikera na inanibidi naye nimuangalie 

kwa jicho la tatu kwani anaweza kuwa ni 

kikwazo kikubwa cha mimi kuwa na 

David.Kwa sasa ambapo nina mpango 

mkubwa na David sintakubali mtu yeyote awe ni kikwazo katika kuufanikisha 

mpango wangu wa kuwa na Yule 

kijana.Ngoja kwanza nione mwenendo 

wao na kama nikiona Tamia anakuwa ni 

kikwazo I’ll take her out of the 

picture.Kwa ajiliya david niko tayari kwa 

lolote lile” akawaza Vicky akavuta pumzi 

ndefu na kuwasha gari aaondoka 

 “ Nahisi moyo kunikereketa sana 

nikivuta taswira walipo David na Tamia 

muda huu.Yawezekana wakawa 

wamekumbatiana kimahaba,yawezekana 

Tamia akawa katika kifua cha David hivi 

sasa.Ouh No ! siwezi kukubali hali hii 

iendelee.David is mine and I don’t want to 

share him with anybody….Lazima nitafute 

namna ya kuweza kuwatenganisha David 

na Tamia na ninatakiwa kulifanya hili 

mapema sana kabla urafiki wao haujaota 

mizizi.” Akaendelea kuwaza Vicky 

 “ Natamani mida hii ningekuwa 

kifuani kwa David nikijivinjari 

naye.Mawazo haya ndiyo yanayonifanya 

nitake kuufanya haraka mpango 

wangu.Ngoja niende moja kwa moja kwa 

Chino nikajaribu kuongea naye nione 

kama anaweza kunisaidia.Nataka mpango 

huu uende haraka ili niweze kumiliki zile 

mali pamoja na David.Natamani sana nammi nianze kuitwa the boss lady.” 

akawaza Vicky na kuendesha gari moja 

kwa moja hadi katika kituo cha mafuta 

kinachomilikiwa na Chino akaomba 

kuonana naye lakini haikuwezekana kwa 

kuwa Chino hakuwepo nchini na 

angerejea baada ya wiki mbili.Hakuwa na 

namna nyingine ya kufanya zaidi ya 

kumsubiri hadi atakaporejea .Akaingia 

garini na kuondoka zake 

********************* 

 Baada ya kutoka katika ofisi za 

kanisa alikoenda kuonana na viongozi 

wake wa dini kwa ajili ya kupata ushauri 

wa namna ya kuweza kuitengua ndoa 

yake,Robin akaelekea moja kwa moja hadi 

shuleni anakosoma 

Penina.Kilichompeleka pale ni kuonana na 

mwalimu Lucy.Ilimlazimu kusubiri kidogo 

kwani mwalimu Lucy alikuwa katika kikao 

cha waalimu.Baada ya dakika kama 

ishirini hivi toka amewasili pale,mwalimu 

Lucy akatokea na akastuka baada ya 

kumuona Robin akiwa amekaa katika sofa 

za kupumzikia wageni. 

 “ Wow !.” akasema na kumfuata 

Robin akamshika mkono kisha akafungua mlango wa ofisi yake wakaingia akaufunga 

mlango na kumkumbatia Robin kwa nguvu 

 “ How are you my king” akasema 

mwalimu Lucy huku akimmwagia Robin 

mabusu mfululizo 

 “ I’m ok my queen.Unaendeleaje ? 

 “ Ninaendelea vizuri 

sana.Sikutegemea kama ungeweza kufika 

hapa mida hii” akasema mwalimu Lucy 

 “ Nimeshindwa kufanya kazi 

imenibidi nije niione kwanza sura yako 

ndipo mambo mengine yaendelee” 

akasema Robin na wote wakaangua 

kicheko. 

 “ Acha utani wako Robin.” 

 “ Anyway tuachane na hayo.Kwanza 

samahani kwa kuja bila taarifa na 

ninashukuru kwa kunipokea” akasema 

Robin na kumfanya mwalimu Lucy 

azidishe kicheko.Robin akaendelea 

 “Nimekuja kwa mambo mawili 

makubwa.Moja ni kukupa taarifa kwamba 

nimetoka kuonana na padre asubuhi hii 

.Nimeongea naye kwa kirefu sana 

,nimemueleza matatizo yote na amekubali 

kwamba nina vigezo vyote ambavyo 

vinafaa kuomba utenguzi wa ndoa 

yangu.Amenipa maelekezo ya kufuata na 

tayari nimekwisha anza hatua za awali.Ni mchakato mrefu kidogo na unaweza 

ukachukua muda lakini ninachoshukuru 

ni kwamba hata viongozi wa dini 

wamenielewa na wamekubaliana nami 

kwa hiyo uhakika wa suala hili kufanikiwa 

ni mkubwa japo litachukua muda 

.Sintachoka kumlilia Mungu suala hili 

lifanikiwe haraka ili mimi na wewe 

tuyaanze maisha yetu haraka 

iwezekanavyo.Vile vile nilikwenda 

kuonana na Vivian asubuhi ya leo 

kumuweka wazi kwamba tuanze taratibu 

za kutengua ndoa yetu.Kwa bahati nzuri 

hata yeye mwenyewe kumbe alikuwa na 

mawazo kama yangu ya kutaka ndoa yetu 

itenguliwe ili aweze kufunga ndoa na huyo 

mume wake .” akasema Robin 

 “ What happened when she saw you? 

Akauliza Lucy huku akitabasamu 

 “ Alistuka sana.Hakutegemea kabisa 

kuniona pale.” 

 “ Vipi maendeleo yake? Is she happy? 

Does she miss you? Akauliza Lucy 

 “ She is fine and happy.Anaonekana 

kuyafurahia sana maisha yake.Mimi 

hanikumbuki hata kidogo amekwisha 

nitoa kabisa katika akili yake” akasema 

Robin.Ukimya mfupi ukapita Robin 

akaendelea  “ Jambo la pili lililonileta hapa 

nataka twende Usa river.” 

 “ Usa river?!!..Mwalimu Lucy 

akastuka sana. 

 “ Ndiyo Lucy.Nataka twende Usa 

river katika kituo kile ulikomuacha 

Angela.Nataka tuanze mara moja safari ya 

kuutafuta ukweli kuhusiana na Angela” 

 Kalamu aliyokuwa ameishika 

mwalimu Lucy ikamponyoka ,viganja vya 

mikono vililoa jasho 

 “ Robin I’m so scared…I don’t think 

I’m ready” akasema mwalimu Lucy. 

 “ Ninafahamu hilo Lucy lakini lini 

basi utakuwa tayari? Uliamua kurejea 

Tanzania kwa ajili ya suala hili na toka 

wakati huo mpaka sasa bado haujapata 

ujasiri wa kuweza kuutafuta ukweli.Lucy 

muda ni huu,tuutumie kuutafuta 

ukweli.Mimi niko hapa na nitakusaidia 

kuutafuta na kuupokea ukweli.Nitakupa 

nguvu ya kuyakubali majibu yoyote 

tutakayoyapata” Akasema Robin 

 Mwalimu Lucy akainama na kuwaza 

ILimchukua zaidi ya dakika tatu Lucy 

kuinua kichwa akasema 

 “ Robin I’m not sure about this ,lakini 

sina namna nyingine ya kufanya ,twende 

Usa river.Siwezi kuukimbia ukweli.Jambohili nililifanya mwenyewe kwa hiyo lazima 

nikubaliane na ukweli wowote 

nitakaoupata” akasema mwalimu Lucy 

huku akiinuka na kuchukua mkoba wake 

akamuomba Adrian waongozane kwanza 

kuelekea nyumbani kwake ambako 

alijifungia chumbani kwake akakaa 

kitandani na kutafakari kwa kina kama ni 

kweli yuko tayari kwa suala lile mwishowe 

akaamua kuwa jasiri.Akabadili nguo 

wakaingia garini na kuondoka kuelekea 

Usa river 

 “ Lucy nafahamu suala hili ni gumu 

kwako lakini hatuna namna nyingine ya 

kufanya lazima tuutafute ukweli 

kuhusiana na Angela.Lazima tufahamu 

kama angela yuko hai na kama yuko hai 

yuko wapi? Kama ikitokea tukiambiwa 

kwamba alifariki lazima tukubaliane na 

ukweli huo na tusonge mbele. “akasema 

Robin 

 “ nakubaliana nawe Robin lakini 

moyoni nina wasi wasi sana.Ninakijutia 

kitendo kile nilichokifanya usiku 

ule.”akasema Lucy 

 “ Lucy kila kitu huwa kinatokea kwa 

sababu maalum kwa hiyo usijilaumu sana 

.Hukuwa na namna nyingine ya kufanya 

kwa wakati ule.” Akasema Robin  “ Robin siri hii unaifahamu wewe 

pekee,hakuna ambaye nimewahi 

kumueleza chochote kuhusu jambo 

hili.Kwa heshima niliyo nayo hivi sasa sijui 

nitauficha wapi uso wangu endapo jamii 

ikigundua kwamba niliwahi kumzaa mtoto 

nikamtelekeza na kukimbia.Please Robin 

naomba suala hili asilifahamu mtu 

mwingine yeyote zaidi yako” 

 “ Usijali Lucy.Hii ni siri yangu na 

hakuna yeyote atakayefahamu” akasema 

Robin na safari ikaendelea.Lucy alizama 

katika mawazo mengi na picha ya kila 

kilichotokea usiku ile ikamjia.Alikumbuka 

namna alivyosimama katika geti la kituo 

kile cha kulelea watoto akatazama huku 

na huko na kuhakikisha hakuna mtu 

anayemuona halafu akamuweka mwanae 

Angela katika geti na kuanza kukimbia. 

 “ Nilimtelekeza mwanangu ambaye 

nimehangaika naye kwa miezi tisa 

tumboni.Vipi kama nilipoondoka alibaki 

akadhuriwa na wanyama au hata wadudu 

wabaya? Ee Mungu nisamehe sana kwa 

kosa hili nililolifanya usiku ule.Ninalijutia 

kosa langu na ninaomba kama mwanangu 

yuko hai unikutanishe naye tena. “ 

akaomba kimya kimya huku akidondosha 

machozi.  “ Lucy tafadhali usilie.Kuwa jasiri.” 

Akasema Robin 

 “ Robin ninajitahidi sana kuwa jasiri 

lakini ninashindwa.Picha nzima ya maisha 

yangu ya huko nyuma imenijia na 

kuniumiza sana.Mambo niliyoyafanya 

usiku ule yananiumiza mno.Sijui nitafanya 

nini iwapo mwanangu alifariki dunia.” 

Akasema Lucy huku akiendelea 

kudondosha machozi 

 “ Lucy tumekaribia sana kufika.Are 

you sure you want to do this? Akauliza 

Robin walipokaribia kufika Usa river 

 “ Ndiyo Robin.Hakuna namna 

nyingine ya kufanya.Lazima niufahamu 

ukweli” akasema Lucy na safari 

ikaendelea. 

 Walifika usa river na kushika njia 

inayoelekea katika kituo cha kulelea 

watoto.Picha za haraka haraka zikamjia 

Lucy akikumbuka namna alivyokuwa 

akikimbia katika barabara hii baada ya 

kumtelekeza mwanae.Hatimaye wakafika 

katika geti kubwa jeusi la kituo kile 

 “ We’re here.Sasa futa machozi ili 

usionekane kama ulikuwa unalia.” 

Akasema Robin.Lucy akafuta machozi na 

Robin akapiga honi.Mlinzi akatoka na kuja 

kuwaonana nao na kuwauliza shida yao wakajieleza kwamba walihitaji kuonana 

na mkuu wa kituo.Mlinzi Yule akafungua 

geti wakaingia ndani na moja kwa moja 

wakaelekea katika ofisi ya mkuu wa kituo 

kile.Alikuwa ni mwanamama mmoja 

mnene sana na mwenye sauti 

laini.Wakasalimiana na kuwakaribisha viti 

waketi 

 “ Karibuni sana jamani.Niwasaidia 

nini? Akauliza Yule mama ambaye kwa 

jina alifahamika kama Iluminata Lameck. 

 “ Mama mimi ninaitwa Adrian na 

huyu mwenzangu hapa anaitwa mwalimu 

Lucy ni mmiliki wa shule ya St,Lucy 

english medium” 

 “ Ouh kumbe wewe ndiye mmiliki wa 

ile shule.Nimefurahi sana kukutana 

nawe.Shule yako ni mojawapo ya shule 

bora kabisa hapa Arusha na katika ukanda 

huu.Hongera sana” akasema bi Iluminata 

 “ Ahsante sana Nashukuru” akasema 

Lucy 

 “ Robin na mwalimu Lucy karibuni 

sana katika kituo chetu cha kulelea 

watoto.Hapa tunalea watoto wale wadogo 

kabisa ambao wanaokotwa au wale ambao 

wamefiwa na mama zao angali wakiwa 

wachanga sana.Sijui niwasaidie nini? 

Akasema Bi Ilimunata  Robin akamtazama mwalimu Lucy 

aliyekuwa kimya kisha akasema 

 “ Mama Kuna jambo limetuleta hapa 

.Yapata miaka ishirini imepita sasa kuna 

msichana mmoja wa kazi ambaye alipewa 

ujauzito na mtoto wa mwajiri wake na 

akafukukuzwa hapo nyumbani.Binti huyo 

hakuwa na ndugu yeyote hapa mjini wa 

kuweza kumsaidia lakini alisaidiwa na 

wasamaria wachache hadi alipojifungua 

salama mtoto wake wa kike.Kwa kuwa 

hakuwa na kazi wala mahala pa kuishi 

ilimuwia ugumu sana msichana huyo 

kuweza kumuhudumia mtoto wake na 

hivyo akaamua kuja kumtelekeza mwanae 

katika geti lenu kisha akaondoka na 

kuendelea na shughuli zake za kutafuta 

maisha.Amekaa na siri hii kwa miaka 

ishirini na ndipo alipoamua kutueleza na 

kutuomba tumsaidie kumpata mtoto 

wake.Kwa kuwa ni mtu wetu wa karibu 

tumeamua kulibeba jukumu hii la 

kumsaidia kumpata mtoto wake na ndiyo 

maana tuko hapa leo.Kwa hiyo mama 

Iluminata tunaomba utusaidie kuufahamu 

ukweli kuhusu mtoto huyu kama aliwahi 

kuokotwa na kulelewa hapa.Nina hakika 

mnazo kumbu kumbu za watoto wote 

mnaowalea hapa.Tutazamie katika kumbukumbu zenu kama katika kipindi 

hicho kuna mtoto aliwahi kuokotwa 

katika geti la kituo chenu. ” akasema 

Robin. 

 Bi Iluminata akakaa kimya kwa 

muda akawatazama Robin na Lucy kisha 

akasema 

 “ Poleni sana kwa mzigo mzito 

aliowatwisha huyo ndugu yenu.Kwa kweli 

mimba zisizotarajiwa kwa hawa mabinti 

zetu limekuwa ni tatizo sugu sana siku 

hizi.Hapa kituoni tuna watoto zaidi ya sita 

ambao wazazi wao wamewatupa na 

wakaokotwa na wasamaria wema.Tatizo 

hili linachangiwa na kutokuwa na uelewa 

wa kutosha kuhusu masuala ya mahusiano 

na mimba za utotoni.Nina hakika binti 

huyo wakati alipoipata mimba hiyo 

alikuwa badi ni msichana mdogo kabisa na 

ndiyo maana alipoona ugumu wa kumlea 

mtoto akaamua kumtelekeza katika geti 

letu.Ninaweza nikamsifu kwa kufanya 

hivyo japokuwa siwezi kuhalalisha 

kitendo alichokifanya lakini hii ni afadhali 

kuliko angeamua kumtupa chooni au 

kumnyonga na kumuua kama wafanyavyo 

baadhi ya wanawake.Pamoja na hayo kuna 

weza kuwa na tatizo kidogo katika 

kulipatia ufumbuzi suala hilo.Nasema hivyo kwa sababu kituo hiki kimekuwa 

kinamilikiwa na wamiliki tofauti tofauti 

kabla ya sisi kungia hapa kwa hiyo 

hatuwezi kujua kama huko nyuma 

walihifadhi kumbu kumbu zote za watoto 

ama vipi.Tatizo lingine kubwa ni kwamba 

jengo la utawala la kituo hiki liliwahi 

kuungua moto lote na kila kilichokuwamo 

kiliteketea kwa hiyo kama kulikuwa na 

kumbu kumbu za nyuma zote 

ziliteketea.Baada ya kuungua moto kituo 

hiki kilikaa zaidi ya miaka miwili ndipo 

tulipokuja sisi na kukikarabati na 

kukifungua upya kwa hiyo hapa tulipo 

kituo hiki ni kipya na tunazo kumbu 

kumbu ambazo tumeanza kuzihifadhi sisi 

tu .Hatuna kumbu kumbu zozote za miaka 

ya nyuma.” Akasema Iluminata.Mwalimu 

Lucy akahisi miguu kumuisha nguvu 

kutokana na kauli ile.Matumaini yote ya 

kupata taarifa za mwanae Angela 

yalitoweka. 

 “ Dah ! Kwa hiyo hakuna sehemu 

nyingine ambako tunaweza tukapata 

kumbu kumbu za watoto mnaowatunza 

hapa? Akauliza Robin 

 “ Hakuna sehemu yoyote nyingine 

mnakoweza kuzipata.Kumbu kumbu zote 

huwa tunazihifadhi hapa kuanzia tarehe waliyopokelewa hapa,na maendeleo yao 

yote kwa ujumla.” 

 “ Tumekwama na hatuna tena namna 

nyingine ya kufanya.Sijui hali ya Lucy 

itakuwaje.Namuonea huruma 

sana,anateseka mno” akawaza Robin 

 “ Lakini kuna jambo nimekumbuka 

ambalo sina hakika kama linaweza 

kuwasaidia lakini si vibaya kujaribu” 

akasema Ilimunata 

 “ Ni jambo gani hilo mama? Akasema 

Robin 

 “ Kuna mama mmoja ni mtu mzima 

kidogo kwa sasa anasumbuliwa na 

maradhi ya miguu.Alikuwa mfanyakazi 

wetu hapa na baada ya kuona amechoka 

na hataweza kumudu majukumu yake 

tuliona ni bora kama 

tutampuumzisha.Huyu amekuwa 

mfanyakazi katika kituo hiki kwa miaka 

mingi toka akiwa msichana na mpaka sasa 

amekuwa mtu mzima.Nina hakika kama 

mkimuona huyu anaweza akawa na 

kumbu kumbu zozote kuhusiana na huyo 

mtoto.Sina hakika sana kama anaweza 

akakumbuka lakini si vibaya kujaribu.” 

Akasema Iluminata na kuwaelekeza akina 

Robin mahala anakoishi huyo 

mama,wakaagana na kuelekea huko  “ Robin nguvu zimeniisha kabisa na 

nimechanganyikiwa.Matumaini ya 

kumpata mwanangu yametoweka na sina 

hakika ya kuonana naye tena hata kama ni 

mzima.NInaumia mno kwa jambo hili” 

akasema mwalimu Lucy kwa huzuni. 

 “ Lucy usife moyo.Bado haujafika 

wakati wa kukata tamaa.Bado tutaendelea 

kumtafuta Angela na ninakuhakikishia 

tutampata tu.Kaza moyo tuongeze juhudi 

za kumtafuta” akasema Robin 

 “ Maelezo ya Yule mama 

yamenikatisha tamaa kabisa.Hapa nilipo 

nahisi moyo wangu ni kama vile unakatwa 

vipande vipande.Sifahamu ni kitu gani 

kitakachoweza kuniponya jeraha hili 

ndani ya moyo wangu” akasema Lucy 

 “ Lucy sintachoka kukwambia 

kwamba huu si muda wa kujilaumu.Huu ni 

muda wa kuwekeza katika kumtafuta 

Angela na kufahamu yuko wapi.Ni kipindi 

ambacho kinahitaji ujasiri mkubwa 

sana.Mimi niko pamoja nawe katika suala 

hili na sintakuacha hata sekunde moja na 

ninakuhakikishia nitakushika mkono pale 

utakapochoka na tutatembea bega kwa 

bega mpaka tuhakikishe Angela 

amepatikana.” Akasema Robin  “ Ninashukuru sana Robin kwa 

msaada huu mkubwa wa kuamua kulivalia 

njuga suala hili.NIngekuwa peke yangu 

nisingeweza kufanya chochote.Ahsante 

sana” akasema mwalimu Lucy na Robin 

akaongeza mwendo akifuata maelekezo 

waliyopewa 

 Hatimaye baada ya mzunguko wa 

karibu saa moja na dakika kadhaa 

walifanikiwa kufika nyumbani kwa Bi 

Elizabeth kaaya mama ambaye 

waliekezwa kwamba anaweza akawa na 

kumbu kumbu kuhusiana na 

Angela.Walipokelewa na kukaribishwa 

ndani na baada ya muda mama mmoja 

mtu mzima akaingia pale sebuleni 

akitembea kwa kukusaidiwa na 

fimbo.Robin na Lucy wakasimama na 

kumsalimu kwa adabu.Wakajitambulisha 

walikotoka na kisha wakamueleza bi 

Elizabeth kile kilichowapeleka 

pale.Aliwasikiliza kwa makini sana na 

Robin alipomaliza kutoa maelezo Bi 

Elizabeth akakaa kimya akavuta kumbu 

kumbu za nyuma na kusema 

 “ Ni kweli mimi nimefanya kazi 

katika kituo kile kwa miaka mingi sasa.Ni 

hivi majuzi tu ndiyo nimestaafu baada ya 

kuanza kusumbuliwa na miguu.Watoto wengi waliopita katika kituo kile 

wamekulia katika mikono yangu kwani 

kituoni pale huwapokea watoto wadogo 

sana.Hata nyumba hii mnayoiona 

nimejengewa na mmoja wa watoto 

ambaye amepitia katika mikono 

yangu.Alipofanikiwa akanikumbuka na 

kunijengea nyumba.Kuhusu huyo mtoto 

unayemsema ninashidwa kupata kumbu 

kumbu vizuri kwa sababu watoto 

wanaookotwa na kuletwa pale kituoni ni 

wengi .lakini hata hivyo..” akakaa kimya 

kidogo kisha akasema 

 “ Lakini kuna kitu 

nimekumbuka.Kuna siku moja mimi 

sikuwa katika zamu ya usiku lakini 

nilipofika asubuhi nikakuta kuna kichanga 

kimeokotwa nikaelezwa kwamba 

kiliokotwa katika geti .Kuna mtu 

alikwenda akakitelekeza pale.kilikuwa ni 

kitoto chenye afya na kichangamfu 

sana.Wote tulikipenda sana.Nakumbuka 

wakati ule mmiliki wa kituo kile alikuwa 

ni Bi Melanie.Nimesahau jina lake la 

mwisho kwani umepita muda mrefu 

sana.Melanie alimpenda sana Yule mtoto 

na akampa jina la Sanya.Bado 

ninalikumbuka sana jina lile.Tulimlea 

vizuri Yule mtoto na baadae Melanie na familia yake walipoondoka kurejea kwao 

waliondoka naye .Huyo ndiye mtoto 

ninayemkumbuka ambaye niliambiwa 

aliokotwa katika geti la kituoni 

kwetu.Sasa sijui kama atakuwa ndiye huyo 

mnayemtafuta au vipi.” Akasema Bi 

Elizabeth.Robin akashusha pumzi baada 

ya maelezo yale yaliyojitosheleza kwani Bi 

Elizabeth alionekana kutokuwa na kumbu 

kumbu nyingine kuhusiana na mtoto huyo 

 “ Bibi tunashukuru sana kwa 

maelezo yako ambayo angalau yametupa 

mwanga Fulani .Kidogo tumeanza kuwa na 

matumaini kwamba yawezekana mtoto 

huyo akawa hai.Na endapo tungeweza 

kupata jina kamili la huyo mama 

ingekuwa rahisi sana kwa sisi kuweza 

kumtafuta na kumpata huyo mtoto.Hata 

hivyo tunakushukuru sana kwa maelezo 

hayo na tunakuomba endapo kuna kitu 

kingine utakikumbuka basi utawasiliana 

nami kwa namba hii ya simu” akasema 

Robin huku akimpatia kadi yenye namba 

zake za simu.Mwalimu Lucy naye 

akafungua pochi yake na kuhesabu 

shilingi laki moja na nusu akampatia bibi 

Yule kisha wakaagana na kuondoka  “ Angela is alive.Thank you Lord” 

akasema Robin wakiwa garini 

 “ Robin ninashindwa niseme nini 

,kidogo sasa ninaweza kuvuta pumzi 

kwani nina uhakika mkubwa kwamba 

mtoto huyo aliyemsema Bi Eliza ni 

Angela.Lakini swali la kujiuliza ni je yuko 

wapi? Akasema Mwalimu Lucy 

 “ Hapo ndipo panapoumiza kichwa 

lakini lazima tumpate tu” akasema Robin 

“ Kidogo ninaanza kuwa na matumaini ya 

kuweza kumpata mwananyu Angela 

japokuwa bado sina uhakika mkubwa 

sana lakini kutokana na maelezo ya bi 

Elizabeth Kaaya kuna sauti inaniambia 

kwamba Angela ni mzima.Kinachoniumiza 

akili yangu kwa sasa,ni je kama ni mzima 

yuko wapi? Akawaza mwalimu Lucy 

wakiwa ndani ya gari wakirejea baada ya 

kutoka kuonana na bi Elizabeth 

 “ Kwa maelezo ya Bi Elizabeth ni 

kwamba huyu aliyekuwa mmiliki wa kituo 

hicho kwa wakati huo aliyemkumbuka 

kwa jina moja tu la Melanie alimpa 

Angela jina la Sanya.Ningefahamu jina la 

pili la huyo mama ingekuwa rahisi hata 

kumtafuta kwa kutumia mtandao kwani 

teknoloji aimekua sana siku hizi lakini 

hilo haliwezekani kwani endapo ukimtafuta kwa jina hilo la Melanie kuna 

mamilioni ya akina Melanie duniani 

.Ninapofika hapa ninajikuta nikiishiwa 

nguvu kabisa kwani uwezekano wa 

kumpata Angela unazidi kuwa mdogo .” 

Akaendelea kuwaza Lucy 

 “ Kama Melanie aliondoka na Angela 

na kwenda naye nchini kwao basi sina 

hakika kama Angela atatamani kurejea 

tena Tanzania.Kwanza mpaka sasa si raia 

wa hapa na nina hakika kwa sasa tayari 

amekwisha fahamishwa kwamba 

aliokotwa kwa hiyo hana haja ya kurejea 

Tanzania kwani hawajui wazazi wake na 

hana mtu yeyote anayemfahamu huku.Ee 

Mungu nitafanya nini niweze kuungana 

tena na mwanangu Angela?.Mateso 

ninayopata ni makubwa mno na ninadhani 

yanatosha kabisa kulipia dhambi hii 

kubwa niliyoitenda” akawaza Lucy 

 Walielekea moja kwa moja 

nyumbani kwa Robin ambako waliandaa 

chakula cha mchana pamoja na kisha kula 

wakaelekea bustanini kupumzika 

 “ Siku ya leo imeanza vizuri kwa 

matumaini .Kwanza mwanzo mzuri wa 

kuitengua ndoa yangu na Vivian.Kitendo 

cha viongozi wa dini kuonyesha 

kukubaliana na hoja zangu kimenipa matumaini kwamba jambo hili linaenda 

kumalizika na kila mmoja atakuwa huru 

.Pili ni mwangaza japo mdogo kuhusiana 

na Angela na kwasasa afadhali kidogo 

tunaweza kuvuta pumzi na kusema 

kwamba Angela yu hai.Tatizo linalokuja ni 

kwamba yuko wapi?Tutampataje? Hilo 

ndilo jambo ambalo tunatakiwa tulitafutie 

ufumbuzi kwa sasa.” Akasema Robin 

 “ Ni kweli Robin.Kwa sasa kidogo 

tunaweza kuwa na uhakika kwamba 

Angela ni mzima lakini linapokuja swali la 

wapi alipo na tutampataje tunarudi pale 

pale mwanzo tulipokuwa.Kwa mujibu wa 

maelezo ya bi Elizabeth ni kwamba 

Melanie aliopoondoka nchini aliondoka na 

huyo mtoto ambaye sisi tunaamini ni 

Angela ambaye kwa wakati huo alikuwa 

amepewa jina la Sanya.Hatufahamu huyo 

Melanie ni raia wa nchi gani.Kama 

tungeweza kumpata huyu mtu ingekuwa 

rahisi kwetu kumtafuta lakini hatuwezi 

kumtafuta kwa sababu hatulifahamu jina 

lake la pili ni nani.Kama kweli ni mzima 

huko aliko sasa hivi Angela lazima 

atakuwa ni msichana mkubwa na pengine 

tayari ameolewa na pengine tayari 

amekwisha ifahamu historia yake kwamba 

aliokotwa na anafahamu kwamba hana ndugu yeyote huku Tanzania na hana 

mpango wa kurudi tena.Nimekuwa kimya 

kwa muda mrefu nikiwaza kuhusiana na 

suala hili na kuna jambo nimelifikiria 

 “ Jambo gani Lucy? 

 “ Nimeamua kuinua 

mikono.Tusiendelee kupoteza muda 

katika suala hili wakati tuna mambo 

mengi ya msingi ya kushughulikia kwa 

ajili ya maisha yetu ya usoni.Kama ni 

mapenzi ya Mungu kutuunganisha naye 

tena basi itakuwa hivyo lakini tuachane na 

jambo hili kwa sasa.Tutapoteza muda 

mwingi sana lakini hakuna matunda 

yoyote.Hili litabaki kuwa ni jeraha la moyo 

wangu na niko tayari kulivumilia hadi 

mwisho wa uhai wangu.Nililifanya jambo 

hili mwenyewe na nitakabiliana na athari 

zake mimi mwenyewe kwa hiyo kwa sasa 

naomba tuelekeze nguvu na akili zetu 

katika jambo lililo mbele yetu yaani 

kuboresha mahusiano yetu na hatimaye 

tufanikiwe kufunga ndoa na Mungu 

atatubariki tutapata watoto wengine na 

familia yetu itakuwa na furaha sana.Lets 

forget about Angela” akasema mwalimu 

Lucy.Robin akamtazama kwa sekunde 

kadhaa na kusema  “ Lucy umeongea kitu cha msingi 

sana lakini kwangu mimi bado moyo 

wangu hauko tayari kukata tamaa 

mapema namna hii.Leo ni siku ya kwnza 

tumeanza kulifuatilia jambo hili na 

hatupaswi kukata tamaa.Ni kweli 

ukiliangalia suala hili namna lilivyokaa 

linakatisha tamaa lakini nakuomba 

tusikate tamaa.Tuendelee kumtafuta 

Angela bila kuchoka.Nina hakika kabisa 

siku moja tutaonana tena na Angela na 

katika mambo ambayo atahitaji 

kuyafahamu ni kwa nini 

ulimtelekeza.Najua utamueleza ukweli 

lakini swali atakalokuuliza ni kwamba 

baada ya maisha yako kuwa mazuri 

ulifanya jitihada gani za kuweza 

kumtafuta na kuungana naye tena? Lazima 

tumuonyeshe kwamba jitihada kubwa 

zilifanyika bila kukata tamaa.Haitakuwa 

kazi rahisi kwa yeye kukusamehe mara 

moja kwa kitendo hiki lakini endapo 

akiona juhudi ulizozifanya basi ataridhika 

kwamba ulikijutia kitendo kile na 

ukafanya kila juhudi kumtafuta.Kesho 

nitarejea tena kwa bi Elizabeth kuona 

kama nitaweza kupata taarifa zaidi ,kama 

kuna chochote anaweza akakikumbuka 

.Kuhusu suala la mahusiano yetu ni kweli linatakiwa kupewa uzito mkubwa hasa 

kwa sasa ambapo taratibu zimeanza za 

kuitengua ndoa yangu na Vivian.Pamoja 

na hayo kuna jambo ambalo nimekuwa 

ninalifikira.Ni kuhusu namna ya 

kumwambia Penina.” Akasema Robin na 

mwalimu Lucy akatabasamu 

 “ Siku zote Penina amekuwa akiota 

kama angeweza kupata mama kama 

wewe.Aliwahi kunitamkia hivyo siku 

moja” 

 “ Really ?!! mwalimu Lucy 

akashangaa 

 “ Kweli kabisa .Alishawahi 

kunitamkia kwamba angefurahi sana 

endapo angepata mama kama wewe kwa 

namna unavyompenda na kumjali.” 

 “ Nimefurahi sana kusikia hivyo 

Robin.Penina ni mtoto ninayempendea 

mno na nimekuwa nikimlea kama mtoto 

wangu kabisa.Nadhani hakuna haja ya 

kuendelea kumficha hadi akasikia toka 

kwa watu wengine kwamba mimi na wewe 

tuko katika mahusiano.Tumweleze ukweli 

“ akasema Lucy 

 “ Litakuwa jambo zuri sana kama 

tukimweleza ukweli jioni ya leo wakati wa 

chakula cha usiku”  “ Hilo ni wazo zuri sana.kama ni 

hivyo tunatakiwa tufanye 

maandalizi.Tuufanye mlo wa leo wa usiku 

uwe ni wa kipekee kabisa “ akashauri Lucy 

na walipokubaliana wote wakaingia 

katika gari na kuondoka kwenda kufanya 

manunuzi ya baadhi ya vitu kwa ajili ya 

kuandaa mlo wa jioni ambao ungekuwa ni 

maalum kabisa kwa ajili ya kuyaweka 

wazi mahusiano yao kwa Penina. 




Vivian aliwahi sana kurejea 

nyumbani .Kutwa nzima alishinda 

mnyonge na mwenye mawazo 

mengi.Alimtaarifu mumewe kwamba 

hakuwa akijiskia vizuri kwa hiyo alirejea 

nyumbani mapema.Dakika kumi tu baada 

ya kurejea nyumbani mumewe naye 

akafika 

 “Umenistua sana uliponiambia 

kwamba hujisikii vizuri nimeona nije 

mara moja kukuona my love.” Akasema 

Tino 

 “ Nashukuru sana mume wangu kwa 

kunijali.” 

 “ Nini hasa kinakusumbua?  “ Mwili wote umekuwa mchovu sana 

leo lakini nimepita kwa Dr.Msona amenipa 

dawa na kwa sasa kidogo najisikia 

afadhali.Umeshindaje leo? 

 “ Nimeshinda salama.Hofu ni kwako 

tu” akasema Tino huku akikaa 

kitandani.Vivian akaamka na kumvua 

viatu na shati ,tino akajilaza kitandani 

 “ Vivian huko kujisikia vibaya 

kulikoanza isije kuwa tayari ni mjamzito” 

akasema Tino na Vivian akatabasamu 

 “ Hapana si ujauzito kwani kama 

ningekuwa na mimba tayari ningejua .” 

akasema Vivian 

 “ Vivian nadhani sasa ni wakati wa 

kuanza kuongelea suala la 

mtoto.Tumekuwa pamoja kipindi kirefu 

sasa lakini mpaka sasa hatujafanikiwa 

kupata mtoto.Nadhani ni wakati muafaka 

kwa sisi kuanza kuliongelea suala hili hasa 

ukichukulia kwamba tayari tumekwisha 

ridhia kwamba tufunge ndoa .” akasema 

Tino 

 “ Tena tukiongelea kuhusu suala hilo 

Tino kuna kitu nataka kukueleza.Leo 

nimeonana na Robin” akasema Vivy 

 “ Umeonana na Robin? Umeonana 

naye wapi? Akauliza Tino 

 “Alinifuata dukani asubuhi.”  “ Ouh ! alikuwa anataka nini? 

 “ Alikuja ili tuongee kuhusu suala la 

ndoa yetu” 

Tino akajiweka vizuri ili kusikia kile 

ambacho mkewe alitaka kumwambia 

 “ Robin amepata mchumba na 

wanataka kufunga ndoa lakini tatizo ni 

kwamba mimi na yeye bado ni wanandoa 

kwa hiyo ametaka tuanze taratibu za 

kuitengua ndoa yetu ili kila mmoja wetu 

aweze kuwa huru kuendelea na maisha 

yake.” 

 “ Hizo ni habari njema sana.Kwa 

hiyo mchakato umekwisha anza? Akauliza 

Tino 

 “ Amesema anakwenda kanisani 

kufuatilia taratibu na atanifahamisha” 

 “Kama na yeye anafikiria kuhusu 

suala hilo hilo basui tumuombe Mungu 

jambo hili lifanikiwe.Ndiyo maana 

nikasema kwamba ni wakati muafaka wa 

sisi kuanza kuongelea masuala ya kupata 

mtoto kwani ninahakika jambo hili 

litafanikiwa tu na tutafunga ndoa” 

 “ Uko sahihi kabisa Tino nadhani 

umefika wakati .Unapendelea mtoto gani 

awe wa kwanza? 

 “ Suala la kuchagua mtoto gani 

azaliwe hilo ni jukumu la muumba mwenyewe lakini nimewahi kusikia 

kwamba kuna namna ya kuweza kufanya 

ili ukapata mtoto wa jinsia 

unayoitaka.Binafsi ninapendelea sana 

mtoto wa kwanza awe wa kiume na wa pili 

awe wa kike.Ninadhani tukiwaona 

wataalamu wa masuala haya ya uzazi 

wanaweza wakatupa ushauri mzuri zaidi 

nini tufanye” 

 “ wow ! kama ni hivyo basi hakuna 

kupoteza muda kesho twende tukaonane 

na hao wataalamu na watufafanulie 

kuhusiana na jambo hilo kama ni la kweli 

ama vipi” akasema Vivian 

*********************** 

 Saa mbili za usiku David alirejea 

nyumbani na moja kwa moja akaelekea 

sebuleni akamsalimu mzee Zakaria na 

kumfahamisha kila kitu namna 

kinavyokwenda.Baada ya maongezi ya 

zaidi ya nusu saa David akaondoka na 

kuelekea chumbani kwake 

kupumzika.Hakujisikia kula usiku huo 

hivyo akaoga na kujitupa 

kitandani.Alikuwa amechoka sana.  Alipitiwa na usingizi haraka na 

akiwa usingizini alihisi akiota kama kuna 

msichana mmoja mrembo sana 

akimpapasa maungoni na kumfanya asikie 

raha ya aina yake.Msichana yule mzuri 

aliyekuwa amevaa gauni refu jeupe 

aliongea kwa sauti laini na iliyopenda 

masikioni mwa David na kumfanya azidi 

kusikia raha ya ajabu.Taratibu akahisi 

kama sehemu zake nyeti zimeguswa na 

yule msichana na zikafura.Akastuka toka 

ndotoni na kukutana na kitu cha ajabu. 

Kuna mtu alikuwa kitandani kwake akiwa 

nusu utupu huku akimpapasa maungoni. 

 “ Vicky ?!!! David akastuka sana 

 “ Shhh !!!..usiongee kwa sauti kubwa 

yule kibwengo ataamka sasa hivi”akasema 

Vicky 

 “ What are you doing in here Vicky? 

 “ Nimekufuata wewe 

David.Nimeshindwa kabisa 

kuvumilia.Mwili wangu nahisi kama vile 

unawaka moto nahitaji kutulizwa 

David.Najua utaniona kama chizi lakini 

uchizi huo umenipa wewe kwa penzi 

ulilonionjesha siku ile.Tafadhali David 

wewe ni mwanaume wa pekee ambaye 

niko tayari kufanya kila niwezalo kwa ajili 

ya kulipata penzi lako.Na ndiyo maana nimemuacha mume wangu chumbani 

kwake na kukufuata wewe huku.Wewe ni 

ua lenye asali tamu na mimi ni nyuki 

niyatefuta asali lazima nikufuate,lazima 

nikug’ang’anie tu.Tafadhali David….” 

Akasema Vicky huku akiivua nguo 

aliyokuwa ameivaa na kubaki 

mtupu.Mwili wa David ukasisimka,damu 

ikamchemka hasa alipokishuhudia kifua 

cha Vicky 

 “ Jaribu lingine hili” akawaza 

david.Wakati akitafakari tayari Vicky 

akamvuta kwake na kuanza kumvua 

fulana aliyoivaa kisha akaanza kumpapasa 

maungoni . 

 “ David najua hatuna uhuru humu 

ndani wala muda wa kutosha ,nakuomba 

tufanye haraka haraka,nikune japo kidogo 

tu na siku nyingine tutatafuta nafasi nzuri 

“ akasema Vicky.David tayari damu 

ilikwisha chemka na Ikulu ilikwisha 

chachamaa .Hakutaka kupoteza muda 

akamvaa Vicky madhabau na kuanza 

kumchezesha Gwaride.Ilikuwa nishughuli 

ya nusu saa lakini iliyomuacha hoi Vicky 

madhahabu.Baada ya kumaliza akava 

haraka haraka na kuondoka kueleka 

chumbani kwake.  “ I’m so stupid !.Nimekubali tena 

kuingia katika mtego wa huyu 

shetani.Nimefanya usaliti mwingine tena 

ndani ya nyumba ya mzee Zakaria…” David 

akajilaumu sana.Kwa dakika kadhaa 

alikuwa amejiinamia akiwaza.Mara akiwa 

mawazoni ukaingia ujumbe katika simu 

,ulitoka kwa Vicky 

“ David sipati neno la kukushukuru 

kwa raha unazonipa.Natamani nipate 

nafasi ya kulala nawe kwa usiku 

mzima.Hata hivyo ahsante hata kwa hiki 

kidogo.Nakupenda kuliko wanaume wote 

wa hii dunia” 

 Ndivyo ulivyosomeka ujumbe 

ule.David akaitoa simu pembeni. 

 “ Lazima nilimalize suala hili haraka 

iwezekanavyo .Nimechoshwa na huyu 

mwanamke.” Akawaza David 

************************ 

Siku tano zimekwisha pita toka Pauline 

alipowasili mjini Moshi.Maisha yake ndani 

ya hoteli kubwa ya kifahari anayoishi 

yalikuwa mazuri na alijitahidi sana 

kufanya kila linalowezekana kujisahaulisha maisha yake ya Arusha na 

kile kilichomsababisha akaondoka 

.Alijitahidi sana kutaka kumsahau David 

pamoja na rafiki yake Tamia ,ambao 

walikuwa ni sababau kubwa ya yeye 

kuondoka Arusha,vile vile alitaka kusahau 

mambo yote yaliyotokea ndani ya familia 

yao na hasa vifo vya mfululizo vya ndugu 

zake vilivyotokea mfululizo kila tarehe 11 

september kila mwaka.Katikahoteli hii 

aliyofikia tayari alikwisha anza 

kuengeneza marafiki ambao wengi 

walikuwa ni wafanyakazi wa hoteli 

hii.Kutokana na haiba yake ya upole 

alipendwa sana na wafanyakazi. 

 Akiwa katika hoteli hii alifanikiwa 

kuokoa maisha ya binti mdogo Macline 

aliyenusurika kuzama katika bwawa la 

kuogelea.Kitendo kile kilimpelekea 

akutane na wazazi wa Macline ambayo 

walitokea kumpenda sana.Ni siku tano 

sasa zmepita toka kutokea kwa tukio lile 

na hajawahi kupata mawasiliano yoyote 

toka kwa Alfred wala mke wake ambao 

walimuahidi kumtembelea mara kwa 

mara. 

 “ Nashangaa kwa nini mpaka leo hii 

Alfred au hata mke wake hawajanipigia 

simu wala kunijulia hali wakati waliahidi kufanya hivyo na wakaniomba wawe ni 

wenyeji wangu hapa Moshi.Tayari 

wamekwisha nisahau? Akajiuliza Pauline 

akiwa amejilaza sofani 

 “ Hapana sina hakika kama 

wanaweza wakanisahau haraka namna hii 

mtu niliyeokoa uhai wa mtoto 

wao.Ninamkumbuka sana Alfred namna 

alivyosisitiza kwamba wanataka wawe ni 

wenyeji wangu.Ninaikumbuka sura ya 

mama yake Macline namna ilivyojaa 

tabasamu kwa kitendo kile cha kumuokoa 

mwanae.Sidhani kama wanaweza 

wakanisahau haraka namna 

hii.Yawezekana kuna sababu 

inayowafanya washindwe kunitembelea 

au hata kunipigia simu.” Akaendelea 

kuwaza Pauline 

 “ Nimeupenda mji wa Moshi.Nadhani 

hapa patanifaa kabisa kuweka makazi ya 

kudumu.Sitaki kurejea tena 

Arusha.Nataka niishi mbali na nyumbani 

.Hapa Moshi si mbali sana na Arusha lakini 

afadhali nitakuwa nimejitenga kilometa 

kadhaa na watu walioniumiza.Haitakuwa 

rahisi kwangu kuonana nao.Vile vile hapa 

Moshi patanifaa kwa sababu baba yangu ni 

mgonjwa kwa hiyo pindi hali yake 

ikibadilika ninaweza kufika Arusha kwa haraka kumuangalia” akawaza na kuinua 

glasi ya wine akanywa kisha akaelekeza 

macho katika luninga alikokuwa 

akitazama filamu 

 “ Kama nimeamua kwa moyo mmoja 

niweke makazi yangu ya kudumu hapa 

Moshi ninalazimika vile vile kufikiria 

namna ya kuwekeza katika vitega 

uchumi.Natakiwa niwe na biashara ya 

kudumu hapa.Katika hili nitahitaji sana 

mtu ambaye anaweza akanipa mwongozo 

wa nini nifanye na kitu gani ninaweza 

nikawekeza hapa Moshi nikapata faida. 

Nina kiasi kikubwa cha pesa benki na 

ninaweza kuanzisha biashara yoyote 

kubwa au hata kiwanda kama nikitaka.” 

Akanyamaza kidogo akatazama tukio 

Fulani katka filamu aliyokuwa akiitazama 

kisha akaendelea kuwaza 

 “ Alfred anaweza akawa na msaada 

mkubwa sana kwangu 

kimawazo.Anaonekana ni msomi mzuri 

.Anaonekana kuufahamu vizuri sana mji 

huu wa Moshi kwa hiyo kama nikimueleza 

wazo langu anaweza akanipa ushauri 

mzuri zaidi.Tatizo linakuja Alfred 

nitamuona wapi?Natamani niende 

nyumbani kwao lakini haitakuwa 

vizuri.Wanatakiwa wao ndio wanitafute.Ngoja nisubiri subiri kidogo 

yawezekana wakanitafuta.” Akawaza na 

mara akaikumbuka sura yenye tabasamu 

ya Alfred 

 “ Wanawake wengine wana bahati 

sana kuwapata wanaume wazuri kama 

Alfred.Kwa muda mfupi niliokaa nao 

nimegundua wanaishi kwa furaha sana na 

Alfred ni mwanaume mwenye kuijali sana 

familia yake.Namuomba Mungu anijalie na 

mimi siku moja niweze kumpata 

mwanaume wa aina hii ya Alfred.Niliamini 

David ndiye Yule ambaye nilikuwa 

ninamsubiri lakini nilijidanganya.I was so 

wrong.David ni mwanaume mshenzi sana 

na hafai hata kidogo.Nilimpenda kwa 

moyo wangu wote na nilikuwa tayari 

kufanya lolote kwa ajili yake lakini badala 

yake akakubali kurubuniwa na Yule 

kahaba Tamia na akanisaliti.Mungu 

atanilipia na ataniletea mwanaume wa 

ndoto zangu . Nahitaji kuanza kujenga 

marafiki wapya na safari hii nitakuwa 

makini sana katika kuchagua 

marafiki.Sitaki marafiki ambao 

wataniumiza kama wale walionitenda kule 

Arusha ………………..” Pauline akastuliwa 

mawazoni na mlio wa simu iliyokuwa 

mezani akainuka na kwenda kuipokea  “ Hallow” akasema Pauline 

 “ Hallow,mapokezi hapa,kuna mtu 

yuko katika laini ya simu anataka kuongea 

nawe,ngoja nikuunganishe naye” akasema 

mwanadada wa mapokezi na hazikupita 

hata sekunde kumi Pauline akaisikia sauti 

ya kiume ambayo alihisi kama amewahi 

kuisikia sehemu 

 “ Hallow Pauline” 

 “ Hallow,nani mwenzangu? 

 “ Unazungumza na Alfred” 

Pauline alitamani aruke ruke kwa furaha 

kwani mtu aliyekuwa akimuwaza dakika 

chache ziizopita ndiye huyo amepiga simu 

 “ Wow Alfred habari yako? 

 “ habari yangu nzuri sana 

.Unaendeleaje? 

 “ Ninaendelea vizuri na 

mapumziko.Macline hajambo> 

 “ Macline na mama yake wote 

hawajambo wanakusalimu sana” 

 “ Nafurahi kusikia hivyo Alfred.” 

Akasema Pauline kikapita kimya kidogo 

 “ Pauline nimekupigia kukuomba 

samahani sana kwani nilikuahidi kwamba 

tungekuja kukutembelea mimi na familia 

yangu lakini tulipatwa na dharura na 

ikatulazimu kwenda nje ya 

mkoa.Tumerejea usiku wa kuamkia leo na nikaona nikujulie hali ila nadhani kesho 

Grace atakuja kukuchuka na utashinda 

nyumbani kwetu kama hautakuwa na 

ratiba nyingine” akasema Alfred 

 “Poleni sana kwa matatizo 

Alfred.Hata mimi nilihisi hivyo kwamba 

lazima mtakuwa mmepatwa na dharura na 

ndiyo maana sikukuona wewe au hata 

mkeo kuja kunitembelea.” Akasema 

Pauline 

 “ Usijali Pauline kuanzia sasa 

utatuchoka wewe mwenyewe” akasema 

Alfred na wote wakacheka kisha Pauline 

akasema 

 “ Alfred unaweza kuwa na nafasi 

jioni ya leo? 

 “ Jioni ya leo?! Alfred akaonekana 

kustuka kidogo 

 “ Ndiyo jioni ya leo.Ninahitaji 

kukuona.Kuna mambo fulani ambayo 

ninataka ushauri na hapa Moshi hakuna 

mwingine ninayemfahamu anayeweza 

kunishauri zaidi yako.” 

 “ Pauline nitakuwa na na 

nafasi.Unataka tunane wapi? Akajibu 

Alfred haraka haraka 

 “ Nataka tuonane hapa hapa hotelini  “ Sawa Pauline nitafika bila 

kukosa.Niambie ni saa ngapi nifike ? 

 “ Kuanzia saa moja jioni tunaweza 

kuonana” akasema Pauline 

 “ Nitafika Pauline bila kukosa” 

akasema Alfred na kukata simu. 

 “ Oh Ahsante Mungu.Mtu ambaye 

nilikuwa nikiwaza nitampataje hazijapita 

hata dakika kumi akapiga simu.Hizi ni 

dalili njema kwamba mambo yangu 

yatakwenda vizuri hapa Moshi.Nina 

uhakika mkubwa nitafanikiwa.” akawaza 

Pauline 

 Kwa upande wa Alfred baada ya 

kukata simu akabaki mdomo 

wazi.Aliduwaa kama mtu ambaye 

anashuhudia jambo fulani ambalo 

hakulitegemea. 

 “ Pauline anataka kuonana na 

mimi.!.Anataka kunieleza jambo gani? 

akawaza 

 “Toka nilipoonana naye mara ya 

kwanza Pauline hajabanduka akili 

mwangu .Ninamuwaza kila 

dakika.Ameichanganya akili yangu sana 

na hili ni jaribu kubwa mno ninakumbana 

nalo na ninasikitika kwamba sina nguvu 

ya kuweza kulishinda.Kwa Pauline lazima 

nikiri kwamba nitaanguka dhambini.Roho wa usaliti ananinyemelea na anaonekana 

kuanza kunizidi nguvu kabisa.Nimeanza 

kumpenda Pauline” Akawaza Alfred 

******************* 

 Papaa Tino magari kama 

alivyozoeleka,mfanya biashara mkubwa 

sana wa magari jijini Arusha aliinua glasi 

yake iliyojaa bia akanywa funda moja na 

kuirudisha chini akaendelea kusoma 

gazeti alilinunua.Hakuwa peke yake pale 

mezani bali alikuwa na rafiki zake watatu 

matajiri wakubwa wanaomiliki migodi ya 

madini ya Tanzanite.Walikutana hapa 

sehemu maarufu sana kwa uoshaji wa 

magari.Walionekana kuongea kwa furaha 

na kubadilishana mawazo kuhusiana naa 

biashara zao.Ghafla Tino akaweza gazeti 

mezani na kusema 

 “ Jamani kuna jambo ninataka 

kuwataarifu” 

 Wenzake wakakaa kimya kusikia ni 

jambo gani analotaka kuwaambia 

 “ Jamani ninataka kufunga ndoa” 

Wenzake wote wakashangilia kwa 

furaha.Ilikuwa ni habari nzuri sana kutoka 

kwa rafiki yao.Walimpongeza sana  “ Shemeji yetu ni mpya au ni Yule 

tunayemjua ? Akauliza Amando mmoja wa 

matajiri wakubwa jjini Arusha 

anayejishughulisha na uchimbaji wa 

madini.Tino akacheka kidogo na kusema 

 “ Shemeji yenu ni Yule 

Yule.Nimekuwa naye kwa kipindikirefu 

sasa kwa hiyo tumeazimia tufunge ndoa” 

 “ Ouh basi vizuri.Tunamfahamu 

shemeji yetu vizuri sana.Hongera sana 

Tino.Pale umepata mke.Yule shemeji ni 

mtulivu na anafajua kutafuta pesa.Tino 

pale umepata mke hongera sana kwa 

uamuzi wako huu wa kutaka kufunga 

ndoa” akasema Paskali ambaye naye ni 

mfanya biashara mkubwa wa madini. 

 “ Lakini Tino mimi kabla ya 

kukupongeza kuna mambo ninahitaji 

kuyafahamu kwanza.Sote hapa 

tunafahamu kwamba Vivian kabla ya kuja 

kwako alikuwa ni mke wa mtu na kwa 

mujibu wa taratibu za dini ni kwamba 

ndoa ikishafungwa hapa duniani 

imefungwa mbinguni pia na ni kifo peke 

yake kinachoweza kuwatenganisha 

wanandoa.Je unataka kufunga ndoa gani ? 

Ya kanisani au ya serikalini? MUme wake 

wa ndoa analifahamu suala hili? .” akaulzia Amando.Tino akanywa funda la 

bia na kusema 

 “ Amando ninalifahamu hilo na kwa 

sasa kinachoendelea ni mchakato wa 

kuitengua ndoa ya Vivian na mume 

wake.Tayari taratibu zimekwisha anza na 

wala msihofu .MUme wake analifaamu hilo 

na hata yeye mwenyewe ndiye 

anayeshughulikia mchakato wa kuitengua 

ndoa yao ili naye aweze kuoa mke 

mwingine.Nmewataarifu ninyi kwanza 

watu wangu wa karibu ili mfahamu ni kitu 

gani kinachoendelea.Pindi mchakato huu 

wa kutengua ndoa ya Vivian ukikamilika 

basi masuala ya ndoa yatafuata haraka 

sana.Nina hamu sana ya kupata mtoto 

ndugu zangu.Ninataka nimpate mrithi wa 

mali zangu lakini ninataka mtoto 

anayetokana na ndoa halali .NImeshndwa 

kuzaa mtoto na Vivian kwa sasa kwa 

sababu kisheria yeye bado ni mke wa mtu” 

akasema Tino.Wenzake wakaendelea 

kumpongeza na kumpa moyo na 

kumuahidi kumpa ushiriano mkubwa 

sana katika suala lile.Pascal na mwenzake 

maarufu kwa jina la Kimaro wakaondoka 

na kumuacha Tino na Amando 

wakiendelea kupata knywaji.  “ Tino nilikuwa nahitaji sana akina 

Pascal waondoke ili nipate nafasi ya 

kuzungumza nawe jambo moja la msingi 

sana ” akasema Amando 

 “ Jambo gani Amando? 

 “ Ni kuhusiana na mpango wako huu 

uliotueleza wa kutaka kufunga ndoa.” 

 “ Kwani kuna tatizo gani? akaulizia 

Tino.Amando akanywa funda la bia na 

kusema 

 “ Tino kuna jambo limekuwa 

linanirereketa kwa muda mrefu sana 

lakini nimeshindwa kupata ujasiri wa 

kukueleza nadhani leo hii ni wakati 

muafaka kabisa wa kuliweka wazi suala 

hili.” 

 “ Amando ni suala gani hilo mbona 

unanipa wasiwasi? Akasema Tino 

 “ Kama unakumbuka awali 

nilikuuliza kama una uhakika wa kile 

unachotaka kukifanya na ukanijbu 

kwamba hauna shaka hata kidogo na suala 

hili na kwamba kila kitu kinakwenda 

vizuri.Ninataka kukuuliza tena una 

hakika unatafuta mrithi wa mali zako 

kupitia kwa Vivian? 

 Tino hakuonekana kupendezwa na 

swali lile akauliza  “ Mbona sikuelewi Amando? Sasa 

ulitaka nitafute mtoto na nani wakati 

Vivian ndiye mke wangu? 

 “ Usinielewe vibaya Tino na hapa 

tunaongea mambo mazito sana kwa 

mustakabali wa maisha yako wewe kama 

rafiki yangu” 

 “ Ok Amando hebu nieleze kuna 

tatizo gani mimi kupata mtoto na Vivian? 

Taratibu za kutengua ndoa yake 

zinaendelea kwa hiyo atakuwa huru na 

tutafunga ndoa” 

 “ Una hakika Vivian ana uwezo wa 

kukupatia mtoto? Akauoiza Armando 

Swali lile likambabaisha kidogo Tino 

,akanywa funda kubwa la bia na kusema 

 “ Armando kwa kweli maneno 

uliyoanza kuyatamka yananipa wasi wasi 

sana.Umeanza kutumia pombe gani siku 

hizi? 

 “ Sijalewa Tino na naomba 

unisikilize vizuri.Nitakwambia ukweli 

hata kama mimi na wewe tutakorofishana 

kwa sababu siku zote ukweli si mtamu 

hata kidogo.” Akasema Amando na Tino 

hakujbu kitu akabaki anamtazama 

 “ Mkeo Vivian hana uwezo wa 

kukupatia mtoto” akasema Amando.Tino 

akamuangalia rafiki yake kwa macho makali bila kusema chochote.Armando 

akaendelea 

 “ Mlipoanza mahusiano yenu Vivian 

aliwahi kutoa mimba mara mbili nadhani 

hakuwa tayari kuzaa kwa wakati ule kwa 

hiyo alipotoa mimba kwa mara ya pili 

inasemekana aliyemtoa alikosea kwa hiyo 

kukawa na matatizo katika kizazi na hivyo 

ili kuokoa maisha yake ikalazimika 

kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kabisa 

kizazi.Upasuaji huu ulifanyika wakati 

wewe ukiwa Japan kufuatilia magari na 

uliporudi akakuambia kwamba 

alifanyiwa upasuaji kuondoa 

uvimbe.Ulikuwa ni uongo.Mkeo 

amekuficha kuhusu jambo hili na 

amekupa matumaini hewa ya kwamba 

atakuzalia mtoto.Hana uwezo huo.Najua 

hutaniamini lakini ukitaka uhakika zaidi 

onana na Dr.Fadhili pale Fadhili hospital 

yeye ndiye aliyefanya upasuaji huo na 

kwa kuwa ni rafiki yangu wa karibu 

alinieleza kuhusu jambo hilo.Sikuweza 

kukueleza jambo hili siku zote kwa 

kuhofia kutetereka kwa ndoa yenu lakini 

kutokana na jambo analotaka kulifanya 

sasa siwezi kuwa mnafiki lazima niseme 

ukweli ili wewe mwenyewe uamue 

kwamba kama utamuoa Vivian basi ujue kwamba hautapata mtoto kamwe labda 

uzae nje ya ndoa” akasema Armando. 

 Taratibu Tino akainua glasi yake 

iliyojaa pombe akanywa funda moja na 

ghafla likatokea tukio ambalo hakuna 

aliyelitarajia.Baada ya kunywa funda lile 

kwa kasi ya aina yake akampiga Armando 

na glasi ile kichwani .Wakati Amando 

ameinama akiugulia maumivu kwa 

kukatwa na glasi ile Tino akanyanyuka na 

kutoa bastora 

 “ Mnafiki mkubwa wewe ! leo 

nakuua…” akasema Tino huku 

akitetemeka kwa hasira.Ghafla wakatokea 

vijana wawili ambao wote ni wafanya 

biashara wa madini na wanafahamiana 

sana na Armando nao wakatoa bastora zao 

wakamelekezea Tino 

 “ Weka chini bastora yako 

,tutakumaliza sasa hivi…” wakasema 

vijana wale.Eneo lile linapendwa sana na 

wafanya biashara wa madini kuja kuosha 

magari yao kwa hiyo taarifa zikasambaa 

haraka kwamba kuna mtu anataka 

kumuua Armando.Watu zadi ya kumi 

wakatokea eneo lile na sita kati yao 

walikuwa na bastora na wote 

wakamuelekezea Tino ambaye bado alikuwa amemuelekezea Armando 

bastora. 

 Taratibu huku akivuja damu 

Armando akainuka bila kuogopa 

 “ You cant shoot me Tino..Hawa 

uwaonao hapa ni jeshi dogo sana ambao 

nikiwaamuru wakumalize sasa hivi 

hautachukua hata sekunde mbili.From 

now on,me and you we’re over lakini 

ukweli tayari unaufahamu na siku moja 

utayaamini maneno yangu..” akasema 

Armando na kutembea kuelekea katika 

gari lake huku vijana wale wakimsindiiza 

.Lilikuwa ni tukio fupi ambalo hakuna 

aliyelitazamia .Baada ya Armando 

kuondoka Tino akapiga meza kwa hasira 

ikaanguka chini kisha akatoka kwa kasi 

hadi lilipo gari lake ambalo tayari 

lilikwisha oshwa akaingia na kuondoka 

kwa hasira maeneo yale.. 

Moja kwa moja Tino akaelekea nyumbani 

kwake.Hakutaka kupitia sehemu nyingine 

yoyote ile.Mtumishi wa ndani alistushwa 

sana na namna Tino alivyorejea .Hakuwa 

katika hali yake ya kawaida 

aliyomzoea.Tino akaingia chumbani 

kwake akajifungia 

 “ Ghhaaaaaahhh!!!!..akapiga ukulele 

kwa hasira huku akiangusha vitu.Alikuwa na hasira kali mno.Akasimama mle 

chumbani akitafakari akakosa jibu akahisi 

kama vile miguu inaisha nguvu akakaa 

chini na kuanza kuyakumbuka maneno 

aliyoambiwa na Armando.Picha ya tukio 

zima ikamjia akajikuta akizidi kuishiwa 

nguvu. 

 “ Mkeo Vivian hana uwezo wa 

kukupatia mtoto” maneno haya ya 

Armando yakaendelea kujirudia kichwani 

mwa Tino. 

 “ Mlipoanza mahusiano yenu Vivian 

aliwahi kutoa mimba mara mbili nadhani 

hakuwa tayari kuzaa kwa wakati ule na 

alipotoa mimba kwa mara ya pili 

inasemekana aliyemtoa alikosea kwa hiyo 

kukawa na matatizo katika kizazi na ili 

kuokoa maisha yake akalazimika 

kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kabisa 

kizazi.Upasuaji huu ulifanyika wakati 

wewe ukiwa Japan kufuatilia magari na 

uliporudi akakuambia kwamba 

alifanyiwa upasuaji kuondoa 

uvimbe.Ulikuwa ni uongo” Bado maneno 

yale ya Armando yakaendelea kumjia 

kichwani na kumuumiza sana  “ Nakumbuka ni kweli nilipotoka 

safari ya Japan nilikuta mke wangu 

amefanyiwa upasuaji na akaniambia 

kwamba alifanyiwa upasuaji ule wa 

haraka ili kuondoa uvimbe tumboni” 

akawaza Tino 

 “ yawezekana Tino akawa anasema 

ukweli? Akajiuliza 

 “ Hapana,ninamuamini sana mke 

wangu na hawezi akanifanyia jambo kama 

hilo.Ni juzi tu tumetoka kumuona daktari 

wa masuala ya uzazi na akatushauri 

tufanye nini kama tukitaka kumpata 

mtoto wa kiume.Vivian alikuwa ni 

mwenye furaha kubwa na wala hakuwa na 

hata chembe ya wasi wasi.Kama angekuwa 

na tatizo hilo alilolisema Armando 

asingekubaliana na wazo langu la kutaka 

tuzae mtoto.Lazima angetoa visingizio 

lukuki lakini yeye alilifurahia sana wazo la 

kuzaa mtoto na yuko tayari hata 

sasa.Ninafahamu kuna watu hawapendi 

kuona mimi nikifunga ndoa na Vivian na 

mmoja wa watu hao ni 

Armando.Wanamfahamu Vivian ni 

mwanamke ambaye anajua sana kutafuta 

pesa kwa hiyo wananionea wivu wanataka 

nikorofishane naye ili wananicheke.Katika 

hilo wameshindwa na hawatapata nafasi ya kunitenganisha na Vivian kamwe” 

akawaza Tino na taratibu akahisi kuanza 

kupata nguvu akainuka na kukaa 

kitandani 

 “leo nimefaamu kwamba binadamu 

ni kiumbe mbaya sana .Sikutegemea hata 

siku moja kama Armando mtu ambaye 

nilikuwa nikimchukulia kama ndugu 

angeweza kunitamkia maneno kama yale 

na kutaka kuniharibia maisha yangu.Sitaki 

urafiki naye tena .Siwezi kuwa na rafiki 

mnafiki kama yule.” Akawaza Tino na 

kukumbuka namna alivyomuelekezea 

Armando bastora 

 “ Aliniudhi sana Yule jamaa.Mimi 

huwa sipendi mambo ya kipuuzi 

.Awashukuru wale marafiki zake ama 

sivyo nigemfanyia kitu kibaya sana leo” 

akaendelea kuwaza Tino akatoka na 

kwenda jikoni akachukua chupa ya pombe 

kali na kuanza kunywa kwa fujo 

 “ Ngoja tu ninywe mvinyo kwa 

sababu Yule kenge ameniudhi sana 

leo.Tayari amekwisha niharibia siku 

yangu kabisa” Tino akaendelea kuwaza na 

mara simu yake ikaita .Alikuwa ni Pascal 

rafiki yake 

 “ Hallow Pascal” akasema Tino baada 

ya kuipokea simu  “ Tino nini kimetokea? Nimepigiwa 

simu na vijana na kuambiwa kwamba 

tulipoondoka pale car wash kumetokea 

jambo la ajabu sana.Tafadhali niambie 

nini kimetokea? 

 “ Pascal naomba mumpe onyo yule 

jamaa kwamba mimi huwa sitaki 

kufuatiliwa mambo yangu hususan 

mambo yangu ya ndani ya 

kifamilia.Ameniudhi sana na ashukuru 

vijana wake ama sivyo tungekuwa 

tunaongea mambo mengine mida hii.Mimi 

si mtu wa kuchezea hovyo hovyo” 

 “ Nini kimetokea Tino? Kitu gani 

kimesababisha mkagombana? 

 “ Muulize Armando atawajibu .Mimi 

siwezi kuwaeleza chochote” akasema Tino 

kwa hasira 

 “ Tino wewe na Armando ni marafiki 

wa muda mrefu sana .Naomba tafadhali 

mtulize hasira na tukae chini tuongee 

kuhusu masuala haya na tuyaweke 

sawa.Haipendezi kwa watu kama sisi 

kuonekana tunagombana mpaka kufikia 

hatua ya kutishiana maisha.Hii si picha 

nzuri hata kidogo kwani sisi ni watu 

tunaoheshimika sana.Mimi nitaandaa 

kikao na tutakaa tuyazungumze masuala 

haya na tuyamalize.” Akasema Pascal  “ Pascal naomba usipoteze muda 

wako tafadhali.Mimi siwezi kuhudhuria 

kikao hicho.Sitaki kabisa kukaa katika 

kikao na mtu asiyenitakia mema.Armando 

hawezi kusimama na kumzushia kashfa 

mke wangu.” 

 “ Kwani alisema nini Tino? Akauliza 

pascal 

 “ Armando anadiriki kusimama na 

kunieleza wazi wazi eti ninajidanganya 

kutaka kufunga ndoa na Vivian eti 

kwamba mke wangu hana uwezo wa 

kuzaa.Yeye ni nani hadi anitamkie 

maneno haya? 

 “ Alitamka maneno hayo? 

 “ Ndiyo Pascal.Hayo ndiyo maneno 

yaliyonipandisha hasira hadi nikajikuta 

nimeichomoa bastora yangu.” 

 “ Dah ! pole sana Tino.Hakufanya 

vizuri kutamka maneno kama 

hayo.Msamehe Tino na hasira zikipungua 

tutakaa na kuyamaliza masuala 

haya.Atalazimika kukuomba msamaha” 

akasema Pascal 

 “ Pascal sihitaji msamaha wake.Mimi 

na Armando tumefika mwisho sitaki tena 

kuwa na rafiki kama yule.Hata aseme nini 

katu sintomsamehe.Ni heri nikawa na 

urafiki na setani kuliko kuwa na urafiki na mtu kama Armando” akasema Tino kwa 

hasira 

 “ Tino tafadhali usiwe na hasira 

hivyo ndugu yangu.Armando amekosea na 

kama rafikiyo jaribu kutafuta namna ya 

kumsamehe.Urafiki huu umejengwa kwa 

miaka mingi na hauwezi kuisha kwa siku 

moja” 

 “ Pascal nakuapia kwamba hadi 

naingia kaburini sintaongea tena na 

Armando” akasema Tino.Pascal akakaa 

kimya kidogo na kusema 

 “ Tino kuna jambo linanishangaza 

kidogo.Wewe na Armando mmeanza 

urafiki wenu muda mrefu sana kabla hata 

mimi na wewe hatujahamiana.Napata 

kigugumizi kidogo kuhusiana na suala 

hili.Ninamfahamu vizuri sana Armando 

mpaka ameamua kutamka maneno haya si 

bure.Hebu jaribu kukaa na Armando na 

kuliongeela suala hili.Ninamfahamu sana 

Armando ni mtu mwelewa sana na ni 

msomi mzuri

Ni mtu mwenye kupima 

jambo kabla ya kulisema.

Usikasirike bure

.Kaa na Armando na umuhoji kuhusiana 

na kauli yake hiyo aliyoitoa.

Huenda ni 

kweli kukawa na kitu kama hicho 

anachokisema.” Akasema Pascal na kuzidi 

kumpandisha hasira Tino

  “ Kumbe na wewe huna tofauti na 

Yule mshenzi mwingine.

Nyote akili zenu 

ziko sawa.

Kama umeamua kumfuata 

mjinga mwenzako sawa.

Mimi siwahitaji 

kabisa katika maisha yangu .

Endeleeni na 

masha yenu na mimi ninaendelea na 

maisha yangu .” akasema Tino na kukata 

simu 

 “ Kumbe hata huyu naye anaungana 

na Yule mwingine !!.

Nashukuru Mungu 

kwa kuniwezesha nikawatambua wanafiki 

ambao kutwa kucha wamekuwa wakiwaza 

kuniona nikiporomoka.

Ninawaapia 

nitaishi maisha yangu bila ya wao na 

wataniona namna nitakavyofanikiwa” 

akawaza Tino na kuendelea kunywa 

pombe ile kali. 

 ********************* 

 Vivian alirejea nyumbani haraka 

sana baada ya kutaarifiwa na msichana 

wake wa kazi kwamba Tino hakuwa 

katika hali yake ya kawaida.

Vivian 

alistuka sana alipomkuta mume wake 

amelala sebuleni hajiwezi kwa pombe kali 

alizokuwa amekunywa.

Haraka haraka 

akaanza jitihada za kumsadia kupunguza 

nguvu ya pombe aliyokunywa.

Tino alitapika sana na Vivian akamchukua na 

kwenda kumlaza sehemu yenye hewa ya 

kutosha. 

 Vivian alishangazwa sana na kitendo 

kile cha mumewe Tino kulewa namna ile 

.Haikuwa kawaida yake kulewa kiasi 

kile.

Akachukua simu yake na kumpigia 

Armando ambaye ni rafiki mkubwa wa 

Tino ili kufahamu kama kuna tatizo lolote 

lililompelekea Tino akalewa kiasi 

kile.

Simu ya Armando ikaita bila 

kupokelewa na baadae haikupatikana 

tena.

Vivian akazidi kushangaa.

Akazitafuta 

tena namba za Pascal rafiki mwingine wa 

Tino akapiga lakini hali ikawa ile ile simu 

yake haikupokelewa 

 “ Kuna nini leo? Mbona hata marafiki 

wa Tino hawapokei simu wakati si 

kawaida yao? Lazima kutakuwa na jambo 

linaloendelea hapa si bure.

Toka 

nimemfahamu Tino sijawahi kumuona 

akiwa amelewa namna hii.” Akawaza 

Vivian na kuendelea kumsaidia Tino ili 

aweze kupata nafuu 

********************

  Ilimlazimu Pascal kusitisha shughuli 

zake na kwenda kuonana na Armando ili 

kufahamu kile kilichotokea na 

kusababisha yeye na Tino kukwaruzana 

kiasi cha kutishiana maisha. 

 “ Armando hebu nieleze nini hasa 

kilichotokea? Nimewasiliana na Tino na 

amenipa majibu ambayo sikuyatarajia 

kabisa.” Akasema Pascal 

 Armando bila kuficha chochote 

akamueleza Pascal kila kitu na kumuacha 

akishangaa 

 “ Dah ! haya ni mambo mazito 

sana.

Ninamshangaa sana Tino kwa 

kuhamaki badala ya kutulia na 

kulitafakari kwa kina jambo hili.

Lakini 

Armando una uhakika na jambo hili? 

 “ Nina uhakika mkubwa sana Vivian 

hana uwezo wa kuzaa mtoto.

Mimi shida 

yangu ilikuwa ni kumtafadhalisha Tino ili 

kabla hajangia katika ndoa na Vivian 

afahamu ni jambo gani analokwenda 

kukutana nalo na asiwe na matumaini ya 

kupata mtoto.

Kwa kuwa hajataka kusikua 

hakuna haja ya kuhangaika naye 

tena.

Ninachoshukuru ujumbe umefika “ 

akasema Armando kwa masikitiko



Saa moja za jioni juu ya alama ilimkuta 

Alfred katika geti la hoteli alikofikia 

Pauline.Hakutaka kabisa kuchelewa miadi 

hii ya muhimu.Alisimamisha gari 

maegesho akajitazama na kuhakikisha 

amependeza vya kutosha kisha akashuka 

garini na kuelekea moja kwa moja 

mapokezi ambako alijitambulisha 

kwamba ni mgeni wa Pauline ambaye 

alipigiwa simu na kufahamishwa kwamba 

mgeni wake tayari amekwisha wasili 

.Pauline akatoa maelekezo Alfred 

apelekwe katika ukumbi wa chakula 

akamsubiri kule.Baada ya dakika kumi 

Pauline akashuka ghorofani akaelekea 

katika ukumbi wa chakula aliko 

Alfred.Mara tu Alfred alipomuona Pauline 

,akasimama wakasalimiana halafu 

akamvutia kiti Pauline akaketi. 

 “ Karibu sana Alfred” akasema 

Pauline 

 “ Mimi ndiye ninayepaswa 

kukukaribisha kwa sababu wewe ni mgeni 

wetu na sisi ndio wenyeji wako kwa hiyo 

napenda kuchukua fursa hii kusema 

Karibu Pauline” akasema Alfred na wote 

wakaangua kicheko.  “ Anaendeleaje Macline na mama 

yake? Akauliza Pauline 

 “ Wanaendelea vizuri .Wana hamu 

sana ya kuonana nawe” akasema 

Alfred.Muhudumu akafika na kuwaandalia 

vinywaji kisha maongezi yakaendelea 

 “ Vipi mapumziko yako 

yanakwendaje? Akauliza Alfred 

 “ Ninaendelea vizuri .” 

 “ Nafurahi kusikia hivyo” akasema 

Alfred 

 Baada ya ukimya mfupi Pauline 

akasema 

 “ Alfred sitaki kuchukua muda wako 

mwingi sana usiku wa leo kwani nafahamu 

ninyi watu wenye familia zenu mnaishi 

kwa sheria.Ukichelewa kurejea nyumbani 

bila sababu ya msingi basi unaweza 

ukaibuka mgogoro mkubwa.Sitaki hilo 

litokee kwenu kwa hiyo I’ll be quick “ 

akasema Pauline 

 “ Pauline usihofu chochote kuhusu 

mimi.Mke wangu ni mwelewa sana na 

isitoshe kazi zangu mimi huwa 

zinaniruhusu hata kufanya kazi usiku kwa 

hiyo usiogope .Hakuna haja ya 

haraka.Tuna muda wa kutosha usiku wa 

leo” 

 Pauline akatabasamu na kuuliza  “ Kwani unafanya kazi gani Alfred? 

 “ Mimi ni daktari wa moyo katika 

hospitali ya KCMC.Wewe je unafanya kazi 

gani? akauliza Alfred 

 “ Mimi ni mfanya biashara” akasema 

Pauline 

 “ Ouh ndiyo maana umeweza 

kumudu gharama za hoteli hii kubwa.” 

Akasema Alfred wote wakacheka halafu 

kikapita kimya kifupi 

 “ Mkeo anafahamu kama umekuja 

kuonana na mimi usiku huu? Akauliza 

Pauline,. 

 “ Hapana hafahamu chochote kama 

nimekuja kuonana nawe jioni hii.” 

 “ Ok tuachane na hayo ya 

wanandoa.Alfred nimekuita kwa sababu 

nahitaji msaada wako.” Akasema Pauline 

halafu akanywa juice kidogo 

 “ Ndiyo Pauline .Nijambo gani 

unataka nikusaidie? Akauliza Alfred 

 “ Nilipokuja hapa Moshi nikitokea 

jijini Arusha nilikuwa na dhumuni moja tu 

la kupumzika na kisha nirejee nyumbani 

Arusha kuendelea na shughuli zangu za 

biahara.Baada ya kukaa kwa siku hizi 

chache hapa Moshi,nimejikuta nikipata 

mtazamao mpya na nimebadili mawazo 

..Nimepapenda sana hapa Moshi na kwa hiyo ninataka niweke makazi yangu ya 

kudumu hapa.” Akanyamaza kidogo na 

kutabasamu baadaya kuuona uso wa 

Alfred ulivyochanua kwa tabasamu pana 

kwa kuisikia kauli ile ya Pauline. 

 “ baada ya kufanya maamuzi hayo na 

kwa sababu mimi bado si mwenyeji sana 

wa mji huu wa Moshi nimeona nimtafute 

mtu ambaye kidogo anaufahamu mji huu 

ili aweze kunishauri ni uwekezaji gani 

ninaweza nikaufanya hapa Moshi ambao 

utaniingizia faida..Hicho ndicho kitu 

nilichokuitia hapa Alfred.Si lazima unipe 

jibu sasa hivi lakini unaweza ukafanya 

uchunguzi wako na ukanipa jibu siku 

yoyote” akasema Pauline.Alfred aliyekuwa 

akinywa bia aina ya Serengeti akainua 

glasi yake iliyojaa kinywaji akanywa funda 

kubwa na kusema 

 “ Pauline kwanza kabisa napenda 

nikushukuru kwa kunichagua mimi ili 

nikushauri katika suala hili kubwa.Vile 

vile siwezi kuelezea furaha yangu kwa 

hicho ulichokitamka kwamba unataka 

kuhamia mjini Moshi.Nimefurahi sna na 

ninaamimi hata family ayangu itafurahi 

pia.Mji huu ni mzuri na hata mimi 

nilipofika hapa sikuwa nimetegemea 

kukaa muda mrefu sana lakini kadiri nilivyozidi kupazoea nilijikuta napapenda 

na sikutaka kuhama tena.Kwa hivi sasa 

nimekwisha weka makazi ya kudumu 

hapa Moshi.Tukirudi katika jambo la 

msingi kuhusiana na nini unaweza 

kuwekeza.Mimi ni daktari na nitakushauri 

kwamba wekeza katika afya.Asikushauri 

mtu ukawekeza katika kitu 

kingine.Wekeza katika afya na itakulipa.” 

Akasema Alfred na kunywa funda la 

kinywaji kisha akaendelea. 

 “ Katika afya kuna sehemu nyingi za 

kuwekeza kulingana na mtaji ulio 

nao.Unaweza ukafungua duka la 

madawa,hospitali au kama mtaji wako ni 

mkubwa kidogo ninakushauri fungua 

kituo cha kufanya vipimo vya afya 

pekee.Hapa utaweka mashine kama CT 

scan,Ultra sound,na vipimo vya magonjwa 

yote vitapatikana hapo na kwa gharama 

nafuu sana.Ninakuhakishia kwamba kama 

ukifanya biashara hii lazima utapata faida 

kubwa.Kwa hapa mjini Moshi kuna 

changamoto kubwa sana ya kitu kama 

hiki.Nimeona namna watu 

wanavyohangaika kupata vipimo kama 

CTscan n.k na wakati mwingine 

hulazimika kusafiri hadi Arusha kufuata 

vipimo.” akasema Alfred  “ Alfred nakushukuru sana kwa 

ushauri wako huo mzuri.Sikuwahi 

kufikiria hata siku moja kuhusu kufanya 

uwekezaji katika eneo hilo la afya.Unajua 

wengi wetu na hasa sisi wanawake 

tunapotaka kufanya biashara huwa 

tunaangalia sana mambo ya urembo na 

kusahau afya.Nitalifanyia kazi suala hilo 

lakini nitakachokuomba ni kunifanyia 

mchanganuo wa gharama halisi ya kituo 

hicho ili niweze kuanza mchakato wa 

kutafuta fedha .Sitaki kuchelewa 

sana.Nataka kuanza maisha mapya na kila 

kitu kipya” akasema Pauline 

 “ Unataka kuanza maisha mapya? 

You want to forget the past? Alfred 

akauliza.Pauline akatabasamu na kusema 

 “ Alfred let us not talk about 

that”akasema Pauline 

 Waliendelea na maongezi hadi 

ilipotimu saa sita za usiku wakaagana 

Alfred akaondoka zake.Ulikuwa ni usiku 

wenye furaha kubwa sana kwa 

Pauline.Alfred alimpa mawazo mengi na 

kuipanua sana akili yake. 

 “ Ninamshukuru sana Mungu kwa 

kunikutanisha na Alfred.Amenipa mawazo 

mengi mazuri na nina hakika kama 

nikiyafanyia kazi basi maisha yangu yatakuwa mazuri sana .Nilifanya vizuri 

sana kuondoka Arusha.kama 

ningeendelea kukaa kule nisingeweza 

kupata mawazo mazuri kama haya.” 

Akawaza 

******************** 

 Imetimu saa saba za usiku bado Tino 

yuko macho.Hakuwa na usingizi hata 

kidogo .Kwa sasa alijsikia vizuri kidogo 

kwani tayari pombe ilikwisha muisha 

japokuwa mwili haukuwa na nguvu 

kabisa.Alivuta kumbu kumbu ya tukio 

zima lilitokea siku ya jana na kuuma meno 

kwa hasira. 

 “ Nilifanya jambo la kijinga sana 

jana.Sifahamu ilikuwaje hadi nikafanya 

ujinga wa namna ile.Ninakijutia kitendo 

kile.Vipi kama kwa bahati mbaya risasi 

ingefyatuka na kumpata Armando? Muda 

huu ningekuwa katika mikono ya dola na 

maisha yangu tayari 

yangeharibika.Natakiwa niwe makini sana 

wakati wa kufanya maamuzi.Kuamua kwa 

pupa kunaweza kumsababishia mtu 

matatizo makubwa sana kama yaliyotaka 

kunitokea jana.” Akaendelea kuwaza Tino. “ Mimi na Armando tumekuwa 

marafiki kwa kipindi kirefu sana na 

amekuwa ni mtu wangu wa 

karibu.Amenisaidia ushauri katika 

mambo mengi ya kuhusu maisha na 

biashara kwa ujumla.N mtu mwenye 

mchango mkubwa katika kunifiksha hapa 

nilipofika .Sielewi ni shetani gani 

alinipanda na kunifanya nimtakie maneno 

mazito kama yale ya kuuvuja urafiki 

wetu.Ninaumia sana kila nikiyakumbuka 

maneno niliyomtamkia Armando.Kila mtu 

alikuwa ananishangaa sana kwa jambo 

nililolifanya.” Akawaza Tino halafu 

akageuza kichwa na kumtazama mke 

wake Vivian aliyekuwa amelala fofofo. 

 “ What if Armando was right? 

Akajiuliza Tino 

 “ Armando ni rafiki yangu mkubwa 

na sina hakika kama anaweza akatamka 

maneno yale mazito kwa dhumuni la 

kunitenganisha na mke 

wangu.Yawezekana kukawa na ukweli 

katika kile alichokisema.Yawezekana mke 

wangu nikweli hana uwezo wa kuzaa 

mtoto.Hili si suala la kupuuza hata 

kidogo.Nilitakiwa kabla ya kuanza 

kugombana na Armando nilitafakari suala 

hili na kulifanyia uchunguzi.Hata hivyo itanilazimu kulifanyia uchunguzi wa siri 

jambo hili kwani hata mimi kuna mambo 

siyaelewei elewi.Wanawake wakati 

mwingine ni watu wanaotembea na siri 

nyingi na inawezekana kabisa alifanya 

kitendo hicho cha kutoa mimba.” Akawaza 

 “ Kama ni kweli sijui nitafanya nini 

kwa sababu ninamuamini mke wangu 

kuliko mtu yeyote yule.Naomba jambo hili 

lisiwe kweli..” Akawaza Tino huku 

akiendela kumtazama mkewe 

**************** 

 Saa nne za asubuhi siku iliyofuata 

ilimkuta Tino katika hospitali ya Dr 

Fadhili.Hospitali hii ni maarufu sana kwa 

kutibu magonjwa ya wanawake.Tino 

alikwenda hadi mapokezi na akaomba 

asaidiwe aonane na Dr Fadhili.Muuguzi 

aliyekuwa mapokezi akaingia ofisini kwa 

Dr Fadhili akamueleza kwamba Tino 

alihitaj kumuona na akamwambia asubiri 

hadi mgonjwa aliyekuwemo mle ofisini 

atakapotoka ndipo Tino aingie. 

 Ilichukua zaidi ya dakika kumi kwa 

mgonjwa aliyekuwamo ofisini 

kutokai.Muuguzi akamchukua Tino na kumuingiza katika ofisi ya Dr Fadhili 

bingwa wa magonjwa ya wanawake. 

 “ Hallow Dr.Fadhili” akasema Tino 

 “ Hallow ndugu yangu habari yako? 

Akasema Dr Fadhili 

 “ habari nzuri sana.” 

 “ karibu sana .Nikusaidie nini? 

 “ Dr Fadhili nina hakika 

unanifahamu” akasema Tino 

 “ Ninakufahamu vizuri Tino 

japokuwa hatuna ukaribu.Hata gari langu 

la sasa nililinunua katika duka lako” 

Akasema Dr Fadhili 

 “ Nashukuru sana nimekutanana 

mmoja wa wateja wangu.usiache kupita 

kunamzigo mpya umewasili” akasema 

Tino na wote wakacheka kidogo kisha 

Tino akasema 

 “ Dr Fadhili kuna jambo limenileta 

hapa .Si la ugonjwa lakini linahusiana na 

mke wangu .Anaitwa Vivian.” 

“Ninamfahamu vizuri sana mke 

wako.”akasema Dr Fadhili. 

“ Ouh nafurahi kusikia hivyo. Dr 

Fadhili kutokana na biashara yangu ilivyo 

kuna nyakati huwa ninasafiri sana 

kwenda kufuata magari huko japan na 

hata Ulaya.mwaka huu mwezi wa pili 

nilikuwa safarini japan mke wangu akanitaarifu kwamba amefanyiwa 

upasuaji mdogo hapa katika hospitali yako 

wa kuondoa uvimbe tumboni.Siku chache 

zilizopita kuna mtu aliniuma sikio 

akanieleza kwamba upasuaji ule 

aliofanyiwa mke wangu haukuwa wa 

kuondoa uvimbe bali aliondolewa kizazi 

baada ya kutoa mimba vibaya na kizazi 

chake kupata hitilafu.Sikutaka kuziamini 

taarifa hizo haraka kwa hiyo imenilazimu 

kuja kwako moja kwa moja ili kuufahamu 

ukweli wa taarifa hizi.tafadhali dr fadhili 

naomba unifahamishe ukweli kuhsu 

jambo hili” akasema Tino.Dr fadhili 

akalifunika faili lililokuwa mezani pake 

akamtazama Tino kwa sekunde kadhaa. 

 “ Tino mkeo Vivian ni kweli aliwahi 

kufika hapa hospitali akiwa 

anasumbuliwa na maumivu ya 

tumbo.Tulimpima na hakuwa na ugonjwa 

wowote tukampatia dawa za kutuliza 

maumivu akaondoaka.Baada ya siku mbili 

akaja tena na safari hii maumivu yalikuwa 

makali sana na ndipo aliponieleza ukweli 

kwamba alitoa mimba na anahisi 

aliyemtoa mimba ile aliitoa vibaya na 

ndiyo chnzo cha maumivu 

yale.Tulimfanyia tena vipimo na kugundua 

kwamba kulikuwa na tatizo katika kizazi chake kwa hiyo ili kuokoa maisha yake ni 

lazima kizazi kiondolewe.Kwa kuwa 

ninafahamu yeye ni mke wa mtu 

nilimuuliza kama mume wake anafahamu 

kuhusu jambo hilo na yuko tayari tufanye 

upasuaji akanijibu kwamba mume wake 

yuko safari nje ya nchi lakini analifahamu 

suala hilo na kwamba hata suala hilo la 

kutoa mimba ile mlikubaliana wote.kwa 

majibu yale ikanilazimu kumfanyia 

upasuaji tukaondoa kizazi .Nimeshangaa 

sana kusikia kwamba hukulifahamu suala 

hili” akasema Dr fadhili.Tino kijasho 

kilimchuruzika usoni. 

 “ Armando was right. Kumbe Vivian 

ni mwanamke mshenzi sana na hafai 

kabisa kuwa mke.Ameua mwanangu 

asiyekuwa na hatia .Kila siku amekuwa 

akinipa matumaini hewa ya kunizalia 

mtoto wakati akifahamu fika kwamba 

uwezo huo hana” akawaza Tino halafu 

akainua kichwa akamtazama Dr Fadhili na 

kusema 

 “ Dr fadhili nakushukuru sana kwa 

taarifa hii ambazo zimenipa uhakika wa 

kile nilichokisikia.Tafadhali ukipata nafasi 

pita tena dukani kwangu kuna mzigo 

mpya umeingia.,”  “ nashukuru sana Tino.Nitapita hivi 

karibuni kuja kuangalia gari jipya:” 

akasema Dr fadhili akaagana na tino 

akaondoka zake. 

 Ilimchukua zaidi ya dakika tano 

kuwasha gari na kuondoka pale 

hospitali.mambo aliyoambiwa na Dr 

fadhili yalimumiza sana 

 “ najuta kumfahamu 

Vivian.Mwanamke huyu ni shetani 

kabisa.Majuta kumpenda.Alimkimbia 

mume wake na kuja kwangu na 

akamtelekeza mwanae mdogo kabisa na 

hajawahi hata kwenda kumuona 

tena.Huyu mwanamke ana roho ngumu 

kama jiwe.Kibaya zaidi ametoa mimba 

zangu mbili.Ameua watoto wangu wawili 

wasio na hatia.hana sifa ya kuwa mama na 

ndiyo maana hakuwa tayari kuzaa watoto 

na wala haumii kuhusu mwanae 

aliyemtelekeza.Kila siku amekuwa 

akinidanganya kwamba atanizalia watoto 

kumbe hata kizazi hana .Nilimpenda sana 

Vivian lakini kwa sasa nimemchukia 

ghafla na sina hakika kama nitaweza 

kumsamehe kwa kitendo alichokifanya” 

akawaza Tino 

 “ Nakumbuka niliwahi kumpata 

mwanamke mmoja mzuri sana aitwaye mwalimu Lucy.Yule mwanamke alijaliwa 

uzuri wa kipekee,heshima na adabu na 

alikuwa na sifa zote za kuwa mke.kwa 

tama zangu nikamtenda 

vibaya,nikamuacha na kumchukua Vivy 

.Niliruka jivu nikakanyaga moto.Najuta 

kwa nini niliamua kuachana na Lucy.Sijui 

hata nitamuona wapi na hata kama 

nikionana naye sina hakika kama anaweza 

akanisamehe kwa kitendo 

nilichomteda..Nadhani Mungu 

ananiadhibu kwa mambo niliyomfanyia 

Yule mwanamke aliyenipenda kwa dhati 

ya moyo wake.Nilidanganywa na mng’ao 

wa Vivian nikadhani nimepata almasi 

kumbe nimeokota chupa..najuta mimi. ” 

Akawaza Tino huku akikata kona na 

kuingia Mtoni bar.Alihisi 

kuchanganyikiwa na alichokuwa 

akikifikiria kwa muda huo ni kunywa 

pombe tu 

Papaa Tino magari kama alivyozieleka 

jijini Arusha Alikuwa ni mteja mzuri wa 

baa hii ya Mtoni.Mara nyingi hupendelea 

sana kufika hapana akiwa ameongozana 

na wafanya biashara wenzake kupata 

kinywaji .Ujio wake wa mapema siku hii 

uliwashagaza kidogo hata wahudumu 

waliokuwa wakishughulika na usafi .Kwa vile walimfahamu waliendelea 

kumuhudumia kwa kinywaji.Hata hivyo 

unywajiwake haukuwa ule wa 

kawaida.Aliagiza bia na kunywa kwa 

fujo.Kila mtuanayemfahamualijiuliza 

kulikoni Tino anywe namna ile jambo 

ambalo haikuwa kawaida yake.Mpaka 

ilipotimu saa saba za mchana Tino 

alikuwa amelewa chakari.Alikuwa 

akicheza muziki na kuwakumbata 

wahudumu hovyo.Ilikuwa ni hali ya 

kushangaza sana.Vituko vilipozidi 

ikamlazimu meneja wa baa achukue 

jukumu la kuwaatarifu rafiki za Tino 

kuhusu mwenzao .Mtu wa karibu sana na 

Tino anayemfahamu ambaye amezoea 

kuwaona wakiwa pamoja mara kwa mara 

ni Armando na kwa kuwa alikuwa na 

namba zake za simu akampiga 

akamfahamisha kuhusu hali ya Tino na 

vituko anavyovifanya.Armando hakuwa na 

namna ya kumsaidia kwa wakati huo 

kwani alikuwa merererani katika 

biashara zake za madini.Alichokifanya ni 

kumpigia simu Vivian na kumfahamisha 

kuhusu hali ya Tino na kumtaka aende 

mara moja akamchukue 

 “ jamani Tino amepatwa na kitu 

gani? Mbona amebadilika ghafla hivi? Ametoa wapi tabia hii ya kunywa pombe 

kupindukia? Akajiuliza Vivian akiwa 

ndani ya gari akielekea Mtoni bar. 

 “ Nina wasiwasi lazima kuna jambo 

linalomsumbua na kumfanya awe mlevi 

kiasi hiki.Jana alikunywa pombe 

kupindukia na leo hii amerudia tena 

kunywa kama jana.Jambo gani limemsibu 

mume wangu ? Si kawaida yake kunywa 

pombe namna hii.Ninaanza kuwa na wasi 

wasi kwamba yawezekana hata kuna watu 

wakawa wamemchezea ili awe mlevi kiasi 

hiki kwa sbabau haiwezekani abadilike 

ghafla namna hii” akaendelea kuwaza 

Vivian. 

 Vivian alifika Mtoni bar na toka 

akiwa mbali aliweza kushuhudia vituko 

alivyokuwa akifanya mume wake.Alikuwa 

amelewa kupita kiasi huku 

akiwakumbatia hovyo wahudumu wa baa 

na kuwapiga mabusu.Viviana akastuka 

sana kwa vitendo vile kwani toka ameanza 

kuishi na Tino hata siku moja hakuwahi 

kumuona akifanya vituko kama vile 

 “ Mungu wangu aibu gani hii!! 

Akawaza Vivian akiwa amejishika mdomo 

na taratibu akamfuata mume wake 

 “ Tino twende nyumbani 

ukapumzike” akasema kwa upole.Tino akageuka na kumtazama Vivian na uso 

ukajikunja kwa hasira 

 “ Umenifuata hadi huku wewe 

shetani? Nakwambia ondoka hapa sitaki 

kukuona!! Akapaaza sauti 

 “ Tino umelewa sana naomba twende 

nyumbani tafadhali ukapumzike.Tabia 

gani hii umeianza ya kulewa mapema 

namna hii? Akasema Vivian na mara Tino 

akamkosa kofi na kutokana na kulewa 

sana akaanguka chini ,akaumia sana. 

 “ Ninatoka damu kwa sababu yako 

wewe mwanamke.Nakwambia 

utanitambua mimi ni nani mwaka huu ” 

akasema Tino. 

 Vivian machozi yalikuwa 

yanamtoka.Akawaomba baadhi wa 

wanaume waliokuwepo pale wamsaidie 

kumshika Tino na kumpandisha garini ili 

aweze kumpeleka nyumbani.Haikuwa 

shughuli ndogo kumkamata Tino lakini 

walifanikiwa kumpakia garini na Vivian 

akampeleka hadi nymbani ambako vijana 

wawiliwalioongozana naye wakimshikilia 

Tino asiweze kuleta fujo ndani ya gari 

wakamshusha Tino na kumpeleka hadi 

chumbani.Vivian akamtibu jeraha 

aliloumia halafu akampandisha kitandani 

kulala.Akamtazama mume wake namna alivyosawajika akatoka mle chumbani na 

kuanza kulia 

 “ Kitu gani kimempata mume wangu? 

Kwa nini amebadilika namna hii? Hapana 

si bure lazima kuna tatizo.Kama hakuna 

tatizo kata biashara zake basi lazima kuna 

mkono wa mtu.Lakini kama kuna tatizo 

kwa nini haniambii? Siku zote amekuwa 

muwazi sana kwangu na amekuwa 

akinieleza kila kitu kinachomsibu katika 

bisahara zake na hata kama ana ugomvi na 

mtu lazima anieleze lakini cha ajabu toka 

jana hajanieleza chochote kama kun 

ajambolinamsibu na badala yake ameanza 

kunywa pombe kupindukia.” Akawaza 

Vivian halafu akakumbuka picha ya 

viytuko vya Tino kule Mtoni bar 

 “ Sijawahi kupata aibu kubwa kama 

ile.Mume wangu ambaye anaheshimika 

mji mzima leo hii amegeuka na kuwa 

kituko .Akiwashika shika hovyo 

wahudumu.Aibu kubwa sana hii.Kibaya 

zaidi akaanza kunitolea hata mimi 

maneno ya kejeli na matusi 

makubwa.Kuna tatizo gani hapa? 

Ninamfahamu sana Tino hata alewe vipi 

hajawahi kunitolea neno lolote la kashfa 

kama alivyofanya leo.Ninaanza kuwa na 

wasi wasi kwamba yawezekana hapa kuna mkono wa mtu.Haiwezekani mambo haya 

yatokee wakati huu ambao tuko katika 

maandalizi ya ndoa yetu. Hili si suala dogo 

,lazima nilipe uzito mkubwa sana na 

lazima nilishughulikie kikamilfu 

mpakaniufahamu ukweli.Kwanza 

nitamuuliza Tino aniambe ni kitu gani 

kilichomsibu na baada ya hapo nitajua 

nini cha kufanya na hatua za 

kuchukua.”akawaza Vivian 

******************* 

 Siku zilikwenda kwa kasi na 

hatimaye mtu ambaye Vicky madhabu 

alikuwa anamsubiri kwa hamu kubwa 

akarejea nchini.Huyu ni Chino kijana 

mwenye mwili mwembamba lakini hatari 

sana.Taarifa za kurejea kwa Chino 

alizipata jionikutoka kwa mmoja wa 

wafanyakazi wa Chino na asubuhi na 

mapema akajiandaa na kuondoka kwenda 

kuonana na Chino. Bado dhamira yake ya 

kutaka kumuua mzee Zakaria ilikuwa pale 

pale.Kadiri siku zilivyozidi kwenda ndivyo 

alivyozidi kupagawishwa na David .Kwa 

penzi alilokuwa akipewa na David alikuwa 

tayari kufanya lolote ili mradi afanikishe 

mpango wa kuwa naye.  “ Sijawahi kupagawishwa na 

mwanaume kiasi hiki hadi nikafikia hatua 

ya kutaka kuua kwa ajili yake.David 

amenifanya niwe chizi wa 

mapenzi.Ninataka niwe huru 

naye.Ninataka nimmiliki na kusiwe na 

kizingiti chochote kile.Kwa sasa kizingiti 

kikubwa ni huyu Zakaria.Ananikera sana 

Yule mzee.Kila siku ninaomba niamke 

nimkute amekufa lakini kila nikifungua 

macho namkuta ananitazama kama 

Kenge.Lazima nimuondoe ili nibaki huru 

kufanya mambo yangu.Nataka niwe huru 

kujivinjari na kijana anayoiweza kazi” 

akawaza Vicky akiwa njiani kuelekeq kwa 

Chino. 

 “ Najua ninafanya dhambi kubwa 

lakini sina namna nyingine .Kuna nyakati 

katika kuitafuta furaha ya maisha 

unatakiwa ufanye maamuzi magumu 

sana.Na haya ninayotaka kuyafanya ndiyo 

maamuzi magumu.Hakuna njia nyingine 

ya kufanya zaidi ya kumuua Yule 

mzee.Sipati picha namna maisha yangu 

yatakavyokuwa baada ya huyu mzee 

kuondoka.Nitakuwa tajiri mkubwa na 

nitakuwa huru na David.” Akaendelea 

kuwaza  Alifika katika kituo cha mafuta 

kinachomilikiwa na Chino na ambako 

ndiko iliko ofisi yake.Aliombwa asubiri 

kwa muda kidogo kwani Chino alikuwa na 

mgeni ofisini kwake.Baada ya dakika 

ishirini mgeni Yule akatoka na Vicky 

akaingia. 

 “ hallow Chino” akasema Vicky 

 “ ouh Vicky madhahabu ! Karibu 

sana “akasema Chino huku akiinuka na 

kusalimiana 

 “ Ahsante sana Chino” akajibu Vicky 

huku akiketi kitini 

 “ Leo ni bahati kubwa sana kumpata 

mgeni kama wewe asubuhi 

hii.Sikutegemea hata siku moja kama 

ungeweza kunitembelea hapa ofisini 

kwangu” akasema Chino 

 “ Ninashukuru sana Chino.Nilifika 

hapa kuonana nawe nikaambiwa uko 

safarini na jana nilipopata taarifa za 

kurejea kwako sikutaka kupoteza muda 

nikaona nije asubuhi hii kuonana nawe 

.”akasema Vicky 

 “ karibu sana Vicky.Ni kweli nilikuwa 

safari na nimerejea jana.Vipi mambo 

yanakwendaje? 

 “ mambo yanakwenda vizuri sana ..” 

akasema Vicky  “ karibu sana Vicky.Nikusaidie kitu 

gani? Akauliza Chino 

 “ Chino nimekuja hapa kwako 

ninashida kubwa sana na ni wewe tu 

unayeweza kunisaidia”akasema Vicky 

 “ Ndiyo Vicky ninakusikia.Ni jambo 

gani hilo unataka nikusaidie? 

 “ Nadhani unafahamu kwamba 

ninaishi na mzee Zakaria.Kwa siku za hivi 

karibuni mimi na mwanae Pauline 

tumekuwa katika misuguano 

mikubwa.Hatuna maelewano kabisa ndani 

ya nyumba.Pauline anafahamu kwamba 

baba yake kutokana na hali yake kuzidi 

kuwa mbaya anaweza akafariki na kama 

ikitokea akafariki basi nitarithi utajiri 

wake wote kitu ambacho Pauline hataki 

kitokee.Amekuwa akinituhumu kwa 

mambo mengi sana kiasi cha kumfanya 

hata baba yake kunichukia na kwa sasa 

mimi na mzee Zakaria hatua maelewano 

mazuri.Chino mimi na Zakaria tumetoka 

mabali na nina mchango mkubwa katika 

utajiri wa Zakaria kwa hiyo siko tayari 

kuona kwamba sina chochote katika mali 

za Zakaria .Nimezipata tetesi kwamba 

Zakaria anataka anioe katika urithi wa 

mali zake zote na kumuweka mwanae 

Pauline.kama hilo likitokea basi nitakuwa masikini mkubwa kwani sintapata kitu 

chochote kwa namna ninavifahamu Yule 

mtoto.Kwa hiyo basi kuna jambo 

nimekuja kukuomba unisaidie” akasema 

Vicky na kukaa kimya kidogo halafu 

akaendelea 

 “ Chino ninataka kumuua Zakaria” 

akasema Vicky na kukaa kimya.Chino 

akamuangalia kwa makini halafu akatoa 

pakitiya sigara na kuchomoa sigara moja 

akawasha na kuanza kuvuta . 

 “ Umenisikia Chino? Akauliza Vicky 

 “ Ninakusikia Vicky endelea:” 

akasema Chino huku akipuliza moshi 

mwingi hewani 

 “ Nimefikia uamuzi huo wa kumuua 

Zakaria li niweze kurithi mali zote 

.Nimefikiria sana watu ambao wanaweza 

wakanisaidia katika suala hili nikaona 

nije kwako nikuletee mpango huu ili 

tuujadili na kuona namna tutakavyoweza 

uufanikisha.Chino huu ni mpango mzuri 

na una pesa nzuri sana kama ukifanikiwa” 

akasema Vicky.Chino akavuta tena sigara 

akapuliza moshi na kusema 

 “ Vicky sina hakika kama umekuja 

sehemu sahihi .Mimi si muuaji na 

nimeshangaa sana unaponieleza jambo 

kama hili.Nilidhani una jambo lingine la maana sana kumbe ni hilo,tafadhali 

naomba uende ukatafute watu wengine wa 

kukusaidia katika mpango wako na si 

mimi.Nina biashara zangu za kuniingizia 

pesa za kutosha na sijihusishi na mambo 

kama hayo na wala siwafahamu watu 

wanaojihusisha na vitendo hivyo.” 

Akasema Chino 

 “ Chino Please naomba unisaidie 

ndugu yangu.Faida itakayopatikana 

haitakuwa ya kwangu peke yangu hata 

wewe utafaidika pia.Najua kazi hii ni ya 

hatari sana na niko tayari kukulipa kiasi 

chochote cha pesa utakachohitaji ili mradi 

tu uniondolee Yule mzee”akasema Vicky 

 ‘Vicky nirudie mara ngapi 

kukwambia kwamba mimi sijihusishi na 

mambo kama hayo? Aliyekuelekeza 

kwangu amekudanganya.Mwambie 

akuelekeze kwa mtu sahihi na si mimi.” 

Akasema Chino huku akijiandaa kuinuka 

 “ Chino naomba unipe dakika mbili 

tuongee tafadhali.”akasema Vicky , Chino 

akakaa. 

 “ Chino ninajua si rahisi kukubali 

kwamba unaweza kuifanya kazi hii lakini 

mpaka nimekuja kwako ninauhakika 

kwamba unaweza 

kunisaidia.Ninakufahamau wewe ni mtaalamuu sana katika kazi hizi kwa hiyo 

sina wasiwasi hata kidogo kwamba 

nimekose anjia.Nimekuja kwa mtu 

sahihi.C’mon Chino hebu tuache 

kuzungushana na tuweke biashara mezani 

tuone kama tutaelewana ama vipi.This is 

the real deal.Utatengeneza fedha nyingi 

sana kupitia kazi hii ” akasema 

Vicky.Chino akamtazama kwa muda wa 

kama dakika mbili halafu akasema 

 “ Inaonekana unanifahamu 

vyema.Lakini ninakuonya kwamba 

kunifahamu mimi ni kujiweka katika 

hatari kubwa.Ni watu wachache sana 

wanaonifahamu mimi na mambo 

yangu.Anyway tuachanane na 

hayo.Unataka mpango huu utekelezwaje? 

Akauliza Chino 

 “ Nimefikiria njia nzuri ya kuweza 

kuufanikisha mpango huu ni kwa 

kutengeneza tukio la uvamizi. Katika 

uvamizi huo mzee Zakaria atapigwa risasi 

na kuuawa.” Akasema Vicky.Chino 

akafikiri kidogo na kusema 

 “ kwa hesabu ya haraka haraka 

unadhani nanaweza kutengeneza shilingi 

ngapi katika mpango huo? Akauliza Chino  “ Kusema ni kiasi gani inaniwa 

ugumu kidogo .Just be free.Nname your 

price” akasema Vicky 

 “ Millioni mia mbili zinaweza 

kupatikana? Akauliza Chino 

Bila kusita Vicky akasema 

 “ Ndiyo zitapatikana,ili mradi 

mpango utimie” akasema Vicky 

 “ Good,basi huu ni mpango 

mzuri.Sasa naomba unipe muda nilifikirie 

hili suala na kuona namna ya kulitekeleza 

halafu nitakupigia simu kukuomba 

tuonane na hapo ndipo tutakapoongea 

vizuri kwa undani” akasema Chino na 

kuchukua namba za simu za Vicky 

wakaagana Vicky akaondoka 

 “ Sasa ninaanza kupata matumaini ya 

mpango wangu kufanikiwa.Haikuwa rahisi 

kumshawishi Chino akubali mpango ule 

lakini ninashukuru ameonyesha 

kukubali.Kwa kiasi cha pesa anachokitaka 

lazima atakubali kuifanya hii kazi.si kiasi 

kikubwa ukilinganisha na faida 

nitakazopata.Nitabakiwa na utajiriwote 

wa Zakaria na zaidi ya yote nitampata 

kijana adimu sana kupataikana zama hizi 

David.” Akawaza Vicky akiw a ni mwenya 

furaha isiyo kifani  “ bado siku chache David atakuwa 

wangu.Halafu nimekumbuka kitu,bado 

kuna huyu mtoto tamia ambaye David 

ameonekana kuanza kumpenda sana.Huyu 

hawezi kunisumbua .Nitamuweka kando 

haraka sana.Nataka mimi nibaki huru na 

David pia awe huru ndipo tuufungue 

ukurasa mpya kati yetu” akaendelea 

kuwaza Vicky 

Baada ya kutoka ofisini kwa Chino,moja 

kwa moja Vicky madhahabu akaelekea 

kwa Safia ambaye ndiye rafiki na mshauri 

wake mkubwa .Safia aliona namna uso wa 

Vicky ulivyokuwa na tabasamu kubwa 

akagundua lazima kuna jambo 

lililomfanya Vivky akawa ni mwenye 

furaha namna ile 

 “ Enhe Vicky.,hebu nieleze 

mwenzangu nini kimekufanya ukawa na 

furaha namna hii leo? Akauliza Safia.Vicky 

akamshika mkono wakatoka nje 

 “ Safia nimetoka kuonana na Chino” 

akasema Vicky 

 “ Really?! Safia akashangaa 

 ‘ Ndiyo.Nimetoka kuongea naye sasa 

hivi” 

 “ Amesemaje? Akauliza 

 “ Haikuwa kazi rahisi kumshawishi 

akubali lakini amekubali ingawa ameniambia nimpe muda aweze kufikiria 

vizuri halafu atanijibu.” 

 “ Hizo ni habari njema 

sana.Hakuuliza maswali umejuaje kama 

yeye anafanya kazi hizi? 

 “ Aliuliza lakini nlimjibu vizuri na 

akaridhika.Hapa nilipo nina furaha sana 

kwani mipango yangu inakwenda vizuri.” 

Akasema Vicky.Safia akafikir kidogona 

kuuliza 

 “Lakini Vicky ninataka kukuuliza 

kwa mara nyingine tena ila naomba 

usinielewe vibaya.Ni kweli umekusudua 

kufanya hili jambo? Ghafla lile tabasamu 

usoni kwa Vicky likapotea 

 “ Safia nimedhamiria kufanya hili 

jambo tena haraka iwezekanavyo kabla 

hata Pauline hajarejea .Nina hamu sana ya 

kuwa huru niyaendeshe maisha yangu 

namna ninavyotaka na njia pekee ya 

kuniweka huru ni kwa kumuondoa Yule 

mzee.Sintaweza kuwa huru kama Zakaria 

ataendelea kuwa hai.Usihofu safia niko 

makini sana katika jambo hili na 

litafanikiwa tu.Nikifanikiwa mimi 

tumefanikiwa sote.Nakuahidi Safia baada 

ya mambo kukamilika nitakuweka katika 

nafasi ya juu sana.Nitakuwezesha uwe na 

duka lako kubwa na hautajishughulisha tena na biashara hii ya saluni.Mimi na 

wewe tumetoka mbali sana na siwezi 

kukutupa.Vuta subira ,muda si mrefu 

maisha yako yatabadilika kabisa pale 

nitakapoanza kuitwa the boss 

lady”akasema Vicky wakacheka na 

kugonganisha mikono. 

 “ safia leo mimi si mkaaji sana 

nimepita hapa kukupa taarifa hizo njema 

na kukutaarifu uanze kujianda kwa 

maisha mapya muda si mrefu sana toka 

sasa”akasema Vicky wakaagana 

akaondokazake. 

 “ Dah ama kweli kuna watu 

wanaichezea bahati sana.Vicky 

amebahatika kuolewa na 

bilionea,japokuwa ni mzee lakini 

anampenda sana na anampatia kila 

anachokihitaji .Pamoja na yote hayo bado 

Vicky hajaridhika na anataka kumuua 

mzee wa watu.Huu ni ukatili mkubwa sana 

.haya mambo anayotaka kuyafanya 

yatamtokea puani siku moja” akawaza 

Safia baada ya Vicky kuondoka 



 Maandalizi ya kufungua hospitali 

itakayokuwa maalum kwa vipimo 

mbalimbali yalianza kwa kasi.Pauline 

alipata msaada mkubwa sana kutoka kwa 

Alfred.Tayari alifanikiwa kukodi jengo la 

ghorofa mbili ambalo atalitumia kwa 

hospitali hiyo na ukarabati wake 

ulikwisha anza. 

 Ni siku ya jumamosi iliyotulia baada 

ya kutoka kukagua maendeleo ya 

ukarabati wa jengo Pauline aliamua 

kupumzika.Kama kawaida yake alikwenda 

kupumzika katika bwawa la 

kuogelea.Akiwa amezamisha mawazo 

yake katika kitabu cha hadithi 

alichookuwa anasoma mara mtu 

akasimama pembeni yake.Pauline 

akageuka na kumtazama mtu Yule 

akakutana na mwadada mmoja mzuri sana 

mwenye tabasamu la kuvutia.Hakuwahi 

kumfahamu mwanadada 

Yule.Wakatazamana 

 “ Hi “ akasema Yule mwanadada. 

 “ Hi “ akajibu Pauline 

 “ Samahani kwa kukusumbua” 

akasema Yule mwanadada kwa kiingereza 

chenye lafudhi ya Marekani.Alionekana 

kutofahamu kabisa Kiswahili.  “ Bila samahani.Karibu” akasema 

Pauline huku akitabasamu na Yule 

mwanadada mwenye nywele ndefu zenye 

rangi ya dhahabu akatabasamu pia 

 “Naitwa Sanya McNill natokea 

Philadelphia Marekani” akasema Yule 

mwanadada 

 “ Ouh Sanya nafurahi sana 

kukufahamu.Mimi naitwa Pauline.Ni 

mwenyeji wa Arusha lakini niko hapa 

Moshi kwa mapumziko.Karibu sana 

Tanzania” 

 “ Ahsante sana Pauline.Nimefurahi 

nimeongea nawe leo.Kwa siku kama tatu 

hivi nilizokaa hapa nilitamani sana kupata 

mtu wa kuongea naye kubadilishana 

mawazo .Nilitamani sana kupata nafasi ya 

kuongea nawe lakini unaonekana ni mtu 

mwenye shughuli nyingi nyingi kila 

wakati” akasema Sanya.Pauline 

akatabsamu 

 “ Ni kweli Sanya nina mradi wangu 

ninaushughulikia hapa Moshi na ndiyo 

maana ninaonekana kuwa na shughuli 

nyingi kila wakati” akasema auline 

 “ Unajishughulisha na biashara gani 

Pauline” akauliza Sanya 

 “ Mimi ni mfanya biashara 

ninajishughulisha na biashara mbali mbali za mavazi na urembo lakini kwa shapa 

Moshi ninataka kufungua hospitali kwa 

ajili ya vipimo” akasema Pauline 

 “ Ouh nafurahi sana kusikia 

hivyo.Mimi mwenyewe ni daktari pia” 

akasema Sanya na kumfanya Pauline 

atabasamu.. 

 “ Nimefurahi sana Sanya kusikia 

kwamba na wewe ni 

daktari.Unashughulika na magonjwa yapi? 

 “ Mimi ninashughulika na magonjwa 

ya mifupa.Ninafanya upasuaji na kuunga 

mifupa” akasema Sanya.Tayari walikwisha 

zoeana sana na Pauline. 

 “ Dr Sanya utakuwepo hapa 

Tanzania kwa muda gani? akauliza 

Pauline 

 “ Hapa Tanzania nitakuwepo kwa 

muda wa miezi mitatu.Nilikuja na kundi la 

wenzangu kwa dhumuni la kupanda 

mlima Kilimanjaro lakini wenzangu tayari 

wamekwisha ondoka na mimi nimebakia 

hapa kuna kazi ambayo natakiwa kwenda 

kuifanya Arusha na baada ya hapo 

nitaendelea na mapumziko yangu “ 

akasema Sanya 

 “ Hata mimi ni mwenyeji wa Arusha 

pia.Endapo utahitaji msaada wa kuhusiana 

na Arusha nitakusaidia .” akasema Pauline  “ Nimefurahi kukutana na mkaazi wa 

Arusha kwani nilihitaji sana kumpata 

mwenyeji ili anielekeze mambo Fulani 

Fulani.Nitafurahi sana kama kwa siku 

moja ndani ya wiki ijayo tutapata nafasi ili 

twende wote Arusha.Unasemaje kuhusu 

hilo? Akauliza Sanya.Kabla Pauline 

hajajibu kitu mara akatokea 

Alfred.Pauline akasimama 

 “ Alfred karibu sana.Mbona umerudi 

kimya kimya bila hata kunitaarifu kama 

umerudi? Akauliza Pauline 

 “ Sikutaka kukupa wasi wasi kwa 

sababu naelewa ulikuwa na wasi wasi 

mwingi sana kama nitafanikiwa ama vipi” 

akasema Alfred.Pauline akamgeukia 

Sanya 

 “ Sanya huyu ni rafiki yangu sana 

anaitwa Dr Alfred.Yeye ni daktari wa 

moyo katika hospitali ya KCMC hapa 

Moshi.Alfred huyu ni rafiki yangu 

anatokea Philadelphia Marekani anaitwa 

Dr Sanya Mcnill.Naye anaishi hapa hapa 

hotelini” Pauline akafanya 

utambulisho.Alfred na Sanya 

wakasalimiana kisha Pauline akaagana na 

na Sanya kwa miadi ya kuonana tena 

kesho yake kwani alikuwa na maongezi 

muhimu sana na Alferd.Wakapanda hadichumbani kwa Pauline.Toka 

wamefahamiana ilikuwa ni mara ya 

kwanza Alfred anaingia chumbani kwa 

Pauline. 

 “ Pole na safari Alfred.Natumia 

kinywaji gani? akauliza Pauline 

 “ Kwa leo naomba whisky tafadhali” 

akasema Alfred huku akiilegeza tai 

yake.Pauline akachukua chupa kubwa ya 

whisky akaiweka mezani na kumimina 

katika glasi mbili wakaanza 

kunywa.Alfred akapiga funda moja na 

kusema 

 “ Pauline una bahati sana ya kupata 

marafki madaktari” akasema Alfred na 

wote wakacheka. 

 “ Kwa kweli ni bahati sana .Mpaka 

sasa nimekwisha kutana na madaktari 

wawili.Hii ni ishara kwamba hata mimi 

nilitakiwa niwe daktari” akasema Pauline 

na wote wakacheka 

 “ By the way nimefika salama Dar es 

salaam na nimerudi na habari njema” 

akasema Alfred na kuufungua mkoba 

wake akatoa bahasha kubwa 

 “ Kila kitu kimekwenda vizuri sana 

na kibali tayari kimepatikana.Nimepata 

msaada mkubwa wa rafiki zangu walioko 

wizarani na ndiyo maana sijachukua muda mrefu.Kilichobaki kwa ngazi ya kanda na 

mkoa kujakufanya ukaguzi na kujiridhisha 

kwamba vigezo vimezingatiwa .” akasema 

Alfred na kutoa nyaraka kadhaa toka 

katika ile bahasha akamkabidhi Pauline 

ambaye alishindwa kujizuia kwa furaha 

aliyokuwa nayo akajikuta akiinukana 

kwenda kumkumbatia Alfred kwa nguvu 

 “ Ouh Alfred sijui nikushukuruje 

jamani kwa msaada wako huu mkubwa” 

akasema Pauline na kumbusu Alfred kisha 

wakatazamana na kitu Fulani kikapita kati 

ya macho yao .Taratibu Alfred akausogeza 

mdomo wake karibu na na mdomo wa 

Pauline ,akatoa ulimi wake na Pauline 

hakua na kipingamizi naye akatoa wake 

wakaanza kunyonyana ndimi.Ghafla mwili 

wote wa Pauline ukapigwa na kitu kama 

chaji za umeme na akajikuta 

akimkumbatia Alfred kwa nguvu zaidi 

huku wakinyonyana ndimi.Hii ni fursa 

ambayo Alfred alikuwa akiitafuta sana na 

aliitumia kikamilifu.Alianza kumfanyia 

Pauline utundu na kadiri dakika 

zilivyosonga Pauline akajikuta hajiwezi 

tena na anahitaji apatiwe huduma .Kwani 

mwili wote ulimchemka kwa ashki.Alfred 

taratibu na kwa manjonjo akamtoa 

Pauline nguo moja moja akabaki mtupu.Naye pia akatoa nguo na kazi 

ikaanza.Chumba cha kulala kilibadilika na 

kugeuka kuwa Edeni ndogo kwa raha 

walizokuwa wakipeana Pauline na 

Alfred.Mzunguko wa kwanza ukamalizika 

na kuwaacha wote wakiwa hoi.Pauline 

akafunika macho kwa aibu 

 “ Unaogopa nini Pauline? Akauliza 

Alfred huku akihema kwa nguvu 

 “ Alfred ninaona aibu sana kwa hiki 

tulichokifanya.Sikuwa nimetarajia kabisa 

kufanya kitu kama hiki hasa na mtu kama 

wewe ambaye kwanza ninakuheshimu 

sana na pili ni mume wa mtu.” Akasema 

Pauline.Alfred akabaki kimya akimtazama 

Pauline halafu akasema kwa sauti ndogo 

 “ Hii ni mara ya kwanza katika 

maisha yangu nimemsaliti mke wangu.” 

 “ I’m so sorry Alfred.Mimi ni chanzo 

cha haya yote kutokea.Ni mimi 

niliyesababisha hadi ukamsaliti mkeo.I’m 

so sorry Alfred” akasema Pauline akijutia 

kitendo kile walichkifanya.Alfred 

akamuinamia na kutaka kumbusu lakini 

Pauline akamzuia 

 “ Stop that Alfred.!!.” akasema 

Pauline 

 “ Pauline tafadhali usijilaumu kwa 

hili lililotokea.Inshort I’ve been dreaming for this to happen.We both wanted this to 

happen ,right?” Akasema Alfred 

 “ Are you crazy Alfred? Are you 

happy about this? Akauliza Pauline 

 “ Pauline I’m not sorry for this na 

wala sijuti.Naomba niwe muwazi kwako 

kwamba nilikuwa nikiota kwa jambo hili 

kutokea na leo nina furaha sana kwamba 

limetokea na huu utakuwa ni mwanzo wa 

ukurasa wetu mpya mimi na wewe” 

akasema Alfred 

 “ Alfred are you drunk? Akauliza 

Pauline akimshangaa Alfred 

 “ I’m not drunk 

Pauline.Ninachokingea kinatoka 

moyoni.Pauline I love you.I real do..” 

akasema Alfred .Pauline akainuka na 

kumtazama kana kwamba ni mara ya 

kwanza wanaonana 

 “ Toka siku ya kwanza niliyokutia 

machoni Pauline ,nimekuwa nikiishi na 

mzigo mzito sana moyoni 

mwangu.Niliitafuta kwa hamu fursa hii ya 

kuweza kukutamkia kwamba 

ninakupenda na …………….” kabla 

hajaendelea Pauline akamkatisha 

 “ Stop Alfred.Wewe ni mume wa mtu 

na una mke mzuri tu.Kwa nini uweke 

mawazo yako kwa wanawake wengine ? Tafadhali mpende mke wako.Ana kila sifa 

ya mke bora.Mtunze naye atakupatia kila 

unachokihitaji.Usielekeze macho nje kwa 

wanawake wengine hawatakusaidia kitu 

zaidi ya kukubomolea nyumba yako.Hiki 

kilichotokea leo ni bahati mbaya tu na 

hakitajirudia tena “ akasema Pauline 

 “ Pauline ni kweli nina mke mzuri na 

mwenye kila sifa nzuri lakini sifahamu 

nini kimetokea na kunifanya nikupende 

namna hii.amlaumu Mungu kwa nini 

hakunikutanisha nawe mapema kabla ya 

Garce.Tafadhali Pauline naomba 

unikubalie niwe na urafiki wa siri mimi na 

wewe ” akasema Alfred na kumfanya 

Pauline acheke kidogo 

 “ Alfred kitu unachotaka kufanya ni 

hatari sana na kina madhara 

makubwa.Sitaki matatizo na mke wako na 

zaidi ya yote sihitaji mpenzi ambaye ana 

mke wake.Ninahitaji kuwa na mwanaume 

ambaye yuko huru na ambay…..” kabla 

hajamaliza alichotaka kukisema Alfred 

akamsogelea na kuanza kumpiga mabusu 

.Pauline akajikuta akishindwa kumzuia na 

haukupita muda wakaingia katika 

mzunguko wa pili. 

 Ulikuwa ni usikuwa aina yake kwa 

Alfred na Pauline.Wote wawili walishindwa kulishinda jaribu lile kubwa 

wakajikuta wakianguka dhambini na 

kumsaliti mke wa Alfred.Kwa penzi 

alilopewa na Alfred Pauline alishindwa 

kuendelea na msimamo wake na akajikuta 

akilikubali ombi la Alfred la kutaka wawe 

na mahusiano ya siri. 

 Saa nne za asubuhi siku iliyofuata 

Alfred akarejea nyumbani 

kake.Alionekana mchovu sana hii 

ilisababishwa na kazi kubwa aliyoifanya 

usiku.Grace mke wake akampokea kama 

kawaida yake na kumpiga 

busu.Akamuandalia maji akaoga kisha 

akajitupa kitandani. 

 Hali aliyokuwa nayo Alfred ikampa 

wasi wasi mke wake . 

 “ Alred jana amelala wapi? Ni kweli 

alilala hospitali? Mbona hakunitaarifu 

kama atalala hospitali wakati siku zote 

kama kuna udharura na anahitajika 

hospitali usiku huniambia na hata 

arejeapo hunisimulia kila kilichotokea 

huko hospitali lakini leo hii imekuwa 

tofauti sana.Alirejea jana kutokea Dar es 

salaam alikoenda kufuatilia kibali cha 

hospitali ya Pauline na bil ahata 

kupumzika akaniambia kwamba 

anampelekea Pauline kibali hicho .Cha walishindwa kulishinda jaribu lile kubwa 

wakajikuta wakianguka dhambini na 

kumsaliti mke wa Alfred.Kwa penzi 

alilopewa na Alfred Pauline alishindwa 

kuendelea na msimamo wake na akajikuta 

akilikubali ombi la Alfred la kutaka wawe 

na mahusiano ya siri. 

 Saa nne za asubuhi siku iliyofuata 

Alfred akarejea nyumbani 

kake.Alionekana mchovu sana hii 

ilisababishwa na kazi kubwa aliyoifanya 

usiku.Grace mke wake akampokea kama 

kawaida yake na kumpiga 

busu.Akamuandalia maji akaoga kisha 

akajitupa kitandani. 

 Hali aliyokuwa nayo Alfred ikampa 

wasi wasi mke wake . 

 “ Alred jana amelala wapi? Ni kweli 

alilala hospitali? Mbona hakunitaarifu 

kama atalala hospitali wakati siku zote 

kama kuna udharura na anahitajika 

hospitali usiku huniambia na hata 

arejeapo hunisimulia kila kilichotokea 

huko hospitali lakini leo hii imekuwa 

tofauti sana.Alirejea jana kutokea Dar es 

salaam alikoenda kufuatilia kibali cha 

hospitali ya Pauline na bil ahata 

kupumzika akaniambia kwamba 

anampelekea Pauline kibali hicho .Cha ajabu hakurejea tena mpaka asubuhi hii 

na hakuna maelezo yoyote alikuwa 

wapi.Something is wrong ” akawaza Grace 

.Akaingia chumbani akachukua simu yake 

na kuzitafuta namba za Dr Kisusa ambaye 

ni rafiki mkubwa wa Alfred akampigia 

simu kumuuliza kama walikuwa na zamu 

ya usiku jana hospitali.Dr Kisusa akamjibu 

kwamba hawakuwa na kazi zozote usiku 

wa jana.Taa nyekundu ikawaka kichwani 

kwa Grace 

 “ Kama hawakuw ana kazi jana 

usiku,Fred amelala wapi? There is 

something is going on.Kuna mabadiliko 

nimeanza kuyaona kwa Alfred toka 

alipoanza ukaribu na Pauline.Anautumia 

muda mwingi sana akiwa na Pauline kwa 

kisingizio kwamba anamsaidia katika 

mradi wake anaotaka kuufungua wa 

hospitali.Ninapata mashaka kidogo na 

ukaribu huu yawezekana kuna kitu 

kinaendelea kati yao? Akajiuliza Grace 

 “ Hapana,niamuamini Alfred.Hawezi 

akanifanyia kitu kama hicho.NI 

mwanaume anayejielewa sana na huwa 

hana tamaa.Hata Pauline pia ni msichana 

mwenye heshima sana na sina hakika 

kama anaweza akakubali kufanya jambo 

kama hilo wakati akifahamu kabisa kwamba Alfred ni mume wa mtu.Ngoja 

niachane na hisia hizi mbaya nimsubiri 

Fred akiamka atanieleza alikuwa wapi 

jana” Akawaza Grace 

******************* 

Kwa takribani saa nzima sasa Pauline 

amekwisha amka lakini alihisi uchovu 

mwingi na kushindwa kuondoka 

kitandani.Uchovu ulitokana na shughuli 

kubwa iliyofanyika usiku ule. 

 “ ama kweli usiku wa jana haukuwa 

wa kawaida.Alfred ni mwanaume wa 

shoka.Ana pumzi kama farasi na 

amenipeleka mizunguko kadhaa bila 

kuchoka.Sikutegemea kama angeweza 

kuwa mahiri namna ile.” Akawaza huku 

akitabasamu 

 “ nashindwa hata kuelewa ilitokeaje 

mimi na lfred tukajikuta tukifanya mambo 

yale.Sikuwahi kuhisi kama ningekuja 

kumvulia nguo zangu kwa namna 

tulivyokuwa tukiheshimiana lakini jana 

imekuwa tofauti kabisa.Ouh gosh why am I 

so weak? Akajiuliza Pauline 

 “ Hata hivyo Alfred alinipeleka 

mawingunina kunirudisha.Alinipa kila 

aina ya raha.Usiku wa jana ni mojawapo ya usiku ambao sintousahau katika 

maisha yangu na umenisaidia sana 

kunipunguzia maumivu yale niliyoumia 

baada ya kutendwa na David.Japokuwa 

nilifurahia kitendo kile lakini bado moyo 

wangu unaugulia ndani,kwani nilifanya 

kitendo kile na mume wa mtu?.Kibaya 

zaidi nilimkubalia Alfred kwamba tuwe na 

mahusiano ya siri bila ya mke wake 

kufahamu..Ouh my Gosh why I did that? 

Why I was so stupid? Akajiuliza na 

kuinuka akakaa ktandani 

 “ Nimefanya kosa kubwa sana na 

mke wa Alfred akiligundua hili ataumia 

sana.Ananipenda na kuniamini na isitoshe 

yeye na Fred wanapenda mno na familia 

yao ina amani na furaha .Endapo jambo 

hili likifahamika furaha yote katika 

familia ya Alfred itatoweka.Hakutakuwa 

na amani na upendo tena na yote hii ni 

kwa sababu yangu.Kwa nini nimekuwa 

mjinga kiasi hiki kukubali kirahisi 

kumvulia nguo mume wa mtu wakati 

maumivu ya kuchukuliwa mpenzi 

ninayafahamu fika? Akajiuliza pauine 

huku machozi yakimlenga. 

 “ Nilimpenda sana David na nilikuwa 

tayari kufanya lolote kwa ajili yake lakini 

nilikuja kuumizwa sana baada ya Tamia ambaye ni rafiki yangu mkubwa 

kunizunguka na kuanzisha mahusiano na 

David.Mateso niliyoyapata yamenifanya 

hadi nikaondoka Arusha na kuja hapa 

Moshi.Nilikimbia kukwepa maumivu zaidi 

na vile vile kutafuta kuponya kidonda 

nilichoumizwa .Ninayafahamu maumivu 

ya kuibiwa bwana kwani yamenikuta 

mimi mwenyewe na mpaka sasa hivi bado 

ninaendelea kutibu majeraha ya 

moyo.kwa namna nilivyoumizwa sitaki 

kuona mtu mwingine akiumia kama 

nilivyoumia mimi kiasi cha kuwachukia 

wanaume na mapenz kwa ujumla.” 

Akawaza Pauline 

“ Pamoja na kuumizwa kote bado 

ninajikuta nikisahau maumivu yote kwa 

haraka sana na kuanguka tena kwa mume 

wa mtu.Kibaya zaidi Alfred amepofuka 

kabisa kwangu na hasikii wala haoni.Yuko 

tayari kufanya jambo lolote kwa ajili 

yangu.Cha kusikitisha zaidi hata mimi 

mwenyewe ninajihisi kutokuwa na nguvu 

za kupambana na jaribu hili kubwa 

kuwahi kukutana nalo katika maisha 

yangu.Tayari Alfred ameanza kuniingia 

katika mishipa ya mwili wangu na 

ninaogopa kwamba sintakuwa na uwezo 

wa kujizuia tena.”  “ Lakini kwa nini nimefikia hatua 

hii? Kwa nini nimejitumbukiza katika 

mahusiano na mume wa mtu? .akiwa 

kitandani amejinamia akiwaza mara 

kengele ya mlango ikalia .Akainuka na 

kwenda kuufungua mlango.Akakutana na 

sura yenye tabasamu ya Sanya 

 “ ouh Sanya !! akasema Pauline 

 “ Pauline !!”akasema Sanya huku 

wakipeana mikono 

 “ Umejuaje kama niko chumba 

hiki?akauliza Pauline 

 “Nimelazimika kwenda kuuliza 

mapokezi wakanielekeza” 

 “ karibu ndani Sanya…” akasema 

Pauline na kumkaribisha Sanya ndani 

 “ Samahani sana kwa kukusumbua 

Pauline.” Akasema Sanya 

 “usijali Sanya.Nilikwisha amka 

kitambo nilikuwa nimekaa tu.habariza 

toka jana? 

 “ habari nzuri sana.Nimeboreka sana 

kukaa peke yangu chumbani nimeona nije 

kukuuliza kama utaenda kutembelea 

mradi wako wa hospitali ili 

tuongozane.Nina hamu ya kuzunguka 

mjini Moshi”  “ Nitakwenda baadae kidogo 

kutembelea mafundimtutaongozana wote 

”akasema Pauline. 

 Walikunywa chai pamoja na saa sita 

za mchana wakaondoka kwenda kuangalia 

maendeleo ya mradi wa hospitali.Sanya 

alifurahi na kumpongeza Pauline kwa 

juhudi zile kubwa na akaahidi kumsaidia 

kwa kila hali kuhakikisha mradi ule 

unakamilika.Baada ya kutoka katika 

mradi ule wakaelekea moja kwa moja 

katika hoteli moja kubwa iliyo katikati ya 

mji wa Moshi kujipatia chakula. 

 “ Sanya ulisema kwamba unataka 

kwenda Arusha.Lini umepanga kwenda 

huko? Akauliza Pauline wakati wakipata 

chakula cha mchana 

 “ Ndiyo ninahitaji sana kwenda 

Arusha kuna mambo Fulani ninataka 

kuyashughulikia lakini nahitaji sana 

kwenda na mwenyeji anayepafahamu 

vyema ndiyo maana nilikuomba kama 

utapata nafasi tuongozane kwenda huko.” 

 “ Usijali Sanya.Mimi niko tayari 

kuongozana nae kuelekea Arusha .” 

 “ Ahsante sana Pauline.Unafahamu 

sehemu inaitwa Usa river? Akauliza Sanya 

 “ Usa river ninapafahamu 

sana.Nimezaliwa Arusha nimekulia Arusha kwa hiyo ninaifahamiu kila 

sehemu ya Arusha.” 

 “ safi sana.Pale usa river kuna kituo 

cha kulelea watoto wadogo.Unakifahamu? 

akauliza Sanya 

 “hapana sikifahamu hicho kituo 

lakini tutaulizana tutaelekezwa.”akasema 

Pauline 

 “ ahsante sana Pauline.Nitashukuru 

sana kwa msaada wako” akasema Sanya 

wakaendelea kula na baada ya muda 

Sanya akauliza 

 “ Wazazi wako wote bado wako hai? 

 “ Ni baba pekee aliye bado hai lakini 

mama amekwisha fariki” 

 “Pole sana Pauline: akasema Sanya 

 “ Ahsante sana .Ni kazi ya Mungu 

siku zote haina makosa.Vipi wewe wazazi 

wako wote bado wako hai? Pauline naye 

akauliza.Sanya akanywa juice kidogo na 

kusema 

 “ hiyo ni sababu iliyonifanya nije 

Tanzania ” akasema Sanya na kunyamza 

kidogoakanywa funda la juice kisha 

akasema 

 “ Ninaishi Marekani kwa sasa lakini 

asili yangu ni Tanzania” 

 Pauline akashangaa sana .  “ Wow ! kwa hiyo wewe ni 

mtanzania? Akauliza Pauline 

 “ japokuwa ni raia wa marekani 

lakini asili yangu ni Tanzania.Nilizaliwa 

Tanzania.Baba na amama yangu wote ni 

watanzania.Kwa bahati mbaya sana 

sikubahatika kuwafahamu wazazi 

wangu.Nilielezwa na walezi wangu 

kwamba niliokotwa katika geti la kituo 

cha kulelea watoto wadogo usa river 

nikiwa bado mdogo sana. Nililelewa pale 

Usa river na aliyekuwa mmiliki wa kituo 

hicho kwa wakati huo nakwa bahati nzuri 

akatokea kunipenda sana .Muda ulipofika 

wa yeye kurejea nchini kwao Marekani 

alinichukua na mimi nikaongozana naye 

nikiwa bado mdogo.Ninamshukuru sana 

mama Yule na familia yake kwani 

wamenilea kwa upendo mkubwa mno na 

hata siku moja sikuwahi kujihisi ni tofauti 

na wao.Nimesomeshwa vizuri na mpaka 

sasa nina maisha yangu mazuri na 

ninajitegemea .Kwa mudamrefu 

nimekuwa nikitafakari sana kuhusu 

wazazi wangu na mwishowe nimeamua 

kuja Tanzania kuitafuta asili yangu.Nataka 

nijaribu bahati kama ninaweza kuwapata 

wazazi wangu japokuwa sina hakika lakini sivibaya kujaribu.”akasema Sanya.Pauline 

akavuta pumzi ndefu na kusema 

 “Pole sana Sanya .Nilipokuona 

sikuwahi kuhisi kama una asili ya 

Tanzania na pili sikuhisi kama unaweza 

kuwa na historia ya kuhuzunisha namna 

hii”akasema Pauline.Sanya akatabasamu 

na kusema 

“ Mara ya kwanza nilipoambiwa 

kuhusu historia yangu nililia 

sana.Nilimlalamikia sana Mungu kwa nini 

mimi nifanyiwe hivi na wazazi 

wangu.Baadae niliona hakuna sababu ya 

kulia badala yake ninapaswa kumshukuru 

Mungu kwa sababu ndiye aliyeniwezesha 

nikawa hai.Nilipotupwa pale kituoni 

ningeweza hata kuuawa. Au hata mtu 

aliyenitupa angeweza kuniua na kunitupa 

jalalani lakini kwa maongozi ya Mungu 

nikaenda kutupwa katika geti la kituo na 

malaika wa Mungu wakanisimamia na 

kunilinda hadi 

nilipookotwa.Nilimshukuru sana Mungu 

kwa zawadi hii ya uhai na nilichobaki 

nikimuomba anipe moyo wa 

kusamehe.Niwasamehe wazazi wangu na 

siku moja aweze kunikutanisha 

nao.Hatimaye baada ya miaka mingi 

kupita nimewasamehe wazazi wangu na nimekuja rasmi kuwatafuta ili niweze 

kuwafahamu na kuungana nao.Kwa hiyo 

Pauline mmi ni mtanzania,nimezaliwa 

hapa na wazazi wangu wako ndani ya nchi 

hii.Sina hakika kama bado wako hai ama 

wamekufa lakini ninamuomba Mungu kila 

siku wazazi wangu wawe hai na niweze 

kukutana nao”akasema Sanya. 

 “ Sanya nimekosa neno la kusema 

kwa simulizi hii ya maisha yako 

uliyonisimulia.Inatia simanzi 

sana.Ninachoweza kukupongeza ni 

kwamba umefanya uamuzi sahihi wa kuja 

kuwatafuta wazazi wako.Binafsi 

ninakuahidi ushirikiano wangu mkubwa 

katika suala hili na ninakuhakikishia 

kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu 

kuhakikisha kwamba kama wazazi wako 

bado wako hai 

wanapatikananaunaungananao tena” 

Akasema Pauline 

 “ Ahsante sana Pauline kwa 

ushirikiano wako huu mkubwa.Nina 

bahati sana ya kukutana na mtu kama 

wewe.By the way umeolewa ?akauliza 

Sanya.Pauline akacheka kidogo na kusema 

 “ Hapana bado sijaolewa” akajibu 

Pauline  “ Ouh Pauline,msichana mzuri kama 

wewe kwa nini mpaka sasa bado 

hujaolewa? Yule uliyekuwa naye jana ni 

mchumba wako? Akauliza sanya 

 “ Dr Alfred ? 

 “ Simkumbuki jina lake lakini yule 

uliyeondoka naye jana tulipokutana 

jioni”akasema Sanya. 

 “ Ni Dr Alfred.Yule si mchumba 

wangu.Ni rafiki yangu nimekutana naye 

hapa hapa Moshi” akasema Pauline 

“ ouh ! nilipowaona nikafikiri mna 

mahusiano kwa namna 

mlivyochangamkiana.Mtu yeyote 

akiwaonalazimaatajua ninyi ni 

wapenzi.mnapendeza sana mkiwa 

pamoja”akasema Sanya,Pauline 

akashindwa ajibu nini akabaki 

anatabsamu.Aliogopa kumwambia ukweli 

Sanya kwamba Fred ni mume wa mtu. 

 “ mwishoni mwa wiki hii tutakwenda 

Arusha na tutaanza kulifanyia kazi suala 

lako”akasema Pauline kwa nia ya kutotaka 

kuongelea kuhusu Dr Alfred.Siku ile 

ukawa ni mwanzo wa urafiki mkubwa kati 

ya Pauline na Sanya 

******************Vivian za kutaka kufahamu mume wake 

alikuwa anasumbuliwa na tatizo gani kiasi 

cha kugeuka kuwa mlevi kupindukia bado 

Tino aliendelea kusimamia kauli yake 

kwamba hana tatizo ila ameamua tu 

kustarehe kwa kunywa pombe.Hali hii 

ilimtesa sana 

Vivian na hakujua afanye nini ili aweze 

kulifahamu tatizo la mume 

wake.Alijitahidi sana kuonyesha mapenzi 

ya hali ya juu lakini kadiri siku zilivyozidi 

kwenda ndivyo hali ya Fred ilivyozidi 

kubadilika . 

 Ni siku ya alhamisi saa tano za 

asubuhi , Tino akawasili katika shule ya 

Mwalimu lucy.Aliegesha gari katika 

maegesho na kuvuta pumzi ndefu. 

 “ Sikuwahi kufikiria kabisa kama 

siku moja nitamtafuta Lucy lakini sina 

ujanja lazima nimtafute. Lazima nionane 

naye.Ni yeye tu anayeweza kuiweka sawa 

akili yangu.” Akawaza Tino na kuchukua 

chupa ya uturi akajipulizia ili harufu ya 

pombe isiweze kusikika. 

 “ Lucy alinipenda kwa moyo wake 

wote .Sikuwa mkamilifu kwake lakini 

alinivumilia sana kwa kuwa 

alinipenda.Pamoja na mambo yote mazuri aliyonifanyia bado nilimdharau na 

kumuona hafai.Nilimuacha Lucy 

nikadanganywa na uzuri wa 

Vivian.Nilidhani nimeokota almasi kumbe 

nilidanganywa na mnga’o na si almasi bali 

chupa.I was so stupid.Lazima nionane na 

Lucy,nimuombe msamaha kwa 

yaliyotokea wakati ule na kama 

ikiwezekana tuyarejeshe mapenzi 

yetu.Japo ni muda mrefu hatujaonana 

lakni nina hakika kabisa kwamba Lucy 

bado ananipenda .” akawaza Tino na 

kufungua mlango wa gari akashuka 

 “ lakini nina hakika na hiki 

nnachotaka kukifanya? Akawaza Tino 

akasita kidogo na kuinama akafikiri 

 “ lazima nionane na Lucy..Siwezi 

ondoka bila kuona naye”akawaza Tino na 

kupiga hatua kuelekekea katika jingo la 

utawala ambako alielekezwa ilipo ofisi ya 

mkurugenzi wa shule .Kulikuwa na watu 

wawili waliokuwa wakisubiri kuonana na 

mwalimu Lucy na baada ya watu wale 

kumaliza shida zao ikafuata zamu ya 

Tino,akaufungua mlango taratibu na 

kuingia ndani.Mwalimu Lucy akapatwa na 

mshangao mkubwa sana kwa kumuona 

Tino pale ofisini kwake.Hakusema kitu 

akasimama na kubaki akimshangaa.  “ hallow Lucy ! akasema Tino 

 “ You ?!!..siamini machoyangu .” 

 “ habari yako Lucy”akasema Tino 

 “ what brings you here Martin? 

Akauliza mwalimu Lucy. 

 “ Nimekuja kukutembelea 

Lucy.Habari ya siku nyingi? Akasema Tino 

huku akivuta kiti na kuketi 

 “ Martin tafadhali naomba 

usikae.Sijakuruhusu ukae katika kiti 

changu “akasema mwalimu Lucy 

 “ Lucy najua hukutegemea kabisa 

kuniona mahala hapa na ndiyo maana 

umhamaki kiasihiki.Ninaomba samahani 

sana kwa kuja ofisini kwako bila 

taarifa.Nisamehe sana lakini sijaja hapa 

kwa shari,nimekuja kwa nia nzuri ya 

kukusalimu na kukujulia hali kwani ni 

muda mrefu umepita 

hatujaonana.”akasema Tino.Mwalimu 

Lucy akacheka kidogo na kusema 

 “ Ninacheka kutokana na watu 

wanavyokosa aibu.Sikutegemea kabsia 

kwa mtu kama wewe martin kwa mambo 

uliyonifanyia kunifuata hapa ofisini 

kwangu.hahaha.aa”akasema Lucy 

nakumaliza kwa kicheko .Martin akainuka 

kitini “Lucy nimekueleza kwamba 

nimekuja hapa si kwa shari bali kwa nia 

njema kabisa ya kukusalimu na kujua 

unaendeleaje.Kwani kuna ubaya 

kutembeleana hata kama tumetengena? 

Sidhani kama kuna ubaya wowote lakini 

kama hutaki kuniona ofisini kwako sawa 

ninaondoka zangu” akasema Tino na 

kuanza kupiga hatua kuondoka.Alipofika 

mlangoni Lucy akamuita 

 “ Martin come back here.”akasema 

Lucy na Martin akageuka na kurudi tena 

ofisini 

 “ Najua mpaka umeamua kunifuata 

hapa si bure kuna jambo 

limekuleta.Nieleze kilichokufanya 

ukanyanyua miguu yako hadi hapa 

kwangu. “ akasema Lucy 

 “ Lucy najua ukiniona hapa unasikia 

kichefu chefu kwa hiyo sitaki kukukwaza 

so I’ll be quick”akasema Tino 

 “ Ni kweli uamuzi wa kuja hapa 

kwako haukuwa uamuzi rahisi lakini 

imenilazimu kuja na kikubwa kilichonileta 

hapa kwako ni kutaka kutafuta amani na 

wewe.Tuyamalize masuala yale yaliyopita 

na tuendelee kuishi kwa amani.” 

 “ Are ou crazy Martin? akauliza Lucy  “ Lucy naomba nisikilize japo kwa 

dakika kumi tu.Nafahamu sistahili hata 

kupata dakika moja ya kuongea nawe kwa 

mambo niliyokufanyia na nimekuja hapa 

rasmi kukuomba samahani kwa kila kile 

nilichokufanyia kiwe kidogo ama 

kikubwa.Nisamehe sana Lucy.Kuna 

mambo mengine niliyafanya kwa 

kuongozwa na ujana na tamaa.Nilifanya 

mambo mengine bila kujua athari 

zake.Baada ya miaka mingi kupita sasa 

ninaziona athari zake.sikupaswa kufanya 

vile nilivyokufanyia Lucy kwa hiyo 

narudia tena kukuomba unisamehe 

sana”akasema Tino 

 “Martin umemaliza ulichotaka 

kuniambia? Akauliza Lucy 

 “ Nimemaliza Lucy.Ni hilo tu 

nililotaka kukueleza.Nahitaji sana 

msamaha wako Lucy” akasema Tino 

 “ Ok nimekusikia Martin .Sasa 

naomba uinuke na uufungue mlango ule 

utoke na usithubutu tena kukanyaga 

katika ofisi hii.Iswear I will never forgive 

you..!!”akasema Lucy 

 “ Lucy najua bado una hasira namimi 

lakini naomba utafute ndani ya moyo 

wako unisamehe kwa yale yote 

yaliyotokea.Ninaomba kama hutajali tuwe marafiki hata kutembeleana au kujuliana 

hali tu.Naomba unipe nafasi hiyo tena Lucy 

ya kuwa rafiki yako wa kawaida 

tu”akasema Tino.mwalimu Lucy 

akatabasamu na kusema 

 “ Unaiona pete hii? Akauliza Lucy 

huku akimuonyesha Tino pete katika 

kidole chake 

 “ tayari kuna mwanaume aliyeiona 

thamani yangu na akanifuta machozi na 

majeraha ya moyo ,akanipandisha hadi 

katika kilele cha juu kabisa cha mawingu 

na kunifanya ni mwanamke mwenye 

furaha kuliko wote na akanivisha pete hii 

ya uchumba.Kwa hivi sasa mimi ni 

mchumba wa mtu na sihitaji tena marafiki 

kama wewe.Umebakki sehemu ya histora 

yangu kwa hiyo usitegemee mimi kuwa 

naurafiki tena na wewe sikuhitaji tena 

katika maisha yangu .Zaidi ya 

yote…”akasema Mwalimu Lucy na 

kuufungua mkoba wake akatoa 

makaratasi fulani 

 “Nimetoka hospitali sasa hivi 

kupima.I’m pregnant.”akasema huku 

akimpatiaTino makaratasi yale ya 

hospitali.Tinoalibakiamesimama 

ameduwaa kamaaliyepigwa na 

umeme.Midomoilikuwa inamcheza cheza  “nadhani sasa unakubaliana nami 

kwamba sikuhitaji Tino katika maisha 

yangu.Hivi sasa nina maisha mengine 

kabisa na yenye furaha .Nilikupa nafasi 

katika moyo wangu ukaichezea kwa hiyo 

sihitaji hata uwe rafiki yangu wa 

kawaida.Kama hutajali naomba uondoke 

nina kikao na waalimu sasa hivi” akasema 

mwalimu Lucy.Tino alihisi miguu 

kumuisha nguvu.Aliumia sana moyoni na 

hasa pale Lucy alipomweleza kwamba ana 

ujauzito.Taratibu akajizoa zoa na 

kuufungua mlango akatoka 

 “ Stupid !! akasema Lucy baada ya 

Tino kutoka. 

 “ mwanaume hana haya 

huyu.Sikutegemea kama siku moja 

angethubutu kuja kunitembelea .Eti 

anatafuta urafiki..Nilimpa nafasi 

akaichezea akauvunja kabisa moyo wangu 

nakunifanya nikaichukia dunia na watu 

wake na leo anathubutu kuja na kuniomba 

msamaha..Lakini nimempa vidonge vyake 

na hatathubutu kunitafuta tena..” akawaza 

mwalimu Lucy.. 

 Tino aliingia ndaniya gari lake 

akaegemea kiti .Kichwa kilijaa mawazo 

mengi  “ I was wrong..iwas so 

wrong.Kumuacha Lucy nilifanya maosa 

makubwa sana.”akawaza na kwa mbali 

machozi yakamlenga.Akawasha gari na 

kuondoka zake. 

 “ Lucy ni mjamzito ! akaendela 

kuwaza 

 “ Kauli ile 

iliniingiamoyonikamamwibana 

kunichoma sana.Kamanisingeachananaye 

kwa hivisasa tayari tungekuwa na watoto 

hata zaidi ya mmoja .Kwa kwelinilikosea 

sana.I was wrong” akawaza 

 “ Kwa Lucy hakuna mategemeo 

tena.Tayari amekwisha endelea namaisha 

yake na ana furaha sana.hakuna wa 

kumlaumu zaid ya kujlaumu mwenyewe 

kw aujinganilioufanya .kwa sasa natakiwa 

nijipange upya nijue nini nitafanya.Kuna 

kitu kimoja ninachotakiw akufanya sasa 

hivi” akawaza Tino. 

Baada ya kuondoka shulenikwa Lucy,Tino 

akaelekea mojakwa moja dukani kwake . 

“ Ninajilaumu sana kwa ujinga 

nilioufanya wa kukorofishana na marafiki 

zangu hasa Armando.Katika wakati kama 

huu yeye angekuwa ni mshari wangu 

mkubwa sana.Nilifanya kosa kubwa sana 

na ninatakiwa kumtafuta na kumuomba msamaha.Mambo aliyonieleza ni ya kweli 

kabisa lakini niliongozwa na hasira 

nikamtukana na hata kufikia hatua ya 

kumtishia bastora.” Alipowaza kuhusu 

jambo hili picha ya kilichotokea siku ile 

ikamrudia akajilaumu sana.Haraka 

haraka akachukua simu yake na 

kuzitafuta namba za simu za Armando na 

kupiga.Simu ikaita na kukatika bila 

kupokelewa,akapiga tena lakini ikawa vile 

vile haikupokelewa. 

 “ Inawezekana bado ana hasira na 

mimi kwa maneno machafu 

niliyomtamkia.What am I gong to do? 

Akajiuliza Tino ,akachukua tena simu na 

kujaribu kupiga lakini bado iliita tu bila 

kupokelewa.. 

 “ lazima nimtafute Armando 

nimuombe msamaha kwa ujinga ule 

nilioufanya.Kwa wakati kama huu yeye ni 

mtu muhimu sana na ninamuhitaji mno” 

akawaza Tino huku akiinuka akaingia 

katika gari lake na kuelekea moja kwa 

moja katika hoteli inayomilikiwa na 

Armando akamuulizia na kuambiwa 

kwamba yuko Mererani katika shughuli 

zake za madini. 

 “ Nitamfuata huko huko 

Mererani.”akawaza Tino na kujaza gari mafuta akaanza safari ya kuelekea 

Mererani kumtafuta Armando 

 “ Ninajuliza sana kwa nini Vivian 

aamue kufanya jambo kamalile na kutoa 

mimba bila ya kunishirikikisha? Hakuwa 

tayari kulea watoto? Hakuwa na imani 

kwamba ninampenda kwa dhati 

?Natamani nipate nafasi ya kumuuliza 

sababu zilizomfanya akaamua kutoa 

mimba na hatimaye akaondolewa kizazi 

na kupoteza uwezo wake wa kuzaa watoto 

tena.” Akawaza Tino akiwa katika 

mwendo mkali akielekea Merererani 

kumtafuta rafiki yake Armando 

 “Nilimpenda sana Vivian na 

nilimpatia kila alichokihitaji.Anabadilisha 

magari kama nguo .Nimemnunulia hadi 

gari la milioni mia mbili na hamsni.Kama 

anapata mambo haya yote kwa nini basi 

hakutaka kunizalia walau hata mtoto 

mmoja na badala yake akaenda kuua 

watoto wangu? Kibaya zaidi amekuwa 

akinidanganya kwamba anataka tufunge 

ndoa ili anizalie watoto wakati anafahamu 

kabisa akwamba uwezo huo wa kunizalia 

watoto hana,kwa nini anidanganye? 

Akaendelea kuwaza huku safari 

ikiendelea  “ Hakuna sababu ya msingi 

anayoweza kunipa iliyomfanya akatoa 

mimba wakati anapata kila kitu na uweo 

wa hata yeye kwenda kujifungulia ulaya 

upo..Picha ya haraka haraka unayoweza 

kuipata ni kwamba Vivian hakutaka kuwa 

na mtoto.Hataki kulea na h ii inamaanisha 

kwamba hafai kuwa mke.Hafai kuwa 

mama. Na ndiyo maana alikwenda kutoa 

mimba.Nakumbuka wakati ninamchukua 

toka kwa Yule bwana wake wa zamani 

alimuacha mtoto wake akiwa mdogo sana 

.Ninachoshukuru Yule bwana wake 

alikuwa ni mtu mstaarabu sana kwani 

angeweza hata kumshitaki Vivy kwani 

mtoto wao bado alihitaji uangalizi wa 

mama yake.Toka nimemchukua Vivian 

hadi leo hii sijawahi hata siku moja 

kumsikia akimzungumzia huyo mwanae 

aliyemtelekeza.Huyu mwanamke 

nishetani kabsia na hafai hata kidogo 

kuwa mke.Ninadhani ni kwa maongozi ya 

Mungu nimeweza kulitambua hili angali 

mapema kabla sijakula kiapo cha 

ndoa.Kwa sasa suala la ndoa yangu naye 

halipo tena na kilichobaki ni kuanza 

maandalizi ya kuachana naye.kwa kuwa 

hatuna kifungo chochote kinachotufunga 

mmi na yeye haitaniwia ugumu sana wa kuachana naye.Nitatafuta mwanamke 

mwingine mwenye mapenzi ya kweli nasi 

huyu mlaghai anayejali pesa na 

mali..”akaendelea kuwaza Tino 

 Hatimaye Tino akafika Mererani na 

kuanza jitihada za kumtafuta Armando na 

saa saba za mchana akafanikiwa 

kumpata.Armando alifurtahi sana 

kuonanana Tino kitu ambacho 

Tinohakukitegemea .Aasitisha 

shughulizake wakaongozana hadi hotelini 

kupata chakula. 

 “ Armando nimekupigia simu zaidi 

ya mara kumi hujapokea.”akaanzisha 

maongezi Tino 

 “ Utanisamehe Tino nilishuka 

shimoni kwa hiyosikuwa na simu.Mpaka 

sasa badosijaichukua simu yangu.”akajbu 

Armando 

 “ Mawazoni nikajua bado unahasira 

kutokana na yale mambo 

yaliyotokea”akasema Tino na kumfanya 

Armando aangue kicheko 

 “ Nilikwisha yasahau yale mambo na 

kamwe siwezi kukasirika kwa ajili ya 

kitendo kile.Yale ni mamboya kawaida 

kutokea kwa wanaume hivyo 

sikushanga.Nilitegemea tungeyamaliza 

mambo yale kiume muda ukiwadia Mambo yanakwendaje lakini?akauliza 

Armando.Tino akavuta pumzi ndefu na 

kusema 

 “ Armando nimelazimika kuja 

mwenyewe kukutafuta na kukuomba 

msamaha sana kwa jambo la kijinga 

nililolifaya siku ile.” 

 “Tino please stop..yale 

mamboyamekwisha pita na hatutakiwi 

kuyazungumza tena” akasema Armando 

 “ Armando tafadhalinaomba 

unisikilize .Nimechoma mafuta hadi huku 

kuja kukuomba msamaha kwa kitendo 

cha siku ile.Baada ya kukaa na kujitafakari 

nimegundua ujinga nilioufanya.Nisamehe 

sana Armando.” Akasema Tino na 

kuchukua glasi ya bia akanywa kidogo na 

kuendelea 

 “Ulichoniambia ni kitu cha kweli 

kabisa.Nilifanya uchunguzi na nikagundua 

kwamba ni kweli mke wangu alitoa mimba 

na akaondolewa kizazi na hana uwezowa 

kupata mtoto tena katika maisha yake 

yaliyobaki.Armando wewe ni rafiki wa 

kweli,wewe ni zaidi ya rafii,ni zaid ya 

ndugu.Unanipenda na unanithamini ndiyo 

maana ukawa tayari kunieleza jambo lile 

gumu. Ni bahati mbaya sana nililichukulia 

jambo lile kwa hasira kwani si jambo jepesi kulitamka wala kulisikia na ndiyo 

maana yakatokea yale 

yaliyotokea.Armando nisamehe sana 

ndugu yangu na tuyafute yale yote 

yaliyotokea tuendelee na urafikiwetu 

kama zamani.Toka nimelifahamu suala 

hili nimechanganyikiwa na sioni nani 

ambaye ana weza akanishauri nini nifanye 

kwa wakati huu mgumu.Nimebaki 

ninakunywa tu pombe ili kuondoa 

mawazo.Armando tafadhali nipokee tena 

ndugu yako wewe ndiye rafikiyangu na 

mshauri wangu mkubwa.Ninakuhitaji 

sana katika kipindi hiki” akasema 

Tino.Armando akanywa funda kubwa la 

bia na kusema 

 “ Martin ,mimi na wewe tumetoka 

mbali sana kabla hata hujafahamiana na 

Vivian.Ninakufahamu vizuri sana kwa hiyo 

urafiki wetu hauwezi ukavunjika ndani ya 

siku moja wala kwa suala dogo kama 

lile.Uamuzi wa kukueleza ukweli kuhsu 

suala hili la mkeo haukuwa rahisi kwani 

niliamini kwamba ni uamuzi wenye athari 

kwanza kwako na mkeo na pia mimi na 

wewe na mimi na mkeo.Lakini kwa 

kuuthamini urafiki wetu na kwa kuwa 

sikufurahishwa na kitendo alichokifanya 

mkeo niliamua liwalo na liwe nikakueleza ukweli na yakatokea yale yaliyotokea na 

ninashukuru kwamba umefanya 

uchunguzi na umegundua kwamba 

nililokwambia ni jambo la kweli 

kabisa.Hili ni suala zito sana linalohusu 

mustakabali mzima wa maisha yako ya 

sasa na mbeleni kwa hiyo unatakiwa 

kufanya maamuzi kwa makinisana.” 

akasema Armando akanywa tena funda 

lingine la bia akaendelea 

 “ baada ya kuufahamu ukweli 

,umefanya maamuzi gani? Akauliza 

Armando 

 “Kusema ukweli mpaka sasa hivi 

bado sijaamua nini cha kufanya na ndiyo 

maana nimekutafuta kwa ajili ya ushauri” 

akasema Tino 

 “ Martin sisi tunaweza tukakushauri 

lakini maamuzi makubwa yanatakiwa 

kutoka kwakowewe mwenyewe. “akasema 

Armando 

 “ Mimi nilichokifikiria ,Yule 

mwanamke hanifai tena.laiti kama 

angenishirikisha katika suala hili kidogo 

ningemuelewa lakini amelifanya jambo 

hili kwa siri na siku zote amekuwa 

akaniahidi kwamba baada ya kufunga 

ndoa atanizalia watoto ndiyo maana 

unaona nilifurahi sana baada ya kusikia kwamba hata mumewe anataka ndoa yao 

itenguliwe.Nilifurahi kwa kuamini 

kwamba ile ndoto yangu ya siku nyingi ya 

kupata watoto wangu inakwenda 

kutimia.Sikujua kumbe niliuziwa chupa 

badala ya almasi.Alichokuwa anakitafuta 

Viviani ni kuishi maisha mazuri ya anasa 

nasi kulea familia ..Tungebahatika 

kufunga ndoa nisingekuwa na ujanja tena 

na angeendelea kutafuta visingizio vya 

mara kwa mara kuhusu kutoshika 

mimba.Kwa ufupi nimedhamiria kuachana 

naye”akasema Tino.Armando akamuita 

muhudumu akamuomba awaongezee 

vinywaki kisha akasema 

 “ Ni uamuzi mgumu lakini wenye 

faida na manufaa kwako.Usinichukie kwa 

kusema haya lakini ukweli nikwamba yule 

mwanamke hakufai hata kidogo hasa 

utokana na mambo aliyoyafanya.Huyu 

shida yake yeye si kulea watoto wala 

familia shida yake yeye ni kupata maisha 

mazuri tu na ndiyo maana alidirki hata 

kumkimbia mume wake na kuja kwako 

akifuata maisha mazuri .Alimuacha 

mumewe na mwanae mdogo kabisa 

ambaye alihitaji sana malezi 

yake.Mwanamke yule hastahili kuwa mke 

na wala hafai kuwa mama kwa hiyo nakupongeza kwa hilo uliloamua 

kulifanya na ninakuomba usirudi 

nyuma.Najua kutakuwa na kugawana 

baadhi ya mali kwa sababu umeishi naye 

kwa kipindi kirefu lakini si mbaya sana ili 

mradi uachane naye na uyaanze maisha 

yako mapya. Tafuta mwanamke mzuri 

ambaye anafaa kuwa mke na uoe akuzalie 

watoto uishi maisha mazuri na yaliypojaa 

furaha.”akasema Armando vinywaji 

vikaongezwa wakaendelea na maongezi 

huku wakipata vinywaji.Urafiki wao 

ulirejea kama zamani 




Baada ya Tino kuondoka ,mwalimu 

Lucy akajiegemeza katika kiti chake na 

kuzamamawazoni. 

 “ Yule baradhuli ameniharibia siku 

tayari.Sikuwahi kufikiria hata siku moja 

kama iko siku anaweza akadiriki 

kunitafuta.Sijui kafikiria nini hadi 

akaamua kuja halafu bila aibu anataka eti 

tuwe marafiki.Hana hata aibu kabisa Yule 

mjinga kwa mambo aliyonitendea leo hii 

anataka mimi na yeye tuwe marafiki? 

Katu jambo hilo haliwezekani hata kidogo 

.Kwa sasa tayari nina maisha yangu mengine yenye furaha.Ninaamini huyu 

niliyempata hataniumiza tena.Namuomba 

sana Mungu anisaidie yasinitokee kama 

yaliyonitokea huko nyuma lakini nina 

imani kubwa na Robin kwamba hawezi 

kuniliza kama walivyoniliza wengine .” 

Mara sura ya Robin ikamjia akatabasamu 

 “ Nimemkumbuka sana Robin 

,nilitaka nikaonane naye jioniya leo nimpe 

taarifa hizi nzuri lakini siwezikusubiri 

hadi jioni rngoja nikamfanyie surprise 

ofisini kwake..Sijui atazipokeaje taarifa za 

huu ujauzito.Ee Mungu nisaidie yasije 

yakanitokea kama ya kule 

nyuma.Ninampenda sana Robin na ndiyo 

maana nimejitoa kila kitu kwa ajili 

yake.Hatukuwa tumepanga kuhusu jambo 

hili lakini nimejikuta siwezi kujizuia tena 

na ninataka mapenzi yetu yashamiri zaidi 

siku hadisiku na njia pekee ya kuzidi 

kuyapa nuru mapenzi yetu ni kwa kupata 

mtoto na Robin.Nimekuwa nikitamani 

sana kupata mtoto mwingine baada ya 

kumpoteza Angela lakini sikuwaamini 

tena wanaume hadi alipotokea Robin 

ambaye moyo wangu umemuamini na 

nimeaamua kwa ridhaa yangu mwenyewe 

kuzaa naye mtoto. “ akawaza mwalimu Lucy na kuchukua mkoba wake akatoka 

kuelekea ofisini kwa Robin 

 Alipokewa vizuri sana na 

mwanadada aliyekuwa mapokezi na kwa 

bahati nzuri Robin alikuwepo ofisini.Lucy 

akaufungua mlango wa ofisi ya Robin 

akaingia 

 “ Lucy ! Robin akashangaa.Hakuwa 

ametegemea kama Lucy anageweza kufika 

pale ofisini kwake mida ile.Akainuka na 

kumkumbatia akambusu kisha akamshika 

mkono hadi katika sofa lililokuwamo mle 

ofisini wakaeti. 

 “ Sikutegeema kabisa kama 

ungeweza kufika hapa mida hii” akasema 

Robin 

 “ Imenilazimu kuja Robin na 

samahani kwa kuja bila taarifa.” 

 “usihofu Lucy hii ni ofisi yako pia.” 

 ‘” Ahsante Robin.Kuna mambo 

mawili yaliyonileta hapa kwako.la kwanza 

si la muhimu sana lakinisi vibaya 

nikakufahamisha.Tino amekuja leo ofisini 

kunijulia hali” 

 “ what !! Tino amekufuata leo? 

Alikuwa anahitaji nini? akauliza Robin 

 “ hakuwa na jambo la maana 

lililomleta alidai kwamba amekuja 

kunijulia hali na eti anataka tuwe marafiki wa kawaida”akasema Lucy.Robin 

akacheka kidogo na kusema 

 “ Ulimjibu nini? 

 “ I sent him away.Nilimueleza ukweli 

kwamba kwa hivi sasa tayari nina mtu 

wangu na ananipenda na nikamuomyesha 

pete hii hapa kdoleni.” Akasema 

Lucy.Robin akatabasamu na kumshika 

Lucy mkono 

 “ Ulifanya vizuri Lucy. Kwa mambo 

aliyokufanyia hapaswi kabisa hata 

kukusogelea.Ningekuwa karibu 

ningemcha vibao” 

 “ hakuna haja ya kufanya hivyo 

Robin.Dunia itamfunza.”akasema Lucy 

 “ Kabla hujanieleza jambo la pili hata 

mimi nina jambo zuri ninataka kukueleza 

.” akasema Robin 

 “ jambo gani Robin? 

 “ Nmepigwa simu na padre benedict 

Sambui yeye ndiye anayeshughulikia 

masuala ya wanandoa na amenitaarifu 

kwamba shauri letu limemfikia mezani 

kwake na alitaka nifike ofisini kwake 

kesho asubuhi niaonane naye.Mambo 

yanakwenda vizuri sana na 

inavyoonekana suala hii haliwezi 

kuchukua muda mrefu sana kwani 

vigezovyote vya kuifanya ndoa yangu itenguliwe vipo wazina kwa mujibu wa 

maelezo ya Padre Benedict ni kwamba 

suala hili halitaweza kuchukua muda 

mrefu sana kama tunavyodhani kwa 

sababu siku hizi sheria zimerahisishwa 

sana tofauti na zamani.kwa hiyo 

tutegemee mambo mazuri siku si nyigi 

sana:” akasema Robin 

 “ Hizoni habari njema sana .Mungu 

atatusimamia Robin na suala hili 

litakwisha.Tutakuwa pamoja muda si 

mrefu sana Robin” akasema Lucy 

 “ haya niambiekuhusu jambo la pili 

ulilotaka kuniambia”akasema Robin.Lucy 

akamshika Robin mikono yake na kusema 

 “ Robin tafadhali naomba kabla 

sijakueleza kuhusu suala hili 

unihakkishie kwamba hautakasirika wala 

kunichukia.” 

 “ Siwezi kufanya hivyo Lucy.kwa nini 

nikasirike? Nieleze ni suala gani hilo? 

akauliza Robin 

 “ I’m pregnant “ 

 Robin akamtazama Lucy kwa 

mshangao na kumfanya aogope 

 “ Lucy tell me it’s a joke”akasema 

Robin  “Its real..I’m pregnant.”’akasema 

Lucy huku akimuangalia Robin kwa wasi 

wasi 

 Robin akaipeleka mikono yake 

katika tumbo la Lucy akalishika halafu 

akamkumbatia Lucy kwa furaha kubwa. 

*********************** 

Saa kumi za jioni siku ya jumatano Vicky 

madhahabu akiwa katika gari lake 

akirejea nyumbani simu yake 

ikata.Mpigaji alikuwa ni Chino.Vicky 

akaishika simu huku mikono ikaloa jasho 

kwani alikuwa akiisubiria simu ile kwa 

hamu kubwa.Akaegesha gari pembeni ya 

bara bara na kubonyeza kitufe cha 

kupokelea 

 “ Hallow Chino habari ya siku mbili 

tatu? akasema Vcky baada ya kupokea 

simu 

 “ habari nzuri sana 

Vicky.Nimekupigia kukutaarifu kwamba 

tuonane kesho saa nne za asubuhi ofisini 

kwangu”akasema Chino 

 “ Sawa Chino nitafika lakini vipi ule 

mpango wetu utafanikiwa? Akauliza Vicky  “ Vicky mambo kama yale hatuwezi 

kuongea katika simu.Fika kesho ofisni ni 

kwangu tutaongea na tutaona kama 

utawezekana ama vipi.” Akajibu Chino 

 “ Sawa Chino nitafika bila kukosa’ 

akasema Vicky na Chino akakata simu 

 “ Dah ! mambo yameiva.Najua Chino 

amekubali kuifanya ile kazi lakini hawezi 

kunionyesha moja kwa moja kwamba 

yuko tayari.Yule mzee siku zake 

znahesabika.Natamani hata leo hii Chino 

angeimaliza kazi na mimi nibaki 

huru.Sipati picha siku nikiwa huru 

kuyaongoza maisha yangu namna 

ninavyotaka ,nitakuwa na kila kitu 

ninachokihitaji katika hii dunia na zaidi 

sana nitakuwa na David.Ngoja nivumilie tu 

siku hizi chachezilizobaki.Nina hakika 

ndani ya wiki moja au mbilli zijazo jina 

langu litabadilika toka Vicky madhahabu 

hadi the boss Vick.”akawaza Vicky na 

kuliingiza gari barabarani akaendelea na 

safari ya kuelekea nyumbani 

 “ Toka siku ya jumatatu David 

amekuwa adimu sana 

kupatikana,anaondoka asubuhi sana na 

kurejea usiku na hata ofisini kwake 

hakai.Jana ndipo nimefanikiwa kuonana 

naye mchana .Ninahisi yawezekana akawa ananikwepa nisionane naye .Yule 

kijana amenifanya chizi.Yaani nikiiona tu 

sura yake nachanganyikiwa na ndiyo 

maana najikuta nikishindwa kujizuia na 

ninajikuta nikimkumbatia na kumwagia 

mabusu.Jamani kumbe kupenda sana ni 

ugonjwa.Sikutegemea kama siku moja 

nitakuja kuchanganyikiwa na mapenzi 

kama nilivyochanganyikiwa kwa David.” 

Akawaza Vicky na kuanza kukumbuka 

toka siku ya kwanza alipomuona David 

kisha akatabasamu 

 “ David alikuwa amechakaa sana 

,hakuwa anatazamika kabisa .Siamini eti 

David Yule ambaye niliona kinyaa hata 

kuisikia sauti yake leo hii niko tayari hata 

kuua kwa ajili yake.Ama kweli uzuri wa 

kitabu ni ndani na si jalada la nje.Sasa 

nimejua kwa nini Pauline 

alichanganyikiwa kabisa aliposalitiwa na 

David hadi akaamua kuondoka kabisa 

Arusha.NInaomba asirudi kabisa Yule 

mjnga hadi nitakapokamilisha mambo 

yangu.Nataka atakapopata taarifa za 

msiba wa baba yake na akirejea akute 

tayari nimemiliki kitu .Leo hii hii 

ninaanza mikakati ya kuhakikisha 

kwamba ninarithishwa kila kitu” akawaza Vicky na kuendelea na safari yake 

kuelekea nyumbani 

 Aliwasili nyumbani saa moja na nusu 

za jioni,na moja kwa moja akamfuata mzee 

Zakaria sebuleni alikokuwa amekaa 

akitazama Luninga akamkumbatia na 

kumbusu. 

 “ I mssed you so much my 

darling”akasema Vicky 

 “I missed you too Vicky..siku yako 

imekwendaje? Mbona leo umewahi kurudi 

tofauti na siku nyingine? 

 “ Nimekukumbuka sana mume 

wangu na ndiyo maana nikaona niwahi 

kurudi kuja kukaa nawe.Muda mrefu 

kidogo hatujautumia tukiwa pamoja 

kutokana na kutingwa sana na kazi na 

ndiyo maana kuanzia sasa ninataka 

nisifanye kazi nyingi ili nipate muda 

mwingi wa kutosha kukaa nawe.You 

missed me ? 

 “ Ofcourse I missed you my angel.I do 

miss you every second”akasema Zakaria 

na Vicky akambusu. 

 “ Zakaria twende tukaoge”akasema 

Vicky 

 “ Mimi tayari nimeoga Vicky wewe 

nenda ukaoge utanikuta hapa”  ‘ C’mon darling..nina hamu sana ya 

kwenda kuoga na wewe.Twende basi 

mume wangu”akasema Vicky na kumshika 

mkono mzee zakaria wakaongozana hadi 

bafuni wakaingia katika jaccuzi .Wakiwa 

ndani ya maji Vicky akapeleka mkono 

wake sehemu nyeti za mzee zakaria na 

kuanza kuzichezea lakini hakukuwa na 

mstuko wowote. 

 “bastard !! yaani ninaishi kama 

ninaishi na msukule humu ndani.Zee 

zimahaliwezi kufanya chochote..Your days 

are numbered you pig.Siwezi kuteseka 

namna hii kila siku.Umri wangu si wa 

kuishi kwa mateso kama haya.” Akawaza 

Vicky 

“ My dear,nimeonana na daktari 

amenipima na na kuna dawa nimeagiziwa 

toka ulaya ambazo zinaweza kunirejesha 

nguvu zangu.Najua unateseka sana kuhusu 

hilo lakini nakuahidi kwamba muda 

wowote dawa hizo zikifika nikaanza 

kuzitumia basi hali itakuwa nzuri na 

utafurahi kama zamani”akasema zakaria. 

 “ Mume wangu usijali kuhusu 

hilo.Ndoa ina milima ya kupanda na 

kushuka.Haya tunayopitia ni majaribu tu 

katika ndoa na tutayashinda.Mungu yupo 

pamoja nasi na tutashinda.Nakupenda sana mume wangu na jambo kama hili 

mimi haliniumizi kabisa kwa sababu 

upedno wa kweli unatoka moyoni.Upendo 

huvumilia na mimi ninavumilia yote 

mume wangu kwa sababu nakupenda kwa 

dhati”akasema Vicky 

 “ ouh Vicky,unajua sana kunikosha 

moyo wangu na ndiyo maana 

ninamshukuru Mungu kila siku kwa 

kukupata mwanamke kama wewe. Ni 

wanawake wachache sana ambao 

wanaweza wakawa na moyo wa kuvumilia 

kama wewe.Ninakupenda sana mke 

wangu na ninakuomba sana uendeleena 

moyo huo huo usibidilike”akasema 

Zakaria 

 “Siku tuliyokula kiapo kanisani 

tuliapa kwamba kwamba tutapendana 

katika shida na raha na hiki ndicho 

kipindi chenyewe cha kuonyeshana ule 

upendo wa dhati.Ninatimiza kiapo change 

cha ndoa na ninakuahidi nitakupenda siku 

zote” 

“Ahsante sana Vicky..Ninashukuru 

sana mke wangu”akasema Zakaria. 

Walipomaliza kuoga wakarejea 

chumbani na Vicky akaelekea jikoni 

kumuandalia Zakaria chakula yeye 

mwenyewe.  “ Mjinga sana Yule mzee.hana hata 

aibu eti kuna dawa zinakuja toka 

uingereza.Anamfanya nani mtoto mdogo? 

Nguvu zimepotea zimeshapotea na hawezi 

chochote.hata wakati bado ana nguvu zake 

hakuna alichokuwa anakifanya zaidi ya 

kunipapasa tu.Vijana kama David ndio 

wanaojua kukuna kisawa sawa 

.Ninachotakiwa kukifanya hapa ni 

kuitumia vizuri nafasi hii ili kabla hajafa 

nikahikishe tayari nimeandikishwa mali 

zote” akawaza Vicky akiwa jikoni 

akiandaa chakula. 

 “ Tukiwa bafuni nilimshika nyeti 

zake na mawazo yakawa mbali sana 

nilihisi kama vile ninamchezea 

David.jamani sijawahi kuchanganyikiwa 

namna hii mimi Vicky” akawaza 

 Baada ya kumaliza kupata chakula 

cha usiku hawakuwa na cha ziada zaidi ya 

kwenda chumbani kwao 

 “Sijamuona david siku ya pili leo.Ana 

matatizo gani?akauliza mzee Zakaria. 

 “ Nilionana naye jana alikuja dukani 

kwangu.Amekuwa na kazi nyingi sana za 

kufuatilia wiki hii.Yule kijana ulifanya 

vizuri kumuajiri ni kijana makini sana 

katika kazi yake.”  “ Ni kweli kabisa Vicky.Ninashukru 

sana kwa kukutana na kijana muaminifu 

kama Yule.Toka nimemkabidhi kazi,vitabu 

vinaonyesha kwamba mapato yamepanda 

sana na ameokoa pesa nyingi ambazo 

zilikuwa zinaibiwa na wafanyakazi wasio 

waaminifu.Amenifurahisha sana na ndiyo 

maana ukaona nikamzawadia lile gari la 

kifahari ambalo nililiagiza kwa ajili yangu 

mwenyewe.” Akasema Zakaria 

 “Vipi kuhusu Pauline, Umewasiliana 

naye? Akauliza Vicky 

 “ Mpaka leo hii bado sijawasiliana 

naye.Nashangaa kwa nini hajanipigia 

kunijulisha kama yuko salama ama 

vpi.Lakini ngoja tumuache atulize kichwa 

chake,anatakiwa ayafurahie maisha yake 

kwa uhuru.kwa sasa sina wasiwasi hata 

kidogo kuhusu biasahara kwa sababu 

yupo david na anafanya vizuri ”akasema 

Zakaria 

 “ Zakaria kuna kitu ninataka 

tuongee.kwa sasa ambapo Pauline yuko 

mbali na hatujui kama atarejea ama 

vipi,yawezekana akaamua kuendelea na 

maisha yake huko aliko.Mimi ni mkeo na 

hizi mali zote ni zetu lakini pamoja na 

hayo unafahamu mimi na Pauline 

tusivyielewana na ananitazama kwa jicho la chuki akijua mimi ni mpitaji tu na 

sitakiwi kabisa kuhusika na kitu chochote 

kuhusina na mali zako.kwa nini basi 

katika wakati huu ambao hayupo na 

hatujui kama atarejea tena usinithibitishe 

kisheria kabisa kwamba niwe msimamizi 

mkuu wa mali zako zote? Akauliza Vicky 

 “Hilo niwazo zuri na la msingi 

sana.Yawezekana leo na kesho mimi 

nikaondoka duniani na ninavyomfahamu 

Pauline unaweza ukapata shida 

sana.Sitaki hata kama nikifa leo ubaki 

uteseke Vicky.Ninashukuru 

umenikumbusha jambo la msingi 

sana.Wiki hii nitaanza kulifuatilia suala 

hili na nitaweka miradi yetu yote chini ya 

usimamizi wako ili hata kama nikifariki 

leo basi kusitokee mgogoro kati yako na 

pauline..” 

 “ Ahsante sana zakaria.Kila siku 

huwa ninasema kwamba wanaume wote 

wangekuwa kama wewe dunia ingekuwa 

sehemu nzuri sana kwa 

kuishi..”akasemaVicky huku akimwagia 

zakaria mabusu 

 “Mipango yangu yote inakwenda 

vizuri.Nitahakikisha kabla ya kifo chake 

niwe tayari msimamizi mkuu wa miradi na mali zote” akawaza Vicky huku akikisugua 

sugua kifua cha Zakaria 

 “ Liangalie kwanza lilivyolala kama 

nguruwe” akawaza Vicky akimtazama 

Zakaria 

****************** 

 Ni saa tatu za usiku David bado yuko 

ofisni kwake akimalizia kazi. 

 “ Nimekuwa na kazi nyingi sana wiki 

hii.Toka wiki iliyopita sijaonana na 

Tamia.Naona kama akili yangu haifanyi 

kazi vizuri bila ya kwenda 

kumuona.Ameikamata akili yangu na 

ndiyo maana namuwaza kila 

sekunde.Ngoja nipite usiku huu 

nikamsabahi ndipo nielekee 

nyumbani.”akawaza David akazima 

kompyuta yake na kufunga ofisi .kabla 

hajaingia garini akapitia katika 

supermarket iliyoko chini ya jengo lile 

akanunua maua mazuri pamoja na kadi . 

 “ Tamia loves suprises . Simwambii 

kama ninakwenda .Nataka kumuonyesha 

namna ninavyomjali” akawaza David 

akaingia garini na kuondoka kuelekea 

kwa Tamia.  “ Nimemkumbuka sana Pauline.Sijui 

nitatatafuta neno gani la kumwambia ili 

aweze kunisamehe kwa namna 

nilivyomuumiza.Nilimuumiza sana Yule 

msichana na yote ilisababishwa na 

Vicky.Namuombea Mungu huko aliko siku 

moja apate mwanaume wa maisha yake na 

awe na furaha tele.Natamani nipate nafasi 

ya kuongea naye na kumuomba msamaha 

lakini naogopa hata kumpigia simu kwa 

mambo niliyomfanyia.Pauline ni sababu 

ya mimi kuwa hivi nilivyo leo.Aliniokota 

mavumbini akanitakatisha nikapendeza 

lakini nikaja kumuumizasana.” Akawaza 

David. 

 “ anyway ukurasa wangu na Pauline 

nimekwisha ufunga na kilichobaki sasa 

hivi ni mimi kuangalia maisha yangu 

nikiwa na Tamia.Nina mpango wa 

kumtambulisha kwa mzee Zakaria 

amfahamu.Sina tena haja ya 

kujificha.Nataka urafiki wetu uwe wazi 

kabisa na kama hakuna kipingamizi 

kingine basi tufunge ndoa na kuishi 

pamoja.Ninataka nitulie na mwanamke 

mmoja ninayempenda ambaye ni 

Tamia.Nitazungumza naye jambo hili 

nisikie naye ana maoni gani” akawaza David akikata kona kuingia katika mtaa 

anakoishi Tamia. 

 Alifika nyumbani kwa 

Tamia.Akashuka garini na kutazama kama 

geti limefungwa.Mlango mdogo wa geti 

ulikuwa wazi akausukuma na kuingia 

ndani.Alikwisha izoea nyumba hii kwa 

hiyo hakuwa na wasi wasi hata 

kidogo.Ndani kulikuwa na gari mbili moja 

ya Tamia na nyingine hakuifahamu ni ya 

nani.Taa zilikuwa zinawaka kuashiria 

kwamba Tamia yupo.Akafika katika 

mlango wa kuingilia sebuleni ambao taa 

zilikuwa zinawaka na kwa mbali sauti ya 

muziki ikasikika.Bila wasiwasi 

akakinyonga kitasa na mlango 

ukafunguka.Sebuleni hakukuwa na mtu . 

 “ Hello my angel I’m home ! akasema 

David aktegemea kusikia sauti ya Tamia. 

 “ yawezekana ametoka kidogo na 

ndiyo maana hata geti hakufunga” 

akawaza David na mara akapata wazo la 

kwenda kutazama chumbani.Akiwaana 

maua yake mkononi akaelekea moja kwa 

moja hadi chumbani akastuka kidogo 

alipofika katika mlango wa Tamia na 

kusikia kiilio kikitokea ndani ya chumba 

kile.Akatega sikio kusikia vizuri ni 

kilikuwa ni kilio cha kimahaba.  “ Tamia anatazama filamu ya ngono 

leo !! yawezekana amezidiwa sana kwani 

hatujakutana toka wiki iliyopita”akawaza 

David huku akitabasamu na kukinyonga 

kitasa cha mlango.Ghafla maua aliyokuwa 

ameyashika yakaanguka chini .Alihisi 

miguu kumuisha nguvu akajiegemeza 

ukutani.Alichokiona mle chumbani 

hakuwa ametegemea kama siku moja 

angekishuhudia.Tamia alikuwa kitandani 

akiwa na mwanaume wa kihindi akiwa 

amekunjwa kama samaki wakiwa nje 

kabisa ya ulimwengu huu na wala 

hawakujua kama kuna mtu ameingia 

ndani.David akapatwa na akili ya haraka 

haraka akachukua simu yake na kuanza 

kuwapiga picha na ndipo Yule jamaa 

alipostuka baada ya kuona mwanga wa 

kamera ya simu.Akakurupuka kitandani 

na kumvamia David akaanza 

kumporomoshea makonde .David kwa 

hasira alizokuwa nazo naye akaanza 

kumporomoshea makonde mazito mazito 

yule jamaa kiasi cha kumfanya uso wote 

utapakae damu.Tamia alikuwa analia 

akiwaomba wale jamaa waache 

kugombana.Yule jamaa wa kihindi 

alianguka chini akigala gala huku 

akiugulia kwa maumvu makali kwa kipigo alichopewa na David.Tamia aliishiwa 

nguvu akakaa chini akilia.David 

akamfuata pale chini akamuinamia na 

kumtazama kwa hasira 

 “ David I’m sorry !! akasema Tamia 

huku akilia .David hakumjibu kitu 

akatoka mle chumbani na kuingia ndani 

ya gari lake 

Jasho lilimtiririka mwilini akawasha 

kiyoyozi ili kujipooza na joto alilokuwa 

analihisi.Kwa dakika kadhaa hakujua 

afanye nini.Picha ya Tamia akiwa 

kitandani na Yule jamaa wa kihindi 

ikamuumiza sana akajikuta akiupiga 

usukani kwa hasira 

 “ Ouh Tamia kwa nini lakini 

umenifanyia hivi? Akajiuliza 

 “ Sikuwahi kumpenda mwanamke 

yeyote kama nilivyompenda Tamia.Kwa 

namna nilivyompenda tayari nilikwisha 

anza kufikiria hata kufunga naye ndoa. 

Ouh jamani kwa nini Tamia akanifanyia 

hivi? Kitu gani amekikosa kwangu? Kama 

ni mapenzi nilimuonyesha ya kiwangio 

cha juu sana na akakiri mwenyewe 

kwamba mimi ni mwanaume ambaye 

alikuwa ananitafuta kwa muda mrefu sasa 

kwa nini aamue kutembea na wanaume 

wengine kama mimi ndiye niliyekuwa nikimfikisha? Akajiuliza David.Hakutaka 

kukaa sana pale akawasha gari na 

kuondoka 

 “ I wish nilichokiona mle ndani 

ingekuwa ni ndoto .Tamia amenivunja 

kabisa moyo wangu!..David akasikitika 

sana 

 “ Ukiacha siku niliyohukumiwa 

kwenda gerezani kwa kosa ambalo 

sikulifanya,jambo la pili lililoniumza ni 

hili la leo.Nilimpenda na kumuamini sana 

Tamia kumbe mwenzanu ni chui aliyevaa 

ngozi ya kondoo.” Akaendelea kuwaza 

David wakati akirejea numbani 

 “ Hakujua kama nitakwenda kwake 

leo hii na ndiyo maana akaamua kumleta 

Yule jamaa mle ndani.Jamani Tamia 

amekosa kitu gani hadi akawa na tabia 

kama hii? Kwa sura ni msichana mzuri 

ambaye huwezi kudhani anaweza kuwa na 

mambo machafu kamahaya.Lakini sipaswi 

kumlaumu mtu yeyote kwa hili ,natakiwa 

kujilaumu mimi mwenyewe kwa kuwa 

mjinga na kujikuta nikikubali kurubuniwa 

kirahisi namna hii na Tamia.Aliniteka akili 

sikusikia wala sikuona . I was so stupid !!. 

 “ Nadhani hii ni adhabu nimepewa 

kutokana na namna nilivyomtenda 

Pauline.Alinipenda sana akanijali na kunithamini lakini nikajikuta nikimuweka 

pembeni na kukubali kirahisi kuingia 

katika mtego wa Tamia.Pauline alinionya 

kuhusu Tamia lakini nikampuuza.Sasa 

yale yote aliyoyasema nimeyashuhudia 

kwa macho yangu.Najuta sana kwa 

kuipoteza bahati ya kuwa na Pauline 

msichana aliyenipenda kwa moyo wake 

wote,akanijali na kunithamini 

.Nilimuumiza sana kwa sababu ya huyu 

kahaba.” David aliwaza mambo mengi 

sana hadi alipofika nyumbani na moja kwa 

moja akaelekea chumbani kwake 

akajifungia na kujitupa kitandani.Baada 

ya kutulia akaanza kuhisi maumivu katika 

zile sehemu Yule jamaa alimtandika 

makonde .Picha ya tukio zima ikamjia tena 

akainuka na kukaa. 

 “ Ninaamini huu ni mpango wa 

Mungu kunionyesha kwamba msichana 

ambaye nilidhani ananifaa kumbe hanifai 

kabisa.NInaaminini mpango wa Mungu 

kwa sababu sikuwa na wazo la kwenda 

kwa Tamia leo hii usiku lakini nilipata 

wazo lile ghafla tu.Ahsante Mungu kwa 

kuniepushia matatizo.Nashukuru kwa 

kumfahamu mwenzangu katika hatua za 

mwanzo kabisa za mapenzi yetu.” 

Akawaza halafu akatoka akaeleka jikoni akachukua chupa ya maji ya kunywa 

akarejea chumbani. 

 “ Nimeumizwa na jambo hili lakini 

siwezi kukaa na kulia kana kwamba 

maisha yangu yamefika mwisho.Bado 

maisha yanaendelea.Mimi ni kijana wa 

kiume na kuumia moyo ni sehemu yangu 

ya maisha kwa hivyo suala hili halipaswi 

kunirudisha nyuma kiasi cha kushindwa 

kufanya mambo yangu ya kawaida. 

Nimekwissha pitia mambo mengi magumu 

na ya kukatisha tamaa kuliko hili .I have to 

move on.Nina hakika bado kuna mambo 

mengi mazuri yanakuja huko 

mbeleni.Ninachotakiwa kukifanya kwa 

sasa ni kuwa muangalifu sana kwa 

wanawake.Kama nisingeligundua hili 

mapema ningeendelea kuwa katika 

orodha ya wanaume wa Tamia huku 

nijidanganya kwamba niko peke yangu 

kumbe ametupanga kama 

abiria.Sikubaliani na ule msemo usemao 

kwamba samaki mmoja akioza basi wote 

huoza .Ninaamini kwamba dunia hii bado 

imejaa wanawake wengi wenye heshima 

na mapenzi ya kweli.Nitamuomba Mungu 

aniangazie na siku moja nitafanikiwa 

kumpata mwanamke ambaye ndiye 

ambaye Mungu amenipangia niwe naye.” Akanywa maji kidogo na kujilaza 

kitandani 

 “ Namsikitikia sana Tamia kwani 

wakati yeye akinilaghai kwa kunitamkia 

kwamba anipenda,mimi nilimpenda kwa 

moyo wangu wote.Anyway ngoja niufunge 

rasmi ukurasa wangu na Tamia na 

nielekeze akili yangu kata kazi.” Akawaza 

David na kujilaza kitandani na mara 

akakumbuka kitu 

 “ Baada ya kuufunga ukurasa wangu 

na Tamia sasa ninahamia kwa Vicky 

nataka niachane naye pia ili niweze kuwa 

huru.Huyu naye siku zake zinahesabikana 

uovu wake wote lazima ukome.Nataka 

nijiweke mbali kabisa na wanawake” 

akawaza 

********************* 

 Vicky madhahabu aliamka asubuhi 

na mapema ili kufanya shughuli za usafi 

wa nyumba,lakini kabla hajafanya 

chochote akaenda katika mlango wa 

chumba cha David akagonga lakini 

hakujibiwa,akamfuata mfanyakazi wa 

ndani akamuuliza kama amemuona David 

,mtumishi yule akamjibu kwamba David 

ameondoka asubuhi sana  “ Kitu gani kinachoendelea kuhusu 

David? Kwa nini kila siku anaondoka 

alfajiri na mapema na kurejea hapa usiku? 

Nina wasi wasi yawezekana akawa 

anakwepa kuonana na mimi.David 

amebadilika hakuwa hivi kabisa.Hata 

hivyo bado hataweza kunikwepa 

daima.Muda si mrefu sana atakuwa wangu 

na sintaumiza kichwa tena kuwaza yuko 

wapi kwani atakuwa nami muda wote” 

akawaza Vicky huku akiendelea na 

shughuli zake za usafi. 

 “ Leo ninakwenda kuonana na 

Chino.Nitapata muafaka kuhusu ule 

mpango wangu .Sitaki jambo hili lichukue 

muda mrefu sana.Kama kuna uwezekano 

hata kesho jambo hili lifanyike .”akawaza 

Vicky akiwa bafuni.Kisha jiandaa 

akaondoka zake kuelekea dukani kwake 

halafu akaelekea ofisini kwa Chino 

 “ Vicky unajali sana muda.Kwa 

namna ninavyowafahamu wanawake 

,nilitegemea ungefika hapa saa tano au saa 

sita badala ya saa nne” akasema 

Chino.Vicky akacheka kidogo na kusema 

 “ C’mon Chino.Nitachelewaje kwa 

jambo la muhimu kama hili? Akauliza 

Vicky huku akivuta kiti na kuketi.Chino 

akatoa sigara akaiwasha na kupiga mikupuo kadhaa akapuliza Moshi na 

kumgeukia Vicky 

 “ Vicky karibu sana.Ninashukuru 

umefika.Kabla hatujaendelea na kile 

nilichokuitia hapa kuna swali naomba 

nikuulize. 

 “ Uliza Chino” 

 “ Una hakika na unachodhamiria 

kukifanya? 

Bila kupepesa macho Vicky akajibu 

 “ Ndiyo nina uhakika Chino na wala 

sina wasi wasi hata kidogo” akasema 

Vicky.Chino akamtazama kwa makini 

machoni na kusema 

 “ Ni kweli 

umedhamiria.Nimeyatazama macho yako 

nimelingundua hilo.Lakini naomba 

nikuulize tena kwamba kwa nini unataka 

kufanya hivi? 

 “ Chino nilikwisha kwambia toka 

siku ile kwamba ninataka maisha ya 

kujiongoza mwenyewe bila kuongozwa na 

mtu yeyote.Ninataka nirithi mali zote za 

yule mzee ili niwe huru na mambo yangu” 

akasema Vicky 

 “ Ni hilo tu? Akauliza Chino 

 “ Ndiyo ni hilo Chino “ akajibu 

Vicky.Chino akapiga mikupuo kadhaa ya 

sigara na kusema  “ Nilihitaji kupata uhakika kwa mara 

ningine tena kutoka kwako kama kweli 

una nia ya dhati ya kulifanya jambo 

hili.Nimekuita hapa leo kukutaarifu 

kwamba mimi na timu yangu baada ya 

kulijadili suala hili tumekubali kuifanya 

hii kazi .” 

 “ Wow ! thank you Chino” akasema 

Vicky kwa furaha 

 “ Lakini kabla ya kuifanya hiyo kazi 

nadhani unakumbuka kiasi cha malipo 

tuliyokubaliana mwanzo? 

 “ Nikakumbuka kila kitu Chino na 

wala suala hilo lisiwape 

wasiwasi”akasema Vicky 

 “ Sawa kama unakumbuka basi 

vizuri.Kwa hiyo tunahitaji mzigo utufikie 

kabla ya kuikamilisha kazi hiyo.” 

 “ Chino naomba tuelewane.Mimi 

ninataka kazi yangu ifanyike na ninyi 

mnataka pesa.Siwezi kuwapatia mzigo 

wote kabla ya kazi kufanyika? Si kwamba 

sikuamini.Nnakuamini sana lakini 

nitaamini vipi kama kazi yangu itafanyika 

ninavyotaka? I cant take that risk.” 

 “ So wat are we going to do? Akauliza 

Chino 

 “ Nitakachofanya nitawapatia nusu 

ya mzigo na baada ya kazi kukamilika vizuri basi nitawamalizia kiasi cha pesa 

kilichobaki.” Akasema Vicky.Chino 

akafikiri kidogo na kusema 

 “ Ok sawa.Tuletee hiyo nusu ya 

mzigo ili tuanze maandalizi ya kazi.Nusu 

itakayobaki naomba tupatiwe siku 

itakayofuata baada ya kazi 

kufanyika.Narudia tena tukiikamilisha 

kazi yako hatutaki kusubiri zaidi ya saa 

ishirini na nne kupatiwa mzigo 

uliobaki.Endapo ukitufanyia usanii basi 

usitulaumu kwa kitu 

tutakachokufanyia.Utakosa kila kitu” 

 “ Usijali Chino.Hakuna usanii 

wowote.Ninachotaka mimi kazi yangu 

ifanyike na tumalizane kila mmoja 

akaendelee na maisha yake.” 

 “ Good.Kitu kingine ni kwamba 

jambo hili ni siri kubwa na hatakiwi mtu 

mwingine yeyote kufahamu.Hata awe ni 

rafiki yako namna gani tafadhali 

usimweleze chochote kuhusu suala hili.Hii 

ni siri yako hadi unaingia kaburini.” 

Akasema Chino 

 “ Usijali kuhusu hilo 

Chino.Anayefahamu kuhusu jambo hili ni 

mimi na wewe tu” 

Chino akawasha sigara nyingine akapiga 

mikupuo kadhaa kisha akasema  “ Lini unataka kazi hii ifanyike? 

 “ Hata leo hi kama ikiwezekana” 

akajibu Vicky na kumfanya Chino acheke 

kidogo 

 “ kwa leo haitaezekana 

Vicky.Yanatakiwa maandalizi.Endapo 

utatuletea mzigo wetu mapema kabla ya 

jumapili basi kazi hii tutaifanya siku ya 

jumapili usiku.” 

 “ Good.Jumapili itakuwa siku nzuri 

sana kwani sote tutakuwa nyumbani.Kwa 

hiyo mmekwishapanga mtafanyaje? 

Akauliza Vicky.Chino akavuta tena sigara 

na kusema 

 “ Tutavamia nyumba yenu saa nne za 

usiku na tutamaliza kila kitu.Siku hiyo 

hakikisha kwamba mmelala mapema sana 

ili tusipate taabu wakati wa kuingia 

ndani.Tumekwisha fanya uchunguzi na 

tumegundua kwamba pale nyumbani 

kwenu hakuna mlinzi kwa hiyo hakuna 

kitakachotuzuia kuingia.Kazi yetu ni 

kumuua mume wako lakini hata wewe 

lazima upate majeraha kidogo ya kupigwa 

na ninakuweka wazi kwamba yale ni 

mapambano na endapo kutakuwa na mtu 

yeyote ambaye ataonekana kuwa 

kipingamizi cha sisi kuutekeleza mpango 

wetu sisi tutamuondoa pamoja na mzee.Tunapokuwa kazini hatuna huruma 

hata kidogo.Ndani ya nyumba yenu 

mnaishi watu wangapi? 

 “ Niko mimi ,Zakaria,mtumishi wa 

ndani na kijana mmoja anaitwa 

David.Hawa wote hawawezi kuwa 

kipingamizi cha mpango huu.” 

 “ Sawa Vicky nimekueleza mapema 

ili usitulaumu kwa kile kitakachotokea 

endapo kuna yeyote kati ya hao ambaye 

ataweka kizingiti..” akasema Chino 

akamuelekeza Vicky mambo kadhaa ya 

kufanya halafu wakaagana Vicky 

akaondoka zake. 

 “ Dah ! wanawake jamani.Anapata 

kila kitu toka kwa bwana wake lakini bado 

haridhiki anataka kumuua mumewe ili 

aweze kurithi mali zote .Sikupenda 

kuifaya kazi hii lakini kwa kuwa ina pesa 

nono ngoja tu niifanye.I’ll kill that man” 

akawaza Chino baada ya Vicky kuondoka 

 Uso wa Vicky haukukaukiwa na 

tabasamu .Alikuwa na furaha ya ajabu 

sana 

 “ Siwezi kueleza furaha niliyo nayo 

leo.Ingawa mtu anaweza akanishangaa 

sana kwamba ninafurahia kuitoa roho ya 

mtu tena mume wangu lakini hawawezi 

kujua ni mateso kiasi gani niliyonayo ndani ya jumba lile na ndiyo maana 

ninaiona siku ya jumapili haifiki haraka 

niondokane na mateso haya 

niliyonayo.Najua nitahuzunika kwa siku za 

awali lakini ndani ya muda mfupi sana 

nitamsahau Zakaria na ili kujisahaulisha 

kabisa kuhusu Yule mzee nitamchukua 

David na tutaenda kupumzika nchi za 

mbali tukirudi huku tayari tutakuwa 

mume na mke.” Akawaza Vicky 

 Moja kwa moja akaelekea kwa shoga 

yake Safia.Akamchukua wakaenda katika 

hoteli wanayopenda kwenda mara kwa 

mara iliyoko Ngaramtoni. 

 “ Vicky kuna jambo gani kubwa kiasi 

cha kunileta huku tuongee? Akauliza Safia 

akitaka kufahamu jambo alilonalo Vicky 

kwani hakuwa amemweleza chochote 

kinachoendelea 

 “ Safia nimetoka kuonana na Chino .” 

 “ Amesemaje? 

 “ Kila kitu kinakwenda vizuri sana na 

tumemalizana tayari” 

 “ Wow ! kwa hiyo kazi inafanyika 

lini? 

 “ Jumapili kila kitu 

kitamalizika.Kuanzia saa nne za usiku kila 

kitu kitamalizika” akasema Vicky  “ Dah ! Hongera sana Vicky kwa 

kuifikia hatua hii.Lakini 

umemtahadharisha awe makini katika 

suala hili kwani ni suala la hatari sana” 

 “ Nimemtahadharisha sana na 

ameniahidi kwamba atakuwa makini 

sana” 

 “ Dah ! Nimekosa neno la kusema 

kuhusu jambo hili.Ninachokuombea ni 

mambo yaweze kwenda vizuri sana na 

uweze kufanikiwa kwani jambo hili ni 

kubwa na kama likienda vizuri basi hata 

sisi tutafaidika pia.” 

 “ Usihofu kuhusu hilo Safia.Baada ya 

wiki moja au mbili hatutakuwa hivi 

tulivyo.Utaingia katika ulimwengu wa 

mamilionea.Nitakupa mtaji mkubwa sana 

na utakuwa tajiri mkubwa.” 

 “ Nitashukuru sana Vicky.” Akajibu 

Safia kisha wakaendelea na maongezi 

mengine namna maisha yao 

yatakavyokuwa baada ya mpango ule 

kukamilika 

 Wakiwa katikati ya maongezi mara 

simu ya Vicky ikaita akatazama mpigaji 

alikuwa ni Tamia 

 “ Hallow Tamia” 

 “ Aunt Vicky shikamoo”  “ Marahaba Tamia hujambo? Mbona 

sauti yako inaonekana kama unalia? Kuna 

tatizo? 

 “ Ndiyo Aunt Vicky kuna tatizo.Uko 

wapi ninahiaji kukuona” 

 “ Niko mbali kidogo kwani kuna nini 

Tamia ,nieleze hata kwa simu kama kuna 

tatizo” akasema Vicky 

 “ Aunt Vicky ni tatizo kubwa siwezi 

kukueleza katika simu” 

 “ Tamia niko mbali na vile vile 

nimetingwa sana na kazi kwa hiyo 

ninaomba unieleze simuni una tatizo gani? 

Nieleze tafadhali usiogope” akasema Vicky 

 “ Aunt Vicky nimegombana na 

David” akasema Tamia 

 “ Umegombana na David.!!! …Nini 

imesababisha mkagombana? Akauliza 

Vicky 

 “ Alini…ali..alini….” Tamia 

akababaika 

 “ ali nini Mbona hunielezi? Nieleze 

nini kimetokea? Akauliza Vicky 

 “ Aunt Vicky ni jambo la aibu hata 

kusema” 

 “ Niambie Tamia hata kama ni jambo 

la aibu.Mimi David ananisikiliza kuliko 

mtu yeyote Yule na ninaweza kuwasaidia 

mkayamaliza mambo yenu”  “ Aunt Vicky David alinikuta 

na..na.na…” 

 “ Alikukuta na nini Tamia? Akauliza 

Vicky 

 “ Alinikuta na mwanaume jana 

usiku!.. 

 “ What ?!..Alikukuta na 

mwanaume????? Akaulzia Vicky kwa ukali 

 “Ndiyo Aunt.Kuna bwana wangu wa 

zamani alinifuata jana nyumbani kwangu 

na akagoma kuondoka akataka nifanye 

naye mapenzi na ili kumfanya aondoke 

ikanibidi nimkubalie na ndipo David 

alipotokea na kutukuta.Ninajaribu 

kumtafuta ili kuongea naye na kumueleza 

hali halisi lakini ninashindwa ,na simu 

yangu hataki kupokea nimejaribu hata 

kutumia namba ngeni lakini akiisikia sauti 

yangu tu anakata simu.Naomba unisadie 

Aunt Vicky niombee kwa David nionane 

naye niongee naye.Yeye ni mwanaume wa 

pekee ninayempenda kulik…………….” 

 “ Stop that kahaba wewe 

!!..Ungekuwa unampenda usingetubutu 

kufanya uchafu wako bila aibu.Sasa 

ninakuambia hivi iwe ni mwanzo na 

mwisho hata kumtaja tena David.Its 

over..Sintakubali kumuona David akiwa 

na kiruka njia kama wewe uliyemaliza mabwana wote wa mji huu.Na siku 

nikikukuta na David utanitambua mimi ni 

nani …Kaa mbali kabisa na David” 

akasema kwa ukali Vicky madhahabu na 

kukata simu 

 “ Vicky kuna nini” akauliza Safia 

 “ Ni Yule msichana wa David anatwa 

Tamia.David amemfumania na mwanaume 

ndani sasa ananiomba nimuombee 

msamaha kwa David.Hii ndiyo fursa 

niliyokuwa ninaisubiri sana.Nilikuwa 

naumiza kichwa sana nitafanya nini 

kuwatenganisha David na Tamia? Lakini 

ninashukuru mambo yananyooka 

yenyewe.Nyota yangu inawaka sana wiki 

hii na ndiyo maana kila ninachokifanya 

kinakwenda vizuri.Kwa sasa David 

amebaki wangu peke yangu” akasema 

Vicky na kuuagiza muhudumu alete 

shampeni ili wanywe kwa furaha 

aliyokuwa nayo. 




ENDELEA Saa tano za asubuhi akiwa ofisini kwake 

David akapigiwa simu na mzee Zakaria 

ambaye alimuomba arejee nyumbani mara amoja kuna jambo la muhimu 

anataka waongee. 

“ Mzee ana tatizo gani? Akajiuliza 

David baada yam zee Zakaria kukata simu. 

“ Hata siku moja mzee Zakaria 

hajawahi kuniita kwa dharura namna 

hii.Kuna nini numbani? .Ninahisi lazima 

kuna tatizo.Yawezekana amezidiwa na 

ugonjwa? Akaendelea kujiuliza David 

akiwa ameegemea kiti chake. 

 “ Lakini sauti yake haionyeshi kama 

amezidiwa na ugonjwa.Au amepata taarifa 

kuhusu mimi na Vicky? Nina wasi wasi 

sana yawezekana tayari amepewa umbea 

kwamba nina mahusiano na mke 

wake.Ouh Mungu wangu nitafanya nini 

mimi kama ni kweli atakuwa amefahamu 

kinachoendelea? Nilifanya kosa kubwa 

sana kumkubalia Vicky matakwa yake na 

kujiingiza katika upuuzi ule.” Akawaza 

David akachukua kitambaa na kujifuta 

jasho akainuka kitini na kuvaa koti lake 

lakini miguu ikawa mzito kutembea 

akakaa juu ya meza. 

 “ Mbona nafsi yangu inasita kabisa 

kwenda kuonana na mzee Zakaria? 

Nitamweleza nini kama ni kweli 

amegundua kuhusu mimi na Vicky 

tunamzunguka? Lakini haya yote yamesababishwa na ujinga wangu.Mzee 

Yule ameniamini na ananithamini kama 

mwanae lakini shukrani yangu kwake ni 

kutembea na mke wake? I’m so 

stupid.Sikupaswa kabisa kufanya 

vile.Anyway ngoja niende nikamsikie 

anachotaka kunieleza.Kama ni kweli 

atakuwa amegundua kuhusu mimi na 

Vicky sintakuwa na namna nyingine ya 

kufanya zaidi ya kuondoka pale kwake 

kwani sintaweza tena kumtazama usoni 

Yule mzee .Nadhani mwisho wangu wa 

kuishi Arusha umekaribia sana.Nimeishi 

kwa kipindi kifupi lakini tayari 

nimekumbana na mambo mengi 

makubwa.Nimemuumiza 

Pauline,nikaumizwa na Tamia na 

nikajiingiza katika mahusiano na Vicky 

madhahabu.Nimeanza kulichoka hili 

jiji.Ninahisi kama vile maisha yangu 

hayajapangwa yawe hapa .Sifahamu 

nitakwenda wapi lakini siwezi tena 

kuendelea kukaa hapa .Nafsi yangu 

inanisuta sana kwa ujinga nilioufanya” 

akaendelea kuwaza David akishuka ngazi 

kuelekea katika gari lake la kifahari 

alilozawadiwa na mzee Zakaria 

 “ Mzee Yule amenizawadia gari hili la 

kifahari kutokana na namna anavyonipenda na kuniamini lakini 

sijaliona hilo na nimediriki kumsaliti kwa 

kutembea na mke wake.Dhambi hii 

itanitesa kwa miaka mingi sana.” 

Akafungua mlango wa gari akaingia ndani 

na kuelekea nyumbani.Akiwa garini Vicky 

akapiga simu akaipokea 

 “ Hallow Vicky ! akasema David 

 “ Hello darling ! akasema Vicky 

 “ Vicky please stop..Sitaki utamke 

jina hilo .Nikwambie mara ngapi kwamba 

sitaki uniite jina hilo? Just call me David.” 

Akasema David kwa sauti iliyoonyesha 

ukali kidogo 

 “ Basi samahani David.Unajua 

ninashindwa kujuzia kabisa kwa namna 

ulivyonichanganya.” Akasema Vicky 

 “ Unasemaje? Akauliza David 

 “ David una matatizo gani? Mbona 

unanijibu hivyo leo? Au ni kwa sababu ya 

ugomvi wako na Tamia? Akauliza Vicky 

 “ Vicky niko barabarani ninaendesha 

nitakupigia baadae kidogo nikipata 

nafasi” akasema David na kukata simu 

 “ Mwanamke shetani huyu 

amenisababisha nikafanya mambo 

ambayo sikuwahi kufikiria 

kuyafanya.Hana aibu hata chembe.Najua 

mwisho wangu naye umekaribia sana.Kama Mzee Zakaria ananiita kwa ajili 

ya suala hilo basi huu utakuwa ni mwisho 

wangu na Vicky.” Akawaza David akiwa na 

hasira na mara akamkumbuka Tamia 

 “ Sitaki hata kukumbuka kuhusu 

tukio lile la jana usiku.Nitukio baya 

kuwahi kunikuta katika maisha yangu ya 

kimapenzi …Ninachoshukuru ni kwamba 

mambo kama haya ya kuvunjika moyo 

nimekwisha yazoea kwa hiyo hata suala 

hili halitachukua muda litafutika kichwani 

kwangu na nitamsahau Yule paka shume 

asiyetosheka na alichonacho.Ninadhani 

labda kwa upande huu wa mapenzi 

nisimame kwanza kwa sababu sina bahati 

kabisa.” akawaza David 

 Alifika nyumbani na kabla hajaenda 

kuonana na mzee Zakaria akaenda 

kwanza chumbani kwake akakaa 

kitandani . 

 “ Mwili wote unanitetemeka .Ni kweli 

nina hatia ndiyo maana ninatetemeka 

namna hii.Lakini hakuna namna ya 

kulikwepa jambo hili.Nimefanya 

mwenyewe upuuzi huu lazima 

nikakabiliane nao.” Akawaza na 

kulifungua kabati lake la nguo.Chini 

kabisa ya kabati lile kulikuwa na mfuko 

wa nailoni akauchukua mfuko ule na kutoa suruali moja ya jeans kuukuu 

pamoja fulana kuukuu akavitazama 

 “ Hivi ndivyo ambavyo ninaweza 

kusema ni vya kwangu.Nilipotoka 

gerezani sikuwa na kitu chochote zaidi ya 

nguo hizi.Nitakapoondoka nitaondoka na 

nguo zangu hizi nilizokuja nazo.Kwa 

kitendo cha aibu nilichokifanya sistahili 

hata kuvaa mavazi yanayotokana na pesa 

ya mzee Zakaria.” Akayarudisha mavazi 

yale katika ule mfuko wa nailoni akafunga 

kabati na kuelekea ghorofani kuonana na 

mzee Zakaria 

 “ Karibu sana David” akasema mzee 

Zakaria akimkaribisha David katika 

sebule yake kubwa 

 “ Ahsante sana mzee “ akajibu David 

huku akiwa na wasi wasi mwingi 

 “ David samahani nimekutoa katika 

kazi muda huu kuna masuala kama mawili 

hivi makubwa nimekuitia hapa.” Akasema 

Zakaria akanyamaza kidogo halafu 

akaendelea 

 “ Kwanza kwa siku zaidi ya tatu 

hatujaonana,kuna tatizo gani? Kila 

nikikuulizia naambiwa umekwisha 

ondoka au kama ni usiku ninaambiwa 

bado hujarejea.Kuna tatizo gani kijana 

wangu hatuonani? Akauliza Zakaria.  “ Mzee hakuna tatizo lolote lakini 

kwa siku kadhaa sasa nimekuwa nikiwahi 

sana kuondoka na kuchelewa kurudi 

kutokana na kuwa na kazi 

nyingi.Nimekuwa nikiwahi asubuhi katika 

kiwanda cha mikate kwenda kufanya 

uhakiki mimi mwenyewe kuhusiana na 

idadi ya mikate iliyozalishwa na nikitoka 

hapo huelekea kiwanda cha maziwa 

kuhakiki kiasi cha maziwa 

kilichopokelewa.Niligundua kuwapo kwa 

udanganyifu katika takwimu ndiyo maana 

nimeamua kufuatilia mimi mwenyewe 

kuhakiki kila kitu” akasema David na uso 

wa mzee Zakaria ukapambwa na 

tabasamu pana sana 

 “ Ndiyo maana ninakupenda 

David.Sijawahi kupata kijana mchapa kazi 

kama wewe.Nimefurahishwa sana na 

juhudi zako za kazi.Katika muda mfupi 

ulioanza kazi umeokoa kiasi kikubwa cha 

pesa,Ninakushukuru sana David .Endelea 

na moyo huo na siku moja nakuahidi 

kukufanyia mambo makubwa sana.” 

Akasema Zakaria 

 “ Ahsante nashukuru sana mzee” 

akajibu David 

 “ Jabo la pili ambalo nimekuitia hapa 

ni kwamba mimi kwa sasa hali yangu ni kama unavyoniona.Ninahitaji sana 

mapumziko .Pauline naye kwa sasa 

hayupo na hatuelewi kama atarejea lini 

Kwa hali hiyo basi kuna jambo 

nimelifikiria.NInataka kumuweka mke 

wangu Vicky kama msimamizi mkuu wa 

mali zangu zote .Ninataka kufanya hivi ili 

hata kama ikitokea mimi nikaaga dunia 

leo basi kusiwe na mgogoro kati ya 

Pauline na mama yake mdogo Vicky.Hata 

hivyo nimeona nisilifanye kwanza jambo 

hili hadi nikueleze na nisikie wewe una 

ushauri gani katika suala hili.Hebu 

niambie wewe unalionaje jambo hili? 

Akauliza mzee Zakaria.David akastuka 

sana lakini akajizuia kutokuonyesha 

mshangao wowote mbele ya mzee Zakaria 

 “ Huyu mzee anataka kufanya jambo 

gani tena? Yaani kumpa Vicky umiliki wa 

mali zote? Akajiuliza 

 “ David una mawazo gani juu ya 

jambo hili?” akauliza Zakaria 

 “Mzee huu ni mtihani mkubwa 

umenipa “ akasema David 

 “ David huu si mtihani bali ni 

majukumu yako .Wewe ndiye 

ninayekuamini sana katika kila kitu kwa 

hiyo siwezi kufanya jambo kubwa kama 

hili bila kusikia kwanza ushauri wako Wewe ni mshauri wangu mkubwa na 

chochote utakachonishauri nitakisikia na 

kukifanyia kazi kwa hiyo usiogope 

kunishauri jambo lolote” akasema 

Zakaria.David akakohoa kidogo halafu 

akasema 

 “ Mzee kwa kuwa umenipa nafasi 

hiyo nikushauri ,basi ushauri wangu ni 

kwamba usifanye jambo hilo kwa sasa 

hadi hapo Pauline atakaporejea .Hata 

hivyo bado ninadhani Pauline anatosha 

kabisa kuweza kuwa msimamizi mkuu wa 

miradi yako yote.Ni msicana mwenye akili 

sana katika biashara.Madam Vicky 

ameshindwa kuonyesha ufanisi katika ile 

biashara yake ya madini hadi imelazimu 

kuongezewa pesa nyingine nyingi ,kwa 

hiyo sina hakika sana kama anaweza 

akalibeba jukumu hili kubwa.Mzee una 

miradi mingi tu mikubwa na inayohitaji 

usimamizi makini sana na nikiwapima 

Pauline na madam Vicky,bado Pauline 

anafaa zaidi kulio madam.Utanisamehe 

lakini kwa kusema hivi “ 

 “ David ninashukuru sana kukupata 

kijana kama wewe.Kwa miaka mingi 

nimekuwa nikimuomba Mungu anijalie 

niweze kumpata mtoto wa kiume mwenye 

akili na upeo kama wewe lakini kwa bahati mbaya mwanangu wa kume 

alifariki .” 

 “ Pole sana mzee” akasema David 

 “ Ahsante sana.Ni kazi ya Mungu.Ila 

namshukru Mungu kwani amenijibu ombi 

langu .Baada ya mwanangu kufariki 

amekuleta wewe.Ninashukuru sana kwa 

usahuri wako mzuri na ninakuahidi 

kwamba nimeupokea na 

sintaupinga.Jambo hili hata mimi 

nimelifikiria sana na ndiyo maana 

nikaamua nikuite kwanza kabla ya 

kufanya lolote.Basi nitalisitisha suala hili 

hadi Pauline atakaporejea lakini naomba 

usimweleze kitu chochote mama yako 

kama tumelijadili suala hili,” 

 “ Mzee ninashukuru sana kwa 

kuniamini.Ninakuahidi kwamba 

sintakuangusha.Nitafanya kazi kwa bidii 

kubwa sana.” 

 “ Ahsante sana David.By the way 

kuna jambo ninataka kukuuliza ingawa 

sina hakika kama utakuwa tayari 

kunijibu.” 

 “ Niko tayari mzee” akasema David 

 “ Siifahamu historia yako na sitaki 

uniambie hadi hapo utakapokuwa tayari 

lakini kuna jambo moja ambalo nataka kulifahamu.Kabla ya kupatwa na maatizo 

yale ulikuwa na mke? Akauliza Zakaria. 

 “ Hapana mzee sikuwa nimeoa ila 

nilikuwa na rafiki wa kike lakini baada ya 

kufungwa gerezani urafiki wetu uliishia 

hapo.” 

 “ pole sana David.Vipi kwa sasa una 

mpango gani wa kutafuta rafiki wa kike? 

 “ Kwa sasa akili yangu yote 

ninaielekeza katika kazi .Baadae ninaweza 

kufikiria kuhusu suala hilo lakini 

ninamuomba Mungu, aniangazie niweze 

kumpata mwanamke ambaye atakuwa na 

mapenzi ya kweli,Siku hizi ulaghai mwingi 

sana.” Akasema David 

 “ Unayosema ni ya kweli kabisa 

David.Siku hizi kinachoangaliwa zaidi ni 

pesa na mali.Nadra sana kupata mapenzi 

ya kweli iku hizi.Ila mimi ninamshukuru 

sana Mungu kwa kunipatia mke bora 

ambaye ananijali na kunipenda sana hasa 

wakati huu wa matatizo.Nitafurahi sana 

kama na wewe ukifanikiwa kumpata 

mwanamke wa aina hii ambaye 

atakupenda si kwa sababu ya sura yako 

nzuri ama kwa sababu ya pesa zako bali 

akupende toka moyoni na ukimpata 

mwanamke wa namna hiyo David 

usimuache.Mlete kwangu na mara moja mimi nitagharamia harusi.Ninataka uishi 

maisha mazuri bila ya kuruka ruka na 

wanawake hawa wa Arusha kwani 

magonjwa mengi sana siku hizi” akasema 

mzee Zajkaria 

 “ Mzee nakushuru sana kwa ushuri 

wako.Nakuhakikishia endapo nikimpata 

utakuwa wa kwanza kumfahamu” 

akasema David 

 “ Ahsante kwa hilo.Jambo lingine 

ninaomba kama una tatizo lolote lile 

ambalo hauwezi kumwambia mtu yeyote 

Yule usisite kuniambia.Muda wowote 

nitakuwa tayari kukusikiliza na 

kukusaidia kwa lolote” akasema mzee 

Zakaria kisha akamumba David 

akaendelee na kazi zake 

 “ Thank you Lord…..!! akasema David 

akiwa amekaa kitandani chumbani kwake 

baada ya kumaliza maongezi na mzee 

Zakaria. 

 “ Ahsante Mungu .Niliogopa sana 

nilidhani tayari amekwisha lifahamu suala 

langu na Vicky.Tayari nilikwisha jiandaa 

kwa kuondoka hapa.Hata hivyo yoho 

inaniuma sana kwa mambo niliyomfanyia 

huyu mzee.Sikupaswa kabisa kumfanyia 

hivi mtu ambaye ananipenda ananithamii 

na kuniheshimu zaidi ya baba yangu mzazi.” Akawaza David na kushindwa 

kujizuia kudondosha machozi mengi.Alilia 

sana kisha akaingia bafuni akaoga na 

kubadili mavazi akajiandaa kwa ajili ya 

kurejea kazini.Kabla hajatoka mle 

chumbani simu yake ikaita.Zilikuwa ni 

namba ngeni 

 “ Hallow “ akasema David 

 “ hallow naongea na David ?”ikauliza 

sauti ya mwanamke upande wa pili 

 “ Ndiyo ni mimi.Naongea na nani? 

 “ Naitwa Safia,ni rafiki mkubwa sana 

wa Vicky madhahabu” 

 “ Ouh Safia ,nikusaidie nini? 

 “ David nahitaji sana kukuona.Kuna 

jambo la maana sana ninataka kuongea 

nawe” akasema Safia 

 “Safia ni jambo gani hilo? Hatuwezi 

kuongea simuni? 

 “ Hapana David hatuwezi kuongea 

simuni.Naomba tuonane jioni ya 

leo.Nitakupigia simu saa kumi na mbili za 

jioni kukuelekeza mahala pa 

kukutana.Tafadhali naomba kama 

utakuwa na shughuli muda huo 

uziahirishe kwanza na uje unisikilize japo 

kwa nusu saa” akasema safia .David 

akafikiri kidogo kisha akasema  “ Sawa Safia nitakuja kuonana 

nawe.Utanielekeza ni wapi tukutane” 

 “ Ahsante David.Jambo lingine 

naomba Vicky asifahamu kabisa kama 

unakuja kuonana na mimi” 

 “ Sawa Safia sintamweleza chochote” 

akajibu David na kukata simu 

 “ Huyu Safia anataka nini kwangu? 

Hata siku moja sijawahi kuonana naye 

nashangaa imekuaje leo anataka kuongea 

nami.Hawa ni rafiki zake Vicky 

yawezekana anataka kunifahamisha kitu 

kuhusu Vicky “ akawaza David huku 

akufunga mlango wa chumba chake 

akatoka na kuingia garini 

 “ Au yawezekana akawa amefahamu 

kuhusu kinachoendelea kati yangu na 

Vicky? Akaujiuliza akiwa ndani ya gari 

 “ Yawezekana kabisa anataka 

kuniambia kuhusu jambo hili.Yawezekana 

Vicky akawa amemwambia kuhusu mimi 

nay eye.Anyway nitakwenda kuonana 

naye kujua anachoniitia kwa msisitizo 

namna ile.Anaweza kuwa na jambo la 

muhimu la kuniambia” akawaza 

 “ Hakuna siku niliwahi kutetemeka 

na kuogopa kama leo.Nilishindwa hata 

kumtazama mzee Zakaria usoni kwa aibu 

.Sitaki tena kitendo kile kijirudie.Lazima nitafute namna ya kuyavunja mahusiano 

yagu na Vicky haraka sana kabla ya mzee 

Zakaria hajagundua kitu.Halafu kuhusu 

ule mpango aliokuwa anaufikiria Zakaria 

eti amfanye Vicky kuwa msimamizi mkuu 

wa miradi yote kautoa wapi? Hapana hili 

si wazo lake kabisa,lazima ni wazo 

lililotoka kwa Vicky.Amefanya vizuri 

kunishirikisha na ameukubali ushauri 

wangu. Vicky hana roho ya ubinadamu 

kabisa.Laiti ningekuwa na uwezo 

ningemuachanisha kabisa na mzee 

Zakaria.” Akawaza na kuuma meno kwa 

hasira 

******************* 

David alirejea ofisini kwake kuendelea 

na kazi.Dakika mbili toka ameingia mle 

ofisini mlango wake ukagongwa 

akamruhusu mgongaji ingie 

ndani.Hakuamini alichokiona mbele yake. 

 “ You ???? akauliza kwa 

mshangao.Akaweka kalamu chini na 

kusimama 

 “ What are you doing here Tamia? 

Akauliza David  “ David I’m sorry” akasema Tamia 

huku akilia.Alikuwa amesawajika 

sana.Macho yake mazuri yalikuwa 

mekundu na ilionyesha wazi alikuwa 

amelia sana.Nywele zake nzuri zilikuwa 

zimetimka na alionekana dhahiri kwamba 

alikuwa na matatizo 

makubwa.Hakuonekana kama ni yule 

Tamia mwenye muonekano na uzuri wa 

kipekee kabisa . 

“ Please Tamia don’t say 

anything..Sitaki kusikia chochote toka 

kwako .Ulichokifanya kimetosha kabisa “ 

akasema David 

“ David Please naomba unisikilize” 

“ hapana sitaki kusikia chochote 

toka kwako Tamia.Kitendo ulichokifanya 

jana hakivumiliki na siwezi kuusamehe 

kwa kitendo kile.I loved you Tamia with 

all my heart ,kitu gani ulikikosa toka 

kwangu? I gave you everything lakini 

haukutosheka hadi ukanisaliti kwa 

wanaume wengine.Pauline alinikanya 

kuhusu wewe nikampuuza kwa 

kudhaninakuonea wivu lakini nashukuru 

nimekushuhudia kwa macho yangu 

mwenyewe bila kuambiwa na mtu” “ David I’m sorry..” akasema Tamia , 

akaanguka miguuni kwa David na 

kulia.David akamshika akamuinua 

 “ Tamia mimi nimekwisha kusamehe 

lakini katu siwezi kurudiana nawe 

tena.Nilikupa nafasi moja ukaichezea na 

ninashukuru nimetambua mapema 

kwamba wewe si muaminifu na hunifai 

hata kidogo.” Akasema David huku 

akimtazama Tamia kwa macho makali 

sana. 

 “ David nimekosa naomba 

unisamehe mpenzi wangu.Sintarudia tena 

kosa lile.Ni shetani tu alinipitia nikajikuta 

nikifanya vile.Nisamehe David “ Tamia 

akaendelea kuomba msamaha 

 “ Tamia hakuna maneno ambayo 

unaweza ukayatumia kunibadili msimamo 

wangu.It’s over between us.Nenda 

kaendelee na maisha yako 

uliyoyazoea.Kitu kimoja ambacho 

kinaniumiza ni kwamba All the men are 

playing you,but me I loved you with all my 

heart.Hukulitambua hilo kwa hiyo 

samahani sana naomba utoke ofisini 

kwangu nina kazi nyingi za kufanya” 

akasema David.Tamia hakuonyesha dalili 

zozote za kutoka mle ofisini akaendelea 

kulia.David akapiga simu kwa walinzi ambao walifika haraka akawaomba 

wamtoe Tamia mle ofisini kwake. 

 “ Tamia alifanya kosa kubwa 

sana.Nilimpenda kwa dhati ya moyo 

wangu lakini kwa kitendo 

nilichokishuhudia jana kamwe sitaweza 

kurudiana naye hata kidogo” akawaza 

david na kuendelea na kazi zake 

****************** 

 Saa tisa za alasiri gari la Vivian 

likafunga breki nje ya nyumba moja nzuri 

iliyozungukwa na migomba 

mingi.Akashuka garini na kuelekea 

mlangoni akabisha hodi na mwanamke 

mmoja mnene akamkaribisha ndani kwa 

furaha kubwa. 

 “ Vivy karibu sana.” 

 “Ahsante sana Doreen.habari za 

toka wiki iliyopita? 

 “ habari nzuri sana.Vipi wewe 

unaendeleaje? 

 “ Mimi ninaendelea hivyo hivyo .” 

 “ Shemeji Tino hajambo? Akauliza 

Doreen 

 “ Mhh ! hajambo” akasema Vivian 

 “Mbona umeguna kuna nini ?  “ Doreeni nimekuja ndugu yangu 

kukuomba ushauri.Mambo kwangu si 

mazuri hata kidogo” 

 “Kuna tatzo gani tena 

Vivian?Mmegombana? 

 “ Ni bora hata tungegombana 

tungesuluhisha yakaisha lakini kuna 

tatizo kubwa” 

 “ kama hamjagombana kuna tatizo 

gani Vivy?akauliza Doreen.Vivian akainua 

glasiiliyojaa juice akanywa na kusema 

 “Baada ya kuishi kwa muda mrefu na 

Tino hatimaye tuliazimia kwamba tufane 

taratibu za kufunga ndoa.kwa kuwa mimi 

na Robin kishera bado ni wanandoa 

inabidi kwanza ndoa yetu intenguliwe na 

kanisa ndipo tuweze kuruhusiwa kufunga 

ndoa tena.kwa bahati nzuri hata Robin 

naye tayari ana mchumba wake ambaye 

anatakakufunga naye ndoa kwa hiyo 

tukaonna tukakubaliana na taratibu za 

kuitengua ndoa yetu zikaanza.Wakati 

taratibu zikiendelea ghafla limeibuka 

jambo moja la ajabu sana ambalo 

linanitesa kila siku.”akasema Vivian na 

kunyamaza kidogo halafu akaendelea 

 “ Tino amebadilika ghafla na 

amekuwa mlevi kupindukia.Hakuwahi 

kuwa mlevi kiasi hiki. Doreen nimechanganyikiwa na sielewi nifanye 

nini.Ndoa yangu imeingia 

mdudu.Nimejitahidi kwa kila namna 

kumuuliza kama kuna tatizo gani 

linamsumbua lakini hunijibu kwamba 

hana tatizo lolote ameamua kunywa 

pombe.Doreen ninateseka sana mwenzio 

na hali hii na sijui nifanye nni.Nimekuja 

kwako kutaka ushauri ndugu yangu 

nifanye kitu gani.Ninampenda sana Tino 

na nikifanya mchezo naweza nisimpate.’ 

Akasema Vivian. 

 “ dah ! hili suala kweli gumu.Vipi 

kuhusu marafiki zake umekwisha jaribu 

kuwasiliana nao na kuwalezea kuhusu 

jambo hili? 

 “ Nimejaribu kuwasiliana na 

marafiki zake lakini hata nao hawanipi 

majibu yenye kueleweka wote wanadai 

kwamba anawafahamu chochote kuhusu 

matatizo ya Tino” 

 Doreen akafikiri kwa muda na 

kusema 

 “ Vivian lazima kuna tatizo hapa si 

bure.Ninavyomfahamu Tino hawezi kuigia 

katika mambo ya ulevi bila kuwa na 

matatizo.Yawezekana labda akawa na 

matatizo katika biashara zake.”  “ Katika biashara hakuna tatizo 

lolote kwani kila kitu ninakifahamu kwa 

hiyo mpaka sasa hakuna tatizo lolote 

lililotokea.” 

 “kama hakuna tatizo lililotokea hata 

katika biashara zake nini basi inaweza 

kuwa chanzo cha yeye kujitumbukiza 

katika ulevi? Akauliza Doreen. 

 “ Hilo ndilo swali 

linalonikondesha.Nimejiuliza sana 

nimekosa majibu.Nimekuja hapa kuomba 

ushauri kwako nifanye nini kuhusu suala 

hili” akasema Vivian 

 “ kwa kweli Vivy inaniwia vigumu 

sana kufahamu kwa haraka Tino anaweza 

kuwa anasumbuliwa na tatizo gani,lakini 

wewe unamfahamu kwa undani zaidi na 

unaweza ukajua tatizo lake.” Akasema 

Doreen 

 “ Doreen mimi kwa mtazamowangu 

ninahisi hapa lazima kuna mkono wa 

mtu.Haiwezekani kabisa kwamba suala 

hili liibuke ghafla namna hii hasa wakati 

huu ambao tumeanza mipango yetu ya 

kufunga ndoa.Kuna watu ambao 

hawapendezwi na jambo hili na wanataka 

kufanya kila linalowezekana ili mimi na 

Tino tusifunge ndoa.”akasema Vivian  “ Hilo ninaweza kukubaliana nalo 

kwani sisi binadamu hatupendani na 

yawezekana kabisa kuna watu ambao 

hawafurahi kukuona ukiwa pale kwa Tino 

ukifurahia maisha.Ni wanawake 

wengiwanaitafuta bahati kama hiyo 

hawaipati .” 

“Umeonaeeenh!!!..Nina hakika 

kabisa kwamba lazima kuna mtu ambaye 

anataka mimi na Tino tuchukiane 

,tukorofishane na mipango yetu ya 

kufunga ndoa ishindikane kabisa lakini 

nitapambana na yeyote yule ambaye 

anataka kuniharibia maisha 

yangu.”akasema Vivian kwa hasira 

 “ Kwa hiyo umefanya maamuzi gani 

? Akauliza Doreen. 

 “ Kuna shoga yangu mmoja anataka 

kunipeleka pangani kwa mganga wake 

Fulani ambaye ana uwezo wa kumfunga 

kabisa mume .Huyu mganga anao uwezo 

wa kukuonyesha hata mwanamke ambaye 

anatembea na mumeo 

naukamshughulikia.Doren kwa namna 

ninavyompenda Tino niko tayari kwa 

lolote .” akasema Vivian.Doreen 

akanyamaza akafikir I na kusema  “ Wazo lako ni zuri lakini kabla 

hujaelekea huko Pangani nina ushauri 

mdogo:” akasema Doreen 

 “ Binafsi siwaamini sana waganga 

hawa wa kienyeji ,lakini kama una hakika 

wanaweza kukusadia si vibaya kujaribu 

,lakini kama una hakika kwamba mumeo 

ana mwanamkemwingine ambaye 

anamfanya awe hivi fanya kwanza 

uchunguzi ili uwe na uhakika kama ni 

kweli kunakitu hicho ndipoo uamue nini 

cha kufanya.”akasema Doreen 

 “ Doreen ninalokwambia nina 

uhakika nalo kabisa kwamba lazima kuna 

mwanamke ambaye anataka kuvunja 

nyumba yangu sasa nataka nimkomeshe 

kabisa ili akome kuvamia wanaume wa 

watu.” 

 “ Ninakubaliana nawe Vivy kwamba 

yawezekana kabisa kwamba Tino ana 

mwanamke lakini fanya kwanza 

uchunguzi ili kujua je ni kweli ? jambo hili 

ni kubwa na si la kuchukulia kwa 

pupa.Umakini mkubwa unahitajika 

”akasema Doreen. 

 “ Sasa nitamchunguza vipi Doreen? 

Akauliza Vivian 

 “ kwanza kabisa usimuonyeshe 

kwamba unahisi ana mwanamke mwingine.Wewe endelea kumuonyesha 

mapenzi kama kawaida.Kesho asubuhi 

akiondoka anza kumfuatilia .usitumie gari 

lako ili asije akakustukia.Tumia gari la 

kukodi na mfuatilie kutwa nzima nina 

hakika utaufahamu ukweli.Ahirisha kila 

kitu kaa sasa na ushugulikie suala hili ili 

uufahamu ukweli wote wa jambo 

hili”akasema Doreen 

 “ Ahsante sana Doreen kwa ushauri 

wako ndiyo maana sijataka ushuri 

kwamtu mwingine zaidi yako kwani siku 

zote wewe ndiye unayenipa ushauri mzuri 

sana”akasema Vivian 

 “ Vivian vipi k uhusu mwanao 

unamtembelea kujua maendelo yake? 

Akauliza Doreen 

 “ Ndiyo nilimtembela shuleni 

kwao.Ni msichana mkubwa sasa hivi . 

Kinachonisikitisha ni kwamba baba yake 

amemuharibu sana.Amemlisha sumu kali 

na ananichukia kupita maelezo.Hataki 

hata kuniona” akasema Vivy 

 “ yah itachukua muda kidogo ili 

kujenga tena mahusiano naye.Haiwezi 

kuwa rahisi na hasa kutoka na mazingira 

uliyoondoka lakini usikate tamaa utafika 

muda mtasawazisha mambo na 

hatakuchukia tena.”  “ Doreen nilifanya kosa kubwa sana 

kuondoka na kumuacha mwanangu 

kipindi kile ,lakini sikuwa na namna 

nyingine ya kufanya,hata hivyo bado 

sijakata tamaa.Nitaendelea kujaribu 

kutafuta ukaribu naye na hasa kwa wakati 

huu ambao maisha yangu ni 

mazuri.”akasema Vivian .Waliongea 

mambo mengi sana na ilipofika saa kumi 

na mbili za jioni Vivian akaondoka zake 

kurejea nyumbani. 

******************* 

 Muziki laini wa ala ulisikika ndani ya 

chumba cha Pauline.Tayari kiza kilianza 

kutanda angani .Alikuwa amelala katika 

sofa akitazama filamu na katika meza 

ndogo kulikuwa na chupa ya mvinyo laini. 

 “ Nashukur u kila kitu kinakwenda 

vizuri.Ukarabati unakwenda vizuri na 

unakaribia kumalizika.Taratibu zote 

zimefuatwa na 

zimekamilika.Ninamshukuru sana Alfred 

kwa msaada wake mkubwa kwani ndiye 

aliyenipawazo hili akanisaidia kufuatilia 

vibali vyote na mpaka sasa mambo 

yanakaribia kufika mwishoni 

badoaanisaidiana nitaendelea kuhtaji sana msaada wake kwani sina uelewa 

wowote wa masuala hya ya afya.” Akawaza 

na kunywa mvinyo kidogo. 

“ Baada ya awamuya kwanza 

kumalizika kinachofuata sasa hivi ni 

kuanza kushughulikia upatikanaji wa 

mashine nvifaa vyote vinavyohitajika.Ni 

fedha nyingi sana lakini nitahakikisha 

ninazipata zote.Wiki ijayo nitakwenda 

Arusha nitaanza kushughulikia kupata 

mkopo mkubwa benki. Natumai baba 

atanisaidia sana katika suala hili na 

atafurahi kuona namna akiliyangu 

ilivyopanuka katoka biashara...haya yote 

ni matokeo ya kuamua kuondoka Arusha 

na kuj….” Pauline akastuliwa toka 

mawazoni na kengele ya mlagoni 

akainuka na kwenda kuufungua mlango 

akakutanana sura yenye tabasamu ya 

Alfred. 

“ Alfred ! karibu sana.”akasema 

Pauline na kukumbatiana na Alfred 

wakapeana mabusu 

 “ hatujaonana toka jana.Tulikuwa na 

operesheni kubwa tatu za kufanya 

.Nimefika nyumbani jioni hi na kutoka 

nikaona nije kukutazama unaendeleaje.I 

missed you so much Pauline” akasema 

Alfred  “ I missed you too Alfred.Pole sana 

na kazi” 

 “ Ahsante sana Pauline. Vipi 

ukarabati unaendeleaje? 

 “Kila kitu kinakwenda 

vizuri.Niliwatembelea mafundi 

wanaendelea vizuri sana” akasema 

Pauline 

 “ Vizuri sana . kwa kuwa hatua ya 

ukarabati inakwenda vizuri kinachofuata 

sasa ni kuanza kushughulikia suala la 

vifaa.Itatulazimu kusafiri kwenda hadi 

kwa watengenezaji kuangalia mashine 

tunazozihitaji.usiogope nitakuwa nawe 

katia suala hili na nitakusaidia kutafuta 

mashine nzuri..” akasema Alfred. 

 “ Wow ! hizo ni habari nzuri sana 

.Hata mimi muda mfupi uliopita nilikuwa 

nafikiria kuhusu suala hilo la mashine na 

vifaa.Jumamosi ya wiki hii nitakwenda 

Arusha.Nina mpango wa kuanza kufuatilia 

mkopo mkubwa benki .Mashne 

zinazohitajikani ghali mnokwa hiyo pesa 

nyingi inatakiwa..” 

 Alfred akataka kusema kitu lakini 

simu iliyoko mezani ikaita na kumfanya 

Pauline ainuke na kwenda kuipokea 

.Akataarifiwa kwamba ana mgeni wake 

mapokezi.  “ Kuna mtu ananitafuta mapokezi 

ngoja nikamuangalie”Pauline 

akamwambia Alfred kisha akashuka 

kwenda kuonana na mgeni wake.Hakuwa 

na miadi q kukutana na mtu yeyote hivyo 

alijuliza maswali mengi ni nani aliyekuwa 

anamtafuta 

 Alipotokeza eneo la mapokezi 

akahisi miguu ikimuisha nguvu 

alipokutaisha macho na Grace mke wa 

Alfred 

 “ My Gosh ! Grace is here !!!..akawaza 

Pauline 

“ Pauline !! akasema kwa furaha Grace 

baada ya kumuona Pauline . 

 “ Grace ! akasema Pauline kisha 

wakakumbatiana 

 “Karibu sana Grace.Anaendeleaje 

mwanao? Akauliza Pauline 

 “ Anaendelea vizuri sana.Vipi wewe 

unaendeleaje? Akauliza Grace 

 “ Ninaendelea vizuri sana pia.Karibu 

sana” akasema Pauline 

 “ Pauline kwanza samahani sana kwa 

kukuvamia bila kukupa taarifa.Nimetoka 

sehemu Fulani hapo karibu nikaona ni 

vyema kama nikapita hapa kukujulia hali 

vile vile nataka nikukaribishe nyumbani kwangu jumapili kwa chakula .” akasema 

Grace 

 “ Grace nashukuru sana kwa 

kunimtebelea.Usihofu kabisa kuhusu 

taarifa.Unakaribishwa hapa muda 

wowote .Nimefurahi saan kukuona na 

ahsante sana kwa kunikaribisha 

nyumbani siku ya jumapili lakini 

utanisamehje sana kwani jumamosi hii 

nitakuwa na safari ya kuelekea 

Arusha.Kuna rafiki yangu ametoka 

Marekani ameiomba niongozane naye 

kuelekea Arusha.Nadhani nitakaporejea 

nitapata muda mzuri sana wa kuja kwako 

na kushinda kutwa nzima.” Akasema 

Pauline 

 “ Ouh basi usijali Pauline.Kama 

utakuwa na safari hata utakaporejea 

tutakualika nyumbani kwetu.We love you 

so much.By the way mradi wako 

unaendeleaje? Akauliza Grace 

 “ Mradi unaendelea vizuri sana 

ukarabati unaendelea vizuri pi 

,namshukuru sana Alfred kwani yeye 

ndiye aliyenipa wazo la kuanzisha mradi 

ule na amenisaidia sana mpaka hatua hii 

ulipofika.“ akasema Pauline na Grace 

akatabasamu  “ Pauline mimi si mkaaji sana 

,nimepita mara moja kukujulia hali 

nadhani tutaonana utakaporejea.Lakini 

kabla sijaondoka,can you show me your 

room.Nataka mara nyingine nikifika hapa 

nipite moja kwa moja bila kuuliza 

mapokezi.Kuna usumbufu 

mwingi,maswali mengi sana” 

 Pauline alihisi haja ndogo inataka 

kumtoka kwa namna alivyostuka baada ya 

Grace kusema anataka kukifahamu 

chumba chake.Haraka haraka akajitahidi 

kutabasamu ili kuuficha mstuko alioupata 

 “ Ni kweli Grace,kuna usumbufu 

mwingi mapokezi .Wanajali sana usalama 

wa wateja wao na ndiyo maana taratibu 

zao ni ndefu hadi uruhusiwe kuonana na 

mtu wako .Twende nikakuonyeshe 

chumbani kwangu,karibu sana. “ akasema 

Pauline na kuongozana na Grace kuelekea 

chumbani kwake. 

 “ Ama kweli leo nimeumbuka .Sijui 

nini kinakwenda kutokea Grace akimkuta 

Alfred mume wake chumbani 

kwangu.Ouh Mungu nisaidie katika suala 

hili.Mtafaruku mkubwa sana unakwenda 

kutokea huku chumbani na sina namna ya 

kuweza kumzuia Grace asiingie chumbani 

kwangu.Nadhani tayari amekwisha hisi kwamba mume wake yuko hapa au 

alikuwa anamfuatailia na ndiyo maana 

amekuja mida hii?.Jamani aibu gani hii 

ninakwenda kuipata leo !! Niwakati kama 

huu ndipomtu unapohitaji sana muujiza 

utokee ” akawaza Pauline huku 

wakipanda ngazi kuelekea chumbani . 

 “ Pauline hoteli hii ni nzuri sana 

nimeipenda na hasa ilivyo safi.Inavutia 

mno.Nimeipenda sana” Grace akamstua 

Pauline kutoka katika mawazo 

mazito.Walikuwa wanapanda ngazi lakini 

Pauline miguu ilikuwa inagongana,mwili 

ulikuwa unamtetemeka ,hakuwana nguvu 

kabisa lakini akajikaza kwa kujitegemeza 

katika mbao za pembeni mwa ngazi. 

 “ Ni kweli Grace..wanajitahidi sana 

kwa usafi “ akajibu Pauline kwa ufupi. 

 “ Tunazidi kukaribia sana chumbani 

na mwili wote hauna nguvu hata 

kidogo.Dah ! leo ninaumbuka vibaya 

sana.Sijawahi pata aibu ya namna hii 

katika maisha yangu.Sijawahikufumwa na 

mume wa mtu hata mara moja.Nadhani 

tayari Grace amekwisha hisi kuna kitu 

kinaendelea kati yangu na mume wake na 

anafahamu kabisa kwamba mume wake 

yuko hapa na inawezekana hata gari la 

mume wake ameliona katika maegesho.Ningejua ningemweleza ukweli 

toka mapema kwamba mume wake yuko 

hapa asingekuwa na wasi wasi na mimi na 

angenionani mtu mkweli.Nahisi alikuwa 

ananitega kuona tabia yangu kama ni 

mkweli na muaminifu.Mpaka hapa tayari 

nimekwisha haribu kila kitu na hakuna 

tena muujiza wowote.Kilichobaki ni bomu 

tu kulipuka. Laiti ningekuwa na simu 

ningeweza hata kumpigia simu Fred na 

kumwambia akajifiche.” Alipokumbuka 

kuhusu simu akapata wazo la ghafla 

 “ Grace,japokuwa una haraka 

naomba ukae hata dakika kumi tu walau 

tuongee.I feel so bored sina mtu wa 

kuongea naye.Nitashukuru sna kama 

ukinipa kampani kidogo.” Akasema 

Pauline.Grace akatabasamu na kusema 

 “ Sawa Pauline.Sikuwa na mpango 

wa kukaa sana lakini kwa kuwa 

umeniomba nitakaa nawe kwa dakika 

kama kumi tu nataka nikamuwahi mtoto.” 

 “ Ahsante sana Grace.Naomba basi 

unisubiri dakika mbili nikachukue 

kinywaji pale chini” akasema Pauline na 

kabla Grace hajasema chochote tayari 

alikwisha geuka na kuanza kushuka kwa 

kasi kubwa hadi mapokezi ambako 

aliomba simu na kupiga chumbani kwake..  “ Hallow” akasema Alfred baada ya 

kupokea simu 

 “ Fred ni mimi Pauline.Grace yuko 

hapa na ameng’angania nimlete chumbani 

kwangu.Nimemsimamisha kidogo ili 

nipate nafasi ya kurejea mapokezi kupiga 

simu.She knows you are here,tafadhali 

namoba ufungue mlango na utoke kwa 

kutumia mlangoule wa kwenye lifti sasa 

hivi” akasema Pauline 

 “ Sawa Pauline.Ahsante kwa taarifa” 

Akasema Alfred na kuutupa mkono wa 

simu mezani. 

 “ Dah ! mwili wote unanitetemeka 

kama vile nina homa.Hili tukio la leo ni 

fumanizi la aina yake.Lakini nilimweleza 

Alfred toka awali kwamba mke wake 

anaweza akagundua kuhusu jambo hili 

akakataa kunisikiliza na haya ndiyo 

matokeo yake.Leo tumefumwa vizuri 

sana.Natamani ningekuwa na mabawa 

niruke mara moja na kupotea niepuke 

aibu hii” akawaza Pauline halafu akaenda 

baa na kuchuku chupa moja ya mvinyo 

akaanza kupanda ngazi kueleka chumban 

kwake 

 “ Samahani Grace 


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog