IMEANDIKWA NA : PATRICK CK
******************************************
Simulizi : The Football
Sehemu Ya Kwanza (1)
Msafara wa rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania,uliwasili katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es
salaam.Dr Vivian Sebastian Matope
rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania akashuka garini akiwa
amevalia suti ya rangi nyeupe
iliyompendeza vilivyo.Kichwani
hakuwa amebadili mtindo wake
wa nywele.Dr Vivian hakupenda
kuweka madoido katika nywele
zake.Alipenda kuzipunguza na
kuzifanya fupi.Alikuwa na mwili
mwembamba wastani na
kumfanya awe ni mmoja kati ya
marais wanawake wazuri zaidi
duniani.
Akiwa katika ulinzi mkali Dr
Vivian alianza kuelekea ndegeni
huku akisalimiana na kuagana na
baadhi ya viongozi waliofika pale
uwanjani kumuaga.Alipomaliza
kuagana na viongozi mbali mbali
akamuita pembeni mkurugenzi wa
idara ya idara ya usalama wa taifa
ndugu George Mzabwa
“George umefikia wapi
kuhusu lile suala ?Kuna chchote
kimepatikana mpaka leo? Akauliza
Dr Vivian
“Madam president lile suala
bado gumu lakini tunaendelea
kulifanyia kazi.Mpaka sasa bado
hatujafikia hatua ya kuridhisha na
ndiyo maana umeona nimekuwa
kimya sijafika kwako kukupa mrejesho wowote” Akasema
George.Dr Vivian akamtazama
akatabasamu na kusema
“Nitakaporejea nataka nikute
tayari kuna hatua imekwisha
pigwa ama sivyo nitakuondoa
katika nafasi hiyo na kuwapa
wengine wenye uwezo wa kufanya
kazi kwa kasi kama
ninavyotaka.Sioni sababu ya
kukukwamisha katika
kulishugulikia suala hili wakati
kila kitu unacho.Naomba ulifanyie
kazi hilo nililokwambia na
nitakaporejea nikute aidha ripoti
ya hili suala,au barua ya kuachia
ngazi au nikuondoe mwenyewe
katika nafasi hiyo.Tumeelewana
George? Akauliza Dr Vivian “Nimekuelewa madam
president” akajibu George
“ Good” akasema Dr Vivian na
kupanda ngazi kuingia
ndegeni.Alipofika katika mlango
wa ndege akageuka na
kuwapungia mkono watu
waliokuja kumuaga halafu
akaingia ndegeni
Dr Vivian ni rais wa kwanza
mwanamke kuongoza jamhuri ya
muungano wa Tanzania .Alizaliwa
22 Octoba 1970 akiwa mtoto wa
kwanza wa Kanali Sebastian
Matope na mke wake Getruda
Mazimbo.Alipata elimu yake ya
msingi katika shule ya msingi
Azimio mjini Dodoma ambako
baba yake alikuwa akifanya kazi wakati huo.Alijiunga na shule ya
sekondari ya St Bernadetha
inayomilikiwa na masista wa
shirika la mtakatifu Bernadetha
iliyoko mkoani Kilimanjaro.Lengo
kuu la kujiunga na shule hiyo iliyo
chini ya watawa ilikuwa ni
kujiunga na maishaya utawa.Toka
akiwa mtoto dogo Dr Vivian
aliyapernda maisha yale ya
kitawa.Alisoma katika shule hiyo
hadi kidato cha sita na matokeo
yalipotoka Vivian alifaulu kwa
kiwango cha juu kwa kupata
daraja la kwanza.Matokeo hayo
yalimfanya Vivian abadili lengo
lake la kuwa mtawa na akachagua
kuendelea na masomo ya udaktari
.Aliendelea na elimu ya juu katika fani ya udaktari katika vyuo vikuu
kwenye nchi mbali mbali kama vile
Israel,Cuba,Urusi,Marekani na
China.Mwaka 2007 aliamua
kurejea nchini Tanzania baada ya
familia yake yaani wazazi wake
wote na mdogo wake kuuawa na
watu wasiojulikana.
Baada ya kurejea nchini Dr
Vivian alifanya kazi kama daktari
wa watoto katika hospitali ya taifa
ya Muhimbili.Alianza kujiingiza
taratibu katika siasa na kutokana
na kipawa chake kikubwa cha
uongozi alichokuwa nacho,Dr
Vivian alijikuta akishika nafasi
kadhaa ndani ya chama na hapo
ndipo alipoanza
kujulikana.Daktari huyu mwenye haiba ya kipekee,mwenye urefu wa
5.8.ngozi nyororo na uso
usiokauka tabasamu alifahamika
sana kwa misimamo yake thabiti
isiyoyumba katika yale mambo
anayoyaamini na hasa katika
kusimamia haki za watu wa hali za
chini wanaokandamizwa.
Tabia yake hii ya msimamo
usiotetereka ilianza kuonekana
pale alipokuwa rais wa serikali ya
wanafunzi katika chuo kikuu
kimoja alichosoma nchini
Marekani.Katika chuo hicho kikuu
wanafunzi wenye asili ya Afrika
walikuwa wanabaguliwa na
kutopewa kipaumbele katika
mambo mengi.Haikuwa rahisi
kwake kuweza kushinda nafasi ya rais wa serikali ya wanafunzi na
aliposhinda kitu cha kwanza
alichoanza kukishughulikia ni
suala la ubaguzi uliokithiri hapo
chuoni.Jambo hili lilimletea
misukosuko mikubwa na hata
kuondolewa katika nafasi yake ya
rais wa wanafunzi baada ya
kuonekana anakiuka sheria za
chuo lakini hii haikumkatisha
tamaa kuendelea kuwapigania
wale waliokuwa
wanabaguliwa.Baada ya mvutano
mkali na chuo hicho hatimaye
ushindi ukapatikana na taratibu za
chuo zikabadilishwa,wanafunzo
wote wakawa na haki sawa.Kwa
wale wanaofuatilia mambo ya
nyota,hii ilikuwa ni ishara tosha kwamba nyota ya Dr Vivian ilianza
kung’aa na siku moja ingeweza
kung’aa na kutoa mwangaza
mkubwa
Wakati akiendelea na
masomo yake aliwahi kuchaguliwa
kuwa msemaji wa wanafunzi
wenye asili ya Afrika katika katika
vyuo vikuu vya Marekani na katika
mojawapo ya hotuba aliyowahi
kuitoa katika kongamano
lililofanyika siku ya kuikumbuka
hotuba aliyoitoa mwanaharakati
aliyepigania haki za watu weusi
nchini Marekani Martin Luther
aliyoitoa 28 August 1963,Vivian
aliweka wazi ndoto yake ya
kuliona siku moja bara la Afrika
linatoka gizani na kuwa bara lenye nuru na nguvu.Alieleza
kusikitishwa kwake na
ukandamizwaji na unyonyaji
unaofanywa na mataifa makubwa
yenye nguvu dhidi ya mataifa
masikini ya bara la Afrika.Hotuba
hii iliyojaa msisimko iliwavutia
watu wengi na kumfanya Vivian
ajulikane na kualikuwa katika
makongamano mbali mbali.Katika
mojawapo ya hotuba alizowahi
kutoa aliweka wazi nia yake ya
siku moja kuwa kiongozi na
kuziunganisha nchi zote za Afrika
na kuwa nchi nmoja yenye nguvu
kijeshi na kiuchumi. Alitamani
siku moja awe rais wa kwanza wa
Afrika na kuongoza bara hili lenye
kila aina ya utajiri. Alipofanikiwa kushinda nafasi
ya urais wa Tanzania,Dr Vivian
amefanya mambo makubwa kwa
muda wa miaka miwili ambayo
amekuwa madarakani.Ni rais
mdogo kwa umri ukilinganisha na
marais wengi wa mataifa mengine
lakini mambo makubwa
aliyoyafanya yamewashangaza
wengi.Ni rais asiyesita kuchukua
maamuzi magumu na
asiyetetereka katika maamuzi
yake.Huyu ndiye Dr Vivian rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania
ambaye amepewa jina la utani la
Dr White kutokana na staili yake
ya kipekee ya kupenda rangi
nyeupe kuanzia mavazi yake hadi
magari yanayotumika katika msafara wake.Mara chache sana
huonekana katika mavazi ya rangi
nyingine lakini siku zote huwa
katika mavazi meupe.
Baada ya kuingia ndegeni Dr
Vivian akasalimiana na marubani
na wahudumu wa ndege yake na
kujiandaa kwa ajili ya kuelekea
jijini New York Marekani
kuhudhuria mkutano mkuu wa
umoja wa mataifa unaofanyika kila
mwaka na ambao huudhuriwa na
wakuu wote wa nchi wanachama
wa umoja wa mataifa.Huu ni
mkutano wake wa kwanza
kuhudhuria tangu achaguliwe
kuwa rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.Mkutano
uliopita aliwakilishwa na makamu wa rais na mwaka huu
anahudhuria yeye
mwenyewe.Katika safari hii
aliongozana na mawaziri
wanne,maafisa wengine kadhaa
pamoja na walinzi wake na jumla
msafara wake ulikuwa na watu
ishirini.
Ndege ilikaa katika njia yake
ya kurukia ikaanza kuondoka
taratibu na kuongeza kasi kisha
ikapaa huku viongozi waliofika
pale uwanjani kumuaga rais
wakipunga mikono kumtakia rais
na ujumbe wake safari
njema.Ndege ilipokaa sawa
angani,Dr Viviana akaitisha kikao
na watendaji alioambatana nao
katika safari ile.Walikutana katika chumba cha mikutano kilichomo
ndani ya ndege ile kubwa chenye
uwezo wa kuchukua watu zaidi ya
ishirini.Walijadiliana mambo
kadhaa kuhusiana na safari yao ile
na baada ya takribani saa moja na
nusu kikao kikamalizika wajumbe
wakatoka na rais akaenda katika
chumba chake kupumzika kwani
safari ile ilikuwa ndefu.Akiwa
chumbani akamuita mdogo wake
Theresa.
Theresa Sebastian Matope ni
msichana mwenye weusi wa
kung’aa na umbo la
kupendeza.Wazazi wa Dr Vivian
walimchukua Theresa toka katika
kituo cha kulelea watoto yatima
akiwa mtoto mdogo sana na kumlea kama mtoto wao wa
kumzaa.Kwa hivi sasa ndiye
mwandishi wa hotuba za rais
“Theresa naomba nione
hotuba uliyoiandaa ninayokwenda
kuitoa New York” Akasema Dr
Vivian baada ya Theresa kuingia
mle chumbani kwake.Theresa
akatoka na kwenda kuchukua
kompyuta yake akarejea na
kumuonyesha Dr Vivian hotuba ile
aliyokuwa anaiandaa
“Imebaki sehemu ndogo ya
kumalizia kuhusiana na
mabadiliko ya tabia nchi Afrika”
Akasema Theresa na Dr Vivian
akaipitia hotuba ile taratibu halafu
akasema “Hii ni hotuba nzuri sana
lakini bado haijafikia kiwango
ninachokihitaji.Hii ni hotuba
yangu ya kwanza katika mkutano
huu mkubwa na ninataka iwe kali
na yenye msisimko.Nimezoeleka
hotuba zangu huwa zinakuwa kali
na zenye msisimko.Nataka
viongozi wa dunia waelewe
msimamo wangu na wa Tanzania
katika mambo mbali mbali hivyo
iongeze ukali hotuba hii” akasema
Dr Vivian
“Dada labda uniweke wazi
unataka nilenge maeneo yapi
hasa.Ulinipa mambo ya kuzingatia
wakati wa kuiandaa hotuba hii na
nimeyafuata ,nimelenga mambo ya
uchumi,misaada ya masharti na unyonyaji wa rasilimali
zetu,mabadiliko ya tabia nchi na
mengineyo” akasema Theresa.Dr
Vivian akaitazama tena hotuba ile
na kusema
“Hotuba hii si mbaya,imekaa
vizuri lakini kuna sehemu ambazo
zinahitaji lugha kali zaidi
kuonyesha msisitizo.Hotuba hii
imepoa sana.Lakini usijali endelea
nayo na utakapomaliza niletee
nitaisahihisha
mwenyewe,samahani kama
nimekukwaza” akasema Dr Vivian
“Usijali dada” akasema
Theresa na kuchukua kompyuta
yake ili atoke Vivian akamuomba
asubiri. “Kaa nami kidogo
Theresa,bado tunayo safari
ndefu.Nyakati kama hizi ndipo
tunaweza kukaa na kuongea
mambo yanayotuhusu sisi.Tukifika
marekani kutakuwa na mikutano
mingi hivyo hatutaweza kupata
nafasi nzuri ya kuzungumza
mambo yetu” akasema Dr Vivian
“Ni kweli dada.Japokuwa tuko
pamoja muda mwingi lakini
hatupati nafasi ya kuzungumza
mambo yetu ya kifamilia” akasema
Theresa na kujimiminia juice
katika glasi
“Kabla sijaingia ndegeni
nilikuwa na mazungumzo na
George Mzabwa.Nilimuuliza
amefikia wapi kuhusiana na kazi niliyompa ya kuchunguza mauaji
ya familia yetu.Amekuwa
ananikimbia kimbia kila
ninapotaka kulizungumzia jambo
hili.Jibu alilonipa
halijaniridhisha.Amesema
kwamba mpaka sasa bado
hajafanikiwa kugundua lolote.Ni
miaka miwili imepita sasa toka
nimempa kazi hiyo na ameniudhi
sana.Nimemwambia nitakaporejea
aidha nikute taarifa kwamba watu
waliofanya kitendo kile kiovu
wamepatikana au nikute barua
yake ya kuachia ngazi mezani
kwangu ama sivyo nitamuondoa
na kumpeleka sehemu nyingine
kwani ameshindwa kazi.Sielewi
kuna nini katika jambo hili hadi lishindwe kupatiwa
majibu.Ninafikiria kutafuta mtu
mwingine wa kuongoza idara ya
usalama wa taifa kwa kasi
ninayoihitaji.George hawezi
kuendana na kasi yangu” akasema
Dr Vivian
“Hata mimi nashangaa na
kujiuliza kulikoni katika suala hili?
Inawezekajane mpaka leo hii
hakuna taarifa yoyote kuhusiana
na wauaji wa familia yetu?Jeshi la
polisi wamefanya
uchunguzi,usalama wa taifa pia
lakini mpaka leo hii hakuna
chombo chochote kilichotoa
majibu ni nani waliua familia yetu
na kwa nini.Vyombo hivi vyote
viwili wanazo rasilimali za kutosha kuwawezesha kufanikisha
uchunguzi wa jambo hili lakini
mpaka leo wameshindwa kubaini
watu waliofanya unyama ule.Hapa
kuna kitu kinatia shaka dada”
akasema Theresa
“Tuachane na hayo
nitayashughulikia nitakaporejea
kwani suala hili kwa sasa
linaonekana kama fumbo gumu
lisiloweza kufumbuka.Nitalivalia
njuga mimi mwenyewe na safari
hii lazima nitapata majibu,lazima
fumbo hili lifumbuke” akasema Dr
Vivian na kumuomba Theresa
amletee juice ya mchanganyiko wa
matunda kinywaji anachokipenda
sana. “Nathan kanipigia simu leo
asubuhi na kunitaarifu kwamba ile
kazi yake aliyokwenda kuifanya
Uswisi imemalizika na hivyo
atanifuata New York na baada ya
mkutano kumalizika tutarejea
wote Da es salaam kuendelea na
maandalizi ya ndoa yetu.Theresa
siwezi kueleza furaha niliyonayo
kwani imebaki miezi mwili tu na
mimi niingie katika ndoa na
mwanaume ninayempenda kwa
dhati.Hata hivyo kuna kitu nataka
kukisikia toka kwako.Watu
wanaongeaje huko mitaani
kuhusiana na ndoa yangu na
Nathan? Nilitaka jambo hili liwe la
kimya kimya lakini watu
wamefukunyua hadi wakagundua ninataka kufunga ndoa”Akauliza
Dr Vivian huku
akitabasamu.Theresa akanywa
funda la juice halafu akasema
“Japokuwa Nathan ulikuwa
naye katika kipindi chote cha
kampeni na kuzunguka naye nchi
nzima lakini bado watu
hawamfahamu vizuri ni
nani.Nimekuwa napitia baadhi ya
maoni ya watu mtandaoni na
nimeona watu wanahoji kwa nini
rais wao aolewe na mtu wa kutoka
nje ya nchi?Tanzania imejaa vijana
wa kila aina wasomi na wabobezi
wa mambo mbali
mbali,haujawaona hao wote hadi
moyo wako ufunguke kwa mtu wa
taifa lingine?Lakini haya yasikuogopeshe ni mawazo tu ya
watu yanayotokea katika mijadala
mbali mbali inayoendelea huko
mitandaoni” akasema Theresa .Dr
Vivian akatabasamu nba kuuliza
“Wewe je una maoni gani?
“Kuhusu nini dada Vivi?
“Kuhusu mimi na
Nathan.Nakufahamu wewe huna
tabia ya kuficha kitu bali husema
kweli toka moyoni.Sijawahi kupata
maoni yako kuhusiana na hili suala
langu na
Nathani.Unaliongeleaje?Nathani ni
mwanaume ambaye naweza
kusema kwamba ninampenda kwa
dhati ya moyo wangu lakini je
unadhani watu wangu
watampenda na kumkubali?Tafadhali kuwa
muwazi kwangu.You are my
sister” akasema Dr Vivian
“Dada ,mapenzi kama yalivyo
hayachagui rangi,umri hata
taifa.Moyo unaweza kufunguka
kwa mtu yeyote awe
mweusi,mweupe n.k.Wewe
umeufungua moyo wako kwa
Nathan na hakuna ubaya wowote
lakini….” Theresa akasita kidogo
akanywa maji ya matunda na
kuendelea
“Umeomba nikueleze ukweli
wangu na nitakueleza ukweli
wangu japo hautakuwa mzuri sana
lakini lazima niuseme kwa kuwa
umeomba.Hakuna mtu
atakayeweza kukuzuia usiolewe na Nathan mwanaume unayempenda
kwa dhati ya moyo wako lakini
ndoa hii ingekuwa na tija zaidi
kama Nathan angekuwa ni
mtanzania.Anaweza akabadili
uraia wake na kuwa mtanzania
lakini damu yake bado ni
Marekani.Kama akiwa mumeo
yeye ndiye atakayekuwa mshauri
wako mkuu kwa mambo mbali
mbali hivyo anapaswa awe ni mtu
anayeipenda Tanzania na
kuifahamu vyema,ayafahamu
matatizo ya waTanzania na
yamguse ili aweze kukushauri
vizuri namna ya kuzitatua
changamoto mbali mbali
unazokumbana nazo katika kazi
yako.Nathani yeye ni mmarekani na Tanzania ameifahamu kwa
sababu yako tu na sina hakika
kama anaweza kuwa mshauri
mzuri katika masuala yanayohusu
Tanzania.Ikitokea akashindwa
kukushauri au akakushauri vibaya
mzigo wote wa lawama utakuwa
juu yako.Lakini haya ni mawazo
yangu tu na usiyachukulie kama
ndiyo mtazamo wa
watanzania.Nathan ni kijana mzuri
na sioni kama ana tatizo lolote”
akasema Theresa
“Theresa ahsante sana.Ndiyo
maana huwa ninapenda kukuomba
ushauri.Una mtazamo wa
mbali.Unafaa sana kuwa mshauri
wa rais na nitalitazama hilo siku za
usoni.Umezungumza mambo ya msingi na ambayo sikuwa
nimeyafikiria kabla sijakubali
kuolewa na Nathan.Vipi kuhusu
wewe na yule mtu wako Damian?
Bado mnaendelea na ugomvi
wenu? Kwa nini masuala yenu
msiyatafutie ufumbuzi na
kuyamaliza ili msonge mbele kwa
amani?
“Dada Vivi kuna mambo
mengine hayafai
kuyalazimisha.Nimetafakari sana
na kugundua mimi ndiye
niliyekuwa nalazimisha penzi
wakati mwenzangu hana muda
nami.Kila wakati mimi ndiye
niliyekuwa nikipiga magoti
kuomba msamaha hata kama si
mimi niliyekosa.Lengo lilikuwa ni kunusuru penzi letu kwa kuwa
Damian nilimpenda zaidi ya
ninavyoweza kueleza.Lakini ulifika
wakati nikasema imetosha na
nikaamua kila mmoja aendelee na
maisha yake.Niliumia mwanzoni
but now I’m happy.Nina amani ya
moyo na ninasubiri yule ambaye
ameumbwa kwa ajili yangu
ajitokeze.Naamini yupo mahala
fulani na muda ukifika nitampata”
akasema Theresa
“Hongera kwa maamuzi
hayo.Mimi nilitamani sana
kukushauri hivyo toka awali lakini
sikutaka kuingilia masuala
yako.Unapoona uko katika
mahusiano halafu wewe ndiye
mwenye kuumia kila siku na mwenzako hajali basi chukua
hatua haraka,huo uhusiano
hautakufikisha mahala
kokote.Natumai tayari umepata
somo la kutosha na utakuwa
makini safari hii kutafuta
mwanaume yule ambaye atakufaa
katika maisha yako.Ukikosea
kuchagua utaumia sana.Mapenzi
yanaumiza mno.Kuna nyakati hata
mimi ninawaza kuhusu Nathan
kama hatutakuwa na migogoro
pindi tutakapofunga ndoa.Nataka
nielekeze akili yangu katika
kuwasadia watanzania
walionichagua na kuwatatulia kero
zao na nitakuwa na muda mdogo
sana wa kushughulikia masuala ya
mapenzi.Hiki hawezi kuwa kikwazo kwa Nathan na kikaleta
mgogoro kati yetu?Laiti Mungu
angeweza kunionyesha maisha
nitakayoishi nikiwa na Nathan
ningeweza kufanya maamuzi lakini
Mungu ametuficha na hatuelewi
chochote kuhusu dakika ijayo”
akasema Dr Vivian
“Usiwe na wasi wasi
dada.Nathan ni kijana mzuri,mpole
na hana matatizo.Lakini …”
Theresa akasita
ENDELEA
Usiwe na wasi wasi
dada.Nathan ni kijana mzuri,mpole
na hana matatizo.Lakini …”
Theresa akasita
“Lakini nini Theresa? Mbona
umesita? Sema unachotaka
kukisema” akasema Dr
Vivian.Theresa akafikiri kidogo na
kusema
“Nothing.Ngoja nikuache
upumzike,mimi naenda kuimalizia hotuba hii halafu na mimi
nipumzike” akasema Theresa na
kuchukua kompyuta yake akatoka
mle chumbani.
“Theresa alitaka kuniambia
nini halafu akasita? Akajiuliza Dr
Vivian baada ya Theresa kutoka
mle chumbani
“Theresa si mtu wa kuficha
jambo,au aliona halina maana
ndiyo maana akaamua kuachana
nalo.Hata hivyo kuna jambo
amelizungumza la maana sana
kwangu na sikuwa nimelitilia
maanani hapo kabla.Nikiolewa na
Nathan yeye ndiye atakayekuwa
mshauri wangu katika mambo
mengi lakini atanishauri kitu gani
kama haifahamu vyema Tanzania wala matatizo ya watanzania?
Akajiuliza
“Nimetoka mbali na Nathan na
ninamfahamu vyema.Hata kama
haifahamu vizuri Tanzania wala
matatizo yake lakini nina imani
atanishauri vizuri kwani ni kijana
mpole na mwenye busara ya hali
ya juu.Sina shaka hata kidogo na
upendo wake kwangu na hata
mimi ninampenda mno na ndiyo
maana hata aliponitamkia kwamba
anataka kunioa niliruka ruka kwa
furaha.Mengi yatasemwa lakini
sitakiwi kuyasikilza.Natakiwa
kuziba masikio na kuyapuuza
kwani huyu ndiye chaguo
langu.Nathan ameingia katika kila
mshipa wa mwili wangu” akawaza na kuinuka kitandani akachukua
kompyuta yake akafungua mahala
anakohifadhi picha na kuzitazama
picha za gauni lake zuri atakalovaa
siku ya harusi yake,akatabasamu
“Sipati picha namna
nitakavyopendeza ndani ya gauni
hili lililobuniwa na mbunifu
chipukizi wa mavazi wa
kitanzania.Naamini
nitakapoonekana nimelivaa gauni
hili jina lake litapaa ulimwenguni
kwani wengi watataka kufahamu
nani alibuni vazi zuri kama hili.”
Akatabasamu na kuanza kutazama
picha nyingine za wabunifu mbali
mbali wa mavazi ya harusi
Alipotoka chumbani kwa
rais,Theresa akaenda katika moja wapo ya ofisi zilizomo ndani ya
ndege hii kubwa akachomeka
spika za masikioni katika
kompyuta yake akaanza kusikiliza
muziki.Uso wake ulionyesha
mabadiliko
“Mambo tuliyozungumza na
dada Vivi yameniharibia kabisa
siku yangu.Kwanza ni kuhusu yule
mchumba wake Nathan.Moyo
wangu haumkubali kabisa na hata
mwenyewe analifahamu hilo na
sijui kwa nini simpendi.Kila
nimuonapo karibu na dada amani
hutoweka kabisa.Najua
wanapendana lakini moyoni
mwangu hana kibali.Si kwamba
ninamchukia ila ninaona hafai
kuwa na Vivian.Nilitaka nimueleze hivyo dada lakini nikasita kwani
asingefurahia maneno hayo.Hata
hivyo siwezi kuingilia mapenzi
yao.Kama wanapendana acha
waoane lakini ningefurahi sana
kama dada yangu angeolewa na
kijana mtanzania” akawaza
Theresa na kufumbua macho
baada ya mlango kufunguliwa na
mtu kuingia mle ofisini.Alikuwa ni
waziri wa mambo ya nje
“Theresa nimekufuata
wewe,kuna kitu nataka
unisaidie.Naomba uipitie hii
hotuba yangu na uirekebishe kama
kuna mapungufu” akasema waziri
huyo na kutoka .Theresa
akaendelea kusikiliza mziki huku
akiipitia hotuba ile ya yule waziri na mara kumbu kumbu fulani
ikamjia akaacha kazi aliyokuwa
anaifanya akajiegemeza kitini
“Ni miaka zaidi ya kumi sasa
imepita lakini bado picha ya
yaliyomkuta baba haijafutika
kichwani na inanitesa kila
uchao.Nilikuwepo na nilishuhudia
kila kilichotokea.Najiuliza kwa
nini mimi?Kwa nini Mungu
akanichagua mimi niyashuhudie
yale yote? Naamini Mungu ana
sababu zake na ndiyo maana
katika watu wote ambao
walimzunguka baba alinichagua
mimi na kunibebesha mzigo huu
mzito.Kila siku ninapolikumbuka
jambo hili mwili wote hupata
baridi.Bado ile milio ya risasi zilizochukua uhai wa baba,mama
na kaka Kelvin ninaisikia
masikioni kila nilalapo.Nimebaki
natembea na siri hii nzito ambayo
hakuna anayeifahamu hata dada
Vivian hafahamu chochote , Ni mimi
pekee ninayefahamu sababu ya
baba ,mama na kaka Kelvin
kuuawa.Ni kwa sababu ya
Football” Machozi yakamtoka
“Nimekuwa najilazimisha
kutaka kulisahau jambo hili lakini
nimeshindwa.Ninaogopa kuliweka
wazi suala hili kwa ajili ya usalama
wangu na dada.Ninaogopa hata
kumueleza dada Vivian kwani
yanaweza kumkuta kama
yaliyomkuta baba .Waliomuua
baba walikuwa wanaitafuta hiyo football ni vipi endapo mpaka sasa
wakawa bado wanaitafuta?
Nitayaweka hatarini sana maisha
ya dada nikimueleza kuhusiana na
hili suala.Ngoja niendelee kulibeba
na itakuwa ni siri yangu pekee na
Mungu wangu.Nimeibeba na
kutembea na siri hii kwa zaidi ya
miaka kumi na nitaendelea
kutembea nayo.Yawezekana wale
jamaa bado wanaendelea
kutuchunguza.Sina hakika kama
watakuwa wamekata
tamaa.Lazima watakuwa
wanachunguza kwa siri ili kujua
football iko wapi.Lakini hii football
ni kitu gani?Ina siri gani ndani
yake?Baba hakuwahi kunieleza
chochote kuhusiana nayo.Ninavyofahamu mimi mkoba
ule uliopewa jina la football asili
yake ni nchini Marekani ambako
kila asafiripo rais wa Marekani
huwa anasafiri nao na ndani yake
kuna mambo ya siri ya kiusalama
kuhusiana na mambo ya
nyuklia.Hapa Tanzania rais Anorld
alianzisha mtindo wa kutembea na
begi kila anakoenda na akalipa
jina la football na baba ndiye
aliyekuwa mbebaji wake mkuu,je
kulikuwa na siri gani humo ndani
yake? Akajiuliza Theresa na
kukumbuka zikamrejesha mbali
JUNE 2007 – DAR ES SALAAM
Saa tatu za usiku familia ya
Kanali Sebastian Matope wamekaa
sebuleni wakitazama filamu baada
ya kumaliza kupata mlo wa
usiku.Theresa akainuka akaenda
chumbani kwake na kurejea na
bahasha ya khaki akampatia baba
yake
“Nini hii,mchango? Akauliza
kanali Sebastian.Theresa hakujibu
kitu akatabasamu.Baba yake
akaifungua na kukuta ni ripoti ya
matokeo ya mtihani.Akaipitia na
kutabasamu
“Theresa hujawahi
kuniangusha hata mara
moja.Safari hii tena umeshika namba mbili.Hongera
sana.Unastahili zawadi kubwa kwa
bidii kubwa unayoionyesha
shuleni” akasema Kanali Sebastian
na kumpa mkewe ripoti ile naye
aipitie
“Zawadi gani utanipatia safari
hii baba? Theresa akauliza.Kanali
Matope akafikiri kidogo na
kusema
“Kwa kuwa umenifurahisha
sana kwa matokeo haya mazuri
nitasafiri nawe kwenda nje ya
nchi”
“Kweli baba? Akauliza
Theresa kwa furaha
“Ndiyo.Kesho rais ana safari
ya kwenda Misri.Kuna kikao kifupi
cha marais wa nchi zinazopitiwa na mto Nile na kwa kuwa mto Nile
chanzo chake ni Tanzania basi rais
wetu naye atahudhuria kikao
hicho.Wakati kikao kinaendelea
wewe utapata nafasi ya kuzunguka
katika jiji la Cairo na kama muda
utaruhusu basi waweza pata nafasi
kufika katika mapiramidi na
utajifunza mambo mengi kwa
kuona kwa macho kuliko kusoma
tu vitabuni”
“Ahsante sana baba.Siwezi
kuelezea furaha yangu.Siamini
kama na mimi nitasafiri na rais
hapo kesho”
“Nitakutambulisha kwa rais
na kumueleza juhudi zako katika
masomo.Naamini hata yeye
mwenyewe atafurahi kwani anapenda sana vijana wanaojituma
katika kazi na masomo” Akasema
Kanali Matope na Theresa akaruka
ruka kwa furaha kubwa.
“Nitafutahi sana baba kama
nitapata nafasi ya kwenda
kujionea mapiramidi kwani
tumekuwa tunayasoma katika
historia.Itakuwa ni somo zuri sana
kwangu kuyashuhudia ana kwa
ana na nitakuja vile vile
kuwasimulia wenzangu maajabu
hayo makubwa ya
dunia.Tutakwenda sote huko
katika mapiramidi? Akauliza
Theresa
“Hautaongozana na mimi
Theresa ila nitakutafutia mtu
kutoka ubalozi wetu ambaye atakutembeza katika sehemu
mbali mbali za jiji la Cairo na kama
nafasi itapatikana basi
atakufikisha hadi katika
mapiramidi”
“Jamani baba kwa nini
usitafute nafasi tukaongozana
wote?Nitafurahi sana nikiwa nawe
mtu niliyemzoea ili iwe rahisi hata
kuuliza maswali”
“Hata mimi ningefurahi sana
kama ningepata nafasi ya
kukutembeza katika jiji la Cairo
lakini kazi yangu
hainiruhusu.Natakiwa kuwa
karibu na rais muda
wote.Usiogope mtu
nitakayekutafutia atakuwa
anaongea kiswahili na utamuuliza kitu chochote utakacho” akasema
Kanali Matope
“Kwani baba lile begi ambalo
huwa unalibeba kila unaposafiri
na rais lina nini ndani
yake?Hakuna mtu mwingine
anayeweza kukusaidia
kulibeba?Sijawahi kuona mtu
mwingine analibeba zaidi yako”
akasema Theresa na kumfanya
baba yake atabasamu
“Lile si begi kama mabegi
mengine.Lile ni begi maalum
linaitwa football”
“Football?? Theresa
akashangaa na kuangua kicheko
“Ndiyo linaitwa Football.Najua
umeshangaa kusikia jina hili
linalomaanisha mpira wa miguu lakini haimaanishi kama begi hili
linabeba mpira wa miguu.Mle kuna
mambo ya siri na hubebwa na mtu
ambaye amekula kiapo cha
kuhakikisha kwa vyovyote vile
hata kutokee nini football
linakuwa salama.Kulibeba begi lile
lazima upitie mafunzo maalum ya
komando na kufuzu kwa kiwango
cha juu.Lengo ni kuhakikisha
anayelibeba begi lile anakuwa ni
mtu mwenye mbinu na uwezo
mkubwa wa kujilinda na kuilinda
football.Asili ya jina hili ni
Marekani ambako rais wa
Marekani ana begi lake ambao
husafiri nalo kila aendako na
mataifa mengine yakaiga mtindo
huo japokuwa kila taifa lina jambo lake linalowekwa ndani yake
lakini mara nyingi huwa ni siri za
nchi zinazohusiana masuala ya
usalama.Hata hivyo muda wangu
wa kustaafu umekaribia na kuna
mtu mwingine anayeandaliwa
kushika nafasi yangu.Nadhani
nimejibu swali lao” akasema
kanali Matope
“Ndiyo nimekuelewa
baba.Kumbe jukumu ulilolibeba ni
kubwa na la hatari sana”
“Ni jukumu kubwa na la hatari
lakini ulinzi wake ni wa kutosha na
wa uhakika.Pamoja na uwezo
wangu mkubwa wa kujilinda na
kuilinda football lakini kuna
walinzi wanne ambao kazi yao ni kunilinda mimi na hilo begi”
akasema Kanali Matope
“Nini kitatokea endapo begi
hilo litapotea?akauliza Theresa na
kanali Sebastian akacheka
“Football haiwezi
kupotea.Tumekula kiapo cha
kuhakikisha tunailinda hadi tone
la mwisho la damu yetu kwa hiyo
unapolibeba begi kama lile basi
uhai wako unauweka rehani ili
kulilinda.Siku zote football ni
salama pengine kuliko hata rais”
akasema kanali Sebastian
“Baba ahsante ngoja niende
nikajiandae kwa hiyo safari ya
kesho” akasema Theresa
“Theresa kesho vaa mavazi ya
kawaida na usibebe mzigo mkubwa kwani ni safari ya siku
moja tu.Chukua vitu vichache
utakavyovihitaji kwa masaa
machache” akasema kanali
Sebastian.
**************
Mkutano wa wakuu wa nchi
zinazopitiwa na mto Nile
ulimalizika jijini Cairo Misri na saa
kumi na mbili za jioni rais wa
Tanzania akaagana na mwenyeji
wake ambaye ni rais wa Misri
akaondoka kurejea
Tanzania.Ilikuwa ni safari nzuri
sana kwa Theresa ambaye alipata
nafasi ya kutembelea sehemu mbali mbali za kihistoria
zinazopatikana jijini Cairo
Katika safari ya kurejea
Tanzania walikuwepo pia
waandishi nane wa habari
wanaotoka nchini Marekani
wakielekea nchini Tanzania lakini
kwa bahati mbaya walichelewa
ndege yao hivyo ikawalazimu
kuomba lifti katika ndege ya rais
ili wawahi ratiba yao ya kuandika
habari kuhusiana na mbuga za
wanyama zinazopatikana nchini
Tanzania.Rais alifurahishwa sana
na namna waandishi wale
walivyojitolea kutaka
kuifahamisha dunia juu ya vivutio
mbali mbali vya utalii
vinavyopatikana nchini Tanzania.Ndani ya ndege rais
alifanya mazungumzo na
waandishi wale na walijadiliana
mambo mbali mbali kuhusu
ukuzaji wa utalii nchini na namna
ya kutangaza vivutio vilivyopo
nchini Tanzania.Baada ya
maongezi ya takribani saa moja na
nusu waandishi wale wakamuacha
rais apumzike nao wakaenda
kuchukua nafasi zao.Ni safari ya
takribani masaa matano hivyo
hakukuwa na maongezi mengi mle
ndegeni na kila mmoja alikuwa
amejipumzisha baada ya uchovu
wa kutwa nzima.Hakuna
aliyetegemea kama kulikuwa na
hatari yoyote mbele yao Safari iliendelea hadi jijini
Nairobi ambako ndege ya rais
ililazimika kutua kwa dharura
baada ya marubani kubaini
kwamba ndege imepungukiwa
mafuta na walikuwa na wasi wasi
mafuta yaliyopo yasingetosha
kuwafikisha Dar es
salaam.Yaliibuka mabishano
makali kati ya walinzi wa rais na
marubani wakihoji kwa nini ndege
ya rais ipungukiwe mafuta?
Ilimlazimu rais kuingilia kati
mabishano yale na mafuta
yakawekwa kisha safari
ikaendelea
Muda mfupi baada ya kuingia
katika anga la Tanzania,ghafla
kukatokea jambo lililowastua walinzi wa rais.Sehemu ya jikoni
kulianza kufuka moshi.Iliwalazimu
walinzi wawili wa rais kwenda
haraka sana eneo la jikoni kwenda
kuangalia chanzo cha moto ule na
mara ikasikika milio ya risasi na
kuibuka kizaazaa kikubwa mle
ndegeni.Wale jamaa walioingia
ndegeni kama waandishi wa
habari wakainuka na kukimbilia
eneo la jikoni na baada ya muda
kila mmoja wao akawa na silaha
kali.Wote walionekana ni watu
wenye mafunzo makubwa sana ya
kupambana kwa kutumia
silaha.Walianza kushambuliana na
walinzi wa rais na kuua watu
hovyo mle ndegeni.Mara tu risasi
za kwanza ziliposikika na kuzua taharuki,Kanali Sebastian
alichukuliwa haraka sana pamoja
na football na kukimbizwa katika
chumba cha rais ambacho
kinaaminika ni salama
sana.Hakumuacha nyuma Theresa
“Nini kimetokea huko nje?
Rais akauliza kwa wasi wasi huku
jasho likimtiririka
“Tumevamiwa” akasema
mmoja wa walinzi wa rais huku
akimvisha rais fulana ya kuzuia
risasi
“Tumevamiwa na ani?
Akauliza rais kwa woga
“Mzee tunatakiwa tukuondoe
haraka sana humu ndegeni kwani
hawa jamaa…...” Hakumaliza
sentensi yake kwani ikaanza kusikika milio ya risasi karibu na
chumba cha rais.Watu wote mle
ndani ya chumba cha rais walivaa
fulana za kuwakinga na risasi
pamoja na miavuli mgongoni
tayari kabisa kwa kuondoka mle
ndegeni.
“Mheshimiwa rais
tuondoke,tayari hawa jamaa
wamekaribia.Tunakushusha chini
kwa mwavuli”
“Hapana.Kitu cha kwanza
tuhakikishe football iko
salama.Kabla ya kunitoa mimi
lazima kwanza tuhakikishe
Sebastian na football ametoka
humu ndegeni” akasema rais
“Mheshimiwa rais jukumu letu
kubwa ni kuhakikisha unakuwa salama.Wewe kwanza halafu
wengine watafuata” akasema
mmoja wa walinzi wake akiwa
amemshika mkono rais
“Hapana kwanza footb…….”
Kabla hajamaliza sentensi yake
ukatokea mlipuko wa baruti na
kuusambaratisha mlango wa
kuingilia mle chumbani mwa rais
na risasi zikaanza
kumiminwa.Walinzi wa rais nao
wakajibu mapigo kwa kumimina
risasi wakimkinga rais
asishambuliwe.
‘Seba run..!!! akapiga kelele
rais na kwa kasi ya aina yake
Sebastian akamshika mkono
Theresa akamvuta wakaingia
jikoni huku mlinzi wake mmoja akiwa nyuma yao.Sebastian
alifahamu vyema ndege hii ya rais
na mfumo wake wote wa
usalama.Pale jikoni kulikuwa na
mlango unaoingia chumba cha
stoo.Wakaingia na kulifunua zuria
katikati ya stoo kulikuwa na
mlango mdogo unaofunguliwa kwa
namba.Akabonyeza namba kadhaa
haraka haraka na mlango
ukafunguka.Kulikuwa na ngazi ya
kushuka chini.Akaingia na
kumshika mkono Theresa
wakaingia ndani na kushuka ngazi
kuelekea chini.Ghafla milio ya
risasi ikasikika mle stoo.
“The football !!!!..akapiga
kelele mmoja wa wale jamaa
aliyeingia stoo na kukuta mlango umefunguliwa na kuna ngazi za
kushuka chini.Wenzake watatu
wakaja na kuungana naye kisha
kwa haraka wakaanza kushuka
chini kuifuata ile ngazi
waliyotumia akina Sebastian
kushukia chini
Sebastian na mwanae Theresa
na mlinzi mmoja walifika katika
sehemu ya kufungulia mlango wa
dharura wa ndege ambao ni
maalum kwa ajili ya kumuokoa
rais.Wakiwa wanajadiliana ghafla
wakatokea wale jamaa na kuanza
kuwarushia risasi.Umahiri wa
Kanali Sebastian na mlinzi wake
katika silaha ulisaidia kiasi cha
kuwafanya wale jamaa wajifiche
na Sebastian akautumia mwanya huo kubonyeza sehemu ya
kufungulia mlango wa dharura
ukafunguka.Mara ghafla wale
jamaa wakaibuka wote watatu kwa
pamoja toka mahala walipokuwa
wamejificha na kuanza kumimina
risasi.Kanali Sebastian akamshika
mkono mwanae Theresa na
kuruka nje.Sebastian hakumuachia
Theresa katika upepo ule mkali na
giza nene,walishuka kwa kasi
kubwa na mara mwavuli aliokuwa
ameuvaa kanali Sebastian
mgongoni ukafunguka na
wakaanza kushuka chini taratibu.
Kumbukumbu ile ikamfanya
Theresa ahisi baridi ghafla na
woga mkubwa.Akatoka mle katika
ofisi akaenda kuzunguka zunguka ndegeni kuhakiki kwamba hakuna
mtu yeyote wa kumtilia shaka mle
ndani ya ndege.Kumbu kumbu ya
tukio lile lililotokea kwa miaka
kumi iliyopita ilimstua
mno.Alibadilishana mawazo na
walinzi wa rais halafu akaenda
kuketi kitini.Alihisi hali yake
kuanza kubadilika
“Miaka zaidi ya kumi imepita
sasa lakini bado naona kama tukio
lile limetokea jana.Bado ninakuwa
na woga mkubwa kila ninaposafiri
na rais.Mimi na baba ndiyo pekee
tulitoka salama katika ile ndege
kwani ilianguka karibu na wanja
wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro na wote waliokuwemo
ndani walifariki dunia.Kwa sasa ni mimi pekee niliyebaki hai ambaye
ninafahamu nini kilitokea usiku
ule.Ni tukio la kutisha sana ambalo
halitaweza kamwe kunitoka
kichwani mwangu.Siwezi
kulisahau giza lile nene kama vile
tuko jehanamu. Namshukuru sana
baba kwani alipambana kwa kila
alivyoweza hadi akafanikiwa
kuniokoa vinginevyo na mimi
ningekufa kwani hakuna yeyote
aliyekuwa ananijali zaidi yake”
akaendelea kuwaza
“Watu wale waliofanya lile
shambulio walikuwa na lengo la
kuipata football lakini baba kwa
umahiri alifanya kila awezalo na
kuhakikisha hawafanikiwi lengo
lao na football ikawa salama.Hii inaonyesha ni namna gani begi lile
lilivyokuwa na thamani kubwa
sana.Limebeba mambo mazito
.Hata rais mwenyewe alipotakiwa
awe wa kwanza kutoka mle
ndegeni alisema hawezi kutoka
yeye kabla football haijatoka
ndegeni.Wote waliipa football
uzito mkubwa sana.Kuna siri gani
ndani ya hiyo football?Liko wapi
lile begi?Nakumbuka tulipofika
chini tulitua katika msitu mmoja
uliokuwa karibu na makazi ya
watu.Sikumbuki ilikuwa saa ngapi
ila tulitembea hadi tulipoikuta
barabara kuu.Baba akaniambia
kwamba pale tulipo palikuwa ni
usa river.Tulilala pale na asubuhi
siku iliyofuata tulipanda basi hadi Dar es salaam.Baba alikuwa na lile
begi na baada ya hapo sikuwahi
kuliona tena.Sifahamu amelificha
wapi ila aliniachia mkufu huu
wenye msalaba wa dhahabu na
kunitaka niutunze na niuvae kwa
siku zote za maisha
yangu.Alinielekeza nimpatie
mkufu huu rais atakayekuwepo
madarakani baada ya miaka kumi
kupita toka ajali ile kutokea.Rais
aliyepo madarakani baada ya hiyo
miaka kumi kupita ni mwanae
Vivian.Alihisi kwamba mwanae
anaweza kuwa rais kwa kipindi
hiki? Hata hivyo nimeogopa
kumpatia dada Vivian huu mkufu
kwa kuhofia maisha yake.Naamini
mkufu huu una jambo kubwa na ndiyo maana akaniomba niutunze
na nije kumpa rais wa
sasa.Nimekuwa najiuliza maswali
mengi sana kuhusiana na mkufu
huu,je una muunganiko wowote na
football?Begi lile la football baba
alilificha wapi? Au alilirejesha
ikulu?Kila mara maswali haya
yamekuwa yanakifanya kichwa
changu kigonge kwani sijawahi
pata majibu yake.Baba ameniachia
mzigo mzito sana na sijui nitautua
vipi au nani nimtwishe? Akawaza
Theresa na kumbu kumbu
nyingine ikamjia.
NOVEMBER 2007 – DAR ES
SALAAM
Imekwisha pita miezi minne
toka ilipotokea ajali ya ndege ya
rais na kuua watu wote
waliokuwemo ndani yake
isipokuwa kanali Sebastian na
Theresa pekee.Kanali Sebastian
alipata wakati mgumu sana kwani
vyombo vya uchunguzi ambavyo
vilimuhoji sana kuhusiana na
kilichotoka katika ajali ile na
namna alivyoweza
kusalimika.Pamoja na kuhojiwa
sana lakini Kanali Sebastian
hakuwahi kuweka wazi kwamba
alinusurika yeye na Theresa.Mara
zote alisimama katika msimamo
wake mmoja kwamba aliyenusurika katika ajali ile
alikuwa ni yeye peke yake na
hakutaka kumuhusisha kabisa na
Theresa.Kama mtu pekee
aliyekuwa amelibeba begi la siri
maarfu kama football alihojiwa
mahala liliko begi hilo na
hakuwahi kueleza
ukweli.Alichokieleza na ambacho
hakikuwa kweli ni kwamba walinzi
wawili wa rais waliasi na kutaka
kumuua rais na kikatokea kizaa
zaa ndegeni na alipotaka kutoroka
na mkoba ule wa football ulipigwa
risasi na ili kuokoa maisha yake
akaamua kuachia na kuruka nje .
“Mpaka leo sielewi ni kwa nini
baba hakutaka kuweka wazi
kuhusiana na kile kilichotokea ndegeni na kuhusu ile
football.Hajawahi mweleza mtu
yeyote mahala alikoificha.Kwa nini
aliamua kuificha badala ya
kuirejesha serikalini wakati akijua
kabisa kwamba kuna siri za
serikali mle ndani? Kwa nini afiche
siri za nchi? akajiuliza Theresa
“Ninajiuliza maswali haya
lakini siwezi kuyapatia majibu.Mtu
pekee ambaye angeweza kuwa na
majibu sahihi ni baba lakini
hayupo.Hapo ndipo huwa
ninachoka na kuamua kuliacha
suala hili kama lilivyo na
kuendelea kuibeba siri hii hadi
siku nitakapoingia kaburini japo
naamini baba alikuwa namakusudi yake kufanya vile
alivyofanya” akawaza
“Lakini ni kweli niko tayari
kuendelea kuibeba siri hii hadi
kaburini? Nimekuwa najiuliza
swali hili mara kadhaa lakini kila
ninapomuangalia dada najikuta
sina namna ya kufanya zaidi ya
kuendelea kuibeba japo baba
alinitaka nimpatie rais wa sasa
mkufu huu.Sina hakika kama alijua
mwanae ndiye atakayekuwa rais
wa Tanzania baada ya kipindi cha
miaka kumi.Hapana sintamueleza
Vivian kwani kufanya hivyo ni
kumuweka hatarini.Baba alitolewa
uhai wake kwa sababu ya jambo
hili na hata mimi nilinusurika
kuuawa kwa sababu kwanza nilikuwa mwanafunzi na pili baba
hakuwahi kuweka wazi kwamba
nilikuwemo katika ndege ile ya
rais.Kama ningejulikana lazima
ningeuawa pia” akaendelea
kuwaza Theresa na machozi
yakamtoka akawahi kuyafuta ili
mtu yeyote asigundue kwamba
alikuwa katika mawazo mazito
“Masikini familia yangu
waliuawa kikatili mno na
nilishuhudia kila kitu.Mpaka leo
bado picha za mauaji yale zinanijia
usingizini.Bado namuona baba
akianguka na kufa huku
akimiminiwa risasi kama
mnyama”
Theresa akashindwa kuyazuia
machozi yasimtoke.Kumbu kumbu ya namna walivyouawa wazazi
wake ilipomjia.
April Hudson Mubara mjane
wa rais Anorld Mubara alirejea
nchini akitokea Marekani
alikoenda mapumzikoni baada ya
kifo cha mume wake.Moja kwa
moja alienda kuishi katika shamba
lao lililokuwepo katika kijiji cha
mchangawima Chalinze.Alitaka
apumzike sehemu yenye utulivu
mkubwa.Baada ya kufahamu
kwamba amerejea nchini Kanali
Sebastian alimpigia simu na
kumtaarifu kwamba atakwenda
kuonana naye kumpa pole kwani
toka yalipofanyika mazishi ya rais
Anorld hawakuwahi kuonana
tena.Bi April alikubali kuonana na Kanali Sebastian kwani alikuwa
mtu wa karibu sana na mumewe
na wakapanga siku ya
kuonana.Siku ilipofika Kanali
Sebastian akaichukua familia yake
yote ili kwenda kumpa pole Bi
April kwa kifo cha mume wake.
Wakiwa wameikamata
barabara inayoelekea katika
shamba la rais Anorld,mara kwa
mbele wakakuta kizuizi cha askari
na magari mawili ya askari
yameegeshwa pembeni.Ni eneo
lililokuwa kimya sana na
hakukuwa na watu eneo hili na
mahala polisi walipoweka kizuizi
chao kulikuwa na vichaka vichaka.
“Hawa askari wanafanya nini
huku? Mbona wameweka kizuizi kwani kuna magari yanakuja huku
zaidi ya machache yanayokwenda
katika shamba la rais Anorld?
Akauliza mke wa kanali
Sebastian.Alionyesha wasiwasi
“Barabara hii inakwenda
katika shamba la rais.Inawezekena
wanaimarisha ulinzi ili kuzuia
watu wasiotambulika kwenda
katika nyumba ya rais wakati huu
ambao bi April yupo huku kwa
mapumziko” akasema kanali
Sebastian
“Hata kama ni ulinzi kwa nini
wasilinde askari wachache?Mbona
hawa wako zaidi ya kumi?
Akauliza mke wa Sebastian na
askari mmoja akasimama kati kati
ya barabara akanyoosha mkono akamtaka kanali Sebastian
asimamishe gari.Taratibu
akapunguza mwendo na
kusimamisha gari pembeni ya
barabara kama
alivyotakiwa.Akafungua mlango na
kushuka ili ajitambulishe kwa
askari wale na wamruhusu apite
lakini alipopiga hatua kama tatu
kuwaendea,ghafla ikasikika milio
ya risasi.Kanali Sebastian
akaanguka chini.Ndani ya gari mke
wake, ,mwanae Kelvin na Theresa
walipatwa na mshangao mkubwa
sana kwa kitendo kile.Haraka
haraka Kelvin akashuka garini ili
kumkimbilia baba yake
aliyeanguka pale chini lakini
alipotaka kumuinamia baba yake naye akachezea mvua ya risasi na
kuanguka karibu na baba yake
“Theresa hawa si
polisi.Tafadhali fanya
nitakavyokuelekeza.Jifiche chini ya
kiti na usiinue kichwa hadi
nitakapokuelekeza.Ninataka
kulirudisha nyuma gari hili ili
tujaribu kujiokoa vinginevyo
watatuua” Akasema mke wa kanali
Matope na kukaa sehemu ya
dereva akaukamata usukani na
kuweka gia ya kurudi nyuma kisha
akakanyaga pedeli ya mafuta na
kwa kasi ya aina yake gari likaanza
kurudi nyuma.Askari kama
watano wakaanza kulikimbiza lile
gari huku wakirusha risasi lakini
kwa ujasiri mkubwa Getruda Matope mke wa kanali Sebastian
matope akafanikiwa kulirudisha
gari nyuma na kupata sehemu ya
kugeuza na kisha akaliondoa kwa
kazi kubwa.Theresa aliyekuwa
amejificha chini ya kiti cha nyuma
akainua kichwa baada ya kusikia
mama yake anakoroma.
“Mama” akaita Theresa na
kugundua kwamba mama yake
alikuwa anatokwa na damu
mdomoni.Alikuwa amepigwa risasi
tumboni.Ghafla akakanyaga breki
kwa nguvu na gari likaserereka
hadi katika shamba la
mpunga.Getruda alikuwa anavuta
pumzi kwa taabu sana na damu
ikimtoka mdomoni “mama !! akaita Theresa huku
akilia
“Theresa…r..un..ruuuuun..!!
“Hapana mama.Siwezi
kukuacha hapa peke yako !!
akasema Theresa
“Run..Thr..ru…rr…runnnnn!!
akasema Getruda kwa taabu na
kuvuta pumzi ndefu akaangukia
usukani.Theresa akaliona vumbi
kubwa nyuma yao linakuja kwa
kasi akajua ni zile gari mbili za
askari akafungua mlango na
kushuka akaanza kukimbia
akikatisha katika shamba la
mpunga.Alihisi miguu yake haina
nguvu lakini akajitahidi kwa kadiri
alivyoweza hadi alipolipita shamba la mpunga na kuingia katika
shamba la michungwa.
Akaweka mikono masikioni
mwake na kuhisi kutetemeka
mwili
“Bado nasikia milio ie ya risasi
masikioni mwangu hadi leo
hii.Kwa mara ya pili nilinusurika
kuuawa.Bila ujasiri wa mama na
mimi hivi sasa ningekuwa mfu”
akawaza na kufuta machozi
“Nahisi baba alitabiri kifo
chake kwani wiki moja tu kabla ya
kifo chake ndipo aliponipa huu
mkufu wenye msalaba.Aliamini
hataweza kufika wakati huu na
ndiyo maana akanibebesha mimi
siri kubwa iliyo katika msalaba
huu na laiti kama ningejulikana basi ningekwisha
uawa.Nitaendelea kuubeba huu
msalaba hadi siku naingia
kaburini.Nitakapofungua tu
mdomo wangu na kuropoka
chochote ndio utakua mwisho
wangu,sintabaki salama”
akaendelea kuwaza Theresa na
kuinuka akaelekea bafuni akalia
machozi mengi sana halafu
akanawa uso na kujipaka poda
upya usoni ili asitambulike kama
alikuwa analia.Akavaa miwani
myeusi kuficha macho yake na
kurejea kukaa akaendelea na kazi
zake huku dege likiendelea
kuchana anga kuelekea New york
Marekani.
OFISI ZA USALAMA WA TAIFA
– DAR ES SALAAM
Shughuli ziliendelea kama
kawaida katika jengo hili la ofisi za
usalama wa taifa.Baada ya kurejea
toka uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere
kumuaga rais,mkurugenzi wa
idara ya usalama wa taifa George
Mzabwa akahudhuria vikao viwili
vya kazi halafu akaenda kujifungia
ofisini kwake.Alijiegemeza kitini
na kuzama mawazoni.Aliwaza sana
na halafu akachukua karatasi
akaanza kuandika.Alipomaliza
akasoma kile alichokiandika
akaridhika na kuiweka karatasi ile katika bahasha na juu ya bahasha
ile akaandika
TO MADAM PRESIDENT.Akaiweka
mezani barua ile halafu akafunga
mlango kwa funguo na kusimama
kati kati ya ofisi.Akaitazama ofisi
yake ,akatoa bastora na kuitazama
kwa uchungu
Wafanyakazi wa ofisi hii ya
usalama wa taifa wakiwa
wanaendelea na shughuli zao za
kawaida walistushwa na mlio wa
risasi.Shughuli zikasimama ghafla
na wote wakijiuliza nini
kimetokea.Tahadhari zikaanza
kuchukuliwa haraka kubaini risasi
ile imelia toka wapi ndani ya jengo
lile.Wakati wakijiuliza huku kila
mmoja akiwa katika tahadhari kubwa na ulinzi ukiwa
umeimarishwa katika sehemu zote
za kuingilia na kutokea,Stella
katibu muhtasi wa George Mzabwa
alishuka ngazi huku akikimbia na
kupiga kelele.Akatoa taarifa
kwamba amesikia mlio wa risasi
katika ofisi ya George.Haraka
haraka watu wakakimbilia ofisini
kwa George na kujaribu kugonga
mlango lakini hakukuwa na mtu
yeyote aliyeitikia toka
ndani,wakapiga simu ya George
ikaita bila kupokelewa hivyo
ikawalazimu kuuvunja mlango na
kuingia ndani wakamkuta George
Mzabwa amelala sakafuni damu
ikimvuja na pembeni yake
kulikuwa na bastora.Hakuwa na uhai na ubongo wake
ulisambaa.Alikuwa amejipiga
risasi kichwani.Uchunguzi
ukafanyika ili kuona kama
shambulio lile lilifanywa na mtu
kutokea nje lakini hakukuwa na
dalili zozote za kuonyesha kama
George alishambuliwa kutokea
nje.Hili lilikuwa ni tukio
lililomshangaza kila
mmoja.Hakuna aliyefahamu
sababu ya George kujiua kwani
muda mfupi uliopita alikuwa na
uso wenye furaha kabisa na
hakuonyesha kama ana tatizo
lolote.Juu ya meza yake kulikutwa
barua aliyomuandikia rais muda
mfupi kabla ya kifo chake. Polisi walitaarifiwa wakafika
kwa haraka na baada ya
kujiridhisha kwamba George
alijiua mwenyewe wakaondoka na
mwili wake kuupeleka hospitali
kwa ajili ya kuuhifadhi na taratibu
nyingine kabla ya kuukabidhi kwa
familia yake
************
Dr Vivian akiwa
amejipumzika katika chumba
chake huku dege likiendelea
kupasua anga kuelekea
Marekani,simu iliyomo mle
chumbani inayotumia mtandao wa
intanet ikaita.Akainua mkono wa
simu na kuipokea “Hallow” akasema Dr Vivian
“Madam president pole na
safari ni mimi Dr Makame”
akasema makamu wa rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania
“Ahsante Dr Makame.Sisi tuko
angani tunaendelea na
safari.Mnaendeleaje huko?
“Habari za huku si njema
sana.Kuna tukio limetokea ambalo
nimeona ni vyema nikikujulisha
mapema”
“Nini kimetokea Dr makame?
“George Mzabwa mkurugenzi
wa idara ya usalama wa taifa
amefariki dunia”
“George amefariki dunia?!! Dr
Vivian akastuka “Ndiyo mheshimiwa
rais.Nimeletewa taarifa hizo na
nimezithibtisha kupitia inspekta
generali wa polisi” akasema Dr
makame na rais akavuta pumzi
ndefu
“Amefariki vipi?Amepata
ajali?
“Amejipiga risasi kichwani
mheshimiwa rais”
Uso wa Dr Vivian ulionyesha
mstuko mkubwa.Hakuwa
ametarajia kusikia habari kama ile
“Madam president” akaita
makamu wa rais baada ya kuona
kumekuwa kimya.
“Nimestushwa sana na taarifa
hizi.Imekuaje hadi George
akachukua maamuzi hayo magumu ya kujiua?akauliza Dr
Vivian
“Hilo ni jambo
linalomshangaza kila
mmoja.Hakuna aliyetegemea kama
angeweza kuchukua maamuzi
kama haya ya kujiua.Tulikuwa
wote uwanja wa ndege asubuhi
tukasalimiana na alikuwa vizuri
tu,hakuonyesha tatizo
lolote.Hatujui nini kilimsibu hadi
akachukua mamauzi haya,hata
hivyo kuna barua imekutwa
mezani kwake ambayo
amekuandikia wewe.Tunadhani
aliiandika muda mfupi kabla
hajajiua” “Ameniandikia barua? Kuna
yeyote ameifungua na kuisoma?
Akauliza Dr Vivian
“Hapana madam president
hakuna aliyeifungua.Imefungwa
ndani ya bahasha”
“Good.Ihifadhi hadi
nitakaporejea”
“Sawa madam president”
“Jambo lingine,nataka
ufanyike uchunguzi kwa mara
nyingine wa kina kujiridhisha
kama kweli George Mzabwa
amejiua au kuna watu
waliomuua.Inashangaza sana kwa
mtu kama George kuchukua
maamuzi haya magumu”
“Sawa madam president
nitaelekeza hivyo.Nawatakieni
safari njema”
“Ahsante sana Dr Makame
kwa taarifa.Hakikisha uchunguzi
huo unafanyika haraka.Kuanzia
nyumbani kwake,ofisini kote
kupekuliwe ili sababu ya George
kujiua ijulikane” akasema Dr
Vivian na kukata simu
“George amejiua …” akasema
na kuzidi kushangaa
“Lakini kwa nini afanye hivi?
Kwa nini ajiue?Kwa nini iwe sasa?
Kuna kitu gani kimemkwaza
?akaendelea kujiuliza maswali
“Jambo hili linahitaji
uchunguzi wa kina kubaini sababu
ya kujiua.Nitaisoma hiyo barua aliyoniandikia kujua alichokisema
lakini nimestuka
sana,sikutegemea kama anaweza
akafanya jambo kama hili”
akawaza Dr Vivian
“Au yale maneno
niliyomwambia asubuhi pale
uwanja wa ndege yamemkwaza?
Nilimtaka nitakaporejea nikute
ripoti ya uchunguzi au nikute
barua yake ya kuachia nafasi
yake.Yawezekana amefikiria sana
na akaamua kujiua.Apumzike kwa
amani huko aliko kwani hata hivyo
alikuwa katika orodha ya viongozi
ambao utendaji wao wa kazi
haujaniridhisha.Nitatafuta mtu
mahiri na mchapakazi
atakayechukua nafasi yake na atakayekuwa tayari kufanya kazi
kwa kasi ninayoitaka.Kipimo cha
mtendaji ninayemtaka ni kutegua
kitendawili cha vifo vya wazazi
wangu.Haiwezekani mpaka leo hii
yapata miaka kumi suala hili
limeshindwa kupata
majibu.Limekuwa ni fumbo
lililoshindwa kufumbuliwa.Tuna
vyombo mahiri kabisa kwa
uchunguzi lakini kwa nini
wameshindwa kubaini nani
aliteketeza familia yangu?Halafu
kuna hili begi ambalo baba
alikuwa analibeba enzi za utawala
wa rais Anorld liko wapi? Lilipotea
rais Anorld alipofariki katika
ajali?Nahisi hivyo kwani hata rais
aliyefuata baada ya Anorld hakuwahi kuwa na lile begi ambalo
rais Anorld alikuwa anatembea
nalo kila aendako.Mfumo ule
uliigwa toka marekani ambao wao
ndani ya begi hilo wanaloliita
football kuna nuclea codes lakini
sisa hatuna nyuklia je kwa nini rais
Anold alikuwa anatembea na begi
lile kila aendako?Siri gani alikuwa
anatembea nayo?Swali lingine
ambalo bado mpaka leo sijapata
majibu yake ni je baba aliokoka
vipi toka katika ndege ile ya
rais?Maelezo aliyotoa baba
hayajawahi kuniingia akilini.Bado
naamini kuna vitu vinakosekana
katika maelezo yake aliyoyatoa
kwa vyombo vya uchunguzi baada
ya ajali.Kwa bahati mbaya nyumba yake iliungua moto muda mfupi
baada ya kufariki kwahiyo hakuna
mahala kokote tunakoweza kupata
taarifa zake zozote.Laiti
kungekuwa na nyaraka zake
zozote tungeweza kuzichambua na
kugundua kama kuna jambo
alikuwa analificha.Hili jambo kweli
ni fumbo gumu na ili kulifumbua
ninahitaji mtu jasiri na mahiri
ambaye anaweza kulishughulikia
jambo hili na kulipatia majibu.Kwa
miaka takribani miwili sasa tangu
nilipompa George alishughulikie
jambo hili hakuna majibu yoyote
na badala yake leo amejipiga risasi
na kufa.Ukiacha hii miaka miwili
niliyompa George,vyombo vya
uchunguzi vimelichunguza jambo hili kwa miaka zaidi ya kumi sasa
na mpaka leo hakuna majibu
yoyote.Kuna nini hapa?Hii
inanifanya nizidi kuamini kwamba
kuna kitu kimejificha katika jambo
hili na sintachoka hadi nihakikishe
nimeufahamu ukweli na wahusika
wanakamatwa na kufikishwa
mbele ya sheria” akawaza Dr
Vivian na kutoka mle chumbani
akamuita Edwin Swai mmoja kati
ya washauri watatu wa mambo ya
usalama wakaenda katika chumba
cha mazungumzo ya faragha
“Edwin kuna taarifa
nimeipokea muda mfupi uliopita
toka Dar es salaam ambayo si
nzuri.George Mzabwa amefariki
dunia” akasema Dr Vivian “George amefariki dunia?Nini
kimemuua?Amepata ajali?Akauliza
Edwin naye akishangazwa na
taarifa zile
“Hajapata ajali amejiua kwa
kujipiga risasi”
“Amejipiga risasi?
“Ndiyo amejipiga risasi ofisini
kwake”
“Oh my God !! akasema Edwin
kwa masikitiko
“Inasikitisha lakini pia
inashangaza sana kwa maamuzi
haya aliyoamua kuyachukua
George.Mungu ampumzishe kwa
amani” akasema rais
“Amen” akajibu Edwin .
“Kufuatia tukio hilo nahitaji
kuiziba nafasi ya George hivyo nahitaji kumpata mtu mahiri sana
ambaye anaweza kuiongoza idara
ya usalama wa taifa kwa umahiri
mkubwa.Utendaji wa George
haukuwa umeniridhisha hata
kidogo na hata hivyo nilikuwa
katika mipango ya
kumuondoa.Wewe umekuwa
katika mambo haya ya usalama
kwa muda mrefu hivyo naamini
unawafahamu watu wengi wazuri
na wanafaa kuongoza idara ya
usalama wa taifa,ninakuomba
upendekeze watu watatu
unaowaamini na mimi nitachagua
mmoja” akasema Dr Vivian
Edwin akafikiri kwa muda
kisha akasema “Sawa madam president
nitajitahidi kulifanyia kazi hilo
jambo kuanzia sasa na hadi
tutakaporejea Dar es salaam
nitakukabidhi mafaili ya watu
watatu nitakaowapendekeza kwa
ajili ya kuziba nafasi ya George
Mzabwa” akasema Edwin
“Nitashukuru sana.Zingatia
sihitaji tu mtu wa kuziba nafasi
bali nahitaji mtu ambaye
anafahamu nini anakifanya na
anayeweza kufanya kazi zake kwa
umahiri mkubwa sana.Idara ya
usalama wa taifa ni idara nyeti
kwa nchi hivyo hatuwezi kuiweka
kwa mtu kwa kuwa ni rafiki yetu
bali anatakiwa mtu mwenye uwezo wa kuiongoza kwa weledi
mkubwa” akasema Dr Vivian
“Nitalizingatia hilo
mheshimiwa rais katika
mapendekezo yangu
nitakayokupa” akasema Edwin
“Good.Jambo la pili nahitaji
kupata mpelelezi mahiri sana kuna
kazi nyeti nataka anisaidie
kuifanya.Naamini unaweza
ukamfahamu mpelelezi yoyote
mahiri sana hivyo nisaidie niweze
kumpata” akasema Dr Vivian
“Madam president tunao
wapelelezi wengi mahiri hapa
nchini.Wapo waliobobea katika
chunguzi za ndani,wapo wabobezi
katika chunguzi za kimataifa,tunao
wa kila aina.Sijui unahitaji mpelelezi mwenye sifa zipi?
Akauliza Edwin
“Edwin itakuwa vyema kama
nikikuweka wazi kuhusu jambo
ninalotaka kulichunguza.Nataka
kuchunguza na kuupata ukweli
kuhusiana na mauaji ya familia
yangu.Nadhani unafahamu kama
familia yangu iliuawa kwa siku
moja na na mpaka leo hii imepita
miaka zaidi ya kumi hakujawahi
kutolewa ripoti yoyote ya
uchunguzi na wala hakuna
aliyewahi kukamatwa kuhusiana
na mauaji yale.Jambo hili limebaki
kuwa kama fumbo gumu
kulifumbua.Jeshi la polisi,usalama
wa taifa wote wamelichunguza
jambo hili na mpaka leo hakuna ripoti yoyote.Nahitaji mtu wa
kuweza kulifumbua fumbo hili.Mtu
ambaye anaweza kutafuna mfupa
huu uliowashinda wengi.Hata
kama ni mtu wa kutoka nje niko
tayari kumlipa kiasi chochote cha
fedha ili mradi uwe na uhakika
kwamba ana uwezo wa kulifumbua
fumbo hili.Sitaki kuamini eti suala
hili limeshindwa kupatiwa
ufumbuzi hadi leo kama Marekani
walivyoshidwa hadi leo hii kupata
ufumbuzi kuhusiana na mauaji ya
wanamuziki Tupac na Christopher
Wallace.Bado nina matumaini
makubwa kwamba endapo
utafanyika uchunguzi wa kina
walioufanya mauaji haya lazima
watapatikana.Hayakuwa mauaji ya bahati mbaya waliotekeleza
mauaji yale walikuwa na sababu
zao na ninataka kufahamu hiyo
sababu ndiyo maana nahitaji mtu
mahiri sana ambaye nitampa kila
nyenzo atakayohitaji ili aweze
kufanikisha uchunguzi huu”
Akasema Dr Vivian.Edwin Swai
akakuna kichwa kidogo na kusema
“Mheshimiwa rais
nakubaliana nawe kwamba hili
suala la kifo cha kanali Sebastian
ni gumu na kama ulivyosema
uchunguzi wake umechukua zaidi
ya miaka kumi.Nadhani huu ni
uchunguzi uliokuwa mrefu zaidi
kuwahi kufanyika hapa nchini na
kama kwa muda huo wote
hawajapata wahusika basi ni wazi hawataweza kufanikiwa
kuwapata.Wazo la kumtafuta
mpelelezi ambaye ataweza
kulifumbua fumbo hili ni wazo zuri
na hata mimi nakubaliana nalo
lakini..” akasita kidogo
“Mbona umesita Edwin?
Akauliza akauliza Dr Vivian
“Kwa uchunguzi mkubwa
kama huu anahitaji mtu mwenye
umahiri wa pekee.Kwa wale
ninaowafahamu mimi sina uhakika
kama kuna mmoja wao anaweza
kuwa na sifa ya kulichunguza suala
hili.Kuna mtu mmoja ambaye yeye
anaweza kukusaidia katika jambo
hili.Anaitwa Meshack Jumbo.Huyu
mzee aliwahi kuiongoza idara ya
ujasusi wa kimataifa kwa miaka mingi na kwa ufanisi
mkubwa.Huyu nina imani anaweza
kukutafutia mtu sahihi
atakayekufaa” akasema Edwin
“Anapatikana wapi huyo
Meshack Jumbo?
“Anaishi Dr es
salaam.Amekwisha staafu kazi na
kwa sasa anapumzika
anajishughulisha na shughuli zake
ndogo ndogo.Ninaweza
kumuandaa ili mkutane muongee
tutakaporejea Dar es salaam”
Dr Vivian akafikiri kidogo na
kusema
“Sawa nahitaji kuonana
naye.Usimweleze chochote
kuhusiana na haya niliyokwambia.Nitamwambia mimi
mwenyewe”
“Sawa madam president”
akasema Edwin na kutoka mle
katika kile chumba.Rais
akazunguka zunguka ndegeni
kuzungumza na watu alioongozana
nao na mara akamuona Theresa
na kustuka kidogo
Sawa madam president”
akasema Edwin na kutoka mle
katika kile chumba.Rais
akazunguka zunguka ndegeni
kuzungumza na watu alioongozana
nao na mara akamuona Theresa
na kustuka kidogo
“Kuna tatizo Theresa,mbona
umejitenga huku peke
yako?akauliza
“Hapana dada Vivian.Sina
tatizo lolote ni uchovu tu” akajibu
Dr Vivian akaketi katika kiti cha
pembeni yake
“Nakufahamu vizuri
Theresa,kama kuna jambo
linakusumbua au limekukwaza huwa unapenda kujitenga na
kukaa peke yako.Niambie tafadhali
kama kuna tatizo lolote.Au
umekwazika na yale maneno
nilikwambia kuhusiana na ile
hotuba? Akauliza Dr Vivian
“Dada Vivi sina tatizo
lolote.Nimeamua nikae hapa
nitafakari mambo yangu .Kama
ningekuwa na tatizo ningekwisha
kueleza” akasema Theresa
“Bado tuna safari ya saa
kadhaa jitahidi basi upate nafasi ya
kutosha ya kupumzika.Tukifika
New York nitakuwa na mambo
mengi ya kufanya kwa hiyo nafasi
ya kupumzika ni finyu sana”
akasema Dr Vivian huku akiinuka na mara akakumbuka kitu na
kukaa
“Nimepewa taarifa na
makamu wa rais muda mfupi
uliopita George Mzabwa amefariki
dunia”
“George amefariki?! Theresa
akastuka
“Ndiyo kafariki.Amejipiga
risasi ofisini kwake”
Theresa akamtazama dada
yake kwa mshangao
“Kwa nini amefanya hivyo?
Kwa nini kachukua maamuzi hayo
ya kujitoa uhai? Akauliza
“Hakuna anayejua kwa nini
amechukua maamuzi
haya.Nimeagiza uchunguzi wa kina
ufanyike kubaini sababu ya yeye kujiua.Kwa upande mwingine
nahisi labda yale maneno
niliyomwambia pale uwanja wa
ndege wakati naondoka
yalimkwaza na akaamua kujiua
kwani nimeambiwa kuna barua
ameniandikia.Nahisi ndani ya
barua hiyo atakuwa ameeleza
sababu ya kuchukua maamuzi ya
kujiua” akasema Dr Vivian
akanyamaza kidogo na kusema
“Mkurugenzi wa idara ya
usalama wa taifa ni mtu mkubwa
na mpaka achukue maamuzi ya
kujiua lazima ipo sababu kubwa na
nzito.Hata hivyo tusubiri
uchunguzi ufanyike na tutafahamu
kwa nini alichukua maamuzi
yale.Jambo lingine nimeamua kumtafuta mpelelezi mwenye
uwezo mkubwa wa kulichunguza
suala la vifo vya familia
yetu.Lazima tuwapate wale
walioiteketeza familia yetu.Bado
sijakata tamaa na siwezi kuamini
eti jambo hili
limeshindikana.Nimeamua
kulivalia njuga mimi mwenyewe
hili jambo na nitahakikisha jambo
hili linafika mwisho.Nitakaporejea
Dar es salaam nitaonana na mtu
ambaye atanisaidia kumpata mtu
mpelelezi mahiri wa kuifanya kazi
hii” akasema Dr Vivian na kurejea
chumbani kwake
“Hili suala linazidi kuchukua
sura mpya na kuzidi
kuniogopesha.George Mzabwa kujitoa uhai si kwa bahati
mbaya.Kuna sababu kubwa.Hisia
za dada zinaweza kuwa kweli
kwamba yale maneno
aliyomueleza asubuhi wakati
anaondoka yamechangia kwa yeye
kujitoa uhai lakini kama suala la
kifo cha baba limesababisha ajitoe
uhai basi suala hili lina siri kubwa
ndani yake.Yawezekana labda
kuna kitu alikigundua na ambacho
hawezi kukiweka wazi na ndiyo
maana akachukua maamuzi ya
kujiua.Unapozungumzia kifo cha
baba unazungumzia pia football
lile begi alilokuwa analibeba na
ambalo mpaka leo hii hakuna
anayefahamu liko
wapi.Nilichonacho hapa ni huu msalaba pekee ambao alinitaka
nisiutoe shingoni mwangu hadi
nitakapomkabidhi rais wa wakati
huu na hakunipa maelezo yoyote
ya kina.Mwili
unanitetemeka,natamani
nimueleze dada Vivian ukweli
lakini naogopa” akawaza Theresa
“Ni mpelelezi gani huyo
anayeweza kulifumbua fumbo hili
lililowashidna hata idara ya
usalama wa taifa? Natamani
nimuone na nina imani hata yeye
mwenyewe hatafika popote
ataishia njiani.Mimi sintafumbua
mdomo wangu na nitaendela
kukaa na siri hii .Sitaki
kuhatarisha uhai wangu na wa
dada yangu Vivian.” Akaendelea kuwaza Theresa huku dege
likiendelea kupasua anga
NEW YORK - MAREKANI
Saa moja za jioni kwa saa za
Marekani ambayo ni saa tisa za
usiku kwa saa za Afrika
mashariki,dege la rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania liligusa
ardhi ya jiji la New york
Marekani.Dr Vivian na ujumbe
wake walipokewa kwa mujibu wa
itifaki na kupelekwa katika hoteli
waliyopangiwa kufikia ambako
rais na ujumbe wake wote
walifikia.Rais hakutaka hata
mmoja aliyeongozana naye
akafikie sehemu nyingine.Baada ya kuoga na kupumzika rais na
ujumbe wake wakapata chakula
cha usiku na kisha akawa na
mazungumzo na balozi wa
Tanzania nchini Marekani.Balozi
alimtaarifu rais kwamba wale
watu aliomtaarifu kwamba
walihitaji kuonana na kuzungumza
naye kuhusiana na mambo kadhaa
ya uwekezaji nchini Tanzania
watakuja usiku ule kuonana
naye.Rais hakuwa na kipingamizi
hivyo akakubali kuonana na hao
wawekezaji.
Wakati rais na balozi wa
Tanzania nchini marekani
wakiendelea na mazungumzo
wakafahamishwa kwamba kuna
watu wanne walikuwa wamefika kwa ajili ya kuuonana na
rais.Balozi akamtaarifu rais
kwamba watu aliokuwa
amemweleza wamefika na rais
akawakaribisha.Ulikuwa ni
ujumbe wa watu wanne.Kiongozi
wa ujumbe ule alijitambulisha
kama Jing wang halafu
akawatambulisha na wenzake
alioambatana nao ambao ni Ling
Huang,Peng Li na wote hawa
walitoka nchini China.Mwisho
akamtambulisha Kim Yung Su
mjumbe maalum wa rais wa Korea
Kaskazini .
Dr Vivian akatabasamu baada
ya Jing wang kufanya utambulisho
ule ingawa kwa ndani alistuka sana kusikia katika ujumbe ule
kuna mtu anatoka Korea kaskazini
“Karibu sana Jing wang na
ujumbe wako.Nafurahi kuonana
nanyi” akasema Dr Vivian
“Hata sisi tunafurahi kuonana
kuonana nawe mheshimiwa
rais.Kwa kuwa umechoka kwa
safari ndefu tutajitahidi
mazungumzo yetu yawe mafupi”
akasema Jing na kunyamaza baada
ya mlinzi kuingia mle ndani na
kumnong’oneza rais kitu
“Mr Nathan amewasili yuko
mapokezi” akasema yule mlinzi
kwa kunong’ona
“Apelekwe chumbani nina
mazungumzo na wageni wangu
sasa hivi” akasema rais na yule mlinzi akatoka na rais akamtaka
Jing aendelee
“mheshimiwa rais
,utatusamehe kwa kuingilia ratiba
yako kwa ujio huu usio rasmi
lakini kutokana na umuhimu wake
imetulazimu kumuomba balozi
wako atusaidie tuweze kuonana
nawe kwani tunafahamu utakuwa
na majukumu mengi hapa New
York na tusingeweza kupata nafasi
ya kuonana na
kuzungumza.Tunashukuru sana
kwa kukubali kuonana
nasi.Mheshimiwa rais sisi ni
wawakilishi wa wafanya biashara
wakubwa wenye makampuni
makubwa toka China.Nadhani
dunia nzima inafahamu juu ya urafiki wa China na Tanzania
lakini kwa usiku huu hatukuja
kuzungumzia juu ya China na
Tanzania bali tumemsindikiza
mwenzetu huyu ambaye ni mmoja
wa wajumbe wa kutoka Korea
Kaskazini wanaohudhuria
mkutano wa umoja wa mataifa
lakini yeye amekuja na salamu
maalum kutoka kwa rais wa Korea
Kaskazini.Tumeongozana naye
kwa sababu isingekuwa rahisi yeye
kuja kuonana nawe moja kwa moja
hata hivyo naomba niseme
machache .Nchi ya Korea Kaskazini
iko katika mageuzi makubwa ya
kiuchumi kwa sasa kwa hiyo
wanatafuta mashirikiano ya
kibiashara na mataifa mbali mbali na wanaelekeza nguvu kutafuta
masoko ya bidhaa zao,kununua
malighafi na kuwekeza barani
Afrika.Kutokana na Korea
kaskazini kufahamika sana katika
harakati zake za kijeshi nchi nyingi
zinasita au kutotaka kuwa na
mashirikiano yoyote na Korea
kaskazini hivyo kutulazimu China
kuwasaidia wenzetu
kuwaunganisha na marafiki zetu
mbali mbali duniani.Tanzania kwa
sasa inafanya mageuzi makubwa
ya kiuchumi na kwa kuwa ina sera
nzuri za kuvutia wawekezaji
,wafanya biashara kutoka Korea
kaskazini wamependa sana kuwa
na mashirikiano ya kibiashara na
Tanzania lakini nchi hizi hazina mashirikiano ya kibiashara kwa
sasa hivyo panahitajika sehemu ya
kuanzia na kikao hiki ni sehemu ya
kuanzia.Kwa hiyo mheshimiwa
rais naomba nisiwe msemaji mkuu
wa kikao hiki na nimuachie Kim
Yung Su ana mengi atakueleza
alichotumwa na kiongozi wake”
akasema Jing Wang
“Karibu sana Kim” akasema
Dr Vivian.
“Ahsante sana mheshimiwa
rais.Kama alivyosema Jing Wang
ninatokea Korea Kaskazini na
nimetumwa salamu maalum toka
kwa rais wetu.Kwanza anakupa
pongezi nyingi kwa mafanikio
makubwa ambayo Tanzania
imeyapata kwa muda mfupi uliokaa madarakani.Umeonyesha
dira na mfano kwa viongozi wengi
duniani.
Korea Kaskazini inajulikana
sana duniani kote kwa harakati
zake za kijeshi hasa msuguano kati
yake na Marekani unaotokana na
majaribio ya silaha kali.Msuguano
huu umesababisha lakini nchi
nyingi zisitake kuwa na
mashirikiano ya kibiashara kwa
kuogopa vikwazo toka nchi kubwa
zenye nguvu na tajiri
duniani.China imekuwa ni
mshirika mkubwa wa kibiashara
wa Korea Kaskazini.Zipo pia nchi
nyingine zinazofanya biashara na
sisi kama vile Russia.Kwa upande
wa Afrika kuna Burkina faso n.k.Kwa sasa nchi yetu iko katika
mageuzi makubwa ya
kiuchumi.Tunataka kuukuza
uchumi wetu uwe imara na ili
kufanikisha hilo imetulazimu
kubadili sera zetu za
uchumi.Tumeanza kukaribisha
wawekezaji toka nje jambo ambalo
halikuwepo hapo kabla.Kama
haitoshi wafanya biashara wetu
sasa wanaruhusiwa kutoka na
kwenda kufanya uwekezaji katika
nchi nyingine pia.Tumeona fursa
kubwa ya kuimarisha
mashirikiano zaidi na Tanzania
kwani tumegundua kuna fursa
nyingi za kuwekeza na nchi zote
mbili zikafaidika.Wafanya
biashara wa Korea Kaskazini wako tayari kuwekeza nchini Tanzania
katika viwanda vya nguo
vitakavyotumia pamba ya
wakulima wa Tanzania na hivyo
kuachana na kuagiza guo
zilizotumika toka Marekani na
mataifa ya ulaya.Hivi karibuni
Tanzania mmetangaza ugunduzi
mkubwa wa mafuta na gesi na
Korea kaskazini tunahitaji sana
mafuta safi ambayo kwa sasa
tunayapata kutoka China”
akanyamaza kidogo halafu
akasema
“Haya yote niliyoyaeleza ni
madogo lakini kubwa zaidi ni
kwamba Korea Kaskazini inataka
kufanya uwekezaji mkubwa katika
uchimbaji wa madini ya Uranium.Tanzania ina kiwango
kikubwa sana cha madini ya Urani
na mpaka sasa hakuna uwekezaji
wowote uliokwisha fanywa
kutokana vikwazo na masharti
yaliyowekwa na umoja wa mataifa
kuhusiana na uchumbaji wa
madini ya Urani.Tunahitaji sana
Urani kwa ajili ya kuzalisha nishati
ya umeme wa uhakika kwa
viwanda vyetu hivyo basi
tunahitaji madini haya kwa
kiwango kikubwa.Uwekezaji huu
mkubwa katika madini haya ya
Urani utaupaisha sana uchumi wa
Tanzania.Mheshimiwa rais kwa
kuwa muda wetu ni mfupi hizo
ndizo salamu nilizotumwa na
kiongozi wetu niziwasilishe kwako nina imani umezipokea na
kiongozi wetu angefurahi sana
kusikia jibu zuri toka kwako
kuhusiana na hizi salamu zake”
akasema Kim Yung Su.Dr Vivian
akawatazama wale watu mle ndani
kwa zamu halafu akasema
“Ahsanteni sana kwa kuja
kuniona.Ujumbe wenu umefika na
nimezipokea salamu.Tanzania na
china tuna urafiki mkubwa wa
tangu enzi za waasisi wa mataifa
yetu mawili.Biashara kati ya China
na Tanzani ni kubwa sana hivi sasa
na kiwango cha uwekezaji
kimeongezeka kwa nchi zote
mbili.Korea Kaskazini hatujawahi
kuwa ma mahusiano ya kibiashara
japokuwa tuna mahusiano ya kibalozi na balozi wa Korea
kaskazini yuko nchini Tanzania
japokuwa Tanzania hatuna balozi
wetu Korea kaskazini na hata
mahusiano ya Tanzania na Korea
kaskazini ni madogo sana siku
hizi.Ni mara ya kwanza kusikia
kwamba Korea kaskazini
wanataka kufanya biashara na
Tanzania.Hili si jambo rahisi
kulifanyia maamuzi kutokana na
sera na mwonekano wa nchi hii
machoni pa dunia.Japokuwa Korea
kaskazini wameamua kubadili
sera zao za kiuchumi lakini bado
inaendelea kuwekewa vikwazo
mbali mbali na umoja wa mataifa
kutokana na sera zake za
silaha.Sitaki kuingia katika mambo ya kisiasa ya nchi yako Kim bali
nataka nijielekeze katika hili suala
mlilolileta kwangu kutafuta
mashirikiano ya kibiashara na
uchumi.Hili ni wazo jema na mimi
binafsi nimelipokea.Tanzania vile
vile tuko katika mageuzi makubwa
ya kiuchumi kwa hiyo
tunakaribisha uwekezaji toka
sehemu mbali mbali ili mradi uwe
ni uwekezaji wenye kuleta faida
kwa nchi yangu na watu
wake.Tunalima pamba nyingi na
litakuwa jambo lenye manufaa
makubwa endapo tutapata
viwanda vingi vya nguo kutakuwa
na soko la uhakika kwa pamba ya
wakulima wetu na hivyo kuinua
kilimo cha pamba kwa hiyo wazo la kuwekeza katika viwanda vya
nguo ninalikaribisha kwani lina
tija kwa wakulima wangu na
ninataka Tanzania iwe kinara
katika uzalishaji wa nguo barani
Afrika.Kuhusu Tanzania kuiuzia
mafuta na gesi Korea Kaskazini
hilo halina tatizo kwani tuna
hazina kubwa sana ya mafuta na
gesi na bado tunaendelea
kugundua gesi zaidi katika maeneo
mbali mbali.Korea kaskazini
mmeonyesha nia ya kutaka
kuwekeza katika madini ya Urani.”
Akanyamaza kidogo na kuvuta
pumzi ndefu na kusema
“Ni kweli Tanzania tuna
karibu ratili milioni 70 za madini
ya Urani na bado utafiti unaendelea katika sehemu
nyingine mbali mbali na mwelekeo
unaonyesha kwamba kuna
uwezekano wa kupata kiasi
kingine kikubwa zaidi cha madini
ya Uranium.Pamoja na kuwa na
kiwango kikubwa cha madini ya
Urani lakini mpaka leo bado
hatujafanya uwekezaji wowote na
hatujanufaika chochote kwa
uwepo wa madini haya nchini
kwetu.Kumekuwa na shinikizo
kadhaa toka kwa umoja wa mataifa
na toka nchi tajiri kutishia
kutuwekea vikwazo vya kiuchumi
endapo tutaanza uchimbaji na
biashara ya Urani.Shinikizo
zinatoka sehemu mbali mbali ili
tusichimbe madini ya Urani.Nilipoingia madarakani
nimewaelekeza wataalamu wangu
wapitie upya sera yetu kuhusu
madini haya ya urani na kutoa
mapendekezo nini tufanye ili
tuanze uchimbaji na kunufaika na
rasilimali tuliopewa na
Mungu.Mmeonyesha nia ya
kujenga mgodi mkubwa wa madini
haya ya Urani ni wazo zuri.Nitakaa
na wataalamu wangu tutalijadili
hilo halafu tutawaelezeni nini
tumeamua”
“Ahsante sana mheshimiwa
rais kwa kutupokea na kuzipokea
salamu za mkuu wetu.Kama
nilivyosema awali kwamba ujio
huu umebisha hodi na rais
angependa sana kujua kama tulipobisha hodi tulifunguliwa
mlango na kukaribishwa ndani?
Akauliza Kim huku
akitabasamu.Dr Vivian naye
akatabasamu na kusema
“Tanzania ni rafiki wa kila
mmoja.Hatuna maadui.Maadui
zetu ni wale wanaopinga
maendeleo yetu na kukwamisha
kusonga mbele.Wale wote
wanaokuja kwetu kwa nia njema
ya kuwekeza tunawakaribisha kwa
mikono miwili.Tanzania
hatufungamani na upande wowote
na hiyo ndiyo sera yetu toka
wakati wa muasisi wa taifa
letu.Hatuchaguliwi marafiki wala
mtu wa kufanya naye biashara na
tunaweza kufanya biashara hata na Korea kaskazini japokuwa
hatukubaliani nao kuhusiana na
sera zake za silaha na majaribio ya
makombora inayoyafanya lakini
milango iko wazi kwa mtu yeyote
kuja kuwekeza Tanzania ili mradi
uwe ni uwekezaji wenye manufaa
kwetu na si wale wanaokuja
kuchukua rasilimali zetu na
kutuacha masikini” akasema Dr
Vivian.Waliendelea na maongezi
na baadae wakaagana na moja kwa
moja akaelekea chumbani
kwake.Alielekeza kutosumbuliwa
tena kwani alihitaji
kupumzika.Aliingia chumbani
kwake na kumkuta Nathan
amejilaza kitandani.Nyuso zao
wote zikachanua kwa tabasamu.Dr Vivian akamfuata Nathan pale
kitandani wakakumbatiana na
kuanza kubusiana.Kila mmoja
alionekana kuwa na hamu sana na
mwenzake
“Nath…” Dr Vivian akataka
kusema kitu Nathan akamzuia
“Tutaongea baadae lakini
kwanza tumalize shughuli
muhimu” akasema Nathan huku
mikono yake yenye nguvu
ikiendelea kukivinjari kifua cha
Vivian ambaye taratibu alianza
kuzidiwa kutokana na utundu wa
Nathan.Alishindwa kujizuia
ikamlazimu amuachie Nathan
afanye kile alichokikusudia Ulikuwa ni mtanange wa
dakika arobaini na Nathan
alimpeleka Dr Vivian vilivyo.
“Ninajivunia sana kuwa na
mwanaume kama wewe una nguvu
za ajabu .Unanifikisha pale
ninapotaka.Ahsante sana Nathan”
akasema Dr Vivian na kumbusu
Nathan
Waliongea mambo mengi
yanayowahusu kuhusiana na ndoa
yao na maisha yao ya usoni na
mara Nathan akauliza
“Nilipokuja niliambiwa
kwamba kuna wageni
unazungumza nao faragha.Ni
wageni gani hao?
“Nilikutana na ujumbe wa
wafanyabiashara wa China wakiwa wameambatana na mjumbe
maalum wa rais wa Korea
Kaskazini” akasema Dr Vivian na
kumstua Nathan
“Walikuwa wanataka nini?
Akauliza
“Korea kaskazini wanataka
kuanzisha mahusiano ya
kibiashara na Tanzania
.Tumezungumzia kuhusu
uanzishwaji wa viwanda vya nguo
na lingine kubwa wanataka
kuwekeza katika uchimbaji wa
Uranium”
“Umewapa jibu gani?
“Tanzania inakaribisha
wawekezaji toka sehemu mbali
mbali duniani na sioni tatizo kwa
wawekezaji toka Korea kaskazini kuwekeza Tanzania.Nitajadiliana
na wenzangu tuangalie suala hili
kwa mapana zaidi.Wewe una
maoni gani kuhusu jambo hili?
Unatarajia kuwa mume wa rais na
utakuwa ndiye mshauri wangu
mkubwa.Nipe maoni yako katika
jambo hili”
“kwa upande wangu sina
kipingamizi chochote katika
kukaribisha uwekezaji nchini
Tanzania ila lazima muwe makini
na watu wanaotaka kuja
kuwekeza.Uwekezaji wowote
kutoka Korea Kaskazini na hasa
katika madini ya Urani utaiweka
nchi ya Tanzania pabaya sana
kimataifa.Kwanza kuwa mshirika
tu na Korea kaskazini ambayo ina maadui wengi inaweza kuiletea
mtatizo Tanzania lakini kwenda
mbali zaidi na kuwaruhusu
wachimbe madini ya Urani
kutaongeza mgogoro.Korea
kaskazini wapo katika msuguano
mkubwa na mataifa makubwa
kutokana na sera zake za
utengenezaji wa makombora na
inadaiwa wana makombora
kadhaa ya nyuklia na wakipata
madini hayo ya urani wataongeza
nguvu katika kutengeneza silaha
za nyuklia na watazidi kuwa tishio
kwa dunia.Hilo ni jambo
mnalopaswa kulitazama kwa
macho sita.Si suala la kufanyia
mzaha” akasema Nathan
“Nini basi ushauri wako? “Tanzania bado ni nchi
masikini,bado inahitaji misaada
toka mataifa makubwa
yaliyoendelea.Sitaki kuona
ukiingiza nchi yako katika
matatizo au migongano na mataifa
wafadhili.Nashauri uachane kabisa
na hao wakorea.Watawawekeni
katika matatizo makubwa.
Tanzania itawekewa vikwazo vya
kiuchumi,mtafungiwa kuuza nje
bidhaa zenu na kunyimwa
misaada.Hili likitokea uchumi wa
Tanzania utayumba sana” akasema
Nathan
“Tanzania ni nchi huru na
haiwezi kupangiwa taifa la kufanya
nalo biashara .Tutafanya biashara
na yeyote yule ambaye tutaonana ana maslahi kwetu.Tumechoshwa
na huu ukandamizwaji
unaofanywa na haya mataifa
makubwa.Ni wakati wa Afrika
kusimama na kuungana kupinga
huu unyanyasaji mkubwa
unaofanywa na haya mataifa
yakiongozwa na nchi yako
marekani.Mungu katupa rasilimali
zitufaidishe kwa nini tunakatazwa
kuzitumia?Kwa nini tuendelee
kuwa masikini wakati utajiri
tunao?Utajiri wetu unaporwa na
sisi tunaachiwa mashimo na
hazina za hawa wakubwa
zinaendelea kunona kwa madini
wanayoyachuma toka
kwetu.Siwezi kuivumilia hali kama
hii iendelee.Afrika lazima tufaidike na rasilimali Mungu alizotupa
kuliko kuacha zichukuliwe na
hawa wakubwa na sisi kubaki
masikini” akasema Dr Vivian.
“Tuachane na hayo Vivian huo
ulikuwa ni ushauri wangu.Tujikite
katika mambo yanayotuhusu sisi
wawili.Tuna maisha yanatusubiri
baada ya kufunga ndoa kwa hiyo ni
muda muafaka wa kupanga
kuhusu maisha yatu ya
baadae.Halafu mpenzi wangu
kuna jambo ninataka kukuuliza”
“Uliza Nathan na samahani
kwa sauti ya juu niliyoitoa
kutokana na lile suala.Unajua
linapokua suala la maslahi ya
Tanzania huwa ninaweka uzito
mkubwa sana” “Usijali mpenzi.Wewe hivi
sasa ni rais wa nchi na
ikimpendeza Mungu baada ya
miezi miwili toka sasa tunaweza
kufunga ndoa.Ninajiuliza kuhusu
suala la familia,namaanisha
watoto.Umekwisha wahi kulifikiria
hilo kuhusu namna tutakavyoweza
kupata watoto wetu?
Swali lile likaonekana
kumstua Dr Vivian.Akafikiri
kidogo na kusema
“Nathan naomba tuliache hilo
suala tutalizungumza siku
nyingine huu si wakati wake”
akasema Dr Vivian
“Vivian huu ni wakati wetu
mzuri wa kulizungumza hili
jambo.Muda uliobaki ni mdogo na kutokana a kutingwa na mambo
mengi kuna uwezekano tusipate
nafasi ya kuliongelea.Kabla ya
kuingia katika ndoa tunapaswa
kulizungumza na kupata muafaka
ili lisituletee mgogoro huko
mbeleni”akasema Nathan
“Nimekuelewa Nathan lakini
sijui nikujibu nini” akasema Dr
Vivian na kuiamisha kichwa
akafikiri kidogo halafu akasema
“Kwani lazima kuwa na
watoto?
Nimekuelewa Nathan lakini
sijui nikujibu nini” akasema Dr
Vivian na kuiamisha kichwa
akafikiri kidogo halafu akasema
“Kwani lazima kuwa na
watoto?
“Ulazima upo mpenzi tena
mkubwa.Watu wawili
mnapoungana na kuwa mwili
mmoja kwa kufunga ndoa,kikubwa
kinachotarajiwa ni kupata watoto
na kutengeneza familia yenye furaha.Kama hakuna tatizo lolote
la kimaumbile kwa mmoja kati ya
wanandoa basi watoto ni
lazima.Hilo ni agizo tumepewa na
Mungu kwamba nendeni
mkazaane muijaze
dunia.Mnapofunga pingu za
maisha Mungu anawatumia
kuendelea kazi yake ya uumbaji
kwa kuwajalia watoto” akasema
Nathan
“Bila watoto ndoa haiwezi
kuwa na furaha? Dr Vivian
akauliza
“Ndoa inaweza kuwa na
furaha bila watoto lakini endapo
hakuna tatizo lolote linaloweza
kutuzuia kupata watoto kwa nini tusizae?Mbona umeuliza maswali
hayo huna mpango wa kuzaa?
“Nathan naomba niwe mkweli
kwako kwamba sina wazo la kuwa
na mtoto hasa kwa wakati
huu.Kwa hivi sasa akili yangu
nimeielekeza katika kuwahudumia
waTanzania.Sitaki niingie katika
jambo lingine lolote
litakalonifanya nishindwe
kuwatumikia watu wangu
walionichagua kwa mapenzi
makubwa.Suala la mtoto itabidi
lisubiri labda hadi hapo
nitakapomaliza kipindi changu cha
uongozi” akasema Dr Vivian
“Hapana mpenzi hatuwezi
kusubiri hadi muda huo.Kwa sasa
una miaka 47,ukimaliza kipindi chako cha kwanza cha uongozi
utakuwa na miaka
50.Ukichaguliwa katika kipindi cha
pili utakuwa na miaka 55 unataka
upate mtoto wa kwanza ukiwa na
umri huo wa uzee?
“Nathan naomba unielewe
kwa sasa nina majukumu mazito
kwa nchi yangu na sintakuwa na
muda kulea mtoto.Utanisamehe
sana kwa hilo.Kama ni mtoto wapo
wengi tunaweza kuchukua wawili
au watatu katika vituo vya kulelea
watoto yatima tukawalea kama
watoto wetu kwa maopenzi
makubwa”
“Hapana Vivian.Sitaki mtoto
asiye wangu.Nataka kulea mtoto
wa damu yangu na si mtoto wa kuokota.Kama unaona kutakuwa
na ugumu kulea nizalie mtoto na
mimi nitalea mwenyewe wakati
ukiendelea na majukumu yako ya
urais” akasema Nathan.Dr Vivian
akamtazama na kusema
“Hilo haliwezeka ni
Nathan.Bado siko tayari kuwa
mama na pengine sitakuwa mama
katika maisha yangu yote”
Jibu lile la Dr Vivian
likaonekana kumkasirisha sana
Nathan.
“Vivian kwa nini
unanifanyia?Kwa nini hutaki kuzaa
mtoto na mimi? Kuna faida gani ya
kuingia katika ndoa ambayo
haitakuwa na uzao?Nakupenda
mno Vivian lakini kwa msimamo wako juu ya suala la mtoto
umenifanya nijifikirie mara mbili
kama kweli tuko tayari kuingia
katika ndoa.Umenishangaza sana
Vivian” akasema Nathan.Vivian
akasimama na kumtazama Nathan
kwa muda akasema
“Nathan nakupenda sana zaidi
ya unavyoweza kufikiri lakini siko
tayari kwa sasa kuwa na mtoto
hivyo basi una fursa mbili za
kuchagua.Aidha wewe na mimi
tuishi bila mtoto au tuachane
ukatafute mwanamke
atakayekuzalia mtoto.Chagua moja
mimi niko tayari kwa lolote”
akasema Dr Vivian.Nathan
akasimama na kutaka kumshika
mkono lakini Dr Vivian akamzuia “Usinishike tafadhali.Naomba
ufahamu kwamba mimi ni
mwanamke nisiyependa
kuyumbishwa na mtu
yeyote.Katika maisha yangu
ninamuogopa Mungu pekee na si
mwanadamu yeyote.Nataka mtu
ambaye nitaolewa naye awe ni mtu
atakayeendana na mimi na
misimamo yangu.Ninaomba
uchague kati ya hayo mawili
niliyokwambia.Au nikuchagulie?
Akauliza Dr Vivian kwa ukali
“Vivian mpenzi nakuomba
haya mambo yasifike huko
tafadhali.Mimi na wewe hatupaswi
kufika hatua kama hiyo ya
kulumbana kiasi hiki.Haya mambo
yanazungumzika na tukae chini tuzungumze.Tumetoka mbali na
tusianze kukorofishana kwa
wakati huu ambao tuko karibu
sana kuifikia ile ndoto yetu ya
kufunga ndoa na kuwa kitu
kimoja.Siko tayari kutengana nawe
kwa sababu nakupenda lakini
suala la mtoto naomba ulifikirie
mpenzi wangu,ni la muhimu
sana.Hatuwezi kamwe kuwa na
furaha katika ndoa yetu bila kuwa
na watoto.” akasema Nathan
“Nathan unaonekana bado
hujanifahamu vyema.Nimekupa
fursa ya kuchagua lakini
umeshindwa kufanya hivyo na
badala yake bado unaendelea
kunichefua.Sasa nisikilize kwa
makini.Mimi ni rais na ninaongoza waTanzania zaidi ya milioni
hamsini kwa hiyo akili yangu yote
nimeielekeza huko.Walinichagua
kwa mapenzi makubwa na wana
imani kubwa na mimi kwamba
nitawasaidia kuboresha maisha
yao.Watoto wa watanzania ni
watoto wangu pia hivyo natakiwa
kuhakikisha kwamba wako salama
kila siku na wana afya
njema.Natakiwa kuhakikisha
wanapata elimu iliyo
bora,natakiwa kuhakikisha wazazi
wao wana maisha mazuri na yaliyo
bora kwa hiyo kila dakika ambayo
Mungu ananijalia kuishi
ninaielekeza katika kutatua kero
za watanzania na ndiyo maana
mara nyingi hata usiku silali ninakesha nikifanya kazi kwa
ajiliya watanzania masikini hivyo
sintakuwa na muda wa kulea
mtoto.Pamoja na kukuelewesha
huko lakini bado umeonyesha
kwamba hauko tayari kuishi bila
mtoto na mimi siko tayari kuwa na
mtoto hivyo katu hatutaweza kuwa
na amani katika hiyo ndoa
yetu.Kwa sababu hiyo ninaona kitu
cha msingi ni mapenzi yetu kuishia
hapa.Ile safari yetu na zile ndoto
zetu zote ziishie hapa.Inaniuma
lakini sina namna nyingine ya
kufanya kwani Tanzania ni
muhimu zaidi kwangu kuliko
mapenzi.Siku zote huwa ninasema
nchi yangu kwanza na mambo
mengine baadae” “Vivian !! akasema Nathan
kwa mstuko mkubwa
“Nathan tafadhali usiseme
chochote.Inuka chukua kila kilicho
chako uondoke”
“hapana Vivian,usifanye
hivyo.Punguza hasira tulimalize
hili suala.Usichukue maamuzi
kama hayo.Mimi nawe hatupaswi
kufika huko”
“Nathan nimekwisha tamka na
mimi nikitamka neno huwa
sitengui kauli yangu hivyo
nakuomba uinuke uondoke.Kila
kitu chetu kimeishia hapa.Kama ni
kuzungumza tutazungumza siku
nyingine lakini si leo.Naomba
uniache nina mambo mengi ya
kufanya kwa nchi yanguTanzania.Nina watu zaidi ya
milioni hamsini ninawaongoza
kwa hiyo sitaki kumizwa kichwa
na mtu mmoja.Naomba uinuke
uondoke kabla sijawaita walinzi
wangu wakutoe humu kwa nguvu”
akasema Dr Vivian.Nathan hakuwa
na ujanja kwani anamfahamu
vyema Dr Vivian akiamua jambo
hivyo akainuka taratibu akavaa
nguo zake
“Vivian natumai hizo ni hasira
tu lakini utakapokuwa umetulia
yatafakari niliyokwambia ni
mambo ya muhimu
sana.Ninaondoka ila tutaonana
tena kesho,nitakuja
tuzungume.Mimi na wewe
anayeweza kututenganisha ni Mungu pekee hivyo suala la mimi
na wewe kutengana naomba
uliondoe kichwani kwako.Katu
haliwezekani” akasema Nathan na
kutoka mle chumbani.Dr Vivian
akaketi kitandani na kuinamisha
kichwa machozi yakamtoka
“I’ve lost him! Nimempoteza
mwanaume niliyempenda kuliko
wote” akawaza Dr Vivian
“Lakini sipaswi kuumia kwani
nimelazimika kufanya hivi kwa
ajili ya nchi yangu.Nampenda mno
Nathan lakini sijui nimepata wapi
nguvu za kuweza kumtamkia
maneno mazito kama yale.Siku
zote nimekuwa dhaifu sana kwake
na kila analoniambia nimekuwa
nalitekeleza ila leo nimepata nguvu na ghafla tu nimezima ndoto
yetu ya kuwa pamoja milele katika
ndoa.Bado miezi miwili tufunge
ndoa lakini hilo halitanipa shida
ila siwezi kuingia katika ndoa na
mtu ambaye haendani na
misimamo yangu.Ndoa yetu
haitakuwa na amani kwani kila
siku atakuwa ananidai mtoto na
mimi siko tayari kuwa na mtoto
kwa sasa.Sitaki kabisa mambo
yatakayonifanya nikapoteza
mwelekeo katika kazi
yangu.Ninawaongoza watu wengi
hivyo kichwa changu kinahitaji
utulivu mkubwa.Sitaki mambo ya
mapenzi yanifanye nishindwe
kutekeleza majukumu yangu kama
rais.” Akawaza Dr Vivian “Nadhani mambo ya mapenzi
si fungu langu.Sina bahati katika
upande huo.Kila ninapojaribu
huishia kuumia na
kulia.Enough.Sitaki kuendelea
kupoteza muda kwa mambo ya
mapenzi.Nina ndoto nyingi za
kutimiza kwa nchi yangu na si
kusumbukia mambo ya
mapenzi.Nadhani ni vyema kama
nitaishi mwenyewe.Nimekuwa mtu
nisiye penda kuyumbishwa na mtu
yeyote toka utoto wangu
namuomba Mungu anisaidie
niendele kuwa na msimamo thabiti
na nisiyume katika maamuzi
yangu ninayoyafanya.Nathan
alikuwa ni furaha yangu,alinipa
tabasamu usoni kila palenilipomuona lakini kuna kitu
kimoja nimekigundua kwake
ananipenda mimi na si
Tanzania.Theresa aliniambia kitu
kimoja cha msingi
sana.Alinikumbusha kama Nathan
anaweza kuwa mshauri mzuri
kwangu.Kwa hili nililoliona muda
mfupi uliopita hawezi kuwa
mshauri mzuri hata kidogo kwa
kuwa hana mapenzi na
Tanzania,haijui Tanzania na wala
hayafahamu matatizo ya
waTanzania” akawaza
NEW YORK - MKUTANO WA
BARAZA KUU LA UMOJA WA
MATAIFA
Mkutano ambao huchukiliwa
kama ndio mkusanyiko mkubwa
kabisa wa viongozi wa
dunia,unaofanyika kila mwaka
katika makao makuu ya umoja wa
mataifa yaliyopo New York
Marekani,ulifunguliwa rasmi na
katibu mkuu wa umoja wa mataifa
ndugu Alfredo Perez.Viongozi
kutoka mataifa karibu yote
wanachama wa umoja huu
walihudhuria wakiwemo wale wa
kutoka mataifa makubwa kama
Marekani,China,Urusi,Ujerumani,U
faransa,Uingereza.Miongoni mwa marais waliohudhuria mkutano
huu walikuwepo pia ambao ni
mara ya kwanza kuhudhuria kama
rais wa Tanzania Dr Vivian
Matope.
Katibu mkuu wa umoja wa
mataifa Alfredo Perez aliwasilisha
taarifa ya mwaka ya utendaji wa
chombo hicho .Baada ya hotuba ya
uwasilishwaji wa iliyosheheni
mambo lukuki ,marais wa kutoka
mataifa mbali mbali walianza
kutoa hotuba zao
Hotuba kubwa iliyokuwa
inasubiriwa kwa hamu ni ya rais
wa Marekani,Mike Straw.Wengi
walitaka kusikia
atakachokizungumza rais huyu
mwenye kujulikana sana kwa kusema hovyo,kutoa matamshi
yasiyo na staha na kupenda
ubaguzi hasa kwa nchi za bara la
Afrika. Ujumbe wa Tanzania
ulirejea katika hoteli walikofikia
kwa mapumziko na chakula cha
mchana kabla ya kurejea tena
katika ukumbi wa mikutano
kuendelea na kikao.Siku hii Dr
Vivian alionekana kuwa tofauti na
alivyozoeleka.Usoni pake hakuwa
na lile tabasamu watu walilozoea
kuliona hali iliyowafanya watu
walio karibu naye kujiuliza
kulikoni
Baada ya kurejea hotelini kwa
mapumziko,Dr Vivian alielekea
chumbani kwake kupumzika na
akamtaka Theresa amfuate “Dada Vivi una tatizo lolote
leo? Akauliza Theresa
“Kwa nini Theresa?
“Hauko katika hali yako ya
kawaida tuliyokuzoea.Kuna tatizo
lolote?
Dr Vivian akafikiri kidogo na
kusema
“Nimeachana na Nathan”
“Nini? Akauliza Theresa kwa
mshangao
“Nimeamua kuachana na
Nathan.Mimi na yeye kila mtu
atafuata maisha yake”
Theresa na Dr Vivian
wakatazamana kwa muda halafu
Theresa akauliza
“Kwa nini umechukua
maamuzi haya dada Vivi? “Ah ! nimelazimika kufanya
hivyo.Sikuwa na namna nyingine”
“Nieleze tafadhali nini
kilitokea ? akauliza Theresa
“Jana usiku tukiwa katika
mazungumo kuhusiana na ndoa
yetu na mambo mengine ya maisha
aliniuliza swali lililoleta mtafaruku
na nikachukua maamuzi haya”
“Aliuliza swali gani?
“Aliniuliza kuhusu suala la
kupata mtoto”
“Mtoto? Mtoto yupi? Theresa
akauliza
“Alitaka kufahamu ninafikiria
nini kuhsu kupata mtoto.Anataka
mara tukisha funga ndoa tuzae
mtoto.Mimi sina tabia ya kuficha
nikamueleza ukweli kwamba kwa sasa sina wazo la kuwa na mtoto
labda hadi hapo nitakapomaliza
kipindi changu cha uongozi.Nina
mambo mengi ya kushughulikia
kwa sasa na siwezi kupata muda
wa kulea.Kulitokea kupishana kwa
maneno na nikaona isiwe taabu
kila mmoja achukue hamsini zake
tumalizane nikaweka nukta katika
kitabu chetu na
kukifunga.Nafahamu tulikaribia
sana kuifikia ndoto yetu ya muda
mrefu lakini yawezekana labda
hatukuwa tumepangiwa kuwa
pamoja”
“Dah ! lakini dada naona kama
maamuzi haya umeyafanya kwa
haraka sana.kwa nini msikae
mkazungumza? “Hakuna tena muda wa kukaa
kuzungumza Theresa.Nimekwisha
amua hivyo na huo ndio msimamo
wangu hautabadilika.Sitaki
kuumiza kichwa na mapenzi
nikashindwa kuwatumikia
waTanzania.Nahitaji kufikiria
maisha ya watu ninaowaongoza na
si kumuwaza mjinga mmoja!!
Akasema Dr Vivian kwa hasira
“Tuachane na hayo,ile hotuba
umeifanyia marekebisho
niliyokuelekeza?Ratiba
inaonyesha usiku wa leo natarajia
kutoa hotuba yangu”
“Iko tayari dada”
“Good.Naomba niipitie”
akasema Dr Vivian na Theresa akampatia hotuba ile Dr Vivian
akaipitia
“Iko vizuri.Imekaa vizuri sana
ahsante.Mambo yote muhimu
yapo” akasema Dr Vivian
“Dada bado nataka
tuzungumze kuhusu hili suala lako
na Nathan.Unadhani ni maamuzi
ya busara kuachana kwa sasa
wakati mmebakiza miezi miwili
mfunge ndoa?
“Theresa tafadhali sitaki
kuzungumza kuhusu Nathan kwa
sasa.Nimekwisha fanya maamuzi
na huwa sina ndimi mbili.Nikisema
hapana ni hapana.Kuhusu
gharama za maandalizi
yaliyofanyika zisikuumize kichwa
,hakutakuwa na ndoa tena kwa hiyo yoyote aliyetoa mchango
wake atarejeshewa.Nenda
kapumzike Theresa usiku wa leo
nitatoa hotuba yangu kesho
nitakuwa na mikutano mbali mbali
ba kesho kutwa nitakutana na
waTanzania wanaoishi hapa
Marekani ,nitazungumza nao na
siku itakayofuata tutarejea
nyumbani” akasema Dr Vivian.
**************
Baada ya mapumziko ya
mchana viongozi walirejea tena
katika ukumbi wa mikutano na
jioni hii viongozi kadhaa
walitarajia kuzungumza.Miongoni
mwa viongozi waliopangiwa kuzungumza jioni hii ni rais wa
Marekani vile vile rais wa
Tanzania ambaye angehutubia
kwa mara ya kwanza
Viongozi walianza kutoa
hotuba zao wakizungumzia
mambo mbali mbali ya nchi zao na
dunia kwa ujumla.Saa moja na
dakika kumi ikafuata zamu ya rais
wa Marekani kutoa hotuba yake.Ni
hotuba iliyokuwa inasubiriwa sana
na watu wengi.Katika hotuba yake
alizungumzia mambo mengi na
halafu akaligeukia bara la Afrika
“Katika hotuba yake asubuhi
ya leo” akasema Mike Straw
“Katibu mkuu wa umoja wa
mataifa alieleza kwa urefu
kuhusiana na mambo kadhaa yanayolikumba bara la afrika kwa
sasa na kwa kirefu amezungumzia
athari za mabadiliko ya tabia nchi
zilizolikumba bara la Afrika na
kuyataka mataifa makubwa
yanayoongoza kwa viwanda kutoa
fedha nyingi kama fidia kwa nchi
za afrika ambazo zimeathirika kwa
kiasi kikubwa kutokana na gesi za
viwandani zinazozalishwa na
mataifa makubwa yanayoongoza
kwa viwanda duniani.Naomba
mnisikie vizuri viongozi wenzangu
wa dunia” akasema na kunyamaza
kidogo akawatazama viongozi
wale ukumbini halafu akaendelea
“Si kweli hata kidogo kwamba
sisi mataifa makubwa ndio chanzo
cha mabadiliko ya tabia nchi yanayolikumba bara la Afrika kwa
sasa.Ni kweli tunazalisha hewa
ukaa kwa wingi toka katika
viwanda vyetu na tumeanza
kuchukua hatua katika hilo lakini
matatizo haya yanayosemwa
kutokea Afrika yangepaswa
kuanzia kwetu sisi ambao ndio
wazalishaji wakubwa wa hewa
ukaa inayotajwa kwenda kuliathri
bara la Afrika.Tungepoteza misitu
yetu ,tungekuwa na ukame
mkubwa,mito ingekauka na
uzalishaji wa mazao ya chakula
ungepungua,lakini hali haiko
hivyo.Misitu yetu ipo tena
mikubwa na inastawi,vyanzo vya
maji bado vinaendelea
kububujisha maji mwaka hadi mwaka,mito yetu inaendelea kujaa
na kutiririsha maji na hakuna
tishio la kukauka kwa hiyo si kweli
kwamba sisi ndio tunaosababisha
ukame ,misitu kupotea,mvua
kutokunyesha barani
Afrika.Matatizo haya yote
yamesababishwa na waafrika
wenyewe.Kwa sababu ya ufinyu
wao wa kufikiri,wanaharibu misitu
ya asili ambayo ni chanzo kikubwa
cha mvua ,wanalima katika vyanzo
vya maji na kusababisha vyanzo
hivyo kukauka ,mito
inakauka,mvua hainyeshi tena,na
hata ikinyesha mara nyingi
inakuwa chini au juu zaidi ya
kiwango hivyo kupelekea
uzalishaji wa mazao kushuka na njaa kuenea katika kila pembe ya
bara la Afrika.Yote haya
yanasababishwa na uvivu wa
kufikiri na kutokuona
mbali.Ukiharibu leo mti uliodumu
kwa zaidi ya miaka mia moja
unategemea nini? Nawaambia
Afrika njaa ,ujinga ,umasikini
vitaendelea kuwatafuna kama
hamtachukua hatua za dhati
kufanya mabadiliko ya haraka
kuhakikisha mnalinda uoto wenu
wa asili kwa ajili ya watoto wa
watoto wenu.Bara lile la kijani
lililokuwa na vijito vyenye
kutiririsha maji kila kona,sasa
limegeuka jangwa na hata nyasi za
kulisha mifugo yenu
mnakosa.Badilikeni Afrika na muache kutafuta visingizio ili
mlipwe fedha na mataifa ya nje
wakati mazingira mmeyaharibu
wenyewe”Akanyamaza kidogo na
kuendelea na hotuba yake
“Baada ya kuliharibu bara lao
kwa kulifanya jangwa sasa
wanakimbia kwa mamia kwenda
nchi za Ulaya kutafuta
maisha.Huko mnakoenda mnataka
mkayaharibu mazingira kama
mlivyofanya katika nchi zenu?
Suala la wahamiaji toka nchi za
Afrika limekuwa ni ajenda katika
kila mkutano,mimi naona ni
upuuzi mkubwa na hatuwezi
kupoteza muda wetu kuwajadili
watu ambao hawawezi kujiongoza
wao wenyewe,hawawezikuyatawala mazingira yao
wenyewe na hawawezi kuwa na
mtazamo wa mbali wa kujua
kwamba wakiyaharibu mazingira
wanayaharibu pia maisha
yao.Wanapigana wenyewe kwa
wenyewe kugombea madaraka na
kusababisha matumizi makubwa
ya fedha kuwahudumia
wakimbizi.Ninawambia viongozi
wenzangu hasa wale wa mataifa
ambayo yamekuwa yakiwapokea
na kuwapa hifadhi hawa watu
wanaokimbia nchi zao,muache
haraka kufanya hivyo.Wakamateni
wote na muwarejeshe katika nchi
walikotoka.Ni wakati wa waafrika
kupambana na maisha yao
wenyewe.Wakianzisha vita watafute wenyewe namna ya
kupata suluhu.Tukiendelea
kuwapokea wakimbizi wao na
kuwapa hifadhi bara zima la Afrika
litahamia huku na mnajua nini
kitakachotokea? Watazaana huku
na kuwa kizazi kikubwa kiasi
kwamba baadae watoto wa watoto
wetu watapata shida ,watakosa
sehemu za makazi kwahi hawa
waafrika ni watu wenye kuzaana
bila mpangilio “ akanyamaza
halafu akaendelea
“Imenilazimu kuzungumza
maneno haya makali si kwamba
ninawachukia waafrika la
hasha,bali nataka waufahamu
ukweli na wajitambue.Tusiendelee
kuwapa maneno matamu kila mara lazima tuwaambie kwa ukali
ili wazinduke toka katika usingizi
waliolala.Viongozi wa Afrika
imarisheni demokrasia katika nchi
zenu ,heshimuni katiba zenu na
msing’ang’anie madaraka kwani
mmekuwa ndiyo vyanzo vya
migogoro mingi.Nchi yangu
imeanza kubadili sera zake za nje
hususan kwa bara la
Afrika.Tunataka tupunguze
misaada yetu na tutaielekeza kwa
nchi zile tu ambazo zitastawisha
demokrasia na utawala
bora.Viongozi wale ambao
watavunja katiba za nchi zao kwa
lengo la kujiongezea muda wa
kutawala au kutawala nchi zao
kwa mabavu hawataonja hata senti moja toka kwa
Marekani.Anzeni pia kujifunza
kujiendesha bila kutegemea
misaada ya kutoka nje.Waambieni
watu wenu wasikimbilie Ulaya bali
wabaki katika nchi zao na wafanye
kazi.Huku wanakokimbilia hakuna
maisha ya bure.Si lengo la
marekani kuingilia masuala ya
ndani ya nchi zenu lakini natoa
onyo kwa kiongozi yoyote ambaye
atang’ang’ania madarakani au
kutawala kwa mabavu bila kufuata
katiba sisi hatutasita kumtoa
madarakani kwa nguvu ili
wananchi wake waishi kwa
amani.Nawafahamu maraisi
kadhaa wa Afrika ambao
wamezigeuza ikulu za nchi zao kuwa kama nyumba zao za
kudumu,siku zao
zinahesabika.Nawaonya
waheshimu katiba na waondoke
madarakani.Ninawaonya vile vile
baadhi ya maraisi ambao
wanafadhili kushirikiana na
vikundi vyenye kuleta machafuko
na hasa ugaidi hamtabaki
salama.Tunawafahamu na
tunaendelea kuwafuatilia na muda
ukifika nawahakikishia
tutawaondoa bila
kigugumizi.Kama mmeshindwa
kujiongoza wenyewe basi
itatulazimu kuja kuwatawala tena”
rais Mike akanyamza baada ya
viongozi wa kutoka bara la Afrika
kusimama na kutaka kutoka nje ya ukumbi kufuatia matamshi yale
makali ya kuudhi.Juhudi
zikafanyika na kuwasihi wabaki
ukumbini na wakatii na hotuba
ikaendelea.
“Kitendo kilichotaka
kufanywa na viongozi wa kutoka
Afrika kinadhihirisha yale
niliyokuwa nayasema muda mfupi
uliopita kwamba viongozi hawa
hawapendi kuelezwa ukweli.Kwao
ukweli ni kutukanwa,mtawezaje
kukuza demokrasia katika nchi
zenu kama hamtaki
kukosolewa?Lazima muwe tayari
kuambiwa ukweli hata kama
unauma na muupookee,hiyo ndiyo
demokrasia.Afrika bado kuna
ombwe kubwa la uongozi na kama kusipofanyika mabadiliko
makubwa ya kiuongozi basi
matatizo ya bara hili
hayatakwisha.Afrika inahitaji
viongozi wenye mtazamo
mpya,wanaokubali kukosolewa na
wakajirekebisha” akanyamaza
baada ya minong’ono kuzidi.Baada
ya ukumbi kutulia akaendelea
“Dunia inaendelea
kupambana na matizo ya ugaidi
toka katika vikundi vya kigaidi
vinavyoendelea kuibuka kila
uchao na kutishia amani ya
dunia.Mashambulio kadhaa
tunaona yametokea katika bara la
Ulaya na watu wasio na hatia
wamepoteza maisha yao.Jijini
London kwa mfano ,watu kadhaa wamepoteza maisha yao kwa
vitendo vya ugaidi,nchini ufaransa
vile vile na nchi kadhaa za
Ulaya.Vitendo hivi vinavyoendelea
kushamiri siku hadi siku
vinaonyesha kwamba bado kuna
kazi kubwa ya kufanya ili
kuutokomeza kabisa ugaidi
duniani.Wakati juhudi za
kupambana na makundi haya ya
ugaidi zikiendelea,kumeibuka
kitisho kingine kwa amani ya
dunia ambacho ni Korea
Kaskazini.Kwa muda mrefu sasa
taifa la Korea kaskazini limekuwa
likijiimarisha kijeshi kwa
kutengeneza silaha kali za
maangamizi na makombora ya
masafa marefu.Kama haitoshi taifa hilo limekuwa likifanya majaribio
ya makombora na kuleta wasiwasi
mkubwa kwa nchi majirani zake
na kwa usalama wa dunia.Taarifa
za kiintelijensia zinaonyesha
kwamba Korea Kaskazini wanayo
hazina kubwa ya makombora ya
masafa marefu yanayoweza
kuvuka bara hadi bara.Umoja wa
mataifa umekuwa unachukua
hatua mbali mbali za kuiwekea
vikwazo Korea Kaskazini katika
harakazi zake za kujimarisha
kijeshi lakini pamoja na vikwazo
hivyo bado taifa hili limekuwa
kiburi na linaendelea na
utengenezaji na kujaribu
makombora yake.Ni siku mbili tu
kabla ya mkutano huu kuanza,Korea Kaskazini
wamefanya jaribio kubwa la
Kombora lililopita juu ya kisiwa
kilicho chini ya Japan.Huu ni
uchokozi mkubwa na
usiovumilika.” Akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Wakati Marekani na jumuiya
za kimataifa wanaendelea na
jitihada za kuidhibiti Korea
Kaskazini juu ya mpango wake wa
silaha kali,yapo mataifa ambayo
kwa makusudi kabisa wameamua
kuiunga mkono Korea Kaskazini.”
Akanyamaza tena kwa muda
“Jana usiku muwakilishi wa
rais wa Korea kaskazini
amekutana na mmoja wa marais
wa kutoka nchi moja ya Afrika na wakaongelea kuhusiana na
kuanzishwa kwa mashirikiano ya
kibiashara baina ya nchi zao na
kama haitoshi walizungumza pia
kuhusiana na kuiuzia Korea
Kaskazini madiniya
Uranium.Niliposema awali
kwamba baadhi ya viongozi wa
Afrika wana matatizo sikuwa
nawatukana bali nilikuwa
namaanisha na hiki kilichotokea
jana usiku ni mfano tosha.Kama
kiongozi wa nchi hii ana akili
timamu anawezaje kuahidi kuiuzia
Korea Kaskazini madini hatari ya
Uranium wakati akijua kabisa
kwamba Korea kaskazini
wanataka kuyatumia madini hayo
kutengeneza silaha za nyuklia ambazo ni tishio kwa
dunia?Ninatoa onyo kwa kiongozi
huyo ambaye sitaki kumtaja lakini
yumo ndani ya ukumbi huu na
ananisikia, asithubutu kufanya
biashara yoyote na Korea
kaskazini.Tunaendelea
kumfuatilia kwa karibu
sana.Akikaidi onyo hili atakuwa
amejiingiza katika matatizo
makubwa sana.Hatutavumilia
kitendo chochote cha kufifisha
juhudi za kimataifa za kuizuia
Korea Kaskazini isiendelee
kutengeneza makombora na silaha
za maangamizi.Narudia tena
tutachukua hatua kali mno kwa
taifa hili masikini la Afrika lenye
kutaka kuanzisha mahusiano na Korea Kaskazini” Aliongea kwa
ukali rais Mike straw.
Aliendelea kuongelea pia
masuala mengine na kisha
akamalizia hotuba yake iliyoja
ubabe na maneno ya kuudhi.
Baada ya hotuba ile ya rais wa
Marekani kumalizka zikafuata
hotuba nyingine mbili toka kwa
rais wa Equado na Mauritius halafu
ikafuata zamu ya rais wa Tanzania
kutoa hotuba yake.Alipanda
jukwaani na kuanza kuhutubia
Baada ya hotuba ile ya rais wa
Marekani kumalizka zikafuata
hotuba nyingine mbili toka kwa
rais wa Equado na Mauritius halafu
ikafuata zamu ya rais wa Tanzania
kutoa hotuba yake.Alipanda
jukwaani na kuanza kuhutubia
“Katibu mkuu wa umoja wa
mataifa na viongozi wengine wa
mataifa mlioko hapa,ni mara
yangu ya kwanza kuhutubia katika
mkutano huu mkubwa na
adhimu,na ni heshima kubwa kwangu kusimama mbele yenu
baba na mama zangu” akasema
huku akitabasamu na kupigiwa
makofi
“Nilikuwa nimejiandaa kutoa
hotuba hii hapa” akaiinua hotuba
aliyokuwa ameindaa na
kuionyesha halafu akaiweka chini
“Lakini sitaitoa hotuba hii na
badala yake nitasema maneno
machache” akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Viongozi wa dunia mlioko
hapa,naomba mfahamu kwamba
kuzaliwa Afrika si bahati mbaya,si
dhambi na wala si mkosi .Mungu
aliyetukuka ndiye aliyeamua
kuwepo na Afrika
,Asia,Ulaya,Amerika na mabara mengine.Ndiye aliyeamua
waafrika,wazungu,wachina
waarabu na akaona
inampendeza.Kuwabagua,kuwadh
arau kwa namna yoyote ile
waafrika au watu wa bara lingine
waliumbwa na Mungu yule yule
aliyekuumba wewe ni kudharau
uumbaji wake Mungu na
kumkosoa kwamba alikosea katika
uumbaji.Mimi ni
mwafrika,ninajivunia kuwa
mwafrika na ninamshukuru
Mungu kuniumba mwafrika na
katika maisha yangu
sintomdharau mtu kwa sababu ya
mahala atokako au kuwa na rangi
tofauti na mimi.Huu ni ubaguzi wa kiwango cha juu mno” akanyamaza
baada ya makofi mengi kupigwa.
“Mmemsikia rais Mike straw
aliyetoka kutoa hotuba yake hapa
muda si mrefu sana.Ni hotuba
iliyojaa dharau na ubaguzi
mkubwa kwa waafrika.Nathubutu
kusema kwamba hii ni hotuba ya
kiwango cha chini mno niliyowahi
kusikia inatolewa na rais wa taifa
kubwa kama hili na ninasema bila
kuogopa kwamba hii ni aibu
kubwa kwa taifa kama Marekani
ambalo linajinasibu kuwa kinara
wa demokrasia duniani” Makofi
yakapigwa akaendelea
“Nimesoma Marekani katika
moja ya vyuo vikuu,nilibahatika
kuwa rais wa serikali ya wanafunzi.Niligundua wanafunzi
wenye asili ya Afrika walikuwa
hawapewi kipaumbele katika chuo
nilichosoma hivyo nikapambana
na kuhakikisha kunakuwa na haki
na usawa kwa wanafunzi wote.Hili
lilifanikiwa lakini kwa kupitia
mambo magumu mno ambayo
sitaki kuyaeleza hapa.Katika
mojawapo ya hotuba niliyowahi
kuitoa katika kongamano la
kumkumbuka mwanaharakati
mtetea haki za weusi Martin
Luther niliwahi kueleza ndoto
yangu ya kuiona siku moja Afrika
iliyoungana na kuwa moja.Hii
ndiyo Afrika waliyoiota viongozi
wetu mashupavu walioikomboa
Afrika,Mungu awarehemu.Viongozi hawa akina
hayati mwalimu Nyerere,Nkrumah
na wengine wengi walitaka kuwa
na Afrika moja ambayo ndiyo
itakuwa suluhu ya matatizo
yetu.Tukiwa wamoja tutakuwa na
nguvu na kupiga hatua za haraka
kimaendeleo.Leo hii ninarejea
tena kuitamka ndoto yangu ya
kutaka kuiona Afrika ikisimama na
kuwa moja” makofi mengi
yakapigwa
“Amkeni viongozi wa
Afrika.Simameni tuungane na
kuwa na sauti moja yenye nguvu
kuweza kupinga ukandamizwaji
unaofanywa na mataifa makubwa
yakiongozwa na
Marekani.Tumesikia matamshi ya kubeza waafrika na viongozi wao
kutoka kwa rais wa
Marekani.Dharau hizi
zinasababishwa na ubinafsi wetu
sisi viongozi wa mataifa ya
Afrika.Laiti kama tungekuwa na
nguvu moja tungekuwa na nguvu
ya kupambana na mtu yeyote yule
awe mkubwa au mdogo.Narudia
kuwaasa tena baba na mama zangu
mlioko hapa leo ni wakati wa
Afrika kuungana na hiyo ndiyo njia
pekee ya kuondoa kauli kama hizi
za kejeli kwetu na ubaguzi
mkubwa tunaofanyiwa.Mwana wa
Afrika Mu’ammar Gaddafi alikuwa
na ndoto kama yangu ya kuiona
siku moja Afrika inaungana na
kuwa moja lakini hakupendwa na wakuu wa mataifa makubwa na
wakafanya kila wawezalo
wakamuua.Niwaulizeni enyi
viongozi mnaotoka mataifa
makubwa yenye kukomaa
kidemokrasia,baada ya
kumuondoa Gaddafi nchi ya Libya
iko salama?Mmewapa wana Libya
demokrasia mliyowaahidi
wataipata baada ya kumng’oa mtu
mliyemuita dikteta? Hao watu
wanaokuja kwa mamia katika nchi
zenu kutafuta maisha mazuri ni
matokeo ya harakati zenu
mnazofanya katika Afrika”Makofi
mengi yakapigwa.Dr Vivian
akaendelea
“Bara la Afrika linaitwa bara
masikini lakini Afrika si masikini.Ni bara tajiri pengine
kuliko yote.Umasikini wetu
unasababishwa na wizi
unaofanywa na mataifa makubwa
kwa kubeba rasilimali zetu na
kwenda kuzitajirisha nchi zao na
kutuacha katika umasikini
mkubwa.Mungu ametupatia mali
nyingi,kila pembe ya Afrika kuna
mali lakini mnakuja kwa kujifanya
mnawekeza na kuchuma mali zetu
kisha mnatuachia mashimo na
huku hazina zenu zinanona kwa
madini yetu.Pamoja na wizi huu
mkubwa bado mnatudharau na
kutuita kila aina ya majina ya
dharau.Ninasimama hapa mbele
yenu baba na mama zangu na
ninasema bila woga kwamba wizi huu wa madini yetu na mali
nyingine umefika mwisho katika
nchi yangu.Ninawaomba na
viongozi wengine wa Afrika
mniunge mkono ili tuweze
kufaidika na mali ambazo Mungu
ametupa katika maeneo
yetu.Tanzania ni nchi
huru,tunajiendesha wenyewe na
hatutaki kuchaguliwa marafiki au
watu wa kufanya nao
biashara.Hatutaki kupangiwa na
taifa lolote kuhusu namna ya
kutumia rasilimali zetu.Mali ni za
kwetu tutaamua wenyewe namna
ya kuzitumia au tumuuzie
nani.Nataka kumpa salamu rais wa
Marekani na washirika wake
kwamba mimi naweza kuwa rais mdogo kuliko wote na wanaweza
kuniona dhaifu lakini nina
msimamo usioyumba.Nikisema
hapana ni hapana.Sina ndimi mbili
na huwa sigeuki nyuma nikifanya
maamuzi.Siogopi vitisho vyovyote
toka taifa lolote lile kubwa au
dogo.Kama alivyosema Mike straw
nimefanya mazungumzo na
mjumbe wa rais wa Korea
kaskazini jana usiku.” Minong’ono
ikaanza kusikika mle ukumbini
“Nawaeleza bila kuwaficha
kwamba rais ambaye Mike straw
hakumtaja jina na alimtolea
maonyo makali ni mimi na
nilikutana na mjumbe kutoka
Korea Kaskazini jana usiku
tukafanya mazungumzo kuhusiana na kuanzisha kwa mashirikiano ya
kibiashara baina ya nchi
zetu.Narudia tena kuweka wazi
kwamba nitaendelea na
mazungumzo na Korea Kaskazini
na kama tutafikia makubaliano
basi tutawauzia madini ya
Uranium ambayo tunayo mengi
sana nchini kwetu.Si Korea
Kaskazini pekee bali taifa lolote
lile ambalo litataka kufanya
biashara na sisi
tunalikaribisha.Tunachokitaka ni
madini yetu yatunufaishe.Sihofii
vikwavyo vyenu vya kiuchumi au
hata kunyimwa misaada yenu
ambayo ndiyo imekuwa kigezo
kikuu cha kutunyonya.Mimi na
wananchi wangu tutafunga mikanda na kuanza safari ya
kujitegemea.Itatuchukua muda
kufikia nchi ya kujitegemea lakini
watoto wa watoto wetu watakuja
kunufaika na maamuzi yetu ya leo
na kutusoma katika historia
namna tulivyokataa unyonyaji na
kuamua kufanya maamuzi
magumu kwa manufaa
yao.Nitasimama mbele ya watu
wangu na nitawaongoza katika
safari hii na nitahakikisha
ninawafikisha salama katika nchi
ya maziwa na asali isiyohitaji
kujiendesha kwa misaada ya
mabeberu.Kwenu viongozi wa
Afrika na waafrika kwa ujumla
wakati wa kufanya mapinduzi na
kuondokana na unyonyaji wa mataifa makubwa umefika.Amkeni
toka usingizini tuungane na tuanze
kwa pamoja safari ya kujitegemea
kiuchumi.Tukuze biashara baina
ya nchi na nchi na hatimaye bara
zima .Tukuze pia biashara na wale
ambao watakuwa tayari kutuunga
mkono katika safari hii kama vile
China na wengine
watakaojitokeza.Kwa viongozi wa
umoja wa mataifa ninawaomba
muwe na nguvu.Msikubali taifa
moja liwe na nguvu na sauti kubwa
ndani ya chombo hiki kikubwa na
kushinikiza kufanyika mambo
watakavyo wao.Japo
tunatofautiana kiuchumi lakini
mbele ya chombo hiki tunapaswa
kuwa sawa.Kama mtaendelea kuipa upendeleo wa kipekee
Marekani kwa sababu ya mchango
wake mkubwa,chombo hiki
kitapoteza dira na hakitakuwa na
maana yoyote,kitakuwa ni chombo
cha Marekani kukandamiza
mataifa madogo na ninawaomba
viongozi wa mataifa mengine
kususia mikutano kama hii
ambayo inakuwa haina tija yoyote
kwa nchi zetu” akanyamaza na
kushangiliwa
“Ndugu katibu mkuu wa
umoja wa mataifa na viongozi wote
wa mataifa mlioko hapa,machache
niliyotaka kuyazungumza ni
hayo.Narudia tena kuwakumbusha
viongozi wenzangu wa Afrika na
wale wa nchi zisizokubaliana na ukandamizwaji unaofanywa na
mataifa makubwa tuunganishe
nguvu na hata ikiwezekana tuwe
na sisi na umoja wetu na hata jeshi
letu ili asitokee mtu yeyote
mkubwa au mdogo akatutisha
kutokana na uwezo wake.Siku zote
nitasimama katika ukweli na
sintochoka kumkosoa yeyote awe
mkubwa au mdogo.Ahsanteni sana
kwa kuniskiliza,Mungu awabariki”
Dr Vivian akamaliza kutoa maneno
yake machache na ukumbi
ukasimama kumshangilia.Ni
viongozi wachache tu waliobaki
vitini wameketi.Hotuba ile fupi
iliwakuna wengi hasa viongozi wa
kutoka Afrika. Baada ya kutoa hotuba ile Dr
Vivian hakutaka kuendelea kukaa
pale ukumbini akawaamuru watu
wake waondoke zao wakarejea
hotelini.Akawaita wote katika
ukumbi wa chakula na
kuwashukuru kwa kasi kubwa
walizofanya na kisha akawaeleza
kitu kilichowashangaza.
“Tunarejea Tanzania usiku
huu”
Wote wakastuka lakini
hakuna aliyehoji kwani wote
wanafahamu msimamo wa kongozi
wao.Wakaanza kujiandaa kwa ajili
ya kuondoka.Ni Theresa pekee
aliyemfuata Dr Vivian chumbani
kwake “Dada mbona ratiba
inaonyesha kwamba bado kuna
mikutano kadhaa ambayo
unapaswa kuihudhuria.Kuna
mkutano umeandaliwa na Kenya
kuhusiana na Malaria,na vile vile
kuna mkutano umeandaliwa na
India kuhusiana na kupunguza vifo
vya wajawazito wakati wa
kujifungua”
“Yote hiyo haina umuhimu
kwetu.Tunarejea nyumbani usiku
huu” akasema Dr Vivian.
“Sawa dada.Hata hivyo
hongera sana kwa hotuba kali
uliyoitoa.Dada umeishangaza
dunia kwa ujasiri wako.Wakati
tunarejea nilikuwa napitia maoni
mitandaoni kuhusiana na hotuba yako.Inaongelewa zaidi kuliko
hata hotuba ya rais wa
Marekani.Wengi hata wamarekani
wenyewe hawajafurahishwa na
hotuba iliyojaa matamshi ya
kibaguzi ya rais wao na ndiyo
maana ulipoamua kumjibu wengi
wamefurahi na kukupongeza kwa
ujasiri wa kuweza kusimama na
kumpa za uso Mike straw”
akasema Theresa na Dr Vivian
akatabasamu.
“Sikuwa nimepanga
kuyazungumza yale lakini
kutokana na hotuba ile ya kishenzi
ya Mike straw iliyojaa ubaguzi
mkubwa na kejeli kwa waafrika
nililazimika kutoa hotuba ile
kumjibu.Theresa wakati wa kuwaogopa hawa viongozi
wakubwa umekwisha hivi sasa ni
jino kwa jino.Ni wakati wa Afrika
kusonga mbele”
“Dada umeamsha upya ari ya
waafrika na ninatumai kila
mwafrika aliyeisikia hotuba yako
atabadili mtazamo na kujenga
uzalendo kwa nchi zao.Mjadala
mwingine unaoendelea hivi sasa ni
kuhusiana na Tanzania na Korea
Kaskazini.Ni kweli dada
umedhamiria kuanzisha
mahusiano na Korea Kaskazini na
kuwauzia madini ya Urani?
Theresa akauliza.
“Samahani sikuwa
nimekushirikisha katika hili
suala.Jana usiku nilipokea ujumbe wa watu wanne na miongoni mwao
alikuwepo mmoja kutoka Korea
Kaskazini.Huyu alikuwa ni
mjumbe maalum aliyetumwa na
rais wa Korea kaskazini
.Tulizungumza masuala kadhaa na
kubwa lililobeba mazungumzo
yetu ni mashrikiano ya kibiashara
baina ya nchi zetu .Wafanya
biashara wa Korea Kaskazini
wanataka kuwekeza nchini
Tanzania kwa kuanzisha viwanda
vya nguo lakini serikali ya Korea
kaskazini wanataka kuanzisha
mgodi mkubwa wa kuchimba
madini ya Urani.Nilizipokea
salamu hizo na sikuwa nimetoa
jibu lolote kwao lakini kwa namna
alivyoniudhi Mike straw nimeamua kuendelea na mchakato
wa kuanzisha mashirikiano na
Korea Kaskazini.Nafahamu nchi
itaingia katika matatizo makubwa
ya kiuchumi lakini tutakipita hiki
kipindi kigumu.Sisi ni taifa
masikini lakini tukisimama imara
na kulinda kilicho chetu,kujenga
biashara ya ndani pamoja na za
kikanda,kutumia vizuri mapato ya
serikali,kujiwekea akiba kubwa ya
chakula nina uhakika tutavuka
salama.Kinachonishangaza Mike
straw amefahamu vipi kuhusu
mazungumzo yangu na wale
wageni? Nimejiuliza sana swali hili
nimekosa jibu.Je Marekani
wamekuwa wananifuatilia? Kama ndiyo kwa nini? Hili suala lazima
lichunguzwe” akasema Dr Vivian
“Dada Vivi,suala hili linanipa
hofu sana.Tukiwekewa vikwazo
vya kiuchumi nchi itayumba sana
na lawama zote zitakuja kwako”
akasema Theresa
“Usiogope
Theresa.Nimekwisha amua kuingia
vitani na nitawaongoza watanzania
katika vita hii.Tutavuka
salama.Nitawafikisha kule
mnakohitaji kufika.Vikwazo
lazima viwepo lakini haviwezi
kuturudisha nyuma.Palipo na nia
pana njia.Usiwe na hofu Theresa
dada yako niko imara na huwa
sitetereki.Nenda kaanze kujiandaa
turejee nyumbani” akasema Dr Vivian na Theresa akatoka kisha
rais akamuita Edwin Swai.
“Hongera sana madam
president kwa hotuba nzuri
ambayo naweza kuiita ni hotuba ya
kimapinduzi.Ulipokuwa jukwaani
unatoa hotuba ile mikono yangu
ilikuwa kifuani mwili ukinisisimka
na hali hiyo iliwapata wengi.Kila
mtu ameshangazwa na ujasiri
wako.Hotuba kama hizi tulizoea
kuzisikia kwa viongozi wale
majasiri wasiowaogopa hawa
wakubwa kama akina mzee
Mugabe,Gaddafi n.k” akasema
Edwin na Dr Vivian akatabasamu
“Ahsante sana
Edwin.Nimekuita hapa kwa
masuala mawili.Kwanza ni kukujulisha kwamba hatuna
sababu ya kuendelea kuk hapa
hasa baada ya matamshi yale ya
kibaguzi toka kwa rais wa
Marekani.Najua ratiba yetu
inatuelekeza bado kuna mikutano
kadhaa nahitaji kuhudhuria lakini
siwezi kuhudhuria mkutano
wowote tena.Sitaki kuendelea
kukaa ndani ya nchi hii inayonuka
ubaguzi huku yenyewe ikiwa
kinara wa kunyooshea wenzake
kidole”
“Madam president mimi
nadhani ungempuuza tu yule
jamaa.Dunia nzima wanamfahamu
ni mropokaji .Tukiondoka
mapema na kuiacha mikutano haitaleta picha nzuri kwa wale
walioandaa”
“Edwin hatulali Marekani,leo
tunarejea nyumbani.Tayari
nimeanzisha vita na siwezi
kuendelea kukaa katika ardhi ya
adui ni mbaya hata kiusalama”
akasema Dr Vivian.
“Jambo lingine ni kwamba
jana nilifanya mazungumzo na
mjumbe wa rais wa Korea
Kaskazini lakini sikuwa
nimefanya maamuzi yoyote
kuhusiana na ombi lao la kutaka
kuwepo kwa mashirikiano ya
kibiashara baina ya nchi zetu mbili
na vile vile kuhusu ombi lao la
kutaka kuwekeza katika uchimbaji
wa madini ya Urani.Nililipokea ombi lao na nilitaka kwanza
nikakae na baraza langu la
mawaziri pamoja na washauri
wangu tulijadili hili suala lakini
kwa maneno aliyoyatamka Mike
straw usiku huu nimeamua
kufanya mashirikiano na Korea
Kaskazini”
“Madam Pres…..”
“Edwin sitaki ushauri wowote
katika hilo suala.Jambo lingine
nataka uchunguzi wa kina
ufanyike kujua ni kwa namna gani
rais wa Marekani amepata taarifa
za mimi kukutana na mjumbe wa
rais wa Korea Kaskazini jana usiku
na hata mambo
tuliyoyazungumza.Nimeshangaa
sana” akasema Dr Vivian. “Madam president
inawezekana kuna moja wao
alikuwa anarekodi mazungumzo
yenu.Yawezekana kati ya watu
wale kuna mmoja alikuwa
mpelelezi.watu wako wa usalama
wanapaswa kufanya kazi ya ziada
kuanzia sasa kuwachunguza watu
wote unaokutana nao.Yawezekana
kabisa wengine wakawa ni
wapelekezi wanakuja
kukuchunguza.Unahitajika
umakini mkubwa sana.Hta hivyo
tukisema tulichunguze jambo hili
itatuchukua muda mrefu kitu
ambacho hatuna.Kwa muda huu
mfupi sidhani kama tutaweza
kugundua chochote” akasema
Edwin.Dr Vivian akainamisha kichwa akafikiri kwa muda halafu
akasema
“Achana na hilo
suala.Mjiandae tuondoke”
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Safari ya saa kumi na tano
ilihitimishwa pale ndege ya rais
ilipotua katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius
Nyerere.Tayari ni saa saba za usiku kwa saa za Afrika
mashariki.Toka uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere
rais akaelekea moja kwa moja
ikulu ambako aliagana na watu
alioongozana nao katika safari ile
akaenda chumbani kwake
kupumzika.Baada ya kuoga
akamshukuru Mungu kwa
kumfikisha nyumbani salama
halafu akakaa kitandani
“Hii ilikuwa ni safari yangu
mbaya kabisa lakini nashukuru
nimeweka msimamo wangu kwa
dunia.Kuna msemo unapendwa
sana siku hizi wanasema
nimeliamsha dude.Na kweli dude
limeamka haswa.Nimeingia katika
mgogoro mkubwa na Marekani ambao ni wadu wetu wakubwa wa
maendeleo,wanachangia fedha
nyingi kila mwaka katika bajeti
yetu.Hii hainisumbui sana
japokuwa kama nchi tutayumba
lakini lazima tuingie vitani ili
tuweze kujifunza kujitegemea.Hii
misaada ndiyo inayotulemaza na
kutufanya tuwe wanyonge na
kushindwa hata kupiga kelele pale
tunapoibiwa huku tukiona au hata
pale
tunapokandamizwa.Nitawaelewes
ha watanzania nitawaomba
tuungane pamoja katika safari hii
ya kuelekea kujitegemea na kama
tukiunganisha nguvu na kuwa kitu
kimoja tutavuka salama.Mimi
sintabadili msimamo wangu na sintageuka nyuma nimeamua
kwenda mbele na lazima tuende
mbele.Dunia tayari imenielewa na
imeelewa msimamo wangu
kwamba Tanzania sasa imeamka
na hatutaki tena mzaha katika
rasilimali zetu na hatutaki
kupangiwa nani wa kufanya naye
biashara.Ndani ya kipindi kifupi
nitasimamisha shughuli zote za
uchimbaji wa madini zinazofanywa
na makampuni ya kigeni na
tutapitia upya sera na sheria zetu
za madini na kuweka sheria na
masharti mapya ili Tanzania ianze
kunufaika na rasilimali
zake.Mikataba yote ya madini
lazima ifumuliwe na kuandikwa
upya.Endapo kuna kampuni yoyote itakayopingana na jambo hili
itafungashiwa virago ndani ya
kipindi kifupi.Hii ni vita kwa hiyo
kuanzia sasa natakiwa kuongeza
ulinzi wangu mara dufu pamoja na
wale wanaonizunguka.Kitendo cha
rais wa Marekani kupata taarifa za
kukutana na kufanya mazungumo
na mjumbe wa rais wa Korea
Kaskazini kimenifanya nigundue
kwamba siko salama.Watu wa
usalama lazima walifanyie
uchunguzi hili jambo haraka sana.”
Akawaza na kujilaza kitandani
“Nataka kesho bila kuchelewa
mchakato wa mazungumzo na
Korea kaskazini uanze mara
moja.Asubuhi nitakuwa na kikao
cha dharura cha baraza la mawaziri na nitatoa maelekezo ili
jambo hili lisichelewe.Kuna jambo
lingine nimekuwa nalifikiria
nikiwa njiani.Kwa nini
nisizungumze na hawa Korea
Kaskazini watujengee kinu cha
nyuklia hapa nchini kwa ajili ya
kuzalisha nishati ya umeme? Kama
madini ya Urani tunayo kwa nini
basi tushindwe kuyatumia
kuzalisha umeme na kuwa na
nishati ya uhakika kwa viwanda
vyetu na ikiwezekana hata tuuze
nje ya nchi?Tukiwa na umeme wa
uhakika utachochea viwanda vingi
kujengwa na hivyo nchi kupiga
hatua kiuchumi.Hili ni jambo la
msingi na ninaona ushirikiano na
Korea kaskazini unaweza ukawa na manufaa makubwa kwa
Tanzania.” Akawaza Dr Vivian.
**************
Bado rais wa Tanzania Dr
Vivian Matope aliendelea kuviteka
vyombo vya habari Tanzania na
sehemu mbalimbali
duniani.Asubuhi hii kila gazeti
liliandika habari zake.Mitandaoni
bado watu waliendelea na
mijadala mbali mbali kumuhusu
huyu rais na mambo aliyoyaongea
katika kikao cha baraza kuu la
umoja wa mataifa na kubwa likiwa ni mashirikiano ya Tanzania na
Korea kaskazini.
Ni kawaida ya Dr Vivian
kuamka asubuhi na kusali kabla ya
kuelekea katika mazoezi halafu
akaoga na kujiweka tayari kwa
ajili ya kuikabili siku.Saa mbili na
nusu rais akaingia ofisini kwake
tayari kwa kuanza kazi.Saa nne za
asubuhi akaingia katika kikao cha
dharura cha baraza la mawaziri
Wakati Dr Vivian akiongoza
kikao cha baraza la mawaziri
,Edwin Swai mshauri wake wa
masuala ya usalama alikuwa garini
kuelekea Mbezi kuonana na
Meshack Jumbo mkurugenzi
mstaafu wa idara ya
ujasusi.Aliwasili nyumbani kwa Meshack Jumbo na kujitambulisha
kwa walinzi wakamruhusu apite
akaelekea ndani ambako
alipokewa na mke wa Meshack
Jumbo akamkaribisha
sebuleni.Mama yule mchangamfu
akamkirimu Edwin kahawa halafu
akaagiza mtumishi wake akamuite
Meshack Jumbo aliyekuwa katika
shughuli ya kukagua mifugo
yake.Aliposikia Edwin amekuja
akaacha shughuli zake akarejea
sebuleni
“Karibu sana Mr Swai”
akasema Meshack Jumbo baada ya
kusalimia.Mkewe akamletea maji
ya nanasi kinywaji anachokipenda
sana kisha akatoka na kuwaacha
wanaendelea na maongezi “Vipi maisha yanakwendaje
Meshack? Akaanzisha
mazungumzo Edwin.Meshack
Jumbo akatabasamu na kusema
“Maisha yanakwenda vizuri
sana.Kustaafu ukiwa umejiandaa
ni kutamu sana.Nina mashamba
yangu yanazalisha mavuno ya
kutosha,nina mifungo mingi ya
kutosha na hivi sasa niko katika
mipango ya kuanzisha kiwanda
kidogo cha kusindika mvinyo wa
matunda.Kwa ujumla maisha ni
mazuri.Vipi nyie huko serikalini
mnaendeleaje na Dr Vivian?
“Tunaendelea vyema ingawa
mambo si mepesi kama ujuavyo Dr
Vivian ni rais mwenye msimamo
mkali sana.Husimama katika yale mambo anayoyaamini hata kama
hayana tija kwake lakini akiamini
kitu fulani huwa habadiliki”
akasema Edwin
“Ni mara ya kwanza Tanzania
tunaongozwa na rais mwanamke
tena kijana bado,unaonaje
utendaji kazi wake? Hiyo
misimamo yake mikali unadhani
inaleta tija au anafanya hivyo
kuwadhihirishia watu kwamba
anaweza ili wamuogope kwa kuwa
ni mwanamama?akauliza Meshack
Jumbo
“Kuna watu huwa dhaifu
lakini hujitutumua na kujifanya
majasiri ili kuficha udhaifu wao wa
ndani.Isije kuwa na rais wetu naye
yuko hivyo kwani sijabahatika kufanya naye kazi na simfahamu
vyema” akaongeza Meshack
“Dr Vivian ni kiongozi na
ninaweza kusema ni mwanamama
shupavu na jasiri sana.Kwa sisi
tulio karibu naye tunamfahamu
vyema na wakati mwingine
tunashangazwa na ujasiri
wake.Akiamua jambo huwa
hageuki nyuma.Akitaka jambo liwe
basi litakuwa.Hii ni tabia yake toka
akiwa mdogo kwa mujibu wa
maelezo yake yeye mwenyewe na
wale wanaomjua toka angali
mdogo.Kwa ujumla naweza
kusema kwamba ni rais
anayetufaa zama hivi.We need
some one strong and powerfull and
that someone is Dr Vivian.Mpaka sasa bado sijaona udhaifu wake
wowote katika kufanya maamuzi”
“I see” akasema Meshack
Jumbo na kunywa maji ya nanasi
kisha akauliza
“Niliitazama hotuba yake
aliyoitoa juzi usiku katika kikao
cha umoja wa mataifa hata mimi
nilistushwa sana na hotuba
ile.Nimekuwa nairudia rudia ile
hotuba mara kwa mara ili niweze
kumfahamu vyema huyu rais
ambaye ni mdogo pengine kuliko
maraisi wote duniani.Haijazoeleka
kwa rais wa kutoka nchi za afrika
kusimama hadharani na
kumshambulia rais wa Marekani
kama alivyofanya Dr Vivian.Ujasiri
kama huu walikuwa nao waasisi wetu wa afrika akina mwalimu
Nyerere na wenzake ambao
hawakuthubutu kumuonea aibu
yeyote yule ambaye anaendekeza
vitendo vya kibaguzi.Viongozi
wetu wengi wa kizazi cha sasa
hawana ujasiri huo wa kusimama
na kuwakemea viongozi wa
mataifa makubwa kama
alivyofanya Dr Vivian na huu ni
udhaifu mkubwa sana wa
kiuongozi ila nashukuru rais wetu
ameonyesha njia.Nimeipenda sana
hotuba ile na ninaweza kusema ni
hotuba bora kabisa niliyowahi
kuisikia toka kwa kiongozi wa
Afrika kwa miaka ya hivi
karibuni.Tumezikosa sana hotuba
kama hizi ambazo tungeweza kuzikia kwa mzee Mugabe au mzee
Gadaffi Mungu amrehemu.Hawa ni
viongozi wachache wa Afrika
ambao walikuwa na uwezo wa
kusimama na kukemea mataifa
makubwa.Mungu amuongoze rais
wetu asije kuyumba katika
misimamo yake.By the way kuna
hili suala la mahusiano na Korea
kaskazini.Rais Mike straw
alilizungumza kwa ukali sana na
baadae Dr Vivian akakiri kwamba
ataanzisha mahusiano na Korea
kaskazini.Ninyi mlio karibu na rais
mmelichukuliaje suala hili au
mmemshauri nini? Akauliza
Meshack Jumbo.
“Hili suala hata sisi kwa mara
ya kwanza tumelisikia akilitamka rais wa Marekani na baadae Dr
Vivian akakiri kwamba ni kweli
amefanya mazungumzo na
mjumbe wa kutoka Korea
Kaskazini.Tulipofika New York rais
alikuwa na maongezi na wageni
wanne na mmoja wa wageni hao
alitokea Korea Kaskazini.Dr Vivian
hakumueleza mtu yeyote
walichoongea hadi pale
alipotamka katika hotuba
yake.Tunachojiuliza ni namna rais
wa Marekani alivyopata taarifa za
mazungumzo yale kati ya Dr Vivian
na mjumbe wa rais wa Korea
kaskazini” Akasema Edwin
“Lazima kuna udhaifu
mkubwa katika ulinzi wa rais.Kuna
mahala uliachwa mwanya na wakaweza kudukua mazungumzo
ya rais na hao wageni wake”
akasema Meshack Jumbo
“Usemalo ni la kweli kabisa
Meshack na hata mimi nimehisi
hivyo na rais pia amekiri hivyo na
ameagiza vyombo vyake vya
usalama vilishughulikie hili suala
haraka sana”
“Edwin,marekani si taifa la
mchezo.Wamepiga hatua kubwa
sana katika teknolojia na
wanawekeza fedha nyingi katika
ulinzi wa taifa lao.Ninahisi
wanamchunguza rais wetu kwa
muda sasa kutokana na mienendo
yake.Lazima walikuwa na wasi
wasi naye na ndiyo maana
wakaanza kumchunguza.Idara zinazohusika na ulinzi wa rais
zinapaswa kuwa macho sana hasa
kwa sasa ambapo ameingia katika
msuguano na Marekani.Kama
ameamua kuanzisha mahusiano na
Korea kaskazini tutakuwa
tumejiweka kati kati ya Korea
kaskazini na Marekani na
kuongeza msuguano.Sisi ni taifa
masikini na hatuna uwezo wowote
wa kupambana na Marekani
kijeshi tutajikuta sehemu mbaya
kama nchi.Sikosoi maamuzi au
mtazamo wa rais kuhusu ushirika
na Korea Kaskazini ila nina wasi
wasi na usalama wetu.Ninyi
washauri wake hamjaliona hilo?
Akauliza Meshack “Mzee Jumbo suala hili ndiyo
kwanza limeibuka na hata
mazungumzo rasmi hayajafanyika
kati ya Korea kaskazini na
Tanzania.Hivi sasa kuna kikao cha
baraza la mawaziri kinaendelea
ikulu na nina imani suala hili
litajadiliwa pia na kufanyiwa
maamuzi ila rais yuko tayari
kabisa kwa jambo hili.Utakapofika
wakati wetu wa kumshauri
tutatimiza wajibu wetu kwa
kumshauri kwa upana sana
kuhusu jambo hili na athari zake”
“Tafadhali liangalieni sana hili
jambo na mumshawishi vizuri rais
lakini sikieni pia maoni na
mtazamo wake yawekana kuna
kitu kizuri amekiona japokuwa kama atafanya maamuzi hapaswi
maamuzi ya pupa tutajikuta
sehemu mbaya” akasema Meshack
Jumbo
“Tutalizingatia hilo mzee
Meshack” akasema Edwin
“Tuachane na hayo.Naamini
mguu huu wa mapema namna hii
haukuwa kuja kunijulia hali”
akasema Meshack na wote
wakacheka
“Tunatamani sana
kuwatembelea wazee wetu
wastaafu na kuchota maarifa lakini
majukumu yanatubana,kama
ujuavyo kuwa karibu na rais.Hata
hivyo nimefurahi sana kupata
wasaa wa kuja kwako asubuhi hii
ya leo japokuwa kuna jambo limenileta hapa” akasema Edwin
na wote wakacheka
“haya niambie umeniletea
nini? Akauliza Meshack Jumbo
“Nimetumwa na rais” akasema
Edwin na kunyamaza kidogo
akamtazama Mzee Jumbo ambaye
alitoa kicheko kidogo
“Rais amekutuma? Akauliza
“Ndiyo nimetumwa na rais
anahitaji kukuona” akasema
Edwin
“Anahitaji kuniona? Kuna
nini?
“Hajanieleza kuna nini ila
amenituma nikutaarifu kwamba
anahitaji sana kuonana nawe “
Mzee Jumbo akafikiri kidogo
na kusema “Nimeshangazwa kidogo na
wito huo wa rais,kwani nilistaafu
kazi kabla hajaingia madarakani
na sina hakika kama ananifahamu”
“Mzee Meshack,yule ni rais wa
nchi na anao uwezo wa kupata
taarifa za mtu yeyote
amtakaye.Yawezekana hajawahi
kukuona lakini anazo taarifa zako
na ndiyo maana anahitaji
kukuona” akasema Edwin
“Anahitaji kuniona lini?
“leo hii.Nimekuja kukuchukua
ili twende ikulu ukaonane naye”
“Leo hii? Meshack Jumbo
akashangaa
“Mbona ghafla sana.Kuna
tatizo lolote? “Sifahamu kuna nini mzee
wangu lakini inaonekana kuna
jambo la muhimu sana hadi rais
wa nchi aamue kukuita
ikulu.Yawezekana kuna ushauri
anauhitaji” akasema Edwin.Mzee
Jumbo akatafakari kidogo na
kusema
“Sawa Edwin.Ngoja nijiandae”
akasema Meshack Jumbo na
kwenda kujiandaa.Edwin
akautumia muda huo kupitia
jumbe mbali mbali alizotumiwa
katika simu yake.Moja kati ya
jumbe alizotumiwa ni video fupi
inayoonyesha viongozi toka nchi
za Japan,Uingereza na Ujerumani
wakilaani hotuba ya rais wa
Tanzania na kuahidi kuungana na Marekani kuichukulia hatua kali
sana Tanzania endapo itaendelea
na azma yake ya kutaka kuanzisha
mashirikiano na Korea Kaskazini.
“Things are starting to get
ugly.Sijui suala hili litatupeleka
wapi” akawaza Edwin
Mzee Meshack Jumbo
alipokuwa tayari akatoka akiwa
amevaa suti ya rangi nyeusi na
kuingia katika gari la Edwin
wakaondoka kuelekea ikulu
kuonana na rais
“Nani mkuu wa idara ya
usalama wa taifa kwa sasa ?
akauliza mzee Jumbo
“Alikuwa ni George Mzabwa”
akajibu Edwin
“Alikuwa? “Ndiyo.Alikuwa ni George
Mzabwa lakini baada ya kifo chake
bado hajateuliwa mwingine kuziba
nafasi yake”
“Amekufa?
“Inamaana hujasikia bado
kilichotokea?
“hapana sijasikia
chochote.Mimi ni mfuatiliaji sana
wa habari za nje kuliko za hapa
nyumbani”
“George Mzabwa alijiua kwa
kujipiga risasi ofisini kwake juzi”
“Alijiua? Kwa nini alifanya
hivyo? Akauliza mzee Jumbo
“Hakuna anayefahamu sababu
ya kujiua kwake.Uchunguzi
unaendelea” “Hii ni ajabu sana kwa mtu
mkubwa kama huyu kujiua.Lazima
kuna sababu kubwa.Yawezekana
labda rais ananiitia suala hilo?
“Sifahamu anachokuitia rais”
akasema Edwin na safari
ikaendelea.
*************
Kikao cha dharura cha baraza
la mawaziri kilichoanza saa nne za
asubuhi kilimalizika saa nane za
mchana.Kikubwa kilichojadiliwa
katika kikao hiki ni kile
kilichotokea katika mkutano mkuu
wa baraza la umoja wa mataifa na
vile vile suala la kuanzishwa kwa
mashirikiano na Korea kaskazini lilichukua nafasi kubwa.Wengi wa
mawaziri walionyesha wasi wasi
wao mkubwa juu ya kuanzishwa
kwa uhusiano na Korea kaskazini
wakihofu kuitumbukiza nchi
katika matatizo
makubwa.Mawaziri waliomba
kutokuharakishwa kwa jambo lile
hata kama lina manufaa kwa
nchi.Pamoja na mawaziri wengi
kuonyesha wasi wasi kuhusu suala
hili na hoja mbali mbali nzito
kutolewa kuhusiana na athari za
kuwa na mashirikiano na Korea
kaskazini lakini bado rais Dr
Vivian aliendelea kusimama katika
msimamo wake wa kuanzisha
mahusiano na Korea kaskazini na
akamuuagiza waziri wa mambo ya nje kuanza mara moja
mawasiliano na mwenzake wa
Korea kaskazini ili mzungumzo
baina ya mataifa haya mawili
yaanze mara moja.Baada ya kikao
kumalizika rais akawa na
mazungumzo mafupi na makamu
wa rais ofisini kwake.
“Dr Makame ,kuna taarifa
yoyote iliyopatikana hadi sasa kwa
nini George mzabwa alijiua ?
akauliza rais
“Mheshimiwa rais mpaka sasa
hakuna taarifa yoyote
iliyopatikana kwa nini George
alijua.Uchunguzi unaendelea lakini
nategemea makubwa yapo katika
barua hii aliyokuandikia.Tunahisi
yawezekana amekueleza lolote” akasema Dr Makame na kuitoa
bahasha toka katika mfuko wa koti
na kumkabidhi rais
“Una hakika hakuna
aliyefungua barua hii? Akauliza Dr
Vivian
“Hakuna mheshimiwa
rais.Nimeitunza mimi mwenyewe
na hakuna ajuaye
kilichoandikwamo”
“Good.Ahsante Dr
Makame.Kaendelee na shughuli
zako tutaonana baadae” akasema
rais na Dr Makame akatoka. Dr
Vivian akaifungua na kuisoma
barua ile
Kwako mheshimiwa rais Rejea mazungumzo yetu leo
asubuhi.Umenitaka hadi
utakaporejea,tayari niwe na majibu
ya ile kazi uliyonipa.
Mheshimiwa rais kazi
uliyonipa si nyepesi na mpaka hapa
nilipo nimekosa jibu la kukupa
lakini kwa ufupi ni kwamba
nimeshindwa kupata majibu ya hili
suala na hiyo ni aibu kubwa kwa
kiongozi mkubwa kama
mimi.Sijafanikiwa kujua nani
waliua familia yako na kwa nini.
Mheshimiwa rais,nakushauri
usipoteze muda wako kwa ajili ya
suala hili kwani hutoweza kupata
majibu yake.Hili suala ni fumbo
kubwa na gumu kulifumbua.Nakushauri achana
nalo.
I failed you madam president
and I’m sorry for that.Siko tayari
kushushwa cheo kwa kushindwa
kupata majibu ya suala hili ambalo
nimetumia kila aina ya uwezo nilio
nao lakini nimeshindwa kulipatia
majibu
Nakushukuru kwa imani
kubwa uliyokuwa nayo kwangu
mheshimiwa rais.Pamoja na
kukuangusha lakini naomba
familia yangu iendelee kuangaliwa
na kupewa matunzo
George Mzabwa
Dr Vivian akahisi kulengwa na
machozi baada ya kuisoma barua ile akainama na kuweka mikono
kichwani.
“Ningejua nisingemwambia
yale maneno.Nimesababisha
akajitoa uhai” akawaza
“Hata hivyo kitu alichokifanya
ni cha kijinga.Hakupaswa kujitoa
uhai.Kama suala hili ni gumu na
ameshindwa kupata majibu
alipaswa kunieleza na kwa pamoja
tungeamua nini tufanye lakini yeye
akachagua kutoa uhai.Naionea
huruma familia yake,nitahakikisha
inahudumiwa kwa kila kitu na
nitakwenda kesho kutoa pole kwa
familia”
Dr Vivian akatolewa
mawazoni baada ya mlango
kufunguliwa akaingia Edwin Swai “Samahani mheshimiwa rais”
akasema Edwin baada ya kuuona
mstuko wa rais
“Karibu Edwin.Take a sit”
akasema Dr Vivian
“Mheshimiwa rais kama
utakumbuka tulipokuwa
tunaelekea New York kuna jambo
uliniomba nikakwambia kwamba
nitakuletea mtu”
“Ndiyo nakumbuka
Edwin.Umekwisha mpata?
“Ndiyo madam
president.Meshack Jumbo yupo
hapa toka asubuhi”
“Ahsante sana Edwin.Naomba
nikaongee naye katika faragha”
“Sawa mheshimiwa rais”
akasema Edwin na kutoka akampeleka Meshack Jumbo
katika chumba cha maongezi ya
faragha.Baada ya dakika tano rais
akaingia.Meshack Jumbo
akasimama wakasalimiana
“Shikamoo mzee Meshack
Jumbo”Dr Vivian akamsalimu
mzee Jumbo kwa adabu
“Marahaba Dr Vivian.Pole na
majukumu”
“Ahsante sana mzee
Jumbo.karibu sana na samahani
kwa kukusumbua”
“Usihofu mheshimiwa rais,sisi
wastaafu tunaheshimu sana wito
wa rais kwa hiyo usione kama vile
umenisumbua bali ni heshima
kubwa umenipa” akasema
Meshack “Ahsante sana baba.Nafurahi
kusikia hivyo.Vipi maisha ya
kustaafu yanakwendaje?
“Maisha mazuri.Baada ya
kustaafu utumishi wa umma
nimejikita katika kilimo na
ufugaji.Nina mashamba yangu
yanazalisha mazao ya kutosha ,vile
vile nina mifugo
ng’ombe,kuku,mbuzi bata na
nguruwe.Kwa ujumla maisha ni
mazuri” akasema Meshack
“Hongera sana.Nitakuja
kukutembea siku moja kujifunza
mambo mengi toka kwako”
“Karibu sana mheshimiwa
rais” akasema Meshack “Mzee Meshack mimi na wewe
nadhani ni mara yetu ya kwanza
tunakutana”
“Kweli mheshimiwa rais.Mimi
nimestaafu kazi kabla hujaingia
madarakani kwa hiyo
hatufahamiani”
“Sikuwa nikikufahamu hadi
pale Edwin Swai alipokutaja kuwa
unaweza kuwa na msaada
kwangu”
“Edwin ni kijana wangu
nimewahi kufanya naye kazi
ananifahamu vyema.Ni msaada
gani unauhitaji?
“Labda nikupe historia kidogo
ndipo nikueleze ninachohitaji.Nina
uhakika utakuwa unamfahamu
Kanali Sebastian Matope” “Ndiyo ninafahamiana naye
japokuwa sikuwa na ukaribu sana
naye ila tunafahamiana kwani sote
tulikuwa watu wa karibu na
rais.Kifo chake kiliniumiza sana.”
“Wakati baba na familia yangu
walipouawa mimi nilikuwa
masomoni nje ya nchi.Nilirejea
nyumbani kuwazika familia
yangu.Japokuwa ni miaka mingi
imepita sasa lakini bado
nakumbuka namna baba na familia
yangu walivyouliwa kwa kupigwa
risasi nyingi hasa baba.Ripoti ya
madaktari wanasema risasi zaidi
ya sabini zilimuingia
mwilini.Yalikuwa ni mauaji ya
kinyama mno”
“Pole sana mheshimiwa rais”
Ahsante mzee Meshack.”
Akasema Dr Vivian na kutulia
kidogo halafu akaendelea
“Hadi ninaingia madarakani
hakukuwa na na mtu yeyote
ambaye amewahi kukamatwa
kutokana na mauji ya familia
yangu.Mara tu nilipoingia
madarakani nilitaka nipewe ripoti
ya uchunguzi lakini hakukuwa na
ripoti yoyote zaidi ya kutupiana
mpira mara hili mara lile ndipo
nilipolazimika kuitumia idara ya
usalama wa taifa kulichunguza hili
suala.Miaka miwili imepita toka
nilipokabidhi jukumu hilo kwa
idara ya usalama wa taifa na
kumtaka mkurugenzi George
Mzabwa alishughulikie kwa karibu sana na ahakikishe suala hili
linapatiwa majibu.Juzi wakati
ninaelekea New York kuhudhuria
mkutano mkuu wa umoja wa
mataifa nilionana na George
uwanja wa ndege nikamwambia
kwamba nitakaporejea nikute
ripoti mezani kwangu ama sivyo
nitamuondoa katika nafasi yake na
kumpa mtu mwingine.Kwa bahati
mbaya George akajitoa uhai kwa
kujipiga risasi.Nimejiuliza sana
kwa nini vifo vya familia yangu
viwe ni kama fumbo lisiloweza
kufumbuka? Niliamua kulivalia
njuga hili jambo na ndipo
nilipomuomba Edwin anisaidie
niweze kumpata mpelelezi yeyote
mahiri wa nje au ndani ya nchi aweze kulichunguza hili jambo na
kujipatia majibu.Edwin alilipima
hili jambo na akasema kwamba
kuna mtu mmoja ambaye anaweza
akawa na msaada mkubwa sana
kwangu ambaye ni wewe hivyo
nikamtaka mara tutakaporejea
Dar es salaam akutafute nionane
nawe.Nashukuru umekuja mzee
wangu ninahitaji sana msaada
wako.Nahitaji unisaidie kumpata
mpelelezi mahiri ambaye ataweza
kulifumbua hili fumbo ambalo
polisi na idara ya usalama wa taifa
wameshindwa kulifumbua kwa
zaidi ya miaka kumi sasa.Hili ni
jambo la kwanza kubwa.Jambo la
pili ninataka mtu wa kuongoza
idara ya usalama wa taifa kwa muda wakati natafuta mtu wa
kuziba nafasi ya George
Mzabwa.Nimefikiria sana ni nani
ninaweza kumpa nafasi hiyo lakini
mpaka sasa sijaona nani anaweza
kunifaa hivyo nimeona nikuombe
unisaidie kuongoza idara ya
usalama wa taifa kwa muda wakati
ninaendelea kutafuta taratibu mtu
anayeweza kuziba nafasi
hiyo.Mzee Meshack umewahi
kuongoza idara ya ujasusi ya taifa
ambayo uliiongoza kwa mafanikio
makubwa,una uzoefu wa kutosha
katika masuala ya usalama.Nina
uhakika unaweza kunifaa sana
hasa kwa wakati huu ambao
nimeingia katika msuguano
mkubwa na mataifa makubwa.Nina imani tayari umekwisha sikia kile
kilichotokea New York katika
mkutano mkuu wa umoja wa
mataifa hivyo basi nchi inahitaji
ulinzi thabiti na intelijensia
kubwa.Idara ya usalama wa taifa ni
muhimu sana kwa wakati
huu.Mzee Meshack tafadhali
naomba usiseme
hapana.Ninakuomba kama binti
yako kama rais wako unisaidie
kwa mwaka mmoja tu na ndani ya
muda huo tayari nitakuwa
nimepata mtu maalum wa
kuiongoza hiyo idara na wewe
utakwenda kupumzika.Nakuomba
sana mzee wangu” akasema Dr
Vivian “Mheshimiwa rais sijui nianzie
wapi lakini naomba nianze na hilo
suala la pili.Kwanza nataka
nikushukuru sana mheshimiwa
rais kwa heshima ya kuniita hapa
ikulu.Pili ninashukuru sana kwa
kuniona ninaweza kuwa na
msaada bado japokuwa umri
umesogea.Pamoja na hayo
utanisamehe sana rais wangu
kwamba kwa sasa siko tayari
kurejea katika kazi.Nilianza kazi
hii nikiwa kijana mdogo na nusu ya
umri wangu nimeitumia katika hii
kazi kwa hiyo ni wakati wangu wa
kupumzika.Hata mke wangu sina
hakika kama anaweza kukubali
jambo hili kwani muda wote
ambao nilikuwa kazini alikuwa ananikosa sana na hivi sasa ana
furaha kwa kuwa niko karibu naye
kila wakati.Mheshimiwa rais wapo
vijana wengi mahiri wanaoweza
kuziba nafasi hiyo ila niko tayari
kwa ushauri muda wowote
nikiombwa”
“Mzee Meshack nafahamu
vijana wengi wazuri lakini hawana
uzoefu kama wako.Ni mwaka
mmoja tu kisha utaendela na
mapumziko yako.Kama ni mama
ndiye kikwazo nitakwenda
kuzungumza naye mimi na
nitamuomba akuruhusu kwani hili
ni suala la kitaifa.Niko hapa kwa
niaba ya watanzania.Wameniweka
hapa niwaongoze kwa hiyo
ninapokuomba uiongoze idara ya usalama wa taifa kwa mwaka
mmoja ni watanzania
wanakuomba hivyo.Tafadhali
mzee wangu nakuomba sana
unisaidie kwa hilo”
Meshack Jumbo akafikiri tena
kidogo na kusema
“Mheshimiwa rais sioni neno
ninaloweza kusema kukataa tena
ombi lako hilo.Sisi ni sawa na
wanajeshi wa akiba hivyo itokeapo
vita tunavaa gwanda tunabeba
silaha na kuingia katika
mapambano kupigania
nchi.Nitakusaidia kwa huo mwaka
mmoja ulioniomba japokuwa kuna
mambo ambayo lazima tuyajadili”
“Ahsante sana mzee Meshack
Jumbo.Sijui nikushukuruje kwa kukubali kwako.Kitu chochote
utakachokihitaji utakipata mzee
wangu na nitajitahidi kukuwekea
mazingira mazuri ya kufanya kazi
yako.Nahitaji idara ya usalama wa
taifa ile iliyokuwepo wakati ule”
akasema Dr Vivian
“Usijali mheshmiwa rais
nitafanya kazi kwa kutumia uwezo
wangu wote.Kuhusu suala la
kwanza uliloniomba nikusaidie
kupata mpelelezi wa kuweza
kukusaidia kutafuta majibu ya
watu walioua wazazi wako.Suala
hili linahitaji mtu maalum.Kuna
kijana mmoja anaitwa Mathew
Mulumbi.Huyu aliwahi kufanya
kazi katika idara ya ujasusi
alikuwa ni tegemeo kubwa kutokana na umahiri wake lakini
baadae akapata matatizo na
kuamua kuacha kazi.Nina imani
utakuwa umemsikia kwani ndiye
muhusika mkuu katika lile sakata
la Peniela” akasema Meshack na Dr
Vivian akatabasamu
“Niliwahi kulisikia sakata hilo
wakati nikiwa ujerumani wakati
huo nikiendelea na
masomo.Alifanya kazi kubwa na
alifahamika dunia
nzima.Nakumbuka mwisho wa
sakata lile walioana”
“Ni kweli walioana lakini
wameachana” akasema Meshack
“Wameachana?Dr Vivian
akashangaa “Ndiyo wameachana na
Mathew amerejea hapa nchini
.Kwa sasa ana shughulikia ujenzi
wa kiwanda chake cha
kutengeneza vipuri vya magari na
mashine mbalimbali.Kitakuwa ni
kiwanda kikubwa cha kuchonga
vipuri hapa nchini”
“Nini hasa sababu ya
kuachana kwao?
“kwa maelezo aliyonipa
Mathew ni kwamba Peniela ndiye
chanzo cha ndoa yao kuvunjika
kwani alianzisha mahusiano na
bilionea mmoja huko Paris
walikokuwa wakiishi.Baada ya
kuachana Mathew amerejea
nyumbani ambako anawekeza
katika kiwanda” “Dah ! so sorry for him.Kwa
hiyo unaamini anaweza kufaa
kuifanya kazi hii?
“Ndiyo ninamuamini sana.Ni
mahiri katika kazi zake na
hajawahi kushindwa katika kazi
yoyote aliyowahi kupewa”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Anapatikanaje huyo
Mathew? Unaweza kunipa namba
zake za simu niwasiliane naye?
“Hapana mheshimiwa rais hilo
haliwezi kuwa wazo zuri.Kuna
namna ya kumshawishi Mathew
akubali kufanya kazi yako.Kwa
sasa hayuko tena katika hizi kazi
na anawekeza katika biashara
zake kwa hiyo itahitaji mtu
maalum wa kuweza kumshawishi aweze kukubali.Nitaifanya hiyo
kazi na nitajitahidi hadi
nihakikishe nimemleta hapa
kwako” akasema Meshack Jumbo.
Maongezi kati ya rais na
Meshack Jumbo yalichukua zaidi
ya saa moja kisha wakaagana.
“Kidogo sasa ninaanza kuwa
na matumaini baada ya Meshack
Jumbo kunihakikishia kwamba
Mathew anao uwezo mkubwa wa
kulifumbua fumbo lililoshindwa
kufumbuliwa la wazazi wangu
kuuawa.Kingine kizuri ni kwamba
amekubali kuiongoza idara ya
usalama wa taifa kwa mwaka
mmoja.Sijui kwa nini nimekuwa na
imani kubwa na yule mzee
japokuwa nimeonana naye leo hii.Nilipomuona tu nikahisi amani
moyoni naamini idara hii ikiwa
chini ya yule mzee kwa mwaka
mmoja itakuwa na mabadiiko
makubwa sana kitu ambacho
ninakihitaji” akawaza Dr Vivian
baada ya Meshack Jumbo
kuondoka.
*************
Baada ya nchi za Uingereza
,Ujerumani,Ufaransa na Japan
kutoa matamko yao kulaani
majaribio ya makombora
yanayoendelea kufanywa na Korea
Kaskazini na kuionya nchi ya
Tanzania dhidi ya kuanzisha mashirikiano na Korea Kaskazini
,nchi za China Korea Kaskazini na
Urusi nazo kwa pamoja zikatoa
tamko ambalo walizionya nchi
kubwa kutothubutu kuigusa
Tanzania kwa namna yoyote ile
kwani ni nchi huru na iachwe
itumie rasilimali zake kwa
manufaa ya wananchi wake.
Tamko hili lilizidi kukoleza
moshi ulioanza kufuka na
kulifanya suala hili lizidi kuteka
vichwa vya habari duniani.Baada
ya matamko hayo kutolewa na nchi
hizo tatu,waziri wa mambo ya nje
wa Marekani naye akajitokeza
mbele ya waandishi wa habari na
kulaani tamko hilo la nchi hizo tatu
na kuzishutumu kwa kuikumbatia nchi ya Korea kaskazini.Aliliita
tamko hilo kuwa ni la kipuuzi na
akazionya nchi hizo kwamba
Marekani haitasita kuzichukulia
hatua kali ikiwamo kuvunja
mahusiano yake ya kidiplomasia
na nchi yoyote ambayo inaendelea
kuiunga mkono Korea Kaskazini
Muda mfupi baada ya tamko
hilo la waziri wa mambo ya nje wa
Marekani kutolewa,nchi za Irani
,Venezuela ,Cuba na India nazo
zikatoa matamko kuiunga mkono
Tanzania juu ya kutumia rasilimali
zake bila kuingiliwa na taifa lolote.
Edwin alimrejesha Meshack
Jumbo nyumbani.Alizungumza
kwa kifupi na mke wake halafu
akaondoka kuelekea mahala
kunakojengwa kiwanda cha
kuchonga vizuri vya magari na
mashine mbali mbali
kinachomilikiwa na bilionea
Mathew Mulumbi.
Aliwasili katika eneo
kunakojengwa kiwanda hicho
ambako shughuli zilikiwa
zinaendelea.Akashuka garini na
kuelekezwa mahala aliko Mathew
akamfuata
“Mzee Jumbo karibu
sana.Mbona umekuja kimya
kimya? Akauliza Mathew “Nimeogopa kukujulisha kama
ninakuja kuogopa kupewa sababu
lukuki kutokana na kazi nyingi
ulizonazo” Akasema Meshack
Jumbo huku akitoa kicheko na
Mathew naye akacheka,akanawa
mikono na kumpeleka Meshack
Jumbo katika kibanda cha
kupumzikia
“karibu sana mzee Jumbo.Nina
imani umekuja kujua kuhusiana na
zile mashine za kiwanda chako cha
mvinyo” akasema Mathew
“Hapana Mathew,ulikwisha
nieleza kwamba zinakuja kwa meli
hivyo sina wasi wasi zitakapofika
utanijulisha.Nimekuja kwa jambo
lingine kabisa” akasema mzee Jumbo na kunyamaza kidogo
halafu akasema
“Rais ameniita ikulu nilikua
na mazungumzo naye”
Sura ya Mathew ikabadilika
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment