Simulizi : The Football
Sehemu Ya Tatu (3)
Rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzanai Dr Vivian Matope
alilazimika kuahirisha kuhudhuria
msiba wa aliyekuwa mkurugenzi
wa idara ya usalama wa taifa
George Mzabwa kutokana na
maombi ya balozi wa Marekani
nchini Tanzania na balozi wa
umoja wa Ulaya walioomba
kuonana naye kwa
mazungumzo.Kwa sababu ya uzito
wa hayo mazungumzo rais
akamtuma makamu wa rais
amuwakilishe katika msiba huo
Saa nne na nusu balozi wa
Marekani nchini Tanzania
Abraham Clerck aliwasili ikulu na
kupokewa na rais
“Karibu sana mheshimiwa
balozi” akasema Dr Vivian
“Nashukuru mheshimiwa rais”
akajibu Abraham.Baada ya
maongezi mafupi ya utangulizi
hatimaye balozi Abraham
akajielekeza katika kile
kilichomleta
“Mheshimiwa rais kwanza
kabisa utanisamehe kwa
kukuvurugia ratiba zako leo hii
.Sikuwa nimepanga kuja kukuona
lakini imenilazimu kuja na
ninashukuru kwa kukubali
kuonana nami” akasema balozi
Abraham “Mheshimiwa rais
imenilazimu kuja kukuona baada
ya kuelekezwa hivyo na serikali
yangu nije nizungumze nawe
mambo mawili makubwa.Jambo la
kwanza ni mahusiano unayotaka
kuyaanzisha na Korea
Kaskazini.Mheshimiwa rais
mahusiano haya hayatakuwa na
manufaa yoyote kwa nchi ya
Tanzania zaidi ya kuiingiza nchi
katika matatizo.Korea Kaskazini
imewekewa vikwazo vya kiuchumi
na taifa lolote ambalo
litashirikiana na Korea Kaskazini
litahesabika kama msaliti kwa
mataifa mengine wapenda amani
duniani.Taifa hili la Korea
Kaskazini wamekuwa wakitengeneza silaha kali za
maangamizi na bila kujali
marufuku na vikwazo iliyowekewa
na umoja wa mataifa wameendelea
kufanya majaribio ya makombora
katika bahari ya Pacific na
kuwatishio kwa nchi jirani zake na
kwa usalama wa dunia.Wakati
dunia yote ikipaaza sauti kukemea
vitendo hivi vya Korea Kaskazini
serikali ya Tanzania inataka
kuanzisha mahusiano nayo na hata
kutamka wazi wazi kwamba
itawauzia Korea kaskazini madini
ya Uranium ambayo Korea
kaskazini wanataka kutayatumia
katika kutengeneza silaha za
nyuklia.Wakati mkutano wa
baraza kuu la umoja wa mataifa ukiendelea Korea kaskazini
imefanya majaribio mawili ya
makombora na kusababisha hofu
kubwa hasa kwa Japan.Kwa hivi
sasa umoja wa mataifa
unatafakari kuwaongezea vikwazo
zaidi Korea kaskazini kufuatia
kiburi chake na kuendelea kufanya
majaribio ya makombora” akatulia
kidogo na kuendelea
“Mheshimiwa rais nimetumwa
kuja kukwambia ufikiri upya
kuhusu mpango wako wa kutaka
kuanzisha mahusiano ya aina
yoyote na taifa hili la Korea
kaskazini.Tunafahamu Tanzania ni
nchi huru na haiwezi kuchaguliwa
marafiki lakini si Korea
kaskazini.Hili ni taifa adui wa kila mtu hapa duniani.Kuamua
kushirikiana na taifa hili ni
kuwasaliti wapenda amani kote
duniani na kujiweka katika
matatizo makubwa kwani lazima
nchi yako itawakewa vikwazo vya
kiuchumi.Tanzania ni nchi
masikini bado haijapiga hatua
kubwa kiuchumi ,bado inategemea
misaada na mikopo toka mataifa
makubwa na hasa
Marekani.Tanzania haina viwanda
vya kutosha inategemea bado
kuagiza baadhi ya bidhaa zake nje
ya nchi.Kwa ujumla Tanzania bado
inazihitaji sana nchi tajiri.Kuamua
kushirikiana na Krea Kaskazini
Tanzani itawekewa vikwazo vya
kiuchumi na kurudisha nyuma juhudi zake za kujiondoa katika
umasikini.Tanzania na Marekani
ni marafiki wa muda mrefu na
kama kuna tatzo lolote basi
tunaweza kukaa
tukazungumza.Marekani ni
mchangiaji mkubwa wa miradi ya
maendeleo na hata bajeti kuu ya
serikali kwa hiyo Tanzania kuingia
katika mgogoro na Marekani
kutaiathiri sana kwani serikali ya
Marekani italazimika kukata
misaada yake kwa Tanzania.Miradi
yote ya maendeleo
itasitishwa.Mheshimiwa rais
nimeombwa nikutaarifu kuhusu
jambo hilo na ufikirie upya wazo
lako la kuungana na Korea
Kaskazini. Jambola pili ni kuhusiana na
makampuni ya Kimarekani
yaliyowekeza hapa
Tanzania.Endapo utaendelea na
maamuzi ya kutaka kushirikiana
na Korea Kaskazini basi
makampuni ya Kimarekani
yaliyowekeza hapa nchini
yataondoa uwekezaji wao mkubwa
na kupeleka katika nchi
nyingine.Hilo likitokea serikali
itakosa kodi,wananchi watakosa
ajira na nchi itayumba sana. Korea
Kaskazini hawezi kufanya
uwekezaji mkubwa kama
uliofanywa na Wamarekani.Kwa
ujumla hakuna faida yoyote
inayoweza kupatikana kutokana
na mashirikiano na Korea Kaskazini zaidi ya hasara
.Mheshimiwa rais bado iko nafasi
ya kuliweka sawa jambo
hili.Serikali ya marekani
inakaribisha kama utahitaji
mazungumzo juu ya jambo
hili.Tanzania inaihitaji sana
Marekani zaidi ya Marekani
inavyoihitaji Tanzania.Pamoja na
hayo serikali ya Marekani imeahidi
iko tayari kuongeza fedha katika
miradi mingi ya
maendeleo.Imeahidi kuongeza
mara nne zaidi ya kiwango
inachokitoa sasa hivi endapo
Tanzania itaachana na mipango ya
mashirikiano na Korea
Kaskazini.Mheshimiwa rais hii si
fursa ya kuiachia .Serikali ya Marekani haijawahi kuahidi kutoa
fedha nyingi kiasi hiki kwa taifa
lolote duniani na inafanya hivi kwa
mara ya kwanza kwa Tanzania
endapo tu mtakuwa tayari
kuachana na Korea
Kaskazini.Marekani haijawahi
kuibembeleza nchi yoyote duniani
lakini inafanya hivyo kwa
Tanzania kwa kuwa wamarekani
wanawapenda sana watanzania na
ndiyo maana hata katika orodha ya
watalii wanaokuja kila mwaka
wamarekani wanaongoza.Hatutaki
kuona Tanzania ikiingia katika
matatizo.Mheshimiwa rais
usikubali kuiacha ofa hii kubwa
.Hii nifursa kubwa ya Tanzania
kupiga hatua.Usikubali kutengwa na jumui ya kimataifa hivyo kama
utakuwa tayari basi mazungumzo
yaanze mara moja ili kuona ni
maeneo gani hasa mngependa
yapewe kipaumbele katika msaada
huo mkubwa utakaotolewa na
serikali ya Marekani.Mheshimiwa
rais hayo ndiyo mambo
niliyotumwa hapa kwako
nashukuru kwa kunisikiliza”
akasema balozi Abraham.Dr Vivian
akatabasamu na kusema
“Nakushukuru sana
mheshimiwa balozi kwa kuja na
kunifikishia ujumbe.Napenda
kukufahamisha kwamba ujumbe
wako nimeupokea kwa mikono
miwili lakini kwa bahati mbaya
umekuja kwa kuchelewa sana.Tayari watanzania
tumekwisha fanya maamuzi
.Tayari tumeamua kufanya
mashirikiano na Korea Kaskazini
.Tayari nimefanya mazungumzo na
rais Kim wa Korea Kaskazini na
tumekubaliana kuanzisha
mashirikiano ya kibiashara na
uchumi baina ya nchi zetu na vile
vile mashirikiano ya
kijeshi.Tanzania ni taifa masikini
kama mnavyoliita lakini umasikini
huu umetokana na unyonyaji na
wizi mkubwa
mnaotufanyia.Mnabeba rasilimali
zetu na kutuacha masikini halafu
mnarudi na kutudanganya kwa
misaada ambayo imetokana na
faida mliyoipata kutokana na mali mliyochuma huku
kwetu.Watanzania tumeamka toka
usingizini na hatutaki hayo mambo
yajirudie tena,tumechoka kuibiwa
rasilimali zetu.Tumesema basi na
kuanzia sasa tunataka rasilimali
tulizonazo zitunufaishe
watanzania sasa na vizazi vijavyo
hivyo basi tumeamua kuanza upya
na kwa kuanzia tutaanzisha
mashirikiano na Korea Kaskazini
.Jambo hili halitawapendeza
mataifa makubwa walioshika
uchumi wa dunia na hivyo
tunatishiwa sana kwamba
tutawekewa vikwazo vya kiuchumi
na nchi itayumba.Nalifahamu hilo
na ninafahamu tutapitia wakati
mgumu kama nchi lakini tutasimama imara na tututavuka
salama.Tunaanza safari ya
kuelekea kujitegemea kama nchi
bila kutegemea misaada au
mikopo ya wafadhili” akanyamza
kidogo akamtazama Abraham
aliyekuwa anavua miwani mara
kwa mara na kufuta macho
“Kwa hiyo balozi Abraham
,katika suala la kwanza
hakutakuwa na mazungumzo
yoyote baina ya Tanzania na
Marekani au nchi nyingine
yoyote.Tumeamua kusonga mbele
na hatutarudi nyuma
kamwe.Waeleze wakuu wako
kwamba Dr Vivian ameamua
kuwaongoza watanzania katika
vita ya uchumi ili Tanzania iweze kujitegemea na kuhusu
mashirikiano na Korea Kaskazini
yako pale pale na hatutarudi
nyuma.Suala la pili ni kuhusiana
na wawekezaji wa Marekani wa
hapa nchini.Kweli kuna
makampuni makuwa ya
kimarekani yamewekeza hapa
Tanzania katika sekta mbali
mbali.Yapo yanayochimba
madini,yapo yaliyowekeza kwenye
mafuta na gesi na sehemu nyingine
mbalimbali.Tayari nimekwisha
waagiza wanasheria wangu kuanza
mchakato wa namna
tukakavyoweza kusitisha
mikataba na makampuni haya
.Nafahamu hili ni jambo
litakalowaudhi sana wamarekani lakini hatuna namna nyingine ya
kufanya .Tunahitaji marafiki na
wawekezaji lakini si wale
wanaokuja kutunyonya na kutaka
kututawala kwa hiyo tutavunja
mikataba yote na tutafuta
wawekezaji wengine au
tutahifadhi mali zetu hadi pale
tutakapojenga uwezo wa ndani wa
kuweza kuchimba” akasema
rais.Balozi Abraham akavua
miwani akafuta machoni na
kusema
“Mheshimiwa rais utakuwa
umefanya kosa kubwa sana kama
ukifanya hivyo.Utaiharibu
Tanzania.Nimeishi hapa kwa muda
wa miaka mitatu na nimetokea
kuwapenda sana watanzania,ninafahamu matatizo
yao na endapo ukifanya hivi
unavyotaka kufanya utawaingiza
katika matatizo
makubwa.Marekani inafadhili
miradi mingi mikubwa hapa
nchini,ipo miradi ya
afya,elimu,maji,nishati ,miundo
mbinu na hii yote inasaidia
mamilioni ya watanzania.Endapo
Marekani itajitoa kufadhili hii
miradi yote watu wengi
wataathirika sana.Serikali ya
Korea Kaskazini haina uwezo wa
kuyafanya haya yote
yanayofanywa na Marekani hapa
nchini Tanzania.Mheshimiwa rais
tafadhali naomba ulifikirie tena suala hili.” Akasema balozi
Abraham
“Mheshimiwa balozi ,naomba
tafadhali tusiendelee kuliogelea
hili suala.Tayari nimekwisha weka
wazi msimamo wangu na wa
tanzania na sipendi kuendelea
kurudi rudia maongezi .Naomba
unifikishie salamu zangu kwa rais
Mike straw na umueleze haya
niliyokueleza bila kupunguza hata
neno moja” akasema Dr Vivian na
kusimama akampa mkono balozi
Abraham
“Ahsante sana balozi kwa
kunitembelea.Nomba umsalimu
sana Mike straw” akasema Dr
Vivian na kumsindikiza balozi nje
akaondoka zake. “Wameanza kutapa tapa hawa
jamaa.Eti wataongeza misaada
mara nne ya ile wanayoitoa
sasa.Hii inaonyesha wazi ni namna
gani wanavyofaidika na rasilimali
zetu.Kama si hivyo
wasingehangaika namna hii kutoa
matamko ya vitisho na sasa
wanaona sitishiki na matamko yao
na wanataka kujaribu kuja na
maneno matamu.Sintogeuka
nyuma ili niwe jiwe,nimeamua
kusonga mbele na nitahakikisha
ninaivusha nchi katika vita
hii.Mwisho umefika wa
kunyanyaswa na mataifa
makubwa” akawaza Dr Vivian na
kutaarifiwa kwamba balozi wa
umoja wa ulaya amefika “Huyu naye nina imani
atakuwa amekuja kuzungumza
mambo haya haya” akawaza Dr
Vivian na kuelekeza balozi huyo
akaribishwe ndani
***************
Mathew na Theresa waliwasili
katika kijiji cha Mchangawima na
kuelekezwa lilipo shamba la rais
Anorld Mubara.Kulikuwa na
barabara nzuri ya lami kuelekea
katika shamba hilo.Miti mizuri
iliyotoa maua mazuri ilipandwa
kandoni mwa barabara
ile.Mandhari ilikuwa ya kuvutia
sana Walifika katika geti la kwanza
kulikokuwa na askari wawili
wakasimamishwa na kuulizwa
wanakoelekea.Mathew na Theresa
wakajitambulisha kwamba
wanatoka ikulu na walikuwa na
maagizo ya rais kwenda kwa bi
April,wakaruhusiwa kupita
“Ulinzi mkali sana mahala
hapa.” Akasema Mathew.Theresa
alikuwa kimya kabisa na
hakuongea kitu.Mwili ulikuwa
unamtetemeka kwa ndani
alipokumbuka siku
waliyoshambuliwa na wazazi wake
kuuawa miaka kumi
iliyopita.Walilikuta geti la pili
wakakaguliwa na kuamriwa
kuacha silaha zao.Bastora mbili za Mathew zikaachwa pale hadi
wakatakapotoka.Hakuna
aliyeruhusiwa kuingia na silaha
katika nyumba ya Bi April
Walifika katika geti la tatu na
walinzi wawili walivalia suruali
nyeusi na mashati meupe
wakafungua geti wakawaonyesha
sehemu ya kuegesha gari na
mtumishi aliyevalia nadhifu
akawasili wakakaribishwa
sebuleni.Lililkuwa ni jumba jumba
kubwa la ghorofa nne.Ukimya
ulikuwa mkubwa eneo hili
Walikirimiwa vinywaji na
baada ya dakika chache akatokea
mama mmoja mzungu
“Karibuni jamani” akasema
mama yule kwa kiswahilisafi.Mathew na Theresa
wakasimama wakamsalimu kwa
adabu
“Nimefurahi sana kupata
wageni leo.Mara chache huwa
natembelewa na watu huku
shambani.Labda wakati wa
sherehe za kitaifa huwa nafuatwa
na kualikwa”akasema bi April
huku akitabasamu.
“Huku kunaitwa shambani
lakini ni sehemu tulivu mno.Hewa
safi na ukimya mkubwa tofauti na
huko mjini tulikosongama
kulikojaa moshi wa magari na gesi
za viwanda.Hatuwezi kupata hewa
safi kama inayopatikana huku”
Akasema Mathew “Usemayo ni ya kweli .Watu
wanakimbilia mjini lakini kumejaa
ghasia.Msongamano
,kelele.uchafuzi wa hewa n.k.Kwa
ujumla maisha ya huku ni mazuri
mno.Haya niambieni nyie ni akina
nani na mmetokea wapi?
“Mimi naitwa Theresa na huyu
mwenzangu anaitwa Mathew.Mimi
ninafanaya kazi ikulu na huyu
mwenzangu anafanya kazi katika
idara ya usalama wa taifa”
Bi April akastuka kidogo kwa
utambulisho ule.
“Karibuni sana.Mimi naamini
mnanifahamu .Naitwa April
hudson Mubara,mjane wa rais
Anorld Mubara.Mneniletea nini
Theresa na Mathew? “Ahsante sana mama kwa
kutupokea na kwa makaribisho
mazuri.Tumekuja kwako
kuzungumza nawe mambo
machache yanayohusiana na
hayati rais Anorld Mubara”
akasema Mathew.April
akaonekana kusita kidogo halafu
akasema
“Nilidhani jambo hili
limemalizika kumbe
bado.Nimekwisha hojiwa na
wengine wengi lakini
walipoondoka hawakuwahi kurudi
tena hapa kunipa mrejesho .Haya
Mathew unahitaji kufahamu nini
kuhusiana na marehemu mume
wangu? “Mama ni miaka zaidi ya kumi
sasa toka ilipotokea ajali
iliyochukua uhai wa mumeo
Anorld Mubara.Kwa muda huo
wote uchunguzi wa ajali ile
haujawahi kukamilika.Mtu pekee
ambaye angeweza kutusaidia
kufahamu kilichotokea ni kanali
Sebastian Matope ambaye naamini
unamfahamu na ambaye ndiye
pekee aliyenusurika katika ajali
ile”
“Kanali Sebastian
ninamfahamu vyema sana”
akasema bi April
“Kanali Sebastian alifariki
miezi michache baada ya mumeo
kufariki katika ajali,na matukio
yote haya mawili la kifo cha mumeo na kifo cha Kanali
Sebastian hayajaweza kupatiwa
majibu hadi leo hii.Vifo hivi
vimekuwa ni kama fumbo gumu
lisiloweza kufumbuka.Rais Dr
Vivian alipoingia madarakani
amelifufua jambo hili na kutaka
uchunguzi ufanyike kufahamu nani
walimuua baba yake na tayari
uchunguzi umeanza kufanyika
.Mimi ni mmoja wa watu
tunaochunguza suala hili na
tunaanzia katika ajali ile ya ndege
iliyomuua rais Anorld Mubara”
Akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Japo jambo hili limekuwa ni
fumbo gumu lakini kuna
mwangaza mdogo sana tumeanza kuuona ambao unaweza
kutupeleka mahala tunakoweza
kupata ukweli wa ile ajali ya
ndege.Tumegundua kwamba
kulikuwa na watu kumi na tisa
ndege ilipoondoka hapa Dar es
salaam kuelekea Misri na wakati
wa kurudi watu waliongezeka
kwani kulikuwa na waandishi wa
habari nane walioomba lifti katika
ndege ya rais baada ya kuchelewa
ndege yao.Ilipotokea ajali
alinusurika mtu mmoja tu na
wengine wote walikufa lakini
kinachoshangaza taarifa ya watu
waliofariki katika ajali hiyo
haionyeshi kama kulikuwa na
waandishi hao wa
habari.Tumegundua kwamba waandishi hao wa habari
walisaidiwa na mtu na mtu mmoja
anaitwa Fakrim Alnasor aliyekuwa
mfanyakazi katika shirika la ndege
la American airways na siku
chache baada ya ajali kutokea
alihamishiwa New york.Uchunguzi
unaonyesha kwamba huyu Fakrim
ni jasusi wa shirika la ujasusi la
Marekani CIA.Tumeanza kuona
chembe chembe za Marekani
kuhusika katika ajali ile kupitia
shirika lake la ujasusi la
CIA.Uchunguzi unaendele a hivi
sasa ili tuweze kumpata huyu
Fakrim lakini tumejiuliza sababu
ya Marekani kuhusika katika suala
hili na kumuua rais Anorld
Mubara.Lazima kuna sababu iliyowapeleka kufanya hivyo na
ndiyo tunaitafuta hivyo tumekuja
hapa kwako kwa kuwa wewe ni
mke wa rais Anorld yawezekana
kuna jambo ambalo unaweza kuwa
unalifahamu halikuwa na kawaida
ambalo linaweza kusababisha
Marekani kufanya kitendo kile
kibaya.Yawezekana kuna siri
fulani aliwahi kukupa tunaomba
utueleze ili itusaide katika
kutafuta chanzo cha kifo chake”
akasema Mathew
“Mmenistua sana vijana.Kwa
miaka hii yote nimekuwa nikilia
nikiomba siku moja ukweli kuhusu
kifo cha mume wangu ujulikane
lakini hakuwahi kutokea mtu
yeyote aliyenipa taarifa yoyote kuhusiana na ajali ile na hata
nilipouliza kama uchunguzi tayari
nikaambiwa kwamba uchunguzi
bado unaendelea.Nimehoji hadi
nikaamua kukaa kimya
nikamwachia Mungu .Hiki
mlichonieleza leo ni kitu
kilichonistua sana na hata mimi
nimeanza kuuona mwanga katika
kupata majibu ya nani walimuua
mume wangu.Hata hivyo
umeniomba nikwaeleze kama
kuna siri yoyote au kuna kitu
chochote ambacho si cha kawaida
inaweza kupelekea Marekani
washiriki katika kumuua mume
wangu ,ukweli ni kwamba Anorld
hakuwa ananishirikisha katika
masuala yake nyeti.Kitu kimoja ambacho namlaumu sana ni usiri
wake katika hata mambo yale ya
hatari.Hata kama kuna jambo
linamsumbua lakini akirudi
nyumbani haionyeshi kama ana
tatizo lolote.Msiri wake mkubwa
alikuwa ni Kanali Sebastian
Matope.Huyu ndiye mwenye
kufahamu siri nyingi za Anorld na
laiti kama angekuwa hai angekuwa
na msaada mkubwa sana kwenu na
tungeufahamu ukweli.Siku
alipouawa alikuwa anakuja
kwangu kuniambia jambo fulani la
siri lakini hakuweza kufika kwani
aliuawa njiani na watu
wasiojulikana”akasema bi April
Mazungumzo kati yao
yalidumu kwa zaidi ya dakika arobaini na Mathew alipoona
hakuna chochote wanachoweza
kukipata toka kwa yule mama
wakaagana na kuondoka.
“Sishangai kwa nini uchunguzi
huu umechukua zaidi ya miaka
kumi na hakuna kilichowahi
kupatikana.Bado ni fumbo zito”
akasema Mathew baada ya
kuondoka kwa Bi April
“Nilikushauri toka mwanzo
Mathew kwamba tusipoteze muda
kwa jambo hil………..”Akasema
Theresa na simu ya Mathew
ikaita,alikuwa ni Meshack Jumbo
“Hallow mzee” akasema
Meshack
“Uko wapi Mathew? “Niko njiani narejea Dar es
salaam.Nimetoka kuonana na bi
April mjane wa rais Anorld.Kuna
taarifa yoyote?
“Ndiyo nimepigiwa simu sasa
hivi na Jimmy ameniambia
kwamba Fakrim amepigwa risasi
na kufariki hapo hapo muda mfupi
uliopita”
Mathew akashusha pumzi
“Amepigwa risasi?Mathew
akashangaa
“Ndiyo”
“Kapigwa risasi na nani?
“Kwa maelezo aliyonipa
Jimmy,anasema kwamba
aliwatuma vijana wake
wamfuatilie na kumteka Fakrim ili
wamuhoji lakini usiku huu wakati anakaribia kufika nyumbani
kwake watu waliokuwa na
bunduki walijitokeza katika gari
lililokuwa linamfuatilia na
kummiminia risasi kisha mmoja
wao akashuka na kuliendea gari la
Fakrim ili kuthibitisha kama kweli
amekufa na ndipo vijana wake
wakaanzisha mashambulizi
kuwashambulia wale jamaa ambao
walifanikiwa kukimbia na
kutokomea kusikojulikana huku
yule mmoja aliyeshuka akipoteza
maisha.Vijana wa Jimmy
walifanikiwa kuipata simu ya
Fakrim pamoja na kompyuta yake
ndogo.Hivi sasa wanakwenda
kuifanyia uchunguzi hiyo simu na
kompyuta kuona kama kuna kitu chochote wanaweza kukipata cha
kutusaidia.Tafadhali njoo mara
moja hapa nyumbani” Akasema
Meshack Jumbo.Mathew akavuta
pumzi ndefu.
“Kuna nini Mathew? Theresa
akauliza baada ya kuona
mabadiliko katika uso wa Mathew
“Fakrim ameuawa”
“Ameuawa? Lini?
“Muda mfupi uliopita”
“Nani kamuua?
“Bado haijulikani .Ameuawa
akirejea nyumbani
kwake.Tutapata taarifa kamili
baadae” akasema Mathew
“Mathew hili suala si
jepesi.Linakoelekea ni suala
linazidi kupanuka .Ninazidi kuwana hofu kuhusu hatima ya maisha
yetu” akasema Theresa
“Hili lililotokea linazidi
kutupa uhakika kwamba Fakrim
alikuwa anahusika na jambo hili
na tayari waliomtuma
wameshtushwa na mahala
tulikofika katika uchunguzi wetu
na ndiyo maana wameamua
kumuua.Naamini wengi
waliochunguza hili suala
hawakufika katika sehemu
tulikofika sisi na kugundua uwepo
wa waandishi wa habari waliopata
lifti katika ndege ya rais kwani
balozi Zubery anasema hakuna
aliyewahi kwenda kumuhoji yeye
chochote kuhusiana na ajali ile
kwani kwa zaidi ya miaka mitano
SEHEMU YA 16
ENDELEA
Hili lililotokea linazidi
kutupa uhakika kwamba Fakrim
alikuwa anahusika na jambo hili
na tayari waliomtuma
wameshtushwa na mahala
tulikofika katika uchunguzi wetu
na ndiyo maana wameamua
kumuua.Naamini wengi
waliochunguza hili suala
hawakufika katika sehemu
tulikofika sisi na kugundua uwepo
wa waandishi wa habari waliopata
lifti katika ndege ya rais kwani
balozi Zubery anasema hakuna
aliyewahi kwenda kumuhoji yeye
chochote kuhusiana na ajali ile
kwani kwa zaidi ya miaka mitano alikuwa hospitali
anatibiwa.Tumegundua kwamba
Fakrim ndiye aliyewasaidia hao
waandishi wa habari kupata lifti
katika ndege ya rais na huyu
Fakrim ni jasusi wa CIA kwa hiyo
kuna mkono wa CIA katika ajali ile
na ndiyo maana mara tu ilipotokea
ajali Fakrim aliondolewa Misri
akapelekwa New York baada ya
kuikamilisha kazi
aliyotumwa.Hatimaye baada ya
miaka kumi tumegundua uhusika
wake katika suala hii na
wamemuua haraka ili tusiweze
kupata taarifa zozote toka kwake
na kuzidi kulifanya suala hili kuwa
gumu.Usiogope Theresa mambo
ndiyo kwanza yameanza.Huko tuendako kutakuwa kugumu zaidi
lakini nitakulinda kama
nilivyokwisha kuahidi.Twende
tukaonane na Meshack Jumbo”
akasema Mathew
****************
Mathew na Theresa waliwasili
nyumbani kwa Meshack Jumbo
akawakaribisha kibarazani na bila
kupoteza muda mazungumzo
yakaanza
“Karibuni sana.Naona uko na
binti mrembo hapa,ni nani huyu?
Nitambulishe tafadhali” akasema
Meshack Jumbo huku akitabasamu
“Anaitwa Theresa Matope ni
ndugu wa rais na ndiye mwandishi wake wa hotuba.Zile hotuba zake
nyingi ambazo huwa unazisikia
zimejaa msisimko mwandishi
wake ni huyu.Rais amenipa
Theresa awe ni msaidizi wangu
katika kazi hii ninayoifanya na
ahakikishe hakuna mkwamo
wowote ninaoupata” akasema
Mathew na kumtazama Theresa
“Theresa huyu ni mzee wangu
anaitwa Meshack Jumbo.Aliwahi
kuwa bosi wangu katika idara ya
ujasusi na sasa amestaafu lakini
rais amemuomba amsaidie
kuiongoza tena idara ya usalama
wa taifa kwa mwaka
mmoja.”akasema Mathew na
Theresa akainuka na kwenda
kumpa mkono Meshack “Nimefurahi sana kukufahamu
Theresa.Kwa kuwa uko karibu na
Mathew basi tutakuwa tunaonana
mara kwa mara” akasema Meshack
Jumbo
“Hata mimi nimefurahi
kufahamiana nawe mzee
Meshack.Mathew amekuwa
anakutaja mara kwa mara”
akasema Theresa
“Kuna lolote mmelipata huko
mlikoenda? Meshack Jumbo
akamuuliza Mathew
“Tulikwenda kuonana na bi
April Hudson Mubara mjane wa
rais Anorld.Tulitaka kufahamu
endapo kuna kitu chochote
anaweza akatueleza cha kutusaidia
katika uchunguzi wetu lakini hatukuweza kupata chochote
kwani April anadai Anorld hakuwa
anamshirikisha katika mambo
yake .Mshirika mkuu wa rais
Anorld ambaye alikuwa
anayafahamu mambo yake meng
hata yale ya siri ni kanali Sebastian
Matope.Hatukuweza kupata
chochote kutoka kwake na tukiwa
njiani tukirudi unanipa taarifa ile
ya kustusha kuhusu
Fakrim”akasema Mathew
“Hata mimi nilistuka
nilipopewa taarifa ile na
Jimmy.Nimejiuliza kwa nini
Fakrim auawe leo? Waliomuua ni
nani? Ni majambazi?Baada ya
kutafakari nimegundua
waliomuua Fakrim wamenifanya hivyo kwa sababu maalum na
kubwa kuna jambo wanalificha na
hivyo inatupa sisi picha kwamba
Fakrim alikuwa anahusika na kwa
namna fulani katika ajali ile ya
ndege ya rais Anorld.Yawezekana
CIA au watu wanaomtumia
wamefahamu kwamba tayari
amefahamika na njia pekee ya
kuendelea kulifanya jambo hili
kuwa fumbo ni kumuua ili tusipate
chochote toka kwake.Mathew ule
mwanga mdogo uliousema jana
kwamba umeanza
kuonekana,unazidi kuongezeka na
tukiufuata kwa umakini tunaweza
kufika nuruni.Unaweza kufanikiwa
kulifumbua fumbo hili” Akasema
Meshack Jumbo “Jimmy hajakupigia tena
kukupa habari zaidi kuhusiana na
Fakrim?
“Hapana bado lakini
namuamini ni mtu wangu wa
karibu.Atatusaidia sana” akasema
Meshack Jumbo na kusimama
“Mathew kama hutojali kuna
kitu naomba ukanisaidie katika
maktaba yangu.Kuna jambo
limenishinda” akasema Meshack
Jumbo
“Theresa naomba nimuibe
Mathew mara moja kuna kitu
nataka akanisaidie katika
kompyuta yangu maktaba.Unajua
sisi tumekwisha kuwa wazee,ila
anarudi sasa hivi,jisikie nyumbani tafadhali” akasema Meshack
Jumbo
“Usijali mzee hakuna tatizo”
akasema Theresa na Mathew
akaongozana na Meshack Jumbo
wakaelekea ndani hadi katika
maktaba ya Meshack.
“Mathew nimekuleta huku ili
tuzungumze.Sikutaka tuzungumze
mbele ya Theresa.Kuna mambo
mawili ambayo nataka nikueleze
kwanza ni kuhusiana na wazo la
kumshirikisha huyu mwanadada
Theresa katika operesheni hatari
kama hii.Hili si wazo zuri hata
kidogo.Sikatai kwamba unahitaji
mtu wa kukusaidia lakini si
Theresa.Hafai kuongozana nawe
hata kidogo kwani jambo hili linaonyesha kwamba lina mtandao
mrefu na linawahusisha hadi CIA
kwa hiyo ni jambo la hatari
sana.Unahitaji msaidizi ambaye
ana uwezo mkubwa wa kujilinda
na kukulinda hata wewe kitu
ambacho huyu Theresa
hana.Nakushauri ukitoka hapa
mrejeshe ikulu akaendelee na
shughuli zake za kumuandikia rais
hotuba na kama kuna kitu
chochote utakihitai toka kwake
utawasiliana naye na si
kuongozana naye.Nadhani
umenielewa Mathew” akasema
mzee Jumbo
“Nimekuelewa mzee Jumbo na
hata mimi nimekwisha liona hilo
na nilikuwa nina mawazo kama hayo.Jambo hili ni pana sana
nakumuweka Theresa karibu
yangu ni kumuweka katika hatari
zaidi.Nitaachana na
Theresa.”akasema Mathew
“Good.Jambo la pili ni
kuhusiana na mauaji ya
Fakrim.Muda mfupi kabla hajafika
hapa Jimmy Snow amenipigia simu
na kunieleza kwamba mmoja kati
ya watu waliokuwa wanamsaidia
kumchunguza Fakrim ni binti yake
Camilla ambaye anafanya kazi
FBI.Anasema kwamba baada ya
mauaji yale kutokea Camilla na
wenzake walifanikiwa kuchukua
simu na kompyuta kama
nilivyokueleza .Wamevifanyia
uchunguzi wa haraka haraka na kugundua kwamba mtu wa
mwisho kuzungumza na Fakrim
katika simu alikuwa ni Nathan
Carter ambaye walipomchunguza
vizuri wamegundua kwamba ni
mchumba wa rais wa Tanzania
.Wakati wakiendelea na uchunguzi
kuhusiana na Nathan Carter kuna
jambo likatokea,Camilla tayari
ameingia matatizoni kufuatia
kuonekana katika eneo la tukio
akichukua kompyuta na simu ya
Fakrim kwani yeye ndiye
aliyekuwa kiongozi wa vijana
waliotumwa kwenda
kumchunguza Fakrim.Tayari
ameanza kusakwa ili ahojiwe kwa
hiyo Camilla amekimbilia Mexico
na toka hapo atakwenda hadi Cuba na lengo ni kutafuta njia ya kuweza
kukimbilia nchini Urusi aliko baba
yake.Nimemshauri Jimmy kwamba
kwa nini Camilla asije nchini
Tanzania ili asaidiane nawe?
Camilla anaweza kuwa msaada
mkubwa sana kwako katika
operesheni hii.Jimmy amekubali
na atawasiliana na Camilla
atakapokuwa amefika
Havana.Endapo akikubali litakuwa
ni jambo jema sana kwetu.Una
wazo gani kuhusu hilo?
“Sina cha kuongeza hapo
mzee.Umefanya kitu kizuri
kumshauri Jimmy kuhusu Camilla
kuja Tanzania.Naamini atakuwa na
msaada mkubwa
kwetu.Kilichonistua zaidi ni kusikia kwamba Nathan Carter ni
jasusi wa siri wa CIA.Huyu ni
mchumba wa rais Dr Vivian na
inaonekana amepandikizwa
makusudi kabisa karibu na rais
kwa lengo maalum” akasema
Mathew
“Kama Nathan ni CIA basi ni
wazi alikuwa na kazi maalum.CIA
wana mbinu nyingi sana za kuweza
kupata taarifa mbali mbali
wanazozitaka kwa hiyo si kitu cha
kushangaza kuona kwamba hata
Nathan aliwekwa hapa kimkakati”
akasema Meshack
“Kwa mujibu wa maelezo
aliyonipa Theresa,Nathan na Dr
Vivian kwa sasa wana mgogoro
katika mahusiano yao na mipangya ndoa yao
imevurugika.Nimeshuhudia leo
Nathan akimpigia simu Theresa na
akagoma kupokea kwa agizo la
rais.Sijajua nini sababu ya
mgogoro huo.Nadhani kuna
ulazima wa kuuchimbua uhusiano
huo wa Dr Vivian na Nathan kujua
namna ulivyoanza na pengine
tunaweza kufahamu lengo la
Nathan.Yawezekana kutokana na
kuzama mapenzini Dr Vivian
hamjui mpenzi wake ni mtu wa
aina gani kwani mapenzi ni
upofu.Wakati tukiendelea
kumchunguza Nathan Dr Vivian
hapaswi kufahamishwa
chochote.Uchunguzi utafanyika
kimya kimya.Kingine tutakachokifanya ni kuhakikisha
Nathan anakuja
Tanzania.Nitazungumza na
Theresa yeye atafanya mipango ya
siri ili Nathan aweze kuja Tanzania
kwa siri bila ya Dr Vivian kujua.Dr
Vivian akifahamu kwamba mdogo
wake amefanya jambo hili kwa siri
linaweza kuleta mgogoro baina
yao lakini litatusaidia sisi kuweza
kumchunguza na kumfahamu
vyema Nathan ni nani.Niachie
suala hili nitalifanyia kazi”
akasema Mathew halafu wakarejea
mahala walikomuacha Theresa
Mathew na Theresa wkaaga na
wakaondoka.
Kwa mujibu wa maelezo
aliyonipa Theresa,Nathan na Dr
Vivian kwa sasa wana mgogoro
katika mahusiano yao na mipango
ya ndoa yao
imevurugika.Nimeshuhudia leo
Nathan akimpigia simu Theresa na
akagoma kupokea kwa agizo la
rais.Sijajua nini sababu ya
mgogoro huo.Nadhani kuna
ulazima wa kuuchimbua uhusiano
huo wa Dr Vivian na Nathan kujua
namna ulivyoanza na pengine
tunaweza kufahamu lengo la
Nathan.Yawezekana kutokana na
kuzama mapenzini Dr Vivian
hamjui mpenzi wake ni mtu wa
aina gani kwani mapenzi ni
upofu.Wakati tukiendelea
kumchunguza Nathan Dr Vivian
hapaswi kufahamishwa
chochote.Uchunguzi utafanyika
kimya kimya.Kingine
tutakachokifanya ni kuhakikisha
Nathan anakuja
Tanzania.Nitazungumza na
Theresa yeye atafanya mipango ya
siri ili Nathan aweze kuja Tanzania
kwa siri bila ya Dr Vivian kujua.Dr
Vivian akifahamu kwamba mdogo wake amefanya jambo hili kwa siri
linaweza kuleta mgogoro baina
yao lakini litatusaidia sisi kuweza
kumchunguza na kumfahamu
vyema Nathan ni nani.Niachie
suala hili nitalifanyia kazi”
akasema Mathew halafu wakarejea
mahala walikomuacha Theresa
Mathew na Theresa wkaaga na
wakaondoka.
ENDELEA
Ni siku iliyotawaliwa na
vikao mfululizo vya
kazi.Kwanza Dr Vivian
alikutana na kufanya mazungumzo
na balozi wa marekani nchini
Tanzania halafu akakutana pia
nakufanya mazungumzo na balozi
wa umoja wa Ulaya.Wote hawa
walikuja kuzungumza naye
kuhusiana na mpango wake wa
kutaka kuanzisha mahusiano na
Korea Kaskazini.Waliwasilisha
salamu za viongozi wao lakini
walirejea kama walivyokuja kwani
msimamo wa Dr Vivian
haukubadilika.Aliwasisitizia
kwamba azma yake ya
kushirikiana na Korea Kaskazini
iko pale pale.Baada ya kuonana na mabalozi wale alikutana na
watendaji kadhaa wa serikali
halafu akakutana na mjumbe
maalum toka kwa rais wa Iran
aliyemtumia salamu
maalum.Katika salamu zake,rais
wa Iran alimuhakikishia Dr Vivian
kwamba yeye na serikali yake
watamuunga mkono katika
mpango wake wa kutaka
kuanzisha mashirkiano na Korea
Kaskazini.Alipomaliza maongezi
na mjumbe huyo maalum kutoka
kwa rais wa Iran,alitaarifiwa
kwamba rais wa China alikuwa
katika laini ya simu kwa ajili ya
mazungumzo.Dr Vivian
akaahirisha kwenda kula chakula cha mchana ili kuzungumza na rais
wa China
“Mr Wang Jing Xu habari yako”
akaanzisha maongezi Dr Vivian
“Habari nzuri kabisa Dr
Vivian.Habari za Dar es salaam?
“Huku kwema.Habari za
Beijing?
“Hapana siko Beijing.Niko
hapa New york kuhudhuria
mkutano wa baraza kuu la umoja
wa mataifa lakini nategemea
kuondoka mara tu
nitakapohutubia hapo kesho”
Akasema rais Wang
“Mimi tayari nimekwisha
ondoka baada ya kutoa hotuba
yangu na sikupata wasaa wa
kuweza kusalimiana nawe” “Usijali Dr Vivian,nimekupigia
kwanza kukupa pongezi nyingi
kwa hotuba yako nzuri uliyoitoa
katika baraza kuu la umoja wa
mataifa.Ni hotuba nzuri na uliitoa
kwa wakati na sehemu
sahihi.Afrika ilisubiri sana kupata
kiongozi mwenye msimamo na
mtazamo kama wewe.Pamoja na
vitisho kuhusiana na vikwazo vya
kiuchumi ambavyo Tanzania
inatishiwa kuwekewa,nakuomba
usilegeze msimamo wako.Usirudi
nyuma hata hatua moja.Shikilia
msimamo wako hapo hapo
uliposhika.Utakapolegeza
msimamo litakuwa ni anguko
lako.Kwa vile umeamua kuingia
katika vita hii,silaha yako kubwa ya kwanza ni msimamo.Usijaribu
kuweka chini silaha yako hiyo na
endelea kupambana hadi ushindi
upatikane.
China tuko nyuma yako na
tutakuunga mkono katika kila
hatua na hata katika hotuba yangu
nitakayoitoa mbele ya baraza kuu
la umoja wa mataifa nitaweka wazi
msimamo wa China kuhusiana na
kuiunga mkono Tanzania kufaya
biashara na taifa lolote duniani
bila kuwekewa mipaka.Siku zote
China itasimama upande wa
Tanzania.Marekani wametishia
kuwasilisha vikwazo kwa umoja
wa mataifa kwa ajili ya kuweka
vikwazo vikali vya kiuchumi kwa
Korea Kaskazini na nchi washirika wake ikiwamo Tanzania lakini sisi
China tutatumia kura yetu ya
turufu kuhakikisha hilo jambo
halifanikiwi.Hatuko tayari kuona
Tanzania inawekewa vikwazo eti
kwa sababu ya kulinda na kutumia
rasilimali zake.Nchi yoyote
itakayothubutu kuichokoza
Tanzania kwa namna yoyote ile
iwe ndogo au kubwa itakutana na
mkono wa China na tutamuadhibu
vikali.Tutaungana na mataifa
ambayo yako tayari na
yametangaza kuiunga mkono
Tanzania dhidi ya vitisho vya
Marekani na washirika wake na
tutahakikisha tunaisaidia
Tanzania kwa kila namna tutakavyoweza ili iweze kukua
kiuchumi
Rais wa Korea kaskazini
amenipigia simu na kunieleza
kwamba mlizungumza kwa kirefu
simuni kuhusiana na kuanzishwa
kwa mashirikiano baina ya nchi
zenu. Nimefurahishwa na hatua
ambazo umeanza kzichukua
kuhusiana na suala hili .Popote
patakapokuwa na mkwamo na
kuhitaji msaada usisite kuniomba
msaada na nchi yangu iko tayari
muda wowote kukusaidia.Naomba
pia utumie mashirikiano hayo
utakayoyajenga na Korea
Kaskazini kuishawishi serikaliya
Korea Kaskazini kuhusiana na
majaribio yake ya makombora katika bahari ya Pacific” akasema
rais Wang
“Nakushukuru sana
mheshimiwa rais kwa kuniunga
mkono.Binafsi nimeamua kuingia
katika vita hii kubwa ya uchumi
dhidi ya mataifa makubwa na
nitasimama imara sintageuka
nyuma.Nashukuru mataifa rafiki
ambayo yanasimama na sisi katika
vita hii yakiongozwa na
China.Endeleeni kutuunga mkono “
akasema Dr Vivian
“Rais Kim alinieleza
kuhusiana na ombi lako la kutaka
kujengewa kinu cha nyuklia kwa
ajili ya kuzalisha nishati ya
umeme.Hilo ni wazo zuri sana na
endapo likifanikiwa litaweza kuleta mageuzi makubwa sana ya
kiuchumi nchini
Tanzania.Ninaliunga mkono na
niko tayari kushirikiana na Korea
Kaskazini katika kujenga kinu
hicho muhimu sana kwa uchumi
wa Tanzania.Mipango yako hii
itaipaisha Tanzania kiuchumi
licha ya tishio la vikwazo”
“Ni kweli mheshimiwa Wang
,nimezungumza na rais Kim
kuhusiana na kujengewa kinu cha
nyuklia hapa nchini Tanzania ili
tuweze kujitosheleza kwa nishati
ya kutosha ya umeme kwani
Tanzania kwa sasa tunafanya
mageuzi makubwa ya kiuchumi na
tunajenga viwanda vingi hivyo
nishati ya uhakika ya umeme inahitajika .Tunayo hazina kubwa
ya madini ya Urani kwa hiyo
tunataka kuwa wazalishaji
wakubwa wa umeme katika
ukanda wa Afrika mashariki kwa
kutumia madini ya Urani.Rais Kim
amelipokea wazo langu na
ameahidi kulifanyia kazi” akasema
Dr Vivian na kuendelea na
maongezi mengine na
walipomaliza maongezi yao Dr
Vivian akaelekea kupata chakula
cha mchana
Walipotoka nyumbani kwa
Meshack Jumbo,Mathew na
Theresa walielekea moja kwa moja
katika hoteli moja maarufu
ambayo Mathew hupenda sana
kwenda kupata chakula.Ni hoteli
iliyoko kandoni mwa bahari kwa
hiyo mchana huu kulikuwa na
upepo mzuri .Mathew alipenda
sana kula samaki na ndiyo maana
hupenda kuja katika hoteli hii
inayosifika kwa kupika vizuri aina
mbali mbali ya samaki.Chakula
walichoagiza kikaletwa wakaanza
kula taratibu huku wakipulizwa na
upepo wa bahari “Theresa kuna mambo mawili
nahitaji kuzungumza nawe”
akaanzisha mazungumzo Mathew
“Kwanza kabisa ninapenda
nikushukuru sana kwa msaada
mkubwa ambao umenisaidia toka
jana tulipoanza kulishughulikia
hili suala.Umenisaidia nimeweza
kupata nyaraka mbali mbali
ambazo nisingeweza kuzipata
kama ningekuwa mwenyewe.Hata
hivyo suala hili linazidi kuchukua
sura mpya kila uchao na mpaka
hivi sasa linaonekana kuwa ni
suala linalovuka mipaka ya
nchi.Marekani inaonekana
kuhusika katika jambo hili ingawa
bado hatuna uhakika mkubwa
hadi hapo utakapofanyika uchunguzi .Kwa hapa tulipofika
suala hili limeanza kuonyesha si
suala rahisi na huko tuendako
kunaonekana kuwa na giza nene
na hatari kubwa kwa hiyo
nimefikiria sana na nimeona
itakuwa vyema endapo nitakuacha
ukaendelee na shughuli zako za
kawaida na mimi niendelee peke
yangu na uchunguzi
huu.Nimefanya hivyo kwa sababu
sitaki kukuweka katika
hatari.Umeona mwenyewe kadiri
tunavyoendelea kulichunguza hili
suala ndivyo mambo mengi
yanavyozidi kuibuka na hivyo
kuzidisha hatari kwa upande
wetu.Kuwa karinu na mimi si suala
zuri kwa sasa kwani hawa watu wanaohusika na matukio yote
mawili ya kuanguka kwa ndege ya
rais na kuuawa kwa baba yako ni
mtandao mrefu na wanaweza
wakafahamu kwamba tayari
tumeanza kuwafuatilia kwa hiyo
watajihami.Sitaki uingie katia
matatizo hivyo kuanzia mchana
huu utarudi ikulu.Nitampigia simu
Dr Vivian na kumtaarifu kuhusu
suala hili.Endapo nitahitaji msaada
wowote kutoka kwako
nitakujulisha lakini si kwa
kuongozana huku nje kama hivi
.Muda wowote hatari inaweza
ikatokea na tukashambuliwa hivyo
unahitajika uwe ni mtu mwenye
uwezo wa kujilinda na kumlinda
mwenzako” akasema Mathew Ukapita ukimya mfupi kidogo
,Theresa akasema
“Nilikuwa naisubiri kwa hamu
kubwa kauli hii kwani jambo hili
limeniogopesha mno toka mwanzo
ila sikuwez kumkatalia dada
aliponiomba niungane nawe
nikusaidie.Siwezi kusema hapana
kwani ni kitu nilichokisubiri hivyo
nakushukuru kwa maamuzi hayo
na endapo utahitaji kitu chochote
kile nitakuwa tayari kukusaidia”
akasema Theresa na Mathew
akatabasamu
“Nafurahi kusikia
hivyo.Usikasirike pale
nitakapokusumbua hata usiku wa
manane” “Usihofu Mathew.Nitakuwa
nalala jicho moja huku nikiamini
kwamba kuna mtu yuko nje halali
anafanya kazi ya kutafuta ukweli
kuhusiana na wazazi wetu na
nitakuombea sana”
“Ahsante.Jambo la pili ambalo
nataka liwe ni baina yangu mimi
na wewe na asifahamu mtu
mwingine yeyote na hasa dada
yako Dr Vivian.”
“Ni jambo gani hilo?
“Uliniambia kwamba Dr
Vivian na mpenzi wake
wamekorofishana?
“Ndiyo wamekorofishana
.Kuna nini kwani?
“Ninahitaji huyo mpenzi wa Dr
Vivian aje Tanzania.Unaweza kunisaidia kumfanya aje Tanzania
haraka?
Theresa aliyekuwa anaipeleka
glasi ya kinywaji mdomoni
akaishusha na kuiweka
chini.Alionekana kushtuka
“Unamtaka Nathan? Kwa nini ?
“Ninamuhitaji awepo hapa
Tanzania karibu na Dr Vivian”
akasema Mathew
“Mathew itakuwa vyema
endapo utanieleza kusudi la
kumtaka Nathan aje Tanzania ili
nikiridhika nione nitafanya nini
kulitekeleza hilo”
“Theresa kwa kuwa nahitaji
sana msaada wako nitakueleza
ukweli ila nakuomba sana sana hii
iwe ni siri yako na usimueleze mtu yeyote hata Dr Vivian”akasema
Mathew
“Sina kawaida ya kumficha
jambo dada yangu lakini kama
kutakuwa na ulazima wa kuficha
basi itanibidi kufanya hivyo. Ni
jambo gani hilo nieleze Mathew
nina hamu ya kulifahamu”
akasema Theresa.Mathew
akanywa funda moja la mvinyo na
kusema
“Kuna tetesi japo hazina
uhakika bado kwamba Nathan
ambaye ni mchumba wa dada yako
,ni jasusi toka shirika la ujasusi la
CIA”
“What ?! Theresa akashangaa
na kuweka kijiko chini
“Tafadhali usistuke Theresa.” “Lazima nistuke
Mathew.Nathan ni mpelelezi?
“Kuna tetesi hizo kwamba ni
jasusi wa CIA na kuna uwezekano
yuko katika shughuli maalum hapa
Tanzania kwa hiyo tunahitaji
kumchunguza ili kuupata ukweli
kama kweli yeye ni CIA na
ametumwa kufanya kazi gani hapa
Tanzania? akasema Mathew.
“Mathew nimeogopa sana kwa
hili uliloniambia.Ni vigumu sana
kuamini lakini kwa namna
nilivyokuwa namuona yule jamaa
sikuwa namuelewa elewa na
ninaweza kukubaliana nawe
kwamba ni mpelelezi na yuko hapa
kwa shughuli maalum” “Kama nilivyokwambia
Theresa kwamba ukiingia katika
kazi hizi kuna mambo mengi ya
kuogofya na kushangaza
utakutana yao kama hili la
Nathan.Naamini hata Dr Vivian
hawezi kukubali kama Nathan
mchumba wake ni jasusi wa
CIA.Hata hivyo tunatakiwa kupata
uhakika kwanza kama kweli ni CIA
na ametumwa kufanya kazi gani
ndipo tutamueleza rais”
Theresa akamtazama Mathew
kwa uoga.
“Unataka nifanye nini
Mathew? Akauliza kwa sauti ya
woga
“Jana tukiwa garini alikupigia
simu lakini hukupokea.Nataka umpigie simu na kuzungumza naye
umwambie kwamba unataka
umsaidie ili aweze kurudiana na
dada yako na ili kufanya hivyo
itamlazimu aje Tanzania.Jiweke
upande wake na asigundue
chochote kama hiki ni kitu cha
kupanga.Mweleze kwamba
asimpigie simu Dr Vivian
kumjulisha kama anakuja
Tanzania bali iwe ni siri yenu”
akasema Mathew
“Nini kitatokea atakapokuja?
“Atakapokuja wewe utakuwa
umemaliza kazi yako na litabaki
jukumu langu kumchunguza na
endapo nitahitaji msaada wako
wowote nitakujulisha” akasema
Mathew “Nitajitahidi kufanya hivyo
lakini nimeogopa sana
Mathew.Sikutegemea kabisa
kusikia habari kama hii” akasema
Theresa
“Usiogope tafadhali
.Unapaswa kuwa jasiri sana ili
tuweze kulifanikisha suala hili”
Theresa akafikiri kidogo na
kuuliza
“Mathew unadhani dada
Vivian yuko katika hatari?
“Inawezekana.Kama Nathan ni
CIA basi lazima yuko karibu na
dada yako kwa shughuli maalum
na hii inatoa picha kwamba Dr
Vivian hayuko salama lakini usiwe
na hofu kwani muda si mrefu
tutalifahamu jambo hili na kumuondoa Dr Vivian katika
hatari” akasema Mathew na
Theresa hakuweza kuendelea tena
kula kutokana na woga
alioupata.Ukimya ukatanda
mezani,Mathew akaendelea kula
kimya kimya.Baada ya muda
Theresa akasema
“Nina wazo Nathan.”
“Karibu”akasema Mathew
“Umenitaka nirejee ikulu
nikaendelee na shughuli zangu za
kawaida lakini sitaki kurejea ikulu
kwa sasa nataka niutumie muda
huu kupumzika.Dada akikuuliza
mweleze kwamba bado uko na
mimi.Unaweza kunisaidia kwa hilo
tafadhali? “Usijali Theresa nitakusaidia
ila jitahidi kwa kila uwezavyo
Nathan aweze kuja Tanzania.”
“Kuhusu Nathan hilo lisikupe
shida kwani atakuja Tanzania
.Nitafanya kila niwezalo na
atakuja”
“Basi usitie shaka nami
nitafanya kama ulivyoniomba
sintamueleza chochote Dr Vivian”
akasema Mathew na kuendelea
kula .Baada ya kumaliza kula
wakaondoka moja kwa moja hadi
nyumbani kwa Theresa .Mathew
akamuacha hapo na kuondoka
zake.
“Nimestuka na kuogopa sana
kusikia kwamba Nathan ni
CIA.Anatafuta nini kwa dada? Kuna kitu gani ametumwa akichunguze?
Akawaza Theresa baada ya
Mathew kuondoka
“ Kwa mujibu wa maelezo ya
dada n kwamba alianza mapenzi
na Nathan wakati angali anasoma
chuo.Inawezekanaje Nathan awe
anamchunguza kwa muda huo
wote? Na kama anamchunguza ni
kuhusu nini?Hili jambo
linachanganya sana lakini ngoja
nimuachie Mathew alichunguze
halafu tutaufahamu ukweli.”
Akawaza na kuchukua simu yake
akazitafuta namba za Nathan na
kutaka kumpigia akasita
“Ninasita kabisa kumpigia
huyu jamaa.Halafu ni vipi endapo
dada Vivi akifahamu kwamba nimemzunguka na kufanya
mawasiliano na Nathan bila ya
yeye kujua wakati wamekwisha
achana?Hii inaweza kuleta
msuguano kati yetu .Lakini
nisipofanya hivyo Mathew
atashindwa kufanya uchunguzi
wake na hatutajua nia ya Nathan
kwa dada Vivi.Ngoja nimpigie simu
na kitakachotokea tutaeleweshana
huko mbele ya safari” akawaza
Theresa na kumpigia Nathan.Simu
ikaita bila kupokelewa na
kukatika.
“Ni saa tisa mchana huku
kwetu ambapo ni asubuhi kwa
Marekani ,yawezekana Nathan
akawa amelala bado.Ngoja
nimjaribu tena.Kabla hajapiga simu yake ikaita alikuwani
Nathan,Theresa akaipokea
“Hallow Nathan” akasema
Theresa
“Habari yako
Theresa,samahani sikuweza
kupokea simu yako nilikuwa
bafuni .Habari za Dar es salaam?
“Huku kwema kabisa.Habari
za New york?
“Huku kwema pia.Nimekuwa
najaribu kukupigia lakini
haupokei simu yangu.Kwa nini
Theresa?
“Utanisamehe sana
Nathan.Sikuweza kupokea simu
zako lakini si kwa makusudi bali ni
kutokana na kubanwa na jukumu
lingine wakati uliponipigia.Siwezi kushindwa kupokea simu yako na
hata wewe unafahamu hilo.Vipi
unaendeleaje na dada Vivi? Kuna
hatua yoyote mmeifikia hadi hivi
sasa?
“Hakuna chochote
tulichoongea hadi sasa kwani
Vivian hataki kupokea simu
yangu.Nimejaribu sana kumpigia
ila hapokei kabisa na katika laini
zake nyingine amenifungia.”
“Dah ! lakini Nathan hebu
nieleze nini hasa chanzo cha wewe
na dada kuingia katika mgogoro
kwa wakati huu ambao
mmebakisha miezi miwili tu
mfunge ndoa?
“Theresa kilichotokea na
kutufarakanisha ni kitu kidogo sana huwezi kuamini.Ni kuhusiana
na mtoto.Nilitaka kufahamu
msimamo wake kuhusiana na
kuzaa mtoto tutakapofunga ndoa
na hapo ndipo ugomvi ulipoanzia
na mwisho akasema kwamba kila
mmoja aendelee na maisha
yake.Mpaka sasa bado siamini
kama kweli eti mimi na Vivian
tumetengana” akasema
Nathan.Theresa akavuta pumzi
ndefu na kuuliza
“Nathan naomba uniambie
kitu kimoja.Je unampenda kweli
Vivian?
“Ninampenda zaidi ya
ninavyoweza kukueleza.Siwezi
kuuelezea upendo wangu kwake.Ni
zaidi ya upendo” “Kama kweli unampenda kiasi
hicho basi usimuache aende.Tafuta
namna ya kulipigania penzi lenu
ambalo mmetumia muda mrefu
kulijenga.”
“Najitahidi sana Theresa
kutaka kulipigania penzi letu
lakini inaonekana mwenzangu
tayari amekwisha fanya maamuzi
na unajua dada yako alivyo akisha
amua jambo huwa harudi
nyuma.Msimamo wake umebaki
ule ule kwamba kila mmoja
aendelee na maisha yake”
Ukapita ukimya kidogo na
Theresa akasema
“Nathan mimi sijafurahishwa
kabisa na hiki kilichotokea kati
yenu na niko tayari kusaidia ili jambo hili likae vizuri.Nitafanya
kila lililo ndani ya uwezo wangu
kwani Theresa hawezi
kunishinda.Nitazungumza naye na
atanielewa”
“Kweli Theresa? Akauliza
Nathan
“Kweli kabisa.Nimeumizwa
sana kuona mmefikia hatua
hii.Penzi lenu lilikuwa ni mfano wa
kuigwa na kila mtu alitamani kuwa
kama ninyi.Sitaki mapenzi yale
yaishie hewani.Nathan wewe ndiye
pekee mwanaume unayemfaa dada
yangu,hivyo nitaingilia kati na
kuliweka sawa hili jambo na
mambo yataendelea kama
yalivyopangwa” “Nashukuru sana Theresa kwa
hilo unalokwenda kulifanya.Hapa
nilipo nimechanganyikiwa na sijui
nifanye nini kwani marafiki zangu
wote wamekwishajiandaa na
wengine tayari wamekata hadi
tiketi wakijiandaa kwa safari ya
kuja Tanzania katika harusi yangu
kwa hiyo nashindwa namna ya
kuwaeleza kwamba hakutakuwa
na harusi tena.Tafadhali naomba
unisaidie Theresa na ndiyo maana
nimekuwa nakupigia simu
nikitaka kukuomba msaada wako
kwani nafahamu uwezo wa
kuliweka sawa jambo hili unao”
“Mimi nitakusaidia Mathew
kama nilivyokuahidi lakini kuna
kitu kimoja unapaswa kukifanya” “Ni kitu gani Theresa?
“Unapaswa kuja Tanzania
haraka iwezekanavyo lakini njoo
kimya kimya bila ya kumtaarifu
Vivian na wala usimpigie
simu.Mimi nitamaliza kila kitu na
halafu utamshangaza kwa kutokea
ghafla.Nitakupa maelekezo yote
utakapofika huku lakini jitahidi
sana kuja Tanzania haraka
iwezekanavyo.Suala hili haliwezi
kutatuliwa na wewe ukiwa mbali
.Unapaswa kuwa karibu ili
muweze kuonana na kuongea ana
kwa ana”
“Hilo si tatizo Theresa.Ninao
uwezo wa kuja haraka
iwezekanavyo.Kwa kuwa suala hili
ni la muhimu sana kuliko mambo yangu mengine,kaka yangu ana
ndege yake binafsi nitaongea naye
asubuhi hii kama naweza kutumia
ndege yake kuja Tanzania.Endapo
akikubali basi hadi kesho saa nne
au tano asubuhi nitakuwa
nimefika Dar es salaam.Theresa
suala hili ninalipa umuhimu
mkubwa mno.Vivian ni kila kitu
katika maisha yangu.Niko tayari
kukosa kila kitu maishani lakini
nimpate yeye tu.Kwa umuhimu
wake huo nitakuja Tanzania
haraka sana.Nataka
nikudhihirishie namna gani Vivian
alivyo muhimu kwangu.” Akasema
Nathan
“Sawa Nathan basi endelea
kufanya taratibu za safari kama utapata ndege binafsi au utapanda
ndege za abiria utanijulisha ila
jitahidi kwa kila uwezavyo uweze
kufika hapa Tanzania haraka
uwezavyo” akasema Theresa na
kukata simu na kuitupa kitandani
“Kwa namna anavyoongea
utadhani kweli ana mapenzi
makubwa sana kwa Vivian kumbe
ana kitu anakitafuta na ndiyo
maana amefurahi sana kusikia
kwamba ninataka kuwaunganisha
tena na Vivian.Amefurahi kwa
kujua kwamba endapo
wakirudiana basi mipango yake
itaendelea kama kawaida.Mambo
kama haya ndiyo yanayonifanya
nisiweze kumweleza mtu yeyote
hata dada kile ninachofahamu kuhusiana na kuanguka kwa ndege
ya rais Anord au hata kifo cha baba
na zaidi sana Football.Tena
nimekumbuka itanibidi
kumuomba dada ulinzi kwani nina
wasiwasi kwa siku hizi mbili
ambazo nimekuwa na Mathew na
nimekuwa nauliza uliza maswali
na kutaka nyaraka totauti tofauti
kuhusiana na ajali ya ndege ya rais
ninaweza kuwa nimeanza
kumulikwa kwani huwezi kujua
nani anakufuatilia nyuma kama
ambavyo ni vigumu kuamini kama
Nathan ni jasusi wa CIA.” Akawaza
Theresa.
Kwa upande wa Mathew
baada ya kuachana na Theresa
akaenda mahali kunakojengwa kiwanda chake kufuatilia
maendeleo ya ujenzi halafu
akarejea nyumbani.Kitu cha
kwanza alichokifanya alipofika
nyumbani ni kumpigia simu rais
Dr Vivian
“Habari yako Mathew”
Akasema Dr Vivian
“Mheshimiwa rais samahani
sana kama nimekuvurugia
shughuli zako kwa simu hii”
“Hapana usijali kabisa
Mathew haujaharibu chochote
isitoshe ukinipigia ninafurahi zaidi
kwani mimi kutokana na kutingwa
sana na kazi ninashindwa hata
kukupigia.Vipi maendeleo yako?
Akauliza “Ninaendelea vyema
mheshimiwa rais.Nimekupigia
kuomba kuonana nawe usiku wa
leo kama hautakuwa na jukumu
lingine la kikazi”
“Mimi nipo kazini kila wakati
Mathew na sina muda wa
kupumzika.Hata usiku huwa
ninafanya mikutano kwa njia ya
simu na watendaji wangu.Hata
hivyo niko tayari kusimamisha
shughuli zangu nyingine zote kwa
ajili yako.Unahitaji kuonana nami
kuanzia saa ngapi?
“Kuanzia saa mbili za usiku
mheshimiwa rais”
“Kama ni saa mbili za usiku
kwa nini basi usiwe mgeni wangu
na tukaungana kwa chakula cha usiku huku tukiendelea na
maongezi?
“Hakuna tatizo kwa hilo
mheshimiwa rais “
‘Sawa Mathew nakutegemea
muda huo wa saa mbili za usiku”
“Ahsante mheshimiwa rais”
akasema Mathew na kukata simu
halafu akampigia Meshack Jumbo
Ahsante mheshimiwa rais”
akasema Mathew na kukata simu
halafu akampigia Meshack Jumbo
“Mzee kuna lolote umepata
kutoka kwa Jimmy kuhusuCamilla?
Akauliza
“Ndiyo Mathew.Jimmy
amekuwa ananipigia kila pale
anapowasiliana na
Camila.Amenitaarifukwamba
Camilla yuko ndegeni hivi sasa
anaelekea Havana Cuba.Kutoka
pale ndipo atakapoanza kutafuta namna atakavyoweza kufika
Tanzania”
“Sawa mzee.Basi akifika
Havana asubiri pale mimi
ninafanya mpango wa usafiri wa
ndege ya kwenda kumchukua hapo
Havana na kumleta Dar es
salaam.Peniela ana shirika lake la
ndege linaitwa Penny
air.Nitamuomba msaada wa ndege
ikamchukue Camilla pale Havana
na kumleta Tanzania.Kitu kigumu
ilikua ni kutoka Marekani
anakotafutwa na kwa kuwa tayari
amekwisha ondoka Marekani basi
hakuna shaka atafika salama
Tanzania.” “Una hakika Peniela anaweza
akakubali kukusaidia?Meshack
Jumbo akauliza
“Ndiyo mzee.Hawezi kukataa
kwani mimi ndiye chanzo cha haya
mafanikio yake yote
aliyonayo.Usihofu kuhusu hilo
mzee.Mtaarifu Jimmy amueleze
Camilla kwamba akifika Havana
atulie hapo kwani ndege
inakwenda kumchukua kumleta
moja kwa moja Tanzania”
“Sawa Mathew.Vipi kuna
maendeleo yoyote ?
“Nimezungumza na Theresa
na amesema kwamba atafanya ila
awezalo kuhakikisha Nathan
anakuja Tanzania.Vile vile usiku
wa leo ninakwena kuonana na rais.Tayari nimekwisha zungumza
naye na amekubali tuonane usiku
wa leo.Kikubwa ninataka kujua
kuhusu mahusiano yake na
Nathan.Nataka kuchunguza kama
kuna kitu maalum Nathan
anachokitafuta toka kwa rais”
“Vizuri Mathew lakini kuwa
makini sana unapozungumza na
rais.Usimpe nafasi ya kugundua
kama unamchunguza
Nathan.Tumia ufundi mkubwa
katika kuuliza maswali
yako.Kingine cha muhimu wewe na
raisi wote mko karibu umri
sawa.Jizuie isitokee tamaa yoyote
kati yenu .”akasema Meshack
Jumbo na Mathew akacheka
kidogo “Usihofu mzee.Mimi
unanifahamu na hata utendaji kazi
wangu unaufahamu.”
“Ni angalizo nilikuwa natoa
Mathew.Sawa tutawasiliana tena
baadae utanijulisha kuhusiana na
hiyo ndege itakayokwenda
kumchukua Camilla.” Akasema
Meshack na kukata simu
“Mzee Jumbo ana wasiwasi
labda naweza kujikuta nimevutiwa
na rais” akawaza Mathew na
kucheka huku akizitafuta namba
za simu za Peniela akampigia.
“Hallo Mathew habari yako”
“Nzuri Peniela.Kabla
sijaendelea uko na mpenzio?
“Hapana kwa nini? “Sitaki ugomvi naye ndiyo
maana nikauliza mapema kama
uko naye karibu ili nikate simu”
“Hapana siko naye hapa
karibu.Unasemaje Mathew?
‘Kwanza kabisa ni kuhusiana
na siku ya kuzaliwa Anna Maria.”
“Ndiyo ni jumatatu
ijayo.Zimebaki siku mbili tu keshi
jumamosi na jumapili .”
“Umekwisha mnunulia zawadi
niliyokuomba?
“Tayari nimemchukulia ila
nimeificha hadi siku ya sherehe”
“Good”
“Bado hauna mpango wa kuja
Paris?
“Hapana siwezi kuja
Peniela.Nimetingwa sana huku” “Bado unafanya kazi ya rais
Vivian?
“Peniela naomba tusiende
huko.”
“Samahani nilitaka
tukujua.Anyway kwanini umepiga
simu?
“Juzi uliniuliza kama kuna
kitu unaweza ukanisaidia”
“Ndiyo nilikuuliza kama kuna
kitu naweza kukusaidia katika
kazi yako ukasema hapana”
“Sikuwa na kitu cha kuomba
kwa wakati huo lakini kwa sasa
ninahitaji msaada wako.”
“Unahitaji nini Mathew?
“Kuna mwadada mmoja
anaelekea Havana Cuba hivi sasa
na anahitajika kuja Tanzania.Ninaomba msaada wa
ndege ya kwenda kumchukua
Havana na kumleta Tanzania”
Ukimya wa sekunde kadhaa
ukapita Peniela akauliza
“Anaitwa nani? Ni mpenzi
wako?
“Anaitwa Camilla.Si mpenzi
wangu bali ni mtu muhimu sana na
maisha yake yako
hatarini.Tafadhali nakuomba
unisaidie Peniela huyu mtu aweze
kufika salama Tanzania” akasema
Mathew.
“Sawa Mathew naomba unipe
taarifa kamili za huyo mtu halafu
nitajua nini cha kufanya” “Ahsante Peniela nitakupa
taarifa zake baadae kidogo”
akasema Mathew na kukata simu
“Asingeweza kukataa.Pamoja
na kutengena lakini Peniela bado
ananipenda sana .Anyway sitakiwi
kuyawaza hayo kwa sasa.Ngoja
nijipumzishe kabla ya kwenda
kuonana na rais usiku wa leo”
akawaza Mathew na kujipumzisha
kitandani
***************
Saa moja na dakika ishirini za
jioni Mathew akiwa mbele ya kioo
chake kikubwa akijitazama kwa
mara ya mwisho kama
amependeza vya kutosha.Ni kweli alikuwa amependeza vya
kutosha.Usiku huu alikuwa
amevaa suti nyeusi iliyomkaa
vyema tayari kabisa kukutana na
rais Dr Vivian.Alionekana kweli
alikuwa bilionea kutokana na
mavazi yale ya gharama kubwa
aliyovaa.
“Sasa niko tayari kuonana na
mkuu wa nchi.Ikulu si mahala pa
kwenda umevaa hovyo hovyo.Ile ni
sehemu kubwa sana na ukienda
pale kuonana na mkuu wa nchi
unatakiwa uwe umejiandaa
vilivyo” akawaza Mathew huku
akimalizia kujipulizia uturi mzuri
wa gharama kubwa halafu
akaondoka kuelekea ikulu.Akiwa
njiani aliwasiliana na Theresa kuhusiana na jukumu alilokuwa
amemkabidhi la kuhakikisha
Nathan anakuja Tanzania bila ya
Dr Vivian kufahamu
chochote.Theresa alimjulisha
Mathew kwamba tayari
amekwisha wasiliana na Nathan na
kwa muda ule tayari alikwisha
anza safari ya kuja Tanzania.
“Theresa anafanya kazi nzuri
sana lakini itakuaje endapo dada
yake atafahamu kwamba yeye
ndiye aliyemuita Nathan
Tanzania?Utaibuka mgogoro kati
yao lakini nitaumaliza.Lazima
tumfahamu Nathan ana kitu gani
anakichunguza kwa rais.Nina
uhakika mkubwa kama Nathan ni
CIA basi ukaribu wake na Dr Vivian ni kwa ajili ya jambo fulani.Usiku
wa leo nitakapozungumza na rais
kuna kitu ninaweza nikakipata
kuhusiana na Nathan” akawaza
Mathew
Aliwasili ikulu saa mbili
kasoro dakika tatu kwa kuwa
alikuwa tayari na kibali cha
kumuwezesha kupita kuonana na
rais muda wowote hakupata shida
akaruhusiwa kuingia ndani ya
ikulu na kupokelewa kisha
akapelekwa moja kwa moja
sebuleni kwa Dr Vivian ambaye
kwa muda huo alikuwa chumbani
kwake naye akijiandaa.Baada ya
dakika zipatazo kumi akatoka
akiwa amependeza kwa gauni refu
jeupe lenye nakshi za kung’aa. “Mathew karibu sana.Umefika
kwa wakati”
“Ahsante sana mheshimiwa
rais.Ninaheshimu sana muda na
ndiyo maana nimefika kwa wakati
ule tuilokubaliana” akasema
Mathew
“Umependeza sana usiku wa
leo” akasema Dr Vivian huku
akitabasamu
“Hata wewe pia umependeza”
akasema Mathew na bila kupoteza
muda Dr Vivian akamkaribisha
katika chumba cha chakula
kulikokuwa kumeandaliwa
chakuls kizuri kwa ajili yao
“Vipi shughuli zako
zinakwendaje? Namaanisha
biashara zako” akaanzisha mazungumzo Dr Vivian wakati
wakipata chakula
“Shughuli zangu zinakwenda
vizuri.Wapo watu wanaosimamia
biashara zangu kwa hiyo hata
kama ninakuwa na majukumu
mengine sina wasiwasi”
“Unashughulika na biashara
gani?
“Kwa sasa ninajenga kiwanda
cha kuchonga vipuri vya magari na
mashine mbali mbali.Kitakuwa ni
kiwanda kikubwa hapa nchini”
“Oh ! Nimesikia kuhusiana na
kiwanda hicho.Kumbe ni cha
kwako!Hongera sana Mathew kwa
uwekezaji huu mkubwa
ulioufanya.Uko peke yako au una
ubia na mtu? “Hiki ni kiwanda changu na
ninakimiliki kwa asilimia mia
moja .Sina ubia na mtu yeyote”
akasema Mathew.
“Hongera sana .Umefanya
jambo la muhimu kuamua kuleta
uwekezaji huu mkubwa hapa
nyumbani kwani naamini
ungeweza kuupeleka sehemu
yoyote lakini ukaamua kurejea
nyumbani.Serikali yagu
inawahitaji sana wawekezaji
wazalendo kama ninyi na itafanya
kila iwezalo kuhakikisha
inawetengenezea mazingira
mazuri ya uwekezaji na unafuu wa
kufanya biashara”akasema Dr
Vivian “Nilipoachana na Peniela
nilitafakari sana kitu cha
kufanya.Nilitamani sana kufanya
uwekezaji hapa
nyumbani.Niliwatafuta washauri
wa kibiashara na wakanishauri
kuwekeza katika kiwanda cha
kuchonga vipuri vya magari na
mashine.Kwa hivi sasa hatuna
kiwanda cha kuchonga vipuri
mbalimbali vya magari na mashine
hivyo nikaamua kuwekeza
huko.Hata hivyo bado ninafanya
utafiti wa kuwekeza pia katika
kiwanda cha sukari ili kuongeza
upatikanaji wa sukari hapa
nchini.Nimewapa jukumu hilo
wataalamu wangu na wanalifanyia
kazi wakikamlisha utafiti wao basi nitaweza kuanza kujenga kiwanda
cha sukari pia”
“Unanifurahisha sana Mathew
kwa namna ulivyo na mtazamo wa
mbali.Nchi yetu kwa sasa bado ina
uhitaji mkubwa wa sukari.Bado
hatujaweza kujitosheleza kwa
sukari yetu inayozalishwa ndani
kwa hiyo tunalazimika kuagiza
kiasi cha sukari kutoka nje ya nchi
ili kuweza kukidhi
mahitaji.Endapo tutakuwa na kiasi
cha kutosha cha sukari basi pesa
tunazotumia kuagizia sukari nje ya
nchi tutazitumia kwa shughuli
nyingine.Nakuhakikishia
ushirikiano mkubwa sana katika
uwekezaji huo wako.Nitakupa
upendeleo mkubwa ili viwanda vyako viweze kukua na kuzalisha
ajira nyingi” akasema Dr Vivian
“Ahsante sana mheshimiwa
rais” akasema Mathew
“Mimi ndiye ninayepaswa
kukushukuru wewe kwani licha ya
kuwa na shughuli nyingi za
uwekezaji lakini umeamua kuacha
shughuli zote na kuja kunifanyia
kazi yangu.Ninapaswa
kukushukuru mno.”
“Usijali mheshimiwa rais.Hii
kazi imekwisha ingia katika
damu,ni kama daktari hata kama
amestaafu lakini bado haachi
kutibu watu.Japokuwa siko tena
katika shughuli hizo lakini
nilishindwa kusema hapana baada ya kuliona tatizo ulilonalo na
linanihitaji mno mimi”
“Ahsante.Ungeweza kusema
hapana lakini ulikubali kwa moyo
mmoja.By the way kuna
maendeleo yoyote hadi hivi sasa?
Akauliza Dr Vivian
“Maendeleo yapo japokuwa
nisingepeda kusema chochote kwa
sasa kwani ni mapema mno ila
mwanga upo na baada ya siku si
nyingi nitakuja na kukueleza kila
kitu.Kwa sasa naomba unipe muda
niendelee kulichunguza hili
jambo”
“Hakuna tatizo katika hilo
Mathew utanieleza pale
utakapoona inafaa mimi kujua lakini kwa mtazamo wako unaona
kuna dalili za kufanikiwa?
“Dalili zipo kwani hatua
tuliyopiga mpaka sasa ni nzuri na
kuna mwanga mdogo umejitokeza
ambao tukiufuata unaweza
ukatufikisha mahala pazuri japo
suala hili ni gumu mno na ndiyo
maana mpaka sasa majibu yake
hayajapatikana na limebaki kuitwa
fumbo gumu.Pamoja na ugumu
wake lakini nakuhakikishia
mheshimiwa rais kwamba
nitafanya kila niwezalo
kuhakikisha kwamba ninaupata
mzizi wake na kuwapata
waliomuua Kanali Sebastian”
Dr Vivian akamtazama
Mathew kwa muda na kusema “Ninajivunia kuongoza taifa
lenye watu kama wewe
Mathew.Kwa sasa nchi yetu
inapitia changamoto nyingi na
watanzania hasa vijana
wanapaswa kuwa na uzalendo
mkubwa kwa nchi yao.Tanzania
inahitaji mshikamano mkubwa
kuliko wakati mwingine
wowote.Nadhani umekwisha sikia
mambo yanayoendelea kati yetu
na mataifa makubwa tajiri
yakiongozwa na Marekani”
“Nimesikia mheshimiwa rais”
“Kwa hiyo mambo
hayatakuwa rahisi na tunapaswa
watanzania kuwa kitu
kimoja.Tunapaswa kuimarisha
uwekezaji wa ndani,kuimarisha biashara ya ndani na baina ya nchi
zetu za Afrika ,tunapaswa
kuyatumia vyema mahusiano yetu
ya kikanda kwa kufanya
biashara.Kwa ujumla tunayo safari
ndefu kuelekea kujitegemea kama
nchi.Tunapaswa kuachana na
misaada ya wafadhili ambayo
inatufanya tuwe watumwa na
kufuata kila sharti
wanalotupa.Nimedhamiria
kuiondoa Tanzania katika
utegemezi na hilo litafanikiwa
endapo watanzania wote
tutaungana na kuwa kitu
kimoja.Ndiyo maana nakupongeza
sana Mathew kwa kuamua kuja
kuwekeza nyumbani.Tunahitaji
wafanya biashara wazawa kama wewe.Tunahitaji kujitosheleza
kwa bidhaa ndani ya nchi na kuuza
nje.”
“Mheshimiwa rais hii ni vita
kubwa tuko nayo kwa sasa lakini
nakuhakikishia kwamba vita hii
tutashinda.Watanzania pia
wamechoka kuwa tegemezi wa
mataifa makubwa na wanataka
kujitegemea.Haitakuwa rahisi
lakini tutashinda.Tuko pamoja”
“Ahsante Mathew kwa
maneno hayo mazuri ya kutia
moyo.Wengi wameungana
nami,hata maraisi wa nchi nyingi
wamenipigia simu na kunitaka
nisilegeze msimamo wangu
niendelee kupambana na kuitoa
Tanzania katika utegemezi.Mungu ametupa rasilimali nyingi hivyo
tunapaswa kufaidika kwa uwepo
wa rasilimali hizo katika nchi
yetu.Kesho kwa kupitia wazee wa
Dar es salaam nitalihutubia taifa
na kuweka wazi kwa watanzania
hali tutakayopitia na kuwataka
kuungana katika mapambano haya
makubwa ya kiuchumi.Bila
kuchukua maamuzi magumu nchi
hii itabaki katika umasikini na
kutegemea ufadhili.” Akasema Dr
Vivian.Walimaliza kula chakula
wakaenda kukaa sehemu maalum
kwa ajili ya maongezi.
“Mathew ahsante sana kwa
kuungana nami kwa chakula usiku
huu.Sasa ni wakati wa maongezi
kuhusiana na kile ambacho ulisema unataka
tuzungumze.Karibu”
“Ahsante sana mheshimiwa
rais kwa chakula kizuri na kutenga
pia muda kwa ajili ya
mazungumzo.Kikubwa
kilichonileta hapa kwako ni kutaka
kukufahamu wewe”
“Me?! Dr Vivian akaonyesha
kustuka kidogo
“Ndiyo mheshimiwa
rais.Nahitaji kukufahamu vyema”
Dr Vivian akacheka kidogo na
kusema
“Kwa nini unataka
kunifahamu Mathew?
“Ninafanya kazi yako kubwa
na ya hatari kwa hiyo nahitaji
kukufahamu vizuri” “Ukinifahamu mimi
kutakusaidia nini katika kazi
yako? Una wasi wasi na mimi?
“Mheshimwa rais sina wasi
wasi wowote nawe lakini
ninahitaji tu kukufahamu vizuri na
hata wewe pia endapo ukihitaji
kufahamu chochote kuhusu mimi
niko tayari kukueleza chochote”
akasema Mathew.Dr Vivian
akamtazama Mathew kwa muda na
kusema
“Mathew nashindwa niseme
nini,hata hivyo ni kitu gani hasa
unachohitaji kukifahamu toka
kwangu?
“Nataka kufahamu maisha
yako kwa ujumla na zaidi sana
tujikite katika maisha yako ya kimahusiano” akasema Mathew na
Dr Vivian akacheka
“Unataka kufahamu maisha
yangu ya kimapenzi? Akauliza na
kucheka tena
“Ndiyo mheshimiwa rais”
“Mathew wewe ni mtu wa
kwanza kutaka kufahamu kuhusu
maisha yangu ya kimapenzi.Hata
hivyo kwa kuwa nilikuahidi
kwamba nitakuwa tayari kukupa
msaada wa kila aina basi sina budi
kukueleza lakini kabla sijakueleza
chochote nataka kufahamu,hii ina
mahusiano yoyote na hili
unalolichunguza?
“Hapana mheshimiwa rais
halina mahusiano yoyote.Hii ni
kwa ajili yangu binafsi” akasema Mathew na Dr Vivian akatoa tena
kicheko.Alionekana kufurahishwa
na jambo lile
“Sijui nikueleze nini Mathew
kuhusu maisha yangu ya
kimahusiano unayotaka
kuyajua.Kwa ujumla naweza
kusema kwamba sina bahati
katika upande huo kwa hiyo sina
maelezo marefu” akasema Dr
Vivian na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Labda nikuanzie mbali
kidogo.Toka nikiwa mdogo
nilitamani sana kuwa
mtawa.Sikutaka kuwa na
mahusano ya
kimapenzi.Niliyapenda maisha
yale ya upweke na kumtumikia Mungu.Nilipomaliza shule ya
msingi nilijiunga na shule ya
sekondari ya masista kwa lengo la
kutaka kuitimiza ndoto yangu ya
kujifunza maisha ya kitawa.Kila
mtu alitegemea kwamba siku moja
ningekuwa mtawa lakini mara tu
baada ya kumaliza kidato cha sita
nikapata mtazamo mpya.Nikataka
kuwa daktari wa
binadamu.Nilitaka sana kutibu
watoto hivyo nikajikuta ndoto
yangu ikibadilika na sikuendelea
tena na maisha yale ya utawa
badala yake nikaendelea na
masomo ya udaktari.Mpaka
wakati huo sikuwa nimewahi
kukutana na mwanaume yeyote au
kuwa katika mahusiano yoyote ya kimapenzi.Nilipokuwa chuo kikuu
nchini Marekani ndipo
nilipokutana na Nathan.”
“Nathan ni nani? Mathew
akauliza kama vile
hafahamuchochote kuhusu Nathan
“Huyu ni mpenzi
wangu.Alikuwa mpenzi wangu”
“Alikuwa mpenzi wako?Hauko
naye tena?
“Tumekwisha achana.Hatuko
tena katika mahusiano.”
“Unaweza kunieleza namna
ulivyokutana na Nathan? Mathew
akauliza na bila kupepesa macho
Dr Vivian akajibu
“Nilipewa nafasi ya kutoa
hotuba kwa niaba ya wanafunzi
wenzagu katika sherehe za kuwakaribisha chuoni wanafunzi
wapya.Ilikuwa ni hotuba nzuri na
niliitoa kwa kujiamini sana na
baada ya kutoa hotuba ile
nilipongezwa na watu mbali
.Mmoja wa watu waliokuja
kunipongeza alikuwa ni
Nathan.Alijitambulisha kwangu
kwamba ni mwanafunzi wa mwaka
wa pili pale chuoni lakini yeye
alikuwa anasomea mambo ya
mawasiliano.Alikuwa ni kijana
mzuri sana.Alikuwa na nywele
nzuri zenye kung’aa,ngozi laini
,macho mazuri,sauti nzuri na
alionekana kuwa ni kijana
mwerevu na mnyenyekevu
sana.Sifahamu nini kilinitokea
lakini nikajikuta nikimpenda Nathan toka nilipomuona.Kwa
mujibu wa maelezo yake aliyonipa
baadae baada ya kuwa wapenzi ni
kwamba hata yeye pia alikuwa
amenipenda toka siku ya kwanza
nilipoingia chuoni.Urafiki ukaanza
kati yetu na alinisaidia sana
kuyazoea maisha ya pale chuoni na
akanisaidia pia kuifahamu nchi ya
marekani.Nathan alikuwa anatoka
katika familia yenye kujiweza
kifedha,kaka zake wawili
walikuwa ni mchezaji wakubwa na
maarufu wa mpira wa kikapu na
walikuwa na utajiri mkubwa hivyo
waliiwezesha familia yao kiuchumi
kwa kuwafungulia miradi mbali
mbali.Kwa mara ya kwanza katika
maisha yangu nilijikuta nikizama na kuyafurahia mapenzi.Nathan
alinisaidia sana na nilitokea
kumpenda mno.Hata alipomaliza
chuo na mimi kuendelea na
masomo katika vyuo vikuu mbali
mbali vya nchi nyingine bado
ukaribu wangu na Nathan ulikuwa
mkubwa sana.Alikuwa na uwezo
wa kuja walau mara moja au mbili
kila mwezi kuja kuniona
chuoni.Nilijiona mwanamke
mwenye bahati sana na hata
wanafunzi wenzangu walinionea
wivu kwa kuwa na mwanaume
anayenijali kama Nathan.”
Akanyamaza kidogo na baada ya
sekunde kadhaa akaendelea
“Hayo yalikuwa ni mahusiano
yangu ya kwanza kabisaTanzania
alikuwa ni mwanaume wangu wa
kwanza kuingia naye mapenzini na
alinifanya nijione ni mwanamke
bora kabisa duniani.Nilipomaliza
masomo yangu ya udaktari
alinisaidia nikapata kazi katika
hospitali moja kubwa nchini jijini
Washington DC ambako nilifanya
kazi hadi pale walipofariki wazazi
wangu ndipo nilipoamua kurejea
nyumbani na aliyenishauri kurejea
nyumbani ni Nathan.Nilianza kazi
katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili na baadae nikaanza
kujiingiza katika siasa na kisha
nikagongea urais na nikashinda na
kuwa rais wa kwanza mwanamke
kuiongoza jamhuri ya muungano
wa Tanzania
Nilianza kazi
katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili na baadae nikaanza
kujiingiza katika siasa na kisha
nikagongea urais na nikashinda na
kuwa rais wa kwanza mwanamke
kuiongoza jamhuri ya muungano
wa Tanzania.Tulikwisha anza maandalizi ya harusi yetu lakini
kuna mambo yametuingilia hapa
kati na kutulazimu kuweka nukta
katika mapenzi yetu.Ninaomba
usiniulize kuhusu kitu
kilichosababisha mimi na Nathan
tukakorofishana na kuhitimisha
safari yetu ndefu” akasema Dr
Vivian na kucheka kidogo
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais kwa maelezo hayo lakini bado
utaendelea kunivumilia kwa
maswali yangu.Nataka kufahamu
mchango wa Nathan katika
masuala yako ya kisiasa.Alikuwa
na mchango wowote?
“Nathan alikuwa na mchango
mkubwa sana katika harakati
zangu za kisiasa.Kuna nyakati nilitaka kukata tamaa baada ya
kukumbana na vikwazo kadhaa
kwanza kwa uchanga wangu katika
siasa na pili kwa kuwa ni
mwanamke lakini Nathan alinipa
moyo sana na kunifanya nisikate
tamaa nikaendelea na harakati
zangu hadi nikawa rais.Ni mtu
mwenye mchango mkubwa sana
katika harakati zangu za
kisiasa.Aliniunga mkono katika
kampeni zangu na kuzunguka
nami nchi nzima na mara nyingine
alidiriki kusimama jukwaani
akaninadi na kuwafurahisha sana
watu kwa kiswahili chake cha
kuunga unga.Nadhani nimejibu
swali lako.Nathan ana mchango mkubwa sana katika maisha yangu
ya kisiasa”
“Kwa sasa Nathan anafanya
kazi gani?
“Ni mhandisi katika kampuni
moja inaitwa A.D electronics iko
Marekani lakini inafanya kazi
katika nchi mbali mbali.Nathan si
mtu wa kutulia sehemu moja
amekuwa anasafiri safiri kwenda
nchi mbali mbali kufanya kazi za
kampuni yake” akasema Dr Vivian
“Mtu kama huyu mwenye
mchango mkubwa katika maisha
yako lazima kuna sababu kubwa
sana iliyosababisha mkatengana
hasa katika wakati huu ambao
mlikaribia sana kuitimiza ndoto
yenu ya kufunga ndoa.Nimesikia kwamba ilibaki miezi mwili pekee
mfunge ndoa.What real happened?
“Mathew hili jambo linaumiza
sana si kwangu tu bali kwa kila
mtu aliye karibu yangu.Kila mtu
alikuwa na mategemeo makubwa
sana kwamba ndoto yangu ya
muda mrefu ya kuolewa na Nathan
itatimia ndani ya muda wa miezi
miwili toka sasa lakini ndoto hiyo
imetoweka.Hakuna tena ndoa kati
yetu.Hii inaniumiza sana hata
mimi lakini sina namna nyingine
ya kufanya na ndiyo maana
nikasema awali kwamba sina
bahati katika mapenzi kwani ndoa
yangu imeota mbawa katika hatua
za mwisho.Maandalizi yote ya
harusi yangu yamekwisha kamilika lakini inasikitisha
kwamba hakutakuwa na ndoa
tena.Kuna nyakati ninafikiria
yawezekana labda nilifanya kosa
kuamua kuachana na maisha ya
utawa na ndiyo maana maisha
yangu ya kimapenzi hayana
mafanikio”
“Hapana Dr Vivian usiwaze
hivyo.Kuhitilafiana katika
mahusiano ni kitu cha kawaida na
mapenzi kuvunjika si mkosi.Ni
mambo ambayo lazima
tukubaliane nayo kwamba yapo na
yanaweza kutoka katika uhusiano
wowote ule.Nitazame
mimi.Nilikuwa na mwanamke
ninayempenda sana ambaye
niliyatoa maisha yagu kwa ajili yake lakini tumekuja
kukorofishana na kila mmoja sasa
ana maisha yake.Iliniumiza kwa
sababu nilikuwa nampenda mno
Peniela lakini sasa tayari nimezoea
na maisha
yanaendelea.Nilichojifunza katika
mahusiano ni kwamba kama
unaona hauna furaha katika
uhusiano wako,huna haja ya
kuendelea kulazimisha na kuutesa
moyo muache aende.Nenda
katafute furaha yako ya maisha
sehemu nyingine.Kwa hiyo Dr
Vivian usijilaumu sana kwa
maamuzi uliyoyafanya.Baada ya
muda utazoea na maisha
yataendelea.Some day you’ll be
happy again” “Me ! happy? Akauliza Dr
Vivian huku akicheka kidogo
“Ndiyo Dr Vivian.Usikate
tamaa siku moja naamini
utampata mtu atakayeikamilisha
furaha yako”
“Sina hakika kama hilo
litatokea.Hakuna mwanaume
ambaye anaweza kutaka kuwa na
mwanamke kama mimi.Kwa sasa
sitaki kuelekeza macho yangu
huko bali nataka niielekeze akili
yangu katika kuwatumikia
watanzania.Furaha yangu ni
kuwatumikia waoa.Ninapopita na
kuona nyuso zao zikiwa na furaha
hiyo ndiyo furaha yangu.Mapenzi
yangu yako kwao kwa hiyo sina
muda wa kupoteza kwa ajili ya kumuhudumia mwanaume
mmoja.Nina watu zaidi ya milioni
hamsini ninaowaongoza na siwezi
kupata muda wa kumuhudumia
mpenzi” akasema Dr Vivian
“Hiyo ndiyo sababu uliamua
kuachana na Nathan?
“Sipendi kuzungumzia hilo
Mathew lakini hiyo ni moja wapo
ya sababu.Nataka nitumie muda
wangu mwingi kuwahudumia
watanzania.By the way how’s
Peniela? Akauliza Dr Vivian
“Peniela anaendelea
vizuri.Tunawasiliana bado na tuna
mtoto anaitwa Anna
Maria.Tuliamua kwa hiari yetu
kuachana na kila mmoja
akaendelee na maisha yake kwa hiyo hatuna ugomvi,bado
tunaendelea kushirikiana katika
mambo mbali mbali na bado ni
marafiki wazuri pia.Tayari ana
mume mpya na ninaliheshimu
hilo”
“Vipi kuhusu wewe una
mipango gani? Umeoa au
unatazamia kuoa mwanamke
mwingine?Dr Vivian akauliza
“ Kwa sasa sina mategemeo
hayo ya kuoa au kutafuta
mwanamke mwingine.Nimekuwa
muoga kidogo baada ya mahusiano
yangu na Peniela kuishia njiani”
akasema Mathew na kucheka
kidogo
“Unaweza ukaniambia nini
kilisababisha mkatengana? Au na wewe hauki tayari kuliongelea hilo
kama mimi? Akauliza Dr Vivian na
wote wakacheka
“Mimi huwa sifichi
kitu.Tulitengana kwa sababu ya
Peniela.Alianzisha mahusiano na
bilionea mmoja ambaye anamiliki
kiwanda cha magari.Sikutaka
kumkwaza kwani walionekana
kuzama mapenzini sana na hivyo
nikaamua tuachane ili aendee na
huyo mpenzi wake lakini
tuliachana kwa wema tu,hatuna
tatizo lolote tunaendelea
vizuri”Akasema Mathew na
kikapita kimya kifupi.Dr Vivian
akasema
“Nadhani kwa upande huo wa
maisha ya kimahusiano tumemaliza.Kitu gani kingine
ambacho ungependa kukifahamu
kuhusu mimi?
“Bado kuna kitu kimoja
ambacho ningetaka kukifahamu.Je
akija Nathan leo na kukuomba
msamaha hata kama si yeye
aliyekosa utakuwa tayari
kumsamehe na kurejesha mapenzi
yenu?
“Mathew nadhani bado
hujanifahamu vizuri.Mimi ni
mmoja wa wale watu ambao
hawana ndimi mbili.Nikisema
hapana ni hapana.Huwa sibadilishi
kauli.Nimeamua kuachana na
Nathan kwa hiyo hakuna tena
tegemeo la mimi na yeye
kurudiana.Nimekwisha weka nukta” akasema Dr Vivian na
ukimya mfupi ukapita
“Mheshimiwa rais nadhani
tumeongea vya
kutosha.Ninashukuru sana kwa
kunipa nafasi hii ya kuzungumza
na kukubali kuzungumzia masuala
yako binafsi tena kwa uhuru
mkubwa bila kuficha.This means a
lot to me” akasema Mathew
“Usijali Mathew.Ahadi ni deni
na nilikuahidi kwamba chochote
utakachokitaka utakipata lakini
nataka kujua,haya tuliyoyaongea
leo yanakusaidia nini? Yana
muingiliano wowote na kazi
unayoifanya? Akauliza Dr Vivian
“Mheshimiwa rais nilihitaji tu
kukufahamu wewe ni mtu wa aina gani na ukitaka kumfahamu mtu
vizuri basi yafahamu maisha yake
ya kimahusiano.Baada ya
mazungumzo haya nimekufahamu
wewe ni mtu wa aina gani.Hii
inanisaidia sana katika kazi zangu
kwa kujua ninafanya kazi na mtu
wa aina gani”
Dr Vivian akatabasamu na
kusema
“Umenifahamu mimi ni mtu
wa aina gani? Can you be honnest
with me?
“Kwanza nimefahamu wewe ni
rais wa watu.Hauna ubinafsi na
maamuzi yote unayoyafanya ni
kwa ajili ya watu.Unaipenda
Tanzania kiasi ambacho
hakielezeki na ndiyo maana umekuwa unafanya maamuzi
magumu hata katika maisha yako
binafsi kwa ajili ya kuwatumikia
watanzania.Mwisho kabisa
nimefahamu wewe ni rais ambaye
hauyumbi na haukubali
kuyumbishwa.Nitafanya kazi
yangu uliyonipoa kwa kuzingatia
hayo niliyoyafahamu” akasema
Mathew
“Ahsante kwa kuyafahamu
hayo.Ninashukuru sana kwa kuja
kunitembelea na unakaribishwa
muda wowote hapa ikulu na
nitakuwa tayari kutenga muda
kwa ajili ya kukusikiliza na kujua
maendelo yako.Nitapenda sana
kukaa nawe na kubadilishana
mawazo si katika kazi hiiniliyokupa bali hata katika
masuala mengine ya nchi,biashara
n.k.” akasema Dr Vivian na
kusimama
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais kwa heshima hii
kubwa.Nitakapohitaji tena
kukuona sitasita kufanya
hivyo.Naomba sasa nikuache
upumzike na mimi nikaendelee na
mambo mengine.Kabla sijaondoka
kuna jambo nilikuwa
nimesahau.Kuna mtu mmoja
anatoka Cuba lakini ni raia wa
marekani anaitwa Camilla Snow
anakuja hapa Tanzania.Huyu
nitakuwa nashirikiana naye katika
uchunguzi wangu.Huyu ni rafiki
yangu sana na amewahi kufanya kazi FBI lakini kwa sasa
amekwisha acha na anafanya
shughuli zake
binafsi.Nimemuomba aje anisaidie
katika uchunguzi wa jambo hili na
amekubali hivyo ninakuomba
unisaidie ili aweze kuingia hapa
nchini bila matatizo na aweze
kupata kibali cha kuishi hapa
nchini” akasema Mathew
“Hakuna tatizo kuhusu hilo
Mathew.Nitatoa maelekezo kwa
watu wangu walifanyie kazi hilo na
ataruhusiwa kuingia na kuishi
hapa nchini kwa muda
atakaohitaji.Nilikuahidi chochote
utakachokihitaji utakipata kwa
hiyo usiwe na hofu yoyote
kuhusiana na hilo jambo.Camilla snow ataingia nchini bila
matatizo.Utanitaarifu ni lini
atakuja nchini”
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais kwa msaada huo
mkubwa.Nitawasiliana nawe na
kukupa taarifa zote kwa kina”
akasema Mathew na rais
akamsindikiza hadi katika gari
lake akaondoka kuelekea nyumani
kwake.
Mara tu Mathew alipoondoka
Dr Vivian akachukua simu na
kumpigia Theresa.
“Hallo Theresa,umekwisha
lala?
“Hapana bado ila ninajiandaa
kulala” “Nimekupigia kukujulisha
kwamba Mathew ametoka hapa
muda si mefu.Nimekuwa naye kwa
chakula cha usiku na baada ya
hapo tukawa na maongezi kidogo”
“Amekuja kukueleza mahala
alikofikia katika uchunguzi wake?
“Hapana Theresa alikuja kwa
dhumuni lingine kabisa.Alitaka
kufahamu kuhusu mahusiano
yangu na Nathan.Amenidadisi
mambo mengi kuhusu mimi na
Nathan”
“Umemueleza kila kitu?
“Imenilazimu kumueleza kila
kitu isipokuwa sababu ya mimi na
Nathan kutengana.Nimeshindwa
kuelewa sababu ya Mathew kutaka
kufahamu masuala yangu binafsi ya kimahusiano.Hebu nieleze kuna
chochote katika uchungzi wake
ambacho kimemfanya atake
kunifahamu mimi na maisha yangu
ya ndani?
“Hakuna dada.Niko naye
muda wote na kila kitu tunafanya
pamoja na hakuna chochote
kinachohusiana nawe na wala
hajaniambia kama anataka kuja
kuonana nawe.Yawezekana labda
anatafuta nafasi” akasema Theresa
na kucheka kidogo
“Theresa huu si wakati wa
utani.Mathew hakuonekana kama
ni mtu anayetafuta nafasi.Ni wazi
alikuwa na sababu maalum ya
kutaka kufahamu kuhusu
mahusiano yangu na Nathan.Nakuomba jaribu
kumchunguza ufahamu nia na
dhumuni la kutaka kunifahamu
kiundani na kuyafahamu
mahusiano yangu.Fanya kila
uwezalo kulifahamu hilo kwani
amenipa wasiwasi kidogo”
akasema Dr Vivian.
“Usijali dada niachie hilo
jukumu na nitalifanikisha ila
nikutoe wasiwasi Mathew si mtu
mbaya na hata kama alitaka
kukufahamu basi ni kwa lengo
zuri.Kama kungekuwa na tatizo
lolote basi angekwisha
nifahamisha kwani kila kitu
anachokifanya huwa
ananishirikisha” “Sawa Theresa lifanyie kazi
hilo nataka kufahamu.Halafu kitu
kingine kesho nazungumza na
wazee wa Dar es salaam kama
utapata nafasi ningependa
uniandalie hotuba lakini kama
hautaweza basi usijali nitaanda
mwenyewe” akasema Dr Vivian na
kuagana na Theresa.
Mara tu alipokata simu
Theresa akampigia Mathew
“Hallow Theresa habari za
usiku huu?
“Habari nzuri Mathew.Uko
wapi?
“Niko njiani naelekea
nyumbani nimetoka ikulu kuonana
na rais” “Amenipigia simu muda mfupi
uliopita kuhusiana na
mazungumzo yenu ana wasi wasi
sana kama yale mliyozungumza
yana mahusiano yoyote na
uchunguzi unaoendelea kuufanya
lakini nimemtoa wasi wasi
kwamba asihofu hakuna kitu kama
hicho”
“Good.Nimezungumza naye
nilitaka kufahamu kuhusu yeye na
Nathan.Nashukuru amekuwa
muwazi kwangu na hajanificha
kitu japokuwa sababu ya
kutengana kwao hajanieleza”
akasema Mathew
“Kuna chochote ambacho
umefanikiwa kukipata kuhusu
Nathan katika mazungumzo hayo? “Kuna vitu kadhaa nimevipata
ninakwenda kuvifanyia kazi halafu
nitakuja kukujulisha kesho.Vipi
kuhusu Nathan unawasiliana naye?
“Ndiyo kama nilivyokueleza
awali kwamba tayari amekwisha
anza safari.Anakuja na ndege
binafsi ya kaka yake na kesho mida
ya saa nne au saa tano hivi
atawasili.Nitakujulisha kila kitu”
“Ahsante sana Theresa kwa
msaada huo ila kumbuka kwamba
jambo hili ni siri yangu na wewe.Dr
Vivian hapaswi kufahamu
chochote kuhusiana na jambo hili”
akasema Mathew
“Nalizingatia hilo Mathew na
hata Nathan nimemueleza hivyo
kwamba Dr Vivian hapaswi kufahamu chochote kuhusiana na
safari yake ya kuja Tanzania”
“Good.Uwe na usiku mwema
Theresa tutaonana kesho”
“Ahsante.Usiku mwema nawe
Mathew” akajibu Theresa na
kukata simu.
“Mambo yanakwenda
vizuri.Nina uhakika tukimfuatilia
Nathan kuna mwanga utapatikana”
akawaza Mathew na hakuelekea
nyumbani kwake bali akaenda
moja kwa moja nyumbani kwa
Meshack Jumbo
“Karibu Mathew” Meshack
Jumbo akamkaribisha Mathew
nyumbani kwake
“Ahsante mzee.Natumai
utanichoka kwa ujio wangu wa usiku” akasema Mathew na wote
wakacheka
“Usijali kijana.Haya niambie
kwa mvao huo lazima umetoka
ikulu” akasema Meshack Jumbo na
wote wakacheka
“Hujakosea mzee.Nimetoka
kuonana na mkuu wa
nchi.Tumepata chakula cha usiku
pamoja halafu tukawa na
maongezi kidogo.Nilitaka
kufahamu kuhusiana na
mahusiano yake na Nathan.”
Meshack Jumbo akakaa vizuri
na kusema
“Kabla hatujaendelea
nimepokea simu toka kwa Jimmy
akinipa taarifa za Camilla.Tayari
amekwisha wasili Havana Cuba na anasubiri maelekezo yetu.Sikutaka
kukutaarifu kwani nilijua utakuwa
ikulu kama ulivyokuwa
umenitaarifu” akasema mzee
Meshack na kumpatia Mathew
maelezo yote aliyopewa na Jimmy
kuhusu Camilla.Mathew akampigia
simu Peniela na kumpa maelekezo
hayo kuhusiana na Camilla halafu
akaendelea na maongezi na
Meshack
“Tayari nimekwisha muachia
jukumu lote Peniela na
atalishughulikia.Tuendelee na
maongezi yetu.Nimekuwa na
mazungumzo na rais kuhusiana na
maisha yake binafsi ya mahusiano
na ninashukuru kwamba rais
amenipa ushirikiano mkubwa amenieleza mambo mengi binafsi
bila kunificha.Katika mazungumzo
yetu kuna mambo
nimeyagundua.Nathan amekuwa
na mahusiano na Dr Vivian toka
wakiwa chuoni .Wamesoma chuo
kimoja na urafiki wao ulianzia
huko.Ninajiuliza swali je wakati
wanasoma Nathan tayari alikuwa
amejiunga na CIA? Na kama ndiyo
kuna kitu alikuwa anakichunguza
kwa Dr Vivian au alitokea tu
kumpenda? Inawezekana labda
Nathan akawa ni CIA lakini akawa
hana jambo lolote baya na Dr
Vivian bali ana mapenzi ya kweli
kwake lakini lazima tujiridhishe
kwa hilo kwa kufanya
uchunguzi”akasema Mathew “Hilo linawezekana Mathew
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment