IMEANDIKWA NA : PATRICK CK
***************************************************************
Simulizi : Scandle (Kashfa) (2)
Sehemu Ya Kwanza (1)
*****************
Mchungaji Adam alirejea kanisani akaonana na Nabii Kasiano na akamueleza hatua ambazo amekwisha chukua ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kuwashirikisha gazeti la Fuku Fuku katika kumtafuta kigogo anayemuharibu mwanae.Nabii Kasiano akamtaka waanze maombi.Wachungaji na watu wengine wachache wakaitwa kujumuika katika maombi hayo.
Yalikuwa ni maombi yaliyodumu kwa saa mbili na mara Nabii Kasiano akawaomba wasimame na wamshukuru Mungu kwa muujiza alioutenda.Wakaimba na kushukuru bila kujua ni muujiza gani
“Wakati wa maombi Mungu amenionyesha nabii wake mahala alipo mtoto.Ninawahakikishia Mungu wa majeshi hashindwi na chochote.Mtoto yuko salama na amenitaka niwaambie wazazi wake wasihofu mtoto yuko salama” akasema Nabii Kasiano aliyekuwa ameloa shati lake huku jasho likimtiririka.Akawataka mchungaji Adam na mke wake aliyefika wakati maombi yakiendelea wamfuate ofisini kwake
“Adam na mke wako
mnapitia kipindi kigumu sana lakini Mungu anawapenda na atasimama nanyi.Endeleeni kusimama katika imani kwani ni kutokana na imani yenu hiyo binti yenu yuko salama.Watu wabaya walitumiwa na shetani kutaka kuwavuruga na kuwapoteza imani lakini Mungu wetu aliye hai amesimama nanyi na amenionyesha mahala alipo mtoto wenu” akasema Nabii Kasiano
“Mtoto wenu yuko
Morogoro.Amefichwa katika hoteli moja ya kifahari” akasema na kuwatajjia jina la hoteli hiyo na chumba
“Mtakapofika msionyeshe kumkasirikia bali pigeni magoti muombe kisha mumchukue na mrudi naye nyumbani.Safari ya kwenda Morogoro inaanza sasa hivi na mtatumia gari langu.Msimweleze chochote mtu yeyote hadi pale mtakapokuwa mmempata mtoto wenu halafu mtatoa ushuhuda wa kile Mungu alichowatendea.Mimi nitaendelea kudumu katika maombi,nitainua mikono yangu kumlilia bwana hadi pale mtakapokuwa mmerejea” akasema Nabii Kasiano na bila kupoteza muda mchungaji Adam na mkewe wakachukua gari la Kasiano na safari ya kuelekea Morogoro ikaanza.
Mara tu
walipoondoka,Kasiano akachukua simu na kuzitafuta namba Fulani akapiga
“Tayari ameanza
safari.Anatumia gari langu” akasema Kasiano na kukata simu
************
Saa moja za jioni Kasiano akiwa bado kanisani kwake akiendelea na huduma akafuatwa na mmoja wa wachungaji wa kanisa lake akamjulisha kwamba wamepokea taarifa kwamba mchungaji Adam Watwila na mke wake wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jioni hiyo wakati wakielekea Morogoro.Ikamlazimu nabii Kasiano kusimamisha ibada na kuwatangazia waumini kuhusiana na taarifa ile ya kustusha kuhusu kifo cha mchungaji Adam Watwila na mke wake.Kanisa likalipuka kwa vilio lakini Nabii Kasiano
akawataka wasilie bali
wadumu katika maombi kwani kanisa linapitia kipindi kigumu
Mlango wa chumba alimokuwa Naomi ulifunguliwa taratibu,Naomi ambaye tayari alikwishapitiwa na usingizi akastuka na kuamka baada ya mkono wa mtu kumgusa mguu wake.Alikua ni nabii Kasiano,haraka haraka akainuka na kukaa kitandani
“Karibu mpenzi.Mbona umeingia kimya kimya hivyo? Akauliza Naomi
“Sikutaka kukustua ndiyo maana nikaingia kimya kimya.Unaendeleaje hapa? Akauliza Kasiano
“Ninaendelea vyema.Vipi wewe unaendeleaje? Umeonana na baba anaendeleaje?Zoezi la kunitafuta
linakwendaje?akauliza Naomi maswali mfululizo.Uso wake ulionyesha wasi wasi mwingi
“Naomi nafahamu wewe ni
jasiri na ninakuomba uwe
jasiri”
“Mbona unaniogopesha Kasiano? Akauliza Naomi
“Usihofu Naomi kila kitu kitakuwa sawa”
“Nini kinaendelea huko nyumbani? Baba umeonana naye? Naomi akauliza Naomi.Nabii Kasiano akamshika mabegani akamtazama kisha akasema “Naomi kuna jambo limetokea nataka unihakikishie kwamba utakuwa jasiri.Nakufahamu wewe ni jasiri hivyo nataka ujasiri wako uutumie wakati huu” akasema Nabii Kasiano
“Kasiano mbona unazidi kunipa hofu? Kama kuna tatizo lolote niambie tafadhali.Ninatafutwa na polisi?
“Hapana hautafutwi na
polisi”
“Sasa kuna tatizo gani limetokea? Nieleze tafadhali” akasema Naomi.Kasiano akamtazama halafu akasema
“Mchungaji Adam na
mkewe wamepata ajali jioni ya leo wakati wakielekea Morogoro” Kasiano akanyamaza akamtazama Naomi ambaye alistuka na kuweka mikono kifuani huku akihema haraka haraka.Kwa sekunde chache tu tayari macho yake yalijaa machozi
“Kasiano niamie tafadhali kama wazazi wangu ni wazima.Niambie ukweli usinifiche” akasema Naomi huku akimwaga machozi
“Naomi nyamaza usilie tafadhali naomba uwe jasiri”
“Kasiano niambie tafadhali wazazi wangu ni wazima? Akauliza Naomi,Kasiano akamtazama kwa muda halafu akasema
“They’re all dead” akasema Kasiano na Naomi akaanguka na kupoteza fahamu.Kasiano akawaita walinzi wake wakaanza kumpepea Naomi ambaye baada ya muda akazinduka na kuanza tena kulia.Kasiano akamkumbatia na kujaribu kumtuliza
“Kasiano I need to go home.Please let me go home” akasema Naomi huku akilia
“Nyamaza kulia
Naomi.Nafahamu hii ni taarifa mbaya lakini naomba ujikaze”akasema Kasiano
“Please Kasiano I need to
go home ! Naomi akaendelea kusisitiza
“Naomi hautakwenda
nyumbani kwa sasa hadi pale muda utakapofika”
“Kwa nini Kasiano?
“Tayari taarifa za kupotea kwako zimekwisha sambaa sehemu mbali mbali,ndugu karibu wote wanafahamu kuwa umepotea hivyo basi utakapoonekana yataanza maswali mengi kutaka kujua mahala ulikokuwa.Jambo lingine polisi tayari wanazo taarifa za kutoweka kwako na watakaposikia kwamba umeonekana wanaweza wakataka kukuhoji kujua mahala ulikokuwa na kama ulikuwa umetekwa nyara au vipi.Katika mahojiano hayo unaweza ukajisahau na kutamka mahala ulipokuwa na hii itakuwa mbaya zaidi kwetu hasa mimi.Nitaingia katika matatizo makubwa sana”akasema Kasiano
“Nini unamaanisha
Kasiano? Akauliza Naomi
“Namaanisha kwamba
hautahudhuria mazishi ya wazazi wako”akasema Kasiano na sura ya Naomi ikabadilika
“Are you crazy? Akauliza
Naomi kwa sauti kali
“Yaani wazazi wangu wote wamefariki dunia halafu nisiende kuhudhuria mazishi yao? Akauliza Naomi kwa ukali
“I’m not crazy Naomi.I mean it ! akasema Kasiano
“You are crazy Kasiano.Huwezi ukamaanisha kitu kama hicho.Wazazi wangu wamefariki na mimi ni mtoto wao wa pekee halafu nisiende kuhudhuria mazishi yao ? Hilo ni jambo lisilowezekana kabisa !
akasema Naomi
“Utanisamehe Naomi
lakini hivyo ndivyo itakavyokuwa.Wazazi wako watazikwa bila ya wewe kuwepo.Utaunganishwa moja kwa moja na kila kitakachokuwa kinaendelea msibani ukiwa hapa” akasema Kasiano na macho ya Naomi yakajaa tena machozi
“Kwa nini unaifanyia hivi Kasiano?
“Ni kwa sababu nataka kujilinda mimi.Nikikuruhusu uende msibani itakuwa ni mbaya zaidi kwa upande wangu” akasema Kasiano
“So I’m your prisoner now ! akasema Naomi
“Naomi this is for our own good.Wazazi wako wamekwisha fariki na hakuna tena kitu cha kuhofia.Nataka nikuhamishie nje ya nchi utaenda kusoma na kushi huko.Sitaki uishi tena hapa Tanzania” akasema Kasiano
“Kasiano mpenzi nimekuelewa hata mimi ninataka kwenda kuishi huko nje ya nchi lakini nataka uniachie nikawazike kwanza wazazi wangu na baada ya hapo utafanya kila unachokitaka”
“Naomi kwa nini hutaki kunielewa? Nimekwambia hilo halitawezekana.Utaendelea kukaa humu ndani kwa siku kadhaa na utakapotoka humu moja kwa moja utakwenda uwanja wa ndege na kuondoka nchini !
“Kwa nini Kasiano
unanifanyia hivi? Siku zote umekuwa ukiniambia kwamba unanipenda lakini leo nimegundua kwamba yale yote uliyokuwa unaniambia ni uongo mtupu.Hunipendi na kila ulichokuwa unanifanyia ni kwa sababu ulikuwa unanitumia kwa manufaa yako.Kwa sasa baada ya mambo kuanza kuharibika sina thamani tena kwako ! akasema Naomi kwa uchungu
“Si hivyo
Naomi.Ninakupenda sana na ndiyo manaa niko tayari kukuhamishia Ulaya ukaishi huko.Yote niliyokufanyia ni kwa sababu ya upendo wangu mkubwa kwako.Naomba uniamini Naomi kwamba ninakupenda mno” akasema Kasiano
“Liar ! akafoka Naomi
“Ninajuta kukutana nawe Kasiano.Umeyaharibu maisha yangu na sasa nimekuwa hatari kwako na sina thamani tena.You used me.Ulinitumia kuuza dawa za kulevya .Unanisafirisha kwenda nchi mbali mbali kila mara na kunibebesha mzigo ambao ni dawa za kulevya unadhani sifahamu? Hukunipenda bali ulikuwa unanitumia kwa manufaa yako lakini baada ya yote niliyokufanyia leo hii unanifanyia hivi? Unaniweka mateka hutaki nikawazike wazazi wangu ! Akauliza Naomi kwa ukali
“Naomi please !
“Najiuliza wazazi wangu walikwenda kutafuta nini Morogoro wakati mtoto wao nimetoweka na sijulikani nilipo? Ninaanza kupata wasiwasi kuhusu vifo vyao kama ni ajali ya kweli au ni ajali ya kutengenezwa ! akasema Naomi na kumtazama Kasiano
“Kasiano you killed them ! akafoka Naomi
“No I didn’t !
“You killed them.Baba asingekubali kwenda Morogoro wakati mwanae nimetoweka na sijulikani
nilipo ! My parents were killed ! akasema Naomi
“Kasiano hata kama ukikana lakini naamini kabisa wazazi wangu wameuawa na wewe lazima umeshiriki katika kuandaa mauaji hayo.Ninakufahamu wewe ni katili na baada ya baba kuelezwa kila kitu kuhusu mimi tayari alikuwa ni mtu hatari kwako na ndiyo maana mkapanga mipango na kumuua.Kwa nini Kasiano ukafanya ukatili huu mkubwa?Kwa nini ukanifanyia hivi? Akauliza Naomi huku akilia.Kasiano akamtazama Naomi halafu akasema
“Sikiliza Naomi.Umetaka kuufahamu ukweli hivyo nataka nikwambia ukweli.Sikiliza kwa makini ! akasema Kasiano
“Kwa sasa unajiona uko kawaida lakini ukweli ni kwamba maisha yako yamebadilika.Tayari umeingia katika dunia nyingine hatari.You are now in drug world.Ukisha ingia katika dunia hii there’s no turning back.Japo wewe hufahamu lakini unafuatiliwa sana kila wakati kuhakikisha kwamba hauwi tatizo au kikwazo kwa wale wote wanaofanya biashara hii.Kosa dogo tu ambalo unaweza ukalifanya litayagharimu maisha yako na utaondolewa haraka sana na hapa ninamaanisha kuuawa.Hii ni sababu iliyonifanya nitumie fedha nyingi kuhakikisha maisha yako shuleni yanakuwa siri kubwa ili wazazi wako wasifahamu chochote.Hakuna aliyetegemea kama Yule mwalimu mkuu niliyekuwa namtumia angefariki dunia na akaja mwalimu mpya akaharibu kila kitu kwa kumjulisha baba yako kuhusu maisha yako shuleni na kwa kufanya vile tayari iliwaka taa nyekunud na kukuweka katika hatari kubwa kani tayari suala limekwisha fika katika vyombo vya dola na kama wakifanya uchunguzi wanaweza wakagundua mambo mengi na kuniweka mimi na wenzangu katika hatari kubwa na ndiyo maana nikachukau hatua hizi kwanza kukuondoa haraka pale shuleni na pia kuhakikisha wazazi wako hawawi kikwazo kwako na katika biashara yetu.Naomi wewe ni mtu unayefahamu siri zangu nyingi hivyo kwa namna yoyote ile napaswa kukulinda na kuhakikisha unakuwa salama.Nina heshima kubwa hapa nchini.Nina kanisa kubwa hapa
Hakuna
anayeufahamu upande wangu wa pili lakini wewe umebahatika kuufahamu na umeyafahamu baadhi ya mambo yangu ninayoyafanya likiwamo hili la biashara ya dawa za kulevya.Kwa haya uliyobahatika kuyafahamu kuhusu mimi wewe tayari ni jukumu langu hivyo sitaki kukuweka katika matatizo na wala sitaki nijiweke mimi katika matatizo ndiyo maana kuna wakati ukifika ninalazimika kufanya maamuzi magumu sana kwa ajili ya kukulinda wewe na kujilinda mimi mwenyewe.Mchungaji Adam ni mtu ambaye nimefanya naye kazi kwa muda mrefu.Mimi naye tunaelewana na sikufikiria kama siku moja ningeweza kufanya kitu kama hiki kwake lakini imenilazimu kumuondoa kwa sababu tayari amekwisha kuwa mtu hatari kwangu.Ameanza kuyachimba maisha yako na kama haitoshi tayari anashirikiana na gazeti moja linaloandika taarifa za uchunguzi kumtafuta mtu ambaye amekuwa akigharamia maisha yako ya kifahari pale shuleni na hii inamaanisha kwamba ananitafuta mimi.Unadhani nini kingetokea endapo angefahamu kuwa ni mimi ndiye niliyekuwa ninagharamia maisha yako pale shuleni?Mambo yangekuwa mabaya kwetu hivyo nikachukua hatua ya kumuondoa angali mapema kabla hajawa hatari kwetu.Utanisamehe Naomi lakini imenilazimu kufanya haya niliyoyafanya.That’s how we live in this world,that’s who we are.We’re monsters ! akasema Kasiano na kwa hasira Naomi akamvamia na kuanza kumnasa makofi
“Monster ! Monster ! akapga kelele Naomi Kasiano akamshika mikono
“Stop Naomi ! akasema
kwa ukali
“Kwa nini umekatili maisha ya wazazi wangu Kasiano? Kwa nini usingeniua mimi na kuwaacha wazazi wangu waendelee kuishi? Akauliza Naomi kwa ukali
“Ninakupenda Naomi na
ndiyo maana sitaki uingie katika hatari yoyote !
“Umeyaharibu maisha yangu shetani mkubwa wewe uliyejificha katika neno la
Mungu.Ninaapa Kasiano labda uniue lakini nikitoka hapa nitakwenda kuanika mambo yako yote hadharani.Nitawaeleza watanzania kile unachokifanya huku ukijificha katika mwavuli wa dini shetani wewe ! akasema Naomi
“Naomi tafadhali naomba uyafute mawazo hayo kichwani kwako ! akasema Kasiano
“Umeyaharibu maisha yangu na kama haitoshi umewaua wazazi wangu ambao hawana kosa lolote.I hate you Kasiano and I must destroy you ! Ninafahamu mambo yako yote unayoyafanya na lazima niyaanike kwa watu wakufahamu wewe ni nani shetani mkubwa wewe ! akasema Naomi na Kasiano akakasirika akamnasa kofi akaangukia kitandani
“Chunga ulimi wako Naomi.Mimi si mtu wa kutishwa na panya mdogo kama wewe ! akasema Kasiano ambaye tayari alikwisha pandwa na hasira.Akamfuata Naomi pale kitandani akamkaba shingo
“Naomi kamwe usithubutu kucheza na mimi.Bado hujanifahamu vizuri.Mimi ni mtu mbaya sana I’ll destroy you Naomi before you destroy me ! akasema kwa hasira
Kasiano
“You are a devil ! akasema Naomi kwa taabu na Kasiano akamuachia akaenda akaegemea kabati akainamisha kichwa akawaza halafu akainua kichwa akamtazama Naomi na kusema
“Naomi tafadhali usitake mwisho wetu uwe mbaya.Tumetoka mbali mimi nawe,tumekuwa na nyakati nyingi za furaha pamoja,please just this once try to understand what I’m doing is for your own good.Ninakupenda Naomi and I don’t want to hurt you ! akasema Kasiano.Huku akilia
Naomi akajibu
“Kasiano maisha yangu yamekwisha haribika,tamaa zangu za maisha ya kifahari zimeniponza na siwezi kutimiza ndoto zangu tena,siwezi kuwa na maisha ya kawaida tena.Umeniumiza mno kwa kuwaua wazazi wangu.I’ll never forgive you for this.Naomba ufahamu kwamba I’m not scared to die anymore.Kama unataka kuniua fanya hivyo lakini nikifanikiwa kutoka hapa umekwisha ! Nitaanika kila kitu unachokifanya !
“Aaaaghhh !! akapiga kelele za hasira Kasiano na kuchukua chupa ya mvinyo akaipiga chini ikavunjika vipande vipande akamtazama Naomi kwa hasira
“Kwa nini unataka nikuharibu Naomi?
“Umekwisha yaharibu
maisha yangu na kilichobaki ni kuniua tu ! akasema Naomi
“Ouh Naomi ! Naomi ! kwa nini unanilazimisha nifanye kitu ambacho sikukusudia kukifanya? Akafoka Kasiano huku Naomi akiendelea kumwaga machozi.
Kasiano akamtazama
Naomi halafu akatoka ndani ya kile chumba.Baada ya dakika tatu wakaingia watu wanne.Naomi akashikwa akafungwa mikono kwa nyuma akabandikwa gundi ya nailoni mdomoni ili asiweze kupiga kelele halafu akavishwa mfuko kichwani akatolewa akaingizwa katika buti ya gari likaondoka.
“Sipaswi kumlaumu mtu haya yote nimeyataka mimi mwenyewe.Nilikubali kuingia katika mahusiano na Kasiano baada ya kushawishiwa kwa fedha na maisha ya kifahari.Nilidhani Kasiano ananipenda kwa namna alivyokuwa ananigharamia kumbe alikuwa ananitumia katika biashara zake.Niliondoka shuleni na kusafiri kwenda nchi mbali mbali bila wazazi wangu kufahamu na huko kote nilikuwa nikipeleka dawa za kulevya.Alichoniumiza zaidi ni kuwaua wazazi wangu.Hawakuwa na kosa lolote.Sioni tena sababu ya kuendelea kuishi bila ya wazazi wangu.Najua huku wanakonipeleka wanakweda kuniua.I’m not scared anymore,I’m ready to die.Ninataka nikaonane na wazazi wangu huko waliko niwaombe msamaha” akawaza
Naomi akiwa katika buti ya
gari akipelekwa mahala asikokujua
Wakati vijana wake wakiondoka na Naomi kwenda mahala alikoelekeza,Nabii Kasiano akaondoka kuelekea nyumbani kwake huku kichwa chake kikionekana kujaa mawazo.
“Yule binti anamaanisha anachokisema na kama nikimuachia lazima atakwenda kuharibu kila kitu.Lazima ataanika siri zangu zote.Haya ndiyo matatizo ya kufanya kazi na watoto wadogo.Wana faida zake na hasara zake pia.Imeniuma kumpoteza Naomi kwa sababu ni binti niliyeanza kumpa mafunzo na tayari alikwisha ifahamu biashara na
kinachonifurahisha zaidi Naomi ana ujasiri mkubwa.Nilitegemea angekuwa ni mtu muhimu sana kumtumia kibiashara lakini imekuwa tofauti.Anyway sihitaji hatari yoyote katika biashara zangu.Ngoja tu nimuondoe nitapata msichana mwingine ambaye atachukua nafasi yake” akawaza Kasiano **************
Mazishi ya mchungaji Adam Watwila yalihudhuriwa na watu wengi sana kwani ni mtu aliyefahamiana na watu wengi.Kikubwa kilichozua minong’ono msibani ni kutoonekana kwa mwanae wa pekee Zoe.Ni mtu mmoja tu aliyefahamu mahala alipo naye ni Nabii mkuu Kasiano Muyenzi.
Ibada ya mazishi iliongozwa na Nabii Kasiano na katika mahubiri yake aliwataka watu kuwa na uvumilivu na kudumu katika maombi hata pale wanapopitia magumu katika maisha yao.Katikati ya mahubiri akafumba macho kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“Ndugu
waombolezaji,ninazitazama nyoyo zenu,zimeumia kwa kifo cha ghafla sana cha mchungaji Adam.Bwana amenionyesha namna nyoyo zenu zinavyosononeka kwa kumchukua mtumishi wake huyu lakini ameniambia kwamba amesikia kilio na maombi yenu kuhusu binti yetu Zoe mtoto wa mchungaji Adam.Siku mbili zilizopita Zoe binti wa mchungaji Adam alitoweka shuleni katika mazingira ya kutatanisha sana.Mimi na baadhi ya wachungaji wakiwamo Adam na mke wake tulizama katika maombi kumuomba Mungu
amrejeshe binti yetu akiwa mzima na wakati tukiomba Bwana akaniambia nimwambie mchungaji Adam asihofu mwanae ni mzima ! akasema Nabii Kasiano
“Baada ya kipindi cha maombi kumalizika niliwaita ofisini kwangu Adam na mke wake na kuwaeleza kile ambacho bwana alikuwa amenituma niwaambie.Wakati nikiwapa ujumbe Adam akaniambia kwamba bwana amemfunulia mahala alipo mwanae.Aliniambia kwamba ameonyeshwa njozi kuwa binti yake yuko Morogoro amefichwa katika hoteli moja ambayo hakunitajia jina lake.Aliniomba nimuazime gari langu kwani gari lake lilikuwa na matatizo na lisingeweza kwenda safari ndefu,na bila kupoteza muda yeye na mke wake wakaanza safari ya kuelekea Morogoro na baadae jioni tukapata taarifa kwamba wamepata ajali na wamepoteza maisha.Baada ya kupata taarifa hizo niliwaomba waumini wangu tusihuzunike kwani bwana amemchukua mtumishi wake na toka wakati huo nimekuwa katika maombi mazito kumuomba bwana anifunulie mahala aliko Zoe na muda mfupi uliopita bwana ameniambia kwamba ameiona huzuni yenu na akanifunulia kwamba binti atarejea nyumbani” Makofi mengi yakapigwa
“Shetani amejaribu kuitikisa nyumba ya mchungaji Adam lakini ameshindwa na binti atarejea nyumbani haleluya !
Maneno yale ya Nabii
kasiano yalileta faraja kubwa kwa ndugu na jamaa waliokuwa na maswali mengi kuhusiana na mahala alipo Zoe.Hatimaye baada ya ibada ndefu miili ya mchungaji Adam na mkewe ikazikwa na usiku wa siku hiyo ndipo Zawadi Mlola alipomchoma Naomi sindano ambayo ilimuharibu akili.
************
Saa kumi na mbili za asubuhi msichana mmoja asiyefahamika alikutwa katika kituo cha basi akionekana kuwa na matatizo ya akili kwani alikuwa anazungumza mwenyewe na kuna wakati alikuwa akivua nguo na kubaki mtupu.Haikujulikana mara moja msichana yule ametokea wapi na hakuna aliyemjali.
Kituoni pale kulikuwa na watu wawili waliokuwa wakifuatilia nyendo za Yule msichana bila watu kuwagundua.Saa mbili za asubuhi likafika gari pale kituoni wakashuka watu wanne na kumchukua Yule binti wakaondoka naye na moja kwa moja wakampeleka
katika kanisa la injili ya wokovu lililo chini ya nabii Kasiano Muyenzi.
Saa nne za asubuhi Nabii Kasiano akafika kanisani na kukuta wachungaji wakiendelea kumuombea msichana Yule ambaye alikuwa amefungwa kamba mikononi.
Nabii Kasiano akaenda ofisini kwake na kuwasiliana na ndugu za marehemu mchungaji Adam akawajulisha kwamba Zoe amepatikana
lakini hali yake si nzuri kwani amekumbwa na mapepo akawataka wafike pale kanisani.Nabii Kasiano akaungana na wachungaji wengine katika maombi na wakati wakiendelea kuomba zikafika gari nne wakashuka ndugu wa mchungaji Adam na kuingia kanisani ambako walimkuta Zoe akiwa amezungukwa na wachungaji wakimuombea.Wote
walistushwa na hali ile aliyokuwa nayo kwani alionekana ni mtu mwenye matatizo ya akili.Alikuwa anacheka na kuzungumza mambo yasiyoeleweka.Ndugu baada ya kuiona hali ile ya wakamuomba Nabii Kasiano wamchukue Zoe wampeleke hospitali.Nabii Kasiano akawaomba wamuachie yeye atagharamia matibabu yote .Zoe alichukuliwa akapelekwa hospitali kuu ya Mtodora ambako alipokewa na kuanza kufanyiwa uchunguzi.Wakati ndugu wakisubiri kupata majibu kutoka kwa madaktari,ilitokea taharuki kubwa hospitalini hapo baada ya Zoe kujirusha kutoka ghorofani na kufariki dunia.
Dakika chache baada ya tukio lile kutokea ujumbe mfupi ukaingia katika simu ya Nabii Kasiano
“It’s done,she’s dead”
“Thank you” akajibu Kasiano
“Ameyataka
mwenyewe.Kitabu chake kinafungwa rasmi.Jina lake
litaondolewa katika kila
sehemu
lilikoandikwa.Nitahakikisha hakuna kumbu kumbu yake yoyote inayobaki.Pale mwili wake utakapooza kaburini hakutakuwa na kumbu kumbu yake hata moja itakayokuwa imebaki duniani” akawaza Nabii Kasiano
BAADA YA SIKU MOJA
Muuguzi Zawadi Mlola alifikishwa mahakamani akituhumiwa kumuua mpenzi wake wakati wa ugomvi uliotokea nyumbani kwa muuguzi huyo.Kesi yake ilisomwa halafu akarudishwa katika gereza la
Uwangwa.Wakati akirejeshwa gerezani alimuona askari magereza akisoma gazeti lenye kichwa cha habari kilichomstua kidogo
“Mgonjwa wa akili ajirusha ghorofani”
Chini ya habari ile kukawa na picha ikionyesha umati wa watu wakiwa wamejaa wakiishuhudia maiti ya msichana anayedaiwa kuwa mgonjwa wa akili aliyejirusha kutoka ghorofa ya saba katika hospitali ya Mtodora na kufariki dunia.Pembeni ya picha ile kubwa kulikuwa na picha ndogo ya msichana anayedaiwa kujiua.Zawadi akastuka baada ya kuiona picha ile ndogo akamuomba Yule askari amuazime lile gazeti akaisoma habari ile akakuta ni habari habari iliyomuhusu msichana anayeitwa Zoe Adam ambaye alipatwa na matatizo ya akili baada ya wazazi wake kufariki dunia katika ajali.
“Hapana,huu ni uongo.Msichana huyu ndiye Yule ambaye nilipelekwa kumchoma sindano .Zoe hakuwa na matatizo ya akili.Nimeshiriki katika kumuua huyu binti kwani ni mimi niliyemchoma sindano iliyomuharibu akili.Siwezi kukubali kishi na jambo hili.Lazima hawa watu watafutwe wakamatwe na washtakiwe kwa mauaji” akawaza Zawadi.
Usiku mzima hakuweza
kupata usingizi na siku iliyofuata alimuomba askari mmoja amsaidie kumpigia simu wakili anayemtetea ambaye alifika pale gerezani na Zawadi akamweleza kile alichomuitia pale. “Nilichokuitia hapa hakihusiani na kesi yangu lakini nataka unisaidie kufikisha taarifa sehemu Fulani kwa ndugu za Yule msichana aliyejirusha kutoka ghorofani hospitali ya Mtodora akidaiwa kuwa ni mgonjwa wa akili” akasema Zawadi
“Msichana Yule si mgonjwa wa akili.Ninamfahamu vyema na ninafahamu kila kilichomtokea.Hakuwa mgonjwa wa akili.Ninaomba ufikishe taarifa kwa ndugu zake ili wanitafute na mimi nitawapa ukweli wote ili haki ipatikane”akasema Zawadi Ujumbe wa Zawadi ulifika kwa ndugu wa Zoe na wao pia wakamtaarifu Nabii Kasiano kuhusu taarifa ile ambaye aliahidi kulifuatilia lile jambo
Asubuhi na mapema siku iliyofuata alifika mtu mmoja pale gerezani na kuonana na Zawadi.Hakuwa anamfahamu mtu Yule na moja kwa moja akahisi ni ndugu wa Zoe
“Sikiliza Zawadi nimekuja hapa kukupa angalizo.Tumepata taarifa kwamba unataka kuzungumza na ndugu wa Zoe kuwaeleza ukweli.Nimekuja kukupa onyo kwamba usithubutu kufanya hivyo.Tunakufuatilia na ukithubutu kusema chochote tutakumaliza.Sisi tunao uwezo wa kuingia hata gerezani na kukumaliza.Ukitaka kuendelea kuwa hai chunga sana ulimi wako.Huo ndio ujumbe niliokuletea” akasema Yule jamaa na kuondoka akimuacha Zawadi akitetemeka kwa hofu.Hakujua wale jamaa wamezipataje taarifa zile.
Saa nne za asubuhi walifika ndugu za mchungaji Adam kuonana na Zawadi lakini wote walibaki vinywa wazi baada ya Zawadi kukana kumfahamu Zoe.Aliwataka radhi kwa kuwasumbua na ndugu wale wakaondoka kwa hasira
**************
“Suala la Naomi limekwisha lakini kuna watu wachache wamebaki ambao wanaweza wakaliendeleza suala hili.Ni gazeti la
Fukufuku.Adam aliwapa kazi ya kuchunguza mtu ambaye alikuwa na mahusiano na mwanae na tayari wamekwisha anza uchunguzi wao.Nataka wafuatiliwe kwa makini kila wanachokifanya na waondolewe taratibu mmoja mmoja bila kuleta mashaka yoyote kama kuna mkono wa mtu” Nabii Kasiano alimpa maelekezo kiongozi wa kundi hatari la Black Mafia ambalo hulitumia katika shughuli zake mbali mbali
Lidya Kipara mwandishi mahiri wa habari za kiuchunguzi alianza rasmi kuchunguza suala lile la kupotea kwa Naomi au Zoe Adam na kisha kupatikana akiwa na matatizo ya akili na baadae kujirusha kutoka ghorofani na kupoteza maisha.Kwa bahati mbaya wakati akifanya uchunguzi wake hakujua kama anafuatiliwa kila anachokifanya.Nyumbani kwake kulifungwa kamera za siri na alikuwa anafuatiliwa kwa saa ishirini na nne kila anachokifanya,gari lake pia liliwekwa kamera ya siri na vifaa vya kunasa maongezi na kumuonyesha mahala aliko,simu yake ilidukuliwa na ilifuatiliwa kwa saa ishirini na nne,kila simu aliyopiga ilisikilizwa na mtu aliyempigia kuchunguzwa.Zoezi la kumfuatilia Lidya lilidumu kwa miezi kadhaa kisha Black Mafia wakawasilisha taarifa ya uchunguzi wao na baada ya kuipitia taarifa ile Kasiano akatoa maelekezo kwa viongozi ambao ni Paul Lewis na John Mkizi
“Nimeipitia taarifa ahsanteni kwa kazi nzuri mliyoifanya.Huyu mwandishi Lidya anaonekana kupiga hatua katika uchunguzi wake na kwa hapa alipofikia hatuwezi kumuacha akaendelea mbele zaidi tunatakiwa kumuondoa yeye na wale wote anaoshirikiana nao.Mipango ya kumuondoa ianze mara moja.Nataka muandae mpango ambao itaonekana huyu mpenzi wake aliyenaye ambaye hapa katika taarifa mmemtaja anaitwa ……..” akasema Nabii Kasiano akaichukua tena taarifa akalitafuta jina la mpenzi wa Lidya
“Anaitwa Papi Gosu Gosu.Nataka ionekane huyu ndiye aliyemuua Lidya.Nataka utaalamu wa hali ya juu mno utumike katika jambo hili na kila kiumbe hai kiamini ni kweli Gosu Gosu ndiye aliyemuua Lidya” akasema Kasiano
“Nimekuelewa mzee lakini kuna jambo ambalo haliko katika taarifa hiyo na ambalo linaweza kuwa na tatizo kidogo kwetu” akasema John Mkizi “Jambo gani John? Akauliza Kasiano
“Kuna mtu anaitwa Mathew Mulumbi anajitokeza katika picha”
“Mathew Mulumbi?
Akauliza Kasiano
“Hili si jina geni.Who is he?
“Huyu ni jasusi nguli,historia yake inaonyesha ni mtu hatari sana” akajibu Paul
“Mathew Mulumbi
anatokeaje katika picha hii?
Kasiano akauliza
“Licha ya kwamba ni jasusi lakini pia ni bilionea.Ana
makampuni kadhaa makubwa hapa nchini na Papi Gosu Gosu ndiye msimamizi wa biashara zake zote.Endapo tutamtumia Gosu Gosu katika jambo hili tunaweza kujikuta tukikabiliana na Mathew Mulumbi”
“John nimesema kwamba
nataka jambo hili lifanyike na kumuaminisha kila kiumbe hai kwamba Gosu Gosu ndiye aliyemuua mpenzi wake.Mathew akiwa ni miongoni mwa viumbe hai naye lazima aamini hivyo”akasema Kasiano
“Mkuu sikushauri sana kumtumia Gosu Gosu katika jambo hili.Tunaweza tukatengeneza ajali au hata uvamizi lakini tukamuweka Gosu Gosu nje ya hili jambo”akashauri John
“Paul na John mnaniangusha.Black Mafia mnao uwezo mkubwa wa kufanya kila kitu sehemu yoyote.Hampaswi kumuhofia mtu yeyote.Wa kuhofiwa pekee ni Mungu ambaye anatupa uhai huu lakini ukiacha Mungu hakuna binadamu anayeweza kutupa hofu.Huyu Mathew Mulumbi ni takataka tu na anaweza akakunjwa
kama karatasi.Sikilizeni tunaendelea na mpango wetu wa kumuua Lidya na mzigo woe ataubeba Gosu Gosu.Akisha ingia gerezani tutatengeneza mpango mwingine wa kumuua humo humo gerezani na hakutakuwa na hatari yoyote.Huyo Mathew Mulumbi where is he now? Akauliza Kasiano
“Kwa sasa hatufahamu mahala alipo”
“Nataka mumtafute na
kujua mahala alipo.Go to all your sources and dig deeper find him.Kama yuko hai ndani ya dunia hii lazima apatikane.Nataka mpaka jioni ya leo muwe tayari mnafahamu mahala alipo ! akasema Kasiano na akina Joh wakaondoka
“MathewMulumbi !
akasema Kasiano na kuvuta pumzi ndefu akaichukua kompyuta yake akaingia mtandaoni kumtafuta ni nani.Alipata taarifa nyingi za kumuhusu Mathew na alihisi shati lake likiloa jasho
“Kumbe huyu si mtu wa mchezo mchezo.Taarifa zake zinaogopesha lakini mimi sipaswi kuwa na hofu.Ninayemuhofia ni Mungu pekee na hakuna mwanadamu katika dunia hii anayeweza kuninyima usingizi.Pamoja na umahiri wake,lakini huyu Mathew Mulumbi bado ni mtu mdogo sana kwangu na hawezi kunitisha hata kidogo” akawaza Kasiano
Jioni ya siku ile akapokea taarifa kutoka kwa John kwamba baada ya uchunguzi wao wa kina wamebaini Mathew yupo nchini Japan katika visiwa vya Okinawa.
“Good.Tutamfuata huko huko na kumleta nyumbani halafu tutammaliza.Kwa sasa endeleeni na mipango ya kumuua Lidya” akasema Kasiano
Wiki mbili baadae Lidya aliuawa akiwa jijini Arusha alikomsindikiza mpenzi wake Gosu Gosu katika uzinduzi wa tawi jipya la kampuni yao.Baada ya mauaji hayo Gosu Gosu akakamatwa na kufunguliwa kesi ya mauaji.
DAR ES SALAAM - TANZANIA
SASA…………….
“Watu wasiojulikana wakiwa wamejihami kwa
silaha nzito alasiri ya leo wamevamia msafara wa magari ya polisi waliokuwa wanampeleka mtuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya na mauaji Mathew Mulumbi katika gereza la Uwangwa na kufanikiwa kumtorosha.Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo watu hao waliokuwa wamefunika nyuso zao walivamia msafara huo wa polisi mita chache baada ya kuvuka daraja la Nyerere wakashambulia askari na kisha kumtorosha mtuhumiwa huyo na kumpakia katika helkopta na kuondoka naye kuelekea mahala kusikojulikana.Mpaka sasa jeshi la polisi halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.Usiku wa kuamkia leo Mathew Mulumbi ambaye ni mfanya biashara mkubwa anayemiliki makampuni kadhaa hapa nchini alikamatwa baada ya polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kuvamia makazi yake na kukamata kiasi kikubwa cha dawa za kulevya na katika tukio hilo miili miwili ya watu waliouawa ilikutwa ndani ya nyumba hiyo.Wakati huo huo jeshi la polisi linawashikilia Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo na Kamishna Jenerali wa magereza nchini Chambao Mnenge kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio la kuuawa kwa mkuu wa gereza la Uwangwa”
Hii ilikuwa ni habari iliyopewa uzito mkubwa na vituo mbali mbali vya luninga na redio katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku.Nabii Kasiano aliitazama taarifa ile akiwa na mke wake Rita sebuleni ndani ya jumba lao la kifahari.
“Mpaka sasa jeshi la polisi wako kimya na hawajatoa taarifa yoyote ! akasema kwa ukali Kasiano
“Yawezekana hata wao jambo hili limewachanganya sana ndiyo maana wanataka kulichunguza kwa undani hawataki kukurupuka” akasema Rita
“Mathew Mulumbi !
akawaza Nabii Kasiano na kuvuta pumzi ndefu akafikiri
halafu akauliza
“We had him.Tayari
tulikwisha mvisha kitanzi.Nani hawa wamemtorosha? Akauliza na kumtazama mkewe
“Rita what do you think?
Kabla Rita hajajibu mlinzi akaingia na kumjulisha Kasiano kwamba kuna mgeni amewasili akatoa ruhusa akaribishwe ndani.Sekunde chache baadae mlango wa sebuleni ukafunguliwa akaingia jamaa mmoja mrefu mwembamba .
“Karibu jemedari” akasema Kasiano huku akitabasamu
“Ahsante sana Kasiano” akajibu Yule jamaa ambaye kwa jina anaita Apollo Semba mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania na ni mmoja wa washirika wakubwa sana wa Nabii Kasiano.
“Pole na safari Apollo na samahani kwa kukurejesha nyumbani” akasema Kasiano
“Usijali Kasiano.Jambo hili ni muhimu mno kwani mambo yakiharibika hata biashara zetu zote zitaharibika ndiyo maana uliponiambia mambo yameharibika
nikaahirisha kila kitu na kurudi haraka” Akasema Apollo na Rita akaingia mle sebuleni na chupa ya pombe kali na glasi akasalimiana na Apollo.Hii ni sebule maalum kwa ajili ya Kasiano pekee na wageni wachache maalum ndio hukaribishwa katika hiyo sebule.Wakati Apollo akizungumza na Rita,Kasiano akachukua simu na kupiga
“Paul mko wapi? Apollo keshafika tunawasubiri ninyi”
“Tuko karibu mzee ndani ya muda mfupi tutakuwa hapo” akajibu Paul Lewis kiongozi wa kundi hatari la
Black Mafia nchini Tanzania.
Hazikupita dakika kumi wakawasili watu watatu,Paul Lewis,John Mkizi na Dennis Lome
“Karibuni makamanda wangu” akasema Kasiano na wote wakajumuika kupata mvinyo ule mkali.
Dakika kama kumi na tano baadae akawasili Keofasi Mabula naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi.Keofas au Keo kama anavyofahamika na wengi ni mmoja wa mawaziri wachache wenye ukwasi mkubwa.Kasiano akampokea na kumkaribisha sebuleni akasalimiana na watu aliowakuta mle na baada ya maongezi mafupi Kasiano akafungua kikao
“Ndugu zangu karibuni sana katika kikao hiki muhimu mno.Sintakifungua kwa sala kikao hiki kwani hakina mambo yanayomuhusu Mungu” akasema na kunyamaza kidogo.
“Imekuwa vyema
mmehudhuria nyote na hata Apollo alikuwa na safari lakini nimemrejesha baada ya kufika Nairobi kutokana na umuhimu wa kikao hiki” akanyamaza tena na kuendelea
“Naamini nyote mpaka sasa mnafahamu kilichotokea na kwa Apollo ambaye alikuwa safarini nimekwisha muhadithia kila kitu” akanyamaza tena
“Nakumbuka wakati tunaandaa mauaji ya Lidya,Paul na John walinishauri kwamba tusimtumie Gosu Gosu kama muuaji na nilitaka kufahamu kwa nini wakanieleza kwamba ana mahusiano na mtu anaitwa Mathew Mulumbi” akanyamaza tena kwa sekunde kadhaa
“Nakumbuka nilicheka
kidogo na kuwauliza ni nani huyo Mathew Mulumbi ambaye anaweza akasababisha tukashindwa kutekeleza mipango yetu? Wakanieleza kwamba ni mmoja wa majasusi nguli kuwahi kutokea hapa Tanzania.John alirudia mara ya pili kuniomba tusimtumie Gosu Gosu kwa sababu ni mtu wake wa karibu sana lakini nilipuuza na nikaagiza mipango yetu iendelee kwani kama hatuwezi kutetemshwa na nchi basi mtu mmoja hawezi kuwa kikwazo kwetu.Leo nataka nikiri kwenu kwa mara ya kwanza kwamba nilifanya kosa kukataa ushauri mzuri ulitolewa na vijana wangu.Mimi ni mkubwa wenu nyote lakini si kila wakati nitakuwa sahihi katika maamuzi hivyo mnisamehe sana kwa haya yanayotokea leo” akasema Kasiano
“Laiti ningekuwa nabii wa kweli ningeweza kuona kile kinachokuja kutokea mbele lakini kama mnavyojua tena………” akasema Kasiano na wote sebuleni wakangua kicheko kikubwa.
“Tuweke utani kando.Ndugu zangu tumekutana hapa ili tujadiliane kuhusiana na hiki kilichotokea na kutafuta muafaka.Kikubwa ni kinachotawala kikao hiki ni Mathew Mulumbi.He’s a big threat to us and he’s still at large.Paul hebu tupe picha ya hatari ya huyu jamaa kwetu ! akasema Kasiano.
“Mipango yetu ilikwenda vizuri na Mathew akarejea nchini na kama tulivyokuwa tumetazamia alikwenda Arusha akaonana na Gosu Gosu ambaye alimueleza kila kitu.Tulisubiri kuona hatua atakazozichukua Mathew na kama tulivyotarajia alianza uchunguzi na tukaamua kumuondoa lakini akanusurika kwa namna ya ajabu sana katika bomu tulilolitega garini.Kunusurika kuuawa kulifungua ukurasa mpya na akajipanga vizuri kukabiliana nasi.Aliungana na Dr Fabian na mke wake katika kuwatafuta watu waliomtengenezea Gosu Gosu kesi ile.Naweza kusema kwamba tayari wamekwisha piga hatua kubwa na hadi wamefanikiwa kumpata Zawadi Mlola ambaye anafahamu mambo kadhaa kuhusu Naomi .Kuna mambo ambayo lazima Zawadi alimwambia Mathew lakini kwa bahati nzuri kitu pekee anachokifahamu Zawadi ni kumchoma Naomi sindano iliyomuharibu akili.Hafahamu chochote zaidi ya hapo.Mkuu alitoa maelekezo kwamba Mathew na wenzake wasiendelee zaidi ya hapo walipofika na ndipo tulipotenegeneza lile tukio na akanaswa bila kutumia nguvu lakini kwa namna ya ajabu tumempoteza.Kuhusu hatari Mathew ni hatari kwetu kwa sababu tayari kuna mambo amekwisha yafahamu na anaendelea kuchimba zaidi na kwa sasa baada ya kunusurika atakuwa ni kama mbogo aliyejeruhiwa.Anafahamu jina lake tayari limechafuka ile sifa yake nzuri aliyokuwa nayo hapa nchini imetoweka hivyo atataka kujisafisha na njia pekee ya kusafisha jina lake ni kuwatafuta wale waliomtengenezea kesi ile yaani sisi hivyo atatumia kila mbinu aliyonayo kuhakikisha hilo linafanikiwa.Kwa hiyo kama ulivyosema mkuu kwamba he’s a big threat to us” akasema Paul ukimya mfupi ukapita
“Haikuwa rahisi kumpata Mathew Mulumbi na kumuingiza katika mtego wetu.Imenigharimu millions of money hivyo sitaki fedha hizi zote zipotee bure.Lazima tuhakikishe Mathew anapatikana .Huyu mtu si hatari kwangu pekee bali kwetu sote.Naibu waziri kuna nini kwa upande wako?Jeshi la polisi mmefikia wapi hadi sasa katika kulichunguza suala hili? Akauliza Kasiano
“Nilikuwa Dodoma na
nimewasili Dar es salaam jioni hii baada ya kuniita na mpaka sasa bado sijapata taarifa za kina kuhusiana na tukio hili” akasema naibu waziri Keofas
“Muda mfupi kabla hamjafika tulikuwa tunatazama taarifa ya habari na karibu vyombo vyote vya habari havina taarifa za kina kuhusiana na hilo tukio lakini kuna kituo kimoja wamejaribu kuwahoji baadhi ya mashuhuda walioshuhudia tukio hilo likitokea” akasema Rita
“Ukiwasikiliza baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo unapata picha kwamba jambo hili limefanywa na watu wataalamu mno.Walijipanga vyema ndiyo maana wakaweza kuwastukiza polisi na wakamchukua Mathew” akasema Rita
“Picha nyingine ambayo inakuja hapa ni kwamba hawa
jamaa walipata taarifa ya kuhamishwa kwa
Mathew,kutoka ndani ya jeshi la polisi.Wasingeweza kujiandaa kama wasingekuwa na taarifa zenye uhakika” Kasiano akasema.Kengele ya mlangoni ikalia akainuka Rita akaenda kufungua mlango akakutana na mlinzi wa Kasiano akiwa ameongozana na mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai David
Chamwino.Wote wakasimama na kumkaribisha David
“Samahani ndugu zangu kwa kuchelewa”akasema David “Usijali David” akasema Kasiano na Rita ambaye ndiye aliyekuwa muhudumu wa kikao kile akamuhudumia David kinywaji alichohitaji.Baada ya kunywa funda moja akalegeza tai halafu akavua koti.
“Tunaweza
kuendelea”akasema David
“David hujachelewa sana.Kikao ndiyo kwanza kimeanza na tunajaribu kulichambua tukio hili lililotokea kutafuta majibu ya nani waliofanya tukio lile na wapi alipo Mathew Mulumbi?Tunachokiona hapa katika tathmini yetu ya haraka haraka ni kwamba watu waliofanya tukio lile walikuwa na taarifa zenye uhakika kwamba Mathew Mulumbi anahamishwa kupelekwa gereza la Uwangwa na wakajipanga kumteka.Tunaamini taarifa hizo lazima watakuwa wamezipata kutoka ndani ya jeshi la polisi” akasema Kasiano
“Hilo linawezekana kabisa.Hawakufanya kwa kubahatisha walifahamu kile walichokuwa wanakifanya” akasema David Chamwino “Swali linaloibuka hapa ni je serikali ndiyo iliyocheza mchezo huu? Akauliza Nabii Kasiano
“Mkuu sina hakika kama serikali wanahusika katika jambo hili”akasema naibu waziri Keofas
“Kwa nini Keo?akauliza Nabii Kasiano
“Niko serikalini na kila kinachoendelea ndani ya jeshi la polisi ninakifahamu hivyo kama kungekuwa na mpango wowote wa serikali kumtorosha Mathew
ningefahamu.Mkumbuke
vilevile Rais alitangaza vita kali dhidi ya dawa za kulevya lakini mafanikio yake yamekuwa madogo kutokana na kutokuwepo na ushirikiano baina ya nchi za SADC na vile vile hata ndani ya nchi tangu alipotangaza vita hakujawahi kamatwa muuzaji yoyote mkubwa zaidi ya kukamatwa watu wadogo wadogo.Kukamatwa kwa Mathew Mulumbi na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kinaipa serikali picha kwamba kikosi vilivyowekwa kwa ajili ya kupambana na dawa za kulevya kinafanya kazi hivyo basi kwa namna yoyote ile hawawezi wakakubali kumpoteza mtu muhimu kama Mathew.Au unasemaje
David?” akasema naibu waziri Keo
“Uko sahihi mheshimiwa naibu waziri.Hakuna mahala ambako serikali inaonekana kushiriki katika tukio hili.Yule jamaa ni jasusi na ana marafiki wengi katika idara hiyo yawezekana marafiki zake ndio waliomtorosha” akasema David
“Kwa hoja hizo hata mimi nakubaliana nanyi kwamba serikali haina sababu yoyote ya
kufanya tukio kama lile la kumtorosha Mathew Mulumbi.Tunatakiwa kufanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunawafahamu waliofanya tukio lile” akasema Kasiano
“Mkuu kuna kitu
nakifikiria” akasema Paul Lewis mkuu wa kundi la black Mafia.
“Karibu Paul” akasema Kasiano
“Baada ya Mathew kukamatwa tumeipata simu yake na katika kufuatilia watu aliokuwa anawasiliana nao tumekuta amekuwa akifanya mawasiliano na mke wa Rais mstaafu Dr Fabian anayeitwa Ruby Kelelo.Ninahisi huyu mwanamke anaweza akatusaidia kufahamu mahala alipo Mathew” akasema Paul
“Mnafahamu mahala
alipo? Akauliza Kasiano
“Nilitoa maelekezo waendelee kumtafuta kwani ametoweka na hajulikani alipo.Ngoja niwasiliane na watu wangu kama wamefanikiwa kupata chochote kuhusu huyu mwanamke”akasema Paul na kuchukua simu akawasiliana na watu wake halafu akakata simu na kusema
“Mpaka sasa hajulikani mahala alipo.Hata hivyo nina wazo.Tunaweza kumtumia Dr Fabian kufahamu mahala alipo mke wake.Kwanza kabisa tunatakiwa kumuua Kamishna Chambao.Huyu hatuna sababu ya kuendelea kumshikilia kwani ni hatari kwetu.Tayari kuna kitu anakifahamu kuhusu sisi kwa sababu aliwasiliana na Dennis Lome kwa simu akimtaka amkabidhi Deus kwa vijana tutakaowatuma kwake.Japo anaweza akaogopa kulisema hilo kwa kuogopa kuvujishwa kwa video chafu ya mke wake lakini maji yanaweza yakamfika shingoni na akaamua kusema ukweli hivyo basi tumuondoe haraka kabla hajaleta madhara.Tutamuua usiku wa leo kwa kumpulizia hewa ya sumu.Baada ya Chambao kufariki dunia David atakwenda kumuhoji tena Dr Fabian na kumwambia kwamba atamsaidia kumtoa katika kesi ile kama atasaidia kuonyesha mahala alipo mke wake ambaye tukimpata tutakuwa tumepiga haua kubwa kufahamu mahala alipo Mathew Mulumbi”
“Ni wazo zuri” akasema
David Chamwino
“Excellent idea.Tujipange kwa ajili ya hilo usiku wa leo.David tunakukabidhi jambo hili utalishughulikia ili tufahamu mahala alipo mke wa Dr Fabian”
“Sawa mkuu” akajibu David
“Jamani kuna swali ambalo nimekuwa najaribu kujiuliza” akasema Rita
“Je kulikuwa na ulazima wowote wa kumuhamisha Mathew Mulumbi kutoka kituoni alikokuwa anashikiliwa akihojiwa na kumpeleka katika gereza la Uwangwa? Akauliza Rita na watu wote wakatazamana
“Swali lako mama Rita lina msingi sana.Lazima tujiulize kama kweli kulikuwa na ulazima wa kumuhamisha Mathew Mulumbi leo” akasema Paul Lewis
“Naibu waziri unasemaje kuhusu hilo?Unadhani kulikuwa na ulazima wowote kwa Mathew Mulumbi kuhamishwa leo kupelekwa gereza la Uwangwa?akauliza Kasiano
“Nadhani DCI anaweza
akatupa maelezo mazuri zaidi kwani yeye alikuwa hapa karibu mimi nilikuwa Dodoma” akasema Keo
“David kulikuwa na ulazima wa kumuhamisha Mathew Mulumbi kwenda katika gereza la Uwangwa leo? Akauliza Kasiano na David akafikiri kidogo na kusema
“Naweza kusema ndiyo na hapana.Ndiyo kwa sababu kwa namna tulivyotengeneza tukio lile Mathew Mulumbi anaonekana kama ni mmoja wa wafanya biashara wakubwa kabisa ambao serikali imekuwa ikiwatafuta siku nyingi na vile vile wanafahamu kwamba Yule ni jasusi ana uwezo mkubwa wa kufanya jambo lolote hata anapokuwa kizuizini,ana uwezo mkubwa wa kucheza na silaha na ana mbinu nyingi za kutoroka hivyo basi lazima wachukue
hatua za kuhakikisha anawekwa sehemu salama.Hapana kwa sababu ulinzi ni mkubwa pale kituoni na hakukuwa na ulazima wa kuhofu kuhusu kutoroka kwa mtuhumiwa”
“Kwa hiyo Mathew alihamishwa kwa sababu za kiusalama? Akauliza Rita “Nahisi hivyo” “Unahisi” akasema Kasiano
“Ndiyo nahisi hivyo kwa sababu sikushirikishwa katika mchakato wa kumuhamisha Mathew bali nilipokea maelekezo kwamba Mathew anatakiwa kuhamishwa kupelekwa katika gereza la Uwangwa na kama tutaendelea kumuhoji basi ni akiwa gerezani”
“Nani alitoa maelekezo hayo? Akauliza Naibu waziri Keofas
“Maagizo hayo yalitoka moja kwa moja kwa IGP” “IGP? Akauliza Kasiano “Ndiyo na hata yeye mwenyewe alilazimika kuwepo wakati wa kumuhamisha Mathew akitaka kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa”
“Guys mtanisamehe kwa maswali yangu” akasema Rita
“Usihofu Rita uliza” akasema Keofas
“Nataka kufahamu mchakato ulivyo tangu mtuhumiwa anapokamatwa hadi kufikishwa mahakamani” akasema Rita
“Kwa kawaida watuhumiwa wote wanapokamatwa huwekwa mahabusu wakati wakiendelea kuhojiwa. Kw kkwa Mathew ilikuwa tofauti.Alikamatwa usiku na kupelekwa kituoni kuhojiwa na kabla hajamaliza kuhojiwa akahamishiwa gerezani”akasema David
“Bado kuna ukakasi katika suala hili David na ukakasi upo katika uharaka wa kumuhamisha Mathew kutoka kituo cha polisi kwenda gerezani” akasema Rita
“Rita kuna kitu una kizunguka na hutaki kukiweka wazi.Naomba nikusaidie kukiweka wazi.Rita ana mashaka na mkuu wa jeshi la polisi kwa maelekezo yake ya kumuhamisha Mathew” “Exactly ! akasema Rita
“Nini hasa wasi wasi wako Rita? Akauliza David
“Ni kuhusiana na uharaka wa kumuhamisha Mathew na uwepo wa kiongozi huyo mkuu wa jeshi a polisi wakati Mathew anahamishwa.Hii imewahi kutokea hapo kabla? Rita akauliza
“IGP anaweza akawepo
sehemu yoyote ile kwani polisi wote wako chini yake hivyo si
kitu cha ajabu kuwepo wakati Mathew Mulumbi anahamishwa” akasema DCI David Chamwino
“Jamani naomba
tumridhishe Rita yeye bado ana duku duku na suala hili.Napendekeza tumfanyie uchunguzi IGP tujiridhishe.Paul mtalifanyia kazi hilo.Fuatiliani mazungumzo yote ya IGP kwa siku ya leo na mfahamu watu aliowasiliana nao ili tuone kama anahusika kwa namna yoyote ile na jambo hili” akasema Kasiano
“Sawa mkuu tutalifanyia kazi.Halafu kuna Yule mgonjwa Zawadi Mlola ambaye bado yuko
hospitali.Alimpigia simu Mathew Mulumbi akamtaka akaonane naye hospitali kuna mambo anataka akamueleze nini maelekezo yako? Akauliza Paul
“Mtoeni pale hospitali na hakikisheni anawaeleza kile alichomueleza Mathew Mulumbi.Mkisha pata maelezo yake muueni ! akasema Kasiano.
Kikao kiliendelea na mikakati kadhaa ikaweka kwa ajili ya kuhakikisha
wanampata Mathew Mulumbi
Mathew Mulumbi
alihamishiwa nyumbani kwa Zarina kama alivyokuwa ameshauri.
“Thank you so much ladies kwa haya mliyonifanyia.Ninyi ni mashujaa wangu” akasema Mathew wakiwa sebuleni kwa Zarina
“Mathew kwa sasa endelea kupumzika tukuandalie chakula kisha….”
“No thank you Zari.Huu ni muda wa kazi chakula baadae”
“Mathew you need to eat first ! akasema Ruby
“Thank you ladies.Naomba tusipoteze muda.Najua hamkuniokoa ili kuja kunificha bali kuendeleza ile kazi tuliyokwisha ianza.Ruby naamini tayari umekwishamueleza Zari kila kitu kinachoendelea”
“Ninafahamu kila kitu tayari” akasema Zari
“Good.Tunaendelea pale tulipokuwa tumeishia.Wale jamaa baada ya mpango wao kushindwa kufanikiwa lazima wataongeza nguvu zaidi katika kujiimarisha na kuhakikisha siwi kikwazo au hatari kwao.Mambo yatakuwa magumu kuliko ilivyokuwa awali hivyo tujiandae.Ruby kwa upande wako kuna chochote umekipata zaidi ya
pale tulipoachia? Akauliza
Mathew
“Ndiyo Mathew.Ulinipa kazi ya kudukua simu ya kamishna Chambao na nilifanya hivyo nikafanikiwa kunasa mazungumzo kati yake na mtu ambaye hakutaja jina lake lakini alijitambulisha kwamba yeye ndiye mwenye video chafu ya mke wake na akatishia kuisambaza video
hiyo kama Chambao hatatekeleza kile atakachomuelekeza” akasema Ruby na kuifungua kompyuta yake akacheza mazungumzo ya Kamishna Chambao na Yule mtu aliyemtaka amkabidhi Deus kwao.
“Nilijua tu kuna kitu hakiko sawa.Kwa nini mzee Yule akaamua kufanya vile? Kwa nini asingewasiliana nami na kunieleza ukweli ingetusaidia sana kuwapata hawa jamaa ! akasema Mathew
“Nilipoyapata mazungumzo haya
nikakutafuta simuni ili nikujulishe lakini hukuwa ukipatikana” akasema Ruby
“Wakati huo tayari nilikwisha ingia katika mtego wa wale jamaa na nilikuwa katika mikono ya polisi.Waliponikamata walichukua simu yangu na kila nilichokuwa nacho ndiyo maana sikuweza kupatikana tena hewani”
“Naamini utatueleza nini kilitokea lakini kabla ya hapo kuna jambo nataka kukufahamisha”akasema Ruby
“Baada ya kukutafuta simuni bila mafanikio tuliamua kulala tukitegemea tutaonana kesho asubuhi lakini usiku wa manane ukaingia ujumbe katika simu yangu kutoka kwa mtu nisiyemfahamu” akasema Ruby na kumuonyesha
Mathew jumbe za Yule mtu. “Baada ya kuupokea ujumbe kutoka kwa mtu huyu ambaye nimempa jina la Zero tulijadiliana na Fabian na kuamua kutokudharau ujumbe ule hivyo nikaondoka mimi na watoto usiku ule ule kwenda mafichoni.Leo asubuhi akanitumia tena ujumbe mwingine” akasema Ruby na kumuonyesha Mathew ujumbe mwingine uliotumwa na Zero akimtaka ajifiche.
“Baada ya kupata ujumbe huo sikuwa na namna nyingine nikalazimika kuomba msaada kutoka kwa Rais Festus na akakubali ndipo tulipoandaa mpango wa kukuokoa kwa kuwatumia makomando wa
SNSA.Kwa ufupi hivyo ndivyo ilivyokuwa hadi sasa” akasema Ruby na Mathew akavuta pumzi ndefu na kabla hajasema lolote Zari akarejea akiwa na sahani iliyojaa nyama za kuku
“Guys tuendelee na mipango huku tukipata nyama.Tunahitaji nguvu” akasema Zarina
“Thank you Zari”akasema Mathew
“Kwa upande wako nini hasa kilitokea?Mara ya mwisho uliponipigia uliniambia unakwenda kumtazama Zawadi halafu ukaniambia tena kuna kitu umekipata kinaweza kutusaidia baada ya hapo hatukuwasiliana tena” akasema Ruby
“Nilionana na Zawadi akaamua kunieleza ukweli kwamba Naomi Bambi si jina halisi la Yule msichana ambaye alimchoma sindano ya kumuharibu akili bali jina lake halisi anaitwa Zoe something like that ! akasema Mathew
“Anadai kwamba analo
faili lenye taarifa za kumuhusu Zoe na amenielekeza mahala alikolificha ndani ya nyumba yake ya zamani.Kwa kuwa sikuwa na vifaa vya kuniwezesha kuingia mle ndani usiku ule niliamua kwenda nyumbani kuchukua vifaa na nilipofika ndipo nikakamatwa na
polisi.Tukilipata hilo faili
tunaweza kufahamu mengi kuhusiana na huyo msichana.Hukupata picha yoyote inayofanana na ile picha niliyoichora ya Naomi? Akauliza Mathew
“Nimejaribu lakini sijaweza kupata picha wala taarifa zozote za kuhusiana na Naomi Bambi.Imekuwa vizuri tumefahamu kuwa jina lake lingine ni Zoe labda tujaribu kumtafuta kwa kutumia jina hilo la Zoe” akasema Ruby
“Natakiwa kwenda katika ile nyumba ya Zawadi ya zamani na kulichukua faili ambalo lina taarifa za Zoe.Baada ya kulipata litatusaidia kumfahamu huyo msichana ambaye sakata hili lote limeanzia kwake” “Right now? Akauliza Zari
“Yes right now.Nahitaji silaha na usafiri.Una silaha
gani hapa kwako? Akauliza Mathew
“Ninazo baadhi ya silaha” akasema Zarina na kuondoka kwenda kuleta silaha alizonazo.
“Mathew una hakika hutaki kupumzika hata kidogo kabla ya kwenda huko? Akauliza Ruby
“Nina majeraha na ninahisi maumivu hasa katika mguu wa kushoto lakini hatuna muda wa kupumzika.Wale jamaa hawalali wanakesha wanafanya kazi kuhakikisha wanazuia mipango yoyote inayofanywa dhidi yao hivyo na sisi hatupaswi kulala.Tunapaswa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunawafahamu ni akina nani” akasema Mathew na Zari akarejea akiwa na sanduku lenye silaha.Mathew akachagua bastora mbili
“This is embarrassing” akasema Mathew
“Nini Mathew? Zari akauliza
“Do you have any new tshirt ? Hii fulana yangu imechafuka damu” akasema Mathew na Zarina akatabasamu akaenda chumbani kwake na kurejea na fulana nne Mathew akavua fulana aliyokuwa amevaa na Zari akaonyesha mstuko kutokana na mwili wa Mathew kujaa makovu ya majeraha aliyowahi kuyapata.Mathew hakumjali akachagua fulana moja iliyomtosha vizuri halafu akajaribu kutembea kidogo na kuhisi maumivu makali katika mguu wake wa kushoto
“Are you okay Mathew? Akauliza Ruby
“I’m fine” akajibu Mathew
“Sasa naweza kwenda.Ninyi mtabaki hapa.Tutawasiliana vipi kama kukiwa na tatizo lolote? Akauliza Mathew
“Mathew I’m gong with you ! akasema Zarina
“Zari please this is war.Hawa watu tunaowatafuta ni wauaji na hawana huruma hata chembe.Kuja hapa kwako tayari tumekuweka katika matatizo hivyo sitaki kukuweka katika matatizo zaidi” akasema Mathew
“Mathew ninaongoza idara nyeti kabisa hapa nchini ambayo jukumu lake ni kupambana na watu kama hawa.Usinione hivi ukadhani siwezi kazi.Nimepewa ukurugenzi wa SNSA kwa kuwa nimepitia mafunzo ya kutosha na ninaifahamu vyema kazi hii.Huwezi kwenda peke yako huko Mathew nitaongozana nawe” akasema Zari na kwenda chumbani kwake akabadili mavazi aliyokuwa amevaa akavaa suruali inayofanana na sare za jeshi ,akavaa na fulana ya kuzuia risasi kisha akavaa koti jeusi na kofia,akachuka kofia nyingine akampelekea Mathew
“Ruby hii ni simu yangu utabaki nayo kwa ajili ya mawasiliano.Usipokee simu yoyote zaidi ya simu nitakayopiga mimi.Kama utataka kuwasiliana nasi pia utanipigia katika namba hizi” akasema Zari na kumuelekeza Ruby kisha wakaondoka kuelekea katika nyumba ya Zawadi Mlola Zari akiwa ni dereva
“Kwa muda gani umekuwa
katika hii kazi? Akauliza Mathew wakiwa garini
“Nina miaka saba sasa katika kazi hii.Nimepata mafunzo nchini Urusi na China.Vipi kuhusu wewe kwa muda gani umekuwa katika kazi hii?
“Ni muda mrefu.Nusu ya maisha yangu hapa duniani nimekuwa katika kazi hii”akajibu Mathew wakapishana na gari mbili za askari polisi wakiwa doria na Mathew akaziweka sawa bastola zake
“Askari kadhaa wamefariki katika lile shambulio hivyo kuna doria kubwa leo kuwatafuta watu waliofanya tukio lile lakini usiwe na hofu nitakufikisha kokote kule
unakotaka kwenda” akasema Zari
“Thank you.Nimewaweka katika hatari lakini jambo hili ni muhimu mno.Hawa jamaa ni watu hatari sana na wanatumia nguvu kubwa
kujificha wasijulikane na hii ndiyo inayonipa nguvu ya kutaka kuwatafuta na kuwafahamu zaidi.I’ll protect you” akasema Mathew
“Kwa namna walivyoandaa
lile tukio wakikuhusisha na dawa za kulevya na mauaji ni wazi hawa jamaa wana uwezo na mtandao mkubwa.Ninahisi hata ndani ya jeshi la polisi tayari wana watu wao” akasema Zarina
“Lazima ni mtandao uliopenyeza mizizi sehemu mbali mbali muhimu na ndiyo mana mambo yao yanafanikiwa.Tutawafahamu mtandoa wao wote hakuna atakayebaki” akasema Mathew
Mathew alimuelekeza Zari sehemu ya kuegesha gari.
“Mahala tunakoenda si mbali sana kutokea hapa,utabaki garini mimi nitakwenda mahala hapo kuchukua faili ndani ya dakika chache nitakuwa nimerejea” akasema Mathew
“Mathew sikuambatana
nawe kwa ajili ya kuwa dereva wako bali kufanya nawe kazi hivyo tunakwenda pamoja huko katika hiyo nyumba kuchukua faili” akasema
Zarina
“Fine” akasema Mathew wakashuka kisha wakaanza kutembea kwa miguu kuelekea katika nyumba ya Zawadi Mlola.Walipita nyumba kadhaa na hatimaye wakafika katika eneo Fulani kulikuwa na mwangaza hafifu kwani nyumba mbili hazikuwa zikiwaka taa
“Nyumba yenyewe ni ile pale.Get ready.Wakati mimi ninafungua kufuli la getini wewe utakuwa ukihakiki usalama.Nyumba hii haijakaliwa na mtu kwa miaka kadhaa hivyo basi majirani wakisikia geti linafunguliwa wanaweza wakapatwa na ushawishi wa kujua nani anafungua” akasema Mathew kisha wakatembea kwa tahadhari hadi katika geti
“Mhhh ! Mathew akaguna baada ya kuona alama za matairi ya gari pale getini. Mathew akachukua vifaa vya kufungulia makufuli akaanza kazi ya kufungua kufuli lile ambalo halikuchukua muda mrefu
likafunguka.Akalisukuma geti wakaingia ndani akatoa kurunzi na kumulika kwani kulikuwa na giza.Wakitembea kwa tahadhari kubwa wakaukaribia mlango wa kuingilia sebuleni,Mathew akatoa funguo bandia na alipotaka kuuchomeka katika kitasa akiamini mlango umefungwa akastuka baada ya kugundua mlango ule haujafungwa.
“Mbona mlango uko wazi?
Akajiuliza
“Yawezekana ni vibaka walivunja mlango wakaingia na kuiba” akawaza na kwa tahadhari akaufungua mlango ule wakaingia ndani.Sebuleni hakukuwa na kitu hata kimoja zaidi ya makaratasi yaliyosambaa sakafuni.
“Sebule mbona tupu?
Akauliza Zari
“Vibaka wamekomba kila kitu humu ndani” akajibu Mathew kisha akaanza kupiga hatua kuelekea katika mlango wa chumba cha kulala
“Where’s the file? Akauliza Zari
“Katika chumba cha kul….” Akasema Mathew huku akiusukuma mlango wa chumba cha kulala na mara taa ikawaka mle chumbani na Mathew akapatwa na mstuko mkubwa baada ya kumuona mwanamke akiwa amefungwa katika kiti.Miguu yake ikafunga breki ya ghafla.Mwili ulizidi kumsisimka baada ya kugundua kwamba mwanamke Yule ni Zawadi Mlola akiwa amefungwa bomu tumboni.
“Zawadi ! akasema
Mathew kwa mshangao
“Mhhh !! Mhhhh ! Zawadi akaguna hakuweza kuzungumza kwani alikuwa amebandikwa gundi ya karatasi mdomoni.
“Jesus Christ ! akasema na kumstua Zarina ambaye naye alisogea karibu kuchungulia kitu kilichomstua Mathew.Zarina alihisi kama haja ndogo inataka kumtoka baada ya kumuona mwanamke akiwa amefungwa kitini huku akiwa na bomu.
“Mhhh ! mhhh ! Zawadi akaendelea kuguna.
“Zari we must save her ! akasema Mathew
“Mathew this is very dangerous !
“We have to try.We can’t
leave her like this ! akasema Mathew
“Una utaalamu wa kutegua mabomu? Akauliza
“Nina utaalamu kidogo.I’ll try to save her” akasema Mathew na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani.
“Mhhhh !! Mhhhhh !
Zawadi akaendelea kuguna
“Shhh ! Stay tight Zawadi I’m going to help you” akasema Mathew na kuanza kumsogelea Zawazi
“Mathew ! akaita Zari lakini Mathew hakumjali akaendelea kumsogelea Zawadi akiwa katika tahadhari kubwa.Taratibu akambandua gundi aliyokuwa amebandikwa mdomoni
“Mathew go ! Run ! akapiga kelele Zawadi
“Stay calm Zawadi we’re
going to help you ! akasema
Mathew
“Mathew tayari wanajua mko hapa.Huu ni mtego !
Tazama juu ya mlango ! akasema Zawadi na Mathew akageuka akatazama juu ya mlango ambako aliona kidude kikiwaka taa nyekundu.Ilikuwa ni kamera
“Zawadi faili liko wapi? Akauliza Mathew
“Wamelichukua ! akajibu Zawadi na Mathew akajisi kama nyundo inagonga kichwa chake mara akapata wazo
“Naomi Bambi jina lake
halisi ni nani? Akauliza haraka haraka
“Zoe Adam Watwila ndilo jina lake.Mathew wametega ile kamera ili kuangalia kila anayeing……”akasema Zawadi na Mathew akasikia mlio Fulani kutoka katika ile fulana yenye bomu aliyokuwa amevalishwa Zawadi na kwa kasi ya umeme akageuka na kuruka akatoka ndani ya kile chumba.
“Zari run !! akasema Mathew na mara tu alipomalizia kutoa mguu sebuleni ukasikika mlipuko akamrukia Zari na kumuangusha chini.
Zilipita sekunde kadhaa kisha Mathew akajaribu kuuvuta mguu lakini ulikuwa umegandamizwa na
tofali.Akasogeza matofali yale haraka haraka na kuutazama mguu wake ulikuwa unavuja damu.Bado kulikuwa na vumbi kubwa eneo lile na moshi.
“Zari ! Zari ! akaita Mathew na Zari akainua kichwa
“Are we safe? Akauliza Zari akiwa amechafuka vumbi.Mwili ulikuwa unamtetemeka
“We have to go
Zari.Umeumia sehemu?
Akauliza Mathew akijaribu kumuinua
“Nahisi ganzi kwenye mguu” akasema Zari.Mathew akamsaidia kunyanyuka kisha wakatoka.Mguu wa kulia wa Mathew ulikuwa unavuja damu.
Mlipuko ule ulipelekea watu wafungue milango ya nyumba zao kutazama kuna nini kimetokea.
“Jitahidi Zari tuondoke eneo hili kabla watu hawajajaa na kunitambua kwani taarifa zangu zimesambaa kila mahali” akasema Mathew akiwa na bastola mkono wa kulia huku mkono wa kushoto akimtegemeza Zari aliyekuwa akitembea kwa kuchechemea.Walifika katika gari lao Mathew akashika usukani wakaondoka
“Oh Thank you Lord ! akasema Zari na kuvuta pumzi ndefu
“That was so close to death ! akasema tena Zari
“Yah ! akasema Mathew
“Ndiyo maana
nilikutahadharisha awali kwamba hii ni vita.Hawa jamaa wamejipanga vilivyo kukabiliana nasi na kwa tukio hili wamedhihirisha namna walivyo hatari.Walifahamu lazima nitakwenda pale hivyo wakajiandaa kunimaliza.Maskini Zawadi ! akasema Mathew
SAA MBILI ZILIZOPITA
Moja ya ghala la kuhifadhia dawa la hospitali ya Katihar lilianza kuwaka moto na kuzua taharuki kubwa hospitalini pale.Watu wakaanza kukimbia hovyo kujaribu kuzima moto ule ambao haukujulikana chanzo chake.Askari wawili wakiwa nje ya chumba alimolazwa Zawadi mara akatokea jamaa aliyevaa koti jeupe kama daktari akawaomba askari wale wakasaidie katika tukio lile kwani kuna watu wanataka kutumia nafasi hiyo kuiba madawa.Askari wale bila kujua kama ule ulikuwa mtego wakatoka haraka haraka na bunduki zao kuelekea mahala unakowaka moto.Mara tu walipoondoka watu wanne wakafika katika chumba alimo zawadi na haraka haraka mmoja wao akamziba pua kwa kitambaa kilichowekwa dawa maalum na Zawadi akapoteza fahamu kisha wakamtoa mle ndani wakaondoka naye.Hakuna aliyeweza kuwatilia shaka kwani walikuwa kulikuwa na heka heka kubwa sana pale hospitali.Jamaa wale walimuingiza Zawadi katika gari kisha wakaondoka wakiwaacha watu wakiendelea na jitihada za kuuzima moto.
Zawadi alipelekwa katika nyumba Fulani akashushwa garini na kuingizwa ndani akawekewa kichupa Fulani puani akapiga chafya mfululizo
“Pole sana Zawadi” akasema jamaa mmoja aliyekuwa na ndevu nyingi.
“Jamani naombeni
msiniue ! akalia Zawadi baada ya kuziona sura za wale jamaa “Sikiliza Zawadi hatutakuua kama utatueleza ukweli.Uko tayari kusema ukweli?
“Niko tayari nitawaeleza kila kitu” akasema Zawadi huku akitetemeka
“Good.Jana usiku ulimuita Mathew Mulumbi
hospitali.Nini ulimweleza? Akauliza Yule jamaa mwenye ndevu
“Tafadhali jiokoe mwenyewe kwa kusema ukweli ama sivyo tutakuua Zawadi” akasisitiza Yule jamaa
“Ni kweli nilimpigia simu
Mathew na kumtaka aje hospitali nilitaka kumueleza ukweli kuhusu Naomi Bambi”
“Hicho ndicho tunataka kufahamu.Ulimweleza nini?
“Ni kuhusu faili”
“Faili lipi”
“Faili lenye maelezo ya Naomi ambalo nililihifadhi pale nyumbani kwangu nikamuelekeza akalichukue”
Wale jamaa wakamchukua
Zawadi hadi katika makazi yake ya zamani akawaonyesha mahala alikolificha lile faili
ambalo bado Mathew hakuwa amelichukua.
“Ahsante Zawadi kwa faili hili lakini pamoja na hayo bado hatutakuacha hai.Wewe na huyo shetani mwenzio lazima mfe” akasema Yule jamaa kisha Zawadi akazibwa mdomo kwa gundi halafu akafungwa barabara katika kiti na mara jamaa mmoja akaingia mle ndani akiwa na fulana iliyofungwa milipuko akavalishwa halafu ikategwa kamera ya siri ya kuwawezesha kuona kila atakayeingia mle ndani
“Kwa heri zawadi.Tutakutana huko mbele ya safari ! akasema Yule jamaa kisha wakaondoka “Tuna hakika Mathew lazima atafika hapa kulifuata hili faili na akifika tu hatatoka hai.Leo ni mwisho wake”
akasema Yule jamaa wakiwa garini
*************
Mlango wa mahabusu alimokuwamo Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo ulifunguliwa akaingia mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai David Chamwino.
“David ! akasema Dr
Fabian alishnagaa kidogo kwa
David kumfuata usiku ule
“Dr Fabian usishangae kuniona hapa muda huu.Saa
ishirini na nne sisi tuko kazini” akasema David
“Unataka nini usiku huu? Umekuja kunitoa nirudi nyumbani? Akauliza Dr Fabian na David akacheka kidogo
“Kurudi nyumbani bado Dr Fabian hata hivyo kuna jambo nataka tulijadili mimi nawe.Yawezekana bado hujapata taarifa lakini Mathew Mulumbi ambaye tulikuwa tunamshikilia kwa makosa ya dawa za kulevya na mauaji ametoroshwa jioni ya leo na watu wasiojulikana”
“Ruby ! Huyu lazima ni
Ruby amefanya jambo hilo! Akawaza Dr Fabian
“Dr Fabian katika mahojiano yetu leo asubuhi ulificha kuhusu mashirikiano yako na Mathew na hii ilitufanya tuamini unahusika katika mauaji yale ya Deus Mtege.Kwa ushahidi uliopo unatosha kabisa kukuingiza katika kesi hii mbaya ya mauaji na dawa za kulevya.Dr Fabian hii ni kashfa kubwa kwa mtu mwenye heshima kubwa kama wewe.Ninataka kulimaliza hili jambo kimya kimya ikiwa ni pamoja na kuufuta ushahidi wote unaokuangamiza katika kesi hii lakini kwa sharti moja tu”
“Sharti gani? Akauliza Dr Fabian
“Nataka utusaidie kumpata Mathew Mulumbi”
“Deus sihusiki na jambo lolote katika haya ninayotuhumiwa nayo na lingine ni kwamba sifahamu alipo Mathew Mulumbi” akasema Dr Fabian
“Katika maelezo yako asubuhi ulisema kwamba mkeo ni mtu wa karibu sana na Mathew.Tunaweza kumtumia huyo kufahamu mahala alipo Mathew Mulumbi” akasema David
“Ni kweli mke wangu na Mathew ni watu wa karibu sana lakini hawezi kushiriki katika mpango huo wa kumteka Mathew” akasema Dr Fabian na David akatoka baada ya dakika chache akarejea akampatia Dr Fabian simu yake
“Mpigie mke wako! akasema David
“Hapana siwezi kumpigia ! akasema Dr Fabian
“Dr Fabian nina nia ya dhati ya kukusaidia katika jambo hili lakini siwezi kukusaidia kama nawe hautatupa ushirikiano wa kumtafuta Mathew Mulumbi”
“Dr Fabian nakufahamu
wewe ni mtu safi na ninataka sana kukusaidia kukuondoa katika kesi hii lakini lazima nawe unisaidie tuweze kumpata Mathew na mzigo wote ubaki kwake.Tafuta namna yoyote ya kumpata mke wako ambaye tunaamini anaweza kuwa na mawasiliano na Mathew Mulumbi” akasema David na Dr Fabian akazama mawazoni
“Siwezi kumuuza Ruby hata kama itanigharimu kwenda gerezani.Nina uhakika ni yeye aliyefanya tukio hili la kumteka Mathew na kwa pamoja lazima watahakikisha wanawapata hawa jamaa.”akawaza Dr Fabian “Dr Fabian ! akaita David
“David kama unataka
kunisaidia nisaidie tafadhali lakini siwezi kumuingiza mke wangu katika jambo hili” akasema Dr Fabian
“Dr Fabian nakuomba kwa mara ya mwisho tusaidie kufahamu mahala alipo mkeo ili tuweze kumfuata na kujua kama ana mawasiliano na Mathew Mulumbi na wewe ubaki huru.Endapo utashindwa kusaidia juhudi za kumsaka na kumpata Mathew Mulumbi nakuhakikishia Dr Fabian mambo yatakuwa mabaya sana na nitashindwa namna ya
kukusaidia.Nilikuonyesha zile video ambazo zinakuonyesha ukiwa na Mathew Mulumbi ni ushahidi mkubwa unaoweza kukuangamiza Dr Fabian” akasema David
“David nani waliokupatia video zile? Akauliza Dr Fabian
“Siwezi kukwambia ni nani.Kwa kuwa umeshindwa kutoa ushirikiano utaendelea kusota hapa na kuanzia kesho mashitaka yataanza kuandaliwa na utafikishwa mahakamani kwa kushirikiana na Mathew Mulumbi katika mauaji ya watu wawili” akasema David na kutoka
“Pamoja na nia ya hawa jamaa ya kutaka kuniangamiza lakini ninamuamini sana Mathew Mulumbi.Kama ametoroshwa basi lazima ni mpango wa Ruby na kama anashirikiana na Ruby lazima watahakikisha wananitoa katika kitanzi hiki.Lazima watafanya kila lililo ndani ya uwezo wao kuniokoa.Hawa watu ni wabaya sana,mtandao wao ni mkubwa na lazima tuwafahamu nini wanachokifanya hadi wanatumia nguvu kubwa namna hii kuwadhibiti wale wote wanaowafuatilia ! akawaza Dr fabian
********************
Mathew na Zari walirejea na kumstua Ruby kwa namna walivyokuwa wametapakaa vumbu huku kila mmoja akiwa na majeraha
“What happened Mathew? Akauliza Ruby
“Tumsaidie kwanza Zari ameumia” akasema Mathew na Zarina akamuelekeza Ruby mahala kilipo kisanduku cha huduma ya kwanza haraka haraka akakileta kisha Mathew akaanza kumuhudumia Zari majeraha aliyoyapata.Baada ya kumganga Zari,Ruby naye akamganga Mathew majeraha na kisha wakamueleza Ruby kile kilichotokea.
“Vita inazidi kupamba moto” akasema Ruby
“Kama ilivyo kawaida yao hawa jamaa muda wote wanakuwa mbele yetu na kuvuruga kila kitu tunachokifanya” akasema Mathew na ukimya ukapita
“Tumerudi pale pale tulipokuwa” akasema Zarina
“Hapana.” Akasema
Mathew na wote wakageuka kumtazama
“Haturudi nyuma
tunasonga mbele japo kwa hatua ndogo.Vita hii ni ngumu lakini kadiri wanavyozidi kufanya kila jitihada za kuturejesha nyuma ndivyo wanavyojikuta wakitupeleka mbele” Mathew akanyamaza kidogo baada ya kumuona Zari amefumba macho akihisi maumivu
“Zari haya ndiyo maisha yetu.Utatusamehe kwa kukuingiza katika dunia yetu lakini unapaswa nawe ujifunze
kuishi maisha yetu” akasema Mathew
“I’m fine Mathew.Msiwe
na wasiwasi wowote”akasema Zari
“Good.” Akasema Mathew na ukimya mfupi ukapita
“Faili hilo walilolichukua lingekuwa na msaada mkubwa sana kwetu” akasema Zari “Kabla bomu
halijalipuka,Zawadi alinitajia jina halisi la Naomi
Bambi.Anaitwa Zoe Adam
Watwila” akasema Mathew
“Hapo ni pazuri kwa kuanzia”akasema Ruby
“Zoe ni jina lake lakini Adam Watwila ndiye mzazi wake.Ruby anza kumtafuta Adam Watwila tufahamu mahala alipo” akasema Mathew na Ruby bila kupoteza muda akaanza kucheza na kompyuta yake.Wakati Ruby akiendelea na zoezi la kutafuta taarifa za Adam Watwila ,Zari akatoka nje
“Are you sure she’ll be okay? Akauliza Ruby
“She’ll be fine.Anaonekana hajawahi kukutana na mikiki mikiki kama hii.Ngoja nikamtazame ! akasema Mathew na kutoka akamfuata Zari akamkuta amekaa kibarazani akionekana kuwa na mawazo mengi.
“Can I sit? Akauliza Mathew na Zari akatikisa kichwa kukubali Mathew akaketi karibu yake
“Zari I know y…..”
“Mathew I’m fine ! akajibu Zari kabla Mathew hajamaliza alichotaka kukisema
“No you are not.Tukio lile limekustua na kukuogopesha sana ! akasema Mathew na ukimya wa sekunde kadhaa ukapita na macho ya Zari yakaanza kudondosha machozi
“Please don’t cry ! akasema Mathew
“Mathew that was so close to death ! Sikujua kama tungekuwa hai hadi sasa !
akasema Zari
“Hawa watu ni magaidi? akauliza
“I don’t know yet ! akajibu
Mathew
“Mathew hawa watu ni magaidi.Kitendo walichokifanya usiku wa leo ni cha kigaidi.Kumfunga bomu Yule mwanamke na kisha kumlipua ndivyo wafanyavyo magaidi ! akasema Zari
“Nimekuwa nikipambana na magaidi kwa miaka mingi hapa ndani na hata nje ya nchi ninafahamu mbinu zao ninafahamu namna wanavyopanga mipango yao lakini hawa jamaa kwa namna wanavyofanya mipango yao nina uhakika si magaidi.Kilichotokea usiku huu ni kwamba walifanikiwa kumteka Zawadi aliyekuwa hospitali ingawa sijui
wamewezaje kwa sababu kuna askari polisi wanaomlinda.Baada ya kumpata nina uhakika walimtesa na akawaambia kuhusiana na lile faili alilokuwa amenielekeza nikalichukue na baada ya hapo ndipo walipomfunga lile bomu kwani walikuwa na uhakika lazima nitakwenda pale kulifuata” akasema Mathew na kukaa kimya kidogo
“Zari mambo kama haya yataendelea kutokea kadiri tunavyondelea kupambana na hawa watu hivyo nataka nipate jibu lako kama utakuwa tayari kuendelea kushirikiana nasi.Kama hautakuwa tayari nitaelewa na tutaendelea mimi na Ruby” akasema Mathew.Zilipita sekunde kadhaa za ukimya Zari akasema
“I’m in”
“Thank you so much Zarina welcome to the show" akasema Mathew na ukimya ukatawala
“Mathew how come you
are not scared to die? Akauliza Zari
“Kwa nini umeuliza hivyo
Zari? Mathew naye akauliza “You saw a woman with a bomb lakini bado ukamfuata bila kuonyesha woga wowote, aren’t you scared to die and leave your family alone? Akauliza Zari na Mathew akatoa kicheko kidogo
“Scared to die ? akauliza Mathew
“I’m not scared to die.Katika kila misheni ninayoifanya ninamtanguliza Mungu anilinde dhidi ya watu hawa waovu hivyo kama ikitokea nimekufa basi ni mapenzi yake.Katika misheni ili ufanikiwe usiwaze sana kuhusu kifo.Jitoe mhanga,pita hata pale ambapo wengine hawawezi kupita.Nadhani umenielewa”
“Nimekuelewa Mathew”
akajibu Zari na ukimya mwingine ukatanda
“Do you have a family? Akauliza Zari
“Four children” akajibu Mathew kwa ufupi “A wife?
“Divorced” akajibu tena kwa ufupi
“Ouh ! so sorry ! akasema
Zari
“Zari let’s not talk about that.Twende tukamtazame Ruby kama kuna kitu amekipata kuhusu Adam Watwila” akasema Mathew wakarejea kwa Ruby
“Everything okay? Ruby akauliza
“Yah,everything’s fine.Umepata chochote kuhusu
Adam Watwila? Akauliza Mathew
“Ndiyo.Adam Watwila alikuwa mchungaji akihudumu
katika kanisa la injili ya
wokovu.Yeye na mke wake
walifariki dunia kwa ajili ya gari wakiwa safarini kuelekea Morogoro.Hakuna taarifa nyingi za kumuhusu yeye” akasema Ruby
“Mwendelezo wa
vifo.Naamini vifo vya wazazi wa Naomi ni mwendelezo wa hawa jamaa katika kuficha mambo yao.Kitu gani alikifahamu huyu Naomi ambacho kimesababisha watu wote hawa kupoteza maisha? Akauliza Mathew na ukimya mfupi ukapita
“Kwa sasa imekwisha kuwa usiku tupumzike na kesho asubuhi tutaanzia nyumbani kwa mchungaji Adam yawezekana kuna mambo tunaweza kuyafahamu kuhusiana na Naomi.Kwa usiku huu tupumzike hadi kesho.Imekuwa ni siku ndefu yenye matukio mazito” akasema Mathew
“Kuna yeyote anayehitaji chakula? Akauliza Zari
“I’m hungry” akasema Mathew na Zarina akaelekea jikoni.Ruby akachukua simu yake maalum akapiga na kutaja namba zake za utambulisho akaunganishwa na Rais
“Hallo” akasema Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais habari za usiku huu”
“Nzuri kabisa Ruby.Nina hamu sana ya kutaka kujua kile kinachoendelea hadi hivi sasa” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais kwa sasa tunaendelea kupanga mikakati kadhaa na hakuna hatua iliyopigwa.Nadhani kuanzia kesho mambo ndipo yataanza rasmi”akasema Ruby
“Ruby naomba mjitahidi sana katika kuwatafuta watu hawa !
“Nakuhakikishia mheshimiwa Rais lazima tutawapata”
“How’s Mathew?
“Anaendelea vizuri”
“Good”
“Mheshimiwa Rais vipi wanangu wanaendeleaje?
“Wanao wako salama
usiwe na hofu yoyote” akajibu Festus
“Ahsante sana mheshmiwa
Rais.Kuna taarifa yoyote kuhusiana na Fabian?
“Taarifa niliyoipata ni kwamba bado anaendelea
kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.Ruby I’m sorry I can’t do anything right now to save him.Ni wewe na Mathew ambao mnapaswa kufanya kila juhudi kuhakikisha mnamsaidia Dr Fabian.Mimi nikiingilia jambo hili nitaonekana nina husika pia”
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais tutajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha tunalimaliza jambo hili na Fabian anakuwa huru” akasema Ruby na kuagana na Rais
“How’s he? Akauliza Mathew aliyekuwa amesimama nyuma ya Ruby bila yeye kufahamu.Ruby akastuka na kugeuka ghafla “Umenistua sana Mathew ! akasema Ruby
“Sorry.How’s Fabian? Mathew akauliza
“Bado anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa mahojiano.Mathew ni sisi ambao tunatakiwa kumsaidia mzee Yule vinginevyo atakuwa katika hatari” akasema Ruby Mathew akamsogelea akamshika begani na kusema
“Ruby I give you my word,we’ll save your husband !
“I trust you Mathew” akasema Ruby
“Wanao wako wapi? Mathew akauliza
“Wako ikulu.Ni sehemu pekee ambako naamini wanaweza kuwa salama” akajibu Ruby
“Ruby I’m sorry.Mimi ndiye chanzo cha haya yote.Mlikuwa mkiishi kwa amani na furaha hadi nilipojitokeza na kuwaingiza katika matatizo haya.Nakuahidi Ruby kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba hali hii inakwisha na mnarejea kuishi maisha yenu ya furaha” “Mathew ..” akaita Ruby “Unasemaje Ruby? Akauliza Mathew na Ruby akafikiri kidogo kisha akasema
“Sifahamu kitu gani nilitaka kukisema.By the way how’s Peniela.Mnawasiliana?
“Sijawasiliana naye kwa muda mrefu lakini naamini yeye na watoto wanaendelea vizuri.Pale mambo yatakapokuwa yametulia nitawasiliana naye kujua maendeleo yao” akasema Mathew
“Do you still love her? Ruby akauliza
“Hata kama ninampenda lakini mimi naye tumekwisha fika mwisho na hivi sasa anaendelea na maisha yake ya furaha na yawezekana tayari amekwisha mpata mwanaume wa maisha yake.Bado ninamuheshimu kama mama wa watoto wangu lakini kuhusu mapenzi mimi naye huo ukurasa tumekwisha ufunga
“Nini sasa mipango yako? Ruby akauliza
“Kuhusu nini?
“Utaishi mwenyewe hadi
lini? Huhitaji mwenza?Akauliza Ruby.Mathew akainamisha kichwa akafikiri na kusema “Kamwe sintajisamehe kwa kukuacha uende Ruby”
“Mathew tafadhali usiseme hivyo”
“It’s true.It wasn’t easy for me to let you go.Ulipoondoka uliacha moyo wangu na jeraha ambalo halitaweza kupona hiyo ndiyo sababu sitaki kuingia tena katika mahusiano mengine.Yawezekana haya ndiyo maisha niliyopangiwa kuishi” akasema Mathew na Ruby akafuta machozi
“Mathew kwa nini lakini ukachukua maamuzi kama yale? Nilikupenda Mathew na nilikuwa tayari kuishi nawe maisha ya aina yoyote.Hata mimi uliniumiza sana” akasema Ruby
“Ilinilazimu kufanya vile Ruby kwa sababu sikujua itanichukua muda gani kurudi tena nyumbani.Nisamehe kwa maumivu uliyoyapata.Lakini hayo yamekwisha pita.Umeolewa sasa tena na mtu mwenye heshima kubwa hivyo tusijaribu kwa namna yoyote kutaka kufukua makaburi.Kilichobaki kwa sasa ni kutazama maisha ya mbele” akasema Mathew
“Mathew nakubali
nimeolewa and I have a family which I love so much lakini sijawahi acha kukupenda hata mara moja.Wewe utaendelea kuwa mwanaume wa pekee kabisa kuwahi kutokea katika maisha yangu.Hata Fabian hilo analifahamu” akasema Ruby na wote wakabaki kimya
“What about her? Akauliza Ruby
“Nani? Mathew naye
akauliza
“Zari.Unamuonaje?
“She’s strong.Anaweza akakabiliana na mikiki mikiki”
Mathew akajibu
“Isn’t she beautiful? Akauliza Ruby
“Una maana gani kuuliza hivyo Ruby?
“Sikupangii maisha yako Mathew lakini kama utahitaji mwanamke wa kuanzisha naye mahusiano,ninakushauri awe Zari”
“Kwa nini Zari? Mathew akauliza
“Anakufaa
sana.Ninakufahamu vizuri Mathew Mulumbi ndiyo maana nikasema kwamba Zari ni mwanamke anayeweza kukufaa sana”
“Hana mume?
“It’s complicated”
“Complicated? How !
“Zari ana tatizo la uzazi.Mchumba wake baada ya kugundua kwamba Zari hana uwezo wa kumzalia mtoto amemuacha.She’s going through a very tough time right now.Try to be close to her.Can you do that for me? Akauliza Ruby.Wakati Mathew akitafakari nini cha kujibu Zari akatokea na kuwataka wakapate chakula
“I’ll see what I can do” akajibu Mathew wakati wakiinuka kuelekea ndani kupata chakula
***********
Simu ya nabii mkuu
Kasiano iliita akainua mkono akaichukua akatazama mpigaji kisha akainuka akakaa na kuipokea
“John nadhani tayari
Mathew Mulumbi amekwisha fariki dunia” akasema Kasiano “Mkuu imeshindikana” “What?!
“Amenusurika kwa mara nyingine tena” akasema John Mkizi
“That’s not true John!
“Ni kweli mkuu.Mathew amenusurika katika mlipuko wa bomu tulilokuwa tumelitega nyumbani kwa Zawadi”
“John hamkujipanga
vizuri?Mbona mlinihakikishia kwamba kila kitu kimepangwa vizuri na kwamba Mathew akiingia hatatoka? Akauliza Kasiano
“Mkuu tulijipanga vizuri.Tuliweka kamera ndani ya kile chumba ili Mathew au mtu yeyote akingia basi tumuone mara moja kisha tutegue bomu lakini Yule jamaa aliweza kufanikiwa kutoka ndani ya kile chumba kama upepo wote tunashangaa”akasema John
“We missed him again ! akasema kwa ukali Kasiano
“I’m sorry Sir ! akasema John na Kasiano akakata simu kwa hasira akaitupa kitandani
“Nini kimetokea? Akauliza Rita mke wake aliyestuka toka usingizini na kumkuta mume wake akizungumza na simu “Mathew Mulumbi
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment