Search This Blog

Friday 7 April 2023

SCANDLE (KASHFA) (3) - 2

  

Simulizi : Scandle (Kashfa) (3)

Sehemu Ya Pili (2)


tena?Rais Festus naye akauliza


“Hapana mheshimiwa


Rais sijawasiliana nao tena”


“Good.Tusubiri tuone nini wanapanga kukifanya lakini naamini kabisa kwamba vita


haijakwisha hadi pale watakapompata Mathew Mulumbi” akasema Rais


Festus


“Mheshimiwa Rais naamini mpaka sasa umekwisha faya tafakari ya kutosha.Kama wakipiga simu tafadhali kubali matakwa yao”


“Mzee Simba,msimamo wangu hauyumbi hata kidogo.Siwezi kuwaogopa watu hawa.Siwezi kuwapa nafasi ya kuichezea ofisi hii hivyo kama watakupigia waambie wakasambaze hizo picha mimi siwezi kuwapa hicho wanachokihitaji”


“Sawa mheshimiwa mwenyekiti nimekuelewa.Kama wakipiga nitawaeleza hivyo”


“Jana uliwasiliana na mzee Titus kuna chochote ulimweleza kuhusu picha zile?


“Hapana sijamweleza chochote”


“Good.Usimweleze yeyote


kitu chochote kile subiri hadi pale watakapoziona picha hizo mtandaoni wale jamaa watakapozisambaza” akasema Raus Festus na kuagana na mzee Simba


“Katu siwezi kusalimu amri kwa wale jamaa.Ninamuombea Mathew Mulumbi uponaji wa haraka ili amalizie vita hii na ninaapa kama akifanikiwa kuwapata hawa jamaa adhabu watakayoipata ni mbaya sana.Hakuna atakayejua wamekwenda wapi wote watakwenda katika jela ya siri na huko watafungwa hasi siku watakapoaga dunia.Wataishi kwa mateso makali na hawataliona jua tena katika maisha yao ! akawaza Rais Festus na kujiandaa kwenda kufanya mazoezi ya asubuhi




**************


Habari kubwa iliyotawala vichwa vya habari vya magazeti ni Rais kukiri kuwa na mtoto wa nje na nyingine ni ya mauaji ya mfanya biashara mkubwa wa vipuri vya magari aliyeuawa na watu wasiojulikana akiwa dukani kwake pamoja na wafanya kazi wake.Habari nyingine ambayo ilipewa uzito ni ile ya kifo cha mchungaji Lucas wa kanisa la injili ya wokovu aliyeteketea kwa moto yeye na familia yake.


Wakati nabii Kasiano akiyapitia magazeti asubuhi simu yake ikaita alikuwa ni Paul


“Paula habari za asubuhi”


“Nzuri kabisa mkuu”


“Kuna taarifa gani mpya?


“Tayari tumekwisha anza maandalizi ya misheni ya leo tunachokisubiri ni ramani ya jengo hilo.Kama umeipata tayari tunaitaka ili tuifanyie kazi” akasema Paul


“Paul endeleeni na maandalizi bado sijaipata ramani hiyo mipango inaendelea kumpata mtu ambaye analifahamu jengo hilo na pale atakapopatikana nitakufahamisha” akasema Kasiano


“Leo ni leo,iwe mvua iwe jua lazima Mathew Mulumbi apatikane.Amenitesa sana huyu mtu nimekosa usingizi chakula hakishuki kwa sababu yake.Kwa namna yoyote ile leo lazima Mathew apatikane ! akawaza nabii Kasiano **************


Mathew Mulumbi


alifumbua macho na kumkuta Ruby akiwa amelala katika sofa lililokuwa ndani ya kile chumba alicholazwa.Mashine mbali mbali zilikuwa zimemzunguka ili kuisaidia mifumo mbali mbali ya mwili wake ifanye kazi.Akamtazama Ruby aliyekuwa katika usingizi mzito


“Namuonea huruma sana


Ruby anapitia kipindi kigumu mno.Ninajuta kwa nini nilimshirikisha katika hili jambo.Natakiwa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha yeye na fami..aagh ! Mathew akataka kuinuka akae lakini akahisi maumivu makali tumboni na muda huo huo muuguzi akaingia haraka


“Kaka Mathew usiinuke


tafadhali endelea kulala na kama kuna kitu chochote unakihitaji basi utabonyeza


kitufe hiki hapa na muuguzi kama hayuko humu chumbani atakuja mara moja.Unajisikiaje kwa sasa? Akauliza Yule muuguzi “Ninaendelea vizuri ila bado nina maumivu tumboni”


“Usihofu yatakwisha maumivu hayo” akasema Yule muuguzi


“Naomba umuamshe Ruby


tafadhali” akasema Mathew na Yule muuguzi akamfuata Ruby akamuamsha taratibu.Ruby alifumbua macho na kuyaelekeza kitandani akamkuta Mathew amekwisha amka akainuka haraka haraka akamfuata


“Mathew! Akasma Ruby kwa furaha


“Sijui nimpe Mungu Zawadi gani kwa maendeleo haya mazuri”akasema Ruby


“Hata mimi ninamshukuru sana Mungu kwa kunirejeshea uhai wangu.Tangu nimeanza kazi hii ya ujasusi kwa mara ya kwanza nilihisi ninakufa.Zari yuko wapi? Akauliza Mathew na Ruby akamuomba Yule muuguzi ampigie simu Zari kumtaka afike mara moja pale chumbani


“Unajisikiaje kwa sasa?


“Ninaendelea vizuri sana isipokuwa bado nina maumivu zile sehemu nilizokuwa nimejeruhiwa” akasema Mathew


“Pole sana Mathew,tukio


lile lilikuwa baya sana na wote tulikuwa na wasiwasi mno na kumlilia Mungu asikuchukue kwa muda huu ambao bado tunakuhitaji mno.Hatukukueleza usiku ulipozinduka lakini Rais naye alikuwepo hapa hadi upasuaji ulipomalizika ndipo akaondoka” akasema Ruby “Rais alikuwepo hapa? “Ndiyo.Alikuja akakaa nasi hapa akahakikisha upasuaji umemalizika ndipo akaondoka” akajibu Ruby na mlango ukafunguliwa akaingia Zari


“Mathew ! akasema Zari na kumfuata Mathew pale kitandani


“Natamani niruke ruke kama mtoto mdogo kwa furaha niliyonayo kwa maendeleo haya mazuri.Mungu ni mwema siku zote na husikiliza maombi ya wote wanaomuomba hata wale wakosefu kama mimi” akasema Zari kwa hisia na machozi yakaanza kumlenga


“Yazuie machozi yasitoke Zari.Huu ni wakati wa kumrudishia Mungu utukufu kwa kunirejeshea tena uhai kwani kwa tukio lile ningeweza kupoteza maisha” akasema Mathew na Zari akapiga magoti pembeni ya kitanda cha Mathew akasema “Mathew thank you”


“Ahsante sana kwa kuyaokoa maisha yangu,nina deni kubwa sana kwako ambalo sijui nitalilipaje” akasema Zari kwa hisia na kama kawaida yake anapokuwa katika hisia kali machozi humtoka


“Zari usilie tafadhali.Toka siku ya kwanza uliposisitiza utaongozana nami kila sehemu ninakoenda nilikuahidi kukulinda na ndivyo nilivyofanya.Kuna wakati nilitaka kumpoteza Ruby niljifunza kuanzia hapo kuwalinda watu wangu kwa gharama yoyote pale tunapokuwa katika misheni” akasema Mathew


“Ninakosa maneno ya kusema Mathew Mulumbi kwa jambo ulilolifanya”


“Zari bado tuko vitani hivyo tuyaweke pembeni mambo hayo hadi pale tutakapokuwa na uhakika vita tumeimaliza.Mmefikia wapi hadi hivi sasa katika kuwasaka wale jamaa? Akauliza Mathew


“Mathew tafadhali kwa sasa usiwaze chochote kuhusu


mapambano.Kwa muda huu tumejielekeza katika kuhakikisha unapona na unakuwa katika afya njema ndipo mambo mengine yaendelee” akasema Ruby


“C’mon ladies tuko vitani na hatuwezi kusimama baada ya mpiganaji mmoja kujeruhiwa.Mapambano lazima yaendelee.Call me a doctor now ! akasema Mathew


“Mathew naomba uelewe afya yako ni kitu muhimu mno.Wewe ndiye kiongozi wa mapambano haya ndiyo maana tunataka kuhakikisha unakuwa katika afya njema kwanza kabla ya kuendelea na mapambano”akasema Zari “I’m fine! Akasema Mathew na kutaka kuinuka akakunja uso kwa maumivu


“Mathew please don’t be sturbon.Umepigwa risasi tatu na umefanyiwa upasuaji mkubwa.Jipe muda wa mapumziko.Tuachie kila kitu sisi tutaweka mambo sawa.Usiwe na hofu yoyote” akasema Ruby


“Ruby you don’t know these people.They’re vey dangerous than you think.Call me a doctor I need to get out of here now ! akasema Mathew


na Zari akampigia simu Dr Fred ambaye alifika mara moja


“Unaendeleaje Mathew Mulumbi?


“Dr Fred niko vizuri naomba tafadhali uniruhusu niondoke hapa.Kuna mambo mengi ya kufanya yananisubiri ! akasema Mathew


“Mathew kwa sasa haitakuwa rahisi kukuruhusu ukaondoka kutokana na afya yako ilivyo.Tumekufanyia upasuaji mkubwa jana kuondoa risasi tatu mwilini mwako upasuaji huo umechukua takribani saa tano.Naomba utupe muda kidogo tuendelee kuangalia maendeleo yako halafu tukijiridhisha kwamba unaendelea vizuri tutakuruhusu utoke lakini kwa leo haitawezekana.Tunaomba siku chache tu”


“I don’t need days I need


to be discarged now ! akasema Mathew


“Mathew hatuwezi kukuruhusu leo kama nilivyokwambia.Mheshimiwa Rais alikuja mwenyewe jana hapa na akanieleza umuhimu wako kwake na kwa nchi pia akatutaka mimi na wenzangu kuhakikisha tunafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha tunaokoa maisha yako.Mathew wewe ni mtu


muhimu sana hivyo nakuomba vumilia kidogo ili hali yako iwe nzuri kisha utakwenda kuendelea na shughuli zako” akasema Dr Fred


“Dr Fred nitakaa hapa kwa siku ngapi? Akauliza Mathew


“Siwezi kusema utakaa hapa kwa siku ngapi lakini pale tutakapojiridhisha kwamba hakuna tatizo katika afya yako tutakuruhusu utoke.Mathew turuhusu tukuhudumie na kuhakikisha unakuwa salama”


“Ahsante Dr Fred” akasema Mathew na Dr Fred akatumia dakika chache kumpima kisha akatoa maelekezo kadhaa kwa muuguzi halafu akatoka


“Umemsikia daktari alivyosema Mathew” akasema Ruby na Mathew akafumba macho halafu baada ya muda akasema


“Sawa mmeshinda”


“Thank you Mathew.We’ll take a good care of you” akasema Zari na Mathew akawa kimya kwa muda akiwaza halafu akasema


“Nataka kufahamu kuhusu


tukio la jana”


“Mathew tafadhali usiwaze mambo hayo japo kwa muda huu ambao uko kitandani” akasema Ruy


“Japo nipo kitandani lakini misheni haiwezi kusimama.Mambo lazima yaendelee.Mmekwisha gundua ni namna gani wale jamaa waliweza kujua kuwa tuko pale tunazungumza na mchungaji Lucas? Akauliza Mathew


“Mathew ulielekeza tuchunguze kama kuna kamera za siri zimefungwa ndani ya ile nyumba”akasema Zari


“Ndiyo nilihisi hivyo kwa sababu wale jamaa wasingeweza kujua kama tuko pale kama hawakuwa wakitutazama katika kamera” akasema Mathew 





“Nilituma timu ya wataalamu kwenda katika nyumba ile kuchunguza kama kuna kamera za siri zimefungwa na kilichotokea kilitushangaza sote”


‘Nini kilitokea? Akauliza Mathew na kufumba macho kwa maumivu


“Mathew una


maumivu.Tafadhali pumzika” akasema Zari


“Nimekwisha zoea


maumivu hiki ni kitu kidogo sana.Endelea nini kilitokea?


“Walipofika walikuta nyumba ikiwaka moto”


“Nyuma iliwaka moto? How?


“Hakuna anayejua nini kilisababisha moto huo.Watu wetu walipofika mahala hapo walikuta nyumba inateketea kwa moto”


“Bastard ! akasema Mathew na kufumba tena macho kwa maumivu “Lazima walijua kuna kitu ndani ya ile nyumba ndiyo maana wakaamua kuichoma moto.These people are very smart.Hawataki kuacha alama yoyote nyuma! akasema Mathew


“Nimepitia magazeti ya leo imeandikwa habari hiyo ya mchungaji kuteketea kwa moto lakini hawajasema kuhusu


risasi magazeti yote yameandika kwamba Lucas na familia yake wameteketea kwa moto ambao unadaiwa kusababishwa na kulipuka kwa mtungi wa gesi”akasema Zari “Hawa jamaa wanao


uwezo wa kutaka habari gani iandikwe katika magazeti na iandikwaje.Wana hela na hakuna wanachoshindwa kupindisha.Vipi kuhusu zile picha za Rais wamezisambaza tayari?Mathew akauliza


“Hapana mpaka sasa hazijasambazwa”akajibu Ruby


“Kwa nini hawajasambaza wakati Rais amekataa kufuata matakwa yao?


“Hatujui kwa nini mpaka sasa hawajasambaza zile picha”


“Hawa watu


wanashangaza sana.Nini kimetokea?


“Hatujui yawezekana wakawa wameogopa”akasema Ruby


“Kuogopa? Hawa jamaa hawafahamu nini maana ya neno kuogopa.Kuna kitu lazima kimetokea ndiyo maana hawajasambaza zile picha” akasema Mathew


“Mathew kuna jambo


lingine.Nilipata ujumbe jana pia kutoka kwa Ziro”


“Ziro alikutumia tena ujumbe?


“Ndiyo” akajibu Ruby


“Can I see it? Akauliza Mathew na Ruby akamuonyesha ule ujumbe kutoka kwa Ziro


“Huyu Ziro anaonekana ni mtu ambaye yuko na hawa jamaa lakini anatusaidia sisi kwa kutupa taarifa za mipango yao.Kwa nini anatupa taarifa?Tukimpata huyu mtu anaweza akatusaidia sana kuufahamu mtandao huu.Ruby hakuna namna unavyoweza kufanya kumpata huyu Ziro? Akauliza Mathew


“Mathew hawa jamaa


wanatumia teknolojia ya hali ya juu sana.Ni wataalamu na wanajitahidi kuhakikisha wanayaficha mawasiliano yao ndiyo maana wanaweza hata kutumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa.Nimejitahidi sana kumfuatilia kutaka kumfahamu lakini sijafanikiwa” akasema Ruby


“Anaonekana yuko upande wetu na anatusaidia,kwa nini basi asitupe taarifa zinazoweza kutusaidia kulifahamu kundi hili la Black Mafia na mtandao mzima wa wafanya biashara wa dawa za kulevya hapa nchini? Akauliza Zari


“Mimi nadhani huyu mtu yuko undercover na anakwenda taratibu ili asije akagundulika.Muda utakapofika tutamfahamu tu.Kuna majasusi wengi wamejipenyeza katika mitandao hii ya dawa za kulevya na haowamekuwa ni msaada mkubwa katika kupata taarifa za haya magenge.Hata huyu Ziro kwa namna anavyotupa taarifa naamini ni mmoja wao.Tumpe nafasi aendelee na misheni yake na pale ambapo ataona kuna haja ya kutusaidia basi atafanya hivyo.Sisi tuendelee na mipango yetu.Swali linaloibuka wamefahamuje kama niko hapa?akauliza Mathew


“Hatujui wamefahamuje”


akajibu Zari


“Kuna kitu nilimwambia Zari jana usiku kwamba katika hili la picha za faragha za Rais kuna kitu cha kujifunza.Rais mwenyewe amekiri kwamba mahusiano yake na Zandile ni ya siri kubwa sana na wanaofahamu jambo hilo ni watu wake wa karibu.Anahisi kati ya watu wake wa karibu kuna mmoja au kadhaa wanaoishirikiana na hawa watu tunaowatafuta ndiyo maana wakaweza hata kufanikisha kupatikana kwa zile picha.Ninakubaliana na Rais kwamba hawa jamaa wanaweza kuwa wamepenyeza hata watu wao miongoni mwa watu wake wa karibu na ndiyo maana inakuwa rahisi siri zake kuvuja.Tunatakiwa tuchukue tahadhari sana tunapomueleza Rais kuhusu maendeleo na mipango yetu ” akasema Ruby


“Ruby uko sawa hata mimi ninahisi hivyo.Nina wasi wasi kwamba hata taarifa za uwepo wangu hapa SNSA zinaweza kuwa zimetoka kwa mmoja wa watu wa Rais.Isingekuwa rahisi kwa Black Mafia kujua kama niko hapa bila kupewa taarifa kutoka katika chanzo chao.Rais alikuja na walinzi


wangapi jana usiku? Akauliza


Mathew


“Sifahamu alikuwa na watu wangapi lakini humu ndani alikuwa na walinzi wanne”


“Wachunguzeni hao


walinzi wa Rais aliokuwa nao humu ndani jana usiku ili tujue kama taarifa hizi za mimi kuwepo hapa zimetoka kwa mmoja wa watu hao”akasema Mathew


“Kuna kitu nimekumbuka.Jana wakati Rais anatoa damu”akasema Zari na Mathew akamkatisha “Rais alitoa damu? “Ndiyo alitoa damu.Ulipoteza damu nyingi hivyo ilihitajika damu kwa haraka na kwa bahati nzuri Rais akawa na kundi la damu ambalo wewe unaweza ukapewa hivyo basi akatolewa damu ukaongezewa”akasema Zari


“Dah ! Nifikishieni shukrani nyingin kwake kwa wema huu alionitendea” akasema Mathew


“Endelea Zari na kile ulichotaka kukisema” akasema


Mathew


“Nilikuwa nasema kwamba wakati Rais akitoa damu kuna mmoja wa walinzi wake alitufuata mimi na Ruby tukiwa katika chumba cha mapumziko akatuuliza kama


kuna kitu tunahitaji


nikamwambia kwamba hatuhitaji chochote hakuondoka akauliza tena kwamba Yule mtu ambaye yuko katika chumba cha upasuaji ni nani? Hatukumjibu chochote kwani tayari Rais alikuwa ametoka katika chumba alimokuwa anatolewa damu.Sielewi kwa nini mtu Yule alikuja kutuuliza swali lile.Kwa wakati ule hakuna aliyekuwa anafikiri sawa sawa wote akili zetu tulizielekeza kwa Mathew lakini sasa baada ya mawazo haya ya Ruby ndipo akili yangu imefunguka na nimelikumbuka hili jambo”


“Hoja ya Ruby ina msingi sana itabidi ufanyike uchunguzi kuwachunguza wale walinzi wa Rais aliokuja nao


jana usiku hapa hospitali” akasema Mathew


‘Sawa Mathew tutafanya hivyo”akasema Zari


“Ruby nilikuomba


unitafutie taarifa za Yule mrembo Zandile kuna chochote umekipata?Mathew akauliza


“Kuna mambo tulielezwa na Rais Festus mwenyewe kuhusiana na mahusiano yake na Zandile” akasema Ruby na kumuelezea Mathew kila kitu walichoelezwa na Rais Festus kuhusu namna alivyokutana na Zandile


“That’s not enough.Dig deeper.Nataka taarifa za kina kuhusiana na Zandile na si mahusiano yake na Rais Festus” akasema Mathew


“Sawa Mathew nitafanya hivyo”


“Turejee katika ujumbe wa Ziro kwamba tayari wamekwisha fahamu mahala nilipo na wanakuja kunifuata.Nini mipango yenu?




“Tumelijadili hilo na tumekubaliana kwamba utakaa hapa hapa SNSA kwani ulinzi ni wa uhakika.Kuna walinzi wenye silaha na ukiacha hao upo mfumo wa kisasa sana wa ulinzi wa kielektroniki.Kama hao jamaa watavamia hili jengo hawatatoka salama” akasema Zari


“Zari nayaheshimu sana mawazo yenu na ninakubali ulinzi wa hapa ni mkubwa na wa uhakika lakini naomba tuzingatie ushauri wa Ziro kwamba niondoke mahala hapa.Hawa jamaa si wa kufanyia mzaha.Ni kikundi hatari na hakuna mahala wanakoshindwa kuingia.Kitu cha msingi ni kutafuta sehemu salama nikapumzike kisha baada ya hapo yafanyike maandalizi kabambe kabisa kuwasubiri hao jamaa watakapokuja basi wakute tumejiandaa tunawasubiri tuwape mshangao wa mwaka na asitoke hata mmoja wao.Find me somewhere safe.Kule katika shamba la makomando si salama tena kwani Rais alifika kule akiwa na walinzi wake ambao tunaamini yupo mmoja wao au kadhaa wanashirikiana na hawa black Mafia.Nataka sehemu nyingine ambako nitapata nafasi nzuri ya kupumzika” akasema Mathew


“Tunazo nyumba zetu za SNSA lakini sitaki twende huko.Msijali tutapata nyumba salama” akasema Zari na Dr Fred akaingia tena akawataka watoke ili aweze kumpima mgonjwa


**************


Asajile Mlabwa mkurugenzi wa idara ya kupambana na ugaidi


Tanzania aliwasili katika ofisi za taasisi ya mama Bella mke wa Rais Festus.Alipokewa na mmoja wa walinzi akamuongoza katika ofisi ya mama Bella ambako aliwakuta


mama Bella akiwa na mkuu wa


jeshi la polisi Tanzania Yeremia Mwaipopo


“Mama Bella” akasema Asajile na kumpa mkono wakasalimiana halafu akasalimiana pia na Yeremia ambaye tayari walikuwa wanafahamiana


“Asajile karibu sana katika ofisi zangu.Nadhani ni mara


yako ya kwanza kufika hapa” “Ndiyo mama Bella ni mara ya kwanza ninafika hapa ofisini kwako” “Ahsante sana kwa kufika Asajile.Kuna jambo la muhimu sana nimekuitia hapa”


“Ndiyo mama” akasema


Asajile kwa adabu


“Jambo lenyewe linamuhusu mheshimiwa Rais” akasema Bella na kunyamaza kidogo halafu akamueleza Asajile kuhusiana na picha zile za faragha za Rais na Asajile akastuka sana


“Watu hao ni washenzi kabisa.Wametoa madai yoyote?akauliza


“Ndiyo wametoa madai.Wanamtaka Mathew Mulumbi”


“Mulumbi huyu jasusi aliyekamatwa na unga wa kulevya?


“Ndiyo”


“Yule jamaa nadhani bado anasakwa na jeshi la polisi” akasema Asajile huku akimtazamaYeremia


“Ndiyo bado anasakwa na jeshi la polisi”akasema Yeremia


“Kwa nini wakatoa madai ya kumtaka mtu ambaye bado anasakwa na jeshi la polisi na hajulikani alipo?akauliza Asajile


“Rais anafahamu mahala alipo Mathew na hao jamaa wanajua Rais anafahamu kila kitu ndiyo maana wakata madai hayo.Asajile suala hili ni pana” akasema Bela na kumueleza Asajile kuhusiana na sakata zima la kupotea kwa Mathew Mulumbi.Asajile alibaki na mshangao mkubwa


“Baada ya kukueleza hayo yote sasa turejee katika kile ambacho tumekuitia hapa.Rais amegoma kutekeleza madai ya hao jamaa


“Amegoma? Asajile akashangaa


“Ndiyo amegoma.Yuko


tayari picha hizo zisambazawe”


Bella akamueleza kwa kina Asajile kuhusu athari za picha zile za faragha za Rais Festus kama zitasambazwa.


“Baada ya kukupa maelezo marefu juu ya suala hili nataka nikuulize swali Asajile je uko tayari Rais wako adhalilike kwa picha zake za faragha kusambazwa? Bella akauliza


“Hapana mama siko tayari kwa hilo.Siko tayari Rais wangu ninayemuheshimu na kumpenda adhalilike ! akasema Asajile


“Good.Sote hapa hakuna


aliye tayari picha hizo za Rais zisambae.Nimezungumza na hao jamaa na kuwaomba wasitishe mpango wao wa kuzisambaza picha hizo kwani ninashughulikia maombi yao ili waweze kumpata Mathew Mulumbi.Nimeungana na IGP katika suala hili na ndiyo maana unamuona hapa.Tunafanya jambo hili kwa siri bila Rais kujua.Atashangaa suala hili limemalizika kimya kimya na hatajua nini kimetokea hivyo hii ni siri yetu kubwa sana.Asajile nadhani umeyasikia yale yote niliyokueleza na umenielewa hivyo ninakuomba niko chini ya miguu yako ukubali kujiunga nasi kuzuia picha zile zisisambazwe.Tafadhali Asajile” akasema Bella.Asajile akafikiri kwa muda halafu akasema


“Sitaki Rais adhalilike na niko tayari kushiriki katika mpango huo jap ni kitu cha hatari sana endapo Rais atafahamu ! akasema Asajile


“Ahsante Asajile kwa kukubali.Nakuhakikishia kwamba Rais hatafahamu chochote”akasema Bella


“Asajile usihofu ndugu yangu tunayafanya haya kumsaidia Rais”akasema Yeremia


“Asajile katika suala hili kuna msaada tunahitaji kutoka kwako”


“Kitu gani mnakihitaji mama Bella? Akauliza Asajile


“Tunafahamu mahala alipo Mathew Mulumbi .Yupo katika ofisi za SNSA.Tunataka kutuma watu waingie hapo na kumchukua ili tumkabidhi kwa hao jamaa na tumalize hili jambo lakini hilo jengo lina ulinzi na ili tuingie humo ndani lazima tumpate mtu ambaye analifahamu vyema atupe maelekezo.Kuna mtu anaitwa Frank Kangole aliwahi kufanya kazi SNSA kwa sasa anashikiliwa katika gereza la siri ambalo liko chini yako.Tunataka utusaidie kumpata huyo mtu atusaidie” akasema Bella


“That’s impossible ! Hilo ni suala gumu sana” akasema Asajile


“Hicho ndicho tunataka utusaidie Asajile.Mtu huyo ni muhimu sana kumpata ili atupe maelekezo na tuweze kutuma watu wetu SNSA kumchukua Mathew Mulumbi


na tulimalize hili jambo”akasema Bella


“Frank Kangole ni kweli amefungwa katika gereza la


siri ambalo liko chini ya idara yangu.Huyu ni mfungwa ambaye nilipewa maelekezo maalum na Rais mwenyewe kwamba akae hapa hadi pale atakapoona yeye mwenyewe inafaa ndipo atamuachia na anafuatilia kwa karibu sana taarifa zake.Siwezi kwa namna yoyote ile kumtoa hapo gerezani” akasema Asajile “Asajile huyu mtu aliyekueleza mama Bella ni muhimu sana katika misheni hii.Shida yetu ni moja tu atupe taarifa za namna ya kuweza


kuingia katika jengo hilo la SNSA ambalo yeye analifahamu vyema” akasema Yeremia


“Hakuna mtu mwingine ambaye mnaweza mkampata na akatoa taarifa hizo? Akauliza Asajile


“Idara hii ya SNSA ni ya siri na ni vigumu sana kuweza kuwafahamu hata watumishi wa idara hiyo.Frank ndiye pekee ambaye tunaamini anaweza akatusaidia sana” akasema Bella


“Ugumu ni namna ya kumtoa Frank hapo gerezani.Rais akifahamu kuwa Frank ametolewa gerezani utaibuka mgogoro mwingine” akasema Asajile


“Usiwe na hofu


Asajile,hata kama likitokea la kutokea mzigo wote nitaubeba mimi.I can handle him ! akasema Bella


“Wasiwasi wangu mwingine ni kwamba Frank hawezi kutoa ushirikiano bila kuahidiwa kitu.Atajua taarifa mnayoihitaji ni ya muhimu sana kwenu hivyo lazima atataka apewe kitu fulani kwanza ndipo akubali kutoa taarifa hiyo mnayoihitaji” akasema Asajile


“Unadhani ni kitu gani anaweza akahitaji?Money? akauliza Bella


“Freedom” akasema


Asajile


“Ili atoe taarifa hiyo lazima atahitaji kuwa huru”


“Give him


freedom”akasema Bella


“Samahani mama Bella


lakini mimi sina nguvu hiyo ya


kumuachia mfungwa yeyote katika gereza hilo la siri.Mwenye nguvu hiyo ni Rais peke yake”


“Nina maanisha kama Frank akitaka uhuru huo muhakikishie kwamba pale atakaposaidia watu wetu wakaweza kuingia SNSA basi atakuwa huru” akasema Bella “Hapo sijakuelewa mama


Bella” akasema Asajile


“Ni hivi Asajile.Frank ataondolewa gerezani kwa muda ili kumuhakikishia kwamba atakuwa huru pale atakapotoa ushirikiano.Utamkabidhi kwetu tutazungumza naye na kumshawishi akubali halafu baada ya kutupa maelezo tunayoyataka tutamuondoa” akasema Yeremia na Asajile akapata mstuko mkubwa


“Una maanisha tumuue?


Akauliza Asajile “Ndiyo.Baada ya


kufahamu siri hii lazima tumuondoe kwani hatuna uwezo wa kkumuachia huru na tukimrejesha gerezani bado ataendelea kuwa hatari kwetu hivyo lazima tutamuondoa ili kufuta kabisa ushahidi wowote ! akasema Bella


“Kama akiuawa utakuwa ni mgogoro mwingine tena,unaweza ukafanyika uchunguzi na na mzigo wote utaniangukia mimi” akasema


Aasjile


“Usihofu Asajile.Frank ataondolewa kitaalamu sana halafu atarejeshwa gerezani akiwa tayari amekufa” akasema Bella 



“Isitoshe Rais atapata taarifa kwamba kuna mfungwa amefariki ghafla gerezani na hawezi akafuatilia kwani ana mambo mengi sana kwa wakati huu na hawezi kupoteza muda kuchunguza kifo cha


mfungwa mmoja” akasema Yeremia


“Asajile tunayafanya haya kwa ajili ya kumnusuru Rais na aibu kubwa ambayo ataipata endapo picha hizo zitasambazwa”Bella akaendelea kusisitiza.Baada ya mashauriano Asajile akakubali kwenda kumtoa Frank Kangole gerezani


Baada ya Asajile na IGP Yeremia kuondoka Bella akampigia simu Kasiano akamjulisha kuhusu mambo yanavyokwenda halafu Kasiano akamtuma Naibu waziri Keofas kumfuata Asajile Mlabwa ofisini kwake kwa ajili ya kwenda kumchukua Frank **************


Zari aliwasili ikulu kuonana na Rais kama alivyokuwa ameomba


“Karibu sana Zari” akasema Rais Festus


“Nashukuru mheshimiwa


Rais” akasema Zari


“Awali ya yote ninataka kujua maendeleo ya Mathew


Mulumbi”


“Tunamshukuru Mungu Mathew anaendelea vyema na anakushukuru sana kwa msaada wa damu” “Nimefurahi kusikia anaendelea vizuri,namuombea apone haraka”


“Mheshimiwa Rais nimekuja hapa kwa mambo mawili makubwa.Kwanza tunataka kumuhamisha Mathew Mulumbi”


“Kumuhamisha?Mnataka


kumpeleka wapi? Akauliza Rais Festus


“Tunataka kumpeleka sehemu salama zaidi.Tumefikia uamuzi huu baada ya kujadili kwa kina na kumshirikisha hata Mathew mwenyewe hivyo nimekuja hapa kuomba msaada wako” akasema Zari


“Hamuamini kama SNSA kuna usalama? Nadhani ni sehemu yenye ulinzi wa kutosha na zaidi ya yote pale wapo madaktari ambao watamuhudumia kwa saa ishirini na nne”


“Mheshimiwa Rais hatuna imani na mtu yeyote kwa sasa hata ndani ya SNSA tunaamini hawa jamaa wanaweza kuwa wamepenyeza mizizi yao.Taarifa zinaweza zikafika kwa hawa jamaa kwamba Mathew Mulumbi yuko pale SNSA na wanaweza wakafanya kila wawezalo kuhakikisha wanammaliza”


“Kama mmeafikiana Mathew Mulumbi ahamishwe mimi siwezi kuwa na kipingamizi.Ninachotaka kujua mnampeleka wapi ambako kutakuwa salama zaidi ya SNSA? Akauliza


“Nimekuja utusaidie katika hilo mheshimiwa Rais.Tunahitaji makazi salama” akasema Zari “Kule katika shamba la mazozi la makomando nako hakuko salama tena?


“Hatuna imani na kule pia.Hatutaki kukaa sehemu moja kwa muda mrefu tunahisi hata kule wanaweza kuwa tayari wamepagundua tunataka sehemu nyingine” akasema Zari na Rais Festus akainamisha kichwa akafikiri kwa muda akasema


“Sehemu pekee ambako


ninaweza kuwasaidia kwa sasa ambako naamini ni salama ni katika ile nyumba niliyomnunulia Zandile.Ni sehemu salama na kuna vyumba vya kutosha.Mathew Mulumbi anaweza akakaa hapo na kupona taratibu.Kuhusu matibabu hakuna tatizo kwani ataendelea kutibiwa na mdaktari wa SNSA”


“Ahsante sana mheshimiwa Rais”


“Saa ngapi mnataka kumuhamisha Mathew?


“Baadaye leo alasiri” akajibu Zari


“Sawa.Kuna muhudumu wangu nitampa maelekezo ya kufanya maandalizi katika hiyo nyumba kabla hamjahamia hapo”


“Do you trust her?akauliza Zari


“Yes I do.Ni muhudumu wangu wa muda mrefu na nimekuwa nikimtumia hata kumuhudumia Zandile awapo hapa nchini” akajibu Rais Festus


“Vipi kuhusu


ulinzi?akauliza Zari


“Kuna walinzi ambao hulinda usiku na mchana”


“Hatutawahitaji walinzi hao tutalindwa na makomando wetu wa SNSA.Unatakiwa uwaondoe mahala hapo kabla sisi hatujaingia” akasema Zari


“Sawa nitafanya hivyo hata mimi sina imani sana na walinziwangu hawa”akasema


Rais Festus


“Kuna jambo la pili ambalo limenileta hapa mheshimiwa Rais”akasema Zari na kunyamaza kidogo “Kufuatia sintofahamu kuhusu namna picha zako za


faragha zilivyopigwa tunahisi kwamba miongoni mwa watu wako wa karibu kuna mmoja au kadhaa wana mahusiano na hawa watu tunaowatafuta”


“Hilo unalolisema Zari hata mimi nimekuwa nalifikiria.Kama nilivyowaeleza kwamba hadi sasa sijapata majibu ni kwa namna gani picha zile zilipigwa na kuwafikia wale jamaa.Mahusiano yangu na Zandile ni ya siri mno na wanaofahamu ni watu wachache ninalazimika kuamini lazima kuna watu


wangu wa karibu wamehusika katika picha zile na siri zangu nyingine” akasema Rais Festus


“Mheshimiwa Rais tunataka kuwachunguza watu wako wa karibu kubaini nani ana mahusiano na hao jamaa.Tunataka kuanza na wale walinzi wako ambao


ulikuja nao jana usiku pale SNSA”


“Kwa nini mnataka kuanza na wale? Kuna kitu mnahisi kutoka kwa mmoja wao? “Ndiyo mheshimiwa


Rais.Tungeomba tupate taarifa zao ili tuweze kuwachunguza na kubaini mienendo yao” akasema Zari


“Lakini wale walinzi niliokuwa nao jana ni miongoni mwa wale ninaowaamini sana”


“Mheshimiwa Rais huu si muda wa kumuamini mtu.Yeyote hata Yule wa karibu yako anaweza akakumaliza” akasema Zari


Rais Festus akachukua simu na kumpigia kiongozi wa timu ya walinzi wa Rais akamtaka amtumie mara moja mafaili ya walinzi wanne aliokuwa nao ndani ya jengola SNSA alipokwenda usiku.Baada ya dakika chache akapigiwa simu kwamba tayari taarifa hizo zimekwisha tumwa.Akatazama taarifa zile katika kompyutayake halafu Zari akaziweka katika diski mweko


“Ahsante mheshimiwa


Rais kile kilichonileta hapa nimekikamilisha” akasema


Zari


“Nitawasiliana nawe baada ya maandalizi katika hiyo nyumba kukamilika” akasema Rais Festus na kuagana na Zari akaondoka


“Nitasikitika mno kama miongoni mwa wale walinzi wangu ninaowaamini sana na kuwashirikisha hata mambo yangu binafsi atatokea mmoja wao akawa anatoa taarifa zangu kwa hao jamaa tunaopambana nao” akawaza Rais Festus




Asajile Mlabwa na naibu waziri wa mambo ya ndani Keofas Mabula waliwasili katika jengo ambalo ni gereza la siri.Ndani ya ukuta mkubwa uliolizunguka eneo hilo kulikuwa na nyumba mbili za makazi vile vile kulikuwa na jengo kubwa mithili ya bohari la kuhifadhia bidhaa na ndani ya jengo hilo kulikuwa na chumba maalum chenye lifti ya kushuka mita mia nne chini ya ardhi ambako ndiko limejengwa gereza hilo la kisasa kabisa ambako watu wale hatari kabisa kwa nchi kama magaidi na wahalifu sugu hufungwa kwa maisha yao yote.Magari mawili yaliyokuwa yanaongozana yaliingia hadi ndani ya jengo hilo la bohari Asajile akashuka na kumtaka Keofas abaki garini.


Ndani ya jengo lile kulikuwa na vyumba vitatu vya ofisi akaenda katika chumba kimojawapo ambako kulikuwa na watu wawili wakasimama na kumsalimu.


“Namuhitaji namba 72


sasa hivi tafadhali” akasema Asajile na mmoja wa wale jamaa akainuka akaeleka katika chumba cha lifti akashuka chini kwenda kumleta mfungwa namba 72.


“Keep if off book.Nitamrejesha baadae” akasema Asajile na jamaa aliyebaki ndani ya ile ofisi akazima kamera.Baada ya dakika tano Frank Kangole akaletwa akiwa amefungwa pingu,Asajile akamchukua


hadi katika gari lake akamuingiza wakaondoka.Baada ya kutoka gerezani walielekea hadi katika nyumba moja ambako walifunguliwa geti wakaingia,Frank akashushwa garini na kuingizwa ndani bado alikuwa na pingu mkononi.Asajile akamtaka Keofas wazungumze pembeni


“Mtu ambaye nimetumwa nikukabidhi ni huyu.Tafadhali naomba kila kitu kiwe kimekamilika kabla ya saa kumi na moja jioni ya leo kwani kila siku saa moja jioni ripoti hutumwa kwa Rais kuhusu wafungwa wote walioko katika gereza.Nadhani maelekezo yote umekwisha pewa na mama Bella”


“Nitajitahidi kwa kila


niwezavyo ili kabla ya muda huo mambo yawe yamekamilika”


“Sawa baada ya kukamilisha mipango yote utanijulisha kisha tutakutana hapa” akasema Asajile kisha wakaelekea katika chumba alimokuwamo Frank


“Hello Frank.Huyu hapa ni naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi anaitwa Keofas Mabula.Nimekutoa pale gerezani kuna kazi ndogo tunataka utusaidie” akasema Asajile.Frank akawatazama halafu akasema


“Nini mnahitaji?


“Kuna kitu tunataka kuchukua ndani ya ofisi za SNSA .Wewe umewahi kufanya kazi SNSA unalifahamu vyema jengo lile tunataka kutuma watu waingie mle ndani hivyo tunataka utusaidie kutupa maelekezo ya namna watu tunaotaka kuwatuma watakavyoweza kuingia humo ndani na kukamilisha kazi tutakayowatuma” akasema Asajile.Frank akawatazama halafu akasema


“Mnataka msaada wangu muweze kutuma watu wenu ndani ya jengo la SNSA? Akauliza Frank


“Ndiyo.Tunataka utusaidie katika hilo suala kwa kuwa wewe umefanya kazi SNSA na unalifahamu vyema jengo hilo” akasema Asajile


“Ninao uwezo wa kuwasaidia namna mtakavyoweza kuingia humo ndani lakini mtakuwa tayari kwa kile ninachokitaka? Akauliza Frank


“Unataka nini Frank? Akauliza Asajile


“Nata nitoke gerezani”


“Usihofu utakuwa huru baada ya kuikamilisha hiyo kazi tunayokupa” akasema Asajile na Frank akaangua kicheko kikubwa


“That simple? Msinione mimi ni mjinga kiasi hicho.Ninafahamu mnachotaka


kunifanyia.Ninataka barua ya kuniachia huru yenye sahihi ya Rais vinginevyo siwezi kuwasaidia kwa chochote” akasema Frank


“Sikiliza Frank.Rais ndiye aliyetoa maelekezo wewe ufungwe gerezani kutokana na uhalifu mkubwa ulioufanya.Wewe tayari ni hatari kwa nchi na maisha yako yataishia mle gerezani.Kwa namna yoyote ile Rais hawezi akakuachia huru lakini sisi tunaweza kukusaidia ukatoka gerezani.Mimi ni naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi ni vipi kama nikikusaidia ukaweza kuondoka hapa nchini na kwenda kuanza maisha mapya nje ya nchi.Utapewa pesa ya kutosha ya kuanzia.Ninao uwezo wa kukusaidia kwa hilo” akasema Keofas


“Uchaguzi ni wako Frank chagua aidha uendelee kukaa gerezani kwa maisha yako yote au ukubali kufanya kile tunachokueleza na uwe huru.Hili ni dirisha ambalo hupaswi kuliacha Frank na kama ukiiacha nafasi kama hii haitatokea tena.Ukifungwa katika lile gereza la siri umesahaulika kwani ni sawa na kuwa tayari umekwisha kufa kwani si ndugu marafiki au familia yako watakaojua mahala ulipo” akasema Asajile.


“Nitawaaminije kama haya mnayonieleza ni ya kweli?Show me something so that I can believe you.Mkinionyesha kitu kama fedha nitakawaamini” akasema Frank


“Frank hapo ulipo hivi sasa wewe ni mfungwa.


Tutakachofanya sisi ni kukuondoa hapa nchini kimya kimya kwa kuwa uwezo huo tunao na kukusaidia fedha ambazo utakwenda kuanzia maisha mahala tutakapokupeleka nje ya Tanzania”akasema Keofas


“Mtanilipa kiasi gani kwa kazi hiyo? Akauliza Frank


“Kiasi kikubwa cha kutosha kwenda kuanza maisha nchi


tutakapokupeleka” akasema


Keofas


“Show me money


first.Kama nikiridhika nazo basi nitawasaidia hicho mnachokitaka” akasema Frank.Asajile akamtaka Keofas wakazugumze


“Huyu jamaa anamaanisha anachokisema hatafanya kitu chochote kama hajaziona fedha.Can you get money anywhere? Kama ungeweza hata kuazima mahala akaonyeshwa akaridhika halafu baadae zitachukuliwa na kurejeshwa zilikotolewa.Bila kufanya hivyo hataweza kuwa na msaada wowote kwetu” akasema


Asajile


“Kuhusu pesa ondoa shaka kabisa nitapata.Kwa kuwa muda unakwenda naomba niondoke naye ili nikakamilishe suala la fedha kisha tukamilishe mipango” akasema Keofas


Keofas akamchukua Frank wakaondoka wakaelekea hadi katika nyumba ambako alielekeza Paul Lewis


“Frank huyu anaitwa Paul utakuwa naye hapa mimi ninakwenda kushughulikia suala la fedha kisha nitarejea hapa.Tafadhali tuokoe muda wakati ninashughulikia suala la fedha endelea kumueleza kila kitu Paul kuhusu jengo hilo” akasema Keofas


“Sintasema chochote kama sijaziona fedha.Unataka niseme chochote weka fedha mezani” akasema Frank na Keofas akaondoka **************


Baada ya saa mbili Keofas akarejea akiwa na sanduku lililokuwa na dola za Marekani akalifungua na Frank akatabasamu akachomoa bunda moja akalichunguza kama ni bandia halafu akalirudisha mahala pake.


“Fedha hizo hapo ambazo zinakuwezesha kwenda kuishi katika nchi yoyote.Kama umeridhika basi ni wakati wako wa kutueleza kile tunachokitaka” akasema Keofas.


“Good.Let’s do this” akasema Frank na kuinua juu mikono yake iliyokuwa imefungwa pingu akitaka zifunguliwe.


“Sasa nataka kufahamu kile mnachokitaka ndani ya SNSA” akasema Frank na


Keofas akamueleza kila kitu


“Nimekuelewa lakini naomba niwaweke wazi kwamba jengo la SNSA ulinzi wake ni mkali sana.Si jengo ambalo unaweza ukavamia kirahisi.Lina ulinzi mkubwa” akasema Frank na kuwaeleza akina Keofas kuhusiana na mfumo wa ulinzi ulivyo pale SNSA.Akapewa karatasi akachora ramani ya jengo lilivyokaa na njia za kuweza kufika kwa urahisi eneo la afya ambako ndiko aliko Mathew Mulumbi.Majadiliano yalichukua zaidi ya saa nne lakini kila walivyojitahidi kujadili bado waliendelea kukutana na ugumu.


“C’mon Frank.Tuonyeshe njia rahisi ambayo tunaweza kuitumia bila kupoteza watu wetu ! akasema Keofas akionekana kuchoka


“Hakuna namna


mtakayoweza kuingia ndani ya jengo hili bila mapambano aidha na walinzi au na silaha zinazoendeshwa kielektroniki.Nimewapa njia tatu ambazo mtachagua ni njia ipi mnaweza mkaitumia kuingia humo ndani” akasema Frank


“Lazima ipo njia rahisi ya kutuwezesha kuingia humo ndani” akasisitiza Keofas


“Hakuna njia rahisi.Kama mnataka kuingia na kumchukua huyo mtu mnayemtaka fuateni maelekezo yangu.I’m done here ni wakati wako sasa wa kutimiza ahadi yako” akasema Frank


“Not so fast.Utaendelea kukaa hapa wakati ninalishughulikia suala lako”


“Ni vipi kama


nikigundulika sipo gerezani na nikaanza kusakwa?


“Usihofu tumekwisha maliza kila kitu” akasema


Keofas


“Frank twende nikakuonyeshe chumba utakachokitumia kupumzika”


“You keep me here?


Nataka hotelini ! akasema Frank


“Frank hapa ndipo sehemu salama unapotakiwa kuwepo kwa sasa.Utahudumiwa kila kitu unakachokitaji.Hautakaa kwa muda mrefu nitakuondoa hapa nchini” akasema Keofas na kusimama,akamtaka Frank amfuate akamuoneshe chumba cha kupumzika.Keofas alitangulia mbele akafuata Frank akiwa amelibeba sanduku la fedha na nyuma yao akawepo Paul.


Ghafla Paul akatoa sindano ndogo kutoka katika mfuko wa koti lake.Ilikuwa na dawa ya kijani ndani yake,akamrukia Frank na kumchoma sindano ile shingoni.Frank akageuka ghafla lakini Paul alikuwa mwepesi akamuwahi ngumi nzito ya uso akaanguka chini,kisha wote wawili wakamgandamiza pale chini.Frank alichomwa sindano yenye sumu kali sana na hakuchukua muda mrefu akafariki dunia.Baada ya kukamilisha zoezi lile haraka haraka akafungwa katika mfuko mkubwa na Keofas akampigia simu Asajile akamjulisha kwamba kazi imemalizika halafu wakaupakia mwili ule wa Frank katika gari la Paul wakaondoka


**************


HatimayeMathew


Mulumbi alihamishwa kutoka SNSA na kupelekwa katika nyumba ya Rais.Ilikuwa ni nyumba kubwa na nzuri yenye vyumba vingi.Tayari kulikuwa na muhudumu maalum


aliyewekwa na rais kwa ajili ya kuwasaidia kazi kwa muda watakaokuwepo pale.Walinzi


wa Rais waliondolewa na


makomando wa SNSA


wakashika usukani wa ulinzi wa nyumba ile.


Ruby na Zari bila kupoteza muda wakachagua chumba kimoja wakaandaa ofisi ambayo wataitumia kuendesha operesheni yao walipohakikisha kila kitu kimekaa sawa wakaenda kumtazama Mathew


“Ahsanteni sana kwa namna mnavyoshughulika kuhakikisha ninakuwa salama” akasema Mathew


“Hata hivyo hakuna muda wa kupumzika kazi lazima iendelee.Nataka kujua wapi tumefikia?Nini kinaendelea? Akauliza Mathew


“Kwa sasa ninaendelea kuwachunguza wale walinzi wa Rais kujua kama kuna mmoja wao anawasiliana na hawa jamaa tunaowatafuta.Vile vile ninaendelea kumchimba zaidi Zandile”akasema Ruby


“Hatuna tena kitu kingine cha kuchunguza zaidi ya hao walinzi?Mathew akauliza


“Kwa sasa hatuna Mathew” akasema Zari na ukimya ukatawala


“Ladies give me a minute


to think.I’ll call you ! akasema Mathew Ruby na Zari wakatoka


Mathew akafumba macho


na kuzama katika tafakari nzito.Alirejesha kumbukumbu ya toka walipoanza kulichunguza lile suala hadi tukio lililopelekea akapigwa risasi nyumbani kwa mchungaji Lucas.Baada ya kurejesha kumbu kumbu ya tukio lile kwa zaidi ya mara moja akataka kuinuka akahisi maumivu makali na muda huo huo muuguzi akaingia akamtaka alale.Mathew akamtuma awaite akina Ruby ambao walifika mara moja


“Nimetafakari sana na nimeona lile tukio pale nyumbani kwa Lucas ni zuri kuendelea na uchunguzi wetu.Kama nilivyowaambia awali kwamba ile nyumba ya mchungaji Lucas lazima itakuwa ilifungwa kamera za siri na ndiyo maana wale jamaa wakaweza kugundua kwamba tuko pale tunazugumza naye kuhusu kifo cha mchungaji Adam.Hawataki kifo cha mchungaji Adam kichunguzwe.Wana hofu kuna kitu kinaweza kugundulika ndiyo maana hata siku ile tulipokwenda kumuuliza nabii mkuu Kasiano kuhusiana na sababu ya Adam kwenda Morgoro tulifuatwa shuleni na kushambuliwa.Leo tena tumezungumza na Lucas kuhusu kifo cha Adam wakamuua.Kuna kitu katik akifo cha mchungaji Adam” akasema Mathew


“Ninalazimika kuamini kama kuna kamea za siri zilifungwa nyumbani kwa mchungaji Lucas basi si yeye peke yake anayechunguzwa bali ni wachungaji wote.Nataka tuweke mtego mdogo ili tupate uhakika kama ni wachungaji wote wa kanisa lile wanachunguzwa.Katika ile orodha ya wachungaji tumchague mmoja tumpigie simu na mpigaji amwambie anataka kumpa taarifa za sababu za kifo cha mchungaji Lucas.Amdokeze kwamba Lucas hakufa katika ajali ya moto kama inavyodaiwa bali kuna sababu nyingine.Mpigaji aweke miadi ya kuonana na mchungaji huyo sehemu


Fulani ili amueleze kila kitu kuhusu kifo cha mchungaji Lucas.Kama kweli wanafuatiliwa mawasiliano yao basi hao jamaa wanaowafuatilia wataingiwa na hofu kubwa na lazima watachukua hatua za kumdhibiti huyo mchungaji ili asionane na mtu aliyempigia simu na hiyo.Baada ya kujiridhisha kuwa wanafuatiliwa ndipo tutaanza kutafuta majibu ya swali la kwa nini wanafuatiliwa? Mathew akanyamaza


“Ni misheni ya hatari kwani hao jamaa watakachokifanya ni kuua hivyo tunapaswa kujiandaa vilivyo kumlinda huyo mchungaji.Hapo lazima tujipange vizuri sana” akasema Mathew na kufumba macho


akisikitika


“Nini Mathew? Akauliza Ruby


“Nani ataongoza misheni hiyo? Hii ni misheni ya hatari sana kwani sisi tunawawekea mtego hao jamaa na wao wanaweza wakatuwekea mtego pia.Msisahau hawa jamaa ni watu hatari sana hivyo….”Mathew akakatishwa na Ruby 



“Mathew kuna kitu ambacho hatukuwa tumekujulisha” akasema Ruby “Kitu gani?


“Baada ya tukio la jana tuliamini utachukua muda hadi upone na urejee katika misheni hii hivyo tukamuomba Nawal aje atusaidie wakati wewe ukiendelea kupona taratibu”


“Nawal?! Mathew akashangaa


“Ndiyo” akajibu Ruby


“Umepataje mawasiliano yake?Niliwahi kukuuliza ukasema hujui mahala aliko na huna mawasiliano naye ! “Nisamehe Mathew


nilidanganya” akasema Ruby na Mathew akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema


“Amesemaje Nawal baada ya kumuomba aje atusaidie?


“Amekubali na hivi sasa yuko ndegeni akija huku Tanzania.Tunategemea awasili hapa kuanzia saa kumi na moja za jioni” akasema Ruby


“Anyway sitaki kuzungumza chochote kwa sasa,kama Nawal akifika atakuwa na msaada mkubwa sana kwani Yule ni mmoja wa


watu ninaowaamini katika mapambano”


“Mathew najua hujafurahi kwa kutokukushirikisha suala hili la kumuita Nawal lakini hatukuwa na namna nyingine ya kufanya kwani misheni inatakiwa kuendelea na hatuna mtu mwingine ambaye tunaweza kumuamini atashika nafasi yako zaidi ya


Nawal.Mimi na mwenzangu Zari hatuna uwezo mkubwa kama mlio nao wewe na


Nawal”


“Usihofu Ruby hakuna


kilichoharibika isitoshe hata mimi muda mfupi uliopita nilikuwa namfikiria Nawal kama angekuwa karibu angetoa msaada mkubwa sana katika misheni hii.Ulifanya kitu kizuri kumuita” akasema Mathew


“Ahsante sana Mathew.Kuhusu kumpigia simu mchungaji kuna namna ninavyoweza kufanya ili nitumie simu yangu lakini hao jamaa kama wakinitafua basi ionekane ni simu kutoka nje ya mkoa” akasema Ruby


“That’s why I love you Ruby.Tumia uchawi wako katika suala hilo” akasema Mathew na Ruby akatoka kwenda kuchukua kompyuta yake


“Zari mara tu Ruby atakapofanikiwa kumshawishi huyo mchungaji kuonana naye jioni ya leo basi utawaandaa makomando wetu kwa ajili ya


misheni hiyo jioni ya leo” akasema Mathew


“Mathew utanisamehe but


I’m not going” akasema Zari “You are not going? Mathew akauliza


“Yes I’m not going.I trust only you hivyo kama wewe haupo na mimi siwezi kwenda kokote”


“Sikiliza Zari unaniamini mimi na mimi ninamuamini


Nawal.She’s good” akasema Mathew


“Utanisamehe Mathew I trust only you” akasema Zari


“Okay.Siwezi


kukulazimisha kama hujisikii kwenda huko” akasema Mathew na Ruby akaingia akaketi sofani na kuanza kazi.


“Kuna mchungaji anaitwa Zabron Mukigwa naye ni mmoja wa wachungaji wa kanisa la injili ya wokovu anayeshughulika na masuala ya maendeleo ya wanawake na vijana wa kanisa hilo.Tumpigie huyu” akasema Ruby


“Sawa.Mpigie simu” akasema Mathew na Ruby akachukua simu yake akampigia mchungaji Zablon na kuweka sauti kubwa ili kila mtu mle ndani asikie


“Hallo” akasema mtu


aliyepokea simu upande wa


pili


“Hallow.Natumai nazungumza na baba mchungaji Zabron Mukigwa”


“Ndiyo mimi.Nikusaidie nini mpendwa? Akauliza mchungaji Zabron


“Baba mchungaji kwanza kabisa poleni sana kwa msiba wa mchungaji Lucas”


“Ahsante sana.Ni mapenzi ya Mungu”


“Baba mchungaji ninaitwa Marietha kuna jambo nataka nikufahamishe kuhusu kifo cha mchungaji Lucas”


“Kitu gani mpendwa?


Akauliza mchungaji Zabron


“Mchungaji Lucas


hakufariki katika ajali ya moto kama inavyodaiwa”


“Lucas na familia yake walifariki kwa ajali ya moto jana usiku”akasema Zabron


“Baba mchungaji nataka kuonana nawe kuna mambo mazito nataka nikueleze kuhusu kifo cha Lucas na familia yake naamini katika simu hautaweza kunielewa” akasema Ruby na kukawa kimya


“Baba mchungaji” akaita Ruby


“Umenistua sana Marietha”


“Tafadhali naomba


tuonane baba mchungaji ili nikueleze kila kitu ninachokifahamu kuhusu kifo cha mchungaji Lucas”


“Kwa leo tuna mkesha wa kumuombea marehemu Lucas na familia yake hivyo sintakuwa na nafasi ya mazungumzo”


“Baba mchungaji naomba


tuonane jioni ya leo kabla ya mkesha kuanza.Nitakufuata hapo hapo kanisani,tutazungumza kwa dakika chache kisha utaendelea na ratiba zako” akasema Ruby na baada ya muda Zabron akasema


“Kuna mgahawa uko hapa kanisani.Tuonane hapo saa kumi na mbili za jioni.Utakapofika utanijulisha nami nitakufuata” akasema mchungaji Zabron


“Ahsante sana baba mchungaji tutaonana hiyo jioni” akasema Ruby na kukata simu


“Very good.Kama


watakuwa wanafuatilia mazungumzo hayo basi hivi sasa watakuwa wanajiandaa namna ya kumdhibiti mchungaji Zabron.Watakuwa wameingiwa hofu kwamba Zabron anakwenda kuelezwa siri ya kifo cha mchungaji Lucas.Tayari tumemuweka hatarini mchungaji Zabron hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunamlinda.Hawataweza kumuua kwa sasa kwani lazima watataka kumfahamu mwanamke huyo ni nani na watataka pia wampate ili waweze kumuhoji kwani wanaamini kwa namna lazima ana mahusiano na sisi.Nataka watumwe sasa hivi makomando hapo kanisani wakaanze kuchunguza eneo ambalo mchugaji Zabron na Ruby wamepanga kukutana.Wakiwa katika eneo hilo la kanisa wanatakiwa kuchunguza kama kuna mtu yeyote ambaye watamtilia shaka na watoe taarifa.Naamini kama haojamaa wamefuatilia mazungumzo kati ya Ruby na mchungaji Zabron naopia watatuma watu wao hapo kanisani hivyo lazima watu wetu wawe makini sana kuwabaini watu hao haraka” akasema Mathew na Zari akampigia simu mkuu wa makomando akamtaka afike pale mahala walipo mara moja akiwa na makomando nane




**************


Paul Lewis alirejea katika ofisi yao na kuwaita viongozi wengine wa Black Mafia katika kikao cha dharura


“Nimetoka kuonana na mtu ambaye amewahi kufanya kazi katika idara ya SNSA na analifahamu vyema jengo hilo lilivyo na kubwa ni kupata ramani ya jengo na jinsi tunavoweza kuingia humo ndani na kumchukua Mathew Mulumbi.Amenichorea ramani ya jengo ilivyo lakini kuna ugumu namna ya kuweza kuingia hmo ndani.Si jengo ambalo linaweza kuingilika kirahisi kutokana na ulinzi mkali uliopo mahala


hapo.Kuna walinzi zaidi ya kumi ambao wametawanyika sehemu ya nje ya jengo hilo wakilinda usiku.Ukiacha walinzi hao wa nje kuna silaha zimefichwa sehemu mbali mbali ya jengo ambazo


zinaendeshwa kwa k0mpyta na hizi ndizo hatari kabisa lakini jamaa amezionyesha katika ramani mahala zilipo” akasema Paul na kuzitoa ramani zile akawaonyesha wenzake wakaanza kuzijadili


“Kwa ujumla kuna ugumu mkubwa wa kufika mahala alipo Mathew Mulumbi na ugumu wenyewe unasababishwa na silaha hizo ambazo zinaendeshwa kwa kompyuta” akasema Paul na kuwatazama wenzake


“Pamoja na ugumu unaoonekana kuwepo lakini kwa namna yoyote ile leo lazima tuingie katika jengo hilo na kumchukua Mathew Mulumbi.Sisi ni zaidi ya jeshi hivyo hatupaswi kuogopa.Kuna kitu kingine ambacho mnapaswa kukifahamu kwamba jengo hilo la SNSA haliko mbali sana na ikulu hivyo ni eneo ambalo lina ulinzi mkali na kuzidi kulifanya zoezi la kuingia ndani ya jengo hilo kuwa gumu.Hata hivyo kuna njia moja tu ambayo inaweza ikatusaidia kuingia ndani ya hilo jengo.Tutatumiwa E bomb”akasema Paul na kunyamaza kwa muda


“Linaitwa Electromagnetic Bomb au kifupi e bomb.Hili ni bomu ambalo likipigwa mahali Fulani basi vifaa vyote vya kielektroniki vilivyoko eneo hilo haviwezi kufanya kazi tena.Umeme utakatika,magari yatazima,simu hjazitafanbya kazi.Kwa ujumla mfumo mzima wa kielektroniki wa mahala hapo hautafanya kazi kwa muda Fulani.Kwa kuwa SNSA kila kitu chao kinaendeshwa kielektroniki basi hakuna kitu kitakachoweza kufanya kazi na hivyo kutupa sisi nafasi ya kuweza kuingia na kumchukua Mathew Mulumbi” akasema Paul na majadiliano kuhusiana na suala lile yakaendelea.


Wakati majadiliano yakiendelea mtu mmoja akamfuata Paul na kumuita pembeni


“Kuna nini Damas?


Akauliza Paul


“Paul kuna tatizo subject


6” akasema Damas


“Tatizo gani? Akauliza


Paul


“Kuna mazungumzo nimeyapata ambayo ni vyema ukayasikiliza” akasema Damas na kuongozana na Paul hadi katika kompyuta yake akacheza mazungumzo yale aliyokuwa ameyapata.Sura ya Paul ikabadilika baada ya kusikiliza mazungumzo yale


“Haya mazungumzo umeyapata saa ngapi? Akauliza Paul



kesho,





“Dakika chache zilizopita” akajibu Damas


“Good job Damas nitumie rekodi hii katika kompyuta yangu halafu endelea kumfuatilia na chochote utakachokipata nijulishe tafadhali” akasema Paul na kuelekea ofisini kwake akampigia simu nabii Kasiano lakini simu iliita bila kupokelewa,akapiga mara ya pili simu haikupokelewa


“Mkuu Kasiano


yawezekana leo ametingwa na mambo mengi ndiyo maana hapokei simu.Hata hivyo kama mkuu wa Black Mafia lazima nifanye maamuzi ambayo naamini hata mkuu Kasiano angeyafanya” akawaza Paul na kurejea katika chumba cha mikutano walimokuwemo wenzake


“Ndugu zangu kuna jambo lingine limejitokeza.Damas amenasa maongezi kati ya subject 6 ambaye ni mchungaji Zabron na mwanamke mmoja ambaye hatujaweza kumfahamu bado” akasema Paul na kuwachezea wenzake yale mazungumzo kati ya mchugaji Zabron na Ruby wakasikiliza


“Ninaamini mwanamke huyu ni mmoja wa wale wanaoshirikiana na Mathew Mulumbi kwani ni wao pekee wanaofahamu mpaka sasa kwamba Lucas aliuawa kwa risasi kabla ya nyumba yake kuteketezwa kwa moto.Kwa kuwa usiku wa leo tuna misheni ya kwenda kumchukua Mathew Mulumbi SNSA basi tutakuwa na misheni nyingine pia ya kumchukua mwanamke huyu anayekwenda kuonana na mchungaji Zabron”


“Lakini nini hasa malengo ya mwanamke huyo kwenda kumueleza mchungaji Zabron kwamba Lucas aliuawa kwa risasi? Akauliza John Mkizi


“Hata mimi sifahamu nini hasa malengo yao ila tutafahamu baada ya kumpata.Jamani hawa watu wanazidi kusogea karibu.Nahisi kuna harufu wameinusa pale kanisani ndiyo maana wanacheza mahala hapo.Ninataka kuanzia jioni ya leo tuanze kuwafagia tukianza na kiongozi wao Mathew.Tukimpata pia mwanamke huyo atatuongoza waliko


wenzake.Nawakumbusha kwa namna yoyote ile mwanamke huyo hatakiwi kuuawa bali tunatakiwa kumpata akiwa hai ili aweze kutuonyesha walipo wenzake” akasema Paul


“Vipi kuhusu mchungaji Zabron? Jamaa mwingine akauliza


“Huyu anatakiwa aachwe hai pia.Ameuawa mchungaji Lucas jana na leo hii akiondolewa mwingine watu wataanzza kuwa na maswali nini kinaendelea kwa wachungaji wa kanisa lile na


jeshi la polisi linaweza likaanza uchunguzi wake jambo ambalo mkuu hataki litokee hivyo kwa sasa mchungaji Zabron ataachwa hai ila tuendelee kumfuatilia kwa karibu sana kwani maneno ya Yule mwanamke kuhusu kifo cha Lucas yataendelea kumtesa sana” akasema Paul


“Katika matukio kadhaa yaliyopita hawa jamaa kila waendako wamekuwa wakitanguliza mtu au watu na nyuma yao kuna timu ya ziada kwa ajili ya kutoa msaada hivyo tusilisahau hilo ili wale tutakaowatuma huko wawe na timu ya msaada endapo kutatokea mashambulizi kwa sababu naamini mwanamke huyo kama anashirikiana na akina Mathew hatakuwa peke yake” akasema John


“Nalifahamu hilo tutatuma timu ya watu saba.Watu watatu wataendesha zoezi la kumchukua mwanamke huyo na watu wengine wanne watakuwa nyuma yao ili kutoa msaada” akasema Paul na mipango ikaanza kuandaliwa mara moja ya namna misheni zile mbili zitakavyoweza kutekelezwa kwa pamoja




**************


Cosmas na Marcello makomando kutoka SNSA


waliwasili katika kanisa la Injili ya wokovu ambalo kwa siku hii huzuni kubwa ilikuwa imetanda kufuatia kifo cha mchungaji Lucas.Waumini walikuwa wengi sana eneo lile na ndani ya jengo la kanisa ibada ilikuwa inaendelea.Kama walivyopewa maelekezo Cosmas na Marcello wakaelekea katika mgahawa uliokuwa mbali kidogo na jengo la kanisa.Ni mgahawa mzuri sana ambao hutoa huduma ya chakula kwa waumini ambao hufurika kwa mamia pale kanisani .Hawakuingia na gari mahala pale.Kazi waliyokwenda kuifanya pale ni kufanya uchunguzi na maandalizi ya misheni inayotarajiwa kufanyika pale jioni.Kila mmoja alichukua meza yake na kuagiza kile alichokitaka huku wakiendelea kufanya uchunguzi na kuwasiliana na wenzao bila kugundulika


Baada ya saa mbili toka Cosmas na Marcello wawasili katika kanisa la injili ya


wokovu,makomando wengine wawili wakiwa na masanduku kama watu waliotoka safari walifika katika hoteli kubwa iliyoko pembeni mwa kanisa lile inayojulikana kama twin tower hoteli.Ni hoteli inayomilikiw ana nabii Kasiano na ilikuwa na majengo mawili yenye ghorofa kumi na tano kila moja


Tayari walikwisha pewa maelekezo na wenzao waliokuwa eneo lile na kuchagua chumba kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa.Baada ya kuingia katika chumba chao kikubwa bila kupoteza muda maandalizi yakaanza.Masanduku yao yakafunguliwa wakatoa kamera na kuzifunga wakielekeza katika mgahawa mahala ambako Ruby na Zabron walipanga kukutana kisha wakaunganisha bunduki zao za masafa marefu na kuziweka tayari


**************


Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia ikitokea Riyadh Saudi Arabia kupitia Addis Ababa Ethiopia iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dare s salaam.Nawal alikuwa ni miongoni mwa abiria waliokuwemo katika ndege hiyo.Baada ya kushuka na kukamilisha taratibu zote za uhamiaji,Nawal alipokewa na makomando wawili waliotumwa uwanjani hapo kumpokea na moja kwa moja wakampeleka mahala walikokuwa akina Mathew


Nawal na Ruby wakakumabatiana kwa furaha halafu akamtambulisha kwa Zari wakasalimiana


“Nafurahi kukuona tena Ruby.Unazidi kupendeza” akasema Nawal kwa furaha ya kumuona tena Ruby


“Nawal karibu tena Tanzania.Nimefurahi mno kukuona” akasema Ruby


“Tuna mengi ya kuzungumza Ruby lakini kwanza nataka kujua hali ya Mathew.Anaendeleaje? Yuko hospitali gani? Akauliza Nawal


“Mathew anaendelea viziri kwa sasa na anahudumiwa hapa hapa ndani” akasema Ruby


“Yuko hapa hapa ndani?


“Ndiyo”


“Nipeleke haraka tafadhali nikaonane naye” akasema Nawal na kuongozana na Ruby kuelekea ghorofa ya juu kabisa aliko Mathew


“Mathew anafahamu kama ninakuja?Nawal akauliza


“Ndiyo nimelazimika kumweleza hivyo anafahamu kama unakuja na amefurahi” akajibu Ruby


Walifika katika chumba alimo Matew Ruby akaufungua mlango wakaingia ndani.Nawal alisimama kwa sekunde kadhaa akimtazama Mathew halafu akamfuata pale kitandani akapiga magoti


“Nawal karibu sana nimefurahi kukuona tena” akasema Mathew “Mathew Mulumbi


sikutegemea siku tukionana utakuwa katika hali hii” akasema Nawal huku akifuta machozi


“Usijali Nawal.Haya ndiyo maisha yetu na mambo kama haya ni ya kawaida kitu cha kushukuru ni kwamba uhai bado upo.Nitapona na nitarejea katika hali yangu ya kawaida” akasema Mathew


“Ninamshukuru sana


Mungu kwa kukunusuru katika tukio hili.Waliofanya kitu kama hiki lazima watalipa ! akasema Nawal akiwa amepiga magoti pembeni ya kitanda cha Mathew huku ameishika mikono yake.


“Vipi maendeleo yako kwa sasa? Akauliza Nawal


“Kwa sasa ninaendelea vizuri kama unavyoniona lakini nitakuwa hapa kitandani kwa siku kadhaa ndiyo maana Ruby akalazimika kukuita uje uchukue nafasi yangu.Kuna misheni kubwa inaendelea” akasema Mathew


“Nini hasa kilitokea Mathew hadi ukapigwa risasi? Akauliza Nawal


“Nilirejea nchini baada ya kuishi nchini Japan kwa miaka mitatu na niliporejea hapa nikakuta kuna mambo yametokea.Ruby mueleze


Nawal kila kitu ili apate picha ya kile kinachoendelea” akasema Mathew na Ruby akamueleza Nawal kila kitu kilichokuwa kimetokea hadi Mathew alipopigwa risasi


“Hapo ndipo tulipofikia


Nawal katika sakata hili” akasema Ruby baada ya kumaliza kumueleza Nawal


“Nimekosa maneno ya


kusema lakini nawapa pole nyote kwa mambo haya mazito mliyoyapitia.Nimeumia sana kwa kilichomtokea Gosu Gosu na Dr Fabian.Nimeumia pia zaidi kwa kutoshirikishwa mapema katika jambo hili.Mimi japokuwa niko mbali lakini ni mwenzenu.Ni ndugu yenu.Mkumbuke Dr Fabian alinipa uraia wa Tanzania hivyo basi mimi ni mtanzania na ninaipenda sana nchi hii” akasema Nawal


“Nawal utanisamehe kwa kutokujulisha mapema kuhusu jambo hili lakini bado hatujachelewa ndiyo maana uko hapa” akasema Ruby


“Nawal sisi ni watu wa kazi na japokuwa umekuwa na safari ndefu kuanzia saa kumi


na mbili za asubuhi lakini hakuna muda wa kupumzika kwani kuna misheni muhimu jioni ya leo” akasema Mathew na Zari akamueleza Nawal kwa kina kuhusiana na misheni ile


wanayokwenda kuifanya jioni ile


“Nawashukuru sana ndugu zangu kwa mapokezi mazuri,mimi na Mathew tunafahamiana vyema ni watu wa kazi na kama alivyosema hatuna muda wa kupumzika.Nionyesheni chumba nikabadili mavazi nijiandae kwa misheni ya jioni ya leo” akasema Nawal na Ruby akampeleka katika chumba walichomuandalia ili aweze kujiandaa **************


“Faru 2&3, this is Faru 7.Kuna watu watatu wanaelekea upande mliko.Wafuatilieni nyendo zao hao jamaa tafadhali” akasema mmoja wa wale makomando waliokuwa katika chumba cha hoteli ya Twin tower wakiwa wamezielekeza kamera na bunduki zao katika mgahawa ambako Ruby alipanga kukutana na mchungaji


Zabron


“Tumekupata


Faru7.Tumekwisha waona hao jamaa tayari” akasema Faru 2


Wale jamaa walikwenda kukaa katika meza na kuagiza vinywaji baridi.Baada ya dakika mbili mmoja wao akatoka pale mezani wakabaki wawili na baada ya muda mfupi tena akaondoka mwingine akabaki mmoja.


“Faru 2,mmoja wa hao jamaa aliyetoka hapo mezani ana kifaa cha mawasiliano sikioni na anazungumza na mtu hivi sasa.Hakuna shaka hawa ni wenyewe” akasema


Faru7 aliyekuwa ghorofani na mwenzake wakiwa na kamera


zenye uwezo mkubwa wakifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea pale mgahawani.Faru 2 na3 baada ya kupewa uhakika kwamba wale jamaa yawezekana ni watu waliokuwa wanawatafuta wakaendelea kuwafuatilia kwa makini sana




Mmoja wa wale jamaa aliondoka pale mgahawani akaelekea getini “Namba5,mmoja wa wale jamaa anakuja eneo lako,amevaa suruali nyeusi koti jeusi na kofia”


“Nimekupata


Faru7.Nimekwishamuona” akasema mmoja wa makomando aliyekuwa eneo la getini ambako kulikuwa na makomando watatu.


Yule jamaa alitoka nje kabisa ya geti akaelekea katika gari moja lenye rangi ya bluu akaingia ndani ya gari hilo na baada ya dakika chache akatoka halafu akaelekea tena mgahawani.


Kiza kilianza kuingia pale ambapo gari la makomando wa SNSA lilipowasili katika


eneo la kanisa la injili ya wokovu.Katika eneo la maegesho ya magari kulikuwa na magari mengi ya waumini waliofika katika mkesha wa sala wa kumuombea mchungaji Lucas.Gari lile likaelekezwa mahala pa kuegesha na muongozaji wa magari


“Tayari tumefika kanisani” akasema Nawal aliyekuwa amevaa gauni refu na kufunika kichwa chake kwa kitambaa laini chekundu.


“Tumekupata vizuri elekea moja kwa moja mgahawani kila kitu kinakwenda vizuri”


akasema Namba 3 aliyekuwa eneo la getini


Mlango wa gari ukafunguliwa Nawal akashuka na kwa kuwa alikwishapewa ramani nzima ya mahala pale akaelekea moja kwa moja katika mgahawa.Ndani ya gauni refu alilolivaa alikuwa na bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti na katika mkoba wake alioushika mkononi kulikuwa pia na bastola


Kwa kupitia kifaa cha mawasiliano alichokiweka sikioni Nawal alielekezwa sehemu ya kwenda kukaa na muhudumu akafika


akamuhudumia kinywaji baridi


Macho ya Faru 2&3 yalikuwa kwa wale jamaa waliowahisi ni Black Mafia kuona ambacho kingetokea pale ambapo Nawal angewasili lakini hakukuwa na chochote kilichotokea,waliendea kupata vinywaji na maongezi


“Nawal sasa toa simu iweke sikioni uonekane kama vile unapiga simu lakini mimi ndiye nitakayempigia simu mchungaji na kumjulisha kwamba tayari nimefika hapo” Ruby akamwambia Nawal


kupitia kile kifaa cha mawasiliano alichokweka


sikioni


Nawal akatoa simu na kuiweka sikioni na muda huo huo Ruby naye akampigia simu mchungaji Zabron “Hallo” akasema Zabron


“Baba mchungaji Marietha ninaongea,tayari nimefika niko hapa mgahawani ninakusubiri,nimevaa gauni jeusi na kitambaa chekundu kichwani” akasema Ruby


“Ahsante kwa kufika ninakuja huko sasa hivi” akasema mchungaji Zabron na


Ruby akakata simu


Mara tu Ruby alipokata simu na Nawal akaitoa simu sikioni mmoja wa wale jamaa aliyekuwa mezani simu yake ikaita akaipokea akazungumza.


“Mpango umefanikiwa inaonekana walikuwa wanafuatilia mawasiliano ya mchungaji na tayari wamejua kwamba mtu anayetaka kuonana naye tayari amekwisha wasili.Baada ya sekunde chache mmoja wa wale jamaa aliyekuwa ameondoka mezani akarejea na wakaonekana wakijadiliana kitu.Makomando walikwisha jiandaa vyema na walikuwa makini kufuatilia kila kitu kilichokuwa kinaendelea mahala pale


Zilipita dakika kumi na mbili mchungaji Zabron akawasili pale mgahawani akaangaza angaza eneo lile na mara akamuona mwanamke Yule aliyekuwa amevaa gauni jeusi na ushungi mwekundu akamfuata


Katika gari lililokuwa limeegeshwa nje ya uzio wa kanisa ambalo makomando waliokuwa eneo le getini walikuwa wanalifuatilia,wakashuka watu wanne na kuelekea ndani haraka haraka hawakujua kama kuna makomando waliokuwa wanawafuatilia


“Hello Marietha” akasema mchungaji Zabron na kumpa mkono Nawal


“Hallo” akasema Nawal na mchungaji Zabron akastuka kidogo kwani sauti ya Nawal ilikuwa tofauti kidogo na ya Yule mwanamke aliyempigia simu


Mara tu mchungaji Zabron alipokaa kitini,mmoja wa wale jamaa wawili waliokuwa mezani akasimama akaeleka upande wa maliwato na Faru 2 akamfuata.Yule jamaa hakwenda maliwato bali alisimama sehemu na macho yake aliyaelekeza mahala walipokaa Nawal na Zabron.Hakumtilia mashaka mtu aliyekuwa nyuma yake na mara akajikuta akiguswa na kitu kama chuma tumboni.


“Tulia hivyo hivyo ulivyo utafuata maelekezo nitakayokupa” akasema Faru 2 na kwa haraka akaichukua bastora ya Yule jamaa lakini ghafla Yule jamaa aliyekuwa mwepesi sana akamtandika Faru2 kichwa halafu akamsindikiza na ngumi faru 2 akatetereka na kutaka kuanguka Yule jamaa akapata nafasi ya kukimbia huku akiwasiliana na wenzake.Faru 2 akageuka kwa haraka na kumtandika risasi kadhaa kwa kutumia bastora yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti Yule jamaa akaaguka chini.Mwenzake aliyekuwa amebaki mezani naye akasimama ghafla na kuchomoa bastora yake kabla hajafanya chochote Nawal alikwisha muona akamsukuma mchungaji Zabron akaanguka chini na kwa kasi ya aina yake akachomoa bastora kutoka katika mkoba wake na kuachia risasi kadhaa Yule jamaa akaanguka.Watu waliokuwa wakipata chakula na vinywaji eneo lile wakaanza kukimbia.Faru3 naye macho yake aliyaelekeza kwa mmoja wa wale jamaa aliyekuwa nyuma ya mnazi akamuwahi kwa risasi kadhaa na kummaliza.Makomando waliokuwa ghorofani wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea pale mgahawani walizitumia vyema bunduki zao za udunguaji kuwakabili wale jamaa wengine wanne waliotokea nje ya geti wakielekea mgahawani na mmoja baada ya mwingine wakajikuta wakienda chini.


Nawal alikuwa mwepesi sana kufumba na kufumbua tayari alimpiga pigo mchungaji Zabron akapoteza fahamu muda huo huo Faru 2 akatokea akamuiua na kumuweka begani na kuanza kuondoka mahala pale kabla watu hawajajaa kwani makelele ya watu waliokuwa wakikimbia eneo lile yalisikika na kuwafanya wengine waliokuwa kanisani wakiendelea na ibada kutoka kuja kushuhudia kitu gani kilikuwa kimetokea.Ili waweze kuondoka kwa urahisi eneo lile Faru3 akazidungua taa mbili kubwa na eneo likawa na mwangaza hafifu kisha wakaondoka kwa kasi


Upande wa nje wa


kanisa,kioo cha pembeni cha gari walilokuja nalo wale jamaa lililokuwa limeegeshwa nje ya uzio wa kanisa kikapigwa ngumi na mmoja wa makomando waliokuwa eneo la getini kikavunjika na jamaa aliyekuwa ndani ya gari akanyooshewa bastora na kutakiwa kuinua mikono yake akatolewa katika gari na kupelekwa katika gari la makomando.


Kulikuwa na makelele


mengi eneo lile la kanisa na watu walielekea mgahawani ambako watu saba walikuwa wamepigwa risasi.Nawal akiwa na mchungaji Zabron pamoja na wale makomando wakaingia katika gari lao na kuondoka.Misheni ilikuwa imekamilika




**************


Ibada ilisimama kwa muda


katika kanisa la injili ya wokovu,vilio vilitawala kila kona baada ya watu saba kupigwa risasi katika mgahawa wa kanisa.Nabii Kasiano naye akatoka kwenda kushuhudia kile kilichokuwa kimetokea katika mgahawa wa kanisa lake.Alistuka baada ya kuitazama miili ile.


“Hawa lazima ni vijana wa Black Mafia nini kimetokea hapa? Akajiuliza halafu akatoa maelekezo ya kuitwa askari polisi mahala pale kuja kufanya uchunguzi wa kile kilichotokea akaelekea ofisini kwake alikoiacha sdimu yake na kukuta watu kadhaa waliompigia simu na mmoja wapo akiwa ni Paul.Akampigia simu Paul lakini simu yake haikupatikana akampigia John msaidizi wa Paul lakini naye simu yake haikupatikana “Kuna kitu gani kinaendelea? Akajiuliza halafu akampigia simu Keofas Mabula


“Mkuu nimejaribu kupiga simu yako zaidi ya mara mbili inaita bila kupokelewa” akasema Keofas


“Niliisahau ofisini kwangu na kutwa nzima ya leo


tulikuwa katika ibada ya kumuombea Lucas.Keofas kuna mauaji yametokea hapa katika mgahawa wa kanisa.Watu saba wameuawa ambao nahisi watakuwa ni vijana wa black Mafia.Kuna kitu chochote Paul amekueleza kinaendelea?


“Paul nilikuwa naye na kwa pamoja tulimuhoji Frank na akatupa maelekezo kisha tukaachana yeye akaenda kuendelea na mipango ya misheni ya usiku wa leo sijawasiliana naye tena kujua nini kinaendelea”


“Nafurahi kusikia mlilimaliza suala la Frank.Basi nahisi hivi sasa watakuwa wamekwenda katika misheni ya kumchukua Mathew Mulumbi ndiyo maana hawapatikani simuni.Nataka ushughulikie hili jambo lililotokea hapa kanisani jioni hii.Nataka ijulikane ni majambazi walivamia na wakauawa na walinzi wangu” akasema nabii Kasiano akampa




Mchungaji Zabron


alishushwa garini baada ya kuwasili katika makazi ya muda ya akina Mathew.Ruby na Zari walikuwepo nje kuwapokea na kumpa pole Nawal


“Ahsanteni sana lakini hii ilikuwa ni misheni ndogo tu.Ninawashukuru makomando kwa namna walivyokuwa wamejipanga na kurahisisha zoezi” akasema Nawal wakaelekea ndani


Mchungaji Zabron ambaye


tayari alikwisha rejewa na fahamu akaingizwa katika sebule na baada ya dakika chache Ruby na Zari wakaingia katika kile chumba . “Mchungaji Zabron pole sana” akasema Ruby na mara Zabron akaitambua sauti ile


“Wewe ndiye niliyekuwa naongea nawe simuni.Nawaomba msiniue ndugu zagu mimi ni mtumishi wa Mungu sina chochote cha kuwapa ! akasema mchungaji Zabron


Zari akamuinua na kumtaka awafuate moja kwa moja wakaelekea katika chumba alimo Mathew Mulumbi.Mchungaji Zabron akastuka sana baada ya kumkuta Nawal mle chumbani,aliingiwa na woga mkubwa.


“Ndugu zangu nawaomba mnisamehe kama kuna kitu nimewakosea mimi ni mchungaji tu.Ni masikini sina chochote cha kuwapa.Nawaomba sana ! akasema Zabron Zari akamuelekeza aketi.Nawal akapandisha kitanda na Mathew akamtazama mchungaji Zabron halafu akasema


“Mchungaji Zabron mimi ninaitwa Mathew Mulumbi naamini jina hili umekwisha wahi kulisikia sehemu kwani kwa siku kadhaa zilizopita limetawala sana katika vyombo vya habari” akasema Mathew na bado mchungaji Zabron aliendelea kushangaa.


“Yule pale uliyekutana naye kule kanisani anaitwa Nawal,Yule pale ni Zari na huyu hapa ni mke wa Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo nadhani unamfahamu” akasema Mathew.Bado mchungaji Zabron alikuwa katika mshangao


“Mchungaji Zabron tafadhali naomba uwe na amani na ninakuhakikishia hapa uko sehemu salama.Hatujakuleta hapa kukuumiza au kukufanya chochote bali ni kwa ajili ya usalama wako hivyo basi ondoa woga” akasema Mathew


“Ninyi ni akina nani? Ni polisi? Wana usalama? Akauliza Zabron


“Sisi tunashughulika na usalama wa nchi” akasema Mathew na kumpa ishara Ruby aendelee


“Baba mchungaji


tumekuleta hapa kwa ajili ya mahojiano muhimu na samahani kwa kutumia njia hii lakini hatukuwa na namna nyingine ya kuweza kukupata kwa mahojiano zaidi ya kufanya hivi” akasema Ruby


“Kuna mwandishi mmoja wa habari anaitwa Lidya aliuliwa na mchumba wake ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha maisha gerezani kwa kosa hilo la mauaji.Mtu huyo anaitwa Gosu Gosu ni mwenzetu.Hakutenda kosa hilo la mauaji kama inavyodaiwa bali aliangushiwa mzigo ule na watu asiowafahamu.Sisi kama wenzake tulianza kuwatafuta watu waliomuangushia kesi ile ya mauaji na kumsababisha akafungwa gerezani” Ruby akanyamaza baada ya mlango kugongwa akaingia Kendrick akawajulisha kwamba Yule dereva waliyemchukua katika gari lililowaleta wale jamaa waliouawa pale kanisani tayari amekwisha fikishwa pale ndani.Nawal na Zari wakatoka wakawaacha Mathew na Ruby wakiendelea na mahojiano na mchungaji Zabron


Ruby alimueleza mchungaji Zabron mambo yaliyotokea baada ya kuanza uchunguzi huo na watu ambao wamekwisha poteza maisha kutokana na suala lile.Uso wa mchungaji Zabron ulionyesha mshangao na woga mkubwa


“Pamoja na yote tuliyokwishayapata katika uchunguzi wetu kuna suala moja ambalo tulitaka kulifanyia uchunguzi wa kina nalo ni sababu ya mchungaji Adam Watwila kuamua kwenda Morogoro siku ambayo mwanae alikuwa ametoweka na hajulikani alipo.Tulimfuata mchungaji Lucas nyumbani kwake bila kumpa taarifa na akatupokea tukamuuliza maswali akatujibu na wakati tukiendelea na mahojiano wakatokea watu ambao walifanya shambulizi la ghafla na kuwaua Lucas na familia yake na huyu jamaa hapa Mathew akajeruhiwa kwa risasi.Alipigwa jumla risasi tatu mbili tumboni na moja katika kalio”akasema Ruby


“Pole sana”


“Ahsante”


“Tulijiuliza wale jamaa wamefahamuje kama tuko pale tunazugumza na mchungaji Lucas? Tukahisi yawezekana kuna kamera za siri zimefungwa katika ile nyuma


ya Lucas tukarejea tena ili kuchunguza tukakuta nyumba inawaka moto.Kwa hiyo baba mchungaji ukweli ni huo kwamba Lucas aliuawa kwa risasi kabla ya moto kuwashwa” akasema Ruby.Mchungaji Zabron midomo ilimcheza akataka kusema kitu akashindwa


“Tulijiuliza maswali mengi” Ruby akaendelea


“Ndipo tukaamua kukupigia simu na kuomba kuonana nawe lengo likiwa ni kuchunguza kama hawa jamaa wanafuatilia pia mawasiliano ya wachungaji wengine na kile tulichokihisi ndicho kilichotokea wale jamaa waliweza kunasa maongezi yetu simuni na lengo lao lilikuwa ni kukumaliza ili tusiweze kukueleza ukweli lakini hawakujua kama na sisi tumejipanga vyema na kuwamaliza wao kabla ya kukumaliza.Pole sana baba mchungaji” akasema Ruby


“Baba mchungaji naamini umemsikia vyema Ruby amekueleza kwa undani kila kilichotokea”


“Nimemuelewa na hapa nilipo nimechanganyikiwa kwa haya mambo mazito niliyoyasikia”


“Baada ya kuyafahamu


hayo yote swali linaloibuka ni je kwa nini hawa jamaa wanawafuatilia? Kwa sasa tumekwisha amini kwamba wachungaji wote wa kanisa la Injili ya wokovu wanafuatiliwa mawasiliano yao,na nina uhakika mkubwa kwama hata nyumba yako lazima itakuwa na kamera za siri wanafuatilia


kila unachokifanya” akasema Mathew


“Hata mimi ndugu zangu sielewi ni mara ya kwanza ninasikia kutoka kwenu kwamba ninafuatiliwa lakini sijawahi kuhisi kitu kama hicho katika maisha yangu ! akasema Zabron


“Baba mchungaji hawa jamaa ambao tunawatafuta na ambao wanawafuatilia wewe na wenzako,wanajihusisha na genge la wauza dawa za kulevya ndiyo maana tunataka kujua kwa nini wanawafuatilia ninyi watumishi wa Mungu?Kitu gani mnakifahamu ambacho mnafuatiliwa msikiseme? Akauliza Mathew


“Ndugu zangu haya


ninayoyasikia leo ni mageni kabisa na sifahamu chochote.Hii taarifa ya kufuatiliwa ni mara ya kwanza ninaisikia hapa.Mimi nimeajiriwa na kanisa na hata nyumba ninayoishi ni ya kanisa,gari la kanisa hivyo sina kitu chochote ambacho kinaweza kikamfanya mtu anifuatilie kunichunguza.Sina biashara yoyote ninayoifanya na hata watu ninaowasiliana nao au kuwakaribisha nyumbani kwangu ni waumini wa kanisa.Kwa ujumla asilimia tisini ya shughuli zangu na mawasiliano yangu ni kwa ajili ya kazi yangu ya kichungaji na kidogo huwa nikipata nafasi ninakwenda kutembelea shamba langu,mke wangu anashughulika na kilimo cha mpunga.Mimi ni mtu masikini tu nimetoka kijijini nikaenda kusomea uchungaji na nilipomaliza mimi na wenzangu watatu akiwamo Lucas tulianza kutumika katika kanisa la injili ya


wokovu” akasema mchungaji


Zabron


“Baba mchungaji kwa sasa familia yako iko katika hatari kubwa hawa jamaa wanajua tumekuchukua na tutakueleza ukweli hivyo tunataka tukusaidie na vile vile wewe utusaidie sisi.Kama kuna kitu unakifahamu tueleze tafadhali”


“Sifahamu chochote ndugu zangu ningewaeleza”


“Haiwezekani ! akasema Mathew kwa sauti ya juu kidogo halafu akafumba


macho baada ya kuhisi maumivu


“Easy Mathew ! akasema Ruby


“Mchungaji Zabron,


lazima ipo sababu ya ninyi wachungaji wa kanisa la injili ya wokovu kufuatilia.Hawa watu wanawafuatilia kwa siri bila ninyi kujua,wanafuatilia maisha yenu,faragha zenu,mawasiliano yenu na kila mnachokifanya.Swali linakuja kwa nini wafanye hivyo?Lazima ipo sababu ya msingi inayowapelekea wao wafanye hivyo.Hawawezi wakapotea muda kuwafuatilia kama hakuna sababu ya msingi”


“Kama iko sababu ya wao kutufuatilia na kuchunguza maisha yetu basi ni wao wanaijua na ndiyo maana wanafanya kwa siri bila sisi kufahamu” akasema Zabron


“Baba mchungaji ninakuomba jipe muda tafakari kwa kina jambo hili lazima utapata jibu.Lazima ipo sababu” akasema Mathew na Ruby akamtoa Zabron mle chumbani


“Jamani nataka kuzungumza na familia yangu kuwajulisha kwamba niko salama”akasema mchungaji Zabrn


“Kwa sasa hautaweza kufanya hivyo kwani utakapotumia tu simu yako basi jamaa watajua mahala ulipo na watakufuata kuja kukumaliza hapa hapa” akasema Ruby na kumpeleka Zabron katika chuma kimoja akamtaka apumzike na komando mmoja akawekwa kumlinda.


Wakati Mathew na Ruby wakiendelea kumuhoji mchungaji Zabron,Katika chumba kingine Nawal na Zari walikuwa wanaendelea na zoezi la kumuhoji yule dereva aliyechukuliwa kutoka katika gari la wale jamaa.Alikuwa amefungwa kamba katika kiti jasho likimtiririka huku akihema haraka haraka


“Relax,take a deep breath ! Nawal akamwambia


“Jamani msiniue ! akasema Yule dereva na mara Ruby akaingia akaelekeza wampeleke Yule dereva katika chumba cha Mathew Mulumbi.Akafunguliwa mikono akapelekwa katika chumba alimo Mathew


“Jina lako nani? Akauliza Ruby


“Naitwa Gabriel”


“Gabriel unafanya kazi wapi?


“Mimi ni dereva” 




“Gabriel sisi utuonao hapa si watu wabaya, kuna taarifa tunahitaji kutoka kwako.Kama utaamua kutoa ushirikiano na kutueleza ukweli basi itakuwa ni pone pone yako lakini kama utaamua kuwa kiburi nakuhakikishia utajiweka katika wakati mgumu sana na utatufanya tutumie nguvu kitu ambacho hatupendi kukifanya”akasema Mathew


“Jamani naombeni


msinitese niko tayari kuwaeleza kila mnachokitaka”


“Good” akasema Mathew na kumfanyia ishara Ruby aendelee


“Gabriel unafanya kazi gani?


“Mimi ni dereva”


“Dereva wa kampuni gani? Akauliza Mathew


“Nina gari langu nalikodisha”


“Gabriel jioni ya leo ulikuja na wenzako kanisani.Nataka utueleze kwa kina kuhusiana na ninyi,shughuli zenu nani kiongozi wenu na wapi mnakojificha?Tueleze ukweli


tafadhali ili we salama yako.Ukitudanganya nakuhakikishia utakuwa umejiweka katika mazingira magumu sana kama alivyokwambia Mathew” akasema Ruby na Gabriel akawatazama kwa woga


“Anza kutueleza tafadhali ! akasema Zari


“Sikilizeni niwaambie ukweli ndugu zangu wale jamaa siwafahamu”


“Gabriel narudia tena kukuonya kwamba endapo utathubutu kutudanganya utapata taabu sana ! akasema


Ruby


“Naambia ukweli jamani wale jamaa siwafahamu”akasema Gabriel na Ruby akachukua simu ya Nawal akachukua alama za vidole za Gabriel akaenda katika kompyuta yake na kumtafuta akampata


“Gabriel Sawaza,una miaka 32 kazi yako ni dereva”akasema Ruby akisoma maelezo ya Gabriel


“Gabriel nataka utueleze ukweli kuhusu ninyi shughuli zenu,makazi yenu na nani kiongozi wenu? Akauliza Ruby “Ninawaambia ukweli jamani wale jamaa siwafahamu” akasema Gabriel


“Gabriel kwa mara ya mwisho nakuomba tafadhali tueleze ukweli” akasema Ruby


“Nieleweni ndugu zangu ninawaambia ukweli mtupu” akasema Gabriel.Nawal akamsogelea na kumtandika ngumi mfululizo damu zikaanza kumtoka


“Mtaniua jamani


ninawaeleza ukweli”akalia


Gabriel


“Tuambie ukweli ! akasema Zari


“Nawaambia ukweli jamani wale watu siwafahamu ! Akasema Gabriel


“Hatuna muda wa kupoteza kwa watu kama hawa ! akasema Nawal na kumminya yule jamaa


korodani zake akapiga kelele kubwa


“Sema ukweli ! akasema


Zari


“Mpeni nafasi aseme” akasema Mathew


“Gabriel nakutahadharisha kwamba usiposema ukweli utapata taabu sana na yawezekana usilione tena hata jua la kesho” akasema Mathew


“Kaka naomba mnisikilize niwaambie ukweli bila kuwaficha” akasema Gabriel


“Haya tueleze” akasema Mathew na Gabriel akafuta damu zilizokuwa zinamtoka mdomoni kufuatia kipigo cha ghafla kutoka kwa Nawal halafu akasema


“Mimi ni dereva wa gari.Nina gari langu ambalo hukodishwa kwa shughuli mbalimbali.Leo nilifuatwa na watu wawili wakaniambia kuna mgonjwa wanakwenda kumchukua katika kanisa la injili ya wokovu.Niliwatajia bei wakaniahidi kunilipa zaidi ya kiasi kile kiasi


nilichowaambia” akanyamaza akafuta damu


“Waliponichukua kijiweni


tulienda katika ofisi ya kampuni ya filamu inaitwa African Picture nikawasubiri wakaingia ndani na baada ya…….”


“Subiri kwanza umesema


African Picture? Akauliza Mathew


“Ndiyo walinipeleka hapo tukawachukua wenzao watano tukaondoka hadi kanisa la injili ya wokovu,wakashuka watatu wakaenda ndani na baada ya muda akarejea mmoja wao na kuzungumza na wenzake kwamba bado


hajafika.Sikutaka kufuatilia mazungumzo yao nilichokuwa nasubiri ni kukamilika kwa


kazi yao ili nilipwe pesa yangu.Baadaye wakashuka wale jamaa wengine wanne wakaelekea ndani nikaendelea kuwasubiri hadi nilipojikuta mikononi mwenu.Nasema ukweli kabisa kaka yangu wale jamaa siwafahamu ! akasema Gabriel.Mathew akamtazama kisha akawaambia


“Mpeni barafu aweke hapo alipoumia.He’s telling the truth” akasema Mathew na Gabriel akatolewa mle ndani akapelekwa katika chumba alichokuwamo mchungaji Zabron


“Tulifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea pale kanisani na alichokisema huyu jamaa ndicho kilichotokea.Kuna kitu kimoja amekitamka Gabriel kwamba baada ya kukodishwa akapelekwa katika kampuni ya kutengeneza filamu ya African pictures ambako waliwachukua wenzao watano wakaelekea kanisani.Swali linalokuja hapa ni kwa nini watu hao watokee katika ofisi za African pictures? Kuna mahusiano gani kati ya African pictures na black Mafia? Akauliza Mathew


“Kuna kitu kingine kilichonistua baada ya kusikia akitaja African pictures.Kuna mtu nilikutana naye Japan anaitwa Sindisiwe Duma.Katika kisiwa nilichokuwa naishi nilikuwa mwafrika peke yangu hivyo nikakutanishwa na Sindi akaniambia kwamba ametokea Afrika kusini na walikuwa pale Okinawa kwa ajili ya kurekodi kipande cha filamu ambacho yeye Sindi ndiye muhusika mkuu.Nilirejea Tanzania kwa kutumia ndege yao.Ni kampuni kubwa na wana ndege yao kubwa ambayo wanaitumia kuwasafirisha wasanii na vifaa kwenda sehemu mbali mbali duniani kurekodi filamu zao.Nataka tuichunguze hiyo kampuni ya African pictures nani mmiliki wake? Ruby hebu fanya kazi hiyo na tuweze kumfahamu mmiliki wa hiyo kampuni.Kama hao jamaa anaosema Gabriel walitokea hapo lazima tupachunguze” akasema Mathew na Ruby akaanza kucheza na kompyuta yake.


“African pictures imeingia katika ubao wetu nimestuka kidogo kwani nina rafiki yangu Sindi katika hiyo kampuni” Mathew akatolewa mawazoni baada ya Ruby kutoa mguno wote wakageuka ku mtazama.


“Mfumo wa SNSA


haupatikani ! akasema Ruby


“Haupatikani? Akauliza


Zari


“Ndiyo haupatikani “ akasema Ruby.Zari naye akajaribu kujiunga lakini mfumo wa SNSA haukuwa


ukipatikana


“This is weird.Nini kimetokea? Akauliza Zari huku akiichukua simu yake


“Au wamegundua


tunatumia mfumo huo na wakatuondoa? Akauliza Mathew


“Hapana si rahisi kugundua” akasema Ruby.Zari naye akatoa mguno


“Kuna nini Zari?Mathew akauliza


“Kila simu ninayopiga SNSA haipatikani.Kuna nini kinaendelea? Akauliza Zari akiendelea kujaribu kupiga simu lakini kila simu aliyoipiga haikupatikana


“Haya ni


maajabu,haijawahi kutokea watu wote SNSA wakazima simu kwa mara moja,hata simu za mezani hazipatikani” akasema Zari




**************


Umbali wa kilometa moja kutoka jengo la SNSA karibu


kila kitu cha kielektroniki kilizima.Umeme ulikatika,magari yalizima,simu hazikufanya kazi,mifumo yote ya kompyuta haikufanya kazi.Hii ilitokea baada ya Black Mafia kupiga bomu la kielektroniki ambalo kazi yake ni kuzima kila kifaa cha kielektroniki katika eneo husika.


Ulikuwa ni mshangao mkubwa sana kwa wafanya kazi wote wa SNSA hawakuwahi kushuhudia kitu kama kile kikitokea.Taharuki kubwa ikatanda katika jengo lile na watu walichanganyikiwa hawakujua wafanye nini.Hakukuwa na njia yoyote ya kuweza kuwasiliana hakukuwa na kitu chochote kilichokuwa kinafanya kazi.Wakati taharuki ikiwa imetanda na watu hawajui wafanye nini,wakajikuta wakivamiwa na kundi la watu wasiowafahamu.Lilikuwa ni tukio la ghafla sana ambalo hawakulitegemea.


Black Mafia walivamia jengo la SNSA na ndani ya muda mfupi wakafanikwia kuwaweka chini ya ulinzi wafanyakazi kadhaa na kuwakusanya sehemu moja.Kwa kuwa ramani tayari walikuwa nayo kundi moja lilielekea upande wa afya kwa ajili ya kumchukua Mathew Mulumbi na wengine wakaendelea na ulinzi wa wale mateka pamoja na kulidhibiti jengo.Upande wa afya kulikuwa kimya na hakukuwa na mtu hata mmoja.Walifungua kila


mlango kila kabati lakini


Mathew Mulumbi hakuwemo.Walirudia mara ya pili kutafuta lakini


hawakumpata.Kundi lililokwenda upande wa hospitali likarejea kuungana na wenzao waliokuwa wamewashikilia mateka wafanyakazi.


“Sikilizeni kwa makini ! akasema Paul


“Yeyote atakayeonyesha mahala alipo Mathew Mulumbi itakuwa ni salama yake na tutamuacha hai ! akasema Paul aliyekuwa amevaa kofia ya kufunika uso wake.Watu wote wakabaki kimya


“Hakuna anayefahamu mahala alipo Mathew Mulumbi? Akauliza Paul kwa hasira.Ghafla akamuinua mmoja wa wafanyakazi akampigisha magoti na kumuwekea bunduki kichwani.


“Nieleze ukweli mahala alipo Mathew Mulumbi !


“Simfahamu Mathew


Mulumbi ! akajibu yule mwanamke na bila huruma Paul akamtandika risasi akaanguka na kufa pale pale.


“Naombeni mfahamu


hatuna utani tutaua mmoja baada ya mwingine hadi pale mtakapotueleza mahala alipo Mathew Mulumbi ! akafoka Paul


“Nafahamu Mathew Mulumbi yuko humu ndani nataka mnioneshe mahala alipo !Wapi amejificha? Akauliza Paul lakini hakuna aliyemjibu


“Narudia tena kuwauliza wapi alipo Mathew Mulumbi? Akauliza Paul na ukimya ukaendelea.Bila mzaha akaizinga bunduki yake na kuachia risasi watu watatu wakaanguka na kufa


“Nitaua mmoja baada ya mwingine.Wapi alipo Mathew Mulumbi? Akauliza tena lakini hakuna aliyemjibu


“Kwa mara ya mwisho wapi alipo Mathew Mulumbi? Akauliza Paul na kuzidi kukasirika akamuinua tena mtu mwingine


“Mathew Mulumbi


alikuwa hapa anatibiwa yuko wapi? Akamuuliza


“Sifaha….” Hakumaliza sentensi akamchapa risasi akaanguka na kufa.John Mkizi akamfuata Paul na kumnong’oneza kitu kisha


Paul akamuinua mwanamama mmoja aliyekuwa anatetemeka na kumnyooshea bunduki


“Nani kiongozi wenu hapa?akauliza “Za..z..zz..Zari” “Zari?


“Ndiyo”


“Nataka unionyeshe huyo Zari ni nani?akasema Paul na kumuelekeza mmoja wa vijana wake aliyekuwa ameshika taa ya chemli amuongoze Yule mama ili akamuonyeshe Zari ni nani.Waliwakagua watu wote mle ndani


“Zari hayuko hapa ! akasema Yule mama na Paul akamuelekezea bunduki “Onyesha alipo Zari !


“Kweli hayupo hapa !


“Amekwenda wapi?


“Hakuwepo hapa ofisini usiku huu ! akasema mwingine


“Nani humsaidia majukumu yake kama hayupo


? akauliza Paul na kumuelekezea Yule mama bunduki.


“Lutengano ! akasema Yule mama akiwa amefumba macho kwa woga


“Lutengano please stand up ! akasema Paul


“Nitahesabu mpaka tatu na kama hutajitokeza watu wanne watapoteza maisha” akaanza kuhesabu na mara Lutengano Mwaijumbe msaidizi wa Zari akasimama akafungwa pingu,wakachukuliwa tena watu wengine wanne wakafungwa pingu na kuwekwa pembeni.Paul akamuita John pembeni wakazungumza


“Tumemkosa Mathew Mulumbi.Hayuko hapa ! akasema Paul


“Paul tusikate tamaa mapema yawezekana kuna


sehemu amefichwa ndani ya hili jengo lao”


“Mathew alikuwa hospitali akitibiwa lakini hayupo.Lazima kuna mahala amepelekwa nje ya hapa.Tusiendelee kupoteza muda tuondoke tukawahoji hawa jamaa tuliowapata watatueleza mahala alipo


Mathew Mulumbi ! akasema


Paul


“Hawa wengine


tunawafanyaje? Akauliza John “Kill them all




“Wako wengi Paul na milio ya risasi ikisikika inaweza ikawavuta watu au askari kufika mahala hapa”


“Nini ushauri wako? Akauliza Paul


“Tuwaache tuondoke na hawa wachache” akasema John.Paul akafikiri kwa muda halafu akasema


“Sawa tusipoteze muda wakusanye vijana tuondoke mahala hapa” akasema Paul na kutoka katika begi lake alilokuwa amelivaa akatoa kopo moja akang’oa kifuniko na moshi ukaanza kutoka kisha akapiga mbinja mara tatu na vijana wa Black Mafia waliokuwa wameshika ulinzi sehemu mbali mbali za jengo lile wakashuka haraka na wote wakakutana nje ya jengo.John akahakikisha kama wote wako salama kisha wakaondoka sehemu ile wakitembea kwa miguu.Magari yao walikuwa wameyaacha mbali na mahala pale hivyo wakatembea kwa miguu kuyafuata.Kulikuwa na giza na baadhi ya sehemu walizopita walisikia watu wakiendelea kushangaa kile kilichotokea.




**************


Kitendo cha mifumo yote ya SNSA kupotea na simu hata moja kutokupatikana


kiliwashangaza sana akina


Mathew


“Hii si kawaida na haijawahikutokea hata mara moja.Ninakwenda SNSA kujua nini kimetokea.Lazima kuna kitu kimetokea si bure” akasema Zari


“Zari sikushauri uende huko.Tusubiri hadi asubuhi tutajua nini kimetokea” akasema Ruby


“Tunautegemea mfumo wa SNSA katika kuendesha misheni yetu hivyo lazima tujue nini kimetokea huko.Zari chukua makomando wawili nenda nao SNSA ujue kuna tatizo gani” akasema Mathew na bila kupoteza muda Zari na makomando wawili wakaondoka kuelekea SNSA


Akiwa njiani bado Zari aliendelea kujaribu kupiga simu SNSA lakini hakukuwa na mafanikio yoyote kila simu aliyojaribu kupiga haikupatikana.


“Nini kimetokea leo?Haijawahi kutokea simu zote zisipatikane ! akawaza Zari huku gari likienda kwa kasi kubwa kutokana na barabara ile kuwa na magari machache


Ghafla dereva akapungua mwendo wa gari baada ya kuona vimuli muli vya magari ya askari polisi yakiwa yamesimama mbele na kufunga barabara huku kukiwa na watu wengi .


“Kuna nini kimetokea pale? Akauliza Zari huku akizidi kuwa na wasi wasi


Akajitokeza askari mmoja akanyoosha mkono na kulitaka gari la akina Zari lisimame pembeni.Zari akashuka akamfuata Yule askari


“Afande kuna nini kimetokea hapa?


“Mama kuna kitu kimetokea huko mbele na haruhusiwi mtu au chombo chochote cha moto kuelekea huko kwa sasa”


“Nini kimetokea? Akauliza Zari kwa wasiwasi


“Hatujui nini kimetokea lakini kama unavyoshuhudia eneo hilo lote lina giza na kikubwa zaidi hakuna mawasiliano,hakuna gari linawaka hakuna kompyuta inafanya kazi kwa ujumla hakuna kifaa chochote cha kielektroniki kinachofanya kazi eneo hilo.Uchunguzi unaendelea kwa sasa kujua nini hasa kimetokea lakini wakati uchunguzi huo unaendelea tunaendelea kuwatoa watu eneo hilo kwa ajili ya usalama wao” akasema Yule askari na Zari akarejea garini


“Kuna nini kimetokea madam? Akauliza mmoja wa makomando na Zari akamuelezea


“Hii mbona inaonyesha kama ni dalili za EMP? Akasema Yule komando


“EMP?akauliza Zari


“Ndiyo.Hizo ulizoeleza ni dalili zake.Bomu hilo linapopigwa huzima kila kitu cha kielektroniki kwa umbali fulani kutegemea na nguvu yake.Mabomu kama haya hutumika katika misheni mahsusi kabisa ! akasema Yule komando na mara Zari akastuka


“Oh my God ! SNSA” akasema Zari


“Kutoka hapa hadi SNSA si mbali na kama bomu hilo limepigwa eneo hili basi lengo lilikuwa SNSA na ndiyo maana mifumo yote SNSA imezima ! akasema Zari na haraka haraka akampigia simu Rais Festus


“Zari umeniwahi nilitaka nikupigie nijue maendeleo yenu” akasema Rais Festus


“Mheshimiwa rais kuna


tatizo limetokea naamini tayari umejulishwa”


“Nimejulishwa tayari kile kilichotokea eneo ambalo si mbali sana na hapa ikulu nimekwisha elekeza uchunguzi ufanyike mara moja kujua nini hasa kmetokea?


“Mheshimiwa Rais


tunaamini kilichotokea hapa ni kitu kinaitwa EMP”


“EMP? Rais akauliza


“Ndiyo mheshimiwa rais


hili ni bomu la kielektroniki ambalo likipigwa sehemu basi huzima kila kifaa cha kielektroniki na kupigwa bomu hilo eneo hili tunaamini ililengwa SNSA” “Jesus Christ !


“Mheshimiwa rais niko


hapa kuna kizuizi cha askari na hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia eneo la tukio.Ninaomba unisaidie niweze kupita hapa na kwenda SNSA kujua nini hasa kimetokea huko” akasema Zari na Rais akamuomba ampe muda mfupi alifanyie kazi ombi lake.Baada ya dakika chache askari mmoja akamfuata Zari na kugonga kioo cha gari


“Mama umeruhusiwa unaweza ukaenda huko unakotaka kwenda lakini gari utaliacha hapa” akasema Yule askari.Zari na makomando wawili wakashuka garini na kutembea kwa miguu kuelekea SNSA.Eneo lote lilikuwa na giza na kulikuwa na askari polisi wakipita nyumba hadi


nyumba kujua kama athari zilizotokea vile vile


walikuwepo watalaamu wa kutoka mamlaka ya mawasiliano na idara mbali mbali kujua nini hasa kilichokuwa kimetokea.


Walifika katika geti la kuingilia SNSA na kukuta kuna askari kadhaa nje Zari akajitambulisha kwamba yeye ndiye mkuu wa idara ile akaruhusiwa kuingia ndani.Wafanyakazi wa SNSA walikuwa wamekusanywa sehemu moja na wengi wakilia kwa kile kilichokuwa kimetokea.Zari akawafuata na walipomuona vilio vikazidi “Nini kimetokea hapa Ezekiel?Zari akamuuliza mmoja wa wafanyakazi


“Mkurugenzi hatujui nini kimetokea lakini ghafla tu umeme ulikatika,kila kitu kikaacha kufanya kazi kuanzia simu,kompyuta na hata tulipojaribu kuwasha jenereta la akiba halikuwaka.Wakati tukijiuliza kilichotokea tulivamiwa na watu tusiowafahamu wakatukusanya na kikubwa walichotaka kukijua ni mahala alipoMathew


Mulumbi.Wenzetu kadhaa wameuawa wakiwamo walinzi karibu wote waliokuwa nje na kama haitoshi wameondoka na wenzetu wengine akiwamo Lutengano ! akasema Ezekiel na Zari akahisi kama kichwa chake kimekuwa kizito ghafla.Ilikuwa ni taarifa iliyomstua sana.Zari akawapa pole na kuwapa moyo kwama wenzao waliotekwa watapatikana halafu akaelekea ndani ya jengo na kuikuta miili ya watu kumi na sita ikiwa imelazwa.Walinzi wote waliokuwa eneo la nje wakilinda usiku ule waliuawa pamoja na wafanyakazi wengine.



Paul na wenzake walirejea katika makao yao makuu wakiwa na mateka wao waliowachukua SNSA.Taarifa ya kwanza ambayo aliipata Paul baada ya kuwasili ofisini kwao ni kuuawa kwa watu wao saba waliotumwa katika kanisa


la injili ya wokovu kwenda kumteka mwanamke ambaye alikuwa na miadi ya kuonana na mchungaji Zabron.Ilikuwa


ni taarifa iliyomstua sana.Alichukua muda akiwa ofisini kwake akitafakari kilichotokea usiku ule


“Misheni zote mbili zimeshindwa kufanikiwa na tumejikuta pale pale tulipokuwepo hatujui mahala alipo Mathew Mulumbi na badala yake tumewapoteza watu saba.Hiki ni kitu cha kustusha sana.Huyu Mathew Mulumbi nahisi anatumia uchawi kwa sababu haiwezekani kila tunapokaribia kumkamata anatuponyoka na hata katika majaribio kadhaa ya kumuua amenusurika kwa namna ya ajabu kabisa.Tumelazimika hadi kutumia EMP lakini tumeshindwa kumpata.Jana tuliambiwa kwamba hali yake ilikuwa mbaya na alikuwa anapatiwa matibabu palepale SNSA lakini leo hayuo amekwenda wapi? Akajiuliza Paul


“Natakiwa kumfahamisha Kasiano kilichotokea.Naamini lazima atakasirika sana kwa hiki kilichotokea hasa kumkosa Mathew Mulumbi” akawaza Paul halafu akachukua simu yake aliyokuwa ameiacha ofisini akaiwasha na kumpigia nabii Kasiano


“Paul nimekutafuta muda mrefu hukuwa unapatikana wewe wala msaidizi wako John.Nataka kujua nini kinaendelea huko? Akauliza Kasiano


“Mkuu tulikuwa na


misheni mbili usiku huu wa leo ndiyo maana mimi na mwenzangu hatukuweza kupatikana simuni” akasema Paul na kumueleza Kasiano kuhusiana na misheni zile mbili namna walivyozipanga na kile kilichotokea


“Paul ninashindwa niseme nini kwa haya unayonieleza.Sikutegemea kusikia mambo kama haya kutoka kwako.Kuhusu hili suala la Zabron hukupaswa kufanya maamuzi yoyote bila kunishirikisha.Ona kilichotokea sasa.Tumepoteza vijana saba na Zabron hajulikani alipo.Ni afadhali kama yangetokea haya halafu tumpate Mathew Mulumbi


lakini tmepoteza watu na Mathew Mulumbi


hajapatikana! We have nothing ! akafoka Kasiano


“Mkuu japokuwa tumemkosa Mathew Mulumbi lakini tunao watu tumewapata kutoka kule SNSA ambao watatueleza kila kitu kuhusu Mathew na mahala alipo” akasema Paul


“Paul umezidi kulifanya jambo hili liwe gumu zaidi.Ninaona kadiri siku zinavyokwenda mbele tunazidi kumfanya Mathew atusogelee na kwa sasa wamekwisha anza kucheza pale kanisani”


“Nakuahidi mkuu kwamba


tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunampata


Mathew ! akasema Paul


“Na iwe hivyo Paul.Watumie hao watu uliowachukua SNSA na uhakikishe Mathew Mulumbi anapatikana ! akasema Kasiano na kukata simu kwa hasira


“Nilijua tu mkuu hatafurahishwa na hiki kilichotokea.Hata hivyo tumejitahidi kadiri tuwezavyo lakini lazima nikiri kwamba


Mathew Mulumbi ametuzidi maarifa” akawaza Paul na kumuita John ofisini kwake


“John nimezungumza na mkuu simuni hajafurahishwa na kushindwa kumpata Mathew.Nataka uwaandae wale watu tuliowapata kule SNSA tuanze kuwahoji na watueleze kile wanachokifahamu kuhusu Mathew Mulumbi” akasema


Paul na John akatoka


“Kwa nini tunashindwa kumpata Mathew Mulumbi? Akajiuliza Paul na mara akapigiwa simu na John akamjulisha kwamba kila kitu tayari kimeandaliwa.Paul akiwa na hasira akatoka na kuelekea katika sehemu wanayoitumia kwa kuwahoji watu mbali mbali


**************


Mathew alielekeza tena mchungaji Zabron apelekwe katika chumba chake.


“Mchungaji Zabron naamini tayari umekwisha tafakari vya kutosha na una


kitu cha kunieleza” akasema Mathew


“Ndugu yangu kama


nilivyokueleza awali kwamba sifahamu chochote kinachowafanya hao watu nisiowafahamu watuchunguze mimi na wenzangu” akasema mchungaji Zabron


“Mchungaji Zabron lazima kuna kitu ambacho kinawafanya hawa jamaa wawachunguze na kuwafuatilia maisha yenu.Narudia tena kusema kwamba hawa watu wanaowafuatilia wana mahusiano na wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya,kitendo cha kuwafuatilia ninyi kinatufanya tuamini kuna kitu mnakifahamu kuhusu watu hao na biashara yao ya dawa za kulevya” akasema Mathew na sura ya mchungaji Zabron ikabadilika akasimama


“Ninaapa kwa jina la Mungu aliye hai sijawahi kujishusisha na watu hao na wala biashara yoyote haramu.Tangu ujana wangu nimekuwa nikimtumikia Mungu kwa uaminifu mkubwa ! akasema mchungaji Zabron kwa sauti ya juu


“Mchungaji Zabron pamoja na hayo unayotueleza lakini bado tunataka kufahamu kwa nini watu hawa wanawafuatilieni wewe na wachungaji wenzako?Lazima ipo siri ambayo inawafanya wawafuatilie.Tuambie tafadhali ni kitu gani hicho? Lengo letu ni kutaka kukusaidia wewe na wenzako ili yasiwakute kama yaliyomkuta Lucas” akasema


Mathew


“Sijui nitumie lugha gani ndugu zangu mniamini kwamba haya ninayowaeleza ni ya kweli” akasema mchungaji Zabron


“Mchungaji wewe ni mtumishi wa Mungu na tunakuheshimu sana.Hatutaki kutumia nguvu kupata kile tunachokihitaji kutoka kwako.Naomba ufahamu hii ni kwa faida yako pia lakini kama hautakuwa tayari kushirikiana nasi basi tutalazimika kutumia nguvu” akasema Mathew “Hata kama mkitumia nguvu majibu yangu hayatabadilika kwani ninachokisema ni kitu cha kweli na kama mtumishi wa Mungu nitasimama katika ukweli.Mungu wetu aliye hai ndiye anayeufahamau ukweli na ananiona hivi sasa mtumishi wake nikisimama katika ukweli.Sifahamu chochote.Siwafahamu watu hao ni akina nani na wala sina mahusiano nao yoyote yale.Kama ningekuwa na mahusiano nao kwa nini ningeendelea kufanya kazi hii ya kichungaji?Ningekuwa tajiri hivi sasa na ningekwisha achana na uchungaji na kuendelea na biashara hiyo” akasema mchungaji Zabron



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog