Simulizi : Scandle (Kashfa) (2)
Sehemu Ya Nne (4)
halafu akachukua kisu na
kukizamisha katika mguu wa
Thomas mahala
palipoungua.Thomas akapiga
kelele kubwa ya maumivu.Zari
akafumba macho.Alihisi mwili
unamtetemeka.Mathew
akakichomoa kisu na kutaka
kukichoma tena katika mguu
“Nitasema ! Nitasema !
akalia Thomas.Mathew
akamfunga jeraha lile
lililokuwa linatoa damu nyingi
“Tueleze haraka kuhusu
Black Mafia” akasema Mathew “Sisi ni wauaji.Ni kundi
kubwa na tunatumwa sehemu
mbali mbali kuua ! akasema
Thomas
“Nani kiongozi wenu hapa
Tanzania?
“Simfahamu.Alvaro ndiye
anayemfahamu”
“Utatupeleka katika
makazi yenu”
“Sipafahamu mimi ni
mgeni hapa.Nimekuja wiki
mbili zilizopita”
“Uliingiaje hapa nchini?
Akauliza Mathew “Nipelekeni hospitali
tafadhali”
“Hakuna hospitali kama
hutaeleza ukweli ! Utakufa kwa
maumivu !
“Mathew huyu mtu
anasema kweli ! akasema Zari
“Hapana anadanganya !
akasema Mathew kwa ukali
“Mathew huyu ni mtu
pekee ambaye anaweza
akatuongoza kufahamu waliko
wenzake hatupaswi
kumpoteza.Tumpatie
matibabu kwanza ndipo tuendelee kumuhoji” akasema
Zari
“Fine.Mpigie simu daktari
aje ampatie matibabu huku
huku shambani na mara tu
akipata matibabu nitaendelea
na mahojiano,lazima atasema
ukweli ! akasema Mathew
“sawa Mathew”akajibu
Zari na kumpigia simu daktari
kutoka SNSA akamtaka afike
katika shamba la mazoezi ya
makomando.Mathew
akamuinua Thomas na
kumpeleka ndani.
************
Kiza kilianza kuingia pale
gari moja lilipowasili katika
nyumba anayoishi Martha
Mwailule.Mlinzi wa kimasai
aliyekuwa amekaa pembeni ya
geti akalisogelea gari lile na
kioo kikafunguliwa.
“Habari yako Masai”
akasema mmoja wa watu
waliokuwamo ndani ya ile gari
“Nsuri.Niwasaidie nini?
“Tuna shida na Martha
tumemkuta? Akauliza Yule jamaa aliyekuwa amevaa
miwani huku akitafuna kitu
“Ninyi ni nani wake?
Akauliza mlinzi Yule
“Sisi ni wageni
wake.Tunaomba kuonana naye
tafadhali kama yumo ndani”
“Subiri dakika moja”
akasema mlinzi na kuingia
ndani baada ya dakika mbili
akatoka akiwa ameongozana
na mwanamke mmoja mnene
wastani ambaye alilisogelea
gari
“Karibuni jamani” “Ahsante sana.Habari za
jioni”
“Nzuri.Nimeambiwa
mnanitafuta”
“Ndiyo tumekufuata hapa
nyumbani utatusamehe kwa
kuja bila taarifa lakini sisi ni
waandishi wa habari kuna
mambo tumekuja hapa
kuzungumza nawe”
“Mambo gani?! Akauliza
Martha akionyesha mshangao
“Martha tunaweza kupata
sehemu tukakaa na kuzungumza? Haipendezi
kuzungumza namna hii”
“Haya karibuni ndani”
akasema Martha na
kumuelekeza mlinzi
kuwafungulia wageni geti
wakaingia ndani na
kukaribishwa sebuleni
“Karibuni
jamani.Nimestuka kidogo kwa
kutembelewa na waadishi wa
habari muda kama huu.Ninyi
mmetokea wapi ndugu zangu?
“Utatusamehe kwa kuja
bila taarifa.Sisi ni waandishi
wa habari wa kujitegemea” “Sawa niwasaidie nini?
Akauliza Martha
“Kuna mambo tumekuja
kuyafahamu kuhusiana na
maisha ya mwanao ” akasema
mmoja wa wale jamaa na sura
ya Martha ikabadilika
“Nini mnataka
kukifahamu kuhusu
mwanangu?
“Tunataka kufahamu
kuhusu maendeleo yake kwa
sasa”
“Mtanisamehe ndugu
zangu lakini maisha ya mwanangu ni mambo binafsi
na sidhani kama yanapaswa
kufuatiliwa na waandishi wa
habari.Mimi ni nani hadi
mnifuate kuniuliza maisha ya
mwanangu” akasema Martha
akionekana kuwa mkali
kidogo.
“Usihofu Martha tunataka
kufahamu maendeleo ya
mwanao baada ya kuanza
kupatiwa matibabu .Tuna
taarifa kwamba alikuwa
ameingia katika matumizi ya
dawa za kulevya vipi
maendeleo yake kwa sasa? “Kaka zangu nawaomba
sana maisha yangu
hayawahusu kabisa.Kwanza
mmefahamuje jina langu?
“Martha kwa sasa
unafanya kazi wapi?
“Jamani kwa nini
mnanilazimisha niwaeleze
kuhusu maisha
yangu?Mnataka nini
kwangu?Au ninyi ni
majambazi?
“Hapana sisi si majambazi
ila ni watu tunaokufahamu
vyema.Tunafahamu umewahi
kufanya kazi katika wizara ya maji kama katibu muhtasi wa
aliyekuwa waziri wa maji wa
wakati huo ambaye kwa sasa
ni Rais Festus
Mayungulu.Tunafahamu kuwa
hata mtoto huyu ulizaa na
Festus lakini hayo yote ni
maisha binafsi na hatupaswi
kuyaingilia lakini tunataka
kufahamu uliacha kazi wizara
ya maji baada ya kupata
mimba je vipi kuhusu maisha
yenu kwa sasa wewe na
mtoto,je Rais Festus
anawagharamia? Akauliza na
sura ya Martha tayari ilikwisha badilika.Alipatwa na mstuko
mkubwa.
“Kaka zangu naomba
muondoke hapa nyumbani
kwangu haraka sana.Sitaki
kuwaona hapa wambea
wakubwa ninyi.Maisha yangu
na mwanangui yanawahusu
nini?
“Kwa hiyo dadaMartha
unakiri kwamba mtoto huyu
uliyenaye ni wa Rais Festus
Mayungulu?
“Hata kama ningezaa na
Rais ninyi inawahusu nini? “Rais ni kioo chetu hivyo
tunahitaji kuyafahamu maisha
yake na kama kiongozi wetu
,kama baba yetu anatakiwa
kuwa mfano wa kuigwa na
sehemu ya kwanza ambapo
anapimwa ni katika matunzo
na malezi ya familia.Je
mwanao anafahamu kama
baba yake ni Rais Festus?
Martha akasimama na
kwenda kuufungua mlango
“Ahsanteni kaka
zangu.Nawaomba muondoke
na msirudi tena hapa !
akasema kwa ukali “Tunashukuru Martha
.Tunaondoka laki..”
“Hakuna lakini odokeni
haraka sana ! akafoka Martha
na waandishi wale wakatoka
na kuingia katika gari lao
wakafunguliwa geti na
kuondoka
“Masai umewaona hawa
jama sitaki waruhusiwe tena
kukanyaga mahala
hapa.Wakija tena hapa piga
mkuki ! akasema Martha kwa
hasira akimuelekeza mlinzi
wake “Ee Mungu wangu siri
imefichuka.Jambo hili
nimelificha kwa miaka mingi
lakini duniani hakuna siri
hatimaye waandishi wa habari
wamelinasa tena wanazo
taarifa hadi mwanangu
ameathirika na dawa za
kulevya.Nimestuka sana ,mwili
wote unanitetemeka.Najiuliza
nini hasa lengo lao la kuja
kunihoji kuhusu maisha
yangu? Wanataka kuandika
katika magazeti yao ya udaku?
Akajiuliza Martha
“Ngoja nimjulishe Festus
jambo hili ili achukue hatua za haraka” akawaza Martha na
kuchukua simu akazitafuta
namba za simu za Rais Festus
akampigia.Simu ikaita bila
kupokelewa akapiga tena
ikapokelewa
“Martha nimekwisha kupa
taratibu za kuwasiliana nami
kwa nini unanipigia simu
muda huu? Akauliza Rais
Festus
“Festus ninafahamu
taratibu lakini kuna tatizo
limetokea ndiyo maana
nimekupigia”
“Tatizo? “Ndiyo kuna tatizo”
“Tatizo gani? Akauliza
Festus
“Muda mfupi uliopita
nimefuatwa hapa na waandishi
wa habari”
“Waandishi? Wanataka
nini? Akauliza Festus
“Wamekuja kuniuliza
maswali kuhusu maisha yangu
na mwanangu Joel” akasema
Martha
“Martha
sijakuelewa.Waandishi wa
habari watakufuataje wewe kukuuliza kuhusu maisha yako
na ya mwanao? Wewe una
faida gani
kwao?Ninachofahamu
waandishi hujielekeza kwa
watu wenye majina makubwa
sasa ujio wao kwako
umenishangaza”
Martha akavuta pumzi
ndefu halafu akasema
“Festus tayari siri imevuja”
“Unasema?
“Siri tayari
imevuja.Wanafahamu kuhusumimi na wewe,tayari
wanafahamu kuhusu Joel
kuwa ni mwanao na
wanafahamu amejiingiza
katika matumizi ya dawa za
kulevya.Wanafahamu kila
kitu” akasema Martha na
ukimya ukatawala
“Festus ! akaita Martha
“Martha umenistua
sana.Sikutegemea kusikia
habari kama hii”
“Hata mimi nimestuka
sana sikutegemea kabisa” “Wamefahamuje hili
jambo? Akauliza Festus
“Hata mimi sifahamu”
“Walikuwa wangapi hao
waandishi wa habari? Akauliza
“Walikuwa wawili wote
wanaume”
“Walikwambia wanatoka
chombo gani cha habari?
“Walisema ni waandishi
wa kujitegemea”
“Jesus Christ ! hili jambo
limevujaje na kuwafikia
wanahabari? Mbona tumejitahidi kulifanya siri kwa
muda mrefu? Akauliza Festus
“Festus wewe una nguvu
kubwa hivyo nakuomba
limalize suala hili.Mimi na
mwanangu sitaki tuanze
kuandamwa na vyombo vya
habari tutaumia sana hivyo
fanya ufanyavyo watafute
watu hawa uzungumze nao au
fanya vyovyote vile ili jambo
hili limalizike kwani linaweza
kukuwekea doa kubwa katika
kazi yako”
“Watu hawa walisema
wanataka nini? Hawakusema kama wanahitaji fedha au kitu
chochote?
“Hapana hawakusema
wanahitaji chochote”
“Martha hebu nipe picha
kamili nini hasa hao jamaa
walitaka kukifahamu?
“Kikubwa walichokuwa
wanataka kukifahamu ni kama
unashiriki malezi ya mtoto”
“Dah ! Jambo hili
limenichanganya sana Martha.
Naomba nikupigie simu
baadae kidogo” “Sawa Festus lakini
nakusisitiza tena kwamba
fanya kila uwezalo kuhakikisha
unalimaliza jambo hili.Sitaki
mimi na mwanangu tuanze
kuandikwa magazetini”
akasema Martha na kukata
simu
Festus aliegemea meza
baada ya simu ile
kukatwa.Alihisi kichwa
kinamzunguka.Ilikuwa ni
taarifa iliyomstua mno
“Hii ni moja ya siri zangu
kubwa ambayo nimejitahidi
kuificha hadi hivi sasa mwanangu ni mkubwa na hata
mke wangu Bella hafahamu
chochote.Hawa waandishi wa
habari wameijuaje? Au ni
Martha anataka kunifanyia
mchezo akawaeleza waandishi
wa habari ili wanitoe fedha
?Nahisi hivyo kwa sababu
sifahamu siri hi imevuja vipi”
akawaza
“Lakini Martha hawezi
akafanya hivyo kwani anaishi
maisha mazuri na anapata kila
kitu anachokihitaji na hata
mwanangu
ninamuhudumia.Nimemuweze
sha kiuchumi kwa kumfungulia miradi mbali
mbali hivyo pesa kwake si
tatizo hata kidogo.Isitoshe
Martha ananipenda sana na
hana sababu ya kunifanyia
jambo kama hili.Swali
linalokuja ni nani basi
aliyeifahamu siri hii halafu
akaiuza kwa waandishi wa
habari? Au ni Joel? Akajiuliza
“Lakini Joel hafahamu
kama mimi ni baba
yake.Nilikubaliana na Martha
jambo hili liwe siri yetu na Joel
asifahamishwe chochote hadi
pale nitakapokuwa nimemaliza
kipindi changu cha urais.Nahisi yawezekana Joel
amechimba na akajua kuwa
mimi ni baba yake na akaanza
kuropoka kwa watu na taarifa
zikawafikia waandishi wa
habari ambao sasa wameanza
kulichunguza hili jambo
kuutafuta ukweli.Nifanye nini?
Akaendelea kujiuliza
“Ningewafahamu
waandishi hao ni akina nani
ningeweza kuwatafuta na
kuzungumza nao tukalimaliza
hili jambo kimya kimya lakini
hata Martha naye
hawafahamu.Natakiwa
kufanya kila lililo ndani yauwezo wangu kuhakikisha
jambo hili halifiki kwa
wananchi na ikibidi hata
nguvu inaweza kutumika
kuhakikisha jambo hili
linazimwa” akawaza akiwa
amejaa hasira
“Ngoja kwanza nimpigie
Salvatory nimuite hapa yeye
anaweza akanishauri vizuri
nini nifanye.Amekuwa ni
mshauri wangu mkubwa wa
mambo yangu mengi
ninamuamini katika hili
anaweza akanishauri vizuri
pia” akawaza na kuchukua
simu akampigia Salvatory Tarimo na kumtaka afike ikulu
mara moja
Nabii mkuu Kasiano
alipewa taarifa na Paul kwamba tayari vijana wake walikwenda kuonana na Martha na ameonyesha mstuko mkubwa sana.Mara tu baada ya kuzungumza na Paul akampigia simu mama Bella “Kasian” akasema Bella “Mama Bella habari za muda huu”
“Njema kabisa.Kuna
taarifa gani? Akauliza Bella
“Mama nimekupigia
kukujulisha kwamba tayari nimekutana na timu yangu tumepanga mikakati na utekelezaji
umeanza.Tumeamua kuanza na lile la mtoto.Muda mfupi uliopita vijana wangu wametoka kuonana na Martha wamemuhoji na amestuka mno”
“Hata mimi nilihisi mambo tayari yameanza kuharibika kwani tukiwa mzani tunakula chakula Festus alipigiwa simu na kuinuka akaenda kuzungumza chumbani na hajarejea tena mezani.Naamini Yule mwanamke wake atakuwa amempigia kumjulisha kuhusu kufuatwa na hao watu wako”
“Inawezekana ikawa hivyo mama”
“Nini hatua inayofuata?
“Hatua ya kwanza ilikuwa ni kumstua Festus ili ajue siri yake imevuja.Baada ya hapo tunaingia katika hatua ya pili ambayo ni kuandaa taarifa na kuitoa gazetini.Kwa kuwa muda huu tayari magazeti mengi yamekwisha anza kuchapwa basi taarifa hii tutaishughulikia kesho na kuhakikisha inatoka katika magazeti ya kesho kutwa.Ninakuhakikishia mama itakuwa ni habari yenye msisimko mno” akasema Kasiano
“Sawa Kasiano kazi nzuri.Baada ya kombora hilo la kwanza nitawapa maelekezo mengine ya kufanya kabla ya kulirusha kombora la pili la maangamizi makubwa” akasema Bella
“Hata sisi tumepanga hivyo mama kwamba hatutarusha kombora la pili hadi pale tutakapoona namna kombora la kwanza lilivyofanikiwa” akasema Kasiano na kuagana na Bella *************
Salvatory Tarimo mshauri wa masuala binafsi wa Rais aliwasili ikulu kama alivyoitwa na Rais Festus na kuelekea katika sehemu ya mazungumzo ya faragha
“Salva utanisamehe kwa usumbufu muda huu” “Usijali mheshimiwa Rais”
“Salva nimekuita nina tatizo kubwa na ninahitaji mno ushauri wako lakini kabla ya yote ninataka nikukumbushe kwamba wewe ni mmoja wa watu ninaowaamini mno na mambo yangu mengi nimekuwa nikikushirikisha ili unishauri na kila unaponipa ushauri nimekuwa nikiufanyia kazi.Ninachotaka kukueleza ni moja ya siri yangu kubwa na ninakushirikisha kwa kuwa ninakuamini kwamba hii itaendelea kuwa siri na haitavuja” akasema Festus
“Ahsante sana kwa kuniamini mheshimiwa Rais ninakuahidi sintathubutu kuvunja uaminifu huo” akasema Salvatory
“Ahsante Salva” akasema Rais Festus na kuvuta pumzi ndefu
“Nitakuanzia mbali kidogo wakati nikiwa waziri wa maji” akasema Festus na kumuelezea Salva namna mahusiano yake na Martha yalivyoanza hadi alivyopata ujauzito na kuacha kazi
“Martha na mwanae
wanaishi maisha mazuri na wanapata kila kitu.Nimemjengea jumba zuri,nimemfungulia miradi mikubwa mikubwa yote hii ni katika kuhakikisha wanaishi maisha bora.Kwa bahati mbaya kijana wangu Joel alijiingiza katika starehe za kupindukia akiwa bado mwanafunzi na kujikuta akiingia katika matumizi ya dawa za kulevya.Kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu ili aweze kuachana na madawa hayo” akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“Usiku huu nimepigiwa simu na Martha akanijulisha kwamba kuna waandishi wa habari wametoka nyumbani kwake wakitaka kufahamu kuhusu maisha yake na mwanae.Kwa mujibu wa Martha ni kwamba wanahabari hao tayari wanafahamu kila kitu kana kwamba walikuwa wanafuatilia kila kilichokuwa kinaendelea kati yetu.Hilo ndilo hasa jambo lililo nistua na kunilazimu nikuite hapa muda huu unishauri nifanye nini?
“Pole sana mheshimiwa
Rais lakini na mimi kuna mambo nataka kuyafahamu.Je kuna mtu mwingine tofauti na nyie wawili aliyekuwa anafahamu kuhusu jambo hili?
“Naamini hakuna kwani
tulikubaliana iwe siri yetu wawili na imekuwa hivyo hadi sasa”
“Unadhani waandishi hao wamelifahamuje jambo hili? “Sifahamu”
“Walisema kama kuna kitu wanakitaka?
“Hapana hawakusema
chochote”
“Mheshimiwa Rais hili si suala dogo.Ni jambo kubwa ambalo linaweza kuweka doa kubwa katika uongozi wako.Wewe ni Rais mwenye sifa kubwa na watanzania wanakupenda sana,toka umeingia madarakani hakujawahi kutokea kashfa yoyote kubwa ambayo imeelekezwa kwako lakini hii kama itafika kwa wananchi itakuwa ni kashfa yako ya kwanza.Mheshimiwa Rais wewe ni kama baba na ukiwa kiongozi mzuri hukosi maadui.Unao maadui wengi ambao usiku na mchana hawalali wanakufuatilia na kuchunguza umekosea wapi ili wapate kukuchafua.Kwa bahati mbaya mpaka sasa hawajapata jambo lolote baya la kukuchafua na wamelipata hili watalipa uzito mkubwa sana. Mke wako analifahamu hili?
“Hapana hafahamu
chochote”
“Hilo ni tatizo lingine.Umewaficha familia yako jambo hili na watakapolipata kwa waandishi
wa habari familia itayumba.Doa la pili utaonekana umemtelekeza mtoto kiasi kwamba akatumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya kwa kukosa malezi.Hii ni kashfa kubwa pia.Mheshimiwa Rais hili si suala jepesi hata kidogo.Kwa hili lazima ukubali umekosea”
“Ndiyo maana nikakuita hapa Salva ili unishauri nifanye nini” akasema Festus
“Mheshimiwa Rais kuna mambo mawili ambayo naweza kukushauri” Salva akanyamaza kidogo “Kwanza hakikisha familia imelifahamu jambo hili kabla ya kulisoma katika magazeti au katika mitandao ya kijamii”
“Una maanisha nimweleze mke wangu?
“Ndiyo.Unapaswa uwe wa kwanza kumueleza mkeo na kumuomba msamaha kwa hiki ulichokifanya.Familia inapaswa kukusamehe kwanza.Usione aibu kuomba msamaha mheshimiwa Rais kwani hapa tunatafuta namna
ya kuilinda pia na familia yako.Wakikuelewa wakakusemehe na amani ikarejea basi hao watasimama nyuma yako pale utakapojitokeza mbele ya umma na kuwaeleza ukweli kuhusu jambo hili”
“Sijakuelewa vizuri Salva una maanisha nini kujitokeza kwa umma?akasema Festus
“Mheshimiwa Rais hakuna anamna lazima ujitokeze mbele ya umma wa watanzania na ulieleze jambo hili.Ni hivi,naamini waandishi hao watakuwa wamejipanga kuichapisha habari hii katika magazeti yao hivyo basi kabla hawajafanya hivyo wewe utawawahi na kulieleza jambo hili kwa wananchi na habari yao itakuwa imekufa.Hawatakuwa tena na sababu ya kuendelea kuichapisha habari hiyo kwani tayari kila mtu atakuwa anaifahamu.Faida ya jambo hilo ni kwamba watanzania watakusikia na kukuelewa.Utaonekana ni kiongozi jasiri ambaye umediriki kujitokeza mbele ya wananchi wako na kukiri kukosea.Nakuhakikishia mheshimiwa Rais jambo hili badala ya kukuangamiza litakujenga zaidi japo litazungumzwa kwa siku mbili tatu lakini maisha yataendelea familia itakuwa na amani na utakuwa umeutua mzigo mzito” akasema Salvatory
“Salva ni kweli unanishauri nilizungumze jambo hili la aibu mbele ya watanzania walioniweka madarakani?
“Ninakushauri hivyo mheshimiwa Rais.Ni vyema kama watanzania watalisikia jambo hili kutoka katika kinywa chako badala ya kulipata kwa mara ya kwanza katika
magazeti.Ukilizungumza wewe mwenyewe halitakuwa kashfa lakini ukisubiri likaandikwa kwanza na magazeti itakuwa ni kashfa kubwa hivyo wawahi hawa wanaotaka kukuchafua waonyeshe ni namna gani ulivyo jasiri,rais unayeweza kuanguka lakini ukainuka na kujifuta vumbi ukaendelea na safari,utawaonyesha ni baba bora ambaye unaweza ukakosea lakini ukaiangukia familia yako ukaiomba msamaha.Hili jambo litakupandisha juu badala ya kukushusha chini kama
wabaya wako wanavyotaka iwe”
“Dah ! Umenipa wakati mgumu sana Salva !
“Ni jambo gumu lakini
lazima lifanyike.Hii itakuwa ni mfano mzuri hata kwa wanaume wengine ambao wamewahi kuwaficha wake zao kuhusiana na watoto wa nje na watapata ujasiri wa kuwaeleza wake zao ukweli”
“Hakuna namna nyingine unadhani ninaweza kufanya labda kuwatafuta waandishi hao kuzungumza nao na kufikia makubaliano naweza hata kuwapa fedha au nafasi serikalini ili kuwaziba mdomo”
“Mheshimiwa Rais hii siri tayari imevuja.Waandishi wangapi utawapa nafasi serikalini? Ukitaka kuwapa fedha utaharibu kabisa mambo kwani wataandika kuwa umetaka kuwapa fedha ili kuwaziba midomo.Hii ni vita mheshimiwa Rais hivyo silaha pekee unayoweza kuitumia ni kwa kujitokeza na kueleza ukweli lakini ukweli huo uanze katika familia.Baada ya hapo utamuelekeza mkurugenzi wako wa habari aandae kipindi maalum kesho asubuhi kupitia luninga yoyote ile ambayo ina watazamaji wengi na katika kipindi hicho utaongozana na familia yako na utaeleza ukweli.Mke wako naye ataeleza kwamba amekwisha kusamehe kwa kitendo kile na hana tatizo lolote na mtoto uliyemzaa nje.”
“Ahsante sana Salva kwa ushauri huu.Naomba unipe muda na mimi niutafakari halafu nitajua nini cha kufanya” akasema Festus na kuagana na Salva
“Ushauri wa Salva ni mzuri lakini ugumu unakuja pale alipodai kwamba nimweleze ukweli Bella.Hilo ni jambo gumu sana kulifanya.Siwezi kumueleza ukweli mwanamke Yule ambaye namfananisha kama chui mwenye ngozi ya kondoo.Hata kama nikimueleza ukweli hatakuwa tayari kunisikia.Yuko tayari kuniona nikididimia.Lakini kama angeweza kukubali akanielewa basi ushauri wa Salva ungefaa mno” akawaza Festus
“Nashindwa nifanye nini? Nikitokea bila kuwa na mke wangu maswali yatakuwa mengi zaidi na nitadhalilika badala ya kutatua suala hili” Festus akaendelea kuwaza.
“Lakini kwa nini nisijaribu kuzungumza naye? Pengine anaweza akanielewa na suala
hili likawa jepesi.Mimi ni mwanaume sipaswi kumuogopa mwanamke ngoja nimfuate Bella” akawaza Festus na kuelekea chumbani kwa mke wake akagonga mlango
“Nani? Akauliza Bella
“Ni mimi” akajibu Festus na baada ya sekunde chache mlango ukafunguliwa na Festus akaingia ndani
“Unataka nini Festus? Akauliza Bella na Festus akamfuata na kumkumbatia akambusu.
“Festus what do you want?
Akauliza Bella lakini Festus bado aliendelea kuipitisha mikono yake katika sehemu mbali mbali za mwili wa mke wake mara Bela akamsukuma
“Festus huwezi ukaingia tu chumbani kwangu na kutaka kufanya ukitakacho ! akasema Bella kwa ukali
“I’m sorry Bella sikuja kwa ajili ya jambo hilo lakini nimejikuta nikipatwa na hisia baada ya kukuona”
“Ungeniona wa thamani kwako usingenifanyia haya unayonifanyia” akasema Bella “Bella tuachane na hayo.I need to talk to you”
“Talk to me? Bella akauliza
“Ndiyo Bella kuna jambo nataka kuzungumza nawe and
please let’s talk like civilsed people” akasema Festus na Bella akaufunga vizuri mkanda wa nguo yake ya kulalia akaenda kuketi katika sofa dogo lililokuwamo mle chumbani akitazamana na Festus
“Haya nieleze unachotaka kunieleza”
“Bella najua mimi na wewe tuko kwenye mgogoro mzito,hatuna mahusiano mazuri japo watu hawalifahamu hilo lakini ninakushukuru kwa kuwa umeendelea kushiriki katika mambo mbali mbali kama mke wa Rais”
“Nini unakitaka Festus? Akauliza Bella
“Nina tatizo kubwa na ninahitaji msaada wako”
“Msaada.Mhn ! akasema
Bella na kutoa mguno
“Ndiyo nahitaji msaada wako”
“Leo nimekuwa wa msaada kwako? Festus nimekusaidia sana hadi ukafanikiwa kuingia ikulu lakini ulipokalia kiti ukageuka nyoka na kutaka kuniuma hata mimi mwenyewe.Leo unahitaji msaada wangu?
“Bella tuyaweke hayo kando kwa sasa.Ni kweli ninahitaji msaada wako” akasema Festus.Bella akamkazia macho
“Najua anachotaka kunieleza.Maji yamemfika shingoni” akawaza Bella
“Nini unahitaji? Akauliza Bella
“Kuna jambo nahitaji kukueleza.Tafadhali naomba unisikilize hadi mwisho” akasema Festus “Nakusikiliza”
“Ahsante”
“This is so hard but I have to do it” akawaza Festus halafu akaanza kumuelezea mke wake tangu wakati akiwa wizara ya maji namna alivyokutana na Martha wakaanzisha mahusiano na Martha akapata ujauzito.Bella akaonyesha mstuko mkubwa kana kwamba hajui chochote akaikunja sura kwa hasira
“Festus wewe ni mtu mbaya sana ! akasema Bella kwa ukali
“Kwa nini ukanifanyia vile.Kitu gani ulikosa kwangu hadi ukaamua kuzaa na huyo kahaba wako?
“Bella ni tamaa tu wakati ule na ndiyo maana nimekuja kwako kukueleza ili uweze kunisamehe jambo hili”
“Festus imetosha.Unajua kabisa kwamba siwezi kukusamehe”
“Kwa nini usinisamehe Bella? Mbona wewe umenikosea mara nyingi tu na nikakusamehe kwanini unashindwa kunisamehe mara hii moja niliyokukosea?
“Kwanza kwa nini unanieleza mambo haya sasa?akauliza Bella “Bella suala hili limevuka mipaka na sasa limekuwa ni suala la familia” “Suala la familia?
“Ndiyo”
“Ukahaba uufanye wewe
halafu liwe ni suala la familia?
“Sikiliza Bella” akasema Festus na kuvuta pumzi
“Jambo hili lilikuwa siri kubwa lakini siyo siri tena kwani tayari waandishi wa habari wamekwisha lifahamu hili jambo na wameanza kulichunguza”
“Kama wamelifahamu mimi nifanye nini?
“Waandishi wa habari hawa naamini watakuwa wanatumiwa na wabaya wangu
kunichafua kisiasa.Nikichafuliwa mimi,ninyi pia mtachafuka hivyo basi nimelazimika kukueleza ukweli kuhusu jambo hili na kukuomba msamaha ili usimame nami katika hili jambo” akasema Festus na Bella akaangua kicheko.
“Bella mimi nawe hatutazamani machoni lakini katika hili naomba tuweke tofauti zetu pembeni na tuungane.Nakuhitaji mno katika jambo hili.Nakuhitaji Bella kuliko wakati wowote.Jambo hili likiwafikia wananchi litakuwa ni doa kubwa sana kwangu na kwenu pia” akasema Festus
“Festus usitake kutuingiza na sisi katika madhambi yako.Jambo hili halituhusu sisi.Ulifanya mambo yako kwa kujificha gizani,yamekufika shingoni na unataka mimi na familia yangu tusimame nawe.Naomba uniondolee upuuzi wako.Simama wewe mwenywe katika jambo hili” akasema Bella “Bella please !
“Festus tafadhali naomba uondoke chumbani kwangu nahitaji kupumzika.Tafuta
namna ya kulimaliza suala hili wewe mwenyewe.Huoni aibu kuja kunieleza uchafu kama huo halafu unaniomba eti nisimame nawe.Simama pake yako ! akasema Bella kwa ukali “Bella ! akasema Festus “Festus toka chumbani kwangu tafadhali nahitaji kupumzika ! akasema Bella
Festus akainuka na kutoka mle chumbani akiwa amefura hasira
“Haya ndiyo mambo
ambayo sikuyataka.Nilijua tu kuja kwa huyu mwanamke na kumueleza ukweli hatanielewa na badala yake nimejidhalilisha tu.Nimezidi kuyakoroga mambo! Akawaza Festus na kuelekea chumbani kwake akampigia simu
Salvatory
“Mheshimiwa Rais”: akasema Salva
“Salva nimefanya kama ulivyonishauri nimezungumza na mke wangu lakini mambo hayajaenda vizuri” “Nini kimetokea?
“Tumeshindwa
kuelewana.I’m alone in this” akasema Festus
“Dah ! nimekosa maneno ya kusema mheshimiwa Rais.Mkeo alikuwa mtu muhimu sana katika jambo hili.Hakuna namna unayoweza ukamshawishi akakuelewa?
“Salva hakuna haja ya kuendelea kung’ang’ania kuwa naye.Naomba unishauri ninatokaje hapa nilipokwama? Akauliza Festus
“Mheshimiwa Rais usijali hata bila familia yako bado lazima ujitokeze mbele ya umma na uwaeleze kuhusu jambo hili.Kwa namna yoyote ile lazima uwe wa kwanza kulieleza kabla ya hao jamaa hawajalichapisha magazetini.Naamini umenielewa mheshimiwa Rais”
“Nimekuelewa
Salva.Ahsante kwa ushauri” akasema Festus na kuagana na Salva
“Dah ! hili jambo kwa nini limeibuka wakati huu? Nani huyu ambaye anataka kunichafua? Akawaza na kumpigia Gidion Benson mkurugenzi wa habari wa Rais akamtaka waonane mara moja
Baada ya dakika chache Gidion ambaye bado alikuwa ofisini kwake akiendelea na majukumu yake akafika kwa Rais
“Gidion ninataka uandae kipindi kesho asubuhi katika kituo cha luninga ambacho kina watazamaji wengi” akasema Festus na kumpa maelekezo ya namna anavyotaka kipindi hicho kiwe.
Mathew Mulumbi
aliufungua mlango wa chumba ambamo Thomas alikuwa anapatiwa matibabu na daktari aliyeitwa na Zari
“Dr Fred vipi maendeleo
ya huyu jamaa? Akauliza Mathew
“Hali yake bado si nzuri,ameungua sana.Ilikuaje akaungua kiasi hiki?
“Unadhani atachukua muda gani kupona? Akauliza Mathew
“Siwezi kusema chochote kwa sasa hali yake inazidi kubadilika na kuwa mbaya zaidi” akasema Dr Fred
“Nini ushauri wako?
“Nashauri tumpeleke
katika kituo chetu pale makao
makuu tukamuhudumie hapa sina vifaa vya kutosha kutibu majeraha kama haya”akasema DrFred na Mathew akaenda kujadiliana na akina Zari kuhusu kumpeleka Thomas makao makuu ya SNSA.
“Bado siafikiani na wazo la
kumpeleka Thomas SNSA.Hili ni misheni ya siri na tunaotakiwa kuifahamu ni watu wachache sana.Endapo huyu Thomas akipelekwa ofisi kuu SNSA watataka kujua ametokea wapi na nini kimempata.Ushauri wangu ni kumtuma Dr Fred akachukue vifaa vyote anavyovihitaji kwa ajili ya kumuhudumia Thomas aje amuhudumie Thomas akiwa hapa hapa ! akasema Mathew
“Wazo la Mathew lina msingi sana” akasema Ruby.Zari akamuita Dr Fred akamuelekeza akachukue vifaa
na dawa anazohitaji kwa ajili ya kumuhudumia Thomas na arejee mara moja.Mara tu Dr Fred aliporejea katika chumba alimo Thomas akasikika akipiga ukelele wa kuomba msaada akina Mathew wakakimbia na walichokikuta mle ndani kiliwashangaza.Thomas alikuwa amejichoma mkasi katika koo na alikuwa anamwaga damu nyingi
“Amefariki ! akasema Dr
Fred akionekana kutetemeka
“DrFred nini kimetokea? Akauliza Mathew kwa ukali
“Amejichoma na
mkasi.Niliporejea humu ndani baada ya kuitwa na mkurugenzi nimemkuta akiwa
katika hali hii”
“Aaaaggghhh !! Mathew akasema kwa hasira na kupiga
“Hii imetokeaje DrFred? Akauliza Zari
“Hata mimi ninashangaa kwani nilimuacha humu huyu jamaa akiwa katika hali mbaya.Sikuwa na wasiwasi wowote kama angeweza kufanya kitendo kama hiki.Aliponiona nimetoka akachukua mkasi na kujiua” “Yawezekana alijaribu kujifanya hali yake ni mbaya wakati akitafuta nafasi ya kuweza kujitoa uhai” akasema Dr Fred huku mwili ukimtetemeka.Mathew akamfuata na kumshika bega.
“Dr Fred usijilaumu kwa hiki kilichotokea.Hakuna aliyejua kama jambo hili litatokea” akasema Mathew
“Ahsante sana Mathew” akajibu Dr Fred na Mathew akatoka ndani ya kile chumba
Ruby akamfuata
“Mathew haya mambo kwa nini yanakuwa hivi? Tumewapoteza watu wawili muhimu ambao wangeweza kutusaidia kufahamu waliko wenzao” akasema Ruby
“Ruby msikate tamaa.Hiki kilichotokea leo kuwapoteza watu hawa wawili ni ishara kubwa ya watu tunaokabiliana nao ni watu hatari na wamekula kiapo cha kutokutoa siri lakini pamoja na kuwapoteza wote wawili tumefanikiwa kufahamu uwepo wa kundi la Black Mafia.Tumefanikiwa kujua kuwa watu hawa tunaowatafuta ni mtandao unaojihusisha na dawa za kulevya.Hii ni hatua kubwa na tunatakiwa kuanzia hapo.Tukilifahamu vyema kundi hili la Black Mafia tunaweza kujua kwa hapa Tanzania nani kiongozi wake?
“Mathew nina hofu tunavyozidi kuchelewa ndivyo Fabian anavyozidi kuwa hatarini.Masikini Fabian sijui hali yake ikoje huko mahala anakoshikiliwa” akasema Ruby “Ruby usiwe na wasiwasi hata kidogo.Nimekwisha kuahidi na ninarudia tena kukuahidi kwamba tutamuondoa Dr Fabian katika kitanzi hiki”
“I do trust you Mathew but how are we going to help him? Hatuna chochote cha kutusaidia kujua mahala walipo hawa watu ! akasema Ruby
“Ruby naomba uniamini tafadhali.I don’t know how butI promise you we’ll save Dr Fabian” akasema Mathew. “Mathew kadiri tunavyoendelea ndivyo mambo yanavyozidi kuwa magumu zaidi kwetu.Ukuta kati yetu na hawa jamaa unazid kuwa mgumu kuupanda”
“Ruby niamini ninachokwambia kwamba tuko karibu sana.Hata kama kuna ukuta mkubwa kati yetu lakini tutatoboa shimo na tutapita.Usikatishwe tamaa na hawa jamaa waliojitoa uhai.Si kila wakati tutakuwa washindi au kumaliza misheni yetu haraka kuna nyakati tunashindwa na kuna nyakati tunapata ugumu mkubwa hivyo lazima tuwe tayari kukabiliana na hali zote lakini vyovyote itakavyokuwa lazima tutawapata watu hawa” akasema Mathew na kila mmoja akawa kimya akiwaza lake
“Kuna kitu najiuliza Mathew” akasema Ruby “Kitu gani Ruby?
“Wale jamaa walifahamuje kama mmekwenda katika shule alikosoma Naomi
Bambi? Akauliza Ruby.Mathew akakuna kichwa kidogo halafu akasema
“Hata mimi nimekuwa
najiuliza swali hilo bado sijapata majibu”
“Hebu angalia Mathew
katika kila tunalolifanya hawa jaama wanakuwa mbele yetu,wanafahamuje mipango yetu? Akauliza Ruby na ukapita ukimya.Ruby akafungua mlango akachungulia nje kama kuna mtu anakuja halafu akarejea tena ndani
“Mathew do you trust her? Akauliza Ruby
“Nani?
“Zari.Do you trust her?
“Yes I do.Kwa nini unauliza hivyo?
“Nina wasi wasi naye sana”
“Kwa nini Ruby?Kuna kitu chochote amekifanya kinakupa wasiwasi?
“Siwaamini sana hawa viongozi wa
SNSA.Unakumbuka wakati ule wa Devotha.Hawa jamaa kama wameweza kupenyeza mizizi yao ndani ya serikali hawawezi
kushidwa kuingiza mizizi yao SNSA”
“Una maanisha Zari anaweza kuwa anashirikiana nao?
“Ninahisi hivyo na hilo linawezekana.Hebu angalia Mathew kwa nini kila tuna chokifanya hawa jamaa wanakifahamu? Lazima
watakuwa wanapewa taarifa kwa siri”
“Ruby hizo ni hisia tu lakini sidhani kama zina ukweli wowote.Zari nimemfahamu kwa muda mfupi na sina hakika kama
anaweza akafanya jambo kama
hilo”
“Mathew please wake up.Mathew Mulumbi ninayemfahamu mimi hakuwa mtu wa kumuamini mtu haraka namna hii”
“I’m the same Mathew Mulumbi and I do trust her.Ningekwisha fahamu kama angekuwa anashirikiana na hawa jamaa lakini nina uhakika Zari hawezi” “Mathew please naomba
tufanye uchunguzi ili tujiridhishe kama kweli Zari hashirikiani na hawa jamaa
“Unataka tufanye uchunguzi gani Ruby?
“Nataka turudi kule katika ile nyumba na kama jamaa wakituvamia tena basi tutakuwa na uhakika mkubwa kwamba wamepata taarifa tumerejea na hapo tutaanza kumchunguza Zari kila anachokifanya.Lazima kuna mtu anafanya mawasiliano ya siri na hawa watu”
“Ruby tutarejea kule kama ulivyoshauri lakini naomba uniamini kwamba Zari hahusiani na hawa jamaa” akasema Mathew
“Nahitaji kujiridhisha
Mathew.Mume wangu yuko mahabusu lazima nifanye kila niwezalo kumsaidia”
“Tunafanya kila linalowezekana Ruby na ninarudia tena kukuhakikishia kwamba tutamtoa Dr Fabian
na kulisafisha jina lake” akasema Mathew na kumfuata Zari akamueleza kwamba wanataka kurudi katika nyumba yake
“Kule ni hatari sana Mathew.Wale jamaa wanaweza wakarudi kuwatafuta wenzao.Nina uhakika mkubwa kwamba lazima watakuwa wanawatafuta wenzao tuliowateka na kuwaua” akasema Zari
“Zari we have to go back.Kama watakuja itakuwa vyema tutakabiliana nao.Waelekeze makomando kwamba tunarejea na wasogee pale karibu na nyumba yako halafu wajifiche kusubiri kama kutakuwa na jambo lolote” akasema Mathew na maandalizi ya kuondoka yakaanza mara moja.Miili ya wale jamaa waliofariki ikahifadhiwa sehemu kwa ajili ya makomando kuja kuichukua na kwenda kuitupa.
Mtaa anaoishi Zari ulikuwa kimya ni sauti za mbwa tu ndizo zilisikika.Ni eneo ambalo wengi wa wanaoishi ni watu wenye kipato kikubwa.Mita kama mia mbili kutoka geti la nyumba ya Zari kulikuwa na magari mawili yameegeshwa
Gari la Zari lilipofika katika nyumba yake geti likafunguka wakaingia ndani
“Geti limefunguliwa na gari moja limeingia ndani.Nahisi wamerudi” Jamaa mmoja aliyekuwa katika mojawapo ya zile gari mbili akiwa na kiona mbali akitazama katika geti la nyumba ya Zari alitoa taarifa ya kile alichokiona.
“Good job Weed.Sasa tuwaache wapumzike halafu tutawastukiza” akasema mtu aliyekuwa upande wa pili wa simu
Mathew alikuwa wa kwanza kushuka garini akiwa na bastora mkononi na baada ya kujiridhisha kwamba kuna usalama akawaruhusu akina Zari nao wakashuka.Ruby alielekea ndani,Mathew na Zari wakazunguka nyumba yote wakaikagua kama ni salama na baada ya kuridhika kwamba ni salama wakaelekea ndani ambako walipitia kumbu kumbu za kamera kuangalia kama wakati hawapo kuna mtu aliingia mle ndani lakini kamera za siri zilizofungwa kuzunguka nyumba ile hazikuonyesha kama kuna mtu yeyote aliyejaribu kuingia mle ndani
“Kuko salama kabisa hakuna tatizo lolote” akasema Zari
“Sawa nadhani ni wakati wa kwenda kupumzisha vichwa ili tukiamka kesho tupate mawazo mapya wapi pa kuanzia” akasema Mathew,Zari na Ruby kila mmoja akaelekea katika chumba chake kupumzika Mathew akabaki sebuleni akiwa na bastola zake tayari kukabiliana na yeyote ambaye angevamia
“Kwa nini Ruby anahisi Zari anaweza kuwa na mawasiliano na hawa jamaa tunaowatafuta?Nadhani ni hisia zake tu lakini Zari hawezi akashirikiana nao.” Akawaza Mathew na kujaribu kuvuta picha ya Zari
“Zari nimenusurika naye matukio mawili sina hakika kama anaweza kuwa ana mahusiano na hawa jamaa.Katika tukio lile la bomu kule kwa Zawadi Mlola tungeweza kuteketea sote wawili.Kama angekuwa na mahusuano nao wangemueleza kuhusu uwepo wa bomu na katu asigekubali kwenda sehemu ambako anajua anaweza akapoteza maisha.Ngoja niachane na mambo haya nijielekeze katika mipango ya kuwasaka hawa jamaa” akawaza halafu
akazima taa ya sebuleni akachungulia nje kisha akarudi kukaa sofani
“Black Mafia” akasema kwa sauti ndogo
“Hawa ndiyo watu tunaopambana nao.Kwa mujibu wa rafiki yake Zari aliyetupa taarifa za kuhusiana na kundi hili anadai ni kundi ambalo kazi yake ni kufanikisha biashara ya dawa
za kulevya na vile vile kuwalinda viongozi wakuu wa mitandao hiyo.Who is the druglord here in our country? Akajiuliza
“Ili kumfahamu kiongozi wao ni nani hapa nchini kuna ulazima wa kulifahamu kwa undani kundi hili ambalo linatajwa kuwa hatari na linatajwa kama ni jeshi la wauza unga.Wapi nitapata
taarifa zaidi za hawa jamaa?Nikiufahamu mtandao wa kundi ulivyo itakuwa rahisi kumfahamu kiongozi wao hapa nchini” akawaza na kuinuka akaenda kuchungulia nje hakukuwa na mtu akarejea sofani
“Kama ningekuwa na mawasiliano na Nawal naamini angeweza kunisaidia katika jambo hili kwani yeye ana watu wake katika idara mbali mbali za usalama nchini Marekani na angeweza kunisaidia kupata taarifa za kutosha za kundi hili.Sina mawasiliano yake na sijui yuko wapi”akaendelea
kuwaza.Kijiusingizi kilianza kumnyemelea Mathew Mulumbi akaiweka bastola zake kifuani akafumba macho.
Zari akiwa tayari amepitiwa na usingizi akastuka baada ya kusikia simu yake ikiita.Akaichukua na kutazama aliyekuwa anampigia akakuta ni kutoka kwa makomando waliokuwa wameegesha gari lao mbali kidogo na nyumba ile kama walivyokuwa wameelekezwa.
“Gibson” akasema Zari kwa sauti ya uchovu
“Mkurugenzi kuna
tatizo.Gari mbili za polisi ziko nje ya nyumba”
“What?
“Kuna gari mbili za polisi ziko nje ya nyumba na ninawaona wanajadiliana namna ya kuingia ndani na wengine wana silaha”
“Jesus ! akasema Zari na kutupa shuka akatoka mbio akauvamia mlango wa Ruby
akamuamsha.Mathew
akastuka baada ya kusikia mtu akikimbia akaziweka sawa bastola zake
Na mara akatokea Zari akihema kwa kasi
“Kuna nini Zari?
“Mathew kuna
tatizo.Nimejulishwa na
makomando kwamba kuna
magari mawili ya askari polisi yamekuja hapo nje na sasa wanajadiliana kuhusu kuingia ndani”
“They already know I’m here.We need to get out now ! Kuna mlango wowote wa kutokea kwa nyuma?
“Upo mlango lakini lazima kote kutakuwa na askari.Kuna sehemu ambako tunaweza kwenda kujificha please follow me” akasema Zari kisha wakakusanya kila kitu walichokiona cha muhimu wakaelekea chumbani kwake na kubonyeza kidude Fulani katika kabati la nguo ikawaka taa ya bluu halafu akalielekeza jicho lake katika taa ile na mara kabati lile likajigawa sehemu mbili ukatokea uwazi na kuwataka akina Mathew kupita katika uwazi ule akabonyeza kitufe kingine kwa ndani kabati lile likajifunga wakashuka ngazi na kukuta kuna chumba kikubwa na kizuri.Kulikuwa na choo, jiko na vitu vyote muhimu vya kumuwezesha mtu kuishi kule chini bila matatizo
“Chumba hiki ni maalum pale kunapouwa na hatari yoyote.Hakuna anayeweza kuhisi kama kuna chumba mahala hapa.Wataingia watatafuta bila kumpata mtu wataondoka zao” akasema Zari
“Hatuwezi kujificha huku kwa muda mrefu we need to do something ! akasema Mathew
“Ni kwa muda tu halafu tutaondoka” akasema Zari “I have an idea” akasema Ruby na kuchukua simu yake ambayo huitumia kuwasiliana na Rais akampigia
“Ruby unaendeleaje?
“Ninaendelea vyema mheshimiwa Rais.Vipi wanangu wanaendeleaje?
“Wako salama wanaendelea vyema”
“Mheshimiwa Rais nimekupigia kuomba msaada
wako.Niko hapa yumbani kwa Zari lakini kuna gari mbili za askari polisi zimefika hapa nadhani tayari wanafahamu Mathew yuko hapa.Naomba tafadhali tusaidie kuwaondoa askari hawa ili tuweze kuondoka mahala hapa” akasema Ruby
“Mmezingirwa na askari?
“Ndiyo mheshimiwa Rais.Tumezungukwa na askari.Tunahitaji msaada wako” akasema Ruby
“Sawa Ruby nimekuelewa” akasema Rais Festus na kukata simu na bila kupoteza muda
akampigia mkuu wa jeshi la polisi
“Yeremia kuna askari polisi wamezingira nyumba ya mkurugenzi wa SNSA.Naomba tafadhali uwaondoe askari hao haraka sana mahala hapo”
“Sawa mkuu ! akajibu Yeremia mkuu wa jeshi la polisi
Jumba la Zari lilizungukwa na ukuta mkubwa wa matofali na juu yake zikapita nyaya zilizounganishwa na mfumo wa ulinzi hivyo kuwapa ugumu askari polisi kuingia mle ndani.Wakati wakiendelea kujadiliana namna ya kuingia humo ndani mara kiongozi wa kikosi kile cha askari akapokea taarifa ya kuwataka waondoke haraka sana eneo lile.Askari wote wakapigwa na butwaa baada ya kuamriwa kurejea katika magari yao na kuondoka.Zari akapigiwa simu na makomando akajulishwa kwamba askari tayari wameondoka.
Kitendo cha askari kuondoka ghafla kiliwashangaza sana wale jamaa waliokuwa katika magari mawili wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea yumbani kwa Zari wakadhani labda kuna taarifa mpya wameipata hivyo nao wakalazimika kuwasha magari yao kuwafuata askari wale walioondoka kwa kasi eneo lile
“Ahsante Ruby.Sasa tuondoke zetu.Tunarejea kule shambani kwa makomando ambako ni salama zaidi.Hapa si salama tena” akasema Mathew kisha wakatoka na kupakia vitu muhimu katika gari wakaondoka. *************
Ni asubuhi nyingine.Kitu cha kwanza alichokifanya Rais Festus baada ya kutoka mazoezini ni kupitia magazeti yote ya siku na hakukuwa na gazeti hata moja lililoandika habari yake.
“Kama alivyoshauri Salva natakiwa kuwawahi kabla habari hii haijatoka gazetini.Najua nitajidhalilisha lakini ni vyema wananchi wakaisikia taarifa hii kutoka kwangu mimi mwenyewe kuliko kuipata kupitia magazeti” akawaza na kumpigia simu mkurugenzi wake wa habari kumuuliza maandalizi ya kipindi yanavyokwenda akajulishwa maandalizi yalikuwa yanaendelea vizuri.
“Wapenzi watazamaji wa kipindi cha Mchaka Mchaka wa asubuhi leo tuna kipindi maalum kabisa.Kama mnavyoona tumeondoka studio na tumekuja hapa ikulu.Kwa mara ya kwanza leo tangu kipindi hiki kianzishwe tutakuwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kama mgeni wetu.Tutapata kifungua kinywa pamoja naye huku tukizungumza mambo mbalimbali kuhusu maisha na kazi zake kwa ujumla.Karibu ndugu mtazamaji ufuatilie mahojiano yetu na Rais asubuhi hii.Ni kipindi cha kwanza kabisa kufanya mahojiano na Rais ikulu kuhusu maisha na kazi zake”
Beatrice Ngaga mtangazaji wa kipindi maarufu cha Mchaka Mchaka aliwajulisha watazamani wa kipindi hicho kuhusu mahojiano na Rais Festus Mayungulu.
“Mpenzi mtazamaji kama nilivyokueleza awali kwamba tunayemsubiri kwa sasa ni mheshimiwa Rais aweze kuwasili na kipindi chetu kianze.Kuna mambo mengi ambayo tutazungumza na mheshimiwa Rais na kama muda utaruhusu basi tutachukua maswali machache kutoka kwa watazamaji na kumuuliza Rais.Narudia tena kukusisitizia kwamba hiki ni kipindi cha kipekee kabisa na hakijawahi kutokea hivyo usiende sehemu yoyote,mjulishe na mwenzako aliye nyumbani ofisini au kokote aweze kutazama au
kusikiliza kipindi cha mchakamchaka wa asubuhi” Beatrice mtangazaji mwenye makeke mengi akaendelea kuwajulisha watazamaji kuhusu kile kinachoendelea
Hatimaye mgeni waliyekuwa wanamsubiri Rais Festus akawasili na kukaribishwa katika kipindi.
“Wapenzi watazamaji mgeni wetu wa leo kama nilivyowajulisha ni mheshmiwa Rais na tayari amekwisha fika hivyo kipindi chetu kinakwenda kuanza rasmi” akasema Beatrice na mazungumzo yakaanza
“Nilitegemea ungekuja na mama Bella” akasema Beatrice
“Bella alitarajia naye kuwepo hapa lakini ameamka leo hajisikii vyema hivyo anaendelea kupumzika.Naamini kitaandaliwa kipindi kingine na yeye atashiriki” akasema Rais Festus
Bella akiwa chumbani kwake alijulishwa na mmoja wa wasaidizi wake kwamba Rais alikuwa katika kipindi cha moja kwa moja cha Mchaka Mchaka ambacho kilirushwa kutokea pale ikulu.Haraka haraka akawasha luninga na kuanza kutazama kile kilichokuwa kinaendelea.
“Mbona sijajulishwa uwepo wa kipindi hiki? Akajiuliza na kuchukua simu akampigia mkurugenzi wa mawasiliano wa Rais “Shikamoo mama”
“Gidion mbona
hujanijulisha kuhusu uwepo
wa kipindi hiki kinachoendelea hivi sasa? Akauliza Bella
“Mama hayo yalikuwa ni maagizo ya rais mwenyewe”
“Kuna jambo gani ambalo linaongelewa katika kipindi hicho?
“Ni mahojiano ya kawaida kuhusu maisha ya kawaida ya Rais pamoja na kazi zake za kila siku”
“Gidion siku nyingine kama kuna jambo la namna hii lazima na mimi nijulishwe.Mimi ndiye mke wa Rais ninapaswa kujua kila kinachoendelea hapa.Umenielewa Gidion? “Nimekuelewa mama”
“Good.Naomba hii
isijirudie tena ! akasema kwa ukali Bella na kukata simu na kuendelea kufuatilia kipindi kile.
Kipindi kilikuwa kizuri na mambo mengi yalizungumzwa.Rais Festus na watangazaji walizungumza kwa urafiki mkubwa.Watangazaji walikuwa huru kuuliza swali lolote walilotaka na Rais akalitolea majibu.
“Mheshimiwa Rais
kimekuwa ni kipindi kizuri sana lakini muda wetu umekuwa mchache naamini siku nyingine tutapanga muda mrefu zaidi ili tuweze kuzungumza kwa undani mambo mengi.Kabla hatujahitimisha mazungumzo yetu kuna lolote ambalo unataka kuwaeleza watanzania? Akauliza Beatrice “Ndiyo lipo” akajbu Festus
“Karibu mheshimiwa Rais” “Kuna jambo ambalo watanzania hawalifahamu na leo ninataka kuliweka wazi kwani mimi pia ni binadamu na kuna nyakati huwa ninakosea”
“Anataka kusema nini huyu? Bella ambaye bado aliendelea kufuatilia mazungumzo yale akajiuliza
“Narudia tena sisi kama binadamu si wakamilifu,tuna mapungufu yetu na hata mimi pia nina mapungufu yangu na ninataka kutumia fursa hii kukiri madhaifu yangu na kupitia mimi wengine wanaweza wakajifunza” akasema Festus na kunyamaza kidogo.
“Mimi ni baba wa watoto watatu lakini kupitia kipindi hiki ninataka kuweka wazi
kwamba nina mtoto wa nje pia”
Bella alihisi kama nyundo nzito imetua kichwani kwake baada ya kuisikia kauli ile ya Rais.
“Oh no ! akasema Bella kwa masikitiko
“Niliwahi kuwa na mahusiano ya siri na mwanamke mmoja ambaye sintapenda kumtaja hapa na katika mahusiano hayo tukapata mtoto wa kiume.Kwa kuhofia aibu nililificha jambo hili na sikutaka familia yangu walifahamu.Nilikosea sana kuuficha ukweli huu” akasema Festus
Wakati Festus akiendelea kujieleza kuhusiana na mtoto wake wa nje ya ndoa simu ya Bella ikaita alikuwa ni Kasiano “Mama Bella nini kinaendelea? Nimefuatilia mazungumzo ya Rais kama ulivyonitaka na nimestushwa sana na alichokifanya kukiri kwamba ana mtoto wa nje ya ndoa.Hivi sasa habari inaandaliwa ili itoke katka gazeti la kesho ! oh my God ! akasema Kasiano
“Kasian simamisha kila kitu.Hakuna habari tena hapa kwani kisha maliza kila kitu.He’s so smart lakini asidhani ameshinda kwani vita bado vinaendelea.Amelikwepa kombora hili lakini hataweza kulikwepa kombora linalokuja” akasema Bella
“Nini kinafuata tena mama Bella? Akauliza Kasiano
“Nitakutumia mawasiliano ya katibu mkuu wa chama chake atatumiwa zile picha nilizokutumia Festus akiwa na Zandile. Mzee huyo aambiwe kwamba picha hizo na video havitasambazwa endapo Festus atakubaliana na matakwa yenu.Wanamtegemea sana Festus katika uchaguzi ujao kwani anakubalika sana na watu wengi hivyo kwa namna yoyote hawatakubali achafuke na nina uhakika watamshawishi akubaliane na matakwa yenu.Hiyo ndiyo namna ya kulitumia kombora la pili.Kama nalo likishindwa kufanya maangamizi tutakwenda na kombora la tatu ambalo ni kubwa zaidi” akasema Bella
“Sawa mama tutafanya hivyo” akajibu Kasiano
“Vijana wa mjini wanasema mkeka umechanika na kweli huu mkeka umechanika.Amekwepa kombora la kwanza lakini hajui kama kuna kombora kubwa zaidi linakuja” akawaza
Bella
************
Habari ya Rais Festus Mayungulu kukiri kuwa na mtoto wa nje ya ndoa ilizua mjadala mkubwa sana na kuwafanya watu wasahau tukio lingine kubwa la Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhuska katika mauaji ya mkuu wa gereza la Kimondo Arusha akishirikiana naMathew Mulumbi ambaye anaendelea kutafutwa na jeshi la polisi.
Katika kambi ya mazoezi ya makomando wa SNSA
,Mathew na Ruby walijulishwa na Zari aliyekuwa amekwenda ofisini kutazama mambo yanavyokwenda,watazame luninga Rais alikuwa anahojiwa.Wakati mahojiano yale yakiendelea yalipita maandishi yakisomeka Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo afikishwa mahakamani kwa kuhusika katika mauaji.Ruby alimwaga machozi mengi baada ya kuisoma taarifa ile
“Ruby naomba uniamini kwamba tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunamtoa DrFabian katika jambo hili na kulisafisha jina lake.Nina uhakika mkubwa tumekaribia sana”
“Mathew tumechelewa na tayari Fabian amefikishwa mahakamani.Itakuwa vigumu sana kuweza kumuondoa katika hili jambo.Hawa watu wana nguvu kubwa na wanaweza wakafanya lolote walitakalo”
“Niamini nikwambialo Ruby kwamba japo
amefikishwa mahakamani
lakini kesi hii ni yangu mimi na hakuna kitakachoendelea hadi pale nitakapopatikana. Ni sisi kujitahidi kwa kadiri tuwezayo kuhakikisha tunawapata hawa watu haraka”
“How? Akauliza Ruby
“Mathew unatafutwa na polisi na oh Jesus ! akasema Ruby kwa masikitiko.
“Ruby please toka nimekufahamu sijawahi kukuona ukikata tamaa.Naomba uwe na uhakika kwamba tutalimaliza jambo hili.Usikate tamaa wakati huu” akasema Mathew
“Nitashindwaje kukata tamaa Mathew wakati mume wangu kafikishwa mahakamani na watoto wangu sijui wako katika hali gani? Akasema Ruby na kuanza kulia
“Ruby kulia hakutasaidia kutatua jambo hili”
“Mathew please let me cry ! akasema Ruby na Mathew akatoka akamuacha peke yake akamfuata Kendrick akamtaka waondoke wakaingia garini na kuondoka bila kumueleza wanakoelekea
Profesa Simoni Themba au kwa jina maarufu Simba akiwa
ofisini kwake katika ofisi kuu ya chama ambacho anakiongoza Rais Festus Mayungulu akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu “Hallo” akasema Simon
“Habari yako mheshimiwa katibu mkuu”
“Nzuri.Nazungumza na nani? Akauliza Simon
“Mheshimiwa katibu mkuu kuna ujumbe nimekutumia katika barua pepe yako naomba kufungua uusome tafadhali halafu nitawasiliana nawe ndani ya muda mfupi”
“Wewe ni nani? Akauliza mzee Simba lakini simu ilikatwa
“Sipendi sana watu wa namna hii.Kwanza ametoa wapi namba zangu?Wahuni kama hawa wananifanya nibadili namba zangu mara kwa mara” akawaza mzee Simba akiwa amekasirika.
“Anasema amenitumia
kitu katika barua pepe ngoja niangalie” akawaza Profesa Simon na kuifungua kompyuta yake akakuta kweli kuna barua pepe imetumwa.Akaifungua na kukuta kuna maelezo
“Fungua picha hizo nilizokuambatanishia zitazame halafu tutazungumza”
Profesa Simon
akazifungua picha zile na kujikuta akitetemeka mwili
“Festus ?!! Profesa Simon akahamaki na kuvua miwani yake akachukua kitambaa akafuta macho
“Yawezekana macho yangu yananidanganya.Ni kweli hiki ninachokiona au? Akajiuliza Profesa Simon akavaa tena miwani yake halafu akaenda kuufunga mlango wake na kurejea tena katika kompyuta yake akaanza kuzitazama zile picha
“Mungu wangu ! akasema na kushusha pumzi
“Nimestuka sana.Huyu ni Rais Festus.Oh my God ! akawaza Profesa Simon akizishuhudia picha za Festus akiwa faragha na mwanamke mmoja mrembo
Wakati akiendelea kuzitazama picha zile simu yake ikapigwa alikuwa ni Yule mtu aliyempigia simu awali
“Profesa umeupata ule ujumbe? Akauliza Yule jamaa “Wewe ni nani lakini?
“Nataka ujibu mzee umeupata ujumbe niliokutumia?
“Unajua athari ya hiki unachokifanya wewe? Akauliza Profesa Simon
“Ndiyo maana
nimekutumia wewe mzee ili uwe wa kwanza kuzitazama picha hizo.Naamini umekwisha mtambua mtu huyo kwenye picha na hizo ni chache ninazo nyingine na video pia.Huyo ni kiongozi wa chama chenu na ambaye mnategemea apeperushe bendera ya chama chenu katika uchaguzi mkuu ujao.Unadhani kuna mtu anaweza akamchagua mtu wa namna hii pindi picha hizi zikifika kwa wananchi? Akauliza Yule jamaa
“Nini unakitaka wewe mtu? Unadhani utatutisha kwa picha kama hizi za kutengeneza?
“Hizo si picha za kutengenza mzee.Ni picha halisi na hata ukimuuliza
kiongozi wako atakiri ni kweli”
“Nini unakitaka?
“Ninataka kusambaza
picha hizi lakini kabla sijasambaza nataka kufanya mazungumzo na Rais kama anaweza akakubaliana nasi basi hii itabaki siri na hakuna atakayefahamu chochote” “Kwa nini usimtafute wewe mwenyewe hadi upitie kwangu?
“Mnamtegemea yeye
awavushe katika uchaguzi hivyo kama mnataka mgombea wenu abaki salama zungumza naye na akubali matakwa yangu kama asipokubali basi kabla jua halijazama siku ya leo picha zake zitasambaa na litakuwa ni anguko lake kubwa na chama chenu pia.Nitawasiliana nawe baada
ya saa mbili kutoka sasa na kama bado hamjachukua hatua zozote basi picha na video zitasambaa mtandaoni” akasema Yule jamaa na kukata simu
“Festus ! Festus ! Festus ! nini hiki unakifanya? Akasema Profesa Simon na kugonga meza kwa hasira
“Ni saa chache zilizopita Festus amejitokeza na kukiri kuwa na mtoto wa nje ya ndoa.Mjadala mkubwa tayari umeibuka na wapinzani wetu wanaitumia nafasi hiyo kuonyesha kwamba hafai kuongoza.Kabla hiyo haijapoa linaibuka tena hili la picha chafu.Huyu Festus amekumbwa na shetani gani? Ni mtu ambaye sote tuliamini ni msafi na hana doa lakini kumbe nyuma ya pazia ni mtu mwenye uchafu mwingi.Mambo kama haya hayakupaswa kufanywa na mtu kama yeye.Hayakupaswa kufanywa na kiongozi mkuu wa nchi.Hii ni aibu na ni anguko kwa chama chetu kama picha hizi zikivuja” akawaza Profesa Simon
“Hapana ngoja nimfuate
sasa hivi.Hili jambo ni zito mno.Haliishii tu kwa Rais linagusa hadi uhai wa chama” akawaza Profesa Simon huku akiipakia kompyuta yake katika mkoba akachukua simu na kumpigia Rais Festus
“Mzee Simba” akasema
Festus
“Festus uko wapi?
“Niko ikulu !
“Usitoke tafadhali ninakuja hapo sasa hivi” akasema Profesa Simon
“Kuna nini mzee Simba? “Tafadhali mwenyekiti ninakuja hapo sasa hivi kuonana nawe.Kama una ratiba yoyote ya kuonana na mtu au kwenda mahala ahirisha tafadhali hadi utakapoonana na mimi” akasema Profesa Simba na kuingia katika gari akamuelekeza dereva ampeleke Ikulu
“Karibu mzee Simba” akasema Festus baada ya profesa Simba kuwasili ikulu
“Ahsante sana mwenyekiti” akasema Profesa Simon na kumtazama Festus kwa mshangao “Kuna nini mzee Simba?
“Mwenyekiti naomba
tukae faragha kidogo kuna kitu cha muhimu mno ambacho nataka tuzungumze” akasema Profesa Simba na Rais Festus akampeleka katika chumba cha mazungumzo ya faragha “Kuna nini mzee Simba?
“Festus sitaki kuchukua muda wako mwingi nitajielekeza moja kwa moja katika suala la msingi.Kufuatia yale uliyoyatamka katika kipindi cha mchakamchaka asubuhi ya leo,huko mtaani kumekuwa na mjadala mkubwa sana”
“Lakini mzee
nilichokizungumza ni ukweli mtupu”
“Nakubaliana nawe
kwamba jambo ulililolifanya ni zuri na japo wapinzani wetu wanataka kuligeuza kukuchafua kwamba hufai uongozi lakini kwa kiasi kikubwa wananchi walio wengi wanakuunga mkono kwa ulichokifanya kusema ukweli” akasema Profesa Simba “Ahsante kwa hilo”
“Mwenyekiti hilo limepita tuwaache watu wajadili lakini kuna lingine kubwa zaidi” akasema na kuufungua mkoba wake akaitoa kompyuta akaikunjua halafu akafungua katika sehemu ya kuhifadhia picha akamtaka Rais Festus asogee atazame.Mara tu alipozitazama zile picha kalamu aliyokuwa ameishika mkononi ikaanguka.Midomo ilimtetemeka akashindwa kuzungumza.
“Mwenyekiti” akaita Profesa Simon
“Umezipata wapi hizi picha? Akauliza Festus huku sauti ikiwa na kitetemeshi
“Nimepigiwa simu na mtu akaniambia kwamba amenitumia faili katika anuani yangu ya barua pepe akanitaka nilifungue na nilipolifungua nikakutana na picha hizi.Nataka kufahamu je picha hizi ni za kweli au ni za kutengeneza? Akauliza Profesa Simon lakini Festus hakuweza kujibu
“Naona ninakaribia kupatwa na uchizi.Siamini hiki ninachokiona.Hizi picha wamezipata wapi?Kitu gani kinaendelea jamani? Ni nani hawa wanaotaka kuniharibia namna hii? Akajiuliza
“Festus ! akaita Profesa
Simon kwa sauti ya juu “Nataka unithibitishie kuhusu hizi picha ni halisi au ni za kutengeneza?
“Sifahamu mzee Simba picha hizi zime…oh ! Dah ! akasema Festus na kushika kiuno.
“Kwa hiyo unakiri hizi ni picha halisi?
“Ndiyo ni picha halisi mzee”
“Bwana wa majeshi ! akasema Profesa Simon na kumtazama Festus
“Kwa nini Festus? “Sikiliza mzee Simba sifahamu picha hizi zimepigwaje lakini naamini ni mpango wa wabaya wangu kutaka kunichafua.Walianza na suala la kuzaa njeya ndoa lakini nikawawahi.Bado haitoshi wameamua kuja na picha hizi Dah !
wamenimaliza” akasema Festus
“Festus hili suala ni zito sana.Mimi mwenyewe nusura nianguke nipoteze fahamu baada ya kuziona picha hizi.Hii ni kashfa kubwa mno na haitaishia kwako tu bali itatugharimu hata chama na ndiyo maana niko hapa.Nafahamu hizi ni njama chafu lakini lazima tukabiliane nazo”akasema Profesa Simon
“Mzee Simba akili yangu imesimama na ninashindwa nini cha kufanya !
“Sikiliza Festus huyu jamaa aliyenitumia picha hizi anataka kuzugumza nawe ili muweze kufanya makubaliano na kama mkielewana basi
jambo hili litabaki kuwa siri hakuna
atakayejua.Ninakushauri msikilize anataka nini na kama kuna uwezekano wa kumpatia anachokitaka mpatie ili jambo hili limalizike.Ninazo namba zake hapa” akasema Profesa Simon na kupiga zile namba simu ikaita
“Hallow katibu”akasema yulejamaa upande wa pili
“Nataka uzungumze na
Rais na useme kile unachokihitaji kutoka kwake ! akasema profesa Simon
“Mheshimiwa Rais!
Akasema Yule jamaa
“Shetani mkubwa wewe ! akasema kwa ukali Rais Festus
“Festus ..! akaita Profesa Simon na kumfanyia ishara atulize jazba
“Nini unakitaka kwangu? Akauliza Rais Festus
“Mheshimiwa Rais naanimi umekwisha ziona picha na katibu mkuu amekwisha kupa maelezo.Sitaki kujitambulisha mimi nani lakini nataka tu ufahamu kwamba ninazo picha nyingi na video pia ukiwa faragha na mrembo Zandile Wepener.Nina kusudia kuzisambaza katika mitandao
ya kijamii lakini sintafanya hivyo kama mimi nawe tutafikia makubaliano” “Nini unakitaka?
“Nataka kitu kidogo sana.Namtaka Mathew Mulumbi ! akasema Yule jamaa
“Mheshimiwa Rais ninamtaka Mathew Mulumbi
kabla ya saa kumi alasiri ya leo na kama usipotimiza hilo basi kufika saa kumi na mbili za jioni picha hizo unazoziaona na nyingine nyingi zitasambaa katika mitandao yote ya kijamii.Nitakupigia simu kupitia katibu mkuu wako baada ya saa mbili kutoka saa ili kujua kama umetekeleza maagizo yangu ! akasema Yule jamaa na kukata simu.Festus akahisi miguu inaisha nguvu akaketi kitini.
Profesa Simon na Rais Festus
walijikuta wakiwa kimya kila mmoja akimtazama mwenzake.Festus alihisi miguu ikimtetemeka .Alistushwa mno kwa kile alichokisikia kutoka kwa katibu mkuu
“Mwenyekiti” akaita profesa Simon lakini Rais Festus hakusikia.Akili yake ilikuwa mbali
“Mwenyekiti ! akaita Profesa Simon lakini bado hakusikika akalazimika kugonga meza ndipo Rais Festus alipoinua kichwa
“Samahani mzee Simba nilikuwa mbali mno kimawazo.Nimechanganyikiwa mzee wangu sijui nifanye nini”
“Mwenyekiti huu si muda wa kuchanganyikiwa wala kuhamishia akili yako sehemu nyingine.Ni muda wa kutumia akili yako yote katika suala hili.Unatakiwa ujielekeze katika kutafuta suluhu ya hili jambo lililojitokeza” akasema Profesa Simba.Ukapita ukimya wakaendelea kutazamana
“Mwenyekiti ! akaita tena profesa Simon na Festus akainua kichwa akamtazama
“Naomba unieleze
mwenyekiti wangu ilikuaje ukafanya kitu kama hiki?Hukujua madhara yake?Mambo kama haya yanafanywa na vijana wadogo na si mtu mkubwa kama wewe.Wewe ni kiongozi wa nchi.Nashindwa hata niseme nini.Hii ni aibu kubwa” akasema Profesa Simon akiendelea kumtazama Rais Festus
“Hii ni aibu mwenyekiti wangu tena ni aibu kubwa mno.Ni kashfa kubwa hii ambayo haijawahi kutokea toka nchi hii imeumbwa.Tumezoea kusikia zinavuja picha za wasanii na watu wengine wenye majina lakini haijawahi kutokea kwa kiongozi mkubwa wa nchi akakumbwa na kashfa kama hii.Mwenyekiti usinione nimekuwa mkali,ni kwa sababu jambo hili linakwenda kukizamisha chama chetu.Nataka tutafute suluhu ya jambo hili kabla wapinzani wetu hawajalipata.Wakilipata tumekwisha! Jambo hili licha ya kuleta athari kwa chama lakini pia litaibomoa familia yako.Unadhani nini kitatokea mkeo na watoto wakiziona picha kama hizi? Akauliza Profesa Simon
“Mzee Simba nashindwa niseme nini.Hili jambo limenichanganya mno na sikulitegemea kabisa. Dah ! akasema Festus na kuinamisha kichwa
“Festus nieleze ukweli niko hapa kwa ajili ya kukusikiliza na kwa pamoja tutatafuta suluhu ya hili jambo” akasema Profesa Simon
“Huyo mwanamke
uliyemuona pichani anaitwa Zandile Wepener nina mahusiano naye”akasema Festus na kunyamaza tena
“Nimekuwa na mahusiano
naye ya siri kwa muda sasa” “Lakini mwenyekiti hukujua kama jambo hilo
linaweza likavuja na kukuletea matatizo?Hukuogopa kama mkeo angeweza kufahamu jambo hilo?
“Mzee Simba umekuwa
mlezi wangu katika siasa kwa miaka mingi naomba nikueleze ukweli.Mimi na mke wangu kwa sasa hatuna maelewano mazuri japo kwa nje tunaonekana kama ni watu wenye kupendana lakini ndani tunaishi kama Paka na Panya.Sitaki kuingia kwa undani zaidi katika suala hilo lakini ni kutokana na matatizo yaliyo katika ndoa yangu ndiyo maana nikajikuta nikiingia katika mahusiano na Zandile na nimefanya jambo hilo kuwa siri kubwa sielewi nani kapiga picha hizi na amepigaje”akasema Rais Festus
“Mwenyekiti hukupaswa
kufanya hivi ulivyofanya hata kama wewe na mkeo mna mgogoro,ungesubiri hadi pale utakapomaliza muda wako wa urais.Kama chama tunakutegemea sana Festus katika uchaguzi ujao na wewe unalifahamu hilo lakini ni nani ambaye atakuwa tayari kumuweka madarakani Rais mwenye tabia za kupenda wanawake na hadi kufikia hatua ya kupigwa picha na makaha….”
“Enough !! akasema Rais Festus na kugonga meza meza kwa hasira
“Kama umekuja hapa kuzungumza naomba
tuzungumze lakini sitaki na sintavumilia ukiendelea kunikashifu ! Hapa unazungumza na Rais wa Tanzania !akasema kwa ukali Rais Festus na kutazamana na profesa Simon
“Festus samahani
nilikosea nikajisahau kama niko ikulu ninazungumza na Rais.Nisamehe kwa hilo lakini nimefikia hatua hii kutokana na uzito wa hili jambo.Mimi
ninalitazama suala hili kwa mtazamo wa kichama zaidi.Festus wewe ni mtu ambaye tunakutegemea mno kubeba bendera yetu na kutuvusha katika uchaguzi mkuu ujao na hata wapinzani wetu wanakuogopa lakini kwa haya mambo mawili ambayo yamejitokeza kwanza ni lile la kuzaa nje ya ndoa na pili ni hili la picha hizi na huyu mrembo tunawapa wapinzani wetu kitu cha kusema kama ambavyo tayari wamekwisha anza kuzungumza kuhusu lile suala la kuzaa nje ya ndoa wakilipata na hili lingine watatumaliza” akasema Profesa Simon
“Lakini mzee Simba haya ni maisha yangu binafsi.Mimi ni mwanadamu kama wengine japo………..”
“Festus samahani kwa kukukatisha ! akasema Profesa
Simon
“Wewe ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ! Hadhi yako inakufanya uwe tofauti na sisi.Wewe ni kiongozi wetu,baba yetu,watu
zaidi ya milioni sitini tunakutanguliza mbele,tumeiweka nchi yetu mabegani mwako hivyo wewe ni mtu wa tofauti kabisa na sisi.Unapoingia katika jumba hili tukufu sahau kuhusu maisha ya kawaida kama sisi.Kazi inayokuleta hapa ni moja tu kuwatumikia wananchi ! akasema profesa Simon
“Nimechoka na hayo maneno yako mzee
Simba,pamoja na kazi zangu za urais lakini pia nina familia,ninatakiwa kuwa na muda nao,ninatakiwa kuwa na muda wa kupumzika, ninahitaji pia faragha kama wanadamu wengine msitake kuhalalisha kwamba Rais hana maisha binafsi ! akasema Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais tutoke katika upande huo tuje katika hili lililoko mezani”akasema mzee Simba
“Ndiyo maana nikasema
kwamba haya ni maisha yangu binafsi”
“Hiyo si kauli ya kuzungumza mwenyekiti wangu.Mambo haya yamekwisha tokea na kitu cha msingi ni kujaribu kutafuta namna ya kutoka hapa tulipokwama na twende mbele.Mimi kama nilivyokueleza kwamba ninalitazama jambo hili kwa jicho la kichama.Tunataka mtu ambaye tutampa bendera yetu aipeperushe awe ni msafi asiye na makondokando lakini wewe tayari umekwisha anza kusemwa semwa .Hili tu la kuzaa nje ya ndoa tayari limekwisha haribu taswira yako kwani Rais ni mtu ambaye anapaswa kuwa mfano kuanzia ndani ya familia yake.Ukianza kusemwa semwa vibaya huko nje ujue kwamba kinasemwa pia chama ndiyo maana niko hapa kuhakikisha kwamba inatafutwa njia ya haraka ya kulimaliza hili suala lisifike kwa wananchi.Nakushauri kama kuna kitu hawa jamaa wenye hizi picha wanakitaka na kiko ndani ya uwezo wako wape tafadhali jambo hili limalizike na maisha yaendelee” akasema profesa Simon.Rais Festus akachukua dakika moja akitafakari halafu akasema
“Yule jamaa aliyekutumia hizi picha anataka nimkabidhi kwao Mathew Mulumbi”
“Mathew Mulumbi?Who is he?
“Humfahamu Mathew Mulumbi?
“Ni nani huyo mtu? Simfahamu”
“Mathew ni jasusi ambaye ameyatoa maisha yake katika kupambana na magenge ya wahalifu na magaidi hapa nchini”
“Unafahamu mahala alipo huyo Mathew? Kama unafahamu mahala alipo mkabidhi kwao ili jambo hili liishe mheshimiwa Rais.Mimi nilidhani labda wanataka kitu kikubwa sana kumbe wanamtaka mtu mmoja tu mkabidhi kwao mwenyekiti jambo hili limalizike mara moja na amani irejee”akasema Profesa Simon
“It’s not that simple ! akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
usilifanye jambo hili kuwa gumu.Hata ukilipeleka kwa washauri wako wote watakushauri kama ninavyokushauri mimi kwamba wape hao jamaa hicho wanachokitaka na wewe uendelee kuwa na amani.Kuna watanzania zaidi ya milioni hamsini tunakaribia milioni sitini hivyo basi ukimtoa mtu mmoja kwa ajili ya kuhakikisha unakuwa salama hakuna tatizo.Tunachoangalia hapa ni salama yako wewe na chama pia.Ni goli moja tu unalotakiwa kulifunga mheshimiwa Rais na mpra utamalizika tukiwa na ushindi mnono” akasema profesa Simon
“Mzee Simba jambo hili si rahisi kama unavyolitazama wewe.Mathew Mulumbi ni mtu muhimu sana kwa nchi hi” akasema Festus na profesa Simon akamtazama kwa mshangao
“Kuna kundi fulani la watu ambao wanafanya mambo ya kihalifu hapa nchini.Wanaua watu,wanapandikizia watu kesi hasa wale ambao wanawafuatilia kuwachunguza au ambao wanafahamu mambo yao.Umesikia kilichomtokea Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo”
“Ndiyo ni kitu cha kushangaza sana”akajibu mzee
Simba
“Basi ile ni kazi ya kikundi hicho.Dr Fabian na Mathew walikuwa wanashirikiana katika kukichunguza kikundi hicho cha hao wahalifu na ndipo yakawafika haya yaliyowafika.Walipandikiziwa kesi mbaya ya dawa za kulevya na mauaji.Wewe unamfahamu vyema mzee Fabian ni mtu muadilifu na hawezi akashiriki katika mambo machafu kama hayo anayotuhumiwa nayo na leo hii amefikishwa mahakamani hanakosa lolote Yule mzee lakini yote haya yamewezekana kwa sababu ya nguvu ya hawa jamaa.Ninafahamu walichokuwa wanakifanya Mathew na Dr Fabian hivyo sikuwa tayari kuwaacha wakapotelee gerezani ikanilazimu kufanya mpango wa kumteka Mathew Mulumbi”
“You did what ?!! akauliza Profesa Simon
“Umenisikia vizuri mzee Simba,nilitengeneza mpango wa kumtorosha Mathew Mulumbi ili aweze kuendelea na zoezi lake la kuwasaka hao jamaa.Lengo la kuwatengenezea Mathew na Dr Fabian kesi ile mbaya ya dawa za kulevya na mauaji ni kwa ajili ya kuwaondoa katika ramani kwani tayari walikwisha anza kuwa na mwanga kuhusu watu hao hivyo basi nikatengeneza mpango ule wa kumtorosha Mathew na hivi sasa anaendelea na zoezi la kuwasaka hao jamaa”
“Mheshimiwa rais
ninatamani niseme kitu lakini ninaogopa kwani hapa niko katika jengo tukufu ila naomba utambue kwamba kile kilichofanyika ni uhalifu na wewe umeshiriki pia.Askari
polisi wetu wamemwaga damu
yao katika tukio lile”
“Nalifahamu hilo mzee Simba na sikuwa mjinga kukubali jambo lile lifanyike kama halina manufaa kwa nchi.Hawa watu ninaowazungumzia ni watu wabaya sana na hatari kwa usalama wa nchi” akasema Rais Festus halafu ukapita ukimya
“Tayari wanafahamu nimehusika katika kumtorosha Mathew Mulumbi na ndiyo maana wameyaelekeza mashambulizi kwangu.Wanayachunguza
maisha yangu na kutafuta
mambo ambayo wanaweza
wakayatumia ili kunishinikiza nimtoe kafara Mathew Mulumbi.Mzee Simba huu ni mtandao mpana mno unaowahusisha hadi watu wangu wa karibu”akanyamaza akainamisha kichwa kwa muda kisha akasema
“Jana jioni nilipigiwa simu na mwanamke niliyezaa naye akanijulisha kwamba alifuatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni waandishi wa habari wakamuhoji kuhusu mahusiano yetu na mtoto.Walitaka walitumie jambo hilo kunichafua ndiyo maana nikawahi kulisema mimi mwenyewe kabla yao.Mwanzoni nilidhani ni wabaya wangu wa siasa ndiyo wanaotaka kunichafua lakini suala hili la leo la hizi picha limenifumbua macho kuwa kumbe niko katika mapambano na lile genge la wahalifu ambao Mathew anawasaka.Wanataka kutumia picha hizi ili wanifumbe mdomo na niwakabidhi Mathew Mulumbi na pindi nikiwakabidhi Mathew basi vita hii itakuwa imekwisha kwani hakuna mwingine ambaye ataendelea kuwatafuta hawa jamaa.Nikiwakabidhi Mathew Mulumbi kama wanavyotaka nitakuwa nimeinua mikono na kukubali kushindwa na mimi hata siku moja sijawahi kukubali kushindwa mzee Simba” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais mpaka hapa suala hili ilipofika lazima ukubali kushindwa.Huwezi kushinda katika jambo hili.Kubali kuwapa hao jamaa kile wanachokihitaji.Kubali kuwapa ushindi ili maisha yaendelee na nchi iwe na amani.Endapo utashindwa kukubaliana nao hawa jamaa na ukaacha wakasambaza picha hizi mitandaoni nchi itatikisika.Siwezi kuelezea aibu hii kubwa na siwezi kuelezea ni athari gani tutazipata kama chama ndiyo maana nakuomba ufanye kila linalowezekana ili jambo hili limalizike.Kama unafahamu alipo huyo jamaa Mathew Mulumbi basi mkabidhi kwa hao watu wanaomtaka”
“Naona hujanielewa mzee Simba.Hawa watu wanaelekea kushindwa katika hii vita na ndiyo maana wanamtaka Mathew ambaye ndiye aliyesimama mstari wa mbele kuwasaka.Wameingiwa na hofu na wanajua kama
wakimpata Mathew Mulumbi basi vita itakuwa imekwisha.Jambo lingine ni kwamba nikikubali matakwa yao kama unavyonishauri nifanye basi itakuwa ni ishara ya kuinua mikono na kuweka silaha chini na pambano litakuwa limekwisha hao jamaa watachukua ushindi na wakichukua ushindi basi wataendesha nchi hii vile watakavyo.Watanilazimisha nifanye kila wanachokitaka,watanilazimish a nipindishe sheria za nchi kwa manufaa yao,kwa ufupi ni kwamba nitakuwa mtumwa wao.Wao watakuwa wameishika nafasi hii ya urais na mimi nitakuwa hapa kama picha tu.Sijui kama unanielewa mzee Simba” akasema Rais Festus
“Ninakuelewa
mheshimiwa Rais.Hili jambo ni gumu sana.Unayosema ni sahihi lakini kwa upande wangu bado nalitazama jambo hili kwa jicho la kichama zaidi.Kwa chama lina athari kubwa mno.Festus tunakutegemea mno kama chama.Una mtaji wa wafuasi wengi na kwa namna unavyopendwa na watu tulitegemea ushindi wa zaidi ya asilimia themanini lakini kama jambo hili litavuja basi chama kitakuwa na wakati mgumu sana kwani sina hakika kama watakubali kukupa tena bendera ya chama uipeperushe katika uchaguzi mkuu ujao.Endapo picha hizi zikisambazwa tutakuwa tumewapa nguvu kubwa washindani wetu kisiasa kupata sababu ya kuzungumza na kutushinda ndiyo maana bado ninarudi pale pale kwamba wape hao jamaa kile wanachokihitaji jambo hili liishe.Hutapoteza kitu kama ukiwapa mtu huyo mmoja wamtakaye.Kama ni majasusi nchi ina majasusi wengi huwezi kuendelea kumng’ang’ania mtu mmoja tu” akasema profesa Simon.
“Hebu fikiria pia mheshimiwa Rais ni aibu gani ataipata mwanamke Yule uliyekuwa naye faragha? Ni aibu gani wataipata familia yako? Akauliza profesa Simon.Rais akamtazama halafu akasema
“Nadhani umefika wakati wa watanzania kutofautisha urais na maisha binafsi ya rais”
“Mheshimiwa Rais
sikuelewi
unachokizungumza.Nimekwis ha kueleza hapo awali kwamba wewe ni kiongozi mkubwa,unaongoza watu zaidi ya milioni hamsini hivyo huwezi kuwa na maisha ya kawaida kama wengine.Maisha hayo utayapata pale utakapokuwa umestaafu lakini kwa sasa unatakiwa ujielekeze katika kuwatumikia watu.Mambo kama haya unayoyafanya yanalichafua jengo hili,yanaichafua ofisi tukufu ya Rais,yanakichafua chama na yanawaumiza watanzania na hasa wanachama wa chama chetu wanaokupenda wanaokuunga mkono na wanaokuombea” akasema kwa ukali Profesa Simon
“Mzee Simba ninakuheshimu sana.Umekuwa mwalimu wangu chuo kikuu,na umekuwa pia mwalimu wangu katika siasa.Kuna jambo ambalo nataka kukwambia ambalo naamini halitakufurahisha wewe na wanachama wengine” akasema Festus huku akimtazama Profesa Simon kwa macho makali.
“Sintainua mikono kusalimu amri kwa hawa jamaa.Sintawapa kile wanachokihitaji yaani Mathew Mulumbi.Siwezi kuwa mtumwa wao.Niko tayari kwa kila wanachotaka kukifanya lakini si kusalimu amri !
“You are not serious Mr President !
“I am serious Mzee
Simba,very serious ! akajibu Rais Festus na Profesa Simon akamtazama kwa mshangao.
“Mheshimiwa Rais
unalichukulia rahisi hili jambo lakini ni jambo zito.Naomba uchukue muda ulitafakari kwa kina na ufanye maamzi sahihi.Angalia mustakabali wako,angalia mustakabali wa nchi na wa chama chako.Hebu pata picha ya namna utakavyo aibika.Festus nakuhakikishia kama picha hizi zitasambaa na ukasikia watu wanavyokusema vibaya utatamani ujitoe uhai ! akasema Profesa Simon
“Mzee Simba sina haja ya kutafakari mara mbili.Nimekwisha fanya maamuzi kwamba nitaendelea kupambana na hawa watu hadi mwisho wangu au wao lakini katu sintaweza kunyanyua mikono na kusalimu amri! akasema Rais Festus na katibu mkuu profesa Simon akaendelea kumtazama huku akihema haraka haraka
“Lazima tulijadili jambo hili katika chama”akasema “Hakuna haja mzee Simba.Mawazo yangu hayatabadilika.Siogopi niko tayari kuibeba aibu hiyo kubwa. Mwanamke Yule ambaye umemuona katika zile picha anaitwa Zandile Wepener anaishi AfrikaKusini.Aliwahi kuwa mke wa mfalme wa Eswatini kabla ya kuachana na kwa sasa niko naye.Ninampenda na sioni aibu kuipigania furaha yangu kwani kwa sasa yeye ndiye furaha yangu yeye ndiye mfariji wangu,yeye ndiye kila kitu kwangu ! Nitasimama hadharani na nitakiri kwamba nina mahusiano na Zandile ! akasema Rais Festus
“Festus shetani gani amekuingia kichwani kwako?
Nani amekuroga namna hii? Huoni namna unavyojidharaulisha wewe na huyo mwanamke unayedai unampenda?
“Nitapata aibu tena kubwa lakini katu siwezi kuinua mikono.Nitaendelea kupambana hadi kuhakikisha nimewatia mikononi hawa jamaa ! akasema Rais Festus wakabaki wanatazamana
“Mzee Simba nadhani tumemaliza.Ninakushukuru sana kwa kunifikishia taarifa hii pamoja na maagizo ya hao jamaa ambayo siko tayari kuyatekeleza.Kwa sasa tusubiri kile watakachoamua kukifanya.Walisema watazisambaza picha hizo jioni ya leo kama sintakuwa nimetekeleza maagizo yao hivyo tusubiri hadi muda huo picha hizo na video zitakaposambazwa! Akasema
Rais Festus
“Mwenyekiti sintaondoka hapa hadi pale tutakapopata muafaka wa hili jambo! Lazima maamuzi magumu yafanyike !
“Tayari nimekwishafanya maamuzi magumu ya kukubali aibu itakayopatikana pale picha hizo zitakaposambazwa.Hakuna tena maamuzi mengine magumu nitakayoweza kuyafanya zaidi ya hayo.Siko tayari kukubali matakwa ya hao jamaa !
“Festus lifikirie jambo hili kwa kina.Nitakupigia tena simu baadaye kujua maamuzi yako au vinginevyo italazimika kuitishwa kikao cha dharura cha viongozi kujadili jambo hili! Akasema Profesa Simon huku akiikunja kompyua yake na kuiweka mkobani wakaagana akaondoka
Rais Festus baada ya kuagana na Profesa Simon akarejea ofisini kwake na kuelekeza asisumbuliwe wala asiruhuwie mtu yeyote kuingia ofisini kwake hadi pale atakapotoa maelekezo.Alivua koti akalegeza tai na kukaa kitini
“Nilipokuwa nagombea
urais nilijua si kazi nyepesi na nitakutana na magumu mengi lakini sikuwahi kuhisi siku
moja ningekutana na wakati mgumu kama huu ninaokutana nao sasa.Nimeingia katika vita kubwa na watu hatari kabisa ambao wameyagundua hata mambo yangu ya siri kabisa ambayo nilidhani hayajulikani
! Akawaza
“Nilidhani nimemaliza
kazi baada ya kulimaliza lile suala la kuzaa njeya ndoa kumbe ndiyo nimechokoza vita.Nilitetemeka mno nilipoziona picha zile nikiwa faragha na
Zandile.Wamepigaje zile picha?Nahisi watu hawa wameanza kunifuatilia muda mrefu sana na na wakagundua mahusiano yangu na Zandile wakaweka kamera za siri wakafanikiwa kupata zile picha.Hii inaanza kunipa wasiwasi kwamba yawezekana hata miongoni mwa walinzi wangu au watu wa karibu ninaowaamini wapo wanaoshirikiana na hawa jamaa na wanawapa taarifa
zangu za siri.Watu wanaofahamu mahusiano yangu na Zandile ni wachache tena wale wa karibu mno ninaowaamini.Lazima kati yao lazima yupo mmoja wao au zaidi ambaye ametoa siri hii na hata kuwezesha watu hawa kuweka kamera za siri mle ndani na kupata picha zile.Dah ! akawaza na kushika kichwa
“Taa nyekundu imekwisha waka na kunitahadharisha kwamba siko salama.Lazima kuanzia sasa nichukue tahadhari kubwa kwa usalama wangu na kila ninachokifanya lakini natakiwa kufanya uchunguzi wa kina kufahamu ni nani ambaye anatoa taarifa zangu kwa hawa jamaa.Hilo itakuwa la kwanza lakini la pili ninarudi katika matakwa ya hawa jamaa.Wanamtaka Mathew Mulumbi ! akawaza na kusimama akaenda dirishani
“Hapa ndipo ninapochanganyikiwa.Nikimto a Mathew Mulumbi ina maanisha kwamba nimeshindwa vita na wataendelea kutoa madai mapya kila wakati.Nitakuwa mtumwa wao jambo ambalo silitaki.Lakini nisipotekeleza kile wanachokitaka basi watazisambaza picha zangu.Ni aibu kubwa mno hii ambayo haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu kwa picha za faragha za Rais kusambazwa mitandaoni” Rais Festus akaendelea kuumiza kichwa chake kwa mawazo
“Picha zile zikisambaa utakuwa ni mwisho wangu wa maisha ya siasa.Hakuna atakayekubali kunipa ridhaa ya kuongoza tena.Nitakuwa nimekiaibisha na kukiangusha chama changu mno.Familia yangu sijui watapita wapi.Hizi ni picha ambazo zitadumu mtandaoni milele na milele na aibu hii nitakwenda nayo kaburini” akaendelea kuwaza akahisi joto akaivua kabisa tai yake
“Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu natakiwa kufanya maamuzi magumu mno.Maamuzi ambayo nitayafanya kwa sasa ndiyo yatakayotoa picha ya safari
yangu ya kisiasa.” Akarejea kitini
“Hawa jamaa ni mtandao hatari na lazima wana watu wao hata hapa ikulu.Wanao watu wao wamenizunguka na hata kuniua wanaweza.Siwezi kukubali kuwapa nafasi watu hawa ya kuendelea kutamba na kufanya mambo yao wanayoyataka kama vile hakuna uongozi.Siwezi kukubali kuwa mtumwa wao
wa kufanya kila watakachonitaka nikifanye.Watu hawa wameharibu maisha ya watu wengi.Hivi sasa tayari Dr Fabian amefikishwa mahakamani na watafanya kila linalowezekana kuhakikisha anaishia gerezani na hata Mathew Mulumbi kama nikikubali matakwa yao na kuwakabidhi lazima aidha watamuua au watamkabidhi polisi na kuhakikisha anafikishwa mahakamani ambako lazima atafungwa.Siwezi kukubali hicho wanachokitaka yaani kumkabidhiMathew kwao.Niko tayari kuibeba aibu hii kubwa hadi siku ya kufa kwangu ili kumpa Mathew nafasi ya kuendelea kuwachunguza hawa jamaa kuwafahamu ni akina nani na kuwafagia kabisa.Nina uhakika akina Mathew wamekwishapiga hatua kubwa hivi sasa ya kuwafuatilia hawa jamaa na ndiyo maana nao wanafanya kila wawezavyo kuweza kumpata Mathew Mulumbi ambaye ndiye kinara wa timu inayowasaka.Pamoja na aibu kubwa ambayo nitaipata lakini siku moja watanzania watakapojua kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia nina uhakika mkubwa wataniona shujaa” akawaza Rais Festus na kuitazama ofisi yake
“Naamini muda si mrefu
kutoka sasa ofisi hii itakuwa chungu mno na si ajabu ndani ya siku chache zijazo nikawa nje ya ofisi hii lakini nilikula kiapo cha kuwatumikia watanzania na ndivyo nimekuwa nikifanya na lazima nihakishe watanzania wanakuwa salama muda wote.Siwezi kukubali kikundi cha watu wachache waibuke na kuleta hofu kwa wananchi,wanaua,wanabambi ka kesi kwa sababu tu wana mtandao mpana lazima nihakikishe ninakifyekelea mbali kikundi hiki na kuufumua kabisa mtandao wao wote na haya lazima yafanyike nikiwa bado nina nguvu ya Rais” akawaza na kuanza kuzunguka zunguka mle ofisini.
“Niko tayari kwa ajili ya kufanya maamuzi magumu mno ambayo yataathiri maisha yangu kwa kiasi kikubwa.Vipi kuhusu Zandile atalipokeaje jambo hili yawezekana ukawa ni mwisho wa mahusiano yangu naye,nawaza kuhusu watoto wangu namna watakavyolichukulia jambo hili lakini lazima nikubali kwamba nitapoteza mambo mengi.Nitapoteza vitu vingi na kubwa zaidi ni imani ya watanzania kwangu.Kwa maamuzi haya magumu sintakuwa sawa tena na yawezekana nikajikuta nimebaki mwenyewe lakini lazima niyafanye na katika hili sitaki ushuri wa mtu yeyote.Ninafanya kile chenye faida kwa nchi” akaendelea kuwaza huku akikaa juu ya meza
“Kabla ya kufanya chochote natakiwa kwanza kuzungumza na Mathew Mulumbi kumueleza kuhusu jambo hili na maamuzi ambayo nimeyachukua.Nataka wajue kwamba tuko vitani na tunapigana na watu hatari mno” akawaza na kuchukua simu yake akampigia Zari
“Mheshimiwa Rais! Akasema Zari baada ya kupokea simu
“Zarina nataka kufahamu maendeleo yenu.Mnaendeleaje?
“Tunaendelea vizuri mheshimiwa Rais”
“Nafurahi kusikia hivyo.Uko wapi hivi sasa?
“Niko hapa ofisini nimekuja kuangalia mambo yanavyokwenda hapa” akasema Zari
“Sawa Zari imekuwa vyema uko karibu na hapa.Njoo mara moja hapa ikulu ninakusubiri” akasema Rais na kukata simu
Baada ya kutoka ikulu kuonana na Rais,Profesa Simon Themba akarejea ofisini kwake.Aliubamiza mlango wa ofisi yake kwa nguvu na kwenda kuketi sofani.Baada ya dakika mbili katibu wake muhtasi akaufungua mlango akaingia ili aweze kumpa taarifa muhimu
“Nancy not now.Kama
kuna chochote cha kunieleza naomba unieleze baadae tafadhali” akasema Profesa Simon na Nancy akatoka.
“Hili jambo la Festus litanipasua kichwa changu.Amekumbwa na balaa gani huyu mtu? akawaza Profesa Simon
“Sikutegemea kabisa kama Festus ageweza kufanya mambo kama haya anayoyafanya.Amejidhalilisha sana na amekivua nguo chama.Kama picha zile zikivuja na kusambaa kwa wananchi lazima kamati ya maadili ikae na kumjadili.Kiongozi mkubwa kama Yule anapaswa awe mfano.Kama picha zile zikivuja basi wananchi hasa wapinzani wetu lazima watataka Rais naye aadhibiwe kama wanavyoadhibiwa wananchi wengine wa kawaida kila picha
zao za faragha zinapovuja.Mimi bado najielekeza upande wa chama heshima ya chama itashuka
sana na tutapata kazi kubwa mno kumnadi mgombea wetu.Tulikwisha amini kwamba hatutakuwa na kazi kubwa katika uchaguzi mkuu ujao ya kumnadi mgombea wetu kwani ana kila sifa nzuri lakini kwa hili tutakuwa na kazi ngumu mno.Oh festus ! Festus! Kwa nini lakini ameshindwa kutulia? Akajiuliza profesa Simon akiwa ameweka mikono kichwani.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment