Simulizi : Scandle (Kashfa)
Sehemu Ya Nne (4)
“Kamishna nafahamu
jambo hili limekuumiza sana lakini kama alivyosema Mathew Deus ni mtu muhimu sana katika kuwatafuta hawa jamaa kwani tayari ana mawasiliano nao” akasema Dr Fabian.Kamishna Chambao akafikiri kisha akasema
“Unataka kumtumiaje huyu shetani? Akauliza Chambao
“Nitamtaka ampigie simu huyo jamaa anayempa
maelekezo na sisi tutaifuatilia simu hiyo na kufahamu mahala alipo huyo jamaa kisha tutamfuata mahala hapo” akasema Mathew
“Vyovyote vile mtakavyofanya lakini I don’t want to be part of this anymore.Siwezi kushirikiana na mtu ambaye ametembea na mke wangu.Tafadhali naomba mnirudishe nyumbani ! akasema Kamishna Chambao
“Kabla hatujaondoka hapa kuna jambo nataka kukuomba Kamishna”
“Unataka nini Mathew?
“Nitahitaji kuzungumza na mke wako.Kuna mambo ambayo nahitaji kufahamu kutoka kwake”
“Mathew bado unahisi mke wangu anashirikiana na hawa jamaa? Akauliza Kamishna Chambao
“Kamishna kuna mambo
bado yananipa ukakasi na ninahitaji kumsikiliza na yeye pia.Suala hili ukiliangalia kwa undani kuna mambo ambayo mke wako anahitaji kuyatolea ufafanuzi.Kama hutajali ningeomba umpigie simu tufahamu mahala alipo,mimi nitakwenda kuzungumza naye” akasema Mathew “Kamishna ni jambo gumu lakini naomba umsikilize Mathew anachoshauri” akasema Dr Fabian.Kamishna Chambao akavuta pumzi ndefu halafu akawasha simu yake aliyokuwa ameizima.Ziliingia jumbe nyingi mfululizo.Wakati akizitafuta namba za simu za mke wake mara ikaingia simu akalazimika kuipokea.
“What ?!! akasema kwa mstuko Kamishna Chambao.
“Haiwezekani !! akaendelea kusema huku akihema haraka haraka “S..s..sawa ninakuja ! akasema Chambao na kushusha pumzi.Midomo ilikuwa inamtetemeka
“Kuna tatizo lolote
Kamishna Chambao? Akauliza Dr Fabian
“My wife ! akasema Kamishna Chambao akitetemeka
“Kafanya nini mke wako? Akauliza Mathew
“She’s dead !
“Dead?! Dr Fabian na
Mathew wakashangaa
“Nini kimesababisha kifo chake?
“Nimeambiwa ameanguka kutoka ghorofani” akasema Chambao
“Imetokeaje akaanguka? Akauliza Mathew
“I don’t know.Nahitaji kwenda hospitali kuthibitisha kama taarifa hizi ni za kweli”
akasema Kamishna Chambao na kuanza kuoka nje kuelekea katika gari
“I’ll go with you” akasema Dr Fabian naye akaanza kutoka Mathew akamuita
“Mheshimiwa Rais mimi nitabaki na Deus nataka kufanya mawasiliano na Yule jamaa aliyemuamuru kumuua Gosu Gosu.Tutaifuatilia simu yake mahala alipo kisha nitamfuata.Jioni ya leo tutakutana nyumbani kwako nitakupa mrejesho” akasema Mathew
“Mathew unafikiria nini kuhusu kifo cha ghafla cha mke wa Kamishna?Unadhani ni kifo cha kawaida? Akauliza Dr Fabian
“Mzee hiki si kifo cha kawaida.Kwa maelezo aliyonipa Deus inaonyesha wazi kwamba tukio la kurekodi video ile lilipangwa na mke wa Kamishna lazima alikuwa anafahamu.Naamini kuna mahusiano kati yake na hawa jamaa na ninaamini wao ndio waliomuua.Imekuwa bahati mbaya sana amefariki kabla ya kumfanyia mahojiano pengine tungeweza kugundua kitu.Hata hivyo mwangaza tulioupata unatia moyo” akasema Mathew
“Sawa Mathew tutakutana
jioni.Please be very carefull” akasema Dr Fabian na kuondoka.
Baada ya Dr Fabian na Kamishna Chambao kuondoka,Mathew akamfuata Deus chumbani akamfungua pingu.
“Kuna taarifa ambazo si nzuri tumezipata muda mfupi uliopita” akasema Mathew “Taarifa gani? Akauliza Deus
“Mke wa Kamishna
Chambao amefariki dunia”
“Nini?! Deus akastuka
“Mke wa mzee Chambao amefariki dunia.Inadaiwa kwamba ameteleza kutoka ghorofani akaanguka na kupoteza maisha”
“Mungu wangu ! akasema Deus
“Deus kuna kitu ambacho ninakiona katika maelezo uliyonipa kuhusu mahusiano yako na mke wa Chambao.Sina uhakika bado lakini kuna kila dalili kwamba mke wa mzee Chambao alikuwa na mashirikiano na hawa jamaa na walimtumia yeye ili kukushawishi ukaingia katika mahusiano naye kisha ikarekodiwa video ile mkifanya mapenzi kwa malengo ya kuitumia katika mikakati yao.Walifahamu Gosu Gosu lazima atafungwa gerezani hivyo maandalizi ya kumuua yalianza mapema kabla hajaingia gerezani na ndiyo maana alipoingia tu gerezani ukaelekezwa kufanya mipango ili auawe” akasema Mathew na Deus akainamisha kichwa akisikitika
“Deus huu si wakati wa kuendelea kusikitika.Mambo yamekwisha haribika na kinachoendelea kwa sasa ni kuhakikisha tunawatafuta na kuwapata watu hao” akasema Mathew
“Mathew I’m so scared.Hawa jamaa wanaweza wakanifuata na mimi wakaniua au hata familia yangu” akasema Deus
“Ndiyo maana tunahitaji kuwatafuta kabla hawajafanya hivyo.Hata hivyo usihofu tutakulinda wewe na familia yako ili mradi uwe tayari kushirikiana nasi” akasema Mathew
“Mimi niko tayari kushirikiana nanyi kwa namna yoyote katika kuhakikisha hawa jamaa wanapatikana.Ni akina nani hawa watu? Akauliza Deus
“Deus tutaongea baadae kwa sasa tuna kazi ya kufanya.Twende ukaoge ubadili mavazi kisha tuingie kazini” akasema Mathew na kumuelekeza Deus bafuni
Wakati Deus akioga,Mathew akampigia simu Ruby akampa taarifa za kile kilichotokea
“Mhh ! Mathew jambo hili mbona linaaza kuogofya.Kama kweli mke wa mzee Chambao alikuwa na mashirikiano na hao jamaa basi mtandao huu ni mkubwa na hatari” akasema Ruby
“Ruby kwa sasa tunao watu wawili ambao wanaweza wakatusaidia katika jambo hili.Tunaye Zawadi ambaye
tunamuomba Mungu amsaidie
aweze kupona,vile vile tunaye Deus.Huyu kama nilivyokueleza amekuwa na mawasiliano nao hivyo nitaanza kwa kumtumia huyu Deus kuwasiliana na huyo mtu wake na wakati akipiga simu nitakutaka uifuatilie namba atakayopiga ili tufahamu mahala alipo nimfuate” akasema Mathew halafu akachukua bastola tatu,mbili za kwake na moja kwa ajili ya Deus.Akamchagulia pia nguo akampa avae kwani Deus hakuwa amekwenda Dar es salaam na nguo nyingine
yoyote zaidi ya sare za jeshi la magereza
“Are you ready? Mathew akamuuliza
“I’m ready” akajibu Deus na Mathew akampatia bastola wakaingia garini na kuondoka
“Kama kweli Yule mama alitumika kunishawishi alinifanyia kitu kibaya sana.Ameyaharibu maisha yangu.Amenifanya nikafanya mambo ya hatari kubwa na kwa sasa niko katika hatari kwanza ya kupoteza kazi na hata kufungwa gerezani.Familia yangu watabaki wanateseka.Najuta kwa nini nikakubali kushawishika na kuingia katika mtego wa Yule mama? Akawaza Deus wakiwa garini
“Mathew watu hawa ni akina nani? Akauliza
“Hata mimi siwafahamu watu hawa ni akina nani na tunaendelea na juhudi za kuwasaka,ninachofahamu mimi ni kwamba watu hawa wamejipanga vyema na wana nguvu ya kufanya chochote” akasema Mathew
“Unadhani kwa nini Gosu Gosu anataka kuuawa? Akauliza Deus
“Gosu Gosu hakuua mtu bali ulikuwa ni mpango uliotengenezwa kitaalamu sana hadi ikaonekana Gosu Gosu ndiye muuaji lakini aliyemuua Lidya si Gosu Gosu.Hawa watu wanaotaka kumuua ndio waliotekeleza mauaji yale ya Lidya na kumuangushia mzigo.Gosu Gosu na Lidya walikuwa wapenzi”
“Kwa hiyo kilichomponza Gosu Gosu ni kuwa na mahusiano na huyo Lidya”
“Ndiyo.Hicho ndicho kilichomponza lakini hakuua”
“Nini sababu ya kumuua Lidya? Akauliza Deus
“Hicho ndicho ambacho
tunakitafuta hivi sasa na hawa jamaa wanajitahidi kwa kila namna kuificha sababu ya mauaji hayo isijulikane ndiyo maana mzigo wa mauaji akaangushiwa Gosu Gosu” akasema Mathew
“Vipi kuhusu familia yangu?
“Usiofu watakuwa salama” akajibu Mathew na simu yake ikaita alikuwa ni Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais” akasema Mathew baada ya kupokea simu
“Mathew lini utaacha mambo hayo ya Rais? Nimekwisha kueleza niite Dr
Fabian inatosha”
“Samahani Dr Fabian” akasema Mathew
“Nimepokea simu kutoka kwa mtu amejitambulisha kama Sajenti Linus kutoka Katihar hospital anadai ulimuachia namba zangu ili anipigie”
“Ndiyo mzee nilimuachia namba zako ili akupigie kukujulisha maendeleo ya Zawadi.Yeye ndiye kiongozi wa kikosi kilichotumwa pale hospitali kumlinda Zawadi” akasema Mathew
“Basi amenipigia kunijulisha kwamba upasuaji umemalizika na Zawadi tayari amekwisha pelekwa katika wodi na amezinduka”
“Hizo ni habari njema sana.Kwa sasa niko na Deus ninataka awasiliane na Yule mtu ili nifahamu mahala alipo halafu nitaelekea Kichangani kuzungumza na Zawadi.Vipi kuhusu mzee Chambao anaendeleaje? Akauliza Mathew
“Hali ya Chambao si nzuri.Amechanganyikiwa.Sual a hili limemchanganya sana.Amepumzishwa katika chumba hapa hospitali ya Mtodora kwani alipoteza fahamu baada ya kuiona maiti ya mke wake.Nimemuacha hospitali kwa sasa ninaelekea nyumbani” akasema Dr Fabian
“Sawa mzee tutawasiliana baadae” akasema Mathew na kukata simu
Safari ikaendelea kimya kimya hadi walipofika sehemu moja yenye msongamano mkubwa wa magari,Mathew akaiwasha simu ya Deus halafu akampigia Ruby na kumtaka ajiandae kwa ajili ya kufuatilia simu ile atakayopiga Deus.Mathew hakukata simu,ilibaki hewani ili Ruby aweze kusikiliza kile kitakachozungumzwa.
Deus akaitafuta namba ya Yule mtu ambaye huwasiliana naye akampigia lakini simu hiyo haikuwa ikipatikana.
“Try again” akasema Mathew na Deus akajaribu tena kuipiga ile namba lakini haikupatkana.
“Amezima simu.Tayari anafahamu mambo yameharibika” akasema Mathew na kumpigia Ruby
“Ruby inaonekana jamaa amekwisha fahamu mambo yameharibika na hapatikani tena simuni.Ninakutumia namba yake ya simu jaribu kuifuatilia namba hii tufahamu ni ya nani na yuko wapi.Mimi ninaelekea Kichangani kujua maendeleo ya Zawadi” akasema Mathew na kumtajia Ruby namba za yule mtu akawasha gari wakaondoka. “Tunaelekea wapi? Akauliza Deus
“Sehemu Fulani” akajibu Mathew
Mathew aliwasili Katihar Medical College and Hospital na kufahamishwa kwamba upasuaji aliofanyiwa Zawadi ulikuwa na mafanikio na tayari Zawadi alikwisha zinduka kutoka usingizini.Mathew akapelekwa katika chumba alimokuwa amelazwa Zawadi ambacho kilikuwa kinalindwa na askari.Mathew na daktari walipoingia mle chumbani,Zawadiakafumbua macho na moja kwa moja akamtambua Mathew
“Kaka umekuja” akasema Zawadi bado sauti yake ilikuwa dhaifu
“Unaendeleaje kwa sasa? Akauliza daktari
“Mwili hauna nguvu na ninahisi maumivu” akasema Zawadi.Daktari akampima halafu akatoka akamuacha azungumze na Mathew “Pole sana Zawadi”
“Ahsante sana kwa kuniokoa.Bila wewe ningeuawa leo.Wewe ni nani? Ni polisi? Akauliza Zawadi
“Naitwa Mathew Mulumbi ninashughulika na usalama wa taifa” akasema Mathew
“Mimi umenifahamuje? Akauliza Zawadi
“Zawadi ninashukuru unaendelea vyema lakini unahitaji kupumzika hivyo sitaki kuchukua muda wako mwingi.Kuna jambo ninataka kulifahamu kutoka kwako na ndiyo maana nilikufuata pale nyumbani”
“Jambo gani? Akauliza Zawadi
“Unamfahamu mtu anaitwa Naomi Bambi? Akauliza Mathew na sura ya Zawadi ikaonyesha mstuko kidogo
“Naomi Bambi? Akauliza Zawadi
“Ndiyo.Unamfahamu?
akauliza Mathew na Zawadi akafumba macho akionekana kuwa katika maumivu
“Naomi Bambi ! akasema Zawadi kama vile anajaribu kukumbuka
“Naomi Bambi ! akasema tena Zawadi na macho yake yakaanza kuloa machozi “Nieleze tafadhali kama kuna chochote unakifahamu kuhusu Naomi Bambi” akasema Mathew na kumfuata akamfuta machozi
“Tell me please”akasema Mathew
“Naomi ni sababu ya mimi kufika hapa nilipo leo.Ni sababu ya maisha yangu kuharibika”akasema Zawadi
“Nieleze tafadhali” akasema Mathew
“Siku moja Jerome
aliniambia kuna kazi nzuri ambayo nikiifanya itanipatia fedha nyingi .Nilimuuliza ni kazi gani akasema kuna mgonjwa natakiwa kumchoma sindano.Kwa kuwa aliniambia nitalipwa fedha nyingi nilikubali kuifanya hiyo kazi na usiku wa manane nikachukuliwa nikiwa nimefungwa kitambaa cheusi usoni nikapelekwa mahala nisikokujua.Nilitolewa kitambaa baada ya kuingizwa ndani ya chumba Fulani nikamuona binti mmoja akiwa amelala kitandani,macho yake yalikuwa mekundu na nywele zilikuwa timu timu.Mikono yake na miguu ilikuwa imefungwa kitandani.Alinitazama kwa macho makali hadi nikaogopa.Jerome akaniletea dawa Fulani akanitaka nimchome Yule msichana.Mimi taaluma yangu ni muuguzi na nilipoitazama dawa ile nikauliza mgonjwa yule anaumwa nini nikaambiwa kwamba nimchome ile dawa kwani ndiyo kazi iliyonipeleka pale nikafanya kama nilivyoelekezwa.Baada ya kuifanya ile kazi nikapewa hundi ya shilingi milioni thelathini.Nilistuka kwa kupewa fedha nyingi kiasi kile kwa kazi ndogo niliyoifanya” Zawadi akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“Siku iliyofuata nilikwenda benki na kuweka fedha zile katika akaunti yangu na jioni yake akaja Jerome nikamuuliza sababu za kulipwa fedha nyingi kiasi kile
akaniambia ni kwa ajili ya kununua ukimya wangu.Nilishangaa nikamuuliza ukimya upi? Akanijibu ni kwa sababu ya Yule msichana niliyemchoma ile sindano.Nilimtaka anieleze kuhusiana na Yule msichana ni na nani na kwa nini nilimchoma ile sindano.Jerome akanieleza kwamba msichana Yule anaitwa Naomi Bambi na dawa ile niliyomchoma ni kwa ajili ya kumuharibu akili.Nilimuuliza Jerome sababu za kutaka msichana Yule aharibike akili lakini hakunieleza na akanionya kama nikithubutu kufungua mdomo wangu kusema chochote nitakuwa nimenunua kifo changu” Zawadi akanyamaza akafumba macho na baada ya muda akaendelea
“Sikupendezwa na kitendo kile tukaanza kugombana na kwa bahati mbaya Jerome akateleza vibaya na kujigonga ukutani akafariki.Nilikutwa na hatia ya kuua bila kukusudia nikafungwa gerezani” akanyamaza tena na machozi yakamtoka
“Jikaze Zawadi nieleze kila kitu” akasema Mathew “Nikiwa gerezani nilitembelewa na mtu mmoja akaniuliza kama ninakumbuka alichonieleza Jerome kuhusu Yule msichana Naomi Bambi nikamjibu ninakumbuka akanionya kwamba kuna watu wanaweza wakafika gerezani kunihoji kama ninamfahamu Naomi Bambi lakini nisithubutu kufungua mdomo wangu kutamka chochote ninachokifahamu.Nikajulishw a kwamba kifungo changu kitakapokuwa kimemalizika sintarejea tena katika ile nyumba niliyoikuwa naishi
bali nitapelekwa katika nyumba nyingine sehemu nyingine ambako nitaanza maisha mapya”
“Kuna mtu yeyote
aliyekufuata gerezani na kukuhoji kuhusu Naomi Bambi? Akauliza Mathew
“Hakuna aliyenifuata kunihoji” akajibu Zawadi
“Nilimaliza kifungo changu nikachukuliwa na mtu akanipeleka katika nyumba mpya pale Kichangani akanikabidhi baadhi ya vitu vyangu muhimu kama kadi zangu za benki nk.Sikuwahi kufuatwa na mtu yeyote kuulizwa chochote hadi ulipofika leo hii na tukio lie likatokea. Kwa nini unataka kufahamu kuhusu Naomi Bambi? Akauliza Zawadi
“Kuna kitu kingine chochote unachoweza kukumbuka kuhusu Naomi? Akauliza Mathew
“Naomi nilimuona mara moja tu tena usiku nikamchoma sindano na sijawahi kumuona tena” akasema Zawadi
“Zawadi ninashukuru sana kwa maelezo haya uliyonipa”
“Nani amekuelekeza kwangu kwamba ninamfahamu Naomi Bambi? Umeniweka katika matatizo makubwa.Tayari nilikuwa nimetulia na ninaendelea na maisha yangu vizuri lakini umekuja na kuharibu kila kitu”
“Zawadi usihofu utakuwa salama.Nje ya chumba hiki kuna askari polisi wanakulinda usiku na mchana na hakuna yeyote atakayekufuata hapa kutishia maisha yako.Nataka kufahamu kuhusu mpenzi wako Jerome.Alikuwa ni mtu wa namna gani? Nani waliokuwa washirika wake? Akauliza Mathew.Zawadi akafumba macho na baada ya sekunde chache akasema
“Jerome sikumfahamu kiundani.Sikuwahi kufahamu kufahamu kazi aliyokuwa anaifanya,sikuwafahamu marafiki zake,sikuwafahamu ndugu zake kitu kimoja tu nilichompenda alinijali sana.Kila nilichokihitaji hata kama ni ghali kiasi gani alinipatia bila kusita kwani fedha alikuwa nayo ingawa hakuwahi kunieleza anafanya biashara gani” akasema Zawadi na kunyamaza kidogo
“Kuna kitu nimekumbuka,sina hakika kama alikuwa ni mtanzania”
“Kwa nini unasema hivyo Zawadi?
“Ni kutokana na lafudhi yake na Kiswahili chake hakikuwa kimenyooka” akasema Zawadi
“Unalifahamu jina la ukoo wake?
“Hapana .Jina ninalolifahamu ni Jerome sifahamu jina lingine” akasema Zawadi
“Ahsante Zawadi.Kuna kitu kimoja ambacho ninaomba unisaidie halafu nitakuacha upumzike” akasema Mathew na Zawadi akainua mguu kidogo akagugumia kwa maumivu Mathew akamsaidia kuuweka vizuri mguu wake
“Nini unahitaji? Akauliza Zawadi
“Ulifanikiwa kumuona Naomi Bambi.Unaweza ukanielezea muonekano wake ulikuaje? Akauliza Mathew
“Imekuwa ni muda mrefu
sasa”
“Jaribu kukumbuka.Fumba macho
vuta picha ya usiku ule ulpomuona” akasema Mathew na Zawadi akafumba macho kisha akaanza kumuelezea Mathew muonekano wa Naomi huku Mathew akifuata maelekezo yale na kuchora katika karatasi.Zawadi alijitahidi kumuelezea Mathew kile alichokikumbuka kuhusu Naomi Bambi.
Baada ya kumaliza kuchora,Mathew akamuonyesha zawadi ile picha na mstuko mkubwa ukaonekana machoni pake.
“Umenistua
sana.Umewezaje kuchora picha kama hii kwa kufuata tu maelezo? Sura ya Naomi niliyemuona usiku ule ni hii hii isipokuwa nywele zake hazikuwa ndefu kiasi hicho” akasema Zawadi na Mathew akafanya marekebisho katika ile picha.
“Hii ndiyo sura niliyoiona usiku ule.Hii ndiyo sura halisi ya Naomi Bambi” akasema Zawadi
“Zawadi ninakushukuru sana kwa msaada wako huu mkubwa.Ninakuhakikishia utakuwa salama na baada ya kupata nafuu utapelekwa katika sehemu salama” akasema Mathew
“Hujanieleza kwa nini unatafuta taarifa za Naomi?
“Zawadi utakapopata nafuu nitazungumza nawe kwa
kirefu zaidi lakini kwa sasa endelea kupumzika.Narudia tena usihofu kuhusu usalama.Kuna askari wanakulinda hapa saa ishirini na nne” akasema Mathew na kumpatia namba zake za simu ili awasilianae naye pale atakapohitaji chochote halafu akamuaga na kutoka.
Akamchukua Deus wakaingia garini na kuondoka
“Kwa mbali ninauona mwanga Fulani japo unakuja na kutoweka.Bado kuna kiza mbele.Zawazi amesema kwamba alifanikiwa kumuona Naomi mara moja tu na akamchoma sindano ambayo lengo lake lilikuwa ni kumuharibu akili.Kwa nini Naomi akaharibiwa akili tena kwa kutumia gharama kubwa? Zawadi anasema kwamba alipewa shilingi milioni thelathini kwa ajili tu ya kumchoma Naomi sindano.Lazima ipo sababu kubwa ya Naomi kufanyiwa hivi.Je yuko wapi kwa sasa? Mathew akatolewa mawazoni na Deus
“Mathew nini kinaendelea kwa sasa? Ninakufuata tu bila kujua wapi tunakwenda” Akauliza Deus
“Chukua simu mpigie tena yule jamaa kama anapatikana” akasema Mathew na Deus akachukua simu akampigia Yule jamaa bado simu yake haikuwa ikipatikana.
“Deus hautaweza kurejea Arusha kwa leo.Bado tuna kazi kubwa ya kufanya hapa Dar es salaam.Kumbuka hawa jamaa wana video yako na wanaweza wakaisambaza mtandaoni ili kuudanganya umma kwamba mke wa kamishna alijiua baada ya video yake chafu kuvuja hivyo hakuna kufumba macho hadi tuhakikishe tumewapata hawa jamaa”
“Mathew kila nikisikia kuhusu video hiyo mwili wote unanitetemeka.Ni fedheha kubwa sana kama video ile itasambazwa” akasema Deus
Mathew akiwa na Deus waliwasili nyumbani kwa Dr Fabian baada ya kutoka hospitali.Deus akakaribiswa chumba cha mapumziko halafu Mathew,Dr Fabian na Ruby wakakutana ofisini kwa Ruby ambako ndiko mipango yote ilikuwa inafanyika.
“Zawadi anaendeleaje? Akauliza Dr Fabian
“Ninamshukuru Mungu Zawadi anaendelea vyema na nimefanikiwa kuzungumza naye.Nilimtaka anieleze kuhusu Naomi Bambi na akanipa maelezo ya kile anachokifahamu kuhusu Naomi” akasema Mathew na kuwaeleza akina Ruby kile alichoelezwa na zawadi kuhusu Naomi.
“Mpaka hapo kuna kitu kimoja tu ambacho nimekipata
kwamba Naomi hakuwa na
matatizo yoyote ya akili hadi pale alipochomwa dawa ambayo ililenga kumfanya aonekane ni mgonjwa wa akili.Nini sababu ya kufanya hivyo? Je Naomi yuko wapi kwa sasa? Hayo ni maswali ambayo yanahitaji majibu.Naamini hapo ndipo alipoishia Lidya akauawa.Suala hili la Naomi linaoekana ni suala kubwa na ndiyo maana alikuwa analichunguza kwa bahati mbaya hakufanikiwa kuzungumza na
Zawadi.Tumepiga hatua moja zaidi ya pale alipoishia Lidya na tumefahamu kuwa Naomi hakuwa na matatizo ya akili.” akasema Mathew
“pamoja na mwangaza huo unaoanza kuonekana kwa mbali lakini badi ngoma ni nzito.Giza bado ni nene”akasema Dr Fabian
“Kwa upande wangu kuna kitu nimekigundua”akasema
Ruby
“Ile namba ya yule mtu ambaye amekuwa akiwasiliana na Deus akitaka amuue Gosu Gosu ni namba ile ile ambayo ilikuwa ikiwasiliana na Kishada kwa njia ya ujumbe mfupi” akasema Ruby na wote wakatazamana
“We have him
then.Umefuatilia wakati akiwasiliana na Kishada alikuwa mahala gani?
“Wakati akiwasiliana na Kishada mtu huyo alikuwa hapa Dar es salaam” akasema
Ruby na kumuonyesha Mathew ramani ikionyesha mahala alipokuwa huyo mtu aliyewasiliana na Kishada
“Good job
Ruby.Ninakwenda mahali hapo kujua nini kinaendelea na pengine ninaweza kupata kitu cha kuweza kutusaidia.Kabla sijaondoka sikuwa nimemaliza mambo ya hospitali.Kwanza ni kuhusiana na mchumba wa Zawadi.Nilipo mdadisi alisema kwamba anahisi mchumba wake huyo hakuwa mtanzania kutokana na lafudhi yake na Kiswahili kisichonyooka.Ninataka ufuatilie kesi ya Zawadi ili ufahanu mtu aliyemuua alikuwa anaitwa nani halafu umfuatilie tumjue kwani ni mmoja wa hawa jamaa.Vile vile kwa kutumia maelezo ya Zawadi niliweza kuchora sura ya Naomi na Zawadi akakubali inafanana sana na Naomi.Nataka uitumie picha hii kumtafuta Naomi”akasema Mathew na kumpatia Ruby ile picha ya Naomi aliyoichora.
“Wow ! she looks so young
! akasema Ruby na Dr Fabian akasogea naye akaitazama ile picha
“Ni kweli anaonekana ni msichana mdogo.Kuna nini kwa huyu msichana mdogo hadi roho za watu zimepotea namna hii? Akauliza Dr Fabian
“Usiofu mzee lazima tutagundua siri iliyoko nyuma ya pazia” akasema Mathew
“Vipi kuhusu huyu Deus,unakwenda naye?
“Hapana atabaki hapa.Is
there any problem? Akauliza
Mathew
“Hakuna tatizo lolote” akasema Dr Fabian kisha Mathew akaondoka
“Natamani sana kufahamu kuna nini kinaendelea kuhusu huyu Naomi Bambi.Kwa nini akaharibiwa akili?Je kuna kuna kitu walikuwa wanakificha kisijulikane hadi wakaamua kumuharibu binti huyo akili? Akajiuliza Mathew
“Mwelekeo si mbaya.Muda si mrefu tutapata mwangaza wa kilichopo nyuma ya jambo hili”akawaza
*************
Tayari nyumbani kwa
Kamishna Jenerali Chambao kulijaa watu waliofika kuungana na familia baada ya kupata taarifa za msiba wa mke wake.Kamishna Chambao
akiwa amekaa na waombolezaji waliofika kumfariji simu yake ikaita,zilikuwa ni namba ngeni katika simu yake akapokea “Hallow” akasema Chambao
“Kamishna Jenerali Chambao naomba usogee mahala ambako hakuna watu tuzungumze tafadhali”
“Wewe ni nani? Akauliza Chambao
“Naomba ufanye hivyo mzee.Nina jambo muhimu nataka kuzungumza nawe kuhusu mkeo” akasema Yule jamaa na Kamishna Chambao akasogea pembeni mahala kusiko na watu “Wewe ni nani na unataka nini? Akauliza “Kamishna naomba
unisikilize vizuri sana” akasema Yule jamaa
“Nakusikiliza”
“Kwanza pole sana kwa msiba mzee wangu” “Ahsante”
“Mzee Chambao kuna jambo nataka kulifahamu kuhusu mkeo ambalo naamini hulifahamu na yawezekana
ikawa ni sababu ya kifo chake.Mkeo hakuwa muaminifu alikuwa akiisaliti ndoa yenu.Alikuwa na mahusiano na mmoja wa viongozi wa moja ya gereza kubwa hapa nchini.Kuna video chafu ambayo mkeo alijirekodi akifanya mapenzi na huyo mpenzi wake wa pembeni” akasema Yule jamaa na Kamshna Chambao akamkatisha
“Tayari ninalifahamu jambo hilo!! akasema Chambao kwa ukali
“Kumbe tayari
unalifahamu jambo hilo,basi naomba nikujulishe kwamba mimi ndiye ninayo video hiyo na ninakusudia kuisambaza mtandaoni ili watu wafahamu uchafu aliokuwa anaufanya mkeo.Kamishna naamini bado hujaitazama video hiyo na ukiitazama utapoteza fahamu.Haifai kutazamwa” akasema Yule jamaa na Kamishna Chambao akahisi kama kisu kikali kinaukata moyo wake.Akauma meno kwa hasira na kusema
“Nakuonya tafadhali usithubutu kufanya hivyo.Usithubutu kumdhalilisha mke wangu kiasi hicho!! Akafoka Kamishna Chambao.
“Sintafanya hivyo mzee kama mimi nawe tutaingia makubaliano”
“Nini unakitaka shetani wewe? Akauliza Kamishna Chambao
“Ninamuhitaji mkuu wa gereza la Kimondo Deus Mtege”
“Unamtaka Deus?
Kamishna Chambao akauliza
“Ndiyo namtaka Deus
Mtege.Yuko hapa Dar es salaam na wewe unafahamu mahala alipo hivyo namuhitaji.Nitatuma vijana wangu watakuja nyumbani kwako kumchukua.Nataka ndani ya saa mbili kutoka sasa niwe nimempata.Kama ukipuuza maelekezo yangu nitaiachia video hiyo ambayo naamini hata wewe utachukua maamuzi kama aliyoyachukua mke wako.Fuata maelekezo yangu na video hiyo haitasambazwa.Clock starts now ! akasema Yule jamaa na kukata simu.Kamishna
Chambao alihisi miguu ikimtetemeka.Alibaki amesimama mahala pale akiwa hajui nini cha kufanya
“Hawa mashetani
hawatanii na wanaweza kweli wakaisambaza mtandaoni video ya mke wangu akifanya mapenzi na Deus kama nikiwapuuza.Siwezi kukubali jambo hilo likatokea kwani nitakayedhalilika ni mimi na familia yangu.Ngoja nimkabidhi Deus kwao.Hata hivyo nina hasira naye mno kwa kitendo alichonifanyia.Kama watamuua watakuwa
wamenilipia kisasi.Anastahili adhabu kali sana yule jamaa !
Baada ya tafakari ya kama dakika kumi Chambao akampigia simu Dr Fabian
“Kamishna unaendeleaje? Akauliza Dr Fabian
“Tayari nimekwisha rejea nyumbani na ndugu wamekwisha anza kuwasili.Kesho ndipo tutakaa na kupanga taratibu za mazishi.Ahsante sana Dr Fabian kwa kuwa nami karibu katika jambo hili zito”
“Usijali Chambao huu ni msiba wetu sote”
“Dr Fabian ninataka kufahamu mahala alipo Deus”akasema Chambao
“Deus? Akauliza Dr Fabian kwa wasi wasi kidogo “Ndiyo.Yuko wapi?
“Deus yuko hapa nyumbani kwangu”
“Ninamuhitaji nina mazungumzo naye ya kikazi.Kuna mambo nimetaarifiwa yametokea katika gereza lake hivyo nataka kuzungumza naye namna ya kuyashughulikia” akasema Kamishna Chambao
“Are you sure? Akauliza Dr
Fabian kwa wasi wasi
“Usiwe na hofu Dr
Fabian,trust me” akasema Kamishna
“Unataka aje hapo nyumbani kwako? Akauliza Dr Fabian
“Ndiyo ninataka afike hapa nyumbani kwangu kwani siwezi kutoka mida hii.Unaweza kunisaidia kwa hilo? Akauliza Kamishna Chambao
“Usijali nitakusaidia lakini Kamishna nafahamu bado una hasira kubwa na Deus so please don’t do anything stupid ! Bado tunamuhitaji sana katika kuwasaka hawa jamaa ! akasema Dr Fabian
“Dr Fabian nakuomba ondoa hofu ndugu yangu siwezi kufanya jambo lolote la kijinga.Mambo haya tutayamaliza kiutu uzima.Vipi Mathew kuna hatua zozote amekwisha piga katika kuwasaka hawa jamaa? Akauliza Kamishna Chambao
“Bado anaendelea kuwasaka na pale atakapokuwa amepiga hatua yoyote tutakujulisha” akasema Dr Fabian na kuagana na Chambao akamfuata Deus akamtaka ajiandae kuna sehemu anaelekea.Hakumweleza kama anakwenda nyumbani kwa Kamishna Chambao.Deus aliagana na akina Ruby kisha
akaingia katika gari la walinzi wa Dr Fabian na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Kamishna Chambao.
“Sina hakika na hili jambo” akasema Ruby baada ya Deus kuondoka
“Jambo gani? Akauliza Dr Fabian
“Kumruhusu Deus kwenda kuonana na Chambao wakati kama huu si suala zuri hata kidogo.Anything can happen. Chambao bado ana hasira kali sana na Deus” akasema Ruby
“Ruby sisi hatahusika na chochote kile kitakachotokea.Kama akimuua it’s up to him ! akasema Dr Fabian
Mathew aliifuata ramani aliyopewa na Ruby inayoonyesha mahala alipokuwa mtu aliyekuwa anawasiliana Kishada kuhusu mauaji ya Gosu Gosu na kujikuta amefika Dar es salaam Casino and hotel. “Kwa mujibu wa ramani niliyopewa na Ruby, huyo jamaa alikuwa hapa.Sehemu kama hizi huzipenda sana watu wanaojihusisha na mipango mbali mbali ya kihalifu,watu wa madawa ya kulevya,majambazi nk.Tayari ninaanza kupata picha ya hawa jamaa ni watu wa aina gani” akawaza Mathew na kuvuka geti akaelekea maegesho.Mara tu alipozima gari dirisha likagongwa akawaona akina dada watatu wakiwa wamevalia nusu utupu wakimsubiri ashuke
“Hawa makahaba hawajui mwenzao niko kazini” akawaza Mathew na kuiweka sawa bastora yake akashuka.Wale makahaba wakamsogelea na kila mmoja akaanza kumuonyesha umbo lake.
“Thank you all but I don’t need any of you tonight” akasema Mathew na kutoa noti kadhaa akawapatia wale akina dada waliokuwa wamemganda kisha akaelekea katika sehemu ya kukatia tiketi halafu akaingia ndani ya kasino. “Watu ni wengi sana humu ni vigumu kufahamu huyo jamaa atakuwa upande gani.Vile vile kuna sehemu ya watu maalum” akawaza Mathew na kuzunguka zunguka sehemu mbali mbali za kasino lile.Akachukua simu na kumpigia Ruby
“Ruby Yule jamaa alikuwa ndani ya Dar es salaam Casino and hotel.Tayari niko humu ndani kuna watu wengi sana ni vigumu kujua mahala alipo.Mwambie Deus ajaribu tena kupiga ile namba ya simu ya Yule jamaa halafu uifuatilie kama yuko humu ndani” akasema Mathew
“Mathew kuna jambo limetokea wakati umeondoka” akasema Ruby kwa wasi wasi
“Kumetokea nini? Akauliza Mathew
“Kamishna Chambao
amepiga simu muda si mrefu akasema anamuhitaji Deus nyumbani kwake”
“Anamtaka Deus? Akauliza Mathew akionekana kushangaa
“Ndiyo alisema ana maongezi naye muhimu ya kikazi nyumbani kwake” akasema Ruby
“Mmemruhusu Deus
akaondoka? Akauliza Mathew
“Ndiyo.Walinzi wa Dr Fabian tayari wamempeleka nyumbani kwa Kamishna” akasema Ruby
“Ruby that’s a big mistake. Kamishna Chambao bado ana hasira kubwa sana na hataki hata kulisikia jina la
Deus.Kama tusingefanya jitihada za kumnyang’anya bastora angeweza kumuua baada ya Deus kukiri alikuwa anatembea na mke wake.Kitendo cha kumtaka aende nyumbani kwake kinanipa mashaka makubwa na hatujui anakusudia kumfanya nini.Deus mwenyewe anafahamu kama anakwenda nyumbani kwa Chambao? Akauliza Mathew
“Hapana hafahamu” akasema Ruby
“Ruby hapa lazima kuna kitu si bure” akasema Mathew “Fabian pia aliingiwa na wasi wasi akamtahadharisha kuhusu jambo hilo lakini Chambao akamuhakikishia kwamba hana nia mbaya na Deus bali kuna masuala ya kikazi wanataka wayazungumze”
“Ruby misheni tayari imevurugika natakiwa kuwahi nyumbani kwa Kamishna Chambao kwenda kumuokoa
Deus.Naamini kabisa Chambao hana mipango mizuri kwa David.Ninakwenda huko kuhakikisha Deus ana kuwa salama kwani bado tunamuhitaji sana.Nitakujulisha nikifika huko” akasema Mathew
************
Gari la walinzi wa Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo lilifika nyumbani kwa Kamishna Jenerali wa magereza Chambao Mnenge.Nje ya nyumba ile kulikuwa na magari mengi yameegeshwa na watu walikuwa wamesimama katika makundi.Deus alipafahamu nyumbani kwa Kamishna Chambao na walipofika pale alistuka sana
“Tumefuata nini hapa? Akauliza Deus
“Hapa ndipo
tulipoelekezwa tukulete” akasema mmoja wa walinzi wale
“No ! No ! Please I don’t want to get in there ! akasema
Edger kwa wasiwasi “Maelekezo tuliyopewa na mheshimiwa Rais ni kuhakikisha tunakufikisha kwa Kamishna Jenerali Chambao ana mazungumzo nawe ya kikazi” akasema mmoja wa walinzi,akashuka akaingia ndani ya nyumba na baada ya dakika chache akatoka akiwa ameongozana na kamishna Chambao.Deus alipomuona Kamishna Chambao aliingiwa na hofu kubwa.Deus akatakiwa kushuka garini na Dr Fabian akamkaribisha “Karibu sana Deus” “Ahsante
mzee”akasemaDeus sauti yake
ikiwa na kitetemeshi.Kamishna akawashukuru wale walinzi wakaondoka.
“Deus nimekuita ninahitaji msaada wako hapa nyumbani kuna mambo mengi ya kusaidia halafu baadae tutazugumza mambo ya kazi.Kwa sasa kuna mzigo nitaomba ukanisaidie kuuchukua” akasema Chambao na kumtaka Deus amfuate wakaenda katika gari Fulani aina ya land cruiser V8 ambalo kulikuwa na watu wawili nje wamesimama.
“Anaitwa Deus Mtege mtaongozana naye kwenda kushughulikia ule mzigo” Kamishna akawaambia wale jamaa wawili waliokuwa nje ya lile gari.Deus akafunguliwa mlango akaingia ndani ya gari na gari likaondoka
Kamishna akajaribu kupiga zile namba za Yule mtu
aliyempigia lakini hazikupatikana “Yale mambo ya Deus yamenikumba na mimi.Hawa jamaa wataniendesha kama gari bovu,wataniamuru nifanye kila wakitakacho kwa kutishia nisipofanya hivyo watasambaza video hiyo ya mke wangu.Ngoja kwanza nimalize msiba wa mke wangu kisha nitajua nini nifanye.Siwezi kukubali kuwa mtumwa wa watu hawa ! akawaza Kamishna Chambao ************
Mathew Mulumbi aliwasili nyumbani kwa Kamishna Chambao.Kutokana na uwingi wa magari yaliyokuwa yanafika pale nyumbani kwa Kamishna kuliwekwa watu wawili waliokuwa wakiongoza magari yaliyokuwa yakiingia na kutoka.Mathew akaelekezwa sehemu ya kuegesha halafu akashuka na kuelekea ndani.Akasimama sehemu na kuangaza angaza kama angeweza kuonana na Kamishna Chambao lakini watu walikuwa wengi akalazimika kuingia ndani ya nyumba akamuuliza jamaa mmoja aliyekuwa na faili akampeleka nyuma ya nyumba ambako Kamishna Chambao alikuwa anazungumza na wazee Fulani.Alipo muona Mathew akawataka radhi wale wazee na kuinuka akamfuata
“Mathew karibu sana” akasema Chambao
“Ahsante mzee.Pole sana” akasema Mathew
“Ahsante” akasema
Chambao na kumchukua Mathew hadi katika chumba kimoja kilichokuwa na sofa mbili wakaketi
“Mathew nimefarijika sana kukuona hapa.Vipi kuna maendeleo yoyote katika kuwatafuta wale mashetani? Akauliza Kamishna Chambao “Mpaka sasa bado kuna hatua ndogo sana tumeipiga katika kuwatafuta hawa jamaa.Kuna mambo nimeanza kuyagundua japo yanaleta mwangaza mdogo lakini kwa ujumla bado kuna giza nene mbele yetu” akasema Mathew na Kamishna Chambao akainamisha kichwa
“Kamishna Chambao
nimetaarifiwa kwamba Deus amekuja huku kwako.Yuko wapi? Nahitaji kuzungmza naye” akasema Mathew “Deus? Akauliza Chambao kwa mshangao kidogo “Kamishna tafadhali namuhitaji Deus kuna masuala ya msingi nataka kuzungmza naye.Where is he? Akauliza tena Mathew
“Deus alifika hapa.Nilimuhitaji kuna masuala ya kikazi nilitaka kuzungumza naye lakini baada ya kufika hapa kuna kazi nimemuomba anisaidie hivyo ameondoka na vijana wangu kwenda kuchukua mzigo
Fulani”
“Amekwenda wapi?
Nielekeze nitamfuata huko” akasema Mathew “Mathew huniamini ninachokwambia? Kama unamuhitaji Deus msubiri hapa atarejea ! akasema Kamishna kwa sauti ya juu kidogo
“I’m curious ! Kuna watu wengi sana hapa msibani na wengine hawana kazi yoyote wanapiga soga na kucheza karata kwa nini ukawaacha hao wote na kumuita Deus aje akusaidie?
“Mathew sihitaji mahojiano nimekwisha kwambia Deus yupo na kama unamuhitaji msubiri atarejea muda si mrefu.Sihitaji maswali tena kuhusu Deus” akasema kamishna akimtazama Mathew kwa macho ya ukali “Una lingine lililokuleta hapa au ni hilo tu? Akauliza “Kamishna nilikutazama machoni ulidhamiria kumuua Deus na kama tusingekunyang’anya ile
bastola hivi sasa tayari Deus angekwisha uawa.Nafahamu bado una hasira naye na ndani mwako bado roho ya kulipiza kisasi haijakutoka.I still need him to find these devils.Kama kitu chochote kibaya kitamtokea Deus you’ll be responsible and you’ll answer to me ! akasema Mathew
“Are you threatening me Mathew?
“This is not a threat Sir,it’s the truth ! Kama una mpango wowote mbaya kwa Deus sitisha mara moja kwani madhara yake ni makubwa.Umenielewa mzee? Akauliza Mathew
“Mathew mimi huwa
sipendi kutishwa na vijana wasio na adabu kama wewe.Nina mzigo mzito hivi sasa wa kuondokewa na mke wangu halafu unakuja bila adabu na kuanza kunitolea vitisho ! Who are you? Akafoka Kamishna Chambao “Kamishna nimekueleza ukweli.Nataka ndani ya saa moja Deus awe amerejea nyumbani kwa Dr Fabian ama sivyo usinione mbaya ! akasema Mathew “Mathew get out now ! akafoka Kamishna Chambao na Mathe akafungua mlango akatoka na kumuacha Kamishna Chambao akihema haraka haraka.Mara tu
alipotoka ndani ya kile chumba akachukua simu akampigia Ruby. “Mathew umemuona
Deus?
“Ruby kuna kitu hakiko sawa hapa”
“Kwa nini Mathew? “Nakuomba udukue simu ya Kamishna tufahamu watu aliowasiliana nao kabla ya kupiga simu na kumuhitaji Deus” akasema Mathew na kwenda katika gari lake
akisubiri kupata taarifa kutoka kwa Ruby
“Nimechanganyikiwa.Huy u Mathew anaweza akafahamu kuwa nimewasiliana na wale jamaa na kufuata maelekezo yao ya kumkabidhi Deus.Natamani nimweleze ukweli Yule kijana lakini naogopa wale jamaa wakijua wanaweza wakaachia video hiyo ya mke wangu na kunidhalilisha.Sitaki kudhalilika,sitaki mke wangu adhalilike.Kwa nini lakini mke wangu aliamua kufanya kitu kama kile? Kwa sasa naamini kabisa kwamba alitumiwa na hawa jamaa kumpata Deus ili mipango yao ya kumuua Gosu Gosu ifanikiwe.Jambo hili litanipasua kichwa changu kwa mawazo ! akawaza Kamishna
Chambao
“Sasa nifanye nini? Tayari nimekwisha mkabidhi Deus kwa wale jamaa kama walivyotaka na sifahamu watamfanya nini lakini chochote watakachomfanya anastahili kwani amenifanyia jambo baya mno ! Potelea mbali ngoja niliache suala hili kama lilivyo na si Mathew wala mtu mwingine yeyote atakayenifanya chochote” akawaza Chambao na kutoka mle ndani
Wakati Mathew akisubiri jibu kutoka kwa Ruby simu yake ikaita zilikuwa ni namba ngeni akaipokea
“Hallow” akasema Mathew
“Hallow
Mathew,unazungumza na
Zawadi”
“Zawadi.Unaendeleaje?
akauliza Mathew “Ninaendelea vizuri.Mathew nimeomba simu kwa daktari nikupigie kuna jambo ninataka kukueleza”akasema Zawadi. “Nakusikiliza Zawadi” akasema Mathew “Utanisamehe kuna jambo sikuwa nimekueleza uliponiuliza kuhusu Naomi Bambi”akasema Zawadi “Usijali Zawadi kama kuna jambo lolote unalo naomba
unieleze tafadhali” akasema
Mathew
“Mathew siwezi kukueleza simuni.Nakuomba tafadhali kama una nafasi uje hapa hospitali nikueleze” akasema
Zawadi
“Sawa Zawadi ninakuja hapo sasa hivi” akasema Mathew na kuwasha gari akaondoka.Akiwa garini akampigia simu Ruby “Ruby nimepata dharura kidogo.Nimepigiwa simu na Zawadi amesema kuna jambo anataka kunieleza ambalo anasema ni muhimu.Ninamfuata hospitali kumsikiliza.Kama kuna chochote utakipata katika simu ya mzee Chambao utanijulisha” akasema Mathew “Mathew una hakika kweli kuna jambo anataka kukueleza? Nina wasi wasi yawezekana labda anatumiwa na hawa jamaa ili uende hospitali na wakufanyie shambulio la kustukiza.Hawa jamaa nimewaogopa sana” akasema Ruby
“Ruby
usihofu.Ninamuamini Zawadi”
“Sawa Mathew
nitakujulisha kile nitakachokipata katika simu ya mzee Chambao” akasema Ruby
Mathew alifika katika hospitali ya Katihar akaelekea moja kwa moja katika chumba alimo lazwa
Zawadi.Alisalimiana na walinzi akawauliza kama kuna tatizo lolote lakini hakukuwa na tatizo.Akaingia ndani ya chumba ,Zawadi hakuwa amelala.
“Hallow Zawadi” akasema
Mathew
“Mathew ninashukuru umefika.Kuna jambo sikuwa nimekueleza lakini baada ya kutafakari sana nimeona nikueleze linaweza kuwa na msaada kwako” “Nakusikiliza Naomi” akasema Mathew
“Ulinifuata na kuniuliza kuhusu Naomi
Bambi.Nilikueleza kwamba nilipelekwa na Jerome aliyekuwa mpenzi wangu kwenda kumchoma sindano msichana huyo.Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuonana naye ana kwa ana lakini sura yake nilikwisha iona hapo kabla” akanyamaza kidogo halafu akaendelea “Msichana Yule jina lake si
Naomi Bambi.Aliitwa Zowe
Adam Watwila” akasema
Zawadi
“Umefahamuje jina hilo? “Siku mbili kabla Jerome hajanipeleka kumchoma sindano Naomi Bambi, alikuja kwangu akiwa amelewa sana akaniomba nimuhifadhie mkoba fulani,kesho yake alipoondoka nikaufungua mkoba wake na ndani nilikuta faili lina nyaraka za hospitali zenye picha ya msichana anaitwa Zowe zinazoeleza kwamba msichana Yule alikuwa na maradhi ya akili.Siku ya pili nilipopelekwa kumchoma sindano Naomi ndipo nikagundua kwamba
Yule msichana Zowe niliyemuona katika lile faili la Jerome ndiye Yule niliyekwenda kumchoma ile sindano japo alikuwa anaitwa jina lingine la Naomi Bambi.Sijajua kwa nini alikuwa na majina mawili lakini jina lake halisi ni Zowe kwa sababu kulikuwa na nakala ya cheti cha kuzaliwa
katika lile faili” akasema
Zawadi
“Zawadi una uhakika na hiyo taarifa unayonipa?
“Ndiyo nina uhakika na sijawahi kumweleza mtu yeyote jambo hili.Nimeona nikwambie wewe pengine linaweza kukusaidia katika uchunguzi wako”akasema
Zawadi
“Unaweza ukakumbuka
Nyaraka hizo zilitoka hospitali gani? Akauliza Mathew “Siku iliyofuata baada ya kumchoma sindano Naomi,alikuja Jerome na kunitaka nimpatie ule mkoba wenye faili lakini kabla sijampatia ndipo ulipotokoea ule ugomvi uliopelekea kifo chake.Hata hivyo kuna sehemu
ndani ya nyumba yangu ya
zamani nililificha faili hilo na nina uhakika bado lipo.Nitakuelekeza ukalichukue.Naamini linaweza likawa na msaada kwako” akasema Zawadi
“Zawadi nitashukuru sana kama utanisaidia niweze kulipata hilo faili ambalo naamini litakuwa na msaada mkubwa sana” akasema Mathew na Zawadi
akamuelekeza mahala
alipolificha faili hilo katika ile nyumba yake ya zamani. “Kuna chochote kingine ambacho unakumbuka kinaweza kunisaidia? Akauliza
Mathew
“Kwa sasa ni hilo tu kama kuna lingine lolote nitakumbuka nitakujulisha lakini nakuomba Mathew utimize ahadi yako ya kuhakikisha ninakuwa salama baada ya kutoka hapa hospitali” akasema Zawadi
“Kuhusu usalama usiwe na shaka Zawadi kwani tayari unaona kuna askari wenye silaha wanakulinda na hata ukitoka hapa utakwenda kukaa sehemu salama,naomba uniamini” akasema Mathew akamuaga Zawadi na kuondoka.Aliingia garini akampigia simu Kamishna Chambao ili kufahamu kama Deus amekwisha rejea lakini simu haikupokelewa. “Bado nina wasi wasi sana na usalama wa Deus.Kwa nini Chambao amekataa kupokea simu yangu? Akajiuliza Mathew na kumpigia simu
Ruby
“Hallo Mathew”
“Ruby ulifanikisha ile kazi niliyokupa? Akauliza Mathew “Hapana Mathew.Niliiacha kwa muda nikaenda kuwabebembeleza watoto.Kwa sasa hali ni tofauti na wakati ule Mathew.Kwa sasa mimi ni mama hivyo ninawajibika pia kuwaangalia watoto.Baada ya muda nitarejea tena ofisini kuendelea na kazi.Vipi huko kuna kitu umekipata? Akauliza
Ruby
“Ndiyo kuna jambo kubwa nimelipata.Niko njiani ninaelekea sehemu Fulani na baada ya kutoka huko nitakuja moja kwa moja nyumbani kwako” akasema Mathew “Kuna nyakati natamani
jambo hili limalizike haraka ili Ruby na familia yake waendelee na maisha yao kwa amani.Tangu nimemshirikisha katika jambo hili kuna mambo mengi ameyaweka pembeni.Kwanza ni kwa familia yake.Muda ambao alipaswa kuwa na watoto wake anautumia katika kushughulikia jambo hili,pili nimemuingiza katika hatari na sasa analazimika kutokutoka ndani.Jambo hili likimalizika nijatiweka mbali kabisa nao” akawaza Mathew “Kabla ya kwenda katika nyumba ya zamani ya Zawadi natakiwa kwanza kwenda nyumbani kwangu kuchukua zana za kuniwezesha kuingia mle ndani.Natakiwa vifaa vya kufungulia mlango nk.Ngoja kwanza niende nyumbani kwangu nikachkue vifaa halafu nitaelekea katika ile nyumba ya Zawadi” akawaza Mathew
**********
Alipokaribia kufika nyumbani kwakeMathew aliona vimuli vumuli vya magari ya polisi karibu na nyumba yake.
“Mbona kuna magari ya polisi karibu na nyumba yangu? Akajiuliza Mathew na kusimamisha gari akachukua simu na kumpigia Victor lakini simu yake haikupatikana.
“Mbona ninaanza kupatwa na wasiwasi? Simu ya Victor haipatikani na magari ya polisi ninayaona karibu na nyumbani kwangu” akawaza Mathew.
“Ngoja nikaangalie kuna nini kimetokea pale.Yawezekana kuna ajali imetokea au kuna tukio la ujambazi” akawaza Mathew na kuwasha gari akaelekea nyumbani kwake. Utepe wa njano wa kuwazuia watu kupita ulizungushwa katika geti la kuingilia ndani na ulinzi uliimarishwa.Mathew akasimamisha gari akashuka na kuwafuata askari polisi akawasalimu
“Naitwa Mathew Mulumbi ndiye mmiliki wa nyumba hii.Nini kimetokea hapa? Akauliza Mathew na askari wote wakamtazama kwa mshangao
“Wewe ndiye mmiliki wa nyumba hii? Akauliza mmoja wa askari
“Ndiyo mimi” akajibu Mathew na mmoja wa askari akamtaka apite wakaeleka ndani
Kulikuwa na askari katika nyumba ya Victor na wengine walikuwa katika nyumba yake kubwa
“Kuna nini kimetokea hapa kwangu? Akajiuliza Mathew akiwa ameogozana na
Yule askari hadi ndani.Askari Yule aliyeongozana naye akapiga saluti kwa mkuu wake na kumjulisha kwamba Yule aliyeongozana naye ni Mathew Mulumbi mmiliki wa ile nyumba
“Wewe ndiye Mathew
Mulumbi? Akauliza Yule kiongozi wa askari “Ndiyo.Kuna nini kimetokea hapa afande? Akauliza Mathew
“Mathew Mulumbi
kuanzia sasa uko chini ya ulinzi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na mauaji” akasema Yule kamanda “What? Mathew akasema kwa mstuko na kuupeleka mkono wake mahala ilipo bastora yake mara akasikia vyuma vikilia.Askari walikuwa wanaweka sawa bunduki zao
“Oh my God ! akasema
Mathew
“Mathew Mulumbi uko
chini ya ulinzi kuanzia sasa hivyo inua mikono yako juu tafadhali ! akasema Yule kamanda na Mathew akainua mikono juu askari mmoja akamsogelea na kumfunga pingu akazichukua bastora zake pamoja na simu.Tayari kulikuwa na waandishi wa
habari wakimpiga Mathew picha
“Afande nani kawapa taarifa hizo kuwa mimi ninajihusisha na biashara za dawa za kulevya? Hamnifahamu mimi ni nani? Akauliza Mathew na Yule kiongozi wa kikosi kile cha askari akawataka askari kumpandisha Mathew ghorofani moja kwa moja hadi chumbani kwake.Alipigwa na butwaa baada ya kukuta paketi za dawa za kulevya zikiwa kitandani.Makabati ya nguo yalikuwa wazi na nguo zilikuwa zimesambaa chini.Chumba chote kilivurugwa mno.Kilichomstua zaidi ni kasiki lake ambalo huhifadhi vitu muhimu pamoja na fedha lilikuwa wazi na ndani yake kulikuwa na paketi za dawa za kulevya. “Hapana hii si kweli hata kidogo ! akasema Mathew
“Mathew Mulumbi tunazo taarifa zako muda mrefu kwamba unajihusisha na biashara hii ya dawa za kulevya lakini tulikuwa tunakutafuta na leo hii tumekupata.Huu mzigo wote tumeukuta chumbani kwako” akasema Yule mkuu wa kikosi na kutoka mle chumbani wakaelekea katika chumba kingine ambacho kilikuwa na askari kadhaa ndani.Kabla ya kuingia mle ndani Mathew akahisi harufu ya damu.Mara tu walipoingia ndani ya kile chumba Mathew akastuka baada ya kuikuta miili miwili ikiwa juu ya meza.Mwili mmoja ukiwa ni wa Deus Mtege mkuu wa gereza la Kimondo na mwili mwingine ukiwa ni wa Victor mwangalizi wake wa nyumba.Miili yote miwili ilikuwa tupu na mwili wa Deus ulikuwa umepasuliwa tumbo,utumbo wote umetupwa nje na ndani ya tumbo kukaonekana pakiti za dawa za kulevya zikiwa zimepangwa kiustadi.Mathew alichanganyikiwa.
“Hii ni njozi au ni kitu cha kweli? Akajiuliza huku waandishi wa habari wakiendelea kumpiga picha.Mathew akachukuliwa na kupelekwa katika mojawapo ya magari ya polisi yaliyokwepo pale nyumbani kwake.
“Ee Mungu naomba
unifumbue macho yangu.Hiki kitu ninachokishuhudia ni cha kweli au niko njozini?
Akaendelea kuwaza Mathew huku upekuzi ukiendelea ndani ndani ya nyumba yake “Hapana hii si njozi.Hili ni tukio la kweli kabisa.Deus ameuawa na Victor pia ! akawaza Mathew na machozi yakamtoka.
“Wamemuua Victor !
Maskini Victor alikuwa kijana mpole sana asiye na tatizo na mtu.Nimekaa naye kwa muda mrefu na amekuwa ni kama mdogo wangu wa damu” akawaza Mathew kwa uchungu “Nafahamu haya yote yamefanywa na wale wale jamaa niliokuwa nawachunguza.Kweli hawa jamaa si watu wa kufanyia mchezo hata kidogo.Wameniwahi na kuniingiza katika kesi mbaya ya dawa za kulevya na mauaji.Kwa hapa sina ujanja kesi hii waliyoniangishia ni kesi mbaya mno.Kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimeingiza ndani mwangu.Kasiki langu likafunguliwa na dawa za kulevya zikaingizwa ndani yake.Ni Gosu Gosu pekee anayefahamu namba za kufungulia kasiki langu lakini licha ya namba ili kasiki lifunguke lazima niweke kidole gumba kwa ajili ya kusomwa alama.Aliyefungua kasiki langu ametoa wapi alama zangu za vidole? Naweza kusema haya ni maajabu makubwa.Kibaya zaidi ni kesi ya mauaji.Wamemuua Deus na kumleta hapa kwangu kisha kumpasua ili ionekane nilikuwa nataka kuutumia mwili wake kusafirishia dawa za kulevya.Huu ni ukatili mkubwa sana.Hawa watu ni mashetani wakubwa.Dah ! Bado siamini kama jamaa wameniwahi na kunifanyia namna hii.Wameamua kuniangamiza kabisa” akawaza
Mathew
***********
Saa nane za usiku simu ya Ruby ikatoa mlio wa ujumbe mfupi.Akainuka kitandani akaichukua simu na kuusoma ujumbe ule ulitoka kwa mtu ambaye hakumfahamu.Ujumbe ule ulimstua sana.
“Run ! They’re coming for you !
Aliurudia tena kuusoma ujumbe ule hakuuelewa ikamlazimu amuamshe mume wake akamuonyesha ujumbe ule.
“Ni nani huyu mtu?
Akauliza Dr Fabian
“Simfahamu ni namba
ngeni kabisa katika simu yangu”akajibu Ruby “Ana maanisha nini kwa ujumbe huu? Akauliza Dr
Fabian
“Ngoja nijaribu kumpigia nimfahamu ni nani” akasema Ruby na kupiga ile namba lakini
haikupatikana.Akampigia simu Mathew lakini naye simu yake haikupatikana.
“What’s going on? Kwa nini Mathew amezima simu
yake? Akauliza Ruby
“Mathew hawezi kuzima simu yawezekana akawa mahala ambako mtandao wa simu si mzuri au simu yake imeisha chaji” akasema Dr
Fabian
“Nini unashauri kuhusu ujumbe huu? Akauliza Ruby “Inaniwia ugumu kusema chochote kwa sababu hatumfahamu aliyetuma ujumbe ni nani na ana malengo gani.Nadhani usubiri hadi pale atakapokuwa anapatikana halafu atatuleza kwa nini ametuma ujumbe kama huu.Au yawezekana mtumaji alikosea kutuma na ujumbe huu ukafika kwako” akasema Dr Fabian.Ruby akatafakari kidogo na kusema “Fabian kumbuka tuko katika mapambano na watu hatari ambao hatuwafahamu ni akina nani nahisi kama ujumbe huu haujakosea njia.Mtumaji ameulenga kwangu moja kwa moja” akasema Ruby
“Kama kweli amekulenga wewe kwa nini basi asipige simu na kujitambulisha yeye ni nani na …” akanyamaza Dr Fabian baada ya ujumbe mwingine kuingia katika simu ya Ruby akaufungua akausoma “Please run.They’re coming for you !
“Ujumbe ule umejirudia tena na mtumaji akiwa ni yule Yule mmoja.Fabian tusipuuze ujumbe huu yawezekana ukawa na maana” akasema
Ruby
“Jaribu kumtumia ujumbe huyo mtu aliyekutumia ujumbe muulize yeye ni nani na kwa nini amekutumia ujumbe wa namna hii? Akauliza Dr Fabian
“Who are you? Ruby akaandika ujumbe na kuutuma “I warn you, run ! They’re after you ! ujumbe wa majibu ukarejea
“Who are they? Ruby
akauliza lakini hakujibiwa akaanza kuingiwa na wasi wasi “Fabian hatutakiwi kumpuuza mtu huyu.Kuna kila dalili kwamba anajaribu kunionya kuhusu hatari iliyo mbele yangu.Yawezekana wale jamaa tunaowachunguza wananifuatilia” akasema Ruby “Huyo mtu aliyekutumia ujumbe huu kwa nini hataki kusema yeye ni nani? Amefahamu vipi kama kuna watu wanakufuatilia? Usihofu mke wangu hakuna tatizo lolote.Kuwa na amani hakuna anayeweza kuingia hapa kwani kuna ulinzi wa kutosha” akasema Dr Fabian na Ruby akarejea tena kitandani ingawa bado alikuwa na mawazo mengi sana.Akajaribu kumpigia simu Mathew kwa mara nyingine lakini simu yake haikupatikana. “Mathew ana tatizo gani hadi simu yake haipatikani? Au amepatwa na tatizo huko alikoenda kumfuata Zawadi? Nakumbuka nilimuonya yawezekana huu ukawa ni mtego amewekewa na alipoenda huko akapatwa na matatizo ndiyo maana hapatikani simuni” akawaza Ruby na kunyanyuka akamuamsha Dr Fabian ambaye tayari alianza kupitiwa na usingizi
“Fabian tafadhali naomba tusiupuuze ujumbe huu.Ninahisi kuna tatizo.Niliwasiliana mara ya mwisho na Mathew akanitaarifu kwamba anakwenda kuonana na Zawadi kuna taarifa anakwenda kumpa nikamuonya kwamba awe makini kwani ule unaweza kuwa ni mtego na mara tu atakapofika hapo atakutana na wale jamaa.Kitendo cha simu yake kutokupatikana kinanipa wasiwasi.Naamini lipo tatizo na huyu mtu ameamua kunijulisha mapema ili nichukue tahadhari.Fabian hawa si watu wa kufanyia mzaha hata kidogo” akasema
Ruby
“Kwa hiyo unashauri nini? Akauliza Dr Fabian “Find somewhere safe for me and my kids.Baada ya kujiridhisha kwamba hakuna hatari yoyote tutarejea hapa lakini kwa usiku huu hatuwezi kuendelea kulala hapa na kuwaweka watoto katika hatari” akasema Ruby
“Ndiyo maana sikutaka Mathew akushirikishe katika jambo hili kwani nilifahamu ukiingia katika hatari basi familia nzima itakuwa hatarini” akasema Dr Fabian “Fabian hayo yamekwisha pita.Tafadhali tufanye haraka tuwaondoe watoto mahala hapa” akasema Ruby na Dr Fabian akakuna kichwa “Fabian hujawahi kunieleza lakini nafahamu una mahala pako pa siri ambako anaweza ukajificha pale kunapotokea hatari kwake na familia yake.Take us there” akasema Ruby.Dr Fabian akampigia simu mmoja wa walinzi wake aliyekuwepo usiku ule akamtaka aandae gari kwa safari ya dharura.
Haraka haraka Ruby
akapakia nguo na vitu vyote vya watoto ambavyo wangevihitaji kisha wakaingia garini na kuondoka. Baada ya dakika zipatazo arobaini wakawasili katika nyumba Fulani ambayo ilikuwa mara ya kwanza kwa Ruby kufika.llikuwa ni nymba nzuri wakakaribishwa ndani “Ruby hapa ni mahala salama kwa wewe na watoto kuwepo kwa sasa.Ni nyumba yangu ya siri na ina ulinzi wa kutosha” akasema Dr Fabian na kumzungusha Ruby kaika sehemu kadhaa za nyumba ile.
Baada ya kuhakikisha Ruby na watoto wako salama,Dr Fabian akaondoka kurejea katika makazi yao ya
kawaida
“Hapa ndipo ninapomchukia Mathew.Amemuingiza mke wangu katika hatari na sasa familia nzima iko katika hatari kubwa” akawaza Dr Fabian na kuchukua simu akajaribu kumpigia Mathew lakini simu yake haikupatikana. Ruby alihakikisha watoto wake wamelala na yeye akapanda kitandani lakini hakuweza kupata usingizi.Akachukua kompyuta
yake na kuanza kuifuatilia ile namba iliyomtumia ujumbe lakini ni namba ambayo haikuwa imesajiliwa “Aliyenitumia ujumbe huu ni mmoja wao kwani wamekuwa na tabia ya kutumia laini za simu ambazo hazijasajliwa.Laini za simu ambazo hazijasajiliwa haziruhusiwi kutumika hapa nchini lakini hawa jamaa wanazitumia.Je mitandao ya simu ambayo hawa jamaa wanaitumia hawajui kama kuna laini za simu ambazo hazijasajiliwa zinatumika? Akaijiuliza Ruby na kukumbuka kitu “Mathew alinipa kazi ya kudukua simu ya Kamishna Chambao.Ngoja niendelee nayo” akawaza Ruby na
kuendelea na zoezi lile.Kwa kutumia mfumo wa SNSA aliweza kudukua mawasiliano ya Kamishna Chambao na kupitia namba moja moja ambazo Kamishna Chambao aliwasiliana nazo kabla ya kupiga simu kwa Dr Fabian akimtaka Deus na simu ya
mwisho ambayo Chambao alipigiwa kabla ya kumpigia Dr
Fabian ilimtoa Ruby Jasho.Aliyasikiliza mazungumzo yale na kuyarudia
“Ndiyo namtaka Deus Mtege.Yuko hapa Dar es salaam na wewe unafahamu mahala alipo.Nitatuma vijana wangu watakuja nyumbani kwako kumchukua.Nataka ndani ya saa mbili kutoka sasa niwe tayari nimempata.Kama ukipuuza maelekezo yangu nitaiachia video hiyo ambayo naamini hata wewe utachukua maamuzi kama aliyoyachukua mke wako.Fuata maelekezo yangu na video hiyo haitasambazwa.Clock starts now!
“Mathew alikuwa sahihi kwamba Kamishna Chambao hakuwa na malengo mazuri na Deus.Kumbe alipigiwa simu na wale jamaa na kumtaka amkabidhi Deus kwao na kama akipuuza basi wangesambaza video ya mke wake.Hii ilikuwa ni nafasi nzuri ya kuwakamata hawa jamaa lakini kwa nini Chambao akakubali maelekezo yao na kumkabidhi Deus? Kwa nini asingetueleza jambo hili na sisi tungefuatilia na kuwatia nguvuni hao jamaa waliotumwa kwake kwenda kumchukua Deus? Akajiuliza
Ruby
“Yule mzee amefaya jambo la kijinga sana” akawaza Ruby na kujaribu kumtafuta Mathew simuni lakini bado hakuwa anapatikana
“Where are you Mathew?
Are you in trouble? Akajiuliza na kuanza kuifuatilia ile namba ya simu iliyowasiliana na Kamishna Chambao “Damn ! akapiga meza kwa
hasira
“Haijasajiliwa tena ! akasema Ruby akachukua simu yake na kumpigia mume wake Dr Fabian “Fabian tayari umefika nyumbani? Akauliza “Ninakaribia kufika nyumbani.Kuna nini?” akajibu
Dr Fabian
“Kuna jambo
nimelipata.Chambao amemuuza Deus” akasema Ruby na kumueleza Dr Fabian kile alichokipata katika simu ya Kamishna Chambao “Ruby una hakika na hiki ulichokipata? Akauliza Dr
Fabian
“Ndiyo Fabian” akajibu Ruby na Dr Fabian akavuta pumzi ndefu
“Sikutegemea kama
Chambao angeweza kufanya kitu cha kijinga namna hii.Kwa kuwakubalia wanachokitaka tayari amekubali kuwa mtumwa wao na atafanya kila watakachomuamuru kwa kuogopa video ya mke wake kusambazwa.Where is Mathew? Akauliza Dr Fabian kwa hasira
“Mpaka sasa Mathew
hapatikani simuni” akajibu
Ruby
“Inatakiwa tukae tushauriane kuhusu jambo hili.Nifahamishe pale Mathew atakapokuwa amepatikana simuni.Umemfuatilia huyo jamaa aliyewasiliana naye ukajua mahala alipo? Akauliza
Dr Fabian
“Ni mtandao ule ule ambao laini zao hazijasajiliwa hivyo ni vigumu kujua ni nani” akasema Ruby “Wakati tunamsubiri Mathew endelea kuchimba
zaidi” akasema DrFabian
**********
“Dar es salaam”
Ndivyo alivyoanza msomaji wa taarifa ya habari ya saa kumi na mbili za asubuhi katika kituo kmoja kikubwa cha runinga “Jeshi la polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya usiku wa kuamkia leo limemkamata mmoja wa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya hapa nchini.Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuvamia makazi ya kigogo huyo,mkuu wa kikosi hicho cha kupambana na dawa za kulevya nchini Safari Twaijuka alisema kwamba walivamia makazi ya kigogo huyo mkubwa wa dawa za kulevya baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna mzigo mkubwa wa dawa za kulevya umeingizwa ndani ya nyumba
hiyo.Jeshi la polisi pia linamshikilia mfanya biashara huyo kwa mauaji ya watu wawili na mmoja wao akiwa ni mkuu wa gereza la Kimondo lililoko Arusha .Tuungane na mwandishi wetu kwa taarifa zaidi” akasema mtangazaji na taarifa ya mwandishi aliyeambatana na jeshi la polisi eneo la tukio ikawekwa.
“Ni usiku wa saa sita
lakini jeshi la polisi kitengo
cha kupambana na dawa za kulevya nchini hawalali wako kazini wakiendelea kupambana na wafanya biashara a dawa za kulevya .Usiku huu kitengo hicho kimevamia makazi ya mmoja wa kigogo wa biashara hiyo hapa nchini bilionea Mathew Mulumbi ambaye ni mmiliki wa makampuni kadhaa hapa nchini na kukamata shehena kubwa ya dawa za kulevya.Niko hapa na mkuu wa kitengo cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya hapa nchini kamanda
Safari Twaijuka.” Akasema Yule mwandishi na kumsogelea kamanda Safari
“Kamanda Safari
unalizungumziaje tukio hili la leo? Akauliza mwandishi
“Kama mnavyoona ndugu waandishi wa habari kwamba usiku wa leo tumemkamata mmoja wa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya hapa nchini anayejulikana kama Mathew Mulumbi ambaye ni mmiliki wa makampuni
kadhaa makubwa hapa nchini.Tulipata taarifa kwamba kuna mzigo mkubwa wa dawa za kulevya umefichwa hapa hivyo tukavamia na kufanikiwa kukamata kilo zaidi ya mia mbili ambazo tunaamini ni dawa za kulevya zilizokuwa zimefichwa katika chumba cha kulala cha kigogo huyo.Pamoja na kukamata mzigo huo mkubwa wa dawa za kulevya ndani ya nyumba hii pia tumekuta miili ya watu wawili wakiwa wameuawa .Tumeweza kumtambua mmoja wa watu waliouawa ni mkuu wa gereza la Kimondo lililoko Arusha Kamishna msaidizi wa magereza Deus Mtege.Mtu mwingine bado tunaendelea na jitihada za kumtambua ni nani.Mmoja wa watu hao wawili alikuwa amepasuliwa tumbo,kuondolewa utumbo kisha kujazwa pakiti za dawa za kulevya tayari kwa kusafirishwa.Inaonekana hii imekuwa ni moja ya njia zao za kusafirisha dawa za kulevya kwa kuua watu na kujaza dawa katika matumbo yao kisha kuwasafirisha kwenda mahala wanakojua wao.Ni ukatili mkubwa sana umefanyika.Tutaendelea kumfanyia mahojiano mtuhumiwa na kuufahamu mtandao wake wote kwani tunaamini hayuko peke yake.Tunatoa wito kwa wananchi tuendelee kushirikiana na jeshi la polisi katika vita hii ya dawa za kulevya hapa nchini.Toeni
taarifa za wafanya biashara wakubwa kama hawa wanaoingiza dawa za kulevya hapa nchini na kuharibu watoto wetu wakati wenyewe wakiishi maisha mazuri” akasema Kamanda Safari huku picha ya dawa za kulevya zilizokutwa chumbani kwa Mathew zikionyeshwa vile vile zikaonyeshwa picha miili miwili iliyofunikiwa ikitolewa ndani ya nyumba ile na kuingizwa katka gari la polisi Dr Fabian aliyekuwa
akitazama taarifa ya habari baada ya kutoka mazoezini alijikuta akiangusha glasi ya maji aliyokuwa ameishika mkononi kwa mstuko mkubwa alioupata baada ya kutazama taarifa ile.Kwa sekunde kadhaa akajikuta akishindwa hata kuinua mguu wake.
Dr Fabian Kelelo alibaki amesimama kWa sekunde kadhaa akihisi kama viungo vya mwili wake havifanyi kazi akaingiwa na hofu kubwa.Taratibu akajaribu kuinua mguu wa kulia ukainuka,akainua mguu wa kushoto ukainuka,akatikisa mikono ikatikisika,akashuka pumzi
“Thank you Lord !
akasema huku akihisi joto la ghafla na jasho jembamba kuanza kumtiririka
“My pills” akasema na kutembea haraka haraka kuelekea chumbani kwake akafungua kabati na kutoa kopo la dawa haraka haraka akachukua vidonge viwili akameza halafu akavua fulana ambayo tayari ilikwisha loana jasho akajilaza kitandani. “Mstuko nilioupata ni mkubwa ndiyo maana hali hii imenitokea.Dah ! bado nashindwa kuamini taarifa ile niliyoitazama kama ni ya kweli.Mathew Mulumbi ! akawaza Dr Fabian na kuinuka akakaa.
“Ee Mungu nini hiki kinaendelea hapa nchini kwetu? Nani hawa wanaofanya mambo ya kutisha namna hii? Akaendelea kuwaza Dr Fabian.Akawasha luninga iliyokuwamo chumbani akakuta tayari taarifa ya habari imemalizika na kilichokuwa kinaendelea ni usomaji wa vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali ya siku hiyo
“KIGOGO DAWA ZA
KULEVYA MBARONI,BILIONEA MUUZA UNGA
AKAMATWA,JASUSI NGULI AFANYA MAUAJI YA
KINYAMA …….Hivi ni baadhi tu ya vichwa vya habari vilivyopamba kurasa za mbele za magazeti karibu yote ya siku ile.Dr Fabian akaweka mikono kifuani alihisi mapigo ya moyo kumwenda kasi isivyo kawaida akachukua simu haraka haraka akampigia daktari wake na kumtaka afike nyuumbani mara moja.Baada ya kuwasiliana na daktari wake akampigia pia simu Ruby “Goodmorning Darling” akasema Ruby “Goodmorning
angel.Mnaendeleaje huko? “Sisi tuko salama.Fabian are you okay:? Akauliza Ruby baada ya kuhisi kuna utofauti katika sauti ya mume wake “My love I’m not okay” akasema Dr Fabian na Ruby akastuka
“Kuna nini Fabian? Akauliza Ruby kwa wasiwasi.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu na kusema “My love,anza kujiandaa
kwa safari”
“Safari?! Ruby akashangaa “Safari gani Fabian?
Akauliza
“You are leaving today” akasema DrFabian “Leaving? Ruby
akashangaa
“Ndiyo
mpenzi,mnaondoka wewe na watoto baadae leo,ninafanya taratibu za usafari ili muweze kuondoka hapa nchini na kwenda nje ya nchi.Hali ya usalama si nzuri hapa Tanzania” akasema Dr Fabian “Fabian
sijakuelewa.Naomba maelezo
ya kina tafadhali ! akasema
Ruby
“Ruby tafadhali naomba tusiweke mabishano katika jambo hili ambalo ni muhimu sana kwa usalama wako na watoto.Siwezi kukubali kuwaweka katika hatari” akasema Dr Fabian “Fabian tumekwisha
lizungumza hili jambo na tukakubaliana kushirikiana na Mathew katika kuwatafuta hawa jamaa na kumsaidia Gosu Gosu aweze kutoka gerezani na tayari kuna mwanga umekwisha anza kuonekana.I’m sorry Fabian siwezi kuondoka na kukimbia nje ya nchi kwani itakuwa ni sawa na kuwasaliti ndugu zangu.Mathew ananitegemea sana mimi katika jambo hili”
akasema Ruby “Ruby you don’t understand what’s gong on !.Please naomba tusilifanye suala hili kuwa gumu” akasema Dr Fabian “Fabian wewe ndiye
unayelifanya jambo hili liwe gumu.Mathew ananihitaji sana katika jambo hili na siwezi kuondoka nikawaacha ndugu zangu.Nitasimama nao ! akasema Ruby
“Ruby hawa watu ambao Mathew anawatafuta ni watu hatari mno zaidi ya unavyofikiri” akasema Dr
Fabian
“Nafahamu Fabian lakini sina sababu ya kuwahofia.I’m
not scared at all ! akasema
Ruby
“Ruby like it or not you are leaving the country today ! akasema DrFabian kwa ukali “No ! I’m not going anywhere ! akajibu Ruby
“Ouh Ruby why are you so sturbon ! akasema Dr Fabian kwa sauti ndogo na kuvuta pumzi ndefu
“Sikiliza Ruby.Sikutaka kukwambia lakini umenilazimsha nikueleze.Something
happened last nght”
“What happened? Akauliza Ruby na Dr Fabian akawa kimya
“Fabian what happened?
Akauliza Ruby kwa wasiwasi “Ni kuhusu Mathew ! “Nini kimemtokea
Mathew? Is he okay? Akauliza
Ruby kwa wasi wasi “Jana usiku tulikuwa tunamtafuta Mathew hakuwa anapatikana kumbe kuna masahibu makubwa yalikuwa yamemkuta” akasema Dr Fabian
“Nini kimemkuta Mathew?
Tafadhali naomba unieleze Fabian usinifiche.Is he dead?
Akauliza Ruby
“He’s not dead” “Kama hajafa nini kimemkuta? “Yamemkuta kama yaliyomkuta Gosu Gosu lakini safari hii mambo yakiwa mabaya zaidi kwa upande wake.Hawa watu wameamua kummaliza kabisa” “What happened? Akauliza Ruby na Dr Fabian akamueleza kila kitu kilichotokea.Kwa sekunde kadhaa Ruby alishindwa kuongea kitu akabaki kimya akihema haraka haraka. “Ruby are you there?
Akauliza Dr Fabian “Fa..Fa..Fab…Fabian I….” Ruby akababaika akashindwa aseme nini.
“Oh my God ! akasema Ruby na kuanza kumwaga machozi.
“Ruby ! Ruby please don’t cry ! akasema Dr Fabian “Fabian I need a minute ! akasema Ruby na kukata simu akaingia bafuni na kuanza kulia hakutaka watoto wasikie akilia.
“Mathew !..... My Mathew !...oh God why him ? ! akaendelea kulia Ruby Mlango wa bafuni ukagongwa,Ruby akafuta machozi akidhani labda ni mmoja wa wanae akaenda kuufungua akakutana na Rhoda mtumishi wake anayemsaidia kuwalea wanae. “Unasemaje Rhoda? “Nimepigiwa simu na mheshimiwa Rais amenitaka nije nikutazame nihakikishe uko salama” akasema Rhoda “Niko salama usijali” akasema Ruby “Amesema nikupe simu uzungumze naye” “Nitampigia” akajibu Ruby na kuufunga mlango “Dah ! kweli hawa jamaa ni watu hatari mno.Sikuhisi kama wanaweza wakafanya jambo kama hili.Tayari wamemtengenezea Mathew kashfa kubwa sana ya mauaji na dawa za kulevya.Alianza
Gosu Gosu na sasa ni Mathew.Hawa wote watapotelea gerezani.I won’t
let that happen ! Siko tayari Mathew afungwe gerezani.Kwa namna yoyote ile lazima nihakikishe nimemtoa Mathew katika kashfa hii kubwa ! akawaza Ruby “Huu si wakati wa kumwaga machozi hata kama nimeumia kiasi gani.Hawa ndugu zangu wawili lazima nihakikishe ninawapigania !
Ruby akachukua simu na kumpigia Dr Fabian
“Are you okay my love? Dr Fabian akauliza
“Fabian lazima niwe mkweli kwamba nimestushwa na nimeumizwa mno kwa jambo hili lakini …” akasema Ruby na kunyamaza baada ya Dr Fabian kumkatisha
“Ruby hawa jamaa ni watu hatari mno.They can do anything,they can destroy anyone ! baada ya kuiona hatari hiyo ndiyo maana nimeonea ni vyema wewe na watoto mkaondoka kwenda nje ya nchi ! akasema Dr Fabian
“Ahsante kwa kutujali Fabian lakini siwezi kukimbia.Mathew na Gosu Gosu ni ndugu zangu na lazima nisimame kidete kuwapigania.Wananihitaji mno kwa sasa hivyo sintaogopa na kukimbia”
“Ruby please, najua wewe huwezi kuogopa lakini hii ni kwa ajili ya watoto wetu.Hawa watu lazima wanafahamu unashirikiana na Mathew katika kuwatafuta hivyo ukae ukijua kwamba hata wewe hauko salama.Muda wowote na wewe wanaweza wakakufanya chochote kama walivyowafanya Mathew na Gosu Gosu !
“Fabian kukimbia si suluhisho.Hawa jamaa ni mtandao mkubwa na kama wakikuhitaji huna pa kukimbilia wanaweza wakakufuata sehemu yoyote.Suluhisho pekee ni kupambana nao na kuwashinda ! akasema Ruby
“Ruby hawa watu hatuwezi kupambana nao.Tumejaribu lakini tazama yaliyotokea.Wanaonekana wako hatua nne mbele yetu.Wanafahamu kila kitu zaidi yetu na wako makini katika kuhakikisha hakuna mwanadamu ambaye anaibuka na kuwa hatari kwao ndiyo maana wale wote ambao wamejaribu kuwatafuatilia aidha wameuawa au wamepotelea gerezani kama Gosu Gosu na sasa ni zamu ya Mathew Mulumbi.Ruby sitaki kuendelea na jambo hili.Nimenawa mikono na ninamlaumu sana Mathew kwa kutuingiza katika hatari hii kubwa ! akasema Dr Fabian
“Nisikilize Fabian.Mathew na Gosu Gosu nimekuwa nao kabla mimi nawe hatujafahamiana .Ni ndugu zangu na siwezi kuwaacha hasa kwa wakati huu ambao wananihitaji kuliko wakati wowote.Kwa hiyo mimi siwezi kuondoka nitabaki hapa kuwatafuta hawa watu ni akina nani na kuwasaidia hawa ndugu zangu wawili.Ninataka wewe uondoke na watoto kwenda nje ya nchi!
“Ruby sintaruhusu jambo hilo.Wewe ni mke wangu na siwezi kukuacha ukaingia katika hatari.Kama ni kuondoka tunaondoka sote hakuna atakayebaki ! akasema
Dr Fabian
“Sikiliza Fabian.Kama kweli unanipenda na kunijali kama unavyodai please let me do this for my brothers .Nafahamu hili ni jambo gumu lakini lazima nilifanye”
“Ruby unajiweka katika hatari kubwa.Naomba unisikilize tafadhali ! akasema Dr Fabian
“Ninakuelewa Fabian
lakini katika hili utanisamehe mume wangu.Tayari nimekwisha fanya maamuzi na hakuna anayeweza kunibadili maamuzi yangu” akasema Ruby akionekana kutokuyumba katika msimamo wake
“Ruby my love these people are very dangerous why don’t you understand me?! Akauliza Dr Fabian
“Fabian wewe ndiye hutaki kunielewa.Nimekwisha kwambia I’m not scared of them.Ninachokuomba make
sure the kids are safe.Kuhusu mimi usiwe na hofu I’ll take care of myself” akasema Ruby
“Ruby hata kama ukisema unataka kuwatafuta hawa jamaa bado itakuwa vigumu sana kwako kwani uko peke yako na huna msaada wowote.They’ll kill you” akasema Dr Fabian
“Ninayo sehemu ya
kuanzia.Yule mtu aliyenitumia ujumbe kunionya kwamba wananifuata ndiye nitakayemtafuta.Naamini kuna kitu anakifahamu na ndiyo maana akanipa angalizo” akasema Ruby
“Ni vipi kamaMathew ndiye aliyekuwa anatuma ujumbe ule baada ya kuona hatari kubwa inakukabili?
“Hapana Yule si
Mathew.Nitamtafuta nijue ni nani na yuko wapi.Naamini lazima anawafahamu watu hao na atanisaidia niweze kuwapata”akasema Ruby
“Ni vipi kama ukishindwa kumpata huyo mtu?
“Kichwa changu kimejaa mipango.Nikishindwa kumpata nitatafuta namna nyingine lakini ninachokuomba darling hakikisha watoto wameondoka hapa nchini.Take them somewhere safe” akasema Ruby
“Ruby I’m coming there.Nataka tulizungumze suala hili kwa undani” akasema Dr Fabian
“Sawa.Kuwa makini Fabian” akasema Ruby na kukata simu
“Nitafanya nini kumshawishi Ruby akubali kuondoka hapa nchini kwa ajili ya usalama wake na watoto? Hawa watu ni hatari mno na maisha yetu sote tayari yako hatarini.Ngoja nimfuate huko huko .Lazima aondoke hata kwa kutumia nguvu.Mimi ni mume wake na ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.Ruby ni mwanamke wa ajabu sana.Anafahamu hatari iliyoko mbele yetu lakini haogopi na yote hii ni kwa sababu ya Mathew Mulumbi.Bado anampenda sana Mathew.Hata kama anampenda Mathew lakini ni mke wangu kwa sasa
hivyo atafuata kile ninachokiamua mimi !
akawaza Dr Fabian na mlango wa chumba chake ukagongwa alikuwa ni mlinzi wake aliyemjulisha kwamba daktari wake amekwisha fika
Daktari alifika na vipimo vyote akampima Dr Fabian na kumtaka afike hospitali kwa vipimo zaidi.Dr Fabian akamtaka daktari atangulie naye atafika baadae kwani kwa wakati ule alikuwa na safari kidogo.Wakati akijiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na mke wake Ruby,mlinzi wake akamfuata akamjulisha kwamba kuna askari polisi wamefika pale kwake wana mazungumzo naye.Mara tu aliposikia neno askari polisi alihisi kama moyo wake unataka kutoka kwa namna ulivyobadili mapigo yake na kuanza kwenda kwa kasi isiyo ya kawaida.Haraka haraka akachukua simu na kumpigia Ruby
“Fabian” akasema Ruby
“Ruby it’s getting ugly.Nimejulishwa kwamba polisi wamefika hapa.Nahisi kuna kitu wanataka kunihoji kuhusu Mathew.Ninakwenda kuonana nao nitakujulisha baadae wamefuata nini” akasema Dr Fabian na kukata simu
“Ninajuta sana kwa Mathew kuniingiza katika jambo hili na kuyafanya maisha yangu yawe ya mashaka namna hii.Ngoja nikaonane na hao askari nijue kilichowaleta hapa kwangu” akawaza Dr Fabian na kuelekea sebuleni walikokuwa wale askari polisi waliofika.Mara tu alipoingia
sebuleni askari polisi wale sita wakasimama na kutoa salamu “Karibuni sana vijana wangu.Poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa” akasema Dr Fabian baada ya kuketi sofani
“Tunashukuru mzee”
wakajibu askari wale na kiongozi wa timu ile ya askari akajitambulisha yeye mwenyewe halafu akawatambulisha askari wengine alioongozana nao kisha akamjulisha Dr Fabian kile kilichowapeleka pale kwake.
“Mheshimiwa Rais nadhani tayari umekwisha sikia katika vyombo vya habari asubuhi ya leo kuhusiana na
tukio lililotokea usiku wa kuamkia leo” akasema mkuu wa wale askari
“Kuna matukio mengi
yametokea usiku wa leo sasa sijui ni tukio lipi
mnalizungumzia” akasema Dr Fabian
“Usiku wa kuamkia leo
jeshi la polisi kitengo cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kimemkamata mmoja wa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya hapa nchini ambaye ni mmliki wa MGC Ltd anaitwa Mathew Mulumbi.Ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa sana hapa nchini na vile vile aliwahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi hapa nchini lakini kumbe ni mmoja wa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya.Mzigo mkubwa wa dawa za kulevya umekamatwa nyumbani kwake na kama haitoshi kuna tukio pia la mauaji limefanyika ndani ya nyumba yake ambapo watu wawili walikutwa wameuawa kwa kupigwa risasi.Mmoja wa watu waliokutwa wameuawa ndani ya nyumba hiyo ni Kamishna msaidizi wa magereza ambaye pia ni mkuu wa gereza la Kimondo lililoko Arusha anaitwa Deus Mtege.Mtu mwingine bado hajatambulika ni nani.Mwili wa Deus Mtege ulikuwa umepasuliwa tumbo kuondolewa utumbo na kisha kupakia madawa ya kulevya ndani yake tayari kwa kuyasafirisha.Ni moja ya tukio baya kabisa” akasema Yule kamanda.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu na kusema
“Ni kweli hili ni tukio baya kabisa.Hata mimi nimestuka sana nilipolisikia.Ninamfahamu Mathew Mulumbi amesaidia sana katika mambo mengi ya kiusalama hapa nchini na hata nilipokuwa madarakani alinisaidia sana.Nimeshangaa kwa hiki alichokifanya.Lakini nimeshangaa zaidi kwa uwepo wenu hapa tukizunguzmia suala hili.Nataka kufahamu je linahusiana vipi na mimi? Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais hauna mahusiano ya moja kwa moja na jambo hili lakini unahitajika katika ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai kwa mahojiano” akasema kamanda Yule na mstuko mkubwa ukaonekana usoni pa Dr Fabian
“Mnanishangaza
sana.Mimi ninahusiana vipi na mambo aliyoyafanya Mathew Mulumbi? Akauliza Dr Fabian kwa wasiwasi
“Usihofu mzee,hakuna kitu kibaya.Kuna maelezo machache ambayo utayatoa na maswali machache utaulizwa”akasema Yule kamanda
“Sawa naomba nimpigie simu mke wangu nimjulishe kuwa ninahitajika polisi” akasema DrFabian na kuelekea chumbani kwake akachukua simu na kumpigia Ruby
“Ruby mambo yanazidi kuwa magumu.Ninahitajika ofisi ya DCI ”
“Jesus ! akasema Ruby “Ninakwenda huko kujua nini wameniitia” akasema Dr Fabian
“I’m coming too” akasema
Ruby
“Hapana Ruby
usije.Nitakujulisha kila kitakachoendelea.Nitakuwa na mwanasheria hivyo usijali kila kitu kitakwenda vizuri” akasema Dr Fabian
“Fabian …” Ruby akataka kusema kitu lakini Dr Fabian akamzuia
“Don’t say anything Ruby I’ll be fine.Ndiyo maana nikakushauri kwamba uondoke nchini wewe na watoto kwani hili jambo lim…..”
“Fabian tumekwisha
limaliza hilo.Siwezi kuondoka nchini kuwakimbia hawa jamaa tusiowafahamu.Yawezekana wao wana nguvu ya kufanya chochote wakitakacho lakini safari hii wamekutana na kisiki.Nenda kawasikilize wanasemaje halafu uje ujadili jambo hili kwa kina” akasema Ruby na kuagana na Dr Fabian
“Najitahidi kuonyesha ujasiri wa kupambana na hawa watu lakini kwa ndani ninatetemeka.Nina hofu kubwa.Hawa watu wanatisha mno.Kitu walichomfanyia Mathew kinaogofya.Hawana mzaha na wale wote wanaowafuatilia na wanawatumia kila mbinu kuwapoteza kama walivyofanya kwa Gosu Gosu na sasa ni Mathew. Wanajua kujipanga na mipango yao yote inakwenda vizuri na hawaachi alama nyuma yao inayoweza kuwatambulisha wao ni akina nani.Hata mimi nimekwisha julikana ninashirikiana na Mathew na niko katika hatari ndiyo maana Yule mtu nisuyemfahamu alinitumia jumbe jana kwamba nikimbie wananifuata.Siwezi kumpuuza. Yule mtu ujumbe wake una maana kubwa kwangu.Ananifahamu na hakutaka niingie katika hatari.Je ni Mathew ndiye aliyekuwa anajaribu kunionya kuwa nikimbie? Ninapaswa kumtafuta mtu huyu na kumfahamu ni nani anaweza akawa na msaada mkubwa kwangu kwa sababu lazima anawafahamu hawa watu ni akina nani.Jana nilijaribu kumtafuta lakini naye ametumia namba ya simu ambayo haijasajiliwa kama wanavyotumia hawa jamaa na kufanya kazi ya kumtafuta iwe ngumu.Hata hivyo lazima nihakikishe ninamfahamu ninaamini ni mmoja wao.Lazima ipo sababu ya kunipa onyo lile ili kuniepusha na wale jamaa.Mtu mwingine ambaye anaweza akanisaidia katika uchunguzi wa kuwabaini hawa mashetani ni Kamishna Chambao.Huyu alipigiwa simu na hawa jamaa jana usiku na kumtaka ahakikishe anamkabidhi Deus kwao na alifanya hivyo.Yeye anaweza akatusaidia katika kuwafahamu hawa watu.” Akawaza Ruby.
************
Haikufahamika walipataje taarifa za Rais mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Fabian Kelelo kufikishwa katika ofisi ya mkurugenzi upelelezi wa makosa ya jinai nchini lakini msafara wa magari ya Rais mstaafu ulipowasili katika ofisi hizo ulikuta waandishi wa habari tayari wamekwisha fika.
“Wamepataje taarifa watu hawa kwamba ninafika hapa leo? Akajiuliza Dr Fabian akiwa ndani ya gari lake.Geti lilikuwa wazi magari yakaingia ndani kisha Dr Fabian akashuka akaongozana na askari polisi wakaelekea ndani na moja kwa moja wakaingia katika ofisi ya DCI David Chamwino.
“Mheshimiwa Rais ! akasema David akisimama na kumsalimu Dr Fabian
“David ! akasema Dr Fabian na David akamuelekeza aketi katika sofa zilizokuwamo mle ofisini.
“Karibu sana mheshimiwa Rais.Tuna muda mrefu kidogo hatujaonana.Vipi maisha ya ustaafu? Akauliza David huku akitabasamu
“Maisha ya usatafu ni mazuri.Kwa ujumla ninaendelea vyema.Vipi ninyi mnaendeleaje na majukumu yenu hapa? Akauliza Dr Fabian ambaye alijitahidi kuificha hofu aliyokuwa nayo
“Tunashukuru
tunaendelea vyema mheshimiwa Rais” akajibu David na ukimya mfupi ukapita
“Mheshimiwa Rais tumekusumbua asubuhi hii kuna mambo ambayo tunahitaji kuyafahamu kutoka kwako.Naomba twende katika chumba cha mahojiano tafadhali”akasema David na kutoka ndani ya ile ofisi wakaelekea katika chumba cha mahojiano ambacho kulikuwa na meza kubwa na viti nane.
“Karibu mheshimiwa Rais” akasema David na kumuelekeza Dr Fabian kiti cha kuketi.Baada ya dakika mbili wakaingia watu wengine watatu jumla ndani ya chumba kukawa na watu wanne.Mlinzi wa Dr Fabian hakutakiwa kuingia mle ndani akabaki nje. “Dr Fabian tumekuita hapa kuna mambo ambayo tunahitaji kuyafahamu kutoka kwako.Tunaomba utupe ushirikiano mkubwa mheshimiwa Rais” akasema David
“Nitawapa ushirikiano kwa chochote kile mnachokihitaji” akasema Dr Fabian
“Ahsante sana” akasema David na ukimya mfupi ukapita
“Mheshimiwa Rais
tunataka utueleze namna unavyomfahamu Mathew Mulumbi” akasema David
“Mathew Mulumbi?
Akauliza Dr Fabian
“Ndiyo .Unaweza ukatueleza namna unavyomfahamu? Akauliza David.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu akafikiri kidogo na kusema
“Mathew Mulumbi
nilimfahamu wakati nikiwa Rais.Ni wakati ule lilipotokea shambulio la kigaidi ambapo mke wangu aliuawa sambamba na wake wengine wa marais.Yawezekana hamfahamu lakini ni Mathew Mulumbi ndiye aliyeongoza wenzake katika kuwasaka wahusika wa mauaji yale na wengine wakauawa wengine mpaka sasa wako magerezani wakitumikia vifungo virefu kwa kujihusisha na ugaidi.Mathew Mulumbi amewahi kufanya kazi katika idara ya ujasusi lakini kwa sasa anajishughulisha na biashara” akasema Dr Fabian
“Unafahamu ni biashara zipi anazifanya? Akauliza
David Chamwino
“Naomba niwe muwazi kwenu ndugu zangu kwamba simfahamu kiundani Mathew Mulumbi lakini ninachofahamu ni mfanya biashara na anamiliki makampuni kadhaa makubwa hapa nchini”
“Ukaribu wako naye ukoje kwa sasa? Dr Fabian akaulizwa
“Ukaribu wangu na
Mathew? Akauliza Dr Fabian
“Ndiyo.Unaweza
ukatueleza ukaribu wenu ulivyo kwa sasa? Akauliza
David
“Mathew si mtu wangu wa karibu sana lakini amekuwa ni rafiki wa familia kutokana na ukaribu wake na mke wangu.Wamekuwa marafiki kwa muda mrefu hata kabla sijafahamiana na mke wangu”akajibu Dr Fabian
“Ulikuwa unafahamu kama Mathew Mulumbi
anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya? Akauliza David.
“Hapana sijawahi kusikia jambo hilo.Ninachofahamu mimi ni kwamba anamiliki makampuni lakini biashara ya dawa za kulevya sijawahi kusikia” akajibu Dr Fabian
“Mke wako ambaye
umedai ni mtu wa karibu na Mathew Mulumbi hajawahi kukueleza chochote kuhusiana na Mathew kujihusisha na masuala ya dawa za kulevya?
“Hapana hajawahi
kunieleza na nina uhakika
mkubwa halifahamu jambo
hilo”
“Kwa nini una uhakika hafahamu?
“Kwa sababu kama angekuwa analifahamu jambo hilo angekwisha nieleza.Sisi tunaishi katika misingi ya uwazi na ukweli hatufichani jambo lolote” akajibu Dr Fabian.David akalifungua faili na kutoa picha akaiweka mezani
“Huyu mtu pichani unamfahamu? Akauliza David
“Ndiyo ninamfahamu.Ni mkuu wa gereza la Kimondo lililoko Arusha” akajibu Dr
Fabian
“Huyu naye mna ukaribu wowote?
“Hapana hatuna ukaribu wowote” Dr Fabian akajibu
“Umewahi kuonana naye ana kwa ana? Akauliza David na Dr Fabian akababaika kujibu
“Mheshimiwa Rais umewahi kuonana na huyu mtu ana kwa ana?akauliza David
“Ndiyo.Nimewahi kuonana naye” akajibu Dr Fabian “Unaweza ukakumbuka lini ilikuwa mara ya mwisho kuonana naye?
Dr Fabian akaonekana kuzama mawazoni
“Mheshimiwa Rais! Akaita
David
“Sikumbuki lini nimekutana naye lakini ilikuwa zamani” akajibu Dr Fabian.David akachukua picha nyingine akamuonyesha
“Huyu naye unamfahamu? “Huyu ni Kamishna Chambao Mnenge.Ni rafiki yangu wa muda mrefu”
“Lini mmeonana au kuwasiliana?
“Nilionana naye jana”
“Unaweza ukatueleza mlizungumza nini mlipoonana? Akauliza David
“Yalikuwa ni mazungumzo ya kawaida”
“Mlionana wapi?
“Nilimfuata ofisini kwake jana asubuhi”
“Ulikuwa peke yako ulipokwenda kuonana na Kamishna Chambao? Akauliza David
“Ndiyo nilikuwa peke yangu.David kitu gani unakilenga kwangu? Kama kuna kitu mahsusi unataka kukifahamu kutoka kwangu niambie na si kuniuliza maswali yenye mitego.Sisi wote ni watu wazima,nenda kwenye kitu cha msingi tafadhali ili tuokoe muda” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais mstaafu Dr Fabian ninakushukuru kwa ushirikiano ulioutoa kwa kujibu vizuri maswali niliyokuuliza lakini hata hivyo kuna mambo ambayo umeshindwa kuyaweka wazi na ambayo yanatuongezea udadisi na kutufanya tutake kukuhoji zaidi” akasema David
“Umeniuliza maswali nimekujibu yote hakuna swali hata moja ambalo sijawajibu” akasema Dr Fabian
“Dr Fabian ninamaanisha ninaposema kuna mambo unayaficha .Ngoja niliweke sawa jambo hili.Siku ya jana ulikwenda kuonana na Kamishna Jenerali wa Magereza Chambao Mnenge ofisini kwake.Katika safari hiyo ulisema kwamba ulikuwa
peke yako lakini ukweli ni kwamba ulikuwa umeambatana na mtu mwingine ambaye ni Mathew Mulumbi” akasema David
Sura ya Dr Fabian
ikabadilika baada ya kusikia Mathew Mulumbi akitajwa kuongozana naye kwenda kwa Kamishna Chambao
“Hatufahamu mliongea nini na Kamishna Chambao ingawa umesema ni mazungumzo binafsi lakini muda mfupi baada ya ninyi kuondoka,Kamishna Chambao naye aliondoka na kuelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ambako alipanda helkopta ya kukodi na taarifa zinaeleza kwamba alielekea jijini Arusha na moja kwa moja
katika gereza la
Kimondo.Hatufahamu alichokwenda kukifanya kule Arusha lakini tunachofahamu ilikuwa ni safari ya ghafla
ambayo hakuwa ameipanga kwani tunayo orodha ya shughuli za siku ambazo alitakiwa kuzifanya Kamishna Chambao lakini katika orodha hiyo hakuna mahala kunaonyesha alikuwa na safari ya kwenda Arusha” akasema
David na kumtazama Dr Fabian
“Hatujui kilichompeleka Arusha lakini alipomaliza kile kilichompeleka kule na kuondoka hakuwa peke yake bali aliongozana na mkuu wa gereza la Kimondo Kamishna msaidizi wa magereza Deus Mtege na wakaelekea Dar es salaam ambako walielekea nyumbani kwa Chambao na baadae wewe ukiwa na Mathew Mulumbi mlifika nyumbani kwa Chambao mkamchukua Deus na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Mathew Mulumbi ambako baadae mwili wa Deus ulikutwa akiwa ameuawa” akasema David
“That’s not true ! akafoka
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais mstaafu,ninayazugumza haya nikiwa na ushahidi wa kutosha na si mambo niliyoyabuni” akasema David na kufungua kompyuta ndogo iliyokuwepo mezani akacheza moja ya video
“Hii ni video inayowaonyesha wewe na Mathew Mulumbi mkiwasili katika ofisi ya Kamishna Chambao,ingawa awali ulidai kwamba ulikwenda peke yako” akasema David na kucheza tena rekodi ya pili
“Hii ni video ambayo inamuonyesha Kamishna Chambao akishuka katika helkopta akitokea Arusha akiwa na Deus Mtege” akasema David na kucheza tena video nyingine
“Hii inawaonyesha wewe,Mathew
Mulumbi,Kamishna Chambao na Deus mkitoka nyumbani
kwa Kamishna Chambao
mkaingia garini na hii video ya mwisho inawaonyesha
mkiingia katika makazi ya Mathew Mulumbi.Baadae
Deus alikutwa akiwa amefariki dunia ndani ya nyumba hiyo ya Mathew Mulumbi na kama haitoshi kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimekutwa ndani mwake” akasema David na ukimya ukatanda mle ndani
“Kumbe tulikuwa
tunafuatiliwa na kurekodiwa kila tunachokifanya ! Mizunguko yetu yote ya jana wanaifahamu na baada ya kuwadanganya kwamba sikuongozana na Mathew Mulumbi kwenda kwa Kamishna Cjhambao nimezidi kujiweka katika kona mbaya.Hili suala linaonekana kunikumba hadi mimi.Hawa jamaa wanataka kutuunganisha wote katika mauaji ya Deus.Ninakwendda kupotea kama
Mathew.Nitafanya nini kuhusu Ruby? Naye lazima atakuwa katika hatari kubwa sana.Lazima aondoke hapa nchini haraka” akawaza Dr Fabian na kutolewa mawazoni na David
“Dr Fabian katika maelezo yako ulificha kuhusu kuongozana na Mathew Mulumbi kwenda kuonana na
Kamishna Chambao jana asubuhi na pili ni kuonana na Deus Mtege.Ulikiri kumfahamu Deus lakini ukadai hukumbuki lini ulionana naye.Kwa ushahidi wa video tulio nao unakuonyesha ukiwa naye siku ya jana.Kwa nini hukukata kukiri kuwa ulionana naye siku ya jana? Akauliza David.Dr Fabian akabaki kimya
“Dr Fabian kutokana na maelezo yako kujichanganya tunashawishika kwamba kuna kitu unakifahamu kuhusiana na Mathew Mulumbi na hivyo tutaendelea na mahojiano yetu baada ya muda mfupi”akasema DCI na kutoka ndani ya kile chumba baada ya kupokea ujumbe katika simu yake kwamba kamishna Jenerali wa Magereza Chambao Mnenge tayari amefika.
“Mzee Chambao karibu sana” akasema David na kumkaribisha kamishna Chambao ofisini kwake
“Mzee kwanza naomba
nichukue fursa hii kukupa pole nyingi kwa kifo cha mkeo.Naamini jeshi la polisi litakamilisha uchunguzi wa kifo chake haraka”
“Ahsante nashukuru”akasema Chambao
“Kamishna tunafahamu uko katika kipindi kigumu lakini tumelazimika kukuita hapa ili tukuulize maswali machache kisha tukuache ukaendelee na taratibu za msiba” akasema David na Kamishna Chambao akaitika kwa kichwa.David akainuka akamtaka amfuate wakaenda katika chumba kingine cha mahojiano ambako watu wengine wanne wakajiunga nao.Mmoja wao akampa David faili akalifungua na kutoa picha
“Kamishna Chambao unaweza ukamtambua mtu huyu pichani? Akauliza
David.Kamishna Chambao akaishika ile picha akaitazama halafu akaiweka mezani
“Hapana simfahamu”
akajibu
“Look again” akasema David na Kamishna akaitazama tena halafu akatikisa kichwa “Simfahamu huyu mtu” akasema Chambao.
“Kamishna Chambao una uhakika humfahamu huyu mtu? Hujawahi kumuona sehemu yoyote? Akauliza David
“Hapana simfahamu na sijawahi kumuona.Ni nani huyu mtu? Akauliza Kamishna Chambao
“Anaitwa Mathew Mulumbi ni mmoja wa wafanya biashara wakubwa hapa nchini anayemiliki kampuni inaitwa MGC Ltd.Jana usiku jeshi la polisi kitengo cha kuzuia na kupamba na dawa za kulevya walipata taarifa kwamba ndani ya nyumba Fulani kuna kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimefichwa,wakavamia nyumba hiyo na kukamata kiasi kikubwa cha dawa za kulevya na kumkamata pia miliki wa nyumba hiyo ambaye ni huyu pichani anayejulikana kama Mathew Mulumbi.Hii ni taarifa ambayo imetawala kila chombo cha habari siku ya leo” akasema David
“Sijapata nafasi ya kutazama habari au kufuatilia mitandao ya kijamii ninashughulikia msiba wa mke wangu” akasema Kamishna Chambao.David akafungua faili na kutoa picha nyingine akamuonyesha kamishna Chambao
“Huyu unamfahamu?
“Ndiyo.Anaitwa Deus
Mtege ni mkuu wa gereza la
Kimondo Arusha” akajibu
Kamishna Chambao
“Unaweza kukumbuka lini umeonana naye? Akauliza David
“Nimeonana naye jana” “Ulionana naye wapi?
“Nilifanya ziara ya kustukiza katika gereza la Kimondo jana”akasema Kamishna Chambao.
“Kuna sababu yoyote
iliyokufanya ufanye ziara ya kustukiza katika gereza la Kimondo?
“Kimondo ni gereza kubwa na linachukua wahalifu sugu kwa hiyo limekuwa ni gereza lenye matatizo mara kwa mara
na nilitaka nistukize ili niweze kujionea mwenyewe namna
hali ilivyo pale gerezani”akajibu Chambao
“Nini kilifuata baada ya kumaliza ukaguzi wako katika gereza hilo la Kimondo?
“Baada ya kumaliza ukaguzi nilirejea Dar es salaam” akajibu Chambao
“Deus ulimuacha Arusha?
Akauliza David na swali lile likaonekana kumbabaisha Kamishna Chambao akabaki kimya
“Kamishna Chambao”
akaita David
“Samahani kichwa changu kimejaa mambo mengi.Deus nilimuacha Arusha” akajibu Chambao
“Kuna taarifa zozote ulizipata jana kwamba Deus ameonekana hapa Dar es salaam? Akauliza David
“Hapana sijapata taarifa zozote.Deus nilimuacha Arusha akiendelea na majukumu yake.Kama alikuja hapa Dar es salaam ni kwa ajili ya mambo yake binafsi na si mambo ya kikazi” akajibu Kamishna Chambao
“Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo una ukaribu naye? Akauliza David
“Ndiyo.Dr Fabian ni rafiki yangu sana tangu wakati akiwa Rais na hata sasa baada ya kustaafu bado ni marafiki”
“Unakumbuka ni lini mara yako ya mwisho kuonana naye?
“Nadhani ni wiki mbili
zilizopita”
“Mlionana wapi?
“Nilimfuata katika makazi yake kumtembelea”akajibu Kamishna Chambao na David akavuta pumzi ndefu akamtazama Chambao halafu akasema
“Kamishna Chambao
maswali mengi niliyokuuliza umetoa majibu ya uongo.Nilikuuliza maswali ambayo majibu yake ninayafahamu nikitegemea ungenieleza ukweli mtupu lakini sifahamu kwa nini umeamua kutokusema
ukweli.Nilichokuitia hapa ni kuufahamu ukweli kisha nikuache uende zako lakini kwa kunidanganya umenishawishi nitake kukuchuguza zaidi”akasema David Chamwino
“David yote niliyokueleza ni ukweli mtupu.Siwezi kukudanganya” akasema Kamishna Chambao.David akainuka na kuifungua kompyuta yake akamsogelea
Chambao
“Kamishna Chambao kuna video ambazo naomba uzitazame halafu tutaendelea na mahojiano” akasema David na kucheza video ya kwanza
“Hii ni jana asubuhi,Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo akiwa ameongozana na Mathew Mulumbi wakiwasili makao makuu ya jeshi la magereza ilipo ofisi yako na hapa walikuja kuonana nawe” akasema David na Kamishna Chambao akapatwa na mstuko mkubwa sana.
“No ! This is not true.Sijaonana na Dr Fabian
jana ! akasema Chambao kwa ukali
“Usijali mzee Chambao tunakwenda taratibu” akasema David na kucheza tena video nyingine
“Hii ni dakika chache baada ya Dr Fabian na Mathew kuondoka ulitoka ofisini kwako ukaingia garini na kuelekea uwanja wa ndege wa Julius Nyerere” akasema na Kamishna Chambao macho yakamtoka
“Hii hapa ni video ukiingia katika helkopta na safari ya kuelekea Arusha ikaanza” akasema David na Kamishna Chambao midomo ikamtetemeka.David hakumjali akacheza tena video nyingine
“Hii ni video nyingine ikionyesha helkopta uliyopanda ikitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ukitokea Arusha”
Video ilionyesha helkopta ikitua mlango ukafunguliwa akashuka Kamishna Chambao akiwa ameongozana na Deus Mtege
“Ulirejea Dar es salaam ukiwa umeongozana na Deus Mtege na hukumuacha Arusha kama ulivyodai nilipokuuliza” akasema David na kucheza video nyingine
“Hii inaonyesha baada ya kutoka uwanja wa ndege mkaelekea nyumbani kwako” akasema Deus na kucheza tena video nyingine
“Dr Fabian na Mathew walikufuata nyumbani kwako
na katika video hii mnaonekana wewe,Mathew Mulumbi,Deus na Dr Fabian mkiingia garini na kuondoka” David akanyamza kidogo halafu akacheza video nyingine
“Hii video inawaoyesha mkiingia katika makazi ya Mathew Mulumbi” akasema David na ukimya mfupi ukapita
“Safari ya mwisho ya Deus iliishia hapa katika nyumba ya Mathew” akasema David na kumuonyesha Chambao picha za mwili wa Deus Mtege akiwa ameuawa nyumbani kwa Mathew.Kamishna Chambao akapatwa na mstuko mkubwa
“Deus alikutwa ndani ya nyumba ya Mathew Muumbi akiwa ameuawa na kama unavyoshuhudia katika picha pakiti za dawa za kulevya zilikuwa zimepakiwa tumboni tayari kwa kusafirishwa” akasema David na kurejea katika kiti chake
“Kamishna Chambao
baada ya kushuhudia video hizi zote naamini nitakapokuja kukuhoji tena utakuwa tayari kunieleza ukweli mtupu.Kwa sasa nakuacha upumzike kwa dakika chache na utafakari kwa kina jambo hili” akasema David kisha wakatoka mle ndani
“Nimekwisha ! Fabian na Yule kijana wake wameniingiza katika tanuru la moto.Wamenishawishi nikashirikiana nao na sasa yamenikuta haya.Nimempoteza mke wangu na kama haitoshi tayari na mimi nimevishwa kitanzi.Nitafanya nini kujitoa katika kitanzi hiki? Najilaumu sana kumsikiliza Fabian.Laiti ningejua kama yatatokea haya nisingekubali kuwafuatilia hawa jamaa.Ni watu hatari na sasa wanakwenda kunipoteza na mimi pia kama walivyompoteza Yule kijana kule gerezani.Mathew Mulumbi pia ameingia katika matatizo makubwa na sina hakika kama atasalimika katika jambo hili.Najuta ! akawaza Kamishna Chambao baada ya David na watu wake kutoka mle chumbani *************
Taarifa za bilionea na jasusi nguli Mathew Mulumbi kukamatwa akihusishwa na biashara ya dawa za kulevya na mauaji ya mkuu wa gereza la Kimondo zilienea kwa kasi ya upepo.Ilikuwa ni taarifa iliyowastua watu wengi waliomfahamu na wasiomfahamu Mathew Mulumbi .
Akiwa katika nyumba
alikopelekwa kwa ajili ya usalama wake na wanae,Ruby alikosa utulivu.Taarifa ya kilichomtokea Mathew bado iliendelea
kumtesa.Kilichomchanganya zaidi ni kitendo cha mume wake Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo kuitwa katika ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai kuhojiwa.Kila wakati alikuwa anaitazama simu yake kusubiri kupata mrejesho kutoka kwa mume wake kuhusiana na kilichojiri katika mahojiano lakini simu ilikuwa kimya.Alichanganyikiwa.
Akiwa bado katika tafakari nini cha kufanya mara ukaingia ujumbe katika simu yake.Akaufungua haraka haraka akidhani unatoka kwa mume wake lakini ujumbe ule haukutoka ulikuwa na neno moja tu
“Hide” (jifiche)
“Huyu ni Yule Yule mtu wa jana aliyenitumia ujumbe kunitahadharisha kwamba ninafuatiliwa” akawaza Ruby
“Lakini ni nani huyu mtu? Akajiuliza halafu akaandika ujumbe
“Who are you?
Akautuma.Alihisi mwili ukimtetemeka kwa hofu akisubiri majibu.Baada ya dakika mbili ukaingia ujumbe mwingine ukisomeka
“Hide”
“Can you help me? Akauliza Ruby
“I can’t.Hide ! ukasomeka ujumbe mwingine
“Oh my God ! What I’m going to do? Akajiuliza na kuvuta pumzi ndefu
“Siwezi kukaa hapa
nikisubiri hatari inikute.Yawezekana hawa jamaa tayari wamekwisha fahamu mahala nilipo na ndiyo maana huu mtu anajaribu kunionya nijifiche.I need to do something.Kitu cha kwanza ninatakiwa kufahamu kinachoendelea kule alikoenda Fabian” akawaza Ruby na kuchukua simu akampigia simu mlinzi wa Dr Fabian
“Nicholas uko na Dr Fabian? Akauliza Ruby
“Hapana mama.Mzee yuko ndani bado wanaendelea na mahojiano na mimi sijaruhusiwa kuingia ndani kujua kinachoendelea lakini kwa dalili ninazoziona hapa mambo si mazuri kwa mzee.Nitakujulisha kila kitakachokuwa kinaendelea hapa” akasema Niko
“Sawa Niko kama ukiweza kumpata hata kwa sekunde chache naomba nizungumze naye tafadhali” akasema Ruby na kukata simu
“Kuna kila dalili kwamba Fabian anaweza akahusishwa katika ile kashfa iliyomkuta Mathew.Ni wazi wale wote ambao wanajaribu kuwafatilia hawa watu,hawabaki salama.Aidha wanauawa au yanawapata kama yaliyowapata Mathew na Gosu Gosu na sasa sifahamu hatima ya mume wangu na hata mimi
mwenyewe .Nina hofu kubwa
lakini sitakiwi
kuogopa.Natakiwa kupambana kuwasaidia hawa ndugu zangu” akawaza Ruby halafu akaenda haraka chumbani kwake akafungua sanduku kubwa na kutoa kisanduku kidogo.Akakifungua na kutoa simu.Akaishika na kuvuta pumzi ndefu
“Sina namna nyingine,hii ndiyo njia pekee ninayoweza kuitumia kwa sasa kupata msaada” akawaza na kuiwasha ile simu maalum kabisa ambayo si rahisi kudukuliwa.Ni simu maalum ambazo wanazo marais wastaafu,mawaziri wakuu wastaafu na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wastaafu.Simu hizi huwawezesha kuwasiliana na Rais moja kwa moja na hutumika pale tu kunapokuwa na suala kubwa la usalama wa nchi.Kila mwenye simu hiyo hupewa namba maalum ya kumtambulisha ili kumuwezesha kutambulika pale atakapopiga.Ruby alikuwa na simu hii kwa kuwa aliwahi kuongoza idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi(SNSA)
Ruby akaandika namba Fulani na kupiga simu ikaanza kuita.Baada ya sekunde chache ikapokelewa na akatakiwa kutaja namba zake za utambulisho ,akataja na kutakiwa kusubiri kidogo halafu akasikia sauti ambayo aliitambua vyema
“Ruby” ikasema sauti ya upande wa pili
“Mheshimiwa Rais !
akasema Ruby “Kuna nini Ruby?
“Mheshimiwa Rais nahitaji kukuona sasa hivi” akasema Ruby
“Njoo ikulu mara moja” akasema Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Festus Mayungulu ambaye alishika madaraka baada ya Dr Fabian kumaliza kipindi chake cha miaka mitano na hakutaka kugombea tena kwa kipindi kingine.Kila simu ile inapotumika Rais hulazimika kumpa mpigaji umuhimu mkubwa kwani lazima kuna
suala muhimu la usalama wa
taifa
Bila kupoteza muda Ruby akakusanya nguo na vifaa vya watoto wake akaweka katika masanduku mawili akamtaka mtumishi wake akayaweke garini akawajulisha walnzi wake kwamba wanaelekea ikulu.
“Ee Mungu nisaidie niweze kufika salama ikulu kwani hawa jamaa wanaonekana wako mbele yetu katika kila hatua tunayoipiga” akaomba Ruby huku akiwa makini kutazama nje kama wanafuatiliwa.
************
Ruby aliwasili ikulu na kupokewa na Rais Festus Mayungulu.Watoto wa Ruby wakachukuliwa na watumishi na kupelekwa katika makazi ya Rais halafu Ruby na Rais wakaenda katika chumba cha mazungumzo ya faragha
“Ruby nimefurahi kukuona.Karibu sana ikulu.Anaendeleaje Dr Fabian?
“Mambo si mazuri mheshimiwa Rais ndiyo maana niko hapa”
“Kuna nini Ruby?
Nimelazimika kuahirisha kikao muhimu sana ili niweze kuzungumza nawe” akasema Rais Festus.
“Mheshimiwa Rais nimekuja kuomba msaada wako baada ya maji kunifika shingoni” akasema Ruby na Rais Festus hakujibu kitu akaendelea kumtazama
“Mheshimiwa rais naamini umewahi kumsikia Mathew Mulumbi”
“Ndiyo nimekuwa
nikimsikia mtu huyu kwa muda mrefu,nimesikia kazi alizozifanya lakini sijawahi kuonana naye ana kwa ana”
“Naamini tayari umekwisha sikia pia kuhusu tukio lililotokea jana usiku likimuhusisha yeye” akasema Ruby
“Nilishangaa sana baada ya kupata taarifa hizo.Huyu mtu alitambulika kama mzalendo wa hali ya juu lakini kumbe anajishughulisha na biashara haramu ya dawa za kulevya huku akijificha katika kivuli cha ujasusi.Nimesikitika sana kwa kitu alichokifanya” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais labda ningeanza kukupa historia kuhusu mimi na Mathew Mulumbi na namna ninavyomfahamu” “Unafahamiana naye?
“Ndiyo ninafahamiana naye sana” akajibu Ruby na kuanza kumueleza Rais Festus namna alivyokutana na Mathew Mulumbi na operesheni ambazo wamewahi kuzifanya pamoja.
“Ni historia yenye kusisimua sana lakini pamoja na hayo yote aliyoyafanya ameharibu kwa kushiriki katika biashara ya dawa za kulevya na mauaji.Narudia tena imenisikitisha sana” akasema Rais Festus
“ Kazi ya mwisho aliyoifanya Mathew Mulumbi ni ile aliyoifanya nchini
Marekani ambako aliishangaza dunia nafikiri unakumbuka alichokifanya kule”akasema Ruby
“Ninakumbuka sana na
siku ile nilidondosha machozi nilipomtazama kijana wa kitanzania akifanya jambo kubwa kama lile.Ruby mazungumzo yetu haya ni kuhusiana na Mathew Mulumbi au kuna suala lingine la kitaifa? Kama hakuna jambo lingine zaidi ya kumzungumzia mhalifu Mathew Mulumbi basi yatakuwa ni matumizi mabaya sana ya laini hizi muhimu kabisa mlizopewa” akasema Rais Festus
“Nalifahamu hilo mheshimiwa Rais lakini ningeomba univumilie niendelee kukueleza kile kilichonileta hapa” akasema Ruby
“Endelea”
“Ahsante sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kunywa funda dogo la maji kulainisha koo halafu akasema
“Baada ya kazi ile aliyoifanya Marekani,Mathew Mulumbi alipotea na hakuna aliyejua mahala alikoenda hadi hivi majuzi aliporejea nchini na kukuta mmoja wa watu wake wa karibu na msimamizi mkuu wa biashara zake anaitwa Papi Gosu Gosu amefungwa gerezani”
“Gosu Gosu ni nani? Hili
jina si geni sana masikioni mwangu”
“Huyu ni mshirika wa karibu sana wa Mathew Mulumbi na amekuwa
akishirikiana naye katika operesheni mbali mbali”
“Alifungwa gerezani kwa kosa gani? Akauliza Rais Festus
“Kwa kosa la mauaji ya mwandishi wa habari”
“Nimewahi kuisikia hiyo
kesi”
“Mathew alikwenda
Arusha kumtembelea Gosu Gosu ambaye alimueleza ukweli wa tukio lililosababisha akafungwa maisha gerezani hivyo kumlazimu Mathew kuanza kufanya uchunguzi kubaini ukweli”
“Sijakuelewa Ruby.Ukweli upi Gosu Gosu alimweleza Mathew hadi akalazimika kuanza kufanya uchunguzi wakati uchunguzi ulikwisha fanyika na mahakama ilimkuta
na hatia kwa kosa la mauaji na kumuhukumu kifungo cha maisha gerezani? Akauliza Rais Festus
“Ni kweli Gosu Gosu
alikutwa na hatia kwa kosa la mauaji na kufungwa maisha gerezani lakini kwa mujibu wa Gosu Gosu hakufanya tukio lile” akasema Ruby
“Hakuua? Rais Festus akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
Rais”akajibu Ruby na Rais
Festus akatoa kicheko kidogo
“Ukienda leo gerezani na kuanza kusikiliza mtu mmoja mmoja kila mfungwa atakwambia kwamba hakutenda kosa bali amesingiziwa.Hicho ni kitu cha kawaida”
“Yawezekana ikawa hivyo lakini Gosu Gosu hakuua kama ilivyodaiwa” akasema Ruby
“Kama hakuua ilikuaje mahakama ikamkuta na hatia na kumuhukumu kifungo? Naziamini mahakama zetu zinatenda haki”
“Mahakama ilitimiza wajibu wake kama kawaida na ilitenda haki wala haikumuonea Gosu Gosu kwani iliridhika na ushahidi uliokuwepo kwamba alitenda kosa lakini ukweli ni kwamba hakutenda lile kosa”
“Hapo ndipo unaponichanganya Ruby”
“Tafadhali naomba
uendelee kunisikiliza mheshimiwa Rais” akasema Ruby na Rais Festus akatingisha kichwa kumpa nafasi aendelee
“Mathew Mulumbi
aliamua kuanza kuutafuta ukweli wa kuhusiana na kile alichoelezwa na Gosu Gosu” akasema Ruby na kumueleza Rais kile ambacho kilimtokea Mathew Arusha mara tu alipoanza uchunguzi wake.Sura ya Rais ikaonyesha mshangao kidogo
“Baada ya kunusurika katika tukio lile,Mathew alirejea Dar es salaam akanitafuta na kwa pamoja tukashirikiana katika kuutafuta ukweli wa jambo hili kwani tayari taa nyekundu ilikwisha waka” akasema Ruby na kumtazama Rais Festus “Mwanamke aliyedaiwa kuuawa na Gosu Gosu alikuwa mwandishi wa habari za uchunguzi.Tuliamini yawezekana kazi yake hiyo ya habari za uchunguzi ndiyo iliyosababisha kifo chake.Tulianza kuchunguza na tukabaini kabla ya kifo chake alikuwa anachunguza jambo lililomuhusu msichana anayeitwa Naomi Bambi ambaye mpaka sasa bado jitihada za kumtafuta kumfahamu ni nani zimegonga mwamba.Hakuna taarifa zake zozote katika mifumo yote ya usajili ya serikali.Tulibaini pia kwamba Lidya alikusudia kwenda kuonana gerezani na mtu anayeitwa Zawadi Mlola.Huyu alikuwa muuguzi na alifungwa gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia na ndiye aliyekuwa na taarifa za kumuhusu Naomi.Kwa bahati mbaya Lidya hakufanikiwa kuonana na huyo
Zawadi.Tulifuatilia na kugundua kwamba Lidya alikuwa anashirikiana na watu watatu katika uchunguzi wa jambo hilo kwanza ni mbunge
Jonas Sabuni ambaye alifariki katika ajali ya moto.Mwingine anaitwa Susan Ibobwe ambaye alikuwa ni mkurugenzi wa kampuni ambayo Lidya alikuwa anafanya kazi.Huyu naye alifahamu na kusaidiana na Lidya katika uchunguzi lakini naye tayari amekwisha fariki dunia.Mwingine ni Paul Kabose ambaye naye tayari amekwisha fariki dunia.Mtu pekee ambaye alikuwa anataarifa za kumuhusu Naomi Bambi alibaki kuwa Zawadi Mlola.Tulimfuatilia na kugundua alimaliza kifungo chake na kutoka gerezani tukagundua anaishi eneo la Kichangani na tukafanikiwa kumpata lakini likatokea shambulio Zawadi alitaka kuuawa Mathew akafanya jitihada akamuokoa.Zawadi alipigwa risasi kadhaa pajani”
“Wait ! akasema Rais
Festus
“Kuna jambo
nimelikumbuka.Nilipigiwa simu na Dr Fabian akaniambia anaomba ulinzi katika hospitali ya Katihar kuna ndugu yake amepigwa risasi na watu wasiojulikana na anahofu wanaweza wakafika hapo hospitali kummalizia.Niliwasiliana na IGP nikampa maelekezo ya kumsaidia Rais mstaafu na akafanya hivyo akawasiliana na mkuu wa kituo cha polisi Kichangani wakatumwa askari hapo hospitali kumlinda huyo mtu aliyepigwa risasi.Ndiye huyo Zawadi? Akauliza Rais Festus
“Ndiyo mheshimiwa Rais ni huyo Zawadi” akajibu Ruby
“Hapo hapo hospitali
Mathew alimuhoji Zawadi kuhusiana na Naomi Bambi lakini alitupa mwanga mwanga mdogo sana”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment