IMEANDIKWA NA : PATRICK CK
***************************************************************
Simulizi : Scandle (Kashfa) (3)
Sehemu Ya Kwanza (1)
“Bado naendelea kujiuliza
kwa nini wale jamaa
hawajasambaza zile picha?
Wameogopa? Nahisi hivyo
watakuwa wametafakari na
wameogopa kufanya hivyo kwa
hofu kwamba wangesakwa kwa nguvu kubwa hadi
wapatikane” akawaza na
kukumbuka kitu
“Ngoja niwasiliane na
akina Mathew niwajulishe
kuwa picha bado
hazijasambazwa na niwatake
wafanye haraka zaidi
kuwasaka hawa jamaa”
Rais Festus akachukua
simu yake akazitafuta namba
za Zari akampigia
“Mheshimiwa Rais”
akasema Zari na Rais Festus
akastuka “Zari are you okay?
“Yes I’m okay Mr
President”
“No you are not.Niambie
tafadhali kuna tatizo lolote?
“It’s Mathew”
“Mathew kafanya nini?
“Amepigwa risasi”
“Nini?
“Amepigwa risasi
mheshimiwa Rais”
“Saa ngapi?
“Usiku huu” “Vipi hali yake?akauliza
Rais
“Hali yake si nzuri.Yuko
katika chumba cha upasaji
hapa SNSA madaktari
wanaendelea na jitihada za
kuokoa maisha yake” akasema
Zari
“Zari ninakuja hapo mara
moja” akasema Rais Festus
“Sawa mheshimiwa Rais”
akajibu Zari na Rais akakata
simu
“Mathew Mulumbi
amepigwa risasi ! It’s getting ugly ! akawaza Rais
Festus.
“Nadhani hii ndiyo sababu
wale jamaa hawajasambaza
zile picha kwa sababu wanajua
wamekwisha mpata Yule
waliyekuwa
wanamtafuta.Wanajua
wamekwisha muua” akawaza
na kutoa maelekezo kwa
walinzi wake kujiandaa.Akavaa
haraka haraka na kuelekea
katika gari msafara wa magari
manne ukaondoka usiku ule
kuelekea ofisi za SNSA ambazo
hazikuwa mbali sana na ikulu. “Bora angepigwa risasi
mtu mwingine lakini si
Mathew
Mulumbi.Tunamtegemea sana
Mathew katika vita hii.Endapo
ikitokea ameuawa basi
litakuwa ni pigo kubwa sana
kwetu.Mathew anatakiwa
apone ili aendeleze
mapambano haya” akawaza
Festus akiwa garini
Ruby akiwa na makomando wa wawili waliwasili ofisi kuu za SNSA akapokewa na Lutengano aliyetumwa na Zari
“Karibu mama
Ruby.Naitwa Lutengano ni mkurugenzi msaidizi wa SNSA” akasema Lutengano na kumpa mkono Ruby
“Ahsante sana.Yuko wapi
Zari”
“This way madam” akasema Lutengano na kumuongoza Ruby kuelekea ndani.Baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi na Ruby wakati wa uongozi wake wakastuka kumuona tena pale usiku ule na kujiuliza kitu gani kinachoendelea.Moja kwa moja Lutengano akampeleka Ruby upande wa Afya iliko hospitali inayohudumia wafanyakazi wa SNSA. Ni hospitali iliyosheheni kila kitu.
Zari alipomuona Ruby akamfuata akamkumbatia kwa nguvu na wote wawili machozi yakawatoka
“Tell me he’s still alive ! akasema Ruby
“Bado yuko katika chumba cha upasuaji.Madaktari wanaendelea na upasuaji” akasema Zari na kumshika mkono Ruby wakaenda kuketi sofani.
“Zari nini kimetokea? Ilikuaje hadi Mathew akapigwa risasi? Akauliza Ruby
“Nashindwaa hata nianzie wapi Ruby.Bado mwili wangu unanitetemeka kwa kile kilichotokea”
“Nieleze tafadhali ! akasema Ruby na Zari akafuta machozi na kusema
“Mimi ndiye niliyepaswa aidha kuwa ndani ya chumba cha upasuaji muda huu au niwe tayari nimepoteza maisha.Risasi zile alizopigwa Mathew zilielekezwa kwangu.He saved my life ! akasema Zari na Lutengano akamfuata
“Nimejulishwa Rais amefika” akasema Lutengano na Zari akafuta machozi “Ruby ninakwenda kumpokea Rais” akasema Zari na kushuka chini kwenda kumpokea Rais na kukutana naye akielekea ndani.
“Mheshimiwa Rais karibu sana” akasema Zari
“Ahsante Zari.Where is he? Akauliza Rais
“This way please” akasema Zari na kumuongoza Rais kuelekea ndani.Watu wote
waliokuwa kazini ndani ya
ukumbi mkubwa wakasimama baada ya Rais kutokea
“Habari za usiku huu ndugu zangu.Poleni sana na majukumu ya kila siku” Rais Festus akawasalimu
“Nimekuja mara moja kuonana na mkurugenzi wenu siku nyingine nitakuja tena tukae tuzungumze nisikie matatizo yenu kama yapo.Kwa sasa endeleeni na kazi na hongereni sana kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama” akasema Festus kisha akaongozana na Zari wakaelekea upande wa afya “How’s he? Akauliza Rais
Fstus
“Bado upasuaji unaendelea” akajibu Zari
“Are you sure he’s going to make it?
“I don’t know mr
President” akajibu Zari
“Ruby ! akasema Rais
Festus baada ya kufika katika chumba cha mapumziko na kumkuta
Ruby.Wakakumbatiana
“It’ s okay Ruby.Dont cry.He’ll be fine” akasema Rais Festus na kumgeukia Zari
“Tangu upasuaji umeanza kuna taarifa zozote kutoka kwa madaktari? Akauliza Rais Festus
“Hapana hawajatoa taarifa yoyote” akajibu Zari
“Nani kiongozi wa madaktari?
“Dr Fred !
“I need to talk to him !
“Mr President ! akasema
Zari
“Zari I need to talk to him now ! I want to tell him how important this man is so that they do all they can to save his life” akasema Rais Festus kwa sauti ya juu.Zari akainuka akaenda katikachumba cha upasuaji akabonyeza kengele na baada ya sekunde chache mlango ukafunguliwa na muuguzi aliyekuwa amevaa mavazi maalum
“Mwambie Dr Fred ,Rais yuko hapa anataka kuzungumza naye sasa hivi” akasema Zari.Baada ya dakika chache Dr Fred akatoka katika chumba cha upasuaji akaelekea katika chumba cha mapumziko alikokuwa Rais
“Mheshimiwa Rais” akasema Dr Fred
“DrFred samahani
nimekutoa katika upasuaji
“Usijali mheshimiwa
Rais”akasema Dr Festus
“Mnaendeleaje na
upasuaji? Akauliza Rais
“Tunaendelea.Tayari
tumekwisha toa risasi mbili zilizokuwa tumboni lakini limejitokeza tena tatizo lingine.Kuna damu nyingi inaendelea kuvuja tunaendelea kutafuta kujua mahala inakovuja damu hiyo tuweze kuizuia” akasema DrFred
“Dr Fred kwanza ninakushukuru wewe na wenzako wote kwa jitihada mnazoendelea nazo kuokoa maisha ya Mathew lakini nataka nikwambie jambo moja kwamba huyu mtu ambaye mnahangaika kuokoa maisha yake ni mtu muhimu mno kwangu na kwa nchi pia na ndiyo maana umeniona hapa usiku huu.Nataka nikuombe wewe na timu yako kufanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya huyu mtu.Mimi nitakuwepo hapa hadi upasuaji utakapokamilika na chochote kile ambacho kitahitajika uniambie kitapatikana na hata kama ni kuongeza madaktari na vifaa nieleze tafadhali” akasema Rais Festus
“Ahsante sana mheshimiwa Rais.Ninakuahidi tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunaokoa maisha ya Mathew” akasema DrFred na kurejea katika chumba cha upasuaji
“Ladies najua jambo hili limetustua sote lakini nawaomba tuwe na imani tumuombe Mungu amlinde Mathew.Tuwe na imani na madaktari watafanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya Mathew Mulumbi” akasema Rais Festus kisha wakaelekea katika ofisi ya Zari
“Zari nini hasa kilitokea hadi Mathew akapigwa risasi? Akauliza Rais Festus.Zari akafuta machozi na kuanza kuwaelezea kilichotokea nyumbani kwa mchungaji Lucas.
“Walifahamuje kama mko pale? Akauliza Ruby na mara Zari akakumbuka kitu
“Find..if..t.t.ther..e is hidden cameras !
Maneno yale aliyoambiwa na Mathew yakajirudia kichwani kwake
“Kuna kitu Mathew
Mulumbi aliniambia wakati tukiwa njiani kuja huku hospitali lakini kwa wakati ule nilikuwa nimechanganyikiwa na sikutilia maanani lakini sasa ninaanza kuelewa kile alichokimaanisha”
“Alisemaje
Mathew?Akauliza Rais Festus
“Aliniambia nitafute kamera za siri nadhani alimaanisha ndani ya ile nyumba kuna kamera za siri zimefungwa na watu waliofunga kamera hizo za siri walikuwa wanafuatilia kila kinachoendelea na ndiyo maana wakaweza kujua kama tuko pale wakaja mara moja na kufanya mauji yale.Mtu wa kwanza kabisa kuuawa alikuwa ni mchungaji Lucas na waliwahi kumuua ili
asiendelee kuzungumza nasi” akasema zari
“Zari tuma timu ya wataalamu wa ufundi waende haraka sana ndani ya hiyo nyumba wafanye uchunguzi kama kuna kamera za siri
humo ndani”akasema Rais festus
“Mheshimiwa Rais kuna uwezekano mpaka sasa polisi watakuwa wamepata taarifa za mauaji hayo na watakuwa eneo
la tukio.Watu wetu hawataweza kuingia mle ndani” akasema Zari “Hata kama wakikuta kuna askari polisi wamekwisha fika watoe taarifa na mimi nitatoa kibali waingie ndani wafanye kazi yao.Lazima tujue kama kuna kamera za siri zimefungwa ndani ya hiyo nyumba”akasema Rais Festus na Zari akaenda kutoa maelekezo kwa timu ya wataalamu wa kamera wakaondoka kuelekea nyumbani kwa mchungaji
Lucas na Zari akarejea ofisini
“Jamani kuna jambo bado lina ukakasi” akasema Ruby “Tuna imani kabisa kwamba waliofanya mauaji hayo ni watu kutoka kundi la Black mafia ambao ndiyo tunapambana nao.Ninajiuliza kuna nini hadi Black Mafia wafunge kamera za siri nyumbani kwa mchungaji Lucas.Kwa nini wamfuatilie kupitia kamera? Akauliza Ruby
“Kweli hapo
panachanganya sana lakini ngoja kwanza tujiridhishe kama kweli kuna kamera za siri humo ndani ya nyumba ya mchungaji halafu tutajua nini cha kufanya” akasema Rais Festus
“Kabla hajauawa mchugaji Lucas kuna kitu gani alikuwa amewaeleza? Ruby akauliza
“Mazungumzo yetu ndiyo kwanza yalikuwa yameanza.Tulimuuliza kuhusu sababu ya mchungaji Adam kusafiri na kuna mambo alitueleza.Alisema kwamba siku ile yeye na baadhi na wachungaji waliitwa kushiriki katika maombi maalum ya kumuombea mtoto wa mchungaji Adam aliyekuwa ametoweka shuleni katika mazingira ya kutatanisha.Wakati wakiendelea na maombi nabii mkuu Kasiano akasimamisha maombi na kuwaeleza kwamba Mungu amempa maono wakati tukiomba na kumuonyesha kuwa mtoto yuko salama.Baada ya hapo mchungaji Adam na mke wake wakaelekea ofisini kwa nabii Kasiano na yeye Lucas hakujua kilichoendelea tena hadi pale alipopata taarifa kwamba Adam na mke wake wamefariki kwa ajali ya gari wakati wakielekea Morogoro” akasema Zari
“Awali ulipojifanya mwandishi na kumuuliza nabii Kasiano kuhusu safari ya Adam alidai kuwa yeye ndiye aliyemtuma Morogoro kwa shughuli za kikanisa.Tulikuwa tunajiuliza inawezekanaje mchungaji Adam kuacha kumtafuta mwanae aliyepotea na badala yake akafunga safari ya kwenda Morogoro?Sasa nimepata picha kwamba Nabii Kasiano baada ya kuonyeshwa maono ya kinabii kwamba mtoto wa mchungaji Adam yuko salama ndipo akamtuma kwenda Morogoro na inawezekana alikuwa katika mwendo mkali sana ili aweze kufika Morogoro na kurejea ili aweze kumtafuta mwanae na ndiyo maana wakapata ajali mbaya wakafariki dunia.Lakini
swali ninalojiuliza kwa nini hakumuacha mke wake aendelee kumfuatilia mtoto wao na yeye akaenda Morogoro peke yake badala ya wote kuongozana katika safari hiyo? Akauliza Ruby
“Tulimuuliza mchungaji
Lucas kama kulikuwa na shughuli yoyote ya kikanisa iliyomlazimu Adam kwenda Morogo……………” akanyamaza
Zari baada ya simu yake kuita
“Hallow”
“Madam unahitajika Afya” akasema muuguzi na Zari akiwa ameongoza na Rais Festus na Ruby wakatoka mbio kuelekea upande wa Afya moja kwa moja ofisini kwa Dr Fred
“Kuna nini Dr Fred? Akauliza Rais Festus
“We need
blood.Tumeishiwa damu na mgonjwa bado anapoteza damu nyingi”
“Bado hamjafanikiwa kujua sehemu inakovuja ndani kwa ndani? Akauliza Rais Festus
“Tunaendelea mheshimiwa Rais.Tunaendelea
kulishughulikia hilo ndiyo maana tunaomba msaada wa damu tumeishiwa”
“Ni damu ya kundi gani mnaihitaji?
“Mathew ni kundi B- hivyo anapokea damu kutoka kundi B- au kundi O- tu”
“Mimi ni kundi O- hivyo hakuna muda wa kupoteza.Nitoeni damu awezekewe Mathew mara moja” akasema Rais Festus na taratibu za kutoa damu zikaanza mara moja.
************
Kwa zaidi ya saa moja
mama Bella mke wa Rais
Festus alikuwa katika simu akizungumza na mtu na
maongezi yao yalionekana
kujaa mahaba mazito.Sauti
ilikuwa ya chini na
laini.Wakati Bella akiendelea
na mazungumzo simuni mara
akasikia mlio katika simu yake
kuashiria kuna simu ilikuwa
inapigwa.
“Patrick samahani naomba
nikate simu,kuna simu
nyingine nataka
kuipokea.Nitakupigia tena
baada ya muda mfupi”
akasema mama Bella na
kukata simu halafu akaipokea
simu ile nyingine “Kelvin” akasema mama
Bella
“Mama ulinipa maelekezo
kwamba nikujulishe kila
mahala anakoenda Rais”
“Ndiyo Kelvin”
“Mama tumekuja hapa
kwenye ofisi Fulani panaitwa
SNSA.Kuna hospitali kubwa
humu ndani na Rais hivi sasa
anatolewa damu”
“Anatolewa damu?!
Akauliza Bella kwa mshangao
“Ndiyo mama.Anatolewa
damu.Nimesikia kuna mgonjwa amejeruhiwa kwa
risasi anaitwa Mathew ambaye
kwa sasa yuko katika chumba
cha upasuaji na hali yake
inasemwa si nzuri,nadhani
anatoa damu kwa ajili hiyo”
“Kelvin una hakika
umesikia vizuri jina hilo la
mgonjwa anayefanyiwa
upasuaji?
“Ndiyo mama.Nimesikia
wakimtaja kwa jina hilo la
Mathew” akasema Kelvin
“Ahsante sana Kelvin
endelea kufanya uchunguzi
zaidi upate taarifa za kutoshaza mgonjwa huyo halafu
utanijulisha.One more
thing,umenifurahisha sana
Kelvin kwa kazi yako nzuri
,nitakupa mara tatu zaidi ya
kiasi kile nilichokuahidi
kukupa” akasema Bella
“Ahsante sana mama
nashukuru” akasema Kelvin na
Bella akakata simu
“Ni kweli hiki
nilichokisikia au niko ndotoni?
Ngoja kwanza nipate uhakika
zaidi” akawaza Bella na
kuchukua simu akampigia
nabii Kasiano “Mama Bella”akasema
Kasiano
“Kasiano nataka kufahamu
kuna tukio lolote limetokea
usiku huu linahusisha vijana
wako? Akauliza Bella
“Ndiyo mama.Nilipata
taarifa kwamba kuna watu
wamekwenda kwa mmoja wa
wachungaji wa kanisa langu na
wanamuhoji mchungaji huyo
kuhusiana na kifo cha
mchungaji Adam.Katika
nyumba zangu zote wanakoishi
wafanyakazi kuanzia
wachungaji na wanafanyakazi wengine kumefungwa kamera
za siri ambazo zinafuatiliwa
kwa saa ishirini na nne na
watu wa Black Mafia.Lengo ni
kuhakikisha kwamba hakuna
yeyote anayegeuka na kuwa
hatari kwangu.Baada ya
kupata taarifa hiyo nilitoa
maelekezo kwa vijana kwenda
kulimaliza hilo jambo.Kuna
nini mama Bella hadi
ukaniuliza? Akauliza Kasiano
“Mathew Mulumbi
alikuwemo katika hiyo
nyumba’ akasema Bella“Mathew Mulumbi?!
Kasiano akashangaa
“Ndiyo.Kwa bahati mbaya
amejeruhiwa kwa risasi na kwa
sasa anapatiwa matibabu
katika ofisi za SNSA”
“SNSA?
“Ndiyo.Nimepata taarifa
hivi sasa kuwa Mathew yuko
huko na anapatiwa
matibabu.Festus amejulishwa
kuhusu hilo tukio naye
ametoka hapa na kuelekea
huko SNSA na hivi
tuzungumzavyo anatoa damu
kwa ajili ya kuwekewa Mathew ambaye amepoteza damu
nyingi.Kasiano tumempata
Mathew.Muda si mrefu vita
itamalizika na amani itarejea”
akasema Bella
“Mama Bella nakushukuru
mno kwa taarifa hii njema kwa
sasa ni kuanza mipango ya
kuhakikisha tunafanikiwa
kuingia hapo SNSA na
kummaliza kabisa Mathew
Mulumbi .Huyu pekee ndiye
wanayemtegemea na kama
tukifanikiwa kumuondoa huyu
mtu basi ushindi utakuwa
wetu.Usiku huu huu
maandalizi ya kuingia ndani ya jengo hilo yanaanza na mpaka
kufika kesho asubuhi tayari
tutakuwa na mpango wa
kutuwezesha kuingia na
kummaliza Mathew Mulumbi”
akasema Kasiano
“Kasiano vita hii nataka
ifike mwisho,sitaki kusikia
tena kuna kosa lolote
limetokea na tukashindwa
kummaliza huyo Mathew
Mulumbi.Sitaki kusikia hadi
kufika kesho jioni kuna
kiumbe hapa duniani kinaitwa
Mathew Mulumbi.Nadhani
umenielewa Kasiano” “Nimekuelewa mama”
akasema Kasiano na Bella
akakata simu
“Siamini kama
tumefanikiwa kumpata mtu
ambaye amekuwa akituumiza
vichwa vyetu sana.Nitawapa
zawadi hao jamaa
waliofanikiwa kumpiga risasi
huyo Mathew Mulumbi.Wao
ndiyo wamesababisha
tukaweza kufahamu alipo huyu
mtu” akawaza Bella
“Baada ya kumuondoa
Mathew sasa tutamgeukia
Festus.Lazima atafanya kila tutakachomuelekeza akifanye !
akaendelea kuwaza
************
Wakati Rais Festus
akiendelea kutolewa damu
kwa ajili ya kumuwekea
Mathew Mulumbi,Zari na
Ruby walikuwa katika chumba
cha mapumziko na kila moja
akiwa mawazoni.
“Mam do you need
anything” sauti ya kiume
ikasikika, Zari na Ruby wote
wakainua vichwa na kumuona
moja wa walinzi wa Rais
akiwatazama “No thank you” akajibu
Zari
“Samahani kwa
kuuliza.Huyu mtu ambaye
yuko kwenye upasuaji ni nani?
Akauliza Yule mlinzi wa
Rais.Kabla Zari hajajibu simu
yake ikaita .Alikuwa ni
kiongozi wa ile timu ya wa
wataalamu waliotumwa
kwenda katika nyumba ya
mchungaji Lucas kuchunguza
kama kuna kamera za siri
zimefungwa humo ndani
“Hallo Jacob” akasema
Zari “Mkurugenzi tumefika
hapa mahala ulipotuelekeza
lakini kuna tukio limetokea
hapa”
“Kuna tukio gani hapo?
“Nyumba uliyotutuma
inateketea kwa moto hivi sasa”
“Inawaka moto?
“Ndiyo mkurugenzi.Kuna
moto mkubwa unawaka hapa
na tayari vikosi vya zimamoto
na uokoaji vimekwisha fika
vinaendelea na kazi ya kuuzima moto huu mkubwa”
akasema Jacob
“Thank you Jacob.Rudini
ofisini” akasema Zari
“Kuna nini? Akauliza Ruby
“Nimetaarifiwa na ile timu
niliyoituma kwenda
kuchunguza ile nyumba kama
kuna kamera za siri ndani yake
kuwa nyumba hiyo kwa sasa
inawaka moto
“Inawaka moto? Ruby
akauliza
“Ndiyo.Inawezekana
jamaa walihisi penginetungeweza kurejea na kufanya
uchunguzi kubaini kama kuna
kamera za siri na wakaamua
kuichoma moto”akasema Zari
“Inawezekanaje hawa
jamaa wakawa wanafahamu
kila tunachotaka kukifanya?
Wamegundua kama akina
Mathew wamekwenda
kumuhoji mchungaji Lucas na
wakaenda
kumuua,wamegundua kuna
watu wanakwenda kuchunguza
ile nyumba kama kuna kamera
za siri wakawahi kuichoma
moto.Niliwahi kumueleza
Mathew wasiwasi wangu
kuhusianana huyu Zari .I
don’t trust her.Haiwezekani
kila tunapopanga mpango
Fulani tarifa zake zinavuja na
na jamaa wanawahi kufahamu
kabla hatujafika.Kama Mathew
Mulumbi akifariki I swear I’ll
kill her ! akawaza Ruby akiwa
amekasirika kupita kifani.
“Lakini kama Zari ana
mahusiano na hawa jamaa kwa
nini wakataka
kumuua?Ametueleza kuwa ni
Mathew ndiye aliyeyaokoa
maisha yake leo kwa kumkinga
na risasi.Hapana sina hakika
kama Zari ana mawasiliano na hawa jamaa.Sasa wanajuaje
mipango yetu? Akajiuliza Ruby
na mara akaingia Rais Festus
“Pole mheshimiwa Rais”
Zari na Ruby wakampa Rais
pole
“Ahsanteni
sana.Nawaomba tusichoke
tuendelee kumuombea
Mathew na Mungu atasikia
maombi yetu” akasema Rais
Festus na kuwataka walinzi
wake waende nje wawaache
peke yao mle ndani
“Mheshimiwa Rais
tumepokea taarifa kutoka kwa wale wataalamu niliowatuma
kwenda kufanya uchunguzi
katika ile nyumba ya
mchungaji Lucas kama kuna
kamera za siri kwamba
nyumba hiyo hivi sasa
inateketea kwa moto” akasema
Zari
“Inateketea moto? Rais
akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Nyumba hiyo kwa sasa
inateketea kwa moto”
“Wamejuaje kuna watu
wanakwenda kuchunguza ile
nyumba?” akauliza Rais Festus “Mheshimiwa Rais hata
sisi sote tunashangaa namna
walivyoweza kugundua kuna
watu wetu wanakwenda hapo
na wakaichoma nyumba moto”
akasema Zari
“Hawa watu wanatumia
nguvu za giza” akasema Rais
Festus
“Kama hawatumii nguvu
za giza katika mambo yao basi
lazima kuna watu wao hata
hapa SNSA ambao wanawapa
taarifa kwa sababu
haiwezekani tumeliamua
jambo hili hapa halafu linawafikia hawa
jamaa.Imenishangaza
sana.Kuweni makini sana
katika hili suala msiwape
taarifa zozote watu wale
ambao hamuwaamini.Sina
imani kabisa hivi sasa kwani
hawa jamaa wameweza
kupenyeza mizizi yao sehemu
mbali mbali” akasema Rais
Festus na kuwataka akina
warejee ofisini.
“Ladies kama
mnavyoshuhudia wenyewe
mambo yanavyokwenda
wenzetu hawalali katika
kuhakikisha wanashinda vita hii hivyo sisi pia hakuna
kulala.Tutafanya kazi usiku na
mchana.Ninajua mmeumizwa
mno na tukio hili la kuumizwa
Mathew lakini vyovyote vile
itakavyokuwa lazima kazi
iendelee.Hawa jamaa
watafanya kila wawezalo
kuturudisha nyuma lakini katu
tusikubali kurudishwa nyuma
na washeni hawa.Tunapaswa
kuendelea kupambana bila
kuchoka.Wakati madaktari
wakiendelea na jitihada za
kuokoa maisha ya Mathew sisi
tuendelee na kazi”akasema
Rais Festus “Mheshimiwa rais tukio
hili lililotokea ni kubwa.Kama
si kwa Mathew Mulumbi
kujitoa mhanga na kupigwa
yeye risasi badala yangu hivi
sasa ningekwisha poteza
maisha.Utanisamehe
mheshimiwa rais kwa sasa
akili yangu haijakaa sawa bado
na siwezi tena kuendelea na
chochote hadi nitakapofahamu
hatima ya Mathew Mulumbi”
akasema Zari
“Zari please !
“Utanisamehe
mheshimiwa Rais.Kwa sasa kipaumbele kinatakwia kuwa
ni kwa Mathew
Mulumbi.Siwezi kupepesa
macho kusema kwamba yeye
ndiye kinara wetu katika
misheni hii na siwezi kuficha
kwamba bila yeye misheni au
vita hii itakuwa imefika
mwisho.Si mimi wala Ruby
anayeweza akafanya yale
anayoyafanya Mathew
Mulumbi” Akasema Zari
“Zari is right Mr
President.Tusimamishe kila
kitu kwa sasa na tujielekeze
katika kuhakikisha Mathew
Mulumbi anapona.Lolotelinaloweza kufanyika basi
lifanyike ili Mathew apone”
akasema Ruby
“Sawa
nimewaelewa”akasema Rais
Festus kisha wakaenda katika
chumba cha mapumziko
kusubiri madaktari waweze
kumaliza upasuaji
“Wanangu wanaendeleaje
mheshimiwa Rais? Akauliza
Ruby na Rais Festus
akachukua muda kidogo
kujibu halafu akasema “Ruby kuna jambo ambalo
sikuwa nimekueleza” akasema
Rais na Ruby akastuka sana
“Kuna nini mheshimiwa
Rais? Akauliza Ruby
“Kuna jambo ambalo
sikuwa nimekueleza.Watoto
wako hawako hapa Tanzania”
“Hawako Tanzania?
Akauliza Ruby kwa mshangao
mkubwa
“Niliwapeleka kwa Rais wa
Rwanda ambaye ni rafiki
yangu mkubwa” akasema Rais
Festus “Kwa nini mheshimiwa
Rais ukafanya hivyo bila
kunijulisha?
“Usihofu Ruby wanao
wako salama kabisa.Sikutaka
ijulikane kuwa wanao wako
ikulu wangekuwa katika hatari
zaidi ndiyo maana
nikawahamisha kimya kimya
kuwapeleka kwa Rais wa
Rwanda.Ninawasiliana naye
kila siku na wanaendelea
vyema usiwe na hofu yoyote”
akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
hukutakiwa kufanya hivyo bila kunishirikisha kwanza
mimi.Umenichanganya zaidi!
Akasema Ruby
“Ruby ulinikabidhi watoto
wako niwahifadhi na
kuhakikisha wanakuwa salama
na ndivyo
nilivyofanya.Nimewapeleka
mahala ambako watakuwa
salama.Naomba uniamini
katika hilo na watoto wako
salama kabisa” akasema Rais
Festus
“If anything happens to
them I’ll never forgive you !
akasema Ruby “Hakuna chochote
kitakachotokea kwa wanao
Ruby niamini” akasema rais
Festus na ukimya ukatawala
wote wakiendelea kutafakari
huku wakisubiri kupata taarifa
kutoka kwa madaktari.
“Mheshimiwa Rais
unadhani kwa nini hadi sasa
wale jamaa hawajaweza
kuzisambaza picha zako kama
walivyokuwa wamekusudia?
Akauliza Zari
“Hata mimi nimekuwa
najiuliza sijapata jibu ni kwa
nini hawajasambaza zile picha zangu kama walivyokuwa
wametishia kufanya”
“Unadhani wameogopa
kufanya hivyo?
“Sijui kama wameogopa au
nini kimetokea lakini
ninachojua ni kwamba
mapambano
hayajakwisha.Kama
hawajasambaza leo hata kesho
au siku nyingine yoyote
wanaweza wakasambaza lakini
hata siku moja hawawezi
kuogopa lazima tuendelee
kupambana” akasema Rais
Festus “Lazima ipo sababu
iliyowafanya hao jamaa
wakaacha kusambaza picha
hizo kama walivyokuwa
wamekusudia” akasema Zari
“Kwa vyovyote vile
watakavyofanya lakini
haturudi nyuma nimekwisha
kubali kubeba aibu ile lakini
sintainua mikono na kukubali
kushindwa vita” akasema Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais
samahani kwa hiki
nitakachouliza yawezekana ni
jambo binafsi sana lakini kama itakupendeza unaweza
ukanipa jibu”akasema Ruby
“Uliza Ruby usihofu”
“Wewe na Zandile
Wepener.Ilikuaje mkaingia
katika mahusiano? Akauliza
Ruby “Msiniambie
mmeanza kuchunguza
mahusiano yangu na Zandile”
akasema Festus
“Hapana mheshimiwa
Rais hatuwezi kufanya
hivyo.Ninahitaji tu
kufahamu.Mimi ni mmoja wa
watu wanaomfuatilia sana
Zandile hasa katika mavazi na niliposikia kwamba uko naye
katika mahusiano nilihisi hadi
nywele zangu
zinasisimka.Zandile ni
mwanamke mrembo mno.How
did you guys meet? Akauliza
Ruby na kwa mara ya kwanza
tangu amefika pale usiku ule
Rais Festus akatabasamu
“Kuingia katika mahusiano
na Zandile halikuwa jambo
jepesi.Kwanza ni mwanamke
mwenye jina kubwa
duniani,ukiachana na utajiri
wake sifa kubwa iliyowahi
kumtambulisha duniani ni
kuolewa na kuachana na mfalme wa Eswatini ndoa yao
ikiwa na miaka miwili tu.Kama
mnafuatilia habari
mtakumbuka ni namna gani
habari hiyo ilivyotawala katika
vyombo mbali mbali vya
habari duniani na umaarufu
wa Zandile ukapaa
mawinguni” akasema Rais
Festus
“Ninyi ni watu wangu na
leo nitawapa siri ila naomba
nitakayowaeleza yabaki humu
humu yasitoke nje”
“You can trust us mr
President” akasema Ruby “Kwanza kabisa mimi na
mke wangu kwa muda mrefu
sasa hatuna maelewano
mazuri.Kuna mgogoro
mkubwa kati yetu na sitaki
kulizungumzia
hilo.Ninawashauri kabla ya
kufunga ndoa kwa wale ambao
bado,mjitafakari mara mbili
mbili kama kweli huyo
uliyenaye anakufaa.Ukikosea
utateseka hadi
kaburini.Tunaulizwa swali na
wanaotufungisha ndoa
kwamba Fulani bin Fulani uko
tayari kumpoke Fulani kuwa
mumeo au mkeo na tunajibu ndiyo.Lile neno ndiyo ni
kubwa mno japo ni rahisi sana
kulitamka.Kama huna uhakika
na mtu anayekutaka mfunge
naye ndoa tafadhali usitamke
ndiyo.Hayo ndiyo
tunayokutana nayo katika
ndoa.Ni mambo
mazito.Tukirudi katika swali
uliloniuliza ni kwamba Zandile
nilikutana naye nchini Afrika
kusini katika mkutano wa
SADC ulifanyika nchini
humo.Wakati nikizungukia
mabanda ya wafanya biashara
waliofika katika mkutano huo
kuonyesha na kutangazabiashara zao nilimkuta Zandile
katika banda la shirika la
hifadhi la taifa akipata taarifa
mbalimbali kuhusiana na
vivutio mbali mbali
vinavyopatikana nchini
Tanzania.Wakati huo bado
alikuwa ni mke wa mfalme na
akajitambulisha kwangu
tukasalimiana akaniambia
kwamba amefurahi sana kwa
taarifa alizozipata katika
banda la hifadhi za taifa na
mimi nikatumia nafasi hiyo
kumkaribisha sana nchini
Tanzania na akaahidi atakuja
kutembea.Siku moja nikapigiwa simu na
kufahamishwa kwamba mke
wa mfalme wa Eswatini
anataka kuja kutembelea
Tanzania nikaelekeza taratibu
zifuatwe na akafika
akapokelewa kama mke wa
kiongozi wa nchi akatembezwa
katika hifadhi mbali mbali na
alifurahi sana.Aliporejea kwao
Eswatini akanipigia simu
akanijulisha kwamba
ameipenda sana Tanzania na
angependa awe na makazi yake
hapa.Mimi nilimkubalia na
kuahidi kumsaidia hivyo
nikanunua jumba moja kubwa kandoni mwa bahari kwa jina
langu na nikamtumia picha
akalitazama akafurahi sana na
baada ya wiki mbili akaja tena
Tanzania lakini safari hii
alitaka iwe ni ziara ya kimya
kimya na asitangazwe kwani
hakutaka watu wajue kama
yuko Tanzania.Alifikia katika
jumba lile nililokuwa
nimemnunulia akalipenda
sana.Jioni ya siku hiyo
akanialika tukapate chakula
cha usiku.Wakati huo tayari
mgogoro kati yangu na mke
wangu umepamba moto
nikajikuta nikivutiwa sana na Zandile.Licha ya uzuri wake
lakini ni mwanamke mwenye
adabu nyingi,anajua kujali na
hata kubembeleza pia mambo
ambayo niliyakosa sana katika
ndoa yangu.Nakumbuka
nilimuomba tukakae nje
tupunge upepo na mambo yote
yalianzia siku ile”
“So did you uhm….did
you…….” Ruby akataka kuuliza
kitu
“Yes we did it kama una
maanisha mapenzi.Tulifanya
usiku ule na huo ukawa ni
mwanzo wa mke wangu
kuhama chumba baada
yakugundua kwamba
nimekutana kimwili na
mwanamke mwingine.Mimi na
Zandile tulitokea kupendana
mno na akawa akija Tanzania
mara kwa mara nadhani hiyo
ni sababu kubwa iliyovunja
ndoa yake na mfalme wa
Eswatini.Hakuwahi kutamka
hadharani sababu ya ndoa
yake kuvunjika bali
kilichosemwa tu ni Zandile
kukosa uaminifu ila sababu
kubwa ni hiyo.Baada ya
kuachana na mume wake
mapenzi yetu yamezidi kupamba moto na Zandi
amekuwa akija Tanzania
karibu kila mwisho wa
wiki.Wanaolifahamu jambo
hili ni watu wangu wa karibu
sana na imekuwa ni siri kubwa
lakini nashangaa kwa namna
picha zile zilivyopigwa”
akasema Rais Festus
“Dah ! Simulizi hii
inasisimua sana mheshimiwa
Rais.Mama Bella anafahamu
kama uko na Zandile?
“Anafahamu kuwa niko
katika mahusiano na
mwanamke fulani lakini hajui kama ni Zandile.Hata kama
akifahamu haitaharibu
chochote katika mahusiano
yangu na Zandi kwani
tumekwisha kubaliana kuwa
tuendelee kubaki kama mume
na mke hadi pale
nitakapokuwa nimemaliza
muhula wangu wa urais kisha
kila mmoja ataendelea na
maisha yake” akasema Rais
Festus
“Mheshimiwa rais kama
mfalme wa Eswatin alifahamu
kuhusu mahusiano yako na
mke wake na wakaachana kwa
sababu hiyo hudhani labda katika suala hili la picha
anaweza kuwa anahusika?
Akauliza Zari
“Sina hakika na mfalme
Yule hana sababu ya kufanya
hivyo.Hili jambo limefanywa
na hawa wahuni majambazi
wakubwa na ninaapa
kuwasaka hadi mtu wao wa
mwisho”
“Unadhani Zandile
atalichukuliaje suala hili la
kusambaa kwa picha zenu za
faragha? Ruby akauliza
“Bado sijamfahamisha
chochote kuhusiana na suala hili lakini itanilazimu
kumfahamisha ili ajue
kinachoendelea na hata kama
picha hizi zitavuja basi awe
akifahamu” akasema Rais
Festus
Nabii Kasiano alifika katika hospitaliya Mtodora ambako miili ya marehemu mchungaji Lucas na familia yake ilipelekwa.Ilikuwa imeungua vibaya sana kwa moto kiasi cha kutoweza kutambulika.Akiwa na mke wake Rita walionyeshwa miili ile ya marehemu na Kasiano akatoa machozi.Akainua mikono juu na kuomba halafu
wakarejea katika gari lao na kuondoka akamuelekeza dereva wake awapeleke katika nyumba iliyoungua ya mchungaji Lucas.Nyumba yote ilikuwa imeteketea na hakuna hata kitu kimoja kilichookolewa.Hawakukaa
sana eneo lile wakarejea nyumbani
“Lucas alikuwa bado kijana sana na ni mmoja wa wachungaji aliyekuwa anapendwa mno na watu na hata mimi nilimpenda sana.Nasikitika mwisho wake umekuwa namna hii.Sikuwahi kutegemea kabisa kama siku moja ningeyaondoa maisha ya kijana Yule.Yote haya yamesababishwa na Mathew Mulumbi.Usingizi aliolala sasa pone pone yake asiamke kwani akiamka mateso atakayoyapata ni makubwa mno.Hakutakuwa na kumkabidhi kwa jeshi la polisi nitahakikisha ninamuua mimi mwenyewe kwa mkono wangu.Hajawahi kutokea mtu aliyewahi kunisumbua mimi na mtandao wangu kama huyu jamaa.Baada ya kumuondoa nitaendelea na vita na Rais nataka apige magoti na kuinua mikono juu na hapo ndipo tutakapofanya shughuli zetu kwa amani bila kusumbuliwa na kitu chochote ! akawaza Kasiano
“Rita nimeumia sana
baada ya kuiona miili ya Lucas na familia yake.Sikutegemea kama mwishowa Lucas ungekuwa namna hii” akasema Kasiano wakiwa chumbani baada ya kuwasili nyumbani kwao
“Kasiano tumefanya mengi na tumeondoa uhai wa watu wengi pia ila kwa hili la Lucas hata mimi imeniumiza sana.Tafadhali nakuomba uhakikishe Mathew Mulumbi anapatikana kwani yeye ndiye chanzo cha haya yote yaliyotokea leo na kutulazimisha kumpoteza Yule mchungaji kijana” akasema
Rita
“Mathew Mulumbi saa zake zinahesabika.Hana muda mrefu kuanzia sasa kama bado ataendelea kuwa hai huko aliko.Nataka suala hili lifike mwisho ! akasema kwa hasira Kasiano na kunyamaza baada ya simu yake kuita walikuwa ni walinzi wake wakamjlisha kwamba kuna mgeni wake amefika,akatoka kwenda kumpokea,alikuwa ni DCI David Chamwino akamkaribisha katika sebule yake.
“Pole sana Kasiano kwa haya yaliyotokea leo” akasema David’
“Ahsante sana
David.Mambo yanazidi kubadilika kila siku lakini tunaelekea mwishoni.Vipi kwa upande wako mambo yanakwendaje?
“Kwa upande wangu mambo yanakwenda vizuri kama mlivyosikia tayari Dr Fabian amekwisha fikishwa mahakamani na kesi imeanza kusomwa.Kitu cha msingi ni kuhakikisha Mathew Mulumbi anapatikana kwani yeye ndiye
muhusika mkuu katika kesi
hii”
“Akipatikana
hatutamkabidhi kwa jeshi la polisi.We’ll kill him ! akasema Kasiano
“Tukimuondoa Mathew
kesi ya Dr Fabian haitakuwa na nguvu na anaweza akaachiwa huru”
“I don’t care lakini ninachokihitaji ni Mathew Mulumbi aondoke kabisa katika picha hii.Hawa wengine akina Fabian hawana madhara makubwa na tunaweza tukawaondoa taratibu au tukawafunga kabisa midomo yao wakabaki kimya.Kama tumeweza kumpa joto Rais wa nchi na akakiri makosa yake hadharani hatuwezi kushindwa kuwanyamazisha watu kama akina Fabian wasio na nguvu yoyote.We’re powerfull people David.Ni mtu mmoja tu ambaye anatuumiza vichwa vyetu huyu Mathew Mulumbi lakini naye hana muda mrefu”Simu ya Kasiano ikaita akajulishwa kwamba mgeni wake mwingine amewasili huyu alikuwa ni naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Keofas Mabula.
“Ndugu zangu karibuni sana na mtanisamehe kwa kuwasumbua usiku huu ambao ni muda wa mapumziko” akasema Kasiano
“Kasiano hakuna muda wa mapumziko.Sisi muda wote tuko kazini hivyo usione kama vile umetusumbua.Sisi ni watu wako hivyo kuwa huru kutuita muda wowote na kutuhabarisha au kutupa kazi” akasema David Chamwino “Ahsanteni.Nadhani
tuendelee na kikao na wale watakaochelewa watakuta sisi tunaendelea.Nimewaiteni usiku huu kuna taarifa ninataka kuwapeni ambayo ni nzuri.Ni kwamba tumefanikiwa kujua mahala aliko Mathew Mulumbi”
“Mmefanikiwa kujua mahala aliko Mathew Mulumbi? Akauliza Keofas
“Ndiyo Keo” akajibu Kasiano na kujulishwa kwamba kuna mgeni mwigine alikuwa amewasili huyu alikuwa ni Paul Lewis.
“Karibu Paul bado hujachelewa kwani tumeanza kikao muda mfupi uliopita” akasema Kasiano
“Usiku huu nilijulishwa kuwa kwa mmoja wa wachungaji wangu kuna watu wawili wanamfanyia mahojiano kuhusiana na kifo cha mchungaji Adam.Nilijua moja kwa moja watu hao wametumwa au wana mahusiano na Mathew Mulumbi nikawaagiza vijana wangu wafike haraka sana mahala hapo na kuwaondoa wote.Vijana wamefanya kazi nzuri sana leo na walifika kwa haraka wakamuondoa Lucas familia yake na wale jamaa waliofika kumuhoji Lucas.Baadae nikapewa ushauri na Paul kuwa tuichome moto nyumba ile ili watu wasijue kama Lucas na familia yake wameuawa kwa
risasi na ndilo tukio lililotokea usiku huu.Hakuna anayefahamu kama kabla ya kuchomwa moto Lucas na familia yake tayari walikwisha uawa kwa risasi”akanyamaza kidogo
“Baadaye nikapata taarifa kutoka kwa vyanzo vyangu vya taarifa kwamba mtu aliyepigwa risasi katika nyumba ile ni Mathew Mulumbi na amepelekwa katika ofisi za SNSA ambako anapatiwa matibabu na hali yake si nzuri.Kama mtakumbuka mara ya mwisho tulipokutana niliwaeleza kuhusu mashirikiano ya Rais na idara hii ya siri.Huko ndiko aliko Mathew Mulumbi kwa sasa.Nimewaiteni hapa usiku huu kuwapeni taarifa hizo kwamba tunakaribia kufika mwisho wa vita hii hivyo tunapaswa kujipanga vizuri kuhakikisha tunaimaliza vyema vita hii na kupata ushindi.Kikubwa hapa ni kutengeneza mpango wa namna ya kuvamia SNSA na kumchukua au kumuua kabisa Mathew Mulumbi.Kama ataendelea kuwa hai baada ya upasuaji huo basi lazima ataendelea kuwepo hapo SNSA akitibiwa na hiyo ni nafasi yetu ya kuvamia mahala hapo na kumchukua” akasema Kasiano.
“Sijui niseme nini kwa mafanikio haya makubwa.Nitachinja ng’ombe na kununua mvinyo ghali kabisa pale tutakapokuwa tumefanikiwa kumuondoa huyu Mwewe” akasema Keofas
“Hawa SNSA ofisi zao ziko wapi? Akauliza David Chamwino
“Kwa maelekezo
niliyopewa ni kwamba jengo la ofisi zao liko karibu na ikulu” “Kama wako karibu na
ikulu basi eneo hilo ni eneo hatari sana.Ulinzi wa maeneo yote ya kuzunguka ikulu ni mkubwa hivyo kama kuna mpango wa kuvamia ofisi hizo kumchukua Mathew lazima tujiandae kweli kweli” akasema Paul Lewis
“Ndiyo maana wakawepo
Black Mafia.Hawa si watalii wamekuja hapa kufanya kazi na nyakati kama hizi ndipo kazi yao inapaswa kuonekana.Ndani ya kundi hilo kuna watu wengi wenye ujuzi na uwezo mkubwa kuna watu ambao ni majasusi,kuna wanajeshi kuna wataalamu wa
kila aina na hata wale waliowahi kuwa makomando nao wapo.Wanalipwa fedha nyingi sana hivyo lazima wafanye kazi tena yenye ufanisi bila kujali wanaifanyia wapi.Hata kama ingekuwa ni kwenda kumchomoa Mathew kutoka ikulu sina shaka na uwezo wa Black Mafia ! akasema Kasiano
“Sikuwahi kuisikia idara
hii hapo kabla na mara ya
kwanza kuisikia ilikuwa kwako
.Nimejaribu kufanyauchunguzi wangu na
nimefanikiwa kumpata mtu
ambaye amewahi kufanya kazi
mahala hapo lakini kwa sasa
amekwisha achana na kazi
hiyo ana kampuni yake ya
ulinzi.Huyu anaweza
akatusaidia sana kufahamu
namna jengo hilo lilivyo na
namna ya kuweza kuingia
humo ndani” akasema Keofas
“Safi sana Keo.Tunapaswa
kumtumia mtu huyo.Fanya
mpango wa kuonana naye kiasi
chochote atakachokihitaji
tutampatia” “Vipi kuhusu zile picha za
Rais? Mbona hazijasambazwa?
Akauliza David na Kasiano
akawaeleza namna ilivyokuwa
na wote wakakubaliana na
mawazo yale ya
Kasiano.Wakaendelea na
majadiliano mengine na kisha
wakatawanyika na kuondoka.
************
Hatimaye baada ya kupita
saa sita tangu Mathew
aingizwe katika chumba cha pasuaji mlango wa chumba
cha upasuaji ukafunguliwa na
Dr Fred pamoja na madakari
wengine waliokuwa
wanamfanyia Mathew upasuaji
wakatoka na wote wakaelekea
alikokuwa Rais na akina Zari
“Poleni sana madaktari”
akasema Rais Festus
“Ahsante mheshimiwa
Rais” wakaitika madaktari
wale na Rais akawaelekeza
waketi “Mheshimiwa Rais
upasuaji umekamilika na
tumefanikiwa kuziondoa risasi
zote tatu.Mbili zilipigwatumboni na moja katika
kalio.Kwa bahati nzuri risasi
zile hazikuweza kuleta
madhara makubwa
tumboni.Wote tulihofia
kuharibiwa kwa viungo kama
ini,uti wa mgongo nk lakini
kote huko kulikuwa salama ila
kilichofanya upasuaji uchukue
muda mrefu ni kutokana na
kuvuja kwa damu ndani ya
mwili na tumechukua muda
mrefu kuitafuta sehemu
iliyokuwa ikivuja na
tulifanikiwa kuipata na
kuiziba.Kwa ujumla upasuaji ulikuwa na mafanikio”
akasema Dr Fred
“Ninawashukuru sana Dr
Fred na wengine wote kwa
namna mlivyoweza kujituma
na kufanikisha upasuaji huu
mkubwa.Mmeokoa maisha ya
mtu muhimu sana kwa nchi
yetu.Ni kutokana na umuhimu
wake ndiyo maana hata mimi
niko hapa muda
huu.Ninachowaomba
madaktari muwe karibu sana
na mgonjwa kuhakikisha
anapata nafuu ya
haraka.Nitaomba orodha yenu
nyote na kesho nitamtuma msaidizi wangu awaletee kila
mmoja tsh milioni 5 lakini
nawaomba kitu kimoja ndugu
zangu hiki kilichofanyika hapa
leo kiwe siri na asitokee mtu
yeyote akavujisha siri hii kwa
mtu yeyote huko nje.Huyu mtu
maisha yake yako hatarini
sana na wanaomtafuta
wakifahamu yuko hapa
hawatashindwa kuja kuvamia
mahala hapa na
kumuua.Tumeelewana ndugu
zangu? Akauliza Rais na
madaktari wakamuitikia
“Nashukuru sana kwa
kunielewa.Je ninaweza kuruhusiwa kwenda
kumtazama mgonjwa kwa
sasa? Najua hawezi
kuzungumza lakini nataka
nimuone sura yake tu
inatosha.Ni mtu wangu wa
muhimu sana” akasema Rais
Festus akavalishwa mavazi
maalum na kupelekwa katika
chumba alimo Mathew
Mulumbi.Alikuwa
amezungukwa na mashine
nyingi zilizokuwa
zimeunganishwa katika mwili
wake kwa ajili ya kumsaidia.
“Pona haraka Mathew.Kila
kitu kimesimama.Vita imesimama tunakusubiri
wewe.Pona haraka shujaa
wangu uje umalizie kazi
uliyokwisha ianza” akasema
Rais Festus kisha akatoka mle
ndani
“Zari vipi kuhusu ulinzi wa
mahali hapa?
“Ulinzi ni wa uhakika sana
mheshimiwa Rais’
“Good.Kama mkihitaji
ulinzi zaidi nijulishe nami
nitaleta walinzi zaidi”
“Hakuna haja mheshimiwa
Rais ulinzi ni wa uhakika sana hapa” akasema Zari
wakamsindikiza Rais hadi
katika gari lake akaondoka
kurejea ikulu.
Baada ya Rais kuondoka
Zari akaomba kuingia katika
chumba alimo Mathew
Mulumbi,alipoziona mashine
zile zilizonganishwa mwilini
mwa Mathew machozi
yakaanza kumtoka
“Why you Mathew
MulumBi? Why now? Akauliza
Zari huku akilia
“Niliwahi kukuuliza kwa
nini huogopi kufa ukanipa jibu ambalo mpaka leo siwezi
kulisahau.Nimekufahamu siku
chache zilizopita lakini nakiri
sijawahi kukutana na mtu wa
pekee kama wewe.Mathew
nashindwa nikuelezeaje .Nina
deni kubwa kwako Mathew
tafadhali nakuomba amka
haraka ili nikulipe deni hili
ambalo hakuna kiasi cha fedha
kinachoweza kutosha
kulilipa.Get well quick Mathew
Mulumbi” akasema Zari na
kushindwa kuendelea kukaa
mle chumbani akatoka akilia.
“Kwa leo sintakwenda
kumtazama Mathew ninaweza nikapoteza fahamu” akasema
Ruby kisha wakaenda ofisini
kwa Zari.
“Zari kuna kitu nimekuwa
nakiwaza”
“Kitu gani Ruby?
“Upasuaji aliofanyiwa
Mathew ni mkubwa na
anaweza akachukua siku
kadhaa ktandani.Kwa
ninavyomfahamu Mathew
akipata nafuu tu anaweza
akataka kuendelea na kazi kitu
ambacho ni hatari sana kwa
afya yake” “Kwa hilo nakubaliana
nawe Ruby.Mathew hata
akifanikiwa kuamka sasa hivi
anaweza akataka kwenda
kazini.Nini ushauri wako
katika hilo? Akauliza Zari
“Ushauri wangu ni
kwamba hatuwezi kuendelea
kumsubiri Mathew hadi
atakapopona kwani hawa
tunaowatafuta hawana muda
wa kusubiri wao kila sekunde
kila dakika kila saa kila siku
wako vitani kuhakikisha
wanaondoa vikwazo vyote
katika biashara zao hivyo
lazima mapambano yaendelee.Kuna mtu anaitwa
Nawal”
“Nawal ? akauliza Zari
“Ndiyo.Huyu ni rafiki yake
Mathew amewahi kufanya kazi
CIA na kwa sasa anafanya
biashara.Ni mtu ambaye
tunaweza kumtumia katika
operesheni hii wakati Mathew
akiwa kitandani.Nawal ni mtu
jasiri sana na nimewahi
kushiriki naye katika misheni
Fulani” akasema Ruby
“Yuko wapi huyo Nawal?
Akauliza Zari “Kwa sasa anaishi nchini
Saudi Arabia.Amekwisha
achana na masuala ya ujasusi
na anafanya biashara lakini
nikimueleza kuhusu Mathew
atakuja hata usiku huu huu
kama ataweza”
“Una mawasiliano yake?
“Ndiyo nina mawasiliano
yake”
“Tafadhali wasiliana naye
kama anaweza akaja haraka
itakuwa vyema sana
tukasaidiana katika
mapambano haya” “Nawal ni mwanamke
mwenye ujasiri mkubwa kama
Mathew naamini anaweza
akawa na msaada mkubwa
kwetu” Ruby akastuka baada
ya mlio wa ujumbe mfupi
kusikika.Akaitoa katika mkoba
wake na kuonyesha mshangao.
“Ni mara ya pili leo
kitendo hiki kinafanyika cha
kuwasha simu yangu wakati
nimeizima” akasema Ruby
“Yawezekana ina hitilafu”
“Hapana haina hitilafu
y0yote.Hii hufanywa na
wabobezi katika teknolojia.Unaweza ukaiwasha
simu ya mtu hata ukiwa mbali
au ukawasha kamera na
kumpiga picha akiwa
hafahamu ukiifahamu
teknolojia unaweza ukacheza
nayo utakavyo” akasema Ruby
na kuufungua ujumbe
ulioingia
“Zero again ! akasema
Ruby
“Anasemaje Zero?
Akauliza Zari na sura ya Ruby
ikabadilika baada ya kuusoma
ujumbe aliotumiwa “Kuna nini Ruby? Akauliza
Zari na Ruby akampa ujumbe
ule ausome
“They’re coming for
him.Take him out of there !
“Tayari wamefahamu
Mathew yuko hapa ! akasema
Ruby
“How ? akauliza Zari
“I don’t know how”
akasema Ruby
“What are we going to do?
Akauliza Zari
“Alituma ujumbe akinitaka
niondoke pale nyumbanikwako na kweli watu wakaja
kuvamia.Hata katika hili
nalazimika kumuamini.Hivi
sasa watakuwa wanajiandaa
kuja hapa kummaliza Mathew”
“Ruby kwanza tujiulize
imewezekanaje watu hawa
wakapata taarifa zetu na
kufahamu mahala alipo
Mathew? Bila kutafuta na
kufahamu ni namna gani
wanapata taarifa zetu bado
Mathew atakuwa katika hatari”
akasema Zari “KItu cha kwanza ni
kumuondoa Mathew mahala
hapa” akasema Ruby na simu
ikaita Zari akaipokea.
“Ruby tunatakiwa haraka
sana.Hali ya Mathew
imebadilika ghafla! Akasema
Zari kisha wakatoka mbio
kuelekea hospitali
Katika chumba cha mikutano ndani ya jengo zilimo ofisi za Black Mafia,Paul Lewis alikutana na viongozi wenzake wa kundi hilo hatari kabisa baada ya kutoka katika kikao cha dharura nyumbani kwa nabii Kasiano
“Nimetoka katika kikao cha dharura usiku huu kwa mkuu.Kuna habari njema” akasema Paul
“Mathew amepatikana” akasema Paul na nyuso zote ndani ya kile chumba cha mikutano zikatabasamu.
“Hizo ni habari njema sana.Amepatikana wapi? Akauliza John Mkizi
“Katika tukio la usiku huu nyumbani kwa mchungaji Lucas alikuwemo pia Mathew Mulumbi na ni mmoja wa watu waliojeruhiwa.Kwa sasa anapatiwa matibabu katika ofisi za SNSA nasikia wana hospitali yao hapo hapo katika
jengo lao na hali yake si nzuri.Kuna uwezekano anaweza akapotea hata maisha”akasema Paul na kunyamaza kidogo
“Baada ya kufahamu mahala alipo Mathew sasa tunaanza kuandaa mpango wa namna ya kuweza kuingia ndani ya jengo hilo na kumchukua.Ninasubiri kupata taarifa na ramni za jengo hilo la idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi lakini wakati tunaendelea kusubiri tuanze kujiandaa kwani itakuwa ni misheni kubwa kwasababu tunaamini jengo hilo lina ulinzi wa kutosha mbaya zaidi haliko mbali sana na ikulu na
kama mnavyofahamu eneo lile lote la karibu na ikulu lina ulinzi mkali hivo tunatakiwa kuandaa mpango kabambe kabisa wa kutuwezesha
kuingia ndani ya jengo hilo na kuondoka na Mathew Mulumbi au kummaliza akiwa humo humo ndani” akasema Paul na mawazo mbali mbali yakaanza kutolewa kuhusu namna ya kuweza kuingia katika jengo la SNSA kumchukua Mathew
************
Gari la naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi mheshimiwa Keofas Mabula lilisimama nje ya geti la nyumba iliyozungushiwa ukuta mfupi na juu yake kukawa na uzio wa vyuma.Alifika mahala hapo baada ya kutoka nyumbani kwa nabii Kasiano walikokuwa na kikao cha dharura.Mlinzi wa nyumba ile aliyekuwa ameshika mbwa mkubwa akalisogelea gari na kabla hajalifikia simu yake ikaita akaipokea na kupewa maelekezo ya kufungua geti akalifungua haraka haraka gari la naibu waziri likaingia ndani.Katika kibaraza alikuwepo jamaa mmoja mnene wastani akiwa amevalia fulana na kaptura .Keofas akashuka garini na kumfuata Yule jamaa wakasalimiana halafu wakaeleka ndani
“Mheshimiwa naibu waziri umenistua ulivyosema unakuja kwangu usiku huu” akasema Yule jamaa
“Martin nimelazimka kuja hapa kwako usiku na samahani kwa usumbufu”
“Bila samahani karibu sana” akasema Martin
“Nina shida ndugu yangu nimekuja nataka unisaidie” “Shida gani mheshimiwa?
“Wewe uliwahi kufanya kazi SNSA naamini utakuwa unalifahamu vyema jengo lote namna lilivyokaa na njia zote hata zile za siri za kuingilia ndani ya jengo hilo”akasema Keofas
“Mheshimiwa, mimi
nilikuwa mlinzi wa nje na mara chache niliingia ndani kwenda kuonana na mkurugenzi hivyo kwa kiasi kikubwa mambo ya ndani ya jengo lile siyafahamu sana.Kuna nini mheshimiwa naibu waziri unakitafuta ndani ya jengo hilo?akauliza Martin
“Kuna mtu muhimu
anashikiliwa hapo SNSA bila kosa lolote ndiyo maana nataka nitume vijana wangu wakamchomoe kabla hawajaanza kumtesa” akasema Keofas
“Ouh kama ni hivyo basi kuna mtu ambaye kama ukifanikiwa kumpata angeweza kukusaidia sana.Anaitwa Frank Kangole.Huyu amewahi kufanya kazi SNSA kwa muda mrefu na ni mtu ambaye nina uhakika mkubwa sana anaweza akakusaidia katika hilo jambo”
“Nitampataje huyo Frank? Akauliza Keofas
“Kwa sasa Frank hayuko tena SNSA amefungwa katika gereza la siri.Alifanya kosa kubwa aliwasaidia majambazi kuingia na kupora mamilioni benki kwa kutumia mfumo wa SNSA”
“Gereza la siri?! Keofas akashangaa
“Ndiyo.Hufahamu kama kuna gereza la siri?
“Hapana.Ni mara ya kwanza ninasikia kutoka kwako kwamba Tanzania kuna gereza la siri.Liko wapi hilo gereza? Nani wanafungwa huko?Akauliza Keofas.
“Mheshimiwa naibu waziri unanishangaza kwa
kutokufahamu uwepo wa
gereza hilo la siri wakati wewe uko katika wizara ya mambo ya ndani ambayo mnahusika na magereza yote yaliyoko hapa nchini” akasema Martin
“Martin ni kweli sifahamu uwepo wa gereza hilo la siri.Katika wizara yetu hatuna magereza ya siri ndiyo maana hilo unalolisema limenishangaza kidogo.Liko wapi hilo gereza?
“Hata mimi sifahamu
lilipo hilo gereza la siri lakini ukitafuta mahala lilipo huwezi kushindwa kulipata.Nakuhakikishia mheshimiwa naibu waziri kama ukimpata huyo jamaa anaweza akakupa taarifa nyingi za kuhusu SNSA na anaweza hata akakusaidia kumtoa huyo mtu wako.Tumia nafasi yako kulitafuta hilo gereza na ukilipata onana na huyo jamaa atakusaidia”akasema Martin
“Ninashukuru Martin kwa ushauri wako utanisaidia sana” akasema Keofas na kuagana na Martin akaondoka.
“Ni mara ya kwanza ninasikia kuhusu uwepo wa gereza la siri.Nani anasimamia gereza hilo ni SNSA? Nani wanafungwa huko? Akajiuliza Keofas akiwa garini
Baada ya kutoka nyumbani kwa Martin alielekea moja kwa moja nyumbani kwake na kitu cha kwanza alichokifanya baada ya kufika nyumbani kwake ni kumpigia simu nabii Kasiano
“Keofas kuna habari gani? Akauliza Kasiano
“Nimetoka kuonana na Martin Yule jamaa nilikwambia amewahi kufanya kazi ya ulinzi SNSA”
“Ndiyo kuna chochote umekipata toka kwake? Akauliza Kasiano
“Martin amenieleza kwamba kwa kiasi kikubwa kazi zake zilikuwa ni ulinzi wa nje lakini amenielekeza kwa mtu anaitwa Frank Kangole ambaye amewahi kufanya kazi SNSA ila kwa sasa amefungwa katika gereza la siri.Umewahi kusikia kuhusu uwepo wa gereza hilo la siri hapa nchini?Keofas akauliza
“Hapana sijawahi kusikia uwepo wa gereza hilo”
“Basi huko ndiko alikofungwa huyo Frank ambaye kama tukimpata atatusaidia sana katika mpango wetu wa kuingia SNSA na kumchomoa Mathew Mulumbi” akasema Keofas
“Kama kweli lipo hilo gereza basi hakuna tatizo tutalitafuta na kulifahamu mahala lilipo.Nakuhakikishia Keofas tutalipata hilo gereza” akasema Kasiano na kuagana na Keofas
“Gereza la siri.Liko wapi hapa nchini? Nisiumize kichwa sana ngoja niwasiliane na Bella yeye anaweza akatusaidia kutafuta kujua kuhusu uwepo wa gereza hilo,anafahamu mambo mengi sana ya nchi
hii” akawaza Kasiano na kumpigia simu Bella
“Kasiano unasemaje?
Akauliza Bella ambaye tayari alikuwa usingizini na kuamka baada ya simu yake kuita
“Mama Bella samahani kwa usumbufu nimekupigia kuomba msaada kuna mahala tumegonga kisiki na tunahitaji msaada wako”
“Nini mnahitaji
Kasiano?akauliza Bella
“Bado tunaendelea kutengeneza mpango namna ya kuingia SNSA,kuna mtu amewahi kufanya kazi katika idara hiyo anaitwa Frank Kangole ambaye amefungwa katika gereza la siri.Hapo ndipo tumekwama mama ni mara yangu ya kwanza kusikia uwepo wa gereza hilo la siri.Tunahitaji msaada wako ili tuweze kumpata huyo mtu” akasema Kasiano “Umesema gereza la siri?
“Ndiyo mama”
“Mhh ! hata mimi sijawahi kusikia kitu kama hicho.Ngoja nipige simu mbili tatu nitafute taarifa nitakupigia tena baadae kama nitakuwa nimepata chochote” akasema Bella na kukata simu akainuka na kukaa kitandani
“Huyu Mathew Mulumbi
ambaye anatufanya tushindwe kulala usingizi ninaapa lazima apatikane” akawaza Bella na kuzitafuta namba za Yeremia Mwaipopo mkuu wa jeshi la polisi akampigia
“Mama Bella”akasema
Yeremia
“Yeremia samahani kwa usumbufu usiku huu.Kuna kitu nataka unisaidie”
“Ndiyo mama Bella
nikusaidie nini?Kuna taarifa zozote umezipata kuhusu Mathew? Akauliza Yeremia huku akiinuka kitandani na kutoka chumbani
“Tayari tumefahamu Mathew yuko SNSA na anapatiwa matibabu hapo baada ya kujeruhiwa kwa risasi usiku huu.Hata Festus alikwenda huko usiku huu kumjulia hali”
“Safi sana.Nini mipango ya kumpata baada ya kufahamu mahala alipo?
“Tunaendelea na mipango ya kutuma waingie humo SNSA wamchukue Mathew Mulumbi tumkabidhi kwa hao jamaa na mambo yamalizike”akasema Bella
“Bella nina vijana mahiri kabisa ndani ya jeshi la polisi ambao ninaweza kuwatumia kwenda kumchukua Mathew Mulumbi kama yupo SNSA”
“Hilo ni jambo la hatari sana Yeremia.Hatutaki kulihusisha jeshi la polisi katika mpango huu.Tutatafuta vijana wengine ambao wataweza kuingia humo ndani ya SNSA na kumchukua Mathew
Mulumbi.Nimekupigia kukuuliza kama unafahamu uwepo wa gereza la siri hapa nchini” akasema Bella
“Gereza la siri? Akauliza Yeremia huku akiinuka na kutoka chumbani “Ndiyo.Una taarifa zake?
“Nimewahi kulisikia hilo
gereza lakini liko chini ya idara ya kupambana na kudhibiti ugaidi.Gereza hilo ni maalum kwa ajili ya kuwafunga magaidi na watu wengine hatari kwa nchi”akasema Yeremia
“Kuna mtu anashikiliwa katika gereza hilo ambaye anaweza akasaidia katika mpango huo.Unadhani nani ninaweza kuzungumza naye akanisaidia? Akauliza Bella
“Zungumza na mkurugenzi wa idara ya kupambana na
ugaidi anaitwa Asajile Mlabwa.Yeye anaweza akakusaidia sana katika hilo” akasema Yeremia
“Nakushukuru sana Yeremia”
“Bella nashauri wakati unazungumza na Asajile tuwe wote ili suala hilo liwe na uzito mkubwa” akasema Yeremia
“Sawa Yeremia ninaomba mawasiliano yake huyo Asajie
ili niwasiliane naye na
kumuomba kuonana naye asubuhi” akasema Bella na kukata simu.Baada ya muda Yeremia akamtumia Bella namba za simu za Asajile Mlabwa mkurugenzi wa idara ya kupambana na ugaidi Bella hakuchelewa akampigia simu
“Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili baada ya simu kupokelewa
“Mkurugenzi Asajile habari za usiku huu”
“Nzuri
kabisa.Nazungumza na nani?
“Mimi ni Bella mke wa Rais”
“Mama Bella?! Asajile akashangaa
“Ndiyo Asajile.Samahani kwa kukuamsha usiku huu.Nina mazungumzo nawe nataka tuonane kesho”
“Hakuna tatizo mama
Bella.Unataka nikufuate ikulu?
“Hapana.Nitakuelekeza mahala tutakapokutana” “Sawa mama Bella”
“Ahsante sana Asajile usiku mwema”akasema Bella na kukata simu
“Sikutaka jambo hili lihusishe watu wengi lakini kadiri muda unavyozidi kwenda tunajikuta tukilazimika kuogeza watu katika mtandao huu.Huyu Asajile imekuaje mpaka leo hii hajaingia katika mtandao wangu? Anatakiwa awepo katika mtandao wangu huyu mtu anaonekana ni mtu muhimu mwenye msaada” akawaza Bella na kujlaza kitandani
Zari na Ruby walifika kwa haraka katika chumba
alimokuwa amelazwa Mathew “Nini kimetokea? Zari akamuuliza mmoja wa wauguzi aliyekuwa anakimbia kuingia katika chumba alimo Mathew
“Mkurugenzi tunawaomba msubiri kwanza hapo nje” akasema Yule muuguzi na kuufunga mlango akina Zari wakabaki nje
“Mungu wangu nini kimetokea humo ndani? Akauliza Ruby midomo ikimtetemeka
“I can’t stay here.I’m going in ! akasema Zari na kuufungua mlango akaingia ndani na kuwakuta madaktari wakiwa katika heka heka za khakikisha hali ya Mathew inakaa sawa.Zari na Bella wakakaa pembeni na kuwaacha madaktari wafanye kazi yao.
Baada ya dakika kumi na tano hali ya Mathew ikawa vizuri
“Mkurugenzi usihofu mgonjwa anaendelea vizuri.Kulitokea tatizo kidogo lakini tumelitatua na sasa anaendelea vyema.Msiwe na hofu yoyote tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha mgonjwa anapona” Dr Fred akawaeleza akina Zari
“Ahsante sana Dr Fred,tulipata wasiwasi mkubwa” wakajibu Zari na Ruby kisha wakatoka mle ndani.
“Nahisi mwili unaishiwa nguvu kabisa” akasema Zari
“JItahidi Zari huu si wakati wa kuishiwa nguvu.Mathew anatutegemea sana kwa wakati huu”akasema
Ruby
“Tunafanya nini kuhusiana na ule ujumbe wa Ziro? Akauliza Zari
“Ujumbe ule si wa kupuuza.Lazima wamekwisha fahamu mahala alipo Mathew Mulumbi na wanajiandaa kuja mahala hapa kummaliza”
“Wamejuaje kama Mathew
yuko hapa?Zari akauliza
“Hakuna anayejua lakini kitu kikubwa kwa sasa ni kuanza mipango ya kumuondoa Mathew mahala hapa”akasema Ruby
“Itabidi tupate ushauri wa daktari kama itafaa
kumuhamisha Mathew katika
hali hii”
“Zari hatuna namna lazima tumuondoe Mathew hapa” akasema Ruby
“Ruby hali ya Mathew ni kama unavyoiona amefanyiwa upasuaji mkubwa na anahitaji uangalizi mkubwa wa madaktari.Tazama muda mfupi tu uliopita kumetokea tatizo katika mfumo wake wa upumuaji hivyo hatuwezi kumuondoa hapa kwa haraka kama unavyotaka.Bado anahitaji kuwepo hapa hadi tutakapohakikisha amepata unafuu mkubwa”akasema Zari
“Zari wewe mwenyewe umesoma ujumbe uliotumwa na Ziro hawa watu tayari wamejua Mathew yuko hapa lazima watakuja hapa.Unataka Mathew auawe? Akauliza Ruby
“Sina maana hiyo Ruby lakini hatuwezi kuwaogopa watu hao na kuhatarisha maisha ya Mathew Mulumbi.Tunao ulinzi wa kutosha mahala hapa.Wewe umewahi kuwa mkurugenzi wa hapa na unafahamu ulinzi wa jengo hili ulivyo.Ulinzi hapa ni mkubwa sana,ukiacha walinzi tulionao waliosambaa katika kila kona kuna silaha kali zimewekwa sehemu mbali mbali za hili jengo ambazo zinaendeshwa kielektroniki.Silaha hizo zimefichwa na watu hao watakaovamia jengo letu hawajui zilipo hivyo basi kama wakijidanganya wavamie hapa tutawamaliza kama wadudu.Hili ni jengo hatari kabisa kuthubutu kuvamia.Nakuomba Ruby usiwe na wasi wasi Mathew atakuwa salama.Tusubiri kwanza apate nafuu halafu tutamuondoa hapa kumpeleka sehemu salama zaidi” akasema Zari
“Sawa Zari” akajibu Ruby
“Nina maswali mengi kuhusu huyu Ziro ni nani hasa? Umekwisha jaribu kumtafuta na kujua ni nani? Akauliza Zari
“Simfahamu huyu Ziro ni nani lakini ninachofahamu yuko katika mtandao wa hawa jamaa tunaowatafuta Black mafia”akajibu Ruby
“Kama yuko katika mtandao wao iweje basi anatusaidia kwa kutupa taarifa zao?Ni wazi ni mtu ambaye anakufahamu hasa wewe na kila pale kunapokuwa na
mpango wowote wameupanga dhidi yako anakupa taarifa mapema ili uchukue tahadhari”akasema Zari
“Hata mimi ninashindwa kuelewa kwa nini anatusaidia? Ninachohisi huyu mtu atakuwa ana mahusiano na sisi na huko aliko he or she’s undercover” akasema Ruby
“Huyu mtu lazima atakuwa anakulinda sana wewe kwa sababu hakuna mwingine ambaye amewahi kumtumia ujumbe wa tadhari zaidi yako.Think
Ruby.Tunaweza tukafanikiwa kumfahamu ni nani huyu mtu” akasema Zari
“Hawa ni watu
wanaotumia teknolojia ya hali ya juu kuhakikisha hawajulikani ni akina nani lakini iko siku atajitokeza tu au ataacha mwanya tutamfahamu ni nani.Kwa sasa tujielekeze kwa Mathew,huyu Ziro kama yuko upande wetu basi ataendelea kutupa taarifa kila pale tunapokuwa katika hatari.” akasema Ruby
“Ulinieleza kuna mtu unaweza ukawasiliana naye akafika kuja kutusaidia.Kama una mawasiliano naye huyo mtu wasiliana naye tafadhali ili aje mara moja.Tunahitaji msaada” akasema Zari
“Ahsante kwa kunikumbusha” akasema Ruby na kufungua sehemu anakohifadhi namba za watu akatafuta namba ya simu ya Nawal akapiga
“Ruby ! akasema Nawal baada ya kupokea simu
“Nawal habari za usiku huu?
“Nzuri kabisa.Vipi maendeleo yako?
“Sisi huku mambo si mazuri ndiyo maana nimekupigia usiku huu”
“Kuna nini Ruby ? Nawal akauliza
“Mathew yuko katika hatari kubwa”
“Mathew?Yuko Tanzania? Akauliza Nawal
“Ndiyo amerejea Tanzania lakini amekutana na matatizo makubwa na muda mfupi uliopita ametoka kufanyiwa upasuaji baada ya kupigwa risasi”
“Mathew amepigwa risasi?
“Ndiyo Nawal”
“Nani kafanya tukio hilo?
“Sikiliza Nawal ninakuomba uje Dar es salaam tunahitaji sana msaada wako.Kuna mambo mazito yanayoendelea hapa.Utakapofika nitakueleza kwa kirefu sana kile kinachoendelea hapa”
“Kuja hapo nitakuja Ruby.Gosu Gosu naye anaendeleaje?Uko naye hapo karibu?
“Gosu Gosu naye alipatwa na matatizo.Amefungwa kifungo cha maisha gerezani”
“Kifungo cha maisha? Nawal akashangaa
“Ndiyo Nawal.Amefungwa kifungo cha maisha.Nawal utakapokuja huku nitakueleza kila kitu kilichotokea”
“Ruby umenistua
sana.Kwa kuwa Rais aliyepita alinipatia uraia wa Tanzania basi sintapata tatizo lolote kuingia hapo nchini.Kesho nitakuja Dar es salaam”
“Nashukuru
Nawal.Utakapoanza safari utanijulisha” akasema Ruby wakaagana.
“Amekubali na atafika hapa nchini kesho”Ruby akamjulisha Zari
“Itakuwa vizuri sana akifika ili aendelee pale ambapo ameishia Mathew.Unadhani kuna ulazima wa kumjulisha Rais kuhusu jambo hilo? Akauliza Zari
“Kuna kitu nataka nishauri.Kuanzia sasa tusimshirikishe Rais katika mipango yetu hasa ya kuhusiana na Mathew Mulumbi” akasema Ruby na
Zari akashangaa
“Kwa nini
Ruby?Humuamini Rais?
“Sina tatizo na Rais ila tatizo langu liko kwa watu wanaomzunguka.Tukirejea
katika lile sakata la picha zake za faragha hata yeye mwenye Rais amekiri hafahamu ni namna gani picha hizo zimepigwa kwa sababu kwanza mahusiano yake na Zandile ni ya siri kubwa na wanaofahamu jambo hili ni watu wachache sana tena watu wake wa karibu.Nahisi miongoni mwa watu wake hao wa karibu yupo mtu anayetumiwa na hawa jamaa na ndiyo maana wanapata siri zote za
Rais.Tukimfahamisha kuhusu Mathew na kama kuna mtu wake wa karibu anaweza akafuatilia na kufahamu mahala tutakakompeleka na hawa jamaa watapata taarifa.Tutakuwa watu wa kuhama hama mpaka lini? Ninashauri tuanze kufanya mambo yetu kwa siri sana bila kushirikisha watu wengi akiwemo Rais”
“Ni vipi kama akigundua tumefanya mambo bila kumshirikisha? Atakasirika sana” akasema Zari
“Atakasirika ndiyo lakini tutamueleza ukweli kwa nini tumefanya hivyo tulivyofanya” akasema Ruby
“Kwa nini tusimueleze wakati huu?akauliza Zari
“Zari that’s not a good idea.Tukimueleza Rais kwamba tunamuhamisha Mathew Mulumbi lazima atataka kufahamu mahala tunakompeleka na anaweza akataka kwenda kumtembelea kujua maendeleo yake na huko hatakwenda peke yake kwani kila aendako Rais huongozana na walinzi na wasaidizi wake na kama miongoni mwao yupo mmoja ambaye atakuwa ana mahusiano na hao jamaa tunaowatafuta basi atapeleka taarifa kwao na maisha ya Mathew yatakuwa mashakani.Ninashauri tuwe majasiri katika jambo hili na kama akituuliza Mathew amepelekwa wapi tutamjibu yuko sehemu salama na tutamueleza sababu kwa nini hatukumshirikisha” akasema Ruby
“Ruby nashauri
tumshirikishe Rais katika suala hili.Nitakwenda mimi ikulu na kuzungumza naye atatuelewa.Isitoshe ni yeye ambaye tutamuomba atusaidie kupata makazi salama kwa ajili ya Mathew” akasema Zari wakaendelea kujadiliana na kukubaliana na wazo lile la Zari
Kitu cha kwanza
alichokifanya Rais Festus baada ya kufumbua macho saa kumi na mbili kasoro dakika saba asubuhi ni kuchukua simu na kumpigia Zari
“Zari nataka nijue maendeleo ya Mathew Mulumbi” akasema Rais Festus
“Mathew Mulumbi
anaendelea vizuri mheshimiwa Rais.Alizinduka na madaktari wamekuwa wakifuatilia kwa karibu sana maendeleo yake.Mpaka sasa hali yake
inaendelea vizuri”akajibu Zari
“Ahsante kwa taarifa hii nzuri.Tafadhali msiondoke hapo SNSA hakikisha Mathew anapata matibabu ya hali ya juu nataka apone haraka akaendelee na shughuli yake ya kuwasaka hawa mashetani ! Nikipata wasaa ninaweza kuja kumjulia hali hapo baadae”
“Hakuna haja mheshimiwa
Rais,sisi tuko hapa na kama kuna tatizo lote litatokea tutakujulisha haraka sana.Halafu mheshimiwa Rais ninataka kuja kuonana nawe baadae kuna masuala nataka kuzungumza nawe”akasema
Zari
“Nashukuru
Zari.Tutaonana hiyo baadaye” akasema Rais Festus na kukata simu
“Maendeleo mazuri ya Mathew Mulumbi ndicho kitu pekee nilichohitaji kukisikia asubuhi hii” akawaza huku akiinuka kitandani na kujinyoosha halafu akakumbuka kitu akachukua simu na kumpigia mkurugenzi wake wa habari
“Shikamoo mheshimiwa
rais”
“Marahaba.Gidion
umepitia magazeti ya leo tayari? Hakuna taarifa yoyote mbaya? Akauliza Festus
“Mheshimiwa Rais tayari ninayo magazeti yote ya leo na kubwa lililoandikwa ni lile suala lako la mtoto wa nje.Ukiacha hilo hakuna habari yako nyingine” “Ahsante Gidion” akajibu Rais Festus ambaye kwa kawaida yeye si mpenzi sana wa kusoma magazeti.
“Kwa nini wale jamaa hadi asubuhi hii hawajasambaza picha zangu? Wameogopa au kuna kitu gani kinaendelea? Akawaza na kuchukua tena simu akazitafuta namba za katibu mkuu profesa Simon akampigia simu ikaanza kuita
“Afadhali leo simu yake inaita nilikwisha anza kupata wasiwasi”
“Mheshimiwa Rais” akasema profesa Simon “Mzee Simba shikamoo”
“Marahaba.Unaendeleaje?
“Nimekutafuta sana jana hukuwa unapatikana simuni kuna tatizo gani lilikupata?
“Simu yangu ilipata matatizo kidogo mheshimiwa Rais”
“Tayari nilikwisha anza kuingiwa na hofu”
“Usihofu mheshimiwa
Rais ni matatizo madogo tu” “Sawa mzee
Simba.Ninataka kufahamu kama wale jamaa waliwasiliana nawe tena siku ya jana.Nimeshangaa kwa nini mpaka sasa hawaja sambaza zile picha kama walivyokuwa wamekusudia endapo nisingetimiza madai yao”
“Mheshimiwa Rais hata mimi ninashangaa kwa nini hawajasambaza.Nilidhani labda umekubali madai yao”
“Hapana siwezi kukubaliana nao kabisa.Msimamo wangu haubadiliki mzee Simba”
“Nini basi nini kimetokea hadi wakashindwa kusambaza picha?akauliza profesa Simon
“Hujawasiliana nao
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment