Search This Blog

Friday, 7 April 2023

SCANDLE (KASHFA) (3) - 5

   

Simulizi : Scandle (Kashfa) (3)

Sehemu Ya Tano (5)




Fernando


“Dr Fernando unaufahamu msimamo wangu siwezi kuzungumza na hao watu na nitawasaka mmoja baada ya mwingine hadi mtu wa mwisho” akasema Festus


“Festus sikushauri uendelee na vita na hawa jamaa.Wamenihakikishia wanafahamu mambo yako mengi na wana ushahidi,hata suala la kuzaa na mdogo wake Bella


wanalifahamu,wanafahamu kuhusu amri uliyoitoa nikaachiwa baada ya kukamatwa na wale wanyama hai,wanafahamu mambo mengi ya siri ambayo yanaweza yakakuweka katika


matatizo makubwa.Nakushauri wasikilize kile wanachokitaka na amani itawale.Maliza kipidi chako cha uongozi ukapumzike usitake kupata nishani ya ushujaa katika hili jambo litakuingiza pabaya.Tazama


hili la picha lilivyoibua mjadala mkubwa nchini na wataendelea kuanika mambo yako moja baada ya lingine na kabla hawajayamaliza utakuwa nje ya hilo jengo jeupe na yawezekana ukawa mahakamani kwa matumizi mabaya ya ofisi ya Rais” akasema Dr Fernando na ukimya ukapita Rais Festus akatafakari


“Nini hasa wanachokitaka hao jamaa? Akauliza Rais Festus


“Protection! Akajibu Dr Fernando


“Protection?! Rais Festus akashangaa


“Ndiyo.Wanataka


wahakikishiwe watafanya biashara zao kwa amani na uhuru bila matatizo yoyote”


“Siwezi kuwa Rais ninayewalinda wauza dawa za kulevya.Katika kiapo nilichokula hakuna mahala nilikoapa kwamba nitawalinda na kuwatetea wauza dawa za kulevya.Niliapa kuilinda na kuitetea katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na hakuna mahala katika katiba hiyo wametajwa wauza dawa za kulevya”akasema Rais Festus kwa ukali “Festus !


“Dr Fernando naomba


kwanza tumalize suala la wale mateka.Wametoa sharti gani la kuwapata? Akauliza Rais Festus


“Wanataka mchungaji mmoja aliyekamatwa na watu wako katika kanisa la injili ya wokovu aachiwe huru hana kosa na hahusiki na kitu chochote” akasema Dr Fernando


“Mchungaji?! Rais Festus akashangaa


“Ndiyo.Huyo akiachiwa basi mateka wengine nao wataachiwa huru” akasema DrFernando


“Dr Fernando huyo mchungaji ana mahusiano gani na hao jamaa? 



“Ni katika kuhakikisha watu wasio na hatia wanakuwa huru ndiyo maana wakadai kwamba huyo mchungaji


alichukuliwa hana kosa lolote”




“Kwa hiyo una uhakika huyo mchungaji akiachiwa wale mateka wengine nao wataachiwa huru? Akauliza


Rais Festus


“Wote wataachiwa huru” akasema Dr Fernando


“Nipe dakika chache nitafute mahala alipo huyo mchungaji halafu nitakujulisha” akasema Rais Festus na kukata simu akavuta pumzi ndefu


“Mimi nizungumze na wauza dawa za kulevya ! akasema Festus akiwa amekunja uso “Eti wanataka amani ili wafanye biashara yao kwa uhuru.Utakuwa ni ujinga uliopitiliza kukubaliana na matakwa yao ! akaendelea kuwaza


“Lakini nisipokubaliana nao wametishia kuendelea kusambaza mambo yangu ya siri na kunichafua.Nimestuka sana baada ya Dr Fernando kunitajia mambo ambayo wanayafahamu hawa jamaa na ambayo yakitoka kwa wananchi yataniweka katika sehemu mbaya sana.Kuna mambo ambayo nimeyafanya kwa kutumia nguvu yangu kama Rais kwa mfano pale alipokamatwa DrFernando nilitumia nguvu yangu kulimaliza suala lake.Wanafahamu pia kuhusu kuzaa na mdogo wake Bella.Hizi ni kashfa kubwa ambazo zikiwafikia wananchi basi maisha yangu katika siasa yatakuwa yamefikia mwisho.Je nikubaliane na kile wanachokitaka yaani niweke silaha chini na kukubaliana nao? Akajiuliza *****************


Zari na madaktari watatu walifika kwa haraka katika kambi ya akina Mathew.


“Mkurugenzi kidonda cha Mathew kimefumuka na anatakiwa arejeshwe tena hospitali” akasema DrFred baada ya kumchunguza Mathew


“Hamuwezi


mkamuhudumia hapa hapa nyumbani? Akauliza Zari


“Hapana kwa hapa hatuwezi anatakiwa sehemu yenye vifaa na hapa hakuna kifaa hata kimoja” akasema Dr Fred


“Leteni vifaa vinavyohitajika hapa hapa nyumbani,Mathew ni mtu anayetafutwa sana sasa hivi na hatuwezi kumpeleka katika hospitali yoyote.Sehemu pekee ambako tulipategemea ni SNSA lakini napo si sehemu salama tena kumpeleka Mathew.Dr Fred nakuomba muende SNSA chukueni kila


kitu kinachohitajika katika kumuhudumia Mathew na tutageuza chumba kimoja humu ndani kuwa hospitali ya muda” akasema Zari


“Sawa mkurugenzi” akasema Dr Fred na kutoka haraka kwenda kuchukua vifaa kama alivyoelekezwa na Zari


“Mathew hali yako bado si nzuri sana na kuanzia sasa utafuata ushauri ule wa daktari utakaa kitandani na sisi tutaendelea kufanya kila kitu.Naomba utuamini” akasema Nawal


“Jamani msiwe na wasi wasi kuhusu mimi” akasema


Mathew


“Mathew please ! akasema


Zari


“Sawa.Hakikisheni Yule mwandishi anasema kila kitu”


“Mwandishi? Zari akashangaa.Ruy akamweleza kila kitu kuhusu Patrick CK


“Wakati tunawasubiri madaktari warejee nitakwenda kumuhoji Yule mwandishi” akasema Nawal


“Tunakwenda wote.Ruby


take care of Mathew” akasema Zari kisha wakatoka na kwenda katika chumba alimokuwemo Patrick.Mlango ulipofunguliwa akaiona sura ya Nawal akapatwa na mstuko mkubwa sana.


“You ?!


akauliza.Hakuyaamini macho yake


“I remember you.A woman from Dubai kumbe uko na hawa jamaa? Who are you? Akauliza Patrick


“Save your breath Patrick ! akasema Nawal akiwa katika sura isiyo na masihara


“Patrick nimepewa dakika chache sana za kuzungumza nawe na ninaomba uzitumie vyema dakika hizo,tunataka utueleze ukweli mtupu kwani hapa ulipofika ni sehemu yako ya mwisho.Ni wewe mwenyewe utakayeamua hatima ya maisha yako,kama unataka kuendelea kuishi na kuyafurahia maisha au kama unataka kutangulia katika hukumu ya haki.Utaendelea kubaki hai kama utaeleza ukweli lakini hatutasita kukutanguliza kwenye haki kama utasema uongo” akasema Nawal na Patrick akaonyesha hofu kubwa


“Kitu gani mnataka kufahamu kutoka kwangu?Nitawaeleza kila kitu jamani ila msiniue! Akasema Patrick.Nawal akaichukua bahasha ile yenye picha za Patrick na Bella akaiweka mezani.Alipoziona tena zile picha akaanza kutetemeka midomo kwa woga


“Kule nyumbani kwako Mathew alikuuliza kuhusiana na picha hizi na hukutoa jibu.Tunataka maelezo ya hizi picha” akasema Nawal


“Huyu uliyepiga naye hizi picha ni nani? Akauliza Zari


“Nitawaeleza jamani lakini nawaomba hili jambo liishie hapa hapa”akasema Patrick


“Tueleze Patrick huyu mwanamke pichani ni nani?Ni mke wako? Zari akauliza tena


“Huyu ni..ni….n….”Patrick akababaika


“Sema ni nani? Nawal


akauliza kwa sauti kali


“Ni …..” Patrick akataka kusema akasita


“Tafadhali usitake tutumie nguvu.Tueleze haraka sana huyu ni nani?


“Ni..Dah !


Nawal akachomoa kitu kidogo kama msumari kutoka katika suruali yake na kwa nguvu akakichoma katika bega la Patrick halafu akakizungusha,Patrick akapiga kelele kwa maumivu makali aliyoyapa.


“Nani huyu mwanamke? “Ni Bella mke wa Rais ! akasema Patrick na kwa nguvu Nawal akakivuta kile chuma na damu ikaanza kumwagika


“Picha hizi ni halisi au ni picha za kutengeneza? Akauliza Nawal


“Ni picha halisi ! akasema Patrick akiwa ameweka mkono begani kuzuia damu isiendelee kumwagika


“Katika picha hizi kinachooneka ni watu wawili walio mapenzini.Ni kweli hiki tunachokiona pichani? Nawal akauliza Patrick akatikisa kichwa kukubali


“Haya ni maajabu ya karne,wewe ! akasema Zari


“Ilikuaje hadi ukaingia katika mahusiano na Bella? Akauliza Nawal


“Nitawaeleza jamani lakini naomba msinitese ! akasema Patrick


“Eleza haraka sana!


“Nilifuatwa na mtu akaniuliza kama ninaweza kazi ya kumuandikia hotuba mke wa Rais nikakubali na kuanza kazi.Nilikuwa nasafiri naye mara kwa mara na hotuba zake zote mimi ndiye mwandishi wake.Taratibu tukajikuta ukaribu wetu ukizidi na tukawa na mahusiano lakini ni yeye aliyenishawishi!


“Natamani nikuharibu sura yako !Unawezake kukubali kufanya kitu kama hicho? Unajua hatari uliyonayo? Kwa nini umejitafutia matatizo wewe kijana?Unadhani Rais akiziona picha kama hizi utabaki salama? Zari akauliza ‘Naombeni mnisaidie ndugu zangu niko chini ya miguu yenu picha hizi zisisambae.Ninawaahidi nitazichoma moto na sintaendelea tena na mahusiano na mama Bella!


“Sisi hatukuzuii kuendelea na mahusiano yako kwani hatujui mmetoana wapi lakini tunachokueleza ni ukweli kwamba ulichokifanya si kitu kizuri hata kidogo.Umenunua hatari kubwa.Endapo picha kama hizi zikimfikia Rais umekwisha ! Hautabaki salama”


“Naombeni msaada wenu


ndugu zangu ! akalia Patrick


“Hadithi yako ni ya kwanza kutumiwa na kampuni ya Afrifcan pictures kutengenezea filamu.Ilikuaje hadi hadithi yako ikachaguliwa? Akauliza Nawal


“Sikufahamu uwepo wa


kampuni ya African Pictures hadi pale nilipotakiwa na mama Bella kumpa baadhi ya hadithi nilizowahi kuandika akazipitia na akachagua hadithi ya Before I die akaniambia hadithi ile itatumika kutengeneza filamu na hapo ndipo akanifahamisha kuhusu uwepo wa kampuni ya African Pictures.Alinikabidhi kwa mtu ambaye ndiye meneja wa kampuni hiyo tawi la Dar es salaam”


“Anaitwa nani huyo meneja? Zari akauliza


“Anaitwa Lethabo Dlamini”


“Umesema ni Bella ambaye alichagua moja ya filamu zako itumike katika kutengeneza filamu,nataka kufahamu Bella ana nafasi gani katika kampuni hii ya African pictures? Ninauliza hivyo kwa sababu kwa mujibu wa maelezo yako anaonekana ana sauti na maamuzi katika hii kampuni” akasema Nawal.Patrick akakaa kimya


“Patrick tafadhali usitake tuanze kukuvunja vunja na kukuharibu vibaya,tueleze ukweli! Akasema Zari


“Bella ni mmoja wa watu wenye hisa katika kampuni hii” akajibu Patrick,Nawal na


Zari wakatazamana “Umesema Bella ni mmoja wa wanahisa nani wengine wamiliki wa hii kampuni? Nawal akauliza


“Kuna mtu anaitwa


Bandile Dlamini yuko Afrika kusini,Roberto Zullo na Martyina Durante wote hawa wako Afrika kusini na kuna watu wengine wawili ambao wanatajwa kuwa na hisa nyingi ila majina yao huwa hayatajwi na siwafahamu ni akina nani” akasema Patrick


“Katika taarifa tuliyonayo inaonyesha mmiliki wa kampuni hii ya African pictures ni wanandoa Roberto Zullo na mke wake Martina Durante.Wewe umejuaje kama kuna wanahisa wengine? Nawal akauliza


“Ukweli ni huu ninaowaambia mimi kwa sababu ndiye ninayesimamia maslahi ya Bella katika kampuni hii hivyo ninafahamu mambo mengi kuhusiana na hii kampuni” akasema Patrick


Wakati wakiendelea na mahojiano Ruby akaingia na kuwajulisha kwamba Dr Fred amekwisha rejea na maandalizi ya chumba yamekwisha anza


“Ruby kuna watu amewataja Patrick kwamba wanamiliki kampuni ya African pictures naomba utusaidie kuwachunguza” akasema Nawal na kumpa


Ruby majina yale ya wamiliki wa kampuni ya African


pictures.Zari na Ruby wakatoka wakamuacha Nawal akiendelea kumuhoji Patrick


“Umewahi kusikia jina


Black Mafia likitamkwa mahala kokote? Akauliza Nawal na Patrick akafikiri kidogo halafu akasema


“Hapana sijawahi kulisikia jina kama hilo”


“Kumbuka vizuri


Patrick.Nitakapo rejea nataka nikute tayari una jibu” akasema Nawal na kutoka


Ruby alilazimika kumpigia simu Jabu rafiki wa Mathew ili kuomba msaada wa taarifa za wale wamiliki wa kampuni ya African Pictures ambao wote ni raia wa Afrika kusini “Mathew Mulumbi” akasema Jabu


“Halo Jabu ninaitwa Ruby ni rafiki wa Mathew Mulumbi na amenipa maelekezo nikupigie simu nikuombe msaada”


“Kitu ganiMathew


Mulumbi anakihitaji? Akauliza Jabu


“Taarifa za watu watatu raia wa Afrika kusini,Roberto Zullo,Martina Durante na


Bandile Dlamini” akasema Ruby na Jabu akasikika akishusha pumzi.


“Kuna kitu gani kinaendelea huko Tanzania hivi sasa? Unaweza ukanieleza tafadhali? Akauliza Jabu


“Jabu utanisamehe kwa vile sina mamlaka ya kukueleza kile kinachoendelea sasa hivi hapa Tanzania.Ni Mathew pekee ambaye anaweza akakueleza” akajibu Ruby


“Sawa.Hawa jamaa watatu sina haja ya kuchukua muda mrefu kutafuta taarifa zao


kwani tayari ni watu wanaofahamika kwa vyombo vya usalama hapa Afrika kusini.Robert0 Zullo na Martina Durante ni mtu na mke wake.Ni wakulima wakubwa wa zabibu na wana kiwanda kikubwa cha kutengeneza mvinyo utokanao na Zabibu.Bandile Dlamini ni bilionea anamiliki


makampuni makubwa ndani na nje ya nchi.Hawa watatu wote ni wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya hapa Afrika kusini” akasema Jabu na Ruby akahisi kama jiwe zito limemgonga kichwani “Umesema ni wafanya


biashara wa dawa za kulevya? Akauliza Ruby


“Ndiyo.Wote watatu ni wafanya biashara wakubwa na kwa lugha zao wenyewe wanaitwa ni miungu wa dawa za kulevya.Ni watu wazito hawa na hata serikali haiwagusi kwani makampuni na biashara zao kwa ujumla zimeajiri mamia ya watu ambao wanaweza wakapoteza ajira zao endapo hawa jamaa watakamatwa” akasema Jabu “Jabu umewahi kusikia kuhusu kundi linaitwa Black Mafia? Akauliza Ruby


“Hapana sijawahi kusikia kundi kama hilo” akajibu Jabu


“Jabu ahsante sana kwa


taarifa hizo nitazifikisha kwa Mathew” akasema Ruby na kukata simu akashusha pumzi halafu akatoka akawafuata akina Nawal waliokuwa katika chumba ambamo Mathew alikuwa anapatiwa matibabu akawaita Nawal na Zari


“Nimezungumza na Jabu


nilimuomba anisaidie kutafuta taarifa za wale watu ambao Patrick anadai wanahisa katika kampuni ya African pictures na jibu alilonipa linastua sana.Anadai wale jamaa ni wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya nchini Afrika kusini”


Ukapita ukimya mfupi halafu Nawal akasema


“Kama watu hao ambao wanatajwa kumiliki kampuni hiyo ni wafanyabiashara wa dawa za kulevya,basi Mathew alikuwa sahihi kuhisi kuwa kampuni hii inamahusiano na Black Mafia.Maswali yanayoibuka hapa ni kamba Bella ni mmoja wa wanahisa wa kampuni hii je anafahamu kuwa washirika wake ni wafanya biashara wa dawa za kulevya? Akauliza Nawal


“Wanasema ndege wa kundi moja huruka pamoja,hawa jamaa wasingekubali Bella akawekeza katika kampuni yao kama si mwenzao” akasema Ruby


“Kwa mawazo ya Ruby ni kwamba Bella naye anajihusisha na biashara hii ya dawa za kulevya” akasema Zari


“Ninahisi hivyo kwa sababu hawa jamaa sina hakika kama wangekubali washirikiane naye katika biashara kama si mwenzao” akasema Ruby


“Hapa tena linaibuka suala lingine ambalo lazima tulichunguze nalo kama Bella anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya” Akasema Nawal na mara ukaingia ujumbe katika simu ya Ruby akausoma sura yake ikabadilika


“It’s Zero” akasema


“Anasemaje safari hii? Akauliza Zari na Ruby akampa ujumbe ule ausome


“Evacuate SNSA they’re coming ! Ndivyo ulivyosomeka ujumbe ule kutoka kwa Ziro


Wanawake wale watatu wakabaki wanatazamana


“What are they looking for this time? Akauliza Ruby “Sifahamu nini wanakitaka lakini lazima niende huko haraka sana”akasema Zari


“Zari ni hatari sana kwenda huko sasa hivi.Unaweza ukapiga simu na ukawapa maelekezo watu waliopo hapo waweze kuondoka mara moja eneo hilo” akasema Ruby


“Hapana Ruby lazima


niwepo nihakikishe kila mtu yuko salama.Mimi ndiye kiongozi wao natakiwa kuwa mtu wa mwisho kutoka ndani ya jengo baada ya kuhakikisha wengine wote wako salama.Katika uvamizi wa awali sikuwepo na wakauawa watu sitaki safari hii kupoteza tena mtu yeyote.I need to be there” akasema Zari.Ruby na Nawal bado walionekana kuwa na wasiwasi


“Najua mna wasiwasi but I have to do this” akasema Zari


“Namna gani unakwenda kuwaondoa watu hapo SNSA? Yawezekana kuna watu wao maeneo ya karibu hivyo wakiona watu wakiondolewa ghafla watahisi tayari mpango wao umejulikana.Wakawajulisha wenzao na wakaahirisha mpango wao wa kuvamia” akasema Nawal


“Kuna njia ya chini ambayo tunaoifahamu ni viongozi pekee.Ruby anaifahamu ni njia ya siri sana ambayo hutumika wakati wa dharura kubwa.Njia hii imepita chini na kwenda kutokea katika matumbawe umbali wa mita mia sita kutoka SNSA.Nitawapeleka watu kujificha huko kwani hao jamaa hawataweza kufika huko” akajibu Zari


“Ni plani nzuri sana.Hakikisheni mmezima kila kitu,jamaa watakapofika wasikute mtu hata mmoja wasikute hata taa moja inawaka,wakute jengo liko giza na kimya na tupu.Watakapoingia ndani watashangazwa na hali watakayoikuta na baada ya kuwakosa watu wataamua kuondoka.Bila wao kujua sisi


tutawafuatilia hadi watakapokwenda baada ya kuondoka pale SNSA na baada ya kujua mahala waliko basi tutajipanga namna ya kuvamia na yawezekana tukaomba hata msaada kutoka kwa Rais” akasema Nawal


“Ahsante sana Nawal kwa wazo lako hilo zuri.Kwa kuongezea katika hilo wazo lako lazima tutumie teknolojia ili wasiweze kugundua kama tunawafuatilia.Kuna kifaa kinaitwa mchawi wa usiku.Huyu ni ndege wa bandia aliyetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kufanya ujasusi hasa nyakati za usiku.Kwa muonekano wake anaonekana kama ndege wa kawaida na si rahisi kwa mtu kumtambua mara moja kama si ndege halisi.Macho yake ni kamera mbili zenye nguvu kubwa ya kuweza kutoa picha nzuri hata mahala penye giza.Mara tu watakapokuwa wameingia mahala hapo tutamrusha ndege huyo hadi katika gari lao na kumficha chini ya gari na watakapoondoka ndege huyo ndiye atakayetusaidia kujua mahala wanakoelekea hao jamaa” akasema Zari


“Kwa mpango huu kama ukienda vyema basi naamini tutakuwa tunaelekea mwisho mwa misheni hii.Tutakuwa tunaukaribia ushindi kwani tayari tutakuwa tumefahamu mahala walipo Black Mafia” akasema Ruby


“Tuombe kila kitu kiende kama


tulivyopanga.Tusiendelee kupoteza muda mimi ninakwenda mara moja SNSA na baada ya kufika kule tutawasiliana na kila kitu kitaongozwa kutokea hapa kwa kutumia mfumo wa akiba kwani pale SNSA kila kitu kitazimwa” akasema Zari na kuondoka haraka kuelekea SNSA


“Ruby kwa nini


usimjulishe Rais kuhusu hiki kinachokwenda kutokea SNSA? Akauliza Nawal


“Kwa sasa ni mapema sana kumjulisha Rais kuhusu jambo hili kwani tunaamini kuna watu wake wa karibu wana mawasiliano na hawa watu tunaowatafuta hivyo tukimjulisha watu hao wanaweza wakafahamu mipango yetu na wakaahirisha kila kitu walichopanga kukifanya usiku huu.Tutaendelea na mipango yetu kama tulivyoipanga na pale tutakapokuwa tumefika mwisho ndipo tutamjulisha Rais” akasema Ruby


“Sawa Ruby wakati


tunasubiri Zari afike SNSA nataka tukaendelee kumuhoji Patrick.Tayari tumefahamu kuwa Bella ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya African pictures,na tumejua wamiliki wenzake wa kampuni hiyo wanajihusisha na biashara ya dawa za kuleya tunachohitaji kujua ni je Bella naye anajihusiana na biashara hiyo?Yule jamaa mle ndani anaweza akatusaidia kupata majibu” akasema Nawal wakaelekea katika chumba alimo Patrick


“Patrick nilikuachia swali naamini tayari unalo jibu” akasema Nawal


“Dada yangu naomba uniamini sijawahi kusikia kokote jina Black Mafia likitajwa.Ni mara ya kwanza nimelisikia kutoka kwako” akasema Patrick





“Patrick unafahamu lakini hatari inayokukabili? Umejitumbukiza katika tanuru la moto! Mimi na wenzangu tunaweza kukusaidia jambo hili likabaki siri na Rais hatafahamu chochote,lakini tutakusaidia kama nawe ukiwa tayari kutusaidia”akasema Nawal


“Nini mnataka niwasaidie? Akauliza Patrick


“Ulinitajia wamiliki wa kampuni ya African pictures.Baada ya kufanya uchunguzi tumegundua wote ni wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya”


“Dawa za kulevya?! Akauliza Patrick kwa mshangao


“Ndiyo.Wote ni wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya nchini Afrika kusini.Bella kuwa na ushirika nao tunahisi naye anaweza akawa anajihusiahan a biashara hiyo”akasema Nawal


“Hapana hiyo


haiwezekani.Bella hajihusishi na biashara hiyo ! akasema Patrick


“Tunataka kujiridhisha kama kweli hajihusishi na biashara hiyo kwa sababu washirika wake hawa ambao wanamiliki wote kampuni ya ya African pictures ni miungu wa dawa za kulevya kwa kiigereza wanaitwa drug lords” akasema Nawal


“Sina hakika kama anaweza akajihusisha na biashara kama hiyo.Ninachofahamu mimi anazo biashara zake nyingine mbali mbali lakini si haramu kama hiyo ya dawa za kulevya” akasema Patrick


“Kuna mtandao mkubwa


wa wafanya biashara wa dawa za kulevya hapa nchini ambao sambamba na kusambaza dawa za kulevya wamekuwa wakijihusisha na mambo mengine mbali mbali ya uhalifu ikiwamo mauaji.Umesikia siku chache


zilizopita kuhusu tukio la


kukamatwa Mathew Mulumbi na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya na mauaji,hayo yote yamefanywa na wafanya biashara hao wakitumia kikundi chao kinaitwa Black Mafia” akasema Ruby na kumuelezea Patrick kuhusiana na kundi la Black Mafia na


mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya likiwamo lile la kusambaza picha za faragha za Rais.


“Kwa maelezo haya marefu naamini umepata picha pana ya kile kinachoendela hapa nchini na kwa nini tunataka utusaidie” akasema Ruby “Kama haya unayonieleza ni ya kweli……….”akasema Patrick Nawal akamkatisha


“Yote uliyoelezwa ni ukweli mtupu.Uko tayari kutusaidia? Akauliza Nawal.Patrick akatafakari kidogo halafu akauliza


“Nini hasa mnataka niwasaidie?


“Kampuni ya African


Pictures ambayo Bella ni mmoja wa wamiliki wake tayari tunahisi ina mashirikiano na kundi la Black Mafia na baada ya kugundua kwamba wamiliki wa kampuni hii ni wafanya biashara wa dawa za kulevya hilo limezidi kutupa uhakika mkubwa zaidi kwamba mahusiano baina ya kampuni hii na Black Mafia yapo.Tunachotaka ni kuchunguza kama Bella anajihusisha na biashaa ya dawa za kulevya na kama ana mahusiano na Black Mafia” akasema Nawal na Patrick akazama katika tafakari


“Sikiliza Patrick hili si jambo la kuzama katika tafakari.Tunataka kujua utatusaidia au tufikishe jambo hili la wewe na Bella kwa Rais? Akauliza Nawal


“Nitawasaidia ! Patrick akajibu haraka haraka


“Good.Ni namna gani utatusaidia kumchunguza Bella? Akauliza Nawal


“Kuna msaidizi wa Bella ambaye yeye anafahamu mambo mengi ya Bella huyo anaweza akasaidia.Anaitwa Sarafina ni rafiki yangu sana na ndiye anayefahamu kuhusu mimi na Bella”


“Tutampataje huyo


Sarafina? Akauliza Nawal


“Nitampigia simu Bella na kumwambia kwamba kuna nyaraka za muhimu amtume Sarafina kuja kuzichukua nyumbani kwangu.Atakapofika mtamchukua na kumuuliza maswali kuhusiana na Bella” akasema Patrick


“Unaonekana ni mpango mzuri” akasema Ruby.Nawal akatoka na kwenda kuichukua simu ya Patrick akaiwasha na kumpatia akamtaka ampigie Bella na kuweka sauti kubwa ili Nawal na Ruby waweze kusikia kile watakachokizungumza


“Patrick ! ikasikika sauti ya Bella upande wa pili wa simu


“Mama Bella” akasema


Patrick


“Tangu lini nimekuwa mama yako? Akauliza Bella na Patrick akajilazimisha kucheka


“I like your voice when you act angry ! akasema Patrick


“How’re you Patrick? Are you home? Akauliza Bella “Ndiyo niko nyumbani,nimefika muda si mrefu” akasema Patrick


“Umekula leo mchana?


Akauliza Bella


“Ndiyo Bella”


“Unakula nini usiku huu? Akauliza Bella


“Nilipita pale Rombo Bites nikachukua chakula”


“Pizza again.Kwa nini lakini hutaki nikuwekee mtumishi wa kukusaidia hapo nyumbani?


“Sitaki mtumishi


Bella”akasema Patrick


“Sawa basi endelea kunisubiri pale nitakapkuwa nimeachana na Festus sintapoteza hata siku moja nitaanza kuishi nawe potelea mbali watu watakavyosema na waseme.Mambo yangu na Festus yanakwenda vizuri na ninachokisubiri ni muda huu mfupi amalize kipindi chake cha urais kisha tutaachana rasmi.Endelea kuvumilia kidogo tu” akaema Bella “Ahsante mama..ouh sorry


Thank you Bella” akasema Patrick


“Wewe ! chunga huo ulimi wako”


“Bella kuna nyaraka muhimu hapa nataka uzipate usiku huu uzipitie halafu uzisaini nahitaji kuzipata kesho mapema kabla ya saa nne asubuhi.Naomba umtume Sarafina aje azichukue mara moja hapa nyumbani kwangu” akasema Patrick


“Sawa Patrick ninamtuma atakuja hapo sasa hivi” akasema Bella kisha wakaagana


“Wewe na Bella mmepisha miaka mingapi? Nawal akauliza


“Amenizidi miaka tisa !


“I see ! akasema na kutaka kusema kitu akanyamaza baada ya simu ya Ruby kuita alikuwa ni Rais Festus


“Mheshimiwa Rais” akasema Ruby na kutoka mle chumbani


“Ruby nataka nijue mnavyoendelea hapo” “Mheshimiwa Rais Mathew mshono wake ulifumuka na kwa sasa madaktari wanaendelea kulishughulikia jeraha”


“What? Rais Festus akauliza


“Jeraha la Mathew lilifumuka lakini tayari madaktari wako hapa wanaendelea kumshughulikia”


“Umenistua sana.Vipi hali yake?


“Si mbaya”


“Mathew Mulumbi


anapaswa kupumzika asifanye chochote kwa sasa hadi pale atakapokuwa amepona.Ni mtu ambaye tunamuhitaji sana.Mmefika wapi katika misheni yenu?


“Kwa sasa tunachoendelea nacho ni kuitafuta familia ya Godfrey”akajibu Ruby


“Kuna hatua zozote tayari mmekwisha piga kujua mahala walipo?


“Hapana mheshimiwa


Rais mpaka sasa hatujapiga hatua yoyote”


“Ruby jielekezeni katika kuwasaka hawa maharamia wa


Black Mafia hili suala la familia ya Godfrey linashuhulikiwa na jeshi la polisi na kwa taarifa nilizozipata tayari kuna fununu za mahala walipo na


uhakika wa kuwapata ni mkubwa”


“Sawa mheshimiwa Rais


tunashukuru kwa taarifa hiyo njema” akasema Ruby


“Ruby ningeweza kuja mwenyewe kufuatilia maendeleo ya Mathew Mulumbi lakini siwezi kwa sasa kutokana na sababu za kiusalama.Naomba unijulishe kuhusu maendeleo yake kila wakati”


“Nitafanya hivyo mheshimiwa Rais” akasema Ruby


“Ahsante.Ruby ninataka pia kufahamu ukiacha akina Yeremia ambao tayari wameondoka kama kuna watu wengine mnaendelea kuwashikilia hapo mkiwafanyia uchunguzi? “Ndiyo mheshimiwa Rais kuna watu wawili”


“Ni akina nani hao? Akauliza Rais Festus na Ruby akamueleza kuhusiana na mchungaji Zabron na Yule dereva


“Ruby ninahitaji kuonana na huyo mchungaji Zabron.Nataka kuzungumza naye tafadhali.Godfrey mnaye hapo ili amlete hapa nizungumze naye? Akauliza Rais


“Ndiyo mheshimiwa Rais” “Vizuri.Ninaomba kuzungumza naye tafadhali” akasema Rais na Ruby akamfuata Godfrey akampa simu azungumze na Rais.Baada ya kupewa maelekezo akamrejeshea Ruby simu


“Yuko wapi huyo mtu ambaye natakiwa kumpeleka kwa Rais? Akauliza Godfrey na Ruby akampeleka katika chumba alimo mchungaji Zabron akamvisha mfuko kichwani wakamtoa nje hadi katika gari la Godfrey kisha akaondoka Ruby akarejea katika chumba alimo Patrick


“Ruby tunatakiwa kumrejesha huyu jamaa nyumbani kwake ili akamsubiri huyo mwanamke aliyewasiliane naye na kumtaka amfuate nyumbani kwake” akasema Nawal


“Sawa Nawal,utaongozana na makomando wawili kwenda huko mimi nitabaki hapa


kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri.Tutaendelea kujulishana kila kinachoendelea” akasema Ruby.Nawal na makomando wawili wakamchukua Patrick wakaondoka kuelekea nyumbani kwake


*****************


Godfrey alifuata maelekezo aliyopewa na Rais Festus akafika mahala alipoelekezwa akazima gari akamvua mchungaji Zabron mfuko kichwani akazikata pingu za plastiki alizokuwa amefungwa mikononi


“Nimeelekezwa nikuache hapa watakuja watu kukuchukua na kukurejesha nyumbani kwako.Tahadhari usimueleze mtu yeyote yale uliyoyaona mahala ulipokuwa ama yale uliyoulizwa.Hii ni kwa ajili ya usalama wako” akasema Godfrey


“Hapa ni wapi? Akauliza mchungaji Zabron


“Go ! akasema Godfrey na kumfungulia mlango mchungaji Zabron akashuka akawasha gari na kuondoka akimuacha mchungaji Zabrona amesimama


akishangaa.Dakika mbili baada ya Godfrey kuondoka likafika gari moja na kusimama mbele yake milango ikafunguliwa akashuka jamaa mmoja ambaye Zabron aliweza kumtambua.Alikuwa mmoja wa walinzi wa nabii Kasiano akamtaka Zabron kuingia garini wakaondoka


“Pole sana baba mchungaji” akasema Yule jamaa


“Mungu mkubwa


sana.Mmefahamuje kama niko hapa?akauliza mchungaji Zabron lakini hakuna aliyemjibu chochote safari ikaendelea kimya kimya


Godfrey baada ya kutekeleza maelekezo ya Rais alielekea ikulu kama alivyokuwa ameelekezwa akamjulisha Rais kwamba tayari kazi aliyomtuma ameikamilisha.Rais akamuelekeza aende sehemu Fulani ataikuta familia yake wanamsubiri hapo. *****************


Mchungaji Zabron baada ya kuchukuliwa mahala alipoachwa na Godfrey alipelekwa moja kwa moja nyumbani kwa nabii Kasiano


“Zabron pole sana” akasema Kasiano na kumkumbatia mchungaji Zabron


“Ahsante sana nabii mkuu kwa maombi.Niko hapa ni kwa sababu ya maombi yenu” akasema Zabron


“Zabron tunamshukuru sana Mungu umerejea salama.Nilimlilia sana Mungu akurejeshe ukiwa hai na kati kati ya maombi nikaisikia sauti ya Mungu ikiniambia usifadhaike kwani mchungaji Zabron ni mzima na atapatikana akiwa mzima wa afya.Usiku huu wakati nikifanya maombi nikaoyeshwa mahala ulipo nikawatuma walinzi wangu kwenda kukuchukua”akasema Kasiano na sura ya mchungaji


Zabron ikaonyesha mshangao “Nabii sijui nikushukuruje kwa…”akasema Zabron lakini Kasiano akamkatisha


“Hupaswi


kunishukuru.Sifa na utukufu vyote tumrejeshee mwenyezi Mungu ambaye amefanikisha hili jambo.Najua umechoka na unahitaji kupumzika nataka unieleze kwa kifupi kuhusu mahala ulikokuwa.Unaweza ukakumbuka ni nani waliokuteka? Akauliza Kasiano na mchungaji Zabron akainamisha kichwa chini. “Ninajiuliza je safari ya


Adam na mkewe kwenda Morogoro ilipangwa makusudi ili Adam auawe? Ukitazama kwa kina safari hiyo utagundua kwamba Adam hakuwa ameipanga


bali ilitokea ghafla tena baada ya kuibuka suala la mwanae hivyo ni wazi safari ile ilipangwa makusudi ili aweze kuuawa na kuondolewa kwani tayari alikwisha onekana ni hatari kwao.Baada ya hapo linaibuka swali gumu kujibu je nabii Kasiano anahusika katika jambo hilo la kupanga mauaji ya Adam? Maneno ya Mathew aliyomweleza yakamjia kichwani


“NImeyakumbuka maneno ya yule jamaa Mathew kuhusu Nabii Kasiano.Nimeshangaza kwanza namna nilivyoachiwa huru na nikapewa onyo nisiseme chochote na kinachonishangaza zaidi baada ya dakika chache toka Yule jamaa aniache likatokea gari kuja kunichukua na Kasiano anadai alionyeshwa mahala nilipokuwa akawatuma watu kuja kunichukua.Kuna mkanganyiko wa mambo hapa.Ninaanza kuyaamini maneno waliyoyasema wale jamaa kwamba mimi na wenzangu tunachunguzwa.Ukifuatilia maneno ya wale jamaa utagundua kuna kitu kinaendelea hapa kanisani.Kifo cha mchungaji Adam,mchungaji Lucas na wale jamaa waliouawa nilipotekwa vinanisukuma nijaribu kufanya uchunguzi kujua kama kuna ukweli wowote katika jambo hilo” akawaza mchungaji Zabron na kutolewa mawazoni na sauti ya Kasiano aliyemuita


“Nilipigiwa simu na mwanamke mmoja akaniambia kwamba anataka kuniona anipe taarifa za kilichosabbaisa kifo cha mchungaji Lucas.Nilishangaa kidogo kwa kuwa sote tunajua Lucas na familia yake walifariki kwa ajali ya moto lakini Yule mwanamke akasisitiza ana taarifa muhimu nikapanga kukutana naye mgahawani” akasema mchungaji Zabrin na kumuelezea Kasiano kilichotokea hadi akatekwa nyara


“Baada ya kunichukua


walinivisha mfuko kichwani ili nisiweze kufahamu mahala ninakopelekwa na waliponifikisha katika nyumba yao wakanivua mfuko kichwani nikakutana na watu nisiowafahamu” akasema Zabron


“Unaweza ukakumbuka


picha yoyote ya mahala hapo?Ulitazama dirishani kuna kitu chochote ulikiona nje?Au ulisikia sauti yoyote ile iwe ya adhana au kengele,treni


au magari?”akauliza Kasiano




“Mahala walikonipeleka kulikuwa kimya sana” akajibu Zabron


“Walikuuliza maswali gani? Akauliza Kasiano


“Waliniuliza maswali mengi lakini kubwa walilotaka kulifahamu ni kuhusu mchungaji Adam na familia yake.Nilivyowatazama wale jamaa wanaonekana ni waandishi wa habari”


“Kwa nini unadhani ni waandishi?Kasiano akauliza


“Kwa namna walivyokuwa wanauliza maswali”


“Uliwaeleza nini kuhusu mchungaji Adam”


“Niliwaeleza kile ninachokifahamu kuhusu maisha yake”


“Unaweza ukakumbuka


hata swali moja walilokuuliza?



“Walitaka kufahamu kama mchungajiAdam alikuwa na biashara nyingine nje ya kazi yake ya uchungaji nikawajibu sisi ni watumishi wa Mungu na kazi yetu kubwa ni kumtumikia Mungu hatufanyi biashara.Niliwaambia Adam alikuwa na maisha ya kawaida kama wengine wote tulivyo.Niliwaeleza ukweli namna unavyotulea kama ndugu zako wa damu” akasema mchungaji Zabron


“Zabron pole sana kwa haya yaliyokupata.Kanisa letu


kwa sasa linapita kipindi kigumu.Shetani anatuandama mno ndiyo maana kila leo linaibuka jambo jipya.Nimekwisha wajulisha waumini kwamba njia pekee ya kushinda majaribu haya ni kuzama katika maombi.Naamini umechoka sana nataka ukapumzike tutazungumza kwa kirefu zaidi kesho lakini kuna jambo moja ambalo nataka nikuombe” “Ndiyo nabii”


“Nataka ukae kimya kuhusu jambo hili.Najua wengi watataka kujua mahala ulipokuwa na kama ulitekwa nani waliokuteka.Usimweleze mtu yeyote kitu chochote hadi hapo tutakapowafahamu hawa watu waliokuteka ni akina nani.Ninataka kuleta wapelelezi wa kujitegemea kutoka nje ya nchi ili waweze kutusaidia kufanya uchunguzi tujue watu hao ni akina nani.Nadhani umenielewa mchungaji Zabron” akasema nabii Kasiano


“Nimekuelewa mkuu wangu nitafanya kama ulivyonielekeza” akasema mchungaji Zabron na kuagana na Kasiano akarudishwa nyumbani kwake.


Mara tu mchungaji Zabron alipoondoka,Kasiano akampigia simu Paul


“Paul,tayari mmekwisha waachia wale watu wote?


“Ndiyo mkuu


tumewaachia wote.Familia ya Yule mlinzi wa Rais imekwisha chukuliwa na wale jamaa wengine wa SNSA wamekwisha achiwa pia”


“Good.Paul nataka muendelee kumfuatilia kwa karibu sana huyu mchungaji Zabron kila anachokifanya na kila anayezungumza naye.Ametoka kwa maadui


zetu na hatujui kuna kitu gani wamemwambia na hata yeye mwenyewe anaonekana kuna mambo anayaficha hataki kuwa wazi.Mfuatilieni kwa karibu na kama akionekana kuwa ni hatari kwetu basi aondolewe kimya kimya” akasema Kasiano


“Nimekuelewa mkuu”


“Zoezi la kwenda SNSA usiku huu linakwendaje?


“Linakwenda vizuri mkuu na tuko katika maandalizi ya mwisho” akasema Paul “Vizuri utanijulisha mtakapofanikiwa kumpata huyo mwanamke Zari.Paul tafadhali hakikisha mnafanikiwa kumpata huyo mwanamke ili aweze kutueleza mahala alipo Mathew Mulumbi” akasema Kasiano na kuagana na Paul




*****************


“Niwasaidie kinywaji chochote? Patrick akawauliza akina Nawal baada ya kufika nyumbani kwake


“No thank you.We don’t drink at work” akajibu Nawal


Patrick akaomba kwenda chumbani kwake kubadili mavazi,Nawal akamtaka aongozane na komando mmoja kwenda chumbani kwake kubadili mavazi kama alivyoomba.


Patrick akiwa chumbani kwake simu yake ikaita na jina likatokea Sarafina.Nawal akainuka na kumpelekea simu chumbani


“Hallo Sarafina” akasema


Patick


“Nifungulie geti nimekwisha fika hapa kwako” akasema Sarafina na Patrick kwa kutumia simu yake akalifungua geti Sarafika akaingia ndani


“Ninyi mtabaki hapa chumbani wakati mimi nazungumza naye halafu baada ya dakika chache mtavamia na mtaanza kutuhoji” akasema Patrick na kutoka kwenda kumpokea


Sarafina


“Umenunua gari lingine? Akauliza Sarafina baada ya kukuta gari mbili mle ndani


“Hilo ni gari la rafiki yangu aliliacha hapa.Karibu ndani Sara” akasema Patrick na


Sarafina akaingia sebuleni


“Nilikuwa nakwenda nyumbani kupumzika ndipo mama akanipigia simu akanitaka nije kwako kuchukua mzigo wake” akasema Sarafina


“Samahani sana kwa usumbufu Sarafina.Nipe dakika mbili nikuandalie mzigo wenyewe.Nikuletee kinywaji gani? Akauliza Patrick na Sara akacheka


“Mbona unacheka


Sarafina?


“Kinywaji ninachotumia hapa hauna.Ninatumia vinywaji vikali ambavyo wewe hutumii hivyo ahsante.Labda niletee maji baridi” akasema Sarafina na Patrick akatoka pale sebuleni akaelekea jikoni.Sarafina akiwa ameyaelekeza macho yake katika simu akasikia hatua za mtu akiingia pale sebuleni akainua kichwa na kujikuta akitazamana na mwanamke aliyekuwa na bastola mkononi


“Mamaaa! Akasema na kuangusha simu chini.


“Shhh !! akasema Nawal akimfanyia ishara akae kimya na muda huo huo makomando wengine wawili wakatokea.Haraka haraka Nawal akachukua simu ya Sarafina akaizima halafu akampekua na kuchukua kila kifaa cha mawasiliano alichokuwa nacho halafu akamuiua akampelekea katika chumba cha maktaba akamkalisha kitini.Sarafina alizidi kutetemeka baada ya kumuona Patrick akiingia mle ndani


“Patrick nini kinaendelea? Akauliza


“Sarafina naomba utulie na unisikilize kwa makini sana” akasema Patrick


“Kuna nini jamani?Nimefanya nini mimi?


“Hujafanya chochote Sarafina naomba unisikilize vizuri” akasema Patrick “Hawa jamaa si watu wabaya.wako hapa kuna mambo wanataka kuzungumza nawe na kuomba msaada wako.Tafadhali naomba uwe msikivu”akasema Patrick.


“Ni akina nani hawa? Uko pamoja nao? Sarafina akauliza


“Sara nadhani unaifahamu vyema kampuni ya African Pictures”


“Ndiyo ninaifahamu”


“Unafahamu kama Bella ni mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo? Akauliza Patrick


“Hapana sifahamu kama Bella ni mmiliki wa kampuni hiyo”


“Bella ni mmoja wa wamiliki wa hiyo kampuni”akasema Patrick


“Sifahamu kitu kama hicho na wala hajawahi kuniambia” akasema Sarafina


“Mimi ndiye


ninayesimamia hisa zake katika kampuni hiyo.Kuna wamiliki wengine wawili ambao wako Afrika kusini na baada ya hawa jamaa kuwafanyia uchunguzi wamegundua kwamba jamaa hao ni wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya” akasema Patrick na sura ya Sarafina ikabadilika


“Kwa hapa nchini kuna matukio kadhaa ambayo yametokea kwa siku chache zilizopita” akasema Patrick na kumtajia Sarafina baadhi ya matukio


“Hayo yote yamefanywa na kikundi kinaitwa Black Mafia.Umewahi kusikia mahali jina hilo? Akauliza Patrick “Black Mafia?


“Ndiyo”


“Hapana sijawahi kulisikia jina hilo sehemu yoyote.Ni kikundi cha nini hicho? Akauliza sarafina


“Black Mafia ni kikundi ambacho kazi yake kubwa ni kuwalinda wafanya biashara wa dawa za kulevya na kufanikisha biashara hiyo kufanyika bila vikwazo” akasema Patrick na Nawal akaongezea kwa kumueleza Sarafina kwa undani kuhusu kundi hilo


“Kundi hilo liko hapa nchini kama nilivyokueleza na wanahusishwa na kampuni hii ya African pictures ambayo Bella ni mmoja wa wamiliki wake” akasema Patrick


“Kuna mambo ambayo


Bella amehusika nayo ambayo yamesababisha hawa watu wawepo hapa.Moja wapo ni hili la kuvuja kwa picha za faragha za Rais” akasema Patrick na kumtazama Nawal ambaye alimueleza Sarafina kile walichokigundua kuhusu zile picha za Rais na Sarafina akatoa macho ya mshangao


“Bella anaweza akafanya kitu kama hicho? Akauliza Sarafina


“Ndiyo.Yeye ndiye chanzo cha picha zile kuvuja”


“Bado siamini.Mama Bella anawezaje akakubali aibu kubwa namna hii imkute mume wake? Mnadai ni Bella aliyepiga picha hizo ikawaje zikawafikia hao mnawaita Black Mafia ambao kwa maelezo yenu mnadai walimtaka Rais atekeleze matakwa yao ili wasisambaze picha hizo? Akauliza Sarafina.


“Taarifa za Bella kuhusika katika picha hizo tumezipata kutoka kwa mtu ambaye ndiye aliyefanikisha hadi picha hizo zikapigwa ambaye ni mlinzi wa Rais”


“Hadi mlinzi wa Rais anahusika katika jambo hili?akauliza Sarafina


“Ndiyo.Aliyefanikisha hadi picha za Rais zikapigwa ni mlinzi wa Rais lakini kwa maelekezo ya Bella.Kitu ambacho tunakichunguza kwa sasa ni je baada ya picha hizo kupigwa ziliwafikiaje Black Mafia ambao wanahusika na dawa za kulevya? Je Bella naye anashirikiana nao? Je naye anajihusisha na dawa za kulevya? Hayo ndiyo maswali tunayoyatafutia majibu na tunawaomba wewe na Patrick ambao mko karibu na Bella mtusaidie kumchunguza na kupata majibu hayo.Naamini umesha sikia kuhusu kutekwa nyara kwa familia ya mlinzi wa Rais anaitwa Godfrey asubuhi ya leo”akasema Nawal


“Ndiyo nimesikia jambo


hilo”


“Tunaamini jambo hilo limefanywa na Black Mafia na kwa kiasi kikubwa Bella anahusika.Tunataka kutafuta kitu au ushahidi ambao utamuunganisha Bella na hao wauza dawa za kulevya.Japo tunafahamu tayari kwamba ana ushirika na wafanya biashara wa dawa za kulevya lakini tunahitaji kuchimba na kufahamu kama naye anafanya biashara hiyo ama vipi.Tunataka ninyi watu


wawili mtusaidie katika hilo” akasema Nawal


“Kwa nini jambo hili msilifikishe kwa Rais


mwenyewe?Kama mnao ushahidi wa kutosha kwamba ni Bella ambaye anahusika na picha zile mwelezeni Rais ili aweze kuchukua hatua” akasema Sarafina


“Hili suala ni kubwa ndiyo maana tunataka kulichimba kwa undani zaidi na kupata ushahidi wa kutosha.Bella ni mtu mzito ni mke wa Rais hivyo ili kuthibitisha madai yetu lazima tufanye uchunguzi wa kina na kupata ushahidi wa kutosha na watu ambao tunaamini mtaweza kutusaidia kufanikisha uchunguzi huo ni ninyi wawili”akasema Nawal




“Ni vipi kama nikisema hapana? Akauliza Sarafina


“Sarafina nafahamu wewe ni mtu wa karibu sana wa Bella siri zake nyingi unazifahamu mimi pia ni mtu wake lakini sifahamu mambo yake mengi kama wewe kwani ndiye ambaye umekuwa ukiongozana naye kwenda sehemu mbali mbali,unafahamu ratiba zake unawafahamu watu anaokutana nao na kila anachokifanya.Utafanya makosa makubwa sana kama utakataa kutoa ushirikiano katika uchunguzi wa jambo


hili.Hebu jenga picha familia ya Godfrey ambao wametekwa na hawajulikani kama wako hai au wameuawa,mfikirie Rais mstaafu DrFabian Kelelo ambaye yuko gerezani hivi sasa kwa kesi ya kutengenezwa,hebu fikiria machungu waliyonayo familia ambazo watu wao wameuawa


na kundi hili la Black


Mafia.Lazima tuchunguze na tujiridhishe kama kweli Bella ana mahusiano na kundi hilo.Kama anajihusisha na kundi hilo lazima apate adhabu stahiki.Nakuomba Sarafina tutoe ushirikiano kwa hawa jamaa na tuwasaidie waweze kumamilisha uchunguzi wao” akasema Patrick na Sarafina akatumia muda kidogo kutafakari halafu akasema


“Mnachonitaka nikifanye ni kitu kigumu sana.Bella ni mkuu wangu na inaniwia ugumu kukubali


kumchunguza” akasema


Sarafina na Patrick akajitahidi kumshawishi Sarafina aweze kukubali.


Hatimaye baada ya ushawishi mkubwa Sarafina akakubali kushirikiana na


akina Nawal kumchunguza


Bella


“Nini nitakipata kwa kufanya jambo hili la hatari? Akauliza Sarafina


“Nothing.Hii ni kwa faida ya nchi yako ni kazi ya kujitolea hata sisi ambao tunafanya kazi hii ya hatari hatuna malipo yoyote lakini tunaifanya kwa mapenzi makubwa tuliyonayo kwa nchi hii”akajibu Nawal


“Kazi mnayotaka


niwafanyie ni ya hatari sana.Ni vipi kama nitakamatwa?Nitakuwa nimeharibu kazi na maisha yangu.Lazima kuwekwe kitu mezani ili hata kazi yangu ikiharibika nijue nina kitu nimekipata kitanisaidia katika kuendesha maisha” akasema Sarafina


“Nini unahitaji? Akauliza Nawal


“Nyote mnafahamu namna mambo


yanavyofanyika.Wekeni mezani kiasi cha kutosha mimi niwafanyie kazi yenu”


“Kiasi gani unahitaji? Akauliza Nawal


“Milioni hamsini.Sitaki hundi wala ahadi nataka fedha taslimu” akasema Sarafina


“Sawa utazipata fedha hizo zote lakini utapewa kwanza nusu na baada ya kuhakikisha kazi imefanyika kama tunavyotaka utamalizwa fedha yako yote.Hakikisha unaifanya kazi kama tunavyotaka” akasema Nawal


“Nimesema nataka


taslimu”akasema Sarafina


“Hakuna katika dunia hii anayeweza kukupa fedha hizo zote taslimu bila kwanza kuwa na uhakika kama kazi yake imefanyika ipasavyo.Usiwe na wasiwasi fedha ipo na unaweza ukapata hata zaidi kama kazi yetu ikifanyika tunavyotaka.Utapewa kwanza nusu na kama kazi ikienda vile tunavyotaka basi utapewa kiasi kilichobaki na hata zaidi kama ikitupendeza” akasema Nawal


“Fine.Kitu gani hasa mnataka niwasaidie kukichunguza?akauliza Sarafina


“Tunataka kufahamu mizunguko yote ya Bella,tunataka kujua anawasiliana na akina nani na wanazungumza nini.Tutakupa vifaa Fulani vidogo ambavyo utapewa maelekezo ya kwenda kuviweka ambavyo vitatusaidia kumchunguza Bella” akasema Nawal


“Usiogope Sarafina kazi ambayo tunataka uifanye ni ndogo sana,ukishaweka vifaa hivyo basi kazi yako itakuwa imekwisha na sisi tutakukabidhi malipo yaliyobaki” akasema Nawal “Sawa nitafanya


hivyo.Viko wapi hivyo vifaa? Akauliza Sarafina


“Patrick atakupatia asubuhi.Tutampatia yeye hivyo vifaa na maelekezo halafu atawasiliana nawe na atakukabidhi.Vile vile tutaondoka na simu yako kuna program tunakwenda kuiweka”akajibu Nawal


“Mnaondoka na simu yangu hilo jambo haliwezekani! Akasema


Sarafina


“Ndiyo linawezekana Sarafina.Unataka milioni hamsini au hutaki? Akauliza Nawal


“Ninahitaji”


“Sawa kaa kimya na simu yako utaipata asubuhi” akasema Nawal


“Sawa.Ninaweza kuondoka


sasa? Akauliza Sarafina


“Sarafina na mwenzako nataka kuwaonya kwamba


jambo hili ni la siri sana na msithubutu kulisema kwa mtu yeyote au usijidanganye ukamweleza Bella.Utakuwa umejiweka katika hatari kubwa .Mmenielewa? akauliza Nawal


“Usiwe na hofu Nawal” akasema Patrick.Nawal akatoka ndani ya kile chumba akamuacha Sarafina na Patrick


“I hate you Patrick.How could you do this to me?akauliza Sarafina kwa ukali baada ya Nawal kutoka


“Sarafina huu si wakati wa kulumbana.Jambo hili ni muhimu sana kulifanya.Kama Bella anajihusisha na dawa za kulevya basi sisi sote hatuko salama.Maisha yetu yako katika hatari kubwa sana.Lazima tusaidie kuchunguza kama kweli anajihusisha na biashara hiyo na kama anashirikiana na hao jamaa wa Black Mafia ambao wamekuwa wakifanya mambo makubwa ya uhalifu hapa nchini basi afikishwe kwenye sheria” akasema Patrick





“Do you trust them? Akauliza Sarafina


“Yes I do” akajibu Patrick na Sarafina akainuka


“Ziko wapi nyaraka za Bella nimpelekee usiku huu? Akauliza Sarafina na Patrick akampatia faili lililokuwa na karatasi kadhaa ndani yake


“Utanijulisha kama mzigo wangu utakuwa umefika” akasema Sarafina na kuondoka mle ndani


“Patrick tumemaliza hapa tuondoke tukakupatie fedha na hivyo vifaa” akasema Nawal kisha wakaelekea garini akachukua mfuko kwa ajili ya kumvisha Patrick kichwani “Mpaka sasa bado hamniamini hadi mnivishe mfuko kichwani? Akauliza Patrick


“Huu ni utaratibu wa kawaida tafadhali” akasema Nawal na kumvisha Patrick ule mfuko kichwani ili asiweze kufahamu mahala wanakoelekea wakaondoka kurejea katika kambi yao. *****************


Zari alipofika katika ofisi zao haraka haraka akatoa maelekezo kila kitu kizimwe.Wakati zoezi likiendelea la kuzima kila kitu,Zari akaenda kumchukua ndege ambaye wamempa jina la mchawi wa usiku.Huyu ni ndege wa bandia ambaye ametengenezwa kama ndege halisi ambaye hutumika katika shughuli za ujasusi.Ndege huyo amefungwa kamera zenye nguvu kubwa ya kuweza kupata picha safi hata usiku na vile vile amewekewa vifaa maalum vya hali ya juu vya kuweza kunasa sauti.Baada ya kumchukua ndege Yule akamuwekea betri akamuandaa kwa ajili ya kazi anayotakiwa kuifanya usiku ule.Baada ya kuhakikisha yuko tayari akawasiliana na Ruby akamuwezesha kuingia katika programu ya kumuongoza ndege Yule kwa kutumia mfumo wa akiba halafu


akarushwa na kwenda kutua getini.Baada ya zoezi lile kukamilika Zari akarejea ndani na kuhakikisha kila kitu kimezimwa kisha akawakusanya watu wote


kuwaeleza sababu za kila kitu kuzimwa


“Ndugu zangu nadhani nyote mmestushwa na kitendo cha kuamuru kila kitu kizimwe hapa ndani.Nimepata taarifa kwamba wale jamaa waliotuvamia hapa juzi na kuua wenzetu wanajiandaa kuja kutuvamia tena usiku huu.Hatuwezi kukubali yakatokea kama yale yaliyotokea juzi hivyo tunachukua tahadhari angali mapema kabla hawajaja.Tutakwenda wote kujificha sehemu salama na watakapokuja hapa watakosa mtu na misheni yao itakuwa imefeli” akasema Zari na kumtaka mlinzi mmoja abaki ili azime umeme halafu aondoke zake wengine wote akawataka wamfuate wakaelekea katika njia ya siri ambayo hakuna aliyekuwa anaifahamu zaidi ya Zari peke


yake.Baada ya kuingia ndani ya njia ile ya siri,Zari


akamjulisha Yule mlinzi na umeme ukazimwa kukawa na kiza kinene mahala pale.Zari kwa kutumia tochi ya simu yake akaenda katika chumba cha jenereta lenye mlio mdogo sana akaliwasha na taa zikawaka kwa upande ule wa chini pekee


“Msihofu jamani hakuna mvamizi anayeweza kutufuata huku” akasema Zari na kuwataka wafanyakazi wote wapumzike maboksi ya vinywaji waliyoyabeba yakafunguliwa kila mmoja akapata kinywaji na Zari akaenda katika chumba cha ofisi akampigia simu Ruby akamjulisha kwamba kila kitu kiko tayari.




*****************


Patrick alishushwa garini na kuingizwa ndani baada ya kurejea katika kambi ya akina Mathew halafu akavuliwa mfuko aliofunikwa kichwani.


“Mambo yanakwendaje hapa? Nawal akamuuliza Ruby


“Madaktari wamekwisha maliza kumtibu Mathew jeraha na kwa sasa amelala.Vipi huko mambo yamekwendaje? Akauliza Ruby na Nawal akamueleza kila kitu kilivyokwenda


“Tutapata wapi kiasi hicho kikubwa cha fedha?akauliza Ruby


“Zungumza na Rais mweleze kwamba tunahitaji kiasi hicho cha fedha atutumie mara moja kwa ajili ya kununulia taarifa muhimu.Yeye ana njia nyingi za kuweza kupata fedha hizo kwa haraka” akasema Nawal na bila kupoteza muda Ruby akampigia simu Rais


“Hallo Ruby” “Mheshimiwa Rais tumekwama tunahitaji msaada”


“Msaada gani Ruby?


“Tunahitaji milioni hamsini”


“Milioni hamsini? Akauliza Rais kwa mshangao kidogo


“Ndiyo mheshimiwa Rais”




“Kwa ajili ya nini mnahitaji fedha hizo zote? Akauliza Rais “Mheshimiwa Rais kuna


taarifa tunahitaji kuinunua ni ya muhimu sana na mtu anayetaka kutupa taarifa hiyo anahitaji kiasi hicho cha fedha” akasema Ruby


“Zinahitajika lini fedha hizo?


“Usiku huu mheshimiwa


Rais”


“Usiku huu? Akauliza Rais


“Ndiyo mheshimiwa Rais


tunazihitaji usiku huu”


“Ruby hizo fedha nyingi na kuzipata usiku huu inaweza kuwa vigumu.Kwa nini msisubiri hadi asubuhi nifanye mpango wa kuzipata?


“Mheshimiwa Rais


zinahitajika usiku huu huu” akasisitiza Ruby na Rais akafikiri kidogo kisha akasema


“Hiyo taarifa gani ya kuweza kugharimu kiasi hicho kikubwa cha fedha?


“Ni taarifa muhimu sana mheshimiwa Rais ambayo tuna uhakika kama ikipatikana itatusaidia kuwafahamu hawa watu tunaowatafuta”


“Sawa Ruby naomba


mnipe muda kdogo niangalie namna ya kufanya.Vipi maendeleo ya Mathew Mulumbi? Akauliza Rais


“Mathew anaendelea


vizuri kwa sasa amelala baada ya madaktari kushona tena jeraha lake”


“Sawa utanijulsha kama kutakuwa na mabadiliko yoyote,halafu kuna kitu nataka kukujulisha ni kwamba nimeamua kumuachia huru Yule mchungaji baada ya kugundua kwamba hana hatia yoyote na kuendelea kumshikilia mtumishi wa Mungu kama Yule tunafanya makosa makubwa.Watafuteni maharamia wa dawa za kulevya na msiwashikilie watu kama hawahusiki na mtandao huo.Utawajulisha wenzako kuhusu hilo” akasema Rais na kukata simu Ruy akabaki na mshangao


“Kuna nini Ruby? Nawal akauliza


“Rais amemuachia mchungaji Zabron aondoke zake”


“Kwa nini amefanya hivyo bila ruhusa yetu? Sisi ndio tuliokuwa tunamshikilia na alipaswa kuwasiliana nasi kwanza kabla ya kumuachia” akasema Nawal wote wakabaki wakishangaa kwa kitendo kile cha Rais




*****************


Baada ya kuzungumza na


Ruby Rais Festus alihisi kuchanganyikiwa “Nitazipata wapi fedha nyingi kiasi hicho usiku huu? Akajiuliza


“Niliwaahidi kuwasaidia kwa kila kitu na lazima nizipate fedha hizo kwani inaonekana taarifa wanayotaka kuinunua ni muhimu sana.Tatizo ni wapi ninaweza kupata fedha hizo kwa haraka? Akajiuliza na mara akakumbuka kitu


“Bella”akasema kwa sauti ndogo


“Huyu ana biashara nyingi na fedha kama hii ni ndogo sana kwake” akawaza Festus na kumpigia simu Bella akamtaka amfuate chumbani kwake mara moja.Bella hakupoteza muda akamfuata Festus chumbani


“Unasemaje


Festus?Umenistua kwa simu yako”akasema Bella huku akikaa pembeni ya Festus “Bella ninahitaji msaada”


“Msaada gani unahitaji Festus?


“Fedha”


“Kiasi gani?


“Milioni mia moja”


“Milioni mia moja? Akauliza Bella


“Ndiyo”


“Kwa ajili ya nini?


“Usitake kujua Bella ninachotaka kujua ni kama unaweza ukanisaidia nikazipata fedha hizo usiku wa leo kisha nitazirejesha kesho” akasema Festus


“Sihitaji uzirejeshe kama unahitaji fedha nitakupa kiasi unachokihitaji” akasema Bella “Ahsante Bella.Ninaweza kuzipata usiku huu? Akauliza Festus


“Ngoja nipige simu mbili tatu halafu nitakupa jibu.Unataka kiasi hicho tu au na zaidi? Akauliza Bella


“Kiasi hicho tu” akasema Bella na kutoka baada ya dakika tatu akarejea.


“Nimepata fedha hizo zinakuja ndani ya dakika kumi zitakuwa zimefika hapa”


“Ahsante sana


Bella.Sikutegemea Kama ningeweza kuzipata fedha hizo usiku huu”


“Festus japokuwa unaniona kama takataka lakini ninaweza kuwa na msaada mkubwa sana kwako.Nataka kufahamu umefikia wapi kuhusu lile wazo la baba la kuonana na wale jamaa?


“Nimetafakari sana wazo hilo lakini bado nafsi yangu imekataa kabisa.Bella ukipita mtaani unaweza ukamwaga machozi namna watoto wa watu wanavyoharibika kwa dawa za kulevya ndiyo maana inaniwia ugumu kubariki biashara hiyo kufanyika hapa nchini” akasema Festus


“Festus tafadhali zingatia ushauri wa baba na uufanyie kazi.Zungumza na watu hawa na mtafikia makubaliano kwani mkiendelea kuwindana utakayeumia zaidi ni wewe.Au nipe mimi nafasi ya kuzungumza nao kwa niaba yako nisikie


wanachokitaka”akasema Bella na Festus akamtazama kwa muda halafu akauliza


“Unaweza ukafanya hivyo? “Ndiyo ninaweza nikazungumza nao kwa niaba yako na tukafahamu nini wanakitaka” 



“Sawa nipe muda hadi kesho asubuhi nitakuwa nimepata jibu nini kifanyike” akasema Festus na Bella akatoka kurejea chumbani kwake


*****************


Nawal alikwenda chumbani kwake akafungua moja ya sanduku lake na kutoa kisanduku kingine kidogo ndani yake kilichokuwa na vifaa vidogo vidogo na kurejea katika ofisi walikokuwa Ruby na Patrick akakifungua kile kisanduku akatoa kifaa kidogo


“Patrick kifaa hiki unakifungua halafu utakuta kuna hiki kidude kidogo kama kijikaratasi.Hiki kijikaratasi kitabandikwa katika koti au nguo ya nje aliyoivaa Bella au katika mkoba na mara tu kitakaposhika nguo hiyo basi kitabadilika rangi na kuchukua rangi ya hiyo nguo na hiki kitatuwezesha sisi kujua mahala kokote anakoelekea” akasema Nawal


“Ni vipi kama akibadili hilo vazi alilovaa au mkoba alioubeba?Kwa nini tusikiweke kifaa hiki chini ya simu yake ambayo anaibeba kila mahala aendako? Akauliza Patrick


“Nawal,anachokisema


Patrick kina msingi.Mimi nadhani tutumie simu.Kwa vile simu ya Sarafina ipo hapa tuiwekee program ambayo itatuwezesha kuweza kuingia katika simu ya Bella na kunasa


mazungumzo yake yote kwani zoezi hili linaweza likatuchukua zaidi ya siku moja” akasema Ruby


“Sawa Ruby ni wazo zuri pia” akasema Nawal na Ruby akaanza kucheza na kompyuta yake akaiingiza program Fulani katika simu ya Sarafina kisha akampa Patrick maelekezo.


“Sarafina ataiwasha program hii pale tu atakapokuwa yeye na Bella pekee.Mara tu atakapoiwasha sisi huku tutajua kama imewashwa na program hiyo itaanza kutafuta na kuipata simu iliyo karibu na kujiunganisha nayo na ikisha jiunga na simu ya Bella itatoa mlio mara tatu na hapo kazi itakuwa imekwisha na atapewa pesa yake itakayokuwa imesalia” akasema Ruby


“That simple? Patrick akauliza


“Ndiyo” akajibu Ruby


“Kwa kazi hiyo pekee mtu anapata milioni hamsini?


“Siyo kazi nyepesi hiyo


Patrick,ni jambo la hatari sana analokwenda kulifanya” akasema Nawal na mara katika kompyuta ya Ruby kukatoka mlio akageuka kutazama


katika program ya Yule ndege maalum mchawi wa usiku kulionekana watu.Ndege Yule alifungwa kifaa maalum cha kuweza kuhisi uwepo wa mtu kwa umbali Fulani.


“Kazi imeanza” akasema


Ruby na kuketi kitini Nawal na Patrick nao wakasogea karibu


Katika geti la kuingilia ndani ya jengo la SNSA kulikuwa na watu sita waliokuwa wamevalia mavazi maalum kama wanajeshi na fulana nzito za kuwakinga na risasi wakiwa na silaha huku vichwani kila mmoja akiwa na kofia ngumu .Eneo lote lilikuwa giza na hakukuwa na hata taa moja ikiwaka.Haraka haraka ikaletwa ngazi ikakunjuliwa na watu wawili wakapanda kwa tahadhari wakarukia ndani na kufungua geti na muda huo huo zikatokea gari mbili na kuegesha nje wakashuka watu kumi na saba wote wakiwa na silaha nzito baadhi wakachukua nafasi na kisha wengine wakaelekea ndani ya jengo.


Hawa watu ni akina nani? Akauliza Patrick


“Black Mafia” akajibu Ruby


“Black Mafia? Hapa wanapovamia ni wapi?


“Ni jengo la idara nyeti ya serikali”


“Hawa mbona


wanaonekana kama wanajeshi? Patrick akauliza


“Ni jeshi la wafanya biashara wa dawa za kulevya” akajibu Nawal


“Dah kweli hawa ni watu hatari sana.Sasa nimewaamini kuhusu kile mnachokisema” akasema Patrick


Ruby kwa kutumia program ya kumuendesha Yule ndege akamshusha akampeleka chini ya mojawapo ya magari yale mawili na kumhifadhi




*****************




Sanduku lililokuwa na shilingi milioni mia moja ndani yake liliwasili ikulu na walinzi wakaliwasilisha kwa Bella naye akaenda kumkabidhi Festus


“Nashukuru sana Bella kwa msaada huu.Sikutegemea kabisa” akasema Festus halafu akampigia simu Godfrey na kumtaka afike pale ikulu mara moja


“Hizi fedha Festus anazipeleka wapi? Akajiuliza Bella


“Lazima nifahamu zinakokwenda”akaendelea kuwaza na kuchukua simu yake akampigia Lucas mlinzi wa Rais lakini simu yake haikuwa inapatikana akapatwa na mshangao mkubwa


“Inashangaza kwa nini


Lucas azime simu yake leo?


Kuna tatizo gani? Akajiuliza


“Ni yeye pekee ambaye ninamtumia katika kumchunguza Festus na hakuna mwingine.Nataka achunguze mahala zinakokwenda hizi fedha” akawaza halafu akamuandikia ujumbe mfupi akimtaka atakapowasha simu ampigie mara moja


Rais Festus akampigia simu Ruby na kumjulisha kwamba tayari fedha zimepatikana na Godfrey atazipeleka muda si mrefu


“Ruby fedha hizi ni nyingi sana hakikisheni zinafanya kazi yenye manufaa” akasisitiza Rais Festus


Godfrey aliwasili ikulu na Rais akampatia fedha zile azipeleke kwa akina Ruby na kumtaka awe makini sana ahakikishe hakuna anayemfuatilia




*****************




Katika jengo la SNSA wale jamaa wavamizi waliokuwa na silaha nzito walifanikiwa kuingia ndani kabisa mwa jengo lakini hawakukuta hata mtu mmoja.Kila kitu kilikuwa kimezimwa.


“Nini kimetokea mahala hapa na kila kitu kimezimwa?Vifaa vyao vipo lakini wenyewe hawapo,wamekwenda wapi? Akauliza Paul aliyeongoza kikosi kile.


“Kwa mujibu wa watu tuliowatuma kuchunguza mahala hapa mpaka wakati tunaondoka kuja huku shughuli zilikuwa zinaendelea nini kimetokea watu hawa wamepotea ghafla? Akauliza


Paul


“Au wale watu wetu wametudanganya hawakuwa mahala hapa? Au labda walikwenda katika jengo lingine sehemu nyingine” akasema jamaa mwingine


“Hapana walikuwa nje ya


jengo hili wakifuatilia kila kinachoendelea hapa kuanzia mchana na wameondoka


baada ya sisi kuanza safari ya kuja huku.Tunachotakiwa kujiuliza wamekwenda wapi watu hawa? Akauliza Paul na kukumbuka kitu akaitoa ramani mfukoni


“Kwa mujibu wa ramani hii aliyoichora Frank kuna chumba kinaitwa chumba salama yawezekana wamekwenda kujificha huko” akasema Paul na kuwachukua watu wake wakaelekea katika chumba hicho salama wakafanikiwa kukipata.Kulikuwa na mlango mkubwa imara sana wakatega mlipuko kisha wakaenda mbali kidogo na mlipuko ule ukausambaratisha ule mlango wakaingia haraka haraka mle ndani lakini chumba kilikuwa kitupu hakukuwa na mtu hata mmoja


“Hawa watu lazima wamekimbia.Haiwezekani asiwepo hata mlinzi mmoja wakati kuna vifaa vya thamani kubwa ndani ya jengo hili” akasema Paul na kupigiwa simu na mmoja wa watu wake akamtaka azunguke nyuma ya jengo lile akaenda haraka na kukuta kuna magari yameegeshwa


“Magari zaidi ya ishirini yameegeshwa huku ! akasema Paul na wote wakabaki wamesimama wakitafakari


“Kuna picha moja ambayo ninaipata.Hawa watu wanaonekana wamekimbia.Swali ni je wamekimbia nini na wamekimbilia wapi? Akajiuliza


“Nashawishika kuamini wamekimbia kwa sababu hawawezi wakaondoka watu wote ghafla bila kuacha hata mlinzi mmoja wakati kuna vitu vya thamani kubwa ndani ya hili jengo.Kuna kompyuta humu ndani zina siri za usalama wa nchi hivyo hawawezi wakaliacha jengo bila ulinzi wowote.Kingine kinachonifanya niamini kwamba jamaa hawa wamekimbia ni uwepo wa magari yao hapa na hii inanidhihirishia kwamba hawako mbali” akawaza Paul na kuwataka watu wake watawanyike tena kwa mara ya pili kuchunguza


“Kama wamekimbia nini kimewakimbiza? Paul akarudia tena kujiuliza swali


“Kuna kitu nimeanza kukihisi.Kutoweka kwa hawa jamaa si bure,Je walifahamu kama tunakuja? Akajiuliza na haraka haraka akawaita watu wake na kuwataka waondoke haraka sana eneo lile


“Huu ni mtego tumetegewa.Hawa jamaa inaonekana kuna mahala wamejibanza wanatutazama na hii ni hatari sana kwetu kwani tunaweza tukashambuliwa bila kujua tunapigwa kutokea wapi.Mahala hapa kuna silaha za siri na tunaweza kusambaratishwa ndani ya sekunde chache” akawaza Paul wakati wakikimbia kuelekea katika magari yao wakaondoka haraka.






*****************




Mara tu Black Mafia walipoondoka katika jengo la SNSA akina Ruby wakajua mara moja kwani tayari ndege wao alikuwa chini ya moja wapo ya gari.Mara tu walipoondoka Ruby akamtumia ujumbe Zari akamjulisha kwamba wameondoka


Mlango wa chumba walimokuwamo akina Ruby ukafunguliwa na wote wakapatwa na mshangao kwa kumuona Mathew Mulumbi “Mathew ! akasema Nawal


Mathew alikuwa anatembea kwa kuchechemea.Wote mle ndani wakabaki wameduwaa wakimtazama


“Sijawahi kuona mtu msumbufu kama huyu MathewMulumbi ! akawaza Nawal.Patrick alipatwa na mstuko na kuingiwa na woga mkubwa baada ya kumuona


Mathew


“Where are we?akauliza Mathew na kuketi kitini.Wote wakabaki wanamtazama


“I’m fine guys.Where are we? Akauliza Mathew na kugeuka akamtazama Patrick


“Why is he relaxing like this? Akauliza


“He’s cooperating” akajibu Nawal na kumueleza Mathew kuhusiana na Patrick na hatua waliyofikia


“Yuko hapa anasubiri fedha toka kwa Rais” akasema


Nawal


“Good.Ahsante kwa ushirikiano wako.Ruby kuna nini kwa upande wako? Akauliza Mathew na Ruby akamweleza kila kitu na mahala walikofikia


“Good job guys.Kwa hili mlilolifanya mmenipa uhakika hata kama nisipokuwepo mnaweza mkafanya mambo makubwa”akasema na kumtazama Patrick


“Hakikisha unafanya kila linalowezekana ili hicho ulichoelekezwa kukifanya kifanikiwe” akasema Mathew “Ruby Mwambie Zari makomando wote wanatakiwa waje hapa ili tuweke mikakati ya kuvamia makazi ya Black Mafia usiku huu wa leo” akasema Mathew


“Mathew kuna jambo


lingine limetokea wakati ukipatiwa matibabu ambalo unatakiwa kulifahamu”akasema Ruby na kumweleza Mathew kuhusiana na Rais kumruhusu mchungaji Zabron kurejea nyumbani


“Kwa nini akafanya hivyo? Akauliza Mathew


“Anadai baada ya kuzungumza naye akagundua kwamba hana kosa lolote na akaamuru aondoke arejee nyumbani”


“Alizungumza naye kitu gani? Tunaopaswa kuzungumza naye ni sisi yeye anahusikaje katika kumuhoji mtu? Akauliza Mathew


“Wote tulishangazwa na jambo hilo” akasema Nawal


“Guys nawapongeza sana kwa kazi nzuri lakini pamoja na maendeleo mazuri ya misheni yetu tunapaswa pia kuhakikisha tunamsaidia Godfrey kujua mahala iliko familia yake.Kadiri muda unavyokwenda ndivyo familia yake inavyozidi kuwa hatarini.Kwa maelezo aliyoyatoa Lucas kuna kila dalili Bella anahusika katika utekwaji wa familia ya Godfrey hivyo kadiri tutakavyo harakisha kufanya uchunguzi kuhusu Bella ndivyo tutakavyoharakisha kuokoa maisha ya familia ya Godfrey” akasema Mathew na kuwataka wahamishie ofisi katika chumba chake kwani alihitaji kujua kila kinachoendelea *****************


Zari na wafanyakazi wengine wa SNSA waliokuwa


wamejificha katika handaki lililo chini ya jengo lile wakatoka lakini Zari hakutaka waendelee tena na kazi akawataka wote isipokuwa walinzi warejee manyumbani kwao kwa hofu ya kuvamiwa tena na wale jamaa.Yeye naye hakupoteza muda akaongozana na makomando wakaondoka kurejea katika kambi yao.


“Bado nitaendelea kumshukuru sana huyu Ziro ambaye mpaka leo hii hatumfahamu.Bila yeye kutupa taarifa mapema leo hii watu wengine wangepoteza maisha” Zari akatolewa mawazoni baada ya simu yake kuita akaipokea


“Hallow” akasema


“Hallow mkurugenzi” ikasema sauti ambayo zari aliitambua


“Lutengano? Akauliza


“Ndiyo ni mimi mkurugenzi” “Gosh ! Uko wapi?


“Niko kwenye gari mkurugenzi ninaelekea nyumbani”


“Unalekea nyumbani?! Zari akashangaa


“Ndiyo.Wale jamaa wametuachia huru na wamekuja kututupa huku mbali kwa bahati nzuri tumepata msaada wa usafiri na sasa tunaelekea nyumbani” akasema Lutengano na Zari akashusha pumzi


“Ilikuaje mkaachiwa huru?


“Hata sisi hatuelewei madam Zari kwani tulichukuliwa tukafunwga vitambaa usoni na kuja kutupwa huku bila kupewa maelezo yoyote”


“Dah ! Ahsante Mungu kwani huu ni kama muujiza.Nyote mko salama kabisa? Akauliza Zari


“Ndiyo sote tuko salama japo tumeumizwa sehemu mbali mbali lakini tuko salama.Hofu yetu ilikuwa kwako kwani wewe ndiye hasa wanayeonekana kukutafuta sana”


“Usiku huu wamevamia tena SNSA lakini hawakufanikiwa kupata mtu yeyote”akasema Zari


“Basi walikuwa wanakufuata wewe kwani ndiye hasa wanayekutafuta wanaamini wakikupata wewe watakuwa wamempata pia Mathew Mulumbi.Madam


sikushauri uende tena hapo SNSA na kama ikiwezekana hamisha kabisa hata ofisi yako au tuhamishe kabisa ofisi kwani wamekwisha zifahamu hawa jamaa” akasema Lutengano


“Hilo ni wazo zuri sana


Lutengano.Nitalifikisha kwa Rais tulifanyie kazi haraka.Naomba wasiliana na Jonathan muelekeze mahala ambapo mtakutana atawafuata


na gari na kuhakikisha kila mmoja amefika nyumbani kwake salama na kama kuna yeyote aliyeumizwa zaidi na anahitaji matibabu kwa usiku huu nijulishe tafadhali”akasema Zari na kukata simu


“Imekuaje wakawaachia akina Lutengano kirahisi namna hii? Akajiuliza Zari


“Nitakutana nao kesho na kuzungumza nao zaidi lakini wazo alilotoa kuhusu kuhamisha ofisi ni wazo la msingi.Idara hii ni ya siri na hata ofisi zake zinapaswa kuwa mahala pa siri pia lakini kwa sasa hakuna siri tena tumekwisha fahamika na hii ni hatari kubwa kwani mahala pale kuna siri nyingi za usalama wa nchi” akawaza Zari


Walifika katika makazi yao na kuwakuta wote wakiwa katika chumba cha Mathew.Habari ya kwanza aliyowapa ni kuachiwa huru kwa wale watu watano waliokuwa wametekwa nyara.


“Kwa nini wamewaachia huru kirahisi namna hiyo? Mathew akauliza


“Hilo ndilo swali ambalo hata mimi nimejiuliza sana sijapata jibu labda tutakapoonana nao wanaweza wakatupa majibu nini kimetokea.Guys kutokana na kuvamiwa mara mbili na hawa jamaa nafikiria kumshauri Rais tuhamishe ofisi mahala pale si pa siri tena” akasema Zari na Mathew ambaye macho yake alikuwa ameyaelekeza kwa Ruby akagundua kuna kitu


“Kuna nini Ruby? Akauliza Mathew


“Inaonekana wale jamaa wamesimama” akasema Ruby


“Mtoe ndege tujue kama kweli wamesimama” akasema Zari na kwa kutumia programu ya kumuongoza Yule ndege Ruby akamtoa na wakaanza kupata picha za mahala pale.Magari yale mawili yalikuwa katika maegesho na hakukuwa na mtu yeyote ndani ya magari yale.


“Inaonekana tayari wamefika kwani magari yameegeshwa na hakuna mtu yeyote ndani ya magari” akasema Ruby


“Safi sana.Unaweza ukajua mahala hapo walipo ni wapi? Akauliza Mathew na Ruby akaanza kucheza na kompyuta yake halafu mara ikatokea


ramani ya jiji la Dar es salaam na mduara mwekundu ukatokeza sehemu Fulani ndani ya Ramani


“Hapa ndipo walipo hao jamaa” akasema Ruby na kuikuza ramani ile


“Tunatakiwa kutuma watu wafuate ramani hiyo ili tuweze


kuipata picha pana zaidi ya mahala hapo ambako wameingia hao jamaa.Yawezekana ndipo yalipo makazi yao au yawezekana kuna kitu wamekwenda kufanya hapo.Zari tuma makomando wawili mara moja wafuate maelekezo watakayopewa na Ruby ili waweze kufika mahala hapo mara moja” akasema Mathew na Ruby akaita makomando wawili Ruby akawapa maelekezo wakaondoka mara moja


“Guys usiku wa leo unaweza kuwa na mambo mazito sana.Makomando wetu wakae katika utayari kwani yawezekana usiku wa leo ukawa ni usiku wao” akasema Mathew




Baada ya kurejea katika ofisi yao Paul bila kuaga mtu yeyote akachukua gari lake dogo na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Kasiano.Wakati wakirejea alimtumia ujumbe Kasiano na kumuomba waonane usiku ule na Kasiano akamtaka mara tu watakapokuwa wamerejea basi amfuate nyumbani kwake wakazungumze


Alifika nyumbani kwa Kasiano akakaribishwa


“Paul hukutaka kunieleza kile kilichotokea katika simu ukasisitiza kwamba unataka kuja kuniona,kitu gani kinaendelea? Akauliza Kasiano


“Mkuu sikutaka kuzungumza mbele ya vijana lakini misheni yetu imeshindwa kufanikiwa”akasema Paul


“Nilijua tu haitakuwa rahisi kuingia tena ndani ya lile jengo”akasema Kasiano “Si hivyo mkuu.Kuingia tumeingia lakini kuna kitu cha ajabu sana kimetokea”


“Nini kimetokea? Akauliza Kasiano kwa wasiwasi na Paul akamueleza kile kilichotokea.Kasiano akamtazama Paul kwa dakika moja halafu Paul akaendelea


“Mkuu hiki kilichotokea kinanipa picha wale watu walikimbia kujificha na walikimbia kujificha kwa sababu walifahamu kuhusu misheni yetu ya kwenda kuvamia pale usiku huu” akasema Paul na ukimya ukatawala.Kasiano akainua glasi yake ya kinywaji akanywa mafunda mawili halafu akasema


“Paul taarifa hii imenistua sana ndiyo maana unaniona ninatumia muda kulitafakari suala hili kwa makini sana.Kuna picha nyingi zinanijia akilini haraka haraka kuhusiana na jambo hili.Watu wote kutoweka asiwepo hata mlinzi na kuacha jengo tupu ni kitu cha kushangaza sana” akasema Kasiano


“Cha kushangaza zaidi mle kuna siri za usalama wa nchi lakini waliondoka wote na kuacha jengo tupu.Mkuu ule ulikuwa ni mtego na ninaamini wale jamaa hawakuwa mbali na yawezekana walikuwa wanatutazama kile tunachokifanya na yawezekana kama tungeendelea kupoteza muda pale wangeweza kutumaliza kwani kuna silaha zimefichwa mle ndani ambazo zinatumika kielektroniki ndiyo maana nikawaondoa watu wangu mara moja mahala pale kuepusha maafa” akasema Paul


“Ulifanya vizuri sana Paul kuwaondoa vijana mahala hapo.Ninachotaka ukifanye kwa sasa tuma vijana wawili warudi tena mahala hapo waangalia kama kuna kazi yoyote inaendelea hivi sasa,waone kama taa zimewashwa tena na walinzi wamerejea.Kama shughuli


zimerejea basi tutakuwa na uhakika mkubwa kwamba walifahamu ujio wenu mahala pale” akasema Kasiano “Tayari nimekwisha tuma watu waende hapo naamini muda huu watakuwa wamefika au wamekaribia” akasema Paul na kutoa simu akampigia mmoja wa watu wake aliowatuma kurudi tena SNSA kuchunguza


“Mkuu tumefika hapa mahala taa zimewaka kama kawaida na ulinzi ni mkali” akajibu Yule jamaa.


“Kila kitu kimerejea” Paul akamwambia Kasiano


“Hakuna kutumia nguvu


kubwa kujiuliza walikuwa wapi ni wazi walikuwa wamejificha baada ya kujua mnakwenda hapo.Swali moja tu ambalo tunatakiwa kulitafutia majibu hivi sasa ni je walifahamuje kama mnakwenda hapo?


“Mkuu hapo jibu ni jepesi lazima taarifa hiyo waliipata kutoka kwetu.Kazi yetu ni kutafuta ni namna gani wameweza kuipata taarifa hiyo hadi wakaweza kuwaondoa watu wote ndani ya jengo”akasema Paul


“Paul watu wako wote unawaamini? Akauliza Kasiano


“Ndiyo mkuu ninawaamini sana”


“Kama taarifa zetu zimeweza kuwafikia hawa jamaa basi ni lazima kuna mtu wetu ambaye anashirikiana nao au kuna namna wamefanya kuweza kupata taarifa zetu.Jambo hili halitakiwi kufika kesho asubuhi lazima tuwe tumepata majibu nini kilitokea na kama kuna mtu anashirikiana nao basi tumjue.Paul tusikubali kuwapa ushindi hawa jamaa kwa namna yoyote ile lazima tuhakikishe tunawaondoa wote.Kilichotokea usiku huu kimenistua sana na sikufichi amani imetoweka ! akasema Kasiano na kunywa tena kinywaji chake


“Paul nataka urejee tena katika ofisi zenu wakusanye watu wako wote sehemu moja,chukua simu zao zote na ichunguzwe moja moja kujua mawasiliano yao,nina uhakika mkubwa sana mtafanikiwa kumpata Yule ambaye anatumika kutoa siri zetu” akasema Kasiano na Paul akaondoka


Mara tu Paul alipoondoka,Kasiano akampigia simu Bella “Kasiano” akasema Bella


“Mama Bella utanisamehe kwa kupia simu muda huu” akasema Kasiano


“Unasemaje Kasiano? Akauliza Bella na Kasiano akamueleza kile kilichokuwa kimetokea usiku ule “Kasiano kwa nini mkafanya kitu cha kijinga kama hicho?Kwa nini mkaenda tena kuvamia SNSA hasa kwa wakati huu ambao


ninahangaika kutafuta suluhu la hiki


kinachoendelea?Kasiano hali si nzuri hasa kwa upande wetu hawa jamaa wanazidi kupata mafanikio zaidi kila uchao na wanazidi kutusogelea ndiyo maana ninajitahidi kuweza kuwazuia wasisogee zaidi ya hapa walipofika lakini mlichokifanya usiku huu kitaharibu juhudi zangu na kufanya mambo yawe magumu zaidi.Nilikuwa karibu sana kumshawishi Rais akae nasi mezani lakini akisikia kwamba SNSA imevamiwa tena itakuwa vigumu kumleta mezani na mambo yatazidi kuwa mabaya” akasema Bella


“Mama Bella mpango ulikuwa mzuri kwani wale watu waliokuwa wanashikiliwa baada ya kuhojiwa walikiri kwamba Zari ndiye anayefahamu mahala alipo Mathew Mulumbi na sehemu pekee ambako tungeweza kumpata Zari ni katika ofisi zao kuu SNSA ndiyo maana ukaibuka mpango huo wa kuvamia tena mahala pale lakini yakatokea hayo yaliyotokea” akasema Kasiano


“Kasiano japokuwa nia


ilikuwa nzuri lakini tayari mambo yameharibika na bila kuchukua hatua za haraka kumtafuta mtu ambaye ametoa taarifa zetu mambo yatakuwa mabaya zaidi.Fix this before sunrise! Akasema Bella


“Ndiyo mama Bella tayari hatua zimekwisha anza kuchukuliwa nimemuelekeza Paul kuchukua simu za watu wake wote zifanyiwe uchunguzi mawasiliano yao ili kubaini ni nani aliyetoa taarifa SNSA” akasema Paul na kuagana na Bella


“Nimestushwa mno na hiki alichonieleza Kasiano kwamba wanahisi kuna mtu ametoa taarifa kwa SNSA kuhusu mpango wao wa kuvamia jengo ndiyo maana wakaweza kutoroka.Kama kuna mtu ndani ya Black Mafia ambaye anatoa taarifa zetu basi hii ni dalili mbaya sana na


anatakiwa asakwe kwa kila namna apatikane kwani yawezekana amekwisha toa taarifa nyingi kwa hawa watu tunaowatafua na yawezekana ndiyo maana mipango yetu inashindwa kufanikiwa kwa sababu yake.Imekuwa vyema wameligundua hili mapema” akawaza Bella na kujaribu kumtafuta Lucas simuni lakini bado hakuwa akipatikana


“Lucas yuko wapi leo? Kwa nini amezima simu? Akaendelea kujiuliza Bella *****************


Godfrey alifika katika kambi ya akina Mathew na kustuka baada ya kumkuta tayari Mathew amekwisha amka.Aliwakabidhi sanduku lile lenye fedha na kutaka kuondoka akidai anatakiwa ikulu lakini Mathgew akamzuia


“Naomba ubaki kwa


dakika chache kuna masuala muhimu nataka tuzungumze” akasema Mathew


“Ningeweza kukaa Mathew lakini nilipewa maelekezo ya kuwasilisha mzigo huu na kuwahi kurejea ikulu kuna kazi inanisubiri”


“Unataka kurejea ikulu?Unawezaje kurejea kazini wakati familia yako haijulikani mahala walipo? Akauliza Mathew na Godfrey akakaa kimya


“Tunataka tujadiliane namna ya kuweza kuipata familia yako.Wale jamaa hawajakupigia simu hadi sasa? Akauliza Mathew


“Hapana hawajanipigia kwani simu yangu waliichukua” akasema Godfrey


“Ulipopewa mzigo huu kuuleta huku ulikuwa ikulu? Akauliza Mathew


“Hapana nilikuwa nyumbani ndipo Rais akanipigia simu nikaenda ikulu akanipa mzigo huu niulete”akajibu Godfrey


“Alikupigia katika simu ipi?Mathew akauliza


“Nina simu nyingine” akajibu Godfrey


“Godfrey kuna kila dalili kwamba Bella anahusika katika tukio la kutekwa familia yako.Tunajiandaa kwa mpango kabambe wa kumchunguza na yawezekana tukafahamu mahala walipo familia yako ninachokuomba usife moyo ila kama kuna kitu chochote unadhani kinaweza kutusadia hata kama ni kidogo unaweza ukatushirikisha tukakifanyia kazi” akasema Mathew na Godfrey akainamisha kichwa kwa muda akazama mawazoni halafu akainua kichwa na kusema


“Naombeni niwe mkweli ndugu zangu kwani sitaki kuendelea kuwapotezea muda wenu ambao mngeutumia kwa mambo mengine muhimu” akasema Godfrey na kunyamaza akamtazama Mathew


“Familia yangu imepatikana” akasema Godfrey na wote mle ndani


sura zao zikapatwa na mshangao


“Wamepatikana? Mathew


akauliza


“Ndiyo wamepatikana” “Wamepatikanaje na wapi?Kuna kitu umewapa watu waliokuwa wanawashikilia wakakubali kuwaachia? Akauliza Mathew na Godfrey akavuta pumzi ndefu


“Mathew


Mulumbi,Ruby,Zari na Nawal ninyi ni ndugu zangu na tangu limetokea tatizo hili la kutekwa kwa familia yangu ninyi mmeonyesha moyo wa dhati wa kusaidia kuwasaka na hivyo naombeni niwe muwazi kwenu.Sifahamu nini hasa kimetokea lakini baada ya kuondoka hapa nikiwa na mchungaji Zabron nilielekezwa na mheshimiwa Rais kumpeleka sehemu fulani nikamuacha hapo halafu nikarejea ikulu na akanielekeza kweda mahala Fulani nikaikuta familia yangu” akasema Godfrey


“Godfrey hatujakuelewa hebu tufafanulie vizuri namna ulivyoweza kuipata familia yako” akasema Zari na Godfrey akarudia tena kuwaeleza kila kitu namna alivyoweza kuipata familia yake


“Hili jambo mbona linachanganya.Unatuthibitishi a kwamba baada ya kuondoka na mchungaji Zabron hapa hukumpeleka ikulu bali ulimpeleka mahala


ulikoelekezwa na Rais halafu ukamuacha hapo?Mathew akauliza


“Ndiyo Mathew nilifanya hivyo kwa maelekezo ya Rais”akajibu Godfrey


“Ulipoipata familia yako hukumuuliza Rais amejuaje kama wako pale na wameachiwaje?


“Hapana sikumuuliza chochote”


“Nini kinaendelea hapa? Mbona kuna mambo yanafanyika ambayo siyaelewi?Akauliza Mathew


“Kweli kuna mambo


yanachanganya.Familia ya Godfrey waliokuwa wametekwa nyara na watu ambao tunaamini ni Black Mafia wameachiwa huru na wakati huo huo wafanyakazi wa SNSA nao pia wanaachiwa huru bila sababu ya kueleweka na bila maelezo ya kutosha Rais anaamua kumrejesha mchungzaji Zabron nyumbani kwake.Mnapata picha gani katika matukio haya matatu? Akauliza Zari


“Mtu pekee ambaye anaweza akatoa majibu yenye uhakika ni Rais,yeye ndiye anayefahamu sababu za kumuachia mchungaji Zabron na akadanganya kwamba amezungumza naye akagundua hana kosa,pili ni yeye aliyempa maelekezo Godfrey aende mahali na ataikuta familia yake hii inatoa picha kwamba Rais anafahamu kwa nini familia hiyo wameachiwa na hii inanifanya niamini aidha yeye au mwakilishi wake amezungumza na hawa watu na wakafikia makubaliano hadi wakaamua kuwaachia huru familia ya Godfrey.Hebu tazameni hii picha tunawatafuta Black Mafia na kwa sasa tunamuhisi Bella mke wa Rais kuwa na mahusiano na hao Black Mafia hamdhani kwamba anaweza kuwa na mkono wake katika jambo hili?akuliza Mathew “Anachokisema Mathew Mulumbi kina msingi sana na inawezekana kabisa Bella akawa na mkono wake katika jambo hili.Kwa kuwa yeye ana mahusiano na hao jamaa yawezekana amefanya namna mateka wote wakaachiwa na inawezekana ndiyo maana Rais akamrejesha mchungaji


Zabron” akasema Ruby


“Kwa hiyo haya yanaonekana kama ni mabadilishano ya mateka” akasema Mathew “Inaonekana hivyo” “Kama ni kweli kwa nini Rais akakubali kufanya kitu kama hicho? Anawezaje kufanya makubaliano na watu ambao anafahamu ni hatari kwa nchi?akauliza Ruby


“Yawezekana anazo


sababu zake za kufanya hivyo” akasema Godfrey


“Hakuna sababu yoyote inayoweza kumfanya akazungumza na hawa jamaa na kuwekeana nao makubaliano ! akasema


Mathew


“Kama ni kweli amefanya hivi atakuwa ametusaliti kwa kiasi kikubwa mno! Akasema Nawal


“Godfrey unaweza ukaenda tunashukuru kwa kila kitu ulichokifanya leo na pole sana kwa masahibu mazito.Wape pole pia familia yako kwa kilichowatokea.Sisi tunaendelea kupambana kuwasaka hawa jamaa na hatutalala hadi mtu wa mwisho atakapokuwa amepatikana” akasema


Mathew


“Kuna chochote ninaweza kusaidia? Akauliza Godfrey


“Ahsante Godfrey uliyoyafanya yanatosha sana,nenda kakae na familia yako wanakuhitaji sana muda huu.Tafadhal usimwelez e Rais chochote kama umetuambia kile ambacho kimetokea” akasema Mathew na Godfrey akaondoka


“Jamani kuanzia sasa Rais si wa kumuamini tena.Anaonekana ni mtu mwenye sura mbili yuko upande wetu na wakati huo huo anafanya mambo ambayo hatuyaelewi.Sisi tunaendelea na misheni yetu kama kawaida ya kumchunguza mke wake na hatutamshirikisha hadi pale tutakapokuwa tumekamilisha uchunguzi wetu.Guys Rais anafahamu mambo mengi kuhusu mke wake lakini anamkingia kifua na hataki aingie katika matatizo.Hakuna aliye juu ya sheria kama mke wake amevunja sheria za nchi lazima aadhibiwe kama wahalifu wengine.Hili halitampendeza Rais na tutaweza kuingia katika mgogoro lakini msihofu migogoro ni sehemu ya maisha yetu” akasema Mathew


“Nilianza kuwa na wasi wasi na Rais pale alipoamua


kulimaliza lile suala la wale jamaa waliokuwa na mpango wa siri wa kumkabidhi Mathew Mulumbi kwa Black Mafia mpango ambao uliongozwa na mke wake Bella” akasema Nawal


“Tusimuwaze sana


Rai……….” Akanyamaza


Mathew baada ya simu ya


Ruby kuita alikuwa ni ziro “Ziro anapiga” akasema Ruby


“Ziro kaamua kupiga? Mathew akauliza wote wakashangaa na bila kupoteza muda Ruby akaipokea na kuweka sauti kubwa ili kila mmoja mle chumbani aweze kusikia atakachokisema


“Hallo who are you? Akauliza Ruby


“I’m the one who’ve been sending you warning messages”


“Thank you.What do you want? Akauliza Ruby


“I’m in trouble and I need your help.They’re searching for me and they’ll soon find me.Please come and get me” akasema Ziro


“Where are you? Akauliza Ruby


“I’m sending you the coordinates where you can get me.7th floor that’s where they are” akasema Ziro


“Okay Ziro send us the coordinates and we’ll come get you” akasema Ruby na kumuuliza ni namna gani watu wao watakavyoweza kumtambua pale watakapoingia ndani akamjulisha kwamba amevaa kofia nyeupe fulana nyekundu na suruali ya jeans ya bluu.Baada ya sekunde tano ukaingia ujumbe katika simu ya Ruby ukiwa na maekelezo kutoka kwa Ziro.


“Wait guys ! akasema Zari


“Kabla haujafanya chochote huu si mtego wa hawa jamaa? Akauliza Zari “Ziro amekuwa akimtumia Ruby ujumbe mbali mbali wa kumuonya sina hakika kama huu unaweza kuwa ni mtego.We need to get her very quick” akasema Mathew


Zari akawaita makomando


wote waliokuwa wamekusanyika pale na kuwataka waanze maandalizi kwani muda si mrefu watatumwa mahala kwenda kumuokoa mtu


Ruby alicheza na kompyuta yake haraka haraka akayatumia maelekezo aliyotumiwa na Ziro kutafuta mahala alipo


“Is this true? Akauliza Ruby


“Kuna nini Ruby?Nawal


akauliza


“Maelekezo haya aliyonipa Ziro yanaonyesha mahala alipo ni pale pale ambako tumewatuma watu wetu wakapatafute na kupafanyia uchunguzi”


“Kweli? Akauliza Mathew na kutaka kuinuka lakini akahisi maumivu na kulala tena




“Ni kweli ndiyo maana nimestuka” akajibu Ruby


“Lakini hatuna sababu ya kushangaa kwani tunafahamu toka awali kwamba Ziro yuko na hawa jamaa.Ametusaidia sana ni wakati wetu na sisi kumsaidia.Wapigie watu wetu simu waulize kama tayari wamekwisha fika hapo mahala tuliowatuma” akasema Mathew na Zari akawapigia simu makomando waliotumwa kufanya uchunguzi kama


tayari wamekwisha fika mahala walikotumwa


“Mkurugenzi tumefika


eneo hili na tulikuwa tunafanya uchunguzi kabla ya kuwajulisha.Nje ya jengo hili la ghorofa saba kuna bango kubwa limeandikwa African pictures Co.Ltd”


“African pictures? Zari akauliza


“Ndiyo mkurugenzi” “Are you sure?


“Ndiyo mkurugenzi”


“Sawa endeleeni na uchunguzi zaidi hakikisheni hamgunduliwi tutawasiliana nanyi baada ya dakika chache” akasema Zari na kukata simu


“African pictures is the place” akasema Zari


“Mathew ulikuwa sahihi kuihusisha hii kampuni na hawa jamaa kabla hata hatujapata maelezo ya Patrick” akasema Nawal na Patrick akasimama


“Samahani ndugu zangu nafahamu sihusiki mahala hapa lakini nimesikia mkitaja jengo la kampuni ya filamu la African pictures.Ninalifahamu jengo hilo ninakwenda mara kwa mara mahala hapo kuonana na


Lethabo.Nimestuka pia kusikia kwamba Black Mafia wanalitumia jengo hilo hilo na wana mahusiano na kampuni hii hivyo nataka nitoe msaada kama nitaruhusiwa”


“Msaada upi unataka kuutoa Patrick”


“Watu mnaowatuma


yawezekana hawalifahamnu vyema hilo jengo ninaweza kuwasaidia kuwapa maelekezo namna ya kufika na kuweza kufika hadi huko ghorofa ya saba mlikoelekezwa na yule aliyewapigia simu” akasema Patrick na Mathew akamtazama kwa muda halafu akamtaka aendelee.Akatoa maelezo ya namna anavyolifahamu jengo lile.Mathew akaelekeza makomando waitwe mle chumbani ili wajadiliane namna ya kuweza kuingia mle ndani ya jengo la SNSA.Kwa msaada wa Patrick makomando wale waliweza kuipata picha ya jengo lilivyo na mjadala ukafanyika namna watakavyoweza kuingia mle ndani na wakakubaliana kuwa na timu mbili moja ikitokea angani na nyingine ikitokea ardhini


“Tutatumia helkopta yetu ambay0 huitumia katika operesheni maalum za usiku kama mnavyojua kwamba


helkopta hii haina mlio hivyo hata pale itakapotua juu ya jengo hawatajua kama kuna helkopta imetua lakini tunahitaji pasiwepo na umeme eneo hilo” akasema kiongozi wa Makomando wa SNSA


“Zari tutawezaje kuuzima umeme eneo hilo? Mathew akauliza


“Tunaweza kuitafuta transfoma ya eneo hilo tukailipua na eneo zima likakosa umeme.Lakini kwa nini tusimuombe Rais awasiliane na uongozi wa shirika la umeme ili umeme ukatwe mahala hapo hadi pale tutakapomaliza operesheni yetu? Akauliza Zari


“Hapana hatuwezi


kumshirikisha katika suala hili.Ruby itafute transoma ya eneo hilo tujue mahala ilipo na tutawatuma watu wetu wakailipue na eneo lote kukosa umeme kabisa”


“Kuna jambo lingine” akasema Patrick


“Wale jamaa wana


jenereta kubwa la akiba ambalo hujiwasha lenyewe kila pale umeme unapokatika hivyo ili mpango huo ukamilike lazima kuhakikisha jenereta hilo nalo linadhibitiwa ili hata umeme ukikatika basi jenereta lisiwake na eneo liendelee kuwa na kiza” akasema Patrick


“That’s a good idea Patrick.Jenereta hilo linatakiwa kuharibiwa kabla umeme haujakatika.Tuelekeze namna ya kufika mahala lilipo jenereta hilo” akasema Mathew


“Nataka tutumie njia rahisi ambayo itamuwezesha mtu wenu kuingia na kuharibu jenereta.Mimi ninafahamika pale na ninaweza kuingia muda wowote niutakao bila matatizo.Nitaongozana na mmoja wa makomando wenu na nitamuelekeza mahala ilipo jenereta.Akishaingia mle ndani hakuna atakayemtilia shaka kwani ataonekana aidha ni msanii kwa sababu kuna shughuli za kurekodi hufanyika hata usiku au ataonekana ni mmoja wa wafanyakazi na ataelekea moja kwa moja lilipo jenereta ambalo huwa liko mbali kidogo na jengo atamaliza kazi halafu atawasubiri wenzake” akasema Patrick


“Hilo ni wazo zuri sana na kwa kuwa wewe unaweza ukaingia pale ndani bila matatizo nashauri uende na makomando wanne ambao watawasafishia njia wenzao watakaotumia njia ya ardhini na kuhakikisha hawakutani na kikwazo chochote.Can you do that?Mathew akauliza


“Yes I can” akajibu Patrick wakajadiliana namna ya kufanya halafu mpango mzima wa namna watakavyoingia ukajadiliwa upya. “Ninakwenda na


Makomando” akasema Nawal


“Hapana Nawal utabaki hapa makomando watakwenda wenyewe” akasema Mathew


“Nataka nikajielekeze kumuokoa Ziro.Yawezekana makomando wakakabiliana na upinzani mkali na wakajikuya wakijisahau kumuokoa


Ziro,mimi hilo ndilo litakuwa lengo langu kwani huyo mtu ni muhimu mno” akasema Nawal


“Hilo niwazo zuri.Jiandae pia nawe uelekee huko na kuhakikisha Ziro anakuwa salama tunamuhitaji sana” akasema Mathew na makomando wanne wakaondoka na


Patrick,wengine sita wakafuatia nyuma yao na wengine ambao walitakiwa kupita juu wakaisubiri helkopta yao iwasili ili nao wondoke.


*****************


Akiwa njiani akirejea ofisini kwake Paul alimpigia simu John msaidizi wake “John kuna tatizo kubwa ambalo tunatakiwa kulishughulikia usiku huu” “Tatizo gani Paul?


“Kuna mtu anayetoa taarifa zetu kwa hawa jamaa.Kitendo cha kuwakosa watu wote wa SNSA usiku huu kinaonyesha wazi walipata taarifa ya ujio wetu na wakajificha.Mipango yetu imekiwa inashindwa kufanikiwa kwa sababu ya huyo mtu ambaye lazima tumtafute tumjue ni nani” “Hata mimi ninahisi hivyo.Tutatumia njia gani kumpata?akauliza John


“Tutakusanya simu za watu wote na kuzifanyia uchunguzi”


“Nilianze zoezi hilo sasa hivi? John akauliza


“Hapana nisubiri ninakuja hapo tutalifanya zoezi hili kwa pamoja.Kuna mtu yeyote ambaye unaweza ukamuhisi?akauliza Paul na John akatafakari kidogo na kusema


“Sina uhakika mkubwa Paul lakini unakumbuka tuliwahi kumtumia Yule mwanadada Ilwazi kumfuata Mathew Japan na kumrejesha nyumbani.Baada ya Mathew kurejea hapa nchini Ilwazi alijitahidi sana kujiweka karibu naye na ndiye aliyetusaidia kupata alama za vidole za Mathew zilizotusaidia kufungua kasiki la Mathew na kuweka ule unga wa kulevya”


“Unahisi Ilwazi anaweza akawa ndiye anayetoa taarifa zetu? Paul akauliza


“Ndiyo maana nikasema kwamba sina uhakika kama ni yeye anayeweza akafanya kitu kama hicho lakini kila kitu kinawezekana.Ni yeye ambaye aliwahi kuwa karibu na Mathew Mulumbi na yawezekana katika ukaribu ule akajikuta akisahau kama yuko kazini akampenda Mathew na anatumia kila njia kumsaidia” akasema John


“Siwezi kukataa John kwani hilo pia linawezekana.Hebu jaribu kuzungumza naye na umueleze kwamba kuna mtu anauza taarifa zetu na leo hii lazima apatikane kama ni yeye lazima atastuka sana na atachanganyikiwa”akasema Paul na kukata simu


John baada ya kuzungumza na Paul akatoka katika ofisi yake na moja kwa moja akaelekea katika sehemu ya mapumziko akamkuta Ilwazi na kumtaka wazungumze kidogo


“Ilwazi kuna jambo limetokea usiku huu.Misheni ya kuvamia SNSA imeshindwa kufanikiwa.Tunahisi kuna mtu miongoni mwetu ambaye anashirikiana na hawa jamaa akina Mathew Mulumbi na anawapa taarifa zetu.Tunataka kuchunguza na kumfahamu mtu huyo.Baadaye tutakuomba utusaidie kufanya uchunguzi wa nani ambaye unahisi anaweza kuwa anahusika katika kutoa taarifa zetu” akasema John


“Ni nani ambaye hajui hatari inayotukabili na akafanya jambo kama hilo? Huyu lazima asakwe kwa kila namna na akipatikana apewe adhabu kali ili liwe fundisho kubwa kwa wengine” akasema Ilwazi


“Hicho ndicho tunachotaka kukifanya” akasema John


“Nini unataka nikifanye kumsaka huyo mtu?


“Tutakuelekeza baadae kwa sasa endelea kufanya uchunguzi kimya kimya”akasema John na kuondoka


“Tayari


nimegundulika.Kitendo cha John kunifuata na kunipa taarifa hizi kinaonyesha wazi kwamba tayari wamekwisha anza kuwa na wasi wasi na mimi na wananichunguza.Sitakiwi kundelea kuwepo hapa natakiwa kuumaliza huu mchezo leo” akawaza Ilwazi halafu akaenda kukaa na wenzake akayasoma mazingira baada ya dakika chache akatoka akaelekea maliwato.Mara tu baada ya kuingia chooni akavuta maji halafu akafungua dirisha akachungulia nje na kuliona bomba la maji akapenya dirishani na kulikamata lile bomba akashuka nalo hadi katika vyoo vya ghorofa ya chini akafungua moja ya dirisha la choo akaingia,hakukuwa na mtu yeyote akatoka mle chooni akaenda katika sehemu kulikojificha akapiga simu kwa akina Ruby halafu akaingiza kirusi katika simu yake kisha akarejea ghorofa ya juu kujumuika na wenzake.


Dakika chache baadaye Paul akarejea na kuwakusanya wote katika chumba cha mikutano


“Nina machache ya kuzungumza nanyi” akasema Paul


“Usiku huu wa leo tulikuwa na misheni ya muhimu sana ambayo kama ingefanikiwa tungempata mtu ambaye anafahamu mahala aliko Mathew Mulumbi na wenzake.Kwa bahati mbaya misheni hiyo haikuweza kufanikiwa kwani tumekuta jengo la SNSA likiwa tupu hakuna hata mtu mmoja kitu ambacho si cha kawaida.Baada ya sisi kuondoka mahala hapo nilituma tena watu kwenda kuchunguza na wakakuta shughuli zinaendelea kama kawaida.Hii inaonyesha watu wale walifahamu kama tunakwenda mahala pale na wakajificha.Walipataje taarifa zetu hiyo ndiyo sababu tuko hapa” akanyamaza na kuwatazama wenzake


“Lazima yupo mtu miongoni mwetu anayetoa siri zetu ndiyo maana mipango yetu inashindwa kufanikiwa.Kila tunapopanga jambo linashindwa kufanikiwa kutokana na hawa jamaa kupata taarifa zetu haraka.Leo lazima tumjue mtu anayeuza taarifa zetu hivyo kuanzia sasa nataka watu wote msalimishe simu zenu tukazichunguze kujua nani anayetusaliti kwa kutoa taarifa zetu.Hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kutoka humu ndani hadi zoezi litakapokamilika” akasema Paul na simu zote zikakusanywa.Katika mlango wa kutokea ndani ya kile chumba walisimama watu watatu wakiwa na bunduki kuhakikisha hakuna mtu atakayetoka


Simu zote baada ya kuchukuliwa zikapeleka katika ofisi ya Paul kwa ajili ya kuchunguzwa.


“Nataka tuanze na simu ya


Ilwazi” akaelekeza Paul na Ilwazi akaitwa akaonyesha simu yake ikaunganishwa na kompyuta na sekunde chache baada ya kuunganishwa kukasikika mlio katika kompyuta na kitu Fulani kikajitokeza.Sekunde chache kukatokea tena kitu cha kushangaza mafaili yaliyomo ndani ya kompyuta yakaanza kufutwa kwa kasi kubwa kila mtu ndani ya kile chumba akachanganyikiwa hakuna aliyejua nini kimetokea.


“Nini kimetokea? Akauliza Paul baada ya kompyuta nyingine pia kuanza kutoa mlio huku mafaili yakifutwa.


“Hatujui mkuu nini kimetokea” akasema jamaa mmoja huku akijaribu kubonyeza vitufe katika kompyuta yake kujaribu kusimamisha kile kilichokuwa kinaendelea bila mafanikio.


“Please stop this now ! akafoka Paul na juhudi za kuzuia kile kilichokuwa kimetokea zikaendelea


“Mkuu hiki ni kirusi na tayari kimekwisha sambaa katika mfumo wetu kukidhibiti kwa haraka itakuwa vigumu”akasema mmoja wa wale jamaa


“Kirusi kimeingiaje katika mfumo wetu? Akauliza Paul kwa ukali


“Hili tatizo limeanza baada ya simu ya Ilwazi


kuunganishwa na kompyuta


hii”


“Call Ilwazi here now ! akafoka Paul na Ilwazi akaitwa akapelekwa katika ofisi ya Paul


“What have you done? Akauliza Paul kwa hasira


“Nothing ! akajibu Ilwazi


“Ilwazi nakuuliza nini umefanya? Akauliza Paul


“Niambieni nini kimetokea? Akauliza Ilwazi


“Kuna kirusi kimeingia katika mfumo wetu na inasadikiwa kimetokea katika simu yako” akasema mmoja wa wataalamu wa kompyuta waliokuwa wanahangaika kudhibiti kirusi kile


“I have no idea” akasema Ilwazi


“Ilwazi naomba unieleze ukweli kuhusu kirusi hiki ama sivyo nitakuua ! akasema Paul


“Sifahamu chochote”


akajibu Ilwazi na Paul akainua bastola yake akamnyooshea


“Nakupa sekunde


thelathini unieleze kuhusu kirusi hiki katika simu yako kimetoka wapi? Akauliza Paul mkono wake ukitetemeka kwa hasira


“Sifahamu chochote Paul kuhusiana na hicho kirusi” akasema Ilwazi na Paul akataka kusema kitu lakini umeme ukakatika.Mle ndani ya ofisi ya Paul kulikuwa na mwangaza mdogo uliotoka katika kompyuta zilizokuwa zinaendelea kuwaka kwa kutumia umeme wa betri.Kawaida umeme ukikatika ndani ya sekunde tano jenereta hujiwasha lakini ilielekea sekunde ya thelathini bila jenereta kuwaka


“What’s going on? Akasema Paul na kufungua mlango wa ofisi yake na kusema kwa sauti kubwa


“Tazameni jenereta lina tatizo gani ! 




Mara tu Paul alipogeuka na kuufunga mlango wa ofisi yake ukasikika mlio wa risasi.Mlio ule wa risasi ilikuwa ni ishara kwa Ilwazi kwamba tayari akina Mathew wameingia.Kama kimbunga akazunguka na teke la mguu wa kulia likakipiga kiganja cha mkono wa Paul uliokuwa na bastola ikaruka na wakati huo huo mguu wa kushoto ukatua


katika shingo ya Paul na kumsukuma hadi ukutani.Kwa kutumia mwangaza mdogo wa kompyuta Ilwazi aliiona bastola ya Paul ilipoangukia akataka kuifuata lakini Paul akawa mwepesi akamrukia teke zito lililompata Ilwazi kisawa sawa akaanguka chini akamsogelea na kumtandika tena teke lingine zito la tumbo Ilwazi akagugumia kwa maumivu.Paul akaiendea bastola yake akainama ili kuiokota lakini akapigwa na kiti akageuka haraka na kukiokota kiti kile akakirusha kwa Ilwazi halafu akaiokota ile bastola na kumnyooshea


“Drop the gun ! sauti ya mwanamke ikamuamuru Paul


“Drop the gun slowly and put your hands behind your head ! sauti ile ikamuamuru tena.Kulikuwa na mwanamke katika mlango wa ofisi ya Paul akiwa na bunduki na miwani ya kumuwezesha kuona kwenye giza.


Taratibu Paul akabonyea


chini ili aiweke chini bastola kama alivyoamriwa na mara tu alipoiweka chini kwa kasi ya ajabu akatumia mkono wa kulia kuchomoa bastola nyingine kiunoni lakini kabla hajaitumia tayari Nawal alikwikiona kitendo kile na kuizinga bunduki yake risasi mbili zikatoka na kuupiga mkono wa Paul uliokuwa na bastola akaanguka chini.Kwa haraka akamfuata pale chini na kuipiga teke bastola ile ikaenda mbali na Ilwazi aliyekuwa amelala chini akainuka taratibu.Nawal akageuka haraka na kumnyooshea bunduki


“Don’t shoot I’m Ilwazi” akajitambulisha na Nawal akayatazama yalemavazi akagundua ni Ziro


“Amekuumiza huyu jamaa? Akauliza Nawal


“Ameniumiza


kidogo.Ahsanteni mmefika kwa wakati muafaka kabisa kwani kama mngechelewa tayari walikwisha nibaini”


“This is not over Ilwazi !! akasema Paul kwa ukali uliochanganyika na maumivu na mara wakaingia makomando wawili mle ndani ya ofisi ya Paul Nawal


akawaelekeza kumfunga pingu Paul


Kiongozi wa makomando


naye akaingia ndani ya ofisi ya Paul


“Huyu ndiye Ziro mwanamke ambaye tulikuja kumuokoa” Nawal akamwambia


“Naitwa Ilwazi.Huyu jamaa hapa ndiye kiongozi wa kundi hili.Nimeingiza kirusi katika mfumo wao na nimechukua taarifa zao zote nimehamishia katika hifadhi yangu.Kwa sasa ninachohitaji ni kuonana na Mathew Mulumbi.Nataka nikazungumze naye” akasema


Ilwazi.


Mkuu wa kikundi kile cha makomando akaelekeza Paul apelekwe katika helkopta


halafu akawasiliana na akina Mathew


“Misheni tumeikamilisha na tumelidhibiti jengo,tumewastukiza bila wao kutegemea ndiyo maana hatujapata upinzani mkubwa.Wameuawa watu kumi na moja na wengine wamewekwa chini ya ulinzi vile vile tumempata kiongozi wao ambaye amejeruhiwa kwa risasi na analetwa hapo” akasema komando mkuu


“Vipi kuhusu Ziro mmefanikiwa kumpata? Akauliza Ruby


“Tumempata yuko salama japo ameumizwa kidogo” akajibu komando mkuu


“Kwa sasa waleteni hapa


Ziro na huyo kiongozi wa Black Mafia,makomando wengine


endeleeni kulidhibiti jengo hilo hadi mtakapopata maelekezo mengine” akasema Ruby


Simu za wale jamaa ambazo zilikuwa zimekusanywa kwa ajili ya uchunguzi zote zikachukuliwa na vitu vingine kama kompyuta ya Paul na simu yake halafu Ilwazi akapelekwa katika helkopta iliyokuwa juu ya jengo lile akaondoka


kuelekea katika kambi ya akina


Mathew


Wakati upekuzi ukiendelea katika ghorofa ya juu ya jengo lile ambayo ilikuwa inatumiwa na Black Mafia,Ghorofa ya tatu kulikokuwa na ofisi ya meneja wa kampuni ile tawi la Tanzania Lethabo Dlamimi,Patrick na makomando wawili walikuwa wanafanya upekuzi na kuchukua vitu mbali kwa ajili ya kwenda kuvifanyia uchunguzi wakavipakia katika gari la Patrick na kuondoka kurejea katika kambi ya akina Mathew




*****************


Ilikuwa ni furaha kubwa kwa Mathew na wenzake baadaya kupokea taarifa kwamba jengo lililokuwa linatumiwa na kikundi cha Black Mafia limedhibitiwa na kiongozi wao kukamatwa.


“Tujipongeze kwa kazi kubwa tuliyoifanya hadi kufanikisha jambo hili” akasema Zari


“Muda wa kupongezana bado kwani kazi haijamalizika.Tumeidhibiti ofisi ya kundi hatari kabisa lililofanya mauaji na mambo mengi mabaya hapa nchini kwetu lakini bado tuna kazi ya kumtafuta kiongozi wao ni nani hapa nchini? Tukilifanikisha hilo na kumkamata kiongozi mkuu wa mtandao wa biashara za kulevya hapa nchini basi tutapongezana lakini kwa sasa bado tuko katikati ya


mapambano”akasema Mathew




“Kwa kuwa tayari kiongozi wao amekamatwa na analetwa hapa ninashauri tuwaondoe makomando wetu mahala pale na tuombe msaada kutoka kwa Rais wapelekwe askari wakalinde jengo hilo na asiruhusiwe mtu yeyote kuingia ndani hadi pale maelekezo yatakapotolewa” akasema Zari


“Hilo ni wazo zuri.Ruby mpigie simu muombe atume askari polisi mahala hapo wakalinde hadi hapo tutakapokuwa tumekamilisha uchunguzi wetu” akasema Mathew


“Ni vipi akiuliza sababu za kuvamiwa kwa jengo hilo? “Mweleze kwa kifupi kwamba ni mwendelezo wa misheni yetu ili ajue kwamba hata kama akituzunguka lakini sisi hatukati tamaa,njia ikifunga kulia tutapita kushoto,akizuia kushoto tutapia kulia.Hatuzuiliki ! akasema Mathew na Ruby akampigia simu Rais


“Ruby ! akasema Rais Festus


“Mheshimiwa Rais samahani kwa usumbufu” “Bila samahani


Ruby.Unasemaje? Akauliza Rais Festus


“Mheshimiwa Rais tunaomba msaada wako” “Ndiyo.Nini mnahitaji?


“Tunaomba msaada wa


askari kulinda jengo linalotumiwa na kampuni ya kutengeneza filamu ya African pictures”


“Kuna nini katika jengo hilo?


“Ni katika mwendelezo wa misheni yetu mheshimiwa Rais.Tutakupa taarifa kamili pale tutakapokuwa tumekamilisha kila kitu lakini kwa usiku huu tunaomba jengo hilo lilindwe na askari polisi na asiruhusiwe mtu yeyote kuingia ndani ya jengo hilo hadi pale tutakapotoa maelekezo”


“Ruby nini hasa ambacho kimetokea katika jengo hilo?


“Mheshimiwa Rais ninaomba nisikueleze chochote kwa sasa naomba utuvumilie hadi pale tutakapokuwa tumefanikisha misheni yetu.Mheshimiwa Rais kwa sasa jengo hilo liko chini ya udhibiti wa makomando wetu na ndani kuna watu kadhaa wanashikiliwa tunaomba


wachukuliwe wakahifadhiwe kituo cha polisi vile vile kuna maiti kadhaa tunaomba zikahifadhiwe hospitali hadi hapo tutakapokuwa tumekamilisha misheni yetu” akasema Ruby


“Ruby nitatekeleza ombi lenu lakini ninataka asubuhi nipate taarifa kamili ya kile kilichotokea hapo na kusababisha watu hao kuuawa na wengine kukamatwa.Lazima sababu ya kukamatwa kwao ijulikane” akasema Rais


“Tutakujulisha kila kitu mheshimiwa Rais tunaomba muda kidogo” akasema Ruby


“Vipi Mathew


anaendeleaje? Akauliza Rais Festus


“Kwa sasa anaendelea vizuri japokuwa bado amepumzika” “Good.Usisahau nataka taarifa kesho asubuhi” akasema Rais Festus na kukata simu


Zari akampigia simu komando mkuu na kumjulisha kwamba polisi watafika pale muda si mrefu watawakabidhi jengo hilo pamoja na maiti na watu wote waliokamatwa kisha wao wataondoka mara moja mahala hapo


*****************


Helkopta ya makomando


ilitua katika sehemu ya mbele ya nyumba ile walimokuwamo akina Mathew.Akashushwa Ilwazi, Nawal akamshika mkono na kumuongoza kuelekea ndani halafu akashushwa Paul aliyekuwa amefungwa mikono yake kwa nyuma akiwa amechafuka damu,huku akigugumia kwa maumivu makali.


“Hongera sana Nawal kwa kazi kubwa na nzuri” akasema


Ruby aliyewapokea Nawal na Ilwazi


“Ilwazi pole sana.Mimi ndiye Ruby ambaye umekuwa ukinitumia ujumbe mbali mbali wa kunionya .Karibu sana hapa ndipo mahala tulipoweka kambi yetu”


“Ahsante sana Ruby nimefurahi kuonana nawe,tutazungmza mengi lakini kwanza nataka kuonana na Mathew Mulumbi”akasema Ilwazi wakamuongoza hadi katika chumba alimokuwamo Mathew.Mathew akastuka sana baada ya kumuona Ilwazi mwanamke ambaye amekuwa akiwatumia ujumbe mbali mbali kuwapa taarifa za mipango ya Black Mafia


“Sindi ?!! akasema


Mathew kwa mshangao


“Mathew Mulumbi ! akasema Sindi na kumfuata Mathew pale kitandani akapiga magoti pembeni ya kitanda


“Mathew Mulumbi pole sana ! akasema Sindi


“Sindi ni wewe kweli au niko ndotoni”


“Ni mimi” akajibu Sindi


“Imetokeaje hii?Sikuwahi kuota hata mara moja kama jambo hili linaweza likatokea.Sikuwahi kuota kama Sindi….oh my God nashindwa niseme nini” akasema Mathew


“Relax Mathew Mulumbi” akasema Nawal na Sindi akasimama akawageukia akina Nawal


“Naitwa Sindisiwe au Sindi kwa kifupi”


“Hatukujua jina lako hivyo tukakuita Ziro” akasema Ruby


“Ni Mathew pekee


aliyekuwa ananifahamu lakini naye hakujua kama ni mimi niliyekuwa nawasiliana na Ruby”akasema Sindi


“Kitu pekee ambacho tulikifahamu ni kwamba mtu huyo tuliyempa jina la Ziro lazima atakuwa na mahusiano na sisi na anatufahamu vyema ndiyo maana anatusaidia.Tulijua lazima itatokea siku tutamfahamu na sasa uko mbele yetu.Ahsante sana kwa msaada wako mkubwa” akasema Mathew


“Mimi ni msanii wa


kuigiza lakini kazi yangu ni ujasusi”akasema Sindi na wote wakabaki wanamtazama kila mmoja akiwaza lake


“Ninafanya kazi katika idara ya siri ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya Afrika kusini.Idara hii ya siri iliundwa baada ya idara zilizokuwepo awali kuonekana kushindwa kudhibiti biashara hiyo ambayo imekuwa ikipanuka kila uchao.Baada ya idara hiyo ya siri kuundwa tulianza kuwafuatilia wafanya biashara wakubwa wa dawa za


kulevya nchini Afrika kusini na mmoja wao ambaye mimi nilipewa kazi ya kumchunguza ni bilionea Bandile Dlamini” Akasema Sindi na kunyamaza kidogo


“Bandile Dlamini anamiliki biashara kubwa kubwa katika miji mbali mbali nchini Afrika kusini lakini chanzo cha utajiri wake ni biashara ya dawa za kulevya.Haikuwa rahisi kumchunguza lakini


nilijitahidi na katika uchunguzi wangu niligundua kwamba Bandile ana mashirikiano na kampuni tatu zilizoko Afrika kusini ambazo mmiliki wake anaitwa Peniela Mwaulaya” akasema Sindi na sura ya Mathew ikabadilika


“Umesema Peniela


Mwaulaya? Akauliza Mathew


“Ndiyo.Nilitegemea kuuona mstuko huo usoni pako pale utakapolisikia jina hilo likitajwa”akasema Sindi


“Lazima nistuke kwa sababu Peniela alikuwa mke wangu japo kwa sasa tumekwisha achana lakini ndiye mama wa watoto wangu na utajiri wake ameupata kihalali.Nimeshangaa kusikia kwamba ana mashirikiano na hawa watu wa dawa za kulevya” akasema Mathew


“Kuna jambo ambalo nataka nikueleze Mathew Mulumbi najua hutapendezwa


nalo lakini lazima nikwambie”




“Sema usihofu


Sindi”akasema Mathew


“Kwa sasa Peniela na Bandile wana mahusiano ya kimapenzi” akasema Sindi


“Hilo si jambo la kunishangaza kwani tayari mimi na yeye tumekwisha achana na siwezi kumpangia nani awe naye katika maisha yake kama ameamua kuwa na mahusiano na huyo bilionea wa dawa za kulevya mimi hainihusu.Endelea Sindi” Mathew akasema


“Baada ya kuanzisha mahusiano na Peniela,Bandile anatumia kampuni hizo za Peniela kutakatishia fedha zake chafu za dawa za kulevya.Nilimfuata Peniela jijini Paris Ufaransa anakoishi nikamweleza kuhusu Bandile akanielewa na akaahidi kunisaidia.Aliniambia kwamba Bandile na wenzake wana mpango wa kuanzisha kampuni ya kutengeneza filamu itakayojishughulisha na utengenezaji wa filamu ndani ya bara la Afrika pekee itakayojulikana kama African pictures.Akaniambia kwamba ataniunganisha na kampuni hiyo kama mwigizaji na wakati huo huo nikiendelea na kazi yangu ya uchunguzi kwani wale jamaa walikuwa na mipango ya kuitumia kampuni hiyo katika shughuli zao za kusambaza dawa za kulevya barani Afrika na kwingineko duniani”Sindi akanyamaza kidogo


“Peniela alifanya kama alivyoniahidi kwani ni kweli kampuni hiyo ilianzishwa na mimi nikawa mmoja wa waigizaji wa kwanza kabisa kuajiriwa na kampuni hiyo.Kabla ya kuajiriwa walinifanyia usaili na wakakiona kipaji changu wakasema ninafaa na hapo ndipo wakaniambia kwamba nitacheza kama muhusika mkuu katika filamu inaitwa before I die iliyoandikwa na mwandishi wa kutoka hapa hapa Tanzania anaitwa Patrick .Wakati tukiendelea kurekodi vipande vya filamu hiyo,yalifanyika mabadiliko katika hadithi na kuonyesha kwamba kuna baadhi ya vipande tutakwenda kuvirekodi nchini Japan.Nilihoji sababu ya hadithi ile kubadilika na ndipo nilipoitwa na kuelezwa kwamba hadithi imebadilika kutokana na kazi maalum ambayo natakiwa kwenda kuifanya nchini Japan.Nilihoji


ni kazi gani hiyo nikaelezwa kwamba kuna mtu natakiwa kumfuata huko na kuhakikisha ninamshawishi kurejea Tanzania nikaambiwa kwamba mtu huyo anaitwa Mathew Mulumbi.Nilistuka kidogo kwa sababu katika maelezo ya Peniela alinieleza kwamba aliwahi kuwa na mahusiano na Mathew Mulumbi.Wale jamaa wakanieleza ukweli kwamba kutokana na umahiri niliouonyesha katika uigizaji wanadhani ninaweza kufaa kuajiriwa katika kundi linaitwa


Black Mafia.Niliuliza Black Mafia ni kitu gani ndipo wakanieleza kazi zake na wakanitisha kwamba kwa kuwa tayari nimefahamu siri ya kampuni ile ya filamu basi sina uchaguzi zaidi ya kukubali kufanya kile watakachonituma nikifanye kwa malipo ya mara tatu zaidi ya fedha ambayo nilikuwa ninalipwa.Hamuwezi amini ndugu zangu lakini malipo yangu kwa mwezi mmoja ni shilingi milioni mia moja na hamsini.Hawa jamaa ni matajiri wakubwa wana pesa kama mchanga” akanyamaza tena


“Nilianza kushirikiana na


Black Mafia nikiwa katika kitengo cha mawasiliano na kabla ya kwenda Japan nikawasiliana na Peniela nikamjulisha kuhusu mpango ule walionao dhidi ya Mathew Mulumbi na akanisisitiza kwamba kwa namna yoyote ile nihakikishe mipango yao haifanikiwi.Kwa kuwa Peniela ndiye aliyenisaidia nikaweza kuingia hadi ndani ya Black Mafia na kuwachunguza bila wao kunifahamu nilikubali kuifanya kazi hiyo ya kuhakikisha kwamba kwa namna yoyote ile Mathew Mulumbi haiingii katika matatizo kama wale jamaa walivyokuwa wanapanga” Sindi akameza mate kulainisha koo halafu akaendelea


“Mipango ilifanywa na tukaelekea Japan katika kisiwa cha Okinawa ambako ndiko ilifahamika Mathew alikuwa amekwenda mapumzikoni” akasema Sindi na Mathew akamkatisha


“Kwa hiyo kukutana kwetu kule Japan ulikuwa ni mpango maalum? Mathew akauliza




“Ndiyo ulikuwa ni mpango maalum.Hata maafisa wale wa uhamiaji waliokufuata nyumbani ulikokuwa ukiishi ulikuwa ni mpango umetengenezwa na hata kama ungejaribu kuomba kuongeza tena muda wa kuendelea kuishi usingekubaliwa lengo ni ili urejee nyumbani


Tanzania ambako walikuwa wameandaa mpango wa kukuua.Mpango ulifanikiwa na ukarejea nyumbani na kama walivyokuwa wametegemea baada ya kupata taarifa za Gosu Gosu ukaelekea Arusha ambako nako wana watu wao na mipango ya kukuua ikafanyika lakini haikufanikiwa.Uliporejea Dar es salaam kama unakumbuka nilikufuata nyumbani kwako na kama utakumbuka uliniuliza namna nilivyofahamu mahala unakoishi nikakudanganya kwamba nimeelekezwa na mtu kumbe ulikuwa ni mpango maalum wa maandalizi ya kukutengenezea kesi ya dawa za kulevya na mauaji lengo likiwa ni ili ufungwe kifungo kirefu gerezani.Hukulijua hilo lakini ni mimi niliyechukua alama zako za vidole kwa ajili ya kufungulia kasiki lako na kupiga picha kadhaa za chumba chako ambazo zilitumika kuandaa mpango wa kukupandikizia dawa za kulevya” akasema Sindi na kunyamaza baada ya sura ya Mathew kubadilika


“Mathew nilikuwa kazini na kazi yangu ilikuwa kuhakikisha ninafanya maandalizi ya mpango mkubwa wa kupandikiza dawa za kulevya nyumbani kwako na baada ya kukamilisha wakaendelea na mpango huo hadi ulipokamatwa .Baada ya wewe kukamatwa walianza kutafutwa pia wale ambao ulikuwa unashirikiana nao na wa kwanza aliyekuwa anatafutwa ni Ruby na kwa kuwa nilikuwa na mawasiliano yake nikamtumia ujumbe wa kumuonya aondoke mahala alipokuwa”


“Niliupata ujumbe huo na ujumbe mwingine wote ulioendelea kunitumia” akasema Ruby


“Sindi ahsante sana kwa maelezo hayo uliyotupa ambayo yametufumbua macho na sasa tumepata picha pana ya jambo hili.Yale uliyotueleza tukiunganisha na yale ambayo tunayafahamu tunapata karibu asilimia tisini ya misheni yetu imekamilika bado asilimia kumi pekee tukamilishe misheni hii.Tunachohitaji kufahamu nani kiongozi wa kundi hili hapa Tanzania? Mathew akauliza


“Mathew kwa hilo hata mimi sifahamu kwani mambo yao wanayafanya kwa siri kubwa na nilikuwa naendelea kuchunguza ndipo likatokea hili lililotokea leo”akajibu Sindi


“Hongera sana Sindi kwa kazi kubwa uliyoifanya umetusaidia sana tukafika hapa tulipofika” akasema Mathew na kumtaka Ruby amweleze Sindi mahala walipokuwa wamefikia katika uchunguzi wao.


“Baada ya kujua tayari wamenigundua nilipandikiza kirusi katika mfumo wao ambacho kimechukua mafaili yao yote na kuyatuma kwangu hivyo tunaweza kupitia mafaili hayo na kupata picha pana zaidi ya namna wanavyofanya biashara zao namna mzigo unavyoingia apa nchini unavyosambazwa na kwenda nje ya nchi.Taarifa hizo zote tayari tunazo.Kuhusu kiongozi au viongozi wao sifahamu ni akina nani.Paul ndiye anayefahamu kila kitu na kwa kuwa tunaye hapa kwa nini asitueleze nani kiongozi wao? Akauliza Sindi


“Mleteni hapa ndani aseme kila kitu” akasema Mathew na Paul akaletwa “Nawal uwanja ni wako


hakikisha anasema kila kitu” akasema Mathew na Ruby akaichukua simu ya Paul akaanza kuifanyia uchunguzi


“Paul una risasi mbili ndani ya mkono wako nafahamu maumivu ya risasi ikiwa mwilini na ninakuona unavyoteseka.Tutakusaidia kukupatia matibabu lakini ni pale tu ambapo utatueleza ukweli.Nataka kufahamu nani kiongozi wenu hapa Tanzania? Akauliza Nawal lakini Paul hakufungua mdomo wake kusema chochote


“Paul ni ukweli pekee utakaokusaidia kwa sasa.Hauna ujanja kwani tayari wenzako wote wamekamatwa na wengine wameuawa.Ofisi yenu iko katika mikono yetu kwa sasa na tunaendelea kuwachunguza.Taarifa zenu zote tunazo.Nataka tuokoe muda tueleze nani kiongozi wenu hapa Tanzania? Akauliza Nawal na Paul akaendelea kuufumba mdomo wake.Nawal akagandamiza mahala alipokuwa amepigwa risasi Paul akatoa kilio kwa maumivu makali aliyoyapata.


“Tueleze ukweli na tukuondolee maumivu haya Paul”


“Kill..kil..ll..meeee ! akasema Paul na Nawal akagandamiza tena mahala pale penye risasi Paul akaendelea kulia


“Kuna kitu nimekipata” akasema Ruby


“Huyu jamaa


amewasiliana na watu wawili mara ya mwisho ambao majina yao yameandikwa mkuu na lingine John.Hawa ni watu ambao amewasiliana nao usiku huu” akasema Ruby


“Umewasiliana na mtu ambaye umemuandika mkuu ni nani huyo? Akauliza Nawal lakini bado Paul aliendelea kukaa kimya.Nawal


akaendelea na zoezi la kumuongezea Paul maumivu makali


“Oh my God ! akasema Ruby kwa mshangao


“Kuna nini Ruby?Mathew


akauliza


“Namba hii yenye jina la mkuu imesajliwa kwa jina la Kasiano Muyenzi ambaye ndiye kiongozi wa kanisa la injili ya wokovu” akasema Ruby na wote mle ndani wakabaki wanatazamana walipatwa na mshangao mkubwa


“Kama vile tulivyokuwa


tunahisi kuhusu kanisa la injili ya wokovu sasa mambo yameanza kujidhihirisha yenyewe.Kama huyu jamaa ambaye ni mkuu wa kikundi cha Black Mafia amekuwa akiwasiliana na Kasiano basi kuna mahusiano kati yao.Nawal endelea anatakiwa aeleze mahusiano yake na Kasiano.Ruby endelea kupekua simu yake tufahamu zaidi.Angalia kama ana mawasiliano yoyote na Bella” akasema Mathew na Nawal akachukua koleo dogo na kumuita komando mmoja akamshika barabara na kuupanua mdomo wake Nawal akalishika jino moja na kutumia nguvu akaling’oa.Paul akapiga kelele kubwa huku damu nyingi ikimtoka mdomoni.


“Sema kila kitu Paul kwani mambo haya ndiyo kwanza yameanza” akasema Nawal lakini bado Paul aliendelea kulia huku damu ikimwagika mdomoni.


“Tunaendelea” akasema Nawal akang’oa jino lingine.Paul aliyekuwa amefungwa kitini akaruka ruka na kiti kwa maumivu makali aliyoyapata.


“Huyu anaonekana mbishi anajifanya amezoea maumivu.Tunaomba tuondoke naye tupe dakika chache atazungumza” akasema komando mkuu na Mathew akatikisa kichwa ishara ya kukubali na makomando wakamchukua Paul wakatoka naye mle ndani


“Naona ni kama muujiza namna mambo yalivyokuja kuunganika huku mwishoni” akasema Zari


“Mathew ulikuwa sahihi pale ulipoibua swali kuhusu Kasiano kuhusika katika vifo vya mchungaji Adam na Lucas”akasema Ruby “Kutokana na mtiririko wa matukio ulivyo niliamini lazima kasiano ama kanisa lake wana mahusiano na hiki kikundi ndiyo maana nikaelekeza kwamba achunguzwe ili tuujue ukweli na leo Mungu ametusaidia tumeweza kuufahamu ukweli.Kasiano na …” akanyamaza Mathew baada ya mlango kufunguliwa akaingia Patrick akiwa amebeba kompyuta alizozitoa katika ofisi ya Lethabo


Dlamini.Alipatwa na mstuko mkubwa sana pale alipomkuta Sindi mle chumbani


“Ilwazi?! Akasema kwa mshangao


“Hello patrick! Akasema Sindi


“Mnafahamiana? Mathew


akauliza


“Ndiyo ninamfahamu


Ilwazi ndiye anayecheza kama Latoya muhusika mkuu katika


filamu ya before I die.Nimeshangaa sana kumkuta hapa”


“Jina langu ni Sindisiwe na si Ilwazi kama mlivyofahamu.Mimi ni mpelelezi na nilikuwa katika kampuni ile kwa kazi maalum na hawa unaowaona humu ndani ni washirika wangu”


“Jesus Christ ! akasema Patrick


“Next time be very carefull with pretty women ! Mathew akasema.Patrick akawaeleza kuhusu zile kompyuta na vifaa walivyochukua katika ofisi ya Lethabo.


“Kazi nzuri


Patrick.Umejitolea kuifanya kazi ya hatari lakini imesaidia sana katika misheni hii.Hatutakusahau kwa msaada huu mkubwa ulioutoa” akasema Mathew


“Lazima nisaidie kwa kila namna niwezavyo kwani nimejikuta nikitumika bila kujua na hilo limeniumiza sana.Bella amekuwa akinitumia kwa faida yake na mbaya zaidi akanitumia katika sehemu mbaya kabisa kusimamia maslahi yake yatokanayo na biashara ya dawa za kulevya bila mimi kujua.Siwezi kumsamehe katika hili ndiyo maana nimejitolea kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anakamatwa” akasema Patrick


“Tumefanikiwa kugundua jambo lingine.Paul ambaye ndiye mkuu wa kundi la Black Mafia amekuwa na mawasiliano na nabii mkuu Kasiano Muyenzi wa kanisa la injili ya wokovu.Hili kanisa tumekuwa tukilihisi toka mwanzo kuhusika na mambo machafu na sasa ukweli umeanza kuonekana.Tunaendelea kuchimba zaidi mahusiano ya Paul na Kasiano” akanyamza Mathew baada ya mlango kufunguliwa Paul akaingizwa mle ndani akiwa hatazamiki.Hakuwa na nguo zaidi ya bukta ya ndani na mwili wake wote ulibadilika rangi na kuwa mwekundu kwa kuvuja damu.Mathew akatabasamu


“Hawa ndio wazee wa kazi napenda kufanya kazi na watu wa namna hii.Mambo kama haya alikuwa anayafanya Gosu Gosu” akawaza Mathew huku akitabasamu


“Yuko tayari kuzungumza” Komando mkuu akawajulisha akina Mathew huku akimketisha Paul kitini.


“Anza kuzungumza ! akasema Nawal


“Kasiano…..”akasema Paul na kunyamaza akavuta pumzi ndefu


“Kasiano ni kiongozi wetu” akasema Paul na Mathew akahisi mwili wote unamsisimka.


“Tueleze kila kitu kuhusu shughuli zenu na mambo ambayo mmekuwa mkiyafanya” akasema Mathew na Paul akaanza kuwaeleza kila kitu kuhusu kundi lao la Black Mafia akaeleza mambo ambayo wamekuwa wakiyafanya namna wanavyoingiza dawa za kulevya na kuzisafirisha kwenda nje ya nchi.Akawataja watu wakubwa walioko katika mtandao wao ambao wengine ni viongozi serikalini na wengine wafanya biashara wakubwa.Alieleza namna walivyotengeneza kesi ya Gosu Gosu na namna walivyowaua wale watu wawili na kuwaficha ndani mwa Mathew ili ionekane yeye ndiye aliyehusika na mauaji yale.Paul alieleza mambo mengi hadi alipokamatwa usiku ule.


“Umetupa maelezo mengi ambayo yatatusaidia sana bado kuna kitu kimoja ambacho tunataka kukifahamu.Kasiano anashirikiana na akina nani kuongoza genge la wafanya biashara wa dawa za kulevya hapa nchini?akauliza Mathew “Sifahamu.Mimi kwa kiwango changu cha mwisho ni kwa Kasiano na sifahamu watu wengine wanaoendelea huko mbele japo nafahamu kuna mtu mwingine ambaye ni mkubwa zaidi yake lakini simfahamu mtu huyo” akasema Paul


“Paul tueleze ukweli ama sivyo tutakurejesha tena kwa wale jamaa” akasema Mathew


“Ninasema kweli jamani naomba msinirejeshe kwa wale jamaa.Nimewaeleza ukweli mtupu sijaficha hata kitu kitu kimoja” akasema Paul


“Zari waite madaktari waje wamuhudumie mara moja tutaendelea naye baadaye” akasema Mathew na Paul akatolewa mle chumbani.


“Mmesikia alichokisema Paul.Ni mambo mazito sana” akasema Mathew


“Hapa nilipo nahisi mwili wangu wote unanitetemeka sikutegemea kama tungeweza


kufichua jambo kubwa kama


hili”


“Haikuwa rahisi hapa


tulipofika lakini bado tuna kazi ya kufanya.Tumeambiwa na Paul kwamba kuna mtu ambaye ni mkubwa zaidi ya Kasiano.Kazi tuliyobaki nayo ni kumchunguza Bella jukumu ambalo tumemuachia Patrick” akasema Mathew


“Patrick tumekupa jukumu zito ambalo lazima uhakikishe unalikamilisha ili tuweze kuikamilisha misheni yetu kwa asilimia mia moja.Nina uhakika mkubwa kama Bella ana mahusiano na Black Mafia lazima atakuwa na mahusiano pia na Kasiano na kesho asubuhi baada ya kugundua kile kilichotokea usiku huu lazima watawasiliana na hicho ndicho ambacho tunakihitaji sana.Ndugu zangu sina uhakika bado lakini nina kila sababu ya kuamini kwamba kiongozi wa mtandao wa wafanya biashara wa dawa za kulevya ambaye Paul hamfahamu atakuwa ni Bella lakini lazima kwanza tujiridhishe.Hakuna kulala usiku huu tunaendelea na kazi ya kuchambua taarifa zote ambazo Sindi amezipata kutoka katika kompyuta za black mafia na hadi kufika asubuhi tuwe tayari na taarifa za kutosha kuhusu hawa jamaa” akasema Mathew na Patrick akainuka


“Ninawashukuru sana Mathew Mulumbi na wenzako kwanza kwa kunishirikisha katika mpango huu na kunipa na mimi nafasi ya kuweza kutoa mchango wangu mdogo.Pili ninawashukuru kwa kunifumbua macho kwani nilikuwa natumika bila kujua na siku moja ningeweza kutumbukia shimoni na kupotea lakini ninyi mmenisaidia kufahamu kile kinachoendelea.Ninawashukur u sana na ninawaahidi kufanya


kila niwezalo ili kazi mliyonituma ikamilike” akasema Patrick na kuwaaga akina Mathew akaondoka.


Kama alivyoelekeza


Mathew,hakukuwa na muda wa kupoteza kazi ikaanza mara moja kuchambua taarifa zile walizozipata kutoka katika kompyuta za akina Paul.


“Sikujua kama tunapambana na mtandao mkubwa namna hii.Maelezo aliyoyatoa Paul yameufanya hadi mwili wangu uhisi baridi.Sikutegemea kama mtandao ungekuwa mkubwa kiasi hiki.Hawa jamaa walikuwa wamejizatiti vilivyo ndiyo maana wakafanikiwa kufanya kila walichokitaka.Kwa bahati mbaya hata wateule wa Rais nao ni miongoni mwa watu waliomo katika mtandao huu.Kitu cha kusitisha zaidi ni kiongozi mkubwa wa kiroho kama Kasiano kushiriki katika mambo haramu kama biashara ya dawa za kulevya na mauaji.Hii ni kashfa kubwa sana kuwahi kutokea hapa nchini.Kumekuwa na minong’ono ya chini chini watu wakiwatuhumu baadhi ya watumishi wa Mungu kujihusisha na biashara haramu lakini hakuna aliyewahi kukamatwa akituhumiwa kujihusisha na mambo hayo.Kasiano atakuwa ni kiongozi wa kwanza kukamatwa na hili litakuwa ni doa kubwa sana kwa viongozi wa kiroho” akawaza Mathew “Ninamshukuru sana


Peniela ambaye alimpandikiza Sindi katika mtandao wa hawa jamaa na kwa Sindi sijui nitamshukuruje kwani amefanya kazi kubwa sana kuniokoa na hatari.Sikujua kilichokuwa kinaendelea kumbe nilikuwa katika hatari kubwa.Sikujua kama nilikuwa ninawindwa hadi wakajua kama nilikuwa Okinawa na wakanifuata hadi kule na kama walivyokuwa wamepanga nilifanikiwa kurejea nyumbani na ndipo mipango ya kuniua ilipoanza na hatimaye leo hii tumefikia hatua hii” akaendelea kuwaza Mathew




*****************


Saa kumi na mbili za asubuhi mlango wa chumba cha Bella ukagongwa akainuka na kwenda kuufungua.Tayari alikuwa anafahamu mtu aliyekuwa mlangoni akamfungulia mlango na Sarafina akaingia.


“Utanisamehe mama kwa


kushindwa kuleta zile karatasi jana niliharibikiwa gari na nkajikuta simu yangu imeisha chaji” akasema Sarafina na Bella akatoa kicheko


“Nilijua tu hautaweza kurudi” akasema Bella na kuchukua faili alilokuja nalo Sarafina na wakati akiendelea kuzipitia nyaraka


zilizokuwemo ndani ya lile faili Sarafina akaitoa simu yake akaiwasha ile programu iliyowekwa na akina Ruby na kujifanya anatafuta kitu katika simu yake na mara ukasikika mlio mara tatu


“Is that your phone? Akauliza Bella


“Ndiyo mama” akajibu Sarafina na Bella akaendelea kuzipitia zile nyaraka


Mara tu Sarafina alipoiwasha ile program iliyowekwa katika simu yake,Kompyuta ya Ruby iliweza kutoa mlio Fulani na mshale ukaanza kuzunguka ikitafuta na mara kukasikika tena mlio na mduara wa kijani ukatokea Ruy akatabasamu


“Tayari tumeipata simu ya


Bella na kuanzia hapa tunaweza kusikia simu zote anazopiga au kupigiwa,tutasoma ujumbe wote anaotuma au kutumiwa tutaweza kuona kila kinachofanyika katika simu yake” akasema Ruby


“Safi sana.Sasa mpigie simu Patrick mjulishe kwamba mpango umekwenda vizuri na ampigie simu Lethabo” akasema Mathew na Zari akampigia simu Patrick akamjulisha kwamba tayari Sarafina amekwisha ifanya kazi yake.Baada ya Ruby kukata simu Patrick akampigia simu Lethabo Dlamini na kumuuliza kama tayari amepata taarifa kuhusu kampuni ya African pictures kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.Taarifa ile ilimstua sana Lethabo na bila kupoteza muda akampigia simu Bella


“Simu ya Bella inaita mpigaji Lethabo Dlamini” akasema Ruby na Bella akapokea simu


“Hallow Lethabo” akasema


Bella


“Mama Bella nimepokea taarifa ambayo imenistua kidogo nataka kupata uhakika kutoka kwako”


“Taarifa gani Lethabo? Bella akauliza


“Nimetaarifiwa kwamba kampuni yetu ya African pictures imewekwa chini ya ulinzi wa polisi kuanzia jana usiku.Umekwisha pata taarifa hizo? Akauliza Lethabo


“Hapana sijapata taarifa hizo.Nani amekupa taarifa hizo?


“Nimetaarifiwa na Patrick” “Yeye amezipata wapi


taarifa hizo? Akauliza Bella


“Sifahamu amezipata wapi”


“Naomba uniachie suala hilo nilifuatilie niufahamu ukweli halafu nitakupigia baada ya muda mfupi” akasema Bella na kukata simu akampigia Patrick


“Anampigia simu Patrick” akasema Ruby


“Hallo Bella” akasema


Patrick baada ya kupokea simu “Patrick nataka kufahamu


ulikozipata taarifa za ofisi za African Pictures kuvamiwa na polisi” akasema Bella


“Nimepigiwa simu na mmoja wa waigizaji asubuhi hii akaniambia kwamba amewahi kwenda ofisini lakini amekuta jengo limezingirwa na askari polisi ndipo nikamjulisha Lethabo ili kujua kuna nini kimetokea hadi jengo lizingirwe na askari polisi” akasema Patrick na ukimya ukatawala “Bella! Akaita Patrick “Patrick nitakupigia baadaye” akasema Bella na kukata simu halafu akampigia Kasiano


“Anapiga tena simu na safari hii kwa Kasiano


Muyenzi” akasema Ruby


“Mama Bella” akasema Kasiano


“Kasiano kuna taarifa zozote umezipata kuhusu kampuni ya African pictures? Akauliza Bella


“Hapana sijapata taarifa zozote.Kuna nini? Akauliza Kasiano


“Kampuni iko chini ya ulinzi wa polisi” akasema Bella


“Chini ya ulinzi wa polisi?! Kasiano akauliza


“Ndiyo.Imewekwa chini ya ulinzi.Nini kimetokea hapo usiku wa jana hadi polisi wakavamia? Akauliza Bella


“Hapan sifahamu chochote”


“Kasiano wasiliana na watu wako ujue kile kilichotokea ili tujue namna ya kulimaliza suala hili”


“Mama Bella umenistua mno kwa taarifa hizo.Ndani ya jengo lile kuna ofisi za Black Mafia ni sehemu ambako kwa namna yoyote ile jeshi la polisi hawatakiwi kuingia na kugundua kile kinachoendelea” akasema Kasiano


“Kasiano huu si muda wa mahubiri.Please fix this immediately” akasema Bella na kukata simu


Mathew akainua mikono juu kumshukuru Mungu.


“Tunakushukuru ee Mungu wa mbinguni ambaye umetuwezesha kupata kile ambacho tumekuwa tunakitafuta kwa jasho na damu” akasema na kuwatazama wenzake ambao nyuso zao zilijaa tabasamu


“Hatimaye sasa tuna uhakika kwamba Bella ana mashirikiano na Kasiano na hatuna shaka tena kwamba Bella ndiye kiongozi wa mtandao huu wa dawa za kulevya hapa Tanzania” akasema Mathew


“Ninashindwa kuyazuia machozi kunitoka kwa furaha niliyonayo” akasema Ruby


“Nini kinafuata baada ya kazi hii kubwa? Akauliza Zari


“Ni wakati wa Rais kuufahamu ukweli wote.Wakati tukimjulisha ukweli mheshimiwa Rais tunaendelea kumfuatilia Bella kwani kwa sasa amechanganyikiwa na hajui kama anadukuliwa hivyo basi atawapigia washirika wake kuwapa onyo kwamba mambo yameharibika” akasema Mathew na Ruby akampigia simu Rais halafu akampa Mathew simu azungumze naye


“Hallo” akasema Rais Festus


“Mheshimiwa


Rais,Mathew hapa ninaongea”


“Mathew nimefurahi


kuisikia sauti yako asubuhi hii.Vipi maendeleo yako? Akauliza Rais



**********

“Ninashukuru ninaendelea vyema mheshimiwa Rais” “Nafurahi kusikia hivyo.Wenzako wote wanaendelea vyema?


“Wote tuko salama mheshimiwa Rais”


“Mathew jana usiku nilipigiwa simu na Ruby akaniomba jambo Fulani nikalitekeleza na nikaomba nipate maelezo asubuhi.Nini kinaendelea hivi sasa katika misheni yenu?


“Mheshimiwa Rais umefika wakati wa kufahamu kila kitu hivyo nimekupigia kukuomba uje hapa ili tukufahamishe kile ambacho tumefanikiwa kukipata”


“Sawa ninakuja sasa hivi” akasema Rais


“Tujiandaeni Rais anakuja muda si mrefu” akasema Mathew




*****************




Rais hakupoteza muda akawasili katika nyumba yake ambako akina Mathew walikuwa wameweka kambi ya muda.


“Karibu sana mheshimiwa Rais” akasema Ruby aliyewaongoza wenzake kwenda kumpokea Rais na kumuongoza hadi katika chumba alimo Mathew Mulumbi.Mara tu Rais alipoingia mle chumbani Mathew akasimama akamsalimu


“Nimefurahi sana kuwakuta nyote mkiwa salama na mnaendelea vizuri” akasema Rais Festus


“Sote tuko salama kabisa mheshimiwa Rais” akasema Mathew


“Nimekuja kwa haraka baada ya kupokea ujumbe wenu”


“Tunashukuru


sana.Tumekuita hapa asubuhi hii kukupa taarifa za kukamilika kwa zoezi letu tulilokuwa tunaendelea nalo la kuusaka mtandao wa dawa za


kulevya hapa nchini” akasema


Mathew


“Mmefika mwisho? Tayari mmewafahamu? Akauliza Rais Festus kwa mshangao


“Mheshimiwa Rais zoezi limekamilika.Naomba Kelvin aletwe hapa mara moja” akaelekeza Mathew na Kelvin mmoja wa walinzi wa Rais akaletwa mle chuumbani alikuwa amevimba na kufungwa bandeji sehemu mbali mbali za mwili


“Mheshimiwa Rais huyu ni Kelvin mlinzi wako”


“Ndiyo ninamfahamu.Kwa nini yuko hapa? Kwa nini mmemfanya hivi? Akauliza Rais


“Tunaanzia sakata la zile picha zako za faragha mheshimiwa Rais” akasema


Mathew


“Baada ya uchunguzi tuligundua kwamba huyu ndiye aliyefanikisha kwa picha zile kupigwa kwa maelekezo ya mkeo Bella” akasema Mathew na sura ya Rais ikabadilika


“Kelvin na Bella? Akauliza


Rais Festus


“Kelvin mueleze Rais ukweli wote.Usifiche hata kitu kimoja” akasema Mathew na


Kelvin akaanza kumueleza Rais kila kitu namna alivyokuwa anatumiwa na Bella hadi alivyotumwa kuwapelekea watu waliotega kamera za siri ndani ya ile nyumba na kumpiga Rais picha za faragha


“Nisamehe sana mheshimiwa Rais nimekosea mno ni tamaa ya fedha iliyonipelekea nikafanya kitu cha namna hii” akasema Kelvin.Rais Festus akamtazama kwa hasira


“Kelvin haya unayonieleza ni mambo ya kweli? Akauliza Rais Festus


“Ndiyo mheshimiwa Rais” akajibu Kelvin


“Kelvin unaonekana umeteswa sana.Niambie ukweli kama hawa jamaa wamekutesa na kukuelekeza uje uniambie mambo haya uliyonieleza” akasema Rais


Festus


“Mheshimiwa Rais


niliyokueleza ni ukweli mtupu” akasema Kelvin


“Kwa nini Kelvin umenifanyia hivi?Licha ya kwamba ni mlinzi wangu lakini nilikuamini na kukufanya kama kijana wangu.Nimekusaidia mambo mengi na kukuweka karibu yangu nikakushirikisha siri zangu kwa nini ukafanya mambo kama haya? Kwa nini ukayaharibu maisha yako? Akauliza Rais Festus “Mheshimiwa Rais nimekosea sana.Nimeponzwa na tamaa ya pesa hivyo sina namna yoyote ya kujitetea.Ninastahili adhabu” akasema Kelvin na Rais Festus akaendelea kumtazama kwa hasira


“Muondoeni mbele ya macho yangu kwani nitamuharibu haribu ! akasema Rais Festus kwa hasira


“Nilijua kuna watu wa karibu yangu wamehusika kwa kiasi kikubwa katika zile picha za faragha lakini sikuwahi kufikiri kama Kelvin ni mmoja wao.Ni kijana ambaye nilimuamini sana na kubwa zaidi nilimchukulia kama mwanangu.Siamini kama leo hii ndiye aliyenigeuka kwa tamaa ya fedha na kunisababishia aibu hii kubwa niliyoibeba” akasema Rais Festus


“Mheshimiwa Rais usiyaweke maisha yako kwa mwanadamu kwani hujui kile anachokiwaza moyoni mwake. Hata Yesu Kristu alisalitiwa na mmoja wa watu wake wa karibu kwa fedha.Naamini sasa umepata picha pana kuhusu lile sakata la picha zako za faragha”akasema Mathew


“Nimeumizwa sana kusikia kwamba ni mke wangu ambaye amefanya kitu kama kile.Sikutegemea kabisa.Japokuwa mimi na yeye tumekuwa katika mgogoro lakini hakupaswa kunifania hivi alivyofanya.Sikuwahi kuhisi kama Bella ni mwanamke mbaya kiasi hiki!


akasema Rais Festus “Mheshimiwa Rais mambo hayakuishia hapo”akasema Mathew na kuelekeza Paul aletwe ndani ya kile chumba


“Mheshimiwa Rais huyu anaitwa Paul Lewis tumemleta hapa jana usiku.Paul huyu ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania nataka umueleze ukweli kuhusu ninyi ni akina nani na nini shughuli zenu,eleza kila kitu bila kuficha” akasema Mathew


“Mheshimiwa Rais mimi ni kiongozi wa kundi la Black Mafia ambalo limekuwepo hapa nchini na kufanya mambo mengi maovu” akasema Paul na kumueleza Rais kwa kina kuhusu kundi la Black Mafia na mambo ambayo wamewahi kuyafanya,namna walivyohangaika kumtafuta Mathew Mulumbi na akamalizia kumueleza ukweli Rais kwamba kiongozi wao kwa hapa nchini ni nabii Kasiano wa kanisa la injili ya wokovu


“Kasiano?! Akauliza Rais kwa mshangao


“Ndiyo mheshimiwa Rais”


“Una hakika na hicho ukisemacho kijana? Kasiano ndiye kiongozi wenu? Akauliza Rais Festus


“Ndiyo mheshimiwa


Rais.Ndiye kiongozi wetu lakini naamini kuna wengine wakubwa zaidi ambao siwafahamu” akasema Paul


“Mathew hiki anachokisema huyu jamaa ni kitu cha kweli? Akauliza Rais


Festus


“Mheshimiwa Rais


anachokisema ni kitu cha kweli kabisa” akasema Mathew na kumueleza Rais namna walivyoweza kuvamia jengo lile la kampuni ya kuengenza filamu na akamtambulisha Sindi kwa Rais


“Nimewahi kusikikia tarifa zako kutoka kwa Ruby kumbe wewe ndiye Ziro.Ahsante sana kwa kazi kubwa na ya hatari uliyoifanya hadi suala hili likafika hapa” akasema Rais


Festus


“Mheshimiwa Rais baada ya kupata maelezo ya Kelvin na kuunganisha picha za matukio kadhaa tulianza kumfanyia uchunguzi mkeo ili kujua mashirikiano yake na Black Mafia.Kuna jambo kubwa tumeligundua ambalo halitakufurahisha mheshimiwa Rais” akasema Mathew na kunyamaza kidogo akaomba apewe bahasha yenye picha za Bella na Patrick


walizozichukua nyumbani kwa Patrick akampatia Rais ambaye alizitazama na kukunja sura


“Mheshimiwa Rais tuligundua kwamba mkeo Bella ana mahusiano na huyo kijana anaitwa Patrick ni mwandishi wa vitabu vya riwaya” akasema Mathew


“Ninalifahamu suala hili” akasema Rais Festus na kuzirejesha picha zile katika bahasha huku watu wote mle ndani wakimtazama kwa mshangao


“Unalifahamu jambo hili?


Mathew akauliza


“Naona nyote mmeshangazwa na kutostuka kwangu baada ya kuziona picha hizi.Ni kweli jambo hili si geni kwangu ninalifahamu.Ninayafahamu mahusiano haya ya Bella na huyu kijana.Kama nilivyowaeleza awali kwamba mimi na Bella hatuna mahusiano mazuri hivi sasa na kitu tunachokisubiri ni mimi nimalize kipindi changu cha urais ili tuweze kuachana na kila mmoja akaendelee na maisha yake.Hivi sasa kinachofanyika ni maigizo tunaonekana tuko pamoja kama watu wenye mapenzi makubwa lakini ukweli mimi na Bella mapenzi yamekwisha zamani”


“Nini ilikuwa sababu ya mgogoro wenu?Mathew akauliza


“Kila mmoja anamtupia mpira mwenzake lakini ni Bella aliyesababisha haya yakatokea.Niligundua mahusiano yake na huyu kijana aliyepiga naye picha nikapatwa na hasira nikaanzisha mahusiano na mdogo wake na tukapata mtoto mmoja,na hapo ndipo mgogoro ulipozidi.Naomba nisiliongelee zaidi jambo hilo vijana wangu.Bado ninahisi msisimiko mkubwa wa mwili kwa mambo niliyoyasikia kutoka kwa huyu kijana.Watu ambao ametaja kuwa wanashirikiana nao ni watu ambao si rahisi kuamini.Nabii Kasiano ni mtu mwenye heshima kubwa sana hapa nchini,kila kunapofanyika hafla yoyote ambayo inawahitaji viongozi wa dini na Kasiano naye hualikwa.Sikuwahi kuhisi kama anaweza akajihusisha na mambo kama haya ya aibu.Sikujua kama naibu


waziri Keofas naye alikuwa ni mmoja wao,David Chamwino huwezi ukategemea naye akawa katika mtandao huu ! akasema Rais Festus


“Mheshimiwa Rais katika kumchunguza mkeo tuligundua kwamba ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya kutengeneza filamu ya African


Pictures.Wamiliki wengine ni


Roberto Zullo,Martina


Durante na Bandile Dlamini.Baada ya kuwachunguza tukabaini kwamba hawa wote ni wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya nchini Afrika kusini na kitendo cha Bella kushirikiana nao kikatupa picha yawezekana naye akawa anajihusisha na biashara hiyo ya dawa za kulevya hivyo tukaweka mtego na hiki ndicho tulichokipata” akasema Mathew na kumtaka Ruby kucheza mazungumzo ya Bella na Lethabo Dlamini.


“Hii ni sauti ya Bella !


akasema Rais Festus


“Huyo aliyekuwa anazungumza naye anaitwa Lethabo Dlamini ndiye meneja mkuu wa kampuni hiyo kwa hapa Tanzania” akasema Mathew na Ruby akacheza tena mazungumzo ya Bella na Kasiano.


“Is this real? Rais Festus akauliza


“Ndiyo mheshimiwa Rais.Kwa mazungumzo hayo tayari tumepata uhakika mkubwa kwamba Bella na Kasiano wana mashirikiano na kwa pamoja wanaendesha mtandao huu mkubwa wa dawa za kulevya hapa nchini.Mheshimiwa Rais mkeo amejihusisha katika suala la uhalifu hivyo lazima achukuliwe hatua kali kama wahalifu wengine.Najua jambo hili ni gumu lakini lazima litekelezwe hakuna namna tutakavyoweza kupindisha ! Mathew akatoa angalizo


“Mathew uko sahihi.Bella na wenzake wote lazima wakutane na mkono wa sheria.Kuna jambo ambalo nataka mlifahamu” akasema Rais na kuwaeleza akina Mathew kile kilichotokea hadi familia ya Godfrey pamoja na wale mateka wa SNSA kuachiwa huru


“Nadhani mnaweza kuona namna mwanamke huyu alivyo nyoka.Alitaka kunichota akili na mimi nikajikuta nikimuamini.Mtanisamehe kwa kile nilichokifanya vijana wangu” akasema Rais Festus


“Mheshimiwa Rais kwa


hapa tulipofika tunalikabidhi kwako suala hili ili jeshi la polisi waendelee na hatua nyingine za kiuchunguzi na kuwatia nguvuni wahusika wote wa mtandao huu.Tutakukabidhi pia taarifa zote tulizozipata kutoka kwa Black Mafia ambazo zinaeleza namna dawa za kulevya zinavyoingia hapa nchini”akasema Mathew


“Vijana wangu nimekosa maneno mazuri ya kuzungumza na sijui nitumie neno gani kuwashukuru kwa hiki mlichokifanya.Huu ni zaidi ya uzalendo kwa taifa lenu.Kwa hiki mlichokifanya mmesaidia mamia ya vijana wasiweze kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya.Baada ya kazi hii kubwa sasa ninawaomba mpumzike na mniachie jambo hili nikaanze kulifanyia kazi.Nina kazi ya kumuapisha mkuu mpya wa jeshi la polisi leo nitakuja tena kuzungumza nanyi baadaye” akasema Rais na kuondoka akiwa amejaa hasira.Wakati akiingia katika gari akamuita Zari akazungumza naye jambo


Fulani kwa dakika mbili halafu akaondoka


“Tumemaliza


kazi.Tumeibua kashfa kubwa sana” akasema Mathew na wote wakamfuata pale kiandani wakamkumbatia kwa furaha halafu Zari akawaomba atoke aende SNSA


******************


Saa nne na dakika kumi za asubuhi,Rais alimaliza


kumuapisha mkuu mpya wa jeshi la polisi na kama ilivyo ada akapewa nafasi ya kuzungumza machache.Uso wa Rais Festus kwa siku hii haukuwa na tabasamu na wengi walidhani ni kutokana na lile tukio la picha zake za faragha kusambaa ndiyo maana tabasamu limepotea usoni kwake.


Aliposimama ili kusema machache,Rais alianza kwa kuwatambua baadhi ya


viongozi wote waliohudhuria hafla ile


“Ndugu zangu kuna mambo machache ambayo


kupitia hafla hii nataka kuwajulisha watanzania.” Akanyamaza kidogo na kila mmoja alikuwa kimya akimsikiliza kwa makini “Katika hotuba yangu ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa SADC moja ya mambo ambayo niliyazungumzia kwa mkazo mkubwa ni vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya.Nilieleza kwa kirefu namna biashara hii inavyozidi kushamiri kila uchao katika nchi za SADC na athari zake kwa kizazi chetu na nikawaomba wakuu wenzangu wa nchi wanachama wa SADC waniunge mkono katika vita hiyo kwani Tanzania peke yake hatutaweza kushinda kama nchi nyingine zitalega lega.Naomba niwaeleze ukweli ndugu zangu watanzania kwamba pamoja na wito ule lakini mpaka sasa bado sijapata uungwaji mkono kutoka kwa viongozi wa mataifa mengine ya SADC na hivyo kufifisha juhudi zetu kama taifa za kupambana na biashara hii haramu ya dawa za kulevya” akanyamaza kidogo halafu akaendelea


“Hata hapa nchini mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya yamelega lega na hayana kasi ile ambayo niliitazamia.Bado dawa za kulevya zimeendelea kuingia nchini na kuendelea kuathiri vijana wetu.Ndugu watanzania wenzangu napenda kukiri kwenu kwamba vyombo vilivyopewa dhamana ya kuendesha mapambano hayo havijafanya kazi yake ipasavyo baada ya viongozi na watumishi wake kwa asilimia kubwa kuwa ni washirika wa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya hapa nchini na hivyo kuifanya vita niliyoitanganza kushindwa kufanikiwa.


Ndugu watanzania watu wanaoendesha biashara hii ni watu wazito.Wamo viongozi wa serikali tena wenye nafasi kubwa,wapo vingozi wa taasisi mbali mbali za umma,wapo wafanya biashara wakubwa,wapo pia hadi viongozi wa dini.Ndugu zangu vita dhidi ya biashara hii ni vita ngumu na ili kuishinda unapaswa kujitoa mhanga” akanyamaza kidogo


“Kama mtakumbuka jana zimesambazwa picha zangu za faragha ambazo zimezua gumzo kubwa sana si Tanzania pekee bali duniani kwa ujumla.Kuvuja na kusambaa kwa picha zile ni moja ya matokeo ya kusimama imara dhidi ya wale wanaojihusisha na biashara hiyo.Sitaki kuzungumzia sana suala hilo lakini niseme kwa ufupi kwamba kabla ya picha zile kusambaa nilipigiwa simu na watu hao wakaniambia wanazo picha zangu na watazisambaza kama sintatekelea maelekezo yao.Sikuwa tayari kutekeleza kile walichonitaka nikifanye na wakazisambaza picha hizo na kutishia kuendelea kuanika hadharani masuala mengine yanahusiana na maisha yangu binafsi lengo likiwa ni kunichafua na kunikatisha tamaa.Pamoja na jitihada hizo zao lakini sikukata tamaa na leo ninasimama mbele yenu kuwajulisheni kwamba timu ndogo ya vijana wazalendo ambao walijitoa kufa na kupona kupigana vita hii pamoja nami wamefanikisha kuufumua mtandao kubwa wa wafanya biashara wa dawa za kulevya hapa nchini” Makofi mengi yakapigwa halafu Rais akaendelea


Ndugu zangu hamuwezi kuamini kwamba hata ndani ya ukumbi huu wamo watu ambao wanajulikana kama miungu wa dawa za kulevya na mmoja wao ni mke wangu Bella” Rais akanyamaza baada ya watu wote ndani ya ukumbi ule kupigwa na butwaa


“Msishangae sana ndugu zangu huo ndio ukweli.Mke wangu ni mmoja wa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya hapa nchini.Sikulifahamu hilo hadi asubuhi ya leo vijana walipofanikiwa kumgundua” akasema Rais.Bella alikuwa ameketi kitini alihisi miguu imeisha nguvu.


“Si huyu tu mwingine ambaye hamuwezi kuamini kwamba ni mmoja wa viongozi wa mtandao wa dawa za kulevya hapa nchini ni kiongozi mkubwa wa kidini,nabii mkuu Kasiano Muyenzi” Rais akanyamaza baada ya Bella kuanguka na kupoteza fahamu,haraka haraka akatolewa mle ndani ili kwenda kupatiwa huduma ya kwanza.


“Msijali ndugu zangu mambo kama hayo mtayaona mengi” akasema Rais Festus


“Wapo watu wengi ambao wanashiriki katika mtandao huu.Mkuu mpya wa jeshi la polisi kazi yako ya kwanza ambayo nataka uishughulikie ni kuhakikisha kwamba hawa wote wanaohusika na dawa za kulevya wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.Mtandao huu haujihusishi na dawa za kulevya pekee yake bali mambo mengi ya kihalifu ikiwamo mauaji.Tunao ushahidi wa kutosha


kuthibitisha kile ambacho wamekuwa wanakifanya.Watu wengi wamekwisha uawa na mtandao huu,na wengine kutengenezewa kesi wakafungwa magerezani mmoja wao ni Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo ambaye yuko gerezani hivi sasa akiendelea na kesi yake ya dawa za kulevya na mauaji,mwingine ni kijana anaitwa Gosu Gosu.Huyu amefungwa maisha gerezani kwa kosa la mauaji lakini ukweli hakufanya mauaji hayo bali alitengenezewa kesi na hawa jamaa.Visa ni vingi vilivyofanywa na hawa jamaa waliokuwa na kikundi chao walichokuwa wanakitumia katika kufanikisha mipango yao ya kihalifu kinaitwa Black Mafia” akasema Rais na


kumuita mkuu mpya wa jeshi


la polisi


“Ninakukabidhi majina haya na ushahidi mwingine wote utaupata,nataka pale nitakapomaliza kutoa hotuba yangu watu hawa wote wawe wamekamatwa na wa kwanza akiwa mke wangu”akasema Rais Festus na mkuu Yule wa jeshi la polisi akachukua majina yale na kutoka nje ya ukumbi akaanza kutoa maelekezo ya watu wale kukamatwa mara moja.




*****************


Saa nane za mchana Ruby akarejea katika kambi ya akina Mathew na kuwataka wamfuate kuna mahala wanaelekea.Walipotoka nje wakakuta helkopta ya SNSA ikiwasubiri wakaingia bila kuambiwa wanakoelekea Kutoka katika kambi yao ya muda moja kwa moja wakaelekea hadi nyumbani kwa Mathew Mulumbi.Wote wakashangazwa na hali waliyoikuta mahala hapo.Kulikuwa kumepambwa vizuri.Kulikuwa na watu kadhaa mahala pale wakiendelea na maandalizi ya sherehe na wengine walionekana kama walinzi


“Haya ni maajabu.Who did this? Akauliza Mathew baada ya kushuka katika helkopta “I did” akajibu Zari


“Wewe ndiye umefanya haya? Kwa nini hukuniambia?


“Ni maelekezo ya Rais” akajibu Zari


Moja kwa moja Mathew akaelekea katika nyumba ya mbwa wake Bravo akamkumbatia kwa furaha kubwa


Wakati wakiendelea kuburudika kwa vinywaji wakiwa nje mara vikasikika


ving’ora vya gari la polisi wote wakapatwa na wasiwasi


“Nini kinaendelea hapa


Zari? Akauliza Mathew lakini Zari akamtaka asiwe na hofu.Geti likafunguliwa na msafara wa Rais ukaingia mahala pale.Akashuka garini na kupokelewa na akina Mathew


“Mathew tayari nimekwisha muelekeza mkurugenzi mkuu wa mashtaka kuifuta mara moja kesi inayomkabili DrFabian Kelelo na nimeelekeza mashtaka yaliyokuwa yameandaliwa dhidi yako yafutwe mara moja.Tayari taratibu za jambo hilo zimeanza lakini kwa mchana huu nimekuja hapa kuungana nanyi katika mapokezi ya Gosu Gosu ambaye tayari nimemuachia huru kwa mujibu wa mamlaka niliyonayo kikatiba” akasema Rais Festus.Mathew kwa furaha aliyoipata akawakumbatia wenzake “We did it” akasema Ruby


“Mheshimiwa Rais tunakushukuru sana kwa msamaha huu ulioutoa kwa mwenzetu”akasema Mathew “Ninyi ndio mliomsaidia mwenzenu.Mmepambana na kuufahamu ukweli wote hivyo siwezi kuendelea kumuacha gerezani mtu ambaye hana hatia yoyote” akasema Rais Festus na wote wakainua vichwa vyao baada ya kuiona helkopta ikielekea mahala pale.Taratibu helkopta ikatua katika bustani.Kila mmoja alikuwa na hamu sana ya kumuona Gosu Gosu.Mlango wa helkopta ukafunguliwa wakashuka jamaa wawili halafu akashuka Papi Gopsu Gosu.Mara tu aliposhuka kitambaa kilichofunika bango kubwa kikavutwa na maandishi makubwa yakaonekana WELCOME HOME GOSU GOSU.


Gosu Gosu alishindwa kuyazuia machozi ya furaha kumtoka akasalimiana na Rais halafu akamfuata Mathew akamkumbatia kwa furaha kubwa


“Thank Mathew


Mulumbi,Thank you brother” akasema GosuGosu


“Welcome home brother” akasema Mathew


Gosu Gosu akasalimiana na akina Ruby na wa mwisho alikuwa Nawal halafu wote wakaelekea katika hema lililokuwa limeandaliwa vyakula na vinywaji.Kabla ya kufanyika kitu chochote Ruby akafanya maombi kumshukuru Mungu kwa kuwawezesha kukamilisha misheni yao ya kuufumua mtandao wa dawa za kulevya.Rais Festus hakuwa na muda mrefu pale hivyo akaomba aseme machache ili aweze kuondoka


“Gosu Gosu karibu tena nyumbani.Sote tumefurahi sana kukuona tena.Naomba nikufahamishe kwamba hawa wenzako ndio waliofanikisha wewe ukatoka gerezani.Walifanya kazi usiku na mchana,wamekumbana na hatari nyingi,Mathew Mulumbi amenusurika kifo mara kadhaa na tukio la mwisho amepigwa risasi tatu lakini bado hakukata tamaa wameendelea kupambana hadi kufanikiwa kuwapata watu waliokutengenezea ile kesi.Sina mengi ya kusema kwa leo zaidi ya kukukaribisha sana nyumbani” akasema Rais Festus na Gosu Gosu akapewa nafasi ya kusema machache


“Mimi ni mwanajeshi,ni


mpiganaji ni mtu jasiri lakini leo hii nimekuwa kama mtoto mdogo nimeshindwa kuyazuia machozi ya furaha kuendelea kunitoka” akanyamaza na kufuta machozi halafu akaendelea


“Nilipoteza matumaini baada ya kufungwa maisha gerezani kwa kosa ambalo sikulitenda.Nikiwa gerezani nilikutana na mchungaji ambaye alinifundisha kuhusu ukuu wa Mungu na kuniomba nisikate tamaa nimkabidhi Mungu matatizo yangu naye atanipigania.Nilimlilia Mungu na kumuomba anisaidie siku moja ukweli uweze


kujulikana.Leo hii ninashuhudia kwenu kwamba Mungu anajibu maombi.Ninasema hivyo kwa sababu nikiwa sina hili wala lile Mathew Mulumbi alifika gerezani kitu ambacho sikukitarajia.Nililia machozi mengi siku hiyo kumshukuru Mungu kwani kwangu ulikuwa kama muujiza.Mathew alinihakikishia kwamba atafanya kila awezalo kuhakikisha ninatoka gerezani.Leo hii nilipopewa taarifa kwamba nimeachiwa huru nimelia machozi mengi ndiyo maana mnaona macho mekundu namna hii.Nashukuruni sana ndugu zangu kwa kila mlichokifanya kuhakikisha ninatoka gerezani.Haikuwa rahisi kama alivyosema Rais na sijui nitawalipa nini ndugu zangu.Ahsant…..”Gosu Gosu akashindwa kumalizia alizidiwa machozi.Nawal akainuka akamfuata akamkubatia na kumfuta machozi.Mathew akasimama ili kutoa neno la mwisho kabla ya Rais kuondoka


“Aliyenipa taarifa za Gosu Gosu kufungwa aliitwa Victor ni kijana ambaye nimetoka naye mbali hakuwa na ndugu hapa mjini mimi ndiye niliyekuwa ndugu yake na nikamjengea nyumba ile pale mnayoiona lakini jamaa walimuua kikatili sana.Mheshimiwa Rais sisi unaotuona hapa ni familia moja na kila pale mmoja wetu anapokuwa na matatizo husimama pamoja kama familia kumsaidia ndiyo maana umeona tulivyofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunamsaidia mwenzetu Gosu Gosu ili aweze kutoka gerezani .Tunashukuru pamoja nasi amejiunga Zari karibu sana katika familia yetu.Tulipoanza misheni hii hatukujua kama tungeweza kukutana na mambo makubwa kama tuliyokutana nayo,tumeweza kuibua mtandao mkubwa kabisa wa dawa za kulevya hapa nchini,tumewaibua wale miungu wenyewe wanaosimamia biashara nzima na mtandao wote.Mheshimiwa


Rais vita hii haijakwisha bado.Hii ni vita endelevu na baada ya hawa wataibuka tena wengine na wengine kitu cha msingi ni kujenga taasisi imara za kuendesha vita hii vinginevyo haya yote tuliyoyafanya yatakuwa bure.Nashauri pia taasisi hizi za dini zifanyiwe uchunguzi mkubwa kabla ya kusajiliwa kwani kuna mengi yamejificha huko.Kuna baadhi zinatumika kama mwavuli wa kuficha mambo maovu kama kanisa la injili ya wokovu.Sitaki kuingilia uhuru wa kuabudu lakini mheshimiwa Rais kuna ulazima mkubwa wa kufanya uchunguzi wa kina na zile taasisi za kidini ambazo zitabainika hazina sifa zifutwe mara moja.Kitendo cha nabii mkuu Kasiano ambaye ana maelfu ya waumini hapa nchini kujihusisha na dawa za kulevya na mauaji kimetia doa kubwa kwa taasisi za kidini.Mwisho nakushukuru mheshimiwa Rais kwa kusimama nasi wewe ndiye shujaa wetu kwani ulikubali kuibeba aibu ile kubwa ili mipango yetu ifanikiwe kama ungekubali kutekeleza matakwa yao ungenikabidhi kwao na ninaamini hivi sasa wangekuwa wameniua na misheni isingefika hapa ilipofika hivyo hatujakuangusha mheshimiwa Rais aibu uliyoibeba imeleta matokeo haya yote” akasema Mathew na kukaa akasimama


Zari


“Naombeni japo dakika mbili nami niseme machache” akasema Zari na kunyamaza kidogo


“Tangu nimejiunga na SNSA huu ni mkasa wangu wa kwanza mkubwa kunipata lakini ninaomba nikiri kwako mheshimiwa Rais sijawahi kukutana na watu majasiri wenye ari ya kazi kama hawa Mathew na wenzake.Nimejifunza kitu kikubwa kutoka kwao.Hawakati tamaa,kwao mlango wa kushoto ukifungwa wanapita kulia,wa kulia ukifungwa watapita juu ili mradi wahakikishe wanafikia malengo yao.Shukran za


kipekee kabisa nataka nimpe


Mathew


Mulumbi.Mheshimiwa Rais huyu ni kiumbe wa ajabu sana ni binadamu wa kwanza nimekutana naye ambaye haogopi kifo.Mathew Mulumbi alidiriki kumsogelea mwanamke aliyekuwa amefungwa bomu ambalo lilikuwa karibu kulipuka kwa lengo la kupata taarifa na alihakikisha ameipata taarifa hiyo na sekunde chache baada ya kupewa taarifa hiyo bomu likalipuka.Picha ile haiwezi kufutika kichwani kwangu.Hilo linaweza kuwa dogo lakini kubwa zaidi kwangu ni namna alivyoweza kunikinga na risasi tatu ambazo zilitakiwa kunipata mimi,na pengine kama asingefanya vile hivi sasa ningekwisha poteza maisha.I don’t know how to pay him for what he did.Amenusurika kupoteza maisha yake kwa ajili yang………” Zari akashindwa kujizuia akaangua kilio.


“Vijana wangu nimewasikia nyote na ninawaahidi kuyafanyia kazi yale yoe mliyonishauri na ninawahakikishia vita hii dhidi ya biashara ya dawa za kulevya imeibuka upya.Mtasikia hatua nitakazochukua.Zari ofisi za SNSA zitahama kutoka mahala pale zilipo kwani zimekwisha fahamika na litajengwa jengo maalum kabisa na idara hii ambayo imeonesha matokeo mazuri itasukwa upya na kuwa bora zaidi.Ruby nimekwisha tuma ndege kwenda Rwanda kuwachukua watoto wako na kuwarudisha nyumbani .Ahsanteni sana vijana wangu naombeni niwaache mpongezane na tutaendelea kuwasiliana” akasema Rais wakamsindikiza hadi katika gari lake akaondoka


BAADA YA WIKI 1


Mathew na wenzake


waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Wote kwa pamoja walimsindikiza Sindi aliyekuwa anaodoka kurejea nchini kwao Afrika kusini baada ya kukamilisha kazi yake.Sindi alipenda kuendelea kubaki Tanzania lakini alitakiwa na viongozi wake kurejea nchini Afrika kusini baada ya wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya


Roberto Zulo na mkewe Martina Durante bila kumsahau Bandile Dlamini kukamatwa na kikosi cha siri cha kupambana na dawa za kulevya nchini Afrika Kusini.


“Mathew ningependa sana kuendelea kukaa hapa Tanzania lakini natakiwa nyumbani kwa majukumu mengine hivyo lazima niondoke.Ninawashukuru sana nyote kwa ushirikiano wenu mkubwa hadi mtandao huu wa dawa za kulevya umefumuliwa naweza kusema barani Afrika kwani hawa watu wote waliokamatwa ndio waliokuwa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya barani Afrika”akasema Sindi na kuagana na kila mmoja aliyefika kumsindikiza pale uwanjani na kuingia ndani kusubiri ndege aweze kuondoka.Mathew na wenzake hawakuondoka hadi walipohakikisha ndege aliyopanda Sindi imeondoka ndipo walipoondoka.


BAADA YA MIEZI 7


Bado kashfa kubwa ya


baadhi ya viongozi wa serikali na wa dini kujihusisha na dawa za kulevya iliendelea kutawala katika vyombo vya habari.Mahakama ilifurika watu kila watuhumiwa hao walipofikishwa mahakamani.Hatimaye baada ya kesi kuunguruma kwa muda wa miezi saba mahakama iliwakuta na hatia watuhumiwa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na mauaji hivyo kuwahukumu vifungo vya maisha gerezani


na wengine miaka thelathini.Bella,nabii Kasiano na mke wake Rita,Paul Lewis,John Mkizi,Apolo Semba,David Chamwino na wengine 40 walihukumiwa vifungo vya maisha huku wengine 53 wakihukumiwa vifumbo vya miaka thelathini gerezani.




****************


Miezi miwili tangu hukumu itolewe kwa akina Bella,Mathew Mulumbi na wenzake waliendelea na maisha yao kama kawaida.Akiwa nyumbani kwake akipumzika akafika mjumbe kutoka kwa Rais akampatia bahasha iliyotoka kwa Rais.Mathew akaifungua na kukuta kuna karatasi na bahasha nyingine ndani yake.Karatasi ile iliandikwa na Rais


“Nimetumiwa barua hiyo


na nabii


Kasiano.Nimekutumia nakala yake naomba uisome tahadhali” aliandika Rais Mathew akaifungua


bahasha ile ndogo na kukuta kuna barua ndani yake akaanza kuisoma.




Mheshimiwa Rais amani kwako


Ninaandika barua hii nikiwa katika majuto makubwa.Sikutegemea kama maisha yangu yangeweza kubadilika na kuwa namna hii.Sikutegemea kama maisha yangu yataishia katika jumba hili.Ninaandika barua hii nikiwa ndani ya chumba kidogo chenye mwanga hafifu,godoro kuu kuu na kitanda kilichojaa kunguni,sipati usingizi usiku nakesha nikilia kumuomba Mungu utokee muujiza.Sikuyazoea maisha haya.Nilizoea kulala ndani ya chumba kikubwa juu ya godoro nene na mashuka masafi yenye kunukia,chumba kilikuwa na ubaridi kutoka katika kiyoyozi.Niliishi maisha kama niko peponi na maisha kama haya ya gerezani nilikuwa nayasoma magazetini au kutazama katika filamu


Mheshimiwa Rais ninaandika


barua hii ili ujumbe huu ufike kwa watanzania kwani nimeamua kukiri makosa yangu kwao.Nakiri kwako na kwa watanzania kwamba mimi sikuwa nabii wa kweli bali nilikuwa nikitumia nguvu za giza katika kanisa langu na kufanya miujiza mikubwa iliyowavuta waumini kujaa kwa wingi.Sina nguvu yoyote ya kinabii na yale maono yote ya kinabii niliyokuwa nawaeleza waumini kwamba nimefunuliwa ni uongo na mengine yalikuwa ni matukio ya kutengeneza ili kuwaminisha watu kwamba nina nguvu kubwa za kinabii.Nimemkosea Mungu na nimewakosea sana watanzania.Nilichukua fedha za watu masikini na kuzitumia kwa maisha ya anasa.Nataka niwausie watanzania kwamba watumishi wa namna hii bado wapo wengi na wanaendelea kuibuka kila uchao na kila mmoja anakuja na mtindo wake wa miujiza nawaomba wajihadhari nao,wengi ni matapeli na hawana nguvu ya kimungu ndani mwao wanafanya miujiza kwa nguvu za giza.


Kanisa langu lilitumika kama mwavuli wa kuukinga mtandao mkubwa wa wafanya biashara wa dawa za kulevya ambao ndio walioniingiza katika mambo haya ya unabii wa uongo.Japo tumehukumiwa vifungo karibu wote lakini bado wananchi wana maumivu makubwa tuliyowasababishia.Tumefanya mambo mengi maovu,vijana wengi wameathirika kwa dawa za kulevya tulizoziingiza hapa nchini na nchi nyingine.Tumefanya mauaji ya watu na mambo mengine maovu katika jamii.Nikisema nieleze yale tuliyoyafanya ninaweza kuandika kitabu cha kurasa elfu moja lakini itoshe tu kusema kwamba mimi na wenzangu tumefanya maovu mengi na ninataka kutumia nafasi hii kuwaomba msamaha watanzania kwa yale tuliyowafanyia.Ni mambo mabaya sana.Tulikuwa wakatili na hatukujua maumivu waliyokuwa wakiyapata watu huku tukiendelea kufurahia maisha kama tuko peponi.


Tunastahili adhabu hii na hata zaidi na ninaamini kuna adhabu kubwa inatusubiri baada ya kuyaacha maisha haya ndiyo maana nimeamua kuwaomba radhi watanzania.


Ninamalizia barua yangu hii kwa kuwaomba watanzania wawe wazalendokwa nchi yao wawe na uchungu na kuipigania nchi yao kama wale vijana tuliopambana nao wakatushida Mathew Mulumbi na wenzake.Tumefanya majaribio kadhaa ya kumuua yeye na wenzake lakini hawakukata tamaa waliendelea kupambana na mwisho wakaibuka washindi.Nawaomba watusamehe mimi na wenzangu


kwa yale tuliyowafanyia


Mheshimiwa Rais naomba


kama itakupendeza toka ndani mwa moyo wako uguswe na utupunguzie japo adhabu hii ya kifungo cha


maisha


Mungu akubariki


Mungu awabariki watanzania Mathew akaikunja barua ile na kuirudisha katika bahasha na uso wake ukachanua tabasamu.


“Mbona unatabasamu


hivyo? Akauliza Zari aliyekuwa ametokea ndani akiwa na sinia la matunda Mathew akampa barua ile akaisoma


“Imekuwa vyema ameamua kukiri makosa yake.Mathew tumeingia katika historia kwa kuibua kashfa kubwa ya viongozi wa dini na serikali kujihusisha katika biashara ya dawa za kulevya “Katika maisha yangu


sintalisahau jambo hili.Ilikuwa ni kashfa kubwa sana” akasema Mathew na kunyamaza baada ya simu yake kuita zilikuwa ni namba za nje ya nchi


“Hallow” akasema Mathew


“Kaka mnaendeleaje? Ikasema sauti ya upande wa pili na Mathew akatabasamu


“Gosu Gosu habari za Qatar?


“Hapa kwema tunaendelea vyema na mapumziko yetu ila tunajiandaa kwenda Miami Marekani kuendeleza mapumziko yetu” akasema Gosu Gosu


“Sawa Gosu Gosu endelea kupumzika unastahili mapumziko marefu kwa yale uliyopitia.Vipi Nawal hajambo?


“Hajambo ametoka kidogo


lakini anaendelea vizuri” akajibu Gosu Gosu


“Gosu Gosu tunashukuru umetukumbuka lini unarejea nyumbani? Akauliza Mathew “Sijajua bado nataka niendelee kupumzika na muda ukifika nitarejea” akajibu Gosu Gosu


“Msalimu sana Nawal sisi hapa tunajiandaa kwenda katika sherehe ya kuzaliwa kwa watoto wa Ruby”


“Wasalimu sana Ruby na


Dr Fabian” akasema Gosu Gosu na kuagana na Mathew ambaye alitazamana na Zari wakatabasamu kisha wakaelekea ndani


TAMATI



0 comments:

Post a Comment

Blog