Simulizi : I Was Wrong | Nilikosea
Sehemu Ya Tano (5)
nimekuchelewesha” akasema Paulie “ Hapana Pauline.” Akajibu Grace
wakaelekea moja kwa moja hadi katika
mlango wa chumba cha Pauline
“ Nnahisi haja ndogo inataka
kunitoka kwa namna ninavyoogopa kwa
kile kinachokwenda kutokea humu ndani
kama Fred hatakuwa amewahi
kutoka.Help me Lord” Akawaza Pauline na
kukinyonga kitasa cha mlango
ukafunguka.
“ Karibu ndani Grace.” Pauline
akamkaribsha Grace ndani.Akapata nguvu
baada ya kutomuona Alfred mle
chumbani.Akashusha pumzi
“ Thank you Lord..!! akashukuru
kimya kimya
“ Wow ! Chumba chako kizuri sana
Pauline.Hii hoteli nimeipenda sana.”
Akasema Grace na kuketi sofani.Pauline
akammiminia mvinyo katika glasi na
kumpatia.Kabla ya kuanza kuywa Grace
akaomba aelekezwe mlango wa
choo,akaingia chooni na baada ya muda
akatoka wakaendelea na maongezi.
“ Pauline nakupongeza sana kwa
uamuzi wako wa kubaki hapa Moshi na
kufungua mradi ule mkubwa.Umefanya
maamuzi yenye kufaa .Licha ya kwamba
utatengeneza faida lakini utasaidia watu wengi kwa upande wa vipimo” akasema
Grace
“ Ahsante sana Grace.Anayepaswa
kushukuriwa sana ni Alfred ambaye
alinipa wazo hili la kuanzisha mradi
huu.i”akasema Pauline huku akitoa
tabasamu kubwa.
Waliendelea na maongezi na baada
ya kama dakika kumi na tano hivi,Grace
akaaga Pauline akamsindikiza hadi
mahala alikoegesha gari akaondoka
“ Ahsante Mungu kwa kunisaidia
katika suala hili gumu.Leo nilikuwa
ninaumbuka .Nashukuru kwa kupata wazo
lile la kumpigia simu Fred na kumtaka
aondoke.Dah ! siamini kabisa kama suala
hili limekwisha salama .Sina hamu na kitu
kingine chochote nataka nikajifungie
nilale mwili wote bado unanitetemeka”
akawaza Pauline na kurejea chumbani
kwake akajitupa kitandani
“ Nina uhakika mkubwa kwamba
Grace tayari amekwisha hisi kitu kuhusu
mimi na mume wake na ujio wake wa
ghafla haukuwa wa bure.Alikuja kutafuta
ushahidi.Ninahisi alimfuata mumewe
nyuma nyuma ili kufahamu anaelekea
wapi.Aliposema kwamba anataka
akakifahamu chumba changu alikuwa na uhakika kabisa kwamba Fred yuko
chumbani.Dah ! mwili wote bado
unanitetemeka.I have to put an end to this
relationship with Alfred .Yule ni mume wa
mtu na tayari mke wake amekwisha anza
kuwa na wasi wasi.Yawezekana Fred
ameonyesha mabadiliko makubwa na
ndiyo maana mke wake amestuka na
kutakakujua kinachoendelea.Sitaki tena
kuendelea na ujinga huu tunaofanya.Mke
wa Fred tayari ameanza kuteseka kwa
sababu yangu.Ndoa yake inaanza
kutetereka kwa sababu yangu.Hapana
siwezi kukubali jambo hili liendelee.Leo ni
mwisho wangu na Fred..” akawaza Pauline
na kumimina mvinyo katika glasi.
“ Ouh Fred ! Fred ! tayari umeniingia
katika mishipa ya damu yangu .Nilikuja
Moshi nikiyakimbia mapenzi lakini huku
nako nimejikuta nikianguka tena
mapenzini.What am I going to do ?
akajiuliza Pauline na kunywa mvinyo wote
uliokuwemo katika glasi na mara mlango
ukagongwa ,akainuka na kwenda
kuufungua .
“ Alfred !!!..” akasema Pauline kwa
mshangao
“ I’m back my love” akasema Alfred
huku akitabasamu “ Fred please go home to your wife”
akasema Pauline
“ Pauline I’m sorry kwa kukuweka
katika wasi wasi.Nimerudi kwa sababu
moja tu kuja kuangalia kama hakukuwa na
matatizo yoyote huku nyuma” akasema
Alfred
“ Everything was fine Alfred”
“Ouh thank you Lord” akasema
Alfred
“ Fred what we’re doing is not
right.We have to stop this immediately
.Mke wako tayari amekwisha anza kuhisi
kwamba kuna kitu kinaendelea baina
yetu.Tafadhali Fred naomba tuachane na
huu mchezo.Leo hii alikuja hapa akiwa na
uhakika kabisa kwamba uko hapa kwangu
na akanitaka nimlete chumbani kwangu
apajue nikashindwa kukataa kwani kama
ningekataa angejua lazima kuna kitu
kinaendelea.Nilihisi kutokwa na haja
ndogo.Sijawahi kutetemeka na kuogopa
kama nilivyoogopa leo.Alfred I beg you let
us stop this” akasema Pauline.Alfred
akamsogelea Pauline akamshika mkono
na kusema
“ Pauline my love please don’t say
that.You know how much I love you my
angel.Kwako nimechanghanyikiwa na sielewi wala sintasikia la mtu
yeyote.Pauline hatuwezi kuuvunja urafiki
wetu.We love each other so
much.Kilichotokea leo ni taa ya kutuonya
kwamba tuwe makini lakini si kuuvunja
uhusiano wetu.Pauline I’m not ready to
end this relationship .Ninakupenda kiasi
ambacho siwezi kukueleza kwa hiyo sahau
kabisa mimi kuachana nawe.Nimenja asali
sasa ninataka nichonge mzinga
kabisa.Lakini nakuahidi nitakuwa
muangalifu sana ili nisije nikakuweka
katika matatizo.Yawezekana kuna mahala
niliteleza na kusababisha mke wangu
akawa na wasi wasi.I promise you it won’t
happen again.Nitajitahidi sana kujizuia
nisionyeshe mabadiliko yoyote yale ili
kumfanya Grace asistuke na sisi tuendelea
na mambo yetu kama kawaida.” Akasema
Alfred
“ Why are you doing this to your
wife? Akauliza Pauline
“ pauline ni kwa sababu
ninakupenda sana.kwa mke wangu
ninapata kila kitu lakini moyo wangu
umekupenda na nimeshindwa
kujizuia.Usinielwe vibaya si kwamba nina
tamaa ama vipi lakini imenitokea tu .” “ Ouh Fred ! sijui umenipa nini.Yaani
nikiuona tu akili yangu inahama kabisa na
kila nilichokuwa nakiwaza kinapotea.”
Akasema Pauline
“ Come here my love” akasema
Alfred na kumvuta Pauline karibu yake
akamkumbatia na kumbusu.
“ I love you Pauline so much.”
Akasema Fred na kumbusu Pauline
“ I love you too Alfred,I love you so
much”
“ Jumamosi hii nitakupeleka
Arusha.”
“ No ! Fred No ! You don’t have to do
that”
“ Usiogope Pauline nitakupeleka
Arusha. I want to spend time with you
there”
“ Fred hapana.Mke wako atakustukia
na itakuwa mbaya kwetu.tayari
nimekwisha mwambia kwamba
ninakwenda Arusha jumamosi hii akisikia
na wewe pia unakwenda huko basi
atafahamu kabisa kwamba tunaongozana ”
“ Pauline naomba tusiweke mjadala
katika jambo hili.Nitakupeleka
Arusha.Please dont say no !” akasema
Alfred.Pauline akajikuta hana uwezo wa
kumkatalia Alfred. “ Sijui Alferd amenipa nini kiasi cha
kushindwa kumkatalia jambo lolote
atakaloniambia.Muda mfupi uliopita
nilikuwa nawaza kuachana naye lakini
sasa hivi sitaki hata aondoke .Nini hiki
kinanitokea jamani? Akajiulzia Pauline
akiwa amekilaza kichwa chake kifuani
kwa Alfred .
“ I’m not crazy ! with my own eyes I
saw Alfred going in that hotel.Hata gari
lake nililikuta maegesho.Ni wazi kabisa
Alfred alikuwa amekwenda kwa Pauline
.lakini kwa nini sikumkuta chumbani kwa
Pauline? Akajiuliza Grace akiwa njiani
kuelekea nyumbani kwake baada ya
kutoka hotelini kwa Pauline
“ Lazima kuna kitu kinaendelea kati
ya Pauline na mume wangu.Alfred
amebadilika sana tofauti na
ninavyomfahamu.hakuwa na tabia ya
kuondoka bila kuaga nanimemfuatili
nikamuona kabisa anaingia ndani yahoteli
ile anamoishi Pauline .Nina hakika kabsa
alikwenda kuonana na Pauline..Ouh my gosh I’m confused !..” akaendelea kuwaza
Grace.
“ Kuna kitu
nimekumbuka.Nilipoingia mle chumbani
kwa Pauline nilikuta kuna chupa ya
mvinyo na glasi mbili na zote zilikuwa na
mvinyo ndani yake.Inaonekana muda
mfupi uliopita kabla ya mimi kuingia
alikuwa na mgeni wanakunywa.nahis
mgeni huyo anaweza kuwa ni mume
wangu.Lakini kama alikuwa na
mumewangu mbona sikumkuta mle
chumbani? Alijificha wapi? Niliingia hadi
chooni lakini hakuwemo.Na je kama
hakuwa kwa Pauline alikuwa wapi? .Garce
akaendelea kujuliza maswali mengi
akakosa majibu.Akafika nyumbani kwake
na kukaa sebuleni akitazama filamu lakini
akili yote ilikuwa kwa Pauline.
“ Kuna kitu nimekumbuka.Wakati
tunapanda kwenda chumbani kwa Pauline
ghafla akasimama na kuniambia kwamba
nimsubiri akachukue kinywaji cha
kusindikiza maongezi yetu.lakini
nilipofika chumbanibkwake nikashangaa
kwa kuzikuta chupa tatu za mvinyo
mezani.Kama kulikuwa na mvinyo
chumbani kwa nini basi akachukue chupa
nyingine? Akajiuliza Grace. “ Ninahis kwamba Pauline alirejea
kaunta kwa lengo la kumtaarifu Alfred
kwamba niko pale hotelini na yeye
aondoke mara moja.Nakubaliana kabisa
na jambo kwamba inawezekana Fred
alitahadharishwa aondoke mara moja mle
chumbani.Ouh sasa nimeanza kupata
picha .” Akatabasamu
“ huu ndio mchezo
walionichezea.Nilijiuliza sana kwamba
Fred alijificha wapi? Kumbe aliwahi
kutoka kabla sijafika mle
chumbani.Ninakubaliana na hili kwa
sababu wakati ninaondoka gari lake
halikuwepo tena pale maegesho,he was
already gone.Ouh Alfred kitu gani
kimekupelekea ukanifanyia hivi?
Akawaza Grace na kuumia sana moyoni
“ lakini ngoja niendelee kuwafuatilia
kwa siri .Nitafahamu tu kamakuna kitu
kinaendelea .Nisiendelee kujiumiza kwa
sasa bila ya kuwa na ushahidi wa
kutosha.kama ni kweli mume wangu
ananisaliti basi iko siku ukweli
utajulikana tu.wanasema siku za mwizi ni
arobaini iko siku arobaini yao
itafika.Nitaumia sana kama nikigundua
kweli mume wangu amenisaliti .I’ll never
forgive him for that” akawaza Grace na kuendelea kutazama filamu.Kichwa chake
kilijaa mawazo mengi sana.
Saa tano na dakika tatu kengele ya
getini ikalia kuashiria kulikuwa na
mtu,akainuka na kwenda kuchungulia ni
nani aliyekuwa anagonga akaliona gari la
mume wake.
“ He’s back”akamfungulia geti Fred
akaliingiza gari ndani
“ bado hujalala? Akauliza Fred.Sauti
yake ilionyesha wasi wasi kwa mbali
“ Nitalalaje bila ya kuhakikisha
umerudi salama mume wangu?
Ulipoondoka hukuniambia unaelekea
wapi kwa hiyo siwezi kulala kabla
hujarejea nyumbani ili nihakikishe kama
uko salama”
“ Ahsante sana Grace.Sorry
niliondoka ghafla bila kuaga.Sikutegemea
kama ningechukua muda mrefu ” akasema
Alfred na kumbusu mke wake.
“ Ulikwenda hospitali? Akauliza
Grace
“ Kuna mgonjwa ambaye nilikwenda
kumtembelea lakini kabla ya kwenda
huko kwa mgonjwa nilipita kwanza
hotelini kwa Pauline .Nilitaka kujua
maendeleo ya mradi kwani nina siku tatu
sijakwenda kuutembelea mradi wake.Baada ya hapo nikaenda kumtazama
mgonjwa.”
“ Anaendeleaje Pauline?akauliza
Grace
“ Anaendela vizuri sana na mradi
wake unaendelea vizuri pia ukarabati
unakaribia kumalizika na kinachobaki ni
kuagiza vifaa tu” akasema Fred.
“ Amekubali kweli alikwenda
kuonana na Pauline.Yawezekana labda ni
kwa sababu ya kumpenda sana.Alfred
ndiyo maana ninaona wivu kwa ukaribu
alio nao na Pauline.Yawezekana hakuna
chochote kinachoendelea kati yao zaidi
yya urafiki wa kawaida .Lakini hata hivyo
ninapaswa kujiridhisha kwamba hakuna
kitu kinachoendelea baina
yao.Nitaendelea kuwafuatilia.” akawaza
Grace.
***********************
Wingi wa kazi alizokuwa nazo uliifanya
siku yake kuwa fupi sana. Saa kumi na
moja na dakika arobaini ukaingia ujumbe
mfupi katika simu yake uliotoka kwa Safia.
“ Tukutane saa moja za jioni baa
mpya inaitwa Kemi bar ipo Kimandolu.” David akausoma ujumbe ule kisha
akaiweka sehemu mezani akaendelea na
shughuli zake.Ilipotimu saa kumi na mbili
na nusu za jioni akafunga ofisi na kutoka
kuelekea sehemu walikopanga waonane
na Safia.
“ Huyu Safia anataka kunieleza
jambo gani ? Akajiuliza akiwa garini
kuelekea Kimandolu.
“ Sijawahi kumuona hata mara moja
na nina hakika ni Vicky aliyempa taarifa
zangu.Au yawezekana anataka kunieleza
kitu kuhusiana na kinachoendelea kati
yangu na Vicky” akaendelea kujiuliza
David.
“ katika maisha yangu kitu kikubwa
ambacho nitakijutia siku zote ni kitendo
cha kukubali kutembea na mke wa mzee
Zakaria.Hiki ni kitendo kibaya sana na
kinaninyima amani kunifanya nishindwe
hata kumtazama mzee Yule
machoni.Ananilea na kuniamini kama
mwanae na badala yake nimeingiwa na
tamaa na nikakubali kuingia katika mtego
wa Vicky.Ninakijutia mno kitendo
hiki”akapunguza kidogo mwendo wa gari
“ kwa kuwa nimelifahamu kosa langu
ninachotakiwia kukifanya si kuendelea
kufanya mchezo huu wa kijinga.Ninatakiwa kuachana kabisa na
Vicky madhahabu.Potelea mbali
litakalotokea na litokee tu lakini sina
namna zaidi ya kuachana naye haraka
sana.kwa namna alivyoniganda Yule
mwanamke najua haitakuwa kazi rahisi
lakini lazima niwe na msmamo na
nisimamie maamuzi yangu.” Akawaza
David
Saa moja na dakika kumi na nne
akawasili Kimandolu katika baa mpya
aliyoelekezwa na Safia.Akatafuta kiti na
kuketi akaagiza kinywaji akaendelea
kunywa wakati akimsubiri Safia.
‘” Sijawahi kuonana na Safia na sijui
kama hata yeye ananifahamu.Lakini
atakapofika lazima atanipigia simu”
Akawaza David na baada ya kama dakika
mbili hivi mwanake mnene wastani
akatokea na kumfuata David pale mezani
“ hello David”akasema yule
mwanamke bila wasi wasi na ilionekana
kabisa alikuwa akimfahamu vyema David
“ hallow “ akajibu David kwani
hakuwa akimfahamu yule mwanamke
“ Natumai hatujawahi kuonana hata
mara mpja.Naitwa Safia”akasema yule
mwanamke “ Ouh Safia.Karibu sana.Ni kweli
hatujawahi kuonana lakini nimeshangaa
umenifahamu vipi? Akauliza David
“ Mimi ninakufahamu vizuri David “
akasema Safia
“Nimefurahi sana kukutana nawe
jioni hii.Maisha yanakwendaje? Akauliza
David
“maisha yanakwena vizuri.Kila kitu
kinakwena vizuri sana.” Akasema
Safia.Muhudumu akafika na kuwahudumia
na kisha wakaendelea na maongezi
“Nilistushwa kidogo na mwito wako
wa dharura nikaahirisha shughuli zangu
zote za jioni ya leo nikaitika
mwito”akasema David
“ Ninashukuru sana David kwa
kukubali ombi langu na samahani pia kwa
kuvuruga ratiba yako lakini suala
nililokuitia hapa ni suala zito na kama
lisingekuwa na uzito katu
nisingekusumbua”akasema safia.
“ Ndiyo na kusikiliza Safia” akasema
David.Safia akanywa juice halafu
akatazama huku na huko kama kuna
yeyote anayewasikia kisha akasema
“ Mimi na Vicky ni marafiki wakubwa
na urafiki wetu umeanza toka tukiwa
shule.Baadae mwenzangu alifanikiwa kuolewa na mzee Zakaria na maisha yake
yakadilika.Pamoja na maisha yake kuwa
mazuri lakini bado hajanitupa.Amekuwa
akinipatia misaada mingi na
ameniwezesha sana kufika hapa nilipofika
.Hata mradi nilionao sasa hivi ni yeye
alinikopesha pesa .Siwezi kusema mambo
yote aliyonisaidia,kwani ni mengi sana.”
Akanyamaza kidogo akameza mate na
kuendelea
“ Kwa muda mrefu nimekuwa ni
mshauri wake mkubwa katika mambo
yake mengi na nimekuwa ni msiri wake
pia.Jambo lolote ambalo hawezi
kumweleza mtu mwingine yeyote
hunieleza mimi kwa hiyo ninayafahamu
mambo yake mengi sana..” akanyamaza
kidogo na kuendelea
“ pamoja na kuwa mshauri wake wa
kila jambo analotaka kulifanya lakini kuna
mambo mengine ambayo sikubaliani naye
na ndiyo maana nimekuita hapa ili
kukueleza kuhusu suala moja kubwa
ambalo sijakubaliana naye”
“ Ndiyo nakusikilza safia” akasema
David akiwa na hamu ya kutaka kusikia
kile ambacho safia anataka
kumwambia.Moyoni alihisi lazima litakuwa ni suala la mahusiano yake na
Vicky
“ najua baada ya kukueleza suala hili
mimi na Vicky urafiki wetu utafikia
mwisho na tutageuka maadui wakubwa
lakini ni bora kuwa maadui kuliko
kushiriki katika jambo kama hili.”
“ Ni jambo gani hilo Safia? Akauliza
David
“ kwanza kabisa naomba niikuweke
wazi kwamba Vicky aliolewa na mzee
Zakaria kwa kufuata pesa na mali na si
kwamba ana mapenzi ya dhati na Yule
mzee.Baada ya mzee Zakaria kuanza
kusumbuliwia na maradhi ,tabia ya Vicky
ikabadilika sana.Alianza kubadilisha
wanaume kwa kisingizio kwamba mzee
Zakaria hana tena nguvu na uwezo wa
kumridhisha .Baada ya kuruka ruka na
wanaume mbali mbali hatimaye ukatokea
na mkaanzisha mahusiano.Hakuna mtu
mwingine anayefahamu kuhusu
mahusiano yenu zaidi yangu.Kutokea
kwako kumembadilisha kabisa
Vicky.David umemchanganya kabisa rafiki
yangu Vicky.Sijawahi kuona Vicky akiwa
amechanganyikwia namna hii na
mwanaume kama ilivyotokea
kwako.Ninamfahamu vizuri kuliko mtu yeyote Yule na ninapokwambia kwamba
amechanganyikiwa kwa jili yako
ninamaanisha kweli kachanganyikiwa na
hasikii la mtu juu yako.”akasema safia
akanyamaza kidogo . David akasema
“ Safia ni kweli nilijikuta nikiingia
katika mapenzi na Vicky lakini najilaumu
sana kwa kitendo kile cha kumzunguka
mzee Zakaria ambaye ananipenda na
kuniamini sana.Hata hivyo ninataka
nisitishe kabisa hiki tunachokifanya
kwani si kitu kizuri hata kidogo” akasena
David.
“ David si kwamba nakulaumu kwa
ulichokifanya kwa sababu najua haikuwa
ridhaa yako wewe kuingia katika
mahusiano na Vicky.Ninamfahamu Vicky
alivyo hata kama ungekataa angefanya
kila namna kuhakikisha anakupata.Ni
wanaume wengi tu wamekwisha nasa
katika mitego yake.Hata hivyo sijawahi
kuona akidata kwa mwanaume kama
ilivyotokea kwako.” Akanyamaza tena
kisha akasema
“ Siku moja Vicky alinifuata
akanichukua akanipeleka mahala kwa
ajili ya maongezi.Aliniambia jambo
ambalo sikuwa nimelitegemea kama
nitakuja kulisikia likitoka katika mdomo wake.Mpaka leo siamini ni shetani gani
amemkumba Vicky na kumfanya awe
namna hii” akasema safia
“ alikueleza jambo gani? akauliza
david
“ Alinieleza kwamba …” Safia akasita
kusema
“ Alikueleza nini safia? Akauliza
David
“ Alinieleza kwamba ..kutokana na
ugonjwa unaomsumbua mzee Zakaria
ameishiwa kabisa nguvu za kiume na
hawezi tena kumridhisha.Akanieleza
namna ulivyomchanganya kwa penzi la
kiwango cha juu unalompatia.Akaniambia
kwamba anatamani awe nawe kila
wakati,anatamani muishi pamoja kama
mume namke ..”
“ What ?!! david akashangaa
“Subiri kwanza niendelee david”
akasema safia
“ Vicky akasema kwamba anatamani
sana kama angeachana na mzee Zakaria
na akaishi na wewe lakini hilo
haliwezekani kwa sababu yuko katika
ndoa na mzee zakaria na akisema aondoke
kimya kimya basi ataukosa utajri mkubwa
wa mzee zakaria kwa hiyo akaja na
uamuzi .” “Aliamua kitu gani? Akauliza David
“Alisema kwamba anataka mpango
ambao utamuwezesha yeye kuupata
utajiri wa mzee Zakaria na papo hapo
wewe na yeey muishi kama mume na mke
kwa hiyo akaona njia pekee ni kumuua
mzee Zakaria” akasema Safia. Badala ya
kushangaa David akacheka kidogo
“ Safia thata not true.NInamfahamu
Vicky japokwa ni kwa muda mfupi lakini
sina hakika kama anaweza akafikia hatua
hiyo ya kumuua mzee Zakaria” akasema
David
“ David ninachokueleza ni kitu cha
kweli kabisa .Ninamfahamu Vicky zaidi ya
unavyomfahamu wewe kwa hiyo
ninachokueleza ni kitu cha kweli na wala
si jambo la kufanyia masihara hata
kidogo.Vicky amedhamiria kumuua mzee
Zakaria na mipango tayari imekwisha
fanyika kinachosubiriwa ni utekelezaji
tu.Hakuna mtu mwingine anayelifahamu
suala hili zaidi yangu na nimekueleza kwa
kuwa nafsi yangu inanisuta na
sikubalianai hata kidogo na kitu
anachotaka kukifanya huyu rafiki yangu.”
“ Oh mungu wangu ! akasema David
“ kwa hiyo amepanga kumuua vipi
mzee Zakaria? Kwa sumu? Akauliza david “ Tayari amekwisha ongea na mtu
mmoja anaitwa Chino ambaye ni jambazi
mkubwa .Wamepanga kwamba tukio hilo
lifanyike siku ya jumapili kuanzia saa nne
za usiku.Chino na kundi lake watavamia
nyumba ya mzee Zakaria na kumpiga
risasi.Itaonekana kama ni tukio la
ujambazi.Baada ya hapo Vicky atarithi kila
kitu na atakuwa huru kuishi maisha yake
akiwa na wewe” akasema Safia.
David akainama akazama katika
mawazo mengi .
“ David ! akaita Safia na kumstua
kutoka mawazoni
“ Nimekuita hapa nikueleze kuhusu
jambo hili ili kwa pamoja tuweze kuzuia
lisitokee.Tumzuie Vicky asiweze kufanya
jambo hili baya.”
“ Safia ahsante sana kwa kunieleza
jambo hili kubwa na zito.Najua haikuwa
rahsi kwako kumsaliti rafiki yako na
kuvujisha siri hii.Vicky ameingiwa na
shetani gani hadi akafikia hatu hii ya
kutaka kumuua Yule mzee? Sikufichi Safia
sijawahi kuona mwanamke ambaye
anatunzwa na kupatiwa kila
anachokihitaji kama Vicky.Lakini pamoja
na hayo bado hatosheki anamuibia mzee
Zakaria pesa nyingi sana na mwishowe amefikia hatua ya kutaka kumuua..Dah !
Nimestuka sana.”’
“ Ndiyo hivyo ilivyo David.”
“ Safia hapa nilipo kichwa changu
kinanizunguka na sijui nifanye
nini.Ninaomba uniache kwanza
nikapumzishe akili yangu na halafu
nitakupigia simu kesho kukueleza nini
ufanye .” akasema David
“ David kumbuka hii ni siri kubwa
sana na asifahamu mtu mwingine yeyote
Yule na wala Vicky asifahamu chochote
kama tayari unafahamu kuhusu mpango
wake”akasema Safia
“ Usijali safia nitajtahidi sana
kulifanya siri jambo hili na hatafahamu
mtu yeyote” akasema David
Baada ya maongezi kidogo david
akaondoka kwa makubaliano ya kuonana
tena kesho yake
“ Nimestushwa sana na jambo
alilonieleza Safia.Vicky ni shetani na hana
kabisa roho ya ubinadamu.Kumuua
mumeo wa ndoa ili arithi mali ! Dah !
inashangaza sana.Nimekuwa nikisikia
mambo haya katika simulzi na sikuwahi
kuhisi kama siku moja ninaweza
kulishuhudia suala hili .” akawaza David
akiwa ndani ya gari “ Sasa nimepata picha.lazima
atakuwa ni Vicky aliyemshawishi mzee
Zakaria kwamba amuandikishe kisheria
kama msimamizi wa mali zake
zote.Kumbe alikuwa na nia yake lakini
sasa ataumbuka.Mipango yake yote
haitafanikiwa.Utajiri anaoutafuta hata
kwa kumwaga damu hataupata kamwe.
Nitahakikisha mpango huu haufanikiwi
kwa namna yoyote ile.Ni bora nife mimi
kuliko afe Yule mzee.I will save him. I need
to find Pauline immediately .” Akawaza
david na kuchukua simu yake akazitafuta
namba za simu za Pauline akapiga lakini
simu haikuwa ikipatikana.
“ Amezima kabisa simu.hata kama
hatakuwepo nitahakikisha mpango huu
wa Vicky haufanikiwi.mwisho wake
umefika.Ni wakati sasa wa kulipiza kisasi
kwa kila ovu alilomfanyia Zakaria na
familia yake. Nilikuwa ninatafuta sana
namna ya kuweza kuachana naye na sasa
kila kitu kimejileta chenyewe.This is the
end of Vicky Madhahabu….”akawaza
David.
“ Sijawahi kuwa na usiku mrefu kama huu
katika maisha yangu.” Akawaza David na
kuinuka kitandani akatazama saa
yake.Ilikuwa ni saa nane za usiku lakini bado hakuwa amepata usingizi.Kichwa
chake kilijaa mawazo mengi sana.
“ Natafakari lakini ninashindwa
kupata jibu kwa nini utoe uhai wa
binadamu mwenzako kwa sababu ya mali?
Ama kweli binadamu wamegeuka wakatili
kuliko hata wanyama
mwitu.Ukimuangalia Vicky na mambo
anayoyafanya katu huwezi kuamini.Lakini
arobaini yake imekaribia sana.”
David akaichukua simu yake
akazitafuta namba za Pauline akapiga
lakini bado ya simu ya Pauline haikuwa
ikipatikana.
“ yawezekana hataki tena
mawasiliano na mtu yeyote ndiyo maana
ameamua kuizima kabisa simu yake.Au
atakuwa amebadili hata namba yake ya
simu ili aweze kusahau kabisa
kilichotokea.Pauline ni mtu muhimu sana
ambaye ninatakiwa kumpata.Anatakiwa
kufahamu kile kinachoendelea hapa
nyumbani kwao.”
Baada ya kutafakari sana David
akaamua kumuandikia ujumbe ili kama
ikitokea akawasha simuyake aupate..
“ Hata kama bado ana hasira na mimi
natunai akiupata ujumbe huu lazima
atanipigia simu.Huu si wakati wa kulumbana ni wakatiw a kuweka tofauti
zetu pembeni ” akawaza David na kujilaza
kitandani na mara kumbu kumbu Fulani
ile ambayo humtesa sana pindi
akiikumbuka ikamjia kichwani
“ Ninapoondoka hapa leo hii mimi si
baba yako na wala sikutambui kama
mwanangu.Ukimaliza kifungo chako usitie
mguu nyumbani kwangu .Nikikuona
nyumbani kwangu nitakuchapa risasi.”
Maneno haya yakajirudia kichwani
kwa David
“ Ouh No! nitafanya nini ili niweze
kulisahau kabisa tukio lile? Limekuwa
likinitesa kila mara.Sitaki kukumbuka
kabisa siku ile ambayo baba yangu
alinitamkia maneno yale nikiwa gerezani.”
Akainuka na kukaa.Machozi
yakamdondoka
“ kwa nini baba yangu anichukie
namna ile na kunitamkia maneno yale
makali ? Alipandikizwa chuki mbaya sana
kiasi cha kunichukia kiasi kile.Anyway
someday I’ll be back home and I will save
my father.I will show him that he was
wrong about me..” Akawaza David ****************
Saa mbili za asubuhi Tino alikwisha
amka .Haikuwa kawaida yake kuamka
asubuhi namna hii.
“ Kaamka asubuhi asubuhi lazima
kuna mahala anakwenda.Leo lazima
niufahamu ukweli” akawaza Vivian
akimtazama mumewe akivaa halafu
wakaenda kunywa chai pamoja
“ Nitachelewa kurudi Leo na
yawezekana nisirudi kabisa.” akasema
Tino. Viviana akamtazama na kuuliza
“ Tino whats going on? Mbona siku
hizi umebadilika kasi hiki? Akauliza
“ Nimebadilika nini Vivian?
“ Hukuwa namna hii.Ulikuwa
unaniamabia kila kitu ,kama una
tatizo,kama una safari lakini kwa hivi sasa
mambo yamekuwa tofauti
kabisa.Hunielezi chochote na hata kama
una tatizo linabaki kuwa ni siri yako.Mimi
ni mkeo na ndiye mtu wako wa karibu
kabisa kwa hiyo ni haki yangu kujua kama
una tatizo ama vipi.Unaniambia tu
kwamba utachelewa kurudi au waweza
usirudi kabisa na huniambii unakwenda
wapi na kwa nini usirudi.Tafadhali Tino
kama kuna tatizo naomba unieleze kuliko kuendelea kuniweka katika wakati
mgumu kiasi hiki” akasema Vivian.Tino
akamalizia chai katika kikombe chake
akanyakua funguo zake akaelekea katika
gari lake akaingia na kuondoka.Vivian
naye akainuka na kukimbi a chumbani
kwake akachukua funguo ya gari lake na
kutoka akaanza kumfuata mume wake.
“ Leo lazima nitafahamu kila
kitu.Nitamfuatilia kila mahala anakoenda
“ akawaza Vivian akiendelea kumfuatilia
mume wake kwa makini
Kituo cha kwanza cha Tino baada ya
kutoka nyumbani ilikuwa ni dukani
kwake.Akashuka garini na kuingia
dukani.Vivian alisimamisha gari umbali
wa kama mita mia mbili hivi halafu
akashuka na kutembea hadi katika baa
moja iliyoko karibu na duka la Tino
ijulikanayo kama Lasana Bar.Pale
panaegeshwa taksi bubu nyingi,akachagua
taksi moja ambayo ingemfaa kwa shughuli
yake akaingia na kisha taksi ile ikaenda
kuegesha si mbali sana na dukani kwa
Tino.
“ Dada kuna mtu tunamsubiri?
Akauliza dereva taksi
“ Kuna mtu tunahitaji kumfuatilia.”
Akajibu Vivian. Baada ya dakika thelathini toka Tino
aingie dukani akatoka na kuingia katika
gari lake akaondoka.
“ Tulifuate lile gari”akasema Vivian
“ Yule ni papaa Tino magari
“akasema Yule dereva taksi
“ Ni mume wangu.usiogope
Mfuate.Lakini kuwa makini sana
asigundue kama anafuatiliwa” akasema
Vivian
“ Wewe kumbe ndiye mke wake?!!
Yule dereva akashangaa sana
“ kwani vipi? Sifai kuwa make wake?
“ Unafaa sana shangazi nilihitaji tu
kufahamu” akasema Yule dereva taksi na
kuendelea kumfuata Tino.
Tino aliikamata barabara kuu ya
Arusha Moshi huku Vivian na Yule dereva
taksi wakiendelea kumfuata kwa nyuma
bila ya yeye kuwa na habari kama
anafuatiliwa.
Safari iliendelea hadi wakafika Usa
river na Tino hakuonyesha dalili zozoteza
kusimama .
“ Huku anakwenda wapi? Ni lazima
mwanamke wake atakuwa huku..au
amepanga akutane na mwanamke huku
mbali ili wasionekane” akawaza Vivian Hatimaye wakafika Bomang’ombe na
Tino akapunguza mwendo na kukata
kushoto..
“ Anaelekea nyumbani kwao.Hii ni
njia inayoyoeleka nyumbani kwa wazazi
wake.Mbona hakuniambia kama
anakwenda nyumbani kwao? Ama kweli
Tino amebadilika sana.Lakini nijambo
zuri kama anakwenda kwao ili
tukakutane kwa wazazi wake niwaeleze
tabia ya mtoto wao.Yawezekana tukapata
suluhu .” akawaza Vivy na kumuelekeza
dereva aendelee kumfuatilia Tino.
Kama alivyokuwa amehisi ndivyo
ilivyokuwa.Tino alikuwa anaelekea
nyumbani kwa wazazi wake wanaoishi
Bomang’ombe.
Vivian akamlipa dereva dereva pesa
yake halafu akashuka garini na kwenda
kugonga geti.Aliyefungua ni mdogo wake
Tino ambaye alifurahi sana kuonana na
Vivian
“ Ouh wifi !!akasema Yule mdogo
wake Tino wakakumbatiana
“ karibu sana wifi yangu..Kwema
huko Arusha?akauliza
“ Arusha kwema kabisa haika”
“ Karibu sana Wifi
yangu.Umeongozana na kaka naye amewasili muda si mrefu .” akasema Haika
na kumshika mkono wifi yake wakaelekea
sebuleni.
“ Vivian ?!!..Tino akashangaa baada
ya kumuona mke wake pale kwao
“ Kumbe ulikuwa na safari ya kuja
huku ? Si ungeniambia kama unakuja kwa
sababu hata mimi nilikuwa nimepanga leo
nije kumsalimu mama.” Akasema
Vivian.Tino akamtazama kwa macho
makali na kusema
“ Hukuwa na ratiba ya kuja huku
ulikuwa unanifuatilia.Ulidhani kuna
mahala ninakwenda? Akauliza Tino kwa
ukali
“ Ndiyo nilikufuata kutaka kujua
unakwenda wapi.kama ulikuwa unakuja
huku kwa nini usingeniambia? Akauliza
Vivian naye kwa ukali kidogo
“ kwanini unataka kila kitu
nikwambie?
“ kwa sababu mimi ni mkeo na
ninapaswa kufahamu kila kitu
unachokifanya ! akasema Vivian kwa sauti
ya juu
“ Unataka kufahamu kila
ninachokifanya !!.Wewe unanieleza kila
unachokifanya? Akauliza Tino “ Sijawahi kukuficha kitu.Chochote
ninachokifanya.Kila kitu
ninakueleza..”akasema Vivian
“ Una hakika na unachokisema?
‘Ndiyo nina hakika nacho.Hakuna
siku nimewahi kukuficha kitu chochote.”
“ Jamani kuna nini humu? Akauliza
mama yakeTino aliyetokea ghafla
palesebuleni.Wakati Tino na mke wake
wanawasili yeye hakuwepo alikuwa
shambani
“ Mama shikamoo” Vivian
akamsalimu mama mkwe wake
“marahaba mama hujambo?
Kisha salimiana wote wakaketi
“ Niliuwa shambani nikapigiwa simu
na Haika kwamba nyote
mmekuja,nikastuka kidogo kwa nyote
kuja kwa pamoja.Nilipokuja nimesikia
mabishano kuna nini kimetokea? Akauliza
mama yake Tino
“ hakuna tatizo mama bali sikujua
kama mwenzangu naye anakuja
huku.Nilishangaa ndiyo nikawa namuuliza
kama alikuwa na safari ya kuja huku kwa
nini hakuniambia? Akasema Tino
“ Hapana mama si kweli
anavyokwambia Tino.Kuna tatizo “
Akasema Vivian “ mama anakudanganya huyu
hakuna tatizo lolote.Kama ana tatizo basi
ni lake binafsi lakini mimi na yeye hatuna
tatizo” akasema Tino
“ Mama kuna tatizo kati yetu na
limekuwa jambo jema sote tuko hapa
,tulizungumze suala hili” akasema Vivian.
“Mama usipteze muda wako hakuna
tatizo lolote”akasisitiza Tino
‘ jamani hebu tuelewane.Nyote mko
hapa na kama kuna tatizo basi tuongee na
tuliweke sawa.Tino ulinipigia simu jana na
ukaniambia kwamba una tatizo na utakuja
leo kuongea name.Ni tatizo gani hilo?
Ndilo hilo analolisema mwenzako?
Akauliza mama yake Tino
“ Mama ,mimi matatizo yangu ni
mengine kabisa.kama yeye ana tatizo basi
aliweke wazi tulisikie”akasema Tino
“ Vivy hebu tueleze kuna tatizo gani
mama yangu? Akauliza mama Tino
“ Mama ,Tino anaogopa kuweka
wazi lakini ni kweli kabisa ndani kwetu
kuna matatizo na yeye ndiye tatizo”
“Mimi ?!! Tino akahamaki
“ Ndiyo wewe ni tatizo” akasema
Vivian.Tino akasimama tayari alianza
kupandwa na hasrira “’Unasema mimi ni tatizo? Akauliza
kwa ukali.Mama yake akamtuliza akakaa
chini
“ Jamani kama mmekuja hapa mna
matatizo hebu tukaeni kama watu wazima
tuongee na tutaweke sawa matatizo
yenu.Vivi hebu sema kuna tatizo
gani?akauliza mama Tino
“ Mama ,mimi na Tino tumekaa
kipindi kirefu sasa na hakujawahi kutokea
na tatizo lolote.Hivi majuzi sote kwa
pamoja tuliazimia kwamba sasa umefika
wakati wa sisi kufunga ndoa na kuishi
kihalali kabisa.Wakati ninaanza kuishi na
Tino nilikuwa ndani ya ndoa kwa hiyo
mpaka sasa mimi ninatambulika kama ni
mke halali wa Yule mume wangu wa
zamani.Ili mimi na Tino tuweze kufunga
ndoa,inalazimu kwamba mimi na mume
wangu ndoa yetu itenguliwe na
kanisa.kwa bahati nzuri hata mume
wangu wa zamani naye alikuwa na
mawazo kama ya kwangu na tayari naye
amepata mchumba na tukakubaliana
kwamba tuanze taratibu za kutengua ndoa
yetu.Wakati taratibu zikiendelea ghafla
mwenzangu akabadilika tabia.Akaanza
kuwa mlevi wa kupindukia.Anakunywa
pombe hadi anajisahau.Kuna nyakati haonekani nyumbani hata siku mbili na
hatoi maelezo yoyote.Nyumba yetu haina
amani tena na hakuna chochote
tunachokiongea wala kukipanga.Muda
wote huwa amekasirika na hataki
kuulizwa kitu chochote.Akiamka ni yeye
na pombe.Leo hii unamuona katika hali hii
ni kwa sababu alijua anakuja kwako ndiyo
maana hajanywa pombe lakini siku zote
mida kama hii huwa amelewa chakali.”
Vivian akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“ Kutokana na tabia yake kubadilika
ghafla nimelazimika leo hii kumfuata ili
kujua anakwenda wapi kwani katika simu
yake kumekuwa na jumbe kadhaa toka
kwa wanawake mbali mbali.Mama nina
hakika mwanao tayari ana
mwanamkemwingine na ndiyo maana
hataki niliseme hili mbele yako” akasema
Vivian
“ Umemaliza? Akauliza Tino
akionyesha wazi kukerwa sana na maneno
yale ya Vivian
“ Jamani mbona siwaeleweni nyie
watoto? Mna matatizo gani? Tino haya
anayoyasema mkeo ni ya kweli ?
“ Ameeleza vizuri sana kuhusu
kilichotokea na kinachoendelea.Ni kweli nimekuwa nikilewa sana kwa siku hizi
mbili tatu lakini nimefikia hatua hii kwa
sababu yake yeye mwenyewe.Sikuwa na
tabia ya kulewa hovyo hata wewe mama
unanifahamu lakini nimeshindwa
kuvumilia na ili niondoe mawazo
niliyonayo inanilazimu ninywe pombe”
akasema Tino
“ Usinisingizie mimi wakati wewe
ndiye mwenye matatizo.Kuna kitu gani
unachokikosa kwangu hadi ukaenda
kutafuta wanawake huko nje? Akasema
Vivian kwa ukali
“ Tino mkeo amekwisha eleza tatizo
lake na wewe tueleze tatizo gani
linakufanya wewe ufikie hatua ya kunywa
pombe kiasi hicho? Kuna kitu
amekukwaza? Akauliza mama yake Tino
“ Mama kwa kuwa sote tuko hapa
hakuna haja ya kuficha kitu na kwa kuwa
yeye mwenyewe amekiri kwamba kuna
tatizo na akanilaumu mimi kwamba ndiye
chanzo cha tatizo sasa ni bora tuweke wazi
kila kitu ili tujue kitakachoendelea.”
Akasema Tino.Akanyamaza akavuta pumzi
ndefu na kusema
“ Mama ni kweli alivyokwambia Vivy
kwamba bila kushawishiwa na mtu
tuliamua sisi wenyewe kwa hiari yetu kwamba umefika wakati wa sisi kufunga
ndoa na kuishi pamoja.Hatukuwataarifu
kuhusu suala hili kwa sababu tulisubiri
kwanza taratibu za kutengua ndoa ya
Vivian na mume wake wa zamani
zikamilike.Wakati tukilisubiri hilo
nikapata taarifa za kustusha kidogo “
akanyamaza kidogo ,akaendelea
“ Niliumwa sikio na watu
wanonipenda kwamba mke wangu hana
uwezo wa kuzaa”
Sura ya Vivian ikabadilika baada ya
kusikia kauli ile.Tino akaendelea
“ Kipindi chote tulichokaa pamoja
nimekuwa nikimsisitiza sana kuhusu
suala la kupata mtoto lakini akasema
kwamba atanizalia mtoto pindi tukifunga
ndoa.Nilivumilia kwa sababu ninampenda
sana mke wangu na ndiyo maana
nilipopewa taarifa hizi sikutaka
kuzikubali mara moja ikanilazimu nifanye
utafiti ili nifahamu kama nilichoambiwa ni
cha kweli ,na nikathibitishiwa bila chenga
kwamba Vivian alikuwa na tabia ya kutoa
mimba kwa sababu hakuwa tayari kuzaa.
Mara ya mwisho alipotoa mimba aliumwa
sana na ikagundulika kwamba alitoa
mimba vibaya na kulikuwa na sifa katika
kizazi chake kwa hiyo akafanyiwa upasuaji wa kuondoa kizazi .Wakati huo
mimi nilikuwa nje ya nchi katika safari
zangu za kibiashara na Vivy akanificha
akaniambia kwamba amefanyiwa upasuaji
wa kuondoa uvimbe ndani ya tumbo.Kwa
muda wote huu Vivy amekuwa
akinidanganya kwamba atanizalia mtoto
pindi tukifunga ndoa wakati akijua kabisa
kwamba hana uwezo wa kuzaa….”
Ghafla Vivian akaanguka chini
akapoteza fahamu………………….
Vivian akapatiwa huduma ya kwanza
akazinduka.Bado hakuonekana kuwa
katika hali nzuri hivyo kuwalazimu Tino
na mama yake wampeleke hospitali ili
aweze kuchunguzwa afya yake.Alipelekwa
katka hospitali ya St Joseph mjini moshi
ambako alipumzishwa kwa muda.Wakati
madaktari wakiendelea kumuangalia
,Tino na mama yake walikuwa wamekaa
nje wakisubiri madaktari wamalize kazi
yao
“ Tino yale mambo uliyoyasema pale
ndani ni mambo ya kweli? Akauliza mama
yake
“ Mama yale ni mambo ya kweli
kabisa.Vivian ni mke wangu na siwezi
kumsemea uongo.Hata mimi
nilipoambiwa suala hili kwa mara ya kwanza nilistuka sana na ilikuwa vigumu
kuamini kama linaweza kuwa
kweli.Nilikorofishana hadi na marafiki
zangu walionipa taarifa hizi lakini badae
nikaona ni bora niutafute
ukweli.Nilionana na daktari ambaye
alimfanyia Vivian upasuaji huo wa
kuondoa kizazi na akanihakikishia
kwamba ni kweli mke wangu hana uwezo
tena wa kuzaa.Jambo hili mama
liliniumiza mno .Unajua kwa kwa miaka
mingi kiu yangu kuibwa ni kupata
mtoto.Ninazo mali nyingi nani basi
atakuwa mrithi wangu ? Niliumizwa mno
na ndiyo maana nikaanza kunywa pombe
kupoteza mawazo.Leo nilikuja ili
kukutaarifu kuhusu suala hili na
kukueleza kuhusu maamuzi yangu
nitakayochukua lakini kumbe Vivian naye
alikuwa ananifuata kwa nyuma akidhani
labda ninakwenda kwa mwanamke
mwingine.Sina mwanamke mwingine na
kama ningehitaji kuwa na wanawake
wengine ningekwisha kuwa nao wengi au
hata kuwa na watoto wengi tu wa nje
lakini sijafanya hivyo kwa sababu
ninampenda sana mke wangu,lakini kwa
hili alilolifanya itanilazimu kufikiri mara mbili tena kama mimi na yeye tunaweza
kuendelea tena ama la” Akasema Tino
“ Pole sana Tino.Najua jambo hili
limekuumiza sana lakini ninakushauri
usichukue maamuzi yoyote kwa sasa.Ni
mapema sana bado kufanya maamuzi
yoyote.Suala hili linatakiwa lijadiliwe na
muafaka ufikiwe.Kukosa mtoto si sababu
ya ninyi kutengana au kuwa ni chanzo cha
ugomvi ndaniya nyumba.Kama kweli
mnapendana kwa dhati mnaweza mkaishi
maisha yenu yenye amani na furaha hata
kama hamna watoto.Kuna watoto wengi tu
wasio na wazazi mnaweza mkamchukua
mmoja mkamtunza na akawa mtoto
wenu.” Akasema mama yake Tino
“ Sijui mama kama tunaweza
tukaishi tena kwa amani kama
mwanzo.Kinachoniumiza zaidi ni kwamba
Vivian alinificha kuhusu suala hili na
akawa ananihakikishia kila siku kwamba
atanizalia watoto pindi tukiingia katika
ndoa.Alifahamu kabisa kwamba tukiingia
katika ndoa sintakuwa na ujanja tena
kwani sintaweza kumuacha ,Hili
limeniumiza sana.Ingekuwa vizuri kama
angenieleza ukweli toka mapema ili nijue
lakini amenificha na kunidanganya.Mama
mwanamke huyu hafai kabisa.Kama ameweza kunificha kuhusu jambo hili ,ni
mambo mangapi basi atakuwa
amenidanganya? Ninahitaji mwanamke
ambaye nitamuamini kwa kila jambo
ambaye hatanificha kitu chochote kile
hata kiwe kigumu namna gani lakini huyu
amekuwa ni mlaghai..She’s there for my
money only.”
“ Tino baba,hebu naomba upunguze
hasira na baada ya kutoka hapa
tutakwenda kuliongelea suala hli na
kufikia maamuzi.Ni kweli mkeo amekosea
kukuficha kuhusu suala hili na
ninamlaumu kwa hilo lakini bado mnayo
nafasi ya kuyaweka mambo yote pembeni
na kuanza upya maisha yenu huku
mkifahamu kabisa kwamba hamtakuwa
na mtoto wa damu yenu.Ninafahamu
mnapendana sana na mmekaa muda
mrefu bila mataizo ya aina yoyote
ile.Tafadhali Tino usifikirie kabisa
kumuacha mkeo Anakupenda sana”
“ Upendo ?!! Tino akaonekana
kuanza kupandisha sauti kidogo
“ Hakuna upendo hata kuidogo
mama.Mwanamke huyu hanipendi kabisa
.Kama kweli angekuwa ananipenda
asingethubutu kutoa mimba na kuua
watoto wangu wasio na hatia.Hata kama ukimtetea vipi ,Vivian hafai na hawezi
kuwa mama.Huko alikotoka kwa mume
wake wa zamani alimuacha mtoto mdogo
kabisa na akakikimbia umasikini wa
mume wake na kufuata utajiri wangu.Ni
mwanamke ambaye anathamini pesa
kuliko kitu chochote kile.Mama
ninamfahamu Vivian kuliko mtu mwingine
yeyote kwa hiyo hakuna haja ya
kumtetea.Mimi nimekwisha fanya
maamuzi yangu na sintarudi nyuma
tena.Nimeishi naye muda mrefu kama mke
wangu na niko tayari kugawana naye kila
kilicho changu lakini si kuendelea kuishi
naye kama mke wangu tena.” Akasema
Tino
“Tino tusiongee mambo haya
makubwa hapa hospitali.Tutaongea
tukifika nyumbani.Nimempigia simu
mjomba wako anakuja toka Machame na
kwa pamoja tutalijadili suala hili na
kupata muafaka.” Akasema mama Tino
“ Hahaha ! mama hakuna muafaka
utakaopatikana.Tayari nimekwisha fanya
maamuzi yangu na siwezi
kuyabadilisha.Imetosha sasa kuishi
maisha ya ulaghai.Ninataka nijipange upya
kuanza maisha yangu na mtu mwngine
ambaye ninaweza nikamuamini na si huyu.Kwa hiyo hakuna haja ya
kuwasumbua akina mjomba ,hakuna
watakachokibadilisha katika maamuzi
yangu” akasema Tino na mama yake
hakusema kitu tena
Uso wa Pauline haukukaukiwa
tabasamu wakati anakagua maendeleo ya
ukarabati wa nyumba atakayoitumia
kufungulia hospitali maalum ya vipimo .
“ Namshukuru Mungu kila kitu
kinakwenda vizuri kwa sasa ni kuanza
kuandaa pesa kwa ajili ya kununulia
mashine na vifaa vingine.Ni pesa nyingi
inahitajika .Nina kiasi cha pesa benki
kinatohsa sana kuanzia na vile vile
nitaongea na na baba naye lazima
ataniongezea kiasi fulani cha pesa na kiasi
kingine nitakopa benki,.Nataka jumamosi
nikienda Arusha nianze taratibu za kupata
mkopo.Najua siwezi kuchukua muda
mrefu kwa sababu baba anafahamika sana
katika mabenki yote kwa hiyo ndani ya
wiki moja tu nina hakika nitakuwa nimepata pesa ninayoihitaji” akawaza
Pauline
“ Nimemkumbuka sana baba
yangu.Natamani kujua maendeleo yake
.Najua hata yeye ana hamu sana ya
kunisikia na kujua ninaendelea vipi.Kimya
changu lazima kitampa wasi wasi mkubwa
sana.Nikifika hotelini leo lazima nimpigie
simu nimjulie hali.” Akawaza na mara
akakumbuka kitu
“ Nikirudi Arusha lazima nitakutana
na David.Sitaki kabisa hata kumtia
machoni Yule kijana.Alinifanyia kitu
kibaya na kuniumiza vibaya sana.Ninataka
nimsahau kabisa katika maisha
yangu.Lakini kwa upande mwinginge ni
yeye aliyenifanya nikaondoka Arusha na
kuja huku Moshi ambako nimepata wazo
lingine zuri la biashara na akili yangu
imepanuka sana.Kwa sasa mimi si Pauline
Yule ambaye alimfahamu wiki kadhaa
zilizopita.” Akasimama na kuegemea
nguzo
“ Lakini kwa nini ninaogopa kuonana
naye? Kwa sasa anaendelea na maisha
yake na mpenzi wake Tamia na
ninawatakia kila la heri katika mapenzi
yao na kwa hiyo sipaswi kabisa kuogopa
kuonana naye.Kuanzia sasa sitakiwi kumkimbia hata kidogo .I’ll face
him.Natakiwa kumuona ni mtu wa
kawaida kabisa” akawaza Pauline
Baada ya kutoka katika ukaguzi
akapita madukani ambako alinunua
baadhi ya vitu alivyovihitaji kisha
akarejea hotelini .Kitu cha kwanza
alichokifanya ni kufungua begi lake
akachukua simu akaitazama na kisha
akaiwasha.Jumbe nyingi zikaingia katika
simu yake hakushughulika nazo moja kwa
moja akazitafuta namba za simu za baa
yake akapiga
“ Hallow Pauline? Akasema mzee
Zakaria baada ya kupokea simu
“ Baba shkamoo”
“ Marahaba mwanangu habari za
huko uliko? Mbona kimya sana?
Nimekuwa ninajiuliza sana sababu ya
wewe kuizima kabisa simu yako na
kutokutaka kabisa kuwasiliana na sisi”
akasema mzee Zakaria
“ Baba utanisamehe kwa hilo lakini
nilikuwa sehemu ambayo mtandao
haupatikani kirahisi ndiyo maana
nikashindwa kuwasiliana
nawe.Unaendeleaje baba? Akauliza
“ Ninaendelea vizuri sana.Hali yangu
inazidi kuboreka.Kwa sasa ninapumzika tu na kufanya sughuli ndogo ndogo
,siumizi kichwa tena kwani David
ananisaidia sana katika masuala ya
kibiashara.Pauline ulikuwa sahihi sana
kunitaka kumuajiri David.Ni mtu sahihi
kabisa.Anafanya kazi zake vizuri sana na
kwa uaminifu mkubwa na mpaka sasa
amekwisha okoa pesa nyingi sana
zilizokuwa zinapotea kwa kukosa
usimamizi. Akasema mzee Zakaria na
Pauline Akakaa kimya
“ Pauline ! akaita mzee Zakaria
baada ya kuona mwanae amekuwa kimya
sana
“ Nipo baba” akajibu
“ Vipi maendeleo yako kwa ujumla?
“ Ninaendelea vizuri sana na wala
usihofu kitu baba”
“ Nafurahi kusikia hivyo” akasema
mzee Zakaria
“ Baba nimekupigia kukujulia hali na
kukutaarifu kwamba kesho jumamosi
nitakuja Arusha kuna jambo ninataka kuja
kuongea nawe .Vile vile ninaweza
kuambatana na rafiki zangu mmoja ama
wawili.” akasema Pauline
“ Ouh ! hizo ni taarifa nzuri sana.Kwa
kweli nitafurahi sana kukuona
Pauline.Ninahitaji sana kukuona.Karibu tena nyumbani.Nitamwambia dada yako
wa kazi aanze kukuandalia chumba chako
haraka pamoja na cha wageni wako”
akasema mzee Zakaria
“ Haya ahsante baba nadhani
nitakupigia tena hiyo jumamosi” akasema
Pauline na kukata simu.Akapata wazo la
kuanza kuzisoma jumbe zile nyingi lakini
wakati akisoma akakutana na ujumbe
uliotoka kwa David ambao ulimstua
kidogo.Akausoma na kuurudia tena kwa
mara ya pilI na ya tatu.
“ Huyu David ana maanisha nini
kunitumia ujumbe kama huu? Mbona
simuelewi? Akajiuliza kisha akaamua
kumpigia.
“ Hallo Pauline.Mzima? Siamini kama
nimeisikia tena sauti yako” akasema David
baada ya kupokea simu ya Pauline
“ David sitaki maneno mengi
,nimeamua kukupigia simu baada ya
kuupata ujumbe wako ambao
umenishangaza kidogo na wala sijakupigia
simu kwa ajili ya jambo lingine kwa hiyo
naomba tafadhali unieleze maana ya
kunitumia ujumbe wa namna hii” akasema
Paline
“ Pauline kwanza nashukuru kwa
kuamua kunipigia.Nimeona nikutumie ujumbe ule ili kukutaka kama uko
karibuna Arusha basi urejee nyumbani
mara moja,there is something going on
here.You must be there before Sunday”
akasema David
“ David kuna nini kiasi cha kunitaka
nirejee haraka nyumbani? Mbona baba
nimeongea naye muda si mrefu na
anaendelea vizuri tu? Kuna tatizo gani
lingine?
“ Kuna jambo kubwa linendelea
huku .Pauline najua mmi na wewe kwa
sasa tuna tofauti zetu lakini naomba
tuziweke pembeni kwa wakati huu na uje
Arusha mara moja.This is for you,your
father and your family” akasema David
“ David kuna jambo gani? Kwa nini
usinieleze kwenye simu?
“ Siwezi kukueleza simuni
Pauline.Tafadhali naomba uje Arusha
mara moja.Na tafadhali usimwambie
chochote mzee Zakaria wala madam Vicky
kama nimekwambia chochote.This is
between us” akasema David
“ David mbona unaniogopesha?
Akasema Pauline
“ Usiogope Pauline ila jitahidi sana
kwa namna yoyote ile uje Arusha kabla ya
jumapili” akasisitiza David.Pauline akabaki kimya kidogo akafikiri kisha
akasema
“ David are you sure its something
serious ??
“ Very very serious” akasema David
“ Ok sawa.Kwa mara nyingine tena
ninalazimika kukuamini lakini make sure
its real something very serious.” Akasema
Pauline
“ Nakuhakikishia Pauline its
something very serious”
“ Sawa nitakuja jioni ya leo badala ya
kesho kama nilivyokuwa nimepanga “
akasema Pauline
“ Ahsante sana nashukuru Pauline
kwa kunielewa. Ninakusubiri jioni ya
leo.By the way how are yo………………”
David hakumaliza sentensi yake Pauline
akakata simu
“ Amekata simu !!! lakini nashukuru
kwamba amenielewa.” Akawaza David
Baada ya kukata simu Pauline
akabaki katika mawazo mengi
“ Ni jambo gani ambalo David
atakuwa ananiitia Arusha kiasi akaweka
msisitizo mkubwa namna hii? Lazima
kutakuwa na suala kubwa ambalo
limetokea na ambalo hataki mtu mwingine
alifahamu zaidi yangu.Itanilazimu niende Arusha jioni ya leo badala ya kesho kama
nilivyokuwa nimepanga.kwa msisitizo ule
lazima kuna kitu si bure.Itanibidi
nimtaarifu Sanya kuhusu safari hii ya
dharura .Vile vile nimtaarifu Alfred kwani
alitaka kuongozana nami kwenda Arusha
kesho lakini haitawezekana tena kwani
mimi ninaondoka leo jioni” Akawaza
Pauline kisha akazitafuta namba za simu
za Alfred akampigia.
“ Hallo my queen” akasema Alfred
baada ya kupokea simu.Pauline
akatabasamu na kusema
“ You have your queen at home
Alfred so please don’t call me queen.”
Akasema huku akitoa kicheko kidogo
“ Vyovyote vile itakavyokuwa you
are,and you’ll forever be my queen.”
Akasema Fred
“ Any way tuachane na hayo Fred
siwezi kushindana nawe.Nimekupigia
kukutaarifu kwamba nimepata dharura
natakiwa Arusha jioni ya leo kwa hiyo ile
safari yetu tuliyoipanga kesho
haitakuwepo tena.I’m so sorry for that
Alfred najua ulitamani sana kuongozana
nami Arusha.” Akasema Pauline “ Pauline you don’t have to be
sorry.Nitaongozana nawe jioni ya leo
kwenda Arusha” akasema Alfred.
“ Stop that Alfred.What we are doing
is not right ..” akasema Pauline
“ Pauline tafadhali tusibishane
kuhusu hili.Nitangozana nawe jioni ya leo
kwenda Arusha” akasema Alfred
“ Sawa Alfred kama umesisitiza
hivyo” akasema Pauline kisha akaagana na
Fred kwa miadi ya kukutana saa kumi na
mbili za jioni kwa ajili ya kuanza safari ya
kuelekea Arusha
“ Kuna nyakati ninaogopa sana kwa
namna Alfred alivyokufa akaoza
kwangu.Hasikii la mtu tena juu
yangu.Yuko tayari kwa lolote lile.Nina
wasi wasi ndo ayake itaingia katika
mgogoro mzito muda si mrefu.Mke wake
ataumia sana kwa kitakachotokea lakini
nitafanya nini sasa? I’m in love too with
Alfred and I cant let him go…Kwa muda
huu mfupi ameniingia katika kila mshipa
wa mwili wangu .I know I’m doing the
wrong thing but I don’t have the power to
say No to Alfred..” akawaza Pauline kisha
akatoka chumbani kwake akaelekea
chumbani kwa Sanya kumtaarifu kuhusiana na safari ile ya dharura.Sanya
akakubali kuongozana naye jioni ile
*********************
Alfred alirejea nyumbani kwake saa
kumi na moja za jioni akaoga haraka
haraka kisha akachukua sanduku lake
dogo na kuanza kupakia baadhi ya vifaa
vyake muhimu.
“ Una safari? Akauliza Grace
aliyeingia ghafla mle chumbani.Wakati
Fred aliporejea nyumbani mke wake
hakuwepo. Fred akastuka
“ Ouh my love ,umenistua sana
ulivyoingia ghafla kama malaika”
Akasema na kumkumbatia akambusu
“ Mbona unapakia una safari?
Akauliza Grace
“ Ndiyo nina safari.Nimeitwa kwa
dharura hospitali ya Serian Arusha.Kuna
mgonjwa anahitaji upasuaji wa haraka
usiku wa leo” akasema Alferd huku
akiendelea kupakia nguo na vifaa vyake
vidogo vidogo
“ Pole sana.” Akasema Grace
“ Ahsante sana. Mke wangu”
“ Lini utarejea ? akauliza Grace “ Sina hakika ndiyo maana
nimechukua nguo za kutosha siku mbili
tatu “ akajibu Alfred kisha akaagana na
mke wake akaingia garini na kuondoka.
Mara tu alipoondoka mke wake naye
akaingia katika gari lake na kuanza
kumfuatilia.Bila kujua kama anafuatiliwa
moja kwa moja Alfred akaelekea katika
hoteli anakoishi Pauline.Akaegesha gari
na kushuka akapanda ghorofani
“ Nilijua tu lazima atakuja
hapa.Pauline aliniambia kwamba atakuwa
na safari ya kuelekea Arusha kesho ghafla
Fred naye anakuja na kuniambia amepata
safari ya dharura kwenda Arusha.hawa
watu kuna mchezo wananicheza.Ngoja
nione kitakachoendelea” akawaza Grace
akiwa ameegesha gari upande wa pili wa
maegesho ya pale hotelini .
Baada ya dakika kama kumi hivi
akamshuhudia Alfred akiwa ameongozana
na Pauline na msichana mwingine ambaye
hakumfahamu wakaingiza mabegi katika
gari la Alfred kisha wakaondoka
“ Nilijua tu lazima kuna kitu
kinaendela kati ya Fred na
Pauline.Wanaelekea Arusha.” Akawaza
Grace huku akiangusha machozi… *************************
Mpaka saa kumi na moja za jioni hali ya
Vivian ilikuwa nzuri na madaktari
walithibitisha kwamba anaweza akarejea
nyumbani kwani hakuwa akisumbuliwa
na kitu chochote .
“ Pole sana Vivian” akasema Tino
lakini Vivian hakujibu k itu
“ Madaktari wamekwisha toa ruhusa
.Tunaweza kuondoka .Tutaelekea kwanza
nyumbani kwa mama kuna maongezi ya
kifamilia na halafu tutaelekea Arusha”
akasema Tino
“ Martin sitaki kabisa kwenda
sehemu yoyote .Ninataka kurudi
nyumbani Arusha.Nirudishe
nyumbani”akasema Vivian
“ Vivian kuna mambo mengi
ambayo tunatakiwa kuyajadili kama
familia.Tutapitia kwanza nyumbani kwa
mama halafu tuelekee nyumbani Arusha.”
“ Martin nimekwambia kwamba
siendi sehemu yoyote ile.Nataka kurudi
nyumbani Arusha.Kama kuna mambo ya
kuongea tutakwenda kuongea huko huko
nyumbani” akasisitiza Vivian
“ Sawa Vivian kama hivyo ndivyo
unavyotaka basi tutakwenda Arusha.Jiandae tuweze kuondoka”
akasema Tino kisha akatoka nje na
kuongea na mama yake kidogo halafu
wakaingia ndani wakamsaidia Vivian
kutembea hadi garini kisha wakaondoka
pale hospitali.
“ Nani kamueleza Martini kuhusu
suala hili ?.Ama kweli dunianihakuna
hakuna siri ya watu wawili.Hakuna mtu
aliyekuwa akifahamu kitu chochote
kuhusiana na jambo hili.Kumbukumbu
zangu hazinionyeshi kama nimewahi
kumueleza mtu mwingine yeyote
kuhusiana na suala hili.Nilifanya jambo
lile kimya kimya na aliyefahamu ni daktari
na wale wauguzi wawili .Sijui sirihii
imevujajena kumfikia Tino.” Akawaza
Vivan akiwa ndaniya gari
“ Nilikuwa najiuliza sana sababu ya
Tino kubadilika ghafla namna hii kumbe
ni baada ya kuzipata taarifa hizi.Ni nani
lakini aliyemwambia? Ama kweli kuna
watu ambao hawataki kutuona mimi na
Martin tukiishi maisha ya furaha.Kwa sasa
baada ya Martin kuligundua jambo
hili,sina ujanja tena its over.Hakuna kitu
ambacho ninaweza kumweleza
akanielewa.Hakuna neno ninaloweza
kulitumia kumuomba msamaha na akakubali kunisamehe.” Akaendelea
kuwaza Vivian
“ Nilimuangalia usoni Martin wakati
akimueleza mama yake.Nina hakika
kabisa kwamba hakuna tena muafaka wa
aina yoyote iIe unaoweza kupatikana kati
yetu.Martin amedhamira
kuniacha.Nimehangaika naye kwa muda
mrefu sana na tumechuma mali za
kutosha siko tayari kukubali kuachwa na
Martin halafu akaja mwanamke mwingine
na kuanza kutumia mali nilizotolea jasho
mimi.Ni bora tukose wote” akawaza Vivian
.
Walifika hadi Bomang’ombe
nyumbani kwa wazazi wa Tino
wakamshusha mama yao halafu bila
kupoteza wakati wakaendelea na safari ya
kuelekea Arusha.Safari ilikuwa ya kimya
kimya ni sauti ya muziki tu iliyokuwa
ikisikika .
“ Nitauficha wapi uso wangu kwa
aibu hii kubwa nitakakayoipata baada ya
kuachana na Martin? Nitachekwa kila
kona na hasa ikigundulika kwamba sina
tena uwezo wa kuzaa.Japokuwa nitakuwa
na mali lakini sintakuwa na furaha tena
katika maisha yangu.Hapana sitaki hilo
litokee.Mjimzimawananijua kama mke wa Tinomagari itakuaje ikisikika kwamba
nimeachwa kwa kutokuzaa? Akawaza
Vivian huku gari likienda kwa kasi
Walifika eneo la kikatiti ambako
kulikuwa na mteremko halafu kilima
kidogo.Hakukuwa na magari mengi jioni
hii kwa hiyo mwendo waliokuwa
wakishuka nao ulikuwa mkali.Kutokea
Arusha kulikuwa na gari moja kubwa la
mizigo liilobeba kontena likishuka kwa
kasi.
“ This is it ..! akawaza Vivian na
ghafla akafanya kitendo ambacho Tino
hakuwa amekitarajia.Kwa kasi ya ajabu
Martin alipigwa ngumi moja usoni na
kisha kwa kasi ya aina yake akaurukia
usukani na kuunyonga kuelekea upande
ule wa lile gari la mizigo lilikokuwa
linateremka kwa kasi na mara kukapotea
kishindo kikubwa.Ilikuwa ni ajali mbaya.
********************
Kiza kilikwisha tanda angani na
safari ilikuwa inaendelea.Alfred
aliyekuwa katika usukani aliendesha gari
kwa mwendo wa kawaida hakutaka
kuendesha kwa mwendo mkali.Safari
ilitawaliwa na maongezi na vicheko. “ Pauline ,tayari umepanga nitafikia
wapi Arusha ? Akauliza Alfred
“ Utafikia nyumbani kwetu” akasema
Pauline
“ Hahahaa..!! unataka mzee wako
anikate shingo? Akatania Fred
“ Hapana Fred.Nyumba yetu ni
kubwa na ina vyumba vya kutosha
tu.Hakuna haja ya kulala hotelini wakati
sehemu ya kulala ipo” akasema Pauline
“ Lakini Pauline unafahamu dhumuni
langu kubwa la kuongozana nawe kuja
Arusha.ninataka niutumie muda wote wa
weekend hii nikiwa nawe.Huoni kama
nyumbani kwenu hilo halitawezekana?
Akauliza Fred
“ Fred wewe na Sanya ni wageni
wangu ,mimi ndiye mwenyeji wenu kwa
hiyo ni jukumu langu kuhakikisha
kwamba mnapatiwa kila kitu
mnachokihitaji.Usihofu kitu Fred.Kila kitu
kitawezekana.Tutapata muda mwingi na
mzuri wa kuwa pamoja.”akasema Pauline
na mara Fred akafunga breki ya ghafla
wote wakastuka baada ya kusikia
kishindo kikubwa sana.Mbele yao
kulitokea ajali mbaya.
“ What happened? Akauliza Sanya
huku mwili wote ukimtetemeka “ Kuna ajali mbaya imetokea kule
mbele .Gari mbili zimegongana”akasema
Alfred kisha akaegesha gari pembeni ya
barabara.Pauline na Sanya waliogopa sana
walikuwa wanatetemeka na hasa
Pauline.Kishindo alichokisikia
kilimuogopesha sana.
“ Twendeni tukatoe msaada
yawezekana kukawa na majeruhi tuwahi
kuwakimbiza hospitali”akasema Sanya
kisha wakashuka garini na kuanza
kukimbia kuelekea eneo la ajali.Kishindo
kile kikubwa kilivuta watu wengi eneo lile
ndani ya muda mfupi tayari
walikwishafika eneo la ajali tayari kwa
kutoa msaada ama ungehitajika.Ndani ya
gari ndogo kulikuwa na watu wawili
ambao walisadikiwa kuwa ni mke na
mume na hali zao zilikuwa mbaya
sana.Watu walijitahidi kwa kadiri
walivyoweza na wakafanikiwa
kuwachomoa majeruhi.
Akiwa ni mmoja wa watu waliosaidia
kuwaokoa majeruhi wale wa ajali,Alfred
akapendekeza wapakiwe katika gari lake
ili waweze kuwahishwa haospitali.Kwa
haraka wakasaidiana na kuwapakia
majeruhi wale katika gari la Fred Pauline
akashika usukani wakaondoka kwa kasi . Katika wale majeruhi wawili ni
mwanamke ambaye alikuwa anagugumia
kwa maumivu makali huku akitaja jina la
Penina.Yule mwanaume alikuwa
anakoroma kwa mbali na hali yake
ilionekana mbaya zaidi.haikuwa rahsi
kuwatambua majeruhi walekutokana na
kuchafuka damu.Wakiwa ndani ya gari
Sanya na Alfred waliendelea na jitihada za
kuizuia damu isiendelee kuwavuja
majeruhi wale wakati Pauline alikuwa
katika usukani wa gari akijaribu
kuendesha kwa kasi na tahadhari kubwa
kuwahi hospitali.
Hatimaye waliwasili katika hospitali
ya mkoa ya Mount Meru ambako
majeruhiwakapokelewa na kukimbizwa
katika chumba cha wagonjwa
mahututi.Alfred na Sanya
wakajitambulisha kama ni madaktari na
wakaomba waruhusiwe kujumuika na
madaktari wenzao ili kuwasaidia majeruhi
wale.Kila aina ya msaada ilihitajika usiku
ule kwa ajili ya kuokoa maisha ya
majeruhi wale hivyo Alfred na Sanya
wakaruhusiwa kujiunga na madaktari
wenzao wa hospitali ya Mount Meru katika
kuwasaidia majeruhi . Pauline alibaki nje akiwasubiri akina
Alfred wamalize kazi yao.Akiwa pale nje
akaona ni vyema amjulishe baba yake
kwamba tayari amekwisha wasili Arusha
akachukua simu yake na kumpigia mzee
Zakaria
“ Hallo Pauline“akasema mzee
Zakaria baada ya kupokea simu
“ baba nimekupigia kukutaarifu
kwamba niko Arusha tayari”
“Uko Arusha?akashangaa mzee
Zakaria
“ Ndiyo baba.Niko Arusha”
“ Mbona uliniambia kwamba
unakuja kesho?
“ Ndiyo nilikuambia hivyo lakini
nikabadili mawazo nikaona nije jioni ya
leo .Lakini kwa sasa niko hapa Mount
Meru hospitali.”
“ Kuna nini hapo
hospitali.Unaumwa? Mzee Zakaria
akauliza kwa wasi wasi
“ Hapana siumwi baba.Kuna watu
tumewaleta hapa wamepata ajali.Rafiki
zangu nilioambatana nao ni madaktari
kwa hiyo wanasaidia katika kuokoa
maisha ya majeruhi hao” akasema Pauline
“ Poleni sana.Nimestuka nikadhani
labda wewe ndio mwenye matatizo.” “ hapana baba si mimi .Naomba
umwambie dada aniandalie chumba
changu pamoja na chumba kimoja cha
wageni nina wageni wawili wote
watafikianyumbani.” Akasema Pauline
kisha akaagana na baba yakena kukata
simu.Mara akapata wazo
“ Sijui nimpigie na David
nimfahamishe kwamba nimekwisha
wasili? Akajiuliza
“ Ngoja nimpige tu nimjulishe
kwamba nimefika.Niko mwenyewe hapa
nje nimeboreka sana.lakini moyo unasita
sana kumpigia tena Yule jamaa kwa
mambo aliyonifanyia.Anyway tu ngoja
nimpigie” akawaza Pauline na kuchukua
simu yake akampigia David
“ Hallo Pauline.Umekwisha
fika?akauliza David mara tu alilipopokea
simu
“ Siku hizi hata kujuliana hali hakuna
moja kwa moja unauliza kama
nimekwishafika” akasema Pauline
“ I’m sorry Pauline.Unajua nikipata
simu yako huwa ninachanganyikiwa
kidogo.”akasema David
“ Kinachokuchanganya nini au
unaona aibu kwa mambo uliyoyafanya?
Akauliza Pauline.David akabaki kimya “ anyway David.Niko hapa Mount
meru hospitali”
“Mount Meru? Kuna nini?unaumwa?
akauliza David
“ Hapana siumwi ila kuna watu
wamepata ajali tumewaleta hapa
hospitali” akasema Pauline
“ Ok Pauline ninakuja hapo sasa
hivi”akasema David
“ David anahisi aibu kubwa kwa
jambo alilonifanyia na ndiyo maana kila
akisikia sauti yangu anahisi
kuchanganyikiwa.Anyway yeye awe na
amani kabisa na Tamia wake kwani mimi
tayari nimekwisha endelea na maisha
yangu.Alfred amenisahaulisha machungu
yote niliyoyapata baada ya kuumizwa na
David.Amenifuta machozi yote na
kunfanya nitabasamu tena.Japokuwa ni
mume wa mtu lakini ameonyesha kunijali
na kunithamini and I’m happy with
him.Ninafahamu kwamba kutatokea
mgogoro mkubwa katika ndoa yake hasa
pale Grace mke wake atakapogundua
kuhusu mahusiano yangu na mume wake
lakini sina namna nyingine ya kufanya
nimekwisha nasa kwa Fred na moyo
wangu tayari umempenda.”akawaza
Pauline.na kukumbuka siku ile ambayo Grace almanusura amfume mume wake
ndani ya chumba cha Pauline
“ Dah ! Ama kweli siku ile niliogopa
sana.Sikuwahi kutetemeka kama siku
ile.Kufumwa na mume wa mtu si kitu
kidogo.Ni aibu kubwa na hasa kwa mtu
ambaye mnaheshimiana na kuaminiana
kama Grace.Pamoja na kwamba alimkosa
Fred siku ile lakini nina uhakika tayari
atakuwa amekwisha hisi kwamba kuna
kitu kinaendelea kati ya mume wake na
mimi.Lakini kitu kinachonishangaza na
kunifanya nijiulize maswali mengi kwa
nini Fred aamue kumsaliti mke wake
ambaye ana karibu sifa zote.Ni mzuri
pengine kuliko hata mimi,ana roho zuri,ni
mkarimu kupindukia ,kwa nini basi
aamue kumuaacha na kuning’ang’ania
mimi? Je kuna vitu anavikosa kwa mke
wake lakini anavipata kwangu? Anyway
siku moja nitamuuliza sababu iliyomfanya
aamue kumsaliti mke wake..Ila wanaume
mhh!!!..mimi wa kwangu pamoja na
kumpenda kwa moyo wangu wote lakini
akanisaliti tena na rafiki yangu na leo hii
mume wa rafiki yangu anamsaliti na kuja
kwangu..hahaah this is funny.Ninashindwa
kuwaelewa wanaume.Ni kitu gani hasa
wanakitafuta kwa mwanamke? Kwa sababu utakuta mtu ana mke wake mzuri
sana lakini bado hatulii na anaruka ruka
hovyo .”akaendelea kuwaza Pauline na
mara David akampiga simu na kumuuliza
mahala alipo,akamuelekeza na baada ya
muda David akatokea .Wakatazamana
kwa sekunde kadhaa kisha David akasema
“ Pole sana Pauline.Nini kimetokea?
Ulipata ajali? akauliza David
“ Hapana David Si mimi niliyepata
ajali.Wakati tukija Arusha gari ya mbele
yetu ilipata ajali eneo la kikatiti hivyo
kutulazimu kuwabeba majeruhi wa ajali
na kuwakimbiza hapa hospitali .Kwa
bahati nzuri watu nilioongozana nao wote
ni madaktari kwa hiyo wameungana na
madaktari wenzao wa hapa Maount Meru
wanawasaidia majeruhi”akasema Pauline
“Vipi hali zao?
“ wameumia sana,na hasa Yule
mwanaume ameumia zaidi na sina hakika
kama anaweza akapona lakini tumuombee
ili apone.Ilikuwa ni ajali mbaya sana
kuwahi kuishuhudia.”akasema Pauline
kisha kukawa kimya.Ni Pauline ndiye
aliyeanzisha maongezi
“ Vipi maendeleo yako? Kazi
zinakwendaje? “Ninaendelea vizuri sana na hata
kazi zinakwenda vizuri.Vipi wewe
unaendeleje?
“ Ninamshukuru Mungu.Anazidi
kunipa nguvu na uhai kila siku.I’m still
breathing,I’m still smilling,life goes
on”akasema Pauline huku
akitabasamu.David akabaki kimya
hakutaka kuongea tena.
“ By the way how is Tamia ? Akauliza
Pauline na kumfanya David ainame kidogo
akafikiria halafu akainua kichwa na
kusema
“ I don’t know how she’s doing “
akajibu
“ You don’t know? What kind of
boyfriend are you? Akauliza kwa
mshangao Pauline
“ We’re not together anymore..
“ What?!! Akauliza Pauline kwa
mshangao
‘ You are not together anymore?
Akauliza tena
“ yes !
“ hahahhaa..unanidanganya tena
David.Haiwezi kuwa kweli.”akasema
pauline
“ Sikudanganyi Pauline ni kitu cha
kweli kabisa mimi na Tamia tumekwisha tengana.” Akasema David.Pauline
akamtazama machoni akaamini kile
alichokuwa anakisema David
“ What happened?akauliza huku uso
wake umejaa tabasamu
David Akakaa kimya kidogo akafiri
na kusema
“ Ulikuwa sahihi kwa yale
uliyoniambia kuhusu Tamia.Nilimfuma na
mwanaume ndani”
“ Oh Thank you Lord..Kile
nilichokisema na hatimaye kimekuwa
kweli.” Akawaza Pauline huku akihisi
furaha ya ajabu sana kwa kile
alichokisikia.
“ David nina hakika sasa utakuwa
umejifunza .Siku nyingine ukiambiwa
kwamba hapa kuna moto basi
usikimbilie.Yatakukuta kama
yaliyokukuta kwa Tamia.Yule ni rafiki
yangu toka muda mrefu tukiwa shule
ninamfahamu vizuri kuliko mtu mwingine
yeyote na ndiyo maana nikawa mkali sana
na kumtaka hata asikuzoee lakini
ukanipuuza na matokeo yake ndiyo
hayo.Anyway tuachane na hayo mambo
kwani hata tukiongea sana hayatusaidia
kitu tena.Ninachoshukuru ni kwamba
umenipa funzo kubwa na ninathubutu kukiri kwamba umenifumbua akili yangu
kwa kiwango kikubwa sana.Kama
usingenifanyia vile nisingeweza kuwa na
wazo la kuondoka hapa Arusha na akili
yangu isingefunguka.Lakini ulinifanya
nikaondoka na nimekwenda mahala
nimejifunza maisha mapya na nimepata
mawazo mapya ya maisha .Kwa kifupi
ninaweza kusema kwamba I’m not a cry
baby anymore.I know how to fight now
and above all I’m happy.”akasema Pauline
“ Ninafurahi kusikia hivyo kwa
sababu hilo ndilo lilikuwa ombi langu
kubwa kwamba uwe na masha mazuri na
yenye furha.” Akasema David
“ David badala ya kukulaumu mimi
ninasema ahsante sana kwani machozi
niliyoyadondosha kwa ajili yako
yamegeuka asali na ninailamba kwa
furaha kubwa.thank you david..”akasema
Pauline na mara simu ya Alfred aliyokuwa
nayo Paulineikaanza kuita.Aliyepiga
alikuwa ni mke wake.Pauline akaitazama
simu ile ikiita aliogopa sana.
“ Grace anapiga .Hapana siwezi
kuipokea simu hii.Sitaki Grace ajue kama
mimi na mumewe tuko pamoja “ akawaza
Pauline na simu ikaita na kukata bila kupokelewa.Ikapiga kwa mara ya pili bila
kupokelewa.
“Mbona hupokei hiyo simu” akauliza
David
“ Hii ni simu ya rafiki yangu aliyeko
ndani ya chumba cha upasuaji
akiwahudumia wale majeruhi.”akasema
Pauline kisha akaiweka simu ile ya Fred
katika yake .
“ Mchana uliniambai kuna suala
zito.what is it? Can you tell me now?
akauliza Pauline
“ Ni kweli pauline kuna jambo kubwa
lakini hapa si mahala pake pa
kuliongelea.kesho tutapata muda mzuri
wa kukaa na kupanga kuhusu jambo hilo.”
“ kwa nini hatuwezi kuongea sasa
hivi? akauliza Pauline
“ Pauline usijali tutaongea kesho.Ni
suala linalohitaji utulivu mkubwa”
akasema David kisha wakaendelea
kusubiri
Saa sita na dakika nane Alfred na
Sanya wakiwa wameongozana na baadhi
ya madaktari wa hospitali ya mount meru
wakatoka ndani ya chumba cha
upasuaji.Madaktari wale wa Mount Meru
wakawashukuru akina Alfred kwa msaada mkubwa waliojitolea.Pauline akawafuata
akawapokea
“ hallow Fred.What happened”
akauliza Pauline
“ Ilikuwa ni ajali mbaya
sana.Mwanamama ameumia sana
tumelazimika kumkata miguu yote kwani
mifupa ilisagika sana na isingewezekana
kabisa kuungwa tena .Mkono mmoja pia
umekatwa .mwanaume pia amepoteza
miguu yote miwili“
“ I’m so sorry”akasikitika sana
pauline
“By the way this is David my
brother.” Pauline akamtambulisha David
kwa akina Fred
“ David hawa ni marafiki zangu.Huyu
anaitwa Dr Fred na huyu hapa anaitwa Dr
Sanya.Fred ni daktari wa moyo katika
hospitali ya KCMC na Dr Sanya ni daktari
wa mifupa anatokea nchini marekani.”
David akasalimiana na Fred kisha
akamgeukia Sanya wakasalimiana
“ ouh mygosh ! what a beautifull
woman…I’ver seen such ana angel !!
akawaza david akimkodolea macho sanya.
Pauline akawaongoza Alfred na Sanya
katika gari ,David naye akaelekea katika
gari lake wakaondoka “ Sanya !!..what a beautifull
woman.Sifahamu ni kwa nini nimestuka
sana baada ya kumuona .Yawezekana ni
kwa sababu ya uzuri wake. Nimekutana
na wanawake wengi wazuri lakini huyu
amepitiliza.Ameustua moyo wangu
ghafla”akawaza David akiwa ndaniya gari
wakielekea nyumbani.
Walifika nyumbani kwa akina
Pauline,David aliyekuWa ametanguliA
mbele na gari lake akshUka na kufungua
geti ,Pauline na wageni wake wakaingia
kisha akawafuata na kuwakaribisha ndani
.Chakula kikaandaliwa wakala na kwa
kuwa walikuwa wamechoka sana wote
wkahitaji kwenda kupumzika. Alfred
akapelekwa katika chumba
kilichoandaliwa maalum kwa ajili
yake,Sanya akaenda kulala na Pauline.
”Pauline chumba chako kizuri sana”
akasema Sanya
“ Ahsante sana Sanya.Jisikie
nyumbani.” Akasema Pauline.Sanya
akamuomba Pauline wapige magoti wasali
sala fupi kabla ya kulala.Pauline akakubali
wakasali sala fupi ikiwa ni pamoja na
kuwaombea majeruhi wale wa ajali
uponaji wa haraka. “ Tukiwa pale katika chumba cha
upasuaji kuna watu wengine wawili
waliingizwa kwa ajili ya upasuaji wa
dharua nao pia wamepata
ajali,inaonekana Tanzania kiwango cha
ajali ni kikubwa sana” akasema Sanya
“ Ni kweli Sanya.Ajali hapa nchini
kwetu zinapoteza maisha ya watu wengi
sana.Vipi Marekani kiwango cha ajali ni
kikubwa?
“ kwa marekani magari ni mengi
sana ukilinganisha na huku na ajali pia
zipo lakini si kwa kiwango hiki.Hapa
nilipo nina zaidi ya mwaka mmoja
sijahudumia mgonjwa wa ajali aliyeumia
kama hawa wa leo.Ajali zipi ndogo ndogo
naza kawaida.Hawa majeruhi wa leo
wameumia kiasi cha kutisha
sana.Ninawahurumia hasa Yule
mwanamke kwa kupoteza miguu yake
yote miwili na mkono wake mmoja.Sijui
maisha yake yatakuwaje baada ya ajali
ile.” Akasema Sanya
“ Inasikitisha sana” akasema Pauline
“ Tuachane na hayo.Kwa nini
hujalala chumba kimoja na Alfred wakati
ninyini wachumba? Akauliza
Sanya.pauline akatasamu na kusema “ Ndiyo ni wachumba lakini kwa mila
za kwetu hairuhusiwi kulala pamoja hadi
hapo mtakapofunga ndoa na ndiyo maana
Alfred ameandaliwa chumba chake peke
yake.Vipi kuhusu wewe una mchumba?
Akauliza Pauline
“ Hapana sina mchumba
bado.Sehemu kubwa ya maisha yangu
nimeitumia katika masomo na sikuwa
nikihitaji kujiingiza katika mapenzi
.Historia yangu ilinifanya nielekeze nguvu
zote katika masomo na kuyajenga kwanza
maisha yangu na kuachana kabisa na
michezo hiyo ya mapenzi.Nilitaka
nisimame mwenyewe kwa miguu yangu
na siku moja niweze kuja kuwatafuta
wazazi wangu na kama ni masikini basi
niweze kuwaondoa katika lindi la
umasikini.” Akanyamaza kidogo akafikiri
halafu akamtazama Pauline na kuuliza
“ Pauline una hakika ninaweza
kufanikiwa kweli kuwapata wazazi
wangu? .
Pauline akainuka akamshika bega na
kusema
“ Usijali utawapata wazazi wako
Sanya.Kama bado wako hai nina hakika
kabisa kwamba utawapata.Jambo la msingi ni kumtanguliza Mungu mbele na
kila kitu kitafaniwa” akasema Pauline
“ Ahsante sana kwa kunipa moyo
Pauline japokuwa kuna nyakati ninakata
tamaa kama ninaweza kuwapata wazazi
wangu ndani ya watu milini arobaini na
tano wa Tanzania.” Akasema Sanya
“ Sanya usikate tamaa hata
kidogo.Niamini nikwambiavyo kwamba
utawapata wazazi wako” akasema Pauline
“ Pauline unanifurahisha sana kwa
namna unavyojiamini.” Akasema Sanya
“ Sanya katika maisha haya lazima
ujiamini katika kila jambo .Nimejifunza
kuhusu faida za kujiamini kwa hiyo
usihofu kesho asubuhi tutakwenda
kwanza hospitali kujua maendeleo ya
wagonjwa wetu wale na halafu tutaelekea
usa river kuanza harakati za mwanzo za
kuwatafuta wazazi wako” akasema
Pauline
“ Ahsante sana Pauline.Yule kaka
yako anaitwa nani ? Nimemsahau jina”
“ Anaitwa David..”
“ Ouh ! jina zuri sana David.Naye
tutaambatana naye kesho?
“ Sina hakika kama ataambatana
nasi.David ni mtu mwenye kazi nyingi
sana.Yeye ndiye msimamizi wa biashara zetu zote kwa hiyo ni mtu mwenye
shughuli nyingi kila wakati.” Akasema
pauline
“ Nimempenda kwa namnaalivyo
mcheshi na mwenye adabu
nyingi.Ametupokea na kutuhudumia
vizuri sana.Mke wake atakuwa na bahati
sana ” akasema Sanya.Pauline
akatabasamu
“ David bado hajaoa “ akasema
Pauline.Sanya akaonyesha mshangao
“ Wewe hutaki kuolewa na yeye
hataki kuoa,mnasubiri nini wakati mna
kila kitu ? Wewe tayari una mchumba
nayeye pia nina hakika tayari ana
mchumba.Wakati ni huu Pauline” akasema
Saya.Pauline hakujibu kitu zaidi ya
kucheka
“ Sanya anaonekana kuanza
kuvutiwa na David.Nilimuangalia toka
tukiwa sebuleni namna alivyokuwa
anamuangalia.Inaonekana wazi kabisa
kwamba amevutiwa naye.Ni afadhali
David akawa na sanya kuliko kuwa na mtu
kama Tamia.Nimefurahi san akusikia
kwamba wamekorofishana na
Tamia.Natamani sana kama angempata
Sanya lakini David ninamfahamu ni mtu
asiye na msimamo hata kidogo .Anaweza akamuumiza sana mtoto wa watu ambaye
bado hajaingia katika ulimwengu wa
mapenzi n kuyafahamu mateso yake”
Akawaza Pauline
Mara tu Alfred alipoingia chumbani
simu yake ikaita.Alikuwa ni mke wake
aliyepiga.Fred akasita kuipokea lakini
mwishowe akaamua kuipokea
“ Hallow Grace my love” akasema
Fred
“ Hallow Fred..unaendeleaje?
Nilikupigia simu lakini
hukupokea.Nilitakanihakikishe kama uko
salama kwani nilipata taarifa za kutokea
kwa ajali mbaya usiku huu”
“ Nilikuwa katika chumba cha
upasuaji uliponipigia.Ajali hiyo
unayoisema ilitokea kwa gari lililokuwa
mbele yetu ambalo liligongana na gari
kubwa la mizigo ikatulazimu kuwachukua
majeruhi na kuwawahisha katika hospitali
ya Mount Meru kwa matibabu kwani hali
zao hazikuwa nzuri.Baada ya kufika
hospitali ikanilazimu kuungana na
madaktari wa Mount Meru kuwafanyia
majeruhi upasuaji kwa hiyo ulipopiga
nilikuwa katika chumba cha upasuaji
,simu alikuwa nayo Pauline.” “ Simu alikuwa nayo
Pauline?!!!!...akauliza Grace na kumstua
sana Fred
“ Mungu wangu ! nimejisahau
nimeharibu kila kitu” akawaza Alfred
“ Fred !! akaita Grace kwa ukali
“ Unasema simu alikuwa nayo
Pauline yupi? Akauliza Grace
“ Picha imekwisha ungua hakuna
namna nyingine ya kufanya zaidi ya
kumueleza ukweli kwamba niliongozana
na Pauline.Nimekwisha haribu kila
kitu”akawaza Fred.
“ Grace utanisamehe mke wangu
sikukjtaarifu kama katika safari hii
niliongozana na Pauline .Aliposikia nina
safari ya Arusha akaomab tongozane wote
kwanihata naye alikuwa na safari ya kuja
hku ” akasema Alfred.Kikapita kimya
kidogo Grace akasema
“ Ok kwa sasa uko wapi?Hotelini au
bado uko hospitali?
“ Kwa sasa niko nyumbani kwa
akina Pauline.Wana nyumba kubwa kwa
hiyo ameniomba nifikie kwao.” akasema
Alfred.Kikapita tena kimya cha sekunde
kadhaa Grace akasema
“ Fred unakumbuka wakati unaniaga
uliniambia kwamba una dharura ya kwenda Serian hospital kuna upasuaji wa
dharura unafanyika usiku huu.Sasa mbona
upo kwa akina Pauline badala ya seriani
katika upasuaji?
“ Upasuaji ule umeahirishwa hadi
kesho” akajibu Alfred na kumfanya Grace
aangue kicheko
“ Haya Ahsante sana Fred.Nakutakia
usiku mwema na kazi njema.Ninakupenda
sana” akasema Grace na kukata
simu.Alfred bado aliendelea kuishikilia
simu
“ Dah ! ama kweli siku ya kufa nyani
miti yote huteleza.Imekuaje nikajisahau
na kumtaja Pauline? Nimeharibu kila kitu
na Grace tayari amekwisha pata
kithibitisho tosha kwamba mimi nina
mahusiano na Pauline.Nimefanya kosa
kubwa na sijui nitamweleza nini Grace
aweze kunielewa.” Akawaza Alfred akiwa
ameinamisha kichwa
“ Nimekwisha haribu ninatakiwa
kutafuta namna ya kuliweka sawa suala
hili.Mipango yangu yote tayari
imevurugika .Hata hivyo natakiwa
kutafuta namna ya kulimaliza jambo
hili.Nilimdanganya na ili kuendelea
kuulinda uongo wangu wa kwanza
ninalazimika kumdanganya tena.Sifurahii kumdanganya danganya Grace lakini kwa
aajili ya Pauline niko tayari
kudanganya.Hata mimi nimechoka na
maisha ninayoishi na ninahitaji
uhuru.Ninahitaji mtu ambaye na mimi
nitampenda kwa moyo wangu wote na
mtu huyo tayari amekwisha tokea naye ni
Pauline.Ni wakati wangu na mimi
kuyafurahia mapenzi.Grace atanisamehe
lakini itafika wakati itanilazimu
nimueleze ukweli kuhusu mimi na
Pauline.” Akawaza Alfred.
“ Hizi nyumba zinaficha mambo
mengi sana ndani yake na ndiyo maana
watu wanaweza kuona wanandoa
wakicheka na kufurahi lakini hawajui
kinachoendelea ndani ya nyumba yao ni
kitu gani.Mimi na Grace tumekuwa ni
mfano wa kuigwa kwa namna
tunavyoonekana katika jamii lakini
hakuna aneyjua nini kinachoendelea
ndani mwetu.” akawaza
“ Ngoja niachane na mawazo haya
kwani yataniharibia kabisa mapumziko
yangu ya mwisho wa wiki ambayo
nimepanga yawe mazuri sana nikiwa na
Pauline.Kilichotokea kimekwisha tokea na
siwezi kurudi nyuma tena” Akawaza na
kulala
Taarifa za ajali iliyotokea eneo la
kikatiti iliyolihusisha gari dogo na lingine
kubwa la mizigo zilianza kusambaa kwa
kasi kubwa jijini Arusha hasa kutokana na
mtu aliyepata ajali ile kuwa ni mtu
maarufu sana.Tino Magari alifahamika
mno jijini Arusha.Akiwa katika baa na
wafanya biashara wenzake wa madini
Armando rafiki mkubwa wa Tino alizipata
taarifa hizi za ajali hii na kustuka
sana.Hakutaka kuziamini taarifa zile moja
kwa moja hivyo kumlazimu kukimbia hadi
katika hospitali ya mount Meru ili
kuthibitisha taarifa zile kama ni za
kweli.Alithibitisha ni kweli rafiki yake
alipata ajali mbaya na amepoteza miguu
yake yote miwili.Alilia sana .
Taarifa zikaendelea kusambaa
karibu kila kona ya jiji.Saa saba na dakika
kama kumi na nane hivi Robin akapigiwa
simu na mmoja wa marafiki zake ambaye
akamfahamisha kwamba mke wake wa
zamani Vivian amepata ajali mbaya sana
yeye pamoja na mume wake Tino na hali
zao ni mbaya sana.Robin hakutaka kuziamini taarifa zile ikamlazimu
kumpigia simu kamanda wa polisi mkoa
wa Arusha ambaye ni rafki yake na
kumuuliza kuhusu habari zile naye
akamthibitihia kwamba ni kweli Tino
magari na mke wake Vivian walipata ajali
mbaya na wamekimbizwa katika hospitali
ya mkoa ya Mount Meru.
“ Sifurahii kilichotokea lakini
ninaamini hiki ni kibao Mungu
amewachapa kwa mambo waliyoyafanya.”
Akawaza Robin kisha akampigia simu
mwalimu Lucy na kumfahamisha
kuhusiana na taarifa zile .kwa kuwa
ilikuwa ni usiku sana wakapanga kwamba
siku ya kesho waende wakawatazame
Tino na Vivian hospitali.
*********************
Siku ya jumamosi ilianza vizuri
sana.Asubuhi hii kiubaridi kilikuwa kikali
kama kawaida ya jiji la Arusha..David
aliamka asubuhi na mapema na kuwahi
kazini kama ilivyo kawaida yake na
kuwaacha watu wote wamelala.Dakika
chache tu baada ya kuondoka Vicky
madhahabu akaamka na kwenda kugonga chumbani kwa David lakini hakuwepo
akamfuata msichana wa kazi akamuuliza
kama amemuona David akataarifiwa
kwamba alikwisha ondoka kitambo sana
Taarifa za kurejea kwa Pauline
hazikuwa taarifa nzuri kwake.Zilimtesa
usiku kucha na kumnyima usingizi.
“ Nina bahati mbaya sana na huyu
mtoto.Kitu gani kimemrudisha? Akajiuliza
Vicky
“ Lakini hata kama akirejea hakuna
kitakachoharibika.Kila kitu kitaendelea
kama kilivyopangwa na kama
ikiwezekana hata yeye anaweza
akaondolewa kabisa ili kuondoa kabisa
kila aina ya kikwazo katika mipango
yangu” akaendelea kuwaza kisha akarejea
chumbani kwake na kumfuata mzee
Zakaria kitandani
“ Darling,nimefurahi sana kwa
Pauline kurejea.Alikueleza alikwenda
wapi kupumzika? Akauliza
“ Hakuniambia alikuwa wapi lakini
alichoniambia kwamba anakuja mara
moja kuna suala la kibiashara anataka
kuja kuzungumza na mimi halafu
ataondoka tena.Amekuja na marafiki zake
wawili “ akasema mzee Zakaria Saa mbili za asubuhi Pauline na
Sanya walikwisha amka.Wakati Sanya
akijiandaa Pauline akatoka na kwenda
chumbani kwa Alfred akagonga,Alfred
akafungua mlango wakakumbatiana kwa
furaha kubwa na kubusiana.
“ How was your night Fred? Akauliza
Pauline
“ Ulikuwa ni usiku mzuri sana japo
picha za wale majeruhi wa ile ajali
zilinitesa sana lakini kwa ujumla nimelala
vizuri sana.Vipi wewe?
“mimi pia nililala vizuri sana na
ningefurahi zaidi endapo ningelala nawe
lakini kwa mazingira ya hapa ndani
isingewezekana ila usijali tutapata muda
wa kutosha wa kula bata kabla ya kurejea
Moshi .Jiandae siku ya leo tuna ratiba
ndefu .Tutaanzia hospitali,Sanya anataka
kwenda kuwatazama wale majeruhi wa
ajali,halafu tutaelekea usa river na kisha
tukitoka hapo ni mwendo wa kula bata
mpaka jioni”akasema Pauline kisha
akatoka na kurejea chumbani kwake
akajiandaa kisha wote kwa pamoja
wakajumuika mezani kwa ajili ya kupata
mlo wa asubuhi
“ David yuko wapi? Akauliza sanya
wakiwa mezaniwakipata kifungua kinywa “ David si rahis kumpata mida
hii.Tayari amekwiha elekea kazini.Baade
kama tunaweza kumualika kwa chakula
cha mchana.” akasema Pauline na mara
akatokea mzee Zakaria akiwa
ameongozana na Vicky.
“ hallo vijana hamjambo? Akasalimu
mzee Zakaria.Wote wakasimama na
kumsalimu kwa heshima
“ Nimefurahi sana kuwaoneni vijana
wangu na karibuni sana.Mimi naitwa mzee
Zakaria ni baba mzazi wa Pauline na huyu
hapa ni mama yake mdogo Pauline
anaitwa Vicky.kwa pamoja
tunawakaribisha a sana hapa nyumbani
kwetu.Jisikieni nyumbani.Marafiki wa
Pauline ni watoto wetu pia na
tunawapenda sana”akasema Zakaria
“ Tunashukuru sana mzee”akasema
Fred
“ Baba hawa ni marafiki zangu.Huyu
anaitwa Alfred ni daktari wa moyo kutoka
hospitali ya KCMC na huyu hapa ni Dr
Sanya yeye anatokea Marekani ni daktari
wa mifupa.” Pauline akafanya
utambulisho.Mzee Zakaria akafurahi sana
kukutana na vijana wale .kwa kuwa bado
ilikuwa ni asubuhi hawakuongea mambo
mengi wakakubaliana kukutana usiku kwa ajili ya chakula ili wapate nafasi ya
kuongea mambo mengi zaidi.
Kisha pata kifungua kinywa Pauline
na wageni wake wakaingia garini na
kuondoka kuelekea hospitali ya Mount
Meru.
“ Familia yako ni wakarimu sana.”
Akasema Fred wakiwa garini.Pauline
hakujibu kitu akatabasamu.Hakukuwa na
maongezi mengi garini hadi walipofika
hospitali ya Mount Meru .hali za majeruhi
wale bado hazikuwa nzuri .
Kutoka pale hospitali safari ya
kuelekea Usa river katika kituo cha
kulelea watoto wadogo kuutafuta ukweli
kuhusu wazazi wa Sanya ikaanza.
“ Tunakwenda kufanya nini Usa river?
Akauliza Alfred
“ Tunamsindikiza Sanya kuna kitu
anahitaji pale Usa river” akasema Pauline
“ Pauline nilisahau kukwambia
.Grace alipiga simu jana usiku”
“ Alipiga? Kuna tatizo lolote?
Akauliza Pauline kwa wasi wasi
“ Hakuna tatizo alihitaji tu kujua
kama niko salama” akasema Fred
“ Anafahamu kama mimi na wewe
tumeongozana kuja Arusha? Akauliza
Pauline “ Ilinibidi nimweleze ukweli kwamba
tumeongozana wote kuja Arusha”
akasema Fred
“ Ouh Fred ! Fred ! Kwa nini
ulimwambia? Ulifanya kosa kubwa
sana.Hukupaswa kumueleza jambo
hilo.Mkeo amekwisha hisi kuna kitu
kinaendelea kati yetu ,huoni kwamba
atazidi kuwa na uhakika kwamba hisia
zake ni kweli mimi na wewe kuna jambo
linaendelea kati yetu? Akasema Pauline
“ Usihofu kuhusu hilo Pauline.Hata
kama akigundua hataweza kunirudisha
nyuma.Nimekwisha aamua kuwa na wewe
na hakuna wa kuubadili msimamo
wangu.” Akasema Alfred.Pauline
akamtazama akatabasamu na kusema
“ Fred inaonekana hujawahi
kuumizwa na mapenzi na hujawahi
kutendwa ndiyo maana unadiriki kusema
hivyo.Grace akigundua kwamba mimi na
wewe tuna mahusiano ataumia
sana.Nakwambia Fred maumivu ya
kutendwa na mpenzi ni makali kuliko
maumivu ya kukatwa na kisu na hasa pale
unapoumizwa na mtu ambaye unampenda
,unamjali na kumthamini na ambaye
umemuamini na kumkabidhi moyo
wako.Ninayasema haya kwa sababu nimeyapitia.Yamenikuta na ninayafahamu
vyema na ndiyo maana ninakwambia
kwamba ni mateso makubwa sana .Sitaki
mateso kama yale yamkute mwanamke
mwenzangu na kumfanya akate tamaa
kabisa ya maisha .” akasema Pauline.
“ Kumbe kuna mtu amewahi
kukuumiza Paulne.Kwa nini hjawahi
kuniambia? Nataka kufahamu ni nani
huyo ambaye anathubutu kukufanyia
hivyo malaika kama wewe? Ni mwanaume
wa aina gani huyo ambaye anaweza
kuichezea dhahabu hii ya thamani kubwa
karibu na moto? akauliza Alfred.Pauline
akatabasamu na kusema
“ Tuachane na hayo Fred.Ni mambo
yaliyopita na imebaki historia.Ila
ninaogopa sana kumuumiza Grace.Ni
mwanamke ambaye hastahili kabisa
kuumizwa kwa namna yoyote ile”
akasema Pauline
“ laiti Pauline angejua ni mateso
kiasi gani niliyonayo mimi angenionea
huruma sana wala asingethubutu kusema
kwamba Grace ataumia akigundua
kwamba mimi na yeye tuna
mahusiano.Kuna ule msemo unaosema
kwamba ukisema unaumwa halafu
ukakutana na wanaoumwa kweli kweli basi utapona bila hata dawa.Pauline
anadai ameumizwa lakini angejua namna
nilivyoumizwa mimi angenionea huruma
sana..” Akawaza Alfred
“ Itabidi mnifundishe Kiswahili ili na
mimi nisikie kile
mnachokiongea.Kiswahili inaonekana ni
lugha tamu sana.Naangalia namna nyuso
zenu zilivyo na tabasamu mkiongea na
ninatamani sana kufahamu
mnachokiongea “ akasema Sanya ambaye
muda mwingi alikuwa kimya akiwasikiliza
akina Pauline wakiongea bila kujua
wanaongea nini
“ Usijai Sanya tutakufundisha
Kiswahili .Ni lugha nyepesi sana kujifunza
na kuielewa “ akasema Pauline.Safari
ikaendelea kimya kimya
Walikaribia sana kufika Usa river.
“ Sanya tumekaribia sana kufika Usa
river.je kuna mabadiliko yoyote? Akauliza
Pauline
“ Mabadiliko gani Pauline? Akauliza
Sanya
“ Yawezekana labda ukawa
umebadili mawazo kuhusiana na hiki
unachotaka kukifanya”
“ Hapana Pauline siwezi kubadili
mawazo .Nimesafiri kutoka marekani hadi huku kwa ajili ya jambo hili kwa hiyo
lazima niufahamu ukweli.” Akasema
Sanya.Pauline akawasha taa ya kushoto
kuashiria kwamba anatoka njia kuu na
kuingia katika barabara inayoelekea
katika kituo cha kulelea watoto wadogo.
“ Pauline kwani kuna nini
kinaendelea? Mbona siwaelewi? Sanya
anataka kufanya nini? Akauliza Alfred
“ Hata nikikueleza sasa hivi
hutanielewa Fred.Nitakueleza tukipata
nafasi nzuri” akasema Pauline na
kupunguza mwendo walipowasili katika
geti kubwa la kituo hiki.Mlinzi
akawafungulia geti wakaingia ndani.
“ Alfred naomba uendelee kutusubiri
humu ndani ya gari hatutachukua muda
mrefu sana” akasema Pauline kisha yeye
na Sanya wakashuka na kuingia katika
jengo la utawala.
********************
Saa nne na dakika kumi na saba
Robin akawasili ofisini kwa Mwalimu
Lucy.Hakukuwa na mtu mwingine ofisini
mle hivyo Robin akapita moja kwa moja “ Hello my love .Unaendeleaje?
akauliza Robin huku akimbusu Lucy
“ Ninaendelea vizuri sana Robin”
akasema Lucy.Robin akamshika tumbo na
kutabasamu
“ How is my little prince doing?
Akauliza na kumfanya Lucy atabasamu
“ Umejuaje kama ni mwanaume?
“ Hisia zangu zinanituma kwamba ni
mwanaume.” Akasema Robin
“ Can we bet? Akauliza Lucy huku
akitoa kicheko kidogo
“ Yes we can.” Akajibu Rbin
“ What if you loose.?
Robin akakuna kichwa na kusema
“ I’m not going to loose. Ila ikitokea
hivyo utachagua mwenyewe nini cha
kunifanya”
“ You will be my slave for two weeks
.Deal? akauliza Lucy
“ Deal “ akajibu Robin na wote
wakacheka.
“ Ok tuachane na hayo .Unaendeleaje
mpenzi?
“ Ninaendelea vizuri sana Robin.Ila
sikuweza kupata usingizi tena baada ya
kupata taarifa zile za kuhusiana na ajali ya
Martin na Vivian” “ Oh my love hutakiwi kukosa
usingizi kwa ajili ya mtu kama Yule.Nina
hakika Mungu amempiga kibao kidogo
yeye na mke wake” akasema Robin
“ Robin ninamuonea huruma sana
Martin na Vivian.Watu wanaielezea ajali
hiyo kwamba iilikuwa mbaya sana.”
Akasema Lucy
“ Mimi wala sijaumizwa kabisa na
kilichowapata.Vivian alinifanyia kitu
kibaya sana mimi na mwanangu na mpaka
leo hii sijasahau kashfa ,matusi na dharau
alizozitoa kwangu achilia mbali
kumtelekeza mwanae ” Akasema Robin
“ Hata mimi Martin aliniumiza sana
ikiwa ni pamoja na kunipiga na kunitolea
kashfa kibao lakini pamoja na hayo yote
nmejikuta ninamuonea huruma sana .
Pamoja na yote aliyokukosea Vivian, lakini
bado ni mama wa mwanao na mpaka sasa
anatambulika kama mkeo wa ndoa kwa
hiyo unapaswa kumuonea huruma na
kumfariji kwa lililompata.Naomba tuende
hospitali tukawatazamae”akasema Lucy
“ Lucy mida hii si ya kuwatazama
wagonjwa .Hatutaweza kuruhusiwa
kuwatazama.Tusubiri mpaka jioni ndipo
tukajaribu kama tunaweza kupata nafasi
ya kuwatazama. “ akasema Robin “ Sawa Robin kama umeamua hivyo.
Penina anafahamu chochote kuhusiana na
ajali iliyompata mama yake?
“ Hapana bado sijamueleza
chochote” akasema Robin
“ Anatakiwa kufahamishwa ili ajue
kinachoendelea.”
“ Nitamfahamisha jioni ya leo ila kwa
sasa nimekuja kukuchukua kuna sehemu
nataka twende” Akasema Robin
“ Unanipeleka wapi Robin?
“ It’s a surprise .” akajibu Robin
“ Ouh Robin unapenda sana
suprises” akasema mwalimu Lucy huku
akiinuka akavaa koti lake kisha wakatoka
mle ofisini wakaingia katika gari la Robin
na kuondoka.
**********************
Kabla ya kwenda ofisini kwake Vicky
madhahabu alielekea moja kwa moja hadi
ofisini kwa Chino kumpelekea kiasi cha
pesa walichokuwa wamekubaliana kabla
ya kazi haijafanyika.
“ Karibu sana Vicky.Imekuwa vizuri
umewahi kwani ungechelewa kidogo
ungenikosa.” Akasema Chino “ siwezi kuchelewa kabisa katika
jambo la muhimu kama hili” akasema
Vicky.
“ Umekuja kamili? Akauliza Chino
“ Ndiyo Chino.Nimekuja kamili kama
tulivyokubaliana” akasema Vicky na
kuliweka mezani sanduku dogo na
kulifungua.Chino akatoa sigara akaiwasha
na na kuivuta kisha akapuliza moshi
mwingi hewani.Akatoa bunda moja na
kulishika akaziangali noti zile nyekundu
nyekundu halafu akalichukua sanduku lile
akalifungia katika kasiki kubwa
lililokuwamo mle ofisini kwake kisha
akarejea mezani
“ Hutaki kuhakikisha kama ziko
sahihi? Akauliza Vicky
“ Ninakuamini huwezi
kunidanganya” akasema Chino akavuta
tena sigara na kusema
“ Ahsante Vicky kwa kutimiza
ahadi.Umeonyesha ni namna gani
ulivyodhamiria kuhusu jambo
hili.Ninakuahidi kwamba kila kitu
kitakwenda kama vile tulivyopanga.Kabla
ya saa sita za usiku kesho kila kitu
kitakuwa kimekamilika na utabakiwa na
utajiri wote” akasema Chino huku
akipuliza moshi mwingi wa sigara. “ Nitashukuru sana Chino lakini hata
hivyo kuna tatizo kidogo limejitokeza.”
Akasema Vicky
“ Tatizo gani Vicky? Akauliza Chino
“ Kuna Yule mtoto wa Zakaria
aliyekuwa amesafiri ,amerejea jana usiku
akiwa na rafiki zake.” Akasema Vicky
“ Unadhani kunaweza kuwa na tatizo
lolote kwa kurejea kwake? Akauliza Chino.
“ Sina hakika kama kunaweza
kutokea tatizo lolote.Nimeona ni vizuri
nikakufahamisha ili ufahamu mle ndani
kutakuwa na watu wangapi”
“ Ahsante kwa taarifa hizo lakini
hicho si kikwazo kabisa kwetu.Kama
nilivyokueleza awali kwamba sisi
tunakuja kwa lengo moja tu la kumuua
mzee Zakaria na kama kutatokea kizingizi
chochote sisi tutakiondoa.Awe mtoto wake
au awe nani sisi tutamuondoa”.akasema
Chino na kumuogopesha Vicky
“ Chino kuna Yule kijana mmoja
anaitwa David tafadhali naomba hata
iweje msimdhuru.Ni mtu muhimu sana
kwangu” akasema Vicky
“ Kama ni mtu wa muhimu kwako
basi fanya mpango asiwepo nyumbani
mida hiyo vinginevyo kama akiwepo na
akatuletea kigingi sisi tutamvunja hata miguu.Hatuna mchezo tuwapo
kazini.Tumeelewana? ” akasema Chino na
kupuliza moshi mwingi
“ sawa chino nitajitahidi kufanya kila
linalowezekana ili David asiwepo
nyumbani mida hiyo” akasema
Vicky.Chino akamtazama kwa makini na
kusema
“ So this is it.Kumbuka mzigo wetu
uliobaki tunauhitaji kesho kutwa baada ya
kumaliza kazi.” Akasema Chino
“ Ninakumbuka Chino siwezi
kusahau “
“ Good.basi sisi ni wage ni wako
kesho usiku.Kama kutatokea mabadiliko
yoyote nitaarifu kabla ya saa sita mchana
kesho .Baada ya saa sita mchana siku ya
kesho sintapatikana katika simu tena”
akasema Chino akaagana na Vicky
akaondoka zake.
“ Mambo yameiva.Hata kama Pauline
amerejea lakini hakuna
kitakachoharibika.Kila kitu kitakwenda
kama kilivyopangwa.Lazima kesho
Zakaria auawe tu.” Akawaza Vicky akiwa
garini baada ya kutoka kwa Chino
Kama ilivyo kawaida yake moja kwa
moja baada ya kutoka kwa Chino
akaelekea kwa shoga yake Safia. “ Kuna habari mpya Vicky ? akauliza
Safia
“ Kama kawaida angu Safia huwa
sikosi habari mpya.Nimetoka kuonana na
Chino na tayari nimempa kiasi cha pesa
alichokitaka kabla ya kuanza kazi kwa
hiyo kesho kila kitu kitakamilika.Shoga
yangu vuta subira kidogo na baada ya siku
chache sana mambo yetu yatabadilika .”
“ Mimi nakuombea heri Vicky
ufanikiwe kwani ukifanikiwa wewe hata
mmi pia nimefanikiwa” akasema Safia.
“ Ila kuna tatizo limejitokeza
“ tatizo gani tena Vicky?
“ si tatizo kama tatizo ila linaweza
kuwa tatizo kama nisipolichukulia kwa
uzito.Pauline amerejea jana usiku”
akasema Vicky
“ Amerejea? Safia akaonyesha
kushangaa
“ Ndiyo Safia .Amerejea jana usiku”
“ Kwa hiyo utafanya nini?
“ Hakuna cha kufanya.Kila kitu
kitakwenda kama kilivyopangwa.Chino
anasema kwamba ikitokea kama Pauline
au mtu mwngine yeyote Yule ataonekana
kuweka kizingiti basi naye pia
watamuondoa haraka sana kwa hiyo
Pauline naye kama akitaka kuleta kujua kwake naye pia ataondolewa vile vile“
akasema Vicky huku akitabasamu na
kuendelea
“ Ila nimemuonya kuhusu David
kwamba kwa namna yoyote ile hatakiwi
kuguswa kwani mpango huu wote ni kwa
ajili yake.”akasema
“ Basi tuombe kila kitu kiende kama
kilivyopangwa na maisha yetu yabadilike”
akasema Safia
“ Usihofu shoga yangu.Maisha yetu
yatabadilika muda si mrefu sana.Basi
mimi naomba niondoke nielekee dukani
kwani sikuwa nimepita hata dukani”
akasema Vicky na kuagana na Safia
akaondoka
“ Shetani mkubwa we,hutafanikiwa
kabisa katika mipango yako.” Akasema
Safia baada ya Vicky kuondoka kisha
akachukua simu yake na kumpigia David
akamfahamisha kila kitu alichoelezwa na
Vicky.
******************
Watu walifurika katika hospitali ya
mkoa ya Mount Meru ili kuwajulai hali
papaa Tino magari na mkewe Vivian.Taarifa za ajali waliyoipata
ziliwastua wengi hivyo kuwafanya wafike
hapa kutaka kujua maendeleo yao.
Pamoja na watu kufika kwa wingi
bado hakuna aliyeruhusiwa kuingia katika
vyumba walimolazwa majeruhi kwani
bado hali zao hazikuwa nzuri.
****************
Pauline na Sanya waliufungua mlango
mkubwa wa kuingilia katika jengo kubwa
la utawala la kituo kile kikubwa cha
kulelea watoto wadogo walioachwa na
mama zao wakati wa kujifungua ama
waliookotwa baada ya kutupwa na wazazi
wao.Walikaribishwa na mwanadada
aliyekuwapo mapokezi na wakaeleza
shida yao ya kuonana na mkuu wa kituo
kile.Waliombwa wasubiri kwa muda
kwani mkurugenzi wa kituo kile alikuwa
amekwenda katika nyumba ya malezi
kuwaona watoto.
Baada ya dakika kumi akaingia
mama mmoja mnene akatambulishwa
kwamba ndiye mkurugenzi wa kituo kile
na akawakaribisha akina Pauline ofisini
kwake. “ karibuni sana katika kituo
chetu.Niwasaidie nini? Akauliza Yule
mama
“ Mama mimi ninaitwa Pauline na
huyu mwenzangu anaitwa sanya.Mimi ni
mwenyeji wa Arusha na mwenzangu yeye
anatokea nchini Marekani.Kuna jambo
kubwa ambalo limetuleta hapa” akasema
Pauline
“ Ndiyo Pauline.Ni jambo gani hilo?
“ Jambo lenyewe linamuhusu huyu
mwenzangu nadhani itakuwa vyema kama
akikuelezea yeye mwenyewe japokuwa
hajui Kiswahili.” Akasema Pauline na
kumwambia Sanya aeleze tatizo lake.
“ Kama Pauiline alivyosema ninaitwa
Sanya na ninatokea nchini Marekani.Ni
raia wa Marekani lakini asili yangu ni
Tanzania.Mlezi wangu ambaye amenilea
toka nikiwa mdogo aliwahi kuishi hapa
Tanzania kwa miaka kumi na aliwahi
kumiliki kituo hiki cha kuelelea watoto
wadogo hadi alipomaliza muda wake wa
kuishi hapa nchini na kurejea Marekani.”
Akanyamaza kidogo na kuendelea.
“ Sikuwa nimefahamu kuhusu
historia yangu hadi pale nilipokuwa
mkubwa kabisa ndipo mama mlezi
aliponieleza ukweli kuhusiana na asili yangu.Aliniambia kwamba niliokotwa
katika geti la kituo hiki baada ya
kutelekezwa na mzazi wangu nikiwa bado
mdogo sana na inakadiriwa nilikuwa na
umri wa kati ya wiki moja au mbili na
nikaanza kutunzwa hapa.Kwa bahati nzuri
mama mlezi na familia yake walitokea
kunipenda na walipoondoka kuerejea
Marekani wakanichukua nikaondoka nao
na hadi leo ninaishi Marekani na ni raia
wa kule.” Akanyamaza kidogo kama ilivyo
kawaida yake kuongea kwa vituo halafu
akaendelea.
“ Kwa miaka kadhaa sasa baada ya
kuufahamu ukweli kuhusu asili yangu
nilikuwa ninatafakari jambo hili kwa
undani na mwaka huu nimeamua kuja
Tanzania ili kujaribu kutafuta bahati kama
ninaweza kuonana na wazazi wangu kwa
hiyo nimeona sehemu ya kwanza ambayo
nimeona inaweza kunifaa kuanzia ni hapa
mahala ambako ndiko niliokotwa na
kulelewa.Nina hakika mtu aliyenitupa
ambaye sifahamu kama ni mama yangu au
ni nani baada ya kujitafakari anaweza
akagundua kwamba alifanya kosa na
akaamua kutaka kufahamu kama mtoto
aliyemtupa yu hai ama vipi kwa hiyo
sehemu ya kupata taarifa hizo ni hapa pekee.Ninatumai umenielewa na unaweza
ukanisaidia kufuatilia katikakumbu
kumbu zenu kama kama kuna kuna mtu
yeyote amewahi kuja hapa kuulizia mtoto
aliyetelekezwa” akasema
Sanya.Mkurugenzi akavua miwani yake na
kuchukua kitambaa akayafuta macho yake
ambayo yalionekana kuloa machozi.
” Sanya historia yako imenifanya
nitoe machozi kwa sababu mtu aliyefanya
kitendo hiki cha kukutupa alifanya
kitendo kibaya sana na hakujua kama siku
moja unaweza ukawa namna hii.Jangalie
sasa ni msichana mkubwa na mrembo
sana.Nina hakika hata yeye mwenyewe
akikuona sasa hivi anaweza asiamini
kama ni wewe Yule ambaye alikutupa
getini.” Akasema mkurugenzi kisha
akavaa miwani yake
“ Sanya karibu sana Tanzania,karibu
sana nyumbani.Ninakupongeza sana kwa
uamuzi wako wa kuamua kuja Tanzania ili
kuitafuta asili yako na kuwatafuta wazazi
wako.Huu si uamuzi rahisi kuufanya hasa
ukikumbuka kwamba mzazi wako
alikutupa wakati huo lakini pamoja na
kitendo hicho alichokifanya bado
umeamua kumtafuta na kuungana
naye.Nakupongeza sana na ninakuahidi kukuunga mkono na kukupa kila aina ya
ushirikiano hadi nihakishe kwamba
umefanikiwa kumpata mzazi wako.”
Akasema mkurugenzi
“ Nitashukuru sana mama” akajibu
Sanya
“ Lakini pamoja na hayo ni miaka
mingi sasa imekwisha pita toka mlezi
wako alipoondoka na baada yake kituo
hiki kumekuwa na wamiliki kadhaa kwa
hiyo kupata kumbu kumbu za nyuma
inakuwa ngumu sana.Kinacholeta ugumu
zaidi ni kwamba jengo hili la utawala
liliwahi kuungua moto na kuteteketeza
kila kilichokuwemo .Ni sisi ambao
tulilikarabati na kuanza tena kulitumia
kwa hiyo hatuna kabisa kumbu kumbu
yoyote ya nyuma tuliyonayo.” Akasema
mkurugenzi.
Kauli ile ikaonekana
kumnyong’onyeza kabisa Sanya na ni wazi
alikata tamaa.
“ hakuna tena tumaini “ Sanya
akamwambia Pauline
“ lakini kuna jambo lingine ambalo
sina hakika sana kama linaweza kuwa na
msaada” akasema mkurugenzi.
“ Tueleze mama linaweza kuwa na
msaada “ akasema Pauline “ Zimepita wiki kadhaa sasa walikuja
hapa watu wawili ambao walikuwa
wanatafuta taarifa za mtoto ambaye
historia yake inafanana na ya kwako
Sanya.Walidai kwamba kuna ndugu yao
aliwahi kumtelekeza mtoto katika geti la
hapa kituoni na akakimbia kwa hiyo
wamekuja kutafuta taarifa za mtoto
huyo.Nao pia niliwaeleza kama
nilivyowaleza ninyi kwamba kuna ugumu
wa kupata kumbu kumbu za nyuma ”
akasema mkurugenzi
“ Ouh Ahsante Mungu..Ni akina nani
hao? Unafahamu mahala walipo? Akauliza
Sanya
“ Sanya ninapatwa na ugumu kidogo
wa suala hili kwa sababu ipo tabia ya
wazazi ambao hawataki kulea watoto wao
ama kutokana na uwezo au sababu
nyngine huja na kuwatelekeza katika geti
la kituo chetu.Tunao watoto zaidi ya
watano sasa ambao tumewaokota
wametelekezwa katika geti letu.Kwa hiyo
sina hakika kama mtoto waliyekuwa
wakimtafuta ni wewe au kuna wengine
ambao nao walitekekezwa getini wakati
huo.” “ Unawafahamu watu hao mahala
walipo? Waliacha kumbu kumbu zao?
Akauliza Sanya
“ Sifahamu mahala waliko wala sina
mawasiliano yao lakini niliwaelekeza kwa
mama mmoja ambaye amewahi kufanya
kazi katika kituo hiki kwa miaka mingi
sana ambaye kwa sasa ni mtu mzima sana
na anasumbuliwa na maradhi.Sifahamu
kama walifanikiwa kuonana naye na
aliwaambia nini kwani hawajawahi
kurejea tena hapa” akasema mkurugenzi
“ Huyo mama anaishi wapi ?
Unaweza kutuelekeza tukamuone?
yawezekana akawa na taarifa zinazoweza
kutusaidia kuwapata wazazi wangu.Kama
amefanya kazi hapa kwa muda mrefu
yawezekana kuna mambo anaweza
kuyafahamu yanayoweza kunisaidia
kuwapata wazazi wangu.” akasema Sanya
“ninaweza kuwapelekea hadi mahala
anakoishi kwani kwa kuwaelekeza
mnaweza mkapotea”
“ Tutashukuru sana mama kwa
msaada wako” akasema Pauline kisha
mkurugenzi akaongozana nao wakaingia
garini na kundoka kuelekea nyumbani
kwa Bi Elizabeth ambaye aliwahi kufanya
kazi katika kitu hiki kwa miaka mingi. “ Kwa nini huku Tanzania vitendo
vya utupaji watoto vimeshamiri sana?
Akauliza Sanya wakiwa garini
“ Kuna sababu nyingi zinazopelekea
watu kuamua kuwatupa watoto wao
lakini kubwa ni mimba zisizotarajiwa.Hiki
ni chanzo kikubwa cha wazazi kuamua
kuwatupa watoto wao kwani
wanapojifungua wanajikuta hawana
uwezo wa kuwahudumia watoto wao kwa
hiyo huamua kuwatupa.Wengine huenda
mbali zaidi na kuamua kuwaua kabisa
watoto na kuwatupa jalalani” akasema
Mkurugenzi
“ Hakuna elimu ya uzazi inayotolewa
mashuleni au hata kwa wale ambao
wamekosa elimu ya darasani ? akauliza
tena Sanya
“ Elimu ya uzazi inatolewa mashuleni
lakini nadhani inahitaji kutiliwa mkazo
zaidi ili iwafikie watu wengi hususan
wale ambao hawakupata bahati ya
kwenda shule” akasema Mkurugenzi.
“ Nimeguswa sana na suala hili na
pengine nikirudi marekani ninaweza
nikafanya kitu Fulani kwa ajili ya kusaidia
kutoa elimu ya afya ya uzazi mashuleni
n.k.Inawezekana kabisa kwamba wengi
wa wanaofanya hivi wanakosa elimu sahihi ya masuala ya uzazi na mahusiano”
akasema Sanya
“ Pamoja na ukosefu wa elimu ya
uzazi “ akasema Alfred ambaye muda
mwingi alikuwa kimya
“ Umasikini wa kipato nao una
mchango mkubwa sana kwa watu
kuwatupa ,kuwaua ama kuwatelekeza
watoto wao.Hata kama mama amepata
elimu ya uzazi ikatokea labda amepata
mimba bila kukusudia mfano kwa
kubakwa ama sababu nyingine na
akajifungau mtoto huku akiwa hana
uwezo wa kumtunza Yule mtoto wengi
suluhisho lao huwa ni kuwatupa ama
kuwaua watoto wao.” Akasema Alfred
“ Dr Alfred ameongea kitu cha msingi
sana kwamba yawezekana umasikini wa
kipato unachangia kwa kiwango kikubwa
sana kwa tabia hizi za utupaji watoto
kuota mizizi.Inawezekana hata mama
yangu alinitupa kutokana na sababu kama
hiyo ya umasikini” akasema sanya
“ Sanya unasema kwamba mama
yako alikutupa? Akauliza Fred kwani
hakuwa akifahamu chochte
“ Ndiyo Dr Alfred .Mama yangu
alinitelekeza katika geti la kituo kile
tulichotoka na ndiyo maana nimekuja Tanzania kutaka kuitafuta asili yangu na
kuwafahamu wazazi wangu.Pauline
hajakwambia?
“ hapana Pauline hajanieleza
chochote.Pole sana.” Akasema Alfred
“ hakuna haja ya kunipa
pole.Tunatakiwa kumshukuru Mungu kwa
kuniweka hai mpaka hii leo kwani katika
makuzi bila ya mama mengi yangeweza
kutokea lakini kwa uweza wake mimi
hapa leo hii nina afya njema kabisa ,nina
jitegemea mwenyewe,nina elimuya
kutosha na zaidi ni mrembo si ndiyo?
Akasema Sanya na wote ndani ya gari
wakacheka.
“ Mungu ana njia nyingi za kukuinua
ndiyo maana baada ya kutafakari kwa
miaka mingi nimemsamheme mama
yangu kwani yawezekana Mungu ana
mipango na mimi na alitaka nipite njia hii
ili aweze kunitumia kwa mipango yake na
sasa ninaanza kuona kitu ambacho Mungu
anataka nikifanye kwa watu wake. “
akasema Sanya.Wote ndani ya gari
wakawa kimya wakimsikiliza
“ Hata kama nisipowafanikiwa
kuwapata wazazi wangu ,Lazima nirudi
Afrika,lazima nirejee Tanzania kuna mambo mengi ambayo natakiwa
kuyafanya huku”
Maongezi yalikuwa mengi ndani ya
gari na hatimaye wakajikuta wamefika
nyumbani kwa Bi Elizabeth kaaya mama
ambaye amefanya kazi katika kituo kile
kwa miaka mingi toka usichana wake hadi
alipokuwa mzee.
Walishuka garini na kwenda kubisha
hodi wakakaribishwa ndani na mama
mmoja wa makamo.
“ Sisi tunatoka katika kituo cha
malezi ya watoto ambako Bibi Elizabeth
amefanya kazi kwa miaka
mingi.Tunashida naye kubwa” akasema
mkurugenzi
“ Elizabeth ni shangazi yangu na kwa
bahati mbaya hamtaweza kuonana naye
kwa sasa kwani ana siku ya tano leo
amelazwa hspitali anaumwa sana na hali
yake si nzuri hata kidogo.Anasumbuliwa
na figo” akasema Yule mama .Sanya
akashika kichwa ,taarifa ile ilimkatisha
tamaa kabisa.Hakukuwa tena na namna
nyingine ya kufanya zaidi ya kuondoka
pale na kuelekea katika hospitali ambako
Elizabeth alikuwa amelazwa. Kabla
hawajatoka mle ndani Sanya akavutiwa na
picha zilizokuwa juu ya kabati akaainuka na kuanza kuzitazama.Akaiona picha moja
iliyomvutia akaichukua akaitazama na
kutabasamu
“ Huyu ndiye Elizabeth? Akauliza
“ Ndiye mwenyewe” akajibu
mkurugenzi
“ Basi huyu aliyepiga naye picha hii
ndiye mama yangu mlezi” wote
wakaitazama picha ile ambayo Elizabeth
alipiga na mama mmoja wa kizungu kisha
wakaondoka kuelekea hospitali
“ Sanya usikate tamaa tafadhali
.Tumtangulize Mungu mbele katika suala
hili na kama ni mapenzi yake basi
atafanikisha jambo hili” akasema Fred.
Elizabeth alikuwa amelazwa katika
hospitali ya mkoa ya Mount Meru .Kwa
muda waliofika hali ya Elizabeth ilizidi
kuwa mbaya zaidi iliyowaogopesha hadi
ndugu zake na walikata tamaa
kabisa.Baada ya kuiona hali ile Sanya
alikata tamaa ya kuweza kupata taarifa
zozote kuhusiana na wazazi wake kwani
mtu aliyemtegemea labda angeweza
kumpa mwanga hakuweza kufumbua hata
macho.Walirejea mahala walikoegsha gari.
“ Tayari nimekata tamaa ya
kuwapata wazazi wangu.kwa hali ya Elizabeth ilivyo sina hakika kama anaweza
akapona.” Akasema Sanya
“ usiseme hivyo Sanya na wala
usikate tamaa.Mungu ni muweza na
Elizabeth anaweza akapona”
“ Mimi ni daktari na ninafahamu mtu
ambaye hawezi kupona.Mpaka hapa
nadhani nimeshindwa .Kilichobaki ni
mimi kujipanga upya kwa mambo
mengine “ akasema Sanya
“ Kwa nini tusitumienjia ya
matangazo? Akauliza Fred
“ Ukitangaza leo hii wanaweza
wakatokea wanawake zaidi ya elfu moja
na likaanza tena zoezi la kupima vinasaba
na unaweza ukafanya zoezi hilo ambalo
litagharimu muda na mwisho wa siku
ukashindwa kumpata mama
yako.Nadhani tukubali kwamba mpaka
hapa hakuna tena namna nyingine ya
kufanya.Kuungana tena na wazazi wangu
ni vigumu sana” akasema Sanya.Ghafla
Mkurugenzi akakumbuka kitu
“ Kuna kitu nimekumbuka !.akasema
“ Umekumbuka nini Mkurgenzi”
akauliza Pauline
“ Nimekumbuka kitu.Katika watu
wale wawli waliokuja pale ofisini
wakiulizia taarifa za Yule mtoto niliyewaelezeni kuna mmoja
alijitambulisha kama mmiliki wa shule
moja kubwa hapa mjini inaitwa St
Lucia.Nadhani si vibaya kama tukimuona
na huyu anaweza akawa na msaada
mkubwa kwetu” akasema mkurugenzi
“ Kama uliwaelekeza kwa Elizabeth
na hawakurejea tena kwako ni wazi
kwamba hawakufanikiwa kupata
walichokuwa wanakitafuta.Nadhani
hakuna haja ya kuendelea kuumiza
kichwa kwa jambo hili.Si suala rahisi hata
kidogo .Tuachane nalo na tuendelee na
mambo mengine.” Akasema Sanya.Pauline
akamtazama na kusema
“ Sanya unakata tamaa mapema
sana.”
“ Pauline suala hili liko wazi kabisa
kwamba ni gumu na linahitaji muda mrefu
sana.Kama ningekuwa na viza ya muda
mrefu ya kuniwezesha kuishi hapa
Tanzania basi ningejipa moyo kwamba
ningeweza kuwapata wazazi wangu lakini
sina muda mrefu sana na isitoshe nina
kazi zinanisubiri Marekani kwa hiyo zoezi
hili inabidi lisimame.Lakini siku moja
nitarejea Tanzania kama nilivyoahidi na
nitafanya mambo makubwa “ akasema
Sanya.Pauline na wenzake hawakuwa tenana neno la kuweza kumshawishi Sanya
.Pauline akawasha gari wakaondoka
“ Kwa sasa tunaelekea wapi?
Akauliza Sanya
“ kwa sasa tunamrejesha
mkurugenzi ofisini kwake Usa river halafu
tuendelee na ratiba nyingine” akasema
Pauline
“ Pauline sitaki tena kwenda usa
river.Wasiliana na David kama anaweza
kuwa na muda mchana huu ili nipate naye
chakula ninyi mtaenda Usa river na
tutaonana mkirejea jioni kwani najua
mna mambo mengi ya kufanya jumamosi
hii kama wapenzi.Mimi nitakuwa na David
nataka vile vile anitembeze ndani ya jiji
hili nilifahamu vizuri.” akasema Sanya na
kumtazama Alfred ambaye alikuwa
anatabasamu.
Pauline akachukua simu na
kumpigia David akamuomba aende
Silvano hoteli ambako atamkuta Sanya
anamsubiri ili waweze kupata wote
chakula cha mchana.Hii ilikuwa ni fursa
ambayo David hakuwa ameitarajia
kabisa.Alitamani sana kuipata nafasi ya
kukaa na Sanya na kuongea lakini hakujua
angeanza vipi kwani bado alikuwa
anamuogopa Pauline.Alikatisha mkutano wake mchana huo na baadhi ya wafanya
biashara na kuchoma mafuta kumuwahi
sanya Silvano hotel
Sanya aliachwa Silvano akiendelea
kumsubiri David ,Pauline na Alfred
wakawarudisha mkurugenzi pamoja na
Yule ndugu yake na bi Elizabeth.
Wakati akimsubiri David,Sanya
aliendelea kupata kinywaji huku kichwa
chake kikionekana kuvurugika kabisa
“Sitaki tena kuendelea na zoezi hili
kwani mpaka hapa limekwisha
shindikana.Kikubwa ni kwamba
nimejitahidi kufanya jitihada za kumtafuta
mama yangu lakini imeshindikana.Sina
hakika kama huko aliko bado yuko hai au
hata ananikumbuka na ana hamu ya
kuonana nami. Nina hakika hana tena
habari na mimi na hanikumbuki
tena.yawezekana labda anajua siko hai
.Hakunihitaji katika maisha yake na ndiyo
maana akanitupa .Ninamshukuru Mungu
kwamba nina watu wengi ambao
wananipenda na wanayafanya maisha
yangu yawe na furaha bila hata wazazi
wangu.Ngoja niachane na mambo haya na
nielekeze mawazo yangu katika mambo
mengine ya maisha yangu na hususan
David “ akawaza Sanya “ Kuna kitu nimekiona kwa David
ambacho sijakiona kwa wanaume wengi
katika sehemu nyingi nilizopita.Ana kitu
Fulani ambacho wengi hawana
.Ninakumbuka jana alivyotupokea
akatukaribisha ,anaonekana ni mtu
mwenye moyo wa aina yake…”
“ Hallow Sanya” Sauti ikasikika
nyuma yake na kumtoa Sanya katika
mawazo mengi akageuka na kutazama
nyuma yake.Akastuka sana.Alikuwa
anatazamana na sura yenye tabasamu ya
David.
“ David umenistua sana.Nilikuwa mbali
kimawazo .Sikujua kama utatokea kwa
nyuma”akasema Sanya
“ Pole Sanya kwa kukustua.Hoteli
hii ina sehemu mbili za maegesho.habari
za toka jana? Toka tulipoachana jana
usiku hatujaonana tena.Niliwahi sana
kuondoka asubuhi na kuwaacha bado
mmelala.” Akasema David
“ Pauline alinieleza na amekusifia
sana kwa utendaji wako wa kazi .Hongera
sana” akasema Sanya
“ahsante sana Sanya” akasema David
na kuvuta kiti akaketi Muhudumu akafika wakaagiza chakula
.Wakati wakisubiri chakula wakaendelea
na maongezi
“ Karibu sana Arusha sanya.karibu
sana Tanzania” akasema David.Sanya
akatabasamu na kusema
“ Nadhani ungeniambia karibu
nyumbani kwa sababu mimi Tanzania ni
nyumbani “
“ Wewe ni raia wa Tanzania? David
akashangaa
“ Kwa sasa mimi ni raia wa
Marekanani lakini asili yangu ni
Tanzania.Nimelizaliwa Tanzania.Wazazi
wangu ni watanzania.Nilihamia Marekani
nikiwa mdogo sana na maisha yangu yote
nimeishi kule” akasema Sanya na
kumfanya David atabasamu
“ Ouh ! nimefurahi kusikia
hivyo.Kwa hiyo hapa Tanzania unatokea
mkoa gani? Akauliza David.
“ Sina hakika sana na asili ya wazazi
wangu lakini yawezekana ni
Arusha.”akajibu Sanya.David akashangaa
kidogo na kuuliza.
“ kwani wazazi wako hawajakueleza
wao wanatokea mkoa gani ? “ kwa bahati mbaya sijawah
kuwaona wazazi wangu”akasema Sanya na
kuzidi kumshangaza David
“ Wametangulia mbele za haki?
Akauliza
“ Sina hakika kama wametangulia
mbele za haki lakini historia yangu
inaonyesha kwamba mimi niliokotwa
baada ya kutelekezwa na mama yangu
katika geti la kituo cha kulelea watoto
wadogo Usa river nikiwa na kama wiki
moja au mbili hivi baada ya
kuzaliwa.Nimelelewa katika kituo kile
pale usa river na kwa bahati nzuri mlezi
wangu alinipenda sana na alipomaliza
muda wake wa kuishi hapa nchini
akanichukua na nikaenda kuishi naye
Marekani.Nimeishi kule mpaka sasa
nilipoamua kuja Tanzania kujaribu bahati
yangu kama ninaweza kuwapata wazazi
wangu”akasema Pauline.David
akamtazama na kumuonea huruma sana
na akasema
“ Pole sana Pauline kwa historia
hiyo.Mungu atakusaidia na utafanikiwa
kuungana tena na wazazi
wako.Ninakuhakikishia utawapata tena
wazazi wako” akasema David na
kumfanya Pauline atabasamu “ Wewe na dada yako Pauline
mnafanana sana.Nyote ni watu ambao
hampendi kukata tamaa kabisa.Hata
Pauline alikuwa ananiambia hivyo hivyo
unavyoniambia”akasema sanya na wote
wakacheka
“ Pauline umekutana naye wapi
mkajuana? Akauliza David
“ Nimekutana naye Moshi katika
hoteli niliyofikia .Nilikuja na wenzangu
kutembelea mbuga za wanyama na
kupanda mlima Kilimanjaro.baada ya
kumaliza ziara yetu wenzangu waliondoka
lakini mimi kwa kuwa nilikuwa na kazi ya
kufanya nikabaki na katika hoteli
niliyofikia mjini Moshi nikakutana na
Pauline.Nilipomuona nilivutiwa sana
kujenga naye urafiki,kwa bahati mbaya
siku za mwanzo alikuwa ni mtu mwenye
shghuli nyingi lakini baadae nikazoeana
naye na tukawa marafiki.Nilifurahi
aliponiambia kwamba yeye ni mwenyeji
wa Arusha nikamuomba kwamba siku
atakapokuja Arusha aongozane nami ili
niweze kuja kuanza zoezi la kutafuta
taarifa za wazazi wangu.Kwa bahati nzuri
jana alinifuata na kuniambia kwamba
amepata safari ya dharura ya kuja arusha
hivyo nikaongozana naye pamoja na mchumba wake Dr Alfred.” David
akastuka sana aliposikia kwamba Alfred
na Pauline ni wachumba lakini hakutaka
kuonyesha mstuko ule mbele ya Sanya
akatabasamu na kusema
“ Vipi mchakato wa kuwatafuta
wazazi wako umekwisha anza?akauliza
David.Sanya akanywa juice halafu
akasema
“ Leo asubuhi tumekwenda usa river
katika kile kituo nilikolelewa.Nimeonana
na Mkurgenzi wa kituo kile na kwa bahati
mbaya sana hakuna taarifa zozote ambazo
zingeweza kunisaidia kukutana na wazazi
wangu.Mkurugenzi Yule ana roho nzuri
sana kwani alitupeleka kwa mama
mmmoja aitwaye Elizabeth ambaye
amewahi kufanya kazi katika kituo kile
kwa miaka mingi toka akiwa msichana
ambaye tulitegemea kwamba anaweza
akawa na kitu chochote anachokifahamu
kuhusu mimi lakini kwa bahati mbaya
sana mama huyo ni mgonjwa mahututi
amelazwa hospitali anasumbuliwa na figo
na muda wowote anaweza akafariki.Zoezi
limekuwa gumu sana na linakatisha
tamaa” akasema sanya akionekanakabisa
kukata tamaa “ Sanya usikate tamaa.kwa vile
umekuja huku Tanzania kuwatafuta
wazazi wako nakushauri usiondoke bila
kuwaona wazazi wako.Sisi tupo
tutakusaidia kwa kila namna hadi jambo
hili lifanikiwe”akasema David na
kumfanya Sanya atabasamu
“ Nimefurahi sana kwa namna
mnavyonipa moyo .Nimeamini yale
maneno kwamba watanzania ni watu
wakarimu sana “akasema Sanya
“ Suala hili ni kubwa kwa hiyo
hutakiwi kabisa kukata tamaa na sisi
kama rafiki zako tunatakiw a tukushike
mkono na kuhakkisha kwamba
unafanikiwa kuungana tena na wazazi
wako .Nakuhakikishia kwamba
tutawasaka kokote waliko na kama wako
hai basi tutawapata tu.Hata kama si leo
lakini siku yoyote ile lazima
wapatikane.”akasema David
“Ninakosa neno la kusema David
kwa ukarimu wenu.Tayari nilikwisha kata
tamaa kabisa na kuamua kuachana na
suala hili lakini umekuja wewe na
nimepata tumaini jipya la kusonga mbele
kuwatafuta wazazi wangu.”akasema
sanya.Muhudumu akafika na chakula walichoagiza akawandaalia meza
wakaendelea kula taratibu
“ Sikuhisi kabisa kama historia ya
Sanya inaweza ikawa namna
hii.Ukimtazama hudhani kama asili yake
ni Tanzania.Mtoto anang’aa kama
Beyonce .kwa kweli hapa lazima nichange
karata vizuri na mtoto huyu
simuachi.Nitafanya kila niwezalo hadi
nihakikishe nimempata .Ninachotakiwa
kukifanya kwa sasa ni kuwa mstari wa
mbele kumsaidia katika zoezi la kuwasaka
wazaziwake ingawa sijui nitamsaidiaje
lakini nitajarbu kila njia niwezayo.Sanya
yuko tofauti sana na Yule kahaba
Tamia.Huyu ni msichana mwenye heshima
zake,ana elimu nzuri na anajtambua
.Hata maongezi yake yanaonyesha wazi
kwamba ni mtu mwenye akili ya kiwango
cha juu sana tofauti na msichana kama
Tamia.”akawaza David huku akimtazama
sanya kwa kuibia
“ David mbona unanitazama hivyo ?
Kuna kitu unataka kuniuliza?
“ uhmmm.hapana sanya nilikuwa
natafakari tu.”
“ Unatafakari nini? Akaulzia
sanya.David akasema “ Natafakari kuhusu mama yako
lazima atakuwa mrembo sana”akasema
David na kumfanya sanya acheke kicheko
kikubwa.
“kwa nini umeseam hivyo david”
“kama wewe ni mzuri hivi
unategemea maaa yako atakuaje?lazima
atakuwa ni mzuri mara mbili
yako”akasema David na kuzidi kumvunja
mbavu Sanya
“ David ninatamani sana kumfahamu
mama yangu .Inawezekana hayo
unayoyasema yakawa kweli na mama
yangu akawa ni mrembo
kupindukia”akasema Sanya na kuzama
ghafla katika mawazo na baada ya muda
akasema
“ Unaifahamu shule inatwa st Lucia?
“ Ndiyo ninaifahamu”akasem David
“ Basi nitapenda unipeleke siku ya
jumatatu.”
“ usijali nitakupeleka.Kuna mtu
unakwenda kumuona pale?
“ Ninataka nikaonane na mkuu wa
shulehiyo”
“Unafahamiana naye?
“hapana sifahamiani naye.Kuna
mradi ninafikiria kuuanzisha mara tu
nitakaporejea marekani.Nimegundua kwamba matukio ya utupaji watoto hapa
Tanzania ni mengi na hii inachangiwa na
ukosefu wa uelewa wa kutosha wa elimu
kuhusu afya ya uzazi na mahusiano.Vile
vile nimegundua kwamba kiti kingine
kinachochangia kwa tabia hii ya utupaji
wa watoto kuongezeka ni umasikini wa
wazazi.Nimepanga kuanzisha shirika
ambalo kazi yake itakuwa ni kusambaza
elimu ya uzazi na mahusiano mashuleni na
vile vile litakuwa na jukumu la kuwasaidia
wanawake masikini kujikwamua
kiuchumi.Hili si jukumu dogo lakini
nitakaporejea marekani nitachangisha
fedha na kutafuta watu ambao wataniunga
mkono ili nipate fedha za kutosha za
kuendesha shirika hilo.Hilo si jukumu
dogi lakini nitahakikisha
ninalikamilisha.Mimi nilitupwa lakini
nikabahatika kulelewa na familia tajiri
ambayo imenifikisha hapa nilipo.Kama si
bahatio hii hvi sasa sijui ningekuwa wapi
.Lakini kabla ya kuanzisha shirika hili
nitapenmda sana kwanza kutembelea
katikamakazi ya watu masikini .Kuna
mambo nnatak akujifunza.” Akasema
Sanya
“ Sanya nimefurahishwa sana na
wazolako nma ninakuahidi ushirkianao wangui mkubwa katiak sualahili
.Nitakusaidia kwa kila kitu
unachokihitaji.Jumatatu nitakupeleka
katika shule unayotaka kwenda na kisha
nitakutemeba sehemu mbalimbali za jinji
hili la Arusha ,nitakupeleka katika sehemu
zenye makazi duni ambako utajifunza
mambo mengi. “akasema David
Robin alimchukua mwalimu Lucy
hadi katika hoteli moja kubwa iliyokuwa
nje ya jiji la Arusha.
“ Robin huku tunakuja kufanya nini?
Akauliza Lucy wakati wakiingia katika
hoteli ile kubwa.Robin akageuka na
kumtazama Lucy akasema
“ We’ll spend the weekend here”
Lucy akapatwa na mshangao kisha
akamkumbatia Robin kwa nguvu na
kumpiga busu
“ Ouh Robin nimekosa neno la
kusema .Thank yopu.Thank yopu so much
my love” akasema Lucy huku akifuta
machozi yaliyomtoka
“ Robin leo umeniweza kweli
.Sikujua kama tunakuja hapa .Kweli hii ni syuprise kubwa kwangu” akasema
Lucy.Bado machozi yaliendelea kumtoka.
“ Usilie Lucy.Bado kuna suprises
kwako” akasema Robin
“ Another surprise? Lucy
akashangaa.Robin akaegseha gari na
kushuka haraka akaenda kumfungulia
Lucy mlango akamshikamkono wakaeleka
ndan I ya hoteli.Tayari alikwisha weka oda
ya chumba ,hivyo moja kwa moja
muhudumu akawaogoza hadi katka
chumba chao kilichokuwa katika ghorofa
ya tatu.
Ndani ya chumba kulikuwa na kila
kitu ambacho Lucy anakitumia kuanzia
mafuta,uturi hadi vipodozi.Akamtazama
Robin na kumkumbatia.
“ Kweli Robin leo hii umeamua
kunifanyia surprise.Sikutegemea kabisa
kam aungeweza kunifanyia hivi” akasema
Lucy na kuchukua kitambaa
akafutamachozi
Robin akaagiza waletewe vinywaji
kisha wakakaa kitandani.
“ Robin kabla hujanieleza chochote
naomba niseme kwamba leo nimefurahi
sana.Kutoka nje ya mji sehemu kimya
kama hii ni kitu ninachokipenda
sana.Nilikuwa nina panga kufany akitu kama hiki lakini umeniwahi .Ninasema
ahsante sana.Nimefurahi sana “ akasema
Lucy
“ Lucy sikujua kama unapenda jambo
hili ila kwa sasa baada ya kujua basi
tutalifaya mara nyinhi tu.Ila kwa leo kuna
jambo maalum nililokuletea hapa”
akasema Robin
“ Robin unanifanya hadi ninaogopa
kwa suprises zako.” Akasema Lucy.
Robin akaenda katika kabati la nguo
akalifungua na kutoa sanduku dogo na
kuliweka kitandani
“ Kuna nini humu Robin? Akauliza
Lucy.
“ My love hii ni surprise ya kwanza
kwako kwa siku ya leo .Ninakuoba
ulifungue sanduku hili wewe mwenyewe
kwa mkono wako na utazame kilichomo
ndani” akasema Robn
“ Robin hebu nieleze kwanza
,uilijuaje kama kuna sanduku mle
kabatini? Robin akatabasamu na kusema
“ Nilifika hapa hapo kabla na
nikaanda kila kitu .Fungua hilo sandulu
Lucy” akasema Robin.Huku mikono
ikimtetemeka akalifungua sanduku lile na
ndani yake akakutana na bahasha kubwa. “ Ichukue hiyo bahasha na usome
kilichomo ndani yake” akaelekeza
Robin.Lucy akaifungua ile bahasha akatoa
karatasi iliyoonekana kama cheti na
kuanza kuisoma na mara akaruka kwa
furaha na kumkumbatia Robin.Machozi
mengi yakamtoka.Alikuw ana furaha
iliyopitliza.Alitaka kila neno zuri
alioliofahamu kwa kweli ilikuwa ni siku
yakeya futraha kubwa mno .Baada ya
dakika zaidi ya kumi za kupandwa na
wazimu wa furaha akaanza kutulia
“ Robin my love siku nyingine
usinifanyie suprises kama hii.Utaufanya
motyo wangu upasuke kwa furaha.”
Akasema Lucy huku akiendelea
kudondosha machozi.Robin akachukua
kitambaa na kumfuta machozi halafu
akasema
“ Leo asububi nlipigiwa simu
kwamba ninahitajika katika ofisiya
askofu.Sikupoteza muda nikafika kabla
hata ya muda nilotakiw
akufika.Nilifanikiw akuonana na askofu
ambaye alinieleza kwamba lile ombi langu
la kutenga ndoa yangu na Vivia tayari
majibu yakeyalikuwa yamerudi.Kwa hivi
sasa kanisa limerekebisha sheria na
taratibu zake na ukichanganya na ukuaji wa teknolojia mambo hayachukuio mud
amrefu kutolewa maamuzi na isitoshe
viopngozi wakubwa wa kidini
wamekasimiwa majukumu ya utoa
maamuzi katika kesi kama hizi kwa niaba
ya kiongozi mkuu wa kanisa .Baada ya
suala langu kufika katikameza ya vongozi
wa juu wa kanisa na kulijadii kwa kina
hatmaye walifikia maamuzi na uamuzi
walioufikia ni wa kukubaliana na ombi
langu la kutaka kuitengua ndoa yanguna
Vivian ka hiyo rasmi sasa mimi na Vivian
si wanandoa tena na kila mmoja
anaruhusiwa kuoa au kuolewa.”Robini na
Lucy wakakumbatiana tena kwa furaha
kubwa na kupongezana kwa ushindi ule
mkubwa
“ Lucy nilipatwa na furaha ya ajabu
sana na ndiyo maana nikafanya haya yote
niliyoyafnya .Hii ni siku yetu kubwa
sana.Nisiku ya furahakubwa katika
maisha yetu.Huu ni mwanzo mpya kati
yetu “ akasema Robin.Huku bado machozi
yakiendelea kumtoka Lucy akasema
“ Robin nimeksoa neno la kusema
.Badio siamini kama jambo hili ni
kweli.Nilidhai labda ingecbhukua miaka
hata zaidi ya m itatu kukamilika lakini
imenishagaza kw anama jambo hili lilivyokwenda haraka haraka.Mungu
ashukuriwe sana”
“ Lucy kama nilivyokueleza awali
kwamba mambo ndaniya kanisa
yamebadilika sana na kingine kilichowapa
urahisi viongozi wa juu kulitolea maamuzi
suala hili ni namna jambo lenyewe
lilivyo.Namna Lucy alivyovunja kiapo
chake cha ndoa na kunitelekeza mimi na
mtoto.Niwazi kwamba
hakustahilikuendelea kuwa mke wangu.”
Akasema Robin kisha akainuka na kwenda
tenakatika kabati akalifngua na kutoa
kijikasha kidogo akakifugua na kutoa pete
nzuri akaishka mkononi na kupiga goti
moja mbele ya Lucy.
“ Nimewahi kuteswa na mwanamke
na nikakata tama kabis aya kupenda tena
lakini nilipokutana na wewe nikakivuna
kiapo change na kuufugua myo wangu
kwako.Toka nilipokutana nawe umekuwa
ni furaha ya maisha yangu,taa imulikayo
maisha yangu,dirana mwelekeo wa
maisha yangu,umekluwa ni kila kitu
kwagu na kwa mwanangu Penina.Kwetu
umekuwa ni kama ua zuri ambalo
huchanua kila siku na kusambaza harufu
nzuri ya manukato .Lucy mmi na
mwanangu Penina tunakuhitaji sana katika maisha yetu na nimepiga gotri
mbele yako kukuomba jambo moja tu.Will
you merry me ?
Midomo ya lucy ikamtetemeka
akashindwa kuongea ,macho yake yalijaa
machozi.
“ Will you merry me Lucy ? akauliza
“ Yees..!!!...Yes ‘ akajibu Lucy.Robin
akainuka wakakumbatiana kwa nguvu
“ basi imetosha Lucy,usilie tena.” Robin
akambembeleza Lucy ambaye macho yake
yalijaa machozi
“ Robin niache nilie.Ninakumbuka
shida na mateso niliyoyapitia na siamini
kama leo hii nimefikia hapa.Machozi
yananitoka kwa furaha niliyonayo kwani
niliamini kwamba maisha yangu yamejaa
mikosi na labda sintampata mwanaume
ninaye muhitaji katika maisha yangu
atakayenipenda kwa moyo wake wote
.Mungu bado ananipenda na amekuleta
wewe Robin.Umenipandisha hadi
uwinguni na kunifanya nijione ni
mwanamke wa pekee na mwenye bahati
kubwa.Sina hakika kama kuna mwanamke
mwingine ambaye amewahi kuvishwa
pete mbili za uchumba na
mwanaumemmoja”akasema Luvy na wote wakaangua kicheko wakakumbatiana
tena.
“ Robin wewe umelifanya hilo.Pete
hii uliyonivisha leo ni pete ya pili.”
Akasema Lucy.Robin akamtazama
akambusu na kusema
“ Nilifanya hivyo makusudi
Lucy.Pete ya kwanza nilikuvalisha wakati
ule ambao bado nilikuwa ni mume wa
Vivian tukisubiri ndoa yetu itenguliwe na
kanisa.Sikujua zoezi lile la utenguzi
lingechkua muda gani na ndiyo maana
nikakuweka alama ili kila atakayekuona
ajue kwamba tayari una mwenyewe.Kwa
sasa niko huru .Si mume wa mtu tena na
ndiyo maana nimeamua kukuvisha pete
nyingine rasmi nikiwa mtu huru ambayo
hii mbadala wake utakuwa ni pete ya
ndoa.” akasema Robin na kuitoa pete ile ya
zamani akamvisha mpya.
“ Robin kuna jambo moja ninataka
kukuomba mpenzi wangu.”akasema Lucy
“ Omba chochote Lucy nitakupatia”
“ Ili furaha yangu ya leo ikamilike
ninaomba tukawatembelee Vivian na
Martin hospitali tuwape pole .Kwa nyakati
tofauti waliwahi kuwa wapenzi wetu.Mimi
nilikuwa na martin na wewe ulikuwa na
Vivian.Najua wametutenda na kutuumiza sana lakini huu ni wakati wa kuyaweka
pembeni yale yote waliyotufanyia na
kwenda kuwajulia hali.Tayari tumekwisha
kipata tulichokuwa tunakihitaji kwa hiyo
hakuna haja ya kuendela kuweka visasi .”
akasema Lucy .
“ Lucy wewe ni mwanamke mwenye
moyo wa kipekee kabisa.pamoja na yote
ambayo Martin amekufanyia lakini bado
unamuonea huruma?”akasema Robin
“ Robin sisi ni binadamu na sote
tunakosea.Hata wao pia walikosea na
tunaagizwa kwamba tunapokosewa
tunatakiwa kuwasamehe
waliotukosea.Hata kama tukilipa kisasi
haitatusaidia chochote.Tusahau yaliyopita
na tuwasamehe.” Akasema Lucy
“ Robin nitakwenda hosptali
kuwaona lakini ni kwa sababu yako
tu.Sikuwa tayari kabisa kwenda
kumtazama tena Vivian nikikumbuka
mambo aliyonifanyia.”akasema Robin
“Ahsante kwa kunikubalia ombi
langu mpenzi wangu.Mungu akubariki
sana” akasema Lucy.
********************** Ni saa mbili za usiku ,nyumbani kwa
mzee Zakaria familia imekutana mezani
kwa chakula cha usiku ambacho
kiliandaliwa maalum kabisa kwa ajili ya
Pauline na wageni wake .Mzee Zakaria
alitaka apate wasaa wa kufurahi tena na
mwanae na vile vile kuwafahamu marafiki
aliokuja nao.Mezani walikuwepo Mzee
Zakaria , mkeweVicky madhahabu ,David
,Sanya na mtumishi wa ndani.Pauline na
Alfred hawakuwepo mezani.Toka
walipoachana na Sanya mchana
hawakurejea tena na hawakumfahamisha
mtu yeyote walikuwa wapi
Baada ya kupata chakula kile kizuri
wote wakajumuika katika chumba cha
mapumziko kwa maongezi
“ Sanya karibu sana hapa
kwetu,karibu sana Tanzania.”akasema
mzee Zakaria
“ Ahsante sana baba nashukuru”
akajibu Sanya
“ Mimi kama nilivyojitambulisha
asubuhi,ninaita Zakariaa ,ni baba mzazi
wa Pauline na huyu hapa ni mke wangu
anaitwa Vicky.Yule pale kijana wangu
David ambaye tayari umekwisha
mfahamu.karibu sana katika famliaya
pauline’”akasema mzee zakaria na maongezi yakaendelea.Waliongea mambo
mengi sana hadi ilipotimu saa tano za
usiku mzee Zakaria akaonekana kuchoka
akaenda zake kulala.David na sanya pia
wakaagana na kila mmoja akaingia
chumbani kwake kulala.
“ Pauline yuko wapi leo? Akajiuliza
David.Akachukua simu na kujaribu
kumpigia lakini namba ya simu ya Pauline
haikuwa ikipatikana.
“ Ananishangaza sana
Pauline.Amezima simu bila kutujulisha
yuko wapi.Pauline amebadilika
sana.Lakini nisimlaumu kwani ni mimi
ndiye niliyechangia sana katika
mabadiliko haya kwa mambo
niliyomfanyia.”akawaza David akiwa
amekaa kitandani
“ Kumbe yeye na Fred ni wapenzi ?
Nimefurahishwa na jambo hili.Fred
anaonekana ni kijana mzuri ,msomi,na
anampenda Pauline.Nina hakika
hatamuumiza kama nilivyofanya
mimi.Pauline na mimi tutabaki kuwa na
mahusiano ya kaka na dada.”
Akatabasamu na kuvua fulana yake
akajilaza kitandani.
“ Pauline inaonekana
amechaganyikiwa kabisa na penzi la Alfred na ndiyo maana amesahau hata lile
suala ambalo nilimuitia .Tulikubaliana leo
tutafute wasaa ili nimueleze kwa ufasaha
kila kitu kinavyokwenda lakini
ameonekana kulisahau kabisa jambo
hili.Ninahisi yuko mahala yeye na mpenzi
wake Alfred wakijivinjari.”akainuka na
kukaa
“ Kesho ndiyo Jumapili siku ambayo
Vicky amedhamiria kuutekeleza mpango
wake wa kumuua mzee Zakaria.Hata kama
Pauline hatakuwepo sintakubali jambo
hilo litokee.Nitamlinda mzee
Zakaria.Nitafanya kila linalowezekana
kuhakikisha kwamba jambo hili
halifanikiwi na huu utakuwa ni mwisho
wa Vicky.Mwisho wake utakuwa wa aibu
sana.Mambo yake yote yatawekwa
hadharani.” akaendelea kuwaza David
“ Kesho itakuwa ni siku mbaya , sijui
nini kitatokea lakini namuomba Mungu
jambo hili analotaka kulifanya Vicky
lisifanikiwe.Nilitaka Pauline alifahamu
jam…” David akastuka toka mawazoni
baada ya kusikia mlango wake
unafunguliwa.Ni kweli kuna mtu aliingia
mle ndani.Alikuwani Vicky madhahabu.
“ Vicky ?!!! akasema David “Shhhh.!! Usipaaze sauti
nimemtoroka Yule mzee nikamwambia
kwamba ninakuja kuongea na Sanya.”
Akasema Vicky kwa sauti ndogo
“ Vicky tafadhali naomba usinitafutie
matatizo nenda chumbani kwako!!
Akafoka David
“ David usiwe mkali mpenzi
wangu.Nimeshindwa kuvumilia
David.Mwili wote unawaka moto na siwezi
kulala bila ya kuguswa nawe.Tafadhali
David nakuomba hata kwa dakika chache
tu.Lile zee kule ndani halitajua chochote .”
Akasema Vicky.
“ Vicky tafadhalinaomba uondoke na
ureje chumbani kwako.Siwezi kufanya
kitendo hicho na wewe leo tena ndani ya
nyumba ya mzee Zakaria.Kama unanihitaji
tafuta siku nyingine na si leo hii” akasema
David lakini ghafla Vicky madhahabu
akamrukia pale kitandani na kuanza
kumvua bukta kwa nguvu
“ David kwa nini unapenda nitumie
nguvu katika jambo kama hili wakati
unafahamu kabisa hali yangu ilivyo na
wajibu wako kwangu ambao tulikwisha
kubaliana? Akauliza Vicky .
“ Vicky nimesema kwamba siwezi
kufanya kitu hicho unachotaka tufanye.Nimesema kwamba siko tayari
kwa leo tena ndani ya nyumba hii.Kwa
nini humuogopi mumeo? Hata kama
unachepukalakini lazima umuheshimu
.Tafadhali toka rudi chumbani kwako”
akasema David huku akijinasua kutoka
katika mikono ya Vicky.
“David mbona unataka kuniudhi
mpenzi wangu? Kwa nini unakuwa hivyo?
Akasema Vicky akiendelea kumbembeleza
David
“Vicky wewe ndiye ambaye hutaki
kunielewa ninapokwambia kwamba hicho
unachokitaka leo hii hakiwezekani
kabisa.”
“ David mwenzako nina hali mbaya
sana na wewe unaendelea kuniumiza
zaidi.Leo sitoki humu ndani bila ya
kuguswa nawe.” Akasema Vicky huku
akiivua nguo ya ndani na kuitupa
pembeni.
“ Huyu mwanamke leo amedhamiria
.Hapana siko tayari kufanya kitendo
hiki.Imetosha sasa” akasema David na
kuchomoka akitaka kutoka mle ndani
lakini Vicky akamuwahi na kumdaka
mkono akamvuta.Purukushani ikaanza
mle chumbani kati ya David na Vicky Hatimaye Vicky akafanikiwa
kumuangusha chini David na kumkalia
juu..
“ David mpenzi wangu kwa nini
lakini unataka tutumie nguvu? Tafadhali
naomba tumalizane na mimi niondoke
zangu.Dakika chache tu David”.
“ Vicky hivi tunavyofanya
tutawafanya watu watusikie na kila kitu
kitaharibika wakitugundua na taarifa
zitamfikia mzee Zakaria.”
“Yote haya yamesababishwa na
wewe David.Unafahau kabisa ni namna
gani ninakuhitaji David lakini umekuwa
unanikwepa kila siku.Tafadhali naomba
penzi lako kwa dakika chache tu” akasema
Vicky
“ haya Vicky umeshinda tusiendelee
kulumbana hadi tukasikika huko
nje.Nitafanya hivyo unavyotaka lakini
naomba nikuweke wazi kwamba kitendo
hiki sijakifurahia kabisa.” Akasema David
huku akiivua bukta yake na kuzidi
kuyapandisha mashetani ya Vicky ambaye
alishindwa kuvumilia akamvuta
wakaenda sofani .
Kukuru kakara zile chumbani kwa
David zikamstua Sanya aliyekuwa katika chumba cha Pauline ambacho hakikuwa
mbali na chumba cha David.
“ Kuna nini kinaendelea ? Mbona
ninasikia vishindo vya kugongwa ukuta na
vitu kuanguka?Kuna watu wanagombana?
Akajiuliza halafu akafungua mlango
akachungulia nje hakukuwa na mtu lakini
akasikia kama sauti za
watuwakibishana.Akatoka na kwenda
kutega sikio katika mlango wa chumba
cha David akasikia kama kuna watu
wanagombana.
“ David anagombana na nani?
Akajiuliza na kusimama pale mlangoni
kwa dakika mbili
“ Huu ninaofanya hapa ni ujinga
mkubwa.Ni vipi iwapo kuna mtu anataka
kumdhuru David? Ngoja nihakikishe”
akawaza Sanya na kukishika kitasa cha
mlango ambao haukuwa umefungwa kwa
funguo akaufungua mlango kidogo na
kuchungulia ndani na kukutana na kitu
kilichomstua sana
“ David !!,.. Aunt?!!! Akajiuliza huku
amepigwa na butwaa .David na Vicky
walikuwa sofani watupu wakifanya
mapenzi. Taratibu akaufunga mlango na
kutoka akarejea chumbani
kwake.Akayafikicha macho “ Hapana siko
usingizini.Nilichokiona si ndoto bali ni
kitu cha kweli kabisa.David na mama yake
mdogo Pauline walikuwa wanafanya
mapenzi.Ninayaamini sana macho yangu
na nilichokiona ni kitu cha kweli kabisa na
si cha kuhadithiwa.” Akawaza Sanya huku
akihisi mwili ukimtetemeka kwa uoga kwa
kitu alichokiona.
“ Nimeogopa sana kwa kitu
nilichokiona.David anatembea na mama
yake mdogo ? Mke wa baba yake ambaye
ni sawa na mama take !! Halafu
wamejiachia bila wasi wasi hata bila hata
kufunga mlango,wanajiamini nini?
Wangefanya nini kama wangekutwa na
Pauline au baba yake? Tena inaonekana
huu ni mchezo wameuzoea na ndiyo
maana hawana wasi wasi hata
chembe.Nashukuru nimegundua mapema
kwamba David ni kijana mshenzi kabisa
na hanifai hata kidogo.Tayari nilikwisha
tokea kumpenda na nilichokuwa
ninahitaji ni kumfahamu vizuri lakini kwa
hiki nilichokiona leo hii,David hanifai
kabisa.Lazima nimwambie Pauline kuhusu
suala hili.Lazima afahamu uchafu
unaofanyika ndani ya numba
yao.Nimekuzwa katika msingi ya ukweli na kukataa uovu kwa hiyo Pauline lazima
afahamu kila kinachoendelea humu
ndani.”akaendelea kuwaza Sanya
Dakika kumi walizitumia David na
Vicky kumaliza mzunguko mmoja kisha
Vicky akavaa haraka haraka.
“ Thank you so much david.”
Akasemahuku akimbusu
“ Vicky sitaki jambo hili lijirudie
tena.Naomba leo iwe ni
mwisho.Nimekubali kufanya hivi kwa
kuogopa mgeni chumban ikwa Pauline
asije akatusikia tunalumbana vinginevyo
ningekufurusha vibaya” akasema David
“ Kwa nini unanifanyia hivi
David.Unamuogopa Pauline? Au
unamuogopa huyu mmarekani?
Nimekuona ulivyokuwa
unamuangalia.Ninakuonya David kama
una mawazo naye yafute kabisa.Kwa sasa
wewe ni wangu peke yangu” Akasema
Vicky.David hakumjibu kitu akamuangalia
kwa hasira.Vicky akambusu na kutoka mle
chumbani akaondoka
“ Huu ni ukosefu mkubwa sana wa
adabu lakini hii ya leo ni ya mwisho kwani
kuanzia kesho hatadiriki tena kufanya
kitu kama hiki.I hate you Vicky….I hate
you so much!!..akawaza David na kuufunga mlango wake kwa funguo
……………….
******************
Chumba namba 76 Katika hoteli kubwa ya
Kobe village ilyoko nje kidogo ya jijila
Arusha, kilikuwa na mwanga mdogo wa
bluu na muziki laini ulisikika kwa
mbali.katika kitanda kikubwa
kilichokuwamo mle chumbani watu
wawili walionekana kuwa katika mahaba
mazito.
“ Pauline sijui nikueleze nini kwa
furaha kubwa niliyonayo leo hii kwa
kupata nafasi hii ya kuwa nawe
hapa.Nilikuwa ninatafuta sana kupata
nafassi kama hii furaha kwa muda mrefu
na hatimaye sasa nimefanikiwa kuipata
toka kwako.Pauline wewe ni wa kipekee
kabisa.Ahsante sana”
“ Alfred ,hata mimi ninapaswa
kukushukuru kwani umenifuta machozi
na kukiponyesha kidonda nilichokuwa
nacho moyoni.Sikuwa na uhakika kama
kidonda nilichoumizwa kingeweza kupona
ndani ya muda mfupi lakini baada ya
kukutana nawe sihisi tena maumivu Ahsante sana Alfred” akasema Pauline
,Alfred akambusu na kusema
“Si mara ya kwanza unanitamkia
suala hilo la kuumizwa.Ni nani
aliyekuumiza moyo wako mtoto mzuri
kama wewe? Ni nani huyo ambaye
anathubutu kukutoa chozi?akauliza Alfred
“ Fred hayo yamekwisha pita.kwa
sasa yamebaki historia.Ninanchokiangalia
sasa ni maisha yangu ya mbeleni nikiwa
na mwanaume wa kipekee kabisa kuwahi
kukutana naye.Thats you Alfred.Pamoja
na hayo bado kuna kitu kinanisumbua
sana na kuninyima raha kila
nikikifikiria”akasema pauline
“ Nini kinakunyima raha Pauline?
Tafadhali niambie mpenzi wangu.Niko
tayarikwenda hadi mwisho wa dunia
kuitafuta furaha yako.Niambie tafadhali
nini kinakutatiza? Akauliza Alfred huku
akizichezea nywele za Pauline
“ Alfred ni kuhusu mkeo
Grace.Ninaogopa sana endapo siku moja
atagundua kwamba mimi na wewe tuna
mahusiano ya siri.Grace ni mwanamke
mpole na anayekupenda sana.Mnaye
mtoto mzuri na mnaishi kwa amani.Sitaki
niwe kikwazo cha kuivuruga familia
yako.Ninafahamu maumivu ya kusalitiwa na mtu unayempenda kwa hiyo sitaki
jambo kama hilo limkute Grace.Ndiyo
maana ninakosa raha kabisa kila
nikiliwaza hilo kwanininakupenda sana
david na sitaki nikukose katika maisha
yangu ” Akaema Pauline
“ Paline hilo si suala la kuhofu hata
kidogo.Mimi ndiye mwenye uamuzi wa
nini nifanye kuhusiana na maisha yangu
.Nimekupenda na nitakuwa nawe na
hakuna wa kunizuia kukupenda.Grace
hawezi kunizuia kuitafuta furaha ya
maisha yangu kwa hiyo usimuhofie
kabisa.Agundue asigundue potelea mbali
nimekwisha amua liwalo na
liwe”akasema Alfred.Pauline
akamuangalia ,akatabasamu halafu
akaupeleka mkono wakae kifuani kwa
Alfred akasema
“Why are you doing this to your wife?
Why are you hurting her?
“ Pauline tafadhali naomba tuachane
na mambo hayo ya Grace.Tuzame zaidi
katika mapenzi yangu mimi na wewe”
akasema Alfred
“ Fred ,mimi tayari nimezama
mapenzini na mume wa mtu ambaye
haonyeshi kujali kama kwa kufanya hivyo
anamuumiza mkewe .Ninataka kufahamu unajisikiaje ukiona mkeo anadondosha
machozi kwa sababu ya kitendo hiki
tunachokifanya? Ni vipi kama na wewe
ukigundua kwamba mkeo amekuwa na
mahusiano na mwanaume mwingine?
Akauliza Pauline.Alfred akanyamaza
akatafakari kidogo kisha akasema
“ Pauline I real don’t care if she’ll get
hurt or not. Kikubwa kwangu ni kwamba
nimekupata wewe mwanamke ambaye
unanipa furaha ya moyo niliyokuwa
naitafuta kwa muda mrefu sana.”akasema
Fred.Pauline akamtazama tena kwa
makini akaguna kidogo kisha akauliza
“ Do you real love her?
“ Paline si watu wote unaowaona
wako katika ndoa ukadhani wanapenda.”
“ Nijibu swali langu Fred.Do you love
your wife?
“ I don’t” akajibu Fred na kumstua
sana Pauline
“ Fred !!akasema pauline na kuinuka
akakaa.
“ Pauline ndiyo maana nikakwambia
kwamba tuachane na masuala ya mimi na
Grace na tuongelee masuala yetu.”
Akasema Alfred ” Fred umenistua sana.Yaani kwa
macho makavu kabisa unadiriki kusema
kwamba humpendi mkeo !!!
“ Ndiyo Pauline.Ulitaka kuufahamu
ukweli basi ukweli ndio huo.I don’t love
her at all”
“ This is weird “ akasema Pauline
kwa sauti ndogo.Kikapita kimya kifupi
Pauline akauliza
“ why are you doing this to her? Are
you punishing her? Kuna kitu amewahi
kukukosea Alfred?
“ Ouh pauine kwa nini unataka sana
kufahamu kuhusu Grace? Nimekwambia
tuachane naye atatuharibia usiku wetu
mzuri.”
“ Fred ninahitaji kujua kila kitu kwa
sababu tayari nimekwisha zama katika
penzi lako nasitegemei kutoka lakini
ninaogopa kama umethubutu kutamka
kwamba humpendi mkeowa ndoa basi
hata mimi unaweza ukaniacha muda
wowote pindi ukipata mwanamke mzuri
zaidi yangu”akasema Pauline
“Pauline tafadhali usiwaze mawazo
kama hayo.Mimi ninakupenda kwa moyo
wanguwote na ndiyo maana unaniona
ninafanya mambo haya yote kwa ajili ya
jambo moja tu kubwa.Kuwa na wewe maishani.Nimekueleza ukweli wa moyo
wangu ili ujue kwamba simpendi mke
wangu na ninakupenda wewe tu na
kamwe katika maisha yangu siwezi
kukuacha hata siku moja”
“ hebu nieleze Fred,mkeo
amekufanya nini hadi umchukie kiasi
hiki? Nina hakika kabisa kwamba ulifunga
naye ndoa kwa sababu ulimpenda na
uliona kwamba anakufaa kwa sababu
huwezi kula kiapo na mtu usiyempenda.”
Akasema Pauline.Alfred akanyamaza na
kumtazama OPauline kwa makini
halafuakasema
“ Do you real want to know the
truth?akauliza Fred
“ Yes I do” akajibu Pauline.Fred
akavuta pumzi ndefu kisha akasema
“ Kuna watu wasiozidi watano tu
ambao wanaufahamu ukweli huu ambao
ninataka kukueleza.Ni ukweli ambao
hatakiwi kufahamu mtu mwingine yeyote
zaidi ya sisi watano lakini kwa kuwa
ninakupenda imenilazimu nikueleze tu.”
Fred akanyamaza kidogo kisha akasema
“ Me and Grace we’re not married..”
akasema Fred na kumstua Pauline
“ You are not married?How come?
Mbona mnavaa pete za ndoa? “ Pauline ndiyo maana nilikwambia
kwamba tuachane na haya mambo.Ni
mambo magumu kuyaelewa.” Akasema
Fred
“ Fred umenishangaza sana.”
Akasema Pauline
“ Pauline tafadhali naomba tuachane
na hayo mambo kwa sasa.Nilichokueleza
kinatosha na ninaomba iwe ni siri
yako.Kama siku nyingine tukipata wasaa
nitakueleza kwa undani zaidi kila kitu
kuhusu mimi na Grace lakini kwa sasa
naomba tuachane na hayo mambo ili usiku
wetu usiharibike” akasema Alfred na
Pauline hakutaka kuuliza tena
“ Inawezekanaje Fred na Pauline
wasiwe wanandoa wakati wanavaa pete za
ndoa? Hapana bado siamini.Lakini kwa
namna nilivyomtazama macho yake
wakati ananieleza inawezekana ikawa
kweli kwani dunia hii imejaa mambo
mengi sana ya ajabu kama yake
yanayotokea katika familia yetu ila
mwaka” akawaza Pauline na
kumkumbuka baba yake.
“ halafu nimekumbuka baba alisema
kwamba ataandaa chakula usiku wa leo
kwa ajili yetu.Najua watakuwa
wametutafuta sana kwani sijawapa taarifa zozote kwamba sintakuwepo.Halafu
nilipanga pia kuonana na David mchana
wa leo ili anieleze kuhusiana na hicho kitu
kikubwa alichosema anataka
kunieleza.Nitaonana naye hata
kesho.natumai leo hii atakuwa amepata
wasaa mzuri wa kuwa na sanya.Nitafurahi
sana kama watakuwa wapenzi kwani
Sanya anaonekana wazi kuanza kuvutiwa
na David.” akawaza Pauline.
********************
Kumepambazuka siku ya
jumapili.Saa kumi na mbili za asubuhi
ilimkuta Sanya akiwa tayari macho.Alipata
usingizi wa mang’amu ng’amu .Tukio
alilolishuhudia usiku chumbani kwa
David lilimkosesha usingizi kabisa.
“ kwa nilichokiona jana
usiku,ninaogopa hata kukaa karibu na
David.Anawezaje kumtazama baba yake
usoni kwa mambo ya aibu
anayoyafanya?..Siwezi kulifumbia macho
jambo hili lazima nimtaarifu Pauline ajue
kinachoendelea ili watu hawa wakanywe
waachane na mchezo wao.Huu ni ukosefu
mkubwa sana wa adabu” akawaza Sanya Ilitimu saa nne za asubuhi lakini
bado David hakuwa ametoka chumbani
kwake.Alihisi uchovu na vile vile kichwa
chake kilikuwa na mawazo mengi sana na
kubwa lilikuwa ni kuhusiana na mpango
wa Vicky wa kumuua mzee Zakaria
mpango ambao ulipangwa kutekekezwa
usiku wa siku ile ya jumapili
“ This is the day..Kila kitu
kitakamilika leo kwa mujibu wa mipango
ya Vicky.Nasikitika mpaka mida hii
sijafanikiwa kumueleza Pauline kile
kinachokwenda kutokea” akawaza na
kuchukua simu yake akazitafuta namba za
simu za Pauline akapiga lakini bado simu
haikuwa ikipatikana.
“ Pauline atakuwa wapi? Kwa nini
ameizima kabisa simu yake
wakatinilimweleza kwamba kuna jambo
kubwa ambalo anatakiwa kulifahamu?
Anyway hakuna kitakachoharibika hata
kama hayupo.Ila niltamani sana alifahamu
jambo hili mapema kabla halijatokea.”
David akampigia safia akamuuliza
kama kuna mabadiliko yoyote katika
mpango wa Vivcky lakini mpaka muda huo
Vicky hakuw amemtaarifu kama kuna
mabadiliko yoyote katika mpango wake. “ David leo lazima kila kitu ifanyike
kwani tayari amekwisha lipa kiasi
kikubwa cha pesa.lakini ngoja nimpigie
nimuulize kama kuna mabadiliko yoyote’
akasema safia na baada ya dakika tatu
akampgia David akamfahamisha kwamba
tayari ameongoe na Vicky na hakuna
mabadiliko yoyote
“ Good .Kilichobaki hapa ni
kujiandaa kwa ajili ya usiku wa leo.Leo
lazima uovu wote wa Vicky ufike mwisho
na mimi nibaki huru kwani baada ya
kuachana na Tamia tayari amekwisha
sema kwamba hataki kuniona nikiwa na
mwanamke mwingine.Tayari tayari
nimekwisha mpenda Sanya na hata yeye
ameonyesha muelekeo mzuri na safari hii
sifanyi makosa.Ni lazima nimpate Sanya.Ni
mwanamke ambaye nina hakika ndiye
atakayenifaa katika maisha yangu kuliko
hawa walaghai wengine ambao kwao pesa
na mali ni vitu walivyoweka mbele zaidi”
akawaza David kisha akainuka akafungua
mlango akatoka nje akasalimiana na dada
wa kazi akamuuliza kama amemuona
Sanya akaambiwa kwamba Sanya bado
hajaamka.David akashangaa kidogo
akaenda hadi katika mlango wa chumba
cha Pauline akagonga na Sanya akaufungua.Alistuka sana alipokutanisha
macho na David.
“ Habari za asubuhi Sanya.Mbona
umestuka namna hiyo uliponiona?
Akauliza david huku akitabasamu.Sanya
akajitahidi kutabasamu kisha akasema
“Nilidhani ni Pauline amerejea na
ndiyo maana nilistuka baada ya kukutana
na wewe badala ya Pauline.Una taarifa
zake zozote? Akauliza Sanya
“hapana sina taarifa zake
zozote.Nimejaribu kumtafuta katika simu
lakini hapatikani”
“ Atakuwa na mpenzi w ake
wanafurahia mapumziko ya wiki” akajibu
Sanya.
“ Sanya tunaweza kutoka baadae
kwenda sehemu kwa chakula cha
mchana? Akauliza David
“ Ahsante david lakini kwa leo
sintatoka kabisa nataka nipumzike tu
ndani.” Akasema Sanya na hakuonekana
kutaka maongezi marefu akamuomba
David amuache akaendelee kupumzika
“ Sanya ana nini leo? Mbona
anaonekana hana furaha hata kidogo?
Halafu Mbona alistuka sana aliponiona?
Siku ya jana alikuwa ni mwanamke
mchangamfu sana na mwongeaji lakini leo ameonekana mkimya na asiyetaka
maonegzi mengi.Anyway ngoja nimuache
apumzike “akawaza David akaelekea
chumhani kwake ambako akakuta ujumbe
katika simu yake,uliotoka kwa Vicky
madhahabu.
“ David nakushukuru sana mfalme
wangu kwa jana usiku.Ulinifanya nikalala
usingizi mzuri sana.Samahani sana kwa
maneno niliyokutamkia jana kuhusu
sanya.Usiku wa leo nimekuandalia
chakula cha usiku sehemu Fulani maalum
kwa ajili yako na Sanya Pekee.Naomba
unipe jibu tafadhali kama utakuwa tayari
kuongozana na Sanya kwenda kwa
chakula cha usiku katika sehemu
niliyowaandalia”
“ Tayari anaanza maandalizi ya
mipango yake.Anataka jioni ya leo mimi
na Sanya tusiwepo hapa ili aweze
kutekeleza mpango wake.”akawaza David
halafu akaandika ujumbe wa kumjibu
“ Asante Vicky lakini hatuna mpango
wa kutoka leo.Niko nyumbani
ninapumzika”
Ujumbe ule ukamstua Vicky ambaye
alikuwa anatafuta namna ya kuhakikisha
kwamba wakati wa shambulio litakalofanyika usiku,David hatakuwepo
nyumbani
“ Huyu kijana Mbona anaaza
kuniweka roho juu ? Endapo akiwepo basi
anaweza akadhurika kwani anapenda
sana ushujaa.Ninavyomfahamu atajitahidi
kupambana na akina Chino na kama
walivyoniweka wazi ni kwamba yeyote
atakayeonekana kuwa kikwazo kwao
lazima watamuondoa tu.Nitafanyaje basi
ili asiweze kuwepo hapa wakati wa
uvamizi? Akajiuliza
“ Nimepata wazo.Nitalazimika
kumpeleka Zakaria mapema sana
chumbani kulala na hivyo watu wote
wataelekea vyumbani kwao kulala.Sitaki
jambo lolote limfike David mwanaume
ninayempenda kuliko wote na haya yote
ninayafanya kwa ajii yake” akawaza Vicky.
Muda ulisonga kwa kasi kubwa na
hatimaye jua likazama na kiza kikachukua
nafasi yake.Ilimlazimu Vicky kunywa
mvinyo mkali ili kuondoa sura ya wasi
wasi aliyokuwa nayo.Pamoja na kunywa
mvinyo ule mkali lakini bado aliendelea
kuwa na wasi mwingi.Hakuna aliyejua
wasiwasi wake ulitokana na nini zaidi ya
David pekee. Saa nane nusu za usiku Pauline na
Alfred wakarejea nyumbani na
wakajumuika mezani na wenzao kupata
chakula cha usiku.Ujio ule wa Pauline na
Alfred ulimchanganya sana Vicky na
kumfanya azidi kuwa na wasi wasi.
“ Huyu shetani naye ametokea wapi?
Kwa nini amekuja muda huu ambao
mambo yanakaribia? Akajiuliza Vicky.
“ Vyovyote itakavyokuwa lazima
mpango ukamilike leo hii.lazima Zakaria
auawe tu.Nina hakika muda huu Chino na
kundi lake watakuwa njiani
wanakuja.Ngoja nifanye haraka haraka
nimpeleke Zakaria chumbani.”akawaza
Vicky
“I missed you all so much”akasema
Pauline.Mzee Zakaria akatabasamu na
kusema
“We missed you too Pauline.Mlikuwa
wapi? Tulipatwa na wasi wasi kidogo”
“ Kuna mahala nilikwenda na Alfred
.Sanya unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri sana
Pauline.”akajibu Sanya maongezi
yakaendelea wakamaliza chakula na mzee
Zakaria akaomba waelekee katika
ukumbi wa mapumziko kwa maongezi ya
hapa na pale “ Pauline naomba sisi tuelekee
chumbani kuna jambo ninataka kuongea
nawe.” Akasema sanya kisha Pauline
akaomba samahani akaondoka na Sanya
wakaelekea chumbani.
“ Guys imekuwa ni siku ndefu sana
nadhani hakuna haja ya kuwa na
maongezi marefu na kumchosha
mzee.Nadhani na ninyi pia mngeenda
kupumzika ili kumpa mzee nafasi ya
kupumzika”akasema Vicky
“ Hakuna tatizo kama tukiendelea na
maongezi kidogo na mzee.Isitoshe
anahitaji sana kufahamiana na mkwewe
Dr Alfred”akasema David na kumfanya
mzee Zakaria kushangaa
“Mkwe wangu?
“Ndiyo mzee.Utanisamehe kwa
kuwahi kukujulisha suala hili kabla ya
Pauline lakini hakuna
kilichoharibika.Pauline amekuja na mkwe
wako na ninadhani amekuja
kumtambulisha rasmi kwako”akasema
david.
“ Ouh hii ni habari njema
sana.Pauline alinipigia simu na kuniambia
kwamba ana jambo kubwa anataka
kuongea na mimi kumbe alikuwa anakuja
kumtambulisha mkwe wangu.karibu sana Dr Alfred .Nimefurahi sana
kukufahamu”akasema mzee Zakaria
akainuka na kwenda kumpa mkono Dr
Fred wakapogezana.
“Mungu wangu hapa hakuna dalili za
maongezi kumalizika sasa hivi.Nitawezaje
kumuondoa David hapa ? nadhani muda
huu Chino yuko karibu sana kufika
inakaribia saa nne na nusu sasa”akawaza
Vicky halafu akamgeukia David.
“ david kwa kuwa umekwisha
mtambulisha shemejiyo kabla ya
muhusika mwenyewe kumtambulisha
kwanini basi usiwape nafasi mtu na
mkwe wake waendelee na maongezi na
kufahamiana zaidi?
“ Hapana Darling.David naye
anatakiwa amfahamu vyema shemeji yake
,kwa hiyo anatakiwa kuwepo
hapa.”akasema mzee Zakaria
“ Ouh Mungu wangu nitafanya nini
sasa ? kila mpango wa kumuondoa David
mbona unashindikana? Akawaza Vicky
akainuka na kuelekea chumbani
“ Nadhani muda wa tukio
umekaribia sana ndiyo maana Vicky
anahaha namna hii .Ee Mungu tusaidie”
akawaza David “ Sanya samahani sana jana sikuweza
kurudi.Kuna mahala tulikwenda mimi na
Alfred na tukashindwa kabisa
kurudi.Unaendeleaje? Nadhani
haukuboreka kabisa kwa kukuacha peke
yako.” akasema Pauline baada ya kuingia
chumbani
“ Usijali Pauline hata mimi nilielewa
kwamba kuna mahala mlikwenda
kufurahia mapumziko.Mimi niko salama
sina tatizo lolote na wala
sijaboreka.Nimekuta filamu nyngi humu
chumbani nakutwa nzima ya leo
nimeshinda ninatazama.Vipi mambo
yalikwendaje huko ? akauliza
Sanya.Pauline akatabasamu na kusema
“ Mambo yalikwenda vizuri sana.
Tulikuwa na wakati mzuri na
kufahamiana zaidi kwani mimina Alfred
hatuna muda mrefu katikamahusiano
yetu..” Akasema Pauline
“ Nafurahi sana kusikia hivyo
japokuwa bado naendelea kukusisitizia
kuhusu suala la kuolewa kama kweli
mnapenda kwa dhati nasi kuchezeana.”
Akasema Sanya na kumfanya Pauline
acheke kidogo.
“ Tuachane na hayo Pauline kuna
jambo ambalo nimekuitia hapa.” Sanya akanyamaza akamtazama pauline halafu
akaendelea
“ Pauline nitakuwa muwazi kwako
na ninaomba unisamehe kama nitakuudhi.
Lakini sualahili siwezi kulifumbia macho
hata kidogo.Kuna kitu kimenisikitisha
sana hapa ndani kwenu” akasema Sanya
“ Sanya anataka kusema nini? Kuna
kitu amegundua kuhusu mimi na Alfred?
Pauline akajiuliza.Sanya akaendelea
“ Jana usiku kuna jambo
nimelishuhudia humu ndani limenifanya
nikose kabisa usingizi.Sijalala usiku wa
leo nimekesha nikitafakari na siwezi
kulifumbia macho jambo hili hata kidogo
na lazima nikueleze ukweli”
“ Sanya ni jambo gani hilo ,nieleze
tafadhali” akasema Pauline kwa wasiw asi.
“ Kama unakumbuka jana baba
alituandalia chakula maalum cha
kutukaribisha ,baada ya chakula tulikuwa
na maongezi kidogo na halafu kila mmoja
akaelekea chumbani kwake kulala.Nikiwa
chumbani nilianza kusikia vishindo kama
watu wakigombana ikanilazimu kutoka
chumbani ili kuona kama ni kweli kuna
watu walikuwa
wanagombana.Nililazimika kufuatilia
vishindo vile na kugundua vilitoka katika chumba cha David.Niliogopa sana kwani
nilihisi labda David kavamiwa chumbani
ikanilazimu kuufungua mlango wa
chumba chake ili nijue kinachoendelea na
nikakutana na kitu ambacho niaibuhata
kukisimuliza.” akasema Sanya na
kunyamaza.
“ Uliona nini Sanya? Akaulizia Paline
“ Ni jambo la aibu lakini lazima
tuuseme ukweli ili kulikomesha jambo hili
lisijirudie tena”
“ Niambie Sanya uliona nini?
“ Nilimkuta David na mama yako
mdogo wakifanya mapenzi”
“ Ouh my God !! akasema Pauline
.Alistuka sana
“ samahani sana pauline kwa
kukuambia jambo hili ambalo nina hakika
limekustua sana lakini hakuna namna
nyingine ya kufanya zaidi ya kulisema
.Hata mimi limenistua na kunikosesha
usingizi usiku .kwa nini david afanye
hivi? Kutembea na mama yake mdogo?
Hili ni jambo la aibu sana kwake na kwa
familia yenu yote.Anawezaje kufanya
jambo kama hili? Akauliza sanya.Pauline
akainama akatafakari
“ Pauline nimekueleza hili ili uweze
kulifanyia kazi na kuwakanya wasiendelee kufanya uchafu wao tena ndani ya
nyumba ya baba yako na kibaya
zaidiwanafanya kwa kujiamini kabisa bila
hata kufunga mlango.Nivipi kama
wangekutwa na baba? David anajitafutia
laana kubwa .Kitedo anachokifanya katu
hakivumiliki hata kidogo .Wewe kama
ndugu yake unatakiwa umkanye aachane
kabisa na suala hili baya analolifanya
kabla hajagundulika na kuichafua familia
yenu..Nilitokea kumpenda sana David na
nilimuona ni kijana mwenye adabu zake
lakini kwa hili nililomshuhudia analifanya
nimemshusha thamani kabisa na hafai
hata kidogo” akasema sanya ambaye hata
uso wake ulionyesha kwamba alikuwa
amekerwa sana na kitendo kile cha David
“ Mungu wangu aibu gani hii jamani?
Akawaza Pauline
“ Nilikwisha hisi kitu kama hiki toka
zamani lakini sikuwahi kupata nafasi ya
kuwanasa kwaniwalikuwa wanafanya
mambo yao kwa siri sana ila walisahau
kwamba siku zote za mwizi ni arobaini
hatimaye wamebainika
wanachokifanya.Kwa kitendo hiki hata
mimi nimemchukia sana David.Kumbe ni
kijana mshenzi kiasihiki na hafai kabsa
hata kuendelea kukaa humu ndani.Kwa nini lakini amfanyie baba mambo kama
haya wakati baba anampenda na anamlea
kama mtoto wake? Hapana suala hili
halivumiliki hata kidogo” akawaza Pauline
na macho yake yakaonekana kujaa
machozi
“ Pauline samahani sana kwa
kukueleza jambo hili ambalo najua
limekuumiza sana lakini sina namna
nyngine ya kufanya zaidi ya kukueleza
ukweli .” akasema Sanya
“ Sanya ahsante kwa kunieleza
ukweli.Wewe ni rafiki wa kweli.Angekuwa
ni mwingine asingekubali kunieleza
waziw azi kwa kuogopa kuniudhi lakini
wewe umejitoa muhanga na kunieleza ili
kuikomesha tabia hii chafu.Ninaomba
samahani sana kwa ulichokiona ambacho
najua kimetia doa katika ile taswira nzuri
uliyokwisha ipata kwa familia yangu.Huu
ni uchafu ulipotiliza na usiovumilika hata
kidogo.najuta ni kwa nini nilimkaribisha
Daid humu ndani.Mimi ndiye
niliyesababisha haya yote kutokea.”
“ Pauline unasema nini? Sanya
akashangaa
“ Sanya naomba nikuweke wazi
kwamba David si ndugu yetu kabisa na
wala hatufahamu ametoka wapi,hatuifahamu historia yakewala
familiayake .Hivi sasa ndiyo tumeamza
kuzifahamu tabia zake.”
“ Pauline unanishangaza sana ”
“ najua utashangaa sanya lani huo
ndio ukweli.David si mtoto wa familia
hiinawalahatuna nasaba naye lakini kwa
namna tunavyoishi naye si rahisi kabisa
kujua kwamba si mtoto wa familia yetu.
Ilivyotokea hadi akafika hapa ni kwamba
aliwahi kumsaidia baba alipopatwa na
matatizo wakati akiendesha gari.Baba
yangu anasumbuliwa na matatizo ya
sukari na shinikizo la damunasiku
hiyoalipatw ana matatizo njiani hivyo
David alimsaida na alionyesha uaminifu
mkubwa sana kwani siku ile baba alikuwa
na milioni nyingi ambazo angeweza
kuondoka nazo lakini hakutumia fedha
zile na akaziwasilisha salama.Kitendo kile
kilitufanya tumuamini sana na hasa mimi
.Hakuwa na makazi wala ndugu hapa
Arusha kwani siku hiyo hiyo alikuwa
amema;liza kifungo chake
gerezani.Nilimuonea huruma na
kumchukua akaja kuishi nasi hapa.Baadae
tukagundua kwamba ana taaluma ya
biashara na kwa kuwa tulihitaji mtu wa
kutusaidia katika masuala ya biashara tukampa kazi na akaifanya kazi yake
vizuri sana na kwa uaminifu
mkubwa.Baba akamuamini na kumfanya
kuwa msimamizi wa biashara zake
zote.David alikuwa ni kijana mzuri na
mchapakazi sana hadi pale alipoanza
kuwa na ushirika na mama mdogo”
“ ushirika na mama yako mdogo? !!
akauliza sanya
“ Ndiyo sanya.mama yangu mdogo ni
mwanamke ambaye kwake yeye vitu
vyenye thamani ni pesa na mali tu na
ndiyo maana mimi na yeye katu
hatuelewani.Toka ameolewa na baba
amekuwa akifuja sana mali za baba
alizozihangaikia kwa muda mrefu .Huyu
mwanamke ndiye aliyembadilisha David
na kumfanya awe hivi alivyo.
“ Unataka kuniambia kwamba huyu
mwanamke ndiye aliyemshawishi David
hadi akakubali kufanya kitendo kile cha
aibu? Ni mwanamke wa aina gani huyu?
“ Nina uhakika huo kwa sababu
ninamfahamu vizuri mama mdogo,si
mwanamkemwenye sifa nzuri na kila mtu
alishangaa sana pale baba alipoamua
kumuoa huyu mwanamke baada ya mama
kufariki.Nina uhakika mkubwa ndiye
aliyembadilisha David kwani mwanzoni alikuwa ni kijana mzuri na mwenye tabia
njema “ akasema Pauline.
“ kama ni hivyo basi mwanamke
huyu hafai hata kidogo lakini pamoja na
hayo kwa nini David akubali kuingia
katika ujinga wa namna hii? Kwa nini
akubali kirahisi kufanya uchafu huui?
Akauliza sanya
“ Ninamfahamu vizuri David ni
mmwanamume dhaifu sana kwa
wanawake na ni rahisi sana
kushawishika.Sikuwa nimepanga
kukueleza jambo hili lakini ni vyema kama
ukijua.Mimi na david truliwahi kuwa
wapenzi japo kwa siku chache.”
” kweli ?!! sanya akashangaa sana.
“ kweli sanya .Nilitokea kumpenda
sana David toka mara ya kwanza
nilipomuona licha ya uchakavu
wake.Nilimuweka moyoni na nilimpemda
kwa dhati kabisa.kwa bahati mbaya david
akanisaliti kwa kutembea na rafiki yangu
mkubwa Tamia.Niliumia sana na ndiyo
maana nikaamua kuondoka kabisa Arusha
na kwenda kupumzika Moshi ambako
nilikutana na Alfred ambaye amenifuta
machungu yote niliyoumizwa na David
kwa hiyo miminisababu nyingine ya Alfred
kuwepo hapa nyumbani” “ Pole sana Pauline.kwa nini
hukunieleza jambo hili hapo kabla? Hata
mimi nilipomuona david nikatokea
kuvutiwa naye sana lakini bada ya
kushuhudia akifanya uchafu ule jana na
haya maneno uliyonieleza leo sina hamu
naye hata kidogo na hanifai
kabisa.Hujachunguza ni kwa nini
alifungwa gerezani? Ametokea wapi?
Familia yake iko wapi? Akauliza Sanya
“ Hapana hatujawahi kuchunguza
mambo hayo yote na hata yeye mwenyewe
hataki kabisa kuongelea hayo mambo
.Kwa kuwa tunamuamini tuliamua
kuachana naye na tusimuulize chochote
hadi hapo yeye mwenyewe atakapokuwa
tayari kutueleza” akasema
“ Mlifanya kosa kubwa Pauline
kumkaribisha ndani mtu ambaye
hamuijuia historia yake.Mnaweza
mkamkaribisha na mhalifu akawafanyieni
kitu kibaya sana”akasema Sanya.
“ Usemayo ni ya kweli Sanya.lakini
haya yote yalisababshwa na upendo
wangu mkubwa kwake.Kama nisingetokea
kumpenda David kwa kipindi kile
asingekuwa hapa nyumbani na kutuletea
aibu hii. Lakini mwisho wake umekaribia
sana na sintauvumilia kabisa ujinga huu anaoufanya.Lazima aondoke hapa
nyumbani haraka iwezekanavyo.
Laz…………..” kabla hajamaliza sentensi
yake ikasikika milio mitatu ya
risasi.Pauline na Sanya wakastuka na
kuogopa sana.Baada ya dakikamoja
ikasikika tena milio mingine ya risasi
safari hii ikiendelea mfululizo.
“ Sanya tumevamiwa !! akasema
Pauline huku akitetemeka
“ Mungu tusaidie”akasema Sanya
,wakafungua mlango wa choo na kujificha
humo.Milio ya risasi iliendela kurindima
kwa zaidi ya dakika ishirini halafu kukawa
kimya na baada ya kama dakika tano hivi
toka risasi zile zikome wakasiika watu
wakiongea na mlango w a chumba cha
Pauline ukafunguliwa.
“Hakuna mtu humu” ikasikika sauti
ya mtu mmoja
“ Angalia sehemu zote hadi
chooni.Wengine wanaweza kukimbilia
wakajificha huko.i’ akasema mwingine.
Pauline na Sanya wakakumbatiana
kwani walijua muda wao umefika.
“ Ee Mungu tuokoe”akasema sanya
huku akilia na mara mlango ukapigwa
teke na kufunguka wakaingia watu wawili. “ Simameni “ Mtu Yule akatoa
amri.Pauline akafumbua macho na
kukutana na askari wawili wenye silaha.
“ Tafadhali tokeni humu ndani.Mko
salama sasa.Kuna yeyote aliyeumia?
Akauliza mmoja wa wale askari.Hakuna
aliyeweza kujibu wote walikuwa
wanatetemeka.Askari wakawachukua na
kuwapeleka sebuleni. Ghafla Pauline
akajikuta akiangua kilio kikubwa baada ya
kuona askari wamembeba David
wakimtoa nje akiwa amechafuka
damu.Alikuwa amepigwa riasasi..
Kelele aliyopiga Pauline ilikuwa kubwa
ikawalazimu maaskari wawili kumchukua
na kumtoa pale sebuleni wakampeleka
chumbani kumtuliza.Alikuwa
anaweweseka huku akiongea maneno
yasiyoeleweka..Sanya aliishiwa nguvu
akakaa chini.Mwili wote ulikuwa
unamtetemeka.Pale sebuleni kulikuwa na
watu wawili ambao walikuwa
wameanguka chini na hawakuonekana
kuwa na uhai tena .Mzee Zakaria alilazwa
sofani akipatiw a huduma na Alfred hali
yake ilikuwa mbaya kutokanana mstuko
alioupata..
Mara askari wakawaingiza watu sita
wakiwa wamefungwa pingu na wawili kati yao wakivuja damu kutokana na majeraha
ya risasi.
“ Mna hakika hakuna tena jambazi
mwingine aliyesalia ? akauliza kiongozi
wa kikosi kile cha askari
“ hakuna afande”akajibu mmoja
wapo
“ Mmezunguka nyumba yote na
kuhakikisha kwamba hakuna mtu
aliyejificha?
“ Ndiyo afande.Tumepekua kila
mahala na hakuna jambazi yeyote
aliyefanikiwa kutoroka wala kujificha.”
Akasema Yule askari.
“ kazi nzuri sana.Silaha zao zote
zimechukuliwa?
“ ndiyo afande.” Akajibu Yule askari
kiukakamavu.
“ wachueni hao majeruhi
muwakimbize hospitali,wale ambao
hawajajeruhiwa wapelekwe moja kwa
moja kituoni bila kumsahau muhusika
mkuu.” Akaamuru askari kiongozi.
Vicky madhahabu akatolewa
chumbani na kuletwa sebulnei akiwa
amefungwa pingu.Macho yake yalijaa
machozi na alikuwa analia akiomba
aachiwe huru kwani hana kosa lolote. “ Mpakieni garini na mumpele moja
kwa moja kituoni muuaji mkubwa huyu”
akaamuru kiongozi na bila kuchelewa
Vicky madhahabu na wale watuhumiwa
wengine wanne ambao hawakujeruhiwa
wakapakiwa garini na kupelekwa moja
kwa moja kituoni.Wale majeruhi wawili na
wale watu wengine wawili waliokuwa
wamelala pale sebuleni ambao
hawakuonekana kuwa na uhai
wakapakiwa katika gari lingine la polisi na
kupelekwa hospitali
“ Mzee anaendeleae? Askari mkuu
akamuuliza Alfred..
“ bado hali yake si nzuri
sana,anatakiwa akimbizwe hospitali”
akasema Alfred
“ gari la wagonjwa liko njiani
linakuja.Jitahidi kadiri ya unavyoweza
kunusuru uhai wake hadi hapo gari la
wagonjwa litakapofika”
.Alfred akainuka na kumfuata sanya
aliyekuwa amekaa chini hana nguvu
“ Sanya polesana kwa tukio hili la
kustukiza ambalo najua limekustua
sana.Sote tumestushwa sana na tukio hili
lakini tunashukuru askari wamewadhibiti
wale wahalifu na hakuna hatari tena. kwa
sasa tuna hatari moja iliyobaki mbele yetu.Mzee Zakaria amepatw a namstuko
mkubwa sana na mapigo yake ya moyo
yako chini mno.Tunatakiwa kuhakikisha
anakuwa salama hadi hapo gari la
wagonjwa litakapowasili” akasema Alfred
.Sanya bado alionekana kuwa katika ile
hali ya taharuki kwa tukio lile.
“ Sanya tafadhali nakuomba
sana.Jitahidi unisaidie .Tunafanya hivi
kwa ajili ya Pauline” akasema Alfred na
kumshika Sanya mkono akamsaidia
kuinuka wakaenda kusaidiana kumpatia
huduma mzee Zakaria .
Gari la wagonjwa likawasili ndani ya
muda mfupi wakampakia mzee Zakaria
na kumkimbiza hospitali.Sanya na Alfred
nao pia waliambatana na gari la wagonjwa
kuelekea hospitali.
Upekuzi mkubwa ukafanyika kwa
mara ya pili ndani ya nyumba ya mzee
Zakaria ilikuhakikisahkwamba hakuna
hatari yoyote na kisha wakabaki askari
kadhaa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi
mahala na wengine wakandoka kuelekea
hospitali kufuatilia hali ya mzee Zakaria
na wale majeruhi wengine pamoja na
Pauline ambaye alionekana kupatw ana
mstuko *****************
Imekwisha timu saa nane za usiku na
madaktari wa hospitali ya St Gasper
wakisaidiana na Alfred na sanya
walifanikiwa kuyarejesha mapigo ya moyo
ya mzee Zakaria katika hali yake ya
kawaida japokuwa bado hakuwa na uwezo
wa kuongea.Mashine zilionyesha kwamba
mifumo yote ya mwili ilikuwa inafanya
kazi vizuri.Madaktari wakapongezana kwa
kufanikiwa kumuondoa mzee Zakaria
katika hatari.Alfred akataarifiwa kwamba
Pauline naye alikuwa amepumzishwa kwa
muda katika hospitali ile baada ya kupata
mstuko alipomuona kutokana na tukio lile
la kustusha.
Alfred na sanya wakaenda katika
chumba alichopumzishwa Pauline ambaye
mara tu alipowaona alitaka kujua hali ya
baba yake na David
“ Mzee hali yake inaendelea vizuri na
mapigo yake ya moyo yamerudia hali yake
ya kawaida.Hayuko tena katika hatari kwa
hiyo usihofu.Kuhusu David sina habari
zake kwa sasa kwani amepelekwa katika
hospitali kuu ya mkoa kwa hiyo ninataka kuelekea huko kujua maendeleo yake”
akasema Alfred
“ Ee Mungu msaidie David aweze
kupona” akaomba Pauline huku machozi
yakimtoka
“ Usilie Pauline.Kilichopo hapa ni
kumuombea sana David aweze
kupona.he’s a hero.He saved your father”
akasema Alfred huku naye akishindwa
kuyazuia machozi kumtoka.
“ Fred mlikuwa wote pale sebuleni
nini hasa kilitokea?Wavamizi wale ni
akina nani na waliingiaje mle
ndani?akauliza Sanya
“ hata mimi bado mwili
unanitetemeka nikikumbuka tukio
lile.Mlipoondoka tuliendelea na maongezi
yetu na hatukujua kumbe kuna watu
wanatuvamia.Tukiwa hatuna hili wala lile
mara ghafla tukasikia milio mitatu ya
risasi karibu sana na
palenyumbani.Wakati tunajiuliza kama
risasi zile zimelia wapi pale nyumbani au
nyumba ya jirani wakatokea watu wawili
wakiwa na bunduki.Walituamuru wote
tulale chini lakini David akawahi
kumrukia mzee Zakaria na mara nikasikia
milio ya risasi mfululizo.Nilikuja
kufumbua macho baada ya kusikia sauti za askari na ndipo nilipomuona David akiwa
ametapakaa damu mwili mzima.wale
jamaa wawili walioingia pale sebuleni
wakiwa na silaha waliuawa na
polisi.David is a hero,he saved your father”
akasema Alfred.Pauline akaangua
kilio.Sanya akambembeleza anyamaze.
“ Ouh David.He saved my father
again” akasema Pauline huku akilia kwa
uchungu
“ Pauline nyamaza kulia
,tunachotakiwa ni kumuombea kwa
Mungu ili aweze kupona .Kitendo
alichokifanya ni cha kishujaa sana .kama
asingekuwa yeye hivi sasa tungekuwa
tunaongea mambo mengine.Endelea
kupumzika Pauline sisi tunakwena
kufuatilia maendeleo ya David “ akasema
Fred
“ Fred tunakwenda wote.lazima na
mimi nikajue maendeleo ya David”
akasema Pauline huku akiinuka kitandani
“ Una hakika hali yako inaruhusu?
Akauliza David
“ Ndiyo David.hapa nilipumzishwa
kwa muda tu kutokana na mstuko
nilioupata lakini hali yangu sasa ni
nzuri.lakini kabla ya kuondoka nataka
kwanza nikamuone baba yangu niridhike kwamba anaendelea vizuri” akasema
Pauline kisha wote wakatoka na kueleka
katika chumba alimolazwa mzee
Zakaria.Hawakuruhusiwa kuingia mle
chumbani bali alimtazama kupitia kioo
cha mlangoni.Daktari aliyekuwa
akimuhudumia Zakaria akamuhakikishia
Pauline kwamba baba yake anaendelea
vizuri sana na asihofu kitu
Hawakuwa na gari hivyo
ikawalazimu kuomba msaada wa gari pale
hospitali ili liwapeleke hospitali ya mkoa
alikopelekwa David.
“ Alfred polisi wanasema watu wale
waliotuvamia ni akina nani? Wamekwisha
tambuliwa? Akauliza Pauline
“ Mpaka sasa bado hawajasema
chochote kwani uchunguzi bado
unaendelea lakini niliwasikia katika
maongezi yao wakipongezana kwamba
hatimaye baada ya kumtafuta kwa muda
mrefu sasa wamempata.Inaonekana watu
wale walikuwa ni majambazi na walikuwa
wanawindwa sana na askari .Uchunguzi
utakapokamilika tutajua kila kitu ila kuna
kitu kingine unatakiwa ukifahamu,mama
yako mdogo naye amechukuliwa na
polisi.” “ Amechukuliwa na polisi?!! Kwa
nini? Pauline akashangaa sana.
“ Hatufahamu ni kwa nini na polisi
hawajatoa maelezo yoyote .Yawezekana
labda wamemchukua kwa ajili ya
mahojiano na baadae wanaweza
wakamuachia” akasema Alfred
“ Alfred bado mwili unanitetemeka
nikikumbuka picha ile ya David akitolewa
mle ndani akiwa ametapakaa
damu.Ninamuomba Mungu amvushe
katika hili kwani natakiwa nimshukuru
kwa kumuokoa baba yangu.Hata David
kama binadamu wengine ana mapungufu
yake lakini binafsi nimemsamehe yale
yote aliyonikosea na kuikosea familia
yetu.Alfred I don’t want him to die”
akasema Pauline na kuangua tena kilio.
“ Pauline tafadhali usiendelee
kulia.Huu ni wakati wa kusimama imara
kwa ajili ya kaka yako David.Kulia
hakutasaidia kitu chochote.Tunatakiwa
tusimame imara katika maombi na Mungu
amponye David.Hiki ni kipindi kigumu
sana kwa familia yako lakini tuko hapa
pembeni yako tutasimama pamoja nawe
hata katika nyakati zile ngumu
sana.”akasema Alfred “ Alfred ninashukuru sana ila
ninasikia uchungu sana kwani
nimemtamkia David maneno mengi
mabaya sana ,nimemtolea laana za kila
aina .Ninajilaumu sana kwa maneno
niliyoyatamka juu yake hata kama
alinikosea.Natamani nipate nafasi ya
kumuomba msamaha.I don’t want him to
die ”akasema Pauline na kuendelea kulia
Walifika katika hospitali kuu ya
mkoa wakataarifiwa kwamba David
alikuwa katika chumba cha upasuaji na
madaktari waliendelea na jitihada za
kuokoa maisha yake kwa kumfanyia
upasuaji wa kuondoa risasi.Alfred
akawaongoza akina Pauline wakaenda
kukaa nje ya chumba cha upasuaji
wakisubiri taarifa toka kwa
madaktari.Usiku huu hali ya Arusha
ilikuwa ni ya ubaridi,Alfred akavua koti
lake na kumpatia Pauline halafu akavua
shati na kumpatia Sanya ,yeye akabakiwa
na fulana ya ndani ..
“ Thankyou Alfred”akasema Pauline.
“ Ouh David why always him? He
saved my father once and this time he
saved him again.Nina deni kubwa sana
kwake na ndiyo maana ninamuomba
Mungu amsaidie aweze kupona.Ninaapa sintamnyanyasa tena na wala sintamsema
vibaya .Nitamuheshimu kama kaka yangu
.Huyu ni mtu muhimu sana kwa familia
yetu.Pamoja na yote aliyoyafanya kwangu
na kwa baba lakini bado tuna deni kubwa
kwake na tunatakiwa kumuhesabu kama
mmoja wa wana familia yetu na si mtu
baki.” Akawaza paulinena kufuta machozi
,akamkumbuka mama yake mdogo
“ kwa nini polisi wanamshikilia
mama mdogo? Yawezekana anahusika
katika tukio hili? Ninamfahamu mama
mdogo ni mtu anayependa sana maisha ya
anasa lakini sidhani kama anaweza
akafikia hatua ya kushirikiana na
majambazi kuja kuiba kwani anapata kila
kitu anachokitaka.Najua wamemchukua ili
wamfanyie mahojiano kwani .Kitu kingine
ninachojiuliza askari wale walitokea wapi
na kufika pale nyumbani haraka namna
ile na kufanikiw akuwadhibiti wale
majambazi? Nimejiuliza sana swali hili
nimekosa majibu.Au yawezekana
walikuwa katika doria na wakawastukia
watu wale na kuwafuatilia na
kuwavamia,.au inawezekana kuna raia
mwema alitoa taarifa kwa polisi
kuhusiana nakuwepo kwa mpango wa
kuvamia nyumba yetu hivyo wakaweka mtego.Kama yupo mtu huyo tunastahili
kumjua na kumpa zawadi kubwa.Askari
wale pia wanastahili sifa na pongezi kwa
namna walivyopamba na watu wale na
kuwadhibiti.”akaendelea kuwaza Pauline
wakiwa wamekaa nje ya chumba cha
upasuaji
“ Kuanzia sasa inatubidi tuweke
ulinzi mkali palenyumbani .Tulijiamini
sana kwamba tuko salama na ndiyo maana
hatukusumbuka kutafuta walinzi.Lakini
kwa tukio la leo tayari nimepata somo
.lazima tutafute walinzi.Kuna makampuni
mengi ya ulinzi tutatafuta kampuni moja
watulindie nyumba yetu.Nitamshauri baba
tufunge kamer…………”Pauline akastuliwa
toka mawazoni baada ya mlango wa
chumba cha upasuaji kufunguliwa na
kitanda kikatolewa kikiwa na mgonjwa
juu yake.Wote wakasimama na
kuwakimbilia wauguzi waliokuwa
wakikisukuma kitanda kile na kutaka
kufahamu kama mgonjwa yule alikuwa ni
david lakini wakataarifiwa kwamba
badoDavid alikuwa katika
upasuaji.Wakaendelea kukaa pale nje
wakisubiri.
****************** Vicky madhahabu alipiga ukele
mkubwa palemlango wa mahabusu
ulipofunguliwa ili aingizwe ndani ya
chumba cha mahabusu wa kike.Askari
alioongozana nao hawakumjali
wakamsukumia ndani na kuufunga
mlango ule imara.Vicky alikaa chini na
kuendelea kulia kilio kikubwa na mara
akatokewa mwanamke mmoja
aliyekuwamo mle mahabusu akamshika
nywele na kumuinua.Vicky akainua uso
wake kwa hasira iliamtazame mtu
aliyemuinua na mara akajikuta
anatazamana na mwanamke mmoja
mnene mwenye nywele timutimu ambaye
katika mikono yake alijichora michoro.
“ Wewe mwanamke nakuomba
unyamaze na usitupigie kelele humu
ndani.Tumekaa tunatafakari namna ya
kujikomboa na matatizo yetu na wewe
unatupigia kelele.Nasema nyamaza haraka
sana”akasema Yule mwanamama
aliyeonekana mshari
Vicky alimtazama kwa dharau juu
mpaka chini kisha akaendelea kupiga
kelele akitaka atolewe mle mahabusu
kulimokuwa na harufu mbaya .Yule mama
akamfuata tena na safari hii bila kumsemesha akamnasa vibao vitatu vikali
na Vicky akaanguka chini.
“ Nimekwambia hatutaki kelele zako
humu ndani.”akasema Yule mama.Vicky
akaogopa ma hakulia tena.Yule mama
akamfuata pale chini.
“ Ni mara yako ya kwanza kuingia
mahabusu?akamuuliza
“ Ndiyo ni mara ya kwanza”
“ Umefanya nini hadi ukaletwa
humu? Unaonekana unatoka familia tajiri
wewe” Akauliza Yule mama lakini Vicky
hakujibu kitu.Machozi yaliendelea
kumbubujika.Yule mwanamke akaamua
kuachana naye.
“ Nimekwisha mimi Vicky.I’m totally
finished.Mambo yote
yameharibika.Nimechanganyikiwa kabisa
na sijui nifanye nini.Mipango yangu yote
imeshindikana.Nini kimetokea ?Askari
wale wamejuaje kuhusu tukio lile? “ Vicky
madhahabu akainama na kufuta machozi
“ Ama kweli nimecheza pata
potea.Sikutegemea kabisa kama jambo hili
lingefika hapa lilipofika.Ouh masikini
mimi jamani ntafanya nini? Akina Chino
wamekosea wapi ? Lazima kuna mtu
aliyevujisha siri hii kwa askari.Ni nani basi
aliye fanya hivyo? Hakuna mtu mwingine aliyekuwa akilifahamu jambo hili zaidi ya
Safia.Yawezekana jambo hili limevuja kwa
akina Chino. Nimechanganyikiwa na sijui
nifanye nini.Maisha yangu
yameharibika.Polisi tayari wanafahamu
kila kitu.Ee Mungu nisaidie mimi
jamani.Ninakwenda kuangamia.”akawaza
Vicky na kuanza tena kulia kwa sauti
kubwa.
TWENDE KAZI
Saa kumi na moja za alfajiri upasuaji
ulikamilika na David akatolewa na na
kupelekwa katika wodi ya uangalizi.Akina
Pauline walifuatana na wauguzi wale
waliokisikuma kitanda hadi katika wadi
ya wagonjwa waliotoka katika
upasuaji.Hawakuruhisiwa kuingia ndani
wakabaki nje ya wodi.Pauline alikuwa
anatetemeka kwa woga.
“ Pauline David will ok.He will fight
this.Be strong “ Alfred akampa moyo
Pauline.Baada ya daktari kuhakikisha
kwamba mashine zote anazotakiwa
kufungwa David ili kumsiaidia kwa
wakati huo zilifanya kazi vizuri akawaita
akina Pauline ofisini kwake. “ Poleni sana lwa matatizo
yaliyowakuta.” Akaanzisha maongezi
daktari.
“ Ahsante sana Daktari” wakajibu
kwa pamoja
“ Nimewaiteni hapa kuwapeni taarifa
za mgonjwa wenu.David alipigwa risasi
tano katika sehemu mbalimbali za mwili
wake.Risasi moja ilimpata katika bega
lake la kushoto ,risasi nyingine ikampata
maeneo ya karibu na nyonga .Nyingine
ikampiga katika paja na mbili alipgiwa
tumboni.Upasuaji wa kuziondoa risasi zile
umechukua muda mrefu lakini nafurahi
kuwataarifu kwamba tumefanikiwa na
risasi zote zimeondolewa mwilini mwa
David .” akasema daktari.
“ Ouh thank God” akasema Pauline
akiwa ameifumbata mikono yake kifuani.
“ Kwa hiyo vipi maendeleo yake kwa
sasa? Akauliza Pauline
“ kwa sasa ni mapema sana kusema
chochote kwani bado mgonjwa yuko
katika usingizi.Tunasubiri
atakapozinduka tumpime na tuanze
kufuatilia maendeleo yake ndipo
tunapoweza kusema chochote lakini kwa
upande wetu sisi kama madaktari
tumefanya kila lililowezekanakuhakikisha kwamba upasuaji unafanikiwa na endapo
litatokea la kutokea basi yatakuwa ni
mapenzi ya Mungu.” Akasema Daktari
“ daktari samahani lakini kwa
kuuliza swali hili .Is he going to make it?
Akauliza Pauline
“ kama nilivyowaeleza awali
kwamba upasuaji umefanyika vizuri lakini
hii haina maana ya moja kwa moja
kwamba mgonjwa wenu anaweza akapona
ama akafariki .Ninaomba niwe
muwazikwenu kwamba kwamba nafasi ya
kupona au vinginevyo ni hamsini kwa
hamsini.Kwa wakati huu ambao
tunaendelea kumuangalia mgonjwa wenu
kwa ukaribu zaidi ni wakati wa kuzidisha
maombi.Simameni katika maombi
tumombee ndugu yetu kwani jitihada za
madaktari pekee hazitoshi.Tumtangulize
Mungu mbele na nina hakika ndugu yenu
David atapona.” Akasema daktari na
kuwataka akina Pauline warejee
nyumbani wakapumzike
“ David I don’t want to go home. !
akasema Pauline
“ Pauline we have to go home.!!
Madaktariwanaendelea kumuangalia
David.usiku mzima tumekesha hapa
unahitaji mapumziko na tutakuja tena baadae.David will be ok”akasema
David.Pauline akakubali wakakodisha
taksi ili iwapeleke nyumbani kwani tayari
kulikwisha pambazuka
“ Kuna kanisa lolote maeneo ya hapa
karibu? Akauliza Sanya.Pauline
akamuelekeza dereva taksi awapaleke
kanisani kwanza kabla ya kuelekea
nyumbani.
Milango ya kanisa ilikuwa wazi na
watu walikwisha anza kuingia kanisani
kwa ajili ya ibada ya kila siku
alfajiri.Sanya akashuka garini na kuingia
kanisani.
“ Huingii kanisani kumshukuru
Mungu kwa kutuokoa na tukio la jana?
Alfred akamuuliza Pauline
“ Mbona nawe huendi kushukuru?
Pauline naye akauliza.
“ Nina dhambi nyingi sana.Sistahili
hata kuingia ndani ya nyumba ile ya
Mungu” akasema Alfred.
“ Vijana nyumba ya Mungu nikwa
ajili ya watu wote na hasa wenye
dhambi.Mungu anawakaribisha nyote
.”akasema dereva taksi ambaye umri wake
ulikuwa mkubwa tofauti na akina
Fred.Pauline na Alfred wakatazamana hawakuonge a kitu tena wakabaki kimya
wakimsubiri Sanya atoke kanisani.
Baada ya kuingia kanisani Sanya
akapiga magoti na macho yake
yakaonekana kuwa na machozi
“ Ee Mungu baba nimekuja mbele
zako kukushukuru kwa kutukinga na
mkono wako dhidi ya wale watu waovu
waliokuwa na nia ovu.Unatupenda sana na
ndiyo maana hujaruhusu watu wale
watudhuru.Ninakuomba ee baba umponye
David.Usimchukue katika kipindi
hiki.Ninampenda na ninamuhitaji sana
katika maisha yangu.Mjalie mzee Zakaria
uponaji wa haraka na uwape faraja familia
yake hasa Pauline katika kipindi hiki
kigumu wanachokipitia.Wewe ni muweza
na neno lako moja tu linaweza kuigeuza
dunia hivyo nakuomba tamka neno lako
moja tu na David aweze kupona.Ahsante
Mungu,ahsante ksa nafasi hii..Amen.”
Sanya akamaliza maombi yake na kutoka
kanisani akarejea garini wakaondoka
kuelekea nyumbani.
“ Baada ya kushuhudia kitendo kile
David alichokuwa anakifanya na Vicky
nilimchukia sana na sikutaka hata
kumuona tena katika macho yangu lakini
nilikuwa najidanganya.David ndiye hasa mwanaume ambaye nilikuwa
ninamuhitaji katika maisha yangu
mwanaume ambaye yuko tayar kuutoa
uhai wake kwa ajili ya
wengine.Ninajilaumu kwa kumuhukumu
kabla sijamfahamu vizuri.Sintachoka
kumuomba na kumlilia Mungu amuondoe
katika hatari na amponye kwani
ninamuhitaji sana.David ameniingia
moyoni mwangu kwa kasi na siwezi
kushindana na nguvu hii kubwa
inayoniaminisha kwamba David ndiye
hasa mwanaumeni nayepaswa kuwa
naye.Nina hakika safari yangu ya kuja
Tanzania ni kwa ajiliya kunikutanisha
naye.Kuna uwezekano mkubwa
nikawakosa wazazi wangu lakini
nikafanikiwa kumpata mwanaume wa
maisha yangu ambaye ni David.”akawaza
Sanya.
“Kitendo alichokifanya David ni cha
kishujaa sana kwani aliona ni bora kama
angekufa yeye lakini mzee Zakaria
apone.Nadra sana katika dunia ya leo
kuwapata watu wa namna hii ambao wako
tayari kuyatoa maisha yao kwa ajili ya
wengine.”akaendelea kuwaza
Sanya.Walifika nyumbani na kila mmoja
akaingai chumbani kupumzika Saa nne za asubuhi kamanda wa
polisi wa wilaya akawasili nyumbani kwa
mzee Zakaria akiwa ameongozana na
askari wengine kadhaa.Walizunguka
nyumba nzima wakachunguza na kisha
wakaingia ndani.Kamanda akataka
kuonana na familia ya Zakaria .Pauline
akajitambulisha halafu akawatambulisha
na akina Alfred.Kamanda wa polisi wilaya
naye akawatambulisha baadhi ya maafisa
alioambatana nao halafu akaelekeza
dhumuni la kufika pale.
“ Nimekuja hapa kwanza kuwapeni
pole kwa tukio lile la jana.Binafsi mzee
Zakaria ni rafiki yangu na nimeguswa sana
na tukio hili kama mlivyoguswa ninyi kwa
hiyo naomba mfahamu kwamba hamko
peke yenu katika jambo hili wengi
tumesikitishwa sana na
kilichotokea.Kama kamanda wa polisi wa
wilaya nimekuja kuangalia mazingira ya
tukio na vile vile kuongea nanyi jambo
moja la muhimu ambalo sina hakika kama
mnalifahamu tayari.Tulifahamu toka
mapema kuwapo kwa shambulio hili na
hivyo tukajipanga vizuri kuweza
kuwadhibiti wahalifu hao.Taarifa ya
kuwepo kwa shambulio hili tulipewa na
David.” “ David !!.Pauline akauliza kwa
mshangao
“ Ndiyo.Taarifa za kuwapo kwa
shambulio tulizipata toka kwa
David.Alikuja mwenyewe kituoni na
kutufahamisha kuhusiana na mipango ya
kuwapo kwa shambulio hili lililotokea.”
Kamanda akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“ Tukio lililotokea jana lilipangwa na
mke wa mzee Zakaria aitwaye Vicky ”
Pauline akastuka sana kwa taarifa ile
“ mama mdogo ?!! Pauline akasema
kwa mshangao..
“ kwa mujibu wa David ni kwamba
Vicky mke wa mzee Zakaria amekuwa
akimuhujumu sana mume wake kwa
kumuibia pesa nyingi sana ambazo
amekuwa akizificha katika akaunti zake
mbalimbali.Katika maelezo aliyotupatia
David ,alikiri kwamba yeye si mtoto wa
familia hii bali alipewa hifadhi na mzee
Zakaria .Alisema kwamba mara tu
alipoanza kuishi hapa mzee Zakaria
alitokea kumuamini na akamkabidhi
biashara zake azisimamie.Mara tu
alipoanza kuzisimamia biashara za mzee
Zakaria Vicky akamfuata na kumtaka
washirikiane katika baadhi ya mambo ambayo lengo lake ni kumuhujumu mzee
Zakaria.Alimuahidi mambo mengi sana
ikiwa ni pamoja na maisha mazuri kama
atakubali kushirikiana naye.David
alikubali kushirikiana naye lakini moyoni
alikuwa na lengo la kutaka kumfahamu
Vicky kwa undani zaidina kufahamu kila
anachokifanya nyuma ya mgongo wa mzee
Zakaria.Baade Vicky alianza kumtaka
David kimapenzi.Kwa kuwa alikuwa na
lengo lake David akakubali na hivyo
wakawa na mahusiano ya siri .Vicky
akamuamini David na alimfahamisha kila
kitu anachokifanya.Kwa kumtumia David
,Vicky alifanikiwa kuchukua mkopo
mkubwa wa mamilioni benki bila ya mzee
Zakaria kujua na kuzihifadhi katika
akaunti yake ambayo David anaifahamu
.Vile vile anasema kuna mambo
mengiambayo aliyagundua kwa Vicky.kwa
siku za hivi karibuni aligundua mpangowa
Vicky wa kutaka kumuua mzee Zakaria ili
aweze kurithi mali zote.Taarifa za kuwepo
kwa mpango huo alizipata kupitia kwa
rafiki mkubwa wa Vicky aitwaye
Safia.Mara tu alipozipata taarifa zile David
akaja kwetu na kutueleza kila kitu na sisi
tukaanza kujiandaa.Mtu ambaye Vicky
alimtumia katika mpango huo ni jambazi sugu aitwaye Chino ambaye sisi jeshi la
polisi kwa muda mrefu tumekuwa
tunamsaka lakini tulikosa ushahidi wa
kuweza kumtia hatiani lakini hatimaye
jana tulifanikiwa kumnasa
..Tunamshukuru sana David kwani licha
ya kuokoa uhai wa mzee Zakaria lakini pia
ametusaidia sana kumkamata mshukiwa
sugu wa ujambazi hapa Arusha.” Kamanda
akanyamaza kidogo na kuendelea
“ kwa sasa upelelezi unaendelea na
ukikamilika Vicky atapandishwa
mahakamani kujibu mashitaka
atakayokuwa anakabiliwa
nayo.Tunachokiomba kutoka kwenu ni
ushirikiano wenu wa hali na mali ili
kuhakikisha kwamba wale wote
waliohusika katika jambo hili
wanachukuliwa hatua stahiki.Endapo
kuna jambo lolote ambalo mnadhani
tunatakiw a kulifahamu kuhusu Vicky
msisiste kutueleza nasi tutalifanyia
kazi.Rafiki wa Vicky aitwaye Safia yeye
tayari anatusaidia katika upelelezi wetu
na tunamuombea David aweze kupona
kwani ni mtu muhimu sana katika kesi
hii.Tuzidi kumuombea sana ili Mungu
ampe nafuu ya haraka na aweze kupona ”akasema Kamanda na kuagana na akina
pauline wakaondoka zao.
“ David alinipigia simu na kunitaka
nije haraka Arusha kun jambo kubwa
anataka kunitaarifu.Nadhani jambo
lenyewe alilotaka kunitaarifu ni hili.”
Akasema pauline
“Alikutaarifu kuhusu jambo hili?
Sanya akashangaa
“ Hakupata nafasi ya kunieleza kama
jambo lenyewe lakini alikuwa na nia ya
dhati ya kunieleza.Ni mimi ndiye
niliyepuuzia.”akajilaumu Pauline
“ Mwiliwote unanitetemeka ,bado
siamini.Mama mdogo ?!! akasema pauline
“ Yaani pamojana maisha ya hali ya
juu aliyokuwa anaishi lakini bado
hakuridhika na akataka kumuua baba ili
arithi mali? Akasema kwa uchungu
Pauline na kuangua kilio.Sanya na Alferd
wakambembeleza
“Ninalia kwa uchungu mkubwa
nikikumbuka namna baba alivyokuwa
anampenda na kumjali Vicky.Alimpatia
kila alichohitaji lakini haya ndiyo malipo
yake? Akazidi kulia
“ Basi Pauline.Imetosha usilie
tena.Tunachotakiwa kukifanya kwa sasa
ni kumuombea sana David apone kwani kama alivyosema kamanda David ni mtu
muhimu sana katika kesi hii inayomkabili
Vicky.David anafahamu vitu vingi sana
kuhusiana na Pauline kwa hiyo akipona
atakuwa na msaada mkubwa sana.”
Akasema Alfred
“ I was wrong about David.Nilikosea
sana kumuhukumu kabla ya kujua nini
dhumuni la alichokuwa
anakifanya.”akasema Pauline na
kuendelea tena kulia ikawalazimu akina
Alfred kufanya kazi ya ziada
kumbembeleza.
********************
Saa kumi na mbili za asubuhi siku ya
jumatatu Robin na Lucy wakaondoka
katika hoteli ile waliyokaa kwa siku
mbili,Robin akampeleka kwanza Lucy
halafu naye akaelekea kwake kujiandaa
kwa ajili ya siku ile ya kazi.Alipofika
nyumbani alimkuta Penina akijiandaa kwa
ajili ya kwenda shule wakasalimiana
“ Baba siku nyingine na mimi
mnichukue niende na ninyi huko
mlikokwenda.kwa nini mliniacha ?
Akauliza Penina “ Kuna mambo ambayo mimi na
mama yako mdogo Lucy tulikuwa
tunayazungumza ambayo yalihitaji kuwa
sehemu tulivu sana”akasema Robin
“ Mlikuwa mnaongelea mambo gani?
Unaweza ukaniambia? Akauliza
hukuakicheka na kumfanya Robin naye
acheke.walikwisha zoea kutaniana
“Ni mambo ya watu wazima
yanayotuhusu mimi na mama yako
mdogo” akajibu Robin
“ Baba ni lini mwalimu Lucy
atahamia hapa na kuishi nasi? Nina hamu
sana ya kuishi naye ” akasema
Penina.Robina akacheka kidogo na
kusema
“ Usijali Penina.Tunaendelea na
mipango hiyo na itakapokuwa tayari
nitakutaarifu.lakini mambo yanakwenda
vizuri sana ” akasema Robin.penina
akatabasamu
“ Pamoja na hayo kuna mambo
mawili ninataka kukutaarifu”
“ Ni mambo gani baba? Akauliza
Penina.Robin akamshika mkono Penina
wakaenda kukaa sebuleni.
“ Penina nafahamu kwamba wewe na
mama yako hamna mahusiano
mazuri.Aliniacha angali ukiwa mdogo sana na katika muda huu wote hadi hivi sasa
hajawahi hata kukutembelea kujua
unaendeleaje.Ninafahamu hasira
ulizonazo juu yake kwani kitendo
alichokifanya ni kibaya .Alikuacha wakati
ambao ulimuhitaji sana.Pamoja na hayo
yote bado ukweli utabaki pale pale
kwamba ndiye mama yako mzazi.Ndiye
aliyekuleta hapa duniani.Hakuna mama
mzazi mwingine ”akasema Robin
“ Baba unataka kusema nini?
Akauliza Penina kwa wasi wasi
“ Penina mimi na mama yako mdogo
Lucy tuna nia ya dhati ya kufunga ndoa na
kuishi pamoja lakini kikwazo kilikuwa ni
kwamba mimi na mama yako bado
tulikuwa katika ndoa.Ili tuweze kufunga
ndoa ili tulazimu kuitengua kwanza ndoa
yetu.Tuliwasilisha suala hili katika idara
zinazohusika na ninafuraha kukujulisha
kwamba tayari wamekwisha lifanyia
maamuzi suala letu na ndoa yangu mimi
na mama yako imetenguliwa rasmi kwa
hiyo niko huru sasa kumuoa mama yako
mdogo Lucy.”akasema Robin.Penina
akatoa tabasamu kubwa sana
“ Nimefurahi sana kusikia hivyo
baba.Ninampenda sana Aunt Lucy na
nitafurahi sana kuishi naye kwani naye ananipenda sana.Naomba baba mfanye
haraka mfunge ndoa ili tuanze kuishi na
Aunt Lucy”akasema Penina
“ Penina ninashukuru kama
umelipokea suala hili kwa furaha.Hivi
karibuni tutaanza maandalizi ya ndoa yetu
na tutakapoanza tutakutaarifu mara moja”
akasema Robin.Ukapita ukimya mfupi na
kisha akasema
“ Ukiacha na hilo ,kuna jambo lingine
pia ninataka kukutaarifu ingawa sizuri .”
“Jambo gani tena hilo baba mbona
unataka kunipotezea furaha yote
niliyoipata? Akauliza penina
“ Ni kuhusu mama yako mzazi”
akasema
“ Mama ?! mama yupi tena?
“ penina kama nilivyotangulia
kukueleza awali kwamba pamoja na yote
aliyotukosea mama yako lakini bado
ataendelea kuwa mama yako mzazi kwani
ndiye aliyekuleta duniani.Hata kama ndoa
yangu na yeye imetenguliwa lakini bado
ataendelea kuwa mama yako tu.”
“ Baba naomba nikuweke wazi
kwamba sitaki kusikia chochote kuhusu
mama .Aliniacha nikiwa mdogo na hata
siku moja hakutaka kufuatilia maendeleo
yangu .Nimekosa upendo wake kwa hiyo hata mimi sihitaji kujua chochote kuhusu
yeye.Ni kweli atabaki kuwa mama yangu
aliyenileta hapa duniani lakini hatapata
upendo wowote toka kwangu.Siwezi baba
!! akasema penina
“ Penina nafahamu uchungu ulionao
na hata mimi pia aliniumiza sana lakini
nimekwisha msamehe.”akasema Robin na
kumfanya penina atoe kicheko kidogo
“ baba unathubutuje kumsamehe
mtu kama mama? Alikuumiza sana
,alikudharau na kukukimbia wakati huna
kitu leo hii unadiriki vipi kumsamehe?
Hapana baba mimi siwezi kumsamehe
hata kidogo.Atabaki kuwa mama yangu
mzazi lakini hatapata kabisa upendo
wangu” akasema Penina
“ Penina naomba unisikilize.lengo la
kukueleza hivi ni kutaka kukufahamisha
kwamba mama yako amepata ajali mbaya
sana ya gari na amelazwa hospitali na hali
yake ni mbaya sana.Pamoja na kwamba
ametukosea sana lakini kwa wakati huu
wa matatizo tusahau yote yaliyotokea na
tushikamane naye,tuonyeshe upendo
kwake kwani anahitaji sana faraja
.”akasema Robin
“ Amepata ajali ?!! “ Ndiyo amepata ajali mbaya na kwa
mujibu wa taarifa ni kwamba hali yake si
nzuri hata kidogo.”
“ Umekwenda kumuona? Akauliza
Penina
“ hapana bado sijaenda
kumtazama.Ninataka twende wote
.Atafarijika sana akituona sote
tumekwenda kumjulia hali.”akasema
Robin.Penina akainama akafikiri kwa
muda na kusema
“ sawa baba tutakwenda kumuona
.lakini ninakwena kwa sababu yako tu ”
akasema Penina
“ Ahsante sana penina.Ahsante
sana.Tutakwenda kumtazama jioni baada
ya kutoka masomoni.”akasema Robin
***********************
Japokuwa usiku mzima walikesha
hospitali,lakini bado Pauline
hakuonekana kuwa na usingizi hata
kidogo ingawa macho yake yalikuwa
mazito.Wakati Alfred na Sanya wakiwa
vyumbani wakipumzika ,Paulinealikuwa
amekaa sebuleni akitafakari.Alifikiria
mambo mengi sana namna familia yao
inavyokumbwa na majanga ya mara kwa mara lakini kubwa zaidi ni hili tukio la
uvamizi lililopangwa na mama yake
mdogo.Akainuka sofani akaenda ukutani
na kuitungua picha kubwa ambayo baba
yake mzee Zakaria alikuwa amepiga na
Vicky
“ Shetani mkubwa huyu ,sura yake
haistahili kabisa kuonekana ndani ya
nyumba hii.Toka mwanzo alipoingia humu
ndani roho yangu ilimkataa kabisa huyu
mwanamke na ndiyo maana mimi na yeye
hatukuelewana.Nilijua kabisa kwamba
hakuwa mtu mwema na hakuwa na nia
njema na baba.Hakumpenda baba bali
alifuata pesa zake tu.Nilijaribu mara
kadhaa kumueleza baba kuhusiana na
namna huyu mwanamke anavyotapanya
mali lakini baba sijui alipewa nini kwani
hakuwa akisikia la mtu yeyote kuhusu
Vicky. Ametuingizia hasara kubwa sana
kutokana na matumizi yake mabaya ya
pesa.Hakuridhika na yote aliyokuwa
anayapata akaona ni vyema kama
akimuua kabisa baba ili arithi kila
kitu.Ninamshukuru sana David kwani
kama si yeye basi hivi sasa baba yangu
tayari angekwisha uawa na mali zote
zingepotelea mikononi mwa Yule shetani
asiye .David ni kama malaika aliyetumwa na Mungu kuja kumlinda baba kwa sababu
ni mara ya pili sasa anamuokoa na
majanga.Mara yakwanza alimuokoa
katika ajali na sasa hivi amemuokoa toka
mdomo wa kifo.kama si yeye hivi sasa
nyumba hii ingetawaliwa na vilio vingi
kwani tayari baba angekwisha
fariki.Risasi alizostahili baba amezibeba
David.Huyu ni kijana wa ajabu sana.
“akawaza Pauline
“ Lakini David ametokea wapi?
familia yake iko wapi? Alifungwa gerezani
kwa kosa gani? Kwa nini hataki kuweka
wazi kuhusu historia yake? Akaendelea
kuwaza Pauline
“ Baada ya tuko la jana nadhani kuna
ulazima wa kumfahamu David kiundani na
kuifahamu pia familia yake mahala
walipo.Katika hali kama hii wanatakiwa
wafahamu hali ya mtoto wao ikoje.Halafu
kinachonipa wasiwasi ni endapo ikatokea
labda David akafariki dunia kitu ambacho
siombi kitokee tutawafahamuje familia
yake? Mungu amjalie David apone na
safari hii lazima atuonyese ilipo familia
yake ili nao wafahamu mahala mtoto wao
alipo.”akaendelea kuwaza Pauline na
mara simu yake ikaita,zilikuwa ni namba
ngeni “ hallow” akasema Pauline
“ hallow ninaitwa Sakina ninapiga
simu kutoka St Gasper
hospitali.Ninaongea na nani tafadhali?
“ Unaongea na Pauline.Kuna habari
gani hapo hospitali ? baba yangu mzee
Zakaria anaendeleaje? Akauliza Pauline
kwa wasiwasi
“ Usihofu Pauline baba yako
anaendelea vizuri sana na ndiye
aliyetuomba tukupigie simu hii” akasema
Yule muuguzi
“ Amesema mnipigie simu? akauliza
Pauline huku uso wake ukiwa na
tabasamu
“ Baba yako alipoamka asubuhi hii
ametaka kufahamu kama uko salama
,tukamuhakikishia kwamba uko salama
lakini bado haamini na anahitaji
kukuona.Kwahiyo Pauline naomba uje
hapa hospitali baba yako anahitaji
kukuona”akasema Yule muuguzi
Pauline akaenda kuwastua akina
Alfred na kuwaomba wajiandae kwa ajili
ya kwenda hospitali kuonana na mzee
Zakaria
Ndani ya dakika ishirini tayari
walikwisha jiandaa na kuondoka kuelekea
hospitali kuonana na mzee Zakaria. “ Hakuna taarifa zozote za kuhusiana
na maendeleo ya David ?akauliza Sanya
“ Hapana ,mpaka sasa hivi hakuna
taarifa zozote kutoka hospitali.Tukitoka
kumtazama baba tutaenda kujua
maendeleo yake” akasema Pauline
“ Ee Mungu tunaomba umponye
David,tunamuhitaji sana” akasema Sanya
kwa sauti ndogo huku macho yake
yakilengwa na machozi.Pauline akageuka
akamtazama
“ I can see her eyes.She’s in
love.Anampenda David na ameumia sana
kwa kilichotokea.She’s the right woman
for David.Nitahakikisha ninafanya kila
linalowezekana hadi Sanya na David
wawe pamoja.Hii ni zawadi kubwa
ambayo nitampatia David.”akawaza
Pauline
Walifika hospitali wakashuka garini
na kuelekea moja kwa moja katika
chumba alimolazwa mzee Zakaria
aliyekuwa amekaa akizungumza na
wauguzi ambao walitoka baada ya akina
Pauline kuwasili.Pauline akamfuata na
kumkumbatia kwa nguvu.
“ Ouh my daddy ! akasema Pauline “ Pauline my queen” akasema mzee
Zakaria na wote wawili machozi
yakawatoa
“ Pole sana baba.Pole sana “akasema
Pauline
“ Wewe ndiye unayepaswa kupewa
pole.Unaendeleaje?
“ Ninaendelea vizuri sana baba.Vipi
wewe maendeleo yako? Akauliza Pauline
“ Ninamshukuru Mungu ninaendelea
vizuri .Nilipoamka niliwauliza madaktari
kama familia yangu wote wazima
wakaniambia kwamba mko salama
sikuamini nikataka hadi niwashuhudie
kwa macho.Nashukuru nimewaona nyote
lakini kuna mtu mmoja sijamuona
hapa.David yuko wapi? Akauliza mzee
Zakaria akina Pauline wakatazamana.
“ Mbona mnatazamana? David yuko
wapi? Tafadhali niambieni kama kuna
tatizo “ akasema kwa wasi asiwasi
“ Daddy just relax everything is fine”
akasema Pauline akijaribu kumtuliza baba
yake.
“ Pauline kuna kitu unanificha.David
yuko wapi? Halafu mama yako mdogo
yuko wapi? Nilitegemea angekuwa hapa
karibu yangu mida hii lakini
sijamuona,whats going on?akauliza mzee Zakaria.Pauline akaogopa kusema
kilichotokea akabaki kimya
“ Dr Alfred tell me what’s going on?
Nini kilitokea jana? Ninachokumbuka ni
kwamba tulisikia milio ya risasi na wakati
tunajiuliza risasi zile zililia wapi mara
tukavamiwa na watu wawili waliokuwa na
silaha na wakatuamuru tulale
chini.Ninakumbuka nilirukiwa na David
na kilichofuata nikasikia milio ya risasi na
sikujua tena nini kiliendelea.Tafadhali
nieleze nini kilitokea? Majambazi wale
waliotuvamia walichukua nini? Akauliza
mzee Zakaria
David akamtazama Pauline halafu
akageuka akamtazama Sanya kisha
akamueleza mzee Zakaria kila
kilichotokea usiku ule.Mzee Zakaria
akashindwa kujizuia kutokwa na machozi
“ So it was him again.He saved me
again!! Ouh David !!..”akasema mzee
Zakaria .Pauline akampiga piga mgongoni
“ be strong daddy” akasema Pauline
“ Where is he now? Anaendeleaje
David? Akauliza mzee Zakaria
“ Kwa sasa yuko hospitali kuu ya
mkoa anapatiwa matibabu.Jana usiku
amefanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi
mwilini mwake na upasuaji ulifanikiwa .kwa hvi sasa yuko chini ya uangalizi wa
madaktari.” Akasema Dr Alfred.Mzee
Zakaria akamtazama na kusema
“ Dr Fred wewe ni daktari,please tell
me the truth,is he going to live ?? akauliza
mzee Zakaria
“ david will be ok.he’s going to
live”akasema Alfred kwa kujiamini ili
kumpa moyo mzee Zakaria.
“ tafadhali nipelekeni nikamuone
kijana wangu “akasema mzeeZakaria na
kutaka kuinuka kitandani
“ Mzee bado unahitaji kuwa katika
mapumziko na pindi madaktari
wakiridhika kwamba unaendelea vizuri
basi watakuruhusu na tutakupeleka
kumtazama David.usihofu mzee david
yuko chini ya uangalzi makini sana na
atapona na hata sisi tunaendelea
kumfuatilia kwa karibu sana” akasema
Alfred na mara simu yake ikaita alikuwa ni
mke wake akatoka mle chumbani akaenda
nje
“ Fuatilieni hali ya David na kama
anapata matibau anayostahili kama kuna
uwezekano tumpeleke nje ya nchi.Sitaki
kumpoteza kijana wangu.” Mzee Zakaria
akamwambia Pauline “ mama yako mdogo naye yuko
wapi? Anamuuguza David?Mzee Zakaria
akauliza
“ daddy kuna jambo ambalo nadhani
unapaswa kulifahamu kuhusu mama
mdogo”
“ Ni jambo gani Pauline?Nieleze
tafadhali.Yuko salama?
“ Yuko salama usihofu” akasema
Pauline na kuvuta pumzi ndefu
“ kamanda wa polisi wa wilaya
alikuja nyumbani leo akaongea
nasi.Ametuambia kwamba majambazi
wote waliofanya tukio lile la kutuvamia
walidhibitiwa.wawili waliuawa na
wengine wanashikiliwa na polisi.Alisema
kwamba kiongozi wa majambazi wale
anaitwa Chino ambaye anamiliki vituo
kadhaa vya mafuta hapa jijini Arusha”
“ Chino ?!! Mzee zakaria akashangaa
“Ndiyo baba”
“ Basi haya ni maajabu.Mbona Chino
ni kijana ambaye tunafahamiana sana?
Kwa nini amfanyie vile? Zakaria
akashangaa
“ kwa mujibu wa kamanda wa polisi
ni kwamba Chino alitumwa kuifanya hiyo
kazi kwa malipo manono. “ Alitumwa?..alitmwa na nani aje
anivamie mimi na familia yangu?
“ alitumwa na mama mdogo Vicky”
akasema Pauline na kwa sekunde kadhaa
mzee Zakaria akabaki anamtazama
mwanae kana kwamba ameona kitu cha
kutisha
“ Vicky ?!! akauliza Zakaria kwa
mshangao
“ Ndiyo .Ni mama mdogo Vicky ndiye
aliyemtuma Chino na lengo lake lilikuwa
ni kukuua ili arithi mali.Kwa hivi sasa
anashikiliw ana polisi na pindi
upeleleziukikamilika atapandishwa
mahakamani”akasema Pauline na mara
mzee Zakaria akaanguka
kitandani.Pauline akapiga kelele kubwa
kuomba msaada.Alfred na madaktari
wengine wakangia mle ndani mbio kujua
kilichotokea.Haraka haraka akina Pauline
wakatolewa mle chumbani na kisha mzee
Zakaria akapakiwa katika kitanda na
kukimbizwa katika chumba cha dharura.
“ Pauline nini kimetokea? Akauliza
Alfred lakini Pauline hakuweza kujibu kitu
alikuwa anatetemeka
“ Sanya nini kimetokea mle
ndani?Alfred akamuuliza sanya “ Mimi sifahamu Pauline na baba
yake walikuw wanaongea nini kwa sababu
sifahamu lugha ya Kiswahili.Kuna mambo
walikuwa wanaongea na mara mzee
Zakaria akaanguka ghafla” akasema Sanya
“ Pauline ulimwambia nini mzee
Zakaria?akauliza Alfred .pauline
hakuweza kuongea alikuwa anatetemeka
.David akamchukua na kumpeleka sehemu
ya kupumzikia .
Baada ya nusu saa daktari akaomba
kuona na akina Alfred
“ Hali ya mzee inaendelea
vizuri,alipatwa na mstuko
.Ninachowaomba katika wakati huu,mzee
asielezwe jambo lolote la kustusha.Hata
kama kuna mwanafamilia alipoteza
maisha katika shambulio basi mzee
asielezwe kwanza kwani endapo akipata
tena mstuko mwingine kuna hatari kubwa
ya kumpoteza.Nimewaiteni ili kuwapeni
hilo angalizo.Jaribuni kuangalia maneno
ya kumwambia mzee.Kwa sasa ataendelea
kuwa chini ya uangalizi wetu hadi hapo
hali yake itakapokuwa nzuri” akasema
daktari.
“ Ahsante Mungu !akasema Pauline
kimya kimya Baada ya maelezo yale ya daktari
wakaondoka na kulekea katika hospitali
ya mkoa kufuatilia hali ya David.Bado
hawakuruhusiwa kuingia lakini daktari
aliwahakikishia kwamba David
anaendelea vizuri na aliwataka warejee
tena jioni pengine wangeweza kupewa
nafasi ya kuiingia na kumuona kama hali
yake bado itakuwa inaendelea kuwa nzuri.
Saa kumi na moja za jioni
Robin,mwalimu Lucy wakiwa
wameambatana na Penina wakawasili
hospitali kuu ya mkoa kwa dhumuni la
kuwajulia hali Vivian pamoja na Tino
magari,Kisha egesha gari wakashuka na
moja kwa moja wakaelekea eneo la
mapokezi ambako waliuliza na
kuelekezwa mahala walikolazwa Vivian na
mumewe Martin.Tayari walikwisha tolewa
katika chumba cha wagonjwa mahututi na
kila mmoja aliwekwa katika chumba
chake .
Walianza kwanza katika chumba
alimolazwa Martin.Marafiki zake kadhaa
walikuwamo mle chumbani wakimjulia hali na wengine walikuwa nje ya chumba
wakisubiri kupata nafasi ya kuingia .
“ watu ni wengi waliokuja kumtazam
Fred,unadhani tutapata nafasi ya
kuruhusiwa kuingia ndani na muda
unazidi kwenda? Robin akamuuliza Lucy
Kabla Lucy hajajibu kitu,akashikwa
bega.
“ Lucy !! akasema Yule mtu
aliyemshika bega
“ Armando !! akasema Lucy na
wakasalimiana
“ Habari za siku nyingi ?
“ habari nzuri sana Lucy.Vipi
maendeleo yako ?
“Ninaendelea vizuri sana .Poleni
sana na matatizo” akasema Lucy
“ Tumekwisha poa Lucy.kwa kweli
walipata ajali mbaya sana.Ni ajabu kabisa
hata leo hii kuwa bado wako hai ingawa
wameumia sana.Martin amekatwa miguu
yote miwili,mke wake yeye amepotea
miguu yote miwili pamoja na
mkono”akasema Armando rafiki mkubwa
wa Martin
“ dah ! ama kweli ilikuwa ni ajali
mbaya sana”akasema Robin “ By The way Armando nilisahau
kukutambulisha,huyu anaitwa Robin ni
mchumba wangu .Robin huyu anaitwa
Armando ni rafiki mkubwa wa Martin.”
Lucy akafanya utambulisho.Armando na
Robin wakashikana mikono
wakasalimiana na kisha Armando
akawaongoza Robin na Lucy kuingia mle
chumbani akawatoa watu wote
waliokuwampo mle mchumbani
wakabaki akina Lucy pekee.Tino magari
alikuwa amelala kitandani,uso ukiwa
umemvimba kutokana na majeraha
makubwa aliyoyapata.Haikuwa rahisi
kumtambua kwa haraka.Aliumia sana.
“ Tino,Lucy amekuja kukutazama”
akasema Armando.
“ Karibu Lucy !! akasema Tino kwa
sauti ya chini sana.Lucy akamsogelea
palekitandani na kumuinamia
“ Martin pole sana”akasema Lucy
huku machozi yakimdondoka
“ ahsante sana Lucy kwa kuja
kuniona.Nashukuru Mungu nimesalimika
katika ile ajali,Yule shetani alitaka
kuniua..Alidhamiria kuniua.”akasemaTino
lakini Lucy hakuweza
kumuelewa.Akamtazama Armando “bado hali yake si nzuri sana na toka
asubuhi amekuwa akiongea maneno hayo
hayo yasiyoeleweka.” Armando
akamfahamisha Lucy.
“ basi sisi ngoja tuondoke tutakuja
tena siku nyingine kumjulia hali
Martin.”akasema Lucy kisha wakatoka mle
chumbani .Bado machozi yaliendelea
kumtoka
“ Its ok Lucy.Martin atapona
tu”akasema Robin
“ Robin namuonea huruma Martin
ameumia sana.Amewahi kuniumiza sana
wakati Fulani lakini kwa hali niliyomuona
nayo leo hii nimeshindwa kujizuia
kudondosha machozi.Ameumia mno”
akasema Lucy wakaongozana hadi katika
chumba alimolazwa Vivian.Marafiki
kadhaa wa Vivian walikuwepo nje ya
chumba kile na wengi walionekana kuwa
na nyuso zenye huzuni.Walikuwa
wamesimama kivikundi wakiongea .Mara
tu Lucy na Robin walipotokeza baadhi ya
watu waliowafahamu wakaanza
kusemezana
Ndani ya chumba kile kulikuwa na
watu wawili tu,Lucy na Robin
wakaingia.Vivian alikuwa amelala
kitandani na kichwani hakuonekana kuwa na majeraha makubwa kama
ilivyokuwa kwa mumewe Martin.Aliweza
kuongea japo bado alionekana kuwa na
maumivu makali sana.
“ hallo Lucy ! Pole sana”akasema
Robin.
“ Robin umekuja kunitembelea..!
Mimi maisha yangu
yameharib…………”Vivian akashindwa
kuendelea kuongea akabubujikwa na
machozi
“ Vivian nyamaza usilie “akasema
mwanamke mmoja aliyekuwa
akimuhudumia huku akimfuta machozi.
Pamoja na kubembelezwa anyamaze
lakini bado Vivian aliendelea kububuji
kwa na machozi.Robin akamsogelea na
kukaa katika kitanda akachukua
kitambaa na kumfuta machozi.Mwalimu
Lucy akamshika mkono Penina .
“ Nyamaza usilie Vivy.” Akasema
Robin.
“ Robin nashukuru umekuja
kunitembelea. Mungu ameniadhibu kwa
mambo niliyokufanyia .” akasema Vivy na
kuendelea kulia
“ Vivy kwa hali yako hii hutakiwi
kulia tafadhali.Jikaze usilie hii ni ajali
kama ajali nyingine na ingeweza kumpata mtu yeyote Yule kwa hiyo usijilaumu sana
kwa kilichotokea” akasema Robin.Vivian
akamfanyia ishara Yule mama
anayemuuguza asogee akamumba awatoe
Lucy na Penina nje ili abaki na Robin
pekee.
“ Robin nimetaka tubaki peke yetu
kuna jambo ninataka kukwambia”
akasema Vivian japo alionekana bado ana
maumivu makali na aliongea taratibu kwa
sauti ndogo .
“ Vivian huu si wakati muafaka wa
kuzungumzia jambo lolote.Tusubiri hadi
hapo utakapopona ndipo utanieleza
unachotaka kunieleza kwani hata mimi
kuna mambo ninaaka kuzungumza nawe
.Tukiachana na hayo pole sana kwa ajali
hii mbaya.Ilitokeaje ajali hii? Akauliza
Robin
“ Robin naomba unisikilize kwani
sina hakika kama nitaipata tena nafasi ya
kuongea nawe.” Akasema Vivian
“ Kwa nini unaema hivyo Vivy?
“ Robin maisha yangu yameharibika
kabisa na yote hii ninajua ni adhabu
kutoka kwa Mungu kwa mambo
niliyokufanyia.Nilikufanyia mambo
mabaya sana na kibaya zaidi ni kitendo
cha kumtelekeza mwanangu. Nilikiuka kiapo changu cha ndoa kwa sababu ya
kuukimbia umasikini wako nikafuata
maisha mazuri lakini pamoja na kupata
maisha mazuri niliyokuwa nayakimbilia
sijawahi kuwa na furaha.Robin ni mimi
ndiye niliyesabisha ajali ile itokee kwa
sababu nilitaka tufe.Mimi na Martin tuna
mgogoro mkubwa na ndoa yetu inaweza
ikavunjika muda wowote . Sikuwa tayari
kuachana na Alfred na ndiyo maana
nikasababisha ile ajali makusudi ili tufe
wote lakini Mungu akaniadhibu kwa kosa
lile .Ninachukua nafasi hii kukuomba sana
msamaha wewe kwa yale yote
niliyokukosea na ninakuomba uniombee
pia msamaha kwa mwanangu Penina.Sina
hakika kama atanisamehe kwa sababu
sikuwahi kuwa mama kwake licha ya
kumleta duniani.Nilimkimbia wakati
akiwa mdogo kabisa na sik………..”
“ Basi imetosha Vivian.” Robin
akazuia Vivian asiendelee tena kuongea
“ Tafadhali usiendelee kuongea Vivy
unajiumiza sana.Mambo hayo yamekwisha
pita na tutayaongea ukishapona.Kwa sasa
si muda muafaka wa kuliongelea jambo
hili.” Akasema Robin
“ Robin naoma unisamehe sana
mume wangu,najua nilikukosea sana na kukuumiza sana lakini naomba
unisamehe.Hebu nifunue shuka
unitazame” akasema Vivian na Robin
akamfunua shuka akastuka sana.Vivian
hakuwa na miguu tena.Miguu yake yote
miwili ilikatwa.Robin akadondosha
machozi
“ Pole sana Vivian !! akasema
“ Robin hali yangu ndiyo hii kwa
sasa.Maisha yangu yote yamebaki
hivi.Nimekuwa mlemavu wa maisha.Sina
miguu tena na sasa ninauona umuhimu
wako.Robin ninawahitaji sana kwa wakati
huu wewe na mwanangu.Tafadhali
naomba unisamehe Robin na tuendelee na
kuishi kiapo chetu cha ndoa.Ninakuahidi
kwamba pamoja na hali yangu hii ya
ulemavu nitawapenda ninyi nyote na….”
“ Vivian naomba tafadhali usiumize
kichwa chako kwa mambo haya.Kitu
kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha kwanza
unapona na baada ya hapo ndipo
tutayazungumza mambo mengine kama
hayo.Jitahidi kwa sasa kuepuka mawazo
kama hayo.Naomba nikwambie vile vile
kwamba nimeambatana na
Penina.haikuwa kazi rahisi kumshawishi
aje akuangalie kutokana na mambo
uliyomfanyia. “ Yuko wapi mwanangu?
“ Yuko hapo nje pamoja na mama
yake mdogo.” Akasema Robin .Pamoja na
maumivu yake yote lakini Vivian
akaonyesha mstuko aliposikia Robin
akimtaja mama mdogo wa Penina
“ Mama mdogo yupi?
“ Mwanamke ambaye ninatarajia
kufuga naye ndoa hivi karibuni” akasema
Robin
“ Robin tafadhali usiniache.Mimi
ndiye mkeo wa ndoa.Tafadhali Robini
najua nimekukosea sana lakini
ninakuahidi kwamba nitakuwa muaminifu
kwako na nitaw………………”
“ Stop that Vivian..!!! akasema Robin
kwa sauti ya juu kidogo
“ Ninaomba matatizo haya yasiwe
kigezo cha kutaka kunivurugia maisha
yangu.Pamoja na kwamba unaumwa lakini
naomba nikuweke wazi kwamba sina
mpango wa kurudiana na wewe .Vivian
wewe ni mwanamke katili na hufai kuwa
mke.Vivian sikutaka kukueleza kuhusu
jambo hili hadi hapo utakapokuwa
umepona lakini umenilazimisha
niliseme.Mimi na wewe si wanandoa
tena.Tayari ndoa yetu imetenguliwa na
kanisa kwa hiyo kila mtu hivi sasa ni huru Olewa na mwanaume wa maisha yako
mwenye mali uliyemkimbilia na mimi
ninamuoa mwanamke ambaye Mungu
amenipangia niwe naye katika maisha
yangu.Mwanamke anayenijali na
kunithamini.Mwanamke mwenye mapenzi
ya kweli na mvumilivu katika hali zote za
maisha ambaye nina hakika hawezi
kunikimbi hata kama nikiwa kipofu
leo.Ninachokishukuru kutoka kwako ni
kunizalia binti mzuri mwenye akili
ambaye ulishindwa kumpa malezi na
upendo kama mama na ukakimbilia
utajiri.Samahani kwa maneno haya
makali Vivy ambayo sikupaswa kabisa
kukueleza hasa kwa wakati huu ambao
unaumwa lakini sina namna nyingine zaidi
ya kukueleza ili ufahamu kwamba mimi
na wewe its over.Nimekuja kukutazama si
kwamba bado ninakupenda ila ni kwa ajili
ya kukuaga na kukutakia maisha mema.”
Akasema Robin na kuinuka kitandani
“ Robin !!!...akalia Vivian lakini Robin
hakumjali akafungua mlango akamuita
Penina na Lucy wakaingia mle ndani na
kumkuta Vivian akilia
“ What happened? Akauliza Lucy
.Robin akamshika mkono Peninakumsogeza karibu na kitanda “ Vivian ,Penina huyu hapa amekuja
kukupa pole” akasema Robin.Vivian
akafuta machozi na kumtazama
“ Ouh Penina !!..”
Penina alibaki anamuangalia hakujua
aseme nini
“ Penina mwanangu naomba
unisamehe sana kwa mambo yote
niliyokukosea na …..” akasema Vivian na
kushindwa kuendelea akaanza kulia
.Robin akatazamana na Lucy kisha
wakapeana ishara watoke nje na
kumuachia nafasi Penina ya kuongea na
mama yake.Penina naye akatoka
kuwafuata.
“ Penina tumekuachia nafasi uweze
kuongea na mama yako .Rudi ndani
ukaongee na mama yako” akasema Robin
“ Baba siwezi.Nitaongea naye nini ?
Sina cha kuongea naye” akasema Penina.
“ Penina hii ni nafasi pekee umeipata
kwa miaka mingi ya kukaa japo kwa muda
mfupi na mama yako na uongee naye.Kwa
wakati huu anahitaji sana faraja na
unaweza kuongea naye jambo lolote
lile.Atafurahi sana kusikia sauti yako.Neno
lolote utakalomwambia atafurahi.Ongea
naye kitu chochote” akasema Mwalimu
Lucy “ Nenda kaongee naye sisi
tunakusubiri hapa nje” akasema
Robin.Penina akaufungua mlango na na
kuingia ndani
******************
Saa kumi za jioni akina Pauline
wakaanza tena safari ya kuelekea
hospitali.Safari hii walianzia hospitali kuu
ya mkoa kumtazama David kabla ya
kuelekea kwa mzee Zakaria.
“ Alfred mchana tulipokuwa na baba
kule hospitali nani alikupigia simu?
Akauliza Pauline wakiwa garini
wakielekea hospitali
“ Alikuwa Grace”
“ Anataka nini?
“ Alitaka kujua maendeleo yangu na
lini ninarejea Moshi” akajibu Alfred.
“ Ok good” akasema Pauline na safari
ikaendelea.
“ Kwa siku hizi chache nilizokaa na
Alfred ninajiona ni kama vile tayari Fred
ni mume wangu.Ni mwanaume anayenifaa
sana huyu .Nina hakika hata leo hii
nikimtambulisha kwa baba lazima atamkubali tu.Lakini tatizo ni mume wa
mtu.Ni hapo tu panaponiumiza
kichwa.Siyo siri tena kwa namna
nilivyotokea kumpenda Alfred ni lazima
nitaingia katika vita ya kumgombania
mume wa mtu.Sina ujanja tena
nimekwisha nasa mtegoni na siwezi
kujinasua .Najua Grace ataumia sana
lakini sina namna nyingine mimi na yeye
lazima tuingie katika mapambano ya
kumgombania Alfred.” Akawaza Pauline.
Waliwasili hospitali na kufululiza
moja kwa moja kwa daktari ambaye
aliwapa taarifa nzuri kwamba kwa
mchana wa siku ile David alizinduka na
kuongea kidogo lakini kwa wakati ule
alikuwa amechomwa sindano ya usingizi
ili dawa kali anazotumia ziweze kufanya
kazi .Kwa ujumla daktari alithibitisha
kwamba maendeleo ya David yalikuwa
mazuri.Hizi zilikuwa ni taarifa nzuri sana
kwa akina Pauline.
Daktari akawaruhusu kuingia
kumtazama David lakini kwa sharti la
kuingia mmoja mmoja mle chumbani tena
wakiwa na mavazi maalum.Wa kwanza
kuingia mle ndani ya chumba alikuwa ni
Sanya.David alikuwa amelala usingizi
mzito ,Sanya akamsogelea na kumshika mkono.Akamtazama kwa makini na
kusema
“ David najua hata ukiwa usingizini
utayasikia maneno haya
ninayokutamkia.Ni maneno yatokayo
ndani kabisa mwa moyo wangu.David sijui
nianzie wapi lakini ninachoweza
kukisema ni kwamba nilikuja Tanzania
kwa dhumuni la kuwatafuta wazazi wangu
na sikujua kama nitakutana na
mwanaume wa kwanza
kumpenda.Nimekutana nawe na ghafla
sana bila kujua sababu nimetokea
kukupenda sana.Nina hakika safari yangu
ya Tanzania ilikuwa ni maalum kwa
kunikutanisha nawe kwani kwa muda
mrefu nilijizuia kuingia mapenzini
nikimuomba Mungu anijalie niweze
kumpata kijana mwenye sifa
ninazozihitaji na sifa nyingi kati ya hizo
unazo wewe David.Ninakupenda
David..Ninakupenda sana na sintoacha
kumlilia Mungu usiku na mchana akupe
uponaji wa haraka ili niweze kupata nafasi
ya kukueleza haya nikwambiayo sasa
huku ukinitazama machoni.”
Sanya akatoka mle chumbani huku
akifuta machozi.Pauline akamkumbatia na
kumpa moyo mkono.Akamtazama kwa makini na
kusema
“ David najua hata ukiwa usingizini
utayasikia maneno haya
ninayokutamkia.Ni maneno yatokayo
ndani kabisa mwa moyo wangu.David sijui
nianzie wapi lakini ninachoweza
kukisema ni kwamba nilikuja Tanzania
kwa dhumuni la kuwatafuta wazazi wangu
na sikujua kama nitakutana na
mwanaume wa kwanza
kumpenda.Nimekutana nawe na ghafla
sana bila kujua sababu nimetokea
kukupenda sana.Nina hakika safari yangu
ya Tanzania ilikuwa ni maalum kwa
kunikutanisha nawe kwani kwa muda
mrefu nilijizuia kuingia mapenzini
nikimuomba Mungu anijalie niweze
kumpata kijana mwenye sifa
ninazozihitaji na sifa nyingi kati ya hizo
unazo wewe David.Ninakupenda
David..Ninakupenda sana na sintoacha
kumlilia Mungu usiku na mchana akupe
uponaji wa haraka ili niweze kupata nafasi
ya kukueleza haya nikwambiayo sasa
huku ukinitazama machoni.”
Sanya akatoka mle chumbani huku
akifuta machozi.Pauline akamkumbatia na
kumpa moyo “ Usijali Sanya David atapona tu”
akasema Pauline na kisha ikafuata zamu
yake kuingia mle chumbani
Wote watatu walifanikiwa kuingia
chumbani mle kumtazama David na kwa
kuwa hawakuwa na kitu kingine cha
kufanya pale hospitali walijiandaa
waondoke na kuelekea hospitali ya St
Gasper alikolazwa mzee Zakaria.Kabla
hawajaondoka Sanya akawakumbusha
akina Pauline kitu
“ Mnawakumbuka wale wagonjwa
wetu wa ajali? Kwa nini kabla
hatujaondoka tusiende kuwatazama na
kujua hali zao zinaendeleaje?
“ Ni kweli kabisa.Kwa sasa wakati
tuna hakika kwamba David hayuko tena
katika hatari nadhani ni jambo jema kama
tukienda kuwatazama wale wagonjwa
wetu kama tayari wamekwisha anza
kupata nafuu” akasema Alfred na baada ya
kwenda katika gari wakaelekea katika
wadi walikolazwa akina Vivian.Walifika
katika chumba cha Tino lakini kulikuwa
na watu wengine ambao walikuwa
wakisubiri kupata nafasi ya kumjulia hali
na tayari muda ulikuwa umekwenda sana
na tayari watu walianza kutakiwa
kuondoka “ Kwa hapa hatutaweza kupata
nafasi ya kuingia.Twendeni tukajaribu
kwa Yule mwanamama” akashauri Pauline
wakaondoka kuelekea katika chumba
alimolazwa Vivian.
Nje ya chumba cha Vivian hakukuwa
na watu wengi,kwani tayari wengi wa
waliokuja kumtazama tayari walikwisha
ondoka.Katika mlango walisimama watu
wawili mwanaume na mwanamke.Pauline
akawasalimu na kuwauliza kama kuna
mtu mle ndani .Yule mwanaume
akawaaambia kwamba mgonjwa anaongea
na mtoto wake
“ Ninyi ni ndugu zake? Akauliza Yule
mwanaume mtanashati
“ Hapana sisi si ndugu zake ila sisi
ndio tuliowachukua kutoka mahala
walikopata ajali na kuwakimbi za hapa
kwa hiyo tumekuja kujua maendeleo yao”
akasema Pauline
“ Ouh ahsanteni sana.Wagonjwa
wote wawili wanaendelea vizuri japokuwa
wamepoteza baadhi ya viungo vya mwili
lakini wanaendelea vizuri.” Akasema Yule
mwanaume
“ Yah ilikuwa ni ajali mbaya sana”
akasema Pauline “ By the way ninaitwa Robin na huyu
hapa anaitwa Lucy mke wangu ” Yule
mwanaume akajitambulisha
“ Nafurahi kuwafahamu.Ninaitwa
Pauline na wale pale ni wenzangu ambao
nimeambatana nao” akasema Pauline
“ Wewe ni mwenyeji wa Arusha?
Akauliza Lucy na mara simu yake ikaita
akasogea pembeni
“ Mimi ni mwenyeji wa hapa Arusha
lakini usiku ule wa ajali ile mimi na
wenzangu tulikuwa tumetokea Moshi.”
Akasema Pauline na kuendelea kusimama
pal e nje wakimsubiri mtu aliyekuwamo
mle chumbani atoke ili waingie.Sanya na
Alfred walikuwa wamesimama kwa mbali
kidogo wakiongea.
“ Aliyesema duniani wawili wawili
hakukosea kabisa .Yule msichana
amefanana mno na Lucy kwa kila kitu
isipokuwa yeye amekuwa ni mweupe
zaidi..Dah ! wamefanana mno..” akawaza
Robin akiwa ameyaelekeza macho kwa
Sanya.Pauline akatazama saa yake ya
mkononi na kusema
“ Nadhani tutakuja tena siku
nyingine kwani muda unakwenda sana na
tunaye mgonjwa mwingine tunayekwenda kumtazama” akasema Pauline na kisha
yeye na akina Fred wakaondoka.
“ Mhhh !!.huku si kufanana kwa
kawaida.Yule msichana na Lucy
wamefanana sana.Wamefanana macho
midomo na hata kutembea.Sijui kama
Lucy amemchunguza Yule msichana vizuri
na kuona namna walivyofanana.Mhh !!
akawaza Robin wakati akina Pauline
wakiondoka kuelekea katika gari
lao.Mlango ukafunguliwa Penina akatoka
“ Baba twendeni tuondoke.Aunt Lucy
yuko wapi? ” akasema Penina
“ Lucy anaongea na simu.Umeongea
na mama yako? Mmeongea nini?
“ Hakuna kitu cha maana
tulichokiongea .Alinitaka nikae karibu
naye na akawa anaongea mambo ambayo
siyaelewi .Ananiambai eti nikuombe ili
usije ukamuacha bali umrudishe tuishi
pamoja.” Akasema Penina.
“ Wewe ukamjibu nini? Akauliza
Robin
“ Sikumjibu kitu nikabaki
ninamuagalia tu.” Akasema Penina
“ Wewe unasemaje? Tumrudishe
mama yako nyumbani tuishi naye?
Akauliza Robin na kumfanya Penina atoe
kicheko kidogo “ Baba mbona unanitega wakati jibu
unalifahamu? Mwanamke ambaye
anakufaa na ambaye mimi ninamuhitaji ni
Aunt Lucy pekee na hakuna
mwingine.Kwani mama alipokukimbia si
alikwenda kuolewa? Basi akae na hao hao
matajiri aliowakimbilia ” akasema Penina.
“ Mhh ! itachukua muda mrefu kwa
Penian kumsamehe mama yake.Vivian
hayupo kabisa kichwani kwa Penina.Haya
ndiyo malipo ya mambo
aliyoyafanya.Alimkimbia mtoto kwa
wakati ambao alimuhitaji sana ,alihitaji
mno malezi ya mama lakini naye
amekataliwa kwa wakati ambao anahitaji
sana mapenzi ya mtoto.Ukimfanyia mtu
ubaya nawe utalipwa kadiri ya ubaya
uliomfanyia.Ni wakati wake wa kujuta
sasa kwa kila alichokifanya.Kama
asingekimbia kwa wakati ule na
akavumilia tukashikamana na hivi sasa
angekuwa anaishi maisha mazuri
anayoyataka lakini alikimbia umasikini
kumbe akasahau kwamba Mungu
aliyenipa mimi umasikini ndiye aliyempa
utajiri huyo mwanaume aliyemkimbilia. .”
akawaza Robin .Lucy akarejea
wakaondoka zao. ****************
Wakiwa garini wakielekea St.Gasper
hospitali kumtazma mzee Zakaria,simu ya
Alfred ikaita.Alipotazama jina la mpigaji
akastuka sana akamuomba Pauline
aegeshe gari pembeni ili aweze kuongea
na ile simu.Pauline akaegesha gari
pembeni na Fred akashuka.
“ Hallow mzee shikamoo ! akasema
Fred huku uso wake ukonekana kuwa na
matone ya jasho
“ Fred ni mambo gani hayo uliyoanza
kuyafanya? Akauliza mtu Yule upande wa
pili wa simu
“ Mambo gani mzee? Akauliza Fred
“ Fred ninakuomba urejee haraka
sana Moshi kwa mkeo.!! Akasema kwa
ukali Yule mzee
“ Amekupigia simu akakueleza
kwamba nimeondoka?
“ Ndiyo.Kwa nini unamfanyi a hivi
mkeo?
“ Mzee nimekuja huku Arusha kwa
dharura,nilihitajika katika hospitali ya
Serian mara moja” “ Tafadhali usinidananye Fred.Mimi
ninafahamu kila kitu zaidi yako.Tayari
nimewasiliana na hospitali ya Serian na
wamenihakikishia kwamba hawajakuita
na wala hakuna mgonjwa wa dharura wa
moyo.Tafadhali naomba urejee Moshi
haraka sana!!!
Alfred akakaa kimya
“ Alfred unanisikia? Akauliza Yule
mzee kwa ukali
“ Ndiyo mzee nimekusikia.”
“ Vizuri.Saa mbili usiku leo nitapiga
simu nyumbani kwako nataka nikusikie
ukiwa Moshi.!!! Akasema kwa ukali Yule
mzee na kukata simu.Alfred akatoa
kitambaa na kujifuta jasho kisha akarejea
katika gari.Sura yake ilikuwa imebadilika
“ Fred nini kimetokea? Mbona
umebadilika hivyo? Akauliza Pauline
“ Pauline I’m sorry lakini jioni ya leo
natakiwa kurejea Moshi” akasema Fred
“ Unarejea Moshi? Kuna tatizo gani?
“ NInahitajika hospitali kuna
dharura”
“ Kwani huwezi ukawadanganya
kwamba uko mbali na huwezi kufika kwa
haraka? Akasema Pauline
“ Hapana Pauline.Lazima nirejee
Moshi leo” akasema Alfred “ C’mon Alfred please don’t leave us.I
need you here.” Akasema Pauline lakini
Alfred hakuweza kubadili msimamo wake
“ Nadhani sasa uvumilivu wangu
umefika mwisho.Ni wakati wa kumaliza
kila kitu .Siko tayari kuendelea kuvumilia
tena upuuzi wa namna hii.Siko tayari
kuendelea kuteseka namna hii” Akawaza
Alfred
Saa tatu za usiku Alfred akawasili
nyumbani kwake Moshi.Mkewe Grace
ndiye aliyemfungulia geti akamkaribisha
ndani .Tayari mtoto wao alikwisha lala
kitambo
“ Pole na safari darling” akasema
Grace
“ Nashukuru sana G.Habari za hapa?
Akauliza Fred
“ Habari za hapa nzuri sana.habari za
Arusha ?” akajibu Grace huku akimsaidia
mume wake kuvua viatu halafu akamvua
shati na kumuongoza hadi chumbani kwao
wakaingia bafuni wakaoaga halafu
wakapata chakula kisha wakapanda
kitandani
“ So you called him? Akauliza Alfred
wakiwa kitandani “ I’m sorry.sikuwa na namna
nyingine ya kufanya kwani leo ni siku
yako “akasema Grace
Alfred hakuonekana kutaka tena
maongezi akageuka upande wa pili kwa
dhumuni la kulala lakini Grace akamgeuza
na kumbusu.
“ Grace I’m sorry kwa leo hatuwezi
kufanya nimechoka sana’” akasema Fred
“ Pole sana Fred laknileo hii ni siku
yako na hatuwezi kuacha.kwa mwenzi
mzima nimekuwa ninaisubiria siku hii.
Tafadhali Fred ,japo kidogo tu” akasema
Grace
“ Grace siwezi kwa leo nimechoka
sana.May be next time” akasema Fred.
“ Fred please ! Ukiacha leo
nitakusubiri tenakwa mwezi mzimahadi
mwenzi ujao.Pleae darling !! akasisitiza
Grace lakini Fred hakuwa tayari.Grace
akakasirika sana na kumtazama Fred kwa
hasira
“ Whats wrong with you Fred ?!!
Akauliza Grace baada ya jitihada zake zote
zote za kumshawishi Alfred wafanye
mapenzi usiku ule kushindikana
“ Grace nimekwambia nimechoka
sana na kwa leo.Naomba unielewe”
akasema Afred .Grace akamtazama kwa hasira na huku akilengwa na machozi
akasema
“ Alfred nadhani ni wakati sasa wa
kuelezana ukweli.Ni kweli umechoka or
its because of her? Akauliza Grace.
“ tayari bomu limelipuka.She knows
everything ”akawaza Alfred .
“ Alfred answer me !!unadhani
sifahamu mambo unayoyafanya na
Pauline? Ninajua kila kitu.Ninajua kabisa
kwamba hukuwa umeitwa Serian bali
ulikwenda kula raha na
Pauline.Ninafahamu kila kitu
mnachokifanya nanimeumia sana .”
Akasema Grace kwa hasira.Fred hakujibu
kitu
“ kwa nini A lfred unanifayia hivi?
Kwa nini lakini unaniumiza kiasi hiki?
Akauliza Grace huku akilia.
“ Nilikuamini sana Fred na siku
tegemea kabisa kama siku moja ungeweza
kunifanyia kitu kama hiki.You are a
monster Fred.!! A monster !! akasema
Grace huku akimpiga Fred na mito ya
kulalia.Fred akamdaka mikono yake
“ Stop calling me a monster !!
akasema Fred kwa ukali
“ between me and you who is a
monster??? Akauliza David huku akitweta kwa hasira.Grace hakujibu kitu
akaendelea kulia.David akakaa kitandani
na kuinama akajishika kichwa akatafakari
na kusema
“ Grace kama ulivyosema awali
kwamba ni wakati wa kuelezana ukweli na
nitakueleza ukweli bila
kukuficha”akasema Alfred huku kifua
chake kikiwa kimeloa jasho
“ Ni kweli sikuwa nimekwenda
Serian kama nilivyokueleza.Nilikuwa n a
Pauline” akasema Alfred.Grace akainuka
na kuanza kumpiga Alfred makofi
“ How could you do this to me
Fred??!! Akauliza Grace huku akilia na
kuendelea kumpiga Fred makofi
“ Stop that Grace!! Akasema david na
kumsukuma Grace akaangukia kitandani
“ Ni kweli mimi na Pauline tuna
mahusiano and to be honest our
relationship is going deeper” akasema
Alfred
“ Please Alfred don’t hurt me please
”akasema Grace huku ameuweka mkono
wake kifuani sehemu uliko moyo na
machozi yakimtiririka
“ You wanted the truth and I’m
telling you the truth” akasema Fred na kumtazama Grace aliyekuwa amekaa
kitandani akilia
“ Grace mimi na wewe tumeishi
pamoja kwa miaka mingi sasa na katika
muda huo wote tumevumiliana na
hakukuwa na mgogoro wa aina yoyote ile
lakini leo hii naomba nikuweke wazi
kwamba siwezi tena kuendelea na aina hii
ya maisha tunayoishi.I can t do this
anymore Grace.” Akasema Fred na
kumstua Grace
“Unataka kusema nini i Fred?
Akauliza Grace
“ I’m sorry Grace but I have to leave
you”
Grace akastuka na kumtazama Fred
kamavile anatazama kitu cha kutisha
“ You are leaving me?? Grce akauliza
kwa ukali
“ yes .I’m leaving you”akajibu Fred
“ No you can’t do that.Huwezi
kuniacha kwa sababu ya Yule kahaba.No
Fred you can’t do that to me!!! Akalia
Grace.
“ Yes I’m leaving you for her .I’m
tired of this.I want to start a new life with
Pauline.Haya si maisha ninayoyahitaji na
ninevumilia sana hadi hapa nilipofika
lakini siwezi kuendelea zaidi ya hapa.Tafadhali naomba unielewe
Grace.Please let me go and find my
happiness.Furaha yangu ninaipata kwa
Pauline”akasema Fred
Ghafla Grace akainuka na kuanza
kutupatupa vitu mle chumbani kwa hasira
.Ikamlazimu Fred kufanya lazi ya ziada ya
kumdhibiti.
“ Unafanya nini Grace?!! Tafadhali
hebu tulia!! Akasema Fred na kumuweka
Grace kitandani.Grace alikuwa
anatetemeka kwa hasira
zisizomithilika.Aakavua ngo zote na
kubaki mtupu akaanza kugala gala pale
kitandani akilia.Alionekana kama
kuchanganyikiwa..
“Grace !! Grace !!..akaita Fred lakini
ghafla Graceakainukana kuzama Fred
kibao .Fred akamuinua na kumnasa vibao
viwili vikali
“ Unanipiga? Akauliza Grace akiwa
amefura kwa hasira
“ nakuuliza Fred unanipiga?!! Kw a
nini umenipiga? Akauliza Grace
“ Grace nimekupiga ili uachane na
mambo yako ya kitoto.Nataka tuzungume
kama watu wazima.Sijawahi kukupiga
hata siku moja lakini ukinilazimisha leo
hii nitakufunza adabu” akasema Fred. “ You want to kill me?!! Go ahead kill
me.!!..Akasema Grace ka hasira na kuanza
kulia ..Fred akamsogelea na kumshika
mabegani kisha kwa sauti ya upole
akasema
“Grace tafadhali naomba unisikilize.”
“ Fred you are killing me my
love…..Please don’t kill me !! akasema
Grace
“ Grace naomba unikilize..Me and
you we can talk about this,right? Akasema
Fred kwa sauti ya kubembeleza.
“ No Fred huna tena cha kuniambia
kwani kila kitu kiko wazi .She’s everything
to you now but I swear you can’t be with
her..”akasema Grace
“ Grace kwa nini unataka kuyafanya
mambo haya yawe magumu? akasema
Fred
“ Fred kitu gani umekikosa kwangu ?
baada ya miaka hii yote kw anini ubadilike
leo hii? Tumevumiliana kwa muda mrefu
sana iweje uniache leo hii? Iwont let that
happen!! Akasema Grace
“ Grace unafahamu kabisa ni kwa
miaka mingapi nimekuvumilia na hata
siku moja sijawahi kukutamkia
lolote.Nimefanya kila kitu ambacho
nimetakiwa kukifanya na sijawahi kulalamika hata siku moja.Unadhani ni
nani ambaye angekubali kufanya kama
nilivyofanya mimi? Nakuapia hakuna
anayeweza kufanya kitu kama hicho .
Maisha yenu ni mazuri tu na kila
mlichokuwa mnakitafuta mmekipata.Ni
wakati wangu na mimiwa kuitafuta furaha
ya maisha yangu.Tafadhali Grace
naombeni mnipe nafasi hii na mimi
niweze kufurahia maisha yangu na
mwanamke ninayempenda “akasema
Alfred
“ Fred nimesema hapana.!! Huwezi
kuniacha “akasema Grace kw a hasira.Fred
akainuka na kumtazama grace halafu
akasema
“ Grace I’m tired of lying to the world
that we’re married while we’re not! Hata
kama ukikataa mimi nitaondoka
tu.Nimekwisha fanya maamuzi na lolote
litakalotokea na litokee tu.kama utajiua ni
juu yako lakini mimi sihusiki na kitu
chochote !! akasema Fred.Grace akafuta
machozina kumtazama Fred
“ Fred unanilazimisha nikwambie
mambo mengine ambayo sikutaka
kukueleza lakini kwa hapa tulipofika
lazima nikueleze.”akasema Grace “Unataka kunieleza nini Grace?
Hakuna utakachonieleza kitakachobadili
msimamo wangu.”Akasema Fred huku uso
wake ukionyesha wasi wasi kidogo.
“ The moment you leave me..you will
die!! Akasema Grace
“ Are you going to kill me?!! Akauliza
Fred
“ Not me ! I won’t kill you because I
love you.” Akasema Grace
“ Who is going to kill me then? Your
daddy? Akauliza Alfred
“ No ! my daddy won’t kill you.Siku
ile ulipokubali kuvaa pete ya ndoa katika
kidole chako na kutamka yale maneno
kilikuwa ni kiapo chako na ambacho
ukikiuka lazima ufe.Alfred sikudanganyi
lakini ukilipuuza jambo hili sintakuwa na
namna nyingine ya kukusadia.You must
die and because I love you so much I will
die too.Siwezi kuisjhi bila wewe.Tafadhali
naomba usifanye hivyo Fred ili uniokoe
na mimi.Mtotowangu bado
mdogo”akasema Grace
“ Tafadhali usinitishe
Grace.Anyeamua siku ya kufa kwa mtu ni
Mungu peke yake na si mwanadamu au
mtu mwingine yeyote.Hilo ulilolisema
haliwezi kunirudisha nyuma hata kidogo”akasema Fred.Grace akamtazama
na kusema
“ Show me your hands” Fred
akamuonyesha mikono yake
“ Where is the ring?
“ Nimeivua.I don’t want to pretend
anymore ” Akasema Fred na Grace
akamtazama kwa macho makali kisha
akasema
“ Katika safari yako yakwendana
kurudi umenusurika ajali ama ulipatwa na
tatizo lolote baya ukiw a Arusha? Akauliza
Grace.Alfred akatafakari kidogo kisha
akajibu
“ Ndiyo.Tulivamiwa nyumani kwa
akina Pauline na majambazi i .How do you
know? Akashangaa Alfred
“ Fred you were supposed to die
.Pone pone yako ni kwamba hukuwa
umeirudisha pete ile kwangu ama sivyo
ungeuawa.Endapo ukithubutu kufanya
hivyo unavyotaka kufanya I swear
hautamaliza siku moja you must die”
akasema Grace.
“ Ouh my God !!..yawezekana ni kweli
hili analolisema Grace? Akawaza Fred
.Grace akamsogelea na kumshika bega.
“ Fred najua nimekustua
sana.Sikutaka kukueleza kuhusu jambo hili lakini umenilazimisha nikueleze..Fred
I love you so much na hata mimi sifurahii
maisha haya tunayoshi lakini nitafanya
nini? najua unahitaji sana uhuru najua
unahitaji sana kuishi maisha yenye uhuru
na mwanamke unayempenda na ndiyo
maana nimekuwa nijitahidi sana kufanya
kila niwezalo ili uweze kuwa na furaha
katika maisha yako .Tafadhali Fred
usifanye hivi.Utajiletea matatizo na sisi
sote tutakuwa matatizoni.tafadhaIi
nakuomba utulie na tuendelee kuishi
kama zamani.”akasema Grace.
“I need to talk to your father!!
Akasema Fred na kuchukua simu
akazitafuta namba za simu za baba yake
Grace akampigia
“ hallo Fred.Umekwisha wasili
Moshi?
“ Mzee kuna tatizo kubwa na
ninahitaji sana kukuona.kesho mimi na
Grace tutapanda ndege na kuja kukuona
mara moja” akasema Fred
“ hamha haja ya kupanda ndege
kunifuata kwani hata mimi ninaelewa
kuna tatizo na nimekwisha jiandaa kesho
nitakuja huko Moshi kuwaoneni.”
Akasema baba yake Grace “ sawa mzee” akajibu Fred na kukata
simu .Jasho liliendelea kumtiririka
mwilini.
“ dah sikujua kama mambo
yangekuwa namna hii.kwa nini lakini
niliamua kujiingiza katika maisha haya na
kujitia kitanzi mimi mwenyewe?
Nitajiokoaje na janga hili linalonikabili ?
Najuta ! najuta kumfahamu
Grace.”akawaza Fred
“ Ni kweli niliweka nadhiri ya kuishi
na Grace kwa maisha yangu yote hadi kifo
kitutenganishe.laiti kama ningefahamu
kama nadhiri ile ni kisu kitakacho nichinja
mimi mwenyewe,katu nisingekubali
kabisa kuyatamka maneno yale.”
Akaendelea kuwaza Fred.
“ Maneno aliyoniambia Grace yana
ukweli ndaniyake na kama nikiyapuuza ni
kweli ninaweza kupatwa na janga au hata
kupoteza maisha.Nikweli wakati
ninaelekea Arusha kulitokea ajali katika
gari la mbele yetu na hata tukiwa kule
Arusha nyumbani kwa akina Pauline
tulivamiwa na majambazi ambao kama si
kwa msaada wa polisi wangeweza kutuua
sote.Nikithubutu kumrudishia pete hii
Grace ninaweza kupatwa na janga kubwa
.lakini siwezi kukubali kumkosa Pauline hata iwe vipi..Kwa ajili yake niko tayari
kwa lolote.Ngoja kesho nitakapoonana na
huyu mzee nitajua kila kitu kuhusu hatma
ya maisha yangu..Nimechoshwa na maisha
haya na litakalotokea na litokee tu”
akawaza Fred.
Nyumba ya mzee Zakaria ilikuwa kimya
kama vile hakukuwa na watu.Sanya na
Pauline walikuwa sebuleni wakitazama
filamu wakati mtumishi wa ndani
akiendelea na shughuli za usafi wa
vyombo.
“ The house is too big for us.Watu
wote waliokuwa wakiichangamsha
nyumba hii hawapo.Baba ,David na hata
Yule shetani Vicky.”akawaza Pauline na
sura ya Alfred ikamjia
“ Ouh Alfred I miss you already.Kwa
nini lakini ukaondoka na kuniacha peke
yangu? Sasa ninaanza kuona adha ya
kuzama katika mapenzi na mume wa
mtu.Nimekaa na Fred kwa siku hizi chache
tayari nilikwisha mzoea na kuhisi kama
vile tayari ni mume wangu.Nitafanya nini
basi ili niweze kummiliki Fred awe wangu
peke yangu? Nitawezaje kumuondoa Fred
kwa mke wake? Akajiuliza auline na
kuinuka akaenda jikoni na kuchukua
chupa ya mvinyo akajimiminia katika glasi.Sanya akamtazama bila kusema
chochote alikuwa ameelekeza macho yake
luningani akitazama filamu
“ Mambo haya ya kuzama mapenzini
na mume wa mtu nilikuwa nayatazama
katika filamu na sikutegemea kama siku
moja na mimi yatanikuta.Sasa yamenikuta
na nitalazimika kuingia katika vita ya
kumgombania mwanaume kwani sina
ujanja tena lazima nipambane kumpata
Alfred.Hili si jambo zuri hata kidogo lakini
nitafanya nini na mimi Alfred nimekufa
nikaoza kwake na ndiye mwanaume
ambaye ninamuhitaji katika maisha
yangu? I must fight to get him.Hata kama
nitamuumiza mwanamke mwenzangu
lakini ninachokihitaji mimi ni kumpata
Fred tu.”akawaza Pauline huku akiendelea
kupata mvinyo taratibu.
“ Pauline ! akaita Sanya
“ Kuna jambo nataka kukuuliza na
ninaomba unieleze ukweli.”akasema
sanya
“ Uliza chochote sanya nitakujibu”
akasema Pauline
“ Ulinieleza kwamba uliwahi kuwa
katika mapenzi na David na akakutenda
mkaachana.Badouna hisia zozote juu yake? Bado una mpenda?akauliza
Sanya.Pauline akatabasamu na kusema
“ kwa nini umeuliza hivyo Sanya?
“ Nnahitaji tu kufahamu”
“ Ni kweli niliwahi kuzama katika
penzi zito na David na akaniumiza sana
alipotembea na rafiki yangu mkubwa
Tamia na ilikuwa ndiyo sababu ya mimi
kuondoka na kwenda Moshi ambako
nilikutana na Alfred ambaye kwa muda
mfupi alifanikiwa kuyatibu majeraha
yangu yote niliyoumizwa na
David.Kukujibu swali lako ni kwamba
David ni mtu muhimu katika maisha
yangu lakini kwa sasa sina hisia naye
zozote za kimapenzi.Kwa sasa David ni
kama kaka yangu .Yaliyopita yamekwisha
pita”akasema Pauline
“ Nashukuru Pauline kwa kuwa
muwazi kwangu.Huyo rafiki yako ambaye
David alikusaliti naye yukoje ? Ni
mrembo?akauliza tena Sanya
“ Anaitwa Tamia.Ni msichana
mrembo sana lakini hawezi kukufikia
wewe hata robo.” Akasema Pauline na
kumfanya Sanya atabasamu.
“ Tatizo la Tamia “ Pauline
akaendelea “ ni msichana ambaye anatamani kila
mwanaume mzuri anayepita mbele yake
na hatulii na mwanaume
mmoja.Nilimuonya David kuhusu kuwa
mbali na Tamia hakunisikia lakini baadae
akakubalina na kilie
nilichomwambia.Alimfumania Tamia
akiwa na mwanaume ndani wakifanya
mapenzi.”
“ kweli ?!!..Sanya akashangaa
“ Kweli kabisa.Alimfumania na
mwanaume chumbani”
“ Dah ! Ikawaje baada ya hapo?
Akauliza sanya
“ Kilichofuata wakaachana na kila
mmoja akaendelea na maisha yake”
Sanya akavuta pumzi ndefu na
kuuliza tena
“ kwa hiyo unataka kuniambia David
kwa sasa hayuko katika mahusiano na
mwanamke mwingine?
“ Sina hakika kama ana mwanamke
mwingine.Nina hakika David yuko huru”
akasema Pauline na kumfanya Sanya
atabasamu
“ Pauline uhhmm…”Sanya akataka
kusema kitu lakini akasita
“ Unataka kusema nini Sanya?
Usiogope” “ Uhhmm..!! utajisiaje kama mimi na
David tukawa na mahusiano?
Uso wa Pauline ukatengeneza tabasamu
kubwa
“ Hilo ni jambo ambalo nimekuwa
nikiliota usiku na mchana
litokee.Nitafurahi sana kama likitokea”
Akasema Pauline
“ Pauline nimefurahi kusikia hivyo
na ninaomba nikuweke wazi kwamba
ninampenda sana David.Ninampenda kwa
moyo wangu wote.Nilipomshuhudia
akifanya kitendo kile na mama yako
mdogo nilikasirika sana na nikatoa
maneno makali juu yake lakini ilikuwa ni
hasira tu.Toka ndani ya moyo wangu
ninampenda sana David na ninaamini
ndiye hasa mwanaumeambaye Mungu
amenipangia niwe naye.Ninaamini
kwamba safari yangu ya kuja Tanzania
ilikuwa maalum kwa ajili ya
kunikutanisha na mwanaume wa maisha
yangu ambaye ninaamini ni
David.”akasema Sanya.pauline akainuka
alipokuwa amekaa na kwenda
kumkumbatia Sanya kwa furaha
“ Ouh Sanya !! pamoja na matatizo
yote niliyonayo umeufanya uso wangu
ujae tabasamu tena.Nimefurahi sana.Toka siku ya kwanza nilipokuona nilijua tu
wewe ndiye mwanamke ambaye ungemfaa
sana David.Baada ya kusikia kwamba
amekorofishana na Tamia niliamini huu ni
mpango wa Mungu ili mkutane.Sikujua
kumbe hata wewe ulikuwa umetokea
kumpenda David “akasema Pauline kwa
furaha kubwa.
“ Sanya mimi nitafanya kila
linalowezekana hadi nihakikishe wewe na
David mnakuwa pamoja .hata kama
ukishindwa kuonana na wazazi wako basi
utafanikiwa kumpata mwanaume
unayempenda” akasema Pauline.
*******************
Saa kumi na mbili za asubuhi
iliwakuta Pauline na Sanya katika geti la
kuingilia hospitali kuu ya mkoa wa
Arusha.Kisha shuka garini wakaelekea
moja kwa moja katika wodi ya uangalizi
maalum ambako walipewa taarifa
kwamba tayari David alikwisha ondolewa
huko na kupelekwa katika wadi ya
kawaida baada ya hali yake kuwa nzuri.
Hii ilikuwa ni taarifa nzuri sana kwa
Pauline na Sanya ambao waliongozana na muuguzi hadi katika chumba
kilichoandikwa Private 12 alimolazwa
David.
David alikuwa amelala, muuguzi
Yule akamuamsha.
“ David ndugu zako wamekuja
kukusalimia”akasema muuguzi.David
akafumbua macho na kukutana na sura
zenye tabasamu za Pauline na Sanya.Kwa
furaha Pauline akamfuata pale kitandani
akamkumbatia.
“ Ouh David !!..akasema Pauline
“ Pole sana David.Unaendeleje?
akauliza Pauline.
“ Ninaendelea vizuri sana
.Namshukuru Mungu amenirejeshea uhai
tena.Nilikwisha chungulia kifo.” Akasema
David .Sanya akamsogelea karibu
“ Pole sana David.” “ akasema Sanya
huku machozi yakimtoka
“ Usilie Sanya.Mimi sijambo
.Ninawashukuru kwa maombi yenu na
Mungu amenirejeshea tean uhai wangu.”
akasema David kwa sauti ndogo. .
“ David ninashindwa kujizuia kulia
kutokana na namna tulivyoogopa baada ya
tukio lile.Ulipigwa risasi tano na kuwa hai
na kuweza kuongea nasi mida hii ni kwa uweza wa Mungu tu.Tulimlilia sana na
amesikia kilio chetu” akasema sanya
“ Msiogope tena.Madaktari
wamenihakiksihia kwamba siko tena
katka hatari na ninaendelea vizuri
sana.Niambieni mzee Zakaria yuko wapi?
“ mzee yupo na anaendelea vizuri ”
akajibu Pauline
“ Nashukuru kusikia hivyo.Nilikuwa
nawaza sana kama mzee ni mzima.Wale
jamaa walikuwa na lengo la
kumuua.Ahsante Mungu kama lengo lao
halikufanikiwa.Dr Alfred naye yuko wapi?
“ Alfred ameondoka jana kuelekea
Moshi .Aliitwa kwa dharura “ akajibu
Pauline.
“ Hakuna mtu mwingine yeyote
aliyedhurika katika shambulio lile?
Akauliza David
“ Hakuna aliyedhurika .David you
saved us.Bila wewe sote
tungeamia”akasema Pauline na
kushindwa kujizuia kuangusha machozi.
“ Basi usilie Pauline.Tumshukuru
Mungu kwa kutukinga na jambo lile baya.”
Akasema David kisha akina Pauline
wakamtayarishia uji . “ Madam Vicky naye yuko wapi?
Akauliza david .Pauline na Sanya
wakaangaliana.
“ tafadhalini niambieni Vicky yuko
wapi?akauliza tena David
“ Vicky anashikiliwa na polisi kwa
hivi sasa akihusishwa na tukio lile”
akasema Pauline
“ Ouh Ahsante Mungu.Nilikuwa na
wasi wasi labda ametoroka”akasema
David
“ Mwanamke yule ni katili sana”
akasema David
“ David tayari tunafahamu kila siku
kilichotokea.Kamanda wa polisi
amekwisha tueleza kila kitu.”akasema
Pauline
“ Amewaeleza kila kitu?
“ Ndiyo David.Kila kitu tunakifahamu
.David kuna mambo mengi sana ya
kuongea ukishapona lakini kwa sasa
naomba niseme samahani sana kwa
kupuuzia wito pale uliponiambia kwamba
kuna kitu cha muhimu unataka
kuniambia. Sikujua kama ulitaka
kunieleza jambo kama hili“ akasema
Pauline.
“ Usijali Pauline.Nilitaka
kukufahamisha kuhusu jambo hili kabla halijatokea lakini hayo yamekwisha pita
sasa hivi.Tutaongea zaidi nikitoka humu ”
akasema David.
*****************
Saa tano za asubuhi Helkopta ikatua
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro.Mzee Damian Mwamba
mmoja wa mabilionea wakubwa afrika
mashariki akashuka .Alikuwa amevaa koti
refu jeusi lililoendana na kofia nyeusi ya
mduara aliyoivaa kichwani.Mkononi
alikuwa na fimbo ndefu yenye nakshi za
dhahabu.
Alitembea taratibu akiwa
ameambatana na walinzi wawili
waliovalia suti nzuri nyeusi .Nje ya uwanja
wa kimataifa wa Kilimanjaro gari aina ya
range rover E vogue yenye rangi nyeusi
ilikwisha andaliwa.Mzee Damian mwamba
akafunguliwa mlango na kuingia kisha
gari lile la kifahari likaondoka na safari ya
kuelekea mjini Moshi ikaanza.
Dakika kama ishirini baadae
akawasili mjini Moshi na kuelekea moja
kwa moja nyumbani kwa Alfred. “ What happened my queen? mzee
Damian akamuuliza mwanae Grace mara
tu baada ya kufika kwao na kumuona
akiwa amevimba macho hali iliyoonyesha
wazi kwamba alikuwa amelia sana usiku .
“ Usijali baba ni mambo ya
kawaida.Karibu sana”akasema Grace
“ Grace wewe ni roho yangu na
hatakiwi kabisa mtu yeyote Yule kukutoa
chozi” akasema mzee Damian
“ Tell me did Alfred hurt you?
Akauliza Damian.Grace hakujibu kitu
akabaki anatoa machozi na mara akatokea
Alfred akitokea chumbani.Mzee Damian
akamtazama kwa hasira na kumnyoshea
fimbo
“ I warned you,my daughter is my
souls and she shouldn’t get hurt in
anyway..Why did you hurt her?? Akauliza
kwa ukali huku uso wake ukionyesha
hasira za wazi .David hakujibu kitu
akabaki anamtazama.
“Nimekuuliza Alfred kwa nini
umemliza mwanangu? Akauliza mzee
damian
“ mzee nadhani ungekaa kwanza ili
tuweze kuongea kuhusu mambo haya ”
Akasema Alfred.Mzee Damiana akaendelea kumtazama kwa hasira na
kusema
“ Kabla ya kukaa nnarudia tena
kukuonya kwamba hii iwe ni mara ya
mwisho kwa mwanangu kudondosha
chozi.!! Akasema kwa ukali mzee damian
na kukaa
“ Grace please bring me my whisky
please !! akasema mzee mwamba na Grace
akamletea chupa kubwa ya pombe
akammiminia katika glasi akanywa halafu
akasema
“ habari za hapa?
“ Shikamoo mzee” akasema Alfred
“Marahaba.Nimewaulizeni habari za
hapa? Akasema mzee Mwamba.Fred na
Grace wakatazamana
“ Mbona hamnijibu? Nielezeni mna
tatizo gani? Nimevunja ratiba zangu zote
kwa ajili ya kuja kuwasiliza kwa hiyo
naombeni mnisaidie kuokoa muda kwani
kila dakika moja inayopotea ninapoteza
millions of money…lakini kabla
hamjanieleza chochote nataka niseme
wazi kwamba Alfred sijapendezwa kabisa
na kile ulichokifanya na ninakuonya
kwamba iwe ni mara ya mwisho .Tabia hii
imeanza lini ya kumdanganya mkeo
kwamba unakwenda Arusha kikazi wakati unakwenda kutumbua raha na mwanamke
mwingine? Honestly nimechukizwa sana
sana na jambo hili na ninaomba iwe ni
maraya mwisho kutokea.Sitaki tena
kusikia kuhusu jambo hilo.Sitaki tena
Grace adondoshe chozi.Unajua chozi la
mwanangu lina gharama gani? Do you
know? Akauliza mzee mwamba.Alfred
hakujibu kitu
“ You don’t even know.Sasa kwa nini
unamliza mwanangu wakati thamani ya
chozi lake huijui? Nasema iwe ni mara ya
kwanza na ya mwisho.Tumeelewana
Alfred? akauliza mzee Mwamba lakini
Fred hakujibu kitu.Alikasirishwa na
maneno yale ya mzee Damian
“ Tumeelewana Fred? Akauliza tena
“ ndiyo mzee” akajibu Fred
“Good.sasa nielezeni matatizo yenu
kabla ya mimi sijaongea chochote”
akasema mzee mwamba
Alfred na Grace wkatazamana.
“ Mwambie sasa wewe si ndiye
uliyemuita? Akasema Grace
“ Mwambie wewe ,” Alfred na Grace
wakaaza kutupiana mpira.mzee mwamba
akacheka halafua akajimiminia mvinyo
katika glasi akasema “ Kama mmeshindwa kunieleza basi
ngoja niseme ya kwangu.”akasema mzee
Mwamba
“ Baba hatujashindwa kukueleza.Ni
kweli mimi na Alfred tuna tatizo kubwa na
ndiyo maana amekuita hapa”
“Nielezeni basi nitatizo gani hilo?
Akasema damian na kumuita mmoja wa
walinzi wake aliyekuwa amesimama
mlangoni akamwambia ampate pakiti la
sigara akatoa sigara kubwa akaiwasha na
kuanza kuvuta
TAMATI
0 comments:
Post a Comment