Simulizi : The Football (2)
Sehemu Ya Nne (4)
kazi moja” akasema Meshack
Jumbo.Maneno yale yalionekana
kumuingia kamanda Anangisye
lakini bado akawa na mashaka
“Naona unashindwa kufanya
maamuzi.Ngoja nimpigie simu rais
nimueleze hali halisi halafu yeye
atatoa maelekezo.Hili jambo ni dogo sana na halipaswi kumfikia
rais ila kwa kuwa huniamini ngoja
nimjulishe ” akasema Meshack na
kuchukua simu yake akaanza
kuzitafuta namba za rais
“Usipige simu hiyo tafadhali
mzee.Nitaonekana mtu
nisiyefahamu majukumu yangu”
akasema Anangisye
“Nini maamuzi yako basi?
Nahitaji kujua kwani muda
unakwendea mbio”
“Mtatumia muda gani
kumfanyia mahojiano?
“Siwezi kukisia muda kwani
inategemea na ugumu wa mtu ila
tunajitahidi sana isichukue muda
mrefu” “Sawa ninakukabidhi
mtuhumiwa uondoke naye lakini
naomba apewe uangalizi wa hali ya
juu sana kwani tuhuma
zinazomkabili ni kubwa.Hata hivyo
mtaongozana na timu ya vijana
wangu ili punde tu mtakapomaliza
mahojiano wamchukue
mtuhumiwa na kumrejesha
kituoni mara moja”
“Hapana kamanda Anangisye
hatuwezi kuongozana na vijana
wako.Mahala tunakompeleka
Mathew kwa maojiano ni mahala
pa siri na hapaswi mtu asiyehusika
kupafahamu.Usihofu chochote
baada tu ya kumaliza upande wetu
tutamrejesha sisi wenyewe na
kumkabidhi kwenu.Mimi ndiye ninayebeba dhamana yote hivyo
nawaomba muendele kutusibiri
hapa hapa ili tukimaliza mahojiano
basi mtuhumiwa aletwe hapa moja
kwa moja”
Kamanda Anangisye
akakubali Meshack Jumbo
aondoke na Mathew.Akaamuru
afunguliwe pingu za miguuni ila
mikono ikabaki imefungwa na
Meshack akapewa funguo ya
kufungulia pingu
“Ahsante sana
kamanda.Tunaonana hapo baadae”
akasema Meshack baada ya
kukabidhiwa Mathew
Meshack ,Mathew na Austin
wakaingia katika gari la
Mathew,Amarachi na Camilla wakaingia katika lile gari
walilokuja nalo wakaondoka
wakiwaacha askari wakishangaa
wasielewe nini kimetokea
Meshack ,Mathew na Austin
wakaingia katika gari la
Mathew,Amarachi na Camilla wakaingia katika lile gari
walilokuja nalo wakaondoka
wakiwaacha askari wakishangaa
wasielewe nini kimetokea
“Ahsante sana mzee” akasema
Mathew
“You don’t have to thank
me.Ni wajibu wangu kufanya hivi
kwani mimi ndiye niliyekufanya
ukakubali kufanya kazi hii hivyo
napaswa kuhakikisha unakuwa
salama”
“Pole sana Mathew” akasema
Austin
“Ahsante Austin.Umepataje
taarifa zangu? Umekutana wapi na
mzee Jumbo? Akauliza Mathew
“Mimi ndiye niliyempigia simu
na kumtaka anisaidie tuweze kukuondoa katika mikono ya
polisi” akasema Meshack
“Nina deni kubwa kwako mzee
jambo.Nilikuwa nimekwama na
sikujua ningewezaje kutoka katika
mikono ya polisi.Tuhuma ile ni
nzito na huu ungekuwa ni mwisho
wangu.Mzee nakuahidi sintofumba
jicho hadi nihakikishe wale wote
waliofanya tukio lile la mauaji ya
Dr Robert wanapatikana”
“Tutayazungumza haya
Mathew lakini kwa sasa nataka
kujua wapi tunaelekea? Tunahitaji
sehemu salama ambako Mathew
atakaa kwa sasa” akasema
Meshack Jumbo
“Tunaendelea nyumbani
kwangu.Usalama pale ni wa uhakika halafu hakuna anayeweza
kuhisi kama Mathew yuko pale”
akasema Austin.Meshack Jumbo
akachukua simu akampigia dereva
wake akamjulisha kwamba
atachelewa kidogo na kumtaka
aingie hotelini apate kinywaji na
atakapomaliza mambo yake
atamjulisha.
Walifika nyumbani kwa
Austin wakakaribishwa ndani.
“Vijana ahsanteni sana kwa
kulifanikisha zoezi la kumuokoa
Mathew toka mikono ya polisi na
tumefanikiwa kumpata bila
kumwaga damu.Hata hivyo
nitawaacha kwa muda kuna
mambo ambayo bado nahitaji
kuyaweka sawa.Nitarejea hapo baadae kidogo.Austin I need your
car.Nahitaji kurejea tena kule
hotelini liliko gari langu.Natakiwa
kurejea tena ikulu usiku huu kuna
suala muhimu la kukamilisha”
akasema Meshack Jumbo na sura
za Mathew na Austin zikaonyesha
wasi wasi
“Msihofu I’ll be fine.Kamanda
Anangisye na askari wake bado
wako nyumbani kwa Mathew
wanatusubiri kwa hiyo nataka
kuitumia fursa hii kukamilisha
baadhi ya mambo muhimu kabla
suala hili halijafika ngazi za
juu.Nitakapomaliza nitarejea na
tutaungana sote kuhakikisha
jambo hili linafika mwisho”
akasema Meshack Jumbo na Austin akamtaka Amarachi ampeleke
Meshack Jumbo hotelini alikoacha
gari lake.
“Sasa uko huru Mathew.Pole
sana”akasema Austin baadaya
Meshack kuondoka
“Ahsante Austin.Sikutegemea
kabisa kukutana nawe katika
mazingira haya”
“Kila kitu ni kwa maongozi ya
Mungu.Hata mimi sikutegmea
kabisa kama ningekutana nawe
kaka hadi pale mzee Meshack
aliponipigia simu na kunijulisha
kwamba uko katika matatizo na
hivyo tunahitaji kukusaidia
kukutoa katika mikono ya
polisi.Nilishangaa kwani niliamini
uko Paris na mke wako sikujua kama uko hapa Dar es salaa”
akasema Austin
“Nimekwisha rejea Tanzania
na ninaendelea na shughuli zangu
za biashara.Kulitokea matatizo
katika ndoa yangu na Peniela
tukaachana.Vipi wewe maisha
yako yanakwendaje?
”Namshukuru Mungu mambo
yangu yanakwenda vyema na kwa
sasa tumefungua kiwanda kingine
hapa Tanzania cha kutengeneza
mvinyo.Kwa ujumla kila kitu
kinakwenda vyema”
“Nafurahi kusikia hivyo”
akasema Mathew.Austin akatoka
na kurejea na chupa kubwa ya
mvinyo akawamiminia Mathew na Camilla katika glasi na
kuwakaribisha
“Hakuna majeraha yoyote
mliyoyapata katika rabsha ile?
Akauliza Austin
“Hapana Austin.Hakukuwa na
vurugu yoyote ile, kila kitu
kilifanyika kwa amani.Tulitii kila
walilotuambia kwani tusingeweza
kupambana na askari wale wengi
wenye silaha za moto.By the way
huyu anaitwa Camilla snow ni
rafiki yangu anatokea Marekani na
yuko hapa nchini kwa ajili ya
kusaidiana nami katika kazi
ninayoifanya ya
uchunguzi.Samahani kwa
kutokutambulisha mapema” akasema Mathew na kumgeukia
Camilla
“Camilla huyu anaitwa Austin
January ni mmoja wa marafiki
zangu ambaye tumewahi wote
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi na sasa kila mmoja
anafanya shughuli zake binafsi.”
Austin na Camilla
wakasalimiana
“Mathew nadhani ni wakati
sasa wa kufahamu ni kitu gani
kinachoendelea .Unachunguza
jambo gani hadi ukajikuta katika
dhahama hii kubwa? Akauliza
Austin.Mathew akavuta pumzi
ndefu na kutafakari kwa sekunde
kadhaa akasema “Sikuwa nimetarajia kama
ningeweza kurejea kufanya
shughuli hizi za uchunguzi tena
kwani tayari nimekwisha jiwekeza
vya kutosha katika biashara.Lakini
alinifuata mzee Meshack na
kuniambia kwamba rais anahitaji
kuniona.Mzee Meshack tuna
mawasiliano mazuri kwani
ninamsaidia kupata mashine kwa
ajili ya kiwanda chake cha
kutengeneza bidhaa za maziwa
anachotaka
kukifungua.Nilikwenda kuonana
na rais kama alivyonitaka na
akanieleza alichoniitia.Alinitaka
nimsaidie kuchunguza chanzo cha
baba yake kuuawa na nani
waliomuua.Kifo cha baba yake kilitokea yapata miaka kumi
iliyopita na mpaka sasa hakuna
taarifa yoyote iliyowahi kutolewa
kuhusiana na mauji yale wala
wauaji kupatikana.Limekuwa ni
kama fumbo gumu.Sikutaka
kuifanya hiyo kazi lakini mzee
Jumbo akanishawishi na kuniomba
sana nikubali kuifanya hivyo
nikakubali.Nilianza kwanza kwa
kuchunguza ajali ya ndege
iliyomuua rais Anorld Mubara
kwani nilihisi kuna muunganiko
kati ya kifo cha Kanali Matope na
ile ajali.Hapo ndipo mambo
yalipoanza” akanyamaza akanywa
mvinyo kidogo na kuendelea
“Niligundua kwamba mpaka
leo hakuna taarifa ya chanzo cha kuanguka kwa ile ndege ya rais
kwani kisanduku ambacho
huhifadhi taarifa zote za
mwenendo wa ndege hakikuwahi
kupatikana.Hii ilinipa mshangao
sana kuhusiana na kutoonekana
kwa kisanduku hicho cheusi
kwasababu mahala ndege
ilipoangukia si sehemu ambayo
kisanduku hakiwezi
kupotea.Ndege ya Rais ilipata ajali
wakati akirejea kutokea nchini
Misri katika kikao cha wakuu wa
nchi zinazopitiwa na mto
Nile.Niligundua kwamba wakati
wakirudi kutokea Misri ndani ya
ndege hiyo kulikuwa na watu nane
walioomba lifti baada ya
kuchelewa ndege yao.Watu hao walikuwa waandishi wa habari
wakitokea Marekani wakielekea
Tanzania kufanya vipindi katika
moja wapo ya mbuga zilizopo hapa
nchini.Baada ya ajali kutokea na
kutangazwa kwamba watu wote
waliokuwemo ndegeni walikufa
miili ya watu hao
haikupatikana.Hii ilizidi
kuniwashia taa nyekundu kwamba
hapa kuna jambo kubwa”
akanyamaza akanywa kinywaji
tena na kuendelea
“Niligundua pia kwamba mtu
aliyewaombea lifti waandishi hao
wa habari Fakrim Alnasor
alihamishiwa nchini Marekani siku
chache baada ya ajali ile ya ndege
kutokea.Katika kumfuatilia mtu huyo nikagundua kwamba alikuwa
na mawasiliano na mtu mmoja
anaitwa Nathan ambaye ni
mchumba wa rais Dr
Vivian.Niliomba msaada kwa rafiki
zangu waliokuwa nchini Marekani
wa kumfuatilia huyo jamaa na mtu
aliyeifanya hiyo kazi ni huyu
Camilla.Fakrim aliuawa wakati
akiingia nyumbani
kwake.Iligundulika kwamba
Fakrim alikuwa ni jasusi wa
CIA.Baada ya kugundua kwamba
Nathan alikuwa na mawasiliano na
huyo mtu ilitulazimu kutumia
ujanja na kumleta Nathan hapa
nchini bila rais kufahamu.Kwa
wakati huo rais na huyo mchumba
wake walikuwa katika mgogoro mkubwa na hata ndoa yao
waliyokuwa wanatarajia kuifunga
ilikuwa imesitishwa.Nathan alikuja
Tanzania lakini wakati
nikimfanyia uchunguzi aliuawa na
mdogo wake rais anaitwa
Theresa.” Akanyamaza kwa
sekunde kadhaa na kuendelea
“Nilitaka kifo cha Nathan kiwe
siri lakini wakati tukielekea
kuuficha mwili huo tukavamiwa na
watu ambao wanatumia sare na
vifaa vya jeshi la polisi na
kutushambulia nikaomba msaada
toka kwa rais na wale wavamizi
wakatoweka.Usiku huo huo
nyumba ya mzee Jumbo ikavamiwa
na kuchomwa moto na wale wale
jamaa na ndipo nilipogundua kwamba walikuwa wanaifuatilia
saa ya Nathan ambayo baadae
nilimkabidhi rais na iko ikulu hadi
sasa.Tuligundua kwamba Nathan
alikuwa na mawasiliano na George
Mzabwa aliyekuwa mkurugenzi wa
idara ya usalama wa taifa aliyejiua
kwa kujipiga risasi.Tulihitaji
kumchunguza George na
tukampata mke wake ambaye
alitupeleka katika nyumba yao
ambayo George huhifadhi nyaraka
zake za siri katika
kasiki.Tulipolifungua kasiki
tukagunuda kuwepo kwa risiti za
benki.Risiti hizo zilionyesha
kwamba George alitoa kiasi
kikubwa cha fedha katika benki ya
Escom tawi la Tanzania na kuziweka katika akaunti tatu
tofauti zilizopo katika hiyo benki
ya Escom ambazo tuligundua ni za
kampuni ya kuchonga madini ya
vito ambayo mke wake Herieth ni
mkurugenzi.Tulimpata Herieth
tukamuhoji na akatuelekeza kwa
mkuu wake Ranbir Kumar ambaye
angeweza kutupa majibu ya
maswali yetu.Tulipomfuata Ranbir
yeye na Herieth wakakimbia kwa
gari na wakati tukiwafukuzia
wakauawa.Kesho yake tukaitwa
ikulu na rais akazuia tusiendelee
tena na uchunguzi tuliokuwa
tunaufanya.Kwa kuwa ni yeye
aliyekuwa ametupa kazi hii
ililazimu kutii wito wake na
nikaazimia kurejea tena katika shughuli zangu za biashara lakini
baadae akanipigia simu Theresa
akaniambia kwamba kuna
mwanadada yuko pale ikulu ni
mgeni na ana wasiwasi
naye.Ikatulazimu kumfanyia
uchunguzi huyo mwanadada na
kugundua kwamba taarifa zote
alizotoa hazikuwa za kweli.Katika
maelezo yake alidai kwamba yeye
ni mtoto wa nje wa rais Anord
Mubara jambo ambalo si kweli
kwani hawana mahusiano
yoyote.Tuligundua hata elimu
anayodai kuwa nayo si kweli
kwani tulifuatilia katika vyuo
anavyodai kusoma lakini
hakuwahi kusoma
huko.Tulipomfuatilia nyumbani kwake tukagundua kwamba
alikuwa na mawasiliano na waziri
wa mambo ya nje wa nchi Dr
Robert Mwainamela na balozi wa
Marekani hapa nchini.Tulifanya
jitihada hadi tukafanikiwa
kumpata Dr Robert na kumfanyia
mahojiano na ndipo tulipogundua
kuwepo kwa mpango wa kumuua
waziri wa mambo ya nje wa
Marekani Helmet Brian mara tu
atakapotua katika uwanja wa
ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere.Mpango huu umesukwa
na serikali ya Marekani
wakishirikiana na watu wao wa
hapa Tanzania.Marekani wana
mtandao mkubwa hapa Tanzania” “Hebu subiri kidogo
Mathew.Marekani wanataka
kumuua waziri wao wa mambo ya
nje ndani katika ardhi ya Tanzania
kwa nini? Akauliza Austin
“Kuna msuguano unaoendelea
hivi sasa duniani kati ya Korea
kaskazini na Marekani na
kilichozidisha msuguano huo ni
baada ya Tanzania kutangaza
kuanzisha mashirikiano ya
kibiasharana na Korea Kaskazini
na kuiuzia madini ya Urani kitu
ambacho Marekani hawakiafiki
kwa hiyo wamekuja na mpango
huo wa kumuua waziri wao wa
mambo ya nje hapa Tanzania na
kudai kwamba mauaji hayo
yamefanywa na watu waliotumwa na Korea Kaskazini na kwa njia
hiyo watapata sababu ya
kuishambulia Korea kaskazini kwa
kigezo cha kulipiza kisasi.Baada ya
kugundua mpango huo mimi na
wenzangu tukaandaa mpango wa
kuzima shambulio hilo na
kumuokoa waziri
Helmet.Ulichosikia kimetokea
usiku huu pale uwanja wa Julius
Nyerere ni mimi na wenzangu
tunahusika nalo na tukafanikiwa
kumuokoa waziri
Helmet.Tulimchukua Helmet hadi
nyumbani kwangu kisha nikaenda
kuonana na rais nikamueleza kila
kitu kuhusiana na kilichotokea
nikamkabidhi kwake Helmet
aweze kumuwekea ulinzi kwani naamini Marekani watatumia kila
njia kumuua.Nilipotoka hospitali
kuonana na rais nikapigiwa simu
na mmoja wa vijana wangu
niliowaacha nyumbani wakimlinda
Dr Robert kwamba wamevamiwa
na watu wenye silaha na vijana
wawili wameuawa na watu hao
wameingia ndani.Nilifika mara
moja nikakuta nyumba
imezingirwa na askari polisi
wakaniweka chini ya ulinzi kwa
mauaji ya Dr Robert.Wale watu
waliovamia nyumbani kwangu
walimuua Dr Robert .Hiyo ndiyo
hali halisi hadi mlipokuja kunitoa
katia mikono ya polisi” akasema
Mathew.Austin akachukua glasi yake ya kinywaji akagugumia
mvinyo wote
“Pole sana Austin.Ni masahibu
makubwa yaliyokupata .Sikujua
kama kuna mambo makubwa
namna hii yanaendelea nchini
kwetu.”
“Ni mambo makubwa Austin
ambayo ukisimuliwa huwezi
kuamini.Marekani wametengeneza
mtandao mkubwa hapa nchini
wanaoutumia kwa shughuli
zao.Kitu ambacho tayari nina
uhakika nacho ni kwanza
Marekani walishiriki katika
kuiangusha ndege ya rais Anorld
na kumuua kwani kwa mujibu wa
taarifa ya daktari aliyefanya
uchunguzi miili ya marehemu ni kulikuwa na matundu ya risasi
katika baadhi ya miili ya
marehemu na hii inaonyesha
kwamba kulikuwa na shambulio
kabla ya ndege
kuanguka.Hatujafahamu bado
sababu ya wao kufanya hivyo ila
tutafahamu kwa kuwa bado
tunaendelea kuchunguza.Pili
shirika la ujasusi la Marekani
wamekuwa wakimfuatilia rais Dr
Vivian kwa muda mrefu toka
angali anasoma chuo kikuu nchini
humo.Walimpandikiza Nathan
ambaye alianzisha mahusiano ya
kimapenzi lakini lengo lake
lilikuwa ni kumchunguza.Mpaka
sasa bado hatujafahamu ni kitu
gani hasa ambacho Marekani wanakichunguza kwa Dr
Vivian.Inaonekana kuna jambo
ambalo wanalichunguza kwa
miaka hii yote bila
kuchoka.Tunapaswa pia kufahamu
kama kuna siri yoyote anayo Dr
Vivian anayo ambayo inawafanya
Marekani wamfuatilie kwa muda
huu mrefu.Hayo ni mambo mawili
ambayo lazima tuyatafutie majibu
yake ila kwa sasa tuna jambo
ambalo tunapaswa kulifanya kwa
haraka nalo ni kuwapata
waliomuua Dr Robert kwani ni
wazi wamefanya hivyo kwa sababu
maalum.Kuna jambo walikuwa
wanalificha lisijulikane.Watu hawa
wako makini sana na kibaya zaidi
wanafahamu kila ninachokifanya.Walifahamu kuwa
sipo nyumbani na Dr Robert yuko
pale kwangu na wakavamia
wakamuua na muda huo huo
askari wakapewa taarifa na mimi
kuangushiwa mzigo wote wa
mauaji.Naamini hiki ni kitu
kilichopangwa na ndiyo maana
nikakueleza awali kwamba safari
hii nimeingia katika anga za watu
wenye nguvu.Mtandao wa hawa
jamaa ni mrefu na wanaweza
wakafanya jambo lolote kwa
wakati wowote wautakao na ndiyo
maana wamefahamu kuhusu Dr
Robert na wakamuua” Mathew
akanyamaza baada ya simu yake
kuita.Akastuka sana “Dah ! Nimesahau hadi kuzima
simu.Hii ni hatari kwani watu
hawa wanaweza wakanitafuta kwa
kutumia mawimbi ya simu na
wakafahamu niko mahala gani”
akasema na kuitoa simu yake
mfukoni na kustuka alipoziona
namba zilizompigia.Ni namba
alizokuwa anazifahamu
“Peniela!! Akasema Mathew
kwa mshangao
“Hizi ni namba zake za simu
ambazo hutumia akiwa
Tanzania.Inawezekanaje atumie
namba hizi wakati yuko Paris
Ufaransa? Au kuna mtu mwingine
ambaye anazitumia badala yake?
Akajiuliza Mathew na kuamua
kuipokea ile simu. “Hallow ” akasema
“Mathew habari yako”ikasema
sauti ya upande wa pili ambayo
Mathew aliitambua ni ya Peniela
“Peniela?! Akauliza kwa
mshangao
“Ina maana huifahamu hii
sauti ni ya nani? Akauliza Peniela
“Ninaifahamu ila nimestuka
kwa kuona unatumia hizi namba
ambazo huzitumia ukiwa Tanzania
wakati wewe uko Paris Ufaransa”
“Niko Tanzania Mathew.”
“Uko Tanzania? Umekuja
muda gani wakati mara ya mwisho
nilizungumza nawe ukiwa Paris
Ufaransa?
“Nimepata dharura na
kuamua kuja mara moja Tanzania.Tutazungumza baadae
kwa sasa ninaondoka hapa
Bandarini Dar es salaam hivyo
nakuomba tukutane nyumbani
kwangu.Kokote uliko nakuomba
usitishe shuguli zako na tukutane
nyumbani”
“Unasema uko bandarini Dar
es salaam? Mathew akashangaa
“Ndiyo,nimetokea
Zanzibar.Ndege zimezuiwa kutua
katika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere kwa muda kufuatia tukio
lililotokea uwanjani hapo mapema
usiku huu hivyo ikatulazimu
kwenda kutua Zanzibar na kutoka
pale nikachukua boti hadi dar es
salaam.Naomba tukutane Mathew nina mazungumzo muhimu sana
nawe”
“Umekuja na Anna Maria?
Akauliza Mathew
“Ndiyo niko naye siwezi
kumuacha” akasema Peniela
“Ahsante sana nakuja hapo
sasa hivi.Ahsante sana kwa
kunileta furaha yangu ya maisha”
akasema Mathew na kukata simu
akamtazama Austin kwa uso
uliojaa furaha na tabasamu kubwa.
“She’s here.!! Akasema kwa
furaha
“She’s here!!Peniela is here in
Tanzania!! Akasema Mathew huku
akiinuka
“ Austin we have to go see her
right now” “Mathew subiri
kwanza.Uliniambia kwamba
uliwasiliana na Peniela akiwa
Paris Ufaransa imekuaje akaamua
kuja Tanzania ghafla hivi ?Ujio
wake huu unanipa mashaka isije
kuwa anatumiwa” akasema Austin
“Usihofu Austin.Lazima kuna
jambo kubwa na la dharura
lililomfanya Peniela akaja
nchini.Ninamfahamu vyema
Peniela hawezi katu kutumiwa na
mtu yeyote kunizunguka
mimi.Tumeachana lakini she’s
very royal to me.Inawezekana
labda Anna Maria amekataa
kusherehekea siku yake
yakuzaliwa bila mimi na ndiyo
maana Peniela akaamua kuja tanzania.Yule bi bilionea sasa na
anaweza akaenda kokote
anakotaka muda wowote.Anayo
ndege yake binafsi yenye kasi
mara mbili ya kasi ya sauti”
akasema Mathew
“Pamoja na hayo Mathew
lazima tuchukue tahadhari kwa
jambo hili.Ujio huu wa haraka wa
Peniela lazima una jambo”
“Sikiliza Austin,kama
nilivyokueleza kwamba tuligundua
George Mzabwa alikuwa na
akaunti katika benki ya Escom
ambayo Peniela ni mmoja wa
wamiliki.Escom bank inamilikiwa
na watu watatu ambao ni Andrew
Pillar,mwanae Anderson Pillar na
Peniela.Tuligundua kwamba kampuni ya kuchonga madini ya
vito ambayo mke wa George
alikuwa mkurugenzi ina
mashirikiano ya kibiashara na
kampuni moja ya Marekani ya
kutenegeza saa za
mkononi.Kampuni hiyo ya saa
ndiyo walioingiza kiasi kikubwa
cha fedha katika akaunti ya
George.Kampuni hiyo ya
kutengeneza saa za mkononi ina
mahusiano na kampuni ya A.D
Electronics ambayo inamilikiwa
kwa siri na serikali ya Marekani
kupitia shirika lake la ujasusi la
CIA.Baada ya kugundua hayo
nilimwambia Peniela anisaidie
kufanya uchunguzi kubaini kama
mpenzi wake Anderson na baba yake Andrew Pillar ni mawakala
wa CIA.Sijapata mrejesho wowote
toka kwake hadi muda huu
aliponipigia simu na kunijulisha
kuwa yuko Dar es
salaam.Ninaamini safari yake ya
ghafla kuja Tanzania ina sababu
kubwa.Twende tukaonane naye”
akasema Mathew
“Mpaka hapa nimekuelewa
Mathew.Twende tukamuone
yawezekana kweli akawa na
taarifa muhimu za kutusaidia”
akasema Austin wakatoka na
kuingia katika gari la Austin
wakaondoka
“Huku njiani yatupasa tuwe
makini sana Mathew kwani wewe
bado ni mtuhumiwa” “Usihofu kuhusu hilo”
akasema Mathew
“Nini sababu ya CIA
kutengeneza mtandao wake hapa
Tanzania? Kuna jambo gani
wanalitafuta? Austin akauliza
“Hilo ndilo swali ambalo mimi
na wenzangu tumekuwa
tunalitafutia majibu” akajibu
Mathew
“Vipi kuhusiana na watu
waliomuua kanali Sebastia
Matope? Umefikia wapi katika
kuwabaini?
“Mauaji ya Kanali Sebastian
Matope hayakuibuka tu hivi hivi
bali yana sababu yake.Ili kupata
sababu ya kwa nini aliuawa
inapaswa kwanza kujua kwa nini rais Anorld aliuwa? Inasemekana
Kanali Matope ndiye pekee
aliyenusurika katika ile ajali ya
ndege iliyomuua rais Anorld
Mubara na miezi michache baadae
akauawa.Katika uchunguzi wangu
nimebaini kuna siri ambayo kanali
matope na rais Anorld walikuwa
wanaifahamu na hiyo ndiyo
iliyopelekea vifo vyao.Kanali
Matope alikuwa ndiye mbebaji
mkuu wa begi la rais lililopewa
jina la football.Begi hilo lilikuwa
na siri ambazo rais alikwenda nazo
kila mahala alikoenda na lilibebwa
na mtu moja tu ambaye ni kanali
Matope.Baada ya ajali ile Football
halikuwahi kuonekana tena na
hakuna ajuaye mahala lilipo.Mpaka sasa uchunguzi
unaonyesha wazi kwamba CIA
wanahusika katika kuratibu ajali
ile ya ndege ya rais lakini bado
sijafahamu kwa nini.Ili kupata jibu
kwa nini walifanya vile tunapaswa
kuingia katika vita na shirika
kubwa la ujasusi duniani
CIA.Tuufahamu mtandao wao
tuufumue na tutapata majibu ya
maswali yetu” akasema Mathew na
Austin akawa kimya.Baada ya
muda akasema
“Mathew pole sana hata hivyo
nakupongeza kwani kazi
uliyoifanya katika kipindi hiki
kifupi ni kubwa.Umegundua
mambo mengi mazito.Kuanzia
hapa tutashirikiana sote.Lazima tulifikishe hili suala mwisho”
akasema Austin
“Ahsante Austin kwa kuamua
kujiunga nami.Jambo hili ni kama
fumbo kubwa ambalo wengi
wameshindwa kulifumbua lakini
naamini safari hii litafumbuliwa”
akasema Mathew
“Kutokana na mtiririko wa
mambo ulivyo,toka ulipoanza
kulichunguza hili suala ni wazi
watu hawa tayari wamekwisha
kufahamu.Unapambana na watu
ambao wanakufahamu lakini
wewe hujawafahamu bado.Hii ni
mbaya kwani muda wowote
wanaweza wakafanya chochote
bila wewe kutarajia.Ni muhimu kuchukua tahadhari ya kutosha”
akasema Camilla
“Anachokisema Camilla ni kitu
cha kweli kabisa.hawa watu tayari
wanakufahamu na ndiyo maana
wamethubutu hata kufahamu
kwamba hauko nyumbani na Dr
Robert yuko pale hivyo wakavamia
wakamuua.Mathew kuna
umuhimu wa kuchukua tahadhari
kubwa kama Camilla alivyoshauri”
akasema Austin na Mathew
akaitika kwa kichwa akionekana
kujawa mawazo
WASHINGTON DC
Saa tisa za alasiri kwa sasa za
Marekani,Will Gadner mkurugenzi
wa shirika la ujasiri Marekani CIA
aliwasili katika ikulu ya Marekani
kufuatia wito wa haraka wa rais
Mike straw.Moja kwa moja
akaeleka katika ofisi ya rais
“Will Gadner
karibu.Sintakuwa na maneno
mengi kwa sasa.Nataka kufahamu
nini kimetokea Tanzania? Kwa nini
operesheni haikufanikiwa?
Akauliza Mike straw ambaye sura
yake ilibadilika kwa hasira nyingi
alizokuwa nazo.Alionekana wazi
kulemewa na mzigo wa mambo.Will Gadner akarekebisha
koo na kusema
“Hakuna aliyetegemea kama
kungetokea jambo kama lile kila
kitu kilikwisha andaliwa vizuri na
kilichokuwa kimebaki ni
kutekeleza mpango wetu”
“Will sihitaji siasa hapa
.Nataka sababu kwa nini mpango
wa kumuua Helmet Brian
haukufanikiwa? Akauliza Mike
kwa ukali
“Mheshimiwa rais naomba
unipe nafasi nikueleze kile
kilichotokea.Nakushauri tuwe
watulivu ili tuweze kutafuta
suluhu ya hili jambo” akasema
Gadner na Mike hakujibu kitu.Will
akaendelea “Kilichotokea Dar es salaam
kimetushangaza sote.Bado
tunaendelea na uchunguzi kubaini
kilichotokea lakini kuna taarifa
tayari tumezipata kutoka
Tanzania.Waziri wa mambo ya nje
wa Tanzania ambaye ni mmoja wa
watu wetu na ambaye tulimtumia
sana katika kuandaa operesheni
hii ameuawa muda mfupi tu baada
ya shambulio kutokea na waziri
Helmet kutoweka.Inaaminika
kwamba alitekwa na kwenda
kuuawa na maiti yake imekutwa
kwa mtu aitwaye Mathew
Mulumbi.Hii inatupa picha
kwamba watu waliofanya
shambulio lile walipata taarifa za
kuwepo kwa mpango wa kumuua Helmet kutoka kwa Dr
Robert.Tuliopata taarifa hizi
tumetafuta kumjua huyu Mathew
ambaye inadaiwa ndiye aliyemuua
Dr Robert ni nani? Tumegundua
kwamba anaitwa Mathew Mulumbi
aliwahi kufanya kazi katika idara
ya ujasusi ya tanzania lakini kwa
sasa anajishughulisha na
biashara.Wakati nakuja huku
nikapata taarifa nyingine kwamba
Mathew Mulumbi ndiye aliyefanya
shambulio lile uwanja wa ndege
wa Julius Nyerere na kuvuruga
mpango wetu.Taarifa hiyo toka
110C inasema kuwa Helmet Brian
ni mzima wa afya na kwa sasa
amekabidhiwa kwa rais Dr Vivian
na yuko ikulu” Sura ya Mike straw
ikabadilika kwa taarifa ile ya Willy
Gadner.Akashika kichwa na
kuvuruga nywele
zake.Alichanganyikiwa
“Hii ni taarifa mbaya ambayo
sikuwa nimetegemea kuisikia.Kwa
mara ya kwanza taifa kubwa
duniani kama Marekani linazidiwa
maarifa na nchi ndogo masikini
kama Tanzania.Nchi hii ni
mshirika wa Korea Kaskazini
ambaye ni hasimu wetu mkubwa
na kwa kuwa tayari wameifahamu
mipango yetu basi tayari
wamepata fimbo ya kutuchapia”
Akainamisha tena kichwa na
kuzama katika tafakari baada ya
muda akasema “Gadner kwa nini lakini
ukaruhusu ufanyike uzembe na
kusababisha maadui zetu
wazifahamu mbinu zetu za
mapambano?
“Mheshimiwa rais ,hakuna
uzembe uliofanyika,kila kitu
kilikwenda vizuri lakini hatuelewi
kwa namna gani Mathew aliweza
kugundua kuhusu mpango
huu.Tutafahamu hayo uchunguzi
utakapokamilika lakini kuna suala
lingine ambalo si zuri sana pia”
akasema Gadner.Sura ya Mike
ikazidi kuonyesha woga
“Msichana Olivia ambaye
tulimpandikiza ikulu ili awe
karibu na Dr Vivian ametoweka na hafahamiki mahala aliko.Jitihada
za kumsaka zinaendelea”
“Oh Mungu wangu !! akasema
Mike straw kwa masikitiko
“Yawezekana akawa
ametekwa nyara au tayari naye
ameuawa? Akauliza
“Bado hatuna uhakika
mheshiwa rais ila uchunguzi
unaendelea” akasema Gadner na
ukimya ukatanda halafu baada ya
muda akasema
“Huyu ni mtu wetu wa pili
anapotea nchini Tanzania na wote
ni wale mliowapandikiza karibu na
rais.Hii inatupa picha ya wazi
kwamba tayari mbinu zetu
wamekwisha zifahamu.Gadner
hatuwezi kuendelea namna hii.Amekwisha fahamu kwamba
tunamchunguza na ndiyo maana
watu wetu wote wanauawa na hii
ina maana kwamba tumeshindwa
kumzuia rais Vivian asianzishe
mahusiano na Korea
Kaskazini.Tumekosa sababu ya
kuishambulia Korea Kaskazini na
yote hii ni kwa sababu ya mipango
yako mibovu.Nilikuamni sana
lakini umeniangusha Gadner.Si
mimi pekee uliyeniangusha bali
umewaangusha wamarekani wote
kwani Korea kaskazini ni adui wa
wamarekani wote.” Akasema Mike
na kuinamisha kichwa akafikiri
kwa muda akamtazama Willy
Gadner na kusema “Najaribu kutafakari ni vipi
endapo Dr Vivian akaufahamu na
kuamua kuuanika mpango wetu
tulioupanga wa kumuua Helmet
Brian?Hili liitakuwa jambo baya
sana kisiasa.Hatutaaminiwa tena
na wananchi na hili ni anguko
langu kubwa kisiasa.Nimeshindwa
kuwalinda wananchi wangu kama
nilivyowaahidi na kuiruhusu
Korea kaskazini kuendelea
kujiimarisha kijeshi na kuzidi
kutishia amani ya Marekani”
akasema Mike na kunyamaza kwa
muda kisha akaendelea
“Helmet Brian ni mmoja wa
watu wangu wa karibu
sana.Tumesoma chuo kimoja na
tulianza pamoja harakati zetu za siasa na ana mchango mkubwa
sana kwa mimi kufika hapa
nilipofika leo.Kiti hiki cha rais ni
yeye ndiye aliyekuwa anatakiwa
akikalie kwani ndiye aliyekuwa
chaguo la wengi ndani ya chama
lakini aliposikia kwamba na mimi
nipo katika mbio za kuwania urais
akajitoa na kuniunga mkono mimi
na hivyo nikapata nafasi hii ya
kuwa rais.Helmet si rafiki tu bali ni
zaidi ya ndugu na maaumuzi ya
kumuua hayakuwa rahisia
kwangu.Itakuaje endapo
atafahamu kuwa mimi ndiye
niliyeidhinisha
auawe?Nimechanganyikiwa Willy
na sijui nifanye nini.Hebu nishauri
nifanye nini kwani ninaweza kuchukua maamuzi magunu
sana.Ninaweza kutuma kikosi
kikavamie ikulu ya Tanzania na
wamchukue Helmet .Uwezo huo
ninao lakini siwezi kufanya hivyo
ila pale nitakapokuwa sina njia
nyingine nitalazimika kufanya
hivyo” akasema Mike kwa hasira
“Mheshimiwa rais,jambo hili
linahitaji umakini mkubwa
sana.Mpaka hapa tayari Dr Vivian
amekwisha fahamu mipango yetu
ya siri na anaweza akaanika kila
kitu kwa dunia na kutufanya
tudharaulike sana.Ipo namna ya
kuweza kujaribu kumnyamazisha
Dr Vivian na kumzuia asifanye
chochote na akafuata kila
tutakachomtaka afanye” “Enhe nakusikiliza” akasema
Mike
“Niliwahi kukueleza kwamba
CIA tumekuwa tunamfuatilia Dr
Vivian kwa muda mrefu sasa toka
alipoanza kusoma hapa Marekani
Kuna sababu maalum iliyotufanya
tumfuatilie kwa karibu kwa muda
huu mrefu na bado tunaendelea
kumfuatilia” Willy Gadner
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Dr Vivian alihamia Marekani
kuendelea na masomo yake ya
udaktari akitokea nchni Cuba
alikokuwa anasoma.Akiwa Cuba
ambako aliishi kwa miaka
minne,Dr Vivian alikutana na mtu
mmoja anaitwa Said Bazharan raia wa Syria ambaye naye alikuwa
nchini humo kwa ajili ya
masomo.Familia ya Said ambao ni
watu matajiri sana wanaomiliki
visima kadhaa vya mafuta
walikuwa wanachunguzwa kwa
tuhuma za kusaidia vikundi
kadhaa vya kigaidi
vilivyounganisha nguvu kwa ajili
ya kupambana na serikali ya
Syria.Urafiki wa Said na Vivian
ulikuwa mkubwa na hatimaye
wakawa wapenzi na katika
mapenzi yao Vivian akapata
ujauzito.Familia ya Said
haikupendezwa na kitendo kile
cha mtoto wao kumpa mimba
mwanamke ambaye kwanza si wa
dini yao na pili ni mwafrika.Ili wa Syria ambaye naye alikuwa
nchini humo kwa ajili ya
masomo.Familia ya Said ambao ni
watu matajiri sana wanaomiliki
visima kadhaa vya mafuta
walikuwa wanachunguzwa kwa
tuhuma za kusaidia vikundi
kadhaa vya kigaidi
vilivyounganisha nguvu kwa ajili
ya kupambana na serikali ya
Syria.Urafiki wa Said na Vivian
ulikuwa mkubwa na hatimaye
wakawa wapenzi na katika
mapenzi yao Vivian akapata
ujauzito.Familia ya Said
haikupendezwa na kitendo kile
cha mtoto wao kumpa mimba
mwanamke ambaye kwanza si wa
dini yao na pili ni mwafrika.Ili kujaribu kuliweka sawa suala hilo
Said alimshawishi Vivian abadili
dini ili aweze kukubalika na
familia yake lakini Vivian hakuwa
tayari kwa hilo.Baada ya
kujifungua mtoto wa kike ambaye
alipewa jina la Nasrat shinikizo
toka kwa familia ya Said
liliongezeka na Said akapata
taarifa za siri kwamba kuna watu
wametumwa nchini Cuba kwa ajili
ya kuwaua yeye ,Vivian na mtoto
wao Nasrat.Said akamueleza
Vivian jambo lile na kwa pamoja
wakapanga mpango ambao Said na
Nasrat wakatoroka na kwenda
nchini Palestina na kwa bahati
mbaya akagunduliwa.Alipofahamu
kuwa tayari amegundulika mahala alikoenda kujificha na kwamba
kuna watu waliokuwa
wanamfuatilia
wamuue,akamtelekeza mwanae
Nasrat katika kituo cha watawa na
muda mfupi baadae nyumba
aliyokuwa akiishi ikalipuliwa kwa
bomu na Said Bazharan hakuwahi
kuonekana tena na wengi
waliamini kwamba alifariki katika
ule mlipuko.Baadae uchunguzi wa
CIA ulibaini kwamba Said hakufa
katika ule mlipuko bali ni mzima
na alipoondoka alikwenda
kujificha nchini Syria na huko
alianzisha kikundi cha kigaidi
ambacho kinashirikiana na
kikundi cha IS kupambana na
serikali ya Syria na sasa anajiita Samir Alzahir”Willy Gadner
akanyamaza kidogo na kisha
akaendelea
“Licha ya kutoka katika
familia yenye kuhusishwa na
kufadhili ugaidi,lakini CIA
walianza kumfuatilia Said baada ya
kugundulika kuwa na mawasiliano
na mwanamfunzi mmoja kutoka
Iraq aliye lipua bomu katika chuko
kikuu kimoja hapa Marekani na
kuua wanafunzi
sitini.Tulichunguza nyenzo zake
hadi pale alipokimbia Cuba.
Alipoanza harakati zake za
kupambana na serikali ya Syria
watu wengi waliuawa wasio na
hatia wakiwamo watoto.Hii
ililazimu serikali ya Marekani na washirika wake kuamua kuingilia
kati.Wanamgambo wanaomtii Said
au Samir kwa sasa walifanya
shambulio kubwa na kuua
wanajeshi zaidi ya arobaini wa
majeshi ya pamoja kwa hiyo
serikali ya Marekani inamsaka
kwa udi na uvumba hadi
sasa.Baada ya kutoka Cuba,Dr
Vivian alikuja kuendelea na
masomo yake hapa Marekani na
kwa kuwa tayari CIA walikwisha
anza kumchunguza aliyekuwa
mpenzi wake Said Bazharan
aliyetoweka ililazimu kuanza
kumchunguza Dr Vivian pia
tukiamini kuwa lazima watakuwa
wanawasiliana.Hivyo basi
akapandikizwa mtu ambaye alianzisha urafiki naye na baaade
wakawa wapenzi na huyu ni
Nathan ambaye amepotea.Pamoja
na kumchunguza Dr Vivian kwa
muda mrefu hatujafanikiwa mpaka
leo kunasa mawasiliano yake na
Said.Hii ndiyo sababu CIA
tunaendelea kumchunguza Dr
Vivian tukiamini kwamba kupitia
kwake tutaweza kufahamu mahala
alipo Said.Baada ya maelezo hayo
marefu turejee katika suala
letu.CIA tumefuatilia na kugundua
kwamba mtoto wa Dr Vivian yuko
hapa Marekani
anasoma.Alipokabidhiwa kwa
watawa,Nasrat alibatizwa
akabadilishwa jina na sasa anaitwa
Florentina dawson” Uso wa rais Mike straw
ukajenga tabasamu kubwa na
kusema
“Hizo ni habari nzuri sana.CIA
mnafanya kazi kubwa na nzuri
mno na ndiyo maana ni shirika
kubwa la ujasusi
duniani.Mnastahili pongezi
kubwa.Dr Vivian anafahamu lolote
kuhusiana na huyu
mwanae?Anajua kama yuko hapa
Marekani?
“Nasrat aliokotwa na watawa
baada ya kutelekezwa na baba
yake ,akapelekwa nchini Israel
akabatizwa akabadilishwa jina na
baadae akaletwa Marekani
kusoma.Said wala Dr Vivian
hawafahamu alipo mtoto wao” “Una uhakika Gadner kwamba
hata Dr Vivian hana taarifa zozote
kuhusu mwanae?
“Ndiyo mheshimwia rais.Hii ni
siri kubwa aliyonayo Dr Vivian na
hata nchini mwake hawafahamu
kama aliwahi kuwa na mtoto.Hata
ndugu zake hawafahamu
chochote”
“Safi sana.Kwa hapo Dr Vivian
tumemuweka
kwapani.Hatafurukuta tena.Nataka
kupata taarifa zote za kuhusiana
na huyo binti haraka sana kabla ya
kufika saa mbili usiku wa
leo.Nataka usiku wa leo
nizungumze na Dr Vivian na
kufanya naye makubaliano ili
kwanza aturejeshee waziri wetu Helmet Brian ,pili asithubutu
kufungua mdomo wake na
kuiambia dunia kwamba ni sisi
tuliopanga kumuua waziri wetu
Helmet.Tatu ajiondoe katika
mashirikiano na Korea
Kaskazini.Mwisho awaachie huru
watu wetu wawili walipotea nchini
mwake ambao nina uhakika
mkubwa kwamba anafahamu
mahala walipo.Akikubali kufanya
haya basi tutamuunganisha na
mwanae Florentina na kama
akipuuza basi nitatishia kuanika
siri yake hii kubwa kwa dunia
jambo ambalo hatakubali
lifanyike.Hatakuwa tayari
ajulikane kwamba amewahi kuzaa
na gaidi na akatelekeza mtoto kwani jambo hili litampunguzia
heshima yake aliyoijenga kwa
watu wake na dunaini kwa
ujumla.Kwa hapa Dr Vivian hana
njia nyingine zaidi ya kuweza
kufanya kile tutakachomtaka
akifanye.Nataka nipate taarifa zote
za kuhusiana na huyo mtoto kabla
ya saa mbili usiku wa leo na
ninaomba kuanzia sasa CIA
muweke walinzi wa kumlinda
Florentina.Mumfuatilie kila
mahala aendako na kujua nyendo
zake zote”akasema Mike ambaye
uso wake ulianza kuonyesha
tabasamu
“Mheshimiwa rais tunaweza
kufanya hivyo lakini njia hiyo si
muafaka na haitakuwa na tija kwetu japo inaweza kumfanya Dr
Vivian akakubaliana nasi katika
baadhi ya mambo” akasema Will
Gadner
“Kwa nini unasema hivyo
Willy?akauliza Mike straw
akionekana kutokufurahishwa na
kauli ile ya Willy Gadner
“Kufahamu mahala aliko Said
Bazharan au Samir Alzahir kama
anavyojulikana sasa si sababu
pekee kwa CIA kuwekeza nguvu
kubwa katika kumchunguza Dr
Vivian .Ipo sababu nyingine kubwa
zaidi”
“Kuna jambo lingine?akauliza
Mike straw kwa mshangao
“Ndiyo mheshimiwa rais”
akajibu Will Gadner halafu ukafuata ukimya mfupo.Will
gadner akaonekana kufikiri jambo
“Ni jambo gani hilo Gadner?
Tafadhali naomba unifahamishe”
akasema Mike straw
Gadner akavuta pumzi ndefu
na kusema
“Dr Vivian kuwa rais wa
Tanzania si jambo lililokuja hivi
hivi bali ni kitu kilichoandaliwa
kwa muda mrefu” akanyamaza
kwa sekunde kadhaa kisha
akaendelea
“Dr Vivian alipoanza masomo
yake nchini Marekani akitokea
Cuba alianzisha harakati za
kutetea wanafunzi wenye asili ya
afrika waliokuwa wakibaguliwa
katika vyuo vikuu mbali mbali vya hapa Marekani na kwa ujasiri
wake alianza kuwavutia watu
wengi wakiwamo baadhi ya
viongozi wa mataifa.Mmoja wa
viongozi aliyeonyesha kuvutiwa
sana na harakati za Dr Vivian
alikuwa ni rais wa Cuba wa wakati
huo Alfredo Marcus.Huyu aliwahi
hadi kumualika Dr Vivian nchini
mwake na kufanya mazungumzo
naye ya siri.Hatujui walizungumza
nini lakini mwezi mmoja baada ya
rais Alfredo kumualika Dr Vivian
nchini Cuba alifanya ziara nchini
Tanzania ambako alikuwa na
mazungumzo na rais wa Tanzania
ambaye ina mashirikiano
makubwa na nchi ya Cuba toka
enzi za waasisi wa mataifa haya mawili.Baada ya kutoka nchini
Tanzania rais Alfredo akaelekea
nchini China ambako alifanya
mazungumzo na kiongozi wa China
kisha akarejea nchini mwake.Ziara
hizi mbili alizozifanya katika nchi
za Tanzania na China zilikuwa na
lengo la kuwashawishi waweze
kumuandaa Dr Vivian aweze kuwa
rais wa Tanzania kwani kuna kitu
kikubwa alikiona kwake.Mipango
ya kumuandaa Dr Vivian kuwa rais
wa Tanzania ilianzia hapo.Aliwahi
kutoa hotuba yake katika moja ya
makongamano aliyowahi kualikwa
na katika hotuba yake hiyo aliwahi
kueleza nia yake ya kutaka
kuiunganisha Afrika na kuwa kitu
kimoja.Alisema kwamba ana ndoto ya kuwa mtawala wa kwanza wa
Afrika iliyoungana na kuwa
moja.Alipotoa hutuba ile tayari
alikwisha fahamishwa kwamba
anaandaliwa kuja kuwa mtawala
wa Tanzania siku za usoni.”
Akanyamaza na Mike akachukua
kitambaa akavua miwani na kufuta
macho yake,Willy akaendelea
“Miaka miwili baadae
ukafanyika uchaguzi na rais
aliyekuwepo madarakani wakati
huo alimaliza muda wake akaingia
madarakani rais Anorld Mubara
ambaye naye alirithishwa mpango
ule wa kumuandaa Dr Vivian kuwa
rais wa Tanzania hapo
baadae.Katika mwaka wa pili wa
uongozi wake rais Anorldalitembelea nchini Cuba na kule
akakutana na wanasayansi ambao
walimuomba rais Anorld
kuwekeza katika kiwanda cha
kutengeneza gesi kwa ajili ya
matumizi ya hospitali na rais
akawakaribisha nchini
Tanzania.Ujenzi wa kiwanda hiki
ulikuwa wa siri na ni watu
wachache tu waliokuwa
wakifahamu mahala kilipojengwa
kiwanda hicho.Kiwanda hicho
kilikuwa kinazalisha gesi
inayotumiwa mahospitalini lakini
kwa kiasi kikubwa walikuwa
wanatengeneza gesi ya sumu
ambayo walikuwa wanaisafirisha
nchini kwao kwa lengo la kujihami
kwani Marekani walikuwa wametishia kuishambulia Cuba
kijeshi.Siri hii ilijulikana baada ya
gesi hiyo kuvuja wakati
ikisafirishwa na kuua watu wote
waliokuwemo ndani ya meli
iliyokuwa ikisafirisha gesi hiyo
kwenda Cuba.Uchunguzi
ulipofanyika ikagundulika
kwamba gesi hiyo haikuwa gesi ya
mahospitalini bali ilikuwa ni gesi
ya sumu yenye uwezo wa kuua
kwa muda mfupi sana baada ya
mtu kuivuta. Serikali ya Cuba
ilificha ukweli wa jambo hili na
badala yake ikatoa sababu
nyingine ya uongo kuhusiana na
watu wake kufariki ndani ya
meli.Baada ya tukio hilo rais
Anorld alikifunga kiwanda hicho na kuondoa wanasayansi wote
waliokuwa wakifanya kazi nchini
Tanzania.Funguo za kuingilia
katika kiwanda hicho alikuwa nazo
yeye mwenyewe pamoja na
nyaraka zote muhimu za
kutengenezea gesi hiyo ya sumu
alizichukua na kwa bahati mbaya
wale wanasayansi wote waliokuwa
wakifanya kazi nchini Tanzania
walifariki kwa ajali ya ndege
wakati wakirejeshwa kwao kwa
hiyo siri ya mahala kilipo kiwanda
hicho cha kutengeneza gesi ya
sumu ilibaki kwa rais Anorld na
baada ya hapo ndipo alipoanza
kutembea na mkoba alioupa jina
fotball ambao ulikuwa na siri zote
za kuhusiana na kiwanda hicho.Mkoba ule ulikuwa na ulinzi
mkali na mbebaji mkuu alikuwa ni
kanali Sebastian Matope ambaye ni
baba yake na Dr Vivian.”
Akanyamaza tena kwa muda kisha
akaendelea
“Baada ya CIA kufanya
uchunguzi wake na kubaini jambo
hilo tulianza mikakati ya kulipata
lile begi au football kama
walivyokuwa
wakiliita.Tulifanikiwa
kuwapandikiza watu wetu katika
ndege ya rais Anorld wakati
akirejea Tanzania akitokea nchini
Misri alikoenda kuhudhuria kikao
cha wakuu wa nchi zinazopitia na
mto Nile lakini hatukufanikiwa
kulipata hilo begi la football kwani kanali Sebastian Matope
alifanikiwa kutoroka nalo
ndegeni.baada ya ….”
“Subiri kidogo
Gadner.Unataka kuniambia
kwamba serikali ya Marekani
wanahusika katika kifo cha rais
Anorld Mubara? Akauliza Mike
straw
“Ndiyo mheshimiwa
rais.Marekani ndiyo iliyomuua rais
Anorld Mubara”
Mike straw akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Kwa nini sikuwahi
kufahamishwa kuhusiana na
jambo hili hadi leo hii?
“Mheshimiwa rais haya ni
mambo ya siri kubwa na sisi tunaofahamu tumeapa kulinda siri
hii katika kipindi chote cha uhai
wetu lakini leo hii nimevunja
kiapo changu kwa kukueleza
jambo hili” akasema Willy
“Tutazungumza baadae
kuhusu suala hili,endelea na lile
suala tulilonalo sasa” akasema
Mike baada ya tafakari
“Baada ya kufanikiwa kutoka
salama ndegeni tuliendelea
kumfuatilia Kanali Sebastian
Matope ili kufahamu mahala
alikolificha lile begi tunalolitafuta
lakini hatukuweza kuambulia
chochote na hadi sasa hatufahamu
mahala alikolificha hivyo
tulazimika kumuua kwani alikuwa
tayari kueleza kile kilichotokea ndegeni.Baada ya kumuua kanali
Sebastian kila kitu kimebaki
siri.Hakuna anayejua nini kilitokea
ndani ya ndege ile ya
rais.Tunaamini kwamba Dr Vivian
kuna kitu anafahamu kuhusiana na
siri hii na mahala kilipo kiwanda
kile cha kutengeneza gesi ya sumu
lakini mpaka sasa hatujafanikiwa
kupata kitu chochote.Mtu wetu
ambaye ni Nathan alijitahidi kwa
kila namna alivyoweza
kumchunguza Dr Vivian kuhusiana
na suala hili lakini hakuweza
kupata kitu chochote.Bado
tunaamini kwamba tukiendelea
kumfuatilia Dr Vivian tutagundua
mahala kilipo kiwanda hicho cha
kutengeneza gesi ya sumu ambacho ni hatari sana kwa
Marekani.Ziara ya kwanza ya Dr
Vivian baada ya kuwa rais ilikuwa
nchini Cuba.Alifanya mazungumzo
na rais wa sasa wa Cuba na
mojawapo ya mambo
waliyoyazungumza ni kukifungua
tena kiwanda hicho.Tunazo taarifa
za uhakika kuhusiana na hilo
lakini Dr Vivian hakuweza kutoa
jibu la moja kwa moja kwamba
amekubali kukifungua tena
kiwanda hicho.Kwa sasa jambo hili
linakuwa hatari zaidi endapo
mashirikiano kati ya Tanzania na
Korea Kaskazini yatafanikiwa
kuanzishwa.Korea kaskazini
inaweza ikatumia gesi hiyo kwa
ajili ya kutengeneza silaha za maangamizi.Tuko katika hatari
kubwa mheshimiwa rais na bado
Dr Vivian ametushika
pabaya
Tuko katika hatari
kubwa mheshimiwa rais na bado
Dr Vivian ametushika
pabaya.Tunaendelea
kumchunguza taratibu ili tuweze
kufahamu mahala kilipo kiwanda
hicho na tukiteketeze.Tunaweza
kumtumia mtoto wake kwa ajili ya
kumlazimisha afanye kile
tunachokitaka lakini kama
ujuavyo Dr Vivian ni mmoja wa
binadamu wenye kujiamini kwa
kiwango cha juu sana na ana kiburi
kikubwa kwa hiyo anaweza
akapata hasira na kuamua kufanya
mambo ambayo hatukuwa
tumeyakusudia.Anaweza akaamua
kushirikiana na Cuba au Korea
Kaskazini katika kutengeneza gesi ile ya sumu na
kutushambulia.Jambo lingine ni
kwamba tayari ameanzisha
uchunguzi kuhusiana na nani
waliomuua baba yake kanali
Sebastian Matope.Kazi hiyo
amempatia Mathew Mulumbi
ambaye kama nilivyokueleza awali
amewahi kufanya kazi katika idara
ya ujasusi Tanzania na tayari
amekwisha piga hatua kubwa
katika uchunguzi wake na kuna
mambo ambayo tayari amekwisha
yagundua ambayo yatampelekea
katika kugundua kwamba
Marekani walihusika katika ajali
ile na kumuua rais Anorld
Mubara.Kwa kuwa alitumwa na
rais kuifanya kazi hiyo lolote analoligundua katika uchunguzi
wake anamueleza pia rais wake”
“Unamaanisha tayari Dr
Vivian ana taarifa za Marekani
kuhusika katika ajali ile? Akauliza
Mike
“Hatuna uhakika bado lakini
kwa kuwa Mathew alitumwa na Dr
Vivian afanye uchunguzi basi ni
lazima atakuwa anamueleza kila
hatua anayoipiga.Huyo Mathew
ndiye aliyemuokoa Helmet”
“Mungu wangu !! akasema
Mike straw
“Mnasubiri nini
kumshughulikia huyo mtu ambaye
ni wazi anaonekana ni hatari
kwetu? Kwa nini mmemuacha hai
mpaka hivi sasa? Hamuoni kwamba akipata ushahidi wa
Marekani kuhusika katika kifo cha
rais Anorld itakuwa ni mbaya sana
kwa upande wetu?Willy tafadhali
usiruhusu jambo hili liendelee
mmalize mtu huyo haraka sana”
akasema Mike
“Si rahisi namna hiyo
mheshimiwa rais” akasema Will
Gadner na Mike akamtazama kwa
hasira.
“Kwa nini si rahisi? CIA mna
kila kitu.Unao watu mahiri
wanaoweza kufanya kazi yoyote
sehemu yoyote duniani na isitoshe
tayari umekwisha tengeneza
mtandao nchini Tanzania.Kwa nini
mnashindwa kummaliza huyo mtu mmoja ambaye anaweza kuwa
hatari kwetu? Akauliza Mike straw
“Kama nilivyokueleza
mheshimiwa rais kwamba huyu
jamaa aliwahi kuwa jasusi na
anafahamu mbinu zote za kujihami
na isitoshe imegundulika ana
shirikiana na watu waliomo ndani
ya CIA na FBI na mipango yote
itakayopangwa basi ataifahamu
mara moja.Tunachoendelea
kukifanya kwa sasa ni kuwabaini
watu anaoshirikiana nao kutoka
CIA ambao wanampa siri
zetu.Tunataka tuubaini pia
mtandao wake wote na kujua ni
mambo gani ambayo tayari
anayafahamu kuhusiana na
Marekani.Baada ya hapo ndipo tutakapotafuta namna ya kuweza
kumuondoa.Bado tunamuhitaji
mtu huyu kwani kupitia yeye
tunaamini tunaweza kufahamu
mambo mengine ambayo
tumekuwa tukiyatafuta hivyo wazo
la kumuua kwa sasa si muafaka”
Mike straw akamtazama Will
Gadner kwa hasira na kusema
“Willy ninakuamini sana
ninaomba usitake nipoteze imani
na wewe kwa kushindwa
kutekeleza majukumu yako
ipasavyo.Sioni sababu yoyote ya
kumuacha hai huyu jamaa ambaye
ni hatari sana kwa nchi yetu.Kama
tayari amekwisha fahamu
kuhusiana na mambo
tuliyoyafanya wanaweza wakatuanika kwa dunia
nikafahamu mambo yanayofanywa
kwa siri na Marekani.” Akasema
Mike na kunyamaza baada ya simu
ya Will Gadner kuita na kuomba
atoke nje kwenda kupokea kwani
ilikuwa ni simu muhimu.Baada ya
dakika tatu akarejea ndani
“Mheshimiwa rais kuna
taarifa ambazo si nzuri kutoka
Tanzania” akasema Willy Gadner
“Kuna taarifa gani Willy?
Akauliza Mike
“Nimetaarifiwa kwamba wale
watu wetu ambao tulikuwa
tumewaweka kwa ajili ya kumuua
Helmet na baadae wakamatwe na
kukiri kwamba wametumwa na
Korea kaskazini wote wametiwa nguvuni jijini Dar es salaam”
akasema Willy na Mike akavuta
pumzi ndefu
“Mambo gani haya yanatokea?
Akasema kwa sauti ndogo
“Gadner haya yote yanatokea
kwa sababu ya uzembe wako.Licha
ya kufahamu umuhimu wa suala
lile lakini wewe na wenzako
hamkujipanga vizuri.Sasa mambo
yote yanaanza kutugeukia.Nataka
ukakae na watu wako na kabla ya
saa nne za usiku nakutaka uje tena
hapa ukiwa na mpango ni namna
gani mnashughulikia suala la
Tanzania.Nataka suala hili
limalizike mara moja.Sitaki
Marekani iendeshwe na nchi
ndogo masikini kama Tanzania.Sitaki wamarekani
waishi kwa hofu.Kama ni kumuua
rais wa Tanzania na hao wote
wanaoshirikiana naye mimi niko
tayari nileteeni mapendekezo na
nitasaini.Tusiendelee kupoteza
muda hapa nataka ukakae na watu
wako mlijadili suala hili kwa
upana wake na kama
nilivyokuambia kabla ya saa nne
za usiku uwe hapa tayari na ukiwa
na mpango wa namna ya kulitatua
suala la Tanzania.Huu ni mtihani
wako wa mwisho ninakupa nafasi
ya mwisho kurekebisha makosa
yako kama ukishindwa na hili
ntakuondoa na kumpa nafasi yako
mtu nitakayeona anafaa kwa kazi
hiyo.Unaweza kwenda” akasema Mike straw na Will Gadner
akainuka akachukua mkoba wake
akafungua mlango akatoka.Mike
straw akachukua chupa ya mvinyo
akamimina katika glasi
akagugumia wote na kuvuruga
nywele.
“Nilimuamini sana Willy
Gadner lakini mpaka hapa
anaonekana ameshindwa kufanya
kazi yake vyema.Ameniingiza
katika matatizo makubwa na sijui
nitatokaje.Ngoja nisubiri muda
huo niliompa nione kama atakuja
na mpango mzuri vinginevyo
nitamuondoa na kumpa nafasi
yake mtu mwingine na kisha
nitafanya vile nitakavyoona
inafaa” akawaza Mike straw baada ya Will gadner kutoka ofisini
kwake.
“Dr Vivian !! akasema kwa
sauti ndogo huku amekuja sura
yake
“Binti mdogo kama Dr Vivian
hawezi kukisumbua kichwa
changu namna hii.Kama
akiendelea kuwa kiburi
nitamuondoa kwani uwezo huo
ninao ! akawaza Mike akiwa
amekunja sura kwa hasira
“Lakini kuna mambo
ameyazungumza Will Gadner
yanaonekana kuwa na
msingi.Inahitajika akili kubwa
kukabiliana na Dr Vivian na si
nguvu.Kwa hapa tulipofika ni wazi
kwamba ametuweka kwenye kona na ili kujiondoa inahitaji busara na
akili nyingi.Natakiwa kutuliza
kichwa changu na kama
nikiliendea jambo hili kwa haraka
ninaweza kuharibu kila
kitu.Nitafanya nini basi? Akawaza
Mike straw na kuminina tena
mvinyo katika glasi akanywa
wote.Mlango ukafunguliwa
akaingia mmoja wa mawaziri
akitaka kumuona lakini Mike
akamuomba waonane baadae
kwani kwa wakati huo alikuwa
katika kushughulikia jambo
zito.Alizunguka zunguka mle
ofisini akiwaza na baada ya muda
akapata wazo
“Suala hili haliwezi kumalizwa
kwa simu wala kwa vitisho.Natakiwa kuonana ana kwa
ana na Dr Vivian na kuzungumza
naye na hii ina maana kwamba
natakiwa kwenda Tanzania haraka
iwezekanavyo.” Akaketi kitini
“Hili ni wazo zuri.Natakiwa
kwenda Tanzania mara moja.Sina
namna kwa vyovyote vile lazima
niende Tanzania.Lazima nionane
na Dr Vivian ana kwa ana
nizungumze naye na tuyamalize
haya mambo” akawaza Mike na
kuchukua simu na kuitisha kikao
cha dharura ili kujadili suala lile la
yeye kwenda Tanzania
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Kikao cha dharura kati ya rais
na wakuu wa vyombo vya ulinzi na
usalama kilichokuwa maalum kwa
ajili ya kujadili tukio lililokuwa
limetokea uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere usiku huo
kilimalizika na wajumbe wakatoka
kwa ajili ya kwenda kutimiza
majukumu waliyopewa na
rais.Wakati akielekea katika ofisi
yake,Dr Vivian alisimama kwa ajili
ya mazungumzo na mkuu wa
majeshi na wakati wakiendelea
kuzungumza akatokea mkuu wa
jeshi la polisi nchini Inspekta
jenerali John Aminiel Mkoka “Madam president ninaweza
kuzungumza nawe kwa dakika
kadhaa? Kuna suala la muhimu
sana nataka nikujulishe” akasema
John Mkoka na rais akamuomba
radhi mkuu wa majeshi ili aweze
kuzungumza na mkuu wa jeshi la
polisi nchini
“John kuna tatizo gani?
Akauliza rais
“Nimepokea simu kutoka kwa
mmoja wa askari wangu akisema
kwamba mtuhumiwa wa mauaji ya
waziri wa mambo ya nje hayuko
tena katika mikono ya polisi”
Taarifa ile ikamstua sana Dr
Vivian “Mathew hayupo katika
mikono ya polisi? Ametoweka vipi?
Akauliza rais kwa mshangao
“Baada ya kupokea taarifa
hiyo nimempigia simu kamanda
wa polisi kanda ya Dar es salaam
na kumtaka anipe taarifa kwa nini
mtuhumiwa huyo hayuko tena
katia mikono ya polisi na baada ya
kufuatilia amenijbu kwamba
Mathew amechukuliwa na mkuu
wa idara ya usalama wa taifa
Meshack Jumbo kwa ajili ya
kumfanyia mahojiano na ameahidi
kwamba akishakamilisha
mahojiano naye atamrejesha
katika mikono ya
polisi.Mjheshimwia rais huyu
mtuhumiwa amefanya mauaji makubwa ya kiongozi na anapaswa
kuwa katika mikono ya polisi kwa
nini Meshack Jumbo amchukue
bila kupata ruhusa au kufuata
taratibu? Kama kuna jambo
alihitaji kulifahamu kutoka kwa
Mathew angefuata taratibu
lakini…..” Mkuu wa jeshi la polisi
nchini Inspekta jenerali John
Aminiel Mkoka akanyamaza baada
ya Meshack Jumbo kutokea.Wote
wakageuka kumtazama.Dr Vivian
akamtazama kwa jicho kali sana na
Meshack hakuonyesha kujali
akamfuata.
“Meshack ! akaita rais kwa
ukali
“Madam president “ Meshack
Jumbo akaitika “Twende ofisini kwangu !!
akasema Dr Vivian na kuongozana
na Meshack Jumbo kuelekea ofisini
kwake.
Walipoingia ofisini wote
wawili wakasimama
wakitazamana
“What have you done
Meshack?!! Akauliza Dr Vivian
“Mheshimiwa rais kuna
mambo mawili nataka
nikujulishe.Kwanza ni kuwa wale
watu watatu ambao ulinipa picha
zao kwamba ndio walotumwa kuja
kumuua waziri Helmet Brian
tayari wamekamatwa na
wanashikiliwa mahala salama hivi
sasa kwa ajili ya kuanza mahojiano
nao.Hii inaonyesha ushupavu wa vijana wetu wa usalama wa taifa
namna wanavyoweza kufanya kazi
kwa haraka na kwa ufanisi
mkubwa.Napenda kukuhakikishia
mheshimiwa rais kwamba idara hii
tayari imerudi katika ubora wake”
akajigamba Meshack Jumbo.
“Jambo la pili ni kwamba
tayari tumekwisha andaa makazi
ya muda ya Helmet
Brian.Nimekuja kumchukua na
kumpeleka kwenda kupumzika”
akasema Meshack
“Ahsante kwa kazi nzuri
Meshack lakini hukunijbu swali
langu nililokuuliza kwamba
umefanya nini usiku huu?Ulidhani
sintafahamu? “Kuna nini mheshimiwa rais?
Akauliza Meshack Jumbo
“Umempeleka wapi Mathew?
Akauliza rais
“Mathew?
“Ndiyo Mathew.Umemchukua
kutoka mikononi mwa polisi na
kumpeleka kusikojulikana.Toka
awali nilikwisha kuona
hukukubaliana na mpango wangu
kuhusu Mathew.Kwa hili
ulilolifanya umevuka mstari na
umenidharau.Oh Meshack don’t
force me to destroy you old
man,just bring back Mathew and
I’ll let you go” akasema Dr Vivian
huku akiuma meno kwa hasira
“Napenda kufanya kazi na
watu wanaonitii na kufuata maagizo yangu .Sipendi
wasaliti.Kwa hiki ulichokifanya
umekuwa ni msaliti
kwangu.Nimekushirikisha mambo
yangu binafsi nikiamini kwamba
wewe utakuwa upande wangu
lakini umenisaliti na kuamua
kumsaidia Mathew wakati
ukifahamu fika kwamba yule ni
mtu hatari sana
kwangu.Sikutegemea kama
ungekuwa namna hii Meshack
Jumbo.Ninakuheshimu sana mzee
wangu hivyo ninachokuomba ni
kitu kimoja tu kwamba mrudishe
Mathew katika mikono ya polisi
halafu nitakuacha uende zako na
nitatafuta mkuu mwingine wa
idara ya suala wa taifa.Siwezi kabisa kuendelea kufanya kazi
nawe.Tayari umekwishaonyesha
picha mbaya kwamba si
muaminifu na hutaki kufuata
maagizo na maelekezo yangu”
Akasema Dr Vivian.Meshack Jumbo
akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Madam president,ni kweli
nimemchukua Mathew toka
mikononi mwa polisi.I’m so sorry
for that but I had no choice.Mimi
na wewe sote tunafahamu kwamba
Mathew hana kosa lolote na
anakwenda kupotea bure.Kesi ile
innaweza kumuweka gerezani kwa
muda wote wa maisha yake
uliobaki.Kama nilivyokueleza
awali kwamba Mathew ni kijana
wangu na ninamchukulia kama mwanangu kwa hiyo siwezi
kukubali kuona akiangamia bila
sababu.Siwezi kuishi kwa amani
katika maisha yangu yaliyobaki
kama Mathew atafungwa gerezani
kwa kosa ambalo hakulitenda.You
can live with that but I cant!
Akasema Meshack Jumbo
“Oh my God !! akasema Dr
Vivian kwa sauti ndogo
“Meshack huu si utani hata
kidogo.Nakuamuru umrejeshe
Mathew haraka sana katika
mikono ya polisi kwani bila
kufanya hivyo utafanya mambo
yazidi kuwa magumu.Nakuonya
kwa mara ya mwisho Meshack
mrejeshe Mathew katika mikono
ya jeshi la polisi ili mimi na wewe twende sawa vinginevyo
hautaamini kile
nitakachokufanyia” akasema Dr
Vivian
“Madam president huu si
utani.Mathew hatarejea tena
katika mikono ya jeshi la
polisi.Siwezi kukubali kijana
wangu akaangamia hivi hivi wakati
amefanya kila juhudi kuifanya kazi
yako uliyompatia.Kwa nini hauna
huruma Dr Vivian? Mathew
alikubali kuacha shughuli zake
zote na kwa heshima yangu
akakubali kuifanya kazi yako tena
bila hata malipo lakini leo hii
amegeuka adui kwako na unataka
kumuangamiza ? Siwezi kukubali
hilo litokee.Niko tayari kuimwaga hata damu yangu kwa ajili ya
kuhakikisha kwamba Mathew
anakuwa salama.Fanya uwezacho
madam president.Kama unaweza
kuniua usisite kufanya hivyo au
kama ni kunifunga gerezani ni
sawa kwangu lakini nitakuwa na
amani ya moyo kwamba Mathew
yuko salama” akasema Meshack na
Dr Vivian akaendelea kumtazama
kwa hasira
“Meshack why are you doing
this? Akauliza
“Because it’s the right thing to
do” akasema Meshack
“Madam president nafahamu
wasiwasi wako kwamba Mathew
anaweza akafahamu mambo
ambayo hutaki ayafahamu lakini yule ni kijana mwelewa
sana.Ukimuelewesha jambo
anakuelewa na ninakuhakikishia
madam president kwamba
Mathew ni mtu ambaye
unamuhitaji sana katika kazi
zako.Ni mtu ambaye hutakiwi
kumpoteza kabisa kwani kuna
mengi utahitaji akufanyie.Mpaka
sasa bado hajafahamu kama ni
wewe uliyemfanyia haya na
endapo akijua kwamba wewe
unahusika katika hili lililotokea
narudia kukuhakikishia madam
president kwamba utakuwa katika
hatari kubwa sana.Hata kama
akiwa gerezani Mathew anao
uwezo wa kuweza kukuangusha
kwani ana mtandao mrefu.Mathew amefanikiwa kuufahamu mpango
wa siri wa kumuua Helmet Brian
jambao ambalo hata idara yetu ya
ujasusi haikuweza kulifahamu na
yeye kwa kusaidiana na wenzake
wachache wamefanikiwa
kumuokoa waziri huyo.Unadhani
nini kingetokea endapo mpango
huo wa Marekani ungefanikiwa? Ni
wazi kwamba mpango wa
mashirikiano na Korea Kaskazini
ungeota mbawa kwani Korea
ingeingia katika vita na Marekani
lakini ni Mathew aliyefanikisha
hilo kutokea.Madam president
unamuhitaji sana Mathew hasa
kwa wakati huu na si
kumuangamiza.Kama unaona kuna
jambo lolote la siri ambalo anahitaji kulifahamu kuhusu wewe
basi unaweza ukamueleza
mapema ili alifahamu na
ninakuhakikshia kwamba Mathew
ni muelewa na atakusikiliza”
akasema Meshack
Dr Vivian akainamisha kichwa
akatafakari kwa muda na kabla
hajasema lolote simu ya mezani
ikaita akataarifiwa kwamba rais
wa Korea Kaskazini Kim Hun Yu
alikuwa katika laini ya simu ya
moja kwa moja kwa ajili ya
kuzungumza naye
“Rais wa Korea kaskazini yuko
katika laini ya simu hivi sasa
anahitaji kuzungumza
nami.Mpeleke kwanza Helmet
Brian akapumzike na halafu urejee hapa bado nina mazungumzo
nawe.Hakikisha usalama upo wa
kutosha kwani CIA wameeneza
mtandao wao hapa nchini”
“Usihofu kuhusu usalama
madam president” akasema
Meshack na rais akatoka mle
ofisini akaelekea katika chumba
cha mazungumzo ya moja kwa
moja.
Meshack Jumbo akaeleka
katika sebule ya rais alikokuwa
waziri Helmet Brian
“Mheshimiwa waziri vipi
maendelo yako?Kuna tatizo lolote
la kiafya unahisi? Yawezekana
labda kuna mahala uliumia katika
purukushani ile” “Ninajisikia vizuri sana
sijaumia na sihisi maumivu
sehemu yoyote”akajibu Helmet
“Vizuri sana.Tayari
maandalizi yamekamilika na
nimekuja kukuchukua kukupeleka
mahala pa siri utakapoishi kwa
muda utakaokuwa hapa Tanzania
ambapo ni mahala salama zaidi”
akasema Meshack Jumbo
“Asante sana.Nani
wanaonipeleka huko mahala
ninakotakiwa kwenda? Akauliza
Helmet
“Mimi na vijana wangu wa
usalama wa taifa”
“Mathew hayupo? “Hapana Mathew hayupo
mheshimiwa waziri”akajibu
Meshack
“Utanisamehe lakini
namuhitaji Mathew yule kijana
aliyeniokoa kule uwanja wa ndege
na akanikabdhi kwa rais awemo
katika timu ya watu wako
watakaonipeleka huko mahala
mnakotaka kunipeleka” akasema
Helmet Brian
“Mheshimiwa waziri kwa sasa
Mathew hawezi kupatikana kwani
yuko katika shughuli
nyingine.Ninaomba uniamini
nimekuja na vijana wenye uwezo
mkubwa wa kukulinda na ndio
watakaokuwa wakikulinda huko
mahala utakakokuwa kwa hiyo nakusihi usiwe na hofu yoyote”
akasema Meshack
“Si kwamba siamini uwezo wa
vijana wako lakini ninamuamini
sana Mathew na ndiyo maana
ninataka awepo wakati
ninapelekwa mahala mnakotaka
kunipeleka”
“Naomba uniamini Helmet
kwamba utakuwa salama bila hata
Mathew kwa hiyo usihofu
chochote.”Meshack akasisitiza
“Na mimi naomba niwe wazi
kwamba sitoi mguu wangu hapa
bila kumuona Mathew.Rais yuko
wapi nahitaji kuzungumza naye”
“Kwa sasa rais ana
mazungumzo muhimu kwenye simu,hivyo itakulazimu kusubiri
hadi atakapomaliza”
“Hakuna shaka nitaendelea
kusubiri” akasema Helmet na
Meshack Jumbo akatoka na
kuchukua simu yake na kumpigia
Mathew.
Hakuna shaka nitaendelea
kusubiri” akasema Helmet na
Meshack Jumbo akatoka na
kuchukua simu yake na kumpigia
Mathew.
“Hallow mzee Meshack”
“Mathew niko hapa ikulu na
ninahitaji msaada wako.Kabla ya
yote napenda kukujulisha kwamba
rais alinipa karatasi yenye picha za
watu watatu ambao waliletwa
nchini kwa ajili ya kumuua Helmet
Brian akanitaka tuwatafute hao
jamaa na tayari wote watatu
wamekamatwa na wako sehemu
salama tunataka kuwafanyia
mahojiano” “Hizo ni habari
njema.Hongera sana mzee kwa
uharaka huo mkubwa wa
kuwakamata watu hao.Ila nina
ombi moja kwako.”
“Omba Mathew”
“Endapo itawezekana naomba
nipewe nafasi ya kuwafanyia
mahojiano hao jamaa”
Meshack Jumbo akanyamaza
kimya alishindwa ajibu nini
“Mzee Meshack” akaita
Mathew
“Mathew nimekaa kimya
nikitafakari nikupe jibu gani lakini
nitajitahidi kufanya kila niwezalo
ili uweze kuipata nafasi hiyo ya
kuwafanyia mahojiano hao
jamaa.Tukiachana na hilo rais alinitaka niandae makazi ya siri
kwa ajili ya Helmet Brian kwa
muda wote atakaokuwa hapa
Tanzania.Tayari makazi yake
yameandaliwa na nimekuja hapa
ikulu kumchukua kumpeleka huko
lakini amegoma hatakwenda
kokote kule hadi akuone.Anataka
na wewe uwepo katika timu
itakayomtoa hapa ikulu
kumpeleka mahala alikoandaliwa
kukaa.Nakuomba sana Mathew
unisaidie kwa hilo ili Helmet
aweze kukuona na akubali
kuondoka hapa ikulu.Anakuamini
wewe pekee” akasema Meshack
Jumbo
“Mzee Meshak kwa sasa
nimeondoka pale nyumbani kwa Austin ninakwenda kuonana na
Peniela.Amewasili usiku huu na
amenitaka nikaonane naye.Kuna
masuala ya muhimu sana
nilimuomba anisaide kufanya
uchunguzi na ninakwena kupata
majibu.Labda nikitoka huko ndipo
niweze kuja ikulu kumchukua
Helmet”
“Ouh sawa
Mathew.Utakapomaliza huko kwa
Peniela utanijulisha na mimi
nitazungumza na rais kuhusu suala
hili ili ukija uweze kuruhusiwa
kuingia moja bila wasiwasi”
“Ahsante mzee nitawasiliana
nawe baadae.Vipi kuhusu polisi?
Hakuna tatizo lolote hadi hivi sasa?
Akauliza Mathew “Hakuna tatizo niachie lile
suala nitalimaliza” akasema
Meshack Jumbo na kuondoka
kuelekea katika sebule ya rais
aliko Helmet Brian
akamfahamisha kwamba tayari
amewasiliana na Mathew na
atafika pale
*******************
Akina Mathew waliwasili
nyumbani kwa bilionea Peniela.Ni
jumba kubwa lililokuwa na ulinzi
wa kutosha.Walinzi
wakawaruhusu wapite na baada ya
kushuka garini wakapokewa na
mtumishi wa ndani
akawakaribisha sebuleni.Baada ya dakika mbili akatokea
Peniela.Akawasalimia wote kwa
kuwakumbatia na kuketi sofani
“Karibuni sana na samahani
kwa kuwasumbueni usiku huu”
akasema Peniela
“Usijali Peniela.Naomba
kwanza nikutambulishe kwa hawa
wenzangu nilioambatana nao.Huyu
hapa anaitwa Austin January ni
rafiki yangu wa muda mrefu
tumewahi kufanya kazi pamoja na
sasa anajishughulisha na biashara
zake.Yule pale ni Camilla Snow
ambaye nilikuomba ndege
ikamchukue Havana.Yeye
anafanya kazi FBI lakini kwa sasa
yuko hapa nchini nikisaidiana
naye katika uchunguzi ninaoufanya” akasema Mathew na
kuwageukia akina Austin
“Jamani huyu ndiye
Peniela.Mimi naye tuliwahi kuwa
wapenzi lakini kwa sasa kila
mmoja anaendelea na maisha yake
ila tuko vizuri hatuna tatizo
lolote.Tuna mtoto mmoja anaitwa
Anna Maria” akasema Mathew na
Peniela akatabasamu .
“Karibuni sana .Nimefurahi
kuwafahamuni” akasema Peniela
“Yuko wapi Anna Maria?
Akauliza Mathew
“Yuko chumbani kwake
amelala.Amechoka sana safari
ilikuwa ndefu.Utaonana naye
kesho” “Hapana siwezi kusubiri hadi
kesho.Nipeleke mara moja
nikaonane naye sasa hivi” akasema
Mathew na Peniela akainuka
akampeleka Mathew katika
chumba cha Anna Maria aliyekuwa
amelala usingizi mzito.Mathew
akainama akambusu usoni
“I love you my
princess.Welcome to your beloved
country.This is where you belong”
akasema Mathew taratibu na
kumfunika vizuri mwanae
wakatoka mle chumbani na
Peniela akamshikamkkono
wakaingia katika sebule nyingine.
“Poleni sana kwa safari
ndefu.Imekuaje ukaamua kuja ghafla namna hii? Mathew
akaanzisha mazungumzo
“Sikuwa nimepanga kuja
Tanzania lakini ilinilazimu kuja
kwa dharura.Nilistuka tulipozuiwa
kutua katika uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere.Tuliambiwa uwanja
umefungwa kwa muda hivyo
tukatue Zanzibar.Nini hasa
kimetokea hapa Tanzania usiku
huu?Peniela akauliza
“Waziri wa mambo ya nje wa
Marekani Helmet Brian alitaka
kuuawa pale uwanja wa ndege
usiku wa leo na ndiyo sababu
uwanja umefungwa kwa muda ili
kupisha uchunguzi na kuhakikisha
ni salama kwa ndege kutua” “Nani waliotaka kumuua
waziri huyo? Akauliza Peniela
“Ni hadithi ndefu kidogo lakini
ni Marekani wenyewe ndio
waliotaka kumuua waziri wao ili
wasingizie Korea Kaskazini na
wapate sababu ya
kuishambulia.Vipi kuhusu wewe
unaendeleaje? Sikupata mrejesho
wowote toka kwako kuhusu ile
kazi niliyokuomba unisaidie”
akasema Mathew
“Mathew nashindwa nianzie
wapi lakini kwanza napenda
nikushukuru sana kwa
kunifumbua macho.Nilikupinga
mwanzoni lakini baada ya kufanya
uchunguzi nilifahamu mambo
ambayo sikuwa nimeyajua kuhusu Anderson na baba yake Andrew
Pillar” Akasema Peniela na
kumvutia zaidi Mathew
“Uligundua nini?akauliza
Mathew
“Mathew kabla sijakueleza
chochote vipi kuhusu wale rafiki
zako hawataboreka kule sebuleni
peke yao? Maelezo yangu ni
marefu kidogo” akasema Peniela
“Usijali endelea”akasema
Mathew.
“Ulinitaka nifanye uchunguzi
katika akaunti ya George Mzabwa
na vile vile kuwachunguza
Anderson na baba yake Andrew
Pillar.Ninaye mtu wangu
anayeshughulikia maslahi yangu
ndani ya Escom Bank kwa hiyo nilimtumia huyo kuweza kufanya
uchunguzi.Majibu aliyonipa ni
kwamba George Mzabwa amekuwa
akipokea fedha kutoka kampuni ya
kutengeneza saa ya Flamingo na
kiasi cha mwisho kulipwa kilikuwa
shilingi milioni mia saba na
sabini.George Mzabwa aliziondoa
fedha hizo kutoka katika akaunti
yake na kuziweka katika akaunti
tatu tofauti za kampuni ya
kuchonga madini ya vito ya
Tanbest Gemstone ltd ambayo
wamekuwa wakifanya biashara na
kampuni ya Flamingo.Katika
akaunti zile tatu za kampuni ya
Tanbest ambazo George aliweka
fedha,zilitolewa kama
ifuatavyo.Akaunti ya kwanza fedha zilitolewa na mtu anaitwa
Ranbir Kumar.Zilikuwa shilingi
milioni sabini.Akaunti ya pili fedha
zilitolewa na kuingizwa katika
akaunti ya Robert Mwainamela na
baadae zikatolewa zote.Zilikuwa
shilingi milioni mia sita na
hamsini.Akaunti ya tatu fedha
kiasi cha shilingi milioni hamsini
zilitolewa na Ranbir Kumar.Huo
ndio mtiririko wa fedha ulivyo
katika akaunti ile uliyoniomba
niichunguze” akasema Peniela na
kunyamaza kidogo halafu akasema
“Ulinitaka pia niwachunguze
Anderson na baba yake
Andrew.Nilifanya kama
ulivyoniagiza.Kwanza nilianza
kumchunguza Andrew Pillar.Nilimfuata nyumbani
kwake.Kwa muda mrefu Andrew
alikuwa ananitaka kimapenzi na
nikaamua kuitumia fursa hiyo
kuweza kupata taarifa
unazozihitaji” akasema Peniela
“I’m sorry.” Akasema Mathew
“Sorry for what? Akauliza
Peniela
“Nimekufanya ukarejea tena
katika yale maisha yako ya awali
ya kutumia mwili wako kupata
taarifa”
“Usijali kuhusu hilo.Yale ndiyo
maisha yangu na nimekwisha
yakubali.Nitakapolazimika
kufanya hivyo ili kupata taarifa za
muhimu sintasita ” akasema Peniela na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Nilimuwekea dawa ya
usingizi katika kinywaji na akalala
kama mfu nikapata nafasi ya
kufanya uchunguzi wangu.Kwanza
nilichunguza kompyuta
yake.Niligundua Andrew amekuwa
akitoa maelekezo katika kampuni
za Flamingo na ile ya A.D
Electronics.Amekuwa akiwatuma
kazi wakurugenzi wakuu wa
kampuni hizi mbili jambo
lililonifanya nijiulize maswali
kuhusu nguvu yake katika
kampuni hizi mbili.Nimechukua
barua pepe zake nimezihifadhi
katika hiki kihifadhi data na
utazipitia pengine zinaweza kuwa na msaada wowote kwako.Kutoka
kwenye kompyuta nikafungua
droo ndogo iliyoko pembeni mwa
kitanda na kukuta kuna hati mbili
za kusafiria.Moja ina jina la Edwin
Washington na nyingine ina jina la
Andrew Pillar na zote mbili zikiwa
na picha ya Andrew.Nikaendelea
kujiuliza maswali kuhusu jina
halisi la Andrew na kwa nini awe
na pasi mbili za kusafiria zikiwa na
majina tofauti?Nikarejea tena
katika kompyuta na kukuta kuna
barua pepe zimeingia na
mojawapo ilitoka kwa mtu anaitwa
Willy gadner ambayo ilimtaarifu
kuwasiliana na ofisi kuu kuna
tatizo limetokea Tanzania.Hizo
barua pepe zote nimekuwekea katika kihifadhi data hicho
nilichokupatia.Nilichunguza pia
kuhusu uhusika wa Andrew Pillar
katika kampuni za Flamingo na A.D
Eletronics nikagundua kwamba
kampuni hizi zote mbili
zinamilikiwa na mtu mmoja
anaitwa Edwin Washington
ambaye ndiye huyo huyo Andrew
Pillar.Nilikwenda pia nyubani kwa
Anderson lakini wakati nikifanya
uchunguzi kumbe Anderson
ameweka mtambo maalum wa
kufuatilia kila kinachoendelea
chumbani kwake wakati hayupo
na hivyo akagundua kwamba
nilikuwa napekua chumba chake
na kufunga kila kitu kwa kutumia
simu yake.Baadae akaja mle chumbani lakini nilifanikiwa
kumpiga na kitu kichwani
akapoteza fahamu na ndipo
nilipoamua kuondoka Paris
haraka na kuja Tanzania.Hayo
ndiyo niliyofanikiwa kuyafahamu
na ninakushukuru sana Mathew
kwa kunisaidia kuwafahamu wale
watu kuwa ni waongo na kuna
mambo mengi
wanayaficha.Ninachotaka
kufahamu,ni kitu gani hasa
kinachoendelea kuwahusu
wao?akauliza Peniela
“Peniela kwanza kabisa
nashukuru sana kwa kazi hii
kubwa na ya hatari uliyoifanya
ambayo itatusaidia sana katika
uchunguzi wetu.Kwa ufupi tu kwa kuwa hatuna muda wa kutosha
nitakueleza kwa kifupi.Kuna
mtandao wa CIA hapa Tanzania
ambao umetengenezwa kwa
malengo maalum.Mtandao huu
ndio uliohusika na kifo cha rais
Anorld Mubara ambaye alifariki
katika ajali ya ndege.Rais Dr Vivian
aliniomba nimsaidie kufanya
uchunguzi kuhusiana na nani
waliomuua baba yake kanali
Sebastian matope.Baada ya kuanza
kuchunguza ndipo nilipogundua
kwamba Marekani wanahusika
katika kifo kile na nikabaini kuna
mtandao wa CIA hapa nchini na
unawahusisha hadi viongozi
walioko serikalini na mmoja wa
watu hao alikuwa ni mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa
ambaye alijiua kwa kujipiga risasi
vile vile waziri wa mambo ya nje
Dr Robert Mwainamela ambaye
ameuawa usiku huu na mauaji
yake yamefanyikanyikia nyumbani
kwangu na mimi kubebeshwa
mzigo huo wa mauaji ya huyo
waziri”akasema Mathew
“Unatuhumiwa kwa mauaji?!!
Peniela akauliza kwa mshangao
“Ndiyo nina tuhuma za
kumuua waziri wa mambo ya nje”
“Hivi sasa unatafutwa?
Akauliza tena Peniela
“Nilikuwa katika mikono ya
polisi lakini nimeondolewa kwa
muda .Tuachane na hayo ambayo
kwangu ni mambo ya kawaida.Baada ya kumchunguza
George Mzabwa ndipo tukagundua
kwamba ana akaunti katika benki
ya Escom ambayo na wewe ni
mmoja wa wamiliki ndipo
nilipokuomba msaada wako
unisaidie kuchunguza lengo likiwa
ni kuufahamu mtandao wote wa
CIA hapa nchini.Umefanya kazi
nzuri sana na sasa twende
tukaungane na akina Austin na
kwa pamoja tujadiliane nini
tufanye” akasema Mathew
“Mathew kabla hatujaenda
huko kuonana na wenzako
nakuomba samahani sana kwa
mambo yale mabaya
niliyokutendea.I did many awfull
things to you and I’m so sorry for that” akasema Peniela lakini
Mathew akamzuia asiendelee
“Penny tutazungumza mambo
hayo kwa wakati wake na isitoshe
hayo yote ni mambo yaliyokwisha
pita.Kwa sasa tujielekeze katika
mambo makubwa yanayotukabili”
akasema Mathew
“That woman Camilla is she
your lover? Akauliza Peniela
“Peniela naomba tuachane na
hayo mambo kwa
sasa.Tutazungumza baadae”
akasema Mathew kisha wakatoka
na kuelekea sebuleni
walikokuwapo Austin na Camilla
“Samahani kwa kuwaacha
wenyewe kuna mambo ambayo Peniela alikuwa ananieleza”
akasema Mathew
“Kwanza ni kuhusiana na
uchunguzi wa ile akaunti ya
George Mzabwa.Peniela ni mmoja
wa wamiliki wa Escom bank kwa
hiyo imekuwa rahisi kwake
kuweza kupata taarifa za
kuhusiana na akaunti ile ya
George.Taarifa alizozipata ni
kwamba George aliingiziwa fedha
nyingi kiasi cha shilini milioni mia
saba na sabini kutoka katika
kampuni ya kutengeneza saa ya
Flamingo ya nchini
Marekani.Baadae fedha hivi
alizitoa na kuzitawanya katika
akaunti tatu ambazo zote ni za
kampuni ya Tanbest Gemstone.Katika akaunti ya
kwanza pesa zilitolewa na Ranbir
Kumar kiasi cha shilingi milioni
sabini.Katika akaunti ya pili pesa
zikatolewa na Robert
Mwainamela.Hizi zilikuwa nyingi
kiasi cha shilingi milioni mia sita
na hamsini.Akaunti ya tatu fedha
zikatolewa na Ranbir Kumar kiasi
cha shilingi milioni hamsini.Huo
ndio mgawanyo wa fedha ambayo
George alipokea kutoka kampuni
ya Flamingo.Baada ya kupata
taarifa hizo kuna maswali ambayo
lazima tujiulize na kuyatafutia
majibu.Kwanza tuliambiwa
kwamba kampuni ya Tanbest na
Flamingo zinafanya biashara lakini
fedha kutoka Flamingo zinapitia katika akaunti binafsi ya George
Mzabwa badala ya akaunti ya
kampuni.Akipokea fedha hizo
George huzigawanya katika
akaunti za kampuni hiyo.je Gerge
ndiye mmiliki wa kampuni ya
Tanbest hadi fedha zote zipitie
kwake?Tunaona pia fedha
zilizowekwa katika akaunti tatu za
kampuni ya Tanbest
zinavyochukuliwa.Ranbir Kumar
anachukua kiasi cha shilingi
milioni mia moja na ishirini na
zilizobaki kiasi cha shilingi milioni
mia sita hamsini zilichukuliwa na
Dr Robert.Swali la kujiuliza je Dr
Robert ana uhusiano gani na
kampuni hii hadi awe na uwezo wa
kuingia katika akaunti ya kampuni na kuchukua fedha nyingi kiasi
hiki?Je naye ni mmoja wa wamiliki
wa kampuni hii?Amezipeleka wapi
fedha nyingi kiasi hicho? Akauliza
Mathew na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea.
“Tukiachana na hilo
nilimuomba pia Peniela anisaidie
kuwafanyia uchunguzi wa kina
Anderson pillar na baba yake
Andrew Pillar ili tujue kwa nini
benki wanayomiliki inatumiwa na
Flamingo kupitishia fedha kuja
Tanzania.Peniela amefanya
uchunguzi na amegundua kwamba
Andrew Pillar ana hati mbili za
kusafiria.Moja ina jina la Andrew
Pillar na nyingine ina jina la Edwin
Washington.Alikwenda mbali zaidi na akagundua kwamba Edwin
washington ndiye mmiliki wa
kampuni za Flamingo na A.D
Elecronics.Sasa tumepata picha
kwamba kampuni hizi zote mbili
ziko chini ya serikali ya Marekani
kupitia shirika lake la ujasusi la
CIA na moja kwa moja Andrew au
Edwin vyovyote anavyojiita ni
jasusi wa CIA.Ili kulithibtisha hilo
Peniela amekuja na na barua pepe
ambazo alizitoa katika kompyuta
ya Andrew” akasema Mathew na
kuchukua kompyuta ya Peniela
akachomeka kile kifaa cha
kuhifadhi kumbu kumbu na barua
pepe zile ambazo Peniela
alizichukua kutoka katika
kompyuta ya Andrew Pillar zikajitokeza na kompyuta akapewa
Camilla akaanza kuzipitia.
“Willy gadner? Akauliza baada
ya kusoma barua pepe ya mwisho
“Huyu ni mkurugenzi wa
CIA.Hapa hakuna shaka kwamba
Andrew ni jasusi wa CIA” akasema
Camilla baada ya kuzipitia zile
barua pepe
“Oh my God ! kwa nini
sikuliona hili toka mapema? Watu
hawa walikuwa na lengo gani
kwangu? Akauliza Peniela
“Usihofu Peniela watu hawa
walikuwa wanataka kukutumia tu
kwa faida zao.Imekuwa vyema
umewafahamu mapema” akasema
Mathew “Baada ya kugundua kuhusu
hilo nini kinaendelea? Austin
akauliza
“Tunachotakiwa kukifanya
kwa sasa ni kuhakikisha tunaupata
mtandao wote wa CIA hapa
nchini.Ninaamini fedha zile
ambazo Dr Robert alizichukua
zilikuwa ni kwa madhumuni ya
kufanikisha mipango mbali mbali
ya CIA hapa nchini.Kampuni hii ya
Tanbest ni kichaka tu cha
kupitishia fedha za CIA.Inatakiwa
kuchunguzwa sana” akasema
Mathew
“Kwa kuwa Peniela tunaye
hapa ambaye ni mmoja wa
wamiliki wa benki ya Escom
ninashauri tuendelee kudukua ili tuweze kufahamu zaidi kuhusiana
na hii kampuni ya Tanbest ambayo
inaonekana ndiyo inayotumika
kupitishia fedha za CIA kuja
Tanzania kufadhili operesheni
mbalimbali za CIA kwa kigezo cha
kufanya biashara na kampuni ya
Flamingo.Ninaweza kuingia katika
mtandao wa benki hii na kudukua
zaidi ili tufahamu zaidi kuhusiana
na hii benki” akasema Camilla.
“Hilo ni wazo zuri
sana.Peniela utamsaidia Camilla
kuingia katika mtandao wa benki
yenu na kudukua taarifa muhimu
za kutusaidia” akasema Mathew na
bila kupoteza muda Camilla
akaanza kazi yake ya
udukuzi.Wakati Camilla akiendelea Peniela akamuomba
Mathew wakaongee
chumbani.Wakawaacha Camilla na
Austin sebuleni wakaenda
chumbani kwa Peniela.
“Unasemaje Peniela? Akauliza
Mathew
“Mathew mimi na wewe
tumetoka mbali.Ninathubutu
kukiri kwamba wewe ni kama
malaika ambaye Mungu alikutuma
uje unikomboe.Nimefika hapa
nilipo kwa sababu ya jitihada
zako.Kama usingeyatoa maisha
yako kupambana kufa na kupona
kwa ajili yangu leo nisingekuwa
Peniela huyu ambaye dunia nzima
inaniheshimu.Mathew sipati neno
zuri la kueleza ni jinsi gani nimeumizwa na mambo
niliyokutendea.Baada ya
kugundua kwamba Anderson na
baba yake walinifanya nikaachana
nawe kwa faida yao wenyewe
nimeumia sana.Nimejiona ni kwa
jinsi gani nilivyokuwa mjinga kwa
kuacha mbachao kwa msala
upitao.Nikiwa angani nilimuomba
sana Mungu anifikishe salama
Tanzania ili niweze kukwambia
maneno haya ana kwa ana
kwamba ninaomba sana msamaha
wako kwa mambo yale
niliyokukosea.Najua una moyo wa
kipekee kabisa na utatafuta namna
ya kunisamehe.Fahamu kwamba
nafasi yako moyoni mwangu bado
ipo japo sijui kama ..” “Peniela stop that.” Akasema
Mathew.
“Kwa sasa kuna mambo
makubwa
yanayonikabili.Ninakabiliwa na
tuhuma za mauaji na kama si kwa
jitihada za mzee Meshack Jumbo
ningeozea gerezani.Kuna mambo
makubwa yanaoendelea hapa
nchini.Mpaka sasa bado
sijafanikiwa kufahamu mahala
ilipo football,maisha ya rais Dr
Vivian yanaonekana yako hatarini
na mimi ninapaswa kumuokoa”
akasema Mathew
“Mathew mimi niko pamoja
nawe katika suala hili na
tutapambana bega kwa bega hadi
tuhakikishe tunamaliza masuala haya salama na ninaomba uniahidi
kitu kimopja tu kwamba baada ya
mambo haya kumalizika basi
tutazungumza kuhusu masuala
yetu mimi na wewe”
“Sawa tutazungumza”
akasema Mathew
“Thank you so much
Mathew.Sasa nisikilize kwa
makini.Nimekuita huku pembeni
kwa jambo mahsusi ambalo
sikutaka kukueleza mbele ya wale
wenzako kutokana na unyeti
wake” akasema Peniela
“Kuna siri ambayo bado
hujaifahamu kuhusu kampuni ya
Tanbest gemstone ltd.Hii ni
kampuni inayomilikiwa kwa siri
na rais Dr Vivian matope”Sura ya Mathew ilionyesha
mstuko mkubwa kwa taarifa ile
toka kwa Peniela
“No that’s not true !! akasema
Mathew huku akitoa kicheko
kidogo
“Ninamfahamu Dr Vivian ni
mmoja kati ya viongozi wachache
waadilifu sana katika bara hili la
Afrika na hawezi kamwe
kujihusisha na kampuni kama hii
ambayo inatumiwa na Marekani
katika kufadhili operesheni zake
chafu nchini Tanzania”akasema
Mathew
“Mathew ndiyo maana
nikakwambia kwamba hili jambo
ni siri kubwa na wengi
hawalifahamu.Nimeamua kukwambia wewe ukweli na
ninaomba uniamini” akasema
Peniela na Mathew akamtazama
kwa sekunde kadhaa
“Peniela we’re at very serious
situation right now so I don’t need
any joke” akasema Mathew
“Mathew this is not a
joke.Please trust me.Kampuni hii
ya Tanbest gemstone ltd mmiliki
wake ni Vivian Matope”
“Dr Vivian ?!! akauliza Mathew
ambaye bado alikuwa katika
mshangao mkubwa sana.
“Mathew najua taarifa hizi
zimekustua sana lakini huo ndio
ukweli”akasema Peniela
“Peniela sijawahi kutilia
shaka taarifa yoyote ile uliyowahi kunipa lakini ninapatwa na wakati
mgumu kukuamini katika
hili.Tanbest ni kampuni ambayo
inatumiwa na Marekani katika
kupitisha fedha ambazo
wanazitumia katika operesheni
zao chafu hapa Tanzania.Iweje Dr
Vivian asilifahamu hilo? Akauliza
Mathew
“Mathew kama hujawahi
kuniamini huko nyuma katika
jambo lolote naomba uniamini
katika hili.Ni kweli Dr Vivian
matope ndiye mmiliki wa kampuni
ya Tanbest” akasema
Peniela.Mathew bado aliendelea
kumtazama kwa macho ya
mshangao “Peniela are you sure about
this?
“Ndiyo Mathew.Nina uhakika
na hili ninalokwambia.Kama bado
huniamini nakuomba ufanye
uchunguzi na utabaini kwamba
sisemi uongo” akasema Peniela na
Mathew akashika kiuno
alionekana kuwa na mawazo
mengi.
“Kampuni hii tunaituhumu
kwa kutumiwa na Marekani
kupitia CIA kupitishia fedha chafu
zinazofadhili operesheni
mbalimbali za CIA hapa nchini na
sikuwahi kuhisi kama inaweza
ikamuhusisha Dr Vivian.Hata hivyo
uchunguzi wa kutosha unatakiwa kufanyika ili kubaini ukweli wa
jambo hili” akasema Mathew
“Ukiachana na hilobado kuna
jambo lingine ambalo naamini
bado hulifahamu”akasema Peniela
na kumtazama Mathew
“Dr Vivian ana akauntiya siri
katika benki ya Escom ambayo
huhifadhi fedha nyingi isiyolipiwa
kodi.Viongozi wengi kutoka
mataifa mbali mbali huficha fedha
katika benki hii na Dr Vivian ni
mmoja wao” akasema Peniela
Ilimchukua Mathew dakika
moja kusema chochote.
“Peniela haya mambo
uliyonieleza yamenistua sana na
sikutegemea kuyasikia masikioni
mwangu.Sijui nifanye nini”akasema Mathew na kurejea
sebuleni walikowaacha Austin na
Camilla
“Kuna chochote
kimepatikana? Akauliza Mathew
“Hapana bado” akajibu
Austin.Mathew akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Kuna jambo ambalo
nimeelezwa na Peniela limenistua
sana”
Camilla akaacha kazi
aliyokuwa anaifanya na
kumgeukia Mathew
“Ni jambo gani? Akauliza
Austin “Peniela amenieleza kwamba
kampuni ya Tanbest Gemstone inamilikiwa kwa siri na rais Dr
Vivian matope”
Wote wawili Austin na Camilla
wakapatwa na mshangao mkubwa.
“Mathew hizi ni taarifa nzito
sana.Peniela ana uhakika nazo?
“Ndiyo nina uhakika nazo
lakini kama mnazitilia shaka
ninawaomba mfanye uchunguzi na
mtaubaini ukweli” akasema
Peniela kwa kujiamini.
“Mathew do you trust her?
Akauliza Austin.Mathew
akamtazama Peniela halafu
akasema
“I do”
“Peniela ni mmoja wa
wamiliki wa benki ya Escom
ambayo Tanbest wana akaunti pale kwa hiyo ni rahisi kwake
kufahamu kuhusiana na benki hii
lakini pamoja na hayo lazima
tujiridhishe kwamba ni kweli Dr
Vivian ndiye mmiliki wa hii
kampuni? Kama ndiyo anafahamu
kinachoendelea kupitia kampuni
yake? Swali lingine ambalo
nimejiuliza baada ya kupata
taarifa hii ni je George Mzabwa
anaingiaje katika kampuni hii?Dr
Robert naye anahusika vipi katika
hii kampuni hadi afikie hatua ya
kuingia katika akaunti ya kampuni
na kuchota fedha?Haya ni maswali
ambayo yanaweza kutusaidia
katika kuufahamu ukweli wa
jambo hili.Ukiacha hilo kuna
jambo lingine” akasema Mathew na simu yake ikaita akasogea
pembeni kuipokea.Alikuwa ni
Meshack Jumbo
Hallow mzee Jumbo”
“Mathew umefika wapi?
Tayari umekwisha anza safari ya
kuja ikulu? Akauliza Meshack
Jumbo
“Hapana mzee Jumbo bado
sijaanza safari ya kuja
huko.Nimekuja kuonana na
Peniela”
“Mathew kama nilivyokueleza
kwamba Helmet Brian amegoma
kuondoka hapa ikulu bila ya
kukuona wewe hivyo nakuomba
uahirishe shughuli zako nyingine
na uje mara moja hapa ikulu
tuweze kumuondoa Helmet hapa na kumpeleka mapumzikoni”
akasema Meshack Jumbo
“Mzee kuna jambo ambalo
nataka nikushirikishe”
“Jambo gani Mathew?
“Kuna kitu nimekipata
ambacho kimenistua kidogo.Kuna
hii kampuni ya kuchonga madini
ya vito ya Tanbset Gemstone ltd
ambayo tumegundua na
mashirikiano ya kibiashara na
kampuni ya kutengeneza saa ya
Flamingo iliyoko
Marekani.Kampuni hii ya Flamingo
na kampuni ya A.D Electronics
aliyokuwa anafanya kazi Nathan
zote ni kampuni zilizo chini ya
serikali ya Marekani kupitia
shirika lake la CIA.Flamingo wamekuwa wakinunua madini ya
vito kutoka kwa kampuni ya
Tanbest lakini kitu cha kushangaza
tumegundua kwamba kuna fedha
kiasi cha shilingi milioni mia saba
na sabini ziliweka katika akaunti
ya George iliyo katika benki ya
Escom kutoka kampuni ya
Flamingo na baadae George
alizitoa fedha hizo akaziweka
katika akaunti tatu tofauti ambazo
tulipozifuatilia tukagundua zote ni
akaunti za kampuni ya
Tanbest.Tumechimba zaidi na
kugundua kwamba katika moja ya
akaunti hizi tatu ambazo George
aliweka kiasi cha shilingi milini
mia sita na hamsini fedha hizo
zilichukuliwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi Dr Robert
Mwainamela.Tumejiuliza maswali
Dr Robert au George wanahusikaje
na kampuni hii ya Tanbest?George
Mzabwa na Dr Robert Mwainamela
wote walikuwa katika mtandao wa
CIA kwa hiyo ni wazi Marekani
wanaitumia kampuni ya Tanbest
kupitishia fedha zao chafu kwa ajili
ya kufadhili operesheni zao mbali
mbali hapa nchini.Kikubwa zaidi
kilichonistua ni kwamba kampuni
hii ya Tanbest mmiliki wake ni rais
Dr Vivian matope”
“What ?!! Meshack Jumbo naye
akapatwa na mshangao mkubwa
“Mathew una hakika na hilo
unalolisema?akauliza “Ndiyo mzee Jumbo.Nina
uhakika nalo.Nimelipata toka kwa
mtu ambaye siwezi kumtilia
shaka” akasema Mathew
“Una ushahidi wowote wa
kumuonyesha Dr Vivian kwamba
ndiye mmiliki wa hiyo kampuni ya
Tanbest?
“Ninalifanyia kazi hilo suala
na nitakapopata ushahidi
wakutosha nitakujulisha” akasema
Mathew.Ukimya wa sekunde
chache ukapita kisha Meshack
Jumbo akasema
“Mathew jambo hili ni zito
hivyo ninakuomba
usiliharakishe.Nenda nalo taratibu
na ulifanyie uchunguzi wa kina na
upate ushahidi wa kutosha wa kumuhusisha rais Dr Vivian na
hiyo kampuni.Yawezekana ikawa
ni njama iliyotengenezwa
kumchafua hivyo kuwa makini
sana na taarifa kama hizi.Wakati
ukiendelea na uchunguzi wako
nakuomba uje hapa ikulu ili
tuweze kumuondoa Helmet Brian
hapa na kumpeleka sehemu
salama halafu utaendelea na
uchunguzi wako.Umenielewa
Mathew?
“Nimekuelewa mzee”
“Ahsante sana.Kama kuna
chochote ambacho unaona
ninaweza kukusaidia basi usisite
kunieleza na mimi nitakusaidia ili
uweze kuukamilisha uchunguzi
wako.Nakuomba mara moja hapa ikulu” akasema Meshack Jumbo na
kukata simu.Mathew akawafuata
wenzake
“ Nimeitwa ikulu mara
moja.Nahitajika kwenda
kumchukua waziri Helmet Brian
na kumpeleka sehemu
salama.Amegoma kutoka ikulu
hadi anione” akasema Mathew
“Mathew una uhakika na
hicho walichokueleza? Usije kuwa
unawekwa mtegoni ili
wakukamate tena” akasema Austin
“Hapana huu si
mtego.Meshack Jumbo hawezi
kunidanganya.Lazima litakuwa ni
jambo la kweli” akasema Mathew
na kuwataka waendelee kuchunguza wakati akielekea
ikulu
“Mathew are you sure you
want to go there? Peniela
akamuuliza Mathew wakati
akiingia garini
“Ndiyo Peniela.Nadhani
unanifahamu vyema kuliko mtu
yeyote mimi huwa siogopi.Usihofu
I’ll be fine” akasema Mathew na
kuwasha gari lake akaondoka
kuelekea ikulu
*****************
Dr Vivian alimaliza
mazungumzo na rais Kim Hun Yu
na mara tu alipotoka akakutana na
Meshack Jumbo akimsubiri “Jumbo bado uko hapa?
Hujampeleka Helmet
kupumzika?akauliza Dr Vivian
“Madam president we need to
talk”
“Not right now Jumbo.I have
some many important things to
do.Take Helmet to safe house then
come back and we’ll talk” akasema
DrVivian ambaye alionekana kuwa
na haraka
“Mheshimiwa rais tuna tatizo
kidogo kuhusu Helmet” akasema
Meshack na kumfanya Dr Vivian
asimame akamtazama kwa muda
halafu akamtaka waelekee katika
chumba cha maongezi ya faragha.
“Kuna nini Meshack? Helmet
ana tatizo gani? Akauliza Dr Vivian “Helmet amegoma kuondoka
hapa hadi atakapomuona Mathew”
“Is he crazy?!!
“Hayo ndiyo masharti yake
aliyoyatoa kwamba hatanyanyua
mguu wake hapa ikulu hadi
atakapomuona
Mathew.Hamuamini mtu yeyote
zaidi ya Mathew ambaye ndiye
aliyemuokoa kutoka katika ule
mpango wa kumuua”
“Oh my Gosh ! akasema Dr
Vivian na kushika kiuno.
“I told you madam president
that we still need him.Mathew
bado ana msaada mkubwa kwetu”
“Ninakwenda kuzungumza na
Helmet kwamba Mathew hataweza
kupatikana na nitampa ulinzi mkali kuelekea huko mahala
anakopelekwa hata wanajeshi
ikibidi.Simuhitaji Mathew hapa
tena.Ninataka kusikia Mathew
yuko katika mikono ya polisi”
akasema Dr Vivian huku akianza
kupiga hatua
“Madam president don’t do
that” akasema Meshack na Dr
Vivian akasimama
“Tayari nimemuhakikishia
Helmet kwamba Mathew yuko
njiani anakuja na hivi tuongeavyo
tayari nimekwisha wasiliana naye
atafika hapa ikulu muda wowote”
“What ?!! How can you do that
Meshack?Kwa nini
unanipuuza?Kwa nini hutaki
kufuata kile ninachokuelekeza?Nimekuelekeza
kwamba Mathew arejeshwe katika
mikono ya polisi lakini umepuuza
na badala yake unamruhusu aje
hapa ikulu.Unataka kunijaribu?
Akauliza Dr Vivian kwa hasira
“Si hivyo madam
president.Sina nia ya kukujaribu”
“Kama huna nia ya kunijaribu
kwa nini unafanya mambo
kinyume na maelekezo yangu?
“Nilidhani tulikwishalimaliza
hili suala la Mathew na
tukaelewana” akasema Meshack
Jumbo
“Meshack hatukuwa
tumeelewana chochote.Msimamo
wangu uko pale pale kwamba
Mathew arejeshwe haraka sana mikononi mwa polisi na
afunguliwe mashtaka ya mauaji.I
want Mathew to disapear !!
akasema Dr Vivian kwa
hasira.Akamtazama Meshack
Jumbo kwa macho makali
“Madam presdient kuna
jambo ambalo nataka
nikufahamishe”
“kama ni kuhusu Mathew
sitaki kusikia tena nataka
arudishwe katika mikono ya polisi
ndani ya dakika thelathi kutoka
sasa vinginevyo nitakuharibu
Meshack.Mimi sijaribiwi.Ni mtu
mbaya sana ukitaka kujaribu
nguvu yangu hivyo kama unataka
usalama na mimi mrudishe Mathew haraka sana kwa polisi!!
Akafoka Dr Vivian
“Madam president jambo
ulilotaka Mathew asilifahamu
tayari amekwisha lijua” akasema
Meshack na kumstua Dr Vivian
“Unasemaje?
“Nnasema kwamba lile jambo
ulilotaka Mathew asilifahamu
tayari amekwisha lifahamu”
“Sikuelewei unachokisema
Meshack.Amejua jambo
gani?akauliza Dr Vivian
“Mathew tayari amefahamu
kwamba wewe ndiye mwenye
kampuni ya Tanbest Gemstone ltd”
Sura ya Dr Vivian ilionyesha
mstuko mkubwa sana na kwa
sekunde kadhaa alibaki mdomo wazi akashindwa aseme
nini.Walitazamana kwa muda
halafu akatoa kicheko kidogo
“Hicho mbona
kichekesho?Kampuni ya Tanbest?
Inajushughulisha na nini hiyo
kampuni kwani siifahamu kabisa”
akasema Dr Vivian
“Madam president japokuwa
midomo yako inakana kuifahamu
kampuni hii lakini sura yako
inaonyesha wazi mstuko ulio upata
kwa hiyo tusiendelee kupoteza
muda hali kila kitu kiko
wazi.Kampuni hii ya Tanbest
imekuwa inatumiwa na kampuni
ya Flamingo ambayo inamilikiwa
na CIA kupitishia fedha kwa ajili ya
operesheni zake chafu nchni Tanzania.Hizi operesheni zote za
Marekani zinazofanyika hapa
Tanzania fedha zake zinapitia
katika kampuni hii.Taarifa zote
Mathew anazo na hivi sasa yuko
njiani kuja hapa ikulu and he need
answers,I also need answers!!
Kwa mara ya kwanza Meshack
Jumbo akamshuhudia Dr Vivian
mwanamke anayetajwa kuwa na
ujasiri wa ajabu, midomo
ikimtetemeka akishindwa kujibu
swali
“Madam president please
trust me and tell me the truth.Is
this company yours?!! Akauliza
Meshack Jumbo lakini Dr Vivian
alibaki kimya hakujibu kitu “Mheshimiwa rais toka
mwanzo nilikueleza kwamba
unaweza kuniamini na kunieleza
siri yoyote ile na mimi nitakuwa
msiri wako.Mpaka sasa Mathew
hajui kama amri ya kumuua Dr
Robert Mwainamela imetoka
kwako.Hii ni siri ambayo
nitakwenda nayo
kaburini.Ninakuonyesha ni kwa
namna gani unavyoweza
kuniamini heshimiwa rais.Mimi
sipaswi kuwa adui yako bali
unapaswa kunifanya mtu wako wa
karibu kwani ninayafahamu
mambo mengi ya kiusalama
ninafahamu namna ya kuweza
kuyamaliza mambo kimya kimya
na hata marais wote niliofanya nao kazi awali wamenitumia sana
katika mambo yao ya siri.Hata hili
la Mathew ninaweza kulimaliza na
mambo yakaenda vizuri ili mradi
unieleze ukweli bila
kunificha.Niweke wazi baadhi ya
mambo ambayo unadhani
ninapaswa kuyafahamu” akasema
Meshack Jumbo
Dr Vivian akainamisha kichwa
akafikiri kwa muda na kusema
“Nataka nionane na Mathew
pindi akifika hapa”
“Sawa madam president”
akasema Meshack Jumbo kisha
rais akatoka na kuelekea sebuleni
alikokuwa amekaa waziri Helmet
Brian “ Helmet Brian” akasema Dr
Vivian
“Mheshimiwa rais” akasema
Helmet
“Kama nilivyokueleza awali
kwamba tutakupeleka sehemu
salama ya kukaa kwani hivi sasa
Marekani watakuwa wanakusaka
kila kona.Ninaamini tayari
wamekwisha fahamu kwamba
mpango wao umeshindwa
kufanikiwa hivyo watakutafuta
kwa udi na uvumba na ndiyo
maana nimeagiza upelekwe
sehemu salama ambako utaishi
huko hadi tutakapopata ushahidi
usio na shaka kwamba ni kweli
Marekani walipanga mpango wa
kukuua.Nimeambiwa kwamba umegoma kuondoka hadi
utakapomuona Mathew” akasema
Dr Vivian
“Ahsante sana mheshmiwa
rais,ni kweli nimekataa kuondoka
hapa hadi nitakapomuona yule
kijana Mathew.Nimetokea
kumuamini sana kwani ndiye
aliyeyaokoa maisha
yangu.Mheshimiwa rais yule kijana
ni mahiri sana na Tanzania ina
bahati mno kuwa na mtu mahiri
kama yule” akasema Helmet na Dr
Vivian akatabasamu
“Watu watatu ambao
walitumwa kuja Tanzania kwa kazi
ya kukuua tayari wamekamatwa
na muda si mrefu tutaanza
kuwahoji ili tupate taarifa za kutosha kutoka kwao.Hao ndio
watakaotupa ukweli kuhusu
mpango huu” akasema Dr Vivian
na tabasamu likajengeka usoni
kwa Helmet Brian
“Vyombo vyako vya ulinzi
vinafanya kazi nzuri sana hadi
vimeweza kuwakamata watu hao
ndani ya kipindi kifupi.Tafadhali
naomba watu hao wahojiwe hadi
waseme ukweli.” Akasema Helmet
na ukimya mfupi ukapita kisha
Helmet akasema
“Nimewaza sana kwa nini
watake kunitoa kafara? Nimekuwa
mtiifu sana kwa nchi yangu na
nimefanya kila lililowezekana kwa
ajili ya nchi yangu lakini malipo
yangu ndiyo haya.Nimeumizwa sana na hili
jambo.Kinachonisikitisha zaidi ni
kwamba Mike straw ni rafiki yangu
mkubwa sana na nina hakika
jambo hili analifahamu lakini
hakufanya chochote na akabariki
niuawe.Mheshmiwa rais naomba
unisaidie kupata ushahidi usio na
shaka kuhusu hili jambo halafu
nitajua nini cha
kufanya.Wamarekani wanapaswa
kufahamu serikali yao ilivyo na
watafanya maamuzi” akasema
Helmet
“Siwezi kumtetea Mike straw
lakini unapokalia kiti kama hiki
kuna nyakati unajikuta
unalazimika kufanya maamuzi
ambayo hukuwa umefikiria kuyafanya.Ninaamini hata Mike
hakupenda kufanya hivi lakini
alilazimika kufanya hivyo kwa
maslahi mapana na taifa
lake.Sitaki kuhalalisha
alichokifanya lakini kuna nyakati
sisi kama marais tunalazimika
kufanya maamuzi magumu kama
hayo” akasema Dr Vivian
“Nalifahamu hilo Dr
Vivian.Nafahamu ugumu wa
kukalia hicho kiti lakini kwa Mike
hakupaswa kunifanyia kitu kama
hiki hasa baada ya mambo yote
niliyomfanyia.Mimi ndiye
niliyepaswa kuwa rais wa
Marekani lakini kutokana na
urafiki wetu mkubwa niliamua
kujitoa katika mbio za kuwania urais na kumpa yeye nafasi lakini
amesahau hayo hote na anataka
kuniua.Nimemshauri sana kutumia
busara katika suala la Korea
Kaskazini lakini Lengo lake ni
kuanzisha vita na ndiyo maana
anafikia hatua ya kufanya
maamuzi kama haya.Marekani
hatuwezi kukubali kuwa na rais
kama huyu lazima nihakikishe
nimemuondoa madarakani”
akasema Helmet na Dr Vivian
akatabasamu
“Tatizo kubwa alilonalo rais
wenu ni kukosa busara na kufanya
maamuzi ya hasira bila kufikiri
athari za maamuzi
anayoyachukua.Matamshi yake
hayamuonyeshi kama anafaa kuwa rais wa Marekani.Kwa miaka yote
marais wa taifa hili kubwa duniani
wamekuwa ni mfano kwa maraisi
wa mataifa mengine kwa matendo
na maamuzi yao lakini kwa huyu
amekuwa ni tofauti sana.Amekuwa
ni rais mwenye matamshi na kauli
za hovyo sana kuwahi kutokea
katika taifa la Marekani na
kuifanya heshima ya taifa hili
machoni pa mataifa ishuke.Sikuwa
nimepanga kuingia katika
mashirikiano na Korea Kaskazini
na wala siungi mkono mpango
wake wa kutengeneza makombora
lakini kauli za dharau kutoka kwa
Mike straw zilinifanya nikubali
kufanya mashirikiano na Korea
kaskazini.Kwa sababu ya kauli zake za dharau dunia hivi sasa
imegawanyika sehemu mbili nchi
zinazoiunga mkono Marekani na
nchi zinazounga mkono Korea
Kaskazini.Pamoja na mgawanyiko
huo bado anataka kuanzisha vita
na Korea kaskazini na hii inaweza
kupelekea kuzuka kwa vita
inayoweza kuitwa ya tatu ya dunia
kwani mataifa yanayoiunga mkono
Marekani yatapigana na yale
yaliyotanganza kuiunga mkono
Korea kaskazini na hii
itasababisha maangamizi
makubwa dunaini kwani mataifa
mengi yana umiliki wa silaha kali
na mengine ya silaha za
nyuklia.Nimetoka kuzungumza na
rais wa Korea kaskazini sasa hivi anasema kwamba ameyaweka
majeshi yake katika tahadhari
baada ya kupata taarifa kwamba
kuna mipango ya siri ya Marekani
kuishambulia nchi yake.Kim Yun
Hu ameapa kutumia silaha zake
kali kuiangamiza Marekani.Korea
Kaskazini ina makombora yenye
kubeba vichwa vya nyuklia na
uwezo wa kuishambulia
Marekani.Damu itamwagika kila
kona ya dunia”akasema Dr
Vivian.Helmet akainamisha kichwa
akazama mawazoni.Baada ya
dakika moja akasema
“Unachokisema mheshimiwa
rais ni kitu cha kweli kabisa na
mimi kama waziri wake wa
mambo ya nje nimekuwanikijitahidi sana kuepuka jambo
hilo lisitokee kwani namfahamu
vizuri Mike ni mtu ambaye hana
uvumilivu hata kidogo na ilikuwa
ndoto yake ya muda mrefu siku
moja kuishambulia Korea
kaskazini na sasa anatafuta kila
njia ya kuitimiza ndoto yake.Ni
mimi pekee ambaye nimekuwa na
uwezo wa kusimama na kumtaka
atumie busara katika suala la
Korea kaskazini.Kwa sasa amebaki
na watu wanaomsikiliza kwa kila
jambo anaweza akaingia katika
vita na Korea Kaskazini.Wakati
mwingine ninahisi yawezekana
labda ametaka niuawe kwa kuwa
nilikuwa nampinga sana katika
suala la kutaka kuanzisha vita na nikijitahidi sana kuepuka jambo
hilo lisitokee kwani namfahamu
vizuri Mike ni mtu ambaye hana
uvumilivu hata kidogo na ilikuwa
ndoto yake ya muda mrefu siku
moja kuishambulia Korea
kaskazini na sasa anatafuta kila
njia ya kuitimiza ndoto yake.Ni
mimi pekee ambaye nimekuwa na
uwezo wa kusimama na kumtaka
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment