Simulizi : The Football (2)
Sehemu Ya Tatu (3)
“Majibu ya maswali haya yote
anayo Dr Robert” akasema Camilla
“Tusipoteze muda wakati mtu
wa kutujibu yupo.Twende
tukaanze mahojiano lazima
tuufahamu ukweli” akasema
Mathew na wote wakaingia katika
chumba alimo DrRobert ambaye tayari alikuwa amerejewa na
fahamu .Alipowaona Mathew na
Camilla wakiingia mle ndani
akakunja sura na kuwatazama kwa
hasira
“Mashetani wakubwa
ninyi.Nini maana ya kunifanya
hivi?Ninaombeni mnifungue
mkono wsangu haraka sana”
akasema Dr Robert kwa ukali
.Mathew akavuta kiti na
kuketi,Camilla akasimama karibu
na mlango.
“Vijana naombeni mnifungue
haraka sana mkono wangu.Mimi ni
mtu mkubwa na sipaswi kufanyiwa
hivi.Mnataka nini toka kwangu?
Nani kawatuma mnifanyie
hivi?Kama mnataka pesa
niambieni nitawapa kiasi chochote
kile mnachokihitaji lakini
msinifanyie udhalilishaji wa
namna hii.Napaswa kuheshimiwa
utu wangu.Kwa wadhifa nilionao
sipaswi kufanyiwa kitu kama hiki
na vijana wadogo kama ninyi !!
akasema kwa ukali Dr Robert.Bado
Mathew aliendelea kumtazama
bila kumsemesha chochote
“Vijana nawahakikishieni
mnajiweka katika hatari kubwa
sana kwa hiki mnachokifanya
kwani mpaka hivi sasa tayari
vyombo vya ulinzi vinafahamu
kwamba niko hapa na muda
wowote mtavamiwa hapa na
adhabu mtakayoipata ni kubwa
sana.Hata hivyo ninaweza kuwasaidia kama mtajutia kosa
lenu na kunifungua haraka sana”
akasema Dr Robert na kumtazama
Mathew aliyekuwa amekaa karibu
yake akimtazama bila kusema
chochote.Dr Robert akapandwa na
hasira
“Say something bastard !!!
akasema kwa ukali
“Nani kawatuma mnifanyie
hivi? Anawalipa kiasi gani kwa
ujinga huu mnaoufanya? Akauliza
tena kwa ukali
“Dr Robert naomba uwe
mtulivu mzee wangu.Hatuna shida
kubwa nawe ila tumekuleta hapa
kwa kutumia njia hii tunahitaji
kuzungumza nawe kuhusu
masuala fulani muhimu.Hakuna yeyote anayefahamu kama uko
hapa na wala hakuna yeyote
atakayekuja kukuokoa hivyo ni
kitu kimoja tu kitakachokuokoa na
kukufanya utoke humu salama ni
ushirikiao wako kwetu.Tupe
majibu ya kweli kwa kila
tutakachokuuliza.Ukifanya kama
tunavyotaka utatoka hapa salama
salimini lakini ukileta ukaidi na
kiburi nakuhakikishia kwamba
hautatoka salama hapa
ndani.Hautaliona tena jua la kesho
na mipango yako yote
hautaikamilisha” akasema Mathew
na sura ya Dr Robert ikaonyesha
woga mkubwa hasa kwa namna
Mathew alivyokuwa anazungumza
kwa kituo bila wasi wasi wowote “Nadhani ni jambo la busara
endapo tutajitambulisha kwako
sisi ni akina nani ili twende
sawa.Mimi naitwa Mathew
Mulumbi.Nimewahi kufanya kazi
katika idara ya ujasusi ya Taifa
lakini kwa sasa ninafanya kazi
zangu binafsi.Yule pale anaitwa
Camilla Snow anatokea marekani
na anafanya kazi FBI.Kwa pamoja
tunafanya kazi ya uchunguzi
tuliyopewa na rais Dr Vivian hivyo
kila tunachokifanya rais ana
taarifa nacho”
Dr Robert akaonyesha mstuko
mkubwa
Dr Robert akaonyesha mstuko
mkubwa
“Rais ndiye aliyewatuma
mnikamate na kunileta hapa?
Akauliza kwa ukali
“Hajatutuma tukukamate ila
tunatekeleza kazi aliyotupa na kwa
hiyo ana taarifa za sisi kukuchukua
na kukuleta hapa”
“No that’s not true!! akasema
DrRobert
“Kama hauamini sasa
utaamini hapo baadae.baada ya
kutufahamu sisi ni akina nani
tuelekee katika mazungumzo yetu
narudia tena kukuomba
mheshimiwa waziri kwamba
tunafahamu kila kitu kuhusu wewe
kwa hiyo usithubutu
kutudanganya.Usijaribu kutuudhi
kwani utaomba ukutane na mtoa
roho kuliko kutukorofisha
sisi.Hatuna huruma tunapokuwa
katika utekelezaji wa majukumu yetu.Hiyo ni tahadhari tumekupa”
akasema Mathew
“Go to hell!! Akasema Dr
Robert na Camilla aliyekuwa
amesimama akiwa na kompyuta
yake akainua kichwa na
kumtazama Dr Robert.Mathew
akatabasamu na kukaa sawa kitini
kisha akasema
“Tutaona nani atakayekuwa
wa kwanza kwenda huko
unakonitaka niende” akasema na
kumtazama kwa macho
makali.Tayari alikwisha anza
kukasirika kufuatia Dr Robert
kuanza kuonyesha kiburi
“Dr Robert kwanza kabisa
nataka kukujulisha kwamba Olivia
au Tausi kama anavyojiita hayup tena duniani amekwisha fariki na
kama hautakuwa na ushirikiano
kwetu basi wewe ndiye
utakayefuata”
Sura ya Dr Robert ikaonyesha
mstuko mkubwa sana na uso wake
uliloa jasho.Mathew akaendelea
“Olivia au Tausi tumegundua
alikuwa ni jasusi toka shirika la
ujasusi la CIA na amepandikizwa
ikulu kwa kazi maalum ya
kumchunguza rais.Marekani
wamekuwa wanamchunguza rais
wetu kwa muda mrefu sasa toka
angali anasoma chuo kikuu nchini
humo.Walimpandikiza jasusi
mwingine anaitwa Nathan na
akaanzisha mahusiano ya
kimapenzi na Dr Vivian na huyo Nathan kwa sasa ni
marehemu.Baada ya Nathan
kupotea ameletwa tena huyu Tausi
au Olivia ambalo ndilo jina lake
halisi. Tumegundua kwamba jana
jioni Tausi aliwasiliana nawe
pamoja na balozi Abraham Clerk
na mkakutana nyumbani
kwake.Leo hii asubuhi
umewasiliana naye tena na hata
mchana huu ulikuwa unawasiliana
naye bila kujua kama ulikuwa
unawasiliana nami kwani tayari
Tausi alikwisha kufa.Tumekuta
ramani ya jiji la Dar es salaam
chumbani kwa Tausi na katika
kompyuta yake tumekuta kuna
ramani ya uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere.Nimewasiliana na balozi Clerk kwa kutumia simu
yako na akasema kwamba vijana
wako tayari wanakusubiri kwa
maelekezo kwani mtu wenu
anakaribia sana kufika.Nataka
utueleze nani mnayemtegea
kuwasili na nini mipango yenu?
Akauliza Mathew.Dr Robert
alikuwa ameinamisha kichwa
“Dr Robert nadhani
umenisikia naomba unipe
jibu.Nani mnayemtegemea
kuwasili na na mpango wenu ni upi
ambao mmekuwa mnauandaa
wewe na balozi Clerk? Akauliza
tena Mathew lakini Dr Robert
hakujbu kitu.
“Mathew ! akaita Camilla na
kumpa ishara Mathew waende nje “Huyu hataweza kutueleza
chochote na kwa kuwa ni mtu wetu
wa muhimu sana hatupaswi
kutumia njia zetu za kumuhoji kwa
kumtesa kwani tunaweza
kumuumiza wakati bado
tunamuhitaji kuna mamboa mengi
tunapaswa kuyafahamu toka
kwake” akasema Camilla
“Anaonekana kuwa kiburi
sana lakini kiburi chake leo
kitakwisha ” akasema Mathew
“Mathew nina wazo” akasema
Camilla
“Kama nilivyosema kwamba
huyu Dr Robert hataweza
kutueleza chochote kwa sasa na
hatupaswi kutumia njia zetu za
kumfanya mtu aweze kufungua mdomo wake kwani ana taarifa
muhimu sana za kutusaidia hivyo
ushauri wangu ni kumlazimisha
aongee kwa kutumia familia
yake.Wakati ukimuhoji mimi
nilikuwa nadukua taarifa
zake.Nimegundua kwamba ana
watoto wawili mapacha wanaitwa
Juliana na Julieth wanasoma
St.Patrick international
School.Tuwatumie watoto hao
wawili kumlazimisha
azungumze.Tumtishie kuwadhuru
wanae na hatakubali kabisa
watoto wake wadhurike na
atasema kila kitu” akasema
Camilla
“Ni wazo zuri japo sipendi
sana kuwahusisha watoto katika mambo kama haya lakini kwa hapa
tulipofika hatuna namna lazima
tufanye hivyo.Ngoja niende huko
mimi mwenyewe,wewe endelea
kuwachunguza hawa jamaa tujue
ni akina nani na wametoka wapi
na kwa nini wako hapa nchini.”
akasema Mathew na kuelekea
chumbani kwake akajiandaa
haraka haraka .Alivaa suti nzuri
nyeusi akachukua gari lingine la
kifahari miongoni mwa magari
yake sita na kabla hajaondoka
akaitafuta namba ya simu ya shule
wanakosoma watoto wa Dr Robert
na kwa kutumia simu yake ya
mkononi akapiga akaomba
kupewa namba za mkuu wa shule
akapewa na akaipekua simu ya Dr Robet akaiona ile namba ya mkuu
wa shule ipo akamuandikia
ujumbe mfupi akimjulisha
kwamba anamtuma mtu kwenda
kuwachukua watoto wake Juliana
na Julieth kuna dharura ya
kifamilia.Alipoutuma ujumbe ule
akaondoka
“Mpango gani ambao Dr
Robert na marekani wanaupanga
kuutekeleza? Ni nani
wanayemtegemea awasili leo?
Haya ni maswali yaliyoumiza sana
kichwa cha Mathew
“Dr Vivian amezungukwa na
nyoka watupu .Dr Robert ni mmoja
wa watu anaowaamini mno na hata
alidiriki kukasirika nilipotaka
kumfanyia uchunguzi.Rais alikosea sana kunizuia nisimfanyie
uchunguzi Dr Robert,hakufahamu
mtu anayempigania ni mtu wa aina
gani.Huyu ni mtu mwenye sura
mbili na inawezekana Dr Vivian
hajalitambua hilo bado.Yeye
anaifahamu sura moja tu ya mtu
mwadilifu na mzalendo anayefaa
hata kuwa rais wa nchi.Sura ya pili
imejificha na inahitaji kazi ya ziada
kuing’amua lakini kwa sasa tayari
nimekwisha ing’amua na sina
shaka kwamba Dr Robert
anashirikiana na CIA .Kupitia
kwake tutaweza kupata mwanga
kuhusiana na huu mtandao ambao
CIA wameujenga hapa nchini na
nini kusudi lao.” Akawaza na
kukumbuka kitu “Mpaka sasa sijapata
mrejesho wowote toka kwa
Peniela.Ana tatizo gani?
Aliniambia atanipigia simu lakini
mpaka sasa bado sijapata simu
yake.Ngoja niendelee kuvuta
subira yawezekana bado
hajakamilisha lile zoezi na
anahitaji muda” Mathew
akaondolewa mawazoni baada ya
simu yake kuita.Zilikuwa namba
ngeni kabisa katika simu yake
akaitazama vizuri akagundua ni
namba za Dr Robert. Akajua lazima
atakuwa ni Camilla akaipokea
“Hallow” akasema
“Mathew ni mimi Camilla
nimelazimika kutumia simu hii ya
Dr Robert” “Usijali Camilla.Kuna tatizo
lolote?
“Nimechunguza majina ya
wale watu tuliyoyakuta katika
mkoba wa Dr Robert nimegundua
kwamba yale si majina yao halisi ni
majina bandia.Wale wote watatu ni
raia wa Korea Kusini
.Nimewasiliana na yule rafiki
yangu kule Marekani anisaidie
kutafuta taarifa zao kama
wanashirikiana na CIA ama
vipi.Ninapata wasiwasi
yawezekana wakawa
wanashirikiana na CIA”
“Kazi nzuri sana
Camilla.Endelea kuwafuatilia tujue
kama nao ni CIA.Mimi ninakaribia
kufika katika shule wanakosoma watoto wa Dr Robert.Ukipata
taarifa yoyote kabla sijarejea
utanijulisha”
“Sawa Mathew nitafanya
hivyo” akasema Camilla na kukata
simu
“Hawa jamaa wanazidi
kuniumiza kichwa.Kuna kitu gani
wanakipanga hapa
Tanzania?Wametoka wapi na kwa
nini watumie majina bandia?Hata
hivyo lazima tutajua kila kitu
wanachokipanga.Haitaanza siku ya
kesho kabla kila kitu hakijawekwa
wazi”akawaza Mathew
akapunguza mwendo wa gari na
kukata kona akifuata barabara
inayoelekea katika shule ya
kimataifa ya St Patrick .Toka kwa mbali shule hii iliweza kuonekana
uzuri wake
“Hi ni shule ya kimataifa hasa
ndiyo maana wanasoma watoto wa
watu wazito” akawaza Mathew
akiyafurahia mazingira ya shule ile
Alifika katika geti la shule
likafunguliwa na mlinzi aliyevaa
sare za kampuni binafsi ya
ulinzi.Mathew akashusha kioo na
kusalimiana na yule mlinzi
aliyetaka kufahamu shida
yake.Mathew akajieleza kwamba
anatoka kwa waziri wa mambo ya
nje na mkuu wa shule tayari ana
taarifa zake.Yule mlinzi akaingia
katika kibanda chake akachukua
simu na kupiga katika ofisi ya
mkuu wa shule akauliza kama mkuu wa shule ana taarifa za mtu
kutoka kwa waziri wa mambo ya
nje,akaombwa amruhusu
apite.Mathew akaruhusiwa kupita
akaelekezwa liliko jengo la
utawala iliko ofisi ya mkuu wa
shule
Aliegesha gari katika
maegesho iliyokuwa karibu na
jengo la utawala akashuka na
kufuata kibao kilichomfikisha
katika ofisi ya mkuu wa
shule.Aligonga mlango wa ofisi ile
na sauti ya mwanadada ikamruhsu
aingie akakutana na mwanadada
mmoja mweupe mwenye nywele
nyeusi zenye
kung’aa.Wakasalimiana na
Mathew akaomba kuonana na mkuu wa shule ambaye tayari ana
taarifa zake.Bila hiyana yule
mwanadada akamruhusu Mathew
afungue mlango wa mkuu washule
akaingia ndani na kukutana na
mama wa makamo akamsalimu
kwa adabu na kujitambulisha
kwamba ndiye aliyetumwa na
waziri wa mambo ya nje ya
nchi.Mwalimu yule hakupoteza
muda akainua simu na kupiga
simu kwa mwalimu wa darasa na
kumtaka awapeleke wale watoto
wawili ofisini kwake tayari kwa
kuondoka.Haukupita muda mrefu
Julieth na Juliana wakawasili na
Mathew akakabidhiwa akaagana
na mwalimu mkuu pamoja na yule
katibu muhtasi wa mkuu wa shule akaongozana na wale watoto hadi
katika gari lake la kifahari
akawafungulia mlango wakaingia
ndani na kuondoka pale shuleni.
“Sipendi sana kuwaingiza
watoto katika mambo kama haya
kwani wao hawana kosa lolote ila
kuna nyakati ambazo inatulazimu
kufanya hivi ili kuweza kupata
taarifa za muhimu.Dr Robert anazo
taarifa za muhimu sana lakini
hataweza kuzitoa bila kutishia
maisha ya watoto wake” akawaza
Mathew huku akiwatazama wale
watoto wawili pacha wazuri
wakiwa wamekaa kiti cha nyuma
wakiwa hawana wasi wasi wowote
“Watoto wachangamfu sana
hawa wananikumbusha mwanangu Anna Maria.Baada ya
seke seke hizi kumalizika lazima
niende Paris kumtembelea na
kujua maendeleo yake” akawaza
Mathew
***************
Aliwasili nyumbani
kwake,akawakaribisha ndani wale
watoto wakapewa vinywaji na
kuwadanganya kwamba baba yao
atawafuata pale muda si mrefu.
“Camilla kuna kingine
chochote umekigundua kuhusu
wale jamaa? Mathew akauliza
“Hapana, bado sijapata
mrejesho wowote toka kwa yule rafiki yangu wa kule Marekani”
akasema Camilla
“Sawa .Muda unakwenda mbio
na hatujui huyo mtu
wanayemtarajia atafika saa
ngapi.Ni wakati wa kuanza
kutafuta majibu.walete watoto
chumbani kwa baba yao” akasema
Mathew
“Mathew naomba kwa
vyovyote itakavyokuwa
tusiwaumize hawa watoto”
akasema Camilla
“Nalifahamu hilo Camiila
lakini ikinilazimu kuwafanya
chochote ili kumfanya Dr Robert
atupe kile tunachohitaji kukisikia
basi nitafanya ila nitajitahidi
kujizuia kutokufika huko.Tusipoteze wakati Camilla
walete watoto chumbani” akasema
Mathew halafu akatangulia
chumbani aliko Dr Robert
akaufungua mlango na kuingia
ndani.Dr Robert alikuwa amejilaza
kitandani bado akiwa amefungwa
pingu mkononi.Alipomuona
Mathew akainuka na kukaa
“Hallow Dr Robert.Nimerejea
tena lakini safari hii siko peke
yangu nimekuletea wageni”
akasema Mathew na mlango
ukafunguliwa Camilla akaiangia
ndani akiwa ameongozana na
Juliana na Julieth
Dr robert alihisi roho inataka
kumtoka baada ya kuwaona
watoto wake pale.Watoto wake nao wakastuka wakataka
kumkimbilia baba yao lakini
Camilla akawazuia.
“Dady what are you doing
here? Akauliza Julieth
Dr Robert alitaka kusema kitu
akashindwa.Midomo ikabaki
inamtetemeka.Uso ukaloa
jasho.Akamtazama Mathew kwa
hasira na kutaka kuinuka Mathew
akatoa bastora na kumtaka
atulie.Watoto wale walipoona baba
yao anaelekezewa bastora
wakaanza kulia Camilla
akawanyamazisha.Dr Robert huku
akitetemeka kwa hasira akasema
“Fenyeni mnachotaka
kukifanya kwangu lakini msiwaguse watoto wangu
tafadhali!!
“Dr Robert hatukuwa na
sababu ya kuwaleta watoto wako
hapa lakini kiburi chako
kimetufanya tuwalete na
tukuonyeshe kwamba tunao
uwezo wa kufanya chochote .Hata
hivyo hatukusudii wala hatuna
sababu ya kuwadhuru watoto
wako unaowapenda lakini
ukitulazimisha kufanya hivyo
hatutasita kuwadhuru mbele yako
ukishuhudia” akasema Mathew na
kumsogelea Dr Robert
“Nitazame vizuri machoni Dr
Robert.Sitanii kwa kile
ninachokisema.Endapo hautatupa
ushirikiano nitabadilika na kuwa mnyama.Usitake kuniona wakati
nimekasirika kwani nitawakata
wanao pumzi kikatili sana nawe
ukishuhudia!! Akasema Mathew na
kumtaka Camilla awatoe mle
chumbani wale watoto
“Dr Robert mimi pia ni mzazi
nina watoto na siwezi kukubali
hata siku moja kuwaweka watoto
wangu katika hatari.Nitafanya kila
niwezalo kuwaokoa
wanangu.Waonyeshe wanao
kwamba wewe ni baba bora kabisa
na ambaye uko tayari kufanya
jambo lolote kwa ajili
yao.Watazame wanao ni wacheshi
wana furaha na wana malengo
makubwa ya maisha yao.Usitake
kunilazimisha nikayakatisha malengoyao.Nieleze kile
ninachokitaka na wanao
watakuwa salama”
“Shetani mkubwa wewe !!
Watoto wangu wamekufanya nini?
Waache watoto wangu haraka sana
waondoke.Kama unashida na mimi
usiwahusishe wanangu!!
“Sikiliza DrRobert kwa sasa
hauko katika nafasi yoyote ya
kutoa amri.Unachotakiwa kufanya
kwa sasa ni kufuata kile
nitakachokuamuru.Utakapofanya
ninavyokuelekeza basi wanao
wataendelea kuwa salama.Nataka
kufahamu wewe na wenzako akina
Tausi na balozi Clerk mna mpango
gani mnaopanga kuufanya leo? Nani mnayemtarajia kuwasili jioni
ya leo?
Dr Robert hakujibu kitu
akabaki kimya
“Dr robert naomba
usinipotezee wakati.Nijibu haraka
maswali yangu”
“mwanaharamu mkubwa
wewe.Niue tu lakini usitegemee
kupata kitu chochote toka
kwangu.Niue mjinga
wewe!!Unadhani kwa kuwaleta
watoto wangu hapa utanifanya
nikwambie unachokitaka?
Unapoteza muda wako bure
kijana.Mimi si mtu rahisi kama
unavyodhani” akasema kwa ukali
Dr Robert Mathew akamtazama halafu
akatazama saa yake ilikaribia sa
kumi na moja za jioni.Akafungua
mlango na kumtaka Camilla
awalete watoto wa Dr Robert mle
chumbani.Mathew akamshika
Julieth
“Nataka nikuonyeshe kwamba
nina maanisha ninachokisema
.Nitaanza na huyu halafu
nitamalizia na yule mwingine
,atakuja mama yao na kama bado
hautataka kutupa tunachokitaka
tutaendelea kuwamaliza ndugu
zako mmoja baada ya
mwingine”akasema Mathew na
kumtaka Julieth amtazame baba
yake “Kiburi chako Dr Robert
kinayaondoa maisha ya mwanao
Julieth” akasema Mathew na
kuiweka bastora kichwani kwa
Julieth ambaye alikuwa analia.Dr
Robert alikuwa anatetemeka mwili
na kuuma meno kwa hasira kali
alizokuwa nazo.
“Tano !! Mathew akaanza
kuhesabu
“Nne !! akaendelea kuhesabu
huku Julieth akitoa kilio.
“Kijana tafadhali nakuomba
waache wanangu.kama unashida
na mimi niue mimi na si
wanangu.hawana kosa lolote.Niue
mimi tafadhali na uwaache huru!!
Akasema Dr Robert huku macho yake yakionekana kuwa na
machozi.
“Tatu !! Mathew akahesabu
“ Baba wape kitu
wanachokitaka wasituue !!
akasema Julieth huku akilia.Dr
Robert alikuwa anahema kwa kasi
na michirizi ya machozi
ikaonekana machoni pake
“Mbili !!
Julieth akaongeza
kulia.Mathew akamtazama Dr
Robert kwa hasira
“Moj..”
“Basi !! Basi !! Usimuue
mwanangu !! akapiga ukelele Dr
Robert
Mathew akamsukuma
pembeni Julieth akaanguka chini Camilla akamuinua na
kumbembeleza anyamaze,Mathew
akamfuata Dr Robert
“Haraka sana nieleze ama
sivyo nitawatoa uhai wanao sasa
hivi!! Akafoka
“sawa sawa nitakueleza kila
kitu lakini naomba unihakikishie
kwamba wanangu watakuwa
salama”akasema Dr Robert huku
machozi yakimtoka.Mathew
akamfanyia ishara Camilla awatoe
mle ndani wale watoto
“Haya anza kunieleza!!
Akafoka Mathew baada ya watoto
wa Dr Robert kutoka mle ndani.Dr
Robert akavuta pumzi ndefu na
kwa sauti yenye kitetemeshi
akasema “Nataka uniahidi kitu kimoja
kabla sijakueleza chochote”
akasema Dr Robert
“Unahitaji nini?
“Nikikueleza kile unachotaka
kukifahamu tayari nitakuwa
ninajihesabu mimi ni
mfu.Ninaomba unihakikishie ulinzi
mimi na familia yangu na
nitakueleza kila kitu” akasema Dr
Robert.Mathew akamtazama na
kusema
“Nieleze kwanza kila kitu na
nikiona uzito wa hicho
utakachokuwa umenieleza basi
nitaamua kama nikusaidie au vipi
lakini kwa sasa siwezi kukuahidi
chochote” akasema Mathew .Dr Robert akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Helmet Brian waziri wa
mambo ya nje wa Marekani
anawasili jioni ya leo” akanyamaza
“Endelea ! akafoka Mathew na
maco yake yalitisha kwa namna
alivyokasirika.Dr Robert
akaonekana kusita kuendelea.
“Dr Rober…..” Mathew akataka
kusema ktu lakini Dr Robert
akamuwahi
“Nitakueleza” akasema na
kumeza mate
“Inapangwa mipango ya
kumuua mara atakapofika hapa
Dar es salaam” akasema na
kunyamaza akatazama chini “Mnataka kumuua waziri wa
mambo ya nje wa marekani?
Akauliza Mathew.Alishangazwa
sana na taarifa zile.Dr Robert bado
aliendelea kutazama
chini.Akamsogelea Dr Robert na
kumshika kichwa akamuinua
“Dr Robert tafadhali naomba
unieleze nielewe.Nani wanataka
kumuua waziri wa mambo ya nje
wa Marekani na kwa nini?
Akauliza Mathew lakini bado Dr
Robert hakutaka kujibu
“Nakuhakikishia DrRobert
safari hii sintahesabu mpaka
tano.Nitawaondoa wanao mmoja
baada ya mwingine!!
“Tafadhali naomba usiwaguse
tena wanangu.Mpaka sasa umekwisha wapa mstuko mkubwa
sana na sijui nitafanya nini
kuwasahaulisha tukio hili la
kinyama ulilolifanya !! akasema Dr
Robert
“Narudia kwa mara ya mwisho
kama unataka wanao waendelee
kuwa hai nieleze nani wanataka
kumuua waziri wa mambo ya nje
wa Marekani na kwa nini?
“Helmet Brian anataka
kuuawa na marekani”akasema
DrRobert
“Anataka kuuawa na
Marekani?!! Mathew akashangaa
“ndiyo ”
“Kwa nini Marekani watake
kumuua waziri wao wa mambo ya
nje? Dr Robert akawa kimya
“Nataka jibu Dr Robert kwa
nini marekani watake kumuua
waziri wao wa mambo ya nje?
“Kwa sababu wanataka
kupata sababu ya kushambulia
Korea Kaskazini”
“Mmepangaje kumuua Helmet
Brian?
“Kuna watu tayari wako hapa
nchini wameletwa kwa ajili ya hiyo
kazi ya kumuua Helmet.Watu hao
baada ya kufanikisha mauaji hayo
watakamatwa na wakihojiwa
watadai kwamba wametumwa na
Korea Kaskazini wamuue waziri
Helmet na hicho kitakuwa ni
kigezo cha marekani kuanzisha
vita na Korea kaskazini” “Tumekuta karatasi yenye
picha tatu katika mkoba
wako.Tumeyachunguza majina ya
watu hao na kukuta ni majina
bandia,je watu hao ndio
waliotumwa kuja kumuua waziri
Helmet? Akauliza Mathew
“Ndiyo ni hao”
“wanatokea nchi gani?
“Mimi sifahamu bali jukumu
langu lilikuwa ni kuhakikisha watu
hao wanaingia,niwatafutie hoteli
za kukaa na kuwapanga kila
mmoja na eneo lake” akasema Dr
Robert.Mathew akamtazama kwa
hasira na kusema
“Dr Robert wewe ni mtu
mkubwa mwenye heshima kubwa
sana ndani na nje ya nchi.Kwa nini umeshiriki katika mpango kama
huu wa mauaji ya mtu mkubwa
kama huyu wakati unafahamu fika
kuwa jambo hili litaleta mvutano
mkubwa sana kati ya nchi yetu na
Marekani? Kama umeweza
kushiriki katika kupanga mauaji
ya kiongozi huyu wa Marekani
utashindwaje kushiriki katika
mauaji ya rais wetu kama
ukishawishiwa na pesa? Akauliza
Mathew lakini Dr Robert hakujibu
kitu akainamisha kichwa
“Mimi nawe bado tuna
mzungumzo marefu hapo
baadae.Kwa sasa nataka unieleze
mlivyopanga kutekeleza mauaji ya
Helmet” akasema Mathew “Siwezi kukueleza zaidi ya
hapa,sitaki mpango huu uvurugike
kwani unanitegemea sana mimi na
endapo usipofanikiwa na
wakafanya uchunguzi wakafahamu
kwamba ni mimi ndiye chanzo cha
mpango kushindwa kufanikiwa I’m
dead” akasema Dr Robert.
“Dr Robert mpaka hapa tayari
mpango huu umeshindikana.Siko
tayari waziri wa mambo ya nje wa
marekani auawe katika ardhi ya
Tanzania.Lazima nifanye kila
niwezalo kuhakikisha mpango huu
haufanikiwi hivyo naomba
tusipoteze wakati nieleze mpango
mzima wa mauaji namna
mlivyoupanga” Dr Robert akafikiri kidogo na
kusema
“Hapana siwezi kukueleza
chochote”
“Dr Robert usitake niwaite
tena watoto wako humu chumbani
na ushuhudie namna uhai
unavyowatoka” akasema Mathew
na kauli ile ikamuogopesha Dr
Robert akalazimika kumweleza
Mathew ukweli wote.Baada ya
kuelezwa namna mpango wote
ulivyopangwa Mathew akamfuata
Camilla
“Wanaendeleaje watoto?
“Wamelala.Wamepatwa na
mstuko mkubwa”
“Hatukuwa na namna
nyingine ya kumfanya Dr Robert aongee zaidi ya kuwatumia watoto
wake.Hata hivyo amefunguka kila
kitu.Jioni ya leo anawasili waziri
wa mambo ya nje wa Marekani
Helmet Brian.Kuna mpango wa
kumuua unaandaliwa na seriali ya
marekani”
Camilla akastuka na
kumtazama Mathew kwa
mshangao
“Marekani wanataka kumuua
waziri wao wa mambo ya nje? Kwa
nini wafanye hivyo?
“Kwa mujibu wa maelezo ya
Dr Robert ni kwamba Marekani
wanatafuta sababu ya kuanzisha
vita na Korea kaskazini.Wale watu
tuliokuta picha zao katika karatasi
kwenye mkoba wa Dr Robert ni wadunguaji walioletwa hapa
nchini kwa ajili ya kazi hiyo ya
kumuua Helmet.kwa maelezo ya
Dr Robert ni kwamba baada ya
kutekeleza mpango wa mauaji ya
Helmet watu hao watakamatwa na
watakiri kwamba wametumwa na
serikali ya Korea Kaskazini na
hapo Marekani watakuwa
wamepata sababu ya kuishambulia
Korea Kaskazini kwa kigezo cha
kulipiza kisasi kwa mauaji ya
waziri wake wa mambo ya nje”
akasema Mathew
“Mathew tafadhali tusiruhusu
jambo hili likatokea katika ardhi
ya Tanzania.Kwa namna yoyote ile
lazima tumuokoe Helmet Brian”
akasema Camilla “Ndiyo Camilla.Katu jambo hili
haliwezi kutokea na lazima
tulizime jaribio hili kwa gharama
zozote” akasema Mathew na
kumpigia simu Hamis Chuma
akamtaka aje na kijana mmoja
“Kwa hiyo tunafanyaje
kumuokoa Helmet asiuawe?
Akauliza Camilla
“Bado tunaye Dr Robert .Huyu
atatusaidia katika kuuvuruga
mpango huu wa mauaji.Kwa
kumtumia yeye atatusaidia kuingia
ndani ya uwanja wa
ndege.Tutakuwa na magari mawili
na ndani ya gari moja tutatega
bomu.Kwa kuwa tutakuwa
tumeongozana naye
hatutakaguliwa.Muda mfupi baada ya Helmet Brian kuwasili bomu
hilo tutakalolotega garini
litalipuka na kuzua kizaa zaa
kikubwa pale uwanjani na huo ni
wakati wetu sisi wa kumchukua
Helmet Brian na kuondoka
naye.Katika mpango huo kuna
maisha ya watu yanaweza kupotea
lakini hatuna namna lazima kwa
gharama zozote tumuokoe Helmet
na tuiokoe dunia kuingia katika
vita nyingine kubwa isiyoweza
kuelezeka kwani mataifa
washirika wa Korea kaskazini
hawatakaa kimya wakiomba
mshirika wao anashambuliwa
hivyo wataingia vitani.Washirika
wa marekani nao wataingia pia
vitani na vita hiyo itazidi kutanuka.Lazima tuzuie dunia
kutumbukia katika janga lingine
kubwa” akasema Mathew na
Camilla akaukubali mpango
ule.Mathew akaelekea katika
chumba alimo Dr Robert.
“Dr Robert nisikilize kwa
makini.Mimi na wenzangu
tumeazimia kuuvuruga mpango wa
kumuua waziri Helmet
Brian.Hatuwezi kukubali mauaji
haya yakafanyika katika ardhi ya
Tanzania.Kama ni kumuua
wakamuulie katika ardhi yao na si
hapa kwetu.Ninakushangaa sana
Dr Robert kwa kukubali kuingia
katika mpango huu bila ya kupima
athari zake kwa nchi na kwa
dunia.Pamoja na hayo utafuata maelekezo yetu.Kwanza utampigia
simu balozi wa marekani na wale
wote ambao mnashirikiana nao
katika mpango huu na wajulishe
kwamba kila kitu kinakwenda
kama kilivyopangwa.Waambie
kwamba ulipatwa na dharura na
ndiyo maana hukuweza
kuwasiliana nao.Baada ya hapo
mpigie simu mkeo mjulishe kuwa
watoto uko nao hivyo
asihofu.Ukimaliza upande huo wa
mawasiliano tutaelekea uwanja wa
ndege kumpokea Helmet na
utatumia uwezo wako wote katika
kuhakikisha kwamba mimi na
vijana wangu tunaingia uwanja wa
ndege bila matatizo wala
kukaguliwa.Ukithubutu kufanya chochote kinyume na maelekezo
yetu basi hutawaona watoto
wako.Tumeelewana?? akauliza
Mathew na Dr Robert akaitika kwa
kichwa.Mathew akamfungua pingu
na kumpa simu yake
akamuelekezea bastora na
kumtaka apige simu wakati
amesimama pale ili aweze kusikia
anachokizungumza.Dr Robert
akafanya kama alivyoelekezwa
akapiga simu na alipomaliza
Mathew akaichukua simu na
kumtaka ainuke na kumpeleka
chumbani kwake katika kioo na
kumtaka ajiweke vizuri kwani
alikuwa amesawajika sana
Wakati Dr Robert akijiandaa
Hamis Chuma na kijana wake mmoja wakawasili kwa kutumia
piki piki.Mathew akamuita Camilla
na kumtaka amsimamie Dr Robert
wakati anajiweka sawa akaenda
kuonana na akina Hamis
“Ahsanteni sana kwa kufika
kwa wakati” Mathew akawaambia
akina Hamis.
“Tumeamua kutumia piki piki
ili kufika kwa wakati kama
ulivyotutaka.” Akasema Hamis
Chuma,Mathew akawaongoza
sebuleni na bila kupoteza wakati
akawaeleza alichowaitia
“Kuna kiongozi mmoja
ambaye anatakiwa kuuawa lakini
kazi yetu sisi ni kwenda
kumuokoa.Ni kiongozi mkubwa.Ni
waziri wa mambo ya nje wa Marekani.Tukio hilo tutalifanya
katika uwanja wandege wa Julius
Nyerere ambayo ni sehemu yenye
ulinzi mkali.Wanaopanga
kutekeleza mpango huo wana
utaalamu mkubwa hivyo
operesheni hii ni operesheni yenye
kuhitaji matumizi makubwa ya
akili,ujuzi na uzoefu.Naomba
niwaweke wazi ndugu zangu
kwamba hii ni operesheni yenye
hatari kubwa kwa hiyo yeyote
ambaye anahisi hatakuwa tayari
aweke wazi angali mapema”
“Mathew sisi ni wazee wa kazi
na hizi ndizo kazi zetu.Sote hapa
tumepitia jeshi,tunafahamu mbinu
zote za mapambano na katu
hatuogopi kupambana.Kwetu kucheza na silaha ni kama vile
kuchezea simu kwa hiyo kwa niaba
ya wenzangu nakuhakikishia
kwamba tuko tayari ,tupe kazi
tuifanye” akasema Hamis
“Good” akasema Mathew na
kuwaelekeza akina Hamis namna
mpango ule wa kumuokoa Helmet
utakavyokuwa.Akaingia chumbani
kwake na kumkuta tayari Dr
Robert amekwisha
jiandaa,akachagua suti tatu na
kuwapelekea akina Hamis.Akatoa
katika gereji gari mbili aina ya
Mercedece benz.Akalitazama
mojawapo ya gari kwa uchungu
“Gari langu jipya kabisa
linakwenda kuteketea lakini kwa
ajili ya kuokoa mtu muhimu asiuawe.” Akawaza na
kumuelekeza Kijana wa Hamis
azifanyie usafi zile gari halafu
akamchukua Hamis wakaeleka
katika chumba cha siri cha
kuhifadhia silaha wakachagua
silaha ambazo
zingewasaidia.Wakachukua
mabomu mawili na kwenda
kuyatega katika gari moja kati ya
zile mbili watakazotumia usiku
ule.
“Sikujua kama una hazina ya
silaha kali nzito kama hizi”
akasema Hamis Chuma wakati
wakilitega bomu ndani ya gari
“Mimi hupenda kuhifadhi
silaha kama hivi kwa sababu hujitokeza operesheni za dharura
kama hizi” akasema Mathew
Walipomaliza maandalizi
Mathew akaenda chumbani alimo
DrRobert na kumtaka waondoke.
Muda umefika Dr
Robert,twende tuondoke tuelekee
uwanja wa ndege” akasema
Mathew na kumtaka Camilla abaki
pale nyumbani akiwalinda watoto
wa Dr Robert.Kabla hawajaondoka
Dr Robert akataka kuwaona
watoto wake.
“Zingatia yale yote
niliyokuagiza na utawaona tena
wanao ila ukifanya kinyume na
maelekezo hautawaona tena
wanao wazuri” akasema Mathew
wakaelekea katika magari.Mathew na Dr Robert wakaingia katika gari
moja,Hamis Chuma na kijana wake
aliyejulikana kama Gidion
wakaingia katika gari lingine
lililokua na bomu na safari ikaanza
kuelekea uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere.
Hali katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Julius Nyerere
Dar es salaam ilikuwa ni ya utulivu
mkubwa na ndege ziliendelea
kutua na kupaa kama
kawaida.Magari mawili ya akina
Mathew yaliwasili uwanjani hapo
na kwa kumtumia Dr Robert
walifanikiwa kuingia ndani ya uwanja ambako kulikuwa na gari
tano zimejipanga kwa ajili ya
msafara utakaomchukua waziri
Helmet Brian kutoka pale uwanja
wa ndege.Gari walilokuwa
wamepanda Mathew na Dr Robert
likasimama mbele kabisa ya
magari ya msafara na lile
walilopanda Hamis chuma na
kijana wale lililokuwa na bomu
likaenda kuegeshwa pembeni ya
magari mengine.Kijana aliyekuwa
na Hamis chuma akashuka katika
lile gari na kwenda kuingia katika
gari walilokuwamo Mathew na Dr
Robert na kukaa katika kiti cha
dereva,Mathew na Hamis Chuma
wakaongozana na Dr Robert
kuelekea mahala ambako wangempokelea Helmet
Brian.Tayari maafisa kadhaa wa
ubalozi wa Marekani na kutoka
wizara ya mambo ya nje walikuwa
wamewasili pale uwanjani
akiwemo pia balozi wa Marekani
nchini Tanzania Abraham
Clerk.Alimvuta pembeni Dr Robert
wakazungumza kwa takribani
dakika kumi na kisha wakaja
kujiunga na wenzao.
Tayari kiza kimekwishatanda
angani wakati ndege iliyombeba
waziri wa mambo ya nje wa
Marekani Helmet Brian ilipogusa
ardhi ya Tanzania.Mlango
ukafunguliwa wakashuka maofisa
wanne wakapokewa na balozi wa
Marekani nchini Tanzania nadakika tatu baadae Helmet Brian
akashuka ndegeni akiwa
amezungukwa na walinzi wake
watatu.Alipokewa na balozi wa
marekani nchini,wakasalimiana na
kisha akamtambulisha kwa
DrRobert ambaye ndiye mwenyeji
wake naye akamtambulisha
Helmet watu kadhaa waliokuwepo
pale uwanjani kumpokea halafu
wakaanza kutembea kuelekea
ulipo msafara wa magari tayari
kwa kuondoka pale uwanjani.
Mita kama hamsini hivi kabla
ya kuufikia msafara wa magari
kikasikika kishindo cha mlipuko
wa bomu na moto mkubwa
ukatokea katika gari lililokuwa
limeegeshwa pembeni ya magari ya msafara.Taharuki kubwa
ikazuka na watu wakaanza
kukimbia hovyo ili kuokoa maisha
yao.Mara tu mlipuko ule
ulipotokea Hamis Chuma
akamuwahi Dr Robert na
kumdhibiti.Walinzi wa Helmet
Brian wakamchukua kiongozi wao
na kuanza kumkimbiza
kumrejesha ndegeni lakini Mathew
tayari alikwishakiona kitendo kile
akachomoa bastora mbili zote
zenye kiwambo cha kuzuia sauti na
kuanza kuwamiminia risasi wale
walinzi wakaanguka chini na
Helmet akajikuta akiwa peke
yake.Alistuka na kuogopa
akageuka nyuma akamuona
Mathew akimfuata akiwa na bastora mbili,mwili
ukamtetemeka.Mathew akamvaa
na kumpa pigo moja kali
akaanguka na kupoteza
fahamu.Akamuinua akamuweka
begani na kuanza kukimbia naye
hadi katika gari lake.Hamis Chuma
ambaye tayari alikuwa amekwisha
fika garini akiwa na Dr Robert
akamfungulia buti ya gari
wakamuingiza Helmet na
kuondoka.Kiza kikubwa
kilikuwepo pale uwanjani watu
wakikimbia kwenda mbali na
uwanja.Akina Mathew hawakupata
wakati mgumu kutoka kwani
sehemu zote za mageti hazikuwa
na walinzi kwani karibu kila mtu
alikuwa amekimbia kuokoa maisha yake.Walifanikiwa kutoka
salama nje ya uwanja ule na safari
ya kuelekea nyumbani kwa
Mathew ikaanza.
“Hakuna
aliyejeruhiwa?Mathew akauliza
“Hapana wote tuko salama”
akasema Hamis
“Good” akasema Mathew na
kumtazama Dr Robert ambaye
alikuwa ameloa jasho mwili mzima
“Nimepoteza gari langu zuri
lakini tumefanikisha kumuokoa
waziri Helmet.Operesheni
imekuwa rahisi zaidi ya
nilivyotegemea japokuwa
imegharimu baadhi ya maisha ya
watu.Pamoja na hayo
tumefanikiwa kuepusha dunia na vita ya tatu ya dunia ambayo
ingeibuka kama Helmet angeuawa
na Marekani kuanza kuishambulia
Korea kaskazini” akawaza Mathew.
Hakukuwa na maongezi
yoyote garini hadi walipofika
nyumbani kwa Mathew,Camilla
akafungua geti wakamshusha
Helmet na kumuweka
sebuleni,bado hakuwa
amezinduka
“Hamis nashukuruni sana kwa
kazi yenu kubwa usiku huu wa leo
hadi tumefanikisha kuokoa maisha
ya huyu mtu ambaye alikuwa
hatarini kuuawa lakini bado kuna
kazi moja bado nahitaji kutoka
kwenu.Nahitaji ulinzi kwa usiku
wa leo hapa nyumbani kwangu.” “Usihofu kuhusu hilo
Mathew.Hata ukitaka mwaka
mzima sisi tuko tayari kukufanyia
kazi.Nitawaongeza vijana wangu
wawili katika kuongeza nguvu
zaidi” akasema Hamis
Mathew akaingia ndani na
kumkuta Dr Robert akiwa amevua
shati huku jasho likiendelea
kumtiririka .Mathew akachukau
chupa ya mvinyo na kummiminia
katika glasi akanywa wote na
kuhitaji tena mwingine akanywa
wote.Mathew akamtaka ainuke
akampeleka katika kile chumba
alichokuwa amemfungia
“Nimefanya kama
mlivyonitaka
nifanye,nimewasaidia mmefanikisha mpango
wenu.Msingeweza kuingia mle
uwanjani bila mimi.Kwa kuwa
mmepata mlichokihitaji ni zamu
yenu sasa kunisaidia na mimi
kwani tayari maisha yangu yako
hatarini,muda wowote ninaweza
kuuawa.Mpango huu ulikuwa ni
wa siri kubwa lakini mimi ndiye
niliyeuharibu.Bila msaada wenu
mimi na familia yangu
tutaangamia”akasema Dr Robert
“Mimi na wewe bado
hatujamaliza mazungumzo yetu”
akasema Mathew na kumfunga
pingu
“Tafadhali naomba msaada
wenu.” Akasema Dr Robert lakini Mathew hakujibu kitu akageuka
kuondoka
“Naomba usiondoke
tafadhali,nisikilize!! Akasema
DrRobert na Mathew akageuka
“Nakuomba tafadhali
usimueleze Helmet jambo lolote
kuhusu Marekani kutaka
kumuua.Kwa kuwa tayari
umefanikiwa kumuokoa fanya
utaratibu aondoke nchini arejee
kwao na asifahamu chchote.Kuna
mambo makubwa nitakueleza
endapo utafanya kama
ninavyokuomba” akasema Dr
Robert .Sura yake ilionyesha woga
mkubwa.Mathew akaubamiza
mlango na kutoka akaenda sebuleni alikokuwapo Camilla
akimpa msaada Helmet kuzinduka.
“Wanaendeleaje watoto?
Akauliza
“Wanaendelea vyema.Pole
sana”
“Ahsante .Tumefanikiwa
kumuokoa Helmet lakini maisha
ya watu kadhaa
wamepotea.Sifahamu ni wangapi
ila kuna watu wamekufa” akasema
Mathew
“Ahsante sana kwa kuokoa
uhai wa mtu ambaye alitakiwa
kuuawa bila kosa lolote.Usijali
kuhusu hao waliopoteza maisha
yao.Katika kila vita lazima kuna
watu wasio na hatia watapoteza
maisha” akasema Camilla na mara Helmet akazinduka.Akina Mathew
wakamsaidia na akarejea katika
hali yake ya kawaida.
“Ninyi ni akina nani? Hapo
nipo wapi? Akauliza
“Usihofu mheshimiwa
waziri,uko sehemu salama”
akasema Mathew na Helmet
akaanza kuvuta kumbu kumbu
akakumbuka kilichotokea usiku
ule katika uwanja wa ndege wa
Julius Nyerere
“Ulitokea mlipuko pale
uwanja wa ndege,nani waolitega
mlipuko ule na kwa kusudi gani?
Walikuwa wananilenga mimi?
Akauliza Helmet halafu
akamtazama Mathew kwa macho
makali “Wewe !! Nimekukumbuka!!
Nilikuona na bastora.Uliwaua
walinzi wangu ..!!Ninyi ni akina
nani? Akauliza Helmet kwa wasi
wasi
Mathew akammiminia mvinyo
katika glasi akanywa
“Naitwa Mathew
Mulumbi.Nimewahi kufanya kazi
na idara ya ujasusi ya Tanzania
lakini kwa sasa ninafanya shughuli
zangu binafsi.Huyu mwenzangu
anaitwa Camilla Snow.Ni raia wa
Marekani na anafanya kazi FBI?
“FBI ?!! akauliza Helmet kwa
mshangao
“Ndiyo” akajibu Camilla“Wewe !! Nimekukumbuka!!
Nilikuona na bastora.Uliwaua
walinzi wangu ..!!Ninyi ni akina
nani? Akauliza Helmet kwa wasi
wasi
Mathew akammiminia mvinyo
katika glasi akanywa
“Naitwa Mathew
Mulumbi.Nimewahi kufanya kazi
na idara ya ujasusi ya Tanzania
lakini kwa sasa ninafanya shughuli
zangu binafsi.Huyu mwenzangu
anaitwa Camilla Snow.Ni raia wa
Marekani na anafanya kazi FBI?
“FBI ?!! akauliza Helmet kwa
mshangao
“Ndiyo” akajibu Camilla “Kuna nini kinaendelea hapa?
Umekuja kufuata nini huku
Tanzania? Akauliza Helmet.
Mathew hakupoteza muda
akamueleza kuhusiana na mpango
wa kumuua ulioandaliwa na
serikali ya marekani.Helmet
akainuka na kupandwa na hasira
“Hapana si kweli hata
kidogo.Serikali ya marekani
haiwezi kufanya kitu kama
hicho.Huu ni uongo wa mchana!!
Akasema na kuibinua meza kwa
hasira
“Huo ni uongo mkubwa!! Rais
Mike ni mtu wangu wa karibu na
hawezi kupanga kuniua mimi!!
Akazidi kufoka “Mheshimiwa waziri amini
tunachokueleza ni kitu cha kweli
kabisa na ndiyo maana tumefanya
kila juhudi kukuokoa” akasema
Camilla.Waziri Helmet
akawatazama kwa sekunde
kadhaa na kuuliza
“Mmefahamuje kuhusiana na
mpango wa kuniua? Akauliza na
sasa alionekana kuanza kutulia
“DrRobert ndiye aliyegundua
mpango huo na akatujulisha.Kwa
pamoja tumeshirikiana naye
katika mpango huu na kukuokoa”
akasema Mathew.Helmet
akainamisha kichwa akazama
katika mawazo mengi .Mathew
akainuka na kwenda katika
chumba alimokuwemo Dr Robert “Sikiliza Dr
Robert.Nimemueleza Helmet
kuhusu mpango wote uliokuwa
umepangwa wa kumuua lakini
sijakutaja kama nawe unahusika
badala yake nimekutaja kama
ndiye uliyegundua kuwepo kwa
mpango ule na ukatujulisha na
tumeshirikiana katika
kumuokoa.Nimefanya hivi ili
kukulindia heshima yako na hivyo
ujiandae kunieleza mambo mengi
zaidi pale nitakapokuja
kuzungumza nawe baadae”
akasema Mathew na kutoka mle
chumbani akaelekea sebuleni na
kumkuta waziri Helemt akiwa
amejiinamia akionekana kuwa na
mawazo mengi “Bado siamini.Nchi yangu
ninayoitumikia kwa moyo wangu
wote ndiyo wanataka kunitoa
kafara kwa ajili ya kupata sababu
ya kuishambulia Korea
kaskazini.Na wewe Camilla uko
hapa Tanzania kwa dhumuni
gani?Kuna kazi yoyote umetumwa
huku?akauliza Helmet
“Niko hapa Tanzania kwa
mambo binafsi nimekuja kwa huyu
mpenzi wangu na kwa bahati nzuri
jambo hili likanikuta na
tukashirikiana pamoja” akasema
Camilla na kumtazama Mathew na
wote wakatabasamu
“Naomba simu niwasiliane na
familia yangu niwajulishe kwamba
niko salama” akasema Helmet “Hapana mheshmiwa
waziri,utapata nafasi ya kupiga
simu pale utakapokuwa katika
sehemu salama zaidi”
“Sehemu salama? Helmet
akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
waziri.Nitakukabidhi katika
mikono salama zaidi” akasema
Mathew na kuchukua simu
akampigia rais
“Mathew siwezi kuzungumza
nawe kwa sasa nataka kuingia
katika kikao kizito cha
dharura.Kuna mambo makubwa
yametokea usiku huu.Naomba
unitafute baadae!! Akasema Dr
Vivian “Mheshmiwa rais tafadhali
naomba usikate simu”
“Unahitaji nini Mathew?Kama
una shida nimekwambia nitafute
baadae kwa sasa ninasubiriwa
katika kikao muhimu sana”
“Mheshimiwa rais ninahitaji
kukuona sasa hivi.Nina jambo
kubwa nataka nikueleze na siwezi
kusubiri hadi hapo baadae.Ni
muhimu sana”
Dr Vivian akafikiri kidogo na
kusema
“Unataka kuja ikulu?
“Vipi hali ya Theresa?
“Mathew naomba ujibu swali
nililokuuliza
“Mheshimiwa rais nimeuliza
hivyo ili kama ikiwezekana tukutane pale hospitali alikolazwa
Theresa.Ahirisha kikao hicho kwa
muda kwa kisingizio cha hali ya
Theresa kubadilika ili uweze
kupata nafasi ya kuja tuonane pale
hospitali.Mheshimiwa rais
nisingeweza kuharibu ratiba zako
kama jambo ninalokuitia si la
muhimu” akasema Mathew
Kwa sekunde kadhaa Dr
Vivian akawa kimya akitafakari
kisha akasema
“Sawa tukutane pale hospitali
sasa hivi !!
“Ahsante mheshmiwa rais”
akasema Mathew na kukata simu
akamuita Camilla pembeni
“Camilla tunampeleka waziri
Helmet kumkabidhi kwa rais.Atakuwa katika mikono
salama zaidi akiwa ikulu”
“Vipi kuhusu hapa nyumbani
tutawaacha Dr Robert na wanae
peke yao?
“Hapana hawatakuwa peke
yao.Kuna ulinzi mkubwa upo
hapa.Hamis Chuma na wenzake
wanalinda hapa usiku wa leo.Hata
hivyo hatutachukua muda mrefu
tutarejea bado tuna mazungumzo
na Dr Robert,ameahidi kunieleza
mambo mengi makubwa endapo
nitamsaidia kuondoka nchini yeye
na familia yake”
“Umemuahidi kumsaidia
kuondoka nchini?
“Sijamuahidi chochote lakini
itategemea na uzito wa kile atakachonieleza” akasema Mathew
na kumfuata Helmet
“Mheshimiwa waziri
tunakuondoa hapa kama
nilivyokueleza na tunakupeleka
sehemu salama” akasema Mathew
“Mnanipeleka wapi? Sitaki
mnipeleke katika ubalozi au
taasisi yoyote yenye mahusiano na
Marekani!! Akasema Helmet kwa
hasira
“Hapana hatutakupeleka
huko,tunakupeleka katika mikono
salama ambako Marekani
hawataweza kukupata kirahisi.Sisi
uwezo wetu wa kuendelea
kukuweka salama ni mdogo na
hivyo unahitaji kuwepo katika
mikono yenye uwezo mkubwa zaidi wa kuhakikisha unakuwa
salama.Naamini Marekani
wakisikia uko hai bado na
umefahamu mpango wao wa
kutaka kukuua wataendelea
kukusaka usiku na mchana hadi
wahakikishe wametimiza azma
yao” akasema Mathew na
kumchukua waziri Helmet
wakaondoka na kuacha nyumba
ikiwa chini ya ulinzi wa Hamis
Chuma na vijana wake
“Dr Robert yuko wapi?
“Hatufahamu mahala aliko
kwa sababu ya ule mvurugano
uliotokea pale uwanja wa ndege
baada ya bomu kulipuka”
“kwa hiyo lile bomu ninyi ndio
mliolitega? “Ndiyo.Ilitulazimu kutega
bomu lile kwa lengo la kuzua
taharuki pale uwanjani ili tuweze
kukupata kabla haujatoka nje ya
uwanja ambako kuna watu
walikuwa wameandaliwa
kukuua.Tunawafahamu watu hao
na hoteli walikofikia na usiku huu
tutahakikisha wote
wanakamatwa”
“kwa nini lakini Dr Robert
hakunieleza kuhusiana na mpango
huu wa kuniua? Yule ni rafiki
yangu na kama angenieleza
mapema nisingekuja Tanzania”
“Inawezekana aliupata
mpango ule katika dakika za
mwisho kabisa ndiyo maana hakukueleza mapema” akasema
Mathew na safari ikaendelea.
********************
Taarifa za kulipuka kwa bomu
katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere muda
mfupi tu baada ya waziri wa
mambo ya nje wa Marekani Helmet
Brian kuwasili nchini Tanzania
zilisambaa kwa kasi kubwa na
vyombo vingi vya habari duniani
vilitangaza kutokea kwa tukio lile
.Taarifa zile ziliwasua sana
wamarekani kwani waliamini
tukio lile lilikuwa limemlenga
waziri wao Helmet Brian na wengi
walianza kuinyooshea vidole Korea Kaskazini na serikali ya
Tanzania kwamba wanahusika
katika tukio lile.Dakika thelathini
baada ya shambulio lile kutokea
Mike straw rais wa Marekani
akatoa hotuba fupi kwa taifa yenye
lengo la kuwatuliza na kuwaondoa
hofu wamarekani kufuatia tukio
lile liliotokea nchini Tanzania
“Wamarekani wenzangu”
ndivyoMike straw alivyoanza
hotuba yake
“Muda mfupi uliopita
nimepokea taarifa kwamba
umetokea mlipuko wa bomu
katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere nchini
Tanzania dakika chache baada ya
waziri wetu wa mambo ya nje
Helmet Brian kuwasili uwanjani
hapo.Nilimtuma Helmet
aendeTanzania katika jitihada za
kumshawishi rais wa Tanzania
asitishe mpango wake wa
kuanzisha mashirikiano na nchi ya
Korea kaskazini.
Tunasubiri kupata taarifa
rasmi toka serikali ya Tanzania
kuhusiana na watu wetu kama
wako salama na hakuna yeyote
aliyepoteza maisha katika mlipuko
huo,hata hivyo wakati tukisubiri
taarifa kutoka serikali ya Tanzania
nitatuma kikosi cha watu kumi na
tano kwenda Tanzania
kuchunguza suala hili na kupata
majibu ya uhakika ni nani hasa
waliohusika katika shambulio lile.Suala hili linatuhusu sisi hivyo
linapaswa kuchunguzwa na
vyombo vyetu wenyewe hivyo
naamini serikali ya Tanzania
watatoa ushirikiano kwa watu
wetu ili waweze kufanikisha
uchunguzi wa jambo hili na
mwisho kumleta waziri wetu
Helmet na wote aliombatana nao
nyumbani
Napenda kutoa angalizo kwa
wale wote waliofanya tukio hili
waanze kutafuta sehemu ya
kwenda kujificha kwani
hakutakuwa na huruma kwa
yeyote aliyeshiriki katika jambo
hili la kuhatarisha usalama wa
watu wetu.Taifa lolote lenye
mkono wake katika jambo hili liwe kubwa au dogo litalipa uovu wao
na tutawaonyesha hasira
zetu.Hatutafumba macho hadi mtu
wa mwisho aliyehusika katika
shambulio hili atakapoadhibiwa
vikali.Narudia tena taifa lolote lile
ambalo lina mkono wake katika
jambo hili tutaliharibu vibaya.
Nawaomba wamarekani
muwe watulivu suala hili
linashughulikiwa kikamilifu na
mtafahamishwa kila
kinachoendelea.
Mungu ibariki Marekani
Ilikuwa ni hotuba fupi lakini
iliyobeba ujumbe mzito.Mataifa
mengine yaliungana na Marekani
kutoa matamko ya kulaani
shambulio lile na kutaka hatua kali zichukuliwe kwa yeyote
aliyehusika katika shambulio lile
Mathew na Camilla wakiwa na
waziri Helmet Brian waliwasili
katika hospitali ya Mt Clara
ambako Theresa alipelekwa baada
ya kushambuliwa kwa
risasi.Mathew akashuka na
kuwataka Camilla na Helmet
wabaki garini,akaenda mapokezi
akauliza kuhusu hali ya
Theresa.Dada aliyekuwepo
mapokezi akabonyeza kompyuta
yake na kusoma orodha ya
wagonjwa kisha akasema “Mgonjwa Theresa Matope
hatuwezi kukupa taarifa zake
labda uonane na daktari mkuu wa
zamu” akasema yule mwanadada
na kumuelekeza Mathew ilipo ofisi
ya daktari mkuu wa zamu usiku
ule akaenda haraka na kugonga
mlango akaruhusiwa kuingia
ndani.Alimkuta daktari mmoja
kijana wakasalimiana
akajitambulisha kisha akaeleza
shida yake
“Utanisamehe ndugu yangu
kwani sintaweza kukuruhusu
kwenda kumtazama mgonjwa
huyo hadi hapo utakapopata kibali
cha rais kwani ndiye aliyetoa
maelekezo hayo kwamba mtu
yeyote asiruhusiwe kuingia katika chumba cha Theresa kama si
mwanafamilia .Ni
madaktari,wauguzi na wanafamilia
pekee ambao wanaruhusiwa
kuingia katika chumba alimolazwa
Theresa”
“Daktari mimi ndiye
niliyemleta hapa Theresa baada ya
kushambuliwa na hata rais
mwenyewe ananifahamu
vyema.Naomba tafadhali
uniruhusu ndugu yangu
nikamtazame Theresa” akasema
Mathew lakini msimamo wa
daktari uliendelea kuwa pale pale
kwamba akitaka kumuna Theresa
lazima apate kwanza kibali cha
rais “Ahsante daktari” akasema
Mathew na kuondoka akaelekea
katika gari lake
“Theresa anaendeleaje?
Akauliza Camilla
“Sijaruhusiwa kumuona.Ili
kuingia katika chumba alimolazwa
lazima upate kibali toka kwa
rais.Ameelekeza mtu yeyote
ambaye si mwanafamlia
asiruhusiwe kuingia” akasema
Mathew
“Tunamsubiri nani hapa
hospitali? Waziri Helmet akauliza
“Kuna mtu tunamsubiri hapa”
akajibu Mathew na ukimya
ukaendelea kutawala
garini.Zilipita dakika ishirini toka
wawasili pale hospitali mara kikasikika king’ora cha polisi na
rais akawasili.Mathew akashuka
na kumfuata rais.
“Vipi hali ya Theresa?
Anaendeleaje?Mimi nimezuiliwa
kwenda kumtazama kwa kuwa si
mwanafamilia.Mheshimiwa rais
naomba kibali cha kuweza kufika
na kumuona Theresa bila vikwazo”
akasema Mathew baada ya
kuonana na rais
“Nimetaarifiwa hali yake bado
si nzuri.Ametolewa katika chumba
cha upasuaji ila bado
hajitambui.Nimetoa maelekezo
kwa uongozi wa hospitali
asiruhusiwe mtu yeyote kuingia
katika chumba cha Theresa kama
si mwanafamilia ili kuhakikisha ndugu yangu anakuwa salama ”
akasema rais na akatokea daktari
mkuu wa zamu usiku ule ambaye
alistuka sana alipomuona Mathew
akiwa amesimama na rais
wakizungumza.Daktari yule
akajitambulisha na rais akamtaka
waelekee katika chumba alimo
Theresa
“Daktari” akaita rais wakati
wakielekea katika chumba
alimolazwa Theresa
“Huyu niliyeongozana naye
anaitwa Mathew ni mtu wa karibu
sana na familia yetu kwa hiyo
naomba aruhusiwe muda wowote
akija hapa hospitali kumuona
Theresa” akasema Rais na yule
daktari akaitika kwa adabu Waliingia katika chumba
alimo Theresa bado alikuwa
amezungukwa na mashine kadhaa
zikimsaidia kuendesha mifumo
kadhaa ya mwili ambayo bado
ilikuwa dhaifu.
“Mungu atakuponya Theresa
na utakuwa mzima tena.Siwezi
kujisamehe kwa sababu yote haya
yaliyotokea mimi ndiye
chanzo.Sikumlinda ipasavyo”
akawaza Mathew wakati daktari
akimpa rais maelezo kuhusiana na
maendeleo ya Theresa.Walitoka
mle chumbani na rais akamuomba
Mathew waelekee katika gari lake
kwa ajili ya
mazungumzo.Wakaingia katika gari la rais na Dr Vivian akafuta
machozi.
“Kila nikimuona Theresa
akiwa katika hali ile ninaumia
sana.Nadhani sasa ni wakati
wakufahamu nini hasa
kilichomtokea mdogo wangu? Nani
aliyetaka kuondoa uhai wake?
Tafadhali nieleze Mathew nahitaji
kujua kilichotokea” akasema rais
“Pole sana mheshimiwa rais
lakini nakuhakikishia kwamba
Theresa atapona tu.Sote
tunamuombea na Mungu atasikia
dua zetu na atamponya” akasema
Mathew na rais akafuta tena
machozi.
“Mathew naamini umesikia
kilichotokea usiku huu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere.Kufuatia tukio hilo
nilitakiwa kuwa katika kikao
muhimu sana muda huu kujadili
kilichotokea na hali ya amani hapa
nchini lakini nimelazimika
kuahirisha kila kitu na kuja
kukusikiliza.Naomba tusipoteze
muda nieleze mara moja kile
ulichoniitia hapa” akasema rais
“Kwanza nakupa pole nyingi
kwa matukio yaliyotokea
leo.Ninakushukuru pia kwa
kukubali mwito wangu na kuja
kunisikiliza.Kama nilivyokueleza
ni kwamba nisingeweza kukuomba
uahirishe shughuli zako kama
jambo lenyewe halingekuwa na
umuhimu mkubwa.” “Ni jambo gani Mathew nenda
moja kwa moja katika pointi sitaki
mizunguko kwa muda huu.Kichwa
changu kina mambo mengi sana”
akasema Dr Vivian
“Ni kuhusiana na kilichotokea
uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere.” Akasema Mathew na
DrVivian akamtumbulia macho
“Mimi ndiye ninayehusika na
kilichotokea pale uwanja wa
ndege.Mimi ndiye niliye lipua lile
bomu”
Dr Vivian akamtazama
Mathew kwa mshangao mkubwa
kama vile ni mara yake ya kwanza
anamuona.
“You ?!! akauliza
akimnyooshea kidole “Ndiyo mheshimiwa rais,mimi
ndiye niliyehusika” akasema
Mathew na Dr Vivian akashusha
pumzi.
“Kwa mara ya kwanza
nimekosa neno la kusema!!
Akasema Dr Vivian
“Hutakiwi kusema kitu
mheshimiwa rais mimi ndiye
mwenye kitu cha
kusema.Nimefanya tukio lile kwa
ajili ya kumuokoa waziri wa
mambo ya nje wa Marekani Helmet
Brian asiuawe.Niligundua kuwepo
kwa mpango wa kumuua Helmet
uliopangwa na serikali ya
marekani kwa kushirikiana na
washirika wao wa hapa Tanzania” “Serikali ya Marekani
wanataka kumuua waziri wao wa
mambo ya nje? Akauliza Dr Vivian
kwa mshangao
“Ndiyo madam president”
“That’s not true.Kwanza kwa
nini wafanye hivyo? Hiyo siyo
namna Marekani wanavyofanya
mambo yao”
“Huo ndio ukweli
mheshimiwa rais kwamba
Marekani walipanga mauaji ya
waziri wao wa masuala ya nje kwa
lengo la kupata sababu ya
kuishambulia Korea
kaskazini.Kuna watu ambao
wameandaliwa maalum kwa kazi
hiyo ya kumuua Helmet na baada
ya kumuua Marekani wangetuma wachunguzi wao kuja Tanzania na
wangewakamata watu hao na
baada ya kuwahoji watu hao
wangekiri kutumwa na serikali ya
Korea Kaskazini kumuua Helmet
na hapo marekani wangeanza
kuishambulia Korea kaskazini kwa
kigezo cha kulipiza kisasi”
“Mathew natamani sana
nikuamini lakini naogopa
kukuamini kwa sababu jambo hili
ni kubwa na sidhani kama
Marekani wanaweza kuwa tayari
kumuua waziri wao wenyewe”
“Mheshimiwa rais jambo hili
nina uhakika nalo na nimelipata
kutoka kwa mtu ambaye marekani
wamekuwa wakimtumia kuratibu
hili suala kwa hapa Tanzania ambaye huwezi kuamini
nikikutajia”
“Ni nani? Akauliza rais huku
sura yake ikionyesha wasi wasi
“Ni mtu wako wa karibu
ambaye uko tayari kufanya kila
uwezalo kumlinda.Ni Dr Robert
Mwainamela” akasema Mathew na
mstuko alioupata Dr Vivian
ulikuwa mkubwa sana.kwa dakika
nzima alikuwa anamtazama
Mathew
“I cant believe you Mathew!!
akasema
“Mheshimiwa rais
sikulazimishi uniamini lakini huo
ndio ukweli wenyewe.Dr Robert
ndiye aliyekuwa akiratibu mpango
huo wa kumuua Helmet na amekuwa akitumiwa na serikali ya
marekani katika mipango yake
mbalimbali hapa nchini”
“Mathew are you sure of this?
Akauliza rais
“Madam president kuna kitu
kimoja ambacho hukifahamu
kuhusu mimi,I’m always
right.Nikikuambia mtu fulani
anapaswa kuchunguzwa amini
kuna kitu tayari
nimekiona.Nilikuomba
nimchunguze Dr Robert lakini
ukamtetea kwa nguvu kubwa ila
ungefahamu mambo anayoyafanya
DrRobert nyuma yako ungeanguka
na kuzimia” akasema Mathew.
“Yuko wapi hivi sasa Dr
Robert? “Ninaye bado namfanyia
mahojiano.Kuna mambo mengi
nahitaji kuyafahamu kutoka
kwake na baada ya kukamilisha
uchunguzi wangu nitakuja
kukueleza kama utakuwa tayari
lakini kuna jambo lingine la
muhimu ambalo ningependa
ulifahamu.Mwanamke aliyeletwa
ofisini kwako akitambulishwa
kama Tausi mtoto wa marehemu
mzee Anorld Mubara ni pandikizi
la Marekani na hana mahusiano
yoyote na mzee
Mubara.Ulidanganywa.Tausi
Mubara si jina lake halisi ni jina
bandia.Jina lake halisi anaitwa
Olivia na hata vyeti vyote
alivyokuja kuwaonyesha ni bandia hajawahi kusoma katika shule na
vyuo alivyoorodhesha.Kwa kifupi
ni kwamba Tausi ni pandikizi la
CIA.Baada ya Nathan CIA
wakamleta Tausi.Huyu Tausi na Dr
Robert wamekuwa na mawasiliano
ya karibu na wamekuwa pamoja
katika mpango huu wa kumuua
Helmet Brian.Nafahamu haitakuwa
rahisi kuniamini lakini huo ndio
ukweli na ninaomba ufahamu pia
kwamba Tausi tayari
amefariki,amejipiga risasi na ndiye
aliyempiga risasi Theresa”
“No !! That’s not true !!
akasema Rais
“Ni vigumu kuamini lakini huo
ndio ukweli wenyewe.Sasa twende
katika gari langu kuna kitu nataka nikuonyeshe” akasema Mathew na
kufungua mlango akashuka.Rais
akamtaka amsubiri kwa muda
.Baada ya dakika nne rais
akashuka wakaelekea katika gari
la Mathew,akafungua mlango na
kuwasha taa
“Madam president
ninakukabidhi waziri wa mambo
ya nje wa Marekani Helmet Brian
akiwa mzima na hana hata
mchubuko.Ana hitaji ulinzi
mkubwa kwani bila kufanya hivyo
marekani lazima watamuua”
“Oh Jesus Christ !!akasema Dr
Vivian
“Mheshimiwa waziri
nakuomba ushuke garini.Kuanzia
sasa utakua chini ya uangalizi wa rais yeye atakupa ulinzi wa
uhakika zaidi” akasema Mathew na
waziri Helmet akashuka garini
akasalimiana na Dr Vivian.Mathew
akatoa karatasi mfukoni na
kumpatia rais
“Madam president hawa ni
raia wa kigeni waliotumwa kuja
kumuua waziri Helmet.Majina ya
hoteli walizofikia yameandikwa na
tuna imani bado hawajatoka
nchini.Watu hawa watafutwe
haraka sana wakamatwe na
wataeleza ukweli wote kuhusiana
na mpango huu wa kumuua waziri
Helmet.Ahsante mheshimiwa rais
kwa kunisikiliza” akasema Mathew
na kuagana na waziri Helmet
ambaye aliwashukuru kwa kumuokoa akaingia garini
wakaondoka akimuacha rais akiwa
amesimama akilitazama gari la
Mathew likiondoka.
“Kwa sasa waziri Helmet yuko
katika mikono salama.Kazi yetu
sisi tumeimaliza na kilichobaki ni
jambo la kiserikali
zaidi.Tunakwenda kuendelea na
uchunguzi wetu.Kuna mambo
mengi tunakwenda kuyafahamu
kwa Dr Robert” akasema Mathew
na simu yake ikapigwa alikuwa ni
Hamis Chuma.Mathew akaipokea
haraka
“Mathew ..Mathew..!!.”
akasema Hamis
“Hamis kuna nini? Akauliza
Mathew “Mathew tumevamiwa na
kundi la watu wenye silaha nzito
vijana wangu wawili wote
wameuawa na mimi nimefanikiwa
kukimbia lakini nimejeruhiwa
mguuni kwa risasi.”
“Vipi kuhusu Dr Robert?!!!
Akauliza Mathew
“Sijui kilichoendelea huko
ndani kwani baada ya
kutushambulia mimi nilikimbia na
sijui kilichoendelea” akasema
Hamis
“Hamis uko wapi hivi sasa?
“Tayari nimewaita vijana
wangu wamenichukua
wananipeleka hospitali.Jeraha
linamwaga damu nyingi” “Pole sana Hamis.Mimi
ninaelekea huko nyumbani sasa
hivi”akasema Mathew na kukata
simu akaongeza mwendo wa gari.
“Kuna jambo limetokea
nyumbani.Watu wenye silaha
wamevamia,wameua walinzi
tuliowaacha na kwa bahati nzuri
Hamis Chuma amefanikiwa
kutoroka lakini amejeruhiwa na
risasi mguuni”
“Oh Mungu wangu !! Ni akina
nani hao? Vipi kuhsu DrRobert na
wanae? Akauliza Camilla ambaye
alistushwa sana na taarifa
ile.Mathew hakujibu kitu
akaongeza mwendo wa gari
kuwahi nyumbani kwake “Naamini waliovamia
nyumbani kwangu ni ule
mtandanowa CIA hapa
nchini.Yawezekana tayari
wamefahamu kwamba waziri
Helmet yuko nyumbani kwangu na
wamevamia ili
kumchukua.Lilikuwa wazo zuri
kuamua kumpeleka waziri Helmet
na kumkabidhi kwa rais.Wasiwasi
wangu ni kwa Dr Robert.Endapo
wakimkuta mle ndani
watamchukua na kumtorosha na
sintopata yale mambo yote
muhimu toka kwake” akawaza
Mathew
Waliwasili nyumbani kwa
Mathew na kukuta nyumba yake imezingirwa na askari wenye
silaha
“Askari polisi tayari
wamekwisha pata taarifa za
kilichotokea hapa
nyumbani.Inawezekana majirani
waliwapigia simu na wakafika kwa
haraka kuwadhibiti wale wavamizi
waliovamia” akasema Mathew
huku akifungua mlango na
kushuka.Askari mmoja
akamsimamisha na kumtaka
ajitambulishe yeye ni nani.Mathew
akajitambulisha kwamba yeye
ndiye mmiliki wa ile nyumba na
hakuwepo nyumbani wakati
ilipovamiwa.Mara moja akasikia
vyuma vikilia askari walikuwa wanaweka sawa silaha zao.Mmoja
wa askari wale akamsoglea karibu.
“Mathew Mulumbi uko chini
ya ulinzi kwa mauaji ya waziri wa
mambo ya ndani ya nchi na
kuwateka watoto wake na
kuwafungia chumbani” akasema
yule askari na kumsogelea Mathew
akamtaka ainue mikono
juu.Mathew alihisi miguu
inaishiwa nguvu.Askari yule
akamsogelea akamshika mkono
akamfunga pingu na kumtaka
apige magoti.Mathew hakuwa na
ujanja tayari alikuwa katika
mikono ya polisi.Haraka haraka
akasachiwa na silaha zake zote
zikachukuliwa.Askari
wakalisogelea gari la Mathew na kumtaka Camilla ashuke
garini.Akatii na kufungua mlango
akashuka.Akasachiwa na
hakukutwa na silaha
yoyote.Akapigishwa magoti
pembeni ya Mathew na muda huo
huo askari wakatoka ndani
wakiwa wamebeba mwili katika
machela ukiwa umefunikwa
shuka.Nyuma ya mwili ule
wakatokea watoto wawili wa Dr
Robert Juliana na Julieth wakiwa
wameshikwa mikono na askari
huku wakilia kwa nguvu.Camilla
machozi yakamtoka alipowaona
watoto wake wakilia.
Mathew Mulumbi uko chini
ya ulinzi kwa mauaji ya waziri wa
mambo ya ndani ya nchi na
kuwateka watoto wake na
kuwafungia chumbani” akasema
yule askari na kumsogelea Mathew
akamtaka ainue mikono
juu.Mathew alihisi miguun inaishiwa nguvu.Askari yule
akamsogelea akamshika mkono
akamfunga pingu na kumtaka
apige magoti.Mathew hakuwa na
ujanja tayari alikuwa katika
mikono ya polisi.Haraka haraka
akasachiwa na silaha zake zote
zikachukuliwa.Askari
wakalisogelea gari la Mathew na
kumtaka Camilla ashuke
garini.Akatii na kufungua mlango
akashuka.Akasachiwa na
hakukutwa na silaha
yoyote.Akapigishwa magoti
pembeni ya Mathew na muda huo
huo askari wakatoka ndani
wakiwa wamebeba mwili katika
machela ukiwa umefunikwa
shuka.Nyuma ya mwili ule wakatokea watoto wawili wa Dr
Robert Juliana na Julieth wakiwa
wameshikwa mikono na askari
huku wakilia kwa nguvu.Camilla
machozi yakamtoka alipowaona
watoto wake wakilia. “Yuko wapi hivi sasa Dr
Robert?
“Ninaye,bado namfanyia
mahojiano.Kuna mambo mengi
nahitaji kuyafahamu kutoka
kwake na baada ya kukamilisha
uchunguzi wangu nitakuja
kukueleza kama utakuwa
tayari,lakini kuna jambo lingine la
muhimu ambalo ningependa
ulifahamu.Mwanamke aliyeletwa
ofisini kwako akitambulishwa
kama Tausi mtoto wa marehemu
mzee Anorld Mubara ni pandikizi
la Marekani na hana mahusiano
yoyote na mzee Mubara.Ulidanganywa.Tausi
Mubara si jina lake halisi ni jina
bandia.Jina lake halisi anaitwa
Olivia na hata vyeti vyote
alivyokuja kuwaonyesha ni bandia
hajawahi kusoma katika shule na
vyuo alivyoorodhesha.Kwa kifupi
ni kwamba Tausi ni pandikizi la
CIA.Baada ya Nathan,CIA
wakamleta Tausi.Huyu Tausi na Dr
Robert wamekuwa na mawasiliano
ya karibu na wamekuwa pamoja
katika mpango huu wa kumuua
Helmet Brian.Nafahamu haitakuwa
rahisi kuniamini lakini huo ndio
ukweli na ninaomba ufahamu pia
kwamba Tausi tayari
amefariki,amejipiga risasi na ndiye
aliyempiga risasi Theresa” “No !! That’s not true !!
akasema Rais
“Ni vigumu kuamini lakini huo
ndio ukweli wenyewe.Sasa twende
katika gari langu kuna kitu nataka
nikuonyeshe” akasema Mathew na
kufungua mlango akashuka.Rais
akamtaka amsubiri kwa
muda.Mathew akashuka na
kumuacha Dr Vivian peke yake
garini.Dr Vivian akavuta pumzi
ndefu na kuufunika uso wake kwa
viganja vya mikono
“Oh my God!! Its getting ugly”
akanong’ona
“Nilimzuia Mathew asiendelee
na upelelezi wake baada ya kuona
mwenendo wake si
mzuri.Niling’amua anakoelekea si kuzuri hata kidogo na anaweza
akavuka mstari na akafahamu
mambo ambayo hapaswi
kuyafahamu lakini yule jamaa ni
mkaidi sana na hakubali
kushindwa ameendelea na
upelelezi wake licha ya kumkataza
na tayari amekwisha kanyaga
mstari.Kitendo cha kumshikilia Dr
Robert ni ishara tosha kwamba
amekanyaga mstari na muda si
mrefu anaweza akauvuka jambo
ambalo sitaki litokee.Nilipomtaka
achunguze kuhusu mauaji ya baba
yangu sikutegemea kama angefika
hapa alipofiuka.Naikubali sana
kazi yake,ni mtu shupavu na
amefanya makubwa na anastahili
pongezi hasa kwa hili alilolifanya leo la kumuokoa waziri wa Helmet
Brian asiuawe kwani endapo
mpango huo ungefanikiwa basi
Marekani wangepata sababu ya
kuishambulia Korea kaskazini na
ingeibuka vita kubwa na ule
mpango wetu wa mashirikiano ya
kibiashara na Korea Kaskazini
ungeishia hewani.Namshukuru
sana Mathew kwa hilo lakini sina
budi kutumia uwezo wangu
kumsimamisha asiendelee na
uchunguzi wake kwani mahala
alipofika hatakiwi kuendelea
mbele zaidi.Uchunguzi wa kifo cha
baba ameuweka pembeni na
ameingia katika mambo mengine
kabisa yasiyohusiana na jambo
nililomtaka achunguze.Mdogo wangu Theresa uhai wake
unashikiliwa na mashine hivi sasa
na yote hii ni kwa sababu yake.I
must stop him !! akawaza Dr Vivian
na kuchukua simu akampigia
mkurugenzi wa idara ya usalama
wa taifa Meshack Jumbo.
“Madam president” akasema
Meshack Jumbo baada ya kupokea
simu
“Meshack naomba usogee
pembeni mahala kusiko na watu
nina mazungmzo nawe ya muhimu
sana” akasema rais na baada ya
skeunde chache Meshack akasema
“Endelea madam president”
“Naomba unisikilize kwa
makini na ninaomba yalenitakayoelekeza yafanyike kwa
haraka sana”
“Sawa mheshimiwa rais
nitafanya kama utakavyoelekeza.”
Akasema Meshack Jumbo
“Hivi tuongeavyo waziri wa
mambo ya nje wa Tanzania Dr
Robert Mwainamela anashikiliwa
nyumbani kwa Mathew.Muda
mfupi ujao Mathew atamfanyia
mahojiano na ninaamini kuna
mambo ambayo Dr Robert
atamuleza ambayo Mathew
hapaswi kuyafahamu” akanyamaza
kwa sekunde tano na kuendelea
“Mr Jumbo sitaki jambo hili
litokee.Sitaki Mathew amfanyie
mahojiano Dr Robert.Haraka sana
nataka utume watu nyumbani kwa Mathew wakamuue Dr Robert.Kwa
sasa Mathew niko naye hapa St
Clara hospital na akitoka hapa
atarejea nyumbani kwake
kumuhoji Dr Robert.Siaki amkute
akiwa bado hai.Naomba sana
jambo hili litekelezwe haraka”
akasema Dr Vivian
“Madam president …” akataka
kusema kitu Meshack Jumbo lakini
rais akamzuia.
“Mzee Jumbo nafahamu
unachotaka kukisema lakini
sihitaji maelezo au ushauri
wowote katika hili.Naomba
litekelezwe haraka sana kama
ninavyoagiza,hili si ombi bali ni
amri.Umenielewa Jumbo? “Mheshimiwa rais,wewe ni
kiongiozi wangu ambaye
ninapaswa kutii kila
unachoniagiza lakini katika hili
ninapatwa na kigugumizi
kidogo.Kwanza ni kuhusiana na Dr
Robert.Huyu ni waziri wetu wa
mambo ya nje kwa nini
tumuue?Pili Mathew ni kijana
wangu ninamfahamu vyema
hakurupuki katika kufanya kazi
zake .Anafahamu
anachokifanya,tena kuna
uwezekano mkubwa Dr Robert
akawa anahusika katika suala
analolifanyia uchunguzi hivi
sasa,huoni kama tukimuondoa Dr
Robert atashindwa kupata mambo
muhimu katika uchunguzi wake? “Meshack sitaki kurudia suala
hili mara mbili,naomba ulifanyie
kazi suala hilo na unijulishe
litakapokuwa tayari.Kabla ya
Mathew kurejea nyumbani kwake
nataka Dr Robert awe tayari
amekwisha malizwa na unijulishe
pindi zoezi hilo
likikamilika.Naomba usiondoke
hapo ikulu kwani nitakuwa na
mazungumzo nawe nitakaporejea”
akasema Dr Vivian
“madam president..”
“Meshack fanya hivyo
nilivyokuelekeza tafadhali !!
akasema Dr Vivian na kukata
simu.Akavuta pumzi ndefu
“Yote haya ameyataka Mathew
mwenyewe kwa ukaidi wake.Nilimzuia asiendelee na
uchunguzi akanipuuza na
akaendelea kwa siri na sasa
anataka kuingia mahala
asikotakiwa kufika na sina namna
nyingine ya kufanya zaidi ya
kutumia uwezo wangu kumzuia
asiende mbele zaidi na kufika
huko asikotakiwa”akawaza Dr
Vivian na kushuka garini
akaongozana na Mathew hadi
katika gari lake akafungua mlango
na kuwasha taa
““Madam president
ninakukabidhi waziri wa mambo
ya nje wa Marekani Helmet Brian
akiwa mzima na hana hata
mchubuko.Anahitaji ulinzi mkubwa kwani bila kufanya hivyo
Marekani watamuua”
“Oh Jesus Christ !!akasema Dr
Vivian
“Mheshimiwa waziri
nakuomba ushuke garini.Kuanzia
sasa utakua chini ya uangalizi wa
rais yeye atakupa ulinzi wa
uhakika zaidi” akasema Mathew na
waziri Helmet akashuka garini
akasalimiana na Dr Vivian.Mathew
akatoa karatasi mfukoni na
kumpatia rais
“Madam president hawa ni
raia wa kigeni waliotumwa kuja
kumuua waziri Helmet.Majina ya
hoteli walizofikia yameandikwa na
tuna imani bado hawajatoka
nchini.Watu hawa watafutwe haraka sana wakamatwe na
wataeleza ukweli wote kuhusiana
na mpango huu wa kumuua waziri
Helmet.Ahsante mheshimiwa rais
kwa kunipa nafasiya kunisikiliza”
akasema Mathew na kumpa mkono
waziri Helmet
“Tafadhali naomba
unikumbushe jina lako” akasema
Helmet
“Naitwa Mathew Mulumbi”
“Mathew ahsante sana kwa
kuyaokoa maisha yangu leo.Sina
neno zuri la kukushukuru kwa hili
ulilolifanya.Taifa la Tanzania
linapaswa kujivunia sana kuwa na
mtu mahiri kama wewe.Nifikishie
salamu zangu na shukrani za
pekee kabisa kwa wenzako wote mlioshirikiana katika zoezi hili na
ninawaahidi baada ya sakata hili
kumalizika salama nitahitaji
kuonana nanyi wote niwashukuru
kwa pamoja.” Akasema Helmet
“Ahsante sana mheshimiwa
waziri.Muda wowote ukihitaji
kuonana nami utamueleza rais
naye anajua mahala kwa kunipata”
akasema Mathew na kuagana na
Helmet akaingia garini
wakaondoka akimuacha rais akiwa
amesimama akilitazama gari la
Mathew likiondoka
“Mheshimiwa rais” akaita
waziri Helmet baada ya kumuona
rais Dr Vivian amezama mawazoni
akilitazama gari la Mathew
likipotea “Oh ! Mheshimiwa waziri” Dr
Vivian akastuka
“Pole sana kwa masahibu yote
yaliyokupata.Ni jambo la
kushangaza sana lililofanywa na
serikali ya Marekani.Karibu
Tanzania na hapa utakuwa
salama” akasema Dr Vivian na
kumuongoza Helmet hadi katika
gari lake wakaondoka pale
hospitali kuelekea ikulu
“Mheshmiwa rais bado naona
suala hili kama ndoto.Bado siamini
kama kweli serikali yangu ambayo
ninaitumikia kwa uadilifu mkubwa
wanaweza kupanga mpango wa
kuniua.Inashangaza
sana.Nimejiuliza maswali elfu moja
kwa nini wafanye hivi sijapata jibu hata moja.Nakuomba mheshimiwa
rais uchunguzi wa kina ufanywe
kuhusiana na jambo hili ili ukweli
ubainike” akasema Helmet
“Mheshimiwa waziri,sina
mashaka hata kidogo na Mathew ni
mmoja wa watu ninaowamini mno
na kama amegundua kuwepo kwa
mpango huu wa kukuua
ulioandaliwa na Marekani basi
amini ni kitu cha kweli lakini hata
hivyo uchunguzi wa kina lazima
ufanyike ili tufahamu ni kwa nini
wamefanya hivi.Nitalikabidhi suala
hili kwa vyombo vyangu vya
uchunguzi ili haraka sana
uchunguzi uanze na ukweli
ubainike” akasema Dr Vivian “Ahsante sana mheshimiwa
rais ila naomba kwa muda huu
ambao uchunguzi utakuwa
unaendelea jambo hili liwe siri na
serikali ya Marekani
isifahamishwe chochote.Sitaki
wafahamu kama niko hai kwani
kama walipanga kuniua na
mpango wao ukashindikana
wakijua niko hai watafanya kila
namna hadi wafanikishe mpango
wao.Uchunguzi utakapokamilika
na ukweli kujulikana basi
nitajitokeza”
“Usijali kuhusu hilo
mheshimiwa waziri,nitalizingatia”
“Nashukur sana” akajibu
Helmet na simu ya Dr Vivian ikaita
alikuwa ni Meshack Jumbo “Nipe taarifa
Meshack.Maagizo yangu
yametekelezwa? Akauliza Dr
Vivian
“Ndiyo mheshimiwa
rais,tayari maagizo yako
yametekelezwa na Dr Robert
amekwisha ondolewa”
“Good.Niko njiani ninakuja
ikulu nitakuwa na mazungmzo
nawe hivyo usitoke hapo” akasema
Dr Vivian na kukata simu
akazitafuta namba za mkuu wa
jeshi la polisi nchini Inspekta
jenerali John Aminiel Mkoka
akampigia
“Mheshimiwa rais” akasema
Inspekta jenerali John Mkoka “IGP nimepokea sasa hivi
taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa
idara ya usalama wa taifa Meshack
Jumbo kwamba waziri wa mambo
ya nje ya nchi wa Tanzania Dr
Robert mwainamela ameuawa
nyumbani kwa mtu mmoja ambaye
amewahi kufanya kazi katika idara
ya ujasusi.Naomba tafadhali
elekeza jambo hili lifanyiwe kazi
haraka sana na huyo mtu
aliyefanya ukatili huo asakwe
kokote aliko na akamatwe kabla ya
kesho asubuhi.Onana na Mr
Meshack Jumbo mkuu mpya wa
idara ya usalama wa taifa yuko
hapo ikulu atakuelekeza mahala
yalipofanyika mauaji hayo” “Ahsante sana kwa taarifa hizi
za kustusha mheshimiwa rais.Mr
Jumbo niko naye hapa ikulu
tukikusubiri,ngoja nizungumze
naye mara moja” akasema mkuu
wa jeshi la polisi.
“Good” akajibu Dr Vivian na
kukata simu
Waliwasili ikulu rais
akaongozana na Helmet hadi
katika sebule yake
“Helmet karibu katika makazi
yangu ikulu.Hapa ni sehemu
salama na tafadhali jisikie
nyumbani.Endelea kupumzika
hapa mimi bado nina majukumu
mengine yananisubiri kwa wakati
huu hivyo naomba nikuache kwa
muda tutaonana baadae kidogo “Ahsante sana mheshmiwa
rais.Kabla hujaondoka kuna kitu
kimoja ninaomba
nisaidiwe.Nahitaji kuwasiliana na
familia yangu na kuwajulisha kuwa
niko salama na wasihofu”
“Sawa Helmet,wapo
wahudumu hapa watakusaidia
kwa chochote utakachohitaji”
akasema Dr Vivian na
kutoka.Kabla hajaingia katika
kikao na wakuu wa vyombo vya
usalama akamuita kwanza
Meshack Jumbo wakaingia katika
chumba cha mazungumzo ya
faragha
“Madam president ..” Meshack
Jumbo akataka kusema kitu lakini
rais akamzuia “Thank you
Meshack.Nashukuru kwa
kutekeleza agizo langu”
“madam …”
“Meshack kuna mambo mengi
yananikabili usiku wa leo hivyo
nina muda mchache wa maongezi
nawe na ninaomba unisikie vizuri”
akasema Dr Vivian ambaye sura
yake haikuonyesha mzaha hata
kidogo
“Nimetoka kuonana na
Mathew.Alinipigia simu na
kunitaka nikaonane naye kuna
jambo kubwa anataka kunieleza”
Dr Vivian akanyamaza kwa muda
halafu akaendelea
“Tukio lililotokea usiku huu
pale uwanja wa ndege JNIA anahusika nalo.Yeye ndiye
aliyelifanya”
“Mathew anahusika ?!!
Meshack Jumbo akashangaa.
“Ndiyo.Anadai kwamba
aligundua mpango wa Marekani
wa kutaka kumuua waziri Helmet
Brian hapa Tanzania na lengo lao
ni ili wapate sababu ya
kuishambulia Korea kaskazini”
akasema Dr Vivan na kutoa
karatasi akampa Meshack
“Hao watu watatu unaowaona
picha zao katika hiyo karatasi ni
wadunguaji walioletwa na
Marekani hapa nchini kwa ajili ya
kumuua Helmet.Baada ya
kutekeleza jukumu lao hilo
serikali ya Marekani ingewakamata halafu wangedai
kwamba walitumwa kufanya
hivyo na serikali ya Korea
Kaskazini na hicho ndicho
wanachokitafuta Marekani yaani
kupata sababu ya kuishambulia
kijeshi Korea Kaskazini.Watu hao
bado wako hapa nchini na kabla ya
mapambazuko nataka wawe tayari
wametiwa nguvuni”
“Dah ! Huyu kijana Mathew ni
mtu wa ajabu sana.Amewezaje
kugundua kuwepo kwa mpango
mkubwa kama huu? Akauliza
Meshack
“Marekani wameshirikiana na
watu wetu hapa ndani ili
kufanikisha mpango huo na
miongoni mwao ni viongozi serikalini.Huwezi kuamini Dr
Robert ni mmoja wa watu
waliokuwa wanatumiwa na
Marekani katika kuufanikisha
mpango huo”
“Dr Robert?! Meshack Jumbo
akashangaa
“Ndiyo.Hata mimi nilistuka
sana Mathew aliponiambia.Kumbe
nimezungukwa na nyoka bila
kujua. Dr Robert ni mmoja wa
watu ninaowaamini mno.Uadilifu
wake si wa kutiliwa
shaka.Nilikuwa nafikiria hata
kumpendekeza awe rais pale
nitakapomaliza kipindi changu
kumbe sikujua alikuwa ni chui
aliyevaa ngozi ya kondoo.Mathew
alikuja kwangu na kuniambia amchunguze Dr Robert lakini
nikamkatalia kumbe kuna kitu
tayari alikwishakiona kwa Dr
Robert” akasema Dr
Vivian.Meshack Jumbo
akamtazama Dr Vivian kwa macho
makali na kusema
“Madam president kama
Mathew amefanya mambo haya
makubwa kwa nini basi
ukamfanyia hivi
ulivyomfanyia?Kwa nini ukaamua
kumuua Dr Robert ambaye kumbe
ni msaliti mkubwa na endapo
Mathew angeendelea kumfanyia
mahojiano angeweza kugundua
mambo mengi makubwa?Marekani
wametengeneza mtandao wao
hapa nchini na kama Dr Robert ni mmoja wao basi angeweza
kufunguka na kutuonyesha
mtandao wake.Mathew ana mbinu
nyingi za kumfanya mtu aweze
kufunguka na kutoa taarifa
muhimu lakini hukutaka kumpa
nafasi,kwanza kuendelea na
uchunguzi aliokuwa anaufanya
kuhusu kifo cha baba yako ambao
tayari alikwisha piga hatua
kubwa.Pili hukutaka amuhoji Dr
Robert ambaye ni mtu muhimu
mno na ambaye angewezesha
mambo mengi kujulikana lakini
umeamua auawe.Kwa nini madam
president? Wewe mwenyewe
ulimpa kazi Mathew kwa nini
hutaki afanikiwe kuikamilisha kazi
uliyompa? Nahitaji kufahamu madam president kwa sababu
Mathew ni kama mwanangu na
katika kazi uliyompa aifanye toka
mwanzo nimekuwa nikimsaidia
sana na kwa sababu ya jambo hili
nimepoteza nyumba yangu na
nusura nipoteze maisha yangu na
familia yangu hivyo ninahitaji sana
kuona jambo hili linafika mwisho
na watu hawa kujulikana ni akina
nani na mtu pekee ambaye anao
uwezo wa kulifikisha mwisho
jambo hili ni Mathew ambaye hivi
tunavyoongea atakuwa katika
mikono ya polisi kwa maelekezo
yako mheshimiwa rais.Umetoea
maelekezo kwa IGP kwamba
ahakikishe Mathew anakamatwa
kwa kosa la kumuua waziri wa mambo ya nje Dr Robert
Mwainamela.Madam president
kwa nini unamuangamiza Mathew
wakati unafahamu fika kwamba
siye aliyemuua Dr Robert?Kwa
kesi hii kubwa uliyomtwisha
Mathew ni wazi hawezi kuponyoka
na ninaweza kusema kwamba
ndoto zake zote za maisha
zimeishia hapa kwani ataozea
gerezani,why madam president?
Why are you destroying this
innocent man? Amekufanyia nini
kiasi cha kukasirika na kuamua
kumtenda hivi? Mtu huyu
aliyejitolea kuifanya kazi yako bila
hata kulipwa senti moja kwa nini
umfanyie hivi?Nahitaji majibu
mheshimiwa rais katika suala hili kwa sababu Mathew ni kama
mwanangu hivyo siwezi kukubali
maisha yake yaharibike huku
nikishuhudia na mimi nikiwa
sehemu ya kuyaharibu maisha
yake” akasema Meshack Jumbo
ambaye alionekana kukasirika
sana.Dr Vivian akavuta pumzi
ndefu akatazama chini kwa
sekunde kadhaa alionekana
kufikiria jambo halafu akainua
kichwa akamtazama Meshack
Jumbo usoni na kusema
“Sikiliza mzee Jumbo.Wengi
wanalilia kukalia kiti cha urais
lakini ni kiti cha moto ukikikalia.Ni
mzigo mzito na kuna nyakati
inakulazimu kufanya mambo
ambayo hukuwahi kufikiria kuyafanya ili mambo yakae
sawa.Toka nilipomfahamu Mathew
hivi karibuni sikuwahi kufikiri
kama siku moja ningefanya
maamuzi kama haya niliyoyafanya
leo kwake.Naikubali na kuheshimu
sana kazi yake na mimi pia
ninatamani kuona kazi niliyompa
inafika mwisho lakini
nimelazimika kufanya haya
niliyoyafanya”
“kwanini madam president?
Hicho ndicho pekee ninachotaka
kukifahamu” akasema Meshack
Jumbo
“Mzee Jumbo naomba
tusiendelee zaidi na suala
hili.Tuendelee na mambo
mengine.Tuna mambo makubwa ya kujadili ambayo yanatakiwa
yatekelezwe usiku huu” akasema
Dr Vivian
“Madam president lazima
kwanza suala hili
limalizike.Mathew is like a son to
me so I need to know why you are
destroying him? After all he has
done to you and to this country is
this what he deserves? I need
answers madam president !!
akasema Meshack Jumbo huku
sauti yake ikiwa kali kidogo
“Mr Meshack mimi naweza
kuwa binti yako lakini naomba
usithubutu tena kuongea na mimi
kwa kunikaripia.Chunga sana sauti
yako unapozungumza na
mimi.Hapa unazungumza na rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Umenielewa mr Jumbo?
Akasema Dr Vivian kwa ukali
“I’m sorry madam president”
akasema Meshack Jumbo.Zikapita
sekunde kadhaa Dr Vivian
akasema
I’m sorry madam president”
akasema Meshack Jumbo.Zikapita
sekunde kadhaa Dr Vivian
akasema
“Mathew amekaribia kufika
mahala ambako hatakiwi kufika na
ndiyo maana nimefanya hivi ili
kumzuia asiendelee mbele zaidi na
kufika mahala ambako ni hatari
kwa maisha yake.Amekaribia
kuvuka mstari.Mathew ni aina ya
watu ambao hawakubali
kushindwa katika jambo lolote lile
walifanyalo kwa hiyo ili kumzuia
lazima kwanza aende gerezani na
akitoka huko basi hataweza kuendelea tena” akasema Dr
Vivian
“Madam president
sijakuelewa una maanisha nini
unaposema kwamba Mathew
amekaribia kuvuka mstari?Kwani
ulipompa kazi yako akufanyie
ulitegemea akwame? Au kuna
mipaka ulimuwekea asifike?
Akauliza Meshack.Dr Vivian
akainama akafikiri kidogo na
kusema
“Mr Jumbo kwa kuwa
unahitaji sana kufahamu basi
nitakueleza lakini yote
utakayoyasikia yatabaki hapa
ndani.Endapo kuna lolote
litakalovuja you are dead.You and
your family will all die.You understand me ?!! akauliza Dr
Vivian.Meshack Jumbo
akamtazama kwa muda na kusema
“You are not a killer madam
president and you cant kill me !!
“Kama unadhani hivyo basi
jaribu kunizunguka na utafahamu
vyema mimi ni nani” akasema Dr
Vivian kwa ukali na ukimya
ukatanda mle chumbani.Baada ya
muda akasema
“Kuna mambo ambayo Dr
Robert anayafahamu kuhusu mimi
ambayo endapo angehojiwa na
Mathew ni lazima angemueleza na
sitaki mtu mwingine yeyote
ayafahamu.Dr Robert alikuwa
mshirika na msiri wangu mkubwa
na anayafahamu mambo yangu mengi.Njia pekee ya kuzuia
mambo yangu yasitoke nje ni kwa
kumfumba mdomo.Pamoja na
kumuua Dr Robert Mathew kwa
umahiri wake engeweza
kuchuguza na kugundua nani
aliyemuua ndiyo maana nikaona ni
vyema kama naye akiwekwa
kizuizini kwa muda.Nadhani
mpaka hapo umenielewa kwa nini
nimefanya haya niliyoyafanya”
akasema Dr Vivian.Meshack Jumbo
akakuna kichwa na ukimya
ukatawala mle ndani
“Say something Mr Jumbo!!
Mbona umekuwa kimya ghafla?
Akauliza Dr Vivian “Madam president ..” Meshack
Jumbo akataka kusema kitu
akanyamaza
“Say it Meshack !! akasema Dr
Vivian
“Madam
president,nimehudumu katika
idara hii ya usalama wa taifa kwa
zaidi ya miaka ishirini.Nimefanya
kazi kwa ukaribu na marais wawili
nikiwa kama mkuu wa idara
hii.Kila rais niliyefanya naye kazi
alikuwa na siri zake.Nyingine
binafsi nyingine za
kikazi.Unapokalia kiti hicho
huwezi kutenda mambo yote sawa
lazima kuna mahali unaweza
kuteleza.Rais ni mwanadamu
kama wengine na si malaika hivyo kukosea ni kawaida.Ulipokuwa na
suala kama hili ungeniita
ukanieleza nikakushauri namna
bora zaidi ya
kufanya.Nimeaminiwa na marais
wote niliofanya kazi nao na
sikuwahi
kuwaangusha.Niliwafanyia kazi
zao za siri na mpaka leo hii siri zao
ziko salama hapa kifuani
kwangu.Nawe pia unapaswa
kuniamini mheshimiwa rais.Kama
una suala lolote la binafsi au la
kikazi ambalo ungependa
limalizwe kimya kimya usiogope
kunishirikisha nami nitakushauri
namna bora ya kulimaliza kama
tulivyolimaliza suala la Dr
Robert.Tukiachana na hayo turejee katika suala la Mathew.Naomba
nikuweke wazi mheshimwia rais
kwamba katika hili umekosea sana
kwa haya maamuzi
uliyoyachukua.Laiti
ungenishirikisha ingekuwa rahisi
mimi kuzungumza na Mathew na
yale mambo unayohofia kwamba
angeyafahamu asingeyagusa bali
yeye angeendelea na uchunguzi
wake wa jambo ulilomtuma”
“Meshack tumekwisha
limaliza hilo na sitaki tuendelee
kulijadili kwani sintabadili
msimamo wangu.Mimi ni tofauti
na marais wengine walionitangulia
ambao walikuita na kukueleza siri
zao.Siri zangu ni za kwangu na siko
tayari zivuje na kufika katika mikono ya adui zangu hivyo yeyote
ambaye akionekana kuwa hatari
kwangu basi nitamundoa mara
moja bila kusita.Hata wewe
nikikuona umekuwa hatari
kwangu sintasita kukuondoa
haraka sana kwa hiyo jichunge
sana mzee Meshack nimekuamini
na ninaomba hata siku moja
usivunje uaminifu wangu kwako”
akasema Dr Vivian.
“With respect madam
president what you did to Mathew
is unfair and it is the biggest
mistake you’ve ever done in your
life.Umefanya mambo mengi
makubwa na mazuri lakini kwa hili
umekosea sana.Hukupaswa
kufanya hivi” “Mr Jumbo narudia tena
kukuonya kwamba usinifundishe
namna ya kuifanya kazi
yangu.Nimekwisha fanya maamuzi
na hakuna wa kuyapinga.Naruidia
kwa mara nyingine tena mjadala
kuhusu Mathew nimekwisha
ufunga!!
“Hapana madam
president.Suala hili si dogo na
haliwezi kuchukuliwa kimzaha
mzaha.Mjadala kuhusu Mathew
bado mrefu na hatujafikia
muafaka.Wewe ni rais na unao
uwezo wa kufanya jambo lolote
ulitakalo ndani ya nchi lakini kwa
mara nyingine nakuhakikishia
kwamba kwa hili la Mathew
umekosea sana.Hukupaswa kabisa kuingia katika vita na
Mathew.Akifahamu kuwa ni wewe
ndiye uliyemfanyia haya Iswear
you are finished.Ninamfahamu
Mathew vyema ni kiumbe mbaya
sana akikasirika”
“Are you threatening me Mr
Jumbo? Akauliza Dr Vivian kwa
ukali.Tayari alikwisha kasirika
“I’m not threatening you
madam president,I’m telling you
the truth.What you did is totaly
wrong and once Mathew find out
that it is you behind everything
that’s heppening to him,you are
finished.You’ll go down madam
president!! Akasema Meshack
Jumbo.Dr Vivian huku akivuta
pumzi haraka haraka akasema “Don’t say another word
Jumbo or I’m going to destroy you
as well !!
“No you cant madam
president !! akasema Meshack
Jumbo
“There is a button under that
table.Once I push it my men will be
here in a second and will take you
away and that’ll be the end of
you.Dont force me to destroy you
old man.I don’t want to hear the
name Mathew again,you
understand me mr Jumbo?!!
Akauliza Dr Vivian akiwa amejaa
hasira
“Madam president naomba
nikuweke wazi kwamba Mathew ni
kijana wangu na alikubali kufanya kazi yako kwa sababu ya heshima
yangu.Siwezi kukubali kuona
akiangamia bila kosa lolot…..”
kabla Meshack hajamaliza sentensi
yake Dr Vivian akabonyeza kitufe
chini ya meza na ghafla walinzi
wanne wa rais wakaingia mle
ndani kwa kasi kubwa
‘That’s a mistake madam
president.If you lock me up then
you are finished.You need me so
badly right now.I’m the only one
who can get you out of this mess
you are in right now!! Akasema
Meshack Jumbo.Dr Vivian
akamtazama kwa makini na
kuwataka wale walinzi wake
watoke nje “Thank you madam president
!! akasema Meshack baada ya wale
walinzi wa rais kutoka
“Mshukuru malaika wako ana
nguvu sana kwani ni mara chache
nimefanya maamuzi na
kuyabatilisha.Wakati mwingine
nikikwambia lazima
unisikilize.Wewe ni mkubwa
kiumri lakini kimamlaka mimi ni
mkubwa wako hivyo unapaswa
kunitii hata kama nina umri sawa
na mwanao !! akasema Dr Vivian
“I’m sorry madam president .It
wont happen again” akasema
Meshack
“Na iwe hivyo” akasema Dr
Vivian “Kuhusu huyu kijana wako
Mathew.Hata mimi sifurahii
kumfanyia hivi na ni moja wapo ya
maamuzi magumu sana ambayo
nimewahi kuyafanya kama
rais.Nafahamu Mathew hana kosa
lolote lakini siwezi kumuacha huru
kwani lazima ataendelea
kuchimba na kufahamu mambo
ambayo hapaswi kuyafahamu na
mimi sitaki siri zangu
zijulikane.Kwa hiyo basi Mathew
lazima asimamishwe kwa muda
lakini hapo baadae ataachiwa
huru.Mjadala kuhusu yeye
unaishia hapa na suala hili ni mimi
na wewe pekee tunaolifahamu.Siri
hii ikivuja nitajua ni wewe na huo
utakuwa ni mwisho wako Meshack Jumbo.Je bado una dukuduku
lolote kuhusu suala hili?
“Hapana mheshimiwa
rais.Ninakubaliana na maamuzi
yako kwani kuna nyakati kama
kiongozi unalazimika kufanya
jambo ambalo hukuwa umepanga
kulifanya.Nimekutazama machoni
mheshimiwa rais hata wewe
umeumizwa na jambo hili lakini
hakuna namna.Tukubaliane na
kilichotokea tusonge mbele”
“Good ! Tuachane na hayo ya
Mathew.Hatukuwa tumemaliza
suala la Helmet Brian.Nataka kabla
ya mapambazuko ya kesho wale
watu watatu ambao nilikupa
karatasi yenye picha zao wawe
tayari wamekwisha tiwa nguvuni.Nataka wahojiwe na
tufahamu nani
aliyewatuma.Ukiacha hilo
namkabidhi kwako Helmet
Brian.Nataka afichwe mahala pa
siri sana.Mnazo sehemu zenu
ambazo huwa mnahifadhi watu
muhimu.Marekani lazima
watataka kufahamu mahala alipo
na hawatachoka hadi wahakikishe
wamempata hivyo basi jitahidi
kwa kila namna uwezavyo
kuhakikisha
hawafanikiwi.Tukifanikiwa kupata
ushahidi wa kutosha kwamba
kweli Marekani walikuwa na
mpango wa kumuua Helmet
tutakuwa tumepata fimbo ya
kuwachapia na tutawanyamazisha kelele zao.Hivyo basi naomba
fanya kila uwezavyo hakikisha
tunafanikiwa kuwapata hao jamaa
waliotumwa kumuua
Helmet.Ninakukabidhi jukumu hili
kwa kuwa ninakuamini na nina
imani kwamba Helmet yuko katika
mikono salama” akasema Dr
Vivian
“Mheshimiwa rais,waziri
Helmet tutamuhifadhi mahala
salama na pa siri.Watu wachache
tu wanaoweza kufika mahala
hapo.Hao wadunguaji walioingia
nchini kwa kazi moja ya kumuua
Helmet nakuhakikishia kabla ya
kufika asubuhi watakuwa
wamepatikana.Pamoja na hayo
mheshimiwa rais kuna jambo nataka kukushauri ila naomba
usikasirike”
“Jambo gani Meshack?
“Jambo hili ambaye angeweza
kulikamilisha kwa ufanisi mkubwa
ni aliyeligundua ambaye ni
Mathew.Tayari anafahamu mambo
mengi kuhusiana na mpango huu
hivyo endapo angeshiriki
ingependeza zaidi” akasema
Meshack
“Meshack umeniomba
nisikasirike na mimi sintakasirika
ila nataka nikuweke wazi kwamba
kwa sasa hakuna namna yoyote ya
kumsaidia Mathew.Habari yake
imekwisha.Katika idara yako ya
usalama wa taifa wapo vijana
wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa kama
Mathew hivyo nakuomba usiwe na
hofu.Tunao watu wengi mahiri
sana kwa hiyo tumuweke Mathew
pembeni kwa sasa na tuwatumie
watu wengine.Tumeelewana
Meshack? Akauliza Dr Vivian
“Sawa madam president”
akajibu Meshack
“Good.Nataka suala la
kuwatafuta wale jamaa lianze
mara moja vile vile shughulikia
sehemu ya kumuhifadhi
Helmet.Ninaingia katika kikao na
nitakapomaliza kikao naomba
nipate mrejesho mahala ulikofikia”
“Sawa mhesimiwa rais”
akasema Meshack Jumbo
wakatoka na rais akaelekea katika kikao cha dharura alichokiitisha
kwa lengo la kujadili kile
kilichokuwa kimetokea jioni
katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere. Kabla
ya kikao kuanza rais akamuita
mmoja wa walinzi wake
akamnong’oneza jambo
“Nataka weka vijana wawili
wamfuatilie Meshack
Jumbo.Nataka kujua kila
anachokifanya kuanzia usiku wa
leo.Nataka nipewe taarifa kila
baada ya nusu saa.Achunguzwe
anakwenda wapi na anakutana na
kina nani” akasema Dr Vivian na
kuendelea na kikao
Meshack Jumbo baada ya
kuachana na Dr Vivian,akaenda katika sebule ya rais alikokuwepo
Helmet Brian na kumkuta
akizungumza na simu akamfanyia
ishara akate mazungumzo yale na
bila kupoteza muda Helmet
akakata simu
“Helmet Brian,naitwa
Meshack Jumbo mkurugenzi wa
idara ya usalama wa taifa.Idara
yangu imekabidhiwa na rais
jukumu lote la usalama wako hivyo
usihofu uko katika nchi na mikono
salama.kwa sasa endelea
kupumzika wakati makazi yako
yanaandaliwa.Nitakuja baadae
kukuchukua na kukupeleka
mahala salama utakapoishi”
“Mnaniondoa hapa ikulu?
Helmet akashangaa “Ndiyo mheshimiwa
waziri.Usihofu utapelekwa sehemu
salama zaidi ya hapa ambako ni
watu wachache tu wanaopafahamu
tofauti na hapa ikulu ambapo ni
sehemu wanapoingia watu wengi
na hivyo hakuna usiri.Serikali ya
Marekani hawapaswi kufahamu
mahala ulipo”
“sawa Meshack” akajibu
Helmet
“jambo lingine” Meshack
akaendelea
“Hutakiwi kupiga simu kwa
mtu yeyote nchini kwako”
“Niliwasiliana na mke wangu
na kumjulisha kwamba niko
salama na kumuondoa hofu ila
nimemtaka asimueleze mtu mwingine yeyote kama niko
salama” akasema Helmet
“Ulifanya kosa.Hupaswi
kuwasiliana na mtu yeyote hata
familia yako kwani kuna
uwezekano mkubwa wakawa
wanachunguzwa na makachero wa
Marekani.Utawaweka katika hatari
kubwa.Utafika wakati utawasiliana
nao lakini si sasa” akasema
Meshack Jumbo na kutoka mle
sebuleni
“Siwezi kuwa sehemu ya
kuyaharibu maisha ya
Mathew.Siko tayari kuona kijana
yule akiangamia lazima nitafute
namna ya kumuokoa.Siamini kama
Dr Vivian anaweza kuwa na roho
ngumu ya kikatili namna hii kiasi cha kuamua kuyaharibu maisha ya
Mathew wakati akijua kabisa
kwamba hajatenda kosa
analotuhumiwa nalo.Kuna kitu
gani anakiogopa Mathew
asigundue kuhusu yeye? Dr Robert
lazima kuna siri kubwa
anaifahamu je ni siri gani hiyo?Dr
Robert alikuwamo katika mtandao
wa Marekani hapa nchini je Dr
Vivian hakulifahamu hilo?Kuna
mambo mengi ya kuyafahamu
hapa lakini ngoja kwanza
nishughulikie suala a kumtoa
Mathew katika mikono ya polisi
ambalo lazima lifanyike usiku huu
huu.Hata kama ni kuvamia kituo
cha polisi na kumtoa Mathew
lazima ifanyike hivyo ili mradi Mathew aokolewe.Kuna mambo
mazito kuhusu rais Dr Vivian
ambayo lazima tuyafahamu.Kuna
siri kubwa anaificha lakini
tutaitafuta hadi tuifahamu”
akawaza Meshack Jumbo na
kuingia chooni akachukua pochi
yake akatoa laini ya simu
akaiweka katika simu yake
akazitafuta namba fulani akapiga.
******************
Savanna 5 star hotel,moja kati
ya hoteli kubwa jijini Dar es
salaam,usiku huu ilijaa
wateja.Watu huwa wengi sana
katika hoteli hii hasa nyakati za
usiku kutokana na huduma zake nzuri.Vyakula vya mataifa mbali
mbali hupikwa na hivyo
kuwafanya wageni kutoka mataifa
mbali mbali kufika hapa kupata
vyakula vya asili yao.Ukiacha
huduma nzuri za chakula na
malazi,wengi hupenda kufika hapa
kupata mvinyo safi uitwao
Amarachi.Ni mvinyo
unaotengenezwa kwa matunda na
ambao umejizolea sifa kemkem
hasa kutokana na ladha yake nzuri.
Austin January anayemiliki
hoteli hii kwa pamoja na mke wake
Amarachi,akiwa amekaa na kundi
la wageni wakitokea nchini
Sweden wakiufurahia mvinyo
Amarachi,simu yake ikaita.Akaitoa
mfukoni na kutazama mpigaji.Hakuna jina lililojitokeza
katika kioo cha simu bali kulikuwa
na namba.Austin alipoziona namba
zile akastuka sana,akainuka
mahala alipokuwa amekaa
akasogea pembeni mahala kusiko
na watu.Simu ile ilianza kuita kwa
mara ya pili akaipokea
“Hallow mzee” akasema
Austin sauti yake ikionyesha
wasiwasi kidogo
“Hujambo Austin?
“Sijambo mzee shikamoo”
“marahaba.Vipi maendeleo
yako?
“Maendeleo yangu
mazuri.Nimestuka sana kuona
namba zako mida hii” “C’mon Austin kwa nini
ustuke?
“Mara nyingi nionapo namba
zako huwa ninastuka sana sijui
kwa nini”
“Usihofu Austin.Ninyi ni vijana
wangu na ndiyo maana huwa sitaki
kuwapigia simu mara kwa mara
kwani nafahamu mzionapo namba
zangu katika simu zenu huwa
mnastuka sana”
“Ndiyo mzee.Namba zako
hufanya mioyo yetu iende
mbio.Tuachane na hayo mzee
wangu habari za siku nyingi?
“Austin utanisamehe sina
muda mrefu wa maongezi nawe
nimekupigia ninahitaji msaada
wako wa haraka sana” akasema Meshack na kupitia spika za simu
akasikia Austin akishusha pumzi
“Msaada upi unauhitaji mzee?
Akauliza Austin
“Kuna mtu nahitaji
kumuondoa katika hatari kubwa
aliyomo.Endapo nisipofanya
juhudi za kumuondoa katika hatari
hiyo nitampoteza.Nahitaji sana
msaada wako kwa hilo” akasema
Meshack Jumbo
“Mzee kwa sasa nimekwisha
achana na hizo shughuli na
nimejiajiri katika shughuli zangu
binafsi.Labda nikusaidie kutafuta
kijana mwingine akusaidie katika
jambo hilo”
“Austin ninafahamu kwamba
kwa sasa unajishughulisha na shughuli zako binafsi lakini bado
ujuzi na uzoefu wako uko pale pale
hivyo ninakuomba unisaidie
katika kazi hiyo.Ukichelewa
nitampoteza kijana wangu.Ninao
vijana wengi ambao ningeweza
kuwaomba msaada lakini
nimekuchagua wewe kwani
ninaufahamu uwezo wako”
akasema Meshack.Ukatawala
ukimya na baada ya muda Austin
akauliza
“Ni nani huyo unayehitaji
kumuokoa,kafanya nini na yuko
wapi?
“Ni Mathew Mulumbi”
akasema Meshack na Austin
akastuka
“Mathew?! Austin akashangaa “Ndiyo.Ni Mathew”
“Kafanya nini?
“Alikuwa katika operesheni
fulani na akagundua jambo kubwa
lakini akawekewa mtego na sasa
yuko katika mikono ya polisi hivyo
nahitaji mtu wa kwenda
kumuokoa toka mikononi mwa
polisi” akasema Meshack jUmbo
“Mzee,huyu Mathew alikwisha
achana na hizi shughuli kama mimi
na anajishughulisha na shughuli
zake pia.Mara ya mwisho
nilikutana naye Paris akiwa na
mke wake Peniela amekuja lini
hapa nchini?
‘Tutazungumza baadae Austin
kwani kwa sasa muda unazidi
kwenda na endapo tutachelewa tunaweza kumpoteza” akasema
Meshack
“Kama ni Mathew basi niko
tayari kufanya kila niwezalo
kumuokoa.Yule ni mtu aliyewahi
kunisaidia sana wakati
fulani.Tayari amekwisha pelekwa
kituo cha polisi? Akauliza Austin
“Hapana bado ameshikiliwa
nyumbani kwake upekuzi
unafanyika” akasema
Meshack.Baada ya sekunde kadhaa
Austin akasema
“Mzee nina ushauri mmoja
ambao unaweza kutusaidia
tukampata Mathew bila kutumia
nguvu.”
“Ushauri gani huo? “Wewe uliwahi kuwa mkuu
wa idara ya usalama wa taifa na
una heshima kubwa sana katika
idara ile.Una mawasiliano na mkuu
wa sasa wa idara ya usalama wa
taifa?
“Kuna jambo ambalo sikuwa
nimekutaarifu Austin.Mkuu wa
idara ya usalama wa taifa
amefariki alijipiga risasi na rais
ameniteua mimi niongoze idara hii
kwamuda.Kwa sasa mimi ndiye
mkuu wa idara ya usalama wa
taifa”
‘That’s not true” akasema
Austin
“Its true.Rais aliniomba
nimsaidie kuiongoza idara hii kwa
muda wa mwaka mmoja hadi hapo atakapokuwa amempata mtu
ambaye atafaa kuiongoza idara hii”
“Kama ni hivyo basi kazi
itakuwa rahisi sana.Wasiliana na
kamanda wa polisi kanda maalum
ya Dar es salaam na mwelekeze
kwamba Mathew aliwahi fanya
kazi idara ya usalama wa taifa kwa
hiyo unamuhitaji kwa ajili ya
mahojiano halafu atakabidhiwa
kwa jeshi la polisi baada ya
kumfanyia mahojiano.Waambie
kuna suala zito la usalama wa nchi
ambalo tunahitaji kumuhoji
Mathew.Kwa kufanya hivyo
tunaweza kumchukua Mathew bila
kutumia nguvu” akasema Austin
Waambie
kuna suala zito la usalama wa nchi
ambalo tunahitaji kumuhoji
Mathew.Kwa kufanya hivyo
tunaweza kumchukua Mathew bila
kutumia nguvu” akasema Austin
‘Wazo lako ni zuri sana Austin
lakini ni gumu kulitekeleza.Rais tayari analifahamu jambo hili kwa
hiyo kutakuwa na ugumu
kuruhusu tumchukue Mathew”
“Mzee kama wewe ni mkuu wa
idara ya usalama wa taifa basi una
nguvu kubwa sana ya kuweza
kumuokoa Mathew.Uko wapi hivi
sasa?
“Niko ikulu lakini muda si
mrefu nitatoka” akasema Meshack
“Mzee tumia nguvu yako
kumuokoa kijana wako”
“Austin kama ningekuwa na
uwezo wa kumsaidia Mathew
nisingekupigia simu kukuomba
msaada.Do what you have to do to
rescue Mathew.Hata kama ni
kuvamia kituo cha polisi basi fanya hivyo ili mradi Mathew awe huru”
akasema Meshack
“Mzee hatupaswi kufika
huko.Hiyo ni hatua kubwa sana
ambayo itakuwa ya mwisho baada
ya jitihada nyingine zote
kushindikana.Hivyo basi
utachagua aidha kumsaidia
Mathew au kumtii rais”
“Austin..!! akasema Meshack
akionyesha kukerwa na kauli ile ya
Austin
“Mzee muda unakwenda na
unatakiwa ufanye uchaguzi aidha
umsaidie Mathew na kumtoa
katika mikono ya polisi au umtii
rais na kijana wako apotee” Ukapita ukimya wa sekunde
kadhaa halafu Meshack Jumbo
akauliza
“Uko wapi Austin?
“Niko hapa katika hoteli
yangu”
“Ninakuja hapo sasa hivi”
akasema Meshack na kukata simu
akatoka na kumuelekeza dereva
wake waelekee Savana 5 star hotel.
“Mawazo ya Austin ni
mazuri.Ninaweza kutumia nguvu
yangu kama mkuu wa idara ya
usalama wa taifa na kumuokoa
Mathew.Hawa vijana bado akili zao
zinachemka na wanafikiri haraka
haraka sana kuzidi mimi ambaye
tayari umri wangu
umekwenda.Nadhani napaswa kulizingatia wazo hili na kulifanyia
kazi .Lakini nikiamua kufuata
wazo la Austin nitajiingiza katika
matatizo makubwa na rais na
ndiyo maana Austin akaniambia
kwamba ninapaswa kuchagua
nimsaidie Mathew au nimtii rais na
kumuacha Mathew akiangamia.”
Akawaza Meshack akiwa garini
“Mathew hana kosa lolote na
kwa kosa hili alilotuhumiwa nalo
anaweza kufungwa hata kifungo
cha maisha gerezani.Siko tayari
kuona kijana yule ambaye
alijitolea kuifanya kazi ya rais kwa
moyo mmoja anaozea
gerezani.Kwa hiyo basi ninachagua
kumsaidia Mathew.Potelea mbali
kama nitakuwa nimetangaza vita na rais kwa maamuzi yangu haya
lakini lazima nimsaidie Mathew”
akawaza Meshack na kuchukua
simu akampigia katibu muhtasi
wake na kumtaka amtafutie namba
za kamanda wa polisi kanda
maalum ya Dar es salaam.Baada ya
dakika tano akatumiwa namba zile
na bila kupoteza muda akapiga
“Hallo” ikasema sauti ya
upande wa pili
“Kamanda unazungumza na
Meshack Jumbo mkurugenzi wa
idara ya usalama wa taifa”
“Nikusaidie nini mkurugenzi?
“Nilimpa taarifa mheshmiwa
rais usiku huu kuhusiana na
kuuawa kwa waziri wa mambo ya
nje Dr Robert Mwainamela mauaji yanayosadikiwa kufanywa na
Mathew Mulumbi na kwa taarifa
niliyoipata hivi punde ni kwamba
tayari amekwisha tiwa nguvuni”
“Ndiyo mkurugenzi.Huyu
kijana Mathew tayari amekwisha
tiwa nguvuni na sasa utaratibu
unafanyika kumpeleka katika
kituo cha kati cha polisi” akasema
kamanda wa polisi kanda maalum
ya Dar es salaam
“Kamanda,huyu jamaa aliwahi
kufanya kazi katika idara ya
usalama wa taifa na kuna mambo
muhimu tunahitaji kuyafahamu
toka kwake kwa hiyo tunahitaji
kumfanyia mahojiano.Baada ya
kumfanyia mahojiano basi
tutawakabidhi muendelee na taratibu nyingine za upelelezi na
mashtaka hivyo naomba
asipelekwe kwanza kituoni ili
tumfanyie mahojiano hapo
nyumbani kwake”
“Sawa mkurugenzi.Sisi sote
tunafanya kazi moja kulinda nchi
yetu kwa hiyo mtaruhusiwa
kumfanyia mahojiano huyo jamaa
na mtakapomaliza mtatukabidhi
mhalifu huyo kwa ajili ya
kuendelea na taratibu
nyingine.Ninampigia simu sasa
hivi kiongozi wa kikosi
kilichotumwa nyumbani kwa
Mathew ili awaruhusu watu wako
wamuhoji hapo hapo nyumbani
kwake” akasema kamanda wa
polisi “Ahsante sana kwa
ushirikiano wako kamanda”
akasema Meshack Jumbo na
kukata simu.
“Wazo la Austin ni zuri sana”
akawaza Meshack huku safari
ikiendelea
Meshack Jumbo aliwasili
Savana 5 star hotel akampigia
simu Austin akamfahamisha
kwamba tayari amekwisha
fika.Austin akamtaka amfuate
ofisini kwake.Meshack akashuka
na kuelekea katika jengo la hoteli
akahakiki kwanza usalama wake
halafu akapanda lifti hadi ghorofa
ya tatu ziliko ofisi akaitafuta ofisi
ya mkurugenzi akagonga na
mlango ukafunguliwa na mwanamke mmoja mwenye sura
iliyojaa tabasamu
“Shikamoo mzee”
“Marahaba nahitaji kuonana
na ndugu Austin January”
“Karibu ndani”
Meshack akaingia ndani ya
ofisi na kukutana na Austin
“Karibu sana mzee
wangu.Nafurahi tumeonana tena
baada ya kitambo kirefu”
‘Hata mimi nimefurahi
kukutana tena nawe
Austin.Nilipata wazo la kukutafuta
ila sikuwa na uhakika kama bado
unatumia ile namba yako hivyo
nilipiga kwa kubahatisha.Vipi
maendeleo yako? “Nendelea vyema.By the way
huyu ni mke wangu anaitwa
Amarachi” Austin akafanya
utambulisho
“Amarachi huyu anaitwa
Meshack Jumbo ni mkurugenzi wa
idara ya usalama wa taifa.Ni mzee
ambaye amenilea mimi na wengi
tuliopita katika idara hii na
tunamuita baba”
“Nafurahi kukufahamu mzee
Meshack” akasema Amarachi
“Mimi pia nafurahi sana
kukufahamu Amarachi” akasema
Meshack na kumgeukia Austin
“Austin tutatapa wasaa wa
kutosha kuzungumza mambo yetu
ya maisha hapo baadae lakini kwa sasa tujadili namna ya kumsaidia
Mathew”
“Kama nilivyokueleza mzee
kwamba tunapaswa kutafuta
namna nzuri ya kumsaidia Mathew
.Wazo lako la kuvamia na kufanya
si muafaka kwa sasa.Tayari
amezungukwa na polisi wenye
silaha na sisi tuko wachache hivyo
hatutaweza kupambana nao ndiyo
maana nakushauri kutumia nafasi
yako kama mkuu wa idara ya
usalama wa taifa kuweza kumtoa
Mathew katika mikono ya askari
bila mapambano au kumwaga
damu” akasema Austin
“Ahsante kwa wazo lile zuri na
kama nilivyokufahamisha tayari
nimewasiliana na kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es
salaam na kumwambia kwamba
tunamuhitaji Mathew kwa
mahojiano kabla hawajampeleka
kituoni.Hivi sasa watakuwa
wanatusubiri sisi kwa hiyo
tunatakiwa kufanya haraka.Nipe
maoni yako tufanyaje kuweza
kumtoa Mathew pale?
“Good.Tukifika pale
utajitambulisha halafu utaomba
upewe nafasi ya kumuhoji Mathew
na baada ya muda utaomba
uondoke naye kwa ajili ya kwenda
kumuhoji zaidi na Mathew
hatarejea tena mikononi
mwao.Mpango huu ni mzuri lakini
una athari pia na athari kubwa
itakuwa upande wako kwani itakulazimu kubeba mzigo wote
wa kupotea kwa Mathew.Utaingia
katika msuko suko mkubwa sana
kiasi cha kuhatarisha hata
kupoteza kazi yako kwa hiyo mzee
kabla hatujaenda huko unapaswa
kutafakari na kufanya maamuzi
kama uko tayari kubeba dhaman
hii kubwa”
Meshack Jumbo akainamisha
kichwa na kutafakari kwa muda
akasema
“Mathew ni kijana wangu na
siko tayari kumuacha akiangamia.I
must do everything to save him.I’m
ready.let us go ! akasema
Meshack.Austin akampa ishara
Amarachi akalibeba begi
lililokuwa juu ya meza.Meshack akataka kusema kitu lakini Austin
akamuwahi
“It’s ok .She’s coming with
us.She’s good at this” akasema
Austin wakatoka nje ya ofisi na
Meshack akapata wazo
“Austin kuna jambo linanipa
wasi wasi kidogo”
“ Jambo gani mzee?
“Rais tayari anazo taarifa za
kushikiliwa kwa Mathew na kabla
ya kuja hapa kulitokea hali ya
kutokuelewana kati yangu naye
kuhusiana suala hili la Mathew
kukamatwa.Ilinilazimu
kukubaliana naye ili niweze
kupata nafasi ya kutoka na
kumsaidia Mathew,hata hivyo
baada ya sintofahamu ile kutokea rais hana imani nami kwani tayari
anaelewa msimamo wangu kuhusu
suala hili na anajua Mathew ni
kijana wangu hivyo siwezi katu
kukubali atiwe nguvuni na hawezi
kuniacha hivi hivi lazima atakuwa
ameweka watu kunifuatilia kujua
ninafanya nini.Ili kuepuka mpango
wetu kuvurugika tusitumie gari
langu.Tutumie gari lako Austin”
akasema Meshack
“Ahsante kwa kuling’amua
hilo mzee Meshack.Tutatumia gari
langu usihofu” akasema
Austin.Wakatokea upande wa
nyuma na kuelekea hadi katika
maegesho maalum ya viongozi wa
hoteli ile wakaingia katika gari la
Austin na kuondoka.Baada ya kuondoka Meshack akachukua
simu na kumpigia dereva wake
akamtaka aendelee kumsubiri
kwani bado ana mazungumzo
muhimu na mtu aliyemfuata pale
hotelini
“Mzee nini hasa
kinachoendelea?Mathew amefanya
nini hadi ashikiliwe na
polisi?Austin akauliza
“Austin kuna mambo
makubwa yanayoendela hapa
nchini kwa sasa na Mathew
alikuwa katika kuchunguza na
ndipo masahibu haya
yalipomkuta.Anashikiliwa na jeshi
la polisi kwa tuhuma za mauaji ya
waziri wa mambo ya nje wa
Tanzania Dr Robert Mwainamela” “Mathew amemuua waziri wa
mambo ya nje wa nchi?Austin
akashangaa
“He didn’t do it.He didn’t kill
him” akasema Meshack
“kama hakumuua kwa nini
ashikiliwe na polisi?
“kama nilivyokueleza Austin
kwamba kuna mambo makubwa
yanayoendelea hapa nchini hivi
sasa na Mathew yupo katika
uchunguzi.Hiki kilichomtokea ni
harakati za watu wenye nguvu
kutaka kumpoteza kwani tayari
amekwisha gusa maslahi ya watu
wakubwa.Kwa hiyo basi ni jukumu
letu sisi kufanya kila tuwezalo
kuhakikisha tunamuokoa kwani
bila kufanya hivyo huu utakuwa ni mwisho wake” akasema Meshack
Jumbo.Austin aliyekuwa katika
usukani akavuta pumzi ndefu na
kuuliza
“Jambo gani Mathew
analichunguza? Amewahi
kukueleza?
“Kuna jambo kubwa alilokuwa
analichunguza na ndani ya
uchunguzi huo yameibuka mambo
mengine makubwa ambayo
yamemuweka katika matatizo
haya makubwa aliyonayo.Tutapata
wasaa wa kuzungumza hapo
baadae lakini kwa sasa
tuhakikishe kwanza tunamuokoa
Mathew” akasema Meshack
“Nafahamu Mathew ni mfanya
biashara mkubwa hivi sasa na hadi kuamua kuacha shughuli zake za
biashara na kurudia kuifanya kazi
hii si kwa ajili ya fedha,lazima
kuna jambo zito lililompelekea
akafanya hiyo kazi” akasema
Austin
“Hakufanya kazi hii kwa ajili
ya kipato.Ipo sababu
iliyompelekea aifanye hii
kazi.Pamoja na kwamba kwa sasa
tayari anajishughulisha na
shughuli zake za biashara lakini
kazi hii bado iko damuni mwake
na ndiyo maana alilazimika
kuingia tena uwanjani pale
alipoona kuna ulazima wa kufanya
hivyo.Nataka niwaweke wazi
vijana wangu kwamba mwisho wa
kazi hii ni pale utakapokuwa umefariki dunia lakini kama bado
unavuta pumzi basi utaendelea
kuifanya kazi hii kila pale
itakapojitokeza.Tazama mimi
tayari nimekwisha staafu lakini
nimelazimika kurejea tena
ofisini.Tuachane na hayo vipi
maendeleo yako?
“Ninaendeleea vizuri .Mimi na
mke wangu tumewekeza sana
katika biashara ya mvinyo uitwao
Amarachi jina la mke wangu
ambaye ndiye aliyeugundua na
tayari tumejenga kiwanda kingine
hapa Dar es salaam cha
kutengeneza mvinyo huo kwa hiyo
tuna viwanda viwili hivi
sasa.Tumejenga pia hoteli mbili
kubwa hapa jijini dar es salaam kwa ujumla tunaendelea
vyema.Nina kila sababu ya
kumshukuru Mungu kwa
mafanikio haya makubwa”
akasema Austin
Safari iliendelea huku
wakizungumza mambo kadha wa
kadha hadi walipokaribia kufika
nyumbani kwa Mathew.Austin
akapunguza mwendo baada ya
kunekana umati wa watu uliofika
eneo la karibu na nyumba ya
Mathew kushuhudia kile
kilichokuwa kimetokea
pale.Austin akapiga honi na watu
waliokuwa wametanda barabarani
wakasogea pembeni na kulipisha
gari lipite.Magari kadhaa ya polisi
yalikuwa yameegeshwa huku polisi wenye silaha wakiwa
wametanda kila kona kuizunguka
nyumba ya Mathew
“Austin ulisema kweli kwa
ulinzi huu wa askari tusingeweza
kupambana nao.Ulinzi ni mkali
sana” akasema Meshack Jumbo na
Austin akasimamisha gari kwani
kulizungushwa utepe uliozuia
watu kuvuka.Wakashuka garini na
Meshack akajitambulisha kwa
kamanda wa polisi mkoa wa
kipolisi Mzizima Anangisye
Mwalukosi ambaye alikuwepo
mahala pale
“Mzee,taarifa zako tayari
ninazo na tunakusubiri wewe
uhojiane na mtuhumiwa ili tuweze kuondoka naye” akasema
kamanda Anangisye.
“Ahsante sana
kamanda.Kutokana na umuhimu
wake huyu jamaa imenilazimu
kuja mwenyewe na vijana wangu
ili tuweze kumuhoji kuhusiana na
masuala kadhaa muhimu.Naomba
dakika ishirini tu kisha
nitamkabidhi kwenu” akasema
Meshack na kuongozana na
kamanda Anangisye hadi sebuleni
walikokuwapo Mathew na Camilla
wakiwa wamefungwa pingu huku
wakilindwa na askari wenye
silaha.Mathew alikuwa amefungwa
pingu mikononi na miguuni
“Mtuhumiwa huyu hapa ila
utatusamhe mzee kwani hatutaweza kumfungua pingu
kwani tumeambiwa ni mtu
hatari.Utamfanyia mahojiano
akiwa amefungwa hivyo hivyo”
akasema Anangisye
“Usijali kamanda.Ahsante
sana.Naomba sasa askari mtupe
nafasi na sisi tufanye kazi yetu
halafu tutawaachia muendelee na
taratibu zenu” akasema Meshack
na askari wakatoka mle sebuleni.
“Pole sana brother” akasema
Austin
“Good to see you Austin”
akasema Mathew
“Jamani huu si muda wa
salamu.Tuna muda mchache sana
hivyo tujielekeze katika suala la kumtoa Mathew hapa” akasema
Meshack
“Mzee, I didn’t kill Dr
Robert.This is a set up!! Akasema
Mathew
“I know
Mathew.Tutazungumza baadae
lakini kwa sasa tutafute namna ya
kumtoa Mathew katika dhahama
hii iliyomkuta.Tuna dakika kumi
na saba tu kutoka sasa” akasema
Meshack
“Mzee mimi nadhani
tuendelee na ule mpango wetu
tuliokuwa tumepanga.Ongea na
kamanda wa polisi mwambie
kwamba mtuhumiwa amekataa
kutoa ushirikiano hivyo unaomba
umchukue umpeleke katika ofisi zenu mkatumie njia zenu za
kumuhoji halafu utamkabidhi tena
kwao baada ya kumaliza
kumuhoji.Hiyo ndiyo njia rahisi ya
kuweza kumtoa Mathew hapa
kwani hatutaweza kupambana na
polisi hawa waliotanda kila kona
ya nyumba hii” akasema Austin
“Hapana.Hatupaswi kufanya
hivyo.Tutamuweka mzee Jumbo
katika matatizo makubwa na
anaweza kufungulia mashtaka kwa
kumtorosha mtuhumiwa wa
mauaji ya waziri .Tusimpe mzee
matatizo ambayo hakuwa
ameyatarajia.Hili ni tatizo langu na
sitaki mtu mwingine apate
matatizo kwa ajili
yangu.Ninachowaomba kwa sasa ni kujaribu kufanya kila
linalowezekana kumsaidia
Camilla.Hapaswi kwa namna
yoyote ile kuingia katika mikono
ya polisi” akasema Mathew
“Mathew sikiliza .Kwa hapa
tulipofika hili si suala lako peke
yako.Ni suala letu sote kwa hiyo
hatuwezi kukuacha peke
yako.Lazima tukutoe hapa utake
usitake.Mimi nitaubeba mzigo
wote huu.Kumbuka kwamba ni
mimi ndiye niliyekuingiza katika
kazi hii kwa hiyo siwezi kukubali
hata kidogo jambo kama hili
likutokee.Niko tayari na nitabeba
dhamana hii.Lazima tukuondoe
hapa” akasema Meshack Jumbo Mathew akataka kusema kitu
lakini Austin akamzuia
“Usiseme chochote
kaka.Tuache tufanye kazi yetu.This
is our mission now” akasema
Austin
Zilipita dakika kumi mlango
ukafunguliwa Meshack Jumbo
akatoka na kumfuata kamanda
Anangisye.
“Afande,huyu jamaa amekuwa
mgumu sana kufunguka na kuna
kila dalili hataweza kusema
chochote.Kuna jambo ambalo
tunahitaji kulifahamu toka kwake
linalohusu usalama wa nchi lakini
hayuko tayari kufunguka.Kama
ujuavyo huyu jamaa amewahi
kufanya kazi katika idara ya ujasusi hivyo si rahisi kumfungua
kwa muda huu mchache.Kwa
sababu hiyo basi nina ombi moja
kwako”
“Ndiyo mzee” akasema
Anangisye
“Ninataka kuondoka na huyu
mtuhumiwa ,tunakwenda naye
katika sehemu yetu maalum kwa
ajili ya kufanyia mahojiano.Kwa
hapa hata kama tukitumia usiku
mzima hatutaweza kupata
chochote toka kwake.Katika
chumba chetu cha mahojiano kuna
vifaa maalum vya kutuwezesha
kumfumbua mdomo mtu yeyote
yule na hasa wale wagumu kama
huyu.Baada ya kupata kule
tunachokihitaji basi tutamkabidhi kwenu tena.Ninaomba hivyo kwa
sababu taratibu zenu za kipolisi
zikianza itakuwa kazi ngumu
kwetu kumpata na kumuhoji hivyo
basi tunataka tumalize kila kitu
kabla hamjaaanza taratibu za
kumshitaki” Kamanda Anangisye
akainamisha kichwa kwa muda
akatafakari na kusema
“Mzee suala lako ni la msingi
mkubwa lakini siwezi kulitolea
maamuzi ya moja kwa moja hadi
hapo itakapotolewa ruhusa kutoka
kwa wakuu wangu.Huyu tayari ni
mtuhumiwa wa mauaji ya waziri ni
vipi endapo atapotea katika
mikono yako? Nani ambaye
atakuwa katika matatizo?Jibu ni
rahisi ni mimi.Mzigo wote utaniangukia mimi.Naomba
usubiri mzee nimfikishe kwanza
sehemu husika na halafu ufuate
taratibu za kuweza kumpata kwa
mahojiano” akasema Kamanda
Anangisye
“Kamanda Anangisye mimi na
wewe tuko idara tofauti lakini
jukumu letu ni lile lile yaani
kulinda nchi na raia wake kwa
hiyo ninaomba
uniamini.Mtuhumiwa hawezi
kupotea katika mikono yetu.Sisi ni
watu makini na tunafahamu
tunachokifanya”
“Mzee Jumbo ninakuamini
lakini kila kitu kina taratibu
zake.Hili suala si gumu lakini
tufuate taratibu zilizowekwa na si kufanya kienyeji enyeji kisha
tukawekana katika matatizo!!
Akasema Kamanda Anangisye
“Naomba nikufahamishe
jambo moja kamanda
Anangisye.Leo jioni kumetokea
shambulio la bomu katika uwanja
wa ndege wa Julius Nyerere
likimlenga waziri wa mambo ya
nje wa Marekani.Watu kadhaa
wanadaiwa kupoteza maisha na
hadi hivi sasa waziri huyo wa
mambo ya nje wa Marekani
hajulikani mahala alipo.Mathew
anazo taarifa muhimu sana za
kuhusiana na shambulio hilo na
ambazo zinaweza kutusaida
kuwafahamu waliofanya hilo
shambulio na mahala alipo waziri huyo aliyetoweka.Ninyi
mnamshikilia Mathew kwa tuhuma
za mauaji na akishafikishwa
kituoni taratibu za kufuata ili
kumuhoji zina mlolongo mrefu na
sisi tunahitaji kupata taarifa kwa
haraka.Naomba uniamini ili
tukamilishe kazi yetu na kisha
tutamkabidhi kwenu akiwa mzima
wa afya.Hatupaswi kuwekeana
vizingiti wakato sote tunafanya
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment