Simulizi : The Football
Sehemu Ya Pili (2)
kidogo aliposikia kwamba
Meshack Jumbo ametoka kuonana
na rais
“Amekuitia kitu gani?
Akauliza Mathew
“Kuna mambo yanayoendelea
hapa nchini kwa sasa hivyo aliniita
kupata ushauri wangu”
“Ni kuhusiana na lile suala la
Korea kaskazini?Naona linazidi
kuchukua sura mpya kila uchao”
“Hatukuzungumza sana suala
hilo ila kuna mambo mengine
mawili aliyoniitia” “Mzee Jumbo nina imani
umekuja kunieleza kuhusiana na
maongezi yako na rais but I’m not
interested.Mimi siko tena katika
haya mambo.Kama kweli hilo ndilo
lililokuleta hapa naomba usipoteze
wakati wako mzee
wangu.Nitakuwa na muda kama
tutazungumza mambo ya
kibiashara” akasema Mathew.
“Mathew nafahamu hutaki
tena kusikia haya mambo ya
wanasiasa na ndiyo maana
nimekuja mwenyewe hivyo
naomba unipe dakika kama tano
tu unisikilize.Japokuwa sote kwa
sasa tumeachana na hizi kazi but
I’m still your boss so you have to
listen tome !! Huu utajiri wako usikufanye ukawa kiburi” akasema
mzee Jumbo kwa sauti ya juu
kidogo Mathew hakujibu
kitu.Meshack akaendelea
“Kuna mambo mawili
aliyoniitia rais leo.Moja ni
kuhusiana na kifo cha mkurugenzi
wa idara ya usalama wa taifa
George Mzabwa aliyejipiga risasi
ofisini kwake.Mheshimiwa rais
ameniomba nirudi kazini kwa
muda wa mwaka mmoja
nikaiongoze idara ya usalama wa
taifa kwani mpaka sasa bado
hajapata mtu wa kuweza
kuiongoza idara hiyo
atakayemuamini hasa kwa wakati
huu ambao nchi inahitaji ulinzi mkali sana”Meshack akanyamaza
na Mathew akauliza
“Kuna sababu yoyote ya huyo
mkurugenzi kujiua?
“Mpaka sasa hakuna sababu
yoyote iliyogunduliwa kwa nini
alijiua japokuwa uchunguzi bado
unaendelea.”
“Umekubali kurejea kazini?
Mathew akauliza
“Mathew kustaafu si mwisho
wa utumishi.Sisi ni sawa na askari
wa akiba pale tunapotakiwa
kurejea katika mapambano kwa
ajili ya nchi basi hatuwezi
kukataa,hivyo nimekubali kurejea
tena kuifanya kazi aliyoniomba
mheshimiwa rais” akajibu
Meshack “Lakini kuna watu wengi
ambao wangeweza kuziba nafasi
hiyo na rais angeweza kuwachagua
na akakuacha mzee
ukapumzike.Umelitumikia taifa
kwa miaka mingi ni wakati wako
wa kupumzika sasa” akasema
Mathew
“Ni kweli Mathew wapo watu
wengi tu wanaoweza kufanya hiyo
kazi lakini hawana uzoefu mkubwa
kama mimi na ndiyo maana rais
ameomba nimsaidie kuziba nafasi
hiyo kwa mwaka mmoja .Nadhani
kuna mambo ameona hayaendi
sawa.Nimeridhia ombi lake na
nitaifanya hiyo kazi kwa muda huo
alionitaka” “Sawa mzee.Kama umeamua
kurejea kazini kwa ombi maalum
la mheshimiwa rais mimi
nakutakia kila la heri katika
majukumu yako ila
nakukumbusha kwamba zama
zimebadilika sana tofauti na
wakati ule ambao ulikuwa
kiongozi.Teknolojia imepanuka
sana zama hizi” akasema Mathew
“Nalifahamu hilo Mathew na
ninao uzoefu wa kutosha isitoshe
hata afya bado inaruhusu.Jambola
pili aliloniitia rais linafanana na
hili la kwanza.Rais anahitaji
kukuona.Anahitaji msaada wako”
“Me ?!! akauliza Mathew kwa
mshangao halafu akacheka kidogo “Mimi nimekwisha achana na
haya mambo kwa hiyo mweleze
kwamba siwezi kuwa na msaada
wowote kwake” akasema Mathew
“Ninalifahamu hilo mathew na
nimekuja hapa mimi mwenyewe
kukuomba ukaonane na
rais.Nafahamu umeachana na haya
mambo na nisingeweza kuja hapa
kama jambo analokuitia rais
lisingekuwa la muhimu.Please my
son nakuomba nenda ukamsikilize
rais anachokuitia.Kuna jambo zito
ambalo anahitaji msaada na ni
wewe pekee unayeweza
kumsaidia.Nakuomba sana
Mathew” akasema mzee Meshack
“Lakini mzee wewe
unafahamu fika kwamba mimi kwa sasa sishughuliki na hayo mambo
tena bali nimejikita katika
biashara kwa hiyo mwambie rais
kwamba siwezi kuwa na msaada
wowote kwake.Kuna watu wengi
sana katika idara ya usalama wa
taifa,polisi n.k kwa nini
asiwatumie hao wote hadi anitake
mimi ? Tayari nimeingia katika
maisha mapya kwa hiyo siwezi
kurudi tena katika hizo kazi mzee
wangu,utanisamehe sana”
“Mathew nakuomba kijana
wangu muonyeshe heshima mkuu
wa nchi na uitike tu wito wake wa
kutaka kukuona.Nenda kaonane
naye usikie anachokuitia halafu
umweleze kwamba kwa sasa
haujishughulishi na hayomambo.Moja ya msingi wa kazi
yetu ni nidhamu kwa uongozi wa
juu kwa hiyo usidharau wito wa
kiongozi wako,nenda kamsikilize
usikie anakuitia nini.Mimi
nilipoitwa sikujiuliza mara mbili
nikaenda haraka na kusikia
alichoniitia” Akasema Meshack
Ilimchukua Mathew zaidi ya
dakika mbili kutafakari halafu
akasema
“Mzee umeniweka katika
wakati mgumu sana lakini kwa vile
nina kuheshimu na umekuja
mwenyewe kuniomba itanibidi
niende kuonana na rais na
kumsikiliza anachokitaka.Lini
anataka nionane naye? “Anakuhitaji sasa
hivi.Nitakupeleka”
“Ananihitaji sasa hivi? Kwa
nini isiwe wakati mwingine au
hata kesho? Kwa sasa nina ratiba
nyingine si unaona shughuli
zilivyopamba moto hapa ?
“Ahirisha shughuli zako kwa
sasa twende ukamsikilize rais
halafu utakuja kuendelea na
shughuli zako” akasema Meshack
Jumbo.Mathew akatoa maelekezo
kadhaa kwa mkandarasi kisha
wakaondoka
“Ahsante sana Mathew kwa
kukubali kwenda kuonana na
rais.Hii ni heshima kubwa
umetupa mimi na rais”akasema
Meshack Jumbo “Nimekubali kwa heshima
yako mzee wangu lakini angekuja
mwingine nisingekubali.Ni jambo
gani hasa ambalo rais ananiitia
unaweza kunidokeza?
“Itakuwa vyema kama yeye
mwenyewe atakueleza.By the way
mnawasiliaan na Peniela? Meshack
Jumbo akauliza
“Tunawasiliana .Hatuna
ugomvi na isitoshe tuna mtoto
mmoja,binti mzuri anaitwa Anna
Maria hivyo hata kama hatuko
pamoja lakini tunaunganishwa na
mtoto hivyo mawasiliano yapo
lakini ni kuhusiana na maendeleo
ya mtoto tu” “Pole sana kwa kilichotokea
kwenye ndoa yako” akasema mzee
Jumbo
“Ni mambo ya kawaida
kutokea katika ndoa” akajibu
Mathew kisha safari ikaendelea
kimya kimya
Walifika ikulu na rais
akataarifiwa kuwasili kwao na
alipomaliza kikao na wageni wake
akawakaribisha Meshack na
Mathew katika chumba cha
maongezi ya faragha
“Karibuni sana.Natumai
Meshack umemleta Mathew
Mulumbi” akasema Dr Vivian huku
akitabasamu “Hujakosea mheshimiwa
rais,huyu ndiye Mathew Wilibroad
Mulumbi” akasema Meshack
“Mathew karibu
sana.Nimefurahi kukutana nawe”
akasema Dr Vivian
“Hata mimi pia nimefurahi
sana kuonana nawe mheshimwia
rais” akasema Mathew
“Ni mara ya kwanza
tunaonana Mathew.Ahsnate kwa
kukubali wito wangu ingawa
nafahamu Mzee Meshack alipata
wakati mgumu kukushawishi
ukubali kuja kuonana nami”
akasema Dr Vivian na wote
wakacheka
“Uko sahihi mheshimiwa
rais,haikuwa rahisi kukubali lakini kwa heshima kubwa kwako na
kwa mzee imenilazimu kuitika
wito wa mkuu wangu wa nchi
hivyo nimeacha shughuli zangu
zote na kuja kuonana nawe”
akasema Mathew
“Nashukuru sana.Mapema leo
nilikuwa na mazungumzo marefu
na Meshack na nina imani
amekudokeza yale
tuliyoyazungumza” akasema Dr
Vivian
“Amenidokeza baadhi ya
mambo lakini kwa upana zaidi
nategemea kusikia toka kwako”
“Itakuwa vyema kama
nikikuanzia mbali kidogo ili upate
picha kamili ya kile nilichokuitia
hapa.Ni siku mbili tu zimepita toka mkuu wa idara ya usalama wa taifa
George Mzabwa ajiue kwa kujipiga
risasi ofisini kwake.Mpaka sasa
bado uchunguzi unaendelea
kubaini sababu ya George
kujiua.Kufuatia kifo hicho bado
sijapata mtu sahihi wa kuweza
kuiziba nafasi yake kwani pamoja
na kujiua lakini utendaji wa
George haukunivutia na nilikuwa
katika mpango wa kumondoa na
kumuweka mtu
mwingine.Nimelazimika
kumuomba mzee Jumbo anisaidie
kuiziba nafasi hiyo kwa mwaka
mmoja wakati nikiendelea
kutafuta mtu anayeweza kufaa
kuongoza idara hii kwa weledi
mkubwa.Namshukuru mzee amekubali kwa moyo mmoja na
kuacha shughuli zake zote kuja
kuifanya kazi hii.Narudia tena
kukushukuru mzee
Meshack.Mungu azidi kukupa umri
mrefu na nguvu” akasema Dr
Vivian na Mzee Meshack
akainamisha kichwa kushukuru
“Mathew naamini kwamba
tayari umekwisha sikia msuguano
uliopo baina ya nchi yetu na
mataifa makubwa.Wakati huu
ninahitaji nchi iwe katika ulinzi
imara na ndiyo maana ujuzi na
uzoefu wa watu kama ninyi
unahitajika sana.Lakini wewe
Mathew nimekuita kwa suala
lingine tofauti na hilo” akanyamaza tena kidogo huku
akiendelea
“Nadhani jina la Kanali
Sebastian Matope si geni kwako”
“Sina kumbu kumbu nzuri ya
jina hilo labda unikumbushe”
akasema Mathew
“Kanali Sebastian Matope
alikuwa mpambe wa rais ambaye
kazi yake kubwa ilikuwa ni
kulibeba begi lenye siri za rais
lililopewa jina la Football
wakililinganisha na lile begi la rais
wa Marekani atembealo nalo kila
aendako ambalo nalo linaitwa
football.Rais Anorld Mubara
alifariki katika jaali ya ndege
akitokea nchini Misri na kanali
Sebastian inaaminika ndiye pekee aliyenusurika katika ajali hiyo
iliyotoa uhai wa wote walikuwemo
ndegeni.Baada ya kunusurika
katika ajali ile baba hakumaliza
miezi sita akauawa yeye,mama na
mdogo wangu Kelvin.Inasemekana
waliuawa wakiwa njiani kwenda
kumtembelea bi April Mubara
mjane wa rais Anorld Mubara.Toka
yamefanyika mauaji hayo
imekwisha pita miaka zaidi ya
kumi na mpaka leo hakuna taarifa
yoyote kuhusiana na nani
aliyefanya mauaji yale ya
kinyama.Baada ya kuingia
madarakani niliagiza idara ya
usalama wa taifa kufanya
uchunguzi wa suala hili na muuaji
apatikane lakini imepita miaka miwili toka nilipotoa kazi hiyo na
hakuna majibu yoyote.Juzi
nilipokuwa nakwenda Marekani
nilimweleza mkuu wa idara ya
usalama wa taifa kwamba
nitakaporejea kutoka marekani
nikute tayari wana taarifa
kuhusiana na mauaji ya familia
yangu lakini nilichokikuta ni hii
barua aliyoiandika George muda
mfupi kabla ya kujipiga risasi”
Dr Vivian akamkabidhi
Mathew ile barua akaisoma halafu
Dr Vivian akaendelea
“Umeona mwenyewe
alichokiandika George.Amekiri
kwamba suala hili ni gumu na
amenisisitiza kuachana nalo kwani
sintaweza kupata majibu.Yawezekana kweli suala
hili nigumu kwani zaidi ya miaka
kumi hakuna ufumbuzi wowote
uliopatikana.Binafsi bado siamini
kama suala hili limeshindikana
kupatiwa ufumbuzi.Bado nina
imani kwamba jambo hili haliwezi
kuachwa liende kimya kimya.Baba
aliuawa na lazima wauaji wapo na
sababu ya kumuua ipo hivyo
lazima tuwafahamu hao
waliomuua na sababu ya
kumuua.Nimeamua kulivalia njuga
suala hili mimi mwenyewe hadi
ufumbuzi upatikane na ndiyo
maana nikamuomba mzee Jumbo
anisaidie kutafuta mtu maalum
mwenye sifa za kipekee ambaye
anaweza kulifumbua hili fumbo ambalo wenzake wameshindwa
kulifumbua.Mzee Meshack amekiri
kwamba mtu huyo maalum ni
wewe ambaye umeonekana unafaa
na unaweza kuutafuna mfupa
uliowashinda wengine” akasema
rais na Mathew akataka kusema
kitu rais akamzuia
“Mathew nafahamu
unachotaka kukisema lakini
nakuomba usikitamke bali
naomba ukubali kunisaidia
kulifumbua fumbo hili
gumu.Nisaidie kama ndugu
yako,kama rafiki
yako.Sikulazimishi unisaidie ila
nakuomba unisaidie niweze
kupata ukweli kuhusu mauaji ya
wazazi wangu waliouawa bila huruma.Baba alipigwa risasi zaidi
ya sabini mwilini mwake.Huu ni
ukatili ulipotiliza.Ingia katika
viatu vyangu na uone machungu
ninayoyapatra kila ninapofikiria
kuhusu suala hili.Kinachoniumiza
zaidi kwa nini vyombo vya
uchunguzi vimeshindwa kuwapata
wauaji? Akasema Dr Vivian na
macho yake yakalengwa machozi
“Inaumiza sana mheshimiwa
rais.Huu ni ukatili mkubwa mno”
akajibu Mathew
“Ni zaidi ya ukatili na ndiyo
maana nakuomba Mathew
unisaide katika hili suala.Nina
imani kubwa kwako kwamba
unaweza ukalifumbua hili
fumbo.Ninakuomba Mathew tafadhali usiseme hapana.Wewe
ndiye tumaini langu la mwisho
katika kuupata ukweli wa suala
hili.Ukikataa wewe sintaweza
kujua nani waliwaua wazazi wangu
kikatili namna ile.Nitakuwezesha
kwa kila kitu unachokitaka ili kazi
yako isiwe ngumu” akasema Dr
Vivian
ndiye tumaini langu la mwisho
katika kuupata ukweli wa suala
hili.Ukikataa wewe sintaweza
kujua nani waliwaua wazazi wangu
kikatili namna ile.Nitakuwezesha
kwa kila kitu unachokitaka ili kazi
yako isiwe ngumu” akasema Dr
Vivian
“Mathew” akaita mzee
Meshack Jumbo
“Mheshimiwa rais ameomba
sana.Tafadhali angalia uzito wa
jambo hili.Fikiria mateso
anayoyapata moyoni mwake kila
siku akifikiria mauaji yale ya
kikatili ya wazazi wake.Ingiwa na
moyo wa huruma na ukubali
kumsaidia dada yako.Wote ni vijana umri wenu unalingana na
anakuomba umsaidie kama rafiki
,kama ndugu yako.Mheshimiwa
rais anahitaji msaada mkubwa hivi
sasa kutoka kwetu na ndiyo maana
hata mimi nimeamua kuachana na
kila kitu na kuja
kumsaidia.Nakufahamu Mathew
hujawahi kuacha wahalifu
wakatamba.Hauko hivyo.Tafadhali
nakuomba kwa mara nyingine tena
kubali kumsaidia rais.Mimi na
yeye tutakuwa nyuma yako na
kukusaidia katika kila
utakachokihitaji” akasema
Meshack Jumbo.Mathew
akainamisha kichwa akaisoma
tena barua ile iliyoandikwa na
George Mzabwa halafu akainua kichwa akamtazama rais na
kusema
“Siwezi kulikataa ombi lako
mheshimiwa rais na huyu mzee
wangu ambaye mimi kwangu ni
kama baba yangu”
Dr Vivian akainuka na kumpa
mkono Mathew
“Mathew ahsante sana.Sijui
nikuelezaje furaha niliyonayo kwa
kukubali kwako kulishughulikia
suala hili lililowashinda wengi”
Akasema Dr Vivian na
kumshukuru pia mzee Meshack
“Mzee Meshack
ninakushukuru sana kwa kumleta
Mathew.Nina uhakika mkubwa
kwamba sasa suala hili linakwenda kupatiwa majibu” akasema Dr
Vivian kwa furaha
“Mheshimiwa rais na mzee
wangu Jumbo naomba niwaweke
wazi kwamba japokuwa
nimekubali kuifanya kazi hii lakini
haiwezi kuwa rahisi na ni mapema
sana kuwa na matumaini yoyote
makubwa ila nawaahidi nitafanya
kila nitakaloweza kuhakikisha
ninapata majibu ya nani walifanya
mauaji hayo na kwa nini.Ni
kawaida yangu kila ninapoingia
katika operesheni fulani basi huwa
nahakikisha nimechimbua hadi
mzizi wake.Ninaamini hata katika
jambo hili sintafumba ukope hadi
ninakikishe nimelichimba na
kuupata mzizi wake.Palenitakaposhindwa au nitakapohitaji
msaada nitwaeleza” akasema
Mathew
“Nafahamu hili si suala jepesi
na ni hatari kubwa sana ndiyo
maana nikasema kwamba
chochote utakachokihitaji
nitakupatia.Kuwa huru kusema
chochote utakachokihitaji”
akasema Dr Vivian
“Nashukuru mheshimiwa
rais.Kabla ya kuanza rasmi
kulishughulikia suala hili naomba
unipe muda niweke kwanza
mambo yangu sawa ili
nitakapoanza kulishughulikia hili
jambo nisiingiliwe na mambo
mengine binafsi.Nitakapokuwa
tayari nitakuja kukuona na kukueleza kwamba sasa ninaanza
rasmi kazi”
“Ahsante Mathew.Jipe muda
wa kutosha kuyapanga mambo
yako na utakapokuwa tayari
utanijulisha.Nitakupa namba
yangu ya simu maalum ambayo
hutumiwa na viongozi wakuu na
wale wa kimataifa pekee kutokana
na umuhimu wako na una ruhusa
ya kupiga muda wowote unaotaka”
akasema Dr Vivian
“Kesho asubuhi nitakuja
kukuona kwani tayari nitakuwa
nimeweka sawa mambo yangu na
kesho hiyo hiyo kazi itaanza”
akasema Mathew
“Utapewa kibali maalum cha
kukuwezesha kuingia hapa ikulu muda wowote bila kuzuiliwa na
mtu.Nataka kazi hii isiwe mzigo
kwako hivyo chochote unachoona
kinaweza kukusaidia nieleze na
nitakusaidia” akasema Dr Vivian
na kuagana na Meshack Jumbo na
Mathew wakaondoka.Baada ya
akina Mathew kuondoka Dr Vivian
akamuita Theresa ofisini kwake
ambaye alifika mara moja.
“Karibu Theresa.Nimekuwa na
mfululizo wa vikao toka asubuhi
na sijapata nafasi ya kuonana
nawe.Mambo yako yanakwendaje?
Akauliza Dr Vivian
“Ninaendelea vizuri
dada.Nashughulikia hotuba yako
katika mkutano madaktari hapo
kesho kutwa” “Good.Nimekuita hapa
kukufahamisha kwamba tayari
nimempata mtu atakayeziba nafasi
ya George anaitwa Meshack
Jumbo.Ni mstaafu huyu ila aliwahi
kuongoza idara ya ujasusi wa taifa
kwa ufanisi mkubwa sana.Ni mtu
mwenye uzoefu wa kutosha na
nimemuomba anisaidie kuongoza
idara ya usalama wa taifa kwa
mwaka mmoja amekubali.Kingine
ni kwamba nimempata mtu
ambaye atafanya uchunguzi
kuhusiana na mauaji ya baba
anaitwa Mathew Mulumbi.Huyu
ndiye aliyeshiriki katika lile sakata
la Peniela kama utakumbuka”
“Wow ! Nalikumbuka lile
sakata.Umemtoa wapi? Yule jamaa nakumbuka alioana na
Peniela,amekubali vipi kuja
kuifanya hii kazi?Lazima
umemuahidi kumlipa fedha nyingi
sana kwani yule jamaa ni bilionea”
akasema Theresa
“Haikuwa rahisi kumpata hata
hivyo yeye na Peniela wamekwisha
achana .Kila mmoja kwa sasa ana
maisha yake.Yule jamaa ni mtu
mwelewa sana na sijui kwa nini
Peniela alikubali kumuacha
mwanaume kama yule aende
zake.Hata hivyo napaswa
kumshukuru sana Meshack Jumbo
kwani kwa kiasi kikubwa ndiye
aliyefanikisha mimi kuonana na
Mathew.Kuhusiana na fedha bado
hatujakubaliana ni kiasi gani atahitaji kwani bado hajaanza kazi
rasmi hadi atakapoweka sawa
mambo yake.Theresa nina imani
kubwa kwamba suala hili
linakwenda kupata majibu”
“Kama ni yule jamaa basi hata
mimi nina uhakika mkubwa
kwamba fumbo hili linakwenda
kufumbuliwa.Kama ungekuwa na
wazo hili toka zamani hivi sasa
tungekwisha jua nani
walioteketeza familia
yetu.Hongera sana dada kwa hatua
hii kubwa.Tumtakie kila la heri
aifanye vizuri kazi hii kwani ndani
yake inaonekana kujaa hatari.By
the way Nathan alinipigia simu
akadai kwamba amejitahidi
kukupigia simu toka asubuhi bila mafanikio.Anaomba umpigie”
akasema Theresa
‘Theresa tayari nimeweka
nukta katika mahusiano
yetu.Nimetafakari sana na kuona
nitajiweka katika matatizo
makubwa na ninaweza kushindwa
kufanya shughuli zangu hivyo
sintaweza kujigawa huku
nihudumie watanzania na huku
nimhudumie mume.Kuna
wanawake hawajaumbwa kuolewa
na mimi ni mmoja wao nadhani
ndiyo maana nilipenda sana kuwa
mtawa wakati nikiwa mdogo”
akasema Dr Vivian
“Dada..” Theresa akataka
kusema kitu Dr Vivian akamzuia “Don’t say anything
Theresa.I’ve never given up in
anything in my life and this is my
first time.Zaidi ya watu milioni
hamsini wako chini ya uangalizi
wangu.watoto wao wanapaswa
waende shule ,wapate elimu
bora,wananchi wangu bado
wanaishi maisha duni ambayo
nahitaji kufanya kila juhudi
kuyaboresha,kutengeza ajira
zaidi,unafuu wa maisha
upatikane,akina mama wajifungue
salama,sitaki hata mwanamke
mmoja apoteze maisha wakati wa
kujifungua.Uzazi unapaswa kuwa
salama.Nchi inapaswa kuwa na
chakula cha kutosha,wakulima
wanahitaji tija katika kilimo chao.Vijana wanamaliza vyuo
vikuu wanahitaji ajira haya ni
machache kati ya mengi ambayo
napaswa kuyashughulikia kwa
hiyo siwezi kuwa na muda wa
kuhudumia mume” akasema Dr
Vivian
“Haya yote uliyoyasema dada
ni ya kweli lakini hata wewe
unahitaji kuwa na maisha yako nje
ya urais.Unahitaji furaha,unahitaji
mtu wa kukuliwaza na kutuliza
kichwa chako,unahitaji
mume,kama Nathan hakufai basi
tafuta mwanaume mwingine”
akasema Theresa
“Theresa ungekuwa umekalia
hiki kiti ungenielewa nina
maanisha nini.Nathan ni mwanaume mzuri lakini nadhani
mimi si chaguo sahihi
kwake.Mitazamo yetu haiendi
sawa.Itakuwa vyema kama
nitakuwa mwenyewe si lazima
niwe na mume ili kichwa changu
kikae sawa.Usiku wa leo
nitakutana na Evans mwenyekiti
wa maandalizi ya harusi yangu na
nitampa rasmi taarifa ya kusitisha
shughuli zote za kuhusiana na
maandalizi ya ndoa yangu na
Nathan na kila aliyetoa mchango
wake arudishiwe” akasema Dr
Vivian
“Dada ni suala la mtoto pekee
ndilo limepelekea ukafanya
maamuzi haya magumu au kuna
sababu nyingine hutaki kuiweka wazi?Yamekuwa ni maamuzi ya
ghafla sana” akasema Theresa
“Theresa labda nilikuwa na
upofu wa penzi na sikuweza kuona
mbele kuna nini lakini maneno
yako uliyonieleza tukiwa ndegeni
yalinitoa upofu na kunifanya
nifikirie sana na kufanya maamuzi
haya.Usihofu kitu mdogo wangu
things will be fine.Nenda
kaendelee na shughuli
zako.Nilitaka nikueleze hayo
mambo mawili” akasema Dr Vivian
na Theresa akatoka
*************
“Ninatoa onyo kwa taifa lolote
lile kubwa au dogo ambalo linaungana na Korea kaskazini
kwamba waache mara moja
kufanya hivyo ama sivyo
yatawakuta matatizo
makubwa.Marekani itawahesabu
kama maadui zake na hatutasita
kuziwekea vikwazo vigumu sana
na ikibidi hata kutumia nguvu za
kijeshi.Ninaonya kwa mara ya
mwisho waache kabisa
mashirikiano yoyote na Korea
Kaskazini kabla hayajawafika
makubwa”
Hii ilikuwa ni kauli ya rais
Mike straw wa Marekani aliyoitoa
kufuatia mgogoro unaoendelea
kufukuta kati ya nchi yake na
Korea kaskazini “Sijui nini utakuwa mwisho
wa suala hili.Endapo hatua za
haraka za kulitafutia ufumbuzi
jambo hili hazitachukuliwa dunia
itajikuta sehemu mbaya
sana.Tanzania tutajikuta kati kati
ya mataifa makubwa.Marekani na
washirika wake hawataki Tanzaia
iwe na mashirikiano na Korea
kaskazini na kuiuzia madini ya
Urani lakini ziko nchi ambazo
zinasimama na Tanzania kama vile
China,Urusi,Iran n.k.Hawa wote ni
wapinzani wakubwa wa
Marekani.Hapa kuna shughuli
pevu.Hizi nchi zinazosimama
upande wa Tanzania nazo zina
uwezo mkubwa kijeshi.Endapo
Marekani na washirika wake watajaribu kwa namna yoyote
kuishambulia Tanzania kuna
uwezekano mkubwa wa kuibuka
vita ya tatu ya dunia.Mungu
aepushe mbali jambo hilo
lisitokee.Maelfu ya watu wasio na
hatia watapoteza maisha” akawaza
mathew akiwa sebuleni kwake
akitazama taarifa ya habari toka
shirika la habari la uingereza BBC.
Aliwahi sana kurejea
nyumbani siku hii.Tayari
alikwisha weka sawa mambo yake
na alikuwa tayari kuanza kuifanya
kazi ya rais.Katika meza ndogo
iliyokuwa mbele yake kulikuwa na
chupa ya mvinyo na glasi.Pembeni
yake alikuwa na kompyuta yake
mpakato na kitu alichokuwa anakifanya katika kompyuta ile
toka aliporejea nyumbani ni
kutafuta taarifa za Kanali
Sebastian Matope.Taarifa nyingi
alizozipata ni kuhusiana na yeye
kunusurika katika ajali ya ndege
ya rais Anorld Mubara.Nyingine
zinahusiana na kifo
chake.Hakukuwa na habari za
kutosha kuhusiana na maisha yake
“Kanali Sebastian hana taarifa
nyingi mtandaoni zinazoeleza
maisha yake binafsi.Hii inaonyesha
kwamba hakuwa mtu maarufu na
ameanza sana kuandikwa katika
mitandao baada ya ajali ile ya
ndege .Nahitaji kumfahamu yeye
binafsi alikuwa ni mtu wa namna
gani na ili kupata taarifa zake natakiwa kuonana na familia
yake.Nitaonana na Dr Vivian kesho
ili niweze kupata taarifa kamili
kuhusiana na baba yake. Kwa
kuanzia uchunguzi wangu kuna
maswali ambayo natakiwa
kujiuliza na kuyapatia
majibu.Kwanza Kanali Matope
alinusurika vipi katika ile ndege ya
rais iliyoanguka?Taarifa zinasema
kwamba ni yeye pekee aliyeweza
kutoka salama ndani ya hiyo ndege
lakini haijaelezwa kwa kirefu ni
vipi alitoka salama.Ninavyofahamu
mimi,endapo kutakuwa na tatizo
lolote katika ndege ya rais kiasi
cha kuhatarisha usalama wa rais
basi yeye huwa ni mtu wa kwanza
kuondolewa ndegeni kwa namna yoyote ile na kisha watu wengine
hufuata.Hata kama rais yuko na
familia yake huondolewa kwanza
na halafu familia yake
hufuata.Ndege ya rais
imetenegzwa maalum ili hata
kama kukitokea tatizo lolote iwe
rahisi kumuokoa rais,najiuliza
ilikuaje Kanali Matope akatoka
ndegeni kabla ya rais?Uchunguzi
lazima uanzie hapo” akawaza
Mathew na kunywa funda la
mvinyo na kuendelea kutafakari.
“Swali lingine ambalo
linahitaji majibu ni kwamba kanali
Matope alikuwa ndiye mbebaji
mkuu wa begi la rais lenye siri za
nchi lililopewa jina la
Football.Sifahamu kulikuwa na siri gani ndani ya hilo begi ila naamini
lazima kulikuwa na siri kubwa na
ndiyo maana rais alienda nalo kila
mahala aendako na mbebaji mkuu
alikuwa ni Kanali Sebastian
Matope.Je begi lile liko
wapi?Alifanikiwa kutoka nalo
ndegeni? Na kama
ndiyo,amelikabidhi ikulu? Kama
hapana kwa nini? Nifahamuvyo
mimi mtu anayebeba football
anakuwa amekula kiapo cha
kuhakikisha inakuwa salama hata
uhai wake ukiwa shakani na huwa
analindwa hivyo sitaki kuamini
kwamba Kanali Sebastian Matope
alinusurika katika ajali ile na
kuipoteza football kitu alichoapa
kukilinda hata ikimlazimu kuutoa uhai wake.Nitahitaji kulifahamu
hili pia” akanywa tena mvinyo na
kuendelea na tafakari.
“Jambo la tatu ambalo
natakiwa kulifahamu ni chanzo
cha ajali ya ndege ya
rais.Uchunguzi wa kisanduku
cheusi cha kuhifadhi kumbu
kumbu za mwenendo wa ndege
unaonyesha nini kilikuwa chanzo
cha kuanguka kwa ndege ya rais?
Nikipata majibu ya mambo haya
matatu ninaweza kupata sehemu
ya kuanzia” Akawaza na kuichukua
tena barua ambayo George
Mzabwa alimuandikia rais
akaisoma
“Katika barua hii George
anamuonya rais kwamba aachane na suala hili kwani ni gumu na
hataweza kupata majibu ya kile
anachokitafuta.Je kuna kitu
chochote kisicho cha kawaida
alichokigundua ? Sidhani mtu
kama George anaweza akachukua
maamuzi ya kujiua bila
sabab…..”Mathew akatolewa
mawazoni baada ya simu yake
mtandao wa Skype kuita katika
kompyuta.Haraka haraka
akaipokea baada ya kuona mpigaji
ni binti yake Anna Maria.
“Hallo my princess how’re
you?
“I’m fine dady.How’re you?
“I’m fine.How’s your mom
doing? “She’s also fine.We miss you so
much.When will you visit us?
“Oh my princess I can’t say
when but I promise I’ll come very
soon to visit you”
“Next week is my birthday,will
you come?
“I’m sorry my princess I wont
come but I’ll send you a very good
gift.Is your mother there with you?
“Yes she’s here”
“Tell her to call me on my
mobile right now”
“Ok dady .I love you”
“I love you too my princess.Be
a good daughter to your mother”
akasema Mathew na simu
ikakatwa na muda huo huo simu yake ya mkononi ikaita.Alikuwa ni
Peniela
“hallow Penny” akasema
Mathew
“Hallow Mathew.Mambo vipi?
“Mambo poa
kabisa.Mnaendeleaje?
“Tunaendelea vizuri.Wewe
unaendeleaje?
“Ninaendela vizuri.Anna
Maria ameniuliza kama nitakuja
katika siku yake ya kuzaliwa”
“Ni wiki ijayo.Are you coming?
“I’m sorry I’m not coming.I
have something very important to
take care over here”
“That something is important
than your daughter’s birthday
party? “Si hivyo Penny lakini ni
jambo la muhimu sana”
Peniela akavuta pumzi ndefu
na kuuliza
“Umerejea tena katika kazi
zako za zamani?
“Ndiyo.Sikutaka lakini
imenibidi nimsaidie rais”
“President Vivian? Are you
working for her?
“Peniela haya ni masuala
yangu binafsi na hupaswi
kuyaingilia.Ninacho kiomba kwako
unisaidie kumnunulia Anna Maria
zawadi yoyote nzuri sana kwa
niaba yangu.Can you help me do
that?
Peniela akafikiri kidogo na
kusema “Sawa nitafanya hivyo”
“Thank you”
“Kwa hiyo unashugulika na
suala gani huko kwa rais?
“Peniela haya ni mambo
yangu hupaswi kujua”
“Can I help? Akauliza Peniela
“No you can’t.Peniela wakati
tunaachana tulikubaliana kwamba
hakuna wa kuingilia maisha ya
mwenzake.Wewe unayo maisha
yako na bilionea wako na mimi
nina maisha yangu hivyo jitahidi
sana kuangalia maisha yako.Kiss
my daughter for me”
akasemaMathew na kukata simu
“Nasikitika sana kukosa
sherehe ya kuzaliwa mwanangu
Anna Maria.Ni mara ya kwanza ninaikosa.Lakini sijaikosa kwa
makusudi bali ni kutokana na
jukumu zito alilonipa rais”
akawaza Mathew
iku mpya imeanza na
tayari rais wa jamhuri
ya muungano wa
Tanzania Dr Vivian Matope
amekwisha jiandaa tayari kwa
kuikabili siku.Akiwa katika
chumba cha chakula akipata
kifungua kinywa na walinzi na
wasaidizi wake alikuwa anapitia
habari mbali mbali katika
magazeti ya hapa nchini na habari
kubwa iliyotawala karibu magazeti
yote bado ilikuwa ni msuguano
unaoendelea kati ya Korea
kaskazini na Marekani huku Tanzania ikijikuta kati kati ya
mzozo huo.Wakati akiendelea
kupitia magazeti,simu yake
maalum ikaita ,akaitazama na
mpigaji alikuwa ni Mathew
akaipokea haraka
“Hallow Mathew,habariz a
asubuhi?
“Habari nzuri mheshimiwa
rais.Nimekupigia kukujulisha
kwamba tayari mambo yangu
nimekwisha yaweka sawa na leo
ninaanza kazi.Asubuhi hii ninakuja
kukuona.Kuna mambo kadhaa
nitayahitaji toka kwako”
“Ahsante sana
Mathew.Nitakupa kila
utakachohitaji.Niko hapaninakusubiri” akasema Dr Vivian
na Mathew akakata simu
“Sifahamu utendaji kazi wake
lakini ,Mathew ananipa matumaini
makubwa katika jambo hili na nina
uhakika kuna hatua kubwa
ataipiga.Nitampa ushirikiano
mkubwa ili aweze kufanikisha
jambo hili” akawaza Dr Vivian
huku akiendealea kupata kifungua
kinywa taratibu na kusoma
magazeti mbali mbali.Alipomaliza
akaelekea ofisini kwake tayari
kuanza kazi.Mtu wa kwanza
kuonana naye ofisini kwake
asubuhi hii alikuwa ni waziri wa
mambo ya nje ambaye alipewa
kazi maalum ya kuhakikisha
mchakato wa mazungumzo kati ya Tanzania na Korea kaskazini
unaanza mara moja.
“Dr Robert,natumai utakuwa
na taarifa za kunipa asubuhi ya
leo” akasema Dr Vivian
“Ndiyo mheshimiwa rais,ni
kuhusiana na kazi uliyonipa jana
mheshimiwa rais” akasema Dr
Robert
“Kwa kushirikiana na balozi
wa Korea Kaskazini hapa Tanzania
nimefanikiwa kufanya
mazungumzo na waziri wa mambo
ya nje wa Korea
Kaskazini.Tumezungumza mambo
mengi kuhusiana na mchakato wa
kuanzishwa kwa mazungumzo ya
mashirikiano ya kibiashara baina
ya nchi zetu mbili kama ulivyonielekeza.Korea kaskazini
kupitia kwa waziri wao wa mambo
ya nje wamelipokea jambo hili kwa
mikono miwili na muda mfupi
uliopita nimetoka kuzungumza
tena na waziri wa mambo ya nje
wa Korea Kaskazini na amanipa
habari njema kwamba tayari
amemfikishia salamu zako rais
Kim Yun Hu wa Korea Kaskazini na
ambaye ameomba kuzungumza
nawe jioni ya leo kuhusiana na
masuala kadhaa muhimu kabla ya
kuanza kwa mashirikiano rasmi
baina ya nchi hizi mbili” akasema
Dr Robert
“Hizi ni taarifa njema sana
kwa kuanzia siku ya leo.Ahsante
Dr Robert kwa kazi nzuri.Kwa sasa endelea kushughulikia maongezi
hayo na rais Kim Hu jioni ya leo”
akasema Dr Vivian
“Sawa mheshimiwa rais.Hawa
jamaa wanaonekana wana nia ya
dhati ya kutaka kufanya
mashirikiano ya kibiashara na sisi
na ndiyo maana mambo
hayachelewi.Hawana muda wa
kupoteza.Hata hivyo mheshimiwa
rais tunapaswa kujiridhisha zaidi
kama kweli tunahitaji
mashirikiano haya na Korea
kaskazini .Jambo hili linaendelea
kuleta mvutano mkubwa na dunia
inajigawa katika pande mbili wale
wanaounga mkono Marekani na
wale wanaounga mkono Tanzania
kuwa na mashirikiano na Korea Kaskazini.Nchi yetu imewekwa
kati kati na imekuwa maarufu
ghafla kwani inazungumziwa
duniani kote” akasema Dr Robert
“Dr Robert hatuna haja ya
kujitathmini mara ya
pili.Tunahitaji kufanya biashara na
Korea kaskazini.Pamoja na kelele
zote zinazopigwa lakini msimamo
wangu bado uko pale pale kwamba
Tanzania na Korea Kaskazini
lazima zishirikiane
kibiashara.Mashirikiano haya
naamini yatakuwa na tija kwa
taifa.Kaendelee kufanya
maandalizi kwa ajili ya mkutano
wangu na Kim leo jioni” akasema
Dr Vivian baada ya simu kuita na
kutaarifiwa kwamba Mathew Mulumbi amefika.Rais akaelekeza
apelekwe katika chumba cha
maongezi ya faragha.Hakupoteza
muda akatoka na kwenda kuonana
na Mathew
“Hallow Mathew karibu
sana.Habari za toka jana? Dr Vivan
akaanzisha maongezi
“Habari nzuri kabisa
mheshimiwa rais.Nimefanikiwa
jana kuweka sawa mambo yangu
na sasa nimekuja rasmi kuanza
kazi”
Uso wa Dr Vivian ukachanua
kwa tabasamu halafu akasema
“Ahsante sana Mathew kwa
kuamua kuahirisha shughuli zako
na kuifanya kazi yangu.Hii ni
heshima kubwa umetupa mimi na familia yangu.Vitu gani utavihitaji
katika kazi hii nikuandalie mara
moja?
“Kwa sasa nitahitaji vitu
vichache.Baada ya kutafakari sana
sehemu ya kuanzia uchunguzi wa
suala hili nimeona nianzie katika
ajali ya ndege ya rais Anorld
Mubara.Kwanza nitahitaji kuipata
ripoti ya uchunguzi wa chanzo cha
ajali ya ndege ile ambamo Kanali
Sebastian alikuwemo na
akanusurika peke yake.Ninaamini
uchunguzi ulifanywa na ripoti yake
kutolewa hivyo ningependa
niipitie nijue chanzo cha ajali
ile.Jambo la pili ninahitaji kupata
nakala ya maelezo aliyoyatoa
Kanali Sebastian katika mahojiano yake na jeshi la polisi.Nataka
kufahamu aliwezaje kutoka salama
peke yake ndani ya ndege
ile?Jambo la tatu nataka kufahamu
kuhusiana na begi ambalo alikuwa
analibeba Kanali Sebastian
lililopewa jina la
football.Inaaminika kwamba
kulikuwa na siri kuwa ndani ya ule
mkoba nataka kujua mahala ulipo
ili tujue ni siri gani hasa
iliyokuwamo ndani yake? Jambo la
mwisho ninahitaji kumfahamu
vyema Kanali Sebastian Matope
alikuwa ni mtu wa namna
gani.Maisha yake yalikuaje na
alipendelea mambo gani zaidi na
kama kuna sehemu ninaweza
kupata kumbukumbu zake itakuwa vyema zaidi ili nione kama
kuna kitu ninaweza kukipata cha
kutusaidia kufahamu sababu ya
kifo chake” akasame Mathew.Dr
Vivian aliyekuwa anamtazama kwa
makini akameza mate na kusema
“Nimekuelewa Mathew na
nitahakikisha hivyovyote
ulivyoomba vinapatikana kwa
haraka sana kabla ya saa nane
mchana wa leo.Taarifa ya
uchunguzi wa chanzo cha ajali ya
ndege iliyomuua rais Anorld
sijawahi kuipata lakini nitaiomba
kutoka vyombo husika na
nitapewa.Nina imani ipo.Jambo la
pili ni maelezo aliyoyatoa Kanali
Sebastian kwa polisi baada ya
kunusurika katika ajali.Haya pia ni rahisi kuyapata na nitaagiza
yaletwe hapa mara moja.Jambo la
tatu ni kuhusu football.Hapa
kutakuwa na ugumu kwani hili
begi halipo.Nilipoingia
madarakani sijawahi kuliona hilo
begi na hata mtangulizi wangu
hakuwahi kunieleza chochote
kuhusiana na Football na wala
hata naye hakuwa nalo.Hakuna
anayejua iko wapi hivyo inabidi
kuifanyia uchunguzi iko
wapi?Jambo la nne na la mwisho
umetaka kumfahamu Kanali
Sebastian alikuwa mtu wa aina
gani na kama kuna mahala
unakoweza kupata kumbukumbu
zake .Ningeweza kumuelezea baba
alikuwa ni mtu wa aina gani lakini muda wangu mwingi nimeutumia
katika masomo hivyo sikuwa
napata muda mzuri sana wa kukaa
nyumbani kwa hiyo sintaweza
kumuelezea baba kwa undani
sana.Hata hivyo ninaye mdogo
wangu anaitwa Theresa huyu
amekuwa na baba muda mwingi
na anaweza akamuelezea vizuri
zaidi.Kuhusiana na kupata
kumbukumbu za baba ni kwamba
muda mfupi tu baada ya kifo chake
nyumba yake iliungua moto ambao
chanzo chake hakikujulikana na
kuteketeza kila kitu kilichokumo
ndani yake kwa hiyo hakuna
mahala kokote tunakoweza kupata
kumbu kumbu zake.Hii inaonyesha
ni kwa namna gani hili jambo lilivyokuwa gumu na ndiyo maana
limekuwa ni kama fumbo
lisiloweza kufumbuka.Pamoja na
ugumu huo lakini nakuomba
Mathew jitahidi kuweza kulipatia
majibu.Kuna mambo mengi
yamejificha katika jambo hili”
akasema Dr Vivian
“Mheshimiwa rais jambo hili
si rahisi kama ulivyosema na kwa
namna lilivyokaa linaonekana ni
suala pana sana na lenye
mkanganyiko wa mambo.Lakini
nakuhakikishia kwamba nitafanya
kila lililo ndani ya uwezo wangu
kuweza kupata majibu ya fumbo
hili.Ninaweza kuonana na
Theresa? “Theresa unaweza kuonana
naye.Yupo hapa ikulu ndiye
mwandishi wa hotuba zangu”
Akasema Dr Vivian na kuinua simu
akampigia Theresa akamtaka afike
ofisini kwake mara moja
“Kuna vitu vingine ambavyo
ungevihitaji Mathew?Mfano silaha
au mtu wa kukusaidia katika
uchunguzi wako?akauliza rais
“Hivyo nilivyokuomba ndivyo
ninavihitaji kwa sasa na endapo
kutakuwa na vitu vingine ambavyo
nitavihitaji nitakujulisha .Silaha
ninazo na sihitaji mtu wa
kunisaidia kwa sasa ila
nitakapohitaji nitakueleza”
“Are you sure? “Yes madam president I’m
sure” akajibu Mathew
“Kiasi gani cha fedha
utakihitaji kwa shughuli hii nzima?
“Fedha?! Mathew akashangaa
na kutabasamu
“Namaanisha malipo
yako.Utahitaji nikulipe kiasi gani
kwa kazi hii?akauliza rais na
Mathew akacheka kidogo na
kusema
“Sihitaji chochote
mheshimiwa rais.Ninazo fedha za
kunitosha.Hili lilikuwa ni ombi
maalum toka kwako na kwa mzee
Meshack.Kama alivyosema
Meshack Jumbo jana kwamba
nimsaidie dada yangu na ndivyo
ninavyofanya.Kwa hiyo usiwaze kabisa kuhusiana na malipo”
akasema Mathew na Dr Vivian
akamtazama kwa mshangao na
kuuliza
“Mathew una uhakika
hauhitaji fedha za kukusaidia?
Kabla Mathew hajajibu kitu
mlango ukafunguliwa akaingia
Theresa
“Theresa karibu
sana.Nimekuita ukutane na
Mathew Mulumbi.Huyu ndiye
atakayetusaidia kulitafutia
ufumbuzi lile fumbo
lililoshindikana kufumbuka.Ndiye
atakaye fanya uchunguzi wa
walioteketeza familia yetu.Mathew
huyu ni mdogo wangu anaitwa
Theresa ndiye mwandishi wa hotuba za rais” Dr Vivian akafanya
utambulisho.Mathew akasimama
na kumsabahi Theresa
“Mathew karibu sana
.Nimefurahi kuonana nawe”
akasema Theresa
“Ahsante sana Theresa.Ni
furaha yangu kukutana nawe pia”
akajibu Mathew
“Mathew kama ujuavyo mimi
nina kazi nyingi sana,vikao
haviishi,natembelewa na wageni
wengi kila siku kwa hiyo kuna
nyakati unaweza ukanihitaji au
ukahitaji msaada wangu na
kunikosa.Kutokana na umuhimu
wa suala hili ninakukabidhi
Theresa utakuwa naye
akikusaidia.Kuna mambo mengi utayahitaji mfano taarifa mbali
mbali hivyo huyu ndiye
atakayekusaidia kuzipata.Theresa
utahakikisha kila anachokihitaji
Mathew anakipata na endapo kuna
kitu kitakushinda basi utanijulisha
mara moja.Mimi nitakuwa
nikiwasiliana nanyi mara kwa
mara kujua maendeleo yenu”
akasema Dr Vivian na kunyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Mathew nakuomba mlinde
sana Theresa kwa kadiri
uwezavyo.Awali ulisema kwamba
huhitaji mtu yeyote wa kukusaidia
katika kazi hii lakini nimeona
jukumu hili ni zito sana na huwezi
kulifanya peke yako bila
msaada.Sitaki ufike mahala ukakwama na ndiyo maana
ninakukabidhi mdogo wangu wa
pekee kusaidia na kukuwezesha
shughuli zako ziende vizuri kwa
hiyo mlinde sana .Hili jambo ni la
hatari sana .Usikubali akaingia
katika hatari yoyote.Kama kuna
taarifa au nyaraka zozote
unazihitaji yeye atakusaidia
kuzipata.Yeye anafahamika na
anaweza akaingia sehemu yoyote
ile kwa jina langu.Narudia tena
kukuomba Mathew mlinde
Theresa” akasema Dr Vivian na
kumgeukia Theresa
“Theresa hautasafiri kwenda
sehemu yoyote kwa sasa kwa ajili
ya kumsaidia Mathew.Weka
pembeni majukumu yako yote kwa muda.Hotuba zangu nitaandika
mwenyewe.Mathew amejitolea
kuifanya kazi hii bila hata kulipwa
senti moja kwa hiyo na sisi kama
familia tunapaswa kumpa
ushirikiano mkubwa.Kuna tatizo
lolote katika hilo? Akauliza rais
“Hakuna tatizo dada.Mimi
niko tayari kumsaidia
Mathew.Isitoshe hili ni jambo la
familia hivyo na sisi tunapaswa
kushiriki”
“Ahsante sana .Mathew
nawatakia kila la heri ila kumbuka
kwamba jambo hili kutokana na
unyeti wake lazima lifanyike kwa
usiri kwani hatujui ni akina nani
wanahusika” akasema Dr Vivian “Ahsante sana mheshimiwa
rais.Narudia tena kukuahidi
kwamba nitajitahidi kwa kila
namna ninavyoweza” akasema
Mathew huku akisimama na
kupeana mkono na rais akatoka
mle ndani ya chumba akamuacha
rais na Theresa wakiongea halafu
Theresa akatoka na kumtaka
Mathew waelekee ofisini kwake
“Nimefurahi kuonana nawe
Mathew.Karibu sana ofisini
kwangu” akasema Theresa baada
ya kuingia ofisini kwake
“Ahsante sana Theresa”
akajibu Mathew.Theresa akapakia
kompyuta yake katika mkoba
pamoja na baadhi ya vitu vyake na
kumtaka Mathew waondoke. “Tunaelekea wapi?
“Katika ofisi nyingine” akajibu
Theresa kwa ufupi. Theresa
alimtaka Mathew amfuate kwa
nyuma na gari lake kisha
wakaondoka maeneo ya ikulu
“Nina mashaka na Mathew
kama kweli ataweza kulifumbua
fumbo hili ambalo limeshindwa
kufumbuliwa na vyombo vya
uchunguzi kwa miaka kumi
sasa.Naona kama vile ana
hatarisha maisha yake kwa
kujiingiza katika hili suala.Kijana
mzuri sana yule sipendi kumuona
akipata matatizo.Sijapendezwa na
mpango wa dada wa kutaka
kulifufua suala hili ambalo kwa
sasa limetulia.Mambo mengi yataibuka na kutuweka katika
hatari kubwa sana.Sintamweleza
mtu yeyote hiki
ninachokifahamu.Itaendelea
kubaki siri yangu” akawaza
Theresa na kuushika msalaba
ulikokuwa shingoni.
“Naamini msalaba huu una siri
kubwa ndani yake ndiyo maana
baba akaamua kunipatia na
kunisisitiza niulinde sana.”
Akawaza Theresa
Gari la Theresa lilisimama nje
ya geti jekundu na haukupita muda
geti hilo likafunguliwa na gari la
Theresa likaingia ndani na Mathew
naye akafuata .Ndani ya nyumba
hii kulikuwa na uzuri wa
kipekee.Nyasi za kupendeza zenye ukijani wa kung’aa zilipandwa kila
kona na kukatwa kwa ustadi
mkubwa.Miti ya aina mbali mbali
yenye maua ya kupendeza
ilipandwa kulizunguka jumba hili
na kulifanya liwe na mandhari ya
kupendeza sana.Alikuwepo kijana
mmoja aliyeonekana akifanya kazi
ya kumwagilia na kuhudumia
bustani.Theresa akasimamisha
gari mbele ya nyumba iliyokuwa
na rengi nyeupe na kuezekwa kwa
vigae vya rangi nyekundu.
Akashuka na Mathew naye
akashuka na kumfuata
“Mathew hapa ni nyumbani
kwanu.Karibu sana.Hapa ndipo
nyumbani kwa Kanali Sebastian
Matope.Rais Dr Vivian naye ameishi katika nyumba hii hadi
alipopata urais.Nyumba ya zamani
ilikuwa upande ule kule chini
lakini iliungua moto hivyo hii
nyumba ni mpya” Akasema
Theresa huku akimuonyesha
Mathew mazingira ya nyumba ile
nzuri
“Nimeyapenda
mazingira.Mmejitahidi sana
kuyaboresha” akasema Mathew
“Baba mzee Matope alikuwa
anapenda sana mazingira na sisi
tumefuata nyayo zake.Ile miti yote
unayoiona katika bara bara ya
kuja huku nyumbani ameipanda
yeye.Karibu ndani mathew.Hapa
ndipo tutakapoweka ofisi yetu ya
muda.Pale ikulu hapana usiri lakini tukiwa hapa tutafanya
shughuli zetu kwa usiri” akasema
Theresa na kuingia
ndani.Waliingia katika chumba
kimoja kizuri kilichokuwa na
samani za kupendeza za ofisi.
“Hii ni ofisi yangu ya
nyumbani.Vivian kabla ya kuwa
rais hii ndiyo ilikuwa ofisi
yake.Kuna kila kitu
utakachokihitaji humu kasoro
silaha” akasema Theresa na wote
wakacheka
“Nadhani bila kupoteza wakati
tuanze kazi” akasema Mathew
“Dada aliniambia kwamba
nikusaidie kwa chochote kile
utakachokihitaji kwa hiyo nina kusikiliza wewe,niambie nini
unahitaji?
“Ahsante.Nilimuomba rais vitu
vinne.Kwanza taarifa ya chanzo
cha ajali ya ndege ya rais
Anorld,pili nakala ya maelezo ya
kanali Sebastian baada ya
kunusurika katika ile ajali ya
ndege,tatu ni begi alilokuwa
analibeba kanali Sebastian
maarufu kama Football,niliomba
vile vile kama kuna sehemu
naweza kupata kumbu kumbu za
kanali Sebastian na mwisho
nilitaka nimfahamu kanali
Sebastian ni mtu wa namna gani
.Rais ameniahidi kunitafutia
taarifa ya uchunguzi wa chanzo cha
ajali ya ndege ya rais Anorld pamoja na nakala ya maelezo ya
kanali sebastian aliyoyatoa baada
ya kunusurika ajalini.Kuhusu
Football amesema kwamba begi
lile halijawahi kuonekana toka
ajali ilipotokea.Kuhusu kumbu
kumbu za kanali Sebastian
nimeambiwa hakuna
kumbukumbu zozote kwani
nyumba yake iliungua moto baada
ya yeye kuuawa.Mwisho kabisa
nilitaka nimfahamu baba yenu
alikuwa ni mtu wa aina gani na
akasema kwamba jukumu hilo
atakuachia wewe kwa kuwa
umekuwa na kanali Matope kwa
muda mrefu na hivyo unaweza
ukamuelezea kwa upana
zaidi”akasema Mathew na kumtazama Theresa kwa muda na
kusema
“Kanali Sebastian Matope
hakuuawa kwa bahati
mbaya.Mauaji yake yalikuwa
yamepangwa na lazima kuna
jambo lipo nyuma yake hivyo
nataka nianzie uchunguzi wangu
mbali kidogo katika ajali ya ndege
ya rais.Nataka kufahamu aliwezaje
kutoka salama katika ndege
ile?Ninavyofahamu mimi endapo
kutatokea tatizo lolote la
kuhatarisha usalama wa rais
ndegeni,aidha hitilafu au uvamizi
wowote basi rais huwa ni mtu wa
kwanza kuondolewa ndegeni.Hata
kama yuko na familia yake lakini
yeye hupewa umuhimu mkubwa kwanza.Katika ajali ile kanali
Sebastian Matope alinusurika peke
yake.Nikipata jibu la namna
alivyotoka ndani ya ndege nitapata
mwanga kwa nini aliuawa.Wakati
nikisubiri taarifa hiyo nataka
nimfahamu huyu kanali Sebastian
alikuwa ni mtu wa aina gani?
Wakati ajali ile ya ndege ilipotokea
Vivian alikuwa masomoni nje ya
nchi kwa hiyo wewe ulikuwepo
hapa,je kuna jambo lolote aliwahi
kukueleza ambalo unahisi
linaweza kutusaidia katika
uchunguzi wetu? Akauliza Mathew
“Kwa kuanzia mimi si mtoto
wao wa kunizaa.Walinichukua
katika kituo cha kulelea watoto
yatima nikiwa mdogo sana.Naambiwa niliwa na umri wa
miaka miwili.Taarifa zinasema
kwamba Kanali Sebastian Matope
hakuwahi kuwafahamu wazazi
wake na alikulia katika kituo cha
kulelea watoto yatima hivyo
alipenda sana kutembelea vituo
vya kulelea mayatima kila pale
alipokuwa na nafasi.Inaelezwa
kwamba kuna siku alikwenda na
mke wake katika kituo
nilichokuwa nalelewa na
walipotaka kuondoka niliwalilia
sana ikabidi waombe kuondoka
nami na toka hapo wakawa ndio
wazazi wangu.Wamenilea kwa
mapenzi makubwa kama mtoto
wao wa kumzaa.Nimekuwa nao
karibu hivyo ninawafahamu vyema.Baba alikuwa ni mtu mpole
na mwenye upendo.Japokuwa
alikuwa ni mwanajeshi tena
aliyewahi kupitia na kufuzu
mafunzo ya komando lakini
arudipo nyumbani hutambua
kuwa yeye ni baba .Hakuwa na
marafiki wengi kutokana na muda
mwingi kuutumia katika kazi
zake.Baba alikuwa mjenzi vile vile
na inasemekana ile nyumba yake
iliyoungua ni yeye
aliyeijenga.Alikuwa mpenda
mazingira pia.Hayo ndiyo
machache ninayoweza kuyaeleza
kuhusiana na baba” “Ahsante sana.Hakuna
chochote alichowahi kukueleza
baada ya kunusurika ndegeni? Hakuwahi kuwaelezeni namna
alivyonusurika?
“Hakuwahi kutufafanulia bali
alieleza kwa ujumla tu kwamba
alinusurika ndegeni kwa kutumia
mbinu za kijeshi.Yawezekana
labda alimfahamisha mama ila
mimi hakuwahi kunieleza”
“Siku ile alipouawa ilikuwa
jumapili,wewe ulikuwa
wapi?Ulimuona akiwa katika hali
gani?
“Siku ile mimi nilikwenda
kuhudhuria ibada na nilichelewa
kurudi kwa sababu kulikuwa na
harambee na laiti ningewahi
kurudi ningeambatana nao na
mimi ningekufa kwani walinisubiri
sana na walipoona wanazidi kuchelewa wakaondoka na
kuniacha.Alikuwa kawaida na
hakuonekana kuwa na tatizo
lolote” akasema Theresa.
“Siku ile ndege ya rais
ilipopata ajali walikuwa wanatoka
nchini Misri katika mkutano.Siku
moja kabla ya safari ile
alikuaje?Kuna kitu chochote
unakikumbuka ambacho
hakikuwa cha kawaida kwake?
“Jioni ya siku ile nilikuwa naye
sebuleni tukipata chakula pamoja
na hakuonyesha utofauti wowote
.Alikuwa kawaida kama siku zote”
akajibu Theresa
Jioni ya siku ile nilikuwa naye
sebuleni tukipata chakula pamoja
na hakuonyesha utofauti wowote
.Alikuwa kawaida kama siku zote”
akajibu Theresa
“I see” akasema Mathew na
kukaa kimya kidogo na kabla hajasema chochote simu yake
ikaita.Alikuwa ni rais Dr Vivian
“Rais anapiga” akasema na
kuipokea
“Hallow mheshimiwa rais”
akasema Mathew
“Mathew just call me Dr
Vivian.Kila wakati mheshimiwa
inachosha masikio.Nimekupigia
kukupa taarifa kuhusiana na ile
taarifa uliyoiomba ya uchunguzi
wa chanzo cha ajali ya ndege ya
rais Anorld.Taarifa nilizozipata
zimenistua .Nimeambiwa kwamba
taarifa hiyo haipo kwa sababu
uchunguzi wa kubaini sababu ya
kuanguka kwa ndege ya rais
haukuwahi kukamilika kwa kuwa
kisanduku cheusi maalum kwa ajili ya kuifadhi taarifa za mwenendo
wa ndege hakikuwahi kuonekana”
“Hakijawahi kuonekana?
Mathew akashangaa
“Mathew nilipokuambia
kamba suala hili ni fumbo gumu
nilikuwa namaanisha na sasa
umeanza kuona ugumu
wake”akasema Dr Vivian
“Kweli Dr Vivian hili suala ni
fumbo.Hainiingii akilini eti
kisanduku hicho muhimu kipotee
kisionekane na halafu isiwekwe
wazi na jambo hili likabaki kuwa
ni siri.Halafu cha kushangaza ni
kwamba ndege ile iliangukia
sehemu tambarare kabisa iweje
kisanduku hicho
kisionekane?Ingekuwa imeanguka katika maji au katika milima
mikubwa hapo kidogo tungeweza
kukubaliana na hilo jambo lakini
hata hivyo ipo namna ya
kukitafuta kisanduku hicho
.Naamini kuna kitu hapa katika hii
ajali ya ndege ya rais na ndiyo
maana nikaamua kuanza
uchunguzi wangu kutafuta kwa
nini ndege hii ilianguka.Nina hisi
lazima kisanduku hicho
kiliondolewa makusudi na
kufichwa ili kuzuia chanzo cha
ajali ile kujulikana.Kama tukiweza
kufahamu chanzo cha ajali hiyo
basi tutaweza kupata urahisi wa
kujua kwani nini kanali Sebastian
aliuawa na waliomuua ni akina
nani.Naamini mauaji ya Kanali Sebastian chanzo chake kimeanzia
mbali” Akasema Mathew
“Mathew nadhani mwanzo tu
umeona utata ulipo hivyo nakusihi
kuwa makini sana wakati
unalichunguza hili jambo.Si jambo
rahisi”
“Nalifahamu hilo mheshimiwa
rais,naomba unisaidie basi nipate
maelezo ya kanali Sebastian
wakati nikitafakari kuhusiana na
hilo suala la kupotea kwa
kisanduku cha kuhifadhi kumbu
kumbu za ndege” akasema Mathew
“Sawa Mathew nimekwisha
agiza niletewe hiyo taarifa na mara
tu itakapofika nitakujulisha mara
moja” akasema rais na kukata
simu “Kuna nini Mathew?akauliza
Theresa
“Nilimuomba rais anisaidie
nipate taarifa ya uchunguzi wa
chanzo cha ajali ya ndege ya rais
Anorld na majibu aliyonipa
yanashangaza sana.Inadaiwa
uchunguzi huo wa kubaini sababu
ya ndege hiyo kuanguka
haukufanikiwa kwa sababu
kisanduku cheusi ambacho
huhifadhi taarifa za mwenendo wa
ndege hakikuwahi kuonekana
eneola ajali’
“Kimekwenda wapi? Nani
kakichukua? Theresa akauliza
“Hakuna mwenye jibu hilo
lakini ni wazi kiliondolewa
makusudi ili chanzo cha ajali hiyo kisijulikane.Theresa suala hli
linaonekana ni kubwa.Chanzo cha
kifo cha baba yenu kimeanzia
mbali.Ninatakiwa kulichimbua
hadi mzizi wake ili kuupata
ukweli”
Theresa akafikir kidogo na
kusema
“Mathew hili suala limeanza
kuniogopesha .Kwa nini
tusiachane nalo kama lilivyo?Sitaki
familia yetu iingie katika hatari
tena”akasema Theresa
“Theresa hili si suala
dogo.Watu waliofanya kitendo
hicho cha kuondoka na kisanduku
hicho ni watu wanaoelewa kitu
wanachokifanya na wana sababu
ya kufanya hivyo.Mimi huwa nikigundua mambo tata kama hili
katu siwezi kukubali kuliacha
likapita hivi hivi.Lazima
nilichimbue jambo hili hadi mzizi
wake na hadi niupate
ukweli.Usihofu kuhusu hatari
mimi nimekwisha zoea na kwa vile
utakuwa karibu yangu nakuomba
uwe jasiri “ akasema Mathew
“Ninaogopa sana Mathew .Kwa
hiyo nini kinafuata baada ya hapa?
“Taa nyekundu imeniwakia
katika ajali ya ndege ya
rais,naamini kuna jambo
limejificha hapo hivyo uchunguzi
unatakiwa kijikita zaidi hapo
katika ajali” akasema Mathew
“Kama hicho kiboksi ambacho
huhifadhi taarifa zote za mwenendo wa ndege hakipo
utachunguza vipi?Theresa akauliza
.Mathew akafikiri na kusema
“Nahitaji kufahamu aliyekuwa
balozi wa Tanzania nchini Misri
wakati huo”
“Unahitaji kuzungumza naye?
“Ndiyo kuna mambo nahitaji
kuzungumza naye” akasema
Mathew na Theresa akazungumza
na mtu simuni na baada ya muda
akakata simu na kumtazama
Mathew
“Nimeambiwa nisubiri kwa
dakika chache nitajulishwa”
akasema Theresa
“Nini unahitaji kufahamu
kutoka kwa huyo balozi? Na vipi
iwapo….” Hakumaliza alichotaka kukisema simu yake ikaita
akazungumza kwa muda wa
dakika tatu kisha akaagana na
aliyekuwa anaongea naye akakata
simu na kumgeukia Mathew
“Nimetaarifiwa kwamba
aliyekuwa balozi wa Tanzania
nchini Misri wakati wa rais Anorld
alipofariki ni Alhaj Zubery
Msokwa.Nimeelekezwa anaishi mji
wa kale Kigamboni
“Good.Twende tukaonane
naye” akasema Mathew wakatoka
na kuingia katika gari la Theresa
wakaondoka
“Natamani Mathew
asifanikiwe katika suala hili na
akate tamaa aachane nalo.Ni suala
la hatari kubwa na ninaamini maisha yetu yatakuwa hatarini
pindi ikibainika kwamba
tumeanza kulifuatilia hili
jambo.Ninaogopa ila sijui nifanye
nini kumkwamisha huyu jamaa
asiendelee na kulichimba hili
jambo.Yeye amedhamiria kuupata
ukweli na nikimtazama machoni
anamaanisha kile
anachokisema.I’m so scared”
akawaza Theresa wakiwa njiani
kuelekea kwa Alhaj Zubery
Msokwa aliyewahi kuwa balozi wa
Tanzania nchini Misri wakati rais
Anorld anapata ajali.
“Kisanduku cheusi
hakikuwahi kuonekana eneo la
ajali.Hii inawezekana vipi?Mathew
akajiuliza “Suala la kupotea kwa
kisanduku cheusi linashangaza
sana hasa kutokana na mahala
ndege ilipoangukia kuwa ni
sehemu tambarare.Ingekuwa
katika maji labda ingeniingia
akilini lakini siwezi kukubali eti
kisanduku kisionekane sehemu
kama ile.Kuna jambo gani
linafichwa kuhusiana na ajali ile?
Naamini kisanduku hicho
kimeondolewa makusudi kabisa ili
sababu ya kuanguka kwa ndege ile
isijulikane.Kingine
kinachonishangaza ni kwa nini
jambo hili limefanywa siri?Kuna
watu ndani ya serikali wanahusika
na ajali ile na ndiyo maana hili
jambo likafichwa lisijulikane? Hapa kuna siri kubwa .Napaswa
kuongeza umakini sana katika hili
jambo.Nikifanikiwa kugundua
kilichotokea hadi ndege ya rais
ikaanguka nitakuwa nimepiga
hatua kubwa sana katika
kufahamu kwa nini kanali
Sebastian aliuawa.Hili jambo
haliwezi kufanywa na mtu mmoja
bali na mtandao mkubwa
waliojipanga vyema” akawaza
Mathew
Safari iliendelea hadi
walipofika katika nyumba
aliyoelekezwa Theresa kwamba
ndipo anaishi Alhaj Zubery
Msokwa.Mathew akashuka garini
na kwenda kugonga geti na baada
ya muda mlango mdogo ukafunguliwa na binti mmoja
akajitokeza akawasabahi
“Niwasaidie nini? Akauliza
“Hapa ndipo nyumbani kwa
Alhaj Zubery Msokwa? Akauliza
Mathew
“Ndiyo hapa.karibuni sana”
akasema yule msichana na
kufungua geti .Theresa akaingiza
gari ndani halafu wakakaribishwa
sebuleni.Baada ya muda akatokea
mama mmoja wa makamo
“Karibuni jamani” akasema
yule mwanamama mweupe sana
na aliyeonekana kama
amechanganya damu.
“Ahsante sana,habari za hapa?
Wakajibu Mathew na Theresa kwa
pamoja “Za hapa nzuri sijui nyie huko
mtokako” akauliza
“Huko ni kwema
kabisa.Samahani kwa kuwavamia
bila taarifa” akasema Theresa
“Bila samahani.Karibuni sana”
“Ahsante.Mimi naitwa Theresa
Matope na huyu mwenzangu
anaitwa Mathew.Sote ni
wafanyakazi wa ikulu” akasema
Theresa.
“Oh ! karibuni sana.Mimi
naitwa Zaina Moskwa.” Akajibu
yule mama na mara yule dada
aliyewapokea akina Mathew
akatokea akiwa na sinia lenye glasi
mbili za juisi na sambusa nne
akawakaribisha “Tunafurahi kukufahamu
Zaina.Tumekuja hapa kutaka
kuzungumza na Alhaj Zubery
Msokwa ambaye naamini ni baba
yako”
“Ndiyo ni baba yangu.Mimi ni
mtoto wake wa mwisho.Watoto
wake wengine wote wako Arabuni
na mimi ndiye niko hapa
kumuhudumia kwani mama yetu
alikwisha tangulia mbele za
haki.Kwa sasa baba anasumbuliwa
na maradhi mbalimbali.Alipooza
upande wa kulia ingawqa kwa sasa
hilo si tatizo sana kwani anaendela
vyema,anasumbuliwa vile vile na
sukari na shinikizola damu.Utu
uzima nao unachangia ” “Dah ! pole sana.Vipi hali yake
kwa sasa? Akauliza Mathew
“Kwa sasa anaendelea vizuri
ila tatizo ni mkono ndio
unaomsumbua”
“Pole Zaina hii ni mitihani ya
maisha.Mungu akupe wepesi wa
kuweza kumuuguza mzee”
akasema Theresa
“Nashukuru Theresa”
akasema Zaina na ukimya wa
sekunde kadhaa ukapita
“ Maradhi haya yalimuanza
wakati gani? Mathew akauliza
“Alianza kuumwa angali akiwa
balozi wa Tanzania nchini
Misri.Alipata ajali ya gari na
kulazwa kwa muda mrefu
hospitali.Amekaa kwa muda wa miaka zaidi ya saba nchini Israel
na Mungu akamjalia akapata nafuu
ndipo tuliporejea nyumbani
Tanzania.Toka wakati huo
amekuwa ni mtu wa nyumbani
.Mlitaka kuzungumza naye jambo
gani? Akauliza Zaina
“Kuna jambo fulani liliwahi
kutokea kama miaka kumi
iliyopita wakati yeye akiwa ni
balozi wa Tanzania nchini Misri
hivyo tunataka kujua kama
anaweza kuwa anakumbuka
chochote kuhusiana na hilo jambo”
akasema Mathew
“Mh ! baba amekuwa na tatizo
la kupoteza kumbu kumbu.Kuna
wakati anakuwa mzima kabisa na
kumbu kumbu zake zinakuwa sana lakini kuna nyakati anapoteza
kumbu kumbu na hata mimi
mwenyewe huwa ananipotea na
kuniuliza mimi ni nani.Hata hivyo
nisiwakatishe tamaa mnaweza
mkajaribu bahati yenu na mkapata
kile mhachokitaka kwani kuna
wakati kumbukumbu zake huwa
zinakaa vizuri na hukumbuka
mambo mengi hata ya zamani”
akasema Zaina na kuwataka akina
Mathew wamfuate wakaelekea
bustanini ambako walimkuta mzee
mmoja aliyevaa kofia nyekundu
akiwa amekaa sofani mahala
palipotengenezwa maalum kwa
ajili ya kupumzika.Ilikuwa ni
bustani nzuri .Mkononi mwake
alikuwa na kitabu cha dini akisoma.Alipomuona Zaina na
wageni akafunika kitabu kile na
kukiweka pembeni
“Baba nimekueletea wageni”
akasema Zaina huku akitabasamu
“Karibuni” akasema mzee
Zubery
“Shikamoo mzee” Mathew na
Theresa wakamsalimu
“Marahaba vijana.karbuni”
“Ahsante mzee.”wakasema na
kuketi katika viti vilivyokuwapo
eneo lile maalum kwa kupumzika.
“Baba hawa wageni wametoka
ikulu ,watajitambulisha wenyewe
na wataeleza kitu gani
kilichowaleta hapa kwako”
akasema Zaina “Karibuni vijana.Wanasemaje
ikulu?
“Mzee mimi naitwa Mathew na
huyu mwenzangu anaitwa
Theresa.Sote ni wafanyakazi wa
ikulu.Tumekuja hapa kwako kuna
mambo tunataka utusaidie
kukumbuka”
“Mambo gani? Akauliza mzee
Zubery
“Uliwahi kuwa balozi wa
Tanzania nchini Misri wakati wa
uongozi wa rais Anorld Mubara”
“Ndiyo nimekuwa balozi wa
Tanzania Misri miaka kumi na
tatu.Nilikuwa balozi kabla hata
rais Anorld hajaingia
madarakani.Hata mke wangu wa
pili nilimpata huko huko.Nilistaafu baada ya kupata ajali na
nikashindwa kuendelea tena na
kazi”
“Pole sana mzee na hongera
kwa kukaa kipindi kirefu katika
ubalozi nchini Misri.Kazi yao
ilikuwa nzuri na ndiyo maana
ukaachwa sehemu moja kwa
miaka mingi.Mzee Zubery kama
utakumbuka rais Anorld alifariki
katika ajali ya ndege akitokea
nchini Misri katika kikao cha
marais wa nchi zinazopitiwa na
mto Nile.Katika ajali hiyo watu
wote walifariki dunia.Chanzo cha
ajali hiyo mpaka leo hajifahamika
.Ukiwa kama balozi ulimpokea rais
Anorld na ujumbe wake hadi
walipoondoka.Kuna chochote unachoweza kukumbuka ambacho
unahisi hakikuwa cha kawaida
katika safari ile ya rais? Mathew
akauliza.Kwa kutumia mkono
wake wa kushoto mzee Zubery
akafuta mdomo wake kwa
kitambaa na kusema
“Niliwapokea rais Anorld na
ujumbe wake, wakahudhuria
kikao ambacho na mimi
nilihudhuria na baadae jioni
akaondoka salama.Aliondoka
salama na kuelekea Jamaica lakini
ndege yake ikaanguka
baharini.Nasikitika sana.Watu wa
Jamaika wamempoteza rais mzuri
sana.Alikuwa na mahusiano
mazuri na Tanzania” akasema mzee Zubery .Mathew na Theresa
wakatazamana.
“Hiyo ndiyo hali yake.Huwa
anapoteza kumbukumbu na
kuongea mambo ya ajabu ajabu
lakini kuna wakati kumbukumbu
zake hukaa sawa na huongea
mambo mengi ya
maana.Anafahamu mambo mengi
sana.Anawafahamu viongozi wengi
wa Afrika waliowahi kupita”
akasema Zaina
“Kwani ninyi mmetoka nchi
gani? Zambia?Mzee Zubery
akauliza
“Ndgu zangu tayari mambo
yameharibika hapa na hamtaweza
kupata kile
mnachokihitaji.Nawashauri niachieni mawasiliano yenu na
baadae akikaa sawa nitamuuliza
kile mlichomuuliza na akiniambia
chochote nitakujulisheni.”
Akasema Zaina.
“Nadhani hilo ndilo la
msingi”akasema Mathew na
kubadilishana namba zake za simu
na Zaina kisha wakaondoka
“Nashukuru hatujapata
chochote toka kwa huyu mzee na
ninaomba aendelee kupoteza
kumbukumbu hivyo hivyo. Sitaki
kabisa jambo hili lifanikiwe kwani
litatuweka mimi na dada katika
hatari kubwa” akawaza Theresa
“Nini kinafuata baada ya
hapa? Tumeshindwa kupata chochote toka kwa yule mzee”
akasema Theresa
“Bado nafikiria kitu cha
kufanya .Nilimtegemea sana Alhaji
Zubery lakini naye ndiyo hivyo
tena kumbukumbu zinakuja na
kupotea” akasema Mathew na
simu ya Theresa ikaita.Akakunja
sura baada ya kutazama
mpigaji.Simu ikaita na kukatika
bila kuipokea.
“Mbona hupokei? Akauliza
Mathew
“I don’t want to talk to him”
akasema Theresa .Mathew
akatabasamu na kuuliza
“Ni mpenzi wako?
“Hapana ni mpenzi wa dada” “Kwa nini basi hupokei simu
yake kama ni shemeji yako
anakupigia? Pokea umsikilize”
“Sitaki kuingilia mambo
yao.Wamekwisha achana na dada
Vivian hataki tena kuendelea na
mahusiano naye kwa hiyo
ananisumbua mimi kutaka
nimsaidie warudiane”
“Nini sababu ya kutengena
kwao?
“Wanajua wenyewe.Dada
hajawahi kunieleza”akasema
Theresa
“Mambo ya mahusiano ni
magumu na yanahitaji uvumilivu
wa hali ya juu.Kama bado
hujaingia katika ndoa nakushauri
umuombe sana Mungu akujalie umpate mwanaume sahihi
kwako.Endapo hautakuwa na
uhakika na huyo mpenzi uliyenaye
usiingie katika ndoa” akasema
Mathew
“Nalielewa hilo Mathew na
niko makini sana .Niliamua
kuvunja mahusiano na mpenzi
wangu niliyekuwa naye
nilipogundua kwamba mimi na
yeye htuwezi kwenda sawa”
“Good.Ulifanya vizuri
sana.Usilazimishe mapenzi.Ni heri
uwe mwenyewe na amani ya moyo
kuliko kuwa katika mapenzi ya
maigizo.Nimekuwa katika ndoa
ninayafahamu vyema mambo haya
na laiti nikipata nafasi nitafungua
darasa huko mbeleni la kuwafunisha watu maisha ya ndoa
yalivyo”
“Oh kumbe umeshaoa?
Akauliza Theresa huku
akitabasamu
“Nilioa lakini kwa sasa
tumekwisha tengana .Maisha ya
ndoa naweza kusema ni mazuri
lakini si rahisi.Si maisha ya
kukimbilia.Muombe sana Mungu
wako akujalie umpate mchumba
mwema.Ukipata pasua kichwa
atakupasua hadi moyo”akasema
Mathew
“Unaonekana umepitia
mambo mengi katika ndoa
yako.Tukipata nafasi utanieleza
mikasa uliyokutana nayo katika
ndoa .Unao………………”Theresa akanyamza baada ya simu ya
Mathew kuita.Akaitoa mfukoni
akatazama mpigaji alikuwa ni
Zaina
‘Zaina anapiga” akasema
Mathew na kuipokea
“Hallow Zaina” akasema
“Mathew kama nilivyokueleza
kwamba kumbu kumbu za baba
huwa zinakuja na
kupotea.Mlipotoka tu kumbu
kumbu zake zimekaa sawa na
akasema niwaite ili ajue
mlichokuwa mnakitaka
nikamwambia mmekwisha ondoka
hivyo nikamuuliza lile swali
ulilokuwa umemuuliza”
“Enhee ! amesemaje? “Amesema kwamba baada ya
rais kumaliza kikao chake
alielekea uwanja wa ndege na
kuna kitu anasema kilitokea hapo
uwanja wa ndege ambacho
hakikuwa cha kawaida.Anasema
kuna waandishi nane wa habari
waliokuwa nchini Misri ila
hakumbuki walitokea nchi gani
lakini walikuwa wanaelekea
Tanzania waliomba nafasi katika
ndege ya rais na wakaruhusiwa
kupanda.Anasema kwamba hiki
alikiona ni kitu cha ajabu sana
kwake.Anasema kwamba yeye
ndiye aliyewaombea lifti kwa rais
naye akakubali.Kingine
anachokikumbuka ambacho
anasema kimemsikitisha sana ni kwamba katika msafara ule wa
rais kulikuwa na binti mzuri
aliyekwenda Misri
kutembea.Amemsahau jina lake ila
anakumbuka binti huyo alikuwa
mcheshi sana .Alipewa maelekezo
kwamba amtafutie mtu wa
kumtembeza jijini Cairo ili ajifunze
mambo mbalimbali ya kihistoria
yaliyomo katika jiji
hilo.Anasikitika kamba binti yule
naye alifariki katika ajali ile.Hayo
ndiyo aliyoweza kuyakumbuka
kwa sasa.Kama kuna kingine
atakachoweza kukumbuka tena
nitakujulisha” akasema Zaina
“Ahsante sana Zaina kwa
taarifa hiyo.Kama kuna chochote
kingine atakueleza naomba unijuze tafadhali” akasema
Mathew na kuagana na Zaina
Ahsante sana Zaina kwa
taarifa hiyo.Kama kuna chochote
kingine atakueleza naomba unijuze tafadhali” akasema
Mathew na kuagana na Zaina
“Anasemaje Zaina? Theresa
akauliza
“Mzee Zubery kuna mambo
amekumbuka.Anadai kwamba
baada ya rais Anorld kumaliza
kikao jijini Cairo na akiwa
anajiandaa kurejea Tanzania
kulitokea waandishi wa habari
walioomba lifti katika ndege ya
rais na yeye ndiye aliyewaombea
kwa rais wakakubaliwa .Anasema
kwamba hiki hakikuwa kitu cha
kawaida kwake japokuwa yeye
ndiye aliyewaombea lifti hiyo.Vile
vile anakumbuka kwamba katika
msafara wa rais kulikuwa na binti
mwanafunzi aliyekwenda nchini Misri kujifunza mambo
mbalimbali,naye alifariki katika
ajali hiyo”
Uso wa Theresa ulionyesha
wasi wasi na mstuko mkubwa
akajitahidi ili Mathew asigundue
“Mathew una uhakika na yule
mzee?Kwa namna alivyo sina
hakika kama tunapaswa
kumuamini.Akili yake haipo sawa”
akasema Theresa
“Lakini Zaina ndiye
anayemfahamu vyema baba yake
na ana uhakika kwamba hizi
kumbu kumbu ni
sahihi.Asingeweza kunipa taarifa
ambazo anajua kabisa kwamba si
za kweli” akasema Mathew “Yule mzee kweli kuna
nyakati kumbukumbu zake
zinakaa sawa.Ni kweli
alichokisema.Kulikuwa na
waandishi nane wa habari wakati
tunarejea Dar es salaam.Binti
mdogo aliyemsema nilikuwa
mimi.Nimweleze Mathew ukweli?
Akawaza
“Theresa kuna jambo nataka
ulifanye” akasema Mathew na
kumtoa Theresa mawazoni
“Sema Mathew unahitaji nini?
“Nataka kufahamnu wakati
rais Anorld anaondoka kuelekea
Cairo Misri alikuwa ameongozana
na akina nani? Kulikuwa na watu
wangapi katika msafara wake? Naamini kumbu kumbu hizi zipo
nisaidie kuzipata”
“Sawa Mathew ngoja
nilishughulikie hilo” akasema
Theresa na kwa kuwa gari
zilikuwa zinakwenda taratibu
kutokana na foleni ndefu
akachukua simu na kuzungumza
na mtu fulani akaomba
aangaliziwe idadi ya watu
walioorodheshwa wakati rais
Anorld alipokwenda Cairo Misri.
Baada ya dakika tano simu ya
Theresa ikaita,akazungumza kwa
dakika mbili halafu akamgeukia
Mathew
“Wakati anaelekea Cairo Misri
rais Anorld alikuwa ameongozana
na mawaziri wawili,wasaidizi ,marubani,wahudumu na
walinzi.Jumla ya watu ndegeni
walikuwa kumi na nane”
“Good.Kwa hiyo kama
kulikuwa na jumla ya watu kumi
na nane walioondoka na ndege ya
rais na ukijumlisha na wale
waandishi nane wa habari jumla ya
watu waliokuwemo ndegeni
wakati wa kurejea nyumbani ni
ishirini na sita.Kanali Sebastian
Matope alinusurika hivyo jumla ya
maiti ambazo zinapaswa kuwa
zilipatikana ni ishirini na tano.Ili
kupata uhakika zaidi kama taarifa
hii ya mzee Zubery ni sahihi
nataka kujua ni maiti ngapi
zilipatikana baada ya ndege
kuanguka? Fuatilia taarifa hiyo nahitaji kujua”akasema Mathew na
Theresa akachukua tena simu
akazungumza na mtu na kusubiri
na baada ya dakika tatu akapigiwa
simu akaongea kwa muda halafu
akamgeukia Mathew
“Nimepewa taarifa kwamba
maiti zilizopatikana katika ajali ya
ndege ya rais Anorld ni kumi na
saba”
“Kumi na saba?
“Ndiyo.Kumi na saba pekee”
“Inawezekanaje kuwe na maiti
kumi na saba wakati ndani ya
ndege walikuwepo watu ishirini na
sita na aliyesalimika ni kanali
Sebastian pekee? Kulipaswa kuwa
na jumla ya maiti ishirini na tano” “Hiyo ndiyo taarifa iliyopo
Mathew kwamba maiti zilipatikana
kumi na saba tu”
“Inashangaza sana.Kwa hiyo
watu tisa hawajulikani walipo”
akasema mathew
“Mathew nilikueleza toka
awali kwamba usimuamini sana
yule mzee kwani ana matatizo
katika kumbu kumbu zake.Kichwa
chake hakiko sawa.Hakukuwa na
watu zaidi ya wale walio
orodheshwa.Kama kungekuwa na
watu zaidi basi maiti zao
zingepatikana lakini ukipiga
hesabu inaonyesha wazi kwamba
hakukuwa na watu wa ziada.Ndege
iliondoka na watu kumi na nane na
baada ya ajali kutokea zikapatikana mati kumi na saba
,na baba pekee ndiye
aliyesalimikana hivyo hesabu
kuwa watu kumi nane.Usiumize
kichwa kwa taarifa za yule
mzee.Hao watu nane anaodai
walikuwemo ndegeni wako wapi?
Akauliza Theresa.Mathew akabaki
kimya
“Nimestuka sana na hadi
mikono inanitetemeka kusikia
kwamba maiti zilizo patikana ni
kumi na saba.Mimi sikuwahi
kuingizwa katika hesabu za watu
waliokuwemo ndani ya ndege na
wala sikuorodheshwa sehemu
yoyote kwa hiyo baba ndiye pekee
anayejulikana kuwa ndiye
aliyenusurika .Watu nane wako wapi? Ni akina nani?Walitoka vipi
ndani ya ndege? Ninavyokumbuka
mimi na baba ndio tulikuwa wa
kwanza kutoka ndegeni.Kuna
wengine walifuata baada ya sisi?
Akajiuliza Theresa
“Theresa” akaita Mathew
“Unasemaje Mathew? Akauliza
Theresa
“Kama unavyoona suala hili
linavyozidi kupanuka ,kuna kitu
kimejificha na lazima
tukijue.Japokuwa mzee Zubery
kumbu kumhu zake kuna wakati
haziko sawa lakini hatuwezi
kumpuuza.Kuna kitu kinanituma
nimuamini.Hata hivyo kuna jambo
lingine nataka unisaidie
kulifahamu” “Sema Mathew unahitaji nini?
“Nataka nipate majina ya watu
waliofariki katika ndege
hiyo.Unaweza kuyapata?
“Ndiyo Mathew.Pale ikulu
tuna kumbu kumbu zote” akasema
Theresa na kuchukua simu
akapiga na kuomba apatiwe
majina ya watu wote waliofariki
katika ajali ile ya ndege ya rais.
Waliwasili nyumbani kwa
Theresa ambako ndiko waliweka
ofisi yao.Theresa akapigiwa simu
akataarifiwa kwamba majina yote
ya watu waliofariki katika ajali ya
ndege ya rais yametumwa katika
akaunti yake ya barua pepe.Mara
moja akaifungua na kumpatia
Mathew majina yale,akayapitia na kutoa kitambaa akafuta uso wake
ulioonekana kuloa jasho.
“Theresa mimi nakwenda
kupumzisha kwanza kichwa
nilitafakari hili suala kwa undani
zaidi kwani ni suala gumu na
linalohitaji utulivu mkubwa.Ni
muda mrefu kidogo umepita
sijakabiliana na suala gumu kama
hili.Nitakujulisha endapo kuna
chochote nitahitaji” akasema
Mathew
“Vipi kuhusu ile taarifa ya
polisi ya maelezo ya baba?Si
uliomba kuipata nayo?
“Ndiyo ikipatikana utanitumia
katika barua pepe yangu. Rais
kama atakupigia akikuuliza
tulikofikia usimueleze chochote kwani bado ni mapesa sana kumpa
taarifa yoyote” akasema Mathew
huku akiinuka ,Theresa
akamsindikiza hadi katika gari
lake akaondoka
“Nashukuru sana Mathew
ameanza kukata tamaa mapema
kulifuatilia suala hili.Naomba
kuendelee kuwa na mkwamo hivi
hivi ili asifanikiwe kugundua
chochote.Naamini watu wale bado
hawajalala,wako macho hivyo
muda wowote wakigundua
kwamba wanachunguzwa basi
wataibuka tena na maisha yetu
yatakuwa mashakani.Nilinusurika
kifo ndani ya ndege baba
akaniokoa,nikanusurika tena kifo
kwa mara ya pili na mama akaniokoa.Safari ya tatu sijui nani
ataniokoa.Sitaki kabisa kuingia
katika mikonona wale jamaa
tena.Watu wale si watu wa
kawaida.Ni makatili sana na nina
aamini mtandao huu
unawahusisha hata watu waliomo
serikalini kwani baba aliuawa na
watu waliovaa mavazi ya askari
polisi na hata magari yao yalikuwa
ya polisi .Na hata baada ya kuuawa
nasikia wao polisi ndio walichukua
miili na kuipeleka hospitali kwa
madai kwamba wameuawa na
watu wasiojulikana.Nina wasi wasi
hawa jamaa bado wanaendelea
kumchunguza dada kwa siri
wakijaribu kufahamu kama kuna
chochote anakifahamu kuhusu Football na amekuwa salama hadi
sasa kwa kuwa hajui chochote na
nitakapo thubutu kufumbua tu
mdomo wangu kumueleza
wanaweza wakamuua” akawaza
Theresa baada ya Mathew
kuondoka
“Najiuliza bado,hii football ina
siri gani hadi damu nyingi namna
ile imwagike bila huruma? Halafu
orodha inaonyesha kwamba wale
waliokufa wote ni watanzania
hakukuwa na mgeni hata
mmoja.Hii inaonyesha kwamba
wale jamaa waliojiita waandishi
wa habari na baadae wakageuka
magaidi na kuiteka ndege ya rais
walipona na hakuna hata mmoja
aliyepoteza maisha.Inaonekana wale jamaa walichokuwa
wanakitafuta ni football pekee na
ndiyo maana nahisi baada ya baba
kuruka na kuondoka waliona
hakuna umuhimu wa kuendelea
kubaki ndegeni kwa kuwa
walichokuwa wanakitafuta
hakikuwepo kwa hiyo wakatoka
ndegeni na kuiacha
ikaanguka.Najiuliza je
waliochukua kisanduku cheusi cha
kuhifadhi kumbu kumbu za
mwenendo wa ndege ni wale
jamaa au ni akina nani?Dah !
mambo haya ni magumu sana na
ndiyo maana sitaki
yaamshwe.Kuna mambo mengi
hapa yamejificha” akaendelea
kuwaza Theresa Kwa upande wa Mathew bado
kichwa chake kilikuwa na mawazo
mengi sana baada ya kuondoka
kwa Theresa
“Mwanzo umeanza kwa
mgumu na bado naona giza
nene.Japokuwa bado nipo gizani
lakini kuna hatua niliyopiga
ambayo inanifanya niamini
kwamba ajali ile ilikuwa na
walakini.Haikuwa ajali ya
kawaida.Naamini hivyo baada ya
kutoweka kwa kisanduku cha
kuhifadhi mwenendo wa ndege na
waliofanya hivyo hawakutaka
sababu ya ndege ile kuanguka
kujulikana.They’re very smart.Huu
lazima ni mtandao mrefu wa watu”
akawaza mambo mengi hadi alipofika nyumbani kwake na
kwenda moja kwa moja chumbani
akaketi kitandani
“Alhaj Zubery amemweleza
Zaina kwamba kuna watu wanane
waliomba lift katika ndege ya
rais.Hizi ni taarifa za kweli? Hali ya
mzee yule inatia shaka
kumuamini.Halafu akasema
kwamba kulikuwa pia na binti
mdogo ndegeni.Mbona sikuona
jina lake katika orodha ya watu
waliokuwemo ndegeni? Orodha ile
inaonyesha wafanyakazi wote
waliokuwemo ndegeni ni wa ikulu
pamoja na wahudumu wa ndege na
hakukuwa na jina la binti
mdogo.Naingiwa na wasi wasi
kidogo kuhusiana na kumuamini yule mzee yawezekana hakuna
ukweli wowote katika hizi taarifa”
akawaza Mathew na kuwasha
kompyuta yake
“Lakini Zaina ndiye
anayemfahamu baba yake vizuri
na anamfahamu ni wakati upi
kumbu kumbu zake huwa sawa na
wakati gani zinapotea .Mpaka
aamue kunipa taarifa hizi ina
maana ana uhakika baba yake
alikuwa sawa sawa.Niamini lipi?
Akaendelea kuwaza Mathew
“Itanilazimu kurejea tena kwa
alhaj Zubery.Natakiwa
kuthibitisha taarifa hizi.Japokuwa
ana matatizo katika kumbu kumbu
zake lakini kuna kitu kinaniambia
kwamba yule mzee anaweza kuwa na msaada kwangu.Lazima nirejee
tena kwake” akawaza na kuchukua
simu akalitafuta jina la mama
Anna na kumpigia
“Hallow” ikasema sauti ya
upande wa pili
“Hallow mnaendeleaje?
Anaendeleaje Anna? Mathew
akauliza
“Anna anaendelea vyema”
“Umekwisha mchukulia
zawadi niliyokuomba?akauliza
Mathew
“Nitamchukulia usij……………..”
Ghafla katika spika za simu
ikasikika sauti ya mwanaume
akiongea kwa ukali akimuuliza
Peniela
“Unazungumza na ani? “Ni baba yake Anna Maria”
akajibuPeniela
“Nipe simu,nataka
kuzungumza naye” akasema jamaa
yule kwa ukali
“Hapana achana naye hana
tatizo anataka kujua maendeleo ya
mwanae” akajibu Peniela na
wakasikika wakinyang’anyana
simu halafu sauti ya kume
ikasikika
“Hallow ndugu.Tafadhali
nakuomba uwe na heshima.Huyu
si mkeo tena .Umekwisha achana
naye kwa hiyo jitahidi kuheshimu
maisha yetu.Nakuomba usimpigie
tena simu .Ukitaka kujua
maendeleo ya mwanao mpigie
mtumishi wa ndani anayemuangalia.Unaingilia
faragha za watu mimi na mke
wangu kwa sasa tunafanya
mapenzi.Natumai utalizingatia
hilo” akasema yule jamaa na
kukata simu.Mathew hakutaka
kukasirika kwa jambo lile
akatabasamu na kutikisa kichwa
akajilaza kitandani
“Sitaki malumbano na huyu
jamaa ambaye anaonekana
hajiamini.Anasumbuka bure mimi
na Peniela tumekwisha achana na
hakuna mategemeo ya kurudiana
tena.Kilichobaki kati yetu ni mtoto
tuliyezaa pamoja.Siwezi
kumlaumu sana kwani ni wivu
mkali alionao kwa mke wake
lakini hata ampe nini Peniela kwake nitabaki ni mwanaume wa
pekee kabisa .Sitakiwi kuwaza
sana hili jambo ngoja nielekeze
akili yangu katika kazi ngumu
iliyoko mbele yangu” Akawaza
Mathew Imekwisha timu saa moja na
nusu za jioni wakati rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr Vivian Matope
alipofahamishwa kwamba rais wa
Korea kaskazini Kim Yun Hu
alikuwa tayari katika laini ya simu
kwa ajili ya mazungumzo. Rais
akaelekea katika chumba cha mikutano ya moja kwa moja
kilichokuwa na runinga tatu
kubwa akabonyeza runinga namba
moja na rais Kim Yun Hu
akaonekana runingani.
“Mheshimiwa rais Kim,habari
yako? Akaanzisha mazungumzo Dr
Vivian
“Habari nzuri kabisa Dr
Vivian.Ni heshima kubwa kwangu
kuzungumza nawe mida hii
kuhusiana na masuala kadhaa
muhimu kwa mustakabali wa nchi
zetu mbili.Kwanza kabla ya yote
napenda kukushukuru sana kwa
kumpokea mjumbe wangu
niliyemtuma kwako na
ukamsikiliza.Vile vile napenda
nichukue nafasi hii kukupongeza sana kwa msimamo wako
usioyumba na kwa maamuzi
makubwa ya kutaka kuanzishwa
kwa mashirikiano ya kibiashara
baina ya nchi yako na Korea
kaskazini.Nilifurahi sana
niliposikia kwamba umeagiza
kuanzishwa kwa mchakato wa
kuanzishwa kwa mashirikiano
baina ya nchi zetu.Hii ni hatua
kubwa kwa Tanzania katika
maendeleo yake ya
kiuchumi.Nafahamu maamuzi haya
uliyoyafanya yatailetea Tanzania
matatizo makubwa na hadi hivi
sasa kelele na vitisho vingi
vimetolewa na vinaendelea
kutolewa na mataifa
makubwa.Silaha yako kubwa ni msimamo wako .Simama imara na
usiyumbe.Watakutisha sana
kuhusiana na vikwavo vya
kiuchumi lakini nakuomba
usiwasikilize wewe endelea
mbele.Ukitaka nchi yako ipige
hatua usigeuke nyuma angalia
mbele.Nchi hizi tajiri hazipenzi
nchi kama Tanzania ipige hatua
kimaendeleo kwani kuna mambo
mengi wanafaidika na hali ya hivi
sasa ya Tanzania.Hivyo endelea na
msimamo wako huo huo kwani
mpaka hivi sasa wewe tayari ni
mshindi.Umewatoa jasho na ndiyo
maana toka ulipotoa hotuba yako
kule New york wanashindwa hata
kulala.Kingine cha muhimu
unapaswa kuzidisha ulinzi mara dufu.Hawa jamaa wanaweza
wakapanga mipango ya kukuua
hata kwa kuwatumia watu wako
wa karibu.Usimuamini mtu yeyote
kuanzia sasa.Umeingia katika vita
ya uchumi ambayo ni ngumu sana
kwani unapigana na mataifa
makubwa yenye nguvu kubwa
kiuchumi na hata kijeshi.Binafsi
ninakuahidi ulinzi dhidi ya taifa
lolote lile litakalotishia amani ya
Tanzania.
Kama
yatafanikiwa,mashirikiano yetu
yatakuwa ni yenye faida kwa
pande zote mbili.Kwa sasa Korea
Kaskazini tuko katika mageuzi
makubwa ya kiuchumi.Tunataka
kuwa taifa kubwa lenye nguvu kijeshi na kiuchumi pia na
mahasimu wetu hawapendezwi na
hilo.Tunawekeza sana katika
viwanda na uchumi wetu kwa sasa
unakua kwa kasi kubwa na kuzidi
kuwapa hofu mataifa mahasimu
wetu na ndiyo maana vikwazo
vinaongezeka kila wakati lakini
sisi hatujali tunasonga
mbele.Tumeimarisha sana
biashara na nchi za bara la Asia na
sasa tunataka kupanua wigo wa
biashara na kuanza kushirikiana
na nchi za Afrika.Tuna viwanda
vingi na tunatengeneza nguvo,vifaa
vya elektroniki,magari,ujenzi na
vinginevyo.Tunahitaji masoko
mapya ya bidhaa zetu na vile vile
tukaribisha bidhaa nyingine toka kwa nchi washirika wetu wa
kibiashara pia tunauhitaji wa
malighafi kama vile pamba kwa
ajili ya viwanda vyetu vya
nguo,tunahitaji chuma na mafuta
safi.Tunahitaji pia kwa kiasi
kikubwa madini ya Urani kwa ajili
ya kuboresha vinu vyetu vya
nyuklia na kutengeneza umeme wa
uhakika kwa viwanda vyetu.Kwa
hiyo basi mashirikiano kati ya
Tanzania na Korea Kaskazini
yatakuwa na faida kubwa sana kwa
nchi zote mbili.Wawekezaji wa
kutoka Korea Kaskazini
wanapenda kuja Tanzania
kuwekeza katika viwanda vya
nguo,kusindika mazao ya kilimo
na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima na hivyo kumpatia
mkulima wa Tanzania tija katika
kilimo chake na sekta ya kilimo
kwa ujumla ambayo ndiyo
inayoajiri watu wengi
itapanuka.Tunataka kuwekeza vile
vile katika viwanda vya
kutengeneza vifaa vya
kielektroniki kama vile simu
n.k.Tunataka vile vile kuwekeza
katika mafuta.Tunahitaji sana
kupata mafuta safi na kama
haitoshi tunataka kuwekeza katika
sekta ya madini kwa kujenga
kiwanda cha kukata na kuongeza
thamani ya madini ya vito na hata
kuchenjua mchanga wa madini
hapo hapo nchini Tanzania kuliko
uwekezaji unaofanywa sasa hivi na makampuni ya kimarekani na
ulaya ambayo huchota madini na
kuyapeleka kwao kuyaongeza
thamani na kupata faida kubwa na
kuzidi kuiacha Tanzania kuwa
masikini.Mwisho tunataka kujenga
mgodi mkubwa wa madini ya
Urani ambayo tutayanunua kwa
bei nzuri na kuifaidisha sana
Tanzania.Madini haya
hatutayatumia kwa ajili ya ajili ya
kutengeneza silaha za nyuklia
kama mataifa makubwa
wanavyodai bali tunayatumia kwa
ajili ya kuzalisha nishati ya
umeme.
Mheshimiwa rais,mpaka hapo
unaweza kuona kwamba
uwekezaji toka Korea kaskazini utakuwa na faida kubwa kwa
Tanzania kwani sisi lengo letu ni
kusaidia uchumi wa Tanzania ukue
tofauti na mataifa mengine
yanayowekeza na kuchuma mali za
watanzania na kwenda
kuyafaidisha mataifa
yao.Makampuni makubwa ya
Marekani na Ulaya wanachimba
madini,mnafaidikaje?Hamjui hata
kiwango cha madini
kinachochimbwa na hampati pato
stahili.Sisi watanzania ni kama
ndugu zetu kwani wamesimama
pamoja nasi hata baada ya kupewa
vitisho vya kuwekewa vikwazo
hivyo tunahitajika kufaya
uwekezaji wenye faida kubwa na
kuipaisha Tanzania kiuchumi.Tunataka kubadili aina
ya uwekezaji na tupate faida wote
sawa sawa na ikiwezekana
Tanzania ipate faida.Uwekezaji
wetu utaongeza na kukuza pato la
mwananchi mmoja mmoja
,utaongeza mapato ya serikali na
hivyo uchumi utakua.Kama hiyo
haitoshi tutashiriki pia katika
miradi mingi ya maendeleo kama
kujenga
mabarabara,mashule,mahospitali
n.k. Kwa kuwa tutakuwa na
uwekezaji mkubwa nchini kwako
tuhakikisha kuna kuwa na
mashirikiano makubwa ya
kijeshi.Tutaipatia Tanzania
msaada wa silaha za kisasa kwa
ajili ya kujilinda na maadui,tutatoa mafunzo kwa jeshi la Tanzania na
litakuwa jeshi la kuogopwa Afrika
kutokana na uwezo na zana kali za
kisasa.Tutajenga pia kiwanda cha
silaha na Tanzania itajitosheleza
kwa silaha za kila aina.Yeyote
atakayeigusa Tanzania atakuwa
ameigusa pia Korea Kaskazni na
hatabaki salama kwani
tutamuadhibu vikali” akasema rais
Kim.Dr Vivian aliyekuwa kimya
akisikiliza akasema
“Ahsante kwa maelezo yako
marefu.Nimevutiwa sana na
mkakati huo wa nchi yako kwa
Tanzania. Sisi kama nchi bado ni
masikini na tunajitahidi sana
tuweze kujiondoa katika umasikini
na kufika nchi ya kipato cha kati.Tunazo rasilimali nyingi sana
hapa nchini tuna madini ya kila
aina,vivutio vya kitalii,ardhi
nzuri,bahari,maziwa na mito lakini
pamoja na kuwa na rasimali hizo
zote bado hatujafaidika na uchumi
wetu bado uko
chini.Tumekaribisha wawekezaji
lakini bado hatufaidiki na mali
zetu kwani kinachofanyika ni wizi
mtupu.Wanachota rasilimali zetu
na kutuachia mashimo.Tumeamua
kubadilika na kubadili sera zetu za
uwekezaji.Tunataka rasilimali zetu
zianze kutunufaisha na kila
mtanzania aone faida ya rasilimali
hizi kuwepo nchini kwao.Msimamo
wangu kuhusiana na rasilimali
zetu hautabadilika kwani wakubwa hawa wametunyonya
vya kutosha na sasa
imetosha.Tunataka wawekezaji
watakaotunufaisha na nina imani
Korea Kaskazini watatufaa
sana.Nitawaelekeza wasaidizi
wangu ili mambo haya yaanze
kufanyiwa kazi haraka hakuna
muda wa kupoteza.Nakuhakikishia
mheshimiwa rais kwamba
uwekezaji wa kutoka Korea
Kaskazini unakaribishwa sana na
hakuna kizingiti chochote.Hata
hivyo kuna jambo nataka
kukuomba”
“Omba mheshimiwa rais”
“Pamoja na mambo yote
mazuri ambayo umeyaongea
mazuri yatakayofanywa na Korea Kaskazini,Tanzania pia tunayo
sera ya viwanda na muitikio ni
mzuri kwani tumepata wawezekaji
wengi wa ndani na nje ya
nchi.Tatizo letu mpaka sasa bado
hatuna umeme wa uhakika sana
kuendesha viwanda vingi na hivyo
kuwafanya wawekezaji wengine
wasite kuja kuwekeza.Kwa kuwa
tunayo madini ya Urani hapa
nchini kwetu tunaomba tusaidiwe
kujenga kinu cha nyuklia hapa
nchini kwa ajili ya kuzalisha
umeme wa uhakika na hivyo
kuchochea uchumi”
“Dr Vivian suala hili
linawezekana kabisa na ni jambo
la msingi mno umeliongea.Mkiwa
na kinu cha nyuklia mtakuwa na uhakika wa umeme wa
kutosha.Naomba nilichukue jambo
hili na nilipeleke kwa wenzangu
tukalijadili na naomba nikuahidi
kwamba tutajenga kinu cha
nyuklia hapo Tanzania japokuwa
jambo hili litazidisha msuguano na
mataifa makubwa kwani ni jambo
ambalo hawalipendi”
“Nalifahamu hilo Kim na niko
tayari kusimama nao.Ili
kufanikiwa dhidi ya mataifa haya
makubwa lazima ujifunze kuwa
kiburi”
“Uko sahihi Dr Vivian.Na mimi
kuna jambo nataka
nikuombe”akasema Kim
Nalifahamu hilo Kim na niko
tayari kusimama nao.Ili
kufanikiwa dhidi ya mataifa haya
makubwa lazima ujifunze kuwa
kiburi”
“Uko sahihi Dr Vivian.Na mimi
kuna jambo nataka
nikuombe”akasema Kim
“Karibu” “Kuna makampuni mengi ya
kimarekani yamewekeza Tanzania
.Kama ujuavyo sisi na Marekani ni
mahasimu hivyo hatutaweza
kufanya kazi
pamoja.Ninachokuomba
tukishakubaliana kuhusiana na
biashara na uwekezaji,sitisha
shughuli zote zinazofanywa na
makampuni ya kimarekani na
washirika wake kama
Ufaransa,Ujerumani na uingereza
.Nataka uvunje nayo mikataba na
uyafurushe nchini mwako.Sisi
tutalipa malipo yote ya fidia kama
yatakuwepo kwani naamini lazima
watakwenda kuwashitaki katika
mahakama zao za kimataifa kwa
kuvunja nao mikataba.Usiwe na hofu Dr Vivian hii ni vita ya
kiuchumi kwa hiyo misuko suko
lazima iwepo lakini kamwe
usigeuke nyuma.Sisi tuko nyuma
yako na tutakulinda” akasema rais
Kim
Mazungumzo kati ya Dr Vivian
na Kim yalichukua takribani saa
mbili.Walizungumza mambo
mengi kuhusiana na mipango yao
ya mashirikiano kisha wakaagana
.Rais Kim aliahidi kutuma ujumbe
wa watu nane wakiongozwa na
mawaziri watatu kuja Tanzania ili
kuanza mazungumzo na serikali ya
Tanzania haraka iwezekanavyo
Hii ilikuwa ni jioni ya faraja
sana kwa Dr Vivian.Mazungumzo
kati yake na rais Kim yalifanya uso wake upambwe na tabasamu
kubwa.
“Hii vita itakuwa kubwa sana
.Nitapata misukosuko toka mataifa
makubwa na tajiri ambayo
yamekuwa yakiendeleza unyonyaji
wa rasilimali zetu lakini sintorudi
nyuma.Nimekwisha amua kuingiza
nchi vitani lazima tupambane na
lazima tushinde.Mali ni zetu na
haiwezekani tuwe ombaomba”
akawaza Dr Vivian
*****************
Saa mbili kasoro dakika kumi
na nne za usiku,Mathew alibisha
hodi nyumbani kwa Alhaj
Zubery.Alikaribishwa na mtumishi wa ndani na sebuleni
akamkuta Zaina akiwa
amejipumzisha akitazama runinga
“Mathew karibu tena.Mbona
usiku huu? Zaina akauliza
“Samahani kwa kuwavamieni
usiku huu bila taarifa” akasema
Mathew.
“Usihofu karibu sana
unakaribishwa muda wowote”
Akasema Zaina
“Nashukuru
Zaina.Nimelazimika kurejea tena
kufuatia ile taarifa uliyonipa
mchana.Kuna mambo ambayo
nataka kuyafahamu zaidi toka kwa
mzee kama atakuwa katika hali
nzuri” akasema Mathew “Mathew sijui kama
nitakukwaza lakini ningependa
kufahamu zaidi ni kitu gani hasa
mnachokihitaji toka kwa mzee ili
nione namna ya kusaidia hata
kumuuliza?Nieleze ukweli usihofu”
akasema Zaina
“Kikubwa tunachokichunguza
hapa ni chanzo cha ajali ya ndege
ya rais Anorld.Mpaka leo hakuna
taarifa yoyote iliyopatikana
kuhusina na chanzo cha ajali ile
hivyo tumeanza tena
uchunguzi.Kuna taarifa
zinakanganya.Ndege ilipoondoka
hapa Dar es salaam ilikuwa na
watu kumi na nane na taarifa
uliyonipa mchana toka kwa mze
Zubery inasema kwamba wakati wa kurudi Tanzania kuna
waandishi nane wa habari
waliongezeka wakielekea Dar es
salaam hivyo jumla yao ikawa
watu ishirini na sita.Ilipoanguka
watu wote walikufa isipokuwa mtu
mmoja tu kwa hiyo maiti zilipaswa
kuwa ishirini na tano lakini taarifa
inaonyesha kwamba kulikuwa na
maiti kumi na saba pekee.Maiti
nane hazionekani.Majina ya watu
waliofariki yanaonyesha kwamba
wote ni watanzania na hakuna
mgeni hata mmoja.Taarifa hizi
mbili zinakinzana na ndiyo maana
nimekuja tena kutaka kuonana na
mzee ili kupata uhakika kwamba
taarifa zile alizokupa ni sahihi”
akasema Mathew “Mathew ninamfahamu baba
yangu vizuri .Nafahamu muda gani
yuko vizuri na na muda gani
hayuko sawa.Taarifa ile niliyokupa
alinipa wakati kumbukumbu zake
ziko sawa sawa na nisingeweza
kukupa kitu ambacho najua
hakiko sahihi.Hata hivyo itabidi
kumuhoji tena pengine anaweza
akakumbuka kitu chochote.Ngoja
nikamlete” akasema Zaina na
kuinuka akaelekea chumbani kwa
mzee Zubery baada ya dakika tatu
akarejea akiwa amemshika mkono
baba yake na kumketisha sofani
“Kijana umerudi tena”
akasema mzee Zubery
“Nimerudi tena mzee.Habari
za usiku huu? “Nzuri.Karibu sana.Zaina
amesema kuna mambo bado
unahitaji kuyafahamu toka
kwangu” akasema mzee Zubery
“Ndiyo mzee.Nimelazimika
kuja tena kuomba msaada
wako.Ulisema kwamba kulikuwa
na waandishi nane wa habari
waliomba lifti katika ndege ya rais
wakati anarejea Dar es
salaam.Taarifa zinaonyesha
ilipoondoka Dar es salaam ndege
ilikuwa na watu kumi na nane na
wakati wa kurudi ukijumlisha na
watu hao nane waliomba lifti jumla
kukawa na watu ishirini na sita
ndegeni.Ni mtu mmoja tu aliyetoka
salama ndani ya ndege hiyo
ambaye ni kanali Sebastian matope kwa hiyo ndani ya ndege
kulipaswa kuwa na watu ishirini
na tano.Kinachoshangaza ni
kwamba maiti zilizokutwa ndani
ya ndege ni maiti kumi na saba
pekee na zote ni za watanzania
,hakuna maiti hata moja ya
mgeni.Hili jambo limenichanganya
na ndiyo maana nimeona nije tena
kwako kupata ufafanuzi zaidi
kuhusiana na hao watu nane
uliodai waliongezeka wakati wa
kurejea Dar es salaam ” akasema
Mathew
“Kwanza kabisa naomba
nikusahihishe kwamba wakati rais
Anorld anakuja Misri alikuwa na
watu kumi na tisa ndani ya ndege
kwani mimi ndiye niliyewapokea kule Cairo na si watu kumi na nane
kama unavyosema.Wakati wa
kuondoka waliongezeka watu nane
ambao ni waandishi wa habari na
waliletwa kwangu na mtu mmoja
anaitwa Fakrim Alnasor.Huyu
alikuwa anafanya kazi katika
uwanja wa ndege na nilifahamiana
naye wiki moja tu kabla ya rais
hajafika Misri.Aliniomba
niwaombee lifti watu hao katika
ndege ya rais na nikaongea na rais
akakubali na wakaondoka na
ndege ya rais.Inawezekanaje
kama watu wote walikufa maiti
zao zisionekane?Mzee Zubery naye
akashangaa.Usiku huu alikuwa
anazugumza kana kwamba hana matatizo yoyote ya kupoteza
kumbukumbu
“Huyu Fakrim Alnasor
alikuwa nani?
“Alikuwa anafanya kazi katika
shirika moja la ndege”
“unaweza kuwakumbuka hao
waandishi wa habari walitoka nchi
gani?Mathew akauliza
“Walitoka Marekani na hata
lafudhi yao ilionyesha ni
wamarekani”
“Ulisema kwamba kulikuwa
na binti moja mdogo lakini mbona
jina lake halikuorodheshwa
miongoni mwa watu
waliokuwemo ndani ya ndege?
“Sifahamu kwa nini
hakuorodheshwa ila ninachokumbuka ni kwamba huyo
binti alikabidhiwa kwa mama
mmoja wa pale ubalozini ambaye
nilimpa kazi ya kumtembeza huyo
binti katika sehemu mbali mbali za
Cairo.Mama Swai ambaye hivi sasa
ni marehemu nilimpa hiyo
kazi.Alimtembeza kuanzia Iraq
akaja mpaka maeneo Syria kule ..”
Zaina akamkonyeza Mathew
ishara kwamba tayari
kumbukumbu zimepotea
“Mzee nakushukuru sana
.Nitakuja kukutembelea tena siku
nyingine” akasema Mathew huku
akiinuka na kumpa mkono mzee
Zubery halafu Zaina akamsindikiza
“Zaina ahsante sana kwa
kunisaidia .Naomba usinichoke kila pale nitakapohitaji msaada wa
mzee” akasema Mathew
“Usijali Mathew
unakaribishwa sana muda wowote
ukiwa na jambo lolote.Naamini
sasa umepata uhakiki wa kile
ulichokuwa unakitafuta”
“Ndiyo sasa nimepata
nilichokuwa nakitafuta” akasema
Mathew na kuagana na Zaina
akaondoka
“Nilifanya vyema kurudi tena
kuonana na mzee Zubery sasa
nimeamini kile
alichokisema.Amesisitiza kwamba
kulikuwa na waandishi nane wa
habari raia wa Marekani ambao
walikuwemo ndani ya ndege
yarais.Swali linaibuka wako wapi? Mbona maiti zao hazikuonekana ?
Walitoka salama ndani ya ndege ?
akajiuliza Mathew
“Hapa kuna jambo limejificha
na ili kufahamu natakiwa kwanza
kuwafahamu hawa waandishi wa
habari ni akina nani?Mzee Zubery
amemtaja mtu mmoja anaitwa
Fakrim Alnasor kwamba ndiye
aliyewapeleka kwake wale
waandishi ili awaombee nafasi
katika ndege ya rais” akawaza
“Laiti kumbu kumbu za mzee
Zubery zingekuwa sawa muda
wote angekuwa ni msaada
mkubwa kweli hata hivyo kwa
haya machache aliyoyakumbuka ni
msaada mkubwa kangu.Ngoja
niyafanyie kazi nione matokeo yake lakini naamini kabisa kuna
jambo nitalipata.Halafu
amesisitiza kwamba kulikuwa na
binti mdogo aliyekwenda kufanya
utalii Misri na kufanya jumla ya
watu waliokuwemi ndegeni kuwa
kumi na tisa badala ya kumi na
nane waliorodheshwa.Najiuliza
huyu binti kama ni kweli
alikuwemo aliingiaje ndegeni bila
kuwepo kwa taarifa zake? Ni binti
wa nani ? Na baada ya ajali mwili
wake haukuwahi kupatikana je
alitoka salama ? Na kama alitoka
salama yuko wapi? Akajiuliza
maswali yaliyoendelea
kumchanganya .
“Hili kweli ni fumbo na ndiyo
maana limewashinda waliojaribu kulichunguza.Lakini lazima
niutafune huu mfupa na lazima hili
fumbo nilifumbue”
Mathew alielekea nyumbani
kwa Theresa na kabla hajafika
akachukua simu na kumjulisha
kwamba anakwenda kwake
“Unakuja kwangu? Mbona
umekwisha kuwa usiku?Theresa
akashangaa
“Mimi hufanya kazi usiku na
mchana kwa hiyo kama ulipewa
jukumu la kuwa msaidizi
wangu,inakubidi na wewe ufanye
kazi kama mimi.Amka tafadhali
nimekaribia kufika kwako”
akasema Mathew na kukata
simu.Alifika getini kwa Theresa na
mlinzi tayari alikwisha pewa taarifa akamfungulia geti akaingia
ndani akapokewa na Theresa
“Karibu ndani” Theresa
akamkaribisha Mathew ndani
“Ahsante Theresa.Tayari
ulikuwa umelala?
“Ndiyo nilikwisha lala.Huwa
nalala mapema sana”
“Basi kuanzia sasa ratiba yako
ya kulala itabadilika.Itakulazimu
ujifunze kukesha.Habari za toka
tulipoachana?
“Hakuna habari yoyote zaidi
ya dada kupiga simu na kuuliza
maendeleo yetu na siumueleza
chochote kama ulivyosema”
“Good.” Akasema Mathew
wakati wakiingia katika ofisi ya
Theresa “Kuna habari gani usiku huu?
Theresa akauliza
“Nimetoka tena kuonana na
yule mzee”
“Kweli wewe king’ang’anizi.
Mathew usipoteze muda na yule
mzee hana msaada wowote
kwetu.Hakuna chochote
anachokumbuka zaidi ya
kutuyumbisha kwa kumbu kumbu
zake ”
“Mzee yule yuko sahihi.Ni
kweli ana tatizo la kupoteza
kumbu kumbu lakini kuna wakati
kumbu kumbu zake huwa zinarudi
na anakuwa mzima kabisa kama
alivyosema mwanae Zaina.Usiku
huu nimezungumza naye na kwa
bahati nzuri nimemkuta ametulia na ameendelea kusisitiza kwamba
kulikuwa na waandishi nane wa
habari ndani ya ndege ya rais
wakati anarejea Dar es
salaam.Anasema kwamba yeye
ndiye aliyewaombea nafasi
waandishi hao kwa rais na
wakakubaliwa.Hata yeye
mwenyewe anashangaa kusikia eti
waandishi wale hawakuwemo
katika orodha ya maiti
zilizopatikana baada ya ajali
kutokea.Swali la kujiuliza je wako
wapi? Walikuwemo ndegeni
wakati ajali inatokea au walishuka
njiani? Maswali haya yangeweza
kupata majibu yake katika kile
kisanduku cha kuhifadhia kumbu
kumbu za mwenendo wandege.Ninaamini kisanduku hicho
kiliondolewa makusudi kabisa
kuficha taarifa za ndege hiyo
zisijulikane.Vile vile kuna huyu
binti ambaye Zubery amesisitiza
kwamba alikwemo ndegeni ni
nani na yuko wapi? Je kama
alifariki maiti yake iko wapi?
Halafu kwa nini hakuwahi
kuorodheshwa katika orodha ya
watu waliokuwemo ndegeni?
Akauliza Mathew
“Mathew hapo ndipo huwa
simuamini yule mzee.Kama watu
hao anaosisitiza, walikuwemo
ndegeni wako wapi? Maiti zao ziko
wapi?Huyo binti anayemsema
yuko wapi? Akauliza Theresa “That’s what we need to find
out” akasema Mathew
“Kwanza nataka kumfahamu
huyu Fakrim Alnasor ni nani?
Tukimfahamu huyu anaweza
akatusaidia kufahamu mambo
mengine kuhusiana na hao
waandishi wa habari.Washa
kompyuta yako tumtafute huyu
mtu” akasema Mathew.Theresa
akawasha kompyuta yake na
kuanza kubofya .Baada ya dakika
kama tano hivi akamuonyesha
Mathew
“Kuna Fakrim Alnasor zaidiya
kumi lakini kuna huyu mmoja
ambaye taarifa inaonyesha
kwamba ni raia wa marekani
.Anafanya kazi katika ofisi za shirika la ndege la American
airways na anaishi jijini New York
Marekani”
“Nadhani anaweza kuwa
mwenyewe kwani mzee Zubery
alisema kwamba Fakrim alikuwa
anafanya kazi katika shirika la
ndege .Kuna umuhimu wa
kumchimba zaidi huyu Fakrim
.Kuna kitu tunaweza kukipata toka
kwake”akasema Mathew
“Kama ni mfanyakazi wa
shirika la ndege la American
airways basi sioni shaka yoyote
kwake.Yawezekana kama
mfanyakazi wa shirika la ndege
alilazimika kuwatafutia usafiri
hao waandishi wa habari.Huyu hatakuwa na msaada wowote
kwetu” akasema Theresa
“Kama aliwasaidia
kuwatafutia usafiri hao waandishi
wa habari wako wapi? Walitoka
vyombo gani vya habari? Lazima
tufahamu mambo hayo ili tuwe na
uhakika kama waandishi wale
walikufa na bado wako hai.Kama
walikufa maiti zao ziko wapi?Kama
walipona wako wapi?” akasema
Mathew na kumuaga Theresa
“Mimi ngoja niende tutaonana
kesho ila muda wowote hata usiku
wa manane nikihitaji jambo lolote
nitakupigia simu”
“Usihofu Mathew”
akajibuTheresa na Mathew
akaondoka “Yawezekana labda Fakrim
hana mahusiano yoyote na ajali ile
kwani yeye anafanya kazi katika
shirika la ndege na inawezekana
akawa aliwasaidia tu hao
waandishi kupata usafiri lakini
hata hivyo lazima uchunguzi
ufanyike.Ninachotaka ni kufahamu
hao waandishi walitoka katika
vyombo gani vya habari? Je wako
hai bado au walikufa? Akawaza
Mathew baada ya kuondoka
nyumbani kwa Theresa
Ilipata saa tano za usiku na
hakwenda nyumbani kwake moja
kwa moja bali akaelekea nyumbani
kwa Meshack Jumbo “Karibu sana
Mathew”akasema mzee Jumbo
akimkaribisha Mathew
“Ahsante mzee.Samahani kwa
kuja bila taarifa”
“C’mon Mathew.Hapa ni
nyumbani na unaweza kuja muda
wowote karibu sana.Mimi bado
nilikuwa najisomea vitabu mbali
mbali.Unajua mambo
yamebadilika sana zama hizi
tofauti na wakati wetu hivyo ili
niweze kuimudu vyema nafasi
niliyopewa na rais lazima nijifunze
mbinu mbali mbali za kisasa.Haya
niambie ujio huu wa usiku si kwa
ajili ya kunisabahi” akasema mzee
Meshack “Ni kweli huu si muda wa
salamu .Kuna jambo limenileta
hapa kwako mzee na ninahitaji
msaada”akasema Mathew na
baada ya muda akasema
“Nimeanza rasmi leo ile kazi
ya rais”
‘That’s good” akajibu Meshack
“Kama alivyosema rais
kwamba hili jambo ni fumbo zito
ila kwa siku ya leo walau kuna
mwanga mdogo sana nimeanza
kuuona kwa mbali” akameza mate
kulainisha koo na kusema
“Uchunguzi wangu umeanzia
katika ajali ya ndege ya rais
Anorld.Niliomba nipatiwe taarifa
za chanzo cha ajali ile lakini jibu
nililolipata toka kwa rais ni kwamba hakuna ripoti yoyote ya
uchunguzi kwa kuwa kisanduku
cha kurekodi taarifa za mwenendo
wa ndege maarufu kama
kisanduku cheusi hakikuwahi
kuonekana eneo la ajali kwa hiyo
kilichosababisha ajali ile
hakijulikani”
“Kweli? Meshack Jumbo
akashangaa
“Kweli kabisa mzee.Hata Hiyo
ndiyo taarifa aliyopewa rais baada
ya kutaka apewe ripoti ya
uchunguzi wa ile ajali”
“Haya ni
maajabu.Inawezekanaje
kisanduku hicho kipotee?Halafu
mbona jambo hili limefanywa siri?
Haijawahi kutangazwa kwamba kisanduku hicho kimepotea”
akasema Meshack
“Hata mimi nimejiuliza
nimekosa jibu lakini hii ni picha ya
wazi kwamba kuna kitu kilifanyika
hapa .Baada ya kulifahamu hili
sikuishia hapo nilimtafuta
aliyewahi kuwa balozi wa
Tanzania nchini Misri wakati
ilipotokea ajali ile anaitwa Alhaj
Zubery Msokwa.Huyu ni mtu
mzima sana kwa sasa na ana
matatizo ya kiafya na wakati
mwingine anapoteza kumbu
kumbu japo kuna nyakati
kumbukumbu hurejea na
anakumbuka vitu mbali mbali
vilivyopita.Hata hivyo kuna
mambo amenieleza ambayo yamenifanya nije kwako usiku
huu.Mzee Zubery amenieleza
kwamba baada ya rais Anorld na
rais wa Misri kumaliza kikao chao
alielekea uwanja wa ndege kwa
ajili ya kurejea Tanzania lakini
kulijitokeza kundi la waandishi
nane wa habari waliokuwa
wanaelekea Tanzania lakini kwa
bahati mbaya walichelewa ndege
yao hivyo kuwalazimu kuomba lifti
katika ndege ya rais.Jumla ya watu
waliokuwemo ndegeni wakati
ndege ya rais inaondoka Cairo
walikuwa watu ishirini na saba
.Baada ya ajali aliyetoka salama ni
kanali Sebastian pekee kwa hiyo
basi kulitakiwa kuwe na maiti
ishirini na tano ndani ya ndege lakini cha kushangaza maiti
zilizopatikana ni kumi na saba
tu.Maiti nane hazipo na miongoni
mwa maiti zilizopatikana hakuna
hata maiti moja ambayo ni ya raia
wa kigeni.Najiuliza hao watu nane
wako wapi?Hao waandishi wa
habari wako wapi?Hakuna
anayeweza kutupa majibu haya
hivyo yatupasa kutafuta majibu
sisi wenyewe.”
Akanyamaza.Meshack
Jumboakatafakari kidogo na
kuuliza
“Umesema huyo mzee
aliyewahi kuwa balozi ana tatizo la
kumbu kumbu?
“Ndiyo” “Unawezaje kumuamini mtu
ambaye kumbu kumbu zake
haziko sawa? Kama kweli
kuliongezeka watu nane wako
wapi? Mbona katika orodha ya
maiti hawapo? Nina wasi wasi na
taarifa yake kama ina ukweli
wowote.Kwenye mambo mazito
kama haya hatupaswi kuamini
taarifa nyepesi kama hizo.Nadhani
kitu cha maana hapo ni kufahamu
kilipo kisanduku cheusi.Nani
kakichukua na kwa nini?Hainiingii
akilini eti kilipotea” akasema
Meshack Jumbo
“Mwanzoni hata mimi
nilikuwa na mashaka sana
kuhusiana na taarifa hii ya balozi
Zubery na imenilazimu kurejea tena kwake usiku huu ili
kujiridhisha na taarifa hii na kwa
bahati nzuri nimemkuta akiwa
mzima na kumbu kumbu zake ziko
sawa na akanihakikishia kwamba
alichokisema ni kitu cha kweli
kabisa.Amemtaja pia mtu mmoja
anaitwa Fakrim Alnasor kwamba
ndiye aliyemfuata na kumtaka
awaombee lifti waandishi wa
habari katika ndege ya
rais.Nimejaribu kutafuta taarifa za
huyo Fakrim na zinaonyesha
kwamba ni mfanyakazi wa shirika
la ndege la American airways
anaishi jijini New York.Ni raia wa
marekani lakini amezaliwa
Misri.Hii inanifanya nimuamini
mzee Zubery kwamba anasema kitu anacho kifahamu.Nimekuja
hapa kwako nataka unisaidie
kumfahamu huyu Fakrim ni nani
na kama amewahi kufanya kazi
nchini Misri ili niwe na uhakika
zaidi kama ndiye aliyetajwa na
Alhaj Zubery.Kama ndiye basi
atatusaidia kuwafahamu wale
waandishi wa habari waliopata lift
katika ndege ya rais ni akina nani
na wako wapi.Tukifanikiwa
kumpata huyu nina hakika
atatusaidia sana” akasema Mathew
Lakini Mathew kwa nini
uingie katika kuchunguza chanzo
cha kuanguka kwa ndege ya rais
badala ya kuchunguza nani
walimuua kanali Sebastian
ambayo ndiyo kazi uliyopewa na rais? Mimi naona uachane na hilo
suala la ndege ya rais kwani
linaonekana kuwa na mzunguko
mrefu sana na ujikite katika
mauaji ya Sebastian” akasema
Meshack Jumbo
“Mzee Jumbo mauaji ya
Sebastian hayakuibuka tu yana
chanzo chake na waliomuua wana
sababu zao hivyo nataka nifahamu
nini kilitokea katika ndege ya rais?
Kilichonifanya nitake kuanzia
uchunguzi wangu katika ajali ya
ndege ya rais ni namna kanali
Sebastian alivyotoka salama katika
ndege hiyo.Ninavyofahamu endapo
kunakuwa na kitisho chochote
katika ndege ya rais basi raisi
huwa anakuwa wa kwanza kuondolewa ndegeni lakini hapa
ilikuwa tofauti.Kanali Sebastian
alikuwa wa kwanza kutoka
ndegeni na rais akafika
ndegeni.Huoni hiki ni kitu cha
ajabu mzee? Jambo lingine Kanali
Sebastian alikuwa mbebaji mkuu
wa Football.Mtu anayebeba begi
hili hula kiapo hata kama
kutatokea jambo gani atahakikisha
anailinda Fooftball ambamo ndani
yake huwa kuna siri za nchi.Je
kanali Sebastian alifanikiwa
kutoka salama na football?Kama
alitoka nayo iko wapi?Maswali
haya yamenifanya nianzie
uchunguzi wangu katika ajali ya
ndege ya rais” akasema Mathew Mzee Meshack Jumbo akafikiri
kwa muda kidogo na kusema
“Kuna kitu hata mimi
ninakiona hapo.Kweli kuna
umuhimu wa kutafuta chanzo cha
kuanguka kwa ndege ya rais lakini
nakuhakikishia Mathew hili
halitakuwa jambo jepesi.Huku
tunakoenda tutafukunyua mambo
na mengine ni hatari kubwa
sana.Maelezo uliyonipa
yanaonyesha kuna jambo si la
kawaida katika suala hili.Ninaanza
kuwa na hisia yawezekana hata ile
ajali ya ndege ya rais ikawa ni ya
kupangwa lakini lazima uchunguzi
ufanyike ili kuupata ukweli”
“Ndiyo maana nimekuja
kwako mzee unisaidie.Nafahamu una ukaribu na mawasiliano na
watu kadhaa wa Marekani ambao
wanaweza wakatusaidia kupata
taarifa za Fakrim” akasema
Mathew.Mzee Jumbo akafikiri
kidogo na kusema
“Kuna rafiki yangu mmoja
anaitwa Jimmy Snow.Huyu aliwahi
kuwa afisa wa juu wa FBI lakini
baadae alikimbilia urusi anakoishi
hadi leo baada ya kugundua
mpango wa siri wa kumuua
uliopangwa na CIA baada ya
kumsaidia jasusi mmoja wa Urusi
kupaa taarifa nyeti za sri za
Marekani.Jimmy anaweza
akanisaidia kupata taarifa za huyo
Fakrim.Aliwahi kunipa namba
yake ya simu anayotumia kwa sasa nchini Urusi ngoja niwasiliane
naye kama anaweza kunisaidia”
akasema mzee Meshack na
kufungua kitabu chake
alimoandika namba nyingi za simu
na kutafuta namba ya Jimmy Snow
akaipata akaiandika katika simu
yake na kupiga.Baada yamuda
simu ikapokewa
“Hallow Jimmy” akasema
Meshack baada ya simu
kupokelewa
“Meshack Jumbo habari za
siku?
“Nzuri kabisa Jimmy habari
yako? Unaendeleaje?
“Ninaendelea vyema
.Umekuwa kimya sana” ‘Ni kweli Jimmy nimekuwa
kimya.Kama unavyojua maisha ya
kustaafu”
“Pamoja na kustaafu Meshack,
lakini usitusahau sisi marafiki
zako.Mimi mwenyewe naendelea
vyema hivi sasa nina mpango wa
kutembelea Afrika na ikiwezekana
nitafika Tanzania.Nitafurahi
kuonana nawe Meshack kwani
tumekuwa tunashirikiana kwa
muda mrefu na umenisaidia katika
mambo mengi sana na hasa wakati
ule nilipopatwa na matatizo
uliwahi kudiriki hata kunitumia
fedha za kujikimu”
“Karibu sana Tanzania
Jimmy.Itakuwa ni furaha yangu
kukupokea hapa .Hata hivyo Jimmy kuna jambo nataka
nikujulishe.Nimeombwa na rais
nirudi tena kazini niongoze idara
ya usalama wa taifa kwa muda wa
mwaka mmoja baada ya kifo cha
mkurugenzi wa idara hiyo”
“Oh ! Hongera sana Meshack
kwa kuaminiwa na kupewa tena
jukumu kubwa kama hilo.Naamini
kuna kitu rais amekiona kwako
ndiyo maana akakupa nafasi hiyo
nyeti sana” akasema Jimmy
“Ahsante Jimmy kwa pongezi
hata hivyo nimekupigia kukuomba
msaada wako”
“Msaada gani unauhitaji
Meshack?
“Kuna mtu mmoja anaitwa
Fakrim alnasor ninahitaji kupota taarifa zake.Anafanya kazi katika
shirika la ndege la American
airways yupo New york.Nafahamu
japokuwa uko nchini Urusi lakini
huwezi kukosa mtu ndani ya FBI
akakusaidia kupata taarifa za mtu
huyu.Ni muhimu sana kwangu.”
Akasema Meshack.Jimmy akafikiri
kidogo halafu akasema
“Taarifa zipi unahitaji kuhusu
huyu mtu?
“Nahitaji taarifa zake zote
zinazomuhusu na zaidi kama
amewahi kufanya kazi na kuishi
nchini Misri”
“Sawa Meshack nina vijana
wangu pale FBI watanisaidia
kupata taarifa za kuhusiana na huyo mtu.Vijana wakinitumia
taarifa nitakutumia mara moja.”
“Nakushukuru sana Jimmy”
akasema Meshack na kukata simu
“Suala lako linafanyiwa kazi
na mara atakapopata taarifa
zozote atatujulisha.Nakusihi sasa
nenda kapumzike ili ujiandae na
siku ya kesho” akasema Meshack
jumbo na Mathew akainuka tayari
kwa kuondoka mara mzee Jumbo
akakumbuka kitu
“Mathew kuna kitu
nimekumbuka.Umekwisha fahamu
ni akina nani walifanya uchunguzi
wa ajali ya ndege ya rais?
“Hapana sikuwa nimeliwaza
hilo” “Basi lifanyie
kazi.Wakijulikana watu hawa ni
akina nani wanaweza wakahojiwa
na wakaeleza kilichotokea
kuhusiana na uchunguzi ule”
“Ahsante kwa kunikumbusha
kuhusu jambo hilo mzee.Halikuwa
katika akili yangu kabisa.Nadhani
ni kutokana na kukaa muda mrefu
bila kufanya kazi hizi ndiyo maana
ninasahau hata mambo muhimu
kama haya.Nitalifanyia kazi hilo
jambo kesho asubuhi” akasema
Mathew na kuondoka
Alipoyaacha makazi ya mzee
Meshack Jumbo akampigia simu
Theresa na kumtaka ajitahidi ili
hadi kesho asubuhi awe na majina
ya timu ya wachunguzi iliyochunguza chanzo cha
kuanguka kwa ndege ya rais
“Imekuwa ni siku ndefu lakini
kidogo naona kuna mwanga fulani
japo mdogo sana lakini kama
nikiufuata nitafika mahala fulani”
akawaza Mathew alipoingia
chumbani kwake
“Natamani kupigia simu na
kuzungumza na mwanangu Anna
Maria lakini muda huu ni usiku
mwingi na tayari atakuwa amelala
.Nitampigia simu yaya wake kesho
kama nilivyopewa
maelekezo.Sitaki tena kumpigia
Peniela.Sitaki kuvuruga
mahusiano yake na mpenzi wake
ambaye hapendi nimpigie simu
Peniela” akawaza Mathew na kutazama picha ya mwanae
aliyoitundika ukutani
“Nakupenda sana Anna
Maria.Iko siku nitakuchukua na
utakuja kuishi Tanzania kwani
huku ndiko kwenu na si huko uliko
sasa.Mungu azidi kunipa uhai
mrefu” akawaza na kujilaza
kitandani
******************
Saa kumi na moja na nusu
Mathew aliamka na kitu cha
kwanza alichokifanya ni kupiga
magoti akamshukuru Mungu kwa
kumuamsha salama halafu
akaingia katika chumba chake cha
mazoezi ambako alifanya mazoezi ya nguvu ili kuweka mwili sawa
halafu akaoga na kujiandaa kwa
ajili ya kuikabili siku.Mpishi wake
alitayarisha kifungua kinywa na
kumjulisha na wakati akipata
kifungua kinywa simu yake
kwanza ikaita alikuwa ni Dr Vivian
akaipokea haraka haraka
“Hallo mheshimiwa rais”
akasema Mathew
“Mathew habari za asubuhi?
“Habari nzuri kabisa
mheshimiwa rais.Sijui
umeamkaje”
“Nimeamka salama
kabisa.Sikupata nafasi ya
kuzungumza nawe jana kujua
maendeleo yakoje” “Ninaendelea vyema kabisa
mheshimiwa rais .Jambo hili ni
gumu na ni fumbo gumu kama
unavyosema wewe mwenyewe
lakini ninaendelea nalo.Kama
nilivyokuahidi mheshimiwa rais
kwamba nitajitahidi kwa kila
niwezavyo kuhakikisha kwamba
ninalichimba suala hili hadi mzizi
wake.Kuna hatua kadhaa
nimekwisha zifikia na kuna
mambo kadhaa yamejitokeza na
muelekeo si mbaya ila kwa sasa
sintasema chochote nipe muda na
nikipiga hatua kubwa
nitakujulisha”
“Nafurahi kusikia
hivyoMathew.Ninarudia tena
kukusisitiza kwamba uwe makini sana.Hili jambo lina siri kubwa
ndani yake imejificha.Ukihitaji kitu
chochote usisite kunijulisha mara
moja” akasema rais na kuagana na
Mathew
Mara tu rais alipokata simu
Mathew akampigia simu mzee
Meshack Jumbo
“Shikamoo mzee” akasema
“Marahaba
Mathew.Umeamkaje?
“Nimeamka salama mzee.Vipi
kuna lolote umelipata toka kwa
Jimmy Snow?
“Ndiyo.Amenipigia simu saa
kumi na moja alfajiri.Amenitumia
taarifa za kumuhusu Fakrim
Alnasor.Ninakutumia sasa hivi katika simu yako” akasema
Meshack Jumbo.
“Ahante sana mzee.Naomba
unitumie ili niipitie sasa hivi”
akasema Mathew na kukata simu
akampigia Theresa.
“Habari za asubuhi Theresa?
“Salama kabisa.Umekwisha
amka?
“Tayari nimekwisha
amka.Mimi huamka saa kumi na
moja za alfajri.Vipi kuna habari
yoyote mpya?
“Umefanikiwa kupata yale
majina niliyokutaka uyatafute?
“Bado sijatumiwa ila asubuhi
hii nitayapata”
“Good.Nitakuja hapo
nyumbani kwako asubuhi hii” akasema Mathew na kukata simu
akauona ujumbe wa kutoka kwa
Meshack Jumbo.Akaufungua
akausoma.Yalikuwa ni maelezo
kuhusiana na Fakrim
Alnasor.Maelezo yale yalionyesha
kwamba Fakrim Alnasor alikuwa
na umri wa miaka 49 na raia wa
Marekani aliyezaliwa nchini
Misri.Amesoma nchini Misri na
Marekani na baada ya kuhitimu
shahada yake ya kwanza ya
biashara aliajiriwa na shirika la
ndege la American
airways.Amewahi kufanya kazi
katika ofisi za shirika hili zilizoko
Misri na baadae akahamishiwa
nchini Marekani .Taarifa
inaonyesha kwamba Fakrim ana mke na watoto watatu.Mathew
akatabasamu
“Mzee Zubery alikuwa
sahihi.Huyu ndiye Fakrim
aliyekuwa anamzungumzia.Huyu
ndiye aliyewapeleka kwake wale
waandishi wa habari na kumtaka
awaombee nafasi katika ndege ya
rais.Picha linaanzia hapa” akawaza
Mathew na kuchukua simu
akampigia Meshack Jumbo
anamjulisha kwamba anakwenda
kwake kuonana naye
“Kuna kiti nimekigundua
hapa.Taarifa hii inaonyesha
kwamba Fakrim alihamishwa toka
Cairo kwenda New york Marekani
wiki moja tu baada ya ajali ile ya
ndege ya rais kutokea.Je kuna mahusiano yoyote kati ya kuhama
kwake na ile ajali? Mathew
akajiuliza
Alifika nyumbani kwa
Meshack Jumbo na kumkuta
anapata kifungua kinywa
“Karibu Mathew”
“Ahsante sana mzee” akajibu
Mathew na kumsubiri mzee Jumbo
amalize kupata kifungua kinywa
halafu wakaelekea barazani
“Mzee kwanza nakushukuru
sana kwa taarifa uliyonitumia.Hata
hivyo imenilazimu kuja tena
kwako baada ya kuridhika
kwamba Fakrim huyu ndiye yule
aliyetajwa na Mzee Zubery
.Nadhani sasa hata wewe umeamini kwamba yule mzee
alikuwa anasema kweli”
“Ndiyo.Nimeipitia ile taarifa
na nimeona kuna muunganiko na
yale aliyoyasema huyo balozi.”
“Ahsante.Hata hivyo kuna
mambo bado nahitaji msaada
wako.Huyu Fakrim anapaswa
kuhojiwa ili kufahamu kuhusu
wale waandishi wa habari.Lengo ni
kupata taarifa zao kwa undani ni
akina nani na wako wapi? Kama
wako hai bado walitokaje ndani ya
ndege ya rais?
“Ngoja niwasiliane tena na
Jimmy Snow nione kama anaweza
kutusaidia kwa hilo” akasema
Meshack Jumbo na kumpigia simu
Jimmy “Habari yako Jimmy” akasema
Meshack baada ya Jimmy kupokea
simu
“habari yako Meshack Jumbo”
“Samahani Jimmy kwa
usumbufu.Ninahitaji msaada wako
tena”
“Usijali Meshack,sema
nikusaidie nini?
“Ninahitaji msaada bado kwa
Fakrim”
“Unachunguza nini kuhusu
Fakrim?
“Tunachunguza kuhusu ajali
ya ndege ya rais Anorld iliyotokea
miaka kumi iliyopita.Kunatajwa
kuwepo kwa waandishi nane wa
habari ambao waliomba lifti katika
ndege ya rais wakati akirejea Tanzania akitokea Misri.Baada ya
ajali hiyo kutokea ni mtu mmoja tu
aliyenusurika lakini wengine wote
walikufa.Kinachoshangaza ni
kwamba waandishi hao nane wa
habari maiti zao
hazikuonekana.Ninataka
kufahamu kupitia kwa Fakrim
kwamba waandishi hao ni akina
nani,walitoka vyombo gani vya
habari na kama wako hai
bado.Nahitaji sana msaada wako
kwa hilo” akasema Meshack Jumbo
.Jimmy Snow akavuta pumzi ndefu
na kusema
“Meshack Jumbo wewe ni
rafiki yangu mkubwa na umewahi
kunisaidia sana katika mambo
mbali mbali na siwezi kukataa kukusaidia katika jambo kama hilo
ambalo naamini lina umuhimu
mkubwa kwa nchi yako.Kuna
jambo moja ambalo naomba
nikuweke wazi ambalo ni muhimu
sana kuhusiana na Fakrim
Alnasor” akanyamaza kwa
sekunde kadhaa na kusema
“Fakrim Alnasor ni jasusi wa
shirika la ujasusi la Marekani
CIA.Ni mmoja wa majasusi wa siri
sana waliosambazwa sehemu
mbali mbali duniani.Kama Fakrim
anahusika katika ajali hiyo basi ni
wazi kwamba alikuwa akifanya
kazi za CIA.Tukimgusa Fakrim
tutakuwa tayari tumeingia katika
mgogoro na CIA lakini hata hivyo
nitakusaidia.Ninao bado vijana wangu ndani ya FBI na mmoja wao
ni binti yangu anaitwa
Camilla.Nitawatumia kuweza
kupata taarifa toka kwa Fakrim za
kuhusiana na ajali hiyo ya ndege
ya rais wa Tanzania na hao
waandishi wa habari aliowasaidia
wakasafiri na ndege ya
rais.Nikipewa taarifa yoyote
nitakujulisha”akasema Jimmy
Snow.
“Nashukuru sana Jimmy”
akasema Meshack Jumbo na
kukata simu akamgeukia Mathew
“Mathew kijana wangu,suala
hili si rahisi hata kidogo.Kadiri
linavyozidi kuchimbuliwa ndivyo
mambo yanavyozidi kuibuka na
sijui huko mbele tutakutana na jambo gani.Jimmy Snow anadai
kwamba Fakrim Alnasor ni jasusi
wa CIA”
Mathew na Meshack Jumbo
wakatazamana kwa muda
“Fakrim ni CIA? Mathew
akauliza
“Ndiyo ni CIA”
“Mhh ! Hapa kuna shughuli
.Kama Fakrim ni CIA basi picha ya
kwanza ninayoipata ni kwamba
yawezekana ni CIA ndio
waliomuua rais Anorld” akasema
Mathew
“Ni mapema sana kujenga hoja
hiyo japokuwa siwezi kukataa
kwani inawezekana lakini
tusiharakishe tuchunguze
kwanza”akasema Meshack Jumbo “Mzee Jumbo kama Fakrim ni
CIA basi nina uhakika mkubwa
kwamba wao ndio wanaohusika
katika ajali ile.Hebu jiulize kwa
nini akahamishwa muda mfupi tu
baada ya ajali kutokea?Ni wazi
alikuwepo pale Misri kwa kazi
maalum na kazi yake ilipokamilika
akaondolewa.That’s how CIA
works.Nina uhakika mkubwa huyu
mtu tukimfuatilia kwa ukaribu
tutagundua mengi”
“Jimmy Snow amesema
atawatumia vijana wake walio
ndani ya FBI na mmoja wao
ambaye ni binti yake anaitwa
Camilla na watahakikisha
wanamuhoji Fakrim kuhusiana na
hao waandishi wa habari na ajali ya ndege ya rais na
watakachokipata atatujulisha”
akasema Meshack Jumbo na baada
ya majadiliano Mathew akamuaga
Meshack na kuondoka.
“Kuna dalili za uhusika wa
Marekani katika ajali ile ya ndege
ya rais kupitia shirika lake la
ujasusi la CIA.Fakrim ambaye ni
jasusi wa CIA aliwaombea lifti
waandishi wa habari wanaotoka
Marekani na baadae ndege
ikaanguka na miili ya waandishi
hao haionekani.Baada ya muda wa
wiki moja toka ilipotokea ajali ile
Fakrim akahamishwa na
kupelekwa New York.Kuna kitu
hapa lazima tukifahamu.Huyu
Fakrim ni mtu muhimu sana katika uchunguzi wetu.Lakini suala la
kujiuliza kama Marekani ndio
wanahusika na kusababisha ajali
ya ndege ile na rais Anorld
akafariki dunia kwa nini basi
walifanya hivyo?Walihitaji
nini?Lazima kuna siri imejificha
hapa .Hili ni suala la kwenda nalo
taratibu na kwa umakini mkubwa
sana .Ukweli utabainika kwani
tayari mwanga umeanza
kujitokeza”akawaza Mathew
wakati akielekea nyumbani kwa
Theresa
Alifika nyumbani kwa Theresa
na kumkuta tayari yuko ofisini
“Umechelewa sana kuanza
kazi” akasema Theresa “Kuna sehemu muhimu
nilipita.Kuna taarifa zozote
umepata?
“Ndiyo tayari nimetumiwa
majina ya timu ya watu saba
waliofanya uchunguzi wa chanzo
cha kuanguka kwa ndege ya
rais.Watano kati ya hao waliofanya
uchunguzi huo wanatoka nje ya
nchi na mmoja alitoka kikosi cha
anga cha jeshi la wananchi wa
Tanzania na mwingine ni mhandisi
toka wizara ya mawasiliano.Kwa
bahati mbaya hawa watazania
wawili walioshiriki katika timu hii
wamefariki dunia” akasema
Theresa na kumpatia Mathew yale
majina akayapitia “Hawa watanzania wawili
walioshiriki katika uchunguzi huu
nini sababu ya vifo vyao? Mathew
akauliza
“Hapana sijaelezwa sababu ya
vifo vyao” akajibu Theresa
“Kuna kitu cha ajabu
nimeanza kukiona.Kuna vifo vya
ajabu ajabu vinatokea kwa wale
ambao wanahusika kwa namna
fulani katika hili tukio la ajali ya
dege ya rais.Ukianzia na mzee
Zubery alipata ajali siku chache tu
baada ya ajali ya ndege ya rais
kutokea na toka muda huo
hajawahi kurejea katika hali yake
ya kawaida.Mwanae Zaina
anasema baba yake ametumia
zaidi ya miaka mitano katika matibabu.Hawa jamaa wawili
waliotajwa kushiriki katika
uchunguzi wa ajali ya ndege ile ya
rais nao wamefariki dunia .Hii
inazidi kutupa uhakika kwamba
ajali ile haikuwa ya
kawaida.Tuachane na hao wawili
hebu tuwatazame hawa
wachunguzi waliotoka nje ya nchi
ambao wanatajwa kutokea katika
kampuni iliyotengeza ndege
hiyo.Itafute hiyo kampuni na
uwaulize kuhusiana na hawa
wachunguzi.Tunataka kufanya
mahojiano na walau mmoja wao ili
watuelekeze ni kitu gani
walichokiona katika uchunguzi
wao na tufahamu mazingira ya
kupotea kwa kisanduku cheusi” akasema Mathew na kutoka nje
akazitafuta namba za simu za
mwanadada anayefanya shughuli
za ndani katika jumba la Peniela
akampigia
“hallo kaka” akasema
mwanadada aliyekuwa
anazungumza kwa lugha ya
kifaransa.
“Hujambo Marie?
“Sijambo kaka.Habari za
Tanzania?
“Huku kwema .Mnaendeleaje
nyie hapo Paris?
“Tunaendelea vyema kaka”
“Nashukuru kusikia hivyo
.Anna Maria anendeleaje? Tayari
amekwisha kwenda shule? “Anaendelea vyema,na tayari
amekwenda shule”
“Vipi maandalizi ya siku yake
ya kuzaliwa? Akauliza Mathew
“Bado sijaona maandalizi
yoyote kuanza”
“Sawa Marie,naomba Anna
Maria atakaporejea kutoka shule
unipigie ninahitaji kuzungumza
naye”
“Nitakujulisha kaka
atakaporejea.Lini unakuja
kututembelea?
“Kwa sasa nimebanwa kidogo
na shughuli nyingi na nitakapopata
nafasi nitakuja kuwatembelea”
akasema Mathew na kukata simu
halafu akawa na mazungumzo na
mkandarasi anayesimamia ujenzi wa kiwanda chake.Baada ya hapo
akawa na maongezi na watu
wengine kadhaa wa muhimu
halafu akarejea ndani na kumkuta
Theresa bado anazungumza na
simu.Alizungumza kwa takribani
dakika kumi na tano halafu
akakata simu na kumgeukia
Mathew
“Mathew hili suala mbona
linazidi kuwa gumu?
“Kwa nini Theresa?
“Nimezungumza na kampuni
ya ndege waliyotengeneza ile
ndege ya rais iliyopata ajali
wanasema kwamba hawakuwahi
kutuma mtu yeyote kuja
kuchunguza kuhusiana na ajali ile
ya ndege.Nimezungumza na mkurugenzi wa kampuni hiyo
anasema kwamba yeye ni mgeni
katika nafasi yake akaniunganisha
na mtu mwingine ambaye
alikuwepo wakati ndege ile
inapata ajali lakini naye akakana
kabisa kutuma timu ya wataalamu
kuja kuchunguza chanzo cha
kuanguka kwa ndege ya rais
iliyotengenezwa na kampuni
yao.Anasema kwamba walisikia
kuhusu kuanguka kwa ndege ile
lakini hawakuwahi kupewa taarifa
rasmi na serikali au hata kuitwa
kufanya uchunguzi.Nilimuuliza
kuhusiana na kutoonekana kwa
kisanduku cheusi cha kurekodi
taarifa za ndege na akashangaa
sana.Nilimtajia majina ya wale ambao wanatajwa kwamba
walikuja kufanya uchunguzi na
akakana kuwa na watu kama hao
katika kampuni yao.Tumekwama
tena”akasema Theresa.Mathew
akavuta pumzi ndefu
“Dah ! Kweli hili suala ni
fumbo zito.Kwa hiyo taarifa hii
iliyokaa katika kumbukumbu za
serikali si ya kweli.Nani
aliyeidhinisha timu hii ifanye
uchunguzi? Kila kitu kuhusiana na
ajali ile ya ndege ni uongo
mtupu.Kuna mambo mengi
yanafichwa na ndiyo maana jambo
hili limebaki kuwa ni fumbo
lisiloweza kufumbuliwa.Kila
aliyejaribu kufanya uchunguzi
alifika mahala akashindwa kuendelea lakini mimi
sintoshindwa nitahakikisha
ninafika mwisho” akasema
Mathew na kuinama akafikiri
kidogo na kusema
Kila
aliyejaribu kufanya uchunguzi
alifika mahala akashindwa kuendelea lakini mimi
sintoshindwa nitahakikisha
ninafika mwisho” akasema
Mathew na kuinama akafikiri
kidogo na kusema
“Tuachane kwanza na hayo
mambo.Hili suala linapaswa
kushughulikiwa kwa umakini
mkubwa.Tuende nalo hatua kwa
hatua.Kabla ya kuja hapa nimetoka
kufuatilia taarifa za kuhusiana na
Fakrim.Kwa taarifa nilizopata toka
marekani ni kwamba Fakrim ni
raia wa Marekani mwenye asili ya
Misri. Anafanya kazi katika shirika
la ndege la british airways na
amewahi kufanya kazi katika ofisi
za shirika hili zilizopo Cairo Misri
na baadae akahamishiwa nchini Marekani.Taarifa inaonyesha
alipata uhamisho wiki mja tu
baada ya ndege ya rais
kuanguka.Kikubwa nilichokipata
kuhus Fakrim ni kwamba ni jasusi
kutoka CIA.Kwa kutumia watu
wetu walioko New york Marekani
tumeomba atafutwe huyu Fakrim
na ahojiwe kuhusiana na wale
waandishi wa habari na kuhusiana
na kuanguka kwa ndege ya
rais.Wakifanikiwa kumpata na
kumuhoji basi tutapata mambo
yatakayotusaidia sana .Mpaka
hapa kunaanza kujitokeza chembe
chembe za Marekani kuhusika
katika kuanguka kwa ndege ile ya
rais.Wakati tukisubiri taarifa
kutoka New York kwa watu wetu wanaotusaidia kuna kitu
ninahitaji”
“Unahitaji nini Mathew?
“Nahitaji kuonana na mjane
wa rais Anorld”
“Sifahamu chochote kuhusu
yule mama ngoja nipige simu
niulize” akasema Theresa na
kupiga simu akapewa maelekezo
halafu akamtazama Mathew
“Nimeelekezwa kwamba
mama huyu anaitwa April Mubara
na kwa sasa anaishi katika shamba
lake lililoko katika kijiji cha
Mchangawima Chalinze Pwani”
“Good.Twende huko sasa
hivi.Tumuhoji pengine kuna kitu
tunaweza kugundua” “Kitu gani unakihitaji toka
kwa huyo mama? Unadhani kuna
lolote analoweza katusaidia?
“Ni mtu muhimu na anaweza
akawa na jambo la kutusaidia.Yule
ni mjane wa rais na yawezekana
akawa anafahamu mambo mengi
ya siri aliyoelezwa na mume wake
.Najaribu kutafuta kiini cha
Marekani kuhusika katika ajali
ile.Je kama kweli ni wao walikuwa
wanatafuta nini?Kwa nini wamuue
rais Anorld?Yawezekana yule
mama akawa anafahamu kitu”
akasema Mathew wakatoka na
kuingia katika gari la mathew
wakaondoka kuelekea Chalinze
kuonana na April Mubara mjane
wa rais Anorld huku sura ya Theresa ikioyesha wasiwasi
mkubwa sana
“Mathew hili jambo limeanza
kuniogopesha sana.Kwa haya
mambo niliyoyaona toka jana
nimeanza kuwa na
hofu.Inawezekana jambo hili
likawa kubwa zaidi ya uwezo
wetu.Kama Marekani imeanza
kujitokeza katika suala hili
inawezekana likawa ni suala
lililovuka hadi mipaka ya
nchi.Najiuliza vile vile hao
waliokuwepo serikalini kabla ya
dada Vivian kuingia madarakani
kwa nini hawakulishughulikia hili
suala na kuliacha liendelee kuwa
fumbo?Uchuguzi wa kuanguka kwa
ndege ya rais umeishia hewani,uchunguzi wa mauaji ya
baba umeishia hewani na viongozi
wako kimya,kuna nini hapa?
“Theresa hili suala kama
ulivyosema linaonekana kuvuka
mipaka ya nchi lakini haliwezi
kunishinda.Hata kama Marekani
wamehusika ninachohitaji
kukifahamu ni sababu ya wao
kufanya hivi
walivyofanya.Hawawezi kufanya
peke yao lazima kuna watu wa
humu nchini walioshirikiana nao
.Nakusihi usihofu nitakulinda”
akasema Mathew na uso wa
Theresa uliendelea kuonyesha
wasiwasi
“Tunaenda tena mahala
walikouliwa wazazi wangu.Sielewi nifanye nini.Natamani nimueleze
Mathew ukweli lakini
naogopa.Ngoja tu niendelee kukaa
na siri yangu.Waliofanya mambo
haya ni mtandao mrefu na wenye
nguvu na endapo wakigundua
kwamba na mimi nilikuwepo
katika matukio yote mawili lazima
wataniua haraka sana kwani pekee
ndiye niliyebaki hai ninayefahamu
nini kilichotokea.Naamini bado
wanaendelea kuitafuta
football.Hapaswi mtu yeyote
kufahamu siri hii.” Akawaza
Theresa.
****************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment