Simulizi : Scandle (Kashfa) (3)
Sehemu Ya Nne (4)
“Nataka nikujulishe kwamba..” akasema na kunyamaza akamtazama Yeremia
“Nataka nikujulishe kwamba nimetengua nafasi ya mkuu wa jeshi la polisi Tanzania na kuanzia muda huu Yeremia Mwaipopo si mkuu wa jeshi la polisi Tanzania na ninamvua vyeo vyote alivyonavyo.Atakayechukua nafasi hiyo nitamtangaza hapo baadayeo ! akasema Rais Festus na kukata simu.Yeremia alihisi kama nyundo kubwa imetua kichwani kwake akapiga magoti na kuinamisha kichwa
“Nilikuonya Yeremia kwamba nitafanya maamuzi magumu sana dhidi yako.Kuanzia sasa wewe si mkuu wa jeshi la polisi tena na nimekuvua vyeo vyako vyote utabaki kuwa askari wa kawaida ! akasema Rais Festus kwa ukali
“Mheshimiwa Rais huwezi ukanifanyia hivi.Kwa nini unataka kuniua mheshimiwa Rais?Umesahau yale yote mazuri niliyoyafanya mpaka unanifanyia hivi?Nimekuwa msaidizi wako mtiifu kwa muda mrefu kwa nini leo umenifanyia haya?
“Yeremia mimi na wewe tuna historia lakini kwa sasa tuko vitani na yeyote atakayenisaliti katika vita hii bila kujali ni nani
ninamuondoa hapo hapo na mapambano yanaendelea” akasema Yeremia
“Mathew huyo ni mtu wenu kwa sasa nataka aeleze kila kitu kuanzia mahala iliko simu ya Asajile na watu wanaoshirikiana nao ! akasema Rais festus na
kumtazama Yeremia kwa hasira
“Mathew nataka aeleze kila kitu huyu.Fanyeni kila mnachoweza kuhakikisha anasema kila kitu halafu mtanijulisha ! akasema Rais Festus na kuwaaga akina Mathew akaelekea katika helkopta yake akaondoka. “Yeremia umesikia alichokisema Rais.Kabla hatujafanya chochote nakupa nafasi ya kutueleza ukweli.Tueleze mahala iliko simu,kwa nini ukaificha? akasema Mathew.Bado Yeremia alikuwa amekaa chini haamini kilichokuwa kimetokea.
“Yeremia hatutaki kupoteza muda wetu kwa mara ya mwisho ninakuomba utueleze ukweli ! akasema Mathew lakini Yeremia hakujibu kitu
“Nawal uwanja ni wako.Ana bahati sana huyu ningekuwa katika hali yangu ya kawaida leo angezungumza hadi lugha asizozijua” akasema Mathew na Nawal akawaita makomando wawili akazungumza nao halafu wakaondoka na baada ya muda wakarejea wakiwa na meza kamba na mataulo.Makomando wale wakamfuata Yeremia aliyekuwa amekaa sakafuni akionekana kuchanganyikiwa wakamtaka asimame lakini aliendelea kukaa kana kwamba hakusikia alichoelekezwa.Ghafla akajikuta amenyanyuliwa akataka kuleta vurugu lakini akadhibitiwa na jamaa wale waliojazia vyema miili yao.Ndani ya nusu dakika tayari alikwisha vuliwa nguo akabakiwa na nguo ya ndani halafu akainuliwa na kuwekwa juu ya meza.Nawal alikuwa katika chumba kingine akitengeneza kitu Fulani.
Makomando wale
walimfunga Yeremia katika ile meza waliyoileta huku katika sehemu walikopitisha kamba wakiweka mataulo ili kuzuia ngozi kuchubuka.
“Yeremia tueleze ukweli tafadhali kabla hatujaanza kutumia nguvu ! akasema Mathew lakini Yeremia hakujibu chochote
Nawal akarejea pale sebuleni akiwa na kitu amekitengeneza akachomeka katika umeme na kufanya majaribio ya kugusanisha nyaya zikatoa cheche
“Nafasi ya mwisho
Yeremia” akasema Mathew “Fanyeni mnachotaka
kufanya lakini sintawaeleza chochote ! akasema Yeremia.Nawal akasogea na kuweka waya mmoja katika kidole na waya mwingine akaugusisha katika mdomo.Yeremia akatoa kilio kikubwa sana.
“Simu iko wapi Yeremia?Mathew akauliza.Nawal hakutaka kupoteza muda akarudia tena lile zoezi kwa mara ya pili lakini bado Yeremia hakusema chochote.Kwa hasira Nawal akaivuta ile nguo ya ndani akaichana halafu akagusisha waya mmoja katika uume na Yeremia akalia kama mtoto mdogo
“Simu iko wapi Yeremia? Akauliza Mathew
“Do it again ! akasema Mathew na Nawal akarejea tena lile zoezi.Wakati zoezi likiendelea simu ya Ruby ikaita akaipokea alikuwa ni Zari ambaye aliwataka warejee mara moja katika makazi yao kwani Asajile alikuwa tayari kuzungumza.Ruby akamuita Mathew pembeni akamueleza kile alichoambiwa na Zari.Wakajadiliana kwa muda mfupi na wakakubaliana warejee ili kuzungumza na Asajile.Yeremia akafunguliwa akavalishwa mavazi halafu wakaondoka kurejea katika kambi yao.
***************
Akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi,Bella alijulishwa na msaidizi wake kuhusu taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ikulu kwamba Rais amemuondoa katika nafasi yake mkuu wa jeshi la polisi na kumvua vyeo vyote.Bella akastuka na kutazama mtandaoni ambako aliikuta taarifa ile akampigia Gidion Benson mkurugenzi wa habari wa Rais kumuuliza kama taarifa ile iliyotumwa mtandaoni ni ya kweli akajulishwa kwamba ni kweli.Bella akahisi kutetemea mwili.
“Mambo yameanza
kuharibika kama Yeremia ametolewa katika nafasi yake lazima Rais kuna kitu amekifahamu kuhusu huu mpango wetu” akawaza na kumpigia simu Kasiano lakini simu yake haikupokelewa akampigia Rita akapokea
“Rita nataka kuzungumza
na Kasiano sasa hivi! akasema Bella
“Mama Bella Kasiano kwa sasa yuko katika ibada ya mazishi ya mchungaji Lucas”
“I don’t care, go and get him I need to talk to him now !
akasema Bella kwa ukali Baada ya muda mfupi
simu yake ikaita alikuwa ni Kasiano Bella hakupoteza muda akaipokea
“Kasiano nataka kufahamu
kitu kimoja tu je Asajile tayari ameondolea au bado? Akauliza Bella
“Mama Bella kwa taarifa niliyoipata kutoka kwa vijana kabla sijaingia kwenye ibada ni kwamba bado Asajile hajaondolewa” akajibu Kasiano
“Kwanini Kasiano?
Nimewapa taarifa zote
kwamba Godfrey ndiye anayefahamu mahala alipo kwa nini mpaka sasa hamjakamilisha kazi niliyowapa?Familia ya Godfrey bado haijatekwa kama nilivyoelekeza? Akauliza Bella
“Kila kitu kimefanyika mama Bella kama ulivyoelekeza.Familia ya Godfrey imeshachukuliwa na mchakato wa kumjulisha Godfrey ulikuwa unaendelea.Ngoja niwasiliane tena na vijana nijue wamefikia wapi”akasema Kasiano “Sikiliza
Kasiano,nimepokea taarifa mbaya sasa hivi kwamba Rais
amemvua madaraka mkuu wa
jeshi la polisi nchini mchana huu.Huyu ni mmoja wa washirika wangu na ndiye amenisaidia sana kujua mahala aliko Mathew na hata kumpata Asajile ni yeye aliyenisaidia hivyo kitendo hicho cha Rais kumuondoa katika nafasi hiyo ni kiashiria kwamba tayari Asajile amekwisha banwa na kutaja
watu alioshirikiana nao katika kumuua Frank.Kama amemtaja Yeremia basi hata mimi lazima atanitaja.Sitaki jambo hili lifike huko natoa hadi jioni ya leo Asajile awe ameuawa.Umenisikia
Kasiano?akauliza Bella
“Nimekuelewa mama Bella hilo litatekelezwa” akasema Kasiano na Bella akakata simu kwa hasira.Baada ya sekunde chache akapiga tena
“Mama Bella” akasema
Kasiano
“Kasiano kuna kitu nimekumbuka.Nani ambaye ulimtuma kwenda kwa Asajile kumchukua Frank?
“Nilimtuma naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Keofas Mabula”
“What? Bella akashangaa
“Kwa nini ukamtuma mtu mkubwa kamayule wakati vijana wapo?
“Ilihitaji ushawishi mkubwa kumshawishi Frank
akubali kutoa taarifa ndiyo maana nikamtuma Keofas” “Ulifanya kosa kubwa Kasiano.Asajile hakutakiwa kumfahamu mtu uliyemtuma kwake.Kwa kuwa naamini ameanza kuwataja watu anaoshirikiana nao lazima atamtaja pia Keofas.Hakuna namna nyingine muondoe
naye mara moja! Akasema Bella
“Mama Bella” akasema Kasiano akionekana kustushwa na kauli ile ya Bella
“Kasiano nimesema muondoe Keofas mara moja,kwa kuwa alionana na Asajile na ndiye mtu aliyemchukua Frank kutoka kwa Asajile tayari ni mtu hatari sana kwetu.Endapo Asajile akimtaja anaweza akakamtwa na akiteswa anaweza akaeleza kila kitu.Akikamatwa Keofas tumekwisha so finish him quick ! akasema Bella na kukata simu
“Hawa watu wanaweza wakaniweka mimi katika matatizo kwa kuendelea kumuacha Asajile hai.Mbona mambo yameanza kuharibika? Sikutegemea kama suala hili lingefika hapa lilipofika lakini ukosefu wa umakini wa Asajile umeanza kutugharimu.Ninajuta kwa nini nilimshirikisha katika mpango huu” akawaza Bella halafu akachukua simu akampigia baba yake
“Bella nilikuwa na mpango wa kukupigia lakini nikapata wageni.Mambo gani haya anayoyafanya mumeo siku hizi? Jana tu ametoka kukiri hadharani kuwa ana mtoto wa nje ya ndoa na kabla hilo halijapoa leo hii picha zake za faragha zinavuja.Aibu gani hii!
Nini anataka kutuonyesha?Anataka tufahamu kuwa yeye ni
kidume?Amesahau kwamba yeye ni Rais na watu wote wanamuangalia yeye? Nimekasirika sana Bella ! akasema baba yake kwa ukali
“Baba kuna kitu
kinaendelea hivi sasa na ndiyo maana haya unayoyaona yametokea” akasema Bella
“Kuna kitu gani kinaendelea Bella? Akauliza Dr Fernando Dambara baba mzazi wa Bella.
Bella alimueleza kuhusiana na Mathew Mulumbi alivyoanza kuwachunguza na mahala
walikofika hadi picha zile zikasambazwa
“Kwa hiyo baba sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuzisambaza picha hizo ili kumvuruga na kumfanya ajielekeze zaidi katika suala hilo na kusahau vita inayoendelea ili sisi tupate nafasi ya kuwatafuta hao watu anaowatumia kutusaka” akasema Bella
“Bella nakupongeza kwa akili hiyo uliyoitumia.Wewe ni mwanafunzi wangu mzuri na ninajivunia tofauti na hawa ndugu zako wengine.Lakini kwa nini hukuniomba msaada
wangu muda mrefu
nikusaidie? Suala hili lingekwisha malizika na wala kusingekuwa na tatizo lolote tena” akasema Dr Fernando
“Baba nitakuja kwako kuomba msaada wako pale ambapo nitaona mambo yananiendea vibaya kama hivi sasa”
“Nini unahitaji nikusaidie?
“I need you to back me up.Nafahamu Festus anakuogopa sana hivyo pale mambo yatakapoharibika nataka utumie nguvu yako kunikingia kifua.Najua Asajile anaweza akanitaja na ninaweza nikaulizwa nilifahamuje kama Mathew Mulumbi yuko SNSA nitasema kwamba nilikuomba msaada na wewe ndiye uliyenisaidia kujua kama Mathew Mulumbi yuko SNSA.Mambo yakiharibika baba naomba uinunue hii kesi na uimalize”akasema Bella
“Usijali Bella nafahamu umuhimu wa uwepo wako hapo ikulu na pale mambo yatakapoharibika nijulishe nami nitalimaliza hilo jambo mara moja” akasema Dr Fernando Dambara
“Ahsante baba.Ninaelekea ikulu sasa” akasema Bella na kukata simu
“Nimelazimika
kutengeneza mazingira ya kujikinga mapema kwani sijui nini kitatokea huko mbele” akawaza Bella na kuchukua
mkoba wake akatoka kuelekea ikulu
Mathew na wenzake walipatwa na mshangao mkubwa baada ya kufika katika kambi yao yao na kuikuta familia ya Asajile ikiwa sebuleni.Pamoja nao alikuwepo pia Godfrey mlinzi wa Rais
“Nini kinaendelea hapa? Familia ya Asajile wamefikaje hapa? Akauliza Mathew
“Mathew samahani sana
kwa hiki kilichotokea ninaomba niwe wa kwanza kueleza tafadhali” akasema Godfrey.Ruby akawachukua familia ya Asajile akawapeleka katika chumba kingine
“Asubuhi ya leo baada ya kuileta ile kompyuta niliyotumwa na Rais nilianza safari ya kurejea ikulu nilipigiwa simu na mtu nisiyemfahamu akanieleza kwamba wanaishikilia familia yangu.Nilidhani utani nikaomba wanipe mke wangu nizungumze naye
akanithibtishia kweli wametekwa.Wale jamaa wakanitaka nifuate maelekezo watakayonipa.Walielekeza niende sehemu Fulani nitakuta gari niingie nikafanya hivyo na
nilipoingia katika hilo gari wakanivisha mfuko kichwani sikujua mahala wanakonipeleka.Nilifikishwa katika nyumba mahala walikokuwa wanawashikilia familia yangu na wakanitaka ili niwakomboe familia yangu niwaonyeshe mahala alipo Asajile.Nilifahamu Asajile yuko hapa hivyo
nikawadanganya kwamba Asajile yuko katika kambi ya jeshi na mimi pekee ndiye ninayeweza kwenda kumchukua huko mahala aliko wakanipa maelekezo ya kufanya nikaja mpaka hapa na kumdanganya mlinzi niliyemkuta kwamba Rais amenituma nije kumchukua Asajile kumbe nilikuwa ninampeleka kwa wale jamaa” Godfrey akawaeleza kila kitu kilichotokea baada ya kumfikisha Asajile kwa wale jamaa
“Baada ya kutoka kule tukaenda nyumbani kwangu nikachukua gari lingine halafu tukaenda kwa Asajile kuichukua familia yake na kuileta hapa ndipo tukapata msaada kutoka kwa walinzi tukazungumza na Zari akatueleza kwamba kwa sasa hawezi kuja kwani amebanwa na majukumu ofisini kwake ndipo akawasiliana nanyi na kuwajulisha kwamba tuko hapa” akasema Godfrey
“Pole sana Godfrey kwa
tukio hilo lililokupata” akasema Mathew na kumgeukia Asajile
“Mathew Mulumbi
ninaomba samahani sana kwa kuileta hapa familia yangu hapa bila ruhusa yenu lakini nimelazimika kuwaleta hapa kwani ni sehemu salama kwao kwa sasa.Nisameheni sana na ninaomba muwapokee” akasema Asajile Mathew hakumjibu kitu akabaki anamtazama
“Umegundua sasa kwamba hapa ndiyo sehemu salama? Akauliza
“I’m ready to talk Mathew ! akasema Asajile
“Nini kimekubadili mawazo? Kwa nini umetuacha tukawa na mzunguko mrefu wakati ulikuwa na nafasi ya kutueleza kila kitu mapema? Akauliza Mathew
“Naombeni mnisamehe
sana lakini sikutambua kama niko katika hatari kubwa kiasi hiki.Baada ya Godfrey kuniokoa ndipo nilipogundua kwamba niko katika hatari kubwa na nikaamua kuwaeleza ukweli”akasema Asajile
“Sawa tueleze kile unachotaka kutueleza.Kabla ya yote nataka Yeremia naye aletwe humu ndani” akasema Mathew na Yeremia akaletwa.Wote wawili walipatwa na mshangao wa mwaka walipoonana
“Haya anza kutueleza unachotaka kutueleza”akasema Mathew
“Nilipigiwa simu usiku na mke wa Rais mama Bella akaniambia kwamba anataka tuonane kesho yake yaani jana.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mama Bella kunipigia simu.Jana asubuhi akanipigia tena simu akanitaka nimfuate ofisini kwake nikaenda na kumkuta akiwa na
mkuu wa jeshi la polisi Yeremia Mwaipopo” akanyamaza baada ya Mathew na akina Nawal kutazamana
“Endelea” akasema Mathew
“Bella alinieleza kwamba kuna watu wanazo picha za faragha za Rais na wanataka kuzisambaza.Akasema watu hao wametoa madai ili wasiweze kuzisambaza hizo picha lakini Rais amekataa kutekeleza madai yao hivyo wameamua wao kwa siri kuyatekeleza madai ya hao jamaa ili kuzuia picha hizo za Rais zisisambazawe na wakaniomba niungane nao ili kumnusuru Rais na aibu endapo picha zake zingevuja.Nilikubali kujiunga nao kwani niliamini kitu tunachokifanya ni kizuri kwa ajili ya kuzuia Rais asidhalilike.Wakaniambia kwamba watu hao wenye picha za Rais wanamtaka Mathew Mulumbi ambaye tayari wamekwisha pata taarifa kwamba yuko katika jengo la SNSA.Wakaniambia kwamba kuna mfungwa amefungwa
katika gereza la siri anaitwa Frank wanamuhitaji ili aweze kusaidia kutoa taarifa za namna ya kuweza kuingia
ndani ya hilo jengo na
kumchukua Mathew.Kwa kuwa niliamini ninafanya jambo jema kwa ajili ya Rais nikakubali na kumtoa Frank gerezani nikawakabidhi ili akawape msaada na baadae arudishwe gerezani” akasema Asajile na kunyamaza akatazama chini.
“Nini kiliendelea? Akauliza Mathew
“Walimrejesha Frank
lakini akiwa tayari amefariki na baada ya hapo mzigo wote ukaniangukia mimi na baadaye wakataka kuniua” akanyamaza na kutazama tena chini.
“Ningejua kama mambo yangekuwa namna hii katu nisingekubali kushirikiana nao.Wamenirubuni na kuniharibia maisha yangu” akasema Asajile huku akimtazama Yeremia kwa jicho la hasira.
“Hili jambo mbona linazidi kuwa kubwa.Hadi mke wa Rais naye yuko ndani ! akawaza Mathew na kumtazama
Yeremia aliyekuwa ana hofu kubwa
“Yeremia usiogope tena tayari Asajile ameamua kufunguka na kutueleza kila kitu.Tunachohitaji ni kusikia kwa upande wako pia ukweli wote.Asajile amejieleza vizuri kwamba wewe na mke wa Rais ndio mliomshawishi aungane nanyi katika mpango wenu wa kuzuia picha za Rais zisisambazwe.Nini unataka kutueleza? Akauliza Mathew.Yeremia alikuwa anatetemeka midomo
“Relax Yeremia and tell us the truth” akasema Bella
“Yeremia hakuna haja ya kuficha chochoteni wakati wa kueleza ukweli” akasema Asajile.Yeremia akafikiri kidogo halafu akasema
“Nilipigiwa simu na mke wa Rais” akasema na kunyamaza
“Mke wa rais tena” akawaza Mathew
“Akanitaka niende ofisini kwake nikaenda na kumkuta akiwa na viongozi wawili wa chama.Akanieleza kwamba kuna picha za faragha za Rais ametumiwa katibu mkuu wa chama na watumaji wametishia kuzisambaza picha hizo endapo Rais hatatekeleza madai yao.Akadai kwamba Rais amegoma kutekeleza madai ya wale jamaa hivyo basi wao ameamua kuungana ili kutekeleza madai ya wale jamaa kwa siri na kuzuia picha zile za faragha za Rais kusambaa.Niliona ni jambo jema nikajiunga nao na tukaanza mikakati ya namna ya kutekeleza mpango wa kukupata wewe Mathew ambaye hatukujua ulikuwa wapi.Bella akazungumza na wale jamaa akawataka wasisambaze kwanza picha za Rais ili ashughulikie kumpata Mathew Mulumbi” akanyamaza na baada ya muda akaendelea
“Alinipigia tena simu juzi usiku akaniambia kwamba tayari amefahamu mahala alipo Mathew Mulumbi katika jengo la SNSA akaniuliza kama ninalifahamu gereza la siri kwani kuna mtu anamuhitaji ili kupata taarifa za muhimu nikamjibu kwamba silifahamu gereza hilo nikamuelekeza kwamba liko chini ya idara ya kupambana na ugaidi na kama kuna kitu anahitaji basi amuulize Asajile nikampa namba zake awasiliane naye na tukapanga kuonana kesho yake ofisini kwake.Jana tukakutana na Asajile ofisini kwa mama Bella na yakatokea kama aliyoyazugumza Asajile” akanyamaza kidogo
“Usiku akanipigia simu
Rais na kunitaka nitume askari nyumbani kwa Asajile wakachukue kompyuta zake na simu ili kumchukunguza kujua anashirikiana na akina nani.Niliogopa sana na badala ya kutuma askari wadogo nikaenda mimi mwenyewe nikachukua kompyuta na simu nikaificha kwa kuhofia kujulikana kama ninashirikiana na Asajile.Kwa ufupi ni hivyo.Mimi na Asajile tuliingizwa katika jambo hili na Bella mke wa Rais kwa lengo la kuzuia picha za faragha Rais zisisambazwe” akasema Yeremia
“Kwa nini hamkuyasema haya mapema hadi mkasubiri mambo yakawaharibikia? Akauliza Mathew Mulumbi
“Sisi wote wawili ni watu wa karibu na Rais na hofu yetu kubwa ilikuwa ni endapo Rais angefahamu tuna mpango wa siri tunaufanya angekasirika sana ndiyo maana tukawa kimya lakini kwa sasa kila kitu kimeharibika,picha za Rais zimevuja,kazi tumepoteza hivyo hakuna haja ya kuficha kitu tena” akasema Yeremia
“Ninyi ni wakubwa zangu ni wazee wangu lakini
mtanisamehe kwa maneno yangu lakini hiki
mlichokifanya ni kitu cha kipumbavu.Mnawezaje mkafanya kitu kama hicho watu wakubwa kama ninyi? Hamkujua kama jambo hili linaweza kuvuja na kuwaweka katika matatizo? Isitoshe ninyi ni wateule wa Rais amewaamini sana na kuwapa dhamana mumsaidie,badala yake mnamzunguka na kufanya mambo yenu kwa siri bila yeye kujua.Kama leo hii mmeshawishiwa na mke wa Rais mkakubali kumzunguka Rais na mkawa na mpango wa siri kesho akitokea mtu akawashawishi na kuwataka mshiriki katika mapinduzi ya kumuondoa Rais madarakani mtakataa? Mlichokifanya ni usaliti na mnastahili haya mliyoyapata na hata zaidi! akasema Mathew kwa ukali
“Lakini tulichokifanya ni kwa ajili ya kuzuia Rais asidhalilike kwa picha zake za faragha kusambaa ! akasema Yeremia
“Hiyo siyo sababu ya kujitetea.Hamna utetezi wowote katika hili mlilolifanya.Kama Rais mwenyewe alilijua hilo na akakataa kata kata kukubaliana na madai waliyoyatoa hao jamaa waliokuwa na picha zake ninyi ni nani wa kuwa na uchungu zaidi yake hadi mkawa na mipango ya siri? Mnajua kile kinachoendelea nyuma ya pazia?Mnajua kwa nini Rais alikataa kukubaliana na madai ya hao jamaa na akawa tayari picha zake za faragha zisambazwe? Mnajua kwa nini Rais alikubali kuvumilia aibu hii kubwa aliyoipata? Mathew akauliza
“Nina hasira nanyi kwa kuwa mlikuwa tayari kunitoa kafara kwa hao jamaa na mnajua wangenifanya nini? Wangeniua na hicho ndicho kitu wanachokihitaji” akasema Mathew
“Kikubwa tulichokuwa tunakitaka ni kumuepusha Rais na aibu! Akasema Yeremia
“Wakubwa zangu tuko vitani.Watu tunaopambana nao ni genge la watu hatari wafanyabiasha wa dawa za kulevya wenye kundi lao linaitwa Black Mafia ambao wamekuwa wakiendesha mambo mbali mbali ya kihalifu hapa nchini yakiwamo mauaji,kutengenezea watu kesi kubwa kubwa na wakafungwa kama walivyonifanyia mimi na DrFabian ambaye yuko mahabusu hivi sasa.Kuna mwenzetu mmoja yuko gerezani anatumikia kifungo cha maisha ametengenezewa kesi na hawa jamaa.Jana nimefanyiwa upasuaji baada ya kupigwa risasi tatu na hao hao jamaa.Hii ni vita mbaya sana na mlipaswa kuwa karibu na Rais mkaungana naye badala yake mkazunguka na kuungana na maadui na kwa hili mmemkasirisha sana Rais ndiyo maana akachukua maamuzi magumu kama aliyoyafanya ya kuwavua nyadhifa zenu na muombe mambo yaishie hapa kwani yakiendelea mtaozea gerezani” akasema Mathew
“Mathew nakubali
tumekosea sana japo tulifanya kwa nia njema…” akasema Yeremia lakini Mathew akamkatisha
“Nimesema sitaki kusikia utetezi huo ! akasema Mathew kwa ukali na kufumba macho kwa maumivu aliyoyapata “Relax Mathew” akasema Nawal
“Ninyi nyote hatima yenu inamtegemea Rais.Kwa sasa tutaendelea kuwashikilia hapa tukisubiri maelekezo ya Rais na muombeni sana Mungu wenu labda Rais anaweza akawasamehe lakini kwa hiki mlichokifanya mnastahili haya yaliyowakuta.Stupid ! akasema Mathew kwa ukali
“Mna bahati sana wakubwa zangu mmenikuta katika hali hii ya maumivu makubwa lakini ninaapa sijui ningewafanya nini ! akasema Mathew ukapita ukimya mfupi Asajile akainua kichwa na kusema
“Mathew mimi nimekuwa mtumishi mwaminifu katika kazi yangu na sina rekodi zozote mbaya hii ni mara yangu ya kwanza nimejikuta katika jambo hili na nimeingia baada ya kushawishiwa na hawa watu wawili Yeremia na Bella.Siyasemi haya kama utetezi kwani ninastahili adhabu kwa kosa nililolifanya na simlaumu Rais kwa hatua hii aliyochukua ya kunivua madaraka na kwa hatua nyingine zitakazofuata lakini pamoja na hayo ninataka kukuomba unipe nafasi ya kusaidia japo kidogo katika hili suala.Kuna taarifa ambayo nitakupa inaweza ikasaidia katika kuwapata hao jamaa mnaowatafuta” akasema Asajile na Mathew akafikiri kidogo akauliza
“Taarifa gani unayo unadhani inaweza ikasaidia?
“Baada ya kukubaliana na mpango wa akina Bella kuna mtu alitumwa ofisini kwangu kwa ajili ya kumchukua Frank.Mtu huyo ni naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Keofas Mabula.Huyu ndiye aliyeondoka na Frank na kumrudisha akiwa tayari amefariki dunia.Mkimpata huyu atawapa maelezo mengi.Mtafuteni tafadhali” akasema Asajile
“Naibu waziri Keofas
Mabula? Mathew akauliza
“Ndiyo.Yeye ndiye aliyetumwa kwangu kuja kumchukua Frank na kumpeleka mahala nisikokujua wakamuhoji na kumuua” akasema Asajile
“Keofas naye ni mshiriki katika mpango huu? Yeremia akauliza
“Ndiyo” akajibu Asajile
“Yeremia unajifanya kushangaa hujui kama Keofas ni mmoja wa watu wenu? Mathew akauliza
“Bella hajawahi kunieleza hata mara moja kama Keofas
naye ni mshiriki katika mpango huu.Nilifahamu mpango huu una watu watano tu,mimi,Bella,wale viongozi wawili wa chama na Asajile lakini kumbe Keofas naye yumo.Bella alitengeneza mtandao mkubwa wa jambo hili” akasema Yeremia
“Ahsante kwa taarifa hii Asajile.Kitu muhimu kwa sasa ni kumpata Keofas Mabula.Tunalifanya zoezi hilo lakini ninyi mtaendelea kuwepo hapa tukisubiri maelekezo ya Rais” akasema Mathew na kuelekeza akina Asajile wapelekwe katika vyumba wakapumzike wakati wakisubiri maelekezo ya Rais “Hapa nilipo mwili wote unanitetemeka.Mke wa Rais naye anahusika katika jambo hili! Sikutegemea kabisa” Akasema Nawal
“Ni jambo la kushangaza mno.Hata Rais akisikia atapatwa na mshangao
mkubwa sana.Hakuna
aliyewahi kufikiria kitu kama hiki kinaweza kutokea” akasema Mathew
“Lakini yawezekana walitaka kufanya jambo hilo kwa nia njema ya kuzuia picha za Rais kuvuja” akasema Ruby “Ruby nimekataa huo utetezi.Rais mwenyewe amekubali picha zake zisambazwe wao ni akina nani wa kupingana na Rais? Wawe walifanya kwa nia njema au vinginevyo lakini walichokifanya hakikubaliki.Tuko vitani halafu kumbe kuna watu wa karibu na Rais ambao wanamzunguka na kumkwamisha na ndiyo maana mtaona kila tunapopiga hatua tunajikuta tukirudishwa nyuma ! Nadhani sasa mnauona ugumu wa vita hii”akasema Mathew kwa ukali
“Kuna mambo kadhaa
tunayotakiwa kuyafanya kwa sasa.Kwanza tunatakiwa kumjulisha Rais kuhusu suala hili na atusaidie kumpata Keofas.Kwa namna mtiririko unavyokwenda inaonyesha Keofas ndiye aliyemchukua Frank kutoka kwa Asajile na kumpeleka aidha kwa Black Mafia au kwa watu wengine lakini tukimpata atatueleza vizuri alimpeleka wapi.Jambo lingine ambalo tunatakiwa kulishughulikia ni kuitafuta familia ya Godfrey.Ndugu zangu tusingeweza kufika hapa bila maamuzi magumu ya Godfrey.Nakuhakikishia mdogo wangu tutaipata familia yako.Wakati huo huo Ruby endelea na ile kazi niliyokupa ya kutafuta zile taarifa lakini kabla ya yote mpigie simu Rais nataka kuzungumza naye” akasema Mathew na Ruby akapiga simu kwa Rais ****************
Bella alifika ikulu na moja kwa moja akaelekea katika ofisi ya Rais.Hakuna aliyemzuia akaingia ndani ya ofisi na kumkuta Rais Festus akiwa ameegemea kiti akiwa na mawazo mengi sana.Ni muda mrefu Bella hakuwa ameingia katika ofisi ile ya Rais
“Hello Mr President ! akasema Bella
“Bella karibu” akasema
Festus
“Festus tafadhali suala hili lisikuumize sana kichwa chako.Try to relax.Tabasamu kama kawaida yako” akasema Bella
“Bella huu si wakati wa kutabasamu.Suala hili ni kubwa sana zaidi ya tunavyolichukulia” akasema Festus
“Suala hili litapita Festus.Umesikiliza maelezo yangu niliyoyatoa kwa waandishi wa habari? Akauliza
Bella
“Hapana sijasikiliza kitu chochote.Sitaki leo kutazama luninga wala kusikiliza redio,sitaki kitu chochote” akasema Festus
“Festus usihofu tena,hili jambo tayari nimelikata makali” akasema Bella na kutoa diski mweko akaichomeka katika kompyuta ya Rais na kucheza video ile iliyorekodiwa wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake.Festus akasikiliza hotuba ile na kumgeukia Bella
“Bella hukutakiwa kufanya hivi” akasema Festus
“Festus uliniambia nifanye kila niwezalo kulipunguza makali jambo hili na ndivyo nilivyofanya na kwa sasa anayeonekana mjinga ni yule aliyesambaza picha hizo” akasema Bella huku akimsugua sugua Festus mgongoni
“Festus tutalivuka jambo hili pamoja.Naomba tuendelee kusimama pamoja hadi mwisho wake.Tunachotakiwa ni kuonyesha mshikamano mkubwa” akasema Bella
“Bella ninakushukuru kwa
hili ulilolifanya japo halijamaliza tatizo lakini kwa kiasi Fulani limepunguza ukali wake ila bado suala ni bichi.Kila ninakopita najiona kama niko mtupu” akasema Festus
“Festus kuna taarifa nimeisikia kuhusiana na Yeremia imenistua sana”akasema Bella “Taarifa ipi?
“Je ni kweli umemuondoa katika nafasi yake ya mkuu wa jeshi la polisi na kumvua vyeo vyote? Akauliza Bella
“Ndiyo nimefanya hivyo” akajibu Rais Festus
“Festus kwa nini ukafanya hivyo? Yeremia ni mtu ambaye amekuwa anakusaidia sana katika mambo mbali mbali.Hukupaswa kumfanyia kitu kama hicho” akasema Bella
“Bella nafahamu wewe na Yeremia ni marafiki wa karibu sana na ni wewe uliyenishauri nimchague kuwa mkuu wa jeshi la polisi.Pamoja na ukaribu mlio nao pamoja na uchapakazi wake nimemuondoa katika nafasi yake na kumvua vyeo vyake vyote.Nahitaji kufanya kazi na watu waaminifu.Yeyote ambaye atakwenda kinyume na mimi hata awe nani atakwenda na maji.Kuanzia sasa sintakuwa na huruma na mtu yeyote Yule
atakayenisaliti! Akanyamaza Rais Festus
“Festus ulichokifanya umekosea sana.Yeremia ni mtu ambaye hakustahili hiki ulichomfanyia.Ninakuomba Festus niko chini ya miguu yako give him another chance.Sitaki kujua amekosea wapi lakini nakuomba umpe tena nafasi nyingine.Amelitumikia jeshi kwa muda huu wote amebakisha miaka miwili astaafu unataka astaafu kwa fedheha namna hii?Bella akauliza
“Yeremia hatastaafu akiwa ndani ya jeshi la polisi atakuwa gerezani ! akasema Festus na
Bella akastuka sana
“Kwani kafanya nini hadi umemchukia na kuchukua maamuzi makubwa namna
hii? Akauliza Bella
“Siwezi kukwambia kwa
sasa Bella”
“Yeremia ni kama kaka yangu hivyo nahitaji kujua alichokifanya”akasema Bella
Kabla festus hajasema chochote simu yake ikaita akamtaka Bella kwenda nyumbani atamfuata huko kuzungumza naye.Mara tu Bella alipotoka akaipokea ile simu
“Hallow Ruby” akasema
Rais Festus
“Mheshimiwa Rais ni mimi Mathew.Samahani nataka kujua kama hapo ulipo kuna watu wengine karibu”
“Niko peke yangu ofisini kwangu.Kuna nini Mathew? Akauliza Rais Festus
“Kuna jambo kubwa
ninataka kukueleza ndiyo maana nikataka kwanza kufahamu kama uko peke yako”
“Endelea niko peke yangu” akasema Rais
“Mara tu ulipoondoka kule shambani tulipokea simu kutoka kwa Zari akatutaka turejee hapa Asajile anataka kuzungumza nasi.Tulirejea hapa lakini tukaikuta pia familia yake iko hapa na ndipo tukaelezwa kile kilichokuwa kimetokea” Mathew akachukua muda na kumueleza Rais kila kitu walichoelezwa na akina Asajile na Yeremia.
“Mathew haya
unayonieleza…oh my God ! Rais Yeremia akajikuta akikosa neno la kusema
“Mathew nimekosa neno la kusema nahisi labda masikio yangu yananidanganya kwa hiki nilichokisikia” akasema Festus
“Mheshimiwa Rais mstuko ulioupata kila mtu hapa ameupata nadhani sasa unaweza ukaona ni kwa
namna gani suala hili lilivyo kubwa.Hakuna aliyetegemea kama mama Bella naye angekuwa anahusika katika suala hili”akasema Mathew
“Mathew nimezidi
kuchanganyikiwa na sijui nifanye nini.Hebu nishauri nini tukifanye kwani akili yangu nahisi imekwama.Mambo yaliyoko kichwani kwangu leo ni mengi na makubwa” akasema Festus
“Mheshimiwa Rais kitu cha kwanza ambacho tunataka utusaidie ni kumpata naibu waziri Keofas Mabula.Huyu tunataka tumuhoji tujue alimpeleka wapi Frank baada ya kumchukua kutoka kwa Asajile.Mheshimiwa Rais huyu ni mtu muhimu sana kwetu kumpata tena kwa haraka.Pili tunataka kuitafuta familia ya Godfrey ambao wametekwa.Godfrey ndiye aliyesababisha tukayafahamu haya yote.Tatu kama itawezekana tunataka kumuhoji pia mama Bella” akasema Mathew
“Mathew nakubaliana na mawazo yako.Nitampigia simu Keofas sasa hivi na kuongea naye kujua yuko wapi halafu nitatengeneza mtego ili akamatwe na nitamkabidhi kwenu.Kuhusu Bella huyu nitamuhoji kwanza mimi mwenyewe ndipo nimkabidhi kwenu.Mathew ahsante sana kwa kuniamsha toka usingizini.Nilikuwa nimelala na sikuelewa mambo yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya pazia.Sikujua kama nimezungukwa na nyoka wenye vichwa vya wanadamu.Bila wewe na wenzako haya yote nisingeyafahamu.Kwa kuwa bado kazi inaendelea sitaki kusema sana ngoja nimpigie simu Keofas nijue mahala alipo halafu nitakujulisha akishakamatwa” akasema Rais Festus na kukata simu
“Taarifa hii ni nzito hadi ninahisi joto” akawaza na kwa haraka akazitafuta namba za naibu waziri Keofas Mabula akampigia
“Mheshimiwa Rais shikamoo”
“Marahaba Keofas unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri mheshimiwa Rais” “Keofas nimekupigia kuna jambo nataka tuzungumze,uko wapi sasa hivi?
“Kwa sasa niko hotelini ninapata chakula mheshimiwa Rais”
“Vizuri sana.Nadhani umekwisha sikia kuwa nimemuondoa mkuu wa jeshi la polisi na kumvua vyeo vyake vyote”
“Ndiyo mheshimiwa Rais
nimesikia taarifa hizo”
“Kwa kuwa wewe uko
karibu na maafisa wengi wa polisi ninataka unisaidie kunipa mapendekezo ya nani unadhani anaweza akafaa kupewa nafasi hiyo.Nataka majina matatu.Unaweza ukanisadia kwa hilo?
“Ndiyo mheshimiwa Rais”
“Vizuri sana.Kuna mtu nitamtuma ofisini kwako muda si mrefu atakuja kuyachukua majina hayo”akasema Rais
“Sawa mheshimiwa Rais ninaelekea ofisini kwangu na mtu huyo atanikuta hapo” akasema Keofas na Rais akakata simu halafu akampigia simu mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa akamtaka atume vijana wanne waende katika wizara ya mambo ya ndani ya nchi wakamchukue naibu waziri wa mambo ya ndani Keofas Mabula na wakisha mpata atawapa maelekezo.Kisha toa maelekezo hayo Rais akampigia simu Mathew akampa mrejesho na kumtaka waanze kujiandaa kwani muda si mrefu watampata Keofas.
Rais Festus akatoka ofisini akaelekea moja kwa moja chumbani kwa mke wake Bella.Akaufungua mlango na kumkuta Bella akizungumza na simu na mara tu alipoiona sura ya mume wake akakata ile simu na kuitupa kitandani
“Festus kuna nini?Mbona umebadilika hivyo? Akauliza Bella.
Kwa hasira Festus akamfuata akamkamata mikono akampeleka ukutani na kumkaba shingo
“I’m going to kill you today
! akasema Festus kwa hasira “F.f….fff …estu ! akasema Bella kwa taabu na kumpiga Festus teke katika korodani akamuachia
“Monster ! You want to kill me? Akauliza Bella kwa hasira.Bado Festus alikuwa
ameinama akisikilizia maumivu
“Kitu gani kimekuingia Festus hadi ukaniumiza namna hii? Akauliza Bella na Festus akainuka na kumtazama kwa hasira
“You are a snake Bella.A cobra ! akasema Festus kwa ukali
“Ulidhani sintaifahamu mipango yako? akauliza
“Mipango gani Festus? Akauliza Bella
“Sitaki maigizo yako tayari ninafahamu kila kitu ulichokifanya wewe na hao wenzako Asajile na Yeremia.Tayari wamekiri na kueleza kila kitu mlichokifanya ! akasema Festus akimtazama mke wake kwa macho yaliyojaa hasira
“Kwa nini Bella? Kwa nini ukanizunguka na kufanya haya uliyoyafanya? Akauliza Festus na Bella akabaki kimya.
“Bella sikutegemea kabisa katika watu wote kama nawe unaweza ukawa ni miongoni mwa nyoka wenye vichwa vya wanadamu wanaonizunguka ! akasema Festus
“Okay Festus sit down.Let’s talk.Nitakueleza kila kitu ! akasema Bella kwa sauti yenye kitetemeshi.Aliingiwa na woga mkubwa.
“Kaa chini Festus
nikueleze kila kitu halafu utaamua mwenyewe nini cha kufanya” akasema Bella na Festus akaketi
“Nilifuatwa na katibu mkuu wa chama mzee Simba akiwa na makamu mwenyekiti wakanieleza kwamba kuna mtu amemtumia mzee Simba picha zako za faragha na kumtaka azifishe kwako ili wakupe madai yao.Mzee Simba akanionyesha picha hizo katika komputa yake na kunieleza kwamba umekataa kutekeleza madai ya hao jamaa na hivyo wanakwenda kuzisambaza hizo picha.Wazee wale wakanieleza kwamba endapo picha hizo zitasambazwa kutakuwa na athari kubwa katika chama kwani wanategemea kukusimamisha wewe tena katika uchaguzi mkuu ujao hivyo hawataki uingie katika kashfa ya aina yoyote ile kabla ya uchaguzo.Walinitaka nishiriki katika mpango wa siri wa kuzuia picha zile zisisambazwe.Njia pekee ya kuzuia picha hizo zisisambazwe ni kwa kuwapa hao jamaa kile walichokuwa wanakihitaji yaani Mathew Mulumbi na hapo ndipo tukaanza mipango ya kumtafuta Mathew ili kumkabidhi kwa hao jamaa kuzuia picha zile kusambazwa” akasema Bella na kumtazama Festus aliyekuwa amefura hasira
“I’m sorry Festus tulifanya mambo haya kwa siri bila wewe kujua lakini tulifanya kwa nia njema ya kukuepusha wewe na familia yetu na aibu hii kubwa.Kwa bahati mbaya mpango wetu haujaweza kufanikiwa kwani tulimkosa Mathew Mulumbi na wale jamaa wakazisambaza picha hizo kama walivyokuwa wameahidi”akasema Bella
“Kwa nini Bella ukaamua kufanya jambo kama hili? Kwa nini umeyaharibu maisha yako? Hujui ni kitu gani ulichoshiriki kukifanya.Bella kwa nini lakini?! Akasema Festus huku akigonga meza ndogo kwa hasira
“Bella hakuna namna unayoweza ukajitetea kwa hiki mlichokifanya wewe na wenzako.Nilipopata taarifa hizi kuwa wewe nawe unashiriki katika jambo hili nilidhani labda masikio yangu yananidanganya nilistuka sana kwani katika watu wote sikutegemea kama nawe ungeweza kushiriki katika mpango kama huu.Kama umeweza kuwaunganisha watu wengine ni wakuu wa taasisi nyeti kabisa mkafanya mambo ya kijinga ya kihalifu huwezi ukashindwa hata kuunganisha watu mkaniua! Akasema
Festus
“Festus nilichokifanya ni mwanamke yeyote anayejitambua angeweza kukifanya.Unadhani aibu hii uliyotupa mimi na wanangu ni ndogo?Yote haya umeyasababisha wewe mwenyewe kwa kupenda kwako wanawake.Hii si sawa hata kidogo jambo ufanye wewe halafu aibu tuipate sisi ndiyo maana nikafanya vile nilivyofanya.Japo sikufanikiwa lakini nilijaribu!
“Bella unaongea kama vile
jambo hili ulilolifanya ni jepesi lakini laiti ungejua kinachokuja huko mbele yako ungelia machozi ya damu.Bella umeshiriki katika mauaji.Watu zaidi ya kumi wameuawa katika jengo la SNSA kwa sababu yako wewe na wenzako.Unafikiri damu ya watu hao itakuacha salama?Ninajuta kwa nini nilikutana na kukuoa nyoka kama wewe ! akasema Festus
“Bella umefika mwisho.Umeyaharibu maisha yako wewe mwenyewe.Kwa hili mlilolifanya wewe na wenzako hamtakuwa salama” Festus akanyamaza baada ya simu yake kuita alikuwa ni mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa
“Jonas zoezi limekamilika? Akauliza Rais Festus
“Mheshimiwa Rais kuna
tatizo limetokea”
“Tatizo gani Jonas?
Akauliza Rais huku akitoka nje ya kile chumba cha Bella
“Nimetaarifiwa na vijana kwamba wakati wakielekea wizara ya mambo ya ndani kama nilivyowatuma walipata taarifa kwamba naibu waziri Keofas Mabula ameuawa hotelini muda mfupi uliopita.Vijana wakalazimika kwenda hotelini hapo na kukuta kweli Keofas,mlinzi na dereva wake wote wamepigwa risasi na kuuawa.Inadaiwa waliotekeleza mauaji hayo ni watu wawili waliofika hotelini hapo wakiwa na piki piki na baada ya kufanya mauaji hayo wakakimbia”akasema Jonas mkurugenzi wa idara ya usalama wa Taifa
Taarifa ile iligonga kichwani kwa Rais Festus kama chuma kigumu.Kwa sekunde kadhaa alibaki kimya huku simu ikiwa sikioni
“Mheshimiwa Rais” akasema Jonas
“Jonas ahsante kwa taarifa hii.Jeshi la polisi watafuatilia mauaji hayo na kuwatafuta wauaji” akasema Rais Festus na kukata simu akampigia Ruby na simu ikapokelewa na Mathew
“Mheshimiwa Rais” akasema Mathew
“Mathew mambo
yameharibika.Naibu waziri Keofas ameuawa muda mfupi uliopita akiwa hotelini akipata chakula cha mchana”
“Ameuawa?! Mathew akashangaa
“Ndiyo”
Wakati Rais akiwa nje simu ya Bella ikaita akaipokea haraka haraka alikuwa ni Kasiano
“Kasiano unasemaje?
“Mama Bella nimekupigia kukujulisha kwamba Keofas tayari ameondolewa” akasema
Kasiano
“Ahsante sana
Kasiano.Good job” akasema Bella na kukata simu akashusha pumzi
Rais Festus baada ya kumaliza kuzungumza na simu akarejea tena chumbani kwa Bella
“Sikiliza Bella watu waliokuwa na picha zangu na wakatishia kuzisambaza kama sintatekeleza maelekezo yao ni genge la wauza dawa za kulevya wakilitumia kundi lao linaitwa Black Mafia ambalo limekuwa likiendesha uhalifu mwingi hapa nchini.Nilikataa kutekeleza matakwa yao lakini wewe na wenzako mkakubali kushirikiana na kundi hilo katika kurudisha nyuma vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya Tanzania.Hilo ni jambo ambalo siwezi kukusamehe Bella wewe na wenzako na umeona kile nilichowafanyia wenzako uliokuwa unashirikiana nao.Kinachofuata ni kuwapandisha mahakamani kwa mashitaka ya mauaji.Nitafikiria kukusamehe kama utasaidia kutoa taarifa za kukamatwa kwa viongozi wa mtandao huo wa dawa za kulevya ambao mlikuwa mnashirikiana nao” akasema Festus
“Festus watu hao siwafahamu ni akina nani na ni mara ya kwanza ninasikia kutoka kwako kwamba ni wafanya biashara wa dawa za kulevya.Mimi sikufahamu chochote kama wanazo picha zako za faragha hadi pale aliponifuata mzee Simba akanitaka tushirikiane kuzuia picha hizo zisisambazwe na aliyenipa mawasiliano yao ni mzee Simba nikawapigia simu tena mbele ya mzee Simba nikazungumza nao na kuwataka wasitishe zoezi la kusambaza picha hizo nikawaahidi kushughulikia madai yao”akasema Bella
“Ulifahamu walikuwa wanamtaka Mathew Mulumbi na ukakubali kuwasaidia kumpata ulijua mahala aliko?Ulitegemea ungempata wapi?Ulifahamuje kama anapatiwa matibabu
SNSA baada ya kupigwa risasi?
Ulifahamu vipi kuhusu Frank Kangole kufungwa katika gereza la siri? Nataka majibu tafadhali ama sivyo Bella sintakuwa na huruma nawe hata kidogo”Akasema Festus
“Sikufahamau mahala alipo Mathew Mulumbi na wala sikujua ningempata vipi hivyo nikaomba msaada kutoka kwa baba anisaidie”
“That criminal? Akauliza Festus
“Iwe mwanzo na mwisho
kumuita baba yangu mhalifu ! Isingekuwa yeye wewe usingekuwa mahala hapa” akasema Bella.Festus akaendelea kumtazama kwa macho yaliyojaa hasira
“Kwa hiyo baba yako ndiye aliyekueleza mahala Mathew aliko?
“Alinielekeza kwa kwa naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Keofas Mabula ili anisaidie kutafuta mahala alipo Mathew ! akasema Bella
Festus aliposikia jina Keofas likitajwa akahisi kama vile nyundo nyingine imegonga kichwani kwake “Keofas alinisaidia kutafuta taarifa na kugundua kwamba Mathew Mulumbi alikuwa anapatiwa matibau SNSA.Sifahamu ni namna gani alipata taarifa hizo na ndiye
aliyenisaidia pia kutafuta watu wa kwenda kuvamia mahala hapo kumchukua Mathew Mulumbi.Ili kuingia katika jengo hilo watu hao aliowatafuta walitaka kuipata kwanza ramani ndipo akaniambia kuna mtu amefungwa katika gereza la siri na kama tukimpata huyo anaweza akasaidia kutupa raani ya jengo hilo,nikawasiliana na Yeremia naye akanikutanisha na Asajile ambaye baada ya kumueleza mpango wetu akakubali kumtoa Frank ili aweze kutupa ramani ya jengo la SNSA” akasema bella
“Keofas Mabula ameuawa muda mfupi uliopita na nina uhakika lazima kuna kitu unakifahamu kuhusu mauaji hayo.Kwa nini auawe sasa baada ya mipango yenu kugudulika? Akauliza Festus akiendelea kumtazama Bella kwa macho makali yaliyojaa hasira
“Festus sifahamu chochote kuhusu jambo hilo.Nani kamuua?
“Bella naomba usi….” Akanyamaza festus baada ya simu yake kuita akatoka nje ya chumba kuipokea
Mara tu Festus alipotoka Bella akachukua simu yake na kumpigia baba yake “Bella unasemaje?
“Baba mambo tayari yameharibika nahitaji msaada wako kama
nilivyokuomba”akasema Bella
“Naibu waziri wa mambo ya ndani Keofas ameuawa mchana huu alikuwa katika mtandao wangu na alikuwa mtu hatari kwetu.Tayari Festus anahisi nimehusika katika mauaji hayo na anajiandaa kunichukulia hatua.Nataka umuhakikishie kwamba Keofas alikuwa ni mtu wako na ulimtuma ili anisaidie kufahamu mahala aliko Mathew Mulumbi” akasema Bella na kukata simu haraka haraka baada ya kitasa cha mlango kunyongwa mlango ukafunguliwa Rais akaingia.
“Festus kifo cha Keofas kimenistua sana.I want to help” akasema Bella “Help? Akauliza Festus
“Ndiyo.Nataka kusaidia kuwatafuta watu waliofanya mauaji hayo” akasema Bella
“Bella usitake kucheza na akili yangu!
“Nisikilize Festus.Keofas alikuwa katika mtandao wa baba na ni yeye aliyemtuma anisaidie.Talk to him yeye anaweza akawafahamu watu waliofanya kitendo hicho”
“Family of criminals ! akasema Festus kwa hasira
“Unasemaje Festus?
Akauliza Bella
“Bella siwezi kuzungumza na mtu kama baba yako ! Hawezi kunisaidia chochote ! akasema Festus
“Festus naomba usidharau.Ni kwa nguvu yake yeye ndiyo maana umekalia kiti hicho cha urais hivyo usimdharau.Anaifahamu nchi
hii zaidi yako,ana mtandao mkubwa na uwezo mkubwa wa kukusaidia” akasema Bella
“Kwanza kabisa futa kauli kwamba baba yako ndiye aliyeniweka hapa.Nimewekwa katika ofisi hii na watanzania walioniona ninafaa wakanipigia kura.Hakuna nchi hii mtu au kikundi cha watu wanaoamua nani awe au asiwe
Rais wa nchi”
“Leo ndiyo unalifahamu hilo?So you have power now huh ! akasema Bella
“Bila nguvu ya Dr Fernando unadhani ungepitishwa na chama kugombea urais?Kuna mtu aliyekuwa anakufahamu wewe? Nakushauri Festus talk to him atakusaidia.Ana mtandao mkubwa”akasema Bella
“Mtandao wa kihalifu ! akasema Festus
“Festus let him help you.Nataka akusaidie kuwatafuta hao waliomuua Keofas na hata hao waliosambaza picha anaweza akakusaidia kuwafahamu” akasema Bella
“Bella you are a snake ! akasema Festus na Bella akaichukua simu yake akazitafuta namba za baba yake akampigia na baada ya sekunde chache simu ikapokelewa “Baba shikamoo”
“Marahaba
Bella.Unaendeleaje?
“Baba kuna tatizo limetokea tunaomba msaada wako.Zugumza hapa na Festus” akasema Bella na kumpa Festus simu
“Festus ! akasema baba yake Bella
“Shikamoo mzee”
“Marahaba Festus.Bella ameniambia mnahitaji msaada”
“Sihitaji msaada wowote kutoka kwako miee” akasema
Festus
“Festus kama unahitaji msaada usione haya.Mimi nitakusaidia”
“I don’t get help from criminals! Akasema Festus
“Criminal?! Baba yake Bella akauliza
“Mzee unafahamu kabisa kwamba mimi nawe hatuendi sawa.You know how much I hate you hivyo siwezi kuomba msaada wowote kutoka kwako ! akasema Festus
“Festus sishangazwi na hizo dharau zako lakini ninakusubiri iko siku utanitafuta na kuhitaji msaada wangu.Jambo lingine sijafurahishwa na aibu unayompa mwanangu.Picha zako chafu ukiwa na makahaba zimeniumiza sana.Lini utabadilika Festus na kuacha tabia zako chafu? Kibaya zaidi hukujali hata pale ulipotakiwa kutoa kitu ili kuzuia picha zako zisisambazwe na ukakubali kumbebesha mwanangu aibu zako.Bella aliniomba msaada nimsaidie katika kuzuia picha zile zisisambae kwani ni yeye atakayepata aibu,wewe hujali kitu chochote ! Ni bahati mbaya sana kwamba mpango huo haukufanikiwa lakini alipambana kuificha aibu yako.Sitaki kusikia umemletea matatizo yoyote kwani alichoikifanya ni kwa ajili ya kuificha aibu yako ! Ukitaka mimi nawe tukosane au ukitaka kuifahamu nguvu yangu ni pale nitakaposikia umemfanya chochote mwanangu ! Umenielewa Festus? Akauliza baba yake Bella.Festus hakujibu kitu akamrejeshea Bella simu yake
“Stupid ! akasema
“Baba nitakupigia simu baadaye ! akasema Bella na kukata simu
“Festus tafadhali naomba ukubali baba akusaidie katika suala hili” akasema Bella.Rais Festus akaendelea kumtazama kwa hasira halafu akavua tai yake akaitupa chini
“Aaaaggghhh !! akasema akiendelea kumtazama Bella
“This is not over ! akasema Festus na kutoka akaelekea chumbani kwake
“Aaagghhh !! akagonga meza kwa hasira na kukaa chini akaegemea kitanda
“Sijawahi kupata jaribu kubwa kama hili.Bella ni mke wangu wa ndoa ni mama wa watoto wangu kwa nini akafanya jambo kama hili alilolifanya?
“Festus watu hao siwafahamu ni akina nani na ni mara ya kwanza ninasikia kutoka kwako kwamba ni wafanya biashara wa dawa za kulevya.Mimi sikufahamu chochote kama wanazo picha zako za faragha hadi pale aliponifuata mzee Simba akanitaka tushirikiane kuzuia picha hizo zisisambazwe na aliyenipa mawasiliano yao ni mzee Simba nikawapigia simu tena mbele ya mzee Simba nikazungumza nao na kuwataka wasitishe zoezi la kusambaza picha hizo nikawaahidi kushughulikia madai yao”
Maneno ya Bella yakajirudia kichwani mwa
Festus
“I’m confused ! akawaza na kuchukua simu akampigia katibu mkuu wa chama chake
“Mheshimiwa
Rais”akasema Profesa Simon
“Mzee Simba sihitaji maogezi marefu tayari ninafahamu kila kitu mlichokifanya wewe,makamu mwenyekiti na mke wangu Bella.Ninataka nisikie kwa upande wako nini kilikupelekea ukafanya maamuzi yale na kutengeneza mpango huo wa siri? Akauliza Festus
“Mwenyekiti …. ! akasema mzee Simba na kunyamaza
“Nieleze mzee Simba kwa nini mkafanya jambo kama lile?Unafahamu athari za mlichokifanya? Akauliza Rais festus
“Mwenyekiti kwanza kabisa naomba unisamehe sana kwani ni mimi na makamu mwenyekiti ndio tuliobuni mpango ule na kumshirikisha mke wako.Hakuwa anafahamu chochote na baada ya kumshirikisha mpango wetu akaukubali na tukamuachia yeye mipango yote aifanye ya kumpata Mathew Mulumbi ili tumkabidhi kwa hao jamaa” akasema Profesa Simon
“Mzee Simba
umenisikitisha sana mzee wangu kwa hiki ulichokifanya.Sikutegemea kabisa”
“Mwenyekiti tulilazimika kufanya vile kwa maslahi ya chama” akasema Profesa
Simon
“Hakuna utetezi wowote unaoweza kuutoa mzee Simba unaoweza kuhalalisha kile mlichokifanya.Nataka nikuweke wazi kwamba jambo mlilolifanya limepeleka mauaji ya watu zaidi ya kumi na mchana wa leo naibu waziri ameuawa ikiwa ni mwendelezo wa kile mlichokifanya”
“Mwenyekiti tusamehe sana kwani wakati tunafanya jambo hili hatukujua kama lingeweza kufika hapa
lilipofika na kupeleka vifo vya
watu hao”
“Mzee Simba umekuwa mwalimu wangu kwa miaka mingi na ninakuheshimu sana.Ninakuomba kesho asubuhi wewe na makamu mwenyekiti wasilisheni barua za kujizulu nyadhifa zenu ndani ya chama.Siwezi kufanya kazi na watu ambao siwezi kuwaamini.Huo ni msaada pekee ambao ninaweza kuwasaidia vinginevyo mtakabiliwa na mashaka ya mauaji” akasema Rais Festus na kukata simu
“Maelezo haya ya mzee
Simba na yale ya Bella yanafanana na inaonyesha Bella hakuwa anafahamu chochote hadi alipofuatwa na wale wazee wakamueleza kuhusu mpango ule wa siri wa kumkabidhi Mathew kwa Black Mafia.Kwa upande mwingine Yule mzee Fernando japo namchukia lakini maneno yake yana ukweli ndani yake.Mimi ndiye niliyesababisha haya yote yakatokea.Ukivaa viatu vya Bella lazima utagundua kwamba alifanya vile kujaribu kuficha aibu ambayo familia wangeipata.Watoto japo ni wakubwa sasa lakini hawawezi kuikwepa aibu hii kubwa kwani mimi ni baba yao na hicho ndicho alichokuwa anakikwepa Bella.Alikuwa na kila haki ya kuzuia picha zile zisivuje kuepusha aibu ile kwake familia.Japo mpango wao ulishindwa kufanikiwa lakini bado ameendelea kusimama nami katika jambo
hili na kuamua kulibeba yeye
mwenyewe kwa kudai kwamba yeye ndiye aliyetoa ruhusa mimi niwe na mahusiano na mwanamke mwingine kwa sababu za kiafya ! akawaza Festus
“Wale wazee wawili walichokuwa wanakisema ni sawa kabisa wao wanaangalia maslahi ya chama.Hawakutaka nipate kashfa yoyote kwani wananitegemea katika uchaguzi mkuu ujao na ndiyo maana wakaamua kufanya vile walivyofanya.Yeremia na Asajile nao halikadhalika walishiriki mpango ule wakijua wanafanya kuninusuru mimi na aibu.Yawezekana walifanya jambo hili kwa nia njema ya kuhakikisha siaibiki lakini jambo hili limekwisha ingia katika uhalifu na mauaji na zaidi wamejikuta wakishirikiana na Black Mafia bila kujua.kwa hili walilolifanya Bella na wenzake wanakabiliwa na shitaka la
mauaji lakini je niko tayari mke wangu aende gerezani?Watoto wangu watanielewaje? Wale wazee
wawili mzee Simba na mwenzake makamu mwenyekiti wa chama tuhuma hizi haziwezi kuwaacha
kando,vipi familia za Asajile na Yeremia ambaye amebakisha miaka miwili astaafu?Wazee hawa wamekuwa watiifu kwangu kwa muda mrefu na hawajawahi kunikosea hata mara moja” akawaza Rais Festus na kushika kichwa
“Kuna sauti naisikia ndani mwangu inaniambia niwasamehe wote”akawaza
“Endapo nikiamua kuwasamehe hawa wote akina Mathew ambao wameyaweka maisha yao hatarini kupambana na mtandao huu wa dawa za kulevya watanielewaje? Akaendelea kuumiza kichwa
“Potelea mbali siwezi kuwahukumu wengine kwa makosa niliyoyasababisha mimi.Wasingefanya haya waliyoyafanya kama nisingekuwa na mahusiano na Zandile ngoja niwasamehe.Akina Mathew wataendelea na misheni yao lakini suala hili la akina Bella la mpango wao wa siri ngoja nilifunge kwani linaweza kuniletea matatizo makubwa kwa sababu wanaohusika humu ni watu muhimu kwangu.Jambo lingine nitafuata ushauri wa Bella wa kwenda kuzungumza na baba yake.Mzee Fernando aliwahi kuwa mkuu wa idara ya usalama wa taifa na aliachishwa kazi baada ya kugundulika kuwa anaongoza mtandao wa kihalifu uliokuwa unapora mabenki .Alifungwa gerezani miaka mitano na kutoka akaendelea na mtandao wke wa kihalifu.Ni bilionea mkubwa sana lakini ni mtu hatari vilevile.Anafahamiana na wahalifu wengi na mitandao yote ya kihalifu hapa nchini anaifahamu.Ugomvi wangu mimi naye ni pale alipokamatwa akisafirisha wanyama hai kwenda nje ya nchi na kunitaka nimsaidie na nikatumia nguvu yangu kama Rais kumsaidia.Toka hapo mimi naye hatuna maelewano mazuri na kila mara tumekuwa tukitoleana maneno makali lakini bado ukweli utabaki pale pale kwamba ana mchango wake mkubwa mimi kufika hapa nilipofika.Yeye na wafanya biashara wenzake walichangia kiasi kikubwa mimi kufika hapa lakini wakataka kuitumia ofisi hii watakavyo na huo ndio ugomvi
wangu mkubwa naye.Kwa suala hili nitalazimika kuonana naye anaweza akanisaidia kunipa mwanga kuhusu kundi hili la Black mafia” akawaza Festus na kuchukua simu yake na kumpigia simu katibu mkuu kiongozi
“Mheshimiwa Rais”
“Katibu nataka nikujulishe kwamba nimefanya uteuzi wa mabalozi wawili wapya ambao ni aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi Yeremia Mwaipopo na mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi Asajile Mlabwa.Vituo vyao vya kazi vitatangazwa baadae ” akasema Rais Festus halafu akampigia simu mzee Simba na kumtaka yeye na makamu mwenyekiti wasiandike barua za kujiuzulu tena waendelee na nafasi zao ndani ya chama halafu akainuka akaenda chmbani kwa mke wake
“Bella I’m sorry ! akasema Festus
“Unasemaje Festus? “Samahani kwa kukuingiza katika jambo hili.Nimetafakari na nimegundua ulifanya vile ulivyofanya kwa nia njema ili kuinusuru familia na aibu ya kusambaa kwa picha zile mbaya”akasema Festus.Bella akamsogelea akamshika mkono na kumketisha kitandani
“Festus hayo yamekwisha
pita hivi sasa tuangalie yale yanayokuja.Tuna mambo mengi ya kufanya mbele yetu.Nataka tusimame pamoja katika jambo hili na tutalishinda” akasema Bella “Bella ninataka baada ya jambo hili kuisha tumalize
tofauti zetu na kuishi kwa upendo na amani kama zamani.Kila jambo hutokea kwa sababu maalum na yawezekana hata hili limetokea ili kuturejesha pamoja” akasema Festus na Bella akatoa tabasamu pana
“Nimewasamehe pia
Yeremia na Asajile nimewateua kuwa mabalozi.Nitawapangia vituo vya kazi hapo baadaye” akasema Festus na Bella akamkumbatia kwa nguvu. “Kitu kingine nimekubaliana na ushauri wako ninataka kuzungumza na baba yako hivyo andaa mkutano” akasema Festus na simu yake ikaita akaipokea akajulishwa kuna mgeni amefika akatoka kwenda kukutana na mgeni wake.Baada ya festus kutoka,Bella akaruka ruka kwa furaha halafu akachukua simu akampigia baba yake
“Baba ninakushkuru sana kwa msaada ule.It worked na amesema anataka kuonana nawe.Nataka atakapokuja kuonana nawe mweleze kwamba vita dhidi ya dawa za kulevya hataishinda badala yake itamuingiza katika matatizo makubwa sana.Mshauri aachane na haya anayoyafanya kwani atajikuta akidhalilika zaidi badala ya kushinda” akasema Bella akampa maelekezo baba yake
*****************
Akina Mathew walipokea taarifa kutoka kwa Zari kwamba Rais amewateua Yeremia Mwaipopo na Asajile Mlabwa kuwa mabalozi wapya.Taarifa hii iliwastua sana akina Mathew
“Kwa nini Rais amefanya hivi? kwa nini amewapa ubalozi watu hawa ambao walishiriki katika mpango hatari kabisa?Akauliza Nawal
“Ninampigia simu atueleze” Akasema Ruby
“Hapana usifanye hivyo.Hayo ni maamuzi yake na kama ipo sababu na akiona inafaa anaweza akatueleza lakini hatuwezi kumpangia Rais chochote.Hatujui nini kimetokea hadi akachukua maamuzi haya.Hawa wote wawili ni wateule wake hivyo anao uhuru wa kufanya maamuzi yoyote kuhusu wao.Ukilitazama suala hili kwa undani utagundua kwamba hawa watu wawili Yeremia na Asajile wote wawili waliingizwa katika jambo hili na Bella mke wa Rais.Yawezekana jambo hili limezungumzwa kifamilia na kumalizwa kimya kimya ndiyo maana Rais ameamua kuwasamehe pia na hawa wengine wawili na kuwapa ubalozi.Tuliweke pembeni jambo hili kwani mambo kama haya ni ya kawaida kutokea.Hata mnapokuwa uwanjani kocha anaweza akabadili mfumo wa mchezo na ndivyo alivyofanya Rais lakini hii haituzuii sisi kusonga mbele.Watu wetu wanasota gerezani.Gosu Gosu na mzee Fabian wote wanatutegemea sisi hivyo kwa namna yoyote ile lazima tuwapate watu waliowabambikia kesi ambao ni genge la wauza dawa za kulevya wakilitumia kundi lao la Black Mafia”
“Hili jambo limenikatisha tamaa sana Mathew! Akasema Ruby
“Usijali Ruby mambo yanasonga na tutaimaliza misheni yetu naomba uniamini” akasema Mathew
“Tulitegemea kumpata
naibu waziri Keofas lakini kama mlivyosikia naye ameuawa.Tunahitaji pia kufahamu ilipo na kuikomboa familia ya Godfrey,muda unazidi kwenda na hatuna taarifa zozote” akasema Mathew na kunyamaza akafikiri kidogo kisha akasema
“African picture ni mahala ambako tunahitaji kupachunguza vyema.Lazima tujue kuna kitu gani kinaendelea hapo.Yule dereva tuliyemkamata kanisani alituambia kwamba aliwachukua watu kutokea pale.Tutaweka kambi maalum na kuchunguza kila kinachoendelea hapo lakini kabla ya hapo Ruby nataka unisaidie kumtafuta mtu mmoja ni mwandishi wa riwaya anaitwa Patrick CK huyu ndiye ambaye hadithi yake inatumiwa kutengeneza filamu.Huyu kuna mambo anayafahamu kuhusiana na hii kampuni nahitaji kuzungumza naye” akasema Mathew na kunyamaza baada ya mlango kugongwa na komando mmoja akasema kwamba Asajile na Yeremia walikuwa nje na wanahitaji kuonana na Mathew akawaruhusu kuingia ndani
“Tulikuwa tunatazama luninga na tumestushwa na taarifa za Rais kututeua kuwa mabalozi.Ni jambo ambalo hatukulitegemea kabisa.Hatujui nini hasa kilichomtokea Rais hadi akafanya maamuzi haya lakini tunapaswa kwanza kuwashukuru ninyi wewe Mathew Mulumbi na wenzako
kwa kutufumbua macho kujua
kile
kinachoendelea.Kuonyesha shukrani zetu kwenu tunataka kutoa msaada” akasema Yeremia
“Hongereni kwa maamuzi haya ya Rais ya kuwateua kuwa mabalozi japo hamkustahili.Kitu gani
mnataka kutusaidia? Akauliza Mathew
“Sisi wote wawili mimi na mwenzangu hapa aliyetuingiza katika jambo hili na kuteletea fedheha hii kubwa ni Bella.Yule ni mwanamke hatari kabisa ambaye mnapaswa kumchuguza kwa undani.Wakati Asajile alipokamatwa Bella alinitaka
nitafute mahala alipo ili auawe kwa hofu kwamba angeweza kututaja kuwa tunashirikiana naye” akasema Yeremia “Kama ungefahamu alipo
Asajile ungeweza kumweleza
Bella ili auawe? Akauliza Nawal
“Mimi na Asajile wote tunatoka Tukuyu ni ndugu yangu huyu siwezi kukubali akauawa”akajibu Yeremia
“Yeremia nataka utupe sababu za kwa nini tumchunguze kwa kina Bella?Kuna mambo unayafahamu ambayo unadhani yanaweza yakatusaidia? Mathew akauliza “Nimesema hivyo kwa sababu Bella ninamfahamu kuanzia akiwa mdogo mimi naye tumesoma wote shule na urafiki wetu ukasababisha hadi wazazi wetu wakawa marafiki.Ninaifahamu familia yake.Ninamfahamu baba yake aliwahi kuwa mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa lakini akafungwa gerezani kwa kujihusisha na uhalifu.Anaitwa Dr Fernando ni tajiri mkubwa sana lakini ni mtu katili na ambaye hadi sasa anajishughulisha na mambo ya kihalifu.Kuna wakati aliwahi kukamatw ana nyara za serikali Rais akalazimika kuizima kesi ile kwa kunitumia mimi hivyo Bella ninamfahamu vyema sana.Sababu zinazonipelekea niwatake mumchunguze ni hizi kwanza aliponipigia simu na kuniuliza kama ninafahamu lilipo gereza la siri aliniambia kwamba amepata taarifa kuwa uko SNSA unatibiwa baada ya kupigwa risasi na alifahamu kuwa hata Rais alikuwa SNSA usiku ule swali je alifahamuje?Lazima kuna watu wanaompa taarifa,watafuteni hao.Pili nilipokwenda nyumbani kwa Asajile hatukujua kama Rais alifika pale yeye mwenyewe na kumchukua Asajile nilipofika pale ndipo nikalifahamu hilo na kumjulisha Bella naye akanielekeza nikatazame kumbu kumbu za kamera ili kujua ni nani mlinzi gani aliyekuwa ameongozana na
Rais usiku ule kwenda kwa
Asajile na nikakuta ni Godfrey.Nikamweleza Bella na tazama kilichotokea kesho yake familia ya Godfrey ikatekwa ili kumlazimisha Godfrey.Hamuoni kuna kitu hapa Mathew? Akauliza Yeremia
“Nilipoonana na wale jamaa walioiteka familia yangu,waliniuliza mahala ambako mimi na Rais tulimpeleka Asajile jana usiku na hii inaonyesha wazi kwamba walikuwa tayari na taarifa zote kwamba mimi ndiye niliyempeleka Rais kwa
Asajile usiku” akasema Godfrey.
“Kuna lingine? Mathew akauliza
“Hayo mawili ndiyo ambayo nimeona niwaeleze ambayo naamini yanaweza kuwa na msaada kwenu.Hata katika suala hili la mauaji ya Keofas chunguzeni vizuri kwa nini ameuawa mchana huu baada ya Asajile kuweka wazi kwamba ndiye aliyetumwa kumchukua Frank? Mathew mkiyafanyia kazi haya yanaweza kuwa na msaada mkubwa kwenu” akasema Yeremia na simu
ikaita akaipokea halafu akampa Mathew “Nani? Mathew akauliza “Jabu” akajibu Ruby
“Hallo Jabu ! akasema Mathew
“Mathew nimekutumia
taarifa nilizozipata kuhusu Zandile katika barua pepe yako kama ulivyoomba”
“Ahsante sana Jabu ninakwenda kuipitia halafu nitakupigia baadae” akasema Mathew na kukata simu akawatazama akina Yeremia
“Yeremia na Asajile binafsi ninawashukuruni kwa taarifa hizi ambazo
mmetupa.Naamini kama mngeshirikiana nasi kuanzia mwanzo hivi sasa tungekuwa mbali sana lakini bado hatujachelewa.Mtatusamehe kwa yale yote ambayo mmeyapitia mkiwa hapa.Sisi tunapokuwa kazini hasa katika kutafuta taarifa muhimu huwa tunalazimika kutumia nguvu na ukatili ndani yake lakini kama msingeleta ubishi msingeyapitia hayo.Kwa kuwa Rais amewateua kuwa mabalozi hii ni ishara kwamba mambo yenu yamemalizika na hatuna tena sababu ya kuendelea kuwaweka hapa hivyo mko huru kuondoka hapa na kurejea majumbani kwenu.Vijana wetu watawarejesha manyumbani ila tunachowaomba sisi vijana wenu bado tuko vitani na hawa jamaa hawafahamu mahala tulipo hivyo tunaomba sana jambo hili asilifahamu mtu yeyote.Msimweleze mtu kama tuko tunaishi hapa.Nadhani mmenielewa wazee wangu” akasema Mathew
“Mathew Mulumbi mimi
ni mtu mzima lakini nashindwa kuyazuia machozi kunit0ka” akasema Yeremia
“Nawashukuru sana na
ninawatakia kila la heri.Bado nitaendelea kushirikiana nanyi kwa kila kile nitakachokuwa nacho.Mungu awabariki na Mathew pole sana nakutakia uponaji wa haraka” akasema Yeremia na kukumbatiana na akina Mathew wakaagana na Mathew akaelekeza makomando kutumia gari lao kuwarejesha nyumbani akina Yeremia.
Nabii mkuu Kasiano aliwaongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya mchungaji Lucas na familia
yake waliofariki kwa ajali ya moto kama wengi walivyifahamu bila kujua ukweli kwamba walikwisha uawa kwa risasi kabla ya moto ule kutokea.Mazishi hayo yalihudhuriwa pia na viongozi kadhaa wa serikali na watu wengine maarufu. Wakati mafundi
wakiendelea na zoezi la kufunika makaburi kwa zege,nabii mkuu Kasiano akapewa nafasi ya kusema neno kwa waombolezaji
“Wana wa Mungu
nimepewa nafasi hii niweze kusema maneno machache kwani mengi sana yamesemwa katika siku hii.Tumekuwa na ibada mfululizo toka siku ya jana tukiwaombea marehemu na katika ibada hizo wachungaji,maaskofu na watumishi wengine wa Mungu wametoa mafundisho mengi.Ninachotaka kuwakumbusha ndugu waumini na waombolezaji ni kuwa kanisa letu kwa sasa linapita katika kipindi kigumu sana.Tunapita katika majaribu makubwa na kama tusiposimama imara katika maombi basi shetani atatupepeta kama ngano” akasema nabii Kasiano akanyamaza kidogo “Yanasemwa mengi kufuatia matukio mfululizo yanayoliandama kanisa letu lakini yote hiyo ni mipango ya shetani na ninawahakikishia kwa jina la bwana aliye hai,shetani huyu anayetamani kuliona kanisa la bwana likianguka atashindwa vibaya sana na kanisa litasimama imara kwani limejengwa katika mwamba usiotikisika!
akasema Kasiano na waumini wa kanisa lake wakasimama na kushangilia kwa nguvu Baada ya kumaliza kuzungumza machache na kuwasihi waumini wa kanisa lake kutotetereka Kasiano akaketi na kupisha kwaya ambayo iliendelea na nyimbo za maombolezo wakati wakisubiri shughuli ya kufunika makaburi kwa zege imalizike.Mara tu baada ya kwenda kuketi akafuatwa na mke wake ambaye alimpa kijikaratasi akakikunjua na kukisoma
“Kuna minong’ono mingi kuhusu kupotea kwa mchungaji Zabron” ndivyo kilivyoandikwa kile kijikaratasi.
“Natakiwa kuzungumza na mke wa Zabron mara tu baada ya kutoka hapa ili niweze kumtuliza wakati
tunalishughulikia suala la mume wake” akawaza Kasiano “Naamini wale jamaa walimchukua Zabron kwa nia ya kwenda kumuhoji kuhusu mimi lakini hawatapata chochote.Wachungaji wangu wote hakuna hata mmoja anayefahamu kuhusu upande wangu wa pili,nimewajengea wote utii mkubwa sana na
katika hilo sina wasiwasi hata kidogo.Ninachoomba wasimuue kwani italeta picha mbaya sana kwa kanisa langu.Lakini yote haya yamesababishwa na Mathew Mulumbi.Kwa nini huyu mtu tumeshindwa kumkamata hadi sasa? Kwa nini kila pale tunapopata taarifa za uhakika za mahala alipo tunapomfuata tunamkosa? Nimekuwa
najiuliza swali hili je Mathew anatumia nguvu za giza au nini? Haiwezekani kila jaribio la kumkamata huyu mtu lishindwe kufanikiwa.Mara ya mwisho tulikuwa na uhakika mkubwa kwamba yuko ndani ya jengo la SNSA akipatiwa matibabu lakini tumetumia gharama kubwa kuvamia jengo hilo na tumemkosa.Huyu ni binadamu kweli au ni kivuli tunakitafuta?Kuna nyakati ninaingiwa na mawazo hayo kwamba yawezekana tunatumia nguvu kubwa kupambana na kivuli cha mtu” akawaza Kasiano
Shughuli zilimalizika pale makaburini na watu wakatawanyika.Kasiano akaelekeza mke wa mchungaji Zabron apande katika gari lake “Pole sana mama mchungaji” akasema Kasiano baada ya gari lake kuanza kuondoka pale makaburini “Ahsante sana nabii.Pole na wewe kwani misukosuko unayokumbana nayo ni mikubwa” akasema mke wa mchungaji Zabron “Kama nilivyosema pale mazishini kwamba kanisa linapitia kipindi kigumu sana
hivi sasa,tunajaribiwa na tunapaswa kusimama imara katika imani.Tusichoke kuomba kwani ndiyo njia pekee ya kutuwezesha kuvuka majaribu haya makubwa yanayoendelea katika kanisa letu hivi sasa” akasema Kasiano na ukimya mfupi ukapita halafu akasema
“Mama mchungaji kwanza kabisa ninakupa pole sana wewe na familia yako kwa tukio la kupotea kwa mchungaji Zabron.Kwa sasa baada ya kumaliza msiba wa mchungaji Lucas tunaelekeza nguvu katika kumsaka Zabron.Baada ya kutomuona katika mkesha wa kuwaombea
familia ya Lucas tulidhani amekwenda mahala na atarejea lakini kitendo cha kutomuona mpaka leo hii kinatupa wasiwasi kuhusu mahala aliko hivyo basi kuanzia sasa ninaelekeza nguvu kubwa katika kumtafuta
na kujua mahala aliko.Suala hili litaripotiwa polisi ili uchunguzi uanze mara moja.Nakutoa hofu mama mchungaji.Msiwe na wasi wasi wowote ule kwani mchungaji Zabron atapatikana akiwa mzima wa afya.Nina uhakika mkubwa wa kumpata Zabron akiwa hana tatizo lolote naomba uniamini katika hilo” akasema nabii Kasiano na safari ikaendelea hadi nyumbani kwa mchungaji Zabron ambako alimuacha mke wa Zabron naye akaenda ofisini kwake.
“Endapo Zabron
hatapatikana kwa haraka mambo yatazidi kwa mabaya kwetu.Lazima kila njia itumike kuhakikisha Zabron anapatikana” akawaza Kasiano na kuchukua simu akampigia mama Bella
“Kasiano vipi maendeleo yenu? Akauliza Bella
“Mama Bella kutwa nzima
ya leo tulikuwa katika pilika pilika za mazishi ya mchungaji Lucas ni muda huu nimepata nafasi ya kuingia ofisini na sijapata nafasi hata ya kuzungumza na vijana wangu kujua kile kilichoendelea kwa siku nzima ya leo.Mama Bella kuna jambo ambalo limeanza kuleta minong’ono na kama lisipotafutiwa ufumbuzi wa haraka linaweza kuleta matatizo” akasema Kasiano na kunyamaza kidogo “Jambo lenyewe ni kuhusiana na kutoweka kwa mchungaji Zabron ambaye tunaamini alichukuliwa na wale jamaa ambao kwa asilimia mia moja tunaamini ni mtandao wa Mathew Mulumbi.Jambo hili lilikuwa limefunikwa na msiba wa Lucas na sasa baada ya msiba kumalizika limeanza kushika kasi kubwa na watu wanataka kufahamu alipo Zabron.Mama Bella huyu mchugaji anatakiwa apatikane mara moja ili kutozua sintofahamu nyingine kwani asipopatikana watu wataanza kujiuliza kuna nini katika kanisa hili?
“Black Mafia wamefikia wapi kulichunguza jambo hilo?
Bella akauliza
“Mpaka sasa hawafahamu chochote kuhusu jambo hili.Wameelekeza nguvu zao katika kumsaka Mathew Mulumbi.Kama wakifanikiwa kujua mahala alipo Mathew tunaamini hapo ndipo alipo
mchungaji Zabron” akasema “Wale watu waliochukuliwa SNSA wote wako salama? Hakuna aliyeuawa hata mmoja? Akauliza Bella
“Wote wako salama wanaendelea kuhojiwa” “Vizuri.Nataka wasiendelee tena kuteswa wapumzisheni halafu nitakupigia tena simu baadaye kukupa maelekezo nini cha kufanya.Hili suala la Zabron niachie mimi nitalishughulikia na msilifikishe polisi” akasema Bella na kukata simu
“Mbona Bella amelipokea suala hili kwa wepesi sana? Kuna kitu anakifahamu kuhusu Zabron? Akawaza Kasiano halafu akampigia simu Paul kiongozi wa kundi la
Black Mafia
“Paul nilikuwa na kazi nyingi sana leo nataka unipe pale ambapo mmefikia hadi sasa” akasema Kasiano
“Mkuu mpaka sasa bado hatujapiga hatua zozote tuko pale pale.Tumeendelea kuwahoji hawa jamaa lakini hawajui chochote kuhusiana na Mathew Mulumbi wala mahala alipo.Kwa sasa tunayemtafuta ni mkurugenzi wa SNSA anaitwa Zarina Faheem ambaye kwa mujibu wa hawa wafanyakazi wa SNSA tuliowateka nyara tukimpata huyo tutakuwa tumempata pia Mathew Mulumbi kwani huyu Zarina ndiye anayefahamu mahala alipo Mathew” akasema Paul
“Mikakati ipi mmeiweka ili kumpata huyo Zarina?
Akauliza Kasiano “Mkuu nilikusubiri upate nafasi nikuletee pendekezo kwamba tunakusudia kuvamia tena SNSA”
“Mnataka kuvamia tena SNSA? Akauliza Kasiano kwa mshangao kidogo
“Ndiyo mkuu.Lengo ni kumpata Zari” akasema Paul “Paul sina hakika kama hilo ni wazo zuri.Ni siku moja tu imepita tangu mvamie hapo hapo SNSA na kuua pamoja na kuwachukua mateka baadhi ya wafanyakazi.Haitakuwa rahisi kuweza kuvamia tena hapo kwani ulinzi utakuwa mkubwa”akasema Kasiano “Mkuu kuhusu ulinzi hakuna tatizo kwani hawategemei kama wanaweza wakavamiwa tena ndani ya muda mfupi na wamejielekeza katika kurejesha mifumo yao.Kwa kuwa tayari tunafahamu kila kitu kuhusiana na lile jengo,ramani yake tunayo hatutapata ugumu wowote wa kuingia humo ndani.Tutafanya tukio la muda mfupi sana kwani lengo ni kumchukua tu Zari” akasema
Paul
“Paul hakuna namna nyingine ya kuweza kumpata huyo Zari zaidi ya kuvamia SNSA tena?akauliza Kasiano “Zari anafahamu kuwa anatafutwa hivyo anajificha.Sehemu pekee ambako tunaweza kumpata ni SNSA” akasema Paul
“Paul nataka muandae mpango huo halafu mniletee niuangalie kama hautakuwa na hatari kwetu kabla ya kutoa kibali cha kwenda kuvamia mahala hapo.Hawa jamaa tunapaswa kuwaendea kwa makini sana hasa kwa wakati huu.Mathew Mulumbi tutampata kwa kutumia akili nyingi kuliko nguvu” akasema
Kasiano
“Sawa mkuu nitawasilisha kwako mpango huo” akasema
Paul
“Paul jambo lingine ni kuhusu wale mateka mliowachukua
SNSA.Msiwatese tena wapeni nafasi ya kupumzika hadi nitakapotoa tena maelekezo mengine” akasema Kasiano na kukata simu
“Hatujawahi kusumbuliwa na mtu kama ilivyotokea sasa Mathew Mulumbi kutusumbua kiasi hiki.Lakini naapa hata kama akitusumbua kiasi gani lazima atapatikana kwa gharama zozote zile” akawaza
Kasiano na kuinuka
“Nahisi uchovu mwingi ngoja kwanza nikapumzike akili yangu itulie” Kasiano akainuka na kutoka ofisini kwake akaingia garini kuelekea
nyumbani
****************
Mathew Mulumbi aliipitia taarifa aliyotumiwa na Jabu kuhusu Zandile Wepener na alipomaliza akawatazama wenzake
“Katika taarifa hii ya Jabu hakuna kitu chochote cha kutilia shaka kuhusu Zandile.Taarifa inasema Zandile ni mfanya biashara ana kampuni mbili moja ya mavazi na nyingine ya vipodozi.Ameorodhesha mali kadhaa alizo nazo majumba magari na vinginevyo” akasema Mathew na kunyamaza akarudia tena kuisoma taarifa ile
“Unasemaje Mathew
kuhusiana na taarifa hiyo? Akauliza Nawal
“Namuamini Jabu kama kungekuwa na tatizo kwa Zandile angenieleza.Tuliweke hilo pembeni tuendelee na mipango ya kuitafuta familia ya Godfrey ambao bado hatujui mahala
walipo.Tumewasikia Asajile na Yeremia maelezo waliyoyatoa.Tuna kila sababu ya kuamini kwamba Bella ana mkono wake katika tukio la kutekwa kwa familia ya Godfrey.Kwa mujibu wa
Yeremia,Bella alitaka Asajile auawe ili asiweze kutoa siri kama anashirikiana nao katika mpango wao wa siri kuzuia picha za Rais kuvuja na alitaka sana kufahamu mahala alipo Asajile na asubuhi ya leo familia ya Godfrey ikatekwa ili aweze kuonyesha mahala aliko Asajile.Kwa mtu yeyote hata asiyefahamu mambo ya kipelelezi atagundua kwamba Bella anahusika katika utekaji huu.Ni yeye pekee ambaye anaweza akaonyesha mahala
iliko familia ya Godfrey” akasema Mathew
“Kuna kitu kingine alikizungmza mzee Yeremia naona kina uzito.Alisema tuchunguze tufahamu namna Bella alivyoweza kupata taarifa za rais kwenda katika jengo la SNSA usiku ule ulipopigwa risasi” akasema Godfrey
“Kuna kitu nimekikumbuka ambacho hata mimi na Zari tuliwahi kukijadili.Siku ile Mathew alipopelekwa SNSA kufanyiwa upasuaji baada ya kupigwa risasi,tulijulishwa na Ziro tumuondoe mahala pale kwani wana mpango wa kuja kumuua tukajiuliza taarifa hizo wamezipataje na baada ya tafakari tukawa na wasiwasi na walinzi wa Rais ndipo tukakumbuka kuwa wakati Rais anatoa damu kuna mlinzi mmoja ambaye alitufuata mahala tulipokuwa tumekaa mimi na Zari na kutuuliza maswali akitaka kufahamu mtu aliyekuwa anafanyiwa upasuaji ni nani? Baada ya kuwa na wasiwasi na walinzi wa Rais tukaomba tupate taarifa zao kuwafanyia uchunguzi lakini hatukuweza kubaini chochote”akasema
Ruby
“Nakumbuka nilipigiwa simu na Rais akanitaka nimtumie taarifa za walinzi wanne aliokuwa nao SNSA usiku”
“Ni sisi ndio tuliokuwa tunazihitaji taarifa hizo kwa ajili ya uchunguzi lakini hatukuweza kubaini chochote” “Ni yupi kati ya walinzi hao ambaye mnahisi anaweza kuhusika na kutoa taarifa za Rais? Akauliza Godfrey na Ruby akafungua sehemu katika kompyuta yake akamuonyesha picha “Huyu ni Kelvin.Ni mmoja wa walinzi ambao alikuwa na
Rais usiku ule” akasema
Godfrey
“Huyu ndiye alitufuata akatuuliza kuhusiana na Mathew” akasema Ruby
“Unamuelezeaje huyo
Kelvin? Mathew akauliza “Ni mmoja wa walinzi ambao sina shaka nao hata kidogo lakini kwa maelezo haya niliyoyapata lazima nimfanyie uchunguzi wa kina mimi mwenyewe kubaini kama ndiye ambaye amekuwa akimpa Bella taarifa mbali mbali za Rais.Nitalazimika kwenda ikulu na kumchukua Kelvin halafu nitampeleka mahala kwenda kumuhoji
nijue kama anashirikiana na Bella.Mimi itakuwa rahisi sana kujua kwa vile mimi ndiye mkubwa wake kikazi”akasema
Godfrey
“Ni mpango mzuri.Ushauri wangu ni kwamba utakapomchukua Kelvin utakwenda sehemu tutakapokuelekeza na utawakuta makomando wawili wakikusubiri kisha mtashuka katika gari lenu na kuingia katika gari la makomando hao mtaelekea katika shamba la mazoezi la makomando na huko nataka Kelvin aseme kila kitu kama anashirikiana na Bella” akasema Mathew “Lazima atasema kila kitu ! akasema Godfrey Mathew akawaita makomando wawili na kuwapa maelekezo ya namna mpango utakavyokuwa na bila kupoteza muda wakaondoka kwenda kumsubiri Godfrey mahala walipokubaliana huku Godfrey yeye akielekea ikulu.
“Ruby nini unacho kuhusu
Kasiano na kanisa lake vile vile kampuni ya African pictures? Akauliza Mathew
“Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya maana niliyoipata ambayo inaweza ikatusaidia.Nabii mkuu Kasiano hana rekodi yoyote ya uhalifu,ukwepaji kodi au sifa yoyote mbaya.Ana miliki biashara mbali mbali kama mahoteli,vituo vya mafuta,viwanda viwili vya kutegeneza maji ya kunywa na bishara nyingine mbali mbali
ukiacha hisa alizonazo katika makampuni kadhaa makubwa hapa nchini.Kwa ufupi Kasiano ni tajiri sana.Kuhusu kampuni ya African pictures makao yake makuu yako
Afrika kusini na wamiliki wake ni Roberto Zullo na mke wake Martina Durante.Nimefuatilia taarifa za hawa watu wawili ni matajiri wakubwa na wote wawili wana asili ya Italia lakini kwa sasa wanaishi nchini Afrika kusini.Kwa hapa
Tanzania wana tawi lao hapa Dar es salaam na anayesimamia anaitwa Lethabo Dlamini.Mpaka sasa wamekwisha rekodi filamu moja na nyingine ziko katika maandalizi na filamu ya kwanza imechezwa hapa hapa Tanzania na baadhi ya vipande nje ya nchi ikiandikwa na mtunzi wa kitanzania Patrick CK” akasema Ruby “Hakuna taarifa zozote za maana tunazoweza kuzipata mtandaoni kuhusu hawa jamaa wanajua sana namna ya kujificha.Nitafutie taarifa za Patrick CK,nataka kujua anakoishi na kila kitu kumuhusu yeye lakini kabla ya hapo nataka upige simu nataka kuzungumza na Rais” akasema Mathew na Ruby akampigia simu Rais
“Hallo Ruby” akasema
Rais Festus
“Mheshimiwa Rais ni mimi Mathew hapa ninaongea” akasema Mathew “Mathew natakiwa kukutafutia simu maalum ambayo utaitumia kwa mawasiliano kuliko kutegemea simu moja ya Ruby au Zari.Ni vipi kama wote wawili hawapo na unahitaji msaada kutoka kwangu? Nitalifanyia kazi hilo haraka iwezekanavyo” akasema Rais
“Ahsante sana Rais hilo ni jambo zuri” akajibu Mathew “Mathew imekuwa vyema umepiga kwani hata mimi nilikuwa nataka kuzungumza nawe” akasema Rais “Mheshimiwa Rais
nimekupigia kukujulisha kwamba muda mfupi uliopita nimewaachia huru Asajile na Yeremia wameondoka zao”
“Umewaachia Asajile na
Yeremia? Akauliza Rais “Ndiyo nimewaachia wameondoka zao” “Nani katoa ruhusa ya kuwaachia? Akauliza Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais
hatujasubiri kupata ruhusa yako kwani tayari tumepata taarifa kwamba umewateua kuwa mabalozi hivyo hatukuwa na sababu ya kuendelea kuwashikilia tena ndiyo maana nimewaruhusu wakaondoka zao”akajibu
Mathew
“Mathew japo nimewateua kuwa mabalozi lakini mimi ndiye niliyekuwa ninahitaji kutoa maelekezo ya kuwaachia
au vipi”
“Mheshimiwa Rais hakukuwa na ulazima wowote wa kuendelea kuwashikilia mabalozi wateule kwani hawakuwa wamefanya kosa lolote” akasema Mathew
“Mathew nafahamu wewe na wenzako kazi kubwa
mnayoifanya,nafahamu namna mlivyo katika hatari kubwa,nafahamu pia hamjafurahishwa hasa wewe na maamuzi niliyoyafanya ya kuwateua Asajile na Yeremia kuwa mabalozi.Haikuwa rahisi hata kwangu kufanya maamuzi haya lakini
nimelazimika”akasema Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais
sipingani na maamuzi yako lakini kwa hiki walichokifanya akina Yeremia ulipaswa walau kutushirikisha na sisi ili tufahamu sababu ya kufanya maamuzi yale.Mheshimiwa Rais ni vipi kama mipango yao ingefanikiwa na nikakabidhiwa kwa Black Mafia? Yawezekana hivi sasa ningekwisha uawa baada ya kukabidhiwa kwa watu waliokuwa wananihitaji”akasema Mathew “Mathew nitakapopata nafasi nitazungumza nawe kwa kirefu kuhusiana na maamuzi haya niliyoyafanya.Kwa sasa naomba tuendelee na misheni yetu ya kuwatafuta hawa jamaa.Kuna maendeleo yoyote mpaka sasa?akauliza Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais kwa
sasa tumejielekeza katika kuitafuta familia ya Godfrey ambaye bila yeye tusingeweza kugundua kuhusu ushiriki wa Yeremia katika suala hili na tusingeweza kujua kama mke wa Rais ndiye aliyekuwa kiongozi wa mpango huo wa kunikabidhi kwa wauaji” akasema Mathew
“Mathew kutekwa kwa
familia ya Godfrey hata mimi kumenisikitisha sana na niko tayari kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha familia hiyo inapatikana haraka.Kuna chochote ambacho mmekwisha kipata mpaka hivi sasa kuhusiana na mahala ilipo familia hiyo? Akauliza Rais Festus
“Hapana mheshimiwa
Rais mpaka sasa hatuna taarifa zozote za mahala ilipo familia hiyo ndiyo maana nimekupigia kuomba msaada wako”
“Nini unahitaji Mathew?
Akauliza Rais haraka haraka “Mheshimiwa Rais ninahitaji kuzungumza na mke wako mama Bella kuna maswali ninahitaji kumuuliza” “Bella? Akauliza Rais
“Ndiyo mheshimiwa Rais.Ninataka kuzungumza naye” akasema Mathew na ukimya mfupi ukapita “Mathew unaweza
ukaniambia ni kitu gani unachotaka kuzungumza na mke wangu?
“Mheshimiwa Rais kuna
kila dalili kutekwa kwa familia ya Godfrey kuna mahusiano na ule mpango ulioongozwa na mama Bella wa kutaka kuzuia picha zako zisisambazwe” akasema Mathew na Rais akasema
“Sikiliza Mathew,kile kilichotokea kikiwahusisha mke wangu na akina Yeremia nimekwisha kifunga rasmi na sitaki jambo lile liendelee tena.Nimefanya maamuzi hayo kwa kuzingatia kwamba jambo hili nimelisababisha mimi mwenyewe na walichotaka kukifanya akina Yeremia ni kwa manufaa yangu pia.Walikuwa wanajaribu kunisitiri na aibu kubwa ambayo nimeipata.Kwa maneno haya si kwamba ninaubariki mpango wao lakini walifanya kwa nia njema ndiyo maana nimeona kuwaadhibu nitakuwa ninawaonea nikaamua kuwapa ubalozi Yeremia na Asajile.Kama ningeamua kuliendeleza jambo lile lingefika mbali sana na hawa wote wangekabiliwa na tuhuma za mauaji na unaifahahamu adhabu yake.Mathew hata kama ungekuwa ni wewe ungekubali mke wako mama wa watoto wako akaingia katika tuhuma za mauaji na kufungwa maisha gerezani au kuhukumiwa kunyongwa? Akauliza Rais Festus na ukimya mfupi ukapita
“Mathew naomba jibu tafadhali”akasema Rais
“Mheshimiwa Rais kama mke wangu amevunja sheria za nchi anastahili adhabu kama raia wengine kwani hakuna aliye juu ya sheria”
Rais Festus akavuta pumzi ndefu akauliza “Mathew kama ungekaa mahala pangu na yakakutokea haya ungefanya nini?
Bila kupepesa macho
Mathew akajibu
“Mheshimiwa Rais kitu walichokifanya mama Bella na wenzake japo unadai walikifanya kwa nia njema lakini tayari kimevuka mpaka na kuingia katika uhalifu.Wameshirikiana na genge la wahalifu ambao tunalisaka usiku na mchana,wamesababisha mauaji ya mfungwa Frank na zaidi ya yote wamesababisha watu zaidi ya kumi wakauawa katika ofisi za SNSA achilia mbali uharibifu uliotokea kwa vifaa vya kielektroniki katika eneo walikopiga bomu lile la kielektroniki.Mheshimiwa Rais hakuna namna yoyote watu waliohusika na jambo kama hili wangeweza kusalimika kama ningekuwa mahala pako” akasema Mathew na ukimya ukatawala “Mathew nimekuelewa ndiyo maana nikasema kwamba hata mimi haikuwa rahisi kwangu lakini nimelazimika kufanya hivyo.Bella ni mke wangu bado japo niliwaambia tuna migogoro ya hapa na pale lakini ndiye mama wa watoto wangu na nimelazimika kulifunika jambo hili kwa ajili ya kuilinda heshima ya familia yangu.Nitawatazama vipi watoto wangu ikiwa nitampeleka mahakamani mama yao kwa kosa ambalo mimi ndiye chanzo chake? Mathew nimejikuta katika wakati mgumu sana na ninaamini hata kama ungekuwa ni wewe ungefanya kama nilivyofanya mimi.Naomba tulifunike jambo hili sisi tuendelee na misheni yetu ya kuwasaka genge hili la wauza dawa za kulevya” akasema Rais Festus “With all due respect Mr
President you are doing a very big mistake” akasema Mathew “Mathew tafadhali naomba usijaribu kuvuka mpaka.Kumbuka mimi ni Rais wako hivyo unapaswa kuwa na heshima.Nimekwisha sema kwamba jambo hili nimelifunga rasmi na sitaki ushauri wowote na ninataka maamuzi yangu yaheshimiwe.Kwa sasa endeleeni na misheni yenu nitawasiliana nanyi baadaye kujua mmefikia wapi” akasema Rais na kukata simu Mathew akawatazama wenzake “Mambo magumu”
akasema Mathew na kuwaeleza wenzake mazungumzo yake na rais yalivyokuwa
“Imekuwa vyema umemwambia ukweli kwamba anafanya kosa kubwa sana kwa maamuzi haya aliyoyachukua” akasema Nawal
“Kama yale yote yaliyosemwa na akina Yeremia kuhusu Bella ni ya kweli basi Rais anaishi na nyoka mbaya sana ndani na kama maandiko yanavyosema Mungu aliweka uadui kati yetu na nyoka baada ya kutumiwa na shetani kuwadanganya Adam na Hawa wakamuasi Mungu,Kama Rais wetu anaishi na nyoka n dani nyote mnajua nini kinaweza kutokea hivyo basi ni jukumu letu kumponda kichwa huyo Nyoka”akasema Mathew
“Una maanisha nini
Mathew? Akaliza Ruby
“Hili jambo haliwezi kumalizika hivi hivi.Bella tayari amekwisha ingia katika vitabu vyetu hivyo tutaendelea kumchunguza na kumfahamu kiundani sana na mwisho
atapata stahili yake” akasema
Mathew
“Mathew wazo lako ni zuri lakini naona kama litatuingiza katika mgogoro mkubwa na mheshimiwa Rais” akasema
Nawal
“Mke wa Rais naye ni raia kama sisi hayuko juu ya sheria hivyo basi kama amevunja sheria lazima aadhibiwe kama raia wengine.Msiwe na hofu ninyi mtakuwa nyuma yangu mimi nitawangulieni mbele ” akasema Mathew “Katika maelezo ya Yeremia baba yake Bella anajihusisha na masuala ya kihalifu.Ninahisi yawezekana Bella anapata msaada kutoka kwa baba yake katika kufanikisha haya yaliyotokea.Hamdhani huyo baba yake akawa na mahusiano na Black Mafia? Nawal akauliza
“Tutafanya uchunguzi
tutajua kila kitu kwa sasa tujielekeze katika kuitafuta familia ya Godfrey.Ruby umefanikiwa kupata mahala anakoishi Patrick CK?
“Ndiyo nimepata.Kwa
taarifa zilizosajiliwa hapa anaishi eneo linaitwa Bogota nyumba namba 467 .Ofisi yake iko mtaa wa Osilo jengo la Bimal Plaza chumba 205” akasema Ruby
“Sawa Ruby.Mpigie simu Zari mwambie kwamba tunahitaji magari hapa.Mimi na komando mmoja tutakwenda nyumbani kwa Patrick CK.Nawal utamfuata ofisini kwake kujua kama yuko hapo lengo ni sisi kupata nafasi ya kufanya uchunguzi wa kina nyumbani kwake na pale atakapokuwa ametoka
ofisini utatujulisha atatukuta ndani mwake”
“Ni vipi kama kutakuwa na watu hapo nyumbani kwake? Namaanisha familia yake?Ruby akauliza “Kila kitu kitajulikana hapo hapo tutakapofika na kama familia itakuwepo basi
itakuwa vizuri zaidi”akajibu
Mathew
“Nini hasa ninakwenda kuzungumza na huyo mtu? Nawal akauliza “Kitu chochote kile ili mradi tunataka kuwa na uhakika kuwa yuko ofisini
kwake ili sisi tupate nafasi ya kufanya uchunguzi nyumbani kwake.Zungumza naye kuhusu vitabu vyake Ruby atakusaidia kuvijua vitabu alivyoandika ili uonekane ni shabiki wake” akasema Mathew “Mathew nini hasa unataka kukichunguza kwa huyu mtu? Unadhani ana mahusiano na kutekwa kwa familia ya Godfrey? Ruby akauliza
“Huyu ni mwandishi wa kwanza ambaye hadithi yake imetumiwa na kampuni hii hivyo kuna mambo mengi anayafahamu kuhusiana na hii kampuni ambayo tayari tuna wasiwasi nayo kuwa na mahusiano na Black Mafia ambao tunaamini ndio walioiteka familia ya Godfrey.Huyu jamaa atatupa maelezo ya kina kuhusu kampuni hii”akasema Mathew “Una hakika Mathew huyu jamaa ana taarifa za kutosha kuhusu hii kampuni? Ruby akauliza
“Trust me.Huyu jamaa kuna mengi anayafahamu kuhusu hii kampuni” akasema
Mathew
“Mathew kwa hali yako hii una hakika unaweza ukamudu? Nawal akauliza “I’m fine ladies msiwe na hofu.Nimeshawahi kufanya kazi katika hali mbaya zaidi ya
hii hivyo msihofu”akajibu
Mathew
“Sawa Mathew” akasema
Ruby na kumpigia simu Zari akamuomba msaada wa magari matatu ambayo Zari aliahidi yatafikishwa na makomando muda si mrefu.
****************
Godfrey aliwasili ikulu na kupewa pole na wafanyakazi wenzake kufuatia kutekwa kwa familia yake.Bila kupoteza muda akaenda kuonana na Rais akamueleza kila kitu kuhusiana na wale watekaji na kila kilichotokea.Rais
akamuhakikishia kwamba
suala lile tayari linashughulikiwa kikamilifu na jeshi la polisi
“Kitu ninachokuomba
Godfrey yale yote yaliyotokea leo yabaki kuwa siri yako asifahamu mtu mwingine yeyote.Nadhani umenielewa Godfrey” akasema Rais
“Nimekuelewa
mheshimiwa Rais na nitafanya hivyo”
“Vizuri.Sasa nenda kapumzike tuwaachie jeshi la polisi ambao wanaendelea na uchunguzi na pale watakapokuwa na taarifa zozote watatujulisha lakini angalizo wanaweza wakaja kukuhoji lakini usiwaeleze chochote kama nilivyokwambia” akasema Rais na Godfrey akatoka akamtafuta Kelvin akampata na kumtaka akamsaidie kazi Fulani
“Pole sana Godfrey.Nina uhakika mkubwa kwamba familia yako watapatikana wakiwa wazima wa afya”akasema Kelvin “”Yah.Tuombe Mungu iwe hivyo” akasema Godfrey akiwa katika usukuni
“Hawa jamaa watekaji hawajakupigia simu kudai chochote? Kelvin akauliza
“Hapana hawajanipigia simu kutaka kitu chochote na hiyo inayoniongezea wasi wasi zaidi”akajibu Godfrey
“Usijali Godfrey wanaweza wakakupigia lazima kuna kitu wanakihitaji hao jamaa na kikubwa ni fedha.Huu mchezo wa kuteka watu umeanza kushamiri siku hizi” akasema Kelvin na safari ikaendelea kimya kimya.
Walifika mahala ambako makomando wawili walikuwa
ndani ya gari wakiwasubiri.Godfrey akaegesha gari na kushuka Kelvin naye akashuka,Gidfrey akafunga gari na kumtaka Kelvin amfuate wakaingia katika gari lingine lililoegeshwa pembeni ya barabara lililokuwa na vioo vyeusi.Ndani ya gari waliwakuta watu wawili ambao Kelvin hakuwafahamu.Mara tu gari lilipoanza kuondoka mmoja wa makomando akatoa bastola na kuielekeza kwa Kelvin ambaye alistuka sana
“Inua mikono yako juu haraka ! akasema na Kelvin akainua juu mikono yake.Haraka haraka Godfrey akampekua na kuchukua bastola simu na vifaa vyake vingine vya mawasiliano akaviharibu.
Kelvin alipatwa na mstuko mkubwa hakuelewa ni kitugani kilichokuwa kinaendelea
“Godf…………..”akataka
kusema kitu lakini akabandikwa gundi mdomoni na kuvishwa mfuko kichwani
akaona giza hakujua wapi wanakwenda
****************
Nawal akiwa na mmoja wa makomando waliwasili mtaa wa Osilo na kulitafuta jengo la Bimal Plaza wakalipata.
“Utanisubiri garini ninaelekea ndani na kama utaona hatari yoyote utanijulisha” akasema Nawal hukuakikiweka sawa kifaa chake cha mawasiliano kilichokuwa sikioni.
“Ruby unanipata sawa sawa? Akauliza Nawal
“Ninakupata vizuri Nawal”
“Tayari nimekwisha fika hapa katika jengo la Bimal Plaza ninaelekea ndani ya jengo kumtafuta Patrick”akasema Nawa’
“Sawa Nawal Mathew pia amekusikia kwani naye yuko njiani akielekea nyumbani kwa
Patrick” akasema Ruby
Nawal akashuka na kutembea kuelekea ndani ya jengo.Chumba namba 205 kilikuwa katika ghorofa ya tano na hakutaka kupanda kikwezi(lifti) akapanda kwa mguu hadi ghorofa ya tano akakitafuta chumba 205 na kukipata.Mlangoni kulikuwa na kibao Masimulizi Co.Ltd.Nawal akausukuma mlango na kuingia ndani akatokea sehemu ya mapokezi ambako aliwakuwa akina dada wawili wakampokea kwa tabasamu murua
“Tukusaidie nini dada? Akauliza mmoja wao
“Nina shida ya kuonana na Patrick CK.Nimemkuta? akauliza Nawal
“Una miadi naye? Akauliza mmoja wa wale akina dada
“Hapana sina miadi naye.Nimetokea Dubai na moja ya malengo yangu niliyoweka nikiwa hapa Tanzania ni kuonana naye.Kama yupo mnaweza kunisaidia tafadhali kuonana naye? Akauliza Nawal na mmoja wa wale wahudumu wa mapokezi akamtaka asubiri sofani akapiga simu kwa katibu muhtasi wa Patrick akamueleza kuna mtu anahitaji kuonana na mkurugenzi wao na baada ya muda Nawal akaelekezwa aingie mlango namba 8.Moja kwa moja akaelekea katika mlango alioelekezwa akausukuma na kuingia ndani akakutana na katibu muhtasi ambaye naye kama walivyokuwa wale akina dada wa mapokezi alimpokea vizuri
“Nimewapenda
wafanyakazi wa hapa wamefundishwa namna ya kumpokea mgeni vizuri” akawaza Nawal wakati katibu muhatsi Yule akihifadhi faili katika kompyuta yake halafu akainuka na kumfungulia mlango wa kuingia katika ofisi ya Patrick.
“Karibu sana dada” akasema Patrick
“Ahsante sana.Naamini wewe ndiye Patrick CK” akasema Nawal huku akitabasamu
“Ndiyo mimi.Karibu sana” “Ahsante.Ninaitwa Nawal ninatokea Dubai,nimekuwa nikifuatilia sana vitabu vyako na kuvutiwa navyo nikapanga siku moja nikija Dar es salaam nitakutafuta nikupe hongera zako kwa kazi nzuri”
“Ahsante sana nashukuru.Wewe ni mtanzania?
“Uhm….” Nawal akaguna kidogo
“Hapana mimi si
mtanzania ila nimekuwa nikija Tanzania mara kwa mara nina marafiki zangu wengi hapa na ninaipenda Tanzania.Mimi ni raia wa Saudi Arabia lakini kwa sasa ninaishi Dubai”
Wakati mazungumzo ya Nawal naPatrck CK yakiendelea,Mathew na Kendrick waliwasili Bogota mahala anakoishi Patrick CK.
“Kwa nini mahala hapa
panaitwa Bogota? Akauliza Mathew
“Kuna wakati eneo hili kulikuwa na magenge ya wauza dawa za kulevya hivyo kukawa na mauaji ya mara kwa mara ndiyo maana wanachi wakaamua kupaita mahala hapa Bogota.Kwa sasa kumetulia hakuna tena mauaji kama ya wakati ule na unaona wewe mwenyewe maendeleo makubwa”akasema Kendrick
Waliitafuta nyumba ambayo walielekezwa na Ruby kwamba ndimo anaishi Patrick CK.Kulikuwa na geti la rangi nyeupe.Mathew akamtaka Kendrick kuegesha gari upande wa pili wa barabara mbali kidogo na ile
nyumba.Akaufungua mlango kwa ajili ya kushuka lakini akafumba macho baada ya kuhisi maumivu makali
“Mathew una hakika
unajisikia vizuri?Kama unahisi uko vibaya nitume nitakwenda kuifanya kazi hiyo badala yako” akasema Kendrick
“I’m fine Kendrick” akasema Mathew kisha wakashuka na kuvuka barabara wakaelekea katika geti la nyumba ya Patrick.Kendrick akabonyeza kengele ya getini na kusubiri
lakini hakuna aliyejitokeza kufungua.Mathew akasogea pembeni kidogo ya geti kulikuwa na kisanduku kidogo akakifunua ndani yake kulikuwa na sehemu ya kupitisha kadi na vile vile
kukawa na namba kuanzia sifuri hadi 9
“Ruby we have a problem.Mahala hapa panaonekana hakuna mtu yeyote ndani na nyumba imefungwa geti linafunguliwa kwa kadi na vile vile kuna kisanduku hapa kina namba kuanzia 0-9”
“Hizo namba zinaweza kutumika kufungulia geti endapo kadi imepotea au imeharibika”
“Can you do something?akauliza Mathew na Ruby akamuuliza maswali kadhaa akitaka maelekezo ya kisanduku kile kilivyo na kwa kutumia simu ya Kendrick wakapiga picha na kumtumia Ruby ambaye aliwataka wasubiri kwa muda kidogo ili program yake iweze kutafuta namba ya kuweza kufungulia geti hilo.Wakati wakiendelea kusubiri mazungumzo kati ya Nawal na Patrick CK yaliendelea na walikuwa wanayafuatilia na kusikiliza kila kitu.Baada ya dakika mbili Ruby akamtajia Mathew namba za kuweza kufungulia lile geti na baada ya kuzibonyeza namba zile geti likafunguka wakaingia ndani.
Mandhari ya ndani ya nyumba ile yalivutia sana.Mazingira yalikuwa safi na ya kupendeza.Moja kwa moja Mathew akaelekea mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni na kumtaka Kendrick kuzunguka nyumba ile na kuikagua.Mathew akaufungua mlango ule na kuingia ndani akaangaza angaza sebuleni halafu akatoka na kwenda katika chumba kingine.Milango ya vyumba haikuwa imefungwa Mathew akaingia katika chumba kimoja kimoja na kisha akaingia katika chumba cha kulala
“Hiki ndicho chumba chake cha kulala” akawaza na kufungua droo ya kitanda ambako alikuta kuna makaratasi mengi akajaribu kuyapitia lakini hakupata chochote cha kumsaidia.Akafungua droo ya chini yake na kukuta kuna hati ya kusafiria akaifungua
“Mhh ! anaonekana
amekuwa na safari nyingi nje ya nchi huyu jamaa.Kuna biashara nyingine anafanya huyu jamaa zaidi ya uandishi? Akajiuliza Mathew na kuendelea kupekua hakupata kitu akaenda kufungua kabati la nguo na ndani yake akakuta kuna kasiki dogo.
“Ruby ndani ya hiki chumba cha kulala kuna kabati la nguo na ndani ya kabati hilo kuna kasiki dogo.Nataka
kulifungua kasiki hili” akasema Mathew
“Mathew ili kulifungua kasiki lazima awepo mtu hapo hapo mwenye ujuzi wa kulifungua kwa hapa sintawea kufanya chochote” akasema Ruby
“I can do it ! akasema Kendrick na Mathew akamtaka aingie ndani mara moja akamuonyesha lile kasiki na Kendrick akaanza kucheza nalo.Wakati Kendrick akiendelea kushughulika na
lile kasiki Mathew akatoka na kwenda katika maktaba ambako kulikuwa na makabati ya vitabu yaliyosheheni vitabu vya aina mbali mbali akausukuma mlango na kuingia ndani akaenda mezani ambako kulikuwa na kompyuta akaifungua kompyuta ile na lakini ilihitajika namba ya siri ya kufungulia.
“Ruby nimeingia katika chumba cha maktaba kuna kompyuta mezani lakini inahitaji namba za siri ili iweze kufunguka” akasema Mathew na Ruby akaanza kumpa maelekezo ya kuweza kuifungua kompyuta ile. Na baada ya muda mfupi kompyuta ikafunguka.
“Thank you Ruby” akasema Mathew na kitu cha kwanza alichokutana nacho ni
faili lililoandikwa HOTUBA YA
HAFLA YA KUWEZESHA
VIKUNDI 200 VYA
WANAWAKE.Mathew akaipitia hotuba ile
“Hotuba hii inaonekana ni ya kiongozi Fulani” akawaza Mathew na kufungua tena faili lingine ambalo nalo lilikuwa ni hotuba akaisoma
“Inaonekana huyu jamaa anatumiwa na viongozi kuwaandalia hotuba mbali mbali kwani kuna mafaili mengi ya hotuba katika hii kompyuta” akawaza Mathew na kufungua sehemu nyingine akakutana na vitabu mbali mbali ambavyo alikuwa anaendelea kuviandika.Wakati akiendelea kukagua kompyuta ile akatokea Kendrick na kumjulisha kuwa tayari amekwisha lifungua kasiki. “Ahsante Kendrick” akasema Mathew na kutoka akarejea chumbani akaufungua mlango wa kasiki na ndani yake akakuta kuna mabunda ya fedha na mafaili matano akayachukua yale mafaili na chini yake akakuta kuna bahasha nyeupe.Akaichukua na kuifungua ndani yake akakuta kuna picha akazipitia.Katika picha hizo Patrick alionekana akiwa kitandani kifua wazi na pembeni yake akiwepo mwanamke mmoja akiwa amevaa nguo nyeupe ya kulalia.Picha nyingine walionekana wakiwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiwa ameloa maji walionekana wametoka kuoga.Kulikuwa na picha
nyingine zaidi ya ishirini ambazo ziliwaonyesha wakiwa katika mikao mbali mbali na nyakati tofauti. Kitu kikubwa ambacho mtu yeyote angekigundua mara tu baada ya kuziona picha zile ni kuwa wale wawili ni mtu na mpenzi wake ingawa mwanamke Yule alionekana ana umri mkubwa. “Vijana wa siku hizi sijui kwa nini wanapenda kuwa na mahusiano na watu waliowazidi umri.Yawezekana labda huyu ndiye mkewe,lakini ameshindwaje kutafuta mtu wa umri wake hadi akawa na mahusiano na huyo mama mtu mzima?Stupid !” akasema Mathew na kumpa Kendrick zile picha yeye akalishika faili.Mara tu Kendrick alipozitazama zile picha akapatwa na mstuko mkubwa
“Jesus ! akasema na kumstua Mathew ambaye aliinua kichwa akamtazama “Kuna niniKendrick mbona umestuka hivyo?Mathew akauliza
“I can’t believe this! Akasema Kendrick
“Kuna nini Kendrick.Niambie tafadhali.Unamfahamu mwanamke huyo pichani? Akauliza Mathew
“Mathew humfahamu
mwanamke huyu katika picha? Kendrick akauliza
“Hapana
simfahamu.Wewe unamfahamu? Ni nani? Akauliza Mathew
“C’mon Mathew unasema kweli humfahamu huyu mwanamke pichani? Kendrick akauliza
“Hapana simfahamu” akajibu Mathew
“Oh my God ! Huyu ni mama Bella mke wa Rais” akasema Kendrick
“Bella? Akauliza Mathew kwa mshangao
“Ndiyo.Huyu mwanamke katika hizi picha ni Bella mke wa Rais” akasema Kendrick
“Kendrick are you sure? Akauliza Mathew
“Ndiyo Mathew nina
uhakika” akajibu Kendrick
“Mathew kuna kitu mmekipata kuhusu Bella? Akauliza Ruby na Mathew akamuelezea kuhusu zile picha walizozipata katika kasiki zikiwaonyesha Patrick na Bella wakiwa katika mikao ya kimahaba
“Kama kweli Patrick na Bella wana mahusiano basi hapo ni sehemu ambapo tutapata mambo mengi” akasema Ruby
“Nawal bado uko hapo ofisini kwa Patrick? Mathew akauliza
“Tayari nimekwisha toka niko sehemu nimekaa ninapata kinywaji ninamsubiri atoke ndani.Nilimuuliza mmoja wa wafanyakazi muda wao wa kutoka akaniambia ni saa kumi na mbili kamili na hivi sasa zimebaki dakika chache ufike muda huo.Nitawajulisha pale atakapokuwa ametoka” akasema Nawal kisha Mathew akazihifadhi zile picha mfukoni wakaendelea na upekuzi ndani ya kile chumba. ****************
Kelvin alishushwa garini baada ya kufika katika shamba la mazoezi la makomando wa SNSA akaingizwa ndani ya chumba kimoja akafungwa mikono na kamba katika kiti halafu akavuliwa ule mfuko kichwani na kuondolewa gundi aliyokuwa amebandikwa mdomoni.
“Godfrey nimefanya nini?
Akauliza Kelvin kwa wasiwasi
“Shut up ! akasema Godfrey aliyekuwa anamtazama Kelvin kwa hasira.Baada ya dakika chache komando mmoja akaingia akiwa na kisanduku kidogo chenye visu na vifaa mbali mbali akaviweka mezani Kelvin akaonekana kuingiwa na hofu kubwa
“Kelvin mahala hapa
tulipo ni nje ya jiji la Dar es salaam na hakuna mtu yeyote anayefahamu kama uko hapa. Nimekuleta hapa kwa ajili ya jambo moja tu kupata ukweli kutoka kwako” akasema Godfrey
“Ukweli gani Godfrey? Kwa nini usingeniuliza hadi ukanileta huku?akauliza Kelvin
“Nataka kufahamu mahusiano yako na mke wa Rais” akauliza Godfrey na Kelvin akastuka na kuuliza “Mke wa Rais?
“Ndiyo una mahusiano
gani naye? Akauliza Godfrey
“Sina mahusiano naye yoyote.Yule ni mke wa kiongozi wa taifa sina mahusiano naye yoyote” akasema Kelvin
“Una uhakika Kelvin? Akauliza Godfrey
“Ninasema kweli Gofrey sina mahusiano naye yoyote” akajibu Kelvin
“Kelvin wewe ni mwenzangu lakini kwa siku ya leo sintakuwa na urafiki wowote nawe.Familia yangu wametekwa na mpaka sasa sifahamu mahala waliko hivyo niko tayari kufanya kitu chochote kile kuhakikisha ninaipata familia yangu.Nakuonya tafadhali nieleze ukweli wote vinginevyo utajiweka katika hatari kubwa sana ! akasema Godfrey
“Ninakueleza ukweli Godfrey sina mahusiano yoyote na mke wa Rais” akasema Kelvin
“Yawezekana hauna mahusiano naye ya kimapenzi lakini anakutumia katika kazi zake mbali mbali za siri”akasema Godfrey “Kazi? Kelvin akastukla
“Ndiyo.Hicho ndicho ambacho ninataka kukifahamu” akasema Godfrey
“Hapana Godfrey sijawahi kutumwa kazi yoyote na mama Bella” akasema Kelvin na Godfrey akazidi kupandwa na hasira akamtazama kwa macho makali
“Ulikuwa mmoja wa
walioambatana na Rais juzi usiku alipokwenda jengo la SNSA.Nani aliyempa mama Bella taarifa za Rais kuwepo katika jengo lile na kile alichokwenda kukifanya? Akauliza Godfrey
“Godfrey sifahamu” akajibu Kelvin
“Nakuuliza tena Kelvin nani aliyempa Bella taarifa za Rais kwenda katika jengo la SNSA? Bella ana taarifa zote hadi Rais kutoa damu.Nataka nikueleze ukweli Rais amekasirishwa sana na kitendo hicho na ameniagiza nifanye uchunguzi kubaini nani ambaye amekuwa akitoa taarifa zake kwa mke wake.Kama ni wewe Kelvin nieleze ukweli na nitajua namna ya kukusaidia’ akasema Godfrey
“Godfrey sifahamu chochote.Kama ningefahamu kitu chochoe ningekwambia”
“Kelvin kama unatumiwa na mke wa Rais naomba uwe muwazi ili nikusaidie” akasema Godfrey na Kelvin bado akaendelea kukana kushirikiana na mke wa Rais.Godfrey akawapa Ruhusa wale makomando waliokuwa nao waifanye kazi yao yeye akatoka na kwenda katika chumba kingine akaiwasha simu ya Kelvin na kuanza kuichunguza.Wakati akiendelea na kuichunguza simu ile huku akiziandika namba za simu zisizokuwa na
majina katika karatasi akaingia komando mmoja na kumjulisha kwamba Kelvin yuko tayari kuzungumza.Godfrey akaacha
lile zoezi alilokuwa analifanya akamfuata.Kelvin hakuwa anatazamika usoni.Ni muda mfupi tu lakini tayari macho yalikuwa yamemvimba na moja limefumba
“Duh ! hawa jamaa balaa.Yaani ndani ya muda huu mfupi Kelvin hatazamiki sura” akawaza Godfrey
“Kelvin ! akaita Godfrey na
Kelvin akainua kichwa
“Godfrey kwa nini unanifanyia hivi? Akauliza Kelvin kwa taabu huku akibubujikwa damu mdomoni “Uko tayari kusema ukweli? Akauliza Godfrey
“Nitakueleza Godfrey naomba msinitese tena” akasema Kelvin akakohoa kidogo halafu akasema
“Ni mimi niliyempa Bella taarifa za Rais kwenda SNSA.Mama Bella hunipa
fedha shilingi milioni tatu kila ninapompa taarifa za safari za Rais” akasema Kelvin na kunyamaza akakohoa na kutema damu
“Kwa nini ukakubali kuuza taarifa za safari za Rais?Hujui kwamba safari nyingine za Rais ni za siri na watu wengine hawatakiwi kuzifahamu lakini wewe unatoa siri za safari hizo na hii ina maana kwamba unauweka usalama wa Rais mashakani !
“Nisamehe Godfrey
sikulijua hilo mimi nilijua Yule ni mke wa Rais na yawezekana anahofu labda Rais ana mwanamke wa pembeni ndiyo maana akataka nimpe taarifa zote za safari za Rais” akasema
Kelvin
“Taarifa ipi ya Rais ulimpa mara ya mwisho? Godfrey akauliza
“Taarifa niliyompa mara ya mwisho ni ile ya Rais kwenda SNSA usiku baada ya hapo sijampa taarifa nyingine”
“Jana usiku nilimchukua Rais tukaenda nyumbani kwa mkuu wa idara ya kupambana na ugaidi anaitwa Asajile
Mlabwa na Rais akamchukua tukaondoka naye akampeleka sehemu Fulani na hiyo ndiyo sababu kubwa ya familia yangu kutekwa asubuhi ya leo ili kunishinikiza nionyesha mahala alipo Asajile.Bella hajakueleza chochote kuhusu jambo hilo? Akauliza Godfrey
“Alinipigia simu usiku ule na kuniuliza kama Rais ametoka nikamjibu Rais hajatoka akawa mkali akaniambia kwamba Rais ametoka usiku ule bila sisi kujua akaniambia nichunguze lakini nilipofuatilia nikakuta Rais yuko ndani.Baada ya hapo sikuwasiliana naye tena” akasema Kelvin
“Kelvin familia yangu wametekwa na sijui wako wapi.Kama kuna chochote unakifahamu tafadhali nieleze ukweli ili kuiokoa.”
“Godfrey sifahamu chochote na kama kuna kitu ningekuwa nakifahamu ningekueleza.Kazi yangu mimi ni kumpa Bella taarifa za safari za Rais sifahamu mambo mengine” akasema Kelvin
“Rais amekuwa akikutana mara kwa mara na Zandile Wepener katika nyumba yake kule ufukweni.Je na taarifa za kukutana kwao umekuwa ukimpa Bella? Akauliza Godfrey na Kelvin akawa kimya
“Nijibu Kelvin.Umekuwa
ukimpa Bella taarifa hizo pia? Akauliza Godfrey na Kelvin akatingisha kichwa kukubali.
“Kelvin kwa nini ukafanya hivyo? Kwa nini ukakubali kutoa siri za Rais?Kufuatia tukio la kusambaa kwa picha zake za faragha,Rais amehisi lazima kuna mmoja watu wake wa karibu amehusika katika tukio lile na tayari ameanza uchunguzi wa kulibaioni hilo.Ulifikiria nini Kelvin hadi ukakubali kufanya kitu cha kijinga kama hicho? Akauliza Godfrey
“Ni tamaa ya fedha iliyonipelekea nikakubali kufanya kitu kama hicho na sikujua kama kuna madhara yoyote.Nilichodhani ni mke wa Rais anafanya uchunguzi kujua kama Rais ana mahusiano na mwanamke mwingine” akasema Kelvin na Godfrey akamtazama kwa hasira huku akihema haraka haraka
“Kelvin natamani nikuharibu haribu kwa ujinga ulioufanya.Siamini kama ni wewe Kelvin ninayekufahamu umeweza kufanya hiki ulichokifanya.Yote haya umeyafanya kwa sababu ya fedha? Akauliza
Godfrey,Kelvin akawa kimya
“Nakuuliza Kelvin yote haya ni kwa sababu ya pesa? Kama ulikuwa na shida ya pesa kwa nini usingemuomba Rais fedha au ukaja kwangu nikakusaidia?
“I’m sorry Godfrey” akasema Kelvin
“Sorry won’t help anything ! akafoka Godfrey
“Umefanya jambo baya
sana Kelvin kutoa siri za Rais.Ulikula kiapo cha kumlinda Rais na kutotoa siri zozote za Rais utakazozifahamu umevunja kiapo chako ! akasema Godfrey akiendelea kumtazama Kelvin kwa hasira
“Kama ulimueleza Bella kuhusiana na mahusiano ya Rais na Zandile ni wazi unahusika katika zile picha za faragha zilizosambazwa.Yawezekana wewe ndiye uliyezipiga.Naomba unieleze
ukweli tafadhali ili nitafute namna ya kukusaidia vinginevyo utakuwa katika matatizo makubwa sana Kelvin.Umeyaharibu maisha yako kwa tamaa ya pesa.Nieleze ukweli tafadhali kuhusu zile picha za Rais,nani alipiga? Akauliza Godfrey
“Sifahamu Godfrey.Kama nilivyokueleza mimi kazi yangu ilikuwa ni kumpa Bella taarifa za kila mahala anakoenda Rais hayo masuala mengine ya picha siyafahamu.Sijui picha hizo zimepigwaje” akasema Kelvin
“Kelvin unaendelea kujiweka katika matatizo makubwa.Nieleze ukweli tafadhali angali mapema ninaweza kukusaidia” akasema Godfrey
“Nakueleza ukweli Godfrey sifahamu chochote kuhusu hizo picha.Naomba uniamini” akasema Kelvin
Godfrey akawataka wale makomando wamfungue Kelvin wakamuingiza katika gari wakaondoka kurejea kwa akina Mathew
“Akina Mathew wanatakiwa kumuhoji huyu mtu lazima kuna mambo amekuwa akiyafanya akishirikiana na Bella.Kwa hili la Kelvin nimejifunza kitu kikubwa sana usimuamini mwanadamu na maisha yako.Mwanadamu ni kiumbe anayeweza kubadilika sekunde yoyote.Kelvin ni mmoja wa watu niliowaamini sana na mara nyingi nilikuwa nikimpanga kuwa karibu na Rais kumbe ni mtu hatari kabisa huyu ambaye angeweza hata kutoa siri kwa maadui wa Rais wakaweza kumdhuru.Ameniogopesha sana” akawaza huku akimtazama Kelvin kwa hasira
“Bella naye kwa nini akataka kupata taarifa za mizunguko yote ya Rais kutoka kwa Kelvin? Lazima alikuwa na mipango yake ndiyo maana akawa akimlipa fedha nyingi Kelvin kuweza kumpa taarifa hizo.Yule mwanamke hatari sana” akawaza Godfrey wakiwa garini wakirejea mjini
****************
Paul Lewis na msaidizi wake John Mkizi waliwasili katika makazi ya nabii mkuu Kasiano ambaye tayari alikwisha rejea nyumbani,wakakaribishwa katika sebule ya wageni maalum na Kasiano akaenda kuamshwa
“Paul karibuni sana.Nilikuwa nimejipumzisha mwili umechoka mno.Kwa siku hizi mbili tumekuwa na
pilika pilika nyingi kanisani.Kuna chochote mmeniletea usiku huu? Akauliza Kasiano
“Mkuu kama
nilivyokueleza simuni kwamba tunakusudia kuvamia tena SNSA” akasema Paul
“Paul nini hasa sababu kubwa ya kutaka kuvamia SNSA? Akauliza Kasiano
“Ninauliza hivyo kwa sababu wasiwasi wangu ni kuwa tumevamia jengo hilo uzi tu na kwa sasa wanaendelea na jitihada za kurejea tena katika shughuli zao za kawaida hivyo lazima watakuwa katika ulinzi mkali sana.Naona kama kwenda huko ni hatari zaidi” akasema Kasiano
“Mkuu hata sisi
tumelitafakari hilo lakini tumeona hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kwenda kuvamia tena SNSA.Tumewahoji kwa kina sana wale mateka tuliowachukua SNSA na wote wamekiri kwamba hawafahamu chochote kuhusu Mathew Mulumbi na kwa wengine hawakujua hata kama yuko ndani ya jengo lao.Kwa maelezo tuliyoyapata kutoka kwa Lutengano ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa SNSA ni kwamba tukifanikiwa kumpata Zari basi tutakuwa tumempata Mathew hivyo basi lengo la kutaka kuvamia tena SNSA ni ili kumpata Zari ambaye atatuelekeza mahala aliko Mathew Mulumbi” akasema Paul na Kasiano akainamisha kichwa akafikiri kidogo na kusema
“Tumepitia mambo mengi
kwa wiki hii nzima.Tumepoteza watu kadhaa na wengine muhimu sana kama Keofas.Sitaki tena kupoteza mtu mwingine” akasema Kasiano
“Mkuu tumejipanga vizuri na tunahakika hatuwezi kupoteza mtu yeyote.Tayari tunalifahamu vyema jengo lile na tunajua wapi tupite na
isitoshe hawafikirii kama wanaweza wakavamiwa tena hivi karibuni hivyo tutawashtukiza na kumchukua
Zari” akasema Paul na kumueleza Kasiano kwa kina kuhusiana na mpango wao wa kwenda kuvamia tena SNSA.Baada ya maelezo yale kwa shingo upande Kasiano akawaruhusu waendelee na mpango ule wa kuvamia SNSA *****************
Kiza tayari kilianza kuingia pale Dr Fernando baba yake Bella alipowasili ikulu kwa mwaliko wa Rais.Alipokewa na Bella akamkaribisha sebuleni na baada ya muda Rais Festus akajumuika nao wakazungumza kidogo halafu wakaenda kupata chakula cha usiku na baada ya chakula Dr Fernando akawa na mazungumzo na Rais Festus
“Festus kwanza ninakushukuru kwa kunialika hapa ikulu jioni ya leo na kuniandalia chakula kizuri.Nimefurahi sana” akasema DrFernando
“DrFernando lengo kuu la kukualika hapa jioni hii ni kufuatia mazungumzo yetu ya mchana” akasema Rais Festus
“Festus kwanza kabisa ninakupa pole nyingi kwa hiki kilichotokea.Nafahamu unapitia kipindi kigumu sana kwani matukio mfululizo yamefuatana.Lakini hili la picha limetokeaje Festus? Akauliza Dr Fernando
“Hata mimi sifahamu
jambo hili limetokeaje” akajibu Festus
“Sikiliza Festus sitaki kuingilia faragha zako lakini nakushauri uwe muangalifu sana.Kitendo cha picha hizi kuvuja kinaonyesha ni namna gani hauko salama.Kama wameweza kupata hadi faragha zako basi wanaweza wakafanya chochote mahala kokote.Kuwa makini sana.Lakini Festus kwa nini huachi mambo haya ya kupenda wanawake?Una mke mzuri Bella najua ana matatizo yake lakini unapaswa kumvumilia.Ndoa si lelemama ni kitu kigumu na kinachoweza kuwavusha na kuwafikisha hadi uzeeni ni uvumilivu.Tazama mimi na mama yake Bella ni wazee sasa hivi lakini tumefika hapa tulipofika kwa sababu ya uvumilivu wa mke wangu.Sikatai tumepanda milima na mabonde mengi lakini tuliendelea kushikana mikono hata pale tulipoanguka.Tukio hili liwe funzo kwako na kwa mke wako mmalize tofauti zenu na mfungue ukurasa mpya.Aibu hii mliyoipata ni kubwa mnatakiwa kuitumia vyema aibu hiyo ili iwajenge zaidi.Tuachane na suala hilo tuendelee na mazungumzo yetu ya mchana” akasema DrFernando.Rais festus akafikiri kwa muda halafu akasema
“Kuna jambo kubwa
linaendelea hapa nchini hivi sasa” akasema Rais Festus na kumweleza Dr Fernando kuhusiana na mtandao wa wafanya biashara wa dawa za kulevya wanaousaka
“Tumejitahidi sana kuwasaka lakini hawa jamaa wamejipanga,mtandao wao ni mkubwa na wanapata nguvu kubwa kutoka kwa kikundi chao cha Black Mafia” akaendelea Rais Festus kumweleza Dr Fernando kuhusiana na kundi la Black
Mafia
“Leo asubuhi familia ya mmoja wa walinzi wangu imetekwa nyara na watu ambao tuna uhakika mkubwa ni hao hao Black Mafia na mpaka sasa hatujui mahala walipo.Watu wengine watano walitekwa nyara katika jengo la SNSA na kama haitoshi mchana wa leo ameuawa naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Keofas
Mabula.Kumekuwa na
mfululizo wa mauaji kila uchao” akasema Rais Festus
“Keofas alikuwa ni kijana wangu akinisaidia katika mambo mbali mbali na nilimuomba amsaidie Bella katika mpango wake wa kuzuia picha zako zisisambazwe.Kifo chake kimenisikitisha sana.Nitawasaka watu waliomuua na kuwashikisha adabu” akasema DrFernando
“Ni Black Mafia hakuna wengine !
“Una hakika Festus? Akauliza Dr Fernando
“Ndiyo ni wao.DrFernando wewe una mtandao mkubwa unafahamiana na makundi mengi ya wahalifu hivyo
nataka unisaidie niweze
kuwafahamu hawa watu wako wapi na jinsi gani nitaweza kuwamaliza lakini kwanza ninataka kuwapata watu waliowateka ambao ni familia ya Godfrey na wafanyakazi wa SNSA! akasema Rais Festus kwa hasira na zikapita sekunde kadhaa za ukimya kisha DrFernando akasema
“I’ve been a….criminal kama ulivyosema mchana ingawa huo ni mtazamo wako na nimekusamehe kwa maneno yale kwa kuwa naamini ulitamka maneno yale kwa hasira ulizokuwa nazo.Festus japokuwa mimi si kiongozi wa nchi lakini ninaifahamu nchi hii kuliko hata wewe unavyoifahamu.Ninazo taarifa ambazo hata wewe Rais hauna,ninaifahamu serikali hii na kila aliyemo ndani yake najua unaweza ukashangaa lakini huo ni ukweli.Festus nataka kukuahidi kwamba nitakusaidia kuweza kuwapata watu hao waliotekwa nyara.Ninafahamiana na magenge mengi ya wahalifu na siwezi kushindwa kupata taarifa za mahala waliko watu hao.Tutawapata Festus ondoa shaka” akasema Dr Fernando “Nitashukuru sana kama watu hao wakipatikana kwa haraka” akasema Rais Festus
“Festus kwa uzoefu wangu nilionao katika mambo haya ninataka kukushauri kitu kimoja” akasema DrFernando na kunyamaza kimya kwa muda halafu akaendelea
“Vita dhidi ya dawa za kulevya ni vita ngumu sana na si vita ya kumalizika ndani ya kipindi kifupi cha mwezi mmoja,mwaka mmoja au mitano.Ni vita ndefu na ngumu.Tazama nchi kama Marekani pamoja na jitihada zote ambazo imekuwa inazichukua kukabiliana na biashara hii ya dawa za kulevya lakini bado magenge ya wauza dawa za kulevya yamekuwa yakiibuka kila uchao,bado mitaa imejaa dawa za kulevya.Wao wana vikosi kabisa na bajeti kubwa lakini mpaka leo bado hawajatangaza ushindi dhidi ya biashara hiyo sembuse sisi ambao bado hatujawekeza nguvu ya kutosha?Sitaki kufifisha juhudi zako,sitaki kubeza mapambano
unayoyafanya,umejitokeza na umeonyesha nia ya dhati kitu ambacho marais wengine wengi wa bara hili na duniani wameshindwa kukifanya lakini pamoja na juhudi zako zote
bado vita hii haijaleta matokeo.Bado dawa zinaendelea kuingia nchini,bado vijana wanaendelea kuvuta unga.Unadhani kwa nini umeshindwa kupata mafanikio? Ni kwa sababu hakuna anayekuunga
mkono.Watu uliowaweka
mstari wa mbele katika vita hii ni wanufaika wa biashara hiyo,mtandao huo ni mkubwa sana na si rahisi kuufumua kwa mara moja kama unavyotaka,pili marais wenzako wamekataa kukuunga mkono pia.Wapo baadhi ya marais wa baadhi ya nchi wanashirikiana na wafanya biashara wa dawa za kulevya.Ninawafahamu na ningeweza kukutajia wengine ni marafiki zako lakini ninawasitiri kwa leo.Festus najaribu kukupa picha ili ufahamu kwa kina kuhusu hiki unachotaka kukifanya,nataka uifahamu vyema vita ambayo unataka
kuipigana”akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“Hawa jamaa wana nguvu
na wamezishika serikali za nchi mbali mbali hapa barani Afrika.Yawezekana wewe bado hauko katika orodha yao lakini kama wamewashika watu wako wa karibu basi wewe huwezi kufanya chochote.Festus nimekupa maelezo haya marefu kidogo ili kukupa picha lakini kile ninachokimaanisha ni kwamba You can’t win this war ! akasema Dr Fernando na kumtazama Rais Festus
“Ni lazima niwe mkweli Festus kwamba huwezi ukashinda hii vita.Utapata mafanikio wiki hii lakini wiki ijayo kila kitu kitarudi kama kawaida.Utamuua kiongozi mmoja wiki hii na wiki ijayo akaibuka mwingine.Kitu kibaya zaidi ni kwamba hawa jamaa ukitangaza vita nao damu itakayomwagika ni nyingi mno.Ni wauaji,ni wamwag aji wa damu na hawaogopi.Festus matokeo ya
vita hii ni hasara nyingi kuliko faida” akasema DrFernando na ukimya ukapita
“Nini ushauri wako kama una uhakika siwezi kushinda hii vita? Niache Tanzania liwe ghala na soko la dawa za kulevya? Akauliza Rais Festus
“Festus hebu tazama ndani ya muda huu mfupi wameuawa watu wangapi? Ni vipi kama mapambano haya yataendelea kwa mwezi mzima watu wangapi watauawa?Ninachokushauri zungumza na hawa watu na muelewane” akasema Dr Fernando na Rais Festus akasimama akamtazama
“Niambie humaanishi hicho unachokisema Fernando” akasema Rais Festus
“Ninamaanisha
Festus.Ninakueleza kitu cha kweli kabisa.Hupaswi kuingia katika uadui na hawa jamaa.Jaribu kukaa nao mkazungumza na kufikia muafaka” akasema Dr Fernando na Rais Festus akacheka kidogo
“Mimi nikae nizungumze na hao jamaa? Kamwe haitatokea.Nimekwisha tangaza vita na sirudi nyuma nitaendelea kupambana nao hata kama nitabaki peke yangu katika uwanja wa vita” akasema rais Festus
“Umekwisha shindwa vita hii Festus.Kama ungeshinda au kuwa na dalili zozote za kushinda vita hii usingeniomba msaada.Festus ninakwambia haya kwa kuwa ninawafahamu watu hawa
vizuri,usiingie katika vita nao huwezi kushinda.Sitaki kutoa maamuzi sasa hivi bali tafakari kwa kina shauriana na mkeo na mtafikia muafaka.Mimi ninakwenda kuanza kuwatafuta hao mateka ulioniomba nikusaidie kuwatafuta.Nitawasiliana nawe pale nitakapokuwa nimepata chochote” akasema Dr Fernando na kusimama wakaagana akaelekea katika gari lake akaondoka
“Huyu mzee ana akili finyu sana.Yaani mimi nizungumze na wauza dawa za kulevya? Hilo ni jambo lisilowezekana kabisa ! akawaza Rais Festus wakati akirejea ndani
“Mambo yamekwendaje
huko? Akauliza Bella baada ya Rais kurejea
“Tumezungumza kuna
ushauri amenipa lakini ni ushauri wa kijinga sana” akasema Festus
“Amekushauri nini? Bella akauliza
“It’s a stupid idea” akasema Rais Festus “Sometimes stupid ideas works” akasema Bella
“Amenishauri eti nionane na wafanya biashara wa dawa za kulevya nizungmze nao” akasema Festus
“Kama amekushari fanya hivyo.Baba anawafahamu vyema watu hao ndiyo maana akakushauri usiendelee na vita nao bali mkae mzungumze kwani kama ukiendelea kupambana nao kuna uwezekano mkubwa usiweze kushinda vita hii” akasema
Bella
“Bella nimemwambia hata baba yako kwamba siwezi katu kukaa na kuzungumza na hao jamaa.Nimekwisha weka ahadi ya kupambana nao hadi mwisho lakini nimemuomba anisaidie niweze kuipata familia ya Godfrey yeye anao mtandao mkubwa na ni rahisi kwake kujua mahala walipo”akasema Rais Festus
“Nina uhakika mkubwa anaweza
akawapata.Anafahamiana na watu wengi,anafahamu mitandao yote ya wahalifu hapa nchini na ndiyo maana akakushauri kwamba usiendelee kupambana na hawa jamaa kwani wanaweza wakaendelea kukuchafua na mwisho ukajikuta huna thamani tena.Festus kama hawa jamaa wameweza kuyachimba maisha yako wakagundua siri zako kwamba una mtoto wa nje,wameweza kupata hadi picha zako za faragha hawatashindwa kujua kama umezaa pia na mdogo wangu na hiyo wakiipata itakuwa ni moja ya kashfa mbaya zaidi.Kashfa hiyo itatuondoa hapa Festus.Hakujawahi kutokea Rais ambaye amekuwa na kasha za ngono kama wewe Festus.Tengeneza amani na hao jamaa ili mambo haya yasiendelee vinginevyo tutaendelea kuvuliwa nguo kila uchao” akasema Bella
“Bella naomba tuliweke pembeni suala hilo kichwa changu kitulie kina mambo mengi sana,kwa sasa ninachoomba ni kuipata familia ya Godfrey na wale mateka wa SNSA” akasema Festus na kuelekea chumbani kwake kupumzika.Bella naye akaenda chumbani kwake akampigia simu baba yake
“Baba ninakushukuru jamaa amechanganyikiwa kwa yale uliyomueleza”
“Unadhani atakubali ushauri wangu? Akauliza DrFernando
“Hana namna lazima
akubali ushauri uliompa.Baada ya kupita saa mbili utampigia simu na kumwambia kwamba umekwisha wafahamu watu anaowatafuta na umewasiliana nao.Endelea kumtisha kwamba jamaa wanazifahamu siri zake nyingi na wataendelea kuzianika hadharani kama ataendelea kutaka kupambana nao.Mwambie kwamba wako tayari kuwaachia mateka wanaowashikilia endapo mchungaji Zabron ataachiwa huru.Nitakuelekeza mahala pa kumpeleka mchungaji Zabron utamuelekeza wakamuache hapo na nitakuelekeza mahala ambako wataikuta familia ya Godfrey na wale mateka wengine wa SNSA.Endelea kumsisitiza kwamba akae na watu hao azungumze nao ili kuepusha umwagaji wa damu”akasema Bella
“Sawa Bella hakuna kitakacho haribika.Ila nakushauri kuwa makini sana katika shughuli zako.Kama isingekuwa mimi kwa sasa tayari ungekuwa matatizoni na
kila kitu kingekuharibikia” akasema DrFernando
“Usihofu baba nitajitahidi sana kuwa makini” akasema Bella na kukata simu halafu akampigia Kasiano akampa maelekezo ya kuwaandaa familia ya Godfrey na wale mateka wa SNSA kwa ajili ya kufanyika kwa mabadilishano.
*****************
Saa moja na dakika ishirini Patrick akatoka ofisini kwake na kuelekea maegesho ya magari
“Patrick ametoka
anaelekea katika gari lake” akasema Nawal ambaye bado alikuwa katika jengo la Bimal Plaza akimsubiri Patrick atoke.Baada ya kuhakikisha ameingia katika gari lake na kuondoka Nawal naye akafanya haraka akaelekea katika gari lao wakaondoka kwa haraka kumfuata Patrick.
“Tuko njiani tunamfuatilia” akasema Nawal
akiwa katika gari wakimfuatilia Patrick aliyekuwa peke yake garini
Gari la Patrick lilikata kona na kuingia Rombo bites
“Ameingia Rombo Bites” akasema Nawal
Patrick alitumia dakika saba hapo Rombo Bites kisha akatoka akiwa amebeba mfuko akaingia katika gari lake na kuondoka.
“Safari inaendelea” Nawal akawaeleza wenzake
Bila kujua kuwa anafuatiliwa,Patrick aliendesha gari hadi supermarket akaingia humo ndani na kutumia zaidi ya dakika kumi halafu akatoka akiwa na mifuko mitatu akaingia garini na safari ikaendelea.Kutoka hapo hakusimama tena sehemu yoyote hadi alipofika Bogota mahala anakoishi.Eneo hili la Bogota usiku huu lilichangamka sana kulikuwa na starehe nyingi na watu wengi walipenda kwenda eneo hilo kupumzika baada ya shughuli za kutwa nzima.Moja kwa moja akaelekea nyumbani kwake
“Anaelekea nyumbani kwake” Nawal akawajulisha akina Mathew
“Good job Nawal,sasa mkae katika utayari ili kama kutatokea tatizo lolote mtoe msaada mara moja” akasema Mathew
Kwa kutumia kitanza
mbali Patrick akafungua geti la nyumba yake na kuingia ndani.Nyumba ilikuwa kimya sana akaegesha gari lake akashuka na kuelekea ndani hakuwa na wasi wasi wowote,akaufungua mlango mkubwa wa sebuleni akaingia ndani na kuwasha taa.Akaenda jikoni akaweka vile vitu alivyokuwa amenunua halafu akaelekea chumbani kwake.Akaufungua mlango na kupapasa ukutani akawasha taa.Mara mkoba wa kompyuta aliokuwa ameushika ukamponyoka na kuanguika chini.Mwili ulimtetemeka.Kulikuwa na watu wawili ndani ya chumba chake mmoja akiwa amekaa sofani na mwingine akiwa amesimama katika pembe ya nyumba na wote wakiwa na bastola wamemuelekezea.
“Sit ! akaamriwa na kutokana na woga aliokuwa nao akaanguka na kukaa sakafuni Yule jamaa aliyekuwa amesimama kwenye kona akamsogezea kiti na kumtaka aketi
“Jama…jj..jam…….” Akataka kusema lakini maneno yakashindwa kutoka alikuwa anatetemeka
“Relax ! Take a deep breath ! akasema Mathew na kuinuka akamsogelea
“Hatuko hapa kukudhuru hivyo usiwe na wasiwasi” akasema Mathew na kuichomeka bastola kiunoni.
“Msiniue jamani ninazo fedha nitawapa”
“Hatuko hapa kutafuta fedha.Tumezikuta fedha nyingi katika kasiki lakini siyo kilichotuleta hapa.Tunayekuhitaji ni wewe ! akasema Mathew na Patrick akazidi kutetemeka kwa hofu
“Nawaomba msiniue
jamani ! akasema huku macho yake yakiwa yamejaa machozi “Jina lako nani?
“Naitwa Patrick..Patrick CK”
“Unajishughulisha na nini?
“Mimi ni mwandishi wa vitabu vya riwaya”
“Zaidi ya kazi hiyo ya uandishi kuna kazi nyingine ipi unaifanya inakuingizia kipato?
“Ninajishughulisha na kilimo”
“Good” akasema Mathew
“Unaishi mwenyewe hapa?
“Ndiyo”
“Huna familia?
“Tumetengana” akajibu “Nini sababu ya kutengana?
“Tulishindwa kuelewana” akajibu Patrick ambaye tayari alikuwa ameanza kuondoa ule woga aliokuwa nao
“Patrick CK kama nilivyokueleza kwamba tumekuja hapa kuzungumza nawe mambo kadhaa na ninakutaka uwe mkweli kwani ndiyo itakuwa salama yako.Kama utanidanganya mambo yatakuwa mabaya sana kwako” akasema Mathew na sura ya Patrick ikaonyesha woga mkubwa
“Nitawaeleza ukweli ndugu zangu naombeni msiniumize!
“Nataka unieleze kuhusu kampuni ya kutengeneza filamu ya African Pictures”akasema Mathew “African pictures?
“Ndiyo.Unaifahamu vipi kampuni hiyo?
“Ni kampuni ya kutengeneza filamu ambayo ina makao yake makuu Afrika kusini na hapa Dar es salaam wana tawi lao.Ni kampuni kubwa kuliko zote ya kutengeneza filamu barani Afrika”
“Nani mmiliki wa kampuni hiyo?Mathew akauliza
“Sifahamu nani mmiliki wake”
“Nilikutahadharisha awali kwamba ninataka unieleze ukweli mtupu”
“Ninakueleza ukweli kaka”
Mathew akamtazama kwa
macho makali halafu akauliza “Umewahi kumsikia mtu anaitwa Mathew Mulumbi?
“Ndiyo nimemsikia katika vyombo vya habari”
“Unaifahamu sura yake? Umewahi kumuona?
“Hapana” akajibu Patrick
“Mathew Mulumbi ni huyu
aliyeko mbele yako hivi sasa hivyo tafadhali kuwa muangalifu sana ninapokuuliza kitu.Kama utaendelea kunipa majibu ya uongo nitakuondoa kiungo kimoja kimoja.Usinione hivi ninazungumza kwa upole,I’m a monster ! akasema Mathew akiendelea kumtazama Patrick kwa woga
“Narudia tena kukuuliza nani mmiliki wa kampuni ya filamu ya African Pictures?akauliza Mathew
“Meneja wake hapa
Tanzania anaitwa Lethabo Dlamini” akajibu Patrick
“Ninataka kumjua mmiliki wa kampuni hiyo na si msimamizi wake! Akasema
Mathew kwa ukali
“Sina hakika lakini ninasikia ni raia wa Afrika kusini”
“Humjui? Akauliza Mathew
“Ndiyo simfahamu” akajibu Patrick CK na Mathew akamsogelea akamtandika ngumi moja ya uso akaanguka chini.
“Simfahamu jamani mtaniua bure! Akasema Patrick na Kendrick akamuinua
“Kiongozi gani unayemuandikia hotuba?Mathew akauliza
“Ninamuandikia mke wa
Rais”
“Umeanza lini kumuandikia hotuba mke wa Rais?
“Nina mwaka mmoja
sasa”akajibu Patrick na Mathew akaitoa ile bahasha yenye picha za Patrick akiwa na Bella.Patrick akatetemeka
“Unaweza ukanieleza chochote kuhusu picha hizi?
Akauliza Mathew na Patrick akabaki kimya akitetemeka mara akaanguka kutoka kitini Kendrick akamfuata pale chini kujua kilichomtokea
“Amepoteza fahamu” akasema Kendrick
“Tunaondoka naye.Nawal naomba msogeze gari karibu atakwenda kutueleza kila kitu kambini kwetu” akasema Mathew na Kendrick akambeba Patrick,Mathew akachukua zile picha mafaili na kompyuta wakatoka mle ndani wakafungua geti na tayari akina Nawal walikwisha fika wakamuingiza Patrick garini,kisha Mathew na Kendrick wakaelekea katika gari lao na safari ya kurejea katika makazi yao ikaanza
*****************
Godfrey alirejea tena katika kambi ya akina Mathew,Kelvin akashushwa na kuwekwa katika mojawapo ya chumba
“Amezungumza chochote? akauliza Ruby na Godfrey akamueleza kila kitu alichokieleza Kelvin
“Nimemleta hapa ili aweze kueleza kwa kina zaidi inaonekana kuna mambo mengi anayafahamu huyu jamaa” akasema Godfrey
“Kazi nzuri sana Godfrey” akasema Ruby na kuongozana na Godfrey katika chumba alimo Kelvin,akaelekeza afunguliwe kamba alizofungwa
“Hallo Kelvin” akasema Ruby na kumtazama namna alivyoumia halafu akaenda kuchukua dawa na kumganga majeraha aliyoyapata na kumpa dawa za kutuliza maumivu.
“Pole Kelvin,kwa sasa pumzika tutazungumza nawe baadae kidogo” akasema Ruby na kutoka katika kile chumba
“Kuna maendeleo yoyote kuhusu familia yangu? Akauliza Godfrey
“Mpaka sasa tunaendelea na jitihada za kuwatafuta, akina Mathew wako njiani wanarejea na watakapokuja tutajadili tena tuone kitu gani kifanyike” akasema Ruby “Kadiri muda unavyozidi kwenda ndivyo matumaini ya kuwapata familia yangu wakiwa hai yanazidi kutoweka.Niliwaua watu wao naamini lazima watalipiza kisasi kwa kuwaua familia yangu na kibaya zaidi sina simu ambayo wangeweza hata kuwasiliana nami kunijulisha kuhusu familia yangu”akasema Godfrey
“Godfrey naomba
usihofu.Tuamini tutakusaidia kuipata familia yako” akasema Ruby na kwenda kuendelea na kazi zake
*****************
Mathew Mulumbi na akina
Nawal walirejea katika kambi yao,Patrick ambaye tayari alikwisha rejewa na fahamu akashushwa garini na kuingizwa ndani.
Godfrey akawaeleza kile kilichotokea kwa upande wake
“Good job Godfrey.Bado tunaendelea kushughulikia suala la familia yako usihofu” akasema Mathew na kuelekea katika chumba alimo Kelvin akavuta kiti na kuketi akamtazama Kelvin ambaye alionekana kuwa katika maumivu makali
“Kelvin.Naitwa Mathew Mulumbi na ninataka kukuuliza mambo machache
ninataka unipe majibu sahihi” akasema Mathew
“Umemueleza Godfrey kwamba ulipewa kazi na mke wa Rais ya kumpa taarifa zote za safari za Rais,kama mlinzi wa Rais uliyekula kiapo cha kumlinda Rais kwa gharama zozote zile kwa nini ukakubali kufanya hivyo? Akauliza Mathew.Kelvin akakaa kimya kidogo halafu akasema
“Nakubali nilifanya ujinga mkubwa.Niliingiwa na tamaa ya fedha alizoniahidi kunipa mama Bella na nikakubali kumfanyia kazi yake”
“Alikuahidi kukulipa shilingi ngapi kwa kazi hiyo aliyokupa?
“Kwa kila taarifa ninayompa hunilipa shilingi milioni tatu”
“Hukuwahi kujiuliza mara mbili kwa nini akulipe fedha hizo zote kwa kumpa taarifa za mahala aliko Rais?Ni vipi kama anashirikiana na watu wabaya na wakamdhuru Rais?akauliza Mathew
“Nisameheni jamani ni tamaa iliniponza nikafanya kitu kama hicho” akasema Kelvin.Mathew akamtazama kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“Kelvin pesa peke yake haziwezi kukushawishi ukaamua kuvunja kiapo chako cha kumlinda Rais na ukahatarisha usalama wake.Nieleze ukweli tafadhali lazima kuna jambo lingine ! akasema Mathew
“Hakuna jambo
lingine.Nilihitaji fedha kugharamia matibabu ya mzee wangu hivyo nikakubali kuifanya kazi ile ya mama Bella! Akasema Kelvin
“Ni wewe uliyemweleza
Bella kuhusu mahusiano ya
Rais na Zandile? Akauliza
Mathew Kelvin akawa kimya “Answer me ! akauliza Mathew kwa ukali
“Ndiyo ni mimi ! akajibu Kelvin.
“Nini kilifuata baada ya kumueleza Bella kuhusiana na mahusiano ya Rais na Zandile Wepener? Akauliza Mathew
“Mimi kazi yangu ilikuwa ni kumpa taarifa,mambo mengine sijui” akajibu Kelvin.Mathew akafungua mlango na kumtaka Kendrick amletee kisu.
“Kelvin nataka unieleze ukweli.Baada ya kumpa Bella taarifa za Rais na Zandile nini kilifuata? Akauliza Mathew
“Sifahamu chochote
Mathew” akajibu Kelvin na Kendrick akaingia mle ndani akampa Mathew kisu,Kelvin akazidi kuogopa
“Rais alipigwa picha za faragha bila yeye kujua nataka kujua nani aliyepiga picha hizo kwani picha hizo zilipigwa ndani ya jengo hili hili na mpigaji lazima alishirikiana na mtu wa karibu na Rais na kwa sasa tunalazimika kuamini ni wewe kwa kuwa ndiye uliyetoa siri za Rais kuwa na mahusiano na Zandile.Nataka unieleze ukweli Kelvin ! akasema Mathew
“Sifaham….” Kelvin hakumaliza alichotaka kukisema Mathew akakikamata kiganja chake cha mkono na kukizamisha kisu Kelvin akapiga kelele kubwa.Mathew akakichomoa kile kisu na damu ikaanza kumwagika
“Nieleze ukweli ama sivyo zoezi litaendelea,utapoteza damu nyingi na mwisho utakufa.Niambie ukweli ! akasema Mathew na zikapita sekunde kadhaa Kelvin akigugumia maumvi Mathew akamtandika kofi halafu akakishika kiganja kingine
“Nitakwambia ! akasema Kelvin na Mathew akakiachia kile kiganja akakitupa kisu chini
“Nieleze haraka !
“Baada ya ….” Akasema
Kelvin na kunyamaza akavuta pumzi ndefu
“Baada ya kumpa taarifa za Rais na Yule mwanamke,alinipa watu wawili akataka niwapeleke mahala ambako Rais anakutana na huyo mwanamke nikawapeleka”
“Unawakumbuka watu hao?
“Hapana siwakumbuki”
“Walifanya nini ulipowapeleka mahala hapo? “Waliweka kamera za siri sehemu mbali mbali za hiyo nyumba”
“Mungu wangu ! akasema Mathew na kuendelea kumtazama Kelvin kwa hasira
“Nini kikafuata baada ya hapo?
“Sijui kilichoendelea ila baada ya wiki mbili nikaambiwa niwapeleka tena wale jamaa katika ile nyumba wakaenda kuondoa vifaa vyao vya siri walivyovifunga” akasema Kelvin na kuanza kudondosha machozi
“I’m so fool ! akasema na Mathew akapandwa na hasira akaanza kumvurumishia magumi mfululizo hadi Nawal na Kendrick walipoingia mle ndani na kumshika.
“Imetosha Mathew ! akasema Nawal na mara Mathew akashika tumboni na kukitazama kiganja chake cha mkono kilikuwa kimeloa damu
“Mathew unavuja damu ! akasema Nawal kwa woga wakamchukua Mathew na kumpeleka chumbani,haraka haraka Ruby akampigia simu Zari akamjulisha kuhusu kile kilichomtokea Mathew.
“Ninakuja huko mara moja na madaktari” akasema Zari
“Mathew kwa hali yako hii unatakiwa upumzike.Tuachie sisi kazi tutaendelea nazo”akasema Nawal
“I’m fine.Msihofu kuhusu mimi tujielekeze katika misheni yetu” akasema Mathew ambaye alijitahidi kuficha kama ana maumivu “Mathew usihofu,Zari yuko njiani anakuja akiwa na madaktari” akasema Ruby
“That Bella is a devil.Kelvin amekiri kwamba ndiye anayehusika na kila kitu
kuhusu picha zile za Rais” akasema Mathew “Bella? Akauliza Nawal
“Ndiyo” akajibu Mathew na kuwaeleza yale aliyoelezwa na Kelvin
“Ni jambo gumu sana kuamini” akasema Godfrey “Unamuamini Kelvin? Akauliza Ruby
“Ndiyo,anasema
kweli.Bella ndiye aliyeelekeza picha zile za Rais zipigwe”
“What a devil ! akasema
Ruby kwa hasira
“Kwa nini Rais akamuamini na kusimama kumtetea? Godfrey akauliza
“Ni kwa sababu bado hajamfahamu vyema.Tuendelee kuchimbua zaidi ili tupate mambo mengi zaidi yanayo muhusu huyu Bella.Baada ya aaaghhh ! Mathew akashindwa kuvumilia maumivu
“Mathew umefanya kazi kubwa pumzika tafadhali” akasema Ruby
“Hakuna muda wa kupumzika.Tunachotakiwa kwa sasa ni kuchunguza kama watu hao anaoshirikiana nao Bella ni Black Mafia au ni watu kutoka mtandao wa baba yake kwani tulielezwa kuwa hata baba yake naye amebobea katika mambo hayo ya kihalifu” akasema Mathew “Waliokuwa na picha za Rais na wakamtaka Rais awape kile wanachohitaji tuna hakika ni Black Mafia kwani ndio tuliokuwa tunapambana nao” akasema Ruby
“Kama ni hivyo je Bella na Black Mafia wana mahusiano? Akauliza Nawal
“Tusiende katika hitimisho mara moja.We need to be sure hivyo tunakwenda taratibu tutapanda ngazi moja baada ya nyingine na kukusanya kila
aina ya ushahidi kuthibitisha” akasema Mathew
“Mathew uko sahihi,ni mapema sana kusema chochote kwa sasa” akasema Nawal
“Bring Patrick in here ! akasema Mathew
“Mathew kwa sasa pumzika umekwisha tonesha kidonda chako.Tuachie sisi tutamuhoji”
“No ! Nataka nimuhoji mimi mwenyewe!
“Mathew you are very sturbon.Why don’t you trust us? Akauliza Ruby
“That guy knows
something and I need to question him now ! akasema Mathew
“Mathew ngoja kwanza
daktari aje akutibu jeraha lako halafu tutaendelea na mambo mengine” akasema Nawal
“Fine” akasema Mathew ambaye bado aliendelea kuweka mgandamizo pale katika kidonda palipokuwa panavuja damu *****************
Simu ya Rais Fests ikaita akatazama mpigaji alikuwa ni Dr Fernando,akaipokea
“Dr Fernando”akasema
Rais Festus
“Festus nimekupigia kukupa mrejesho wa ile kazi uliyonituma.Kama nilivyokwambia kwamba ninao mtandao mrefu na ni kazi nyepesi kwangu kuwafahamu watu mnaowatafuta.Nimefanikiwa kuwajua na kuwasiliana nao” “Real? Mapema namna
hii? Akauliza Rais Festus akishangaa
“Nilikwamba Festus nchi hii ninaitazama katika kiganja changu ninafahamu mambo mengi ambayo hata wewe huyafahamu.Tuachane na hayo kazi ya kwanza uliyonituma nikusaidie ni kuwatafuta mateka familia ya mlinzi wako Godfrey na wale jamaa waliotekwa wafanyakazi wa SNSA”
“Ndiyo.Kuna chochote umefanikiwa kukipata? Akauliza Rais Festus
“Ndiyo.Nimefahamu mahala walipo nimezungmza na watu waliowateka”
“My God ! umezungumza
na Black Mafia? Akauliza Rais Festus
“Festus sitaki kwenda kwa kina zaidi lakini nataka kukuhakikishia kwamba mateka wote wako salama kabisa na baada ya kuzungumza na hao jamaa wamenituma nikueleze kitu kimoja wanataka amani” akasema Dr Fernando “Amani ! akasema Festus
“Ndiyo Festus hawa jamaa wanataka amani.Hawataki mapigano yaendelee kwani wanaoathrika na kupoteza maisha katika mapigano haya
ni watu wasio na hatia.Nafahamu hutaki kulisikia hili lakini wanataka kuzungumza nawe na mimi ninarudia tena kukushauri zungumza nao” akasem Dr
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment