Search This Blog

Friday, 7 April 2023

THE FOOTBALL (2) - 2

   

Simulizi : The Football (2)

Sehemu Ya Pili (2)


Tanzania” 

“Mathew tafadhali naomba 

usiendelee zaidi.Tulipoachana 

mimi na wewe tulikubaliana 

kutokufuatiliana katika maisha 

binafsi lakini umeanza 

kunichokonoa.Mambo yangu ya 

kibiashara yanakuhusu 

nini?Mbona wewe una biashara 

zako na sijawahi kukuchunguza? 

Stop that Mathew !! akasema 

Peniela kwa ukali “Peniela naomba usinielewe 

vibaya.Sikuwa na wala sina lengo 

la kukufuatilia lakini haya mambo 

yameibuka katikati ya uchunguzi 

wangu.Kuna mtu mmoja anaitwa 

George Mzabwa huyu alikuwa 

mkuu wa usalama wa taifa na 

alijiua kwa kujipiga risasi.Baada ya 

uchunguzi nimegundua kwamba 

huyu George ana akaunti katika 

benki yenu na aliwekewa fedha 

nyingi na kampuni ya Flamingo 

inayotengeneza saa za thamani 

duniani .George alitoa fedha katika 

akaunti yake na kuziweka katika 

akaunti tatu tofauti za kampuni ya 

kuchonga madini ya vito ya 

Tanbest gemstone ltd ambayo mke 

wa George ni mkurugenzi.Tulipombana 

akamtaja mtu mmoja anaitwa 

Ranbir Kumar kwamba ndiye 

mwenye kampuni hiyo na 

tulipokuwa tunamfuatilia 

ameuawa” 

Mathew akatulia kidogo na 

katika spika za simu akamsikia 

Peniela akihema haraka haraka. 

“George Mzabwa “ Mathew 

akaendelea 

“Alikuwa na mashirikiano na 

shirikka la ujasusi la Marekani 

CIA” 

“Mathew nini hasa 

unachokitafuta?Nieleze 

nifahamu.Mambo ya CIA sijui mimi 

sihusiki nayo.Msaada upi unahitaji toka kwangu ? akauliza Peniela 

akionekana kukasirika 

“Nataka kuwachunguza 

Anderson na baba yake Andrew 

Pillar” 

“Ati nini ?!! akauliza Peniela 

kwa ukali 

“Nataka kuwachunguza 

Andrew na Anderson Pillar na 

ninakuomba unisaidie kuifanya 

hiyo kazi” akasema Mathew 

Peniela akatoa kicheko kidogo 

cha dharau na kusema 

“Mathew japokuwa 

tumetengana lakini 

ninakuheshimu sana lakini 

tunakoelekea unataka kunifanya 

nikuchukie kabisa.Hicho 

unachokisema ni sawa na kunitukana.Mimi nimchunguze 

mpenzi wangu? Ni moja ya njia 

zako za kutaka kutuchafua na 

kuvuruga mapenzi 

yetu?Nakwambia Mathew njama 

zako zimeshindwa hautafanikiwa 

hila zako.Mimi na Anderson 

tunapendana na katu 

hatutatengana!! 

“Peniela naomba unielewe 

tafadhali sina lengo lolote baya 

nawe na wala sitaki kuyaingilia 

maisha yako nayaheshimu 

maamuzi yako ya kuchagua kuwa 

na Anderson lakini hii ni kama 

ajali imetokea hivyo nahitaji 

msaada wako.Uliniomba wewe 

mwenyewe unisaidia na sasa 

nahitaji msaada wako” Lingekuwa ni suala lingine 

ningekusaidia lakini kwa ujinga 

ulionieleza siwezi kukusaidia na 

tafadhali usinipigie simu kama 

hauna kitu cha maana cha 

kuniambia” akasema Peniela kwa 

ukali 

“Peniela naomba unisaidie 

tafadhali ,ni wewe pekee 

unayeweza kunikwamua hapa 

nilipokwama.Kumbuka sikuwahi 

hata mara moja kukataa 

kukusaidia na nilipambana kufa na 

kupona hadi ukafika hapa 

ulipofika.Sijawahi kukuomba 

msaada na leo ni mara ya kwanza” 

“Naheshimu mchango wako 

kwangu Mathew lakini siwezi 

kufanya ujinga huo unaonitaka niufanye.Siwezi kumchunguza 

mpenzi wangu” 

“C’mon Peniela don’t be stupid 

!! akasema Mathew kwa ukali 

“Am I a stupid !! akauliza 

Peniela 

“These people are using you 

Peniela and you dont want to 

know.Tafadhali Peniela kama 

hukuwahi niamini huko nyuma 

please trust me now” 

“Mathew nakuamini sana,ila.” 

“Kama unaniamni 

basinisaidie.Sikiliza Peniela 

japokuwa tumeachana lakini bado 

nakujali kwa kuwa wewe ni mama 

wa mtoto wangu.Usalama wenu 

unapokuwa shakani siwezi kukaa 

kimya lazima nihakikishemnakuwa salama muda 

wote.Utakapopuuzia hili 

ninalokueleza sasa hivi usinilaumu 

pale mambo yatakapoharibika” 

akasema Mathew na ukimya mfupi 

ukapita halafu Peniela akasema 

“Nini unahitaji nifanye? 

“Thank you so much 

.Ninachotaka ukifanye ni 

kuwachunguza Anderson na baba 

yake Andrew Pillar.Nataka 

uchunguze mawasiliano yao 

wanawasiliana na akina 

nani,chunguza marafiki 

zao,chunguza biashara zao 

zote.Chunguza vile vile mahusiano 

ya benki ya Escom na kampuni ya 

Flamingo na mwisho chunguza 

kuhusu mtiririko wa fedha toka kampuni ya Flamingo kwenda 

Tanbest.Nina uhakika mkubwa 

sana kuna kitu utakigundua” 

Penila akavuta pumzi ndefu 

na kusema 

“Nipe muda nione kama 

nitaweza kufanya hiyo 

kazi.Nitakupa jibu baadae.Ila 

naomba ufahamu kwamba 

sijapendezwa na hicho unachotaka 

nikifanye na ninafanya kwa sababu 

umegusia kuhusu usalama wa 

Anna Maria” 

“Ahs………………….” Kabla 

Mathew hajamaliza simu ikakatwa 

“Haikuwa kazi nyepesi 

kumshawishi lakini amekubali na 

ataifanya kazi” Mathew 

akamwambia Camilla “Safi sana” akasema Camilla 

Walipomaliza kupata 

kifungua kinywa wakaondoka 

kuelekea ikulu 

PARIS – UFARANSA 

Tayari zimekwisha pita 

dakika kumi na mbili toka Peniela 

azungumze na Mathew 

simuni.Bado alikuwa amekaa 

kitandani akitafakari 

“Namfahamu vizuri Mathew 

hawezi akaniambia jambo kama 

hili endalo lingekuwa halina 

ukweli.Hana tabia ya kusingizia 

mtu uongo.Tuka tulipoachana 

tumeendelea kuwa marafiki na 

hatuna mgogoro 

wowote.Amekuwa ananiheshmu 

sana na hana mpango wowote wa 

kuingilia maisha yangu na kwa 

hiyo basi lazima nimuamini 

anachokisema.Yawezekana kweli kuna mambo ambayo siyafahamu 

kuhusu Anderson na baba yake 

Andrew.Inawezekana benki hii iko 

kwa malengo maalum na 

inawezekana hata mimi nikawa 

natumiwa bila kujifahamu kama 

Mathew alivyosema.Itabidi 

nitafute namna nitakavyoweza 

kufanya uchunguzi” akawaza 

Peniela na kukumbuka kitu 

“Andrew Pillar” akasema kwa 

sauti ndogo 

“Huyu ni mzee mwenye 

kupenda sana wanawake na hata 

Anderson aliwahi 

kunitahadharisha kutokuwa na 

ukaribu mkubwa na baba yake 

kutokana na tabia zake 

chafu.Andrew amekuwa ananitamani sana na wamewahi 

kunitongoza mara mbili hadi pale 

nilipotishia kumueleza mwanae 

mambo yake machafu.Nadhani hii 

ni fursa ninayopaswa kutumia 

kumpa kile anachohitaji Andrew” 

akawaza Peniela 

“Mathew amenilazimisha 

nirejee yale maisha yangu ya 

zamani nilipokuwa natumwa na 

Team SC41 ambao walikuwa 

wananitumia kuweza kupata 

taarifa nyeti toka kwa watu mbali 

mbali kwa kuwarubuni 

kimapenzi.Tayari nilikwisha 

yasahau maisha yake lakini inabidi 

niyarudie tena.I hate doing this but 

I have to…..” akawaza Peniela na 

kutoka akaelekea moja kwa moja ofisini kwake.Alipoingia ofisini 

kwake akampigia simu Lydie 

mwanadada aliyewahi kuwa 

mtumishi wake wa nyumbani na 

baadae akamuendeleza kielimu na 

kumpatia kazi katika benki ya 

Escom. 

“Lydie nina kzi yangu naomba 

unisaidie kuifanya” akasema 

Peniela baada ya kusalimiana 

“Ndiyo dada nipe hiyo kazi 

nifanye” akasema Lydie 

“Ni kazi ambayo nataka 

uifanye kwa umakini na kwa usiri 

mkubwa” 

“Nitafanya hivyo dada” 

“Ahsante sana .Kuna mteja 

mmoja ana akaunti katika benki 

yetu anaitwa George Mzabwa anaishi Tanzania,aliwekewa fedha 

toka katika kampuni ya Flamingo 

kisha akazisambaza katika akaunti 

tatu tofauti za kampuni ya Tanbest 

ambao ni wateja wetu.Nataka 

uchunguze mtiririko wa fedha 

kutoka kampuni ya Flamingo 

kwenda akauti ya huyo mteja wetu 

George na vile vile nataka ufuatilie 

fedha zilizowekwa katika akaunti 

za Tanbest zimekwenda wapi?nani 

kazichukua?Naomba tafadhali 

unifanyie hiyo kazi ya muhimu” 

“Sawa dada ninaifanya kazi 

yako muda si mrefu na nitazingatia 

usiri kama ulivyonieleza.Kuna 

jambo lolote lingine? 

“Ni hilo tu” akasema Peniela 

wakaagana “Namuamini Lydie ni 

mwaminifu sana kwangu na 

atafanya kama 

nilivyomuelekeza.Sasa nimfuate 

Andrew Pillar” akawaza na kutoka 

akaelekea katika gari lake la 

kifahari.Hakutaka kuongozana na 

dereva wala walinzi 

wake.Alipoingia katika gari lake 

akakizima kifaa ambacho 

humuoyesha kila mahali 

anapokwenda ili kuwarahisishia 

walinzi wake kazi ya kumlinda.Vile 

vile mpenzi wake Anderson Pillar 

hupenda sana kufahamu kila 

sehemu anakoenda 

“Mathew aliniambia kwamba 

Anderson na baba yake 

wananitumia bila mimi kujielewa.Hili linaweza kuwa na 

ukweli wowote?yawezekana kweli 

kuna mambo yanaendelea na mimi 

siyafahamu.Mathew hawezi 

kutunga jambo kubwa kama 

hili.Anadai huyo George ambaye ni 

mteja wa benki yetu ana 

mashirikino na CIA na ana wasi 

wasi kwamba CIA wanatumia 

benki ya Escom kupitishia pesa 

kwa ajili ya operesheni zao nchini 

Tanzania. Mhh ! mambo hayo sijui 

ya CIA na nini wanayafahamu wao 

wenyewe mimi shida yangu kubwa 

ni kuwachunguza na kuwafahamu 

vizuri ili nijiridhishe kwamba 

hakuna mambo yanayoendelea 

nyuma ya pazia bila mimi 

kufahamu.Sitaki kujiingiza katika matatizo hapo mbeleni.Hata hivyo 

nilifanya kosa kubwa kuingia 

katika mapenzi na Anderson bila 

kwanza kumfanyia utafiti na 

kumfahamu vyema.Ingekuwa ni 

kule nyumbani Tanzania 

ningesema alinipa dawa .Mpaka 

leo sielewi nini hasa kilichotokea 

na kunifanya nimpende ghafla 

Anderson na kumuacha Mathew 

mwanaume ambaye aliyatoa 

maisha yake akapambana na 

kunifikisha hapa nilipo leo.Pamoja 

na kuingia kichwa kichwa lakini 

ninampenda sana Anderson hata 

hivyo lazima nimfahamu 

vyema.Huko mbeleni tunaweza 

kuamua kufunga ndoa hivyo 

lazima niwe na uhakika naye” akawaza Peniela akielekea 

nyumbani kwa Andrew Pillar 

Andrew Pillar hakuwa na 

taarifa kama Peniela atakwenda 

nyumbani kwake asubuhi.Akiwa 

bado chumbani kwake akijiandaa 

kwa ajili ya kutoka kuelekea 

katika shughuli zake akapigiwa 

simu na kutaarifiwa kwamba 

Peniela amefika pale nyumbani 

.Alistuka akauliza kama amekuja 

na mumewe akajibiwa kwamba 

amekuja peke yake. 

“Haya mbona 

maajabu?Peniela amekuja peke 

yake nyumbani kwangu?!! Andrew 

akashangaa 

“Amekuja kujitafuta nini 

asubuhi hii ?Muda mrefu hajawahi kukanyaga hapa.Nini 

kimemleta?Ana tatizo 

gani?Andrew Pillar akajiuliza 

maswali bila kupata majibu 

akaenda katika kioo cha 

kujitazamia akarekebisha nywele 

zake zikakaa vizuri halafu akavaa 

haraka haraka 

“Wiki imeanza vizuri kwa 

baraka za kutembelewa na huyu 

malaika Peniela.Nimekuwa 

nikiisubiri kwa hamu kubwa siku 

hii na leo imewadia” akawaza na 

kwenda kujitazama tena katika 

kioo akaridhika amependeza vya 

kutosha akatoka kwenda kuonana 

na Peniela “Oh Peniela karibu sana” 

akasema Andrew .Peniela 

akasimama na kumsalimu 

“Nimestuka kidogo 

nilipoambiwa umekuja nafahamu 

hii ni sehemu ambayo hukuwa na 

mpango wa kufika 

kabisa.Anderson yuko wapi? 

“Tuachane na hayo ya zamani 

Andrew.Nimekuja peke yangu 

Anderson hajafika na wala 

hafahamu kama nimekuja hapa” 

“Hafahamu kama uko hapa? 

“Ndiyo hajui 

chochote.Nimeamua kuja 

mwenywe bila kumjulisha naomba 

uniahidi kwamba hautamweleza 

chochote kuhusu mimi kufika 

hapa” Andrew akainua mkono na 

kusema 

“Nakuahidi sintamweleza 

chochote Andrew” 

“Ahsante” akasema Peniela 

.Alikuwa anaongea huku 

akitabasamu na kubadili mikao 

hali iliyompa wakati mgumu sana 

Andrew Pillar 

“Naamini lazima kuna sababu 

iliyokuleta hapa asubuhi hii” 

“Ndiyo Andrew.Kuna jambo 

limenileta.Nafahamu mimi nawe 

tunazo tofauti zatu lakini 

nimelazimu kuja nikiamini kabisa 

kwamba utanisaidia” 

“Siku zote nimekuwa tayari 

kukusaidia lakini wewe ndiye uliyejiweka mbali nami.Haya 

niambie una tatizo gani? 

Kabla Peniela hajaongea 

chochote Andrew akamtaka 

waelekee ghorofani na kumuagiza 

muhudumu awaandalie 

mvinyo.Sehemu ya juu ya jumba 

hili la kifahari la Andrew kulikuwa 

na sehemu nzuri ya kukaa na 

kuzungumza 

“Karibu Peniela,nieleze 

matatizo yako” akasema Andrew 



Karibu Peniela,nieleze 

matatizo yako” akasema Andrew 

“Andrew kama nilivyokueleza 

awali kwamba nina tatizo la 

kibinafsi zaidi na sitaki Anderson 

au mtu mwingine yeyote afahamu” 

“Usihofu kuhusu mimi 

Peniela.Niamini na chochote 

utakachoniambia kitabaki hapa kifuani kwangu.Hata fahamu mtu 

mwingine yeyote” akasema 

Andrew 

“Ahsante” akajibu Peniela na 

kunywa mvinyo kidogo kisha 

akasema 

“Nilipoanza mahusiano na 

Anderson tayari nilikuwa na mtoto 

mmoja niliyezaa na mume wangu 

wa kwanza anaitwa Mathew” 

“Enhee” akasema Andrew 

akimsikiliza Peniela kwa makini 

“Ni miaka kadhaa sasa imepita 

toka niingie katika mahusiano na 

Anderson na mapenzi yetu 

yamekuwa yakishamiri kila 

uchao.Ninampenda sana na 

ninataka kuzaa naye mtoto” “Oh ! hilo ni jambo jema sana” 

akasema Andrew huku akiachia 

tabasamu pana 

“Uso wako unaonyesha 

tabasamu lakini ndani ya moyo 

wako haukubaliani kabisa na suala 

hilo kwani hukutaka mwanao 

Anderson aoe mwanamke 

mweusi.Unawachukia weusi na 

hata siku za mwanzo za mahusiano 

yetu uliweka upinzani mkubwa.Ni 

kwa sababu hiyo Anderson 

amekuwa ana sifa kufanya 

maamuzi juu ya suala hili la kuzaa 

na mimi.Anderson ananipenda na 

anataka sana kuzaa nami mtoto ila 

anakuogopa” akanyamaza akainua 

glasi ya mvinyo akanywa na kumtazama Andrew aliyekuwa 

akimsikiliza kwa makini 

“Nimekuja kwako Andrew 

kukupigia magoti kukuomba 

uridhie suala hili na sisi tuweze 

kupata mtoto.Niko tayari 

kukufanyia jambo lolote lile ili 

uridhie.Nakuomba sana Andrew” 

akasema Peniela .Andrew Pillar 

akashusha pumzi akatoa paketi ya 

sigara na kutoa moja akawasha 

akavuta mikupuo kadhaa na kutoa 

moshi mwingi halafu akanywa 

funda kubwa la mvinyo na kusema 

“Anderson alipoanza 

mahusiano nawe alipata wakati 

mgumu sana kunieleza 

nimuelewe.Alinihakikishia 

kwamba anakupenda kwa dhati ya moyo wake na nikamtaka 

anionyeshe mwanamke huyo 

anayetaka kumuoa 

nimjue.Nilipokuona hata mimi 

mwili ukanisisimka,nikaona 

halitakuwa jambo jema endapo 

sintamruhusu Anderson awe na 

malaika kama wewe,lakini 

nilimkataza kabisa asizae 

nawe.Sikutaka damu yangu 

ichanganyike na damu 

nyeusi.Sikutaka katika ukoo 

wangu kuwe na chembe chembe 

zozote za mtu mweusi na ndiyo 

maana hadi leo hii bado Anderson 

hajakubaliana nawe kuhusu kuzaa 

mtoto japo anapenda sana kuzaa 

nawe na hawezi kukubali hadi 

hapo nitakaporidhia jambo hilo na anafahamu fika kwamba akifanya 

kinyume na matakwa yangu 

akazaa hata kwa siri nitajua na 

nitamuua huyo mtoto na hata 

mama yake pia.” Akasema Andrew 

na ukimya mfupi ukapita 

“Kwa nini unamfanyia hivi 

mwanao? Peniela akauliza 

“Kama nilivyokueleza 

kwamba ninawachukia watu weusi 

sana!! Akasema Andrew kwa ukali 

“Nalifahamu hilo na ndiyo 

maana nimekuja mwenyewe ili 

tuzungumze jambo hili mimi na 

wewe pekee.Nataka kufahamu 

jambo moja toka kwako” akasema 

Peniela na kunyamaza 

“jambo gani Peniela? “Nataka kujua je na mimi 

unanichukia kama unavyochukia 

watu weusi? 

Kabla hajajibu swali lile 

akavuta sigara iliyobakia na 

kunywa mvinyo kisha akasema 

“Ninawachukia watu weusi 

lakini kwako imekuwa 

tofauti.Sikuchukii Peniela” 

“Kama hunichukii kwa nini 

basi usikubaliane na wazo letu la 

kupata mtoto? 

“Sikuchukii Peniela ila siwezi 

kuruhusu mwanangu akazaa nawe 

kwani unalipia uovu wa watu 

wenye asili yako!! 

Peniela akainuka akaenda 

kuketi katika sofa alilokuwa 

amekaa Andrew,akamtazama nakumshika bega kisha kwa sauti 

laini akasema 

“Niambie Andrew nikufanyie 

nini uridhie jambo hili?Niko tayari 

kufanya jambo lolote 

utakalonitaka nilifanye” 

Mapigo ya moyo wa Andrew 

yalibadilika na kuanza kwenda 

mbio.Peniela akauondoa mkono 

begani akakikuna kidevu halafu 

akaupeleka kifuani na kuushusha 

mapajani na taratibu akaupeleka 

mkono maeneo ya ikulu na 

kukaanza kufura kwa hasira. 

“Peniela acha hivyo tafadhali..! 

akasema Andrew huku akihema 

kwa kasi .Peniela hakumjali 

akaendeleza utundu wake na kufungua mkanda wa suruali 

akafungua zipu 

“Peniela wewe ni mke wa 

mwanan……………” akasema 

Andrew lakini Peniela 

akamuwekea kidole mdomoni 

“Kwa muda mrefu umekuwa 

unanitamani leo nimekuja 

mwenyewe.Fanya kile ulichokuwa 

unakitamani kukifanya kwangu” 

akasema Peniela kwa sauti laini na 

kuitoa ikulu iliyokuwa 

imechachamaa na kwa kutumia 

ulimi wake akaifanyia utundu 

mkubwa na kumfanya Andrew 

atoe miguno kwa raha aliyokuwa 

akihisi 

“Twende chumbani 

kwako.Hapa tunaweza tukakutwa na wafanyakazi wako” akasema 

Peniela .Andrew akavaa vizuri 

wakashuka na kuelekea chumbani 

kwake.Mara tu walipofika 

chumbani Andrew akageuka 

mbogo majeruhi na kumuinua 

Peniela akamtupa 

kitandani.Akavua koti na kulitupa 

chini,akaona shati litachukua 

muda mrefu kulivua akakata 

vifungo na kulitupa.Ndani ya muda 

mfupi tayari alikuwa 

mtupu.Alionekana kama mtu 

aliyechanganyikiwa.Akarukia 

kitandani na kumkuta tayari 

Peniela naye amekwisha toa nguo 

na kubaki mtupu na bila hata 

kupoteza sekunde mtanange 

ukaanza.Dakika kumi na saba zilitosha kumaliza mzunguko wa 

kwanza na Andrew akajitupa 

pembeni akihema kama Simba 

aliyetoka kufukuza windo 

“Pamoja na utu uzima wake 

lakini bado ana nguvu na pumzi 

kama Simba dume.Halafu 

anaonekana alikuwa amenikamia 

sana kwa namna alivyokuwa 

anafanya kwa pupa.Baada ya 

kujichuuza sasa ni wakati wangu 

wa kujilipa” akawaza Peniela 

halafu akageuka na kumbusu 

Andrew 

“Ahsante Andrew.Sikuja kama 

u mjuzi wa mambo kiasi hiki.Hata 

Andrew hakufikii” akasema 

Peniela akavaa suruali yake 

“Unakwenda wapi Peniela? “Nakwenda kuchukua 

vinywaji” 

“Hapana acha mimi niende” 

akasema Andrew na kuvaa 

kaptura yake na fulana akaenda 

kuchukua vinywaji.Aliporejea 

chumbani akakuta Peniela akiwa 

mtupu amejilaza kifudi fudi na 

miguu akiwa ameitanua.Ghafla 

ikulu kukakasirika .Akaweka 

vinywaji na kumfuata Peniela 

akataka kuanzisha mtanange 

mwingine lakini Peniela akamzuia. 

“Andrew mimi nina taratibu 

zangu.kama unatakamzunguko wa 

pili nenda kwanza halafu ndipo 

tuendelee.Sipendijasho” 

Haraka haraka Andrew 

akaingia bafuni kuoga.Peniela akachukua pakiti ndogo yenye 

dawa ya unga akamwagia katika 

mojawapo ya glasi akat8kisa na 

kuhakikisha imekorogeka vyema 

akachukua glasi mbili na kuingia 

nazo bafuni akamtaka Andrew 

ajaze maji katika beseni kubwa la 

kuogea wakaingia ndani ya beseni 

akampa glasi ile yenye kinywaji 

alochoweka dawa.Andrew 

akanywa mafunda kadhaa haraka 

haraka huku Peniela akichezea 

ikulu 

“Peniela wewe ni mwanamke 

mwenye utamu wa hali ya juu 

sana.Naomba tafadhali …….” 

Akanyamaza na kufumba macho 

“Naona macho yanaanza kuwa 

mazito.Nahisi usingizi” “Basi malizia kinywaji twende 

tukalale kwa muda na ukiamka 

tuendelee na mtanange 

mwingine.bado nina hamu sana 

nawe.kiu yangu haijakwisha” 

akasema Peniela na Andrew 

akachukua glasi akagugumia 

mvinyo wote na taratibu akaanza 

kuona giza na kulala usingizi mzito 

“Kwisha habari yake .sasa ni 

wakati wangu” akawaza Peniela na 

kumtoa Andrew akamvuta hadi 

pembeni ya kitanda akamlaza .Kitu 

cha kwanza alichotaka 

kukichuguza ni kompyuta ya 

Andrew,akaitoa katika mkoba 

akaiwasha lakini kulihitajika 

sehemu ya kuweka alama ya dole 

gumba ili iweze kufunguka.Peniela akauinua mkono wa Andrew na 

kuweka kidole gumba katika 

kompyuta ikafunguka.Akafungua 

sehemu ya barua pepe na kuanza 

kuzipitia kwa haraka 

haraka.Nyingi ya barua pepe 

zilikuwa za kazini.Baada ya kupitia 

barua pepe zile akagundua 

Andrew amekuwa akipokea na 

kutoa maelekezo katika kampuni 

ya Flamingo na katika kampuni ya 

A.D Electronics 

“Andrew ana hisa katika 

kampuni hizi mbili ?Barua pepe 

zinaonyesha amekuwa anatoa 

maelekezo kwa wakurugenzi wa 

kampuni hizi mbili.Yawezekana 

labda amewekeza pia katika 

kampuni hizi.lakini hii kampuni ya Flamingo ndiyo aliyoituhumu 

Mathew kwamba ilimtumia fedha 

nyingi mkurugenzi wa usalama wa 

taifa Tanzania ambaye ana 

mashirikiano na CIA”Akawaza 

Peniela huku akizihifadhi barua 

pepe zile katika kifaa chake cha 

kuhifadhia kumbukumbu. 

“Kama ningekuwa na 

utaalamu mkubwa wa mambo 

haya ya kompyuta ningeweza 

kufahamu mambo mengi kutoka 

katika hii kompyta kwani kuna 

mafaili mengi hayafunguki 

yanahitaji programu maalum za 

kuyafungulia.” Akawaza na 

kuiweka kompyuta kitandani 

baada ya kuona funguo ikining’inia 

katika droo ya pembeni ya kitanda.Akaifungua droo ile na 

kitu cha kwanza alichokutana 

nacho ni bahasha nyeupe 

akaifungua ndani na kukutana na 

pasi mbili za kusafiria.Moja 

ilikuwa na jina la Edwin 

Washington na nyingine ilikuwa na 

jina la Andrew Pillar na zote 

zikiwa na picha moja ya Andrew 

“Andrew ana majina mawili?!! 

Akashangaa 

“Sasa naanza kuamini kile 

alichokisema Mathew kwamba 

kuna mambo siyajui kuhusu hawa 

watu.Kwa nini awe na hati mbili za 

kusafiria zenye majina tofauti?Jina 

lake halisi ni nani?akajiuliza na 

kugundua kwamba moja ya pasi ile 

yenye jina la Edwin washington ilitolewa Marekani na nyngine 

yenye jina la Andrew Pillar 

ilitolewa Ufaransa. 

“Marekani anafahamika kama 

Edwin Washington na huku 

Ufaransa anajulikana kama 

Andrew Pillar.kwa nini awe na 

majina mawili.Kuna kitu gani 

anakificha?Akaendelea kujiuliza 

Alipekua ile droo na kukuta 

nyaraka mbali mbali akarudisha 

kila kitu kama alivyokikuta 

akatazama sehemu nyingine 

mbalimbali hakuna cha maana 

alichokipata akarejea tena 

kitandani na kukuta kuna barua 

pepe nyingine 

zimeingia,akazifungua na 

kuzisoma.Moja ya barua pepe ilitoka kwa Willy gadner na 

ilimtaarifu kuwasiliana na ofisi 

kuu kuna tatizo Tanzania.Hii 

ikazidi kumpa wasiwasi Peniela 

akaihifadhi pia barua pepe ile 

katika kifaa chake kisha akaifuta 

kabisa ili Andrew asigundue kama 

barua pepe zake mpya zimesomwa 

“Haya niliyoyagundua 

yanatosha.Naamini yakifanyiwa 

kazi kuna mambo yanaweza 

yakabainika” akawaza Peniela na 

kuifunga kompyuta ile akairudisha 

katika mkoa akampandisha 

Andrew kitandani akamlaza vizuri 

na kumfunika 

“Leo lazima niwafahamu ninyi 

ni akina nani? Akawaza na kuvaa 

vizuri akachukua mkoba wake na kuondoka akarejea ofisini kwake 

na kumpigia simu Lydie 

akamuuliza kuhusu kazi aliyompa 

kama tayari ameikamilisha 

“Naomba nipe saa moja dada 

halafu nitakupa majibu.Bado 

naendelea kuifanya ile kazi” 

“Sawa Lydie nataka 

nikuongeze tena kazi 

nyingine.Nataka unisaidie 

kuwafahamu wamiliki wa kampuni 

za A.D Electronics na Flamingo zote 

za nchini marekani” akasema 

Peniela na kukata simu akaegemea 

kitini 

“ Ningefanya kosa kudharau 

ombi la Mathew.Kuna kitu tayari 

amekwisha kiona kwa Andrew na 

mwanae Anderson.Hata mimi kuna kitu nimeanza kukihisi hakiko 

sawa.Nitajilaumu sana kwa kuwa 

na Anderson endapo nitagundua 

kwamba kuna mambo anayafanya 

nyuma ya mgongo wangu.Ngoja 

nisubiri majibuya Lydie” 

DAR ES SALAAM – TANZANIA 

Iliwalazimu Mathew na 

Camilla kusubiri kwa zaidi ya saa 

tatu kwani asubuhi hii alikuwa 

ametingwa sana na mambo 

mengi.Hatimaye wakakaribishwa 

katika chumba cha mazungumzo 

ya faragha na rais akamkuta humo 

“habari za asubuhi 

jamani.Samahani kwa 

kuwasubirisha kwa muda mrefu”  akasema Dr Vivian aliyeonekana 

kuwa na haraka sana 

“Hakuna tatizo mheshimiwa 

rais” akasema Mathew 

“Mathew sitaki kupoteza 

muda nina mambo mengi sana 

leo.Nataka uniambie kwa nini 

ulidharau mwito wangu jana 

usiku? Akauliza Dr Vivian kwa 

ukali 

“Mheshimiwa rais naomba 

utusamehe sana kwa kutoitika 

mwito wako jana lakini haikuwa 

makusudi.Tulikuwa katika 

operesheni muhimu sana na 

tusingeweza kuiahirisha” 

“Mathew nafahamu kwamba 

nimekupa kazi ya kufanya lakini 

kila pale ninapokuita lazima uitike wito haraka sana.Kitendo 

ulichokifanya jana ni dharau 

kwangu kama rais.Nikikuambia 

acha kila ufanyacho njoo haraka 

unatakiwa utii na uachane na kila 

kitu .Unajua nilikuwa nakuitia 

jambo gani?Ni vipi endapo 

ningekuwa katika hatari na 

ninahitaji msaada?! Akauliza Dr 

Vivian kwa ukali 

‘Tusamehe mheshimiwa rais 

halitajirudia tena jambo kama 

hilo” akasema Mathew.Dr Vivian 

akamtazama kwa macho makali 

akasema 

“Mathew nilikuamini hata 

kabla sijakuona lakini namna 

unavyopeleka mambo yako 

unanifanya niwe na wasi wasi sana.Sijasahau bado jambo 

ulilolifanya kwa Nathan,ukaja tena 

ukataka kumchunguza waziri 

wangu na sasa umefikia wakati 

hata wito wangu 

unaudharau.Sipendi sana 

kudharauliwa kwa sababu tu mimi 

ni mwanamke.Umesahau kuwa 

mimi ni rais wa nchi hii na 

ninapaswa kuheshimiwa!! 

“Mheshim…………….” 

“Sitaki maelezo yoyote 

Mathew.Ninachokuomba kuanzia 

dakika hii lile zoezi 

lisimame.Ulipofika panatosha sana 

na sitaki uendelee zaidi.Nitatafuta 

watu wengine wa kuendelea 

mahala ulikofikia lakini wewe 

sikutaki tena.Nenda kaendelee na shughuli zako za biashara.Ahsante 

sana kwa namna ulivyojitolea 

kuifanya kazi yangu na sitosahau 

mchango wako katika jambo hili” 

“Mheshimiwa rais!! 

“Mathew nimesema sitaki 

maelezo yoyote.Nataka ukabidhi 

ile kadi maalum uliyopewa kwa 

ajili ya kuingilia hapa ikulu na 

sitaki unipigie tena simu .Ahsante 

na nikutakie kila la heri 

.Tukijaliwa uzima tutaonana” 

akasema rais na kusimama 

akatoka.Mathew na Camilla 

wakabaki mle chumbani 

wamepigwa na butwaa 

“Nini kimetokea Mathew? 

Mbona rais anaonyesha kukasirika 

sana? Akauliza Camilla ambaye hakuwa anafahamu kiswahili 

hivyo mazungumzo ya rais na 

Mathew hakuyaelewa 

“Rais hataki tena tuendelee na 

hili suala” 

“Hataki?!! Camilla akashangaa 

“kwa nini? Akauliza 

Kabla Mathew hajajibu 

akaingia mlinzi wa rais na 

kuwasabahi. 

“Nimeelekezwa niwasindikize 

muondoke na kaka nimeambiwa 

unikabidhi kadi uliyopewa” 

akasema yule mlinzi na bila tatizo 

Mathew akamkabidhi kadi 

wakasindikizwa hadi garini 

wakaondoka maeneo ya ikulu 

“Mathew kwa nini 

ukamkubalia rais afanye hivi? Kwa nini ameamua kusitisha uchunguzi 

ambao tayari baadhi ya mambo 

makubwa yameanza kubainika? 

Mathew hili ni kosa kubwa 

amelifanya rais wenu.Hakupaswa 

kufanya vile” akasema Camilla 

“Camilla rais ndiye aliyenipa 

kazi hii na sasa hataki tena 

niendelee nayo” 

“Na wewe uko tayari 

kuachana nayo? 

“Ndiyo Camilla.Sina sababu ya 

kuendeleza uchunguzi wakati 

aliyenipa kazi hataki 

niendelee.Nilijitolea kuifanya hii 

kazi tena bila hata malipo lakini 

kama ameamua tusiendelee ni 

nafuu kwangu kwani ninakwenda 

kuendelea na shughuli zangu za nini ameamua kusitisha uchunguzi 

ambao tayari baadhi ya mambo 

makubwa yameanza kubainika? 

Mathew hili ni kosa kubwa 

amelifanya rais wenu.Hakupaswa 

kufanya vile” akasema Camilla 

“Camilla rais ndiye aliyenipa 

kazi hii na sasa hataki tena 

niendelee nayo” 

“Na wewe uko tayari 

kuachana nayo? 

“Ndiyo Camilla.Sina sababu ya 

kuendeleza uchunguzi wakati 

aliyenipa kazi hataki 

niendelee.Nilijitolea kuifanya hii 

kazi tena bila hata malipo lakini 

kama ameamua tusiendelee ni 

nafuu kwangu kwani ninakwenda 

kuendelea na shughuli zangu za bishara.Usihofu Camilla 

utaendelea kukaa hapa 

nchini,nitakufanyia mpango wa 

kibali cha ukaazi na tutashirikiana 

katika kuendesha miradi 

yangu.Tuachane na hizi kazi na 

tuangalie maisha mengine” 

“Mathew rais amefanya kosa 

kubwa sana .jambo hili si dogo 

wala la kufanyiwa mzaha.Ni jambo 

kubwa na kila uchao linazidi 

kutanuka.Tafadhali kama unaweza 

jaribu kumshawishi tena 

akuruhusu uendelee na 

uchunguzi” 

“hakuna namna tutakayoweza 

kumshawishi rais abadili mawazo 

yake na wala sioni sababu ya 

kufanya hivyo.Kama yeye

 ameamua hivyo basi na iwe.Hata 

hivyo si kwamba suala hili litaishia 

hapa baada ya sisi kuachana nalo 

bali amesema atatafuta wengine 

watakoendelea nalo” 

“Hata akiwatafuta watu 

wengine hawana uzoefu kama 

tulionao sisi.Mpaka sasa uhai wa 

watu umekwisha potea kwa 

sababu ya suala hili.Nimeikimbia 

nchi yangu kwa sababu ya hili 

suala.Kitendo cha kusitisha 

uchunguzi kimeniumiza sana” 

“Usiumie camilla .Haikuwa 

ridhaa yetu bali ya yule aliyetupa 

kazi ndiye aliyeamua kusitisha 

tusiifanye tena kazi yake.Usiogope 

Camilla utaishi maisha mazuri 

hapa Tanzania” akasema Mathew na kuchukua simu yake baada ya 

gari kusimama katika foleni 

akampigia Meshack Jumbo. 

“Mathew habari yako kijana 

wangu” 

“Habari nzuri mzee 

Jumbo.Tayari umekwisha anza 

kazi? 

“Ndiyo Mathew.Niko kazini 

tayari.Mambo yanakwendaje? 

“Mzee sina mengi ya kusema 

kwa sasa ila kwa kifupi tu ni 

kwamba rais amesitisha tena lile 

zoezi” 

“Amesitisha tena?Kumetokea 

nini ? 

“Ni hadithi ndefu mzee 

nitakusimulia tukionana ila 

napenda tu nikushukuru kwa msaada wako mkubwa ulionisaidia 

hadi tukafika hapa” 

“Mathew hebu subiri 

kwanza.Imekuaje hadi rais 

akafanya maamuzi hayo? 

Umekubaliana nayo? 

“Nimelazimika kukubaliana 

nayo kwani yeye rais ndiye 

aliyenipa kazi hiyo na alipozuia 

nisiendelee siwezi 

kupinga.Ninakwenda kuendelea na 

biashara zangu.Nitakutafuta mzee 

wangu tuzungumze vizuri” 

“Mathew jambo hili haliwezi 

kusimama kwa hapa lilipofika 

lazima liendelee.Ninakwenda ikulu 

sasa hivi kuonana na rais lazima 

suala hili tulifikishe mwisho” “Mzee Jumbo ,rais amekwisha 

fanya maamuzi na mimi tayari 

nimekwisha fanya maamuzi ya 

kurejea katika biashara zangu na 

siwezi tena kufanya hii kazi hivyo 

usipoteze muda wako.kama ni 

kuendelea basi tufuteni watu 

wengine wa kuendelea lakini si 

mimi.Kwa heri mzee Jumbo” 

akasema Mathew na kukata simu 

“Mathew una uhakika hutaki 

tena kuendelea kulichunguza hili 

suala na kufahamu ukweli? 

“Sioni sababu ya kuendelea na 

uchunguzi huu ambao rais 

ameanza kuonyesha 

kuupinga.Anataka tufanye 

atakavyo yeye na si kwa mujibu wa 

taratibu zetu hata hivyo hatuwezi kuendelea na jambo ambalo 

muhusika hataki liendele.kama 

wewe ni mkandarasi umepewa 

Kandarasi fulani na aliyekupa kazi 

hiyo akakuzuia usiendelee na kazi 

utaendelea? 

“Lakini Mathew jambo hili ni 

kwa manufaa mapana ya 

nchi.Jambo hili halimuhusu rais 

pekee bali waTanzania wote.kama 

rais hataki,sisi tuendelee kwa 

niaba ya waTanzania” 

“Camilla naomba tu unielewe 

kwamba siwezi tena kuendelea na 

jambo hili.Tujielekeze katika 

mambo mengine muhimu .Wapo 

wengine wataendeleza pale 

tulipofika sisi.Suala hili naomba 

lisikuumize kichwa” “Kichwa lazima kiniume 

Mathew kwani nilikuja Tanzania 

kwa ajili ya kazi hiyo pekee .kama 

kazi iliyonileta haiwezi kufanyika 

hakuna haja ya mimi kuendelea 

kukaa hapa Tanzania” 

“Camilla rais wetu ni mtu 

anayesimama katika maneno 

yake.Akisema hapana ni 

hapana.Hatuwezi kwenda kinyume 

na matakwa yake tutajitengeneza 

uadui naye.Kitu cha msingi 

tuachane na kazi hii kama 

alivyotutaka na tujielekeze katika 

mambo mengine.Tanzania ni nchi 

nzuri na salama kwa 

kuishi.Nitakusaidia kuyaanza 

maisha mengine.Nitakushirikisha 

katika biashara zangu utayafurahia maisha .Tafadhali 

usiwaze kuhusu kuondoka kwa 

kuwa tu ile kazi haiendelei” 

akasema Mathew 

“Mathew sina hakika kama 

nitaweza kufanya kazi nyingine 

zaidi ya upelelezi.Sifahamu 

chochote kuhusu biashara” 

“Usiogope nitakusaidia .Hata 

mimi nilipata wakati mgumu sana 

mwanzoni nilipoamua kuachana 

na hii kazi na kufanya kazi zangu 

binafsi lakini baadae 

nilizoea.Nawe pia utazoea” 

akasema Mathew na safari 

ikaendelea kimya kimya 

“Sijashangazwa na maamuzi 

ya rais kwamba uchunguzi 

usiendelee kwani toka awali  alikwisha onyesha kila dalili za 

kutaka suala hili lisiendelee.Bado 

ana hasira kwa kifo cha 

Nathan.Kwa kuwa yeye ndiye 

mwenye kazi ngoja tuyaheshimu 

maamuzi yake lakini amekosea 

sana.Angeacha suala hili limalizike 

na ukweli ujulikane.Hili ni jambo 

pana sana tofauti na yeye 

anavyofikiri,hata hivyo atatafuta 

watu wengine watakaoendeleza 

pale tulipofikia sisi.Hawatapata 

kazi kubwa kwa sababu 

tumekwisha toboa tundu na 

mwanga mdogo unaonekana” 

akawaza Mathew 

Walifika nyumbani kwa 

Camilla akaingia chumbani kwake 

kupumzika .Wakati Mathew akijiandaa kwenda katika mambo 

yake ya biashara ,simu yake ikaita 

alikuwa ni Theresa 

“Hallow Theresa” 

“Mathew uko 

wapi?Nimekutafuta hapa ikulu 

nikaambiwa tayari umekwisha 

ondoka” 

“tayari nimeondoka 

Theresa.Sikuwa na sababu ya 

kuendelea kukaa hapo baada ya 

dada yako kuzuia tusiendelee na 

ile kazi ya uchunguzi.Naamini 

tayari amekwisha kueleza” 

“Amenieleza nimestuka 

sana.Wewe umeamua nini? 

“Nimeyapokea maamuzi yake 

na nimekubali kutokuendelea tena 

na uchunguzi .Ninarejea tena katika shughuli zangu za kawaida 

za biashara .Ahsante sana Theresa 

kwa ushirikiano mkubwa ulionipa 

na nitatafuta nafasi walau kwa 

chakula tukae tuzungumze mambo 

mengine tofauti na hili kwani 

tayari tumekwisha kuwa 

marafiki.Naamini hautanikatalia 

siku nikikupa mwaliko” 

“Usiogope Mathew muda 

wowote unakaribishwa” 

“Ahsante sana” akajibu 

Mathew.Ukimya wa sekunde 

kadhaa ukapita Theresa akasema 

“Mathew uko wapi? 

“Niko nyumbani lakini nataka 

kutoka kwenda katika miradi 

yangu” “Usitoke hapo nakuja sasa 

hivi.Kuna jambo nataka 

tuzungumze” 

“Sawa nakusubiri” akasema 

Mathew na kukata simu 



Theresa aliwasili nyumbani 

kwa Mathew na kumkuta 

akimsubiri 

“Karibu sana Theresa” 

“Ahsante .Mzungu wako yuko 

wapi? 

“Amepumzika” 

“Mhh ! Theresa akaguna 

“Watu na wazungu wao” 

akasema “Theresa achana na hayo 

mambo.Uliniambia una jambo 

unataka kuzungumza nami” 

“Huachi hata nipumue 

Mathew?Hautaki kuniona hapa 

kwako? 

“Si hivyo Theresa” 

“Kama si hivyo mbona 

unaniharakisha nikueleze kile 

kilichonileta hapa? 

“Basi samahani Theresa 

sikumaanisha hivyo 

unavyofikiri,karibu sana.Tayari 

umekadhi ofisi? 

“Hilo ndilo hasa lililonileta 

hapa kwako”akasema na 

kunyamaza kidogo. 

“Nimefika ikulu mapema leo 

kama dada alivyonitaka nikakutana na huyo atakayekuwa 

anatumia ofisi yangu .Ni 

mwanadada mrembo sana mtoto 

wa rais Anorld Mubara.Baada ya 

kuwa naye kwa saa kadhaa 

nikimuelekeza mambo mbali 

mbali,kuna mambo yamenipa wasi 

wasi kuhusu yule msichana” 

akanyamaza kidogo akamtazama 

Mathew na kuendelea 

“Kuna mambo yamenipa wasi 

wasi kuhusu yule dada anayeitwa 

Tausi Mubara.katika kumuhoji 

aliniambia kwamba hajawahi 

kufika Tanzania na hii ni mara 

yake ya kwanza.Maisha yake yote 

ameishi nchini marekani na ndiko 

alikojifunza kiswahili .Baada ya 

kuonana na rais akanieleza kitu cha tofauti akasema kwamba Tausi 

ni mtoto wa nje wa rais Anorld 

Mubara lakini amelelewa na bi 

April.Nilishangaa kidogo na 

kujiuliza bi April alimleaje wakati 

Tausi hajawahi kufika 

Tanzania?Nilimuuliza pia Tausi 

kama anafahamu maana ya jina 

lake la tausi akasema kwamba 

hafahamu chochote.Nikamuuliza 

nani aliyempa jina hilo la Tausi 

akadai ni baba yake Anorld 

Mubara.Nikamuuliza kama muda 

wote alikuwa anaishi nje ya nchi 

lini ilikuwa ni mara ya mwisho 

kuonana na baba yake?akajibu 

kamba walionana miezi miwili 

kabla ya baba yake hajafariki 

alipokwenda marekani kupima afya yake.Nilimuuliza kama ana 

wafahamu na kuwasiliana na 

ndugu zake waliochangia baba 

akasema kwamba amewahi 

kukutana na mmoja tu anaitwa 

Nancy.Wengine hajawahi kuonana 

nao.Dada alinieleza kwamba 

ameamua kumsaida Tausi baada 

ya kuombwa na bi April 

aliyemfuata jana ikulu” 

Mathew akamtazama Theresa 

kwa muda kisha akasema 

“Theresa umenipa maelezo 

marefu lakini bado sijafahamu ni 

kitu gani hasa unakihitaji toka kwa 

huyu Tausi?Ana tatizo gani? 

“Mathew nimekuja kukueleza 

ili mumchunguze huyu msichana 

ni nani hasa.Anaonekana si mkweli hivyo nimekuja na nakala za vyeti 

vyake vya taaluma ili mnisaidie 

kufanya uchunguzi kwanza kuhusu 

elimu yake na pili kuhusu maisha 

yake” 

“Unahisi amedanganya 

kuhusu elimu yake? 

“Nahisi ametudanganya kila 

kitu kuhusu yeye hivyo nawaomba 

ninyi mliobobea katika mambo 

haya ya uchunguzi mnisaidie 

kumchunguza .Ninaamini kabisa 

kuna kitu hakiko sawa kuhusu 

yule msichana”Mathew akashusha 

pumzi na kusema 

“Unataka kufanya nini baada 

ya kumfahamu? “Hilo ni juu yangu ila 

ninachohitaji ni kumfahamu 

vyema Tausi” 

“Sawa hilo halina tatizo 

tutakusaidia kumchunguza” 

akasema Mathew na kwenda 

chumbani kwa Camilla akamueleza 

kila kitu halafu wakaenda 

sebuleni.Camilla na Theresa 

wakasalimiana .Camilla akaiwasha 

kompyuta yake akachukua kifaa 

cha kuhifadhi kumbu kumbu cha 

Theresa akachomeka katika 

kompyuta yake na kuzipata nakala 

za vyeti vya elimu vya Tausi 

“Amesoma chuo kikuu cha 

Howard” akasema Camilla na 

kuanza kubofya kompyuta yake na 

baada ya dakika kumi akasema “Katika kanzi data ya chuo 

kikuu cha Howard hakuna jina la 

Tausi Mubara.Hawajawahi 

kuhifadhi jina kama hilo” 

“Hilo linawezekanaje wakati 

cheti chake kina jina la Tausi 

Mubara na kimetolewa chuo kikuu 

cha Howard? Theresa akauliza 

“Usihamaki Theresa bado 

tunaendelea kumchunguza.Ngoja 

tuchunguze pia katika hizi shule na 

vyuo alivyoorodhesha kwamba 

amesoma” akasema Camilla 

akaendelea kubofya kompyuta 

yake huku akina Mathew 

wakimtazama.Ilimchukua zaidi ya 

dakika kumi halafu akasema 

“Hivi vyeti vyote ni 

bandia.Huyu Tausi hajawahi kusoma katika vyuo 

alivyoviorodhesha 



amesoma” Akasema Camilla 

“Oh Mungu wangu !! Theresa 

akashangaa 

“Theresa ulikuwa sahihi.Huyo 

msichana ni 

mwongo.Amedanganya ili apate 

ajira ikulu” akasema Mathew 

“Nilikuwa na wasiwasi naye 

sana ndiyo maana nikataka 

kumfahamu vyema .Kumbe ni 

mwongo hana elimu anayodai 

kuwa nayo” akasema Theresa 

“Kwa nini adanganye?Tuanzie 

hapo” akasema Mathew 

“Nadhani kuna ulazima wa 

kumfahamu zaidi.Moja ya nyaraka 

aliyoiambatanisha ina picha yake ngoja tutumie picha hii 

kumtafuta.Leo lazima tuufahamu 

ukweli kuhusu yeye” Akasema 

Camilla na kuchukua picha ile ya 

Tausi akaiingiza katika programu 

maalum ya kutafuta picha na 

ikaanza kutafuta 

“Itachukua muda kidogo 

kwani picha ni nyingi lakini 

inatafuta kwa kasi kubwa” 

akasema Camilla na wote wakakaa 

kimya wakisubiri kompyuta 

imalize kazi 

Ilichukua zaidi ya dakika 

kumi halafu ikatoa mlio na picha 

kubwa iliyofanana na ile ya Tausi 

ikajitokeza. 

“Huyu hapa!! Akasema Tausi “Ni mwenyewe Tausi” 

akasema Theresa 

“Jina lake ni Olivia 

Howard,mzaliwa wa Texas 

Marekani .Baba yake anaitwa 

George Howard na mama yake 

anaitwa Elizabeth Howard.Baba 

yake ni mwanajeshi mstaafu .Huyu 

msichana amedanganya haitwi 

Tausi” akasema Camilla 

“Dada anapaswa kufahamu 

haraka sana kuhusiana na huyu 

msichana” akasema Theresa huku 

akiishika simu yake lakini Mathew 

akamzuia 

“Subiri kwanza usimjulishe 

rais.Lazima kwanza tumfahamu 

kwa kina huyu mtu.Kwa nini atoe taarifa za uongo ? Kwa nini 

amdanganye rais?akauliza Mathew 

“Lazima ana sababu 

maalum.Hawezi kumdanganya 

mkuu wa nchi bila sababu” 

akasema Camilla 

“Ulisema Tausi alipelekwa 

ikulu na bi April Mubara? 

“Dada alinieleza hivyo 

kwamba April Mubara ndiye 

aliyekwenda ikulu jana 

akamuomba amsaidie kumpa kazi 

tausi akidai kwamba ni mtoto wa 

rais Anorld Mubara aliyezaa na 

mwanamke mwingine” 

“Mhh kuna kitu 

kinachanganya hapa,April Mubara 

amemfuata rais akasema kwamba 

Tausi ni mtoto wa nje ya ndoa wa Anorld na yeye ndiye 

aliyemlea.Taarifa tulizonazo 

zinaonyesha kwamba hakuna jina 

Tausi Mubara bali anaitwa Olivia 

Howard.Kwa nini April naye 

alishiriki uongo huu mkubwa? 

Akauliza Mathew. 

“Ili tuzidi kuwa na uhakika 

tufahamu Anorld Mubara alikuwa 

na watoto wangapi,wako wapi na 

kama ikiwezekana tuwasiliane nao 

tufahamu kama wanamfahamu 

huyu ndugu yao Tausi” akasema 

Camilla na kuanza tena kubofya 

kompyuta 

“Ilikuaje hadi ukaanza 

kumuuliza maswali Tausi na 

ukahisi kuna jambo haliko sawa? 

Mathew akamuuliza Theresa “Sikupendezwa na kitendo cha 

dada kunitaka nimpe mtu 

mwingine ofisi yangu hivyo 

nikaanza kumuhoji ili kumfahamu 

ni nani,katokea wapi lakini 

nilivyozidi kumuhoji nikagundua 

kwamba kuna mambo 

aliyoniambia hayakuwa ya kweli 

ndiyo maana nikapata wazo la 

kumchunguza ni kumfahamu 

vizuri” akasema Theresa 

“Nafurahi kushirikiana 

nawe.Theresa umeibua mambo 

mengi .Bila wewe tusingefahamu 

kuhusu Nathan na wala mambo ya 

siri ya George Mzabwa.Leo tena 

umeibua suala lingine muhimu 

sana kuhusu huyu Tausi” akasema 

Mathew Camilla aliendelea kubofya 

kompyuta yake na baada ya muda 

akageuka 

“Tayari.Anorld Mubara 

alikuwa na watoto wawili pekee 

ambao ni Nancy na Jackline 

Mubara.Nancy yuko Marekani na 

Jackline yuko nchini Rwanda 

anafanya kazi katika shirika la afya 

duniani.Huyu ni rahisi 

kumpata.Tupige simu ofisi za WHO 

Rwanda tuombe kuzungumza 

naye” akasema Camilla na bila 

kupoteza wakati zikatafuta namba 

za simu za WHO Rwanda .Theresa 

akapewa apige simu. 

“Hallow” ikasema sauti ya 

upande wa pili. “Hallow,naongea na Jack 

Mubara? Theresa akauliza 

“Ndiyo.Nani mwenzangu? 

“Naitwa Theresa Matope 

nafanya kazi ikulu” 

“Oh Theresa! Nimefurahi 

kukufahamu.Una uhusiano na rais 

Vivian matope? 

“Ndiyo .Ni dada yangu” 

“Oh vizuri.Nikusidie nini 

Theresa? 

“Samahani sana Jack kuna kitu 

nataka kukuuliza.Nataka 

kufahamu kuna ndugu yenu 

ameanza kazi leo hapa ikulu 

anaitwa Tausi Mubara.Anadai 

yeye ana mama yake 

mwingine.Unamfahamu?“Tausi Mubara? Jack 


****************


PARIS – UFARANSA 

Peniela hakutaka tena 

kuendelea kukaa ofisini kwake 

akaondoka kurejea 

nyumbani.Kichwa chake kilijaa 

mawazo mengi.Alipofika 

nyumbani aliyatoa maelekezo kwa 

walinzi na watumishi wake 

kutosumbuliwa na mtu yeyote 

akajifungia chumbani kwake 

.Alichukua albamu kubwa la picha 

akaanza kupitia picha moja moja 

akakumbuka mambo mengi na 

akiwa katika tafakari nzito ya 

maisha yake simu ikaita 

akatazama mpigaji na kwa haraka 

akalitupa pembeni albamu la picha 

na kuipokea ile simu “Hallow Lydie” 

“Dada tayari nimeikamilisha 

ile kazi” 

“Ahsnate sana.Nipe majibu” 

“Nimefuatilia ile akaunti ya 

George Mzabwa.Ni kweli amekuwa 

anapokea fedha kutoka kampuni 

ya kutengeneza saa ya Flamingo 

iliyopo Marekani.Kiasi cha mwisho 

kuingizwa katika akaunti hiyo 

kilikuwa shlingi milioni mia saba 

na sabini .George alizitoa fedha 

hizo na kuziweka katika akaunti 

tatu tofauti lakini zote ni za 

kampuni ya kuchonga madini ya 

vito ya Tanbest Gemstone 

ltd.Kampuni hii inafanya biashara 

na kampuni ya 

Flamingo.Nimefuatilia fedha hizi zilizowekwa katika akaunti tatu za 

kampuni ya Tanbest ,katika 

akaunti moja fedha zilizotolewa na 

mtu anaitwa Ranbir Kumar.Katika 

akauni ya pili fedha zilihamishwa 

na kuingizwa katika akaunti 

nyingine ya Robert Mwainamela na 

baadae zikatolewa zote.Katika 

akaunti ya tatu fedha zilitolewa na 

Ranbir Kumar .Kuhusu ile kazi ya 

pili uliyonipa ya kutafuta wamiliki 

wa kampuni za A.D Electronics na 

Flamingo” 

“Umegundua nini? 

‘Makampuni haya yote mawili 

yanamilikiwa na mtu mmoja 

anaitwa Edwin Washington” 

“Edwin Washington? Peniela 

akashangaa “Ndiyo dada.Edwin 

Washington ndiye mmiliki wa hizi 

kampuni zote mbili” akasema 

Lydie na ukimya mfupi ukatanda 

kisha Peniela akasema 

“Lydie ahsante sana naomba 

asifahamu mtu mwingine yeyote 

kuhusu mambo haya niliyokuomba 

unifanyie” 

“Usihofu dada” akasema Lydie 

na kukata simu.Peniela akavuta 

pumzi ndefu na kuhisi baridi kwa 

ndani 

“Mathew alikuwa sahihi 

kabisa .Andrew na mwanae 

Anderson wana siri 

kubwa.Yawezekana wananitumia 

bila mimi kujielewa kama 

aliyosema Mathew” akawaza “Mathew alisema kwamba 

George Mzabwa aliyekuwa 

mkurugenzi wa idara ya usalama 

wa taifa na baadae akajipiga risasi 

,alikuwa anashirikiana na shirika 

la ujasusi la CIA na kwamba CIA 

wamekuwa wakitumia Escom bank 

ambayo mimi ni mmoja wa 

wamiliki kupitishia fedha zake 

kwa ajili ya operesheni zao nchini 

Tanzania.George amekuwa 

anatumiwa fedha nyingi toka 

kampuni ya Flamingo 

inayomilikiwa na 

Andrew,ninachojiuliza kama 

Flamingo wanafanya biashara na 

kampuni ya Tanbest ambayo 

yawezekana labda George alikuwa 

na hisa kwa nini wasiilipe kampuni moja kwa moja hadi fedha zipitie 

kwanza katika akaunti ya George 

ndipo aziingize katika akunti za 

kampuni ya Tanbest?Kama CIA 

wamekuwa wanapitisha fedha kwa 

kutumia benki ya Escom 

inawezekana kampuni ya Flamingo 

ndiyo inayotumika kupitishia hizo 

fedha ?Kama jibu ni ndiyo ,Andrew 

Pillar ndiye mmiliki wa kampni 

hiyo analifahamu hilo?akajiuliza 

Peniela na kustuka ghafla 

“Oh my God!! Inawezekana 

Andrew akawa ni CIA? Akajiuliza 

na kutazama juu kwa sekunde 

kadha halafu akainuka akavaa na 

kuingia katika gari akaondoka 

peke yake bila walinzi “Lazima nimchunguze pia 

Anderson .Kuna mambo atakuwa 

ananificha.Kauli ya Mathew 

kwamba Anderson na baba yake 

wananitumia bila mimi kujifahamu 

inanifanya niwaze mambo mengi 

sana.Baada ya kumfahamu Andrew 

Pillar ni nani nimeanza kuwa na 

mashaka mengi hata na 

Anderson.Kuna uwezekano 

mkubwa nikafahamu mambo 

ambayo sikuwa nikiyafahamu 

kuhusu hawa jamaa.Namshukuru 

sana Mathew kwa kunifumbua 

macho.Sikuwahi kuhisi chochote 

kibaya kuhusu Anderson na baba 

yake.Kitendo cha Anderson kuwa 

na majina mawili tofauti 

kimenistua sana” akawaza Peniela akielekea nyumbani kwa mpenzi 

wake Anderson Pillar 

Alifahamika nyumbani kwa 

Anderson hivyo hakuna aliyemzuia 

na moja kwa moja akaingia 

chumbani kwa Anderson kwa 

kuwa alikuwa na funguo.Aliangaza 

angaza wapi aanze 

kuchunguza,mara simu yake ikaita 

alikuwa ni Anderson Pillar.Peniela 

akatetemeka na kuogopa 

kupokea.Simu ikaita tena na safari 

hii akaamua kuipokea 

“Hallow Anderson” akasema 

Peniela 

“Peniela mpenzi wangu uko 

wapi? Akauliza .Peniela 

akababaika kujibu “Uko ofisini ? Anderson 

akauliza 

“Hapana siko ofisini 

nimekwisha toka” 

“Uko wapi mida hii? 

“Nimetoka kidogo kuna 

mahala nimekwenda” 

“Sawa mpenzi ,basi ukirejea 

nyumbani kwako unifahamishe 

nataka kuonana nawe” 

“Nitakujulisha” akasema 

Peniela na kukata simu akashusha 

pumzi ,akalisogelea kabati kubwa 

la nguo na kulifungua akaiona 

droo ndogo 

“Nimewahi kumuona 

Anderson akiweka vitu katika droo 

hii.Yawezekana ninaweza kukuta 

baadhi ya vitu vyake vya siri kama nilivyokuta kwa baba yake 

Andrew” akawaza Peniela na 

kuifungua ile droo .Kabla hajagusa 

chochote akasikia mlio wa kitu 

akageuka na kugundua mlio ule 

ulitoka katika kitu mfano wa saa 

kilichokuwa juu ukutani 

kikionyesha namba zikienda kwa 

kasi kubwa na mara namba 

zikasimama kukaonekana sifuri 

mbili 

“Nini kile? Akajiuliza na mara 

sauti ikasikika toika katika kile 

chombo 

“La sortie est verrouuillee !! 

ikiwa na maana mlango 

umejifunga.Haraka haraka Peniela 

akakimbia hadi mlangoni 

akajaribu kuufungua lakini haukufunguka tayari ulikwisha 

jifunga 

“Oh no ! Mambo gani haya 

?akawaza Peniela akiwa 

amechanganyikiwa.Akachukua 

simu yake na kutaka kumpigia 

Anderson lakini kila alipojaribu 

kupiga simu haikutoka 

“Nimeingia choo cha 

kiume.Huku mahala siko.Anderson 

atakuwa ameweka mfumo maalum 

katika chumba chake akiingia mtu 

ambaye haumtambui basi kila kitu 

hujifunga na huwezi kutoka 

.Nimekwama lakini lazima nitafute 

namna ya kujiondoa humu kabla 

Anderson hajanikuta hapa na 

nikakosa jibu la kumpa nimekuja 

kutafuta nini chumbani kwake bila kumjulisha” akawaza Peniela na 

kuliendea dirisha.Lilikuwa ni 

dirisha imara sana,akajaribu 

kuligusa akapigwa na shoti ya 

umeme 

“Dah ! ama kweli ndege 

mjanja hunaswa katika tundu 

bovu.Nimenaswa humu na sielewi 

nitatoka vipi!! Akawaza na kuketi 

kitandani akitafakari namna ya 

kujiokoa.Kabla hajaamua afanye 

nini akasikia mlango unafunguliwa 

akasimama haraka haraka na 

kusogea mlangoni na ghafla 

hakuamini 

alichokiona.Aliyesimama mlangoni 

alikuwa ni mpenzi wake Anderson 

Pillar.Walibaki wanatazamana na 

Peniela alishindwa kuzungumza chochote alikuwa anatetemeka 

kwa ndani 

“Hallow Peniela.Karibu 

mpenzi wangu” akasema Andrew 

lakini bado Peniela aliendelea 

kusimama na hakuongea 

chochote.Anderson akaufunga 

mlango na kumsogelea Peniela 

“Hapa ni kwako Peniela hivyo 

usiwe na wasi wasi ila ulipaswa 

kunieleza ukweli kwamba uko 

hapa na mimi nisingekuwa na 

shida nawe kwani hapa 

unaruhusiwa kuingia muda 

wowote.Kingine naomba nikuweke 

wazi kwamba kuna kamera za siri 

humu chumbani kwangu na kila 

ninapoondoka huwa 

naziunganisha na simu yangu hivyo chochote kinachoendelea 

humu chumbani wakati sipo 

ninajulishwa kupitia simu 

yangu.Ulipoingia ndani 

nilijulishwa na ndiyo maana 

nikakuuliza uko wapi?Nawe 

hukunieleza ukweli 

ukanidanganya ,nikapatwa na wasi 

wasi kwamba ujio wako huu si 

mwema na hivyo nikafunga kila 

kitu kwa kutumia simu” akasema 

Anderson na Peniela akakasirika 

“Kwa nini ukanifanyia hivyo 

Anderson ? Huniamini? Hutaki nije 

chumbani kwako wakati haupo? 

Akauliza 

“Swali hilo nalirejesha 

kwako.Kwa nini ukanidanganya 

nilipokuuliza mahala ulipo?Kwa nini hukunieleza ukweli kwamba 

uko hapa nyumbani kwangu? Kwa 

nini ukaja kwa siri? Kuna nini 

unakitafuta? Tuanzie hapo” 

akasema Anderson.Peniela 

hakuweza kujibu chochote 

“Huna cha kusema Peniela? 

Akauliza Anderson akizidi 

kumsogelea Peniela 

“Kama hutaki kusoma kwa 

hiari yako 

mwenyewe,nitakulazimisha 

kuongea” akasema Anderson 

“Naomba usinikaribie 

tafadhali!! Akasema Peniela na 

simu ya Anderson ikaita akaitoa 

mfukoni na kuipokea.Kadiri 

alivyokuwa anazungumza na yule 

aliyempigia simu ndivyo sura yake ilivyozidi kubadilika.Alipomaliza 

kuongea na simu akamtazama 

Peniela kwa macho makali 

“Umefanya nini nyumbani 

kwa baba? Akauliza 

“Baba yako amekuelekeza 

nilichokifanya? 

“Kwa nini ukafanya vile 

Peniela?Kukupenda huku kote 

tunakokupenda haitoshi hadi 

uanze kutuchokonoa maisha yetu 

ya ndani? 

“Wewe na baba yako wote ni 

walaghai.Kwa nini hamkunieleza 

ukweli kuhusu biashara 

zenu?Mmekuwa mnanitumia kwa 

faida zenu.Mlidhani sintakuja 

kuwagundua?akasema Peniela 

kwa ukali “Peniela tafadhali nakuomba 

sana ,ulichokigundua nyumbani 

kwa baba kibaki siri yako na 

usimueleze mtu mwingine 

yeyote.Ninakupenda sana na 

nitakueleza kila kitu ili mradi 

unihakikishie kwamba suala hili 

litabaki kati yetu na hatafahamu 

mwingine” akasema Anderson 

akimkaribia Peniela ambaye 

alikuwa anasogea taratibu 

kuelekea mlangoni.Anderson 

alilifahamu lengo la Peniela akatoa 

bastora baada ya Peniela 

kuukaribia mlango 

“Usijaribu kutaka kutoka 

Peniela.Ninakupenda sana na 

sitaki kukufanyia chochote 

kibaya.Tafadhali kaa tuzungumze na nitakueleza kila unachotaka 

kukifahamu” akasema Anderson 

“Huyu hajanifahamu bado 

historia yangu.Nikiwa Team SC41 

nilipewa mafunzo ya hali ya juu 

sana.Ngoja nimuonyeshe uwezo 

wangu.Lazima nipambane ili 

kujiokoa” akawaza Peniela na 

ghafla akajifanya ameteleza na 

kutaka kuanguka chini.Anderson 

akaruka hatua mbili kumuendea 

Peniela bila kujua kwamba ule 

ulikuwa ni mtego. 

“Peniel………….” Akasema 

Anderson na kuinama lakini ghafla 

akapigwa teke kali sana 

lililomfanya apepesuke na 

kuanguka chini.Peniela akainuka 

kwa kasi akiwa na chuma mkononi alichokiokota wakati ameanguka 

chini na kumpiga nacho Anderson 

usoni akatoa mguno wa maumivu 

makali.Bila kumpa nafasi 

akamuendea na kumpiga teke kali 

la mbavu na Anderson akaanza 

kulalamika kuvunjwa 

mbavu.Peniela tayari alikwisha 

pandwa na hasira akachukua 

chungu cha maua na kumpiga na 

kukipasua katika kichwa cha 

Anderson akapoteza fahamu. 

Akauinua mtungi wa pili na 

kutaka kumpiga nao Anderson 

mara simu yake ikaita.Alikuwa ni 

yaya wa Anna Maria.Akauacha 

mtungi ule ukaanguka na kuipokea 

simu 

“Hallow” akasema “Dada ,Anana Maria 

amerudishwa nyumbani 

anasumbuliwa na mafua” 

“Nakuja sasa hivi.Andaa nguo 

na vitu vyake kwa ajili ya safari” 

akasema na kukata simu 

akamtazama Anderson aliyekuwa 

amelala akivuja damu.Akapandwa 

na hasira akaanza kumpiga 

mateke ya usoni 

“Kwa sababu yako nilimuacha 

mwanaume aliyenipenda kwa 

dhati ya moyo wake,akayatoa 

maisha yake kwa ajili 

yangu,kumbe hukuwa na mapenzi 

yoyote nami .Wewe na baba yako 

wote ni mashetani 

wakubwa.Nimewachukia sana!! 

Akasema na kumtandika teke kali la tumbo akatoka mle chumbani 

hadi katika gari lake na kuondoka 

kwa kasi.Akiwa njiani akazitafuta 

namba fulani akapiga 

“Donald andaa ndege haraka 

sana nina safari ya ghafla kuelekea 

Tanzania.Ndani ya nusu saa tayari 

nitakuwa hapo” akasema Peniela 

“Sawa mama ndege iko tayari 

muda wote na nitakachokifanya 

hivi sasa ni kujaza mafuta ya 

kutosha kwa safari hiyo ndefu” 

akasema Donald 

Alifika nyumbani kwake na 

kwa haraka akapakia baadhi ya 

vitu vyake vichache akawachukua 

mwanae na mwangalizi wake 

wakaondoka kuelekea uwanja wa 

ndege.Hakutaka kuongozana na mlinzi yeyote .Ndege yake binafsi 

ilikuwa tayari wakapanda na safari 

ya kuelekea Tanzania ikaanza 

“Narudi tena 

Tanzania.Anderson shetani 

mkubwa naamini atakuwa 

amekufa nilimpiga sehemu 

mbaya.Najilaumu sana kwa 

kumuacha Mathew mwanaume 

aliyenipenda kwa dhati .Aliyatoa 

maisha yake kwangu.Lazima 

nifanye kila niwezalo kurudisha 

tena penzi letu kwani naamini 

bado sijachelewa.Mimi ndiye 

niliyemkosea kwa tamaa zangu 

lakini hakuwahi kunikosea hata 

mara moja.Yeye ni chanzo cha huu 

utajiri wangu na ndiye aliyenitoa 

mdomoni mwa mamba na kuyabadili maisha 

yangu.Simjulishi kama 

ninakwenda Tanzania 

nitamjulisha nikifika uwanja wa 

ndege wa Julius Nyerere”akawaza 

Peniela. 

MPENZI MSOMAJI,PENIELA 

ANAREJEA TENA DAR ES SALAAM 

KUFUATIA MASAHIBU 

YALIYOMKUTA CHINI 

UFARANSA.NINI KINAKWENDA 

KUTOKEA KATI YAKE NA 

MATHEW? 

MATHEW ANAKUTANA NA 

CHANGAMOTO NYINGI KATIKA 

UCHUNGUZI ANAOUFANYA JE 

ATAFANIKIWA KUUPATA UKWELI? MAREKANI WANAPANGA 

KUMUUA WAZIRI WAO WA 

MAMBO YA NJE ILI WAPATE 

SABABU YA KUISHAMBULIA 

KOREA KASKAZINI JE 

WATAFANIKIWA MIPANGO YAO” 

ENDELEA KUIFUTAILIA 




Rais wa jamhuri ya muungano wa 

Tanzania Dr Vivian Matope 

alisimamisha shughuli Zake kwa 

muda baada ya kutaarifiwa 

kwamba rais wa Korea Kaskazini 

Kim Yuh Hu alikuwa katika laini ya 

simu kwa ajIli ya mazungumzo ya 

ana kwa ana kupitia runinga.Dr 

Vivian akiwa ameongozana na Dr 

Robert Mwainamela waziri wa 

mambo ya nje wa Tanzania 

wakaingia katika chumba cha 

mazungumzo ya moja kwa moja 

kwa kutumia runinga na bila 

kupoteza muda Dr Viviana 

akaanzisha mazungumzo “Mheshimiwa rais Kim habari 

yako” 

“Habari nzuri sana Dr Vivian 

habari ya Tanzania? 

“Huku kwema 

kabisa.Nimeambiwa uko kwenye 

laini nikaacha shughuli na kuja 

kukusikiliza” akasema Dr Vivian 

“Dr Vivian nimekupigia simu 

ili kukupa taarifa za kile 

kinachoendelea kuhusiana na ule 

mpango wetu wa 

mashirikiano.Muda mfupi uliopita 

kimemalizika kikao kati yangu na 

mawaziri wangu na katika kikao 

hicho tumejadili jambo hili kwa 

upana wake na tumeazimia 

kwamba itatumwa timu ya watu 

hamsini na saba kuja Tanzania wakiwa ni wataalamu katika 

nyanja mbali mbali.Watakuja 

Tanzania kukutana na wenzao na 

kisha kwa pamoja watajadili 

namna bora ya kufanya 

mashirikiano haya yawe ni yenye 

tija kwa nchi zote mbili.Naamini 

ujumbe huo tutakaoputuma 

utapata ushirikiano mkubwa toka 

kwa watu wako utakaokuwa 

umewaandaa kwa ajili ya shughuli 

hii ili kuharakisha suala hili liende 

haraka,hakuna kuchelewa katika 

suala lenye maslahi makubwa 

kama hili” akasema Kim 

“Nashukuru kwa taarifa hiyo 

nzuri mheshimiwa rais 

Kim.Naponda kwa mara nyingine 

tena kukuhakikishia kwamba mimi na serikali tunayo nia ya 

dhati kabisa ya kufanya 

mashirikinao na serikali yako ya 

Koreaka Kaskazini na tayari 

tumekwisha waandaa watu wetu 

kwa ajili ya jambo hilo.Ujumbe 

wako utakapofika utapokelewa 

vizuri na kupewa ushirikiano 

mkubwa kwani ni dhamira yangu 

hata mimi kuona suala hili 

linakwenda haraka haraka na 

mashirikiano haya yanaanzishwa” 

akasema Dr Vivian. 

“Kwa kuongezea hapo Dr 

Vivian” akasema Kim 

“Hivi sasa kuna kelele nyingi 

sana zinapigwa na vitisho 

kutolewa kutoka kwa yale mataifa 

mahasimu wetu na yote hii ikiwa na lengo moja tu la kuhakikisha 

mashirikiano yuetu 

hayafanikiwi.Marekani na 

washirika wake ndio wanaoongoza 

harakati hizo za kuhakikisha 

kwamba hatushirikiani.Wanafanya 

kila wawezalo kuhakikisha 

mpango huu 

haufanikiwi.Nakuomba tafadhali 

usilegeze msimamo wako hata 

kidogo.Hii ni vita na ili kupata 

ushindi lazima maadui zetu 

watumie kila mbinu 

wanayoweza,watatumia maneno 

na vitisho,wakishindwa watatumia 

vikwazo vya 

kiuchumi.Wanafahamu kwamba 

Tanzania bado ni taifa masikini na 

linategemea misaada kutoka mataifa wafadhili kwa hiyo 

wakiweka vikwazo vya kiuchumi 

nchi itayumba na hivyo 

kukubaliana na matakwa 

yao.Wakishindwa hapo katika 

vikwazo vya kiuchumi watatumia 

mbinu ya kuwavuruga kama 

nchi,wanaweza wakaleta mivutano 

na migogoro ndani ya nchi ili 

mvurugane na mshindwe 

kuelewana na wakishindwa pia 

katika hilo watatumia mbinu ya 

kukuondoa madarakani na hapa 

wanaweza hata kukuua na 

wanaweza wakatumia hata watu 

wako mwenyewe.Ninakueleza 

hayo Dr Vivian ili uweze kujiandaa 

kwani Marekani ninawafahamu 

vyema ni nchi yenye kutumia kila aina ya mbinu kufanikisha kupata 

kile wakitakacho.Hawatakubali 

kabisa kushindwa katika hili hivyo 

jiandae kwa misuko suko mikubwa 

lakini usihofu sisi tuko pamoja 

nawe na tutasimama nawe katika 

kila hatua.Tanzania ni nchi tajiri 

kwa rasilimali na ndiyo maana 

nchi nyingi kubwa wanaelekeza 

macho yao huko hivyo suala hili si 

suala dogo” 

“Nalifahamu hilo Kim na 

tayari nimekwisha jiandaa 

kukabiliana nalo kwa namna 

yoyote ile hivyo usiwe na 

wasiwasi.Pale nitakaposhindwa 

nitakuomba msaada.Nazifahamu 

mbinu zao zote chafu na 

tutazikabili”akasema Dr Vivian “Kitu kingine cha muhimu” 

akasema Kim 

“Kuanzia sasa usimuamini 

mtu yeyote.Punguza idadi ya watu 

wale unaowaamini na 

unaowaeleza mipango na siri 

zako.Marekani wana tabia ya 

kuwatumia watu wa karibu 

kuweza kukuangamiza.Watu 

unaowaamini leo wanaweza 

wakakugeuka kesho.Kuwa makini 

sana hasa katika mambo yako ya 

siri”akasema Kim 

“Niko makini sana na hilo 

suala Kim na tayari nimekwisha 

anza kulifanyia kazi”akajibu Dr 

Vivian 

“Vizuri sana.Suala lingine 

ambalo nimelijadili na mawaziri wangu ni kuhusiana na ombi lako 

la kujengewa kinu cha nyuklia kwa 

ajili ya kuzalisha nishati ya 

umeme.Katika ujumbe 

nitakaoutuma nchini 

Tanzania,watakuwepo pia 

wataalamu wa nyuklia ambao 

watakuja kufanya utafiti namna ya 

kuweza kujenga kinu hicho na 

kutoa mapendekezo yao kabla ya 

ujenzi kuanza.Nimezungumza pia 

na rais wa China na kwa pamoja 

tumekubaliana kwamba 

tutashirikiana katika ujenzi wa 

kinu hicho.Mheshimiwa rais 

ninaiona picha ya Tanzania mpya 

miaka michache ijayo .Litakuwa ni 

taifa kubwa lenye nguvu kiuchumi 

na kijeshi pia barani Afrika.Kitu kikubwa cha msingi usikate tamaa 

tuendelee kupambana hadi 

tuhakikishe tunaweka sahihi 

mashirikiano haya.Kwa sasa 

tuwape nafasi wataalamu wetu 

wafanye maandalizi.Ninakuahidi 

ulinzi mkubwa kwa nchi yako 

dhidi ya taifa lolote litakalotishia 

amani ya Tanzania” akasema Kim 

Hun Yu 

Wakati mazungumzo kati ya 

rais wa Tanzania Dr Vivian na rais 

Kim Hun Yu wa Korea Kaskazini 

yakiendelea,Theresa akawasili 

ikulu na moja kwa moja akaelekea 

ofisini kwake 

“Theresa umerejea !! Tausi 

akashangaa kwani walikwisha 

agana “Ndiyo Tausi.Nimerejea tena 

kuna kazi nimekumbuka sikuwa 

nimeikamilisha ni ya muhimu 

sana” akasema Theresa 

“Rais aliniambia kwamba 

kuna kazi unaifanya nje ya ofisi,ni 

kazi gani unaifanya huko?Tausi 

akauliza na Theresa akatabasamu 

“Kuna jambo la kifamilia 

ninalishughulikia ndiyo maana 

nikaomba likizo fupi.Unaendeleaje 

na kazi hapa? 

“Ninaendelea vyema 

japokuwa sijapata ushirikiano 

mzuri toka kwa wafanyakazi wa 

hapa.Kila mmoja yuko na kazi zake 

na hakuna anayenijali nakosa hata 

mtu wa kumuuliza kitu 

chochote.Mpaka sasa sielewi kazi yangu ni ipi .Natamani nimuulize 

rais lakini amekuwa na shughuli 

nyingi leo hata kumuona imekuwa 

kazi ngumu.” 

“Usijali Tausi,hapa ikulu ni 

sehemu yenye pilika pilika nyingi 

sana kwa hiyo kila mmoja yuko 

katika kufanikisha jukumu 

lake,lakini mimi niko hapa kama 

kuna chochote unahitaji nikusaidie 

nitakusaidia” 

“Ninashukuru sana Theresa 

na nimefurahi umekuja.Kuna 

jambo nitaomba unisaidie.Mimi ni 

mtaalamu wa mawasiliano japo 

nina shahada ya mahusiano ya 

kimataifa lakini napendelea zaidi 

kufanya kazi katika sehemu ya 

mawasiliano.Ninaomba unisaidie kuongea na dada yako ili aweze 

kunipangia niende huko katika 

kitengo cha mawasiliano.Unaweza 

kunisaidia kwa hilo tafadhali? 

“Usihofu Tausi 

nitakusaidia.Nitazungumza na 

dada na atanisikia.Hilo ni suala 

dogo sana kwangu nikimueleza 

dada atalifanyia kazi haraka.” 

“Ahsante Theresa nitashukuru 

sana uknisaidia kwa hilo” akasema 

Tausi na baada ya muda Theresa 

akauliza 

“Vipi maisha ya hapa Tanzania 

unayaonaje? 

“Maisha ya hapa ni mazuri ila 

tatizo ni foleni ndefu hasa nyakati 

za asubuhi.Ni changamoto kubwa kuwahi kazini kwa foleni ndefu 

namna ile.” 

“Hapa Dar es salaam unaishi 

wapi Tausi? 

“Nilikuwa naishi na mama 

lakini kwa sasa nimehama kule 

shambani kwake na nimehamia 

Dar es salaam ili nipate urahisi wa 

kuja kazini” 

“Hapa Dar es salaam unaishi 

wapi?Theresa akauliza tena 

“Ninaishi mji mweupe” 

“Oh ! ni sehemu nzuri sana.Ule 

ni mji mpya umejengwa hivi 

karibuni na ni sehemu wanakoishi 

watu wenye uwezo mkubwa 

kifedha.Ulipewa jina la mji 

mweupe kutokana na majengo 

yake karibu yote kupakwa rangi nyeupe.Ninakwenda kule mara 

kwa mara ninao marafiki zangu 

wawili wanaishi kule”akasema 

Theresa 

“Ni pazuri sana hata mimi 

nimepapenda.Nikiw akule najiona 

kama niko Marekani.Ni mji 

uliojengwa kimataifa” akasema 

Tausi 

“Unaishi nyumba gani pale ili 

siku moja nije nikuchukue 

nikutembeze katika jiji hili la Dar 

es salaam ufurahie uzuri wake? 

“Bado sijafahamu vyema 

mitaa ila nyumba ninayoishi ni 

namba 402Block C iko nyuma ya 

kanisa katoliki” 

“Oh Vizuri.Nitakuja 

kukutembelea mwishoni mwa wiki.Unaishi mwenyewe au tayari 

umekwisha pata mwenza? 

Akauliza Theresa na Tausi 

akacheka kicheko kikubwa 

“Sina mwenza ninaishi 

mwenyewe.Vipi wewe umekwisha 

olewa? 

“Hapana bado.Mambo ya 

kimahusiano hayakwenda vizuri 

hivyo bado niko mwenyewe” 

“Vipi rais anaolewa 

lini?Nilisikia mama akimuuliza 

suala la ndoa yake” 

“Alikuwa na mpango wa 

kufunga ndoa lakini mambo 

yamevurugika na ndoa imeota 

mbawa” 

“Nini kilitokea? “Kuna mgogoro ulitokea kati 

yake na mpenzi wake ikabidi suala 

la ndoa lisitishwe kwanza” 

“Masikini.Nini hasa kilitokea? 

“Ni mambo ya kawaida ya 

wapenzi” 

“Mpenzi wake ni mTanzania? 

“Hapana si mTanzania.Ni 

Mmarekani” 

“Hawakuwa wakiishi pamoja? 

“Hapana.Bado hawakuwa 

wakishi pamoja.Tuachane na hayo 

mambo.Twende nikakuonyeshe 

sehemu mbali mbali za hapa ikulu 

na kukutambulisha kwa watu 

wakufahamu.Naomba vile vile 

unipe namba yako ya simu ili tuwe 

na mawasiliano ya mara kwa mara 

ili hata pale utakapohitaji msaada wakati sipo iwe rahisi kuwasiliana 

kukusaidia” 

“Kwa sasa sina 

simu.Nimeambiwa hadi nisajili 

laini.Nitakujulisha nitakapopata 

laini ya simu” akasema Tausi 

Theresa akamuomba Tausi 

amsubiri kwa muda aende 

maliwatoni.Akaufunga mlango na 

kumuandikia Mathew ujumbe 

“Tausi anakaa mji mweupe 

nyumba namba 402 kitalu 

C.Nyumba anayoishi iko nyuma ya 

kanisa katoliki.Anaishi mwenyewe 

na hana simu” 

Baada ya kutuma ujumbe ule 

akatoka akamchukua Tausi na 

kuanza kumzungusha sehemu 

mbali mbali za ikulu Dr Vivian alimaliza 

mazungumzo na rais Kim Hun Yu 

wa Korea kaskazini na kutoka 

katika kile chumba cha 

mazungumzo na akajulishwa 

kwamba balozi wa Marekani 

Abraham Clerk alikuwa 

amefika,akampa maelekezo Dr 

Robert halafu akaelekea ofisini 

kwake na balozi Abraham 

akakaribishwa 

“Mheshimiwa balozi 

Abraham,karibu sana” 

“Ahsante sana mheshimiwa 

rais” 

“Habari za toka jana? 

“Nzuri mheshimiwa 

rais.Nimepata ujumbe wako hivyo 

nimeitika wito wako ulionitaka nifike kukuona.Naamini kuna 

taarifa nzuri” 

“Balozi nimekuitia masuala 

mawili.Kwa kuwa leo nina mambo 

mengi nitaongea kwa kifupi 

sana.jambo la kwanza kwanza ni 

kuhusiana na lile suala la Nathan” 

akanyamaza kidfogo halafu 

akaendelea. 

“Tayari nimekwisha toa 

maelekezo kwa vyombo vyangu 

vya uchunguzi na vinaendelea 

kulifanyia kazi suala hilo ila mpaka 

sasa bado sijapata mrejesho toka 

kwao.Naamini pindi 

watakapokamilisha kazi 

niliyowatuma watanipa taarifa na 

mimi nitakujulisha nini 

wamekipata.Suala la pili ni kuhusiana na ziara ya waziri wa 

mambo ya nje wa 

marekani.Nimepata taarifa toka 

kwa waziri wangu wa mambo ya 

nje kwamba waziri wa mambo ya 

nje wa Marekani atafika hapa 

nchini baadae leo kwa ajili ya 

ziara fupi.Nini hasa kinamleta 

Tanzania? Akauliza Dr Vivian 

“Mheshimiwa rais tukianzia 

na hilo suala la pili .Ni kweli waziri 

wa mambo ya nje wa Marekani 

anakuja Tanzania.Alikuwa na ziara 

ya kwenda Rwanda lakini 

kutokana na mambo 

yanayoendelea hivi sasa kati ya 

Tanzania na marekani 

amelazimika kuahirisha ziara yake 

ya Rwanda na kuja Tanzania.Akiwa hapa atafanya 

mazungumzo na waziri mwenzake 

wa mambo ya nje wa Tanzania 

halafu atakutana na wamarekani 

walioko hapa nchini.Kufuatia 

mvutano unaoendelea hivi sasa 

watu wetu walioko hapa Tanzania 

wameingiwa na hofu kubwa kwa 

hiyo anakuja kuwatuliza 

wamarekani na kuwataka wawe 

watulivu wakati suala hili 

linatafutiwa ufumbuzi.Kabla 

hajaondoka hapa nchini atakuja 

kukuona na atakuwa na 

mazungumzo nawe. Lengo ni 

kutafuta muafaka wa suala hili 

linaloendelea kufukuta hivi sasa” 

akasema Abraham na kunyamaza 

kidogo halafu akaendelea “Tukirejea katika suala la 

kwanza kuhusiana na 

Nathan,ninashukuru kwa jitihada 

ambazo umezifanya za kuanza 

kuchunguza na kutafuta mahala 

aliko lakini nina ombi moja ili na 

sisi tuwe na imani kwamba 

Tanzania inafanya juhudi kubwa 

katika kumtafuta mtu wetu 

nahitaji na sisi tushirikishwe 

katika uchunguzi huo.Ninaomba 

walau kuwe na watu wetu wawili 

watakaoambatana na timu hiyo ya 

wachunguzi na vile vile na mimi 

nitataka niwe nikipewa taarifa za 

namna uchunguzi huo 

unavyoendelea na kila hatua 

inayofikiwa.Ukifanya hivyo 

mheshimiwa rais utatufanya na sisi tuwe na imani kwamba kuna 

kazi kubwa inafanyika ya 

kumtafuta Nathan” akasema Balozi 

Abraham.Dr Vivan akatabasamu 

na kusema 

“Mheshimiwa balozi ,hilo 

unalolitaka ni jambo 

lisilowezekana.Tayari nimekwisha 

kabidhi jukumu hili kwa vyombo 

husika na vinaendelea kulifanyia 

kazi kwa hiyo wewe na watu wako 

mtasubiri hadi vyombo vyangu 

vikalimishe kazi niliyowapa kwani 

hata mimi nikiwapa kazi huwa 

siwaingilii katika kutekeleza 

majukumu yao ya kitaalamu” 

akasema Dr Vivian 

“Mheshimiwa rais nilikueleza 

jana kwamba suala hili tunalipa umuhimu mkubwa sana na kila 

mara nimekuwa nasumbuliwa 

kutaka majibu ya wapi limefikia 

suala la Nathan.Mheshimiwa rais 

huyu aliyepotea ni raia wa 

Marekani na raia yeyote wa 

Mareani akiuawa au kupotea 

katika nchi ya kigeni,lazima 

atafutwe hadi apatikane na 

kurejeshwa nyumbani.Ili tuwe na 

uhakika kwamba Tanzania 

inafanya juhudi katika 

kushughulikia suala hili la Nathan 

nataka na sisi tushirikishwe katika 

uchunguzi huo unaoendelea na sisi 

tutoe mchango wetu.Hatupaswi 

tuachwe nje ya jambo hili 

muhimu.Kutunyima haki ya 

kushiriki katika uchunguzi wa mtu wetu aliyepotea kutatupa wasiwasi 

kama kweli Tanzania ina nia ya 

dhati ya kumtafuta mtu wetu” 

akasema balozi Abraham.Dr Vivian 

akamtazama kwa makini na 

alionyesha kukerwa na maneno 

yale ya balozi Abraham 

“Jamilla Hussein ni 

mwanafunzi wa kiTanzania 

aliyekuwa anasoma nchini 

Marekani aliuwa na watu 

wasiojulikana kwa kupigwa risasi 

mwaka jana.Ulisikia serikali ya 

Tanzania ikidai kushirikishwa 

katika uchunguzi? 

“Mhesh..” balozi Abraham 

akataka kuzungumza lakini rais 

akamzuia “Nijibu balozi ulisikia 

tukiomba kushiriki katika 

uchunguzi au turuhusiwe 

tuchunguze wenyewe? 

“Hapana sikusikia ” 

“Kama sisi hatujawahi 

kuomba kutaka kushirikishwa 

kufanya uchunguzi kwa ajili ya 

watu wetu wanaouawa au 

kufanyiwa matendo yasiyofaa 

katika nchi yenu kwa nini ninyi 

mtake kushirikishwa katika 

uchunguzi nchini kwetu?Kwa nini 

hamuamini au kuheshimu vyombo 

vya uchunguzi vya nchi nyingine? 

Akauliza Dr Vivian 

“Mheshimiwa rais,Marekani 

ina vyombo vya uchuguzi vyenye 

uwezo mkubwa kuliko nchi yoyote ulimwenguni ndiyo maana 

anapopotea au kutekwa raia 

yoyote wa marekani tunakuwa na 

imani sana kama uchunguzi 

ukifanywa na vyombo vyetu 

wenyewe.Tunaomba turuhusiwe 

na sisi tushiriki na tuongeze nguvu 

tukishirikiana na vyombo vya 

uchunguzi vya hapa Tanzania” 

akasema balozi Abraham 

“Mheshimiwa balozi hao raia 

wa marekani wana tofauti na 

binadamu wengine? Wao 

wanavuta pumzi tofauti na hii 

tuvutayo sisi?Wameumbwa kwa 

dhahabu? Kama jibu ni ndiyo basi 

nitaruhusu Marekani waje 

wafanye uchunguzi wao hapa 

Tanzania lakini kama jibu ni hapana,sintaruhusu mtu yeyote wa 

Marekani kuja kufanya uchunguzi 

wowote hapa nchini.Naomba 

muheshimu taratibu na sheria za 

nchi yetu” akasema Dr Vivian kwa 

sauti ya ukali 

“Mheshimiwa rais si kwamba 

hatuheshimu sheria na taratibu za 

nchi hii lakini tunaomba kuwa 

sehemu ya timu ya kufanya 

uchunguzi huo.Mtu 

tunayemuongelea hapa ni raia wa 

Marekani” akasema balozi 

Abraham na Dr Vivian akasimama 

“ Balozi Abraham nimekwisha 

weka wazi msimamo wetu na 

ninaomba tusiendelee tena 

kulijadili hili suala na ninyi mtasubiri hadi hapo uchunguzi 

utakapokamilika” 

“Mheshimiwa rais kuna 

ugumu gani katika kutushirikisha 

na sisi katika uchunguzi huo? 

Tunaomba tuwe na watu wetu 

wawili tu.Suala hili si gumu na 

sioni kwa nini hautaki 

kukubaliana nami.Au kuna kitu 

ambacho hautaki tukifahamu 

katika suala hili? 

Dr Vivian akamtazama 

Abraham kwa hasira 

“Unamaanisha nini 

unaposema kwamba kuna jambo 

sitaki lijulikane katika suala hili? 

Akauliza 

“Sina maana mbaya lakini 

ninashanganzwa na kukataa kushirikisha watu wetu katika 

timu ya uchunguzi wa jambo hili ili 

tuwe na imani na kazi 

inayofanyika” 

Dr Vivian hakujibu kitu 

akaenda mezani kwake akainua 

simu na kupiga baada ya sekunde 

kadhaa mlango ukafunguliwa na 

wakaingia walinzi wake wanne 

“Msindikizeni balozi katika 

gari lake aondoke hapa ikulu 

haraka sana na ninatoa maelekezo 

kwamba balozi Abraham 

asiruhusiwe kuingia tena hapa 

ikulu kuanzia leo !! akasema Dr 

Vivian kwa ukali 

“Mheshimiwa rais bado 

hatujamaliza!! akasema balozi 

Abraham kwa mshangao.Walinzi wale wakamtaka ainuke na 

aondoke kama alivyotakiwa na 

rais.Balozi Abraham akainuka na 

kuondoka 

“Huyu balozi ananinyima 

amani sana kwa namna 

anavyolifuatilia hili suala la 

Nathan.Maneno aliyoyazungumza 

hapa yanaonyesha wazi kwamba 

kuna kitu tayari wanakifahamu 

kuhusu Nathan.Inaonyesha wazi 

kwamba tayari wanafahamu kuwa 

Nathan amekufa na sasa 

wanatafuta kuthibitisha kama ni 

kweli.Hii itabaki kuwa siri na 

hakuna atakayefahamu jambo 

hili.Mathew na Theresa 

wameniingiza katika mvutano 

mwingine na Marekani ambao sikuwa nimeutarajia.Hili 

linanifanya niwe na hasira sana na 

Theresa ambaye ndiye aliyemuua 

na kusababisha haya yote 

kutokea.Kwa nini alifanya 

vile?Hakujua kama suala hili 

litaleta mtafaruku 

mkubwa?Itanichukua muda mrefu 

kuweza kurudisha moyo wangu 

kwa Theresa na kumsamehe kwa 

hili alilolifanya.Ameniumiza sana 

kwa hiki alichokifanya.Yule 

mwenzake naye badala ya kufanya 

kazi niliyomtuma amekuwa 

analeta mabalaa kila uchao.Mpaka 

sasa amekuwa ni msababishaji 

mkubwa wa matatizo badala ya 

kutafuta nani waliomuua baba 

yangu.Imekuwa vyema nimewasimamisha kuendelea na 

uchunguzi kwani walikokuwa 

wanaelekea ni kubaya.Sitaki tena 

kuendelea na uchunguzi wa hili 

jambo kwani mwisho wake si 

mzuri” akawaza Dr Vivian na 

kuendelea na kazi zake 




Huyu balozi ananinyima 

amani sana kwa namna 

anavyolifuatilia hili suala la 

Nathan.Maneno aliyoyazungumza 

hapa yanaonyesha wazi kwamba 

kuna kitu tayari wanakifahamu 

kuhusu Nathan.Inaonyesha wazi 

kwamba tayari wanafahamu kuwa 

Nathan amekufa na sasa 

wanatafuta kuthibitisha kama ni 

kweli.Hii itabaki kuwa siri na 

hakuna atakayefahamu jambo 

hili.Mathew na Theresa 

wameniingiza katika mvutano 

mwingine na Marekani ambao sikuwa nimeutarajia.Hili 

linanifanya niwe na hasira sana na 

Theresa ambaye ndiye aliyemuua 

na kusababisha haya yote 

kutokea.Kwa nini alifanya 

vile?Hakujua kama suala hili 

litaleta mtafaruku 

mkubwa?Itanichukua muda mrefu 

kuweza kurudisha moyo wangu 

kwa Theresa na kumsamehe kwa 

hili alilolifanya.Ameniumiza sana 

kwa hiki alichokifanya.Yule 

mwenzake naye badala ya kufanya 

kazi niliyomtuma amekuwa 

analeta mabalaa kila uchao.Mpaka 

sasa amekuwa ni msababishaji 

mkubwa wa matatizo badala ya 

kutafuta nani waliomuua baba 

yangu.Imekuwa vyema nimewasimamisha kuendelea na 

uchunguzi kwani walikokuwa 

wanaelekea ni kubaya.Sitaki tena 

kuendelea na uchunguzi wa hili 

jambo kwani mwisho wake si 

mzuri” akawaza Dr Vivian na 

kuendelea na kazi zake 

***************** 

“Hongera sana Mathew kwa 

uwekezaji huu mkubwa 

ulioufanya.Uliponiambia kwamba 

unawekeza katika kiwanda sikujua 

kama unajenga kiwanda kikubwa 

namna hii” akasema Camilla 

wakati wakiendelea na kukagua 

maendeleo ya ujenzi wa kiwanda 

cha kuchonga vipuri vya magari,mitambo na mashine 

mbalimbali kinachomilikiwa na 

Mathew 

“Ahsante sana Camilla.Mimi 

na Peniela tulifanikiwa kuwa na 

utajiri wakubwa.Tulikuwa na 

miradi mingi mikubwa 

iliyotuingizia fedha 

nyingi.Tulipoachana ilitulazimu 

kugawana mali hivyo nikapata 

pesa nyingi sana na nikaamua kuja 

kuwekeza nyumbani Tanzania” 

“Huyo Peniela niliwahi 

kumsikia wakati fulani kwamba 

damu yake ilitumika kutengeneza 

kinga inaitwa Peniela na kujipatia 

fedha nyingi.Peniela alifanya kosa 

kubwa sana kuamua kuachana na 

mwanaume kama wewe”“kwani mimi nikoje Camilla? 

Mbona niko sawa na wanaume 

wengine” 

“Hapana Mathew hauko sawa 

na wanaume wengine.Mimi 

humsoma mtu haraka sana na 

nimegundua u mwanaume wa 

tofauti sana na wengine”Camilla 

akasitisha alichotaka kukisema 

baada ya Mathew kuitoa simu yake 

mfukoni kufuaia mlio wa ujumbe 

mfupi kusikika.Akasimama na 

kuusoma ujumbe ule. 

“Theresa ametuma ujumbe 

akituelekeza anapoishi Tausi” 

akasema na kumtafsiria Camilla 

ambaye hakuwa anaelewa 

kiswahili “Theresa amefanya kazi 

kubwa sana.Nini kinafuata? 

“Kinachofuata kwa sasa 

tunakwenda nyumbani kwa Tausi 

kufanya uchunguzi.Tupite kwanza 

nyumbani kwangu tukachukue 

silaha na zana nyingine za 

kutuwezesha kuingia ndani mwa 

Tausi bila tatizo” akasema Mathew 

na kwa haraka wakaingia katika 

gari wakaondoka kuelekea 

nyumbani kwa Mathew. 

“Hakuna mpaka sasa 

mrejesho wowote toka kwa 

Peniela?Camilla akauliza 

“Mpaka sasa hajapiga simu 

kunipa mrejesho.Sijui kuna 

nini.Nimeanza kuingiwa na 

wasiwasi yawezekana labda mpenzi wake atakuwa 

amemkamata wakati akijaribu 

kuwachunguza.Nimemuingiza 

katika suala la hatari sana” 

akasema Mathew 

“Tumpe muda kidogo 

yawezekana anatafuta nafasi nzuri 

ya kufanya uchunguzi wake.Unajua 

mambo kama haya ya 

kumchunguza mtu yanakuwa 

magumu sana kama huna ujuzi au 

uzoefu wowote wa 

kuchunguza.Inawezekana hajui 

aanzie wapi kuchunguza”akasema 

Camilla 

“Unachosema kinaweza kuwa 

sahihi Camilla lakini kutokana na 

mtiririko wa mambo ulivyo kuna 

uwezekano mkubwa Anderson Pillar na baba yake Andrew 

wakawa ni CIA na Peniela anaweza 

akajikuta katika matatizo 

makubwa endapo watagundua 

kwamba anawachunguza.Lakini 

pamoja na ugumu na hatari iliyopo 

yeye ndiye pekee tunayemtegemea 

kwani watu ambao wangeweza 

kuwa na taarifa muhimu ambao ni 

George Mzabwa,Ranbir Kumar na 

Herieth Mzabwa wamekwisha 

fariki dunia na hata kampuni ya 

Tanbest Gemstone ltd imeteketea 

kwa moto.Hakuna mahala 

tunakoweza kupata taarifa 

kuhusiana na zile fedha nyingi 

alizotumiwa George kutoka 

kampuni ya Flamingo” akasema 

Mathew na safari ikaendelea Walifika nyumbani kwa 

Mathew wakachukua silaha na 

baadhi ya vifaa ambavyo 

vingeweza kuwasaidia katika kazi 

wanayokwenda kuifanya 

nyumbani kwa Tausi. 

Iliwachukua saa moja na 

dakika ishirini na mbili kuwasili 

eneo la mji mweupe.Huu ni mji 

mpya ambao umejengwa 

pembezoni mwa jiji la Dar es 

salaam.Ni moja kati ya mji wa 

mfano kabisa wenye lengo la 

kupunguza msongamano kati kati 

ya jiji la Dar es salaam kwa hivyo 

ndani ya mji huu kuna kila aina ya 

huduma inayoweza kumfanya mtu 

aifuate katikati ya jiji.Hakukuwa 

na msongamano wa magari katika mji huu hata hivyo Mathew 

aliendesha gari taratibu ili 

kuifurahia mandhari nzuri ya mji 

huu uliojengwa vizuri na kuwekwa 

mandhari nzuri sana za kuvutia. 

Kwa kufuata maelekezo 

waliyopewa na Theresa 

walifanikiwa kufika katika kanisa 

katoliki wakazunguka mtaa wa 

nyuma na kuanza kuendesha gari 

taratibu wakisoma vibao vya 

namba za nyumba zilizokuwa 

pembeni ya mageti ya kila nyumba 

na hatimaye wakafanikiwa kuipata 

nyumba ile waliyoelekezwa na 

Theresa namba 402.Mathew 

akaegesha gari pembeni ya 

barabara wakashuka na kuangaza 

pande zote kama kuna mtu anawafuatilia lakini hakukuwa na 

mtu yeyote aliyekuwa 

anafuata.Watu wachache walikuwa 

wanapita barabarani na kila 

mmoja alijali mambo yake.Mathew 

akalitazama kufuli kubwa 

lililotumika kufunga geti 

akafungua pochi yake ndogo na 

kutoa funguo bandia akachomeka 

katika kufuli lile akajaribu 

kufungua ikagoma akajaribu 

nyingine ikagoma.Alijaribu fuguo 

nne zikagoma na funguoa ya tano 

ikafungua.Wakaingia ndani na 

kuangalia usalama na kama kuna 

kamera yoyote ya ulinzi mahala 

pale.Hakukuwa na dalili zozote za 

kuwepo mtu kulikuwa na ukimya 

mkubwa.Mathew akaelekea mlangoni wakati Camilla akiwa 

makini kaungalia kama kuna mtu 

anakuja pale.Akatoa funguo 

nyingine bandia na kuufungua 

mlango wa sebuleni wakaingia 

ndani. 

Katika meza sebuleni 

wakakuta kuna chupa kubwa ya 

mvinyo,glasi tatu na vichungi vya 

sigara. 

“Inaonekana Tausi alikuwa na 

wageni anakunywa nao kwani 

kuna glasi tatu hapa mezani” 

akasema Camilla.Wakachunguza 

pale sebuleni kisha wakaanza 

kufungua chumba kimojakimoja 

wakichunguza hadi walipofika 

katika chumba cha kulala cha 

Tausi.Ni chumba pekee kilichokuwa kimefungwa kwa 

funguo.Kama kawaida yake 

Mathew akatumia funguo bandia 

na kuufungua mlango wakaingia 

ndani ya chumba kile.Vitu vilikuwa 

vimepangwa kwa ustadi 

mkubwa.Juu ya meza iliyokuwa 

pembeni ya kitanda kulikuwa na 

karatasi mbili kubwa pamoja na 

simu ya mkononi.Mathew 

akazichukua karatasi zile 

wakazifungua.Moja ilikuwa ni 

ramani ya jiji la Dar es salaam na 

katika ramani ile kuliwekwa 

miduara mitatu myekundu katika 

baadhi ya sehemu 

“Ramani ya jiji la dar” Mathew 

akamwambia Camilla “Tausi ana kazi gani na hii 

ramani ya jiji la dar ? Camilla 

akauliza 

“Yawezekana anataka 

alifahamu vyema jiji la Dar ndiyo 

maana akapewa hii ramani.Lakni 

kwa nini hizi sehemu 

amezungushia miduara 

myekundu? 

“Swali hilo hatutaweza 

kulipatia majibu”akajibu Camilla 

na Mathew akaikunjua karatasi ya 

pili ambayo haikuwa na kitu zaidi 

ya hesabu nyingi. 

“Hizi ni hesabu zake alikuwa 

anapiga.Halafu alimweleza 

Theresa kwamba hana simu na hii 

inafanya nini chumbani kwake? Akauliza Mathew huku akiifungua 

na kukuta kuna laini akaiwasha 

“ Hakuna namba yoyote 

iliyohifadhiwa humu katika siku 

ila kuna namba tatu zilipigiwa na 

simu hii jana saa kumi na mbili 

jioni.Leo asubuhi pia kuna namba 

mbili zimepiga katika simu hii.” 

Akasema Mathew 

“Yawezekana Tausi ndiye 

anayeitumia hii simu? Camilla 

akauliza 

“Inabidi tulichuguze hilo 

tufahamu hizi namba zilizopigiwa 

jana ni za nani na hizi zilizopiga leo 

asubuhi ni za nani.Kwa kuwa 

tumeikuta simu hii chumbani 

kwake naamni yeye ndiye 

aliyekuwa anaitumia.kama ni hivyo kwa nini amdanganye 

Theresa kwamba hana simu? Ni 

wazi hataki kujuliikana kama ana 

simu na anaitumia simu hii kwa 

siri hasa akiwa nyumbani.” 

Akasema Mathew na wakaendelea 

kuchunguza mle chumbani 

hawakuweza kupata kitu kingine 

cha kuwasaidia 

“Tuondoke na hii ramani ya 

jiji la Dar na hii simu tukavifanyie 

uchunguzi” akasema Mathew 

wakatoka na kufunga milango 

vizuri wakaondoka.Wakiwa bado 

ndani ya mji mweupe,ujumbe 

ukaingia katika simu ya Mathew 

“Mathew vipi huko? Huyu mtu 

kuna kitu amestuka ghafla na 

anataka kuondoka kurejea nyumbani mara moja.Hapa 

ninajaribu kumzuia zuia kuvuta 

muda.Tayari mmechunguza 

kwake? 

Ikamlazimu Mathew 

kusimamisha gari katika bustani 

ya kupumzika wakalipa kingilio 

wakaingia bustanini,wakanunua 

vinywaji na kutafuta sehemu nzuri 

wakapumzika.Mathew akampigia 

simu Theresa 

“Hallow Mathew vipi 

maendeleo huko?Huyu mtu 

anataka kurejea nyumbani kama 

nilivyokujulisha katika ujumbe” 

“Tumetoka kwake sasa 

hivi.Tumefanikiwa kupata karatasi 

yenye ramani ya jiji la dar na kuna 

sehemu kumezungushiwa miduara myekundu vile vile tumekuta 

simu” 

“Mmekuta simu? Mbona 

aliniambia hana simu?Theresa 

akashangaa 

“Alikudanganya kuna simu 

tumeikuta chumbani 

kwake.Ninakutumia namba sasa 

hivi nakuomba uzifanyie kazi 

haraka tufahamu ni za nani.Kuna 

namba zilipigiwa na hii simu jana 

jioni na nyingine zimepiga kwa 

simu hii leo asubuhi.” 

“Sawa Mathew nitumie hizo 

namba nizifanyie kazi haraka.Kwa 

hiyo huyu mtu huku unaruhusu 

nimuache arudi nyumbani 

?akauliza Theresa “Muache arudi nyumbani 

kwake,sisi tumekwisha 

ondoka”akasema Mathew na 

kumtumia Theresa namba zile 

alizozikuta katika ile simu ya 

Tausi. 

“Tausi samahani kwa 

kukuchelewesha sintaweza tena 

kuongozana nawe kwa chakula cha 

mchana,kuna kazi natakiwa 

kuikamilisha.Utanikuta hapa 

utakaporejea” Theresa 

akamwambia Tausi ambaye 

alionyesha kukasirika kwa kitendo 

kile cha Theresa kumchelewesha 

“Theresa kama ulijua 

haujakamilisha kazi zako 

usingeniambia 

nikusubiri.Umenichelewesaha sana” akasema Tausi na kuinua 

mkoba wake akatoka kwa 

haraka.Theresa akaanza kuifanya 

kazi aliyopewa na Mathew. 

**************** 

Nusu saa tayari imekwisha 

pita toka Mathew na Camilla 

walipowasili katika bustani ya 

kupumzikia kati kati ya mji 

mweupe.IIikuwa ni bustani tulivu 

yenye mandhari ya kuvutia sana 

na walionekana kama hawakutaka 

kundoka mahala pale kwani 

walionekana kuzama zaidi katika 

mazungumzo yao. “Sisi tunaotoka nchi 

zilizoendelea tuna mtazamo hasi 

kuhusu bara la Afrika.Tumezoea 

kuona katika vyombo vya habari 

vya nchi zetu vikionyesha au 

kuandika habari kuhusiana na 

bara hili kujaa mambo mabaya 

kama vile njaa,ukame,mapigano ya 

wenyewe kwa wenyewe na 

mengine mengi yenye kujenga 

taswira mbaya ya bara hili na 

katika mipango yangu sikuwahi 

kufikiria kuja kutembea barani 

Afrika.Matatizo haya yaliyotokea 

yamenifanya nijikute tayari niko 

ndani ya bara hili nchini 

Tanzania.Nimejionea mwenyewe 

maisha ya hapa na nimegundua 

kumbe mengi ya yale ambayo tumekuwa tunalishwa na vyombo 

vyetu vya habari ni uongo 

mtupu.Tanzania ni nchi nzuri 

imejaa amani tele,watu wake ni 

wakarimu na hata lugha yao 

wanayoongea kiswahili ni nzuri na 

inavutia.Natamani nijifunze kwa 

haraka lugha hii ili niweze 

kufahamu nini 

mnachoongea.Nimeipenda 

Tanzania sana na ninafikiria hata 

kuishi hapa kama kutakuwa na 

usalama kwangu”akasema Camilla 

na Mathew akatabasamu 

“Camilla imekuwa vizuri 

umekuja mwenyewe na 

umeshuhudia kwa macho yako 

nchi hii ilivyo nzuri.Ni kawaida 

kwa vyombo vya habari vya nchi tajiri kutafuta na kuandika au 

kutangaza habari zile mbaya 

zinazohusu bara la Afrika na hivyo 

kujenga taswira mbaya kwa watu 

wa mataifa ya nje kuhusu 

Afrika.Ndani ya bara hili la Afrika 

kuna mambo mengi mazuri 

ambayo hayaandikwi.Kuna 

tamaduni nzuri za makabila mbali 

mbali yanayopatikana katika bara 

hili.Kuna vivutio vingi vya utalii 

vinapatikana ,kuna utajiri mkubwa 

wa madini mbali mbali.Sikatai 

kwamba hakuna matatizo.Kuna 

mapigano na mauaji ya wenyewe 

kwa 

wenyewe,njaa,ukame,umasikini 

lakini haya yote si kwa kiwango 

kama kinachoandikwa na vyombo vya habari vya mataifa ya nje.Nchi 

nyingi za Afrika kwa sasa 

wanapambana katika kupiga hatua 

za kimaendeleo,wanafanya 

mageuzi ya kiuchumi ili 

kuboresha maisha ya watu 

wao.Nyakati za chaguzi mbali 

mbali waandishi wa vyombo 

vikubwa vya habari toka nchi 

kubwa huja kwa wingi kuandika 

habari lakini huzipa uzito mkubwa 

habari zile za mapigano 

yanayotokea baada ya uchaguzi ili 

Afrika kuonekane hakuna 

demokrasia na watu wake ni wa 

hovyo.Nimefurahi umekuja 

mwenyewe na umejionea kwa 

macho hali halisi ya mambo ilivyo 

hapa Tanzania.Na hapa ni Dar es salaam,bado haujafika Arusha 

ambako ndiko kwenye kitovu cha 

utalii,ukienda Kilimanjaro,Iringa 

na kote utakakoenda Tanzania 

kuna uzuri wa kipekee 

kabisa.Yatakuwa maamuzi mazuri 

endapo utaamua kuhamishia 

makazi yako hapa Tanzania” 

“Hakuna tatizo kuhusu kuishi 

hapa ila lazima nijiridhishe 

kwanza kuhusu usalama 

wangu.Unajua kwa sasa 

ninatafutwa na CIA na 

hawatapumzika hadi hapo 

watakapohakikisha wamenitia 

mikononi wakinituhumu kwa 

mauaji” 

“Usihofu kuhusu usalama 

wako.Nakuhakikshia Camilla hapa utakuwa salama kabisa wala 

usihofu.Kuna wakati hata baba 

yako amewahi kujificha hapa 

mambo yalipomuharibikia huko 

kwao” 

“Mathew kwa nini unasisitiza 

sana nibaki Tanzania? Camilla 

akauliza .Mathew akatabasamu 

lakini kabla hajajibu chochote 

simu yake ikaita alikuwa ni 

Theresa 

“Hallow Theresa” 

“Mathew tayari nimeifanya ile 

kazi” 

“Good.Umewafahamu wenye 

sile namba? 

“Ndiyo nimewafahamu lakini 

siwezi kukueleza simuni.Mko 

wapi? “Bado tuko katika mji 

mweupe kuna bustani nzuri sana 

hapa ya kupumzika” 

“Sawa.naomba tukutane pale 

Rombo garden tupate chakula au 

ninyi tayari mmekula? 

“Hapana bado.Tukutane hapo 

Rombo Garden tupate chakula kwa 

pamoja .Pale wanachoma nyama 

nzuri sana tumpeleke Camilla 

apate nyama choma na ndizi.Pale 

ni watalamu sana wa kuchoma 

nyama na ndizi”akasema Mathew 

na kukata simu akamtaka Camilla 

waondoke wakakutane na Theresa 

mahala walikopanga wakutane 

“Mathew nilikuuliza swali 

hukunijibu.Kwa nini unataka nibaki Tanzania? Camilla akauliza 

wakiwa garini 

“Hupendi kuishi Tanzania? 

Mathew naye akauliza 

“Pamoja na uzuri,hali ya 

amani,watu wakarimu na 

marafiki,lakini sina mpango wa 

kuishi hapa Tanzania labda kama 

kuna jambo mahususi ambalo 

unadhani linaweza kunifanya 

nibadili mawazo yangu na kubaki 

Tanzania.Nilikuja Tanzania kwa 

kuwa baba alinitaka lakini sikuwa 

na mpango wowote wa kuja 

Afrika” 

“Nadhani tufanye kwanza hii 

kazi na tutakapoimaliza basi 

tutaangalia nini cha kufanya kwa 

sasa ni mapema sana kuzungumza lolote” akasema Mathew na safari 

ikaendelea hadi walipofika Rombo 

garden.Watu walikuwa wengi kiasi 

mchana huu wakipata 

chakula.Mathew na Camilla 

wakatafuta sehemu nzuri wakaketi 

na kukaribishwa na wahudumu 

nadhifu sana.Kwa kuwa walikuwa 

wanamsubiri Theresa 

hawakuagiza kwanza chakula 

badala yake wakaagiza vinywaji 

wakaendelea kunywa huku 

wakibadilishana hili na lile 

“Mathew unahisi kwa nini 

Marekani wanatumia kila aina ya 

mbinu kumchunguza rais 

wenu?Unahisi labda ni huu 

mvutano uliopo sasa uliotokea 

baada ya Tanzania kutangaza kuanzisha mashirikiano na Korea 

Kaskazini ndio sababu ya 

Marekani kumuandama hivi Dr 

Vivian? Camilla akauliza .Mathew 

akainua glasi yake ya kinywaji 

akanywa kidogo na kusema 

“Ukitazama mtiririko wa 

mambo ulivyo,Marekani 

wameanza kumfuatilia Dr Vivian 

toka zamani wakati anasoma chuo 

kikuu nchini Marekani.CIA 

walimpandikiza Nathan 

akaanzisha mahusiano na Dr 

Vivian kwa hiyo mgogoro 

ulioibuka sasa umekuta tayari 

Marekani wanaendelea 

kumchunguza Dr Vivian.” 

“Unahisi kuna kitu au siri 

fulani anayo Dr Vivian kiasi cha Marekani kuchukua muda mrefu 

namna hiyo kumchunguza? 

Camilla akauliza 

“Naamini hivyo.Lazima kuna 

jambo ambalo Dr Vivian 

analo.Marekani hawawezi 

kumfuatilia kwa muda mrefu kama 

hakuna jambo wanalolitaka 

kwake.Mfano walitumia muda 

mrefu kumfuatilia Osama bin 

laden kwa kuwa alikuwa na 

umuhimu kwao.Ipo pia mifano 

mingi ya watu ambao marekani 

kwa kutumia vyombo vyake vya 

uchunguzi imekuwa inawafuatilia 

kwa muda mrefu.Kitendo cha 

kumfuatilia Dr Vivian toka angali 

anasoma kinadhihirisha kwamba kuna jambo wanalitaka toka 

kwake” 

“Unahisi Dr Vivian anaweza 

kuwa ni hatari kwa Marekani 

ndiyo maana wanamfuatilia namna 

hii? 

“Sina hakika na hilo hadi 

litakapofanyiwa uchunguzi lakini 

kwa tathmini ya haraka haraka CIA 

wametumia muda mrefu 

kumfuatilia Dr Vivian ,wametumia 

gharama kubwa katika 

kutengeneza mtandao ambao 

unawagharimu fedha mambo haya 

yote hayawezi kufanyika kama 

jambo alilonalo Dr Vivian halina 

manufaa kwa 

Marekani.Wamemtumia Nathan 

kumchunguza Dr Vivian kwa muda mrefu na baada ya Nathan sasa 

amekuja tena Tausi.Lakini papo 

hapo ninapata wazo yawezekana 

labda marekani hawana uhakika 

na hicho wanachokinguza kwa Dr 

Vivian au tayari amekwishajua 

kwamba anachunguzwa hivyo 

kuficha hicho wanachokichunguza 

na kuwafanya Marekani 

waendelee kumchunguza bila 

kuchoka”akasema Mathew 

“Mathew huoni kama kuna 

ulazima wa kumchunguza rais na 

kufahamu ni jambo gani ambalo 

Marekani wanatafuta toka kwake? 

“Kazi ambayo rais alitaka 

niifanye ni kuchunguza nani 

walimuua baba yake na kwa 

nini.Kwa kuwa tumeamua kuendelea na uchunguzi kwa siri 

bila yeye kufahamu,tumalize 

kwanza hili suala tulilokwisha 

lianza ndipo tuone kama tunaweza 

kumchunguza rais” akasema 

Mathew 

“Math………” Camilla akataka 

kusema kitu lakini akanyamaza 

baada ya simu ya Mathew 

kuita.Alikuwa ni Theresa.Mathew 

akamuelekeza mahala walipo na 

hazikumalizika dakika mbili 

akatokea 

“Samahani kwa kuchelewa” 

akasema Theresa na muhudumu 

akafika wakaagiza waletewe 

chakula.Camilla alionekana 

kukifurahia sana chakula kile cha 

nyama choma na ndizi 




Itanilzimu kujifunza 

utaalamu huu wa uchomaji nyama 

ili kama siku moja nitarejea 

nyumbani na mimi 

nikawafundishe wengine.Huu ni 

utaalamu mkubwa sana wa 

uchomaji nyama,natamani nije 

hapa kila siku kula nyama kama 

sintakuwa mzigo kwenu” akasema 

Camilla na wote wakacheka 

.Waliendelea kula huku Mathew na 

Theresa wakimsimulia Camilla 

mambo mengi mazuri 

yanayopatikana Tanzania.Baada 

ya kula mazungumzo yakaanza 

“Haya tueleze nini umekipata 

katika zile namba ? Mathew 

akauliza Nilipofika ikulu nimemkuta 

Tausi akiwa ameboreka sana na 

alifurahi aliponiona.Hakuna mtu 

aliyekuwa na muda naye.Nilifanya 

kujiweka karibu yake na 

kumsikiliza nikajenga naye 

urafiki.Mpaka hivi sasa bado 

hajapangiwa kazi yoyote na rais na 

amewekwa katika ofisi yangu kwa 

muda ili aweze kuzoea mazingira 

ya ikulu kabla ya kupangiwa idara 

atakayofanya kazi.Ameniomba 

nimfanyie mpango kwa rais ili 

ampangie kazi katika idara ya 

mawasiliano akidai ndicho kitu 

alichokisomea na ana shahada 

katika teknolojia ya 

mawasiliano.Nilimuahidi kuongea 

na dada kuhusu suala hilo na akafurahi.Nilimtaka anipe namba 

zake za simu ili tuwasiliane mara 

kwa mara akadai hana simu” 

“Huyu mwanamke ni mwongo 

mkubwa.Ulipoondoka kueleka 

ikulu tuliendelea kumchunguza na 

Camilla akapata msaada toka kwa 

watu wake wa nchini Marekani na 

tukagundua kwamba Tausi au 

Olivia ambalo ni jina lake halisi 

anafanya kazi CIA” 

“CIA ?!! Theresa akastuka 

“Ndiyo.Hiyo ndiyo sababu 

nilikutaka uipate simu yake 

anayotumia ili tufahamu 

anawasiliana na akina nani.Tausi 

amewekwa pale kwa sababu 

maalum na amekuomba umfanyie 

mpango aende katika idara ya mawasiliano lengo lake ni 

kumchunguza rais na kila 

kinachoendelea ikulu” akasema 

Mathew na Theresa akashika 

kichwa 

“Mathew lazima tumjulishe 

rais kuhusu hili suala!! Akasema 

“Hapana Theresa.Hatuwezi 

kumjulisha kwa sasa halafu 

ukumbuke rais hataki tuendelee 

na uchuguzi wowote hivyo 

atakasirika sana kusikia 

tumepuuza amri yake na 

tunaendelea na 

uchunguzi.Kikubwa cha kufanya 

hapa ni kumchunguza Tausi na 

kupitia kwake tutafahamu mambo 

mengi.Tutafahamu watu 

anaoshirikiana nao hivyokuufahamu mtandao wao wote 

hapa Tanzania” 

“Mathew maisha ya dada 

yangu yapo hatarini.kwa nini 

tusimueleze ukweli ili akachukue 

hatua? 

“Kwa sasa Tausi ndiye pekee 

tunayemtegemea kutuongoza 

kuelekea katika kuufahamu 

mtandao wao.Sikiliza Theresa,Dr 

Vivian amekuwa anachunguzwa na 

marekani kwa muda mrefu hivyo 

lazima tufahamu kwa nini 

wanamchunguza.Kwa kumtumia 

Tausi tutaweza kufahamu ,hivyo 

jambo hili rais hapaswi kulifahamu 

kwa sasa hadi hapo tutakapokuwa 

tumekamilisha uchunguzi wetu” 

akasema Mathew lakini bado sura ya Theresa ilionyesha wasiwasi 

mkubwa 

“Nyumbani kwa Tausi 

mligundua ? akauliza 

“Sebuleni tumekuta chupa 

kubwa ya mvinyo na glasi tatu 

pamoja na kisahani cha kuwekea 

majivu ya sigara.Inaonyesha,jana 

usiku kulikuwa na zaidi ya mtu 

mmoja pale sebuleni wakinywa 

mvinyo.Hii inatupa picha kwamba 

licha ya ugeni ambao Tausi anadai 

kuwa nao lakini tayari anao 

washirika wake hapa Dar es 

salaam.Tulipoingia katika chumba 

chake cha kulala tukakuta kuna 

simu na chini ya simu hiyo 

kulikuwa na karatasi mbili moja 

ikiwa na mahesabu na nyingine ikiwa na ramani ya jiji la Dar es 

salaam.Tulipoichunguza simu 

tukagundua kuna namba tatu 

ambazo alizipigia jana jioni halafu 

kuna namba nyingine mbili 

zimepiga katika simu hii leo 

asubuhi.Umefahamu ni akina nani 

anawasiliana nao?Mathew 

akauliza 

“Nimezichunguza zile namba” 

akasema Theresa na kutoa 

karatasi katika mkoba wake na 

kumpa Mathew ambaye alionyesha 

mshangao mkubwa 

“Dr Robert? Akauliza 

“Ndiyo.Moja kati ya namba 

hizo ni ya Dr Robert” akajibu 

Theresa “Theresa amegundua nini? 

Akauliza Camilla ambaye alibaki 

nyuma wakati Mathew na Theresa 

wakizungumza kiswahili 

“Theresa tayari amepata 

majina ya watu wenye zile namba 

katika ile simu tuliyoikuta 

chumbani kwa Tausi.Kwa mujibu 

wa namba hizi,katika simu ya 

Tausi inaonyesha jana jioni 

aliwasiliana kwanza na April 

Mubara ambaye ni mke wa 

marehemu wa Anorld Mubara .Vile 

vile akawasiliana na Abraham 

Clerk huyu ni balozi wa Marekani 

nchini Tanzania na mwisho 

akawasiliana na Robert 

Mwainamela.Leo asubuhi 

amempigia simu Robert Clerk pamoja na Dr Robet” akanyamaza 

na kumtazama Theresa kwa muda 

halafu akasema 

“Nadhani sasa utakubaliana 

nami kwamba kuna ulazima wa 

kumchunguza waziri wa mambo ya 

nje Dr Robert mwainamela.Huyu 

ambaye wewe na dada yako 

hamtaki achunguzwe mkidai ni 

mtu safi ana mawasiliano na Tausi 

jasusi wa CIA aliyepandikizwa 

ikulu ili amchunguze dada yako. 

Angalia mtiririko ulivyo.Jana 

amewasiliana na Abraham Clerk 

na Dr Robert Mwainamela.Mezani 

tumeuta glasi tatu za mvinyo na 

picha inayokuja ni kwamba 

inawezekana balozi Clerk na Dr 

Robert mwainamela walikuwepo jana nyumbani kwa Tausi” 

akasema Mathew 

“Theresa wewe ni mfanyakazi 

wa ikulu upo karibu na rais muda 

wote na hivyo kuwafahamu 

viongozi wengi,tuambie umewahi 

kumuona Dr Robert akivuta 

sigara? Camilla akauliza 

“Hapana sijawahi kumuona 

akivuta sigara” akasema 

Theresa.Mathew na Camilla 

wakatazamana 

“Theresa nafahamu 

hautapendezwa na hili lakni kwa 

namna yoyote ile lazima tumpate 

Dr Robert” 

“Kama Tausi ni jasusi wa CIA 

na amepandikizwa kwa shughuli 

maalum,unadhani Dr Robert naye ana mahusiano na CIA? Theresa 

akauliza 

“Kitendo cha Dr Robert kuwa 

na mawasiliano na Tausi kinatoa 

picha kwamba wawili hawa wana 

mahusiano fulani.Ili tujue 

wanahusiana vipi lazima tufanye 

uchunguzi” akasema Mathew 

“Vipi kuhusu April Mubara 

ambaye ndiye aliyempeleka Tausi 

kwa rais? 

“Huyu tutamchunguza pia 

lakini kwanza tumchunguze Dr 

Robert” 

“Mimi nina wazo” akasema 

Camilla 

“Kabla ya kuanza na Dr Robert 

kwa nini tusirejee kwa Tausi? 

Alimuaga Theresa kwamba anakwenda nyumbani kwake 

hivyo naamini lazima atakuwa 

nyumbani kwake hivi sasa.Huyu 

anaweza kutusaidia hata kumpata 

Dr Robert kirahisi sana kwani yule 

ni waziri na si rahisi kumpata ila 

kwa kumyumia Tausi anaweza 

akapatikana kwa kuwa tayari 

wana mahusiano” 

“Una maanisha tumteke 

Tausi? Theresa akauliza 

“Ndiyo.Tukimtumia huyu 

tunaweza kumpata kirahisi Dr 

Robert” 

“Hapana sikubaliani na hilo 

wazo la kumteka Tausi” akasema 

Theresa 

“Wazo alilotoa Camilla ni la 

msingi.Tukimpata Tausi tunaweza kufahamu mambo mengi na hata 

itakuwa rahisi kumpata Dr Robert 

na.Nakubaliana na Camilla tuanzie 

kwa Tausi.Tukifika Theresa 

utaingia ndani kwanza halafu sisi 

tutafuata nyuma” 

“Hatukuwa tumekubaliana 

nimfuate nyumbani 

kwake.Atastuka sana kwa nini 

nimemfuta kwake.Hivi sasa tayari 

atakuwa amegundua kwamba 

kuna watu waliingia nyumbani 

kwake wakati hayupi hivyo 

akiniona ghafla nimemfuata 

anaweza akahisi labda ninahusika 

katika suala hilo na maisha yangu 

yatakuwa katika hatari” 

“Usiogope Theresa.Muda wote 

tumezungukwa na hatari lakini kwa kuwa tunafanya kazi hii kwa 

manufaa ya nchi basi Mungu 

anatuongoza na kutukinga na 

hatari.Twende garini” akasema 

Mathew wakainuka na wakaelekea 

katika gari lake,akafungua droo ya 

siri ambayo huhifadhi silaha na 

vitu vingine muhimu vya kazi 

akatoa kiboksi kidogo akalifungua 

na ndani yake akatoa kitu fulani 

kidogo akampa Theresa 

akakiweka sikioni 

“Hiki ni kifaa cha 

mawasiliano.Sote tutakuwa navyo 

masikioni na tutasikia kila 

utakachokizungumza na Tausi na 

endapo tutahisi kuna hatari yoyote 

tutavamia ndani mara moja 

kukuokoa” akasema Mathew na kuwasha kifaa kile ambacho 

kinawezesha mawasiliano kupitia 

vile vidude walivyoweka 

masikioni.Akajaribu na kila kitu 

kikaenda sawa.Theresa akaingia 

katika gari lake na akina Mathew 

wakafuata nyuma wakaelekea 

nyumbani kwa Tausi. 

“Toka nilipomuona Tausi 

nilipatwa na wasiwasi kuhusu 

mienendo yake ni mtu mwenye 

kutafuta ukaribu na rais,kumbe 

hisia zangu zilikuwa kweli.Tausi ni 

jasusi wa CIA aliyepandikizwa pale 

ikulu kwa shughuli maalum.Nini 

hasa wanachokitafuta hawa 

jamaa? Je ni lile begi la football au 

kuna kitu kingine?Nahisi kuna kitu 

zaidi ya football kwani kama alivyosema Mathew hawa jamaa 

wameanza kumfuatilia dada kwa 

muda mrefu toka angali anasoma 

chuo.Walimtumia Nathan kujenga 

urafiki wakawa wapenzi na baadae 

dada akawa rais na kipindi hicho 

chote wamekuwa wakimchunguza 

bila yeye kufahamu.Kuna jambo 

gani dada analo ambalo Marekani 

wanalitafuta kwake? Nadhani kuna 

ulazima wa kumchunguza na 

kuufahamu ukweli.Haiwezekani 

Marekani wakawekeza namna hii 

katika kumchunguza lazima kuna 

kitu.Nitajaribu kuutafuta 

ukweli.Nitajaribu kuutafuta ukweli 

japo nafahamu si rahisi kutokana 

na ukaribu kati yangu na dada 

kupungua kutokana na kitendo nilichokifanya cha kumuua 

Nathan.Dada haonyeshi machoni 

kama amechukia lakini moyoni 

amechukia vibaya sana na alidiriki 

kunitolea maneno fulani mabaya 

ambayo nikiyakumbuka naumia 

sana.Hata hivyo lazima 

nimchunguze ana siri gani” 

akawaza Theresa akiwa garini 

akielekea nyumbani kwa Tausi 

“Halafu kuna jambo lingine 

limenistua sana.Baba aliuawa 

wakati akienda kuonana na bi 

April Mubara shambani 

kwake.Huyo huyo April ndiye 

aliyempeleka Tausi kwa rais 

akadai ni mtoto wa marehemu rais 

Mubara na akadai kwamba yeye 

ndiye aliyemlea tangu akiwa mdogo wakati si kweli hata 

kidogo.Tausi si mtoto wa mzee 

Mubara na amedanganya kila kitu 

kuanzia jina hadi elimu.Ninaanza 

kuwa na mashaka makubwa na 

huyu mama April kwa kushiriki 

kwake katika kumdanganya 

rais.Kwa nini adanganye kwa ajili 

ya kumsaidia Tausi apate kazi 

ikulu? Je naye ana mahusiano na 

hawa jamaa? Kujitokeza kwake 

katika matukio haya mawili 

kunanifanya niwe na maswali 

mengi juu yake.Huyu mama anafaa 

kuchunguzwa ili afahamike kama 

naye anahusiana na CIA kwani 

ameshiriki katika kumsaidia mtu 

wa CIA kuingia ikulu kwa njia ya 

udanganyifu.Natamani nimueleze Mathew jambo hili lakini 

naogopa.Sitaki afahamu siri 

niliyonayo ambayo nimekwisha 

jiapiza kutomueleza mtu yeyote 

hadi siku naingia 

kaburini.Tutakapokuwa tumetulia 

nitatoa mapendekezo yangu kwa 

hawa wenzangu ili mama April 

achunguzwe” 

Theresa akaongeza mwendo 

wa gari baada ya kuwasili katika 

mitaa ya mji mweupe ambako 

hakuna magari mengi 

“Kitendo cha Tausi kuwa na 

mawasiliano na Dr Robert 

kimenishangaza sana.Hoja ya 

Mathew ina uzito mkubwa.Kama 

Tausi ni mgeni amefahamiana vipi 

na Dr Robert hadi wakawa wanapigiana simu? Hapo kuna 

kitu.Laiti ningeweza kusikia 

rekodi ya mazungumzo yao 

ingetusaidia sana kufahamu 

wanachokizungumza.Nilikuwa 

mbishi pale Mathew alipotoa wazo 

kwamba Dr Robert anahitaji 

kuchunguzwa lakini sasa naona 

ipo haja ya kumfanyia uchunguzi 

haraka sana.Ni mtu ambaye 

ninamfahamu vyema ana heshima 

kubwa katika jamii ya ndani na nje 

ya nchi.Uadilifu wake si wa 

kutiliwa shaka na hata watu 

wanahisi kwamba anafaa sana 

kuwa rais pale Dr Vivian 

atakapomaliza muda wake wa 

uongozi.Ni mtu safi ambaye 

hajawahi kuingia katika kashfa yoyote lakini pamoja na usafi wake 

ninaanza kuona kuna mambo 

ambayo bado hatuyafahamu 

kuhusu yeye.Kitendo cha 

kuwasiliana na Tausi ambaye ni 

jasusi wa CIA kimenifanya nianze 

kuwa na mtazamo mwingine 

kuhusu huyu mzee.Hili suala 

naona ni kubwa zaidi ya 

ninavyofikiria.Ngoja tuendelee 

kulichunguza jambo hili hadi 

mwisho.Kuna nyakati sitaki 

Mathew afanikiwe katika 

uchunguzi huu lakini kuna nyakati 

nalazimika kumuunga mkono ili 

alifikishe mwisho jambo hili na 

tuweze kuwabaini chui ndani ya 

zizi la kondoo ni akina nani lakini 

siri yangu hataweza kuifahamu kamwe.Dada alifanya kosa kubwa 

kumsimamisha Mathew asiendelee 

na ule uchunguzi.Yawezekana 

hafahamu kama amezungukwa na 

Simba wanaomuwinda usiku na 

mchana.Halafu kuna jambo 

nimekuwa nalitafakari sana usiku 

ule alikuwa anatuitia jambo gani 

hadi akamtaka Mathew asitishe 

kila anachokifanya na kwenda 

ikulu? Kwa nini kesho yake 

hakumweleza Mathew 

alichomuitia usiku na badala yake 

akamzuia asiendelee tena na 

uchunguzi? Dah ! kuna mambo 

yanakanganya sana lakini ngoja 

tuanze na jambo moja moja 

tukienda na mambo yote kwa 

wakati mmoja tutakwama” akawaza Theresa na kupunguza 

mwendo wa gari baada ya 

kukaribia kufika nyumbani kwa 

Tausi.Akapiga piga sikioni na kuita 

“Mathew unanipata? 

“Nakupata vyema Theresa” 

“Nimekaribia kufika 

nyumbani kwa Tausi kwa mbali 

kidogo naliona gari lake likiwa 

limeegeshwa nje.Anaonekana bado 

yuko ndani” 

“Sawa Theresa,sisi tuko 

nyuma yako usihofu” akasema 

Mathew na taratibu Theresa 

akaegesha gari nyuma ya gari 

analotumia Tausi.Uzio wa 

kuzunguka nyumba anamoishi 

Tausi haukuwa mrefu.Ulijengwa 

kwa matofali na na upande wa juu kukawa na vyuma na mtu aliyeko 

nje aliweza kuona kinachoendelea 

ndani ya uzio.Akiwa ndani ya gari 

Theresa akavuta pumzi ndefu na 

kuufungua mlango wa gari 

“Help me Lord ! akawaza na 

kushuka garini.Alipiga hatua mbili 

kuelekea getini mlango wa 

kuingilia sebuleni ukafunguliwa na 

Tausi akatoka akionekana kuwa 

na haraka sana na kuufunga tayari 

kwa kuondoka lakini mara 

alipogeuka akakutanisha macho 

na Theresa aliyekuwa anaingia 

getini.Alishangaa sana 

“Theresa?!!! Akasema Tausi 

kwa mstuko.Hakuwa ametegemea 

kumuona Theresa pale nyumbani 

kwake muda ule “Tausi !! akaita Theresa huku 

akitabasamu 

“Theresa nilikuacha 

ikulu,umefika saa ngapi huku? 

Akauliza Tausi akiwa amesimama 

bado akishangaa 

“Nilikuambia nina rafiki zangu 

wanaishi huku hivyo kuna mmoja 

wao amenipigia simu anaumwa 

nikaja mara moja kumjulia hali 

nikaona nipite hapa kwako 

nipafahamu.Mbona unanishangaa 

haunikaribishi ndani? 

“Karibu ndani” akasema Tausi 

na Theresa akaingia ndani 

“Hapa ndipo ninaishi Theresa 

karibu sana” 

“Ahsante Tausi.Hii ni nyumba 

kubwa na nzuri sana.Hujihisi mpweke kuishi peke yako katika 

nyumba kubwa kama hii? Theresa 

akauliza 

“Hapana sioni tatizo lolote 

kwa mimi kuishi peke yangu” 

“Baba yako marehemu mzee 

Mubara ana jumba kubwa kule 

maeneo ya viongozi wastaafu kwa 

nini usiishi kule badala yake 

ukaamua kuja kuishi huku peke 

yako? 

“Hata nyumba hii pia ni ya 

baba.Ningeweza kuishi kule lakini 

nimechagua mwenyewe kuishi 

huku napenda sehemu zenye 

ukimya sana” akasema Tausi 

ambae hakuonekana 

kufurahishwa na ujio wa 

Theresa.Ukimya mfupi ukapita Theresa akiikodolea macho chupa 

ya mvinyo iliyokuwa mezani na 

pembeni yake kukawa na glasi tatu 

na kisahani cha majivu ya sigara 

“Tausi unavuta sigara? 

Akauliza Theresa 

“Hapana sivuti sigara.Kuna 

watu walinitembelea jana na 

mmoja wao anavuta sigara” 

akasema Tausi huku akiinuka na 

kuziondoa zile glasi pamoja na 

kisahani cha majivu.Baada ya 

dakika mbili akarejea 

“Theresa tayari umekwisha 

pafahamu nyumbani kwangu 

nadhani ni wakati sasa wa 

kuondoka turejee kazini.Siku 

nyingine nitakukaribisha hapa 

tutashinda kutwa nzima”“Ahsante Tausi.Nahitaji 

kwanza kuingia maliwatoni halafu 

tuondoke” akasema Theresa na 

Tausi akampeleka.Theresa 

akaufunga mlango na kupiga piga 

sikioni 

“Hallow Theresa” akasema 

Mathew 

“Mathew huyu mtu ameanza 

kuonyesha wasi wasi kuhusu ujio 

wangu hapa kwake na anataka 

tuondoke,mko wapi?Imenibidi 

niombe kuja huku chooni ili 

kuvuta muda.Yuko peke yake 

humu ndani mnasubiri nini? 

“Usihofu Theresa tuko tayari 

hapa nje na tunaingia ndani sasa 

hivi.Tafadhali usitoke humo 

chooni” akasema Mathew “Geti la nyumba anamoishi 

Tausi lilikuwa wazi,Mathew na 

Camilla wakaingia ndani.Mathew 

akampa ishara Camilla azunguke 

kwa upande wa nyuma. 

Akiwa chumbani kwake 

akimsubiri Theresa atoke 

maliwatoni,Tausi akasikia kama 

hatua za mtu akitembea katika 

varanda.Akaingiwa na wasi wasi 

akaita 

“Theresa !!! hakujibiwa akaita 

tena 

“Theresa !! bado 

hakujibiwa.Akazifunga vizuri 

nywele zake akainua godoro na 

kutoa bastora yake na taratibu 

akanyata hadi mlangoni na 

kuufungua taratibu na kwa tahadhari kubwa akatazama 

katika varanda lakini hakukuwa 

na mtu.Akatoka na kuelekea 

katika mlango wa maliwato 

akagonga na kuita 

“Theresa !! 

Kutoka ndani ya maliwato 

Theresa akaitika na kumtaka Tausi 

amsubiri 

“Ni wewe ndiye uliyekuwa 

unatembea hapa katika varanda? 

Tausi akauliza 

“Ndiyo ni mimi? Nilikwenda 

kuchukua taulo katika mkoba 

wangu niliouacha sebuleni. 

“Usikae sana 

humo,tutachelewa kazini,rais 

anaweza akanitafuta.Halafu 

ni……………” Hakumaliza alichotaka kukisema mara ghafla akatokea 

Mathew na kumuelekezea bastora 

“Taratibu sana weka chini 

bastora yako halafu ipige teke ije 

kwangu !! akasema Mathew kwa 

sauti kali iso masihara 

“Kumbe ni mtego !! akasema 

Tausi kwa sauti ndogo 

“Nakuamuru kwa mara 

nyingine tena,taratibu weka nchi 

bastora yako na uipige teke ije 

kwangu” akasema tena 

Mathew.Tausi hakuonekana 

kutaka kutii amri aliyopewa na 

Mathew 

“Mathew usimpe nafasi ya 

kutupotezea wakati wetu,kama 

hataki kutii amri mlaze chini” 

ikasema sauti nyingine kutokea kwa nyuma na kumfanya Tausi 

ageuke ghafla na kujikuta 

anatazamana na bastora ya 

Camilla aliyekuwa amesimama 

katika mlango wa nyuma 

“Mungu wangu !! akasema 

Tausi huku akiuma meno kwa 

hasira 

“nakuamuru kwa mara 

nyingine Olivia weka silaha yako 

chini.Nitahesabu mpaka tano na 

kama hautatii nitakuchapa risasi!! 

Sura ya Tausi ilionyesha 

mstuko mkubwa sana baada ya 

kusikia jinala Olivia likitajwa 

“Tano !! akasema Mathew na 

baada ya sekunde kadhaa 

akaendelea 

“Nne !! “Tatu !! 

Ghafla kikatokea kitu 

ambacho hakuna kati yao 

aliyekuwa amekitarajia.Tausi 

aligeuka kama upepo na 

kuvurumisha risasi upande ule 

alikokuwa amesimama Camilla na 

kuruka sarakasi huku aiachia 

risasi kuelekea upande ule 

alikokuwa Mathew,akatua karibu 

na mlango wa maliwato akaupiga 

teke ukafunguka lakini kabla 

hajaingia ndani Mathew 

akajitokeza akaachia risasi 

zilizompata Tausi mguuni.Theresa 

akiwa ndani ya maliwatoni alipiga 

ukelele mkubwa kwa woga 

uliompata baada ya Tausi kuupiga 

mlango Pamoja na kupigwa risasi za 

mguu,Tausi akajivuta akaingia 

maliwato na kuusukuma 

ukajifunga.Taratibu na kwa 

tahadhari kubwa Mathew 

akanyata kuelekea 

maliwatoni.Theresa alipiga kelele 

baada ya Tausi kumuelekezea 

bastora 

“Wewe ni nyoka mkubwa na 

haya yote yametokea kwa sababu 

yako.Watu wako wamenizingira na 

lengo lao ni kunikamata.Siwezi 

kuwapa nafasi hiyo ya kunikamata 

nikiwa mzima.Hata hivyo siwezi 

kuondoka peke yangu,lazima 

tuondoke sote.Jino kwa jino!! 

Akasema Tausi huku akikunja sura 

kwa maumivu aliyokuwa anayapata mguuni baada ya 

kupigwa risasi 

“Tafadhali usiniue 

Taus……………” 

Bila huruma Tausi 

akavurumisha risasi kadhaa toka 

katika bastora yake yenye 

kiwambo cha kuzuia sauti 

zilizompata Theresa akaanguka 

chini.Mlango wa maliwato 

ukapigwa teke na Mathew 

akajitoma ndani na kabla 

hajafanya chochote Tausi 

akajielekezea bastora kichwani na 

kujifumua kwa risasi akafa pale 

pale. 

“Oh No !! akasema Mathew 

kwa mstuko baada ya Tausi 

kujipiga risasi.Alipotupa jicho pembeni akamuona Theresa akiwa 

amelala chini akivuja damu 

nyingi,akamkimbilia 

“Theresa !! Theresa !! akaita 

akijaribu kumtikisa lakini hakuwa 

na fahamu na mapigo ya moyo 

yalipiga kwa mbali 

“No !! Don’t die Theresa !! 

akasema Mathew na kumuinua 

Theresa aliyekuwa anavuja damu 

nyingi akamtoa maliwatoni na 

kumkuta Camilla akiwa 

amesimama katika varanda 

akifunga jeraha lililokuwa linavuja 

damu baada ya moja ya risasi 

iliyopigwa na Tausi kumkwaruza 

katika mkono wake wa kushoto. 

“Theresa !! Camilla akasema 

kwa mstuko alipomuona Mathew amembeba Theresa huku akivuja 

damu 

“Camilla tumuokoe 

Theresa.Huyu shetani kampiga 

risasi.Tumkimbize hospitali” 

akasema Mathew na kutoka 

haraka akakimbia hadi 

garini.Kabla hajatoka Camilla 

alihakikisha Tausi kweli amefariki 

halafu akafunga milango ya 

nyumba ile wakaondoka kwa kasi 

kuelekea hospitali 

“Ee Mungu mponye 

Theresa.Usimchukue katika 

wakati huu bado tunamuhitaji 

sana” Mathew akaomba wakiwa 

njiani wakielekea hospitali 

“Vipi hali yake?Mathew 

akageuka na kumuuliza Camilla aliyekuwa nyuma amemshikilia 

Theresa 

“Bado hairidhishi,mapigo ya 

moyo yako chini sana fanya haraka 

tunaweza kumpoteza” 

“Hapana Theresa hapaswi 

kufa.Mungu amtasaidia atapona!! 

Akasema Mathew akiwa na wasi 

wasi mwingi kuhusu uhai wa 

Theresa 

“Tumjulishe rais? Camilla 

akauliza 

“Tutamjulisha baadae tukifika 

hospitali!! Akasema Mathew 

Walifika hospitali ya Mt Clara 

moja ya hospitali kubwa ya rufaa 

nchini yenye madaktari wazuri na 

vifaa vya hali ya juu.Haraka haraka 

Theresa akashushwa na kukimbizwa katika chumba cha 

upasuaji kwa ajili ya jitihada za 

kuokoa uhai wake.Camilla ambaye 

naye alikuwa amepigwa risasi 

katika mkono wake wa kushoto 

akachukuliwa kwenda kutibiwa 

jeraha lake.Mathew hakuruhusiwa 

kuingia katika chumba cha 

upasuaji akachukuliwa na 

kupelekwa kwa daktari mkuu 

kutoa maelezo.Mathew 

akajitambulisha kama mfanyakzi 

wa ikulu anayefanya kazi chini ya 

ofisi ya rais na yule eliyepigwa 

risasi ni mdogo wa rais.Daktari 

mkuu aliposikia Theresa ni mdogo 

wake rais hakutaka maelezo zaidi 

akainuka haraka wakaongozana 

na Mathew hadi katika chumba cha upasuaji akamtaka asubiri pale nje 

katika viti vya kupumzika.Mathew 

alishindwa kukaa akabaki 

amesimama ameshika kiuno. 

“Nahisi 

kuchanganyikiwa.Naogopa hata 

kumpigia simu rais kumjulisha 

kuhusiana na jambo hili.Sijui 

nitamwelezaje juu ya tukio hili 

lakini haya yote yamesababishwa 

na mimi kukosa umakini na 

maamuzi ya haraka kumlinda 

Theresa.Nilichelewa kumdhibiti 

Tausi hadi akampiga risasi 

Theresa.Nilikuwa na uwezo wa 

kumuua kabla hajaleta madhara 

haya lakini nilisita kufanya hivyo 

nikitaka kumpata Tausi akiwa 

mzima.kwa sababu ya uzembe wangu nimekosa Tausi na kuna 

uwezekano ninaweza kumpoteza 

pia Theresa.Nitajilaumu sana 

endapo Theresa atapoteza 

maisha.Naomba Mungu amponye 

kwani endapo atapoteza maisha 

naamini nitaingia katika mgogoro 

mkubwa na dada yake Dr Vivian” 

akawaza Mathew na kutoka 

mahala alipokuwa amesimama 

akaenda kusimama sehemu 

nyingine 

“Rais anapaswa kutambua 

kwamba amezungukwa na kundi la 

Simba na mbwa mwitu wenye 

kumuwinda na neno moja tu 

linatosha kabisa kumuondoa 

duniani.Marekani wamepandikiza 

watu wao wengi karibu na rais na ninaweza kusema kwamba rais 

wetu yuko katika himaya yao 

wakiamua muda wowote 

kummaliza wanaweza wakafanya 

hivyo” Mathew akaondolewa 

mawazoni baada ya mlango 

kufunguliwa na muuguzi akatoka 

akiwa amebeba nguo zilizotapakaa 

damu akampatia Mathew.Zilikuwa 

ni nguo na vitu vya Theresa 

“Vipi hali yake anaendeleaje? 

Mathew akamuuliza yule muuguzi 

“Ni mapema sana kusema 

chochote.Tusubiri madaktari 

wamalize kazi yao.Vuta subira 

muombe Mungu sana” akasema 

yule muuguzi na kurejea 

ndani.Mathew akazitazama zile nguo za Theresa na machozi 

yakamlenga 

“Ee Mungu sisi sote ni mali 

yako na hakuna wa kukupangia 

nini cha kufanya juu yetu.Unafanya 

ukitakacho na hatuwezi 

kukupinga.Unatoa na kutwaa kwa 

muda uutakao.Pamoja na hayo ee 

Mungu nakuomba usimchukue 

Theresa kwa wakati 

huu.Yaliyomkuta ni katika 

kutekeleza kazi tunayoifanya kwa 

manufaa ya nchi yetu.Mpe nafasi 

ee baba ili aweze kushuhudia 

mwisho wa jambo hili.Nakuomba 

kwa unyenyekevu mkubwa 

ikupendeze iwe hivyo.Amen” 

Mathew akafanya maombi 

mafupi kimya kimya halafu akaelekea katika gari lake 

akazihifadhi zile nguo za Theresa 

na kuegemea kiti 




ENDELEA

Nimeumizwa sana na hiki 

kilichomtokea Theresa.Niliwahi 

kuumia kama hivi siku alipouawa 

Anitha.Theresa alijitoa kwa moyo 

wote kufanya kila kazi 

niliyomtuma hata zile za hatari 

kubwa.Ni mtu asiyeogopa kitu.Kwa 

muda huu mfupi niliokaa naye 

tumejenga ukaribu 

mkubwa.Hakuwa na ujuzi wowote 

wa mambo haya ya uchunguzi 

lakini amekuwa ni msaada 

mkubwa sana kwetu katika 

kufanikisha baadhi ya mambo” 

akawaza Mathew akiwa garini “Ngoja nirejee ndani 

nikafuatilie kwa karibu hali ya 

Theresa” akawaza na kushuka 

garini akapiga hatua mbili na 

kusimama 

“lakini Kwa nini nisimjulishe 

rais kuhusu suala hili?Najua 

hatutaelewana lakini ni vyema 

endapo nitamweleza mapema 

kuliko kusubiri halafu akapata 

taarifa toka kwa watu wengine.Ila 

kabla ya kumjulisha rais natakiwa 

kufanya jambo moja” akawaza 

Mathew na kurejea garini 

akachukua simu yake akampigia 

Hamis Chuma akamuelekeza ilipo 

nyumba ya Tausi akamtaka 

kwenda huko mara moja akaitoe 

ndani maiti ya Tauso na kwenda kuihifadhi sehemu ambako 

haitaweza kugundulika halafu 

asubiri maelekezo mengine.Baada 

ya kutoa maelekezo hayo kwa 

Hamis Chuma akampigia simu rais 

“ Mathew” akasema rais 

akionekana kutokuifurahia ile 

simu toka kwa Mathew 

“Mheshimiwa rais 

ulinielekeza nisikupigie simu 

lakini nimelazimika kukupigia 

kukupa taarifa muhimu.Theresa 

amepatwa na matatizo.Amepigwa 

risasi na kwa sasa yuko katika 

chumba cha upasuaji hapa 

hospitali kuu ya Mt.Clara” 

“Oh my God !! Tukio hilo 

limetokea saa ngapi? Nani kafanya 

unyama huo? Akauliza Dr Vivian “Mheshimiwa rais ni habari 

ndefu kidogo ila siwezi kukueleza 

simuni hadi tutakapoonana ana 

kwa ana” 

Ukimya wa sekunde kadhaa 

ukapita kisha Dr Vivian akasema 

“Mathew naomba 

usinifiche.Niambie ukweli kuhusu 

hali ya Theresa.Is she dead? 

akauliza Dr Vivian.Sauti yake 

ilionekana kujaa woga 

“Mheshimiwa rais Theresa 

hajafa ila hali yake si 

nzuri.Madaktari wanaendelea na 

jitihada za kuokoa uhai wake” 

“Ninakuja sasa hivi hapo 

hospitali.Tafadhali naomba 

nikukute hapo hapo unieleze nini 

kilichotokea hadi ndugu yangu akashambuliwa!! Akasema rais na 

kukata simu 

“Lazima kutaibuka 

kutokuelewana kati yangu na rais 

atakapofika.Ni bora endapo 

sintamweleza nani kampiga risasi 

kwani akijua kilichotokea kila kitu 

kinaweza kikaharibika kwani 

alikwisha tuzuia kuendelea na 

uchunguzi” akawaza 

Mathew.Alirejea tena katika 

chumba cha upasuaji na kumkuta 

Camilla tayari amekwisha tibiwa 

jeraha lake mkononi na amekaa 

nje ya chumba cha upasuaji 

“Pole sana Camilla 

unajisikiaje? 

“Naendela vyema.Ile risasi 

kwa bahati nzuri ilinikwaruza tu katika nyama ila yule mwanamke 

ni hatari sana kwa namna 

alivyogeuka na kuachia risasi 

inashangaza sana.Ana wepesi wa 

ajabu.Sikuwa nimetegemea kabisa 

kama angeweza kufanya vile na 

ndiyo maana risasi ile 

ikanikwaruza mkononi” akasema 

Camilla 

“Marekani wamejiandaa vya 

kutosha na watu wao wote 

wanaowatumia katika operesheni 

zao wamekamilika katika kila 

idara.Sikufichi hata mimi sikuwa 

nimetegemea kama Tausi 

angeweza kugeuka namna ile na 

kufanya shambulio.Hata hivyo 

nasikitika tumemkosa alikuwa ni 

muhimu mno kwetu.Tungeweza kupata mambo mengi muhimu 

toka kwake” akasema Mathew 

“Mathew narudia tena 

kulisema hili,Marekani kuna 

jambo kubwa wanalitafuta hapa 

Tanzania na ndiyo maana 

wamejipanga namna hii.Nini hasa 

wanakitaka? Akauliza Camilla 

“Swali hili tumekuwa 

tunajiuliza mara kwa mara lakini 

tutapata majbu baadae kwa sasa 

tuweke pembeni kila kitu na 

kufuatilia hali ya 

Theresa.Kilichomtokea 

kimeniumiza sana.Hakupaswa 

kuwa ndani ya chumba cha 

upasuaji hivi sasa akipigania 

maisha yake.Nakiri tulifanya 

uzembe hasa mimi nilipaswa kuhakikisha ninamlinda Theresa 

kwa gharama zozote zile.Toka 

awali alikataa suala la kumfuata 

Tausi nyumbani kwake lakini 

tukamlazimisha na yamemkuta 

haya.Ianiuma sana” 

“Mathew haya ni 

mapambano.Hii ni vita na katika 

vita mambo kama haya ni lazima 

yatokee.Theresa ni askari shujaa 

na hata kama ikitokea akapoteza 

maisha anatakiwa atambuliwe 

kama shujaa.Ni kweli umeumia 

hata mimi vile vile lakini huu 

hauwezi kuwa kwisho wa 

mapambano.Lazima tusonge 

mbele.Yawezekana safari ya 

Theresa ikaishia hapa japo 

hatuombi iwe hivyo lakini ikitokea hivyo sisi tuliobaki lazima 

tuendeleze mapambano hadi 

tuhakikishe tunaikamilisha 

operesheni hii” akasema Camilla 

“Nakubaliana nawe Camilla 

suala hili halitaishia hapa lazima 

tulifikishe mwisho ila lazima 

tukubali kwamba kilichomtokea 

Theresa 

hakikustahili.Tulizembea.Kama 

tungeongeza umakini 

asingeshambuliwa” 

“Hapana Mathew hatupaswi 

kujilaumu.Kilichotokea ni ajali na 

hatukuweza kukizuia.Lengo 

lilikuwa ni kumpata Tausi akiwa 

hai ili atupe majibu 

tunayoyahitaji.Japokuwa 

hatukufanikiwa kutimiza lengo lakini tumejitahidi.Tuachane na 

hayo,tayari umekwisha wasiliana 

na rais ukamjulisha kilichotokea? 

Akauliza Camilla 

‘”Tayari nimekwishamjulisha 

na yuko njiani anakuja” 

“Vizuri sana.Nini kinafuata 

baada ya kumkosa Tausi akiwa 

mzima? Camilla akauliza 

“Kwanza tayari nimekwisha 

waagiza vijana wangu wakautoe 

mwili wa Tausi pale kwake na 

kwenda kuuficha mahala ambako 

hakuna atakayeugundua hadi hapo 

nitakapowapa maelekezo 

mengine.Sitaki wenzake wafahamu 

kama Tausi amekufa.Wakifahamu 

hivyo watajificha na tutashindwa 

kuwafahamu hivyo kifo cha Tausi kitakuwa cha kimya kimya.Kitu 

cha pili,simu yake 

tunayo,tutaitumia kumpata Dr 

Robert.Rais atakapfika hapa sisi 

tutaondoka tutakwenda nyumbani 

kwa Tausi,nitamtumia Dr Robert 

ujumbe mfupi wa kutumia simu hii 

ya Tausi na kumtaka afike pale 

nyumbani kwake mara moja na 

hapo tutampata kirahisi sana.leo 

lazima tupate majibu ya maswali 

yetu yote” akasema Mathew 

“Mpango mzuri.Huyu Dr 

Robert tukimpata anaweza 

akatusaidia sana kufahamu 

mambo mengi” akasema Tausi 

halafu kila mmoja akawa kimya 

akiwaza lake 

******************** 

Rais wa jamhuri ya muungano 

wa Tanzania Dr Vivian matope 

aliwasili hospitali ya 

Mt.Clara.Ulikuwa ni ujio wa ghafla 

na hakuna aliyekuwa 

ameutegemea.Daktari mkuu 

aliyekuwa katika chumba cha 

upasuaji akisaidiana na madaktari 

bingwa wengine kuokoa maisha ya 

Theresa akajulishwa kuhusu ujio 

wa rais akatoka mara moja na 

kwenda kumpokea wakaeleka 

ofisini kwake.Hakuruhusiwa 

mpiga picha yeyote au mwandishi 

wa habari katika ziara ile ya ghafla 

ya rais pale hospitali.Daktari mkuu akamjulisha rais kuhusiana na 

maendeleo ya Theresa toka 

walipompokea na jitihada 

zinazoendelea kufanyika kuokoa 

maisha yake. 

“Japo bado hatujui hatima ya 

mgonjwa ni nini lakini napenda 

nikushukuru sana wewe daktari 

kwa niaba ya timu yako ambao 

wanafanya kila juhudi hivi sasa 

kuhakikisha mdogo wangu 

anapona.Hata hivyo naomba 

unieleze ukweli bila kunificha,ipo 

nafasi ya mdogo wangu kupona? 

Nieleze ukweli bila kuogopa” 

akauliza Dr Vivian 

“Mheshimiwa rais ni mapema 

sana kusema lolote kuhusu 

mgonjwa lakini kwa hali yake ilivyo naweza kusema kwamba 

matumaini ya kupona ni hamsini 

kwa hamsini.Hii si kauli nzuri 

kusikia lakini ndio ukweli 

halisi.Mgonjwa amepigwa risasi 

sehemu mbaya sana ila mimi na 

timu yangu tunafanya kila 

tunaloweza kulifanya kuhakikisha 

tunaokoa uhai wa mgonjwa.Kama 

kutatokea lolote baya basi 

yatakuwa ni mapenzi ya Mungu” 

“Ahsante daktari kwa ukweli 

huo.Kingine ninachotaka uniambie 

ni kama kutakuwa na ulazima wa 

kumpeleka mgonjwa nje ya nchi 

kwa matibabu makubwa 

zaidi.Naziamini hospitali za ndani 

lakini endapo utaona upo ulazima wa kumpeleka nje ya nchi usisite 

kunijulisha mara moja” 

“Mheshimiwa rais 

nakuhakikishia kwamba hakuna 

ulazima wa kumpeleka mgonjwa 

nje ya nchi.Tunayo timu nzuri ya 

madaktari bingwa wa kila idara na 

karibu wote wako ndani ya 

chumba cha upasuaji hivi sasa 

wakifanya kila wawezalo kuokoa 

uhai wa Theresa” akasema daktari 

“Nashukuru kwa kunipa 

moyo.Kitu kingine ambacho 

nitakiomba ni usiri.Asiruhusiwe 

mtu yeyoye awe mpiga picha au 

mwandishi wa habari kufanya 

uchunguzi wowote kuhusiana na 

tuko hili.Nitaagiza ulinzi mkali 

uwekwe hapa hospitali na endapo atatoka salama katika chumba cha 

upasuaji basi ni watu maalum 

wachache watakaoingia katika 

chumba atakamolazwa” akasema 

rais na kisha akaongozana na 

daktari kuelekea katika chumba 

cha upasuaji.Nje ya chumba kile 

akawakuta Mathew na Camilla 

.Alistuka alipomuona Camilla 

akiwa amechafuka 

damu.Akawasogelea na 

kuwasalimu 

“Poleni sana” 

“Ahsante mheshimiwa rais” 

wakajibu kwa pamoja.Rais 

akawataka waongozane wote 

kuingia ndani ya chumba cha 

upasuaji kushuhudia kilichokuwa 

kinaendelea.Wakavishwa mavazi maalum na kuingia 

ndani.Walisimama mbali na 

kushuhudia heka heka 

zilizokuwamo mle ndani katika 

kuokoa uhai wa 

Theresa.Hawakukaa sana mle 

ndani wakatoka na rais akatoa 

maelekezo kadhaa kwa daktari 

mkuu na kabla hajaondoka 

akawaomba Mathew na Camilla 

wasogee pembeni wakazungumze. 

“Nielezeni nini hasa 

kimetokea? Nani kampiga risasi 

Theresa? Rais akauliza 

“Mheshimiwa rais huu si 

wakati wake.Tutaongea kwa kirefu 

zaidi hapo baadae lakini kwa sasa 

kipaumhbele ni Theresa apone” “Mathew nilikupa Theresa 

akusaidie katika uchunguzi wako 

na nikakuomba kwa kila namna 

unavyoweza umlinde lakini 

umeshindwa kufanya hivyo na 

kuacha mdogo wangu akapigwa 

risasi na sasa anapigania maisha 

yake.Najuta kwanini niliamua 

kulifanyia uchunguzi suala hili 

kwani limekuwa ni kama mkosi 

kwangu.Toka lilipoanza 

kuchunguzwa kila mara 

yamekuwa yanatokea mabalaa tu 

.Endapo Theresa atapoteza maisha 

mimi ndiye nitakayepaswa 

kulaumiwa kwa kusababisha kifo 

chake kwa kumtoa ashiriki katika 

shughuli za hatari wakati akiwa 

hana ujuzi wowote wa mambo haya ya kiuchunguzi”akasema Dr 

Vivian na mara simu ya Tausi 

ambayo Mathew alikuwa 

ameiwasha ikatetema kuashiria 

kuna mtu anapiga .Mathew akaitoa 

na kutazama mpigaji zilikuwa ni 

namba za Dr Robert.Simu 

ilipokatika akaandika ujumbe 

mfupi 

“Njoo hapa nyumbani kwangu 

mara moja nakusubiri kuna jambo 

limetokea nataka tulijadili kwa 

haraka kabla sijarejea ikulu” 

Akautuma ujumbe ule na 

baada ya sekunde chache ukaingia 

ujumbe 

“Hutakiwi kurejea tena ikulu 

mambo yamekaribia 

sana.Ninakuja hapo kwako sasa hivi nisubiri” Mathew akausoma 

ujumbe ule na kuirejesha simu 

mfukoni 

“Mheshimiwa rais 

,mkandarasi anayesimamia ujenzi 

wa kiwanda changu ananihitaji 

kwa dharura” akasema Mathew 

“Theresa hana maana yoyote 

kwako tena hadi uamue kumuacha 

na kuondoka?akauliza Dr Vivian 

“Si hivyo mheshimwia 

rais.Pamoja na hili lililotokea 

lakini mambo mengine lazima 

yaendele.Ninamjali sana Theresa 

ila kuna dharura imetokea ambayo 

inanihitaji mimi.Nitarejea baadae 

kujua maendeleo yake.kama 

hautajali utakapokuwa na nafasi 

nahitaji kukuona na kukueleza kwa kirefu kuhusu hiki 

kilichotokea leo” akasema Mathew 

na kumtaka Camilla waondoke 

“Umemweleza rais ukweli wa 

kile kilichotokea? Camilla akauliza 

wakati wakiingia garini 

“Hapana sijamueleza.Sitaki 

afahamu kama tunaendelea na 

uchunguzi.Angeona tunamdharau 

kwa kupuuza amri yake 

aliyotutaka tusiendelee na 

uchunguzi tena.Kwa sasa 

hatuhitaji vita na rais kwani ana 

uwezo wa kuzuia tusifanya jambo 

lolote” akasema Mathew 

“sawa.Tunaelekea wapi? 

Camilla akauliza 

“Nyumbani kwa Tausi.Wakati 

tunazungumza na rais simu ya Tausi ikaita na mpigaji alikuwa Dr 

Robert.Nilimtumia ujumbe mfupi 

nikijifanya ni Tausi na kumjulisha 

kwamba niko nyumbani na 

kumtaka afike mara moja tuonane 

kabla sijarejea ikulu.Majibu 

aliyoyatoa Dr Robert 

yalinistua.Alimjibu kwamba 

hatakiwi kurejea ikulu kwani 

mambo yamekaribia.Ni mambo 

gani hayo? Kuna kitu wanapanga 

kukifanya kwa siri? 

“Mathew maneno hayo ni 

ishara tosha kwamba Dr Robert na 

Tausi wana mashirikiano ya 

karibu.Lakini bado yatupasa 

kufahamu ni mashirikiano ya aina 

gani waliyonayo na kama Dr Robert anashirikiana na CIA au 

vipi” akasema Camilla 

“Kwa kuwa anakuja huku 

nyumbani kwa Tausi basi tutapata 

majibu yetu yote.Leo mbivu na 

mbichi lazima zijulikane” akasema 

Mathew na kumpigia simu Hamis 

Chuma kumuuliza kama 

walifanikiwa kuikamlisha ile kazi 

aliyowapa.Hamisi akamjulisha 

kwamba tayari wamekwisha 

imaliza ile kazi na usafi 

umekwisha fanyika hivyo hakuna 

yeyote atakayeweza kugundua 

kwamba kuna mtu aliuawa mle 

ndani 

“Mathew samahani kwa 

kuuliza ila kuna jambo nataka 

kulifahamu vizuri” “Uliza Camilla usihofu” 

“Rais aliupozuia tusiendelee 

na uchunguzi alikueleza sababu? 

“Sababu kubwa ambayo 

ilimfanya asitishe lile zoezi la 

uchunguzi ni baada ya sisi kutotii 

amri yake alipotutaka tuache kila 

kitu na twende ikulu lakini 

tukapuuza” 

“Unadhani hiyo ni sababu 

nzito ya kumfanya asitishe jambo 

kubwa kama hili 

lisiendelee.Kitendo cha sisi 

kutokwenda ikulu kama 

alivyotutaka kingeweza 

kuzungumzwa na kuisha.Ilitosha 

kumweleza kwamba tusingeweza 

kwenda ikulu muda ule kwa kuwa 

tulikuwa katika operesheni ambayo tusingeweza kuiacha na 

kwenda ikulu muda ule.Badala 

yake hakutaka kusikiliza upande 

wetu na kuamua kusitisha 

tusiendelee na uchunguzi 

wetu.Sababu aliyoitoa ni nyepesi 

sana hailingani na maamuzi 

aliyoyachukua” akasema Camilla 

“Unahisi kuna sababu 

nyingine zaidi ya hiyo aliyoitoa? 

Mathew akauliza 

“Nimelitafakari sana jambo 

hili nikaona lazima ipo sababu 

nyingine iliyomfanya Dr Vivian 

akasitisha tusiendelee na 

uchunguzi sababu ya sisi ni 

kupuuza wito wake hana mashiko 

kwani tulikuwa katika kutekeleza 

kazi yake mwenyewe” “Camilla tuachane kwanza na 

hayo mengine japokuwa yana 

msingi na tujielekeze kwanza 

katika jambo lililoko mbele yetu 

na baada ya kulikamilisha 

tutaliweka mezani suala hilo na 

kulifanyia kazi kwani hata mimi 

nilikuwa na mawazo kama yako” 

akasema Mathew 

Waliwasili katika makazi ya 

Tausi maeneo ya mji mweupe.Bado 

gari la Tausi lilikuwepo pale 

pale,wakaegesha kwa mbele yake 

na kushuka geti halikuwa 

limefungwa wakingia ndani.Ile 

michirizi yote ya damu tayari 

ilikwisha safishwa na akina 

Hamis.Milango haikuwa 

imefungwa kwa funguo wakaingia ndani na kitu cha kwanza 

alichokifanya Camilla ni kuingia 

cumbani kwa Tausi akachagua 

mavazi ya Tausi akavaa na 

kuyaficha yale mavazi yake 

yaliyotapakaa damu.Mathew 

akamtaka Camilla aende sebuleni 

akahakiki usalama ili yeye afanye 

uchunguzi katika chumba cha 

Tausi wakati wakimsubiri Dr 

Robert.Mkoba wa Tausi ulikuwa 

mezani na kitandani kulikuwa na 

kompyuta ndogo.Akaufungua 

mkoba ule na kutazama 

kilichokuwamo ndani 

yake.Kulikuwa na vitu vichache 

kama rangi za mdomo na vipodozi 

vile vile kulikuwa na kifaa cha 

kuhifadhia kumbu kumbu.Mathew akakichukua kifaa kile na 

kukichomeka katika kompyuta 

ndogo iliyokuwa kitandani na 

kuanza kuyapitia mafaili 

yaliyokuwamo mle ndani ya kile 

kifaa.Kulikuwa na picha mbali 

mbali za Tausi alizopiga sehemu 

mbali mbali.Mathew akaanza 

kuipekua kompyuta ile ili kuona 

kama kuna kitu anaweza 

akakipata kitakachowafaa 

“Mhh ! Kuna mafaili 

hayafunguki.Ngoja nimpelekee 

Camilla yeye ana utaalamu 

mkubwa wa haya mambo” 

akawaza Mathew na kumfuata 

Camilla sebuleni akampa ile 

kompyuta na kumtaka aikague 

kwani kuna mafaili yamefungwa na yanahitaji programu maalum ya 

kuyafungua.Camilla akaanza kazi 

yake na baada ya dakika tano 

akamuita Mathew 

“Kuna kitu nimekigundua 

katika mojawapo ya mafauli 

yaliyokuwa yamefungwa.Ni ramani 

ya uwanja wa ndege wa kimataifa 

wa Julius Nyerere.Katika ramani 

hii kuna alama ya mstari 

mwekundu umechorwa na sielewi 

ni kwa nini? Akasema 

Camilla.Mathew akaitazama 

ramani ile kwa muda na kusema 

“Tulipokuja mara ya kwanza 

tuliipata ramani ya jiji la Dar es 

salaam chumbani kwa Tausi na 

sasa tumeipata tena ramani ya 

uwanja wa ndege wa kimataif wa Julius Nyerere.Kuna jambo gani 

wanalipanga hawa watu? Akasema 

Mathew akiendelea kuitazama 

vyema ile ramani 

“Mstari huu mwekundu 

umechorwa sehemu wanakopita 

watu mashuhuru kama vile 

viongozi wakubwa wa serikali 

watokapo au kuingia toka nje ya 

nchi.Kwa nini mstari mwekundu 

uchorwe eneo hili pekee?akauliza 

Mathew akiendelea kuitazama ile 

ramani 

“Ukiunganisha ramani hii ya 

uwanja wa ndege,ile ya jiji la Dar 

pamoja na ujumbe ule ambao Dr 

Robert aliuandika kwa Tausi 

kwamba mambo yamekaribia 

unapata picha kwamba kuna jambo linapangwa na hawa jamaa 

aidha katika uwanja wa ndege wa 

kimataifa wa Julius Nyerere au 

katika viunga vya jiji la Dar es 

slaam.Lazima kuna mpango 

mkubwa unaand……………” 

“Shhhhhhh…”Camilla 

akamfanyia Mathew ishara 

anyamaze 

Kupitia dirishani aliliona gari 

moja la kifahari aina ya marcedece 

benzi lenye rangi nyeusi 

likisimama karibu na geti la Tausi. 

“Nahisi ni mwenyewe Dr 

Robert amefika.Wewe utabaki 

hapa ndani.Mkaribishe vizuri 

mdanganye kwamba Tausi yuko 

chumbani kwake na mimi 

ninakwenda kuzungukaikaitika

nyuma ili nichunguze kama 

amekuja mwenyewe au kuna watu 

ameongozana nao.Nitaibukia 

mlango wa mbele na kulimaliza 

zoezi kwa haraka” akasema 

Mathew na mlango wa lile gari 

ukafunguliwa akashuka jamaa 

mmoja mnene aliyevaa suti nzuri 

nyeusi na miwani myeusi kichwani 

alivaa kofia ya mduara. 

“Ni mwenyewe” akasema 

Mathew akatoka haraka kwa 

kupitia mlango wa nyuma 

Mlango wa mbele sebuleni 

ukagongwa na sauti tamu ya 

Camilla ikaitika



Mlango wa mbele sebuleni 

ukagongwa na sauti tamu ya 

Camilla ikaitika 

“Please come in.The door is 

open” akasema Camilla huku 

akijifanya kuwa makini katika kompyuta ile aliyokuwa ameishika 

mkononi. 

Mlango ukafunguliwa na yule 

mgongaji akaingia.Camilla alikuwa 

ameketi sofani bila wasi wasi 

akiwa na kompyuta ya Tausi na 

yule mgongaji alipoingia akaiweka 

komputa pembeni akainua kichwa 

wakatazamana 

“Welcome Sir.Are you Dr 

Robert? Camilla akauliza huku 

akitabasamu 

“Yes I am.Who are you? 

“I’m Carmelita Johson a friend 

of Tausi” Camilla akadanganya 

“Oh Good to see you 

Carmelita” akasema Dr Robert 

huku akimpa mkono Camilla “Good to see you too Dr 

Robert.Let me call Tausi she’s in 

her room waiting for you” akasema 

Camilla na kabla hajapiga hatua Dr 

Robert akamuita 

“ Wait !! 

“Before you call her I want to 

know a few things about 

you.Where do you live? If possible 

can you give me your contacts so I 

can invite you for dinner or a 

drink” akasema Dr Robert 

akionyesha wazi kuvutiwa na 

Camilla ambaye alikuwa ameachia 

tabasamu pana la kichokozi 

“Tausi will give you all my 

details don’t worry” akasema 

Camilla na kumkonyeza Dr Robert kisha akaelekea chumbani kwa 

Tausi 

Mara tu Camilla alipoondoka 

pale sebuleni,mlango mkubwa wa 

mbele ukafunguliwa na taratibu 

akaingia Mathew akiwa na bastora 

iliyofungwa kiwambo cha kuzuia 

sauti. Dr Robert alistuka na 

kusimama huku akitumbua macho 

kama vile amekutana na dudu la 

kutisha 

“Halow Dr Robert !! akasema 

Mathew 

“Who are you?!! Akauliza Dr 

Robert huku midomo 

ikimtetemeka 

“Sit down !! akasema Mathew 

kwa sauti kali.Dr Robert akaogopa 

na kukaa chini na mara akatokea Camilla naye akiwa na bastora 

mkononi.Dr Robert akazidi 

kuchanganyikiwa 

“What’s the meaning of this? 

Where is Tausi?Who are you? 

Akauliza Dr Robert huku 

akitetemeka kwa woga.Mathew 

akampa Camilla ishara 

akamsogelea Dr Robert 

“Please don’t hurt me! I have 

mon….” Hakumaliza sentensi yake 

akapigwa pigo moja la karate na 

kupoteza fahamu . 

“Amekuja peke yake? Camilla 

akauliza 

“Ndiyo amekuja 

mwenyewe.Hakuongozana na 

dereva wala walinzi wake na 

hakutaka kutumia gari la serikali ili asigundulike mambo 

yake.Arobaini yake imewadia leo 

na atatueleza kila kitu” akasema 

Mathew kisha akamtaka Camilla 

aliingize gari lao ndani 

wakampakia Dr 

Robert.Wakalipekua gari lake na 

wakakuta kuna mkoba 

wakaondoka nao 

WASHINGTON DC – 

MAREKANI. 

Ni saa tatu za asubuhi kwa saa 

za Marekani,Mike straw rais wa 

Marekani alipowasili katika ofisi 

za CIA Washington DC.Hii ilikuwa 

ni muda mfupi tu baada ya vyombo 

vya habari vya Korea kaskazini kutangaza kufanikiwa kwa jaribio 

kubwa la kombora la masafa 

marefu lililorushwa na Korea 

Kaskazini katika bahari ya 

Pacific.Kwa mujibu wa vyombo 

hivyo vya habari ni kwamba 

kombora hilo aina ya MQ603 lenye 

uwezo wa kubeba kichwa cha 

nyuklia lilikuwa na uwezo wa 

kufika katika miji ya Marekani 

kama vile San francisco,Los 

angeles na hata Las Vegas.Hizi 

zilikuwa ni taarifa mbaya zilizozua 

taharuki kubwa kwa wamarekani 

na wengi walitaka nchi yao 

kuchukua hatua kazli za haraka 

kuidhibiti Korea kaskazini ambalo 

limekuwa ni taifa tishio kwa 

Marekani. Mike Straw alipokewa na 

mkurugenzi wa CIA Willy gadner 

na kukaribishwa 

ndani.Wafanyakazi wote 

wakasimamisha kazi kwa muda ili 

kusalimiana na rais 

“Habari za asubuhi? rais Mike 

straw akaanza kuwasalimu 

“Ni furaha yangu kubwa 

kuwepo hapa asubuhi hii.Nimekuja 

kuwapongezeni kwa juhudi kubwa 

mnazozifanya kila siku.Mnafanya 

kazi usiku na mchana kwa ajili ya 

usalama wa Marekani na ni kwa 

sababu yenu na vyombo vingine 

Marekani imeendelea kuwa 

salama.Nawaomba msichoke 

endeleeni kujituma katika kazi 

kwani maisha ya wamarekani yako mikononi mwenu.Maadui wa 

marekani wanaongezeka lakini 

hakuna atakayethubutu 

kupambana na sisi 

akatushinda.Nawatakieni kila la 

heri katika utendaji kazi 

wenu.Ahsanteni sana” Mike straw 

akazungumza machache kisha 

akaongozana na Will Gadner hadi 

ofisini kwake 

“Karibu sana mheshimiwa 

rais” akasema Willy 

“Ahsante Willy.Nimelazimika 

kuja mwenyewe kufuatia taarifa 

zilizotoka muda si mrefu ambazo 

nadhani tayari umekwisha 

zisikia.Korea kaskazini wamefanya 

jaribio lingine la kombora katika 

bahari ya Pacific” “Taarifa hizo tayari tunazo 

mheshimiwa rais na tunaendelea 

kuzifanyia kazi ili tujue ukweli 

wake kama kombora hilo la 

MQ603 lina uwezo wa kufika Las 

Vegas kama walivyodai”akasema 

Willy 

“Willy nimeamua kuja 

mwenyewe hapa ili nishuhudie 

kwa macho kile mnachokifanya 

kuhusu suala hili la Korea 

Kaskazini.Katika jambo hili 

tunawategemea sana CIA.Korea 

kaskazini wanazidi kupiga hatua 

kubwa kijeshi kila uchao huku sisi 

tukiendelea kuwatazama na 

kuwaongezea vikwazo ambavyo 

havionekani kuwa na msaada 

wowote.Ndani ya muda mfupi tu tayari wamekwisha fanya 

majaribio mawili ya makombora 

ya masafa marefu.Kim Hun Yu 

haogopi wala hasikii sauti ya 

kiumbe yeyote anayevuta pumzi 

kama yeye.Anafanya kile 

anachokusudia na anaendelea 

kufanikiwa.Kwa muda mrefu lengo 

la Korea Kaskazini ni kutengeneza 

kombora ambalo litafika katika 

miji ya Marekani na kikubwa 

anachokilenga ni kutengeneza 

Kombora la kufika Washington 

DC.Kama tayari wamefanikiwa 

kutengeneza kombora lenye 

uwezo wa kufika Las Vegas muda si 

mrefu wataweza kutengeneza 

kombora la kufika hadi 

Washington DC na hilo kama nilivyosema ndilo lengo lao la 

muda mrefu.Mbaya zaidi ni 

kwamba kombora hilo 

walilolifanyia majaribio lina 

uwezo wa kubeba kichwa cha 

nyuklia.Hiki ni kitisho kikubwa 

sana kwa Marekani .Mimi kama 

rais niliyeapa kuwalinda 

wamarekani dhidi ya uchokozi 

wowote ule siwezi kuacha upuuzi 

huu ukaendelea.Nataka kuiadhibu 

vikali sana Korea kaskazini.Nataka 

kuiharibu Pyongyang !! Nataka 

kuharibu mfumo wote wa silaha 

wa Korea kaskazini.Nataka ibaki 

historia kwamba kuliwahi kuwa na 

taifa linaitwa Korea kaskazini 

katika ramani ya dunia.Uwezo wa 

kuiharibu kabisa Korea Kaskazini au hata kuifuta katika uso wa 

dunia tunao hivyo nataka 

kuanzisha vita ili niweze 

kumchakaza Kim Hun lakini 

lazima iwepo sababu ya kuanzisha 

vita ndiyo maana nikabuni 

ulempango wa kumuua waziri 

Helmet Brian.Nataka kufahamu 

mmefikia wapi kuhusu ule mpango 

wetu kule Tanzania? Akauliza Mike 

Straw. 

“Mheshimiwa rais bado 

tunaendelea na mipango yetu 

nchini Tanzania na ninaweza 

kusema kwamba kila kitu 

kinakwenda vizuri sana.Tayari 

tumefanikiwa kumpandikiza mtu 

mwingine ndani ya ikulu ya Dar es 

salaam ambaye yuko karibu sana na rais na kupitia huyu tutaweza 

kufahamu kila kinachoendelea 

pale.Kuhusu mpango ule wa 

kumuondoa Helmet Brian nao pia 

unakwenda vizuri.Helmet 

atawasili katika uwanja wa ndege 

wa kimataifa wa Julius Nyerere leo 

saa moja za jioni na tayari kila kitu 

kimekwisha andaliwa vizuri na 

hadi kufika saa mbili za usiku 

Helmet tayari atakuwa amekwisha 

kufa.Tuna mawasiliano mazuri na 

watu wa Dar es salaam na sisi hapa 

tuko makini tunafuatilia kwa 

karibu sana kila kinachoendelea 

kule” 

“Ahsante kwa taarifa hizo 

nzuri ila narudia tena 

kukukumbusha kwamba hii ni operesheni kubwa inayohitaji 

umakini mkubwa sana.Sitaki 

kusikia kuna uzembe wowote 

unafanyika katika operesheni 

hii.Makosa au uzembe wa aina 

yoyote ile utakaofanyika katika 

operesheni hii sintauvumilia 

kabisa.Mara tu nitakapopata 

taarifa ya kifo cha Helmet Brian 

nitamuelekeza waziri wa ulinzi 

aadae majeshi wakati nikisubiri 

kupata idhini ya bunge 

kuishambulia Korea Kaskazini” 

akasema Mike 

“Mheshimiwa rais 

nakuhakikishia kwamba 

tunafahamu umuhimu wa 

operesheni hii na hivyo tuko 

makini zaidi ya unavyofikiri.Tumeweka uzito 

mkubwa sana katika suala 

hili.Tayari wadunguaji watatu 

wako Tanzania na ndio 

watakaoikamilisha hii 

kazi.Tutawakamata watu hao na 

baada ya kuwahoji watadai 

kwamba wametumwa wamuue 

Helmet na Korea kaskazini .Kila 

kitu kitakwenda vizuri sana 

mheshimiwa rais” akasema Will 

Gadner 

“Vipi kuhusu yule kijana wetu 

aliyekuwa na mahusiano na rais 

wa Tanzania uliyeniambia 

kwamba amepotea na hajulikani 

alipo,amekwisha patikana? 

“Mpaka sasa bado 

hajapatikana ila uwezekano wa kumpata akiwa hai ni mdogo 

sana.Tunachopambana hivi sasa ni 

kuupata mwili wake.Balozi wetu 

Abrahm Clerk analishughulikia 

hilo suala” 

“Unadhani rais wa Tanzania 

Dr Vivian alimgundua kwamba 

yule kijana ni pandikizi la CIA na 

akamuua? Mike akauliza 

“Kwa hali halisi ilivyo 

mheshimiwa rais kuna uwezekano 

mkubwa sana kwamba tayari 

Nathan atakuwa ametambulika 

kama ni CIA na ndiyo maana tuna 

mashaka aidha atakuwa ameuawa 

au ametekwa na kufichwa mahala 

ili kutoa siri” 

“Juhudi kubwa zinahitajika ili 

kupata taarifa za mahala alipo huyu kijana tujue kama ametekwa 

au amekufa.Pamoja na operesheni 

hii kubwa inayoendelea Tanzania 

lakini wekeza nguvu pia katika 

suala hili ili kujua alipo huyu 

kijana ambaye hatujui kama 

amekufa au ametekwa.kama 

ametekwa anaweza akateswa na 

akatoa siri.Anatakiwa haraka sana 

atafutwe na apatikane”akasema 

rais 

“Tunalishughuliki hilo 

mheshimiwa rais” 

“Vizuri.Kabla sijaondoka kuna 

jambo nataka kulifahamu.Ni 

kuhusiana na huyu rais wa 

Tanzania Dr Vivian.Taarifa 

uliyonipa ni kwamba CIA 

mmekuwa mnafuatilia kwa muda mrefu,lakini bado hujanieleza ni 

kwa nini mnamfuatilia? Kuna kitu 

gani mnakitafuta toka kwake?Ana 

umuhimu gani kwa Marekani hadi 

tuwekeze namna hii katika 

kumfuatilia?akauliza Mike 

“Mheshimiwa rais Dr Vivian ni 

mtu muhimu sana kwa Marekani 

na ndiyo maana CIA tumekuwa 

tunamfuatilia kwa karibu kwa 

muda mrefu.Tumeanza 

kumfuatilia Dr Vivian toka angali 

anasoma chuo kikuu hapa 

Marekani na mpaka sasa bado 

tunaendelea kumfuatilia tena kwa 

karibu zaidi.Kuhusu ni kwa nini 

tunamfuatilia naomba nitafute 

muda nitakuja kukueleza kwa 

kirefu zaidi kwani ni suala lenye kuhitaji muda wa kutosha lina 

maelezo marefu.Kwa sasa naomba 

tuelekeze nguvu katika operesheni 

kubwa inayotukabili” akasema 

Willy gadner 

“Sawa Gadner,nakubaliana 

nawe kuhusu hilo.Kwa kuwa una 

majukumu makubwa 

yanayokukabili ngoja nikuache 

uendelee na operesheni hii 

muhimu ila naomba kuwe na 

mawasiliano ya karibu 

sana,nataka nijulishwe kila 

kinachoendelea Tanzania.Kitu cha 

mwisho ni kuzingatia usiri.Jambo 

hili ni siri kubwa na hapaswi 

kufahamu mtu mwingine 

asiyehusika” “Nitalizingatia hilo 

mheshimiwa rais” akajibu Gadner 

wakaagana na rais akaondoka 

DAR ES SALAAM – TANZANIA 

Bado Dr Robert hakuwa na 

fahamu wakati Mathew na Camilla 

walipowasili katika makazi 

yao.Wakamshusha garini na 

kumuingiza ndani wakamuweka 

katika chumba kilichokuwa na 

kitanda kimoja cha chuma na 

kumfunga pingu mkono mmoja na 

kuifunga katika kitanda.Simu 

nyingi zilikuwa zinapigwa katika 

simu ya Dr Robert ambayo Mathew 

alikuwa nayo lakini hawakupokea 

simu yoyote.Walikaa sebuleni na kuanza kuupekua mkoba wa Dr 

Robert uliokuwa na makaratasi na 

mengi yakiwa ni nyaraka za 

kikazi.Wakati wakiendelea 

kuzipekua nyaraka zile moja moja 

simu ile ya Dr Robert 

ikaita,Mathew akatazama mpigaji 

jina liliandika “balozi Clerk” 

“Balozi Clerk anapiga.Huyu 

nahisi ni yule balzi wa Marekani 

hapa Tanzania” akasema Mathew 

na kuchukua zile namba za simu 

alizozitoa katika simu ya Tausi na 

kuzilinganisha na zile za balozi 

Clerk katika simu ya Dr Robert 

zilikuwa zinafanana 

“Ni mwenyewe.Watu hawa 

wana mawasiliano ya karibu” 

akasema Mathew na kwa kutumia simu ya Dr Robert akamuandikia 

ujumbe mfupi balozi Clerk 

“Niko katika kikao muhimu 

cha dharura na rais hivyo siwezi 

kupokea simu.Nitumie ujumbe 

mfupi” akautuma ujumbe ule na 

baada ya sekunde chache ukaingia 

ujumbe toka kwa balozi Clerk 

“Ukimaliza kikao tafadhali 

tuonane haraka vijana wako tayari 

wanasubiri maelekezo ya mwisho 

kwani muda wa kuwasili mtu wetu 

umekaribia sana” 

Mathew akausoma ujumbe ule 

na kumpa simu Camilla naye 

ausome. 

 “Mathew sasa picha inaanza 

kuja.Ukiunganisha ramani zile 

mbili ile ya uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na ile ya jiji la Dar 

es salaam ni wazi kuna mtu 

muhimu 

wanayemsubiria.Ukitazama 

ramani ya uwanja wa ndege 

kumechorwa mstari mwekundu 

katika sehemu wanakopita 

viongozi wa kitaifa na hii ina 

maanisha kwamba mtu 

anayesubiriwa na hawa jamaa ni 

mtu mkubwa.Tunachokihitaji 

kufahamu ni kwa nini kukawa na 

alama ya mstari mwekundu katika 

sehemu hii wanakopita viongozi 

wakuu wa kitaifa?akauliza Camilla 

“Kuna jambo kubwa 

linapangwa kufanywa na hawa 

jamaa.Huyu mtu wao 

wanayemsubiri ni nani? Ukiongezea katika hoja yako ni 

kwamba,ramani ya jiji la Dar es 

salaam pia ina alama nyekundu 

katika baadhi ya sehemu.Hii ni 

ishara tosha kuna jambo 

linaandaliwa ambalo lazima 

tulifahamu na mtu pekee wa 

kutufahamisha ni 

DrRobert.Camilla endelea kupekua 

nyaraka zake mimi ninakwena 

kumzindua ili atupe majibu” 

akasema Mathew na kuelekea 

chumbani kwake ambako 

alichukua kichupa kidogo akaenda 

chumbani alimo Dr Robert 

akakifungua kile kichupa na 

kukiweka puani kwa Dr Robert. 

Baada ya sekunde kadhaa akapiga 

chafya mfululizo.Mathew

 hakumsemesha chochote akatoka 

na kumfuata Camilla sebuleni 

“Tayari amezinduka.Kuna 

chochote umekipata katika 

nyaraka zake? Akauliza Mathew 

“Nyingi ni nyaraka za kazi 

lakini kuna karatasi moja 

nimeikuta ina picha za watu 

watatu halafu pembeni ya kila 

picha kukawa na jina la hoteli na 

jina ambalo naamini ni la 

mojawapo ya sehemu za jiji hili la 

Dar es salaam” akasema Camilla na 

kumuonyesha Mathew ile karatasi 

ambayo ilikuwa na picha tatu 

kama alivyosema Camilla.Picha ya 

kwanza ilikuwa na jina Kang Chol 

Hwan jina la hoteli ni Silver peak 

na chini yake kukaandikwa barabara ya viwanda.Picha ya pili 

ikaandikwa Kim Kyong Hui jina la 

hoteli likaandikwa Samawati 

beach halafu kukaandikwa Jasmin 

Plaza.Picha ya mwisho ikaanzika 

Pak Pong Ju ambaye hoteli ni 

Samila 5 star na mahali ni 

barabara ya Twiga. 

“Camilla kuna kitu ninakiona 

hapa” akasema Mathew baada ya 

kuitazama ile karatasi.Akachukua 

karatarsi yenye ramani ya Dar es 

salaam akaitazama na kusema 

‘Tulikuwa tunajiuliza maswali 

kuhusu ile miduara myekundu 

katika ramani ya jiji la Dar es 

salaam sasa jibu 

limepatikana.Katika kila picha hizi 

kuna jina la sehemu na sehemu hizo ndizo zimechorwa mistari 

myekundu katika hii 

ramani.Ninahisi hawa jamaa 

wamepangwa katika sehemu hizi 

kwa ajili ya kufanya kazi 

maalum.Kuna ulazima kubwa wa 

kufahamu kitu wanachotaka 

kukifanya hawa jamaa.Halafu 

tunapaswa tuwafahamu hawa 

jamaa ni akina nani? Mathew 

akauliza 


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog