Simulizi : Scandle (Kashfa)
Sehemu Ya Tano (5)
“Alieleza ni nani huyo
Naomi Bambi? Akauliza Rais Festus
“Kwa maelezo aliyotupa ni kwamba aliwahi kumuona Naomi Bambi mara moja tu tena usiku wa manane na alipelekwa mahala alipo kwa kazi moja tu ya kumchoma sindano”
“Sindano ?! Rais Festus akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Kwa mujibu wa Zawadi dawa aliyochomwa Naomi ni kwa ajili ya kumuharibu akili”
“Kumuharibu akili?! Why? Akauliza Rais Festus
“Bado hatufahamu ni kwa nini Naomi akafanyiwa hivyo lakini kwa mujibu wa Zawadi anadai Naomi hakuwa kichaa”
“Mhhh ! Rais Festus akaguna
“Wakati tukiendelea
kuzifanyia kazi taarifa tulizopewa na Zawadi tulipokea taarifa nyingine kutoka gereza la Kimondo” Ruby akanyamaza kidogo
“Katika gereza la Kimondo aliingizwa mtu mmoja anaitwa Kishada.Ukweli ni kwamba mtu huyo hakuwa mfungwa bali aliingizwa gerezani kwa lengo moja tu la kumuua Gosu Gosu kwa sindano ya sumu.Kwa bahati nzuri tayari tulikwisha weka mtu pale gerezani wa kumsaidia Gosu Gosu na aliweza kumpatia Gosu Gosu taarifa za kile kilichopangwa kufanyika dhidi yake.Kwa uhodari wake Gosu Gosu aliweza kupambana na huyo mtu akafanikiwa kumuua na baada ya kumpekua akamkuta na simu ambayo alikuwa anaitumia kuwasiliana na watu waliomtuma akaitumia simu hiyo kuwasiliana na Mathew akamjulisha kile kilichotokea.Taarifa hiyo ikatufanya tuamini jambo lile haliwezi kufanyika bila ya uongozi wa gereza kulifahamu.Jana asubuhi Fabian na Mathew Mulumbi wakaenda kuonana na Kamishna jenerali wa magereza mzee Chambao wakamueleza ukweli na kumuomba awasaidie waweze kumpata mkuu wa gereza la Kimondo kwa mahojiano.Mzee Chambao akakubali na kusafiri hadi Arusha kwa kutumia helkopta akamleta Deus ambaye alipohojiwa kuhusiana na tukio lile kuna jambo likagundulika” Ruby akanyamaza tena kidogo.Rais Festus alikuwa kimya akimsikiliza
“Deus alikiri kumuingiza mtu huyo gerezani lakini alidai ni maelekezo aliyoyapata kutoka kwa mtu asiyemfahamu”
“Mtu asiyemfahamu? !
akauliza Rais Festus kwa ukali
“Alibanwa sana na akalazimika kusema ukweli kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mzee Chambao na mtu huyo aliyekuwa akimpa maelekezo alikuwa na video iliyorekodiwa kwa siri ikiwaonyesha yeye Deus na mke wa Kamishna Chambao wakifanya mapenzi.Mtu huyo alitishia kuisambaza video
hiyo katika mitandao ya kijamii kama Deus asingefaya kile alichomuelekeza.Ili kuepuka aibu ambayo angeipata kama video hiyo ingesambazwa Deus akakubali kufanya kila alichoelekezwa na huyo mtu na kubwa alilomuelekeza ni kumuua Gosu Gosu.Kwanza alijaribu kuwatumia wafungwa ndani ya gereza lakini wakashindwa ndipo walipomuingiza huyo Kishada lakini naye akauwa”
“Dah ! akasema Rais Festus
“Juhudi za kumtafuta mtu huyo ambaye tulibaini alikuwa hapa Dar es salaam zilianza na mara Kamishna Chambao akapiga simu na kumuomba Deus ambaye kwa wakati huo alikuwa nyumbani kwetu akimsubiri Mathew.Mzee Chambao alidai kwamba anataka kuzungumza na Deus mambo muhimu ya kikazi.Fabian aliwatuma walinzi wake wampeleke Deus nyumbani kwa Chambao.Wakati zoezi likiendelea tukamjulisha Mathew kwamba Chambao amemuomba Deus wakazungumze masuala ya kazi na hilo likamstua Mathew akalazimika kuacha kile alichokuwa anakifanya akaenda nyumbani kwa Chambao lakini hakumpata Deus na kukatokea kutokuelewana kati yake na Chambao.Alinipa kazi ya kudukua mawasiliano ya Chambao kwani kuna kitu alikwisha kihisi kuwa hakipo sawa.Wakati akisubiri majibu akapigiwa simu na Zawadi ambaye alimtaka aende hospitali kuna jambo anataka kumueleza.Mathew aliondoka na kwenda hospitali na alipotoka huko akanipigia simu akanijulisha kuwa kuna mambo ya muhimu ameyapata kutoka kwa Zawadi yanayoweza kutusaidia na akasema kuna sehemu anakwenda akitoka huko atakuja moja kwa moja nyumbani kwetu na huo ukawa mwisho wa kuwasiliana naye kwani simu yake haikupatikana tena.Katika udukuzi nilioufanya katika mawasiliano ya Kamishna Chambao niligundua kwamba muda mfupi kabla ya kutupigia simu akimtaka Deus aliwasiliana na mtu Yule Yule aliyekuwa akimpa maelekezo Deus” akasema Ruby akaiwasha kompyuta yake na kucheza maongezi ya Kamishna Chambao na Yule mtu.
“Mhh ! Rais Festus akaguna baada ya kumaliza kusikiliza mazungumzo yale
“Baada ya kuwasiliana na huyo mtu ndipo alipopiga simu akamtaka Deus na akamkabidhi kwa hao jamaa
na baadae akakutwa akiwa amekufa nyumbani kwa Mathew Mulumbi.Nilimtafuta Mathew usiku kucha bila kumpata hadi asubuhi ya leo nilipopigiwa simu na Fabian akanijulisha kwamba Mathew amekamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya vile vile mauaji ya Deus .Mheshimiwa Rais,Mathew Mulumbi hajafanya hiki anachotuhumiwa kukifanya huu ni mchezo umefanywa kitaalamu sana na hawa jamaa tuliokuwa tunawachunguza”
Ruby akanyamaza
“Hili suala ni gumu sana Ruby na hata mimi limenitikisa.Kinachoumiza kichwa ni kwamba jeshi la polisi wamekamata kiasi kikubwa cha dawa za kulevya nyumbani kwa Mathew na kama haitoshi miili miwili imekutwa ndani mwake.Unawezaje kusema kwamba Mathew hahusiki na jambo hili? Akauliza Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
nilianza kwa kukupa historia kuhusu mimi na Mathew Mulumbi hivyo ni mtu ninayemfahamu vizuri sana.He’s a honest man.Hajihusishi na biashara yoyote haramu.Nimekueleza pia kwa kirefu kuhusiana na kile kilichotokea jana.Mathew ameangushiwa mzigo huu mkubwa kwani wote ambao wamekuwa wakiwafuatilia hawa jamaa aidha hufariki dunia au huangushiwa kesi kama ilivyokuwa kwa Gosu Gosu na sasa ni Mathew Mulumbi.Mheshimwa Rais hawa watu ni mtandao mpana sana na wana nguvu na uwezo wa kufanya chochote wakitakacho.Hivi tuongeavyo Fabian amechukuliwa na polisi asubuhi na anahojiwa katika ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai akihusishwa na tukio lile la dawa za kulevya na mauaji.Mheshimiwa Rais unamfahamu vyema Fabian ni mtu ambaye hawezi akajihusisha na mambo kama haya lakini naye anataka kuunganishwa na jambo hili kwanza kumchafua na pili kumpoteza kabisa.Hakuna anayewachunguza watu hawa akabaki salama” akasema
Ruby na Rais Festus akakuna kichwa
“Jana nilipokea ujumbe kutoka kwa mtu nisiyemfahamu ukinitaka nikimbie” akasema Ruby na kumuonyesha Rais ule ujumbe aliotumiwa na mtu asiyemfahamu.Festus akasoma jumbe ambazo mtu Yule asiyefahamika alikuwa anamtumia Ruby
“Ni kutokana na jumbe hizi ililazimu usiku wa manane mimi na familia yangu kuondoka kwenda mafichoni na muda mfupi kabla ya kukupigia simu nilipokea tena ujumbe mwingine kutoka kwa huyu huyu mtu akinitaka nijifiche” akasema Ruby na kumuonyesha Rais Festus ujumbe wa Yule mtu
“Dah ! Suala gumu sana hili” akawaza Festus
“Mheshimiwa Rais nimekuja kwako kuomba msaada.Mimi na familia yangu tuko katika hatari kubwa kwani hata mimi hivi sasa ninawindwa kwani nilishirikiana na akina Mathew kuwatafuta hawa watu.Mheshimiwa Rais naomba uniamini tafadhali nisingeweza kuja hapa kwako kama sina uhakika na haya ninayokwambia” akasema Ruby ukapita ukimya halafu Rais Festus akasema
“Ruby wewe ni mmoja wa watu ambao mmekuwa katika idara nyeti za usalama wa nchi
hii na siwezi
kukupuuza.Mambo
uliyonieleza ni mazito na ni wazi hawa watu ni hatari mno na kama ulivyosema wana uwezo wa kufanya kitu chochote”akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
ukifuatilia maelezo hayo niliyokupa utaona kuna mtandao mkubwa ambao kuna jambo unalificha lisijulikane.Ukianzia kwa Naomi Bambi ambaye
aliharibiwa akili,ukija kwa Lidya ambaye aliuawa na wale wote wote waliokuwa wanashirikiana wakauawa vile vile.Kila ambaye anataka kuwachunguza habaki salama.Gosu Gosu ameishia gerezani na sasa anafuata Mathew na nina uhakika mkubwa Dr Fabian naye lazima ataingizwa katika mkumbo huo” akasema Ruby na Rais akatazama juu na kuvuta pumzi ndefu.Akatafakari kwa dakika moja halafu akasema
“Dr Fabian ni sababu ya mimi kuwepo hapa nilipo.Ni yeye aliyenipigania hadi nikafanikiwa kufika hapa.Haikuwa rahisi.Ndani ya chama kulikuwa na upinzani mkubwa na vigogo walikuwa na watu wao waliowataka washike madaraka lakini ni Dr Fabian ambaye alipima ni nani anafaa akanichagua mimi na akapambana kufa na kupona kuhakikisha ninapita katika michakato yote.Lengo la hawa mashetani ni kumchafua,kumdhalilisha na kuhakikisha anaingia gerezani.I won’t allow that ! akasema kwa ukali Rais Festus na kusimama
“Ruby niambie nini tunaweza kukifanya kuhusiana na hawa watu? Akauliza Rais
Festus
“Mheshimiwa Rais hawa watu lazima wasakwe kwa kila namna na wajulikane ni akina nani na kitu gani ambacho wanatumia gharama kubwa namna hii kukificha
kisijulikane.Kingine ni kuufahamu mtandao wao.Wanaonekana ni watu ambao wamejipenyeza na kuotesha mizizi yao sehemu mbali mbali muhimu na kwa nguvu waliyonayo ndiyo maana wana uwezo wa kufanya chochote wakitakacho.Wana uwezo wa kudukua mawasiliano ,wana uwezo wa kutumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa kitu ambacho hakiwezekani hapa nchini lakini wao wanakifanya na ndiyo maana inakuwa vigumu kuwatambua.Lakini mheshimiwa Rais kabla ya hayo yote ninaomba uisaidie familia yangu.Nataka watoto wangu wawe salama wakati mimi nikiendelea na mapambano na hawa jamaa” akasema Ruby
“Kwa hilo usihofu
Ruby.Watoto wako watakuwa salama na wataishi hapa ikulu ambako ni sehemu salama zaidi hadi hapo jambo hili litakapokuwa limemalizika”
“Ahsante mheshimiwa
Rais.Baada ya hapo tunatakiwa kutafuta namna ya kuhakikisha tunampata Mathew Mulumbi ili tuweze kuendelea kuwasaka hawa jamaa”
“Ruby hapo kuna ugumu mkubwa.Tayari Mathew yupo
katika mikono ya jeshi la polisi akituhumiwa kwa mauaji na dawa za kulevya na nchi nzima inalifahamu jambo hilo.Hapo siwezi kuweka mkono wangu kwa namna yoyote ile bila na mimi kuonekana ninahushirikiana naye.
Kumtoa Mathew Mulumbi kwa sasa itakuwa vigumu sana.Mikono yangu imefungwa na siwezi kuingilia uchunguzi wa jeshi la polisi.Hawa jamaa wamejipanga vizuri mno ni wataalamu wa kupanga mambo yao walijua fika kwamba kwa hili Mathew hawezi kuchomoka”akasema
Rais Festus
“Mheshimiwa Rais bila kumsaidia Mathew Mulumbi na Dr Fabian hatutaweza kuwafahamu hawa jamaa na mambo yao wanayoyaficha hayataweza kujulikana.We have to do anything to save him..! akasema Ruby
“Ngoja kwanza niwasiliane na DCI nijue kinachoendelea hivi sasa katika suala hili” akasema Rais Festus na kuchukua simu akampigia mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai.
“Hallow DCI”akasema
Rais Festus baada ya simu yake kupokelewa
“Naam mzee”
“Nataka kufahamu kwa kina kuhusiana na tuko lililotokea usiku wa leo la Yule mfanya biashara aliyekamatwa na dawa za kulevya” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa raia mwema ambaye alidokeza kwamba kuna mzigo wa dawa za kulevya umefichwa katika nyumba ile ndipo jeshi la polisi kitengo cha kupambana na kuzuia dawa za kulevya kilipovamia nyumba hiyo usiku na kukamata kiasi kikubwa cha dawa hizo.Ni mzigo unaokadiriwa kuwa zaidi ya kilo mia moja na hamsini.Ndani ya nyumba hiyo pia kulikutwa miili miwili ya watu waliouawa mmoja ukiwa ni wa Deus Mtege mkuu wa gereza la Kimondo lililoko Arusha.Usiku huo huo wa jana uchunguzi ulianza na jeshi la polisi lilifanikiwa kupata ushahidi mwingine mzito wa jambo hili ukiwahusisha Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo pamoja na mkuu wa jeshi la magereza hapa nchini.Hawa wawili wanaonekana kushirikiana na Mathew Mulumbi kwa karibu sana na kuna kila dalili kwamba walishiriki katika kupanga mauaji ya Deus Mtege.Tayari wamekwisha itwa hapa katika ofisi yangu na tunaendelea kuwahoji.Kwa ufupi tu hapo ndipo tulipofika mheshimiwa Rais” akasema DCI David Chamwino.
“Ahsante DCI kwa maelezo hayo lakini Dr Fabian ni mtu mkubwa,ni rais mstaafu hivyo lazima mjiridhishe na uhusika wake kabla ya kumuhusisha na jambo hili na kuharibu sifa yake nzuri.Hata kama hahusiki na chochote lakini kitendo cha kumuita mstaafu huyu na kumuhoji kuhusiana na suala la Mathew Mulumbi tayari wananchi watajua lazima ana uhusiano nalo.Nataka maelezo tafadhali kama kweli mlijiridhisha vya kutosha kuhusu uhusika wake” akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais” akasema DCI “Tumepata ushahidi ambao tunaufanyia kazi na kuna kila dalili kwamba wakubwa hawa walihusika kwa namna Fulani katika sakata lile hasa katika kupanga mauaji ya Deus”
“Unaweza ukaniambia ni ushahidi gani huo? Akauliza Festus
“Kuna video tumezipata ambazo zinaonyesha mienendo yote ya Rais mstaafu kwa siku ya jana.Asubuhi ya jana akiwa ameambatana na Mathew Mulumbi walifika katika makao makuu ya magereza wakaonana na Kamishna Chambao na muda mfupi baada ya wao kuondoka Kamishna Chambao akaondoka akaenda uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akapanda helkopta akaelekea Arusha na baadae alirejea Dar es salaam akiwa na Deus Mtege na moja kwa moja wakaenda nyumbani kwake.Baadae Dr Fabian na Mathew walifika nyumbani kwa Kamishna Chambao.Hawakukaa sana wakaondoka wote na kwenda nyumbani kwa Mathew Mulumbi ambako ndiko mwili wa Deus ulikutwa.Mheshimiwa Rais tayari tumeanza kuwahoji DrFabian na Kamishna Chambao lakini kuna mambo wamejichanganya hivyo kutushawishi tuwahoji zaidi na kuwafanyia uchunguzi wa kina.Inaonekana kuna jambo wanalifahamu kuhusiana na mauaji ya Deus.Tutaendelea kuwashikilia kwa mahojiano zaidi” akasema David
“Sawa DCI nimekuelewa lakini naomba mjiridhishe kwa kina kama kweli wazee hao wanahusika na jambo hili vinginevyo tutakuwa tumewadhalilisha sana” akasema Rais Festus
“Tutafanya hivyo mheshimiwa Rais.” akajibu David na Rais Festus akakata simu
Festus akatoa kitambaa mfukoni na kujifuta jasho.
“Mhh ! Ruby hili suala ni zito sana.Uliponieleza nilidhani ni jambo jepesi lakini kwa sasa ninauona uzito wake” akasema Rais Festus
“Yale yote uliyonieleza ndiyo ambayo amenieleza DCI. Kwa mujibu wa maelezo yake anadai tayari wamewaita Dr Fabian na Kamishna Chambao wanaendelea kuwahoji.Anadai wamepata ushahidi mzito unaowahusisha Dr Fabian na kamishna Chambao katika kile anachodaiwa kukifanya Mathew Mulumbi.Wana ushahidi wa video
zinazowaonyesha Dr Fabian na Mathew Mulumbi katika mizunguko mbali mbali ya siku ya jana.Anadai wanayo video ikiwaonyesha Dr Fabian na Mathew wakiwasili katika ofisi ya Kamishna Chambao na hadi Chambao alivyoondoka kwenda Arusha akarejea akiwa na Deus na mwisho ni pale ambapo wote watatu,Dr Fabian,kamishna Chambao na
Mathew Mulumbi wakiwa na Deus wakiingia katika nyumba ya Mathew ambako ndiko Deus alikutwa ameuawa.Haya aliyoyazungumza yanafanana na maelezo yale uliyonipa” akasema Rais Festus
“Yote aliyokwambia ni kweli mtupu.Kumbe walikuwa wanawafuatilia kila wanachokifanya na kuwarekodi ili kutengeneza ushahidi.Mheshimiwa Rais nadhani kwa haya uliyoyapata kutoka kwa DCI umenielewa vyema kile nilichokueleza”
“Ruby nimekuelewa vyema sasa.Hawa watu ni mashetani wakubwa.Tusipofanya kitu Dr Fabian na wenzake watakuwa katika mataizo makubwa sana.Nini unashauri kifanyike? Akauliza rais Festus
“Mheshimiwa Rais,mtu wa kwanza ambaye tunapaswa kuhakikisha anapatikana kwa siku ya leo ni Mathew Mulumbi”
“Kwa nini awe Mathew peke yake? Akauliza Rais Festus
“Mathew Mulumbi ndiye anayelichunguza suala hili.Tukifanikiwa kumpata yeye ndiye atakayehakikisha anaendelea kuwasaka hawa watu na kuwafahamu ni akina nani kwa kuwa tayari kuna mwanga anao.Ni Mathew Mulumbi pekee mwenye uwezo wa kuwatafuta hawa jamaa na kujua kile wanachokificha” akasema
Ruby
“Ruby nakuliana na ushauri wako lakini tatizo ni kwamba Mathew Mulumbi yuko mikononi mwa jeshi la polisi hivi sasa wakimuhoji na baadae watampeleka mahakamani.Ninashindwa kuuona mwanya wowote ambao unaweza ukatusaidia tuweze kumpata.Ruby ninashindwa nifanye nini”
“Mheshimiwa Rais
hatupaswi kusubiri hadi Mathew Mulumbi akafikishwa mahakamani.We have to get him today ! akasema Ruby
“How?! Akauliza Rais Festus
“Mheshimiwa Rais hatuna namna nyingine ya kuweza kumpata Mathew kwa haraka zaidi ya kutumia nguvu kumchukua”
“Ruby wewe umeshakuwa
mkurugenzi wa idara nyesti kabisa SNSA unafahamu mbinu nyingi.Kama kuna mbinu ambayo unadhani inaweza ikatumika kumpata Mathew Mulumbi kwa haraka nieleze tafadhali lakini si matumizi ya nguvu” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais hakuna mbinu nyingine zaidi ya kuvamia na kumchukua Mathew” akasema Ruby na sura ya Rais Festus ikabadilika
“Unataka tuvamie kituo cha polisi? Siwezi kuruhusu hilo lifanyike.Ni jambo baya kabisa ambalo linaweza kupelekea umwagikaji mkubwa wa damu.Kituo cha polisi ni sehemu nyeti kabisa ambako hapatakiwi kwa namna yoyote ile kuchezewa ! akasema Festus
“Mheshimiwa Rais sikumaanisha kuvamia kituo cha polisi.Ninaheshimu kituo cha polisi na siwezi kukushauri tuvamie kituo cha polisi na kumchukua Mathew”
“Sasa unashauri tuvamie wapi na kumchukua Mathew?Mahala alipo ni kituo cha polisi” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais ushauri wangu ni huu.Zungumza na mkuu wa jeshi la polisi na umpe maelekezo kwamba Mathew Mulumbi asilale kituo cha polisi leo hii bali ahamishiwe katika gereza la Uwangwa akakae huko mahala ambako kuna ulinzi mkali.Sisi tutajipanga na kuuvamia msafara huo wakati akipelekwa gereza la Uwangwa kisha tutamchukua Mathew Mulumbi.Mheshimwia Rais hii ndiyo njia pekee ambayo tunaweza kuitumia kumpata Mathew Mulumbi siku ya leo.Tukimkosa siku ya leo tutakuwa tumeshindwa kila kitu” akasema Ruby
“Ruby njia hii inaweza ikasababisha damu kumwagika na wanaoweza wakapoteza maisha kama
tukitumia njia hii ni askari polisi.Bado tunarudi pale pale kwamba sitaki kuwadhuru askari polisi kwa namna yoyote ile ili kumuokoa
Mathew Mulumbi! Akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais katika kulifanikisha jambo hili hatuwezi kukwepa umwagikaji wa damu.Wale watakaopoteza maisha damu yao haitakuwa imepotea bure bali watakuwa wameimwaga damu yao kwa ajili kuwasaidia ndugu zao ambao wanaangamizwa kila uchao na hawa maharamia.Tutahakikisha damu zao hazipotei bure mheshimiwa Rais”
“Ruby unanipa wakati mgumu sana ! akasema Festus
“Mheshimiwa Rais huu ni wakati ambao unapaswa kufanya maamuzi magumu.Watu hawa lazima tuwafahamu ni akina nani kwani mambo wanayoyafanya yanaogopesha.Kama wameweza kutumia laini za
simu bila kuzisajili,kama wameweza kufanikiwa kumuingiza mtu gerezani ambaye si mfungwa,kama wanaweza kumpandikizia kesi mbaya hata ya mauaji mtu yeyote Yule basi watu hawa ni hatari mno na wanaweza wakafanya kitu chochote.Watu hawa wanawafahamu watu wote wanaowachunguza na nina uhakika hata mimi ninafuatiliwa na yawezekana wanafahamu kama nimekuja hapa ikulu na kama wakilifahamu hilo hata wewe tayari utakuwa umeingia matatizoni na wanaweza wakaanzisha vita na wewe mheshimiwa Rais.Tunatakiwa kufanya kila linalowezekana kumpata Mathew Mulumbi ambaye ana uwezo mkubwa wa kuwatafuta na kuwapata hawa jamaa” akasema Ruby
“Why Mathew Mulumbi?
Hatuwezi kupata watu wengine ambao wanaweza wakawasaka hawa watu? Akauliza Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
Mathew Mulumbi tayari amekwisha piga hatua kubwa katika kuwafahamu watu hawa na tayari kuna mwanga anao ndiyo maana ninashauri kwamba tumtumie yeye katika kuwasaka hawa watu”
“Ninasema hivyo kwa
sababu sitaki tuingie katika umwagaji wa damu kwa sababu ya mtu mmoja.Tunaweza tukaunda timu ya watu kadhaa na Mathew Mulumbi anaweza akaisaidia timu hiyo kwa kuwapa mwangaza wa namna ya kuweza kuwapata hawa jamaa.Kwa njia hiyo tutakwepa kumwaga damu.Timu hiyo itafanya kazi
na pale ukweli ukibainika Mathew na wenzake ambao watakuwa wameshikiliwa watakuwa huru” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais ushauri wako si mbaya lakini kwa suala hili bado naendelea kusisitiza lazima tumpate Mathew Mulumbi tena leo.Ninamfahamu vyema,ninaufahamu umahiri wake na uwezo wake katika kushughulika na mambo kama haya.Mathew Mulumbi ndiye anayeweza akafanya kazi kwa haraka na kufanikisha kuwatoa wengine katika kitanzi” akasema Ruby na Rais Festus akazama mawazoni
“Endapo tutaamua
kufanya kama ulivyoshauri unao watu ambao unaweza ukashirikiana nao? Lazima tupate watu ambao wanaweza wakaifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani kama
likitokea kosa lolote basi tutakuwa tumeshindwa vibaya sana” akasema Rais Festus “Tutatumia makomando wa kitengo cha siri cha usalama wa taifa SNSA”
“Unataka kuwashirikisha SNSA katika jambo hili? Akauliza Rais Festus
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ninawafahamu timu ya makomando wa SNSA
nimefanya nao kazi mbali mbali wana uwezo mkubwa na ni pekee ambao wanaweza wakaifanya misheni hii”
“Sijapenda kuwashirikisha watu wengi katika jambo hili kwa kuhofia taarifa kuvuja na sisi sote tukaingia matatizoni.Hebu jaribu kujenga picha ndogo tu endapo jambo hili likashindwa kufanikiwa au hata
likifanikiwa halafu taarifa zikavuja kwamba na mimi nimeshiriki kwa kulibariki lifanyike unadhani nani ambaye atakuwa katika matatizo makubwa?Ni wazi mimi ndiye nitakayekalia kiti cha moto na ninaweza hata kuondolewa madarakani ndiyo maana ninataka kama tukilifanya jambo hili basi lifanyike kwa umakini mkubwa sana” akasema Rais Festus “Mheshimiwa
Rais,nakuomba usiwe na hofu yoyote.Ninachokuomba niunganishe na mkurugenzi wa SNSA na kila kitu kitakwenda vizuri.Kwa pamoja tutaandaa misheni kabambe kabisa na hadi kufika jioni ya leo tutakuwa tumempata Mathew Mulumbi” akasema Ruby
“Ruby haya ni maamuzi yangu ya kwanza magumu kuyafanya tangu nimekalia kiti hiki na ninalazimika kufanya haya kwa ajili ya kumsaidia Dr
Fabian.Sitaki mzee Yule achafuliwe jina lake kwani amefanya mengi mazuri kwa nchi hii na vile vile ni yeye aliyesimama hadi nikafika hapa” akasema Rais Festus na kunyamaza kidogo
“Ruby tufanye kama ulivyoshauri.Tumuokoe Mathew Mulumbi” akasema Festus na kuchukua simu akampigia Zarina Faheem mkurugenzi wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi SNSA.
“Mheshimiwa Rais” akasema Zarina
“Zarina nakuomba hapa ikulu mara moja” akasema Festus
“Sawa mheshimiwa Rais! Akajibu Zarina Rais Festus akakata simu akamgeukia Ruby
“Ruby kuna kitu ninakifikiria.Kama tukifanikiwa kumpata Mathew Mulumbi tutakuwa tumeanzisha vita kubwa na hawa jamaa lazima watahakikisha kwa namna yoyote ile wanampata na kumuua kwani tayari amekwisha kuwa mtu hatari kwao.Kama wakijua na mimi nimeshiriki katika kumtorosha Mathew wanaweza wakaanza kunichimba maisha yangu ya nyuma na wanaweza wakapata mambo yangu ya huko nyuma na kuyaanika kwa watu ili kunichafua au hata kuniondoa madarakani”akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais kuna kitu chochote ambacho unadhani hawa jamaa wakikipata wanaweza wakakitumia katika kukuchafua na kinaweza kukuletea matatizo katika nafasi yako ya urais? Kama kuna kitu chochote naomba uwe muwazi tafadhali ili tuweze kutafuta namna ya kukishughulikia angali mapema” akasema Ruby na
Rais Festus akafikiri kwa muda akasema
“Hapana hakuna tatizo
lolote”
“Good” akasema Ruby
“Wakati tunamsubiri
Zarina afike nadhani ungewasiliana na mkuu wa jeshi la polisi umpe maelekezo ya kuhakikisha siku ya leo Mathew anapelekwa gereza la Uwangwa akalale huko” akasema Ruby
“Hapana Ruby siwezi kuzungumza na IGP suala hili katika simu.Hawa watu nimewaogopa sana.Nitamuita hapa na nitazungmza naye kwa undani.Yawezekana usifurahishwe na maamuzi yangu lakini lazima tumshirikishe pia IGP”
“Do you trust him Mr
President? Akauliza Ruby
“I do.Ni mmoja wa watu wachache ninaowaamini sana” akasema Rais Festus
“Fine.Kama unamuamini hakuna tatizo lakini umuonye kwamba watu hawa si wa kawaida” akasema Ruby na Rais Festus akachukua simu yake ya mkononi akazitafuta namba za mkuu wa jeshi la polisi akampigia
“Shikamoo mheshimiwa Rais” akasema mkuu wa jeshi la polisi baada ya kupokea simu ya Rais
“Marahaba.IGP
ninakuhitaji hapa ikulu mara moja”
“Sawa mheshimiwa Rais ninakuja hapo muda si mrefu” akajibu IGP na Rais akakata simu
*************
Zarina Faheem
mkurugenzi wa SNSA aliwasili ikulu kama alivyotakiwa na Rais.
“Ouh Ruby! Akasema
Zarina kwa furaha baada ya kumkuta Ruby akiwa na Rais.Hakutegemea kabisa
“Zarina ! akasema Ruby wakakumbatiana
“Ni muda sasa hatujaonana.Gosh you look like an angel ! akasema Zarina
“Okay ladies mtapata nafasi baadae ya kuzungumza kwa sasa tujielekeze katika kilichotukutanisha hapa” akasema Rais Festus
“Zarina ninashukuru umefika kwa haraka.Naamini tayari umekwisha pata taarifa za kile kilichotokea usiku wa kuamkia leo”
“Kuna mengi yametokea usiku wa kuamkia leo mheshimiwa Rais”
“Ni kuhusiana na Mathew Mulumbi”
“Ouh Mulumbi yule
bilionea wa dawa za kulevya nimekwisha sikia taarifa zake.Nimesikitishwa sana kwa kitendo alichokifanya.Kwa mtu mwenye hadhi kama yake hakupaswa kabisa kufanya yale aliyoyafanya” akasema
Zarina
“He didn’t do it ! akasema Ruby na Zarina akamtazama kwa mshangao
“Sikiliza Zarina,Mathew Mulumbi hakufanya hayo anayotuhumiwa kuyafanya.Ni jambo ambalo limetengenezwa kwa umakini mkubwa kumchafua na kumpoteza kabisa.Ruby atakueleza kwa kirefu zaidi kuhusiana na jambo hilo lakini nimekuita hapa kwa ajili ya kukupa maelekezo muhimu” akasema
Rais Festus
“Nakusikiliza mheshimiwa Rais”
“Leo kuna misheni nzito na ya muhimu ambayo nataka ifanyike.Tunakwenda kumteka Mathew Mulumbi kwa kuwatumia makomando wa SNSA”
“Oh my gosh ! akasema
Zarina akionyesha mshangao
“Hivi sasa Mathew yuko katika kituo cha kati cha polisi akifanyiwa mahojiano na baadae leo atahamishiwa katika gereza la
Uwangwa.Wakati akipelekwa gerezani makomando watavamia msafara na kumteka.Maelekezo yote atakupa Ruby hivyo nataka uongozane naye hadi SNSA mkajipange vema namna ya kuitekeleza misheni hiyo lakini narudia tena kutoa angalizo kwamba sitaki makosa yoyote yafanyike.Misheni hii ikishindwa kufanikiwa sisi sote tutaingia matatizoni na hasa mimi ndiye nitakayekuwa katika matatizo makubwa sana hivyo nataka umakini mkubwa mno wakati mnatekeleza misheni hii.Naamini mmenielewa” akasema Rais Festus
“Tumekuelewa
mheshimiwa Rais usihofu” akajibu Ruby
“Ahsante sasa mnaweza
kwenda kujipanga kwa ajili ya misheni hiyo na mimi nitaendelea kuwasiliana nanyi kuwapa taarifa zaidi.Kitu kingine ambacho nataka kuwaasa suala hili ni nyeti sana hivyo walifahamu watu wachache” akasema Rais Festus na kusimama akiashiria kumalizika kwa kikao kile “Mheshimiwa Rais
tafadhali hakikisha wanangu wanakuwa salama” akasema Ruby naye akisimama
“Usihofu Ruby.Hapa wako salama” akajibu Rais na akina Ruby wakaondoka kuelekea katika gari la Zarina
“Ruby what’s going on? Akauliza Zarina wakielekea katika gari
“Zari kuna jambo kubwa sana linaendelea hivi sasa ndiyo maana umenikuta hapa
ikulu”
“Linahusiana na Mathew Mulumbi?
“Ndiyo.Nitakueleza kila kitu lakini kwa sasa tuelekee katika kambi ya makomando wa SNSA” akasema Ruby wakaingia garini na Zarina akamuelekeza dereva waelekee katika kambi ya makomando wa SNSA
Wakiwa njiani Ruby akautumia muda huo akamueleza Zarina kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
“Mhh ! hata mimi nimeingiwa na woga.Watu hawa ni akina nani? Akasema Zarina baada ya Ruby kumueleza kila kitu kuhusiana na wale watu wanaowatafuta
“Mpaka sasa hawajulikani lakini tunachokifahamu ni mtandao wa watu wenye nguvu na uwezo wa kufanya chochote”
“Sasa nimeelewa kwa nini
Rais alisisitiza jambo hili lifanyike kwa siri bila ya watu wengi kulifahamu.Ana hofu yawezekana hata ndani ya SNSA watu hao wakawa wamejipenyeza na wakaweka watu wao”
“Inawezekana” akasema Ruby
“Nilipopata taarifa za Mathew Mulumbi kukamatwa akijihusisha na dawa za kulevya pia mauaji nilishangaa sana.Sijawahi kuonana na Mathew ana kwa ana lakini kwa taarifa ninazozisikia kuhusu yeye anaonekana ni mtu ambaye hawezi akajihusisha na mambo kama haya kwani anao utajiri wa kutosha.Nafsi yangu ilisita kabisa kuamini taarifa hizo” akasema Zarina huku safari ikiendelea.
Waliwasili katika kambi ya makomando wa SNSA ambao walifurahi kumuona tena mkuu wao wa zamani Ruby lakini walishangazwa na ujio wake pale.Bila kupoteza muda Zari akawakusanya makomando wale katika chumba maalum
“Habari za asubuhi makamanda.Naamini mnajiuliza maswali mengi kwa kumuona Ruby mahala hapa.Kwa ufupi tu ni kwamba Ruby yuko hapa kikazi.Ni muda mrefu hakujajitokeza kazi nzito hivyo leo tunakwenda kazini” akasema Zari na kunyamaza halafu akamkaribisha Ruby azungumze na makomando wale
“Nimefurahi kuonana nanyi tena ndugu zangu.Nilijitenga nanyi kwa muda lakini mimi bado ni mwenzu na hapa ni nyumbani muda wowote tunarejea na leo nimekuja kuonana nanyi kuna misheni muhimu ambayo tunakwenda kuitekeleza” akasema Ruby na kunyamaza akaunganisha kompyuta yake na luninga iliyokuwa ukutani mbele ya kile chumba halafu akaitafuta picha ya Mathew Mulumbi.
“Anaitwa Mathew
Mulumbi.Wengi wenu naamini mnamfahamu kwa sababu tumekwisha fanya naye kazi kadhaa wakati nikiwa mkurugenzi”akanyamaza akawatazama wale makomando waliokuwa kimya
wakimsikiliza
“Usiku wa leo Mathew amekamatwa nyumbani kwake akituhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na pia imekutwa miili miwili ya watu ndani ya nyumba yake ambao wanadaiwa kuuawa na Mathew.Kwa hivi sasa Mathew Mulumbi anashikiliwa katika kituo cha kati cha polisi.Ukweli ni kwamba Mathew hajafanya mauaji hayo na wala hajihusishi na dawa za kulevya.Huu ni mchezo umechezwa na watu hatari sana ambao Mathew alikuwa anawachunguza.Misheni yetu ya leo ni kumteka nyara” akanyamaza tena na kuwatazama makomando ambao hawakuonyesha hata chembe ya mstuko
“Labda kwa ufupi tu ni kwamba Mathew Mulumbi hajafanya hayo anayotuhumiwa kuyafanya bali kuna watu ambao wamemuangushia mzigo huu mzito kwa lengo la kuvuruga uchuguzi aliokuwa anaufanya dhidi yao.Watu hao ni makini na hatari na mpaka sasa kila aliyejaribu kuwachunguza ameishia kuuawa au kutengenezewa kesi.Mnakumkumbuka Gosu gosu ambaye tulifanya naye kazi SNSA naye pia ni mmoja wa waathirika wa hawa jamaa.Gosu Gosu alikuwa na mahusiano na mwanamke mwandishi wa habari aliyekuwa anawachunguza hawa jamaa na kilichotokea mwanamke huyo akauawa na Gosu Gosu akaangushiwa kesi kwamba ndiye aliyemuua na akafungwa maisha gerezani.Mathew naye alishika kijiti na kuanza kuwasaka hawa jamaa lakini naye ametengenezewa kesi ya dawa za kulevya na mauaji.Si
Mathew pekee aliyekumbwa na upepo wa hawa jamaa bali hata mume wangu Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo naye vile vile anatuhumiwa kushirikiana na Mathew katika biashara hiyo ya dawa za kulevya na mauaji.Misheni yetu ya leo ni kumteka Mathew Mulumbi”Ruby akanyamaza kwa muda
“Misheni imekaa namna hii.Mathew Mulumbi atatolewa katika kituo cha kati cha polisi na kupelekwa katika gereza la Uwangwa.Sisi tutakuwa tumejipanga tayari tukisubiri taarifa na tutaufuata msafara huo.Mara tu baada ya kulivuka daraja la Nyerere ndipo kila kitu kitakapofanyika” akasema Ruby kisha wote wakasogelea katika ramani kubwa ya jiji la Dar es salaam wakaanza kujadiliana namna ya kuitekeleza misheni ile. *************
Mkuu wa jeshi la polisi
Inspekta Jenerali Yeremia Mwaipopo aliwasili ikulu kama alivyotakiwa na Rais.
“Karibu sana IGP nimefurahi umefika kwa haraka” akasema Rais Festus
“Uliponipigia simu nilikuwa karibu na maeneo haya mheshimiwa Rais”
“Awali ya yote nataka kufahamu mahala mlikofikia katika suala la Yule mfanya biashara anayetuhumiwa kujihusisha na biashara dawa za kulevya na mauaji aliyekamatwa jana usiku”
“Mheshimiwa Rais tunaendelea kumuhoji kuufahamu mtandao wake wote na mpaka sasa kuna watu ambao tayari tunawashikilia kwa mahojiano na wengine tunawatafuta.Ambao tunawashikilia hadi hivi sasa ni Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo na mwingine ni Kamishna jenerali wa magereza Chambao Mnenge.Baada ya kumaliza mahojiano na kupata taarifa kamili nitakujulisha mheshimiwa Rais” akasema mkuu wa jeshi la polisi
“IGP nimeamua nikuite hapa kuna jambo muhimu sana ninataka tuzungumze na sikutaka tuzungumze simuni kwani hizi simu haziaminiki siku hizi” akasema Rais Festus
“Ni kweli mheshimiwa Rais simu zimekuwa hazina usiri” akajibu IGP
“IGP ninafahamu wewe ni mshirika wangu na ni mmoja
wa watu ninaowaamini sana katika serikali”
“Nalifahamu hilo mheshmiwa Rais na ninashukuru kwa kuniamini”
“Kubwa ambalo
nimekuitia hapa ni hili suala la Mathew Mulumbi”
“Ndiyo mheshimiwa Rais”
“Mathew Mulumbi ni mmoja wa majasusi nguli kabisa kuwahi kutokea hapa nchini.Ameshiriki katika misheni kadhaa kubwa na katika misheni zote amezimaliza kwa mafanikio makubwa.Amekuwa ni kinara wa kupambana na magaidi na mara ya mwisho aliipandisha Tanzania katika ramani ya dunia kwa kile alichokifanya nchini Marekani.Kutokana na kazi yake hiyo Mathew amejitengenezea maadui wengi ndani na nje ya
nchi.Tukio la jana la kukamatwa akiwa na mzigo wa dawa za kulevya pamoja na mauaji ni la kutengenezwa na wabaya wake lakini Mathew hajahusika na mambo hayo na wala hahusiki katika mauaji ya watu waliokutwa wameuawa ndani mwake” akasema Rais
Festus
“Mheshimiwa rais,mzigo wa kilo zaidi ya mia moja hamsini umekutwa katika chumba chake cha kulala pamoja na miili ya watu wawili ikiwa katika mojawapo ya chumba ndani ya nyumba yake .Sis….” IGP akanyamaza baada ya Rais Festus kumkatisha
“Nalifahamu hilo IGP lakini nakuhakikishia kwamaba Mathew Mulumbi hakufaya hayo huu ni mzigo ameangushiwa ili kumpoteza” akasema Rais na kumpa IGP maelezo ya kina kuhusiana na suala lile la Mathew Mulumbi “Mheshimiwa Rais hili suala linaonekana ni kubwa zaidi ya
tunavyolitazama.Sikufahamu kumbe kuna jambo zito nyuma ya tukio lile” akasema IGP
“Ndiyo maana nikakuita hapa tuzungumze ana kwa ana.Hili suala ni kubwa na tunatakiwa kuchukua hatua za haraka sana kuwafahamu watu hawa ni akina nani na kitu gani wanakificha kisijulikane.Bila kuchukua hatua za haraka Mathew na Dr Fabian tutawapoteza na watu hawa wataendelea kufanya maovu hapa nchini.Dr Fabian amelitumikia taifa kwa uadilifu mkubwa sana na sasa wanataka kumchafua kwamba anajihusisha na dawa za kulevya ndiyo maana wametengeneza ushahidi unaotosha kabisa kumuunganisha na Mathew”
“Mheshimiwa Rais tukiwaacha watu hawa wanaweza wakaleta hatari kubwa sana kwa nchi.Kama wana uwezo wa kumtengenezea mtu kesi mbaya ya mauaji na akafungwa gerezani watu hawa ni genge baya kabisa na wanatakiwa wasakwe haraka kabla hawajaleta madhara makubwa.Hawa ni wachache tu waliofahamika kuuawa lakini ni vipi ambao hatuwafahamu? Yawezekana kuna watu wengi tu wamekwisha uawa na hatuna taarifa.Yawezekana kuna watu wengi wako magerezani kama huyo jamaa Gosu Gosu kwa kesi za kutengenezwa.Kuna uovu mkubwa unafanywa na hawa jamaa bila kujulikana” akasema IGP huku sura yake ikiwa tayari imejikunja kwa hasira.
“Ahsante kwa kunielewa IGP sasa kuna jambo moja ambalo nataka lifanyike”
“Ndiyo mkuu”
“Mathew Mulumbi tayari amekwisha anza uchunguzi wa kuwatafuta hawa watu na tayari kuna hatua amekwisha piga hivyo hatuwezi kumuacha aende gerezani kwani kwa kufanya hivyo tutashindwa kuwapata hawa watu na lengo lao ni kuhakikisha Mathew anakwenda gerezani na huko watapanga mipango ya kumuua ili kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayekuwa hatari kwao.Ninataka Mathew Mulumbi atekwe ” akasema Rais Festus.IGP akavuta pumzi ndefu halafu akasema
“Samahani mheshimiwa
Rais sijakuelewa hapo”
“Mpaka sasa nchi nzima tayari wanafahamu kuwa Mathew Mulumbi anajihusisha na dawa za kulevya hivyo basi ninataka atekwe kutoka katika mikono ya polisi ili akaendelee na uchunguzi wake kuhusianana na hawa watu.Bila Mathew hatutaweza kuwapata hawa watu”
“Mheshimiwa Rais hili suala naona lina ugumu kidogo”
“Usihofu IGP ugumu upo lakini hatuna namna ya kufanya zaidi ya kumchukua Mathew kutoka katika mikono ya polisi.Mpango uko hivi Mathew ataondolewa kutoka katika kituo cha kati cha polisi na kupelekwa katika gereza la Uwangwa.Njiani watavamiwa na Mathew atachukuliwa.Kuna kikosi maalum ambacho tayari kimeandaliwa kwa kazi hiyo na kwa kuwa tayari imekwisha fahamika kwamba Mathew anajihusisha na dawa za kulevya kila mtu ataamini kwamba waliofanya tukio hilo la kumteka ni wenzake wanaojihusisha na dawa za kulevya.Umenielewa IGP?
“Nimekuelewa mheshimiwa Rais”
“Good.Ninataka
ulishugulikie hilo.Ninataka maandalizi ya kumuhamisha Mathew Mulumbi kuelekea gereza la Uwangwa yaanze mara moja ukitoka hapa na ninataka taarifa zote za jambo hilo kuanzia idadi ya askari na njia watakayopita na hata silaha watakuwa nazo ngapi na za aina gani” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais
utanisamehe lakini katika jambo hili yataibuka mapambano kati ya askari na hao watu walioandaliwa kuvamia msafara na ninaweza kuwapoteza askari wangu ! “Hatuwezi kukwepa damu kumwagika katika jambo hili.Lazima wapo askari wetu watakaopoteza maisha yao lakini nakuhakikishia IGP kwamba damu yao haitapotea bure” akasema Rais Festus na majadiliano yakaendelea kisha wakaagana IGP akaondoka kwa ajili ya kwenda kutekeleza maagizo ya Rais.
Baada ya IGP kuondoka,Rais akampigia simu Ruby
“Mheshimiwa Rais” akasema Ruby
“Ruby nimekupigia kukujulisha kwamba tayari nimezungumza na IGP na nimempa maelekezo ya kufanya na hivi tuzungumzavyo amekwenda
kuyatekeleza.Atanijulisha kila kitu nami nitawajulisha.Vipi mmejiandaaje huko?
“Tumejiandaa vizuri mheshiwa Rais.Tayari nimekwisha zungumza na makomando kuhusiana na kile wanachokwenda kukifanya na tayari maandalizi yameanza” “Very good.Ruby narudia kukusisitiza kwamba umakini mkubwa unatakiwa katika misheni hii na makomando hao wajaribu kwa kila watakavyoweza kuepuka kumwaga damu kama hakuna ulazima” akasema Rais Festus
*************
Saa kumi na dakika ishirini,Mathew Mulumbi akiwa amefungwa pingu mikononi alitolewa ndani ya kituo cha kati cha polisi na kuingizwa katika gari la polisi tayari kwa kupelekwa katika gereza la Uwangwa.Waandishi wa habari waliokuwa wamepiga kambi kituoni hapo kufuatilia kile kilichokuwa kinaendelea walijitahidi kuchukua picha mbali mbali za tukio lile na wengi walihitaji kuipata picha ya Mathew Mulumbi wakati akitolewa mle kituoni.
Mathew aliingizwa katika gari maalum la kubebea wafungwa hasa wale hatari akaingizwa katika chumba kilichotengenezwa kwa vyuma vigumu.Mkono wake wa kulia ukafungwa katika pingu maalum iliyokuwamo mle ndani halikadhalika miguu nayo ikafungwa na pingu zenye mnyororo kisha chumba kikafungwa kwa kufuli halafu mlango mkubwa wa nyuma ukafungwa .Bado waandishi wa habari waliokuwepo lile eneo waliendelea kuchukua
picha za tukio lile la Mathew Mulumbi kuhamishwa kutoka kituo cha polisi kwenda katika gereza la Uwangwa.
Taratibu zote zilikamilika na msafara ukaondoka pale kituoni kuelekea gereza la Uwangwa chini ya ulinzi mkali.Ilitangulia piki piki ya polisi kwa ajili ya kusafisha njia halafu likafuata gari la polisi lililokuwa na askari nane
nyuma yake likafuata gari maalum alimo Mathew Mulumbi na mwisho kukawa
na gari lenye askari sita wenye silaha.Mkuu wa jeshi la polisi nchini Yeremia Mwaipopo alikuwepo kushuhudia Mathew Mulumbi akihamishwa
“Karibu wote ni askari vijana sana.Maskini hawajui nini kinakwenda kutokea huko mbele,wengi wao kama si wote wanaweza wakapoteza maisha.Inaniumiza sana lakini hakuna namna nyingine ya kuwasaidia lazima nitekeleze maagizo ya mkuu wangu” akawaza IGP Yeremia na kurejea ndani halafu akamtumia ujumbe Rais Festus na kumjulisha kwamba tayari safari imeanza. *************
“Upo msemo umezoeleka
kwamba steringi hauawi lakini kwa picha hili steringi ameuawa na picha imefika mwisho”akawaza Mathew Mulumbi akiwa ndani gari akipelekwa katika gereza la Uwangwa.
“Jamaa wameniwahi sikutegemea kabisa.Nimekutana na watu wengi hatari lakini hawa jamaa nimewavulia kofia.Ni watu wabaya zaidi ya nilivyofikiri.Wako mbele zaidi yetu.Wanajua kila tunachokifanya na wanatumia
kila njia kuhakikisha hatuwi kikwazo kwao.Wanafahamu wanachokifanya na wanakifanya bila woga.Ni akina nani watu hawa?Kitu gani wanakificha kisijulikane? Wanatumia gharama kubwa kujificha nahisi lazima jambo wanalolificha ni kubwa pia.Nasikitika sana yamenikuta haya kabla sijawafahamu.Tayari nilikwisha anza kupata mwanga lakini jamaa walikuwa mbele yangu kuhakikisha kwamba hawajulikani na wakaniingiza katika kesi hii
mbaya.Wamemuua Victor mtu ambaye nimeishi naye kwa muda mrefu kama ndugu.Wameniumiza sana” akawaza Mathew akiwa garini.
“Hii ni kashfa kubwa sana imenikumba.Mathew
Mulumbi eti ninajihusisha na dawa za kulevya.Mpaka muda huu taarifa zimekwisha sambaa nchi nzima kwamba nimekamatwa na dawa za kulevya.Mzigo ule wa dawa za kulevya uliokamatwa chumbani kwangu ni wa gharama kubwa sana kilo zaidi ya miamoja na hamsini ni pesa nyingi lakini jamaa hawakujali gharama walichokuwa wanakitaka wao ni kunitoa katika picha na wamefanikiwa.Ninapaswa kujilaumu mimi mwenyewe kwa kutochukua tahadhari ya kutosha kwani nilifahamu ninawatafuta watu hatari lakini sikuweka tahadhari ya kutosha.Kingine kinachoniumiza zaidi ni kwamba tayari nimewaweka akina Ruby katika hatari kubwa.Hawa jamaa lazima watakuwa wanafahamu kuwa ninashirikiana nao katika kuwatafuta hivyo lazima nao watakuwa katika hatari.Vile vile Gosu Gosu nani atamsaidia kuweza kutoka gerezani? Kweli picha limekwisha vibaya” akaendelea kuwaza Mathew
Magari yalikwenda kwa
kasi huku piki piki ikitangulia na kuweka magari pembeni ili kuyapisha magari yale ya polisi yapite.
Magari yalifika katika daraja la Nyerere na kuvuka kwa kasi kubwa
“Ni nani anaweza akaendeleza uchunguzi hapa nilipoishia mimi? Kuna mwangaza nimeupata na laiti ningeweza kumpata mtu kama Nawal angeweza kulishughuliia jambo hili kwa kushirikiana na Ruby.Sifahamu alipo Nawal wala sina mawasiliano yake.Hii ina maana kwamba hawa jamaa hawatajulikana? Oh Mungu wangu ! Akawaza Mathew na kutikisa kichwa akasikitika
“Sijawahi kukata tamaa katika maisha yangu lakini safari hii sina ujanja.Mbio zangu zimefika ukingoni.Unahitajika muujiza wa enzi zile za manabii wa kweli kuchomoka katika jambo hili.Pamoja na kugonga ukingoni lazima nifikirie namna ya kuliendeleza suala hili.Siwezi kukubali kubeba mzigo mzito namna hii bila faida y….!! Ghafla kikasikika kishindo kikubwa na gari likayumba Mathew akajigonga katika chuma.Gari likayumba mara ya pili na kuanguka chini likabiringika mara mbili kutokana na mwendo wa kasi llilokuwa linakwenda.Mathew alisikia kwa mbali milio ya risasi halafu taratibu macho yake yakaanza kupoteza nuru akapoteza fahamu
Mlango wa nyuma wa lile gari ukafunguliwa haraka haraka wakaingia watu wawili wakiwa wamevaa mavazi meusi na kufunika sura
zao.Mmoja wao akachomoa bastora na kulipiga risasi kufuli lililofunga mlango wa kile chumba alimokuwamo Mathew .Watu wale wakaufungua mlango na kwa haraka pingu alizofungwa Mathew zikafunguliwa akatolewa nje akiwa hana fahamu na sehemu mbali mbali za mwili wake zikivuja damu.
Magari mawili ya polisi yalikuwa yanawaka moto na askari polisi wakiwa wamelala barabarani wakionekana hawana uhai.Watu wenye bunduki nzito wakiwa wamezifunika nyuso zao walilizunguka eneo lile na mara ikatokea helkopta yenye rangi nyeupe ikashuka chini kidogo na kamba nzito ikashushwa mmoja wa wale jamaa akajifunga kiunoni na kumfunga Mathew kisha helkopta ikaanza kupaa huku kamba ile ikivutwa ndani ya helkopta kwa kutumia mashine ya kuvutia.Wale jamaa wengine ambao wote walikuwa wamezifunika sura zao zisionekane wakaingia katika magari yao na kuondoka kwa haraka eneo lile.
Taarifa za tukio lililotokea Kigamboni mbele kidogo baada ya kuvuka daraja la Nyerere zilianza kusambaa kwa kasi kubwa.Gari la polisi lililojaa askari wakitokea katika kituo kikubwa cha polisi wilaya ya Kigamboni liliwasili eneo la tukio muda mfupi baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mmoja wa askari aliyejeruhiwa.Haraka haraka zoezi la kuwatafuta askari waliojeruhiwa likaanza wakapakiwa katika gari na kukimbizwa hospitali.Gari nyingine nne zilizojaza askari ziliwasili eneo la tukio na haraka Daraja la Nyerere likafungwa kwa muda .Hakuna gari lililoruhusiwa kupita tena zaidi ya magari ya askari ukaguzi mkali ukaanza.
Akiwa ofisini kwake,Rais Festus alipokea taarifa ya kushambuliwa kwa askari
polisi waliokuwa wanamuhamisha mtuhumiwa wa dawa za kulevya na mauaji kutoka kituo cha polisi kumpeleka katika gereza la Uwangwa Kigamboni. “Mungu atusaidie katika jambo hili tusijekuwa tumemwaga damu za vijana wetu bure” akawaza Rais Festus halafu akampigia simu Ruby
“Ruby tayari nimepata taarifa muda mfupi uliopita kwamba shambulio limetekelezwa na Mathew ametoroshwa.Kuna taarifa gani huko kwenu?
“Mheshimiwa Rais tunashukuru sana kwa msaada wako mkubwa.Mambo yamekwenda vizuri kama tulivyopanga na hivi sasa makomando wetu wako njiani
wakirejea kambini.Tumetaarifiwa Mathew amepata majeraha kufuatia gari alilokuwa amepanda kupinduka na amepoteza fahamu lakini atakapofika tutafahamu ni majeraha ya ukubwa gani aliyoyapata” akasema Ruby
“Ruby nataka nirudie tena kukusisitiza kwamba tumefanya maamuzi haya
magumu na kumwaga damu ya
vijana wetu kwa ajili ya
kumuokoa Mathew.Naomba tafadhali damu ya vijana hawa isipotee bure.Nataka Mathew Mulumbi afanye kila awezalo kuhakikisha anawapata hao watu aliokuwa anawatafuta.Nitasikitika sana kama atashindwa kuwapata watu hao” akasema Rais Festus
“Mheshimiwa Rais nakuhakikishia kwamba watu hao watapatikana lakini haitakuwa rahisi kwani baada ya kugundua kwamba Mathew hayuko tena katika mikono ya dola lazima wataingiwa na hofu kubwa na watafanya kila wawezalo kuhakikisha Mathew hawi kikwazo kwao.Pamoja na ugumu utakaokuwepo mheshimiwa Rais nakuhakikishia kwamba tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha watu hawa wanapatikana”akasema Ruby
“Nashukuru kwa
kunihakikishia hilo Ruby”
“Jambo lingine mheshimiwa Rais nataka kufahamu kuhusu hatima ya Fabian.Je ataendelewa kushikiliwa na polisi? “Fabian bado ataendelea kuhojiwa na jeshi la polisi.Ni Mathew Mulumbi pekee ambaye anaweza akawasaidia yeye na mwenzake Kamishna Chambao hivyo hakikisha unamuhimiza kufanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuwapata hao watu na kuwasafisha DrFabian na Chambao”akasema Rais Festus
“Naomba mheshimiwa
Rais uendelee kuhakikisha wanangu wanakuwa salama muda wote.Kwa sasa nitapotea kidogo sintakupigia simu hadi pale nitakapokuwa na shida kubwa zaidi nikihitaji msaada wako” akasema Ruby na kuagana na Rais Festus
***********
Helkopta ya makomando
wa SNSA ilitua taratibu katika sehemu yake ndani ya kambi ya makomando wa idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.Ruby,Zari na mkuu wa kikosi kile walikuwa wamesimama karibu na eneo lile tayari kwa kumpokea Mathew Mulumbi.Ruby alikuwa ameiweka mikono yake kifuani akionekana kuwa na hofu huku nywele zake ndefu zikipeperuishwa na upepo mkali kutoka katika helkopta.Walikuwepo pia madaktari wawili walioitwa na
Zarina kutoka ofisi kuu ya SNSA kwa ajili ya kuwahudumia wale ambao watakuwa wamejeruhiwa katika misheni hiyo
Mlango wa helkopta ukafunguliwa wakashuka makomando wanne halafu wakashusha kitanda alichokuwa amelazwa Mathew ambaye alikuwa ameumia sehemu mbali mbali za mwili pale gari lilipoanguka.Uso wake ulikuwa umechafuka damu kufuatia jeraha alilokuwa amelipata usoni lililokuwa linamwaga damu nyingi.
Ruby akawafuata makomando wale na alipomuona Mathew machozi yakamtoka.
“Mathew ! akaita lakini makomando wale hawakumpa nafasi wakamkimbiza Mathew ndani hadi katika chumba maalum ambako walianza kumpatia huduma na kumganga majeraha aliyokuwa ameyapata.Wakati Mathew akiendelea kupatiwa huduma makomando wengine walianza zoezi la kubandua karatasi zilizokuwa zimebandikwa katika helkopta ile na kuifanya ionekane ni ya rangi nyeupe wakati rangi yake halisi ni nyeusi.
Dakika chache baadae,makomando waliokuwa katika magari nao wakawasili,Ruby na Zari wakawapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya halafu kiongozi wa misheni ile akaenda na akina Ruby pamoja na mkuu wa makomando akawapa
taarifa za namna misheni ile ilivyofanyika.Baada ya kikao
kile kifupi Ruby na Zari wakaenda katika chumba alimokuwa anahudumiwa Mathew.Tayari alikwisha gangwa majeraha aliyoyapata lakini hakuwa amerejewa na fahamu. Ruby akamfuata pale kitandani akamkumbatia na kumwaga machozi
“Ouh Mathew jamani ! siamini kama umetoka katika mkono ya dola” akasema huku akimwaga machozi.Akainua kichwa na kumtazama Mathew halafu akambusu shavuni
“Ruby ! akaita Zarina na Ruby akastuka akainuka na kufuta machozi wakatoka ndani ya kile chumba
“Zari tunatakiwa kuanza maandalizi mara moja ili Mathew atakapozinduka akute kila kitu kipo tayari na misheni iendelee.Ofisi kuu ya misheni hii itakuwa hapa katika kambi ya makomando ambako naamini ni sehemu salama sana.Mimi na Mathew wote tutakaa hapa hadi pale tutakapokuwa tumeikamilisha misheni hii”
“Are you sure? Akauliza
Zari
“Ndiyo Zari”
“Vipi kuhusu Dr Fabian? Atakubali ukae hapa?
“Usihofu kuhusu
Fabian.Hapa tuko vitani hivyo hakuna tatizo” akasema Ruby ukapita muda kidogo halafu Zarina akasema
“Ruby kuna kitu nataka kuuliza na utanisamehe” “Usijali uliza”
“Wewe na Mathew Mulumbi,kuna chochote kinaendelea kati yenu? Akauliza
“Kwa nini umeuliza?
“Niliona namna ulivyomkumbatia Mathew mle chumbani nikahisi yawezekana kuna kitu kinaendelea” akasema Zarina
“Zari siwezi kukuficha kitu mimi na Mathew tumewahi kuwa wapenzi huko nyuma lakini tuliachana ndipo nikaolewa na Dr Fabian” akajibu Ruby na ukimya mfupi ukapita
“Do you still love him?akauliza Zarina
“Haina umuhimu
tena.Mimi naye kwa sasa ni marafiki tu”
“Answer the question
Ruby.Do you still love him? Akauliza Zarina
“Yes I do.Mathew alikuwa ni mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote na nilikuwa tayari hata kuutoa uhai wangu kwa ajili yake lakini hiyo ilikuwa zamani kwa sasa tayari nina maisha mengine.Nina familia ninayoipenda sana na hata yeye amekwisha endelea na maisha yake”akajibu Ruby
“Dr Fabian anafahamu kama wewe na Mathew mmeshawahi kuwa na mahusiano huko siku za nyuma? Zarina akauliza “Anafahamu” akajibu Ruby
“Anachukuliaje kuhusu wewe kufanya kazi kwa ukaribu na Mathew?
“Ni jambo gumu sana kwake.Anafahamu bado ninampenda Mathew lakini hana namna ya kunizuia
nisifanye kazi na
Mathew.Nimekwisha muhakikishia kwamba hata kama bado ninampenda Mathew lakini hakuna chochote kitachotokea kati yetu kwani nafahamu nimeolewa na ninamuheshimu hivyo siwezi kwa namna yoyote ile kumsaliti.Mathew na Gosu Gosu ni ndugu zangu,sisi ni familia moja hivyo kunapotokea tatizo kwa mmoja wetu siwezi kushindwa kusaidia kama ninao uwezo ndiyo maana unaniona hapa” akasema Ruby
“Ahsante Ruby kwa majibu hayo mazuri.Lakini bado kuna kitu ninataka kukifahamu kuhusu wewe na Mathew.Ilikuaje mkaachana halafu bado mnaendelea kuwa na ukaribu mkubwa namna hii?
“Ni hadithi ndefu kidogo lakini ukweli ni kwamba hatukuachana bali Mathew ndiye aliyenitaka niendelee na maisha yangu kwa kuhofia nikiwa naye hataweza kunipa ile furaha ya maisha ninayoitaka.Maisha ya Mathew yamejaa misuko suko mingi hivyo hakutaka maisha yangu yawe katika hatari ndiyo maana akanitaka nitafute mwanaume atakayenipa furaha ya maisha na wakati huo tayari Dr Fabian alikwisha onyesha dalili za kunipenda hivyo nikaamua kuolewa naye”
“Dr Fabian do you love him? Akauliza Zarina
“Yes I do.Nilikubali kuolewa naye akiwa bado ana nafasi ndogo sana ndani ya moyo wangu ambao nafasi yote aliichukua Mathew lakini
nilijitahidi kujifunza kumpenda Dr Fabian na hadi sasa ninampenda sana.Ananijali na kunithamini”
“Are you happy? Akauliza
Zarina
“Zari is this an interrogation or what? Akauliza Ruby na Zari akacheka
“Ruby ninajaribu kujifunza kutoka kwako namna ulivyoweza kupitia vikwazo katika mahusiano lakini ukaweza kuhimili na mpaka sasa una furaha.Mimi kwa sasa ninapitia kipindi kigumu sana katika mahusiano yangu ya kimahusiano” akasema Zarina na kuinamisha kichwa
“Mambo gani unayapitia
Zari? Kama unaweza ukafunguka ninaweza kukusaidia hata mawazo” akasema Zari
“Mpenzi wangu ambaye tumekuwa na mahusiano tangu tukiwa wanafunzi wa sekondari amebadilika siku hizi na kuna kila dalili kwamba muda wowote mahusiano yetu yatafikia mwisho” “Nini tatizo?
“Mtoto”
“Mtoto?! Ruby akashangaa “Ndiyo.Mpenzi wangu
anataka mtoto ndipo tufunge ndoa”
“Kwani kuna ugumu
wowote Zari? Mzalie mtoto kama anavyotaka ili kuokoa penzi lenu.Mmetoka mbali na suala kama la mtoto lisiwatenganishe” akasema Ruby
“Ruby kuna tatizo.Sina uwezo wa kuzaa.Tumezunguka kwa madaktari wengi lakini imeshindikana.Nimetumia dawa za kila namna imeshindikana ndipo mwenzangu alipoamua kutafuta mwanamke mwingine na kumpa mimba.Hivi tuongeavyo tuna miezi miwili hatujaonana.Suala hili linanila akili yangu sana Ruby nashindwa nifanye nini.Kuna wakati niliingiwa na mawazo hata ya kumuua huyo mwanamke lakini nikaondoa wazo hilo kwani Yule mwanamke hana makosa yoyote.Ruby kuna wakati ninajiwa na mawazo mabaya sana na ninahofu siku moja ninaweza kufanya jambo baya hadi watu wakanishangaa” akasema Zarina
“Pole sana Zari.Mambo kama haya yanawatokea wanawake wengi siku hizi na si wewe peke yako.Kumekuwa na wimbi kubwa la wanawake kukosa uwezo wa kubeba mimba siku hizi lakini hii si sababu ya kukufanya unyanyasike wala kukufanya uchukue maamuzi mabaya ambayo hayana faida kwako.Naomba nikueleze ukweli Zarina.Mwanaume huyo hakupendi kama anavyodai.Kama kweli angekuwa na mapenzi ya dhati kwako angekubaliana na hali uliyonayo na nyote mkamshukuru Mungu kwani ndiye mwenye kupanga kila kitu.Imekuwa ni tabia ya wanaume siku hizi kutangaza ndoa pale anapoona mwanamke tayari ni mjamzito.Hiki si kitu kizuri hata kidogo.Je wanawake ambao hawana uwezo wa kubeba mimba hawana haki ya kuolewa? Hili jambo linawakumba wanawake wengi.Ninachoweza kukushauri usishughulike naye endelea na maisha yako na yeye muache aendelee na maisha yake kwani alichokuwa anakitafuta kwako ni mtoto tu.Usiache kumuomba Mungu na ninakuhakikishia kwamba siku moja utampata mwanaume ambaye atakuwa tayari kukuoa hata kama huna uwezo wa kumzalia watoto” akasema Ruby
“Ahsante Ruby kwa ushauri wako.Kidogo ninajiona nimeutua mzigo mzito niliokuwa nimeubeba” akasema Zarina
“Ni kweli ni mzigo mzito sana na ni jambo linaloumiza
mno kwa mwanamke kukosa mtoto lakini inaumiza zaidi pale suala hilo linapogeuka kuwa fimbo ya kukuadhibu.Sahau kuhusu wanaume na jielekeze katika kazi.By the way kuna mchungaji mmoja ametangaza neema kwa wanawake wote ambao hawana waume kwamba kuna upepo sijui unaitwaje utavuma na kuwaleta wanaume kwa wanawake wote ambao bado hawajaolewa na wanahitaji wanaume wa kuwaoa.Yawezekana na wewe ukapitiwa na upepo huo na ukabahatika” akasema Ruby na Zaria akaangua kicheko kikubwa hadi machozi yakamtoka
“Ahsante Ruby kwa kunichekesha.Ni muda mrefu sijacheka namna hii”
“Kitu gani kimekufurahisha namna hiyo?
“Ni hao wanaume
watakaoletwa na upepo ! akasema Zarina na kuangua tena kicheko
“Cheka tu wakati wenzako wanapata wanaume huko ! akasema Ruby naye akicheka
“Ruby unaamini katika mambo hayo?
“Kwa Mungu kila kitu kinawezekana” akasema Ruby
“I believe in God too lakini hili la wanaume kuletwa na upepo limenifurahisha sana.Yawezekana hata huyu wa kwangu aliletwa na kimbunga ndiyo maan….” Akanyamaza Zarina baada ya mmoja wa madaktari kutokea “Mathew amezinduka” akasema Yule daktari
“Ahsante Mungu” akasema Ruby huku akinyanyuka wakatembea haraka kwenda katika chumba alimo Mathew wakaingia na kumkuta Mathew tayari amekwisha rejewa na fahamu
“Mathew ! akasema Ruby kwa furaha na Mathew akapatwa namshangao mkubwa.Hakuamini kumuona
Ruby mahala pale
“Ruby ! akasema Mathew Ruby akamfuata akamkumbatia
“Ee Mungu nitakulipa nini kwa jambo hili kubwa ! akasema Ruby huku macho yake yakilengwa machozi
“Kweli huu ni muujiza mkubwa sana.Sikutegemea kama ningekuona tena Ruby.I thought….I though ….oh my God ! Mathew akashindwa kuendelea na kumkumbatia Ruby kwa nguvu.
“Tell me if this is real !
akasema Mathew
“It’s real Mathew.You are free” akasema Ruby na Mathew machozi ya furaha yakamtoka
“Thank you Ruby.Sikutegemea kabisa.Nakumbuka mara ya mwisho gari lilipoanguka
nilisikia milio ya risasi nikajua jamaa wamekuja kunimaliza kabisa”akasema Mathew
“It was us.Ni sisi tulifanya misheni ile na kukutoa katika mikono ya polisi.You are safe now Mathew” akasema Ruby “Ahsante sana Ruby.Sina cha kukulipa” akasema Mathew
“Mathew for you I can move the mountain.I think you know that” akasema Ruby
“Ouh that’s so sweet” akawaza Zarina aliyekuwa amesimama pembeni akiwatazama
“Watu hawa bado wanapendana sana” akawaza Zarina baada ya Mathew na Ruby kukumbatiana tena. “Mathew kutana na Zarina Faheem.Huyu ndiye mkurugenzi wa sasa wa SNSA.Ndiye aliyechukua nafasi yangu” Ruby akafanya utambulisho
“Hellow Mathew
Mulumbi.Nimefurahi kuonana nawe” akasema Zarina na kumpa Mathew mkono.
“Hello Zari.Hata mimi nimefurahi kukutana nawe.Ahsanteni sana nyote kwa hiki mlichokifanya.Sikutegemea.H apa niko wapi?
“Hapa uko katika kambi ya makomando wa SNSA ni sehemu pakee ambako utakuwa salama kwa sasa”
“No ! I need to go somewhere else.I have my reasons”akasema Mathew
“Mathew hapa ni sehemu ambako tunaamini utakuwa salama zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote” akasema Ruby
“Nalifahamu hilo Ruby lakini sitaki kuwepo hapa.Kama hamuwezi kunitafutia sehemu salama zaidi basi nitatafuta mwenyewe mahala nitakapoona panafaa”
“Mathew don’t be sturbon ! akasema Ruby
“Ni vipi kama tukimpeleka nyumbani kwangu?Ni sehemu salama ninaishi mwenyewe na kuna mfumo mzuri wa ulinzi” akasema Zarina
“Are you sure? Ruby akauliza
“Hakuna tatizo tunaweza kuhamishia ofisi pale nyumbani kwangu”Zarina akashauri
Mathew akaelezwa wazo
lile la Zarina akalikubali kisha maandalizi ya kumuhamisha kumpeleka nyumbani kwa Zarina yakaanza
MWAKA MMOJA ULIOPITA
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Bendera za nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) zilipepea katika jengo ambako unafanyika mkutano wa kilele wa jumuiya hiyo.Jumla ya marais kumi na tano kutoka nchi kumi na sita wanachama wa jumuiya hiyo ya SADC tayari walikwisha
wasili jijini Dar es salaam kuhudhuria mkutano huo ambapo nchi ya Tanzania ilitarajiwa kuchukua uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja.Kabla ya mkutano huo wa marais,kulitanguliwa na mikutano kadhaa ya utangulizi
na washiriki zaidi ya elfu mbili walihudhuria maonyesho ya bidhaa za viwandani kutoka katika nchi wanachama
Rais Festus Mayungulu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndiye aliyeufungua mkutano huo wa kilele na katika hotuba yale aliyoitoa baada ya kukabidhiwa uenyekiti alieleza mambo mengi ambayo Tanzania ingeyafanya katika mwaka mmoja ikiwa kama mwenyekiti
na miongoni mwa mambo
aliyoyasisitiza ni kuhusiana na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya. “Waheshimiwa viongozi siwezi kumalizia hotuba yangu bila kuzungumzia biashara ya dawa za kulevya” akasema Rais Festus na ukumbi ukapiga makofi
“Ndugu zangu marais na wote mnaohudhuria mkutano huu,kwa miaka ya hivi karibuni sote tumeshuhudia kukua na kustawi kwa biashara ya dawa za kulevya katika ukanda wetu wa SADC ,katika bara zima la Afrika na dunia kwa ujumla.Kumekuwa na juhudi mbali mbali zinazofanyika duniani kukabiliana na biashara hii ya dawa za kulevya lakini juhudi hizi zimekuwa zikikabiliana na ugumu kwani wafanya biashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakibuni na kubadili mbinu za usafirishaji kila uchao.
Bara la Afrika limekuwa ni njia ya kupitishia dawa za kulevya kutoka kwa wazalishaji kwenda katika masoko makubwa ambayo ni nchi za Ulaya na Asia.Taarifa zinaonyesha kwamba kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya Cocaine kilipitishwa katika nchi za Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kwenda bara la Ulaya.Nchi za
ukanda wa SADC zimekuwa pia ni njia kuu ya kupitisha dawa za kulevya hasa Heroin kutoka katika nchi za Asia.Licha ya juhudi mbali mbali ambazo zimekuwa zinafanywa na nchi zetu kupambana na kudhibiti
biashara hii lakini mtandao
wake umekuwa ukipanuka siku hadi siku na vijana wetu wengi kuvutiwa na biashara hiyo kwa tamaa ya kupata utajiri wa haraka haraka na ndiyo maana wamekuwa wakikubali kubeba na kusafirisha dawa hizo wakiwa wamezificha matumboni mwao
n.k.Takwimu za dawa zilizokamatwa zinatisha na kutufanya tujiulize maswali je tunafanya juhudi za kutosha kukabiliana na biashara hii inayoendelea kushika kasi kama moto wa nyika? Akauliza Rais Festus akanyamaza kidogo halafu akasema
“Ndugu zangu jibu la swali hili ni kwamba bado hatujachukua hatua za kutosha kudhibiti biashara hii na ndiyo maana imeendelea kustawi.Wote tunafahamu kwamba wanaoendesha
biashara hii si watu wadogo.Ni matajiri wakubwa na wengine ni viongozi wa serikali hivyo kufanya vita hii iwe ngumu zaidi na katika baadhi ya nchi japo
wanawafahamu wanaohusika
na biashara hii lakini wameshindwa kuwachukulia hatua kutokana na watu hao ama kuwa na ukaribu na viongozi wakuu wa nchi hizo,au kuwa na nyadhifa kubwa serikalini au ni watu wenye uwezo mkubwa kifedha na kuheshimika katika jamii zetu
Ndugu marais,wageni waalikwa mabibi na mabwana awali nilitaja kwamba Afrika limekuwa ni lango la kuingizia na kusafirishia dawa za kulevya kwenda katika masoko makubwa ya Ulaya na Asia.Dawa hivi zinapopita katika nchi zetu si zote zinapelekwa nje ya bara letu bali kiasi hubaki kwa ajili ya soko la Afrika ambalo limeendelea kukua kwa kasi kubwa.Wafanya biashara hawa wamekuwa wakiwalenga watu wa kipato cha kati hasa vijana na kuwaingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na zipo taarifa kwamba wakati mwingine wafanya biashara hawa wamekuwa wakigawa
dawa hizi bure zikiwa katika mfumo wa pipi kwa wanafunzi wa shule ili kuanza kuwazoesha kutumia dawa hizi kwa madhumuni ya kukuza soko lao.
Ndugu zangu marais,mabibi na mabwana sisi ambao tumepewa dhamana ya kuwaongoza watu wetu tunapaswa kuhakikisha tunachukua hatua kali na za haraka ili kuokoa kizazi chetu kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya.Kama hali ilivyo sasa ikiachwa iendelee ,miaka kumi ijayo mataifa yetu yatajikuta yakiwa na upungufu mkubwa wa nguvu kazi kwani asilimia kubwa ya vijana ambao ndiyo nguvu kazi watakuwa wamejiigiza katika matumizi ya dawa za kulevya na kama sote tunavyoelewa mtu ambaye amejiingiza katika matumizi ya dawa hizi uwezo wake wa kufanya kazi hupungua au kushindwa kabisa kufanya kazi.Muda wote hufikiria kupata pesa ya kununua dawa za kulevya na kuwafanya wengi wao kutumbukia katika uhalifu.Mtumiaji wa dawa hizi anaweza hata kumuua mzazi wake ili kupata fedha za kununulia madawa hayo.Waheshimiwa viongozi wenzangu kama tusipochukua hatua kali sasa,miaka kumi ijayo bara la Arika halitakuwa sehemu salama ya kuishi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa dawa za kulevya ambao watakuwa wamejiingiza katika uhalifu mkubwa.Kama hilo litatokea tunaopaswa kulaumiwa ni sisi viongozi wa sasa ambao hatuoyeshi kuchukua hatua madhubuti za udhibiti wa biashara hii na simfundishi Mungu kazi lakini ninasema wazi tutastahili adhabu kali pale tutakapoaga dunia hii kwa kushindwa kuwakinga watoto wetu dhidi ya madawa ya kulevya wakati kila kitu kipo katika mikono yetu” akasema kwa msisitizo Rais Festus na kupigiwa makofi mengi
Nataka niwaambie ndugu marais na wote mliohudhuria mkutano huu kwamba sisi Tanzania kama mwenyekiti wa jumuiya hii ya SADC tayari tunao mkakati mzito na tumedhamiria kutumia kila nguvu na uwezo tulio nao katika kuhakikisha tunalimaliza jambo hili la dawa za kulevya katika ardhi yetu.Nawahakikishia tena ndugu zangu tumeamua na hatuna mchezo katika hili.Hii ni vita kama vita nyingine kwani wafanya biashara hawa ni wauaji,hawana huruma hata kidogo hivyo na sisi tumejipanga vyema hatutakuwa na huruma na yeyote anayejihusisha na bishara hii.Baadhi ya wafanya biashara hao wana makundi makubwa
yanayomiliki silaha kali hivyo na sisi tumejipanga kutumia silaha kali zaidi yao kukabiliana nao.
Ndugu zangu narudia tena kuwahakikishia kwamba sisi Tanzania tumedhamiria kuingia vitani dhidi ya watu hawa lakini vita hii haitakuwa na maana au haitaleta matokeo mazuri kama nchi nyingine za SADC hazitachukua hatua za makusudi kabisa za kukabiliana na biashara hii haramu.Tunayo orodha ya wafanya biashara wakubwa katika kila nchi ndani ya SADC na nitamkabidhi kila rais orodha ya wafanya biashara wa dawa za kulevya walio katika nchi yake kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka.Vita hii tutashinda kama nchi zote za ukanda wa SADC tutasimama pamoja.Watanzania tuna methali inasema kidole kimoja hakivunji chawa hivyo basi nahimiza ushirikiano mkubwa na katika kipindi chetu cha uongozi wa mwaka mmoja tutaweka msisitizo mkubwa sana katika suala hilo na kuifanya iwe ni ajenda ya kudumu katika SADC.
Hiyo ilikuwa sehemu ya hotuba ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Festus Mayungulu aliyoitoa katika mkutano mkuu wa SADC
uliofanyika jijini Dar es salaam ambapo nchi ya Tanzania ilikabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.
CAPE TOWN – AFRIKA
KUSINI
Ndege ya kifahari aina ya Airbus A-318 ilitua katika uwanja mkubwa wa ndege ulio katika shamba kubwa la
Zabibu nje kidogo ya jiji la Cape town linalomilikiwa na bilionea Roberto Zullo raia Afrika kusini mwenye asili ya Italia.Kati kati ya shamba hilo kulikuwa na kiwanda kikubwa cha kutengeneza mvinyo wa zabibu uliojizolea umaarufu mkubwa katika nchi za Ulaya.
Mlango wa ndege ukafunguliwa ngazi ikashushwa halafu wakashuka walinzi wanne na kusimama pembeni ya ngazi na baada ya dakika tano mfanyabiashara mkubwa wa dawa za kulevya nchini Mexico bilionea Juan Castillo akashuka akiwa ameongozana na mke wake pamoja na walinzi saba.Roberto Zullo na mke wake Martina Durante wakasogelea ndege ile kuwapokea wageni wao.Juan na Roberto wakasalimiana kwa furaha halafu kila mmoja akamsalimu mke wa mwenzake.Roberto na mke wake wakawaongoza Juan na mkewe kuelekea ndani ya jumba lao kubwa la kifahari.
Dakika kumi na tano baada ya Juan Castillo kuwasili ndege nyingine aina ya Gulfstream G550 ikatua katika uwanja ule akashuka Nabii Kasiano Muyenzi kutoka Tanzania akiwa ameongozana na msichana mmoja mwenye umbo dogo lakini mrembo sana.Roberto na mke wake waliwapokea Kasiano na msichana aliyeongozana naye wakawakaribisha sebuleni ambako waliwakuta Juan Castillo na mke wake.Ilikuwa ni furaha tupu pale sebuleni kwa Juan kuonana na Benard.Dakika chache baadae helkopta ikatua na akashuka bilionea Bandile Dlamini akitokea katika jiji la Pretoria naye akiwa ameongozana na mke wake.Roberto akawapokea na kuwakaribisha ndani .Baada ya kusalimiana Roberto akawakaribisha wageni wake katika sehemu ya
juu ya jumba lake la kifahari kulikokuwa kumeandaliwa chakula maalum kwa ajili yao.Walipata chakula huku wakiendelea na mazungumzo mbali mbali kwani ni muda mrefu hawakuwa wameonana ana kwa ana.Baada ya chakula kila mmoja akapelekwa katika chumba alichokuwa ameandaliwa kwa mapumziko.Wakati wengine wakipumzika,Roberto alimuomba Kasiano wazungumze kidogo
“Nimefurahi tumeonana
Kasiano,habari za Tanzania? Akauliza Roberto
“Tanzania kwema
kabisa,vipi huku mnaendeleaje?
“Sisi tunaendelea vyema pia.Nimeshangaa kidogo kutokumuona shemeji Rita.kwa nini hujaongozana naye?
Kasiano akatabasamu kidogo halafu akasema
“Sijaweza kuambatana na Rita kwa sababu kuna kongamano kubwa la wanawake kuanzia kesho ambalo anatakiwa kuhudhuria”akasema
“Huyu uliyekuja naye ni binti yako? Hongera una binti mrembo sana”Akasema Robert na wote wakacheka
“Anaitwa Zoe Watwila.Si binti yangu” akasema Kasiano na Roberto akapatwa na mshangao
“Una maanisha….”
Roberto akataka kusema kitu Kasiano akamkatisha kwa kutikisa kichwa.Roberto akampa mkono wa pongezi
“Hongera nakupongeza Kasiano wewe huwa hufanyi makosa unapochagua.Mtoto Yule ana uzuri wa ajabu kabisa”
“Ni mtoto wa mchungaji wa kanisa langu na mimi ndiye
ninayemgharamia masomo
yake katika shule ya kimataifa hivyo kila pale ninapohitaji mtu wa kunituliza akili yangu
Zoe huwa karibu” akasema Kasiano
“Kasiano utanisamehe kwa hili nitakalokwambia lakini kwa uzuri wa huyu mtoto jina hilo la Zoe halimfai.Mtafutie jina lingine litakaloendana na uzuri wake” akasema Roberto na kuwasha sigara kubwa akavuta mikupuo kadhaa halafu akasema
“Nimekumbuka kitu.Zoe amefanana japo si sana na
Yule mwanamitindo wa
Marekani Naomi Campbell.Mbadilishe jina muite Naomi jina hilo litaendana na uzuri wake.Muite Naomi
Bambi.Bambi ni jina la
Kiitaliano linalomaanisha msichana mdogo” akasema Roberto na wote wakacheka “Kasiano mtunze sana huyu msichana kwani tunawahitaji sana wasichana wa namna hii katika biashara”
“Hilo ndilo dhumuni langu na ndiyo maana nimekuja naye hapa ili kuanza kumzoesha mazingira taratibu aweze kuwafahamu na kuwazoea marafiki zangu.Nataka kuanza kumuondoa katika maisha yale ya dini aliyokulia na kumfundisha maisha haya ya starehe naamini siku moja atakuwa mmoja wa watu wetu wazuri sana katika biashara” akasema Kasiano. “Ninashukuru Kasiano
kwa ufafanuzi huo ni hicho tu nilichokuwa nataka kukifahamu,nilikuwa najiuliza maswali mengi kuhusiana na Yule binti malaika.Sasa unaweza kwenda kuendelea kupumzika” akasema Roberto na Kasiano akarejea chumbani kwake ambako alimkuta Zoe akiwa kitandani amejilaza akiwa amevalia nguo za ndani zenye rangi nyeupe.Kasiano akahisi mwili wote ukimsisimka baada ya kumkuta Zoe akiwa katika mavazi yale
“Zoe unajua sana
kuivuruga akili yangu !
akasema Kasiano akimtazama Zoe kwa matamanio
“Mbona unanitazama hivyo? Njoo mpenzi nakusubiri” akasema Zoe kwa sauti laini na Kasiano akavua nguo haraka haraka na kupanda kitandani ambako ilipigwa mechi ya haraka haraka ambayo ilimuacha hoi nabii Kasiano
“Zoe sijui nikwambie nini ujue namna ninavyokupenda.Maneno peke yake hayatoshi kueleza namna ulivyoingia na kujaa ndani ya moyo wangu.Ninakuahidi Zoe chochote utakachokitaka utakipata hata kama ukitaka nikununulie ndege mimi niko tayari” akasema Kasiano na Zoe akatoa kicheko kidogo
“Si masihara Zoe,nina maanisha ninachokisema.Chochote utakachokitaka hata kama ukitaka ndege nitakununulia kwani pesa kwangu si tatizo.Ninapesa kama mchanga” akasema Kasiano na Zoe akamkumbatia kwa furaha akammwagia mabusu
“Nina bahati sana kukupata baba askofu..” akasema Zoe na Kasiano akamkatisha
“Zoe mara nyingi nimekwisha kukataza kuniita majina hayo tukiwa faragha.Niite mpenzi au Kasian,au Kasiano inatosha”
“Sawa mpenzi” akajibu Zoe huku akimchezea chezea kifuani
“Mpenzi nimefurahi sana kuongozana nawe katika safari hii.Marafiki zako wakarimu sana lakini utawaambia mimi ni nani wako?akauliza Zoe na Kasiano akatoa kicheko kidogo halafu akainuka akenda mezani akamimina mvinyo katika glasi mbili na moja akampatia Zoe halafu wakagonganisha glasi
“Wewe ni ua la moyo wangu,wewe ni malaika wangu itoshe tu kusema kwamba wewe ni kila kitu kwangu na sioni aibu kukutambulisha hata mbele ya marafiki zangu kwamba wewe ni mpenzi wangu” akasema Kasiano na kumbusu Zoe
“Ninachokuomba Zoe ni
usiri.Jambo hili halipaswi kujulikana.Ninafikiria kukutafutia shule nje ya nchi nitajaribu kumshawishi baba yako akubali na nitakuwa nikikutembelea mara kwa mara huko” akasema Kasiano
“Nitafurahi sana mpenzi” akajibu Zoe
“Kuna jambo lingine nataka kukwambia” “Jambo gani? Akauliza Zoe huku akimtazama Kasiano kwa macho yake malegevu
“Nataka nikubadili jina lako”
“Unibadili jina?
“Ndiyo.Nataka nikufanye wa kimataifa zaidi jina hilo la Zoe si baya lakini nataka nikupe jina zuri zaidi ambalo kama utalipenda basi ndilo uakalokuwa unalitumia bila wazazi wako kufahamu”
“Jina gani unataka kunipatia?
“Naomi Bambi” akasema Kasiano na kumtazama Zoe huku akitabasamu “Unalipenda?
“Ndiyo ni jina zuri”
“Ahsante kwa kulipenda.Tutalizungumza zaidi jambo hilo kwa sasa tupumzike” akasema Kasiano ambaye alionekana kuchoka
Saa kumi na moja za jioni Roberto na wageni wake wakaelekea katika shamba la farasi kulikokuwa na farasi zaidi ya ishirini.Wageni wa Roberto walishuhudia mbio za farasi na michezo mbali mbali ya kutumia farasi.Kijua kilipozama wakarejea katika makazi ya Roberto huku kila mmoja akionekana kuwa na tabasamu usoni kwa burudani ile nzuri.
Chakula cha jioni kiliandaliwa katika bustani huku bendi maalum ya muziki wa mashambani ikitumbuiza muziki mzuri.Hawakuwa peke yao,Roberto alikuwa amewaalika baadhi ya marafiki zake wakajumuika katika chakula kile cha jioni alichokiandaa kwa heshima ya wageni wake.Mvinyo ghali kabisa ndio uliokuwa ukinyweka usiku ule uliokuwa wa kipekee kwa kila aliyekuwepo.Wanamuziki wale walijikuta wakioga noti kwa umahiri wao wa kuwaburudisha wageni kwa nyimbo mbali mbali.Ilipotimu saa saba za usiku wageni wakarejea vyumbani mwao kupumzika kujiandaa na siku inayofuata.
*****************
Saa nne za asubuhi Roberto na wageni wake wakajifungia katika chumba maalum kwa vikao.Ni chumba kilichotengenezwa kwa namna yake ili kukidhi vikao vya siri.Wanawake wao walikwenda kuzunguka sehemu mbali mbali za shamba lile kubwa la Zabibu
“Ndugu zangu nimefurahi sana kwa sote kukutana hapa siku ya leo.Japo tumekuwa tukiwasiliana kwa simu na hata kwa njia ya video lakini ni tofauti na kukutana na namna hii.Nimefurahi tumekutana sote na mkuu wetu Juan Castillo ambaye nilimuomba ahudhurie kikao hiki naye akakubali”Roberto akafungua kikao
Kikubwa nilichotaka tukutane hapa wote ni kuzungumzia masuala muhimu kuhusiana na biashara zetu.Ni vyema kila baada ya muda Fulani tukakutana kama hivi na kuzungumza changamoto mbali mbali tunazokutana nazo katika biashara zetu.Haya ni maelekezo kutoka kwa madam Bella kwamba tukutane na tutafute suluhu ya kukabiliana na vikwazo vinavyoendelea kuibuka katika biashara yetu” akasema Roberto na kunyamaza kidogo.
“Siku mbili zilizopita wakuu wa nchi 16 za jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) walikutana jijni Dar es salaam Tanzania katika mkutano mkuu wa jumuiya hiyo na Tanzania imepewa uenyekiti wa jumuiya kwa
mwaka mmoja.Yawezekana tayari mmefuatilia na kujua kilichoendelea katika mkutano
huo lakini kwa ufupi tu ni kwamba yamesainiwa maazimio kadhaa katika mkutano huo lakini maazimio hayo hayana athari zozote kwetu” akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“Kikubwa ambacho
kinatugusa katika mkutano huo ni hotuba aliyoitoa mwenyekiti mpya ambaye ni Rais wa Tanzania.Hotuba yake haikuwa mbaya lakini aliharibu hapa”akasema Roberto na kuwasha luninga kubwa iliyokuwamo mle ndani akacheza kipande cha hotuba ya Rais Festus Mayungulu aliyoitoa katika mkutano wa
SADC uliofanyika nchini Tanzania
“Hotuba hii ilitolewa kwa lugha ya kiswahili hivyo
naomba Kasiano utoe tafsri ili watu wote humu waweze kuelewa alichokizungumza Rais wa Tanzania” akasema Roberto na Kasiano akaanza kutoa tafsiri ya hotuba ile kwa lugha ya kiingereza.Ilipomalizika sehemu ile ya hotuba ya Rais Festus ambayo alizungumzia kuhusiana na vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya watu wote wakawa kimya wakitazamana
“Ahsante Kasiano kwa tafsiri naamini wote tumeielewa vizuri.Lakini mambo hayakuishia hapo.Walikutana tena faragha na kuendelea kulizungumzia zaidi suala hili na hapo ndipo Rais wa Tanzania alipowakabidhi maraisi wenzake orodha ya wafanya biashara wakubwa wa dawa za
kulevya katika kila nchi.Viongozi hawa wametangaza vita na hii si vita ndogo.Japokuwa si marais wote wako tayari kuingia katika vita hii kwani baadhi yao wanafaidika na biashara hii lakini kwa ushawishi wa serikali ya Tanzania ambayo ndiyo mwenyekiti wa jumuiya kwa sasa watalazimika kuungana katika hii vita hivyo ndugu zangu tuna kazi ya kufanya mbele yetu.Kama wao walivyotangaza vita na sisi lazima tuwe tayari kuingia vitani.Kila mbinu lazima itumike katika kutafuta ushindi wa hii vita.Kikao chetu hiki kijielekeze katika kutafuta jawabu namna tutakavyoweza kukabiliana na hii vita iliyotangazwa.Karibuni kwa mawazo” akasema Roberto
“Ninamfahamu huyu
Rais.Ni rais ambaye hana masihara katika kile
akisemacho.Kama ametangaza vita dhidi ya biashara hii ni wazi ni vita ya kweli hata kama hatapata uungwaji mkono kutoka kwa marais wengine lakini yeye ameapa kuwamaliza wafanya biashara wa dawa za kulevya nchini Tanzania.Tangu ameingia madarakani zaidi ya wafanya biashara mia moja na hamsini wakubwa wamekwisha kamatwa.Rais aliwataka wananchi kuwataja wafanya biashara wa dawa za kulevya na majina mengi yametajwa na yanafanyiwa uchunguzi na ndiyo sababu ya kuwakamata watu wote hao.Rais Festus ni mtu asiyeyumba katika msimamo wake hivyo ninauona ugumu wa hii vita aliyoitangaza” akasema Kasiano
“Ahsante Kasiano kwa kutupa picha pana ya Rais wa Tanzania.Pamoja na misimamo yake na dhamira yake ya kutaka kupambana na biashara hii,lakini hatupaswi kuingiwa na hofu.Yeye si wa kwanza kutangaza vita hii.Mataifa makubwa yenye nguvu kubwa,mbinu na teknoljia kushinda Tanzania yamekwisha tangaza vita lakini biashara hii imeendelea kushamiri kila uchao hivyo hatupaswi kutishwa na mtu mmoja au nchi moja kamaTanzania au nchi za ukanda huu wa SADC” akasema Roberto na kuwasha sigara yake kubwa
“Nimeanza biashara hii nikiwa na miaka kumi na sita” akasema Juan Castillo
“Niliacha shule kutokana na ufukara mkubwa katika familia yetu kiasi kwamba kuna wakati tulikosa hata mlo wa siku.Nimepitia mengi.Sikumbuki ni mara ngapi nimenusurika kuuawa lakini ni mara nyingi.Mwili wangu una makovu mengi ya risasi zilizotaka kunitoa uhai lakini mpaka leo hii niko hai na ninaendelea na biashara.Haikuwa rahisi
kufika hapa nilipofika na ninathubutu kusema kwamba ninaifahamu biashara hii kuliko ninyi nyote hivyo hii vita waliyoitangaza hawa marais ni kitu kidogo sana.Tumekuwa tukipambana na vikosi vya Marekani kwa miaka mingi na ndiyo maana niliamua kuja kuwekeza Afrika.Nchi za Afrika ndiyo kwanza zinaamka usingizini wakati tayari tumekwisha tengeneza mtandao mkubwa
ambao si rahisi kuusambaratisha.Nawahakikis hia ndugu zangu kwamba hii vita ni rahisi sana na wala hatupaswi kushika silaha kupigana” akasema Juan Castillo mmoja wa wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya
“Nchi hizi za SADC zinataka kuungana na kuendesha kwa pamoja mapambano dhidi ya dawa za kulevya,sisi tunachotakiwa kukifanya ni kuuvuruga umoja wao”
“Kivipi Juan? Akauliza Bandiel Dlamini ambaye ni mfanya biashara mkubwa wa dawa za kulevya nchini Afrika kusini.
“Kwa ajili ya biashara zetu tunaihitaji sana
Tanzania,Msumbiji na Afrika kusini.Hawa wote wako katika jumuiya ya SADC hivyo basi tunatakiwa kuleta mvurugano mkubwa katika jumuiya hii na kuwafanya washindwe kuzungumza lugha moja.Wakishindwa kuelewana miongoni mwa nchi wanachama hawataweza kutekeleza vita hii.Tuwajengee chuki raia wa nchi za SADC wachukiane wao kwa wao na wakati wakigombana sisi biashara zetu zitaendelea kama kawaida.Mpango wenyewe ni huu.Hapa Afrika kusini kuna raia kutoka karibu mataifa yote ya Afrika.Tunatakiwa kujenga chuki kati ya Raia wa Afrika kusini dhidi ya wageni na hatimaye wageni waanze kushambuliwa kuchomewa biashara na hata kuuawa.Zoezi hili litawahusu wale wageni wanaotoka nchi za afrika hasa za ukanda wa SADC.Raia wa kutoka nchi nyingine za Asia au Ulaya wasiguswe katika vurugu hizo.Mnalionaje wazo hilo? Akauliza Juan Castillo
“Ni wazo zuri sana hilo.Kweli wewe ni mkongwe katika hii biashara na unazifahamu mbinu nyingi zaidi yetu.Kwa upande wangu nadhani hiyo ni mbinu nzuri sana na ninaiunga mkono” akasema Roberto na wengine wote wakalikubali wazo la Juan Castillo.
“Nawashukuruni sana kwa kulikubali wazo langu.Roberto na Bandile ninyi kwa kuwa mko hapa Afrika kusini mnatakiwa kuanza kulitengenezea mikakati ya haraka jambo hili” akasema Juan
“Jambo hili linatakiwa kuanzia kwa wanasiasa.Wanasiasa wengi ninafahamiana nao na wengi wamekuwa wakinitegemea sana katika masuala ya kifedha kuendesha mambo yao ya kisiasa.Nitawatumia baadhi ya wanasiasa kuanza kupandikiza chuki miongoni mwa raia wa Afrika kusini kwamba wageni hasa wale wa kutoka mataifa ya Afrika wamekuja kuchukua ajira zao na hivyo mkakati wa kuwaondoa kwa kutumia nguvu utaanza.Naamini kampeni hii itafanikiwa sana.Pale watakapoanza kuuawa na biashara zao kuchomwa moto jumuiya ya kimataifa itapaaza sauti kulaani na nchi za kiafrika hazitabaki nyuma lazima zitalaani vitendo hivyo na itajengeka chuki dhidi ya raia wa Afrika kusini walioko katika nchi nyingine za bara la Afrika” akasema Roberto “Baada ya vurugu hizo kuanza nitapaaza sauti kulaani na kwa kuwa mimi ni mwenyekiti wa umoja wa viongozi wa dini Tanzania nitapaaza sauti na kuwataka viongozi wengine wa dini wapaaze sauti zao kulaani jambo hilo na kwa pamoja tutaitaka serikali kuwarejesha nyumbani raia wake walioko nchini Afrika kusini.Kama haitoshi nitakodisha ndege kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani raia wote wa Tanzania na kitendo hicho kitakuwa ni chanzo cha chuki kubwa kwa raia wa Afrika kusini.Mahusiano kati ya taifa na taifa yatapungua na kudhoofisha vita dhidi ya dawa za kulevya ambayo wamedhamiria kuifanya” akasema Kasiano Muyenzi
“Hii ndiyo faida ya kutengeneza mtandao mpana.Huwezi amini sisi hapa wachache lakini tumelishika bara la Afrika na tunaweza kufanya chochote” akasema Juan Castillo na wote wakagonganisha glasi.
“Kwa wale wote ambao mna mahusiano ya karibu na marais au viongozi wengine wakuu wa nchi hakikisheni zoezi litakapoanza basi mnayatumia vyema mahusiano hayo kuwashawishi waweze kuwaondoa raia wao nchini Afrika kusini na kujenga hasira kwa raia wao.Tukiligawa bara la Afrika tutaweza kulitawala vizuri na kuendesha biashara zetu bila matatizo yoyote” akasema
Roberto
“Kuna jambo lingine ambalo nataka kulifanya” akasema Juan Castillo
“Pamoja na kuleta mvurugano huo baina ya nchi za Afrika lakini lazima tujizatiti zaidi kuanzia sasa.Nina kundi langu linaitwa Black Mafia.Hawa nitawaleta wataweka kambi hapa Afrika kusini na Tanzania.Kasiano utawasimamia kwa upande wa Tanzania na kwa hapa Afrika kusini watakuwa chini ya Roberto.Kazi yao hawa jamaa ni kuhakikisha biashara inakwenda vyema na yeyote Yule ambaye ataonekana kuwa kikwazo kwetu basi tunamuondoa haraka sana.Hili kundi limenisaidia sana katika biashara zangu kwa upande wa Amerika.Ni watu waliopitia mafunzo ya hali ya juu sana.Wapo waliowahi kufanya kazi katika idara za ujasusi,wapo waliowahi kuwa wanajeshi,wapo wataalamu wa mawasiliano kwa ujumla kundi hili imesheheni wataalamu katika kila Nyanja.Yeyote ambaye mnadhani ni kikwazo au hatari kwenu basi hawa ndiyo suluhisho.Ni watalaamu wa kumaliza mambo kimya kimya” akasema Juan.
“Jambo lingine ambalo nataka kuwafahamisha ni kwamba ninataka kuanzisha kampuni kubwa ya filamu ambayo itajikita katika kutengeneza filani barani Afrika.Hii itawahusu wasanii wa bara la Afrika pekee.Black Mafia watajificha nyuma ya kampuni hiyo.Kampuni hiyo itakuwa kubwa na yenye ofisi yake kuu hapa Afrika kusini na dar es salaam Tanzania lakini itakuwa ikizunguka katika nchi mbali mbali za Afrika kutengeneza filamu na hiyo itakuwa ni mojawapo ya njia nzuri ya kusambaza mzigo katika nchi za Afrika.Nitatoa ndege mbili kwa ajili ya kampuni hiyo kwa ajili ya kuhakikisha wasanii wanafika sehemu mbali mbali za bara” akasema Juan Castillo.
Kilikuwa ni kikao kirefu na mambo mengi yalijadiliwa katika kikao hicho na kubwa zaidi likiwa ni kuimarisha biashara yao ya dawa za kulevya barani Afrika.
MIEZI MITATU BAADAE
“Asidingi abokufika
ezweni lethu ! (Hatuhitaji wageni katika nchi yetu)
“Aba bantu bokufika lapha bezothatha imisebenzi yethu,bagcwalisa imigwaqo yethu ngezidakamwiza,babulala abantu bakithi,Asibadingi lapha.Abafanele baye lapho bevela khona !(Wageni hawa wamekuja na kuchukua ajira zetu,wanaijaza mitaa yetu dawa za kulevya,wanaua watu wetu.Hatuwahitaji hapa.Warudi walikotoka !)
“Lona ngumyalezo oya kuhulmeni,asizukuphinda sihlanganise abanye.Uma bengakwazi laba bantu bangaphandle ukuthi emazweni abo okuqala sizokwenza lokho thina ngokwetu !
(Huu ni ujumbe kwa serikali kwamba hatutavumilia tena.Kama hawawezi kuwarudisha wageni hawa katika nchi walikotoka tutafanya hivyo sisi wenyewe !
Haya yalikuwa ni maneno ya kiongozi mmoja wa kimila wa kabila la wazulu akizungumza kwa hasira katika mazishi ya wanafunzi watatu waliouawa ka kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa ni wageni.Nyuso za watu wote pale msibani zilionyesha simanzi na hasira kubwa kufuatia mauaji yale
Kiongozi mmoja wa siasa aliyekuwepo pale msibani naye akapata nafasi ya kusema neno kwa waombolezaji
“Mauaji ya namna hii hayakubaliki na hatutavumilia kuendelea kuona watoto wetu wakiuawa kila uchao,hatutavumilia kuona vijana wetu wakikosa ajira huku ajira zikichukuliwa na wageni,Afrika kusini ni kwa waafrika kusini pekee.Hatutaki wageni ambao wanakuja kutuua hatutaki wageni ambao wanakuja kuharibu vijana wetu hatutaki wageni ambao wanakuja kuchukua ajira zetu wakati maelfu ya vijana wetu hawana ajira.Tunaitaka serikali kuchukua hatua za haraka sana kukabiliana na hali hii ama sivyo sisi tuko tayari kuingia barabarani,tutapita nyumba moja baada ya nyingine tutawaondoa wageni wote ! akasema mwanasiasa Yule huku akishangiliwa na kundi la vijana
Kwa siku mbili mfululizo
mauaji yaliendelea kutokea katika jiji la
Johanesburg.Vijana takribani nane waliuawa kwa kupigwa risasi na makundi ya wahalifu ambayo yanadaiwa kuongozwa na raia wa kigeni.Kitendo cha serikali kukaa kimya kilizidi kupandisha hasira kwa wenyeji dhidi ya wageni.Wanasiasa walipiga kelele kuitaka serikali ya Afrika kusini kuchukua hatua za haraka kudhibiti hali ile ya mauaji ya wenyeji lakini bado serikali haikutoa tamko lolote kulaani mauaji yale na hii ilifanya kauli za kuitaka serikali ya Afrika kusini iwaondoe wageni wote nchi Afrika kusini ziliendelea kutolewa na wanasiasa na watu mbali mbali .
Rais Festus Mayungulu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alikuwa Rais wa kwanza barani Afrika kuibuka hadharani na kulaani kauli za kibaguzi zilizokuwa zinatolewa na watu wa Afrika kusini dhidi ya wageni.Katika ukurasa wake wa twitter Rais Festus aliandika
“Tumezisikia.Ni kauli za kibaguzi ambazo hazipaswi kufumbiwa macho na kila mpenda amani duniani.Tunaziomba mamlaka nchini Afrika kusini kukemea kauli hizi zenye mlengo wa kutugawa waafrika”
Ujumbe huo mfupi wa
twitter aliouandika Rais Festus Mayungulu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ilifungua mlango na marais wengine kutoka nchi mbali mbali za kiafrika walianza kuandika katika kurasa zao za twitter wakilaani kauli zile za kibaguzi
DAR ES SALAAM -
TANZANIA
Wakati nchi nyingi za kiafrika zikisimama kulaani kauli na matendo ya kibaguzi dhidi ya wageni ,jijini Dar es salaam nchini Tanzania waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampuni kubwa ya filamu barani Afrika ambayo ilikuwa na ofisi katika majiji ya Dar es salaam na
Johanesburg Afrika kusini.Watu wengi walihudhuria ufunguzi huo wa kampuni kubwa kabisa ya filamu ambayo lengo lake ni kukuza vipaji vya wasanii wa Afrika.Wasanii wa filamu kutoka katika nchi za Afrika mashariki walihudhuria kwa wingi katika uzinduzi huo.
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Theresia Tarimo alitumia fursa hiyo kulaani vikali kauli za kibaguzi za baadhi ya wanasiasa wa nchi ya Afrika kusini dhidi ya wageni kutoka katika mataifa ya Afrika.
Katika uzinduzi huo mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo aliwatangazia wasanii na wote waliohudhuria sherehe hizo za uzinduzi kwamba filamu yao ya kwanza watakayoanza kuicheza itakuwa ni kutoka Tanzania ijulikanayo kama before I die.Aliwatambulisha baadhi ya wasanii wa kitanzania ambao watashiriki katika filamu hiyo na kuwataka wasani zaidi kujitokeza katika usaili kwa ajili ya filamu nyingine wanazotegemea kuzitoa.
Nabii Kasiano Muyenzi
alifuatilia uzinduzi ule akiwa sebuleni katika jumba lake kubwa la kifahari.Wakati uzinduzi ukiendelea alikuwa akiwasiliana kwa njia ya ujumbe mfupi na Roberto Zullo akimfahamisha kile kilichokuwa kinaendelea katika uzinduzi ule huku wakipongezana kwa mafanikio yale makubwa.
JOHANESBURG – AFRIKA
KUSINI
Hatimaye baada ya kauli za raia wa Afrika kusini kuitaka serikali yao kuwaondoa wageni wote wa kutoka mataifa ya Afrika kuonekana kupuuzwa,siku ya jumatatu asubuhi na mapema vijana waliokuwa wamejihami kwa silaha za jadi walianza kupita katika mitaa ambayo waliishi wahamiaji kutoka mataifa mbali mbali ya Afrika, wakiingia nyumba moja moja kuwapiga na kuwadhalilisha wageni hao.Biashara zao pia zilivamiwa kuporwa na kisha kuchomwa moto.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo taarifa zilivyozidi kusambaa na vijana zaidi kujiunga na kundi likawa kubwa.Polisi wa Afrika kusini walijitahidi kuwatawanya vijana wale lakini walioneka kuzidiwa nguvu kutokana na uwingi wa vijana hao.
Taarifa za matukio yale ya kuvama na kupiga wageni zilivuka mipaka ya Afrika kusini na kuanza kusambaa kwa kasi kubwa huku picha za kile kinachofanywa na makundi ya vijana zikionyeshwa na kuzidisha hasira kwa raia wa mataifa mengine.
Hadi ilipotimu saa kumi na mbili za jioni tayari raia kumi na moja kutoka mataifa ya kigeni walikuwa wameuawa na biashara nyingi za wageni zilichomwa moto huku mali zao kama vile nyumba na magari kuharibiwa vibaya sana.Hofu kubwa ilitanda jijini Johanesburg hasa kwa raia wa kigeni wanaotoka katika nchi za afrika
Machafuko yaliingia katika siku ya nne huku idadi ya wageni waliouawa ikifika thelathini na saba na idadi kubwa wakiwa majeruhi. Taarifa zilizopandisha watu hasira mataifa mengi ya kiafrika ni kitendo cha baadhi ya polisi kushirikiana na makundi ya vijana katika kuwapiga wageni.
Rais wa Zambia alikuwa wa kwanza kuwataka raia wake wote walioko Afrika kusini warejee nyumbani ikiwa ni pamoja na kutuma ndege maalum kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani.Hatua hiyo ilizidisha hasira kwa raia wa Zambia na hivyo kususia bidhaa zote zinazotoka Afrika kusini.Mataifa mengine kumi na saba nayo yalitangaza kuwaondoa Raia wake nchini Afrika kusini na kuwarejesha nyumbani.Katika baadhi ya nchi raia wa Afrika kusini walivamiwa kupigwa na mali zao kuharibiwa na katika nchi nyingine wakitakiwa kuondoka kurejea nyumbani kwao.Baadhi ya nchi ziliwarejesha nyumbani mabalozi wao.
Mvurugano mkubwa uliotokea miongoni mwa
mataifa ya Afrika ilikuwa ni ushindi mkubwa kwa mtandao wa wafanya biashara wa dawa za kulevya.Kama walivyokuwa wamekusudia kukosekana kwa maelewano miongoni mwa nchi wanachama wa SADC kulipelekea mipango waliyokuwa wameipanga kuhusiana na kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya kushindwa kufanikiwa hivyo kuwapa uwanja mpana zaidi wa kuendelea na biashara yao bila vikwazo.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Mchungaji Adam Watwila
akiwa katika ofisi yake akiendelea na majukumu yake mara simu yake ikaita hakumfahamu mpigaji akaipokea simu ile
“Hallow” akasema mchungaji Adam
“Hallow nazungumza na mchungaji Adam Watwila? Ikauliza sauti ya mwanamama upande wa pili
“Ndiyo unazungumza na mchungaji Adam Watwila nani mwenzangu?
“Mimi ni mkuu wa shule anakosoma mwanao Naomi Bambi”
“Naomi Bambi?! Akauliza mchungaji Adam kwa mshangao “Ndiyo mchungaji”
“Hapana sina mtoto anayeitwa Naomi Bambi.Mwanangu anasoma
katika shule hiyo lakini anaitwa Zoe Adam Watwila na si Naomi”
“Mchungaji mimi ni mgeni hapa shuleni nina wiki tatu tangu niwe mkuu wa shule hii hivyo bado sijawafahamu sana wanafunzi wa shule hii.Pamoja na hayo ninakuhitaji hapa shuleni baba mchungaji” akasema mwalimu “Kuna tatizo lolote?
“Kuna mambo nataka kuzungumza nawe” akasema mwalimu
“Sawa mwalimu ninakuja sasa hivi” akasema mchungaji Adam na kutoka ofisini kwake akaingia garini kuelekea katika shule ya kimataifa ya wasichana anakosoma mwanae Zoe.Ni moja kati ya shule inayotajwa kuwa na gharama za juu mno nchini Tanzania.
“Kuna nini huko shuleni hadi wananitaka niende? Ni mara ya kwanza wananiita shuleni.Nina wasi wasi kidogo yawezekana kuna tatizo labda kuna malipo hayajakamilishwa lakini kwa mujibu wa nabii mkuu malipo yamekwisha fanyika kwa miaka yote minne atakayosoma Zoe shuleni hapo sasa kuna nini wananiitia? Akajiuliza mchungaji Adam
“Au yawezekana huyo mwalimu kwa kuwa ni mgeni amechanganya majina na badala ya Zoe akadhani mimi ni mzazi wa huyo mwanafunzi anaitwa Naomi” akawaza mchungaji Adam na mara akakumbuka kwamba alikuwa na kikao na Nabii mkuu Kasiano hivyo akalazimika kumpigia simu kumjulisha kwamba ameitwa kwa dharura shuleni anakosoma mwanae
“Kuna nini shuleni? Akauliza Nabii Kasiano
“Mwalimu hajanieleza
lakini inaonekana kuna tatizo kubwa haijawahi kutokea nikaitwa shuleni.Nitakujulisha kila kitu baada ya kufika
shuleni” akasema mchungaji Adam
Alifika katika shule ya kimataifa anakosoma mwanae na kukaribishwa katika ofisi ya mkuu wa shule
“Ahsante kwa kufika mchungaji” akasema mwalimu Sheila Sanibo ambaye ndiye mkuu mpya wa shule ile.
“Ahsante sana mwalimu.Naitwa mchungaji Adam Watwila ninahudumu katika kanisa la injili ya
wokovu” mchungaji Adam akajitambulisha
“Nashukuru mchungaji na samahani kwa kukuondoa katika majuumu yako” akasema mwalimi Sheila
“Usijali mwalimu japo wito wako umenistua kidogo kwani sijawahi kuitwa shuleni hata mara moja.Kuna tatizo lolote? Akauliza mchungaji na kabla mwalimu Sheila hajasema chochote mchungaji akasema
“By the way umejaribu
kuangalia vizuri lile jina la mtoto? Uliniponipigia simu uliniambia mwanangu anaitwa Naomi.Mwanangu anaitwa Zoe Adam Watwila” akasema mchungaji Adam
“Sijakosea mchungaji.Nimejaribu kupitia kumbu kumbu zangu hapa……” akasema mwalimu Sheila na kuchukua faili akalifungua na kusema
“Mwanao aliandikishwa hapa shuleni kwa jina la Zoe Adam Watwila kama unavyodai lakini baada ya kuingia kidato cha tatu jina lake limebadilishwa na sasa anaitwa Naomi Bambi” akasema mwalimu Sheila
“Mwalimu that’s impossible” akasema mchungaji Adam na mwalimu Sheila akamuonyesha faili
“Haya mbona maajabu.Mwanangu anawezaje kubadili jina bila ya mimi kuwa na taarifa?Zoe ndilo jina lake kwa nini aamue kubadili jina bila kutushirikisha sisi wazazi wake?! Akauliza mchungaji Adam ambaye tayari alikwisha anza kupandwa na hasira
“Mwalimu namuomba Zoe
aitwe hapa aje aeleze kwa nini ameyafanya haya?
“Mchungaji,ni kawaida kwa wanafunzi wanapofika kidato cha tatu kuchagua jina ambalo atataka kulitumia atakapokuwa kidato cha nne na ambalo ndilo litakalotumika katika cheti chake cha kumaliza elimu ya sekondari na mwanao alichagua jina Naomi Bambi.Tutamuita na kumuuliza lakini kabla ya hapo kuna jambo la msingi ambalo nimekuitia hapa” akasema mwalimu Sheila na kuinua simu akampigia mwalimu mlezi wa wanafunzi akamtaka afike ofisini kwake mara moja
“Mwalimu kuna kitu gani kimetokea hapa? Akauliza mchungaji Adam na mara mwalimu mmoja mwembamba mrefu akaingia mle ofisini na kumsalimu mchungaji Adam
“Mchungaji huyu anaitwa mwalimu Filomena ndiye mlenzi wa watoto wetu hapa shuleni.Mwalimu Filomena huyu anaitwa mchungaji Adam watwila baba mzazi wa Naomi Bambi”
“Mwalimu stop calling my daughter Naomi.She’s not Naomi she’s Zoe Adam !
akasema kwa ukali mchungaji Adam
“Calm down Mr
Adam.Tuko hapa kujaribu kutafuta suluhisho hivyo naoma tujaribu kudhibiti jazba najua jambo hili limekustua sana lakini tutapata muafaka” akasema mwalimu Sheila
“Samahani mwalimu ni
kweli jambo hili limenistua sana”
“Pole baba mchungaji”akasema Mwalimu Sheila zikapita sekunde chache akasema
“Baba mchungaji
nimekuita hapa kuna tatizo kuhusu mwanao.Kama nilivyokueleza kwamba mimi bado ni mgeni hapa shuleni nina wiki ya tatu sasa.Nililetwa hapa baada ya mwalimu mkuu aliyepita kufariki dunia kwa ajali ya gari”
“Nilipata taarifa hizo.Poleni sana”akasema mchungaji Adam
“Siku tatu zilizopita alikuja kijana nadhifu hapa shuleni akiwa na gari la kifahari.Hakuwa na maelezo mengi akanikabidhi mkoba mdogo nilipoufunga nikakuta ndani yake kuna fedha nikamuuliza ni fedha za nini akaniambia niwaulize walimu wanafahamu.Niliwauliza baadhi ya walimu wachache lakini wakashindwa kunipa majibu kila mwalimu hakuwa tayari kueleza ukweli kuhusu fedha zile ni za nini.Bahati nzuri alijitokeza mwalimu Filomena na kunieleza ukweli wa fedha zile.Nilistuka sana baada ya kupewa maelezo.Fedha ile hapa shuleni iliitwa mshahara wa Naomi.Kila mwisho wa mwezi fedha ile huletwa hapa shuleni na mkuu wa shule huwagawia walimu wote kwa ajili ya kuhakikisha Naomi Bambi anaishi maisha ya kifahari hapa shuleni.Nilijiuliza huyu Naomi Bambi ni nani?.Nilimuuliza mwalimu mlezi kuhusiana na Naomi ni mtoto wa nani? Akaniambia kwamba ni mtoto wa mchungaji nikashangaa kidogo ni mchungaji gani anayeweza kumfanyia mwanae mambo kama yale ya anasa kubwa.Mwalimu akaniambia kwamba Zoe au Naomi ni msichana ambaye amekuwa akiishi kama mtoto wa malkia pale shuleni.Ni mwanafunzi ambaye hapaswi kuguswa au kukemewa.Mwalimu hebu
tueleze kila kitu kuhusu
Naomi” akasema mwalimu
Sheila
“Baba mchungaji,mwanao Zoe au Naomi amekuwa akiishi maisha ya kifahari sana hapa shuleni.Shule hii inafahamika kuwa ni shule ya watoto wa matajiri na ni shule yenye gharama kubwa kabisa hapa nchini lakini pamoja na
utajiri wa wazazi wa watoto wanaosoma hapa bado hawajafikia maisha ya Naomi.She’s the boss here.Walimu hata wanafunzi wanamuogopa kwa jeuri ya fedha aliyonayo.Kwanza kabisa Naomi hali chakula cha mchana wala cha usiku hapa shuleni.Analetewa chakula kutoka katika mojawapo ya hoteli kubwa hapa jijini.Kila unapofika muda wa chakula gari huleta chakula chake maalum kutoka hotelini.Naomi ana uwezo wa kufanya chochote akitakacho hapa shuleni.Mara nyingi amekuwa akiomba ruhusa na kuondoka hata wiki nzima. Naomi alikwisha uweka hadi uongozi wa shule katika kiganja chake.Mkuu wa shule aliyeondoka ni mmoja wa watu ambao walikuwa wanafaidika na fedha ya Naomi.Si mara moja amekuwa hafanyi mitihani na majaribio lakini amekuwa akijaziwa alama za juu na wakati mwingine taarifa ilionyesha ni mmoja wa wanafunzi kumi bora lakini ukweli tunaufahamu sisi.Sisemi uongo baba mchungaji mimi mwenyewe ni mmoja wa watu waliokula sana fedha ya Naomi kwani siwezi kukataa wakati wengine wanachukua.Mwalimu mkuu aliyepita kila mwisho wa mwezi alikuwa anapokea fedha nyingi kutoka sehemu Fulani na kisha huja kutugawia hapa
shuleni walimu wote kwa ajili ya kumuhudumia
Naomi.Uliitwa ni mshahara wa Naomi.Hii ni siri ya walimu na wafanyakazi wa hapa na ndiyo maana Naomi hapa shuleni ni malkia” Mwalimu Filomena akanyamaza baada ya mchungaji Adam kufumba macho na kuanza kufanya maombi akimuomba Mungu amsaidie ampe nguvu kwani jambo lile lilikuwa zito sana kwake.
“Mchungaji” akaita mwalimu Sheila na mchungaji Adam akafumbua macho
“Mwalimu Sheila imenilazimu kumuomba Mungu anipe nguvu kwani naona kama jambo hili linataka kunishinda nguvu. Tuendelee” akasema mchungaji Adam na kujifuta jasho usoni
“Baada ya mwalimu Filomena kunieleza ukweli kuhusiana na zile fedha zilizoletwa zikijulkana kama mshahara wa Naomi nilipata ushawishi wa kuyajua zaidi maisha ya binti huyu mdogo na je wazazi wake fedha hizi zote za kuchezea wanazitoa
wapi? Tulimpekua na kumkuta na dola zaidi ya elfu tano za marekani”
“Jesus Christ ! akasema mchungaji na kuweka mikono
yake kifuani mahala ulipo moyo
“Tulimkuta na simu tatu ambazo thamani yake kila moja ni zaidi ya milioni moja lakini simu hizo zote hazikuwa na laini hivyo hatujui alikuwa anazitumiaje .Tumemkuta na vito vya thamani kubwa ambavyo mpaka sasa hatujui thamani yake.Mchungaji mimi pia ni mzazi hivyo nimeona siwezi kulifumbia macho jambo hili ndiyo maana nimekuita hapa ili tulijadili na utuhakikishie kama unayafahamu haya na kama fedha hizi zote alizonazo mwanao wa kidato cha tatu wewe ndiye unayempatia na je
hizi fedha zinazojulikana kama mshahara wa Naomi wewe ndiye unayezitoa? Akauliza Mwalimu Sheila.Mchungaji Adam akavuta pumzi ndefu na kusema
“Mwalimu Sheila haya yote unayonieleza ni kweli yanamuhusu mwanangu Zoe au ni mwanafunzi mwingine?
“Ni mwanao baba mchungaji.Ni vigumu kuamini lakini huo ndio ukweli wote kuhusu maisha ya mwanao hapa shuleni”akasema mwalimu Sheila
“Mwalimu ninakushukuru sana kwa kujitoa mhanga kunieleza ukweli.Ninashindwa niseme nini na laiti ningekuwa na ugonjwa wa moyo ningeanguka na kufariki hapa hapa kwani jambo hili limenistua mno !
“Pole sana baba
mchungaji” akasema Mwalimu Sheila
“Naomba niwaeleze ukweli mwalimu kwamba mimi
sihusiki na chochote katika hayo mliyoyasema.Mimi nina maisha ya kawaida sana.Kipato changu ni kidogo ambacho kinatokana na kazi yangu hii ya uchungaji na hakiwezi kumudu kumsomesha mwanagu katika shule kama hii ambayo ada yake kwa mwaka mmoja ni sawa na mshahara wangu kwa miaka mitano au zaidi.Mke wangu ni mwalimu wa shule na maisha yetu ni ya kawaida kabisa.Ninaishi katika nyumba niliyojengewa na kanisa kwani sikuweza hata kujenga nyumba ya kuishi.Kusema ukweli Zoe anasomeshwa na kanisa.Upo utaratibu katika kanisa letu kuwafadhili watoto wa wachungaji na waumini wengine katika masomo ndani na nje ya nchi.Zoe alibahatika kupata ufadhili katika shule hii.Haya mambo niliyoyasikia hapa ni mazito na mageni kabisa kwangu.Siamini kama yanafanywa na mwanangu Zoe.Ee Mungu nisaidie katika jambo hili ! akasema mchungaji Adam na kuinamisha kichwa alichanganyikiwa
“Kwa hiyo baba mchungaji unatuthibitishia kwamba si wewe ambaye hutuma fedha hapa shuleni zinazojulikana kama mshahara wa Naomi? Akauliza mwalimu Sheila
“Mwalimu mimi sina uwezo huo.Sina fedha za kuchezea kiasi hicho.Mwanangu Zoe amekulia katika maisha ya kawaida sana na haya mnayonieleza ninayaona kama hadithi”
“Si hadithi mchungaji ni jambo la kweli kabisa.Swali ni nani ambaye anampatia Naomi fedha hizi zote na kwa madhumuni gani? Inashangaza mtoto wa kidato cha tatu kukutwa na zaidi ya shilingi milioni kumi na moja za matumizi yake binafsi.Baba mchungaji mwanao anatakiwa abanwe na aseme ukweli ni nani anayempatia fedha hizi zote?Lazima yupo mtu ambaye anapatia fedha na huyo ndiye ambaye amekuwa akileta fedha hizo shuleni kuwagawia walimu ili kuhakikisha Naomi anakuwa huru kufanya kila akitakacho na ndiyo maana imekuwa rahisi kwake kuondoka hapa shuleni kila pale anapotaka bila kuulizwa na mwalimu yeyote” akasema mwalimu Sheila
“Nimechanganyikiwa mwalimu na sijui nifanye nini.Naomba tafadhali mumuite Zoe aje hapa atueleze ukweli ! akasema mchungaji Adam na mwalimu Sheila akamtuma mwalimu Filomena kwenda kumuita Zoe.Zilipia dakika kumi na tano ndipo mwalimu Filomena aliporejea na habari ambayo si nzuri
“Mkuu,Naomi ameondoka na hakuna anayejua amekwenda wapi.Nimekwenda hadi bwenini kwao fedha na vitu vyake vya thamani vyote
amechukua .Kwa mujbu wa walinzi getini limekuja gari kuja kumchukua muda mfupi baada ya mchungaji kuwasili hapa”
Mchungaji Adam akazidi kuchanganyikiwa
SAA MOJA LIYOPITA
Akiwa darasani kipindi kikiendelea simu ya Zoe ikatetema akaitoa akatazama mpigaji alikuwa ni Nabii Kasiano.Akainuka na kumuomba ruhusa mwalimu akatoka nje akaelekea chooni ambako aliipokea ile simu
“Hallow mpenzi ! akasema Zoe
“Mbona umechukua muda hivyo kupokea simu?
“Nilikuwa darasani.Vipi mbona umenipigia muda huu wa masomo?
“Nimekupigia kukujulisha kwamba jiandae linakuja gari sasa hivi hapo shuleni kwenu ukukuchukua”
“Kuna safari ? Akauliza Zoe
“Tafadhali jiandae Zoe ! akasema Kasiano na kukata sim
“Yawezekana kuna safari imejitokeza”akawaza Zoe na kumtafuta mwalimu wa zamu akamtaka ampatie funguo ya bweni lao kwani wawapo madarasani mabweni yote hufungwa.Naomi alikuwa na sauti hivyo mwalimu alishindwa kumnyima funguo akaenda kupakia vitu vyake muhimu katika sanduku lake dogo na baada ya muda akajulishwa kwamba tayari gari limefika akatoka kupitia geti la upande wa pili ambalo ndilo hulitumia mara nyingi.
Dereva wa gari lile alikwisha pewa maelekezo mahala pa kumpeleka Naomi.Akiwa garini Naomi akamuandikia ujumbe Kasiano akamjulisha tayari amekwisha ondoka shule akamuuliza mahala anakoelekea
“Nimekwisha mpa
maelekezo dereva.” akajibu
Kasiano
“Kuna nini leo mbona Kasiano anaonekana yuko tofauti? Au kuna safari ya ghafla imetokea? Akajiuliza Naomi huku gari likiendelea kukata mitaa.
“Ngoja nitajua kinachoendelea.Mara nyingi akiniita ghafla namna hii lazima kuna safari imejitokeza” akaendelea kuwaza Naomi akafungua mkoba wake mdogo akachuka mkebe wa poda akaanza kujipaka.Hakuwa na wasi wasi wowote
Safari yao iliishia katika jumba moja kubwa la ghorofa moja.Dereva akabeba sanduku la Naomi akamkaribisha ndani.Nyumba ilikuwa kubwa na kimya.Yule dereva aliyeonekana kuifahamu vyema ile nyumba akampeleka katika chumba kikubwa na kizuri akamtaka apumzike
“Nyumba nzuri sana hii” akawaza Naomi kisha akajilaza kitandani.Akavua mavazi yale aliyokuwa ameyavaa na kuvaa mavazi mepesi yaliyoonyesha kila kitu alichokivaa akajiandaa kumsubiri Kasiano.
Zilipita dakika ishirini na mbili,Kasiano akawasili na moja kwa moja akaelekea katika chumba alimo Naomi.Mara tu alipoufungua mlango akastuka baada ya kumuona Naomi akiwa amelala kitandani nusu mtupu.
“Naomi kweli unajua kucheza na akili yangu.Sikuwa nimepanga tufanye chochote leo lakini tayari umeamsha kila kitu” akasema Nabii Kasiano huku akivua nguo zake haraka haraka na kuzitupa chini kisha akapanda kitandani.Alikuwa ni kama fisi mwenye njaa.Walimaliza mzunguko mmoja na Nabii Kasiano akiwa hoi
“Wewe mtoto iko siku utaniua kwa raha hizi unzonipa” akasema Kasiano huku akiinuka wakaenda kuoga pamoja halafu wakarejea chumbani na Kasiano akavaa mavazi yake
“Mpenzi kuna nini leo ukaniondoa mapema namna hii shuleni?Kuna safari? Akauliza Naomi
“Hakuna safari Naomi.Kuna jambo limetokea ambalo nikaona ni vyema nikuite hapa nikueleze”
“Jambo gani limetokea mpenzi? Akauliza
Naomi.Kasiano akavuta pumzi ndefu na kusema
“Uliniambia kwamba mwalimu mkuu alikupekua na kukuta fedha na vito.Basi baba yako ameitwa leo shuleni.Nadhani ameitwa kwenda kuelezwa kila kitu kuhusu wewe”akasema Kasiano na Naomi akastuka akainuka na kukaa
“Baba ameitwa shuleni? Akauliza
“Ndiyo ameitwa shuleni na muda huu naamini tayari atakuwa amekwisha elezwa kila kitu kuhusu wewe ndiyo maana nikakuondoa haraka sana kwani kila kitu kimeharibika”
“Kasiano uliniambia kwamba hakuna tatizo lolote litakalotokea shuleni na …...” “Ni kweli nilikuahidi hivyo Naomi na hakujawahi kutokea tatizo lolote hadi alipokuja
huyu mwalimu mpya ambaye amekuja kuharibu kila kitu.Mwalimu aliyepita nilikuwa namlipa fedha kila mwezi ili awagawie waalimu wenzake wote ndiyo maana ilikuwa rahisi kwako kuweza kutoka muda wowote uutakao lakini huyu wa sasa amekataa fedha hizo na ndiyo maana akamuita mzazi wako.Lakini usijali kila kitu kitakwenda vizuri” akasema Kasiano “Kasiano baba yangu akifahamu jambo hili anaweza akafa kwa mstuko.Nataka umpigie simu umuulize kama kuna chochote ameambiwa kuhusu mimi” akasema Naomi na Kasiano akachukua simu akampigia mchungaji Adam
“Hallo baba askofu” akasema Adam
“Adam hebu nipe taarifa za huko shuleni.Kuna tatizo lolote? Akauliza nabii Kasiano
“Baba askofu kuna mambo makubwa sana huku ambayo sikuwahi hata kuyaota.Shetani anaitembelea familia yangu !
“Kuna nini?
“Ni mambo makubwa
kuhusu binti yangu Zoe.Mambo anayoyafanya hapa huwezi amini kabisa.Nitakuja kukueleza kila kitu nikija huko kwa sasa tunamtafuta kwani ametoweka na hatujui alipo”
“Ametoweka?
“Ndiyo ametoweka na hutujui amekwenda wapi” “Ametowekaje hapo shuleni?Hakuna walinzi?
“Kuna ulinzi wa kutosha lakini dah ! ni mambo makubwa haya baba askofu nitakuja kukueleza”
“Kwa hiyo mmechukua
hatua gani hadi sasa za kumtafuta?
“Kwa sasa tayari tumekwisha toa taarifa kituo cha polisi na tumeambiwa kwamba tusubiri kwa saa ishirini na nne na kama bado hatujamuona kisha turejee tena.Kinachofuata ninataka kwenda katika vyombo vya habari,luninga na magazeti kuomba msaada wa kumtafuta.Nitasambaza pia picha zake katika mitandao ya kijamii ili waweze kutoa taarifa
pale atakapokuwa ameonekana”
“Adam sikushauri utumie mitandao ya kijamii katika kumsaka mwanao.Ninaamini Naomi yuko sehemu Fulani na atarejea nyumbani.Kwa sasa tunachotakiwa kukifanya ni kudumu katika maombi.Tukutane kanisani na tutafanya maombi makubwa leo kumuomba Mungu atuonyeshe mahala alipo Naomi.Nitamlilia bwana wa majeshi anionyeshe mahala alipo mwanao.Najua shetani anataka kuijaribu familia yako hivyo basi njia pekee ya kumshinda ni kudumu katika maombi.Naomba achana na kila kitu tukutane kanisani kwa ajili ya maombi.Bwana atafanya unabii mkubwa sana siku ya leo” akasema Kasiano
“Ahsante baba.Ninakuja kanisani sasa hivi” akasema mchungaji Adam na kukata simu
“Naomi nadhani umesikia mwenyewe kwamba tayari mambo yameharibika” akasema Kasiano huku Naomi
akilia
“Kasiano nina hofu kubwa sana.Nitafanya nini?Baba ataniua !
“Usihofu nitalimaliza suala hili.Wewe utaendelea kukaa hapa hadi pale suala hili litakapokuwa limemalizika”
“Ni vipi kama nitaanza kusakwa na polisi? Tayari baba amekwisha toa taarifa polisi na ndani ya saa ishrini na nne nisipoonekana basi nitaanza kusakwa.Nikikamatwa itakuwa mbaya zaidi kwani kila kitu kuhusu sisi kinaweza kujulikana”
“Usiwe na hofu
Naomi.Kila kitu kiko hapa mkononi mwangu.I’ll handle everything.Wewe endelea kukaa hapa usiwe na hofu
yoyote kila kitu kitamalizika” akasema Kasiano
“Kitu pekee unachopaswa kukifanya usiwasiliane na mtu yeyote Yule.Zima simu yako kuanzia sasa.Kama nikitaka kuwasiliana nawe nitatumia simu hiyo hapo mezani” akasema Kasiano na kumkumbatia Naomi
*************
Mchungaji Adam alifuata ushauri wa mkuu wake nabii Kasiano na kuanza safari ya kurejea kanisani.
“Lazima yupo tajiri ambaye amemuharibu mwanangu.Siwezi kukubali jambo hili lazima nimfahamu mtu huyo ni nani? Akawaza Adam
“Nimekumbuka kuna
gazeti linaitwa Fukufuku.Ni gazeti maarufu sana kwa kufichua maovu mbali mbali katika jamii.Wao wamejikita zaidi katika kuandika habari za kuchunguzi.Ngoja niende hapo wao wanaweza wakanisaidia kufahamu huyu mtu aliyemuharibu mwanangu ni nani.Ningeweza kuweka wapelelezi wa kujitegemea lakini sina fedha ya kuwalipa,ngoja tu nitumie waandishi wa habari kwani hii ni habari kubwa kwao na watahakikisha wanaupata ukweli wa jambo hili na kumuanika hadharani tajiri huyo .Baada ya hapo ndipo nitakapofungua kesi na kuhakikisha haki inatendeka” akawaza mchungaji Adam
Aliwasili katika ofisi za gazeti la Fukufuku na kuomba kuonana na mkurugenzi akamweleza tatizo lake.Mkurugenzi aliyejulikana kwa jina la Susan Ibobwe akamshukuru sana mchungaji kwa kuwaamini wao waifanye kazi ile na kumuhakikishia mchungaji kwamba watafanya kila lililo ndani ya uwezo wao kuhakikisha wanamfahamu huyo kigogo ni nani.
Mara tu baada ya mchungaji Adam kuondoka ,Susan Ibobwe akamuita Lidya Kipara mmoja wa waandishi mahiri kabisa katika habari za kiuchunguzi akamkabidhi kazi ile ya mchungaji Adam
*****************
Mchungaji Adam alirejea kanisani akaonana na Nabii Kasiano na akamueleza hatua ambazo amekwisha chukua ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kuwashirikisha gazeti la Fuku Fuku katika kumtafuta kigogo anayemuharibu mwanae.Nabii Kasiano akamtaka waanze maombi.Wachungaji na watu wengine wachache wakaitwa kujumuika katika maombi hayo.
Yalikuwa ni maombi yaliyodumu kwa saa mbili na mara Nabii Kasiano akawaomba wasimame na wamshukuru Mungu kwa muujiza alioutenda.Wakaimba na kushukuru bila kujua ni muujiza gani
“Wakati wa maombi Mungu amenionyesha nabii wake mahala alipo mtoto.Ninawahakikishia Mungu wa majeshi hashindwi na chochote.Mtoto yuko salama na amenitaka niwaambie wazazi wake wasihofu mtoto yuko salama” akasema Nabii Kasiano aliyekuwa ameloa shati lake huku jasho likimtiririka.Akawataka mchungaji Adam na mke wake aliyefika wakati maombi yakiendelea wamfuate ofisini kwake
“Adam na mke wako
mnapitia kipindi kigumu sana lakini Mungu anawapenda na atasimama nanyi.Endeleeni kusimama katika imani kwani ni kutokana na imani yenu hiyo binti yenu yuko salama.Watu wabaya walitumiwa na shetani kutaka kuwavuruga na kuwapoteza imani lakini Mungu wetu aliye hai amesimama nanyi na amenionyesha mahala alipo mtoto wenu” akasema Nabii Kasiano
“Mtoto wenu yuko
Morogoro.Amefichwa katika hoteli moja ya kifahari” akasema na kuwatajjia jina la hoteli hiyo na chumba
“Mtakapofika msionyeshe kumkasirikia bali pigeni magoti muombe kisha mumchukue na mrudi naye nyumbani.Safari ya kwenda Morogoro inaanza sasa hivi na mtatumia gari langu.Msimweleze chochote mtu yeyote hadi pale mtakapokuwa mmempata mtoto wenu halafu mtatoa ushuhuda wa kile Mungu alichowatendea.Mimi nitaendelea kudumu katika maombi,nitainua mikono yangu kumlilia bwana hadi pale mtakapokuwa mmerejea” akasema Nabii Kasiano na bila kupoteza muda mchungaji Adam na mkewe wakachukua gari la Kasiano na safari ya kuelekea Morogoro ikaanza.
Mara tu
walipoondoka,Kasiano akachukua simu na kuzitafuta namba Fulani akapiga
“Tayari ameanza
safari.Anatumia gari langu” akasema Kasiano na kukata simu
************
Saa moja za jioni Kasiano akiwa bado kanisani kwake akiendelea na huduma akafuatwa na mmoja wa wachungaji wa kanisa lake akamjulisha kwamba wamepokea taarifa kwamba mchungaji Adam Watwila na mke wake wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jioni hiyo wakati wakielekea Morogoro.Ikamlazimu nabii Kasiano kusimamisha ibada na kuwatangazia waumini kuhusiana na taarifa ile ya kustusha kuhusu kifo cha mchungaji Adam Watwila na mke wake.Kanisa likalipuka kwa vilio lakini Nabii Kasiano
akawataka wasilie bali
wadumu katika maombi kwani kanisa linapitia kipindi kigumu
.MWISHO WA SCANDLE SEASON ONE..TUENDELEE NA SEASON 2
MWISHO
0 comments:
Post a Comment