IMEANDIKWA NA : PATRICK CK
******************************************
Simulizi : The Football (2)
Sehemu Ya Kwanza (1)
“Hapana hakueleza chochote
na hakuna anayefahamu
anakwenda wapi.” Akasema mama yule na mara uso wake
ukaonekana kubadilika.Mathew
akagundua kitu usoni pa yule
mama akageuka nyuma na
kukutana na wanawake watatu
waliovaa mavazi marefu na
kujifunika nyuso zao wakabaki
wanaonekana macho pekee.
“Mbona huyu mama
ameogopa baada ya kuwaona hawa
wanawake wakiingia hapa?
Akajiuliza Mathew na ghafla
kukatokea jambo ambalo hakuna
aliyelitegemea.Wale wanawake
watatu waliokuwa wamevaa
magauni marefu kila mmoja
akatoa bunduki ndogo aliyokuwa
ameificha ndani ya gauni lile na
kuanza kuachia risasi na kuwataka watu wote walale chini .Watu wale
walitawanyika haraka sana na
kumbe hawakuwa peke yao
walikuwepo wengine nje na idadi
yao ikaongezeka mle ndani.Ndani
ya sekunde chache watu wote
waliokuwepo eneo lile wakalala
chini wakiwamo Mathew na
Camilla
Mbona huyu mama ameogopa
baada ya kuwaona hawa wanawake
wakiingia hapa? Akajiuliza Mathew
na ghafla kukatokea jambo ambalo
hakuna aliyelitegemea.Wale
wanawake watatu waliokuwa
wamevaa magauni marefu kila
mmoja akatoa bunduki ndogo
aliyokuwa ameificha ndani ya gauni
lile na kuanza kuachia risasi na
kuwataka watu wote walale chini
.Watu wale walitawanyika haraka
sana na kumbe hawakuwa peke yao
walikuwepo wengine nje na idadi yao
ikaongezeka mle ndani.Ndani ya
sekunde chache watu wote
waliokuwepo eneo lile wakalala
chini wakiwamo Mathew na Camilla
ENDELEA
“Tulieni nyote.Hatuna lengo
baya nanyi na wala hatutaki
kumdhuru mtu yeyote” Akasema
mmoja wa wale jamaa aliyekuwa
amejitanda mavazi marefu na
kufunika uso kama
mwanamke.Watu wote walikuwa
kimya wamelala chini kama
walivyoamriwa na wale jamaa
ambao idadi yao ilizidi ishirini na
walikuwa wamezingira katika kila
kona ya nyumba.
“Tunamuhitaji mjane wa
marehemu.Naomba ajitokeze
tafadhali” akasema yule jamaa na kuingia ndani waliko kuwa
wamekaa akina mama.
“Tunamuhitaji haraka sana
mjane wa marehemu !! akaendelea
kusema yule jamaa akiwa katika
chumba walichokuwamo akina
mama wengi.Hakuna yeyote
aliyesimama.Yule jamaa akawapa
maelekezo watu wake wanne
waliokuwa mle ndani ambao wote
walikuwa wamefunika nyuso zao
waingie katika kila chumba
wapekue.Nyumba ya George
Mzabwa ilikuwa na vyumba vinne
vya
kulala,sebule,maktaba,jiko,vyoo na
mabafu.Wale jamaa wakaingia
ndani ya vyumba haraka haraka
kila mmoja na chumba chake wakaanza kupekua lakini
hawakufanikiwa kukipata
walichokuwa wanakitafuta.Yule
jamaa aliyeonekana ndiye kiongozi
wao akasema kwa ukali
“Nataka haraka sana mjane
wa marehemu ajitokeze ama sivyo
tutawateketezeni nyote !!
Pamoja na vitisho vile lakini
hakuna aliyejitokeza.Kwa hasira
akamfuata mama moja akamuinua
“Naomba msiniue jamani !!
akasema yule mama huku akilia
“Nitakuacha hai endapo
utanionyesha mjane wa marehemu
alipo !! akasema yule jamaa kwa
sauti kali
“Hayupo ametoka na hatujui
amekwenda wapi” “Unanidanganya? Nakupa
sekunde kumi unionyeshe mahala
alipo mjane wa marehemu”
akasema yule jamaa
“Naomba uniamini kweli
ametok….” Hakumaliza neno la
mwisho yule jamaa akammiminia
risasi.Akina mama waliokuwepo
mle ndani wakapiga yowe lakini
yule jamaa akawatuliza kwa
kupiga risasi juu akitishia
kuwamaliza wote kama
wangeendelea kupiga kelele.Akiwa
amefura kwa hasira akamuinua
mwanamke mwingine na kumtaka
amuonyeshe alipo mjane wa
marehemu
“ Baba utatuua sote lakini
huyo unayemtafuta hayupo.Ametoka na hatujui
amekwenda wapi” akasema yule
mama huku akitetemeka kwa
hofu.Yule jamaa kwa hasira
akammiminia risasi na kumuua
“Camilla hawa jamaa
wataendelea kuua watu huko
ndani bila hatia.Hizo risasi
zimesikika kuna mtu mwingine
ameuawa.Lazima tufanye jambo
kuwazuia wasiendelee kuua watu”
Mathew akamwambia Camilla kwa
kunong’ona
“Unataka kufanya nini
Mathew? Hawa jamaa wako wengi
na wana silaha kali.Hatuwezi
kupambana nao hata
kidogo.Tuwaache wafanye wanachotaka waondoke” akasema
Camilla
“Kweli wako wengi lakini
hawa ndio wale
tunaowatafuta.lazima tufanye kila
linalowezekana kuwadhibiti”
akasema Mathew
“ Mathew tafadhali usi…”
“Usiogope Camilla.Mimi
ninawafuata” akasema Mathew na
kuinuka akainua mikono juu.Watu
wawili waliokuwa eneo lile
wakamsogelea wakimuelekezea
silaha zao na kumtaka alale
chini,akapiga magoti
“Mimi ni mdogo wa marehemu
na ninaweza kuwasaidia kupata
hicho mnachokitafuta” akasema Mathew.Wale jamaa
wakatazamana.
“ Tafadhali msiendelee kuua
watu,nitawasaidia kupata kile
mnachokitafuta” akasema
Mathew.Mmoja wa wale jamaa
akamuongoza Mathew kuelekea
ndani akiwa ameinua mikono juu
.Akina mama wote walikuwa
wameondolewa kutoka katika
vyumba walimokuwa wamekaa na
kuwekwa sebuleni.Yule jamaa
kiongozi wa wale wavamizi
akageuka na kumuona Mathew
akiingizwa sebuleni akiwa
ameinua mikono juu
“Huyu naye kafanya
nini?akauliza “Huyu ni mdogo wake na
marehemu” akasema yule jama
aliyekuwa nyuma ya Mathew na
silaha
“Piga magoti haraka” akasema
yule kiongozi kwa ukali na Mathew
akapiga magoti.
“Wewe ni mdogo wake na
marehemu?
“Ndiyo ni mdogo wake
Marehemu.Naweza kusaidia
kupata kile mnachokitafuta ila
msiendelee kuua watu .Kitu gani
mnakihitaji? Akasema
Mathew.Yule jamaa akamtazama
kwa hasira na kuuliza
“Mjane wa marehemu yuko
wapi? “Amekwenda kaburini
kuonyeshwa kaburi la mumewe na
kuwasha mshumaa.Jana hakuweza
kushuhudia mazishi ya mume
wake alikuwa amepoteza fahamu”
Mathew akadanganya.Yule jamaa
akamtazama kwa sekunde kadhaa
akamtaka asimame wakaelekea
chumbani kwa George
“Nataka simu za
marehemu.Haraka sana tuonyeshe
mahala zilipo” akasema yule jamaa
“Mnahitaji kwa dhumuni
gani?Ninyi ni polisi?Mathew
akauliza ni swali lile likaonekana
kumkera yule jamaa
“Nakupa sekunde kumi ,kama
ukishindwa kuonyesha zilipo simu
za marehemu nitakumaliza kama nilivyowamaliza hao wanawake
uliowaona wamekufa sebuleni!!
“George ana kasiki la siri
ambalo yeye na mke wake huficha
vitu vyao muhimu na nina hakika
humo ndimo mke wake alimoweka
vifaa muhimu vya mumewe
alivyokabidhiwa baada ya
mumewe kujiua.Kasiki hilo liko
nyuma ya kabati la nguo” akasema
Mathew na kuanza kulisogeza
kabati la nguo ili aweze kupata
nafasi ya kulifungua kasiki alilodai
liko nyuma ya kabati la nguo.
“Hii ndiyo nafasi yangu
ambayo sitakiwi kuipoteza”
akawaza Mathew na kuzunguka
nyuma ya kabati,akatoa bastora
yake haraka haraka halafu kwa nguvu kubwa akalisukuma kabati
likaanguka kwa mbele.Yule
kiongozi wa lile genge la wavamizi
aliliona kabati likianguka akaruka
pembeni kulikwepa na hiyo ndiyo
nafasi Mathew alikuwa
anaitafuta.Kwa kasi ya umeme
akaachia risasi kadhaa toka katika
bastora yake yenye kiwambo cha
sauti na kumfumua yule jamaa
kichwa na kwa wepesi wa aina
yake akaruka na kunyakua
bunduki ya yule jamaa.Kishindo
cha kuanguka kwa kabati
kiliwastua jamaa wengine
waliokuwamo mle ndani na huku
wakikimbia jamaa wanne
wakaingia mle chumbani na
kumkuta Mathew akiwa tayari amejiandaa akiwa na bunuki ya
yule jamaa aliyemuua na
hakufanya ajizi akavurumisha
mvua ya risasi ambazo wale jamaa
hawakuwa wamezitarajia na wote
wanne wakaanguka chini
.Hawakuwa na uhai tena.Akaitupa
ile bunduki na kuchukua nyingine
halafu akamvua mmoja wao kofia
aliyokuwa ameivaa ya kufunika
uso akavaa pamoja na fulana ya
kujikinga risasi na kutoka mle
ndani kwa tahadhari kubwa
akanyata hadi sebuleni na
kuwakuta akina mama peke yao
bila kuwepo wale jamaa
waliokuwa wamewashika
mateka.Kutokea nje akasikia sauti
za magari,akavua kofia ile ya kufunika uso,akatoka na kuwakuta
watu bado wamelala chini
akawapigia ukelel
wainuke,akakimbia kwa tahadhari
hadi nje lakini alikwisha chelewa
wale jamaa walikwisha ingia
katika magari yao na kukimbia
“Wamekimbia !! ikasema sauti
ya Camilla nyuma yake
“Tumewakosa tena” akasema
Mathew
“Iliposikika milio ya risasi
alitoka jamaa mmoja mbio na
kuwaita wenzake kwa ishara na
wote wakatoka na kukimbia .Nini
kimetokea ndani?Nilikuwa na
wasiwasi sana kuhusu usalama
wako baada ya kusikia ile milio ya
risasi” akasema Camilla.Mathew akamsimulia kila kitu kilichotokea
mle ndani
“Watu hawa lazima wana
mahusiano na kile kikundi cha
askari wanotumiwa kufanya
uvamizi.Lazima kuna jambo
wanataka kulificha lisijulikane
ndiyo maana walikuwa wanahitaji
simu za George” akasema Mathew
“Lakini kwa nini iwe sasa?
Kwa nini watafute simu hiyo leo
tena baada ya sisi kufahamu
kuhusu George kuwa na
mawasiliano na Nathan?Tujiulize
maswali haya na yanaweza
yakatusaidia kufahamu mambo
mengi” akasema Camilla
“Ni kweli Camilla,kuna kitu
hata mimi ninakiona hapa.Hawa jamaa walifahamu fika kwamba
tunakuja huku kuonana na mjane
wa marehemu hivyo wakajitahidi
kuwahi kutudhibiti tusipate
tunachokitafuta lakini waliku
ya rais na kifo cha baba
,wangekwisha nimaliza muda
mrefu sana.Hakuna mpaka leo
anayefahamu kama nilikuwemo
katika ile ndege.Wanachofahamu
ni kwamba abiria wote walifariki
.Siri hii haipaswi kujulikana na
lazima nifanye kila niwezalo
kumkwamisha Mathew asiufikie
ukweli” akaendelea kuumiza
kichwa kwa mawazo mengi hadi
alipofika nyumbani kwa George
Mzabwa.Akashuka na kuwasabahi akina mama waliokuwa
wanaokota mchele na kuwaomba
wamuelekeze alipo mke wa
George.Mama mmoja
akamuongoza hadi katika chumba
kilichokuwa na akina mama
sita.Mama mmoja aliyevaa mavazi
meupe alikuwa amelala juu ya
godoro na Theresa akawasalimu
wale akina mama kwa adabu
halafu akaenda kuketi pembeni ya
mfiwa.
“Pole sana mama” akasema
kwa sauti ndogo
“Ahsante sana mwanagu”
akajibu mama yule ambaye bado
macho yake yalikuwa yamevimba
“Mama mimi naitwa Theresa
natokea ikulu katika ofisi ya rais.Kuna mambo yamenileta hapa
kuhusiana na mumeo”
“Ni mambo gani?
“Unaweza ukajikaza tukaenda
kuzungumza hapa nje tafadhali ni
mambo ya siri kidogo”akasema
Theresa na yule mama akainuka
wakaingia katika chumba cha
kulala
“karibu” akasema mke wa
George
“Ahsante sana.Mama mumeo
George alijipiga risasi hivyo nataka
kufahamu umeshakabidhiwa vitu
vyake vyote?Alikuwa na vitu mbali
mbali kama vile simu ,kompyuta
nk.Wameshakuletea vitu hivyo
tayari? “Hapana bado.Alinifuata mtu
mmoja anaitwa Inspekta Msibi
Makwala Msibi akanihoji kama
naweza kufahamu sababu ya
mume wangu kujiua,akaniambia
pia kwamba yeye ndiye
anayesimamia uchunguzi wa suala
la kujiua mume wangu na kuna
baadhi ya vifaa vya marehemu
wanavyo kama hiyo simu na
kompyuta ili viwasaidie katika
uchunguzi wao wa kubaini
kilichosabisha George ajiue na
uchunguzi wao utakapokamilika
watavirejesha”
“Sawa mama naomba twende
ofisini kuna vitu vingine vya
marehemu vya kutambua na
kuvichkua na hawezi kupewa mtu mwingine zaidi yako.Nafahamu
umechoka bado na hauna nguvu
lakini jikaze twende hatutachukua
muda mrefu” akasema Theresa
.Mke wa George akatafakari kidogo
halafu akaomba ajiandae
Wakati mke wa George
akijiandaa Theresa akachukua
simu na kumpigia Dr Vivian.
“Unasemaje Theresa?
Akauliza Dr Vivian baada ya
kupokea simu
“Dada naomba msaada
wako.Nataka kufahamu inspekta
Msibi Makwala msibi anapatikana
kituo gani cha polisi?
“Kuna tatizo lolote na huyo
mtu” “Hapana dada namuhitaji nina
shida naye binafsi “ akasema
Theresa
“Nipe dakika mbili niulize”
akasema Dr Vivian na kukata simu
Mke wa George alipomaliza
kujiandaa wakaongozana hadi
garini wakaondoka.Dakika chache
baada ya kuondoka nyumbani kwa
George ,simu ya Theresa ikaita
alikuwa ni rais.Akapunguza
mwendo wa gari na kuipokea
“Hallow dada” akasema
“Theresa huyo askari
unayemuulizia nimeambiwa yuko
katika ofisi za upelelezi kanda
maalum”
“Ahsante dada nashukuru”
akasema Theresa na kukata simu.Hakutaka kumpa dada yake
nafasi ya kuendeleza
maongezi.Hakukuwa na maongezi
garini hadi walipofika nyumbani
kwa Theresa.Mke wa George
alionekana kuwa na wasi wasi
“mama karibu ndani”
akasema Theresa wakaingia
sebuleni
“Mama utanisamehe kwa
kutokueleza ukweli lakini hakuna
vitu vya marehemu bali nilitaka tu
nikutoe pale nyumbani ili tuweze
kuzungumza mambo ya msingi
kuhusiana na kifo cha mumeo”
akasema Theresa na sura ya mke
wa George ikajikunja kwa hasira
“Mama usikasirike lakini
suala ninalotaka kuzungumza nawe ni muhimu sana kwa
usalama wako na familia yako”
akasema Theresa na kauli ile
ikamstua yule mama.
“Unamaanisha nini
unaposema
hivyo?akauliza.Theresa akakohoa
kidogo kurekebisha koo lake na
kusema
“Tutakayozungumza hapa
naomba iwe ni siri kubwa kati
yangu nawe”
“Mbona unazidi kunipa wasi
wasi?
“Usiogope mama nitakueleza
kila kitu.Kuna uchunguzi
unafanyika hivi sasa kubaini
sababu ya kuanguka kwa ndege ya
rais Anorld Mubara na kusababisha kifo chake miaka
kumi iliyopita.Katika uchunguzi
huo imebainika kwamba
mumeo
George Mzabwa alikuwa na
mawasiliano na watu
wanaosadikiwa kusababisha ajali
ile na kumuua rais Anorld”
Mstuko alioupata mke wa
George ulikuwa mkubwa
“Mume wangu anahusika
katika kuilipua ndege ya rais?
Akauliza
“Bado haijathibitika hivyo
lakini kitendo cha kuwa na
mawasiliano na watu
waliosababisha ajali hiyo
kinaashiria kwamba mumeo
anaweza kuwa alihusika katika
ajali ile.George aliamua kujipiga risasi ili kuilinda familia yake
kwani watu aliokuwa
anashirikiana nao ni watu hatari
na wangeweza hata kuteketeza
familia yote ili kuharibu ushahidi
wasigundulike”
“Oh Mungu wangu !! akasema
yule mama
“Simu ya George” Theresa
akaendelea
“Alikuwa anaitumia kwa
mawasiliano ina ushahidi wa
kutosha wa mawasiliano yote kati
yake na hao wenzake na hiyo ni
hatari kubwa sana kwenu kwani
hao jamaa hawatalala hadi
wahakikishe wameipata simu hiyo
yenye mawasiliano kati ya George
na hao watu .Hamtakuwa salama kwani watu hao watawawinda kila
dakika hadi wahakikishe
wameipata hiyo simu ili kuendelea
kuificha siri yao”
“Kwa hiyo
nifanyaje?Nimechanganyikiwa
sijui cha kufanya”
“Sikiliza mama,mimi ni ndugu
wa rais na ninao uwezo wa
kukulinda lakini kikubwa
unachoweza kukifanya ni
kuhakikisha unaipata hiyo simu ya
mumeo na kufahamu watu
aliokuwa anashirikiana nao
.Nakuahidi kwamba ukifanikiwa
kunipa hiyo simu na tukafanikiwa
kuwafahamu hao washirika wake
nitakuombea ulinzi mkali toka kwa rais na familia yako itakuwa
salama”
“Unanichanganya sana na
sielewi nitaipataje hiyo simu toka
kwa polisi kabla hawajamaliza
uchunguzi wao.Lakini….” akasita
kidogo
Unanichanganya sana na
sielewi nitaipataje hiyo simu toka
kwa polisi kabla hawajamaliza
uchunguzi wao.Lakini….” akasita
kidogo
“Kuna kitu nimekumbuka
labda kinaweza kuwa na msaada
kwako.Tunayo nyumba yetu mpya
ambayo George alipanga tuhamie
baadae iko miembe pacha .Katika
chumba cha kulala kuna kasiki
ambalo alikuwa anahifadhi vitu
vyake vya siri.Inawezekana labda
katika kasiki hilo kuna vitu vya
msingi vinavyoweza kukusaidia
kuwafahamu hao watu aliokuwa
anashirikiana nao.Nilihisi lazima kuna jambo alikuwa ananificha na
sikujua kama linaweza kuwa
jambo kubwa kama hili la
kushirikiana na wauaji wa rais”
“Tunaweza kwenda huko
miembe pacha”
“Hakuna tatizo tunaweza
kwani nahisi yawezekana hata
katika kasiki hilo kutakuwa na
fedha alikuwa anaficha” akasema
mke wa George wakaondoka
kuelekea miembe pacha.Wakiwa
njiani mke wa George akapigiwa
simu na kupatwa na mstuko
mkubwa kwa taarifa aliyopewa
“Mungu wangu !! akasema
“Kuna nini mbona umestuka?
Theresa akauliza “Nimetaarifiwa kwamba kuna
kundi la watu wamevamia
nyumbani kwangu wakiwa na
silaha wakinitafuta mimi na
wameua watu wawili kwa
risasi.Nimeambia alijitokeza mtu
mmoja akadai kwamba yeye ni
ndugu wa marehemu na
akapambana nao akafanikiwa
kuua wavamizi watano na wengine
wakakimbia.Polisi tayari
wamefika na ninatakiwa kurejea
nyumbani mara moja.Ee Mungu
mitihani gani hii inatupata? Mbona
ni mgumu kuzidi uwezo wangu?
Akasema mke wa George akilia
kwa uchungu
“Watu hao ndio wale
niliokuwa nakueleza kwamba mumeo alikuwa anashirkiana
nao.Nadhani sasa umeyaamini
maneno yangu”
“Jamani nitawapeleka wapi
watoto wangu?Mbona George
ametuachia matatizo makubwa
namna hii? Akaendelea kulia mke
wa George
“Usilie mama tutakulinda
.Kitu cha msingi ni wewe kufuata
maelekezo nitakayokupa.Hawa
jamaa lazima watarudi tena na
tena hadi watakapohakikisha
wanapata kile
wanachokihitaji.Nitakuombea
ulinzi kwa rais lakini nawe
unapaswa kunipa ushirikiano ili
tuweze kuwafahamu hao watu ni
akina nani”akasema Theresa na safari ikaendelea huku mke wa
George akiendelea kutiririsha
machozi
“Hizi ndizo athari za kujiingiza
katika makundi hatari kwa tamaa
ya fedha na unapoondoka
unawaachia familia yako matatizo
makubwa kama George
aliyomuachia mke
wake.Namuonea huruma sana
huyu mama hakuwa akifahamu
chochote kuhusu mambo
aliyokuwa anayafanya mume
wake” akawaza Theresa
Kwa maelekezo ya mke wa
George waliwasili eneo la miembe
pacha katika nyumba mpya ya
George.Ilikuwa ni nyumba kubwa
nzuri.Pembeni ya nyumba hiyo kulikuwa na nyumba nyingine
ndogo ambayo aliishi muangalizi
wa ile nyumba kubwa.Mke wa
Georgia akamtaka yule jamaa
amletee funguo za nyumba kubwa
wakaingia ndani
“Nyumba nzuri sana na kuna
kila kitu humu kwanini hamtaki
kuhamia huku? Theresa akauliza
“George hakutaka tuishi
huku.Nahisi alitaka kuifanya kama
sehemu yake ya siri ya kufichia
mambo yake” akasema yule mama
na kuufungua mlango wa chumba
kikubwa cha kulala.
“Hiki ni chumba chetu cha
kulala” akasema yule mama na
kufunua zuria kisha akang’oa
kigae na likaonekana kasiki “Kasiki hili ndilo George huwa
analitumia kuhifadhia mambo
yake ya siri” akasema yula mama
na kuanza kubonyeza namba
kadhaa akijaribu kulifungua
.Alijaribu kubadilisha namba mbali
mbali bila mafanikio.
“Limegoma kufunguka
.Sifahamu namba anayotumia
kufungulia hili kasiki” akasema
yule mama.Theresa
akachanganyikiwa
*******************
Mathew na Camilla waliwasili
ikulu na kukaribishwa sebuleni
kwa rais “Unafahamika sana hapa ikulu
kwani hatujapata usumbufu
wowote wa kuja kuonana na rais”
akasema Camilla wakiwa sebuleni
wakimsubiri rais
“Rais alinipa kibali cha
kuingia hapa ikulu muda wowote
niutakao bila kuzuiliwa na mtu
yeyote ili kurahisisha kazi yangu
kwa hiyo kuingia hapa ikulu ni
kama kuingia chumbani kwangu”
akasema Mathew
“Ni bahati kubwa kuwa na
ukaribu na rais.Mambo yako
mengi yatakwenda vizuri”
akasema Camilla na muda huo huo
akaingia rais Dr Vivian.Mathew na
Camilla wakasimama kwa adabu “karibuni sana.Habari za
jumapili?
“Habari nzuri mheshimiwa
rais,sijui kwa upande wako”
“Hivyo hivyo.Naona
umeniletea mrembo leo” akasema
Dr Vivian na kuachia tabasamu
“Huyu ndiye yule mgeni
wangu niliyekuomba kibali cha
kuingia nchini anaitwa Camilla
snow.Anatokea Marekani na
amekuja kunisaidia katika kufanya
uchunguzi wa lile suala” akasema
Mathew na kumgeukia Camilla
“Camilla huyu ni rais wa
jamhuri wa muungano wa
Tanzania anaitwa Dr Vivian
matope” Camilla akainuka na kwenda
kumpa mkono rais
“Nimefurahi sana kukutana
nawe mheshimiwa rais.U
mwanamke jasiri na usiyeyumba
.Hivi sasa dunia nzima
wanafahamu barani Afrika kuna
kiongozi mmoja mwanamama
mwenye ujasiri wa aina yake.Hii ni
heshima kubwa umetupa
wanawake.Hongera sana
mheshimiwa rais” akasema
Camilla.Dr Vivian akaachia
tabasamu pana sana
“Ahsante Camilla.Ni furaha
kubwa kwangu kukutana
nawe.Kwa kuwa uko karibu na
Mathew basi tutakuwa tunaonana
mara kwa mara kwani hapa ikulu Mathew huja kama nyumbani
kwake” akasema Dr Vivian
“Mathew nipe taarifa za
kilichotokea nyumbani kwa
George” akasema Dr Vivian na
Mathew akamsimulia kila kitu
kilichotokea Dr Vivian akashika
kichwa
“Watu hawa ni akina
nani?Mbona wanatuumiza vichwa
vyetu namna hii?akauliza Dr
Vivian akiwa amekasirika
“Hakuna taarifa zozote toka
polisi kuhusu kuwatambua wale
jamaa tuliowaua jana kule
makaburini? Mathew akauliza
“Mpaka sasa bado sijapata
jibu lolote kutokea
kwao.Nimewapa muda hadi saa saba mchana wa leo niwe
nimepata jibu .Tukiwafahamu ni
akina nani itatusaidia kufahamu
viongozi wao.Sikuwahi kufikiri
kama Nathan anaweza akanifanyia
hivi.Mapenzi yetu yalikuwa
makubwa,yalivuka kiwango cha
kawaida na ndiyo maana nikawa
kipofu,sikuona wala kusikia
kuhusu Nathan.Alinidekeza na
nikajiona ni mwanamke wa pekee
ninayependwa kuliko wote
duniani kumbe alinipofusha kwa
malengo yake.I hope he’s in hell
right now!! Akasema Dr Vivian
kwa hasira
“Ninapata hasira kila
nikimuwaza Nathan.Tuachane na
hayo .Uliniuliza kama nilikuwa na mtu wakati nikipewa majibu ya
zile namba za simu .Kama
nilivyokueleza simuni nilikuwa na
Dr Robert Mwainamela waziri wa
mambo ya nje.Huyu ni mtu
ninayemuamini sana na hawezi
kuwa na tatizo lolote ndiyo maana
nikamueleza kuhusiana na George
kuwa na mashirikiano na CIA.Ni
mmoja wa watu wanaonisaidia
mno nafikiria hata kumpendekeza
urais pale nitakapomaliza muda
wangu,anafaa sana kuwa kiongozi
mkubwa” akasema Dr Vivian
“Mheshimiwa rais,kumekuwa
na uvujaji wa taarifa zetu mbali
mbali na hata tukio lililotokea leo
linadhihirisha hilo.Wale jamaa
walipata taarifa kwamba tayari tumefahamu kuhusiana na George
kuwa na mawasiliano na Nathan
na walifika pale kwa lengo moja
kuhakikisha kwamba wanaipata
simu ya George .Wanafahamu
kwamba tukiipata tutafahamu
mambo mengi.Ukiacha mimi,wewe
na Theresa ambao tunafahamu
kuhusu George kuwa na
mawasiliano na Nathan mtu
mwingine anayefahamu alikuwa ni
Dr Robert.Mheshimiwa rais
nafahamu hautapendezwa na hili
ninalotaka kulisema lakini nahitaji
ufahamu kwamba nataka
kumchunguza Dr
Robert.Ningeweza kufanya hivyo
kimya kimya bila kukueleza
chochote lakini sitaki yaliyotokea kwa Nathan yajirudie tena na
ndiyo maana nimeona kabla
sijafanya chochote niombe kwanza
ruhusa yako.Nafahamu huyu ni
mtu wako wa karibu na
unayemuamini sana lakini
anatakiwa achunguzwe hivyo
naomba ruhusa yako ya kufanya
hivyo” akasema Mathew na sura ya
Dr Vivian ikabadilika akamtazama
Mathew kwa macho makali
“Kwa nini ufanye hivyo
Mathew? Unadhani Dr Robert
anaweza kuwa anashirikiana na
hao watu ? akauliza
“Siwezi kusema moja kwa
moja kwamba anashirikiana nao
lakini tunapaswa kulithibitishahilo kwa kufanya uchunguzi”
akasema Mathew
“Mathew siwezi kamwe
kuliruhusu jambo kama hilo
likafanyika .Dr Robert ni mtu wa
heshima sana katika taifa hili
.Anaheshimika mno ndani na nje
ya nchi na ni mmoja kati ya hazina
ya viongozi tulio nao.Zaidi ya yote
ninamuamini mno na kumfanyia
uchunguzi mtu kama huyu ni kama
kumdhalilisha”
“Mheshimiwa rais,tafadh…..”
“Mathew my word is
final.Nikisema hapana ni
hapana,tena nakuomba
usizunguke na kwenda kufanya
uchunguzi wako kwa
siri.Nikifahamu mimi na wewe tutaingia katika
mgogoro.Namuheshimu sana Dr
Robert na nina muamini pia hivyo
siwezi kwa namna yoyote ile
kuruh…..” Rais akakatisha
alichotaka kukisema baada ya
mmoja wa wasaidizi wake kuingia
na kumtaarifu kwamba kuna
mgeni alikuwa amefika anahitaji
kumuona
“Mathew natumai tumemaliza
na umenielewa.Sitaki uchunguzi
wowote kwa Dr Robert.Nikipata
taarifa zozote toka polisi kuhusu
wale watu nitakujulisha.Ahsante
sana kwa kuja kuniona na sasa
mnaweza kwenda kwani nina
wageni muhimu wamekuja
kunitembelea.Kama kuna lingine lolote nipigie simu” akasema Dr
Vivian na kuinuka akaagana na
akina Mathew wakaondoka
“Siwezi hata kidogo kuruhusu
Dr Robert akachunguzwa.Yule ni
mtu mwenye heshima kubwa sana
na siwezi kumdhalilisha kiasi
hicho.Mathew atafute wahusika
halisi wa hili jambo na si kurukia
rukia hata watu wengine
wasiohusika .Nina mfahamu vizuri
Dr Robert hawezi katu kujihusisha
na mambo ya kijinga kama hayo.Ni
mwanasiasa mzoefu,msomi mzuri
na mwenye kujiweza kimaisha”
akawaza Dr Vivian baada ya akina
Mathew kuondoka.
Mlango wa sebuleni
ukafunguliwa akaingia bi April Hudson Mubara mjane wa rais
Anorld Mubara akiwa
ameongozana na msichana mmoja
mwembamba mrefu wastani
mwenye nywele ndefu.Dr Vivian
akasimama na kuwalaki wageni
wake
“Shikamoo mama” Dr Vivian
akamsalimu bi April kwa adabu
“Marahaba Dr Vivian habari za
siku?
“Nzuri kabisa
mama.Unaendeleaje mama yangu?
“Ninaendelea vyema.Habari za
hapa?Mnaendeleaje nyie?
“Ninaendelea vyema mama”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Utatusamehe kwa kuja bila
taarifa” “Usijali mama.Hapa ni
nyumbani unakaribishwa muda
wowote bila hata kutoa taarifa”
akasema Dr Vivian,wahudumu
wakafika na kuwahudumia wageni
vinywaji na vitafunwa
“Huyu ni mwanangu anaitwa
Tausi”
“Wow ! Tausi.Unaendana
kabisa na hilo jina lako.You are so
pretty” akasema Dr Vivian
“Thank you” akasema Tausi
“Mzee Mubara alimzaa Tausi
na mwanamke mmoja toka Brazil
lakini mimi ndiye niliyemlea akiwa
mdogo na baadae akaenda kuishi
nchini Marekani na ndiyo maana
unaona hafahamu vyema kiswahili
”akasema bi April “Karibu sana
Tausi.Nimefurahi kukufahamu”
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais.Hata mimi pia nimefurahi sana
kukufahamu” akasema Tausi
“Siku hizi umekuwa kimya
sana Dr Vivian.Mbona umenitupa
mama yako namna hiyo?Hata simu
hunipigii siku hizi.Au unasubiri
hadi katika sherehe za kitaifa
ndipo tuonane ?
“Hapana mama,sijakutupa na
siwezi kufanya hivyo.Mambo ni
mengi sana.Wewe umekaa ikulu na
unafahamu namna mzee
alivyokuwa anatingwa na mambo
mengi.Hata hivyo nilifikiri
umekwenda Marekani kutokana
na ukimya mwingi” “Tanzania ndiyo nyumbani
kwangu kwa sasa na si
Marekani.Muda mwingi niko
shambani kwangu napumzika.Pole
na misuko suko iliyotokea
.Nimeona ngoja nije nimpe pole
mwanangu kwani urais ni kazi
ngumu.Usikatishwe tamaa na haya
yanayoendelea kutokea.Wewe
songa mbele wasaidie
waTanzania.Hata hivyo
nakupongeza sana kwa namna
unavyokabiliana na changamoto
mbali mbali unazokutana nazo”
akasema bi April
“Ahsante sana
mama,nashukuru.Kwa ujumla
tunaendelea vizuri.Changamoto ni
nyingi lakini tunazikabili.Nashukuru napata
uungwaji mkono mkubwa toka
kwa wananchi”
“Nafurahi kusikia hivyo .Vipi
kuhusu hili linaloendelea hivi sasa
la mvutano na Marekani,tayari
limekwisha patiwa muafaka?
“mama suala hili halina
muafaka .Tayari nimekiwisha
fanya maamuzi kwamba
nitaendelea na mchakato wa
mashirikiano na Korea Kaskazini”
“Sawa Dr Vivian kama unaona
suala hilo lina maslahi kwa taifa
basi endelea nalo”
“Ndiyo mama kuna maslahi
makubwa kwa nchi yetu kama
tutaanzisha mashirikiano ya
kiuchumi na Korea Kaskazini.Tutafaidika na kukuza
uchumi wetu.Tanzania tunapaswa
tuanze kujitegemea na ili tufikie
huko lazima maamuzi magumu
yafanwe.Tayari nimekwisha fanya
maamuzi hayo magumu na
nitahakikisha ninawaongoza
waTanzania katika safari hii hadi
tufikie kuwa nchi
inayojitegemea.Ni wakati wa
waTanzania kuamua aidha
kuungana nami katika safari hii na
kujikwamua kiuchumi au kubaki
nyuma na nchi kuendelea kuwa
omba omba lakini mimi rais wao
sintageuka nyuma.Sitaki kugeuka
jiwe,nitaangalia mbele daima.Kwa
hiyo mama safari ndiyo imeanza
na tutapitia misuko suko mingi sana.Mataifa tajiri yanaendelea
kutupa vitisho kuhusiana na
kuwekewa vikwazo vya kiuchumi
lakini mimi nasonga mbele.Kuwe
au kusiwe na vikwazo lazima
Tanzania ijitegemee kiuchumi”
akasema Dr Vivian
“Naamini huko aliko baba wa
taifa hili amejaa tabasamu usoni
pake kwa nchi kupata kiongozi
shupavu kama wewe.Endelea na
ari hiyo hiyo kuwasaidia
waTanzania”
“Ndiyo mama,waTanzania
wana shida nyingi sana na
ninayanya haya yote kwa ajili ya
kuwasaidia wao na vizazi vyao”
“Sawa Vivian.Tuachane na
hayo,vipi kuhusu masuala yako ya ndoa?Mmefikia wapi?Mara ya
mwisho tulipokutana uliniambia
kwamba bado maandalizi
yanaendelea”
“Kumetokea matatizo kidogo
kwa hiyo ile ndoa haitakuwepo
tena.Utaratibu unafanywa ili wale
wote waliotoa michango yao
waweze kurejeshewa”
“Pole sana .Nini kimetokea
Vivian na kusababisha haya yote?
“Ni mambo ya kibinafsi zaidi
sipendi kuliongelea kwa undani ila
ndoa ile haipo tena”
“Usijali mwanangu ,Mungu
ana makusudi yake.Kama
imeshindikana sasa,baadae
itawezekana.Vuta subira na
usikate tamaa” “Ahsante mama” akasema Dr
Vivian na ukimya ukatawala.Bi
April akasema
“Dr Vivian,pamoja na kuja
kukujulia hali,lakini nina shida
nyingine imenileta”
“Niambie mama ni shida gani?
“Ni huyu mdogo
wako.Ameamua kuja kuishi nami
hapa Tanzania lakini hana
kazi.Naomba umsaidie apate japo
kijikazi chochote hapa ikulu.Ni
msomi mzuri ana shahada ya
teknolojia ya mawasiliano na vile
vile anayo sahahada ya mahusiano
ya kimataifa.Aliponieleza wazo
lake hilo nikaona nikufuate
mwanangu umsaidie mdogo
wako.Nina sehemu nyingi ambazo ningeweza kumtafutia kazi lakini
nimeamua nije hapa kwako
kutokana na heshima ya mahala
hapa.Mtu anayefanya kazi ofisi ya
rais anakuwa na heshima kubwa”
akasema bi April
“Sawa mama nimekusikia na
ombi lako siwezi kulikataa.Kwa
sababu ya heshima yako na mzee
Mubara,Tausi atapata kazi hapa
ikulu.Nitakuomba Tausi uje kesho
asubuhi saa moja na nusu tayari
kuanza kazi.Njoo na vyeti vyako
vyote ili uhakikiwe na kuingizwa
katika mfumo wa ajira wa serikali”
“Ahsante sana mheshimiwa
rais kwa msaada huo mkubwa”
akasema Tausi “Usijali Tausi.Niite dada
inatosha” akasema Dr Vivian
wakaendelea na maongezi
mengine ya maisha yaliyochukua
zaidi ya saa moja kisha bi April
akasema
“Dr Vivian ,sisi inatubidi
tuondoke tukuache uendelee na
majukumu mengine kwani
tumekuvamia bila taarifa na
kuvuruga ratiba zako .Halafu kabla
sijasahau nina namba mpya ya
simu ninayoutumia hivi
sasa.Ihifadhi tafadhali” akasema bi
April na Dr Vivian akaingia
chumbani kwake akachukua simu
na kuhifadhi namba ya bi April
halafu akawasindikiza hadi nje
wakaagana na kuondoka“Nimefurahi sana
kutembelewa na wageni kama
hawa.Bi April amebaki mpweke
lakini nitahakikisha wale wote
waliomuua mumewe
wanapatikana na kufikishwa
katika sheria” akawaza Dr Vivian
Kwa zaidi ya dakika ishirini
,Theresa na mke wake wa George
Mzabwa walikuwa wanajaribu
kulifungua kasiki bila
mafaniio.Mke wa George Mzabwa
aliyekuwa amechoka alikaa
pembeni na kumuacha Theresa
naye ajaribu kufungua lakini jitihada zake zote hazikuzaa
matunda
“Tuondoke hatutaweza
kulifungua kasiki hili
leo.Nitakwenda kupekua katika
makablasha yake pengine naweza
kupata namba za kufungulia hili
kasiki”
‘hapana lazima tufungue hili
kasiki” akasema Theresa
“Hakuna namna
tutakavyoweza kulifungua hili
kasiki bila kuwa na namba
maalum za kufungulia.Twende
tuondoke nitakujulisha
nikifanikiwa kuzipata hizo
namba,ninasubiriwa nyumbani”
“Hatuwezi kuondoka hapa bila
kasiki hili kufunguliwa” akasema Theresa na kusimama akajishika
kiuno na kutafakari kwa muda
“Hapa sina namna lazima
niombe msaada kwa
Mathew.Nilitaka jambo hili liwe
siri lakini kwa hapa tulipofika maji
yamenifika shingoni.Sina utaalamu
wowote wa kufungua kasiki hili”
akawaza Theresa na kuchukua
simu akampigia Mathew
“Hallow Theresa” akasema
“Mathew kuna jambo
limetokea naomba msaada wako”
“Nini kimetokea Theresa?
Akauliza Mathew kwa wasi wasi
“Siwezi kukueleza simuni ila
nitakuelekeza mahala uje mara
moja kuna jambo la msingi sana
ambalo linaweza kutusaidia” akasema Theresa na Mathew
akasita kidogo
“Mathew” akaita Theresa
“Nielekeze mahala ulipo
Theresa” akasema Mathew na
Theresa akamuelekeza mahala
alipo.Mathew akabadili uelekeo na
kuanza kuelekea mahala aliko
Theresa
“Rais anafanya kazi yetu kuwa
ngumu kwa kuzuia kumchunguza
Dr Robert.Niko kwenye kazi hii
kwa muda mrefu na ninafahamu
mambo mengi na ndiyo maana
sikukurupuka kutaka kumfanyia
uchunguzi Dr Robert .Rais
amekosea sana kuzuia hili
lisifanyike kwani kwa sasa
hapaswi kumuamini mtu yeyote.Mtandao huu ni mpana
sana na yawezekana kuna watu
wakubwa wanahusika pia.Pamoja
na rais kumtetea sana Dr Robert
lakini bado nafsi yangu inataka
kumchunguza kiundani.Mara
nyingi nikiwa na hisia na kitu au
mtu fulani huwa ni kweli.Mara
chache sana hisia zangu hazijawa
kweli.Lazima nitafute namna ya
kumchunguza Dr Robert kwa siri”
akawaza Mathew
Iliwachukua dakika arobaini
na sita kuwasili mahala alipo
Theresa.walishuka garini kwa
tahadhari kubwa wakaenda
kugonga geti likafunguliwa na
jamaa mmoja akawakaribisha
ndani .Gari la Theresa lilikuwepo ndani.Yule jamaa akawapeleka
sebuleni ambako walikuwepo
Theresa na mwanamke mmoja
wameketi
“Mathew karibu” akasema
Theresa
“Theresa kuna tatizo gani?
Akauliza
“Mathew huyu ni mke wa
GeorgeMzabwa” akasema Theresa
“Mke wa George?!! Mathew
akashangaa
“Ndiyo Mathew.Najua
umestuka sana lakini nitakupa
maelekezo hapa baadae kwa sasa
tuelekee katika jambo muhimu
nililokuitia hapa” akasema
Theresa na kumtaka Mathew na
Camilla wamfuate wakaingia katika chumba cha
kulala,akawaonyesha kasiki
lililokuwa katika sakafu ya
chumba
“Hapa ndipo George Mzabwa
huficha nyaraka zake za siri.Nina
uhakika mkubwa kwamba
tukifanikiwa kulifungua tutapata
mambo mengi kuhusiana na
George” akasema Theresa
“Theresa umefikaje
huku?Umewezaje kuyajua haya
yote? Mathew akauliza
“Mathew tafadhali tusipoteze
muda.Tulifungue hili kasiki na
haya mambo mengine
tutazungumza baadae “ akasema
Theresa“Mke wa George hafahamu
namba za siri za kufunguliwa
kasiki hili? Mathew akauliza
“Kama angekuwa
anazifahamu ningekuomba uje
Mathew?Amejaribu namba zote
anazozifahamu lakini
imeshindikana”
“Nini kimetokea hapa? Camilla
akauliza
“Tunahitaji kulifungua hili
kasiki.George alikuwa anaficha
baadhi ya vitu vyake hapa”
akasema Mathew
“Niacheni nilifungue .Ninao
utaalamu wa haya mambo japo
itachukua muda kidogo” akasema
Camilla “Wakati Camilla akijaribu
kulifungua hili kasiki naomba
tuongee Theresa” akasema
Mathew walipofika sebuleni
walimkuta mke wa george
“Mama hawa ni wenzangu
,wote ni wafanyakazi ikulu na
tunashirikiana pamoja”Theresa
akamwambia
“Pole sana mama kwa yote
yaliyotokea.Kuna mambo
makubwa yametokea nyumbani
kwako leo na a……….”
“Tayari nimekwisha pewa
taarifa.Hapa nilipo
nimechanganyikiwa na sielewi
nitafanya nini kulinda familia
yangu” “Usihofu mama.Tutakulinda
kitu cha msingi ukubali
kushirikiana nasi”
“Mwenzenu Theresa
amenielza kila kitu na ndiyo
maana nikamleta hapa.Kitendo
alichokifanya George kushirikiana
na hawa watu waovu
kimenisikitisha sana na niko tayari
kutoa ushirikiano mkubwa kwenu
ili mradi mnihakikishie ulinzi
kwangu na familia yangu”
“Usihofu kuhusu ulinzi
utapata.Juhudi za kuwatambua
wale jamaa waliovamia nyumbani
kwako zinaendelea na kwa bahati
nzuri nilifanikiwa kupambana nao
na kuwaua watano” akasema
Mathew na mke wa George akainuka na kukaa akimtazama
Mathew kwa mshangao.
“Ni wewe ndiye uliyepambana
nao?
“Ndiye mimi”
“Niliambiwa kuna mtu mmoja
alijitokeza na kupambana na hao
wavamizi akafanikiwa
kuwashinda.Nilitamani sana
kumfahamu mtu huyo nimshukuru
kwa jambo la kishujaa
alilolifanya.Nimefurahi kukuona”
“Usihofu mama,uko salama”
akasema Mathew akatoka nje na
Theresa
“Haya nieleze nini
kimetokea?Umemtoa wapi mke wa
George? Mathew akauliza “Mathew naomba usinielewe
vibaya kwa kile nitakachokueleza
lakini ilinilazimu nifanye
hivyo.Mara tu uliponipigia simu na
kunifahamisha kuhusu George
kuwa na mawasiliano na Nathan
na ukataka kupafahamu nyumbani
kwake nilihisi lazima utakuwa na
mpango wa kwenda nyumbani kwa
George kuzungumza na mke
wake.Nilijua lazima ungekwenda
na Camilla na msingefanikiwa
kupata kitu chochote kwani yule
mama aisngekubali kutoa
ushirikiano wowote kwenu hivyo
nikalazimika kwenda haraka
haraka kuzungumza naye,
nikamdanganya na kuondoka
naye.Ili anipe ushirikiano nilimueleza ukweli kuhusu mume
wake kuwa na mashirikiano na
watu wabaya.Lengo kuu lilikua ni
kuitafuta simu ya
mumewe.Alinieleza kwambaa
hakuwa amekabidhiwa vifaa vya
marehemu kwani bado uchunguzi
wa kifo chake ulikuwa
unaendelea.Baadae akakumbuka
kwamba mumewe alikuwa
anaficha baadhi ya vitu vyake
katika hii nyumba yao mpya hivyo
tukaja hapa.Tukiwa njiani kuja
huku akapigiwa simu na
kufahamishwa kuhusiana na
kilichotokea nyumbani
kwake.Tumefika hapa
tumehagaika sana kulifungua lile
kasiki bila mafanikio ndipo nilipoamua kukupigia
simu.Utanisamehe sana Mathew
kwa kufanya jambo hili kimya
kimya bila kukushirikisha lakini
lengo langu ni zuri tu.Chochote
ambacho ningekipata hapa lazima
ningekujulisha tu” akasema
Theresa.Mathew akatumia
sekunde kadhaa kumtazama usoni
halafu akasema
“Nilipaswa nikasirike kwa hiki
ulichokifanya kwani ni kitu cha
hatari sana lakini kwa mara
nyingine tena maamuzi yako
uliyoyafanya yamekuwa na faida
kwetu.Mara ya kwanza ulifanya
maamuzi na kumuua Nathan
nilichukia sana lakini yakaibuka
mambo makubwa likiwamo hili kundi la watu wenye kutumia sare
na zana za jeshi la polisi.Leo tena
umefanya maamuzi ya kwenda
kumchukua mke wa George na
kuna mambo
yamejitokeza.Ulifanya jambo la
maana sana kwani endapo mke wa
George angekuwepo pale
nyumbani kwake sijui nini
kingetokea.Yawezekana
tusingeweza hata kufahamu kama
kuna sehemu ya siri george
alikuwa anahifadhi vitu
vyake.Ninaamini endapo
tutafanikiwa kulifungua hili kasiki
tutafahamu mambo mengi.Ila siku
nyingine usijaribu tafadhali
kufanya mambo kimya kimya bila
kunishirikisha.Mambo haya ni hatari kubwa sana kwako.Laiti
wale jamaa wangefahamu kama
umeondoka na mtu waliyekuwa
wanamtafuta hivi sasa ungekuwa
katika hatari kubwa”
“Samahani Mathew sintarudia
tena”
“Na iwe hivyo” akasema
Mathew
“Nini kilitokea nyumbani kwa
George?akauliza Theresa.Mathew
akamsimulia mkasa wote
“Dah ! poleni sana .Kuna
ulazima wa kufanya kila juhudi
kuwabaini watu hao ni akina nani
kwani wanaonekana ni watu
waliojipanga vizuri na wana uwezo
mkubwa wa kupata taarifa zozote
muda wowote ndiyo maana kila tunachokifanya wao tayari
wanakuwa na taarifa.Kuna watu
wakubwa katika mtandao huu na
tusipowatambua juhudi zetu zote
zitakwamishwa na hili genge
hatari”
“Theresa wakati unapiga simu
nilikuwa nimetoka kuonana na
rais.Kuna jambo lilinipeleka
ikulu.Nilimuuliza rais wakati
anapewa majibu kuhusiana na ile
namba ya George alikuwa na nani?
Rais akajibu kwamba alikuwa na
waziri wa mambo ya nje Dr Robert
Mwainamela.Ninataka
kumchunguza huyo Dr Robert”
“Unahisi ana mahusiano na
hao watu? Theresa akauliza ‘Sina uhakika na hilo lakini
nina wasi wasi naye ndiyo maana
nataka kumchunguza”
“Lakini Dr Robert ni mtu
mwenye heshima zake na hawezi
kujihusisha na mitandao kama hii
ya maharamia” akasema Theresa
“Hata rais naye amenijibu
hivyo”
“Tayari umemwambia
kwamba unataka kumchunguza Dr
Robert?
“Ndiyo imenilazimu
kumweleza .Sikutaka yatokee tena
kama yale yaliyotokea kwa Nathan
hivyo nikamfuata kuomba kibali
chake nimchunguze Dr Robert”
“Amesemaje?
“Amekataa” “Hawezi kukubali .Hata mimi
siafikiani na wazo hilo la
kumchunguza Dr Robert .Kuwa
karibu na rais wakati anapewa
majibu yale ya kuhusiana na
namba za simu za George si sababu
ya yeye kuwa
anahusika.Tuwatafute watu sahihi
lakini Dr Robert ninaweza
kusimama na kumtetea” akasema
Theresa
“Nimewasikia nyote lakini
kwa uzoefu nilionao katika mambo
haya naamini kabisa kuna ulazima
wa kumchunguza Dr
Robert.Mtanisamehe sana kama
nitakuwa ninamvunjia heshima
kwa kutaka kumchunguza Dr
Robert lakini ni kawaida yangu kutokuamini watu”akasema
Mathew
“So how’s she? Theresa
akabadili maongezi
“Nani ?
“Your girl friend”
“Theresa nimekwisha kueleza
kwamba Camilla ni rafiki na
mshirika wangu”
“Mhh !! Theresa akaguna
“Haya tutaona” akasema
“Twende tukamsaidie
Camilla,yawezekana anahitaji
msaada” akasema Mathew
wakaingia ndani.Simu ya Theresa
ikaita akatoka tena nje kwani
mpigaji alikuwa Dr Vivian
“Theresa uko wapi? “Niko sehemu fulani na
Mathew”
“Oh ok.Nakuomba kesho
asubuhi ufike hapa ikulu kuna mtu
nataka umpe maelekezo
machache,atakuwa anatumia ofisi
yako kwa wakati huu ambao
utakuwa unasaidiana na Mathew”
“Umepata mtu mwingine wa
kushika nafasi yangu?Theresa
akauliza
“Sina maana kwamba
ninakuondoa katika nafasi yako.Ni
hivi,amekuja bi April Mubara
mchana huu akiwa na binti yake
akaomba nimpatie kazi hapa ikulu
na mimi kwa heshima ya baba
yake nimeshindwa kumkatalia
hivyo nimemuagiza aje kesho kuanza kazi na kwa wakati huu
ambao hautakuwepo hapa ofisini
basi atatumia ofisi yako wakati
nikitafuta sehemu ya kumuweka.
Halafu nitaomba uwe karibu naye
kwani bado hajui sana kiswahili”
“Ametokea wapi hadi asijue
kiswahili?
“Ametokea Marekani ndiko
alikokuwa anaishi kwa muda
mrefu”
“Sawa dada nitakuja hiyo
asubuhi” akasema Theresa na
kukata simu
“Hii ni mipango ya dada ya
kutaka kuniondoa taratibu katika
ofisi yake.Kitendo nilichokifanya
cha kumuua Nathan bado
kinaniumiza sana.Vyovyote atakavyoamua mimi niko tayari”
akawaza Theresa wakati akirejea
ndani.Bado Camilla hakuwa
amefanikiwa kulifungua lile kasiki
“Ninao utaalamu wa
kuyafungua makasiki lakini hili
limenitoa jasho” akasema Camilla
“Tutapoteza muda mwingi
sana hapa na hatutaweza
kulifungua.Kitu pekee
tunachoweza kufanya hapa ni
kulichimba hili kasiki na
kuondoka nalo” akasema Mathew
“Lakini hatutaweza kufanya
hivyo hadi tuwasiliane kwanza na
mwenye nyumba ili akubali”
akasema Theresa na kumuita mke
wa George wakamuomba
waliondoe lile kasiki ili wakalikate.Haikuwa rahisi kwa
mke wa George kukubali lakini
alikubali na vifaa vikaletwa
likaanza kuchimbuliwa.Ilichukua
zaidi ya saa moja kuweza
kuliondoa
“Theresa wewe utamrejesha
mke wa George nyumbani kwake
na sisi tunakwenda
kulishughulikia hili kasiki na
chochote tutakachokikuta
tutakujulisha” akasema Mathew
“Mathew mke wa George
anahisi mumewe alikuwa
anahifadhi fedha nyingi humu kwa
hiyo kama mtakuta kuna fedha
huyu mama apewe”
“Usihofu Theresa,chochote
kitakachopatikana humu hakuna atakayekigusa” akasema
Mathew,wakalipakia kasiki lile
katika gari wakaondoka.Wakiwa
njiani kurejea nyumbani Mathew
akapigiwa simu na rais
“Hallow Mheshimiwa rais”
“Mathew habari za mchana?
“Nzuri kabisa mheshimiwa
rais”
“Mathew nimepigiwa simu na
waziri wa mambo ya ndani muda
mfupi uliopita anasema kwamba
jeshi la polisi limefanya uchunguzi
wa zile picha na wamesema wale si
askari wao.Ni watu waliotumia
sare za jeshi la polisi lakini si
askari polisi” “Kama si askari polisi basi
lazima wana watu wao ndani ya
jesho la polisi”akasema Mathew
“Mathew nakuomba jitahidi
sana tuweze kuwabaini hawa watu
ni akina nani.Wanazidi kuwa tishio
na wanaonekana ni watu hatari”
“Nitajitahidi mheshimiwa
rais” akasema Mathew na kukata
simu
“Rais amepewa taarifa
kwamba wale sio askari polisi bali
ni watu wanaotumia sare na vifaa
vya polisi”Mathew akamwambia
Camilla
“Marekani kuna jambo kubwa
wanalitafuta Tanzania na ndiyo
maana wametengeneza mtandao
mkubwa na nina imani mtandao huu umetawanyika katika kila
idara nyeti ya serikali .Rais
anapaswa kuwa makini sana
kwani yawezekana hata katika
watu wanaomzunguka kuna walio
katika huu mtandao” akasema
Camilla
“hilo nalikubali kabisa lakini
sisi ndio tunaopaswa kumlinda
kwa kuwa ndio tunaoitambua
hatari iliyopo.Yeye ana uhakika na
ulinzi alio nao lakini hapaswi
kumuamini mtu yeyote kwa
sasa.Hao anaowaamini leo
wanaweza kugeuka nyoka wenye
sumu kali kesho” akasema Mathew
*******************
Dr Vivian akiwa
amejipumzisha akitafakari namna
mambo yanavyokwenda akapewa
taarifa kwamba balozi wa
Marekani amefika
kumuona.Hakuweza kukataa
akaagiza akaribishwe ndani
“Amekuja kutafuta nini tena
huyu balozi? Wanataka
nizungumze lugha gani ili
wanielewe? Wanajaribu kutumia
kila mbinu kunishawishi lakini
hawatafanikiwa” akawaza Dr
Vivian na kujiweka tayari hkwenda
kuonana na balozi
“Balozi Abraham Clerck
karibu sana.habari za jumapili?
“Habari nzuri mheshimiwa
rais,samahani sana kwa kuvamia
bila taarifa”
“Usijali mheshimiwa
balozi,karibu sana”
“Ahsante” akasema balozi
Clerk na rais akamtaka waende
kuzungumza katika chumba cha
mazungumzo ya faragha
“Mheshimiwa balozi,naamini
kuna jambo lililokuleta hapa
mchana huu.Ujumbe gani
umeniletea?
“Mheshimiwa rais nimetumwa
kwako kama muwakilishi wa taifa
la Marekani hapa Tanzania na raia
wote wanaoingia na walioko hapa
nchini wote wako chini
yangu.Nimepigiwa simu na ndugu wa mtu aitwaye Nathan ambaye
nimeambiwa ni mchumba wako na
mko katika maandalizi ya kufunga
ndoa.Ndugu hao wanadai kwamba
Nathan aliondoka na kuja
Tanzania siku mbili zilizopita na
alifika hapa wa kutumia ndege ya
kaka yake ambaye ni mchezaji
maarufu na tajiri wa mpira wa
kikapu.Alipofika aliwajulisha
ndugu zake kwamba amefika
salama Tanzania na toka wakati
huo hawajawasiliana tena.Hii
imewapa wasiwasi mkubwa ndugu
zake na wamejaribu kumtafuta
sana kwa njia ya simu au mtandao
bila mafanikio ndipo walipoamua
kunijulisha mimi kama
muwakilishi wa wamarekani walioko hapa Tanzania ili niweze
kusaidiana na serikali ya Tanzania
kumtafuta.Hii si kawaida yake
kutokuwasiliana na ndugu zake.
Kwa bahati mbaya Nathan
hakufika ubalozini kutoa taarifa za
kufika kwake hivyo sina taarifa
zake na mimi kama kiongozi wa
wamarekani hapa nchini ni
jukumu langu kujua na
kuhakikisha wamarekani wote
wanaoishi au kutembelea hapa
Tanzania wako salama hivyo
Nathan kama raia wa Marekani ni
jukumu langu kufahamu mahala
alipo na kama yuko salama”
akanyamaza kidogo halafu
akasema“Mheshimiwa rais
nimelazimika kuja kwanza hapa
kwako kutokana na mahusiano
yako na Nathan ambaye ni
mchumba wako na mnatarajia
kufunga ndoa hivi karibuni hivyo
kama amekuja Tanzania ni wazi
alikuwa amekuja kwako kwani
hana shughuli nyingine inayoweza
kumleta Tanzania zaidiya
kukufuata wewe mchumba wake
hivyo kamaanakuja Tanzania
lazima akujulishe. Nataka
kufahamu mheshimiwa rais
,Nathan yuko wapi? Yuko
salama?akauliza balozi Abraham
.Dr Vivian akatazamana balozi kwa
muda akatabasamu na kusema “Kwanza naomba
nikufahamishe mheshimiwa balozi
kwamba mimi na Nathan kwa sasa
hatuna mahusiano tena.Tayari
tumekwisha tengana na hata ile
ndoa tuliyotegemea kuifunga
haipo tena.Sielewi kwa nini
amewaficha ndugu zake jambo
hili”
“Mmetengana? Toka lini?
Akauliza balozi Abraham
“Sitaki kuingia ndani zaid
kuhusiana na jambo hilo ila itoshe
tu kufahamu kwamba mimi na
Nathan hatuna tena mahusiano
.Hakuna tena ndoa.Kuhusu kuja
Tanzania sina taarifa hizo na
sijawasiliana naye na hakuwa na
sababu ya kunijulisha kama anakuja Tanzania wakati sina
mahusiano naye tena.Kama alikuja
Tanzania basi ni kwa shughuli
zake binafsi na si kwamba
amenifuata mimi”
“Mheshimiwa rais,halitakuwa
jambo rahisi kuwaeleza hivyo
ndugu zake.Nathan hana shughuli
yoyote ya kumleta Tanzania zaidi
ya kukufuata wewe mpenzi wake”
“Mheshimiwa balozi,nadhani
unanifahamu nilivyo,sina tabia ya
kurudia rudia jambo moja mara
mbili.Nimekwisha sema kwamba
sina mawasiliano wala mahusiano
na Nathan kwa sasa na taarifa za
yeye kuwepo Tanzania ninazisikia
kwa mara ya kwanza sasa hivi toka
kwako.Amekuja kutafuta nini Tanzania wakati mimi na yeye
hatuna mawasiliano? Lazima na
mimi nifahamu alichokuja
kukifanya Tanzania na kama
sintopata sababu ya msingi ya yeye
kuja nitampiga marufuku
asikanyage ardhi ya
Tanzania.Sitaki atumie ukaribu
wangu naye kwa mambo yake
binafsi!! Akasema Dr Vivian kwa
ukali
“Mheshimiwa rais ,kama
unakiri huna taarifa zozote za
kumhusu Nathan basi naomba kwa
kutumia vyombo vyako mtu huyu
atafutwe kokote aliko ili serikali
ya Marekani iwe na uhakika
kwamba mtu wao yuko
salama.Wewe kama rais unao wigo mpana zaidi wa kuweza kupata
kwa haraka taarifa za kumuhusu
mtu yeyote yule.Ni hicho tu
tunachokuomba mheshimiwa rais”
“Kama mna uhakika Nathan
alikuja Tanzania basi nitaagiza
vyombo husika vifanye uchunguzi
na kufahamu yuko wapi”
“Saa ngapi nitegemee majibu
mheshimiwa rais?
“Siwezi kukupa muda
balozi.Pale vyombo vyangu
vitakaponipa mrejesho
nitakujulisha”
“Mheshimiwa rais ningependa
suala hili lisichukue muda mrefu
,naomba ndani ya saa kumi na
mbili toka sasa niwe nimepata
majibu” “Na kama usipopata majibu
katika muda huo utafanya nini?
Akauliza Dr Vivian kwa ukali
“Nina uhakika mkubwa
kwamba ndani ya muda huo lazima
majibu yatakuwa yamepatikana
kuhusu aliko Nathan.Tanzania ina
vyombo mahiri vya uchunguzi
lakini endapo utapita muda huo
bila kupata jibu lolote tutalazimika
kuleta watu wetu kuja kufanya
uchunguzi ili tufahamu mtu wetu
aliko.Raia wa Marekani akipotea
katika nchi ya kigeni kila juhudi
itafanyika kuhakikisha
anapatikana akiwa hai au amekufa
na ndivyo tutakavyofanya kwa
Nathan.Kama sintapata mrejesho
toka kwako basi lazima watakuja hapa watu wetu kuchunguza na
kufahamu aliko Nathan”
Maneno yale ya balozi
Abraham Clerk yakaonekana
kumkera sana Dr Vivian akainuka
akamsogelea balozi Abraham.
“Nisikilize vizuri balozi,mimi
huwa sitishwi na binadamu
anayevuta pumzi kama
mimi.Namuogopa Mungu pekee
anayenipa pumzi.Hakuna mtu
yeyote wa Marekani atakayeingia
hapa nchini kufanya uchunguzi wa
kumtafuta huyo Nathan.Mimi
ndiye mkuu wa nchi hii na neno
langu ni la mwisho!!
“Nimekueelwa mheshimiwa
rais.Mimi naondoka ila nitasubiri
simu yako na muda ninaanza kuuhesabu sasa” akasema balozi
Abraham na kusimama akaondoka
“ Mathew na Theresa
wameiiniza tena katika matatizo
mengine makubwa ambayo sikuwa
nimeyategemea.Walifanya kosa
kubwa kumuua Nathan na hawa
jamaa tayari wamekwisha fahamu
kwamba Nathan ameuawa lakini
wanahitaji wathibitishe kama
kweli amekufa ama
la.Wakifanikiwa kulithibitisha hilo
utakuwa ni mgogoro mwingine
mpya.Sasa nimeona umuhimu wa
kile alichokuwa anakisema
Mathew kwamba jambo hili libaki
siri na lisifahamike.Nadhani hiyo
ndiyo njia pekee ya kuepusha mgogoro na Marekani.Kifo cha
Nathan kitaendelea kuwa siri”
Ilimlazimu Mathew kumuita
Hamis Chuma nyumbani kwake ili
amsaidie kulikata kasiki
walilolitoa nyumbani kwa George
Mzabwa.Hamis na vijana wake
wawili walifika kwa wakati na
wakaanza zoezi la kulikata lile
kasiki.Iliwachukua zaidi ya saa
moja kulikata na hatimaye
wakafanikiwa.Mathew akawalipa
ujira wao wakaondoka
“Ni muda wa kufahamu
ukweli” akasema
Mathew.Hakukuwa na fedha ndani
ya lile kasiki kama alivyosema mke
wa George bali kulikuwa na mafaili
mawili yenye nyaraka mbali mbali halafu kukawa na simu ambayo
alipoichunguza akagundua
kwamba haikuwa na laini ndani
“Mjanja sana huyu .Simu hii
ameitoa laini na hii inaonyesha
kwamba ilikuwa na umuhimu
kwake na ndiyo maana akaja
kuificha huku” Akasema Mathew
na kulifungua faili la kwanza
akaanza kulipitia nyaraka
zilizomo.Kulikuwa na risiti kadhaa
za benki zikionyesha tarehe tofauti
ambazo George alitoa fedha .Kila
risiti ilionyesha kiasi kikubwa cha
fedha .Hakuna risiti iliyoonyesha
chini ya milioni mia moja.Pesa hizo
zote alizitoa katika akaunti ya
benki moja iliyoko kwenye benki
ya Escom tawi la Tanzania. “Pesa nyingi sana hizi.Kwa
hesabu za haraka haraka
inaonyesha fedha hizi si chini ya
milioni mia tano.George alikuwa
na biashara gani ya kumuingizia
kiasi kikubwa namna hii cha
fedha? Akajiuliza Mathew na
kuendelea kupekua nyaraka
nyingine mbali mbali.Katika faili la
pili akakuta risiti tatu zikionyesha
George aliweka fedha katika
kampuni tatu tofauti zote zikiwa
katika benki ya Escom.
“Risiti zinaonyesha kwamba
George alitoa kiasi kikubwa cha
fedha katika akaunti moja na kisha
akaweka tena fedha katika akaunti
tatu tofauti zilizo katika benki hii
ya Escom.George ni mtumishi wa umma,anafanya biashara gani ya
kumuwezesha kuwa na fedha
nyingi kiasi hiki?Kuna risiti zaidi
ya tano hapa na hakuna hata risiti
moja inayoonyesha alitoa chini ya
shilingi milioni mia moja.Nadhani
tuchunguze hii akaunti ni ya
nani.Siamini kama akaunti hii ni ya
George.Kama ni yake basi
tufahamu anafanya biashara gani
hadi awe na fedha nyingi kiasi
hiki.Vile vile tuchunguze na zile
akaunti nyingine ambazo risiti
zinaonyesha kwamba aliweka
fedha” akasema Mathew halafu
akachukua simu akampigia
Theresa akamjulisha
walichokikuta katika kasiki “Ahsante kwa taarifa Mathew”
akasema Theresa na Mathew
akagundua kitu katika sauti yake
“Theresa una tatizo lolote?
“Mathew kuna jambo sikuwa
nimekueleza.Dada ameonyesha
wazi kwamba amekasirishwa na
kile nilichoikifanya kuhusu Nathan
na hanihitaji tena.Ameanza
kuniondoa taratibu ikulu karibu
yake”
“Amekuondoa ikulu? Kivipi?
Mathew akauliza
“Ametafuta mtu mwingine wa
kushika nafasi yangu na kesho
asubuhi amenitaka niwahi
nikamkabidhi ofisi”
“Amepata mtu mwingine wa
kumuandikia hotuba? “Hajasema hivyo lakini huyo
mtu aliyemtafuta ataitumia ofisi
yangu”
“Theresa bado sijakuelewa
vizuri.Kama rais hajatamka
kwamba anakuondoa katika nafasi
yako kwa nini uwe na wasi wasi?
“Amenipigia simu akaniambia
kwamba ananihitaji kesho asubuhi
nifike ikulu nimkabidhi ofisi mtu
mpya na kumuelekeza mambo
kadhaa ya pale ofisini.Ameniambia
mtu huyo anaitwa Tausi Mubara
mtoto wa marehemu Anorld
Mubara.Kuna ofisi nyingi pale
ikulu ambazo angeweza kumpa
huyu mtu wake azitumie lakini
ameacha zote na kuchagua ya kwangu.Hii ni dalili tosha kwamba
hanitaki tena”
“Umeseema amempa kazi
mtoto wa rais Anorld Mubara?
Mathew akauliza
“Ndiyo.Anaitwa Tausi”
“Usiogope
Theresa,hakutakuwa na tatizo
lolote.Dr Vivian hawezi kutafuta
mbadala wako kwani wewe ni
mwandishi mahiri sana wa hotuba
.Fanya kama alivyokuelekeza
.Halafu kesho nitaomba msaada
wako nataka kufuatilia hizi
akaunti katika benki ya Escom
kufahamu ni za nani”
“Sawa Mathew,nikitoka ikulu
tutakwenda kufanya hiyo kazi”
akasema Theresa wakaagana “Nini kinafuata baada ya
hapa? Camilla akauliza
“Kilichopo mezani kwa sasa ni
kuhusu George.Tunapaswa
kumchunguza kufahamu hizi
akaunti za benki ni zake ama za
nani.Kama ni zake tufahamu
ametoa wapi pesa nyingi namna
hii”
“Hilo ni wazo zuri lakini bado
haitoshi.Ni vipi endapo atakuwa na
biashara zake anafanya zenye
kumuingizia kiasi hicho kikubwa
cha fedha?Katika kulipitia faili hili
nimegundua kwamba kuna risiti
zinaonyesha kwamba wiki
iliyopita amelipia makontena
mawili bandarini ambayo
yalikuwa na mzigo wa baiskeli.Najiuliza mtu kama huyu
ambaye risiti zinaonyesha kwamba
ametoa mamilioni ya fedha benki
ameagiza kontena mbili za baiskeli
kwa dhumuni gani? Ana duka la
kuuza baiskeli?Hata kama akiuza
kontena hizo mbili zilizojaa
basikeli haziwezi kumpatia kiasi
kikubwa namna ile cha fedha
tulichokiona katika risiti.Kitu
kingine cha kujiuliza kwa nini
afiche risiti hizi huku ? Kama ana
biashara ya basikeli kwa nini risiti
hizi asigeziweka nyumbani
kwake?Hapa kuna jambo
limejificha?
“Ahsante Camilla kwa kuliona
hilo mimi nimepitia kwa haraka
haraka na sikutilia maanani suala hilo.Kama unavyosema hapa kuna
jambo.Nadhani tufuatilie kontena
hizi zilikwenda wapi ili
tujiridhishe kama kweli kontena
hizi zilikuwa na
baiskeli.Yawezekana labda kuna
mambo mengine tukayagundua
anayoyafanya George.Kwa kuwa
leo ofisi nyingi zimefungwa
itatubidi kazi hiyo tuifanye
kesho.Kwa muda huu wa siku
uliobaki tupate chakula tupumzike
tujiandae kwa siku ya kesho
ambayo naamini itakuwa ndefu
sana.Wewe utaendelea kupumzika
na mimi nitaelekea kuangalia
maendeleo ya ujenzi wa kiwanda”
“Hujaweka mkandarasi? “Mkandarasi yupo lakini
lazima na mimi nifuatilie kwa
karibu maendeleo ya mradi kuona
kama mambo yanakwenda sawa.”
Akasema Mathew
**********************
Mlango wa chumba cha
Mathew uligongwa taratibu na
Mathew ambaye tayari alikwisha
pitiwa na usingizi akastuka toka
usingizini na kitu cha kwanza
alichokifanya ni kupeleka mkono
wake ilipo bastora yake ambayo
huiweka pembeni.Akatazama saa
ilikuwa ni saa tano na dakika kumi
na saba za usiku.Mlango ukagonwa
tena ,akainuka akachukua bastora na kuelekea
mlangoni.Akachungulia katika
kitobo kidogo cha kumuwezesha
kuona mtu aliyeko nje akamuona
Camilla
“Camilla anatafuta nini hapa
muda huu? Akajiuliza na kufungua
mlango
“Camilla!! Akasema Mathew
“Mathew samahani kwa
kukuamsha mida hii” akasema
Camilla akiwa na kompyuta yake
mkononi
“Usijali Camilla.Karibu”
akasema Mathew na kumkaribisha
Camilla chumbani kwake
“Hujalala mpaka mida hii?
Mathew akauliza “Mimi hulala saa mbili au tatu
pekee na muda wote huwa nafanya
kazi.Tulipoachana wewe ukaja
kupumzika ,mimi nimeendelea na
kazi.Nilikuwa nachunguza hii
benki ya Escom”
“Umegundua nini kuhusu
benki hii?
“Nimegundua kwamba awali
benki hii ilikuwa inamilikiwa na
tajiri mmoja wa kifaransa na
ilikuwa inajulikana kama Pazera
commercial bank .Baada ya tajiri
huyo kufariki watoto wake
wakaiuza benki hiyo kwa tajiri
mwingine aliyewekeza sana nchini
Ufaransa anaitwa Andrew Pillar”
“Andrew Pillar?!! Mathew
akashangaa “Ndiyo. Andrew Pillar.Huyu
ndiye aliyeinunua hii benki na
kuibadili jina ikaitwa Escom bank”
“Namfahamu Andrew ni baba
mzazi wa Anderson Pillar
aliyevunja ndoa yangu na
Peniela.Sikujua kama Andrew
ndiye mmiliki wa hii benki.Ama
kweli dunia ni kijiji” akasema
Mathew.
“Sikuishia hapo” akasema
Camilla
“Nimeendelea kuichunguza
zaidi nikagundua kwamba katika
benki hii kuna wanahisa wengine
ambao niAnderson Pillar na
Peniela Mwaulaya”
“Peniela?! Akauliza Mathew
kwa mshangao mkubwa “Ndiyo.Naye ni mmoja wa
wamiliki wa hii benki.Anamiliki
asilimia thelathini na tano ya mtaji
wa hii benki”
“Umewezaje kuyafahamu haya
yote? Mathew akauliza
“Mimi ni mdukuaji mkubwa
sana na hata FBI wamekuwa
wananitumia sana kudukua taarifa
mbalimbali.Ninaweza kuingia
katika mtandao wowote ule na
kuchukua taarifa
ninayoitaka.Nimeweza kuingia
katika mtandao wa benki hii na
kupata taarifa hizi
zote.Nimekwenda mbali zaidi na
kugundua kwamba akaunti ile ya
benki inayoonyesha George alitoa
fedha ilifunguliwa nchini marekani na Geroge mwenyewe na kwa mara
ya mwisho kiasi cha shilingi za
kitandania milioni mia saba na
sabini ziliwekwa katika akaunti
hiyo kutoka kwa kampuni ya
kutengeneza saa za mkononi ya
Flamingo.Nilichunguza tena
kampuni hii ya Flamingo
nikagundua nikampuni pacha na
A.D Electronics kwani mmiliki
wake ni mmoja lakini kama
unavyofahamu kwamba A.D
Electronics ni kampuni iliyo chini
ya serikali ya Marekani kupitia
shirika lake la ujasusi la CIA kwa
hiyo hata hii kampuni ya saa ya
Flamingo nayo vile vile iko chini ya
serikali ya Marekani kwa siri”
akasema Camilla “Nimechimba zaidi”
akaendelea
“Nimegundua kwamba George
alitoa fedha nyingi katika akaunti
yake na kuziweka katika akaunti
tatu tofauti.Nimezifuatilia akaunti
zile nimegundua kwamba zote tatu
ni za kampuni ya kuchonga madini
ya vito ambayo mkewe Herieth
Mzabwa ni mkurugenzi”
Usowa Mathew ulionyesha
mshangao
“Camilla una uhakika na hayo
unayonieleza? Akauliza
“Asilimia mia moja nina
uhakika nayo.Nina utaalamu wa
hali ya juu wa kufanya udukuzi
kama nilivyokueleza” “Herieth
ametudanganya.Anafahamu kila
kitu kuhusu mumewe.Ahsante
sana Camilla kwa kazi hii kubwa
uliyoifanya ambayo imetupa
mwanga katika uchunguzi
wetu.Nimestushwa sana kusikia
kwamba Peniela ni mwanahisa
katika benki ambayo imetumika
kupitishia fedha ambazo naweza
kuziita ni chafu ambazo
zinatumika kufanikisha
operesheni mbali mbali za
Marekani hapa Tanzania.Kwa
kifupi naweza kusema kwamba
Escom bank inatumiwa au
inashirikiana na CIA.Nina wasi
wasi yawezekana hata Anderson
na baba yake Andrew Pillar wote wakawa ni CIA na wanatumia
benki yao kwa ajili ya shughuli
mbali mbali za siri za CIA.Wafanyie
uchunguzi hawa watu wawili
Anderson na baba yake li tujue
kama nao pia ni CIA” akasema
Mathew
“Kwa sasa sina mtu ndani ya
CIA anayeweza kunipa msaada
wowote.Kuna njia moja tu ya
kuufahamu ukweli ambayo sina
hakika kama utaipenda lakini
ndiyo pekee inayoweza kutusadia
kuwafahamu hawa watu wawili ni
akina nani.” Akasema Camilla
“Niambie Camilla ni njia ipi?
“Ni kumtumia Peniela”
“Peniela amezama katika
mapenzi mazito na Anderson na sina hakika kama anaweza
kukubali kunisaidia kumchunguza
mpenzi wake”
“Yawezekana hafahamu
ukweli wa jambo hili.Mpigie simu
uzungumze naye anaweza
akatusaidia na hata mwenyewe pia
itamsaidia kama akimfahamu
mpenzi wake vyema” akasema
Camilla.Mathew akachukua simu
na kuzitafuta namba za Peniela
akataka kupiga akasita
“Piga Mathew” Camilla
akasisitiza.Mathew akabonyeza
sehemu ya kupigia na simu
ikaanza kuita.Simu iliita bila
kupokelewa
“Hawezi kupokea muda
huu”akasema Mathew na mara simu yake ikaanza kuita,alikuwa ni
Peniela aliyempigia,akaipokea
haraka haraka
“Mathew mbona umepiga
usiku mwingi namna hii?
“Samahani Peniela kwa
usumbufu.Uko na mumeo?
“Ndiyo niko naye ila
nimelazimika kutoka chumbani na
kuja kuzungumza nawe huku
mbali kwani akifahamu kama
umenipigia muda huu utaibuka
ugomvi,ana wivu sana Anderson.”
“Samahani sana Peniela kwa
kukusumua usiku huu,si lengo
langu kukuletea matatizo katika
maisha yako na mpenzi lakini
nimekupigia mida hii kwa sababu
nahitaji msaada wako” “Msaada wangu?
“Ndiyo.Unakumbuka ulikuwa
unaniuliza kama kuna chochote
unaweza kunisaidia? Basi nahitaji
sasa msaada wako” akasema
Mathew na Peniela akasikika
akishusha pumzi
“Mathew muda huu si mzuri
kuzungumza mambo
hayo.Nitakupigia simu mimi
mwenyewe kesho asubuhi na
tutazungumza utanieleza unahitaji
msaada gani na kama ni jambo
lililo ndani ya uwezo wangu
nitakusaidia” akasema Peniela na
kukata simu
“Mathew usiogope kumuomba
msaada.Nina hakika hafahamu
chochote kuhusu huyo mpenzi wake na baba yake” akasema
Camilla
“Wakati tunamsubiri Peniela
kesho asubuhi,usiku huu lazima
operesheni iendelee.Mke wa
George kuna mambo anayafahamu
lazima tumfuate na atupe majibu
kuhusiana na mumewe” akasema
Mathew na kumtaka Camilla
akajiandae waelekee kwa Herieth
Mzabwa mke wa George.Wakati
Camilla akijiandaa Mathew
akampigia simu Theresa
akamjulisha kila kitu
walichokigundua na kumtaka
naye ajiandae kwani wanakwenda
wote nyumbani kwa Herieth
“Kwa nini Herieth akaamua
kutudanganya ? Ni wazi hakutaka tuufahamu ukweli ndiyo maana
akaamua kutuambia uongo.Usiku
wa leo utabaki wa kihistoria
kwake kwa yale atakayokutana
nayo” akawaza Mathew huku
akiendelea kujiandaa.Walipokuwa
tayari wakaingia garini na
kuondoka wakaelekea kwanza
kwa Theresa kabla ya kwenda kwa
Herieth
*******************
Watu wachache tu waliokuwa
macho wakati akina Mathew
walipowasili nyumbani kwa
Herieth Mzabwa.Kulikuwa na
ulinzi wa askari polisi kufuatia
tukio lililotokea mchana .Akina
Mathew wakajitambulisha kwa
askari polisi wale na
wakaruhusiwa kuingia
ndani.Mathew akamtaka Theresa
ashuke amfuate Herieth ndani na
amdanganye kwamba kuna
mamilioni ya fedha wameyakuta
katika kasiki hivyo anahitajika
akayachukue.Theresa akaingia
ndani na baada ya kama dakika
kumi akarejea akiwa
ameongozana na Herieth
akamfungulia mlango akaingia
garini wakaondoka. “Habari za usiku huu Herieth?
Akauliza Mathew aliyekuwa katika
usukani.Herieth akastuka
“Unanifahamu jina langu?
“Ndiyo” akajibu Mathew na
safari ikaendelea kimya kimya
“Tunakwenda wapi? Herieth
akauliza
“Theresa hajakueleza
chochote?
“Ameniomba tuongozane
tukaone kilichokuwamo ndani ya
kasiki” akasema Herieth
“Ndiyo tunakwenda
huko.Samahani kwa kukusumbua”
“Bila samahani”akajibu
Herieth halafu kukawa kimya
safari ikaendelea hadi walipofika nyumbani kwa Mathew,wote
wakashuka na kuingia ndani
“Herieth karibu sana.Ahsante
kwa kukubali kuongozana nasi
kuja huku usiku huu.Nitakuwa na
maneno machache sana ya kusema
kwani tayari ni usiku na unahitaji
kwenda kupumzika” akasema
Mathew na kuingia chumbani
akarejea akiwa na mafaili mawili
akayaweka mezani
“Tumefanikiwa kulifungua lile
kasiki lakini hatujakuta fedha
kama tulivyokueleza” Akasema
Mathew akamstua Herieth
“Hamjakuta fedha? Akauliza
“Ndiyo.Hakukuwa na fedha
zozote bali tumekuta vitu vichache
tu.Cha kwanza ni hii simu lakini kwa bahati mbaya haina laini na
hatujafanikiwa kupata chochote
ndani yake.Kingine tumekuta
mafaili hayo mawili yenye nyaraka
mbali mbali.Baada ya kuchambua
nyaraka zilizomo tumekutana na
risiti hizi za benki” akazichukua
risiti zile na kumuonyesha Herieth
“Risiti hizo zinaonyesha
kwamba kwa nyakati tofauti
George alitoa kiasi kikubwa cha
fedha katika akaunti iliyoko benki
ya Escom.Risiti nyingine
zinaonyesha pia kwamba kwa
nyakati tofauti George aliweka
fedha katika akaunti tatu tofauti
zilizopo katika benki hiyo ya
Escom.Tunataka utuambie je
akaunti hii ya mumeo unaifahamu? Akauliza Mathew na Herieth
akazitazama zile risiti na kusema
“Hapana siifahamu akaunti
hii.Nimestuka sana kwa jambo
hili.George hakuwahi kunieleza
chochote kuhusiana na kuwa na
akaunti katika hii
benki.Ninazifahamu akaunti tatu
alizonazo katika benki mbali mbali
na zile ambazo tumewafungulia
watoto wetu na hazina kiwango
kikubwa cha fedha kama hiki
kinachoonyeshwa katika risiti
hizi.Hatuna biashara au mradi
wowote mkubwa kutuwezesha
kuwa na kiasi kikubwa namna hii
cha fedha.Sikujua kama George
kuna mambo ananificha” akasema
Herieth akionekana kushangazwa na risiti zile.Mathew akamtazama
kwa makini sana na kuuliza
“Hizo akaunti tatu ambazo
George aliweka fedha kwa nyakati
tofauti na zote ziko katika benki
hii ya Escom.Unazifahamu?
Herieth akazipitia zile risiti
kwa makini na kutikisa kichwa
“Hapana sizifahamu akaunti
hizi”
“Una hakika Herieth? Theresa
akauliza
“Kama nilivyowaeleza
kwamba jambo hili ni geni kwangu
na George hakuwahi kunieleza
chochote.Alinificha mambo haya
yote.Kama ningefahamu moja
wapo ya hizi akaunti ningewaeleza” akasema Herieth.
Mathew alionyesha kukasirika.
“Sikiliza Herieth,naomba
utueleze ukweli.Una hakika
hauzifahamu hizi akaunti?Una
hakika George hakuwahi
kukushirikisha katika hizi fedha?
Akauliza Mathew
“Jamani nimekwisha waeleza
kwamba sifahamu chochote
kuhusiana na hizi fedha wala
akaunti hizi.Mambo haya yote
nimeyafahamu sasa hivi
kwenu.George alikuwa ananificha
mambo yake mengi ya siri”
“Herieth unafanya kazi gani
na wapi? Mathew akauliza
“Mimi? Herieth akauliza “Ndiyo.Unafanya kazi gani na
wapi?Mathew akarudia swali
“Ninafanya kazi Tanbest
Gemstone” akasema Herieth huku
sauti yake ikionyesha kitetemeshi
“Unafanya kazi gani katika
kampuni hiyo?
“Mimi ni mkurugenzi.Kwani
vipi? Akauliza Herieth akionekana
kustushwa sana na kuulizwa kazi
yake
“Herieth mimi na wenzangu
hawa unaotuona hatulali
tukipambana kwa ajili ya
kuhakikisha nchi inakuwa salama
kwa hiyo pale anapotokea mtu au
kikundi cha watu wakawa kikwazo
katika kufanikisha majukumu
yetu,huwa tunakuwa wakatili sana” akasema Mathew huku
akimtazama Herieth kwa macho
makali na kumuogopesha
“Tumegundua unatudanganya
na umetuudhi
sana.Umetulazimisha tuvae sura za
kazi na endapo utaendelea
kutudanganya yawezekana
usilione jua la kesho”
Kauli ile ikamuogopesha sana
Herieth midomo ikamtetemeka
“Narudia tena kukuuliza
Herieth hizi akaunti unazifahamu?
Herieth hakujibu kitu
akatazama chini
“Ninaomba jibu
Herieth,unazifahamu hizi akaunti?
Mathew akauliza kwa sauti ya juu “Sizifahamu” akajibu .Mathew
akamtazama na kushusha pumzi
“Sikiliza Herieth,tayari
tunafahamu kila kitu ila tunakata
tufahamu zaidi toka kwako ila
umeamua kutudanganya
.Tunafahamu akaunti ile ambayo
mumeo alitoa fedha ni ya kwake
.Mumeo alilipwa fedha nyingi toka
kampuni ya Flamingo
inayotengeneza saa za
mkononi.Baada ya kulipwa fedha
hizo akazitoa na kuziweka katika
akaunti tatu tofauti za kampuni ya
Tanbest ambayo wewe unafanya
kazi kama mkurugenzi.Herieth
naomba niwe wazi kwako kwamba
hapa hauna ujanja na
kitakachokuokoa ni kusema ukweli.Nataka kufahamu
mahusiano ya George na hii
kampuni ya Flamingo.Kwa nini
fedha iwekwe katika akaunti yake
halafu ihamishwe na kuwekwa
katika akaunti za kampuni
yenu?akauliza Mathew
“Mimi sifahamu chochote
kuhusiana na masuala ya fedha za
kampuni yetu”
“Herieth unazidi
kuniudhi.Tafadhali nieleze ukweli
ama sivyo nitakuharibu sura
yako.Sitaki kukupa maumivu
mengine hasa kwa wakati huu
unaoendelea kumlilia mumeo”
“Kweli sifahamu chochote
kuhusiana na hizi fedha za kampuni wala mahusiano ya
George na kampuni unayoisema”
“Muda wa mchezo
umekwisha” akasema Mathew na
kuinuka akaenda chumbani kwake
na kurejea na kisanduku kidogo
akatoa kifaa fulani kidogo mithili
ya mashine ya kunyolea nywele
akakichomeka katika umeme
kikatoa cheche
“Huu ni umeme na endapo
hautakuwa tayari kusema ukweli
nitakuchoma na umeme utasikia
maumivu makali mwili
mzima,utatamani roho ikutoke
lakini hautakufa bali utahisi
maumivu kama uko
jehanamu.Sitaki kufika huko
naomba unieleze ukweli ili ujiepushe na mateso makali.Najua
unaufahamu ukweli ila unatuficha”
akasema Mathew
“Jamani mtaniumiza bure
mimi sifahamu chochote.Japokuwa
ni mkurugenzi lakini jambo hili
silifahamu kabisa.Naomba
mniamini.Kama ningetaka
kuwaficha jambo nisingekubali
kuwapeleka mahala mume wangu
anakoficha siri zake.Naomba
mniamini jamani sifahamu
chochote”
Mathew akampa ishara
Camilla ambaye kwa kasi ya aina
yake akaikamata mikono ya
Herieth akaifunga kamba na
Mathew akakiwasha kifaa kile na
kukigusisha katika ngozi ya Herieth ambaye alipiga ukelee
mkubwa sana.
“Nadhani sasa umeyaona
maumivu yake na hapa ni mwanzo
tu,nitakuwa naongeza chaji kila
wakati hadi utakaposema ukweli”
akasema Mathew
Huku akitetemeka mwili na
machozi kumtoka,Herieth
akasema
“Mtaniua bure jamani
sifahamu choch……” Kabla
hajamaliza sentensi yake Mathew
akakiweka tena kila kifaa mguuni
na Herieth akapiga kelele
“Sema ukweli!! Akafoka
Mathew
“S..ss..sss..ifa..sffaaham….”
“Mathew !! akaita Camilla
“Huyu hatatueleza
chochote.Naomba unipe dakika
tatu tu nimfumbue
mdomo.Hatuwezi kupoteza muda
kwa mtu mmoja” akasema Camilla
na kumfungua Herieth mikono
halafu akafungua kiboksi kile cha
Mathew alichokiweka mezani
akatoa kifaa kidogo kwa ajili ya
kushikia vitu vidogo kijulikanacho
kama koleo akamfuata Herieth na
kumnasa kibao
“Nitazame usoni !! akasema
kwa ukali na kumuinua Herieth
kichwa
“Nimepewa dakika tatu tu za
kumaliza kiburi chako.Nataka
kabla ya muda huo kuisha utueleze
ukweli.Kabla sijaanza kukuharibu naomba utupe ukweli!!! Akasema
Camilla lakini Herieth hakufumbua
mdomo
“Nitahesabu sekunde tano
ufumbue mdomo wako na kusema
ukweli !! akasema Camilla na
kuanza kuhesabu sekunde na
zilipotimu sekunde tano bila
Herieth kufumbua mdomo,mara
ghafla kwa kasi ya umeme Camilla
akaukamata mkono wake wa
kushoto na kukikamata kidole
kidogo cha mwisho kwa kutumia
ile koleo na mlio wa kitu kigumu
kuvunjika ukasikika.Alikuwa
amekikata kidole .Akawahi
kumziba Herieth mdomo asipige
kelele “Huu ni mwanzo tu na kama
hautatueleza tunayoyataka ndani
ya dakika tatu nitamaliza vidole
vyako vyote !! akasema Camilla
kwa ukali.Damu nyingi ilikua
inatoka kwenye jereha .Theresa
aliyekuwa pembeni akishuhudia
kilichokuwa kinaendelea mle
ndani akaogopa sana.Camilla
akaukamata tena kwa nguvu
mkono wa Herieth alioukata
kidole na kukibana kidole cha pili
“Basi !! basi !!! nitasema..”
akasema Herieth kabla Camilla
hajakuondoa kile kidole
alichokuwa anajiandaa kukikata
“Nitasema !!..Nitasema !!
akasema Herieth huku
akiweweseka.Mathew akachukua dawa na kumwagia lile jeraha na
kulifunga damu isiendelee kutoka
“Haya tueleze” akasema
Camilla.Herieth akafuta machozi
akasema
“Kampuni yetu na kampuni ya
Flamingo ni washirika wa biashara
.Tunawauzia madini ya vito kwa
ajili ya kutengenezea saa za
thamani.Kuhusu masuala ya fedha
mimi sifahamu chochote kwani
mimi kazi yangu ni usimamizi tu
na sishiriki kabisa na masuala
yoyote ya kifedha.George na
mkurugenzi mkuu ni marafiki na
ndiyo maana ilikuwa rahisi mimi
kupata kazi katika hii kampuni ila
sifahamu kuhusiana na hayo
masuala ya fedha” “Mkurugenzi wako mkuu
anaitwa nani? Mathew akauliza
“Anaitwa Ranbir Kumar .Huyu
ndiye anayeweza kuwaeleza kila
kitu kuhusiana na fedha na
chochote mtakachohitaji
kufahamu kuhusu hii kampuni”
akasema Herieth
“Unatupeleka sasa hivi mahala
anakoishi huyo mkurugenzi wako”
“Sifahamu anakoishi “
akasema Herieth .Kwa kasi ya aina
yake Camilla akaushika mkono wa
Herieth na kukibana kidole kimoja
kwa koleo.Herieth akapiga kelele
akitaka Camilla asimkate kidole
“Msiniumize jamani.Kweli
sifahamu nyumbani kwa Ranbir
labda naweza kuwasaidia mkaonana naye.Nitampigia simu
na kumjulisha kwamba nina tatizo
na atakuja mara moja” akasema
Herieth na Mathew akatoa simu
yake ana kumtaka amtajie namba
za simu za Ranbir
Kumar,akampigia na simu ikaita
akampa Herieth
“hallow !! ikaita sauti ya
upande wa pili
“Mr Ranbir ni mimi Herieth”
“Herieth !!
‘Ndiyo .Samahani kwa
kukupigia mida hii”
“Herieth kuna tatizo lolote?
“Ndiyo Ranbir nina tatizo ila
siwezi kukueleza simuni naomba
tuonane ni muhimu sana” Ranbir Kumar akasikika
akivuta pumzi ndefu na kuuliza
“Herieth ni tatizo gani ambalo
huwezi kunieleza
simuni?Hatuwezi kuonana kesho?
“Hapana Ranbir.Nadhani
umesikia kilichotokea leo
nyumbani kwangu.Maisha yangu
yako mashakani nahitaji msaada
wako wa haraka.Nisingeweza
kukupigia kama sina shida ya
muhimu”
“Sasa hivi uko wapi ? Ranbir
akauliza
“Niko katika nyumba yetu
nyingine.Sitaki kulala pale
nyumbani ulipo msiba ndiyo
maana nimekuja hapa mahala ambako hapajulikani” akasema
Herieth
“Nieleze mahala ulipo”
akasema Ranbir
“Ninakutumia sasa hivi
ujumbe wenye maelekezo ya
mahala nilipo na namna
unavyoweza kufika” akasema
Herieth na kumpa simu Mathew
ambaye alimuandikia ujumbe
Ranbir na kumtumia.Baada ya
muda Ranbir akapiga.
“Herieth huko ulikonielekeza
sintaweza kufika kwa sababu
umekwishakuwa usiku mwingi na
isitoshe sijawahi fika.Kama
unaweza tukutane pale shimoni
Casino nyuma ya Jamina
Tower.Ukifika hapo nipigie simu
unijulishe”
“Tujiandae tuondoke.”
Akasema Mathew.Herieth
akabadilishwa mavazi kwani yale
aliyokuwa nayo yalikuwa
yamechafuka kwa damu ,akapewa
pia dawa ya kutuliza maumivu
kisha wakaondoka.
“Mmeniumiza sana bila kosa
lolote na kunipa ulemavu wa
kudumu.Sintawasahau wala
kuwasamhehe kwa hili
mlilonifanyia.Sijawahi kukutana
na watu wakatili kama ninyi”
akasema Herieth kwa hasira
akitazama mkono wake
“Haya yote yametokea kwa
sababu ya ubishi wako.Ungeshirikiana nasi
yasingekukuta haya.Jilaumu
mwenyewe na kiburi chako!!
Akasema Mathew na safari
ikaendelea kimya kimya
“Sijawahi kushuhudia mtu
akifanyiwa ukatili mkubwa wa
kukatwa kidole
chake.Nimewaogopa sana hawa
watu wawili.Afadhali Mathew ana
moyo wa huruma lakini huyu
Camilla ni mbaya sana.Ana roho ya
kikatili.Sura yake na mambo
anayoyafanya haviendani kabisa”
akawaza Theresa ambaye alikuwa
kimya sana toka aliposhuhudia
Herieth akikatwa kidole
“Lakini hawa jamaa kweli
wamebobea katika mambo ya uchunguzi.Wamewezaje kufahamu
mambo haya yote kuhusu George
na mkewe?tayari kuna dalili za
Marekani kuhusika katika mauaji
ya baba lakini sitaki Mathew
aufahamu ukweli kwa nini
walimuua.Ni mimi pekee
ninayeufahamu kwa nini baba
aliuawa na nimekwisha jilisha
kiapo cha kutomueleza chochote
mtu yeyote .Nina hakika hata naye
kama ilivyokuwa kwa
waliomtangulia atakutana na giza
nene.Atayafumbua mengi
yaliyojificha lakini hataweza
kuifahamu siri hii niliyo nayo.”
Akawaza Theresa huku gari
likienda kwa kasi kubwa .Walifika shimoni Casino,moja
ya Kasino kubwa lililojengwa chini
ya Ardhi.Mathew akampa simu
Herieth akamtaka ampigie Ranbir
amjulishe kwamba tayari
amekwisha fika.Herieth akampigia
simu Ranbir akamjulisha
amekwisha wasili pale kasino
“Nenda katika maegesho ya
upande wa kusini angalia gari
litakalowasha taa mara tatu
haraka haraka kisha usimame
hatua kumi na tano” Ranbir akatoa
maelekezo.
Herieth akawaeleza akina
Mathew alivyoelekezwa na
Ranbir.Mathew akamtaka
waongozane “Hapana hilo si wazo zuri
Ranbir akiona nimeongozana nawe
atapata wasiwasi.Kama
hauniamini nitaongozana na
Theresa na nikisha onana na
Ranbir nitampa ishara aje
awastue” akasema Herieth.Mathew
akamtazama Theresa
“Ngoja niende naye” akasema
Theresa
“Herieth nakuonya don’t try
anything stupid !! akasema
Mathew .Herieth na Theresa
wakashuka garini wakaanza
kutembea kuelekea mahala
alikoelekeza Ranbir Kumar.Taa za
gari zikawaza mara tatu haraka
haraka na ile ilikuwa ni ishara
kwamba tayari Ranbir amekwisha muona akasimama kama
alivyokuwa ameelekezwa.Baada ya
dakika nne mlango wa gari
ukafunguliwa akashuka jamaa
mmoja mfupi mnene akawafuata
akina Herieth
“Herieth ! akasema
“Ranbir ,samahan sana kwa
kukusumbua”
“Bila samahani .Huyu ni nani?
“Huyu ni rafiki yangu ndiye
aliyenileta hapa anaitwa Theresa”
akajbu Herieth halafu akamgeukia
Theresa
“Theresa naomba ukanisubiri
garini nina mazungumzo ya
faragha na Mr Ranbir” akasema
Herieth na Theresa akageuka akaondoka kurejea garini waliko
akina Mathew
“Herieth kuna nini?Kwanza
pole sana kwa mambo yaliyotokea
leo nyumbani kwako.Uko salama
lakini? Ranbir akauliza baada ya
Theresa kuondoka
“”Ranbir haraka sana ingia
garini tuondoke eneo hili”
akasema Herieth huku akimvuta
mkono Ranbir akimuongoza
kuelekea garini
“Theresa ulisema una tatizo
na nimekuja kukusikiliza.Nieleze
tafadhali tatizo lako”
“Ranbir tafadhali ondoa
kwanza gari tutazungumza huko
mbele baada ya kutoka hapa” akasema Herieth lakini bado
Kumar aliendelea kumtazama
“Ondoa gari Ranbir.Hili si
eneo salama.Kuna hatari kubwa
hapa”
“Sikuelewi Herieth,kuna
hatari gani?Eneo hili upo ulinzi wa
kutosha na ni sehemu salama
ndiyo maana nikaomba tukutane
hapa.Una tatizo gani? Akauliza
Ranbir
“Ranbir kuna watu
wanakutafuta.Wanataka
wakukamate
wakuhoji.Wamenitesa sana hadi
wamenikata kidole”
“Kuna watu wananitafuta?!!
Ranbir akashangaa “Ndiyo.Ondoa gari haraka
nitakueleza kila kitu” akasema
Herieth
“Herieth nashindwa
kukuelewa una maanisha nini?
Hebu jaribu kuwa muwazi nini
hasa kimekutokea?Akina nani
wamekukata kidole?Kwa nini
wananitafuta mimi? Hebu
funguka”
“Yule mwanamke niliyekuwa
naye hapa amekwenda kuwaita
wenzake na muda wowote
watafika hapa.Wanakutafuta
wewe.Wamenitesa sana
niwaelekeze mahala ulipo
na..”Herieth hakumaliza sentensi
yake Mathew na Camilla wakatoea “Hawa hapa wamefika.Ondoa
gari !! akapiga ukelele Herieth na
Ranbir akawasha gari akaliondoa
kwa kasi.Camilla akatoa bastora
yake lakini Mathew akamzuia
“Kuna ulinzi mkali eneo hili
hatupaswi kufanya vurugu
zozote.Twende tuwafuate”
akasema Mathew wakakimbia kwa
kasi kurejea katika gari lao
.Mathew akaliwasha gari na wakati
huo gari la Ranbir lilikuwa
linatoka getini.Mathew akaliondoa
gari kwa kasi kubwa kuwafuata
“I’m so stupid !! Kwa nini
nilimuamini Herieth aende peke
yake? Tayari ametuchezea
mchezo.Lazima kwa namna yoyote
ile tuwapate.Herieth anafahamaukila kitu na ndiyo
maana licha ya kumtesa alikuwa
mgumu sana kufunguka.Lazima
tuwapate kwa namna yoyote
ile.Hawa waatupa ufumbuzi wa
mambo mengi” akawaza Mathew
akiwa ameuma meno kwa hasira
“Wale ni akina
nani?Unawafahamu? akauliza
Ranbir akiwa na wasi wasi
mwingi.Herieth akamueleza kila
kitu.Ranbir aliogopa sana
akageuka nyuma na kuona kuna
gari mbili yuma yao.Akaongeza
mwendo na kukata kushoto
kuingia katika barabara ambayo
usiku huu haikuwa na
magari.Mojawapo ya zile gari mbili zilizokuwa nyuma yao nayo
ikakata kona
“Wanatufuata !! akasema
Ranbir kwa woga.Akamuelekeza
Herieth afungue droo ya gari atoe
simu aiwashe.Herieth akafanya
hivyo na kumpa,akatafuta namba
fulani akapiga
Gari la akina Mathew likiwa
katika mwendo mkali sana mara
simu yake ikaita ,akatazama
mpigaji alikuwa ni rais
“Rais anataka nini usiku huu?
Akajiuliza na kuipokea
“Hallow Mheshimiwa rais”
akasema
“Mathew samahani kwa
kukuamsha mida hii” “Usijali mheshimiwa rais
sijalala bado niko barabarani
naendelea na kazi yangu”
“Usiku wote huu?!
“Ndiyo mheshimiwa rais kazi
zetu hizi hazina muda maalum”
“Sawa Mathew naomba
unisikilize vizuri .Sitisha kwanza
operesheni zako zote ninakuhitaji
hapa ikulu mara moja”
Mathew akastuka
“Mheshimiwa rais tuko katika
operesheni muhimu sana ambayo
inaweza ikatupa mwangaza
mkubwa hivyo hatuwezi kuja huko
sasa hivi hadi hapo
tutakapokamilisha operesheni
yetu” “Mathew hili si ombi bali ni
amri na ninakuonya usijaribu
kuipuuza amri ya rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania !!
“Mheshimiwa rais umetupa
kazi tuifanye na ndicho
tunachokifanya hivi sasa.Kuna mtu
muhimu sana ninamfukuzia
mwenye taarifa za muhimu na
ambaye nikimpata atatusaidia
kufahamu mambo mengi” akasema
Mathew na kukata simu
akamuamuru Camilla aizime
kabisa
“Rais anataka nini? Theresa
akauliza
“Anataka tuachane na kazi hii
haraka tuelekee ikulu”
“Ana tatizo lolote? “Hajasema kama ana tatizo ila
ametoa amri tuachane na
operesheni hii tuwahi ikulu
haraka”
“Yawezekana labda amepatwa
na tatizo au ana jambo la muhimu
la kutuambia ndiyo maana
amesema hivyo”
“Hata kama ana jambo la
msingi sana la kutuambia
atatusubiri hadi hapo
tutakapomaliza operesheni
yetu.Hatuwezi kuwaacha akina
Ranbiri wakapotea wakati tayari
wamekwisha onyesha kwamba
kuna mambo wanayaficha”
“Lakini Math……………!!
“No Theresa.Hatuendi kokote
hadi kwanza tuhakikishe tumewapata akina Kumar.Rais
atatusubiri”akasema Mathew na
kuongeza mwendo wa gari
kulifukuzia gari la akina Kumar
lililokuwa linakwenda mwendo
mkali sana.Kabla hawajafika
katika makutano ya barabara ya
Twiga na Mangaka ghafla kikasikia
kishindo kikubwa .Gari la Ranbir
liliacha njia likagonga nguzo ya taa
ya barabarani na kwa kasi
iliyokuwa nayo ikabiringika zaidi
ya mara tatu halafu ikaangukia
katika mtaro.Umbali uliokuwepo
kati ya gari la Kumar na la kina
Mathew haukuwa mrefu hivyo
ilipotokea ajali ile ilimlazimu
Mathew kufunga breki ya ghafla na
gari likaserereka hadi mtaroni.Hakuna aliyeumia zaidi ya
michubuko midogo
midogo.Milango ilikuwa
imejifunga hivyo jitihada za
kujiokoa zikaanza.Camilla ambaye
upande wake ulikuwa
juu,akakipiga kioo kikavunjika na
kutoka kupitia dirishani na mara
tu alipotoka akaona kitu
kilichomstua.Watu wawili wakiwa
na makoti meusi na mmoja wao
akiwa na bunduki ndogo
iliyofungwa kiwambo cha sauti
wakitokea katika gari la akina
Ranbir lililopata ajali,kisha
wakapanda piki piki na kuondoka
kwa kasi kubwa.Camilla
hakuwajali akaendelea na jitihada za kuwatoa akina Mathew mle
garini
Japokuwa tayari ni
usiku,lakini kishindo
kilichotokana na ajali ya gari lile la
Ranbir kiliwastua watu na ndani
ya muda mfupi ajali ya jali ya gari
lile la Ranbir kiliwastua watu na
ndani ya muda mfupi tayari watu
walikuwa wamefika eneo la ajali
na juhudi za uokozi
zikaanza.Mathew na Theresa
wakasaidiwa wakatoka garini na
Mathew akaelekea katika gari la
Kumar ambako watu walikuwa
wanajitahidi kuwatoa ndani ya
gari.Wa kwanza kutolewa garini
alikuwa ni Ranbir.Tayari alikwisha
fariki.Mathew akajitahidi kusogea karibu zaidi akamchunguza na
kustuka baada ya kugundua
matundu mawili ya risasi katika
paji lauso
“Risasi?!! Akashangaa
“Macho yangu hayajawahi
kunidanganya .Yale ni majeraha ya
risasi.Nani kampiga ris……………….”
Akatolewa mawazoni baada ya
Herieth naye kutolewa garini
akiwa tayari
amekwishakufa.Alilazwa pembeni
ya Ranbir na Mathew akapata
nafasi ya kumchunguza na
japokuwa alikuwa ameloa damu
lakini alifanikiwa kuyaona
matundu ya risasi .Akahisi baridi
ghafla na taratibu akajiondoa
katika lile kundi la watu akaelekea liliko gari lake.Theresa alikuwa
amekaa chini akilia
“Unajisikiaje Theresa ?
“Sijielewi Mathew,nahisi
kuchanganyikiwa”
“Pole sana” akasema Mathew
na kuwaomba vijana waliokuwepo
pale wamsaidie kutoa gari mtaroni
kwa ujira.Ndani ya dakika kumi
walifanikiwa kulitoa gari lile
mtaroni ,Mathew na akina Camilla
wakaingia na kuondoka
“Ranbir na Herieth wote
wamekufa” akasema Mathew na
Theresa akazidisha kilio
“Usilie Theresa hizi kazi
ndivyo zilivyo.Nilikutahadharisha
toka awali kwamba ujasiri
mkubwa unatakiwa hivyo nyamaza kulia shughuli bado pevu”
akasema Mathew na kumgeukia
Camilla
“Kuna jambo sikuwa
nimekueleza Mathew.Nilipotoka
ndani ya gari bado hakukuwa na
watu waliokuwa wamefika eneo la
ajali hivyo nilifanikiwa kuwaona
watu wawili wakitokea katika gari
lile tulilokuwa
tunalifukuzia.Mmoja wa watu wale
niliowaona alikuwa na bunduki
ndogo iliyofungwa kiwambo cha
sauti wakapanda pikipiki yao na
kuondoka kwa kasi
kubwa.Sikuweza kufanya chochote
kwani kwa wakati ule hata mimi
nilikuwa
nimechanganyikiwa”akasema Camilla na Mathew akavuta pmzi
ndefu
“Inawezekana hao jamaa ndio
waliosababisha ajali ile kwani
naamini walikuwa wanawasubiri
akina Kumar na walifahamu
kabisa kwamba anapita njia hii
hivyo toka kwa mbali wakaanza
kuwashambulia kwa risasi na
kusababisha gari kupotea
mwelekeo na kupata
ajali.Ninaamini kabisa watu hao ni
kutoka katika ule mtandao wa CIA
kwani waliofanya jambo hili
wamelifanya kitaalamu sana.Huu
mtandao unazidi kunipasua
kichwa dhangu.Ranbir na Herieth
wasingeweza kukimbia kama
kusingekuwa na jambo wanalolificha tusilifahamu.Kwa
sasa wote wamekufa na tumerudi
katika sifuri.Tungeweza kuwapata
tungefahamu mambo mengi toka
kwao na ndiyo maana wameuliwa
ili kutuzuia tusiweze kupata
chochote.Ninachojiuliza
wamefaamuje kama tulikuwa
tunawafuatilia akina
Ranbir?akauliza Mathew.
“Ninahisi Ranbir baada ya
kugundua kwamba tunamfuatilia
aliomba msaada na ili kulimaliza
hili suala wakalazimika kuwaua ili
kuendelea kuificha siri
yao”akasema Camilla
“Mtandao huu ni mrefu na
ndiyo maana wana uwezo wa kufahamu kila kile
tunachokifanya” akasema Mathew
‘Tumaini pekee lililobaki kwa
sasa ni Peniela ambaye endapo
atatusaidia kutupa taarifa
tunaweza kugundua mambo mengi
kuhusiana na hii benki ya Escom”
akasema Camilla
“Mathew tunakwenda
kumuona dada? Theresa akauliza
“Hapana .Hatuwezi kwenda
usiku huu.Tutakwenda kuonana
naye kesho.Lazima ajifunze
kuheshimu kazi zetu.Alitupa kazi
na atuache tuifanye bila
kutuingilia.Kitendo alichokifanya
usiku huu kututaka tuachane na
operesheni yetu sijakipenda.Kesho
tutakapokwenda kumuona nitamuuliza kwa nini alitaka
tuachane na kile tulichokuwa
tunakifanya?
“Mathew yawezekana ana
tatizo au ana jambo la maana
analotaka kutueleza” Theresa
akasisitiza
“Basi atasubiri hadi kesho”
akajibu Mathew na safari
ikaendelea kimya kimya hadi
nyumbani kwa Theresa
wakamuacha hapo na wao
wakaendelea na safari.Walifika
nyumbani Camilla akamtibu
majeraha yake madogo madogo
aliyoyapata halafu wakaketi
sebuleni
“Mathew nilichokigundua
hapa ni kwamba CIA wameweka mtandao mkubwa hapa nchini
kuna jambo kubwa wanalitafuta
hivyo inatubidi kuongeza
umakini.Mtandao waliotengeneza
una nguvu na umesambaa
sana.Tukio lililotokea usiku huu
linathibitisha hayo ninayoyasema
.Waligundua kwamba
tunawafuatilia akina Ranbir na
kama tungefanikiwa kuwakamata
kuna mambo tungeyafahamu toka
kwao hivyo wakatuma wale watu
wawili wawamalize haraka na
hivyo kuturudisha nyuma.Kila
hatua tutakayopiga toka sasa
lazima tuwe makini mno” akasema
Camilla
“Usemayo ni ya kweli
Camilla.Hii kampuni ya Tanbest Gemstone ltd inatakiwa
kuchunguzwa tuwafahamu
wamiliki wake ni akina ni kwani
inaonyesha wazi kwamba
inatumiwa na CIA kupitisha fedha
kwa ajili ya kufadhili operesheni
mbalimbali wanazozifanya hapa
Tanzania.George aliwekewa kiasi
kikubwa cha pesa na yeye
akakigawa katika akaunti tatu za
kampuni hii ya Tanbest.Itatubidi
tuchunguze fedha hizi
zilizoingizwa katika akaunti za
Tanbest Gemstone ltd zimekwenda
wapi.Kwa ujumla tupate matumizi
ya hizi pesa ili tujiridhishe
kwamba hazitumiki katika
kufadhili operesheni za CIA hapa
nchini hivyo itakuwa ni kazi ya kesho” akasema Mathew
wakaagana na kila mmoja akaingia
chumbani kwake kujipumzisha
.Mathew akarudisha kumbukumbu
ya matukio yote yaliyotokea kwa
siku nzima
“Matukio yote haya
yaliyotokea yanafanywa na
mtandao uliotengenezwa na
Marekani.Ni kitu gani hasa
wanachokitafuta hapa Tanzania?
Toka walipomuua rais Anorld ni
miaka zaidi ya kumi sasa lakini
bado wanaendelea na harakati
zao.Nini wanachokitafuta? Bado
kuna kazi kubwa ya kufanya
kufahamu ni kitu gani
wanakitafuta na kufumua kabisa
mtandaa wote” akawaza Mathew na kutazama saa ilikuwa ni sa
kumi na dakika nane.Akafumba
macho na kuutafuta usingizi
Siku mpya imeanza na
asubuhi hii taifa liliamshwa na
taarifa za kustusha kufuatia vifo
vya mkurugenzi mkuu wa kampuni
ya kuchonga madini ya vito ya
Tanbest ltd na mke wa aliyekuwa
mkurugenzi wa idara ya usalama
wa taifa Herieth Mzabwa
waliofariki katika ajali.Sambamba
na taarifa hiyo kulikuwa na taarifa
nyingine iliyoeleza kwamba ofisi
za kampuni ya kuchonga madini ya
vito ya Tanbest Gemstone ltd zilikuwa zimeteketea kwa moto
usiku huo huo.Taarifa nyingi
zilizoandikwa magazetini zilidai
kwamba Ranbir Kumar na Herieth
walifariki katika ajali wakati
wakielekea katika ofisi yao baada
ya kupata taarifa za kuungua
moto.Taarifa hizi za ofisi za
Tanbest Genstone ltd kuungua
moto zilimstua Theresa na hivyo
kumlazimu kumpigia simu Mathew
Simu ya Theresa ilimuondoa
Mathew usingizini akapokea
“Hallow Theresa”
“Bado umelala Mathew?
Theresa akauliza
‘Ndiyo bado nimelala.Macho
mazito sana”
“C’mon Mathew amka” “Unasemaje Theresa?
‘Umekwisha pata taarifa za
kilichotokea jana usiku?
“Hapana.Nini kimetokea?
“Ofisi za kampuni ya Tanbest
zimeteketea kwa moto usiku wa
kuamkia leo”
“What ?!!
“Ndiyo habari iliyoandikwa
karibu katika magazeti yote”
‘This is weird!! Akasema
Mathew
“Mathew nimekupigia kukupa
taarifa hizo.Mimi najiandaa niende
ikulu kukabidhi ofisi”
“Ahsante kwa taarifa
Theresa.Tutaonana huko ikulu sisi
pia tunakuja ikulu asubuhi hii
kuonana na rais kufahamu alikuwa anatuitia jambo gani jana usiku”
akasema Mathew na Theresa
akakata simu
“Dah ! mambo yanazidi kuwa
mambo.Ofisi za Tanbest
zimeteketea kwa moto.Hii inazidi
kunipa picha kwamba kuna jambo
linafichwa hapa ambalo lazima
tufanye juhudi kulijua.Tayari
wamejua kwamba tunafahamu
kuhusu Tanbest kuwa na
mashirikiano na kampuni ya
Flamingo hivyo baada ya kuwaua
Ranbir na Herieth wameamua
kuteketeza kabisa kampuni hii ili
kuhakikisha kwamba hakuna
nyaraka yoyote tunayoweza
kupatikana.Mapambano yanazidi
kuwa makali.Tayari tumeanza kuwatikisa na ndiyo maana haya
yote yanatokea.Upo usemi
unaosema kwamba giza
linapokuwa nene basi kunakaribia
kupambazuka.Haya yanayoanza
kutokea sasa ni ishara kwamba
tunaukaribia ukweli.Kikubwa
tunachopaswa kukifanya ni
kuongeza umakini zaidi kwani
naamini mida hii watakuwa
wanatuwinda watuondoe”
akawaza Mathew na kutoka
akaenda kugonga chumbani kwa
Camilla na hakukuwa na
mtu.Akasikia sauti ya vyombo
jikoni akaenda na kumkuta mpishi
wake wakasalimiana akamuuliza
alipo Camilla akamueleza kwamba
ameenda kufanya mazoezi ya kukimbia.Mathew akarejea
chumbani kwake kwa ajili ya
kujiandaa kuianza siku.Akiwa
bafuni akasikia mlango wa chumba
chake unafunguliwa
“Nani huyo? Akauliza
“Ni mimi Camilla”
Mathew akaoga haraka
haraka na kutoka akamkuta
Camilla amekaa sofani
“Nimekutafuta nikaambiwa
umekwenda mazoezi” akasema
Mathew
“Nilikwenda kukimbia.Huwa
ninakimbia kilometa kadhaa kila
asubuhi.Vipi wewe umeamkaje?
“Nimeamka salama kabisa”
“Kuna loote toka kwa Peniela?
Akauliza Camilla “Hapana mpaka sasa
hajanipigia simu.Kwa kuwa
aliahidi kunipigia yeye mwenyewe
ngoja nimpe muda na kama
asipopiga hadi saa nne
nitampigia.Hata hivyo kuna taarifa
nyingine nimepewa na Theresa
asubuhi hii kwamba kampuni ya
Tanbest aliyokuwa anafanya kazi
Herieth imeteketea kwa moto jana
usiku.Hii ni picha ya wazi kwamba
kuna jambo linafichwa” akasema
Mathew na Camilla akashusha
pumzi
“Kama nilivyokueleza jana
kwamba vita hii inapamba
moto,hivyo umakini na tahadhari
kubwa vinatakiwa.Watu hawa
tayari wamestushwa na hatua tunazopiga na wanafanya kila
juhudi kuhakikisha hatufanikiwi
malengo yetu.Kama wameteketeza
ofisi za Tanbest ni wazi
wameturejesha kwenye
sifuri.Hawa jamaa wako makini
mno katika kila wanachokifanya”
akasema Camilla
“Ni kweli wameturudisha
nyuma lakini wamezidi kutupa
uhakika kwamba kuna jambo
ambalo hawakutaka
tulifahamu.Tutafuta namna
nyingine ya kuendelea na
uchunguzi wetu na
ninakuhakikishia kwamba lazima
tutafahamu hicho wanachokificha”
“Tunaanzia wapi leo? Camilla
akauliza “Asubuhi hii tunakwenda
ikulu kuonana na rais halafu
tutakwenda bandarini kuchunguza
kuhusu zile kontena mbili
alizoziingiza George ambazo
nyaraka zake zinaonyesha ni
basikeli” Mathew akanyamaza
baada ya simu yake kuita alikuwa
ni Meshack Jumbo
“Mzee Shikamoo”
“Marahaba Mathew habari
yako? Unaendeleaje?
“Naendelea vyema mzee”
“Nimekupigia kukujulia hali
na kukufahamisha kwamba leo
ninaanza rasmi kazi kama mkuu
wa idara ya usalama wa taifa.Hivi
sasa naelekea ikulu na baada ya kutoka kwa rais nitaelekea ofisini
kuanza kazi”
“Ahsante kwa taarifa mzee
Jumbo mimi pia naelekea ikulu
tutakutana huko.Nahitaji kuonana
na rais asubuhi hii”
“Vipi umefikia wapi katika
uchunguzi wako?
“Bado mambo magumu ila
tukionana nitakueleza kila
kitu”akasema Mathew na kukata
simu na kumtaka Camilla
akajiandaa waanze
kazi.Walipojiandaa wakakutana
katika chumba cha chakula kwa
ajili ya kupata chai.Wakati
wakiendelea kupata chai simu ya
Mathew ikaita.Alikuwa ni Peniela “Hallow Peniela” akasema
Mathew baada ya kupokea
“Habari yako Mathew”
“Nzuri .Habari za huko?
Hajambo Anna Maria?
“Anna Maria hajambo
anaendelea vyema.Kesho ni siku
yake ya kuzaliwa”
“Nasikitika sana kwamba
sintoweza kuhudhuria.Nimebanwa
sana”
“Usijali.Jana ulinipigia simu
ukasema kwamba una jambo la
kuzungumza na una hitaji msaada”
“Ndiyo Peniela nahitaji
msaada wako .Kuna mahala
nimekwama nahitaji unikwamue”
“Sema unahitaji nini Mathew? “Nilikueleza kwamba kuna
uchunguzi ninaufanya”
“Ndiyo ulinieleza” Peniela
akadakia
“Uchunguzi wangu
umenifikisha hadi Escom Bank”
akanyamza na baada ya sekunde
kadhaa Peniela akauliza
“Umefika Escom bank?
“Ndio .Nimegundua kwamba
benki hii inamilikiwa na watu
watatu, Andrew Pillar mwenye
asilimia hamsini za hisa ,wewe una
asilimia thelathni na tano na
Anderson Pilla ana asilimia kuni
na tano” akasema
“Baada ya kugundua hivyo
nini basi unachokitaka?Siruhusiwi
kuwa na hisa benki? “Si hivyo Peniela naomba
unisikilize hadi nitakapomaliza”
“Endelea”
“Nimegundua kwamba benki
ya Escom inatumiwa kupitisha
fedha kwa ajili ya shughuli haramu
za serikali ya Marekani nchini
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment