Simulizi : The Football
Sehemu Ya Nne (4)
lakini vipi kuhusu mawasiliano
yake na Fakrim?Wote wawili ni
CIA na Nathan ndiye mtu wa
mwisho kuwasiliana na Fakrim
kwa mujibu wa maelezo
tuliyoyapata.Lazima kuna kitu
hapa tunapaswa kukifahamu
kuhusu yeye.Huyu kwa sasa ni mtu
wetu wa muhimu
sana.Tukimfanyia uchunguzi wa
kina kuna jambo
tutalifahamu.Hawa CIA huwa
hawang’ang’anii sehemu bila
faida.Kitu cha msingi tujaribu
kufahamu lini alijiunga na
CIA.Kama tukigundua kwamba
alikuwa tayari CIA kabla ya
kuanza mahusiano na Dr Vivian basi tutakuwa na uhakika kwamba
kuna jambo analitafuta” akasema
Meshack Jumbo
“Jambo la pili ambalo
nimeligundua kutokana na
mazungumzo yetu ni kwamba
Nathan anafanya kazi katika
kampuni inaitwa A.D
electronics.Nataka tuichunguze
kampuni hii inahusika na mambo
gani ili tuunganishe na kazi
anayoifanya Nathan” akasema
Mathew
“Dr Vivian hajakueleza
inahusiana na mambo gani hii
kampuni?
“Sikutaka kumuhoji kwa
undani zaidi aliponitajia tu jina la kampuni kwangu ilitosha kabisa
na sikutaka kumuhoji kwa undani”
“Ok sawa twende katika
maktaba yangu ndiko iliko
kompyuta yangu” akasema
Meshack Jumbo wakaelekea katika
maktaba yake.Mathew akaitumia
kompyuta ya Meshack Jumbo
kuitafuta kampuni ya A.D
electronics na majibu yaliyokuja
yalionyesha kwamba A.D
electronics ni kampuni kubwa
inayojihusha na utengenezaji wa
vifaa mbali mbali vya kielekroniki
.Wanatengeneza vitu kama
simu,vifaa na programu mbali
mbali za kompyuta na wana
matawi yao karibu sehemu kubwa
ya dunia. “Nathan ni CIA na uwepo wake
katika kampuni hii uanipa
mashaka kidogo inawezekana
akawa yuko hapa katika hii
kampuni kwa kazi maalum kwa
kuwa yeye ni mtaalamu wa
mawasiliano kwa mujibu wa Dr
Vivian.Naomba umpigie simu
Jimmy Snow na umuombe
akusaidie kuichunguza au kama
kuna lolote analofahamu
kuhusiana na hii kampuni ya A.D
Electronics” akasema Mathew na
Meshack Jumbo bila kusita
akachukua simu na kumpigia
Jimmy
Hallow Meshack Jumbo”
akasema Jimmy
“Habari ya saa hizi Jimmy.” “Nzuri sana Meshack Jumbo”
“Jimmy utanisamehe kwa
usumbufu mwingi ninaokupatia
lakini kabla ya kukueleza sababu
ya kukupigia napenda nikujulishe
kwamba tayari inaandaliwa ndege
maalum ya kwenda kumchukua
Camilla kule Havana na rais wetu
tayari amekwisha taarifiwa na
ametoa kibali kwa Camilla kuingia
nchini hivyo usiwe na wasi wasi
kabisa kuhusiana na usalama
wake”
“Hizo ni habari njema sana
Meshack.Bado nazidi kukusisitiza
kwamba naomba usalama kwa
mwanangu Camila uimarishwe
kwani nimekubali aje huko
kutokana na urafiki wetu mkubwa kwa hiyo sitaki kusikia ameingia
katika matatizo yoyote”
“Usihofu kuhusu hilo
Jimmy,Camilla atakuwa salama
naomba uniamini” akasema
Meshack Jumbo.
“Jimmy nimekupigia kuomba
msaada wako tena.Kuna kampuni
inaitwa A.D
electronics.Tumegundua kwamba
Nathan anafanya kazi katika
kampuni hii hivyo tunataka
kuifahamu vyema hii kampuni
.Naomba kama unaw….”
“Meshack ninaifahamu hii
kampuni A.D electronics” akasema
Jimmy
“Hii ni kampuni ambayo
inamilikiwa na serikaliya
Marekani kupitia shirika lake la
ujasusi la CIA japo jambo hili ni siri
kubwa.Kampuni hii imejizolea
umaarufu mkubwa siku za
karibuni ndani ya Marekani
kwenyewe na katika nchi nyingi
kutokana na kutengeneza bidhaa
zenye ubora mkubwa lakini kwa
bei nafuu.Wanatengeneza simu
,kompyuta,programu za kompyuta
na vituvingine mbali mbali vya
kielektroniki.Ni maarufu sana kwa
simu za EZZY ambazo ni simu
ngumu na za kisasa sana
zilizojizolea umaarufu mkubwa
hapa Marekani na duniani kwa
ujumla kutokana na ubora na
uimara wake .Siri kubwa iliyopo
katika bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hii ni kwamba kuna
program maalum za siri huwekwa
ambazo ni vigumu kuonekana au
kugundulika ambazo zinakusanya
taarifa za mtumiaji na
kuwawezesha CIA kuzipata.Kila
unachokifanya katika simu yako
CIA wanakifahamu na hiyo
inawasaidia sana kuwa na taarifa
mbali mbali za watu
wengi.Wamejikita zaidi katika nchi
za uarabuni na ni kampuni
inayoongoza kwa kugawa misaada
mikubwa katika ya kompyuta
mashuleni,viwandani n.k upande
huo wa mashariki ya kati kumbe
wana lengo la kutafuta taarifa.Hii
kampuni imewasaidia sana
kuweza kunasa mambomengi ya wale watu wanaowatafuta .Kama
Nathan anafanya kazi katika
kampuni hii basi hilo si suala la
kushanganza kwani ni kampuni
iliyo chini ya CIA lakini
wanaolifahamu hili ni watu
wachache sana ” akasema Jimmy
Snow
“Ahsante sana Jimmy kwa
taarifa hiyo nzuri.Nitawasiliana
nawe tena baadae” akasema
Meshack Jumbo na kukata
simu.Akafuta jasho katika kipara
chake
“Mathew hili jambo linazidi
kuwa kubwa na ule mwanga
mdogo uliokuwepo unazidi
kuongezeka.Jimmy snow anasema
kwamba kampuni hii ya A.D eletrocnics ikochiniya serikaliya
Marekani kupitia shirikal ake la
ujasusi la CIA.Hili ni mojawapo ya
siri za nchi ya Marekani.Kama
tulivyoona katika yale maelezo
tuliyoyatoa mtandanoi,biadhaa za
kampuni hii zinasifiwa kwa ubora
na bei nafuu.Wanafanya hivi kwa
kuwa kuna ruzuku ya serikali ya
marekani kwa hiyo kampuni hii si
haiko kwa ajili ya kutengeneza
faida.Wanatengeneza simu aina ya
EZZY ambazo ni maarufu sana
nchini Marekani. Jimmy anasema
kwamba katika vifaa
vinavyotengenezwa na kampuni
hii kama vile kompyuta,simu na
vinginevyo kuna programu za siri
huwekwa ambazo si rahisi kugundulika ambazo
huwawezesha CIA kupata taarifa
zote za mtumiaji. Wanatumia
taarifa hizi katika kufahamu
mambo mbali mbali hasa ya watu
wanaojishughulisha na mambo ya
ugaidi na ndiyo maana kampuni hii
imejielekeza zaidi katika nchi za
kiarabu” akasema Meshack Jumbo
“Dah ! kweli hili jambo
linazidi kutanuka.Kama Nathan ni
mfanyakazi wa kampuni hii na
yuko karibu na rais wa Tanzania je
yuko pale kwa ajili ya
kumchunguza rais au ni kwa ajili
ya mapenzi? Akauliza Mathew
“Kama yupo kumchunguza
rais wetu lazima tujiulize kwa nini
afanye hivyo?Kuna sababu yoyote ya Marekani kutaka kumchunguza
rais wetu ? Kama ni kumchunguza
labda waanze sasa baada ya
kuingia katika mgogoro nao lakini
kwa huko nyuma Tanzania na
Marekani hazikuwa na matatizo
yoyote na Marekani wamekuwa
wafadhili wakubwa sana wa
miradi mbali mbali ya maendeleo
katika nchi yetu hivyo sina hakika
kama walikuwa na chochote cha
kuhofia hadi wamchunguze rais
wetu.Uchunguzi wa kina
unahitajika hapa kwani Marekani
wanaweza wakamtumia katika
kupata taarifa muhimu hasa katika
huu msuguano unaoendelea hivi
sasa” akasema Meshack“Mzee ninaamini kwamba
lazima Nathan atatupeleka sehemu
ambako tunaweza kupata mwanga
wa kutosha wa jambo hili ambalo
limeanza kuchukua sura
mpya.Naomba nikuache upumzike
mimi ninaondoka ,nitawasiliana
nawe tena kesho asubuhi kukujuza
kama nimepata taarifa yoyote.Lini
unaanza kazi rasmi?
“Jumatatu nitaanza.Nina siku
mbili za kesho na kesho kutwa
kujiandaa na jumatatu
nitakabidhiwa rasmi ofisi”
“Sawa mzee usiku mwema”
akasema Mathew
“Kuwa makini sana Mathew
hili jambo limeanza kuelekea
sehemu mbaya sana” “Usijali mzee nitakuwa makini
sana” akasema Mathew na kuingia
katika gari lake akaondoka huku
kichwa chake kikiwa na mawazo
mengi sana akachukua simu na
kumpigia Theresa
“ Hallow Mathew” akasema
Theresa kwa sauti ya uchovu
baada ya kuipokea simu ya
Mathew
“Theresa umekwisha lala?
“NdiyoMathew.Unasemaje?
“Ninakuja hapo kwako sasa
hivi”
“Kuna nini Mathew?
“Kuna jambo la muhimu
.Tafadhali usinichoke” akasema
Mathew na kukata simu “Bado akili yangu inaamini
lazima kuna jambo ambalo Nathan
analichunguza kwa rais.Ninaamini
hana mapenzi ya kweli bali
amepandikizwa kwa sababu
maalum.je ni jambo gani hilo?
Lazima nifahamu kuhusu hilo”
akawaza Mathew akiwa katika
mwendo mkali kuelekea kwa
Theresa.
Haikumchukua muda mrefu
kuwasili nyumbani kwa Theresa
kwani usiku huu magari hayakuwa
mengi sana
barabarani.Alifunguliwa geti na
kukaribishwa ndani na Theresa.
“Mathew karibu.Umependeza
sana usiku huu” akasema Theresa “Nilitoka kuonana na rais
kama nilivyokueleza na sijafika
bado nyumbani kubadili
mavazi.Samahani kwa usumbufu
wangu ,nakuomba
usinichoke.Kuna jambo la msingi
sana limenileta kwako usiku
huu”akanyamaza kidogo na
kulegeza tai yake
“You have anything to drink in
here?Nahisi koo likimekauka
“Unahitaji kinywaji gani?
Maji?Theresa akauliza
“Naomba kama kuna wine
tafadhali”
Theresa akaondoka na
kurejea na chupa kubwa ya wine
na glasi mbili akaziweka mezani na kumimina kinywaji kile katika
glasi.Mathew akaigugumia yote.
“Theresa una siku ngapi?
Akauliz aMathew na Theresa
akashangaa
“Ninazo simu tatu.Kuna nini
kwani?
“Ninaziomba hapa siku zako
zote pamoja na kompyuta yako
mpakato na kama una kifaa
kingine chochote ambacho
unakitumia kwa ajili ya
mawasiliano ninakiomba hapa”
akasema Mathew na Theresa huku
akiwa katika mshangao akaenda
chumbani kwake na kurejea na
simu tatu na kompyuta ndogo
mbili.Mathew akazikagua simu zile
na kukuta mbili zina jina la EZZY akahisi mapigo ya moyo wake
kubadilika akazichuka na
kompyuta zile akazitazama na
kukta zote zina jina la EZZy
akamtazama Theresa
“Hizi kmpyuta na hii simu
ulizinunua wapi? Akauliza
“Hizi sikununua, nilipewa na
Nathan”
Mathew akahisi jasho linaanza
kumchuruzika usoni akavua koti.
“Kwani kuna nini Mathew?
Theresa akauliza
“Katika maongezi yangu na
rais usiku huu ”akasema Mathew
“Kuna mambo kadhaa
niliyagundua lakini kubwa ni
kwamba Nathan anafanya kazi
katika kampuni inayoitwa A.D electronics.Imenilazimu kuifanyia
uchunguzi kampuni hiyo kujua
shughuli inayofanya.A.D
electronics ni kampuni ya
kimarekanio ambayo
wanatengeneza vifaa vya
kielektroniki kama vile
simu,kompyuta na programu
mbalimbali za kompyuta.Hizi simu
na hizi kompyuta zote zenye
majina ya EZZY zinategenezwa na
kampuni hiyo na ndiyo maana
Nathan akakupatia” akasema
Mathew na baada ya sekunde
kadhaa akasema
“Kuna siri kubwa katika
kampuni hii anayofanyia kazi
Nathan.Hii kampuni inamilikiwa
na serikali ya Marekani kwa kupitia shirika lake la ujasusi la
CIA lakini hii ni siri kubwa na watu
wachache sana wanalifahamu hilo
ingawa kampuni hii inatajwa
kumilikiwa na matajiri wawili
wakubwa wa Marekani lakini huo
ni uongo kwani mmilki mkuu wa
hii kampuni ni serikali ya
Marekani na ndiyo maana bidhaa
za kampuni hii zina ubora mkubwa
lakini bei yake ndogo.Hii ni kwa
sababu kampuni hii haiko
kibiashara bali kwa lengo maalum”
Sura ya Theresa ikabadilika
baada ya kupata taarifa ile toka
kwa Mathew.
“Katika simu na vifaa
vinavyotengenezwa na kampuni
hii kuna programu za siri zinawekwa ambazo kazi yake ni
kuwawezesha CIA kukusanya
taarifa zote za mtumiaji.Kupitia
program hiyoya siri wana uwezo
wa kufuatilia mawasiliano yako
yote ya simu ,barua pepe n.k Hii ni
njia wanayoitumia siku hizi kwa
ajili ya kubaini watu wenye nia
mbaya na nchi yao kama magaidi
n.k.Unapoanza kutumia simu hizi
wanafahamu kabisa kwamba simu
yao au kompyuta namba fulani
inatumiwa na nani na yuko wapi
na kila siku wanauwezo wa kupata
taarifa zako”
“What ?!! Theresa akastuka
“Ndiyo hivyo Theresa.Hizi
simu zina programu maalum ya siri ambayo huwawezesha kuwa na
kila taarifa ya mtumiaji”
“Oh my God ! akasema
Theresa kwa mstuko
“Mbona umestuka hivyo
Theresa?
“Kama ni hivyo basi dada
atakuwa katika hatari kubwa sana
kwani hata dada naye anatumia
simu hizi.Nathan aligawa simu na
kompyuta hizi kuanzia kwa dada
hadi kwa wasaidizi wake wote na
ndizo wanazotumia kutokana na
ubora na uwezo wake mkubwa”
“Jesus Christ !! akasema
Mathew.
“Mpaka hapa tayari nimepata
picha kwamba Mathew yuko hapa
kwa kazi maalum.CIA wanazo taarifa zote za mawasiliano ya rais
kwa kuwa anatumia simu ile
aliyopewa na Nathan.Kama
aligawa simu na kompyuta kwa
wafanyakazi wote basi lengo lao ni
kubwa .Wanataka wawe na taarifa
nyingi nyeti za kuhusu rais na nchi
kwa ujumla.Mpaka sasa tayari
watakuwa na taarifa nyingi
kuhusiana na kila kinachoendelea
hapa nchini.Rais wetu hayuko
salama kwani hawa jamaa
wanafahamu kila kitu
kinachoendelea ikulu”akawaza
Mathew
“Mathew tutafanya nini
kumlinda rais? Kumbe yule jamaa
ni shetani mkubwa namna hii?
Sikutegemea kabisa kama Nathan ambaye analia kila siku kuwa na
mapenzi makubwa kwa dada
anaweza kuwa hivi.Mathew do
something! Akasema Theresa
“Kama rais na watu wote
wanaomzunguka walipwa simu na
kompyuta za kampuni hii basi ni
wazi ilikuwa ni kwa sababu
maalum ya kupata taarifa
mbalimbali nyeti za rais na nchi
kwa ujumla.Kitu kikubwa cha
kujuliza hapa ni je kitu gani hasa
wanakitafuta?Kwa nini
wanamchunguza rais? Lazima ipo
sababu kubwa” akasema Mathew
na kumtazama Theresa
aliyeonekana kujawa na woga
mwingi “Theresa unaweza ukanieleza
sababu ya Nathan na Dr Vivian
kutofautiana na kuamua kila
mmoja aendelee na maisha yake?
Kama unafahamu naomba unieleze
tafadhali”Mathew akasema
“Sababu kubwa aliyonieleza
dada ambayo ilisababisha
washindwe kuelewana ni
mtoto.Nathan alikuwa anahitaji
mara tu watakapofunga ndoa basi
dada amzalie mtoto lakini dada
alikataa jambo hilo na kudai kwa
sasa ana majukumu mengi na
hawezi kupata muda wa kulea.Kwa
mujibu wa dada,Nathan alimtolea
maneno ambayo hakuyapenda na
ndiyo maana akakasirika na kuamua kutengana” akasema
Theresa
“Sasa nimepata picha.Nathan
hakukurupuka katika kudai Dr
Vivian amzalie mtoto.Tunapaswa
kujiuliza kwa nini iwe sasa? Kwa
nini Nathan hakuwahi kudai mtoto
muda wote ambao walikuwa
katika mahusiano hadi aje adai
mtoto wakati huu ambao Dr Vivian
amekuwa rais?Huoni kwamba
huyu jamaa alifahamu kabisa
kwamba Dr Vivian hawezi
kukubaliana na jambo hilo hivyo
akataka kuanzisha mgogoro kati
yao ili mapoenzi yao
yasiendelee?Ni wazi kwa wakati
huu Dr Vivia ana majukumu mengi
na mazito kama mkuu wa nchi na hataweza kuwa na muda wa
kutosha kulea.Nathan alilifahamu
hilo fika lakini akaamua kuanzisha
mgogoro ili ndoa isifungwe.Kwa
ufupi naweza kusema kwamba
huyu jamaa hana mapenzi yoyote
kwa Dr Vivian bali alikuwa
ametumwa kuifanya kazi maalum
lakini swali linalokuja ni kazi gani
aliyotumwa? Ni uchunguzi gani
aliokuwa anaufanya toka angali
wako chuo?Kuna jambo ambalo Dr
Vivian amewahi kulifanya ambalo
limewafanya CIA waanze
kumchunguza toka wakati
anasoma?akasema
Mathew.Theresa hakujibu kitu
alionekana kuchanganyikiwa “Theresa hivi ndivyo
tutakavyofanya.Kuanzia sasa
usizitumie kabisa hizi simu.Kesho
tutakwenda kutafuta simu
nyingine.Rais pia anapaswa
kuacha mara moja kutumia simu
na vifaa vyote vya mawasiliano
alivyopewa na Nathan.Wale wote
waliopewa vifaa vya mawasiliano
na Nathan wote wanapaswa
kuacha kuvitumia haraka sana
lakini si kwa wakati mmoja ili
kuzuia hawa jamaa wasiweze
kustuka kwa nini imetokea ghafla
hawapati taarifa tena.” Akasema
Mathew
“Mathew lazima tumuonye
dada kuhusu suala hili lazima
aache haraka sana kutumia vifaa hivi vya Nathan.Ikiwezekana hata
usiku huu” akasema Theresa
“Hapana Theresa hatuwezi
kufanya kwa haraka namna
hiyo.Kesho asubuhi mimi na wewe
tutaongozana hadi ikulu tukiwa na
simu mpya na nitajua namna ya
kumueleza rais ili asigundue
chochote kuhusiana na
Nathan.Tafadhali nakuomba
Theresa hili suala ni la siri kubwa
kati yetu na hapaswi mtu
mwingine yeyote kulifahamu kwa
sasa.Tunaofahamu mpaka sasa
kuhusiana na Nathan ni mimi
,wewe na mzee Meshck
Jumbo.Itunze siri hii na
usimweleze mtu yeyote hadi pale
tutakapokamilisha uchunguzi wetu” akasema Mathew na kutoa
laini katika zile simu za Theresa na
kumtaka asizitumie kabisa zile
kompyuta au hata kuhamisha
mafaili katika kompyuta
nyingine.Mathew akaagana na
Theresa akaondoka kuelekea
nyumbani.Alifika nyumbani kwake
saa nane za usiku na kujilaza
kitandani
“Ni kitu gani ambacho Nathan
anakichunguza kwa Dr
Vivian?Kuna jambo ambalo si la
kawaida alilonalo Dr Vivian hata
CIA wamchunguze? Kompyuta zile
zimegawiwa kwa watu wa ikulu na
lengo likiwa ni kupata taarifa za
kumuhusu rais.Wanapata taarifa
zake zote kila siku na wanafahamu kila kitu anachokifanya au
anachopanga kukifanya.Hii ni
hatari sana kwa rais wetu hasa
katika wakati huu ambao ameingia
katika mgogoro na
Marekani.Wanaweza wakamfanya
lolote kwa wakati wowote
wanaotaka kwani wanazo taarifa
zake zote hadi ratiba zake
zote.Nathan ana mambo mengi ya
kuchunguzwa.Ni mtu muhimu mno
kwetu.Hata hivyo kuna umuhimu
wa kumchunguza pia rais
yawezekana kuna jambo fulani la
siri analo na ndiyo maana serikali
ya Marekani wanamchunguza kwa
siri” akawaza
“Kesho itakuwa jumamosi
ndefu sana.Kwanza asubuhi nataka kwenda tena kuona na rais na
kubadilisha simu zake zote pamoja
na kompyuta na kila kitu.Baada ya
hapo nitajiandaa kwa ajili ya
kumkabili Nathan ambaye
anategemea kuwasili saa nne au
saa tano za asubuhi.Kesho lazima
ukweli ujulikane kwa nini
wanamchunguza rais? akawaza
Mathew na kuanza kuutafuta
usingizi
Ni kama ilikuwa kufumba na
kufumbua
kukapambazuka.Mathew alilala
masaa machache sana na kuamka
akajiandaa kwa ajili ya kuianza siku.Alifanya mazoezi ya kutosha
akaoga na kabla ya kupata
kifungua kinywa akampigia simu
rais na kumjulisha kwamba
asubuhi ile angefika ikulu alikuwa
na jambo muhimu la kuzungumza
naye.Alipata kifungua kinywa
halafu akaondoka kuelekea kwa
Theresa.Alimkuta tayari
amekwisha jiandaa kwa kazi za
sikuile.Kama ratiba yao
walivyoipanga wakaondoka
kuelekea katika maduka ya vifaa
vya elektroniki
“Mathew sikuweza kupata
usingizi usiku wa leo.Nilikuwa na
mawazo mengi mno.Lile jambo
nililolifahamu jana kuhusu Nathan
limeninyima amani kabisa”
akasema Theresa
“Usihofu Theresa na ndiyo
maana nikakwambia kwamba
unapoaswa kurejea ikulu katika
shughuli zako za kila siku kwani
kazi hizi zina hatari nyingi mno
ndani yake.Hata hivyo usijali
nitakulinda kila pale utakapokuwa
nami.Nitahakikisha wewe na dada
yako mnakuwa
salama.Ninachokuomba katika hali
kama hii usimuamini mtu yeyote
yule.Hata kama una mpenzi
unayempenda sana usithubutu
kumuamini kwa asilimia mia
moja.Unaona kilichotokea kwa Dr
Vivian? Alimpenda mno Nathan
bila kujua ni mtu wa namna gani.Umakini mkubwa unatakiwa
kuanzia sasa.Kitu chochote
unachoona si cha kawaida
nitaarifu mara moja”akasema
Mathew.Theresa alikuwa
anatazama nje akionekana mwingi
wa mawazo.
“Nilifanya jambo la maana
sana kutokumueleza dada
chochote kuhusiana na siri hii
ninayoifahamu ya Football.Endapo
angekuwa anafahamu hivi sasa
naamini angekwisha uawa
.Natamani kumueleza Mathew
kuhusu siri hii lakini bado
ninaogopa kwani kwa kufanya
hivyo nitakuwa ninayaweka
hatarini maisha yangu na dada kwani hawa jamaa wanadukua
taarifa zetu” akawaza Theresa
“Ngoja jambo hili liendelee
kuwa siri yangu na hatafahamu
mtu mwingine yeyote.Naamini
hata Mathew akifanya uchunguzi
wake hataweza kufahamu kama na
mimi nilikuwemo ndani ya ndege
ile ya rais kwani watu wote
walioniona ndegeni wamekwisha
fariki” akaendelea kuwaza
Theresa.
Walipita katika maduka ya
simu na kununua simu kadhaa za
bei ghali pamoja na
kompyuta.Theresa akapewa simu
mbili na pamoja na kompyuta
mpya mbili .Simu nyingine tatu
pamoja na kompyuta wakaenda navyo ikulu kwa ajili ya kumpatia
rais.
Rais Dr Vivian aliwakaribisha
akina Mathew katika chumba cha
maongezi ya faragha.Hakupenda
kuzungumza na Mathew katika
ofisi yake.
“Karibuni sana.Habari za toka
jana?
“Nzuri kabisa mheshimiwa
rais” akasema Mathew na ukimya
mfupi wa sekunde kadhaa ukapita
kisha Mathew akasema
“Mheshimiwa rasi tumekuja
kwako mara moja kwa dharura na
tunashukuru umetupokea.Kuna
jambo limetuleta hapa”
“Usijali Mathew nilikwisha
sema muda wowote mtakaonihitaji mimi nipo pamoja nanyi kwa hiyo
msisite kuja kuniona kama kuna
jambo lolote lenye ulazima wa kuja
kuniona” akasema Dr Vivian
“Ahsante sana.Mheshimiwa
rais tumekueletea simu tatu na
komputa mbili.Kuanzia sasa
hautatumia zile simu zako za
zamani hivyo nakuomba
ubadilishe simu zako unazotumia
na uanze kutumia hizi
nilizokuletea.Hizi ni simu mpya
kabisa ambazo nimezinunua
asubuhi hii nikiwa na
Theresa.Kompyuta yako
unayotumia sasa hautaitumia tena
bali utaitumia hii niliyokuletea
.Nafahamu swali la kwanza
utakalouliza ni kwa nini? Naomba usiniulize swali hilo kwa sasa
mheshimiwa rais bali naomba
ufanye hivyo nilivyokueleza .Hii ni
kwa ajili ya kuhakikisha unakuwa
salama mheshimiwa rais.Hapo
baadae nitakuja na kukueleza kila
kitu kuhusiana na suala hili”
akasema Mathew
Dr Vivian akachukua muda
kidogo kuwatazama Mathew na
Theresa halafu akaishika
mojawapo ya simu aliyoletewa na
Mathew akaitazama kama kwamba
anaikagua halafu akasema
“Mathew mimi na wewe
hatukuwahi kufahamiana hapo
kabla.Leo ni siku ya tatu kama si ya
nne toka nimekufahamu
.Nilipokuona tu nafsi yangu iliniambia kwamba nimempata
mtu sahihi kwa ajili ya kuifanya
kazi iliyoshindikana kwa zaidi ya
miaka kumi.Nilikuamini kabla
hata ya kukupa kazi hii
uifanye.Ninakuamini sana Mathew
zaidi ya ninavyowaamni hata wale
ninaofanya nao kazi lakini kuna
mambo yameanza kunipa
wasiwasi.Jana umekuja kunihoji
kuhusiana na maisha yangu binafsi
na leo hii unakuja na kunitaka
nibadilishe simu zangu.What’s
going on Mathew? Kuna nini
ambacho hutaki kunieleza?
Sikakatai yawezekana labda kuna
tatizo umeligundua lakini kwa nini
hutaki kunieleza?Nijuze na mimi
nifahamu.Inaniwia ugumu kuweza kukubaliana na mambomengine
kirahisi rahisi bila kufahamu
sababu.Naomba kufahamu
tafadhali hizi zimu zangu zina
tatizo gani?
“Mheshimiwa rais kwanza
ninashukuru kwa kuniamini na
ninakuomba undelee kuniamini na
mimi ninakuahidi kwamba
sintakuangusha.Ninafahamu kiu
yako ya kutaka kujua kila
kinachoendelea katikauchunguzi
wangu lakini kuna mambo
mengine ambayo siwezi kukueleza
kwa sasa hadi hapo nitakapokuwa
nimeyachimbua kwa kina kwa hiyo
nakuomba unipe muda kidogo na
mimi nitakuja kukueleza kila kitu
na mahala nilikofikia lakini kwa sasa itoshe tu kukuomba ukubali
kufanya hiki
nilichokueleza.Naomba ubadilishe
simu zako kuanzia sasa na uanze
kutumia hizi simu nilizokupa
pamoja na hii kompyuta.Tafadhali
sana mheshmiwa rais naomba
ukubali”
“Mathew sijakataa kufanya
hivyo lakini ninachotaka
kufahamu ni je simu hizi zina shida
gani? Akauliza Dr Vivian
“Kama nilivyosema
mheshimiwa rais kwamba ni
mapema sana kusema chochote
kwa sasa.Nipe muda wa siku mbili
nitakuja hapa na kukueleza kila
kitu.Tafadhali sana mheshimiwa
rais.Kama uliweza kuniamini hata kabla hujanipa kazi hii naomba
uniamini pia katika hili” akasema
Mathew.Dr Vivian akafikiri kidogo
na kusema
“ Sawa Mathew nitafanya
hivyo.Ninakuamini na nitaendelea
kukuamini na ninaomba
nisikuharakishe kuja kunieleza
kuhusu maendeleo ya uchunguzi
wako.Endelea kuchunguza taratibu
na pale utakapoona kuna
umuhimu wa mimi kufahamu
chochote unakaribishwa” akasema
Dr Vivian na kumtuma Theresa
aende ofisini kwake akazilete simu
zake.
“Mathew nakuomba kama
kuna jambo lolote ambalo
unaliona si la kawaida ila linaweza kuwa na hatari kwangu au kwetu
basi usisubiri njoo unitaarifu mara
moja na kama kuna hatua za
kuchukua tufanye hivyo mara
moja.Tuko katika wakati mbaya
sana kama nchi” Akasema Dr
Vivian baada ya Theresa kutoka
“Sawa mheshimiwa rais
nitafanya hivyo” akajibu Mathew
“Vipi hakuna sehemu yoyote
uliyokwama kitu chochote?
“Hakuna mheshimiwa
rais.Theresa yuko makini sana
kuhakikisha kwamba hakuna
mahala ninakwama ”
“Halafu nimekumbuka
kitu.Uliniomba nikupatie nakala ya
maelezo ya kanali sebastian toka
polisi aliyoyatoa wakati wa mahojiano baada ya kunusurika
katika ndege .Sijafanikiwa kuipata
taarifa hiyo.Kumekuwa na dana
dana nyingi katika suala hili toka
nilipoomba ripoti hiyo na mpaka
sasa sijaipata.Maelezo niliyoyapata
ni kwamba jalada hilo halionekani
kwani imekwishakuwa ni muda
mrefu na kuna uwezekano jalada
likawa limekwisha fungwa”
akasema Dr Vivian
“Usijali mheshimiwa
rais.Suala hili lina vizingiti vingi
toka mwanzo lakini hatuwezi
kukata tamaa,tutatafuta namna
nyingine ya kuweza kufanya
uchunguzi.Ninachokuomba
nahitaji kupata ripoti ya daktari
aliyefanya uchunguzi kwa miili ya wale waliofariki katika ajali hiyo
kwani kwa maelezo niliyoyapata ni
kwamba ndege hiyo iliwaka moto
baada ya kuanguka.Nahitaji kujua
nini alikigundua katika miili ya
marehemu?
“Sawa Mathew nitajitahidi
kufanya hivyo na mpaka mchana
wa leo nitajitahidi niwe tayari
nimeipata ripoti hiyo” akasema Dr
Vivian na Theresa akarudi akiwa
na simu tatu za rais.Akabilisha
laini za simu na kuziweka katika
simu zile mpya walizoleta
“Ninafanya nini na hizi simu
za zamani?
“Naomba unipatie.Ile
kompyuta yako ya zamani
usiitumie tena bali utaanza kuitumia hii na wala usihamishe
faili lolote kutoka katika ile
kompyuta yako ya zamani”
akasema Mathew na kuzichukua
zile simu za rais kisha wakaagana
na rais,wakaondoka
“Ahsante sana Mathew kwa
kumundoa dada yangu katika
hatari” akasema Theresa
“Theresa bado Dr Vivian
hajatoka katika hatari.Hawa
majasusi wana njia nyingi za
kuweza kufanikisha malengo
yao.Mambo mengi tutayafahamu
tukifanikiwa kumpata Nathan.Saa
ngapi anawasili leo? Umekwisha
wasiliana naye kufahamu atafika
saa ngapi? “Jana aliniambia anatarajia
kufika leo saa nne au saa tano”
“Kama ni muda huo basi
zimebaki dakika kama ishirini hivi
ifike saa nne.Twende tuelekee
huko.Utaratibu ni kwamba ukisha
mpokea utaondoka na gari langu
na utampeleka hotelini
akapumzike na halafu jioni ya leo
utamualika nyumbani kwako kwa
chakula na mazungumzo na mimi
nitautumia muda huo kwenda
kuingia katika chumba chake na
kufanya uchunguzi .Nikisha maliza
nitakujulisha na utaachana naye
kisha tutakutana nikujuze
nilichokipata katika uchunguzi
wangu” “Sawa Mathew.Nikitumia gari
lako wewe utatumia nini?
“Nitatumia taksi.Msisitize
Nathan kwamba safari hii iwe ya
siri kubwa na asimueleze mtu
yeyote kama amekuja hadi hapo
mipango ya kumuunganisha tena
na Dr Vivian itakapokamilika”
akasema Mathew
“Usijali Mathew nitatekeleza
hilo” akasema Theresa na
wakaelekea moja kwa moja hadi
uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Julius Nyerere kwa ajili ya
kumsubiri Nathan.Akiwa pale
uwanjani akawasiliana na Peniela
na kujulishwa kwamba tayari
amekwisha tuma ndege ya kwenda Havana Cuba kumchukua Camilla
Snow .
“Kwa mujibu wa Peniela
ndege iliyomchukua Camilla tayari
imeondoka Havana Cuba saa kumi
na mbili alfajiri ya leo kuja Dar es
salaam kwa hiyo tumtegemee
Camilla kesho alfajiri” akawaza
Mathew wakati wakiendelea
kumsubiri Nathan.Wakiwa hapo
uwanjani Meshack Jumbo akapiga
simu ikamlazimu Mathew asogee
mbali kidogo na Theresa ili aweze
kuzungumza na mzee Jumbo
“Mzee shikamoo”
“Marahaba Mathew habari za
toka jana?
“Nzuri mzee
wangu.Umeamkaje? “Nimeamka salama.Nimeona
kimya nikaona ngoja nikujulie hali
na kujua mambo yako
yanakwendaje”
“Mambo yanakwenda vyema
mzee.Jana nilipotoka kwako
nilipata wazo la kwenda kwa
Theresa na nikakuta anatumia
simu aina ya EZZY zile
zinatotengenezwa na kampuni ya
A.D electronics.Nilimkuta na simu
mbili na kompyuta mbili.Theresa
anadai kwamba vifaa hivyo
alipewa na Nathan kama
zawadi.Anadai kwamba hakupewa
yeye peke yake bali hata rais na
watumishi karibu wengi wa ikulu
walipewa kama zawadi kila mmoja
simu na kompyuta bila kujua kama zina madhara makubwa kwao.
Nilimzuia asiendelee kuzitumia na
nikamueleza hali halisi kwa nini
asitumie tena hivyo vifaa.Hii ni
picha nyingine tunayoipata kuhusu
Nathan kwamba yuko karibu na
rais kwa kazi maalum”
“Kwa hiyo kwa muda huu
wote walikuwa wanapata taarifa
zote za rais..Dah ! akasema
Meshack Jumbo
“Ndiyo mzee.Kwa muda mrefu
sasa wamekuwa wakipata taarifa
zote za rais na watu
wanaomzunguka kwa maana hiyo
wanafahamu kila kitu kuhusiana
na rais na hata yale mambo nyeti
ya nchi .Rais wetu yuko katika
hatari kubwa na hasa kwa sasa baada ya kuingia katika msuguano
na Marekani.Asubuhi ya leo
nimekwenda kununua simu
nyingine mpya na kumpelekea rais
pamoja na kompyuta na kumtaka
aache kutumia zile simu na
kompyuta alizopewa na
Nathan.Haikuwa kazi rahisi
kumshawishi lakini amekubali na
ameachana na zile simu kwa hiyo
kwa upande wa rais hakuna tatizo
tena bado kwa wasaidizi wake na
wale wanaomzunguka.
Tunatakiwa taratibu kuanza
kuziondoa kompyuta zile toka
mikononi mwao pamoja na zile
simu .Uchunguzi ukikamilika na
tukiwa na uhakika wa nini
wanakichunguza tutalifikisha hili suala kwa rais na hatua
zichukuliwe ikiw ani pamojana
kubadili kompyuta na mfumo
mzima wa mawasiliano wa
ikulu”akasema Mathew
“Nimekosa neno la kusema
Mathew.Hili jambo linaumiza
kichwa changu sana toka
nimelifahamu.Ni kitu gani hasa
ambacho wanakichunguza kwa
rais?
“Hilo ni swali ambalo majibu
yake tutayapata baada ya kumpata
Nathan.Yeye ndiye anayejua ni kitu
gani hasa anakitafuta kwa
rais.Hivi sasa tuko hapa uwanja wa
ndege tukimsubiri kwani
alimuahidi Theresa kwamba leo
saa nne hadi saa tano atakuwa amewasili kwani anakuja na ndege
binafsi ya kaka yake.Kutoka hapa
Theresa atamchukua na
kumpeleka hotelini na usiku wa
leo atamkaribisha nyumbani
kwake na hiyo itakuwa ni nafasi
yangu ya kwenda katika chumba
alichofikia Nathan na kufanya
uchunguzi.Endapo nitashindwa
kupata kitu chochote kwa leo
itanilazimu kuweka mtego na
kama mtego huo utashindwa
kufanikiwa basi itanilazimu
kumteka Nathan na kumuhoji”
“Sawa Mathew sina tatizo na
huo mpango wako ila umakini
unatakiwa kwani huyu jamaa naye
ni mtaalamu sana wa haya mambo
kwa hiyo muda wote yuko katika tahadhari kubwa.Vipi kuhusu
Camilla?
“Nimezungumza na Penie…”
Mathew akastuka kidogo baada ya
kutazama katika sehemu ya
kutokea abiria wanaowasili na
kumuona Theresa akiwa
ameongozana na kijana mmoja
mtanashati sana aliyevalia
nadhifu.
“Mathew ! akaita mzee Jumbo
“Mzee mambo
yameiva.Ninamuona Theresa
akiwa ameongozana na kijana
ambaye ninahisi ndiye Nathan na
wanaelekea katika gari langu.Mzee
nakuomba nikuache ili niweze
kuwafuatilia na kuhakikisha
mpango wetu unakwenda kama tulivyopanga” akasema Mathew
huku akitembea kuelekea zilipo
taksi
“Sawa Mathew utanijulisha
baadae kila hatua utakayokuwa
umefikia” akasema Meshack
Jumbo
“Nitakujulisha mzee.Kuhusu
Camilla nimezungumza na Peniela
muda si mrefu na amenieleza
kwamba tayari ndege aliyoituma
kwenda Havana kumchukua
imeondoka saa tano za usiku kule
Havana ambayo ni sawa na kumi
na mbili za alfajiiri kwa saa za
afrika mashariki na safari ya
kutoka Havana hadi Dar es salama
inaweza kuchukua saa ishirini na
mbili au zaidi kwa hiyo tumtegemee Camilla kesho
asubuhi” akasema Mathew na
kuagana na mzee Meshack Jumbo
akamuelekeza dereva aifuate gari
ile waliyopanda Theresa na
Nathan.
*****************
“Karibu sana Dar es salaam
Nathan” akasema Theresa wakiwa
ndani ya gari wakielekea hotelini
“Ahsante Theresa.Gari lako
zuri mno.Ni la kifahari mno.Magari
kama haya hata Marekani
yanaendeshwa na matajiri
wakubwa au viongozi wakubwa
kwani sifa yake kubwa hayapenyi risasi” akasema Nathan.Theresa
akatabasamu na kusema
“Hili si gari langu.Ni gari la
mpenzi wangu mpya anafanya
biashara ya madini na kwa kuwa
amesafiri kwenda nje ya nchi
katika biashara zake ameniachia
nilitumie.Sina uwezo wa kununua
gari kama hii” akasema Theresa
“Hongera sana .Kumbe tayari
una mpenzi mpya tena tajiri”
akasema Nathan na wote
wakacheka.
“Anaendeleaje Vivian?
Akauliza Nathan
“Dada anaendelea
vizuri.Nimekuwa naye jana
tumekaa hadi usiku tunazungumza
kuhusiana na suala lenu na ameniahidi kunipa jibu baada ya
kufikiria.Asubuhi ya leo kabla
sijaenda uwanja wa ndege
kukusubiri nimekutana naye
lakini hatukuzugumza mengi
nilikuwa namuandalia hotuba
fulani”
“Umeonaje muelekeo wake?
Yuko tayari kuweza kurudisha
moyo na kuendelea na mchakato
wa harusi yetu? Theresa
ninampenda mno Vivian na sijui
nikuelezaje namna
ninavyompenda.Sifahamu
nitakupa zawadi gani
utakaponisaidia kuurejesha tena
uhusiano wangu na Vivian”
“Usiogope Nathan niachie hilo
jukumu na nitalimaliza.Vivian hawezi kunishinda .Kitu cha
msingi ni kufuata maelekezo yangu
tu na kila kitu kitakwenda sawa”
“Hivi sasa tunaelekea wapi?
“Tunaelekea hotelini.Utafikia
hotelini utapumzika na baadae
jioni nitakuja kukuchukua
tutakwenda nyumbani kwangu
kupata chakula na nitakupa
mrejesho wa kila
kinachoendelea.Kitu cha msingi
zingatia usiri.Asifahamu mtu
yeyote aliye karibu na dada kama
unakuja Tanzania.Tunao fahamu
kuhusu ujio wako ni mimi na wewe
pekee.Nataka kumshangaza dada
Vivian na hataamini macho yake”
akasema Theresa na kumfanya
Nathan atabasamu. Walielekea moja kwa moja
hoteli Pentagone moja ya hoteli
kubwa jijini Dar es slaam yenye
umbo la pembe tano.Pale Nathan
alichukua chumba .
“Nathan,pumzika hapa mimi
ninakwenda kuendelea na
majukumu mengine na baadae
jioni ujiandae nitakuja kukuchuku
atuende nyumbani kwangu
nitaandaa chakula na
tutalizungumzia suala lenu na
kama ikimpendeza Mungu basi
Vivian anaweza akajiunga
nasi.Ninakwenda kujaribu
kulifanikisha hilo” akasema
Theresa.Nathan akainuka na
kumkumbatia kwa furaha
“Theresa tafadhali nakuomba
fanya kila uwezalo kuhakikisha
ninakutana na kuzungumza na
Vivian” akasema Nathan
wakaagana na Theresa
akaondoka.Mara tu alipoondoka
hoteli Pentagone akampigia simu
Mathew na kumfahamisha kila kitu
kilivyoenda .Mathew
akamuelekeza mahali alipo na
kumtaka amfuate
“Nilipomuona Nathan moyo
wangu ulipatwa na hasira kali.Yule
shetani kumbe kwa muda huu
wote amekuwa anatuchunguza na
kudukua habari zetu.Hana maana
yoyote shetani mkubwa
yule.Anayaweka maisha yetu
katika hatari kubwa.Nilijitahidi kutabasamu nilipokuwa karibu
naye lakini angejua ninachokiwaza
moyoni mwangu angekaa mbali
kabisa na mimi” akawaza Theresa.
Alimfuata Mathew mahala
alikomuelekeza na kumkuta
akipata supu wote wakakaa na
kuendelea kupata supu.
Alimfuata Mathew mahala
alikomuelekeza na kumkuta
akipata supu wote wakakaa na
kuendelea kupata supu.
“Mathew mambo
yamekamilika.Nathan tayari
nimempeleka hoteli Pentagone
amepewa chumba namba 202
ghorofa ya tatu” Akasema Theresa
na kuvuta pumzi ndefu
“Pole Theresa najua haikuwa
rahisi kwako lakini nakuomba
ujenge ujasiri ili Nathan asigundue
chochote.Uso wako ujenge
tabasamu kila wakati.Huyu ni mtu muhimu sana kwetu.Kuna mambo
mengi ambayo tunahitaji
kuyafahamu kutoka kwake.Kazi
yako ni kuhakikisha unakuwa naye
karibu wakati mimi nitakamilisha
jukumu la kumchunguza na
kuhakikisha ninamfahamu ni nani
na nini lengo lake” akasema
Mathew.Wakati wakiendelea
kupata supu simu ya Mathew
ikaita,alikuwa ni Dr Vivian
“Hallo mheshimiwa rais”
akasema Mathew
“Mathew nimeipata ile taarifa
ya uchunguzi wa madaktari kwa ile
miili ya watu waliofariki katika
ajali ya ndege ya rais.Ninakutumia
sasa hivi katika simu yako”
akasema rais “Ahsante sana mheshimiwa
rais.Nitumie ili niipitie” akasema
Mathew
“Kama utahitaji maelezo zaidi
utayapata kwa daktari aliyeongoza
kuichunguza miili ya marehemu
wa ajali ile ya ndege anaitwa Dr
Proches Masawe.Kwa sasa ni
mstaafu na anamiliki hospitali
yake inaitwa tumaini hospital”
akasema Dr Vivian
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais ngoja niifanyie kazi hiyo
taarifa” akasema Mathew na
kumgeukia Theresa
“Asubuhi ya leo nilimuomba
rais anisaidie niweze kupata
taarifa ya madaktari waliofanyia
uchunguzi miili ya marehemu wa ajali ya ndege ya rais
Anorld.Ameipata taarifa hiyo na
atanitumia muda si mrefu.Vile vile
amesema kwamba kwa maelezo
zaidi nikaonane na daktari
anaitwa Proches masawe ana
hospitali yake inaitwa
Tumaini.Nitakupeleka nyumbani
ukaendelee na maandalizi ya
kukutana na Nathan jioni ya leo
mimi nitakwenda kwa Dr Masawe
nikazungumze naye ana kwa
ana.Nataka kupata picha ya
majeraha ya marehemu hao
japokuwa inasemekana wengi
walikuwa wameunguzwa na moto
na wengine vibaya sana hadi
kulazimika kuwatambua kwa
kutumia vinasaba.” akasema Mathew na muda huo huo mlio wa
ujumbe mfupi ukalia katika simu
yake akaufungua na kuusoma.Rais
alikuwa amemtumia ripoti ile ya
madaktari.Mathew akaipitia
haraka haraka na kumuonyesha
Theresa.Wakaingia garini
wakaenda hadi nyumbani kwa
Theresa halafu Mathew
akaendelea na safari ya kuelekea
Tumaini hospitali kuonana na Dr
Masawe.
Alifika hospitali ya Tumaini na
kushuka garini akamuuliza
muuguzi mmoja angewezaje
kuonana na Dr Masawe.Muuguzi
yule akamuelekeza mahala ilipo
ofisi ya Dr Masawe.Mathew
akaenda hadi katika ofisi ile na kukuta kuna watu kadhaa
wamejipanga mstari wakisubiri
kuonana na daktari na walikuwa
wanaingia mmoja mmoja.
“Watu ninaowaona hapa
hawapungui thelathini na bado
wanazidi kuongezeka.Itanibidi
nitafute namna ya kufanya ili
niweze kuonana na huyu Dr
Masawe” akawaza Mathew na
kuondoka eneo lile akamfuata
daktari mmoja aliyekuwa
anazungumza na simu .Akamsubiri
amalize mazungumzo yake halafu
akamsabahi
“Habari yako daktari”
akasema Mathew
“Nzuri kaka habari yako” “Nzuri kabisa” akasema
Mathew na kumuomba daktari
yule kama angeweza kupata nafasi
wakaongea pembeni kidogo.Bila
hiyana daktari yule akamuomba
waelekee nyuma ya mgahawa wa
hospitali.Mathew akamueleza yule
daktari kwamba alikuwa na shida
ya kuonana na Dr Masawe lakini
kuna watu wengi hivyo anaomba
msaada.Bila kusita daktari yule
akakubali kumsaidia Mathew
kuonana na Dr Masawe.Mathew
akamuomba namba zake za simu
na haraka haraka akamrushia
kiasi cha shilingi laki moja na yule
daktari alitabasamu na kuondoka
haraka na baada ya kama dakika
kumi hivi akarejea na kumtaka Mathew amfuate.Waliekea katika
ofisi fulani na walipoingia
wakamkuta mzee mmoja mnene
akiwa amekaa katika kiti cha
kuzunguka mara moja Mathew
akajua yule ndiye Dr
Masawe.Akamsalimu kwa
adabu.Daktari yule ambaye
alimsaidia Mathew kuonana na Dr
Masawe akamtambulisha mzee
yule kuwa ndiye Dr Masawe halafu
akatoka
“Kijana karibu sana” akasema
Dr Masawe
“Ahsante Dr Masawe na
samahani sana kwa usumbufu“
“Usijali kijana
wangu.Nimeelezwa kwamba
umetokea ikulu na nikaacha wagonjwa nikaona nije
nikusikilize”
“Ni kweli mzee.Mimi naitwa
Mathew natokea
ikulu.Nimeelekezwa nije hapa
kwako na rais ili niweze kupata
ufafanuzi wa kuhusiana na jambo
fulani lililowahi kutokea yapata
miaka kumi sasa” akasema
Mathew.
“Ni jambo gani hilo Mathew?
Akauliza Dr Masawe huku sura
yake ikionyesha wasi wasi
“Ni kuhusiana na ajali ya
ndege ya rais Anorld.Kuna hii
ripoti hapa mliitoa kuhusiana na
uchunguzi mlioufanya katika miili
ya marehemu wa ajali ile” akasema
Mathew na kuitoa simu yake akamuonyesha Dr Masawe ile
taarifa akaipitia na kukunja sura
“This is not true !! akasema
kwa ukali
“Kivipi Dr Masawe?
“Huu ni upuuzi mtupu.Hii si
ripoti yetu tuliyoitoa” akasema Dr
Masawe.Mathew naye akashangaa
“Una hakika hii si ripoti yenu
Dr Masawe?
“Ndiyo kijana wangu.Hii si
ripoti yetu.Huu ni upuuzi
mkubwa.Umeitoa wapi ripoti
hii?Nani kafanya hivi?
“Ripoti hii nimetumiwa na rais
mwenyewe na ndiyo maana
nikaamua kuja hapa kupata
uthibitisho kama kweli ni
yenyewe” “Rais amedanganywa .Hii si
ripoti yenyewe.Kuna mchezo
umefanywa hapa kuibadili taarifa
yetu.Hatukutoa sisi ripoti ya aina
hii” akasema Dr Masawe na
kurudia tena kuipitia ile taarifa na
kutikisa kichwa
“Taarifa yenu ilikuwaje Dr
Masawe? Mathew akauliza
“Sikiliza Mathew ni kweli
niliongoza madaktari wengine
wawili katika kuifanyia uchuguzi
miili ya marehemu na baada ya
kukamilisha uchunguzi wetu
tukaandika ripoti na kuikabidhi
kwa wahusika ikiwa imefungwa
kabisa kwani ni nyaraka ya
siri.Kwa hiyo kuna watu huko
serikalini kwa makusudi na kwa manufaa yao wameibadili taarifa
yetu”
“Dr Masawe unaweza
ukanieleza mlichokiandika katika
taarifa yenu ambayo ni halisi
tofauti na hii taarifa bandia ?
Mathew akauliza
“Mathew ningependa sana
kukueleza kuhusiana na taarifa
hiyo lakini hiyo huwa ni taarifa ya
siri na huwa inakabidhiwa kwa
vyombo husika .Nadhani ingekuwa
vyema mngewafuata watu
waliokabidhiwa taarifa hiyo na
kujua kwa nini walibadili taarifa
yetu na kuandika taarifa ya
uongo?akasema Dr Masawe
“Dr Masawe nisingekuja hapa
kwako kama kungekuwa na mahala ninakoweza kupata
msaada.Nimekuja hapa kwako ili
kupata ukweli halisi wa kile
mlichokigundua baada ya kufanya
uchunguzi wenu.Ninaomba sana
unisaidie mzee wangu” akasema
Mathew
“Kijana nasikitika kwamba
siwezi kuongea chochote kuhusu
jambo hilo ambalo tulilikamilisha
na tukatoa ripoti yetu ya
uchunguzi.Walioibadilisha wana
makusudi yao kwa hiyo ni jukumu
lako wewe kama mchunguzi
kufahamu ni nani walibadilisha
hiyo taarifa na kuandika upuuzi
huu mkubwa. Nakushauri Mathew
wafuate wakubwa zako huko
serikalini na uanze kulifuatilia suala hili utagundua mchezo huu
mchafu uliofanywa” akasema Dr
Masawe huku akiinuka.
“Dr Masawe kama hutaki
kuufumbua mdomo wako
kunieleza kuhusiana na kile
mlichokigundua ,ni vipi kama
tutakwenda hatua ya mbele zaidi
na nikayanunua maneno
yako.Unasemaje kuhusu
hilo?Mathew akauliza.Dr Masawe
akang’aka
“Money ? You want to buy me?
Akauliza Dr Masawe
“Sikiliza mzee
wangu.Ninachokihitaji toka kwako
ni maneno yako machahe tu na
wala sihitaji taarifa nzima.Name
your price and I’ll pay you right now” akasema Mathew.Dr Masawe
akafikiri kidogo na kusema
“How much are you going to
pay me?akauliza huku
akitabasamu
“Sema unahitaji kiasi gani?
“Unajua kijana sisi madaktari
huwa haturuhusiwi kutoa
sir………….”
“Dr Masawe!! Mathew
akamkatisha.
“Nafahamu unachotaka
kukisema kwa hiyo tufupishe
mjadala .Just name your price.Kiasi
gani unakihitaji?Two
Million?Three or four?
“Kwa uzito wa taarifa yenyewe
nakuomba uamue mwenyewe utanipa kiasi gani”akasema Dr
Masawe
Mathew hakutaka kupoteza
wakati akachukua simu yake na
kumuomba Dr Masawe namba
zake za simu akamtumia shilingi
milioni mbili.Dr Masawe
alipoziona akasema
“Kijana wewe unafahamu
namna ya kuishi mjini.Nina hisi
lazima utakuwa unatokea Moshi
wewe.” Akasema Dr Masawe na
wote wakacheka
“Ni hivi,mimi na madaktari
wenzangu tulifanya uchunguzi wa
miili ile na tuligundua kwamba
kuna uwezekano mkubwa watu
wale walikufa kabla ya ndege
kuanguka.Uchunguzi ulionyesha walikosa hewa safi na inaonekana
walivuta hewa yenye sumu au
hewa isiyo safi na wengi aidha
walikufa au kupoteza fahamu
kabla ndege haijaanguka.Kingine
tulichogundua ni matundu ya
risasi kwa baadhi ya miili
isipokuwa mwili wa rais wenyewe
haukuwa na tundu la
risasi.Tuliyaandika haya yote
katika taarifa yetu na tukaikabidhi
kwa vyombo vya uchunguzi na
sijui kwa nini wakaamua
kuibadilisha taarifa hii na
kuandika huu upuuzi japo kuwa
sahihi hii ni ya
kwangu.Nimeshangaa sana kama
kuna mambo ya ajabu kama haya
yanaendelea serikalini.Unapaswa kuchunguza na kugundua
waliofanya upuuzi huu walikuwa
na lengo gani” akasema Dr
Masawe.
“Nashukuru sana Dr Masawe
kwa msaada huu mkubwa”
akasema Mathew na kuagana na
Dr masawe na kuelekea mahala
alikoegesha gari lake akaingia na
kujifuta jasho.
“Toka awali nilikuwa na
wasiwasi sana kuhusiana na ajali
ile ya ndege ya rais.Baada ya
kuanza kuchunguza kuhusiana na
ile ajali nimegundua mambo
kadhaa ya kustaajabisha.Kwanza
kisanduku cheusi cha kuhifadhi
mwenendo wa ndege kilitoweka na
kukawa na majina bandia ya watu waliotumwa kuja kufanya
uchunguzi wa chanzo cha
kuanguka kwa ndege ile.Leo tena
linaibuka jambo lingine kwamba
taarifa hii inayodaiwa ni ya
madkatari walioifanyia uchunguzi
miili ya marehemu wa ajali ile ya
ndege si sahihi na
ilibadilishwa.Taarifa hii haielezi
chochote kuhusiana na baadhi ya
miili ya marehemu kukutwa na
matundu ya risasi na haionyeshi
kama watu wale ndani ya ndege
walikufa kabla ndege haijaanguka
na wala kusaidikiwa kuvuta hewa
chafu au hewa yenye sumu .Hii ni
habari mpya kabisa na itanisaidia
sana kufahamu kilichotokea ndani ya ndege ile na kusababisha
ianguke” akawaza Mathew
“Kumeonekana matundu ya
risasi kwa baadhi ya miili,swali
ninalojiuliza ni je kulikuwa na
mashambulizi ndani ya ndege?
Kama ndiyo,nani alikuwa
anashambulia na kwa dhumuni
gani?Hiyo hewa chafu au ya sumu
anayosema Dr Masawe kwamba
inahisiwa walivuta watu
waliokuwamo ndani ya ndege
ilitoka wapi?Nikifanikiwa kupata
majibu ya haya maswali nitakuwa
nimefanikiwa kujua kwa nini
ndege ile ilianguka.Kanali
Sebastian alikuwa ni mtu muhimu
mno katika uchunguzi huu.Endapo
angekuwa hai mpaka sasa angeweza kutusaida kujua nini
kilichotokea ndani ya ndege.Hata
hivyo tayari tumeanza kupata
mwanga mdogo kuhusiana na ajali
ile.Tayari ninafahamukwamba
kulikuwa na kurushiana risasi
ndani ya ndege kabla haijaanguka”
akawaza Mathew
Kutoka Tumaini hospital
,Mathew aliekea moja kwa moja
kwa Meshack Jumbo.
“Mathew karibu sana.Habari
za huko utokako?Meshack Jumbo
akamkaribisha
“Huko kwema kabisa mzee
mambo yanakwenda vizuri”
“Nafurahi kusikia hivyo.Vipi
kuna habari yoyote mpya? “Ndiyo Mzee.Kuna jambo
nimelipata ambalo linaweza
kutusaidia sana katika uchunguzi
.Kwanza kabla ya yote
nikujulishe,tayari Nathan
amekwisha wasili na hivi sasa
yuko hotelini na jioni ya leo
atakwenda nyumbani kwa Theresa
na mimi nitautumia mwanya huo
kwenda kufanya uchunguzi katika
chumba chake.Naamini kuna kitu
lazima nitakigundua katika
chumba cha Nathan.Kuhusu
Camilla kama nilivyokueleza ni
kwamba yuko angani muda huu
anakuja Tanzania tumtegemee
hapa kesho alfajiri” Akasema
mathew “Maendeleo mazuri.Ila
nakushauri uwe makini sana
kuhusu Nathan na umuonye hata
Theresa pia kwamba asifanye
mchezo na yule jamaa.Ni mtu
hatari sana”
“Nitafanya hivyo mzee.Vile
vile tayari nimekwisha mbadilishia
rais simu na sasa hatumii tena zile
simu alizopewa na
Nathan.Kinachofuata kwa sasa ni
kuanza kuziondoa kompyuta zote
na simu ambazo Nathan aligawa
kwa wafanyakazi wa ikulu wale
wanaomzunguka rais.Zoezi hili
likikamilika tutakuwa na imani
kwamba hawataweza tena kupata
taarifa za ikulu japo hawatakata tamaa na wanaweza wakatafuta
njia nyingine” akasema Mathew
“Tuachane na hayo.Leo
asubuhi nilipokwenda ikulu
kuonana na rais nilimuomba
anisaidie niipate taarifa ya daktari
aliyefanya uchunguzi miili ya
marehemu waliofariki katika ajali
ile ya ndege.Rais akanitumia
taarifa ambayo ni hii hapa”
akasema Mathew na kumpa mzee
Meshack ile taarifa katika simu
yake akaisoma
“Hiyo ni taarifa ambayo
inadaiwa ndiyo ya madaktari
walioifanyia uchunguzi miili ya
marehemu walikuwamo ndani ya
ndege.Baada ya kuipata
nilimtafuta daktari aliyeongoza uchunguzi huo anaitwa Dr Proches
Masawe ambaye kwa sasa ni
mstaafu lakini anamiliki hospitali
yake inaitwa Tumaini
Hospital.Nilimuonyesha Dr
Masawe ripoti hii na akastuka sana
akadai kwamba huu ni upuuzi
umefanywa kwani ripoti
waliyoitoa wao si hii.Anadai
kwamba kuna mchezo mchafu
umefanyika na ripoti yao
ikabadilishwa.Nilimuomba
anieleze
walichokigundua.Haikuwa rahisi
lakini nikatumia ushawishi kidogo
na akanieleza kwamba waligundua
kwamba watu wale waliokuwamo
ndegeni kuna uwezekano mkubwa
walikufa au kupoteza fahamu kabla ya ajali kutokea kutokana na
kuvuta hewa chafu au yenye
sumu.Kingine waligundua
matundu ya risasi katika badhi ya
miili ya marehemu.”
“Jesus christ ! akasema
Meshack Jumbo .
“Hili suala mbona linakuwa
hivi?Mbona kila siku linaibuka
jipya? Akasema kwa sauti ndogo
“Kutokana na taarifa hii
niliyoipata toka kwa Dr Masawe
inaonyesha wazi kwamba kuna
jambo lilitokea ndani ya ile
ndege.Kwanza uwepo wa matundu
ya risasi kwa baadhiya miili
inatupa uhakika kwamba
kulikuwa na kurushiana risasi japo
hatujui nani na nani waliokuwa wanashambuliana.Jambo la pili ni
kuhusiana na hiyo hewa chafu au
yenye sumu wanayohisiwa kuivuta
watu waliokuwamo
ndegeni.Tukiweza kuyafumbua
hayo mawili tutakuwa tumepata
ukweli wa kilichosababisha ndege
kuanguka bila hata ya kutegemea
kisanduku cheusi.” Akasema
Mathew.Meshack akafikiri kidogo
na kusema
“Usemayo ni ya kweli Mathew
lakini ni wapi tutapata majibu
hayo?Tungeweza kupata majibu
kama tungeweza kumpata mtu
ambaye alikuwamo ndani ya hiyo
ndege ambaye angetueleza kama
kulikuwa na kurushiana risasi na
ni akina nani waliokuwa wanashambuliana?Kanali
Sebastian alikuwa ni mtu muhimu
sana kwetu.Kama angekuwa hai
angeweza kutueleza nini hasa
kilichotokea lakini naye amefariki”
akasema Meshack Jumbo
“Kuna hawa waandishi
aliowasema Alhaj Zuberi kwamba
walikuwamo ndani ya ndege
ambao mpaka sasa hatujapata
uhakika kama kweli walikuwamo
ndani ya ndege au vipi kwani mtu
pekee ambaye angeweza kutusaia
kuwafahamu ni Fakrim ambaye
naye tayari ameuawa.Dah ! suala
hili linazidi kuwa fumbo
gumu,lakini ngoja tumsubiri
Camilla tuone atakuwa na taarifa
gani za kumuhusu Fakrim.Yawezekana tunaweza
kupata taarifa nzuri ya kutusaidia
kutoka kwake” akasema Mathew
“Mathew nakubaliana
nawe.Jambo hili linazidi
kuchangana mno.Ngoja tumsubiri
Camilla hiyo kesho tujue naye
atakuja na habari gani” akasema
Meshack Jumbo.
Waliendelea na maongezi na
baadae Mathew akaaga
“Mzee nimetaarifiwa kwamba
kuna mizigo yangu imewasili
bandarini kwa hiyo nataka nifike
huko kuanza taratibu za kuitoa
halafu tutaonana labda baadae
usiku nitakapotoka kufanya
uchunguzi kwa Nathan” akasema
Mathew na kuondoka
Ukumbi wa mikutano wa
mwalimu Nyerere ulifurika wazee
wa jiji la Dar es salaam walioitika
wito wa rais wa kufika hapa.Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr Vivian matope alitaka
kuzungumza na taifa kupitia kwa
wazee wa jiji la Dar es
salaam.Ulinzi ulikuwa mkali sana
katika ukumbi huu.Burudani mbali
mbali zilikuwa zinaendelea wakati
wakimsubiri rais awasili.
Saa tisa za alasiri juu ya
alama rais akiwa ameongozana na
makamu wa rais na waziri mkuu
wakaingia ndani ya ukumbi tayari kwa kuwahutubia wazee wa Dar es
salaam.Watu wote ukumbini
wakasimama huku
wakimshangilia rais hadi
alipochukua nafasi yake wimbo wa
taifa ukaimbwa halafu wote
wakaketi.Muongoza shughuli
akamkaribisha kiongozi wa wazee
wa jiji la Dar es salaam aweze
kuzungumza machache na kisha
amkaribishe rais aweze
kuzungumza na watanzania kwa
kupitia wazee wa Dar es
salaam.Mzee Said seif said akatoa
salamu za wazee wa Dar es salaam
na kisha akamkaribisha rais aweze
kuzungumza nao.Makofi mengi
yakapigwa rais aliposimama na
kuelekea katika sehemu iliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya
kutolea hotuba.
“Mheshimiwa makamu wa rais
was jamhuri ya muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa waziri
mkuu wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania,mheshimiwa mkuu
wa mkoa wa Dar es
salaam,waheshimiwa wakuu wa
wilaya za Dar es
salaam,waheshimiwa wabunge wa
Dar es salaam mlioko
hapa,viongozi wa vyama vya siasa
mliopo hapa,wakuu wa vyombo
vya ulinzi na usalama mlioko
hapa,kiongozi wa wazee wa Dar es
salaam mzee Said Seif said,wazee
wote mliopo katika ukumbi huu
shikamooni” Wazee wote wakaitika halafu
akaendelea
“Awali ya yote napenda
kuanza kwa kumshukuru sana
mwenyezi Mungu mwingi wa
rehema kwa kutupa afya njema na
kutuwezesha kukutana hapa leo
hii.Wapendwa wazee wangu
umekuwa ni utaratibu uliojengwa
na viongozi wetu waliotangulia
kwamba kila pale kunapokuwa na
jambo kubwa la kitaifa ambalo
linapaswa kuwafikia watanzania
wote basi hulifikisha kwa
watanzania kwa mtindo huu wa
kuzungumza na wazee.Imezoeleka
wazee wa Dar es salaam lakini
inaweza kuwa wazee wa sehemu
yoyote ile,Arusha Mwanza,Dodoma na kwingineko
kutegemea na mahala alipo
rais.Nimeurithi utaratibu huu
kutoka kwa viongozi
walionitangulia na mimi
nitaendelea nao na kila pale
litakapotokea suala kubwa la
kitaifa nitakuwa nazungumza na
watanzania kwa kupitia kwenu
ninyi wazee” akasema Dr Vivian na
kupigiwa makofi
“Wapendwa wazee
wangu,nimewaiteni hapa kuweza
kuzungumza nanyi masuala
kadhaa yanayohusiana taifa
letu.Awali ya yote napenda kupitia
kwenu kuwafahamisha watanzania
kwamba nchi yetu ni salama,na
hakuna kitisho chochote cha usalama.Mipaka ya nchi yetu bado
iko salama na vyombo vyetu vya
ulinzi viko imara muda wote
kuhakikisha nchi yetu inakuwa
salama kwa hiyo nawaomba msiwe
na hofu yoyote ya usalama
endeleeni kufanya shughuli zenu
kama kawaida”
Wazee wangu kuna mambo
mawili au matatu ambayo nataka
kuzungumza nanyi mchana wa
leo.Kwanza ni kuhusiana na
yaliyotokea katika mkutano wa
baraza kuu la umoja wa
mataifa.Huu ni mkutano wa kila
mwaka ambao hukutanisha
viongozi wa mataifa yote ya dunia
ambayo ni wanachama wa umoja
huu au wawakilishi wao.Mwaka jana niliwakilishwa na makamu wa
rais na safari hii niliamua niende
mwenyewe.Wengi mmesikia
kilichotokea kule
Marekani,vyombo vya habari
vimelitangaza sana,magazeti ya
ndani na nje ya nchi yameandika
sana jambo hili.Naomba kidogo
nieleze japo kwa ufupi nini hasa
kilijiri huko na kuleta
sintofahamu kubwa.
Baada ya kufika Marekani
nilikutana na ujumbe wa watu
wanne watatu wakitoka China
ambao ni wawakilishi wa wafanya
biashara wakubwa wa China na
mmoja alikuwa ni mjumbe
maalum wa rais wa Korea
Kaskazini.Walikuja kwangu tukazungumza mambo mbali
mbali.Mjumbe maalum wa kutoka
Korea Kaskazini alitumwa na rais
wa Korea Kaskazini kuniletea
salamu maalum na katika salamu
hizo rais wa Korea Kaskazini
aliniomba tuweze kuzungumza
kuhusiana na kuanzishwa kwa
mashirikiano ya kibiashara baina
ya nchi zetu.Katika salamu hizo
aliweka wazi kwamba Korea
kaskazini wanahitaji mashirikiano
ya kibiashara na
Tanzania.Wafanya biashara wa
Korea Kaskazini wako tayari
kuwekeza nchini Tanzania katika
sekta mbali mbali na hasa katika
viwanda hasa vya nguo.Vile vile
alionyesha nia ya kutaka kuwekeza katika uchimbaji wa
madini ya Urani ambayo tunayo
mengi hapa nchini.Nilizipokea
salamu hizo ila sikutoa jibu lolote
hadi kwanza nitakaposhauriana na
wenzangu katika serikali ili tuone
kama tunaweza kufanya
mashirikiano hayo na kama
yatakuwa na faida yoyote kwa
Tanzania.
Kesho yake wakati akitoa
hotuba yake, rais wa Marekani
Mike straw alitoa matamshi makali
sana na kuishutumu Tanzania
kuwa na mashirikiano na Korea
Kaskazini na hata kujadiliana
kuhusiana na biashara ya madini
ya Uranium.Hakuishia hapo
alikwenda mbali zaidi na kutoa vitisho vya kuwekewa vikwazo
vikali kwa Tanzania na nchi
nyingine ambazo zinashirikiana na
Korea Kaskazini.Kwa ujumla
hotubayake ilikuwa na matamshi
makali iliyojaa ubaguzi mkubwa
na dharau hasa kwa nchi na
viongozi wa Afrika.Nadhani wengi
wenu tayari mmeisikia hotuba
hiyo ambayo naweza kuiita ni
hotuba ya hovyo sana kuwahi
kutolewa na rais wa taifa kubwa
kama Marekani.
Binafsi sikupendezwa na
shutuma na dharau zile za rais wa
Marekani kwa nchi yangu pendwa
na kwa bara letu la Afrika na ndiyo
maana sikuweza kutoa hotuba
niliyokuwa nimeiandaa kuitoa na badala yake nikaamua kumjibu pia
rais wa Marekani kwa maneno
makali pia.Katika houba yangu
niliweka wazi kwamba tutafanya
mazungumzo na mashirikiano na
Korea Kaskazini endapo
yataoneana kuwa na faida kwa
nchi yetu. Baada ya hotuba yangu
ile ukaibuka msuguano mkubwa
Wazee wangu na watanzania
naomba mfahamu kwamba
kumekuwa na ukandamizwaji
mkubwa sana katika nchi zetu
zinazoendelea kutoka kwa nchi
tajiri zikitutaka tufanye kila
wanachokitaka wao na tukikataa
wanatishia kutunyima misaada ya
kimaendeleo.Nchi zetu nyingi bado
zinaendelea kutegemea misaada kutoka nchi tajiri.Bajeti zetu bado
ni tegemezi kwa kiasi kikubwa na
ni nchi chache sana barani Afrika
ambazo zimejenga uwezo wake wa
ndani lakini nyingi bado
zinategemea nchi wahisani.Hisani
hii inaendelea kutufanya waafrika
tuwe watumwa na umasikini
usiishe katika nchi
zetu.Tunaogopa kufanya maamuzi
magumu kwa ajili ya maendeleo ya
nchi zetu kwa kuogopa kuwaudhi
wahisani wetu ambao wanaweza
wakatunyima misaada endapo
hawataridhika na maamuzi hayo
na hii imetufanya tuendele kuwa
masikini kiazi hata
kizazi.Tunasema kwamba tuko
huru lakini kama huwezi bado kujitegemea kiuchumi na
tunategemea kuendesha nchi zetu
kwa misaada yenye masharti
kutoka mataifa yale makubwa basi
huu si uhuru kamili.Uhuru kamili
ni pale tutakapoweza kujitegemea
kiuchumi kuachana na omba omba
ambayo inaturejesha katika
utumwa wa kiuchumi.Tunazo
rasilimali nyingi lakini
hazitunufaishi kwa sababu hatuna
uwezo wala teknolojia ya
kutosha,hatuna uhuru wa kupanga
bei wa bidhaa zetu za
kilimo.Rasilimali ni zetu lakini
tunapangiwa bei na hawa
wakubwa.Ninawahakikishia baba
na mama zangu na watanzania kwa
ujumla kama hali ikiendelea hivi,dunia itafika mwisho na sisi
tukiwa bado masikini wakubwa .
Wazee wangu wa Dar es
salama na watanzania,matamshi
ya rais Mike straw aliyoyatoa na
anayoendelea kuyatoa
yanaonyesha picha halisi ya hiki
ninachokizungumza.China ni
mshirika mkubwa wa Korea
Kaskazini na wanafanya biashara
kubwa lakini Marekani
haimuongelei China kwa kuwa ni
taifa kubwa kiuchumi na kijeshi
badala yake anatutolea vitisho sisi
mataifa madogo na masikini
kwamba tutakiona cha mtema
kuni tukithubutu kushirikiana kwa
namna yoyote ile na Korea Kaskazini.Huu ni unyanyasaji
ulipovuka mipaka.
Umasikini wetu kama
Tanzania na kama waafrika
unasababishwa na viongozi wetu
waliopo sasa na wale waliopita
kushindwa kufanya maamuzi
magumu kwa ajili ya kufanya
mapinduzi makubwa ya uchumi
kwa nchi zetu na hivyo nchi yetu
kuendelea kuitwa nchi masikini
wakati tuna utajiri wa kila
aina.Siwalaumu sana wazee wetu
kwani walifanya kazi kubwa ya
kupambana wakaikomboa nchi
yetuna kutujengea misingi mizuri
ya amani ,utulivu na mshikamano
lakini sasa umefika wakati wetu
sisi kufanya mapinduzi makubwa ya uchumi na kwa kuwa bado tuko
katika ukoloni wa kiuchumi ambao
kwa kiasi kikubwa uchumi wetu
unamilikiwa na mataifa makubwa
ya nje,lazima tufanye maamuzi
magumu sana.Matokeo ya
maamuzi tutakayoyafanya leo hii
hatutanufaika nayo bali watoto na
watoto wa watoto wetu.Nchi zote
zilizopiga hatua kimaendeleo
zilifanya maamuzi ya kuondokana
na umasikini na wakasimama
katika maamuzi yao na baada ya
vizazi leo hii wamekuwa mataifa
tajiri na nchi nyingine ambazo ni
tajiri sasa hazina rasilimali kama
tulizonazo sisi kwa hiyo hata sisi
tukiamua kuanza leo hii kuchukua
hatua madhubuti juu ya kuubadili uchumi wetu tunaweza” Makofi
mengi yakapigwa
“Nawaambieni ukweli wazee
wangu na watanzania kwamba
tunaweza tukiamua na lazima
tuamue.Hatuwezi kukubali hali hii
ikaendelea.Hatuwezi kuendelea
kuwa omba omba kwa nchi tajiri
wakati tunazo rasilimali nyingi
zimejaa kila kona ya nchi
yetu.Hatuwezi kuendelea
kuruhusu madini yetu na
rasilimali nyingine kuchukuliwa
na wageni kwa kisingizio cha
uwekezaji wakati wananchi wetu
wakiendelea kuwa masikini na
tunaachiwa mashimo.Tunaibiwa
halafu tunaletewa pesa kama
misaada kwa masharti wakati pesa hizo zinatokana na wizi mkubwa
wanaoufanya kwetu.Kufuatia hali
hiyo mimi kama rais wenu
mliyenichagua kwa kura nyingi
sana niwaongoze nimefanya
maamuzi magumu” akanyamaza
kidogo akanywa funda la maji na
kuendelea
“Wazee wangu wapendwa na
watanzania kwa ujumla nimeamua
kuiingiza nchi katika vita ya
kiuchumi.Nimechagua njia ngumu
ambayo wengi hawatapenda
kuipita lakini sisi lazima
tuipite.Nimeamua kuanzisha
mashirikiano ya kibiashara na
Korea kaskazini.Kelele nyingi sana
na vitisho vinatolewa kwa nchi zile
ambazo zinashirikiana na Korea Kaskazini lakini hayo yote
nimeamua kuyaweka kando na
kuamua kushirikiana na nchi hii”
Akanyamaza kidogo baada ya
kusikia kumekuwa na minong’ono
mle ukumbini akawatazama wazee
halafu akanywa maji kidogo na
kuendelea
“Wazee wangu nimefanya
maamuzi haya magumu sana licha
ya vitisho kwa nchi yetu kwa
sababu kubwa moja.Nchi ya Korea
kaskazini licha ya harakati zake za
kijeshi na kufanya majaribio
kadhaa ya makombora baharini
kitu ambacho sisi kama nchi
hatukiungi mkono lakini
wanafanya mageuzi makubwa sana
ya uchumi na uchumi wao unakua kwa kasi kubwa kiasi kwamba
wakubwa hawa wakiongozwa na
Marekani wanaanza kuwa nawasi
wasi kwamba uchumi wa Korea
Kaskazini ukiwa mkubwa sana
taufa hili litakuwa tishio kubwa
kwao na ndiyo maana wanafanya
kila wawezalo kuweza
kuizorotesha Korea Kaskazini
kiuchumi kwa kuweka vikwazo
vya kila mara vya kiuchumi lakini
pamoja na hayo bado uchumi wa
Korea kaskazini umeendelea
kupaa.Wamebadili sera zao za
uwekezaji na sasa wawekezaji
kutoka nchi nyingine
wanaruhusiwa kwenda kuwekeza
na kuna wawekezaji wengi kutoka
China na baadhi ya nchi za Asia.Wana viwanda vingi sana sasa
hivi na wanatengeneza bidhaa
nyingi sana ambazo masoko yake
makubwa ni nchi za Asia ,baadhi ya
nchi za Afrika na Ulaya.Wamekuza
teknolojia yao na wanatengeneza
bidhaa za kielekroniki kwa
teknolojia yao.Haya ni mageuzi
makubwa sana wameyafanya
ambayo hata sisi tunaweza
kuyafanya.Inakadiriwa kama
ukuaji huo wa uchumi wa Korea
Kaskazini utaendelea kama ulivyo
hivi sasa ,kwa miaka kumi ijayo
itakaribiana kulingana kiuchumi
na China.
Ukuaji huo wa kiuchumi wa
Korea Kaskazini unawafanya
wahitaji sana kupata malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda
vyao.Wanahitaji pamba nyingi kwa
kuwa wana viwanda vingi vya nguo
na kama haitoshi watajenga pia
viwanda vya nguo hapahapa
Tanzania na hawatanunua pamba
ghafi bali watajenga viwanda vya
kutengeneza nyuzi na kutengeneza
vitambaa hapa hapa nchini kwa
hiyo watanunua vitambaa kutoka
Tanzania na hiyo itaongeza
thamani ya Pamba ya Tanzania na
kuongeza mapato ya
nchi.Wanahitaji mafuta safi ya
magari na mitambo,wanahitaji gesi
wanahitaji madini na watajenga
kiwanda kikubwa cha kukata na
kuongeza thamani ya madini ya
vito hapa nchini hivyo hakutakuwa na madini yatakayopelekwa nje ya
nchi kukatwa kila kitu kitafanyika
hapa hapa Tanzania.Wanahitaji pia
mazao mengine ya kilimo kama
kahawa n.k.Wanahitaji pia madini
ya Urani kwa ajili ya kuzalisha
umeme wa kutosha wa viwanda
vyao tofautina maneno
yanayosemwa na Marekani na
washirika wake kwamba wanataka
kutumia madini hayo kuongeza
idadi ya silaha zao za nyuklia.
Sisi Tanzania pia tuko katika
mageuzi ya kiuchumi,viwanda
vingi vinajengwa hapa kwa hiyo
tutahitaji umeme wa
uhakika.Nimezungumza na
kiongozi wa Korea kaskazini na
ameahidi kutujengea kinu cha nyuklia hapa nchini kwetu kwa
ajili ya kuzalisha umeme kwani
tunacho kiwango kikubwa cha
madini ya Urani.Endapo
tutalifanikisha hilo Tanzania
tutakuwa wazalishaji wakubwa wa
umeme afrika mashariki na
tutauza umeme mwingine kwa
jirani zetu kwani tutakuwa na
kiwango kikubwa cha umeme.Haya
na mengi ambayo sijayasema hapa
ni picha ya wazi kwamba Tanzania
itanufaika sana kama itaanzisha
mashirikiano ya kibiashara na
Korea kaskazini.Kwa sasa
Marekani ndio wawekezaji
wakubwa hapa Tanzania katika
sekta muhimu kama gesi,na
madini lakini pamoja uwekezaji huo mkubwa walioufanya lakini
bado hatunufaiki chochote,ni wizi
mtupu unaoendelea huko,madini
yetu yanazidi kuisha bila ya sisi
kunufaika.Nimesema imetosha na
sasa tunataka kuanza kunufaika na
madini yetu wenyewe kwa hiyo
basi tutachukua hatua za kupitia
upya sera na sheria zetu za madini
na kwa wakati huo wote
makampuni haya yatasimamisha
shughuli zao hapa Tanzania hadi
hapo tutakapobadilisha sheria
zetu za madini ambazo tunataka
Tanzania inufaike kwa kiwango
kikubwa.Kama kuna kampuni
itakayoshindwa kukubaliana na
sheria zetu mpya milango iko wazi
na wanaruhusiwa kuondoka.Hatubembelezi
mwekezaji tena kwa hiyo yeyote
ambaye hajisikii kuwekeza
Tanzania anaweza kuondoka mara
moja.Tunataka kujenga uwezo wa
ndani ili tuweze kuchimba
wenyewe na kupata faida.
Wazee wangu na watanzania
,tumeanza kuchukua hatua za
kufanya mabadiliko katika uchumi
wetu na baadhi ya hatua hizo kama
vile mashirikiano na Korea
kaskazini hazitakuwa rahisi kwani
hazitawapendeza mataifa tajiri
kwa hiyo tutawekewa vikwazo
vikali vya kiuchumi.Tutazuiwa
kuuza bidhaa zetu katika masoko
ya kimataifa ,tutawekewa vile vile
vikwazo vya kuagiza bidhaa mbali mbali kutoa nje ya nchi,pamoja na
vikwazo vingine vingi lengo ni
kuudhoofisha uchumi wetu ili
tuwapigie magoti.Tutapitia kipindi
kigumu sana katika historia ya
nchi lakini
tutashinda.Nawahakikishia
tunashinda na mimi kiongozi wenu
nitasimama imara na kutangulia
mbele kuwaongoza hadi
nihakikishe nimewafikisha katika
Tanzania ya maziwa na
asali.”Makofi mengi yakapigwa
“Ndugu zangu narudia tena
kuwahakikishia kwamba
tutashinda hii vita japo
ngumu.Lakini hatutashinda kwa
maneo matupu bali kwa
vitendo.Kwanza kabisa sote tunapaswa kutambua kwamba
nchi iko vitani na si vita ya
kushambuliana kwa silaha kali bali
vita ya kiuchumi ambayo ni mbaya
sana.Baada ya kulifahamu hilo kila
mmoja anapaswa aiunge mkono
vita hii na nchi yote inapaswa ije
pamoja .Tukijiunga na kwenda
pamoja kama nchi basi vita hii
haitakuwa ngumu kwetu lakini
endapo tutajigawa wenyewe kwa
wenyewe tutawapa nafasi maadui
zetu kwa hiyo nawaomba sote
tushikamane katika vita hii.Najua
si wote watakubaliana na haya
tunayoyafanya lakini naomba hata
wale wasiokubaliana nasi
wasiwavunje moyo wale ambao
wamekubali kuingia vitani.Tunataka kuiondoa nchi
katika utegemezi kwa hiyo
tutakuwa wakali sana kwa yeyote
atakayejaribu kuturudisha nyuma.
Tunaanza kwa kujenga
biashara ya ndani,tujenge
utamaduni wa kutumia bidhaa
zetu zinazozalishwa na viwanda
vya ndani,tuvae nguo zetu,viatu
vyetu na hivyo kuvijengea uwezo
viwanda vyetu vya ndani.
Tutaimarisha biashara baina ya
nchi majirani na kuzitumia vyema
fursa za kikanda kufanya biashara
na vile vile tutajenga mashirikiano
makubwa na nchi ambazo
zitatuunga mkono katika vita
hii.Tayari nimekwisha pata
uthibitsho kutoka kwa rais wa China ambaye ametangaza rasmi
kutuunga mkono,Urusi wako na
sisi,India,Iran,Venezuela,Mexico,Br
azil,Qatar na nchi nyingine mbali
mbali za kiarabu.Hawa na wengine
ambao wataendelea kutuunga
mkono tutajenga nao mashirikiano
mazuri ya kibiashara na hivyo
uchumi wetu utaendelea
kuiamarika licha ya
vikwazo.Kikubwa zaidi tunapaswa
kufaya kazi kwa bidii sana na
kuhakikisha kila kaya
inajitosheleza kwa chakula na nchi
kwa ujumla na kuweka
akiba.Tujifunze matumizi mazuri
ya fedha tunazozipata.Kuhusu ajira
nawaomba msihofu ndugu
watanzania kwani viwanda vingi vitajengwa na tutazalisha ajira
nyingi.Mambo yote haya
yatafanikiwa endapo
tutashikamana ndiyo maana
narudia tena kuwasisitiza ndugu
watanzania tushikamane sana na
kufanya kazi kwa bidii.Mtuunge
mkono katika kila hatua
tunazochukua kwa manufaa ya
nchi yetu.Endapo tukienda pamoja
tutafanikiwa katika vita hii na
Tanzania itakuwa ni taifa kubwa
kiuchumi Afrika,tutaweza
kujitegemea wenyewe na
hatutayumbishwa na mtu au taifa
lolote”
Hotuba hii ya rais Dr Vivian
ilisimamisha nchi kwa muda wote
aliokuwa anaitoa.Ilikuwa inarushwa mubashara katika
runinga na katika redio zote hivyo
wananchi wote hata wale wa
vijijini waliweza kuipata.Wengi
walifurahishwa sana na hotuba ile
hasa msimamo wa rais kuhusiana
na mageuzi makubwa ya
uchumi.Wengi waliokuwa na hofu
waliondolewa hofu baada ya
kumuona rais wao namna
alivyokuwa amejiamini na
akiongea bila woga wowote.Wengi
waliipongeza sana hotuba ile nzuri
na waliahidi kumuunga mkono
rais katika vita ile ya kiuchumi
aliyoitangaza.
Tayari kiza kimekwisha ingia
na Theresa amekwisha jiandaa
tayari kuelekea hoteli Pentagone
kumchukua Nathan kama
alivyokuwa amemuahidi kwamba
atakwenda kumchukua.Kwa zaidi
ya dakika kumi na tano sasa
Theresa amekuwa mbele ya kioo
kikubwa cha kujitazamia
akijiangalia na uso wake
ukionyesha wasiwasi mkubwa
aliokuwa nao.
“Kuna sauti ninaisikia
inaniambia kwamba nisifanye hivi
ninavyotaka kufanya lakini kila
nikimfikiria Nathan naikumbuka
picha ya risasi zaidi ya sabini alizopigwa baba,namkumbuka
mama alivyoyatoa maisha yake
kuniokoa.Japokuwa bado haina
uthibitisho lakini naamini Nathan
ni mmoja wa watu walio katika
mtandao wa wale walioteketeza
familia yangu na bado anaendelea
kutuchunguza na kusabisha tuishi
kwa wasi wasi.Nikikumbuka
mambo haya ninajikuta nikipata
hasira na kuendelea na mipango
yangu.I’ll never be the same after
tonight but I have to do it to
protect myself and my
sister”Theresa akatolewa
mawazoni na simu ya Mathew
“Hallow Theresa”
“hallow Mathew” “Theresa are you ok? Mathew
akauliza baada ya kugundua kitu
katika sauti ya Theresa
“I’m ok Mathew.Uko wapi?
‘Niko nyumbani kwangu
nimekwisha jiandaa na ninasubiri
simu yako.Nimeona kimya ndiyo
maana nimeamua kukupigia”
akasema Mathew
“Niko hapa nyumbani
ninajiandaa kuelekea hoteli
Pentagone kumchukua Nathan”
“Ok sawa ukishamchukua
utanijulisha kwa ujumbe mfupi”
akasema Mathew na kukata simu
“Miguu yangu mizito hata
kunyanyuka lakini lazima nijikaze
na nikamilishe mpango wangu.Bila
kufanya hivi dada na mimi tutakuwa hatarini” akawaza
Theresa na kuchukua mkoba wake
akaingia garini na kuondoka
kuelekea hoteli Pentagone.
“Ukimuona alivyo kama
malaika kumbe ni shetani nyoka
mkubwa yule.Kwa muda huu wote
amekuwa
anatuchunguza.Amekuwa anapata
taarifa zetu zote na sielewi ni kitu
gani anakichunguza kwetu? Kitu
gani anakichunguza kwa
dada?Kuna nyakati ninafikiri
yawezekana labda bado
wanatuchunguza kufahamu
kuhusu football? Hisia zinanituma
hivyo yawezekana hawa jamaa
wamekaa kimya muda huu wote na
wanatuchunguza.Kama ni hivyo basi Marekani ndio waliomuua rais
Anorld na kuiteketeza pia familia
yangu.Ninashukuru sijawahi
kumueleza mtu yeyote kuhusu siri
hii na kama ningefanya hivyo
wangekwisha tuua mimi na
dada.Nathan ametumwa makusudi
kwa lengo la kutuchunguza lakini
usiku wa leo ni mwisho wa
sarakasi zake” akaendelea kuwaza
Theresa huku sura yake ikijikunja
kwa hasira
Alifika hoteli Pentagone na
kwenda kugonga chumbani kwa
Nathan akafunguliwa na kumkuta
Natha akiwa amekaa sofani
amependeza kwa suti nyeusi huku
uso wake ukiwa na tabasamu.Theresa akavuta pumzi
ndefu na kutabasamu
“tabasamu kwa mara ya
mwisho paka wewe” akawaza
Theresa na kwenda kumkumbatia
Nathan
“Umeshindaje leo?
“Nimeshinda salama
Theresa.Sijui wewe”
“Hata mimi nimeshinda
salama”
“Nilikuwa na hofu pengine
hautakuja tena” akasema Nathan
na wote wakacheka
“Kwa nini nishindwe kuja
wakati ni mimi ndiye
niliyekuomba uje? Akasema
Theresa huku akicheka kidogo “Uko tayari?Tunaweza
kuondoka? Akauliza Theresa
“Niko tayari tunaweza
kuondoka” akasema Nathan
wakatoka mle chumbani
wakaingia katika gari la Theresa
wakaondoka
“Vivian
anaendeleaje?Umefanikiwa
kuonana naye? Nathan akauliza
“Usiwe na haraka hivyo
Nathan,utafahamu kila
kitu”akasema Theresa huku
akitabasamu
“Moyo wangu hautulii kila
nikimuwaza Vivian.Toka
tulipoingia katika mgogoro siko
sawa kabisa” “Ushofu Nathan suala hili
limekwisha malizika na kama
ikimpendeza Mungu usiku wa leo
utakuwa ni usiku wa furaha kubwa
katika maisha yako”
“Kweli Theresa? Akasema
Nathan kwa furaha kubwa
“Mimi huwa ninaongea kwa
vitendo.Twende nyumbani tupate
chakula na kisha mambo mengine
yatafuata ila leo kuna mambo
makubwa.” Akasema Theresa .
Walifika nyumbani kwa
Theresa na Nathan akakaribishwa
sebuleni
“Una nyumba nzuri sana
Theresa”
“Ahsante Nathan.Kabla ya yote
ngoja kwanza niandae chakula tule halafu nikueleze mwanzo hadi
mwisho kuhusu suala lenu”
Akasema Theresa na kwenda
jikoni akaitazama chupa yenye
mvinyo akaishika na akahisi
mikono inamtetemeka.Akaiweka
chupa chini na kuchukua simu
yake akamtumia ujumbe Mathew
akamjulisha kwamba tayari
Nathan alikuwa pale nyumbani
kwake.Akachukua tena chupa ile
akaitazama na kuchukua glasi
akaelekea sebuleni akammiminia
Nathan katika glasi
“Nathan karibu kinywaji mimi
naandaa chakula.Jisikienyumbani”
akasema Theresa na kuondoka
pale sebuleni akaenda kuandaa
chakula . “Mungu atanisamehe kwa hili
nililolifanya lakini sina namna
nyingine ya kufanya.Nina hasira
sana yule kenge.Ni mtu hatari
sana kwetu.Huyu ni nyoka mwenye
sumu kali ambaye anapaswa
kupondwa kichwa haraka sana
kabla hajatujeruhi” akawaza
Theresa.Alionekana kuwa na wasi
wasi mwingi.Aliandaa chakula
mezani na kuelekea sebuleni
kuchungulia.
Nathan alikuwa ameanguka
amelala sakafuni akiwa
amejikunja.Mdomoni alionekana
kutokwa na mapovu mengi huku
akikoroma kwa nguvu.Theresa
akapata ujasiri akamfuata
akajaribu kumtikisa lakini Nathan hakuwa na fahamu na aliendelea
kukoroma kwa nguvu na mara
akawa kimya .Theresa akashindwa
kujizuia akaenda chumbani kwake
akilia.
“Please Lord forgive me.I’ve
killed him !! akalia kwa woga.Mwili
wote ulikuwa unamtetemeka.
“Sikuwahi kuhisi kama siku
moja na mimi nitaingia katika
dhambi kubwa kama hii ya kuua
mtu.Lakini huyu ni mtu hatari sana
kwa usalama wa nchi yetu na kwa
familia yangu.Angeendelea kubaki
hai angetuteketeza wote na kuleta
madhara makubwa kwa
nchi.Sitakiwi kulia,napaswa kuwa
jasiri.Hawa ndio walioiteketeza
familia yangu kikatili sana.Nilikuwepo siku ile na
nilishuhudiwa namna baba
alivyouawa.Lazima nilipe kisasi
kwa ajili ya baba na mama
waliouawa kikatili” akawaza na
kuinuka akaenda jikoni akachukua
chupa ile yenye mvinyo akaenda
kuumwaga wote chooni na kwena
nje akaivunja vunja ile chupa na
kutupa vipande vyake katika
shimo la maji machafu akarejea
sebuleni.Nathan alikuwa ameloa
mapovu na alikuwa ametoa ulimi
nje.Akamtikisa kwa mguu
“He’s
gone”akawaza.Akaichukua glasi ila
ya kinywaji aliyokuwa anaitumia
Nathan na kwenda kuitupa katika shimo la maji taka akarejea
sebuleni
*****************
Mathew alipopata ujumbe wa
Theresa kwamba tayari
amekwisha mchukua
Nathan,hakuwa mbali na hoteli
Pentagone hivyo akawasha gari
akaelekea moja kwa moja hoteli
Pentagone.Usiku huu hoteli hii
ilikuwa inang’aa kutokana na taa
nyingi za kila rangi.akaegesha gari
na kushuka akaelekea
ndani.Kulikuwa na watu wengi
katika sehemu ya chini
kulikokuwa na hoteli na
baa.Kulikuwa na bendi iliyokuwa inapiga muziki wa kiafrika na
kuwaburudisha wageni waliofika
hotelini hapa.Hakuna aliyekuwa
na mashaka na Mathew akapanda
lifti hadi ghorofa ya tatu.Ndani ya
lifti alikuwa peke yake na alipofika
ghorofa ya tatu akashuka akaanza
kutafuta chumba namba 202
ambacho ndicho chumba cha
Nathan.Alikuwa amevalia nadhifu
kabisa akiwa katika suti nzuri ya
kijivu na mkoba mzuri wa
gharama kubwa, alionekana ni mtu
mwenye uwezo kifedha.Alipishana
na watu kadhaa na halafu
akakipata chumba namba
202.Akatazama pande zote na
hakuona mtu yeyote.Kulikuwa
kimya.Akatoa mashine fulani ndogo toka katika mkoba wake
akaigundisha pembeni ya sehemu
ya kupitishia kadi ya kufunguilia
mlango halafu akachukua kadi
fulani akaiingiza katika kile kifaa
alichokigundisha mlangoni na
kubonyeza namba kadhaa na
kusubiri kwa muda wa sekunde
kadhaa na taa ya kijani ikawaka
halafu akaipitisha kadi ile katika
sehemu ya kuwekea kadi na
namba fulani zikajitokeza katika
kile kifaa alichokigundisha
pembeni na mlango
ukafunguka.Taa ilikuwa inawaka
chumbani akaizima haraka halafu
akawasha kifaa fulani kidogo na
mara akaona mwangaza wa bluu
pembeni ya dirisha akasogea na kukiondoa kile kifaa kilichokuwa
karibu na dirisha akakikanyaga
kwa mguu kikasambaratika.Bado
kifaa kile alichokuwa amekiwasha
kiliendelea kutoa mlio akatazama
chini ya kitanda na kuona kuna
mwanga wa bluu akafunua godoro
na kutoa kifaa hicho akakiharibu
vile vile.Baada ya hapo akatoa
kopo fulani akapuliza mle
chumbani na kuvaa miwani
maalum na kuona kitu fulani
kidogo kilichokuwa juu ya meza
ambacho unaweza
ukakidharau.Akakichukua
akafungua dirisha na kukitupa nje.
“Clear” akasema na kuwasha
taa “Kweli huyu jamaa ni
jasusi.Alikuwa amechukua kila
hatua ya kujihami.” Akawaza
Mathew na kuanza kuchunguza.Juu
ya meza kulikuwa na kompyuta
mpakato,akaichukua na kuiweka
katika mkoba wake.Akalifungua
sanduku lake na kumwaga kila
kitu kitandani akaanza kukagua
kitu kimoja kimoja akakutana na
simu tatu,akazichukua zote
akaziweka katika mkoba
wake.Kitu cha mwisho
alichokipata kilikuwa ni kimkebe
fulani kidogo cha rangi nyekundu
akavichukua vyote na wakati
akirejesha nguo katika sanduku
mara simu yake ikaita,alikuwa ni
Theresa “hallow Theresa”
“Mathew uko wapi?
“Niko hapa chumbani kwa
Nathan najiandaa niondoke.Tayari
amekwisha ondoka?
“Mathew nakuomba uje hapa
nyumbani kwangu haraka
sana.Chukua kila unachotaka
kikichukua na uje hapa nyumbani
haraka”akasema Theresa
“Kuna nini Theresa? Nathan
amekwisha ondoka hapo?
“Mathew naomba uje hapa
haraka sana .Kuna tatizo
limetokea”
“Kuna tatizo gani?
“Siwezi kukueleza simuni
Mathew nakuomba uje haraka”
akasema Theresa na kukata simu.Mathew akapakia vitu haraka
haraka katika sanduku na kutoka
mle chumbani akachungulia kama
kuna mtu yeyote pale karibu lakini
hakukuwa na mtu akatoka haraka
haraka na kupitia sehemu ya baa
halafu akaelekea mahala
alikoegesha gari akaondoka hoteli
Pentagone
“Theresa ana tatizo
gani?Nathan amegundua kitu na
anataka kumdhuru? Akajiuliza
huku akiongeza mwendo wa gari
na kuyapita magari kadhaa
“Lazima kutakuwa na tatizo
kubwa .Huyu jamaa ni mtu hatari
alikuwa amejihami sana.Ndani ya
chumba kile kulikuwa na kifaa kile
alichokuwa amekiweka pembeni ya dirisha ambacho kazi yake
ilikuwa ni kuhisi aina ya mtu
aliyeingia chumbani na
kumjulisha Nathan kama kuna mtu
chumbani kwake.Hiki ni kifaa
kinachomchunguza mtu
kibaolojia.Kinahisi hadi harufu ya
mtu.Huyu jamaa atatuongoza
kuelekea kupata majibu ya
maswali yetu” akawaza Mathew
Alifika nyumbani na mara tu
Mathew aliposhuka garini Theresa
akamfuata akamkubatia
“Thank you Mathew for
coming” akasema na kumshangaza
Mathew.
“Theresa kuna atizo gani?
Umenistua sana uliponipigia
nikahisi umepata tatizo kubwa.Yuko wapi Nathan?
ameondoka? Akauliza
Mathew.Theresa alionekana kuwa
na woga mwingi
“Mathew twende ndani
tafadhali” akasema Theresa na
wakaelekea sebuleni.Mathew
akastuka sana baada ya kumuona
Nathan akiwa amelala sakafuni
amejaa mapovu mdomoni na
alionekna hana uhai.
“Nini kimetokea? Akauliza
Mathew huku akimsogelea Nathan
na kutaka kumshika Theresa
akamzuia
“Don’t touch him ! akasema
Theresa na kuzidi kumshangaza
Mathew “Theresa kuna nini ?Nathan
amefanya nini?Mathew akauliza
“He’s dead”
“Dead? How? Mathew akauliza
“Nini kimetokea hapa
Theresa? Akauliza Mathew huku
akiwa amemkazia macho Theresa
“Theresa niambie nini
kimetokea hapa? Nini kimemuua
Nathan?akauliza Mathew lakini
Theresa alishinda kujibu alikuwa
anatetemea midomo
“You did this? Akauliza
Mathew lakini Theresa hakujibu
kitu
“C’mon Theresa answer me
you did this?akauliza kwa ukali na
Theresa akatikisa kichwa
kukubali. “Oh my God !! akasema
Mathew na kumtazama Theresa
kwa hasira
“Kwa nini Theresa?Why
????akauliza Mathew
“Mathew I’m sorry.I had no
choice”
“No choice? Just that? Akauliza
Mathew.
“Mathew I’m sorry.”
“Stop Theresa!! Akasema
Mathew kwa ukali
“How could you be so stupid?!!
Akafoka Mathew
“Kwa nini ukafanya jambo hili
la kijinga bila kupima athari zake?
Akaendelea kufoka
Mathew.Maneno yale ya Mathew yakaonekana kumkera sana
Theresa akapandwa na hasira
“Mathew naomba usirudioe
tena kuniita mimi
mjinga.Nimelazimika kufanya hivi
nilivyofanya kwa usalama
wetu.Huyu mtu ni hatari na wewe
unafahamu.Ameweka maisha
yangu na dada hatarini.Huyu na
mtandao wake ndio waliochukua
uhai wa baba kikatili
sana.Nitawezaje kumuacha hai mtu
kama huyu ambaye anatuwinda
usiku na mchana?Anatafuta taarifa
zetu kila uchao,nimeshindwa
kuvumilia Mathew nimeamua
kuingia katika dhambi ya uuaji
kwa ajili ya kuilinda familia
yangu,kumlinda dada yangu.Unajua ni taarifa ngapi
kuhusu dada zimewafikia
wanaomtafuta usiku na mchana
kupitia huyu mtu? Hukufanikiwa
kuziona maiti za wazazi
wangu,baba alipigwa risasi zaidi ya
sabini,unadhani mwili wake
ulikuaje?Yalikuwa ni mauaji ya
kikatili sana ambayo yalifanywa na
mtandao wa huyu mtu.Siwezi
kumuacha akaenda hivi hivi
nimeamua kumuua.Nimemuwekea
sumu kali katika kinywaji yenye
uwezo wa kuua kwa
haraka.Vyovyote utakavyoamua
kufanya mimi niko tayari kama ni
kunipeleka polisi just do it I’m
ready to pay for what I’ve done”
akasema Theresa.Mathew akainama na kushika
kiuno.Alizama mawazoni
“Mathew do it quick.Call the
police! Akasema Theresa kwa
hasira
“Theresa tafadhali usifanye
utani katika suala kama
hili.Nathan alikuwa ni mtu
muhimu sana katika uchunguzi
wetu na tulitegemea kupata
mambo mengi kupitia kwake na
ndiyo maana nikakuomba ufanye
juu chini aweze kuja nchini .Kama
ni kumuua ningeweza kumuulia
huko huko Marekani lakini
sikutaka afe kwani kuna mambo ya
muhimu sana ninayahitaji kutoka
kwake. Kwa hiki ulichokifanya
tumerudi tena kwenye ziro hatuna tena mwanga.Kama ulikuwa na
mawazo ya kumuua Nathan
ungenieleza mapema ili tusubiri
kwanza baada ya kufanya
uchunguzi wangu ndipo nikuachie
umuue uondoe hasira zako”
“Mathew hawa watu
wameteketeza familia yangu.Hujui
ni uchungu kiasi gani nilionao
baada ya kugundua kwamba huyu
yuko katika mtandao wa watu
waliowateketeza wazazi wetu na
bado anaendelea kutufuatilia
usiku na mchana.Hata wewe
ungekuwa mahala pangu
usingeweza kumuacha hai.Potelea
mbali Mathew kama uchunguzi
utashindikana lakini ili mradi mtu
huyu hatari nimekwisha muondoa duniani na mimi na dada yangu
tuko salama !! akasema Theresa
“Usijidanganye Theresa.Dr
Vivian hayuko salama.Umezidi
kuyaweka maisha yake katika
hatari kubwa kwa hiki
ulichokifanya.Umeongeza mzigo
wa matatizo” akasema Mathew na
Theresa akainamisha kichwa
akafuta machozi halafu kwa sauti
ya upole akasema
“Mathew please help
me.Rightnow I’m don’t know what
I’m going to do” akasema
Theresa.Mathew akamtazama kwa
muda halafu akasema
“Kuna mtu mwingine yeyote
anafahamu au umempigia simu kuhusiana na hiki kilichotokea?
Akauliza Mathew
“Hapana sijamjulisha mtu
yeyote zaidi yako”
“Good” akasema Mathew na
kuinamisha kichwa akafikiri
kidogo na kumtazama tena
Theresa
“Jambo hili tunapaswa
kulifanya liwe siri kubwa ili rais
asilifahamu.Tunapaswa kutafuta
namna ya kuficha huu mwili
usionekane kabisa na mtu yeyote
na hata kama ikigundulika basi
awe tayari hatambuliki” akasema
Mathew
“Una maanisha tukamzike? “Kama ikiwezekana iwe hivyo
itakuwa vizuri lakini tutamzika
wapi usiku huu?
“Mathew sifahamu
chochote.Ninahisi
kuchanganyikiwa tafadhali fanya
kile unachoweza kukifanya uweze
kuuondoa mwili huu na
kuuficha.Akili yangu haifanyi kazi
tena” akasema Theresa huku
akiendelea kumwaga machozi
Mathew akainamisha kichwa
na kuanza kufikiria,akatazama saa
yake ilionyesha ni saa tano za
usiku.Akachukua simu yake na
kuzitafuta namba fulani akapiga na
simu ikapokelewa
“Hallow Casian naomba
kuzungumza na Hamis Chuma mara moja” akasema Mathew na
hakutoa simu sikioni na baada ya
dakika mbili ikasikika sauti nzito
“Bilionea Mathew,habari yako
kaka?
“Nzuri kabisa Hamis.Uko wapi
mida hii?
“Niko sehemu fulani
tunajiandaa kwenda kazini”
“C’mon Hamis hamuachi
shughuli hizo?
“Tukiacha tutaishije ndugu
yangu mji wenyewe huu halafu na
nyie watu wakubwa mmetukimbia
siku hizi hata mawasiliano nasi
hamtaki?
“Si hivyo
Hamis,ninawakumbuka sana watu
wangu lakini naomba muachane na hizo shughuli mimi nitatafuta
namna ya kuwawezesha”
“Ndiyo maana nakukubali
sana Mathew wewe uko tofauti na
wengine.Unapenda kutatua shida
za watu.Haya nieleze mkubwa
wangu kuna nini usiku huu
manaake najua haujanitafuta ili
kunisabahi.Ukinipigia usiku kama
huu lazima kuna kazi unataka
kunipa”
“Ni kweli Hamis kuna kazi
nataka kukupa.Uko na vijana
wangapi?
“Niko na vijana watano”
“Good.Kuna kazi nataka
niwape na nitawalipa vizuri sana
ila nataka muifanye kadiri ya maelekezo yangu” akasema
Mathew
“Usihofu mathew wewe
unajua namna sisi tunavyofanya
kazi zetu.Tukutane wapi?
“Mbele ya Balale Bridge kuna
ghorofa limetelekezwa kwa miaka
mingi.Tukutane pale ndani ya
dakika ishirini.” akasema Mathew
na kukata simu
Theresa nahitaji mfuko
wowote mkubwa au karatasi
kubwa la nailoni pamoja na
kamba” Akasema Mathew.Theresa
akaenda stoo na kurejea na
karatasi kubwa la nailoni na
kamba pamoja na glovu.Mathew
akamlaza Nathan juu ya karatasi
ile halafu akamsachi hakuwa na kitu chochote zaidi ya saa ya
mkononi akaivua na kuiweka
mfukoni.Akamviringisha vizuri
ndani ya ile karatasi na kumfunga
kamba.BadoTheresa alikuwa
analia.
“Mlinzi wako anajua
kuendesha gari?
“Ndiyo anafahamu”
“Good.Mpe funguo mwambie
aende akakuletee mvinyo.Mtume
mbali kidogo sitaki aone wakati
tunautoa mwili huu na kuupakia
garini.Kuna mtu mwingine ambaye
you humu ndani mida hii ?
“Hakuna mtu
mwingine.Mtumishi wangu
amesafiri” akasema Theresa. “Haya fanya haraka
kamuondoe mlinzi pale getini”
akasema Mathew na Theresa
akatoka baada ya dakika tano
akarejea
‘Tayari amekwisha ondoka na
gari.” Akasema Theresa
“Good”akasema Mathew na
kumbeba Nathan hadi katika gari
lake wakampakia katika buti
“Kuna kitu chochote unahisi
hakijakaa sawa hapo ndani?
“Kila kitu kiko safi”
“sasa mpigie simu mlinzi
wako mwambie arudi umepata
dharura kuna mahala
unakwenda”akasema Mathew na
kumpigia simu mlinzi wake akamtaka arudi nyumbani kwani
yeye amepata dharura ametoka
“Now let’s go” akasema
Mathew na kuondoka.
“Wale uliokuwa unazungumza
nao kwenye simu ni akina nani?
Theresa akauliza
“Ni watu wangu”
“Wanafanya shughuli gani?
“Watoto wa mjini”
“Watoto wa mjini? Hawana
shughuli?
“Wanashughulika na
ujambazi” akasema Mathew na
sura ya Theresa ikaonyesha
mstuko mkubwa sana
“Usistuke Theresa.Katika
shughuli zetu huwa tunajikuta
tunafahamiana na watu mbalimbali na kuna wakati huwa
tunasaidiwa na watu kama
hawa.Kuna kazi nyingine ambazo
hatuwezi kuzifanya na huwa
tunawatumia watu kama hawa
wakazifanye.Wao ndio
watakaoshughulikia huu mwili na
hautaonekana tena”
“Do you trust them? Theresa
akauliza
“Relax Theresa.Let me fix this.
akasema Mathew.
CENTRAL INTELLIGENCE
AGENCY (CIA) – WASHINGTON DC
Saa tisa alasiri jijini
Washington DC kikao kilikuwa
kinaendelea katika ofisi za shirika
la ujasusi la Marekani CIA.Ndani ya
chumba cha mikutano kulikuwa na
watu kumi na tatu.Wakati kikao
kikiendelea mlango ukafunguliwa
akaingia mwanadada mmoja
aliyekuwa amevaa sketi fupi na
kufanya kikao kisimame akamuita
mkubwa wake ambaye aliwaomba
samahani wajumbe akatoka nje.
“Kuna nini Monica? Akauliza
“Mr Edger kuna tatizo
limetokea naomba kama hutajali
twende ofisini kwangu” akasema Monica na Edger akaingia tena
katika kile chumba cha mkutano
akawaomba wajumbe wamsubiri
kuna dharura imejitokeza na
atarejea muda si mrefu halafu
akaelekea moja kwa moja ofisini
kwa Monica
“Kuna nini Monica? Akauliza
Edger Brown
“Kuna tatizo limetokea kwa
Cell 12A.” akasema Monica na
kumstua kidogo Edger
“Kuna nini kimetokea?
“Cell 12A aliondoka jana
kuelekea Tanzania na nilikuwa
nafuatilia maendeleo yake.Dakika
chache zilizopita mawasiliano yake
yalikatika” “Nini? Akauliza Edger kwa
mshangao.Monica akabonyeza
kompyuta yake na katika runinga
kubwa iliyokuwamo mle ofisini
kukatokea kitu mfano wa chati
iliyokuwa na mstari mmoja
ulionyooka katikati.
“Mr Brown,Cell 12A alikuwa
katika orodha ya wale maajenti wa
CIA walioingizwa katika mfumo
mpya wa utambuzi ambao
wamefungiwa kifaa maalum ndani
ya miili yao ambacho hurekodi
mwenendo wa mapigo ya moyo na
ambacho huwa kinaunganishwa
kwa saa maalum anayoivaa
mkononi ambayo hutuwezesha sisi
kupata taarifa zake kila wakati na
hapaswi kuivua saa hiyo katika siku zote za maisha yake.Iwe mvua
au jua saa hiyo haitoki mkononi
kwani imetengenezwa maalum na
haipitishi maji wala
haiharibiki.Muda mfupi uliopita
kulitokea tatizo kwa Cell
12A.Nilisikia kengele ya thadhari
ikilia na nilipofuatilia nikagundua
mapigo ya moyo ya Cell12A
yalikuwa yameshuka chini isivyo
kawaida na hii ni ishara kwamba
alikuwa katika hali mbaya na
baadae hali ikawa kama
unavyoona katika chati .Ikiwa hivi
inamaanisha kwamba ajenti huyo
tayari amefariki dunia”
“Mungu wangu!! Akasema
Edger Brown. “Umejaribu njia zote za
kuwasiliana naye zimeshindikana?
“Njia zote za kuweza kupata
mawasiliano yake na kufahamu
yuko wapi zimekatika ghafla na
hakuna inayofanya kazi.Ni saa
yake tu ambayo bado ninaendelea
kuisoma hapa”
“Hizi ni taarifa za kustusha
sana”
“Kitu kingine” akasema
Monica
“Kuanzia leo asubuhi taarifa
kutoka kwa namba 1212 ambaye
ni rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania zimekatika na mpaka
sasa hakuna rekodi zozote kutoka
kwake wala kutoka kwa namba
1214.Wote hawa wawili taarifa zao zimekatika asubuhi ya leo kitu
ambacho kinatia shaka kidogo
halafu hawa ni ndugu.Namba 1214
ni mdogo wake na 1212.”
“Kuna kitu hakiko sawa
Tanzania.Hatua za haraka sana
zinatakiwa kuchukuliwa.Usifanye
chochote ngoja kwanza
niwasiliane na wakuu wangu
niwape taarifa” akasema Edger
brown na kuchukua simu
akawasiliana wakuu wake
akawajulisha kile ambacho
alikuwa ameelezwa na
Monica.Taarifa zile ziliwastua hata
wakubwa wake
“Kitu cha kwanza
unachopaswa kukifanya Mr Brown
wasiliana na 110C huyu atafanya mipango ya kwenda kumnusuru
12A kama yuko kwenye hatari
.Baada ya hapo suala la 1212 na
1214 lianze kushughulikiwa
haraka sana kwani hatuwezi
kuwapoteza hawa hasa kwa wakati
huu.Ni watu muhimu sana.110C
afanye kazi ya ziada kuhakikisha
kila kitu kinakaa sawa mpaka
kufikia kesho jioni.Kitu kingine Mr
Brown endapo kunatokea jambo
kubwa kama hili toa taarifa makao
makuu haraka sana kwa ajili ya
maamuzi ya haraka.Elekeza macho
yako Tanzania ambako ni muhumu
sana kwetu kwa sasa.Tumekaribia
sana kwa hiyo hatuwezi
kushindwa hapa.110C ahakikishe
suala hili halitokei tena.Tunamuhitaji sana 1212
kuliko kawaida” akasema Steven
Camp
Edger brown akarejea katika
ofisi ya Monica haraka
“Monica mpigie simu haraka
110C nahitaji kuzungumza naye”
akasema Edger.Monica akapiga
simu maalum kwa namba 110C na
ilipoanza kuita akampatia Edger
“Hallow 110C
ninazungumza.Naongea na namba
ngapi?
“Unazungumza na Eger Brown
CIA washigton DC.Kuna tatizo
limetokea muda si mrefu na
nimepewa maelekezo kwamba
ulishughulikie haraka sana.Cell
12A aliondoka huku marekani kuelekea Tanzania jana na amefika
leo.Muda mfupi uliuopita
mawasiliano yetu yameonyesha
kwamba mapigo yake ya moyo
yalianza kushuka sana na baadae
yakakatika kabisa.Hii
inatuonyesha kwamba yuko katika
hatari au tayari amekufa kwa hiyo
tunataka ulishughulikie hilo
haraka sana na uhakikishe
anapatikana akiwa katika hali
yoyote ile mzima au
amekufa.Wasiliana nasi kila baada
ya dakika kumi na tano kutupa
taarifa.Monica anakutumia ramani
inayoonyesha mahala alipo 12A
ambako mpaka sasa bado
tunaendelea kumsoma lakini hatuna taarifa za mapigo ya moyo
wake”
“Sawa ngoja nilishughulikie
hilo haraka sana.”
“Jambo la pili” akasema Edger
“1212 na 1214 wamekatika
kuanzia asubuhi ya leo.Fuatilia
ujue kuna tatizo gani?Tunataka
mawasiliano yarejeshwe haraka
sana kabla ya kesho jioni” akasema
Edger
“Sawa Edger ngoja
nishughulikie kwanza hili la 12A”
akasema 110C na kukata simu
DAR ES SALAAM – TANZANIA
“Umepata nini kule chumbani
kwa Nathan? Akauliza Theresa wakiwa wamesimama katika taa
za kuongozea magari za barabara
ya Serengeti.Hakukuwa na magari
mengi katika barabara hii.Taa
zikawaruhusu kupita wakaishika
barabara ya Uwazi.Hii ni barabara
inayopita kandoni mwa bahari na
kwa usiku huu hakuna magari
mengi.Mathew alitaka wawahi
kufika mahala walikopanga
wakutane na akina Hamisi Chuma
“Mathew haukunijibu swali
langu”Theresa akakumbusha
“Nilikuuliza ulipata vitu gani
kule chumbani kwa Nathan.Kuna
chochote ulifanikiwa kukigundua?
“Kuna vitu vichache
nimevipata .Nimepata kompyuta
ndogo,simu tat……………” akasema Mathew na mara akasikia
muungurumo wa
helkopta.Haikuwa juu sana akatoa
kichwa kutazama nje.Helkopta ile
ilikuwa chini chini sana na ilikuwa
inakwenda sambamba nao
Kwa mbali nyuma yao
zikaonekana gari mbili zikija kwa
kasi kubwa sana.Mathew
hakushangaa kwani ni kawaida ya
gari kukimbia katika barara hii
ambayo kwa usiku huu huwa haina
magari mengi.
“Tutakapolimaliza hili suala
nitavipitia vifaa vile na kuona
kama kuna chochote tunaweza
kugundua.”
Piki piki mbili zilizokuwa
zinakwenda kwa kasi kubwa zikawapita kwa kasi na helkopta
ile ikaendelea kutembea juu yao.
“Theresa kuna hali naiona si
ya kawaida hapa.Kuna hizi gari
mbili zinakuja nyuma yetu kwa
kazi kubwa halafu kuna hizi piki
piki mbili zimetupita kwa kasi na
zilipofika mbele yetu zimepunguza
mwendo na ile helkopta naona
inaanza kupaa juu zaidi” akasema
Mathew.Alianza kuhisi hatari.
“Una wasi wasi labda
tunafuatiliwa? Akauliza Theresa
huku akitazama nyuma
“Ninahisi hivyo”akasema
Mathew
“Nani atufuatilie?Hakuna
yeyote anayefahamu kitu chochote kuhusiana na Nathan” akasema
Theresa
“Yawezekana hivyo lakini
ninahisi kuna hali isiyo ya
kawaida” akasema Mathew na
kuachia usukani wa gari akatoa
bastora zake akaziweka
karibu.Theresa akaanza kuhisi
baridi.Aliogopa sana.Ghafla piki
piki zile zikageuza na kuanza
kurudi kwa kasi kubwa na huku
taa zao zikimmulika Mathew na
kumfanya aone kwa taabu
kutokana na mwanga mkali wa taa
toka kwa zilie pikipiki
“Theresa haraka ruka kiti cha
nyuma” akasema Mathew na
Theresa akaruka haraka katika
kiti cha nyuma.Ghafla gari la akina Mathew likaanza kuyumba na
kutaka kuhama njia .Tairi moja la
mbele lilipasuka .Mathew hakuwa
na papara aliushika usukani kwa
nguvu na kulielekeza gari mbele
huku akiondoa mguu katika pedeli
ya mafuta.
“Mathew what’s going on?
Akauliza Theresa kwa wasi
mkubwa baada ya kuona namna
gari lilivyoyumba.Mathew
hakujibu kitu bali aliendelea
kulidhibiti gari na taratibu
likaanza kupunguza mwendo na
kusimama.Gari mbili zilizokuwa
zikija nyuma kwa kasi nazo
zikasimama.Mathew akataka
kushuka garini lakini ghafla
ikasikika milio ya risasi “Mathew tunashambuliwa !!
akasema Theresa kwa wasi wasi
mkubwa
“Theresa lala chini!!! Akasema
Mathew.Kwa haraka akabinua kiti
cha pembeni na chini yake kukawa
na sanduku ambalo alilifungua na
ndani yake kulikuwemo na
silaha.Akachukua kopo moja dogo
mithili ya kopo la dawa ya kuulia
wadudu akangoa kifuniko
akafungua mlango kidogo na
kulirusha kwa nyuma likaanza
kutoa moshi mzito,akachukua
lingine akalirusha na eneo la
nyuma ya gari likawa na moshi
mzito.Akiwa na bunduki ndogo
mkononi akatazama nyuma na hakuona mtu na hakusikia tena
risasi.
“Theresa tuko katika hatari
hivyo usishuke garini.Ngoja
nipambane na hawa jamaa”
akasema Mathew
“Mathew please don’t!!
akasema Theresa na mara ghafla
kwa mbele yao zikatokea gari tatu
za polisi zikiwasha vimuli muli
halafu kwa juu ikatokea tena
helkopta iliyowasha taa ikumulika
gari la akina Mathew.Watu
waliovalia mavazi ya polisi wakiwa
wamejihami kwa silaha na fulana
za kujikinga na risasi wakashuka
ndani ya zile gari mbili na
kujipanga,mmoja aliyekuwa na
kipaza sauti akaanza kupaaza sauti kuwataka watu waliokuwamo
katika lile gari la akina Mathew
washuke garini kabla
hawajashambuliwa
“Mathew what are we going to
do?Hawa polisi wanataka nini
kwetu? akauliza Theresa huku
akilia alikuwa amechanganyikiwa
“Be strong Theresa !!
Tumezungukwa na hawa askari
kila kona.Wote wana silaha kali
hatutaweza kupambana nao,wako
wengi na jaribio lolote la
kupambana nao linaweza
kutuletea matatizo.Hata hivyo
usihofu gari hili ni maalum kabisa
halipenyi risasi hivyo tunaweza
kutafuta msaada wa haraka”
akasema Mathew “Then do something to get us
out of here!! Akazidi kulia Theresa
huku akisali kumuomba Mungu
awaokoe.Mathew akachukua simu
na kupiga zile namba maalum za
rais.
“Hallow Mathew” akasema Dr
Vivian na Mathew akashusha
pumzi baada ya simu yake
kupokelewa
“Mheshimiwa rais ninaomba
msaada wako wa haraka sana.Niko
mahala na Theresa tumezingirwa
na askari polisi kila kona na
wanataka kutushambulia kwa
risasi.Ninaomba msaada wako wa
haraka sana.Kuna gari zaidi ya nne
na helkopta moja iko juu.Fanya
haraka tafadhali” “Unasema mmezingirwa na
polisi?!! Dr Vivian akashangaa
“Ndiyo mheshimwia rais”
“Dada tuokoe! Akasema
Theresa kwa sauti huku akilia
“Huyo ni Theresa?akauliza
DrVivian
“Ndiyo mheshimiwa rais ni
Theresa”
“Oh my God ! ni polisi gani hao
na kwa nini watake
kuwashambulia?kwa nini
wawazingire?
“Mheshimiwa rais fanya
haraka msaada tafadhali.”
Akasema Mathew
“Ok ngoja nione
nitakachofanya.Mko wapi?” “Tuko katika barabara ya
Uwazi karibu na kanisa kubwa la
Jerusalem temple” Akasema
Mathew na kukata simu.Baada ya
kuongea na rais akampigia simu
Hamis
“Mathew tayari tumekwisha
fika hapa mahala tulipokubaliana
tukutane.Uko wapi?
“Hamis nimepata
tatizo.Nimezingirwa na askari na
wanataka
kunishambulia.Tafadhali
naombeni msaada.Niko hapa
karibu na kanisa la Jerusalem
temple.Tafadhali naombeni mje
hapa haraka sana na muanzishe
mashambulizi ili niweze kupata
nafasi ya kutoka” “Sawa Mathew ninakuja hapo
na kikosi sasa hivi” akasema
Hamis
“Mathew what are we going to
do?Hao watu uliowasiliana nao
watawahi kufika kabla ya hawa
polisi hawajatukamata na kukuta
maiti ya Nathan garini? Mathew do
something !!
“Usiogope Theresa.Gari hili
halipenyi risasi na hawataweza
kutupata.Hata hivyo I have to do
something to buy time” akasema
Mathew na kutoa bomu dogo la
kurusha kwa mkono akafungua
mlango kidogo na kulirusha
upande wa mbele karibu na
zilipokuwa na gari za polisi
likalipuka na kuzua taharuki kubwa.Risasi zikaanza kumiminwa
kuelekea katika gari la Mathew na
mmoja wa wale askari akaonekana
kuwazuia wenzake kulishambulia
gari la akina Mathew.
“Hawa polisi wamejuaje
kuhusu sisi hadi wakaamua
kutufuatilia? Kuna mtu pale
nyumbani kwa Theresa aliona
wakati tunapakia maiti ya Nathan
ndani ya gari na akawajulisha
polisi? Akajiuliza Mathew.
Mara ghafla wale polisi
wakaonekana wakiingia katika
magari yao na kuondoka kwa kasi
ya ajabu.Kitendo kile
kiliwashangaza sana akina Mathew “Mbona
wanaondoka?Wanakwenda
wapi?Theresa akauliza
“Hata mimi nashangaa
sana.Wamepewa amri ya
kuondoka ? Mbona ghafla sana
halafu wanaondoka kwa kasi
kubwa namna hii?akauliza Mathew
“Inashangaza sana.” Akasema
Theresa.Kutokea nyuma yao
zikaonekana gari za polisi zikija
kwa kasi
“Wamerudi tena.”akasema
Theresa
“Hawa ni wengine” akasema
Mathew na kuwapigia simu akina
Hamis akawataka wasifike kwanza
eneo lile hadi atakapowapa taarifa Magari matatu yaliyosheheni
askari wenye silaha yakafunga
breki mita kadhaa kutoka katika
gari la akina Mathew.Askari
wakashuka na kuanza kulisogelea
gari la akina Mathew kwa
tahadhari.Walipolifikia mmoja wa
askari akaenda kugonga katika
kioo cha gari na kuwafanyia ishara
wafungue mlango na watoke nje.
“Mathew please don’t get out”
akasema Theresa
“Stay in the car.Ngoja
nishuke.Hawa askari nawaona
wako tofauti sana na wale
wengine.Nikitoka garini funga
milango na chochote
kitakachotokea usifungue mlango” akasema Mathew na kushuka chini
akiwa na bastora mkononi
“Weka silaha yako chini
tafadhali kisha piga magoti na
uinue mikono juu” Mathew
akaamriwa.Bila ubishi akaiweka
chini bastora yake na kuisukumiza
mita kadhaa mbele halafu
akaweka mikono kichwani
“Jitambulishe” akaamuru
askari kiongozi wa kikosi kile
“Naitwa Mathew ninafanya
kazi ikulu.Garini niko na mdogo
wa rais anaitwa Theresa” akasema
Mathew na kuamriwa
kusimama.Askari yule kiongozi
akamfuata
“Naitwa Meja Allan.Nini
kimetokea hapa? Tumepewa taarifa ya kufika hapa kwa haraka
sana kwani ulikuwa umewekwa
chini ya ulinzi wa askari na
walikuwa wanawashambulia”
“Mimi na Theresa tulikuwa
katika safari zetu na ghafla
zikatokea gari mbili zikitufuata
kwa nyuma na mara zikatokea piki
piki mbili zikatupita halafu
zikarejea tena kwa kasi na mara
tairi moja la gari langu likapata
pancha nahisi lilipigwa
risasi.Nikajitahidi kulimudu gari
hadi likasimama na tukaanza
kushambuliwa kutokea
nyuma.Kwa habati nzuri gari langu
hili halipenyi risasi.Tukiwa
tunatafakari nini cha kufanya
zikatokea gari mbili za polisi mbele yetu na wakashuka polisi
wakiwa wamejihami kwa silaha na
kutuamuru kushuka
chini.Ikatokea helkopta ikasimama
juu angani na kutumulika kwa
juu.Nikawasiliana na rais na
kumuomba msaada kwani askari
wale walionekana kutokuwa na
nia nzuri na sisi”
“Una hakika watu hao ni
askari?Wameelekea wapi?
Akauliza Meja Allan
“Ni askari na walikuwa na
mavazi na magari ya askari
polisi.Baada ya ninyi kusikika
mkija na magari yenu mara ghafla
wakaingia katika magari yao na
kuondoka haraka sana.Ni kama vile walipata taarifa ya ujio wenu”
akasema Mathew
Askari wakalikagua gari la
Mathew halikuwa limeharibiwa
zaidi ya matairi yote kutobolewa
kwa risasi
“Huyo mdogo wake rais ana
hali gani? Akauliza Meja Allan
“Amepatwa na mstuko kidogo
na nitaomba mnisaidie kumfikisha
ikulu.Mimi nitabaki hapa
nimeagiza niletewe matairi
nibadilishe niendelee na safari
yangu” akasema Mathew
“Hatuwezi kukuacha hapa
peke yako hasa baada ya tukio hili
kutokea.Tutawapeleka ikulu au
sehemu mnayotaka kwenda na
askari polisi watalilinda gari lako hadi kesho asubuhi
litakapotengenezwa na uchunguzi
kufanyika.Tunatakiwa
kuwafahamu hao askari
waliofanya tukio hili” akasema
Meja Allan
“Meja Allan ninaomba
tuzungumze pembeni kidogo”
akasema Mathew na kusogea
pembeni na Meja Allan
“Afande Allan naomba
nikuweke wazi kwamba niko
katika operesheni fulani nzito
niliyopewa na rais kwa hiyo
kuendelea kukaa hapa ni kuharibu
kila kitu.Nafahamu uko katika
majukumu yako ya kazi lakini rais
akisikia kwamba operesheni
yangu imeshindwa kufanikiwa kwa sababu ya kuzuiliwa hapa
hatafurahi.Ninakuomba afande
kwa kuwa suala hili limekwisha
malizika niacheni niendelee na
operesheni yangu” akasema
Mathew na Meja Allan akafikiri
kwa muda na kusema
“Kumbe sote tuko kundi
moja.Ulitakiwa kujitambulisha
mara moja.Una hakika hauhitaji
msaada wowote ?
“Hapana afande.Ninachoomba
ni kumpeleka yule mwadada ikulu
kwa rais na mimi nikisha maliza
operesheni yangu nitaelekea
huko” akasema
Mathew.Akaongoza na na Afande
Allan wakarejea garini Mathew akafungua mlango na kumtaka
Theresa ashuke
“Theresa utaongozana na
hawa askari watakupeleka ikulu
mimi naendelea kulimaliza lile
zoezi halafu nitakuja ikulu”
akasema Mathew
“Mathew are you
sure?akauliza Theresa
“Usihofu Theresa.”akasema
Mathew .Askari wale
wakamchukua Theresa
wakampakia katika gari lao moja
na kuondoka kuelekea ikulu
wengine wakabaki akiendelea na
kupima.Mathew akawapigia simu
akina Hamis na kuwataka wafike
mara moja ili waendelee na lile zoezi.Hazikupita dakika kumi
wakawasili
“Mathew nini kimetokea
hapa?
“Kuna tukio
lilitokea.Nilivamiwa na watu
wenye mavazi na magari ya polisi
na angani walikuwa na
helkopta.Kwa bahati nzuri gari
langu hili halipenyi risasi
ikanilazimu kuomba msaada na
askari walipotokea wale
waliokuwa wanatushambulia
wakakimbia.Tusipoteze muda
twendeni tuondoke eneo hili.”
akasema Mathew gari lake
likafungwa kamba likaanza
kuvutwa na gari la akina Hamis wakaondoka hadi walipofika
sehemu walikopanga wakutane.
“Haya Mathew ni kazi gani
ulotaka kutupa? Hamis akauliza
“Kuna mwili wa mtu mmoja
nahitaji kuupoteza.Nataka
mkaufiche mahala ambako
hautaonekana.Ninyi ni wataalamu
wa haya mambo tumieni uzoefu
wenu na mwili huu usiweze
kuonekana” akasema Mathew na
kufungua buti ya gari akina Hamis
wakahamisha mwili wa Nathan na
kuuingiza katika buti ya gari lao
kisha Mathew akatoa shilingi
milioni tano katika droo ya gali
lake akawapa wakalivuta gari la
Mathew hadi alipofika katika kituo
cha mafuta akaegesha hapo na kuomba msaada wa ulinzi wa gari
lake hadi kesho asubuhi akaita
taksi na kupanda akaondoka.
“Wale askari polisi walitokea
wapi? Walifahamu kuhusu uwepo
wa mwili wa Nathan mle garini?
Kama ndiyo walifahamu vipi?Kuna
mtu aliona wakati tunaupakia
mwili ule na kutoa taarifa polisi?
Akajiuliza Mathew
“Nimeshangazwa mno na wale
askari polisi.Walianza
kushambulia kwa risasi kitu
ambacho si cha kawaida kwa
askari polisi.Ukitakiwa kusimama
na askari polisi unatakiwa kwanza
ushuke garini ujisalimishe na
ukikataa inawalazimu watumie
nguvu.Askari polisi hawawezi kushambulia kabla hawajatoa
amri ya
kujisalimisha.Watakushambulia
kama umekataa kutii amri na
kuwashambulia.Inaonekana askari
wale walikuja kwa kazi maalum
halafu ni kama vile walipewa
taarifa kwamba kuna askari
wanakuja hivyo wakaondoka
haraka haraka.Hii inanishangaza
sana.Kama walikuwa kazini kwa
nini wakakimbia walipojua kuna
askari wenzao
wanakuja?Ninaanza kuingiwa na
wasi wasi kuhusiana na wale
askari.” Akawaza Mathew na
kumuelekeza dereva ampeleke
kwa Meshack Jumbo. “Umekuwa ni usiku mbaya
sana.Sikutegem…………….” Mathew
akatolewa mawazoni baada ya
simu yake kuita.Alikuwa ni rais Dr
Vivian
“Hallow mheshimiwa
rais”akasema Mathew
“Mathew uko wapi sasa hivi?
“Niko njiani naelekea
nyumbani kwa Meshack Jumbo”
“Nakuomba ikulu haraka
sana” akasema rais na ukata
simu.Mathew akavuta pumzi ndefu
“Mambo yameiva.Dr Vivian
anaonekana kubadilika sana
.Amezungumza kwa hasira
sana.Inawezekana tayari Theresa
amefika ikulu na inawezekana
labda akawa anataka kufahamu kilichotokea.Ninaomba Theresa
asiwe amemueleza chochote
kuhusu Nathan kwani atakuwa
ameharibu kila.Sijui atafanya nini
akisikia kwamba Nathan
amekufa.Dah ! Theresa ameharibu
sana kwa kuamua kumuua
Nathan.Sikutegemea kabisa kama
anaweza akafanya jambo la hatari
kama lile,anway I have to fix it”
akawaza Mathew
Mathew alifika nyumbani kwa
Meshack Jumbo na kukaribishwa
ndani.Meshack Jumbo akahisi kuna tatizo baada ya kuiona hali
aliyokuwa nayo Mathew
“Nini kimetokea
Mathew?akauliza
“Mzee kuna tatizo kubwa
limetokea na sijui nianzie wapi
kukueleza” akasema Mathew
“Nieleze tafadhali.Nini
kimetokea?
Mathew akamueleza mzee
Jumbo kila kitu kilichotokea
kuhusiana na Nathan.
“Mhh! Mzee Jumbo akaguna
“Hili suala linakanganya sana”
Akasema
“Mzee ninahitaji kwenda
kuonana na rais usiku huu
amenipigia simu wakati ninakuja
huku nakunitaka nifike ikulu haraka sana.Yawezekana mambo
tayari yameharibika”
“Atakuwa tayari amefahamu
kilichotokea?
“Sina hakika lakini
uwezekano ni
mkubwa.Yawezekana labda
Theresa amekwisha mueleza kila
kilichotokea na ndiyo maana
akaniita kwa haraka namna
ile.Ngoja nikamsikilize nifahamu
alichoniitia.Kama kuna tatizo
lolote nitalimaliza” akasema
Mathew
“Hili suala la kifo cha Nathan
limebadili kabisa upepo wa hili
suala na sasa limekuwa la
kimataifa.Mzozo kati ya Tanzania
na Marekani utaongezeka haraka sana.Yawezekana mambo
tayari yameharibika”
“Atakuwa tayari amefahamu
kilichotokea?
“Sina hakika lakini
uwezekano ni
mkubwa.Yawezekana labda
Theresa amekwisha mueleza kila
kilichotokea na ndiyo maana
akaniita kwa haraka namna
ile.Ngoja nikamsikilize nifahamu
alichoniitia.Kama kuna tatizo
lolote nitalimaliza” akasema
Mathew
“Hili suala la kifo cha Nathan
limebadili kabisa upepo wa hili
suala na sasa limekuwa la
kimataifa.Mzozo kati ya Tanzania
na Marekani utaongezeka maradufu na watahitaji maelekezo
ya kina kuhusiana na kifo cha mtu
wao.Halikuwa wazo zuri
kumshirikisha yule msichana
Theresa katika operesheni
hii.Toka mwanzo sikuwa
nimeliafiki jambo hili na ndiyo
maana nikakuomba umrudishe
ikulu akaendelee na shughuli zake
za kuandika hotuba.Ona sasa
amekuweka katika hatari kubwa
na kila kitu inabidi kisimame kwa
ajili ya kulishughulkia suala moja
tu la Nathan”
“Mzee ngoja nikamsikilize rais
na nitakujuza chochote
kitakachojiri huko.Naomba
unihifadhie hili begi langu halafu
nitaondoka na gari lako ” akasema Mathew na kuchukua gari la
Meshack Jumbo akaondoka
kuelekea ikulu
“Asemayo mzee Jumbo ni ya
kweli kabisa.Hakukuwa na
ulazima wa kumshirikisha Theresa
katika operesheni hii kwani
ameharibu kila kitu na
kunirudisha nyuma sana.Sijui nini
kitatokea Dr.Vivian akifahamu
kuhusiana na kifo cha mpenzi
wake Nathan.Endapo Marekani
wakifahamu kama Nathan
amekufa basi watahitaji maelezo
ya kina amekufaje.Hili suala
litaleta mvutano mkubwa sana”
akawaza Mathew akiwa garini
kuelekea ikulu kuonana na rais Aliwasili ikulu na kupelekwa
moja kwa moja sebuleni kwa
rais.Dr.Vivian aliyekuwa chumbani
kwake akafahamishwa kuhusu ujio
wa Mathew na baada ya muda
akafika sebuleni.Uso wake
uliionyesha hasira kali.Akawataka
walinzi wake watoke pale sebuleni
na kuwaacha yeye na Nathan
pekee.Dr.Vivian akamtazama
Mathew kwa macho makali na
kusema
“Kuna kitu kimoja tu ambacho
nataka kukifahamu kwa sasa,nini
kimetokea Mathew? Akauliza bila
hata salamu.Wote wawili
walikuwa wamesimama.Mathew
akabaki kimya “Mathew nieleze haraka nini
kimetokea?
“Theresa hajakueleza
chochote? Akauliza Mathew baada
ya Theresa kuingia pale sebuleni
na kwenda kuketi sofani
“Hajanieleza chochote.Toka
amefika hapa analia na kusema
“I’m sorry sister”Nini
kimetokea?Kuna kitu gani
kimetokea ambacho hataki
kunieleza? Tafadhali niambie
Mathew nini kimewakuta
huko?Sijawahi kumuona Theresa
akiwa katika hali hii hata mara
moja na ndiyo maana
nimestuka.Nieleze tafadhali”
akasema Dr.Vivian Mathew akamtazama Theresa
aliyekuwa amejiinamia sofani
.Halafu akasema
“Kuna sehemu mimi na
Theresa tulikuwa tunakwenda
usiku huu kuonana na watu
fulani.Tukiwa njiani nikagundua
tulikuwa tunafuatwa na gari mbili
nyuma yetu halafu juu yetu
kukawa na helkopta na ghafla
zikatokea piki piki mbili zikatupita
halafu zikaanza kurudi kwa kasi na
tairi moja katika gari langu
likapigwa risasi nikajitahidi
kulimudu gari lisiache bara bara
na mara tu gari liliposimama
zikamiminwa risasi kutoka katika
gari zilizokuwa zinatufuata nyuma
yetu na kutoboa matairi yote.Kwa bahati nzuri gari langu halipenyi
risasi hivyo ikawa nafuu
kwetu.Mara kwa mbele yetu
zikatokea gari tatu za polisi na
wakashuka watu waliovalia
mavazi ya polisi na wakiwa
wamejihami kwa silaha
.Walitutaka kushuka garini na
ndipo nilipoamua kukuomba
msaada.Nashukuru sana kwa
kutuma msaada wa haraka kwani
polisi walikifika kwa wakati na
wale wavamizi wakaondoka kwa
haraka sana.Inaonekana walipata
taarifa kwamba askari polisi
wanakuja hivyo wakaondoka
haraka sana.Jambo hili
limenishangaza sana.Najiuliza je
wale walikuwa askari wa jeshi letu la polisi au ni watu waliotumia
sare na vifaa vya jeshi letu? Kama
walikuwa ni polisi kweli kwa nini
wakakimbia baada ya wale askari
wenzao kuwasili?Kuna maswali
hapa bado nayatafutia majibu.Kwa
hiyo mheshimiwa rais hiyio ndiyo
hali halisi iliyotokea usiku huu na
ninakuomba ondoa
hofu.Tunaendelea vizuri japo
mambo yanazidi kuwa magumu”
akasema Mathew.Dr.Viviana
akaenda kuketi sofani.
“Mhh! Jambo hili hata mimi
mwenyewe linanichanganya .Hao
askari ni akina nani na
walifahamuje kuhusu ninyi?Hizo
sare na vifaa vya jeshila polisi walivitoa wapi?Hiyo helkopta
waliyokuwa nayo ni ya polisi pia?
“Sikupata nafasi ya
kuichunguza helkopta lakini
magari na sare ni za polisi”
akasema Mathew
“Sawa, nitaagiza uchunguzi wa
kina ufanyikekuhusiana na askari
hao na tuwabaini ni akina nani au
kama kuna watu wanatumia sare
na vifaa vya jeshi letu kwa kazi zao
binafsi basi tuwabaini lakini hii
inaonyesha kwamba tayari
mmekwisha fahamu na na hii
inaongeza hatari kubwa
kwenu.Inabidi umakini uongezeke
na ikibidi nitawapa ulinzi ili
muweze kuwa salama katika
shuhuli zenu.Hiki kilichotokea leo kimeniwashia taa nyekundu
kwamba hamko salama na
kwamba kwa hizo siku chache
mlizoanza uchunguzi kuna watu
tayari mmekwisha wagusa na ndio
maana wanajitokeza kuwakab…...”
“Sister !! Theresa akasema na
kumkatisha dada yake
“Unasemaje Theresa?
Akauliza Dr.Vivian.Mapigo ya
moyo wa Mathew yakabadilika
“Dada naomba niwe mkweli
.Kuna jambo hatujakueleza
ukweli” akasema na kufuta
machozi
“Jambo gani
Theresa?Dr.Vivian akashangaa “Theresa !! akasema Mathew
huku akimtazama Theresa kwa
macho makali
“ Mathew we have to tell her
the truth.She needs to know”
akasema Theresa
“Not now Theresa !! akasema
mathew kwa sauti ya
juu.Dr.Viviana akazidi kupata hofu
“Kuna nini Theresa? Kuna kitu
gani ambacho nahitaji
kukifahamu? Akauliza Dr.Vivian
“It’s about Nath…..”kabla
hajamaliza sentensi yake Mathew
akaingilia kati
“Madam president ngoja mimi
nikueleze ukweli” akasema
Mathew “No Mathew mimi ndiye
ninayepaswa kumweleza dada kwa
kuwa mimi ndiye niliyetenda”
akasema Theresa
“Jamani mbona nashindwa
kuwaelewa?Kuna nini kimetokea
na mnasita kunieleza?
“Ni kuhusu Nathan”
“Nathan?? Dr.Vivian akastuka
sana.
“Ndiyo dada”
“Nathan…….”
“Madam president let me
explain !! akasema Mathew
“No ! let her explain to me
what happened” akasema
Dr.Vivian na kumsogelea Theresa
“Niambie Theresa kuna nini
imetokea?Nathan kafanya nini? Theresa akafuta machozi na
kumtazama dada yake kisha
akasema
“Nathan is dead”
Dr.Vivian akabaki mdomo
wazi akimtazama Theresa.Kwa
sekunde kadhaa alibaki na
mshangao mkubwa na hakuweza
kuzungumza chochote.Baada ya
muda akasema
“That’s not true !!
“It’s true .He’s dead.I killed
him” akasema na kuzidi
kumchanganya
Dr.Vivian.Akamfuata Mathew
“Mathew hebu niambie
Theresa ana matatizo gani? Mbona
anaongea vitu ambavyo havielewi?
Akauliza Dr.Vivian.Mathew akamshika mkono na kumketisha
sofani.
“Tell me Mathew.What’s going
on? Theresa amepatwa na nini?
Akauliza Dr.Vivian akiwa katika
wasi wasi mkubwa
“Dr.Vivian naomba unipe
dakika chache nikueleze japo kwa
ufupi jambo moja muhimu sana”
“Nieleze Mathew” akasema
Dr.Vivian huku bado sura yake
ikionyesha wasi wasi mkubwa
“Kama nilivyokueleza
kwamba ninataka kuanza
uchunguzi wangu katika ajali ya
ndege ya rais kwani naamini
chanzo cha kuuawa kwa kanali
Sebastian kina mahusiano na ajali
ya ndege ya rais.Nimegundua kwamba wakati ikiondoka hapa
Dar es salaam kwenda Cairo
Misri,kulikuwa na watu kumi na
tisa ndani ya ndege ya rais na
mmoja ambaye inasadikiwa
alikuwa ni binti mdogo hakuwa
ameorodheshwa miongoni mwa
abiria waliokuwamo ndegeni na
mpaka sasa sijafahamu kwa nini
ila bado naendelea kulichunguza
hilo.Wakati wa kurejea Tanzania
kulijitokeza kundi la waandishi
nane wa habari ambao
walichelewa ndege yao na kuomba
lifti katika ndege ya rais na rais
akaruhusu wapande.Hatujui bado
chanzo cha ajali ile lakini taarifa
iliyopo inaonyesha kwamba baada
ya ajali ile miili iliyopatikana ni kumi na saba tu .Miili mingine
haikupatikana.Swali la kujuliza je
iko wapi?hawakufika Tanzania au
walishukia njiani? Bado naendelea
kulifanyia kazi hilo lakini
nimefanikiwa kumfahamu mtu
mmoja anaitwa Fakrim Alnasor
huyu ni mzaliwa wa Misri lakini
ana uraia wa Marekani kwamba
ndiye aliyewaombea lifti hao
waandishi nane wa habari katika
ndege ya rais.Kwa kuwatumia
watu ambao tuna mashirikiano
nao wa Marekani wametusaidia
kuchunguza na kugundua kwamba
Fakrim alihamishwa nchini Misri
muda mfupi baada ya ajali ile ya
rais kutokea na kupelekwa
Marekani.Watu wetu hao walikwenda mbali zaidi na
kugundua kwamba Fakrim
alikuwa ni jasusi wa shirika la
ujasusi la marekani CIA.”
Sura ya Dr.Vivian ikabadilika
baada ya kusikia neno CIA
likitajwa.
“CIA?
“Ndiyo alikuwa ni jasusi wa
CIA na inaonyesha kwamba
alikuwa nchini Misri kwa shughuli
maalum na alipomaliza shughuli
yake akaondolewa.Tuliwataka
watusaidie kumchunguza zaidi
Fakrim kuhusana na hao
waandishi nane wa habari
aliowasaidia wakaingia katika
ndege ya rais lakini kitu cha ajabu
Fakrim alipigwa risasi na kufariki dunia kabla hao watu wetu
hawajampata kwa
mahojiano.Walifanikiwa kuondoka
na simu na kompyuta yake ndogo
na baada ya kufanya uchunguzi
wakagundua kwamba mtu wa
mwisho kuwasiliana na Fakrim
alikuwa ni Nathan”
Dr.Vivian akazidi kuonyesha
uso wa mshangao.
“Nathan?
“Ndiyo madam
president.Nathan alikuwa na
mawasiliano na
Fakrim.Tulimchunguza pia Nathan
na tukagundua kwamba hata naye
ni jasusi wa CIA”
“No ! That’s not true !!
akasema kwa ukali Dr.Vivian “Najua ni jambo gumu
kuliamini lakini tuna uhakika
mkubwa kwamba Nathan ni jasusi
wa siri wa CIA na tunahisi alikuwa
karibu nawe kwa kazi
maalum.Serikali ya Marekani
wanakufuatilia Dr.Vivian kwa
kupitia shirika lake la ujasusi
ambao nao wanamtumia Nathan
kukuchunguza”
“Mathew unazidi
kunichanganya.Mimi ndiye
nnayemfahamu Nathan kuliko
mnavyomfahamu ninyi.Katu
Nathan hawezi kuwa hivyo
unavyosema.Hawezi kuwa
mpelelezi na kibaya zaidi eti
anatumiwa kunipeleleza mimi.Hilo
nalikataa haliwezekani kabisa.Nimetoka mbali naye na
ninamfahamu zaidi ya mtu yeyote
anavyoweza kumuelezea.Labda
uwe unamzungumzia Nathan
mwingine na si huyu ninamfahamu
mimi,my Nathan” akasema
Dr.Vivian
“Ni vigumu kuamini Dr.Vivian
lakini huo ni ukweli na tulikwenda
mbali zaidi kwa kuichunguza hadi
kampuni anayofanya kazi Nathan
ya A.D electronics tukagundua
kwamba ni kampuni ambayo iko
chini ya serikali ya Marekani
kupitia shirika lake la ujasusi la
CIA ingawa hili halifahamiki kwa
watu.Walianzisha kampuni hii kwa
lengo maalum na ndiyo maana
wanatengeneza bidhaa zenye ubora mkubwa lakini kwa bei ya
chini kwa sababu hawako kwa ajili
ya kutengeneza faida bali wana
lengo lao maalum.Katika simu na
kompyuta wanazotengeneza kuna
programu maalum inawekwa
ambayo huwawezesha wao wapate
taarifa zako zote katika kifaa
hicho.Kama unatumia simu basi
mawasiliano yako yote
wanayapata na kama unatumia
compyuta basi wana uwezo pia wa
kupata kila unachokifanya katika
kompyuta yako.Hii inawasaidia
sana kuweza kupata taarifa
mbalimbali hasa za magaidi na
watu ambao wanahatarisha
usalama wa Marekani.Nimegundua
kwamba Nathan alikupa simu na kompyuta zinazotengenezwa na
kampuni yao na si wewe tu bali
aligawa pia kwa watu wote
wanaokuzunguka.Alifanya hivi
kwa sababu maalum na kupata
taarifa zako zote na ndiyo maana
baada ya kuligundua hilo jana
nikaja kubadilisha simu zako ili
taarifa zako ziwe salama”
“Oh my God !! akasema
Dr.Vivian.Alistuka sana
“Una uhakika na hilo jambo
Mathew?
“Ndiyo mheshimiwa rais nina
uhakika nalo”
“Kama ni hivyo kwa nini
hukutaka kunieleza mapema?
“Kwa sababu ingekuwa
vigumu kuamini na hata hivyo bado nilikuwa naendelea na
uchunguzi wangu kuhusiana na
kwa nini Marekani
wanakuchunguza”
“Ulipokuja kunihoji kuhusu
maisha yangu ya kimahusiano
ulikuwa tayari na taarifa
kuhusiana na Nathan kuwa jasusi
na ananipeleleza?
“Ndiyo mheshimiwa
rais,tayari nilikuwa na taarifa hizo
lakini kuna vitu ambavyo nilihitaji
kuvifahamu kutoka kwako”
“Mathew umenisikitisha sana
.Kwa nini ukagundua jambo kubwa
kama hili na ukakaa kimya huku
nikiendelea kuwa katika hatari?
Akauliza Dr.Vivian akionekana
kukasirika . “Madam president si kila
jambo linaloendelea katika
uchunguzi unapaswa kuelezwa
haraka haraka,kuna mambo
mengine ukielezwa haraka
yanaweza yakaharibu uchunguzi
na hasa suala kama hili ambalo
linamuhusisha mtu wako wa
karibu na mtu
unayempenda.Isingekuwa rahisi
kuturuhusu kuendelea na
uchunguzi kwa mtu wako wa
karibu”
“Hapana Mathew ulipaswa
kunieleza na kama ningekubaliana
nawe ningetoa kibali cha
kuendelea kumchunguza na hata
ningeweza kukupa ushirikiano
mkubwa sana wa kusaidia katika uchunguzi wako.Umechukua hatu
gani sasa? Umefikia wapi katika
uchunguzi wako huo?
“Sikutaka kufahamu kitu
chochote kabla sijakamilisha
uchunguzi wangu hivyo
inanilazimu kuongea na Theresa
nikamueleza kila kitu na tukaamua
kumuita Nathan aje Tanzania
kimya kimya bila wewe kufahamu”
Dr.Vivian akakunja sura
baada ya kusikia kauli ile toka kwa
Mathew
“Nathan amekuja Tanzania
bila ya mimi kujulishwa?How
could you do that Mathew?And you
Theresa how can do that to me?
Akasema Dr.Vivian kwa ukali “Mheshimiwa rais tuliamua
hivyo kwa sababu nilitaka nipate
nafasi ya kumchunguza Nathan
bila yeye kufahamu kama
anachunguzwa.Naamini kama
tungekujulisha jambo hili
usingekubali Nathan aje Tanzania
kutokana na mafarakano yenu
hivyo tusingeweza kupata taarifa
zozote za kumuhusu yeye ndiyo
maana nikamuomba Theresa
afanye mpango ili Nathan aweze
kuja kwa siri Tanzani bila
kukujulisha ili nipate nafasi ya
kumfanyia uchunguzi”
“He came? Akauliza Dr.Vivian
“Ndiyo alikuja” “Yuko wapi? Tayari umefanya
uchunguzi wako? Akauliza
Dr.Vivian
“Amekuja asubuhi ya leo na
kwa mujibu wa mipango
tuliyoipanga ni kwamba jioni ya
leo Theresa alimkaribisha Nathan
nyumbani kwake halafu mimi
nikaenda kufanya uchunguzi
chumbani kwa Nathan.Nikiwa
naendelea na uchunguzi wangu
chumbani kwa Nathan nikapigiwa
simu na Theresa akanitaka niende
nyumbani kwake haraka
sana.Nilifanya hivyo na nilipofika
nyumbani kwake…” Mathew
akasita
“Sema Mathew ulipofika
nyumbani kwa Theresa ikawaje? Mathew akageuka na
kumtazama Theresa.
“Tell me Mathew !! akasema
Dr.Vivian kwa ukali akionekana
kuwa na wasiwasi mkubwa
“I found him dead” akasema
Mathew na ukimya
ukatanda.Dr.Vivian akawatazama
Mathew na Theresa kwa zamu
halafu akamfuata Theresa sofani
“Theresa tell me is that true?
Theresa hakujbu kitu bali
akatikisa kichwa ishara ya
kukubali.Dr.Vivian akaweka
mikono
kichwani.Alichanganyikiwa.Akaka
a chini.Alishindwa
kulia,alishindwa kuzungumza
akabaki anamtazama Theresa kwa macho makali yaliyojaa hasira
huku midomo
ikimtetemeka.Akamgeukia
Mathew
“Mathew nakuamini sana
please tell me it’s a joke”
“It’s true madam
president.Nathan is dead”Ghafla
Dr.Vivian akainuka na kwenda
kumvaa Mathew akaanza
kumtandika vibao,Nathan
akamdaka mikono.
“Nilikuamini sana Mathew
kwa nini umenifanyia hivi? Why
you killed him?!! Akauliza Dr
Theresa huku akilia.Dr Theresa
akakaa chini na kuanza kulia
“Dada usimlaumu
Mathew.Yeye alikuwa na lengo zuri tu la kutaka kumchunguza Nathan
lakini mimi ndiye
niliyemuua.Unapaswa kunilaumu
mimi si Mathew.!! Akasema
Theresa
“Get out of my face Theresa !! I
hate you so much.Sikutegemea
kama siku moja unaweza
ukanifanyia jambo baya kama hili?
Why you killed him? Why you
killed an innocent soul? akauliza
Dr.Vivian huku akilia
“Dada nililazimika kufanya
vile kwa ajili ya usalama
wako.Nathan was a
monster.Hakuwa na mapenzi
yoyote nawe bali alikuwa hapa
kwa kazi maalum alizotumwa
kama ulivyoambiwa na Mathew.Hakuna anayejua nini
sababu ya kukuchunguza na
hatujui mpaka sasa amekwisha
pata mambo gani kuhusu wewe”
“Hiyo haikuhalalishi wewe
kumuua Nathan !! akafoka
Dr.Vivian
“Hakukuwa na namna
nyingine ya kuweza kumzuia
Nathan zaidi ya kumuua?Oh God
please give me strength..” akasema
Dr.Vivian na kusimama
“Dada najua nimekuudhi kwa
hiki nilichokifanya .Hata mimi
nakubali sijafanya kitu kizuri
lakini sikuwa na namna nyingine
ya kufanya.Nathan ni mtu mbaya
sana na japokuwa hatuna
uthibitisho bado lakini naamini watu anaoshirikiana nao ndio
waliomuua baba.Siwezi kumuacha
hai mtu kama huyu ambaye
pamoja na kuiteketeza familia yetu
bado anaendelea kutufuatilia.Can’t
you see that Vivian? Akauliza
Theresa ambaye alionekana
kupandwa na hasira
“Sikuwahi kufikiri hata siku
moja kama nitaingia katika
dhambi ya uuaji lakini
imenilazimu kufanya hivyo kwa
sababu ya usalama wangu na
wako.Najua hili ni kosa la jinai kwa
hiyo niko tayari kuipokea adhabu
inayostahili kwa sababu ya kitendo
nilichokifanya.So madam
president call the police now.Mimi
ni muuaji na ninastahili adhabu kama wauaji wengine.Najua
nitafungwa maisha au kifungo
kirefu gerezani lakini nitatumikia
kifungo kwa furaha nikijua uko
salama na nimelipa kisasi vile vile
kwa watu walioteketeza familia
yetu.So make that call now !!!
akasema Theresa.Dr.Vivian
akamsogelea na kumnasa kibao
kikali
“Umefanya makusudi kumuua
Nathan kwa vile unajua kwamba
siwezi kukupeleka mbele ya
sheria? Akauliza Dr.Vivian kwa
ukali
“Dada mimi niko tayari kwa
lolote lile.Siogopi kukutana na
mkono wa sheria na wala usijaribu
kunionea huruma!! “Theresa wewe si damu yangu
na sioni ugumu kukuharibu.I
swear I’ll never forgive you for this
and I’ll destroy you!! Akasema
Dr.Vivian na kuiendea simu kabla
hajainua mkono wa simu Mathew
akamuawahi na kumdaka mkono
akamzuia kupiga ile simu
“Don’t make that call !!
akasema Mathew
“Dr.Vivian suala hili linahitaji
busara kubwa sana na
ninakuomba usichukulie hasira
kwani utashindwa kulimaliza hili
jambo.Usimuhukumu wala
usijaribu kumfanya chochote
Theresa kwani mimi ndiye
niliyemuomba amuite Nathan
huku Tanzania.Kilichotokea kimekwisha tokea na hatuna
namna zaidi ya kukabiliana na
kilichotokea.Najua wewe ni rais na
una uwezo wa kupiga simu hata
sasa na ukaamuru Theresa
akamatwe na hata kama atafungwa
gerezani bado haitamrejesha
Nathan.Theresa amefanya hivi
aliivyofanya kwa upendo mkubwa
alio nao kwako.Ametanguliza
usalama wako mbele ndiyo maana
akaamua kufanya maamuzi haya
magumu .Kutoa roho ya mtu si
jambo rahisi.Badala ya kupoteza
muda kulumbana tutafute suluhu
ya suala hili”
Stay away from us
Mathew.Wewe ndiye sababu ya
haya yote yaliyotokea.Kwanza sitaki tena uendelee na uchunguzi
wako kwani imekuwa ni balaa
tupu na hakuna chochote
unachokipata.Uchunguzi wako
wote unaishia hapa.Sitaki tena
kuendelea na suala hili.Ahsante
kwa msaada wako ambao
umegeuka karaha.Nilitegemea
makubwa sana kutoka kwako
kumbe wewe nawe ni sawa na wale
wale.Kaendelee na biashara zako
sitaki tena uendelee na hii
kazi.Kila mara suala hili limekuwa
linanigharimu maisha ya watu
sitaki kuendelea nalo
tena.Imetosha” akasema Dr.Vivian
kwa hasira
“Dr.Vivian tafadhali
usichukulie hasira.Hili ni suala zito sana na bado linahitaji uchunguzi
wa kina.Tafadhali niache
niendelee na uchunguzi wangu
mpaka mwisho kwani tayari
nimekwisha pata mwanga na
nikiendelea kidogo ninaweza
kupata ufumbuzi na kubaini ni
nani waliwaua wazazi
wako.Tafadhali sana mheshimiwa
rais” akasema Mathew
“Mathew nilikwisha
kutahadharisha hapo awali
kwamba nikisema jambo huwa
sibadilishi kauli yangu.Nimesema
kwamba sitaki kuendelea na hili
zoezi.Imefika mwisho ahsante sana
kwa kila kitu na kwa balaa
ulilolisababisha”
“Mhesh………………” “Stop !! akasema Dr.Vivian
kwa ukali
“Ninachohitaji kusikia ni kitu
kimoja tu toka kwako.Nataka
kufahamu mwili wa Nathan uko
wapi? Nionyesheni uliko mwili wa
mpenzi wangu na wewe
ukaendelee na maisha yako ila
huyu mwenzako aliyejipa
dhamana ya kutoa roho za watu
nitashughulika naye.Hawezi
kukwepa mkono wa sheria!!
“Madam president nakuomba
sana niko chini ya miguu yako
nakuomba usimfanye chochote
Theresa.Kama ni kunipeleka
kwenye sheria nipeleke mimi
ambaye ndiye niliyemuomba
Theresa katika dhambi hii.Kama nisingemuomba anisaidie
kumfanya Nathan aje Tanzania
asingeweza kupata wazo la
kufanya hivi alivyofanya.Kwa hiyo
naendelea kukuomba usimfanye
chochote Theresa.” Akasema
Mathew
“Mathew tafadhali nakuomba
usitake kunijaribu.Mimi ni tofauti
sana na viongozi wengine.Usitake
kunijaribu na ukajikuta
nikikuharibu.Theresa must face
the law.Siwezi kuliacha hili
likaenda hivi hivi” akasema Dr
Vivian.Mathew akamtazama na
kusema
“Una uhakika gani kwamba
Theresa ndiye aliyemuua
Nathan?Ukimfikisha mbele ya sheria unao ushahidi kama ni yeye
ndiye aliyemuua? Ni vipi kama
akisema kwamba ni wewe ndiye
uliyemtuma amuue Nathan?Dunia
nzima kwa sasa inafahamu una
ugomvi na Marekani kwa hiyo
wataamini umemuua Nathan kwa
hasira zako kwa Marekani.Why
don’t we skip that part and do
things right? Akauliza Mathew na
Dr.Vivian akapandwa na hasira
kali
“Unataka kupambana na
mimi Mathew? Unataka
kushindana na mimi? Akauliza Dr
Vivian kwa hasira
“Madam president
utanisamehe sina lengo na wala
siwezi kupambana nawe.Nilichokiongea ni ili
kuliweka suala hili kwa ukubwa
wake na badala ya kukaa
tukilumbana tufikirie namna ya
kuweza kukabiliana na hili suala.”
“Mathew its over.Nimekwisha
kwambia kwamba sitaki tena
kuendelea na wewe na wala
uchunguzi wa suala hili sitaki
kabisa uendelee.Ninachokitaka
mnionyeshe mwili wa Nathan
ulipo.Nionyesheni ulipo mwili wa
mpenzi wangu.Ili tuende sawa
nakuomba unionyeshe ulipo mwili
wa Nathan” akasema
Dr.Vivian.Mathew na Theresa
wakatazamana
“Hamtaki kunionyesha ulipo
mwili wa Nathan? “Madam president,kutokana
na mambo unayoyapitia kwa sasa
hasa msuguano wako na nchi ya
marekani nadhani si vizuri jambo
hili likajulikana.Mpaka sasa
tunaofahamu kuhusu suala hili ni
mimi,Theresa na Meshack Jumbo
ambaye nimemweleza muda mfupi
kabla sijafika hapa.Serikali ya
Marekani itakubana katika kona
kwa kutaka uchunguzi wa kina
ufanyike kuhusu mwili wa
Nathan.Dunia nzima watajua
kwamba nawe unahusika katika
mauaji hayo.Tanzania tutaingia
katika msuguano mwingine
mkubwa .Watatumia kigezo hicho
kukuondoa katika mstari.Uko
tayari kwa jambo hilo kutokea?Nakushauri mheshimiwa
rais jambo hili liendelee kuwa siri
na asifahamu mtu
mwingine.Usiliweke jambo hili
kwa vyombo vya uchunguzi litaleta
shida kubwa”
Dr.Vivian akashika kiono na
kutazama chini.Kwa mara ya
kwanza toka amekuwa rais
alijikuta katika wakati mgumu
sana na alishindwa kufanya
maamuzi
“Sikutegemea kama mnaweza
kuniweka katika wakati mgumu
kama huu.I don’t know what to do”
akasema Dr.Vivian
“Fanya maamuzi Dr.Vivian
muda unakwenda sana” akasema
Mathew “Mathew nimesema sijui
nifanye nini.Mmekwisha haribu
kila kitu.Mmenitwisha jiwe
zito.Mmeniingiza katika vita mpya
ambayo sikiwa nimeitegemea hasa
kwa wakati huu ambao
ninaiongoza nchi katika vita
kubwa .Pamoja na hayo siwezi
kulifumbia macho jambo
hili.Lazima niliweke wazi.Kama
Nathan amekufa lazima nchi yake
ifahamu na lazima mwili wake
upelekwe kwao ukazikwe kwa
heshima .Hiyo ndiyo namna
ninayoweza kulimaliza hili jambo
na mwisho kabisa wale wote
waliohusika katika jambo hili
watachukuliwa hatua kali za
kisheria.Tafadhali naomba mnionyeshe ulipo mwili wa Nathan
nianze taratibu za kuukabidhi kwa
serikali yake” akasema Dr.Vivian
na machozi yakamtoka
“Mathew tafadhali nauhitaj
mwili wa Nathan.Nipeleni mahala
ulipo mwili wake nikashuhudie na
kuamini kama kweli amekufa”
akaendelea kusisistiza Dr.Vivian
“No madam president I wont
do that.Suala hili linapaswa
kuendelea kuwa siri kubwa.Jambo
hili likiwekwa wazi litaleta
msuguano mkubwa sana.Madam
president nakuomba unikubalie
suala hili liendelee kuwa siri yetu”
“Mathew siwezi kulifanya siri
jambo kubwa kama hili.Lazima
niliweke wazi,muuaji afahamike na afikishwe mbele ya sheria”
akasema Dr.Vivian
“Dr.Vivian nakuomba tena
usithubutu kufanya hivyo kwani
utaharibu kila kitu.Mpaka sasa
tuna uhakika kwamba serikali ya
Marekani kupitia shirika lake la
CIA wana mkono wao katika
mambo haya yaliyotokea kuanzia
ajali ile ya ndege ya rais Anorld na
tunaamini hata mauaji ya kanali
Sebastian Matope watakuwa
wanahusika.Tumegundua
wamekuwa wanakufuatilia na
kupata habari zako,hatujui bado
kwa nini wanafanya hivyo lakini
lazima ipo sababu kubwa ya
kudukua taarifa za mkuu wa
nchi.Endapo ukiliweka wazi hili suala na ikajulikana kwamba
Theresa ndiye aliyemuua Nathan
itaharibu kila kitu na tutashindwa
kupata majibu wanachunguza
jambo gani toka kwako.Nakuomba
usikie ushauri wangu ,jambo hili
liendelee kuwa siri yetu.Nafahamu
umeumia sana na kila mmoja wetu
hapa ameumia kwani Nathan
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment