Search This Blog

Friday, 7 April 2023

SCANDLE (KASHFA) (2) - 5

   

Simulizi : Scandle (Kashfa) (2)

Sehemu Ya Tano (5)


“Kibaya zaidi anachonishangaza ni kwamba hataki kuchukua hatua za makusudi kabisa za kulimaliza hili suala.Wale jamaa wametoa sharti jepesi sana kwamba wanamtaka huyo mtu anaitwa Mathew Mulumbi ili wasiweze kuzisambaza zile picha lakini Festus amegoma kwamba hawezi akamtoa Mathew na anataka kupambana na hao jamaa ! akawaza Profesa Simon na kuikunja sura yake kwa hasira


“Laiti ningefahamu mahala alipo huyo Mathew Mulumbi ningewaelekeza hao jamaa wakamchukue na hili jambo liishe kwa sababu Festus haonekani kujali hata kidogo.Analiona jambo hili ni la kawaida sana.Nani kamroga Yule jamaa hadi anashindwa kuwa na mtazamo wa mbali? Kwa nini anashindwa kuona hili ni bomu na muda wowote linaweza likalipuka na athari zake ni kubwa kwake kwa nchi na kwa chama pia?Akawaza profesa Simon


“Ngoja nizungumze na Yule jamaa atupe muda zaidi hata wa siku moja ili tuweze kulishughulikia jambo hili kwa kina na kuhakikisha linamalizika” akawaza Profesa Simon halafu akaichukua simu yake akazitafuta namba za simu za Yule jamaa aliyemtumia picha za Rais Festus akampigia


“Katibu mkuu” akasema Yule jamaa


“Nimekupigia tena ili tuzungumze jambo hili” akasema Profesa Simon


“Unataka tuzungumze kitu gani mzee? Tayari Rais ametekeleza maagizo yangu?


“Ni hilo ambalo nataka tulizungumze”


“Nataka kufahamu maagizo yangu yametekelezwa au bado? Akauliza Yule jamaa


“Bado hajatekeleza kuna ugumu wake katika lile ulilomtaka alifanye na muda uliompa ni mfupi”


“Hakuna cha kuzugumza mzee kama maagizo yangu hayajatekelezwa.Nitafute pale ambapo Rais atakapokuwa ametekeleza agizo nililompa”


“Tafadhali usikate simu” “Mzee naomba usiendelee kunipotezea wakati wangu”


“Sikiliza ndugu yangu jambo hili ni kubwa sana.Linagusa maslahi ya nchi pia.Rais ndiye kiongozi wetu ndiye baba yetu hivyo faragha zake zinapaswa kusitiriwa na si kuanikwa hadharani.Ninakuhakikishia kwamba mimi binafsi nitasimamia na kuhakikisha kwamba Rais anatekeleza kile ulichomtaka akitekeleze lakini naomba utoe muda zaidi il……”Profesa Simon hakumaliza simu ikakatwa “Amekata simu mshenzi huyu ! akasema kwa hasira


“Hawa jamaa


hawatanii.Lazima watafanya kama wanavyotaka kufanya.What are we going to do? Akawaza profesa Simon halafu akampigia simu makamu mwenyekiti wa chama ambaye alikwenda shambani kwake akamtaka amsubiri anamfuata huko huko shambani kwake kuna jambo zito la kuzungumza ************



Zari aliwasili ikulu kama alivyoitwa na Rais.


“Zari karibu sana ikulu nimefurahi kukuona.Wenzako wanaendeleaje? Akauliza “Wanaendelea vizuri”


“Kwanza nataka kujua namna mambo yanavyokwenda.Sijapata nafasi ya kuwauliza kujua mnavyoendelea katika misheni yenu.Wapi mmefika hadi hivi sasa? Akauliza Rais Festus “Mheshimiwa Rais bado tunaendelea lakini mambo yanakuwa magumu.Kila tunapopiga hatua moja wenzetu nao wanapiga mbili lakini maendeleo si mabaya.Tulikofika kunatia moyo” akasema Zari na kumueleza Rais Festus kwa ufupi namna misheni yao inavyokwenda


“Ruby alinitaarifu kuhusiana na nyumba yako kuzingirwa na polisi jana usiku nikawasiliana na mkuu wa jeshi la polisi nikamtaka askari hao waondoke haraka sana.Naamini hakukuwa na madhara yoyote”


“Tunashukuru sana mheshimiwa rais kwa msaada ule mkubwa.Tunaamini askari wale walipewa taarifa kwamba Mathew Mulumbi yumo mle ndani na kilichowachelewesha


kuingia ndani ni ukuta


mkubwa na uwepo wa mfumo wa kisasa wa nyaya za ulinzi juu ya ukuta huo.Baada ya wao kuondoka na sisi tukaondoka tukaenda mafichoni” akasema


Zari


“Nahitaji kuonana na


Mathew Mulumbi” akasema Rais Festus


“Mathew Mulumbi kama nilivyokueleza kwa sasa yuko katika shamba la mazoezi la makomando wetu.Ni mbali kidogo kutoka hapa na Mathew kama unavyojua hawezi kuja hapa ikulu labda uzungumze naye kwa simu” akasema Zari


“Nitakwenda huko aliko sitaki kuzungumza naye kwa simu nataka tuonane ana kwa ana” akasema Rais Festus “Mheshimiwa Rais kama ukienda mahala hapo lazima utaleta ushawishi kwa watu kutaka kujua kuna nini mahala hapo hadi ukaenda? Nashauri uzungumze na Mathew kwa kutumia simu” akasema Zari


“Sitaki kuzungumza naye kwa simu.Nataka kuonana naye ana kwa ana.Kuna suala la muhimu mno ambalo nataka kuzungumza naye.Usihofu tutakwenda kwa kutumia helkopta” akasema Rais Festus na kutoa maelekezo helkopta ya Rais iandaliwe.Zari akamjulisha dereva wake arudishe gari lake ofisini kwake kisha akaongozana na Rais wakaelekea katika helkopta wakaondoka pamoja na walinzi wanne kuelekea katika shamba la mazoezi la makomando wa SNSA aliko Mathew Mulumbi.




**************


Mathew Mulumbi


alimuelekeza Kendrick kusimamisha gari nje ya duka moja la kuuza vipuri vya magari.


“Ingia mle ndani utakayemkuta mwambie kwamba unataka kuonana na Senza.Wakikuuliza wewe ni nani waambie una maagizo yake kutoka kwa Bravo.Kama yupo watakupeleka kwake na utamwambia kwamba nimekutuma nataka kuonana naye” akasema Mathew na Kendrick akashuka akaelekea ndani ya duka lile kubwa la kuuza vipuri vya magari ambalo lilikuwa na wahudumu wanne.Akamfuata jamaa mmoja akamjulisha kwamba anataka kuonana na Senza Yule muhudumu akamuelekeza amfuate jamaa mmoja aliyekuwa amevaa fulana nyekundu


“Karibu kaka” akasema Yule jamaa kwa uchangamfu mkubwa


“Ahsante sana.Kaka nahitaji kuonana na Senza”akasema Kendrick na Yule jamaa akastuka akatazama pande zote halafu akamtaka Kendrick amfuate wakaingia katika chumba


kilichokuwa kinatumika kama


ofisi


“Umesema unataka kuonana na Senza?


“Ndiyo”


“Kwa nini unataka kuonana naye?


“Nina maagizo yake kutoka kwa Bravo”


“Bravo? Akauliza Yule jamaa


“Ndiyo” akajibu Kendrick na yule jamaa akamtaka amsubiri kwa muda mfupi akatoka na baada ya dakika chache akarejea na kumtaka amfuate wakaelekea hadi katika chumba kimoja na yulejamaa akagonga mlango wakaruhusiwa kuingia ndani wakamkuta jamaa mmoja mnene akiwa amekaa kitini huku miguu akiwa ameipandisha juu ya meza.Alikuwa anavuta sigara na chumba kilikuwa na moshi mwingi akamfanyia ishara Kendrick aketi kitini.Akaendelea kuvuta sigara yake huku akitazama mashindano ya farasi kupitia luninga kubwa iliyokuwa ukutani.


“Nina ujumbe wako ! akasema Kendrick baada ya kumuona Yule jamaa hana habari kama kuna mtu mle


ofisini


“Kaka nina ujumbe wako” akasema Kendrick na kusimama


“Sit ! akasema Yule jamaa na Kendrick akaketi.Yule jamaa akavuta sigara akapuliza moshi halafu akauliza


“Umetoka wapi?


“Nina ujumbe wako kutoka kwa Bravo”akajibu Kendrick na Yule jamaa akastuka kidogo


“Bravo?


“Ndiyo”


“Amekutuma nini? “Anahitaji kuonana nawe” “Yeye yuko wapi?


“Yuko hapo nje”


“Yuko nje? Akauliza Yule jamaa


“Ndiyo yuko nje” akajibu Kendrick na yule jamaa akazima sigara yake na kusimama haraka haraka akaongozana na Kendrick wakaelekea katika gari alimokuwamo Mathew.Kioo kikashushwa na Yule jamaa akapigwa na butwaa baada ya kumuona Mathew garini.Haraka haraka akakimbia katika geti akamuelekeza mlinzi afungue gari la akina Mathew likaingia ndani.Mathew akafungua mlango akashuka na Yule jamaa akamkumbatia kwa furaha halafu akampeleka ofisini kwake


“Siamini kama ni wewe.Niliposikia kile kilichokupata nilistuka sana.Kwanza sikujua kama uko hapa nchini kwani muda mrefu hatujaonana!


“Nikweli sikuwepo hapa nchini kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu” akasema Mathew


“Pole sana Mulumbi kwa mambo yaliyokupata” “Ahsante sana Karim”


“Niliposikia kwamba Mulumbi ametoweka nilitabasamu.Mathew you are the ghost.Kwa namna ulivyoweza kuondoka katika mikono ya polisi it’s amazing ! akasema Karim


“Karim sina muda mrefu hapa kwako nimekuja kuomba msaada wako” akasema Mathew


“Nimeingia katika vita na miungu wa dawa za kulevya” akasema Mathew


“Mathew ilikuaje ukaingia katika dunia hiyo?Nilishangaa sana niliposikia kwamba mzigo mkubwa wa dawa za kulevya umekamatwa nyumbani kwako.Nilishangaa sana na kujiuliza imekuaje Mathew akaingia huko?


“Sijawahi kuingia huko.Karim unafahamu kazi zangu unafahamu biashara zangu sijawahi kuingia katika biashara hizo.Kuna suala nilikuwa nalifuatilia linahusiana na Gosu Gosu”


“Gosu Gosu nilisikia kesi yake ya mauaji”


“Gosu Gosu hakufanya


yale mauaji bali aliangushiwa mzigo ule ikaonekana yeye ndiye muuaji”


“Aliangushiwa mzigo na nani? Akauliza Karim


“Sifahamu bado ninaendelea na uchunguzi ambao umenifikisha katika ulimwengu huo wa dawa za kulevya.Niko katika vita kubwa hivi sasa na hao jamaa ndiyo maana yakatokea yale yaliyotokea.Niliwekewa kiasi kikubwa cha dawa za kulevya nyumbani kwangu na kutengenezewa pia kesi ya mauaji.Ukweli ni kwamba I didn’t do it”


“Naelewa Mathew


Mulumbi.Nafahamu mambo


yalivyo pale unapoingia katika dunia hiyo ya wafanya biashara hao.Hiyo ni vita mbaya sana na isiyokwisha.Ukiingia katika himaya ya hawa jaama hawalali hadi wahakikishe wamekuondoa kabisa katika himaya yao hata kama itachukua miaka mingi hivyo sishangai kwa hiki kilichokutokea Mulumbi .Pole sana”


“Nimekuja kwako nahitaji msaada wako Karim” “Anything you need Mathew Mulumbi”


“Kuna kitu nimekutana nacho ambacho nataka msaada wa kukifahamu zaidi.Nataka kufahamu kuhusu kundi linaitwa Black Mafia”


“Black Mafia? Akauliza Karim


“Ndiyo.Umewahi kusikia kundi hilo?


“Labda nikuweke wazi Mathew kwamba ni muda mrefu nimekwisha toka katika ulimwengu huo wa dawa za kulevya na kwa sasa ninajishughulisha na biashara


ya vipuri vya magari na unakumbuka ni wewe uliyenipa ushauri huu hivyo mambo mengi yanayoendelea huko siyafahamu”


“C’mon Karim.I need your help ! akasema Mathew


“Mathew wewe ni mtu wangu wa karibu sana na kama ningekuwa nafahamu chochote kuhusiana na kundi hilo ningekueleza lakini sifahamu chochote”


“Najua bado una rafiki zako huko naomba unisaidie kutafuta taarifa hizi za uwepo wa kundi hilo linaloitwa Black Mafia hapa nchini”


“Hao Black Mafia wanajihusisha na nini hapa nchini?


“Kwa taarifa chache nilizonazo ni kwamba kundi hili lilianzishwa huko Amerika ya Kusini na kazi yake kubwa ni kuwalinda miungu wa biashara hizo na kuhakikisha hakuna kikwazo chochote kinatokea katika biashara.Kundi hilo tayari liko hapa nchini na ninachotaka ni


kupata taarifa zake na vile vile kumfahamu kiongozi wao hapa nchini” akasema Mathew


“Mathew ni mara ya kwanza leo nimesikia kuhusu uwepowa kundi hilo.Naomba uniachie hiyo kazi nitafanya uchunguzi wangu na nitakachokipata nitakujulisha”


“Nitashukuru sana Karim kwa msaada huo.Ningeomba kazi hiyo uifanye haraka kidogo kwani hawa jamaa wanaendelea kunitafuta kwa nguvu kubwa!


“Hadi kufikia leo jioni nitakuwa nimepata majibu na nitakwambia.Bado nina watu wangu huko nitawatumia


kutafuta taarifa za kundi hilo” akasema Karim


“Karim ninakushukuru na ninakutegemea sana ndugu yangu” akasema Mathew akaagana na Karim wakaondoka naMathew akamuelekeza Kendrick sehemu nyingine wanakoelekea.




**************


Helkopta ya Rais ilitua katika shamba la mazoezi la makomando wa SNSA.Ruby na makomando walikuwa wamesimama karibu na mahala ambako helkopta ingetua kwani tayari walikwishajulishwa na Zari kuhusu ujio ule wa Rais mahala pale.Mlango ukafunguliwa wakashuka walinzi wa Rais na kujipanga pembeni halafu akashuka Zari na baada ya muda akashuka Rais Festus,Ruby akasogea akasalimiana na Rais kisha wakaelekea ndani


“Ruy habari za hapa? Akauliza Rais festus


“Habari za hapa ni nzuri na si nzuri vile vile.Nimefurahi sana kukuona mheshimiwa Rais naomba kabla ya yote unipe taarifa za maendeleo ya wanangu.I miss them a lot” akasema Ruby


“Wako salama


wanaendelea vizuri kabisa” akasema Rais Festus


“Do they ask about me and their father?


“Wanauliza ninawaambia mmekwenda safari lakini mtarudi siku si nyingi.They are happy! Akasema Rais Festus


“Naomba tafadhali ukienda unipe simu nizungumze nao.Ninakosa usingizi kila nikiwafikiria wanangu.Kitu kimoja tu ninachokuomba waweke mbali na televisheni wasije wakajua kile kinachoendelea kwamba baba yao anakesi mahakamani” akasema Ruby “Kwa namna Ruby anavyowapenda watoto wake,angefahamu kama hawako hapa Tanzania angezimia.Lakini niliwatoa hapa na kuwapeleka kwa Rais wa Rwanda kwa siri kwa sababu ya usalama wao” akawaza Festus


“Mnaendeleaje hapa? Akauliza Festus


“Hivyo hivyo mheshimiwa Rais tunaendelea japo taratibu


lakini maendeleo si mabaya”



“Amekwishanieleza Zari


kila kitu.Kilichonileta hapa ni kuzungumza na Mathew Mulumbi.Where is he?akauliza Rais


“Mathew Mulumbi alitoka asubuhi na mmoja wa makomando na hakusema anakwenda wapi”


“Hayuko hapa? Akauliza


Rais Festus


“Hayupo”


“Call him.Namuhitaji hapa sasa hivi ! akasema Ris Festus na Zari akachukua simu yake akazitafuta namba za Kendrick akampigia




**************


Baada ya kutoka kuonana na Karim,Mathew Mulumbi alimuelekeza Kendrick waelekee katika kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa kinachomilikiwa na mdogo wa mchungaji Adam Watwila.Wakiwa njiani wakielekea huko kiwandani simu ya Kendrick ikaita “Hallo mkurugenzi” “Kendrick uko wapi?


“Niko barabarani naendesha gari mkurugenzi”


“Uko na Mathew Mulumbi?


“Ndiyo niko naye”


“Mpe simu tafadhali” akasema Zari na Kendrick akampa Mathew simu “Zari” akasema Mathew


“Mathew nataka urudi hapa kambini mara moja Rais yuko hapa anataka kuzungumza nawe”


“Rais?! Mathew akashangaa


“Ndiyo.Rais yuko hapa amekuja kuzungumza nawe jambo muhimu”


“Sawa ninakuja” akajibu


Mathew na kumuelekeza Kendrick warejee katika shamba lao la mazoezi.




**************


Profesa Simon Thema aliwasili shambani kwa makamu mwenyekiti wa chama anachokiongoza Rais Festus.


“Katibu karibu sana” akasema mzee Titus Mgasa


“Nashukuru sana mzee


Titus.Pole na shughuli za kilimo”


“Ahsante.Nimeona leo nina nafasi nije mara moja kuangalia maendeleo ya shamba langu.Vipi kuna habari gani huko ambayo hukutaka kusubiri hadi ukanifuata huku? Akauliza mzee Titus wakati wakielekea katika nyumba iliyokuwepo pale shambani


“Mzee Titus nimeamua kukufuata huku kuna jambo zito” akasema profesa Simon na kuvuta pumzi ndefu


“Unaniogopesha katibu”


“Sikuogopeshi mzee Titus lakini kweli ni jambo zito” akasema profesa Simon


“Nadhani tayari umekwisha pata taarifa za alichokifanya mwenyekiti asubuhi ya leo”


“Mpaka sasa bado


naendelea kutafakari na sijapata jibu kwa nini akafanya kitu kama kile.Kwani kama angekaa kimya kuhusianana mahusiano yake nje ya ndoa angepungukiwa nini? Mbona amejidhalilisha sana? Tatizo la Festus ni kupenda kufanya maamuzi peke yake bila kuwashirikisha wenzake.Kama angekuja kwetu na kutueleza tungempa ushauri nini cha kufanya lakini akakurupuka


mwenyewe kwenda kwenye luninga akaanza kutoa siri zake.Amejishushia heshima na zaidi ya yote anakidhalilisha chama” Akasema mzee Titus


“Mzee Titus hiki alichokifanya mwenyekiti asubuhi ya leo ni kidogo sana.Lipo bomu lingine ambalo likilipuka litatumaliza sisi sote”


“Kuna jambo lingine tena?


Akauliza kwa mshangao mzee Titus


“Ndiyo kuna jambo lingine tena kubwa.Ni bomu” akasema profesa Simon.


“Mchana wa leo nikiwa ofisini kwangu nilipigiwa simu na mtu nisiyemfahamu akaniambia kuna kitu amenitumia katika barua pepe nikafungua na kukutana na kitu ambacho almanusura kinitoe uhai.Mzee Titus kama leo hii ningekuwa na ugonjwa wa moyo ningeanguka na kufa pale pale”


“Ni kitu gani hicho? Akauliza mzee Titus


“Kuna watu hapa karibu? Akauliza Simon


“Hapana watu wote wako shambani wanaendelea na kazi” akajibu mzee Titus na profesa Simon akaifungua kompyuta yake na kumsogezea mzee Titus akamtaka azitazame picha zile.Mzee Titus akazitazama na kuguna akavua miwani na kuisogelea zaidi kompyuta


“Huyu ni Festus? “Ndiyo ni mwenyewe”


“Mungu wa Israel ! akasema mzee Titus kwa mstuko.Akavaa miwani yake akarudia tena kuzitazama zile picha halafu akauliza


“Is this real? Siyo zile za kutengeneza kwa lengo la kumchafua Rais? Akauliza mzee Titus


“Hapana mzee.Hizi ni


halisi na wala si picha za kutengeneza” akajibu profesa Simon na mzee Titus akajikuta akiegemea kiti na kuvuta pumzi ndefu


“Kweli hili ni bomu” akasema


“Ni bomu kubwa la maangamizi”


“Ni nani huyo amekutumia picha hizi na kwa malengo gani?


“Simfahamu na wala


hajajitambulisha ni nani.Baada ya kuzipata picha hizi nikaamua kwenda moja kwa moja ikulu kuonana na mwenyekiti nikamuonyesha” “Akasemaje?


“Hata naye alistuka sana.Nilimtaka akiri kama picha hizi kweli ni halisi na si za kuengeneza akakiri kwamba ni picha halisi si za


kutengeneza”


“Mungu wangu ! akasema mzee Titus


“Alidai kwamba mwanamke huyo unayemuona pichani ana mahusiano naye ya kimapenzi”


“Amekiri hivyo? Akaulia mzee Titus


“Ndiyo.Tuachane na hayo kubwa alilolitaka huyo jamaa aliyenitumia hizi picha ni kuzungumza na Rais na walipozungumza huyo jamaa alimwambia kwamba hatazisambaza picha hizi pamoja na nyingine nyingi alizo nazo kama Rais atakubali kumpatia kile anachokihitaji”


“Anahitaji kitu gani huyo jamaa? Pesa?


“Hapana hahitaji pesa.Anahitaji mtu?


“Mtu? Akauliza mzee Titus


“Ndiyo anamtaka Mathew Mulumbi”


“Mathew Mulumbi?Huyu ambaye amekamatwa juzi na madawa ya kulevya halafu akatoroka?


“Huyo huyo”


“Kwani amekwisha


kamatwa na jeshi la polisi huyo Mathew Mulumbi?


“Hapana bado lakini Rais anafahamu mahala alipo”


“Unanichanganya


katibu.Rais anafahamu mahala alipo kivipi huku jeshi la polisi linamsaka? Akauliza mzee Titus na profesa Simon akamuelezea kile alichoelezwa na Rais kuhusu Mathew. “Maneno haya yametoka kwenye kinywa chake yeye mwenyewe Rais? Akauliza mzee Titus


“Ndiyo”


“Hapa nilipo mwli wangu wote unanitetemeka.Kweli hii ni vita kubwa.Ninachojiuliza hawa jama wamewezaje kupata picha hizi za faragha?


“Hata yeye mwenyewe


bado anajiuliza jambo hili limetokeaje.Anavyohisi hao jamaa tayari wana watu wao hadi ndani ya ikulu ndiyo maana wakaweza kupata picha zile akiwa faragha”


“Baada ya kuelezwa na huyo jamaa kwamba wanamtaka Mathew Mulumbi nini maamuzi ya Rais?


“Hilo ndilo lililonileta hapa kwako.Rais amekataa kukubaliana na matakwa yao”


“Amekataa? Mzee


Titus akashangaa


“Ndiyo anataka kupambana nao” “This man is not serious.Yaani hajatetemeshwa na hizi picha?


“Mwenyekiti amedhamiria kabisa kutaka kupambana na hao jamaa.Mzee Titus jambo hili lina athari kubwa sana kwa chama.Tunamtegemea sana Festus katika uchaguzi mkuu ujao lakini kama jambo hili likivuja basi chama kitazama.Hatuna mtu mwingine ndani ya chama kwa sasa mwenye sifa kama za


Festus”


“Hukumuelewesha hilo jambo?


“Nimemuelewesha lakini ameshindwa kunielewa ndiyo maana nimelileta suala hili kwako ili tusaidiane mawazo.Nimejaribu kuzungumza na huyo jamaa kumuomba muda zaidi amegoma na kudai muda aliotoa unatosha na kama kile anachokitaka hakitakuwa kimetekelezwa ndani ya muda huo basi atazisambaza picha hizi mitandaoni.Nahisi kama akili yangu inafika ukomo kufikiri ndiyo maana nimekuja kwako ili tusaidiane nini tufanye?Festus amekwisha fanya maamuzi na yuko tayari picha hizi zisambazwe bila kujali athari zake”


“Nani kamroga mwenyekiti wetu?Huyu si Festus ninayemfahamu mimi”


“Hata mmi nimeshangaa mno.Sikuwa nikiufahamu upande wa pili wa Rais wetu ukoje. Mzee Titus tutaendelea kulijadili jambo hili kwa upana wake lakini kwa sasa tujielekeze katika kutafuta suluhu ya jambo hili kabla muda uliotolewa haujamalizika.Tufanye kila linalowezekana kwa ajili ya chama kwani aibu ya mwenyekiti wetu ni aibu ya chama pia.Tutaziweka wapi sura zetu kama picha hizi zitasambaa ?


“Nadhani kuna jambo moja ambalo tunatakiwa kulifanya.Tuonane na mke wake”


“Mke wa Rais? Akauliza


profesa Simon kwa mshangao “Ndiyo.Hakuna namna


lazima tuonane na mke wake”


“Mzee Titus I don’t think that’s a good idea”


“Hiyo ndiyo njia pekee kwa sasa tunayoweza kuitumia kumsaidia Festus na pia kukisaidia chama”akasema mzee Titus


“Wasi wasi wangu ni kwamba Festus anaweza asipendezwe na sisi kumfuata mke wake na kumueleza kuhusu aibu hii kabla yeye hajafanya hivyo,utaibuka mgogoro kati yetu”


“Hata kama ikileta matatizo lakini tunajaribu kutatua hili tatizo.Tunajaribu kutafuta suluhu.Hakuna njia nyigine ya kuweza kulimaliza hili jambo zaidi ya kufanya kama wanavyotaka hao jamaa.Yawezekana mama Bella kuna kitu anakifahamu kuhusiana na Mathew Mulumbi hivyo kama tukimshirikisha katika suala hili anaweza akatusaidia kufahamu mahala alipo na sisi tukawasiliana na hao jamaa tukawapa maelekezo wakaenda kumchukua na jambo hili litakuwa limekwisha.Rais atabaki salama na chama pia” akasema mzee Titus


“Mzee Titus kama nimekuelewa vizuri una maanisha kwamba tufanye jambo hili bila kumshirikisha Rais?


“Exactly.Kama Rais amekwisha fanya maamuzi basi hakuna namna tutakavyoweza kumshawishi akakubali kutekeleza matakwa ya hao jamaa.Rais wetu kwa sasa amepofushwa haoni,anasindwa kung’amua athari zilizoko mbele zitakazoletwa na bomu hili kama likilipuka.Lazima afahamu kwamba si kila vita lazima uibuke mshindi kuna nyakati itakulazimu ukubali kushindwa na kuwapa wengine ushindi.Tukimtumia Bella naamini tunaweza kufanikiwa kwani hata yeye mwenyewe hatakubali mume wake apate aibu hii kubwa hivyo kama kuna kitu anakifahamu kuhusu Mathew Mulumbi lazima atatueleza.Kingine ninachotaka tumshirikishe mama Bella ni kama unavyomjua Yule mama ana nguvu sana ana uwezo mkubwa wa kuweza kupata taarifa za mahala aliko Mathew.Najua utatokea ugomvi kati yetu na Festus lakini hakuna namna hapa tunajaribu kulinda taswira ya chama na nchi! Akasema mzee Titus na profesa Simon akakubaliana naye kisha mzee


Titus akampigia simu mama Bella mke wa Rais


“Mzee Titus shikamoo baba”


“Mama Bella nimekwisha kwambia hizo shikamoo zako hizo” akasema mze Titus na wote wakaangua kicheko


“Marahaba Bella unaendeleaje?


“Sisi hatujambo mzee


Titus”


“Mama Bella nafahamu uko katika majukumu yako ya siku lakini nina shida ya dharura nataka kukuona”


“Saa ngapi unataka tuonane mzee Titus?


“Sasa hivi”


“Sawa mzee naomba


unifuate katika ofisi zangu”akasema mama Bella na kukata simu haraka haraka mzee Titus na profesa Simon wakaingia garini na kuondoka


kuelekea zilipo ofisi za taasisi ya mama Bella


***************


Mathew alirejea katika msitu wa mazoezi wa


makomando wa SNSA kama


alivyotakiwa kwa ajili ya kwenda kuonana na Rais.Mara tu baada ya kushuka garini


Zari akampokea na kumuongoza kuelekea kwa Rais


“Mheshimiwa Rais” akasema Mathew na kumpa mkono Rais


“Mathew Mulumbi habari yako.Leo nimefurahi sana nimeonana nawe ana kwa ana na nikakushika mkono” akasema Rais Festus


“Karibu sana hapa katika makazi yetu ya muda mheshimiwa Rais”


“Ninashukuru


nimekaribia” akasema Rais Festus na kunyamaza kwa muda


“Mathew Mulumbi,Zari na Ruby kwa kuwa tuliyekuwa tunamsubiri amekwisha fika hakuna tena kuendelea kupoteza muda.Nimekuja hapa kwanza kujua kile kinachoendelea kufahamu mahala mlikofikia katika misheni hii mnayoendelea nayo.kwa bahati nzuri tayari Zari na Ruby wamekwisha nieleza kwa kirefu kuhusu maendeleo yenu na mahala mlikofikia.Ninawapongeza sana kwa kazi kubwa ngumu


na ya hatari mnayoifanya.Nimeelezwa mara kadhaa mmenusurika kufa.Mahala mlipofika ni pakubwa mno na nimekuja kuwapa moyo kwamba msikate tamaa hiki mnachokifanya ni muhimu sana kwa nchi.Genge hili la wahalifu lazima lisakwe na lisambaratishwe ! akasema kwa hasira Rais Festus


“Mhshimiwa Rais ninakuahidi kwamba tutafanikiwa kulisambaratisha kundi hili kwani hatua tuliyofikia ni nzuri walau kuna mwanga umeonekana na sasa tumeweza kufahamu watu tunaowatafuta ni genge la wafanyabiashara wa dawa za kulevya.Hii si vita nyepesi hata kidogo kwani wao pia wamejihami kwa kila kitu kuhakikisha kwamba hakuna mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo katika biashaa yao ndiyo maana wakaanzisha kundi la Black Mafia ambalo ni kama jeshi lao.Kundi hilo lina watu wenye mafunzo ya juu ya ujasusi,mawasiliano nk.Wanatumia silaha nzito na wanatumia teknoljia ya hali ya juu katika kuhakikisha mambo yao yanakwenda” akasema Mathew



“Kama mtakumbuka


katika mkutano mkuu wa SADC uliofanyika hapanchini ambapo Tanzania ilipewa uenyekiti kwa muda wa mwaka mmoja nilitangaza namna sisi kama nchi tulivyodhamiria kupambana na biashara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikishamiri siku hadi


siku.Niliziomba pia nchi wanachama wa SADC kuungana pamoja katika vita hii kwani nchi moja peke yake haiwezi kushinda hii vita lakini kumekuwa na uungwaji mkono usioridhisha kutoka kwa nchi wanachama wa SADC na kuzorotesha vita hiyo niliyoitangaza.Hapa nchini vile vile tumeendelea na mapambano kwa kusua sua na bado sijaona yale matokeo makubwa niliyoyakusudia kuyaona.Kila ukipita mitaani unawaona vijana wakiwa wamelewa unga na hii ina maanisha kwamba bado unga unaendelea kuingia hapa nchini na biashara inaendelea kama kawaida.Kuzorota kwa vita hii hapa nchini ni ishara kwamba hawa wafanya biashara wana mtandao mpana sana hadi katika vyombo vinavyohusika na mapambano hayo.Hiki mlichokifanya katika siku hizi chache kimewastua mno wameamka na mapambano yameanza” akasema Rais Festus na kunyamaza kidogo baada ya muda akaendelea


“Sielewi wamefahamu vipi lakini tayari wanajua kuwa nimeshiriki katika mpango wa kumtorosha Mathew Mulumbi.Ndiyo maana ninasema hawa jamaa wana mtadao mpana sana nahisi


hata ndani ya SNSA tayari wamekwisha jipenyeza.Mpango ule ulikuwa


wa siri sana lakini tayari wameufahamu na sasa wameyaelekeza mashambulizi kwangu”akanyamaza tena kidogo


“Kuna televisheni humu ndani?


“Ndiyo ipo” akajibu Zari


“Kama mnafuatilia leo asubuhi nilikuwa katika kipindi cha mchaka mchaka ambacho kilifanyika ikulu na katika kipindi hicho niliweka wazi kwamba nina mtoto wa nje ya ndoa na jambo hili limezua mjadala mkubwa sana siku ya leo” akanyamaza tena


“Nikiwa wizara ya maji niliwahi kuwa na mahusiano na mwanamke mmoja na tukapata mtoto wa kiume anaitwa Joel lakini jambo hili tukalifanya siri kubwa hata mtoto huyo hafahamu kama mimi ni baba yake.Kitu cha kushangaza jana mwanamke huyo niliyezaa naye alifuatwa na watu waliojifanya ni waandishi wa habari ambao walianza kumchimba kuhusiana na jambo hilo na maendeleo ya mwanangu ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu baada ya kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.Alinipigia simu akanieleza jambo hilo na nikashangaa sana namna hao jamaa walivyoweza kuzipata


taarifa hizo za siri.Nilimueleza mshauri wangu wa masuala binafsi jambo hilo na akanishauri kwamba wanahabari hao wanataka kuitoa gazetini taarifa hiyo ambayo itauza mno akanishauri niwe wa kwanza kuzungumza jambo hilo mimi mwenyewe kabla waandishi hao hawajaliweka wazi kwa umma ndiyo maana nikaandaa kipindi kile na kutamka lile jambo.Si kwamba nilipenda kufanya vile lakini nililazimika kwani kama wananchi wangelipata kupitia magazeti ingekuwa mbaya zaidi kwa upande wangu.Nilijua nimelimaliza hilo suala na waandishiwa habari hawana tena cha kusema kumbe nilikuwa najidanganya” Zikapita sekunde kadhaa za ukimya halafu akasema


“Nilipigiwa simu na katibu mkuu wa chama changu akataka tuonane akanifuata ikulu na kunionyesha picha zangu za faragha.Ninyi ni vijana wangu hivyo nataka niwaweke wazi kwamba kwa hivi sasa nina mahusiano na mrembo mmoja anafanya shughuli za mitindo anaitwa Zandile Wepener.Nadhani tayari mnamfahamu kwani aliwahi kuwa mke wa mfalme wa Eswatini na walipoachana alitawala sana vichwa vya habari duniani kote.Sitaki kuingia kwa undani zaidi huko kwa vile mmekwisha fahamu niko naye inatosha.Zandile amekuwa akija Dar kila mwisho wa wiki na kufikia katika nyumba niliyonunua na huwa ninapata muda wa kuwa


naye na ananifariji sana.Mambo haya huwa ninayafanya kwa siri kubwa lakini nimestuka baada ya kuletewa picha zangu nikiwa faragha na Zandile.Katibu mkuu alitumiwa picha hizo na mtu asiyemfahamu naye akazileta kwangu.Mtu huyo ametishia kuzisambaza picha hizo katika mitandao ya kijamii kama nisipotekeleza kile anachokitaka.Nilidhani ni waandishi wa habari tena lakini pale aliponitajia anachokitaka ndipo nilipofumbuka macho na kung’amua kuwa niko vitani”


“Nini wanataka hao jamaa? Akauliza Mathew


“You”


“Me? Mathew akashangaa


“Ndiyo Mathew hao jamaa wanataka nikukabidhi kwao ili wasiweze kuzisambaza picha hizo mitandaoni” akasema Rais Festus


“Subiri kwanza mheshimiwa Rais,nataka kufahamu hizo picha ni halisi au ni picha za kutengenezwa? Akauliza Mathew


“Si picha za kutengeneza ni picha halisi.Nimezichunguza kwa makini ni picha halisi nikiwa faragha na Zandile” akasema Rais Festus


“Dah ! hii imekwenda mbali sasa”akasema Zari “Sikilizeni vijana wangu niliwaambia hawa jamaa wana nguvu na wanaweza wakafanya chochote naamini wana watu wao hata miongoni mwa watu wanaonizunguka hivyo basi jambo kama hili kutokea si kitu cha ajabu” akasema Rais Festus


“Nimewaambia kwamba hawa jamaa wamestuka sana kwa hatua kubwa mliyoipiga ndani ya siku hizi


chache,mmefahamu mambo mengi ambayo hawakutaka muyajue ndiyo maana nao pia wanatumia nguvu kubwa katika kuhakikisha wanawazuia msiendelee


mbele.They are very smart wanafahamu Mathew


Mulumbi ndiye kiongozi wa timu hii hivyo wakimpata huyo basi vita itakuwa imekwisha na hakuna atakayewaumiza vichwa vyao tena.Wanazo picha zangu wanajua mimi ni Rais na sintakubali picha zangu zisambazwe mitandaoi


hivyo basi lazima


nitakubaliana na kile wanachokitaka.Wanajua kupanga karata zao vizuri,kwani nikikubali kuwapa kile wanachokitaka basi tayari nitakuwa nimeinua mikono ishara ya kushindwa vita na nitakuwa mtumwa wao.Wataitawala ofisi yangu na nitakuwa ninafanya kila watakachoniamuru.Sintakuwa na nguvu tena ya kupambana nao kwani kila nitakapojaribu kufanya chochote watanikumbusha kwamba wanazo picha zangu za faragha” akasema Rais Fesstus


“Jamaa hao wametoa muda na utakapokwisha bila kumkabidhi Mathew Mulumbi kwao basi picha zangu zitasambazwa mitandaoni.Ni tukio la aibu kubwa kwa picha za faragha za Rais kuvuja.Halitakuwa tukio kubwa tu hapa Tanzania bali dunia nzima” akanyamaza na kuinamisha kichwa kwa sekunde kadhaa halafu akasema


“Nimekuja hapa


kuzungumza nanyi,nilitaka nionane uso kwa uso na Mathew Mulumbi wakati ninamueleza hili kwamba siko tayari kukukabidhi kwa hao jamaa.Siko tayari kukubaliana na matakwa yao na niko tayari kwa picha hizo zisambazwe.Niko tayari kuibeba aibu hiyo kubwa !


“Mheshimiwa Rais ! akasema Mathew na kusimama


“Mathew sit ! akasema


Rais Festus.


“Maamuzi haya


niliyoyafanya ni yangu binafsi,sijaomba na sitaki ushauri wa ushauri wa mtu yeyote.Nafahamu nitapata aibu kubwa ambayo hakuna kiongozi mkubwa amewahi kuipata hapa nchini ila nitavumilia yote lakini kuna jambo moja tu ambalo


limenileta hapa” Rais akamkazia macho Mathew Mulumbi






“Mathew Mulumbi nataka unitazame machoni na unihakikishie kwamba utawaongoza wenzako kuhakikisha kwamba genge hili la wauza dawa za kulevya unaliondoa.Mzigo wa aibu nitakaoubeba ni mzito sana hivyo nataka aibu hiyo iwe na manufaa.Promise me Mathew” akasema Rais Festus “Mheshimiwa Rais,kabla sijakuahidi chochote naomba na mimi uniruhusu dakika mbili niseme kitu” akasema Mathew


“Mathew sitaki unieleze chochote kwa sasa.Nataka uniahidi kwamba utapambana kuhakikisha mtandao wote wa dawa za kulevya hapa nchini unafumuliwa.That’s what I want to hear from you” akasema Rais Festus


“Mheshimiwa Rais naomba usinione mtovu wa nidhamu lakini naomba niseme jambo hili.Wewe ni Rais wa nchi,watanzania wana imani kubwa nawe ndiyo maana wakakupigia kura nyingi uwe kiongozi wao.Kwa namna yoyote ile mim, wenzangu hawa na mtanzania yeyote mwenye mapenzi na nchi yake hawezi akaruhusu picha za faragha za rais wake zikasambaa na akadhalilika.Wanaotaka kufanya hivi ni watu makatili wasio na utu hata chembe.Ukidhalilika wewe mheshimiwa Rais tumedhalilika watanzania hivyo naomba ufahamu mheshimiwa Rais kwamba siafikiani na hicho unachotaka kukifanya japokuwa unakifanya kwa mapenzi makubwa kwa nchi yako.Niko tayari nikabidhiwe kwa hao jamaa ili mambo haya yamalizike na ninaamini hata wenzangu humu ndani wataniunga mkono katika hilo” akasema Mathew


“Mathew kijana wangu si kwamba sifahamu hayo unayoniambia.Nimetafakari sana jambo hili ndiyo maana nikafikia maamuzi haya.Niliapa kwa nguvu zote kupambana na magenge ya biashara ya dawa za kulevya.Sijapata uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wenzangu serikalini na ndiyo maana vita hii imekuwa ikisua sua.Kwa sasa nimepata watu ambao wako tayari kupigana vita hii kikamilifu pamoja nami.Siwezi kuwaacha watu kama hao ambao ni ninyi hapa ndiyo maana siko tayari kukubaliana na matakwa ya hao jamaa ya kumtoa Mathew Mulumbi.Niko tayari kuubeba mzigo wa aibu itakayosababishwa na picha zangu za faragha kusambazwa na hao jamaa na ndiyo maana ninataka mnihakikishie kwamba kwa kila namna itakavyokuwa mtahakikisha mnalifutilia mbali genge hili la wahalifu.Ninyi ni watu ambao kama ningekuwa nanyi muda mrefu basi vita hii ingekwisha malizika lakini bado hatujachelewa” akasema Rais Festus


“Mheshimiwa Rais pamoja na hayo yote lakini naomba ukubali mbio langu kwamba fanya kama watu hao wanavyotaka .Nikabidhi kwa hao jamaa.Kwa kufanya hivyo utakuwa umetusaidia kuingia katika mtandao wao.Tutajipanga vizuri mimi na wenzangu katika suala hili na hii ni nafasi ambayo hatuwezi kuiachia.Tunahitaji sana kuufahamu mtandao wa hawa jamaa mheshimiwa Rais”


“They’ll kill you Mathew Mulumbi why don’t you understand?Umekuwa ni hatari kwao ndiyo maana wanatumia kila njia ili waweze kukupata na wakikupata wewe watakuwa na uhakika hakuna mwingine atakayewapa hofu.Mathew this is my war and I’m willing to sacrifice everything to win it ! akasema Raus Festus


“Mheshimiwa Rais ..”


“Mathew tafadhali sitaki tuendelee na mjadala kuhusu jambo hili.Nimeamua kuja kuwaeleza ili mtambue ukubwa na umuhimu wa vita


hii”


“Tunafahamu


mheshimiwa Rais ukubwa wa hii vita.Ni vita ngumu na hawa jamaa hawalali wala hawakati tamaa hadi pale watakapohakikisha vikwavyo vyote vimeondoka na kwa sasa sisi ndiyo vikwazo vyao hivyo lazima wahakikishe tumeondoka.Tazama mimi ninatafutwa na polisi kwa kukamatwa na dawa za kulevya na mauaji,wewe mheshimiwa Rais mambo ndiyo kama hayo yanayokukabili na yawezekana


yakafuata mengine makubwa zaidi lakini kwa vyovyote vile itakavyokuwa vita hii lazima tuishinde.Nakuhakikishia mheshimwia Rais hata wakitumia mbinu gani lazima genge hili na mtandao wao wote tuufutilie mbali ! akasema Mathew


“Hayo ndiyo maneno niliyokuwa nataka kuyasikia.Sasa naombeni kuanzia sasa muongeze kasi mara mbili zaidi.Wakati wao wakielekeza mashambulizi kwangu ninyi mtaitumia nafasi hiyo kuwasaka.Nadhani mmenielwa Mathew na wenzako”


“Tumekuelewa


mheshimiwa Rais na ninarudia kwa mara nyingine tena kukuhakikishia kwamba mimi na wenzangu hawa tukishirikiana na makomando wetu tutahakikisha tunapambana kwa kila tuwezavyo kuusaka na kuubaini mtandao huo”


“Msisahau vile vile kwamba Rais mstaafu Dr Fabian amefikishwa mahakamani leo na amesomewa shtaka la mauaji,hii yote ni mipango ya hawa jamaa katika kuwamaliza nguvu wale wote wanaowafuatilia hivyo basi ni sisi ambao tunapaswa kumsaidia Dr Fabian” akasema Rais festus na baadaya majadiliano mafupi


akapanda helkopta na kurejea ikulu


**************


Profesa Simon na mzee


Titus waliwasili katika ofisi za mama Bella mke wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.Walipokewa vizuri na kukaribishwa ofisini kwa Bella


“Karibuni sana wazee wangu.Leo nina bahati sana kutembelewa na viongozi wakuu wa chama.Hii hutokea


kwa nadra sana” akasema


Bella


“Ni kweli hii hutokea kwa nadra na ukiona jambo hilo limetokea basi ujue kuna suala zito” akasema mzee Titus na wote wakacheka


“Vipi maisha yanaendaje Bella?


“Sisi tunaendelea vyema na majukumu ya kila siku ya kuijenga nchi” akasema Bella “Tunashukuru kusikia hivyo.Bella hakuna haja ya kupoteza muda mwingi.Tumekuja hapa kuna jambo ambalo tunataka kuzungumza nawe.Hii ofisi yako watu hawawezi kutusikiliza kwa nje? Jambo lenyewe tunalotaka kulizungumza ni zito kidogo” akasema profesa Simon na Bella akawataka watoke mle ndani wakaenda kuketi bustanini


“Hapa kidogo afadhali hakuna atakayetusikiliza” akasema profesa Simon na ukimya wa sekunde kadhaa ukapita


“Karibu profesa kuna jambo gani? Akauliza Bella


“Mama Bella tumekuja kwako ila utatusamehe sana kwa kuja kwako moja kwa moja lakini hakuna namna imetulazimu tufanye hivyo” akasema Profesa Simon “Msijali wazee wangu”


“Ahsante.Leo mchana nilipokea simu kutoka kwa mtu nisiyemfahamu akanielekeza nifungue barua pepe yangu na nikakuta kitu cha kustusha sana”akasema profesa Simon na kufungua sehemu ya kuhifadhia picha katika kompyuta yake akamuonyesha Bella zile picha za mume wake.Bella alipoziona machozi yakaanza kumdondoka akalia kwa kwikwi.Simon na mzee Titus wakaanza kumbembeleza


“Kwa nini wazee wangu mmenionyesha picha kama hizi?Hamjui ni kwa nama gani mmeniumiza wazee wangu! Akasema Bella akiendelea kumwaga machozi


“Mama Bella halikuwa


jambo jepesi kwa sisi na uzee wetu huu kukufuata na kukuonyesha picha kama hizi lakini imetulazimu kuja kwako hivyo tusamehe sana” akasema mzee Titus


“Kuna kitu ambacho unapaswa ukifahamu Bella” akasema Titus na kumpa ishara profesa Simon aeleze


“Mtu aliyenitumia picha hizi anataka kuzisambaza katika mitandao ya kijamii”


“What?!


“Ndiyo mama Bella anataka kuzisambaza katika mitandao ya kijamii lakini amedai yuko tayari kuachana na mpango huo endapo atatimiziwa kile anachokitaka”


“Anataka nini? Pesa?


Akauliza Bella haraka haraka


“Hapana hahitaji fedha” “Nini anahitaji?


“Anamuhitaji Mathew Mulumbi”


“Mathew Mulumbi?


“Ndiyo.Nadhani tayari umekwisha sikia huyu jamaa alikamatwa siku chache zilizopita na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya na mauaji lakini baadae akatoroshwa na watu wasiojulikana”


“Huyu Mathew bado


anatafutwa na jeshi la polisi”


“Mama Bella kuna jambo ambalo yawezekana hulifahamu bado ni kwamba Mathew alitengenezewa lile tukio na watu aliokuwa anawafuatilia ili akamatwe na afungwe gerezani.Kwa bahati mbaya tukio lile lilimuhusisha pia Dr Fabian Kelelo ambaye ni rafiki mkubwa wa Rais Festus .Ulitengenezwa mpango wa kumtorosha Mathew Mulumbi ili aendelee kuwafuatilia hao jamaa na Rais Festus alishiriki katika


mpango huo”





“Wait ! Unamaanisha


Festus alishiriki katika mpango ule wa kumtorosha Mathew Mulumbi? Akauliza Bella


“Ndiyo alifahamu uwepo wa mpango ule hivyo anafahamu mahala alipo Mathew Mulumbi.Hao jamaa baada ya kugundua kuwa Rais anafahamu mahala alipo Mathew Mulumbi basi wakatumia njia hii ya kutishia kusambaza picha zake za faragha ili Rais aweze kuwakabidhi Mathew Mulumbi”


“Ni akina nani hao jamaa?




“Hatuwafahamu ni akina nani” akajibu mzee Titus


“Mama Bella suala hili lina athari kubwa katika chama na ndiyo maana tuko hapa” akasema profesa Simon na kumueleza Bella kwa upana kuhusu athari zitakazojitokeza


pale picha zile za Rais Festus zitakaposambazwa


“Mama Bella pamoja na


athari zote hizo nilizokueleza katika chama lakini mumeo amekataa kukubaliana na matakwa ya hao jamaa na tumekuja kwako kuomba msaada” akasema profesa Titus


“Amekataa?


“Ndiyo amekataa kabisa” “Hii si akili yake ya kawaida.Huyo kahaba aliyenaye amekwisha muharibu akili ndiyo maana hafikirii vitu vya msingi ! akasema Bella


“Hata sisi tunashangaa kwa kutokukubaliana na matakwa ya hao jamaa”


“Nini sasa maamuzi yenu?Bella akauliza


“Tunataka kuokoa chama


chetu dhidi ya aibu kubwa.Tunataka kumuepusha na yeye pia dhidi ya aibu na tunataka kufanya hayo yote kimya kimya bila yeye kufahamu.Tunataka kukutumia wewe mama Bella” akasema mzee Titus


“Kunitumia mimi?


Akauliza Bella


“Ndiyo.Tunataka kukutumia wewe” “Kivipi?


“Tunafahamu nguvu yako una mawasiliano na watu wengi hivyo basi inaweza ikawa rahisi kwako kufahamu mahala alipo Mathew Mulumbi bila Rais kujua.Kama tukifahamu mahala alipo Mathew Mulumbi basi tutawaelekeza hao jamaa ambao watamchukua na jambo hilo litakuwa limemalizika kimya kimya Rais hatafahamu chochote na picha zake hazitasambazwa mtandaoni.Unaonaje mpango huo? Akauliza mzee Tius


“Ni mpango mzuri.Hata


mimi siko tayari kwa picha hizi kusambaa mtandaoni ni aibu kubwa mno lakini siwezi kufanya kazi hii peke yangu nataka tushirikiane sote” “Hicho ndicho hasa tunapaswa kukifanya,lazima sote tushirikiane” akasema mzee Titus


“Vizuri.Kitu cha kwanza nataka kuzungumza na hao jamaa kama mna mawasiliano yao” akasema Bella


“Ninazo namba za Yule jamaa ninaweza nikampigia” akasema Profesa Simon


“Ninataka kuzungumza naye kumuhakikishia kwamba watapata kile wanachokihitaji lakini waongeze muda na wasisambaze picha hizi mtandaoni.Baada ya hapo


nitaandaa kikao na baadhi ya watu muhimu ambao


tutazungumza nao suala hili ambao wanaweza wakafahamu mahala alipo Mathew Mulumbi” akasema Bella na Profesa Simon akampigia simu yule jamaa aliyemtumia zile picha za Rais


“Katibu nilikuelekeza usinipigie simu kama huna


jambo la msingi la kuzungumza nami.Naamini umenipigia simu kuna jambo zuri unataka kuniambia” akasema Yule jamaa na bila kusema chochote profesa Simon akampa simu Bella


“Hallo unaongea na mama Bella mke wa Rais”


“Bella? Jamaa aliyekuwa simuni akashangaa


“Ndiyo.Niko hapa na katibu mkuu wa chama pamoja na makamu mwenyekiti wamenionyesha picha zile ulizowatumia nimeumia sana.Sikuwahi hata kuota kama mume wangu anaweza akafanya jambo la namna hii.Kwa upande Fulani ninawashukuru kwani mmenisaidia kunifumbua macho kuhusu mume wangu lakini nina ombi kwako” akasema Bella


“Nakusikiliza mama Bella”


“Nimeelezwa hapa kwamba mmemuagiza Rais awakabidhi Mathew Mulumbi na ninaamini jambo hilo analishughulikia hivi sasa,ninachowaomba ni kwamba inaweza ikachukua muda kukamilisha hilo ombi le……”


“Mama Bella” Yule jama akamkatisha


“Naomba unisikilize ndugu yangu.Nimesema inaweza ikachukua muda kidogo kulikamilisha jambo


mnalolitaka hivyo basi ninaomba kwanza msizisambaze hizo picha kwani watakaoumia na kupata aibu zaidi ni mimi na watoto.Naombeni sana kwa hili mtusitiri.Pili


ninawahakikishia kwamba mimi nitalishughulikia jambo hili.Ninakwenda kuonana na Rais sasa hivi nikitoka hapa na kumsisitiza umuhimu wa kutekeleza kile mlichomuelekeza na ninawahakikishia kwamba huyo mtu mnayemtaka mtampata lakini ninawaomba sana niko chini ya miguu yenu mtusitiri mimi na wanangu na aibu hii kubwa msisambaze hizo picha japo kwa siku ya


leo.Nawaomba sana” akasema Bella


“Mama hata sisi hatupendi kusambaza picha hizi za Rais


lakini akitupa kile tunachokitaka hakuna atakayesambaza.Ninakupa hadi saa mbili usiku wa leo uhakikishe Mathew Mulumbi amepatikana baada ya hapo sintapokea tena ombi lolote kutoka kwa mtu yeyote na nitaziachia picha hizo.Nadhani umenielewa mama” akasema Yule jamaa


“Nimekuelewa na ahsante kwa kunikubalia ombi langu” akasema Bella na kukata simu.Akashusha pumzi


“Ahsante Mungu.Jamaa kaonekana kunielewa kidogo na amenipa hadi saa mbili za usiku maagizo yake yawe yametekelezwa.Nitaomba tuutumie vyema muda huu kabla ya saa mbili ili kujua mahala alipo Mathew Mulumbi” akasema Bella.


“Mtu wa kwanza kabisa ambaye anaweza akatusaidia ni mkuu wa jeshi la polisi hapa nchini.Huyu hata kama hafahamu chochote lakini ni rahisi kwake kuweza kufahamu kuhusu Mathew kwani ni mtu wa karibu sana na Rais na wanashirikiana kwa mambo mengi.Nitamtaka tuonane naye tutazungumza na atatueleza kile anachokifahamu” akasema Bella na kuchukua simu akampigia mkuu wa jeshi la


polisi


“Madam first lady ! akasema Yeremia


“Mheshimiwa IGP pole na majukumu”


“Nashukuru sana mama


Bella,vipi maendeleo yako”


“Ninaendelea vyema.IGP niko hapa na makamu mwenyekiti wa chama mzee Titus pamoja na katibu mkuu profesa Simon”


“Ouh leo umetembelewa na vigogo wa chama” “IGP vigogo hawa wamekuja kuniona kwa jambo muhimu sana hivyo kama una nafasi ninakuomba uje hapa ofisini kwangu tuna mazugumzo muhimu nawe” akasema Bella na baada ya tafakari akasema


“Sawa Bella ninakuja hapo” akasema Yeremia Mwaipopo na kukata simu


“IGP amekubali na anakuja hapa ili tuzungumze naye”


“Umesema IGP ni mtu wa karibu sana na Rais unadhani hatakwenda kumueleza Rais hiki tunachotaka kukifanya? Akauliza mzee Titus


“Hapana


hatamweleza.Licha ya kuwa ni mtu wa karibu na Rais lakini ni rafiki yangu vile vile na ananiheshimu sana” akasema Bela wakaendelea na maongezi wakati wakimsubiri IGP Yeremia.






Baada ya helkopta ya Rais kupaa na kuondoka,akina


Mathew wakarejea ndani.


“Nahisi hadi kuishiwa nguvu kwa namna hawa jamaa


walivyojipanga na wanavyoendesha mapambano.Najiuliza wamewezaje kupata picha za faragha za Rais? Akauliza Zari


“Kama wameweza


kupenya ulinzi wa rais na hatimaye wakafanikiwa kupata picha hizo za faragha za Rais basi hao jamaa ni hatari mno,wako vizuri” akasema Ruby


“Nilisema wakati Rais yuko hapa na ninarudia tena kusema kwamba vita na wauza dawa za kulevya si vita nyepesi hata kidogo.Ni vita ngumu na mbaya.Ni kwa bahati mbaya


katika nchi zetu za kiafrika bado hatujashuhudia magenge makubwa na hatari yanayojihusisha na biashara


hii lakini ukifika Mexico au Colombia ndipo utafahamu nini ninakizungumzia.Hawa watu ni wakatili mno.Mliwahi kusikia wakati Fulani mfanya biashara mmoja mkubwa wa dawa za kulevya huko Amerika alikamatwa na kuwekwa gerezani lakini alitoroshwa kwa namna ya ajabu kabisa.Lilichimbwa handaki hadi katika chumba alimokuwamo na akatoroshwa.Escobar hakuna asiyefahamu mambo aliyoyafanya nchini Colombia.Kwa nguvu aliyokuwa nayo ilifika hatua akataka hata kugombea urais.Ninachotaka kukuonyesha hapa ni nguvu kubwa waliyonayo hawa jamaa hivyo msishangae kupatikana kwa picha za faragha za Rais.Hii inaonyesha nguvu ya hawa jamaa ni kubwa na wanaweza wakaingia sehemu yoyote.Tutegemee mengi makubwa zaidi !akasema Mathew


“Mathew ulifikiria nini kumwambia Rais akukabidhi kwa hao jamaa? Akauliza Zari


“Hata mimi nilistuka sana.Hivi ulimaanisha kile ulichokuwa unakisema? Akauliza Ruby


“Sifahamu maana ya mzaha.Nilimaanisha kile nilichokisema.Rais wa nchi kudhalilika ni kitu kibaya sana ndiyo maana nilitaka anikabidhi kwao japokuwa naamini ungekuwa ni mwanzo wa kupenyeza mizizi hadi


katika kiti cha Rais na wangemuendesha watakavyo wao lakini tayari nilikuwa na plani yangu”


“Mathew hawa jamaa kama wangekupata vita ingekwisha.Sote hapa tunakutegemea wewe.Wakati unazungumza maneno yale ulijaribu kutufikiria sisi,uliwakumbuka Gosu Gosu na Fabian? Wote hawa wanakutegemea wewe uwaondoe mahala walipo hivi sasa.Wakati mwingine unapofanya maamuzi jaribu kwanza kuwafikiria na wale wanaokuzunguka.Kuna mawili ambayo yangetokea kama Rais angekubali kukukabidhi kwa hao jamaa kama ulivyotaka.Ungeuawa au ungekabidhiwa kwa polisi lakini kuuawa ingepewa kipaumbele zaidi kuliko kukukabidhi kwa plisi wakihofia kujirudia kwa jaribio la kukutorosha.Mathew please


don’t do that gain” akasema Ruby


“Ladies si kwamba


sikufikiria nilipofanya maamuzi yale tayari nilikuwa na mpango.Tuachane na hilo na tujielekeze kwa suala lililoko mezani kwa sasa ambalo ni picha za faragha za Rais.Ni kashfa kubwa kuwahi kutokea katika nchi yetu” akasema Mathew na kusikitika


“Ni kashfa kubwa” akasema Zari


“Hata hivyo nampongeza mheshimiwa Rais” akasema Zari na kucheka kidogo


“Amekwenda maelfu ya


kilometa hadi Afrika kusini na akafanikiwa kung’oa chombo.Zandile Wepener si kifaa cha mchezo.Sisemi kwamba sisi ni wabaya la hasha ila lazima tuwe wakweli


Zandile ni mzuri” akasema Ruby


“Ruby is right.Zandile ni mwanamke mrembo sana ndiyo maana aliweza kuingia katika orodha ya wake za mfalme wa Eswatini na kama tujuavyo mfalme Yule huwa anachagua hasa.Tumpongeze Rais wetu kwa kweli” akasema Zari


“Natamani nimuone huyo Zandile.Ruby unaweza nionyesha picha zake? Akauliza Mathew na Ruby akaenda katika kompyuta yake akazitafuta picha za Zandile na kumuonyesha Mathew


“Mhh ! si mchezo.Kwa hapa mzee wetu alikuwa na haki ya kuvuka mipaka” akasema Mathew huku akitabasamu


“Ruby nataka kumfahamu kwa kina huyu Zandile Wepener.Nahitaji taarifa zake”




“Mathew ! akasema Ruby


“Ruby please.Nataka umchimbe nipate taarifa zake zote unazoweza kuzipata.Nina maana yangu kuzitaka taarifa hizo za Zandile”


“Kuna nini Mathew una hofu naye?


“Siwaamini sana wanawake wazuri kama huyu Zandile.Mara nyingi hutumika katika ujasusi”


“Unadhani Zandile anaweza kuwa jasusi? Akauliza Ruby


“Sina hakika bado lakini inawezekana.Tutafahamu pale tutakapofanya uchunguzi.Japokuwa tuna mambo mengi lakini hili nalo lina umuhimu sana.Sifahamu imetokeaje hadi Rais akajikuta mikononi mwa Zandile lakini tuliweke hilo kando tutaendelea nalo taratibu ” akasema Mathew


“Nilipoondoka asubuhi nilikwenda kuonana na mtu mmoja anaitwa Karimu au jina la kikazi Sinze.Huyu aliwahi kuwa mfanya biashara mkubwa wa dawa za kulevya na ni mimi niliyemshawishi aachane na biashara hiyo baada ya kunusurika kuuawa mara mbili kwa risasi.Kwa sasa ana duka lake kubwa la kuuza vipuri vya magari lakini bado ana watu wake katika mtandao wa biashara ya dawa za kulevya nimemuomba anisaidie kutafuta taarifa za hili kundi la Black Mafia.Ameniahidi kunisaidia kutafuta taarifa hizo na amenihakikishia hadi jioni ya leo atakuwa amezipata.Akifanikiwa atakuwa ametusaidia kwa kiasi kikubwa sana.Baada ya kutoka hapo nikaanza safari ya kuelekea kwa mdogo wake Adam Watwila lakini kabla sijafika huko ndipo nikapigiwa simu kwamba Rais ananihitaji”


“Tumuombee huyo


Karimu aweze kuzipata taarifa hizo kwani hawa jamaa nimewaogopa sana” akasema Zari


“Nini ulitaka kwenda kuzungumza na mdogo wake Adam Watwila? Akauliza Ruby


“Nilitaka nikampe taarifa za mahala tulikofikia.Nilitaka akafahamu kuwa sisi si waandishi wa habari bali ni wapelelezi na ninaamini angeweza kutoa ushirikiano na kama kuna kitu anakifahamu angeweza kutueleza” akasema Mathew


“Guys japokuwa tumeweza kupiga hatua kubwa ndani ya kipindi kifupi kiasi cha kuwapa hofu hawa jamaa lakini tumefika mahali tumekwama.Tumekutana na ukuta mkubwa hivyo lazima tutafute namna ya kutoka hapa tulipokwama.Nataka tupitie kwa umakini sana kila tulichokifanya toka tumeanza kuchuguza hili suala la Naomi Bambi na tuangale namna ya kusonga mbele wakati tunasubiri kupata taarifa za kundi la Black Mafia kutoka kwa Karim” akasema Mathew akachukua kalamu na kuelekea katika ubao mweupe


“Tuanzie katika chimbuko la jambo hili ambalo ni Naomi Bambi” akasema Mathew na kuandika Naomi Bambi ubaoni.


“Alipata ufadhili katika shule ya kimataifa na huko maisha yake yakabadilika hadi pale inapokuja kugundulika na wazazi wake kujulishwa.Baada tu ya maisha yake kufahamika ndipo mfululizo wa matukio ulipoanza” Mathew akachora mstari chini ya jina la Naomi


“Adam na mke wake


walikuwa wa kwanza kufariki ,akafuata Lidya,mbunge,na watu wengine wawili nimewasahau majina lakini nitawapa majina ya X na Y.Wote hawa walifariki dunia wakijaribu kuchunguza kuhusu Naomi Bambi” akanyamaza akautazama ubao ule halafu akasema


“Baada ya sisi kuingia rasmi katika uchunguzi tayari watu kadhaa wamepoteza maisha wakiwamo na watu wao na vifo hivi vyote vimetokea wakati hawa jamaa wakijaribu kuzuia kitu chochote kuhusiana na Naomi Bambi kisijulikane.Kuna kitu kimoja ambacho bado hatujakipatia muafaka na ambacho kimekuwa kinakula sana akili yangu. Jambo lenyewe ni kuhusiana na safari ya mchungaji Adam Watwila.Bado kuna kitu tunakikosa hapa” akasema


Mathew


“Adam aliondoka kwenda Morogoro siku ambayo mwanae wa pekee Zoe au Naomi alitoweka shuleni bila kujulikana mahala aliko.Bado kuna maswali ambayo hatujayapatia majibu mpaka sasa,japo kiongozi wake alitueleza kwamba Adam alikwenda Morogoro kwa shughuli za kichungaji.Tuliwahi kujadili hili na leo nataka tujadili tena.Tupate picha hii.mchungaji Adam anapokea taarifa nzito kama ile ya maisha ya Zoe pale shuleni,halafu ghafla mwanae anatoweka na hajulikani alikoelekea.Adam na mkewe wanaachana na zoezi la kumtafuta mtoto wao aliyetoweka na badala yake wanafunga safari kwenda Morogoro ambayo inadaiwa ni ya safari ya kichungaji.Naiamini sana akili yangu na katika hili inanikatalia kwamba hilo ni jambo lisilowezekana”


“Mathew uko sahihi.Sisi ambao hatumfahamu Zoe na wala hatuna mahusiano naye tunatetemeka mwili baada ya kupata taarifa za maisha yake, iweje mzazi wake ashindwe kutikiswa na taarifa hizo na anaamua kuachana na zoezi la kumtafuta anafunga safari kwenda Morogoro.Kweli haiingii akilini”akasema Zari “Nilisema tulipokuwa


tunajadili awali suala hili kwamba linawezekana katika filamu tu lakini katika uhalisia ni kitu kisichowezekana.Mimi ni mama na msinione niko hapa nanyi lakini sipati


usingizi,silali nikiwawaza wanangu japo wako sehemu salama ni vipi kwa wazazi wa Zoe ambao mtoto wao tena wa pekee ametoweka na hajulikani mahala alipo?Hawakuguswa kwa namna yoyote ile hadi wakaamua kuacha zoezi la kumtafuta na kufunga safari ya kuelekea Morogoro kwenye shughuli za kanisa? Akauliza Ruby


“Au yawezekana mchungaji Adam alipatwa na hasira kwa taarifa kuhusu maisha ya mwanae shuleni akakasirika na akaamua kuachana naye akaendelea na shughuli zake za kichungaji.Kama mzazi yawezekana alichukizwa na matendo yale na kuamua kumuacha akafundishwe na ulimwengu”akasema Zari “Bado nafsi yangu inakataa kabisa.Mimi pia ni mzazi nina watoto lakini hata kama mtoto amekuudhi vipi huwezi kumkatia tamaa na ikitokea ikawa hivyo basi hiyo ni hatua ya mwisho kabisa baada ya mzazi kufanya kila jitihada kumrekebisha mwanae bila mafanikio. Mchungaji Adam hata kama mambo aliyoelezwa kuhusu mwanae ni makubwa kiasi gani hakupaswa kukata tamaa.Ninakataa kabisa kwamba Adam alikasirika kuhusiana na kile alichoelezwa shuleni kwa Zoe na hivyo kuamua kumuacha.


Mkumbuke vile vile tulielezwa na mdogo wake Adam kwamba alipigiwa simu na kaka yake akielekea Morogoro akamwambia kwamba kuna jambo zito atakuja kumueleza atakaporudi. Hakuna jambo lingine alilotaka kumueleza mdogo wake zaidi ya suala hilo la mwanae Zoe.Hapa ninataka picha kwamba wakati anampigia simu mdogo wake alikuwa na haraka sana ya kuwahi akamilishe shughuli iliyompelekea huko kisha arejee kushughulikia suala la mwanae Zoe.Swali je kwa suala hili la kupotelewa na mwanae kulikuwa na ulazima wa kwenda Morogoro? Kwa nini asingetumwa mchungaji mwingine kwenda Morogoro na Adam akaachwa aendelee na zoezi gumu la kumtafuta mwanae aliyetoweka?Mathew akauliza


“Kweli hapo kuna ukakasi mkubwa” akasema Zari


“Nataka tuifahamu shughuli iliyompeleka Adam


Morogoro ilikuwa na umuhimu kiasi gani hadi ikashindwa kuahirishwa au akatumwa mtu mwingine.Majibu tutayapata katika kanisa alilokuwa anahudumu Adam.Ruby tafuta taarifa za kanisa hilo na tufahamu kuna wachungaji wangapi kisha tutafute mchungaji mmoja tumfuate tuzungumze naye naamini tunaweza tukapata kitu Fulani cha kutusaidia” akasema Mathew




Mkuu wa jeshi la polisi Yeremia Mwaipopo aliwasili katika ofisi za taasisi ya mama Bella kama alivyoombwa


“Ahsante sana Yeremia kwa kufika kwa haraka” akasema mama Bella


“Kuitwa na mke wa Rais si jambo dogo hivyo lazima uitike wito kwa haraka sana” akajibu Yeremia na wote wakacheka


“Yeremia karibu sana.Leo nimepata ugeni mzito nimetembelewa na vigogo hawa wa chama” akasema Mama Bella


“Ndiyo maana uliponiambia kwamba uko na wakubwa hawa nimefanya haraka zaidi ya kufika hapa” akasema Yeremia na wote wakaangua tena kicheko


“Yeremia tumekuita hapa kuna jambo la muhimu sana ambalo tunataka kuzungumza nawe.Ni jambo la muhimu lakini ni la siri mno na tumeamua kukushirikisha kwanza wewe kwa kuwa ninakufahamu naamini kile tutakachokizungumza hapa hakitavuja” akasema Bella


“Mama Bella ahsante kwa kuniamini na kuniita hapa kunishirikisha katika hilo jambo”


“Yeremia kama unakumbuka siku chache zilizopita alikamatwa mfanya biashara mmoja mkubwa wa dawa za kulevya na mauaji ambaye alitoroshwa na mpaka sasa hajulikani alipo.Kumekuwa na mambo mengi yakisemwa kuhusiana na jambo hili la Mathew Mulumbi kutoroshwa” akasema Bella na kunyamaza kidogo


“Leo mchana mzee Simba


akiwa katika ofisi yake alitumiwa ujumbe katika barua pepe na mtu asiyemfahamu na alipoifungua barua pepe hiyo alikutana na kitu cha ajabu sana ambacho sisi sote kimetustua mno” akasema Bella na kumpa maelekezo profesa Simona amuonyeshe IGP Yeremia zile picha za faragha za Rais alizotumiwa.Yeremia alipatwa na mstuko mkubwa sana akamtazama Bella “This is………..


“It’s him” akajibu Bella


“Is this real?akauliza Yeremia na Bella akatikisa kichwa.Yeremia akarudia tena kuzitazama zile picha


“Bado nashindwa kuamini kama hiki ninachokiona ni cha kweli”


“Sote tumepatwa na mstuko mkubwa kama uliokupata wewe na bado tunashangaa mpaka sasa lakini hizi ni picha halisi kabisa za Festus na hatujui zimepatikanaje”


“Ama kweli dunia ina mambo” akasema Yeremia


“Mtu aliyetuma hizi picha” akaendelea Bella


“Amesema anataka


kuzisambaza katika mitandao ya kijamii”


“Mungu wangu ! akasema Yeremia


“Ni nani hawa wanaotaka kufanya jambo la kipuuzi kama hili? Yeremia akauliza kwa ukali


“Yeremia hawa watu hawatanii na kweli watazisambaza hizo picha”


“I won’t let that happen ! akafoka Yeremia


“Hawa watu wanatakiwa wasakwe na wakamatwe haraka sana.Huyu ni Rais wa nchi huwezi ukaingilia faragha zake hata kidogo ! akaendelea kufoka


‘Yeremia hatuna haja wala muda wa kupambana na hawa watu.Kwa hivi sasa wao wameshika mpini hivyo tukifanya mzaha watatukata na tutaumia” akasema profesa Simon


“Mnataka tufanyaje?


“Wametoa sharti hawa jamaa kwamba hawatasambaza picha hizi endapo Rais atamkabidhi kwao Mathew Mulumbi”


“Mathew Mulumbi?


Akauliza Yeremia


“Ndiyo wanamtaka


Mathew Mulumbi”


“Kwa nini wanamtaka Mathew Mulumbi?


“Hawajasema ila hicho ndicho wanachokitaka ili wasizisambaze picha hizi.


“Hawa watu ni wajinga sana.Hawajui kama Mathew Mulumbi ametoroka na hajulikani alipo? Mimi ndiye mkuu wa jeshi la polisi na hadi sasa tunaendelea kumsaka na hatujafanikiwa kujua mahala alipo.Kwa nini wamfuate Rais na kumtaka awakabidhi mtu ambaye hajulikani alipo? Akauliza Yeremia


“Festus anajua alipo


Mathew Mulumbi is” akasema Bella


“What?


“Rais anafahamu mahala alipo Mathew Mulumbi” akarudia tena Bella “No! That’s not true !


“It’s true” akasema profesa Simon


“Mathew Mulumbi


alitoroshwa na genge la wafanya bioashara wenzake wa dawa za kulevya na Rais Festus hafahamu chochote naye anatutegemea sisi jeshi la polisi kupata taarifa za mahala alipo Mathew Mulumbi”


“Nimezungumza naye na akakiri kwamba kutoroshwa kwa Mathew ulikuwa ni mpango maalum na yeye alifahamu kila kitu”


“Rais Festus amesema hivyo?


“Ndiyo.Rais amekiri hivyo”




“That’s impossible”


“Yeremia anachokisema profesa Simon ni kitu cha kweli kabisa.Baada ya kupata picha hizo alimfuata akamuonyesha na akakiri kufahamu kila kitu kuhusu mpango ule wa kumteka Mathew Mulumbi” akasema


Bella


“Kama anafahamu


alipo,amekubali kumtoa Mathew Mulumbi kwa hao jamaa? Akauliza Yeremia


“Hapana amekataa na ndiyo maana tumekutana hapa.Hao jamaa wametoa muda na kama Rais asipotimiza matakwa yao ndani ya muda walioutoa basi watasambaza picha hizi” “Ni akina nani hao watu?


“Hakuna


anayewafahamu.Yeremia tumekuita hapa kukushirikisha katika mpango wetu.Rais Festus hii si akili yake ya kawaida kukubali eti picha zake za faragha zikasambazwa.Endapo picha hizi zitasambzwa kwanza itakuwa ni aibu kubwa sana kwa familia.Mimi na watoto tutaumia mno,sijui tutaziweka wazpi sura zetu.Jambo la pili


ni katika


chama.Wanamtegemea Festus awavushe katika uchaguzi mkuu ujao hivyo kama picha hizi zikisambaa litakuwa ni pigo kubwa sana kwao.Hizo ni athari chache tu zitakazotokea endapo picha hizi zitasambazwa hivyo mimi na wazee wangu hapa tumekaa tumejadili na kukubaliana kwamba tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha picha hizo hazisambazwi”


“Mtazuiaje picha hizo zisisambazwe wakati Rais amekwisha kataa kutoa ushirikiano kwa hao jamaa wenye hizo picha? Yeremia akauliza


“Tumekubaliana na hawa wazee wangu kwamba


tutafanya kila tuwezalo kuwapa watu hao kitu wanachokihitaji.Tayari nimezungumza na watu hao na nimewaomba wasizisambaze picha hizo kwani maombi yao yanashughulikiwa na wamenielewa wameahidi kuogeza muda”


“Umewaahidi kuwapatia


Mathew Mulumbi.Do you know where he is? Akauliza Yeremia


“Sifahamu aliko Mathew Mulumbi lakini tutamtafuta na kumpata”


“Bella sishauri jambo hilo lifanyike.Hawa watu wanatakiwa wasakwe na wapatikane wafunzwe adabu namna ya kuheshimu viongozi! Akafka Yeremia


“Yeremia hawa watu ni mtandao mpana na hata kama ukimkamata mmoja wao au wawili au hata kumi lakini bado watazisambaza picha za Rais hivyo basi katika hili lazima tukubali tumeshindwa.Just for once let them win” akasema Bella na


kumtazama Yeremia ambaye


alitikisa kichwa


“Najua viongozi wengi hili la kukubali kushindwa hamlipendi lakini lazima lifanyike ili kumnusuru Rais wetu na aibu hii kubwa.Lazima lifanyike ili kukinurusu chama na aibu hii kubwa.Yeremia hatuwezi kukubali picha hizi zikasambazwa.I swear I’ll kill myself kama picha hizi zitaachwa zisambae.Siwezi kuibeba aibu hii kubwa.As your friend I need your help ! akasema Bella na Yeremia aliposikia neno la kujiua akastuka akamtazama Bella halafu akauliza


“Bella huna haja ya kufika huko katika hatua ya kujitoa uhai.Nitashirikiana nanyi japo nafahamu ni hatari sana kufanya jambo hili kwa siri bila Rais kufahamu” akasema Yeremia


“Ahsante


Yeremia.Tunalazimika kufanya hivi kwa sababu Festus haoni kama kuna tatizo”


“Fine.Nini mnataka nifanye kwa upande wangu? Akauliza Yeremia


“Tunafahamu wewe ni mtu wa karibu sana na Rais na tunaamini utakuwa unafahamu mahala aliko Mathew Mulumbi.Kama unafahamu jambo hilo tusaidie tafadhali tumpate huyu mtu” akasema Bella


“Naomba nikiri kwamba


Rais alinipa maelekezo ya kuhakikisha Mathew Mulumbi anahamishwa kutoka polisi na kupelekwa katika gereza la Uwangwa lakini kabla hajafikishwa huko akatoroshwa.Ni kutoka kwenu leo nimesikia kwamba Rais alikuwa anafahamu kuhusu mpango ule wa kumteka Mathew.Nakiri kwenu wazee wangu na mama Bella kwamba sifahamu chochote kuhusu mpango huo na sifahamu mahala alipo Mathew.Rais hajanishirikisha katika mpango huo” akasema


Yeremia


“Lakini kwa kuwa wewe ni mtu wa karibu na Rais tunaomba utusaidie kutafuta taarifa hizi za mahala alipo


Mathew Mulumbi kwani tukichelewa zaidi ya muda waliotoa,hawa jamaa watasambaza hizi picha” akasema mzee Titus


“Bella wewe uko karibu na Rais kwa nini usimshawishi akakubali kumtoa Mathew Mulumbi? Akauliza Yeremia


“Sitaki ajue kama tayari nimelifahamu jambo hili na atataka kujua nimelifahamu vipi ndiyo maana huu ni mpango wa siri sana tunaufanya” akasema Bella


“Nimekuelewa Bella lakini nina ushauri ambao unaweza ukatusaidia katika jambo hili.Kuna idara moja inaitwa SNSA.Hii ni idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi ambayo iko chini ya Rais.Ninaamini lazima Rais ameitumia idara hii katika huu mpango wa kumtorosha Mathew Mulumbi.Endapo tukifanikiwa kufahamu mahala zilipo ofisi za idara hii basi


tutakuwa tumempata Mathew Mulumbi.Nina uhakika mkubwa sana Mathew yuko SNSA.Kitu kingine kinachoweza kutusaidia kumpata Mathew Mulumbi ni mke wa Rais mstaafu Dr Fabian anaitwa Ruby.Huyu naye ametoweka na hatujui yuko wapi.Huyu Ruby inasemekana amekuwa ni mtu wa karibu sana na Mathew Mulumbi hivyo kama tukimpata tuna uhakika mkubwa sana wa kumpata Mathew.Vile vile huyu Ruby amewahi kuwa mkurugenzi wa SNSA hivyo ninalazimika kuamini kwamba hata naye amehusika katika mpango huu na wote wamejificha SNSA” akasema Yeremia





“Ushauri wako ni mzuri sana Yeremia.Niachieni jambo hilo nitalifanyia kazi kuzitafuta ofisi za idara hiyo.Nina uhakika mkubwa hadi kesho asubuhi ninaweza kuwa nimekwisha pata majibu”


“Jitahidi uweze kuyapata majibu hayo mapema .Lakini hao jamaa wataweza kukubali kuongeza muda zaidi wakati jambo hili linashughulikiwa? Akauliza Yeremia


“Nitazugumza nao na kuwaomba wasubiri ombi lao tunalifanyia kazi.Nitatumia


kila aina ya ushawishi ili wanielewe.You know me”akasema Bella


“Kuna swali najiuliza.Rais tayari amekwisha jiandaa kwa picha zake kusambazwa je ni vipi pale atakapoona kimya na picha zake hazisambazwi?akauliza


Yeremia


“Siri hii itabaki kwa sisi watu wanne tu.Hakuna kumweleza mtu mwingine yeyote na mzee Simba nakuomba uzifute kabisa picha hizo katika kompyuta yako.Rais atashangaa kumekuwa kimya na hatajua nini kimetokea.Hata kama itatokea akagundua huko mbeleni tulichkifanya lakini tayari suala litakuwa limemalizika” akasema Bella


Waliendelea na mazungumzo na kikao kilipomalizika wakatawanyika halafu Bella akachukua simu na kumpigia nabii Kasiano


“Mama Bella” akasema Kasiano


“Kasiano mambo


yanakwenda vizuri japo mtu wetu amekuwa kiburi na hataki kukubaliana na


alichotakiwa kukifanya lakini kwa sasa mambo yanakwenda vizuri” akasema akasema Bella na kumueleza kile kilichotokea na mahala alikofikia




**************


Rais Festus alirejea ikulu na moja kwa moja akaenda kupumzika hakutaka kuendelea na kazi.Kichwa chake kilijaa mawazo.Mara tu alipoingia chumbani kwake akaivua tai na kuitupa chini kwa hasira


“Ndani ya saa chache kutoka sasa picha zangu zitasambaa mitaani,itakuwa ni habari inayoongelewa kila kona.Dah ! aibu kubwa mno hii.Lakini najiuliza wale jamaa wamewezaje kuzipata picha zile? Wamezipigaje? Je walitega kamera za siri na wakaweza kupata zile picha?Wali…aagh ! akawaza na kukaa kitandani


“Hii ni aibu ambayo nitaishi nayo hadi kifo changu lakini ni afadhali nikaishi kwa aibu kuliko kukubaliana na wale washenzi.Naamini Mathew Mulumbi na wenzake watafanya kila wawezalo kuhakikisha wahuni hawa wanapatikana na kufikishwa mbele ya sheria.Lakini hata kama wakipatikana bado aibu yangu itaendelea kuwepo.Dah ! Kuna nyakati ninajuta kwa nini nilianzisha mahusiano na Zandile.Kama nisingekuwa naye haya yote yasingetokea” akawaza na kutazama saa yake.Fulana aliyoivaa ndani ililoa jasho


**************


Taratibu jua lilizama na kiza kikaanza kuchukua nafasi.Rais Festus alikuwa amejifungia chumbani na hakutaka kusumbuliwa na mtu yeyote.Chumbani alikuwa na chupa ya mvinyo mkali akinywa taratibu


Mshale wa saa


ulipoonyesha ni saa moja kamili za jioni hofu ikamzidi.


“Naamini huko mtandaoni tayari kumewaka moto.Hivi sasa tayari picha zangu zimekwisha sambazwa.Sijui nitapita wapi kujificha na aibu hii” akawaza Rais Festus


“Lakini nitaendelea kuhofu hadi lini?Nilikubali mimi mwenyewe wasambaze picha zangu hivyo lazima


nikabiliane na hili jambo.Ngoja kwanza niwasiliane na mkurugenzi wangu wa habari nimuulize kama kuna chochote kimerushwa mtandaoni” akawaza na kuiwasha simu yake aliyokuwa ameizima akampigia Gidion Benson mkurugenzi wake wa habari


“Gidion nataka kufahamu kuna habari yoyote mtandaoni au picha imetoka jioni ya leo kunihusu mimi? Akauliza Rais Festus


“Nimekuwa nafuatilia kwa karibu sana mijadala mitandaoni lakini kubwa mpaka sasa ni kile ulichokizungumza katika kipindi cha Mchaka mchaka.Jioni ya leo hakuna habari nyingine mpya wala picha yoyote”


“Are you sure? Akauliza Rais Festus


“Ndiyo nina uhakika mzee”


“Gidion naomba tumia dakika chache kupita mitandaoni tena kujiridhisha kama hakuna habari yoyote iliyorushwa jioni ya leo ikinihusu mimi.Ndani ya dakika chache unipe majibu” akasema Rais Festus na kukata simu


“Namuamini sana Gidion


lakini ngoja kwanza ajiridhishe kama kweli hakuna picha zilizorushwa mtandaoni jioni ya leo” akawaza Rais Festus


Zilipita dakika kumi Gidion akampigia simu Rais na kumpa mrejesho kwamba hakuna habari yoyote mpya mtandaoni inayomuhusu yeye zaidi ya ile kauli yake ya kukiri kwamba ana mtoto wa nje.Rais festus akashusha pumzi na kwenda kuketi sofani


“Haya mbona maajabu.Kwa nini hawajarusha zile picha hadi muda huu wakati muda waliokuwa wametoa umekwisha pita? Au wamebadili mawazo? Lakini nisijipe moyo kwanza kwani muda bado.Ngoja nisubiri hadi itakapofika saa sita za usiku ndipo nitakapoamini picha hazijarushwa lakini hata kama hazitarushwa leo siyo kwamba mambo yamekwisha vita ndiyo kwanza imeanza.Ngoja niwasiliane na katibu mkuu mzee Simba nimuulize kama amewasiliana tena na wale jamaa” akawaza Festus na kumpigia simu profesa Simon lakini simu yake haikuwa inapatikana.Akajaribu mara ya pili na ya tatu lakini simu yake haikupatikana.


“Hii inashangaza sijawahi kumpigia mzee Simba simu nikamkosa.Nini kimetokea leo? Akawaza


“Ngoja niendelee kusubiri yawezekana baadae akapatikana” akawaza na kuinua glasi ya mvinyo ***************




Kendrick aliingia kwa kasi katika chumba ambako akina Mathew walikuwa na majadiliano kuhusiana na mahala wanakotarajia kwenda usiku ule


“Kendrick kuna nini? Akauliza Zari ambaye alistushwa na ujio ule wa Kendrick


“Mathew come quick you


have to see this ! akasema Kendrick wakatoka haraka wakaelekea katika chumba cha mapumziko ambako makomando walikuwa wanatazama taarifa ya habari


“Kuna nini Kendrick? Akauliza Mathew na muhtasari wa habari ukaisha ikaanza habari kamili


“Watu wasiojulikana alasiri ya leo wamevamia duka la kuuza vipuri vya magari na kuuwa watu sita akiwemo mmiliki wa duka hilo aliyefahamika kama


Karim Hussein”


Mathew alihisi kama nyundo imetua kichwani kwake baada ya kuitazama habari ile.


“Mimi ni sababu ya vifo hivi ! akasema Mathew


“Huyu ndiye mtu uliyemfuata ukamuomba


akusaidie kutafuta taarifa za Black Mafia? Ruby akauliza


“Ndiyo”


“Dah ! akasema Zari


“Wamemgundua alikuwa anawachunguza hivyo wakaamua kummaliza yeye na watu wake.Imeniumiza sana” akasema Mathew na kutoka katika kile chumba cha mapumziko akarejea katika ofisi yao.


“Mathew tunaendelea na mipango yetu? Akauliza Ruby


“Ndiyo tunaendelea na mpango yetu kama tulivyoipanga.Haya yanayotokea hayawezi kutukatisha tamaa.Tunakwenda kuonana na mchungaji Lukas” akasema


Mathew


Mchana wa siku ile


Mathew alimpa maelekezo Ruby ya kutafuta taarifa za kanisa kubwa la injili ya wokovu na katika taarifa za wachungaji wa kanisa hilo Mathew akachagua wamtafute mchungaji Lukas kwani alionekana ni kijana zaidi kuliko wengine ili wapate taarifa kuhusiana na mchungaji Adam.Ruby kama kawaida yake alifanikiwa kufuatilia na kufahamu mahala anakoishi Lucas


Mathew hakutaka kupoteza tena muda akamtaka Zari waondoke kuelekea kwa mchungaji Lucas huku timu ya makomando ikiwa tayari kuwafuatilia kwa nyuma kuhakikish wanakuwa salama


“Ruby endelea kufuatilia kama wale jamaa wataachia picha za Rais kwani muda ambao waliutoa umekwisha pita.Kama kuna chochote


utakipata utatujulisha” akasema Mathe


“Mathew please take care” akasema Ruby


“I will” akajibu Mathew wakati akiufunga mlango wa gari wakaondoka


“Hawa watu wanazidi


kuleta hofu.Kila tunapopiga hatua wanaturejesha nyuma zaidi.Kuna nyakati Napata hofu kubwa sana kwa namna hawa jamaa wanavyoendesha


mambo yao lakini kila ninapomtazama Mathew Mulumbi ninapata matumaini.Pamoja na kunusurika mara kadhaa kuuawa lakini Mathew hajatetereka.Bado anaendelea kupambana”akawaza Ruby baada ya akina Mathew kuondoka




Ilipata saa mbili kasoro 

dakika kumi na nane akina 

Mathew walipowasili katika 

makazi ya mchungaji 

Lucas.Kabla hawajashuka 

garini wakataka kupata 

uhakika kutoka kwa 

makomando kama kuna hatari 

yoyote nyuma yao lakini 

hakukuwa na hatari yoyote hivyo wakashuka garini na 

kwenda getini Mathew 

akagonga na baada ya dakika 

chache geti likafunguliwa 

akajitokeza kijana mmoja 

 “Tumemkuta mchungaji 

Lucas? Akauliza Mathew 

 “Ndiyo yuko 

ndani.Karibuni sana” Yule 

kijana akawakaribisha kwa 

adabu akawafungulia geti 

wakaingiza gari 

 Walikaribishwa sebuleni 

na mke wa mchungaji Lucas 

akafika akawasalimu kwa 

adabu na kuwaomba wamsubiri mume wake kwa 

dakika chache alikuwa 

anamalizia 

maombi.Waliendelea 

kutazama mahubiri ya nabii 

mkuu Kasiano kupitia kituo 

cha televisheni cha kanisa la 

injili ya wokovu. 

 Wakati wakiendelea 

kutazama mahubiri,akatokea 

mchungaji Lucas wakasimama 

na kumsalimu 

 “Karibuni sana wapendwa” 

akasema mchungaji Lucas 

 “Ahsante sana”  “Nimechelewa nilikuwa 

kwenye maombi na 

nilipomaliza nikaambiwa kuna 

wageni wananisubiri” 

 “Utatusamehe mchungaji 

Lucas kwa kuja muda huu na 

vile vile kuja bila 

taarifa”akasema Mathew 

 “Msihofu ndugu 

zangu.Kuweni huru.Nyumbani 

kwangu ni mahala pa huduma 

muda wote bila kujali ni usiku 

au ni mchana.Karibuni 

niwasaidie” 

 “Baba mchungaji sisi ni 

ndugu wa mchungaji Adam Watwila.Mimi naitwa Justin 

na huyu hapa ni mke wangu 

Linah sote tunaishi nje ya 

nchi”akasema Mathew na Zari 

akatabasamu 

 “Ouh karibuni 

sana.Nimefurahi 

kuwaona.Mchungaji Adam 

alikuwa anatumika katika 

kanisa letu na ni mmoja wa 

wachungaji ambaye alipendwa 

na kila mtu.Ameacha pengo 

kubwa” akasema mchungaji 

Lucas 

 “Kuna jambo ambalo 

mpaka leo hii bado hatujapata majibu ndiyo maana tumekuja 

hapa kwako utusaidie kama 

kuna kitu unaweza 

ukakifahamu”akasema 

Mathew 

 “Karibuni” 

 “Mchungaji Adam alipata 

ajali wakati akielekea 

Morogoro yeye na mke 

wake.Mpaka leo hatufahamu 

Morogoro alikwenda kufuata 

nini? Tumeambiwa kwamba 

safari hiyo ilikuwa ya ghafla 

sana.Je unaweza ukafahamu 

Adam na mkewe walikuwa 

wanafuata nini Morogoro? Tusaidie tafdhali kama kuna 

chochote unakifahamu” 

akasema 

 “Kwa kweli hata mimi 

sifahamu sababu gani 

iliyomfanya afunge safari ya 

kwenda Morogoro.Ilikuwa ni 

safari ya ghafla na hata sisi 

hatukujua kama ameelekea 

Morogoro hadi pale tulipopata 

taarifa kwamba amepata ajali 

na kufariki.Tulistuka kwa 

sababu si kawaida yake 

kuondoka bila kuaga 

wenzake.Kama anasafari nje 

ya mkoa hutuaga sote lakini 

siku ile aliondoka bila kuaga mtu yeyote. Ninachokumbuka 

siku ile tukiwa tunaendelea na 

huduma mbali mbali pale 

kanisani tuliitwa na nabii 

mkuu tukashiriki 

maombi.Mtoto wa mchungaji 

Adam alikuwa ametoweka 

shuleni na hakujulikana 

mahala alipo.Baadhi ya 

wachungaji tuliokuwa karibu 

pamoja na waumini wachache 

tukaungana tukafanya maombi 

na wakati tukiendelea kuomba 

nabii mkuu akatuomba 

tumshukuru Mungu kwani 

wakati tukiomba Mungu 

alimfunulia mahala alipomtoto aliyepotea.Baada ya 

hapo Adam na mke wake 

wakaelekea katika ofisi ya 

nabii na sisi tukaendelea na 

shughuli zetu nyingine.Sikujua 

kama Adam aliamua kwenda 

Morogoro baada ya hapo” 

 “Dah ! Ahsante sana 

mchungaji kwa taarifa hii.Je 

hakukuwa na shughuli yoyote 

ya kikanisa ambayo ilimuhitaji 

mchungaji Adam huko 

Morogoro? Akauliza Mathew 

na mchungaji Adam 

akaonekana kutafakari halafu 

akasema  “Sikumbuki kama 

kulikuwa na shughuli yoyote 

ya kikanisa ambayo 

ilimlaz.aaagh ! Ghafla 

ukasikika mpasuko wa kioo na 

mchungaji Adam akatoa 

mguno 

 “Mchungaji ! akaita 

Mathew na kuinuka kutaka 

kumsogelea 

 “Aaaaggh ! mchungaji 

Lucas akatoa mguno kwa mara 

ya pili na michirizi ya damu 

ikaonekana kifuani.Akili ya 

Mathew ikafanya kazi haraka 

haraka akaruka kama mshale na kumrukia Zari aliyekuwa 

amekaa katika sofa karibu na 

mchungaji Lucas na 

kumkinga.Sekunde chache 

baadae mlango ukapigwa teke 

na makomando waliokuwa 

wakiwafuatilia akina Mathew 

wakaingia. 

 “Madam Zari are you 

okay? Akauliza Kendrick 

 “I’m okay.What happened? 

Akauliza Zari 

“Jamaa wanne walikuja 

kwa kasi na piki piki mbili na 

wawili wakaingia ndani haraka 

na kwa namna walivyoingia ndani tulihisi kuna jambo 

tukaja haraka na tayari jamaa 

walikwisha maliza kile 

wallichokuja kukifanya 

wakaruka ukuta na 

kukimbia”akasema Kendrick 

na kumfuata mchungaji Lucas 

lakini tayari alikwisha fariki 

 Zari aliyekuwa amekingwa 

na Mathew akahisi maji maji 

yakimdondokea akastuka 

baada ya kusikia Mathew 

akitoa mguno wa maumivu 

 “Mathew ! akaita Zari 

 “Mathew !! akaita Zari na 

Mathew akajaribu kuinuka lakini akaanguka ndipo wote 

waliokuwepo pale sebuleni 

wakapatwa na mstuko 

mkubwa.Mathew alikuwa 

anavuja damu alikuwa 

amepigwa risasi. 

 “Mathew umepigwa risasi ! 

akasema Zari na kuwaita watu 

wake 

 “Cameras ! akasema 

Mathew 

 “Mathew tunakupeleka 

hospitali ! You’ll be fine” 

akasema Zari huku 

akitetemeka  “Find th….th..t …” Mathew 

akataka kusema kitu 

akashindwa 

 “Guys we’re taking him to 

SNSA hospital right now ! 

akaelekeza Zari na Mathew 

akainuliwa akakimbizwa 

garini.Wakati Mathew 

akiingizwa garini komando 

mmoja akamfuata Zari 

 “Mkurugenzi familia 

nzima wameuawa.Mmoja 

alikuwa upande wa mbele na 

mwingine upande wa nyuma. 

Wauaji walitumia bastora 

zenye viwambo vya kuzuia sauti hivyo wakaweza kuua 

kimya kimya tena kwa haraka 

sana ! 

 “Mungu wangu ! akasema 

Zari huku mwili ukimtetemeka 

 “Tunasubiri maelekezo 

yako mkurugenzi” 

 “Let’s get out of here now ! 

tunaelekea SNSA.Make sure 

no one is following us ! 

akaelekeza Zari na kuingia 

garini kisha wakaondoka kwa 

kasi kubwa kuelekea SNSA. 

 “Mathew ! Mathew ! akaita 

Zari ambaye macho  yake  yalifunikiwa na 

machozi.Mathew akafumbua 

macho na kusema 

 “Cameras…” 

 “Kamera zipi Mathew? 

Akauliza Zari 

 “Find..if..t.t.ther..e is 

hidden cameras ! akasema 

Mathew na kushindwa 

kuendelea fahamu zikampotea 

 “Mathew be strong we’re 

taking you to hospital ! akalia 

Zari 

 “Mathew please ! Zari 

akaendelea kulia  “Drive faster !! Zari 

akamuelekeza dereva 

 “Ee Mungu nakuomba 

usimchukue Mathew kwa 

sasa.Bado tunamuhitaji mno ! 

akaomba Zari huku machozi 

yakiendelea 

kumporomoka.Dereva wa gari 

lile aliendesha gari kama mtu 

asiye na akili nzuri na 

ilimlazimu kuvunja hadi sheria 

za barabarani pale 

alipoendelea na safari wakati 

taa za barabarani zilipomtaka 

asimame na almanusura 

asababishe ajali kubwa lakini 

kwa uhodari wa komando Yule aliweza kuikwepa ajali hiyo na 

safari ikaendelea. 

************** 

 Katika ofisi kuu SNSA 

madaktari tayari 

walikwishapewa taarifa na Zari 

hivyo walikwisha fanya 

maandalizi na walikuwa tayari 

kumpokea mgonjwa .Mara tu 

gari lilipofika Mathew 

akashushwa haraka akawekwa 

katika kitanda akawekewa 

kifaa cha kumsaidia kupumua akakimizwa ndani.Zari 

hakubaki nyuma aliambatana 

na madaktari huku 

akiwasisistiza kufanya kila 

linalowezekana kuokoa maisha 

ya Mathew Mulumbi. 

 “Mkurugenzi tunafanya 

kila tutakachoweza kuokoa 

maisha yake ! akasema Dr 

Fred wakati wakimuingiza 

Mathew katika chumba cha 

mionzi ambako walitumia 

mashine ya X Ray na kuziona 

risasi tatu.Mbili zikiwa 

tumboni na moja ikiwa katika 

kalio la upande wa kulia.Mashine ya kuonyesha 

mgandamizo wa damu ilianza 

kutoa mlio kuonyesha 

mgandamizo wa damu 

unashuka.Madaktari 

wakapasua sehemu katika 

tumbo na damu ikamwagika 

wakaingiza mpira Fulani na 

mashine ikaacha kutoa mlio 

ule.Kulikuwa na heka heka 

katika hospitali ile ya 

SNSA.Mathew akapelekwa 

katika mashine nyingine ya 

mionzi kwa ajili ya 

kuchunguzwa zaidi halafu 

akaingizwa katika chumba cha 

upasuaji.  “Mkurugenzi tunakuomba 

usubiri nje tafadhali” akasema 

DrFred na Zari akatoka ndani 

ya kile chumba akakutana na 

msaidizi wake Lutengano 

Mwaijumbe 

 “Mkurugenzi twende 

ukapumzike tafadhali waache 

madaktari waendelee na kazi 

yao ya kuokoa maisha ya huyu 

mtu ! akasema Lutengano 

 “No Lute.I need to be here 

! The man in there, took a 

bullet for me ! He saved my 

life.Mimi ndiye niliyekuwa 

natakiwa kuwemo ndani ya hiki chumba sasa hivi au 

pengine ningekwisha poteza 

maisha.I need to be here right 

now ! akasema Zari na kulia 

kwa kwikwi. 

 “It’s okay madam.Tuko 

pamoja nawe na mgonjwa 

atapona.Hata hivyo madam 

Zari itakuwa vyema wakati 

upasuaji ukiendelea ukaenda 

kunawa na kubadili 

mavazi.Umechafuka damu” 

akasema Lutengano na 

kumshika mkono Zari 

wakaelekea ofisini kwa Zari 

ambako kuna kabati lake la 

nguo kwa ajili ya dharura.Shughuli zilisimama 

kwa muda pale SNSA wote 

waliokuwepo usiku ule 

walistushwa sana na hali 

aliyokuwa nayo 

mkurugenzi.Zari hakutaka 

mazungumzo akamtaka 

Lutengano amuache 

mwenyewe kwa 

muda.Akajitazama namna 

alivyokuwa amechafuka damu 

akajikuta akipiga magoti na 

kuanza kulia 

 “Ee Mungu damu hii 

katika mavazi yangu 

imemwagika kwa ajili 

yangu.Baba namkabidhi Mathew Mulumbi mikononi 

mwako.Wewe ndiye 

unayefahamu umuhimu wake 

kwetu na kwa nchi 

pia,ninayaweka maisha yake 

kwako mfalme mwenye kutoa 

na kutwaa kwa muda 

uutakao.Ninakuomba baba 

sikia maombi yangu kiumbe 

dhaifu ikupendeze Mathew 

Mulumbi abaki nasi ili tuweze 

kuimaliza kazi tuliyoianza ya 

kupambana na wahalifu hawa 

hatari wenye kutoa roho za 

watu wako bila huruma.Baba 

ninaomba kwa machozi…” Zari 

akashindwa kuendelea na maombi akajikuta akikaa chini 

na kuendelea kulia. 

 “Kwa nini Mathew? Kwa 

nini yeye ndiye apatwe na hili 

janga? Kwa nini muda huu 

ambao anahitajika mno? 

Akawaza Zari akainuka na 

kuelekea bafuni.Ofisi yake 

ilikuwa inajitegemea kila kitu 

kuanzia choo hadi bafu 

akajitazama katika kioo na 

taratibu akaanza kuvua mavazi 

yake 

 “Zimeonekana risasi tatu 

mwilini mwa Mathew na zile 

zote zilinilenga mimi.Nimezoea kuona katika 

filamu namna watu 

wanavyojitoa maisha yao kwa 

ajili ya kuwakinga wengine na 

risasi lakini leo nimeshuhudia 

kwa macho yangu namna 

Mathew alivyofanikiwa 

kuniokoa na kupigwa yeye 

risasi.Nina deni kubwa kwa 

mtu huyu ambaye ameniokoa 

zaidi ya mara 

moja.Nakumbuka katika ule 

mlipuko wa bomu kule 

nyumbani kwa Zawadi 

alinikinga pia na yeye ndiye 

aliyeumia.Mathew ni kiumbe 

wa aina yake nitafanya kila niwezalo kuhakikisha anapona 

! akawaza Zari akaoga haraka 

haraka na kubadili mavazi 

 “Taarifa hii itamstua mno 

Ruby lakini hakuna namna 

lazima nimjulishe” akawaza 

Zari na kuchukua simu 

akampigia Ruby 

 “Zari mmekuwa kimya 

sana hadi nimeanza kupatwa 

na wasi wasi.Mnaendeleaje 

huko? Akauliza Ruby na Zari 

akavuta pumzi ndefu na 

kubaki kimya 

 “Zari ! akaita Ruby  “Zari is everything okay ? 

akauliza Ruby na Zari 

akasikika akilia kwa kwikwi 

 “It’s Mathew” akasema 

Zari 

 “Mathew ! oh my God ! 

Nini kimetokea? Akauliza 

Ruby kwa wasiwasi 

 “Amepigwa risasi ! 

akasema Zari na ukimya 

ukatawala.Baada ya sekunde 

kama hamsini hivi Zari akaita 

 “Ruby are you there? 

Akauliza Zari  “Zari please tell me this is 

not a joke ! 

 “Ni kweli Ruby” akajibu 

Zari zikapita sekunde kadhaa 

za ukimya halafu Ruby 

akauliza 

 “Zari niambie ukweli bila 

kunificha.Is he dead ? akauliza 

Ruby 

 “Hapana lakini hali yake si 

nzuri.Amepigwa risasi tatu 

mbili tumboni na moja katika 

kalio.Madaktari wanaendelea 

na upasuaji hivi sasa hapa 

SNSA”  “I’m coming there ! 

akasema Ruby na kukata simu. 

 “Kwa namna Ruby 

anavyompenda Mathew 

Mulumbi taarifa hii itakuwa 

imemstua mno.Mathew ndiye 

kinara wetu katika……” Ruby 

akatolewa mawazoni baada ya 

mlango 

kugongwa.Akamruhusu 

mgongaji kuingia ndani 

alikuwa ni Lutengano 

 “Unaendeleaje 

mkurugenzi” akasema 

Lutengano msaidizi wa Zari  “I don’t know Lute ! 

akajibu Zari 

 “Kitu gani hasa kimetokea 

mkurugenzi? Yule mgonjwa ni 

nani? 

 “Not now Lute.Nitakueleza 

kila kitu lakini si sasa 

hivi.Bado niko katika mstuko 

mkubwa.Nimenusurika 

kuuawa usiku huu na Yule mtu 

kule ndani ndiye ameokoa 

maisha yangu.Pale 

nitakapokuwa katika nafasi 

nzuri nitakueleza”akasema 

Zari  “Mkurugenzi nimeuliza 

kutaka kufahamu ili kama 

kuna msaada wowote na mimi 

nisaidie” akasema Lutengano 

 “Keep everyone busy.Sitaki 

watu waelekeze akili zao kwa 

Yule mgonjwa kule.Pale 

nitakapokuwa na la 

kuwaambia nitawaambia 

lakini kwa sasa kila mmoja 

aendelee na kazi zake” aksema 

Zari na Lutengano akatoka. 

 “Naona kama kifo 

kinaninyemelea.Kwa siku hizi 

chache kama si kuwa karibu na 

Mathew ningekwisha poteza maisha.I don’t want to die this 

young” akawaza Zari na kutoka 

ofisini kwake akaelekea 

upande wa hospitali ambako 

upasuaji ulikuwa unaendelea 

**************** 

 Gidion Benson 

mkurugenzi wa habari wa Rais 

alimjulisha Rais Festus 

kwamba amepitia mitandaoni 

hakukuwa na habari yoyote 

mpya ya kumuhusu yeye. “Ahsante sana Gidion 

endelea kufuatilia na kama 

ukipata habari yoyote mpya 

kunihusu mimi nijulishe mara 

moja tafadhali.One more thing 

nataka ufanyike uchunguzi 

kwa magazeti yote ambayo 

yatatoka kesho kama kuna 

habari yoyote mbaya 

inayonihusu mimi ukiacha ile 

ya mtoto wa nje” akasema Rais 

Festus na kukata simu 

 “Nini kimetokea? Wale 

jamaa walitoa muda na 

umekwisha pita lakini 

hawajasambaza zile picha 

kama walivyokuwa wametishia.Yawezekana 

wameogopa kufanya hivyo au 

kuna kitu wanataka 

kukifanya.Hawa watu huwa 

hawakubali kushindwa kirahisi 

lazima kuna jambo wanataka 

kulifanya” akawaza Rais Festus 

akachukua simu yake na 

kuzitafuta namba za mzee 

Simba akampigia lakini simu 

yake haikuwa ikipatikana 

 “Hii ni ajabu.Mzee Simba 

hajawahi kuzima simu hata 

mara moja.Yeye ni katibu 

mkuu wa chama na muda wote 

simu yake iko hewani.Nini kimetokea leo? Akajiuliza 

Festus. 

 “Au kuna jambo baya 

limetokea .Au yawezekana 

akawa hata ametekwa na mimi 

sifahamu” akawaza na 

kumpigia simu makamu 

mwenyekiti mzee Titus 

 “Mheshimiwa mwenyekiti” 

akasema mzee Titus 

 “Mzee Titus ninataka 

kuzungumza na katibu mkuu 

lakini hapatikani simuni na si 

kawaida yake.Kuna tatizo 

lolote?  “Nimewasiliana naye mida 

ya saa kumi na mbili za jioni 

tukazungumza na hakuwa na 

tatizo lolote” 

 “Mzee Titus ulipowasiliana 

naye kuna chochote 

alikueleza? 

 “Kuna kazi nilimpa 

anisaidie kuifanya na ndipo 

akanipigia kunipa mrejesho wa 

ile kazi niliyomtuma” 

 “Ahsante mzee Titus” 

akasema Rais Festus na kukata 

simu “Huyu mzee Simba kwa 

nini hapatikani simuni? 

Akaendelea kujiuliza 

 “Nahisi labda amezima 

simu anaogopa kupigiwa na 

wale jamaa waliomtumia 

picha.Hajawahi kuzima simu 

hata mara moja” akawaza Rais 

Festus 

 “Bado naendelea kujiuliza 

kwa nini wale jamaa 

hawajasambaza zile picha? 

Wameogopa? Nahisi hivyo 

watakuwa wametafakari na 

wameogopa kufanya hivyo kwa 

hofu kwamba wangesakwa kwa nguvu kubwa hadi 

wapatikane” akawaza na 

kukumbuka kitu 

 “Ngoja niwasiliane na 

akina Mathew niwajulishe 

kuwa picha bado 

hazijasambazwa na niwatake 

wafanye haraka zaidi 

kuwasaka hawa jamaa” 

 Rais Festus akachukua 

simu yake akazitafuta namba 

za Zari akampigia 

 “Mheshimiwa Rais” 

akasema Zari na Rais Festus 

akastuka  “Zari are you okay? 

 “Yes I’m okay Mr 

President” 

 “No you are not.Niambie 

tafadhali kuna tatizo lolote? 

 “It’s Mathew” 

 “Mathew kafanya nini? 

 “Amepigwa risasi” 

 “Nini? 

 “Amepigwa risasi 

mheshimiwa Rais” 

 “Saa ngapi? 

 “Usiku huu”  “Vipi hali yake?akauliza 

Rais 

 “Hali yake si nzuri.Yuko 

katika chumba cha upasaji 

hapa SNSA madaktari 

wanaendelea na jitihada za 

kuokoa maisha yake” akasema 

Zari 

 “Zari ninakuja hapo mara 

moja” akasema Rais Festus 

 “Sawa mheshimiwa Rais” 

akajibu Zari na Rais akakata 

simu 

 “Mathew Mulumbi 

amepigwa risasi ! It’s getting ugly ! akawaza Rais 

Festus. 

 “Nadhani hii ndiyo sababu 

wale jamaa hawajasambaza 

zile picha kwa sababu wanajua 

wamekwisha mpata Yule 

waliyekuwa 

wanamtafuta.Wanajua 

wamekwisha muua” akawaza 

na kutoa maelekezo kwa 

walinzi wake kujiandaa.Akavaa 

haraka haraka na kuelekea 

katika gari msafara wa magari 

manne ukaondoka usiku ule 

kuelekea ofisi za SNSA ambazo 

hazikuwa mbali sana na ikulu.  “Bora angepigwa risasi 

mtu mwingine lakini si 

Mathew 

Mulumbi.Tunamtegemea sana 

Mathew katika vita hii.Endapo 

ikitokea ameuawa basi 

litakuwa ni pigo kubwa sana 

kwetu.Mathew anatakiwa 

apone ili aendeleze 

mapambano haya” akawaza 

Festus akiwa garini 


MWISHO WA SEASON 2. ENDELEA KUFUATILIA SEASON 3


MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog