Simulizi : Scandle (Kashfa)
Sehemu Ya Tatu (3)
Gosu Gosu akasimama “Wewe ni nani wa kuniamuru mimi? I’m the boss here and you’ll follow my orders. Do you understand?! Akafoka Gosu Gosu na Kishada akatoa kicheko “Kumbe unafahamu
kiingereza.Ngoja nikujibu kwa kiingereza”akasema Kishada akimtazama Gosu Gosu kwa dharau
“My only boss is God who can take my soul at any time.Chawa kama wewe huwezi kwa bosi wangu.You don’t know me young boy so step aside ! akasema Kishada kwa ukali
“Wewe ndiye ambaye hunifahamu mimi ni nan……” Gosu Gosu akasema na kabla hajamaliza sentensi yake ghafla Kishada akarusha ngumi Gosu Gosu akaiona akaudaka mkono ule.Kishada alikuwa mwepesi sana akarusha mguu wake wa kulia ukampata Gosu Gosu kifuani akaanguka chini.
“Huna uwezo wa kupigana nami wewe kijana.Panda ukalale ! akasema Kishada na kukaa kitanda cha chini. Gosu Gosu akajizoa mzima mzima pale chini akamvaa na kumtandika vichwa viwili mfululizo.Kwa haraka Kishada akaukamata mkono wa Gosu Gosu na kuuma.Gosu Gosu akamtandika ngumi nzito akaanguka kitandani.Pamoja na kipigo kile bado Kishada alikuwa mwepesi sana,kwa kasi ya ajabu akainua blanketi lililokuwa limekunjwa akatoa sindano ndogo na kutaka kumchoma nayo Gosu Gosu mkononi,Gosu Gosu akawahi kumkamata mkono.Kwa kutumia mkono wake wa kushoto Gosu Gosu akaziminya kwa nguvu korodani za Kishada na ule mkono uliokuwa umeshika sindano ukalegea kwa maumivu makali aliyoyapata na Gosu Gosu akaitumia nafasi hiyo kwa nguvu akaupindisha mkono wa Kishada ulioshika sindano na kumchoma sindano ile shingoni akaiminya na dawa yote iliyokuwamo ndani yake ikaingia katika mwili wa Kishada. Halafu akamgandamiza chini kwa nguvu.Kishada alifurukuta
lakini taratibu nguvu zikaanza kumuisha na mwishowe akakata roho.Haraka Haraka Gosu Gosu akaichomoa ile sindano akaenda chooni akairushia ndani kisha akafungua maji mengi na sindano ikabebwa na maji. “Dah ! Siamini kama nimefanikiwa kumuondoa huyu muuaji.Kama ningekuwa legelege tayari ningekwisha kufa kwani alikuwa ananitegea nilale ili anichome sindano ile yenye sumu kali ambayo inaua ndani ya muda mfupi sana” akawaza Gosu Gosu na kumtazama Kishada “Nani kamtuma huyu
jamaa kuja kuniua? Akajiuliza “Nina wasi wasi mkubwa hadi Mathew atakapokamilisha uchunguzi wake kama bado nitakuwa hai.Majaribio ya kuniua yamekuwa mengi na baada ya hili la sindao ya sumu kushindikana lazima watatafuta namna nyingine ya kuhakikisha ninauawa.Ee Mungu muwezeshe Mathew awafahamu hawa watu mapema kabla hawajanitoa uhai” Gosu Gosu akatolewa mawazoni baada ya kusikia sauti ya mtetemo wa kitu. “Nasikia kuna kitu kinatetema kama mtetemo wa simu” akawaza na kuanza kumpekua Kishada akamkuta na simu
“Jesus ! akasema kwa mshangao
Katika kioo cha simu kulikuwa na ujumbe mfupi.Akapitisha dole gumba la Kishada nyuma ya simu ikafunguka akausoma ujumbe
ule ulioandikwa neno moja tu
“Done?
Gosu Gosu akatafakari kuhusu ujumbe ule uliotoka katika namba ambazo
hazikuwa na jina
“Ngoja nimjibu nione atakavyojibu huyo mtu aliyemtumia ujumbe huyu Kishada” akawaza Gosu Gosu “Not yet” akaandika na kuutuma ujumbe ule.Baada ya sekunde chache simu ikatetema na ujumbe mwingine ukaingia “Make sure you finish before 1:00 am.The car will be outside waiting for you” ukasomeka ule ujumbe na mwili wa Gosu Gosu ukasisimka
“Be carefull the subject is very dangerous” ukasomeka tena ujumbe mwingine. “Kumbe huyu jamaa
aliletwa hapa gerezani kama mfungwa kwa lengo moja tu la kuniua kisha aondoke gerezani usiku huu huu! Dah ! huu mtandao nimeanza kuuogopa.Ni watu hatari sana hawa.Imekuwa bahati kwangu nimeweza kumuwahi huyu jamaa.Nitatumia simu hii hii kumfahamisha Mathew kuhusiana na jambo hili” akawaza Gosu Gosu. Haraka haraka akaandika namba za Victor katika simu ile akapiga lakini hazikuwa zinapatikana.Akaandika nyingine ambazo aliweza kuzikumbuka kwa haraka na simu ikaanza kuita akashusha pumzi
“Hallow ! ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili wa simu
“Hallow Martha ni mimi Gosu Gosu” akasema kwa sauti ya chini
“Gosu Gosu?! Martha akashangaa “Ndiyo ni mimi” “Oh my God ! umewezaje kupata simu gerezani? Akauliza Martha
“Martha sikiliza nahitaji msaada wa haraka sana.Unanisikia? akauliza Gosu Gosu akizungumza kwa sauti ya chini
“Ninakusikia Gosu Gosu nini unahitaji? Akauliza
Martha
“Ninataka uende pale nyumbani kwangu,utamkuta Mathew Mulumbi mwambie ninahitaji kuzungumza naye” “Mathew is here? Martha akashangaa
“Martha fuata maelekezo yangu.Nahitaji msaada wa haraka sana”
“Sawa Gosu Gosu
ninakwenda huko sasa hivi” akasema Martha na kukata simu.Gosu Gosu akampandisha Kishada kitanda cha juu akamfunika vizuri kwa blanketi akionekana kama ni mtu aliyelala usingizi halafu akaenda kukaa katika kitanda cha chini .Baada ya dakika chache akasikia vishindo vya askari ambao hupita kukagua vyumbani kama wafungwa wote wamo katika vyumba vyao.Gosu Gosu akachukua kitabu akajifanya anasoma.
“Papaa ! akasema mmoja wa askari magereza akiwa na wenzake wamesimama mlangoni
“Afande ! akasema Gosu
Gosu
“Mko salama humu? “Ndiyo Afande tuko salama.Mwenzangu mgeni amejipumzisha kitanda cha juu”
“Sawa.Maliza kusoma
kitabu chako uzime taa ulale ! akaamuru yule msaidizi wa mkuu wa gereza. “Mpango huu wa
kumuingiza gerezani mtu ambaye si mfungwa lazima viongozi wa gereza hili watakuwa wanahusika ndiyo maana ninapatwa na mashaka sana kama nitaendelea kuwa hai siku mbili au tatu
zijazo.Hata hivyo ninamkabidhi Mungu maisha yangu yeye ndiye atakayenipigania” akawaza
Gosu Gosu
DAR ES SALAAM
Martha mmoja wa viongozi wa MGC Ltd anamfahamu vyema Mathew Mulumbi kwani amefanya kazi katika kampuni yake toka ilipoanzishwa.Baada tu ya kupewa ujumbe na Gosu Gosu akaamka na kumuaga mumewe kwamba kuna
dharura imetokea kazini akaingia garini na kuondoka kwa kasi kuelekea nyumbani kwa Mathew Alifika nyumbani kwa Mathew Mulumbi akitegemea kukuta walinzi kama alivyokuwa amezoea lakini akalikuta geti likiwa tupu.
“Hii hali mbona inanishangaza.Hata siku moja hapajawahi kukosekama mlinzi hapa nyumbani kwa Mathew” akawaza Martha na kushuka garini akatazama huku na huku kama kuna mtu maeneo yale halafu akaenda kugonga geti.Alisubiri dakika mbili baada ya kugonga geti lakini hakuna aliyefungua “Sina hakika kama kuna mtu humu ndani.Hata kama Mathew Mulumbi yuko hapa Dar es salama lakini humu ndani hayumo” akawaza Martha na mara akapata wazo akampigia Gosu Gosu
“Martha umeshafika?
Akauliza Gosu Gosu “Nimefika lakini hakuna dalili zozote za kuwepo mtu humu ndani” akajibu Martha.Gosu Gosu akampa namba za simu za Victor akamtaka ajaribu kumpigia na Martha alipopiga simu ikaanza kuita na baada ya sekunde chache ikapokelewa. “Hallow” akasema Martha “Hallow.Wewe ni nani?
Akauliza Victor
“Ninaitwa Martha.Niko hapa getini nimekuja kuonana na Mathew nina ujumbe wake muhimu kutoka kwa Gosu Gosu nataka kumpatia” akasema Martha na Victor
akakata simu halafu akampigia
Mathew
“Unasemaje Victor?
Mathew akauliza
“Bosi nimepigiwa simu na mtu anaitwa Martha anadai yuko getini ana ujumbe wako muhimu kutoka kwa Gosu Gosu” akasema Victor
“Martha? Akauliza
Mathew
“Ndiyo bosi” akajibu Victor na Mathew akainuka akatoka mle chumbani “Amesema yuko getini?
“Ndiyo bosi.Nimfungulie? akauliza Victor
“Hapana Victor usiende getini ninakwenda mwenyewe” akasema Mathew na kwenda katika chumba cha kamera lakini akashangaa kukuta hakuna kamera inayofanya kazi.
“Hakuna hata kamera moja inayofanya kazi” akasema kwa hasira na kutoka akarejea chumbani kwake akamtazama Sindi ambaye tayari alikwisha pitiwa na usingizi akafungua droo yake pembeni ya kitanda akatoa bastola akashuka chini na kuelekea getini kwa tahadhari “Ni nani huyo anayekuja usiku huu na kudai eti ana taarifa muhimu kutoka kwa Gosu Gosu? Huu unaweza kuwa ni mtego wa hawa jamaa kwani kama Gosu Gosu angekuwa na ujumbe wa muhimu lazima angetafuta namna ya kunifikishia mimi mwenyewe na si kupitia kwa mtu mwigine.Hawa jamaa wana mbinu nyingi sana”
akawaza Mathew akielekea getini
Sindi hakuwa amelala usingizi mara tu Mathew alipotoka,akafungua mlango taratibu akamuona Mathew akishuka chini,akarejea chumbani akafungua pochi yake akachukua kopo dogo akaenda katika kasiki la Mathew akapulizia dawa ile halafu akachukua tochi ndogo yenye mwangaza wa bluu akamulika kasiki kukaonekana alama za vidole akachukua karatasi maalum akaiweka katika alama akaibandua na tayari ilikuwa na alama za vidole akaiweka karatasi ile katika mfumo wa nailoni na kuificha katika pochi yake,akafungua tena mlango akasikiliza kama Mathew anarejea lakini ndani kulikuwa kimya akarejea chumbani akachukua kamera ndogo katika pochi yake na kupiga picha za chumba cha Mathew haraka haraka kisha akairudisha kamera ile ndogo katika pochi yake akalala tena kitandani
Mathew alifika getini akapanga tofali tatu kisha akarukia juu ya ukuta akazama nje na kuliona gari likiwa limeegeshwa na getini kulikuwa na mwanamke amesimama.Alipomtazama vizuri yule mwanamke akapatwa na mshangao
“Martha?! Akasema
Mathew na kushuka akaificha bastora yake kiunoni akafungua geti
“Martha” akasema
Mathew na Martha abakaki anamshangaa bila kusema chochote
“Martha ! akaita tena
Mathew na ukimya ule wa Martha ukamstua akaupeleka mkono wake ilipo bastola “Mathew I’m
sorry.Nimeshikwa na butwaa baada ya kukuona.Sikutegemea kabisa kama uko hapa nchini” akasema Martha na Mathew akautoa mkono katika bastola “Martha ingiza gari ndani tafadhali” akasema Mathew na Martha akaingiza gari ndani akashuka garini na kumkumbatia Mathew kwa nguvu.
“Ouh Mathew siamini kama leo nimekuona tena” “Karibu sana Martha” akasema Mathew
akamkaribisha ndani
“Nimestuka sana kukuona hapa usiku huu.Kwema huko utokako?Mathew akauliza “Mathew kuna mengi
tutazungumza lakini kwanza nikupe kile kilichonileta hapa usiku huu.Nimetumwa na Gosu Gosu”
“Gosu Gosu? “Ndiyo.Amenipigia simu akaniambia kwamba nikufikishie ujumbe haraka sana kwamba anataka kuzungumza nawe”
“Martha I don’t understand.Gosu Gosu yuko gerezani amewezaje kupata simu na kuzungumza nawe?
“Hata mimi sifahamu
Mathew”
“Are you sure it’s him?
Akauliza Mathew “Ndiyo Mathew ni mwenyewe kabisa” akasema Martha na kupiga zile namba za simu alizotumia Gosu Gosu simu ikaanza kuita akampatia Mathew
“Hallow Martha” ikasema sauti ya upande wa pili ambayo mara moja Mathew aliitambua ni ya Gosu Gosu “Gosu Gosu ! akasema Mathew na kutoka mle sebuleni akaenda nje hakutaka Martha asikie mazungumzo
yao
“Oh Ahsante
Mungu.Mathew sikiliza kuna jambo limetokea hapa gerezani” akasema Gosu Gosu na kumsimulia Mathew kila kitu kuhusiana na Kishada aliyetumwa kumuua. “Mathew I’m in big trouble right now please save me !
akasema Gosu Gosu
“Relax Gosu
Gosu.Nakuahidi nitakusaidia” “Hii namba ninayoitumia ni namba yake huyu jamaa mtaifuatilia na kumfahamu zaidi vilevile kuna namba nitakutumia ambazo ni za mtu aliyekuwa anawasiliana naye kwa njia ya ujumbe mfupi na kikubwa alitaka kufahamu kama tayari zoezi la kuniua limekamilika” akasema Gosu
Gosu
“Gosu Gosu ahsante sana kwa taarifa hii nzito ambayo naamini itatusaidia sana katika uchunguzi wa jambo hili.Ninachokuomba ndugu yangu endelea kuwa imara usikate tamaa sisi tuko pamoja nawe na tunaendelea kupambana kuhakikisha tunakutoa gerezani” akasema
Mathew
“Mathew sijawahi kuogopa katika maisha yangu lakini kwa mara ya kwanza ninahisi kuwaogopa hawa jamaa.Wanaonekana ni mtandao mkubwa na wanaweza kufanya chochote.Kama wameweza kumuingiza gerezani mtu ambaye si mfungwa kwa lengo la kuniua hawatashindwa kuniua hata kwa risasi au kuniwekea sumu katika chakula.I’m so scared”
“Gosu Gosu usiwe na hofu tayari tumekwisha weka mazingira ya ulinzi wako hapo gerezani na ndiyo maana ukapatiwa taarifa ya kuhusu huyo mtu aliyetumwa kuja
kukuua.Endapo kutatokea jaribio lolote la kutaka kukudhuru basi utajulishwa mara moja”
“Ahsante sana Mathew .Nimefurahi kuzungumza nawe yawezekana hii ikawa ni mara ya mwisho kwani sifahamu kesho nini kitanitokea pale itakapogundulika huyu jamaa ameuawa”
“Usihofu Gosu Gosu
tunajitahidi sana na ninakuhakikishia kwamba utatoka mahala hapo gerezani” akasema Mathew “Ahsante Mathew.Kila la heri lakini kuwa makini unapowafuatilia hawa jamaa” akasema Gosu Gosu na kukata simu.
Mathew akashusha pumzi na kumrejeshea Martha simu yake
“Martha ahsante sana kwa
kunifikishia taarifa hii
muhimu”
“Ninashukuru pia Mathew kwa kukuona tena.Kwa nini umekuja kimya kimya? Bila Gosu Gosu kunipigia simu nisingeweza kujua kama uko
hapa mjini” akasema Martha
“Ninapumzika kwanza
lakini siku chache zijazo
nitakuja ofisini kuangalia
namna mambo yanavyokwenda.Martha nafahamu tuna mengi ya kuzungumza lakini muda huu si muafaka kwa mazungumzo.Nakuahidi tutakutana na tutazungumza mengi siku nyingine” akasema
Mathew
“Ahsante Mathew.Vipi kuhusu Gosu Gosu? Suala la kufungwa kwake limetuumiza mno.Gosu Gosu ni mtu mzuri hana tatizo na mtu na …” akasema Martha na Mathew akamkatisha
“Tunalishughulikia suala lake.Mtajulishwa kila kitu lakini mambo yanakwenda
vizuri”
“Nitafurahi sana kama
Gosu Gosu akitoka gerezani jamani” akasema Martha “Martha tutaendelea kuwasiliana.Nakushukuru tena kwa kuja kwangu usiku huu” akasema Mathew huku akinyanyuka.Martha naye akanyanyuka ingawa alionekana kutaka kuendeleza maongezi.Mathew akamsindikiza hadi garini akaondoka
“Natamani kama ningekwenda kwa Ruby usiku huu huu ili tuanze kufuatilia namba ya simu aliyonipa Gosu Gosu lakini kwa usiku huu haiwezekani yule tayayi ni mke wa mtu na lazima niliheshimu hilo.” Akawaza Mathew wakati akirejea ndani akaenda moja kwa moja chumbani kwake “Watu hawa ni akina nani?
Swali hili linanimaliza akili yangu kila ninapojiuliza.Katika maisha yangu ya ujasusi nimekumbana na watu wengi lakini hawa wako tofauti sana.Wanaonekana wako mbele zaidi yetu kwani kila tunapopiga hatua moja wao wanapiga mbili.Wamejipanga vyema kuhakikisha hakuna
alama wanaiacha nyuma na vile vile hakuna kizingiti kinajitokeza mbele yao” akawaza Mathew “Ninamshukuru Dr Fabian kwa msaada wake ambao umeweza kumuokoa Gosu Gosu.Bila kuzungumza na mkuu wa magereza, Gosu Gosu asingeweza kupewa taarifa ile ya mpango wa kumuua na hivi sasa tayari
angekuwa amekufa.Kwa jambo hili lililotokea la kumuingiza mtu gerezani kumuua Gosu Gosu lazima uongozi wa gereza unahusika kwa kiasi kikubwa. Mpango huu umeandaliwa kitaalamu sana na ndiyo maana ninaamini hawa watu ni majasusi wa hali ya juu na wamejipanga vyema.Baada a mpango wao kushindikana sasa tuna sehemu nzuri ya kuanzia uchunguzi.Tukiweza kuuchunguza uogozi wa gereza la Kimondo hasa mkuu wa gereza hilo ambaye naamini anaweza akatueleza kila kitu kama tukimpata.Haya mambo yote yataanza kufanyika
kesho” akaendelea kuwaza
Mathew
GEREZA LA KIMONDO –
ARUSHA
Kengele ya kuashiria ni muda wa kuamka na kwenda kukusanyika kwa ajili ya kuhakikiwa kisha kuelekea katika majukumu ya usafi ililia na milango ikafunguliwa wafungwa wakatoka vyumbani.Gosu Gosu naye akatoka katika chumba chake na kuungana na wenzake
“Leo ni siku mbaya sana kwangu.Muda si mrefu watagundua mwili wa Yule jamaa na mambo yataanzia hapo.Laiti ningekuwa na uwezo wa kutoroka mahala hapa ningeweza kuondoka lakini siwezi kwani ulinzi ulioko hapa si wa mchezo.Lakini ninamuamini Mathew na nitafuata ushauri wake wa kuwa mvumilivu wakati analishughulikia suala hili” akawaza Gosu Gosu Wafungwa walijipanga mistari na kuanza kuitwa majina.Baada ya uhakiki ule wa asubuhi wote wakatawanyika kuelekea katika kazi walizopangiwa.Kila mtu alishangaa kwa kumtomuona Yule mfungwa mpya lakini hata jina lake halikuitwa.
“Gosu Gosu Yule jamaa aliyeletwa jana yuko wapi? Akauliza mchungaji Peter “Nimemuacha chumbani
amelala” akajibu Gosu Gosu “Mbona jina lake
halijaitwa na hakuna taarifa yoyote ya mfungwa kupotea?Akauliza Peter “Hata mimi sifahamu kwa nini imekuwa hivi lakini nilimuacha ndani akiwa amelala,sikutaka kumuamsha” akasema Gosu Gosu.Hakutaka kuwaeleza watu kwamba mfungwa Yule alikuwa amefariki dunia.
Wakati wakiendelea na usafi askari mmoja akamfuata Gosu Gosu na kumuita. “Mambo yameanza” akawaza Gosu Gosu na kuongozana na Yule askari magereza hadi katika gari la magereza akafungwa pingu na kutakiwa kuingia garini kisha gari likawashwa na kuondoka.Mbele ya gari lile kulikuwa na gari la mkuu wa magereza ambaye asubuhi hii alikuwa anaendesha yeye mwenyewe.Walipofika Arusha mjini mkuu wa gereza akasimamisha gari kisha akawafuata wale askari magereza waliokuwa katika gari la nyuma na kuwakabidhi bahasha iliyojaa fedha akawataka wakatulie mahala wapate supu safi yeye atakapokuwa amemaliza mizunguko yake atawapigia simu ili waweze kurejea gerezani.Gosu Gosu akashushwa kutoka katika lile gari la askari magereza akaingizwa katika gari la mkuu wa gereza akafunikwa mfuko kichwani kisha akalazwa chini huku askari wawili wenye silaha wakiendelea kumlinda,gari likaondoka. Waliliacha jiji la Arusha wakaingia wilaya ya Arumeru na safari ikaendelea hadi walipofika katika eneo la Kikatiti ambako waliiacha barabara kuu wakaingia katika barabara ya vumbi.Waliifuata barabara hiyo huku mkuu Yule wa magereza ambaye asubuhi hii hakuwa amevaa sare za jeshi akiendelea kuwasiliana na mtu katika simu akimpa maelekezo hadi walipofika katika nyumba moja ya ghorofa iliyozungukwa na ukuta wenye rangi nyeupe na ufito wa rangi nyeusi kwa upande wa chini.Geti likafunguliwa na gari lile likaingia.
Gosu Gosu akashushwa
ndani ya gari akaingizwa katik achumba kimoja ndani ya ile nyumba na kukalishwa katika kiti.Mfuko uliokuwa kichwani ukatolewa na akajikuta akiwa amezungukwa na watu wanne wenye silaha ambao hawakuwa askari . “Nilijua tu leo nitakuwa na mtihani mzito sana na yawezekana ukawa ni mwisho wangu.Mkuu a gereza kumbe anashirikiana na hawa jamaa na amenileta huku baadaya jaribio la kuniua kushindwa kufanikiwa” akawaza Gosu Gosu.Baada ya dakika kadhaa mlango ukafunguliwa wakaingia watu wanne na mmoja akaketi kitini wengine wakasimama ukutani.Yule jama aliyekuwa amekaa kitini uso wake ulikuwa na makovu akavua miwani na jicho lake moja lilikuwa limefumba halikuwa linaona
“Tutazungumza kwa ufupi sana” akasema Yule jamaa mwenye sauti nzito
“Jana umeua mtu gerezani na ukaichukua simu yake.Nataka uniambie wapi ilipo hiyo simu? Akauliza Yule
jamaa
“Sifahamu
unachokisema.Sijaua mtu !
akasema Gosu Gosu
“Wewe ni shujaa siyo?
Akauliza Yule jamaa “Kama wewe ni shujaa basi hapa umekutana na mashujaa halisi na hatuna maneno mengi bali vitendo ndivyo vinachukua nafasi kubwa.Unawaona hawa watu wote wako tayari kwa kazi moja tu ya kuhakikisha unatueleza kila kitu.Niambie mahala ilipo simu uliyoichukua kutoka kwa Yule jamaa uliyemuua ili tuokoe muda urejee gerezani ukapumzike”
“Sikuelewi unachokizungumza.Sijaua mtu yeyote” akasema Gosu Gosu kwa ujasiri hakuonekana kuogopa.Yule jamaa akamuangalia kwa hasira “Kwa mara ya mwisho simu iko wapi?
“You go to hell ! akasema
Gosu Gosu kwa dharau “Ahsante.Nilikwambia kwamba hapa maneno yana nafasi ndogo sana.Vitendo ndivyo vinazungumza” akasema Yule jamaa na kutoa ishara Gosu Gosu akachukuliwa kutoka katika kile chumba akaingizwa katika chumba kingine akalazwa kitandani miguu na mikono ikafungwa barabara kwa kamba na hakuweza hata kutikisika likaletwa taulo likawekwa usoni akaanza kumwagiwa maji.Gosu Gosu alitapa tapa kutafuta hewa.Yule jamaa akawataka wasimame Gosu Gosu akakohoa mfululizo “Wapi ilipo simu?
“Go to hell ! akasema Gosu
Gosu na zoezi likaendelea tena Wakati zoezi likiendelea Yule jamaa mfupi aliyekuwa akimuhoji Gosu Gosu akapigiwa simu akatoka nje na baada ya muda akarejea ndani akasimamisha lile zoezi lililokuwa linaendelea
“Simu tayari imepatikana lakini laini haimo ndani yake.Nataka uniambie laini ya simu iko wapi? Akauliza Yule jamaa
“Go to hhhhel ! akasema Gosu Gosu Yule jamaa akatoka akaenda katika chumba alimokuwa amekaa mkuu wa gereza akipata kinywaji “Amesema chochote?
“Hajasema chochote na
kuna kila dalili hatasema kitu” “Tutafanya nini? Akauliza mkuu wa gereza “Tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunaipata laini hiyo.Hataondoka hapa mpaka laini hiyo ipatikane” akasema
Yule jamaa
“Hapana lazima arejee gerezani.Kama ni kuhojiwa ataendelea kuhojiwa kule gerezani.Huyu ni mfungwa na endapo atapatwa na tatizo lolote au kufariki nje ya gereza mzigo wote utaniangukia mimi.Nimemleta hapa ili mtumie njia zenu za kuhoji na muweze kupata taarifa za mahala ilipo simu ambayo tayari imepatikana na kilichobaki ni laini tu”akasema mkuu wa gereza “Mzee huyu mtu si rahisi kufunguka kama unavyodhani.Tumepewa maelekezo tufanye kila linalowezekana kuhakikisha anasema kila kitu” akasema
Yule jamaa
“Ndiyo maana nimemleta hapa ili mtumie mbinu zozote aweze kufunguka lakini hakikisheni kwamba anatoka hapa akiwa salama.Kama ni kumuua atauawa akiwa ndani ya gereza na si njeya gereza” akasema mkuu wa gereza huku akivuta sigara yake na Yule jamaa akarejea tena ndani wakaendelea kumtesa Gosu
Gsu
DAR ES SALAAM
Mathew ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka na
kumuamsha Sindi ambaye
alikuwa katika usingizi mzito “Sindi nataka nikurejeshe kambini,nina kazi muhimu ya kufanya asubuhi hii” akasema Mathew.Sindi akaamka wakaingia bafuni wakaoga haraka haraka kisha wakajiandaa kwa ajili ya kuondoka.
“Mathew nakushukuru sana kwa ukarimu wako.Nimefurahi sana naamini tutaendelea kuwa na nyakati nzuri kama hizi kwa muda nitakaokuwepo hapa Tanzania” akasema Sindi “Usijali Sindi tutaendelea kukutana zaidi na utafurahia uwepo wako hapa Tanzania” akasema Mathew na Sindi akambusu.
“Ahsante Mathew kwa
usiku mzuri” akasema Sindi wakatoka na kuelekea katika gari la Mathew kisha wakaondoka kwenda katika
kambi ya akina Sindi
****************
Kisha mrejesha Sindi kambini kwao,Mathew alielekea moja kwa moja nyumbani kwa Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo.Tayari walinzi walikwisha pewa maelekezo ya kutokumzuia muda wowote atakapofika hivyo akafunguliwa geti na kuingia ndani akapokewa na mtumishi wa ndani akamkaribisha sebuleni.Baada ya dakika kadhaa akatokea
Ruby
“Mathew karibu.Habari za asubuhi” akasema Ruby “Nzuri kabisa Ruby habari za hapa?
“Nzuri”akasema Ruby na kumtaka Mathew waelekee ofisini kwake.
“Jana hukuweza kuendelea
tena na lile zoezi? Akauliza
Mathew
“Mathew naomba nikuulize kitu kimoja” akasema Ruby na kunyamaza kidogo halafu akauliza “Are you sure you want to help Gosu Gosu? “Yes I am.Kwa nini umeuliza?
“Nimeuliza ili nipate uhakika kama kweli unataka kumsaidia Gosu Gosu” “Nisingekuwa hapa kama nsingehitaji kumsaidia Gosu Gosu.Unadhani ninapata usingizi kwa mambo yanayomtokea kule gerezani? Akauliza Mathew
“Mathew kama kweli una
nia ya dhati ya kumsaidia Gosu Gosu jielekeze katika kazi hiyo na waweke kwanza pembeni hao wanawake wako.Ningeweza kuifanya ile kazi jana usiku lakini sikuona sababu ya kuacha kuwahudumia wanangu na kuendelea na kazi wakati mwenzangu umelala unafurahi na mwanamke wako ! akasema
Ruby
“Okay Ruby
nimekuelewa.Tusilifanye suala hili kuwa gumu.I promise it won’t happen again”akasema
Mathew
“Good” akasema Ruby huku akiiweka sawa kompyuta yake
“Dr Fabian yuko wapi? Kuna jambo muhimu nataka kuwaeleza” akasema Mathew na Ruby akachukua simu akampigia Dr Fabian “Darling unaweza kuja hapa ofisini mara moja? There is something important” akasema Ruby na hazikupita dakika mbili Dr Fabian
akaingia na kusalimia na
Mathew
“Kuna kitu gani mmekipata? Akauliza Dr
Fabian
“Kuna jambo muhimu ambalo nyote mnapaswa kulifahamu” akasema Mathew na kunyamaza kidogo “Jana usiku nimezungumza na Gosu Gosu” “Gosu Gosu alikupigia simu?
“Ndiyo”
“How? Amepataje simu
kule gerezani? Akauliza Dr Fabian.Mathew akawaeleza kila kitu alichoelezwa na Gosu Gosu kuhusiana na Yule mtu aliyetumwa kwenda kumuua. “Mungu wangu ! akasema
Ruby
“Maisha ya Gosu Gosu yanazidi kuwa hatarini”
akasema Dr Fabian
“Namshukuru Gosu Gosu kwa kwa uhodari wake wa kupambana na kuweza kummaliza huyo jamaa kwani ametupa sehemu nzuri ya kuanzia.Tunapaswa kumchunguza huyo Kishada vile vile tumchunguze mtu ambaye alikuwa anawasiliana naye kwa njia ya ujumbe mfupi akitaka kujua kama kazi aliyotumwa imemalizika.Pamoja na hayo…” Mathew akanyamaza kidogo
“Jambo hili lazima linawahusisha pia viongozi wa gereza la Kimondo.Mpango huu lazima walishirikishwa na wakaufanikisha kwa kumuingiza gerezani mtu ambaye si mfungwa ili akafanye mauaji.Mkuu wa gereza la Uwangwa lazima ahojiwe katika jambo hili lazima kuna kitu anakifahamu” akasema Mathew na Dr Fabian akakuna
kidevu chake na kusema
“Mathew uko
sahihi.Jambo hili haliwezi likafanywa bila viongozi wa gereza kulifahamu.Nakubaliana nawe kuna ulazima wa kumuhoji mkuu wa gereza la Kimondo.Kama ulivyosema kwamba kumekuwa na majaribio kadhaa ya kutaka kumdhuru Gosu Gosu na hii inatoa picha kwamba kuna mahusiano kati ya uongozi wa gereza na hao wanaotaka kumuua Gosu Gosu”
“What are we going to do?
Akauliza Ruby
“Nina ushauri” akasema
Dr Fabian
“Kamishna jenerali wa magereza hapa nchini ni rafiki yangu sana na ndiye nilimuomba anisaidie kuhakikisha Gosu Gosu anakuwa salama na huyo askari aliyempa ujumbe Gosu Gosu kuwa kuna hatari,lazima atakuwa anatumiwa na mkuu huyo.Nataka kumtumia mkuu huyo wa magereza nchini katika kumpata mkuu wa gereza la Kimondo kwa mahojiano lakini kuna kitu ambacho lazima tukifanye” akasema Dr Fabian “Kitu gani mzee? Akauliza
Mathw
“We have to tell him the truth” akasma Dr Fabian “Tell him the truth?
Akauliza Ruby “Dr Fabian is right.Tunapaswa kumueleza
ukweli ili atusaidie”
“Ni vipi kama naye ana mashirikiano na hawa watu? Akauliza Ruby “He’s an honest man” akajibu Dr Fabian
“Fine” akasema Ruby lakini sura yake haikuonekana kuridhika na ushauri ule wa Dr
Fabian
“Nitampigia simu nimuombe kuonana naye asubuhi hii” akasema Dr Fabian na kutoka akaelekea chumbani alikoacha simu yake “Mathew are you sure you want to do this? Akauliza Ruby baada ya Dr Fabian kutoka mle ndani
“Ruby ,huyu mkuu wa gereza la Kimondo lazima kuna kitu anakifahamu kuhusiana na haya yanayoendelea kwa Gosu Gosu hivyo kumueleza ukweli mkuu wake ndiyo njia pekee ya kuweza kumpata kwa haraka” “Wasi wasi wangu ni vipi kama naye ana mashirikiano
na hao jamaa? Akauliza Ruby
“Ruby muamini mumeo alichokisema kwamba anamuamini huyo mkuu wa magereza” akasema Mathew “No human being is honest these days” akasema Ruby kwa
sauti ndogo
“Unasemaje Ruby?
Akauliza Mathew
“It’s nothing” akajibu Ruby.Mathew akampatia zile namba za simu za Kishada pamoja na zile namba za Yule mtu aliyekuwa anawasiliana naye kwa ujumbe mfupi.Kabla
Ruby hajaanza kuzifanyia kazi
Dr Fabian akaingia
“Amekubali tukaonane naye asubuhi hii.Ninakwenda kujiandaa ili tumuwahi kwani ana majukumu mengi”akasema Dr Fabian na kuelekea chumbani kwake kujiandaa
“Pamoja na kumchunguza huyu mtu aliyetumwa kumuua Gosu Gosu,tunaendelea pia kumfuatilia Zawadi Mlola.Kama alitoka gerezani salama basi kuna mambo mawili aidha amekwisha fariki au ni mzima.Kama ni mzima
tunapaswa kufahamu mahala alipo na kama alifariki tufahamu pia.We need to dig deeper.Find all her bank accounts na kila chenye mahusiano naye” akasema Mathew
“Sawa mkuu wangu
nitafanya hivyo” akasema Ruby huku akitabasamu Dr Fabian akaingia mle ndani na kumtaka Mathew waondoke “Utatujulisha kile utakachokuwa umekipata” akasema Mathew wakaelekea katika gari la Dr Fabian wakaingia na kuondoka wakitanguliwa na gari la walinzi na nyuma yao kukiwa na gari lingine la walinzi.Safari ilikuwa ya kimya kimya.Ni Dr Fabian aliyeanzisha mazungumzo “Mathew umerejea
nyumbani kwa ajili ya Gosu Gosu na utaondoka tena?
Akauliza Dr Fabian “I’m back for good.Sikujua kama Gosu Gosu yuko kwenye matatizo.Nimekuja kufahamu baada ya kufika hapa.Kujibu swali lako sina mpango tena wa kuondoka” akajibu Mathew na sura ya Dr Fabian ilionekana kuna kitu kinamsumbua
“Huyu mzee ana wasi wasi uwepo wangu hapa unaweza kuwa hatari kwa ndoa yake.Bado anaamini labda ninaweza kurudiana na Ruby” akawaza Mathew halafu akasema
“Usihofu Dr Fabian hakutakuwa na tatizo lolote kwa mimi kuwepo hapa nchini.Me and her we’re done” akasema Mathew huku akitazama pembeni.Baada ya muda Dr Fabian akauliza “Do you still love her? “Sir,there is nothing between us! Akajibu Mathew na simu ya Dr Fabian ikaita “Ruby anapiga” akasema na kuipokea
“Hallow Darling ! akasema
Dr Fabian
“Ninaweza kuzungumza na
Mathew? Akauliza Ruby na Dr
Fabian akampa Mathew simu “Hallow Ruby.Kuna
chochote umekipata? Akauliza “Ndiyo Mathew.Yule mtu ambaye alitumwa kumuua Gosu Gosu anaitwa Adili
Mpipe.Ana miaka 38.Elimu yake ni kidato cha nne.Taarifa zinaonyesha huyu mtu ni jambazi hatari sana na amekuwa anatafutwa na jeshi la polisi kwa kuhusika katika matukio mbali mbali ya kihalifu ikiwamo mauaji.Inatajwa kwamba huyu jamaa amekuwa akifanya uhalifu wake katika nchi za Tanzania,Burundi na jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.Imekuwa vigumu kukamatwa kwani akifanya uhalifu katika nchi moja hukimbilia katika nchi nyingine.Hakuna taarifa yoyote ya jeshi la polisi ikionyesha kwamba Adili alikamatwa na kufunguliwa mashtaka kisha akahukumiwa kifungo gerezani” akasema
Ruby
“Good job Ruby.Taarifa hiyo inatupa uhakika kwamba Adili au Kishada kama anavyoitwa hakuwa mfungwa bali aliingizwa gerezani kama mfungwa kwa lengo la kumuua Gosu Gosu.Vipi kuhusu Yule aliyekuwa anawasiliana naye kwa ujumbe mfupi? Akauliza
Mathew
“Namba ile imetumika bila kusajiliwa hivyo ni vigumu kumfahamu nani alikuwa anaitumia”
“Hawa jamaa wana nguvu na uwezo wa kufanya chochote.Jaribu kutafuta wakati akiwasiliana na Kishada mtu huyo alikuwa wapi? Akauliza Mathew “Sawa Mathew”
“Please keep us posted” akasema Mathew na kukata simu
“Ruby anasemaje?
Akauliza Dr Fabian na Mathew akampa maelezo yale aliyopewa na Ruby “Kwa picha ninayoipata huyu Kishada alikodishwa ili kwenda kumuua Gosu Gosu.Nani aliyemkodisha na kumtuma akamuue Gosu Gosu
ndilo swali linalofuata” akasema Mathew
“Mtu aliyekuwa anawasiliana naye ametumia laini ya simu ambayo haijasajiliwa na hii inaonyesha wazi jinsi hawa jamaa walivyo na uwezo wa kufanya chochote na kila wanakopita hawataki kuacha alama nyuma yao” ‘Taratibu tutaupata mwangaza” akasema Mathew na safari ikaendelea
Walifika katika makao makuu ya jeshi la magereza na kuelekea moja kwa moja katika
ofisi ya Kamishna Jenerali wa magereza Chambao Mnenge.Dr Fabian alipokewa kwa heshima kubwa. “Mheshimiwa Rais karibu sana.Nimefurahi umenitembelea leo hii ofisini kwangu” akasema Chambao Mnenge Kamishna jenerali wa Magereza Tanzania baada ya akina Mathew kuingia ofisini kwake
“Ahsante sana kwa
kutukaribisha ofisini kwako kamishna” akasema Dr Fabian “Nimeongozana pia na mmoja kati ya watu muhimu sana kwa nchi hii.Nina uhakika tayari umekwisha mfahamu” akasema Dr Fabian “Sura hii si ngeni machoni kwangu” akasema Kamishna Chambao
“Anaitwa Mathew Mulumbi.Amewahi kufanya kazi katika idara yetu ya
ujas…….”
“Ouh sasa nimemkumbuka.Sura hii si ngeni kabisa na nilikuwa najaribu kutafakari nimeiona wapi hii sura.Mathew Mulumbi karibu sana ofisini kwangu.Ni heshima kubwa kutembelewa na mtu kama wewe” akasema Kamishna
Chambao
“Ahsante sana
Afande”akasema Mathew “Kamishna nafahamu umeahirisha baadhi ya majukumu yako ili uweze kukutana nasi hivyo sitaki kuchukua muda wako mwingi nataka niende moja kwa moja
katika kile kilichotuleta hapa”
“Karibu” akasema
Kamishna Chambao “Kamishna nilikuomba jana msaada kuhusu yule kijana aliyefungwa kule Kimondo Arusha”akasema Dr
Fabian
“Ndiyo tayari nimekwisha weka askari mmoja pale gerezani ambaye anamsaidia kwa siri” akasema Kamishna Chambao
“Ahsante kwa hilo
Kamishna lakini leo nimerudi tena na suala hilo hilo.Kwa ufupi tu ni kwamba Yule kijana amekuwa akifanya kazi bega kwa bega na Mathew na kwa pamoja wamekuwa ni msaada mkubwa sana kwa nchi yetu hata pale ambapo vyombo vyetu vya usalama vimeshindwa kung’amua matukio mbali mbali ya kuhatarisha amani yetu lakini wao kwa ushujaa kabisa wameweza kujitoa mhanga wakapambana kufa na kupona na kuondoa hatari.Unavyomuona hapa Mathew amepitia magumu mengi sana.Usiione sura yake ni angavu lakini akivua shati hutatamani kuona huo mwili wake ulivyo na makovu ya mateso ambayo ameyapitia.Gosu Gosu pia amewahi kunusurika kifo baada ya kupigwa risasi.Kwa ufupi tu vijana hawa ni muhimu mno kwa taifa hili” akanyamaza Dr Fabian kwa sekunde kadhaa halafu akaendelea
“Gosu Gosu alipatwa na mkasa ule na kufungwa gerezani wakati huo Mathew Mulumbi hakuwepo nchini.Baada ya Mathew kurejea nchini aliamua kufanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma zile zilizokuwa zinamkabili Gosu Gosu hadi kupelekea akafungwa maisha gerezani na kuna mambo muhimu ameyagundua katika uchunguzi wake” akasema Dr Fabian na kumgeukia Mathew
“Mathew mueleze Kamishna kile ambacho umekigundua” akasema Dr Fabian na Mathew akamueleza Kamishna Chambao kisa chote cha Gosu Gosu na hatua aliyofikia katika uchunguzi wake.
“Naamini mpaka hapo umenielewa Kamishna” akasema Mathew “Angekuwa ni mtu mwingine nisingemuamini
lakini kwa kuwa ni wewe Mathew Mulumbi ninalazimika kuamini kile unachoniambia japo mwili wote umenisisimka kwa maelezo haya.Ni jambo zito hili.Pole sana kwa kunusurika kifo Arusha”akasema
Kamishna Chambao “Ahsante sana Kamishna” akasema Mathew na baada ya sekunde chache akaendelea “Siku ya jana katika gereza la Kimondo aliingizwa mfungwa ambaye anajulikana kwa jina la Adili Mpipe au kwa jina la utani Kishada ambaye alipelekwa katika chumba anamolala Gosu Gosu.Kwa bahati nzuri kijana uliyemuweka pale gerezani kumsaidia Gosu Gosu alimpa tahadhari Gosu Gosu kwamba kuna mpango wa kumuua kwa kumtumia huyo Kishada ambaye alikuwa na sindano yenye sumu.Usiku wa jana Gosu Gosu alipambana na Kishada na akafanikiwa kumuua kwa kutumia sindano hiyo ya sumu” akasema Mathew na kumueleza Kamishna Chambao namna mpango wa kumuua Gosu
Gosu ulivyokuwa umeandaliwa,Kamishna Chambao akavuta pumzi ndefu “Nimekuwa katika jeshi la magereza tangu nikiwa na miaka ishirini na moja,nimekuwa mkuu wa magereza kadhaa hapa nchini na jambo kama hili sijawahi kulishuhudia wala kulisikia.Ni mara ya kwanza ninasikia kuna mtu ameingizwa gerezani kama mfungwa kwa ajili ya kwenda kutekeleza uhalifu” akasema Kamishna Chambao “Jambo hilo limetokea Kamishna jana usiku.Mpaka sasa kuna taarifa zozote umezipokea kuhusiana na mfungwa aliyefariki gerezani? Akauliza Mathew “Hakuna taarifa yoyote nimepokea kuhusiana na mfungwa kufariki
gerezani”akajibu Kamishna
Chambao
“Hujaambiwa kwa sababu hakuwa mfungwa bali raia wa kawaida aliyeingia gerezani kama mfungwa” akasema
Mathew
“Kamishna nimekuja hapa kwa sababu Mathew ana ombi maalum kwako” akasema Dr
Fabian
“Kitu gani unahitaji
Mathew?”akauliza Kamishna
Chambao
“Suala hili lazima uongozi wa gereza unalifahamu hivyo ninahitaji kumuhoji mkuu wa gereza la Kimondo ili atueleze ni kwa namna gani jambo hili limetokea na awataje watu ambao wameshirikina nao katika jambo hili.Hatuwezi
kulifanikisha hilo bila msaada wako Kamishna” akasema Mathew.Kamishna Chambao akafikiri halafu akasema
“Mambo uliyonieleza
Mathew ni mazito sana na siku zote jukumu letu ni kupambana na waovu.Mimi
niko tayari kukusaidia.Nataka kufahamu namna utakavyomuhoji huyo mkuu wa gereza”akasema Kamishna
Chambao
“Ahsante
Kamishna.Mahojiano hayo yatafanyika kwa siri hivyo ninachohitaji ni mkuu huyo wa gereza la Kimondo afike Dar es salaam kwani mahojiano hayo yatafanyika hapa Dar es salaam”
“Unataka aje Dar es salaam?
“Ndiyo namuhitaji hapa Dar es salaam na ndiyo maana nimekuja kuomba msaada wako ili aweze kufika hapa
Dar” akasema Mathew “Lini unahitaji kumuhoji?
“Leo hii”akasema Mathew
“Leo hii? Kamishna
Chambao akashangaa
“Ndiyo Kamishna” “Kwa leo itakuwa vigumu kwa sababu lazima nimpe taarifa ajiandae na kesho ndipo aje Dar es salaam” akasema Kamishna Chambao “Kamishna suala hili halihitaji kuchukua muda.Kuhusu usafiri usiwe na shaka tunaweza kutafuta helkopta hata ya kukodisha ikaenda Arusha mara moja kumchukua.Unachotakiwa ni kumfahamisha kwamba kuna kikao kazi kinachowahusu wakuu wote wa magereza kuna maelekezo yametolewa na Rais na kikao hicho kinatakiwa kufanyika jioni ya leo hapa Dar
es salaam” akasema Dr Fabian “Mheshimiwa Rais wazo
lako ni zuri lakini kama mkuu huyo wa gereza atakuwa anashirikiana na hao watu waovu akipata wito wa ghafla wa kuja Dar es salaam anaweza akahisi kuna jambo haliko sawa na tunaweza tukakosa kufahamu kile tunachokihitaji kutoka kwake.Ninakwenda mwenyewe huko Arusha.Nitafika gereza la Kimondo bila taarifa.Nitajifanya nina ziara ya kuzungukia magereza makuu yote ya hapa nchini.Nikitoka hapo nitamtaka mkuu wa gereza hilo aingie katika helkopta kisha nitaondoka naye bila kumweleza tunaelekea wapi.Si yeye wala watu anaoshirikiana nao watafahamu tunaelekea Dar.Akifika hapa nitakwenda naye mahala halafu nitawafahamisha na Mathew utafika tutaongozana wote kwenda mahala ambako utamuhoji kisha nitamkabidhi kwako.Akisha hojiwa na kueleza kila kitu ndipo atakaporejea Arusha.Hakuna atakayefahamu kama yuko hapa Dar es salaam.Mnaonaje mpango huo? Akauliza Kamishna Chambao “Ni mpango mzuri sana” akasema Mathew na kunyamaza baada ya simu yake kuita.Alikuwa ni Ruby “Ruby anapiga”
“Pokea msikilize” akasema Dr Fabian na Mathew akatoka
mle ndani akaipokea simu
“Hallow Ruby”
“Mathew kuna jambo nimelipata” akasema Ruby “Nakusikia Ruby nini umekipata? Akauliza Mathew “Nimeendelea kuchimba
kuhusu Zawadi Mlola na kuna mambo
nimeyagundua.Nimefuatilia
kamera za ulinzi za gereza la
Uwangwa alikokuwa amefungwa na nimefanikiwa kumuona zawadi akitoka gerezani kwa kutumia geti B akiwa amevaa suruali ya jeans rangi ya bluu,shati jekundu na koti na alikuwa amebeba mfuko.Baada ya kutoka getini mtu mmoja ambaye nitakutumia picha yake alimfuata akampokea ule mfuko na kumuongoza hadi katika gari funguliwa geti alielekea moja kwa moja katika maegesho ya magari akamfungulia mlango katika gari moja dogo lenye rangi nyeupe wakaondoka
Nimefuatilia namba za lile gari nikagundua kwamba zilikuwa ni namba bandia.Nimejaribu kufuatilia gari lile lilielekea wapi baada ya kutoka gerezani,baada ya kuvuka daraja la Nyerere gari sikuweza kuliona tena”akasema Ruby “Dah ! akasema Mathew “Sikuishia hapo” Ruby akaendelea
“Nimeendelea kumchimba zaidi huyu Zawadi na kugundua kwamba alikuwa na akaunti mbili katika benki mbili tofauti.Akaunti moja ni ile ambayo mshahara wake ulikuwa unapitia na baada ya kufungwa gerezani hakuna fedha yoyote iliyoingia katika akaunti hiyo kwani hakuendelea kupokea mshahara.Akaunti nyingine ni kwa ajili ya kuweka akiba.Siku tatu baada ya kutoka gerezani kiasi cha shilingi million ishirini na nane zilitolewa katika akauti yake iliyo katika benki ya Jacita Comercial kwa njia ya hundi.Baada ya hapo akaunti hiyo haikuwahi kutumika kuweka au kutoa fedha.Miezi mitatu iliyopita ilifunguliwa akaunti nyingine katika benki ya akiba ya wajasiriamali tawi la Kichangani kwa jina la Zawadi Mlola na alipatiwa mkopo wa shilingi milioni tano kutoka katika benki hiyo.Wiki mbili zilizopita katika tawi hilo hilo la Kichangani,fedha zimetolewa katika akaunti yake kwa kupitia mashine ya kutolea fedha.Hayo ni mambo ambayo nimefanikiwa kuyagundua baada ya kuchimba kwa undani kuhusu Zawadi.Naamini yanaweza kutupa picha Fulani” akasema
Ruby
“Ruby ahsante kwa kazi hii kubwa ambayo naamini itatupatia mwanga wa kutosha kuhusiana na alipo Zawadi.Pamoja na ugunduzi huo lakini bado tunahitaji kujiridhisha kuwa Zawadi yuko hai na ni yeye ndiye aliyetoa fedha katika akaunti hiyo.Isije kuwa kuna Zawadi mwingine au kuna mtu anatumia akaunti yake.Katika chumba cha kutolea fedha naamini kuna kamera za siri na endapo tukifanikiwa kupitia kamera hiyo itatusaidia kuweza kumtambua Zawadi.Unaweza ukafanya lolote katika mfumo wa kamera za benki ya akiba ya
wajasiriamali? Akauliza
Mathew “Ile ni benki binafsi,mfumo wake wa ulinzi haujaunganishwa na SNSA hivyo siwezi kuingia” akasema
Ruby
“Sawa Ruby ngoja
niangalie nini tunaweza kufanya.Tafadhali naomba unitumie picha ya Zawadi katika simu yangu” akasema na kukata simu kisha akarejea ndani
“Kila kitu kiko sawa? Akauliza Dr Fabian “Ndiyo mzee kila kitu
kinakwenda vizuri” “Good.Tayari nimewasiliana na kampuni ya kukodisha ndege nimekodisha helkopta moja ambayo itampeleka Kamishna
Chambao jijini Arusha” Dr Fabian akamwambia Mathew.
Walimuaga Kamishna Chambao kwa miadi ya kuwasiliana pale atakapokuwa amerejea kutoka Arusha.Wakati wakishuka kuelekea katika gari Mathew akamweleza Dr Fabian kile alichofanikiwa kukipata Ruby “Haya ni maendeleo mazuri sana.Nini unataka kukifanya baada ya kupata taarifa hizo? Akauliza Dr
Fabian
“Ninahitaji kujiridhisha kama huyo aliyetoa fedha katika tawi hilo la Kichangani wiki mbili zilizopita ni
Zawadi.Ndani ya chumba cha kutolea fedha kuna kamera ya
siri hivyo nahitaji kupitia kumbu kumbu za kamera hiyo.Kwa mujibu wa Ruby ile ni taasisi binafsi hivyo haijaunganishwa na SNSA na imekuwa vigumu kwake kuweza kuingia katika mfumo wa ulinzi wa benki hiyo”
“Mkurgenzi wa benki hiyo ninafahamiana naye.Ninaweza kuzungumza naye na akatoa maelekezo ya kuruhusu ukapitia kumbu kumbu hizo” akasema Dr Fabian “Naomba ufanye hivyo mzee” akasema Mathew
wakaingia garini na safari ya kuelekea katika makao makuu ya benki ya wajasiriamali ikaanza
**************
Mathew na Rais mstaafu
Dr Fabian Kelelo waliwasili makao makuu ya benki ya akiba ya wajasiriamali na kuonana na meneja mkuu ambaye aliwakaribisha kwa
furaha ofisini kwake “Pascal nimekuja ninaomba msaada.Kuna mtumishi wangu mmoja aliiba fedha na kutoweka, nimesikia ameonekana maeneo ya Kichangani katika tawi lenu akitoa fedha katika mashine ya kutolea fedha.Ninajua katika chumba cha kutolea fedha kuna kamera ya siri hivyo ninataka kupata ruhusa kutoka kwako ya kupitia kumbukumbu hizo za kamera na kujiridhisha kama kweli ni yeye.Ni hilo tu lililonileta hapa kwako” akasema Dr Fabian “Mzee hukuwa na haja ya kupoteza muda kunifuata hapa kwa ajli ya jambo hilo ungenipiga tu simu ningetoa maelekezo.Nani unamtuma huko au unakwenda mwenyewe?” akasema Pascal meneja mkuu wa benki ile ya akiba ya wajasiriamali.
“Ni mimi ndiye ninayekwenda huko, mzee anapumzika” akasema Mathew na Pascal akampa barua kuipeleka kwa meneja wa tawi la Kichangani.
“Pamoja na barua hiyo
lakini nitampigia simu vile vile
kumpa msisistizo zaidi ili uhudumiwe mara moja” akasema Pascal wakamuaga na kuondoka
“Mzee ninashukuru sana kwa msaada huu mkubwa,sasa unaweza ukarejea nyumbani kupumzika mimi nitachukua taksi kuelekea
Kichangani.Nitakachokipata huko ntawajulisha” akasema
Mathew
“Mathew nina gari mbili za walinzi badala ya kutumia taksi tumia gari moja”
“Ahsante mzee nitachukua
taksi” akasisitiza Mathew kisha wakaagana na Mathew akatembea kwa miguu hadi katika kituo cha taksi
akamuomba dereva mmoja ampeleke Kichangani.
GEREZA LA KIMONDO -
ARUSHA
Papi Gosu Gosu
alishushwa kutoka katika gari la mkuu wa gereza mara tu baada ya kurejea gerezani akitokea Kikatiti alikopelekwa kuteswa ili aonyeshe ilipo simu ya Kishada.Uso ulikuwa umemvimba kwa kipigo alichokipata kutoka kwa wale jamaa lakini pamoja na mateso yale makali hakuonyesha mahala ilipo laini ya simu ya Kishada.
Akiwa amefungwa mikono kwa pingu Gosu Gosu alipelekwa katika pango maalum ambalo hutumika katika kutoa adhabu kwa wafungwa wakorofi akavuliwa nguo na kufungwa katika mti uliokuwa na alama za damu “Gosu Gosu hii ni nafasi ya
mwisho nataka uonyeshe wapi ilipo laini ya simu uliyoichukua? Akauliza mkuu wa gereza lakini Gosu Gosu hakumjibu kitu “Endeleeni na kazi hadi pale atakaposema mahala ilipo laini ya simu” akasema mkuu wa gereza akiwaelekza askari magereza wawili waliokuwamo mle ndani ambao walichukua fimbo maalum na kuanza kumchapa. Mwili wa Gosu Gosu ulivimba kwa kipigo kile na damu kumchuruzika. “Wapi ilipo laini ya simu? Akauliza mkuu wa gereza kwa hasira lakini Gosu Gosu hakumjibu “Endeleeni hadi atakaposema ! akaamuru mkuu wa gereza na kipigo kikaendelea.
Akiwa amekunja sura kwa hasira simu ya mkuu wa gereza ikaita akaichukua na kutazama mpigaji alikuwa ni Kamishna jenerali wa magereza .Akahisi kutetemeka,akatoka nje na kuipokea ile simu
“Afande ! akasema
“Deus ninakuja hapo gerezani kwa kutumia helkopta nataka maelekezo tafadhali mahala ambako inaweza ikatua kwa salama” akasema
Kamishna Chambao
“Unakuja hapa gerezani? “Ndiyo tayari nimekwisha ingia Arusha na muda wowote
nitafika hapo gerezani” akasema Kamisha “Muelekeze rubani atue katika uwanja wa mpira wa kikapu,nitaweka mtu hapo wa kutoa maelekezo” akasema Deus na Kamishna akakata simu.
“Mungu wangu ! akasema Deus na kuingia ndani haraka haraka akawataka wale askari kusimamisha zoezi lile haraka la kumtesa Gosu Gosu “Mrejesheni katika chumba chake kuna jambo limetokea.Tutaendelea baadae” akasema Deus na Gosu Gosu akafunguliwa akavalishwa nguo na kubebwa haraka haraka kurejeshwa katika chumba chake. Mstuko alioupata Deus ulikuwa mkubwa.Hakutegemea. “Kamishna anakuja
kufanya nini? Halafu kwa nini amekuja bila kutoa taarifa? Hii si kawaida yake.Kila anapotembelea gereza taarifa hutolewa.Hapa lazima kuna kitu si bure” akawaza Deus Mtege na haraka haraka akakimbia nyumbani kwake ambako alivaa sare za jeshi na kukimbia kuelekea katika uwanja wa mpira wa kikapu akawapigia simu maafisa wengine wa gereza kuweka vitu vizuri kwani Kamishna atafika muda wowote.
Helkopta iliyombeba Kamishna jenerali Chambao ilitua katika uwanja wa mpira wa kikapu na Kamishna akashuka akapokelewa na mkuu wa gereza na baadhi ya maafisa wachache waliokuwepo.Wakasalimiana kisha wakaongozana kuelekea katika ofisi ya mkuu wa gereza.
“Karibu sana
Afande,sikujua kama utakuja leo hii” akasema Deus
“Nina ziara ya kuzungukia magereza yote makubwa nchini na nilifanya makusudi kutokutoa taarifa ili kuangalia kile kinachoendelea magerezani.Kila kitu hapa
kinakwenda vizuri? Akauliza
Kamishna Chambao “Kila kitu hapa kinakwenda vizuri” akajibu Deus na kumueleza Kamishna Chambao hali ya gereza kisha wakatoka wakazungukia baadhi ya sehemu za gereza lile kama jikoni na katika baadhi ya vyumba wanavyolala wafungwa.Kisha maliza kuzunguka sehemu mbalimbali wakarejea katika
ofisi ya mkuu wa gereza
“Deus ninakupongeza it Chambao na kuongozana na Deus hadi katika helkopta wakaingia, helkopta ikapaa na kuondoka.
“Nashukuru Kamishna
hajauliza chochote kuhusiana na kile kilichotokea hapa gerezani nadhani hajafahamu
chochote” akawaza Deus
DAR ES SALAAM
Mathew aliwasili katika benki ya akiba ya wajasiriamali tawi la Kichangani akamlipa dereva taksi halafu akaingia ndani.Alijieleza kwamba ni mgeni wa meneja wa tawi akapelekwa katika ofisi ya meneja ambaye alikuwa ni kijana sana,wakasalimiana
“Karibu sana kaka.Taarifa zako tayari
zimefika.Nimepewa maelekezo na meneja mkuu ya kuhakikisha tatizo lako linatatuliwa” akasema yule meneja ambaye kibao kilichokuwa mezani kiliandikwa Amos Themba.Akainuka na kumtaka Mathew amfuate wakaenda hadi katika chumba maalum kwa ajli ya kufuatilia kamera zote za ulinzi za ile benki ambamo waliwakuta vijana wawili,Amos akamkabidhi Mathew kwa wale vijana ili waweze kumsaidia tatizo lake.Mathew akawaelza wale jamaa shida yake na wakaanza kuishughulikia.Haikuwa kazi ngumu kwani tayari Mathew alikuwa na muda ambao Zawadi aliingia ndani ya chumba cha kutolea fedha
Mathew aliyaelekeza macho yake katika runinga ya ukutani na mmoja wa wale jamaa akamuita akaketi kitini. “Tayari unaweza ukaanza kufuatilia,nimerudisha sekunde kadhaa nyuma kabla ya muda ambao mtu huyo aliingia ndani ya chumba cha kutolea fedha” akasema mmoja wa wale vijana
Mlango wa chumba cha
kutolea fedha ulifunguliwa na mwanamke mmoja akaingia ndani ya chumba kile.Alikuwa amejfunga kilemba kichwani na macho yake aliyafunika kwa miwani myeusi.Alitoa fedha na kutoka.Kwa kutumia kamera ya nje Mathew akamfuatilia mwanamke Yule ambaye alikwenda hadi katika maegesho ambako alipanda piki piki na kuondoka.Wakati ikiondoka namba ya piki piki ilionekana Mathew akainakili halafu akawashukuru wale jamaa akatoka.Akamfuata meneja mkuu akamshukuru kwa msaada ule akatoka na kumpigia simu Ruby akampa namba za ile piki piki akamtaka aifuatilie ni ya nani.Alienda kujipumzisha katika duka Fulani na kununua soda baridi wakati akisubiri jibu kutoka kwa Ruby
“Yule mwanamke lazima ni mwenyewe japo alikuwa amejifunga kilemba na miwani lakini hatofautiani sana na Yule kwenye picha niliyonayo” akawaza Mathew
Zilipita dakika kadhaa Ruby akampigia simu na kumjulisha kwamba piki piki ile imesajliwa kwa jina la
Hussein Mlula akampatia na namba zake za simu Mathew akampigia simu ikaita
“Hallow” akasema jamaa
aliyepokea simu
“Hallow Hussein” akasema Mathew kana kwamba ni mtu anayemfahamu vyema.
“Mambo vipi? Akasema Hussein
“Mambo poa.Uko wapi?
“Niko kijiweni.Wewe nani ndugu yangu?
“Unaweza ukaja hapa katika duka limeandikwa Meku karibu na benki ya
wajasiriamali? Akauliza
Mathew
“Ouh hapo kwa
mangi,sawa naja sasa hivi” akasema Hussein
Baada ya muda mfupi piki
piki moja ikawasili pale dukani Mathew akamfuata
“Hussein? Akauliza
“Mambo vipi kaka” akajibu Hussein
“Mambo poa.Hussein
mimi ndiye niliyekupigia simu.Nilipewa namba zako na dada mmoja akaniambia nikifika hapa Kichangani nikupigie utanipeleka kwake” “Ni nani huyo? Mimi nina wateja wengi” akasema Hussen na Mathew akatoa simu yake akamuonyesha picha ya Zawadi
“Ouh kumbe huyu dada.Ni mteja wangu sana.Ana duka lake kubwa la madawa” akasema Hussein na Mathew akapanda katika piki piki
“Nikupeleke dukani kwake au nyumbani?
“Unadhani muda huu atakuwa nyumbani au dukani? “Nadhani tuanzie nyumbani.Si anafahamu kama unakuja leo?
“Ndiyo anafahamu” akasema Mathew
Hussein alimpeleka
Mathew hadi katka nyumba Fulani iliyokuwa na uzio mfupi wa matofali kiasi kwamba ukiwa nje unaweza ukamuona aliye ndani.Kulikuwa na geti la rangi nyeusi na pembeni kidogo na geti kulikuwa na duka.Hussein akasimamisha
piki piki mbele ya duka na kumpigia mkono mwanamke Fulani aliyekuwa dukani akiuza.
“Dada nimekuletea mgeni” akasema Hussein na Mathew akamlipa fedha yake akaondoka.Akatembea hadi dukani
“Karibu” akasema Yule mwanamke dukani
“Ahsante sana.Mimi ni mgeni wako kwa bahati nzuri nimempata Hussein kumbe anafahamu mahala unapoishi na akanileta”akasema Mathew na Yule mwanamke akaonyesha wasiwasi kidogo “Karibu ndani” akasema kisha akamfungulia Mathew mlango akaingia ndani akampeleka sebuleni akampatia glasi ya maji
“Samahani naomba
nikafunge duka ninarejea sasa hivi” akasema Yule mwanadada aliyekuwa amevaa suruali ya jeans ya bluu na fulana ya bluu.
“
“It’s her japo kwa sasa amenenepa sana” akawaza Mathew baada ya kuitazama tena iele picha ya Zawadi katika simu
“Ahsante Mungu nimefanikiwa kumpata Zawadi.Huyu atatusaidia sana kufahamu kile ambacho alikuwa anakichunguza Lidya” akawaza Mathew na Yule mwanadada akarejea “Karibu sana kaka”
“Ahsante.Habari za hapa? Akauliza Mathew
“Hapa kwema
kabisa.Nadhani mwenzangu unanifahamu lakini mimi bado sijakufahamu.Yawezekana tumewahi kuonana sehemu na mimi nimesahau.Naomba unikumbushe wapi tumekutana? Akauliza Zawadi
Mathew aliyekuwa amekaa katika sofa akiangalia dirishani aliona mlango mdogo wa geti ukifunguliwa wakaingia watu wawili wakatembea haraka haraka kuelekea sebuleni.Mathew akastuka
“Kuna wageni
unawategemea leo? Akauliza Mathew
“Hapana.Kwa nini?
“Kuna mlango wa kutokea nyuma? Akauliza Mathew
“Kwani kuna nini? Zawadi akauliza.Mathew tayari alikwisha upeleka mkono ilipo bastola yake iliyofungwa kiwambo cha sauti
“Kimbia haraka ! akasema Mathew na zawadi akabaki amesimama amechanganyikiwa.Mara Mathew akamrukia na kumuangusha chini.Ukasikika mlio wa risasi na vioo vya kabati lililokuwa sebuleni vikavunjika.Mathew alikuwa mwepesi akageuka na kuachia risasi mbili dirishani alikokuwa amesimama jamaa mmoja akaanguka chini.
“Run !! akasema Mathew na Zawadi akasimama akaanza
kukimbia kuelekea nje kupitia mlango wanyuma.Mathew naye akainuka huku akiachia risasi mlangoni akamfuata wakatokea upande wa nyuma wakakimbia hadi katika ukuta.Mathew akamsaidia Zawadi kupanda ukuta akarukia nje wakati akijaribu kupanda ili naye aruke nje ukasikika mlio wa risasi,akageuka na kuwaona watu wawili wakitokea katika ule mlango wa nyuma.Akaachia risasi na watu wale wakarudi ndani akapanda ukuta na kuruka nje.Akamkuta Zawadi akiwa amelala chini akigugumia kwa maumivu ya mguu ulioumia baada ya kuruka
“Zawadi nisikilize.Jitahidi inuka tuondoke mahala hapa.Hawa jamaa watatuua”
“Siwezi mguu wangu umeteguka” akasema zawadi huku akilia.Mathew akafanya maamuzi na kwa haraka akamuinua Zawadi akamuweka mabegani akaanza kukimbia naye mara ikasikika milio ya risasi na Zawadi akatoa mguno.Zawadi alikuwa mzito lakini Mathew alikimbia naye kwa ukakamavu mkubwa.Wakati akikimbia alihisi mgongo wake unaloa,zilikuwa ni damu.
Baada ya kukatisha vichochoro kadhaa Mathew akatokea katika mtaa mwingine.Milio ya risasi iliyosikika ilizua taharuki eneo lile.Mathew akamuweka Zawadi katika kibaraza cha nyumba moja baada ya miguno ya maumivu kuongezeka na ndipo alipogundua Zawadi alikuwa amepigwa risasi mbili pajani na alikuwa amepoteza damu nyingi na hali yake ilikuwa mbaya
“Oh no !! akasema kwa mstuko
“No you cant die Zawadi before you tell me everything !
akasema Mathew
“Zawadi ! unanisikia? Akauliza Mathew
“Ninakufa ! oh ninakufa ! akasema Zawadi na watu wakaanza kusogea wakitaka kujua nini kimetokea.
“Amepigwa risasi na majambazi.Tumsaidie kumpeleka hospitali haraka sana” akasema Mathew na haraka haraka mtu mmoja akajitolea gari Zawadi akaingizwa garini na gari likaondoka kwa kasi kubwa sana.Hali ya zawadi iliendelea kubadilika huku damu nyingi ikimwagika katika jeraha la pajani ambako alipigwa risasi mbili.
“Zawadi ! Zawadi !
unanisikia? Akauliza Mathew na Zawadi akafumbua macho
“Zawadi niambie Naomi
Bambi ni nani? Akauliza Mathew lakini Zawadi hakujibu kitu alikuwa anagugumia kwa maumivu
Alifikishwa katika kituo cha Afya cha Kichangani lakini walimsaidia kuzuia damu isiendelee kutoka wakaelekeza akimbizwe katika hospitali kubwa.Aliingizwa katika gari la wagonjwa likaondoka kwa kasi kubwa kuelekea hospitali.
Hospitali pekee kubwa ambayo ilikuwa karibu na wangeweza kuifikia kwa haraka ni Katihar Medical College and Hospital. Hospitali hii ina chuo kikubwa cha madaktari na hospitali inayosifika kwa kutoa huduma za uhakika
“Ee Mungu msaidie Zawadi aweze kupona.Ninamuhitaji sana kwani ana taarifa za muhimu” Mathew akaomba kimya kimya
Gari la wagonjwa lilikwenda kwa mwendo mkali sana na kufika hospitali ya Katihar ambako tayari taarifa ilikwisha fika kuwa mgonjwa wa risasi anapelekwa.Mara tu gari lilipofika Zawadi akashushwa haraka haraka na kukimbizwa katika chumba cha upasuaji.Wakati madaktari wakiendelea na jitihada za kumsaidia Zawadi, Mathew akatoka nje na kumpigia simu
Ruby
“Mathew nipe habari za huko.Umefanikiwa? akauliza Ruby
“Nimefanikiwa kumpata
Zawadi lakini kuna tatizo limetokea” akasema Mathew na kumueleza Ruby kile kilichotokea
“Dah ! Pole sana Mathew”
“Ahsante Ruby”
“Are you sure she’s going to make it? Akauliza Ruby
“I’m not sure.Tumuombe
Mungu amsaidie apone kwani ni mtu wa muhimu sana kwetu”akasema Mathew
“Who are these people? Akauliza Ruby huku akivuta pumzi ndefu
“I don’t know.Kinachonishangaza ni kwamba wamefahamuje kama niko pale kwa Zawadi? Kwa namna walivyoingia walikuwa na uhakika mkubwa kwamba niko mle ndani.Inaonekana walikuwa wananifuatilia” akasema Mathew “Mathew” akaita Ruby “Unasemaje Ruby?
“Kuna uwezekano mkubwa hawa watu wanafuatilia mazungumzo yetu ndiyo maana wameweza kujua kama unakwenda kwa Zawadi”akasema Ruby
“Hilo linawezekana Ruby kwa sababu watu waliofahamu kuwa ninakuja kumuona zawadi ni wewe na Dr Fabian”akasema Mathew
“Mathew hawa jamaa
wanakufuatilia na bado hatari
haijakwisha.Hivi sasa watakuwa wanafahamu hospitali ulikompeleka Zawadi na wanaweza wakafika hapo muda wowote kummalizia.Zima simu yako toa laini na uitupe” akasema Ruby.
“Sawa Ruby nitafanya hivyo lakini kuna jambo ninalihitaji.Zungumza na Dr Fabian ninahitaji ulinzi wa kutosha hapa hospitali.Hawa jamaa wanaweza wakafika hapa muda wowote kwa lengo la kummaliza Zawadi.Inaonekana kuna jambo analifahamu ambalo hawataki tulifahamu kutoka kwake.Tunatakiwa kumlinda sana Zawadi” akasema Mathew
“Sawa nitafanya hivyo haraka” akasema Mathew na kukata simu.Hakupoteza muda akaizima haraka haraka akachomoa laini halafu akaenda katika pipa la taka taka akaitupa.
“Ruby yuko sahihi.Hawa jamaa wanafuatilia mazungumzo yetu ya simu ndiyo maana wameweza kujua niko pale nyumbani kwa Zawadi.Tayari nimemuweka Ruby katika hatari kubwa.Nitamshauri kwa siku za karibuni hadi tutakapokuwa tumefanikiwa kulitegua fumbo hili asitoke ndani kwani nyumbani kwake uko ulinzi wa kutosha” akawaza Mathew
Akiwa nje ya chumba cha upasuaji akisubiri upasuaji uliokuwa unaendelea kumuondolea Zawadi risasi katika mguu wake,askari nane wenye silaha wakafika wakitokea katika kituo cha polisi Kichangani wakiongozana na daktari.Mathew alipowaona akasimama wakamfuata
“Mathew Mulumbi?
Akauliza kiongozi wa timu ile ya askari na Mathew akaitika kwa kichwa wakasalimiana
“Pole sana” akasema Yule askari aliyejitambulisha kama Sajenti Linus
“Tumepewa maelekezo
kuja kuimarisha ulinzi mahala hapa”
“Ahsanteni sana kwa kufika.Madaktari wanaendelea na zoezi la kumuondolea risasi Yule dada.Mpaka tutakapopata taarifa kutoka kwao bado mgonjwa yuko katika hatari ya kuuawa”akasema Mathew
“Nani wanaotaka kumuua?
Akauliza Sajenti Linus
“Sifahamu ni akina nani” akajibu Mathew na askari wale wakajipanga vizuri kuzunguka chumba cha upasuaji
*************
Helkopta iliyowabeba Kamishna Jenerali wa magereza Tanzania na mkuu wa gereza la Kimondo ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Safari ya kutoka Arusha ilikuwa ya kimya kimya na hakumueleza
Deus mkuu wa gereza la Kimondo mahala wanakoelekea hadi walipojikuta wakitua jijini Dar es salaam.
“Tumekuja kufanya nini
Dar es salaam? Mbona hakuniambia kama tunakuja Dar es salaam? Inaonekana kuna kikao kizito sana leo lakini sina uhakika kama ni kuhusiana na kile kilichotokea gerezani kwani angekwisha niuliza tayari.Kitendo cha kutouliza chochote kinaashiria hajui chochote hadi sasa” akawaza Deus
Walishuka katika helkopta na kuingia katika gari la
Kamishna Chambao wakaondoka na moja kwa moja wakaelekea nyumbani . “Sikukwambia kama
tunakuja Dar es salaam.Tuna kikao kizito kati ya wakuu wa magereza yote makubwa nchini na mheshimiwa Rais.Kwa sasa tunawasubiri wengine wawasili halafu tutakwenda kuzungumza na Rais.Kwa sasa tupumzike kidogo tupate chakula kisha tutaelekea ofisini”
akasemaKamishna Chambao halafu akaenda chumbani kwake akampigia simu Dr Fabian akamjulisha kwamba tayari amekwisha rejea na alikuwa nyumbani kwake na mkuu wa gereza la Kimondo
***********
Katika hospitali ya Katihar bado hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa madaktari kuhusiana na maendeleo ya Zawadi.Chumba cha upasuaji kilikuwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi.Wakati wakiendelea kusubiri upasuaji umalizike,wakatokea walinzi wa Dr Fabian na kumpa Mathew taarifa kwamba Dr Fabian anamuhitaji haraka sana.Mathew akaagana na Sajenti Linus akampa namba za simu za Rais mstaafu Dr Fabian ili kuwasiliana naye kumpa taarifa za kile kitakachokuwa kinaendelea pale hospitali.
Baada ya kutoka hospitali moja kwa moja Mathew alielekea katika makazi ya Dr Fabian alikokuwa anasubiriwa.
“Mathew pole sana kwa hiki kilichotokea” akasema Dr Fabian baada ya Mathew kuwasili akiwa amechafuka damu.
“Ahsante sana mzee”
“Hakuna mahala wamekujeruhi washenzi hawa? Akauliza Ruby
“Nashukuru mimi
sijaumizwa sehemu yoyote” akasema Mathew na kuwasimulia kwa ufupi kile kilichokuwa kimetokea.Dr Fabian akaenda chumbani kwake akatafuta nguo ambazo zinaweza kumtosha Mathew akapata suruali ya jeans na fulana akamletea
“Nenda kaoge badilisha nguo tunasubiriwa na Kamishna Chambao” akasema Dr Fabian na Mathew akaenda bafuni akaoga na kubadili mavazi.
“Ruby kuna chochote
umekipata zaidi? Akauliza Mathew
“Nilipatwa na mstuko mkubwa nilipopata taarifa za kile kilichotokea kule kwa Zawadi nikaacha kila kitu.Nimeogopa sana” akasema Ruby
“Ruby usihofu mimi nitakuwa salama.Endelea kulichimba suala hili na chochote utakachokipata utatujuliza” akasema Mathew na Ruby akampatia simu nyingine
“Nina laini nyingine tatu za simu hivyo nitaachana na ile niliyotumia kuwasiliana naye na nitatumia laini nyingine.Simu hii tayari ina moja ya laini zangu hivyo utaitumia kwa muda kuwasiliana” akasema Ruby halafu akampatia Mathew faili lililokuwa na picha mbali mbali pamoja na diski mweko
“Kila kitu kuhusu Deus kiko humu” akasema Ruby
Mathew na Dr Fabian wakaingia garini na kuondoka kuelekea kwa Kamishna Chambao
“Sikutegemea kama jambo hili lingekuwa kubwa na la hatari namna hii.Watu hawa ni akina nani? Kitu gani wanakificha kisijulikane? Akauliza Dr Fabian
“Kwa namna mambo yao wanavyoyafanya wanaonekana ni mtandao mkubwa na waliojipanga vyema katika kuhakikisha mambo yao hayakwami wala kujulikana.Wako makini sana kuhakikisha wanafuatilia kila kitu kinachoweza kuwaletea madhara hata kama ni kidogo sana.Wako tayari na wana uwezo wa kumuondoa mtu yeyote ambaye ni kikwazo kwao hata kama ni mkubwa na ana nguvu kiasi gani.These people thay can do anything.They’re very dangerous” akasema Mathew na Dr Fabian akaonekana kuanza kuwa na wasiwasi kufuatia maneno ya Mathew
“Mzee nashauri ulinzi ungeimarishwa zaidi pale nyumbani na asiruhusiwe mtu yeyote asiyejulikana au kuwa na miadi maalum kuingia ndani na…….” akasema Mathew na kunyamza kidogo
“Kwa muda huu ambao
bado tunaendelea kuwatafuta hawa watu ni akina nani nashauri Ruby angeendelea kubaki ndani hadi hapo tutakapopata ufumbuzi wa sakata hili” akasema Mathew na Dr Fabian akakohoa kidogo
“Ni wazo zuri hilo.Tayari naye amekwisha ingia katika hatari lakini nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kumlinda.Sintakubali Ruby aingie katika hatari” akasema Dr Fabian na ukimya ukapita
“Mathew kwa muda mrefu umekuwa unakabiliana na mambo haya na una uzoefu wa kutosha.Unadhani hili ni jambo la kigaidi? Akauliza Dr
Fabian
“Kwa mtiririko wa mambo unavyokwenda hakuna dalili za watu hawa kuwa ni mtandao wa kigaidi.Hawa ni watu waliojipanga
vizuri,wenye mafunzo na mtandao mpana.Tumuombee Zawadi apone naamini anafahamu mambo ambayo yanaweza yakatusaidia kutafuta ufumbuzi wa sakata
hili.Ukifuatilia sakata hili
linamuhusu Naomi Bambi na Zawadi ndiye aliyetajwa na Lidya kwamba ana taarifa za kuhusiana na Naomi Bambi” akasema Mathew
“Kitu ninachojiuliza kwa nini mpaka sasa yuko hai? Kwa nini hawajaweza kumuua? Wengine wote waliokuwa na mahusiano na uchunguzi aliokuwa anaufanya Lidya waliuawa” akauliza Dr Fabian
“Nadhani ni kwa sababu hajawahi kufungua mdomo wake kusema chochote kuhusu Naomi.Ni Lidya pekee ambaye alihitaji kuzungumza naye amuhoji kuhusu Naomi lakini kwa bahati mbaya hakufanikisha lengo lake aliuawa kabla hajakwenda gerezani kumuhoji Zawadi nadhani hiyo ni sababu ambayo imemfanya zawadi aendelee kuwa hai mpaka sasa kwani hakuonekana kuwa ni
hatari kwao.Baada ya kugundua kwamba unamfuatilia ndipo wakaamua kumuua kwani tayari alianza kuonekana kuwa kikwazo kwao” akasema Mathew
Walifika nyumbani kwa Kamishna Chambao wakakaribishwa sebuleni.Kamishna Chambao akafahamishwa kuhusu kuwasili kwa wageni akamuacha Deus katika chumba cha mapumziko na kwenda sebuleni.
“Karibuni sana.Nashukuru nimerejea salama na kama mko tayari tunaweza kwenda kuanza kazi”akasema Kamishna Chambao na Mathew akawaeleza namna mpango mzima utakavyokuwa.Mathew na Dr Fabian wakatangulia katika gari na baada ya dakika chache Kamishna Chambao na Deus nao wakatokea,mlango wa gari walilokuwamo Mathew na DrFabian ukafunguliwa na Deus akapiga saluti kikakamavu na kumsalimia kisha wakaingia garini na kuondoka.Bado Deus hakujua wanakoelekea.Uwepo wa Dr Fabian ulizidi kumchanganya
“Kitu gani kinaendelea hapa? Huyu rais mstaafu ana kitu gani na sisi? Au ni yeye ambaye tunazungumza naye? Lakini mbona yeye ni mstaafu? Deus akajiuliza maswali akakosa majibu
“Naiomba simu yako”Mathew akamwambia Deus
“Nini? Akauliza Deus kwa
sauti ya ukali
“Do it Deus” akasema Kamishna Chambao
“Afande nini kinaendelea?kwa nini nimpe smu yangu? Akauliza Deus
“Deus fanya kama ulivyoelekezwa.Mpe simu yako ! That’s an order ! akafoka
Kamishna Chambao na Deus akampa Mathew simu yake akaizima na kuichomoa betri
“Kamishna nawe pia naomba uzime simu yako na toa betri” akasema Mathew na Kamishna akafanya kama vile alivyoelekezwa
“What’s going on here? Akajiuliza Deus.Aliingiwa na hofu kubwa
“Mbona sielewi kinachoendelea.Tangu amekuja Arusha, Kamishna simuelewi elewi.Alinichukua katika helkopta na kunileta Dar es salaam bila kunijulisha kama tunakuja huku.Ameniambia kuna kikao kazi na Rais lakini sioni dalili zozote za kikao na badala yake ametokea Rais mstaafu.Kama haitoshi amechukua na simu yangu akaizima.Nini kinaendelea hapa? Bado Deus aliendelea kujiuliza
Mathew tayari alikwisha toa maelekezo kwa dereva hivyo safari ikawa ya kimya kimya hadi walipofika nyumbani kwake.Akaziandika namba za simu za Victor katika simu aliyopewa na Ruby akampigia na kumtaka afungue geti.Magari yakaingia ndani kisha Mathew akawaongoza Dr
Fabian,Kamishna Chambao na Deus kuelekea ndani.Walinzi wa Dr Fabian wakabaki nje.Mathew aliwataka wabaki sebuleni kwa muda akaenda kuandaa chumba kwa ajili ya mahojiano na baada ya muda akarejea na kuwataka wamfuate hadi katika chumba alichokuwa
amekiandaa.Kulikuwa na meza yenye viti viwili halafu pembeni kukawa na viti vingine viwili akawataka Dr Fabian na Kamishna Chambao waketi halafu akamuelekeza Deus kuketi katika kiti kilichoko mezani.Mathew akawasha kifaa Fulani na kukipitisha mwilini kwa Deus akijaribu kuhakiki kama hana kifaa chochote mwilini ambacho kinaweza kuwa kinamuonyesha mahala alipo.Baada ya kuridhika kwamba hana kifaa chochote Mathew akamtazama na kusema
“Kamishna msaidizi wa magereza Deus Mtege na mkuu wa gereza la Kimondo” akasema Mathew
“I don’t understand what’s going on here.Kamishna nini hiki kinaendelea?Who is this guy? Ananifahmu mimi ni nani? Akauliza Deus kwa ukali
“Naitwa Mathew Mulumbi ninashughulika na usalama wa taifa ! akasema Mathew
“Nataka kufahamu kwa
nini niko hapa? Akauliza Deus “Deus usihofu kuna maswali machache utaulizwa” akasema Kamishna Jenerali Chambao
“Kamishna umenileta Dar es salaam ukidai kuna kikao na
Rais.Hiki ndicho kikao na Rais? Akauliza Deus
“Deus nitakuuliza mawasli na ninaomba unijibu kwa ufasaha.Endapo utashindwa kuonyesha ushirikiano nitalazimika kutumia nguvu .Naomba tusifike huko katika hatua ya matumizi ya nguvu kwani si hatua nzuri kwa mtu mwenye heshima kubwa kama wewe” akasema Mathew
“Nini kimetokea gerezani
Kimondo siku ya leo? Akauliza Mathew
“Hakuna chochote
kilichotokea.Kila kitu kiko kawaida” akajibu Deus
“Una hakika kila kitu kiko sawa? Akauliza Mathew
“Ndiyo.Kwani vipi? Kamishna umekuja gerezani ukajionea hali halisi” akasema Deus.Mathew akafungua faili akatoa picha na kuiweka mezani
“Unamfahamu huyu mtu?
Akauliza Mathew na sura ya Deus ikaonyesha mstuko mkubwa.Alibabaika akashindwa kujibu
“Deus nakuuliza unamfahamu huyu mtu?
“H..hh ..hapana simfahamu” akasema Deus
“Good” akasema Mathew
“Naamini hakuna mfungwa anayeingizwa gerezani bila wewe kuwa na taarifa”
“Ndiyo” akajibu Deus
“Huyu mtu pichani
anaitwa Adili Mpipe au jina maarufu Kishada.Ni jambazi sugu na amekuwa anatafutwa na jeshi la polisi Tanzania kwa kuhusika katika matukio mengi ya ujamabazi wa kutumia silaha hapa nchini vile vile kuhusika katika mauaji.Mtu huyu jana ameingizwa katika gereza la Kimondo kama mfungwa wakati hakuna mahakama yoyote iliyomuhukumu kifungo.Una taarifa hizo? Akauliza Mathew na Deus akazidi kubabaika.Matone ya jasho yalionekana usoni pake.
“Unalifahamu jambo hili
Deus? Akauliza kamishna Chambao
“Hakuna kitu kama
hicho.Jambo hilo haliwezekani kabisa. Mfungwa yeyote anayeingia gerezani lazima awe amehukumiwa kifungo na mahakama” akasema Deus
Mathew akawasha
kompyuta na kuichomeka ile diski mweko na ikatokea video ikimuonyesha Kishada namna
alivyoingia gerezani kama mfungwa.Deus midomo ikamtetemeka.
“Huyu jamaa alitumwa kwa kazi moja ya kumuua mfungwa anaitwa Gosu Gosu ambaye anatumikia kifungo cha maisha gerezani.Alikuwa na sindano yenye sumu kali ambayo angeitumia kumuua Gosu Gosu lakini kwa bahati nzuri lengo lake halikuweza kufanikiwa kwani Gosu Gosu alipambana naye na kumuua” Mathew akanyamaza na kumtazama Deus
“Bado unakataa kwamba
jambo hili halijafanyika katika gereza la Kimondo? Akauliza Mathew Deus hakujibu kitu
“Deus umeulizwa swali jibu ! akasema kwa ukali Kamishna Chambao
“Kamishna hayo yote si kweli ! akasema Deus na Kamishna Chambao akapandwa na hasira
“Unathubutuje kusema hili jambo si la kweli wakati kuna kila ushahidi wa kuonyesha limefanyika? Deus nitamuamuru Mathew atumie nguvu ili uweze kusema ukweli.Vile vile naomba nikuweke wazi kwamba kwa hiki ulichokifanya ni kosa kubwa,nitakufukuza kazi na haitaishia hapo utafunguliwa mashitaka na utafungwa kifungo kirefu gerezani.Kwa nini umekubali kuharibu maisha yako Deus? Kwa nini unataka kuiacha familia yako ikiteseka? Tueleze ukweli na ninakuhakikishia jambo hili litabaki ndani ya chumba hiki na utaendelea na maisha yako kama kawaida” akasema Kamishna Chambao.Deus akainamisha kichwa alionekana kuzama mawazoni
“Deus nafahamu jambo
hili hukulifanya peke yako.Nataka kuwafahamu watu unaoshirikiana nao katika kuandaa jambo hili la kumuingiza jambazi Kishada gerezani na mipango yote ambayo imekuwa ikiendelea ya kumuua mfungwa anaitwa Papi Gosu Gosu” akasema Mathew na Deus akainamisha kichwa
“Deus naomba
nikuhakikishie kwamba kama hautaamua kujisaidia wewe mwenyewe hakuna mwingine atakayekusaidia na usinilazimishe nikatumia nguvu kwani ni hatua mbaya sana.Tueleze ukweli na kama alivyosema Kamishna kwamba ukitueleza ukweli jambo hili litabaki humu ndani na halitafahamika nawe utaendelea na maisha yako kama kawaida” akasema Mathew.Bado Deus aliendelea kuwa kimya
“Deus suala hili linalokukabili ni suala baya.Sikushauri ukakubali jambo hili likavuka kuta za nyumba hii kwani ukikataa kutoa ushirikiano na kueleza ukweli hakutakuwa na namna nyingine zaidi ya kulifikisha jambo hili katika vyombo husika na kwa ushahidi huu uliopo hautakwepa kifungo kirefu gerezani.Umepewa nafasi itumie vyema.Tueleze ukweli.Nani unashirikiana nao katika jambo hili? Akauliza Dr Fabian
Zilipita sekunde karibu hamsini za ukimya na Kamishna Jenerali Chambao akasema kwa ukali
“Deus mbona umegeuka bubu? Huna kitu cha kusema? Akauliza.Deus akainua uso wake na kusema “Sifahamu chochote !
“Kwa kauli hiyo umenilazimisha kufungua sura ya pili” akasema Mathew na kuinama akavuta boksi la chuma akaliweka mezani na kulifungua.Lilikuwa na zana mbali mbali za kutesea.Wakati Mathew akiandaa zana za kutesea Deus akaibinua meza na kupata upenyo akataka kukimbia,Mathew aliyeanguka chini akamuwahi na kumkata mtama akaanguka.Deus alikuwa mtu wa mazoezi akainuka haraka sana na kuinua kiti akamrushia Mathew akakipangua na kumfuata Deus mlangoni alipokuwa anajaribu kuufungua
mlango.Akamtandika teke zito lililomfanya apepesuke kabla hajakaa sawa akapigwa tena teke lingine kali la tumbo akaanguka chini.Mathew akamfuata na kumvurumishia ngumi mfululizo na ndani ya sekunde chache tayari mdomo wake ulijaa damu.
“Mathew imetosha ! akasema Dr Fabian.Mathew akamuinua Deus
“Nilikwambia kwamba awamu hii hautaipenda! Akasema Mathew na kumtandika tena kichwa Deus akaanguka chini.Mathew akachukua pingu na kumfunga mikono halafu akamuinua na kumkalisha kitini.Akachukua mashine Fulani akaichomeka katika umeme akagusanisha vyuma viwili vikatoa cheche.Kamishna Jenerali akavua miwani.Alionekana kuingiwa na hofu
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho utatueleza ukweli? Akauliza Mathew lakini Deus hakujibu kitu aliendelea kububujikwa damu mdomoni Mathew akamgusa
shingoni na vile vyuma viwili
Deus akatoa ukelele mkubwa
“Nani unashirikiana nao? Akauliza Mathew
“Nitasema !! Nitasema ! akasema Deus
“Haya sema haraka sana” akasema Mathew na Deus akavuta pumzi ndefu
“Nani unashirikiana nao? Akauliza Mathew
“Siwafahamu !
“Deus nilikuonya kwamba sitaki mchezo” akasema Mathew na kugusanisha tena ncha za vile vyuma cheche zikatoka
“Nitasema ! Usinichome tena nitasema ! akasema Deus akitetemeka kwa woga
“Eleza kila kitu ! akasema Kamishna Jenerali Chambao
“Siwafahamu watu hao ! akasema Deus na sura ya Mathew ikajikunja kwa hasira akainuka
“Ninasema kweli naomba unisikilize ! akasema Deus
“Endelea lakini tafadhali naomba usifanye mchezo na mimi ! akafoka Mathew.Deus akavuta pumzi ndefu na kusema
“Simfahamu huyo mtu !
“Kwa nini usiwafahamu wakati unashirikiana nao? Akauliza kwa ukali Kamishna Chambao
“Kamishna tumpe nafasi ajieleze” akasema Mathew “Kuna mtu huwa
ananipigia simu na kunitishia na kunilazimisha nifanye vile atakavyo” akasema Deus na kunyamaza akavuta pumzi ndefu
“Hujawahi kuonana naye
ana kwa ana? Akauliza Mathew
“Hapana sijawahi kuonana naye ana kwa ana ! akajibu
“Inawezekanaje mtu akakuamuru ufanye kitu kama hiki wakati hamjawahi kuonana? Deus tafadhali usitufanye sisi watoto wadogo”akauliza Kamishna Chambao
“Nasema ukweli Afande”
“That’s impossible ! akafoka Kamishna Chambao
“Deus kama umeamua
kutueleza ukweli tafadhali sema ukweli wote vinginevyo utakuwa unajidanganya na kulifanya jambo hili lizidi kuwa gumu zaidi” akasema Mathew
“Naombeni mnielewe
jamani sijawahi kukutana na mtu huyo,tumekwa tukiwasiliana kwa simu na ananipa maelekezo”
“Nini hasa ambacho mtu huyo anakihitaji ukifanye?
“Anataka.;…” Deus akanyamaza.
“Anataka GosuGosu auawe”
“Kuna wafungwa wengi gereza la Kimondo.Amewahi kukwambia kwa nini Gosu Gosu peke yake auawe? Akauliza Mathew
“Hapana hajawahi
kunieleza” akajibu Deus “Kwa nini ukakubali kutekeleza maagizo ya mtu usiyemfahamu? Akauliza Mathew na Deus akawa kimya
“Deus eleza tafadhali.Umedai mtu huyo haujawahi kuonana naye ila amekuwa akikupigia simu na kukupa maelekezo.Kwa nini ukakubali kutekeleza maelekezo yake.Is he payig you money? Akauliza Mathew “Hapana hanilipi pesa”
“Kama hakulipi kwa nini ukakubali kufanya mambo haya ya hatari kabisa ambayo yanaweza kukufikisha sehemu mbaya?
“Because I had no choice ! akasema Deus kwa ukali
“Please Deus tell us the real reason ! akasema Dr Fabian.Deus alikuwa anatetemeka midomo na uso wake uliloa jasho.
“Deus ! akasema Mathew
“They have a video..oh my God ! akasema Deus na kuinamisha kichwa
“What video? Akauliza
Mathew na Deus akainua kichwa akamtazama Kamishna Jenerali Chambao
“Kamishna utanisamehe sana mzee wangu ! akasema Deus akimtazama Kamishna Chambao
“Deus nimekuhakikishia kwamba ukitueleza ukweli wote bila kutuficha nitakusamehe na jambo hili
litabaki kati yetu sisi tuliomo humu ndani.Tunataka kumfahamu mtu huyo ambaye umekuwa unawasiliana naye” akasema Kamishna Chambao “Mzee naomba unisamehe
tafadhali”
“Deus eleza ukweli na utasamehewa kama alivyoahidi Kamishna” akasema Mathew.Deus akavuta pumzi ndefu na kusema
“Mzee nimekuwa katika mahusiano na mke wako.Naomba unisamehe mzee ! akasema Deus
Taarifa ile ilipenya kwa kasi masikioni mwa Kamishna jenerali Chambao akainuka na kuanza kumsogelea Deus “Unasemaje Deus? Akauliza Mathew
“Nimekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa Kamishna” akasema Deus na kamishna akainua kiti alichokuwa amekalia akataka kumpiga nacho lakini Mathew akawahi kumzuia.Wakati Mathew akimzuia Kamishna Jenerali Chambao akaichomoa bastora ya Mathew aliyokuwa ameichomeka kiunoni akamnyooshea Deus.Mikono
ilikuwa inamtetemeka kwa
hasira
“Nataka urudie kutamka kile ulichokitamka muda mfupi uliopita ! Tamka kwa sauti masikio yangu yasikie ! akasema Kamishna Chambao
“Kamishna tafadhali weka chini silaha yako ! akasema Mathew
“Nataka huyu shetani arudie kutamka kile alichokitamka ! akasema kwa hasira Kamishna Chambao
“Nisamehe Kamishna ! Ni shetani tu alinipitia ! akasema Deus huku akitetemeka kwa woga
“Sir please put your gun down ! You don’t have to do this.We need him alive ! akasema Mathew
“I don’t care ! Yaani Deus unaweza ukanifanyia mimi hivi? Akauliza Kamishna Chambao
“Nimekutunza kama
kijana wangu,nimekupigania hadi umefika hapa ulipofika na nilikuwa na mipango ya kukusaidia ufike mbali zaidi lakini kwa yote niliyokufanyia haya ndiyo malipo yake? Akauliza kamishna Chambao.Deus alikuwa anatetemeka akiwa amefumba macho.
Dr Fabian aliyekuwa amesimama nyuma ya Kamishna Chambao akanyata taratibu na Kuukamata mkono wa Chambao uliokuwa na bastora akauinua juu.Kwa kasi ya ajabu Mathew naye akamfuata Chambao na kumnyang’anya ile bastora halafu akasaidiana na Dr Fabian Kelelo kumtoa
Kamishna Chambao mle ndani
Mathew akamtaka Dr Fabian ampeleke katika chumba cha mapumziko yeye akabaki na Deus
“Deus tumebaki wawili naomba unieleze ukweli wote bila kunificha hata kitu kimoja.Kwa sasa mimi ndiye msaada wako pekee.Ni kweli una mahusiano na mke wa Kamishna Jenerali Chambao” akasema Mathew na Deus akashusha pumzi
“Ndiyo nina mahusiano ya kimapenzi na mke wa Kamishna Chambao”akajibu
Deus
“Ilikuaje Deus ukaingia katika mahusiano na mke wa
kiongozi wako? Akauliza Mathew
“Haikuwa ridhaa yangu lakini nilishawishiwa nikajikuta nikianguka dhambini na kuanza kutembea na mke wa Chambao.Najutia sana jambo hili”
“Ilikuaje mkajikuta mkianzisha mahusiano na mke wa Chambao? Mathew akauliza.Deus akanyamaza kidogo halafu akasema
“Mke wa Kamishna
Chambao ana kampuni yake ambayo imechukua tenda ya kusambaza baadhi ya vitu katika baadhi ya magereza hapa chini likiwemo gereza la Kimondo hivyo alikuwa akifika mara kwa mara nikajikuta nikizoeana naye tukaanzisha mahusiano.Ni yeye aliyenishawishi hadi tukaanzisha mahusiano” akasema Deus
“Mahusiano yako na mke wa Kamishna Chambao yana mahusiano gani na hiki kilichotokea gerezani? Akauliza Mathew
“Siku moja nilitumiwa video iliyonionyesha nikifanya mapenzi na mke wa Kamishna.Hapo ndipo mambo yote yalianzia” akasema Deus
“Ulitumiwa video? Nani alikutumia?
“Huyo jamaa
ninayewasiliana naye”
“Uliuchunguza ni video halisi au ilitengenezwa kwa lengo la kukutia hofu? “Haikuwa imetengenezwa
ni halisi”
“Nini kikafuata baada ya kutumiwa video hiyo?
“Nilimuuliza mtumaji kama anahiaji fedha akasema hahitaji fedha ila kuna kazi anataka niifanye na akanipa angalizo kwamba endapo nitapuuza au kumweleza mtu yeyote basi wataisambaza video ile mtandaoni.Sikuwa tayari kwa aibu hivyo nikakubali kufuata maelekezo aliyokuwa ananipa”
“Ni muda gani ameanza kukupa maelekezo ?
“Mara tu Gosu Gosu
alipoletwa gerezani.Alitaka auawe hivyo nikawatumia kikundi Fulani cha wafungwa kutekeleza mpango huo lakini ikashindikana kwani Gosu Gosu aliweza kupambana nao akawashinda na kuwaumiza vibaya sana.Baada ya hapo ndipo akataka nimuingize gerezani Adili Mpipe kama mfungwa ili afanye kazi ya kumuua Gosu Gosu kwa sumu lakini naye akazidiwa nguvu na Gosu Gosu akamuua” akasema Deus
“Amewahi kukutajia jina lake huyo mtu? Mathew akauliza
“Hapana hajawahi
kunitajia jina lake wala mahala aliko” akajibu Deus
“Kitu gani kingine alikuelekeza ukifanye ukiacha mpango wa kumuua Gosu Gosu?
“Baada ya kumuua
Adili,Gosu Gosu aliichukua laini ya simu ya Adili akaificha na alichonielekeza ni kuhakikisha laini hiyo ya simu inapatikana haraka sana na akanielekeza nimpeleke Gosu Gosu katika nymba Fulani maeneo ya kikatiti ambako ningemkabidhi kwa watu wamtese ili aeleze mahala alikoiweka hiyo laini ya simu.Nilifuata maelekezo yake nikampeleka Gosu Gosu mahala hapo akateswa sana lakini hakuonyesha ,mahala
ilipo laini ya simu ya Adili” akasema Deus “Nimekueleza ukweli mtupu bila kuficha hata neno mja.I need your help.Hawa jamaa wanaweza wakaniua au wakaidhuru familia yangu.Please help me ! akasema Deus
“Deus ahsante kwa kunieleza ukweli.Pamoja na kunieleza ukweli lakini bado haitoshi.Nitakutaka utusaidie tuweze kumfahamu na kumpata huyo mtu aliyekuwa anawasiliana nawe na kukupa maelekezo ya kumuua Gosu Gosu.Kumpata mtu huyo ndiyo njia pekee ya kuweza kukuondoa katika kifungo alichokufunga.Je upo tayari kushirikiana nasi kumtafuta huyo mtu aliyekuwa
anawasiliana nawe? Akauliza Mathew
“Niko tayari kusaidia kumsaka huyo mtu ambaye amenisababishia nikafanya mambo kama haya ambayo tayari yameniweka katika matatizo makubwa”akasema Deus
“Ahsante kwa maamuzi hayo” akasema Mathew na kutoka ndani ya kile chumba akaenda katika chumba cha mapumziko akawakuta Dr Fabian na kamishna Jenerali Chambao.Alipomuona Mathew akasimama
“Mathew why you took that gun? Ungeniacha nimfumue Yule shetani.Kwa nini akanifanyia hivi? Amefika hapa alipofika kwa sababu yangu lakini badala yake ananifanyia haya? Deus anadiriki kutembea na mke wangu kweli? Akauliza kamishna Chambao. Mathew akamfuata akamshika mkono na kumuomba aketi kitini
“Bado siamini jambo hili” akasema Chambao
“Kamishna kwanza nikupe pole kwa jambo hili ambalo limetustua wote.Hakuna aliyelitegemea.Nimezungumza na Deus amenieleza ukweli” akasema Mathew na kuwaeleza akina Dr Fabian na Chambao kila kitu alichoelezwa na Deus
“Kwa maelezo haya ya
Deus kuna kitu nimekihisi”
Akasema Mathew
“Unahisi kitu gani
Mathew? Akauliza Dr Fabian
“Huu unaonekana ni mpango uliopangwa. Deus anadai kwamba ni mke wa Kamishna ndiye aliyemshawishi hadi akajikuta akiingia katika mahusiano naye.Kuna kitu ninakiona hapa.Kuna uwezekano naye akawa alitumiwa na watu hao kwa ajili ya kumuingiza mtegoni Deus halafu wakarekodi ile video kwa ajili ya kuitumia kumfanya Deus afanye kile wanachokitaka” akasema Mathew
“Mathew you are not serious. Mke wangu hawezi kujihusisha na watu hawa. That’s impossible ! akasema Kamishna Chambao kwa ghadhabu
“Kwa hawa jamaa kila kitu kinawezekana Kamishna” akasema Dr Fabian
“Mheshimimiwa Rais mke
wangu hawezi katu kujihusisha na watu hao.Ni mfanya biashara nimemfungulia kampuni kubwa na kumtafutia masoko ya uhakika,ana pesa ya kutosha na katu hawezi akajihusisha na mtandao wa watu hawa ! Amenisaliti lakini katika suala hili ninaweza kusimama kumtetea.Hawezi akashirikiana na hao watu ! Bado nataka nikamfundishe adabu Yule mshenzi !!
akasema kwa hasira Kamishna Chambao
“Mzee naomba unisikilize tafadhali ! akasema Mathew
“Mathew sitaki maneno yoyote ya kutaka kumtetea
Yule jamaa kwa kitu alichonifanyia! Akasema Chambao
“Baada ya kutueleza ukweli wote,Deus anakuwa ni mmoja wa watu wetu wa muhimu sana kwani tayari ana mawasiliano na hawa watu tunaowatafuta.Ninataka kumtumia katika kuwatafuta watu hao na yeye yuko tayari kutoa ushirikiano kwa sababu yuko katika kifungo cha hawa jamaa” akasema Mathew
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment