Search This Blog

Friday 7 April 2023

SCANDLE (KASHFA) (2) - 2

   

Simulizi : Scandle (Kashfa) (2)

Sehemu Ya Pili (2)


amenusurika tena ! akasema Kasiano


“Again ?! akauliza Rita


“Sifahamu kwa nini mtu mmoja amekuwa akituumiza vichwa kiasi hiki.Kila pale tunapomuingiza katika mtego wetu anaponyoka.Huyu mtu lazima atakuwa anatumia ulozi si bure.Mara mbili amenurika katika mabomu tuliyomtegea.What kind of a man is he? Akauliza kwa ukali Kasiano.Ukapita ukimya halafu Rita akasema


“Darling this man Mathew


Mulumbi,he’s not who we think he is.Ni zaidi ya vile tunavyomdhania.Safari hii tumekutana na mtu wa tofauti na hivyo hata mbinu za kumtafuta lazima ziwe za tofauti pia” akasema Rita


“Rita siamini kama anaweza akatokea mtu mmoja akatuchezea kiasi hiki.I swear we must find him,we must show him who we are ! akafoka Kasiano na kuichukua tena simu akampigia Paul Lewis


“Hallow bosi” akasema Paul


“Paul imetokeaje hadi Mathew Mulumbi akatuponyoka tena? “Samahani kwa hilo bosi” akasema Paul


“Paul yawezekana


mnalichukulia kirahisi sana suala hili.Mathew Mulumbi is very dangerous and if we’re not serious he’ll take us down !


“Samahani sana bosi nakuahidi haiwezi kutokea tena wakati mwingine” akasema Paul.Kasiano alikuwa amefura kwa hasira


“Mmefikia wapi kuhusu mkuu wa jeshi la polisi? Akauliza Kasiano


“Tumedukua simu yake na kufuatilia mazungumzo yake ya siku ya jana amewasiliana na watu wengi lakini kuna kitu kimetupa wasi wasi kidogo.Alipigiwa simu na Rais akamuita ikulu.Baada ya simu ile ya Rais simu iliyofuata aliyoipiga mkuu wa jeshi la polisi ni kwa kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam akitaka mtuhumiwa Mathew Mulumbi ahamishwe kupelekwa katika gereza la Uwangwa na shughuli zote za kumuhoji zitafanyika wakati mtuhumiwa akiwa gerezani.Baadae IGP alimuandikia Rais ujumbe kuwa safari imeanza bila kufafanua ni safari ipi lakini ukiangalia muda ambao ujumbe huo ulitumwa unaendana na muda ambao Mathew Mulumbi aliondolewa pale kituoni.Ni IGP aliyempigia tena simu Rais na kumfahamisha kuhusu kutokea kwa shambulio katika daraja la Nyerere na Mathew Mulumbi kutoroshwa.Rais akaagiza kila juhudi zifanyike kuhakikisha Mathew anapatikana.Simu nyingine zilizofuata ni za kawaida kwa makamanda wa polisi kuwasisitiza ufanyike uchunguzi wa kina na kubaini nani waliofanya shambulio lile.Hapo ndipo tulipofikia bosi” akasema Paul na Kasiano akashusha pumzi


“Ahsante sana Paul walau kidogo joto langu limeshuka kwa hiyo taarifa.Nini mawazo yako katika hayo mliyoyagundua? Akauliza


Kasiano


“Ukiifuatilia taarifa hii utaona kwamba IGP aliitwa ikulu akaenda kuonana na Rais na baada ya hapo ndipo maelekezo ya kuhamishwa Mathew Mulumbi yalipotolewa.Kama haitoshi bado IGP alimtaarifu Rais kwa njia ya ujumbe kuwa safari imeanza.Mwisho akamjulisha kwamba limetokea shambulio.Hizi ni picha ambazo ukiunganisha unaweza ukapata picha kwamba maelekezo ya kuhamishwa kwa Mathew Mulumbi inawezekana yalianzia huko juu lakini bado hatuna uhakika hivyo tunatakiwa kupata uhakika nani aliyempa IGP maelekezo ya kumuhamisha Mathew Mulumbi? Hapa picha inaonyesha ni Rais lakini lazima tuwe na uhakika” akasema Paul


“Paul ahsante sana kwa hatua hii kubwa.Walau kwa sasa tunaanza kuuona mwangaza wa jambo hili.Ahsanteni sana black Mafia kwa kazi kubwa.Japo kuna wakati tunashindwa lakini kwa hili mlilolifanya mmenifurahisha.Endeleeni kuchimba zaidi nitawasiliana nawe tena baada ya muda” akasema Kasiano na kukata simu


“Walau kidogo matumaini yanarudi” akasema Kasiano na kumueleza mkewe kile alichoelezwa na Paul halafu akachukua simu na kumpigia mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai David Chamwino.


“Hallo Kasian” akasema David


“David umelala?


“Ndiyo mkuu tayari nilikuwa usingizini.Kuna taarifa gani?


“Amka David huu si wakati wa kulala.Kuna watu wanataka kutunyang’anya ugali wetu hivyo lazima tupambane nao kuhakikisha hakuna anayethubutu kuchezea chakula chetu.Kuna mambo matatu.Kwanza Mathew ameponyoka kwa mara nyingine tena usiku huu hivyo hatujampata.Pili nataka kufahamu kama ulizungumza na Dr Fabian kama tulivyokuwa tumepanga”


“Ndiyo


Kasian.Nilizungumza naye na hakuweza kutoa ushirikiano wowote hata pale nilipomwambia kwamba nitamsaidia kumuondoa katika suala lile.Nilimpigia simu Paul nikamweleza jambo hilo”


“Sawa endelea na taratibu zako na hakikisha anafikishwa mahakamani.Jambo la tatu ambalo nataka kukwambia ni ule wasi wasi wa Rita kuhusu uharaka wa kumuhamisha Mathew Mulumbi.Black Mafia wamefuatilia na kugundua kwamba IGP aliitwa ikulu na baada ya hapo ndipo maelekezo ya kumuhamisha Mathew yalipotolewa.Baadae mkuu huyo wa jeshi la polisi alimtumia rais ujumbe mfupi akimjulisha kwamba safari imeanza na hapa tunaamini ni safari ya kumuhamisha Mathew kwani muda ulipotumwa ujumbe huo haupishani sana na muda ambao Mathew Mulumbi


aliondolewa kituo cha polisi kupelekwa gereza la


Uwangwa” akasema Kasiano


“Kwa hiyo maelekezo ya kumuhamisha Mathew kumpeleka gerezani yalitolewa ikulu? Akauliza David


“Bado hatuna uhakika kama maagizo hayo yalitoka ikulu lakini ukifuatilia


utagundua kwamba IGP


Yeremia alitoa maelekezo ya kumuhamisha Mathew baada ya kutoka ikulu ambako alikwenda kuonana na Rais.Tunachohitaji kwa sasa ni kupata uhakika kama kweli maelekezo hayo yalitoka ikulu.David I’m going to need your help” akasema Kasiano


“Anything you need


Kasiano” akasema David “Wewe umekuwa ndani ya jeshi la polisi kwa muda mrefu na mambo mengi unayafahamu.Je unafahamu kitu chochote ambacho tunaweza kukitumia ili kumfanya IGP atueleze ukweli maelekezo ya kumuhamisha Mathew Mulumbi yalitoka wapi?Nataka tusitumie nguvu katika suala hili bali tutafute jambo lolote la siri linalomuhusu IGP na tumtishie kwamba tutalianika hadharani kama asipokubali kutueleza ukweli nani alimpa maelekezo ya kumuhamisha Mathew Mulumbi.Nafahamu watu wakubwa kama huyu hawawezi kukosa siri.Do you know anything? Akauliza Kasiano.Ukapita ukimya mfupi halafu David akasema


“Ninazifahamu siri zake chache” akajibu David


“Good.Tell me ! akasema Kasiano


“Miaka minne iliyopita kabla Yeremia hajawa mkuu wa jeshi la polisi,ilitokea kashafa moja kubwa baada ya wafanya biashara wawili wa madini ya vito raia wa Kenya walipouawa na askari wakidaiwa kuwa ni majambazi na ikadaiwa kwamba walikutwa na bunduki ya kivita aina ya AK47 pamoja na silaha nyingine na kiasi cha shilingi milioni hamsini za kitanzania.Ndugu za marehemu hao walikuja juu na kudai kwamba ndugu zao waliouawa hawakuwa majambazi bali walikuwa ni wafanyabiashara wa madini na ushahidi mkubwa ukatolewa.Mimi ndiye niliyetumika kulimaliza sakata lile.Ukweli ni kwamba wale jamaa hawakuwa majambazi.Walikuwa ni wafanya biashara na walipouawa walikutwa na kiasi kikubwa cha fedha kipatacho shilingi bilioni tisa na milioni mia tano hamsini na nane.Fedha hiyo yote ilichukuliwa na kugawanywa kwa askari walioshiriki tukio lile na wengine hivi sasa wamekwisha acha jeshi na ni matajiri wakubwa.Yeremia wakati huo alikuwa ni kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam alichukua kiasi cha shilingi bilioni nne ambazo alizihifadhi katika akaunti ya siri ya mke wake nje ya


nchi.Hii ni moja ya siri zake kubwa ambazo ninazifahamu.Siri nyingine ni kwamba ana mtoto wa nje ya ndoa ambaye aliwahi kuhusika katika mauaji.Ulitokea ugomvi katika klabu akampiga mtu risasi akamuua.Yeremia aliniomba nilimalize suala hilo na mtuhumiwa akaachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi.Nadhani kwa mambo hayo mawili endapo akitishiwa kuwa yataanikwa hadharani lazima ataeleza kama Rais anahusika katika suala hili la


Mathew Mulumbi” akasema David


“Ahsante sana David lakini Yeremia anaonekana ni mtu wako wa karibu sana kiasi cha kukushirikisha katika masuala yake nyeti kabisa.Huwezi kutafuta namna ya kumshawishi akakueleza kama kuna kitu anakifahamu kuhusu kutoroshwa kwa Mathew Mulumbi? Kasiano akauliza


“Kwa sasa mahusiano yetu si mazuri sana baada ya kugundua nina mahusiano na


mwanae wa kwanza ambaye naye ni askari polisi.Hakulipenda hilo na niko hapa katika nafasi hii kwa sababu ninazifahamu siri zake vinginevyo angekwisha niondoa zamani sana” akasema David


“Sawa David taarifa ulizotupa zinatosha sana.Tunaomba utupate jina la mke wake na benki alikohifadhi hizo fedha ili tuanze kuzifuatilia usiku huu huu” akasema Kasiano kisha wakaagana.


“Tunaanzisha vita mpya na


dola.Tunaanza na mkuu wa


jeshi la polisi


Tanzania.Haijalishi vita hii itakwenda hadi wapi lakini lazima Mathew Mulumbi apatikane”Kasiano akamwambia mke wake halafu akachukua simu na kumpigia Paul akampa maelekezo ya kufanya



Saa kumi na moja za alfajiri,Kasiano aliamshwa toka usingizini na simu kutoka kwa Paul Lewis


“Paul” akasema Kasiano kwa sauti iliyojaa uchovu


“Mkuu tumeifanya ile kazi uliyotupatia na tumefanikiwa kuipata akaunti ya mke wa IGP Yeremia nje ya nchi.Ina jumla ya shilingi bilioni nne na milioni sabini” akasema Paul


“Good job Paul.Baada tu ya mapambazuko kila kitu kiendelee kama tulivyokuwa tumepanga” akasema Kasiano na kukata simu.




************


Saa kumi na mbili na nusu za asubuhi simu ya mkuu jeshi la polisi nchini Yeremia Mwaipopo ikaita zilikuwa ni namba ngeni katika simu yake. “Hallow ! akaita Yeremia


“Heshima yako mzee wangu”


“Nzuri kabisa.Nani mwenzangu? Akauliza IGP Yeremia Mwaipopo


“Mzee mimi ni mwandishi wa habari za kujitegemea” akasema Yule jamaa upande wa pili wa simu


“Ndiyo ndugu mwandishi unasemaje asubuhi hii? Akauliza Yeremia


“Mzee nina mazungumzo nawe siku ya leo”


“Ndugu mwandishi ukitaka mazungumzo nami unatakiwa ufuate taratibu rasmi za kiofisi mimi huwezi ukanipigia simu asubuhi nikiwa kitandani na kuniambia kwamba unataka kuonana nami.Hiyo si adabu na sipendi mambo hayo.Ukitaka kuonana na mimi fuata taratibu zilizowekwa ! akasema IGP Yeremia kwa sauti ya ukali kidogo


“Mzee ninazifahamu taratibu hizo lakini shida yangu ni ya haraka kidogo ndiyo maana nikaamua kukupigia simu moja kwa moja”


“Kijana nimekwisha kwambia kama una suala lako na unataka kuniona tafadhali fuata taratibu zilizopo na si kunitafuta kihuni namna hii.Tena nakuomba iwe ni mara ya mwisho kunipigia simu kienyeji namna hii na kuomba kuonana nami ! akasema IGP Yeremia na kukata simu kwa hasira


“Kuna nyakati huwa nawachukia sana waandishi wa habari.Anapiga simu mapema namna hii na anataka kuonana nami akidhani mimi ni mtu unayeweza kunipata muda wowote unaotaka.Hawa ndiyo wale wanaoitwa makanjanja hawajui hata kutafuta habari,hawajui kufuata taratibu ili waweze kupata habari.Ameniudhi sana ! akawaza IGP Yeremia.Kabla hajaiweka simu mezani ikaanza kuita akakunja sura akaipokea kwa hasira


“Wewe kijana ! nakupa onyo usiendelee kunichezea.Nitakutafuta na kukuchukulia hatua kali sana ! Naomba hii iwe ni mara ya mwisho ! akasema IGP na kukata simu akiwa amekunja sura kwa hasira.Baada ya sekunde chache ukaingia ujumbe katika simu yake akaufungua na kuusoma


“Mzee nataka kuzungumza nawe kuhusiana na suala la mauaji ya wale wafanya biashara wa madini miaka minne iliyopita na fedha zilizoko katika akaunti ya mkeo nje ya nchi !


Ujumbe ule ulimfanya IGP Yeremia apatwe na mstuko mkubwa akaurudia kuusoma ujumbe ule huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio kutokana na mstuko alioupata


“Who is this devil? Akajiuliza akiwa amekunja sura


“I’ll destroy this instect ! akasema kwa hasira


“Huyu jamaa anajitafutia matatizo ! akaendelea kuwaza na mara simu ikaanza kuita akaitazama ikiita na kukatika ikaanza kuita tena


“Kijana nakupa onyo la


mwisho kwamba unaelekea katika tanuru la moto.Waliokutuma jambo hili wamekudanganya na utapotea.Acha kufuatilia mambo yasiyokuhusu ! Wenzako kama wewe wamekwisha potea kwa mambo ya udaku kama unayoyafanya wewe ! akasema kwa ukali Yeremia


“Mzee utapokea ujumbe wa maelekezo mahala pa kukutana na endapo usipotokea kwa muda nitakaokuelekeza basi usinilaumu.One more thing,usithubutu kunitisha au kutuma askari kunikamata utakuwa umeharibu sana kwani ndani ya sekunde chache nchi nzima itazifahamu siri zako ikiwamo ya mtoto wako wa nje ya ndoa ambaye alikabiliwa na kesi ya mauaji lakini ukatumia nguvu yako kuimaliza kesi hiyo.Mkeo anafahamu kama una mtoto nje ya ndoa? Akauliza Yule jamaa na kuzidi kumpandisha hasira IGP Yeremia.


“Mzee naomba ufuate


maelekezo nitakayokupa ili tuzungumze na baada ya hapo hutasikia tena simu yangu na kila kitu kitazikwa utaendelea na maisha yako kwa amani” akasema Yule jamaa na kukata simu.Baada ya sekunde chache ukaingia ujumbe uliomuelekeza IGP Yeremia muda na mahala pa kukutana na mtu Yule aliyempigia simu


“Mambo gani haya yananitokea?Huyu jamaa anaongea kwa kujiamini sana inaonekana anao ushahidi wa kutosha.Amezifahamuje siri hizi? Akajiuliza IGP Yeremia


“Huyu jamaa lazima kuna kitu anakihitaji kutoka kwangu na kama nikimkubalia matakwa yake basi nitakuwa mtumwa wake.Lazima nimuonyeshe uwezo wangu kiroboto huyu.Nitamuonyesha mimi ni nani na lazima atanieleza amezipata wapi taarifa hizi ambazo ni siri kubwa.Nitamfundisha adabu ili liwe fundisho kwake na wenzake wenye tabia kama zake za kufuatilia maisha ya watu ! Ninawachukia waandishi wa habari ! akawaza akiwa amefura kwa hasira




****************




Mathew Mulumbi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka asubuhi na kuanza kuzunguka zunguka nje ya nyumba ya Zarina akisubiri waamke hakutana kuwasumbua


“I miss my home.Nilidhani safari hii ninakuja kupumzika nyumbani lakini nimejikuta tena kati kati ya kadhia nzito.Lini maisha haya yatakwisha na mimi niishi maisha ya furaha na amani kama wenzangu? Akajiuliza akiwa amesimama akiwatazama ndege waliokuwa wakiruka na kutua bustanini


“Goodmorning Mr


Mulumbi ! ikasikika sauti ya


Zarina aliyesimama mlangoni Mathew akageuka na kumfuata


“Goodmorning


Zari.Unaendeleaje? “Ninaendelea vyema kabisa.Vipi wewe unaendeleaje?


“Ninaendelea vizuri pia.Ruby amekwisha amka?


“Ndiyo lakini anafanya maombi ya asubuhi”


“Ni vizuri akafanya maombi kwa niaba yetu ili Mungu atutangulie katika siku ya leo ambayo naamini itakuwa ngumu sana.Hatuwezi kushinda vita hii bila kumtanguliza Mungu” akasema Mathew


“Wakati tunamsubiri Ruby nitakwenda kuandaa kifungua kinywa” akasema Zari na kuelekea jikoni Mathew akaenda katika chumba chake kujiweka tayari kuikabili siku.


Baada ya kujiandaa


Mathew akaelekea sebuleni na kuwasha luninga akitaka kufuatilia habari za magazeti ili kupata picha ya kile kinachoendelea mtaani.


Habari kubwa iliyopamba vichwa vyote vingi vya habari vya magazeti siku hii ni tukio la kushikiliwa kwa rais mstaafu Dr Fabian Kelelo kwa tuhuma za mauaji na dawa za kulevya akishirikiana na Mathew Mulumbi.Habari nyingine kubwa ilikuwa ni tukio la kutoroshwa Mathew Mulumbi.


“Sikutegemea kama siku moja Fabian angekuja kuchafuliwa namna hii.Hii ni kashfa kubwa sana amezushiwa ! Halafu hawa waandishi wa habari inaonekana kama vile wanatumiwa na hawa jamaa kwani karibu wote wameiweka habari hii kama habari kuu ili kumchafua Dr Fabian ! akasema Ruby ambaye naye alikuwa anafuatilia habari za magazeti


“Yote haya ni kwa sababu yangu.Nakuahidi Ruby tutalivuka hili.Tualimaliza na Dr Fabian atakuwa huru na tutalisafisha jina lake.Naomba uniamini ! akasema Mathew kisha wakaelekea kupata kifungua kinywa.Baada ya kupata kifungua kinywa wakaingia katika chumba ambacho ndiko mipango yote ya operesheni yao ilikuwa inafanyika


“Ladies leo ndiyo leo.Ni moja ya siku zile ngumu kabisa hasa kwangu.Ninatafutwa na


jeshi la polisi na vile vile ninatafutwa na wale jamaa zetu hivyo tusitegemee urahisi hata hivyo nina uhakika mambo yatakwenda vizuri kwa kuwa tumemuweka Mungu mbele yetu” akasema Mathew


“Mzizi wa haya yote yanayoendelea hivi sasa ni Naomi Bambi ambaye jina lake halisi ni Zoe Adam Watwila” akasema Mathew akichora ubaoni


“Hatufahamu mambo


mengi kuhusu Naomi ila tunachokifahamu ni kitu kimoja tu kwamba hakuwa na matatizo ya akili.Hii ni kwa mujibu wa Zawadi ambaye ndiye aliyemchoma sindano ya kumfanya aonekane ni mgonjwa wa akili.Kwa kuwa ndiye chimbuko la haya yote basi lazima tumchunguze na kumfahamu kiundani sana huyu Naomi au Zoe.Wazazi wake pia wamekwisha fariki hata hivyo leo tunakwenda nyumbani kwao kujaribu kupata taarifa za kina kuhusiana na Zoe.Baada ya hapo tutajua nini kitafuata.Ruby wewe utabaki hapa nyumbani utakuwa unatufuatilia kwa kutuma mfumo wa SNSA.Mimi na Zari tutaingia mtaani.Hata hivyo we are going to need a back up from SNSA” Mathew akatoa maelekezo na bila kupoteza muda Zari akaomba makomando wanne wafike pale nyumbani kwake kwa ajili ya kuwafuata katika mizunguko yao ya siku. ************


Mlango wa chumba cha mahabusu alimo Dr Fabian Kelelo ukafunguliwa akaingia David Chamwino.


“Umeamkaje Dr Fabian? Akauliza David


“David wanakulipa kiasi gani hawa watu ili uniangamize namna hii? Akauliza Dr Fabian


“Sikiliza Dr Fabian mashtaka dhidi yako yanaandaliwa na utafikishwa mahakamani kusomewa


mashtaka ya kushiriki katika mauaji ya mkuu wa gereza la Uwangwa na vile vile kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.Hii ni kesi mbaya Dr Fabian na hakuna namna unavyoweza kuponyoka kifungo kwani ushahidi ni mzito.Kwa mara ya mwisho nataka uniambie wapi alipo mke wako? Ninaamini mkeo anafahamu mahala alipo


Mathew


Mulumbi.Nakuhakikishia kwamba mkeo atakuwa salama kwani tunachokihitaji ni taarifa tu za mahala aliko


Mathew.Last chance Dr Fabian ! akasema David na Dr Fabian akamtazama kwa hasira


“David haya unayoyafanya iko siku yatakurudia ! akasema Dr Fabian na David akatikisa kichwa akisikitika


“Dr Fabian umeipoteza nafasi pekee


uliyoipata.Nitakapotoka hapa sintakuwa na uwezo wa kukusaidia tena hivyo kama una lolote la kusema muda ni sasa ! akasema David lakini Dr Fabian hakumjibu chochote


“Dr Fabian kwa sasa hakuna mwingine anayeweza kukusaidia.Ni wewe pekee unayetakiwa kufanya juhudi za kujitoa kitanzini” akasema David


“Go to hell David !


akasema Dr Fabian kwa hasira




“Dr Fabian usinilaumu mimi tafadhali kwani haya yote umeyataka wewe mwenyewe.Umeshindwa kujisaidia mwenyewe pale ulipopata fursa” akasema David na kutoka mle ndani halafu akarejea


“Kuna kitu nimesahau kukujulisha.Kamishna Jenerali wa magereza Chambao Mnenge amekutwa amefariki dunia kwa mstuko wa moyo” akasema David na kumstua sana Dr Fabian


“Chambao amekufa? Dr


Fabian akauliza


“Ndiyo amefariki dunia kwa shinikizo la damu.Dr Fabian hili suala ni zito sana” akasema David na kutoka.Dr Fabian akaingiwa na hofu kubwa


“Siamini kama Chambao amekufa kifo cha kawaida.Nina wasi wasi jamaa wamemuua kwa kuhofia anaweza akasema kile anachokifahamu kuhusu wao kwani waliwasiliana naye na kumtaka amkabidhi Deus Mtege na wakaenda kumuua.Ni akina nani watu hawa? Akajiuliza Dr Fabian


“Nimeanza kuingiwa na hofu lakini naamini Ruby na Mathew huko waliko hawalali kuhakikisha wanawafahamu watu hawa ni akina nani pamoja na kunitoa katika hiki kitanzi nilichovishwa.Wao pekee ndiyo wanaonipa imani na nguvu ya kuvumilia haya yote.Mungu atawaongoza na watafanikiwa kuwapata wahalifu hawa” akawaza Dr Fabian





Mkuu wa jeshi la polisi aliwasili ofisini kwake.Siku hii hakuonekana kuwa katika hali ya kawaida.Alionekana kusumbuliwa na jambo.Alipoingia ofisini kwake alijiegemeza kitini akavuta pumzi ndefu.


“Bado nawaza Yule jamaa amezifahamuje siri zangu? Akajiuliza


Hili ndilo swali ambalo lilimuumiza mno kichwa toka alipopigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwandishi wa habari.


“Kitu gani anakihitaji huyu mtu hadi akataka tuonane?Watu kama hawa wanachokihitaji mara nyingi huwa ni fedha.Nilifikiria kumuua lakini ni vipi kama anao wenzake na wakalianika suala hili? Akaendelea kujiuliza maswali


“Nina wasi wasi yawezekana miongoni mwetu kuna mtu amevujisha siri hii.Fedha za wale wafanya biashara ziligawanywa kwa watu kumi na wengine hivi sasa tayari wamekwisha acha jeshi wanafanya biashara zao ninahisi kuna mmoja wao amevujisha siri ili kunikamua fedha.Nitahakikisha ninamtafuta na kumfahamu mtu huyo ni nani” akawaza IGP Yeremia Mwaipopo halafu akachukua simu na kumpigia David Chamwino


“Mkuu habari za asubuhi” akasema David baada ya kupokea simu


“Habari nzuri kabisa. David kuna jambo la muhimu sana nataka kukuagiza ulifanye”


“Nakusikiliza mkuu” akasema David


“Nataka uwakusanye wale wote waliopata mgao wa wakenya ninataka kuzungumza nao jioni ya leo.Hakikisha hakosekani hata mmoja ! akasema IGP Yeremia


“Mkuu umenistua


kidogo.Kuna nini kwani? Ni muda mrefu umepita”


“David fanya nilichokuelekeza.Nataka wote wawepo jioni ya leo” akasisitiza Yeremia na kukata simu


“Lazima kuna mmoja wao ambaye ametoa siri hii na lazima nimfahamu ! akawaza na kuitazama saa yake


“Muda ambao Yule jamaa amenitaka nikaonane naye unakaribia.Natakiwa kufanya maamuzi je niende au nisiende? Akajiuliza


“Ngoja niende


nikamskilize vile vile nimfahamu ni nani na anataka nini ! akawaza Yeremia na kutoka akaanza safari ya kuelekea mahala alikoelekezwa na Yule jamaa wakutane




***********




Gari la Zarina lilisimama nje ya nyumba nzuri iliyokuwa ya mchungaji Adam Watwila.Kwa mbali gari la makomando wanne wa SNSA wanaowafuatilia akina Mathew nalo lilisimama.


“Ruby tumefika tunataka kuingia ndani” Mathew aliyekuwa ameweka kifaa cha mawasiliano sikioni akawasiliana na Ruby .Asubuhi hii alikuwa amevaa fulana nyeusi pamoja na jaketi jeusi halafu akavaa kofia nyeusi pia na kidevuni akabandika ndevu bandia ili kubadili mwonekano wake.Zari aliyekuwa amevaa suruali ya jeans nyeupe na raba zenye mchanganyiko wa rangi akafungua mlango akashuka,Mathew naye akashuka wakaelekea getini na kugonga.Baada ya dakika chache msichana mmoja aliyekuwa na mikono iliyoloa maji akajitokeza na kuwakaribisha.


“Hapa ni nyumbani kwa mchungaji Adam Watwila? Akauliza Mathew


“Simfahamu huyo mtu” akajibu Yule msichana


“Kwani wewe ni nani hapa?


“Mimi ni mtumishi wa ndani nimeanza kazi mwezi


uliopita”


“Ouh sawa.Wenyewe tumewakuta? Akauliza Mathew


“Baba yuko kazini lakini mama amesafiri Ulaya”


“Unaweza ukatusaidia namba zake za simu tafadhali? Akauliza Mathew na Yule msichana akaenda ndani baada ya muda akarejea akiwa na karatasi aliyoandika namba za simu wakamshukuru na kurejea garini.Mathew akampa Zari zile namba akaziandika katika yake akapiga simu ikaita


“Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili


“Hallow habari yako ndugu yangu”


“Nzuri kabisa nani mwenzangu?


“Naitwa Zarina ni mwandishi wa habari”


“Ndiyo Zarina unahitaji nini?


“Nina mazungumzo nawe mafupi nimefika hapa nyumbani kwako na kupewa namba zako na mtumishi wako wa ndani.Nielekeze ulipo nikufuate tafadhali” akasema Zari


“Nini unakitaka Zari? “Kuna mambo nataka tuzungumze kuhusiana na mchungaji Adam Watwila” “Mambo gani?


“Hatuwezi kuzungumza simuni.Naomba tuonane tafadhali nakuahidi hatutachukua muda wako mwingi” akasema Zari na Yule jamaa akamuelekeza mahala alipo wakawasha gari na kuondoka.Mathew akawajulisha makomando wale kwamba wanaondoka na waendelee na kazi ya kuwafuatilia






**********




Kwa kufuata maelekezo waliyopewa walifika hadi katika kampuni ya kutengeneza maji kisha Zari akampigia simu Yule jamaa ambaye alitoka na kuwafuata.Zari akafungua mlango


wakasalimiana.Mathew naye akafungua mlango akashuka.Yule jamaa hakuweza kumtambua kutokana na muonekano wake kubadilika kabisa


“Hello.Naitwa Msafiri


Mtwale niko na Zarina” “Karibuni sana” akasema Yule jamaa na kuwachukua akawapeleka ofisini kwake


“Karibuni sana jamani.Mimi naitwa Ezekiel Watwila ndiye mmiliki wa kiwanda hiki cha kutengeneza maji ya kunywa.Ninyi wenzangu mnatokea wapi?


“Kama nilivyokueleza simuni sisi ni waandishi wa habari wa kujitegemea na tumekuja hapa kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na mchungaji Adam Watwila.Kabla ya yote wewe na yeye mna mahusiano yoyote?


“Ndiyo mimi ni mdogo wake.Baada ya kufariki mimi ndiye ninayeishi katika ile nyumba yake na hiki hapa ni kiwanda changu tunatengeneza maji.Kimeanza muda si mrefu sana ndiyo maana mnaona bado ujenzi unaendelea.Nini mnataka kukifahamu kuhusu Adam? Akauliza Ezekiel


“Unaweza ukatueleza kwa


kifupi kilichosabisha kifo cha mchungaji Adam watwila? Mathew akauliza


“Adam alipata ajali akiwa na gari la Nabii Kasiano wakati akielekea Morogoro.Tairi moja la mbele lilipasuka na kwa kuwa walikuwa katika mwendo mkali sana gari lilipinduka mara kadhaa na kupelekea kifo chake yeye na mke wake aliyekuwa ameambatana naye katika safari hiyo”


“Poleni sana”


“Ahsante tumekwisha poa”


“Morogoro alikwenda


kutafuta nini? Zarina akauliza


“Nakumbuka alinipigia simu wakati amefika Mbezi akaniamia kwamba amepata safari ya ghafla ya kwenda Morogoro hivyo akanitaka niende nyumbani kwake kuhakikisha kunakuwa salama hadi atakaporejea.Nilimuuliza anakwenda kufanya nini Morogoro muda ule? Je ni kwa shughuli zake za kichungaji? Akanijibu kwamba atakuja kunieleza kila kitu atakaporejea kwani kuna mambo mazito. Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kuzungumza naye na baadae mida ya saa moja jioni zikaja taarifa kwamba amefariki dunia”akasema Ezekiel


“Ameacha watoto wangapi mchungaji Adam? Akauliza Mathew


“Mchungaji Adam alikuwa na mtoto mmoja pekee aliyeitwa Zoe ambaye naye amekwisha fariki dunia”


“Dah ! nini kilisababisha kifo cha huyo mtoto wake? Akauliza Mathew


“Huyu mtoto alipatwa na


matatizo ya akili”


“Unaweza kutueleza kidogo kuhusiana na huyo mtoto wa mchungaji Adam je matatizo hayo ya akili yalianzaje?


“Huyo mtoto alikuwa anasoma katika shule moja ya kimataifa ya wasichana ya Danisa.Alipata ufadhili kutoka kwa kanisa alilokuwa anahudumu baba yake ambalo lina kawaida ya kuwapatia ufadhili wa masomo katika shule mbali mbali watoto wa wachungaji na watoto wa baadhi ya waumini wasio na uwezo wa kugharamia elimu….” Akasema Ezekiel na kunyamaza kidogo halafu akasema


“Nilipopata taarifa za kufariki wazazi wake nilikwenda moja kwa moja shuleni kwao kwa ajili ya kutoa taarifa na kumchukua kumrejesha nyumbani nilipata


taarifa iliyonistua sana.Niliambiwa kwamba Zoe alitoweka pale shuleni na hajulikani alipo.Niliambiwa kwamba baba yake aliitwa na uongozi wa shule kwa ajili ya kufahamishwa mambo kadhaa kuhusiana na mtoto wake na hapo ndipo mwanae alipotoweka na hakujulikana alikoelekea.Zoe hakuonekana hadi baada ya mazishi ya wazazi wake ndipo alipookotwa kituo cha basi akiwa amechanganyikiwa akapelekwa kanisani kuombewa.Tulitaarifiwa tukaenda mara moja na kumkuta kweli binti yetu akiwa amechanganyikiwa anazungumaza maneno yasiyoeleweka tukawaomba ili tumpeleke hspitali na tunashukuru Nabii mkuu Kasiano akajitolea kugharamia matibabu tukampeleka hospitali.wakati vipimo vikiendelea tukaambiwa kwamba Zoe amewaponyoka waliokuwa wamemshikilia akakimbia na kujirusha ghorofani akafariki dunia.Hivyo ndivyo ilivyokuwa ndani ya wiki moja tukawapoteza familia nzima” akasema Ezekiel


“Poleni sana”akasema Zarina


“Ahsante” akajibu Ezekiel


“Nataka kufahamu je huyu


Zoe alishawahi kuwa na matatizo yoyote ya akili wakati akiwa mdogo?


“Hicho ndicho kinachoshangaza kwani Zoe alikuwa ni binti mwenye akili nyingi sana na hakuwahi kuwa na matatizo yoyote ya akili”


“Kuna taarifa yoyote mliwahi kuipata kutoka kwa madaktari kuhusiana na ugonjwa wa Zoe? Akauliza Mathew


“Nataka kwanza kufahamu ndugu zangu dhumuni lenu ni nini kuhusiana na haya mnayoyauliza? Akauliza


Ezekiel


“Kuna mwenzetu


mwandishi wa habari alifariki dunia kwa kuuawa na mpenzi wake.Katika kupekua baadhi ya nyaraka zake tukagundua kwamba alikuwa analichunguza suala la Zoe Adam Watwila lakini hakuweza kulifikisha mwisho ndipo na sisi tulipoamua kuanza kulichunguza jambo hili na ndiyo maana tumeona tuanze kwanza kwa kumfahamu Zoe ni nani na sisi


tuendelee pale alipoishia” akasema Mathew


“Nawashukuru sana kwa maamuzi hayo mliyoyafanya lakini napenda niwaeleze ukweli ndugu zangu hili suala la Zoe ni suala lenye utata mkubwa sana.Kwanza kabisa baada tu ya Zoe kufariki dunia kwa kujirusha ghorofani siku chache baadae tukafuatwa na mwanasheria mmoja akatueleza kwamba kuna mtu yuko gereza la Uwangwa amemtuma kwamba anazo taarifa za kuhusiana na


Zoe.Tulimfuata mwanamke huyo lakini cha kushangaza tulipofika akabadilika na kukataa kabisa kutueleza chochote.Siku chache baadae akatufuata mwandishi mmoja wa habari nikazungumza naye na nikamueleza pia kuhusiana na yule mwanamke wa gereza la Uwangwa ambaye alidai anazo taarifa za kuhusiana na Zoe akasema atafanya jitihada za kwenda kumuona mwanamke huyo lakini siku chache baadae nikasikia kwamba mwandishi huyo ameuawa na mpenzi wake.Hapo ndipo kila mtu alipoanza kuliogopa jambo hili na watu wakatushauri tuachane nalo kwani tunaweza kumalizika wote.Hakuna aliyejihusiaha tena kufuatilia suala hilo tukaliacha kama lilivyo hadi sasa ambapo mmejitokeza ninyi na kutaka kuliendeleza lakini napaswa kuwatahadharisha mapema kwamba hili jambo ni la hatari na hata sisi wenyewe hatuelewi kuna nini katika jambo hili” akasema Ezekiel.


“Tumekuelewa Ezekiel na tunakuahidi kwamba tutalichunguza jambo hili kwa undani zaidi na kila hatua tutakayoipiga tutakushirikisha na kila pale tutakapohitaji msaada wako tunaomba


tafadhali utusaidie” akasema Mathew


“Mimi niko tayari kuwasaidia kwa lolote mtakalolihitaji muda wowote” akasema Ezekiel


“Ahsante tunashukuru.Tunakuomba pia usimweleze mtu yeyote kuhusiana na haya mazungumzo yetu” akasema Mathew na kuchukua kadi ya biashara ya Ezekiel yenye namba zake za simu kisha wakaondoka na kurejea katika gari lao


“Team B report ! akasema Zari akiwataka makomando wa SNSA watoe taarifa kama wakati wao wako ndani kuna hatari yoyote iliyojitokeza


“Hakuna tatizo lolote kila kitu kiko sawa” akajibu kiongozi wa timu ile


“Ruby unanipata?


Akauliza Mathew huku Zari akiwasha gari


“Ninawapata vyema


kabisa”


“Good.Nadhani


umefuatilia mazungumzo yetu na Ezekiel.Kuna chochote umekipata kufuatia


mazungumzo yale? Mathew akauliza


“Ezekiel ametupa mwanga lakini bado tunarudi palepale kwa Zoe au Naomi Bambi.Huyu ndiye chimbuko


la haya yote yaliyotokea” akasema Ruby


“Kwa upande wangu nimepata picha hata vifo vya wazazi wake yawezekana vilitokea kwa sababu yake.Nina wasi wasi na ajali iliyowaua wazazi wake ! akasema Zari


“Me too.Ajali hiyo nina wasiwasi nayo sana ndiyo maana kituo kinachofuata ni kanisa la injili ya wokovu kubwa ni kutaka kujua kile kilichompelekea mchungaji Adam akafunga safari ya Morogoro tena akiwa na mke wake.Ezekiel alisema kwamba gari ambayo Adam alipata nayo ajali ni ya nabii mkuu Kasiano.Tukifanikiwa kumpata huyu atatusaidia kufahamu kilichompeleka Adam Morogoro” akasema Mathew na safari ya kuelekea katika kanisa la injili ya wokovu linaloongozwa na nabii mkuu Kasiano Muyenzi ikaanza.




***********





Sanora beach hotel ndiko mahala mkuu wa jeshi la polisi nchini Yeremia Mwaipopo alielekezwa kwenda ili akaonane na Yule mtu aliyempigia simu.Alishuka garini na kumpigia simu Yule jamaa


“Tayari nimefika hapa wewe uko wapi? Akauliza


“Nenda mapokezi waambie ni mgeni wa Tuma watakuleta mahala nilipo.Angalizo nakuhitaji wewe peke yako.Usiongozane na mtu mwingine yeyote !


akasema Yule jamaa


“Hilo haliwezekani ! Lazima niongozane na walinzi wangu!


“Mzee fuata nilichokuelekeza.Nakutaka wewe peke yako ! “Tafadhali ni mlinzi mmoja ambaye hana madhara yoyote !


“Ok good.Mlinzi mmoja tu tena utamwelekeza akae mbali” akasema Yule jamaa na kukata simu kisha IGP akamchukua mlinzi wake wakaelekea ndani ya hoteli.Wahudumu wa hoteli walipatwa na mshangao kidogo kumuona mkuu wa jeshi la polisi mahala pale.Aliingia ndani ya hoteli na kuelekea moja kwa moja mapokezi akasalimiana na wahudumu na bila hata kujitambulisha mmoja wa wahudumu akamtaka amfuate.Wakaelekea moja kwa moja katika bustani nzuri sana iliyokuwa na miavuli mingi ya kupumzikia huku upepo mwanana wa bahari ukivuma.Muhudumu Yule alimpeleka Yeremia katika meza ambako aliketi jamaa mmoja akiwa amevaa suti nyeupe na kofia nyeupe ya mduara huku akisoma gazeti.


“Kaka mgeni wako amefika” Muhudumu akamwambia Yule jamaa ambaye aliweka gazeti pambeni akasimama na kusalimiana na Yeremia. “Ahsante kwa kufika mzee! Akasema Yule jamaa huku akitabasamu kwa mbali.Yeremia akamtaka mlinzi wake asogee mbali


kidogo awape nafasi a kuzungumza


“Ninaapa wewe kijana hunifahamu mimi vizuri, nitakupoteza ! Waliokutuma kwangu wamekudanganya ! akasema Yeremia kwa hasira baada ya kumuona mtu aliyempeleka moyo mbio ni kijana sawa na mtoto wake wa kwanza


“Easy ! Easy ! ..” akasema


Yule jamaa ambaye hakuonekana kuwa na wasi wasi wowote.Huku akihema kwa hasira Yeremia akasema


“Nina dakika kumi tu za kuwepo hapa hivyo sema ulichotaka kuniambia ! akasema Yeremia kwa ukali


“Mzee Yeremia mimi ndiye niliyekuita hapa hivyo ndiye ninayepanga muda wa wewe kuwepo hapa ! akasema Yule jamaa na kuzidi kumpandisha Yeremia hasira


“Hivi kwa nini nisichukue bastola na kukamaliza haka kajamaa hapa hapa? Akajiuliza


Yeremia


“Mzee Yeremia nimekuita hapa na samahani kwa kukuharibia ratiba yako ya siku.Nisamehe kwa maneno yote niliyokutamkia wewe ni mzee wangu na ni mtu mkubwa hapa nchini hivyo napaswa kukuheshimu” akasema Yule jamaa na kidogo Yeremia akaanza kupoa


“Mzee nimekuita hapa kukupa taarifa kwamba ninazo taarifa za kuhusiana na lile tukio la wale wafanya biashara wa kutoka Kenya waliouawa hapa Dar es salaam wakidaiwa ni majambazi.Sitaki kupoteza muda kwa hilo kwani unalifahamu.Mzee kwa vile umesema una muda mfupi wa kuwepo hapa kwa nini tuzunguke zunguke wakati kila kitu kinajulikana? Akauliza Yule jamaa


“Lengo la kukuita hapa mzee wangu ni mimi na wewe kujaribu kutafuta namna ya kusaidiana ili jambo hili lisijulikane kwa watu na mimi pia ninahitaji msaada wako.Nakuhakikishia mzee endapo tutakubaliana mimi na wewe you’ll never hear from me again and your secrets will be safe” akasema


Yeremia akafikiri kidogo halafu akauliza


“What do you want?


“Ninachokihitaji ni kitu kidogo mno.Ni neno moja au mawili basi tutakuwa tumemalizana” akasema Yule jamaa akatoa sigara katika pakiti iliyokuwa mezani akawasha na kuvuta


“Usiku wa kuamkia


jana,jeshi la polisi lilimkamata mfanya biashara mmoja mkubwa wa dawa za kulevya hapa nchini anaitwa Mathew Mulumbi.Baadae alasiri


Mathew alihamishwa kutoka kituo cha polisi na kupelekwa katika gereza la Uwangwa na kabla ya kufika gerezani msafara ukavamiwa askari wakauawa na Mathew akatoroshwa na mpaka sasa haijulikani nani waliomtorosha na jeshi la polisi bado halijatoa taarifa yoyote.Uharaka wa


kumuhamisha Mathew


ambaye kwa taarifa tulizonazo bado alikuwa anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi unazua maswali mengi na baada ya kuchunguza tukabaini kwamba amri ya Mathew kuhamishwa uliitoa wewe baada ya kutoka ikulu ulikoitwa na Rais.Ninachotaka kufahamu je kuhamishwa kwa Mathew Mulumbi ni amri kutoka kwa Rais? Akauliza Yule jamaa na Yeremia akababaika kujibu


“Niambie ukweli mzee wangu” akasema Yule jamaa


“Ilikuwa ni amri yangu na


Rais hakunituma chochote.Aliniita ikulu kwa ajili ya masuala mengine kabisa”


Yule jamaa akapuliza moshi na kusema


“Dakika chache baada ya Mathew kuondolewa kitoni ulimtumia ujumbe Rais ukimtaarifu kwamba tayari Mathew amekwisha ondolewa” Yeremia alikosa kitu cha kujibu akabaki anamtazama Yule jamaa kwa hasira


“Tunafahamu kila kitu mzee ndiyo maana ninataka uniambie ukweli”


“Rais hakunituma maamuzi yale yalikuwa ni yangu mwenyewe ! akasema Yeremia


“Ahsante mzee kwa majibu hayo ya uongo.We’re done here lakini usiache kufuatilia magazeti ya kesho asubuhi! Akasema Yule jamaa huku akikusanya vitu vyake pale mezani na kuanza kupiga hatua


“Wait ! akasema Yeremia na Yule jamaa akageuka


“Kwa nini unataka kufahamu? Akauliza


“Usiniulize maswali mzee naomba majibu” akasema Yule jamaa


“Nikikupa majibu


unayoyataka sitaki tena unisumbue or I’ll kill you !


“Nakuhakikishia mzee kwamba ukinipa jibu ninalolihitaji sintakusumbua tena” akasema Yule jamaa.Yeremia akafikiri kwa muda halafu akasema


“Agizo lilitoka kwa Rais !




“Are you sure?


“Yes I’m sure.Rais ndiye aliyenipa maelekezo ya kumuhamisha Mathew Mulumbi kumpeleka katika gereza la Uwangwa na mimi nikayatekeleza” akasema Yeremia


“Alisema kwa nini Mathew ahamishwe?


“Mathew ni jasusi hivyo Rais alihofu kwamba angeweza akatumia mbinu za kijasusi akatoroka ndiyo maana akaelekeza kwamba ahamishiwe gerezani”


“Watu waliomteka Mathew Mulumbi inaonekana walikuwa na mawasiliano na watu ndani ya jeshi la polisi hivyo wakaweza kujiandaa na kuuvamia msafara wakamteka Mathew.Hudhani kwamba mpango huu wa kumteka Mathew Mulumbi ulipangwa ndani ya serikali?


“Kwa nini serikali imteke Mathew Mulumbi? Akauliza Yeremia


“Wewe ndiye unayepaswa


kunijibu kwa sababu kuna kila dalili kwamba mpango wa kumteka Mathew Mulumbi


uliratibiwa ndani ya serikali na ndiyo maana likatolewa agizo kwamba ahamishiwe gereza la Uwangwa na njiani wakavamiwa na kutekwa.Wewe na Rais kuna kitu mnakifahamu kuhusu jambo hili la Mathew kutekwa”


“Sikiliza kijana,mimi nilipewa maelekezo na mkuu wa nchi na mimi nikayatekeleza.Ujumbe niliomtumia Rais mara tu baada ya Mathew kuondolewa


kituoni ni kumjulisha kwamba lile agizo lake tayari limefanyiwa kazi.Sifahamu kama kuna mpango wowote wa serikali wa kumtorosha Mathew Mulumbi.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania amekwisha tanganza vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya hapa nchini hivyo basi hana sababu yoyote ya kumtorosha mtu ambaye ni mfanya biashara mkubwa wa dawa za kulevya .Wapo watu ambao wamemtorosha


Mathew na jeshi la polisi linaendelea kuwasaka” akasema IGP Yeremia halafu wakatazamana kwa muda


“Nimekujibu maswali yako yote na hii itakuwa ni mara ya mwisho mimi na wewe kuonana.Kama ukithubutu kunipigia simu tena au kunifuata ninaapa kwa miungu yote unayoifahamu nitakuua.Nitakuua kijana ! akasema kwa ukali IGP Yeremia


“Mzee nilikuahidi na nitatimiza ahadi yangu.Hutanisikia tena na siri zako zitaendelea kuwa salama ! akasema Yule jamaa


“Na iwe hivyo ! akasema kwa ukali Yeremia na kusimama halafu akakumbuka kitu na kuketi


“Nataka uniambie nani amekueleza mambo haya? Akauliza


“Hilo siwezi kukueleza ni siri yangu” akasema Yule jamaa na kuinuka akakusanya vitu vyake na kuanza kuondoka mahala pale


“Nitampata tu mtu


aliyekupa taarifa hizi ! Yeremia akasema kwa sauti ndogo naye akainuka na kuondoka.




************




“Ruby tumewasili kanisa la injili ya wokovu” Mathew akamjulisha Ruby mara tu walipofika katika kanisa kubwa la Injili ya wokovu. “Hapa tunaweza kupata


taarifa za kutusaidia” akasema Mathew na kumtazama Zari “Are you ready?


“Yes” akasema Zari kisha wakashuka garini na kuangaza angaza eneo lile kama kuna hatari yoyote halafu wakaanza kupiga hatua kuelekea katika ofisi za kanisa.


“Kanisa kubwa sana hili” akasema Mathew


“Maelfu ya waumini hukusanyika hapa kwa ibada kila jumapili” akajibu Zarina


Katika ofisi za kanisa kulikuwa na watu wengi waliofika kwa ajili ya kupata huduma za kiroho.


“Mathew this place is dangerous for you.Kuna watu wengi hapa na yawezakana wakaweza kukutambua japokuwa umebadili muonekano.Niache mimi niende nikazugumze na Nabii Kasiano” akasema Zari


“Mathew Zari is right.Muache yeye aende akazungumze na Kasiano kwani sehemu hiyo ni ya wazi mno na kuna watu wengi” akasema Ruby aliyekuwa akiwasikiliza Mathew na zari waliokuwa na vifaa vya mawasiliano masikioni mwao.


“Fine.Nenda katafute majibu nitakusubiri hapa garini” akasema Mathew na Zari akaondoka kuelekea


katika ofisi za kanisa.Hakuifahamu ofisi ya Kasiano akalazimika kuwauliza akina mama waliokuwa wamesimama wakijadiliana jambo wakamuelekeza akaelekea huko.Kulikuwa na foleni ndefu ya watu waliokuwa wakisubiri kuonana na nabii Kasiano.Akasogea pembeni kidogo na kuwasiliana na Mathew


“Kuna foleni kubwa sana hapa haitakuwa rahisi kuonana na nabii kwa haraka” akasema Zari


“Do something Zari! akasema Mathew na mara zari akamuona mchungaji mmoja


akitokea katika ofisi ya nabii akapata wazo akamkimbilia.


“Bwana asifiwe baba mchungaji” akasema Zari


“Amen.Karibu mwana wa Mungu” akasema mchungaji


“Mchungaji nina shida ambayo nahitaji sana msaada wako”


“Karibu” akasema mchungaji


“Ndani ya dakika


thelathini zijazo ninatakiwa kupanda ndege kwenda nje ya nchi kwa ajili ya usaili wa kazi.Nimekuja hapa kwa ajili ya kubarikiwa na nabii mkuu ili nitakapofika huko mambo yangu yaende vizuri.Kuna foleni kubwa sana na lengo langu linaweza lisifanikiwe.Unaweza ukanisaidia kuonana na nabii mkuu kwa muda mfupi wa


dakika chache tu ili anibariki nikawahi ndege? Akauliza Zari na Yule mchungaji akageuka akaitazama foleni ndefu ya watu wanaosubiri kuonana na Nabii kisha akasema


“Nabii mkuu leo ana maombi ya mtu mmoja mmoja


lakini hata mimi ninaweza kukuombea”akasema mchungaji


“Nashukuru sana


mchungaji nalifahamu hilo lakini kuna suala lingine ambalo nitahitaji ushauri wa nabii mkuu ndiyo maana ninaomba unisaidie niweze kuonana naye.Nitatumia dakika chache sana”akasema Zari


“Sawa twende unifuate!


Akasema Yule mchungaji,Zari akamfuata wakaingia katika ofisi ya Nabii mkuu.Yule mchungaji akamuelekeza mmoja wa wahudumu wa ofisi ile ya nabii mkuu kwamba atakapotoka mtu anayehudumiwa na Nabii basi aingie Zarina ambaye ana dharura.Zari akamshukuru yule mchungaji kwa msaada wake akaendelea kusubiri.Baada ya dakika kumi mlango wa ofisi ya Nabii mkuu Kasiano ukafunguliwa akatoka mwanamama mmoja na muhudumu akamruhusu Zari kuingia.Mara tu alipoingia alimkuta Nabii akiwa amefumba macho ameinua mikono akiomba halafu akafumbua macho na akaonekana kama kustuka kidogo baada ya kugonganisha macho na Zari


“Karibuni mwana wa


Mungu” akasema Kasiano


“Bwana asifiwe mtumishi wa Mungu” akasema Zari


“Amen.Karibu sana” akasema Kasiano na kumuelekeza aketi “Nikusaidie nini?


“Nabii mkuu nimekuja kwako mimi naitwa Zari ni mwandishi wa habari wa kujitegemea”


“Mwandishi wa habari? Akauliza Kasiano


“Ndiyo nabii.Nimekuja kukuona kuna jambo dogo ninataka kuzungumza nawe” akasema Zari


“Samahani sana Zari ninawapenda waandishi wa habari lakini huu ni muda wa kuhudumia watu wenye matatizo mbali mbali.Kuna watu wamefika hapa kuanzia saa kumi na mbili za asubuhi kwa ajili ya kuonana nami niwaombee na kuwatatulia matatizo yao sina muda kwa ajili ya mahojiano kwa sasa ! akasema Kasiano akionekana kutopendezwa na ujio ule wa Zari


“Nisamehe baba,ninaomba dakika tano tu kuna jambo moja dogo ambalo ninataka kuzungumza nawe” “Nini unataka kuuliza?


“Ni kuhusiana na marehemu mchungaji Adam Watwila aliyekuwa akihudumu hapa” akasema Zari na sura ya Kasiano ikaonyesha mstuko kidogo halafu akakunja sura


“Kuna nini kuhusu mchungaji Adam?


“Nimefahamishwa


kwamba alipata ajali wakati akielekea Morogoro akiwa na gari lako.Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba ilikuwa ni safari ya ghafla na hakuna anayefahamu alikuwa anakwenda kufanya nini Morogoro.Kwa kuwa


aliondoka na gari lako je alikueleza sababu ya yeye kwenda Morogoro na mke wake? Akauliza Zari


“Sikiliza Zari.Safari ile mimi ndiye niliyemtuma kwenda Morogoro kwa shughuli za kanisa ndiyo maana nikampa gari langu”akajibu Kasiano “Unaweza ukanieleza ni shughuli gani hiyo ambayo ilimlazimu kuondoka kwa haraka?


“Nani kakwambia kwamba Adam aliondoka kwa haraka?Nani kakwambia kwamba safari hiyo ilikuwa ya ghafla? Akauliza nabii Kasiano kwa ukali kidogo


“Nimezungumza na mdogo wake ambaye ameniambia kwamba alipigiwa simu na kaka yake ambaye ni mchungaji Adam akamjulisha kuwa amepata safari ya ghafla kwenda Morogoro.Kwa mujibu wa mdogo wake huyo alimuuliza Adam anachokwenda kukifanya huko Morogoro lakini hakumweleza bali alimwambia kuna jambo zito atamweleza atakaporejea kwa bahati mbaya hakurejea akafariki njiani”


“Zari unatoka chombo gani cha habari?


“Ni mwandishi wa


kujitegemea” akajibu Zari na Kasiano akashusha pumzi


“Sikiliza Zari.Achaneni na huyo mdogo wake Adam hafahamu chochote.Mimi ndiye niliyemtuma Adam kwenda Morogoro na haikuwa ni safari ya ghafla bali ni safari iliyokuwa imepangwa ila Adam alichelewa kuondoka hapaDar es salaam kutokana na kuwa katika huduma ndiyo maana alikuwa katika mwendo mkali sana” akasema Kasiano


“Ahsante sana baba kwa ufafanuzi huo.Vipi kuhusu mtoto wake Zoe?


“Ndugu yangu naomba sasa unipishe niwahudumie


watu wenye shida mbali mbali


ambao wamekuwa wananisubiri toka alfajiri.Kama una maswali nitafute wakati mwingine.Fuata taratibu zilizopo na maswali yako yote nitayajibu ila kwa leo utanisamehe sihitaji maswali zaidi ! akasema Kasiano


“Baba nashukuru kwa ushirikiano wako”akasema Zari


“Nenda kwa amani”


akasema Kasiano.Zari akatoka mle ofisini.Mara tu alipotoka Kasiano akamzuia akidai ana maombi maalum akafunga mlango na bila kupoteza muda akamtuma muhudumu wake amuite Joseph mmoja wa walinzi wake ambaye alifika mara moja “Joseph


umemuona mwanadada


aliyetoka ofisini kwangu muda mfupi uliopita amevaa suruali ya jeans nyeupe.Follow her and find out who she is ! akasema Kasiano


“Sawa mkuu” akajibu


Joseph


Zari baada ya kutoka kuonana na nabii Kasiano akaelekea maegesho alikomuacha Mathew akimsubiri garini.


“Welcome back Zari.Ruby tunaondoka hapa.Naamini umefuatilia mazungumzo ya Zari na nabii mkuu”Mathew akamwambia Ruby


“Nimewapata vizuri


Mathew”


“Kilichotuleta hapa ni kufahamu kuhusu safari ya ghafla ya mchungaji Adam Watwila kuelekea Morogoro japo nabii mkuu ametoa ushirikiano mdogo lakini hakijaharibika kitu tumefahamu safari ya Adam ilikuwa ni ya kichungaji ingawa bado nafsi yangu haijaridhika.Kituo kinachofuata ni shuleni kwa Zoe” akasema Mathew na Zarina akawasha gari wakaondoka pale kanisani.


“Uuphh ! Haikuwa rahisi kujifanya mwandishi wa habari.Yule nabii ana macho makali sana kiasi nilianza kuingiwa na hofu kwamba yawezekana anafahamu ninamdanganya kwani hawa manabii wana nguvu kubwa ya kuweza kutazama hadi ndani ya mtu” akasema Zari na Mathew akatoa kicheko kidogo


“Manabii wa kweli walikuwa akina Musa hawa wa siku hizi mhh !.Tuachane nao


tujielekeze katika kazi yetu” akasema Mathew


**************


Wakati nabii mkuu Kasiano akiendelea kuwasikiliza na kuwahudumia watu wenye matatizo mbali mbali waliofika osifini kwake kuhudumiwa,ukaingia ujumbe katika simu yake ukitoka kwa John Mkizi


“Mkuu,IGP amekiri kwamba agizo la Mathew Mulumbi kuhamishwa lilitoka kwa Rais



Kasiano akafumba macho akatafakari kwa muda halafu akakumbuka kuna mtu ambaye alikuwa anamsikiliza akamuomba samahani kwamba anatakiwa sehemu Fulani kuna mgonjwa mahututi anataka kwenda kumuombea.Akavaa koti lake na kutoka akawaomba radhi watu waliokuwa wanamsubiri akawataka waje siku inayofuata moja kwa moja akaelekea katika gari lake la kifahari aina ya limousine lisilopenya risasi akafunguliwa mlango na walinzi wake akaingia kisha msafara wake ukatoka pale kanisani.Mara nyingi msafara wake huwa na magari kuanzia sita ya walinzi wake


“Tunaelekea nyumbani” akatoa maelekezo halafu akazitafuta namba za simu za mke wake akampigia na kumtaka arejee nyumbani kuna dharura.Baada ya kuwasiliana na Rita akazitafuta namba Fulani na kuziangalia akavuta pumzi na alionekana kama vile anasita kuzipiga lakini mwishowe


akaamua kuzipiga na simu ikaita


“Kasiano” ikasema sauti ya


mwanamke wa makamo


upande wa pili “Mama Bella shikamoo”


“Marahaba.Unaendeleaje?


“Ninaendelea vyema mama” akajibu Kasiano na ukimya mfupi ukapita


“Unasemaje Kasiano? “Mama nahitaji kukuona” “Lini?


“Leo hii.Kuna suala ambalo nahitaji msaada wako” “Kuna tatizo gani Kasiano?


“Kuna jambo limevuka uwezo wangu ninahitaji msaada” akasema


Kasiano.Zilipita sekunde kadhaa kisha Yule mwanamke akasema


“Uko wapi?


“Ninaelekea nyumbani kwangu”


“Sawa ninakuja hapo baada ya saa moja” akasema Yule mwanamama na kukata simu.Kasiano akashusha pumzi




*************




Mathew na Ruby


waliwasili katika shule ya kimataifa alikosoma Zoe,Zari akashuka na kwenda kujiandikisha katika kitabu cha wageni.Baada ya kujiandikisha, akarejea garini wakafunguliwa geti na kuruhusiwa kuingia ndani.


Joseph mmoja wa walinzi wa Kasiano aliyekuwa anawafuatilia akina Mathew aliegesha gari umbali wa mita kadhaa kutoka pale shuleni halafu akampigia simu nabii Kasiano


“Joseph nipe taarifa!


“Mkuu nimemfuatilia Yule manamke,hakuwa peke yake kuna mtu alikuwa anamsubiri katika gari”


“Dereva wake?


“Hapana si dereva kwa sababu anayeendesha gari ni Yule mwanamke”


“Taarifa gani unataka kunipa? Kasiano akauliza


“Wale jamaa wamekuja


hapa katika shule alikosoma


Zoe”


“Wamekwenda shuleni?


“Ndiyo mkuu”


Ukapita ukimya halafu Kasiano akasema


“Ahsante John endelea kuwafuatilia na unijulishe pindi watakapokuwa wametoka” akasema Kasiano na kukata simu halafu akampigia John Mkizi


“John kuna kazi ya haraka nataka ifanyike.Kuna mwanamke mmoja alifika ofisini kwangu akajitambulisha ni mwandishi wa habari na anatafuta taarifa za mchungaji


Adam,nimemtuma John amfuatilie na amenitaarifu kuwa huyo mwanamke akiwa na mwenzake wamekwenda katika shule alikosoma Zoe.Naamini wanakwenda kutafuta taarifa zake.Nataka uwasiliane na Joseph haraka sana ambaye yuko karibu na shule hiyo muwateke hao jamaa mara tu watakapotoka katika geti la shule na kuwapeleka black site muwahoji tuwafahamu ni akina nani na nini wakachokitafuta.Nina wasi wasi hawa jamaa wanaweza wakawa na mahusiano na Mathew Mulumbi.Naomba jambo hili lifanyike kwa haraka sana ! akasema Kasiano


“Sawa mkuu tunalitekeleza kwa haraka sana ! akasema John






************


Mathew na Zari


walikaribishwa katika ofisi ya mkuu wa shule


“Karibuni sana niwasaidie nini? Akauliza mwalimu mkuu wa shule ile ya kimataifa ya wasichana


“Mwalimu,sisi ni waandishi wa habari tumekuja hapa kutafuta taarifa za mwanafunzi aliyewahi kusoma hapa anaitwa Zoe Adam watwila”


“Zoe Adam Watwila ! akasema mwalimu


“Ndiyo” akajibu Mathew na mwalimu Yule akainua mkono wa simu akampigia katibu wake muhtasi akamtaka amsaidie kutafuta taarifa za Zoe


“Wakati katibu wangu muhtasi anatafuta taarifa hizo,mnaweza kunieleza ni taarifa ipi hasa mnayoitafuta? “Mwanafunzi huyu kwa


sasa amekwisha fariki dunia lakini mazingira ya kifo chake yana utata ndiyo maana tunataka kupata taarifa zake za shuleni kwani taarifa zinatuonyesha kwamba matatizo yake yalianzia hapa shuleni” akasema Mathew na mwalimu Yule mwanamama akainuka akafungua kabati na kutoa faili


“Hili ndilo faili lenye kumbu kumbu za wanafunzi wote wa shule hii waliofariki dunia tangu shule ilipoanzishwa” akalifungua faili lile na kuanza kulitafuta jina la Zoe lakini hakulipata. “Umesema anaitwa Zoe Adam Watwila? Akauliza “Ndiyo mama”


“Hakuna taarifa zake zozote humu ! akasema mwalimu mkuu na kuwatazama akina Mathew kwa mshangao


“Hakuna taarifa zake?Mathew naye akauliza kwa mshangao


“Ndiyo hakuna.Humu ndimo zinakaa kumbu kumbu za wanafunzi wote waliofariki dunia tangu shule imeanzishwa na kuna wanafunzi sita tu waliofariki dunia na kati ya hao hakuna jina la Zoe Adam Watwila” akasema mwalimu mkuu na mara akaingia katibu muhtasi wake na kumjulisha kwamba hakuna taarifa zozote za kumuhusu Zoe katika kumbu kumbu za shule


“Are you sure? Mwalimu mkuu akauliza


“Ndiyo mama nimeangalia zaidi ya mara moja na sijapata taarifa za mwanafunzi huyo” akasema Yule katibu muhtasi


“Check again ! akasema Mathew


“Mna uhakika mwanafunzi huyo amesoma hapa?


“Ndiyo mama amesoma


hapa alikuwa anafadhiliwa na kanisa la injili ya wokovu”


“Kama amesoma hapa kwa nini basi jina lake halipo katika orodha ya wanafunzi waliowahi kusoma hapa? Akauliza mwalimu mkuu


“Hapo hata sisi tunashangaa”Zari akasema


“Je alifariki akiwa kidato cha ngapi? Akauliza katibu muhtasi


“Alifariki akiwa kidato cha tatu”


“Kama alifariki akiwa kidato cha tatu basi lazima kidato cha pili alifanya mtihani wa taifa na lazima jina lake litakuwepo.Ngoja nitazame katika kumbu kumbu za matokeo ya kidato cha pili” akasema katibu muhtasi na kurejea ofisini kwake


“Inashangaza kwa taarifa za huyo mwanafunzi kutoonekana katika kumbu kumbu za shule.Mimi nina miezi mitano tu hapa shuleni na nyuma yangu wamepita walimu wakuu kadhaa ndiyo maana nashangaa kwa nini taarifa za huyo mwanafunzi zikaondolewa katika kumbu kumbu za shule? Akanyamaza mkuu wa shule baada ya katibu muhtasi wake kuingia ofisini.


“Madam katika kumbu


kumbu za shule za kidato cha pili kuna mwaka mmoja kumbu kumbu zake hazipo”


“What’s going on here? Akauliza mwalimu mkuu.Kutoweka kwa kumbu kumbu za Zoe kulimshangaza sana


“Jamani mna uhakika mwanafunzi huyo alisoma shule hii?


“Ndiyo madam.Uhakika zaidi unaweza ukapiga simu katika kanisa la injili ya wokovu ambao ndiyo walikuwa wafadhili wake ukauliza” Akasema Mathew na mwalimu mkuu akamtaka katibu muhtasi wake amtafutie namba za simu za kanisa la wokovu na kwa haraka akaingia mtandaoni akatafuta mawasiliano ya kanisa hilo na kumpa mwalimu mkuu


akawapigia na akathibitishiwa kwamba kweli Zoe Adam Watwila alikuwa anafadhiliwa na kanisa hilo.


“Wanakiri ni kweli alikuwa anasoma hapa sasa kwa nini taarifa zake hazipo? Hata kama mwanafunzi akifariki lazima kuwepo na kumbukumbu lakini kwa huyu hakuna kumbukumbu zozote”


“Madam nina wazo.Kwa nini usiwasiliane na watu wa baraza la mitihani naamini lazima wana kumbu kumbu na wakaweza wakatusaidia kujua kama Zoe alifanya mtihani wa


taifa ”


“Hilo ni wazo zuri tena ninao marafiki zangu kule” akasema mwalimu mkuu na kuinua simu akapiga baraza la mitihani na kuzungumza na mmoja wa marafiki zake anayefanya kazi hapo akamtaka amsaidie kutafuta taarifa za Zoe.Baada ya dakika chache akajibiwa kwamba hakuna taarifa zozote za Zoe katika kumbu kumbu za baraza la mitihani,mwalimu mkuu akazidi kuchoka


“Kuna nini hapa kinaendelea jamani?Haya mbona mauza uza?Taarifa za huyu mwanafunzi zimeyeyukia wapi?


“Mwalimu huyu


mwanafunzi ana jina lingine pia anaitwa Naomi Bambi”


“Naomi Bambi? Akauliza katibu muhtasi


“Ndiyo” Mathew akajibu “Unamfahamu? Mwalimu


mkuu akauliza


“Kuna siku niliwahi kusikia walimu wakizungumza na kulitaja jina hilo lakini sikutilia maanani sana.Nadhani ukiwauliza waalimu waliokuwepo hapa ashuleni kwa muda mrefu kuna kitu watakuwa anakifahamu kuhusiana na huyo mwanafunzi” akasema katibu muhtasi.Mwalimu mkuu akainuka na kuwaomba radhi akina Mathew wamsubiri akaelekea katika ofisi ya waalimu


“Hawa watu ni hatari sana.Wanafahamu wanachokifanya na wanahakikisha hawafanyi makosa.Wamehakikisha wameziondoa taarifa zote za Zoe au Naomi kila mahali ! akasema Zari


“Ruby tuko hapa shuleni lakini tumegonga mwamba.Hakuna taarifa zozote za Naomi Bambi”Mathew akamjulisha Ruby


“Dah ! akasema Ruby


“Lakini bado nina imani tun………..” akasema Mathew na kunyamaza baada ya mlango kufunguliwa na mwalimu mkuu kurejea akiwa ameongozana na mwanamama mwingine mwembamba mrefu


“Huyu ni mlezi wa wanafunzi hapa shuleni na amekuwa katika nafasi hiyo kwa muda mrefu na nilipowauliza kama kuna yeyote anayemfahamu Zoe au Naomi akasimama na kudai yeye anamfahamu.Madam hawa ni waandishi wa habari ambao wanatafuta taarifa za Zoe Adam Watwila lakini kwa bahati mbaya hakuna taarifa yake hata moja katika kumbu kumbu za shule.Unaweza ukatueleza vile unavyomfahamu huyo Zoe? Akauliza mwalimu mkuu


“Inashangaza sana kwa


taarifa zake kuyeyuka lakini nitawaeleza ukweli.Zoe toka alipoanza kidato cha kwanza alikuwa ni mwanafunzi aliyekuwa akiishi maisha ya juu sana kuliko wengine wote hapa shuleni.Aliishi kama mtoto wa malkia” akasema mwalimu Yule na kuwaeleza akina Mathew historia nzima ya Zoe namna alivyokuwa akiishi kifahari pale shuleni.Mwalimu mkuu alibaki mdomo wazi kwani kwake ile ilikuwa ni kama hadithi. “Aliletwa mwalimu mkuu mpya na hapo ndipo mambo yalipobadilika.Yeye hakuwa tayari kupokea fedha hizo kutoka kwa huyo mtu asiyejulikana na akamuita baba yake hapa shuleni na mimi ndiye niliyemueleza baba yake kila kitu kuhusiana na mwanae.Nilitumwa nikamuite Naomi lakini sikumpata kwani alikwisha toweka na huo ndio ulikuwa mwisho wake wa kuonekana hapa shuleni.Jioni ya siku ile tukasikia baba yake amefariki dunia na siku chache baadae tukapata taarifa kwamba Naomi ameokotwa


kituo cha basi akiwa hajielewi akapelekwa hospitali na huko akajirusha ghorofani akafariki dunia” akasema mwalimu mlezi wa wanafunzi na ofisi ikawa kimya.Baada ya muda mwalimu mkuu akasema


“NImekuwa katika kazi hii kwa zaidi ya miaka thelathini na sijawahi kukukutana na


kisa cha namna hii” akasema mwalimu mkuu


“Huyo mwalimu mkuu


ambaye alikataa kuchukua fedha na kumuita mzazi wa Naomi anaishi wapi? Zari akauliza


“Amekwisha fariki dunia” “Dah ! Hili jambo mbona linaniogopesha hata mimi ! akasema mwalimu mkuu


“Mwalimu wewe umekuwa


mlezi wa wanafunzi na unawafahamu vizuri.Unaweza ukakumbuka nani aliyekuwa rafiki mkubwa wa Naomi hapa shuleni? Mathew akauliza


“Naomi alikuwa rafiki wa kila mwanafunzi hapa shuleni lakini kuna watatu ambao walikuwa wanakaa chumba kimoja na katika hao watatu alikuwepo mmoja aliyekuwa karibu naye zaidi na hata darasani walikuwa wanakaa kwa kufuatana.Mwanafunzi huyo anaitwa Salome Mwilo mtoto wa gavana wa benki kuu na alihamishwa shule baada ya Naomi kufariki”


Wakati Mathew na Zari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa shule,zilitokea piki piki mbili kila moja ikiwa na watu wawili wakaenda kuegesha katika mojawapo ya vibanda vya kuuzia vinywaji baridi vilivyokuwa katika upande wa pili wa barabara wakaagiza maji ya kunywa.Hakuna mtu yeyote aliyetegemea kama eneo lile muda mfupi ujao pangegeuka uwanja wa vita.


Mathew na Zari baada ya kuridhika na kile walichokipata wakamuaga mkuu wa shule na kutoka wakaelekea katika maegesho walikoacha gari lao


“Mambo yanazidi kuwa


mambo.Hii taarifa tuliyoipata hapa shuleni ni nzito sana na kwa mbali picha inaanza kujitengeneza yenyewe.Hili suala la Zoe ni kubwa zaidi ya tunavyodhani” akawaza Mathew


“Ruby tumemaliza hapa


tunaondoka.Tafuta taarifa za Salome Mwilo ambaye tumeelezwa alikuwa rafiki wa karibu wa Naomi.Kuna mambo ambayo atakuwa akiyafahamu kuhusu Naomi ambayo yanaweza kutusaidia katika uchunguzi wetu” akasema Mathew


“Sawa Mathew I’m on it !


akajibu Ruby


“Eagle team we’re leaving! Zari akawajulisha makomando wa SNSA akawasha gari na kuelekea getini.Baada ya kufika getini Zari akashuka kwa ajili ya kwenda kusaini kitabu cha wageni na wakati huo geti likafunguliwa na kuwa wazi kwa ajili ya akina Mathew kutoka


Katika kibanda cha kuuza vinywaji baridi,jamaa wawili kati ya wale wanne waliofika na pikipiki walipoona geti limefunguliwa na Zari akisaini kitabu ili watoke, haraka haraka wakaacha vinywaji vyao na kubeba mabegi yao wakavuka barabara wakielekea getini.Zari alimaliza kusaini kitabu cha wageni na kugeuka kwa ajili ya kurejea katika gari lao mara wale jamaa wawili kila mmoja akachomoa bunduki ndogo kutoka katika begi na kuanza kumimina risasi juu.Walinzi wakapatwa na mstuko mkubwa kila mmoja akalala chini.Mathew aliyekuwa garini aliwaona wale jamaa wakikimbia wakielekea getini huku wakipiga risasi juu,mlango wa upande wa dereva ulikuwa wazi kama mshale akaruka nje


“Zari get down !! akasema na kumfuata Zari akamshika mkono na kumvuta nyuma ya gari na wakati huo wale jamaa walikwisha fika getini.


“They’re coming for us.Let’s surprise them !


akasema Mathew na kwa kasi ya ajabu akatoka nyuma ya gari na kuachia risasi kutoka katika bastora yake akamlenga jamaa mmoja kati kati ya paji la uso akaanguka.Mwenzake aliruka katika maua huku risasi zikimkosa.Mara ghafla likatokea gari ambalo lilifunga breki ya ghafla na mlango ukafunguliwa.Alikuwa ni Joseph na alikuwa tayari katika usukani ili mara tu mateka watakapoingizwa garini aweze kuliondoa mara moja. Jamaa wale wawili waliobaki katika vibanda vya maji baridi nao wakakimbia wakielekea getini huku wakipiga risasi juu na mara Yule jamaa aliyekuwa amejificha katika maua akajitokeza na kuungana nao kuvurumisha risasi katika gari la akina Mathew waliokuwa wamejificha nyuma ya gari


“Eagle team tumevamiwa


tunahitaji msaada wa haraka ! Zari akawajulisha makomando wa SNSA.Wale jamaa waliendelea kusogea zaidi katika gari la akina Mathew huku wakitawanya risasi ili kumzuia Mathew asiweze kutumia bastola yake


Mathew akataka kujaribu


kujitokeza ili aweze kukabiliana nao lakini risasi zilizoendelea kuvurumishwa kama mvua zikamzuia.Mara ghafla makomando wa SNSA wakafika wakiwa na gari lao lisilopenya risasi wakiwa na bunduki nzito.Kilikuwa ni kitendo cha ghafla ambacho Joseph na wenzake hawakuwa wamekitarajia.Makomando walianza kuvurumisha risasi kwa wale jamaa.Joseph akaliondoa gari kwa kasi lakini risasi kutoka katika bunduki nzito aina ya HK 416 kutoka kwa mmoja wa makomando


ilipasua kioo na kutua kichwani kwake gari likayumba na kwenda kugonga ukuta,Joseph akangukia usukani


Mivumo ya risasi kuelekea upande waliokuwepo akina Mathew ikakoma baada ya makomando kuwasili,Mathew akamuona mmoja wa wale wavamizi akiwa amejibanza katika kona ya geti hakumkawiza akamtandika risasi kadhaa na kummaliza eneo likawa kimya


“Mathew are we safe? Zari akamuuliza Mathew


“We’re safe.Back up team is here” akasema Mathew na kumshika mkono Zari wakatoka nyuma ya lile gari.


“Madam you are safe now !


akasema mmoja wa makomando. “Imekuaje mkashindwa kung’amua kama kuna watu wanatufuatilia? Akauliza Zari


“Zari mambo hayo ni baadae.Kwa sasa tunatakiwa tuondoke haraka sana kabla wananchi na polisi hawajafika eneo hili.Wapekueni hao jamaa wote chukueni kila walicho nacho tutakwenda kufanya uchunguzi kuwafahamu ni akina nani” Mathew akatoa maelekezo halafu akaelekea katika gari la Joseph akaufungua mlango na kumpekua akamkuta na simu akaichukua halafu akachukua mkasi mdogo maalum kwa kukatia vitu vigumu akakata kidole gumba akakifunga katika kitambaa akarejea katika gari lao ambalo halikuwa na tundu hata moja la risasi licha ya kumiminiwa risasi nyingi kwani ni gari lisilopenya risasi.Zari akawasha gari wakaondoka kwa kasi huku wakiacha taharuki kubwa ikiwa imetanda eneo lile




***********


“Darling kuna tatizo gani? Uliponipigia simu na kunitaka nirejee nyumbani nimestuka na kujiuliza masali mengi kuna nini? Rita mke wa nabii Kasiano akamuuliza mume wake baada ya kuwasili nyumbani na kumkuta mume wake tayari amekwisha rejea


“Samahani Rita kwa kukustua lakini nimelazimika kukuita kuna jambo la muhimu sana” akasema Kasiano na kunyamaza akamtazama mke wake


“Nambie Kasiano kuna tatizo gani?


“Imethibitika kwamba


Rais ndiye aliyetoa maelekezo kwamba Mathew Mulumbi ahamishwe” akasema Kasiano


“Oh my God ! Rita akasema kwa mshangao “Nadhani tayari umekwisha pata picha ya tunakoelekea.Ni wazi huu ulikuwa ni mpango uliotengenezwa ndani ya serikali kumtorosha Mathew Mulumbi na nina uhakika Rais anafahamu mahala alipo hata hivyo tunahitaji kupata uhakika zaidi ndiyo maana nimemuita hapa mama Bella


ili kuzungumza naye jambo


hili”


“Bella anakuja?


“Ndiyo


anakuja.Nimelazimika kumuita hapa kutokana na suala hili kuvuka mpaka.Kwa hapa lilipofika hatuna namna zaidi ya kumuhusisha mama Bella” akasema Kasiano


“Ngoja nifanye maandalizi haraka haraka ! akasema Rita na kuwaita watumishi wa ndani akawapa maelekezo na maandalizi yakaanza mara moja.Wakati maandalizi yakiendelea Kasiano akampigia simu Joseph ili kufahamu kama zoezi la kumteka mwanamke Yule aliyekwenda kumuhoji kuhusu Adam limekamilika lakini simu ya Joseph haikupatikana hivyo akalazimika kumpigia simu John Mkizi na kumuuliza kama zoezi limefanikiwa. “Mkuu nimetuma vijana


wanne wakiwa na piki piki na tayari wamekwisha fika eneo la tukio wakimsubiri mwanamke huyo atoke kwani hadi ninawasiliana nao bado alikuwa ndani”


“Hebu wasiliana nao tena ujue wamefikia wapi” akaelekeza Kasiano


“Nahitaji sana kumfahamu Yule mwanamke ni nani.Hawezi akaibuka tu na kuanza kutafuta taarifa za


Adam na mwanae kwa wakati huu lazima atakuwa na mahusiano na Mathew Mulumbi kwani ndiye ambaye alikuwa katika harakati za kulichunguza jambo hili.Wasisitize kwamba jambo hili ni muhimu mno na sihitaji kosa lolote lifanyike.Nataka mpaka jioni ya leo niwe tayari na taarifa za kutosha kuhusiana na Yule mwanamke.Umenielewa John?




“Nimekuelewa mkuu”

“Good.Keep me posted ! akasema Kasiano na kukata simu akalegeza tai yake

“Leo ni siku ngumu sana.I need something strong ! akawaza na kuelekea katika kabati kunakohifadhiwa chupa za mvinyo akachagua mvinyo mkali akamimina katika glasi akagugumia wote na kufumba macho

“Dah ! akasema kisha akaelekea chumbani kwake.

“Vita na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania haitakuwa vita rahisi.Yeye ni mkuu wa nchi na ana nguvu kubwa kuliko sisi wote na anao uwezo wa kufanya lolote lakini kama kweli ameshiriki katika suala hili la kumtorosha Mathew Mulumbi basi lazima atakuwa anafahamu kila kitu kinachoendelea hivyo lazima tupambane naye kwa namna yoyote ile.Haitakuwa vita rahisi.It’s a victory or death ! akawaza Kasiano na kuvuta pumzi ndefu

“Bahati nzuri kwa upande wetu tumetengeneza mtandao mpana sana ndani ya serikali na kubwa ambalo najivunia ni kwamba kiongozi wetu mkuu ni mama Bella mke wa Rais.Huyu ndiye atakayeongoza mapambano dhidi ya mume wake ndiyo maana ninasema haitakuwa vita nyepesi kwani Rais akilijua hili sote tutaangamia,we need to be very carefull” akawaza Kasiano akachukua simu na kumpigia David Chamwino

“David mambo

yanakwendaje kwa upande wako?

“Huku mambo

yanakwenda vizuri.Maandalizi yanaendelea na kesho Dr Fabian atafikishwa mahakamani”

“Good.Nataka

kukufahamisha vile vile kwamba Yeremia amekiri kuwa alitumwa na Rais kumuhamisha Mathew

Mulumbi na hii inaonyesha upo mpango wa siri ulioandaliwa wa kumtorosha Mathew

Mulumbi.Ninalishughulikia hilo kwa sasa ili kutafuta uhakika wa jambo hili na baada ya hapo ndipo tutajua tufanye nini lakini haitakuwa vita rahisi kama kweli Rais anahusika katika mpango ule wa kumtorosha Mathew Mulumbi” akasema Kasiano

“Usihofu Kasiano kila kitu kitakwenda vizuri” akasema David

“Sawa David endelea na mipango yako tutawasiliana jioni” akasema Kasiano na kukata simu


************


Gari mbili zikitanguliwa na gari la polisi ziliwasili katika makazi ya nabii mkuu Kasiano.Huu ulikuwa ni msafara wa mke wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Bella Mayungulu au jina maarufu mama Bella.

Mama Bella licha ya

kutoka katika familia ya kitajiri lakini anajulikana zaidi kwa utajiri mkubwa alionao yeye

binafsi.Anatajwa kumiliki mashamba makubwa,viwanda,migodi ya madini na yuko katika maandalizi ya kuanzisha shirika lake la ndege litakalojulikana kama Bella Air.Ni mwanamke ambaye jina lake liko vinywani mwa watu kila siku.Amekuwa ni mtu wa kujitolea sana katika mambo mbali mbali ya kijamii,kama vile kusaidia vikundi mbalimbali vya akina mama na vijana,wazee,wanafunzi na walemavu.Ni mwanamama ambaye hupenda kujichanganya na watu wa kila rika.Bella anatajwa kuwa ni mmoja kati ya wanawake wenye nguvu kubwa ya ushawishi na inadaiwa ushawishi alio nao katika jamii ulimsaidia sana mume wake Festus kushinda uchaguzi na kuwa Rais wa

Tanzania.Pamoja na mafanikio hayo makubwa aliyonayo lakini siri kubwa ambayo watu wengi hawaifahamu ni kwamba Bella na mume wake Rais Festu Mayungulu wana mgogoro mkubwa sana licha ya mara kwa mara kuonekana wako pamoja.

Nabii Kasiano na mke wake Rita walimpokea mgeni wao na kumkaribisha ndani katika sebule maalum

“Mama karibu sana” akasema Rita akiwa amepiga goti moja akimkaribisha mama Bella kinywaji

“Ahante sana Rita.Ndiyo maana hujisikia furaha sana nijapo hapa kwenu mu wakarimu mno” akasema Bella na kunywa funda moja

“Kasiano shughuli zako zinakwendaje? Kanisa linakua?

“Ndiyo mama.Kanisa

linakua kwa kasi kubwa na idadi ya waumini inaendelea kuongezeka” akasema Kasiano

“Hizo ni habari nzuri” akasema Bella na kunywa kinywaji.

“Hata hivyo,kuna ulazima wa kwenda kuongeza nguvu zaidi.Kwa sasa kuna ushindani mkubwa.Yameibuka makanisa mengi na waumini wanachanganyikiwa hawajui waende wapi”

“Nakubali mama kuna

ushindani lakini ninachoshukuru ni kwamba kwetu waumini wamekuwa wakiongezeka”

“Bado haitoshi.Kanisa linatakiwa liwe kubwa zaidi.Linatakiwa liwe ni namba moja na kupata waumini wengi zaidi si hapa tu Dar es salaam bali pia hata mikoani na njia pekee ya kuwafanya waliopo waendelee kudumu na kuwavuta wengine zaidi ni kwa kuongeza miujiza na kufanya mambo makubwa zaidi ambayo wengine hawawezi.Hii miujiza ya kuponya walemavu imekwisha zoeleka wewe unapaswa kufanya makubwa zaidi ya hayo ndiyo maana nataka uende tena kozi na ukirudi basi uweze kufanya mambo makubwa sana.Kanisa hili ni mwavuli mkubwa unaotukinga sisi sote” akasema Bella

“Hakuna tatizo katika hilo mama.Neno lako ni amri kwangu na siwezi kusema hapana” akasema Kasiano

“Good.Maandalizi yataanza na pale mambo yakikaa vizuri utajulishwa”

“Sawa mama”

“Haya Kasiano nimekuja

kukusikiliza tatizo lako.Je ni tatizo la kibiashara au la kikanisa? Akauliza Bella

“Ni tatizo la kibiashara mama”

“Sawa hebu nieleze”

“Mama ili kukuza zaidi

soko letu la ndani niliona ni vyema kuanza kuwekeza kwa wanafunzi wa chini na wa kati”akaanza Kasiano na Bella akamkatisha

“Kasiano nilikukataza jambo hilo kwa hapa Tanzania!


“Ndiyo mama lakini kuna jambo nilillifanya ambalo sikujua kama huko mbeleni linaweza kuwa na madhara”

“Ulifanya nini? Akauliza Bella na Kasiano akavuta pumzi ndefu

“Nilianza utaratibu wa kuwaingiza katika mtandao na kuwafundisha kazi mabinti wa umri wa kati na hasa wanafunzi ili wakiwa katika umri mdogo basi wanogewe na fedha na pale watakapomaliza masomo wajikite zaidi katika biashara.Kuwatumia wanafunzi hawa ni wazo zuri sana kwani wanaweza wakapita kiurahisi sehemu mbali mbali wakiwa wamebeba mzigo mkubwa.Nilianza kwanza na msichana mmoja anaitwa Zoe Adam watwila au Naomi Bambi.Huyu binti nilianza kwa kusafiri naye safari kadhaa nje ya nchi halafu nikaanza kumsaifirisha peke yake ili kumpa uzoefu na baadae nikaanza kumpa kiasi kidogo cha mzigo na akaufikisha sehemu husika na tayari nilikwisha mkutanisha na watu mbali mbali na mbinu mbali mbali alizifahamu.Kwa ujumla naweza kusema kwamba nilimuandaa vyema kabisa Yule binti ila ilitokea bahati mbaya baba yake akapata taarifa za kuhusu maisha ya mwanae.Baba yake ni mmoja wa wachungaji wangu na ili kulimaliza suala lile lisiende mbali zaidi nikalazimika kuwaondoa Adam na mke wake na mwisho nikamuondoa Yule binti.Sikuwa na namna nyingine na hapo ndipo matatizo yalipoanzia.Kuna watu walianza kumchunguza

Yule binti lakini nilifanikiwa kuwaondoa wote na mambo yakawa shwari hadi hivi majuzi aliporejea nchini mtu mmoja anaitwa Mathew Mulumbi”

“Mathew Mulumbi ! Huyu ambaye amekamatwa kwa mauaji na jana akatoroshwa?

“Ndiye huyo”

“Ameleta tatizo gani kwako huyu jamaa?akauliza Bella

“Kuna rafiki yake anaitwa Gosu Gosu ambaye tulimtengenezea kesi ya mauaji na amefungwa gerezani Arusha.Mathew aliporejea alianza kuchunguza nani waliomtengenezea kesi ya mauaji rafiki yake na hapo ndipo mvurugano ulipoanza.Amenusurika kifo mara kadhaa hadi tulipotengeneza tukio lile akakamatwa na polisi.Kwa tukio lile namna tulivyolitengeneza tuliamini ulikuwa ni mwisho wa Mathew Mulumbi lakini kwa bahati mbaya jana akatoroshwa na mpaka sasa hatufahamu mahala alipo” akanyamaza kidogo halafu akaendelea

“Mama nimekuita hapa kuomba msaada wako kwani tunaamini Rais Festus ameshiriki katika mpango huo wa kumtorosha Mathew Mulumbi au kama hajashiriki basi kuna kitu anakifahamu kuhusiana na jambo hilo” akasema Kasiano na ukimya ukatanda mle ndani

“Kweli hili ni tatizo” akasema Bella kwa sauti ndogo akanywa kinywaji kidogo halafu zikapita sekunde chache akasema

“Kasiano unao uhakika kama kweli Festus ameshiriki katika mpango huo wa kumtorosha Mathew Mulumbi?

“Sina uhakika bado lakini kwa mujibu wa mkuu wa jeshi la polisi Yeremia Mwaipopo ni Rais Festus aliyempa maelekezo kwamba Mathew Mulumbi ahamishwe kutoka kituo cha polisi apelekwe katika gereza la Uwangwa na kwa namna mchezo ulivyochezwa utaona kabisa watekaji walikuwa na taarifa zote kuhusana na kuhamishwa Mathew.Tunalazimika kuamini kwamba hiki ni kitu kimepangwa ndani ya serikali” akasema Mathew

“Kama ni kweli Festus ameshiriki katika mpango huo basi lazima atakuwa amefahamu kuwa zile tuhuma anazokabiliwa nazo Mathew Mulumbi si za kweli na wanashirikiana kufanya uchunguzi na hii iakuwa mbaya sana kwa upande wetu” akasema Bella

“Mathew tayari amekwisha anza uchunguzi na ndiyo maana tumekuwa tukichukua kila hatua kumdhibiti lakini kila pale tunapomnasa na ndoano yetu amekuwa akichomoka”

“What do you want me to do? Akauliza Bella

“Kwanza kabisa tunahitaji kuwa na uhakika kweli Rais ameshiriki katika jambo hili na mtu pekee ambaye anaweza akatusaidia kupata uhakika huo ni wewe mama” akasema Kasiano

“Dah ! hapo kuna ugumu kidogo.Ngoja niwapeni siri ambayo hamuifahamu.Mimi na Rais kwa sasa hatuna maelewano mazuri.Tuna mgogoro mkubwa wa ndani japo tukiwa nje tunaonekana ni watu wenye furaha lakini ukweli ni kwamba tunaigiza na kumuuliza jambo kama hili itakuwa vigumu sana.Hata hivyo nitatafuta namna ya kufanya kuupata ukweli.Kama Yeremia amekiri alitumwa na Festus nitaanzia kwake.Yule ni rafiki yangu na mimi ndiye niliyemtaka Festus amteue kuwa mkuu wa polisi.Mimi na Yeremia tumesoma darasa moja shule ya sekondari hivyo ni marafiki wakubwa na hawezi kunificha kitu atanieleza ukweli wote kama kulikuwa na mpango wowote wa ndani wa kumtorosha Mathew Mulumbi.Baada ya kupata uhakika huo ndipo tutajua nini cha kufanya” akasema Bella

“Mama ninakushukuru sana kwa hilo.Huyu Mathew Mulumbi amekuwa ni tishio kubwa kwetu tunatakiwa haraka sana tufahamu mahala alipo.Tukimpata huyu mtu basi tutakuwa na amani” akasema Kasiano

“Mimi nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha tunaupata ukweli wa jambo hili.Ninataka pia kufahamu kuhusu Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo ana mahusiano gani na Mathew Mulumbi?Nimesikia naye

anashikiliwa na jeshi la polisi”

“Mathew na mke wa Dr Fabian ni marafiki wakubwa hivyo watatu hawa na baadae wakamuongeza Kamishna Jenerali Chambao Mnenge waliungana katika kufanya uchunguzi wa watu waliosababisha Gosu Gosu akafungwa gerezani.Dr Fabian na Chambao wasingeweza kuachwa kwani tayari wanafahamu kuhusu sisi na ndiyo maana nao wakaingizwa katika suala hili lakini tayari Chambao amefariki dunia na tunaowatafuta hivi sasa ni Mathew na mke wa Dr Fabian”

“Umezungumza kuhusu Ruby mke wa Dr Fabian kuna picha nimeanza kuiona.Nilielezwa na watumishi wetu wa ndani kwamba watoto wa Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo walikuwepo pale ikulu lakini baadae waliondolewa na sikutaka kuuliza wamepelekwa wapi.Baada ya maelezo haya uliyonipa sasa nimeanza kupata picha kwamba yawezekana kweli Festus ameshiriki katika mpango huu wa kumtorosha

Mathew.Festus na Dr Fabian ni marafiki wakubwa na kama Dr Fabian alikuwa anashirikiana na Mathew kuwatafuta basi lazima Festus naye atakuwa analifahamu jambo hili hivyo uhakika wa yeye kushiriki katika mpango wa kumtorosha Mathew ni mkubwa hata hivyo nitafanya uchunguzi wangu kwanza ili nipate uhakika na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya.Nipeni muda hadi jioni ya leo nitakuwa nimepata jibu na tutawasiliana tujue nini tunafanya”akasema Bella na kuchukua simu yake akampigia simu mkuu wa jeshi la polisi Yeremia Mwaipopo

“Madam First lady ! akasema Yeremia

“Yeremia nahitaji kuonana nawe mchana huu.Tunaweza kutana ofisini kwangu tafadhali? Akauliza Bella

“Mama Bella nimebanwa

san…..”

“Yeremia please it’s very important.Naomba tuonane ofisini kwangu”

“Sawa madam Bella ninakuja hapo” akajibu Yeremia

“Vijana wangu naomba

niwaache ili nikaanze kulifuatilia hili suala.Kama kuna kitu Yeremia anakifahamu basi atanieleza na mimi nitawajulisha halafu tutaanzia hapo” akasema Bella na kusimama.Kasiano na mkewe Rita wakamsindikiza

hadi katika gari lake akaondoka

Baada ya Bella kuondoka ,Kasiano akarejea ndani na kitu cha kwanza alichokifanya ni kumpigia simu John Mkizi kupata taarifa kuhusiana na maelezo aliyoyatoa kuhusu kumteka mwanamke Yule mwandishi wa habari aliyemfuata ofisini kwake

“John nipe taarifa umekwisha wasiliana na Joseph? Akauliza Kasiano

“Mkuu kuna tatizo limetokea”

“Nini kimetokea John?

“Simu za Joseph na wale vijana niliowatuma hazipatikani.Nimetuma watu wawili kuwafuata na kujua kama kuna tatizo lolote” akasema John



“Madam first lady,leo ni siku ambayo nina ratiba ndefu sana lakini nimelazimika kukatisha ratiba nyingine ili niweze kuja kuonana nawe kama ulivyoomba” akasema mkuu wa jeshi la polisi

Yeremia Mwaipopo baada ya kuwasili katika ofisi ya mama Bella

“Yeremia utanisamehe kwa kukusumbua nina jambo linanisumbua kidogo” “Usijali Bella”

“Naamini suala linalowaumiza vichwa vyenu

kwa sasa ni Mathew Mulumbi”


“Kweli kabisa.Huyu jamaa anaumiza mno vichwa vyetu.Tunamsaka kwa udi na uvumba na mpaka sasa hatujui yuko wapi”

“Ni suala hilo hilo ambalo nami nimekuitia hapa.Kuna tetesi nimezisikia kwamba wewe na Rais mnahusika katika kumtorosha Mathew Mulumbi.Hizi ni tetesi za

kweli? Akauliza Bella bila kupepesa macho

“Bella hata mimi

nimezisikia taarifa hizo lakini hazina ukweli wowote.Hadi sasa hakuna anayefahamu nani aliyemtorosha Mathew Mulumbi na jeshi la polisi linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watu hao pamoja na Mathew” Akasema Yeremia

“Yeremia nimekuita hapa tuzungumze jambo hili kwa sababu wewe ni mtu wangu wa karibu na tumekuwa tukishirikiana mambo mengi kabla hata Festus hajawa Rais.Naomba unieleze ukweli wa jambo hili.Je wewe na Festus mmeshiriki katika mpango wa kumtorosha Mathew Mulumbi? Akauliza Bella

“Kwa nini unataka kujua Bella?

“It’s because of Festus.Suala hili linaweza kumletea matatizo ndiyo maana ninataka niufahamu ukweli angali mapema ili nijue namna ya kufanya ili jambo hili lisiweze kuleta matatizo kwani Festus akipata matatizo nami pia nitakuwa matatizoni”

“Madam first lady kwa nini usizungumze na Rais kuhusu jambo hili?

“Hawezi akanieleza chochote unafahamu namna Festus alivyo na misimamo yake.Mara nyingi huwa hanishirikishi katika masula yake ya ofisi hivyo naomba unieleze ukweli Yeremia” akasema Bella na Yeremia akaonekana kusita

“Yeremia please tell me the truth ! Bella akasisitiza.

“Yeremia najua unaufahamu ukweli na haijawahi kutokea hata mara moja ukashindwa kunieleza ukweli” akasema Bella

“Bella nitakueleza ukweli lakini naomba kile nitakachokueleza kibaki ndani ya kuta hizi”

“Usihofu nieleze” akasema Bella na Yeremia akavuta pumzi ndefu kisha akasema

“Something is going on.Kuna kikundi Fulani cha wahalifu ambacho bado hakijafahamika kimekuwa kikiendesha mambo yao ya kihalifu na kinaonekana ni kikundi chenye mtandao mrefu hadi serikalini.Kuna mtu mmoja alibambikiwa kesi ya mauaji na amefungwa maisha katika gereza la

Kimondo Arusha.Huyo jamaa ana mahusiano na Mathew Mulumbi” akasema Yeremia na kunyamaza kidogo “Mathew alianza kufanya uchunguzi kuwabaini watu waliomtengenezea rafiki yake kesi ile ya mauji na kupelekea akafungwa maisha gerezani. Toka ameanza kuchunguza amenusurika mara kadhaa kupoteza maisha.Usiku wa kuamkia jana alitegewa mtego na hao jamaa akakamatwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya na mauaji akafikishwa kituo cha polisi.Mathew alikuwa anashirikiana na Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo,Kamishna jenerali wa magereza Chambao Mnenge na mke wa Dr Fabian na wote hao wakajumuishwa katika tuhuma zinazomkabili Mathew wakidaiwa kushirikiana naye katika mauaji na dawa za kulevya ndiyo maana umesikia Dr Fabian na Chambao wamekamatwa na polisi.Baada ya kuzipata taarifa hizo Rais hakuwa tayari kumuona Dr Fabian akiishia gerezani ndipo ukapangwa mpango wa kumtorosha Mathew Mulumbi ili aweze kuwafuatilia hao jamaa na kuwahamu ni akina nani na vile vile kumsafisha Dr Fabian kwani tayari jina lake limekwisha chafuliwa kwa kumuhusisha katika biashara ya dawa za kulevya na mauaji.Kwa hiyo madam first ule ulikuwa ni mpango maalum umepangwa.Kuna

kundi hatari sana kipo hapa nchini kinaendesha mambo yake ya kihalifu na lengo la kumtorosha Mathew ni ili aendelee kuwasaka wahalifu hao ” akasema Yeremia

“Dah ! akasema Bella

“Ni mambo mazito Bella yanaendelea ! akasema Yeremia

“Festus alipata wapi taarifa hizo za Dr Fabian na wenzake kutengenezewa mtego na hao wahalifu wanaotafutwa na Mathew Mulumbi? Akauliza Bella “Ruby ! akasema Yeremia

“Ruby? Bella akauliza

“Ndiyo.Ruby mke wa

DrFabian usimuone vile she’s very dangerous.Anazo taarifa nyingi sana za kiintelijensia za nchi hii.Kabla ya kuolewa na Festus alikuwa ni mkurugenzi wa SNSA”

“SNSA ni kitu gani? Akauliza Bella

“Hufahamu kuhusu SNSA?

“ Ni mara ya kwanza

ninasikia leo jina hilo sijawahi kulisikia hapo kabla” akasema

Bella

“SNSA means Secret National security Agency” akasema Yeremia

“Kwa Kiswahili ni Idara ya siri ya usalama wa ndani wa nchi.You are the first lady kwa nini hufahamu mambo kama

haya? Ipo taasisi hii ya siri ambayo inafanya kazi zake kwa siri kubwa na watu wengi hata ndani ya serikali hawafahamu uwepo wake.Tunaofahamu ni sisi viongozi wa idara nyeti za serikali kwani kuna wakati huwa tunasaidiana pale inapolazimu.Idara hii iko chini ya Rais wa nchi na kazi yake kubwa ni kuhakikisha inaondoa vitisho vyote vya usalama wa nchi kimya kimya na kuhakikisha nchi inakuwa salama.Ruby aliwahi kuwa mkurugenzi wa idara hiyo hivyo anafahamu mambo mengi” akasema Yeremia

“Ofisi zao ziko wapi hao SNSA? Akauliza Bella

“Ninafahamu uwepo wa

idara hii lakini sifahamu mahala zilipo ofisi zao kama nilivyokwambia idara hii ni ya siri na mambo yake yote ni ya siri kubwa”akajibu Yeremia

“Unamfahamu

mkurugenzi wa sasa wa SNSA

?

“Huyu wa sasa nimewahi kumona mara moja tu baada ya kukutanishwa na Rais na simkumbuki hata jina lake na hana mashirikiano na idara nyingine kama ilivyokuwa kwa Ruby.Mambo haya ukimuuliza Festus atakueleza kwa undani kwani yote yako chini yake” akasema Yeremia

“Unadhani hao SNSA watakuwa wametumiwa kumtorosha Mathew Mulumbi? Akauliza Bella

“Sina hakika.Kwa ninavyofahamu SNSA hawana kikosi wenyewe kazi yao ni kuchunguza na kama kuna ulazima wa kutumia nguvu basi hutumia jeshi la

polisi.Mbona una uliza sana kuhusu Mathew Mulumbi? Do you know him? Akauliza Yeremia

“Kama nilivyokwambia

kuna tetesi za Festus kuhusika katika tukio lile ndiyo maana ninataka kulifahamu kwa undani zaidi suala hilo.Nashukuru umenieleza ukweli na nitajaribu kumshauri Festus kuchukua tahadhari na hata wewe pia jitahidi sana kuchukua tahadhari kwani watu wamekwisha anza kuhisi ule ulikuwa ni mchezo na ninyi mmeshiriki”akasema Bella

“Usijali tuko katika tahadhari ya kutosha” akasema Yeremia

“Yeremia ninakushukuru

kwa uliyonieleza.Sitaki kuendelea kukupotezea muda unaweza kwenda kuendelea na majukumu yako mengine.Kama kuna kitu nitakihitaji usinifungie mlango tafadhali”akasema Bella

“Bella wewe ndiye

uliyenisaidia hadi nikafika hapa bila wewe kumshawishi Festus kuniteua kuwa mkuu wa jeshi la polisi hivi sasa ningekuwa bado ninasota huko chini hivyo ninakuthamini sana na ndiyo maana nimeamua kukueleza ukweli huu ambao ni siri kubwa kati yangu na Rais.Muda wowote ukihitaji chochote mlango uko wazi” akasema Yeremia

“Kabla hujaondoka nataka

kuuliza swali la mwisho,unafahamu alipo Mathew Mulumbi? Akauliza Bella na Yeremia akacheka kidogo

“Hapana madam Bella sifahamu mahala alipo

Mathew

Mulumbi.Anayefahamu haya yote ni mumeo Festus.Ukimuuliza yeye anaweza akakueleza ukweli” akasema Yeremia

“Festus hawezi kukubali kunieleza”

“Kwa nini? Hakuamini? Akauliza Yeremia na Bella akatabasamu

“Festus ana tabia moja.She don’t trust women.Hata katika safu yake ya uongozi kuna wanawake wawili tu” akasema Bella huku akicheka na Yeremia naye akaangua kicheko

“Yeremia ninakushukuru

sana kwa kufika,nililokuitia ni hilo tu na nisingependa nikupotezee tena muda hivyo nakuruhusu uondoke” akasema Bella

“Usijali Bella hujanisumbua.Muda wowote ukiwa na chochote kinakusumbua you know where to find me” akasema Yeremia wakaagana akaondoka zake na Bella akarejea ofisini akaketi kitini akavuta pumzi ndefu

“Namlaumu sana Kasiano

kwa kusubiri jambo hili limefika hapa lilipofika ndipo ananijulisha.Nimetulia nikijua kila kitu kinakwenda vizuri lakini kumbe mambo yanakwenda hovyo na kuna mchwa wanaanza kula nguzo za ngome yangu.Hii ni himaya yangu na lazima niilinde kwa nguvu na uwezo wote nilio nao ! akawaza Bella

“Hii itakuwa ni kama vita ya tatu ya dunia.Festus na Mathew Mulumbi kumbe wanashirikiana kuwatafuta watu ambao wao wanaamini ni mtandao wa wahalifu bila kujua kwamba mimi ndiye kiongozi wao hapa nchini na ukanda wote wa Afrika mashariki.Hatua za haraka sana zinapaswa zichukuliwe katika kuwadhibiti Festus na watu wake kwani tukichelewa huu unaweza ukawa ni mwisho wetu ! Ni wakati sasa wa kutumia kila aina ya nguvu tuliyonayo katika mapambano haya” akawaza Bella na kumpigia simu Kasiano akamjulisha kwamba anakwenda tena nyumbani kwake kuna jambo amelipata.


****************


Wakati akimsubiri

Bella,Kasiano akapewa taarifa na John Mkizi kwamba vijana wote waliotumwa kwenda kumteka mwandishi wa habari wameuawa.

“What?! Kasiano

akauliza,alistuka sana

“Mkuu vijana wetu wote waliotumwa kumteka mwandishi wameuawa akiwemo na Joseph”

“Imetokeaje hiyo John?! Akauliza Kasiano kwa ukali

“Kwa mujibu wa

mashuhuda ni kwamba geti la shule lilipofunguliwa,watu wawili waliokuwa katika kibanda cha kuuza vinywaji baridi wakavuka barabara wakikimbia wakiwa na bunduki hku wakipiga risasi juu wakielekea getini na mara likatokea gari lingine likiwa na watu wenye bunduki nzito wakaanza kuwashambulia wale jamaa ambao ni watu wetu na kuwaua wote kisha wakaondoka

“What the hell !! akasema Kasiano na kugonga meza kwa hasira

“John nataka uende wewe mwenyewe mahala hapo na ujue nini kimetokea.I need answers ! nataka kujua watu wangu wameuawa vipi ! akafoka Kasiano na kukata simu

“What’s going

on?akajiuliza Kasiano

“Why my people are not serious? Kila ninapowaambia kwamba hii vita ni mbaya hawaonekani kujali.Mambo wanayachukulia kirahisi rahisi tu na ndiyo maana tunashindwa kufanikiwa ! Kasiano akaendelea kuwaza akiwa anatetemeka kwa hasira

“Nilikuwa sahihi yule mwanamke lazima ametumwa kwangu kunichunguza na lazima atakuwa anashirikiana na akina Mathew.Jamani huyu Mathew Mulumbi nitampataje? Mbona anaanza kuninyima amani kiasi hiki? Anazidi kupiga hatua na kama tukizembea anaweza akaupata ukweli.Hatupaswi kumpa nafasi.Tuna kikosi chenye nguvu black Mafia ,tuna mtandao mpana hadi ndani kabisa ya serikali lakini wapi tunafeli? Kwa nini tumeshindwa kufahamu mahala alipo Mathew Mulumbi na kuzidi kumpa nafasi ya kutukaribia? Akajiuliza Kasiano

“Kamwe mtu mmoja

hawezi akatuyumbisha namna hii.Lazima tutamfutilia mbali yeye na wale wote anaoshirikiana nao ! akagonganisha mikono kwa hasira

“Lakini huyu jamaa ni binadamu wa namna gani ambaye kila tunapomnasa anaponyoka?Naanza kuhisi labda anatumia dawa huyu jamaa si bure.Hata hivyo ninaapa kwamba haitapita siku ya kesho kabla hatujafahamu mahala alipo !

Kasiano akachukua simu na kumpigia Paul Lewis mkuu wa Black Mafia

“Paul kwa nini watu wako wanashindwa kulipa uzito mkubwa hili suala la Mathew Mulumbi?Black Mafia ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba vikwazo vyovyote vinaondolewa na biashara yetu inakwenda vyema kwa nini basi mnashindwa kukiondoa hiki kikwazo kidogo kama Mathew Mulumbi? Akauliza Kasiano kwa ukali

“Bosi tunalishughulikia hilo suala”

“Black Mafia mmelala hamjui kuna watu hawalali wanatusaka usiku na mchana.Mathew Mulumbi na wenzake hawafumbi macho wanatusaka kwa udi na uvumba na anazidi kutusogelea karibu.Mchana huu tayari tumepoteza watu watano akiwamo Joseph mlinzi wangu.Niliwatuma wamteke mwanamke mmoja mwandishi wa habari ambaye alifika ofisini kwangu kuniuliza kuhusiana na kifo cha Adam Watwila na niligundua alikuwa ananiuliza maswali ya mitego na ndipo nikamtuma Joseph amfuatilie ili tumfahamu ni nani.Baada ya kutoka ofisini kwangu mwanamke huyo alikwenda katika shule alikosoma Naomi akijaribu kutafuta taarifa zake nilipotaarifiwa nikamuelekeza John atume vijana wakamteke huyo mwanamke lakini nimepewa jibu kwamba vijana wote wameuawa akiwemo Joseph.Imeniumiza sana kuwapoteza vijana namna hii na kadiri tunavyoendelea kupoteza vijana ndivyo tunavyowaruhusu hawa watu kutukaribia.Nataka Black Mafia mfanye kazi yenu ipaswavyo.Umenielewa Paul?

“Nimekuelewa mkuu”

“Good.Nataka hadi kufikia kesho jioni Mathew Mulumbi awe amekwisha ondolewa katika dunia hii na uwezo wa kutimiza hilo mnao ! Waite watu wako na uwaeleze hatari inayotukabili kwa sasa”akasema Kasiano “Nitafanya hivyo mkuu”

“Jambo lingine nataka ushughulikie mawasiliano ya Joseph.Naamini hao jamaa waliomuua kitu cha kwanza kukimbilia ni simu ili wajue watu ambao anawasiliana nao hivyo haraka sana hakikisha mnashughuikia suala hilo ili wale jamaa wasipate chochote kwani nao ni wataalamu katika teknolojia”akasema Kasiano.




Kwa kutumia kitanza mbali,Zari akafungua geti la nyumba yake wakaingia ndani kisha gari la makomando wa SNSA waliokuwa wakiwafuatilia kwa nyuma nalo likaingia ndani.Zari ambaye tangu lilipotokea shambulio shuleni walikoenda kufuatilia taarifa za Naomi Bambi alikuwa kimya

kabisa,akashuka garini na kuwafuata makomando ambao walishuka haraka haraka.Zari akawatazama huku uso wake ukiwa umefura hasira

“Nataka mniambie kwa nini mmeshindwa kung’amua kama tulikuwa tunafuatiliwa? Akauliza kwa ukali lakini makomando wale hawakumjibu kitu

“We almost got killed ! akasema kwa ukali.Mathew akashuka garini na kumfuata

“Zari please ! akasema Mathew

“Mathew nataka waniambie kwa nini walishindwa kubaini watu waliokuwa wanatufuatilia mpaka tukanusurika kuuawa? Akauliza Zari

“Badala ya kuwalaumu tunapaswa kuwashukuru wameokoa maisha yetu.Bila wao yawezekana wale jamaa wangeweza kutufikia.Ruby mambo ndiyo kwanza

yameanza hivyo hili lililotokea lisikuogopeshe.C’mon let’s go inside we have a lot of things to do ! akasema Mathew na Ruby akatoka akamshika mkono Zari wakaelekea ndani.

“Thank you

gentlemen.You did great today.You saved us” Mathew akawaambia makomando huku akiwapa mkono wa pongezi

“Ahsante sana kaka.Mtatusamehe kwa kushindwa kung’amua watu waliokuwa wanawafuatilia”

akasema kiongozi wa timu ile ya makomando

“Msijali mambo kama haya yanatokea sana.Watu tunaowatafuta wana utaalamu mkubwa ndiyo maana ikawa vigmu kutambua kama wanatufuatilia.Hata hivyo bado mnastahili sana pongezi kwa namna mlivyoweza kulizima shambulio lile” akasema Mathew

“Ni akina nani wale jamaa? Wanaonekana wako vizuri !

“Bado hatufahamu ni

akina nani lakini si watu wa kudharau.Ni wataalamu,wanajua kujipanga vizuri.C’mon guys lets get inside” akasema Mathew na kuongozana na makomando wale wakaingia ndani akawapeleka katika chumba cha mapumziko ambako aliwahudumia vinywaji halafu akawafuata akina Ruby waliokuwa katika chumba cha Zari, akagonga mlango na Ruby akaufungua.

“Mathew karibu ndani” akasema Ruby na Mathew akaingia ndani akamkuta Zari akiwa amekaa chini ameegemea kitanda huku ameinamisha kichwa chake akionekana kukata tamaa.

“Zaria are you okay? Akauliza Mathew



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog