Simulizi : Scandle (Kashfa)
Sehemu Ya Pili (2)
“Mathew ninacho jiuliza kama lengo lao lilikuwa ni kumuua Lidya kwa nini wasigemuua akiwa jijini Dar es salaam? Wangeweza kumfuata nyumbani kwake kwani anaishi peke yake lakini wamesubiri wakati amekuja Arusha ndipo wakamuua” akasema Gosu Gosu
“Gosu Gosu watu waliofanya mauaji hayo ni watu makini na wanaofahamu nini wanakifanya.Walikuwa na sababu zao za kumuua Lidya Arusha wakati ukiwa naye.Hakuna kitu chochote
kingineunachoweza kukumbuka ambacho tunaweza kukiunganisha na mauaji hayo ya Lidya?
Akauliza Mathew “Kwa muda mrefu
nimeishi kwa amani sijawahi kukorofishana na mtu yeyote,mimi nimejikita tu katika biashara” akasema Gosu Gosu.Mathew akatafakari kidogo na kusema
“Gosu Gosu hili suala si dogo.Picha ninayoipata mimi ni kwamba watu hao hawakuwa na lengo la kukuua kwani kama waliweza kuingia
ndani na kumuua Lidya bila wewe kusikia wasingeshindwa kukuua.Kilichofanyika hapa ni kumuua Lidya na kutengeneza tukio ili uonekane wewe ndiye uliyemuua Lidya na lengo ni kupoteza mwelekeo wa uchunguzi.Kwa namna tukio lilivyotengenezwa ni wazi hakuna anayeweza kubisha kwamba hukumuua Lidya na kibaya zaidi ni bastola yako kutumika katika mauaji hayo.Gosu Gosu lazima lipo jambo kubwa nyuma ya mauaji hayo ya Lidya na ili kufahamu kitu gani kilichopelekea kifo
chake italazimu kwanza kumchunguza Lidya mwenyewe.Hakuwahi kukueleza kama kuna jambo lolote la hatari analichunguza?
Akauliza Mathew “Hapana hakuwahi
kunieleza.Lidya alikuwa msiri sana kuhusu kazi yake” akajibu Gosu Gosu
“Ninahisi kuna jambo alikuwa analichunguza na akagundulika ndiyo maana akauawa na wewe ukaangushiwa kesi hiyo ya mauaji.Gosu Gosu nakuahidi nitafanya kila lililo ndani ya
uwezo wangu kuchunguza na kuupata ukweli.Ninakuahidi nitakutoa mahala hapa.Sifahamu na siwezi kukuahidi ni lini lakini amini nitakuondoa mahala hapa.Lazima muuaji wa Lidya apatikane na kuja kutumikia adhabu hii ambayo umeangushiwa wewe” akasema Mathew
“Mathew baada tu ya kukuona nimepata matumaini ya siku moja kutoka ndani ya hili gereza.Tafadhali Mathew naomba uniondoe hapa gerezani.Ni sehemu yenye
mateso makubwa na kuna watu hawanipendi humu wanaweza wakaniua muda wowote” akasema Gosu Gosu na kumueleza Mathew mambo anayokutana nayo mle gerezani
“Pole sana Gosu Gosu.Haya yote yatakwisha pale tutakapokuwa tumempata muuaji na ninakuahidi lazima atapatikana” akasema Mathew na ukimya mfupi ukapita baada ya askari magereza aliyekuwa amesimama pembeni kutazama saa yake
“Gosu Gosu nadhani muda wangu umekwisha.Nataka kufahamu kuhusu Ruby.Yuko hapa nchini au ameondoka?
Akauliza Mathew
“Ruby yupo aliolewa na rais Fabian kelelo”
“Aliolewa na Dr Fabian?
Mathew akauliza
“Ndiyo aliolewa na Dr Fabian” akajibu Gosu Gosu
Askari magereza akawafuata na kumjulisha Mathew kwamba muda wake umekwisha.Wakaagana na Gosu Gosu akachukuliwa akatolewa mle ndani.Mathew
naye akaondoka zake.Alipoingia garini akaegemea kiti na kuvuta pumzi ndefu
“Ee Mungu niongoze niweze kuwapata waliomuua Lidya na kumsababishia Gosu Gosu adhabu ya kifungo cha maisha gerezani” akawaza Mathew na kuwasha gari akaondoka
“Kwa namna tukio lile lilivyotegenezwa hata kama mimi ningekuwa jaji ningeamini kuwa Gosu Gosu amefanya mauaji yale lakini ninamfahamu Gosu Gosu na
ninaamini hajaua.Ni jukumu langu kuhakikisha ninawasaka na kuwapata wale wote waliofanya jambo hili na kumuangushia mzigo Gosu Gosu.Jambo hili haliwezi kufanywa na mtu mmoja lazima upo mtandao tena wa watu makini na wanaojua nini wanakifanya.Haitakuwa shughuli ndogo lakini nitapambana nao.Hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe” akawaza Mathew na kutoka gerezani akashika barabara kurejea jijini Arusha.
“Mauaji yalitokea Kobe village hoteli.Breki ya kwanza ni hapo” akawaza Mathew
************
Kobe village moja ya hoteli kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki iliyoko jjini Arusha ilipewa jina hilo kutokana na muonekano wake kama kijiji.Kulikuwa na nyumba kadhaa ndogo ndogo kwa ajili ya wageni wale ambao hupenda kukaa katika nyumba na kujihudumia kama vile wako nyumbani,vile vile
kulikuwa na majengo pacha marefu yenye ghorofa thelathini kila moja.Ni moja ya hoteli ambayo hufikiwa na mamia ya wageni kila siku kutokana na ubora wake.
Mathew Mulumbi aliwasili katika hoteli hii akaelekea mapokezi akapokewa vyema na wahudumu wenye mafunzo ya hali ya juu ya namna ya kukaribish wageni.Ufikapo katika hoteli hii hata kama ulikuwa na hasira za namna gani utajikuta ukitabasamu kutokana na makaribisho utakayopewa.Mathew
alichagua kufikia katika nyumba ile ile ambayo yalifanyika mauaji ya Lidya,muhudumu akamuongoza hadi katika nyumba ile.
Baada ya muhudumu kutoka Mathew akaanza kuikagua ile nyumba
“Natakiwa kufahamu namna wauaji walivyoweza kuingia ndani ya nyumba hii bila ya Gosu Gosu kuwasikia” akawaza na kuanza kukagua chumba kimoja kimoja na mwisho ikawa ni chumba cha
kulala.Akasimama mlangoni na kutazama kitanda
“Humu ndimo mauaji yalifanyika na kuharibu maisha ya Gosu Gosu” akawaza na kuanza kukagua chumba kile
“Siwezi kugundua chochote inaonekana kuna ukarabati mkubwa umefanyika katika nyumba hii baada ya mauaji ya Lidya kutokea” akawaza wakati akilitazama dari
“Waliofanya mauaji yale lazima ni majasusi wa hali ya juu sana.Hawakuonekana
wakati wakiingia wala wa kutoka” akaendelea kuwaza Mathew akiwa amekaa kitandani
“Nani mmiliki wa hoteli hii? Akajiuliza Mathew na kuinua mkono wa simu iliyokuwamo mle chumbani akapiga mapokezi
“Kobe village hapa idara ya huduma tukusaidie nini?
Ikasikika sauti ya mwanadada simuni
“Ninaomba kuzungumza na Juliana tafadhali” akasema Mathew
“Juliana ametoka kidogo na atarejea muda si mrefu”
“Sawa akirejea anipigie niko nyumba 36 kitalu C” akasema Mathew na kukata simu
Juliana ni mfanyakazi wa hoteli ya Kobe katika sehemu ya mapokezi ambaye alizoeana na Mathew kwa haraka sana wakati alipowasili
“Kumbe Ruby aliolewa na Dr Fabian”akawaza Mathew akiwa amekaa sofani
“Sitakiwi kuumia kwa sababu nilimpa uhuru mimi mwenyewe wa kuendelea na
maisha yake.Amefanya maamuzi mazuri na ninaamini huko aliko hivi sasa ana furaha” akawaza Mathew na simu ya mle chumbani ikaita
“Huyu lazima atakuwa ni Juliana” akawaza Mathew na kuinua mkono wa simu
“Hallow” akasema “Hallow unazungumza na
Juliana hapa mapokezi.Nimekuta ujumbe wako unahitaji kuzungumza nami” akasema Juliana
“Ndiyo Juliana nilipiga simu nikaambiwa umetoka
kidogo.Saa ngapi unamaliza zamu yako?
“Mimi nimekwisha maliza zamu yangu,nilikuwa usiku lakini nimechelewa kuondoka kwa sababu aliyetakiwa kunipokea alipata dharura kidogo hivyo ikanilazimu kuendelea na zamu.Tayari amekwisha fika na mimi ninaondoka sasa hivi”
“Sawa Juliana kabla hujaondoka tunaweza kuzungumza kidogo? Akauliza Mathew
“Hakuna tatizo tunaweza kuzungumza”
“Ahsante sana Juliana.Unaweza ukaja hapa namba 36 kitalu C?
“Sawa ninakuja hapo sasa hivi” akasema Juliana na kukata simu
Haukupita muda mrefu kengele ya nyumba alimo Mathew ikagonga akainuka na kwenda kuufungua mlango
“Juliana karibu sana” “Ahsante.Nimesahau jina
lako unaitwa nani? “Naitwa Mathew
Mulumbi”
“Mathew Mulumbi?! “Ndiyo”
“Hili si jina geni kulisikia” “Umewahi kulisikia wapi? “Sikumbuki nadhani ni
kwenye filamu.Kwani wewe unacheza filamu?
“Hapana mimi si mcheza filamu”
“Unajishughulisha na nini? Akauliza Juliana
“Ni mfanya biashara” “Biashara gani
unashughulika nayo?
“Nina fanya biashara ya viatu.Huagiza viatu kutoka nchi za nje na kuvileta hapa nchini”akasema Mathew
“Hongera sana”
“Ahsante”
“Jambo gani unataka kuzungumza nami?
Nimechoka ninataka nikapumzike”
“Nilitegemea utamaliza zamu yako jioni hivyo nikataka kukuomba unipe kampani kwani nimeboreka sana hapa peke yangu kwa bahati mbaya kumbe zamu yako imemalizika asubuhi” akasema Mathew na Juliana akatoa kicheko
“Samahani sana nimekwisha maliza zamu yangu na hata hivyo isingekuwa rahisi kupata
nafasi ya kuwa nawe hata kama ningekuwa namaliza zamu yangu jioni” akasema Juliana na kumuonyesha Mathew kidole kilichokuwa na pete ya ndoa
“Mimi tayari ni mke wa mtu hivyo kila pale nimalizapo zamu yangu hurejea haraka sana nyumbani kutimiza majukumu yangu kama mke” akasema Juliana
“Hongera sana lakini hata mimi vile vile ni mume wa mtu na sioni ubaya wa kukaa kuzungumza kupata kinywaji
na kubadilishana mawazo” akasema Mathew
“Wewe pia ni mume wa mtu? Mbona sioni pete kidoleni mwako? Akauliza Juliana
“Pete ni utambulisho tu lakini ndoa iko moyoni.Wangapi wanavaa pete vidoleni lakini wanatoka nje ya ndoa zao? Pete nzuri ni ile inayovishwa moyoni.Lakini naomba niwe mkweli kwako kwamba sina mke kwa sasa tumetengana”
“Kwa nini mlitengana?
Akauliza Juliana
“Ndoa zina mambo mengi Juliana tuachane na hayo.Nimeboreka sana nahitaji mtu walau wa kuzungumza naye mambo mbali mbali”
“Nitakutafutia mtu Mathew usijali”
“Sihitaji mtu mwingine nakuhitaji wewe”
“Kwa nini mimi? “Sifahamu lakini
nimevutiwa tu kutaka kuzungumza nawe” akasema Mathew na Juliana akatabasamu kwa mbali
“Niambie kuhusu mumeo ana wivu? Akauliza Mathew
“Ana wivu sana” “Imekuaje akakuruhusu
ukafanya kazi sehemu kama hii ambayo unakutana na watu wa kila aina na wengine ni kama mimi wanaweza wakakuona tu wakavutiwa nawe? Akasema Mathew na Juliana akaangua kicheko
“Mimi ninajielewa kwamba nina mume na ninajiheshimu hivyo hata kama atatokea mtu na kuhishawishi vipi siwezi kukubali”
“Hongera kwa msimamo huo.Kama unajiamini kwa nini
basi unaogopa kukaa nami kwa mazungumzo? ‘
“Ninahitaji kupumzika nimechoka sana”
“Jioni utakuwepo kazini? “Hapana jioni ya leo
sintakuwepo nitakuwa katika mapumziko hadi kesho kutwa asubuhi ndipo nitaingia kazini”
“Basi nitakutembelea nyumbani kwako jioni ya leo.Nielekeze unapoishi tafadhali” akasema Mathew
“Hapana usije nyumbani kwangu mume wangu ni mkali
sana na atanielewa vibaya” akasema Mathew
“Usihofu Juliana nielekeze mahala unapoishi na nitakuwa mgeni wenu jioni ya leo.Usimuhofie mume wako I can handle him” akasema Mathew
“Huyu jamaa mbona king’ang’anizi namna hii? Najaribu kutumia kila mbinu kumkatisha tamaa lakini bado anaendelea kung’ang’ania” akawaza Juliana halafu akamuelekeza Mathew mahala anakoishi
“Ahsante Juliana nitakuwa mgeni wako jioni ya leo” akasema Mathew na Juliana akatoka.
“Nimeupenda msimamo wa Juliana lakini hadi pale nitakapopata taarifa ninazozihitaji kutoka kwake ndipo nitakapomuachia.Sijali kama ana mume au hana.Ninapohitaji taarifa kutoka kwa mtu yeyote lazima niipate.Najaribu kutaka kupata taarifa za kutosha kuhusiana na hoteli hii ninahisi yawezekana kuna mahusiano
kati ya hoteli hii na yale mauaji ya Lidya” akawaza Mathew
*************
Saa moja za jioni,Mathew Mulumbi akiwa na gari lake aliwasili katika nyumba aliyoelekezwa na Juliana.Ilikuwa imezungukwa na ukuta na geti la rangi nyeusi.Mathew akashuka garini na kwenda kugonga geti.Baada ya dakika mbili mlango mdogo pembeni ya geti ukafunguliwa akatokea Juliana.Usiku huu alikuwa
amevaa fulana ya rangi nyeupe na kaptura nyeusi
“Mathew ?!! akasema Juliana kwa mstuko.Hakutegemea kama Mathew angeweza kufika pale nyumbani kwake
“Hallo Juliana” akasema Mathew huku akitabasamu
“Mathew umekuja kweli ! akasema Juliana
“Nilikuahidi kwamba nitafika Juliana.Naweza kukaribia ndani? Akauliza Mathew.Juliana hakumjibu kitu akafungua geti na kumtaka Mathew aingize gari
ndani halafu akamkaribisha sebuleni
“Karibu sana Mathew” akasema Juliana
“Ahsante Juliana” akajibu Mathew na kuketi sofani Juliana akamuhudumia kinywaji
“Sikutegemea kabisa kama ungeweza kufika”
“Mimi huwa sitanii nikikuahidi ninakuja lazima nifike.Vipi mzee yuko wapi? Akauliza Mathew na Juliana akacheka kidogo
“Mbona unacheka Juliana?Nimeingia katika
himaya ya watu hivyo napaswa kujitambulisha kwa wenye mali haraka” akasema Mathew na Juliana akacheka
“Mathew nilikudanganya.Sina mume”
“Huna mume? “Ndiyo sina mume”
“Mbona ulinionyesha pete kidoleni?
“Ile pete ninavaa kwa sababu maalum.Kuna mmoja wa viongozi wa hoteli ile ninakofanya kazi amekuwa akinitaka kimapenzi na kibaya zaidi kigogo huyo amekwisha athirika na virusi vya
ukimwi.Ili kumkataa nimemwambia kwamba nina mume na ndiyo sababu ya kuvaa pete hii lakini kiukweli sina mume ninaishi peke yangu” akasema Juliana
“Pole Juliana.Mambo kama hayo yapo sana sehemu za kazi kwa viongozi kuwataka kimapenzi wafanyakazi na pale wanapokataa hutishia kuwafukuza kazi.Nakupongeza kwa msimamo wako na ninakuomba uendelee hivyo hivyo na kama akiendelea kukufuata mfikishe katika vyombo husika.Watu wa
namna hiyo wanaotumia madaraka yao kuwanyanyasa wengine hawafai kabisa” akasema Mathew kwa msisitizo
“Ahsante Mathew kwa kunipa moyo nitajitahidi kwa kila namna niwezavyo kumkwepa na kama akiendelea na usumbufu wake nitafanya kama ulivyonishauri.Mimi nimekueleza ukweli wangu wote vipi kuhusu wewe.Uliniambia ukweli au nawe ulinidanganya? Akauliza Juliana
“Mimi sikukudanganya nilikueleza ukweli.Sina mke tulitengana”
“Mathew kwani ukinieleza ukweli utapungukiwa kitu gani? Akauliza Juliana
“Tatizo wanawake wamezoea kuambiwa maneno ya uongo na mara zote uongo huwa mtamu sana ndiyo maana hata pale wanapoambiwa maneno ya ukweli hawataki wanataka waambiwe maneno matamu ya uongo.Sikiliza Juliana mimi siko hapa kukutaka kimapenzi bali nimekuja tu kwa maongezi
ya kawaida.Umepika chakula gani hapa ndani kwako?
Akauliza Mathew
“Sijapika chochote humu ndani.Mimi huagiza chakula hotelini” akasema Juliana
“Unaagiza chakula hotelini? Mathew akashangaa
“Ndiyo mbona umeshangaa?
“Kwa nini usipike nyumbani kwako? Akauliza Mathew
“Hurudi nimechoka ndiyo maana huagiza chakula hotelini.Mara chache ninapika lakini kwa zile siku ambazo
hushinda nyumbani” akasema Juliana na kuchukua simu yake akampigia mtu Fulani akaagiza aletewe chakula cha watu wawili.
“Mathew wakati tunasubiri chakula kiletwe ni wakati sasa wa kunieleza kile ambacho umekuwa unataka kunieleza toka mchana” akasema Juliana
“Sina jambo mahsusi nililotaka kukwambia Juliana nilihitaji tu kupata muda wa kuzungumza nawe mambo mbali mbali”
“Mambo kama yapi?
Akauliza Juliana
“Kuhusu maisha ya kila siku”
“Mathew kuwa mkweli yaani msisitizo wote ule ni kutaka tu kuongelea kuhusu maisha?
“Ndiyo nataka tu kuzungumza nawe mazungumzo ya kawaida” akasema Mathew
“Ninyi wanaume ni watu wa ajabu sana.Kwa nini mnapenda kuzunguka zunguka namna hiyo? Kuna ubaya gani ukienda moja kwa moja katika
kusema ukweli wa kile kinachokusumbua moyoni mwako? Kuwa jasiri eleza kile kilichokuleta hapa na usiniambie kwamba umechoma mafuta ya gari lako kuja kuzungumza nami masuala ya maisha”
“Huyu mwanamke tayari amekwisha anza kuwaza mambo mengine kabisa.Mimi sikuja hapa kwa mapenzi lakini yeye anahisi kilichoniletra hapa ni ngono” akawaza Mathew na kabla hajamjibu geti likagongwa Juliana akainuka
“Nadhani chakula kimeletwa tayari” akasema na kuweka vizuri nguo yake kisha akatoka nje.
Sekunde chache baada ya Juliana kutoka nje Mathew akasikia muanguko wa kitu kilichoangukia katika chungu cha maua karibu na mlango.Muanguko ule ukamstua Mathew akainuka na kunyata kuelekea mlangoni akaufungua na kutoka nje.Mathew alipatwana mstuko mkubwa sana baada ya kumuona Juliana akiwa ameanguka chini.
“Oh my God ! akasema na kutoka mbio akamkimbilia na kumkuta Juliana akikata roho.Akajaribu kumsemesha lakini tayari alikwisha fariki dunia.Alikuwa na matundu sita ya risasi kifuani na moja kichwani.
Mathew akatoka mbio akafungua mlango mdogo wa geti na kuchungulia nje lakini hakuona mtu yeyote ambaye angemhisi kufanya mauaji yale akaufunga mlango na kurejea ndani akamuinua Juliana na kumuingiza ndani
“Mauaji haya yamefanywa kama yale ya Gosu Gosu.Nadhani huu ni mpango wa kutaka kuniangushia mzigo wa kesi ya mauji kama Gosu Gosu.Nina uhakika polisi wanaweza wakafika hapa haraka.Natakiwa kuondoka haraka sana eneo hili” akawaza Mathew na kuichukua simu ya Juliana akaizima halafu akachukua begi lake katika gari akaenda bafuni na kubadili mavazi haraka haraka na kujifuta damu katika mikono yake
“Hili tukio sitakiwi kulifanyia masihara kwani linaweza likaniangamiza kama Gosu Gosu na ninaamini mpango wa watu hawa ni kunifanya nionekane muuaji.Alama zangu za vidole ziko katika nyuma hii hivyo hata kama nikikimbia wanaweza wakachunguza alama za vidole na kunikamata.I need to do something” akawaza Mathew na kumfunika Juliana kwa shuka
“Juliana umeuawa kwa sababu yangu.Imeniumiza
sana lakini nakuahidi kwamba nitawasaka wale wote waliokufanyia ukatili huu mkubwa ! akasema Mathew na kufungua sehemu ya nyuma ya gari lake ambako alihifadhi mafuta kwa ajili ya dharura akachukua galoni la mafuta akaenda chumbani kwa Juliana akamwaga mafuta nyumba nzima halafu akachukua mti akaufunga nguo akauwasha na kuurusha ndani halafu akakimbilia katika gari lake.Akachomeka funguo akainyonga ili kuliwasha lakini gari
halikuwaka.Akanyonga mara ya pili lakini halikuwaka.Akili ya Mathew ilifanya kazi haraka haraka na kwa kasi ya aina yake akalinyakua begi lake na kuufungua mlango akaruka nje na kutimua mbio kuelekea nje ya nyumba ile.Mara tu alipotoka nje ukatokea mlipuko mkubwa.Gari lake lilisambaratishwa na bomu.Alianguka chini kwa sekunde kadhaa halafu akainuka na kuanza kukimbia.
Alifika katika baa moja ambayo kulikuwa na muziki wa bendi akakodisha taksi na
kumtaka dereva ampeleke katika kituo cha basi anakoweza kupata gari la kwenda Moshi
“Magari ya kwenda Moshi usiku huu kaka sina hakika kama unaweza ukapata” akasema Yule dereva taksi
“Wewe unaweza ukanipeleka? Akauliza Mathew.Yule dereva akatafakari kidogo na kusema
“Unakwenda Moshi sehemu gani?
“Pale pale Moshi mjini.Ukinifikisha pale nitashukuru sana”
“Kukupeleka Moshi hakuna tatizo,ila tatizo liko kwenye malipo”
“Itanigharimu shilingi ngapi?
“Laki moja na thelathini”akasema Yule dereva Mathew akatoa pochi yake akahesabu shilingi laki moja na nusu akampatia Yule dereva
“Nimekuongeza zaidi haya nipeleke mara moja” akasema Mathew na Dereva huku akitabasamu akawasha gari wakaondoka
“Ee Mungu ahsante kwa kuniepushia kile kifo” akawaza Mathew akiwa garini
“Ni kwa mapenzi ya Mungu nimenusurika katika ule mlipuko lakini jamaa walikusudia kuniua na yawezekana hivi sasa wanajua nimekwisha fariki.Huu ni mtandao hatari sana ambao sipaswi kuwafanyia masihara hata kidogo.Nimewasili jana tu hapa nchini lakini tayari wamekwisha fahamu nimerejea Tanzania na wanafahamu niko Arusha na nimeonana na Gosu
Gosu.Wananifuatilia na wameanza kuingiwa hofu kwamba ninaweza kuwa kizingiti kwao ndiyo maana wakatega bomu lile katika gari.Nashukuru nina utaalamu na mabomu yale ya kutegwa katika gari ndiyo maana niliweza kung’amua haraka uwepo wa bomu baada ya gari kushindwa kuwaka nilipoliwasha.Lakini ni akina nani hawa watu? Kuna kitu gani wanakificha? Hapa wamekutana na chuma kisichotetereka nitapambana nao na nitawafahamu ni akina
nani na kitu gani wanakificha” akawaza Mathew huku akitazama nyuma kama kuna gari linawafuata
************
Safari iliendelea kwa kasi huku ndani ya gari kukiwa na ukimya mkubwa.
“Nilifanya vizuri kurejesha chumba pale Kobe Village kabla sijaenda kwa Juliana.Kama ningekuwa sijarejesha chumba naamini wangenifuata pale hotelini.Mambo ndiyo kwanza
yameanzana wakigundua kwamba nimenusurika katika ule mlipuko wataendelea kuniandama kwani wanaonekana ni mtandao mkubwa.Kwa picha ambayo nimeipata kwa tukio la leo ni Gosu Gosu aliangushiwa mzigo ule wa mauaji ili kupoteza uchunguzi wa kifo cha Lidya kwani kusingekuwa na ulazima wa kufanya uchunguzi wakati muuaji amepatikana na kuna kila ushahidi unaoonyesha kwamba ameua.Kuna jambo kubwa ambalo limepelekea Lidya akauawa na hilo ambalo
lazima nilifahamu.Japokuwa Lidya aliuawa hapa Arusha lakini kazi zake alizifanyia Dar es salaam na hapa Arusha alikuja kwa mapumziko hivyo natakiwa kurejea Dar es salaam ambako naamini ndiko kuna majibu ya kwa nini aliuawa” akawaza Mathew
“Nasikitika sana ni mimi niliyesabaisha kifo cha Juliana.Kama nisingetaka kuzungumza naye asingeuawa.Watu hawa ni wepesi sana na mipango yao wanaifanya haraka haraka.Ndani ya muda mfupi
tayari wamekwisha tengeneza tukio na kulitekeleza.Haya ni mambo ambayo hufanywa na majasusi wa hali ya juu sana” akaendelea kuwaza Mathew
Aliwasili mjini Moshi na kumtaka dereva amuache karibu na stendi kuu ya mabasi.Kutoka pale akatembea kwa miguu na kuipata nyuma ya wageni ambako alichukua chumba na kujiandaa kwa ajili ya safari ya kurejea Dar es salaam siku inayofuata.
DAR ES SALAAM
Saa kumi na moja za jioni basi alilolipanda Mathew liliwasili jijini Dar es salaam.
“Ahsante Mungu kwa kunifikisha salama Dar es salaam” Mathew akashukuru wakati akishuka katika basi na moja kwa moja akaelekea mahala zinakoegesha taksi akakodisha taksi na kumuelekeza dereva ampeleke nyumbani kwake.
“Chimbuko la mauaji ya Lidya liko hapa dar es salaam.Kwa namna yoyote ile lazima nifahamu kwa nini aliuawa na niwapate wauaji ili
niweze kumtoa Gosu Gosu gerezani.Mtu wa kwanza kabisa ambaye nahitaji kumuona ni Ruby.Najua haitaleta picha nzuri kwa Ruby na mume wake lakini sina nia mbaya .Ninahitaji sana msaada wa Ruby” akawaza Mathew
Alifika nyumbani kwake akaoga haraka haraka halafu akachukua gari lingine kutoka gereji na kuelekea katika makazi ya Rais mstaafu Dr Fabian Kelelo.Rais mstaafu Dr Fabian alikuwa ni mmoja wa marais waliowahi kuitawala
Tanzania ambaye aliingia katika historia kwa kutawala kipindi kimoja tu na hakutaka kugombea tena.
Ilimchukua Mathew saa moja na dakika kadhaa kufika nyumbani kwa Dr Fabian.Alisimamishwa getini na walinzi akashusha kioo na kuwasalimu
“Habari zenu wakuu” akasema Mathew
“Nzuri kaka.Tukusaidie nini?
“Nimekuja kuonana na mke wa Rais mstaafu”
“Wewe ni ndugu yake?
“Mimi ni rafiki wa familia”
“Kaka utatusamehe kwa sababu taratibu za hapa ni kwamba haturusu mtu yeyote ukifika muda huu kuingia ndani labda awe ni mtu wa karibu sana na familia au ana miadi maalum na tarifa hutolewa kwetu kuwa tumruhuru.Tunaomba urudi kesho kaka” akasema mmoja wa wale askari
“Ahsanteni wakuu kwa ufafanuzi lakini ninaomba msaada wenu.Naomba mnisaidie kuwapigia simu na
kuwajulisha kwamba Mathew Mulumbi yuko hapa na kama wataniruhusu kuingia sawa kama wakikataa basi nitaondoka na kurejea kesho”
“Umesema unaitwa nani?
Akauliza Yule askari “Mathew Mulumbi”
akajibu Mathew na Yule askari akamtazama kwa makini
“Subiri kidogo kaka”akasema halafu akarejea katika nyumba yao ya ulinzi akainua mkono wa simu na kupiga simu ndani ikapokelewa na mtumishi wa ndani
“Naomba umjulishe mama kwamba kuna mgeni wao yuko hapa getini anaitwa Mathew Mulumbi” akasema Yule askari
Dr Fabian Kelelo na mke wake wakiwa wamejipumzisha katika sofa nje ya nyumba yao mahala ambako hupenda sana kukaa nyakati za jioni na kujadiliana mambo mbali mbali,mara akatokea mtumishi wao wa ndani.
“Mama nimepokea simu kutoka getini wanasema kuna mgeni anaitwa Mathew Mulumbi”
“Mathew Mulumbi? Ruby akastuka
“Ndiyo”
Dr Fabian na Ruby wakatazamana.
“What is he doing here?!
Akauliza Dr Fabian
“I don’t know” akajibu Ruby na kumtaka Yule mtumishi awajulise walinzi wamruhusu Mathew aingie.Dr Fabian akavuta pumzi ndefu
“Anatafuta nini hapa huyu jamaa? Akauliza Dr Fabian naye akionena kustushwa na ujio ule wa Mathew
“Sifahamu.Ngoja tumsikilize kilichomleta” akasema Ruby na kuinuka.Ujio ule wa Mathew uliwastua sana
“Sikutegemea kumuona huyu jamaa hapa nyumbani kwangu.Ujio wake jioni hii haunipi picha nzuri hata kidogo.Huyu jamaa huibuka kama mzimu na kila anapoibuka lazima kuna jambo litatokea.Sitaki kabisa amuhusishe mke wangu katika mambo yake.Kwa sasa Ruby ni mama wa familia na hajihusishi tena mambo yale ya ujasusi” akawaza Dr Fabian
Mathew aliruhusiwa kuingia ndani akaegesha gari mahala kulikowekwa kibao cha maegesho ya magari halafu akashuka na kutembea kuelekea katika jumba kubwa la Dr Fabian.Mlango ukafunguliwa na Ruby akajitokeza.Mathew akasimama wakatazamana kwa muda.Ruby akavuta pumzi ndefu halafu akasema
“Karibu”
“Ahsante Ruby” akajibu Mathew na kuingia sebuleni akaketi sofani.
“Habari za hapa Ruby.Samahani kwa ujio huu wa jioni wa bila taarifa” akasema
“What are you doing here Mathew? Akauliza Ruby
“Hatujaonana muda mrefu Ruby hakuna hata kusalimiana? Akauliza Mathew
“Sema kilichokuleta hapa na uondoke Mathew”akasema Dr Fabian aliyeingia pale sebuleni akiwa ameshika kikombe cha kahawa.Mathew akasimama
“Mheshimiwa Rais shikamoo.Habari za siku nyingi”
“Nzuri Mathew.Karibu sana”
“Ahsante mheshimiwa Rais.Samahani kwa kuwavamia jioni hii tena bila taarifa”
“Usijali.Naamini una jambo la msingi la kufika huku kwetu jioni hii ya leo.Kwanza kabla ya yote napenda kukufahamisha kwamba mimi na Ruby tulifunga ndoa na sasa tuna watoto mapacha wawili,Michael na
Gabriel.Hatukujua mahala uliko ndiyo maana hatukuweza kukupa mwaliko lakini naamini tayari taarifa hizo umezipata na ndiyo maana uko hapa”
“Hongereni sana kwa hatua hii kubwa” akasema Mathew na kumeza mate kulainisha koo
“Mathew nini hasa kilichokuleta hapa usiku huu?
Akauliza Ruby “Nimekuja kuomba
msaada wako” akasema Mathew na Dr Fabian akaweka kikombe chake mezani na
kukohoa kidogo halafu akasema
“Mathew kuna jambo ambalo nataka kuliweka wazi kwako kwamba kwa hivi sasa Ruby si Yule ambaye ulimfahamu miaka mitatu iliyopita.Kwa sasa Ruby ni mke wa mtu na ni mama wa familia hivyo hajishughulishi tena na mambo yoyote yanayohusiana na ujasusi.Ana taasisi yake anaisimamia hivyo sitaki umuingize tena katika mambo yoyote yanayohusiana na kazi zako.Ninatoa angalizo mapema ili kama una mpango
wowote wa kutaka kumuomba akusaidie katika mambo yako ya ujasusi usihangaike kwani hatakusaidia” akasema Dr Fabian
“Dr Fabian..ouh sorry mheshimiwa Rais” akasema Mathew
“Vyovyote vile utakavyoniita sawa tu” akasema Dr Fabian
“Mimi na Ruby tumefahamiana muda mrefu kabla ya wewe kumfahamu na bila mimi usingeweza kumfahamu Ruby.Huyu si rafiki tu bali ni ndugu
yangu.Nimekuja nina shida na sina mtu mwingine wa kunisaidia zaidi ya huyu ndugu yangu” akasema Mathew
“What do you want Mathew? Akauliza Ruby
“Ni kuhusu Gosu Gosu” akasema Mathew
“Oh my God ! Gosu Gosu again ? Nini unakitaka kuhusu Gosu Gosu? Mbona suala hili limekwisha malizika? Akauliza Dr Fabian
“Dr Fabian mimi,Ruby na Gosu Gosu tunaishi kama familia hivyo Gosu Gosu ni sehemu ya familia yetu”
“Nalifahamu hilo Mathew lakini suala lake limekwisha malizika.Alikutwa na hatia katika kesi ya mauaji akafungwa maisha gerezani.Nini unataka kukifahamu? Akauliza Dr Fabian
“Sihitaji kufahamu chochote Dr Fabian kwani tayari ninafahamu kila kitu”
“So what do you need?
Akauliza Ruby
“I need your help” “Msaada gani unauhitaji
Mathew? Akauliza Ruby
“Ninataka kumsaidia Gosu Gosu”
“There is nothing you can do to help him! akasema Dr Fabian
“Mzee naomba unisikilize kidogo” akaomba Mathew
“Endelea Mathew” akasema Ruby
“Nimerejea nchini Juzi na baada ya kupata taarifa za kile kilichomtokea Gosu Gosu nilianza safari usiku huo huo kwenda Arusha na jana nikafanikiwa kuonana na Gosu Gosu gerezani” akasema Mathew na kunyamaza baada
ya kumuona Ruby akifuta machozi
“Gosu Gosu amefungwa gereza la Kimondo lenye ulinzi mkali na ni moja ya gereza hatari kabisa.Maisha ya Gosu Gosu gerezani si salama,kumekuwa na majaribio ya kumdhuru kila mara na kinachomsaidia yuko hai hadi sasa ni kwa sababu ya nguvu alizonazo na ukorofi wake.Inaonekana kuna genge ambalo limepewa kazi ya kumuwinda ili wamuue lakini hadi leo hii hawajafanikiwa na wengine hadi sasa wamekuwa
walemavu.Kwa ujumla tusishangae tukipata taarifa kwamba Gosu Gosu hatunaye kwa sababu usalama wake mle gerezani ni mdogo sana” akasema Mathew na kunyamaza.Ruby akainamisha kichwa akafunika uso kwa viganja vyake.
“Hakuna siku inayopita bila kumuwaza Gosu Gosu.Kinachoniumiza ni kwamba I didn’t do anything to help him.Sikuwahi kuhudhuria mahakamani hata mara moja na sikuwahi hata kwenda kumtembelea
gerezani.Ni aibu kubwa sana hii” akawaza Ruby
“Tunahitaji kumsaidia kwa haraka ili aweze kutoka mle gerezani” akasema Mathew
“Hilo haliwezekani Mathew.Gosu Gosu alitetewa na mawakili nane nguli wa sheria na wakashindwa na hata wao wenyewe wamekiri kwamba kesi ile ilikuwa ngumu sana kwao kwani ulikuwepo ushahidi wa kutosha kuthibitisha kwamba Gosu Gosu alifanya mauaji yale.Mathew tafadhali usipoteze muda wako kwa
jambo hili.Gosu Gosu aliua na mahakama ikatimiza wajibu wake.Hakuna namna ya kuweza kutengua hukumu ile” akasema Dr Fabian
“Dr Fabian mimi si mwenda wazimu,nina akili zangu timamu na ninafahamu kile ninachokisema.Nina kila sababu za kutaka kumsaidia Gosu Gosu aweze kutoka gerezani kwa sababu hakufanya lile kosa la mauaji” akasema Mathew
“Hakuua? Akauliza Dr Fabian
“Ndiyo hakuua!
“Mathew hukuwepo hapa nchini na hujui kilichotokea.Waulize watu waliokuwepo watakueleza kila kitu.Hakuna shaka hata kidogo kwamba Gosu Gosu alimuua Yule msichana na kila mtu analifahamu hilo”akasema Dr Fabian
“Gosu Gosu hakuua.Narudia tena Gosu Gosu hakumuua Lidya”
“Kama si yeye nani alifanya mauaji yale?
“Hilo ndilo ambalo nalifanyia kazi sasa hivi
kufahamu nani aliyefanya mauji yale” akasema Mathew
“Mathew utapoteza muda wako bure ! akasema Dr Fabian
“Dr Fabian nimekuja hapa kuzungumza na Ruby hivyo kama hutajali unaweza ukanipa dakika tano tu nizungumze naye? Akaomba Mathew akionekana kuchukizwa na maneno ya Dr Fabian
“Ruby ni mke wangu mimi na siwezi kukupa ruhusa ya kuzungumza naye faragha.Kama una lolote
unataka kumwambia mweleze mbele yangu nisikie” akasema Dr Fabian
“Endelea Mathew usijali” akasema Ruby
“Kama nilivyosema kwamba nilikwenda Arusha kuonana na Gosu Gosu.Nimeonana naye tukazungumza na amenieleza kwa undani kile kilichotokea na mambo mengine ambayo hajawahi kumueleza mtu yeyote.Nimeridhika Gosu Gosu hakufanya mauaji yale” akasema Mathew
“Who did? Akauliza Dr Fabian
“I don’t know” akajibu Mathew na kumgeukia Ruby
“Sikiliza Ruby.Gosu Gosu aliangushiwa kesi ile ya mauaji ili kupoteza sababu halisi ya kumuua Lidya.Lidya alikuwa ni mwandishi wa habari za uchunguzi na tunahisi kwamba yawezekana kuna jambo alikuwa analichunguza lililosababisha mauti yake.Waliomuua Lidya ni watu hatari sana na unaonekana ni mtandao kwani hata mimi nimenusurika jana kupoteza
maisha jijini Arusha” akasema Mathew na kuwasimulia Ruby na mume wake kile kilichotokea Arusha
“Pole sana Mathew.Tumesikia tukio hilo la mlipuko wa bomu na nyuma kuteketea jijini Arusha lakini hatukujua kama ni wewe unahusika na tukio lile” akasema Ruby
“Polisi hawawezi wakafuatilia namba za gari lako na wakakupata wakakuhusisha na mauaji ya huyo muhudumu wa hoteli aliyeuawa? Akauliza Dr Fabian
“Gari nililolitumia lina namba za bandia” akajibu Mathew
“Mathew I’m so scared.Hili jambo limeanza kunitisha sana” akasema Ruby
“Kuthibitisha kwamba kuna kitu kinachofichwa wauaji waliondoka na kompyuta na simu ya Lidya.Jambo hili Gosu Gosu hajawahi kumueleza mtu yeyote zaidi yangu” akasema Mathew
“What’s your plan?
Akauliza Dr Fabian
“Ili kufahamu wauaji ni akina nani na kitu gani kilichosabaisha wakamuua Lidya nataka kwanza kumchunguza Lidya.Gosu Gosu amenipa namba zake alizokuwa anatumia Lidya na ndiyo maana nimekuja hapa.Nataka kufahamu watu ambao Lidya aliwasiliana nao mara ya mwisho siku alipouawa.Ruby ni hilo tu lililonileta hapa” akasema Mathew.Dr Fabian akageuka na kumtazama mke wake
“Can you do it? Akauliza Dr Fabian
“Yes I can ! akajibu Ruby “Good.Lakini Mathew
nataka tuelewane jambo moja” akasema Dr Fabian na kunyamaza kidogo
“Mke wangu atakusaidia kwa leo hii tu na baada ya hapo sitaki tena umfuate kuomba msaada.Kama utafika hapa iwe ni kwa sababu maalum tena pale utakapokuwa umetoa taarifa na kukubaliwa lakini usije tu hapa kama ulivyokuja leo hii na kudhani utakaribishwa.Sitaki kumuingiza mke wangu katika
msauala yoyote ya hatari.Umenielewa? akauliza Dr Fabian
“Nimekuelewa mzee” akajibu Mathew
“Good” akasema Dr Fabian na kuinuka akaondoka
“Mathew twende katika ofisi yangu” akasema Ruby na kumuongoza Mathew hadi katika ofisi yake ya nyumbani”
“Hongera sana kumbe una watoto mapacha”akasema Mathew
“Mathew please don’t go there.Tufanye kile kilichokuleta hapa halafu
uondoke ! akasema Ruby huku akiiwasha kompyuta yake
“Inaonekana nyote hamjafurahi kwa ujio wangu hapa kwenu” akasema Mathew
“Ulitaka niruke ruke baada ya kukuona tena?akauliza Ruby
“Ruby umebadilika sana.Hukuwa namna hii” akasema Mathew
“Ni wewe ndiye uliyenibadilisha and I hate you.Nakuchukia sana Mathew.Uliniacha wakati ambao nilikuwa nakuhitaji sana”
“Ruby…” Mathew akataka kusema kitu lakini Ruby akamkatisha
“Don’t say anything Mathew.Let’s try to help Gosu Gosu” akasema Ruby na kufuta machozi
“Nilimuumiza mno Ruby kuamua kumuacha lakini sikuwa na namna nyingine.Afadhali sasa ana furaha” akawaza Mathew
“Kuna kitu chochote Gosu Gosu alikueleza kuhusu mimi?
Akauliza Ruby
“Hapana hajanieleza chochote” akajibu Mathew
“Sitaki kumweleza namna Gosu Gosu anavyomchukia kwa kushindwa kufika hata mara moja gerezani kumtembelea” akawaza Mathew huku Ruby akiendelea kucheza na kompyuta yake
“Mathew kumbu kumbu zote za namba hii zimekwisha futwa”
“Zimefutwa? Mathew akashangaa
“Ndiyo zimefutwa katika mtandao lakini kuna namna nyingine ambayo tunaweza kuzipata.SNSA wanahifadhi mawasiliano yote ya simu
kutoka katika mitandao ya simu kila siku hivyo itanilazimu kuingia katika mfumo wa SNSA kuzitafuta kumbu kumbu hizi”akasema
“Fanya vyovyote vile uwezavyo ninachohitaji ni kufahamu watu ambao Lidya alizungumza nao mara ya mwisho” akasema Mathew
Ruby alianza kucheza na vidole vyake kwa haraka haraka.Ilimchukua dakika tano halafu akasema
“Done”akasema Ruby baada ya kumaliza zoezi lile
“Watu watano wa mwisho kuwasiliana na Lidya ni
1. Aarav Patel 2.Vivian Jombe 3.Paul Kabose 4.Susan Ibobwe 5.Jonas Sabuni. “Huyu Jonas Sabuni
alikuwa mbunge na alifariki kwa ajali ya moto.Nyumba yake iliteketea kwa moto na hakuna hata mmoja wa familia yake aliyetoka hai” akasema Ruby
“Dah ! Kuna taarifa zozote za kilichosababisha moto huo?
“Mpaka leo hakuna anayejua nini chanzo cha moto huo”
“Nataka nipate mazungumzo ya mwisho ya Lidya na huyo mbunge Jonas Sabuni” akasema Mathew na Ruby akaanza tena kucheza na kompyua yake.
“SNSA hawawezi kugundua kama umeingia katika mfumo wao? Akauliza Mathew
“Inaonekana umekwisha nisahau mimi ni nani Mathew” akasema Ruby na baada ya
muda maongezi yakaanza kusikika
“Hallow” ikasema sauti ya kiume ambayo ilikuwa ni ya mbunge Jonas Sabuni
“Hallow mheshimiwa” ikasema sauti ya mwanamke ambayo waliamini ilikuwa ya Lidya
“Lidya ningetamani sana kuja kuonana nawe ana kwa ana kwani sipendi sana kutumia simu kuzungumzia mambo yetu lakini nimebanwa sana na shughuli.Ninataka kujua umefikia wapi katika lile suala?
“Lile suala ni gumu sana kaka lakini ninaelekea kupata mwangaza.Kuna mama mmoja anaitwa Zawadi Mlola amefungwa katika gereza la Uwangwa kwa kosa la kuua bila kukusudia ambaye nimebaini anazo taarifa Fulani muhimu zinazoweza kunisaidia katika uchunguzi.Kwa sasa niko Arusha lakini nitakaporejea Dar es salaam nitakwenda kuonana na huyo mama nimuhoji nione kitu gani anakifahamu kuhusu sakata la Naombi Bambi.Kaka bado
kuna giza nene lakini si muda mrefu nitapata mwangaza” akasema Lidya
“Jitahidi Lidya.Nasubiri sana suala hili ili nilipeleke bungeni .Ni moja ya kashfa kubwa sana” akasema Jonas
“Nitajitahidi kaka” “Nitakutumia fedha kiasi
Fulani kesho kama milioni tatu hivi zikusaidie katika shughuli zako na kama kuna kingine chochote utakihitaji utanijulisha” akasema Jonas na kukata simu.
Mathew na Ruby wakatazamana.
“Kwa maongezi hayo inaonyesha kuna jambo Lidya alikuwa analichunguza kuhusiana na mtu anaitwa Naombi Bambi na mbunge Jonas alikuwa anasubiri majibu ya uchunguzi huo ili aweze kuyafikisha bungeni.Kuna maneno aliyatumia Jonas kwamba hii itakuwa ni kashfa kubwa sana. Lidya alikiri kuwa kuna giza nene katika jambo hilo lakini akaahidi kwamba alikaribia kupata mwangaza.Nina uhakika mkubwa kwamba ajali ya moto iliyomuua Jonas
ilikuwa ya kupangwa na waliomuua ni watu wale wale waliomuua Lidya.Waligundua kwamba Lidya na Jonas walikuwa wanashirikiana katika uchunguzi wa suala hilo ndipo walipoamua kuwaondoa wote.Wako makini sana hawa watu katika kuhakikisha jambo hilo au hiyo kashfa inabaki kuwa siri” akasema Mathew na kunyamaza baada ya Dr Fabian kuingia mle ofisini
“Kuna mafanikio yoyote?
Akauliza Dr Fabian “Ndiyo.Kuna mambo
tumeanza kuyapata” akasema
Mathew na kumueleza kwa ufupi kile walichokuwa wamekipata.
“Mhh ! inaonekana kweli kuna jambo limejificha hapa ! akasema Dr Fabian
“Tuendelee” akasema Mathew
“Lidya alimwambia Jonas kwamba aligundua kwamba Zawadi Mlola anazo taarifa ambazo zingeweza kumsaidia katika uchunguzi wake na alipanga kwenda kumuona gerezani lakini hakuweza kufanya hivyo kwani alirejea Dar es salaam akiwa mfu.Vile
vile amemtaja Naomi Bambi.Kwa mujibu wa maelezo ya Lidya sakata au kashfa aliyokuwa anaichunguza inamuhusu huyu Naomi.Nitahitaji kupata taarifa za watu hawa niwafahamu”akasema Mathew
Ruby alianza kucheza na kompyuta yake na hakuchukua muda akapata taarifa za Zawadi Mlola kwani alikuwa anatumia mfumo wa SNSA .
“Zawadi Mlola ana miaka 40.Ni muuguzi kitaaluma.Taarifa zinaonyesha kwamba alifungwa gerezani
kwa kosa la kuua bila kukusudia” akasema Ruby akisoma taarifa ya Zawadi Mlola.
“Vipi kuhusu Naomi Bambi? Akauliza Mathew
“Huyu hakuna taarifa zake zozote.Kama zilikuwepo basi zimekwisha futwa” akasema Ruby
“Ahsante.Kazi ya kwanza kesho nitakwenda gereza la Uwangwa kumtafuta huyu Zawadi Mlola naamini kama nikifanikiwa kuonana naye anaweza akanieleza kuhusu Naomi Bambi.Susan Ibobwe
alizungumza nini na Lidya? Akauliza Mathew.Ruby akacheza na kompyuta yake kisha wakaanza kusikiliza maongezi ya Lidya na Susan Ibobwe
“Hallow Lidya habari yako? Ikasema sauti ya Susan
“Habari yangu nzuri madam Susan”
“Unaendeleaje huko Arusha?
“Ninaendelea vizuri madam”
“Enhe unasemaje Lidya?
“Madam nimekupigia kukuomba msaada wako.Kuna mtu amefungwa katika gereza la Uwangwa nataka kuonana naye.Huyu ni muhimu sana kwani anaonekana anaweza kuwa na taarifa zinazoweza kunisaidia katika uchunguzi wa lile suala la Naomi Bambi’ akasema Lidya
“Nini unahitaji nikusaidie Lidya? Akauliza Susan
“Kwa kuwa unafahamiana na watu wengi nataka unisaidie kunifanyia mpango ili niweze kuonana na huyo mfungwa na kuzungumza
naye.Naamini nikienda mwenyewe ninaweza nikakutana na kigingi” akasema Lidya
“Anaitwa nani huyo mtu unayetaka kuonana naye?
Akauliza Susan
“Anaitwa Zawadi Mlola” “Sawa Lidya
nitalishughulikia hilo.Lini unategemea kurejea Dar es salaam?
“Nitarejea kesho na huyo mama nataka nikaonane naye kesho kutwa”
“Lidya usiwe na wasi wasi.Chochote kile
unachokihitaji nitakusaidia kwani suala hili endapo litakamilika gazeti letu litalifanya gazeti letu kuwa ni moja ya gazeti bora kabisa hapa nchini. Jambo lingine Lidya hili suala unalolichunguza ni zito hivyo basi naomba uendelee kuchukua tahadhari sana.Ukigundulika kwamba unalifuatilia jambo hili utajiweka katika hatari kubwa.Muda wowote ambao ukihisi hatari yoyote nijulishe haraka sana”
“Nitafanya hivyo madam.Hata hivyo niko makini sana”
“Haya Lidya nakutakia kila la heri tutaonana hiyo kesho” akasema Susan na kukata simu.Dr Fabian ambaye nae aliyasikia mazungumzo yale akashusha pumzi
“Susan anaonekana ndiye mkurugenzi wa kampuni aliyokuwa anaifanya kazi Lidya.Huyu naye anafahamu kile alichokuwa anakichunguza Lidya.Naye amekiri kwamba Lidya alikuwa anachunguza kashfa nzito.Tuhamie kwa mtu
wa tatu Paul Kabose” akasema Mathew na Ruby akaanza kutafuta taarifa za Paul Kabose
“Paul ni mhadhiri katika chuo cha uandishi wa habari ambachoLidya alisoma” akasema Ruby na kuweka mazungumzo kati ya Lidya na Paul
“Hallo Lidya” akasema Paul
“Mambo vipi Paul.Ulikwenda kumhoji Yule mtu niliyekuelekeza? Akauliza Lidya
“Ndiyo nilionana naye lakini hafahamu chochote”
“Dah ! suala hili mbona linakuwa gumu namna hii.Tegemeo pekee kwa sasa lililobaki ni Yule mama kule gerezani.Tayari nimekwisha muomba mkurugenzi wangu anifanyie mpango ili niweze kuzungumza na mama Zawadi Mlola.Yeye anafahamiana na wakubwa wengi hivyo itakuwa rahisi mimi kuonana na Zawadi”
“Lidya una hakika huyu mama anaweza kuwa na taarifa za hili jambo? Akauliza Paul
“Paul I’m not sure.Hili suala limekuwa ni kama kucheza karata”
“Lini unarejea Dar es salaam? Paul akauliza
“Narudi kesho”
“Sawa Lidya tutaonana pale utakapokuwa umerudi” akasema Paul na kukata simu.
“Kwa mazungumzo haya ni wazi Paul Kabose na Lidya walikuwa wanashirikiana katika kulichunguza hili suala.Huyu naye anaingia katika orodha ya wale tunaowatafuta” akasema Mathew
Baada ya kusikia mazungumzo ya watu watatu kati ya watano ambao walizungumza na Lidya mara ya mwisho walibaki watu wawili ambao baada ya kupitia mazungumzo yao hayakuhusiana chochote na kile ambacho Lidya alikuwa anakichunguza.Aarav Patel alimjulisha Lidya kwamba viatu alivyoagiza vilikuwa vimefika hivyo apite dukani kwake kuvichukua na Vivian Jombe aliwasiliana na Lidya kuhusu kusuka.Lidya alihitaji kwenda kusuka jioni ya siku
inayofuata na akamuuliza Vivian kama angeweza kumsuka jioni hiyo mara tu atakapokuwa amerejea kutoka Arusha
“Hawa watu watatu Jonas,Susan na Paul ndio wa muhimu zaidi kwani tametupa picha kwamba kuna kitu kilikuwa kinaendelea.Nadhani mpaka hapa mheshimiwa Rais umeanza kuamini maneno yangu kwamba Gosu Gosu aliangushiwa mzigo wa kesi ya mauaji ili kuzuia uchunguzi wa kifo cha Lidya usifanyike” akasema Mathew
“Baada ya kufuatilia mazungumzo hayo ya Lidya na hao watu watatu sasa nimeanza kuona kuna kitu katika suala hili.Nimeanza kukuamini Mathew” akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais si kila wakati nitakuwa sahihi lakini katika jambo hili naomba uniamini nina uhakika mkubwa kwamba niko sahihi Gosu Gosu hakufanya yale mauaji”
“Mathew utanisamehe kama nilikukwaza hapo awali lakini kwa picha inayokuja
inaonyesha wazi kwamba kuna jambo kubwa nyuma ya pazia.Ahsante Mathew kwa kulifahamu hili.Sisi sote tulikuwa tumeaminishwa kwamba Gosu Gosu alifanya mauaji yale.Nini kinafuata baada ya kusikiliza mazungumzo haya?
“Tayari nina sehemu ya kuanzia.Kuna hawa watu watatu ambao waliwasiliana na Lidya mara ya mwisho.Jonas,Susan na Paul.Jonas tunamtoa katika orodha na wanabaki Susan na Paul ambao kesho
nitawatafuta vile vile nitamtafuta Zawadi Mlola ambaye amefungwa katika gereza la Uwangwa.Kuna mambo mengi tutayafahamu kutoka kwa huyu mama kama nitafanikiwa kumuona na kubwa zaidi ni kumfahamu Naomi Bambi ni nani?
Akasema Mathew “Mathew kuna jambo
nataka nikiri kwa niaba ya mke wangu.Gosu Gosu ni mtu ambaye ameshirikiana nawe bvega kwa bega katika misheni mbali mbali muhimu sana kwa nchi na hata amenusurika
mara kadhaa kupoteza uhai wake.Mimi binafsi ni rafiki yangu lakini alipopatwa na haya matatizo mimi na mke wangu tulijiweka kando na hatukumsaidia kwa lolote.Ruby alihitaji sana kwenda walau kuonana naye lakini nilimkataza sikutaka aonekane ana mahusiano na muuaji.Tulikosea sana.Tulipaswa kumsaidia” akasema Dr Fabian na kunyamaza baada ya kumuona Ruby akifuta machozi
“Hata hivyo bado hatujachelewa
kumsaidia.Umetueleza kile kilichotokea Arusha na wewe ukanusurika kuuawa.Ujio wako tayari umewapa hofu hawa jamaa na kitendo cha kwenda kuonana na Gosu Gosu kinamuweka katika hatari kubwa.Umetueleza mambo anayokutana nayo gerezani hivyo nataka kusaidia.Mkuu wa magereza Tanzania ni rafiki yangu nitazungumza naye ili Gosu Gosu aweze kulindwa”
“Ahsante mheshimiwa Rais,hilo ni jambo kubwa sana” akasema Mathew
“Mathew just call me Dr Fabian.Urais nimekwisha achana nao na sasa ni raia wa kawaida kama wewe” akasema Dr Fabian
“Sawa mzee”
“Kuna kingine chochote ambacho unahitaji msaada? “Kwa sasa hakuna lakini
pale nitakapohitaji msaada nitawajulisha.Ahsanteni sana kwa msaada huu mkubwa na mtanisamehe vile vile kama kuna usumbufu wowote niliowasababishia usiku huu kwa ujio wangu wa bila taarifa” akasema Mathew
“Mathew usihofu.Tunafurahi umerejea na tumepata mwangaza wa kile kinachoendelea.Unakaribishw a hapa muda wowote” akasema Dr Fabian
“Ni wakati wangu wa kuondoka nikajiandae kwa ajili ya siku ya kesho” akasema Mathew na kuinuka tayari kwa kuondoka
“Mathew una hakika nyumbani kwako utakuwa salama? Kama unahisi usalama ni mdogo karibu hapa
kwangu kuna usalama mkubwa” akasema Dr Fabian
“Ahsante Dr Fabian nitakuwa salama” akasema Mathew kisha wakamsindikiza hadi katika gari lake akaondoka wakarejea ndani
“You didn’t believe me ! akasema Ruby
“Hayo yamekwisha pita mke wangu” akasema Dr Fabian
“Hukuniamini nilipokwambia kwamba Gosu Gosu hakufanya mauaji yale na
..”
“Ruby I’m sorry.Ni wewe tu na Mathew ambaye mliamini Gosu Gosu hakufanya yale mauaji lakini watu wote pamoja na mimi tuliridhika kwamba alimuua Lidya kutokana na ushahidi mkubwa uliokuwepo.Ni usiku huu ndipo macho yangu yamefumbuka baada ya kusikiliza mazungumzo ya Lidya na mbunge Jonas na wale wengine wawili”
“Kwa hiyo ulisubiri hadi mazungumzo haya yapatikane ndipo uniamini? Kwa nini
ulishindwa kuniamini mimi mke wako?
“I’m sorry Ruby.Nilikosea and It won’t happen again.Naomba tafadhali suala hili lisituletee kutokuelewana malaika wangu.Tuungane pamoja kumsaidia Gosu Gosu.Bado hatujachelewa” akasema Dr Fabian
“Tafadhali naomba ujifunze kuniamini.Sikupendezwa na namna ulivyokuwa unazungumza na Mathew”
“Darling nilihitaji kuzungumza naye namna ile ili
ajue kwamba kwa sasa wewe una majukumu mengine ili asikushirikishe katika misheni zake.Wewe umekwisha achana na hayo mambo kwa sasa ni mke wa mtu na una majukumu mengine ya kulea watoto wetu ndiyo maana nikajaribu kukukingia kifua kwani najua wewe na Gosu Gosu hamuwezi kusema hapana kwa Mathew” akasema Dr Fabian
“Sikukuhitaji unikingie kifua.Mimi ni mtu mzima na ninaweza kujisimamia mwenyewe.Naomba uniamini tafadhali mimi na Mathew
tumekwisha jenga ukuta kati yetu lakini ni mtu anayestahili heshima kubwa sana kwani kama si yeye mimi nawe tusingekutana.Ninapokuwa naye ondoa mawazo kwamba tunaweza tukarudiana.Nimewaacha wanaume wote duniani na kukubali kuolewa nawe hivyo niamini Fabian”
“Nimekuelewa mpenzi wangu na samahani kwa tabia ile niliyoionyesha kwa Mathew.I promise it won’t happen again” akasema Dr
Fabian kisha wakaelekea katika chumba cha chakula
************
“Lile suala ni gumu sana kaka lakini ninaelekea kupata mwangaza.Kuna mama mmoja anaitwa Zawadi Mlola amefungwa katika gereza la Uwangwa kwa kosa la kuua bila kukusudia ambaye nimebaini anazo taarifa Fulani muhimu zinazoweza kunisaidia katika uchunguzi.Kwa sasa niko Arusha lakini nitakaporejea Dar es salaam nitakwenda
kuonana na huyo mama nimuhoji nione kitu gani anakifahamu kuhusu sakata la Naombi Bambi.Kaka bado kuna giza nene lakini si muda mrefu nitapata mwangaza”
Maneno ya Lidya akizungumza na mbunge Jonas yaliendelea kujirudia kichwani kwa Mathew akiwa amejipumzisha kitandani chumbani kwake huku bastola yake ikiwa pembeni tayari kuitumia muda wowote kukitokea tatizo
“Who is Naomi Bambi?
Akajiuliza Mathew
“Huyu anaonekana ndiye muhusika mkuu wa kashfa ambayo Lidya alikuwa anaichunguza.Yuko wapi huyu Naomi na kwa nini hakuna taarifa zake zozote zilizorekodiwa? Uhai wa watu tayari umekwisha ondolewa kwa sababu yake.Kwa namna yoyote lazima nimfahamu huyu Naomi.Kesho mambo yataanza” akawaza Mathew
“Nawakubali hawa jamaa ni wataalamu na wamejipanga vyema lakini safari hii wamekutana na mtaalamu zaidi yao hivyo mpambano
utakuwa mkali sana” akawaza na sura ya Ruby ikamjia kichwani
“Kwa kiasi Fulani ninajihisi amani baada ya kuonana tena na Ruby na kujiridhisha kwamba yuko katika mikono salama lakini bado ana hasira moyoni mwake kwa kitendo changu cha kumuacha.Sikupenda kufanya vile lakini ilinilazimu.Sitakiwi kumfikiria sana Ruby kwa sasa kwani ni mke wa mtu na tayari wana watoto hivyo natakiwa kuweka heshima kubwa
kwake.Tutabaki kuwa marafiki wa kawaida na kama ikimpendeza Mungu iko siku atanipatia mwanamke wa kunifaa” akawaza Mathew na kumkumbuka Sindi
“Nilimuahidi kumtembelea Sindi katika kambi yao.Nitajitahidi kesho kama nikipata nafasi kwenda kumjulia hali”
***************** Mshale wa saa ulionyesha
ni saa kumi na mbili za
asubuhi,tayari Mathew
alikuwa katika chumba cha mazoezi akiweka sawa viungo vyake.Baada ya kumaliza mazoezi akarejea chumbani kwake akaoga na kujiandaa tayari kuikabili siku.Alichagua suti nzuri ya kijivu akavaa na kutabasamu alipojitazama katika kioo
“Niliyakosa sana mambo haya ya kuvaa suti” akawaza kisha akaingia katika chumba chake kidogo cha siri ambako huhifadhi silaha akachukua bastola iliyofungwa kiwambo cha sauti akaiweka ndani ya koti akatoka.Tayari Victor
alikwishaandaa kifungua kinywa na alikuwa anamuandalia Mathew gari ambalo angelitumia kwa siku ile.
“Nyumba imekuwa kimya sana.Gosu Gosu na Lucy waliifanya nyumba hii kuchangamka muda wote” akawaza Mathew wakati akipata kifungua kinywa.Alipomaliza akatoka nje ambako tayari gari lilikwisha andaliwa akaingia na kuondoka
“Kitu cha kwanza natakiwa kupata mawasiliano.Ni muda
mrefu sijaitumia laini yangu ya simu.Natakiwa niende moja kwa moja ofisini kwao wakanifungulie laini yangu baada ya hapo nitaendelea na mizunguko mingine” akawaza Mathew
GEREZA LA KIMONDO – ARUSHA
Saa nne za asubuhi wakati wafungwa wakiwa katika shughuli mbali mbali,gari la magereza likawasili na mfungwa mmoja aliyefungwa pingu za miguu na mikono
akashushwa.Alikuwa mwembamba lakini mwenye macho ya kikatili.Baada ya kusajiliwa akaongozwa na askari magereza kwenda katika chumba alichopangiwa.Wakati akipita kazi zilisimama wafungwa wote wakimtazama.
“Anaitwa Adili lakini anafahamika zaidi kama Kishada.Ni jambazi sugu na muuaji mkubwa.Ni mtu hatari mno huyu jamaa.Msimuone mwembamba ni mkatili mno.Sijui wamewezaje kumkamata na lazima wakati wa kumkamata damu
ilimwagika kwani inadaiwa huyu jamaa anatumia dawa ndiyo maana anafanya mauaji na hakamatwi” mmoja wa wafungwa katika kundi la akina Gosu Gosu waliokuwa na kazi ya kupunguza matawi ya miti akawaambia wenzake na wote wakajielekeza kumtazama Kishada.
“Uwepo wake hapa unaashiria si mahala salama tena.Ninamfahamu huyu jamaa na nimeingiwa na hofu kubwa kumuona” akasema Yule jamaa kisha kazi zikaendelea baada ya Kishada
kupita.Dakika tano baadae mchungaji Peter Msavu ambaye anakaa chumba kimoja na Gosu Gosu akaitwa na kuelekezwa kwamba kuanzia siku ile atahama na kuhamishiwa katika chumba kingine kumpisha mfungwa mgeni ambaye ni Kishada.Alihamisha vitu vyake na kuelekea katika chumba kingine akipishana na mfungwa mpya .
Shughuli ziliendelea na kingora cha kuashiria ni muda wa kujiandaa kwa ajili ya chakula cha mchana
kikalia.Askari magereza mmoja kijana akamfuata Gosu Gosu ambaye alipewa kusimamia shughuli ile ya kukata miti na kumuuliza namna shughuli ilivyokwenda wakati wakizungumza akamvuta pembeni na kumpatia karatasi lililokunjwa.
“Nenda chooni kausome ujumbe huo” akasema Yule askari magereza na kumfanya Gosu Gosu ashangae.Toka amefika katika gereza hili askari magereza wameonekana kuegemea upande wa wale wasiompenda ambao
wamekuwa wakimuwinda usiku na mchana wammalize.Taratibu Gosu Gosu akaelekea chooni akafunga mlango na kuikunjua ile karatasi akaanza kuisoma.
“Kuwa makini mfungwa mpya ameletwa katika chumba chenu na kazi iliyomleta hapa ni kukuua.Usilale katika kitanda cha juu amepewa maelekezo ya kutega sindano yenye sumu ambayo itakuchoma na utakufa haraka”
Gosu Gosu akahisi kijasho kikimchuruzika baada ya kuusoma ujumbe ule
“Kumbe bado hayajaisha.Kunifunga maisha gerezani hawajaridhika na sasa wanataka kuniua kabisa.Hawa jamaa wana mtandao mpana sana na ndiyo maana kumefanyika majaribio kadhaa ya kuniua lakini yameshindikana na sasa wamelazimika kumtuma muuaji.Nadhani hii imechangiwa na ujio wa Mathew hapa gerezani.Mathew anao msemo
wake mmoja hupenda kuusema kwamba Ni mungu pekee atakayeamua kifo chake na si mwanadamu.Leo ninaurejea mimi msemo huo hakuna mwanadamu atakayepanga kifo changu ni Mungu pekee.Nitamuonyesha kazi huyo muuaji aliyetumwa kuniua” akawaza Gosu Gosu akiwa ameukunja uso wake kwa hasira
“Nashangaa imekuaje leo nikapewa tahadhari kwamba kuna hatari inanikabili wakati majaribio kadhaa ya kunitoa uhai yamekwisha fanyika bila
kupewa tahadhari yoyote?Nahisi haya ni mambo ya Mathew.Yawezekana tayari amekwisha tengeneza mtandao wa kunisaidia hapa gerezani.Ninamshukuru sana kama ni yeye aliyefanya hivi kwani hapa gerezani ninaishi bila kujua kama nitaiona kesho” akawaza Gosu Gosu
Baada ya chakula cha mchana wafungwa hupata nafasi ya kupumzika aidha katika vyumba vyao au katika sehemu maalum za kupumzikia.Gosu Gosu hupenda kuutumia muda huu
kupumzika chumbani kwake lakini kwa siku hii aliamua kwenda kupumzika maktaba akitafakari namna atakavyokabiliana na maisha ya pale gerezani
DAR ES SALAAM
Mathew alifanikiwa kufunguliwa laini yake ya simu ambayo hakuwa ameitumia kwa muda mrefu na mtu wa kwanza kabisa kumpigia alikuwa ni Ruby
“Hallow” akasema Ruby
“Ruby ni mimi Mathew.Habari za asubuhi”
“Salama kabisa.Umeshapata mawasiliano?
“Ndiyo.Tayari nimefunguliwa laini yangu”
“Good.Nini kinaendelea hivi sasa? Akauliza Ruby
“Kwa sasa ninaelekea Uwangwa Prison kuonana na Zawadi Mlola nikitoka hapo nitaendelea kuwatafuta wale wengine Susan na Paul” akasema Mathew
“Sawa Mathew.Utanijulisha utakachokipata”
“Ruby” akaita Mathew na kuka akimya
“Unasemaje Mathew?
Akauliza Ruby
“I’m sorry about last night.Sikukusudia kuwakwaza
.Nilichohitaji ni msaada” akasema Mathew
“Mathew ni mimi ninayepaswa kukuomba samahani kwa namna tulivyokupokea jana.Hatukukupokea kama rafiki na mtu wetu wa karibu
bali tulikuona kama jambazi mvamizi.Samahani sana Mathew kwa jambo lile nakuahidi halitajirudia tena” akasema Ruby
“Ruby tuyaweke hayo pembeni yamekwisha pita.Nitakupigia kukujulisha kile kitakachokuwa kimejiri” akasema Mathew na kukata simu
Mathew alifika gereza la Uwangwa akaegesha gari na kuelekea mapokezi akaeleza shida iliyompeleka pale ya kuonana na mfungwa Zawadi Mlola.Taarifa aliyopewa ni
kwamba Zawadi Mlola ni kweli alikuwepo pale gerezani akitumikia kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia lakini tayari alikwisha maliza kifungo chake na kutoka gerezani.Mathew hakuwa na la kufanya akarejea garini na kuondoka pale gerezani.Mara tu alipoliacha geti la gereza akampigia simu Ruby
“Hallow Mathew” akasema Ruby
“Ruby nimetoka sasa hivi gereza la Uwangwa”
“Umefanikiwa kuonana na Zawadi?
“Taarifa niliyoipata ni kwamba Zawadi alimaliza kutumikia adhabu yake ya kifungo na amekwisha toka gerezani.Ninaomba unisaidie kupitia taarifa zake ili nifahamu mahala anakoishi nimfuate” akasema Mathew na Ruby akamtaka asubiri kidogo.Baada ya muda akampigia simu na kumjulisha kwamba Zawadi alikuwa akiishi mtaa wa Konani nyumba namba 46.
“Nimekupata Ruby.Ngoja niende huko sasa hivi” akasema Mathew
“Naomba nifanikiwe kumpata huyu mama kwani anaweza akatusaidia sana katika kulifahamu suala ambalo Lidya alikuwa analichunguza” akawaza Mathew
Aliwasili katika mtaa wa Konani na kuitafuta nyumba aliyoelekezwa kwamba ndiyo aliyokuwa akiishi Zawadi.Majani yaliota kulizunguka geti na hakukuwa na dalili zozote za kuishi mtu
katika nyumba ile.Mathew akalisogelea geti lililoonekana kufungwa muda mrefu akatafuta upenyo na kuchungulia ndani.Aliona gari moja likiwa limegeuka makazi ya ndege.
“Nyumba hii ina muda mrefu haijakaliwa na mtu” akawaza Mathew na kumtafuta mjumbe wa mtaa ule lakini akabahatika kuonana na mke wake.
“Mama nimekuja katika mtaa wenu ninamtafuta mama Zawadi Mlola ni muuguzi wa
hospitali ya Kikoma”akasema Mathew
“Zawadi? “Ndiyo mama”
“Zawadi kweli alikuwa anaishi mtaa huu.Alipata matatizo na kufungwa gerezani baada ya hapo hatujawahi kumuona tena katika mtaa huu.Tulikwenda kumtembelea gerezani tukambiwa alimaliza kifungo na akaachiwa huru lakini hapa nyumbani hatukuwahi kumuona na hatujui yuko wapi.Nyumba yake imegeuka makazi ya popo,hakuna anayeishi hadi
leo watu wanaiogopa wanadai kuna mauza uza”
“Huwezi kuwafahamu ndugu zake au watu wake wa karibu? Mathew akauliza
“Hapana hakuna anayewafahamu ndugu zake” akajibu Yule mama.Mathew hakuwa na la kufanya akarejea katika gari lake akaegemea kiti na kuvuta pumzi ndefu
“Yuko wapi Zawadi Mlola? Ni mzima kweli au amekwisha fariki?” akajiuliza Mathew na kuwasha gari akaondoka.Alisimamisha gari mbele ya nyumba ile ya Zawadi
akashuka na kupiga picha kadhaa halafu akaingia garini na kumpigia simu Ruby
“Mathew umefanikiwa kufika nyumbani kwa Zawadi? Akauliza Ruby na Mathew akamueleza kila kitu.
“Dah ! Nini kinafuata Mathew? Akauliza Ruby
“Kinachofuata ninakwenda kumtafuta Susan Ibobwe” akasema Mathew
“Mathew usinielewe vibaya lakini nimeanza kuwa na wasi wasi sana kuhusiana na watu waliokuwa karibu na Lidya hasa wale waliokuwa
wanafahmu kile alichokuwa anakichunguza” akasema Ruby
“Usihofu Ruby tutapata picha kamili ya jambo hili baada ya kuwatafuta Susan na Paul” akasema Mathew
“Anachokisema Ruby ni kitu cha kweli kabisa.Kuna wasi wasi mkubwa wale wote waliokuwa karibu na Ruby kama bado wako hai.Nisikate tamaa ngoja niwafuatilie hawa watu wawili nijiridhishe kama wako hai” akawaza Mathew
Alifika katika ofisi za gazeti ambalo Lidya alikuwa anafanya kazi gazeti ambalo
linasifika kwa kuandika habari za kiuchunguzi.Taarifa aliyoipata ilimstua kwani Susan alikwisha fariki dunia kwa ajali ya gari akitokea mkoani Morogoro.
“Yale yale aliyoyasema Ruby” akawaza Mathew wakati akiondoka katika ofisi zile za gazeti.
“Susan asingeweza kubaki salama kwa sababu alifahamu kile alichokuwa anakichunguza Lidya.Kwa namna hawa jamaa walivyojipanga katika kuhakikisha siri yao haivuji lazima jambo wanalolificha
litakuwa kubwa sana na kadiri wanavyojitahidi kulificha lisijulikane ndivyo kiu yangu ya kulifahamu inavyoogezeka na lazima nitalifahamu.Kituo kinachofuata ni kwa Paul” akawaza Mathew
Alifika katika chuo cha uandishi wa habari alikokuwa anafundisha Paul Kabose nako taarifa aliyoipata haikumshangaza.Paul Kabose alivamiwa na majambazi nyumbani kwake na kuuawa kwa risasi.Mathew akaondoka na kurejea garini kisha akampigia simu Ruby.
“Kuna habari gani Mathew? Akauliza Ruby baada ya kupokea simu
“Kama vile ulivyohisi Ruby,wale wote waliokuwa na ukaribu na Lidya na waliofahamu kuhusu kile alichokuwa anakifanya wameuawa.Siri yao iko salama” akasema Mathew
“Nilihisi kitu hicho.Kama walimuua Lidya lazima wawamalize na wale wote aliokuwa anashirikiana nao.Tutafanya nini Mathew? Akauliza Ruby
“Ninakuja nyumbani kwako ili tulijadili jambo hili kwa upana zaidi kama hutajali” akasema Mathew
“Karibu Mathew” akasema Ruby
“Ahsante” akajibu Mathew na kuwasha gari akaondoka kuelekea nyumbani kwa rais mstaafu Dr Fabian Kelelo
“Gosu Gosu hakufahamu kile alichokuwa anakichunguza Lidya na kama angekifahamu tayari naye angekwisha uawa kwani wale wote waliokuwa wanalifahamu wameuawa.Inaonekana hawa
jamaa walikuwa wanafuatilia mazungumzo yote ya simu ya Lidya na kuwafuatilia wale wote ambao alishirikiana nao katika uchunguzi wakawamaliza” akaendelea kuwaza Mathew
*********** Mathew aliwasili katika
makazi ya Rais mstaafu Dr
Fabian Kelelo akakaribishwa na Ruby na moja kwa moja wakaelekea katika ofisi yake ya nyumbani.Mathew akamueleza kwa kina kile alichokipata
katika mzunguko wake alioufanya kuwatafuta wale wote waliozugumza na Lidya mara ya mwisho.
“Ruby mambo ndiyo kwanza yameanza.Kuna mengi bado yanakuja kwani hawa jamaa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha kwamba siri yao haivuji.Hawahitaji kizingizi ndiyo maana wanaendelea kuua kila mtu ambaye ataonekana ni hatari kwao”akasema Mathew
“Tumekwama Mathew” akasema Ruby na Mathew akacheka kidogo
“Hawa jamaa tunaowatafuta hawajui neno linaitwa kukwama hivyo na sisi hatupaswi na hatuwezi kukwama.Kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu katika kumtafuta Zawadi Mlola.Tunahitaji kujua kama yuko hai au naye amekwisha uawa kama wengine.Mtaani kwao hawajawahi kumuona tena toka alipofungwa gerezani na hii inamaanisha kwamba alipotoka gerezani hakurudi tena nyumbani kwake.We need to dig deeper” akasema Mathew na kumtazama Ruby
“Kuna kamera katika kila kona ya gereza la Uwangwa.Kwa kuwa SNSA wameunganishwa na mifumo yote ya taasisi za serikali,nataka tuingie katika mfumo wa kamera wa gereza la Uwangwa na tupitie kumbu kumbu za kamera za siku Zawadi alipoondoka gerezani hapo.Nataka kufahamu aliondoka na usafiri gani?
Kama alichukuliwa na gari basi tutalifuatilia gari hilo kujua ni la nani.Kama aliondoka kwa mguu basi tutafuatilia kamera moja moja za umma zilizoko
katika barabara mbali mbali hapa jijini kumtafuta kujua alipotoka gerezani alielekea wapi.Si kazi nyepesi lakini lazima tuifanye kwani Zawadi ndiye pekee anayeweza kutupa mwangaza wa jambo hili kama bado atakuwa hai hivyo lazima tujiridhishe kama yuko hai bado na yuko wapi” akasema Mathew” na Ruby akashusha pumzi
“Kweli si kazi nyepesi.Ni kazi ngumu lakini kama ulivyosema hatuwezi kuikwepa lazima tuifanye” akasema Ruby
“Ni vipi kama tukishindwa kumpata Zawadi? Akauliza Ruby
“Kuna dalili ambazo zinanifaya namini kwamba Zawadi anaweza kuwa hai hivyo tusikate tamaa tufanye zoezi hili hadi pale tutakapojiridhisha kwamba yuko hai au amekufa.Hakuna kulala usingizi hadi pale tutakapolikamilisha jambo hili” akasema Mathew na bila kupoteza muda Ruby akaanza kazi
“You don’t want to tell me?
Akauliza Ruby
“Tell you what? Mathew naye akauliza
“Mahala ulikokuwa” akasema Ruby
“Ruby we have an important job to do.Haya mengine hayana umuhimu sana kwa sasa”
“Yana umuhimu kwangu” akasema Ruby
“Tazama Ruby,wewe kwa sasa tayari ni mke wa mtu,umeolewa na mmoja wa watu wazito hapa nchini.Masuala yangu kwa sasa hayakuhusu sana.Tujielekeze katika
kumsaidia Gosu Gosu” akasema Mathew na Ruby akavuta pumzi ndefu halafu akasema
“Why you did that to me?
Why you dumped me like that? Akauliza Ruby na kuacha kazi aliyokuwa anaifanya na kumgeukia Mathew
“Answer me Mathew ! akasema Ruby
“Ruby wewe mwenyewe unafahamu nilipitia kipindi kigumu sana katika maisha yangu.Matukio yalifuatana mfululizo,nilipoteza kila kitu na nusura ningepoteza pia
maisha yangu.Nilihitaji muda wa kutuliza kichwa na kutafakari kuhusu maisha yangu ni wapi nimetokea na wapi ninaelekea ndiyo maana nikafanya maamuzi yale kwani sikujua ningerudi lini hapa nyumbani na sikutaka kukufanya unisubiri”
“Mathew ulifahamu kabisa nilikula kiapo cha kuwa nawe pekee na kama ungenieleza ningesubiri hata kwa maisha yangu yote.Lakini …..” akasema Ruby na kunyamaza
“Ruby tuachane na hayo mambo yamekwisha pita.Kwa
sasa wewe ni mke wa mtu na ninaliheshimu hilo.Yale yote yaliyopita yabaki historia” akasema Mathew na Ruby akatoa kicheko kidogo na kutaka kusema kitu lakini mlango ukafunguliwa na Dr Fabian akaingia mle ofisini
“Hello Mathew.Karibu sana” akasema Dr Fabiana na kwenda kumbusu mkewe
“Vipi mnaendeleaje hapa? Akauliza Dr Fabian na Mathew akamueleza kile alichokuwa amekipata
“Nilifanikiwa kuzungumza na mkuu wa Magereza
nikamuomba amuwekee Gosu Gosu ulinzi na akaniahidi kufanya hivyo.Kidogo kwa sasa tunaweza kuwa na matumaini kwamba Gosu Gosu atakuwa salama lakini lazima juhudi za kumtoa gerezani ziendelee” akasema DrFabian
“Ahsante sana DrFabian kwa msaada huo mkubwa” akasema Mathew
“Kwa hiyo nini kinaendelea sasa hivi?
Akauliza DrFabian “Kwa sasa zoezi
tunaloendelea nalo ni kumtafuta Zawadi
Mlola.Tunataka kujiridhisha kama bado yuko hai au amekufa na kama yuko hai tujue mahala alipo” akajibu Mathew na Dr Fabian akatoka akiwaacha wakiendelea na zoezi lao.Mara tu Dr Fabian alipotoka simu ya Mathew ikaita alikuwa ni Victor
“Hallo Victor” akasema Mathew
“Bosi kuna mgeni wako amekuja hapa anakutafuta.Nimkaribishe ndani? Akauliza Victor
“Ni nani huyo mgeni?
Sikuwa na miadi ya kuonana
na mtu yeyote leo” akasema Mathew
“Anadai anaitwa Sindi” akasema Victor na Mathew akastuka
“Sindi? Akauliza “Ndiyo mkuu”
“Sawa mkaribishe ndani ninakuja sasa hivi” akasema Mathew
“Ruby nimepata dharura kuna mgeni ambaye sikumtegemea amefika nyumbani nahitaji kwenda kuonana naye.Naomba uendelee na lile zoezi tafadhali nitarejea baadae kidogo.Kama
kuna kitu utakipata utanijulisha” akasema Mathew
“That Sindi.Is she your new woman? Akauliza Ruby
“Ruby please” akasema Mathew
“Go” akasema Ruby na Mathew akafungua mlango akatoka.
“Sindi amefahamuje nyumbani kwangu?Sikuwahi kumuelekeza mahala ninapoishi amewezaje kufika? Sikutaka afahamu mimi ni nani” akawaza Mathew akiwa garini
Mara tu Mathew alipoondoka Dr Fabian akaingia katika ofisi ya Ruby
“Nimemuona Mathew akiondoka.Kuna chochote mmekipata? Akauliza Dr Fabian
“Amepigiwa simu kuna mgeni wake wa muhimu amefika nyumbani kwake hivyo amekwenda kumpokea”akajibu Ruby
“Ouh.Nilidhani kuna jambo mmefanikiwa kulipata”akasema DrFabian na ukimya ukatawala
“Are you two okay?
Akauliza Dr Fabian “Yes.We’re okay don’t
worry”akajibu Ruby na Dr Fabian akatoka mle ofisini
“Nilisikiliza mazungumzo ya Mathew na Ruby bila wao kujua kama nilikuwa mlangoni.Hakuna ubishi kwamba Ruby bado anampenda Mathew.Ninachoshukuru Mathew ni kijana mwelewa na alimkumbusha Ruby kwamba yeye sasa ni mke wa mtu hivyo mambo yao ya zamani
yamekwisha pita na imebaki historia” akawaza Dr Fabian
*********** Mathew alifika nyumbani
kwake na moja kwa moja
akafululiza sebuleni ambako alimkuta Sindi akiwa ametulia sofani akitazama runinga huku akiburudika kwa mvinyo safi wa zabibu unaotengenezwa Dodoma Tanzania.
“Sindi ! akasema Mathew kwa mshangao.Huku akitabasamu Sindi
akanyanyuka na kwenda kumkumbatia.
“Mathew.Nimefurahi kukuona tena” akasema Sindi “Umefahamuje hapa nyumbani kwangu? Akauliza
Mathew baada ya kuketi sofani “Mathew kwa nini
ukanificha kuhusu wewe? Akauliza Sindi Mathew hakumjibu
“Nilimaliza kurekodi kipande changu nikapewa siku saba za mapumziko hapa Tanzania.Niliwaeleza wakubwa wangu kwamba ninatamani sana kuonana
nawe lakini sifahamu mahala unapoishi.Mtunzi wa hadithi tunayotengenezea filamu aliniuliza kama ulinielekeza unakoishi nikamwambia sifahamu unakoishi ila nilipomtajia tu jina akastuka na ndipo aliponiuliza kama nina uhakika na jina nililomtajia.Nilimwambia sijakosea jina.Mshangao wake ulinifanya nihisi kuna kitu kuhusu wewe ndipo nilipomtaka anieleze kama anakufahamu na akaniambia kwamba jina Mathew Mulumbi ni jina maarufu sana
hapa nchini Tanzania.Akanieleza kwamba wewe ni mfanyabiashara mkubwa unayemiliki makampuni kadhaa makubwa hapa nchini.Ni yeye aliyenileta hapa kwako.Nimefurahi Mathew kufahamu nyumbani kwako na pia kuonana nawe tena” akasema Sindi na kutabasamu
“Karibu sana Sindi.Kwa ufupi tu ni kwamba mimi huwa sipendi kujitangaza wala kujionyesha kama nina utajiri mkubwa.Nje ya nyumbani kwangu ninaishi maisha ya
kawaida kabisa kama watu wengine” akasema Mathew
Mazungumzo yaliendelea hadi ilipofika saa mbili za usiku
“Huyu Sindi hana dalili zozote za kuondoka hapa.Anaonekana anataka kulala hapa.Itakuwa vyema sana walau nipate mtu wa kuwa naye humu ndani kwa usiku wa leo.Ngoja nimjaribu kama atakuwa tayari kulala hapa’ akawaza Mathew
“Sindi inakaribia saa tatu za usiku sasa.Unaonaje kama ukilala hapa leo hii halafu
nikakurudisha kambini kwako kesho asubuhi? Akauliza Mathew na Sindi akatabasamu
“Hakuna tatizo Mathew.Kama nilivyokwambia nina mapumziko ya siku saba hivyo hakuna shida naweza kulala hapa” akasema Sindi
“Swala amejileta mwenyewe kwenye mtego” akawaza Mathew na maongezi yakaendelea hadi ilipofika saa nne za usiku Mathew akaongozana na Sindi hadi chumani kwake.Wakiwa katika maandalizi ya mtanange mkali,simu ya Mathew ikaanza
kuita akaichukua na kutazama mpigaji alikuwa ni Ruby
“Hallow Ruby” akasema Mathew
“Mathew are you busy?
Akauliza Ruby “Hapana.Kwa nini
umeuliza? Kuna chochote umekipata?
“Ulisema utarejea tena lakini mpaka sasa sijakuona”
“Ruby nimeshindwa kurejea tena nitakuja asubuhi na mapema.Kuna chochote umekipata? Akauliza
“Hapana bado.Ulipoondoka na mimi
sikuendelea tena na ile kazi ila nitaendelea nayo kesho asubuhi” akasema Ruby
“Sawa Ruby tutaoana tena hiyo kesho asubuhi” akajibu Mathew na kukata simu
“Mathew ninahitaji mvinyo na vipande vya barafu.Unaweza ukaniletea tafadhali? Akaomba Sindi na Mathew akatoka mle chumbani akaelekea jikoni kumletea Sindi kinywaji alichoagiza
Mara tu Mathew alipotoka chumbani Sindi akainuka haraka haraka akafungua
pochi yake na kutoa kifaa Fulani kidogo akakipitisha nyuma ya simu ya Mathew ikfunguka akaandika haraka harakja namba za Ruby katika karatasi halafu akaingiza namba Fulani katika simu ya Mathew halafu akazima na kuirudisha mahala ilipokuwa.Baada ya muda Mathew akarejea akiwa na chupa ya mvinyo .Bila kuelewa kile kilichofanywa na Sindi Mathew akammiminia Sindi mvinyo katika glasi wakanywa na na baadae wakajikuta
wakiingia katika mtanange mkali.
GERZA LA KIMONDO
King’ora cha kuashiria ni muda wa chakula cha usiku kililia na wafungwa wote wakakusanyika katika bwalo la chakula.Toka Gosu Gosu alipopewa taarifa kwamba mfungwa mpya aliyejulikana kwa jina la Kishada yuko pale gerezani kwa ajili ya kumuua yeye, hakuwa na amani kabisa.Kwa siku nzima hakukanyaga chumbani kwake.Alishinda maktaba akijisomea na baada ya kutoka maktaba akaenda katika karakana ya ufundi ambako alikaa huko hadi ulipofika muda wa chakula cha usiku. Katika meza moja iliyokuwa pembezoni kabisa mwa bwalo la chakula mfungwa mpya alikuwa amekaa peke yake akipata chakula.Wafungwa walionekana kumuogopa hivyo kuikimba meza aliyokuwa amekaa na kujikuta akiwa peke yake.Kishada hakujali mtu yeyote aliendelea kula taratibu.
“Gosu Gosu naomba uwe makini sana na Yule mfungwa mpya aliyehamishiwa chumbani kwetu haonekani kuwa ni mtu mzuri” Mchungaji Peter Msavu akamnong’oneza Gosu Gosu wakati wakipata chakula.
“Usihofu mchungaji nitakuwa makini sana” akasema Gosu Gosu na kuendelea kula huku akimtazama Kishada mara kwa mara.Baada ya chakula wafugwa waliendelea na mazungumzo mbali mbali huku wakitazama taarifa ya habari katika runinga kubwa
iliyokuwamo ndani ya bwalo hilo
King’ora cha kuashiria muda wa kwenda kulala kikalia,Gosu Gosu akamuaga mchungaji Peter kisha akaelekea katika chumba chao.Milango yote ya vyumba ikafunguliwa na wafungwa wakaanza kuingia vyumbani mwao.Gosu Gosu alikuwa wa kwanza kuingia chumbani na kwenda kulala katika kitanda cha chini.Hakutaka kugusa kitanda cha juu kutokana na tahadhari aliyopewa.Kishada alikuwa mtu wa mwisho kuondoka bwaloni.Aliingia chumbani kwao na lango likafungwa.Akasimama mlangoni akamtazama Gosu Gosu kwa macho makali akiwa amelala katika kitanda cha chini
“Nani kakupa ruhusa ya kulala katika kitanda hicho? Kishada akauliza kwa ukali.Sauti yake ilikuwa nyembamba yenye kukwaruza.Gosu Gosu akageuza kichwa akamtazama akaendelea kujilaza “Wewe ni kiziwi? Husikii unachoambiwa? Akafoka
Kishada
“Wewe ni nani? Gosu Gosu naye akauliza kwa ukali halafu akainuka na kukaa kitandani “Ondoka haraka sana
katika kitanda hicho na iwe ni mara yamwisho kukigusa ama sivyo nitakuharibu sura yako ! akaendelea kufoka Kishada na
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment