Simulizi : Balaa
Sehemu Ya Nne (4)
Walikuwa
na mateka wengi sana. Sasa walitulia katika kambi yao wakiwa na uhakika wa
kupata mioyo kumi tano kwa siku kadhaa.
***** CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwezi ukapita, bila
tukio lolote lile la kushangaza katika mji wa Kilwa Masoko wala mji wa Kilwa
Kivinje. Baadhi ya watu walianza kusahau matukio ya kutisha yaliyotokea mwezi
mmoja nyuma. Watu walianza tena kutembea usiku. Baadhi ya askari Polisi pia
walisahau kasheshe iliyotokea mwezi mmoja nyuma. Lakini wazazi na ndugu wa watu
waliotekwa hawakusahau kabisa, waliomboleza kila siku juu ya upotevu wa ndugu
zao. Wao walikuwa na mawazo sawa na mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel
Mwaseba, ambaye hakuwa amesahau juu ya vifo na upotevu wa watu kiajabu wa raia
wema na alikuwa kazini kila jua lililokuwa linachomoza. Hatimaye Daniel Mwaseba
sasa alikusanya taarifa za kutosha juu ya sakata hii, na kuingia kazini rasmi.
Jioni moja ilimkuta Daniel Mwaseba katika baa ya Tiga Tisa. Baa ileile iliyokuwa
chanzo cha kifo cha Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Kilwa. Pale Tano
alipoikosa shabaha yake ambayo ilikuwa ni Mwanasheria mlevi na kumuua
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa. Daniel Mwaseba hakwenda kunywa
katika baa ile. Daniel Mwaseba alikuwa kazini. Alikuwa makini kwa kila
kilichoendelea pale Tiga Tisa, alijua lazima atapata kitu kitakachompeleka hatua
nyingine katika upelelezi wake. Naam, Daniel Mwaseba alishakusanya taarifa za
kutosha. Taarifa ambazo zilizomjurisha kwamba, kwa mara ya mwisho Mwanasheria wa
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa alikuwa katika baa hiyo kabla mauti hayajamfata
hadi nyumbani kwake. Bila shaka Israel mtoa roho alitoka naye hapo, hivyo ndivyo
Daniel Mwaseba akivyoamini. Hiyo ndio sababu pekee iliyompeleka Daniel Mwaseba
katika baa ya Tigatisa. Alikaa kwenye kona moja, iliyokuwa gizani kidogo lakini
ilimuwezesha kuona watu wote wanaoingia na kutoka katika baa ile maarufu Kilwa.
Saa nne alikaa pale baa ya Tiga Tisa. Hakukuwa na kitu chochote cha kukitilia
shaka. Baa ilikuwa na ushwari wake uleule alioukuta tangu alivyoingia.
'Mvumilivu hula mbivu' Saa sita ya usiku katika baa ya Tiga Tisa aliingia mtu
mmoja mrefu, mtu ambaye Daniel Mwaseba alimtilia shaka kidogo. Alikuwa jamaa
mmoja mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, alikuwa amevaa vest nyeupe huku chini
akiwa amevaa pensi fupi aina ya timberland. Pamoja na ujabari uliokuwa
unaonekana katika mwonekano wake lakini alikuwa anachemenea mguu mmoja. Sifa
hizo hazikumfanya Daniel Mwaseba astuke sana, mpaka pale Mhudumu wa baa ile
alivyomkonyeza Daniel Mwaseba. Daniel alishaenda katika Baa hiyo mida ya jioni
na kumhoji Mhudumu wa Baa ile. Mhudumu aliyemthibitishia kuwa anamtambua mtu
anayemuhisi kuwa ndiye alimuuwa Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Kilwa.
Mhudumu alimwambia kuwa alimtilia shaka mtu huyo pindi tu alivyoingia katika Baa
ile. Mhudumu alianza kumpeleleza mtu yule kwa siri. Ingawa Mhudumu hakuwa
mtaalamu wa wahalifu, lakini macho ya mtu yule yalimjulisha kwamba yule jamaa
alikuwa Mhalifu! Aliyashuhudia macho mabaya ya jamaa yule yakimwangalia
Mwanasheria mara kwa mara. Na pindi tu Mwanasheria alivyopanda gari lake na
kuondoka, na yule jamaa naye aliondoka. Zilipokuja taarifa kwamba Mwanasheria
kauwawa kwa kisu nyumbani kwake, yule Mhudumu alimtilia shaka sana yule mtu
aliyemwona akimwangalia Mwanasheria kwa jicho baya. Lakini hakuwa na mtu sahihi
wa kumueleza. Upelelezi wa Polisi ulikuwa wa ajabu sana. Hawakwenda kabisa
kupeleleza mahali ambapo Mwanasheria alionekana kwa mara ya mwisho (Tigatisa).
Mhudumu yule aliwasubiri askari waje pale angalau awaambie anachokifahamu kuhusu
kifo cha Mwanasheria, lakini Polisi hawakwenda. Naye hakuwa na amani ya kwenda
kituo cha Polisi kueleza hisia zake, kwanza zilikuwa hisia tu. Mhudumu alikaa na
dukuduku moyoni mpaka leo hii jioni alivyokuja askari huyu kijana, Daniel
Mwaseba. Baada ya Daniel Mwaseba kumchokonoa Mhudumu yule Mhudumu alimueleza
kila kitu Daniel, na kumuhakikishia kuwa anamtambua huyo mtu endapo atatokea
tena katika baa ile. Ingawa Mhudumu alisema huyo mtu hakuja tena katika baa ile
tangu usiku wa tukio lile. Daniel Mwaseba hakuwa na wasiwasi, alimwambia Mhudumu
kuwa atakuwa anaenda Baa kila siku. Na siku atakayoyokea tu huyo jamaa
amkonyeze, kwa bahati nzuri siku ileile Tano alienda TigaTisa, na Daniel Mwaseba
ndipo alipokonyezwa na yule Mhudumu. Daniel Mwaseba pale alipokaa alimuona
vizuri sana Tano. Bila wasiwasi wowote Tano alichagua meza moja iliyokuwa tupu
na kukaa. Yule Mhudumu alienda Kumsikiliza Tano. Kisha alirudi tena kaunta
kuchukua alichoagizwa. Daniel Mwaseba alimshuhudia Mhudumu akipeleka bia mbili
katika meza ya yule jamaa, kisha akaondoka. Daniel Mwaseba alinyanyuka pale
alipokaa na kuifuata ile meza aliyokaa Tano. Ghafla, Tano aliushuhudia ugeni
asioujua katika ile meza yake. Tano alimwangalia kwa umakini mkubwa sana yule
kijana mgeni aliyeivamia meza yake bila kukaribishwa. Yule kijana nae ( ambaye
sisi tunamtambua kama Daniel Mwaseba) alitulia tuli, kama hakuwa amefanya jambo
lolote lile ajabu. Baada kama ya dakika moja ya ukimya, Daniel alimuita Mhudumu
wa Baa ile kwa kutumia ishara ya mkono. Mhudumu alienda kwa mwendo wa taratibu
akiwa anatetemeka, alijua anaitwa ili akayaeleze pale yote aliyomwambia Daniel
Mwaseba kabla. Lakini haikuwa hivyo, alipofika pale Daniel alimuagiza maji
makubwa ya baridi aina ya Kilimanjaro. Wakati Mhudumu akienda kuchukua maji.
Ndipo Daniel alijitambulisha kwa yule jamaa mwenye mwili wa kibabe. "Naitwa
Daniel Mwaseba.." Alivyolitaja tu hilo jina, kwa kutumia macho yake makini ya
kipelelezi, Daniel Mwaseba aliona mstuko alioupata yule jamaa, ulikuwa mstuko
mkubwa ulioiacha sura yake ikiwa katika hali ya kutahayari. Bila shaka Tano
hakutegemea kabisa kukutana na mtu mwenye jina kama lile. Kabla Daniel
hajaongeza kitu chochote, Mhudumu aliyaleta maji ya Kilimanjaro makubwa
aliyoyaagiza Daniel Mwaseba. Akayaweka juu ya meza pamoja na glasi ya wastani.
Mhudumu aliondoka huku uwoga ukitapakaa hadi katika mwendo wake. Daniel Mwaseba
alifungua ile chupa kubwa ya Kilimanjaro, akamimina maji nusu katika glasi,
akanywa funda moja dogo. Alitulia akiyaruhusu maji yale ya baridi kupenya katika
koo lake. Aliyefanya hayo yote kwa umakini mkubwa sana. Kuhakikisha yule jamaa
hafanyi ujanja wowote ule. Kwa upande Tano hakuwa tayari kabisa kulisikia jina
la Daniel wakati ule. Mara nyingi sana alishazisikia sifa na umahiri wa Daniel
Mwaseba katika mapambano. Kwa bahati mbaya zaidi alikuwa amekutana na Daniel
Mwaseba akiwa mgonjwa, mgonjwa wa goti aliloumizwa na Dokta Yusha. Tano alijutia
kitendo cha kuachana na wenzie kimoyomoyo, wangekuwa wote labda wangeweza
kumkabili Daniel Mwaseba na kumzidi mbinu. Tano alitafakari kwa kina afanye nini
ili anusurike katika kisanga kile, lakini hakupata, akili ilikuwa inagoma kabisa
kuwaza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila akiwaza akili ilikuwa inamrudisha palepale mezani na mbele yake alikuwa anatazama na mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba. "Unaitwa nani mwenzangu?" Daniel aliuliza kwa sauti yake ya upole yenye kuonesha urafiki. Jamaa hakujibu, alikaa kimya kama hajaulizwa kitu. "Usinilazimishe nitumie nguvu kijana, nina nguvu za kukufanya chochote!" Sasa Daniel alisema kwa ukali kidogo. Tano alimwangalia tu Daniel Mwaseba, huku akitafuta namna sahihi ya kutoa bastola yake iliyokuwa kiunoni kwake. "Huwezi kuniwahi kwa bastola yako iliyopo kiunoni" Daniel alikijibia kitu ambacho Tano alikuwa anakiwaza tu kichwani kwake. Tano alistuka sana! Licha ya kusomea saikolojia ya wahalifu Daniel Mwaseba alikuwa na kipawa cha kutambua vitu vinavyopita katika kichwa cha Mhalifu. Daniel hakuujari mstuko wa Tano wa Six Killers. Yeye aliuliza swali lengine kabisa . "Kwanini ulimuua Mwanasheria?" Tano hakujibu kitu, aliendelea kuwa bubu. "Naona umeshindwa kunijibu hapa tukiwa kama rafiki, sasa utanijibu mahala pengine tukiwa kama maadui" Daniel Mwaseba alichomoa bastola na kumuonesha Tano kwa siri sana. Hakuna mtu mwengine wa pembeni aliyeweza kuiona ile bastola kwa jinsi alivyooneshwa zaidi ya Tano mwenyewe. "Hii bastola nzuri sana, halafu ina kiwambo cha kuzuia sauti. Naweza nikakufumua kichwa chako kimyakimya bila mtu yoyote kutambua sababu ya kichwa chako kutawanyika! Naomba ufuate nitakachokuelekeza" Uso wa Tano ulistuka sana kutokana na kauli ya kitisho toka kwa Daniel Mwaseba. "Nyanyuka taratibu na utoke nje ya baa hii, nakuomba twende kirafiki, ujanja wowote ule utakaoufanya inamaanisha unakitafuta kifo chako kwa nguvu!" Tano aliishiwa ujanja, hakuwa na chochote cha kufanya, alikutana na mjanja wa wajanja, alitoka nje taratibu huku akifuatwa kwa nyuma na Daniel Mwaseba kwa umakini mkubwa sana. Safari yao iliishia katika nyumba ya kulala wageni aliyofikia Daniel Mwaseba, pembezoni mwa bahari ya hindi, Kimbilio lodge. Huku njiani wakitembea kama marafiki wa kweli. Watu waliopishana nao njiani bila kuhisi hatari yoyote kati ya watu hawa wawili, laiti wangejua vitu vilivyokuwa vinazunguka katika vichwa vya watu hao wawili. Walipoingia tu ndani ya chumba chake, Daniel Mwaseba alimkaribisha Tano kutoka kundi la Six Killers. "Karibu sana rafiki yangu, haya sasa kwa hiyari yako naomba unambie unaitwa nani?" "Kunileta hapa haimaanishi kwamba mimi ni mateka yako, eti kwamba nitakwambia chochote unachojisikia kuniuliza" kwa mara ya kwanza Tano alijibu huku mdomo wake akiubetua kijeuri kwenda juu. "Hahaha kumbe nawe jeuri" Daniel Mwaseba alikuwa anacheka huku akimtazama kwa umakini Tano. Ilikuwa ni kitendo bila kuchelewa, Daniel Mwaseba alirusha teke la haraka lililotua katika goti la Tano, goti lilelile lililojeruhiwa na daktari makini kabisa, Dokta Yusha. Tano alipiga ukelele mkali sana kutokana na maumivu aliyoyapata katika goti, kutokana na pigo lile la teke toka kwa Daniel Mwaseba. "Sipendi kukutesa kijana, naomba unambie kila nitakachokuuliza" Daniel Mwaseba aliongea maneno hayo yakienda sambamba na ngumi mbili nzito zilizompata barabara Tano katika shavu lake la kulia. Ngumi hizo zilileta athari kwa Tano, Damu zilikuwa zinamchuruzika mdomoni. "Utasema husemi?" "Nitasema" Tano alijibu huku akitema rundo la damu. "Safi sana kijana" "Unaitwa nani?" "Tano" "Tano nani?" "Tano wa Six killers" "Sijakuelewa" "Naitwa Tano wa Six killers" "Six killers ndio nini?" Tano alikaa kimya. Daniel Mwaseba alipatwa na hasira juu ya ukimya wa Tano, alirusha ngumi ya nguvu iliyotua katikati ya mdomo wa Tano, ngumi iliyorudisha jibu, meno mawili ya Tano yalidondoka sakafuni. "Six killers ndio nini?" Daniel aliuliza kwa ukali! Tano aliona hana ujanja, ilimpasa afanye kitu ili aweze kujiokoa katika mdomo wa kifo! Kwa nguvu zake zote Tano alisimama. Ingawa alisikia maumivu makali kwenye goti lakini alisimama. Alirusha teke la nguvu lililomkosa Daniel Mwaseba kidogo sana. Bila wepesi wa Daniel Mwaseba kulikwepa teke lile angepata madhara makubwa sana. Tano aliyebadirika na kuwa kama mzimu alirusha ngumi ya nguvu iliyompata Daniel Mwaseba katika bega la kushoto. Tano alikuwa amechachamaa, alikuwa anataka kufa na mtu. Daniel nae akajipanga vyema sasa. Tano wa Six Killers alikwenda mzima mzima kumvaa Daniel Mwaseba. Daniel Mwaseba alimuona vizuri sana, alikuwa ameshajipanga vizuri kimapambano, Daniel alisogea pembeni kidogo, Tano alipita moja kwa moja kwa kasi kubwa sana na kwenda kuuvaa ukuta. Ebwana wee! Alijigonga vibaya sana usoni. Dakika hiyohiyo uso wa Tano ulivimba na kutoa kitu kiitwacho nundu katikati ya paji lake la uso! Tano alipata maumivu yasiyo na kifani, alitumia nguvu nyingi sana kwenda kumvaa Daniel Mwaseba. Tano wa six killers hakuweza kustahamili maumivu aliyokuwa anayapata, alianguka chini mzimamzima. Daniel Mwaseba hakumuonea huruma kabisa. Sasa angalau kidogo alishayajua madhara ya Tano. Hakutaka kumpa mwanya wa kufanya chochote. Alimfata kwa teke la nguvu palepale chini alikokuwa amelala. Teke la kiume lililotua barabara katika kifua cha Tano, Tano alitoa mguno hafifu wa maumivu na kuanza kutoa madonge mazito ya damu mdomoni. "Nakufaa" Tano alisema kwa sauti dhaifu, ama hakika alikuwa amepatikana hasa. Daniel Mwaseba alimjibu, alimjibu kwa teke kali sana la uso. Daniel alikuwa na huruma sana kwa raia wema. Lakini kwa bahati mbaya hakuwa na huruma kabisa kwa wahalifu kama Tano. Uso mzima wa Tano ulitapakaa damu. Tano alijikusanya pale chini, akijitahidi kuvuta pumzi zake za mwisho. Daniel Mwaseba aliinama pale chini alipokuwa amejipweteka Tano, alimshika koromea kwa mkono wake wa kulia. Tano macho yalimtoka pima!, Daniel Mwaseba alimkaba kiasi kwamba alishindwa hata kumeza mate, ama kumeza damu ambazo ndizo zilikuwepo mdomoni mwake. "Six killers ni nini?" Daniel Mwaseba aliuliza kwa nguvu akiwa anaangaliana na Tano. "Hata nisi-po-kwambia uta-ni-fanya n-ini, mi-mi ni mfu ta-ya-ri, nifa-nye utakacho si-kwa-mbii ki-tu" Daniel Mwaseba akajua yule jamaa amegoma kusema. Alimwacha pale, akasogea kwenye kabati lililokuwa ukutani, akafungua na kutoa mkoba wake. Alitoa kamba za katani, kamba alizotumia kumfunga vizuri sana Tano miguuni na mikononi, hakutaka kumuua, alitaka kujua vitu kwanza toka kwa yule jamaa. Alimwacha kamfunga vizuri Tano na kutoka nje ya kile chumba. Hakwenda mbali sana Daniel, alijibana sehemu akiangalia kitatokea nini pale mlangoni.

CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimwacha kamfunga
vizuri Tano na kutoka nje ya kile chumba. Hakwenda mbali sana Daniel, alijibana
sehemu akiangalia kitatokea nini pale mlangoni. Kwa jinsi Tano alivyofungwa
kamba zile na kwa hali aliyokuwa nayo, mimi na wewe tusingeweza kufungua zile
kamba. Lakini Tano wa Six killers hakuwa mimi na wewe. Tano alikuwa nunda kweli.
Tano alikuwa mjuaji, Tano alikuwa jambazi mahiri, Tano alikuwa mbabe, Tano
alikuwa mtemi. Tano alikuwa sugu! Daniel Mwaseba akiwa amejibanza katika mpenyo
katika korido ya nyumba ile ya kulala wageni alishangaa kuuona mlango wa chumba
chake ukifunguliwa na mtu kutokea ndani. Tano alikuwa anaenda taratibu kumfata
Daniel Mwaseba pale chini alipokuwa amelala. Ngoma sasa ilikuwa imemgeukia
Daniel, tena imemgeukia kwa kasi sana! Tano alikuwa anatisha kama mzimu! Tano
alinyanyua guu lake baya la kulia juu, saizi ya kimo cha mbuzi akawa
analirudisha kwa kasi kuelekea katika kifua cha mwanaume, Daniel Mwaseba, Tano
alikuwa anautumia mguu uleule alioumia vibaya sana gotini. Labda Tano alishikwa
na ganzi katika mguu ulipewa jeraha na Dokta Yusha, maana hakusikia kabisa
maumivu ya ule mguu wake mbovu. Akiwa amelala pale chini Daniel Mwaseba aliuona
vizuri sana mguu ule. Ulivyokuwa unashushwa, kwa kasi ya haraka alinyoosha
mikono yake yote miwili na kuudaka mguu ule mbovu, Daniel Mwaseba aliuzungusha
kwa nguvu zake zote. Mguu mbovu wa Tano uliteguka aisee! Tano alianguka chini
akigalagala na kulia mithili ya mtoto mdogo. Alikuwa anasikia maumivu yasiyo na
mfano. Daniel Mwaseba akiwa na ghadhabu aliruka juu na kushuka chini,
aliukanyaga tena mguu mbovu wa Tano palepale kwenye kifuti. Tano alilia kilugha
cha kwao.... "Six killers nd'o nini?" Tano alimwangalia Daniel Mwaseba kwa
hasira sana. Alijitahidi kukusanya mate ya kutosha mdomoni, ingawa kwa shida
lakini aliyapata. Aliyarusha mate yale yote yaliyokuwa yamechanganyika na damu!
Yalitua katikati ya paji la Daniel Mwaseba. Mate yenye mchanganyiko wa damu
mbaya! Kitendo kile cha kijeuri kilizidi kumuuzi Daniel Mwaseba. Sasa alipandwa
na hasira mithili ya kifaru. Hakujiangaisha kabisa kuyafuta yale mate yenye damu
ya Tano. Alirudisha kichwa chake nyuma, kwa nguvu zake zote alikipigisha kichwa
chake katika kichwa cha Tano. Kilikuwa kichwa kweli! Kichwa kilichomwacha Tano
akipiga kelele mithili ya mtu aliyefiwa na baba yake mzazi. Kichwa kilichomwacha
Daniel Mwaseba akiwa nae katapakaa damu usoni. Damu alizozitoa toka katika sura
ya Tano. Ghafla! Mlango wa kile chumba ulifunguliwa kwa nguvu! Watu watatu kila
mmoja akiwa na bunduki mkononi walikuwa wanawaoneshea midomo ya bunduki zao kwa
Tano wa Six Killers na mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba!
Kasheshe! "Naitwa Alfred Duto, afisa wa jeshi la polisi, mko chini ya ulinzi"
Askari mmoja alitamka huku akiwa kashikilia kitambulisho chake cha kazi imara
mkononi. Daniel Mwaseba na Tano wote walinyoosha mikono juu. kila mmoja
akiuchukulia ujio wa askari wale kwa namna tofauti, wakati mpelelezi Daniel
akiupokea ujio wa askari wale kwa tabasamu. Kwa sababu ujio wa Polisi wale
ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kwake. Kwakuwa yeye alikuwa ni askari pia, hivyo
walikuja askari wenzake. Lakini kwa Tano lilikuwa ni pigo kubwa sana, kuingia
katika mikono ya polisi ni kitu alichokuwa hataki hata kufikiria. "Haya tokeni
nje haraka!" Askari mmoja aliamrisha kwa sauti ya amri. "Naitwa Daniel Mwaseba"
Askari wote watatu walistuka kusikia jina hilo. Daniel alishusha mkono mmoja na
kutia mfukoni, alitoka na kitambulisho chake cha kazi. Sasa Polisi wakawa makini
na yule jamaa mwengine. Huku wakitoa midomo ya bunduki zao kwa Daniel. Kumbe
purukushani zao na makelele wakati wanapigana zilisikiwa na Mhudumu kule nje.
Mhudumu ambaye alimpigia simu Meneja wake kumueleza juu ya hofu yake na chumba
namba saba, chumba alichofikia Daniel Mwaseba. Meneja nae aliamua kutoa taarifa
polisi. Sasa walikuwa Askari wanne, wakitoka nje na Mhalifu. Kutoka katika
hoteli ya kitalii ya Kimbilio, hoteli aliyofikia Daniel Mwaseba, haikuwa mbali
kabisa na kituo cha polisi Masoko. Ilikuwa ni pua na mdomo. Walitumia miguu tu
kumfikisha Tano kituoni. Walipofika kituoni Tano aliendelea na Kiburi chake.
Hakueleza kitu chochote zaidi ya kusema yeye anaitwa Tano wa Six Killers.
Alipewa mateso makali sana na askari Polisi. Mateso ambayo hayakumfanya Tano
atoboe siri zake ama siri za kundi la six Killers na mpango wao haramu. Tano
aliendelea kuwa bubu. Alilala kituoni siku ile, huku Daniel Mwaseba akirudi
mtaani kuendelea na upelelezi wa mauaji na kupotea kwa wanafunzi. Huku akiwa na
msamiati mpya kichwani mwake ambao alishindwa kuutambua. 'Six killers' Kesho
yake asubuhi Tano alipelekwa mahabusu, Gereza la wilaya ya Kilwa. Alipakiwa
kwenye gari la polisi akiwa kafungwa pingu mkononi. Huku bunduki mbili
zikitazama kichwa chake. Gari ilioondoka kwa kasi kubwa sana huku ikipiga
ving'ora. Tano alizungusha macho yake huku na huko, kutafuta nafasi ya kutoroka,
na ilikuwa hivyo. Tano wa Six killers akiwa hoehae aliiona nafasi akiyoitafuta.
Tano alijilegeza kidogo ikawa laini kama mlenda kisha akaanguka kwenye bodi ya
gari. Askari wote walipatwa na mshangao mkuu, waliacha kumuelekezea ile midomo
hatari ya bunduki, walimsogelea huku bunduki zao zikining'inia mabegani.
Lilikuwa kosa la mwaka! Tano akiwa kajilegeza vilevile alijirusha nje ya ile
gari na kushuka katika barabara ya lami. Tano alifikia vibaya sana katika
barabara ya lami, kumbuka gari lilikuwa linatembea kwa kasi kubwa sana. Pia Tano
alikuwa amefungwa pingu mikononi. Lakini Tano hakujari hilo hata chembe. Wale
Askari walibaki midomo wazi, na bunduki zao mkononi zikiwa zinawashangaa.
Hawakuwa na ujanja wa kuruka kwa kasi ile, ilikuwa ni zaidi ya hatari. Askari
walipigapiga bodi ya gari ile ili kumuamrisha dereva apunguze mwendo, maskini
dereva hakusikia chochote, mwendo ule ukichanganya na kelele za king'ora,
ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Walimuacha Mhalifu hataru sana njiani, wao
wakiendelea na kasi yao ya kutisha kuelekea gerezani! Tano, kwa sasa alikuwa
ametapakaa damu mwili mzima, akiwa na maumivu kila sehemu ya mwili wake, maumivu
ya kupewa kichapo na Daniel Mwaseba, maumivu ya kuruka katika barabara ya wakati
gari ikiwa kasi, tena na kuangukia kwenye lami. Tano alikuwa na roho ya paka!
Kwa kutambaa ingawa kwa shida sana alijisogeza pembeni ya barabara, alikuwa na
maumivu makali sana, kiasi kwamba alikuwa anashindwa kunyanyuka. Nasema ilimpasa
ashindwe kunyanyuka lakini Tano wa Six Killers alijitahidi kunyanyuka, maana
kuendelea kukaa mahala pale ilikuwa ni hatari sana kwake. Jamaa alijitahidi
kunyanyuka, aliweza, Tano alinyanyuka kwa mwendo wa kusuasua alijisogeza pembeni
zaidi ya barabara. Gari ya polisi ilikuwa inaingia katika viwanja vya gereza la
Kilwa. Dereva alipiga kona kwa mbwembwe nyingi huku akifunga breki kali sana.
Laiti angejua kama mhalifu Tano hakuwepo kule nyuma ya gari. Gari lilisimama.
Taarifa mbaya kabisa ikapenya katika masikio ya dereva. Kwamba mhalifu Tano
alijirusha toka katika ile gari wakati ikiwa katika mwendo mkali. Ilikuwa ni
kitendo bila kuchelewa hata sekunde kumi, dereva alirudi kwa haraka katika
usukani wa gari ya Polisi na kuligeuza gari kwa haraka pia, kurudi pale mahali
ambapo alijirusha Tano. Dakika nne na sekunde thelathini tu zilitosha
kuwafikisha pale, askari walishuka haraka haraka kabla gari haijasimama vizuri
na kuanza kumsaka Tano. Walichakua katika nyasi zote lakini Tano hakuonekana!
Askari waliishiwa nguvu, kwa jinsi Tano alivyojirusha na kufikia na mwendokasi
waliyotumia kurudi pale walitegemea kumkuta Tano palepale barabarani. Hayo
yalikuwa mawazo yao, lakini Tano hakuwepo kabisa pale barabarani, hata dalili tu
kama kulikuwa na kiumbe.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hayo yalikuwa
mawazo yao, lakini Tano hakuwepo kabisa pale barabarani, hata dalili tu kama
kulikuwa na kiumbe. Huko porini Ngome hali ilikuwa ya taharuki sana. Tangu jana
yake usiku Tano alikuwa hajarejea kambini. Waliamini Tano amepotea kama
alivyopotea Sita. Sasa wanapotea vipi, wanaenda wapi, hakuna aliyekuwa na
majibu. Walitafuta sehemu zote walikodhani labda atakuwepo lakini Tano
hawakumpata. Mwishowe walienda mahali ambako Tano aliwaambia ataenda usiku,
katika baa ya Tiga Tisa. Six killers wote wanne walienda katika baa ya Tiga
Tisa. Walikaa meza moja na kuanza kuchunguza mazingira ya pale baa. Hawakupata
lolote la maana. Mwishowe Moja aliamua kumuita Mhudumu mmoja ili amuulizie kama
alimuona jamaa yao hapo. Kwa bahati mbaya Mhudumu aliyemuita Moja nd'o yuleyule
aliyeongea na Daniel Mwaseba kabla. Nd'o yuleyule aliyefanikisha Tano kukamatwa.
Mhudumu muoga sana anapokutana na wanaume kama hawa. Haikuwa kazi ngumu kwa
vijana mahiri wa six killers kutambua kwamba Mhudumu yule anayajua mengi.
Wakaamua nae wamchukue. Kwa bahati mbaya kabisa Mhudumu wa baa ya Tigatisa
akaingia katika mikono isiyo salama. Mikono hatari ya kundi baya na katili sana
kuwahi kutokea katika historia ya Kilwa, kundi la Six Killers. Mhudumu nae
akapelekwa porini bila kujua ukatili wa sehemu anakopolekwa na jamaa wale. Na
majaa hao makatili sasa walikaa sebuleni na kuwaza na kujadiliana nini cha
kufanya baada ya matokeo mabaya sana. Kijana mbishi, kijana mkatili, kijana sugu
kabisa Tano wa six killers alikuwa katika mikoko ya pwani ya makuburi. Alikuwa
amejificha katika mikoko hiyo akiwaza namna salama ya kutoka katika mikoko na
kurudi kambini kwao, porini ngome. Pamoja na uvumilivu wote huo lakini Tano
alikuwa anapita katika maumivu makali sana. Alikuwa na vidonda mwili mzima,
vidonda ambavyo sasa vilikuwa vinapitiwa na na ladha ya chumvichumvi toka katika
mikoko ya pwani. Askari walirudi kituoni, kutoa taarifa kwamba Jambazi
aliyejulikana kwa jina la Tano alikuwa amewarotoka. Kwa haraka sana habari hizo
mbaya zikafikishwa kwa Daniel Mwaseba huku askari wakimwaga mtaani kama njugu
kumsaka Tano wa six Killers. Daniel Mwaseba alipopigiwa simu, hakujibu kitu
chochote kuhusu ile simu zaidi ya kuitikia tu tena kwa sauti ndogo sana. Mpaka
saa sita usiku inaingia ilimkuta Tano pale katika mikoko, muda huo giza lilikuwa
la kutisha sana, usiku ukichanganya na uwepo wa mikoko iliyoshonana. Muda huo wa
saa sita ndipo Tano alishuka juu ya mkoko na kuelekea porini Ngome kwa kupitia
pori kwa pori. Hakujua, Tano hakujua! Nyuma yake hatua kama kumi na saba,
kulikuwa na mtu makini anamfata. Mtu ambaye alilijua lile ficho lake muda mrefu
sana. Mtu huyo hakutaka kumkamata. Shida yake ilikuwa ni kutaka kujua tu uelekeo
wa Tano utakuwa wapi. Yeye alikuwa na shida ya kuyafahamu makazi ya yule jamaa,
aliyejiita Tano. Na sasa ndio alikuwa anafanikiwa kuuona uelekeo wa Tano, na kwa
umakini mkubwa alikuwa anamfuata Tano kwa nyuma, bila Tano kuhisi jambo lolote.
Kwa bahati mbaya kabisa Mhudumu wa baa ya Tigatisa akaingia katika mikono isiyo
salama. Mikono hatari ya kundi baya na katili sana kuwahi kutokea katika
historia ya Kilwa, kundi la Six Killers. Mhudumu nae akapelekwa porini bila
kujua ukatili wa sehemu anakopolekwa na jamaa wale. Na majaa hao makatili sasa
walikaa sebuleni na kuwaza na kujadiliana nini cha kufanya baada ya matokeo
mabaya sana. Kijana mbishi, kijana mkatili, kijana sugu kabisa Tano wa six
killers alikuwa katika mikoko ya pwani ya makuburi. Alikuwa amejificha katika
mikoko hiyo akiwaza namna salama ya kutoka katika mikoko na kurudi kambini kwao,
porini ngome. Pamoja na uvumilivu wote huo lakini Tano alikuwa anapita katika
maumivu makali sana. Alikuwa na vidonda mwili mzima, vidonda ambavyo sasa
vilikuwa vinapitiwa na na ladha ya chumvichumvi toka katika mikoko ya pwani.
Askari walirudi kituoni, kutoa taarifa kwamba Jambazi aliyejulikana kwa jina la
Tano alikuwa amewarotoka. Kwa haraka sana habari hizo mbaya zikafikishwa kwa
Daniel Mwaseba huku askari wakimwaga mtaani kama njugu kumsaka Tano wa six
Killers. Daniel Mwaseba alipopigiwa simu, hakujibu kitu chochote kuhusu ile simu
zaidi ya kuitikia tu tena kwa sauti ndogo sana. Mpaka saa sita usiku inaingia
ilimkuta Tano pale katika mikoko, muda huo giza lilikuwa la kutisha sana, usiku
ukichanganya na uwepo wa mikoko iliyoshonana. Muda huo wa saa sita ndipo Tano
alishuka juu ya mkoko na kuelekea porini Ngome kwa kupitia pori kwa pori.
Hakujua, Tano hakujua! Nyuma yake hatua kama kumi na saba, kulikuwa na mtu
makini anamfata. Mtu ambaye alilijua lile ficho lake muda mrefu sana. Mtu huyo
hakutaka kumkamata. Shida yake ilikuwa ni kutaka kujua tu uelekeo wa Tano
utakuwa wapi. Yeye alikuwa na shida ya kuyafahamu makazi ya yule jamaa,
aliyejiita Tano. Na sasa ndio alikuwa anafanikiwa kuuona uelekeo wa Tano, na kwa
umakini mkubwa alikuwa anamfuata Tano kwa nyuma, bila Tano kuhisi jambo lolote.
Masaa matatu yalitosha kumfikisha jambazi Tano kambini kwao huko porini Ngome.
Bila kujua kabisa kama nyuma yake kulikuwa na mtu ambaye aliyekuwa akikanyaga
kila sehemu ambapo alitoa mguu wake. Mtu huyo akiyemfata Tano kwa nyuma alikuwa
makini sana, asiyeruhusu kufanya makosa katika kazi yake. Mpelelezi namba moja
nchini Tanzania aliyekuwa anaitwa Daniel Mwaseba.
CHANZO:
https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Masaa matatu
yalitosha kumfikisha jambazi Tano kambini kwao huko porini Ngome. Bila kujua
kabisa kama nyuma yake kulikuwa na mtu ambaye aliyekuwa akikanyaga kila sehemu
ambapo alitoa mguu wake. Mtu huyo akiyemfata Tano kwa nyuma alikuwa makini sana,
asiyeruhusu kufanya makosa katika kazi yake. Mpelelezi namba moja nchini
Tanzania aliyekuwa anaitwa Daniel Mwaseba. Daniel Mwaseba alitilia shaka uwezo
wa mtu yule mapema sana. Aliamua kulifatilia kwa nyuma lile gari pale tu
lilipotoka kituo cha polisi likiwa na Tano ndani yake. Daniel Mwaseba
alishuhudia vizuri sana jinsi Tano wa six Killers alivyojirusha wakati gari
linatembea kwa kasi kubwa sana! Daniel alishangaa sana umahiri wa jambazi Tano.
Kwa mwendo uliokuwa linatembea gari lile la jeshi la polisi na kwa jinsi Tano
alivyojirusha angekuwa mtu mtu dhaifu kama mimi na wewe angepasuka vibaya sana.
Lakini Tano hakuwa mimi na wewe, alikuwa mtu hatari zaidi ya hatari yenyewe.
Pamoja na kujirusha namna ile lakini Tano hakuumia kwa kiasi hiko. Daniel
akimshuhudia jinsi Tano alivyokuwa anajikokota na kujificha katikati ya mikoko.
Bila kujua kama alikuwa anafuatwa na mtu nyuma yake. Daniel Mwaseba alihakikisha
hafanyi kosa lolote kama ilivyo ada yake. Na kweli hakufanya kosa. Wakati Tano
wa six killers kajibana katikati ya mikoko, Daniel Mwaseba nae alijibana kwenye
mikoko umbali sio mrefu sana na alipojibana Tano. Alikuwa na uwezo wa kumkamata
lakini hakutaka kumkamata. Nia yake ilikuwa ni kuona uelekeo wa yule jamaa
itakuwa wapi, Daniel Mwaseba alihisi Tano lazima ataenda kwenye maficho yao. Na
hicho ndicho kitu ambacho Daniel Mwaseba alichokuwa anakihitaji sana. Kule kwa
nje mpelelezi Daniel Mwaseba aliizunguka kwa umakini mkubwa ule ukuta mrefu
uliokuwa umezunguka eneo lile. Pamoja na kuzunguka kwake lakini Daniel Mwaseba
hakuipata sehemu muafaka ya kuweza kumruhusu kuingia katika nyumba ile. Ukuta
ulikuwa imara na mrefu sana, kiasi kwamba Daniel Mwaseba pamoja na ujasiri wake
wote lakini hakuona namna ya kuweza kuupanda ukuta ule. Daniel Mwaseba alikaa
chini na kutafakari, akaona bora arejee wakati mwengine ili aweze kuvamia kambi
ile na kuumaliza kabisa mchezo unaofanywa na watu wale. Daniel Mwaseba alirejea
mjini kwenda kujipanga vizuri tayari kwa kuja kuifanya shughuli mzito
atakaporejea tena. Kule ndani kiongozi wa kundi la Six killers, Don Genge
alikuwa anamuuliza maswali Tano, na Tano aliyajibu maswali yote kwa ufasaha na
umakini mkubwa. Kwa jinsi Tano alivyowasimulia jinsi alivyotoka katika mdomo wa
mamba watu wote walibaki midomo wazi. Walimpongeza Tano kwa ushujaa wake. Pamoja
na kumsifia sana Tano lakini taarifa za kuwepo kwa Daniel Mwaseba katika mji wa
Kilwa Masoko zilomstua kila mmoja mle ndani. Katika watu waliokuwemo mle ndani
hakuna aliyekuwa haijui habari ya Daniel Mwaseba. Walikumbuka vizuri sana jinsi
alivyoangamiza na kuteketeza mpango hatari wa angamizo katika mji wa Iringa.
Wahenga walisema subira yavuta heri, na kweli. Saa sita ya usiku alimshuhudia
yule jamaa akitoka kwenye mikoko alipojificha. Masaa yote matatu aliyokuwa
anayatumia kujiburuza kuelekea porini ngome, Daniel Mwaseba alikuwa nyuma yake.
Tano alikuwa kachoka sana, mchoko ulioambatana na maumivu kila sehemu ya mwili
wake. Alikuwa anajiburuza kwa shida sana! Daniel Mwaseba alihakikisha hatoi
ukelele wowote ule wa kuweza kumsitua yule jamaa. Ilikuwa ni mwendo wa
kimyakimya. Porini ilikuwa giza sana, lakini kwa mara nyingine tena Dokta Yusha
aliuona umahiri wa yule jamaa aliyekwenda kwa jina la Tano, pamoja na kuwa
nyang'anyang'a lakini jamaa alichanja mbuga, na kufika kambini kwao. Daniel
Mwaseba kwa macho yake mawili aliushuhudia ukuta mkubwa sana uliojengwa kule
porini. Kimoyomoyo alitabasamu, akijua pale ndipo maficho ya wale watu wabaya.
Sehemu sahihi aliyokuwa anatamani kuijua, na sasa aliijua. Alimshuhudia yule
jamaa akihangaika kubonyeza kitufe fulani pale mlango, na baada ya dakika kama
tano geti lilifunguliwa. Na yule jamaa aliingia ndani ya ule ukuta kwa mwendo
wake uleule wa kujiburuza, kisha geti lilifungwa tena. Daniel Mwaseba
aliyashuhudia yote hayo akiwa kajibanza nyuma ya mti mmoja. Ndani ya nyumba
kundi la Six killers lilikuwa katika mshangao. Walishangaa Tano kurejea tena
kambini. Kila mmoja alikuwa na swali lake la kumuuliza Tano, mtu aliyerudi
kimaajabu sana kambini, akiwa na vidonda kadhaa mwilini mwake, lakini hawakuweza
kumuuliza chochote. Ruhusa ya kuuliza maswali alikuwa nayo kiongozi wa kundi
lile pekee, Don Genge. Huko mkoani Mtwara katika hospitali ya misheni ya Ndanda,
hali za wagonjwa wa Dokta Yusha zilikuwa kidogo zinaendelea vizuri. Angalau
Nasra Mpaukha, mke wa Dokta Yusha na Hasina Omary, mpambe wa Bi harusi na rafiki
kipenzi wa Nasra sasa hali zao zilikuwa zinaleta matumaini. Kwa upande wa Nasra
sasa alikuwa anaweza kupumua mwenyewe bila ya msaada wa mashine. Sasa alikuwa
anaweza kuongea kwa kupapasia ingawa hakuwa na kumbukumbu yoyote ya mambo
yaliyotokea nyuma. Hali ya Hasina ilikuwa mzuri zaidi. Alikuwa anakula na
kuongea kama kawaida na kidogo alianza kurejewa na kumbukumbu ya yaliyotokea
nyuma. Kutengamaa kwa hali za watu hao wawili zilimtia faraja sana Dokta Yusha,
maana aliona dhamira yake ya kwenda Kilwa, kuwakomboa watu wa Kilwa juu ya
sakata lile la kutisha ilikuwa inaelekea kutimia, tena matumaini yaliongezeka
siku baada ya siku. Dokta Yusha aliendelea kukaa hospitalini Ndanda, kuziangalia
hali za wagonjwa wake kwa siku tatu zaidi. Siku ya nne Dokta Yusha alikuwa ndani
ya basi la Nsungia akielekea Kilwa Kivinje. Aliamua kwenda kuanzia kilwa Kivinje
akiamini ndipo mahali sahihi lilipoanzia suala hili na ndipo ataenda kulimaliza.
Gari lilipofika Kilwa Kivinje. Dokta Yusha alikuwa abiria wa wa tatu kushuka
katika basi la Nsungia. Moja kwa moja alianza kutafuta nyumba za mahasimu wake.
Saa nane mchana ilimkuta Dokta yule kijana, Dokta Yusha akigonga bila wasiwasi
wowote katika mlango wa nyumba ya dokta katiri wa kike, Dokta Sharifa Juma.
Dokta Yusha aligonga hodi mara tatu mlango wa Dokta Sharifa Juma, alisimama
kidogo baada ya kugonga ile mara ya tatu akisikilizia ndipo alisikia kelele za
miguu ya mtu ikielekea pale mlangoni ishara kuwa kuna mtu alikuwa anaenda
kufungua ule mlango. Dokta Yusha alijipanga vizuri pale mlangoni, tayari kwa
lolote kitakachotokea pale mlangoni. Mlango ulifunguliwa, msichana mmoja mdogo
mwenye umri kati ya miaka kumi na sita na kumi na nane ndio alienda kufungua ule
mlango. "Shikamoo kaka" Yule msichana alimsalimia Dokta Yusha pale mlangoni.
"Marhaba hujambo binti" Dokta Yusha aliitikia ile salamu huku macho yake
yakiangalia moja kwa moja hadi ndani ya nyumba ile. "Sijambo kaka" Msichana
aliitikia kwa sauti yake ya upole. "Dokta Sharifa nimemkuta?" Dokta Yusha
alitupa karata yake kwa kumuulizia adui yake. Alijitahidi kuuliza kwa sauti ya
kawaida kuficha hasira zake kwa Dokta huyo. "Hapana, dada hayupo" Yule msichana
alijibu. "Kaenda wapi?" Dokta Yusha aliendelea kumuhoji yule dada. "Dada siku ya
tatu leo hajarejea nyumbani, na simu yake haipatikani sijui hata yuko wapi?"
Yule msichana alielezea kwa kirefu. Dokta Yusha akajua mambo sasa yameiva. Kwa
vyovyote Dokta Sharifa na wanaharam wenzie watakuwa sehemu fulani, wakiwa
wanapanga mambo yao, na pengine kuamua kuzima simu kabisa ili kupunguza bugdha
toka kwa watu. Dokta Yusha aliwaza hayo kwa haraka kichwani mwake, huku mdomoni
mwake akitoa jibu. "Sawa binti" "Akija dada nimwambie alikuja nani?" Msichana
yule aliyeonesha dalili ya uwerevu mkubwa aliuliza. "Mwambie alikuja Dokta
makini, Dokta mwadilifu, Dokta mchapakazi, utakumbuka hilo jina?" "Ndo jina lako
hilo? Nitalikumbuka" Msichana alisema huku akitabasamu. Dokta Yusha alimuaga
yule msichana mwerevu anayefanya kazi kwa Dokta katili sana na kuondoka zake.
Sasa alielekea nyumbani kwa Dokta mwengine katili, Dokta Zaidi Kilumba. Huko
alikutana na kijana wa kiume mlangoni. Mdogo wake na Dokta Zaidi Kilumba, naye
alimpa taarifa zilezile kama alizozipata nyumbani kwa Dokta Sharifa Juma, habari
za kutoonekana Dokta Zaidi Kilumba nyumbani kwake kwa siku tatu. Kengele ya
hatari ikagonga kichwani kwa Dokta Yusha. Iweje dokta Zaidi Kilumba na Dokta
Sharifa Juma wote wasirejee nyumbani kwao kwa siku tatu? Kuna nini
kinachoendelea. Dokta Yusha alitamani apafahamu kule katika kambi ya mateso
alikopelekwa kabla, lakini hakuwa anajua kabisa njia ya kumfikisha kule. Dokta
Yusha aliamua kutembelea katika nyumba za wale manesi watano waliokuwemo katika
mpango huu hatari. Aliowaona siku ile na aliwakumbuka vizuri sana. Ingawa kwa
shida lakini alizipata nyumba zao kwa kuulizia kwa watu, nako ujumbe ulikuwa
uleule. Wahusika wote wa mauaji yale ya kikatili walitoweka majumbani mwao kwa
takribani siku tatu. Dokta Yusha aliamua kwenda Kilwa Masoko alihisi labda huko
atapata kitu cha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kumsaidia kujua chochote juu ya sakata hili hatari. Siku hiyo usiku ulivyoingia ndio Daniel Mwaseba alikuwa anarejea tena kule porini, Ngome. Kuona jinsi ya kulisambaratisha kundi hatari la Six Killers. Mchana wa siku ile alienda katika kituo cha polisi Masoko na kupewa baadhi ya vitu akivyovihitaji, ikiwemo na pikipiki kwa ajili ya kumfikisha kule porini. Sasa Daniel Mwaseba akiwa katika chumba chake katika hoteli ya Kimbilio, alivaa suruali nyeusi aina ya jeans pamoja na T-shirt nyeusi yenye matirio ya mpira iliyombana vizuri katika mwili wake. Chini alivaa raba nyeusi vyepesi maalum kwa ajili ya mapambano. Upande wa kulia na wa kushoto kiunoni mwake alikuwa na bastola, moja kila upande. Huku mgongoni akiwa na begi dogo jeusi alimoweka kamba pamoja na zana zingine kwa ajili ya kwenda kukamilisha kazi yake hii hatari. Nyuma ya pikipiki lake aina ya Kawasaki ambalo lilikuwa linamsubiri kwa nje aliweka chuma kikubwa na kizito maarufu kama nanga pamoja na kama ngumu ya mwani. Saa sita ya usiku aliwasha pikipiki yake kwa mwendo wa taratibu na kuelekea porini ngome. Alipofika karibu na ile nyumba Daniel Mwaseba aliipaki pikipiki yake pembeni mbali kidogo na lile eneo la kambi ya kundi la Six Killers. Akihofia kelele za pikipiki yake kuwastua watu waliokuwepo ndani ya kambi ile hatari. Daniel Mwaseba aliifungua ile nanga nyuma ya pikipiki yake. Aliibeba ile nanga hadi pembezoni mwa ukuta mrefu wa kambi ile. Daniel Mwaseba akafikiria namna sahihi ya kuingia mle ndani kwa kutumia ile nanga, lakini aliikosa, alichokuwa anafikiria kuja kukifanya na ile nanga ilikuwa sivyo. Daniel Mwaseba alipiga mahesabu yake vibaya. Akaiacha ile nanga pale chini. Akaamua kupiga hatua za kimyakimya kwenda katika geti la mlango ule. Alihisi labda hapo nd'o patakuwa sehemu sahihi patapomuwezesha kuingia ndani ya kambi ile hatari. Alichunguza kwa makini kama dakika kumi pale getini ili kupata namna ya kuingia mle ndani, lakini bado hakupata sehemu sahihi ya kuingia mle ndani. Six Killers walikuwa wamejipanga vizuri sana kiulinzi na usalama. Daniel Mwaseba aliamua kurejea tena upande wa kushoto alikoiacha ile nanga yake. Alifika hadi pale alipoiacha ile nanga, akaipita tu kama hajaiona na kuelekea mbele zaidi. Alitembea hafi akafika nusu ili aumalize ule ukuta. Aliangalia pembeni, akauona mti mrefu pembezoni zaidi ya ule ukuta. Akili za Daniel Mwaseba zikafanya kazi kwa kasi ya haraka. Mithili ya nyani aliupanda ule mti hadi juu. Kwa kutumia taa zao zenye mwanga hafifu sasa alishuhudia ramani nzima ya ile kambi. Kwa kutumia macho yake Daniel alipima umbali toka pale kwenye mti alikokuwepo hadi kwenye ule ukuta. Ulikuwa umbali mkubwa, lakini aliona inawezekana. Daniel Mwaseba alipitisha uamuzi wa kujirusha toka kule mtini ili adondokee mle ndani.

Kwa kutumia macho
yake Daniel alipima umbali toka pale kwenye mti alikokuwepo hadi kwenye ule
ukuta. Ulikuwa umbali mkubwa, lakini aliona inawezekana. Daniel Mwaseba
alipitisha uamuzi wa kujirusha toka kule mtini ili adondokee mle ndani. Haikuwa
kazi rahisi kama unavyoweza kufikiria. Ilikuwa kazi ngumu sana inayohitaji mtu
wa kufanya hivyo awe na roho ya kijasiri, roho ya kikomando, roho ya paka!
Ambayo bila shaka Daniel Mwaseba alikuwa na roho ngumu zaidi ya hizo. Daniel
Mwaseba alijirusha bwana toka kule mtini. Alielea hewani mithili ya samaki
mkizi. Alipofika ndani ya ile kambi, Daniel Mwaseba alipata maumivu ya mguu
kutokana na umbali ule mrefu aliojirusha. Daniel alisimama kivivu, alijinyoosha
kidogo viungo vyake ili kujiweka sawa. Kabla hajafikiria chochote cha kufanya
alisikia sauti ya ukelele wa miguu kuelekea pale alipokuwa. Ishara kwamba kuna
mtu alikuwa anaelekea pale alipokuwa. Daniel Mwaseba alijibana ukutani
akisaidiwa kwa kiasi kikubwa na giza la usiku. Huku akizishukuru taa za mle
ndani kwa kutoa mwanga hafifu. Akatulia kidogo, akaangaza huku na huko Alikiona!
Daniel Mwaseba alikiona Kivuli cha mtu kikielekea pale alipoangukia awali,
akajua bila shaka alikuwa amesikia kishindo chake kile cha kuchumpa. Daniel
Mwaseba akasimama imara, akijua muda muafaka wa kupambana umefika. Yule jamaa,
ambaye alikuwa Mbili wa Six Killers alisimama pale alipoangukia awali Daniel
Mwaseba, huku akiwa kampa kisogo Daniel. Daniel Mwaseba akaona ile ndio nafasi
pekee ya kuitumia. Alimsogelea Mbili kwa mwendo wa taratibu sana, mwendo wa
kunyata, hakuruhusu kelele yoyote katika msogeo wake, alimkaribia sana Mbili.
Mbili alikuwa kasimama vilevile. Daniel Mwaseba alikunja ngumi, akaurudisha
nyuma mkono wake, mkono ule ambao alikuwa amekunja ngumi aliuleta mbele kwa
nguvu sana, usawa wa uti wa mgongo wa Mbili wa Six Killers. Daniel Mwaseba
alivyotegemea haikuwa hivyo. Ule mkono uliokunjwa ngumi ulikosa wa kumpiga.
Mbili pale aliposimama, ingawa alimpa kisogo Daniel Mwaseba lakini alikuwa
anahisi kila kitu kilichokuwa kinatokea nyuma yake. Kumbuka vijana hawa walikuwa
ni nusu makomandoo, makatili na wanaoweza kucheza na hisia. Ingawa Daniel
Mwaseba hakutoa ukelele wowote ule wa kuweza kumstua mtu hadi anafika pale,
lakini Mbili wa Six Killers alikuwa anasikia makelele makubwa sana, ndio alikuwa
anapigiwa makelele hisiani. Na ile ngumi ya nguvu toka kwa Daniel Mwaseba kwenda
katika uti wake wa mgongo alikuwa ameshaihisi tangu inakunjwa hadi wakati
inarushwa. Kazi ya Mbili ilikuwa ndogo sana, kuruka mbele kwa haraka kwa mtindo
wa sambasoti na alipotua chini walikuwa wanaangaliana na Daniel Mwaseba uso kwa
uso! Balaa! Daniel Mwaseba alistaajabu sana umahiri mkubwa uliooneshwa na yule
jamaa. Lakini alishangaa kwa sekunde i mbili ilipotimia sekunde ya tatu naye
akajipanga vyema, akajua anapambana na mtu asiye wa kawaida. Daniel Mwaseba
alijirusha juu huku mguu wake wa kulia ukitangulia mbele kuelekea katika kifua
cha yule jamaa. Mbili sasa alikuwa amejipanga vizuri, alirudi nyuma kidogo na
kubonyea kwa chini, Daniel alipitiliza jumla na kudondoka vibaya sana baada ya
teke lake kukosa wa kumpiga. Daniel alinyanyuka kwa kusuasua huku yule jamaa
akiwa anamcheka kwa kebehi na dharau. Daniel Mwaseba alijipanga tena, safari hii
akiwa makini zaidi alishachoka dharau za yule jamaa. Lakini kwa bahati mbaya
kabisa hakufanikiwa kufanya alichotaka kukifanya! Ghafla! Taa zenye mwanga mkali
ziliwashwa na uwanja mzima ulikuwa na nuru mithili ya mchana! Balaa Baada ule
mwanga mkali wa taa. Ulioleta nuru mahali pote pale, vikafata vicheko vya karaha
toka mahali ambako Daniel Mwaseba hakuwa anapajua, yeye alisikia sauti tu.
Lakini Mbili wa Six Killers alipatambua vizuri sana mahali ambako vikipotokea
vicheko hivyo. Wakati Daniel Mwaseba akishangaashangaa kutafuta mahali sahihi
vikipotoka vicheko hivyo mara mlango mkubwa wa nyumba iliyokuwa mbele yake
ulifunguliwa. Walitoka watu watatu walioshiba. Miili imara iliyojengeka vizuri
kimazoezi. Vifua wazi huku wakiwa wamevaa pensi za kijeshi zilizo katika mtindo
wa timberland, na T-shirt nyeusi za mpira zilizowabana vyema. Jamaa walimsogelea
Daniel Mwaseba kwa mwendo wa taratibu huku Daniel nae akijihadhari kwa kusogea
nyuma, kinyumenyume. Kwa kasi ya haraka Daniel Mwaseba alichomoa bastola yake
iliyokuwa upande wa kulia wa kiuno chake. Akawa anawaelekezea wale jamaa kwa
zamu, mara kamuelekezea yule jamaa akiyepambana nae kabla, mara akiwaelekezea
wale majamaa watu waliokuwa wanamfata. Wale majamaa hawakujari,
walikuwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wanamsogelea tu Daniel Mwaseba bila uwoga wowote ule. Daniel alirudi nyuma mpaka aliufukia ukuta, akauegemea ukuta huku bastola yake akiwa kaielekeza mbele. Bila kusita wale majamaa watatu walikuwa bado wanamsogelea, bila kusema neno lolote lile. Ilikuwa kama hawaioni ile bastola aliyoishika Daniel Mwaseba. Au labda walikuwa wanaona Daniel Mwaseba kashika kijiti tu kidogo. Hali ilikuwa ya hatari sasa! Jamaa walisogea hadi wakafika pale ukutani, alipokuwa Daniel Mwaseba. Daniel hakutaka kupiga risasi alijua madhara ya kurusha risasi kwa watu ambao asiowajua wamejipanga vipi. Maana kujiamini kwao ilimaanisha wamejipanga vizuri kwa hali ile. Ilibidi asubiri aone watu wale wana nia gani huku akitafuta mpenyo wa kujitoa katika kisanga kile kibaya. "Karibu sana kwenye nyumba ya kifo mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba!" Jamaa mmoja kati ya wale watu watatu waliokuwa wanatoka kule katika mlango wa ile nyumba ndogo alisema kwa nyodo na dharau kubwa sana. Daniel Mwaseba hakujibu kitu chochote alikaa kimya huku akitafuta mbinu ya kutoka salama mahali pale, alitafuta kwa haraka namna ya kujiokoa sehemu ile ya hatari, lakini hakuipata! Ghafla jamaa wale, wote watatu kwa pamoja waliruka juu na huku wakitanguliza mguu wa kulia mbele. Yalikuwa mateke matatu kwa mpigo! Yaliyorushwa kwa ufundi mkubwa sana. Mateke matatu yenye uzito tofauti toka kwa watu watatu tofauti yalitua katika kifua cha mtu mmoja, Daniel Mwaseba. Nguvu ya mateke yale yalimsukuma kwa nguvu Daniel Mwaseba katika ukuta na alijibamiza vibaya sana ukutani! Alisota katika ule ukuta na kudondoka chini taratibu. Kabla hajainuka wale majamaa watatu walisogea kwa kasi pale alipokuwa amedondokea Daniel Mwaseba. Jamaa aliyekuwa amesimama upande wa kulia alirusha teke lengine kwa mguu wake wa kulia, na yule aliyekuwa amesimama upande wa kushoto nae alirusha teke kwa mguu wake wa kushoto, wakati yule wa kati alikuwa amesimama tu akiangalia ujuzi wa wale wenzake. Mashavu yote mawili ya Daniel Mwaseba yalikutana na shurba. Mateke yote mawili yale yalitua katika mashavu ya Daniel Mwaseba. Damu ziliruka toka katika mdomo wa Daniel Mwaseba. Daniel sasa aliona hakuna tofauti, kufa na kuishi vyote ni sawa, akiwa amelegea kidogo kutokana na mapigo ya wale jamaa aliinyanyua bastola yake tayari kwa kufyatua. Alimuelekeza yule mtu aliyesimama katikati ya wenzake, hakuwa na mzaha sasa Daniel, macho yake yalionesha hivyo. Alikuwa tayari kwa lolote! Kwa bahati mbaya kabisa hakuwahi kufanya alichokuwa anataka kukifanya. Yule jamaa aliyekuwa kati aliufyatua mguu wake kwa kasi ya haraka sana na kuupiga ule mkono wa Daniel Mwaseba ulioshika bastola. Kwa macho yake yote mawili Daniel Mwaseba aliishuhudia bastola yake ikiruka angani na kutua katika mikono ya yule jamaa wa kati. E bwanaa wee! Sasa Daniel aliona muda wake wa kuuwawa umefika, ujanja wake umefikia kikomo. Kwa sasa amepatikana! Alikuwa ameingia sehemu hatari sana, zaidi ya hatari yenyewe. Aliwaza hayo, halafu akabadirika, alikuwa anawaza mawazo hasi, yeye alikuwa mti makini sana. Akaitupa kule dhamira ya kushindwa. Siku zote yeye alikuwa ni mshindi! Daniel Mwaseba, alizungusha macho yake kuwaangalia watu wale watatu waliogeuka kama watoa roho kwake. Jamaa wale wawili wakawa wanamwangalia yule jamaa wa katikati aliyekuwa ameishika bastola ya Daniel Mwaseba, imara kwa mkono wa kiume. Daniel akaona ile ndio nafasi pekee ya kuitumia, nafasi ya hatari sana, lakini ilibaki ile tu. Angafanya nini, Daniel Mwaseba alinyanyuka pale chini kwa haraka, asalalee! hakuwahi kufanya hata chembe alichotaka kufanya! Ngumi ya nguvu toka kwa yule jamaa aliyekaa upande wa kulia ilitua katikati ya mwamba wake wa pua. Ngumi iliyompata sawia. Daniel alikaa tena chini bila kupenda. Damu sasa zikiwa zinachuruzika mithili ya bomba kutoka kwenye pua. Jamaa alikuwa anaangalia kwengine lakini aliuona ujanja ukiotaka kufanywa na Daniel Mwaseba. Daniel akajua sasa amepatikana, wale majamaa hawakutaka kumpa nafasi yoyote ile ili afanye anachotaka kufanya. Walikuwa wepesi mithili ya umeme. Pale chini alishika tshirt yake na kuipangusa ile damu iliyokuwa inamtoka puani. Majamaa watatu walimwangalia Daniel Mwaseba kwa tuo, halafu kwa pamoja wote waligeuka nyuma. Katika mlango uleule waliotokea wao kuna mtu mwengine alikuwa anatoka. Daniel Mwaseba nae aliacha kujifuta damu na kumwangalia mtu huyo aliyekuwa anaenda mahali pale. Jamaa alisogea kwa hatua za taratibu huku akinesa kwa madaha mpaka pale walipokuwa wamesimama wale majamaa watatu. Mgeni huyu mpya, mtembea kwa mdenguo. Kwa majina alikuwa anaitwa Don Genge. Mkuu wa vijana wale. Mtu katili kabisa kuwahi kutokea duniani. Na kwa bahati mbaya alikuwa anawaongoza vijana makatili sana! Yule jamaa aliyepambana mwanzo na Daniel Mwaseba nae alisogea pale walipo wale wenzie, sasa walikuwa wanne na Don Genge watano. Macho kumi ya watu makatili yalikuwa yanamwangalia Daniel Mwaseba. Naam! Macho kumi toka kwa watu watano. Daniel Mwaseba alikuwa pale chini akipiga hesabu zake, akitafuta namna ya kujitoa pale lakini hakuona namna yoyote ile. Ama kwa hakika Daniel Mwaseba alikuwa amepatikana. "Hahaha Daniel Mwaseba, una bahati mbaya sana. Umejiingiza mwenyewe katika mdomo wa mamba. Umekifata kifo chako hapa! Huwezi toka salama mahali hapa, tunakuuwa Daniel na tunakutoa moyo!" Don Genge alisema kwa kujigamba sana. Daniel Mwaseba hakujibu kitu, alikuwa anawaangalia tu kwa zamu watu wale watano. "Daniel Mwaseba,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mpelelezi mahiri nchini Tanzania..." Sauti kutoka kule mlangoni ilisikika. Nayo ikitaja jina la Daniel. Daniel Mwaseba alinyanyua sura yake na kumwangalia mtu aliyotoa kauli hiyo, alimtambua vizuri sana. Alikuwa ni yule jamaa aliyepambana nae kule Kimbilio lodge, yule jamaa aliyejirusha katika gari la polisi likiwa katika mwendo mkali. Mhalifu mwenye roho ngumu ya paka! Alikuwa anaitwa Tano! Sasa kundi zima la Six killers lilitimia. Alikuwepo Moja, Mbili, Tatu, Nne, Tano na kiongozi wao Don Genge. Kiukweli Daniel Mwaseba alikuwa katika balaa kubwa sana! "Hahaha eti mpelelezi mahiri nchini Tanzania, mpelelezi mahiri anaingia kichwakichwa kwenye moto namna hii. Ulikuwa unajiona makini sana Daniel Mwaseba, eti Taifa la Tanzania linakutegemea hahaha, Tano ni mahiri zaidi yako. Kwa taarifa yako alikuwa anakuona ulivyokuwa unamfata. Huwezi kumfikia Tano wewe kiakili hata siku moja. Tumekushudia jinsi ulivyojirusha toka mtini. Huna akili za kutuzidi Six killers, huna hata kidogo" Don Genge aliongea kwa kujigamba na kumsifu kijana wake Tano. Daniel Mwaseba aliwaangalia wale watu makatili sana. Aliudhika pia na majigambo yao, lakini kimoyomoyo Daniel Mwaseba alijisemea. 'Mtajuta' "Tummalize sahivi Bosi, tusimcheleweshe" Moja alishauri. "Hatuwezi kumuua haraka namna hiyo Moja, lazima afe kwa mateso makali sana!" Don Genge aliyasema maneno hayo huku akiachia teke kali lililonasa vizuri katika shavu la Daniel Mwaseba. Damu ziliruka hovyo! Daniel alipata maumivu makali sana, lakini hakutaka kuonesha mbele ya maadui zake. Alijikomaza na kwa bahati nzuri Daniel Mwaseba alikuwa mwalimu katika fani ya kuvumilia maumivu.

Huko katika
mji mdogo wa Kilwa Masoko usiku uleule ambao Daniel Mwaseba alikuwa anapata
mateso makali sana kwa vipigo toka katika kundi hatari la Six killers, Dokta
kijana, Dokta makini, Dokta mzalendo, Dokta Yusha alikuwa ameshahaha vya kutosha
katika mitaa yote ya mji wa Kilwa Masoko kuwatafuta madaktari wale hatari kwa
Taifa. Alijaribu kuwatafuta mahali mote ambako alikuwa anaamini wale madaktari
makatili wanaweza kuweka maskani yao bila mafanikio yoyote. Tangu jioni ya siku
ile alipotoka tu Kilwa Kivinje alianza kuwasaka, jioni ilipita bure na sasa
usiku wa manane Dokta Yusha alikuwa bado anahaha. Alipita karika baa zote za
Kilwa Masoko. Baa zilizokuwa hadharani na baa za vichororoni. Alijaribu pia
kupita nje ya nyumba za kulala na kujaribu angalau kuwaulizia watu aliowakuta
nje. Lakini hakupata fununu zozote za maana. Pamoja na hayo yote lakini Dokta
Yusha hakutaka kabisa kuchoka ama kukata tamaa wakati akijua fika kwamba kuna
watu walikuwa wanateseka mahali flani. Funguo pekee ya kufika huko ni kuwapata
wale madaktari makatili watakaomfikisha kule porini. Alitafuta sana, baadae
aliamua kwenda kulala katika nyumba yake ya kulala wageni aliyofikia.
Ndio....Alienda kulala katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi. Dokta Yusha
aliingia chumbani kwake na kujitupa kitandani bila kufanya chochote. Hakuoga,
hakubadili nguo wala kufunga mlango. Alilala chali kitandani huku usingizi ukiwa
umempaa kabisa, alikuwa akiwaza na kuwazua nini cha kufanya. Baada kama ya
dakika kumi za kutafakari Dokta Yusha aliamka. Aliona ule sio muda muafaka wa
kulala. Dokta Yusha aliinuka pale kitandani na kuingia tena mtaani. Safari hii
alikumbuka kufunga mlango. Alitoka nje ya nyumba ile ya kulala wageni. Hatua
kumi na saba tu toka nje ya nyumba ile ya kulala wageni ya Mikumi, Dokta Yusha
alikutana na kitu kilichomshangaza sana. Dokta Yusha alipigwa na mshangao mkuu.
Dokta Yusha alikutana uso kwa uso na Mwanasheria. Mlevi wa ajabu sana kuwahi
kutokea ndani ya mji wa Kilwa Masoko na Tanzania kwa ujumla. Mlevi aliyehusika
mara kadhaa kuokoa maisha ya Dokta Yusha katika hali ya utani. Mlevi ambaye
mchana aliachwa katika hospitali ya misheni ya Ndanda, cha kushangaza sasa usiku
wa manane alikuwa katika mji wa Kilwa Masoko. Dokta Yusha alipatwa na mshangao
mkuu. Mwanasheria mbele ya macho yake, hakuamini kabisa. "Wewe Mwanasheria, upo
huku, umekuja saa ngapi, umewaacha na nani wagonjwa?" Dokta Yusha aliuliza
maswali mfululizo akiwa na wahka mkubwa.
Dokta
Yusha alipatwa na mshangao mkuu. Mwanasheria mbele ya macho yake, hakuamini
kabisa. "Wewe Mwanasheria, upo huku, umekuja saa ngapi, umewaacha na nani
wagonjwa?" Dokta Yusha aliuliza maswali mfululizo akiwa na wahka mkubwa. "Nipo
Dokta, tena jana na leo" pamoja na Dokta Yusha kuuliza maswali kwa hisia kubwa,
lakini Mwanasheria alitoa jibu la utani. "Mwanasheria!" Dokta Yusha aliita kwa
ghadhabu. "Rabeka Dokta" Aliitika. "Acha utani Mwanasheria, umekuja lini hapa,
sasa wagonjwa umewaacha na nani kule hospitali?" Dokta Yusha sasa aliuliza akiwa
ametulia kidogo. "Nimemwona Dokta Kilumba leo, tena sasahivi" Mwanasheria badala
ya kujibu maswali ya msingi ya Dokta Yusha, yeye aliongea kitu kipya kabisa.
"Dokta Kilumba? Umemwona wapi?" Dokta Yusha nae alipatwa na fadhaha kusikia
Mwanasheria ameonana na Dokta Kilumba. Miongoni mwa watu anaowatafuta kwa udi na
uvumba tangu alivyoingia Kilwa. "Nimemwona Dokta pale katika baa ya by night
bar" Mwanasheria alisema huku akiionesha baa hiyo iliko kwa kidole chake.
Haukuwa mbali sana na pale walikosimama, nyumba ya kulala wageni ya Mikumi hadi
katika baa ya Masoko by night. "Twende Mwanasheria, twende haraka" Dokta Yusha
alishauri kwa sauti yenye uharaka. "Usiwe na pupa Dokta, polepole ndio mwendo"
"Unajua sikuelewi Mwanasheria" "Utanielewa Dokta Yusha. Hatuna haja ya kwenda
pale na kumvamia, twende taratibu tujifiche sehemu na kuona uelekeo wake baada
ya kutoka pale" "Sawa Mwanasheria" Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi kwa mwendo
wa taratibu kama alivyoshauri Mwanasheria walienda katika baa ya by night, lengo
lao kuu ni kumuwinda Dokta zaidi Kilumba. Pamoja na ulevi wake uliotukuka lakini
Mwanasheria alionesha busara ya hali ya juu sana. Dokta Yusha aliushangaa sana
umakini wa Mwanasheria mlevi. Sasa Dokta Yusha nae alituliza mori, alipunguza
pupa na kuanza kuwa makini zaidi. Walitoka pale taratibu kuelekea katika baa ya
Masoko by Night. Giza la usiku ule liliwasaidia sana mashujaa wale wawili,
shujaa Dokta Yusha na shujaa Mwanasheria mlevi. Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi
walifika pembeni ya baa ya Masoko by night. Walijibanza pembeni katika kibanda
kidogo cha kuuzia vocha, kibanda kilichokuwa mbele ya duka kubwa la nguo na
vipodozi kuwahi kutokea ndani ya mji wa Kilwa, duka liitwalo Swanaha.com.
Kibanda walichojificha kilikuwa kinamilikiwa na mwanadada mjasiriamali ndani ya
mji wa Kilwa Masoko, alikuwa anaitwa Asma Twalibu. Kutoka pale katika kibanda
cha kuuzia vocha...Mwanasheria mlevi na Dokta Yusha walikuwa wanamshuhudia
vizuri sana Dokta Kilumba. Akiwa amekaa katika meza peke yake huku akinywa bia
baridi aina ya Safari bila wasiwasi wowote. Hakujua kabisa alikuwa karibu na
mtego. Karibu na hatari! Dokta Kilumba alikuwa anawindwa na wawindaji mahiri
sana. Kwa bahati nzuri siku hiyo kulikuwa na 'disco' ndani ya ukumbi wa Masoko
by night. 'Disco' ambalo lilikuwa na faida kubwa sana kwa Dokta Yusha na
Mwanasheria mlevi. Wingi wa vijana wacheza 'disco' waliozagaa pale nje
iliwafanya wasionekane na Dokta Zaidi Kilumba. Hadi kibanda cha vocha kinafungwa
Dokta Kilumba alikuwa bado anapata ulabu na kina Dokta Yusha wamejificha
palepale. Usiku mnene Dokta Kilumba aliinuka pale katika kile kiti chake
alichokalia. Alipepesuka kidogo kutokana na pombe, kisha akakaa sawa. Akapiga
hatua za taratibu kutoka katika uwanja wa baa ile. Alifanya yote hayo huku
akitazamwa kwa umakini na macho manne. Mhudumu wa baa ya Masoko by night
alimkimbilia Dokta Kilumba alitoka kule nje. Dokta Kilumba alikuwa anapepesukia
nje bila kulipa bia alizokunywa pale baa. Mhudumu alipomfikia na kumueleza,
Dokta Kilumba hakuwa mbishi. Alitia mkono mfukoni na kumlipa Mhudumu hela yake.
Baada ya kumlipa Mhudumu yule, Dokta Kilumba akapiga hatua zake za kilevi, huku
akiyumba, hatua za kilevi zilizomfikisha Dokta Kilumba hadi katika gari yake
ndogo, Toyota corolla. Kwa bahati mbaya kabisa, Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi
hawakuwa wamejiandaa kwa jambo hilo. Walitegemea Dokta Kilumba ataondoka kwa
miguu. Wao hawakuwa na usafiri wa aina yoyote ili kumfatilia Dokta Kilumba.
Wakiwa pale nyuma ya kibanda cha vocha walimshuhudia Dokta Kilumba akipanda gari
lake taratibu na kuiongoza gari yake upande wa bandarini (custom). Dokta Yusha
na Mwanasheria mlevi walibaki wakiikodolea macho ile gari aliyopanda Dokta
Kilumba ikishika kasi katika barabara ya lami. Kichwani mwa Dokta Yusha alikuwa
anawaza wafanye nini ile Dokta yule mwanaharamu asiwapotee katika upeo wa macho
yao. Alitafakari harakaharaka bila kupata jibu. Aliamua kushauriana na
Mwanasheria, Dokta Yusha alipoangalia pembeni pale alipokuwa Mwanasheria,
hakuwepo! Alikuwa amebaki peke yake amejibanza pale katika kibanda cha vocha.
Alipoangalia ile barabara alikoelekea Dokta Kilumba, kwa mbali, usawa wa baa ya
Makondeko alimuona Mwanasheria akiwa kwa juu ya pikipiki aina ya boxer akielekea
upande uleule alikoelekea Dokta Kilumba. Taa zilizokuwa zinawaka pale baa,
zilisaidia Dokta Yusha amtambue vizuri Mwanasheria mlevi. Alipigwa na butwaa!
Mwanasheria mlevi juu ya pikipiki? Dokta Yusha alipigwa na butwaa. Hakuelewa
kabisa Mwanasheria mlevi alikuwa ametoka saa ngapi pale nyuma ya kibanda cha
vocha walipokuwa wamejificha. Dokta Yusha pia alipigwa na butwaa, hakuwa
anaamini kabisa kama Mwanasheria mlevi angeweza kuendesha pikipiki. Tena kwa
kasi namna ile. Yalikuwa maajabu hasa! Aliwaza hayo kwa muda mfupi, Dokta Yusha
nae hakutaka kuzubaa, akajua kazi sasa imeiva, ni kuipakua tu. Alimuita dereva
pikipiki za
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kukodi harakaharaka, akapanda nyuma na kumuelekeza kwa kidole kuwa aifate pikipiki aliyokuwa anaendesha Mwanasheria mlevi. Sasa watu wawili wakiwa katika pikipiki mbili tofauti walikuwa wanamfukuzia mtu mmoja, Dokta Zaidi Kilumba. Safari ya Dokta Zaidi Kilumba iliishia katika nyumba ya kulala wageni ya Mjaka. Nyumba safi na ya kisasa ya wageni iliopo katika mtaa wa Tanesco. Dokta Kilumba aliingia ndani, na moja kwa moja alielekea chumbani kwake. Baada ya kubadili nguo na kuoga, dokta Zaidi Kilumba alilala, bila kujua hatari iliyokuwa inamfata nyuma yake. Mwanasheria mlevi nae alipaki nje ya nyumba ile ya kulala wageni, lengo la mwanasheria lilifanikiwa kwa asilimia mia moja, yeye alikuwa anataka kujua mahali anapoishi dokta yule kwa kipindi kile. Na alifanikiwa. Mwanasheria mlevi alitabasamu peke yake alivyokumbuka jinsi alivyoparamia pikipiki ya watu kule Masoko by night, baada ya mwenye pikipiki kuiacha ikiwa na funguo yake, sijui alijisahau ama alikusudia, Mwanasheria hakutaka kujua. Alifikiria pia jinsi mshangao atakaopata mwenye pikipiki, baada ya kurudi na kutoikuta pikipiki yake pale alipoiacha. "Kwa vyovyote atadhani kaibiwa, nitamrejeshea lakini" Mwanasheria akasema kwa sauti ndogo na kujijibu mwenyewe. Dakika mbili baadae pikipiki aliyopanda Dokta Yusha nayo iliwasili. Dokta Yusha alimlipa yule dereva pikipiki pesa yake. Baada ya dereva pikipiki kuondoka. Mwanasheria ndiye alikuwa wa kwanza kuiona pikipiki ile toka mahali alipokuwa, alifurahi alivyoona abiria wa pikipiki ile ni rafiki yake kipenzi, dokta Yusha. Alimfata dokta Yusha aliyekuwa anazubaazubaa tu. Baada ya kuonana. Walikumbatiana kwa furaha. "Kazi nzuri Mwanasheria" Dokta Yusha alimpongeza Mwanasheria. "Ndio majukumu yangu haya Dokta, usihofu" Mwanasheria mlevi nae alijibu kiuhakika. Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walijipanga kwa ajili ya uvamizi. "Sasa mwanasheria tutaingiaje hapa" Dokta Yusha aliuliza huku akimwangalia Mwanasheria mlevi usoni. "Hapa inabidi tujifanye Wateja, ndo njia pekee ya kuingia humu" Mwanasheria mlevi alijibu kwa kujiamini. "Halafu" Dokta Yusha aliuliza tena. "Tukishapewa chumba tutajua jinsi ya kufanya humohumo ndani" Mwanasheria alijibu. "Sawa Mwana" Dokta Yusha na Mwanasheria walienda mapokezi kwa lengo moja tu, la kupata chumba ili wawe karibu na Dokta Zaidi Kilumba. Walifika mapokezi, walikutana na mhudumi wa kike, aliwahudumia vizuri. Mwanasheria na Dokta Yusha wakakodi vyumba viwili. Chumba alichopewa Mwanasheria na chumba alichopewa Dokta Yusha vilikuwa vinaangaliana. Kila mmoja aliingia katika chumba chake. Baada ya kama dakika tatu Mwanasheria mlevi alitoka katika chumba chake ns kwenda kugonga katika mlango wa chumba cha Dokta Yusha. Dokta Yusha alienda kumfungulia, walikaa ndani na kuanza kupanga mambo yao. "Sasa tutajuaje chumba alichpanga yule mwanaharam?" Dokta Yusha aliuliza katika hali ya udadisi mkubwa. "Dokta Kilumba yupo chumba namba 8" Mwanasheria alijibu katika hali yake ileile ya kujiamini. "Umejuaje Mwanasheria kama Dokta Kilumba yuko chumba namba nane?" Dokta Yusha aliuliza huku akiwa amemkazia macho Mwanasheria mlevi. "Nilichungulia katika daftari pale mapokezi wakati tunaandikiashwa" Dokta Yusha sasa alitokea kumhusudu sana Mwanasheria mlevi. Hakukuwa na umbali mkubwa sana kati ya chumba namba nane alichokuwemo Dokta Kilumba na chumba namba kumi na tatu walipokuwepo watu hawa wawili, Mwanasheria mlevi na Dokta Yusha. Kulikuwa na tofauti ya vyumba kama vinne hivi ili kufika katika chumba alichokuwa amepanga Dokta Kilumba. "Tutaingiaje sasa chumbani kwake?" Dokta Yusha aliuliza huku akimwangalia Mwanasheria mlevi usoni. "Tutagonga tu mlango" Mwanasheria mlevi alimjibu Dokta Yusha kwa kifupi. "Je akiuliza nani anagonga akiwa bado hajafungua mlango?" Dokta Yusha aliuliza tena. "Tutasema Mhudumu" Mwanasheria mlevi alikuwa anajibu majibu mafupi huku akiwa na uhakika tele. "Ahaaa..poa twende tukajaribu" Dokta Yusha alikubaliana na Mwanasheria mlevi, bila ya kudadisi sana. Usiku uleule wa maneno Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walitoka katika, chumba namba kumi na tatu, walichopanga na kwenda chumba namba nane, chumba alichokuwa amepanga hasimu wao, adui yao, Dokta Kilumba. Kule ndani Dokta Kilumba baada ya kwenda kujimwagia maji, sasa alikuwa amekaa katika shuka nyeupe iliyokuwa imetandikwa juu ya kitanda kikubwa, ndani ya nyumba ile ya kulala wageni ya Mjaka. Dokta Kilumba alikuwa akisubiri ujio wa mgeni, mwanamke baamedi aliyekubaliana kwenda kustarehe nae alivyokuwa kule baa. Dokta Kilumba akiwa kule baa, alipatana kwa siri, kwenda kufanya mambo ya siri. Alikuwa Baamedi wa Masoko by night, aitwaye Glad na alikuwa amemuelekeza namba ya chumba alichofikia, pia alikuwa ameshampa hela ya usafiri wa kumfikisha pale, na sasa alikuwa anamsubiri tu ili aje kupewa huduma ya siri atakayoilipia. Dokta Kilumba hakutaka kufatana nae wala kukaa nae karibu Glad baamedi, alikuwa anaogopa kuchafua taswira yake ya heshima mbele jamii. Ingawa Alice alikuwa mwanamke mrembo sana, lakini kutokana na kazi aliyokuwa anaifanya (Ya ubaamedi) Dokta Kilumba aliiona kama kazi ya dharau, kazi ambayo yeye kama Dokta anayeheshiwa hakustahili kuambatana na mwanamke wa aina hiyo. Tena akielekea nae katika nyumba ya kulala wageni. "Ngongongo" Mara mlango wa chumba alichokuwa Dokta Kilumba uligongwa, na Dokta Kilumba bila kufikiria alinyanyuka pale kitandani kwa mbwembwe bila tahadhari yoyote na kwenda kuufungua ule mlango. Katika akili ya Dokta Kilumba alikuwa anajua yule mwanamke aliyeongea na kule baa, Glad baamedi, mwanamke aliyekubaliana nae kule katika baa ya Masoko by night ndiye alikuwa anagonga mlango muda ule. Dokta Kilumba aliusogelea ule mlango bila wasiwasi wowote. Akiwa amejifunga taulo jeupe safi kiunoni, huku juu akiwa kifua wazi. Alipofungua tu mlango alikutana na Balaa! Alipigwa na dhoruba kali sana. Alijikuta amesukumwa kwa nguvu na kifua cha kiume cha Dokta Yusha, msukumo ambao ulimrudisha ndani kwa kasi na kumdondosha chini moja kwa moja. Dokta Kilumba hakujiandaa kabisa na tukio lile, alitegemea kukutana na kukumbatiwa na kifua laini cha mrembo Glad, lakini kwa bahati mbaya kabisa alikutana na kitu tofauti, alikutana na kifua kigumu cha kiume, kifua cha Dokta Yusha. Baada ya anguko lililotokana na msukumo wa kifua cha dokta Yusha. Kwa mwendo wa taratibu dokta Yusha alimfata Dokta Kilumba pale chini. Wakati Dokta Yusha akimfata Dokta Kilumba pale chini, Mwanasheria mlevi alibaki pale mlangoni, alikuwa anafunga mlango wa chumba kile cha kulala wageni kwa ndani. Mambo yote hayo yalifanyika kwa muda mfupi sana, na kwa umakini mkubwa pia. Dokta Kilumba alibaki ametumbua macho pale chini, sakafuni. Kichwani mwake yalikuwa yanapita maswali mengi sana, bila ya kuwa na majibu. Ingawa Dokta Kilumba alikuwa anawafahamu vizuri watu wale wawili lakini Dokta Kilumba hakujua kabisa watu wale wametokea wapi baada ya kutoweka kwa muda mrefu, na wamekijua vipi chumba chake. Dokta Kilumba hakupata muda wa kutafakari zaidi, Kofi la nguvu la mkono wa kulia toka kwa Dokta Yusha lilitua katikati ya uso wa Dokta Kilumba. Dokta Kilumba aliona vimulimuli. Kilikuwa kitendo cha ghafla sana na Dokta Kilumba hakutegemea kabisa kufanyiwa vile na Dokta Yusha. Hali ilikuwa tete mle ndani kwa upande wa Dokta Kilumba. Vijana wale wawili makini walikuwa wamembana Dokta Kilumba kisawasawa. Mwanasheria mlevi nae alitoka pale mlangoni na kusogea pale walipokuwa Dokta Yusha na Dokta Kilumba. Siku hiyo Mwanasheria alikuwa hajatia hata tone moja la pombe, lakini mwendo wake ulikuwa wa kilevi. Sauti yake ilikuwa ya kilevi. Ama hakika Mwanasheria mlevi alikuwa ameathiriwa sana na pombe, pombe ilikuwa imeweka kambi ya kudumu katika mishipa yake ya damu. Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga mguu mwengine kule, alikuwa anayumba ndani ya chumba, alikuwa anakwenda mtindo wa zigzag, lakini Mwanasheria alifika alipopakusudia. Pale walipokuwa wale mahasimu wawili, Dokta Yusha na Dokta Kilumba.

ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment