Simulizi : Bonde La Mauti
Sehemu Ya Nne (4)
Ndege ya kisasa kabisa ilitua katika uwanja wa kimataifa jijini New York ikitokea katika nchi ya Braziri. Habiria walio fika siku hiyo walikuwa wengi mno ila kuna watu walioneka tofauti na wengine kuanzia mavazi hadi muonekano wao. Kila mahali waliko pita watu hawakuchoka kuwatazama muonekano wao.Ingawa si kawaida kwa nchi kama Marekani kumkuta mtu akishangaa shangaa ila kwa hili hakika lilioneka kushangaza mno. Huu ulikuwa ni ujio wa kikosi cha kwanza cha N003 kuingia kazini baada ya kutakiwa na jeshi la Wamarekani kusaidia kupambana na kikosi hatari cha Warusi walio kuwa wamewatia jampa jampa waamerika hasa upande wa anga. Kilicho wafanya watu washangae ujio wa watu hawa ni mavazi yao ya kazi ambayo walivaa viumbe hawa kwa hakika walionekana ni washari na hawana muzaha na mtu maana mwendo wao ulikuwa wa kikakamavu. Baada ya kukamilisha itifaki zote katika uwanja huo walitoka hadi nje ya uwanja wa ndege. Hapo waliweza kuzikuta gari za jeshi la marekani zikiwasubiri kwa hamu."N001 kagua gari hizo kabla ya kuzitumia" kifaa alicho kivaa N001 kilimpatia maelekezo pale alipo karibia gari moja wapo aina ya Hama. Uliunyoosha mkono wake na kulishika gari hilo kwa sekunde tano.... Komputa iliyokuwa imeunganishwa kwenye mkono wake iliyo kuwa na muundo wa saa iliandika ripoti nzima ya gari hilo. Baada ya kuwa ameingiza ripoti hiyo alituma matokeo kwa mkuu wake. "lipo salama pandeni muondoke lakini musisahau nilicho watuma" magari ya kijeshi yasiyo pungua matano yalianza safari huku gari lililo mbeba N001 na wenzake wawili likiwa katikati .Safari yao ambayo iliwachukua kutwa nzima hatimaye iliweza kutia nanga kwenye kambi Kubwa ya Navy USA. Iliyo kuwa pembezoni mwa bahari ya Pasifiki. Kama kawaida ya kambi kubwa za kimarekani pale pale kwenye kambi lazima kuna kuwa na huduma za kijamii kama ulaiani yaani pale pale kuna shule,hospitali,mahoteli na kadharika. Baada ya msafara huo kufika katika kambi hiyo waliongozwa na MP hadi katika ofisi ya sp Huyu ndiye msimamizi mkuu wa kikosi cha dharura katika uwanja wa kivita. "Karibuni sana vijana natumaini mmekuja kutimiza jukumu lenu tu katika eneo la hatari ambalo kwetu sisi tumeshidwa kulisogelea maana eneo hilo lina miseri hatari na ambazo zinajiendesha automatik. Mnaweza kuitaza kwa ukaribu video hii. " katika video hiyo. "20216 nazidiwa over naitaji kulidwa . 20216 naitaji msaada haraka adui anashambulia pande zote " hatimaye ndege hiyo ililipuka kabisa baada ya kuyumba na kukosa mwelekeo kwani ilishambuliwa na ndege bora iliyo jua kucheza na anga kwa usahii kabisa., VIDEO IKAZIMWA. "kama mlivyo ona hivyo ndivyo kulivyo chechenya. Askari wengi wamepotea na wengine kutekwa na kundi la kigahídi linalojita eagle fly .Kundi hili linatisha katika masuala ya anga maana hatukuwahi kuangusha hata ndege yao moja zaidi ya sisi kupoteza marubani na ndege. Kazi mtakayo ifanya ikiwa ya kwanza ni hii hapa" Alitumbukiza mkono kwenye koti na kutoa mchoro ulio kuwa ukionyesha mtambo mdogo wa kuongoze makombora ya masafa marefu ya nyukilia. Hakika macho yaliwatoka baada ya kuushuhudia mtambo huo adimu ukiwa mikonon mwa eagle fly. Kazi yao waliona imeanza kuwa nyepesi mno. "kama mlivyo ona picha ya mtambo huu unaitajika ikulu maana ni hatari kumilikiwa wa watu wasio na akili nzuri waweza kuangamiza ulimwengu mzima.kwa hiyo mnaweza kwenda katika kiwanda kilicho katika ili mjiandae na kazi iliyo mbele yangu kesho na mkajionee ndege mpya iliyo udwa na injinia wa anga ana ngozi kama yenu....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakika macho yetu yaliweza kuzitazama ndege za kisasa kabisa ambazo zilionyesha ubora wake hata kwa kuzitazama kwa nje. Hakika hapo ndipo niliweza kuona uhimara wa kikosi hiki cha NAVY maana kwa kawaida unaweza kinadili na meli ila si masuala ya vita vya maji tu na anga wapo vizuri. "Karibuni katika kitengo chetu cha dharura mi naitwa Meja Dori na mi ndo nahusika na masuala ya setlaiti na intanet katika kambi hii." Tulikaribishwa ndani zaidi kwenye chumba hiki chenye ndege hapo ndipo tuliweza kujione kompyuta kubwa na za kisasa zote zikiwa chini ya mwanadada Dori. Doli aliendele kubonyeza kompyuta zile huku akiwa makini zaidi. Nilipo zidi kumtazama niliweza kungundua anaweka program kwenye ndege hizi lakini mambo yalikuwa yamemwendea mrama. Nilimsogerea na kuanza kukagua jinsi anavyo sakinisha program kwa shida nikawa nimegundua kitu kwenye kompyuta yake yaani anacho fanya anaingiza program kwingine kabisa tofauti na alipo kusudia na ndio maana inakataa kusakinishwa kwa wepesi zaidi. Sikusema kitu maana ningeingilia yasiyo niusu. "Yaani hizi program zi nagoma kabisa kuingia kwenye mfumo wake maalum sijui kwanini?" Ali lalama Meja Doris baada ya kujaribu muda mrefu. Ilinibidi nitoke katika chumba hicho cha ndege za kisasa maana niliona pale kwenye kambi kuna wasaliti wengi na niligungua hilo baada ya kuona jinsi kulivyo na mtambo wa kudulufu mifumo ya kompyuta. Baada ya kufika nje ya chumba hiki moja kwa moja nilielekea kwenye chumba ambacho niliandaliwa ili nijipumzishe maana nilikuwa na uchovu wa wiki nzima. Nilipo fika katika chumba hicho nilikikagua kwa umakini ili kusiwe na kamera yeyote ya kunichunguza. Kwa macho sikuweza kugundua kitu cha hatari.Hapo ilinibidi niwashe kompyuta yangu yenye muundo wa saa.Hapa niliweza kugundua kuna vinasa sauti ambavyo vimetegeshwa chini ya kitanda. Sikudhubutu kuvigusa maana nilijua lazima watajaribu kutuchunguza kama ilivyo tabia yao ya kupeleleza mtu wanaye mtilia shaka. Hapo ilinibidi niwatumie ujumbe wenzangu wawe makini na watu hawa maana wanatuchunguza hili hali wametuitaji wao tuwasaidie. Ujumbe uliwafikia watu wangu kwa hiyo taarifa itabidi itumwe kwa ujumbe tu. Kutokana na uchovu nilio kuwa nao nilijitupa katika kitanda na kulala . Nikiwa katika usingizi mzito nilisafiri katika ndoto ya mapigano ambayo ilikuwa hivi. "Virusi mulivyo dugwa ni hatari mno hivyo itawabidi mfanye mazoezi ya kutosha ili muweze kujiongoza wenyewe na zoezi letu lianze na udunguaji wa masafa ya kati. Haya we N001 njoo uanze na hiyo sanamu ipasue kichwa." DR.ERICK aliendelea kutupa maelekezo ya kudungua umbali wa kati. Nili ibeba snahipa na kulala kifudifudi hapo nilihiweka kwenye tageti sanamu hiyo ya kufanyia mazoezi ya ulengaji.Nilibana pumzi kisha mawazo yote nikayaweka kwenye tageti yangu kisha nikabofya na kuvuta traiga risasi iliyo toka iliweza kukipasua kichwa cha sanamu hilo. Nilishutuka toka katika usingizi huku nikihema kwa kasi maana kila nikiota ndoto hizo najuta kuwa Mpelelezi najuta kuwa askari. Hapo nilinyanyuka na kuingia bafuni ili nioge niondoe uchovu.Baada ya kutoka kuoga nilizivaa nguo za kazi maana sikutamani kuishi katika kambi hii yenye waasi na wasio na shukrani. Baada ya kuwa tayari nilitoka katika chumba na kuelekea kwenye chumba chenye ndege ili niweke mfumo mwingine maana sikupenda kufuatiliwa nikiwa angani.,..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipofika kwenye chumba hiki cha kuopalait ndege na kuziingizia program nilimkuta bado meja Dori akiangaika kuweka program kwenye ndege hizi za kijeshi aina ya 5.su-35FLANKER FIGHT. Ndege hizi zina uwezo maalum wa kumtafuta adui umbali wa kilomita 400na kumshambulia Ndege hizi pia zina injini mbili pia zina uwezo wa kubeba silaha mbali mbali pia na maeneo kumi na nne yanayo fugwa siraha kwa ajili ya kushambulia.******[MENGINE UTAYAJUA KAMA UKIIFUATILIA RIWAYA HII HADI MWISHO MAANA NDEGE HIZI ZIMETENGENEZWA URUSI NA NI HATARI ]****** “pole sana meja kwa Meja kwa uchovu wa kucheza na mashine hizi maana tangu asubuhi unaangaika nazo.” **Nili vuta kiti kingine na kukaa karibu naye huku nikiendelea kumuangalia jinsi anavyo endelea kuangaikia program ambazo tayari wabaya wake wamesha mhaki yeye bila kujua .Aliendelea kucheza na kibodi bila kunisemesha kitu chochote maana alijiona anaelekea kumaliza kumbe sivyo kabisa wenzake wapo hatua mbili mbele yake.Na mimi sikutaka kumpa nafasi ya kuendelea kuwa bize ilinibidi kuchombeza tena neno litakalo mutoa kwenye mudi yake ya kuchanganyikiwa na kazi yake ya mtandao. “Meja mbona naweza kukusaidia kazi hii maana mimi nina uzoefu mkubwa kwenye mambo haya na hapo unapoangaika kuisakinisha program hii inaonwa n a maadui na ndiyo maana inakataa kusakinishwa kwenye ndege hizi.Hebu tazama mwenyewe hapa kuna kama computer zaidi ya moja ukiona kitu hiki ujue tayari kuna mvamivi kwenye mtandao wenu hebu itazame kwa makini program yenu ya ulinzi jinsi ilivyo liwa na virus nab ado hayo yoote ujayaona.mi nipo tayari kukusaidia tena bure bila malipo yoyote yale.” Baada ya kuwa nimemwambia mambo yote yale hatimae aliingia mwenyewe kwenye mtego ambao nilikuwa nimedhamilia aingie maana kati ya jkazi nilizo kuwa nimepewa na wakubwa wangu wa kazi ilikuwa imetia kwa asilimia mia bila serikali hii ya Marekani kushutukia mchezo wa BONDE LA MAUTI maana nilipaswa kunyonya msiri zote za kikosi cha NAVY na kuzituma kwenye kambi yetu ili ziweze kufanyiwa kazi inayotakiwa ikiwemo kuioongoza satlite yao kwa faida yetu. “Ni kweli kabisa naona kuna mtu anaingilia mawasilia yetu na inaonekana yupo hapa kwenye kambi hii ,atakuwa ni nani mtu huyu maana ana uzoefu kabisa wa kuibia siri zetu na tayari kaniaribia mfumo wangu wa ulinzi. Na wewe umejuaje mambo hayo na mbona umeingia kwenye mpango huu bila kualikwa maana ni hatari ukikutwa kwenye chumba hiki cha mawasiliano wakati huusiki na mbaya zaidi wewe ni askari wa kukodishwa maana huwa hatuwa amini kabisa katika mambo ya siri kama haya’’ “Kwanini usiniamini ili hali nimekuonyesha mwizi wako aliye kuchelewesha kwenye kazi hii. Na bado nitakusaidia kumkamata na si hayo tu nitakutengenezea ulinzi wa komputa yako ili kuzuia wote wanaoweza kuingilia mfumo huu.Huenda bado hujanijua vizuri nipe nafasi nikwambie mimi ni nani hasa kwenye kompyuta yako hiyo.” Nilitumia maneno ya ushawishi ili niweze kumteka akili yake maana nilikwisha kuona mambo yanaweza kuharibika kama nisipo kuwa makini na maneno yangu maana alionekana kunitilia mashaka . Baada ya kumshawishi kwa muda mrefu hatimaye alinipatia nafasi ya kumtafuta mtu anaye durufu komputa yake.Katika kukagua mtandao niliweza kugundua kwamba kuna mtu anarusha mawasiliano kwenda kwenye kambi ya FLY EAGLE iliyoko URUS hapo nilimuonyesha meja DORI kwamba program hizo si salama tena kwa ndege hizi maana adui amesha gundua udhaifu wetu wote kwenye teknologia hasa ya kompyuta maana anaweza kutudungu akitaka na muda wowote atakao. “Umeshuhudia mwenyewe jinsi mambo yalivyo. je unaweza kunambia mbinu gani ungetumia ili kuzuia huli lisitokee tena katika kambi yenu? .Usijari Meja wacha nikutengenezee program matata ya kuwafumua huko waliko na hawatarudia tena kuingilia mfumo wako huu na salamu zako watazipata huko waliko. “Mbona unanionyesha mambo mazito ambayo sikuwahi kufikilia kama yapo kwenye ulimwerngu huu wa teknologia ? utawafumuaje hili hali hakuna kikosi kilicho tumwa ? Sawa acha nione maajabu yako sasa yalivyo maana sikujua kama utayaweza mambo haya jinsi ulivyo hivyo.”
********************************************* ********************************************* *********************NDANI YA URUSI********************************
“Mkuu mtandao wetu umeanza kusumbua yaani hauleti mambo kama ilivyo kawaida maana naona kuna virusi vinavamia kompyuta zetu nani hatari maana tayari kompyuta tatu zimeliwa na kuzima imebaki masta kompyuta moja tu na watu walio haribu za kwanza ni wa kikosi cha NAVY “ “Nani kaharibu mfumo huu ?Nitamkata kichwa akipatikana na zimeni hiyo master computer mara moja isije ikharibibika “ Wakati wakiendelea na mchakato wa kuzima kompyuta yao hiyo walio kuwa wakiitegemea hapo ndipo uliskikka mlipuko mzito mno ndani ya chumba cha mitambo*****
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara ya mwisho tulikuwa kwenye kambi ya Urusi katika kambi ya EAGLES FLY katika kitengo cha computer system .Tuliona majanga waliyo yapata baada ya kujaribu kudurufu computer za NAVY. **************Baada ya mlipuko ulioiharibu computer yao kubwa kutokea jeshi hili la fly eagle lilibadilisha haraka had disk ya compute yao lakini na yenyewe walikuta tayari imeliwa na virus kwa hiyo hapo waliweza kutambua mtu wanaye pambana naye ni hatari . "Kuanzia sasa jiandaeni kuwapokea wageni wetu waalikwa maana muda si mrefu wanaingi katika anga letu jitahidini muwape ukarimu wa njungu Karanga na korosho msisahau na maboga ya kutosha pia mkumbuke ninahitaji mgeni mmoja habaki hapa maana nina zawadi yake nzuri ya kumpatia ambayo atawapelekea na wanafunzi wake." Aliongea jenerali wa kambi hiyo baada ya kushambulia katika mifumo yake ya computer . *******NDANI YA KAMBI YA NAVY *-********** Ndege za kisasa kabisa zilikuwa zikipakiwa kwenye meli kubwa ya kijeshi kwa ajili ya kusafirishwa na kusogezwa karibu kabisa na kambi ya maadui. "Hakikisha kikosi Chako kinarudi Salama maana kundi hili ni hatari katika masuala ya anga na ndiyo maana mmeitiwa kazi hii ya hatari kwa maana na nyinyi ni hatari kama nyinyi. Baada ya Saa moja mtaingia katika ndege zenu ili mhanze kibarua chenu lasmi kumbuka zipo kambi tatu kabla ya kuingia kwenye kambi kuu ya Fly eagle kwa hiyo mtapaswa kuziteketeza zote ili mweze kujilinda na kila kambi ina nddge zaidi ya hamsini kwa hiyo hangamiza ndege zote zitakazo wafuata." Moja Dori aliwapatia data zots za kambi ya eagle fly na kutoka katika chumba hicho cha mapailot wa kundi la hatari .
*---**-BAADA YA SAA MOJA KUPITA-**-*********** "Kuanzia sasa hakuna kurudi nyuma isipo kuwa kwa amri yangu tu.Kumbukeni hii ni vita na mweye nguvu lazima ashinde na kambi hizi zina taarifa ya ujio ujio wetu kaeni mkao mzuri." N001 alitoa maelekezo na ushaur kwa vijana wake alio fika nao kwenye kambi ya NAVY.. *****-KAMBI YA EAGLE FLY ******** "EAGLE 1 pokeeni wageni we nu wapo angani ." Ndege kumi zilinyanyuka kwa kasi ya ajabu mno na kwenda kuwapokea wageni wao . baada ya dakika kumi tayari walisha wasili Area 1898.9-8+75/ Long way .hakika halo ndipo walipoweza Kujua wageni wao walivyo wakarimu maana ndani ya sekunde kumi mtu ndege zao zilikuwa majivu. "Ndege zetu za utangulizi zimedondoka zote mkuu." GENERAL wakikosi cha eagle alitoa taarifa kwa mkuu wake . "Watumieni kunguru wa kutosha msiwasubirishe maana.watu hawa ni ni hatari mno kwetu.Kunguru weusi ni aina ya ndege ya kivita iliyo na kasi zaidi ambayo ilibuniwa na Mrusi wakati wa vuguvugu la muungano wa Soviet wao wanaipatia jina Cr protec2000 jina utani likiwa kunguru mweusi.Ni ndege isiyo shidwa kuruka hata kama haina mafuta kwa maana inatumia nguvu ya mionzi ya nyuklia ."Maana naona ndo wataweza kucheza nayo " General was kirusi alitoa hamuli yake kisha akaingia chumba cha mawasiliano kutuma ripoti kwa kikosi cha Kunguru weusi. Kila kitu kilimwendea kombo general huyu maana kile alicho kuwa akitazama katika mashine za mawasiliano kilikuwa kipya katika macho yake. Na hapo ndipo alipo pata taharifa mbaya tena.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******Ndege za kikosi cha Eagle zilipamba anga kwa bwebwe nyingi baada ya kupewa fursa ya kutalii anga lao kwa ulinzi. Na hiyo ndiyo nafasi ya kundi la doct ERICK na timu yake kupiga chenga lao kwa wamalekani na hawa EAGLE. Kwa maana misheni yao ilisukwa mapema kwa ajili ya kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja. *****MSITU WA AMAZONI****-* Katikati ya msitu huo mkubwa duniani wenye sifa kede kede .Ukiwa umesheni miti mikubwa ya asili pamoja na wanyama pori. Kulionekana wawindaji wawili wakiwa na siraha zao za moto wakiwa kwenye shughuli zao za uwindaji.Kama ilivyo kawaida ya wawindaji lazima wasome mazingira kwanza kabla ya kuanza kazi yao .Mmoja wa wawindaji hao akiwa kwenye shughuli ya kutega mtego wake wa kukamatia swala alipo inama na kuanza kukata kichaka ghafula katikati ya kichaka hicho aliweza kuliona box jeusi likiwa limefunikwa na vichaka chaka.Mwindaji yule alilisogelea box lile kwa umakini na kuanza kuyaondoa majani yale kwa umakini mkubwa mno.Akiwa anakaribia kuligusa box lile gafla alimuona nyoka aina ya kobra akiwa amtazama kwa matamanio makubwa mno.Ilimbidi arudi nyuma kwa tahathali kubwa mno ili asiumwe na kiumbe huyo mweye hasira nyingi asiye penda kutaniwa.Baada ya kufanikiwa kumuacha kiumbe huyo aliamua kuamisha mitego yake ili na mwenzake asije akagundua siri hiyo ili baadae aweze kurudi na kuangalia kuna nini ndani ya box lile jeusi.Baada ya kukutana na mwenzake alimshauri wahamie eneo jingine akiwa na lengo la kumkwepa mwenzake asigundue siri yake .**;**;*
Baada ya wawindaji wale kupata eneo jingine lililo wafaa waliweka mitego yao ya kuwanasia paa katika eneo hususa kabisa ambalo paa hufika pale kwa ajiri ya kunywa maji wakati wa adhuhuli.Wakiwa bado wapo wanasubilia mawindo yao yaweze kutokeza hapo ndipo mwindaji aliye kuwa ameliona box lile jeusi alipo hamua kumuaga mwenzake kwamba amesahau begi lake mahali alipo kuwa mwanzo hivyo alimuomba amusubili aweze kulejea ndipo waendeleze shughuli iliyo kuwa imewaleta hapo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
URUSI
Baada ya kambi ya eagle flay kuangamizwa yote hapo ndipo kikosi cha NAVY kilipo weza kuitekeleza kanuni hiitwayo plan ZERO wakiwa na lengo la kupoteza ushaidi wa kila kitu kilicho tokea kwenye misheni yao ya siri ya kuwakodi askali toka kundi la BONDE LA MAUTI kwa maana hawakutaka siri itoke kwenye kambi kambi yao na isambae kwa magaidi ambao waliendelea kutisha kwa teknologia hivyo waliamua kutuma ndege za maangamizi ambazo ni maalum kwa kuangamiza ndege ambazo zinapaswa zifiche siri na zisiweze kuonekana tena. “no 002 na 003 chukua nafasi iliyo hapo kushoto maana naona wanahiji kuitekeleza plan ZERO hawa jamaa “(PLAN ZERO ni mpango hasi wa kuficha siri ya jeshi na Mara nyingi watekelezaji na washiriki wa mpango hufa wore ili kulinda siri .Na huo ndo mpango uliokuwa tayari kutekelezwa.) DR Erick aliwapa taarifa ya kujihami wenzake baada ya kugundua ndege za maangamizi zikija katika Ukanda wao ambao walikwisha kuuchukua baada ya kuuwa wameikamilisha misheni yao na hilo alilihisi mapema na ndiyo maana kabla ya kuondoka kwenye kambi ya wana Navy alichukua kila kitu muhimu kitakacho wasaidia kutoroka baada ya kutokea ujanja kama huo kwa hapo aliweza kucheza na akili zao bila wao kujua maana kila kitu kilichopagwa alikipata kupitia vinasa sauti ambavyo mtambo wake aliuseti kwenye komputa yao wenyewe. Ndege hizi za maangamizi baada ya kuwa karibu mita kama mia mbili hapo ndipo zilianza kutupa miseri za kuangushia ndege kwenye ndege hizi tatu zilizo kuwa zimetoka kumaliza misheni. Lakini ndege hizi za kundi la Bonde la mauti hapo ndipo ziliamua kufanya kituko cha mwaka maana zilianza kushuka chini kuelekea kwenye uso wa bahari ya Hindi kwa kasi ya ajabu tofauti na walivyo dhani zinaweza kwenda . Baada ya muda waliweza kuziona ndege hizo tena zikiwa kwenye mwendo wa zigizaga hapo ndipo ndege za maangamizi ziliachia makombola kama mvua ili kuyiteketeza ndege hizi haraka kabisa .Makombora hayo yaliyo tupwa kwa mkupuo yaliweza kuziangamiza ndege zote tatu bila wasi wasi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment