Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

HII NI DUNIA AU KUZIMU? - 1

 







    IMEANDIKWA NA : AHMED JIRIWA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Hii Ni Dunia Au Kuzimu?

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MUAVENGERO.



    Sauti kali ya lango kuu kuu lililokuwa likifunguliwa zilisikika, lango hilo kilikuwa likifunguluwa na mlinzi mmoja mkakamavu aliyeonekana kuijali sana kazi yake. Baada ya lango hilo kufunguliwa, gari moja ya kizamani Land Rover deffender iliyokuwa na rangi ya kibuluu iliyopapatuka kutokana na kupita wakati wake, iliingizwa hapo ndani kwa kasi kubwa huku vumbi kali likitimka. Gari hiyo iliingia hadi ndani ya ule uzio wenye ukuta mrefu kwenda juu kisha kusimama katikati ya ule uzio. Vumbi kali lilitimka hadi kuulifanya lile gari kutoonekana kwa muda mfupi kidogo. Baada ya kutulia kidogo, mlango wa upande wa dereva wa ile gari, ulisukumwa kwa guu lenye nguvu mlango huo ukang'oka pasipo kuleta ubishi, ukadondokea mbali na eneo lile. Hakukuwa na watu wengi ndani ya ilr gari bali kulikuwa na mtu mmoja tu ambaye ndiye aliyekuwa akisabisha vurugu zote hizo. Buti kubwa la kijeshi lenye rangi nyeusi, lilishuka na kuikanyaga sakafu ngumu ya zege la kizamani lililotengenezwa kitambo kingi. Ulikuwa ni mguu mmoja tu ndiyo uliyoshushwa lakini mguu mwingine ulikuwa umebaki garini pamoja na kiwiliwili kizima, kifupi ni kwamba hakuwa ameshuka kabisa chini zaidi ya guu lake hilo moja. Alionekana akiwa amepiga shati gumu lenye mifuko mingi pamoja na pensi safi ya mifuko mingi pia. Alikosa tabasamu mtu huyo, hakuonekana kuwa ni mwenye huzuni ama furaha. Machoni alikuwa amevaa mawani nyeusi ya jua. Aliunyanyua mkono wake uliokuwa umebeba saa kubwa ya gharama, akonekana kuchanganyikiwa kabisa mahali hapo. Aliushusha mkono huo wenye saa kisha kuupandisha tena pengine labda alijua majibu yangeweza kubadilika lakini haikuwa hivyo, muda ulikuwa ni uleule. Masaa yalikuwa yanakimbia kwa kasi kubwa sana kwani muda huo huyo jamaa anaangalia muda, ilikuwa imeshatimu saa 04:23 za jioni, hakuona dalili za kuweza kurudi kwa yule aleyemtuma kazi alichoka kwa asilimia nyingi sana. Bwana yule mwenye mabuti makubwa, alitia mkono wake kwenye moja ya mifuko ya lile shati gumu alilokuwa amelivaa, akatoka na pakiti moja ya sigara, Embasy. Akachomoa sigara moja na kuiweka mdomoni kisha akachukua kiberiti cha gesi, akawasha na kuichoma ile sigara kwa mbele. Alipiga pafu kubwa akatoa moshi mzito nje kisha akairudisha tena kinywani. Akapiga pafu la wastani lakini moshi hakuwa ameutoa wote nje, aliuvuta ndani kwa nguvu sana kabla ya kuanza kuutoa nje kwa utaratibu maalumu. Alionekana kuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana, kichwa chake kilikuwa hakitulii kabisa, shingo lake lilikuwa likigeuka kushoto na kulia dhahiri mtu huyo alikuwa akisubiri jambo fulani mahala hapo. Kila muda alikuwa ana kazi ya shusha pandisha, shusha pandisha ya mkono uliobeba saa. Sigara ile sasa ikawa inateketea pasipo muhusika kushughulikia, hakukumbuka kama kulikuwa na sigara ambayo ilikuwa ikiteketea mikononi mwake. Waswahili hunena ya kwamba subira yavuta heri, Heri ya kusubiri ndiyo iliyomsaidia mtu huyo mwenye mabuti makubwa ya kijeshi kukutwa hapo na kile alichokuwa akikisubiri. Sauti za hatua pamoja na makanyagio ya nguvu yaliyokuwa yanasikika kutokana na mkanyagaji kuwa mzitp au kutembea kwa kishindo kikuu. Mtu huyo alifika mahali hapo akiwa anatweta, ni wazi alikuwa akikimbia ama alikotoja si kwema. Mtu huyo alikuwa ni mweusi wa rangi, mrefu kwrnda juu, mwembamba wa umbo mwenye mwele fupi alizozikata kiafrika. Macho makubwa kiasi. Alifika mahali hapo kisha akasimama mbele ya bwana yule mwenye mabuti makubwa.

    "tumefeli tena" alisema mtu huyo mweusi kisha akatulia tuli akiendelea kuhema kwa nguvu. Yule bwana mwenye mabuti makubwa akajifanya kama yale maneno ya yule bwana yalipita pembeni ni kama hakusikia. Jicho lake pekee ndilo lililokuwa likibadilika hatua kwa hatua, kutoka kwenye weupe kiasi hadi kufikia kuwa mekundu. Ule mkono uliokamata sigara ukawa unatetemeka ni kama sigara ile yenye tumbaku kavu iliyochujwa kitaalamu, ilianza kumuwia uzito.

    "kiongozi, timefeli tena, wale jamaa wamejipanga sana aisee" alirudia tena kauli yake yule mtu mweusi baada ya kuona ya awali haikutiliwa maanani. Jicho kali lililoiva kwa wekundu mithili ya ndege Chore mla pilipili kisha bwana yule mwenye mabuti makubwa aliikunja ile sigara na moto wake kisha akaizamisha kinywani mwake akaanza kuitafuna kwa ghadhabu kuu kabisa, kwa sekunde chache akawa ameitema filter ya ile sigara lakini kila kitu alimeza kuanzia tumbaku sambamba na takataka nyingine. Akasimama kwa kasi kubwa akamsogelea yule bwana mweusi.

    "eti unasemaje wewe mpuuzi?" akahoji yule bwana mwenye mabuti makubwa. Alikuwa mrefu kiasi, mwenye mwili mkubwa uliotuna misuli, hakuwa ni raia wa nchi hii kabisa japo hakuwa mweupe sana. Uliza yake ilikuwa ni kama hajasikia kitu alichokisema yule mtu mweusi tokea mwanzo.

    "tumefeli ki......!"

    "hebu tulia kwanza, unadhani labda naipenda hiyo ngonjera yako? Inaniumiza masikio ila nilitaka nione tu kama mwanzo ulikosema kunipa ripoti ama laa! Kumbe ni kweli, hii kazi niliwapa wapumbavu wasiyojitambua. Kwanini sasa mmefeli ikiwa mliniambia mnaweza kuifanya kazi ile kwa wepesi kabisa?" akahoji huyo bwana akiwa amesimama karibu kabisa na mtu yule mweusi.

    "wale jamaa wamejipanga sana kiongozi ile ngome ngumu haiingiliki, tumejaribu tumeshindwa na wenzangu wote wameuwawa ni Mike pekee ndiyo ametekwa."

    "unataka kuniambia Mike ametekwa wewe?"

    "haa! Kwanini atekwe sasa mbele yako, si nilikuamini sana, aaaagh.....hata nafasi ya kumuuwa hujaipata?" alibwata huyo bwana mwenye mabuti makubwa.

    "nafasi ya kufanya hivyo sijaipata, tulikuwa katika hali ngumu mno hata hivyo nimefanya kazi sana hadi kutoroka" alizidi kujitetea yule mtu mweusi. Yule bwana mwenye mabuti makubwa alikuwa tayari amebadilika kutoka kwenye ubinadamu hadi unyama. Alimzunguuka yule bwana mweusi kisha akasimama nyuma yake huku akiwa amemshika mabega. Akainama kidogo hadi kwenye sikio la upande wa kushoto, akamnong'ononeza.

    "hebu niambie ilikuwaje hadi makazidiwa kipumbavu namna hiyo"

    "bila shaka walikuwa wakituona, kwani sisi tulipofika tu mahali ambapo ndipo tulipanga kufanya mashambulizi, tukajikuta wenzetu wakianza kudondoka mmojammoja hadi tulipokuja kukaa sawa tayari tulishabaki wawili. Hatukurudi nyuma tulipambana kufa na kupona lakini nguvu yetu kubwa ilishapotea tukakosa jinsi. Risasi zilikuja kwetu kama mvua ikabidi tumutawanyike, hilo likawa kosa kubwa sana kwetu. Walimkata Mike kisha kuondoka naye hapo mimi nilikuwa naandamwa sana. Ikanibidi niwatoke na kufanikiwa kukimbia" alieleza kwa ufupi ilivyokuwa yule mtu mweusi. Pumzi nzito zikamtoka huyo bwana mwenye mabuti makubwa, alihema kwa nguvu sana kiasi cha kusababisha harufu mbaya ya sigara kutoka kinywani mwake yote kujaa usoni mwa yule mtu mweusi. Hakuumizwa na ile harufu mbaya ya sigara bali kilichomuumiza ni kuhusu hatma yake mahali hapo. Huyo bwana mwenye mabuti makubwa alikuwa si mtu mwenye utu hata kidogo.

    "eti, ngome yao ngumu sana haiingiliki" aliigiza huyo bwana mwenye mabuti makubwa kisha akaendelea.

    "kwahiyo unaoingilika kwa urahisi ni mk*nd* wako si ndiyo?"

    "ha....hapa....na kiongozi!"

    "ila?" alihoji tena lakini hakusubiri jibu, akaendelea tena.

    "unajua sijajua kama nyinyi ni wazembe kiasi hicho, unajua ni bora hata kufanya kazi na mashoga labda wanaweza kufanya kwa weledi kuliko nyinyi ambao sijajua jina la kuwapatia"

    "nisamehe kiongozi ni makosa yangu lakini naapa, ukinipa tena nafasi sitokuangusha" aliomba msamaha mtu yule mweusi. Yule bwana mwenye mabuti makubwa aliikunja sura sura yake hadi kupelekea kuchora matuta kweye paji lake la uso. Alikichomoa kisu kwa nguvu kutoka kiunoni mwa yule mtu mweusi kisha akamkita nacho mwenyewe cha kufua, akachomoa. Akamchoma kingine cha mbavu upande wa kushoto, akachomoa. Mwisho alichoma cha kwenye mbavu za upande wa kuli kisha akakizunguusha kutokea huko kulia kuja kushoto. Vitu vyote vya ndani vya mtu yule mweusi vikamwagika kwenye sakafu ya kizamani ya eneo lile. Hakuridhika, alimsukuma kwa nguvu sana, ule mwili wa yule mtu mweusi ukajipigiza kwenye bodi la lile gari kisha kudondoka chini kwa kishindo kikubwa.

    "kirahisirahisi tu eti, unaomba kusamehewa. Mpuuzi sana wewe. Nenda kuzimu kwa wapumbavu wenzio nikikuhitaji kwa ajili ya kuja kunipa burudani ya kitandani, nitakutumia ujumbe Shoga wewe. Kumbe ni mara kumi na kadhaa ufanye kazi na kahaba anaweza kukufurahisha kuliko ninyi wapimbavu." akaweka kituo bwana huyo kabla ya kuendelea tena kubwata.

    "Mike, Mike, Mike....si anatatoa siri zetu hadharani huyu mjinga?" alichanganyikiwa kupita kawaida huyo jamaa. Alikitupa kile kisu kwa ustadi mkubwa huyo bwana mwenye mabuti makubwa, kisu hicho kikaenda kukita kwenye shingo la yule mtu mweusi ambaye hakuwa hai tena kisha akatema mate yaliyojaa rangi ya tumbaku akaondoka eneo hilo kwa kasi kubwa mno kuelekea ndani ya jingo kubwa na la kizamani sana ukilitazama kwa nje. Aliufikia mlango mkuukuu akaufungua na kuzama ndani. Lilikuwa ni jingo la kuvutia sana kwa ndani. Bwana yule alipita moja kwa moja ndani kwankuifuata korido ndefu iliyokuwa ikivipita vyumba kadhaa hadi alipofika kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kikisikika sauti za miguno ya mapenzi. Akausukuma mlago wa chumba hicho akaingia ndani bila hata kubisha hodi. Aliwakuta watu wawili wakiwa wanaburudishana kwa ngono. Mwanamke akiwa juu huku mwanaume akiwa chini. Miguno ilikuwa imekolea sana huku huyo mwanamke akionekana kujituma sana juu ya kazi hiyo. Hawakuwa na hofu hata na mtu aliyeingia ndani hapo ma si kama hawakumuona laa hasha, walimuona sana ila hawakuona umuhimu wa kuiacha burudani yao eti, kisa mtu aliyevamia ndani hapo.

    "Benso, tafadhali sitisha huo mchezo, ninashida na Dede kwenye ofisi yangu" alisema bwana yule mwenye mabuti makubwa kisha hakusubiri kusikia hoja yoyote kutoka kwa wazinzi wale, akatoka na kuurudisha mlango kwa nguvu sana. Wale watu waliokuwa wakiburudishana wanaofahamika kwa jina la Benso na Dede, walisitisha ule mchezo kisha Benso akamsukumia Dede pembeni akajinyanyua pale chini.

    "vaa nguo umfuate huyo jamaa sijui anashida gani" alisema Benso huku akiiuzunguusha mkia wake mule ndani pasipo kuwa na shaka lolote lile. Aliziekea nguo zake akavaa kisha kumgeukia Dede pembeni akajinyanyua pale chini..........





    "vaa nguo umfuate huyo jamaa sijui anashida gani" alisema Benso huku akiiuzunguusha mkia wake mule ndani pasipo kuwa na shaka lolote lile. Aliziekea nguo zake akavaa kisha kumgeukia Dede.

    "unashangaa nini wewe?, nenda ukamsikilize huyo jamaa si unajua si kawaida yake kuvamia starehe zetu" alisema Benso ambaye kwa kulikata jina hilo waweza kumuita Ben. Dede alikuwa bado hata hajavaa nguo, alikuwa mtupu kabisa, alimtazama Ben kwa muda kisha akaziendea nguo zake na kuzitia mwilini. Kilikuwa ni kiji sketi kifupi kilichoishia juu ya magoti halafu ndani ya hicho kiji sketi hakuwa amevaa nguo nyingine ya aina yoyote ile. Juu alikuwa amepiga kiguo fulani kidogo tu kilichozuia matiti yake mazuri kwa mbele. Dede alikuwa ni msichana mrembo sana, kuanzia sura hadi umbo lakini hapo ulikuwa huwezi kuamini wala kukubali ukiambiwa huyo binti ni mrembo, labda unaweza kukubali kwa kulitazama umbo pekee lakini sura mh. Dede aliiharibu sura yake kwa kuichora chora picha na mistari ya ajabuajabu huku mgongoni akiwa amepiga chata kubwa la nyoka mkubwa aina ya Cobra. Binti huyo aligeuka kwa madaha kisha akaondoka ndani humo.

    "nini tatizo Bacon?" aliuliza Dede mara baada ya kuingia ndani ya ofisi ya yule bwana mwenye mabuti makubwa aliyefahamika hapo kwa jina moja tu la Bacon. Jibu halikutoka kwa haraka hadi Dede alipojitwalia nafasi ya kuketi.

    "wale wajinga wamefeli tena kumleta yule binti wa Mh. Backa" alisema Bacon.

    "hilo nililifahamu kiongozi" alijibu Dede. Bacon akasema.

    "si hilo tu bali Mike ametekwa pia"

    "eti nini!"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "kama nilivyokuambia" alijibu Bacon huku akionesha kuchanganyikiwa kwa asilimia kubwa sana.

    "haraka sana kiongozi Mike an.....!" hakuimaliza sentensi yake Dede, Simu ya mezani ya kiofisi ilipiga kengele kuashiria kuwa ilihitaji kuleta ujumbe kwa njia ya sauti. Bacon alinyanyua mkonga wa simu hiyo moja kwa moja akaitupia sikioni mwake.

    "ndiyo mkuu?" aliongea baada ya kuiweka simu hiyo sikioni, akatulia kidogo kisha akaendelea.

    "limekuwa ni jambo la kushtukiza sana na ndiyo tuko kwenye mjadala hapa mkuu.......ok, natekeleza ni kwa muda mfupi sana" baada ya kusema hayo, simu hiyo ikarudishwa kwenye kikalio chake kisha Bacon akapumua kwa nguvu sana. Alimtazama Dede kwa nukta kadhaa akaesma.

    "mkuu anajua kuwa Mike ametekwa" kauli hiyo ya kuwa mkuu anajua ilimshtua kidogo Dede lakini mshtuko wake alifanikiwa sana kuuficha, hakupata jambo la kusema lakini Bacon alikuwa nalo.

    "mshtue Ben kisha wape taarifa na wengine wa muhimu tukutane kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya dakika hii hii" alipokomea hapo, Dede alikuwa tayari amekwisha kuamka kwenye kiti, akaondoka hapo kwa mwendo wa kuringa lakini wa haraka sana akapotelea kwenye mlango wa ofisi hiyo kutokea upande wa nje wa hiyo ofisi. Bacon alinyanyua simu yake kubwa ya kisasa kabisa, akaiweka mfukoni mwa kombati yake na kutoka ndani ya kile chumba. Dede alivyotoka mule ofisini, alielekea moja kwa moja kwenye kile chumba ambacho walikutwa wakifanya ngono. Akamkuta Ben aliwa anaifunga Bastola yake ya kizamani sana ambayo ilikuwa inakitako cha kahawiya huku ikiwa na bomba nyembamba ya kutolea risasi. Ilikuwa ni bastola tata sana ya kijapan toleo la kwanza kabisa.

    "anasemaje kiongozi?" aliuliza Benson. Dede alijibu kuwa kiongozi anakuhitaji kwenye ukumbi wa mikutano now. Aliongea hivyo huku akiwa anapita mbio sana. Akatokea kwenye mlango mmoja ambao haukuwa ukifungwa, akatokea upande mwingine huko akawakuta vijana kadhaa wakiwa wanacheza kamari.

    "Beda, ita B1, B2 na Mbega. muda huu tukutane chumba cha mikutano" alisema hivyo lakini hakukaa akapita, akatokea upande mwingine kisha akakamata korido iliyompeleka kwenye chumba kimoja chenye giza kiasi. Akashuka ngazi chache kisha akatokea kwenye ukumbi mkubwa. vijana wawili Ben na Bacon wakiwa wamesimama katikati ya ule ukumbi wakiwasubiri wao. Alipofika hapo na vijana wengine tisa wakatokea kwenye milango tofauti hadi kufika hapo ambapo viongozi wao walikuwa wamesimama.

    "hatuna muda wa kupoteza, tuliowatuma kazi wameharibu utaratibu. Hawakufanikisha kumleta yule binti mbaya zaidi Mike ametekwa hivi tunavyoongea hapa, yuko chini ya askari wa Backa. Mkuu amenitaka niwe Urusi kabla ya kesho na pia amenitaka tukamilishe kazi ya awali kabla ya nyingine kufuata. Nimewaita hapa kwa ajili ya hili." akaweka kituo kikubwa Bacon. Akawatazama wale vijana ambao walikuwa na idadi ya watu kumi na mmoja huku yeye akiwa ametimiza idadi ya watu kumi na wawili kisha akaendelea na pale alipoishia.

    "Dede mimi na wewe tutaondoka pamoja baada ya kikao hiki cha dharula, wewe ni nyoka hivyo najua mauwaji yako ni ya kimya sana. Mike anatakiwa kufa kabla hata ya saa sita ya usiku huu wa leo. Ben wewe unatakiwa kwenda kisiwa cha Madagascar leo hii kwa dokta Lee. Huko utakwenda kuchukuwa mchanganyiko wa kwanza ambao umetengenezwa na huyo Kim. Jamani haya mambo yanatakiwa yatekelezeke leo hii hadi ikifika kesho kuwe na majibu mazuri ambayo mkuu yatampa raha. Tunao waacha hapa. B1, ninyi mtasambaa kama kawaida yenu ili kuhakikisha hakuna kiumbe anapita kwenu. B2, ninyi mtagawana, kaskazini na kusini halafu nyie Mbega mtakuwa mnatazama kote. uweni tu msimhoji mtu msiye mjua. Kazi njema Guys" alikomea hapo Bacon kisha akatoka mule ndani akiongozana na Dede. Kila kitu kiliachwa katiKa ulinzi wa kufa mtu. Kulimwagwa siafu, Mbwa pamoja na Mbega ambao hawa walikuwa ni wadunguaji hatari sana. Haikuwa na watu wengi hii kambi lakini ulinzi wake ulikuwa ni shida sana. Bacon na Dede walikuwa tayari wapo juu ya pikipiki moja kubwa sana. Bacon alikuwa akielekea uwamja wa ndege huku Dede akitakiwa kumuondoa duniani Mike kabla hata haja mwaga siri. Bacon aliachwa kilomita kadhaa kabla ya kufika uwanja wa ndege wa Mark D Air. Akawa anapiga hatua kadha kabla ya kuzifikia Tax zilizokuwa zimepaki kando ya barabara, akaingia kwenye Tax moja ambayo ilichukua jukumu la kumalizia kipande kilichobakia. Dede yeye baada ya kumucha Bacon pale njia panda, aliingia kushoto kwenye barabara ya kwenda Mtoni. Alivuta mafuta kwa fujo pikipiki likaongeza kasi kubwa sana. ilikuwa ni safari ndefu mno, safari ya kuchosha lakini kwa mwanadada huyo, hakuiona kama ilikuwa ni safari kubwa. Hadi inafika mida ya saa tatu usiku tayari Dede alikuwa ameshafika inje ya kisiwa hicho. Alikuwa akikiona kwa mbali kidogo kisiwa hicho cha kuvutia.



    MASAA MATANO NYUMA.



    "mkuu nadhani kwa adhabu tuliyompa ilikuwa ni halali kabisa" alikuja kijana mmoja mbele ya bwana mmoja mwenye ndevu nyingi nyeusi tii kisha kijana huyo kusema kile kilichomleta mahali hapo.

    "mhu! Hebu niambie, amesema kuwa yeye ni nani na anatokea wapi?" aliuliza mtu huyo anayefahamika kwa Jina la Backa. Mzee mmoja mwenye utajiri wa kutisha sana, utajiri ambao ulitokana na kurithi kwa wazazi wake ambao walifariki dunia angali mdogo sana. mzee huyo alishawahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo ndogo ya UNGAMO kipindi kile cha Raisi Julio Mobande. Kwa mtu usiyemjua unaweza kusema kuwa labda mwanasiasa huyo wa zamani, alichuma mali zake kupitia siasa ama vinginevyo vingi vinavyo husiana na siasa lakini ukweli ni kwamba kwenye siasa alifuata haki ya kuwatumikia wananchi tu na ndivyo alivyofanya. Wananchi walikuwa wakimpenda sana mzee huyo kutokana na utendaji wake wa kazi hakuna kiongozi wa nchi aliyekuwa hamjui mh. Backa. Mzee mwenye busara na upendo mkubwa kwa wananchi, huyu siye kiongozi yule anayeamuru wanachi wapigwe kama baadhi ya viongozi wengine wakiserikali alikuwa ni kiongozi mpenda amani na haki kubwa kwa anaowaongoza.

    "tumejaribu kila mateso lakini amegoma kabisa kusema, tumempiga na kupiga hadi kupoteza fahamu bado ameweka ubishi....hataki kabisa!" alieleza yule kijana ambaye alikuwa ni miongoni mwa walinzi wa karibu wa mh. Waziri mstaafu bwana Backa Ramson Backa.

    "hata jina lake pia?" alihoji Backa.

    "kabisa mheshimiwa"

    "nini mmemfanya sasa?"

    "tumempeleka kwenye bwawa la Ruba, acha aogelee nao nadhani kesho atakuwa tayari kusema" alijibu huyo kijana.

    "hapo sawa sasa naomba niitie Tereza mwambie aje muda huu" aliagiza Backa baada ya kuridhishwa na kile ambacho watu wake wamefanya kisha yule kijana kuondoka mahali pale na maagizo mengine. Muda mfupi tu binti mrembo mwenye umbo la kilimbwende alifika mahali ambapo Backa amekaa. Akachukua nafasi kisha akakaa na yeye pia.

    "nimekuja baba" aliitikia wito yule binti akawa makini zaidi kusikia kitu ambacho baba yake ataongea. Backa Ramson Backa, alitulia kimya huku akimuangalia binti yake mithili ya mtu ambaye hakuwa na kitu safi cha kumuambia bali ni kwa kumuona tu, utulivu ule haukudumu sana, mzee huyo akajikohoza kidogo kisha akasema.

    "ni muda sasa sijakutia machoni, tangu asubuhi, ulikuwa wapi mama?"

    "yaani baba hilo tu ndilo lililofanya unitumie mtu wa kuja kuniita mbiombio au kuna jingine!" alihoji Tereza binti mrembo mwenye sura nyembamba na mwili mwembamba wa kuvutia alikuwa akitabasamu.

    "usifikirie hilo ni dogo binti yangu mapenzi niliyonayo kwako ni makubwa sana. Hata marehemu mama yako alikuwa akilifahamu hilo nimekuwa si mwenye furaha ninapokosa kukuona kwa muda hata kama ni wa dakika kadhaa, nimekuwa hivi kwa sababu hakuna mtu mwingine wa kuweza kunipa faraja hili nililifahamu tangu mama yako akiwa hai. Niliamini kuwa wewe ndiye pekee utakayekuwa mtu wa kuniondolea mawazo sasa unadhani naweza kuwa na furaha ya namna gani unapokuwa mbali" alisema Ramson Backa. Tereza akatulia hakutaka kusema kitu alimtazama baba yake kwa muda kidogo kisha akayashusha macho yake chini na kuja kuyainua baada ya Baba yake kuendelea na pale alipokomea.

    "nini kwani kimekufanya usionekane kwa muda wote huo? Sina hakika pia kama utakuwa umekula chakula cha usiku maana muda unazidi kwenda na chakula bado kipo pale mezani"..........



    "asante sana baba yangu kwa kuwa na moyo wa pekee sana kwa binti yako, nilikuwa maabara leo kwa muda sana kiasi cha kunifanya hata kushindwa kula kwa wakati" alisema Tereza.

    "ulikuwa unafanya nini muda wote huo, usitake kuniambia bado unaendelea na utafiti wako?" aliongea kwa kushangaa kidogo huku akijiweka sawa kitini mzee huyo. Tereza akatabasamu kisha akaongea.

    "nadhani hakuna jambo jingine ambalo linaweza kuniweka maabara kwa muda mwingi kiasi chote hicho baba, ninahitaji kuhakikisha hili linafanikiwa la kwanza kabla ya jingine. Nataka kuwa mtu wa kwanza kutoka ndani ya Taifa hili kuweza kutengeneza dawa ambayo itaweza kuzisaidia nchi kame kuboreshea shughuli zao za kilimo. Nataka kuhakikisha dawa hii inawezesha kukuza mazao kwa muda mfupi kuliko ule ambao umezoeleka, hii nataka iwe ya muda mfupi zaidi yaani ni kama muda wa wiki nane tu kwa mazao yasiyohimili ukame kama mahindi na mazao mengine ya chakula ambayo hayawezi kuhimili ukame hii naona itasaidia sana. Pia vilevile nataka dawa hii ninayoitengeneza iwe na uwezo wa kuufanya mmea usiwe wa kunyongea pale tu unapokuwa umeupa dawa hii" aliongea. Muda wote huo wakati Tereza akiwa anaongea, mh. Backa alikuwa ametulia kimya huku akiwa na sura ambayo si ile ambayo ilibeba tabasamu mwanzo. Sura hii ilikuwa imefunikwa na huzuni ya ghafla mno kiasi kwamba Tereza alipatwa na mashaka hakuwa na furaha kabisa huyo bwana.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "nini kimekupata baba mbona upo kwenye hali ambayo si ile niliyoizoea, kuna tatizo?" alihoji Tereza. Backa bado hakuwa na jambo la kusema bali alichokifanya kwa muda huo ni kuinamisha kichwa chake chini kwa muda mfupi kidogo, alipokuja kukiinua alimtazama binti yake kwa macho ambayo yalikuwa na majonzi mazito sana akasema.

    "hakuna kitu kibaya sana duniani ambacho mtu anaweza fanyiwa kwa uonevu. Inauma pale unapoona kile ulichokipigania kwa muda mrefu hakifanikiwi kwa mipango ambayo umeipanga kwa kutaraji jambo fulani lenye faida lije kutokea" yalikuwa ni maneno ambayo Tereza hakuyaelewa kabisa kabisa ikabidi kuhoji ni kitu gani mzee wake huyo anamaanisaha lakini badala ya kujibu kile alichoulizwa Backa aliendelea na maneno yake ya mafumbo kama ada.

    "vita yoyote ngumu inahitaji maandalizi ili vita hiyo uweze kushinda na hata kama maandalizi yatakuwa macahache lakini unaimani ya ushindi wa kishindo kikubwa kwa sababu ulishakuwa na taarifa za vita tangu mapema. Vita siku zote inapiganwa na maadui hakuna marafiki wanaokubali kuingia kwenye vita kijinga jinga labda kama kunamaslahi makubwa ndani yake, utajisikiaje kama utapata taarifa kuwa adui yako amegoma kupigana nawe lakini kuna njia mbadala ya kukupiga ameindaa?" akakoma hapo kisha sura yake akaielekezea dirishani. Bado Tereza alibaki na maswali akiwa ni mwingi wa maswali ya kujiuliza kichwani mwake, kwanini baba yake anaongea yote yale, bado alishindwa kumuelewa kwa asilimia kubwa kabisa. Hakuacha kumwambia kuwa hakuwa akimuelewa. Backa hakutaka kuweka bayana kila kitu kwa binti yake aliogopa sana alikuwa yupo na hofu kubwa ya moyo wake moyo wake ulikuwa ukimuuma sana. Alikuwa akiwaza mambo mengi sana yaliyozidi kumkosesha raha na amani ya moyo. Hata binti yake alipokuwa akimmbembeleza amfafanulie kile alichokuwa akikimaanisha aligoma na kujifanya kama hakusikia kilichokuwa kikiongelewa mahali hapo. Aliyakumbuka maisha yake ya nyuma wakati ni kiongozi, alikumbuka jinsi ambavyo alivyokuwa akiifanya kazi yake kwa weledi mkubwa.

    "maadui wa mtenda haki ni wale wasiyopenda kuitenda haki" alisema kwa sauti ya uchoyo sana kisha akayafinya macho yake yaliyokuwa yakimwaga machozi mtindo mmoja alikuwa amegeukia pembeni hakutaka binti yake ashuhudie kama alikuwa akilia mahali pale. Alijiinamia na kufuta machozi kwa haraka kisha akaamka na kumwambia binti yake inabidi sasa wakale maana ni muda hawakuwa wamepata chakula na haijalishi, hata kama ni usiku ni lazima wale kwani matumbo hayawezi kuvumilia njaa kwa muda mrefu. Aliongoza hadi ilipo meza ya chakula akakaa kwenye kiti huku binti yake naye akijiweka kitini kisha binti mrembo akaja kuwaandalia wakawa wanakula taratibu. Kimya kilikuwa kikubwa sana mahali hapo kilichokuwa kikisikika ni midomo, sahani na vijiko.



    Wakati wao wakiwa wanaendelea kula, bila kujua chochote kile tayari kulikuwa na mtu makini na hatari kuliko hatari yoyote ile, alikuwa akikivamia kisiwa hicho cha Backa kwa siri kubwa na utaalamu wa hali ya juu mno. Hakuwa mwingine mtu huyo alikuwa ni Dede au nyoka kama ambavyo Bacon alimuita. Baada ya kulitelekeza pikipiki lake mahali salama, alipanga mkakati wa kuweza kufika kisiwani pasipo kugundulika. Ulinzi ulikuwa ni mkubwa sana na muda pia ulikuwa umeenda mno ilikuwa inapata saa nne na madakika yake. Alilanda pembezoni mwa ufukwe ule wa bahari akiwa anatazama ni usafiri gani utakaoweza kumfikisha ndani ya kile kisiwa ambacho kilikuwa kikimilikiwa na Backa Ramson Backa ambacho kilikuwa kinakwenda kwa jina la Backa Island. Dede alikuwa ameshavaa mavazi ya kuogele mithili ya samaki, alisogea kwa siri sana sehemu ambayo kulikuwa na watu wengi kiasi hapa akajua kwa vyovyote vile hawezi kukosa usafiri wa kumpeleka huko kisiwani. Wakati akiwa anazunguukazunguuka, aliweza kuona boti ndogo mfano wa pikipiki zile kubwa, hii ilikuwa ni boti iendayo kasi tena ikiwa imefungwa pembeni kidogo ya eneo ambalo lilikuwa na watu wengi. Akajivuta taratibu huku wanaume wenye tamaa wakimkodolea macho wakidhani ni mtu wa palepale labda kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa. Sehemu hiyo ilikuwa imechangamka kidogo, ilikuwa ni fukwe ambayo wengi wa watu walipenda kuitumia sana kwa ajili ya kupoteza mawazo hivyo kwa nyakati za usiku kama hizo huwa pana muziki wa kiaina ambao ulikuwa ukiwapa watu faraja, nyama za kila aina zilichomwa mahali hapo, samaki wakubwa wa kuchoma pamoja na supu ya Pweza na Ngisi wa kuchemsha. Magari ya kifahari yalikuwa yameegeshwa maeneo hayo, ilikuwa ni sehemu iliyochangamka kiasi fulani. Dede alipita hadi maeneo ambayo kulikuwa kukifanyika michezo ya watoto nyakati za mchana hapa alikuta pamepoa kidogo lakini pia hakutaka kujionesha kwa vyovyote vile aliamini hapakosi walinzi. Aliambaa pembeni mwa eneo lile hadi akaja kutokea mahali ambapo palikuwa kimya zaidi huku kukiwa na viboti vingi vidogodogo hapa alijitokeza taratibu lakini kabla hata hajafanya lolote, akatokewa na mtu mmoja aliyekuwa ameshika mtutu wa bunduki.

    "wewe ni nani na kwanini uko hapa?" aliuliza yule mlinzi lakini aliyeulizwa hakujibu na badala yake aliinama chini na kufanya makalio yake yaonekane vizuri kwa jinsi alivyokuwa ameinama. Yule mlinzi akajua kuwa huyo alikuwa ni mwanamke, macho ya tamaa yakamtoka huku moyo wa tamaa ukiwa umemsahaulisha majukumu yake ya ulinzi.

    "kwanini uko hapa wewe mrembo?" alibadilisha swali, sauti pamoja na mtindo mzima wa uliizaji, bunduki yake haikuwa ikimuelekea yule muulizwaji tena.

    "nilikuwa nahitaji Honda moja nizunguuke nayo hapa ufukweni" akasema Dede huku akiamka na kumgeukia yule mlinzi.

    "hapana, muda huu ni ngumu sana huruhusiwi kufanya hivyo ni hatari sana" alieleza mlinzi yule akiwa amekaa kirafiki kabisa bila kujua kama aliyenaye si mtu wa mchezo na alikuwa akimtafutia nafasi tu.

    "kwa mfano nikihitaji, na kukupa kitu ambacho kitakufurahisha kwa usiku huu maana ni muhimu sana mimi kupata hiyo honda...halafu kwanini uko mwenyewe maeneo haya?" alisema yule dada akiwa sasa anamsogelea yule mlinzi na kumshika beka mwisho akamnyuka swali.

    "tuko zamu wenzangu wapo kule wanapata chakula kidogo?"

    "kwani huwa mnakuwa wangapi kwenye zamu hasa?" akatupiwa swali jingine la mtego, kwakuwa alikuwa katika hali ya tamaa mbele ya mtoto huyo, hata hayo maswali aliyokuwa akiulizwa hakuyapa uzito. Alijikuta akiropoka kila kitu hadi idadi ya walinzi ambao huwa wanakuwepo kwenye lindo lao ama kwa hakika penzi hupumbaza na kukutoa kwenye umakini kama tu ukiwa hayawani wa mambo hayo. Dede alimsogelea karibu zaidi yule mlinzi kisha akaachia pigo moja la nguvu sana lililopigwa chini ya kifua, yule mlinzi hakuweza hata kutoa sauti ya maumivu. Alizunguushwa na kukamatwa shingo kisha kuvunjwa akaachiwa chini na gobole lake akiwa hana uhai. Dede alikamata miguu akamburuta hadi kwenye boti moja hivi akamtumbukiza ndani na kumuacha humo kisha yeye akakamata boti ndogo iendayo kasi aina ya Honda akaitia moto ikakubali akapotea nayo vivo hivyo pasipo kuwasha taa. Dakika tatu tu zilitosha kumfikisha kwenye himaya ya Backa aliiacha boti ile umbali kidogo na fukwe ya kile kisiwa ilipo kisha akazama majini. Alikuja kuibukia upande mwingine kabisa wa ile fukwe ambayo ilikuwa ikilindwa na askari wenye silaha kali. Alilala kwenye mchanga huku mwili ukiwa majini akala doria kila upande wa lile eneo alipo hakikisha kuwa pale alipoibukia ni mbali kidogo na ulinzi mkali, akachomoka kwa kasi kubwa hadi kwenye uzio uliokuwa ukilindwa na nyaya hatari sana zenye shoti ya umeme. Abaki pale bila hata kutikisika, alikuwa akifikiria jinsi ya kuweza kukamilisha mauwaji ya Mike na ilikuwa ni lazima afe usiku huo kabla haijafika asubuhi. Mara wakapita askari wawili eneo ambalo yupo yeye, akajibana kimya hadi wakapita pale. Alichokigundua Dede ni kwamba kwenye lindo hilo wapo hadi akari wa kike.

    "natakiwa kuingia humu ndani kwa kupitia sare za hawa askari lazima nihakikishe naondoka na askari mmoja wa.....!" kabla hata haja maliza kuongea hivyo, kukasikika michakacho ambayo ilikuwa ikielekea upande aliopo yeye. Akazidi kujibana pale ili asiweze kuonekana, nguo nyeusi alizovaa ziliweza kumficha vizuri kabisa. Wakati akiwa pale, yule askari ambaye alikuwa ni wa kike ambaye alipita muda mfupi tu na mwenzake, ndiye aliyekuwa akirudi.

    " huyu ni halali yangu sasa" alijisemea mwenyewe huku akimlia nyatunyatu hadi akamkaribia, akamgusa bega la upande wa kushoto kisha akarudi kulia, yule askari akafanya kosa moja la kijinga sana la kugeuka upande ule alioguswa. Pigo moja zito lilitua kwenye mshipa ulijitokeza wa upande wa kulia, sauti ndogo ya mguno ikamtoka yule askari lakini hakuachwa hivyo hivyo, pigo jingine likatua nyuma ya shingo akalegea na kuangukia kwenye mikono mikavu ya Dede. Akaburutwa hadi kwenye ile sehemu ambayo aliitumia kujificha, dakika tatu nyingi dede akatoka akiwa katika muonekano wa yule askari wa kike akatazama saa yake akagundua kuwa muda haukuwa rafiki,.....





    ulikuwa ukimuacha kwa kasi kubwa. Akachukua ule uelekeo wa upande ule ambao askari yule alikuwa akielekea mwanzo, mawazo na akili yake vilimtuma kuwa kule ndiko kulikokuwa na geti la nyuma la kuingilia ndani. Hakuwa amekosea kwani alipofika tu alipokelewa na sauti ya askari wa kiume aliyekuwa amechwa eneo lile.

    "huku hakuna shida tena muda huu acha mimi nirudi kwenye lindo kuu ila hakikisha ukitoka huku unapitia getini ili ulifunge kwa ndani halafu kuwa makini bana huku ni karibu sana na bahari usije ukatokewa na majini" iliongea sauti ya askari yule wa kiume. Dede akajibu kwa sauti ya chini ambayo aliitoa maalumu ili kuficha sauti yake maana hakujua sauti ya askari aliyechukua muonekano wake ikoje. Yule askari wa kiume ni kama alisita kidogo lakini hakubaki sana hapo akaondoka.

    "kama angeendele kubaki ningejua amenitilia mashaka, nisingekuwa na budi zaidi ya kumuuwa" aliwaza Dede huku akiingia ndani ya lile geti kisha kutokea upande wa ndani, akalirudisha kidogo lile geti na kuelekea ndani kabisa ya ule uzio. Alilizunguuka lile jingo huku akiwa tayari amevaa soksi maalumu ya kuiziba sura yake usoni. Alipofika kwenye kona moja alifanikiwa kumuona mtu akija kwa mwendo wa haraka sana akitokea ndani ya jingo lile kubwa upande wa pili, akasubiri pale kwenye ile kona ili kumngojea. Yule mtu alipita pale bila kuwa na umakini wowote ule, akajikuta amezuiwa mbele na mtu aliyevaa mavazi ya askari wa nje ya uzio huku akiwa amevaa soksi ya kutoruhusu sura yake isionekane.

    "vipi tena mbona huku muda huu?" aliuliza yule mtu akiwa na hofu kidogo.

    "nataka kujua yule mateka wa mchana amehifadhiwa wapi?" akasema yule askari feki. yule mtu akashtuka zaidi na kutoa macho. Mateka? Anataka kujua? Kwa nini? Yeye ni nani na kwanini aulize hivyo askari wa nje na mambo ya ndani humu wapi na wapi?" alijiuliza maswali mfululizo yule mtu bila kuwa na jibu lenye kusaidia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "wewe ni nani kwani?" akaamua kuuliza sasa yule mtu.

    "askari wa lindo la usiku" alijibu kwa upole wa juu kabisa bila kuwa na shaka lolote lile.

    "askari wa lindo la nje na mambo ya humu ndani ni wapi na wapi kwanaza hayo mamlaka umepewa na nani wewe au wewe ni mgeni wa hapa?" aliuliza maswali kadhaa mtu yule. Dede badala ya kujibu akatabasamu tabasamu la ndani ya moyo huku sura yake ikiwa haina hata robo ya tabasamu. Alijua hapo amelenga na huyo ndiye atakayempeleka kwenye mateka wake. Hakuwa na muda wa kupoteza tena, mapigo mawili ya nguvu yalitua tumboni mwa yule mtu, akatoa miguno midogo kisha kabla hajafanya jitihada zozote za kujitetea, alishtukia kisu kikiwa kooni mwake huku ncha ya kisu hicho ikiwa imegusa kabisa koo lake.

    "niambie mahali mateka alipo kabla hata sijakiruhusu hiki kisu kitengeneze Ala kwenye shingo lako" alinong'oneza kutokea mgongoni Dede. Yule mtu akajua labda yule askari feki anatania akakukuruka ili kutaka kujinasua, kisu kikazama taratibu kwenye nyama zake za shingo, kilikuwa kinamtoboa.

    "na nase....ma kak....dada nasema" alibwabwaja yule mtu huku akiomba mtu huyo asiyemjua jinsia alegeze.

    "sema haraka kabla sijachukua maamuzi ya kukuuwa tu hata kama hujaniambia" alisisitiza Dede akiwa amelegeza kile kisu kidogo tena alitaka kuambiwa na hali ya ulinzi ilivyo huko ambako mateka huyo amehifadhiwa. Yule mtu alieleza kila kitu hadi hali ya huko ilivyo na jinsi ya kuingia pia. Dede hakuwa akihitaji yote hayo alichotaka kujua hasa ni wapi Mike alipo na ulinzi basi hayo ya kuingia yeye ndiyo atajua.

    "ni niachie basi dada si tayari nimekwisha kuughaarr....!" hakumaliza kuomba kuachiwa yule mtu, kisu kile kilisha zama na kuachwa chini akipigania uhai wake. Dede alinyanyua mkono kama ada yake zilikuwa zimesalia dakika tano tu ili kuweza kutimia saa sita kamili. Akaondoka pale hadi mahali ambapo kwa maelekezo aliyopewa angeweza kumuona mateka wake aliyekuwa ametumwa na kiongozi wake wa kazi kuhakikisha anamtoa duniani. Alifanikiwa kumuona Mike kwa mbali sana tena akiwa katika hali ya kuhangaika ilionesha kuwa alikuwa katika hali ya maumivu kiasi ama makali aliyokuwa akiyapata. Alitoa darubini yake ndogo kisha akaanza kuivuta picha ya Mike taratibu, hakuamini kile alichokiona, Mike alikuwa amejaa Ruba mwili karibia wote kuanzia mahali ambapo maji yale machafu ya lile bwawa dogo la Ruba yalipoishia hadi maeneo ya tumboni. Dede damu zilimkimbia vibaya sana akajikuta akisisimuka kwa kile alichokiona.

    "walikuwa wamepanga kuhakikisha kesho anatapika kila anachokijua, washenzi sana hawa. Ngoja basi nimpunguzie maumivu ili keaho wasipate tabu ya kumuhoji" alisema Dede kisha akatoa ki rasketi mgongoni mwake na kutoka na silaha moja hatari sana yenye mfanano wa nyota, ilikuwa na pembe tatu. Aliizunguusha mkonono huku akisogea kwa mwendo wa haraka kisha akakivurumisha kwa nguvu nyingi sana. Kifaa kile kikawa kinasafiri kwa kasi kubwa sana huku kikipita mule ambapo kilikusudiwa kipite. walinzi ambao walikuwa mule ndani kwenye wavu ule wa nyaya nene na zenye uwazi wa kupita kichwa cha Mbuzi, walikuwa hawana wasiwasi kabisa tena walikuwa kwenye starehe za kupiga pombe kali huku wakiwa wanacheza karata bila shaka. Walikuwa wapo pale kwa kazi moja tu nayo ni kuhakikisha mateka wao ambaye hadi muda huo alikuwa hajajitambulisha hata jina, anapoteza fahamu ndipo wamtoe na kumhamishia kwenye jingo jingine ili kutakapokucha ahojiwe. Hawakuwa wakijua kuwa wakati wao wakiwa wanafurahi kwa michezo ya karata, ndiyo muda huo Mike anapokea nyota ile yenye sumu kali iliyokita nyuma ya shingo na kumfanya aangushe shingo chini na kupoteza maisha. Hawakujua kama huo ndiyo ulikuwa muda wa kumtilia mashaka mateka wao, wao walikuwa na kitu kingine kabisa katika vichwa vyao.



    *******

    *******



    MADAGASCAR.



    "kamanda kuna mtu anakuja upande huu wetu!" alisema mtu mmoja kutokea ndani ya himaya kubwa ya Dr. Lee. Alikuwa kwenye jingo la juu kidogo ambapo ndipo mahali pake pa kazi muda wote. Alikuwa tayari amemuweka mtu huyo kwenye shabaha tayari kufanya chochote pindi amri itakapokuwa imetolewa.

    "anaonekana hana mashaka kabisa na anakuja pasipo kuwa na hofu yaani ni kama anakwenda kwa mke mkubwa" alisema tena yule kijana akiwa na simu sikioni. Baada ya kama dakika moja aliingia mtu mule ndani ya kile chumba ambacho alikuwamo yule kijana. Alikuwa mrefu kwenda juu mwenye sura ngumu yenye makunyanzi, mikono iliyotoka misuli na pua kubwa kiasi. Akachukua darubini na kutazama upande ambao kijana aliyempigia simu alikuwa ameelekeza.

    "nasubiri amri yako kamanda hapa yupo kwenye kumi na nane zangu" alisema yule kijana akiwa amefinya jicho lake moja kwenye bunduki safi kabisa ya R4.

    "hapana anaonekana kuna kitu kinamleta, ngoja tukijue kwanza halafu kama ni kufa atakufa hapa hapa" alisema yule bwana mwenye makunyanzi usoni na pua kubwa huku akiishusha ile darubini kutoka usoni kwake, akaiweka mezani kisha akachukua simu na kutafuta namba ya mtu aliyemkusudia akaiweka sikioni baada ya kuipiga.

    "mpokeeni mgeni yupo Line namba mbili hakikisheni mnamleta kirafiki hadi nyumba ya wageni" alitoa amri yule bwana mwenye makunyanzi kisha akatoka mule ndani kwa haraka kidogo. Wakati Benso akiwa anazidi kulikaribia jingo kubwa la Dr. Lee, tayari wana usalama wa himaya ile walisha muona siku nyingi sana hivyo alikuwa akija tu huku akiwa hana mashaka lakini tayari kulikuwa kumeshatumwa wenyeji kuja kumpokea. Akiwa anakaribia Line namba tatu ambayo ndiyo ya mwisho kabla huja ligusa geti namba moja, alishtukia sauti ya vyuma vikitolewa usala kutoka kwenye silaha zisizoongopa aina ya SMG huku wanaozitoa usalama wakiwa wanasogea taratibu eneo ambalo yupo yeye.

    "mikono juu" amri ilitolewa mahali hapo na yeye bila hiyana akanyanyua mikono. Akasachiwa na kukutwa na bastola moja nene ya kirusi pamoja na kisu kimoja kiunoni. wakavichukua vile vitu kisha kumfunga pingu wakampeleka mahali walipotakiwa kumpeleka. Ben hakukaribishwa kirafiki hata kidogo pia hakuulizwa maswali ya aina yoyote ile kwanza aliambulia kichapo cha nguvu hadi akalegea ndipo alipoachwa hadi siku inayofuata ambayo ndiyo aliahidiwa kupewa salamu na kuulizwa habari za atokako. Alikuwa amepigika kweli, alikuwa hoi vibaya sana.



    SIKU ILIYOFUATA, asubuhi hali ilikuwa imechafuka kwa mh. Backa. wana habari walikuwa wengi sana huku askari pia wakiwa wamezagaa, ni baada ya askari wa lindo la usiku kugundua kuwa askari mwenzao ameuwawa lakini pia mateka pamoja na mfanya kazi wa ndani ya hilo jumba wakiwa wameuwawa. Vifo vilikuwa vya kushangaza sana kwani kila marehemu alikufa kwa namna yake. Askari alikufa kwa namna ya ajabu sana kwani hakukutwa na jeraha hata moja, walihisi huwenda kuwa alikabwa shingo hadi kufikwa na umauti lakini mfanya kazi wa ndani alikufa kwa kisu kilichoachwa kwenye koromeo lake huku mateka akifa kwa silaha za kininja. Hii iliwapa kazi askari kujua, je, muuwaji alikuwa ni mmoja ama laa! Mh. waziri wa zamani alikuwa akifuta machozi mbele ya miili miwili ya marehemu ambayo ilikuwa ikichukuliwa na askari kwa ajili ya kupelekwa hospitali. Mwili mmoja haukumliza sana Backa na badala yake ulikuwa ukimtia ghadhabu kila akiutazama kwani ndiyo pekee uliosababisha yale. Lakini kwa nini yote yale yalikuwa yakitokea? Hakuwa na maadui Backa tangu enzi za uongozi wake, au ni utendaji wake wa kazi ndiwo uliopelekea kuandamwa na watu asiowafahamu? Yote hayo alikuwa akijiuliza mzee huyo ambaye kwa kumuangalia tu kwa macho ungeweza kugundua labda mzee huyo anamatatizo ya kutokuongea, hakuwa mtu wa kuongea sana kwa lugha nyepesi, Backa Ramson Backa alikuwa ni mvivu wa kuongea. Mengi aliwaza, mengi alijiuliza pasipo kupata majibu lakini alipofikia kwenye kuhusu binti yake, hapo akapata mashaka kidogo na kuwaza kuwa huwenda yote yale yanaletwa kwa sababu ya binti yake. Alikumbuka vitisho kadhaa alivyokuwa akivipokea kutoka kwa mtu asiyemfahamu kuwa anashida sana na binti yake na hiyo ni kutokana na kuwa binti yake huyo anakitu cha thamani sana.

    Hapa moyo wake ukapiga kwa nguvu na kufikiri kwa muda kidogo, machozi ya uchungu yakamtoka.

    "ungemtoa binti yako kwa ridhaa yako mwenyewe nadhani wala tusingefikia mbali mheshimiwa" alikumbuka kauli kadhaa za vitisho alizokuwa akizipokea bwana huyo. Kubwa na iliyompa mashaka juu ya hayo yanayomtoke ni ile ya.....basi tutakuwa tukikutembelea hadi pale tutapokubaliana.

    "haya ndiyo matembezi.......!" alijiuliza lakini hakufika mwisho wa sentensi yake ikaelea hewani.

    "hivi ni kwanini haya yote yanatokea mheshimiwa maana hili ni tukio la tatu kutokea lakini bado hujachukua hatua zozote za kiusalama" lilikuwa ni swali kutoka kwa mwanahabari mmoja.

    "ukisema kuwa sijachukua hatua za kiusalama utakuwa unakosea, hatua nimezichukua kubwa sana tangu kutokea kwa tukio lile la awali. Na kuhusu maadui sikuwahi kuwa na maadui hata siku moja enzi za uongozi wangu" alijibu kwa staili hiyo Backa.

    "ni hatua gani za kiusalama ulizozichukua labda mheshimiwa waziri mstaafu?" swali jingine likakita.

    "taarifa zilifika kwa polisi na wakaahidi kufanya uchunguzi wa matukio haya pia nikaongezewa ulinzi wa masaa ishirini na nne.

    "je, wameshajua angalau chanzo cha hili linalokutokea kila siku kiongozi?" sasa maswali yalianza kumkera Backa.

    "hilo swali ni vema kama ungewauliza maafisa wa jeshi la polisi kuliko kuniuliza mimi. Kazi yangu ni kupeleka tatizo na wao kama wanausalama wa raia ni kufuatilia tatizo" alijibu huku akiwa amekunja sura kuwa sasa hahitaji tena maswali lakini mwanahabari bado alizidi kumsumbua na maswali tu.

    "hili tukio lililotokea jana ni tukio kubwa sana na muuwaji ameuwa ndani ya nyumba yako sasa ni hatua gani unachukua maana hiyo ni hatari kwako zaidi?" hili mh. Backa alishindwa kulijibu kabisa aliondoka eneo hilo. Angelijibu kwa namna gani sasa na wakati hata yeye hilo swali anajiuliza kuwa ni kwa namna gani ataulinda usalama wake. Alikuwa amechanganyikiwa kabisa. Aliishia kwenye fukwe yake ya gharama ya juu na kusimama akiyashangaa maji ya bahari yanavyojisukuma mchangani huku yakivigusa viatu vyake pasipo kuyafanya lolote. Alikuja kushangaa ubavuni kwake kukiwa na kiongozi mkubwa wa jeshi la polisi.

    "mh. baadae nitakuhitaji makao makuu ya jeshi la polisi nikiwa na maana nitakuhitaji ofisini kwangu kwa ajili ya kuliongea hili kwa kina kwani hali inazidi kuwa hatari zaidi na usalama wako unazidi kuwa mashakani" alisema yule kamanda wa polisi Inspector General (IGP) wa jeshi la polisi wa nchi ya Ungamo. Mh. Backa alitikisa kichwa kisha kiongozi yule wa polisi kuondoka.

    "hadi muone maji ya shingo yanataka kumzidi mtu ndipo muujue wajibu wenu" aliwaza Backa akiwa anamtazama kiongozi yule mwenye cheo cha juu kabisa kwenye jeshi la polisi jinsi anavyoziparamia ngazi za kumtoa pale.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "naweza kuwa mashakani leo hata kesho, sina imani na ulinzi nilionao tena kama walinzi wote waliokuwepo jana hawajafanikiwa kumuona adui akiingia na kutoka, huu si ulinzi wa kujiaminisha nao kabisa" aliwaza Back alipokuwa anaendelea kuyashangaa maji ya bahari. Alisimama pale kwa muda mrefu sana kisha akapiga hatua tatu akaketi kwenye kiti kimoja pale kwenye ile fukwe yake. Hakutaka kuondoka mahali hapo hadi alipokuja mlinzi wake mkuu.

    "muheshimiwa hapa si salama kukaa peke yako inabidi tuelekee ndani kwa sasa" alisema yule mlinzi. Backa hakusema kitu alikaa hivyo hivyo kimya tu.

    "Muheshimiwa nadhani tungeondoka sasa na ukaelekea ndani" alirudia tena. Backa bado hakutaka kuinyanyua sura yake lakini akasema.

    "hapa si salama kabisa si ndani si nje, kama adui ameweza kuingia na kufanya mauwaji ya mwenzao aliyekuwa kwenye ulinzi wa askari nikitegemea wangemuona, unadhani usalama wangu ni upi sasa" alisema Backa akiwa kwenye majonzi makubwa sana kisha kabla yule mlinzi wake hajasema chochote, Backa akaendelea.

    "Phily, nenda kaniitie Tereza hapa nataka kuonngea naye"

    "lakini kiongozi.....!"

    "nimesema kaniitie Tereza Phily, hata wewe ni wa kunichanganya kiasi hicho? Umekuwa lini jeuri wewe hasa ninapokuagiza jambo" alikoroma Backa kuashiria kuwa hakuwa katika hali ya kawaida kabisa. mh. Backa alichanganyikiwa kwa asilimia kubwa kabisa. Phily aliondoka kwa mwendo wa nusu kutembea nusu kukimbia, alitembea mwendo wa nusu nusu.

    "nimefika baba!" alisema Tereza akiwa anamhurumia baba yake kwa kiasi kikubwa mno. Backa alinyanyuka kwa kasi sana mithili ya mtu aliyepata mshtuko kisha akasema kwa sauti ya upole huku akitembea taratibu pembeni mwa yale maji yaliyokuwa yanakilowesha kabisa kiatu chake bila kujali.

    "nakumbuka marehemu mama yako aliwahi kusema haya. 'ni bora nitangulie mimi nisione mwanagu wa pekee akipitia mitihani ya maisha'. Kiukweli nilikuwa sijamuelewa kwanini alikuwa akiipenda ile kauli hasa ninapokuwa katika hali ya ugonjwa mkubwa. Ni kauli aliyokuwa akiipenda sana na muda mwingine huwa analia na kumuomba Mungu ili afe yeye na mimi nibaki kwa ajili ya kukulea wewe kwasababu alijua ni jinsi gani nilivyokuwa nikikupenda nawe ukinipenda pia. Akafa kweli, alikufa nakumbuka, ndiyo alikufa ningali bado namuhitaji sana" hapa Backa alisema huku akiwa ameyaelekeza macho yake kushoto na alifanya hivyo kuhakikisha jicho lake la kushoto linalotoa machozi kila ahisipo uchungu, halionwi na binti yake huyo. Hakupenda kuona binti yake akimuona kuwa alikuwa akipitia maumivu makali.

    "sasa leo ndiyo nagundua ile kauli yake, nagundua kuwa alikuwa na maana kubwa sana. Najiona mimi mwenyewe tu kwenye malezi yako wakati aliniambia angekuwa akinipa msaada hata kama akifa. Najiona mimi mwenyewe Tereza mwanangu, najiona jinsi ninavyoipoteza ndoto yako ya kuwa mtu maarufu na msaada mkubwa kwa nchi masikini zilizosababishwa na ukame. Naiona elimu yako inavyobadilika kuwa ya maangamizi" alisema mengi Backa hadi Tereza akabaki na mshangao baba yake ameamua kuongea kuwa anajiona jinsi anavyoipoteza elimu yake lakini hajajua anaipoteza kivipi, hajajua kwanini elimu hiyo itapote. Akataka kumuuliza baba yake lakini akakuta anaendelea kuongea.

    "Nilitumia gharama nyingi sana mwanangu kukusomesha kwenye vyuo vikuu duniani kwa kutumia pesa nyingi, haikuwa tatizo kutumia pesa nyingi kwa sababu sijawahi kufikiria kufilisika. Ukafanya vizuri huku ukiwa na nia ya kuja kuwa mwana sayansi mkubwa utakayebobea kwenye mimea mbalimbali na kugundua dawa ambayo itaharibu bakteria wote hatari wanaoidumaza mimea, mazao bila kuleta mavuno. Ukafanikisha ndoto yako kupitia vyuo mbali mbali duniani ikiwemo marekani pamoja na urusi ambako ndiko ulikochukulia shahada yako ya Sayasi ya mimea na madawa ya mimea." akaweka tuo mheshimiwa Backa namna hiyo kisha akazidi kuongea.

    "nahisi kuna watu waliona juhudi zako na uwezo wako tena mtu huyo anatokea huko huko urusi, wanakuhitaji kwa udi na uvumba kwa lengo la kukutumikia vibaya"

    "kwanini unapenda kuhisi kitu ambacho si cha kweli na hakiwezi kuwa kweli hata siku moja" alisema Tereza.

    "Tereza mwanangu, hiki ninachokuambia si kama ninahisi tu bure, kuna mambo kadha wa kadha ndiyo yanayonifanya nihisi hivyo" alisema Backa. Tereza alimshika baba yake mkono kisha akasimama na kusema.

    "tambua kuwa hukuwa na maadui tangu ungali kijana, umekuwa ni mtu wa watu hata ulipokuwa kiongozi hadi ulimaliza muda wako wa uongozi. Hakuna mtu anayekuzungumzia vibaya Haika yote hii pamoja na jiji zina la Pande, huyo ni nani aje leo na kuleta vitisho hivi. Mimi nachukulia ni vikundi vya vijana wa mtaani tu ambao wameamua kuvamia tu, basi"

    "vikundi vya mtaani vinaweza kuvamia tu pasipo kuwa na sababu za msingi wauwe tu na kuondoka na inamaana hata hufikirii kama watu waliokuja kufanya mauwaji jana ni kwa ajili ya kumuuwa mtu wao tu, wewe hujui ni kwanini?" akanyamaza Backa ilikutoa nafasi ya binti yake kuelewa kisha akakamatia palepale na kuendelea.

    "walifanya vile ili kuhakikisha siri zao hazivuji. Ndiyo walijua kuwa ni lazima huyu mateka ningempa mateso hadi aseme ametumwa na nani na kwa lengo gani. Tereza mwanangu, hawa ni watu makini na wanajua wanachokitaka kwangu kama si roho yangu basi ni taaluma yako" alihitimisha. Kwa maelezo yale tu Tereza hakuwa na neno la kuchomekea akabaki kushusha pumzi nyingi sana na kutulia kwa muda. Akamwambia baba yake sasa si muda wa kutulia tena na kutegemea ulinzi wa kumlinda tu bali anatakiwa kuwa karibu zaidi na wana usalama. Na yeye akiwa kama waziri mkuu mstaafu anaamini wanausalama hawawezi kumuacha adhalilike, kwanza ni aibu kubwa kwa kiongozi wa serikali kukumbwa na mambo ya ajabu kila uchao halafu vyombo vya usalama vikae kimya. Backa akamwambia binti yake kuwa asiache kumalizia kile alichokianza, aendelee nacho na yeye anakwenda kuonana na IGP Liyambo ili kuweza kujua njia gani za kutumia ili ajihakikishie usalama kisha moja kwa moja ni lazima akamuone mkuu wa nchi wa kipindi hicho alichowahi kuwapo yeye ambaye licha ya kuwa chini yake kikazi pia alikuwa ni rafiki yake mkubwa sana. Wote hao alitakiwa kukutana nao.



    Kwa upande wa Ben alikuwa tayari amekwisha kuhojiwa na kutoa kila kitu kilichompeleka kule kwa Dr. Lee. Alitoa sababu zote za kufika pale na kuongezea kuwa kilichofanya yeye kufika pale ni kuhitaji mchanganyiko wa kwanza wa sumu ambayo itatakiwa kutumika kwenye michanganyiko miwili ambayo itakuwa ni hatari zaidi kwa maisha ya wanadamu hasa wa Afrika. Baada ya kutoa taarifa hizo Lee akaomba kukutana na mtu huyo ili kuweza kumhoji zaidi. Benny akapelekwa mbele ya mzee hatari sana mzee ambaye hakuwa akionekana sura. Alikuwa amevaa vazi maalumu la kufunika sura huku akiwa kwenye baiskeli maalumu ya kujiendesha yenyewe ya kisasa kabisa.

    "ni nani aliyekutuna umesema kijana?" aliuliza kwa suti ndogo sana iliyotokea kooni...



    "Mr. Bencov" alijibu Benny kwa ufupi.

    "ni mrusi si ndiyo, najua ni mrusi huyo....kwanini anahitaji sumu kwa ajili ya Afrika? Hakuwahi kukuambia kuwa ni kwanini anahitaji sumu kwa ajili ya Afrika?" aliuliza tena baada ya kujiumauama kwa sauti yake ileile ya kutengeneza.

    "hakuwahi kuniambia hata siku moja ila inavyoonekana kuna sababu za msingi sana za yeye kufanya hivyo" alijibu Benny kwa urefu kidogo. Yule mzee aliye ndani ya nguo ndefu ya moja kwa moja aliiamsha shingo yake kwa mikono miwili ambayo ilikuwa imelalia upande wa kushoto wa bega lake kisha akainyanyua sura yake juu ambayo ilikuwa ipo kwenye kinyago kilicholandana na sura yake pana akasema.

    "Lady Devil....waambie wampeleke ndani kisha kwa kutumia mawasiliano aliyomipa huyo kijana niunganisheni na huyo mrusi ili tujadili jambo" akakomea hapo. Binti mmoja mrefu mwenye sura ya urembo iliyovutia, mkononi kuanzia karibu na bega la kushoto hadi karibia na kiungio cha chini, kulikuwa na alama kubwa nyeusi kama ya kuungua kwa moto ilijaa nusu ya mkono mzima kutaka kuuzunguuka. Aliwageukia watu waliokuja na yule mtu pale na kuwaambia wampeleke kwenye chumba safi akapumzike na apewe huduma yoyote atakayoihitaji. Wale watu wakafanya hivyo kwanza walimfungua pingu kisha kumpeleka huko walikotakiwa kumpeleka huku akiwa nyuma ya ulinzi mkali. Walipomfikisha kwenye hicho chumba alikuja binti mwingine huyu alikuwa na asili ya kichina, akawapa amri kuwa chumba hicho alichomo huyo jamaa kinatakiwa kuwa na ulinzi masaa ishirini na nne kisha akaondoka. Tayari mawasiliano yalikuwa yamekwisha kuunganishwa tayari na watu hao walikuwa kwenye maongezi ya siri sana. Maongezi hayo yalikwisha kwa makubaliano maalumu ambayo hakuna aliyejua tofauti na wazungumzaji.



    ******

    ******



    Gari ya kifahari sana yenye rangi nyeusi na vioo vizito visivyoruhusu mtu wa ndani kuonekana na wa nje, ilisimama kwenye makao makuu ya polisi majira ya adhuhuri. Walishuka watu wawili wenye mawani za giza huku wakiwa kwenye suti kali nyeusi, mmoja akaenda kufungua mlango wa nyuma upande wa kulia kisha kuushikilia mlango huo. Mzee mwenye mwele nyeusi tii! Aliyekuwa ndani ya suti ya rangi ya ugoro ya kunyurutika alikishusha chini kiatu chake cha pesa ndefu kilichoshabihiana na rangi ya suti ile kiasi. alisimama na kabla hata ya kupiga hatua tayari ulinzi wa watu wale wawili ulikuwa imara kabisa. akaongozwa njia hadi kwenye lile jingo lililoandikwa kwa maandishi ya kuchonga yaliyosomeka MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI. Wakaingia kwenye mlango wa jingo hilo huku mheshimiwa huyo akipokea salamu kutoka kwa baadhi ya maaskari. Alizama ndani humo kisha moja kwa moja akaingia kwenye ofisi ya mkuu wa polisi kwa kuelekezwa na kwa sababu ujio wake ulikuwa ukitambulika hakuwa na shida sana kuweza kuingia. Alipofika ndani mule ya ile ofisi safi ya kupendeza liyokuwa na hadhi ya kweli kabisa kuweza kukaa bwana huyo mwenye tumbo kubwa kiasi, IGP alisimama na kumpa mkono kisha kumkaribisha kitini kabla ya yeye kukaa pia. Zilifuata salamu za hapa na pale kisha wakaingia moja kwa moja kwenye lile sekeseke.

    "mh. hebu niambie mimi kuna nini tatizo hasa mbona ni wewe tu, kuna mawaziri wangapi wakuu wamestaafu kabla yako na baada yako?" aliulizwa swali la kwanza mh. Backa. Akashusha pumzi nzito kisha akajiweka sawa kabla ya kunyanyua kinywa chake ili kuweza kusema kile anachokijua. Alisema kila kitu anachokijua yeye lakini bado hayakuwa na uzito wa kumshibisha Inspekta Jenerali wa polisi bwana Liyambo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "haya uliyonieleza ndiyo sababu ya yote yanayokutokea mheshimiwa?" akatupa swali jingine IGP swali ambalo lilimfanya bwana Backa kukaa kimya kwanza na kufikiri ni wapi alipokosea au ni kipi hakukisema hapo, ukimya wake ukazalisha swali jingine kutoka kwa jenerali huyo wa polisi.

    "na ni kwanini haya yanatukia kwako na sijasikia mh. Raisi wa sasa na zama zako kuongelea chochote?" hapa sasa Backa akakumbwa na jambo la kushtuka kidogo. Ni kweli alitaka akitoka pale aelekee kwa mh. Raisi bwana Julio Mobande, lakini kwanini aende? Ni mangapi yamemkuta na hakuna hata siku moja ambayo bwana huyo alimpa pole wala kumjulia hali? Hana Luninga? Au hata kama si mpenzi wa kutazama taarifa ya habari, ni msomaji mzuri wa magazeti yule?" Alijiuliza mengi Backa. Akapata picha ya mashaka kidogo na hapo ndipo alipokumbuka hata utendaji wa Rais wake kipindi hicho alipokuwa madarakani. Alikuwa ni mvivu wa kutoa maamuzi, kila kitu walifanya viongozi wa chini yake yeye hakuhusika kwenye jambo lolote lile pia alikuwa akimtaka yeye asaini mikataba mbalimbali pamoja na karatasi zihusuzo unyang'anywaji wa makampuni mbalimbali ambayo mengine yalifuata taratibu katika uwekezaji na mengine machache tu ndiyo ambayo hayakuwa yakifuata taratibu za kiuwekezaji. Hapa ndiyo akakumbuka swali ambalo alishawahi kujiuliza mwishoni kuhusu mkuu wake wa nchi kumpa kipaumbele kwa kila kitu lakini wakati akiwa anajiuliza hivyo alikuwa amekwisha chelewa kila kitu kilikuwa kimeshakamilika. Kubwa na lililomuumiza moyo ni hili analohisi leo linamtesa. Hakutaka kuliweka bayana mbele ya IGP akasema jambo jingine ambalo ndilo linalompa hofu kwa wakati wote. Alisema kuhusu vitisho anavyovipokea kutoka kwa wauwaji na huku wakiwa wanamtaka binti yake. IGP alitulia kidogo lakini wazo la Backa kutaka kwenda kwa mh. Mobande, hili hakuliafiki. Akamwambia ni vema kama angetulia kwanza ili aweze kutafakari kwanza. Backa akaafiki hilo. IGP akamuahidi kumpa ulinzi wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wauwaji wanajulikana. Backa akatoka mule ndani akiwa amenyongea tofauti na alivyoingia. Akaingia garini na kutoweka eneo lile.



    "Mkuu kuna taarifa zimetumwa ofisini muda huu ni za sauti hivyo unaweza kuja kusikiliza" aliongea mtu mmoja mbele ya bwana mmoja mwenye tumbo kubwa lililonawiri, mfupi mwenye kichwa kikubwa na shingo nene. Alipopokea ule ujumbe, alitoka na kuongozana na yule kijana hadi huko ofisini. Alikuta vijana wakiwa katika kazi zao wakifanya hili na lile, akaunganishiwa kifaa maalumu kisha kuvalishwa head phone. Sauti zote zilizokuwa zikiendelea baina ya waziri Backa na IGP zilisikika. Bwana huyo akatoa macho kisha akairudisha ile Head Phone mezani akatoka mule ndani kwa kasi kubwa sana kwenye chumba kimoja hivi ambacho kilikuwa kikubwa na chenye mazagazaga mengi. Akajikalisha kitini kisha kuvuta simu ya mezani hapo akatia namba kadhaa kisha mkonga wa simu akauvuta hadi sikioni.

    "haloo!" sauti nzito ikasikika kutokea upande wa pili wa simu. Bwana yule akashusha pumzi na kusema.

    "lazima kila kitu kiende kwa utaratibu uliopangwa, kazi yako unaijua sawa sawa Tumbo?" aliuliza bwana huyo mwenye kichwa kikubwa na shingo nene, upande wa pili wa simu ukajibu.

    "naijua kazi yangu sawasawa Mh. Mobande na sijawahi kwenda kinyume"

    "hujui Tumbo, laiti ungelikuwa unajua ungekwisha kunijuza yaliyojiri" akasema Mh. Mobande.

    "nilipanga kwenda kumziba kwanza mdomo ndipo nihakikishe kila kitu kinawafikia nyinyi" alisema mtu aliyefahamika kwa jina la tumbo.

    "hapo sawa" akatulia Mh. Mobande Rais wa zamani wa awamu ya pili wa taifa dogo la Ungamo. Akaishusha simu na kuiweka kwenye kikalio chake kisha akayagandisha macho yake ukutani ambapo kulikuwa na kalenda kubwa ya mwaka 2001. Akacheka sana baada ya kuzitazama zile picha ambazo ziliipamba ile kalenda. Hakuridhika, alinyanyuka kutoka pale kitini hadi kwenye ile kalenda akaigusa ile picha kisha akarudi tena kitini huku akicheka kama mwehu.

    "pesa zako zilikutia kichaa wewe mshenzi, kama uliona pesa ni kitu cha thamani na hukuhitaji kiongezeke, ungeachana na siasa. Unaingia kwenye siasa halafu unakuwa kimbelembele na kujifanya unaijua haki kuliko mimi ambaye ndiyo nilikuwa kichwa cha taifa hili, hah hah hah haaa! Ni vijimitego vidogo tu vinawatia mkenge kunguni kama wewe. Acha tuone kama pesa zako zitakuwa na faida kwako, nataka kuona kama zinaweza kukusaidia kwenye hili maana watu walikuwa wanasema kama ukizihamisha pesa zako zote Taifa hili dogo la Ungamo linaweza kutikisika kiuchumi. Na kweli tulikuabudu lakini sasa wanaume tunazihitaji hizo pesa" alisema kwa tambo kubwa bwana Mobande kisha akajilaza kitini na kufumba macho huku AC ikiwa haichoki kumpa faraja ya hali safi ya hewa ambayo ingeweza hata kumpa usingizi kama asingeamua kujinyanyua pale na kuondoka.



    IGP alikuwa amekwisha panga vikosi vingi yeye mwenyewe tena vikiwa ni vikosi vile anavyoviamini sana kisha akavipangia kazi ya kuhakikisha ulinzi kwa muheshimiwa Waziri Backa haupungui. Vilikuwa ni vikosi nambari moja katika jeshi la polisi la nchi hiyo. kulikuwa na vikosi vya silaha na mapigano ya ana kwa ana kisha kulikuwa na vikosi vya mbwa wanaonusa kila aina ya harufu ihusuyo walifu na uhalifu wenyewe, ulinzi ulikuwa umekamilika mno. Inspekta Jenerali Liyambo alifanya hivyo kwa sababu maalumu si kikazi pekee. Backa alikuwa ni mtu aliyempigia kifua sana hadi kuwa katika nafasi ile ya ukuu wa polisi wa nchi, kama si Backa asingefikia pale hilo halipingiki na hicho ndicho hasa kilichomfanya awe kipaumbele kwa kila jambo kuhakikisha anamsaidia. Japo alichelewa kutenda msaada yeye mwenyewe lakini ndiye aliyekuwa akiwahimiza vijana wake waimarishe ulinzi kwa waziri yule mstaafu. Pia tayari alishaanda vijana wawili ambao walikuwa ni Ispekta Moo pamoja na kijana machachari huyu alikuwa ni Ispekta Bogo. Sababu kuu ya kuwaweka mainspekta hawa kazini ni kwamba, vijana wale walikuwa hawashindwi na kazi hata siku moja na ni vijana ambao umakini kwao ni kitu cha kwanza. Wakati akiwa bado ofisini kwake, alishtukia akipokea ugeni wa ghafla, ugeni ambao haukuwa na taarifa kwake hata kidogo. Alikuwa ni waziri wa ulinzi na usalama mh. Bande sir. Huyu ndiye aliyekuwa akiitwa kwa jina la tumbo na Mh. Mobande.

    "karibu sana mheshimiwa" alikaribisha IGP huku akinyanyuka na kutoa mkono wa karibu. ......



    Waziri huyo aliupokea na kuketi kisha hakuwa na jingine la kuongeza zaidi ya kwenda kwenye kile kilichompeleka mahali pale.

    "hongera kwa kuitenda kazi yako kwa weledi mkubwa" alianza kwa kusifia.

    "asnte sana kiongozi huo ni wajibu wetu wana usalama na ulinzi wa raia" alijibu pongezi zile.

    "lakini kwanini hukuomba ushauri kwa wenzi wako na umeamua tu kuchukua maamuzi ya moja kwa moja? Ulifikiria nini labda kutoka kwenye kuwashirikisha wenzako hadi kuamua wewe kama wewe? Vipi kwani, wanakusaliti?" alipiga swali bwana huyo huku akiwa amemkazia macho kiongozi huyo mkubwa wa Jeshi la polisi. Swali lile lilimpa mashaka kidogo lakini mashaka yake hakutaka yawe bayana, akatuliza kichwa na kujibu.

    "nilikuwa nikiwashirikisha wenzangu mwanzo na kuomba ushauri jinsi ya kuweza kukabiliana na hili tatizo, lakini hakukuwa na msaada mkubwa kwa mheshimiwa waziri sasa ile ni aibu kwa Taifa, sisi kama taifa hatuoni kama ni aibu kushindwa kumlinda kingozi wetu au ndiyo tufanye alishapita na yake yamepita?" aliongea kwa hisia kidogo Liyambo lakini alijikuta akipokea kauli iliyomuacha njia panda kutoka kwa kiongozi huyo na hakutakiwa kupinga bali ni kutekeleza na kauli hiyo aliambiwa inatoka ngazi za juu.

    "ilipaswa iwe hivyo lakini kwa vile tunathamini viongozi wetu waliopita, unachotakiwa kufanya ni kupunguza ulinzi kwa Backa nikiwa na maana ya kuwa askari wa silaha wapungue na mapambano pia wapungue kidogo lakini askari wa mbwa pamoja na mbwa wao wanatakiwa kutoka wote na waripoti kituoni, hii ni amri na siyo ombi" alimaliza kusema hivyo Bande Sir kisha alinyanyuka kitini na kuondoka bila hata ya kuaga. Liyambo alibaki kimya huku bumbuwazi likimgubika kwa kiasi kikubwa. Alipatwa mashaka makubwa sana na kauli za waziri.

    "kauli hii inatoka ngazi za juu kabisa........ni amri na siyo ombi!" aliyakumbuka maneno ya Bande Sir. IGP. Anamaamuzi tena makubwa tu lakini amri kutoka kwa mkuu wa nchi hii alitakiwa kuiheshimu sana. Akanyanyua mkonga wa simu na kupiga mahali kisha akatoa amri kuwa kikosi Mbwa kilichopo kwenye lindo kirudi chote na hakita kuwepo lindoni tena pia katika vikosi vitakavyobakia, kila kikosi kibakiwe na askari wane. Hiyo ilikiwa ni amri. Akakata simu kisha kukaa kimya kama mwendawazimu aliyeona dawa itakayo mponya.



    ANTANANARIVO MADAGASCAR.



    Mvutano ulikuwa mkubwa sana kutoka pande mbili kila upande ulitaka kuwa namba moja yaani kila kundi lilitaka kushika nafasi lenyewe. Hiyo ilikuwa ni baada ya yale mazungumzo kufikia muafaka na bwana Bencov kukubali kuja Madagascar kufanya maongezi ya pamoja ambayo yalikuwa na dhima ya muungano pengine.

    "wewe huna uwezo wa kuweza kutengeneza sumu ambayo itatumika kupata huo mchanganyo ili ije kuwa hatarishi kwenye maisha ya watu. Mimi ninauwezo wa kuunda sumu ya awali huoni kama mimi nafaa kuwa kiongozi wa kundi zote mbili?" iliuliza sauti ndogo iliyotokea kooni, hii ilikuwa ni sauti ya Dr. Lee. Sauti ambayo ni ndogo lakini ikitoka kwa watu wake inakuwa kubwa na yenye mamlaka mazito.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ninao uwezo binafsi Dr. Lee. Ni kweli sinauwezo wa kutengeneza sumu lakini ninaouwezo wa kutengeneza silaha hatari sana za kutisha za kibaolojia ambazo kama utafanikiwa kumpiga binadamu kwa risasi moja basi hawezi kuishi wala kuzikwa mwili wake unamenyeka menyeka kwa muda wa masaa sabini na mbili na kupotea kabisa na kubaki mifupa baada ya siku kadhaa" alisema bwana mmoja mrefu mweupe mwenye mwili mkubwa, huyu alikuwa ni Bencov kijana mdogo sana wa Kirusi. Kauli ya Bencov ilimshtua sana Dr. Lee kiasi cha kuipeleka mikono yake yoye miwili na kukikamata kichwa chake kilichoangukia kushoto kama kawaida na kukinyanyua hadi kikakaa sawa. kisha akamtazama vizuri kijana huyo wa kirusi aliyesema kuwa anauwezo wa kutengeneza silaha ya namna ya kutisha hata kwa kuiongelea. Alichezesha kichwa chake bwana Lee ambacho kilikuwa hakiwezi kujizuia kwa muda mrefu bila kuanguka na kulalia kwenye bega kisha akasema yake ikiwa ni kuonesha uwezo wake mbele ya kijana huyo mdogo.

    "nakwenda kukuonesha hiyo sumu ambayo uhatari wake ni mkubwa japo haiwezi kuuwa bali inapoozesha na kumuweka mtu kuwa katika hali ya uzezeta maisha yake yote ya duniani na pia huwa inampa maumivu makali kila baada ya masaa nane mtu atakaye chomwa sindano ya sumu hiyo. Hii ndiyo iliyonifanya nikapewa jina la Dr. Lee mara baada ya kuacha kulitumia jina la Lee Kim. Ukisha kuiona Sumu hiyo pia nitakuonesha madhara yake nawe utanionesha madhara ya hiyo silaha yako" alipokwisha kusema hayo, yule mrusi akakubali kwa kubetua mabega. Dr. Lee alibofya batani moja kwenye ile baiskeli yake, baiskeli ile ikajigeuza na kumtoa pale huku nyuma wale wote waliokuwapo pale wakafuatia. Safari yao iliishia kwenye maabara kubwa kabisa, huko kulikuwa na mitambo na mashine mbalimbali. Kulikuwa na wafanyakazi walio katika mavazi meupe huku wakiwa wamevaa maski za kuzuia harufu kali ya madawa mule ndani. Dr. Lee aliwaelekeza wale jamaa zake wapite mahali na walipopita, hapo walikuja kutokea sehemu nyingine ambayo ilikuwa ni tofauti na huko walikotokea, wakiwa na maski kama za wale wafanyakazi wa mule ndani.

    "hii ndiyo mitambo inayotumika kutengenezea sumu hiyo niliyokuambia, sumu hiyo inatengenezwa kwa vitu vya ajabu mno kama utabahatika kuona. Nifuateni huku" alitoa maelezo Lee kwa watu wale. Wakatoka pale na kuingia kwenye mlango mwingine, aliwaelekeza wale watu njia ya kupita kwani njia alizokuwa akipita yeye ni fupi ambazo ni chombo chake cha usafiri tu ndicho kinachoweza kupita. Walikuja kutokea upande mwingine, huku kulikuwa na joto kali sana na wafanya kazi wa huko walivaa mavazi mepesi mno ya kuteleza na maalumu ya kuzuia kemikali za huko. Hata wao walipofika huko walipewa hayo mavazi kwasababu chumba hicho kilikuwa ni chumba cha uzalishaji hivyo kulikuwa na kemikali mbaya sana ambazo kama zitakuingia mwilini unaweza kupata madhara makubwa. Walifika kwenye kinu kimoja hivi, hapo Bencov alibaki mdomo wazi yeye na watu wake lakini kina Merina au Shetani wa kike na watu wake walikuwa katika hali ya kawaida sana kama hakukuwa na kitu cha kushangaza mbele yao. Kulionekana vichwa kadhaa vya binadamu vikiwa vianasubiri kuingizwa kwenye mtambo mmoja ambao ulikuwa ukivipasua vichwa hivyo. Walikaa hapo kwa muda kidogo huku wakishuhudia kichwa kimoja kimoja kikiingia kwenye mashine hizo. Walizidi kusonga mbele zaidi ya pale.

    "hapa ndipo unapochukuliwa ubongo wa binadamu na kusafirishwa hadi kwenye kile kinu cha rangi ya kibuluu, pale ndipo unapochanganywa na kemikali kisha kusagwa pamoja hadi kwenye ile mashine ya rangi nyekundu pale ndipo inapochemshwa na kuwa uji mzito ambao ukitoka pale ndiyo tunachanganya na kemikali ya mwisho ambayo inaitwa Red Chemical (RC). Tukisha ichanganya, kabla ya kupoa kwanza, inaingia kwenye mashine hii ndogo ikitoka hapo inakuwa katika hali ya kimiminika ambacho tayari ni sumu kamili" alisema mtu mmoja aliyekuwa amevaa tofauti na wafanyakazi wote. Maelezo yale yalitosha kabisa na hakukuwa na swali la kuuliza. Hapo ndipo walipotolewa na kupelekwa kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kimetulia sana. Kilikuwa ni chumba chenye giza zito. Walipoingia tu mule ndani, taa ikawaka. Kulionekana mwili wa mtu mmoja mnene aliyekuwa amelala kitandani mtu huyo alikuwa akilalamika sana huku akijinyonganyonga pale kitandani.

    "sumu ile bwana Bencov ni sumu yenye madhara haya, huyo mtu unayemuona hapo kitandani ni miongoni mwa waliokuwa wafanyakazi wangu lakini hakuwa na uaminifu kwangu kwani wakati mimi natengeneza hii dawa kipindi hicho nikiwa nahangaika kutafuta material mbalimbali pamoja na kuunda kemikali za kutengezea dawa, huyu alikuwa akitoa siri za uandaaji dawa hizo kwa serikali ya nchi hii. Nikajua naishi na mtu hatari kuliko hatari ilivyo, nilimkamata na kumfungia ndani kwa muda wa mwaka mzima alikuwa akiishi katika mateso makali mno, chakula alikuwa akila mara moja kwa siku tena kisichokidhi haja ya tumbo hata la Paka. Nilipanga kumuweka vile hadi siku nakuja kuipata hii dawa. Nilipoifanikisha mwishoni mwa mwaka jana, ndipo nilipoanza kumpa malezi mazuri kwa kumlisha chakula kizuri na bora. Nilifanya vile kwa sababu nilikuwa sijui madhara ya hii dawa kwa kiasi kikubwa na yeye nilitaka kumfanya kuwa jaribio langu la kwanza kwa hii dawa. Mwaka huu mwanzoni ndipo nilifanya jaribio kwenye mwili wake." aliweka kituo Dr. Lee, akatulia kwa muda kidogo. Ilikuwa kama dakika mbili hivi kisha akakoroma kidogo kutokea kooni na kuendelea.

    "ni kwa muda mfupi tu madhara yalianza kumkuta. Alikuwa akipambana na maumivu makali mno hadi nikawa najua labda angeweza kufa lakini haikuwa hivyo. Tukamfanyia uchunguzi na kujua kuwa ni sumu mbaya sana ambayo madhara yake ni kushambulia ubongo kwa kiasi kikubwa na kumfanya mtu kuwa zezeta asiyeweza kutambua kitu chochote kile awapo kwenye kipindi cha maumivu na kweli anaishi kwenye maumivu makali mno ya kukakamaa kwa misuli kila baada ya masaa manane. Hali hiyo ikimkuta huwezi kumkaribia kama unaroho fupi. Misuli inatutumka na kuchora mistari ya kutisha kwenye mwili wake, hapo hakuna hata msuli mmoja unaojificha anakuwa ni kama kiumbe cha ajabu na huwa mzito na mkavu mithili ya mti mkavu. Mwili huwa unabadilika rangi na kuwa mwekundu hadi anaogopesha kumtazama. Hali hiyo inakuwa mwilini mwake kwa muda wa dakika tatu na anaporejea katika hali ya kwaida, kumbukumbu zake hazina mkisio maalumu. Muda mwingine zinarudi na muda mwingine zinagoma kurudi kabisa" alimaliza kuongea Dr. Lee kisha kimya, kimya kilitanda mkoromo ukasikika kutoka kwa Dr. Lee hali ya mshangao ikawakumba wale wageni bwana Bencov na vijana wake wawili Benson na mwingine aliyejichora matatuu kwenye mikono yake yote.

    "msijali jamani yuko salama huyu" aliongea Merina huku akimuamuru kijana mmoja amtoe boss huyo hapo mahali. Kijana akatekeleza kazi aliyopewa, alisogea mbele ya kile kifaa cha usafiri kilichombeba bosi wake kisha akabonyeza vitufe fulani kisha kutoka kule mbele baada ya sekunde chache tu, ile baikeli maalumu ikamtoa Dr. Lee mahali hapo kwa kufuata njia pasipokuongozwa na muongozaji wa aina yoyote.

    "kwahiyo hii sumu inaitwaje sasa?" aliuliza Bencov huku akimuelekea mtaalamu mmoja pale baada ya Lee kuondoka.



    "kutokana na kushambulia ubongo kwa kiasi kikubwa, tumeamua kuipa jina la Brainaptic poison" alijibu huyo mtaalamu. Wakazidi kupitishwa sehemu mbalimbali walipomaliza hapo chumbani kisha walitoka hadi kwenye ukumbi mkubwa sana huko walimkuta tena Dr. Lee akiwa ametulia kitini kwake huku mwili wa yule jamaa ukiwa kwenye kitanda ukiwa umetulia tuli sana. Baada ya wale watu kufika eneo lile, baada ya ule mwili kuwatangulia. Hakukuwa na maongezi mengi bali Merina ndiyo alisimama na kuchukua jukumu la kuongea.

    "kila kitu nadhani kimekamilika kwa upande wake kilichobakia ni kwa upande wako, yule mtu aliyoko pale mbele ndiyo anayetakiwa kuingia kwenye jaribio la silaha yako hiyo ili tuweze kuujua uwezo wako kwenye utengenezaji wa silaha hizo" alihitimisha Merina kisha kumgeukia bwana Bencov. Bwana huyo alibaki kimya bila kusema jambo kisha akamuangalia yule mgonjwa pale mbele ambaye hata kukaa kulimshinda kwa jinsi alivyokuwa amelegea. Mtu ambaye hakuwa akipata huduma zozote za kibinadamu kama kula kuoga na vitu vingine vinavyofanana na hivyo, kula alikuwa akila kwa kutumia mipira maalumu na hata kujisaidia pia alikiwa akijisaidia pasipokujitambua alikuwa akiishi kwa maumivu makali mno. Hakuwa na ugonjwa mwingine unaomsumbua kifupi ni kwamba alikuwa mzima kabisa wa afya lakini hakuwa akijitambua kwa jambo lolote lile. Bwana mdogo Bencov alimtazama yule mtu kwa tuo kidogo kisha akasema.

    "nadhani hamjui sababu za kumtazama huyo mtu," akatulia na kusema tena.

    "silaha yangu sijawahi kuijaribu kwa mgojwa wa kufa muda wowote kama yule, nahitaji mnilete mtu mzima kabisa na mwenye nguvu zake" alipokwisha kutoa tu maelezo hayo, Dr. Lee alimgeukia Merina, Merina alimgeukia kijana mmoja ambaye alikuwa mahali hapo. Kijana yule hakusubiri asimamiwe au aamriwe. Aliondoka kwa kasi kubwa hadi nje, aliporudi alikuwa ameongozana na kijana mmoja ambaye alikuwa akija pale huku akiwa na wasiwasi mkubwa. Haikuwahi kutokea kuitwa ndani ya hilo eneo tena kukiwa na wakubwa zake lilikuwa ni jambo la ghafla na hakulitegemea. Aliletwa hadi mbele ya Dr. Lee.

    "Bencov kijana ni huyu unaweza fanya jaribio lako kwangu sasa nataka kuona, pia unaweza kufanya kwa wote maana hata yule marehemu aliye hai pale kitandani hana anachoniingizia kwa sasa zaidi ya kunimalizia umeme uaotumika kusumia chakula kipitacho kwenye mipira, anatia hasara tu" alisema Dr. Lee. Benco aliomba yule mtu awekwe mbele yake kwa umbali wa kama miguu minne ya mtu mzima kisha akaichuku silaha yake kutoka kwenye begi dogo alilokuwa nalo kijana mdogo anayekwenda kwa jina la Beda. Akaishika vizuri ile silaha ambayo ilikuwa iko na muundo wa bastola fupi mbele ikiwa na mcha ndefu yenye rangi nyekundu. Akachomoa pini fulani chini ya ile silaha kisha kumuelekezea yule mtu aliyeletwa mahali hapo.

    "silaha hii inanguvu kubwa sana Dr. Lee. Msukumo wake ni mkubwa ambao kama uko karibu sana inaweza kukurusha kwa umbali fulani. Ukipigwa na risasi hiyo maeneo yoyote mwilini mwako, unamuda mfupi sana wa kuokoka na kifo" alifafanua Bencov huku akiiruhusu risasi kutoka kwenye tundu la ile bastola. Ilikuwa ni risasi iliyotoka kwa kasi kubwa kisha kumkuta yule mtu. Alirushwa kwa umbali kidogo akarushwa juu mfano wa kimo cha Ng'ombe kisha kurudishwa chini kwa nguvu kubwa huku akitokwa na miguno ya maumivu, kimya kikafuatia. Wote pale walikuwa kimya sana hakuna hata mmoja aliyethubutu kutoa sauti.

    "huu ni mchezo wa kitoto unaonilete Bencov, unajaribu kunionesha sinema za kitoto za kufa kufa, nimekuwahi!" alisema kwa sauti yake ya kutengeneza kama kawaida Dr. Lee mara baada ya yule mtu aliyepigwa kusimama na kushangaa. Bencovu hakujibu kitu badala yake aliigeuza ile bastola yake ya kipekee sana na kumuelekezea yule mgonywa pale kitandani. Akabonyeza trigger, risasi ikatoka kwa kasi kubwa sana na kwenda kutua kwenye kifua cha yule mgonjwa hadi akageuzwa upande mwingine kutokana na kasi iliyotumika. Yule mgonjwa alikumbwa na kitu kama mshtuko hivi, akainuka kidogo akakaa kitako kwa sekunde chache kabla ya kurudi tena kitandani. Bado Dr. Lee aliona hakuna kitu kinachomshangaza pale, akataka kubwatuka tena kwa maneno ya hasira lakini Bencov akamuwahi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hii silaha ni ya kipekee sana, silaha hii haikuwahi kutengenezwa popote duniani hivyo sishangai hata wewe ikikushangaza kwa kuona labda hakuna kitu inafanya" macho yakamtoka Dr. Lee huku akiwa anatazama chini. Akaikamata shingo yake iliyolegea na kumtazama kijana huyo wa kirusi kisha kuiachia shingo yake ikarudi palepale begani.

    "silaha hii niliitengeneza kwa ghadhabu kubwa mno na ghadhabu zangu zisingefutika abadan bila kupata suluhisho la hii silaha. Hapa ninafuraha tena siyo ndogo hata kidogo. Sababu kubwa ya furaha hiyo ni hii silaha" akatulia hapo huku akiwaacha wanaomsikiliza wakiwa hawamuelewi. Baada ya kuvuta pumzi ama kumeza mate, akaendelea Bencov.

    "nimefurahi ama nafurahi kwa sababu nimepata silaha itakayonifanya mimi kulipiza kisasi. ndiyo, ninakisasi kikubwa sana na Taifa dogo la Ungamo, Taifa hili sitalisamehe katika maisha yangu hadi nihakikishe limeangamizwa nami" ilikuwa ni kauli ambayo Dr. Lee hakuilewa kwa asilimia kubwa kubwa sana hivyo ni kama alikuwa na maswali kadhaa kwa kijana huyo mdogo.

    "umekwenda nje ya pale nilipotaka unijibu lakini si nje tu bali pia sijajua kama unaweza kufanya yote mwenyewe kisha uje kuomba msaada kwangu. Nini sababu ya hayo yote?" aliuliza Dr. Lee.

    "najua kuwa ninaswali la kujibu kutoka kwako lakini pia ninasababu za kufika huku nilipofika. Ilikuwa ni lazima ujue sababu za mimi kutengeneza silaha hiyo hatari kwenye maisha ya watu na pili ujue ni kwa nini mimi nimekuja kuhitaji msaada kwako. Kwanza nikwambie tu kwamba silaha hiyo unayoiona ni silaha ambayo madhara yake ni baada ya dakika kumi na tano kisha huleta madhara makubwa kwenye mwili wa kiumbe aliyejeruhiwa na silaha hii. madhara yake huja au hutokea kila baada ya masaa mawili na ifikapo maasaa Sabini na mbili ndipo kiumbe huharibika kabisa na hiyo ni baada ya kupasuka kwa moyo....zimesha fika dakika kumi na tano hebu angalia kwanza" aliongea Bencov kisha akahitaji utulivu ili kuweza kuwapa nafasi wenzake waweze kuona anachokizungumza. Mtu yule aliyekuwa amesimama baada ya kupigwa na ile bastola ya aina yake, alianza kutetemeka taratibu kama mtu ambaye alikuwa akitikiswa. mtetemeko ule ukabadilika ukawa si mtetemeko tena bali ni mtikisiko, alitikisika mwili mzima yule mtu mwisho akapinduka pindu kama Nyati aliyedungiliwa kwa risasi. Akawa anapiga miguu, alikuwa ni kama mtu aliyekuwa akipambana na hatua za mwisho za uhai. Alionesha dhahiri kuwa maumivu aliyokuwa akipambana nayo hayakuwa madogo. Hakuishia kupiga miguu tu bali alianza kupiga kelele mtindo mmoja hadi Dr. Lee mwenyewe akakumbwa na hofu, si yeye pekee bali hata wengine waliokuwa wakitazama ile sinema, walikuwa katika hali ya tofauti mno. Alidumu kwenye kelele zile kwa muda wa sekunde mia moja na thelathini ndipo akatulia tuli. Damu zikachukua nafasi sasa lakini hapo alikuwa halii bali mwili wake ulikuwa ukipanda na kushuka kwa nguvu na kila ulippkuwa ukishuka, ndipo damu zilivyozidi kumtoka. Wakati wakiwa wanaendelea kumshangaa yule mtu, upande wa yule mgonjwa naye mambo yakaanza kuwa magumu. Shida ikaibuka ikawa kama ile ya awali hakuna aliyeacha kugeuza shingo yake na kutazama kule nako. Ukelele mkubwa ukamtoka yule mgonjwa ulikuwa ni ukelele wa ajabu mno.

    "silaha hiyo ilikuwa na uwezo wa kufanya mauwaji ya lile Taifa lakini ingenigharimu sana. Ingenibidi niandae jeshi kubwa na silaha hizi nizitengeneze nyingi kwa ukubwa na nguvu tofautitofauti kitu ambacho kingenifanya nichelewe kutimiza ndoto zangu mapema. Hii ndiyo sababu ya pekee iliyonifanya mimi kuja kuomba msaada kwako wa kuweza kutengeneza sumu au virusi kama itawezekana ili kuliuwa lile taifa kwa mara moja tu na hii silaha iwe ni kwa ajili ya wale ambao wataleta kujua" alijibu swali alilokuwa amelisitisha kijana Bencov. Jibu hili likamfanya Dr. Lee aone kuwa yupo na kijana makini mbele yake na hapaswi kumdharau au hata kudhani anaweza kumgeuka, moyoni akakiri kuwa umoja wao utakuwa na faida kubwa na endapo kweli wakifanikiwa kutengeneza hiyo sumu au hivyo virusi, ni wazi angeweza kuirudishia uhai ndoto yake aliyokuwa akiiota kila siku. Swali ama wazo la kujiuliza lilolomjia kichwani ni je, yeye kama yeye pale amefika mwisho wa kubuni dawa au sumu, ni nani sasa wa kuweza kutengeneza sumu kwa kutumia mchanganyo ambao ameuanza yeye? Hili lilikuwa ni swali lililochukua muda kidogo kwenye kichwa chake likichekechwa na ubongo wake hadi pale jibu lilipokuja kuwa Bencov alikuwa akihitaji tu dawa hiyo ili akaifanyie muendelezo, ni nani sasa anaweza tengeneza hiyo dawa na ilhali yeye akiwa utaalamu huo hana. Hakutaka kuishia kujiuliza mwenyewe tu bali aliamua kumuuliza swali hilo huyo kijana wa Ki rusi.



    "nani atahusika na muendelezo wa kutengeneza hilo angamizo?"

    "hilo lisikutie shaka hata kidogo Dr. Yupo mtu, huyu ni mtalaamu mkubwa sana wa mambo ya Sayansi ya mimea, anauwezo wa kutumia mimea kutengeneza dawa na pia anauwezo wa kutumia hiyo hiyo mimea akatengeneza sumu au kitu kibaya zaidi cha kuweza kuiletea dunia shida. Tulianza kugundua uwezo wa huyo binti, tulipotembelea chuo kimoja cha tafiti na magonjwa ya mimea huko nchini Urusi. Nilimuhusudu sana aje kunisaidia siku moja lakini nilizidi kufanya chunguzi zangu za kutaka kumnasa, nikagundua kumbe anatokea Afrika tana ndani ya nchi husika. Huyo ni binti mdogo sana....!"

    "binti....?" aliuliza kwa mshangao wa aina yake, Dr. Lee, hakuwahi kuamini kama kunaweza kutokea binti akawa ni mzuri kwenye Sayansi yenye faida kubwa kiasi hicho.

    "ndiyo, ni binti mdogo tena ni mtoto wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Taifa la Ungamo" alizidi kufafanua Bencov. Dr. Lee alizidi kushangaa sana. Huyo dkta mwenye uwezo mkubwa kiasi hicho ni binti yaani mtoto wa kike, pia ni zao kutokea Afrika, hili lilizidi kumpa mshangao mkubwa mno, hakuacha mshangao wake uzidi kumshangaza yeye tu bila kupata uhakika wa mambo akazidi kuuliza mzee huyo ambaye muda wote machoni alikuwa amevaa kinyago kilichoyaficha hata macho yake.

    "uanasema anatokea Afrika? Unataka kuniambia kuwa Afrika kuna watu wenye vipawa vya kujua mambo makubwa kama hayo?"



    aliuliza Dr. Lee huku kwa upande mwingine akisahau historia ya maisha yake.



    "ndiyo, ni Afrika. Huyo mtoto sikuwa nikimhitaji sana ila kutokana na kuwa nahitaji kuliangamiza taifa lao wenyewe basi sina budi kwalo ni lazima nimhusishe kwenye hili, ni lazima tumteke ili afanikishe kutengeneza hiyo sumu ambayo itakwenda kulicha taifa lake hoi. Limenikosea sana taifa lile la Ungamo, Ungamo sitakaa niisamehe kwenye maisha yangu yote. Ungamo ilinifanya niishi kwa mashaka makubwa tena bila wazazi, no, nooo, noooo" alisema kwa chuki kubwa sana kijana Bencov alionesha kuwa kuna siri nzito sana baina yake na Taifa la Ungamo.



    "Backa Ramson Backa!" alisema hivyo moyoni, hakutaka sauti yake isikiwe na mtu yeyote pale. Kimya kikatanda tena. Walikuwa wakiitazama tena ile miili ambayo ilikuwa mbele yao ambayo ilikuwa ikivuja damu kama bomba.



    "aiseee!" alistaajabu Dr. Lee baada ya kuyarudisha macho yake kuitazama ile miili iliyokuwa imebadilika rangi na kuwa miekundu kwa damu. Yule mgonjwa ndiyo aliificha kabisa rangi ya mashuka aliyokuwa amelalia na kubaki ikiwa na rangi nyekundu tupu huku sakafu ya mahali hapo ikiwa haitamaniki kwa damu.



    "ndiyo maana nikakuambia kuwa ni hatari sana Dr. Kwani ile sumu inakwenda kusababisha moyo kufeli kusukuma damu, mapigo yake huwa mepesi sana hivyo kupelekea kushindwa kusambaza damu mwilini. Damu itakapokuwa haisukumwi kwenda mwilini, itakuwa inajikusanya kwenye mishipa mikubwa na midogo ya damu. Sasa hapo hiyo kemikali ndiyo inapofanya kazi ya kula misuli hiyo na kufanya damu kumwagi au kubadili mfumo wake wa kazi, hapo ndipo itakapo tika kwenye kila sehemu ya mwili iliyowazi. Itatoka kwenye tundu za pua, kwenye vinyweleo, kwenye mdomo, masikio, macho hata na sehemu za siri. Itakuwa inatoka kwa kasi mno. Tendo hilo linamuweka muathirika katika maumivu ila ndiyo atashindwa kufanya kitu kutokana na damu nyingi kumtoka hivyo ataishia kufanya kama afanyavyo huyo hapo chini" alitulia Bencov akiwa hana hata sura ya tabasamu alikuwa amebadilika sana na alikuwa akipata hasira kubwa mno kila alikimbukapo jina la Backa. Maelezo yale yalikuwa ni ya kushiba mno. Mwili wa yule kijana aliyelala sakafuni ulikuwa hautulii mara ubingilie mara ucheze ilimradi tu kiumbe kile kilionesha kuwa hakikuwa kwenye maumivu madogo.



    "umesema wataishi hivi kwa muda gani?" aliuliza Dr. Lee akiwa amemkubali huyo kijana kwa moyo mkunjufu kabisa. Bencov aligeuka akamtazama huyo mzee aliyeonekana dhoofu wa mwili kisha akajibu kuwa.



    "siku ya leo na kesho ndiyo siku ya maumivu kwao lakini keshokutwa ndiyo itakuwa siku yao ya mwisho kwani ndiyo siku ambayo moyo unakuwa umevimba kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hatua ya kupasuka. Moyo huo utakapopasuka, ndiyo mwisho wa maisha yao lakini kwa masaa yatakayo salia kemikali iliyo mwilini inakwenda kuushambulia mwili wote na hapa watu watazoa mifupa pekee na siyo miili ya watu" alihitimisha Benco. Dr. Lee akabaki kimya tena kama mtoto aliyetishiwa mdudu anayemuogopa kwa kuambiwa kuwa akilia hana bahati. Hapo hakuwa na la kuongeza tena mbele ya huyo kijana alicho kifanya ni kukubali kuwa hakuna tamaa tena hapo bali waungane na kuwa kitu kimoja ili wafanikishe yao kwani hata yeye alikuwa na lake zito ambalo kwa umoja wao watakaouunga anaamini watafanikiwa kwa kiasi kikubwa mno. Kama wasemavyo wengi kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, Lee alihitaji muungano huo ili kuweza kuweka nguvu zao pamoja ili waweze kufanya yote kwa wepesi mkubwa. Watu hao sita walitoka hapo kwenye hilo chumba kubwa wakiwa wanaiacha ile miili ikiwa inashambuliwa na mateso/maumivu na kwenda kwenye chumba kingine kisafi sana chenye kila kitu kwa ajili ya kumpa binadamu raha ya kuwepo hapo. Hewa safi ya humo ndani ilikuwa ikipuliza kwa heshima na taadhima ili kuwafanya watu hao walionawirika kwa ridhiki ya pesa chafu, waweze kukamilisha yale yaliyowapeleka hapo.



    "mh!, mh!" alijikohoza Bencov kisha akamtazama Dr. Lee kabda hajayaacha macho yake kwa mwanadada ambaye tangia kuingia kwa Bencov ndani ya himaya ya Dr. Lee, tabasamu ya tabasamu lilikuwa mtihani.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "sasa tunaweza kuingia kwenye jambo la msingi" alisema Bencov akiwa ameshayahamisha macho yake kutoka kwa Shetani wa kike kisha kuyazunguusha kwa kila mmoja pale ndani. Dr. Lee ndiye aliyekuwa akisubiriwa azungumze kitu mahala pale. Alitulia kwa dakika kadhaa kisha akahema kwa nguvu hadi sauti mithiri ya mtu aliyebanwa na pumu ikamtoka kooni kisha akasema kwa sauti yake ile ya kutokea kooni.



    "weka mezani hiyo ramani ya himaya nzima ya jumba la huyo Backa" Bencov alichukua ramani kutoka kwa kijana wake mmoja akaiweka mezani. Macho ya Dr. Lee yaliipitia ile ramani kwa umakini mkubwa kisha akanyanyua macho yake pasi na kusogeza shingo lake akasema.



    "huyu mtu anaonekana ni tajiri sana, hili eneo ni kubwa mno"



    "ndiyo, ni mtu anayejiweza kupita kiasi, huyo jamaa anapesa ambazo hata kama utaamua kumuibia huwezi kumfilisi. Nakumbuka alitumia utajiri wake kubadilisha muelekeo mzima wa maisha yangu" alijibu Bencov.



    "oooh! Vizuri, haijalishi anapesa kiasi gani au anaulinzi wa aina gani tunachotakiwa ni kumpata binti yake mapema sana ili sisi tuweze kutengeneza hii sumu mapema kwa matumizi bora ya wa afrika" aliongea Lee kama anasimulia wajukuu zake hadithi. Swala likaja ni nani anafaa kuikamilisha hiyo kazi kwa haraka na upesi. Bencov akanadi na kusema vijana wake wapo makini na anawaamini sana hivyo hiyo kazi ataifanya yeye. Dr. Lee akapanda na kusema kuwa ili kuimarisha umoja wao na kuonesha kuwa yuko pamona kwa kila jambo anaomba hiyo kazi apewe yeye ili kumuonesha kuwa hata yeye anavifaa vya kazi. Wakakubaliana kuwa kazi ifanyike hivyo lakini kutokana na Bencov kuwafahamu watu wengi wa nchi ya Ungamo, ajaribu kuwatumia vibaraka alivyovipandikiza huko kwa ajili ya kutoa rai kwa Backa kuwa kwa hiyari yake amtoe binti yake ili kujua ni vipi mtu huyo moyo wake ulivyo lakini pia hapo hapo mtu au watu watakaowatuma wao watakuwa na kazi ya kuchunguza jinsi ya kuvamia ndani ya kisiwa cha waziri huyo wa zamani. Majukumu hayo yakawa hayana mtu wa kuyapinga, walikubaliana na safari ikatakiwa kufanyika siku inayofuata. Jioni ya siku hiyo Merina au Shetani wa kike alikuwa ndani ya chumba chake ambacho mara nyingi huwa humo akiwa ametulia kimya. Alikuwa amekaa kwenye kiti kikubwa cha thamani ya juu sana huku akiwa ameweka gilasi ndefu iliyojaa mvinyo. Miguu yake aliikunja kwa ustadi mkubwa hakuonekana kuwa ni mtu mwenye wasiwasi au mashaka, alionekana ni mtu ambaye alikuwa ameamua kugida mvinyo huo ili akaukabidhi mwili wake kitandani ili siku inayofuata aweze kuamka mapema. Aliikamata gilasi ile kisha akapeleka kinywani taratibu kwa pozi za kike, akapiga funda moja jepesi kisha kuirudisha tena mezani. Akaigamia kiti kile ambacho hata kulalamika kuwa kinaumia ama laa kilishindwa, kilizidi kuubeba mwili huo uliovikwa mabazi mepesi yaajabu ya kulalia ambayo yalikuwa yakionesha kila kilichovaliwa ndani. Bikini nyeupe ilionekena dhahiri mara tu binti huyo anaposimama. wakati akiwa anaendelea kupata hicho kinywaji chenye kilevi, mlango wa kuingilia humo ndani ukafunguka kisha baiskeli ya matairi matatu ikaingia. Hakuwa mwingine bali alikuwa ni bosi wake ambaye alipofika hapo alisimama kwa ghafla sana.



    "my Lady Devil" aliita huyo mzee. Merina aliishusha ile gilasi ambayo alikuwa ameishika mkononi kisha akanyanyua macho yake kumtazama huyo aliyemuita.



    "tungetumia njia ndefu sana hadi kufika kwenye lengo letu lakini kwa hili kila kitu nadhani kitakuwa rahisi" aliaema Dr. Lee.



    "kwanini Boss?" aliuliza Merina.



    "sisi ingetubidi kuingia Tanzania kwa njia ya kusafirisha madawa ya binadamu pamoja na mifugo. Namaanisha kwamba ingetakiwa sisi kupandikiza madaktari wetu kwenye kila hospitali ya Tanzania. Hii ingetutaka kutumia muda mrefu sana wa kulimaliza na pia tusingeweza kuwamaliza wote wajinga wale. Kuja kwa huyu kwetu ni jambo zuri sana na itatupunguzia gharama, tutakapoingia Ungamo tuatahakikisha tunafanya chini juu tuingie Tanzania. Huyo binti anaumuhimu sana kwetu" alisema Dr. Lee huku shingo yake iliyolegea ikiwa imeegamia upande wa kushoto kama ada.



    "unajua unachotakiwa kufanya Merina ukifika Ungamo kwanza ni kuweka kambi ya muda, uchunguze na uapate njia rahisi ya kuweza kuvamia na kuondoka na huyo binti. Bencov atafanya kama tulivyokubaliana pale, hiyo ndiyo itakayokufanya wewe kuweka kambi ya muda huko...nikutakie safari njema yenye mafanikio hapo kesho" alihitimisha Dr. Lee kisha akaondoka mule ndani akimuacha binti yule akiwa anajimiminia kinywaji tumboni mwake taratibu.



    *****

    *****

    Sigara kubwa la gharama lilikuwa likitoa moshi mwepesi mara baada ya kushushwa kutoka kinywani mwa mtu mwenye sifa au waweza sema mtu mwenye kujisikia sana. Moshi mwingi alikuwa akiutoa kutoka kinywani mwake taratibu. Bacon. Ni siku moja baada ya kurudi ndani ya nchi ya Ungamo akitokea Urusi. Mbele ya bwana huyo mwenye sifa na majigambo, kulikuwa na binti mrembo akiyekuwa amejichafua sura yake huyu ni Dede. Bacon alipiga pafu moja kubwa jingine na kuvuta moshi ndani ya mapafu yake kwa kiasi kidogo kisha wote uliobakia kuutoa mdomoni na puani. Akaishusha ile siger na kuikung'uta jivu kwenye chombo maalumu cha kuwekea majivu kisha akamtazama huyo binti.



    "Dede, najua huna furaha kabisa kutokana na kuchelewa kurudi kwa Benson?" aliuliza swali jepesi Bacon. Dede hakujibu kitu alinyanyua macho yake juu na kumtazama kiongozi wake wa kazi. Kabla hata hajasema kitu chochote, Bacon akaendelea.



    "Benson yupo kwenye mpango mwingine na mpango huo uko chini ya mkuu wetu ni mpango wa kuziacha hoi nchi hizi za kiafrika" alitulia kidogo akavuta tena pafu jingine na kutulia akisubiri ule moshi usambae kwenye ubongo wake na kumpa raha.



    "mpango? Mpango upi huo?...inamaana siyo ule ambao tulitumwa na mkuu?" aliuliza mfululizo Dede.



    "ni ule ule ila huu uko na nguvu za watu wawili, mkuu ameungana na Dr. Lee. Umoja wao ndiyo utakaoweza kuturahisishia sisi kumaliza kazi hii mapema" alisema Bacon. Dede akawa bado anamashaka na kitu alichoambiwa hakukielewa kwa asilimia kubwa. Alikuwa na maswali ya kuuliza lakini muda ulikuwa ni mdogo sana hakupata nafasi hiyo kwani Bacon alipigiwa simu na kutakiwa mahali.



    Ilikuwa tayari ni jioni, muda ambo Backa aliuona ni muda wa pekee sana kwake ni muda aliokuwa akifurahi na binti yake baada ya binti huyo kufanikisha kuimaliza kazi yake ya kutengeneza dawa ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa mataifa masikini. Kulikuwa kumeandaliwa hafla fupi kwa ajili ya kufanikisha hilo. Watu wachache lakini wakubwa kidogo na wenye pesa zao walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kuutendea haki mualiko walioupata kutoka kwa tajiri mwenzao.



    "nisema asanteni sana kwa kuweza kufika hapa kwa ajili ya kumpongeza binti yangu kwa kuweza kufanikisha kile ambacho kitakuwa ni msaada na faida kubwa kwenye nchi zetu hizi masikini"...



    alizungumza Backa baada ya kukabidhiwa kipaza sauti na mshehereshaji wa hafla hiyo ndogo. Aliwatazama wageni waalikwa walipo hapo kisha akakisogeza tena kipaza sauti karibu kabisa na kinywa chake akasema.



    "nitakuwa sijafanya la maana sana kama sitakushukuru muheshimiwa Ndungai kwa kuweza kuhudhuria kwenye sherehe hii. Umekuwa ni mtu mwenye majukumu mengi sana lakini kwenye hili umekuwa ni mualikwa pekee uliyefika mapema mno, hii inanipa imani kuwa niko pamoja sana na marafiki zangu" makofi yakapigwa kwa shangwe kidogo kisha kimya kikafuatia. Backa akasema.



    "wapi alipo Tereza, ni vema nimkabidhi kipaza sauti mlengwa ili aseme machache. Tereza alisimama, macho ya watu wote pale yakamtazama yeye, shangwe likaibuka, vifijo na nderemo vikazoa ile nafasi iliyopewa na huyo waziri wa zamani. Kila mmoja pale alikuwa na furaha sana kumuona binti huyo.



    "ni muda mrefu sikupata kumuona huyu binti amekuwa sasa" alijisemea moyoni mzee mmoja mwenye tumbo kubwa, mashavu makubwa na macho yaliyotoka nje kidogo. Alikuwa akifurahi muda wote kwenye ile hafla na huyu ndiye mzee ambaye alionekana akinyanyua mkono juu baada ya kutajwa kwa jina lake na mh. Backa. Tereza alisogea hadi ilipo meza kuu kisha akatoa salamu baada ya kukabidhiwa kile kipaza sauti kisha akavuta pumzi ndani na kuzitoa taratibu.



    "asanteni sana wageni waalikwa kwa kuweza kufika hapa mapema na kuifanya shughuli hii mubashara kufanyika kwa wakati husika, sina kikubwa cha kuwalipa zaidi ya kusema asanteni sana. Kabla sijakwenda kwenye pointi muhimu, niseme jambo moja la muhimu sana kwangu. Nampenda sana baba yangu, nampenda sana kwani baada ya kifo cha mama yangu yeye ndiye aliyehakikisha nakuwa na furaha kila wakati hii inanifanya nijione kama niko na wazazi wangu wote wawili." aliweka kituo hapo Tereza kisha akamgeukia baba yake aliyeko upande wa kuumeni kwake akasema.



    "Mungu akupe maisha marefu baba yangu, mungu akulinde na maadui mh. Backa" kisha akayarudisha macho yake kwa watu waliyoko mbele yake akaendelea.



    "nilikuwa ninandoto kubwa sana ya kuweza kulisaidia taifa langu la Ungamo kwa kutengeneza kitu chenye faida kutoka kwenye elimu yangu. Tangu wakati nipo New Youk nchini Marekani kwenye chuo kimoja cha Sayasi ya mimea ambako ndiko nilikoanza safari ya kuutafuta ujuzi huo kabla sijakwenda nchini Urusi, niliapa kuhakikisha kuwa elimu yangu inakuwa ni kwa ajili ya taifa langu. Niliishi kwa kushinda maabara kwa muda wa miezi mitatu kama siyo minne baba yangu Ramson anajua" alicheka kidogo alipofika hapo. Kimya kilikuwa kizito sana mule ukumbini.



    "sikukata tamaa, niliumiza kichwa na fikira zangu kwa ujumla, nilifanya majaribio mengi hadi nikafanikiwa. Kikubwa kilichopelekea ujio wenu hapa ni kutaka muipatie jina dawa hii ambayo ni zaidi ya mbolea zote mnazo zifahamu ninyi lakini kabla ya jina niwape sifa japo kwa ufupi tu uwezo wa dawa hii. Inauwezo wa kuinyanyua mimea iliyokata tamaa kwa kuzidiwa na ukali wa jua, inauwezo wa kuunawirisha mmea kwa kutumia unyevunyevu wa usiku mkubwa tu bila hata mvua, hii inamaana kuwa hata kama mvua ikigoma kunyesha kwa kipindi kirefu, bado kunauwezekano mkubwa wa kuvuna mazao ya kutosha. Ni faraja kubwa sana kwangu kwani ninaimani nimekwenda kuipa Afrika dawa na kitu pekee cha kuwafanya wana wa Afrika wasilie tena kwa kukosa chakula" alinyamaza, makofi mengi yakarindima, furaha ilikuwa kubwa sana iliyopita kipimo.



    "hakuna kitu kizuri kama hicho ambacho umekileta kwetu na umekuwa ni binti mzuri kwetu pia kabla hata haujafikiria kuiingiza hiyo dawa mtaani" alisema kijana mmoja ambaye alikuwa amekaa pembeni kidogo ya kile chumba cha sherehe. Alikuwa kama amejitenga lakini alikuwa ni moja kati ya wafuatiliaji wazuri tu.



    "Backa hapa umezaa, umelea pia" alisema yule bwana mwenye tumbo kubwa na macho makubwa, aliyefahamika kwa jina la Ndungai ilikuwa ni kwa sauti ya chini mno. Jina la hiyo dawa likapendekezwa na watu wengi wakaliafiki, binti yule akatoka pale mezani na kumpisha baba yake ahitimishe.



    "Asanteni sana kwa kuweza kuifanya hafla hii fupi ifane, niwashukuru wote kwa ujumla pia niseme tu umoja na ushirikiano wenu ndiyo uliozalisha jina la dawa ambayo ni muhimu kwa maisha yetu. Jina limepokelewa vizuri na wengi wa wananchi wa Ungamo watakuwa wanaongea lugha moja hivi karibuni. DATU (Dawa ya Taifa la Ungamo). Ni jina la Taifa hili japo mwenyewe atalipa jina la kisayansi. Nadhani niseme tu asante sana kwa mara nyingine" alihitimisha mh. Backa. Shughuli ikafungwa rasmi na watu wakatawanyika. Baada ya watu wote kuondoka, alibaki Mh. Backa, Tereza, Mr. Ndungai pamoja na kijana wa mzee Ndungai, huyu ndiye yule aliyekuwa ameonekana kujitenga kidogo. Walikuwa wanashuka ngazi kuelekea kwenye fukwe kubwa na ya kifahari sana ya mzee huyo, fukwe inayovutia kukaa na kupoteza mawazo. Upepo mwanana wa fukwe hiyo ulipelekea kuleta hali ya kipekee sana ya lile eneo. Walijigawa makundi mawili, mr. Ndungai alikuwa yupo na mzee mwenzie wakiwa wanateta jambo huku Tereza akiwa na kijana mtanashati wa mr.

    Ndungai.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "hongera sana Tereza kwa kuweza kufanikisha ndoto zako, wewe ni mwanamke shujaa sana, jina lako limekuwa ni la kipekee sana" alitoa pongezi huyo kijana huku wakiwa wanatembea pembezoni mwa maji ya bahari.



    "asnte sana Tamimu.....ni Tamimu eenh!?" alishukuru Tereza huku akiwa hana uhakika na jina alilolitaja kama kweli ni la kijana huyo.



    "ndiyo ni Tamimu, unanikera sana ukijifanya kulisahau jina langu. Kemikali zinakupa uchizi si ndiyo?" alileta mzaha Tamimu, wote wakaangu kicheko.



    "oooh! Vizuri, unajua baba yangu amekuwa mstari wa mbele kwa kila kitu kuhakikisha kuwa nafikia malengo yangu, amejitoa sana yule mzee. Mungu ampe maisha marefu kwa kweli" alisema Tereza.



    "baba yako ni kama baba yangu, baba yangu amekuwa ni mtu wa kuangalia kipawa cha mtu kiko wapi kisha hukikuza. Mimi nilikuwa mtundu sana wa kukimbiza magari na nilipenda sana kuangalia mbio za magari kupitia mitandao hata muda mwingine kutoroka nyumbani na kwenda kushuhudia mashindano. Baba akagundua kuwa nilikuwa na kitu cha ziada kwenye mambo ya magari hivyo alichukua jukumu la kuhakikisha naendeleza kipawa changu. Alinipeleka nchini Marekani huko akanikutanisha na rafiki yake ambaye alikuwa ni raia wa kule. Huyo mzee alikuwa ni mtu mkubwa naweza sema alikuwa ni mmiliki wa kampuni kubwa ya Ferrary. Nikawa chini ya ile kampuni, tulikuwa wengi na kila kijana alikuwa akihakikisha anaonesha kipawa chake ama uwezo alionao. mimi nilikuwa hodari sana kwenye kukimbiza gari. Nilidumu pale hadi nilipofanikiwa kuwa na jina kubwa sana kwenye ile kampuni lakini sikuendelea kuwepo pale nilihitaji kuwa na kampuni yangu mwenyewe ya kutengeneza magari yaendayo kasi" alikomea hapo huyo kijana.



    "unamaanisha kuwa umefanikiwa kutimiza ndoto zako pia?" aliuliza Tereza huku wakiwa wamesimana chini ya mti wa mkoko uliostawi na kumwaga kivuli cha kuvutia.



    "ndiyo, kwasasa mimi nina kamapuni yangu inayokwenda kwa jina la TAMIMU NDUNGAI. RACE (TN. RACE). Gari zote zinazotoka chini ya hiyo kampuni zina nembo hiyo" alisema Tamimu. Tereza alimpongeza sana huyo kijana. Walitazamana kwa muda mrefu sana vijana hao ambao historia yao ni kubwa mno. Katika kutazamana kwao kuna kitu walikumbuka, waliwahi kuishi pamoja kama ndugu kipindi hicho cha nyuma wakiwa bado ni vijana wadogo. Hicho ndicho kilichowafanya kutazamana na kucheka kwa hisia za kweli.



    "ni jukumu letu kama wazazi kuhakikisha ndoto za vijana wetu zinatimia, niliiga kila kitu kuotoka kwako, nami nimefanikiwa kutimiza ndoto za kijana wangu Backa. Sasa ni muda wa kuona vijana wakiwa na furaha maana tumesha wavusha kwenye mto mzito na sasa ni wao tu na kufanya kile ambacho kilikuwa kimelala kwenye damu zao" alikuwa ni mr. Ndungai akiongea maneno hayo. Walikuwa wamesimama kwenye mchanga mwingi wa fukwe hiyo huku macho yao yakiwa yameelekea kule ambako vijana wao wapo. Walikuwa katika furaha kubwa na ya aina yake.



    Furaha ya kweli huleta amani ya moyo, moyo hupata amani pale sura yako inapokuwa imekusanya furaha na kuifanya kuwa ni miongoni mwa vitu vya msingi na vyenye thamani kubwa kwenye maisha yake ya kila siku. Ishi na furaha ili moyo ubakiwe na amani. Amani inapozidi huupa mwili afya ya kweli na kukufanya uishi kwa kujiamini katika maisha yako yote. Nani asiyependa kufurahi na ni nani asiyependa moyo wake ubaki na furaha? Furaha inahitajika kwenye maisha yetu, ni jukumu letu kuhakikisha tunaizaa, kuilea na kuikuza furaha ili ibaki nasi, hapo tutakuwa tumeupa moyo amani nasi kunawirisha miili yetu.



    Ninapoizungumzia furaha ninamaana kubwa sana. wawili wanapokutana na kuongea lugha moja yenye kueleweka nikiwa na maana kuwa wawili wenye kuelewana kwa lugha Moja......





    pia wakawa ni wenye kujadili mambo ya msingi yenye kujenga, huweza kuizaa furaha ya aina yake. Tereza na Tamimu walikuwa ni watu wenye kuelewana tangu wakiwa ni watoto kabisa, hawakuwahi kukwazana na kama ipo siku ambayo mmoja akatokea kumkwaza mwengine, huwa wepesi kuombana msamaha. Ukaribu wao wa muda mrefu ndiwo uliopelekea kuwa wamoja, elimu yao, hata ufahamu wao mkubwa ulikuwa kama ni wenye kulingana. Elimu pekee ndiyo iliyokuwa ikiwafanya wao kuishi mbali bila kuonana, sasa Tamimu amekuwa ni kijana mwenye uwezo mkubwa kifedha huku Tereza naye akiwa ni binti anayeukimbiza utajiri mkubwa pindi tu atakapoiingiza dawa yake mpya aliyokuwa akiitengeza kwa siri kubwa hii ilikuwa ni dawa ya ukuzaji bora wa mifugo kupitia mimea. Ilikuwa ni dawa ya pekee sana ambayo kama ataanza kuitangaza ingeweza kumpa utajiri mkubwa sana duniani. Dawa hiyo aliipa jina la Diet Pills (DP). Ilikuwa ni dawa ya pekee mno ambayo kwa asilimia kubwa ilikuwa ikienda kuwanufaisha wafugaji kote duniani lakini pia wakulima watakwenda kunufaika nayo, ni dawa ambayo aliipa jina hilo la Chakula Dawa kwa kuamini ni dawa ya pekee ambayo mfugo wowote utakuwa unaipata dawa hiyo kupiti chakula ambacho kinatoka kwenye aina yoyote ya mmea baada ya kuchanganya. Dawa ambayo itafanya mifugo isisumbuliwe na magonjwa ya aina yoyote ile pindi mnyama apewapo angali bado hajakumbwa na maradhi. Na kwa upanfe nwingine akitumia malighafi hayo kuunda mbolea ambayo aliipa jina hilo. Kwa pamoja walijikuta wakitazamana kwa tuo kubwa, macho yao yakanena jambo midomo haikupewa nafasi ya kutamka japo neno. Wakati wao wanafanya vile, kwa upande wa wazazi wao, walikuwa wakiwatazama hatua kwa hatua bila kujua kama walikuwa wakitazamwa. Wao walizidi kuwa karibu kwa kutazamana hadi pale Tamimu alipoanza kuzungumza.



    "nilikusubiri kwa muda.........!" hakusubiriwa amalize maneno hayo, neno nilikusubiri lilitosha kumpa taarifa Tereza kuwa hilo lililotaka kuzungumzwa hapo ni jambo ambalo si dogo. Tereza alimuwahi Tamimu kwa kumuwekea kidole chake cha shahada mdomoni mwake akiwa anamtaka asiseme kitu. kisha akamsogelea na kumkumbatia.



    "ni muda mrefu sana Tamimu nilikuwa nikikusubiria, unadhani yale maneno yako ya zamani mimi niloyachukulia mzaha? Niliamini unamaanisha" alisema Tereza akiwa amemkumbatia kijana huyo. Pumzi zao zikatoka na kupotelea kwenye hewa kila mmoja alikuwa akiutazama mgongo wa mwenzake kupitia mabegani, kwa urefu walilingana, hakika walivutia kuwatazama.



    "nakupenda sana Tereza, naomba huu uwe ni mwanzo wa mimi na wewe lakini uwe ni mwanzo wa kutokuja kutengana, uwe wangu kwenye kila njia utakayopita nami niwe nawe kwenye kila hali ya furaha, karaha na mashaka hadi amani ya kweli ije" yalikuwa ni maneno mazito mno kutoka kinywani mwa Tamimu. Maneno hayo yalimfanya Tereza kujitoa kwenye kifua cha kijana huyo kisha kumtazama usoni kwa muda kidogo. Alimtazama sana hadi kutotaka kuamini kama maneno yale ya kishujaa yalikuwa yakitoka kwenye kinywa cha kijana huyo.



    "nakupe.....?" nafikiri alitaka kusema neno nakupenda lakini kauli ile ilizibwa na kinywa cha Tereza kilichouvamia mdomo wake na kuanza kupeana ladha tamu ya kinywaji asilia kitokacho kwenye viywa vyao. Wazee wao waligeuka na kuwapa mgongo vijana wao.



    "nadhani maneno yangu yametimia Backa, nilikuambia kuwa kijana wangu ndiye atakayeoa binti yako" alizungumza mr. Ndungai, mzee mwenye tumbo kubwa na macho makubwa lakini yaliyo na weupe wa kung'aa ndani yake. Alisema huku akiwa ameliweka tabasamu pana lililokuwa limeyavimbisha mashavu yake makubwa kiasi.



    "unahaki ya kujivunia sasa, unamuingiza binti mpole na mpenda watu kwenye ukoo wako" alisema Backa. Cheko kubwa likawatoka wazee wale lilikuwa ni cheko la furaha kubwa. Backa alitaka kunyanyua mdomo ili kusema jambo lakini simu yake ya kiganjani ikamuita. Akaitoa mfukoni na kuipokea japo jina la mpigaji halikujiandika kwenye kioo cha simu ile. Akaitundika sikioni mwake pasipo kuongea jambo, alikuwa akiisikiliza sauti ya mpigaji. Mara sauti nzito ikakita kwenye ngoma za masikio yake.



    "habari yako muheshimiwa?" ilisalimia sauti hiyo.



    "nani mwenzangu maana namba yako haipo kwenye orodha ya watu wanaoishi kwenye simu hii?" aliuliza Backa nae ili kutaka kujua.



    "hah!, hah!, hah!. haaaa! Nilijua tu utauliza, namba yangu kama utapenda unaweza kuihifadhi kwenye simu yako maana nitakuwa nikikupigia kwa kipindi hiki kifupi" alisema mtu wa upande wa pili wa simu bila kutoa jibu la swali aliloulizwa. Backa ikabidi kuuliza tena swali hilo hilo kwa mara nyingine la ni nani wewe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "usitake kumjua mtu ambaye hapendi kujulikana, bora mimi nakujua inatosha" ilisikika sauti ya upande wa pili wa simu.



    "aaaalaaa! Mbona......!"



    "nisikilize kwa umakini muheshimiwa wa zamani" ilikazia hiyo sauti na kuikatisha kauli ya kuchanganyikiwa ya mh. Backa kisha ikaendelea.



    "tunakupa siku tatu tu za kuchagua, hiyo ni moja pili kwenye hilo hilo neno kuchagua, tuanataka ujue kuwa si kuchagua kumtorosha binti yako laa!" ilizidi kuibadilisha hali ya Backa hiyo sauti.



    "tunamtaka binti yako kwa muda huo wa siku tatu kwa hiyari yako mwenyewe, kama itashindikana basi huwenda tukakupa siku nyingine tatu za maumivu labda tutakuwa tumeridhisha nafsi zetu. Kumbuka ni siku tatu tu" ilisisitiza sauti hiyo kisha simu kukatika. Backa alibaki kinywa wazi hakupata jibu wala neno la kuongeza mahali hapo. Nini kimejiri? Likawa ni swali la mr. Ndungai. Bado Backa alikuwa ni kama mtu aliyekumbwa na jambo baya kabisa na kweli lilikuwa ni baya kupitiliza.



    "hii simu ni kutoka wapi Backa mbona hutaki kuongea" alizidi kuhimiza Ndungai aambiwe kitu ambacho mzee mwenzie kimemchanganya ghafla namna ile. Backa hakujibu kitu alichokifanya ni kumkabidhi simu mwenzake mkononi. Ndungai aliitazama ile simu kwenye upande wa namba zilizotumika tayari, alikutana na namba ya ajabu sana, namba aliyokutana nayo ilionekana kuwa ni namba eidha inayotumika kwenye kampuni fulani au taasisi. zilikuwa ni namba tano tu. Macho ya kuuliza yakamtoka Ndungai,



    "mbona hii namba ni ya kampuni ama shirika fulani, kamapuni yake moja imepata matatizo?" alijiuliza hivyo Ndungai kutokana na hali aliyoionesha Backa. Ndungai akajaribu kuipiga hiyo namba labda apate kujua shida ni nini lakini kilichotokea ni kusikika kwa sauti za tip!, tip!, tip!, kuashiria kuwa hakuna majibu yoyote. Ndungai akajikuta akiishusha ile simu kama anayetaka kuitia mfukoni huku macho yake ya kumuuliza mwenzake kulikoni yakiwa yamefotoka fotoo!



    "unanichanganya sasa Backa kama hutaki kusema" aliongea kwa kuchoshwa na hali ya Backa ya kuwa katika hali ya sintofahamu muda wote.



    "wanamtaka Tereza wanasema" alijikuta akisema hivyo, nasema alijikuta akisema hivyo, kwa sababu sauti yake aliitoa akiwa amejichokea chokee!



    "hah hah hah haaa! Backa wewe ni mtu mzima sasa unatishiwa vipi na vitoto vidogo vilivyokosea namba eenh?" alisema kimzaha kabisa Ndungai pasipokujua kucheka kwake kunaweza kumfanya mwenzake alie. Backa alimtazama Ndungai kwa macho makali na yenye mshangao kisha akasema.



    "hivi ni kweli mtu aliyekosea namba huwa anamtaja mtu au ni vipi, ni kweli mpigaji hakujitambulisha zaidi ya kutoa vitisho lakini mbona amesema wananifahamu? Ni kweli watakuwa wananifahamu hao jamaa Ndungai usidharau"



    "hakuna kitu kama hicho, tabia ya watoto kuchezea simu za wazazi wao imekuwa kwa kiasi kikubwa sana za utandawazi, hivyo hata hiyo inaweza kuwa ni hao hao tu" aliongea Ndungai. Backa akaliona hilo lina mantiki kidogo na inawezekana ni kweli alisemalo mzee mwenzake. Hawakuhitaji kuendelea kubaki hapo tena, wakachukua uelekeo wa kurudi ndani. Walikuwa wamewaacha vijana wao wakiwa bado wanayafurahia mahusiano yao yaliyochipua upya. Ndungai alikuwa ametangulia mbele huku Backa akiwa nyuma. Mawazo ya kuwa eti, ni watoto wanaochezea simu za wazazi wao ikamjia, akakumbuka sauti ya yule mtu wa upande wa pili wa simu aliyempigia. Alikuwa ni mtu aliyemiliki sauti nzito iliyodhihirisha kuwa hakuwa mtoto, sasa kama hakuwa mtoto, inamaana mtu huyo alikuwa katika kumaanisha. Mh! akagumia huku akipanda ngazi hadi juu kabisa ya upande mwingine. Walipofika ndani tu, haukupita muda mrefu wale vijana wakawasili. Backa akaikunjua sura yake kwa tabasamu ili kumficha binti yake kutojua chochote lakini Tamimu aligundua kitu, hiki kikamjengea mashaka kichwani mwake lakini hakutaka kujionesha kuwa alikuwa amegundua kitu.





    "baba nadhani mimi niwaache natakiwa kuwahi ofisini jioni hii ili nikaweke mambo sawa kwa nitakayemuacha pale maana kesho naweza kusafiri" aliongea Tamimu. Backa na baba yake wakawa hawana kitu cha kuzuia ikabidi kumruhusu.



    "naomba Tereza anisindikize nadhani nitamrudisha mida ya saa moja hivi za usiku" alisema Tamimu huku akiwa anamtazama moja kwa moja Backa usoni, alijua huwenda baba wa binti yule hakufurahishwa na ukaribu wake na Tereza hivyo akawa na wasiwasi wa kutopewa ruhusa ya kusindikizwa. Ndungai alimtazama Backa aliye katika wakati mgumu wa kuamua je, binti yule amruhusu ama akatae lakini hakuwa na neno la kupinga alicho kifanya ni kutoa rai kuwa ahakikishe anamrudisha nyumbani akiwa salama. Wakaondoka wale vijana lakini Tamimu akawa anajiuliza mambo mengi sana kichwani mwake kuhusu baba wa mpenzi wake.



    "kutakuwa kuna kitu si bure hii" alijisemea moyoni. huku wakiwaachwa wazazi pekee waliokuwa katika hali ya kufarijiana tu hadi muda ambao Tereza anarudishwa nyumbani. Ndungai aliaga kisha kutoka na kijana wake hadi kwenye Helkopta iliyowaleta hapo kisha rubani wao akafanya yake, Helkopta hiyo ikatembea na hewa.



    USIKU NDANI YA JIJI LA PANDE.



    Kwenye jumba moja la orofa tatu ama nne hivi. Kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa na mwanga hafifu sana, kulikuwa na watu watatu. Wawili kati ya hao, walikuwa ni watu wakubwa wenye miili iliyoshiba kupita kawaida ila mmoja alikuwa ni kimbaumbau kama mtu kutoka Somalia. Unaweza kusema labda alikuwa ni dhaifu sana kiafya au kipesa pia la hasha! Alikuwa na pesa lukuki za kuweza kumfanya kuishi maisha yale ayatakayo ndani ya jiji hilo kubwa la Pande. Kulikuwa kuna kitu ambacho kiliwakutanisha watu hao humo ndani na ilikuwa ni kwa siri sana. Wawili walikuwa wamekaa kitandani lakini huyu mmoja alikuwa amesimama, huyo aliyesimama alikuwa ni yule kimbaumbau.



    "kazi ya mkuu nimekwisha kuianza" alisema yule kimbaumbau kwa sauti iliyokinzana na mwili wake, alikuwa na mwili mwembamba na mrefu sana lakini sauti yake ilikuwa nzito kama ya Simba dume anayetaka kuteka himaya.



    "hilo ndilo nilikuwa na mashaka nalo" alisema mtu mmoja kati ya wale wanene.



    "umempa siku ngapi za hiyari?" aliuliza yule mwingine mnene ambaye unene wake ulimzidi huyu wa awali.



    "siku tatu tu kama ambavyo mliniagiza na tatu za maumivu kama akikaidi hiyari" alitamba yule mtu huku akiwa amesimama kwa mtindo wa kutanua miguu ili kuufupisha kidogo urefu wake angalau awe karibu na wenzake kimaongezi.



    "lakini hujamwambia kuwa hizo siku tatu za maumivu atakwenda kumkosa binti yake pia"

    "haikuwa na haja yakumwambia hivyo kwani hata huko kumkosa bibti yake ni maumivu yaliyokusudiwa" alizidi kuunguruma yule bwana mwembamba mwenye sauti nzito.



    "ok, ni vizuri, kingine cha kuongezea ni kwamba kesho asubuhi unatakiwa kwa mh. Rais mstaafu, nyumbani kwake kuna jambo anataka kuteta na wewe" alisema yule mnene kuliko mwenzie kisha kila mmoja akatulia na kunyanyuka, wakatoka mule ndani na kumuacha yule mwembamba pakee. Baada ya kuhakikisha yuko mwenyewe, aliuelekea mlango na kuufunga, akarudi kitandani ambako alijilaza chali ili kulipisha giza, liupite usiku ulioficha.



    Pilika pilika za jiji zilikuwa zikiendelea taratibu, watu wengi walikuwa wakiitendea haki siku hiyo mpya kwa kufanya kazi kwa kujituma. Magari yalikuwa yakipiga honi kila baada ya sekunde kadhaa. Foleni ilikuwa kubwa mno kiasi cha kufanya watu kujiuliza kuna nini mbele, hilo lilikuwa ni jambo jipya kupata kutokea kwenye barabara ya T.H kuelekea Muavengero. Honi sasa zilizidi zilikuwa si zile ambazo watu wengi walikuwa wakizisikia hapo mwanzo. Foleni ile ikawa imesimama kabisa hakuna gari hata moja ambayo ilisogea mbele.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " kuna nini kwani?" aliuliza dada mmoja aliyekuwa amekaa siti ya nyuma.



    "hata sijui lakini naona bila shaka kuna kitu siyo bure" alijibu dada mwingine huyu alikuwa ni wa pembeni yake. Jibu hilo halikumfurahisha hivyo akataka kusimama ili kuona kile ambacho kinasababisha foleni hiyo. Akajikuta akipokea maneno makali kutoka kwa abiria mmoja ambaye alikuwa amesimama baada ya kumkanyaga akajikuta akirudi chini bila matarajio yake. Kitu pekee alichokifanya ni kumuomba dada aliyekaa upande wa dirishani afungue dirisha ili waweze kusikia sauti za huko nje, yule dada akatii dirisha likafunguliwa. Zogo kubwa likasikika kutokea nje sasa. lilikuwa ni zogo kubwa kweli tena huku watu mbalimbali wakikimbilia huko ambako zogo lilikuwa likiwavuta.



    "mtoeni huyooooooo!, mpigeniiiiii! Ndiyo kawaida yake anajifanya kichaa kumbe ni mzima tu!" hizo ni miongoni mwa sauti zilizokuwa zikisika huko nje ya gari alilokuwa amepanda huyo binti ambaye alikuwa na shauku ya kutaka kujua ni nini kimetukia.



    "konda hebu fungua mlango nichukue bodaboda siwezi kuendelea kuwepo hapa nina kazi za watu zinanisubiri" alizungumza dada mmoja aliyekuwa kwenye siti iliyo karibu na mlango, kondakta akamwambia kuwa ashike nauli yake mkononi kama ni vipi. Dada yule hakuwa na ajizi alitoa kiasi cha pesa kinachotakikana kisha akashuka baada ya gari kusimama na mlango wa hiyo gari kufunguliwa. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa kwa konda yule kwani hakukuwa na abiria ambaye alibaki mule ndani akijikuta ameambulia kichwa kimoja tu kilicholipa nauli ndani ya gari zima. Kundi lile likakimbilia mbele zaidi ambako tukio lilikuwepo, watu walikuwa wengi mno lakini kitu cha pekee kilicho acha watu wengi kusahau majukumu yao kwa muda, ni kuhusu mtu aliyeonekana dhahiri kuwa ni kichaa ama mwendawazimu kwa jina zoelefu. Alikuwa amekaa katikati ya barabara akilia kwa uchungu mkubwa kitu alichokuwa akizungumza ni kuwa 'niacheni nife, kwanini mmenicha niendeshe gari bila break, mlikuwa mnajua nyinyi madhara, kama mlikuwa hamjui basi mlikuwa mnamakusudi yenu. Haiwezekani nibaki mimi tu wakati wenzangu waliuwawa kwenye ajali' maneno haya alikuwa akiyatoa kama wimbo fulani kiasi cha watu kuto kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikizungumzwa na huyo chizi. Kijana mmoja mtanashati alijitokeza na kwenda kujifanya kumtoa pale kwa kutumia uzoefu wake na nguvu alizobarikiwa nazo na maulana huku akiongea maneno makali ya unatuchelewesha watu tuna kazi zetu. Alijua labda yule kijana ama mtu wa makamo aliye na biashara zake za kuendelea kutamba ngonjera azijuazo mwenyewe, alikuwa yupo pale kama muigizaji tu. Alimsogelea na kutaka kumshika mkono ili kumtoa. Yule kijana mtaka sifa mbele ya kadamnasi, alijikuta yeye akiwa ni zaidi ya mjinga na majuto makuu kumkuta, alipokea pigo moja maridadi lililopigwa kiufundi sana. Alipinduka chali watu wakabaki wakishangaa, aibu kubwa ilimkumba yule kijana damu zilikuwa zikimchuruzika kutokea puani.



    Lakini wakati hayo yanaendelea asubuhi hiyo, kule kwenye kile chumba cha hoteli ambacho usiku uliopita kulikuwa na kikao ambacho siyo rasmi, yule kijana mwembamba mwenye sauti nzito alikuwa ameshakiacha chumba kile kwa umbali mrefu sana. na kwa wakati huo alikuwa akiingia kwenye jumba kubwa huko Muavengero Kaskazini. Moja kwa moja alijitoma ndani bila kuulizwa na mlinzi wa aina yoyote ile hadi kwenye chumba kimoja. Huko alikaribishwa na kukaa kwenye kiti mbele yake kukiwa na mtu mweusi mwenye nywele za kutafuta kichwani mwake. Alikuwa ni mtu mwenye mwili wa wastani tu, hapo alijaa kwenye kiti vilivyo.



    "Kitema, nimepata taarifa zako jana kutoka kwa Kijazi, ameniambia kuwa kazi umeianza vizuri ya kutoa vitisho kwa Backa?" alisema yule mtu mweusi. Huyu mtu ndiye aliwahi kuwa Rais kipindi cha waziri Backa. Anafahamika kwa jina la Julio Mobande Julio.



    "ndiyo, mkuu kila kitu kimeanza poa" alijibu Kitema.



    "vizuri ni lazima iwe hivyo Kitema kwani pesa nyingi haiokotwi barabarani kama iokotwavyo shilingi mia, pesa nyingi huwa inatafutwa na inahitaji mbinu za utafutaji. Hizi sasa ndiyo mbinu lazima tuli nyambue hili Taifa kwa siri hadi tulimalize, hakuna tutakacho kipoteza sisi" aliwamba huyo jamaa kama muwamba ngoma awambavyo, hakuishia hapo tu bali akauliza pia kama kama nyingi na kujijibu mwenyewe kuhusu Kitema kuupata ujumbe wa kumhitaji nyumbani kwake asubuhi na kwa kuwa amekuja, hii ilimaanisha kuwa ujumbe huo aliupata.



    "kuna hili moja linanichanganya Kitema, ni kuhusu huyu kichaa, kuna mengi anayajua sasa anaweza kunipa shida baadae hebu fanya juu chini uniletee habari za kifo chake hata kama utamuu kwa kumburuta na mashua baharini ni sawa tu." akaweka kituo kisha akaendelea kidogo baada ya kupiga funda dogo la kikombe cha kahawa.



    "anapatikana sana maeneo ya T.H (Talent House). Mtaa huo ndiyo mtaa pekee anaoupenda, pia unaweza kuambaa na barabara ha TH. Ni mwiba huyu mtu, anaweza hata kuchafua jina langu kimataifa. Nenda Kitema, nenda ukamtoe uhai. Pesa nyingi ya kujikimu kwa siku ya leo ipo kwenye mifuko yako ya benk, fanya hima" alikomea hapo kisha akakitwaa tena kikombe cha kahawa na kukisogeza kinywani mwake lakini kabla haja mumunya kilichomo kwenye kikombe kile alijikuta akitabasamu na kukirudisha kikombe mezani ni baada ya kuwashwa na jambo fulani moyoni mwake.



    "kitema. Kutoka kwenye mlizi wa pembeni hadi kuwa muuwaji wangu hatari sana. Hakuna wa kumtisha Julio tena nipo na komandoo ambaye amekwepa mishale mingi bila kumuachia hata jeraha" aliongea hivyo kwa sauti ya chini sana kisha akaachia cheko jepesi na kukitwaa tena kile kikombe cha udongo kilichobakiwa na Kahawa nusu ya kumalizia.



    Watu walizidi kushangaa, wahuni na washangaaji wengi walilibadilisha lile tukio kuwa ni sehemu ya kufurahi huku wengine wakiwaumiza watu kwa kuwaibia.



    "haiwezekani, mbona yuko vizuri sana huyu mtu. Lile pigo ni la mtu aliyewahi kuwa mpiganaji" alijiuliza yule dada aliyeomba kushuka garini akidai kuwa kuna kazi nyingi zilikuwa zikimsubiri. Alivutiwa sana na yule kichaa. Watu waliogopa kumsogelea baada ya kuona ametoa dozi tamu kwa kijana mtanashati. Magari yalizidi kujaa, msafara ulikuwa mkubwa mno kama kulikuwa na mkutano wa mwanasiasa fulani aliyekuwa akijinadi kwa wananchi. Hakuna aliyethubu kupiga hatua kumsogelea, kila mmoja alikuwa akihanya lakini dada yule aliyeshuka garini kwa kuomba, alipiga hatua ndogo ndogo hadi kumfikia yule kichaa akachuchumaa nyuma ya kichaa yule. Watu wakabaki wakikodoa macho kama hawakuamini kumuona binti mdogo tu kuweza kujitoa na kwenda kumkabiri yule chizi. Wakavutika zaidi ili kuona nini kinaweza kujiri, zile sauti za kumuomba yule bwana atoke zilikuwa hazipo tena kila mmoja alikuwa kimya kabisa kutazama.



    "habari yako?" alisalimia yule dada kwa kumnong'oneza yule kichaa sikioni. Hakujibiwa na wala hakubahatika hata kubadili muonekano wa yule kichaa. Akavuta pumzi na kuzitoa kisha akajaribu tena kurusha kete nyingine.



    "huu msafara ni mkubwa sana, huoni kuwa haya ni mazishi ya muasisi wa Taifa hili anakwenda kuzikwa" alisema yule dada. Macho yakamtoka yule kichaa lakini hakuongea kitu, alimgeukia yule dada na kumtazama usoni ni kweli dada yule alikuwa na huzuni kiasi machoni mwake. Yule kichaa alisimama kwa haraka sana, yule dada naye akasimama na kurudi pembeni ya barabara ile na kumtazama yule kichaa aliyekuwa amesimama kikakamavu kabisa na kutembea mwendo wa pole hadi pembeni ya yule dada akapiga saluti kisha akainama na kumnong'oneza yule dada.



    "mbona wewe uko hapa sasa huingii kwenye gari ili uende mazishini?" kama ni mtu mwingine angekunja sura kwa kukumbwa na harufu kali ya kinywa kutoka kwa yule kichaa lakini yule binti hakuonesha kitu chochote na badala yake naye akamuinamia na kumnong'oneza......



    "msafara huu utakwenda taratibu sana hivyo nitakwenda kwa miguu tu" yule kichaa akatabasamu kidogo na kutaka kuondoka kule ambako gari zilikuwa zinatokea, yule dada akamshika bega, kichaa akageuka kwa taharuki kubwa lakini alikutana na tabasamu la huyo dada huku akipokea sauti tamu iliyokuwa ikijitambulisha kwake.



    "naitwa Petii" baada ya hapo kulikuwa hakuna tena maongezi, yule kichaa aliondoka na kumucha yule dada akiwa amesimama pale akimtazama. Gari zilikuwa zimeshaanza kuondoka eneo lile taratibu.



    Huyu dada ni nani, na huyo kichaa naye ni nani? unaweza kujiuliza hivyo lakini unapojiuliza wewe hivyo, kuna mwengine atakuwa na maswali mengi sana kuhusu mkasa huu. Tutajua kila kitu mbele ya safari.



    Kumbuka tu kwa muda huo wakati yule kichaa akiwa anaondoka, kuna vijana wawili waliokuwa wanaongozana na Kitema, ambao tayari walikuwapo maeneo hayo na walikuwa wakifuatilia kila kitu kuanzia wakati yule dada anakwenda kuzungumza na yule kichaa pale barabarani hadi kuagana.



    "si ndiyo yule pale?" aliuliza kijana mmoja kati ya wale wawili.



    "ndiyo mwenyewe kwa maelekezo niliyopewa na boss" alijibu Kitema kisha akasema tena.



    "anatakiwa afe muda huu kamata silaha zenu hakuna kumrembea" alimaliza kutoa amri Kitema, wale vijana wakawa wanapiga hatua ndefu ndefu kuzidi kumkaribia yule kichaa huku mikono yao ikiwa tayari kiunoni kuzipapasa bastola zao. Wakati wakiwa wanakuja kwa kasi wale vijana, dada yule aliona akajenga mashaka makubwa sana kwa vijana wale. Akahisi kitu huku uhatari wa maisha ya yule kichaa akiwa ameupa kipaumbele. Kichaa yule alikuwa yupo kasi kidogo akiwa anatembea huku macho yake yakiwa chini ghafla wale vijana wakatoa mabomba ya bunduki na kumnyooshea yule kichaa, zilikuwa tayari zimetolewa usalama ni kuruhusiwa kufanya mauwaji tu ndiyo zilikuwa zikisubiri. Dada yule aliyejitambulisha kwa jina la Petii, alitoka kwa kasi pale alipo na kukimbilia kule ambako yule kichaa yupo. Wakati akiwa amemkaribia, risasi zikarindima, Petii alikuwa tayari ameshajirusha na kumkumba yule kichaa. wakapindukia barabarani wakabingilia na kujikuta upande wa pili wa barabara huku risasi zile zikikosa kuleta madhara kwa wapita njia wengine. Petii alimkamata yule kichaa mkono akamuonesha wale watu ambao wako upande wa pili wa barabara ambao walikuwa wamekamati bastola mikononi mwao.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "J.M.J!" akasema kwa mshangao mkubwa yule kichaa kisha wakatoka pale kwa kasi kubwa wakikimbilia kwenye chochoro za majumba makubwa huku nyuma wale vijana wakawa nao wakiwafuata kwa kasi kubwa mno huku bastola zao zikiwa hewani. Mjini hapo palichafuka kwa muda mfupi tu. Watu wakawa wanahofu na maisha yao sasa badala ya siku nzuri hii ikawa ni siku mbaya huonekana asubuhi. Wakati wale vijana wakiwa wanakimbiza kwa kufuata nyuma, Kitema alikuwa anatumia mbinu kali za kuhakikisha anakutana nao kwa mbele. Petii na yule kichaa walikimbia hadi kwenye chochoro moja lililokuwa limetenganisha nyumba mbili za wastani hapa wakagawana. Kichaa akabana kulia na Petii akabana kushoto. Wale vijana walipofika pale, walishtukia wakipigiwa mateke silaha zao na kubaki mikono mitupu, kila mmoja akawa na wake. ulikuwa ni mkono wa dakika chache tu wale vijana wakawa chini. Petii alishangazwa na uwezo wa yule kichaa, ulikuwa ni uwezo mkubwa sana tena akiwa anapiga mapigo ya kutotaka kujichosha yaani anapiga mapigo makali sehemu hatari. Hawakutaka kubaki pale walikimbia mbele zaidi lakini wakati wanatoke kwenye uwazi mmoja baada ya kuyamaliza yale majengo yaliyokuwa yamepangana, walipigwa mapigo ya kushtukiza na wote wawili wakajikuta chini. Walipokuja kusimama, walikutana na mtu mrefu mwembamba akiwa hana tabasamu usoni akiwa amekaa mtindo wa kimapambano. Walisimama wote kwa pamoja na kutaka kumvamia lakini yule kichaa akamzuia Petii kisha akasogea yeye mbele. Alikuwa amekunja ngumi kawaida sana, yule Kitema akaja kwa kasi kubwa na kumvamia yule kichaa, alikosea. Pigo alilokutana nalo lilikuwa ni pigo baya sana, pigo ambalo lilimrudisha nyuma kisha kumpatia maumivu makali sana. Rasta za yule kichaa zilikiwa zimemwagika kiasi cha kuziba macho yake. Hakubadili mtindo yule kichaa alikuwa kwenye mtindo uleule wa kukunja ngumi kihasarahasara. Kitema akabadili mtindo na kuja tena, Petii alibaki kuwa mtazamaji tu maeneo yale. Mpambano ulikuwa ni mkali mno, Kitema alikuwa amemzidi yule kichaa kwa hatua kubwa sana japo alijitahidi kurusha makonde kadhaa yaliyo myumbisha Kitema lakini uhodari na mbinu za kikomandoo ndizo zilizokuwa zikimshinda kichaa yule. Alichezea mapigo kama matatu manne ya kumchanganya, kichaa yule akatupwa chini lakini akawahi kujipindua na kusimama, haikusaidia kitu, Kitema aliruka hewani na kumshushia makonde kadhaa ya kifua. Kichaa yule alipinduliwa vibaya sana huku damu nyingi zikimtoka kwa wingi sana. Kichaa yule alikuwa na moyo wa ajabu sana pamoja na kile kichapo lakini hakuacha kujikaza kiume, alisimama tena, Kitema akaja kwa kasi ileile lakini safari hii aliambulia maumivu ya aina yake kwani wakati akiwa anakuja kwa ile kasi ya kutaka kuuwa, Petii alichomoka kutoka pale alipo na kukamata mabega ya yule kichaa ambaye bado hakumjua jina na kijizunguusha kama aliyetaka kubinjuka kavu, kisha akamzawadia kijana huyo mateke mazito ya kifua na ngumi safi iliyopigwa hewani ambayo ilitua kwenye mwamba wa pua. Mguno mkali wa maumivu ulimtoka Kitema huku akirushwa na lile pigo.



    "tusipoteze muda rafiki tuondoke hapa huyu mtu hatumuwezi anauwezo mkubwa sana kutuzidi sisi" alisema Petii kisha wote wakatoka kwa mbio nyingi wakimuacha jamaa akiwa anajizoazoa pale chini. walitoka mbali kabisa na lile eneo, walisimama kwenye gema moja hivi ambalo lilikuwa likielekea kwenye bonde moja kubwa ambalo lilikuwa nje ya mji kidogo. Yule kichaa alimtazama Petii kwa kitambo kingi kisha tabasamu la mbali likamtoka. Rasta zake japo zilikiwa chafu sana lakini bado hazikuuficha uzuri wa kijana yule. Alikuwa ni mzuri bado lakini sababu za kuwa vile hazikujulikana. Petii alimtazama kwa macho ya kumuonea huruma, alitaka kusema kitu ili kujua sababu za kutafutwa vile na kutaka kuuliwa au ni kile kitendo cha kukaa barabarani, halafu pia walisema kuwa ni kawaida yake kuwa msumbufu pale mjini, hili lilikuwa likimuumiza sana Petii. Tabasamu lake la kirembo lilimkaa usoni hadi urembo wake wa asili ukaonekana, alikuwa na mwanya mwembamba uliojitokeza kwenye meno ya juu na kumfanya kuzidi kupendeza zaidi. Alikuwa na mwili uliovimba kwa nyuma huku ukitanuka kwa mtindo wa kupendeza maeneo ya mapajani, suruali aliyokuwa ameivaa iliweza kudhihirisha hilo. Hakuwahi kusema kitu kwa huyo kichaa kwani aliwahiwa yeye.



    "M.Y.S!" alisema huyo kichaa kisha akapiga kavu na kubingilia kwenye lile korongo. Petii alichungulia huku moyoni akiwa anaumia sana. Maisha ya yule mtu hakujua ni kwanini yawe vile, alikuwa ni kichaa na kweli alitambulika hivyo pale mjini. Swali alilojiuliza ni vipi awe na uwezo mzuri tu wa mapambano. ni nani yule. alikuwa akijiuliza sana Petii.



    "M.Y.S!" nini maana ya hizi herufi, au ndiyo amejitambulisha kwangu na huyo J.M.J ni nani?" yalikuwa ni maswali mengi sana aliyojiuliza lakini jibu hakulipata zaidi ya kujipa ushauri mwenyewe tu wa kwamba ni lazima ahakikishe anamjua huyo J.M.J na yule kichaa hatomuita tena kichaa bali atamuita M.Y.S kisha akaamua kuondoka pale huku akijiahidi moyoni kuwa atakuwa anakwenda kumtembelea mahala pale.



    Ni siku ya pili sasa tangu kuingia kwa Merina ndani ya jiji la Pande jiji ambalo alitakiwa kufanya kazi moja tu ya kumteka binti wa Mh. Backa. Jiji hilo lilimpokea vizuri bila shaka yoyote, alikuwa ametulia ndani ya Hoteli moja ya kifahari sana. Kazi ya kumteka binti wa Backa haikuwa kubwa kwake kwani tangu anaingia hapo mjini, alikuwa tayari ameshafanya uchunguzi wa kutosha kwenye jumba au himaya kubwa ya mh. Backa. Moyoni Merina alikiri kuwa Backa hakuwa mtu mdogo, alikuwa ni mwenye ukwasi mkubwa sana wa shilingi na mali, mzee huyo alikuwa akimiliki Kisiwa kikubwa sana ambacho alikinunua kutoka kwenye mikono ya serikali kabla hata hajaingia serikalini kama waziri mkuu Japo hati na makabidhiano rasmi yalifanyika angali yu madarakani. Ila alikuja kukifanyia ujenzi kisiwa hicho mara baada ya kumaliza muda wake wa uongozi na Rais wa kipindi hicho muheshimiwa Julio Mobande akimpa kongole kwa kuweza kumiliki kisiwa kikubwa na kizuri namna ile. Na baada ya kuwa amekamilisha ujenzi wake alikibadilisha jina kisiwa hicho na kukiita B Island au Backa Island. Utafiti wote alioufanya ilikuwa ni kutaka kujua kuhusu ulinzi wa hapo, aligundua kuwa ulinzi uliopo ni mdogo sana ambao hauwezi kumpotezea muda mwingi na alitaka kuhakikisha hadi kazi ya ziada aliyopewa na mkuu inafanikiwa. Kitisho, ndiyo, kitisho kizito cha mtu mwenye hasira kilimkuta tena Backa, hiki si kama kile cha awali cha siku tatu za kuamu la!, hiki kilikuwa hakina mzaha hata kidogo na aliambiwa kuwa kama hatofanya hivyo basi asimlaumu mtu. Kitema alikuwa na ghadhabu za kuzidi mara baada ya kumkosa kichaa ambaye tunamfahamu kwa jina la M.Y.S kisha kuambulia kipigo kilichomfanya kubandika bandeji kwenye pua yake nyembamba iliyokutana na ngumi kavu ya kike. Alichanganya matusi aliyotukanwa na boss wake kwa kumkosa chizi huyo na tena kupata mkong'oto. Akamua kutoa kitisho kibaya zaidi kwa Backa kutokana ni yeye aliyepewa rungu la kutoa vitisho. Julio aliona lilikuwa ni jambo la ajabu sana mwendawazimu kutoa adhabu na kutoroka kifo lakini wahenga huwa wanasema kuwa huwezi kuisifia mvua kama haija kunyea. Mobande alikuwa hajui kilichomkuta Mtu wake huyo anayemuamini lakini siri ya mtungi anayo mwenyewe kata. Backa alijitupa kitini kama mzigo akajizunguusha kwa hasira kama mara tatu hivi alipokuja kutulia alikuwa ni kama mtu anayelia, alikosa la kufanya hali ilizidi kuwa tete sana. Aliukamata mkonga wa simu na kuiweka sikioni huku akibonyezabonyeza namba kwenye vitufe kadhaa.



    "Ndungai, hali inazidi kunitisha ndugu yangu sijui nafanya nini!" alilalamika Backa lakini upande wa pili haukuwa ukifanya jitihada zozote, bado ulilichukulia lile jambo ni kama mzaha fulani hivi.



    "hakuna kitu kama hicho Backa rafiki yangu, hao ni vijana wa mtaani tu wanaokufahamu hakuna zaidi ya hilo, wameamua kukutisha tu hao, mtu mkubwa kama wewe watakufanya kitu gani?" aliongea kimasihara kabisa Ndungai hakujua ni vitisho gani ambavyo alikuwa akikutana navyo rafiki yake. Backa aliishi kimashaka sana kwa muda huo wa siku mbili, maisha aliyaona machungu mno kwa muda huo mchache. Kila akimfikiria binti yake alikuwa akizidi kupata mashaka makubwa.



    "Tereza binti yangu kwanini ni wewe na si mtu mwingine, kwanini ninaishi kwa mashaka hivi...hapana ninakila sababu za kuhakikisha nakulinda mwanangu" aliwaza Mh. Backa alipokuwa amekaa sebuleni kwake akipata kutafakari hili na lile. Macho yake yalikuwa yameilekea luninga kubwa ya bapa lakini picha za kwenye luninga hiyo aliziona kama ni mawingu fulani tu yapitayo. Akakamata kiongozea luninga hiyo na kuizima. akalielekea kabati lake kubwa akalifungua lakini hakuna kitu alichokitoa ndani humo, akarudi kochini akakaa tena. Akapiga kite cha ghadhabu kisha akainuka tena na kuliendea lilelile kabati akatoka na jagi kubwa la maji akaenda kuchukua maji lakini hakuondoka nayo. Backa alikuwa amechanganyikiwa kupita kiasi.



    "hey, hey hey! hebu nipatie maji ya kunywa!" aliagiza Backa mara baada ya kukaa pale kitini tena. Binti aliyegiziwa akaleta maji hayo kisha akaondoka, Backa akabaki akiitazama ile gilasi ya maji kanakwamba anakitu cha kuiuliza.



    Siku hiyo iliisha ikiwa imemuweka Backa katika mashaka sana hadi ilipoingia siku ya tatu asubuhi. Siku hii ilikuwa ni siku ambayo Backa alitakiwa kuitimiza ile amri aliyopewa na mtu asiyemjua. Siku hii ilimuacha Backa na wasiwasi hakujua ni nini kitakwenda kumtokea baada ya kupinga amri za watu hao asio wajua. Kitanda hakupenda kimbebe hadi muda huo lakini mwili wake haukutaka kutoka pale kitandani, akili na mawazo yake yote yalikuwa juu ya maisha yake na vitisho alivyokuwa akivipokea.



    "huwenda kweli walikuwa ni vijana wa mtaani, hawawezi kunichanganya kiasi hiki.....ni kweli bwana ni vijana wa kihuni tu" alijiwazia Backa pale kitandani, mawazo yake yakampa kidogo ahuweni ya kuona hana sababu za kuogopa ama kuwa na hofu kwa watu asiowajua.



    "mimi sijui ni mjinga kiasi gani, nimeishi kwa miaka mingapi hadi leo nije kutishwa kipumbavu na watoto sijui wahuni" alizidi kuwaza bwana huyo. Nguvu za kuamka zikawa sasa zinaanza kumnyemelea, alikuwa katika uchovu mzito wa akili lakini sasa alihisi kupata nguvu fulani.

    akabingilia pale kitandani kama Buma akakaa kitako lakini kabla hajaugusisha mguu wake chini, simu yake ikaita, harakaharaka akainyakuwa na kuitazama kiooni. Lahaula walakuwatta! Mpigaji alikuwa ni yuleyule, ndiyo, alikuwa ni yuleyule mwenye namba ngeni, namba ambayo haikuwa ikifanana na namba ya mtandao wowote aliyowahi kuuona. Akapata hofu, mashaka makubwa yakamshika, hata ule ushauri wa mawazo yake akauona wa kipumbavu na huwenda ulikuwa ukimhadaa. Hawa si vijana wa kihuni hawa. Akawaza kwa kujirudisha kwenye tukio la kweli.



    "wanaweza kuwa ni vijana wa kihuni kweli?" alijikuta akijiuliza pasipo kuipokea kwanza hiyo simu, ni wazi hakuwa na nguvu ya kuipokea hiyo simu lakini kuna shauku ambayo ilimkaa moyoni ya kutaka kujua ni nini kipya ambacho hao jamaa wanataka kumuambia, alipofikiria kuwa huwenda hakuna jingine zaidi ya vitisho, moyo ulisita akaogopa na simu nayo ikakatika. Akapata afadhali akaongea moyoni mwake kauli iliyompa nguvu yeye mwenyewe tu.



    "afadhali hata ilivyokatika" alijipa imani Backa na kutaka kuirudisha simu mahali ilipokuwepo awali, hakuwahi, simu ikaita tena, tena safari hii iliita kwa sifa kubwa sana Backa akajikuta akiichukua ile simu kwa pupa pasipo kutarajia akaipokea, macho yakamtoka akawa hana budi ikabidi tu aiweke sikioni.



    "hah!, hah!, hah!, haaa!" sikuwahi kufikiri kama ingetokea siku moja ukashindwa kupokea simu yangu...wewe ni mtu unayejiamini sana sasa kwa nini unakuwa muoga hivyo?" sauti nzito ikauliza, ilikuwa ni sauti ileile iliyokuwa ikimpa vitisho mheshimiwa Backa. Sauti ambayo kwa wakati huo alikuwa akiiogopa kuliko hata alivyokuwa akijishauri.



    "mbona hunijibu? nimekukera labda? au sauti yangu umeshaichoka ama kuizoea muheshimiwa?" aliuliza lakini hakuishia hapo tu, aliendelea tena.



    "sina cha kukusaidia Backa, umekaidi na kwa kawaida kwetu sisi mtu anayekaidi huwa hatumpi nafasi ya kujitetea" alibadili sauti kwa kiasi kikubwa sana ilikuwa ni sauti ambayo si ile aliyoanza nayo kuongea hii ilikuwa haiko kirafiki wala kimzaha.



    "ngoja uone" akasema.

    "ngoja uone Backa, ngoja uone tu jinsi dunia inavyotakiwa kuwa. Kesho asubuhi utapata salamu" ilikoma hiyo sauti na kukatika kwa simu kabisa. Backa akajikuta ameganda kama nyamafu. Simu aliiona nzito kiganjani mwake ikamtoka mkononi pasipo matarajio yake. Laiti isingelikuwa kuwepo kwake pale kitandani basi ingelipasuka na kusambaratika kwa kupiga sakafuni kwa kishindo kizito. Macho yake yalikuwa yamechora alama moja nyekundu kutokea kushotoni mwa kila jicho. Alifanana na mtumiaji mzuri wa majani maarufu ya Bange, yavutwapo yawapo makavu. Lakini wala yeye si mtumiaji, ila kwa hapo jinsi alivyokuwa, alikuwa ni kama ametoka kutumia bange. Akapumua kwa nguvu nyingi.



    BI. ROZI HOTEL.



    Kimya kizito kilikuwa kimetanda ndani ya chumba kimoja, unaweza kusema labda hakukuwa na kiumbe chochote ndani humo. watu watatu walikuwa wamekaa kwenye viti tofauti, hakukuwa na meza yoyote iliyopo kati yao. ilionekana kulikuwa na kikao muhimu na chenye makusudi mazito ya kukutania mahali hapo.



    "huyu binti anaitwa Merina, hilo linatosha kukufanya umfahamu binti huyu, hakuja hapa eti, kwa sababu ya kukutambulisha tu hapana, bali sababu za kumleta hapa ni kutaka kukuambia kuwa ile kazi ambayo nilikupa siku mbili zilizopita ya kutoa vitisho kwa Backa, inaangukia rasmi kwa huyu dada. Hata kwenda kinyume na wewe hata kidogo kwani yeye ndiye aliyetoa muongozo mzima wa kazi ile" aliongea kwa urefu Jalome, huyu alikuwa ni yule mtu mnene na mkubwa kuliko wote. Alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa Rais wa zamani bwana Mobande lakini huwa haonekani hovyo, ni kwenye mambo nyeti kama hayo tu. Kitema alimtazama yule dada aliyetakiwa kumkabdhi ile kazi, hakukataa nafsini mwake wala hakuonesha dalili yoyote ya kutaka kumpinga. Alijua pia kuwa ile kazi ilikuja kwake kwa sababu tu lakini wapo waliokuwa waendeshaji wakubwa wa kazi hiyo.



    "naitwa kitema, nashukuru kukufahamu Merina" alijilitambulisaha Kijana huyo mkavu. Macho ya Big Jarome yaliwatazama wote kwa pamoja kisha akasema.



    "nadhani hadi hapa tulipofikia ni pazuri kwetu naomba tuiwasilishe kazi yetu mikononi mwako"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "hapana shaka Kitema, nimefurahi nikiwahitaji tena nitawatafuta" alisema Merina kisha kikao hicho kikafungwa Merina akatoka humo ndani akaelekea nje ya hiyo hoteli kubwa na nzuri iliyopo ndani ya jiji hilo la Pande. Alijitia garini na kutoweka.



    "mkuu, walinzi watatu wa usiku wametoweka pasipo kujulikana ni wapi wameekea" aliingia Phili kwenye chumba/ofisi ya mh. Backa iliyopo ndani ya jumba lake siku iliyofuata asubuhi.



    "sijakuelewa Phili unachokimaanisha!?" aliuliza Bcka akiwa na hofu ndani yake. Taarifa ile ilikuwa ni mpya sana kwake, aliwahi kupata taarifa za kuuwawa kwa walinzi wake lakini siyo kupotea.



    "yaani wamepote na inaaminika kuwa wameuwawa kabla ya kupotea kwao" alisema Phili.

    "ah!, ah! Hapo utakuwa unanichanganya zaidi Phili, hebu niweke wazi, wameuwawa au wamepotea?"



    "wameuwawa kwanza kisha kupotea"



    "hapana Phili hao wapo hawawezi kuuwawa wala kupotea, watakuwa wapo msalani au ufukweni. Jaribuni kufanya msako eneo lote kisha uniletee taarifa zilizoshiba" mh. Backa hakutaka kuamini kwa asilimia mia moja eti, kuwa walinzi wake wameuwawa ama kupotea.



    "muheshimiwa, taarifa hiyo ilikuja kwangu baada ya kufanyika msako huo mkubwa mara baada ya kuona baadhi ya walinzi hawaonekani. Hata mimi nilipinga kama wewe lakini nilitewa wakafanya msako na kuniletea vidhibiti, naomba ukashuhudie unyama uliotukia" alitoa maelezo Phili mtu pekee wa karibu wa Backa. Backa hakutia neno tena bali alinyanyuka na kumfuata Phili hadi nje huko ilikuwa ni nusura adondoke. Alikutana na mikono mitatu na kila mkono ulikuwa umekamatishwa silaha yake, damu zilikuwa zimetapakaa kila kona ya eneo lile. Backa akapatwa na mtetemeko mkubwa wa moyo.



    "inamaana ni kweli sasa si ndiyo?" aliuliza kwa sauti pasipo kuamua, alikuwa na lengo la kujiuliza mwenyewe lakini kukanganyikiwa na wingi wa mambo ndiwo uliopekekea kujiuliza kwa sauti hadi mlinzi wake mkuu wa karibu Phili, kuuliza kunani. Akashangaa kuulizwa hivyo hata hivyo hakujibu maana hakujua ajibu ni nini badala yake.



    "umesema walikuwa wangapi?" akauliza.



    "nani muheshimiwa, wauwaji au askari walioondoka...aaam! waliouwawa wakiwa lindoni?" aliuliza Phili naye akiwa amechanganyikiwa.



    "waliotoweka wakiwa lindoni?" akasawazisha swali lake Backa. Phili akajibu kwa mara nyingine kuwa waliouwawa ama kutoweka walikuwa watatu. Backa aliumia sana moyo wake ulikosa nguvu ghafla aliuona kama unataka kutengeneza njia ya kutoka nje ya mwili wake. Lilikuwa ni shambulio la kumtisha sana tena siyo kumtisha tu pekee bali kumpa hofu mazima. Wakiwa wanazidi kushuhudi vile vitu vya kutisha, walijikuta wakifuatwa na askari mmoja ambaye alikuwa lindo kwa muda huo, alikuwa akihema sana kama mtu aliyekuwa akikimbizwa.



    "mheshimiwa, walinzi wote waliokuwa lindo usiku wameuwawa hakuna hata mmoja aliyerudi kituoni na nimepata kushuhudia vitu vya ajabu sana nilipokuwa najaribu kuzunguuka kwenye hili eneo lote....wenzetu wameuwawa muheshimiwa" yalikuwa ni maneno ya mlinzi huyo aliyekuja mahali hapo mara baada ya kupigiwa simu kutoka kiyuoni kwao kuwa hakuko sawa. Backa alichoka, alichoka mwili, akili na kila kitu, hakujibu kitu alijivuta taratibu ili kwenda kuona hicho au hivyo vitu vya ajabu alivyoviona mlinzi. Walikwenda hadi huko.



    "Mungu wangu!" moyo wa Backa ulipiga kikumbo kizito na kubadili mapigo yake. Alishuhudia kifusi cha mikono na miili kama miwili tu ambayo ilikuwa haina kichwa. Kama ingelikuwa sio mhimili wa mlinzi wake wa karibu basi Mh. Backa angedondoka chini, mwili ulimlegea sana, Backa alilia, alilia kweli Backa.



    "haya siyo mauwaji ya kawaida Phili, hawa walitaka kunikomoa....mbona sasa wamefanikiwa kunikomoa, wameniumiza mimi jamani kuna kipi ambacho nimeikosea dunia oouh!" alilia Backa kupita kiasi.



    "Boss!" sauti ya kike iliita. Backa akageuka kwa kasi huku akiwa amekikata kilio chake ghafla.



    "unataka kuniambia nini Marmaa?"

    aliuliza kwa mshangao huku akiwa amesimama imara.



    "dada ame......!"



    "ameuwawa nae pia?" aliuliza Backa.



    "hapana, ametekwa na watekaji wameacha hii karatasi" alijibu Marmaa dada wa kazi ambaye ndiye awaye karibu na Tereza huku akimkabidhi mheshimiwa hiyo karatasi. Backa aliipokea hiyo karatasi huku mikono ikiwa inamtetemeka, aliifunguwa kwa shida alikuwa ni kama amekamata kaa la moto kwa jinsi alivyokuwa akitetemeka. Karatasi ile ikadondoka chini, Phili akaiokota na kuifungua alipotaka kumkadhi, mheshimiwa akamwambia aisome tu. Phili akaisoma kwa sauti.



    "NAJUA BINTI YAKO ANAWEZA AKAGOMA KUIFNYA KAZI YETU KWA HIYARI YAKE, ITATUMIKA SHURTI IKIBIDI KAMA AMBAVYO TUMEKUACHIA MAAFA NYUMBANI KWAKO.....UMEONA MUHESHIMIWA BACKA, KAZI ILIKUWA NI NDOGO SANA KAMA UNGEKUBALI KUTUPA MWANAO MAPEMA. POLE KWA MSIBA MZITO WA KUAMBULIA BAADHI YA VIUNGO VYA WALINZI WAKO. NGOJA TUONE BINTI YAKO ATAKAVYOFANYA, AKIWA KIBURI ITATUBIDI KURUDI TENA ILI TUJE TUONGEE" wakati Phili anamaliza kuisoma hiyo karatasi, Backa alikuwa ameshadondoka tayari na kupoteza fahamu. Walimbeba na kumrudisha ndani na kumfanyia huduma ya kwanza hadi fahamu zilipomrudi. Muda huo huo aliomba kuongea na IGP. Simu ikaletwa akaunganishwa nae.



    "pole sana kiongozi wangu, nimezipata taarifa zako za kutisha hivi niko njiani nakuja" aliongea IGP Liyambo mara baada tu ya simu hiyo kupokelewa. Backa akaishusha hiyo simu na kuomba aunganishwe na Ndungai. Ikaunganishwa.



    "sasa wamefanya kweli Ndungai, wamefanya mauwaji ya walinzi wote wa usiku na wamemteka na binti.......!" alishindwa kumalizia Backa kilio kizito kikakita kwenye ngoma za masikio za Ndungai. Alijisikia vibaya sana alikosa kitu cha kusema, ama kwa hakika mzarau mwiba guu huota tende. Ndungai alikuwa akileta masikhara makubwa sana kwa Backa juu ya habari za vitisho alivyokuwa akivipokea rafiki yake. Simu ilikatika pasipo kutarajia, unafikiri angeongea nini sasa, alijiona ni mnafiki mkubwa sana kwa rafiki yake.



    "kumbe ilikuwa ni kweli?" akajipumbaza kujinga huku akiwa bado katika butwaa kubwa kabisa, alikuwa na uwezo mkubwa pengine wa kuzuia hilo labda kama angelitilia maanani sasa alidharau likatokea, nani mwenye makosa, alijiona ni msababishi wa jambo hilo pia. Wakati Ndungai akiwa anajiuliza maswali mfululizo, kwa upande wa Liyambo ndiyo alikuwa anaingia kwenye himaya ya Backa. waziri mkuu wa zamani. Boti ndogo mbili zilikuwa zikiingia hapo kwa kasi kubwa,





     taarifa ya kutekwa kwa mtoto wa Backa zilisambaa kama 'Ubuge' kwenye kinywa cha Mbuzi. Jiji la Pande na viunga vyake ikiwemo na nchi nzima, walizinyaka hizo taarifa. Lilikuwa ni jambo la kushangaza sana hilo, iweje taarifa hizo zisambae namna hiyo kama vumbi la upupu kwenye upepo. Waandishi wa habari walikuwa wamejaa hapo kwenye jumba la Backa wakitaka kumuhoji kigogo huyo wa zamani lakini nafasi hiyo hawakuipata abadani. Backa aligoma kabisa kutoa ushirikiano kwa waandishi hao, hakuwa na uwezo wa kuweza kuyakabili maswali ya waandishi hao ni kama aliona watakwenda kumuongezea machungu tu.



    "hebu tuambie ilikuwaje hadi mtu ama watu wakavamia na kufanya uhalifu mkubwa pasipo kugundulika?" lilikuwa ni swali la muandishi mmoja wa habari akijaribu kumuuliza mlinzi mkuu wa Backa kama anaweza kuwa anajua chochote. Phili alitulia kidogo kisha akasema.



    "watu waliovamia hapa hawakuwa ni majambazi wa visu na viwembe bali walikuwa ni makomandoo kwani hata sauti za pumzi zao hazikuweza kusikika.



    " kulikuwa kuna visasi labda kwa Backa na watu wengine, wewe ukiwa kama mtu wa karibu zaidi na mheshimiwa?" aliuliza huyo muandishi wa habari.



    "kwa nijuavyo mimi hakuna, mzee alikuwa akiishi vizuri tu na watu siju wakati yupo madarakani labda.....!" alijibu Phili kisha kuiacha kauli yake njiani mara baada ya kupokea wito kutoka kwa bosi wake aliyopo ndani. Akaondoka mahali hapo akimuacha muandishi wa habari kwenye maswali na sentensi za kuungaunga. Labda serikalini alikuwa na maadui? au labda ni wakati yupo madarakani kuna watu walikuwa hawapendi utendaji wake wa kazi? Ndivyo alivyokuwa akijiuliza kijana huyo ambaye alikuwa akihitaji kupata habari safi ya kulipamba gazeti lake lililompa ajira.



    "achana na waandishi wa habari Phili hakuna msaada wowote utakaoupata kutoka kwao, acha wabuni kama walivyobuni za awali juu ya vifo vilivyotokea usiku" aliongea Backa akiwa amekaa kitandani huku drip likiwa linashusha matone mwilini mwake taratibu. Jenerali alikuwa ametulia kimya akimtazama kiongozi huyo ambaye ndiye aliyefanya yeye kuwa hapo kwa asilimia nyingi mno. Alikumbuka kauli nyingi sana za busara za huyo bwana kubwa ilikuwa ni ile ya kumwambia kuwa anapenda watu wanaofanya kazi kwa ajili ya watu wanaowategemea, anapenda kuona kiongozi yeyote yule akifanya kazi kwa ajili ya anaowaongoza na si vinginevyo. Alikumbuka kuwa kupigana kwake kwa nguvu nyingi kazini wakati akiwa ni inspekta wa polisi, kitendo chake cha kuipiga rushwa mateke na kusimama kwenye haki ndicho pekee kilichomfanya Backa akishirikiana na waziri mwenye dhamana ya ulinzi wa kipindi chake cha uongozi, kukaa chini na kuweza kumshawishi raisi aliyopo madarakani hadi kupanda kwa cheo hicho kikubwa bila kuwekewa ngazi wala vizingiti. Haikuwa kazi ngumu kufanya hivyo kwani Backa na mwenzake walikuwa ni watu wenye usawishi na ukaribu mzuri na Rais aliyopo madarakani. Aliapa moyoni mwake Liyambo kuwa atalibeba hilo 'ndundu begani' hadi kieleweke. Tayari alikuwa ameshampa kazi kijana mmoja makini sana ili kuweza kuchimbua jambo hilo kwa siri kubwa huku akimuahidi vingi vinono.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "najua hayo yote yanaletwa na nini muheshimuwa lakini naapa sitakuacha, nitakuwa nawe bega kwa bega hadi tujue nini chanzo" alisema Liyambo huku akiwa amesimama tayari kuondoka humo ndani ya chumba ambacho alipumzikia Backa. Backa alimtazama bwana huyo mwenye uchafu wa vyeo vya kipolisi ambaye alishaanza kusalitiwa na umri taratibu kisha akasema.



    "nimekuwa kama mwana mkiwa sasa, sina ninayetegemea ni wewe kijana wangu. Nitapenda kusikia kila utakachokuwa unachunguza ili nijue nini natakiwa kufanya" kishapo Liyambo alikung'uta makalio na kuondoka. Hakutaka kupitia mlango wa mbele kwani alijua fika waandishi wa habari watakuwa macho kumsubiria, hakutaka kujibu chochote kwa waandishi hao. Alitokea mlango wa nyuma lakini hakuna watu wabishi kama waandishi wa habari hasa pale wanapotaka kupata habari yenye undani zaidi. Alikutana nao huko huko ikabidi kujifanya amevaa mawani ya bati.



    "Afande, unaweza kutuambia chochote labda kutoka kwenye yale aliyokueleza muheshimiwa waziri?" lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa mtoto wa kike aliyekuwa amekamata kinasa sauti mkononi mwake. Hakutoa jibu lolote la kuwaridhisha hao watu bali kitu pekee alichokijibu mahali hapo ni kuwaambia kwamba wamfuate ofisini.



    "kwahiyo afande mnampango gani mwingine kuhusiana na ulinzi wa muheshimiwa ambao kwa sasa unaonekana kuwa mashakani kwa asilimia miamoja na kitu?" maswali mengi na yenye ujazo yalikuwa yakizidi kumiminika kwa Inspekta jenerali, yote ya yote alifanikiwa kuyakwepa na kuwataka waandishi hao waende ofisini kwake.



    Ndungai yeye hakutaka kufanya papara kuelekea kwa rafiki yake, aliamua kutulia na kutafakari mengi juu ya nini afanye maana hiyo sasa imeshakuwa ni shida kubwa. Pia alitaka kuhakikisha anaingia nyumbani kwa Backa kukiwa hakuna waandishi wa habari wala nini.



    *******

    *******

    "muacheni alale kwanza akiamka nadhani tutamkalibisha kwenye himaya hii mpya" sauti nzito ya kiume ilisema mara baada ya Tereza kufikishwa kwenye makazi ya Dr. Lee huko kisiwani Madagascar. Watu walifunga chumba baada ya kuhakikisha binti huyo wamemdhibiti vizuri kisha wakaondoka wote na kuelekea mahali ilipo gari kubwa. Walipofika hapo walishuhudia miili isiyopungua ishirini ikishushwa kutokea garini humo mingi ikiwa haina mkono mmoja na mingine ikiwa imeondolewa mikono yote. Merina alifika hapo mara baada ya kuhakikisha ameonana na bosi wake kisha akatoa maelekezo kuwa miili hiyo moja kwa moja ipelekwe maabara. Hakukuwa na kipingamizi mahali hapo kwani Merina ndiye mwenye sauti ya mwisho mahali hapo baada ya Dr. Lee na Bencov kinyume na hapo hakukuwa na mwingine labda kijana Lonto mwenye sura mbaya yenye makunyanzi.



    "ndiyo maana nakukubali sana Merina, wewe siyo binti wa mchezomchezo kabisa, sikutegemea kama ungeweza kufanya mambo yote mawili kwa wakati mmoja" alisema Dr. Lee baada ya kuzishuhudia maiti hizo karibia ishirini zikiingia hapo maabara.



    "hii inatosha sisi kuweza kutengeneza sumu nyingi ambazo zitaweza kuchanganywa na madawa yatakayobuniwa na huyo binti pindi tu atakapoamka" alisema tena Dr. Lee kisha akatulia akiangalia jinsi miili hiyo inavyozidi kuingizwa. Walisonga mbele zaidi huko walikuta mashine moja ambayo ilishughulika na ukataji wa vichwa tu. Miili kadhaa ililazwa kwenye meza ya hiyo mashine kisha ikawashwa, meza ile ikaanza kusogea taratibu kukifuata kisu. Kichwa kilitenganishwa na kiwiliwili kisha kiwiliwili hicho kilitolewa hapo huku kichwa kikihifadhiwa kwenye jokofu kwa ajili ya kusubiri uzalishaji.



    "kazi inakwenda vizuri kwakweli" alisifia moyoni Dr. Lee huku akiwa anatabasamu kanakwamba kile kilichokuwa kikifanyika pale ni igizo au maandalizi ya wimbo fulani mzuri.



    "Boss, yule binti ameamka tayari" sauti ya kiume ilisema mahali hapo.



    "ok, vizuri, mpekekeni chumba cha chakula akale kwanza mimi nitamkutia huko" alijibu Dr. Lee kisha akaigeuza baiskeli yake akatoka humo ndani. Alijivuta taratubu huku Merina akiwa nyuma yake hadi kwenye chumba kimoja kilichokuwa safi sana huko walimkuta Tereza akiwa amefungwa kamba na kuzibwa mdomo. walipoingia wao muda kidogo, Bencovu nae alitia maguu.



    "hey muwekeeni chakula sasa, mbona mnamuacha akiwa anasubiri" alifoka Dr. Lee. Vijana walileta chakula ambacho kilikuwa kwenye chombo safi kisha kumsogezea. Wakamfungua kamba pamoja na kutoa gundi iliyopo kinywani mwake. Tereza alihema kwa nguvu sana baada ya kutolewa hilo gundi kinywani. Bado alikuwa na maswali mengi sana kuhusu hapo alipofikishwa ni wapi lakini kila akiwaangalia watu waliopo hapo walikuwa na sura tofautitofauti kabisa. Akimtazama yule mzee aliyeamrisha vijana wamuwekee chakula, alikuwa ni kiumbe cha ajabu sana machoni mwake Kinyago cha ajabu kilikuwa usoni kwake huku akiwa haonekani macho wala mdomo. Tereza alijiuliza kuhusu mtu huyo, ni nani maana watu kama hao alishawahi kuwashuhudia kwenye muvi kali sana alizokuwa akipenda kuzitazama ila tofauti ya mtu huyo ni sauti yake. Sauti ilitokea kooni na ilionekana dhahiri kuwa ni ya kutengeneza, kingine ni shingo ya mtu huyo kulegea yaani ilikuwa imelalia begani kabisa. Alipoyahamisha macho yake alimuona mtu mmoja mrefu huyu alikuwa ni mrusi. Alikuwa mrefu na mweupe sana huku akibeba macho yenye mboni kama za Paka ama Chui! Kifupi hapo hakukuwa na mwenye afadhali.



    "karibu chakula binti kisha tuongee machache" alisema Bencov akiwa anamtazama huyo binti machoni. Tereza alikitazama kile chakula, kilikuwa ni chakula kizuri tu tena anachokifahamu lakini tendo kula ndilo lililogoma, hakuwa na ujasiri wa kula hata kidogo mbele ya hizo sura za watu asizozielewa.



    "hey binti kula, unadhani sisi ni watu wabaya kwako, ni watu wazuri na wenye upendo, kula basi" sauti hiyo ilimshtua Tereza kwa kiasi kikubwa sana. Hapo ndipo alipokumbuka kuwa alitekwa na sauti ya mtu huyo ndiyo iliyohusika. Akajua kumbe hakuwa na mzazi wake karibu hapo alipo ni mateka kamili. Sura za wale watu zilimchanganya kupita kiasi kila akitazama alishindwa kuelewa ni kitu gani hasa kilichopelekea yeye kuwa mahali pale. Akiwa anazidi kujiuliza, watekaji wale wanamtaka ale baada ya chakula kuletwa mahali hapo. Hamu ya kula haikuwepo kabisa kila alivyokuwa akilazimishwa kula aliona kama anapigiwa kelele tu mahali pale. Kila mmoja alikuwa akimtaka binti huyo ale lakini ilikuwa ni kazi bure hakuelewa hata kidogo.



    "hivi unafikiri sisi ni wazazi wako labda tukulazimishe kula kama mtoto mdogo" alisema Dr. Lee akiwa ameilaza shingo yake begani kama kawaida. Tereza alimtazama huyo mzee kwa hasira kali mno kisha akayarejesha macho yake kwa wale watu wengine waliopo pale. Akamtazama binti yule ambaye ndiye chanzo cha yeye kuwa pale, akamuona jamaa mmoja mwenye asili ya kikorea kisha akamaliza kwa jamaa mwingine aliyekuwa na sura ngumu iliyo na makunyanzi. Mahesabu yake yakamtuma kuwa anaweza kulianzisha varangati na kupita kisha kutoweka mahala hapo. Akajikurupusha pale kitandani akawapiga vikumbo lakini hakuna hata mmoja aliyetikisika mahali. Yowe kali la maumivu likamtoka baada ya kuchabangwa makofi mawili ya nguvu, shavu lake akaliona kama linaongezeka ukubwa huku michonyoto ya maumivu ikilipa shida shavu lake, kizunguzungu kikamvaa kisha kumwagika chini kama mzigo.



    "mwili wenyewe mwepesi halafu anatusumbua" alikoroma Merina mara baada ya kumzawadia binti huyo makofi hayo ya nguvu.



    "mrudisheni kitandani na hicho chakula chake kiweke mezani akiamka njaa itakuwa imemkamata zaidi ni lazima atakuala tu" alisema Dr. Lee kisha wote wakatoka mule ndani.



    Hali ilikuwa tete sana kwa Inspekta Liyambo mawazo yalikuwa yamemuandama kiasi cha kushindwa kujiona anakitu ambacho si haki kama kitaendelea kubaki moyoni mwake pekee. Hiki kilikuwa ni kizito mno hadi kikafikia hatua ya mkumfanya atulie vizuri kitini. Zilikuwa tayari ni dakika zaidi ya thelathini zimepita tangu kuwa kwenye meza ya chakula huku chakula kikiwa kinamtazama kwa muda mwingi tu. Si kama kilikuwa hakitaki kuliwa na bwana huyo la! bali huyo bwana ni kama hakukiona hicho chakula mahali hapo.



    "kwanini nimekuwa mtu wa namna hii? Nimekuwa msiri sana kwenye jambo hili sasa naliona jinsi linavyokwenda kunielemea" aliwaza Liyambo kisha akakamata gilasi ya maji na kupiga kutu kadhaa na kuirudisha pale mezani na kunyanyuka akaelekea chumbani kwake huko akamkuta mkewe akiwa anasoma kitabu. Kichwani mwake aliwaza kuwa si kama Mkuu wa mchi alikuwa hajui mambo yale, alikuwa anajua lakini kumuelez pia ni wajibu kwake.



    "umeshatoka hapo na chakula changu hukukila hivyo?"....



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    lilikuwa ni swali kutoka kwa mkewe, alijifanya kama hakulisikia lakini haikusaidia kitu akakutana na jingine.



    "haya kuna lipi jingine limejiri huko linalokufanya usile?" hili lilikuwa tofauti kidogo lakini mwisho lilikuwa likilenga lilelile la awali. Liyambo akageuka na kumtazama mkewe kisha akasema,



    "kuna jambo la msingi kidigo napaswa kumshirikisha mkuu wa nchi"



    "utakula ukirudi au ndiyo utakula huko huko kwa mkuu wa nchi?" akauliza tena. Hili Liyambo hakulipa uzito akalipa mgongo bila ya kulijibu na kutoka akijisemea kwa sauti ndogo aliyoisikia mwenyewe.



    "na utu uzima huo bado tu unanionea wivu" akatoka na kuelekea maegeshoni. Gari ndogo aina ya Toyota Mark II ilitiwa moto kisha kutolewa taratibu hadi barabarani. Ilikamata barabara ya K2 kisha kuiacha na kuingia kwenye barabara kubwa inayolekea Majumba mengi, hapa Inspekta akavuta mafuta na kuifanya gari hiyo kuongeza kasi.



    "nilifanya kosa kubwa sana kutompigia simu muheshimiwa hili ni kosa kubwa sana na sujui ni kitu gani hasa kilichofanya hawa jamaa niwaamini kwa namna hii" aliwaza Liyambo baada ya kufika ndani ya ofisi yake muda huo wa jioni. Akavuta simu ya mezani baada ya kuhakikisha kuwa mlango ameufunga vizuri kabisa. Alitaka kuyafanya maongezi hayo kwa siri kubwa bila kujulikana na mtu yeyote. Alipiga namba kadhaa na kuiweka sikioni. Hakujua kama kuna msaliti kila pande na huyu alikuwa anatumia akili nyingi sana kwani akimuona mkuu wake wa kazi anaingia ofisini, basi huweka kinasa sauti kidogo na chenye nguvu mlangoni. Ambacho kinanasa maongezi yote na kuyarusha mahali. Hivyo ndivyo ilivyo na ndiyo maana hata alipokuwa akiongea na Backa kunawatu walijua.



    "Inspekta Jenerali naongea, naomba kuongea na mkuu" alijitambulisha kisha kutoa sababu za kupiga simu hiyo. Mtu aliyepokea hiyo simu akamjibu kuwa mkuu yupo ofisini kwake na amesema hahitaji usumbufu hivyo anaweza kumpigia yeye moja kwa moja moja kama kunashida ya muhimu. Alijibiwa Liyambo na mtu aliyempiga. Liyambo hakusubiri kitu kingine alikata simu na kubonyeza namba moja ambayo ndiyo ilikuwa ikimuunganisha na mh. Rais moja kwa moja.



    "habari yako mkuu?" alisalimia.



    "salama Liyambo nini tatizo si kawaida yako kuja moja kwa moja kwenye 'line' yangu?" aliuliza mh. Rais ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la mh. Mabandu Mbonde.



    "ni kweli mkuu, sikuweza kuliacha hili jambo liendee kulala kwenye moyo wangu tena likiwa hivi, hali imekwenda sivyo ndivyo na ni tete labda niseme hivyo"



    "nini tatizo?" akagandamiza.



    "ni kuhusu mh. Backa mkuu, yuko katika hali mbaya kabisa na amekuwa ni mtu asiyeishi kwa amani ya moyo hata kidogo, niliamua kulivalia njuga kwa kujaribu kuweka askari wa kutosha lakini haikusaidia na nikapokea amri kutoka kwako kuwa nipunguze ulinzi kule nami sikuwa na pingamizi"



    "upunguze ulinzi? Amri kutoka kwangu? Lini sasa mbona kama unajaribu kuleta simulizi hapa Liyambo?" yalikuwa ni maswali mchanganyiko kutoka kwa mh. Mabandu. Yale maneno kuwa alitoa amri ya kupunguzwa kwa ulinzi yalikuwa yakimchanganya sana na pia alijua labda walinzi waliouwawa kule kwa Backa ni walinzi binafsi kumbe walikuwa ni askari wa jeshi la polisi kabisa, aisee!, hilo lilikuwa ni pigo kubwa mno. Lilikuwa ni pigo la aina yake, askari wasiopungua kumi na wawili ama zaidi, waliuwawa tena si kuwawa tu bali hata miili yao haikuonekana zaidi ya viungo pekee. Ilikuwa ni aibu. Aliona kama ni matusi mazito mno alikuwa akitukanwa na watu hao waliyofanya hayo mambo. Hata Inspekta alipotaka kusema kitu alimzuia na kumwambia kuwa, hayo maongezi hayakufaa tena kusikilizika simuni bali aelekee ofisini. Liyambo akafanya hivyo.



    "umesema mimi ndiyo niliyetoa amri ya kupunguza walinzi kwa Backa?" aliuliza mh. Rais mara baada ya Inspekta Jenerali Liyambo kufika ofisini kwa Mh. Mabandu.



    "ndiyo mkuu, alikuja mh. waziri wa ulinzi na kuniambia kuwa walinzi wanatakiwa kupunguzwa, kule na si ruhusa kupeleka walinzi wengi kwa ajili ya ulinzi wa mtu mmoja pekee, nilitaka kubisha lakini nikaambiwa kuwa hiyo ni amri na inatoka kwako mukuu" alieleza IGP.



    "mnataka kunichezea ninyi, mimi siwezi kufanya huo upuuzi hata kidogo. Waziri mzima anafanya vitu vya hatari namna hii....alisema lini hizo habari?" aliongea mengi Mh. Mabandu kisha akauliza.



    " siku mbili kabla ya hili tukio" alijibu IGP.

    Mungu wangu! Hii inaleta picha gani sasa, au....lakini sasa kwanini ulichukua maamuzi mkononi bila kunijulisaha IGP? Mimi na wewe tunamjua Backa vizuri na Backa ndiye aliyefanya wewe ukawa hapo, unafikiri atajihisi nini...ataona kama anatengwa Backa si wa kusononeka Liyambo!"



    "najua mkuu...!"



    "hapana hujui wewe laiti ungejua usingekubali kuamini kauli ya mtu mmoja kuja kuzima maamuzi yako" alimkatisha kisha akatoa amri ya kuhakikisha binti wa Mh. Backa anapatikana ndani ya siku mbili tu kisha akaamuru Ulinzi mkubwa ikiwezekana ataongeza wa kutosha zaidi kwa mh. Backa. IGP akatoka mule ndani akiwa na mkanganyiko mkubwa wa mawazo. Kichwa kilizidi kumuuma zaidi ya awali, huku hivi na huku vile nini, ni lipi na lipi ni nini, akachoka. Aliinyanyua simu yake ya mkononi na kumpigia kijana wake, huyu alifahamika kwa jina la Inspekta Bogo.



    "anza kazi sasa, mimi sielewi naona mafiligisu tu kisha uwe unanitumia ujumbe kila hatua utakayokuwa unapiga" alitoa amri, upande wa pili ukatii lakini pia akatoa kazi ya siri kama hiyo kwa kijana mwingine. Akang'oa gari yake na kutoka kwenye vile viunga vya Ikulu. Lakini wakati yeye anatoka, kuna gari moja ya kifahari sana ilikuwa inaingia hii bila shaka haikuwa mbali na mazingira hayo maana ni punde tu baada ya kutoka ya IGP nayo ikaingia. Ilikaguliwa nje ikiwa ni sambamba na ndani ya gari hiyo kisha ikaruhusiwa kuingia kwenye lango kuu la Ikulu hiyo iliyopo ndani ya jiji la Pande. Akashuka mtu ambaye alionekana viatu tu hadi magotini kisha mtu huyo kuelekea ndani ya hiyo Ikulu.



    ******

    *******

    Majira ya saa kumi za jioni, majira hayo ndiyo ambayo yaliweza kuwa rafiki kwa bwana Ndungai, Boti ndogo ya kifahari ilikita nanga kwenye fukwe ya Backa Island kisha mtu mwenye mwili mkubwa kiasi akashuka akiwa anaitazama anga kwa kunyanyua shingo juu. Alipoishusha shingo yake alilitazama jumba kubwa la rafiki yake mara machozi yakamtoka akayafuta kwa mikono yake na kupiga hatua ndogo ndogo kulielekea jumba hilo. Alifika mahali ambapo Backa alikuwa amejipumzisha akamtazama kwa muda kidogo, machozi mengi yakammwagika lakini alifanikiwa kuyafuta na kujiweka kitini.



    "sikuyajua haya mapema ndugu yangu, sasa naamini dogo ukililetea mzaha lazaa kubwa na kutunga usaha" akatulia. Backa akanyanyua macho na kumtazama huyo mtu mbele yake halafu akainama tena, Ndungai akaendelea.



    "nisamehe sana Backa lakini sitabaki kimya kwenye hili....lakini mimi sidhani kama hili linaweza kufanywa na mtu kutoka mbali Backa" kauli hii ndiyo iliyompa Backa uhai na kumrudisha mahali hapo ni wazi alikuwa maili nyingi kimawazo, akazidi kuyafuatilia maneno ya rafiki yake.



    "hawa watakuwa ni watu kutoka humu humu nchini na bila shaka ni watu wa karibu zaidi ambao walikuwa eidha unafanya nao kazi pamoja au walikuwa na ukaribu na wewe" Backa alizidi kutoa macho. Sasa haya maneno alianza kuyaelewa vizuri japo si mara moja kuyasikia lakini hapa alijikuta akiamini kuwa huenda hilo likawa na ukweli zaidi lakini hakunyanyua mdomo wake kusema lolote, Ndungai akazidi.



    "Ulikuwa una marafiki wengi sana Backa hasa Tanzania, yule waziri mkuu wa kipidi chako alikuwa ni rafiki yako sana yule. hebu jaribu kumueleza hili kama ikishindikana.....lakini haiwezi kushindikana, anaweza hata kukutafutia wapelelezi wa siri wakaja hapa ili kujua ni nani anayehusika na huu mpango kisha wakalipa kwa hili." akakomea hapo kwa muda mdogo tu, akamtazama rafiki yake alipoona amepumua vya kutosha akamalizia kabisa.



    "kama akishindwa kukupa msaada mimi nitajua cha kufanya" alipokwisha kusema hayo akanyanyuka na kutoka mule ndani hadi nje, huko akaelekea lilipo Boti lilomleta mahali hapo, akaitazama bahari kwanza kwa muda mrefu, aliona kama miili ya askari iliyopotea imemezwa humo lakini hakutaka kujipa tabu, kulifikiria hilo ambalo si ndani ya jukumu lake kwa wakati huo alipanda Boti na kuondoka.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Neno msaada ni dogo sana kulitamka lakini msaada unapotendeka kwa vitendo, neno hilo unaweza kulipa thamani kubwa mno ila pale msaada huo unapoukosa kipindi ambacho unauhitaji, hili huwa ni jambo jingine kabisa. Waweza kuiona dunia ni ya wengine waishio kwenye furaha lakini wewe upo tu kama somo kwa wanaotaka kujifunza kuwa huwa kuna matatizo yanayowakabili binadamu. Hili ndilo neno pekee libaloishi kwenye moyo wa bwana mkubwa Backa. Hakuwa na matumaini na msaada kutoka kwenye Taifa lake, aliona wazi akimpoteza binti yake bila kupata msaada wa kumrejesha binti huyo aliyekuwa ndiye kioo chake akitoka akirudi na hata akiwapo nyumbani tu, pasipo kuiona sura ya binti huyo, kwake ni shida. Kwa muda huo amekuwa mwenyewe, ile sura aliyokuwa akipenda kuitazama haikuwepo tena. Alilia sana hadi machozi machache yaishio kwenye kifua cha mtoto wa kiume yakakauka sasa anajikuta kabakiwa na majonzi yaliyojikusanyia huzuni kubwa machoni mwake. Anapowaza kuwa hakuna msaada wala hakuwa amekosea kwani wakati yeye akiwa anadhani msaada kutoka kwa serikali ambayo hata yeye aliitumikia kwa kipindi kingi utakuja, wanaopaswa kumpa msaada wana kumbana na vitisho vikali mno kiasi cha kujitoa kabisa kwenye wazo la kumfikiria Backa. Mh. Raisi Mabandu, anapokea mgeni ghafla kisha mgeni huyu anamtaka aachane kabisa na sekeseke hilo la kumsaidia Backa. Mabandu akasimama kama Rais na kusema kuwa hawezi kuishi na aibu chumbani kwake hivyo akaapa ni lazima amsaidie Waziri huyo wa zamani hadi pale atakapo hakikisha binti wa mheshimiwa huyo anapatikana. Mgeni asiyejulikana, anapiga kasia na kwenda mbali zaidi na kumuambia kuwa anajua IGP Liyambo alitoka hapo na ujio wake ni kuhusiana na mjadala wa kumjadili Mh. Backa. Kama ni hivyo basi aache na kama atakuwa kinyume na hapo ni wazi asisahau uwepo wa binti yake aliyepo masomoni nje ya nchi kwani muda wowote aweza kuwa matatani. Raisi akakumbwa na taharuki kubwa baada ya kuona kuwa hao jamaa hawakuwa na nguvu ndogo pia wanamtandao mkubwa mno. Kama ujuavyo uzito wa damu haulingani na maji na uchungu wa mwana aujuae mzazi, Mabandu akamshirikisha mkewe hizo habari. Mke akamwambia kuwa mwanae akitekwa basi Backa ndiyo ashike nafasi ya huyo binti. Yalikuwa ni matusi kwa mzee wa watu lakini Mabandu hakuwa na kitu cha kuongeza hapo akaamua kutulia huku moyoni akisema Kila Mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake. Akalipotezea kama hakulisikia. Kwa IGP nako mambo yalikuwa ni hayo hayo lakini yeye ilikuwa ni tofauti kidogo maana yeye alipokea ujumbe tu kwenye simu baada ya kupigiwa na mtu asiyemjua kisha kuambiwa asitishe zoezi la kumpa msaada Backa, haikuishia hapo, mtuma ujumbe aliongezea akasema kuwa kama akikaidi ni wazi atazika viungo vya wazazi wake waliopo huko kijijini au awakose kabisa yaani asiwaone machoni mwake. Hili la kuuliwa wazazi lilikuwa ni zito zaidi lakini sifa ya Liyambo ni ubishi na ubishi huo ndiyo uliomfanya kupata hicho cheo cha kuwa mkuu wa Jeshi la polisi ndani ya nchi ya Ungamo. Akataka kujua nani mmiliki wa hiyo sauti ta vitisho hivyo akaituma ile namba kwenye mamlaka husika, mamlaka inayohusiana na masuala ya mawasiliano. Ni kama mtoa onyo alikuwa akimuona kwani akiwa katika harakati za kufanya hivyo, ujumbe mfupi wa maneno ukaingia kwenye simu yake. Akaufungua haraka haraka, ujumbe huu haukuwa na jina wala namba ya mtumaji ulikuja wenyewe tu........



    "kufanya kitu chochote cha kutaka kutufuatilia hilo ni kosa kubwa kuliko hata kulala na mama yako mzazi. Chunga sana" ajabu alipomaliza kuusoma huo ujumbe, simu ikazima. Akaiwasha, washa na wewe lakini simu haikuwaka, inamaana hata huo ushahidi pia unapotea. Akatulia Liyambo na kujiuliza maswali mengi mfululizo ni akina nani hao na wamefanywa kitu gani na Backa hadi kuwa hivyo? Jibu hakulipata na kama angelipata lingekuwa la uwongo au la kujifariji tu. Akaamua kujinyamazia lakini akaapa moyoni kuwa hawezi kuacha kujaribu. Alijipa imani hiyo kwa sababu tayari alishamuingiza Mpelelezi hatari wa jeshi la polisi Inspekta Bogo na hakukuwa na Kenge yoyote aliyekuwa akijua hilo. Akaamua kuelekea nyumbani kwa Inspekta majira hayo ya saa moja usiku ili kumueleza kuwa yeye anakaa pembeni kwanza ili kuwaridhisha hao watekaji wa binti wa mh. Waziri Backa lakini yeye aendelee na kazi kwa usiri mkubwa kwani hakuna anayemfahamu pia akampa simu ndogo mpya iliyo na 'line' mpya pia kisha akamwambia hiyo ni kwa ajili ya kumpa habari za upelelezi wake tu na si vinginevyo, Inspekta Bogo akakubali kwa heshima kubwa kisha wakaagana. Wakati Liyambo akiwa anatoka kwa Inspekta Bogo, huku mh. Backa aliamua kuyatilia maanani maneno ya rafiki yake wa toka zamani na mfanyabiashara mwenzie kuwa hali kwa muda huo imekuwa tete na serikali yake imekaa kimya hivyo hana budi kuomba msaada binafsi kwa rafiki yake wa zamani kutoka Tanzania. Muda huo ndiyo aliikamata hiyo simu na kuiweka sikioni.



    "habari za masiku tele?" salamu ilisikika kutoka upande wa pili wa simu hiyo. Backa akavuta kamasi nyembamba kisha kujibu salamu hiyo kwa sauti kavu iliyolia kwa kitambo kingi, ilikuwa ni sauti iliyokosa rutuba kabisa.



    "si nzuri kabisa ndugu yangu" alijibu Backa mara baada ya kuvuta zile kamasi nyembamba.



    "inaonekana si nzuri kabisa kweli maana sauti yako na muda ulionipigia vinaoana na taarifa hiyo, kunani sasa ndugu yangu....umefiwa?" ukaweka swali upande wa pili ili kutaka kujua zaidi nini kinasababisha. Backa akafunguka mwanzo wa vitisho hadi vitisho kwisha na kuondoka na binti yake. Mtu aliyeko upande wa pili wa simu alisikitika sana tena sana hadi kukosa neno la kusema kwa muda kisha akamwambia kuwa jambo hilo la kuhitaji wapelelezi si dogo ni jambo la kumhusisha mkuu wa nchi na kwa kuwa yeye ni mtu wa karibu sana na Raisi, akamuahidi bwana huyo kuwa muda huo huo anampigia simu mheshimiwa ili kupata nafasi ya kuonana nae hapo kesho. Akamuahidi kuwa hata yeye jibu atalipata kesho hiyo hiyo hata kama ni usiku wa giza. Backa akavuta pumzi ya matumaini na kuamini huwenda msaada wa kupatwa kwa binti yake upo karibu. Aliiamini sana Tanzania, aliamini sana wapelelezi wa Tanzania hivyo hakuwa na mashaka juu ya hilo. Angalau kwa muda huo akapata walau muda wa kuutafuta usingizi japo chakula kiliendelea kugoma kupita kooni. Wakati yeye akiwa anautafuta usingizi, ndani ya Jumba lile la kizamani ndani ya nchi hiyo hiyo ya Ungamo, kulikuwa na kikao kizito mno kuliko uzito wenyewe na kilikuwa kikiendeshwa na vijana watano tu. Kikao hicho cha ghafla kilikuja baada ya ugeni wa ghafla pia kuingia ndani ya ngome hiyo. Ugeni huo ulikuwa ni kijana mdogo wa Kirusi lakini mwenye sauti inayoheshimika na kuogopewa sana na vijana wa hapo himayani. Alikuwa ni Bencov.



    "msione kimya ndugu zangu baada ya kutoa agizo lile la kwenda kumuua yule mpuuzi kule kwa Backa, ukimya ule haukuwa bure kwani nilipokuwa nimeagiza Benson aende kwa Dr. Lee kwa ajili ya kupata mchanganyiko wa awali kwa ajili ya kutengeneza sumu ya kuangamiza hili Taifa, kukazaliwa mambo mengine mapya lakini yenye msaada vile vile kwetu" akanyamaza Bencov. wote mule ndani wakamtazama kanakwamba hawajamuelewa lakini kabla hajaendelea, Bacon akauliza.



    "ni mambo gani hayo?" Bencov akageuka na kumtazama Bacon kwa nukta moja kisha akaendelea.



    "Dr. Lee naye anayake makubwa mno na ameomba tuungane pamoja" aliposema hivyo miguno ikakita mule ndani na sauti za pamoja kutoka



    "kivipi" huku Bacon akimalizia.



    "kwanini umemuamini huyo Dr. Lee mapema kiasi hicho?" kimya kikatanda ndani hapo huku vichwa vya vijana wane vikitikisika juu chini, hii ilimaanisha kumuunga mkono Bacon.



    "nilijua mngesema hivyo, nilijua tu na ndiyo maana nikawahitaji hapa....hivi mnajua ni kwanini Benny alichelewa kuja huku?" akauliza lakini hakusubiri jibu, akaendelea.



    "nilitaka awe shahidi namba moja kwenu ili mjue nini nataka kiwe. Dr. Lee ni mzee sana lakini anaakili nyingi kuliko mchwa, huyo mzee anauwezo mkubwa kuliko nitakavyowahadithieni ninyi hapa. Dr. Lee anauwezo wa kubadili baadhi ya viungo vya binaadamu kuwa sumu ama kemikali mbaya, sasa hiyo amegoma kutuuzia sisi bali ametaka ushirikiano kwani hata yeye anamaswaibu makubwa na anataka kuyatimiza kabla hajafa na ni kwenye moja ya Taifa lililo ndani ya bara hili la Afrika, hakutaka kulitaja ni Taifa gani. Pia Dr. Lee ni mgonjwa sana hawezi kutugeuka yule...Benny nadhani umemshuhudia yule mzee, anataka ushirikiano wa kweli na kwa hili tutashinda sisi na vilevile atashinda yeye kisha kila mmoja anafanya yake" alipokomea hapo watu wote pale wakabaki kimya. Kimya kile kilipokoma, Bencov akawaambia vijana wake watatu wale kuwa kuna kijana anajua na anaweza kuwaambia miili ya askari waliokuwa wakilinda Backa Island wamepotelea wapi, kisha kusema kuwa hiyo yote ni mipango ya Dr. Lee kuhakikisha anajaza dawa za kutosha ili kuja kumpa binti wa Backa kazi ya kumalizia ili waweze kuismbaza dawa hiyo.



    "hivi huyo binti anaweza kuifanya hiyo kazi kweli?" aliuliza Dede baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu. Swali lake halikujibiwa ila alichoambiwa ni kuwa kazi bado haijaanza na kila kitu kitakachokuwa kikihitajika hata kama ni roho ya mtu, watapewa wao kwani Dr. Lee amekabidhi rasmi hiyo kazi mikononi mwake. Vijana wakafurahi na kuahidi kuifanya kazi hiyo kwa nguvu kama wanaweza kupata oda. Bencov akawaambia hao vijana kuwa wazidi kuimarisha ulinzi kila kona na wahakikishe kila anayeingia ndani ya nchi hiyo kama hawamuelewi basi ni kumuondoa duniani mapema sana kabla hajapata mahali pa kulala. Kwa maagizi hayo tu kazi ilionekana si ndogo. Kikao kile kikaisha. Muda ulikuwa umekimbia sana. Kijana aliyeshupaa mwili utadhani hali, alikuwepo hapo kwenye hicho kikao na ndiyo maana kikawa na watu watano. Huyu alikuwa hapo kwa ajili moja tu ya kumuwakilisha raisi wa zamani mh. Julio Mobande.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi ya siku iliyofuata ilikuwa ni tulivu sana huku anga likionesha kila dalili kuwa muda mfupi mbele kungeweza kunyesha mvua. Pamoja na utulivu huo wa siku hiyo lakini kwa Mh. Ndungai hakukuwa na utulivu hata kidogo huyu alikuwa akilia moyoni japo hakuonesha huzuni. Hakujali kabisa kama siku iliyoisha, kijana wake aliingia hapo usiku kutokea nchini China kwa ajili ya kwenda kutafuta Kampuni kubwa ambayo itamsaidia kukuza biashara yake ya magari yaendayo kasi. Mzee huyo alikuwa ni kipenzi sana cha kijana huyo na ndiye aliyehakikisha kijana huyo anakuwa juu kimaisha na hakutaka kumkwamisha hata kidogo kwenye kile anachokihitaji ili tu kuikuza kampuni yake ambayo ilinza kukua kwa kasi baada ya kuingia rasmi kwenye ushindani wa kimataifa. Alimpenda sana kijana wake lakini kwanini sasa usiku uliopita hakujisumbua kwenda kumpokea uwanja wa ndege na ilhali aliujua ujio wake, ulikuwa ndiyo utaratibu aliomjengea kijana wake huyo hasa anapokuwa hajasafiri. Alikuwa akijiuliza sana Ndungai juu ya maswali atakayo kumbana nayo piandi tu atakapoikutanisha sura yake na kijana wake, lazima angetaka kujua hali ya binti anayempenda, lazima angemuulizia tu alikuwa na imani hakupata kusikia habari yoyote ya kutangazwa kuhusu kupotea kwa binti huyo ambaye alikuwa ndiyo moyo wake wa pili. Angejibu nini Ndungai? Ni bora basi angesikia taarifa kwenye vyombo vya habari juu ya upotevu wa binti huyo huwenda asingeulizwa sana mambo mengi angelikuwa akiyajua lakini haikujulikana ni kwanini taarifa ilifichwa kwenye vungu zisizojulikana kama ni za vitanda au za meza kisha kushindwa kutangazwa hata upotevu wa askari waliopotea. Unaweza ukajiuliza yale maswali ya wanahabari yalikuwa ni ya nini sasa, au ndiyo wauwaji wana nguvu nyingi kuliko serikali au serikali ndiyo imezuia zile habari zisirushwe hewani? Nini hii maana yake? Ama kweli hali ilikuwa ngumu sana. Kitu ambacho Ndungai hakukijua ni kuhusu uwepo wa kijana wake hapo sebuleni kwa muda tu na tayari alishamuona jinsi alivyokuwa amekosa raha. Tamimu alijiuliza sababu za mzee wake kukosa raha namna hiyo, akajua labda ni kutokana na yeye kutokujulikana kama amefika hapo ama laa.



    "lakini nilimpigia simu kuwa nimeshafika jana usiku sasa kwanini hivi" alijiuliza Tamimu kisha kuamua kumgutusha kidogo.



    "baba, nipo hapa mbona halafu hauko sawa nini tatizo" aliongea Tamimu lakini mshtuko wa baba yake ulimtisha sana. Ndungai alishtuka mno hakutaka kuiona sura ya kijana wake mahali hapo lakini ndiyo hivyo tena na hakujua jinsi ya kumkwepa.



    "hakuna tatizo kijana wangu nipo hapa nimekumbuka mengi sana yaliyopita toka enzi hizo" alijibu Ndungai akiwa kwenye wasiwasi kidogo. Tamimu akajua hapo anadanganywa lakini alijua jisi ya kuweza kiliweka sawa hilo jambo akaamua kujifanya kupotezea na kwenda sawa na akili ya baba yake.



    "usitake kuniambia kuwa umemkumbuka mama tena" alisema Tamimu huku akionesha tabasamu la mbali. Baba yake akageuka na kumtazama kisha akayarudisha macho yake kule alikokuwa akitazama awali.



    "umejuaje kuwa namkumbuka mama yako hapa? na ni lazima nimkumbuke, unafikiri angekuwepo hapa ungekuwa hivyo wewe, ungekuwa ni mtu unayetulia nyumbani na kutufanya sisi wazazi wako tufarijike kukuona sijajua ni kwanini upendo wa kweli mnawaonesha mama zenu ninyi watoto" aliongea Ndungani na kumfanya Tamimu kutulia kidogo kisha akasema.



    "samahani sana baba yangu kama nimekukosea lakini kumbuka kuwa hii ni moja ya kunifanya niwe mtu maarufu duniani pia nilitaka kutimiza ahadi niliyokuahidi kuwa siku moja gari zangu zitatumika sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya mashindano." akaweka kituo kisha akasema tena.



    "sina muda mrefu sana nitatulia nyumbani kwani tayari nimepata wafanyabiashara wakubwa ambao watakuja kufanya mazungumzo na mimi ya kibiashara pamoja na kufanya majaribio ya gari zangu. Nikisha kamilisha haya baba lazima nimuoe Tereza ili niishi kwa amani sasa" maneno hayo yakawa ni mwiba mkali usiouma bali uliosababisha mshtuko wa aina yake kwenye moyo wa Ndungai kisha kumpa unyong'onyevu wa haja. Kwanini alinyong'onyea baada ya kupata mshtuko? Hili swali ndilo la kwanza kujiuliza moyoni Tamimu kisha kumsogelea karibu zaidi baba yake na kumuuliza. Kwanini ameshtuka kiasi kile. Mzee Ndungai hakuwa na jibu aliloona litakuwa dawa ya kuweka sawa akili ya kijana wake zaidi ya kumwambia ukweli juu ya upotevu wa Tereza, hakujali ni kiasi gani kijana huyo ataumia. Aligeuka na kumtazama kwa nukta kadhaa kisha kufungua kinywa chake kilichozungukwa na ndevu nyingi za busara.



    "kijana wangu, hakuna kilichofanya niikose amani moyoni mwangu kama hiki" kauli hiyo ikamfanya Tamimu kuwa makini zaidi kusikiliza kipi hasa kama sio hicho au chochote kilichomkosesha raha baba yake.



    "Tereza amepotea.....mmh! Hapana, nikisema amepotea nitakuwa bado nauficha ukweli, Tereza ametekwa na watu wasiojulikana sura wala ngozi yao na tulipojaribu kumtafuta, hakuna cha maana sana tulichoambulia zaidi ya kukutana na 'mafigisufigisu' yasiyoeleweka. Ni magiza mawili sasa sijui tangu kutoeshwa kwake" aisee! Kama kuna siku ambayo Tamimu alichoka na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja basi ni siku hiyo. Kijana huyo alizikamata nywele zake zilizo na mchanganyiko wa mataifa mawili tofauti, akazivuruga kisha kumtazama mzazi wake kama vile alikuwa akitaka kumwambia asijaribu kuweka utani mbele ya jambo ambalo maumivu yake hayana kifani lakini sura ya baba yake ilitosha kumuonya na kumwambia kuwa ni tangu lini mzazi akajenga mazoea ya kumdanya mtoto. Tamimu mwenye asili ya kiarabu kwa mama huku akiukomba weusi kidogo kwa mr Ndungai, alimkamata baba yake na kumuuliza ni nini hasa kinachojiri hapo na ni kwanini hakumpa taarifa mapema hadi asubiri ujio wake na kwanini wasimtafute  kwa kila hali hadi wampate,





    kisha hayo akaona hayatoshi akaongeza na kuuliza hatua aliyoichukua baba wa binti huyo.



    "my boy, Tereza hakutekwa na kikundi cha wachunga Ng'ombe, Tereza ametekwa na watu wazito na walidhamiria kufanya huo utekaji. Tulijitahidi kuishirikisha Serikali juu ya jambo hili lakini hakuna lilichofanyika zaidi ya ukimya hadi sasa. Baba wa Tereza amechanganyikiwa sana tena sana hakuna mfariji anayempa faraja zaidi ya kilio, kilio kimekuwa karibu yake zaidi na hicho ndicho kinachompa faraja yenye kupunguza angalau maumivu ndani yake. Amejiona kama ni mtu wa kuja tu ndani ya Taifa hili na si yule aliyekuwa anajitoa si kwa hali bali kwa mali ili tu kuhakikisha Taifa changa linakomaa angalau lifike mahali litambulike kwenye umoja wa mataifa yaendeleayo. Si kitu yote hayo aliyoyafanya na badala yake ameachwa na kutazamwa kama nyumbu wamtazamao mwenzao anavyoshambuliwa na Simba. Hakuna msaada" alieleza Ndungai ikiwa ni pamoja na kutoa majibu ya maswali mengi aliyoyauliza Tamimu. Hakuuliza swali jingine huyo kijana alitoka hapo ndani kwa kasi kubwa sana hadi yalipo maegesho yake ya magari ambayo hakuwahi kuyatumia, akaingia kwenye gari moja lililo na chata kubwa la moto ubavuni huku likiwa na maandishi mazito mekundu yaliyosomeka T.N RACE. Chini kidogo ya ile alama ya moto. Haya yalikuwa ni magari yaliyotengenezwa na kiwanda chake kipya kabisa cha T.N Company na hakuwahi kuyatumia magari hayo hata siku moja. Aliwasha gari hiyo yenye namba U 78 RS kisha kulirudisha nyuma kwa kasi kubwa na kuligeuza kwa kupiga no linda, alipokuja kuliweka sawa tayari lango lililokuwa likifunguliwa kwa kifaa maalumu lilikuwa wazi. Aliiruhusu gari hiyo yenye sauti nzito mithili ya Simba mwenye wivu, ikachomoka kwa kasi kubwa sana hadi baba yake akashika kichwa. Hakuwahi kumuona kijana wake kuwa katika kasi hiyo ya gari hata siku moja.



    "nini anafanya huyu kijana?, anakwenda wapi sasa jamani? alijichapa maswali mawili kisha kuyaacha bila kuyajibu. Tamimu alipotoka hapo nyumbani, alivuka mitaa kadhaa na kuikamata barabara ndogo ya Muavengero kisha kuiacha hiyo barabara na kupita kwenye mtaa wa madukani akaja hadi kwenye makutano ya barabara ya Taifa, akaiyacha hiyo ya Taifa na kukamata barabara kubwa ya Haika, hii ilifahamika kama Haika Road. Hapa ndipo alijikuta akiwakusanya watu na kuwaacha midomo wazi. Alizizunguka gari nyingi sana alizozikuta kwenye barabara hiyo ambazo zilikuwa kwenye foleni kisha akapita kwenye upande ambao si wake kiuendeshaji, akawa anatazamana na magari yanayokuja kwa kasi huku yeye akiwa kwenye kasi kubwa. Alipishana na hizo gari kwa kasi hiyohiyo hadi nyingine zikawa zinasimama tu kumpisha mbabe huyo afanye yake hadi alipoimaliza ile foleni na kuweza kuingia kwenye upande wake, akakanyaga mafuta kwa fujo na kufanya hiyo gari iongeze kasi maradufu, watu walishangaa sana huku wakiulizana maswali ambayo waliyajua wenyewe.



    "ulishawahi kuiona hii gari mahali?" kijana mmoja alikuwa akimtupia swali mwenzake.



    "hapana hii gari ni mpya kabisa machoni mwangu na ni ya kipekee sana" alijibu mwingine.



    "aloo! Kuna watu roho zao ni kama hawatembei nazo jamaa, ule siyo mwendo wa kutumiwa na binadamu mwenye nyama na damu kama mimi na wewe, yule atakuwa na mwili wa plastiki au mbao siyo bure kabisa." alichomekea mwingine lakini wote wakiwa ni kuhusiana na kustaajabia mwendo na uendeshaji wa gari ile ambayo iliacha gumzo pale mjini. Tamimu alikuja kusimama karibu na msitu wa Gonja kisha kutulia kwa muda akitafakari hili na lile pasipo kupata suluhu ya tafakuri yake.



    Wakati yeye akiwa hapo bila kujua ni njia gani anaweza kuipata kuweza kumsaidia mpenzi wake ambaye amepotea ama kutekwa kama taarifa zilizomfikia, Machozi yalikuwa yakimmwagika kupita kiasi, Tamimu alilia kwa sauti ya juu mno. Yote hayo yakiwa yanaendelea, kwa mh. Backa kunazidi kuwa kugumu zaidi baada ya kupokea ujumbe kutoka kwa rafiki yake wa Tanzania kuwa Mkuu wa nchi hiyo ya Tanzania, amegoma kutoa msaada huo huku akiweka hoja za msingi kuwa mambo binafsi hayahusiani na hayo aliyoyataka, akashauri labda kutafuta wapelelezi wa kujitegemea ambao wangeweza kumsaidia zaidi. Ujumbe huo haukuja na suluhu yoyote ile kwa Backa kwani hakuambiwa ni nchi gani inahusika na hao wapelelezi wa kujitegemea hilo likamfanya mh. Backa ajikunyate kama kinda la Njiwa ama kifaranga cha kuku huku akikosa pa kuendea ili apate msaada. Backa anajikuta amechoka na kuchoka zaidi hadi nguvu ya mwili kutaka kumkimbia, ujasiri wa kiume pekee ndiwo uliozizuia nguvu hizo lakini ujasiri huo haukuweza kukizuia kilio, Backa akalia tena, tena na tena hadi akakosa sauti. Lakini muda huo kwa jinsi ulivyokuwa ukikimbia ndivyo ambavyo Ndungai alivyokuwa akipata mashaka na mshawasha wa kutaka kujua ni kipi kimejiri kwa rafiki yake. Au hakutumia njia aliyompa? Aliwaza sana Ndungai kisha akaitazama saa, saa ikamwambia kuwa muda si rafiki kwake na tayari umeshamtupa mkono kwani tayari ilikuwa inakimbilia jioni. Akamfikiria kijana wake ambaye tangu alipoondoka hakurudi na kila alipopiga simu yake ilikuwa haipokelewi, huyu akamchanganya zaidi akaamua kutumia njia ambayo alimshauri rafiki yake lakini hii ilikuwa ni kupiga ikulu moja kwa moja. Akazama ndani na kwenda kwenye simu yake ya ofisi ndogo ya pale nyumbani. akaandika namba mbili tatu ambazo alikuwa na uhakika wa kumpata mhusika mwenyewe. Akaweka sikioni.



    "Haloo!" sauti nzito iliyopata kuwa na utulivu mkubwa ikapokea simu. Ndungai akashusha puamzi inzito kisha akasema.



    "muheshimiwa, Ndungai hapa naongea" akajitambulisha, upande wa pili wa simu ukawaka kwa furaha kisha zikafuata salamu ndefu za marafiki hao na kuulizana habari za siku nyingi tangu kuonana kwao. Baada ya maongezi hayo yaliyotosha kuonesha ukaribu wao wa kirafiki, Ndungai akaenda kwenye mzizi wa kupiga simu hiyo. Akaeleza kile kilichomvuta ama kumlazimisha kupiga simu hiyo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Ndungai nini tatizo la nchi yenu, nimezipata taarifa japo hazikuwa zimeshiba sana lakini inaonesha ni tatizo kubwa kwani hata waziri wangu wa mali asili na utalii amenipa hizo ripoti. Sikuzipa uzito sana kwani niliona ni mambo binafsi tu hivyo sikutaka kuyapa uzito mambo hayo, hebu nishawishi kwa kina" aliongea mmiliki wa sauti hiyo ya upande wa pili ambaye alikuwa ni mh. Rais wa nchi ya Tanzania mh. John Martin. Ndungai hakuacha kumpa maelezo yote kinagaubaga kuanzia mwanzo hadi hapo yalipokomea. Muheshimiwa Martin John, akampa cheo Ndungai kwa kumwambia kuwa kwa niaba yake atalivalia njuga hilo jambo. Moyo wa ndungai ukalipuka lipu kwa furaha, akaona sasa huo ndiyo ulikuwa muda wa kupata uhakika kuwa Tereza angepatikana muda si mrefu. Hakujua kuwa katika mambo kama ahadi huwa hayatabiliki ni muda gani yanaweza kutekelezwa.



    Ahadi si jambo la kulipa asilimia nyingi kwamba punde utakapoahidiwa basi itakwenda kutimia, yeye hakujua ni muda gani ahadi aliyoahidiwa kutoka Tanzania itakwenda kutimia kwasababu hakutajiwa siku wala saa. Siku zikakatika, wiki nayo ikaingia bila matokeo. Ile ahadi akaiona ni kama ahadi butu kwake. furaha iliyokuwa imepamba uso wake ikafifia na kubaki akijiuliza, hivi rafiki yake anagundu au? Ni lazima alikuwa ajiulize hivyo maana tangu kukumbwa na mabalaa, hakuna jambo la suluhu linalopangwa likafika mwisho. Backa alizidi kukonda kwa kuwa mbali na chakula na si Backa pekee bali hali ile iliwaathiri watu wengine. Mmoja akiwa ni mtekwaji na mwingine akiwa ni Tamimu. Wote hao waligoma kabisa kula kwa nafasi zao hali hiyo ikawa ni tishio kwa kila aliyekaribu na watu hao. Ndungai aliogopa kuendelea kushuhudia watu wake wa karibu wakizidi kuteseka kwa njaa na mawazo dhidi ya mpendwa wao, kulikuwa hakuna mkombozi zaidi yake, ndiyo, mkombozi alikuwa ni yeye tu kwani wote walikuwa chini ya jicho kali la kamera linalowafuatilia. Ni nani angekubali kuipoteza familia yake kwa ajili ya rafiki, jibu ni hakuna. Ndungai alichoka haswa na kujikuta akikata tamaa lakini tunaambiwa kuwa siku zote muomba Mungu hachoki na yeyote aombaye kwa dhati basi hupewa. Ni siku hii jioni, Ndungai pasipo mategemeo yake, anapokea simu kutoka Tanzania na kuambiwa kuwa lile ombi lake sasa linakwenda kutimia. Mh. Rais wa nchi hiyo alimwambia kuwa anatuma vijana wawili, hao ndiyo watakaokuja kuifanya hiyo kazi lakini awe makini, asiwe mtu wa kuropoka kwani yaweza kuwa hatari mno. Ndungai akafurahi kupindukia, furaha ile ikavuka mipaka akaona si vibaya akawashirikisha watu wake wa karibu ili nao waweze kufurahi pamoja. Si kama hakuikumbuka ile kauli au onyo alilopewa na mtu aliyempa msaada huo binafsi la, ila aliona kuropoka ni kule kuitoa siri nje ya watu wasiohusika lakini hakujua kuwa kuropoka kwaweza kuwa ni kuitoa siri kifuani mwako na kumpa mwingine, hili hakulijua. Siri ile akampa kijana wake kijana akaahidi kuwafuata watu hao uwanja wa ndege ikiwa ni kuonesha kuwa anahitaji sana msaada wao ili kuweza kumrudisha mpenzi wake nyumbani. Ndungai akamwambia kijana wake kuwa hilo lisimpe tabu kwani watu hao hawatafikia kwa mtu yeyote yule zaidi ya wanapopajua wao. Alipokwisha kufanya maongezi na kijana wake, akarudi nyumbani kwake kisha akamata simu ili kuweza kumpa taarifa zile mh. Backa. Simu ikaita kidogo tu kisha ikapokelewa.



    "Mungu amesikia kilio chetu rafiki yangu" ndivyo alivyoanza Ndungai mara baada ya simu yake kupokelewa.



    "nini kipya tena Ndungai, kunamsaada wowote?" alihoji kwa upole sana Backa, hakuwa na imani na chochote kile yeye alijihesabia kuwa ni wa kupoteza tu.



    "kunatumwa wapelelezi wawili kesho wanaingia ndani ya nchi hii ili kuweza kufanya upelelezi wa kina juu ya sakata hili" akaweka pozi hapo huku akipumua pumzi ya faraja sana kwa kuweza kumpa taarifa nzuri rafiki yake. Backa ni kama alikuwa akirudi tena duniani, ile taarifa ilikuwa ya kipekee sana kwake na hakuitegemea. Hakutaka kuuliza aliwezaje kufanya ushawishi hadi kupewa wapelelezi hao wawili, alichokuwa nacho kwa wakati huo ni furaha pekee. Alitoa shukurani nyingi za dhati sana kwa rafiki yake huyo kisha akaahidi mengi pia kubwa likiwa ni kuiunganisha familia hiyo pingi Tereza atakapopatikana. Simu ikakatwa huku Backa akipata nguvu ya kusimama kutoka kitandani lakini alishindwa kupiga hata hatua kutokana na mwili kuwa dhoofu kwa kukosa chakula kwa masiku mengi ama wiki kadhaa. Akarudishwa tena kitandani kwa kukalishwa na Phili huku akiagiziwa chakula ambacho alikila kwa furaha iliyoletwa na matumaini mapya.



    Ni tofauti, kwani wakati wao wakiwa wanapata matumaini. kwa upande mwingine simu zilikuwa zikifanya kazi kubwa ya kuwaita watu pamoja. Nasema hivyo kwa sababu Ndungai hakujua kama kitendo chake cha kumpigia Backa simu, alikuwa ametengeneza kosa kubwa litakalo wagharimu. Mawasiliano ya Backa yalikuwa yamevamiwa kitambo sana na watu makini ambao walikuwa wakipata taarifa zote ambazo zilikuwa zikitoka kwa simu yake kwenda kwa mtu mwingine na ndiyo maana watu hao wakenda kiurahisi kutoa vitisho kwa mh. Mabandu kutokana na IGP kumwambia Backa kuwa ni lazima taarifa azifikishe ikulu. Mawasiliano yote ya watu hawa yalikuwa yakifuatiliwa kwa ukaribu sana. Watu hao walimfuatilia IGP Liyambo kuanzi anatoka nyumbani kwake hadi ofisini kwake kisha kutoka ofini kwake hadi Ikulu kisha akapewa vitisho Raisi, hata akapewa na yeye kwa wakati wake. Sasa huwenda matumaini ya Backa na watu wake yasiwe ya kudumu.



    MUAVENGERO CASINO



    Ukimya ulikuwa umetawala sana ndani ya chumba kimoja cha Casino hilo kubwa la mjini Pande.Casino lililobeba jina la mtaa huo maarufu wa Muavengero. Watu wawili wanene walionekana wakishuka garini baada ya gari ya kifahari kusimamisha gurudumu zake maegeshoni hapo. walikuwa ni watu wenye suti za gharama sana. watu hao walikuwa ni wenye kufahamika sana, mmoja alikuwa ni swahiba mkuu wa raisi wa zamani bwana Julio, huyu alikuwa ni yule bwana mwenye tumbo kubwa, Jarome. Hapa alikuwa na mwenzake naye pia alikuwa na tumbo kubwa anayefahamika kwa jina la Kijazi. Waliulenga mlango wa kuingilia kwenye hilo Casino na kuingia humo. Walipita njia ambazo zilikuwa si za kuonekana na watu ili kuepuka usumbufu wa hapa na pale. Walikuwa hapo baada ya simu maalumu waliyopigiwa na kiongozi wao wa kazi. Walifika ndani ya kile chumba tulivu wakatwaa nafasi na kuketi kisha kutoa salamu kwa waliowakuta hapo. Muda kidogo akaingia mtu aliyeshupaa mwili huyu alikuwa ni Kitema, mtu pekee anayemuwakilisha Julio Mobande kwa kila kitu.



    "nadhani tumekamilika si ndiyo?" alisema mtu mmoja huyu alikuwa ni yule aliyeshupaa mwili, alikuwa akigeuza shingo yake kuangalia kama kuna kiti kilikuwa kitupu lakini kabla hajajipa jibu yeye mwenyewe kuwa hakuna kiti kilicho kitupu, Kijazi akajibu kuwa nadhani yeye ndiye alikuwa mtu wa mwisho. Akasema.....



    "vikao vyetu si vya kisiasa wala nini, sisi tuko hapa kwa kuhakikisha tunakamilisha mipango yetu iende kama ilivyokusudiwa. Nadhani kukutana kwetu hapa siyo kwa bahati mbaya, hakuna simu inayojipiga yenyewe halafu iwe na lengo moja la kuwakutanisha watu pamoja kama hivi. Simu mliyopigiwa ilikusudiwa na ilikuwa na lengo la sisi kukutana hapa" akatulia na kuwatazama watu wale watatu kwa pozi kubwa. Alikuwepo waziri wa ulinzi mahali hapo, bwana Bande Sir na bwana Kijazi. Kisha Kitema akaendelea.



    "mimi si muimba ngonjera wala mtamba ngano. niende kwenye kusudi. Kuna kiumbe ameyachoka maisha yake ya kuwa hai na anapenda kufa kifo kibaya mno ambacho hakijawahi kutokea duniani. Nadhani ninyi wenyewe ni mashahidi kuwa tukikutana hapa ni mjadala wa kuitoa roho ya kiumbe au viumbe kwa maumivu makali mno ambayo hata malaika mtoa roho hajawahi kuyatumia katika utoaji wake wa roho." akaweka nukta kidogo kisha akaendelea.



    "kuna mtu anafahamika kwa jina la Ndungai. huyu mdudu anatakiwa afe....mh, mh! Siyo afe.....anatakiwa auwawe leo hii hatakama usiku lakini asifike kesho. Kazi hii nakupa Kijazi najua wewe huruma Mungu alikunyima kabisa. Kwanini afe sasa?....anakufa kwa sababu ameanza kuomba wapelelezi kutoka Tanzania"



    "nini!?" taharuki ikawatoka wote pale na kujikuta wakiuliza swali hilo kwa pamoja.



    "hata mimi na kiongozi tulishtuka vivo hivyo lakini kwa sababu aliamua kutupa taarifa kama mtoto atupavyo jino juu ya bati kwa kutegemea Kunguru atalichukua na kumletea jipya, tulitupia mbali mshangao ule na kuamua kuwapigia simu. Wapelelezi hao wakikanyaga tu Tao De Air Port, nataka wawe mikononi mwako bwana Bande Sir. Utachukua vijana wa kazi kisha utaondoka nao kwa ajili ya kwenda kuwapokea wageni hapo kesho kisha nitakupigia simu hiyo kesho nikuelekeze cha kufanya" alimaliza kutoa malekezo lakini kuna hoja ilitoka kwa mheshiwa waziri bwana Bande Sir kuwa huwenda ikawa shida kidogo kama wakianza kumuua Ndungai kwani taarifa zinaweza kuwafikia wapelelezi na wakasitisha kuja wakihisi labda ujio wao umetambulika. Kitema akasema kuwa Ndungai ni mtu ambaye hana kitu kwenye serikali yeye ni mfanya biashara tu na hata kama watu wakijua ni lazima wapelelezi waje kwani kifo chake kitasikika wakati wapelelezi wakiwa safarini. Akawatoa wasiwasi na kuwaambia wasiwe na shaka kila kitu kipo kwenye mpangilio uliokwenda kidato. Kikao kile kikafungwa na wote wakatawanyika eneo lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Boss, unajua hali ya huyu binti ni mbaya sana anaweza kufa halafu tukashindwa kutimiza kitu tulichokipanga?" aliuliza Merina akiwa karibu kabisaba na Dr. Lee. Dokta huyo hakusema kitu alibaki akiwa ametulia tu eneo hilo kama si yeye aliyekuwa akiulizwa lakini ukimya huo haukudumu sana akasema.



    "siku zote hizo nilikuwa nataka kujua anaweza kubadilika au ataendelea kubaki kwenye msimamo wake wa kugoma kula. Zimebakia siku chache sana za kuanza kutengeneza hayo madawa ya maangamizi na mtengenezaji ni yeye. Leo ndiyo itakuwa mwisho wa kumbembeleza na atakuwa akifuata amri tu" alisema Dr. Lee lakini muda huo huo kuna mtu aliingia mule ndani na kusema kuwa hali ya Tereza ni mbaya zaidi na inavyoonekana kuna kitu amekula kwa ajili ya kujiuwa. Taarifa hiyo ikawa mbaya sana kwa Dr. Lee kwani endapo Merina akifa ni wazi Bencov hawezi kumuelewa hata kidogo na si kumuelewa pekee bali hata mpango wake utazembea.



    "hakikisheni anatibiwa haraka iwezekanavyo na hakikisheni mnampa chakula kwa mipira ili arudishe nguvu haraka sana jamani" alifoka Dr. Lee.



    "usiongee kwa jazba Boss unaweza kukosa pumzi halafu ikawa shida" alisena Merina kwani alimjua Boss wake vizuri, afya yake imekuwa ni ya mgogoro tangu kupata matatizo makubwa sana huko nyuma. Hivyo alikuwa karibu na mzee huyo kila wakati ili ahakikishe anakuwa salama muda wote.



    "naogopa sana Merina, naogopa. Tangu nitokewe na hili lililoniweka hivi nimekuwa muoga sana, unafikiri Bencov atanielewa endapo Tereza akifa" alilalama Dr. Lee akiwa anahofu kubwa lakini Merina alimtoa wasiwasi na kumwambia kuwa hali ya Tereza itarudi kuwa salama hivyo asiwe na mashaka, alimsukuma na kumtoa hilo eneo hadi chumbani kwake ambapo alimshusha kutoka kwenye baiskeli na kumuweka kwenye godoro dogo lililokuwa limetandikwa chini na kumuambia apumzike kidogo mahali hapo kila kitu kitakwenda sawa. Dr. Lee alijilaza kisha akafikiri ya mbali sana. Mawazo hayo yalimpa maumivu makali sana, yalimtoa machozi mzee huyo.



    "siwezi kukaa kimya kipumbavu mimi, nitalipa kwa kila kitu, lazima wafe wote walionifanya hivi" alisema kwa sauti yake ya mkoromo, Dr. Lee alikuwa amewekewa koo la bandia, inaonekana alipata matatizo makubwa huko nyuma na kuna sababu zilizopelekea hivyo. Merina alikuwa amelegea mwili tepetepe, wauguzi walikuwa wakihangaika kumpakiza kwenye kitanda maalumu cha wagonjwa. Ni baada ya kupokea amri kutoka kwa daktari makini sana Dr. Cherlin. Cherlin alikuwa na wasiwasi mkubwa sana na maisha ya Tereza, hakujua ni adhabu gani angepewa endapo binti huyo akikumbwa na matatizo makubwa. Ilikuwa ni lazima angepewa adhabu kali sana. Ni lazima Tereza awe salama hata kwa kuazima dokta nje ya nchi.



    "mpelekeni chumba maalumu cha wagonjwa huyo" aliagiza dokta huyo kisha yeye akachukua box dogo na kuelekea huko alikopelekwa Tereza. Alipofika huko alikuta mgojwa amelazwa kitandani vizuri, alimtazama kwa haraka haraka kisha akamsogele akachukua vipimo na kutulia kidogo baada ya kukitazama kifaa kidogo ambacho kilimpa majibu.



    "hakuna kitu chote kinachomsumbua huyu. Anatakiwa kupata chakula cha kutosha, hakula kitu chochote kwa muda wa siku tatu nzima. Mpelekeni mkamlishe kwa njia ya mipira" alitoa maelezo kuhusiana na vipimo vya mgonjwa kisha akaagiza kitu ambacho alitakiwa kufanyiwa Tereza. Hakwenda mbali alikuwa akifuatilia kila kitu dokta huyo alikuwa ni dokta makini sana lakini ndani yake alikuwa ni katili kupita kiasi, roho yake ilikuwa imepoteza haiba ya ubinadamu kabisa.



    "fuatilieni maendeleo yake na kisha muwe mnanipa taarifa kila baada ya muda" aliongea huku akitoka mule ndani.



    Giza lilikuwa limeumeza mchana na kuvimba kwa tambo kubwa, giza lilikuwa limepamba hasa, hakukuwa na mbalamwezi na pia kulionesha kuwa na mawingu kidogo ya mvua. Utulivu ulikuwa mkubwa mno. Kijazi alikuwa akiingia kwenye himaya ya Ndungai. Ilikuwa ni nyumba kubwa yenye ghorofa mbili. Hakuwa ghorofani bwana Ndungai alikuwa upande wa chini, hiyo ikiwa ni baada ya kutoka kuongea na kijana wake. Alikuwa akitoa maneno ya kumtia nguvu kijana wake kwani ule muda wa kijana huyo ambao alikuwa anatoka, ndiyo huyo bwana Kijazi alikuwa akiikaribia nyumba hiyo taratibu. Aliingia hapo na gari nyeusi tupu. Alizipiga hatua kadhaa hadi kuufikia mlango. Akagonga mara moja mbili, mchakacho ukasikika kwa ndani kisha kuguswa kwa mlango lakini mgusaji hakufungua na badala yake aliuliza.



    "kuna kitu chochote umesahau?" hakukuwa na jibu lolote alilopewa mgongewaji, ukimya wa sekunde kadhaa ukagubika. Ndungai akaamua kuufungua huo mlango kwa haraka akidhani ni kijana wake alikuwa anarudi labla kufuata kitu fulani. Kijazi akaingia humo ndani bila ukaribisho, taratiibu sana, alipiga hatua ndogo ndogo hadi sebuleni. Alikuwa hana wasiwasi kabisa Kijazi. Aligeuka huku na huko kama dume la njiwa linalotaka kumliwaza jike. Ndungai ule ugeni haukumfurahia kabisa alikuwa na mashaka nao sana. Mtu huyu alikuwa anamfahamu, ni mfanya biashara huyu, anamfahamu vizuri sana wanakutana sehemu mbalimbali za kibishara kama mikutano ya kibishara, makongomano ya kibiashara na kadhalika. Hapo kwake vipi sasa, tena usiku. Ugeni ule haukumpa raha hata kidogo. Alikuwa kama hamuoni Ndungai alivyoshangaa bwana huyo. Aliingiza mkono mfukoni na kuibuka na Sigara iliyoundwa kwa mkono. Ilikuwa ni bangi hii, aliiwasha pasipo na shaka lolote kisha kuuvuta moshi na kuuwachia angani kwa fujo. Ndungai alitoa macho sana. 'Marijuana' ndani ya nyumba yake? Aisee ilikuwa ni lazima awe na hofu kidogo. Kijazi alipiga pafu jingine kwa fujo na kuuvuta ndani na kuutoa taratibu.



    "kwanini leo mikono inaniwasha namna hii?" sauti nzito ya Kijazi ilitoka kisha kicheko cha kifedhuli sambamba na kumtazama bwana Ndungai.



    "ni vile umepata kuuwa muda mrefu huko nyuma" mbona haya maneno yalikuwa hayaleti picha nzuri kwa Ndungai, aama! Ndungai alitoa macho baada ya kusikia hayo maneno.



    "wewe ni mfanya biashara, au uliwahi kuwa mtu fulani Serikalini?" aliuliza Kijazi huku akiwa amejishika kiuno, alikuwa amemuinamia Ndumgai kidogo ambae alikuwa amekaa pasipo kujua amekaa muda gani.



    "mimi ni mfanya bia.....!"



    "oooh! Ndiyo, nimekumbuka....Ndiyo maana nilikuwa najiuliza ubongoni ni nani anaetakiwa kufa leo, kumbe ni wewe" alisema Kijazi kwa utaratibu sana. huyu mgeni alikuwa akimchanganya sana.



    "mbona sikuelewi wewe, umeingia bila ukaribisho wangu halafu unaongea vitu ambavyo ha.....aaaah!" Ndungai alipiga kelele hiyo mara baada ya kupata maumivu makali sana kwenye sikio. Lilikuwa likining'inia. mshenzi yule mgeni alimkata Ndungai sikio bwana. Damu zilikuwa zikimwagika mahali hapo. Kicheko kikali kilikuwa kikimtoka, alikuwa anacheka tu kila saa. Sikio lilikuwa limekatwa aliumia sana Ndungai, alijaribu kufanya hivyo mara Tatu, yaani alikuwa akilikata sikio lile kama anakata kitu gani sijui. Halafu kilie kitendo kilimfurahisha sana Kijazi. Maumivu makali aliyokuwa akiyapata Ndungai, kwake ilikuwa ni kama kitu cha kumfurahisha sana.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "unajua kwanini nimekata sikio la kushoto?....nimelikata hilo kwa sababu linanguvu sana. Linanguvu ya kusikiliza mambo yasiyolihusu.....halafu inaonekana viungo vyako vimekuponza?....masikini viungo vumeuponza mwili" alikuwa akiongea mithili ya mtu aliyechanganyikiwa. Alikuwa amepiga koti refu jeusi, hilo koti lilikuwa limevaliwa kwa kazi maalumu si kama jambazi wengine wavaavyo. Lilikuwa refu sana hilo koti kiasi cha kufunika viatu kwa kiasi kikubwa. Kijazi alimtazama Ndungai kama anatazama kitu cha ajabu, ni chizi huyu jamaa. Aliikamata nyama ya mdomo wa chini aisee! akapitisha kisu chake kikali. Hakikufanya makosa, ndungai alizunguuka kama mpira wa tufe. Aliumia sana Ndungai, yalikuwa ni maumivu makali mno, damu zilimwagika mtindo mmoja sura ya Ndungai ilikuwa inaaza kutisha. Kijazi alicheka sana na kurukaruka kwa furaha. Aliiweka Bange yake kinywani na kupiga pafu moja kubwa sana kisha akauvuta moshi kwa nguvu sana kwenye mapafu yake. Alisimama ghafla, alikuwa ni kama amegandishwa na umeme vile. Alikuwa ameyafumba macho yake kwa hisia kali mno, alikuwa akiusikilizia ule moshi kwa jinsi unavyompa madini ya kukiharibu kichwa chake ubongoni.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog