Search This Blog

Sunday 22 May 2022

FUTA MACHOZI MPENZI - 3

 





    Simulizi : Futa Machozi Mpenzi

    Sehemu Ya  Tatu (3)



    Wazazi wakachanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka Melania kuanguka chini kama mzigo. Wakamsogelea, pale chini alipokuwa alikuwa kimya kabisa. Kila mmoja akashangaa, wakachukua simu na kuanza kuzungumza na mtu aliyekuwa upande wa pili ambaye aliwaambia kwamba kulikuwa na ajali mbaya ya gari ilikuwa imetokea na mtu aliyekuwa na simu hiyo alikuwa hoi.

    Hawakutaka kuchelewa, wakamchukua Melania na kumpeleka nje ambapo wakampandisha ndani ya gari na kuanza kumpeleka hospitali. Njiani, walijaribu kumpa huduma ya kwanza lakini msichana huyo hakuweza kuzinduka.

    Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika Hospitali ya Maria iliyokuwa Msasani, wakagawana, wengine wakaelekea katika Hospitali ya Palestina alipokuwa amelazwa Godson.

    Walipofika na kuulizia mapokezi, wala halikuwa jambo gumu kumpata kwani tukio hilo lilitokea muda mchache uliopita na ilikuwa ajali mbaya. Wakaelekezwa katika wodi aliyokuwepo na kuambiwa kusubiri.

    “Anaendeleaje?” aliuliza baba yake Godson.

    “Bado hali yake si nzuri! Naomba mtuache kwanza,” alisema daktari kwa harakaharaka kama mtu aliyekuwa akiwahi kitu fulani.

    Walikuwa wakijaribu kuyaokoa maisha ya Godson, alikuwa kwenye hali mbaya, kichwa chake kilichanika mpaka kuzifanya damu kuanza kutoka puani mwake. Watu walishangaa, mbali na kupasuka huko kichwa, bado mwili wake ulikuwa umechunika na kifuani alikuwa na kovu kubwa kwani alipotolewa dirishani, alitolewa nje kupitia kioo cha mbele na kifua chake kuwa kitu cha kwanza kilichofika kwenye barabara ya lami.

    “Atapona?” aliendelea kuuliza baba yake huku machozi yakianza kumtoka.

    Walisubiri mpaka baada ya saa mbili ambapo Bi Pamela na mama yake Godson walipofika mahali hapo ambapo wote kwa pamoja walikuwa wakilia tu. Hakukuwa na mtu aliyeruhusiwa kuingia ndani kwani hali aliyokuwa nayo Godson haikuwa nzuri hata kidogo.

    Baada ya kukaa hapo kwa saa mbili, mlango ukafunguliwa na dakjtari mmoja aliyevalia koti kubwa kutoka huku uso wake ukionyesha kwamba kulikuwa na hali mbaya sana humo ndani alipotoka.

    “We want to see him, how is he?” (tunahitaji kumuona, anaendelea?) aliuliza mama yake Godson huku akifuta machozi yake kwani kama kulia, alilia sana.

    “Hali yake si nzuri, ni lazima tumuhamishe hospitali na kumpeleka Muhimbili,” alijibu daktari huyo, wakati anaongea, mlango ukafunguliwa, Godson alikuwa kimya juu ya machela, ikaanza kusukumwa kuelekea nje ambapo tayari gari la wagonjwa lilikuwa mahali hapo.

    “Godson...Godson kijana wangu...” aliita mama yake Godson huku akilia kama mtoto, wakati akisema maneno hayo, tayari aliiwahi machela na kutaka kumuamsha kijana wake aliyekuwa kimya kabisa.

    “Mama! Subiri tumuwahishe hospitali,” alisema daktari huku manesi wakimsogeza pembeni.

    Safari ya kuelekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikaanza, kila mmoja alikuwa na hofu kwamba hiyo ingekuwa nafasiu ya mwisho kwa Godson kwani kwa jinsi alivyokuwa ameumia, kwa jinsi mwili wake ulivyofungwa bandeji zilizokuwa zimelowanishwa damu, ilionyesha kabisa kwamba asingeweza kuinuka tena pale kitandani alipokuwa.

    ****

    Moyo wa Nicholaus ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kama kweli msichana Melania alimkomoa kwa kuzifuta picha zile katika simu yake na kwenye barua pepe yake. Alikasirika mno, moyo ulimuuma na kila wakati alipokuwa akilifikiria jina la msichana huyo, alihisi kuwa na moyo wa kutaka kulipiza kisa kwa kile alichokuwa amekimfanyia.

    Siku za kwanza hakulala, aliumia, alitamani kuondoka Australia na kwenda Tanzania kwa ajili ya kumkomesha msichana huyo. Moyo wake ulibadilika, mapenzi aliyokuwa nayo kwa msichana huyo yakapotea na chuki kubwa kuutawala moyo wake.

    Hakuonekana kuwa na raha, alikaa huku akionekana kuwa na mawazo tele, kwake, kwa kile kilichokuwa kimetokea kilionekana kuwa kama dharau hivyo ilikuwa ni lazima kuhakikisha kwamba anamkomoa msichana huyoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliendelea kusoma nchini Australia na mwaka mmoja ulipomalizika, akarudi nchini Tanzania. Hakutaka kumtaarifu mtu yeyote, hakutaka kuwaambia wazazi wake kwani alirudi kwa ajili ya kufanya kazi ya kulipa kisasi tu kwa msichana Melania.

    Akaanza kumfuatilia, akagundua kwamba msichana huyo alikuwa kwenye uhusiano na mwanaume mwingine, moyo wake ulimuuma, hakutaka kuona Melania akiwa kwenye uhusiano wowote ule, hivyo akapanga kummaliza mwanaume huyo.

    Kitu cha kwanza kilikuwa ni kumfuatilia, alitaka kujua anapoishi, hilo halikuwa tatizo, akagundua kwamba jamaa huyo alikuwa akiishi Mbezi Beach hivyo kuhitaji msaada kutoka katika Kundi la Black Ninja lililokuwa na makazi Kinondoni kwa ajili ya kukamilisha kazi hiyo.

    “Kitu cha kwanza tunahitaji kumjua huyo mtu,” alisema kiongozi wa kundi hilo aliyejiita Don King.

    “Hakuna tatizo!”

    Akawachukua vijana wa kundi hilo na kwenda nao mpaka Mbezi Beach ambapo wakaanza kumsubiria Godson nje ya nyumba yao, alipotoka ndani ya jumba hilo, vijana wawili wakamfuata, wakalisimamisha gari lake na kuanza kuzungumza naye.

    “Hivi kwa mzee Mkude ni wapi?” aliuliza kijana mmoja, huyu alijiita Dracula.

    “Mzee Mkude? Wala simfahamu mtu huyo,” alijibu Godson huku akionekana kutokuwa na hofu kabisa na watu hao.

    “Humfahamu kweli? Mzee mmoja ana mbwa kumi, tumesikia anaishi huku,” alisema kijana mwingine aliyejiita Lizard.

    “Wala simfahamu!”

    “Basi sawa. tunashukuru!”

    Hawakuoneekana kama watu wabaya, waliongea huku wakiwa na uhakika kwamba waliyekuwa wakiongea naye alikuwa Godson, mtu aliyekuwa akihitajika sana. Kazi yao kwa wiki nzima ilikuwa ni kumfuatilia, walitaka kuhakikisha wanafanikiwa kumuua kama walivyotakiwa kufanya.

    Baada ya siku kadhaa kukatika, ndipo wakaandaa gari lao kubwa aina ya Lori, walikuwa na ratiba yake nzima, walijua kila siku alipokuwa akiamka, breki ya kwanza ilikuwa ni kwenda kazini na jioni alikuwa akielekea gym kabla ya kurudi nyumbani na baada ya hapo anakuwa na mizunguko kadhaa.

    Walichokifanya, kwa kuwa alikuwa akifanya kazi katika Kampuni ya Amazon iliyokuwa katika jengo la Plaza, Ubungo, wakajua kwamba kila siku ilikuwa ni lazima kupitia Barabara ya Shekilango kwenda gym iliyokuwa Mwenge, hakutaka kupita Barabara ya Morogoro na kuunganisha Barabara ya Sam Nujoma kwa kuwa kulikuwa na foleni.

    Walimfuatilia na siku hiyo ndipo walipojipanga. Wakaliweka lori lao maeneo ya Sinza Mori na wengine wakawa wanafuatilia kwa nyuma. Walipofika Palestina wakamwambia jamaa aliyekuwa na lori ajiandae na wale waliokuwa na Godson, mmoja akalipeleka gari lake aina ya coaster mbele ya gari la mwanaume huyo na mwingine akiwa nyuma, wakamuweka mtu kati, ili asione kile kilichokuwa kikija mbele na hata gari lililokuwa likija nyuma.

    Godson hakujua kilichokuwa kikiendelea, hata gari lilipofika Sinza Makaburini, hakuweza kuliona lori lililokuwa likija kwa kasi kule mbele yake. Wakati lori lile likiwa limechochewa, kasi kubwa, alichokifanya dereva wa coster iliyokuwa mbele ni kukata kona kushoto, njia ya kuelekea katika Baa ya Honey Pot na kumwacha Godson peke.

    Godson alishtukia kuliona lori likiwa mbele yake, alijitahidi kutaka kulikwepa lakini hakufanikiwa, liri lile lililokuwa kwenye mwendo wa kasi likalipiga gari lake, kishindo kikubwa kikasikika, watu wakashika vichwa, Godson akatolewa ndani ya gari, akapiga kichwa kwenye kioo cha mbele cha gari lake, kikavunjika, akatupwa nje na kujipigiza kwenye lami, hakujua kilichoendelea baada ya hapo, akabaki kimya kabisa, kila mtu akajua kwamba tayari jamaa alikufa hapohapo.

    ****

    “Tell me the truth, Caspian, tell me the truth,” (niambie ukweli, Caspian niambie ukweli) alisikika msichana mmoja kwenye simu.

    “What do you want me to tell you?” (unataka nikwambie nini?)

    “Who is this Christine?” (huyu Christina ndiye nani?)

    “I don’t know what you are talking about,” (sijui unazungumzia nini)

    “I saw messages, you were chatting with her,” (nimeona meseji ulikuwa unachati naye)

    “You are not serious,” (huna uhakika)

    “I saw it! Let me show you,” (niliona! Acha nikuonyeshee meseji zote)

    Ilikuwa kimbembe, kila kona watu walikuwa wakigombana, siri zilikuwa wazi, wale waliokuwa wakitumia mtandao wa Facebook, hakukuwa na amani tena. Meseji zao zote zilikuwa nje, hakukuwa na siri tena, watu walishindwa kuelewa ni kitu gani kilichokuwa kimetokea.

    Wale waliofanya siri, siku hiyo kila kitu kilikuwa wazi kabisa. Hakukuwa na amani, meseji zote za kimapenzi zilikuwa nje. Mbali na meseji hizo, mpaka picha za watu walizotumiana zilionekana kwenye wall zao.

    Hakukuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kuzifuta meseji wala picha hizo. Watu walilalamika mno, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea. Watumiaji wa mtandao huo wakachanganyikiwa, watu wakajua kwamba kulikuwa na mabosi waliokuwa wakilala na wafanyakazi wao, kulikuwa na wanaume waliokuwa wakilala na watoto wao, yaani kila siri ambayo ilikuwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook, kipindi hicho ilikuwa wazi.

    “Unalia nini?”

    “Kumbe unatembea na rafiki yangu!”

    “Hapana mpenzi! Nani kakudanganya?”

    “Na mlitumiana picha za utupu!”

    “Hapana! Nani kakwambia hayo?”

    “Ingia Facebook!”

    “Kuna nini kwani? Unanichanganya sana.”

    “Nimesema ingia. Julian, sitaki unioe, sitaki tena ndoa, kumbe unatembea na rafiki yangu, tena si huyo tu, marafiki zangu wote umewatongoza, kwa nini? Kwa nini ulilala nao? Halafu leo unasema unataa kunioa? Kwa nini umeuumiza moyo wangu?” alilalamika msichana mwingine.

    Hali iliendelea kuwa mbaya, kila kona kulikuwa na matatizo. Meseji zao za siri zilikuwa wazi, kila mmoja alikuwa na uwezo wa kuingia kwenye akaunti ya mtu yeyote na kufanya kitu chochote kile kikiwa ni kuangalia meseji zote ambazo waliwasiliana.

    Wale waliokuwa kwenye mipango ya kuoana, hakukuwa na ndoa tena, siri zilivuja kwamba wanandoa waliotarajiwa kufunga ndoa, kumbe walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengine.

    Ilikuwa ni kilio dunia nzima, hakukuwa na usalama, kila siri ikawekwa wazi na hakuna aliyejua ni jambo gani lilikuwa limetokea.

    Wakati hayo yakiendelea, ndani ya jengo la Kampuni ya Facebook watu walikuwa wamechanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka hali hiyo kutokea.

    Kuingiliwa kwa mtandao wao na meseji kusomwa, watu wengi walijiua, ilikuwa ni aibu kubwa, wengine wakagundulika kwamba walikuwa wakifanya mapenzi ya jinsia moja, yaani kila kitu kilichokuwa siri kwenye Mtandao wa Facebook, kwa kipindi hicho kilikuwa wazi, na kila mtu akikiona zikiwemo meseji na picha mbalimbali za utupu walizokuwa wametumiana.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakukuwa na aliyejua kitu kilichokuwa kimetokea, hali ilikuwa mbaya, kila mtu aliyekuwa na akaunti katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook alikuwa akilalamika huku kukiwa na taarifa za ndoa nyingi kuvunjika.

    Mark Zuckerberg alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea, marafiki zake walimsumbua kwenye simu kwa kumlalamikia kuhusu kile kilichotokea katika mtandao wake.

    Harakaharaka kikao cha dharura kikaitishwa, vijana waliopewa jina la Pastors, yaani wachungaji wakaitwa kwa ajili ya kujadili ni kitu gani kilikuwa kimetokea. Vijana hao hawakuwa wachungaji hasa, ila walikuwa ni watu waliokuwa na mawazo ya nini cha kufanya katika mtandao huo, mawazo yao yanapokuwa mazuri, hupelekwa kwa The Man ambaye yeye ndiye hutengeneza kwa kutumia utaalamu wake.

    Si Zuckerberg tu aliyechanganyikiwa, kila mtu alionekana kutokuwa sawa. Ndani ya dakika kumi tu, tayari kulikuwa na malalamiko kila kona, tayari wapenzi waliachana, ndoa zilivunjwa na hata baadhi ya kampuni zilianza kufanya mikakati ya kulishtaki kampuni hiyo ambayo ilikuwa chini ya Zuckerberg.

    Kwenye chumba cha kikao, kila mtu alikuwa kimya, meneja, Peters alichanganyikiwa, muda mwingi alikuwa akimwangalia The Man ambaye naye pia alionekana kuwa na hofu kubwa.

    Walijua kwamba wao ndiyo waliosababisha hali hiyo, The Man ambaye ndiye alikuwa mtaalamu wa mtandao huo alitaka kuuzima Mtandao wa MeChat lakini matokeo yake akashtuka kuona link za mtandao huo zikiingiliwa na virusi ambavyo hakujua vilitoka wapi, vikaanza kutafuna codes na mwisho wa siku meseji za siri za watumiaji wa mtandao huo kuwa wazi.

    Wakati kila mmoja ndani ya chumba hicho akimwangalia mwenzake, mlango ukafunguliwa na Zuckerberg kuingia. Kama kawaida yake, alivalia pensi fupi, raba na fulana ya bluu iliyoandikwa Facebook kwa mbele.

    Alipofika, akawaangalia watu wote kumi na nane waliokuwa humo ndani, uso wake ulionyesha ni kwa jinsi gani alichanganyikiwa, alipokea simu nyingi za vitisho ambazo zilimfanya kuona muda wowote ule angefilisiwa kutokana na fidia kubwa walizokuwa wakizitaka watu wengi kulipwa kwa kile kilichotokea.

    “Nini kimetokea?” lilikuwa swali la kwanza alilowauliza watu hao.

    “Hata sisi hatujui!” alisema meneja.

    “Haiwezekani! Haiwezekani mseme hamjui. The Man, nini kimetokea?” aliuliza bosi huyo.

    The Man akabaki kimya, alitamani kumwambia kile kilichotokea lakini moyo wake ulisita kufanya hivyo. Alikiinamisha kichwa chake chini, alikuwa na mambo mengi ya kuongea lakini hakujua angechukuliwaje, hakujua bosi huyo angeweka uamuzi wake.

    “Mimi ndiye niliyehusika,” alisema The Man maneno yaliyomfanya kila mtu kushtuka.

    “Unasemaje?”

    “Mimi ndiye nimesababisha haya!”

    “Kivipi?”

    “Nilitaka niuzime mtandao wa MeChat kama nilivyofanya kwa mingine kwani nilihisi kwamba ungekuwa juu zaidi yetu, watu wangeupenda zaidi ya mtandao wetu,” alisema The Man, maneno aliyokuwa akiyazungumza mahali hapo, kila mmoja alibaki akishangaa.

    “Kwa nini uliamua kufanya hivi? Mimi siogopi ushindani The Man, napenda kuona nikiingia kwenye ushindani kwa sababu ndiyo njia nyepesi ya kudhihirisha wewe ndiye bora, sasa hautaki ushindani, unataka kuwa juu kila siku, ni lini utakua bila ushindani?” aliuliza Zuckerberg huku akimwangalia The Man.

    “Naomba unisamehe bosi!”

    “Nakupa kazi moja. Ndani ya saa mbili, ninataka kila kitu kirudi kama zamani. Wachungaji, fanyeni kazi ya kubuni kipi kifanyike kuwaomba msamaha watumiaji wa mtandao huu. Mkimaliza, mpeni The Man akifanyie kazi na kuwatumia watu. Nataka hilo lifanyike ndani ya masaa mawili tu,” alisema Zuckerberg na kukifunga kikao hicho.

    ****

    William aliusukuka mtandao wake vilivyo, alijua fika kwamba mara baada ya kuuachia hewani ilikuwa ni lazima watu wengine wajaribu kuuingia na kuufanya walivyotaka wao. Aliufanya uwe na muonekano rahisi na wakati haukuwa na urahisi wowote ule.

    Aliviweka virusi vyake kwa ajili ya kuulinda mtandao huo na ndiyo maana hata The Man alipojaribu kuuingia na kufanya mambo yake, akashtukia kuona link ya mtandao wa Facebook zikichukuliwa, virusi vikaenda katika data base ya mtandao huo na kuvuruga kila kitu.

    Alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, baada ya Facebook kuonekana kutokuwa na usalama wowote ule, watu wengi wakauhama na kuhamia katika Mtandao wa MeChat ambao ndani ya siku chache tu tayari ulikuwa na watumiaji milioni mia moja.

    Yalikuwa ni mafanikio makubwa ndani ya siku chache, William akaanza kuingiza kiasi kikubwa cha fedha, akawa mtu maarufu na aliyeheshimika kila kona. Alipendwa, kila mmoja aliona kwamba mtu huyo alitakiwa kuwa kwenye nafasi ya juu kabisa katika ulinzi wa nchi yao.

    Wakati hayo yote yakiendelea, Borya alikuwa akiwasiliana na watu wake. Kila mmoja alitaka kuona mtu huyo akitekwa na kupelekwa nchini Urusi haraka iwezekanavyo, hawakuwa na muda wa kusubiri zaidi kwani kwa jinsi alivyokuwa akiendelea kukaa chuoni ndivyo Wamarekani wangeendelea kujiwekea uhakika kwamba mtu huyo alikuwa mtu wao.

    “Umefikia wapi?” aliuliza jamaa mmoja kutoka Urusi, walikuwa wakizungumza kwenye simu.

    “Bado naendelea.”

    “Unachelewa sana Borya. Hatuna muda, ni lazima tufanye harakaharaka. Leo, saa nne usiku, kutakuwa na sherehe ya uongo ya kuzaliwa ya msichana Catherine, nenda naye mpaka kwenye Ukumbi wa Cassanova na umwambie kwamba huyo Catherine ni rafiki yako. Mkifika huko, mpe maji anywe kwa wingi ili ashikwe na haja ndogo na kwenda chooni kujisaidia. Huko atakutana na watu ambao watamteka kwa kumnusisha kitambaa chenye dawa za usingizi,” alisikika jamaa huyo kwenye simu.

    “Sawa mkuu!”

    “Hakikisha unafanya hilo kwa manufaa ya serikali yako!”

    “Hakuna shida.”

    Alichoambiwa ndicho alichokifanya. Siku hiyo usiku akamwambia William kwamba kulikuwa na msichana ambaye ni rafiki yake alikuwa na akifanya sherehe ya kuzaliwa katika Ukumbi wa Cassanova hivyo kama wangekwenda huko lingekuwa suala jema.

    Mara ya kwanza William alitaka kukataa lakini akahisi kwamba kama angefanya hivyo, rafiki yake huyo angejisikia vibaya hivyo kukubaliana naye kishingo upande.

    Akamwambia Linda kwamba angerudi muda si mrefu kwani hakutegemea kukaa sana huko. Linda akakubaliana naye na hivyo kwenda huko. Ndani ya gari, walikuwa wakizungumza kwa furaha sana, ilikuwa vigumu kuhisi kwamba nyuma ya sherehe hiyo kulikuwa na mpango kabambe wa kuhakikisha William anatekwa na kupelekwa Urusi haraka iwezekanavyo.

    “Borya! Sikutokuwa na muda sana, nitahitaji kupumzika,” alisema William.

    “Haina shida. Mimi mwenyewe nakwenda kwa sababu namuheshimu sana Catherine, vinginevyo nisingekwenda,” alisema Borya,

    Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika ukumbi huo. Nje, kulikuwa na watu wengi, walikuwa Warusi na hao wote walikuwa wamepangwa kwa ajili ya kuhudhuria sherehe hiyo huku wakitakiwa kuhakikisha kwamba William anatekwa na kuondolewa mahali hapo kwenda kufichwa.

    Aliandaliwa daktari ambaye alitakiwa kumchoma sindano William ya kumfanya ashindwe kuzungumza kitu chochote kile, mbali na hilo, pia kulikuwa na mtu maalumu ambaye alitakiwa kumvarisha sura ya bandia, yaani akichomwa sindano na kushindwa kuzungumza, kesho yake asafirishwe kwenda nchini Urusi, na uwanja wa ndege waambiwe kwamba mtu huyo alikuwa mgonjwa, na kwa sababu William asingekuwa na uwezo wa kuzungumza, basi iwe rahisi kwao kumsafirisha.

    “Wewe ni William?” aliuliza msichana mmoja wa Kirusi.

    “Ndiyo mimi!” alijibu William huku akitoa tabasamu pana.

    “Hongera sana. Umetufanya tuunganike pamoja kwenye mtandao wako,” alisema msichana yule huku akipekua kwenye mkoba wake na kutoa kamera, akamuomba wapige picha pamoja.

    “Hakuna shida.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nicola...Njoo tupige picha na William,” alisema msichana huyo huku akimuita rafiki yake ambaye akaungana naye na kupiga picha kadhaa.

    Ilikuwa ni vigumu kugundua kwamba kila kitu kilichokuwa kikiendelea hapo kilipangwa. William hakutakiwa kuhisi kitu chochote kile na hata hao wasichana, wote walipangwa kufanya kile walichokuwa wamekifanya.

    Baada ya picha kadhaa, wakaingia ndani. Huko, kila mtu alikuwa bize na mambo yake, hakukuwa hata na mtu aliyemwangalia William kana kwamba mtu huyo hakuwa ndani ya ukumbi huo.

    Kulikuwa na pombe nyingi, William hakutaka kunywa pombe, alihitaji maji hivyo kuletewa na kuanza kunywa taratibu. Japokuwa walipanga kukaa humo kwa saa moja lakini wakajikuta wakikaa kwa saa nyingi zaidi.

    “Nakuja...” alisema William.

    “Unakwenda wapi?”

    “Chooni! Nakuja sasa hivi!” alisema William na kwenda chooni kwani maji mengi aliyokuwa akinywa, yalimfanya kuhisi mkojo hivyo kwenda kujisaidia.

    “Kazi imekamilika,” alijisemea Borya huku akinyanyua mikono juu kama mtu aliyefunga goli na kushangilia, wenzake wote waliokuwa mule, wakacheka kwani kazi waliyoitiwa, ilikuwa imekamilika.

    William akaingia chooni, akaanza kujisaidia, Hakuwa peke yake, kulikuwa na watu wengine. Hakuhisi kama watu hao walikuwa wabaya, walionekana kuwa watu wazuri tu, wakati akijisaidia, mwanaume mmoja, mwenye mwili mkubwa akasogea kule alipokuwa.

    Bado hakuwa na hofu lakini ghafla akashtukia akishikwa kwa nguvu, mwanaume mwingine akatokea, akamuwekea kitambaa cheupe puani, alipoanza kuvuta pumzi wakati kitambaa hicho kikiwa puani, hapohapo mwili wake ukaanza kukosa nguvu, akalegea, akaona giza mbele yake, akalala, na kilichoendelea baada ya hapo, hakukijua.

    ****

    Gari la kifahari lilipaki nje ya ukumbi wa Cassanova, muziki ulikuwa ukisikika kwa sauti kubwa kutoka ndani ya gari lile, hakukuwa na mtu aliyezungumza lolote lile, wengi walihisi kwamba watu waliokuwa ndani ya gari hilo nao walitaka kuingia ndani ya ukumbi huo lakini haikuwa hivyo.

    Gari hilo halikuondoka, liliendelea kubaki mahali pale mpaka baada ya nusu saa, yaani dakika kadhaa baada ya William na Borya kuingia ukumbini, milango ya gari ile ikafunguliwa na wanaume wawili kuteremka.

    Walikuwa Waarabu, walivalia suti kali nyeusi, nyusoni mwao walikuwa na miwani, muda wote walikuwa wakitabasamu, wakaanza kupiga hatua kuelekea katika ukumbi ule.

    Walipofika mlangoni, wakazuiliwa na mabaunsa waliokuwa mlangoni, hawakuwataka watu hao waingie humo, wakawaambia kwamba sherehe hiyo haikuwahusu hata kidogo.

    “Ila tulialikwa!” alisema jamaa mmoja.

    “Na nani?”

    “Catherine!”

    “Anawajua?”

    “Sasa angetualika kama hatujui?” aliuliza jamaa mmoja.

    “Basi hamruhusiwi kuingia!”

    “Kwa nini sasa?”

    “Kwa sababu haiwahusu!”

    Waarabu wale hawakutaka kukubali, bado walisisitiza kwamba walitaka kuingia ndani ya ukumbi huo kwa sababu walikuwa wamealikwa. Warusi hao hawakujua watu hao walijuaje kama siku hiyo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ya msichana Catherine, hawakuwa na uhakika kwamba Waarabu hao walialikwa kweli au la.

    Wakawasiliana na watu wa ndani na kuwaambia waende pale nje ambapo wakawaambia kuhusu watu hao, na alipoitwa huyo Catherine wa bandia akasema kwamba hakuwatambua watu hao.

    “Siwafahamu!” alisema Catherine huyo.

    “Sasa mualiko tulipata wapi?”

    “Hata mimi sijui! Labda siyo Catherine mimi!” alisema msichana huyo.

    Waarabu wale hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka na kurudi ndani ya gari lao. Nyuso zao zilikuwa kwenye tabasamu pana, walipewa kazi, ilionekana kuwa ngumu lakini baada ya dakika kadhaa za kukaa nje ya ukumbi huo, kazi hiyo ikaonekana kuwa nyepesi, kilichokuwa kimebaki kilikuwa ni utekelezaji tu.



    Baada ya kupita saa kadhaa, Melania akarudiwa na fahamu pale kitandani alipokuwa. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kulitaja jina la Godson. Aliangalia huku na kule, alitaka kufahamu mahali alipokuwa, aliona akiwa juu ya kitanda huku kukiwa na dripu iliyokuwa ikining’inia.

    Kwa jinsi muonekano ulivyokuwa ndani ya chumba kile, akagundua kwamba alikuwa hospitalini. Alifikaje? Hakujua, na kama aliletwa mahali hapo, alikuwa akiumwa nini na kwa nini mpenzi wake hakuwepo? Hakupata jibu.

    Baada ya kukituliza kichwa chake kwa dakika kadhaa ndipo kumbukumbu zikaanza kumrudia. Akakumbuka namna alivyopigiwa simu na kupewa taarifa kwamba mpenzi wake alikuwa amekufa.

    Hapohapo alipokuwa, akaanza kulia huku akiliita jina la mpenzi wake, Godson. Moyo wake uliumia mno, hakuamini kama alikuwa akipita katika kipindi kigumu kama hicho. Huku akiwa analia, nesi mmoja akaufungua mlango wa chumba hicho na kumfuata Melania aliyekuwa hapo kitandani.

    “Godson yupo wapi? Mpenzi wangu yupo wapi?” aliuliza Melania huku akimwangalia nesi huyo ambaye alikuwa akimtuliza anyamaze kwani hapo alipokuwa palikuwa hospitalini.

    Alihisi maumivu makali moyoni mwake, moyo wake ulimwambia kwamba mpenzi wake alikuwa amekufa na ndiyo maana alipigiwa simu na kupewa taarifa. Alitaka kuondoka hospitalini hapo, hakutaka kuendelea kubaki na wakati hakujua hali ya mpenzi wake ilikuwaje.

    Kuondoka halikuwua jambo jepesi, akaambiwa atulie mpaka pale atakaporuhusiwa kwani hali yake haikuwa nzuri kama ilivyotakiwa kuwa. Alikaa hospitalini kwa saa kadhaa ndipo mama yake aliporudi kumjulia hali.

    Alipomuona tu, akaanza kulia, alimwambia mama yake jinsi moyo wake ulivyokuwa kwenye maumivu makali baada ya kusikia taarifa za kifo cha mpenzi wake, Godson. Hapo ndipo mama yake, Bi Pamela akaanza kumbembeleza na kumtaka anyamaze kwani Godson hakufa kama alivyosikia bali alikuwa hospitali akipatiwa matibabu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mama! Niambie ukweli!”

    “Godson hajafa mpenzi! Ni mzima ila madaktari wanaendelea kumpatia matibabu!” alisema Bi Pamela.

    Hakukuwa na kitu alichokihitaji Melania kama kumuona mpenzi wake. Hakukaa sana hospitalini, alipotolewa, kitu cha kwanza kilikuwa ni kwenda hospitalini huko kwa ajili ya kumuona Godson.

    Walipofika, wakaambiwa wasubiri, wakaungana na wazazi wa mwanaume huyo na kuambiwa wasubiri. Muda wote Melania hakuonekana kuwa na furaha, alionekana kuumia mno moyoni mwake.

    Walisubiri kwa siku nzima, wakaambiwa kwamba siku hiyo wasingeweza kumuona hivyo walitakiwa kurudi siku nyingine. Wakaondoka huku wakiwa wamenyong’onyea, nyumbani, Melania alikuwa na hali mbaya, hakula, hakulala, hakufanya kitu chochote kile zaidi ya kukaa na kumfikiria mpenzi wake.

    Ilipofika saa sita usiku, akashindwa kuendelea kukaa nyumbani, akaelekea hospitalini, alitaka kufuatilia kila hatua ambayo mpenzi wake alikuwa akipitia. Hakuruhusiwa kumuona, akarudi kwenye benchi na kutulia hapo.

    Usiku ulikuwa ni wa mateso sana, alilia mno, alipigwa na baridi lakini hakuwa tayari kuondoka mahali hapo. Moyoni mwake hakuhisi kabisa kwamba ajali ile ilikuwa imepangwa, hakuhisi kabisa kama Nicholaus alihusika katika ajali hiyo, kwake aliichukulia kama ajali ya kawaida ambayo ingeweza kumtokea mtu yeyote yule.

    Asubuhi ilipofika, wazazi wa Godson wakafika hospitalini hapo. Walishangaa kumuona Melania akiwa hapo, wakamfuata na kumkumbatia huku wote wakilia. Madaktari hawakutoa tamko juu ya hali aliyokuwa nayo Godson mule ndani, walikuwa watu wa kuwapita huku kila mmoja akionekana kuwa na jambo zito la kuwaambia lakini walishindwa kufanya hivyo.

    Baba yake Godson akaonekana kugundua kitu, jinsi madaktari walivyokuwa wakipitia kutoka ndani ya kile chumba na kuwaangalia, walionekana kuwa na kitu mioyoni mwao, kitu kibaya ambacho hawakutaka watu wengine wakifahamu.

    “Kuna nini?” aliuliza baba yake Godson huku akiwa amemsimamisha daktari mmoja.

    “Hakuna kitu!”

    “Mtoto wangu anaendeleaje?”

    “Anaendelea vizuri,” alijibu daktari huyo huku akionekana kutokuwa na uhakika na kile alichokuwa akikizungumza.

    “Una uhakika?”Daktari hakujibu kitu chochote kile, akaondoka mahali hapo kwenda kuendelea na shughuli zake.

    Kitendo hicho kikawatia hofu, mioyo yao ikapata majibu kwamba Godson alikuwa amekufa chumbani mule hivyo ilikuwa ni lazima madaktari wasite kuwaambia ukweli. Wakachanganyikiwa, Melania akazidi kulia kwa sauti mpaka madaktari wengine walipofika na kuuliza nini kilikuwa kimetokea mpaka Melania alie, wakajibiwa kwamba kulikuwa na dalili zote kwamba mgonjwa wao alikuwa amefariki ndani ya chumba alichokuwa amelazwa.

    ****

    Ilikuwa ni vita ya kumgombea William, kila mmoja alijua kwamba endapo serikali ya Marekani ingekuwa na mtu kama William basi kungekuwa na mambo mengi ambayo yasingekwenda kama yalivyotakiwa kwenda kwani nchi hiyo ingekuwa juu kiteknolojia kitu ambacho kingeifanya dunia kuwa na hofu kubwa juu ya taifa hilo kubwa.

    Mbali na Urusi ambayo kila siku walikuwa wakipambana kuhakikisha kwamba William anapatikana mikononi mwao pia kulikuwa na kundi jingine ambalo usiku na mchana lilikuwa likimuhitaji William, kundi hili lilikuwa ni Al Qaeda, kundi la kigaidi lililokuwa na makazi yao nchini Afghanistan katika Milima ya Tora Bora.

    Kundi hilo lililokuwa likiongozwa na jamaa mwenye roho mbaya, Idriss Al Ghabush lilichanganyikiwa mara baada ya kusikia taarifa juu ya William ambaye alionekana kuwa mtu hatari katika masuala ya kompyuta.

    Ilikuwa ni lazima kupambana na Marekani kwa kutumia kompyuta. Watu wengi wa kundi hilo waliuawa kwa sababu ya masuala ya kompyuta. Wengi walikuwa wakikamatwa kila walipokuwa wakizungumza kwa njia ya simu ambazo zilidukuliwa na wataalamu hao wa IT.

    Marekani ilikuwa na wataalamu wengi wa kutumia kompyuta kitu kilichowapa ugumu kupambana nao. Mara baada ya kuona kwamba wanashindwa na taifa hilo kutokana na nguvu kubwa ya teknolojia, hapo ndipo walipoamua kumtafuta Muhindi aliyeitwa Cashmir Ajay ambaye alilifanya kundi hilo kuwa juu zaidi kiteknolojia kiasi kwamba Marekani ikaanza kupata kazi upya.

    Baada ya kusumbuliwa sana, ndipo ujio wa William ukagundulika. Walijua kwamba huyo alikuwa mtu hatari kutokana na yale aliyokuwa akiyafanya hivyo kuwatuma watu nchini Marekani kwa ajili ya kumfuatilia mtu huyo.

    “Ila kuna taarifa zinasema kwamba hata Warusi wanamfuatilia,” alisema jamaa mmoja.

    “Umejuaje?”

    “Kuna yule mpelelezi wetu kitengo cha KGB ndiye aliyenipa taarifa hizo.”

    “Kwa hiyo nao wapo Marekani?”

    “Ndiyo mkuu!”

    “Hakikisheni mnakwenda huko! Chochote kitakachotokea, fanyani mnalolijua ili mambo yawe sawa,” alisema Ghabush.

    Harakaharaka mawasiliano kati ya Waarabu waliokuwa Afghanistan na Marekani yakafanyika haraka sana. Vijana wengine watatu wakatumwa kuelekea huko kwa ajili ya kukamilisha kile kilichotakiwa kufanywa kipindi hicho.

    Kuingia nchini Marekani hakukuwa na tatizo lolote lile, walijifanya kuwa wanachuo waliokuwa wakienda huko kusoma huku wengine wakijifanya kuwa wafanyabiashara wakubwa.

    Hilo halikuwa tatizo, wakaruhusiwa kuingia ambapo moja kwa moja wakaonana na wenzao na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea. Walichokifanya ni kufuatilia, walipofika chuoni wakagundua kwamba kulikuwa na Mrusi mmoja aliyekuwa karibu sana na William.

    Wakaingiwa na shaka kwamba huyo Mrusi hakuwa mtu wa kawaida, alikuwa karibu na William kwa maslahi fulani, hivyo wakaanza kufuatilia kwa ukaribu. Siku ambayo Borya na William walikuwa wakienda kwenye sherehe ya kuzaliwa ya msichana Catherine, wakawatuma vijana wawili ambao walifika mpaka ukumbini na kutaka kuingia ndani lakini hawakuruhusiwa.

    Hilo halikuwa tatizo, walijua fika kwamba huo wote ulikuwa ni mchezo uliopangwa, ili kuwadanganya, wakajifanya wakiondoka lakini wakaliegesha gari lao sehemu na kuteremka kisha kuanza kufuatilia.

    Ilipofika usiku mkubwa, Warusi wanne wakatoka ndani ya ukumbu ule huku mmoja akiwa amembeba mtu begani, walikuwa na uhakika kwamba huyo alikuwa William, akapandishwa ndani ya gari na kuondoka mahali hapo.

    “Tuwafuatilie,” alisema Mwarabu mmoja, huyo aliitwa Kadesh Saleh.

    Wakaingia ndani ya gari na kuanza kuwafuatilia. Ilikuwa ni safari ndefu kidogo ambayo iliishia ndani ya jumba moja la kifahari lililokuwa likimilikiwa na Mrusi mmoja, mfanyabiashara mkubwa aliyeitwa Petrov Tasha.

    Humo ndani, mara baada ya William kuingizwa, mtu aliyeonekana kuwa daktari akahitaji William apelekwe katika chumba maalumu kwa ajili ya kuvishwa sura ya bandia.

    Hilo halikuwa tatizo, huku akiwa amepoteza fahamu, akapelekwa katika chumba hicho na kuwekwa juu ya meza kubwa. Hapo, ikachukuliwa sura ya bandia ya mtu aliyeonekana kuwa Mrusi kisha kuvarishwa, ngozi yake nyeusi ikaanza kupakwa vipodozi mbalimbali na kubadilika, akaonekana kama Mzungu.

    “Ni lazima achomwe sindano yenye Mitrophynpil,” alisema daktari huyo.

    “Haina shida! Dawa ziandaliwe!”

    “Hiyo si dawa, ni sumu ambayo itavifanya viungo vyake vyote kutokufanya kazi kwa saa sabini na mbili,” alisema daktari huyo.

    “Sawa. Ngoja itafutwe.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kulikuwa na ugumu mkubwa kuipata sumu ya Mitrophynpil lakini ndani ya saa moja, wakafanikiwa na hivyo kumpelekea daktari huyo ambaye bila hofu, akamchoma William sindano yenye sumu hiyo ambayo ingevifanya viungo vyake vyote kutulia, kutokufanya kazi kabisa zaidi ya kichwa.

    “Sasa yupo huru kusafirishwa!”

    Hicho ndicho kilichofanyika, siku iliyofuata, hata kabla suala la William halijaanza kuwa gumzo, wakafanya mipango ya kumsafirisha William kuelekea nchini Urusi, hawakupata tabu kupata tiketi, walipopewa na vibali vyote vya safari, wakaelekea uwanja wa ndege.

    Wakawatafuta watu wengine watatu, hao walitakiwa kujifanya ndugu wa William na walikuwa wakimpeleka ndugu yao nchini Urusi kwa ajili ya matibabu. Ilikuwa vigumu kwa watu kugundua kwamba mtu huyo hakuwa yule waliyekuwa wakimwangalia.

    Sura ilikuwa nyingine, aliyafumbua macho yake lakini alishindwa kuongea kitu chochote kile. Hakuonekana kuwa mtu mweusi, sura pamoja na vipodozi alivyokuwa amepakwa vilionyesha kabisa kwamba William alikuwa Mrusi.

    We have to take him to Russia, he is going to die,” (tunatakiwa tumpeleke Urusi, anakufa) alisema mwanamke mmoja ambaye naye alikuwa Mrusi.

    “Ooh! Very sorry! Can I see his ID, please” (Ooh! Poleni sana! Naweza kukiona kitambulisho chake, tafadhali?) alisema msichana aliyekuwa katika sehemu ya kukagua pasipoti na vibali vingine.

    “This one madam,” (hii hapa mama)

    Mwanamke yule akakichukua na kuanza kukiangalia, ni kweli alionekana kuwa Mrusi aliyeitwa Vladimir Kulich ambaye alionekana kuwa na siku chache za kuishi duniani kutokana na magonjwa mawili yaliyokuwa yakimsumbua, kupooza mwili na kansa ya damu. Baada ya kukiangalia kwa sekunde kadhaa, akawaruhusu wapite huku Wiliam akiwa amewekwa kwenye kiti cha matairi.

    Alikuwa akiona kila kitu kilichokuwa kikiendelea, alitamani kuzungumza na kumwambia mwanamke yule kwamba hao hawakuwa ndugu zake lakini alishindwa kabisa kufanya hivyo.

    Hakutingishika pale alipokuwa, bado sumu aliyokuwa amechomwa iliendelea kuvidhoofisha viungo vyake. Moyoni mwake aliumia mno, hakujiona kuwa tayari kuelekea nchini Urusi ila kwa sababu ya watu hao kumuhitaji, akajikuta akipelekwa huko pasipo kupenda.

    Wakati wao wakipita na kuingia ndani, ya jengo la uwanja huo. Waliofuata walikuwa Waarabu wa kundi la Al Qaeda. Hao walitumwa kwa ajili ya kumsafirisha William kuelekea nchini Afghanistan.

    Walifuatilia kwa karibu kila kitu kilichokuwa kimetokea, tangu usiku uliopita mpaka siku hiyo. Walijua kwamba kama ndege hiyo ingefika Urusi ingekuwa ngumu sana kwao kufanikiwa kumteka William hivyo waliona kulikuwa na umuhimu mkubwa wa kumalizia kila kitu ndani ya ndege.

    Hakukuwa na mtu aliyejua kama asubuhi sana ya siku hiyo baada ya kugundua ndege aliyokuwa akisafirishiwa William, Waarabu hao walionana na wahusika kinyemela na kuwalipa dola laki moja kwa ajili ya kuweka mzigo wao wa silaha na mabomu ndani ya ndege hiyo.

    Kilichobaki kilikuwa ni kuiteka ndege hiyo, kuwaua abiria wote na kumtorosha William.





    Linda alikuwa chumbani, moyo wake ulikuwa na hofu tele, hakujua ni kitu gani kiliufanya moyo wake kuwa namna hiyo, alikosa furaha, amani ikapotea kabisa. Akasimama kutoka kitandani na kuanza kutembea huku na kule, aliogopa kwani kwa kawaida anapokuwa katika hali hiyo basi ilikuwa ni lazima kuwe na jambo baya mbele yake.

    Hakujua ni jambo gani. Kitu cha kwanza kabisa kilichokuja kichwani mwake kilikuwa ni mpenzi wake, William. Akaichukua simu yake na kuanza kumpigia, simu ilikuwa ikiita, iliita na kuita lakini haikupokelewa.

    Akashikwa na hofu zaidi kuona kwamba inawezekana kulikuwa na jambo baya hivyo akamwandikia ujumbe kwamba kama angeuona basi ampigie kwa kuhisi inawezekana alikuwa sehemu yenye kelele ambapo hakuweza kuisikia simu yake ikiita.

    Hakupata usingizi, alijaribu kulala lakini usingizi haikumjia kabisa. Mawazo yelimuendesha, muda ulizidi kwenda mbele lakini mpenzi wake hakupiga simu, hivyo akampigia Borya.

    Kama ilivyokuwa kwa William, hata naye hakupokea simu ile, akashikwa na hofu kwamba inawezekana walipata ajali wakati wakirudi kwani haikuwa kawaida kwa wote wawili kutokupokea simu.

    Usiku huo ukawa wa mateso tele, mpaka asubuhi inaingia William hakuwa amerudi chumbani kitu kilichomfanya kuwasiliana na uongozi wa chuo. Hakukuwa na aliyeamini kile walichoambiwa, haikuwa rahisi kwa William kwenda sehemu na kulala hukohuko. Taarifa za kupotea kwake zikasambazwa chuoni hapo mpaka kuwafikia maofisa wa FBI ambao walipewa jukumu la kumlinda chuoni hapo.

    “What? This is impossible!” (nini? Haiwezekani!) alisikika mwanaume kwenye simu.

    “He got lost,” (amepotea)

    “How?” (kivipi?)

    Maofisa wa FBI walichanganyikiwa, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumtafuta Linda ambaye aliwaambia kwamba usiku uliopita aliondoka na rafiki yake, Borya kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa ya msichana mmoja aitwaye Catherine na baada ya kuondoka, hawakurudi tena.

    “Did you try to reach him?” (ulijaribu kumpigia?)

    “Yes! I did it several times,” (ndiyo! Nilifanya hivyo mara kadhaa!)

    Maofisa hao hawakutaka kukubali, walichokifanya ni kumpigia simu, kama ilivyokuwa kwa Linda, hata kwao simu haikuwa ikipokelewa. Hawakuwa na jinsi, walichokifanya ni kutraki simu yake ili kujua ilikuwa mahali gani. Hilo likafanyika na ndani ya nusu saa, tayari walijua kwamba simu hiyo ilikuwa katika Mtaa wa Livingstone katika ukumbi mmoja ulioitwa Cassanova.

    Maofisa hao wakaelekea huko, walipofika, wakaingia ndani, hakukuwa na mtu, waliangalia huku na kule lakini hawakubahatika kumuona mtu yeyote japokuwa bado GPS yao ilionyesha kwamba simu ya William ilikuwa humo ndani.

    Wakapiga tena, wakasikia simu ikianza kuita chooni, wakaondoka na kuelekea huko, walipofika, waliikuta simu ikiwa chini lakini William hakuwepo mahali hapo, haikuwa simu yake tu bali hata simu ya Borya ilikuwa pembeni yake hivyo wakazichukua na kuondoka nazo.

    Walichanganyikiwa, walijilaumu kwa kutokuwa makini kuhakikisha kwamba William anakuwa kwenye mikono iliyo salama. Waliondoka mpaka katika kituo chao kidogo ambapo kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuchukua simu ya Borya na kuangalia namba alizokuwa amepiga na kupiga.

    Katika uwanja wa namba zilizoingia na kutoka, hakukuwa na namba yoyote ile lakini hilo halikuwatisha kwani waliamini kwamba walikuwa na uwezo wa kugundua namba zozote zile hivyo wakaituma namba yake makao makuu na kuomba kutajiwa namba zilizoingia na kutoka na kama iliwezekana basi wachukue mawasiliano yao yaliyofanyika kwa njia ya sauti.

    “Tupe dakika ishirini!”

    Baada ya dakika ishirini, wakapigiwa simu na kupewa namba zote zilizokuwa zimeingia na kutoka. Hapo ndipo walipopata jibu kwamba mtu aliyekuwa na William alikuwa Mrusi na hata namba ambazo alikuwa akiwasiliana nazo zilitoka katika makao makuu ya Shirika la Ujasusi la KGB nchini humo.

    “Tumekwisha! Kumbe yule kijana alikuwa jasusi!” alisema ofisa mmoja wa FBI, kiongozi aliyeitwa Hugh Jackman.

    “Unasemaje?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakikisheni upekuzi unafanyika kila kona. Bado tunahitaji kumfahamu mtu aliyekuwa akiitumia simu hii kwa undani, kama atakuwa nchini ame ameondoka,” alisema Jackman.

    Hilo ndilo lililofanyika, ilikuwa ni lazima FBI wahakikishe kwamba mwanaume huyo anapatikana haraka iwezekanavyo. Wakarudi chuoni ambapo huko wakachukua picha ya Borya, wakaangalia picha yake na kuanza kuitafuta katika kompyuta zao.

    Nyaraka zake zote zilionekana wazi, ilionyesha ni siku gani aliingia nchini Marekani, alipopitia mpaka kufika katika chuo hicho. Walijilaumu sana, walihisi kwamba Borya alikuwa mtu hatari lakini cha kushangaza hawakuchukua hatua yoyote ile.

    “Hebu alama za vidole zake,” alisema Jackman.

    “Ngoja tuziskani tuone!”

    Wakaichukua simu ile na kuanza kuskani, walitaka kuona alama zake za vidole ili wazitume uwanja wa ndege ambapo hapo wangeangalia kama kwa simu hiyo mtu aliyekuwa na alama hizo za vidole kama aliondoka.

    Hilo halikuwa zoezi la muda mrefu, ndani ya dakika tano, wakapewa alama za vidole ambazo zilitumwa hadi uwanja wa ndege sehemu ya kuingilia abiria ambapo baada ya kuangalia, zilionyesha kwamba mtu huyo alipita muda muda mchache uliopita na kuingia kwenye ndege uya Fly Emirates.

    “Tunakuja!”

    Kila kitu kilichofanyika kwa wakati huo kilifanyika haraka sana. Maofisa hao wakaelekea mpaka uwanja wa ndege, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuangalia picha za kamera kwa siku hiyo. Walipelekwa katika chumba maalumu kilichokuwa na kompyuta nyingi na televisheni na kisha kuonyeshewa picha zote zilizopigwa siku hiyo.

    “Hapohapo! SI alipitia geti hili?”

    “Ndiyo!”

    “Huyu hapa! Yupo na wenzake! Madaktari! Inakuwaje? Nani anaumwa?” aliuliza Jackman.

    “Kwa maelezo yaliyotolewa mwanaume mgonjwa anaitwa Vladimir Kulich. Amepooza mwili mzima,” alisema dada yule ambaye ndiye aliyekagua vitambulisho vyao.

    “Sasa ilikuwaje apite na wenzake? William alikuwa wapi?”

    “Hatujui! Hakukuwa na mtu mweusi waliyepita naye zaidi ya huyu mgonjwa,” alisema dada huyo.

    Jackman akachoka, akashusha pumzi ndefu na kutulia kitini. Kila mmoja alikuwa kimya, alimwangalia mwanaume huyo aliyeonekana kuwa na hasira kupita kawaida. Akaanza kuzungukazunguka ndani ya chumba kile huku akionekana kuwa na mawazo tele.

    Kila mmoja alikuwa akimsikilizia yeye, walitaka kufahamu ni kitu gani kilitakiwa kufanyika kipindi hicho. Baada ya kukaa katika hali hiyo kwa dakika tano, hapohapo akawarudia.

    “Umesema wale waliokuja ni madaktari?” aliuliza.

    “Ndiyo!”

    “Na mgonjwa alitoka wapi?”

    “St. Pius Medical Centre.”

    “Hebu wapigieni simu kuwaulizia kuhusu huyu mgonjwa,” alisema Jackman.

    Hapohapo alichokisema ndicho kilichofanyika. Namba zikatafutwa na kupigwa kwa ajili ya kumuulizia mgonjwa aliyeitwa Vladimir Kulich. Simu ilipopokelewa na kuuliza swali hilo, mtu aliyekuwa huko hospitalini akaangalia majina ya wagonjwa wote waliokuwepo na hata walioruhusiwa, hakukuwa na mgonjwa mweye jina hilo.

    “Hakuna mgonjwa mwenye jina hilo,” alisikika dada wa hospitalini.

    “Huyu mgonjwa ni William!” alisema maneno yaliyomfanya kila mtu kushtuka.

    “Unasemaje?”

    “Huyu mgonjwa ndiye William!” alirudia maneno yake.

    Kila mmoja alimshangaa, hawakuamini kama angesema maneno kama hayo. Walimwangalia mgonjwa yule kwenye televisheni ile, alikuwa Mzungu wa Urusi, muonekano wake haukuonekana kama alikuwa William hata mara moja.

    “Inawezekana vipi?”

    “Kwani huyu mgonjwa alizungumza lolote?”

    “Hapana!”

    “Ndiyo maana nimewaambi kwamba mgonjwa huyu ni Willia,’ alisema Jackman huku akimwangalia mmoja baada ya mwingine aliyekua ndani ya ndege hiyo.

    Kitu alichokitaka ni kujua mahali ndege hiyo ilipofikia, waliamini kwamba safari ya watu hao ilikua ni kwenda nchini Urusi hivyo ilikuwa ni lazima kuhakikisha kwamba hata kabla ya ndege hiyo kuwasili nchini humo basi waweze kuishusha ndege hiyo na kumchukua mtu wao.

    Wakawasiliana na watu wa mamlaka ya anga uwanjani hapo na kupewa taarifa kwamba bado ndege ilikuwa safarini kuelekea Ottawa nchini Canada hata kabla ya kuelekea nchini Urusi.

    “Ilikwishaingia nchini Canada?”

    “Bado! Ndiyo inakaribia!”

    “Ni lazima ishushwe haraka iwezekanavyo,” alisema Jackman.

    Wakati wakiwa wanawasiliana na watu hao, baadaye wakaambiwa kwamba mawasiliano yalikatika na hawakuwa wakiifikia ndege hiyo. Hawakujua watu hao walikuwa wapi, hawakujua kama ndege hiyo ilikuwa safarini au ilipokea hitilafu.

    Wakaendelea kuwasiliana nao, wakaifuatilia kwenye rada na kitu kilichowashangaza wote, ndege hiyo haikuweza kuonekana kwenye rada.

    Hapo ndiupo maofisa wa FBI wakachanganyikiwa zaidi, kikao cha dharura kikaitishwa katika chumba kidogo makao makuu kwa ajili ya kujadili kitu kilichokuwa kikiendelea. Kila mmoja ndani ya chumba hicho alionekana kuwa na hofu tele, walikuwa radhi kupoteza kitu chochote kile lakini si kumpoteza William ambaye alionekana kuwa mkombozi wao mkubwa katika masuala ya teknolojia. Wakati wakiwa kwenye kikao hicho, mara mlango ukafunguliwa na msichana fulani mrembo kuingia huku akiwa na karatasi mkononi mwake, kila mmoja akamshangaa.

    “What is going on?” (nini kinaendelea?) aliuliza jamaa mmoja.

    “A plane carrying William has crashed in the Columbia Mountains,” (ndege iliyomchukua William imepata ajali katika milima ya Columbia).

    Kila mtu aliyesikia maneno hayo akashtuka, hakuamini kama kweli kile kilichozungumzwa kilikuwa kweli au la. Alichokifanya msichana yule ni kuchukua rimoti iliyokuwa ndani ya chumba kile na kuwasha televisheni, kila kituo cha habari kilikuwa kikionyesha tukio hilo.

    Wote kwa pamoja wakajikuta wakishika vichwa kwa huzuni tele, ndege ileile waliyoambiwa kwamba ndiyo iliyombeba William huku akionekana mgonjwa ndiyo iliyopata ajali kwa kuanguka katika milima ya Columbia ambayo asilimia kubwa ilikuwa ni ya mawe iliyokuwa na barafu kubwa.

    “At least one fifty people died,” (watu mia moja na hamsini walikuwa wamepoteza maisha,” yalisomeka maneno makubwa yaliyokuwa yakipita yaliyowafanya watu wote kulengwa na machozi kwani idadi hiyo ya watu ndiyo iliyokuwa ndani ya ndege hiyo kubwa ya Fly Emirates.



    Waarabu watatu wakasimama kutoka katika viti walivyokuwa wamekaa na kuelekea chooni, huko, tayari mizigo yao iliyokuwa na mabomu, bunduki ilikuwa huko. Hakukuwa na mtu aliyeonekana kuwa na hofu nao, walivalia suti na huku mikononi mwao wakiwa wameshika Biblia kitu kilichoonyesha kwamba watu hao walikuwa wachungaji wa Kiarabu ambao walifika nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza Neno la Mungu.

    Hawakuingia chooni wote, waliingia kwa zamu, huko, walipotoka, mmoja akaenda mbele, mwingine akasimama katikati na mwingine nyuma tena wote wakiwa na mabegi ya parachuti migongoni mwao, walihakikisha abiria wote wanakuwa katikati yao.

    Warusi wale walikuwa kwenye viti pamoja na abiria wengine, hawakuhisi kama Waarabu hao walikuwa magaidi, walichukulia kama abiria wengine ambao walikuwa na uhuru wa kutembea huku na huko hapo kwenye ndege.

    “Hey! Listen up,” (Hey! Sikilizeni!) alisema Muarabu mmoja kwa sauti kubwa, watu wote wakanyamaza na kumwangalia.

    Mwarabu huyo hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kutoa bunduki yake, kila mmoja akashtuka, hawakuamini kama kweli ndege hiyo ilikuwa imetekwa na magaidi hao. Wale Warusi waliokuwa na William, walishangaa, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, walikuwa safarini na tayari waliwaambia wenzao kwamba kila kitu kilikamilika, William walikuwa naye na ndani ya saa chache ndege hiyo ingetua Urusi huku wakiwa na mtu huyo.

    Hata kabla hawajafika huko, ndege hiyo ilitekwa na Waarabu ambao kwa kuwaangalia tu walionekana kuwa na roho mbaya, ilikuwa ni afadhali kukutana na mbwa mwitu msituni, tena ukiwa peke yako kuliko kukutana na watu hao.

    “Tumeiteka ndege hii, tunataka wewe ufanye kile tunachotaka ufanye, ukienda kinyume, hatuna budi kukuua,” alisema Mwarabu huyo huku wenzake wawili wakiwa wanazunguka huku na kule.

    “Kitu cha kwanza kabisa ninataka wote mliokuwa humu ndani mlalie viti vyenu huku mkiweka mikono juu,” alisema Mwarabu huyo aliyeitwa Abdul, ndani ya sekunde kumi, kila abiria akafanya hivyo wakiwemo wale Warusi ambao hawakuwa na silaha yoyote ile.

    Abdul akapiga hatua kuwafuata Warusi wale, alipowafikia, akawaambia kwamba huo ulikuwa muda wa wao kuondoka na mtu waliyekuwa wakimuhitaji. Walishangaa, walijua kwamba hakukuwa na mtu aliyejua kama walimbadilisha William kuwa kwenye muonekano mwingine kabisa, sasa Waarabu hao walijuaje?

    Wakati hayo yote yakiendelea, Wiliam alikuwa katika chumba kingine, sehemu ambayo iliwekwa kwa ajili ya wagonjwa waliokuwa vitandani au katika viti vya walemavu. Walichokifanya ni kwenda sehemu hiyo na kumwambia kwamba ilikuwa ni lazima kuondoka naye.

    William alikuwa na maswali mengi ya kuuliza kwamba watu hao walikuwa wakinanani lakini alishindwa kufanya hivyo kabisa kwa sababu hakuwa na uwezo wa kuzungumza neno lolote lile, viungo vyake havikuweza kusogea sehemu yoyote ile.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alichokifanya jamaa huyo ni kulifunga kwa nyuma begi katika kiti hicho cha walemavu na kisha kuanza kukisukuma kuelekea mlangoni tayari kwa kuondoka. Kila mmoja aliyekuwa ndani ya ndege ile alikuwa na hofu tele, kifo kilionekana mbele yao, hawakuona kama wangeweza kupona kwani walijua historia ya Waarabu, waliyakumbuka matukio kadhaa yaliyowahi kutokea, walikumbuka vilivyo tukio la Septemba 11 lililotokea nchini Marekani, hivyo kila mmoja akaanza kusali sala yake ya mwisho.

    “Ni lazima mfe. Hatutaki watu wajue nini kilitokea ndani ya ndege hii,” alisema Abdul na kuwaambiia wenzake kwamba hiyo ilikuwa nafasi ya kuwaua watu hao ili waondoke.

    Hawakutaka kupoteza muda, kila mmoja akashika bunduki yake aina ya AK-47 na kuanza kuwamiminia risasi abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo. Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kabla, marubani hawakujua chochote kile ila baada ya kusikia milio ya risasi, wakatoka kuona nini kikiendelea, nao wakapigwa risasi na ndege kuanza kupoteza muelekeo.

    “Turuke,” alisema jamaa mmoja.

    Hilo ndilo lililofanyika, kiti cha kwanza kilikuwa ni kukisukuma kiti alichokalia William halafu na wao kuruka kwa parachuti. Walipokuwa angani, mmoja akakifuata kiti kile alichokuwepo William na kisha kulifungua parachuti lake kisha na wao kufungua yao.

    Wakati wao wakiendelea kushuka chini, ndege ile ilikwenda na kugonga katika Milima ya Columbia na kulipuka. Walishuhudia kila kitu kilichokuwa kimetokea, mioyo yao ikawa na furaha tele kwani walifanikisha kile walichokuwa wamekikusudia.

    Wakati walipokuwa wakiendelea kushuka, William alipoteza muelekeo, hakuwa kama wao ambao waliamua parachuti liende kutua wapi. Alikaa tu huku akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea, wakati yeye akitua tu, wale Waarabu walitua mbali kabisa, umbali kama wa mita mia moja na hamsini.

    “Ametua kule, tumfuateni,” alisema Abdul mara baada ya kutua chini.

    Hicho kilikuwa kipindi cha baridi kali nchini Canada. Ardhi nzima ilikuwa imefunikwa na barafu kubwa huku kwa mbali theluji ikiendelea kudondoka kwa wingi. Wakavua mabegi yao, hawakutaka hata kukunja maparachuti yao, wakaanza kukimbia kuelekea kule alipotua William.

    Chini kulikuwa na barafu lililochanganyika na theluji nyingi kiasi cha kufikia magotini mwao, walitembea kwa shida sana kuelekea kule alipokuwa William. Walipofika kama hatua mia moja kabla ya kumfikia, wakaona bonde moja kubwa likiwa mbele yao, ili kwenda kwenye upande aliokuwa William ilikuwa ni lazima kulivuka bonde hilo ambalo nalo lilijaa barafu na theluji nyingi.

    “Tufanye nini?” aliuliza Mwarabu mmoja.

    “Ni lazima tuvuke bonde hili kwa gharama yoyote ile,” alisema Abdul na hivyo kuanza kuvuka bonde hilo.

    Ilikuwa kazi kubwa, lilikuwa bonde hatari la Vernian lililoaminika kuwa na wanyama hatari aina ya mbwa mwitu wa kwenye baridi. Hawakuogopa kwa sababu walikuwa na bunduki mikononi mwao, hivyo wakaanza kulivuka.

    Haikuwa kazi nyepesi kulimaliza bonde hilo, walichukua dakika ishirini kushuka bonde na kupandisha. Kitu cha ajabu kabisa mara baada ya kulivuka bonde hilo na kufika kule alipokuwa William, hawakuweza kumuona.

    Kila mmoja alishangaa, waliangalia nyuma, usawa waliokuwepo, pale waliposimama ndipo ambapo William alipokuwa, hawakujua alikwenda wapi kwani kwa jinsi alivyokuwa, hakuwa na nguvu ya kufanya kitu chochote kile.

    “Yupo wapi? Si alikuwa hapa?” aliuliza jamaa mmoja.

    “Hata mimi nashangaa. Jamani! Kiti hiki hapa,” alisema jamaa mmoja, ni kweli, pembeni yao, mbali kidogo kulikuwa na kiti kile cha walemavu, hakikuwa kikionekana vizuri kwa sababu kilifunikwa na theluji zilizokuwa zikidondoka.

    Wakakifuata, juu ya kiti hicho hakukuwa na mtu yeyote yule, walishangaa. Wakaangalia huku na kule, William hakuwepo kitu kilichowachanganya sana. Hawakutaka kukubali, hawakutaka kuendelea kubaki hapo, walichokifanya ni kuanza safari ya kuelekea sehemu yenye miti mingi ambapo waliamini kwamba William alikimbilia huko.

    Hawakuwenda mwendo mrefu, baada ya dakika kumi na tano, wakafika katika sehemu iliyokuwa na nyumba kubwa ambayo asilimia tisini ilitengenezwa kwa mbao, wakahisi kwamba Wiliam alikuwa ndani ya nyumba hiyo, wakaanza kuisogelea huku wakiwa na bunduki zao. Kipindi hicho walikuwa tayari kupambana na kitu chochote kile ambacho kingewafanya kumkosa William.

    ****

    “Who are you?” (wewe ni nani?)

    Lilikuwa swali lililotoka kwa mwanaume aliyekuwa na ndevu nyingi aliyekuwa amevalia koti kubwa lenye manyoya mengi kwa ajili ya kujikinga na baridi, mkononi alishika bunduki yake kubwa aina ya gobole na alikuwa akiongea huku akimwangalia William.

    Huyo alikuwa muindaji aliyekuwa na kazi ya kuwawinda wanyama wengi katika msitu huo ambao ulikuwa ukitawaliwa na barafu jingi kila kipindi cha baridi kama hicho kilipofika.

    Alimwangalia William, alionekana kama mtu aliyehitaji msaada mkubwa. Japokuwa kulikuwa na baridi kali lakini William alivalia nguo nyepesi ambayo ilionyesha kumpa shida hapo alipokuwa.

    Hakujibiwa swali lake, akahisi kwamba kulikuwa na tatizo. Pamoja na hayo yote lakini kichwa chake kilikuwa na maswali mengi kwamba iliwezekana vipi mtu huyo kuwa mahali hapo tena huku akiwa kwenye kiti cha walemavu kitendo kilichoonyesha kwamba hakuwa sawa?

    Hakutaka kuuliza maswali zaidi, alichokifanya ni kumnyanyua William na kuondoka naye mahali hapo. Alipata tabu, kupiga hatua kwenye theluji nyingi kama ile ilikuwa mtihani mkubwa lakini hakutaka kumuacha William, ilikuwa ni lazima aondoke naye, ilikuwa ni lazima amsaidie.

    Hakuchukua dakika nyingi akafika katika nyumba aliyokuwa akiishi. Akaufungua mlango na kuingia ndani. Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kuwasha moto na kumsogeza William kwa ajili ya kupata joto, hakuishia hapo, akamlete chupa za pombe na kumuwekea mbele yake.

    “Why are you here?” (kwa nini upo hapa?) alimuuliza lakini William hakujibu chochote kile zaidi ya kumwangalia.

    “Are you Russian? Can you speak English?” (wewe ni Mrusi? Unaweza kuzungumza Kiingereza?) aliuliza lakini bado jibu la William lilikuwa ni ukimya wake.

    Muda uliendelea kusonga mbele, baada ya dakika kadhaa, akahisi kama nje kulikuwa na watu. Harakaharaka akasogea dirishani na kuchungulia nje. Macho yake yakatua kwa watu waliovalia suti, walikuwa Waarabu watatu ambao walikuwa wakisogea kule nyumba yake ilipokuwa huku mikononi wakiwa na bunduki.

    “Ooh My God,” (Ooh Mungu wangu!) alijikuta akisema kwa kuhamaki. Hata alipofikiria kuhusu gobole lake, ndiyo kwanza lilikuwa na risasi mbili tu zilizobaki.

    “I am a dead man already,” (tayari mimi ni mfu) alisema huku akionekana kukata tamaa.



    Hakukuwa na amani, kila mtu alipagawa mara baada ya kusikia kwamba ndege iliyokuwa imembeba William kuelekea Urusi ilipata ajali, ikaanguka na kulipuka. Taarifa hizo zikasambazwa kila kona, wale waliokuwa hawafahamu kama William alitekwa, wakafahamu kitu kilichowashangaza wengi kwamba ilikuwaje Marekani, pamoja na ulinzi wao wote, Warusi wafike nchini humo na kumchukua William kana kwamba alikuwa mtu wao?

    Wakati watu wakijiuliza hilo, huku nyuma FBI walikuwa wakifanya kila kitu kujua kama kweli wakati ndege ikilipuka, William alikuwa ndani ya ndege au la? Na kama ndege ililipuka, ni kweli ilipata hitilafu angani au kulikuwa na kitu kingine.

    Cha kwanza walichokifanya ni kwenda mpaka eneo ambalo ndege hiyo iliangukia, hapo, walihitaji kupata Black Box, kifaa maalumu kilichokuwa kikinasa mawasiliano ya marubani kwenye ndege ili wajue ndege hiyo ilipata tatizo gani mpaka kulipuka.

    Kifaa hicho kikachukuliwa na kupelekwa Jijini New York yalipokuwa makao makuu ya FBI. Wakaitwa wataalamu wa ndege kutoka katika Shirika la Ndege la Emirates kwa ajili ya kukifungua na kusikiliza kile kilichotokea kwani waliamini kama kweli kulikuwa na tatizo, ilikuwa ni lazima marubani walilizungumzia hilo kama walivyokuwa wakiagizwa.

    Kifaa kikawekwa, kikaunganishwa na kuanza kusikiliza mawasiliano hayo. Hakukuwa na sauti za marubani, walichoweza kusikia ni sauti za watu ambao lafundhi yao ilikuwa ni ya Kiarabu, baada ya muda, milio ya risasi ikaanza kusikika.

    “Ndege ilitekwa,” alisema Jackman huku akiwaangalia watu waliokuwa humo.

    “Sawa. Kama ilitekwa, inamaana Waarabu walijitoa mhanga?”

    “Hilo ni gumu. Kwanza cha kwanza kujiuliza, kama waliiteka, kwa sababu gani? Na kama lengo lilikuwa ni kumchukua William, yupo wapi kwa sasa?” aliuliza Jackman.

    Maswali hayo hayakuwa na majibu, wakawasiliana na Shirika la Kijasusi la CIA na kuwaambia kuwa walitakiwa kufuatilia kila kitu kilichotokea. Hiyo haikuwa kazi kubwa kwa majasusi wa CIA, wakasafiri mpaka Canada, walipofika katika milima ya Columbia, wakateremka na maparachuti kwenda kwenye eneo ambalo ndege hiyo ilipolipuka.

    Wakaanza kuangalia eneo lenyewe, waliangalia angani, walitaka kuangalia umbali ambao ndege hiyo ilipotoka mpaka kuangukia hapo na kulipuka. Wakaanza kufuatilia, wakaanza kuingiza utaalamu wao wa kuchunguza.

    “Wanasema ndege ilianguka, kama kweli ilianguka, kwa maana hiyo itakuwa ilianza kupata hitilafu umbali wa mita mia mbili. Hakuna ndege inayoanguka umbali wa mita mia moja baada ya kupata itilafu, ni lazima itakuwa mia mbili kwenda mbele,” alisema jamaa mmoja, alikuwa akizungumza huku akiwa na darubini mkononi.

    “Na bila shaka ndege hii ilitokea huku,” alisema jamaa mwingine na hivyo kwenda kule ndege ilipokuwa imetokea.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati wakifanya hayo yote, mikononi mwao walikuwa na kifaa maalumu kwa ajili ya kuangalia umbali kwa urefu wa mita, walipofika mia mia mbili, wakajua kwamba hapo ndipo ndege ilipoanza kupata hitilafu.

    “Bila shaka ilianzia hapa, ikaenda kule na kuanguka. Na kama huku ndipo ilipoanza kuanguka, kutakuwa na kitu hukuhuku. Hebu tuangalieni, kuna jambo nahisi. Kama kweli wale Waarabu hawakuwepo kwenye ndege, inamaana waliruka, na kama waliruka, inawezekana walitumia parachuti, kwani ndege inayoanguka, inaweza kuwa angani kwa umbali wa mia mia moja, na kama waliruka, wapo wapi?” alihoji jamaa mmoja, huyu ndiye waliyemuona kuwa mtu wao mwenye uwezo mkubwa wa kufikiria, aliitwa Gibson Charles.

    Walichokifanya ni kuanza kuzunguka huku na kule wakitafuta walichokuwa wakikitafuta kwani walijua kwamba kulikuwa na kitu, Waarabu wasingeweza kuruka kwenye ndege hivihivi, kama waliruka kweli ilikuwa ni lazima walitumia parachuti.

    Walipoona wametafuta bila mafanikio hapo ndipo walipochukua kamera yao ya kisasa iliyofungwa kwenye kifaa kiitwacho drone na hivyo kukirusha angani kwa ajili ya kuchukua picha huku wao wakifuatilia kwenye iPad waliyokuwa nayo.

    Drone ilikwenda huku na kule, ilitafuta kila sehemu, walikaa huku wakiangalia, walifuatilia kwa makini kabisa. Hali haikuwa nzuri mahali hapo, bado theluji iliendelea kuanguka na hawakuacha hata mara moja.

    Kamera ile ilitafuta mpaka ilipofika sehemu ambapo waliona kitu kama kiti kwa mbali, wakaishusha drone kwenda karibu zaidi, wakakiona kitu ambacho waliamini kwamba ni kiti. Walichokifanya ni kuwasiliana na FBI kwanza.

    “Mara ya mwisho William alikuwa kwenye nini? Alikuwa na uwezo wa kutembea?” aliuliza Gibson.

    “Hapana! Alikuwa kwenye kiti cha walemavu,” alijibu Jackman.

    “Ahsante.”

    Wakahisi kwamba kile ndicho kiti alichokuwa William, wakaanza kuelekea kule kilipokuwa. Hakikuwa karibu, ulikuwa ni umbali wa mita mia tano, walipita kwenye theluji nyingi, waliteseka kupiga hatua lakini hawakutaka kurudi nyuma.

    Mbele yao waliyaona mafanikio makubwa, waliamini kwamba iwe isiwe kile ndicho kiti alichokuwa amekalia William. Walipofika umbali fulani, mbele yao kulikuwa na bonde kubwa ambalo walitakiwa kulivuka ndipo wakifikie kile kiti kilipokuwa.

    “Ni lazima tulivuke hili bonde,” alisema Gibson.

    Hawakuwa na jinsi, hicho ndicho walichokifanya, wakaanza kuvuka bonde lile lililokuwa limefunikwa kwa barafu kubwa na theluji. Walitumia dakika kadhaa, wakalimaliza na kuibukia sehemu ambayo haikuwa mbali na kamera yao ya drone ilipokuwa karibu kabisa na kiti, wakaanza kukifuata.

    “Ndicho chenyewe. Kwa hiyo?”

    “Hatujui nini kilitokea. Hebu wasiliana na NASA, ni lazima tupate picha za satalaiti ambazo zitatuonyesha kama kulikuwa na watu, walikuwa wameelekea wapi,” alisema Gibson.

    Haraka sana mawasiliano yakafanyika, ilikuwa ni lazima wajue kile kilichokuwa kimetokea mahali hapo, kama kulikuwa na watu walikwenda wapi, walitaka kujua mahali na waliamini kwa shirika kubwa kama la NASA liliweza kupiga picha ambazo zingewapa urahisi wa kujua mahali walipoelekea watu waliokuwa wakiwatafuta.

    “Mpo wapi?”

    “Canada.”

    “Eneo?”

    “10N latitude, 85W longitude.”

    “Subiri!

    Walitakiwa kusubiri kwa dakika kadhaa, baada ya dakika tano, wakatumiwa picha iliyoonyesha alama nyekundu sehemu ambazo watu walipita ndani ya saa kadhaa zilizopita. Wakafanikiwa kugundua kwamba eneo hilo lilikuwa na watu kadhaa, waliona mistari minne mekundu kuonyesha kwamba kulikuwa na watu wanne waliokuwa wameelekea upande wa Magharibi.

    “Kwa hiyo hao Waarabu walikuwa wanne?” aliuliza jamaa mmoja.

    “Inawezekana. Kama kuna mistari minne, inawezekana walikuwa wanne kwa sababu kwa William, jinsi alivyokuwa, sidhani kama alikuwa na uwezo wa kutembea,” alisema Gibson.

    Wakaelekea huko. Walitembea kwa dakika kama ishirini ndipo mbele yao wakaona nyumba moja kubwa ikiwa imeteketea kwa moto. Waliingia ndani ya nyumba hiyo, hakukuwa na kitu chochote kilichobaki, kila kitu kiliunguzwa vibaya kwa moto, na ndiyo nyumba ambayo William alipelekwa na yule mzee mwindaji.

    ****

    Waarabu walikuwa nje ya nyumba ile, waliamini kwamba mtu waliyekuwa wakimtafuta alikuwa ndani ya nyumba hiyo. Hawakutaka kukaa hapo nje, ilikuwa ni lazima waingie ndani kuhakikisha kama kweli mtu huyo alikuwa humo.

    Silaha zilikuwa mikononi mwao. Wakaingia ndani kwa kuvunja mlango uliokuwa umefungwa kwa ndani, waliangalia huku na kule, William hakuwepo. Hawakutaka kuishia sebuleni tu, wakaingia mpaka vyumbani kuona kama wangemkuta mtu huyo lakini napo hawakumuona.

    Walikasirika, hawakujua mahali alipokuwa, walichokifanya, kama kukosa wote wakaelekea katika gari lililokuwa nje ambapo kulikuwa na dumu la mafuta ya petroli, wakalichukua, wakaimwagia nyumba yote kisha kuichoma moto.

    Waliumia mioyo yao kumkosa William lakini hawakutaka kujali. Walibaki hapo huku wakiiona nyumba hiyo ikiteketea, ilipokwisha yote na kubaki majivu, wakaridhika na hivyo kuondoka mahali hapo huku wakiwa na uhakika kwamba William alikuwa ameteketezwa na moto ndani ya nyumba hiyo.



    Bado hali ya Godson ilikuwa mbaya hospitalini, tangu alipopata ajali, hakuweza kurudiwa na fahamu kitandani alipokuwa. Alitumia mipira kula huku akiwa na mashine ya oksijeni iliyokuwa ikimsaidia kupumulia.

    Pale kitandani alipokuwa, alihuzunisha mno, kila daktari aliyemwangalia, alikiri kwamba hizo ndizo zilikuwa dakika za mwisho za kijana huyo kuvuta pumzi ya dunia hii na baada ya saa chache hasingeweza kupumua tena.

    Wazazi wake na Melania waliendelea kumlilia, kila mmoja alihuzunika mno, hawakuamini kama kweli Godson alikuwa kimya kitandani na wakati jana tu alionekana kuwa na furaha tena na hata walipokuwa wakizungumza, alizungumza kama hakuna jambo baya ambalo lingetokea.

    Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, hakuwa na nafuu, hali yake iliendelea kuwa vilevile, haikubadilika na kuwa na unafuu hata mara moja. Melania alilia na kulia mpaka kufikia kipindi ambacho aliona kama amezoea, kwani kama kulia, alilia sana lakini hakukuwa na kitu kilichobadilika.

    Marafiki zake walifika hospitalini hapo, walimfariji achukulie kila kitu kuwa kawaida lakini haikuwa rahisi kwa msichana huyo. Moyo wake ulichoma, aliumia katika kiasi ambacho alihisi asingeweza kuumia kama kipindi hicho.

    “Mama! Godson atapona kweli?” aliuliza Melania, alionekana kukata tamaa kabisa, moyo wake ulimwambia kwamba ilikuwa ni lazima mpenzi wake huyo afe kitandani pale.

    “Atapona tu!” alisema Bi Sophia.

    “Kweli?”

    “Tumwamini Mungu.”

    Siku zikakatika, baada ya siku nne ndipo wakaruhusiwa kuingia ndani ya chumba alicholazwa Godson, kwa kumwangalia tu, lilikuwa jambo gumu kugundua kwamba mtu huyo alikuwa akipumua, alionekana kama mtu ambaye alifariki dunia saa chache zilizopita.

    Melania akamsogelea, alipomfikia, akamlalia kwa juu na kuanza kulia juu yake huku akimuomba ayafumbue macho yake na amtazame tena kwani alikuwa amekwishafika ndani ya chumba hicho lakini Godson hakuyafumbua macho yake.

    “Mpenzi! Godson mpenzi! Naomba ufumbue macho yako, fumbua macho yako mpenzi unitazame. Nitazame mpenzi, umefumba macho siku nyingi, naomba uyafumbue hata kwa dakika moja unitazame, nitazame mpenzi,” alisema Melania huku akilia kama mtoto, wazazi wake walikuwa wakifanya kazi ya kumbembeleza anyamaze lakini hakunyamaza.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Melani! Nyamaza binti yangu!” alisema mama yake.

    “Inaniuma mama! Inaniuma! Kwa nini Godson, kwa nini Mungu amfanye hivi Godson tena siku ya kunivusha pete ya uchumba?” aliuliza Melania huku akiendelea kulia kama mtoto.

    “Nyamaza Melania,” alisema baba yake Godson.

    Siku zikakatika mpaka siku ya ishirini ilipoingia bado Godson alikuwa kimya kitandani. Ndugu, jamaa na marafiki waliona kwamba huo ndiyoo ulikuwa mwisho wake. Waliwaonea huruma wazazi wao kwani mbali na kaka yake aliyekuwa nchini Ukraine, yeye ndiye alikuwa mtoto pekee aliyeishi nchini Tanzania.

    “Naamini kuna siku atapona tu,” alisema baba yake Godson.

    “Lakini siku zinakwenda baba,” alisema Melania.

    “Uponyaji wa Mungu hauna mipaka, hata kama muda utakwenda, lakini bado hauwezi kuzuia kazi yake kufanya miujiza,” alisema baba yake Godson huku akiwa na imani tele kwamba kuna siku kijana wake angefumbua macho kitandani pale na kupona kabisa. Kwa watu wengine, walipokuwa wakimwangalia Godson, hawakuhisi kama jambo hilo lingeweza kutokea kwani hali yake ilizidi kuwa mbaya kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele.

    ****

    Mwindaji yule alikuwa kimya ndani ya nyumba yake, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya ili kujiokoa katika mikono ya watu hao ambao hawakuonekana kuwa watu wazuri, kwa jinsi walivyokuwa, bunduki walizozishika zilionyesha kabisa kwamba watu hao walikuwa hatari sana.

    Alichokifanya ni kwenda chumbani kwake huku akiwa amemuacha William kwenye kochi sebuleni, huko alipokuwa ndipo alipokumbuka kwamba ndani ya nyumba hiyo, wakati alipokuwa akiijenga, chini aliweka handaki kwa ajili ya kujilinda na maadui.

    Hakutaka kupoteza muda, akarudi sebuleni, akamchukua William, akambeba na kuelekea naye chumbani, huko, akaufungua mpango wa kuingilia ndani ambapo ukifungwa, ilikuwa ni vigumu kujua kama kulikuwa na mlango, akaingia huko.

    Kulikuwa na kila kitu, sebule kubwa huku kwa juu kukiwa na ukuta ambao ndiyo ulikuwa sakafu kwa vyumba na sebule ile ya juu. Alipoingia, akaufunga mlango na kumpeleka William kitandani. Akiwa huko, akaanza kusikika watu wakiingia ndani kwake,watu hao wakaanza kumtafuta huku wakitembea huku na kule, kwa pale alipokuwa, alikuwa na uhakika kwamba watu hao wasingeweza kumuona kwani hata mlango wa kuingilia huko ilikuwa vigumu kugundulika.

    Alitulia huko mpaka pale alipohisi kwamba nyumba hiyo ilikuwa ikiteketea moto. Alilifikiria hilo, likampa uhakika kwamba watu hao hawakuwa watu wema na alifanya jambo la maana sana kumchukua mtu huyo ambaye hakujua alikuwa nani na ilikuwaje aonekane ameruka kwa parachuti na wakati hali yake ilikuwa mbaya.

    “Huyu ni nani?” alijiuliza bila kupata majibu.

    Hakutoka huko, hata watu wale walipoondoka, aliamini kwamba bado walikuwepo mahali hapo. Akafanya mambo yake, kulekule chini alipokuwa akapika na kumnywesha William uji wa moto. Baada ya saa kumi, akasikia wanaume wengine wakifika katika nyumba hiyo.

    Hao walikuwa ni majasusi wa CIA lakini hakutaka kutoka kwani bado mawazo yake yalimwambia kwamba watu hao walikuwa wabaya ambao walifika mahali hapo kwa ajili kuwaua, hivyo hakutaka kutoka huko.

    Walikaa huko kwa siku nzima huku William akiendelea kuwa kama alivyokuwa. Bado mwindaji yule alikuwa na mawazo tele, hakujua mtu huyo alikuwa nani na kitu gani kilitokea mpaka kuwa mahali pale siku hiyo.

    Wakati akiendelea kujiuliza hayo ndipo akaamua kuwasha televisheni na kuanza kuangalia kuona kitu gani kilikuwa kikiendelea. Habari ambayo ilikuwa kubwa katika vituo vingi vya habari ilikuwa ni kutekwa kwa William na kufa katika ajali ya ndege iliyotokea.

    Kila mmoja alihuzunika, lawama za Wamarekani zikahamia kwa Warusi ambao walionekana kutokujali, na walipoambiwa kwamba wao ndiyo walihusika, walibisha na kuhitaji kuletewa ushahidi kwani kama wataalamu wa kompyuta, walikuwa na watu zaidi ya ishirini, tena wote wakiwa na ukali zaidi ya huyo William.

    “We can’t do bullshit,” (hatuwezi kufanya huo upumbavu) alisema waziri mkuu wa nchi hiyo.

    “But the FBI report says you did it,” (lakini ripoti ya FBI inasema mlifanya)

    “No! We are dealing with our business, not theirs,” (hapana! Sisi tunadili na mambo yenu na siyo yao) alisema waziri huyo.

    Maofisa wa CIA waliendelea kupeleleza kila kona kujua mahali alipokuwa William lakini hawakupata jibu, mioyo yao iliumia sana, hawakuamini kama kweli walimkosa mtu huyo. Walikasirika, walijua kwamba Urusi ndiyo walifanya kazi hiyo ya kumteka William na kuondoka naye, walihisi kwamba ili kuwapoteza maboya wakaamua kuilipua ndege ili ionekane William amekufa na wao kumchukua kirahisi.

    Hawakutaka kukubali, hawakutaka kushindwa. Walichokifanya ni kuwasiliana na maofisa wao waliokuwa nchini Urusi na kuwaambia kwamba ni lazima wafanye kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba William anapatikana kwani kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima mtu huyo awe huko.

    Hilo halikuwa tatizo, watu hao waliokuwa humo wakajipanga na kuanza kazi mara moja ili kuweza kumpata mtu huyo. Kila mmoja nchini Marekani alikuwa na uhakika kwamba William angepatikana kwani watu waliokuwa wamewatuma walikuwa wazoefu na kazi yao na uzuri zaidi ni kwamba hawajawahi kushindwa kwenye kila kitu.

    ****

    “Ooh! Is this William? What has hapenned to him?” (Ooh! Huyu ni William? Nini kimemtokea?) aliuliza mwindaji huyo.

    Alishtuka, aliiona taarifa ya habari ikimuonyesha mtu aliyehisiwa kupotea au kufa katika ajali ya ndege iliyotokea nchini Canada. Alipomwangalia mtu huyo kwenye televisheni, aligundua kwamba alikuwa William ambaye alikuwa ndani ya chumba chake.

    Alishindwa kuamini, alimwangalia mara mbilimbili, kwake, hiyo ilionekana kuwa nafasi kubwa ya kushinda mamilioni ya dola kwani baada ya CIA kushindwa, wakaamua kuweka kiasi kikubwa cha fedha kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwa mtu huyo.

    Alijiona tajiri, alipokuwa akimwangalia William, hakumuona William akiwa amelala bali aliziona noti za dola zikiwa kwenye mfuko mkubwa wa fedha pale kochini. Alitamani kuwapigia simu CIA na kuwaambia kwamba mtu waliyekuwa wakimtafuta alikuwa ndani ya nyumba yake.

    Hakuwa na simu ya mkononi, katika maisha yake alikuwa akitumia simu ya mezani na mbaya zaidi wakati nyumba ikichomwa moto, nyaya za simu hizo nazo ziliteketea kitu kilichompa wakati mgumu.

    Hakuwa na haraka sana, alichokipanga ilikuwa ni lazima aondoke mahali hapo na kwenda mjini asubuhi inayofuata kwa ajili ya kwenda kuwapigia simu CIA na kuwaambia kilichokuwa kimetokea ili waje kumchukua mtu wao.

    Hilo likafanyika, baada ya kuwa na mawazo usiku mzima, hatimaye asubuhi ilipofika, akatoka nyumbani kwake kwa kutumia gari lake na kuelekea mjini huku akiwa na furaha tele. Kutokana na wingi wa theluji na barafu ilimchukua mwendo wa saa moja mpaka mjini ambapo akaelekea kwenye kibanda cha simu na kupiga simu.

    “Mmesema kuna dola ngapi kwa atakayefanikisha kupatikana kwa William,” aliuliza mara baada ya simu kupatikana.

    “Tunazungumza na nani?”

    “Nimeuliza kwanza. Kunijua si jambo la muhimu kuliko kujua mahali William alipo,” alisema mzee huyo kwa mbwembwe.

    “Dola milioni mbili” alisema mwanaume kwenye simu, hiyo ilikuwa ni sawa na bilioni mbili kwa pesa ya Tanzania.

    “Sawa.”

    “Unaye?”

    “Ndiyo! Yupo nyumbani kwangu amejaa tele!”

    “Kweli?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo! Njooni kabisa na pesa zangu! Nilimkuta akiwa kwenye kiti, kuna Waarabu walitaka kumuua,” alisema mzee huyo.

    “Sawa. Tunakuja.”

    “Sasa mtajua nilipo.”

    “Tunajua. Tunafika ndani ya nusu saa.”

    Mzee huyo akasubiri alipokuwa, moyo wake ulikuwa na presha kubwa, hakuamini kama ndani ya saa chache zijazo akaunti yake ingetuna na kuwa na dola milioni mbili ndani. Alisubiri, baridi lilimpiga, aliagiza kahawa na kunywa lakini bado aliendelea kuchomwa na baridi lile.

    Kila alipokuwa akizifikiria pesa alizoambiwa kwamba angezipata, alihisi mwili ukipata joto kali. Alisubiri na baada ya dakika kumi na tano, magari mawili makubwa yaliyofanana na Range yakafika mahali hapo, wakamchukua na kuelekea nyumbani kwake.

    Kilichokuwa kikimshangaza ni muonekano wa watu hao, hawakuwa Wamarekani kama alivyodhani bali kila alipowaangalia aliona kwamba watu hao walikuwa Warusi. Alijiuliza sababu ya kuwa hivyo lakini akakosa jibu. Alikumbuka dhahiri kwamba aliambiwa kuwa watu hao wangefika baada ya nusu saa lakini kitu cha ajabu kabisa, watu hao walifika ndani ya dakika kumi na tano tu.

    “Mmh!” alijikuta akiguna.

    Hakutaka kujali sana, kitu alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni pesa tu. Njiani, hakuna kitu alichokuwa akikiulizia kama fedha zake, alitaka kupewa chake kwanza hata kabla hajawaonyeshea mahali alipokuwa William kwani kila alipowaangalia watu hao, alihisi kabisa kama wangembadilikia.

    “Utapewa tu,” alisema mwanaume mmoja.

    “Basi hakuna shida. Nyumbani ni pale,” alisema mzee huyo.

    “Mbona hakuna nyumba.”

    “Ilichomwa moto. Nilimpeleka kwenye handaki langu! Twendeni,” alisema mzee huyo pasipo kujua kwamba watu waliokuwa wamemchukua hawakuwa Wamarekani bali Warusi ambao walikuwa wamezitraki simu za FBI na hivyo alipopiga simu, walizipata taarifa hizo na hivyo kwenda wao kabla ya hao CIA.



    Je, nini kitaendelea?

    Je, nini kitatokea Warusi hao wakimchukua William?

    Je, Godson atapona?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog