Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

HUJUMA - 5

 







    Simulizi : Hujuma

    Sehemu Ya Tano (5)





    “Sasa tunavamia, Fasendy utatangulia kwa sababu bunduki yako inaweza kupiga risasi mfululizo, mimi na Jamir tunakuja, tutatumia kamba hiyo hapo juu mpaka paleleee (akaonesha kwa vidole), pale tutajiachi na kufikia kwenye yale magunia kisha kila mtu atachukua nafasi yake, lakini wakati tunashuka Fasendy utakuwa ukipiga risasi kila unayemtaka ili kuwachanganya hawa Maharamia,” Kamanda Amata akatoa maelekezo na wote wakaitikia, Fasend alruka na kuidaka kamba kwa mkono wake mmoja huku ule mwingie ukifyatua risasi kuwalenga wale jamaa, Jamir na Kamanda nao wakafuatia. Watu waliokuwa katika shughulia hiyo waliacha shughuli zao na kukimbia kimbia huku na huko.

    “Tumeavamiwaaaaa, tumevamiwaaaa,” kijana mmoja alikuwa akipiga kelele bila mpangilio. Kamanda Alijirusha na kutua kwa miguu yake miwili, mtu wa kwanza kuvaana naye alikuwa na bunduki kubwa mgongoni mwake, akampiga kikumbo na yule mtu akaanguka chini chali, alipotaka kujaribu kuinuka alijikuta akipigwa ngwala moja maridadi na kurudi chini kama mzigo, akachomoa bastola kwa haraka akiwa pale chini, akachelewa kwani risasi ya Jamil ilishafumua kichwa chake, Kamanda Amata akaichuku ile bunduki na kujibana sawia nyuma ya maboksi mengi yaliyozagaa katika lile eneo, alipotazama huku na kule alimuona Jamir aliyeshika bunduki yake kwa umakini kabisa lakini hakumuona Fasendy.

    Maharamia wakatoka walikokuwako na kuanza msako wakiwa na silaha nzito nzito.



    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gari ya Shalabah iliingia kwa fujo katika eneo la bandari, na nyuma yake alikuwa akifuatwa na Land cruiser iliyobeba wapiganaji wenye silaha. Shalabah akashuka, kwa mwendo wa nusu kukimbia na nusu kutembea alikutana na Hussein mlangoni akiwapanga vijana wake kumsaka Kamanda Amata.

    “Hussein,” Shalabah akaita.

    “Chief, huyu jamaa katuweza, lakini tutamtia mikononi,” Husseina alimwambia Shalabah.

    “Ila ukumbuke wako watatu,” Shalabah akatoa onyo.

    “Hatuna muda wa kupoteza ni kumsaka, Mr. Lonely hatotuelewa kama tutashindwa kuwadhibiti watu watatu tu, wakati sisi tuna jeshi kubwa la kutosha,”Hussein alikuwa akimwambia Shalaba.

    Mlipuko mkubwa ukasikika upande wa pili, harufu ya baruti ikatapakaa. Shalabah akamwamcha Hussein, akiwa na shotgun mkononi mwake alifungua mlango na kutokea huko kwenye mapambano, alichanganyikiwa alipoona jinsi Kamnada Amata na Jamir wanavyowadhibiti viumbe hao.



    §§§§§

    “Endelea kudhibiti eneo mi nakwenda kuwatafuta wengine,” Kamanda akamwambia Jamir kisha yeye akahamia upande mwingine akiwaacha wake Maharamia wakiapambana na Jamir, Komandoo mwenye hasira kutoka Tanzania.

    Kamanda Amata alteremka ngazi kwenda  chini, akiwa kwenye ngazi, alijikuta akipamiwa nyuma yake, alisukumwa kwa mbele na kujibamiza katika ukuta, alipogeuka kumwangangalia ni nani, alipata konde moja kali lililotua shavuni, akayumba kidogo na kumwangalia vizuri mtu huyo aliyemchapa konde hilo. Konde la tatu kutoka kwa yule mtu halikumpata Kamanda, alilipangua kiufundi kwa kuudaka mkono wa huyo mtu kisha akageuka nao na kuuweka begani akauvuta kwa nguvu na kuvunja mifupa. Yule bwana akalia kwa uchungu. Kamanda Amata akageuka na kumchapa makonde ya maana mpaka yule bwana akalala chini kwa utulivu. Kamanda Amata akaendelea kushuka chini.



    §§§§§

    Ndani ya chumba kikubwa sana kisichokuwa na kitu, kulikuwa na watu kama thelathini hivi wakiwa wamewekwa pamoja, hakukuwa na kiti, wala kitanda, walikuwa wamewekwa tu kama watu waliopo mahabusu. Kati yao kulikuwa na Watanzania ishirini waliotekwa na Maharamia, walikuwa wametulia kimya kabisa, wengine wakicheza karata kupoteza mawazo na wengine wakicheza drafti. Chumba hicho kilichoko chini ya ghala la bandari kilitumika zamani kama stoo ya kuhifadhia vipuli vya meli lakini baada ya kujengwa bandari mpy pale Mogadishu na kuhamisha kila kitu, Maharamia hao walijibinafsishia eneo hilo, hakuna aliyewauliza kwa sababu ndani yao kulikuwa na sauti za wanene. Walihodhi eneo lote hilo, na ukionekana kulifuatilia siku inayofuata ungeamka bila pumzi.

    Mmoja wa wale mateka, mwanajeshi wa jeshi la maji wa Tanzania, alishtuka ghafla kutoka usingizini na kuwakuta wenzake ambao walikuwa wakicheza drafti wakiwa wanaendelea na mchezo wao, hawakuwa na usingizi wala hamu ya kulala, kila mmoja aliwaza hatima yao isiyojulikana.



    “We vipi, mbona unshtua wenzako?” mmoja akmwuliza.

    “Tulieni,” akawaambia huku akiwaoneshea kidole juu kuwapa ishara ya kutega sikio.

    “Nini? Kuna nini?” mwingine aliuliza.

    “Sikilizeni,” aliendelea kuwasisitizia. Wote walitulia lakini hakuna walichokisikia.

    “Ah, achana nae huyo ameshanchanganyikiwa,” mwingine aliyestuka usingizini akajibu kutoka kona ya chumba hicho.

    “Oya, sikilizeni AK-47 inavyolalamika huko, kimenuka!” akawaeleza mara hii akiwa amesimama wima.

    Mabishano ya milio ya bunduki ilianza kusikika kwa ukaribu, wote walinyanyuka, hakuna aliyelala tena, walijua wazi kwa jinsi sauti zile za milipuko ya risasi zilivyokaribia eneo ambalo wapo wao, kwa vyovyote ni vita ya ukombozi.





    §§§§§§

    Kamanda Amata aliruka kwenye ngazi na kutua katika mwimo wa ngazi hiyo na kuserereka nayo kuja chini huku mkononi mwake AK-47 ikilalama na kufumua mtu mmoja baada ya mwingine.

    “Yuko huku!!!” jamaa mmoja aliita kwa nguvu na wenzake waliokuwa juu wakaanza kuteremka chini kumfuata Amata, lakini walijikuta wanagonga ukuta baada kukutana uso kwa uso na Fasendy aliyekuwa amekamata bunduki kubwa aina ya SCAR H (Special operation Combart Assault Rifle), bunduki ya Kibelgiji, alianza kumwaga njugu na kuwarudisha nyuma wale vijana.

    “Rudini msijeee!!!” mwingine aliwazuia wenzake.

    “Kamanda, songa mbele,” Fasendy alipiga kelele huku akirudio juu.

    Wakati yote hayo yakiendelea, Jamir alikuwa amefunga kazi katika upande wa juu, na alijificha mahala ili aone kama kuna yeyote atakayeleta shida, mkononi mwake alitulia na SMG (SubMachine Gun. Eneo lote lilidhibitiwa na watu watatu waliojipanga vyema.

    Fasendy, alikuwa akitembea kwa kunyata kuelekea kwenye ujia mrefu upande wake wa kushoto, huku bunduki yake ikiwa makini mkononi mwake. Mara ghafla alisikia mchakacho wa miguu nyuma yake alipogeuka tu, alikutana na konde zito liliuchana mdomo wake wa chini, akatoa yowe la maumivu. Kabla hajajiweka sawa, konde lingine lilitua shavuni, akajaribu kujitetea mbele ya mtu huyo, lakini ikawa ngumu, alipigwa teke la nyuma ya magoti akajikuta akiiga magoti, na bunduki ikimtoka huku akiachia risasi mfululizo.



    “Mshenzi sana we mwanamke, umetugeuka siyo?” ilikuwa ni sauti ya Shalabah, aliyekuwa akiongea huku akimzunguka kusimama mbele yake.

    “Nani amewasaliti?” Fasendy akauliza.

    “Hujui siyo? Sasa utajua leo, na huyo mwanaume wako huko alikoenda ndiko liliko kaburi lake, hapa hatoki mtu,” Shalabah akajibu.

    “Hata wewe hutoki kama ni hivyo,” Fasendy alijibu kijeuri huku damu zikimvuja katika mdomo wake wajuu uliochanika kwa konde la Shalabah.

    “Sema mko wangapi?” Shalabah akauliza.

    “Hata ukiniua, sintosema Abadan!” Fasendy alijibu kijeuri.

    “Unajifanya jeuri sio?” Shalabah alimwambia na kumshushia kipigo cha nguvu, Fasendy hakuonesha makeke yoyote katika hilo alitulia na kujibwaga chini. Kutoka pale chini Lijizungusha kwa kasi na kumchota ngwala Shalabah, lakini Shalabah alikuwa mwepesi na kujigeuza hewani, kisha akatua kwa miguu yake.

    “Fasendy, tulipokuwa jeshini mimi nilikuwa mkufunzi wako, tangu lini mwanafunzi akamshinda mwalimu?” Shalabah alijisifu.



    §§§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jamir alisikia mabishano hayo ya Shalabah na Fasendy, taratibu akajitoa katika maficho yake akipiga hatua kusogea kule watu hao wanakoongea, kwa kuwa alikuwa akielewa kwa kiasi Fulani lugha ile, alijua Fasendy yuko matatani, hawakuwa na njia ya mawasiliano katika yao watatu, kila mmoja alipigana na kuwasiliana na mwenzake kwa hisia. Jamir alimuona Shalabah lakini kabla hajafanya lolote Shalabah alihisi uwepo wa mtu mwingine, akachomo bunduki yake na kufyatua risasi upande aliokuwa Jamir.

    “Aaaaaaaiiigggghhhh!!!!!” sauti ya mamumivu ya Jamir ilisikika huku akijirusha upande wa pili na kujificha nyuma ya ukuta mwingine.

    “Jamiiiiiiirrrrrrrrrrr!!!!!!” Fasendy alipiga ukelele baada ya jamir kuruka upande wa pili huku akitoa yowe la maumivu.

    “Umemuumiza Jamir!!!” Fasendy alimpigia kelele Shalabah, lakini alizimwa na kofi kali la shavuni.

    “Ndio, nab ado naenda kummalizia kabisa,” Shalabah akamuacha Fasendy pale chini na kukimbilia kwa Jamir, alipofika pale alipoangukia Jamir, hakumuona. Akabaki kapigwa na butwaa, si aliangukia hapa! Akashangaa, hakujua ni vipi au ni wapi jamir katorokea ilhali alikuwa kampiga risasi.



    “Shiiitttt!!!” akapiga kelele na kugeuka kurudi kwa Fasendy, nako akapigwa na butwaa la mwaka Fasendy hayupo pale alipomuacha, hawa ni masehetani au binaadamu? Akajiuliza bila jibu, akatazama huku na kule akaelekea kwenye tundu kubwa la dirisha na kumuona Fasendy akiwa chini kabisa, akainua bunduki yake na kufyatua kumlenga, akachelewa, Fasendy alikwishaingia chini ya lile jengo na kushika ngazi za kuteremkia bondeni.

    Shalabah akateremka kwa kasi kwenda chini huku bunduki yake ikiwa mkononi mwake, akainua simu yake ya upepo.

    “Hussein, wasitoke hao, wanataka kutoroka nimewadhibiti vya kutosha, hawatuwezi,” Shalabah alimwambia Huseein kibonge cha mtu alipokuwa akishuka ngazi kwenda chini, lakini alishangaa sana kuona hajibiwi akaita tena na tena.



    §§§§§

    Kamanda Amata alijikuta akipigwa na kitako cha bunduki, kilimpiga chini kidogo ya shingo akhisi maumivu kwenye uti wa mgongo, aligeuka na konde zito, lililompeleka chini huyo aliyefanya kiotendo hicho, hakumsubuiri aamke, teke kali la usoni lilimgeuza upande wa pili na kumvunja mwamba wa pua, damu na makamasi vilivuja kwa pamoja.

    “Funguo zikowapi?” akamwuliza huku akimfuata, yule jamaa akawa anasota kinyumenyume huku akionesha mkono ndani ya kiofisi Fulani kilichokuwa hapo jirani. Ilioneka ndiye alikuwa mtunza chumba hicho. Kamanda Amata akaingia ndani ya kile kiofisi kwa kurukia miguu miwili na kuutawanya mlango wote, akavuta droo na kuchukua fungu la funguo, akatoka nalo na kujaribu kila inayowezekana kufungua mlango huo, funguo ya tano ilikubali kuufungua, ukafunguka, lakini chumba kilikuwa cheupe hakina mtu, akamgeukia yule jamaa pale nyuma, akakuta hayupo akamuona akimaliziki kwenye kona Fulani ya ujia katika jengo hilo, shabaha madhubuti ndani ya sekunde mbili alimvunja mguu yule bwana akajibwaga chini kama mzigo. Akamuwahi pale pale na kumkamata ukosi wa shati lake.



    “Unanifanya mimi bwege sio?” Akamuuliza, huku akimburuza na kurudi naye mpaka pale, “Chumba kikowapi?” akamtupia swali linguine. Yule jamaa alikuwa akiugulia mguu na pua yake.

    “Sema haraka, sina muda wa kupoteza,” Kamanda alipiga kelele, akamgeuza chali na kumtumbukiza domo la bastola kinywani mwake, yule bwana akapiga kelele za woga huku macho yakiwa yamemtoka pima.

    “Nasema, nnna ssssema!” alibwabwaja, Kamanda akatoa ile bastola, “Malango wa pili kwa ndani kushoto.”

    Kamanda akamsonya na kumchapa kofi kisha akaingia ndani ya kile chumba na kukuta mlango mwingine, uliokuwa ukigongwa kutokea ndani lakini sauti hafifu sana ilikuwa ikitoka hapo kwani mlango ulikuwa ni wa chuma kizito. Akatumbukiza funguo na kufanikiwa kuufungua ule mlango.



    §§§§§

    Hussein alikuwa hajui afanye nini, alikuwa ndani ya chumba cha yale makombora na watu wachache pamoja nao, katika ile manowari kubwa ya JW waliyoiteka, ilikuwa imewekwa mahali maalum ambapo ukija kwa nje huwezi kuiona, kwani walikuwa wameizamisha chini ya bahari na kuifungi kwenye ghala yao iliyopo huko, ghala hiyo ilikuwa na uwezo wa kujazwa maji na kuwa kavu kadiri wanavyoamua wao. Alipokuja Kamanda Amata alikuta imejaa maji yote, lakini wakati wakiwa tayari kuyaondoa yale makombora kulikuwa hakuna hata tone la maji. Tayari makombora mawili yalikwisha ondolewa pale na kuingizwa kwenye ile PARPADOS, meli kubwa iliyoegeshwa nje.

    Hussein, mtu mnene asiye na shindo kwa jinsi alivyonenepa, alikuwa kachanganyikiwa kiasi Fulani. Mkono akiwa kakamata shotgun na wale vija aliokuwa nao wote walikuwa wamekamata silaha za aina mbalimbali.

    “Lazima atakuja huku mbuzi huyu, ni kuutoboa mwili wake kwa risasi mpaka huwe chandarua,” aliwaambia wale vijana na wote wakaziweka tayari bunduki zao.

    Akainua redio yake, ambayo wakati inaongea hakujibu lolote, “Shalabah niko huku chamber, namsubiri huyo mbuzi afike nimmalize,” akamwambia Shalabah.

    Kisha akawageukia wale vijana wake, “Mko tayari?”

    “Yes Boss,” walijibu lakini walionekana wazi kutetemeka, waliona kama sinema inayotukia hapo, na wao wakiwa ni wamoja wa wachezaji sinema hiyo.



    §§§§§§

    DAR ES SALAAM – TANZANIA

    MADAM S aliirudisha simu yake katika mkoba wake mara baada ya kupata taarifa ya kutoroka kwa Balozi wa Somalia. Akasimama na kuliaga jopo la wanausalama waliopo pale. Chiba alibaki kuangalia mawasiliano kama yanaenda vyema.

    Madam S akatoka nje ya jengo la makao makuu ya jeshi, ilikuwa imetimu saa nane za usiku. Akachukua simu yake akabofya namba Fulani na kuiweka sikioni.

    “Scoba, nahitaji helkopta haraka sana, inabidi tufike visiwa vya Zanzibar bila kuchelewa,” akaongea na simu hile.

    “Umesomeka Madam, Uwanja wa ndege wa jeshi tafadhali kikosi namba KJ 603, haraka,” Scoba akajibu simu ile na kisha kujiandaa kwa safari. Alikwishaambiwa kuwa kwa muda huo wote ahakikishe anakuwa ndani ya eneo hilo la uwanja wa ndege wa Jeshi kwani anaweza kupata taarifa yoyote na ndivyo ilivyokuwa.

    Madam S alikuwa katika mwendo wa kasi kuelekea Uwanja wa ndege na wakati huohuo, Gina naye alikuwa katika barabara hiyo kuelekea Uwanja wa ndege.



    Wote wakaingia pale kwa tofauti ya dakika moja na sekunde kumi na tano, walikuta Scoba tayari akilipasha moto Chopa akiwa Keisha funga mikanda ya usalama na amekwishavaa vyombo maalum vya mawasiliano.

    Madam S akakwea na kuketi katika siti ya mbele alkadhalika Gina akajitupa katika siti ya nyuma, Scoba akawapa ishara ya kufunga mikanda vizuri, akampa ishara Madam S ya kuvaa vyombo vya mawasiliano, milango ikafungwa, Chopa likanyanyuliwa kwa umahiri kabisa.

    “Zainzibar, kuna boti iko majini inasafiri kwenda huko nataka tufike kabla yake,” Madam S akamwambia Scoba.

    “Umesomeka, nilifikiri unataka tufanye fishing,” akajibu.

    “Oh, no! hatuwezi fishing Kamanda hayupo, laity angekuwepo tungemuonesha jinsi tulivyo mahiri katika mambo kama haya,” Madam akajibu. Ile Chopa ikaendelea kupasua mawingu juu ya bahari ya Indi kukitafuta kisiwa hicho maarufu kwa zao la Karafuu.

    Ukimya ulichukua nafasi ndani ya Chopa hiyo, wakimtazama kijana huyo mahiri katika kazi hiyo miaka kadhaa akilitawala dude hilo la Kirusi. Wakiwa angani waliona vitu viwili vikiwapita kwa kasi ya ajabu kimoja kushoto na kimoja kulia, ilikuwa ni kasi kuliko kasi unayoijua, wakaona kwa mbele vitu vile vikiwa ka ma kimwondo.

    “Nini kile? Isiwe tumetunguliwa Scoba,” Madam S aliuliza.

    “Usihofu mama, hakuna wa kutuletea shida kati anga letu wenyewe,” akajibu.

    “Sasa kile ni kitu gani?”

    “Usiogope ni watanashati wetu hao ni ndege aina ya kivita aina ya MiG-31E nayokwenda kasi kuliko kasi yenyewe, ina uwezo wa kwenda kilomita 3000 kwa saa moja,” Scoba alieleza.

    “Waoh!” Madam S akashangaa, “Asante sana Jenerali Kamsumi.”



    §§§§§

    ILIKUWA ni furaha mateka wale kutoka ndani ya kile chumba, hawakutegemea hata siku moja kama litatokea, mbele yao mwanaume mkakamavu alisimama akihakikisha wote wanatoka ndani salama.

    “Asante sana, sasa watatukoma washenzi hawa!” mmoja alisikika wakati akitoka katika chumba kile. Wale mateka walitoka na kutawanyika kila kona. Ilikuwa ni balaa kila anayekutwa alichezea kichapo cha maana na kunyang’anywa silaha yake, msako mkali ulianza ndani ya himaya ile, nje ndani, meli kubwa ya PARPADOS iliwekwa chini ya ulinzi pamoja na watu wake wote waliokuwamo ndani.

    Kamanda Amata aliwahesabu wote kwa jumala yao walikuwa kama thelathini na nane hivi, zaidi ya wale ishirini na tano waliotekwa na ile Manowari ya JW kulikuwa na wengine zaidi kutoka Ufaransa, Ubelgiji na nchi za mbali, wote walitekwa meli zao za mizigo na Maharamia hao waliotikisa Dunia.

    Eneo zima lilizingirwa na wapiganaji hao waliookolewa punde tu, wakiwa na hasira, waliwakung’uta vibaya Maharamia waliokutana na o hata wengine kupelekea kukimbia eneo.







    §§§§§§

    Saa ya Kamanda Amata ilimpa ishara ya kuwa kuna ujumbe unaingia, akaiinua na kuiruhusu.



    ….Dakika 85 hakikisha umewaweka watu wako mahali salama, Tai wako njiani msije mkanyakuliwa kama vifaranga vya kuku…

    Ilikuwa ni ujumbe kutoka kwa Chiba, kwa harakaharaka huku akiwa macho huku na kule aliujibu ujumbe ule.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ….hakuna sehemu ya kujificha, tutakuwa ndani ya meli kubwa, wasiiweke kwenye shabaha tafadhali…

    Siwezi kutoka hapa kabla sijatenganisha roho na mwili ya Shalabah, akawaza Kamanda huku akikimbia tarataibu.



    “Kamanda Amata!” ilikuwa sauti ya Fasendy ikiita. Kamanda akageuka nyuma kumtazama mwanamke huyo.

    “Vipi?” akamuuliza.

    “Shalabah!” akajibu. Amata akakza macho mwa Fasendy aliyekuwa akionekana kuwa na maumivu makali.

    “Namtafuta,” akamwambia, Fasendy akampa ishara ya kumfuata, moja kwa moja wakafuata huo ujia mpaka kwenye mlango mmoja uliojitenga peke yake. Fasendy akasimama akamzuia Amata, pumzi yake ilikuwa ikitoka kwa tabu, alionekana kuchoka haraka.

    “Fasendy nini?” Kamanda akauliza wakatia akijiandaa kufungua mlango.

    “Sikia, ukimuua Shalabah, na Hussein kuna boss wao, Mungu mtu asiyeonekana kwa macho ya binadamu, anaitwa Mr Lonely, ukammalizie,” Fasendy alimwambia Amata.



    “Kwa nini unasema hivyo, wewe utakuwa wapi?” akauliza kama mtoto. Fasendy akachomoka mikononi mwa Kamanda na kuteremka ngazi mpaka kwenye mlango mwingine, akampa ishara Kamanda Amata ya kuwa ni hapo, Kamanda hakusubiri, alimpa Fasend ile shotgun kisha akamhesabia moja mpaka tatu na kuubamiza mlango, kisha akaingia mzima mzima na kuruka sarakasi, akiwa hewani wale vijana wa Hussein walimlenga shabaha lakini hawakujua kama hiyo ilikuwa ni janja tu, risasi za Fasendy ziliwamaliza wote watatu na kuwaacha hoi wakiagana na roho zao. Kamanda Amata alipotua chini, konde la kwanza lililtua katika tumbo la Hussein, la pili hapohapo na la tatu.

    “Siku yenu imefika,” akamwambia. Husein hakukubali kufa kizembe, alimpiga kichwa Amata, akayumba na kabla hajajiweka sawa, alipigwa ngwara kali iliyomuondoa sakafuni na kumpeleka hewani kabla ya kutua chini kama kifurushi.

    “Kumbe ni mwepesi namna hii? Sikutegemea na ninashangaa hata umewezaje kumuua Sharon kwa uteke huu,” Hussein, mtu mnene alijigamba huku akiweka sawa suruali yake aliyoivalia tumbo.



    “Aaaaaaiiiiiiiggghhhh!” Sauti ya Fasendy ilisikika. Amata akageuka kutazama kule mlangoni, akamwona Fasendy akiwa kabanwa kabali na mkono wenye nguvu wa Shalabah.

    “Afadhali mmekuja wote kunirahishia kazi,” Amata akasema huku akinyanyuka pale chini. Hussein kwa haraka alirudi nyuma na kurukaruka kwa madaha huku akikunja ngumi zake, akarusha konde moja, Kamanda Amata akailikwepa na kumtandika konde la mbavu mpaka Hussein akaguna, kabla hajauachia mkono wa bonge hilo, alimuongeza ngumi nyingine mbili za nguvu ambazo zote zilitua mbavuni na kumlegeza Hussein, almwachia mkono na kumrukia teke moja kali la kuzunguka lililosukuma mpaka kwenye maboksi akajibwaga huko. Kabla hajanyanyuka Kamnda Amata alimuwahi pale pale na kuukamata mkono wake akauzungusha kwa nguvu ukatawanyika mifupa yake kwa ndani, Hussein alilia kama mtoto.



    “Mwache huyo mwanamke!!” Amata alimwambia Shalaba wakati akimwacha Husseina na kugeukia upande huo.

    “Unasema nini wewe mtoto Changudoa! Unafikiri ulivyowaweza hao na mimi utaniweza? Kwa taarifa yako mimi ndiye niliyemfundisha huyu mwanamke wako michezo yote hii anayoifanya, hapa, sasa kama na wewe unataka kujaribu sogea nikumalize,” Shalabaha akaijigamba mbele ya Amata.

    “Sasa kwa nini unajiwekea ngao huyo mwanamke? Kama unaona unauwezo wa kupambana na mimi muache huyo uje kwa mwanaume hapa shoga wewe,” Kamanda Amata akamtia hasira Shalabah. Shalabah akauma meno na kumtupa Fasendy kwa nguvu kiasi kwamaba hakuweza hata kujizuia. Shalabah akiwa na kisu kikali mkononi mwake alimkimbilia Amata huku akiwa kauma meno.



    “Iyaaaaaaaaaaaa!!!!!” alipiga makelele akiwa kadhamiria kumdidimiza Amata hicho kisu. Kamnada alishajipanga, aliruka hewani na kuzungusha miguu yake, mguu wa kusoto ukapiga mkono wenye kisu, kikaanguka na wa kulia ukatua kwenye shavu la Shalaba, akayupa na kujibamiza kwenye chuma kubwa lililofungwa hapo kwa ajili ya kuinulia vitu vizito.



    9

    “Gina hatutakiwi kumkamata Balozi kwa vitisho au nguvu, kwanza nataka ujue ni wapi anakwenda kama ni hapa ndani ya Zanzibar au ana safari nyingine, cha muhimu ni kuwa asiondoke katika nchi ya Tanzania,” Madam S alimwambia Gina ambaye alkuwa akisikiliza kila kitu.

    “Sawa Madam,” Gina aliichomoa bastola yake na kuipachika vizuri kiunoni, “Sasa tunashukia wapi?” akauliza.

    “Uwanja wa ndege, ningeweza kuwashusha hata Ngome Kongwe lakini usiku huu tutawashtua wananchi,” Scoba alijibu na dakika mojan baadae tayari chopa lile lilikuwa likiweka magurudumu yake juu ya ardhi ya Zanzibar. Madam S akifuatiwa na Gina wakashuka, Scoba akazima injini na kuteremka baadae.

    “Karibu Zanziba Madam ijapokuwa umekuja kwa dharula hata Gahawa hatujaandaa, ila sio mbaya karibu sana,” alikaribishwa na kijana mmoja mtu wa makamo anayejulikana kwa jina moja tu Kwame. Kwame alikuwa ametumwa kikazi Zanzibar miaka miwili iliyopita kutoke idara ya Usalama wa Taifa.



    “Tumekuja kuchukua mzigo kama inabidi,” Madam S akamwambia.

    “Usijali, maagizo yako niliyapata na yanafanyiwa kazi, mzigo lakima muupate,” akajibua Kwame.

    “Ok, usafiri?” Madam akauliza.

    “Kila kitu kipoa Madam,” akajibiwa kisha wote wakaingia ndani ya Range Rover moja ya buluu, Scoba akaketi nyuma ya usukani kwa kuwa yeye wa idara hiyo.

    Walitoka Uwanja wa Ndege na kuchukua barabar ya Nyerere, wakashuka nayo moja kwa moja mpaka hospitali ya Mnazi Mmoj, pale wakaiacha ile barabara ya Kaunda na kuchukua ya kulia. Barabara ya Mtoro mpaka Mkunazini, wakapenye vichochoro.

    “Kijana kuna vichochoro havipitwi na magari utagonga!” Kwame alimwambia Scoba.



    “Usaijali usiku saa hii hakuna wa kugongwa zaidi ya mchawi,” Scoba wakati anamalizia usemi wake alikuwa ameshatoke barabar ya Jamatini, akashuka nayo mpaka ile ya Mizingani, hapo kwa mwendo wa polepole akasimamisha gari yake. Gina akateremka na kutembea kwa miguu kuelekea katika bandari hiyo ndogo. Hakuingia bandarini kwani usiku huo kulikuwa kumefungwa, chini ya mwembe mkubwa kulikuwa na wazee wameketi walionekana kuwa ni walinzi wa eneo, hilo, waliketi wakinywa kahawa, akawaendea ili kupoteza dakika kadhaa hapo akiisubiri ile boti kuwasili.

    Madam S aliitazama saa yake ilikuwa tayari ni saa tisa za usiku, akarudisha mkono chini na kufyatua kitia akajilaza.

    “Bibi stahafu sasa! Tuachie vijana,” Kwame alimtania Madam S.

    “Ah, Rais wenu hataki nistahafu, anataka nizeekee mpaka siku mnikute nimefia mezani ofisini,” akajibu.



    §§§§§

    Jamir alijiinua kwa taabu sana kutoka pale alipoangukia baada ya kupatwa na risasi za Shalabah, damu nyingi zilikuwa zikimvuja, katika sehemu ya mbavu hakuwa na nguvu tena zaidi ya kusota na kujibana nyuma ya ndoo kubwa la takataka, alipoona ukimywa umetawala, akainguka na kutembea kwa tabu huku akiifanya bunduki ya AK 47 aliyoiokota kuwa kama mkongojo wa kutembelea. Alifika sehemu yenye dirisha na kuchungulia nje, alisikia milio kadhaa ya bunduki huku watu wakikimbili kwenye ile meli kubwa iliyoegeshwa gatini. Alijikongoja na kuweza kutoka nje, wakati huo wale wanajeshi waliokuwa wametekwa walikuwa tayari melini, alijikokota mpaka lango la kutokea kule gatini, akapiga mbinja kali, wale askari kule juu ya meli walimuona, lakini hakuwajua kama ni mwenzao au la.

    “Hima himaaaaaa!!!!!” mmoja akaropoka kwa nguvu na Jamir akaitikia, “Tanzaniaaaaaaaaa!!!!!”. Wawili kati yao wakateremka haraka na kwenda kumsaidia. Kwa mbali waliona gari zilizzokuwa zikija zikiwa zimewasha taa, wakajua sasa mambo yameharibika.

    “Kamanda aliyetuokoa hayupo, tutaondokaje bila kumuona?” ubishano ulianza kati yao.



    “Mwambie Nahodha asogeze mbali kidogo japo mita mia tano baharini ila tusiondoke,” mwingine alidakia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Watu wote waliokuwa wakifanya kwenye ile meli walikamatwa na kufungwa kamba na kuwekwa katika chumba kilicho chini karibu na injini.

    Nahodha George, aliyekuwa ndani ya nguo zake nyeupe lakini sasa zilizochafuka na kunuka kwa jasho alikuwa akiuzingisha usukani wa ,eli ile, PARPADOS kuisogeza baharini wakiati wakipanga jinsi ya kumpat Kamanda Amata.

    Jamir alilazwa katika kitanda na mwanajeshi mmoja mwenye taaluma ya udaktari akasogea na msaidizi wake nakuanza kumsaidia.

    “Vipi?” mkuu wa msafara aliuliza.

    “Risasi imeingia pabaya sana  sana sijui kama ataweza kupona labda kwa kudura za Mwenyezi Mungu,” yule Daktari alimweleza mwanajeshi huyo mwenye nyota tatu mabegani mwake ambaye tangu mwanzo ndiye aliyekuwa kiongozi wa msafara huo uliokuwa ukielekea huko bahari ya Kaspian.

    Jamir alifumbua macho akamtazama yule daktari, “Usiumie Dokta, hata nikifa nimeshafanya kazi niliyotumwa, nimeipigania nchi yangu, Tanzania, nimewapinia watu wangu, Watanzania, fanya unaloweza lakini ukishindwa basi muachie Mungu,” Jamir akafumba macho tena.



    §§§§§

    Kamanda Amata kwa haraka, alimuwahi Shalabah na kumchapa makonde kadhaa bila upinzani wowote, Shalabah akaiinua kutoka pale alipokuwa ameegemea, “Usifikiri mimi bwege wewe,” akasema. Alimuwahi Amata akamshika kwa vidole vyake kwenye mifupa ya mabega, Kamanda akasikia maumivu na kuhisi ganzi ikimwingia kwa kasi. Shalabaha akamsukuma nyuma na kumchapa konde moja lililomyumbisha na kumwongezea linguine ambalo lilimpeleka chini.

    “Bado mtoto mdogo wewe kwenye mapigano,” Shalaba alimwambia Amata huku akikamata ukosi wa shati lake na kumpigisha magoti, kwa kutumia goti lake alimpiga kidefuni, Amata akadondokea nyuma, Fasendy aliyekuwa chini hakuweza kuvumilia, aliinuka na kumuwahi Shalabah akamdandia mgongoni na kumng’ata katika mshipa mkubwa wa shingo.

    “Aaaaaaaiiiigggghhhh!!!!” Shalabah akapiga kelele na kumkamata shingo Fasendy kwa nyuma kisha akambinua na kumbwaga upande wa mbele, Fasendy akafikia mgongo, akatoa mguno hafifu wa kukata tama, lakini hakujali, alijinyanyua kiufundi na kuruka sarakasi matata alipita teke moja kali la kuzunguka lakini Shalabah akalikwepa vizuri, teke la pili nalo akalikwepa vilevile, alipotua chini akakuta na pigo kali lililopigwa kwa viganja viwili juu ya matiti yake, Fasendy akasukumwa nyuma kwa nguvu, alipopata nguvu za kusimama, alirudi kwa kasi kumvamia Shalabah.



    “Fasendyyyyyyy!!!!!!!!!” Kamanda Amata alipiga kelele baada ya kuona Shalabah akichomoa kisu kutoka katika biatu chake kikubwa alichokuwa amekivaa, lakini alichelewa, Fasendy alikutana na kisu kikali kilichopenya katika tumbo lake pembeni kabisa chini kidogo ya mbavu.

    “Aaaaaaaaa, ameniuaaaaa…” yalikuwa ni maneno ya mwisho ya Fasendy, akajibwaga chini, kwa nguvu na kile kisu kikabaki mkononi mwa Shalabah. Kamanda Amata akaainuka kama mbogo, Shalabah akafanya mchezo uleule, alikipima kisu kilipate tumbo la Amata barabara, kumbe mwenzake alishausoma mchezo huo. Alimkwepa kwa sentimita chache na kile kisu kikapita pembeni, Kamanda Amata akajiguza na kuudaka mkono wa Shalabah, aliuvuta kwa nguvu na kuusukuma chini, kisha kwa kisigino chake alipiga korodani za Shalabah, yowe likamtoka, akapiga tena kisha akamvuta mbele kwa nguvu na kumuweka sawa, konde moja la uso, la pili na la tatu yalimtoa fahamu kijana huyo mtukutu. Akageuka na kurudi kichwa kichwa, Kamanda Amata akaruka juu na kumnasa shingo kwa miguu yake akampiga kabala ya miguu na kushuka nae mpaka sakafuni. Shalaba alirusharusha miguu na mikono lakini ile kabala ilikuwa balaa, tungeiita kabali namba tisa, Shalabah alilegea na kutulia kimya, shingo yake ikiwa tayari imevunjwa na miguu ya Kamanda Amata. Akanyanyuka na kumuwahi Fasendy, akamuinua kwa mikono yake na kumfanya kama kaka kwa kuegemea mikono hiyo.



    Hussein, akapata uhai ghafla, akazinduka kutoka kwenye mzimio mzito, akamuona Shalabah akiwa kalala chini miguu kaitupa huku na kule ulimi ukimning’inia nje, akaokota bunduki yake iliyokuwa imedondoka si mbali naye, wakatia huo Kamata akiwa na Fasendy akijaribu kumsaidia hili na lile labda atamwamsha, damu zilikuwa zinamvuja kwa wingi. Hussein aliinua ile shotgun na kulenga kisogo cha Kamanda Amata.

    “Bastard!” alitamka maneno hayo huku akiondoa akiingiza risasi chemba. Kamanda Amata aliduwaa akapoteza mtandao wa akili yake kwa nukta kadhaa.







    §§§§§

    Huko nje, lori aina ya Jeifang ziliingia kama kumi hivi na kushusha askari wenye silaha waliovamia eneo lile, wakiwa na bunduki nzitonzito. Walikuja kusaidia wenzao waliozidiwa nguvu na askari wa Kitanzania, walitawanyika huku na huku kwa amri waliyokuwa wakipewa na kiongozi wao aliyekuwa katikati ya lango akiwapa ishara ya mkono kuashiria kushoto ama kulia. Dakika moja baadae wote wakazingira lile eneo na kuazna kusaka kila kona.



    KATIKA ANGA LA SOMALIA

    “...MiG-31E target 1, MiG-31E,” Rubani katika ndege ya pili iliyopewa jina la target 2 alikuwa akimwita yule wa target 1, wakiwa juu mita 23000 au futi 75,500 kutoka usawa wa bahari. Kadiri ya uzoefu wao tayari walikuwa kwenye anga la Somalia, ili kuweza kupata shabaha waitakayo kutoka na kasi ya ndege hizo, walianza kushuka taratibu kutafuata Mogadishu jambo ambalo ni ndani ya dakika tano tu wangekuwa wameifikia.

    Walipohakikisha wameiona ardhi ya Mogadishu walifanya manuva na kila mmoja alikwenda upande wake kwa kuzigeuza ndege hizo ghafla, kisha wakazunguka na mmoja akatokea mashariki huku mingine akitokea Maghalibi.



    “…MiG-31E Target 2 ready to engage,” sauti ya rubani wa ndege ya pili ilimwambia yule wa ndege ya kwanza kuwa yuko tayari kufanya mashambulizi. Wakati huo katika kipimo cha shabaha ndani ya ndege zile kila mmoja aliweka eneo analotaka kulipiga. Kwa sekunde iliyo sawa, wote wakabofya vitufe vilivyo katika mkono maalum kwa kazi hiyo ndani ya ndege hizo. Milipuko mikubwa ilitokea, mmoja ulipiga katika lango kulikokuwa nay ale magari yakishuhsa wapiganaji nwengine na mwingine ulipiga eneo lililokuwa na nyumba ya ghorofa iliyotumika kama ofisi au sehemu ya mikutano yao.



    “Uuuuuuuuuuhuuuuu!!!!!” rubani wa ndege ya kwanza alishangilia kwa shabaha yake, akainyanyua ndege yake na kuipeleka juuu kwa kwa si kaipoiweka sawa akadondosha makombora manne ya maana yakashuka na kusambaratisha kila kilichosimama, ilikuwa ni hali ya kutisha, moto mkubwa ulifumuka na ndege hizo hazikwenda mbali zikilikuwa zikirandaranda maeneo hayo.

    Baada ya kuhakikisha wamesawazisha ndani ya dakika moja waliambiana.



    “MiG-31E target 1, Mission succesifull,” wa kwanza akamwambia mwenzake naye akajibu kwa mtindo huohuo wakimaanisha kuwa kazi yao ilikuwa imekamilika kwa ufanisi. Wakazipindua ndege zao na kuongeza kasi kurudi walikotoka na kuacha wapiganaji wa Maharamia wakiwa wameteharuki kwa hali hiyo, wakiokotana huku na huko.



    §§§§§

    PARPADOS ilipewa amri ya kuondoka haraka karibu na lile eneo la bandari, haikuwa na budi taratibu ilipiga maji kwa makata maji yake na ikazidi kuliacha mbali lile eneo la bandari na kusogea katikati ya bahari.

    Poooooooooooo!!!! Honi nzito ilisikika baharini, wale wanajeshi waliokuwa kwenye deki ya ile meli waliitazma nyuma na mbele wanakoelekea na kuona meli nyingine kubwa kwa mbali. Hawakuitambua sawasawa pia kutokana na giza nene la saa tisa usiku.

    “Unaombwa kusimamisha meli yako hapo kwa usalama wako,” ilikuwa sauti iliyotoka katika ile meli kubwa waliyoikuta imepiga nanga katikati ya maji, Nahodha wa jeshi la maji la Tanzania hakukaidi, alizima injini na ile meli ikapunguza mwendo taratibu.

    BARNATOV LINE, maandishi yaliyosomeka ubavuni mwa meli ile ya kijeshi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Colonel, sisi ni wanajeshi wa Tanzania, tuliokuwa mateka chini y maharamia wa Kisomali,” mkuu wa msafara katika meli ya PARPADOS iliyowabeba wale Watanzania na wenzao alijitambulisha kwa niaba ya wote huku akipiga saluti kwa kanali huyo wa jeshi la Urusi.

    “Sawa, Captain, je watu wetu mna habari nao?” yule Kanali wa jeshi la Urusi akauliza.

    “Ndiyo Kanali wote wako salama kabisa, kama unavyowaona,” akajibu na kisha akawaita wale vijana watano wa jeshi la Urusi, wakapiga saluti kwa mkubwa wao.

    Kanali wa Kirusi akatikisa kichwa kuonesha kuwa ameridhika kwa hali hiyo, “Ok, naweza kuondoka na vijana wangu,” akaomba.

    “Hapana Colonel, inabidi mje muwachukue kule Tanzania kwani hawa walitoka pamoja nasi Tanzania nasi kwa mission maalum Sir,” yule mkuu wa msafara mwenye cheo cha Captain alimjibu.

    “Ok, maadam tumejua wako salama hakuna shida, tutafanya utaratibu wa kuwachukua, asante sana Captain,” yule Kanali wa Kirusi akashukuru na ile meli ikaongeza kasi kuondoka eneo lile. Furaha ya kuokoka kwao ilikuwa dhahiri shahiri nyusoni na mioyoni mwao, waliimba wakacheza wakafungua vinywa vilivyojaa ndani ya meli hiyo na kugida kama hawana akili nzuri.

    Jamir alikuwa kalala kimya kitandani huku macho yake ameyafumba, hakujitikisa wala hakufanya kitu chochote. Mara kwa mara daktari aliyekuwa akimwangalia alikuwa akimpima mapigo ya moyo kuona kama yanapiga au yamesimama. MV PARPADOS iliendelea kukata maji haikusimama mpaka katikati ya bahari, ikapiga nanga na wote wakasubiri, Nahodha wa meli hiyo akatafuta mawasiliano na makao makuu ya jeshi (JW) ili kuomba msaada wa haraka kwani wasingeweza kwenda mbali na meli hiyo.



    §§§§§§§

    Wakati Kamanda Amata akifikiria jinsi ya kujiokoa dhidi ya risasi itakayofyatuliwa na Hussein ambaye alikuwa akikenua meno, “Nimekupata, panya buku wewe!” akitamka maneno hayo, alivuta kifyatulio (trigger) lakini kabla hakijaruhusu risasi kutoka, Kamanda Amata alimshuhudia mtu huyo Kibonge akipaishwa juu na kubwaga kando, damu mithiri ya bomba ilikuwa ikitoka katika kichwa chake. Kamanda Amata akageuka kutazama kule ilikotoka ile risasi. Kidirisha kilichoruhusu mtutu wa bunduki hiyo kupenya kilifunguliwa wazi na mtu mmoja mfupi aliyeshupaa aliteremka na kuruka kwa ndani, akatua kwa miguu yake miwili akasimama. Amata alimtazama lakini hakumjua kwa kuwa alikuwa kavaa sox kuficha uso wake.



    “Vipi, amekufa?” yule mtu akauliza kwa Kiswahili safi, Kamanda akamtazama tu bila kujibu wakati mtu huyo alikuwa akivuta hatua huku bunduki yake ikiwa mgongoni, akaenda pale alipolala Fasendy, akapiga goti na kuweka mgongo wa kiganja chake cha kulia katika shingo ya mwanamke huyo, akasikiliza kwa nukta kadhaa baadaye akamgeukia Amata, “Hajafa,” akamwambia.

    Yule mtu akasimama na kuvua kofia yake usoni, sasa wakatazamana uso kwa uso na Kamanda Amata hakuna aliyekuwa anamjua mwenzie.



    “Naitwa Daud Daud, mwanajeshi wa jeshi la hadhimu la Tanzania, nilikuja Mogadishu kwa operesheni hii lakini mwenzangu aliuawa vibaya na mimi nimiliponywa maisha yangu na huyu mwanamke, hata simjui kwa jina,” akajitambulisha na kutoa maelezo mafupi.

    Kamanda Amata akamtazama yule kijana akahakikisha kuwa kweli ni Mtanzania baada ya kuona bendera ya Tanzania iliyobandikwa kwa juu ya mfuko wa kombati alilovaa.

    “Naitwa Amata Ric,” lakini kabla hajamalizi Daud akamalizia “…Kamanda Amata.” Wote wakacheka na kupeana mikono.

    “Ok Daud tutaongea vizuri, vipi hali ya huko nje kabla hatujatoka?” Amata akauliza.

    “Huko nje kumevurugika, ndege vita za JW zilifika na kufanya kazi kubwa sana ya kusambaratisha ngome yote, utajionea mwenyewe,” Daud akajibu.

    “Ok, tuna tuna kazi tatu, moja ni kumsaidia huyu dada, pili kufungua hayo makombola na kuchukua vichwa vyake, tatu ninahitajin kuonana na kiongozi wa hawa Maharamia anaewapa jeuri, Mr. Lonely,” Kamanda akamwambia Daud.



    Kisha kwa kushirikiana wakaanza kufungua yale Makombora, huko nje moto mkubwa ulikuwa ukiwaka, kwa haraka haraka waliweza kufungua makombora yote nane kwa kuwa mawili tayari yalikuwa yamepakiwa kwenye ile meli PARPADOS.

    Kisha wakafunga hivyo vichwa ambavyo kwavyo kuna mlipuko mbaya sana uliohifadhiwa, na hlilo ndilo bomu lenyewe. Vilikuwa ni vizito, wakavikusanya pamoja.

    Mara mlango ukafunguliwa, Chammeleone akaingia na vijana wake waliokuwa tayari kwa lolote kutokana na silaha walizozibeba.

    Alipiga makofi kumpongeza Amata, “Hongera sana kijana, sasa hapa si pa kukaa, hawa jamaa wako wengi sana, naomba tuondoke haraka,” akawaambia. Kwa kushirikiana na wale wafuasi wake wakabeba vile vichwa na kutoka navyo nje ilhali Kamnda Amata alimbeba mabegani mwake Fasendy, wakatoka ndani ya jengo hilo. Huko nje kulikuwa ni moshi na mioto kila kona, Kamanda Amata aliikubali kazi iliyofanywa na Tai kutoka Tanzania. Wakaelekea kwenye Land Cruiser iliyoegeshwa nje, wakapakia kila kitu na kuondoka eneo hilo.

    Kamanda Amata alitulia kwenye landcruiser huku miguuni mwake amemlaza Fasendy aliyekuwa hajitambui, moyoni alikuwa akifikiria mengi sana, jinsi ya kumpata Mr. Lonely, alijua wazi kuwa huyu ndiye mzizi wa genge hili la wahuni ambao kazi zao ni kuteka meli za mizigo huku wakivunja sheria za kimataifa kwa kuzivamia zikiwa katika maji makubwa, maji ya kimataifa.



    §§§§§§

    DAR ES SALAAM – TANZANIA



    Saa 12:00 asubuhi, gari ya Usalama wa Taifa ilisimama kwenye nyumba Fulani huko Masaki. Wanaume wawili wakateremka na kulijongea lango kuu la nyumba hiyo ya kiongozi wa ngazi za juu katika awamu ya kwanza. Mlinzi wa getini akafungua lango na kuwakaribisha vijana hao waliovalia suti nadhifu sana.

    “Tuna shida na mzee,” mmoja alimwambia yule mlinzi.

    “Shida sasa hivi?” yule mlinzi akauliza.

    “Ndiyo sasa hivi,” mwingine akajibu. Yule mlinzi akainua simu ya mezani hapo katika kibanda chake na kupiga ndani ya nyumba hiyo kubwa ya kifalme akampa ujumbe mtumishi wa ndani naye akamwamsha huyo aliyekuwa mheshimiwa.

    Alipotoka ndani akiwa katika pyjama alikutana na vijana hao, hakuuliza moja kwa moja aliwatambua kwa jinsi walivyoonekana, askari kanzu.

    “Enhe, niwasaidie nini vijana ? mbona asubuhi asubuhi?” akawauliza.

    “Mheshimiwa, sisi ni vijana wa Usalama wa Taifa, tumetumwa kutoka Ikulu, Mzee unatakiwa Ikulu kabla ya saa moja asubuhi, hivi tumetumwa kukuchukua,” mmoja akasema.



    “Ikulu, kuna nini saa hii, mambo ya Ikulu tulishaachana nayo zamani,” akajitetea.

    “Sisi ni wajibu wetu tu kukufikishia ujumbe kama ulivyo, unaitiwa nini utajua hukohuko,” yule kiongozi wa serikali ya awamu ya kwanza akabaki kaduwaa, akarudi ndani na kubadilisha nguo kisha akaondoka na hao vijana kwa kutumia gari waliokuja nayo.

    Asubuhi hiyo, watu kama watano walikamatwa na wengine kuwekwa kizuizini, wakati uchunguzi ukiendelea, hawakutakiwa kutoka hata ndani ya nyumba zao, kila kabrasha lililohusiana na mikataba ya kampuni iliyokuwa ikichimba yale madini kule Msanga mkuu liliwekwa mezani upya na Mkaguzi mkuu wa serikali na kamati ya Bunge walianza kuyapitia tena.



    ZANZIBAR

    Asubuhi hiyo hiyo Gina alikuwa na vijana wengine wawili wa Usalama wa Taifa nje ya hoteli ya Serena pale Zanzibar, tayari kumkamata Balozi wa Somalia ambaye ilionekana alikuwa akishirikiana na Waziri wa Ulinzi kutoa siri za mradi huo na nini kinaendelea.

    Waliingia ndani ya chombo cha kuwapandisha juu, Gina akabonya kitufe namba 4 na kile chombo kikawapandisha.

    Wakafika mlango namba 456 kama walivyoelekezwa na mtu wa mapokezi. Wakagonga mlango mara tu ukafunguliwa. Wale vijana wakaonesha vitambulisho vyao na moja kwa moja wakaingia ndani ya chumba hicho.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Mheshimiwa Mr. Balozi, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakuweka chini ya uangalizi wake kwa muda usiojulikana, hii inatokana na mbinu chafu ulizokuwa ukizifanya kuihujumu nchi hii,” kijana mmoja alimweleza huku akimkazia macho, Mr Balozi aliishiwa nguvu, akajitupa kitandani na kuketi.

    “Mnajua mi ni mtu mkubwa sana, halafu hamuwezi kuniambia hayo mnayoniambia bila kibali kutoka serikalini kwangu,” akalalama.

    “Hatuwezi kukuweka chini ya ulinzi bila serikali yako kujua, inajua na ndiyo iliyoturuhusu,” yule kijana akamwambia. Mr Balozi hakuwa na ujanja, alijiweka tayari na kuondoka chiini ya uangalizi wa vijana hao mpaka kwenye gari ile aliyokuwapo Madam S, Kwame na Scoba, safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Zanzibar ikaanza.

    Pale waliingia naye kwenye Chopa na kumrudisha Dar es salaam ambako alirudishwa nyumbani kwake na kuwekewa ulinzi wa kutotoka kwenda popote mpaka uchunguzi utakapokamilika.

    Halia ilikuwa tete kwa kila aliyejijua kuhusika na sakata hilo, matumbo yalijaa gesi zisizo na sababu, BP za kushika zikaongezeka, lakini katika yote hayo hakuna aliyemuona Bw. Goloko Mikidadi. Kila mmoja alijiuliza yuko wapi mtu huyo aliyewafanya wao kuwa ma-bilionea, hakuna aliyejua kama mwenzi wao, swahiba alikuwa chakula cha samaki wa Mr. Lonely. Hakika zilikuwa siku ndefu mno kwa mabwanyenye hao wenye uchu wa kuliibia Taifa. Hii ilikuiwa ni hujuma, hujuma mbaya kuliko yoyote iliyowahi kutokea.



    Viongozi wenye dhamana na Taifa, haohao tena wanaliibia Taifa hilohilo, wanalihujumu na badala watetee Wanachi bado wanawakandamiza, wakilalia minoti ilhali yule wa kijijini anapiga mwayo wa njaa huku mkono wake akiwa kauweka shavuni bila kujua kesho yake inakuwa vipi.

    Ni hujuma, watu wanapokuwa tayari kupigania Taifa lao, wanaposonga mstari wa mbele wewe unawakabidhi kwa maadui wanauawa wanadhindwa kulipigania Taifa lao, na wewe unakenua meno yote kwa kuchekelea ilhali familia za watu hao zinalia na kuomboleza zikiwa hazijui kesho na keshokutwa zitakuwa mgeni wa nani.







    Waziri wa Ulinzi alikuwa ameketi sebuleni kwake akaiangalia kuninga kubwa kabisa iliyokuwa imening’inizwa ukutani, alivua kofia yake aliyokuwa ameivaa kichwani mwake na kuficha nywele zake zenye asili kama Kiarabu au Kisomali, akaiweka mezani. Ijapokuwa alikuwa na hofu lakini hakupenda kuionesha kwa yeyote, aliendelea kutazama Televisheni, aliendelea kunywa mvinyo wake taratibu. Mara simu yake ikaita kwa fujo, akainyakua na kuitazama kwenye kioo, private number, akasita kuipokea akaiweka tena mezani, akashusha pumzi za nguvu na kuvuta gazeti la Uhuru na kulipekuwa kurasa moja na nyingine kana kawamba hakuwahi kulisoma gazeti hilo.

    Mara ile simu ikaita tena, akainyakua na kuona vilevile private namba, akaipokea kwa taabu na kuiweka sikioni. Akasikiliza anachoambiwa, hakika hakikumfurahisha, akajua sasa ni wakati wowote atakuja kuchukuliwa na kufikishwa panapohusika. Hodi ikabishwa mlangoni, akahisi kuchanganyikiwa. Akajua vijana watakuwa wamefika, afanye nini sasa kama mabilioni kayaficha Uswiss wakati wavuja jasho wanashinda na mlo mmoja na mlo wenyewe bado haukidhi mahitaji ya viini lise, ilimradi tu wamekula kujaza tumbo.



    Aliikumbuka siku aliyoingizwa kwenye sakata hilo, uroho na uchu wa pesa, sasa aliona wazi vikimtokea puani.

    Miaka Sita Iliyopita

    Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa

    JIONI ya siku hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi alichelewa kutoka ofisini kwani alikuwa na kazi nyingi za kumaliza kabla ya safari yake ya kwenda UN kumwakilisha Rais wan chi katika mkutano wa masuala ya usalama hasa katikam nchi za maziwa makuu. Akiwa katika kupangapanga hiki na kile, hodi ilibishwa mlangoni kwake na Katibu wake, Miranda aliingia ndani akiwa na bahasha mkononi, bahasha iliyopendeza kwa rangi na maua, akakbidhiwa, akaipokea na kuichana kuangalia kuna ujumbe gani ndani yake.

    Alikuwa akialikwa kwenye hafla maalumu iliyoandaliwa katika makazi ya Balozi wa Somalia nchini Tanzania, wiki moja inayofuata, akatikisa kichwa kuashiria amekubaliana nao.

    “Isome kisha ijibu uwatumie taarifa,” akamwambia Miranda.

    “Niwaambie nini?” akauliza.

    “Positive,” akajibu kwa mkato akimaanisha kuwa amekubaliana na mwaliko huo.



    Wiki moja Baadaye

    Nyumbani kwa Balozi wa Somalia



    Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi alikuwa ni mmoja kati ya wageni mbalimbali kutoka ofisi tofauti za kibalozi na taasisi zisizo za kiserikali walijumuika katika viwanja vya makazi ya Balozi huyo, ilikuwa ni Cocktail party, mara Balozi akamwendea Waziri wa Ulinzi na kumsalimu kwa makeke na bashasha pembeni alikuwa amefuatana na kijana nadhifu, aliyeonekana kashiba pesa, nywele zake hazikumficha kabisa kuwa yeye ni Msomali, lakini huyu alikuwa tofauti kabisa kwani alionekana kutakata kwa pesa.

    Wakasalimiana wote watatu wakatambulishana kwa majina na shughuli zao.

    “Ndiyo bwana Shalabah, kalibu sana Tanzania,” Waziri wa uUlinzi alimkaribisha kijana huyo kisha mazungumzo yakafuata. Hoja kubwa ilikuwa ni kumjuza Waziri huyo juu ya huo mradi wa Madini ambao unaendelea kati ya wadau mbalimbali waliopo serikalini na waliotoka. Walipenda kumhusisha yeye kwa kuwa ndiye alikuwa mwenye dhamana ya usalama wan chi, alijua kila mpango wa kijeshi katika kurutubisha madini hayo ya Urani yaliyopatikana huko Mtwara, Msanga Mkuu. Aliwasikiliza kwa makini sana, lakini kwa kuwa siku yenyewe ilikuwa fupi akawaomba waonane siku inayofuata mahali Fulani pa utulivu, wakakubaliana kukutana Hoteli Embassy katikati ya jiji usiku wa saa tatu. Walipoagana Mheshimiwa Waziri akapewa bahasha ya khaki, alipoichungulia baadae akiwa nyumbani kwake ilikuwa ni hundi ya milioni tano, bila jasho. Akakenua meno yake kwa furaha ya kujipatia pesa hizo.

    Inaonekana huu mradi una pesa, nitawasikiliza kesho, alijiwazia na kuitupia ile bahasha katika briefcase yake ya kazini.



    §§§§§§

    Ilikuwa ni juu kabisa ya hoteli hiyo, walipoketi watu hawa watatu wakiongea biashara hiyo haramu.

    “Tangu mwaka 1990 tumekuwa katika mradi huu na lengo kubwa ni kupata haya madini ama yawe yamerutubishwa au la, kwa kuwa sisi tunafanya biashara na makundi ya Kimataifa ya Kigaidi na yanayofanana na hayo, tuna miradi mikubwa. Sasa shida yetu ni kuwa tunataka haya madini ambayo yako hapa, kwanza kuna plan gani nayo tunajua, sasa kwa hilo tumeona tusubiri yakishatengenezwa makombora hayo ndiyo tunayataka sisi,” Shalabah alimwambia Mh. Waziri, akabaki anatikisa kichwa kuashiri anaelewa.

    “Sasa hayo yote mmeyajuaje?” akawauliza.

    “Aaah, si nimekwambia tuna watu tangu miaka hiyo waliokuwa wakifanya kazi ya kutuwekea mipango sawa, wakiwemo Mawaziri kadhaa, Katibu wa Wizara ya Madini Bwana Goloko Mikidadi na wengine katika ngazi mbalimbali, sasa tumepata mpango mzima na tumejua kuwa mnayarutubisha na kutengeneza makombora, sisi tunahitaji hayo makombora lakini sasa kama unavyojua hawa wazee wenggine wamestahafishwa, wengine wamefungwa na mambo mengi, tulikuwa na kikwazo kimoja, kulikuwa na mtu ambaye alikuwa ngazi ya juu pale katika bodi ya mradi huo naye aliwekwa na Mwl Nyerere mwenyewe, tukagundua kuwa alikuwa ni Usalama wa Taifa aliyekuwa akitoa siri hizi zote serikalini ndio maana ikapelekea ule mradi kusimamishwa kwa muda kabla ya kuanza tena na ndipo mkataba na kampuni ya Kirusi ukasainiwa, pale tulianza upya tena lakini kwa msaada wa walewale walio nje ambao serikali iliwaondoa kwenye nyadifa zao, tukajipenyeza na kuweza kujua kinachoendelea. Sasa tunataka nawe utusaidie kwa hilo, kujua nini kinaendelea na kwa kuwa information nyingi tunazo sasa ni kuyapata hayo makombola,” akaongea Shalabah.

    Mh. Waziri akabakia kumwangali tu akimsikiliza kwa makini sana na kumwelewa kwa kina vile vile, akaijiweka sawa kitini na kuinua glass yake iliyojaa Whisky aina ya John Walker, alipoishusha akajikuna tumbo lake na kujikohoza kwa minajili ya kusafisha koo lake.



    “Ok, nimekuelewa bwana Shalabah na bwana Balozi, kila kitu kinawezekana, pesa ipo?” akauliza.

    “Pesa kwetu sio ugonjwa Mheshimiwa, tunazo nyingi kama matundu ya chandarua,” Shalabah akajibu na wote wakacheka, kisha Waziri akaendelea, “Ni kweli kama mlivyo na maelezo mengine, mpango nji uleule, na ujue sasa hii sio serikali ya awamu ya kwanza hii ni nyingine, Wanasayansi wetu wa jeshi upande wa milipuko wanashirikiana na wale wa jeshi la Urusi kutengeneza makombora yenye nguvu kubwa nay a masafa marefu ili kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu na ile ya Afrika kwa ujumla.”

    Shalabah alifurahishwa na manenoi hayo, “Sasa tunaweza kupata hayo Makombora? Tufanya biashara ya pesa nyingi na wapigania uhuru kote duniani, lazima tuhakikishe uhuru wetu unapatikana na nchi zetu kutambulika na kupewa haeshima duniani kote,” akaeleza.

    “Na kwa hilo nakuhakikishia nitatoa ushirikiano mkubwa nanyi, kweli lazima tupiganie uhuru wan chi zetu,” Mh. Waziri akaunga mkono.



    Kauli ile ikawashtua kidogo Shalabah na yule Balozi.

    “Msishtuke, mimi kiasili ni Msomali, wazazi wangu waliingia Tanganyika miaka hiyo, kule Arusha, wakajichanganya na Wamburu hivyo ikawa ngumu kutambulika uhalisia wa uraia wao, nimekulia hapa, nimesoma hapa, na mara kadhaa nakwenda Somalia na kuona harakati kubwa za ukombozi, nilipendezwa nazo na nilitamani niwaunge mkono,” akawaeleza.

    “Haujachelewa, wakati ndio sasa!” Balozi akamwambia yule Mheshimiwa.

    “Mimi ni mbunge wa Mburu Magharibi, na nimekuwa jeshini kwa miaka mingi kule Monduli mapaka nachaguliwa kuwa Waziri wa Ulinzi ni mbunge wa Mburu Maghalibi, na hili ni kosa kubwa la Serikali ya Tanzania, haina muda wa kuchunguza uraia wa mtu, ilimradi umeishi miaka mingi, wanakupa ubunge wakitaka, uwaziri kama hivi na kadha wa kadha nah ii itawagharimu sana, siwezi kuacha watu wangu wanateseka kupigania uhuru wao eti kwa sababu ni nchi iliyonilea, never,” akaongea kwa hisia.

    Kauli ile iliwafurahisha wote walikuwapoa hapo, vinywaji vikaagizwa tena na kuku wazima wawili wakaletwa mezani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa sikilizeani, process ya kutengeneza hayo makombora itaanza mwaka ujao na itachukua miaka kama mine hivi mpaka kukamilika kwa sababu ni teknologia mpya inayobuniwa, na awamu ya kwanza tutaangua makombora ishirini na tano mazito, hivyo nitawapa taarifa ya kila kitu,” akawaeleza.

    Kikao hicho kisicho rasmi kilihitimishwa majira ya saa tano usiku kwa makubaliano ya kuunganisha nguvu, Waziri wa Ulinzi wa kipindi hicho alikubali kufanya hujuma hiyo kwa Taifa lililomlea na kumpa maisha bila kujali.



    MIAKA MINNE BAADAE

    MOGADISHU – SOMALIA



    “Sasa inabidi uwe bega kwa bega na bwana Goloko Mikidadi kwani yeye ndiye Master Plan wa mradi huu kwa upande wetu, nimefurahi mlivyofanya mbinu za kumuua yule kizabizabina Chamellaon, sasa mambo ni murua,” Shalabah na Hussein walikuwa kwenye kikao kifupi na wadau hao katika kasri la Mr. Lonely.

    “Bila shaka! Ila kma nilivyowaambia na imeelezwa katika hilo kabrasha, hisyo ni siri ya serikali, mi nimeitoa kwenu, miaka miwili baadae tutafanya jaribio la kwanza la makombora hayo kule Caspian sasa tunafanyaje, hatuwezi kuyauza kama mishikaki lazima tutumie mbinu makini kuyapata,” yule Waziri alieleza.

    “Ndiyo, lazima itumike mbinu ambayo haitaonesha uwepo wa hujuma kati yetu na serikali ya Dodoma,” Goloko alidakia.

    “Sawa, hilo mtuachie sisi tu, sisi ndiyo tunajua la kufanya, lakini mnatuhakikishia kuwa kila kitu ni sawa? Hakuna tena kama akina Chamelleone,” Shalabah alionesha wasiwasi.



    “Usiwe na shaka kijana, mimi ndiye Waziri wa ulinzi, of cause kuna kidudu mtu kimoja hivi na hiki nitakifanyia kazi mapema tu ili ikiwezekana kama si kukiua basi kukiondoa kazini, na ninajua nitafanya nini,” Waziri aliongea huku kauma meno.

    “Nakumaini sana Mheshimiwa,” Shalabah akajibu huku akipigapiga mgongoni.

    Siri za serikali juu ya mpango wa kurutubisha na kufanya majaribio ya makombora hayo ulitolewa na Waziri wa Ulinzi kwa kuuza kwa wafanyabiashara hao wakubwa. Pesa ilifanya kila kitu, ilimnunua kila mtu, pesa ilinunua uzalendo na kuweka usaliti na hujuma mahala pake.

    Wakapeana mikono na kukumbatiana kwa mafanikio ya kazi yao, na sasa ilisubiriwa tu wakati ufike taratibu nyingine ziendelee.



    §§§§§§

    Kamanda Amata alipanda ngazi akifuatana na Daudi mpaka katika mlango mmoja uliondikwa MANAGER, hakugonga aliingia tu moja kwa moja na kuufunga nyuma yake, akatoa kofia yake na Daudi akafanya hivyohivyo. Yule Meneja akashtuka kuwaona watu hao, akasimama kama aliyemrishwa.

    “Vipi? Kuna tatizo?” akauliza huku akihemaa harakaharaka.

    Daudi alitoa bastola yake na kuigongesha mtutu wake juu ya meza ya huyo meneja, huku akimwangalia usoni.

    “Pasingekuwa na tatizo tusingekuja lakini kwa kuwa wewe unajua kuwa sisi tulishakufa basi leo mizimu imekutokea, tunamtaka Mr. Lonely, haraka sana, hakuna maelezo, hutaki kutuambia tunakuua hapahapa, hatuna masihara na mtu,” Kamanda akamwambia na wakati huohuo, Daudi alimvuta mkono na kumsogeza pembeni ya meza yake ili asije kubonyeza kitufe cha kuita walinzi.



    “Hamna tabu, msiniue nitawaeleza anakoishi lakini huyu mtu sijui kama ni mtu kweli, yupo tu kwa jina, yeye haonekani, utamwona tu katika luninga,” yule meneja akajibu kwa kubabaika.

    “Sawa, ni wapi anaishi au hapo ilipo hiyo luninga ni wapi?” Kamanda akauliza.

    “Wadada Jaziira, nyumba yake iko pekee yake baada ya kuyapita maghala ya bandari, imezungukwa na ksitu mdogo wa kupandwa,” akajibu huku akiwa amelowa jasho mwili mzima kwa woga.

    “Asante sana, nikikuhitaji nitakuja tena,” Kamanda alimwambia huku akiuendea mlango. Daudi alifuata nyuma, baada ya Kamanda kutoka nje ya ofisi ile, Daudi alikuwa ametoka nusu akatazama ndani ya ofisi hiyo kama aliyesahahu kitu, akainua bastola yake yenye kiwambo cha sauti, “Hustahili kushi,” akafyatua risasi na kupiga kwenye paji la uso la meneja huyo, akasota ukutani na kuserereka mpaka akaketin chini damu zikimvuja kisogoni. Daudi akachomoa ufunguo na kuufunga mlango kwa njue, akavaa kofia yake kama mwanzo na kuondoka eneo hilo.



    DAR ES SALAAM



    Waziri wa Ulinzi aliteremka kwenye gari yake kwa uchovu akiwa na mawazo lukuki, alipokelewa na mhusika na moja kwa moja akaingia ndani ya Ikulu ya Tanzania, akaongozwa mpaka kwenye ofisi maalum ambayo Mheshimiwa Rais na jopo lake la uchunguzi walikuwa humo. Aliingia kwa kitetemeshi, hakuna aliyemsemesha zaidi ya kugongana macho na Madam S. akaoneshwa kiti akaketi.

    “Mheshimiwa, nilikuheshimu sana kama mmoja wa wasahauri wangu wa ulinzi wan chi hii lakini nasikitika sana kwa yale uliyoyashiriki na kutufanyia hujuma mbaya kama hii, umekuwa mbunge, tukakupa na uwaziri, ndiyo, umefanya kazi nzuri sana katika wizara yako lakini nasikitika kwamba wewe ndiye unayejulikana kwa jina la Mr X katika watu walioshiriki hujuma hii chafu. Kwa nini umewahujumu Watanzania? Wamekukosea nini?” Mheshimiwa Rais alikuwa akiongea kwa uchungu sana, ukumbi wote ulikuwa kimya kabisa ni kiyoyozi tu kilichokuwa na uhuru wa kutoa mlio humo ndani. Waziri wa ulinzi hakuwa na jibu, kwani aliyokuwa akiambiwa alijua kabisa kuwa ni kweli tupu.

    Yakafuata majadiliano marefu katika jopo hilo, na mwisho muafaka ukafikiwa.



    “Sasa wewe ni mtu mkubwa serikalini, tunaendelea na uchunguzi na wakati huu wa uchunguzi, hutakiwi kutoka nje ya mji wa Dar es salaam bila kibali change na popote unapoenda nje mji lazima usindikizwe na watu wa usalama, tunazifunga akaunti zako zote, huwezi kutoa wala kuingiza pesa, kwani imeonekana una akaunti Uingereza na jana imepokea mabilioni ya shilingi, hongera sana, nimemaliza, sio peke yako wapo na wengine wengi,” Rais alimaliza kuzungumza. Waziriwa Ulinzi akawekwa kizuizini akiwa anaangaliwa kwa jicho la karibu kwa kila afanyalo. Serikali ilihakikisha ndani ya saa tano imewakamata wote waliohusika na kuahidi kuwafungulia mashitaka. Lakini mtu mmoja hakupatikana na huyu ni Goloko Mikidadi.



    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majira ya saa sita mchana, chopa za JW ziliwasili katika Uwanja wa Jeshi la Wananchi, familia, ndugu na jamaa za wapiganaji hao zilikuwa hapo kwa ajili ya kuwapokea ndugu zao. Furaha zilitawala, shangwe na hoihoi. Hakuna aliyetegemea kuona tena sura ya nduguye kwa kuwa walikuwa wakijua wazi jinsi Somalia kulivyo, ama wangeishachinjwa au kuuawa kwa jinsi yoyote ile.

    “Karibu nyumbani mpenzi,” ilikuwa ni moja ya sauti kati ya nyingi iliyosikika uwanjani hapo, akimkumbatia mumewe na kumpa busu la mahaba.

    “Sikutegemea kama utarudi baba,” mtoto alimwambia baba yake upande mwingine wa eneo hilo. Mkuu wa Majeshi Jenerali Kamsumi pamoja na mwambata wake walikuwa katika eneo hilo kuwapokea wahanga hao. Wanajeshi wale walijipanga mistari miwili na kumsikiliza Mkuu wao alipokuwa akiwaambia maneno mafupi ya faraja, kisha akawapa likizo ya miezi miwili kila mmoja ili wakapumzishe akili zao kabla ya kurejea kazini.

    Wale wanajeshi watano wa Urusi wangekabidhiwa kwa Balozi wao baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu katika hospitali ya jeshi ya Lugalo. Watu walitawanyika na kuuacha uwanja huo mkiwa kama walivyoukuta, furaha na shangwe zilihamia majumbani mwao, ikiwamo na kupeana zawadi za ushindi.



    §§§§§

    MADAM S aliitoa miwani yake usoni na kuiweka mezani huku mbele yake akiwatazama vijana wake makini wa idara ya kijasusi ya serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chiba, Scoba, Gina, Dr. Jasmine.

    “Hongereni kwa kazi ngumu ambayo imetuumiza vichwa sana kuikamilisha, kila mtu aliifanya kwa upande wake na kwa pamoja tumeikamilisha, nadhani mmejionea wenyewe, kikulacho ki nguoni mwako, hila za Waziri wa Ulinzi kufanya mpaka Kamanda Amata aondolewe kazini ilikuwa ni kuhakikisha njia nyeupe kwa mpango huu wa kidhalimu, kumbe ndiyo Mr. X. Ili kuhakikisha hujama hii inahitimishwa sawasawa, nawapa kazi, nah ii ni kutoka hapa ofisini na siyo mahali popote, nataka wachunguzwe viongozi wote mmoja baada ya mwingine, na ndani ya mwezi mmoja kila mtu aniletee tafutishi zake nini kimegundulika, lazima kuna makandokando,” Madam S aliwapa maagizo vijana wake watiifu kuhakikisha wananusa kila kona ili kujua lolote linaloambatana na hilo. Wakiwa katika mazungumzo hayo, simu yake ya ofisini ikapata uhai, ikaunguruma kwa fujo kama imepewa adhabu kufanya hivyo, akainyakua na kuiweka sikioni, huku akimpa ishara Chiba ahakikishe amerekodi simu hiyo. Madam S alikuwa na tabia ya kurekodi simu zote zinazoingia katika ofisi yake hata iwe ya kirafiki, nah ii ilimsaidia sana hasa anapokuwa anataka kumbukumbu ya jambo Fulani, lakini si hilo tu, huwa anaandika katika kitabu chake cha kumbukumbu mambo yote yanayotukia kwa kila siku yake,

    kikazi na kifamilia.



    “Hallo!” aliita katika simu ile.

    “Kamanda Amata,”

    “Ooh Kamnda, nipe mrejesho, najua kazi umeimaliza na sas bado sikuoni nyumbani nakuhitaji haraka sana,” Madam S alimwambia Kamanda kwenye Simu hiyo.

    “Bado sijamaliza kazi ndio maana sijarudi, nipo hapa na Komandoo wa JW, Daudi aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha, yuko mzima na salama, tutarudi wote nyumbani, lakini pia tuko, Madam, kuna kazi naimalizia mchana huu kisha nitarudi nyumbani.”

    “Usijali Kamanda, nakutakia mema katika kumalizia kazi hiyo, Gina anakumiss sana na anakusubiri kwa hamu,” Madam S akarusha utani ndani ya simu hiyo. Kamanda Amata upande wa pili alicheka sana kisha simu ikakatika.

    Madam akawageukia vijana wake, “Mnasalimiwa na Kamanda, atarudi si muda kuna kazi kidogo anamalizia.”

    Kila mtu alionekana kuwa na furaha kwa kupata habario hizo kutoka kwa Kamanda. 10



    AKIWA NDANI ya suti safi ya rangi nyeusi, kiatu kilichong’azwa kwa Kiwi, nywele zililizowekwa kwa mtindo wa kupendeza, miwani ya jua iliyomkaa vizuri kabisa, Kamanda Amata aliteremka katika gari moja ya gharama sana iliyokuwa ikiendeshwa na mwanamke mrembo kabisa, aliyependeza kwa mavazi yake yenye ving’arong’aro, unaweza kusema ni Muhindi lakini pia utasema ni Mwarabu yote yangewezekana. Gari hiyo aina ya BMW iliegeshwa pembeni tu mwa jumba kubwa la kifahari lenye bustani ya maua ya kupendeza, ukimya ulitawala eneo hilo ni kelelel za ndege tu zilizikika kwa nadra kidogo kutokana na hali ya jangwa ya eneo lile hakukuwa na viumbe kwa wingi, Kamanda Amata hakuona mtu yeyo te katika mazingira ya jumba hilo pweke. Aliiacha gari iliyomleta ikiweka maegesho vizuri, akapanda ngazi kuuelekea mlango mkubwa wa nyumba hiyo, akaitoa simu iliyokuwa mfukoni mwake, simu ya Shalabah, akabofya vitufe fulani Fulani, kisha akashika kitasa cha mlango huo na kuusukuma ndani, ukafunguka, akaingia na kuufunga nyuma yake.



    Mbele yake alilakiwa na sebule kubwa, safi isiyo na samani yoyote, akapepesa macho huku na kule labda ataona mlango eneo hilo lakini hakuona kitu zaidi ya mapicha ya ajabuajabu yaliyotulia ukutani na kufanya ndani humo kuwa mwa kuogofya. Akaitazama tena ile simu, na kuitafuta majina yaliyomo katika orodha, yote hakuyajua hata moja, akaamua kuzunguka sebule ile huku akiangalia kwa makini kila kilichowekwa au kuning’inizwa ukutani. Kati ya masanau na mapicha yote yaliyowekwa juu ukutani, ni sanamu moja tu lilikuwa chini kidogo, sehemu ambayo unaweza kuishika kwa mkono wako bila kufanya jitihada yoyote. Akagusa lile sanamu, mara akaona jicho la sanamu hiyo likichezacheza.

    “Shiiit!” akatamka kwa sauti hafifu, wakati anatoka eneo lile akaligonga lile sanamu bahati mbaya mara kipande cha ukuta kikasogea pembeni, ukabaki uwazi, ujia mrefu uliingia ndani ya uwazi huo, Kamanda Amata akachomo bastola yake na kuingia ndani ya ule ujia, akapita kwa hadhari kubwa sana akitazama milango iliyojipanga katika ujia huo, lakini kila alipoutikisa mmoja hauukuwa na dalili ya kutikisika seuse kulegea. Mlango wan ne kutoka mwisho, aliposimama tu mbele yake ukafunguka, kulikuwa na kijichumba kidogo kiking’azwa na taa hafifu na muziki laini wa kihindi ulisikika taratibu, akatazama kwa makini mle ndani na juu akaona kuna kamera ya usalama.



    Wameniona, akajisemea kwa sauti yake mwenyewe ya kuweza kujisikia yeye tu, akaingia na mara hiyo kijumba kile kikaanza kuteremka chini. Kamanda Amata akateremka kwenye hicho kijumba na kukutana na sebule nyingine kubwa zaidi ya ile, lakini tofauti na ile, hii ilikuwa na kila aina ya samani ya thamani ya juu, viti vyenye nakshi ya dhahabu, viliizunguka meza kubwa sana iliyokuwa hapo, kioo kikubwa cha luninga kilitulia mahala Fulani katika ukuta wa jumba hilo. Mara taa zikawaka zenyewe mle ndani na kufanya mwanga kuwa mkali zidi ya ule wa kwanza. Kamanda Amata akashika bastola yake sawia katika kiganja cha mkono, sauti ya vicheko vya kiume ikaanza kusikika ndani ya sebule ile.

    “Aaaaaa ha ha ha ha…. Karibu sana kwenye Kasri ya wasio hai, umekuwa mgeni wangu wa dharula sana siku hii ya leo ukizingati nilikuwa safarini kuondoka, najua kilichokuleta labda umekuja kumfuata huyu ndugu yako…” ile sauti ikasema hayo. Mara ile luninga ikapata uhai ikaonesha picha ya kuogofya sana, mwili wa Goloko Mikidadi uliokuwa umechomwa kwa vyuma vinene upande mmoja na kutokea upande mwingine, akiwa ameachama kinywa chake na macho yamemtoka.



    “Shiiit” akang’aka Kamanda Amata, ile sauti ikacheka tena.

    “Sasa na wewe utakuwa kama huyu si muda mrefu,” ile sauti iliendelea kuongea.

    “Acha ujinga wako, nimekuja kukumaliza wewe unayefanya biashara haramu za kuiharibu dunia,” Kamnada Amata aliongea huku akiwa ameuma meno.

    “Aaaaaa ha ha ha ha aaaaaa ha ha ha, wacha kunichekesha, tangu lini mfu akafa tena?” ile sauti ikauliza kwa kebehi huku ikitanguliwa na cheko la dharau, lililomfanya Kamanda Amata kufura kwa hasira.

    Aliinua bastola yake na kupiga ile luninga, iksambaratika yote, ikamwagika chini vipande vipande, nyuma ya ile luninga akaona tundu kubwa la kupita hata land cruiser, na kiti kimoja kilicholala chini, mezani palikuwa na kamera ndogo DV Cam, akaruka kile kihunzi na kuingia ndani, akatazama huku na kule akaona mlango mmoja ukiishi kufungwa, akauwahi na kuupiga teke, ukafunguka, akaingia kwa fujo na kuupiga kikumbo mlango mwingine kwa ndani, mara akasikia kelele ya mlio wa injini ya boti iliyokuwa ikiwashwa, akageuka kulia na kuona boti iliyokuwa ikitaka kuondoka, na mtu mmoja alikuwa juu yake, akafyatua risasi ikapiga injini, injini kazima.



    Kamanda Amata hakufanya ajizi, risasi moja ya mgongo katikati ya uti, ikagawanya pingili hizo.

    “Aaaaaaaaa nooooooo!!!!” ilikuwa sauti ya yule mtu akijibwaga upande wa nyuma, Kamanda Amata akajivuta na kumshika akamvuta mpaka nje ya lile eneo lililokuwa na boti akamlaza sakafuni.

    “Leo mfu lazima ufe tena, shetani mkubwa!” Kamanda akamwambia Mr. Lonely.

    “Tafadhali, umeshaniumiza, basi niachie uhai wangu, nitakupa pesa nyingi sana,” akaongea kwa tabu.

    “Wewe umeacha uhai wa watu wangapi mpaka leo?”

    “Nitakupa pesa nyingi,” akalalama.

    “Pesa zako zinanuka,” akafyatua risasi moja na kupiga kwenye paji la uso, Mr. Lonely akalala kimya huku ametoa macho ya mshangao.

    Alikuwa mwembaba mrefu, mwenye ndevu za kuhesabika, upara ulitawala kichwa chake, mavazi yake ya kawaida yangemfanya aonekane ni mmoja wa masikini huko mtaani.

    “Mwisho wa zama zako Mr. Lonely,” Kamanda akasema hayo huku akiipachika ile bastola kwenye mkoba wake ndani ya suti.

    Akauacha mwili ule na kutoka ndani ya jumba lile.



    Nje kabisa alisimama kulitazama jumba hilo la kifahari, akageuka na kuingia katika gari ileile aliyokuja nayo.

    “Twende,” akamwambia yule mwanadada, wakaondoka kuifuata barabara kubwa. Umbali kama wa mita mia moja hamsini, “Simama,” alimwamuru yule dereva mwanadada. Akashuka na kulitazama lile jumba, akinua saa yake na kuizungusha kwenye pete yake ya juu, mlipuko mkubwa ukatokea katika lile jumba, moto na moshi mzito, kishindo kililisambaratisha lile jumba lote lililoitwa la kifahari.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    UWANJA WA NDEGE WA ADEN ADDE – MOGADISHU



    KAMANDA AMATA akiwa amemkumbatia Fasendy dakika chache kabla ya kuagana, aliyashuhudia machozi ya mwanamke huyo mpiganaji yakikifikia kifua chake, “Sina budi kwenda Fasendy, kwa heri, tutaonana tena.”

    “Wapi Kamanda? Hata hii imekuwa ajali tu kukutana, lakini asante kwa kila kitu,” Fasendy akamshukuru Amata.

    “Usijali tutaonana popote duniani sio lazima Somalia wala Tanzania,” Kamnda akamwambia kisha akamtoa kifuani pake, akambusu shavuni, akavua saa yake ya kijasusi saa yenye kufanya mambo mengi sana, akampatia Fasendy, “Unikumbuke,” akamwambia.

    Fasendy naye akampa kibegi kidogo mkononi mwake, “Unikumbuke,” akamwambia. Kisha Kamanda Amata akaagana na Chamelleon na timu yake, akaondoka kuingia uwanjani tayari kwa safari ya kurudi nyumbani.



    ˜˜MWISHO˜˜







0 comments:

Post a Comment

Blog