Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

KITANZI CHA MWISHO - 5

 







    Simulizi : Kitanzi Cha Mwisho

    Sehemu Ya Tano (5)





    GODFREY KYOMUKAMA, lilikuwa ni jina lililotangulia pale katika ule ujumbe kisha ikafuatia anuani yenye namba tano 16841- 5576 ikamalizia na jina la KAMPALA, Kamanda Amata akaelewa ujanja wa marehemu Kajiba, kwa kuwa alijua kuwa atakufa hivyo hakutaka adui wake ajue maana ya namba hiyo kama atakuwa wa kwanza kuipata, lakini Mungu si Athumani wala Athumani si Mungu ile namba ikafikia kwa mkewe kipenzi Yaumi mtoto wa Kizaramo, nae akapata maana ya namba hiyo kwa shoga yake waliyekutana naye mahabusu pale Segerea, Fasendy. Sasa yuko na Kamanda anaiona namba ile kwa ufasaha zaidi anaielewa, Yaumi anaangusha chozi, anamkumbatia Amata na kulia kifuani mwake, “Wewe ni Malaika kwangu, sijui nikupe nini, nahisi umetumwa na Kajiba uko aliko.”

    “Zaina, nyamaza, kazi bado, sasa tumtafute huyu bwana Kyomukama, kadiri ya maelezo yako umesema ni mfanyabiashara mkubwa, basi atakuwa anajulikana sana, tukimpata yeye, najua tutategua na hii namba ya pili, hapo sasa kazi itakuwa imekwisha, napenda tulimalize hili usiku huu ili kesho asubuhi turudi Tanzania tukajue la kufanya, hii namba ya pili ndiyo kila kitu,” Kamanda alimueleza Yaumi huku akiondoka nae eneo lile.



    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ndani ya Kampala, Fasendy aliwasili majira ya saa nane usiku, ilikuwa ni masaa manne tu tangu alipoachana na Matinya pale Dar es salaam na kumhakikishia kumaliza kazi kabla ya alfajiri. Fasendy, komandoo mtoro wa kike kutoka jeshi la Somalia aliweza kusafiri kwa njia yoyote ile ya hatari ilimradi tu atomize azma yake, mafunzo magumu kama hayo aliyapata katika majeshi ya nchi ya Iran alipopelekwa na serikali yake kupata mafunzo hayo kabla ya kuhasi jeshi na kujiunga na vikundi vya waasi, huko mwanamke huyu alifanya vizuri na akawa tegemeo kubwa sana katika jeshi lake. Baada ya kujiunga na waasi kwa miaka kadhaa akagundua kuwa jeshi la Somalia na liel la Iran walikuwa wakishirikiana kumtafuta, hivyo akatoroka na kwenda kusikojulikana, hapo akawa mpiganaji wa kukodiwa, sifa kubwa aliyokuwa nayo ni kuweza kujigeuza katika hali yoyote ile, mpole, mkali, kichaa, kiziwi, bubu au hata mlemavu ilimradi tu atomize anachokitaka. Alipoingia Tanzania kwa kificho na kuweka makazi yake alijulikana kama bubukiziwi, alipanga nyumba mbovumbovu tu huko Buguruni kabla ya kuinunua ile ya Masaki, hakujulikana nini anachofanya lakini wengi walimjua kuwa ni muuza bangi, Malaya wa kuijiuza mwenyewe na kuwauza wasichana kwa minajirti ya kujipatia pesa, polisi wote walimjua kwa mtindo huo. Walipomkamata, mawili, ama walipewa rushwa au walipewa mabinti wafurahie maisha na kisha wakamuacha, Fasendy alikuwa na uwezo wa kupenyeza kazi zake hasa za bangi, sigara na dawa za kulevya mpaka ndani ya ngome za Magereza, hakuna aliyejua kivipi lakini alijulikana kwa hilo.



    Usiku wa siku moja akiwa nyumbani kwake Masaki ambako hata ukikutana nae huwezi kumtambua kama ni Yule wa Buguruni kwa jinsi anavyoonekana tofauti, alifuatwa na watu wawili, mmoja mwarabu na mwarabu na mwingine mswahili lakini aalikuwa akionekana kushiba pesa, wakaongea nae biashara kichaa ya kwenda kutoa mafunzo ya kijeshi kwa vijana wao ambao walikuwa wakiandaliwa kwa mapinduzi ya ghafla, mapinduzi ya kuuondoa uongozi wa Tanzania madarakani ili wenye tama ya madaraka wajitwalie viti hivyo.

    Fasendy akaingia mkataba mnono, akakubali kazi hiyo ambayo kwake ilikuwa ni kama kumfundisha kuku kula mchele.



    Mara baada ya kuachana na Matinya alielekea uwanja wa ndege na kutazama chati ya ndege zinazoondoka usiku huo na muda huo, akafanikiwa kuipata ndege ya shirika la KLM iliyokuwa ikienda Amsterdam lakini ingetua Nairobi, bingo! Alipoona ulinzi umelegalega, aliangalia jinsi ya kuingia ndani ya uwanja huo asijulikane na mtu. Bahati haiji mara mbili, mara gari ya wafanyakazi iliwasili, wakateremka wadada wa kutosha wa idara ya mizigo pale uwanja wa ndege, akamtazama Yule aliyeona analingana nae kwa urefu hata umbo akampata, kabla ya yote akajifanya ana shida na kumuendea, akamuomba pembeni Yule mwanadada akamfuata mpaka kwenye kigiza kidogo, pigo moja kali la karate, likampoteza fahamu Yule mwanadada, Fasendy akayatwa m,avazi ya ile idara, sasa akaonekana kuwa ni mmoja wao, akamlaza vyema Yule aliyemnyang’anya nguo zake na kumfunika kwa baibui aliyovaa hapo awali. Akaliendea geti na kupita bila tabu, tayari alikuwa ndani ya uwanja akiitazama ndege kubwa ya KLM iliyokuwa tayari imewasha taa zake za vimulimuli ikiashiri kuondoka…..





    Karibu yake lilipita gari la zimamoto likiwa njiani kuelekea kule ambako ndege hutumia kuruka, Fasendy, akaitumia nafasi hiyo, akadandia nyuma na kuondoka nalo, lilipofika mwisho wa ile barabara likasimama, Fasendy akajiweka tayari. Dakika tatu baadae lile dege kubwa lilikuwa eneo lile, Fasendy kwa kutumia uzoefu wa kazi yake alikimbia kwa mwendo wa kawaida na kuingia katika uvungu wa ndege hiyo, ni mchezo hatari sana kama haujui kuucheza lakini mwanamke huyu mtukutu aliweza kulifikia tairi la mbele la ndege hiyo na kulidandia kisha kutumia nafasi hiyo kujipenyeza katika eneo maalumu ambalo tairi hilo hujihifadhi mara tu ndege irukapo. Dakika kumi zingine alikuwa tayari angani akisafiri kuelekea Nairobi, alipofika pale alifanya michezo hiyohiyo na kufanikiwa kufika Kampala usiku huo, aliingia mjini kwa usafiri wa kukodi na moja kwa moja kama alivyoelekezwa. Protea Hotel ndipo alipokuwa ameelekezwa kuiwa mtu wake yupo hapo, akafika kaunta na kutumia lugha yake ya ulaghai kujua kama kuna wageni wa aina hiyo wamefki katika hoteli hiyo, jibu lilikuwa hapana lakini Fasendy alijua wazi kuwa Kamanda Amata hawezi kuwa mjinga kutumia jina lake kujisajiri katika hoteli, hivyo aliutumia ujanja wa kuuliza muda gani wageni gani waliingia, hapo akapata jibu, akalipia chumba na kujifanya mmoja wa wageni katika hoteli hiyo, akaingia katika lifti mpaka ghorofa ya juu kidogo, jirani kabisa na chumba cha Kamanda Amata alipopanga na Yaumi, Fasendy alitulia mlangoni akitazama kama kuna yoyote anayekuja pande hizo, alipohakikisha usalama upo, akauchezea mlango ule kwa funguo zake Malaya na kuingia ndani, alipotuhakikisha mlango upo nyuma yake tu, bastola mkononi alifyatu risasi nne kuelekea kitandani akijua kuna mtu aliyelala, lakini alioshangaa hakuna hata sauti ya mguno wa maumivu, akanyata mpaka pale na kulifunua shuka kwa haraka huku bastola yake ikiwa baki mkononi mwake, Fasendy akasonya baada ya kujua kuwa ameshezwa shere, pale kitandani ni mashuka tu yaliyofunikwa kitaalamu kiasi kwamba uingiapo utajua ni mtu kalala.



    Aliishusha bastola yake na kuirudisha kiunoni, kisha akaketi kutafakari afanye nini, hakujua atampata wapi Kamanda, lakini kwa kuwa alijua kuwa hapo ndipo alalapo basi aliamini kwa vyovyote Kamanda atarudi tu, hivyo alitulia kitini na kusubiri.



    §§§§§



    Ulikuwa ni usiku wa hekaheka, kila mmoja kwa upande wake alyaka kuhakikisha usiku huo anakamilisha kazi yake ili kupambazuke na pambazuko jipya. Fasendy alitaka kuhakikisha anammaliza Kamanda Amata kabla ya jua la asubuhi, Madam S na Chiba wanataka kuhakikisha wanakamilisha tafutishi zao kabla ya jua la asubuhi, Kamanda Amata na Yaumi nao wanataka kuhakikisha kabla ya jua la asubuhi wawe tayari wametegua kitendawili hicho tata.

    Kila kona ilikuwa ni mshikemshike, kuanzia Dar es salaam mpaka Kampala.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa usiku wa giza, Chiba aliitazama hundi aliyoipata kutoka katika mkoba wa kazini wa marehemu Jaji Ramson, haikuwa na shaka kama sio zilezile. Hundi hiyo kuanzia mwandiko, saini, vyote vilikuwa vya mtu mmoja, mtu mkubwa serikalini, ‘Anataka nini?’ Chiba alijiuliza. Akatazama hundi nyingine ambazo kamanda Amata alizipata bkutoka kwa Chilungu, kila kitu kilekile isipokuwa ni namba ya hundi tu ndiyo iliyopishana, ‘Hundi za katikati kapewa nani?’ Chiba akazidi kajiuliza. Akaitazama saa yake, ilikuwa tayari imetimu saa nane za usiku, akazikusanya zile hundi zote na kuziweka mahala salama, akainua simu na kumpigia Madam S ambaye muda huo alikuwa nyumbani kwake, wakapanga hili na lile na kuona cha kufanya ili kuukabili mtandao huo ambao mpaka dakika hiyo hawakujua kusudi lao ni nini hata wafanye mauaji kama hayo tena kwa watu muhimu sana serikalini. Baada ya kuongea kwa kirefu na boss wake, Chiba aliiacha nyumba yake na kuingia katika gari kisha kupotelea mitaani.



    Madam S akiwa ndani ya pajama, aliketi sebuleni akimsubiri kijana huyo, haikuchukua muda mrefu aliwasili nyumbani kwa Madam S na kukaribishwa ndani. Mazungumzo ya kikazi yaliendelea, zile hundi zote zikawekwa mezani na wakaziangalia kwa pamoja.

    “Lazima tumchunguze, tumuweke chini ya uangalizi wetu ili kufuatilia nyendo zote, anapotoka na anapoingia mpaka tujue ni biashara gani anaifanya kisha ndiyo tumtie mkononi,” Madam S alimwambia Chiba.



    “Sawa kabisa na nafikiri jibu la Kamanda likifika linaweza kutupa mwanga, kwa maana huu mtandao si wa hawa tu lazima kuna wengine,” Chiba aliongezea.

    “Lo, kweli walisema wahenga, kikulacho ki nguoni mwako, haya tutaona. Ok, nipe ripoti kutoka kwa Kamanda anaendeleaje na Yule mwali? Maana wasije kuwa wamelala badala ya kufanya kazi,” Madam S alimaliza maneno yake na kuuliza swali.

    “Ujumbe wa mwisho aliniambia, ‘Hakuna kulala,’ lakini inaonekana kuwa kuna watu wamejua kuwa Kamanda yuko kule, maana tayari amepambana nao,” Chiba alieleza.

    “Whattt????!!!!” Madam aliuliza kwa mshangao, akatulia kimya kisha akamtazama Chiba, “Nililijua hilo sasa nimeshakuwa na uhakika na kile nilichokuwa nakifikiria.”

    “Kitu gani Madam?” Chiba aliuliza.

    “Wakati Gina ametumwa na Kamanda kwenda kumfanyia utaratibu wa usafiri wa Kampala kuna kijana aliyekuwa akimfuatilia Gina, mimi niliweka kijana mwingine nae atazame kila kitu, akanambia kuwa kijana huyo aliyemfuatili tangu pale nyumbani kwake mpaka uwanja wa ndege alihakikisha anajua kila Gina alichokifanya, na nina uhakika ni huyu aliyetoa taarifa kuwa Kamanda amekwenda Kampala,” Madam S alinyanyuka na kuiendea meza yake ndogo iliyopo hapo sebuleni, akavuta kitoto cha meza na kutoa picha kadhaa, akaja nazo mpaka mezani.



    “Huyu hapa, jamaa alipata picha zake chache japo kwa mbali,” Madam S alimwambia Chiba na kumpa zile picha, Chiba alizitazama kwa makini, “Kazi imekwisha, kesho tu huyu atakuwa mikononi na atasema kila kitu.”

    “Chiba, hawa jamaa wanajua wanachokifanya, kama ni mpango au siri basi ipo ndani ya mioyo ya watu wasiozidi watatu, hawa wengine ni watumwa tu, ukiwabana sana mwisho hawana la kukwambia, lakini wacha tuwalundike ndani kitaeleweka tu,” Madam S alieleza na mara hii kama kawaida yake alikuwa na chupa ya pombe kali akimimina kwake na kwa Chiba, “Cheers!”.



    §§§§§



    KAMANDA Amata alimtazama Yaumi, akatikisa kichwa.

    “Yaumi! Hapa kuna tatizo moja, ili kupata maelezo juu ya huyu Kyomukama lazima turudi hotelini kwa ajili ya kumperuzi kwenye mtandao wa usalama ili tujue anaishi wapi na anafanya kazi gani, hapo sasa ndipo tutampata usiku huu, au vinginevyo kama wewe ungekuwa unakumbukka nyumbani kwake,” Kamanda alimweleza Yaumi, wakahafikiana na safari ya kurudi hotelini ilianza.



    Haikuwachukua mud asana kufika Protea Hotel, moja kwa moja Kamanda aliiendea kaunta, “201 tafadhali,” aliomba funguo kwa kutaja namba ya chumba, wakati akikabidhiwa, alimwuliza tena Yule mhudumu wa mapokezi kama kuna ujumbe wake wowote, jibu alilopewa ni kwamba hakuna lolote.

    Kwa hatua za haraka haraka alipanda ngazi huku akifuatiwa na Yaumi, alipofika mlangoni mwa chumba chake, akasimama kwanza na kutazama tundu la mlango.

    “Kuna mgeni alikuja au amekuja!” alimnong’oneza Yaumi, kwa maana alipokuwa anatoka aliegesha kipande kidogo cha uzi katika tundu la ufunguo, kipande hicho kisingeweza kutoka mahali kilipo kama hakuna funguo iliyoingia tunduni hapo, akaingiza funguo na kufungua mlango akausukuma ndani lakini yeye mwenyewe hakuingia, akasubiri kidogo, Yaumi akiwa nyuma yake akavuta hatua tatu na kujitoma ndani ya chumba.

    “Tulia kama ulivyo!” sauti ya kike ilimwamuru Amata, akatulia kama alivyoambiwa.



    “Mbona mnapenda kuwasumbua wageni vyumbani mwao jamani?” Amata aliuliza.

    “Mgeni wewe? Unafikiri ulivyotoka Dar hatukukuona? Sasa kwa taarifa yako nipo hapa kwa kazi moja tu, kukuua,” ile sauti iliendelea.

    “Usijali, mimi nilishakufa siku nyingi, ila kila anayeniua mara ya pili hufa yeye, nina wasiwasi sana kwa mrembo kama wewe kufuata njia hiyo hiyo,” Kamanda alizidi kumuuzi Fasendy aliyekuwa akijibishana naye.

    “Mxiuuuuu !!!” Fasendy alisonya na kumuwekea bunduki kisogoni. Muda wote Kamanda alitaka bunduki hiyo imguse ili ajue kuwa adui wake yupo jirani na yeye, kichwani mwake akaanza kupanga shambulizi la ghafla, wakati huo alimwambia Yaumi asiingie chumbani amsubiri koridoni akamwachia na bastola moja kwa ajili ya lolote litakalotokea.

    Ubaridi wa mtutu wa bunduki hiyo ulimfanya Amata kusisimka mwili, akiwa bado mikono yake iko juu, alijaribu kufikiri kuwa mwanamke huyo anajiamini nini hata kumsubiri chumbani humo, akajiandaa kwa pambano kali maana alijua fika kuwa huyo si mwanamke wa kawaida.

    Kwa kasi ya ajabu aligeuka na mkono wake wa kuume ukaipiga ile bunduki na kutoka mikononi mwa Yule mwanamke. Fasendy, hakupoteza nukta alipiga mapigo kadhaa ya karate na kumchapa Kamanda Amata ambaye aliangukia upande wa pili wa meza iliyokuwa katikati ya chumba hicho, alihisi kitu kama maji yakitiririka katika maungo ya midomo yake upande wa kuli, alipojifuta akagundua kuwa ni damu, alijiinua haraka lakini kabla hajawa wima, Fasendy alimpiga mtama mmoja maridadi, Kamanda Amata akanyanyuliwa juu lakini kabla hajatua chini alijigeuza na kumshushia teke moja kali lililotu nyuma ya shingo, Fasendy aliyumba kuelekea ukutani, akatumia nafasi hiyo kukanyaga kwa nguvu ukuta na kujirusha samasoti, nukta hiyo hiyo Kamanda Amata nalimuepa na alipotua tu, makonde kadhaa yalimfikia usoni Fasendy akabaki kachanganyikiwa. Kutokana na ile nguo ya kininja aliyoivaa Fasendy haikuwa rahisi kwa Amata kumgundua mwanamke huyo mwenye upara. Fasendy alipanga mapigo makali ya karate na mara akibadilisha mitindo kwa kasi ya ajabu, lakini Kamanda Amata alikuwa akiisoma mikono ya mwanake huyo na kujaribu kuipangua kwa akili yake yote, mapigo kadhaa yalimfikia na kumuumiza lakini mengine aliyapangua kiufundi zaidi. Zilikuwa ni sekunde kama arobaini na tano ambazo zilimuacha Kamanda Amata akiwa hoi sakafuni kwa kichapo kikali toka kwa mwanamke huyo, kwa jinsi mikono ya Fasendy iliyokuwa ikizungushwa hewani kubadilisha aina ya mapigo, kamanda Amata alikuwa akiona si mikono miwili tu bali ni zaidi ya mia moja, hivyo alijaribu kuupangua huu lakini alijikuta akichapwa na mwingine.



    Ilikuwa ngumu kwa Yaumi kuvumilia kipigo kile kutoka kwa huyo mwanamke, aliiweka vizuri bastola yake na kuingia ndani kwa kasi lakini kabla hajatulia, mguu wa nguvu ulitua kifuani mwake na kumwaga chini kama mzigo, bastola iliyo mkononi mwake ikafyatuka na risasi ikifumua kiio cha dirisha, Fasendy akautumia mwanya huo kuchumpa dirishani na kutoka nje ya chumba hicho.

    Kamanda Amata alijizoazoa na kuwahi dirishani, alimuaona Yule mwanamke ninja akiwa chini kama mtu aliyeumia, akaufungua mlango haraka kuteremka ngazi kumuwahi, bastola mkononi, nyuma akifuatiwa na Yaumi aliyekua akitema damu kila apigapo hatua moja. Kamanda Amata alipofika chini hakukuwa na mtu, shetani!

    Akageuka na kumuona Yaumi kajiegemeza ukutani, akamfuata na kumkalisha chini.

    “Nakufa Kamanda!” aliongea kwa shida kiasi kwamba ilihitaji umakini kumsikiliza ili kumuelewa. Baada ya Kamanda Amata kumnyoosha hapa na pale sasa akamuona akichangamka, akamchukua na kumsaidia kutembea mpaka mapokezi akamkalisha, wakati huo tayari gari ya polisi ilikuwa inaingia katika hoteli hiyo baada ya kupata taarifa kuwa kuna uvamizi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shiiit!!!!!” Kamanda aling’aka, akamchukua Yaumi na kupanda juu mpaka chumbani kwake, akafunga kwa ndani, wakachukua mikoba yao ambayo ilikuwa ni michache tu, Kamanda akavua mkanda wa suruali na kuupachika sawia katika moja ya vyuma vya kushikia dirisha hilo, akambeba Yaumi mgongoni na kujining’iniza katika mkanda ule, taratibu ule mkanda ukawa ukijifungua kama rola ya kamba, akatua chini salama salimini alipouachia ule mkanda ukarudi kwa kasi kuelekea pale ulipofungwa na ulipofika mwisho mlipuko mdogo ukatokea na kuuharibu kabisa. kamanda Amata na Yaumi wakazunguka mpaka kwenye maegesho ya magari, Rage Rover nyeupe ilikuwa imeegeshwa, Amata akapasua kioo na kuingia ndani akamfungua Yaumi upande wa pili kisha akabomoa sehemu ya ufunguo na kuzikutanisha nyaya Fulani, gari ikawaka, akakamata usukani na kuondoka eneo hilop la hoteli bila kuwashtua wengine, akiwaacha polisi wakiendelea na upelelezi wao.



    Baada ya mwendo wa kama dakika kumi huku akihakikisha usalama wao, akaegesha gari pembeni, akatoa kompyuta yake ndogo na kuiunganisha na mtandao kisha akaufungua mtandao wa shirika la simu la Uganda (UTL) akaingiza jina Godfrey Kyomukama katika sehemu iliyotengwa kwa minajili ya kutafuta, baada ya sekunde kadhaa majibu yakaja, jina lilikuwa ni lile lile, namba ya nyumba, barabara ya Malcom X Avenue, Namba ya simu pamoja na sanduku la barua vilianishwa. Kamanda Amata hakuwa na haja ya kupiga simu bali ni kwenda moja kwa moja nyumbani kwa mtu huyo, akaingiza gari barabarani na kuanza kuitafuta barabara hiyo.

    Kwa mwendo aliokuwa akitembea na gari hiyo haikumpa shida kuipata barabara hiyo mara tu alipoikanyaga ile barabar ya Kasozi akitokea York Terrace, alikatisha Impala Avenue na kusonga mbele kidogo kisha akapinda kushoto na kuanza kuangalia namba za nyumba zilizojipanga eneo hilo, haikuchukua muda akaiona ile anayoihitaji, akakunja kulia na kusimama getini, wakati anakunja ile kona gari moja ya kampuni ya ulinzi ikawapita na kwenda kuegeshwa mbele, Amata hakuitilia mashaka, akapiga honi, na geti likafunguliwa kidogo, mlinzi akajitokeza na kuuliza shida ya wageni hawa, walipoomba kuonana na Mr Kyomukama ilikuwa ngumu kidogo kutokana na muda wenyewe, lakini walisititiza sana na Yule mlinzi akawasiliana kwa simu ya siri na bosi wake….



    “Muda ni mbaya, mzee hawezi kutoka nje,” Yule mlinzi alimweleza Amata.

    “Mwambie, ni ugeni wake muhimu sana, aamke kama hataki nitamwamsha mwenyewe,” Kamnda Amata aliongea kwa ukali sana mpaka Yule mlinzi akatetemeka.

    “Unajua mheshimiwa, boss huwa hapendi kusumb uliwa mida kama hii, kwa nini msimsubiri? Mbona sasa ni saa kumi na kitu! Bado kidogo tu ataamka,” Yule mlinzi aliongeza mazungumzo.

    “Wewe unanielewa? Mwambie ana ugeni mzito kama hayuko tayari tunaingia wenyewe huko ndani, kama hana habari basi mwambie ana masaa mawili tu ya kuishi, na wanaokuja kumtoa uhai wako njiani” maneno hayo ya Amata yalimuwacha Yule mlinzi hakiwa hoi kwa mshangao, akajiuliza mara kadhaa kama yeye ndiye mlinzi na kazi yake ni kumlinda bosi wake afanyeje pale anapoambiwa kuwa wauaji wa bosi wake wako njiani, akachanganyikiwa, hakujua la kufanya.



    “Tunapoteza muda Kamanda!” Yaumi alilalama, Kamanda akafungua mlango wa gari na Yaumi akatokea upande wa pili, wakafika getini kabisa na kuliacha gari palepale. Yaumi akatoa bastola.

    “Hay we mlinzi, fungua geti haraka! Ukibisha nakufumua ubongo wako”. Ilikuwa ni ganzi, Yule mzee alitazamana na domo la bastola, alibaki akitetemeka na muda huohuo suruali yake ikalowa ghafla, akajitazama, lo, fedheha, haraka haraka akafungua geti. Yaumi na Kamanda wakaingia kwenye bustani kubwa ya maua ya aina mbalimbali, bila kuuliza wakafuata ujia mororo uliotengenezwa kwa mawe safi kulielekea jumba la Godfrey Kyomukama, kwa mwendo wa haraka walimuacha Yule mlinzi palepale akiwa hajui la kufanya.

    Kabla hawajaufikia mlango wa jumba hilo, walisikia kelele za ufunguo kutoka ndani, walipoufikia na mlango ulifunguka, nyuma yake kulikuwa na bwana mmoja mtu wa makamo, mwenye umbo la wastani, mrefu, mweusi ti.

    “Bila shaka wewe ndiye bwana Kyomukama,” Kamanda Amata alianza mazungumzo, Kyomukama alijikuta katika hali tofauti maana alimshuhudia Yaumi akiwa bado na bastola mkononi mwake.

    “Ndiyo mimi, nimewakosea nini hata mje kuniua?” Kyomukama aliongea kwa kitetemeshi.

    “Hatujaja kukuua, na sisi si kazi yetu kuua, tafadhali tuingie ndani na tuna dakika kumi tu, za kumaliza kazi yetu na wewe ni msaada mkubwa sana kwetu kwa sasa, kwa ukarimu wako, utajisifu baadae kwa kuwa inawezekana ukawa umeokoa taifa kubwa,” Kamanda Amata alisema hayo huku tayari akiwa amefika sebuleni kabisa mwa jumba hilo la kifahari lenye kila kitu ndani.



    “Sawa niko tayari, mnataka nini?” Kyomukama aliuliza na wakati huohuo mkewe naye akaungana nao, wote wawili hawa walikuwa bado ndani ya pajama za kulalia.

    “Unamjua Kajiba?” Kamanda aliuliza.

    “Ndiyo, ni rafiki yangu sana Yule, lakini sasa nilisikia ameuawa, sikuhudhuria maazishi yake,” Kyomukama akajieleza.

    “Ok, haina haja juu ya maazishi yake, kwanza hayajafanyika, sasa sisi tumetoka Tanzania, mimi ni mtu wa usalama,” Kamanda akatoa kitambulisho chake kilichomtambulisha kama ACP Jaffary akamuonesha.

    Hapo sasa hali ya nyumba ilibadilika, Kyomukama alionekana kuchangamka sasa pamoja na mkewe.

    “Sasa, kabla hajafa, je aliwahi kukutumia mzigo wowote?” kamnda aliuliza.

    “Ndiyo, alinitumia,” Kyomukama akajibu.

    “Mzigo gani na ukoje?” Kamanda aliendelea na maswali yake, wakati huo Yaumi alikuwa akisubiri kwa shauku kujua kama ndiyo mchezo huo utakuwa umeishia hapo au la.

    “Alinitumia briefcase ndogo nyekundu,” akajibu.

    “Ndani ina nini? Unaweza kunambia?” Kamanda aliendelea.

    “Sijui kilichomo maana alipoutuma kwangu akanipigia simu kuwa nisiufungue mpaka muda utakapofika wa kufanya hivyo, name kwa sababu namuheshimu sana rafiki yangu, sikuufungua.” Kyomukama alijibu kwa ufasaha kiasi kwamba Kamanda Amata aliridhika na majibu hayo.



    “Ok, sasa wakati aliokwambia ndio huu, kwa kuwa muda wenyewe haututoshi, hatuwezi kuufungua hapa, ila huo mzigo unatakiwa kurudi Tanzania,” Kamanda Amata alitulia kidogo, akajishika kiuno na kumtazama Kyomukama, “Lete!” akamuamuru. Kyomukama akaenda zake chumbani kwake na kuitoa ile briefcase kwenye sefu la uficho na kuileta pale sebuleni, akaiweka juu ya meza kila mtu alitupia macho briefcase hiyo.

    “Zaina! Angalia kama ndiyo hiyo,” Amata aliamuru. Yaumi akaichuku na kuigeuza mara mbili, “Yap, ndiyo yenyewe,” akajibu.

    Kamanda Amata akanyamaza ghafla, akatzama dirishani, kisha akarudisha macho yake kifuani mwa Kyomukama, akaona kadoti ka mwanga mwekundu kametua katikati ya moyo wa bwana huyo, ‘Hana hatia,’ alijisemea kichwani mwake kana kwamba kuna anayemwambia, “Chini woteeeee!!!” kamnda alipiga ukulele na wakati huo tayri alikwishamsukuma Kyomukama kwa nguvu zote na kumfaya amuangukie mkewe na wote wawili kujibwaga sakafuni, Yaumi bado hakujua nini kinatokea zaidi ya kusiki ule ukulele, kabla hajakaa sawa, alipigwa mtama mmoja maridadi naye bila kikwazo aliirejea sakafu. Yaumi alisikia kitu kama nyuki kimepita jirani kabisa na sikio lake kisha katika sekunde hiyohiyo kufuatiwa na kelele za kioo kinachopasuka na kumwagika chini kama chumvi. Ilikuwa ni risasi iliyolenga kumuua Kyomukama, hakuna aliyejua kwa nini, lakini Kamanda Amata alifanya kazi ya ziada kuokoa maisha ya bwana huyo. Bado wakiwa sakafuni, Kamanda Amata alitoa ishara ya kuwa wamfuate, akawa anatambaa kuuelekea mlango mkubwa kisha akawaacha wakiwa wamejificha nyuma ya kochi kubwa.

    Akatumi dakika chache kuangalia usalama ikiwemo na kumsaka huyo aliyefyatua risasi hiyo, kutokana na wingi wa maua katika ile bustani haikuwa rahisi kumuona, kumbe hakujua kwamba mdunguaji huyo hakuwa ndani ya wigo bali kwenye mti mmoja uliokuwa nje ya wigo na aliweza kuona vizuri japo hakujua nani ni nani na kutumia bunduki hiyo kubwa kutaka kuleta maafa.

    Kamanda Amata akarudi ndani, akamwambia Yaumi afungue ili kuona kuna nini ndani ya briefcase hiyo kwa maana wangeweza kuondoka kumbe wanachokitaka hakimo humo.

    Lilikuwa kabrasha kubwa, lenye karatasi takribani kumi zilizobanwa vizuri na kufungwa kwa utepe wa dhahabu, chini kabisa ya karatasi zile kulikuwa na karatasi nyingine moja iliyoandikwa kwa mkono, akaitoa na kumpa Kamanda,



    “…Siri hii ni kubwa na ni nzito sana, najua kuwa wenye nayo wanahaha kuitafuta, na ili waipate wanatumia kila mbinu kunibana. Sipo tayari kuwapa, ni heri nife niliokoe taifa langu, wapo tayari kuniua, name niko tayari kufa, siri hii nimeigawanya mimi mwenyewe katika vipande viwili, hiki ni kipande cha kwanza na cha pili kinapatikana kwa namba 0013205…”



    baada ya barua hiyo ndefu mwishoni iliandika urithi wa mali zote za Kajiba. Kamanda Amata akatulia kimya, akaikunja ile karatasi kama ilivyokuwa awali, akairudisha palepale ilipokuwa na kuifunga ile briefcase bila kusoma zile nyaraka nyingine, akamgeukia Kyomukama.

    “Mr Kyomukama, mzigo tumeupata lakini haujakamilika, na Kajiba kasema kuwa sehemu nyingine ya mzigo huu inapatikana katika namba hii,” Kamanda Amata akamuonesha Kyomukama ile namba katika simu yake kwa maana aligundua kuwa ni hiyo aliyoipata katika hifadi ya Kajiba kule nyumbani kwake na hapa kaikuta tena.

    Godfrey Kyomukama, aliitazama kwa makini namba hiyo na kuonesha mshtuko kidogo, kwa mtu wa kawaida asingeweza kuuona mshtuko huo lakini si kwa Kamanda Amata, Kyomukama akamgeukia Amata, “Ndiyo hii ni namba ya gari langu,” akamwambia Kamanda Amata. Amata akasukuti akakosa jibu la kupambanua namba ya gari inahusu nini katika sakata hilo, akamtazama tena Kyomukama, akaona labda anamchezea.

    “Unasema hii ni namba ya gari lako?”

    “Ndiyo,”

    “Liko wapi?” akauliza

    “Hili gari bwana mkubwa lilipata ajali mwezi mmoja uliopita na limeungua moto lote,” Kyomukama akajibu. Kamanda Amata akaishiwa pozi, akatulia kimya, akajitupa kochini, “Naomba maji ya kunywa!” Kamanda akatoa ombi kwa mke wa Kyomukama.



    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    GABRIEL Matinya aligutushwa na kelele za jogoo lililowika mita kadhaa toka kwenye dirisha lake, lilimkatisha usingizi mtamu wa alfajiri uliomchukua punde tu baada ya kumaliza kazi nzito aliyopewa na Marina usiku huo, ndipo alipogundua kuwa bado alikuwa kiunoni mwa mwanadada huyo machachari, motto wa Kitanga. Aliitazama saa yake hakuamini kama ni alfajiri, mpaka hapo hakuwa amepata taarufa yoyote toka kwa Fasendy, alitamani jua lisichomoze lakini huwezo huo hakuwa nao.



    Kama kuna kitu kilikuwa kinamuumiza kichwa sasa kilikuwa ni juu ACP Jaffary, kwa kuwa alijua katika jeshi lake la polisi hakuna mtu huyo, sasa alijaribu kuumiza kichwa kujua ni nani, na wasiwasi mkubwa ulikuwa ni je inakuwaje kama amegundua mpango wao huo.

    Hakuna kingine cha kufanyiwa uamuzi ndani ya kichwa cha Matinya, kila upande aliona umebana, akaamua kujipa masaa kumi na mbili tu kama swala lao likishindikana basi ni kutoroka nchini. Siku hiyo alipanga kuiweka tayari hati yake ya kusafiria na kabrasha nyingine muhimu, alijua akitoka hapo ni moja kwa moja kuelekea Dubai maana huko tayari alikuwa akimiliki jumba la kifahari, lakini alisikitika sana kwa kuwa alijua wazi kuwa lazima amuache Marina, nah ii ilitokana na uzembe kuwa siku zote hakuwahi kumuuliza kama ana hati ya kusafiria, ‘nitamsaidiaje?’ alijiuliza huku akishikashika kiuno cha binti huyo ambaye alikuwa ndani ya usingizi mzito. Mara simu yake ikaita, alipoangalia kiooni ikaonekana No 02, akaiweka sikioni, simu ilikuwa ikimuhitaji kwa kikao cha haraka asubuhi ya siku hiyo. Matinya aliahidi kufika, akavuta moja ya vijitabu vyake vya kumbukumbu akanyofoa karatasi moja na kuandika mambo Fulani, kisha akatia kwenye bahasha na kufunga. Akamuamsha Marina na kumkabidi ile bahasha akimwambia kuwa aamkapo tu aifikishe panapohusika.

    Akanyanyuka tayari kuelekea maliwato lakini Marina akamvuta na kumrudisha kitandani.

    “Beibi wapi jamani bado nakuhitaji,” Marina alilalama kwa sauti ya kichovu.



    “Nna kikao asubuhi hii ngoja niwahi,” Matinya alijibu.

    “Hapana subiri, nipe japo kimoja tu ndio uende jamani,” Marina alijigeuzageuza kitandani katika mtindo ambao Matinya alijikuta anaishiwa nguvu, sehemu za chini zikarudiwa na uhai na kusimama kama mlingoti wa bendera ya chama, akajikuta akikirudia kitanda, kabla hajafika Marina aliifungua miguu yake na kumkaribisha kwa mikono miwili, hakuna linguine zaidi ya wawili hao kuvunja amri ya sita. Marina alikuwa mjanja, alizivuna vyema pesa za Matinya kwa kumpa mapenzi ya kiujana mpaka Matinya akafukuza mkewe ili afaidi penzi hilo, kila alichotaka akapata kwa mwanamke huyo hivyo na wewe hakuwa na budi kurudisha fadhila, nyumba akamjengea, gari akamnunulia, nini kingine. Kila aliposema moyoni nitamuacha kesho, kesho haikufika, kama unavyojua ukionja asali utachonga mzinga, ndivyo ilikuwa kwa Matinya. Kila wakati alikuwa akiitazama simu labda Fasendy atapiga kumpa ripoti lakini haikuwa hivyo, wasiwasi ukamzidi, moyoni akaona hakuna linguine jioni ya siku hiyo lazima aiache nchi, nchi anayoipenda eti, yenye unono wa asali na maziwa, lakini nafsi ilimsuta kuwa kaitendea mabaya, alijuwa wazi kadhia hiyo ikifika mikononi mwa serikali haku linguine bali ni kitanzi, ijapokuwa serikali yetu haitekelezi adhabu hii, lakini kitanzi kilimfika Yaumi kwa hila zao, sasa yaumi hajulikani alipo. Matinya aliona hapo hakuna kingine ila kama itabidi lazima atakula kitanzi na kitanzi hizo si ajabu kikawa kitanzi cha mwisho.

    “We vipi leo!?” ilikuwa ni sauti kali kidogo ya Marina aliyekuwa chini ya tumbo kubwa la Matinya akijishughulisha katika kitanda kilichokuwa kikishangilia mchezo huo, alipiga kelele hizo baada ya kuhisi ghafla kuwa ile kitu imechomoka kumbe sio tu kuchomoka bali imenywea na kuwa kama ya motto, chezea msongo wa mawazo wewe!



    §§§§§



    KAMANDA Amata bado alikuwa hajaelewe kinachosemwa hapo, akamtazama tena Kyomukama.

    “Unasema ni namba ya gari, na gari lilipata ajali tena likawaka moto, ok, hata kama liliwaka moto mabaki yake yako wapi?” Kamanda akauliza.

    “Mabaki yake yapo Kabale ambako ndipo lilipopata ajali baada ya kugongana na lori la mafuta,” Kyomukama akajibu.

    “Sawa sasa hatuna budi kufika Kabale kwa njia yoyote ile,” Kamanda alieleza.

    “Mkuu, kutoka hapa kwa gari ni takribani masaa nane maana pana umbali wa kilomita 337, labdakama tutumie ndege ya kukodi, mimi niko tayari kulipia,” Kyomukama akajitolea, wazo likaafikiwa. Kamanda Amata akaona wazi kuwa muda aliopanga kumaliza kazi hiyo umeshaongezeka, kama atasafiri kutoka hapo kwenda Kabale na kurudi basi inabidi kuongeza masaa mengine kadhaa, hakuwa na budi.

    “Haya Mr Kyomukama, fanya unaloweza tuondoke mara moja, ikiwezekana kabla ya saa nne tuwe tumemaliza kazi,” Kamanda akasema. Bwana Kyomukama akainua simu yake ya mezani na kupiga simu katika mashirika ya kukodi, Mungu si Athumani akapata ndege moja ya watu wane, hivyo wakajiandaa harakaharaka kuondoka. Kamanda Amata akachukua ile briefcase na kuiweka vizuri. Wote watatu isipokuwa mke wa Kyomukama wakatoka nje ya jumba hilo.

    “Samahani, naomba nimuone mkeo mara moja kabla hatujaondoka,” akaomba Kamanda, akarudi ndani na kuwaacha Yaumi na Kyomukama pale nje, sekunde hamsini tu akaungana nao na wote wakaingia katika gari nyingine ya bwana Kyomukama na kutoke geti la upande wa pili na kutokomea zao.



    Uwanja wa ndege wa Kampala ulikuwa umetulia alfajiri hiyo, ni wasafiri wachache walionekana kutoka na kuingia, ilionekana wazi kuwa siku hiyo haikuwa siku ya safari kubwa. Kyomukama aliingiza gari sehemu maalumu na kuiegesha vizuri, kisha wote wakashuka na kuifunga gari hiyo vizuri. Wakati wakielekea mahali ambapo wao wangepata usafiri huo wa chatter Kamanda Amata aliiona tena ile gari ya kampuni ya ulinzi ikiwa imeegeshwa sehemu na ndani hakukuwa na mtu, nywele zikamsimama akajua kwa vyovyote hapo uwanja wa ndege lazima patokee tatizo.

    “Naomba kila mtu awe makini kwa usalama wake,” Kamanda alitoa rai kwa Kyomukama na Yaumi.

    Walipokamilisha itifaki zote, wakaelekea kwenye ndege ndogo iliyokuwa tayari kwa safari hiyo fupi ya kwenda na kurudi, kila mtu akaketi na kufunga mkanda, hakuna lolote lililotokea mpaka ile ndege ilipoacha ardhi. Wote walikuwa kimya hakuna aliyeongea na mwenzake.



    Dakika arobaini baadae walikuwa tayari katika eneo wanalolihitaji, walitua katika kiwanja cha ndege cha kienyeji tu, wakateremka na kukodi tax kuelekea eneo ambalo gari ya Kyomukama ilipata ajali. Hauku mwendo mrefu walifika eneo la tukio, wakiwa wanashuka pale pikipiki moja iliwapita kwa kasi ikiwa na watu wawili juu yake, Kamanda Amata akawa na wasiwasi kidogo hasa alipomuona Yule mtu wa nyuma amebeba briefcase ndogo nyekundu, akatazama na kisha akatulia lakini akili yake haikuwa ikifanya kazi sawasawa. Wakateremka bondeni mpaka walipofikia yale mabaki ya lile gari.

    “Kumbe lilikuwa basi?” aliuliza Kamanda huku akilizungukazunguka lile bodi bovu chakavu lililokuwa limemeguliwa huku au kule na vijana wanaotafuta pesa kwa kuuza vyuma au mabati chakavu.

    “Vipi?” Yaumi aliuliza.

    “Hainipi maana!” Kamanda alijibu.

    “Hii basi nilikuwa naipenda sana, kwa maana hata bodi yake nilitengeneza Tanzania, na Kajiba ndiye aliyesimamia kazi nzima pale Quality Group,” Kyomukama aliwaeleza Kamanda na Yaumi.

    Ilimchukua dakika kumi na tano Kamanda kulizunguka lile basi chakavu kuchunguza hiki na kile, hakuna cha maana alichoona, akaamua kutoka ila basi alichokipata ndicho akifanyie kazi.



    Kijua mwanana kilipendezesha miti iliyokuwa mahali hapo, sauti za ndege nazo zilifanya muziki mtamu. Alipokuwa anaeuka kuondoka ndipo alipoona kitu ambacho kilimpa hisia tofauti, kadiri ya watu jinsi walivyong’oa mabati ya gari hilo, kuna kitu kilibaki upande wa juu ambako kulikuwa ni keria ya kuwekea mizigo kwa ndani, kilikuwa kama kisanduku cha chuma lakini kilichochomewa barabara, Kamanda Amata akakitazama na kurudi kukiangalia, hakifunguki kilikuwa kimechomewa madhubuti kabisa, ili ukitoe pale kilipo ni lazima ukate kwa moto wa gesi, akapatilia mashaka, akamwita Kyomukama na yaumi nao wakatazama kweli kila mtu alihisi kitu. Muda huohuo ukafanyika mpando na kupatikana gesi kwa ajili ya kukatia eneo lile, vijana wakafanya hivyo na kufanikiwa kuondoa kwa usalama kile kijisanduku.

    Kamanda Amata akawaelekeza wale jamaa kukata kwa uangalifu sana, wakafanikiwa na ndani yake wakatoa briefcase nyingine ndogo nayo ni nyekundu kama ile ya kwanza, Kyomukama na yaumi wakabaki kupigwa na mshangao. Kamanda Amata akaigeuzageuza ile briefcase na kumpelekea yaumi aifungue, namba alizojaribu ndizo zikafungua, haiku na tofauti ndani, kulikuwa na kabrasha moja lenye karatasi kama theletini hivi zilitofungwa kwa bahasa ya khaki lakini ikiwa wazi upande wa juu.



    “Kazi imekwisha, tuondokeni,” Kamanda akawaamuru na safari ikaanza kuelekea kule walikoiacha ile ndege, wakiwa njiani ile pikipiki ikawapita tena na watu walewale lakini mara hii hawakuwa na ile briefcase Kamanda akacheka kimoyomoyo.

    Ilikuwa tayari saa mbili kasorobo asubuhi walipofika kwenye ndege yao na kuikuta kama walivyoiacha, wakamlipa detreva tax na kisha wakaiendea ile ndege, kilichoawashangaza hakukuwa na rubani. Kamanda akasimama na kuwazuia Yaumi na Kyomukama, hali ilikuwa siyo yenyewe, mtu mmoja aliyekuwa kwenye uwanja huo pale ofisini alipokwenda kumwangalia alimkuta kalali meza yake, alipomgeuza damu, risasi ilishafanya yake. Kyomukama aliyekuwa jirani na Kamanda Amata alishuhudia jeraha kubwa kifuani mwa Yule mtu, ilikuwa hali ya kuogofya sana. Kamanda Amata bastola mkononi, akafuangua mlango wa pili na kutokea kwa nje, la haula, maiti nyingine ya askari mgambo ilikuwa imekalishwa kwenye benchi ikiwa imeegemea bunduki yake. Kamanda Amata akatazama hali ile akajua walikuwa wakifuatiliwa...



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Damu ilikuwa ikimchemka Kamanda akazunguka na kutokea upande wa pili wa jengo lile, hakukuwa na mtu, akarudisha silaha yake na kuamua kurudi kule kwenye ndege alikomuacha Yaumi. Kyomukama alikuwa katangulia mbele akifuatiwa na Kamanda Amata nyuma yake, walipotokeza tu upande ule, yowe la uchungu lilimtoka Kyomukama, damu ikawa inamtoka begani, ilikuwa ni risasi iliyokata nyama ya bega, Kamanda Amata akaitwaa tena bastola yake akatazama huku na huko akamuona kityu kama kivuli kikitoka sehemu moja kwenda nyingine, akajibana nyuma ya nguzo moja akifikiria jinsi ya kumkabili kiumbe huyo.



    Hakuweza kumsaidia Kyomukama kwa maana alijua kwa kufanya hivyo atakuwa amejiweka peupe, akatoka nguzo moja kwenda nyingine, akafika kwenya ukuta uliokuwa na korido katikati, akajiweka tayari kwa shambulizi la ghafla, akajitokeza na kugeuka kushoto, ndani ya sekunde chache alimuona kiumbe huyo, risasi ya kwanza ilifumua kioo cha dirisha, ya pili ikapiga kwenye mlango, ya tatu ikamparuza kiumbe huyo, akadondosha bunduki yake kubwa huku akitoa mguno wa maumivu. Kamanda Amata hakujali hiyo bunduki, alishajua kuwa sasa kiumbe huyo hana silaha, alikimbiloia upande ule na alipokunja kona tu, kipigo kikali kikamshukia, Kamanda Amata alijilaumu kwa hilo kwa kuwa alikuwa kaingi bila tahadhari. Alijibwaga chini na kujibiringisha huku bastola yake ikimtoka mkononi, alijiinua na kusimama wima, mikono yake ililikinga teke kali na la nguvu kutoka kwa kiumbe huyo, Fasendy.



    Kamanda Amata aliyumba kidogo na kujizungusha akiwa goti moja chini, ngwala maridadi ilimshusha Fasendy kuja chini kabla hajafika kwa kasi ya ajabu Kamanda Ama tayari alijigeuza na kupiga teke kwa nguvu zake zote likatua mgongoni mwa Fasendy wakati akielekea chini, kutokana na nguvu ya teke lile, Fasendy aliinuliwa na kubamizwa ukutani, aligeuka na kumkabila Kamanda kwa mara nyingine, akiwa ameikinga mikono yake katika mtindo wa Lerdrit, Kamanda Amata aliuona mtindo huo, mtindo unaotumiwa sana na makomandoo wa jeshi la Thailand, ni mtindo ambao mpigaji anakushambulia kwa muda mfupi bila onyo na kuutoa uhai wako kwa mapigo machache tu, Kamanda Amata aliona kazi kubwa inayomkabili kupambana na mwanamke huyo, Fasendy, bado alikuwa amejificha uso wake kwa ile ninja aliyoivaa. Kwa kasi ya ajabu, Fasendy aliizungusha mikono yake na kumpelekea shambulizi kali Kamanda Amata, lakini alijikuta anagonga ukuta baada ya kuuona umahiri mkubwa wa Kamanda katika kutumia mtindo wa kichina dhidi ya ule wa Kithai Kusangi-ryuu Kobujustu. Fasendy alijikuta akianguka kama mzigo baada ya kichapo kikali cha dharula kilichompata kutoka kwa Kamanda Amata, sasa hapakuwa na mchezo wala utani. Kamanda Amata alimuendea Fasendy pale chini kabla hajaamka, teke la miguu miwili lilitu kifuani mwa Amata, akaruka samasoti na kusimama wima kabla ya kulikwepa teke kali la Fasendy lililorukwa kiufundi sana. Kamanda Amata akajua hapa anapambana na mjuzi, mjuzi wa mapigano ya mikono mwenye uwezo wa kutumia kila aina ya mchezo.

    “Kamandaaaaa!” ilikuwa sauti ya Yaumi aliyekuwa akiingia eneo lile huku akikimbia na alipofika pale alisimama ghafla baada ya kukuta mchezo ule uliokuwa katikati, hakuelewa nani anampiga nani au nani anapigana na nani.



    Kamanda Amata sasa alikuwa hatamaniki kwa jinsi alivyochafuka vumbi na damu za hapa na pale. Fasendy akiwa chini anagalagala naye hatamaniki, kutoka pale chini Fasendy alisikia kelele ya ule wito, akaamka akatoa ile ninja yake na kubaki kichwa wazi.

    ‘Mwanamke mwenye upara!’ alijisemea Kamanda huku akijiweka sawa. Fasendy alijitoa mzimamzima na kupeleka mapigo kadhaa kwa Amata ambayo yalikingwa kwa ufundi, alipojikuta anishiwa na kupoteza nukta tu konde zito la Kamanda lilitua kwenye shavu la Fasendy, likampepesua, konde linguine likamuweka sawa na la tatu likampeleka chini akiwa hoi, Kamanda Amata akamkanyaga kwa guu lake mgongoni na kusikia yowe hafifu kutoka kwa mwanamke huyo.

    “Kamandaaaaaaaa!” ilikuwa sauti ya Yaumi kwa mara nyingine, “Noooo! Kamanda”

    Kwa wito ule Kamanda alimuacha fasendy akiwa hoi. Yaumi alikimbiulia pale alipolala Fasendy.

    “Fasendy !!!!!” aliita kwa nguvu kabla hajamfikia, Fasendy aliinu uso wake kwa tabu kumtazama mtu huyo, Kamanda Amata alishtuka kusikia jina hilo akasogea pale naye kwa kasi kumwangali mwnamke huyo.

    §§§§§



    Dar es salaam

    Saa 2:29 asubuhi



    MADAM S na Chiba walikuwa katika ofisi yao ya siri huko Mbwamaji, upande wa pili wa mji ng’ambo ya bahari ya Hindi, walikuwa wakijadiliana hili na lile juu ya kifo cha Jaji Ramson. Walikuwa wakijaribu kuunganisha matukio haya ya mauji yaliyotokea katika mtindo wa kufanana, walipokutanisha hundi zote ambazo muuaji wa kwanza alifanyiwa malipo, na ile ambayo Chiba aliikuta katika kabrasha za Jaji Ramson zilishahabiana kila kitu, tayari walishajua hundi hizo ni kitabu cha nani katika benki gani, kilichowaacha hoi ni kuwa anayemiliki kitabu hicho ni mtu mkubwa tu serikali, lakini iweje alipie mauaji ya namna hiyo? Lilikuwa ni swali gumu sana kwao, jibu lilikuwa ni kusubiri tafutishi za Kamanda Amata ili kujua kipi ni kipi na wapi waanzie. Mpaka dakika hiyo hawakuwa na taarifa yoyote kutoka kwa Amata, iliwatia hofu sana, lakini kilichowapa moyo ni kuwa Kamanda Amata bado alikuwa akionekana kwenye mitambo yao ya GPS inayoongozwa kwa satellite, kilichowashangaza ni kuwa usiku alionekana Kampala na asubuhi kadiri ya taarifa zinazotumwa kila wakati na mfumo huo alionekana yuko nje ya Kampala Kilomita 337, walijaribu mawasiliano lakini hawakupata kirahisi.

    “Usihofu, jamaa yuko vizuri naamini atafanikisha, ila inaonekana kazi ni ngumu kuliko tulivyotegemea, nafikiri tyuendelee kumtafuta kwa utaratibu wetu,” Chiba alimwambia Madam S kumtoa hofu. Madam S alitikisa kichwa kuashiria kaelewa, akaendelea kupata kahawa aliyokuwa akijinywea tangu mwanzo.

    “Chiba, cheki vijana wanasemaje katika ufuatiliaji wao,” Madam S alimuomba Chiba, kwa maana jana yake walikuwa wamewaweka chini ya uangalizi watu wawili, IGP Gabriel Matinya na meneja wa idara ya Ushuru na Forodha bwana Gomegwa. Chiba akafanya utyaratibu huo na baada ya dakika chache alipata majibu, akaambiwa kuwa IGP Matinya muda huo ameonekana katika hotel ya New Afrika na tangu ameingia humo ndani ni tayari dakika thelethini zimepita bado hajatoka alkadhalika bwana Gomegwa alikuwa ofisini kwake akiendelea na majukumu mengine. Madam S aliridhishwa na taarifa hizo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande wa pili wa Jiji la Dar es salaam …



    “Leo hii inabidi kontena lile liondoke ili program yetu iende tulivyotaka; mipango yote ipo sawa kwa upande wangu ila bado sijasikia kuhusu wewe mambo yanaendaje katika idara yako ya usalama?” ilikuwa sauti nzito ya huyo anayeitwa namba 02 katika mtandao wao. Matinya alitulia kidogo kama anayetafakari jambo kisha akamgeukia Yule bwana.

    “Sikia bwana mkubwa, upande wa usalama kuna mambo mengi kidogo, lakini kama tulivyojipanga na kuona pamoja mara ya mwisho kuwa kila anayeonekana kujua lolote juu ya hili tunamfuta duniani, tumefanikiwa kumuondoa jana Jaji Ramson, sasa nikishamaliza kusaini zile kabrasha pale bandarini tutammaliza bwana Gomegwa mchana wa leo, vijana wapo tayari na wanafanya kazi nzuri, lakini kuna tatizo moja kubwa sana hapa huu mpango umefika mikononi mwa idara ya usalama wa Taifa,” Matinya aliposema hayo aliona dhahiri mshtuko alioupata huyo namba 02 wao.

    “Unasema idara ya usalama wa Taifa wameshaijua hii kitu?!” Yule namba mbili akauliza.



    “Ndiyo, wameijua na wao sasa wako hjimahima kutafuta hizo kabrasha zilizopotea na hivi sasa wako Kampala, Uganda,” Matinya alieleza.

    “Tumekwisha!” Yule jamaa aliongeza kauli ya masikitiko, akainama chini kama anayeomboleza kifo cha shangazi yake kisha akamgeukia Matinya, “Sasa umechukua hatua gani? Maana katika hili sote tunakutazama wewe!” akaongeza tena kusema.

    “Ni kweli, mi nimejipanga kila idara, na tunavyoongea binti yetu aliyefanya kazi ya kumuondoa Jaji Ramson sasa yupo Kampala kummaliza huyo aliyetumwa na serikali na ikiwezekana azipate hizo kabrasha,” Matinya akaeleza.

    “Ok, hapo nimekuelewa bila shaka, naamini atafanya kitu Yule binti ni profesheno katika kuua iwe kwa mikono au kwa silaha kadiri ya maelezo ya mdau wetu kutoka Uarabuni,” yule bwana alipokwishakusema hayo akajikohoza kidogo kuweka sawa koromeo lake, kisha akaendelea; “Sasa mi naona fanya mpango wa lile kontena kutoka ili lianze safari leo hii kabla ya saa tano, mi nasubiri taarifa zako,” akamaliza. Wakaagana na Matinya kisha kila mtu akajua lake la kufanya.



    §§§§§



    Simu ya bwana Gomegwa iliita, kwanza akaitazama kisha akakenua meno yake kuonesha fuaraha inayokuja ghafla moyoni, ‘Kesho tu naagiza bati Afrika ya Kusini za kumalizia nyumba yangu kule Boko, kisha nimnunulie mama watoto Vitz ya kuende sokoni maana kila siku tunagombania gari moja, aisee Mungu anipe nini, labda kidonda,’ akainyakua ile simu na kuitega sikioni.

    “Mpango wangu wa kazi umefikia wapi, nahitaji kutoa mzigo,” sauti ya upande wa pili ikasema.

    “Hamna shaka ni saini mbili tu mheshimiwa kisha ulete lori kubeba mambo mengine nimeshakamilisha, ila bwana kumbuka ahadi yetu, mkono kwa …..” kabla hajamaliza ile sauti ikamalizia “…Mkono” ile simu ikakatika.



    Dakika tano tu baadae kijana mmoja alifika ofisini mwa Gomegwa na kukabidhiwa lile kabrasha akatoka nalo kuelekea kwenye gari moja aina ya Vox lenye vioo vya giza, ndani yake kulikuwapo na bwana Matinya, akasaini zile karatasi kisha akaambatanisha na hundi ya milioni ishirini, akamrudishia Yule kijana naye akairudisha kwa bwana Gomegwa.

    “Ok sasa leteni Lori lipakie huo mzigo, kule tayari limetoka sasa kuna kijana atawapeleka bandari kavu ili mkalibebe,” akatoa maelekezo huku akitabasamu. Siku hiyo bwana Gomegwa hakuwa na hamu ya kufanya kazi kwani alitamanai kila kitu akimalize siku hiyohiyo kwa ile pesa aliyopewa kwa njia ya hundi hivyo alikuwa akijipanga kutoka ofisini na kuelekea benki ambako angehamishia pesa hizo katika akaunti yake, ‘Milioni ishirini, za cheeee, kazi ya kusaini tu, aaah wacha masikini wafe masikini tu, sie tunapeta ili heshima ije,’ alijisemea moyoni huku akijiweka tai yake vizuri kana kwamba kuna baridi lakini kumbe joto la Dar lilikuwa ni lile lile tu.



    Kila kitu kilikamilika, kontena la akina Matinya tayari lilikuwa juu ya semi tela tayari kwa safari na gari ya kusindikiza iliwekwa tayari na vijana wawili. Matinya akiwa ndani ya ile Vox alikuwa akifurahi sana kuona lori hilo likitoka taratibu kwenye geti mojwapo huko Kurasini na kuingia barabara ya Mandela bila tatizo, kazi imekwisha!



    §§§§§



    “Matinya yuko maeneo ya bandarini ijapokuwa hajashuka kwenye gari, inaonekana kuna fomu au kabrasha anazosaini, bado tunafuatilia nyendo zake,” ilikuwa ni taarifa iliyomfikia Chiba akiwa bado na Madam S naye akaifikisha kwa Madam S kama ilivyo.

    “Hapa kuna jambo Chiba, na nakwambia kweli lazima leo hii kieleweke, leo jua halitui ikibidi basi mtanishika mikono huku na huku kama Waisrael walavyofanya kwa Haruni ili jua lisimame na vita iendelee,” Madam S alisema huku akigongagonga meza yake.

    “Twende mjini hukohuko, maana hapa tuko mbali sana, tatizo ni uhakika tu na wanachokifanya tukishakijua tu hakuna cha wewe nani wala wewe nani,” Madam S aliendelea kulalama huku akiweka bastola zake vizuri kabla ya kuvaa kikoti chake cha suti ambacho huzuia hivyo vyote visionekane.



    Rejea Kabale – Uganda



    “Fasendy ! ni wewe? Siamini macho yangu,” Yaumi alizungumza huku akilia, “Kwa nini Fasendy, kwa nini, ina maana na wewe umeshiriki kumuua mume wangu Fasendy?”

    Fasendy aliinama chini akiwa bado amelala hajiwezi kwa kipigo alichokipata kutoka kwa Kamanda Amata, akainua uso wake uliojaa machozi, akamtazama Yaumi bila kumjua, “Wewe ni nani mpaka unajua jina langu?” Fasendy akauliza. Na muda huohuo Kamanda Amata alifika eneo lile, pale alipolala Fasendy, akamtazama usoni na kutikisa kichwa, naye akaita kwa upole “Fasendy!” ndipo walipokutana uso kwa uso na Kamanda na kila mmoja kumtyambua mwenzake.

    “Umeniuzi, umeniuzi sana!” Kamanda Amata akang’aka na kuiendea bastola yake, akaichukua na kuiweka sawa, ilikuwa na risasi moja tu chembani.

    “Lazima nikuue siwezi kukuacha hai Fasendy,” Kamanda Amata akazungumza kwa sauti.

    “Yaumi, nenda kwa Kyomukama haraka, huyu niachie nimmalize,” Kamanda Amata akakalipa kwa hasira, akamwekea Fasendy bastola kichwani huku akiwa kapiga magoti pale alipolala Fasendy.

    “Niambie nani unayemfanyia kazi?” akamuuliza, Fasendy akabaki kimya hakujibu, “Jeuri siyo? Mi sina haja ya majibu yako kama hutaki kunipa, nakuua,” sekunde hiyohiyo mlio wa kilinda usalama cha bastola ukasikika, Fasendy akaanza kutetemeka kwa hofu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nikueleze wewe kama nani? Kama umemsaidia dada yako mpaka hapa basi una heri maana angeshanyongwa, sijapata kuona kaka anayediriki kuweka maisha yake rehani hasa kwa kumuwekea bastola kichwani mtu mbaya kuliko shetanikichwani mwake sasa,” Fasendy aliongea bila kuogopa. Kamanda Amata aliuma meno, akamgonga na mtutu wa bastola, Fasendy akatulia kimya.

    “Kwa taarifa yako, mimi si kaka wa Yaumi, mimi ni Kamanda Amata kutoka idara nyeti ya uslama wa Taifa, TSA,” kamanda alijitambulisha, kwa jibu hilo Fasendy alipata nguvu ghafla na kunyayuka wima akiwa bado katazamana na domo la bastola, hakuamini anachokisikia, hakuamini anayemuona, kama yeye ni shetani basi hapo alikutana na Malaika mkuu.

    “Sikia Kamanda, si mimi bali ni watu wenu wa juu, wenye uroho wa madaraka ndiyo wanaofanya haya, mimi ni mfanyakazi kama wewe tu, sina linguine, siwezi kukujibu maswali yako ila maadam umepata yale makabrasha na mi nilitumwa niyachukue kwako na nikuue, sasa nakuachia, nenda kayasome utapata siri yote ya jambo hili, kabla hujaniua naomba nimuone shoga yangu kipenzi Yaumi, anayepiagania haki na maisha ya mumewe, ni mwanamke jasiri, shujaa kuliko hata mimi,” Yaumi aliongea huku akitoa machozi ya uchungu, ‘Sijawahi kuona Komandoo akilia’ Kamanda akajisemea, akamkumbuka Fasendy siku walipokutana nyumbani kwake, alivyomkirimia kwa kila jambo, akashuha bastola yake na kuiweka mahali pake, akamwita Yaumi.

    Yaumi akafika mara moja huku nyuma yake akifuatiwa na Kyomukama aliyekuwa amefungwa kitambaa begani.

    Fasendi akawatazama wote watatu kisha akamtazama Yaumi aliyekuwa akilia.



    “Yaumi, mimi sikumuua mumeo wala sikushiriki, nilikuja Tanzania kwa kazi nyingine na ndipo nilipopata taarifa ya kupotea kwa hizi kabrasha zetu, lakini baadae walipoanza kuzitafuta mimi sikuwa katika mpango huo, nilikuwa nasubiri kazi yangu ambayo kesho inaanza huko, mkoa wa Pwani. Tulikutana Yaumi pale Segerea tukawa mashoga nikakupa msaada wangu mwingi mpaka ukafika kujua kuwa kabrasha hizo ziko huku lakini mimi mpaka nakufumbulia ile namba sikuwa najua unatafuta nini wala sikujua kuwa mauaji ya mumeo yanaendana na kazi yetu. Pole Yaumi, leo tumekutana katika mazingira mabaya kabisa ambayo kamwe sikupenda uyashuhudie. Yaumi, wewe ni mwanamke shujaa sana, jasiri na hodari, mwnamke anayejua kumtetea mumewe, nikimaliza kuzungumza haya, Kamanda Amata mtu ambaye nimemsikia tu na sikuwahi kumuona mpaka leo hii ataniua, ila kama ningekkuwa hai ningekusaidia kumuua Yule aliyemuua mumeo kwani ninamjua na ningemuua mbela ya macho yako, kwa heri Yaumi.” Fasendy alimaliza kuzungumza na kila mtu alikuwa kimya wakati huo. Mara kutoka mbali vilisikika ving’ora vya gari za polisi zikija eneo hilo. Kamanda alitazama huku na kule.

    “Yaumi, Kyomukama, ondokeni haraka mkaingie kwenye ndege kabla polisi hawajafika, haraka!” aliposema hayo Kamanda akawaamuru kuondoka, yaumi akampa mkono Fasendy kisha akatokomea kwenye ndege.



    Kyomukama na Fasendy waliingia ndegeni, lo, wakamkuta rubani akiwa kalala kwenye kiti cha abiria akiwa hana uhai, damu ikiwa huku na kule, hali hiyo Yaumi hakuipenda akabaki kachanganyikiwa hana la kufanya.



    Mara akasikia mlio wa risasi kutoka kule alikomuacha Fasendy na Kamanda Amata, Yaumi akainama kichwa akasikitika kwa kifo cha Fasendy, mara akamuona Kamanda Amata akija akikimbia kuelekea ile ndege naye akaingia na kuufunga mlango, alipotazama akamuona Kyomukama kiwa kamuinamia Yule rubani. “Vipi amekufa?” akauliza.

    “Hapana ila anapimua kwa tabu,” Kyomukama akajibu.

    Kamanda Amata hakuona haja ya kuchelewa hakutaka polisi wawafikie, akakaa kwenye kiti cha rubani, ‘nilijifunza zamani sijui kama leo nitaweza,



    IJAPOKUWA alionekana kuwa na wasiwasi lakini hakusahau mafunzo aliyoyapata huko Russia jinsi ya kurusha vijindege kama hivi, alipohakikisha ameketi salama kitini na kumuomba Kyomukama na yaumi nao kuketi sawia wakiwa na mikanda tayari kwa safari, Kamanda Amata alianza kutomasa nobu moja baada ya nyingine, injini haikusita kuanza kazi yake, alipohakikisha imekaa sawa akafyatua mahala pengine na ile chatter taratibu ikaanza kuondoka eneo lile kuelekea kwenye njia ya kuruka au kutua.

    “Kyomukama, mpigie simu mkea mwambie aje uwanja wa ndege na mzigo wangu,” Kamanda Amata alimwambia Kyomukama huku akiwa anaiweka tayari ndege kwa mwendo wa kuruka.



    Polisi walikuwa tayari wamekwishafika eneo hilo na waliishuhudia ndege hiyo ikivuta kasi kwenda kuruka, walijitahidi kuizuia lakini walichelewa kwani walipofika kwenye barabara ya kurukia ndege tayari Kamanda Amata alishainyanyua umbalikama wa futi mia moja kutoka usawa wabahari, wakaishia kuitazama ikipotelea angani.

    Baada ya kuiweka sawa akafyatua mkanda wake na kumgeukia yaumi na Kyomukama.

    “Vipi ameamka?” aliuliza baada ya kumuaona Rubani Yule mwenye jeraha katika mkono wake akiwa ameketi huku kajiegemeza pembeni mwa kiti.

    “Ndio naona ameamka,” yaumi alijibu.

    “Mlete akae hapa kitini ana majukumu ya kufanya,” wakafanya hivyo kadiri ya maelekezo ya Kamanda Amata, Yule rubani akaketishwa na kufungwa mikanda, kwa nguvu ndogo alizonazo akbonyeza hapa na pale na hali ya hewa ndani ya ndege ile ikabadilika, kaubaridi mororo kakachukua nafasi. Yaumi akamkabidhi lile kabrasha Kamanda akiwa amelichukua toka kwa Kyomukama, Kamanda akalipokea na kutoa zile karatasi ndani ya ile bahasha ya khaki na kuzichambua moja baada ya nyingine, akazisoma japo kwa haraka haraka, kwa namna moja au nyingine alipatwa na mshtuko wa aina yake, akabaki midomo wazi kama mtu aliyepigwa shoti ya umeme, akatikisa kichwa kwa masikitiko, akafungua ukurasa unaofuata, akafanya hivyo tena baada ya kusoma lililopo hapo, akafunga lile kabrasha akionekana wazi kuchanganyikiwa, akafumba macho na kutulia tuli kabisa. Aliitazama saa yake ilikuwa tayari saa tatu asubuhi ikikimbilia saa nne, na muda huo alimsikia rubani akiongea japo kwa sauti ya tabu kuwasiliana na watu wa Kampala uwanja wa ndege ili kutua salama.



    Dakika kumi baadae walikuwa tayari katika ardhi ya Kampala, kitu kilichowashangaza ni kufika na kupokelewa na jeshi la polisi kuwaweka wote chini ya ulinzi kwa mauaji yaliyotokea huko Kabale kwenye uwanja mdogo wa ndege, walipotaka kuwatia pingu Kamanda Amata akawazuia, na kuwaambia kwanza wakalete gari ya wagonjwa maana rubani na Kyomukama walikuwa na hali mbaya.

    “Hivi tangu lini mhalifu akajileta kwenye mikono ya dola kama hana akili?” kamanda aliwauliza wale askari, nao wakatazamana, “Sasa hao muwapeleke hospitalini watibiwe na aiulizwe mtu kitu chochote, muwaache huru waendelee na maisha yao ya kila siku, mimi ni mwana usalama kutoka Tanzania, kwa maelezo zaidi juu ya mauaji yel mtaikuta taarifa kwa mkuu wenu wa kazi,” Kamanda akatoa maelezo kisha akatoka na kuwaacha akifuatana na Yaumi mpaka alipo mke wa Kyomukama, Yule mwanamke akamkabidhi lile kabrasha Kamanda Amata akapokea na kumshika mkono Yaumi, wakaingia ndani ya uwanja mkubwa wa ndege. Ilikuwa ni bahati kwao kwa muda huo tayari kulikuwa na ndege ya ATC ikitokea Congo DRC kupitia Kampala kisha kuja Dar es salaam, hivyo wakafanikiwa kupata nafasi katika ndege hiyo baada ya Kamanda kujitambulisha kwao japo kwa uongo kidogo. Kamanda Amata na Yaumi walikuwa wameketi kwenye daraja la kwanza wakati huo yaumi alikuwa amelala kwa uchovu wa mikiki mikiki ya usiku uliopita, Kamanda Amata alikuwa akiperuzi yale makabrasha ili aone nini zaidi kipo ndani.



    ‘MPANGO KABAMBE WA MAPINDUZI YA KWELI’, yalikuwa ni maandishi makubwa yaliyokozwa kwa wino mweusi na kupigiwa mstari yakibeba kabrasha hilo, kwa mikono ya kitetemeshi Kamanda Amata alifungua kurasa moja baada ya nyingine akisoma kwa makini sana juu ya mpango huo uliopewa uzito wa ‘KABAMBE’.

    Mambo mengi, mipango ya kutisha ilikuwa ndani ya kabrasha hilo, sehemu ya kwanza ya mpango huo ilikuwa ni maelezo ya kwa nini mpango huo ukapangwa, nani anahusika katika eneo gani, Kamanda Amata hakuamini anachokisoma, hakuamini majina anayoyaona kwenye orodha hiyo. Majina matatu ya juu kabisa ndiyo yalimshtua zaidi, huyo aliyejiita namba moja, namba mbili na namba tatu wao. Ilikuwa hali ya kuogofya.



    Mpango kabambe ulikuwa ni mpango wa kufanya mapinduzi katika Tanzania ikiwamo kuvunja muungano na kuirudisha Tanganyika, kutokana na kuwa jambo hilo haliwezekani kujadilika iwe bungeni au katika baraza la mawazili, watu watatu wenye ushawishi waliamua kujiweka pembeni ili kuhakikisha linakamilika iwe kwa damu au kwa maji, lakini mpaka hapo ilikuwa tyari ‘kwa maji’ imeshindikana, iliyobaki ni ile ya ‘kwa damu’. Watu wasio na huruma na roho za wenzao walikuwa wameamua kufanya hayo.



    MISITU YA ULUGURUCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    VIJANA wapatao mia tano walikuwa wamefichwa katika misitu minene ya uluguru, hakuna mtu aliyekuwa anajua hilo isipokuwa watu watano tu, mpango ulikuwa ni kuwapa mafunzo ya kijeshi ya kupambana kwa mikono na silaha, ikiwa ni matayarisho ya kuipindua serikali iliyo madarakani, kumuua Rais na nchi kutwaliwa na wao. Vijana hao walioingizwa huko kwa siri miezi kadhaa, walikuwa wakipata mafunzo makali ya upiganaji wa kitaalamu yaani kung fu, judo, karate na mitindo mingineyo, huo ukiwa ni mpango wa awali.

    Baada ya mpango huo kuilipangwa sasa mafunzo ya kutumia silaha za kisasa, makombora,a mabomu ya uzito mbalimbali, kufundishwa mbinu za kivita ili kupambana na vijana wa jeshi la wananchi. Kijana mmoja alitakiwa kupewa mafunzo maalumu ya kudungua ili aweze kumdungua mkuu wan chi na kisha kuendesha mapinduzi hayo ikiwa ni kuteka kila idara nyeti ya serikali.



    Mkufunzi mkuu wa mafunzo hayo ya kijeshi alikodiwa kutoka Somalia, Komandoo wa kike, Fasendy. Walikuwa wakisubiri silaha nzito walizofadhiliwa kutoka nchi Fulani huko ughaibuni, kontena tatu ziliingia bandarini Dar es salaam bila mtu yeyote kushtuka kuwa ndani yake kuna nini, kabrasha za kontena hizo ziliorodhesha vyombo vya nyumbani, na hili lisikaguliwe, walipanga mbinu za kuwahadaa wahusika wenye vitengo ile mzigo upite kiurahisi wakisema ‘kwenye uzia penyeza rupia’. Ilipangwa mara tu vijana hao wakomaapo kimafunzo, waletwe Dar es salaam kwa njia tofauti tayari kutekeleza huo mpango kabambe, na mara baada ya kukamilisha zoezi hilo, tayari wakiwa wamempindua mkuu wan chi basi watangaze utwala mpya utakaoongozwa na Bw. Kadingi G, Kadingisa ambaye katika mpango huo alionekana kuwa ndiye kinara wa kutoa maagizo na kutafuta wafadhili katika mipango mbalimbali, yeye ndiye alikuwa kapewa No 1 ili kumficha jina lake, hakuwa anaishi nchini kwa miaka mingi sana baada ya kutoroka kwa kuhusishwa na kesi ya uhaini, alipojulikana kuwa alikuwa akifadhili wahaini waliotaka kuipindua serikali ya awamu ya kwanza kati ya miaka ya ’70.



    Sasa aliamua kutimiza azma yake kwa njia nyingine katika uongozi wa awamu nyingine, na hasa alipohakikisha kuwa Yule mbaya wake amekwisha aga dunia. Huyu bwana aliyafanya yote hayo akiwa nje ya Tanzania, lakini lengo na mpango wake haukuwa kurudi Tanzania bali kurudi Tanganyika, tayari zilikwishaandaliwa bendera za taifa hilo jipya na mipango mingi ilikuwa imeandaliwa, yeye alitakiwa kuwa rais na wengine kuwa wasaidizi katika idara nyeti.



    Mafunzo yalikuwa yakiendelea katika misitu hiyo na vijana walikuwa wameiva kwelikweli katika idara za makabiliano ya ana kwa ana. Ilikuwa bado siku mbili tu waanze mafunzo hayo ya kutumia silaha chini ya mkufunzi Fasendy.



    §§§§§



    Kamanda Amata alishusha pumzi ndefu akiwa kurasa ya kumi na kitu ya mpango huo ulioandikwa kitaalamu sana, macho yake yalitua juu ya kichwa kilichobeba habari.



    VIONGOZI WATATU WA JUU

    1. Dr. Kadingi G. Kadingisa (Rais) – No 01

    2. Bw. Sikotu O. Sikotu (Makamu Rais) – No 02

    3. Bw. Gabriel Matinya (Waziri mkuu) – No 03



    Hiyo ilikuwa orodha ya juu kabisa ukiachia na mipango mingine. Ilikwishapangwa tarehe ya mapinduzi yenyewe, siku ambayo mkuu wa nchi atakapokuwa katika ziara ya kikazi huko Kagera, auawe wakati huku Dar es salaam kufanyike utekaji wa idara nyeti kama Redio ya Taifa, kituo cha Televisheni cha Taifa ila kubadili matangazo siku hiyohiyo, kuvamia Ikulu, kuteremsha bendera ya Tanzania na kuiweka ile wanayoitaka wao, wakati huo wakidhibiti hapa na pale ambapo pangeleta shida.



    Kamanda Amata aling’amua wazi nani anayetoa siri juu ya safari za mkuu wa nchi, hakuwa na shaka kwa ni mwenye jina ambalo lilifichwa kwa No 2 alikuwa ni waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais mipango na uratibu, No 3 alikuwa ni Inspector General of Police( IGP), ambaye ni mdau mkubwa sana wa duru za usalama nchini.

    Sura ya Kamanda ilibadilika. Akainua saa yake na kuanza kuandika vitu Fulani tayari kuvituma nyumbani ili vifanyiwe kazi. ‘Kajiba alikuwa na kila sababu ya kufanya alilolifanya,’ Kamanda alijiwazia huku akimtazama yaumi aliyekuwa amelewa kwa usingizi mzito.

    Alitikisa kichwa kuonesha siktiko lake juu ya huyu mwanamke aliyeachwa mjane ambaye bado alihitaji mapenzi mazito ya mumewe. ‘Mungu ana maajabu yake,’ alijisemea moyoni alipojiuliza kwa nini siri nzito kama hiyo imfikie Kajiba na si mtu mwingine wa usalama. ‘Walijiamini kupita kiasi kubeba siri hii katika daladala,’ aliendelea kuwa na mawazo. Alitamani kama ashuke muda huo ili akamkamate Matinya na Sikotu kwa mkono wake na vibaraka wote wa kundi hilo, alitamani kama angekuwa jaji awahukumu kunyongwa kwa kitanzi kimoja na kiwe kitanzi cha mwisho, moyo wa hasira ulimkamata mpaka kumfanya koo lake kukauka, akaomba bia kwa mhudumu wa ndege, akaletewa bia aina ya Calsberg, “Hakuna Safari?” aliuliza, akajibiwa hakuna. Akaigugumia yote lakini bado alihisi ana kiu, lakini alichelewa kugundua kuwa kiu inayombana ni kiu ya hasira.

    “Kwani hii ndge inatua saa ngapi?” alimuuliza mhudumu mwingine, akajibiwa asubiri ni dakika arobaini na tano watakuwa tayari nyumbani.



    Dar es salaam- saa 5:45 asubuhi



    FURAHA ilikuwa kubwa kwa bwana Gomegwa baada ya kuhakikisha hundi yake iko salama katika mfuko wake wa shati, alifunga ofisi tayari kuondoka kwenda benki na kisha akapate chakula bora cha mchana au wengi hukiita mlo kamili. Ili asifaidi peke yake alimwita mkewe kipenzi kama surprise ili wajumuike pamoja katia hotel ya Embassy. Alitoka ofisini na kumuachia maagizo sekretari wake kisha akaingia kwenye gari yake, siku hii aliamua kuendesha mwenyewe gari binafsi hakuhitaji mtu kujua kinachoendelea.

    Akiwa kwenye barabara ya kuelekea Samora kuelekea picha ya askari kisha aende benki tawi la Azikiwe, alikuwa akipiga mruzi ndani ya gari yake akifuatisha wimbo uliokuwa ukipigwa ndani ya gari yake, wimbo kutoka Kenya uliokuwa ukiitwa ‘Nchi ya kitu kidogo’, akiwa katika mwendo wa wastani huku ametanguliwa na gari nne mbele na nyuma yake kulikuwa na Toyota Noah nyeusi iliyokuwa ikija polepole, kelele za honi kutoka nyuma zilimshtua kidogo akatazama kwenye kioo na kuona ile Noah ikiomba kupita, Gomegwa akabana pembeni na kuipisha hiyo gari. Ile Noah ikapita upande wa kulia wa gari ya Gomegwa.



    Scogon, tayari alikuwa ameweka bastola yake ikiwa na kiwambo cha sauti katika upenyo mdogo wa dirisha, alipokuwa tayari usawa wa dereva yaani Gomegwa, kidole cha shahada kilitekenya trigger ya Magnum 22, Winchester, ilitii amri, risasi moja ili penya kwenye dirisha wazi la Gomegwa ikapiga usawa wa sikio na kutokea upande wa pili, kisha ile Noah ikaongeza mwendo na kuipita gari ya Gomegwa ambayo ilitembea kwa usahihi mita kumi tu na kuacha njia kabla ya kupanda msingi na kujirusha mpaka kwenye ofisi moja iliyokuwa katika jengo jirani, ikapasua kioo kikubwa na kudondoka eneo hilo. Kama kawaida ya Watanzania, wakaacha shughuli zao na kwenda kushuhudia ajali hiyo. Kutokana na pigo la risasi ile bwana Gomegwa alipoteza maisha palepale.

    “Alikuwa amelala huyu, pombe hizo!” alisikika mzee mmoja muuza karanga akiwaambia wenzake.



    Mbele kidogo Toyota Noah ikasimama, Scogon na Mdumi waliteremka kuja kuhakikisha kama wamemaliza kazi au la, lakini walipoona wakina mama wanalia wakikiambia huku na kule wengine wakitapika, wkajua tayari, kazi imekwisha. Wakarudi garini na kuondoka wakiwa wamejiridhisha na walilolifanya.



    §§§§§



    Saa ya Madam S ilimfinya kushiria kuna ujumbe unaoingia, akaibonya kitu Fulani na kusubiri ujumbe huo…

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “…Kila kitu kimepatikana, Madam, naomba wafuatao wakamatwe mara moja, 1. IGP Gabriel Matinya na Mheshimiwa Sikotu O. Sikotu. Zaidi ya hayo kuna kontena tatu zipo bandarini zizuiwe kutoka na zifanyiwe uchunguzi haraka iwezekanavyo…”



    Huo ulikuwa ni ujumbe uliosubiriwa kwa hamu na mwanamama huyo, ‘Welldone Kamanda’ akajisemea na kuichukua simu yake kutoka mezani…



     Akiwa tayari amekwishapeleke taarifa hiyo tete kwa mheshimiwa Rais, Madam S alikuwa na Baraka zote za kuifanya kazi yake, alitabasamu na kusimama kabla ya kuiacha meza yake, kisha akaliendea kabati moja lililopo ndani ya ofisi yake na kuchukua vitu Fulani Fulani kama miwani yake yenye uwezo wa kunasa picha mjongeo, kinasa sauti kimoja kidogo sana, alipoona yuko sawa kabisa, akampigia simu Inspekta Simbeye.



    “Yes, Madam, niambie,” ilikuwa sauti ya Simbeye.

    “Kuna kazi ya haraka, naomba vijana wako wenye silaha na gari moja tufuatane sasa hivi kuna kontena tatu zimetoka bandarini asubuhi hii zinaelekea Morogoro, zikamatwe na kurudishwa kituoni haraka,” Madam alitoa maelekezo.

    “Hilo tu mama?” Simbeye aliuliza.

    “Hilo la kwanza, la pili unipe jibu kama vijana wameshakwenda,” Madam S alimaliza kwa utanai, kisha akaingia kwenye gari yake, kabla hajaondoka akapiga namba nyingine.

    “Hey Chiba, kumekucha mwanangu, amuru vijana wanaomwangalia Mr Gomegwa wamkamate sasa hivi wamlete kituo cha kati, kisha mheshimiwa Sikotu O. Sikotu akawekwe chini ya ulinzi afikishwe ofisi nyeti mara moja kwa mahojiano, na hao wanaomwangalia Matinya wasimpoteze kwani naye inabidi tukamkamate, afikishwe ofisi nyeti,” Madam S akatoa maagizo kwa kijana wake anayemwamini endapo Kamanda anakuwa nje ya eneo.

    “Copy, Madam S, vijana kazini,” Chiba aliitikia.



    Chiba alipomaliza kupokea simu hiyo tu, mara simu yake ya upande wa pili ikaita,

    “Ndiyo vijana, na mi nilitaka niwapigie sasa hivi, kabla hujanambia unalotaka kunambia, naomba sasa mumkamate Bw Gomegwa na mumlete kituocha kati,” Chiba akatoa maagizo, lakini badala ya kusikia jibu akakutana na ukimya.

    “Chiba, ni kwamba huyu bwana Gomegwa amepata ajali mbaya na kufariki palepale kama dakika kumi hivi, ajali imetokea mtaa wa Samora mpaka tunavyoongea bado shughuli za kutoa mwili wa marehemu kwenye gari zinaendelea,” Yule kijana alitoa taarifa.

    “Ok nimekusoma, nafika hapo sasa hivi,” Chiba alishusha pumzi na kurudisha simu yake mfukoni, kisha akatumia simu nyingine na kumpa taarifa Madam S. kutoka kwa madam S Chiba alibadilishiwa uelekeo na sasa walihitaji kwenda kwa bwana Sikotu.



    Taarifa za kuzuia kontena zinazosafirishwa kwenda Morogoro zilitawanyika katika makutano ya Tazara, Buguruni na Ubungo ili pilisi wa usalama barabarani waweze kuzuia yasipite, kutoka nTazara waliambiwa kuwa wamekwishapita, vivyo hivyo Buguruni mpaka Ubungo, hakuna ujanja, Land Cruiser ya polisi ikiwa na askari sita wenye silaha wakiongozwa na pikipiki moja kubwa la polisi, ving’ora vya nguvu ili magari mengine yaachie njia, ikawa hivyo. Kila mtu barabarani alikuwa akishangaa mwendo mkali wa msafara huo mfupi, hawakujua kinachoendelea.

    Baada ya mwendo mrefu sana, tayari walikuwa wanakaribia maeneo ya Mlandizi, ndipo walipoona gari la kusindikiza makontena hayo, wakalipita na mbele kabisa waliyakuta malori hayo yakipanda mlima wa kuingia Mlandizi, ile pikipiki ikapita kwa kasi na kusimama mbele yake, Yule polisi akashuka na kusimamaisha yale malori yote mawili. Dereva wa lori la kwanza akasimama naye akashuka.

    “Ndio afande, vipi leo unanikamata kwa mtindo mwingine?” Yule dereva akauliza, kabla hajajibiwa ile Land cruiser tayari ilikwishafika na wale askari wakateremka na kuweka ulinzi.



    “Kijana, unasafirisha mzigo gani?” Yule polisi wa pikipiki akauliza, Yule dereva akafungiua makaratasi, Yule polisi akayasoma, yalikuwa yameonesha kuwa mzigo unaosafirishwa ni vyombo vya nyumbani, tena vilikuwa vikienda Mbeya kwa jinsi anuani ile ilivyoandikwa.

    “Naomba tukague,” Yule polisi akaomba, lakini yale makontena yote yalikuwa yamefungwa kwa vifungo maalum. Wakabadili mawazo, na kuamuru kontena zote zirudishwe mpaka kituo cha polisi kati, huko ndiko yakakaguliwe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§



    GABRIEL Matinya, kwa kuwa alikuwa ni mtu wa juu katika dura za usalama nchini, alipata taarifa mapema sana kuwa kuna hizo kontena zinafuatiliwa, akajua waziwazi hapo mambo yameharibika, alitakiwa kufika kituo cha polisi kati haraka iwezekanavyo lakini kichwani aliwaza na kujua kuwa huo usije kuwa mtego wa panya akaahidi kufika haraka iwezekanavyo. Akatafakari kwa kina huku kijasho chembachemba kikimtoka hakujua la kufanya, ‘Hapa sasa hapafai, lililobaki ni kutoroka nchi tu,’ alitoka ofisini kwa kupitia ngazi za nyuma ya jengo, ngazi za dharula ambazo huwa hazitumiki mara kwa mara, akateremka mpaka chini na kutembea hatua za haraka haraka, alipokaribia geti dogo la upande wa nyuma akakutana na WP Magreth, wakasalimiana, Magrerh akamtazama Matinya lakini aliona wazi kuwa hayuko sawa kwa maana si mtu wa kutyoka peke yake hasa akiwa kikazi namna hiyo.



    Matinya hakuonesha kujali, alitoka mpaka barabara ya nyuma akasimamisha tax na kuingia moja kwa moja akaomba impeleke Buguruni Chama, ikawa hivyo. Dakika ishirini baadae, Matinya alikuwa katika gari binafsi, alikwishapata ndege ya kukodi kumfikisha Nairobi kisha pale aondoke kwenda ughaibuni usiku huo. Akanyanyua simu na kumtafuta Marina, hakupenda kabisa kumuacha binti huyu, barafu la moyo wake, akamwambia wakutane Uwanja wa ndege ndani ya dakika thelathini. Matinya alitulia ndani ya gari yake akiendesha taratibu simu yake ikiwa inaita mara kwa mara kila alipoangalia ilikuwa ni simu kutoka kwa Inspekta Simbeye, jina hilo lilikuwa likimuharibia raha yote ya maisha kwa nukta hiyo, ‘Nikifanikiwa kufika Nairobi tu, wamenikosa’. Kwa ujumla Matinya alimsaliti Sikotu kwani alijipanga kutoroka bila kumshirikisha mwenzi wake au bosi wake huyo na wala hakutoa taarifa yoyote juu ya ukamatwaji wa kontena hizo, alitaka aiponye nafsi yake.

    Dakika kumi na tano baadae tayari alikuwa ndani ya jengo la uwanja wa ndege, aliitazama saa yake mara kwa mara huku akiangali kama Marina atakuwa amefika hapo, hamuoni!



    §§§§§



    Hali ya hofu iliingia ghafla ndani ya moyo wa Sikotu, mapigo yake yalisikika wazi yakibadilisha uelekeo pale alipopata taarifa ya ujumbe wa maandishi toka kwa Matinya kuwa ‘Mambo yameharibika, mzigo umekamatwa,’ baada ya hapo kila alipokuwa akipiga simu, wapi hakumpata Matinya wala nani sijui, bahati mbaya hakuwa anajua simu yoyote ya vijana wa Matinya, kijasho kilimtiririka, ofisi ilikuwa na joto japokuwa kipooza hewa kilikuwa kikifanya kazi yake vizuri, alilegeza tai na kufungua baadhi ya vishikizo vya shati lake wakati huo tayari koti lilikuwa halifai mwilini kwake, lilishawekwa pembeni, alishika hiki akashika kile vyote havikuwa na maana kwake, alijishaka kiuno akahema, akimbie? Haiwezekani, kwani hapo nje tu angekutana na dreva wake, afanyeje, hakuna jibu, mara mlango ukagongwa na sekretari wake akaingia na kuurudisha nyuma yake.

    “Mheshimiwa kuna wageni wanataka kukuona,” ilikuwa sauti nyororo ya binti huyo aliyevalia nadhifu.

    Mheshimiwa Sikotu alimtumbulia macho mwanadada huyo kiasi kwamba aliingiwa na woga.

    “Waambie waingie,” alijibu Sikotu kwa shida kidogo huku akijiweka vizuri kitini. Lo, ilikuwa vigumu kuamini anachokiona mbele yake, Mwanamama mkongwe ambaye nywele zake kama hakuzifunika kwa kilemba basi unaweza kusema alijimwagia jivu kidogo kichwani kwa jinzi mvi zilivyocahnganyika na nywele nyeusi, alisimama mbele yake akimtazama.



    “Karibu kiti Madam eehhhnn!” kabla Sikotu hajamaliza, alikatishwa na jibu, “Madam S,” alimalizia mwenyewe.

    “Sijaja kukaa bali nimekuja kukuchukua wewe No 2 wetu ili ukaonane na Rais na kumueleza juu ya mpango ule ambao mlikuwa mmeupanga wewe, Matinya pamoja na mshirika wenu Dr. Kadingi G. Kadingisa mnayemwita ninyi No 1 au ndio Rais wenu wa Tanganyika mnayoitaka,” Madam S aliongea huku sura yake ilionekana wazi kuwa haina msamaha hata kidogo, Sikotu akamtazama mwanamke huyu aliyeaminiwa na Rais hata kupewa kitengo hicho cha juu sana katika usalama wan chi, ‘Rais hakukosea,’ alijisemea moyoni. Bw. Sikotu alionekana akitetemeka wazi, swala la kuonana na Rais lilikuwa ni swala lingine kabisa, hofu kuu ilimtanda kuanzi machoni mpaka miguuni, mfumo wa maji taka wa mwili ukashindwa kufanya kazi sawasawa. Sikotu akajitahidi kusema.

    “Sipo tayari kuonana na mkuu wa nchi, sipo tayari kuning’inia kitanzini na umri huu kwa kashfa hii nzito,” alilalama mara vijana wawili wenye sare ya polisi waliingia ndani ya ofisi hiyo mmoja akiwa na pingu mkononi, akamfuata bw. Sikotu pale kitini ili kumfunga pingu hizo kisha aondoke naye, Sikotu alikuwa kajiinamia mezani, alipoatikiswa aamke hakuamka, walipomgeuza walishuhudia povu jingi mdomoni.

    “Kajiua, shiiiiit!” madam S aling’aka kwa hasira. Sikotu wa Sikotu alijiua kwa kutumia kidonge maalumu chenye sumu inayokuua haraka tu, kidonge hicho hutumiwa sana na majasusi ambao hawako tayari ama kuhojiwa ili kutoa siri Fulani au kukwepa mateso makali ambayo hayaepukiki. Bw. Sikotu alikuwa amechagua njia hiyo kujiondoa duniani. “Bahati yako umejitanguliza mwenyewe,” Madam S aliongea kwa sauti ya chini akiwa anatoka ndani ya ofisi ile na kuwaacha vijana wa jeshi la polisi wakiufanyia kazi mwili wa Sikotu.



    §§§§§



    Matinya alitafutwa kila mahali na wale vijana waliopewa kazi hiyo baada ya kupewa amri na Chiba kumtia nguvuni kwa kibali maalu toka Ikulu, jengo zima la makao makuu ya Polisi Matinya hakuonekana, ilikuwa ni zahama kubwa, kila mtu alishangaa nini kinatokea katika jengo hilo, maana vijana walikuwa wakihaha huku na kule, lakini hola.

    WP Magreth alikuwa akitembea chini ya jengo hilo kuzunguka upande wa pili kwenye ofisi za jeshi la uhamiaji alipopata taarifa ya kutafutwa kwa Matinya, alisimama kwanza, akajiuliza maswali mawili hivi, ‘Nilimuona,’ alijijibu, akatoa taarifa haraka kuwa Matinya aliondoka jengo hilo karibu nusu saa moja nusu saa ilopita kwa tax binafsi, hapo msako mkali ukaanza.



    Marina alikuwa akitoka katika ofisi za uhamiaji tayari amekamilisha hati zake za muda mfupi za kusafiria, alipokuwa akishuka kwenye ngazi za jengo hilo ndipo alipokutana macho kwa macho na WP Magreth, akamkumbuka mwanadada huyu, alimuona mara nyingi katika sakata la Yaumi kipindi hicho, akamtazama kwa chati kisha akaendelea kuteremka zile ngazi, alipogeuka tena bado alimuona Magreth akimfuatilia kwa macho…



    ....mpaka alipoingia katika gari yake na kuondoka, akainua simu ya upepo na kutoa taarifa za mtu huyo ili afuatiliwe, kazi ikafanyika, askari waliovaa kiraia katika gari ya kiraia pamoja na WP Magreth mwenyewe wakamfuatilia Marina ili kujua mwisho wa safari yake.



    §§§§§



    Katika kituo cha polisi cha kati, kontena tatu zilifikishwa uani na kazi ya ukaguzi chini ya askari polisi. Vifungo vya milango vilikatwa na milango hiyo kufunguliwa, kontena moja baada ya jingine lilikaguliwa ili kujua vilivyomo ndani. Upekuzi ukaanza, kila walichokishika kilikuwa ni chombo cha matumizi ya nyumbani, sahani za udongo, vibakuli, vikombe na vitu mbalimbali kama masinki ya chooni. Wale vijana walitoa vile vitu na kuanza kukata tamaa.

    “Mkuu hapa naona ni vitu vya nyumbani tu,” mmoja alimwambia inspekta Simbeye aliyekuwa akisimamia zoezi hilo.

    “Haya, hamia la pili,” aliwaamuru. Wale vijana wakaanza kazi tena kwenye kontena la pili, mambo yalikuwa yale yale, makorokoro ya nyumbani na hakukuwa na linguine la ziada, kazi ikiwa inaendelea.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§



    Kamanda Amata na Yaumi walitoka ndegeni na kukanyaga ardhi ya Tanzania baada ya shughuli nzito ya huko Uganda, alipoifungua simu yake tu akapata taarifa ya kutoroka kwa Matinya lakini ufuatiliaji ulikuwa ukiendelea na ilisemekana kuwa amepanga njama ya kutoroka kwa usafiri wa anga. Kamanda Amata akatulia kwanza na kutafakari mawili matatu akamtazama Yaumi aliyeonekana kuchoka sana, akampa lile kabrasha ndani ya mfuko wa khaki.

    “Shika hili tunza vizuri, usitoke hapa mpaka nitakaporudi,” Kamanda Amata alimwambia Yaumi naye akafanya hivyo.

    Kamanda Amata akajamwendea rafiki yake anayefanya kazi mamlaka ya uwanja wa ndege ambaye anaratibu safari zote za kutoka na kuingia, alimuuliza kama kuna ndege yoyote ambayo imetoka au inatoka kwenda nje ya nchi kwa asubuhi hiyo, akaambiwa hakuna ndege yoyote, hata zile za ndani ni nne tu zilizokwishaondoka, moja imekwenda Mtwara, nyingine Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya, zaidi ya hapo ni zilizoingia tu. Walipotazama orodha ya majina hakuna jina walilolihisi labda limetumika kimagumashi. Simu zikapigwa viwanja vyote vya ndege ambako safari hizo zinaishia ili kumchunguza abiri mmoja baada ya meingine wanaoshuka katika ndege hizo, makachero wa mikoa hiyo wanaoweza kumtambua mtu kwa urahisi walikuwa viwanjani ili kutekeleza agizo hilo. Kamanda Amata alifikiri kwa kina akaona kama katika ndege hizo za ndani mtu huyo hayupo basi kwa vyovyote bado yuko ndani ya Dar es salaam hapo hapo, mara simu yake ikamfinya kuashiria kuwa kuna ujumbe unaingia, akaitazama na kuruhusu ujumbe huo. Akausoma na kuuelewa. Alipokuwa anatoka ndani ya ofisi ya huyo bwana wa mamlka ya Uwanja wa ndege ndipo kwa chini alimuona mtu anayefanana na Matinya kwa mwili na mwendo lakini sura yake ilikuwa tofauti kidogo, nyuma yake kulikuwa na mwanadada ambaye sura yake haikuwa ngeni sana kwa Kamanda Amata. Simu katika ofisi ya bwana huyo ikaita, akaipokea na kuzungumza habari Fulani.



    “Sawa sawa hakuna shida ipe njia ya kuondoka, umesema inaenda wapi?” yule bwana akamuuliza aliyepiga simu. Akajibiwa, wasiwasi kidogo ukamwingia na mashaka juu ya ndege hiyo ya kukodi ambayo taarifa yake imefika punde tu kuwa inaomba njia ya kuondoka.

    “Kamanda! Akamwita,” akamwita, “Kuna ndege ya kukodi hapa inaelekea Nairobi nusu saa ijayo nimepata taarifa sasa.”

    “Naomba isiondoke na nijue abiria waliomo ndani,” kamanda alimwambia Yule meneja.

    “Imekodiwa na bwana Silvanus Kilowoko akiwa na mkewe, ni wao wawili tu,” Yule meneja akaeleza.

    “Sawa, hao ndio ninaowahitaji, bila shaka, asante sana,” Kamanda Amata akateremka kwa kasi zile ngazi za umeme kuelekea chini alikomuona Yule mtu aliyemuhisi ni Matinya. Alipofika chini hakumuona, alitazama huku na kule lakini peupe. Akashikwa begani, alipogeuka akakutana uso kwa uso na Gina.

    “Karibu nyumbani Kamanda,” akamkaribisha.

    “Asante, namsaka boss wako anatoroka nchi,” Kamanda akamwambia Gina.

    “Ndiyo, yupo hapa, WP Magreth kanambia, nimekutana naye hapo chini,” Gina akajibu.

    “Ingia kazini haraka, hakikisha haondoki ndani ya jengo hili,” Kamanda alimwambia Gina, “Una chochote?” akamuuliza.

    “Niko full kinyama mpenzi wangu,” Gina akajibu na wakati huo tayari akatoka eneo hilo na kuingia upande mwingine wa jengo hilo la kuvutia.



    “Silvanus Kilowoko, amepita hapa?” Kamanda akamwuliza mtu wa ukaguzi wa uhamiaji pale uwanja wa ndege.

    “Ndiyo, anaelekea Nairobi yuko na mkewe, anapitia geti namba nane,” Yule bwana alitoa ushirikiano.

    Kamanda Amata akaanza kuliandama geti namba nane, mikononi mwake hakuwa na silaha yoyote, kila aliyemuona alimshangaa kwa jinsi alivyo na eneo alilopo.



    Gabriel Matinya na kimwana wake Marina walikuwa katika pozi la kusubiri kuingia ndegeni walipopata taarifa kuwa ndege hiyo itaondoka baada ya masaa mawili kwa kuwa hakukuwa na njia wakati huo, taarifa hiyo iliwataka waendelee kusubiri palepale walipo na wasiondoke ili kuepusha usumbufu.

    Machale yakamcheza Matinya, akatazama huku na huku na kumwangalia Marina.

    “Lakini beibi, mbona umepanga safari ya ghafla hivyo, mwenzako hata nguo ya kubadilisha sina,” marina alilalama.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usijali, kuna dharula na sikupenda kwenda peke yangu, hata huko tuendako kuna maduka utafanya shopping ya kutosha,” matinya alijibu. Baada ya sekunde kadhaa alinyanyuka na kutazama huku na kule, akaona hali tete ndani ya uwanja huo unaojulikana kama JNIA, aliona sura anazozijua za makachero wa usalama na baadhi ya vijana wake anaowafahamu fika. ‘Hawa kuwatoroka sio shida, ila wangekuwepo wale watatu wale hawatorokeki,’ alijiwazia huku akipanga nini cha kufanya kichwani mwake. Ulikuwa ni msako wa panya, kila choo ndani ya jengo hilo kilifunguliwa hata kama unajisaidia kilipekuwa kuhakikisha mtu huyo haondoki, kila ofisi ilikuwa kwenye hali ngumu, kila mzigo mkubwa ambao ungeweza kuhifadhi binadamu ulifungulia na kutazamwa kwa undani, wakati huohuo mbwa wa polisi nao walikuwa katika wakati mgumu kuliko maelezo wa kunusa harufu ya huyo anayetakiwa baada ya kunusishwa moja ya vitu vyake anavyovitumia mara kwa mara.

    “Marina mpenzi,” Matinya aliita, Marina akageuka kumtazama kibosile wake.



    “Unasemaje dear?” Marina akajibu kwa sauti ya mahaba.

    “Safari ni baada ya masaa mawili, sasa waweza kuzungukazunguka kidogo halafu tukutane hapahapa dakika tisini zijazo,” almwambia Marina, wazo halikupingwa. Matinya akampa kiburungutu cha pesa kama atataka kununua chochote basi afanye hivyo. Marina akatumbukiza burungutu hilo kwenye pochi yake, na kuanza kuvuta hatua akifuata ujia mrefu ambao wasafiri wengine walikuwa wakipita kuelekea eneo la kupumzika wakisubiri usafiri.



    Kutoka pale alipoketi bila kujitikisa, Yaumi alimuona Marina akija kupitia njia hiyo, hakuamini kama ni yeye au anafananisha maana binadamu hasa wa kike wakijipamba urembo wa kichina basi wote hufanana, akamkazia macho, lakini hakutaka Marina amuone hivyo akajificha sura yake kwa mkono kama mtu anayesikiliza simu. Mwendo wa Marina ulionekana ni wa woga kiasi Fulani kwa maana mpaka hapo alishaona kuna kitu hakiendi sawa uwanjani hapo na pia hali aliyonayo dushelele wake ilikuwa tofauti sana. Aliamua kuondoka eneo hilo hata safari yenyewe hakuona umaana wake, alijaribu kupiga simu ya Scogon na Mdumi zote hazikupatikana, alijaribu kupiga tena na tena wapi. Aliamua kutekeleza lile alilojiamulia mwenyewe, alirudisha simu mkobani na kuendelea na safari yake ya kuelekea nje ya jengo hilo, akwa na uhakika kuwa hakuna mwingine anayeweza kumshukia kwa lolote, alitembea kwa kujiamini tu, lakini haikuwa hivyo.



    WP Magreth alimuona Marina akiwa peke yake, akajua kwa vyovyote mwnamke huyo yupo na Matinya na akimbana tu lazima ataonesha Matinya alipo, alianza kumfuata kwa wizi ili asigunduliwe.

    WP Magreth alitoa taarifa kwa wengine wote ili kumkamata mwanamke huyo, kila mmoja akwa tayari kwa hilo. Magreth akateremka taratibu kutoka pale alipo kuja upande wa pili kwenye milango ya kutokea nje. Bahati mbaya au nzuri akiwa kwenye ngazi za umeme kuteremka chini aligeuka kumtaza Marina, hakumuona, akili ikamsimama kwa sekunde kadhaa, ‘ina maana kaniona au imekuwaje?’ alijiuliza, akaangaza macho vizuri ili amuone lakini wapi, hakumuona mwanamke huyo, hapo akaongeza kasi ya kuteremka.

    “Vipi mmemuona?” aliwauliza wale aliowapa maelekezo pale karibu na mlango.

    “Hapana na hapa hajatoka,” wakamjibu.

    “Msakeni,” alitoa amri na vijana wale wakaacha ule mlango na kuingia ndani kumsaka mwanamke huyo.



    §§§§§



    Matinya alipoona kuwa Marina ameshaondoka pale alipokuwa naye, ukawa ni muda wa kujiokoa mwenyewe, ‘kafe peke yako, kama mwanamke ntapata mwingine, lakini nakupenda,’ alijisemea moyoni. Akatoka kwenye lile eneo alilokuwa ameketi na kupita kwenye geti namba nane akaingia kwenye ujia wa kushuki chini uwanjani, akazishuka ngazi kwa haraka, akafika chini na kukuta wafanyakazi wengi wa Swissport wakishughulika kupakia na kupaku mizigo kwenye ndege zilizopo hapo, akawapita na kukunja kushoto, maana alijua fika akipita kulia ataonekana kwa kuwa ni sehemu ya VIP, akapenya penya hapa na pale, akafika mwisho wa jengo. Akajibana na kuangali upande wa maegesho ya magari kama angeweza kulifikia gari lolote na kuondoka nalo, kwakuwa alizijua sura za walio wengi pale nje aliona ugumu wa kufanya zoezi hilo, kila kona aliona vijana wa usalama wametanda akajua kazi ipo, na si ndogo. Akatulia palepale kuangali upepo unaeendaje, mbele yake kulikuwa na geti ambalo hutumika kwa wafanyakazi alitazama na kumuona mlinzi aliyekuwa kasinzia mahali hapo akiwa hana hili wala lile.



    Kamanda Amata alikuwa bado akimsaka Matinya kwa udi na uvumba kila alikopita ilikuwa hola, akajua wazi kuwa sasa ni kazi kubwa maana kwa vyovyote Matinya anatumia mbinu mbalimbali za kujilinda dhidi ya adui wake kwa kuwa naye hiyo ni moja ya kazi yake, umakini unahitajika. Alipita hapa na pale hakuona chochote, simu yake ikaita, akaitazama alikuwa Yaumi akitumia simu ile aliyomuachia kwa muda kutuma ujumbe.

    “Kuna mtu hapa nina wasiwasi naye sana, ni mwanamke, njoo umuone anaweza kukusaidia,” Kamanda Amata akasoma ujumbe huo na kuirudisha simu mfukoni na kuendelea kufanya msakao wake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Marina akiwa katika harakati za kutoka, kwa bahati nzuri alimuona WP Magreth hivyo kwa haraka akawa anatafuta njia ya kujinasua naye kwani kwa kumuona afande huyo sasa alijua kinachoendelea, aliju kabisa kama si Matinya basi yeye atakuwa chambo japokuwa hakujua hasa tatizo ni nini. Alipokuwa katika harakati za kujinasua, akitembea kwa mwendo wa haraka haraka alipita jirani kabisa na Yaumi, ndipo yaumi alipofanya hila kwa manamke huyo,kwanza akikumbuka jinsi alivyomnyanyasa alipokuwa gerezani, alimtegea muguu na kumchota mtama maridadi, Marina alitua chini kama mzigo, mzima mzima,.

    “Askari mzima huna stamina!” yaumi alimwambia, Marina alishtuka kusikia sauti hiyo, alipogeuza uso wake alikutana uso kwa uso na Yaumi, alibaki mdomo wazi.

    “We si umenyongwa wewe?!” marina aliuliza kwa mshangao kwa kuwa kwa kumuona tu yauminalirukwa na akili ghafla.

    “Ee na hapa ulipo wewe ni kuzimu, sasa leo umekutana na mzimu wa yaumi, mwanamke una hila wewe,” Yaumi alisema hayo akiwa kashikwa na hasira kali juu ya mwanamke huyo. Marina alijaribu kujiinua lakini wapi, teke moja kali toka kwa Yaumi lilimrudisha chini, alipotaka kujibu mashambulizi alijikuta anatazamana na mdomo wa bastola kutoka kwa mwanamke mwingine aliyemjua fika, Magreth.

    “Tulia kama ulivyo punda wewe!” Magreth aliunguruma. Alikumbuka jinsi alivyojibiwa kwa nyodo na mwanamke huyo pale Mahakama ya Kisutu miezi kadhaa nyuma. Marina akatiwa pingu, wakati huo wale vijana wawili wa polisi walifika na kumchukua kwa kumshika huku na huku.



    “Najua kwa vyovyote wewe unajua ama Matinya au wafuasi wake wako wapi, haya tuongoze haraka,” Mgreth aliamuru huku akimtulizia kofi moja kali shavuni. Alipogeuka akakutana na Yaumi, japokuwa alimhisi lakini hakumjua vizuri kutokana na jinsi alivyo, Marina akawaongoza skari hao kule aliko Matinya, walipofika hakuonekana Matinya wala nani, hapo ndipo Marina akajua kasalitiwa, akaangusha chozi la uchungu. WP Magreth akatoa taarifa hiyo, vijana wakabana kila kona kuhakikisha haponyoki mtu, Matinya aliwatoa jasho.

    Gina akiwa katika harakati zake za huku na kule, uzuri wake yeye alikuwa hajulikani sana na watu, alimuona Matinya alipokuwa ananyata kumuendea Yule mlinzi pale alipo, mara moja akatoa alama ya kumjulisha kamanda kwa kutumia simu yake, akahakikisha Matinya hapotei machoni pake. Matinya alifika katika kile kibanda cha mlinzi na kumpa pigo moja kali Yule mlinzi mpaka akazirai, Gina alipoona kitendo kile akasikitika sana kwa ukatili huo. Akampa maelekezo Kamanda ya wapi pa kumpata Matinya.



    Kamanda Amata akaingia katika moja ya duka linalouza vitu vya utamaduni, akanunua pama kubwa la miaa akalivaa na kulivutia usoni kisha akanunua sigara na gazeti, akachomoa bastola yake bila mtu kujua na kuifutika ndani ya gazeti kisha akaelekea kule alikoambiwa, alimuona mtu aliyekuwa ndani ya kibanda kile, lakini huyu alikuwa na ndevu kidevuni mwake wakati Matinya daima hana ndevu za kidevuni, kama unavyojua polisi wote wako hivyo. Alimuona Matinya alkitoka ndani ya kibanda kile na kuelekea kunako maegesho ya magari, akamfuata kwa nyuma na wakati huo Gina alikuwa nyuma kabisa akingali kama kuna lolote litakaloleta shida kwa wakati huo. Matinya alifika kwenye moja ya gari za watu waliokuja uwanjani hapo na kufanya uharamia ili kuingia katika gari hilo.

    “Hapana, huwezi kufanya kitu kama hicho mzee, kama wewe wajibu wako ni kulinda usalama wa raia na mali zao sasa kwa nini unataka kuharibu mali ya mtu mwingine? Isitoshe unataka kuiba hilo gari, ukimbilie wapi wakati unayajua madhambi yako mwenyewe,” Kamanda Amata alikuwa akimwangalia Matinya aliyejaribu kujibadili sura yake lakini bado alijulikana na watu hawa.

    Matinya aligeuka na kukutana uso kwa uso na Kamanda Amata aliyekuwa kasimama huku mkono mmoja uko ndani ya gazeti. Hakuwa na la kufanya, mara hiyohiyo suruali yake ililowa kwa chini, akabaki akitetemeka. Kamanda Amata akanyanyua walk talk yake na kupeleka taarifa kwa wanaohusika. Matinya akaona hali mbaya, akataka kujaribu kujikoa kwa namna nyingine.

    “Risasi moja ilichimba udongo milimita kadhaa pembeni mwa kiatu cha Matinya,” Ukijaribu ujanja wowote ule siogopi kukuua, hayawani wewe! Na nakwambia utawataja wote hata kama siwajui, mlifikiri hili ni taifa la kuchezea kama mataifa mengine? Nitahakikisha unafika mbele ya sheria na kupokea hukumu yako, bila shaka ni kitanzi hata kama adhabu hiyo inapigwa marufuku duniani kote basi kitanzi chako kitakuwa kitanzi cha mwisho,” Kamanda akiwa katika kusema hayo tayari vijkana wa kazi walifika.



    “Mtieni pingu! Mnamuogopa kwa sababu bosi wenu? Huyu ni muhalifu kama walivyo wengine na leo atanye debe alikuwa hajui kuwa sheria ni msumeno?” Kamanda aling’aka kwa vijana wa polisi waliokuja eneo lile. Matinya akatiwa pingu na kuswagwa kama ng’ombe, akapakiwa ndani ya Land cruiser ya polisi, humo akakutana na Marina aliyekuwa amechoka kwa machozi. Alipomuona Matinya akiingia ndani ya gari hiyo Marina alishikwa na uchungu akamvamia matinya na kumuuma meno begani kwa hasira.

    “Una haki ya kufanya hivyo maana ulikuwa ukitelekezwa hivyo,” WP Magret alimwambia Marina huku akimtuliza kw kichapo kumlaza chini.

    Ilikuwa ni hekaheka ya waandishi wa habari kupata picha tamu za tukio hilo, kumhoji huyu na Yule ili kupata habari za kuuza na kuwajuza Watanzania ambao hawakuweza kufika hapo. Picha za televisheni, picha za magazeti hazikuwa haba katika hilo. Msemeji wa jeshi la polisi alikuwa kati wakati mgumu wa kukutana na waandishi kila nukta, huyu akitaka kujua lile na lile likitakiwa na huyu.



    §§§§§



    Kamanda Amata na Yaumi walichukuliwa na Gina mpaka kwenye gari aliyowaandalia na kuwahifadhi humo. Wakiwa wanaangalia hekaheka za wanausalama na waandishi wa habari katika hilo ilikuwa ni kama sinema. Kamanda Amata alimtazama Gina.

    “Asante Gina,” alimshukuru.

    “Karibu sana!” Gina alirudisha shukrani hiyo. Walitoka uwanjani hapo na moja kwa moja kuelekea mjini. Walipofika eneo la Mtava baada ya mataa ya Tazara Kamanda alimuamuru Gina kusimamissha gari, nae akafanya hivyo. Dakika moja kioo ch pembeni kikagongwa na mtu kana kwamba anabisha hodi. Gina akashusha kioo na kukutana na mtu asiyemjua.

    “Utatusamehe mara nyingine kwa hili,” Yule mtu akamwambia Yaumi huku akitoa kitu kama sox jeusi mfukoni mwake na kumvika usoni.

    “Elewa kuwa wewe umekwishanyongwa, subiri ufufuke siku ya tatu kutoka sasa kama ilivyoandikwa,” Kamanda Amata alimwambia Yaumi, kisha Yule mtu akamchukua Yaumi na kumuingiza kwe gari nyingine na kuondoka naye.



    Safari ya Kamanda na Gina iliishia katika ua wa kituo cha polisi kati. Vitu vyote katika makontena yale vilikuwa vimemwagwa chini, wakati wao walikuwa wakiishia nusu ya kontena Madam S aliwaambia washushe vitu vyote, lo. Nusu ya mwisho ya kila kontena kulipakiwa silaha za kutisha, silaha za kivita, RPG, mashine gun, shot gun, mabomu ya mkono, mabomu ya kutegwa kwa kutumia saa nay ale ya rimoti, mavazi ya kijeshi yeney kila kitu, redio za mawasiliano, mabomu ya machozi, vinyago vya kuzuia moshi wa sumu, buti za kijeshi, na kila dhana za kivita, kuilikuwa na pikipiki za kwenda kasi zilizofungwa mabomu na bunduki ndogo ndogo ambazo muendeshaji huzitumia kufanya maangamizi. Kila mtu alibaki mdomo wazi, ilikuwa ni shehena ambayo ingetumiwa vizuri na watu waliokomaa katika medani za kivita basi ingekuwa ni vita kubwa sana ndani ya nchi yetu. Walikuwa wanafikiri nini watu hawa?



    Madam S alimkubatia Kamanda Amata kwa furaha pale alipomuona tena.

    “Hisia zako zimelikomboa taifa, the black dog,” Madam S alimwambia Kamanda Amata.

    “Ni moja ya kazi zetu kila tuwapo, nikikusi lazima nikufuatilie,” Kamanda alijibu.

    “Mheshimiwa Sikotu ameamua kujimaliza mwenyewe,” Madam alimwambia.

    “Ana bahati kwa maana angepata hukumu mbaya mbela ya macho ya Watanzania,”Kamanda akajibu. Madam S alimtazama kijana huyo kwa tuo.

    “Yuko wapi Yaumi?” akauliza.

    “Yuko shamba kwa mapumziko na kila kabrasha analo yeye mwenyewe,” Kamanda Amata akajibu kisha wakaondoka pamoja na kuingia kwenye gari ya Gina.

    “AGI ofisi tafadhali,” Madam S alimwambia Gina.

    “Shilingi elfu kumi tu,” Gina alijibu kwa utani huku akiondoa gari yake. Moja kwa moja mpaka katika jengo la JM Mall ambako ndipo zilipo ofisi za kamnda Amata na katibu wake Gina.

    Walimkuta Chiba tayari akiwa pale.

    “Yeah lazima tujipongeze kwa kazi ngumu,” Madam S aliwaeleza, hakuna aliyejua nini kimeandaliwa hapo ofisini zaidi ya Madam S na Gina tu. Ndani ya kujipongeza huko kulikuwa na mazungumzo ya hapa na pale.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    §§§§§



    SIKU MBILI BAADAE

    MAHAKAMA YA KISUTU



    NI JENGO lile lile ambalo lilitumika kumhukumu Yaumi kunyongwa, leo hii Gabriel Matinya, Marina, Scogon, Mdumi, Chilungu na wengine kadhaa walifikishwa hapo kusomewa kesi zao ikiwemo ya mauaji, kuingiza silaha za kivita kinyume na sheria, uhaini na nyinginezo nyingi, wote waliunganishwa katika sakata hilo.

    Ilikuwa ni kesi ya aina yake, watu walijaa ndani na nje ya mahakama hiyo, palikuwa hapapitiki, polisi wa farasi na mbwa walitanda kotekote kuzuia vurugu yoyote inayoweza kutokea eneo hilo.

    Waandishi wa habari walijaa wa magazeti, redio na televisheni kila mmoja alikuwa akitaka kuhakikisha anapata picha nyingine nzuri ya kulipamba gazeti lake.



    Kamanda Amata, Chiba, Gina, na Madam S walikuwa eneo hilo katika hali ya kificho ili kuweza kufuatilia kila kinachoendelea. Kila mtu alionesha jinsi alivyokasirishwa na watu hao, wengine walipiga kelele watolewe ili wawapige mawe mpaka wafe kwa udhalimu wao.



    Hakukuhitajika ushahidi zaidi kwani mwanasheria wa upande wa serikali aliwasilisha, kwanza hundi zilizotumika kwa kumlipa muuaji wa ACP Chonde, Jaji Ramson na Kajiba. Uliwasilishwa ujumbe wa simu uliokuwa ukiagiza kuawa kwa Dr. Omongwe wa jeshi la Magereza. Hundi za rushwa kwa Jaji Ramson na Bw. Gomegwa, hundi hizo zote zilikuwa na saini moja na kitabu cha mtu mmoja ambacho benki ilithibitisha kuwa ni mali ya bwana Sikotu O. Sikotu aliyekuwa waziri, Kabrasha za uingizaji wa silaha hizo na vitu vingi sana vilivyotoa ushahidi kamili vingine hata Matinya mwenyewe hakuwahi kutegemea kama vinaweza kupatikana na kuanikwa hadharani. Picha za vijana walio mafunzoni huko misitu ya Uluguru nazo ziliwasilishwa mahakamani pamoja na mpango mzima wa kambi hiyo.



    Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo aliahirisha mpaka baada ya wiki moja, washitakiwa wote walirudishwa rumande katika gereza la Ukonga wakisubiri siku hatima yao.



    §§§§§



    “Tumewakamata, lakini bado watu wawili ambao wanatakiwa waungane na wenzao katika kesi hiyo,” Madam S aliwaeleza Chiba na Amata pamoja na wengine wachache waliojumuika katika kikao hicho, akanywa maji na kuendelea, “Bw Kadingi wa Kadingisa, kwake hii ni mara ya pili kushiriki katika jaribio hilihili, mwaka ule alitoroka lakini sasa lazima akaletwe, aje hapa ahukumiwe kadoiri ya matendo yake, pamoja na huyo mfadhili wao kutoka Oman.”

    Madam S alikuwa akiongea huku akizunguka meza ile kubwa waliyokuwa wameketi katika mtindo wa duara, ilikuwa kama mwalimu anayewafundisha wanafunzi wake juu ya jambo Fulani.

    “Sawa Madam, hilo limesikiwa na linafanyiwa kazi na ofisi yako makini kabisa inayotambulika kwa kazi zake nzito ndani na nje ya nchi. Lakini huyu mjane Yaumi tunamrudishaje uraiani ilhali watu wanajua kuwa amekwishanyongwa? Na mali zote wamemnyang’anya kwa kuwa ilidhaniwa kamuua mumewe?” Chiba aliuliza.

    “Haina shaka Chiba, Magazeti yataandika na redio zitaeleza ukweli kuwa Yaumi hakuua na yupo huru kisha atarudi uraiani kama raia wengine na ataendesha maisha yake kama mtu mwingine, kuhusu mali zake umepatikana waraka wa maandishi juu ya mali za kajiba zote zilizo ndani na nje ya nchi na huo waraka mwenyewe kajiba aliuficha pamoja na kabrasha hizi akautuma Uganda, hivyo waraka huo utafikishwa kwa mwanasheria na wote waliopora mali watanyanganywa na zitarudishwa kwa mwenyewe yaani Yaumi.” Baada ya Madam kusema hayo wote wakapiga makofi kwa maana walimuonea huruma sana mwanamke huyo.



    BAADA YA SIKU SABA

    MAHAKAMA YA KISUTU



    ILIKUWA ni siku nyingine ambayo iliwajaza watu palepale Kisutu kusikiliza kitakachojiri juu ya kesi hiyo. Tayari vyombo vya habari vilieleza wazi juu ya Yaumi na siku hiyo alijitokeza kwa mara ya kwanza hadharani akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

    “Usiwe na mashaka, upo huru” Kamanda Amata alimwambia Yaumi wakati akishuka kwenye gari kuingia mahakamani hapo kusikiliza kesi na pia kuwa kama mmoja wa mashahidi waliotakiwa kuzungumza siku hiyo. Kilikuwa ni kitu cha kuvutia kwani wengi walishajua kuwa amenyongwa lakini leo hii wamemuona tena Yule aliyeitwa muuaji, gaidi.



    Baada ya kesi kuahirishwa tena kwa mara ya pili watihumiwa walikuwa wakitoka mahakamani kuingia kwenye gari lao tayari kwenda rumande kwani hawakupewa dhamana. Wananchi wenye hasira walikuwa wakitaka kushambulia gari hilo kwa mawe kabla hawajatimuliwa na vikosi vya FFU.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati walipokuwa wakishuka ngazi za jengo hilo, Yaumi alikuwa akitembea polepole kwenye korido kuelekea nje akiongozwa na WP Magreth pamoja naye Kamanda Amata alikuwapo kama mita tano nyuma akibadilishana mawazo na Inspekta Simbeye. Mara kelele kubwa ikasikika upande wa nje wa jengo hilo na watu kutawanyika huku na huko. Kamanda Amata akasimama ghafla, “Yaumi,” akatamka na kukimbilia kule kwenye vurugu akiwa na bastola mkononi, alipofika alibabatizana na Yaumi aliyekuwa akirudi ndani.

    “Kuna nini?” aliuliza.

    “Ameuawa kwa risasi,”



    Kamanda Amata alifika nje na kushuhudia mwili wa Scogon na Chilungu ikiwa chini, damu zikivuja kwa kasi, wameuawa. Watu waliokuwa katika eneo hilo walitawanyika na kufanya duara kubwa kuacha ile miili ikiwa pale chini.

    Polisi waliokuwepo tayari walitawanyika na kuelekea kwenye jengo la jirani kwa maana risasi ile ilionekana imetokea upande wa juu wa ghorofa la Raha Tower.

    Chiba alikuwa wa kwanza kufika juu ya jengo hilo, hakukuta mtu, chini alikuta maganda mawili ya risasi, alipoyaangalitu aligundua ni AK 47 imefanya vitu vyake, ‘Bila shaka huyu ndiye muuaji wa Jaji Ramson’, alijisemea wakati akishuka kurudi chini.



    §§§§§



    Makaburi ya Kinondoni



    AKIWA katika suti nyeusi, akipambwa kwa miwani nyeusi huku kichwa akijiangushia mtandio mweusi, Yaumi alisimama mbela ya kburi la mumewe Kajiba T. kajiba lililokuwa bado lina maua mengi yalioshiria upendo wa wale waliokuja kumzika. Kushoto na kulia kwake walikuwapo watoto wake wawili. Siku hiyo naliipanga maalumu ya kufanya msiba wa mumewe kwa kuwa yeye hakuwa na nafasi hiyo. Dr Omongwe alikuwa ni mmoja aliyemsindikiza.

    Walikwenda watu wane tu, lakini alionekana mtu wa tano. Mwanamke aliyevaaa guo nyeusi juu yake kajizungushia mtandio mweusi vilevile kama Yaumi, alisogea taratibu na kuweka shada la maua juu ya kaburi la Kajiba. Yaumi alimtazama mwanamke huyo hakujua ni nani. Yule mwanamke baada ya kukamilisha zoezi hilo aligeuka nyuma na kujitoa ule mtandio wake wa kichwani na kubaki wazi akiwa na upara tu.

    “Fasendy!!!!” yaumi alijikuta akitamka jina hilo kwa mshangao mkubwa, hakuamini kama anayemuona alikuwa ni fasendy au mzuka wake.

    “Usishangae Yaumi, ila mwenyewe umeona kilichotokea mahakani siku ile, wale watu wawili ndiyo waliomuua mumeo, na mimi kama nilivyokuahidi nimewaua mbele ya macho yako, Scogon, ndiye alimpiga risasi mumeo baada ya Chilungu kumchoma visu, niliona mkanda wa video wa mauaji hayo, lakini sipendi wewe uushuhudie. Nafurahi nimetimiza nililokuahidi,” Fasendy alimaliza kusema hayo na kujitupia mtandio wake kama awali.

    “Fasendy, asante! Naamini ipo siku tutaonana,” Yaumi akamshukuru Fasendy, akaachia tabasamu pana.



    HATIMA



    Baada ya kila kitu kukamilika, Matinya alihukumiwa kunyongwa na wenzi wake wote walihukumiwa kifungo cha maisha jela.

    Ijapokuwa mhaini mmoja na mfadhili wa kundi hilo walikuwa bado kupatikana lakini wote walihukumiwa kifungo cha maisha siku yoyote watakapopatika wawe hai ama wamekufa.

    Yaumi alirudi uraiani, na kuendelea na maisha si katika nyumba ile ya Tabata Kimanga bali nyumba mpya ambayo ndiyo kwanza walipanga kuhamia na mumewe, alimilikishwa biashara zote za mumewe na kuendelea kuwalea na kuwasomesha watoto wake wawili, huku Mr Kyomukama akimsaidia kusomesha mmoja.



    Hiyo ikabaki stori ndani ya walioishuhudia, ikabaki simulizi ndani ya waliyoisoma na kuisikia. Ikabaki kumbukumbu nzito ndani ya Yaumi na watu waliomzunguka.



    §§§§§

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kamanda Amata, Chiba,” Madam S aliita kwa upole, kisha akaendelea baada ya kuona wote wako makini na kusikiliza, “Matinya kanyongwa, Sikotu kajiua mwenyewe, lakini tuna deni moja, kama Kadingi alikuwepo kwenye uhaini wa kwanza na kutoroka na mara hii kahusika tena na hatujampata je hawezi kufanya baya zaidi mara ya tatu?” akauliza.

    “Hilo neno Madam,” Chiba alijibu na Amata akaendelea kujimiminia kinywaji kama kawaida yake.

    “Kwa hiyo mnasemaje? Mi nataka kuwahi saa hizi,” Kamanda Amata akauliza mara baada ya kushusha glasi ile.

    “We mwenyewe unajua! Kamlete mhaini…”



    ««« MWISHO»»»»

0 comments:

Post a Comment

Blog