Search This Blog

Sunday 22 May 2022

MAUAJI YA KASISI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE



    *********************************************************************************



    Simulizi : Mauaji Ya Kasisi

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    HOLY FAMILY BASILICA

    NAIROBI

    HAKUNA mtu aliyeamini anachokiona mbele yake, kila aliyepita njia alitikisa kichwa na wengine kuangusha machozi. Polisi kutoka kituo cha kati cha Nairobi walikuwa hapo mbele ya kanisa hilo kubwa wakifanya uchunguzi wa hili na lile. Mwili usio na uhai ulikuwa umelala chini na majeraha makubwa kifuani yakiwa yameganda damu nzito. Hakuna asiyejua mwili ule ni wa nani, kila aliyepita alisikitika, wengine hata walighairisha safari zao za kazini, vilio vilitawala eneo lile. Kila mtu alionekana kuguswa kwa namna moja au nyingine na mauaji ya Kasisi huyu wa kanisa la Roman Catholic, Rev Fr Frederick Gichuru, hakuna aliyejua kwa nini na ni nani aliyetekeleza mauaji haya ya kinyama. Baada ya kumsachi hakuna cha ziada walichokikuta katika kanzu ya kasisi huyo zaidi ya rozari iliyokuwa mkononi mwake.

    “Bila shaka alikuwa katika sala zake za asubuhi” sauti ya kukwaruza kutoka kwa koplo Otholong’ong’o ilipenya sikioni mwa sajenti Maria Kariuki ambaye kwa muda huo alikuwa bado amepigwa na butwaa. Sajenti Maria alisikitika na kujutia nafsi yake, alijiona kama mwenye makosa mbele ya Mungu kwa kifo hicho.

    “Ndiyo, afande, daima asubuhi kabla ya misa makasisi wa kikatoliki huwa na wajibu wa kusali kwanza wao weyewe” Sajenti Maria alimjibu koplo Otholong’ong’o huku ukungu mzito ukimtoka kinywani mwake kuashiria baridi kali ya mwezi wa sita hapo Nairobi. Bado sajenti Maria alikuwa kajiinamia jirani kabisa na mwili ule akiuangalia kwa makini jinsi ulivyoharibiwa kwa risasi, maganda saba ya Colt 45 yalikuwa mkononi mwake, huku akiyarusharusha alijinyanyua taratibu na kuamuru mwili ule uondolewe na kupelekwa chumba cha maiti cha hospitali ya rufaa.



    EPISODE 01.



    Inspekta Simon Saitoti alimkazia macho sajenti Maria aliyekuwa ameketi mbele yake akiwa na jalada moja la khaki lililoandikwa juu ‘MAUAJI YA KASISI’, alionekana kama mtu ambaye haelewi anachoelezwa, alilivuta jalada lile na kuliperuzi kurasa zake chache kwa dakika kadhaa, kasha akainua macho yake kutazama ukutani ambako kulipambwa kwa picha ya muasisi wa taifa hilo, hayati Jomo Kenyatta.

    “Umesema paroko wa kanisa hilo hamjamkuta, sivyo?” Inspekta Saitoti alimtwanga swali sajenti Maria.

    “Ndiyo afande, na tulipowauliza masista walisema kuwa kawaida wanakuwa na zamu ya kufanya misa za asubuhi vigangoni, hivyo paroko alikuwa amekwenda kigangoni” Maria alijibu kwa ukakamavu wa kipolisi.

    “Ok, mauaji kama haya hayajawahi kutokea hapa kwetu hii ni mara ya kwanza, na naomba sana iwe mara ya mwisho, endelea kufanya uchunguzi wa tukio hili kwa kina ukishirikiana na koplo Otholong’ong’o na mnipe taarifa za kina, ili tuwatie mbaroni wauaji.”

    “Sawa afande” sajenti Maria alisimama na kurudi nyuma hatua mboli na kupiga saluti ikiwa ni kitendo cha kuonesha heshima kwa mkubwa wake kadiri ya nidhamu za kipolisi.



    * * *CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Kijua cha haja kililing’aza jiji kubwa la Nairobi, jiji lenye pilikapilika za kila aina katika ukanda wa Afrika ya Mashariki. Watu walionekana wakitembea na kuvuka barabara kwa haraka haraka kuashiria kuwa ukichelewa tu matatu itakugonga. Bado hali ya ubaridi ilikuwa ikiendelea na kila mtu alionekana kujidhatiti kwa hali hiyo.

    Kwenye kituo kimoja cha basi, mwanaume mmoja mrefu alikua amesimama akisubiri matatu, mara tu matatu moja ikafika na muziki mkubwa ndani yake, akaikaribia na kupanda ndani yake, mkononi alikuwa na mfuko wa plastiki ulioandikwa UCHUMI, bila shaka alikuwa akitoka supermarket, safari yake kwa matatu hiyo iliishia katika kitongoji cha Uthiru Kenoo barabara kuu ya kwenda Uganda. Kwa mwendo wa wastani alivuka kwa kupitia daraja kubwa na kufika upande wa pili wa barabara hiyo ambapo kuna biashara nyingi, aliliendea gari aina ya Hammer lililokuwa limepaki hapo, ndani yake hakukuonesha dalili yoyote ya kuwapo mtu, alifungua mlango kwa kidubwasha maalum na kuuweka ule mfuko katika kiti cha mbele kasha akatokomea kusikojulikana.

    Takribani nusu saa hakuna aliyeisogelea gari ile, mara akaja mtu mwingine mnene wa haja pamoja na mwanamke mmoja mrefu na mwenye mwii ulioumbika vizuri, wakaingia ndani ya gari ile na kujifungia milango.

    “Shit, washakosea tena” alisikika Yule mtu mnene akimwambia Yule mwanamke

    “Nini tena?”

    “Hawako makini na kazi yao, tunawalipa pesa nyingi lakini hawajui nini cha kufanya, nguruwe wakubwa hawa”

    “Kwani nini?” Yule mwanamke alizidi kudadisi

    “Ah, we yaache tu, hutakiwi kujua”

    “Aaa jamani, yani umelala na mimi umenambia vingapi mapaka hili usinambie?”

    “Mambo ya kazi haya, achana nayo”.

    Ile gari ilitiwa moto na kurudi mjini, hakuna ambaye angekaa bila kulitupia macho gari ilo ka jinsi lilivyo na uzuri wa aina yake na gharama yake ndiyo iliyotia kiwewe.

    Moja kwa moja gari ile ilisimama karibu kabisa na mtaa wa Koinange, mtaa unaosifika kwa machangudoa hapo Nairobi.

    “Nitakucheki usiku twende club” mtu mnene mwenye asili ya kihindi alimwambia Yule mwananmke na kumpa noti za shilingi elfu moja moja tano za Kikenya.



    * * *



    Askofu mkuu wa jimbo kuu la Nairobi, Mhashamu Gregory Julius Maina, akiwa ofisini kwake alishikwa na huzuni kubwa kwa habari ya mauaji ya fr Gichuru, alimlilia na kumuombea lakini hakujua ni nini hasa chanzo cha kifo hicho. Alitafakari na kuumiza kichwa, kasha akainua macho yake na kutazama jopo lile la makasisi lililokuwa mbele yake, kila mmoja alikuwa ama akiangusha au akijifuta machozi, ukumbi wa parokia ya Maria Consolatha katika eneo la Westland ulikuwa umetulia kimya kabisa kana kwamba hakukuwa na watu ndani yake.

    “Nawasalimu katika jina la Bwana” Askofu aliwasalimu makasisi wale wapatao kama mia mbili weupe kwa weusi.

    “Amen” waliitikia.

    “Nina masikitiko moyoni, kuwatangazia rasmi kifo ca kasisi mwenzetu padre Frederick Gichuru, paroko msaidizi wa parokia ya Familia Takatifu, kilichotokea leo alfajiri kwa kupigwa risasi saba za kifuani na kupoteza uhai papo hapo” alifuta machozi na kukaa kimya kidogo, kasha akaendelea “Tunalaani vikali kabisa mauaji haya yasiyo na sababu inayoeleweka, hatuna cha kusema zaidi ila sisi kama kanisa tunaiomba serikali na vyombo vyake vya dola vifanye kazi ya kuwatia nguvuni wote wanaohusika, na tunawaomba raia wema wanaojua tetesi yoyote ya kifo hiki kutoa taarifa polisi au hata kwetu ili kusaidia katika kupambana na kadhia hii. Zaidi ya yote Bwana awasamehe kwa maana hawajui watendalo. Ibada ya mazishi itafanyika keshokutwa katika Basilica la Familia Takatifu” alimaliza Askofu kutoa tamko kwa niaba ya kanisa, kisha kuwapatia Baraka na wote wakatawanyika.

    “Baba, pole kwa msiba” Kasisi mmoja alimsalimu paroko wa Basilica la Familia Takatifu ambaye msaidizi wake ndiye aliyeuawa asubuhi hiyo.

    “Tumeshapoa, Mungu mwenyewe anajua”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara gari ya polisi aina ya Land Cruiser iliingia katika viwanja vya kanisa hilo la Conslata, sajenti Maria alikuwa wa kwanza kuteremka, akiwa ndani ya suruali yake ya buluu na shati la buluu bahari alipendeza kwelikweli. Alifanya juu chini kumpata Padre Joe Smith, raia wa Marekani ambaye ni paroko wa Basilica lililotokea mauaji, alipompata alimuomba kuongea naye machache na wote wakaelekea katika ofisi ya parkia hapo Consolatha.

    “Pole sana baba kwa msiba, naitwa sajenti Maria kutoka kituo cha polisi cha kati Nairobi”

    “Asante, tumeshapoa” alijibu Fr Joe Smith kwa Kiswahili chake kinachopendwa na wengi hasa anapotoa mahubiri.

    “Wakati tukio linatokea, wewe ulikuwa wapi asubuhi hiyo?”

    “Mimi nilikuwa nimekwenda kufanya misa ya asubuhi kigangoni”

    “Siku hiyo ni wewe ulitakiwa uwende kigangoni?”

    “Hapana, kadiri ya ratiba siku hiyo haikuwa zamu yangu”

    “Enhe sasa ilikuwaje ukaenda?”

    “Fr Gichuru, usiku wa jana alinambia kuwa yeye hajisikii vizuri, hivyo angependa kubaki parokiani” alimjibu sajenti Maria ambaye alionekana kuandika vitu Fulani kwenye kitabu chake.

    “Je unafahamu lolote kama marehemu alikuwa na ugomvi na mtu, au hali yoyote tofauti iliyokuw katika maeneo yenu kama wachungaji?”

    “Kwa kweli katika siku hizi, kumekuwa na mambo ya ajabu kabisa, kuna watu walikuwa wanakuja sana pale parokiani na kuuliza mambo mengi kwa watoto watumishi, wakati Fulani tulimkuta mtu anapekua Sacristia, walipomuuliza akawachapa makofi.”

    “Mlichukua hatua gani?”

    “Niwaulize ninyi polisi, mimi nilipiga simu polisi na mkaahidi kuja kufanyia uchunguzi lakini bho! Sikuwaona”

    “Sawa, msaidizi wako alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote awe sista au mwingine yeyote?”

    Fr Joe alishtuka kidogo kwa swali hilo. Sajenti Maria akatoa tabasamu lake lisilo nahisia hata kidogo mbele ya watu.

    “Mbona umeshtuka baba?”

    “Eh nikikuuliza wewe kama una mahusiano na kasisi hautashtuka?” wote wakacheka kasha Joe akaendelea “Hakuna kitu kama hicho, kama kipo basi mimi sijui”

    “Haya, asante sana baba, kama nikikuhitaji nitakutafuta” wakapeana mikono na kuagana.



    Sista Rose alikuwa akibubujikwa na machozi mbele ya sajenti Maria.

    “Usilie Sista, ni maswali machache tu nataka kukuuliza”

    “Sawa afande”

    “Wakati mauaji yanatokea wewe ulikuwa wapi?”

    “Muda huo mimi nilikuwa natoka nyumbani kwetu naenda kuandaa misa kanisani…



    Ilivyokuwa

    …Ilikuwa yapata saa kumi na moja na nusu alfajiri, sista Rose alikuwa na zamu ya kwenda kuandaa misa, aliamka na kujiandaa, kisha akiwa ndani ya mavazi ya kitawa alitoka nje ya nyumba ‘coventi’ yao na kwa mwendo wa taribu na rozari yake mkononi alikatisha kauwanja kanakotenganisha nyumba yao na kanisa, mara alisimama ghafla moyo wake ulifanya paaah! Hakujua kwa nini, kwa mbali alimuona Fr Gichuru akiingia kwenye uwanja wa kanisa hilo akiwa kwenye vazi lake jeusi na kofia nyeusi yenye nyoya katikati, alivaa kikasisi hasa na si mara nyingi kuonekana kaika mavazi haya. Alikuwa akitembea taratibu na mara walikutana na sista Rose katikati ya uwanja, wakasalimiana kwa ishara lakini Fr Gichuru alibaki kasimama akimwangalia sista Rose, akamuonesha ishara ya kuwa ainamishe kichwa chake, sista Rose akafanya hivyo na Fr Gichuru akamuwekea mikono kichwani kumbariki, mara mwanga wa taa za gari ukawamulika kutoka getini, hakuna liyejua ni gari ya nani, Fr Gichuru akamuacha Sr Rose aendelee na shughuli yake yeye akaliendea geti…

    Sista Rose alikuwa kajibanza kwenye ua kubwa lililo karibu kabisa na mlango wa kuingilia sakristia, akiangalia kinachoendelea, baada ya mabishano mafupi kati ya Fr Giochuru na wale jamaa waliokuja na ile gari mara alishuhudia kasisi yule akianguka chini kwa kishindo na sauti ya kike iliamuru wengine kupanda garini na kuondoka kwa kasi. Sista Rose alibaki akitetemeka huku machozi yakimwagika na si kumbubujika, alishindwa afanye nini, awaamshe wenzake au aende kumsaidia Fr Gichuru, alikuwa njia panda hakujua afanye nini. Gari ile ilipoondoka alirudi nyumbani kwao akilia na kuwapa taarifa wenzake ambao wote waliamka na kwenda kuona tukio hilo kisha kupiga simu polisi na kwa paroko ambaye alikuwa ameenda kigangoni kwa misa ya alfajiri…



    “Poleni kwa msiba huo mzito” sajenti Maria alitoa pole akiwa na macho makavu kabisa, “Labda sista niambie, unaweza kukumbuka aina ya gari walilokuja nalo?”

    “Kwa kweli ni shida kulikumbuka kwa kuwa kulikuwa na giza na mi nilikuwa mbali kidogo” sista alijibu.

    “Kipi cha pekee unachokumbuka katika tukio hilo?”

    “Sauti ya mwanamke iliyokuwa ikimhimiza mwenzake kumaliza kazi, nilisikia wakitamka jina ‘Black Cheetah’” alimaliza na kutungua kilio.

    “Ok waweza kwenda tutakapokuhitaji tutakupa taarifa.



    * * *

    Black Cheetah, jambazi sugu linalotafutwa na polisi ukanda wote wa Africa Mashariki, linajikuta katika sakata jipya, sakata la mauaji ya kasisi. Kila mtu aliamini kuwa jambazi hilo si bure tu bali linatumia hata nguvu za giza kwa jinsi linavyoweza kuwatoroka polisi katika mazingira ya kutatanisha hata wenyewe kushindwa kujielewa inakuwakuwaje. Hakuna aliyekuwa halijui jina hili, si mtoto wala mtu mzima, jina la Black Cheetah halikuisha midomoni mwao.

    Sajenti Maria alishtushwa kusikia jina hilo likitajwa na sista Rose kuwa aliisikia sauti ya kike ikilitamka katika tukio hilo. Alitafakari akaona kibarua hicho si cha kitoto ni kucheza na mtu au watu waliokomaa kwenye taaluma.

    Black Cheetahm, kama anavyojiita ni kijana mtukutu, mkakamavu, muasi aliyetoroka katika kundi lao la M23 huko mashariki mwa Congo, aliyetokea kuwa jambazi sugu na tishio katika ukanda wote wa Afrika ya mashariki, alikuwa akikodiwa na matajiri wakubwa kutekeleza mauaji au wizi wa kutumia silaha. Mara kadhaa ameshahusishwa na wizi wa benki uliotokea Dar es salaam Tanzania miaka michache iliyopita, mlipuko wa bomu uliotokea Kampala wakati watu wakiangalia mpira na matukio mengi yaliyotukia huko Kenya ambayo hata hatuwezi kuyaainisha hapa, kwa ujumla alikuwa gaidi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwezi mmoja uliopita

    Ngong Hills Hotel-Nairobi

    Gari aina ya Hammer nyeusi ilisogea taratibu katika maegesho ya hoteli ya Ngong Hills, watu watatu, wanaume, wakashuka wakiwa ndani ya suti nyeusi zilizotanguliwa na shati nyeupe, mmoja kati yao mwenye mwili mnene alikuwa akitembea kwa msaada wa fimbo maalum, taratibu waliingia hotelini hapo na moja kwa moja wakaelekea sehemu ya chakula na kuchukua meza yenye viti vine na kuketi, kiti kimoja kilibaki wazi wakaagiza vyakula na vinywaji na kuanza maongezi yao. Maongezi yaliendelea na baada ya muda kidogo kijana mmoja aliingia mahali pale akiwa kavalia koti kubwa la bluu nyeusi akiwa na kofia kubwa aina ya pama, kwa hatua za maringo aliijongea meza hiyo, kila mtu alimuangalia kwa mwendo wake hususan camera za usalama. Alifika katika meza ile na kuvuta kiti kimoja kilichobaki kikimsubiri yeye, akaketi na kuiweka bilauri yake vizuri kabla ya kuimiminia kinywaji kilichokuwa hapo.

    “Yes, Cheetah…” yule bwana anaetembea kwa msaada wa fimbo alimkaribisha

    “Nimeitika wito wako, bwana Bill” Cheetah alijibu.

    “Vizuri, hawa ni wadau wenzangu ambao sote tumekuita ili tukupe kazi maalum” aliendelea

    “Nawasikiliza”

    “Kuna kazi ndogo tunataka utufanyie” alizungumza bwana Wambugu, akajikohoza na kuendelea “Tunataka kitu kinachoitwa Monstrance, kimehifadhiwa katika kanisa kuu la Familia Takatifu hapa Nairobi, of course ni kazi ndogo tu”

    “Hakuna kazi ndogo kama itahitaji kumwaga damu, hasa damu ya watu wasio na hatia” Cheetah alimjibu Wambugu

    “No! hatumwagi damu, ni kujua ilipo na kuichukua basi”

    “Unafikiri tutaipata kwa urahisi kama unavyofikiria? Maana ingekuwa ivyo basi hata wewe ungeenda pale na kuichukua, lakini kama umeniita mimi maana ni kwamba hiyo si kazi ndogo kwa vyovyote lazima vyuma vitaongea” Cheetah alimaliza kauli yake na kuinua bilauri iliyojaa kilevi na kujimiminia kinywani mwake baada ya kulishuighulikia pande la nyama lililokuwa ndani ya sahani hiyo.

    “Hilo nalo neno bwana Cheetah. By the way wewe utajua la kufanya, sisi tunachotaka ni Monstrance basi” alimaliza bwana Wambugu.

    “Ok, tusipoteze muda, mimi nitaunda kikosi kazi kitakachoweza kufanikisha kazi hiyo, lakini mjue kule ni kanisani, wale makasisi wana mazindiko yao, hivyo lazima mnipatie fedha iliyotakata”

    “Ha ha ha ha ha hilo usitie shaka bwanaaa bwana Cheetah” cheko la kivivu lilimtoka yule bwana anyetembea kwa fimbo, kisha akainua simu yake na kubofya namba kadhaa, punde tu vijana wawili waliingia pamwe na briefcase ndogo mkononi, ikawekwa mezani, kwa ishara ya mkono ya mkono yule bwana alimuomba Wambugu kuifungua, baada ya kuzungusha vijinamba Fulani mara yenyewe ilifyatuka kuashiria kuwa kilichopo kiljaa ndani yake kwa kukandamizwa hasa. Naam manoti yenye sura za Moi na Kenyatta yalipangwa na kubanwa katika mabandali kibao, Black Cheetah macho yalimtoka pima.

    “Ukifanikisha kazi basi hata briefcase hii ni mali yako” yule bwana alizungumza kivivu.

    Black Cheetah alitikisa kichwa juu chini juu chini kuashiria amekubaliana nao. Kwa kuanzia alipewa mabandali kadhaa katika mfuko wa plastiki. Waliagana wane hao na Cheetah akaondoka zake akiwaacha wao wakiendelea kutumbua mavyakula yaliyojaa mezani hapo.

    Katika maegesho ya magari, Cheetah aliisogelea gari yake na kusimama kidogo kisha akaangalia uku na huku, hakuona yeyote wala chochote cha kushuku, akaingia na kukaa nyuma ya usukani, milango ikafungwa na vyoo vyote vikabaki juu. Aliufungu ule mfuko wa karatasi na kuhesabu burungutu zile, si haba takribani laki mbili za Kenya, alikenua kwa furaha na kulazimisha tabasamu ambalo halikuendani na uso wake khasilan. Alitia gia na kuyaacha maegesho, baada ya kulivuka geti moja kwa moja aliningia barabara ya Ngong na kurudi katikati ya jiji la Nairobi.

    “Hivi unafikiri tutafanikiwa kuipata?”Wambugu alimwuliza yule bwana anyetembelea fimbo

    “Ha ha ha ha Wambugu unanichekesha sana, kazi iko kwa Cheetah lazima atararua mpaka tuipate, na tukishaitia mkononi yule Don kule Ujerumani atatukatisha kwa pesa nyingi, si ya kitoto” aliongea kwa sauti yake ya kivivu huku mdomoni akitafuna vyakula aina aina.

    “Don!” Wambugu alishangaa

    “Yeah, Don, anaitwa Don Fredrick Schurmann, ni tajiri sana katika mji wa Achen, yeye ndiye anayetaka hiyo Monstrance, amesema tukiifikisha mikononi mwake tutapata pesa nyingi sana, ha ha ha ha !” alimaliza kwa kucheka na kunyanyua bilauri yake iliyojaa mnvinyo wa Sant Raphael.



    * * *

    Katika bar kubwa ya Dagoreti Corner super pub, watu walijaa sana wakiburudika kwa vinywaji, nyama choma huku muziki laini wa The Mushroom ukisikika kutoka katika spika kubwa zilizozunguka eneo hilo. Hakuna aliyefikiria kesho kila mmoja alijiachia kwa starehe zake alizoziona kuwa zinamfaa, ilimradi siku ilipita katika mtindo huo. Katika kona moja ya pub hiyo watu watatu waliketi katika mtindo wa mzunguko mmoja wao alikuwa mwanamke walionekana kana kwamba wana mazungumzo mazito sana, hivyo hakuna mtu ambaye alisogelea eneo lile zaidi ya mhudumu wa pub hiyo, naye alikuja tu kuleta alichoagizwa na kuondoka zake.

    “Ndiyo vijana, kuna kazi ya kuifanya haraka iwezekanavyo” Cheetah alianzisha mazungumzo.

    “Tunakusikia mkuu” sauti pekee ya kike iliiitikia kauli hiyo.

    “Tunatakiwa kuchukua mzigo pale Holy Family Basilica”

    “Mapesa mangapi tukachukue?” aliuliza kijana mwingine aliyeketi hapo.

    “Siyo pesa Bwana Gichui, kuna kitu kinaitwa Monstrance, mnakijua?” Cheetah aliwauliza na wote wakatazamana.

    “Monstrance!?” Mellina Wanjiku alishtuka na kujishika kifua kwa mshangao.

    “Unashtuka nini, unaijua?” Cheetah aliuliza, na yeye alionekana kushtuka kidogo na kuanza kujiuliza kama kapokea mbuzi kwenye gunia safari hii.

    “Naijua Monstrance, ni chombo kitakatifu sana, kukishika kwa hila inaweza kuwa matatizo kwetu” Mellina alijibu kwa upole sana, akatulia kidogo kisha akaendelea “Pamoja na ujambazi ninaoufanya sikuwa kufikiri kuligeukia kanisa, kuna nini kwenye Monstrance hiyo?” aliuliza Mellina

    “Ah vile vitu vya wakatoliki huwa vinatengenezwa kwa dhahabu tu, itakuwa ndiyo wanayoitaka” alijibu Gichui.

    Black Cheetah alijikuta kwenye mtihani mgumu, kama kuna vitu aliviogopa ni miujiza ya Kimungu ambayo mara nyingi aliisoma kati vitabu vitakatifu, mtihani mkubwa! Alijiona amefanya ujinga kutokuuliza nini kilichomo katika monstrance hiyo, je kama wakizikuta nyingi ni ipi ya kuichukua, utata!

    “Cheetah!” aliita Mellina.

    Black Cheetah alishtushwa na wito huo kutoka katika lindi la mawazo, akawatazama wanakikundi wenzake ambao yeye aliona wangefaa kwa kazi hiyo lakini sasa walimfanya hata yeye kushikwa na wasiwasi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok, tunafanya kazi au hatufanyi tuchague moja” aliwapa mtego. Baada ya kutafakari mara mbili mara tatu wote waliamua kuingia kazini kuisaka hiyo monstrance.



    (monstrance ni chombo maalum kinachotumika kwa wakristo hasa dhehebu la katoliki katika ibada za Ekaristi Takatifu kama alhamis kuu na siku ya Ekarist, hutengenezwa ama kwa dhahabu au upakwa rangi ya dhahabu)

    “Ah vile vitu vya wakatoliki huwa vinatengenezwa kwa dhahabu tu, itakuwa ndiyo wanayoitaka” alijibu Gichui.

    Black Cheetah alijikuta kwenye mtihani mgumu, kama kuna vitu aliviogopa ni miujiza ya Kimungu ambayo mara nyingi aliisoma kati vitabu vitakatifu, mtihani mkubwa! Alijiona amefanya ujinga kutokuuliza nini kilichomo katika monstrance hiyo, je kama wakizikuta nyingi ni ipi ya kuichukua, utata!

    “Cheetah!” aliita Mellina.

    Black Cheetah alishtushwa na wito huo kutoka katika lindi la mawazo, akawatazama wanakikundi wenzake ambao yeye aliona wangefaa kwa kazi hiyo lakini sasa walimfanya hata yeye kushikwa na wasiwasi.

    “Ok, tunafanya kazi au hatufanyi tuchague moja” aliwapa mtego. Baada ya kutafakari mara mbili mara tatu wote waliamua kuingia kazini kuisaka hiyo monstrance.



    Miaka kumi nyuma… Al-hamis kuu 1996



    Kanisa la Holy Family lilishehani watu mapaka nje wakifuatilia misa takatifu ya alhamis kuu ambapo yalifanyika maadhimisho ya karamu ya mwisho. Hakukuwa hata na njia ya kupita kuelekea popote kila mtu alipo basi ni hapohapo.

    Katika madhabahu makasisi wapatao sita pamoja na baba Askofu walikuwa wakiendesha misa hiyo kubwa ambayo mwisho wake huwa inakuwa na maandamano ya kuhamisha mwili wa Bwana kuupeleka mahali pengine ili waumini wapate kuabudu. Watu waliketi kimya kumsikiliza baba Askofu Njue mara baada ya misa hiyo kuhitimika

    “Tuna furaha kuwatangazia kuwa mwaka huu tumepokea Monstarnce maalum kwa maadhimisho ya misa maalum. Monstrance hii ambayo ina historia kubwa katika kanisa ilitengenezwa miaka ya 1878 huko Tanzania katika abasia kubwa ya Wabenedictin iliyopo Peramiho. Na ilitolewa zawadi kwa Baba Mtakatifu Leo XIII na kuhifadhiwa pale Roma. Leo hii imeletwa hapa kwetu kwa ajili ya maadhimisho ya jubilee ya miaka mia moja ya Ukristu hapa Kenya. Na itahifadhiwa hapa mpaka tukio hilo litakapokwisha ndipo tutairudisha Roma” alimaliza maelezo yake na kujongea madhabahuni, akainyanyua juu ile Monstrance kubwa iliyokuwa iking’aa kwa rangi ya dhahabu hasa ilipomulikwa na taa zilizowekwa kwa umaridadi ndani ya kanisa hilo, kengele zililia na kisha maandamano kutoka nje ya kanisa yalifanyika mpaka kwenye kikanisa kingine kidogo, ikahifadhiwa hapo na kuacha watu wakipeana zamu za kufanya ibada usiku huo.



    1878

    Mahali Fulani huko Tanzania



    Vibarua wa wakolono walikuwa wakichimba mashimo makubwa kuingia chini ya milima iliyozunguka eneo hilo, huku wakiwa wamesimamiwa na askari hatari wa kijerumani. Kazi ilikuwa ngumu lakini walifanya hivyo hivyo, walitoa mchanga na kuuchekecha kwenye chekeche maalum na wale wazungu waliondoka na udongo walioutaka na kuingia nao katika chumba maalumu na kuuhifadhi.



    Katika milima ile baadaye kulijengwa majengo makubwa na yale mashimo yakawa ndani yake, kila kukicha wazungu wengi walikuwa wakiingia hapo, hawa wakisafiri na hawa wakifika ilimradi shughuli zilikuwa nyingi katika eneo hilo.



    Peter Schurmann alikuwa busy kugongagonga chuma kimoja kilichokuwa katika mtindo wa samaki, jasho lilimtoka mwili mzima lakini yeye hakujali aliendelea na kazi yake, na aliporidhika na kile alichokitengeneza alichukua kitu kama uji mzito wa moto na kumwagia ndani yake kisha akauacha upoe kwa muda. Alipokuja kutoa baadae alipata kituchenye umbo la samaki, akaketi na kuanza kukifanyia nakshinaksh. Hakika kazi ya mhunzi yule ilikuwa safi sana chombo kile kilikuwa kiking’aa sana hasa wakati ambapo kinapigwa na mwanga, kishapo akatengeneza mkitako safi kikubwa na kukiunganisha kwa chini ya chombo kile ili kiweze kusimama chenyewe na kweli ilikuwa hivyo, kisha wakakihifadhi katika kanati maalumu. Yake mashimo yaliyopo kule ndani yote yakafukiwa lakini kilibakishwa chumba kimoja ambacho hicho haruhusiwi kuingia mtu yeyote mpaka leo hii. Katika milima iliyozunguka walisimika vitu kama misalaba mikubwa na kuijengea kwa sementi kali sana ambayo si rahisi kuivunja kwa zana za kawaida tulizozizoea. Kile chombo baada ya kukamilika kilihamishwa na kupelekwa kwao.



    Chombo kile kilipelekwa huko Italia na kuhifadhiwa kati chumba maalum ndani kabisa ya kanisa la Mtakatifu Petro, Vatican. Chombo hicho kilichojulikana kwa jina la Monstrance kilitolewa mara moja tu kwa mwaka na daima kiliwekwa sehemu maalumu ambayo kila mmoja angeweza kwenda kuadudu huko.



    Wiki chache nyuma

    Jomo Kenyatta International Airport



    Rev. Fr Frederick Gichuru aliketi katika viti vya kupumzikia akisubiri muda wake ufike aingie ndegeni kuelekea Roma kwa kazi maalumu. Watu walikuwa ni wengi uwanjani hapo na kila mmoja wao alikuwa na safari yake, hakuna aliyefuatilia mwenzake anafanya nini au anataka nini.

    Tangazo lilisikika kwenye chombo cha kupaaza sauti kuwataka abiria wanaosafiri kwa ndege ya shirika la ndege la uswiss kuingia ndegeni tayari kwa safari. Pembeni ya Fr Gichuru alikaa mtu mmoja mnene aliyeshiba vizuri, inaonekana ndege hiyo yeye aliipanda kutokea Dar es salaam au Kilimanjaro, alimsalimia Fr Gichuru kwa kumpa mkono wake wa kuume.



    * * *CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Na baada ya ndege hiyo kuwa angani mazungumzo baina yao yalichukua nafasi. Mtu huyu mnene alikuwa akielekea Ujerumani kwa shughuli za kikazi na Fr Gichuru nae alikuwa akielekea Roma kwa shughuli za kikazi vilevile. Ndege ilipotua katika uwanja wa kimataifa wa Geneva, ndipo Fr Gichuru alipogundua kuwa yule mtu mnene mwenye sauti ya kivivu alikuwa akitembea kwa msaada wa fimbo. Waliagana na kila mmoja kuchukua njia yake.



    Akiwa kwenye gari iliyokuja kumchukua Fr Gichuru alididimia kwenye kisima kirefu cha mawazo, alijaribu kuyarudisha maongezi yale aliyokuwa akiongea na yule mtu mnene kwenye ndege, ilionekana alikuwa akifahamu vitu vingi labda katika kuzunguka sna nchi mbalimbali za dunia hii, lakini alishtushwa kwa jinsi alivyoizungumzia kwa tuo monstrance ile ambayo Fr Gichuru alikuwa akienda kuifuata ili kuileta Nairobi, Kenya.



    Baada ya itifaki zote za kikanisa kukamilika Fr Gichuru alikabidhiwa ile monstrance, aliitazama kwa udadisi na kuigeuzageuza ‘Kile ni chombo cha thamani sana, hata pale kilipo hakuna aneujua uthamani wake’, maneno ya yule bwana yalimrudiarudia kichwani mwake. Aliiweka juu ya kijimeza kidogo na kufanya ishara ya msalaba kisha akaitumbukiza kwenye kisanduku maalumu kwa kazi hiyo tayari kwa safari. Baada ya chakula cha jioni Fr Gichuru alikuwa katika mazungumzo na makasisi mbalimbali katika ukumbi maalum, wakibadilishana mawazo na pia akiwaalika katika adhimisho la jubilee hiyo.



    Fr Gustav Macker, alikuwa akizungukazunguka katika bustani ndogo iliyo karibu na lango kuu akiongea na simu bila kuchoka kwa lugha yao ya kijerumani, alionekana mara kama anatoa melekezo Fulani, wakati mwingine kama anajibishana na mtu kwa ukali. Alipomaliza alimuona Fr Gichuru akiwa tayari ameketi ndani ya gari akimngoja kwa safari ya uwanja wa ndege.

    “Oh Father, nilikuwa naongea na nyumbani kidogo, tunaweza kwenda?”

    “Ndiyo nipo tayari.”

    Fr Gustav aliondoa gari na kuelekea uwanja wa ndege, njia nzima hakuna aliyeongea na mwenzake, mara kwa mara Fr Gichuru alikuwa akistuka kila alipokumbuka mzigo alioubeba aliingiwa na giza la hofu.

    “Haya Father , mi nakutakia safari njema na Bwana akutangulie” Fr Gustav alimuaga Fr Gichuru, akamkumbati na kumpa mkono kisha yeye akageuza gari na kurudi alikotoka.

    Akiwa ndani ya ndege alikuwa akisoma kitabu chake cha riwaya ya ‘Msitu wa Solondo’ kilitungwa huko Tanzania, kilimvutia sana hasa alipojua kuwa kwa nini wazungu hupenda sana kudadisi mambo, alikuwa mara ancheka mwenyewe, mara anakunja uso, mara anajishika moyoni kuonesha mshtuko basi ilimradi riwaya hiyo ilimkamata vilivyo.

    Baada ya takribani masaa nane angani, ndege ya shirika la ndege la Uswiss ilikanyaga ardhi ya Nairobi na kujiegesha vyema katika maegesho yake. Watu walishuka mmoja baada ya mwingine na mwisho kabisa Fr Gichuru alishuka akiwa na kijisanduku kile mkononi mwake. Alilakiwa na paroko wake Fr Joe Smith na kumuongoza kuelekea kwenye gari aina ya Land Rover 110 Defender mali ya jimbo kuu la Nairobi. Wakati wanatoka pale uwanja wa ndege na kushika barabara kubwa ya kurudi mjini waliipita gari aina ya Hammer iliyokuwa imeegeshwa na mara tu ile gari iliingia barabarani. Ikiwa nyuma kama gari ya tatu hivi ilikuwa aikiifuatilia ile Land Rover 110.

    “Karibu sana Fr Gichuru, safari yako imekuwaje?”

    “Safari imekuwa nzuri sana, lakini kuna kitu Fr kinanitia mashaka sana”

    “Ooh kitu gani tena Fr?”

    Fr Gichuru alimsimulia mazungumzo yote aliyozungumza na yule mtu mnene kule kwenye ndege, juu anavyoijua ile monstrance na jinsio alivyomueleza mara ngapi amewahi kuiona na ni nchi tofauti tofauti na ameahidi kuja Nairobi katika adhimisho hilo la jubilee.

    “Ananitia mashaka sana, kwa nini kila inapokwenda na yeye anaenda, ni kipi kinamvutia?” Fr Gichuru alimuuliza Fr Joe

    “Inategemea kabisa, lakini labda anapenda kuiona inavyopendeza au ni Mkristo kwelikweli anayedumu sana katika imani”

    Walipokaribia katika geti la kanisa ile Hammer iliwapita kwa kasi na kusimama mbele sana. Fr Joe aliichukua monstrance ile na kuihifadhi katika chumba maalumu kilichopo ndani ya nyumba yao.



    2

    1961

    Munichen – Ujerumani



    “Ule ni urithi wa ukoo wetu, babu wa baba yangu alisema lazima tufanye juu chini tukauchukue popote utakapokuwepo” mzee wa zaidi ya miaka themanini alikuwa akiongea na mjukuu wake wakiwa shambani juu ya trekta aina ya Massey Furgasson.

    “Ha, kumbe eee!” Mjukuu wa miaka saba alikuwa akimsikiliza babu yake kwa makini sana.

    “Sasa, wewe mjukuu ndiyo unatakiwa ufanye kazi hiyo, wewe unaonekana mjanja sana”

    “Mimi, ah! Naogopa.”

    “Usiogope, muda ukifika utajua la kufanya. Ila mjukuu wangu wewe unapenda kufanya nini ukiwa mkubwa?”

    “Mimi ningependa kuwa mwanajeshi, nipigane vita.”

    “Ha ha ha ha Mjukuu wangu Gustav, vita si jambo jema. Unajua ni kitu gani nilikuwa nafikiria juu yako?”

    “Hapana niambie babu”

    “Wewe uwe Padre, uongoze kanisa, uchunge kondoo wa Bwana”

    “Ha! Nitakuwa nakunywa divai yote” mjukuu alimjibu babu yake na babu mtu alitungua kicheko kadiri ya mawazo ya mjukuu wake.



    Miaka michache baadae

    Munichen – Ujerumani

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gustav Macker alimaliza masomo yake na kujiunga na seminari kuu ya Mt Augustino iliyopo kati jimbo la Munichen, alikuwa mtii kwa viongozi wake na hata kupendwa na waalimu na walezi wake katika seminari yao. Alimaliza miaka mitano ya falsafa na baada ya kupata stashahada yake alichaguliwa kwenda mji wa Achen hukohuko Ujerumani kuendelea kusoma teolojia kwa miaka mingine mitano, alikuwa ni kijana mpole, mnyenyekevu na mtii kwa kila jambo, daima kila alipoonekana al;ikuwa katika hali ya unyenyekevu wa hali ya juu.

    Siku moja alitembelewa na mtu asiyemjua, baada ya mazungumzo marefu sana walifahamiana kuwa kumbe wao ni ndugu, na sasa huyu ambaye angetakiwa kumwita kaka alikuwa ni mtu mkubwa kwatika mji huo wa Achen.

    “Ndiyo, mimi ni Andreas Schurmman, baba yangu mimi mzee Ernst Schurmman alizaliwa tumbo moja na mama yako Angela Schurmman, wakati wa vita ya pili ya duni ndipo walipopoteza maisha katika mazingira tofauti na wewe ulichukuliwa ukiwa mdogo na babu yako aliyemzaa mama yako, mimi nililelewa na msamalia mwema tu mpaka nimekuwa hivi nilivo.”

    Gustav alitikisa kichwa juu chini kuonesha kuwa aliielewa hiyo safari ya maisha jinsi ilivyokuwa.

    “Umejuaje kama nipo hapa?”

    “Nina rafiki yangu ambaye ni mfanya kazi hapa ndiye aliyeniambia lakini hata yeye hajui kuwa mimi na wewe tuna undugu, ila mimi nilijua kwa kuwa ninalikumbuka jina hili Gustav Macker, karibu sana nyumbani uje unitembelee”.

    Baada ya mazungumzo yao waliagana na kila mtu kubaki na na hamsini zake, ‘Sasa ishu yangu itakamilika’, Don Andreas Schurmann alijiwazia wakati akiingia kwenye gari yake aina ya Mercedes Benz na kuuacha uwanja wa seminari hiyo.



    * * *



    “Hutakiwi kushangaa wala kushtuka” Don Andreas alimweleza Gustav Macker.

    “Sishangai kwa unachoniambia, bali nashangaa kwa nini babu aliweka utajiri huo huko?! Inatia uchungu”

    “Hapana babu yangu alikuwa na akili sana, alikuwa anatafuta mahali salama pa kuihifadhi siri ile ya utajiri kwa kizazi chake cha sasa” Don Andreas akajimiminia glass yake ya pombe kali na kusafisha koo kwa kujikohoza kidogo, kisha akaendelea, “Vatican, ni sehemu yenye usalama sana duniani, na si uongo. Mzee Peter Schurmann aliiweka pale siri ile ya utajiri mkubwa kwa ukoo wake. Sikia Gustav, utakapokuwa Padre nitafanya kila njia uhamishiwe Vatican ili ufanye uchunguzi ujue jinsi gani tunaweza kuipata Monstance ile irudi mikononi mwetu.”

    Gustav aliinama kwa sekunde chache akiangalia sakafu ile ya marumaru safi ambayo ilimruhusu kuiona taswira yake mwenyewe kwa jinsi ilivyokuwa safi.

    “Gustav!” Don aliita, “Usihofu, haya ni mambo madogo sana, na nina hakika tutafanikiwa na kuishi kifalme”. Maneno matamu ya Don Andreas yalianzisha mapigano ya nafsi na roho ndani ya kijana huyu ambaye kanisa liliridhia kumpa ukasisi miezi michache ijayo, ama kweli kwenye mkono wa Mungu hapakosi mguu wa shetani. Mazungumzo ya wawili hao yalikuwa marefu sana na mwishowe makubaliano yalifanyika na mpango mahsusi ukapangwa na tajiri huyo, Don Andreas, kama alivyojulikana.



    Baada ya miezi sita Gustav Macker alipewa daraja la upadre na kuwa kasisi rasmi katika kanisa Katoliki, hakuamini masikio yake alipopata taarifa kuwa kituo chake cha utume kitakuwa Vatican, katika makao makuu ya kanisa hilo.



    * * *

    Dagoreti Corner Super Pub



    Black Cheetah alinyanyuka na kusimama wima na wengine wakafanya hivyo hivyo.

    “Vijana tuingie kazini, tutengeneze pesa” Cheetah aliwaeleza wenzake na wote wakahafiki.



    Walipomaliza vinywaji hivyo waliliendea gari ya Black Cheetah aina ya Subaru na kupotelea mjini. Ilikuwa tayari majira ya saa nne usiku Subaru ile ilipoegeshwa katika maegesho ya viwanja vya Uhuru, wote wakateremka na kupotelea katika club kubwa inayojulikana kama Nairobi by night, humo starehe za aina zote zilikuwa zikipatikana, walijichanganya na wadau wengine wakisubiri mida yao ya kazi ifike ili wafanye wanalolihitaji.



    * * *

    Ilitimu saa sita ya usiku, Cheetah na wenzake walipoegesha gari yao karibu kabisa na jingo la kanisa hilo na kushuka.

    “Hivi nyie mnaosali, hiyo monstrance sijui nini huwa inahifadhiwa wapi?” Cheetah aliwauliza wenzake

    “Kawaida kwenye chumba cha kuvalia makasisi, ambacho huwa ni kanisani” alijibu Mellina wakati Gicui akiliangalia jingo lile kubwa lililojengwa kwa kuta nene ajabu likiwa katikati ya mji wa Nairobi.

    “Ok, nafikiri mmoja wetu aingie huko kwenye hicho chumba halafu wengine waangali usalama wa ndani na nje” Cheetah alitoa oda.

    “Sawa Cheetah!” Gichui aliitikia kama aliyekurupushwa usingizini.



    Dakika chache baadae Gichui alikuwa ndani ya wigo wa kanisa hilo akitalii hapa na pale, akiangalia hiki na kile, usiku mnene usio na mbala mwezi, aliifanya kazi hiyo kwa ustadi hata walinzi hawakugundua chochote, Mellina na Cheetah walibaki nje lakini kila mmoja upande wake, Mellina katika ulinzi wa nje na Cheetah akiwa makini na tayari kumuokoa Gichui kama itatokea la kutokea. Akiwa ndani ya wigo ule Gichui alitembea kwa uangalifu sana akichungulia kwenye vitundu vidogo vilivyojengewa kwenye ukuta huo wa kanisa, ndani aliona tu kataa kekundu kakiwakawaka mithili ya mshumaa, alikaangalia na kukumbuka kuwa pale huwa makasisi wanawekaweka vikombe Fulani, labda ni penyewe. Aliendelea na kutokea upande wa nyuma wa kanisa hilo, milango kadhaa ilikuwako hapo na yote imefungwa imara kabisa kwa vitasa vya kiitaliano, kila aliyoutikisa ulikuwa imara kabisa, akatoa funguo zake zinazofungua kotekote akatumbukiza moja na kujaribu ikagoma, akachukua nyingine akatumbukiza mlango ukakutii amri na kufunguka, akiwa na sox yake kichwani akaingia ndani ya chumba hicho ambako alikutana na makabati mengi ambayo yalimchanganya, kabati kubwa la mbele liliunganishwa na meza kubwa sana iliyofunikwa kwa Formica safi, akatulia na kuatafakari, kabati lipi hasa analolihitaji, kwake aliiona kazi hiyo ikiwa rahisi kabisa ni kiasi cha kufungua makabati tu na kubeba anachotaka kisha kuondoka. Alilijongea kabati hilo kubwa na kujaribu milango yake, ilikuwa wazi, ndani kulikuwa na nguo tu za ibada zinazotumiwa na makasisi....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    * * *

    Fr Frederick Gichuru, alishtuka usingizini, ndoto mbaya ilimsongasonga hata kuufanya moyo wake kwenda mbio, alikaa kitandani na kuitafakari ndoto hiyo hakupata maana, machozi yalimtoka, alipiga magoti mbele ya msalaba na kutulia kimya, baada ya dakika kadhaa alishtuka na kusikia kelele za mlango kama mtu anaufungua kwa kutumia nguvu, alisikiliza kwa makini na kukuguundua kuwa ulikuwa mlango wa Sakristia (sakristia ni chumba kinachojengwa pamoja na kanisa ambacho uhifadhiwa mavazi na vitu mbalimbali vya ibada), mlango ambao Gichui alikuwa akiufungua taratibu sana lakini Fr Gichuru aliusikia kwa kelele. Aliinuka na kuchuku kanzu lake zito jeusi ili kujistiri na baridi kali ya Nairobi, alienda mpaka chumba cha Fr Joe, akamkua mzee huyo anakoroma kwa usingizi mzito akaamua kumuacha, akatoka nje kuelekea kanisani kushuhudia nini kinafanyika, alishtuka na kusimama ghafla alipoona mlango wa sakristia uko wazi, alikibanza kwenye ua kubwa la yugiyugi lililomficha vizuri, ‘wanataka nini?’ alijiuliza asipate jibu, aliangalia lakini hakuona mtu kutoka, alivuta hatua ndogindogo na kuufikia mlango huo, akazipanda ngazi na kuingia ndani, aligeuka huku na huku hakuona mtu isipokuwa milango wazi ya makabati.

    “Tulia apo hapo, usijitikise” sauti ilitoka upande wa makabati ya nyuma.

    Fr Frederick alitulia na kunyoosha mikono yake juu kujisalimisha.

    “Wanaume wanapokuwa kazini wewe hutakiwi kuamka amka” Gichui alimwambia Fr Gichuru, Fr Gichuru aling’ata meno kwa hasira, hakujali kama mtu huyo ana silaha gain alishusha mikono na kugeuka na kutazamana na domo la bastola aina ya Smith and Wesson.

    “Wewe ni nani?” Fr Gichuru aliuliza

    “Usitake kujua” alijibiwa

    Fr Gichuru alimkazia macho Gichui, Gichui alijikuta akiishiwa nguvu na kushusha bastola yake.

    “Kwa nini mnataka kulidhulumu kanisa?” akauliza Fr Gichuru, “Nani aliyekutuma? Na mnataka nini?” kimya kilitawala kati yao, “Sema nitakusaidia, kazi ya kanisa ni kusaidia wahitaji na wenye shida, sema.” Gichui aliinua bastola yake tena na kuondoa kiguu cha usalama kuruhusu risasi ipande juu tayari kabisa kufyatuliwa.

    “Siogopi risasi, maana risasi itaua mwili lakini kamwe haiwezi kuuwa roho” Fr Gichuru alimueleza jambazi yule. Gichui alishusha pumzi bado akimnyoshea bastola kasisi huyo.

    “Sikiliza kijana, weak bastola yako mahali pake uende kwa amani, maadam sijakuona sura yako na hii itabaki kuwa siri yetu mimi na wewe tu,” Fr Gichuru alimaliza na kuanza kufunga makabati yake. Alipogeuka baadae hakumuona yule jambazi mahali pale, akafanya ishara ya msalaba na kurudi nyumbani kwake. Usingizi haukuwako tena mpaka kulipokucha.



    * * *

    “Uuuuh!” Gichui alipumua kwa nguvu baada ya kuingia kwenye gari yao akiwa na wenzake tayari kuondoka.

    “Tupe ripoti” Cheetah alitoa ombi kwa Gichui

    “Haaaa, siamini”

    “Huamini nini, umeona nini huko?” Cheetah alidadisi

    “Makabati makubwa na nguo za kasisi, sijaona monstrance”

    “Lakini Gichui unaonekana kuna kitu hutaki kusema” mellina alidakia kutokapale nyuma ya usukani alikpokaa.

    “Kanisani, si pa kuiba” alijibu, “Nimekutana na Kasisi Gichuru ana kwa ana pale kanisani” akaweka tuo kidogo na kuendelea “Nilijikuta naishiwa nguvu, sikuweza kufanya lolote, akaniruhusu kuondoka”.

    “We bwege kweli, ungembana huyohuyo akueleze” Meliina aling’aka.

    “Mellina mi nashindwa kukueleza, wale jamaa sijui wana dawa!” aliongea kwa mshangao Gichui.

    “Basi, tutarudi kwa nguvu mpya” Cheetah aliwapoza wenzake na kuondoka zao.



    “Una uhakika kuwa hiyo monstrance ipo huku?” Cheetah alimuuliza mtu mnene kwa njia ya simu.

    “Mi siyo mtoto Cheetah, najua na nina uhakika na hilo, hakikisha tunaipata” alijibiwa.

    “Maana jana tumefanya upekuzi mle kanisani hatukuiona” aliendelea kuongea Cheetah

    “hata kama haipo kanisani, lakini ipo maeneo hayo, fanya kila unaloweza uipate” alimaliza mtu mnene na kukata simu.



    “Sasa wajukuu, hapa kilichobaki ni kufanya mbinu zote kumteka Fr Gichuru tumbane mpaka atueleze maana yeye ndiye aliyeuleta ule mzigo” Cheetah aliwaelezawenzake na wote wakaafikiana na kupanga mikakati.



    * * *

    “Baba Joe, leo usiku nimeota ndoto mbaya sana hata nikaamka usiku kusali” Fr Frederick alimueleza Fr Joe walipokuwa mezani wakipata chai.

    “Ni nini tena umeota Fr?” Joe aliuliza

    “Ah, ndoto mbaya sana” alisema huku akitua slesi za mkate katika sahani na kuiinamia meza akitegemeshwa na mikono yake miwili. Fr Joe aliona matone kama matone ya maji yakidondoka juu ya meza hiyo.

    “Fr, ni nini, nieleze nikusaidie” Fr Joe aliinuka kitini na kulmuendea Fr Gichuru huku akimueleza maneno hayo, alitoa kitambaa chake na kumfuta machozi. Fr Gichuru aliinuka kitini pamoja na Fr Joe wakatoka nje kwenye kabustani kadogo na kutembeatembea wakiwa na rozali zao mikononi.



    “Fr Joe! Nililala kama kawaida mara baada ya masifu ya jioni, katikati ya usiku huo niliota nipo Roma makao makuu ya kanisa, nipo juu kabisa ya mnara wa jengo hilo, niliangalia chini palikuwa parefu sana, isingekuwa rahisi hata kuruka, sikuwa na msaada, nililia na machozi yangu yalikuwa ni machozi ya damu, yalitirirka na kulowesha kanzu yangu nyeupe lakini hayakufika chini bali yote yalituama kifuani upande wa moyo wangu. Nilimuona Malaika kasimama mbele yangu mkononi kashika kikombe, akanisogelea akanipa kikombe hicho ambacho ndani yake kulikuwa na divai nyekundu lakini cha kushangaza mlikuwa na risasi ndani yake, akanambia

    ‘Kunywa’, nikasita akanambia kuwa ‘yakupasa unywe’, nilikiangalia kikombe kile, mwsho nilikitwaa na kunywa, nilipomaliza tu nilihisi kizunguzungu na kuanguka kutoka juu ya mnara ule kuelekea chini, lakini kabla sijafika chini nilishtuka kutoka usingizini.

    Mara moja niliitafakari ile ndoto lakini sikupata maana yake, nikapiga magoti kusali, wakati nasali niakaanza kusikia kelele za mlango wa Sakristia ukifunguliwa, kelele zile zilikuwa kubwa mno hata kuyasumbua masikio yangu, nilinyanyuka na kuitwaa kanzu yangu kisha nikaja chumbani kwako nikakukuta umelala, nikakuacha na kwenda kungalia nini kinachotukia huko, lo! Fr Frederick alijishika kifuani na kukumbuka ahadi yake na yule jambazi ‘ibaki kuwa siri yetu’…”

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Oh Bill, aaaah, uuuuh” sauti ya kimahaba iliyoashiria kuwa viumbe hao wapo kwenye ulimwengu mwingine zilitawala chumba kimojawapo katika hotel kubwa inayojulikana kama Plazza Hotel iliyopo katikati ya jiji la Nairobi.

    Bill, mtu mnene alikuwa kitandani akipewa raha na msichana wa Kikikuyu kutoka North Kinangop, binti huyo alihakikisha anampagawisha mzee huyo mpaka ammalize kabisa, na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Bill alikuwa nyang’anyang’a kwa penzi alilopewa na msichana huyo aliyembeba usiku uliopita katika mtaa wa Koinange hapo hapo Nairobi kwa dau la kulipana dola za kimarekani, alimfurahia jinsi alivyomkatia kiuno kwa mitindo ya ajabu hata akafanywa kusahau adhma ya kumtaka msichana huyo kimapenzi.

    Rosemary Wangui alihakikisha anamkamua Bill mtu mnene mpaka tone la mwisho akiwa na lengo moja tu la kuchota madola yake yaliyojaa katika mkoba maalumu wa ngozi.

    Penzi la uongo na muda mfupi liliendelea katika kitanda cha hotel hiyo, hakuna aliyekiogopa kifo, baada ya kuona hawafaidi utamu wa maumbile yao ndipo walipokubaliana kutokutumia kinga ili kutiana hasara roho, hapo sasa ndipo mtu mnene alipoahidi donge nono kwa shughuli aliyopewa na msichana huyo aliahidi kufanya lolote kwa jinsi alivyopagawisha na mtu mnene, Bill.

    “Rose, you are so sweet baby!” Bill alitamka maneno hayo huku akijifunga taulo kuelekea maliwato.

    “Same to you my cock” Rose alimsindikiza Bill kwa macho wakati akielekea maliwatoni huku moyo wake ukimuenda mbio kwa kuuona ule mkoba wa Bill ulioshiba manoti. Dakika chache baadae Bill alitoka maliwato na kuketi juu ya kitanda na kuruhusu minyama ya mwili wake kutikisika kwa jinsi alivyojitupa hapo.

    “Rose!” Bill aliita

    “Yes, Sir!” Rose aliitika kwa adabu ya uongo.

    “Unauona ule mkoba wenye pesa?” Bill alimtupia swali Rose

    “Yeah nauona, vipi?”

    “Nitakupa ule mkoba kama ulivyo, na pesa yake ndani” Bill alizungumza hayo na kumwangalia Rose usoni, Rose hakuamini anayoyasikia kutoka mtu mnene, tabasamu pana lilichanua usoni mwa mrembo huyu, tabasamu la kuuaga umasikini, tabasamu la utajiri wa dharula.

    “Sijaelewa darling” Rose alisema kuonesha kuwa hajaelewa aliloambiwa.

    “Nini hujaelewa? Kwenye ule mkoba kuna dola za kimarekani nyingi tu, nahitaji kukupa wewe pamoja na mkoba wake kama ulivyo”. Rose alibaki kimya, kisha akafungua kinywa chake na kumwambia mtu mnene “Asante,” akamkumbatia na kukutanisha ndimi zao ambazo zilichukua muda kidogo kila moja kuonja ladha ya nyingine. Kisha Bill akamtoa Rose kinywani mwake.

    “Sikia, hakuna ujira usiyo na kazi kwanza” Bill aliongea, akainua glass yake ya pombe ya kirusia ‘Pushkin’ akapiga funda moja na kumtupia jicho Rose aliyejilaza kitandani na kuegamia upande wa mbele wa kitanda hicho kwa kutumia mto wa kulalia.

    “Nakusikiliza” Rose alimwambia Bill mtu mnene.

    “Unamjua huyu?” Bill alimuuliza Rose na kumpa picha ndogo iliyoonekana kwenye kioo cha simu yake kubwa, Rose aliipokea na kuiangalia kwa makini sana kisha akatikisa kichwa kuashiria ameifahamu.

    “Mmh! Namfahamu, kafanyaje?”

    “Namtaka huyu mtu nizungumze nae kirefu, na wewe nataka unifanikishie hilo”

    Rose alibaki midomo wazi, alimwangalia Bill mtu mnene hakummaliza

    “Kivipi?” akauliza

    “Nataka ufanye kila hila ya kike, umlete mahali halafu vijana wangu watawateka wote wawili ila wewe watakuacha nay eye tutamchukua kwa kuwa tuna shida naye” Bill alimueleza kinagaubaga, Rose alionesha woga sana katika hilo, alijifikiria kwa kina, pesa anazitamani, kulitekeleza hilo ni vigumu, ugomvi mkubwa kati ya nafsi yeke ulizuka haikuwa rahisi kwake kuuamua, alinyanyuaka kutoka pale kitandani alipokaa na kuvuta hatua chache kuelekea maliwato alipita mbele ya Bill akiwa mtupu kama alivyozaliwa, Bill alibaki hoi na kushuhudia jogoo lake likiinua taulo kuashiria network imerudi.



    3

    Sajent Maria na koplo Othorong’ong’o walibaki kutazamana hawakuwa na jibu sahihi juu ya mauaji yale, waliperuzi kwa pamoja faili lile walilokabidhiwa na Inspekta Simon Saitoti

    “Kwa maelezo ya Fr Joe, yule paroko, nafikiri tuifanyie kazi hiyo taarifa tuliyopewa” koplo Othorong’ong’o alimueleza sajent Maria aliyekuwa ameketi kwenye benchi huku akiwa na redio call yake mkononi.

    “Uko sahihi, lakini haya maelezo yangekuwa timilifu sana kama tungeonana na marehemu lakini haikuwa hivyo” sajenti Maria alionesha ugumu wa kazi ulipo.

    “Sajenti, hivi tukifanya uchunguzi kwenye mitaa ya vibaka kama Kawangware kule hatuwezi kupata habari yoyote ya huyu Cheetah, ili tupate kwa kuanzia?” koplo Othorong’ong’o aliuliza.

    “Unafikiri Cheetah kwa hadhi yake atakuwa anjificha kule ambako kila mara tunaenda kwa msako, kule wamejaa wahamiaji haramu koplo” sajenti Maria alimjibu koplo Othorong’ong’o, kisha kimya kifupi kikatawala.

    “Nafikiri litakuwa jambo la busara sana tukijaribu njia hiyo, ila twende kiraia zaidi ili tuchangamane nao kisha tuweze kupata habari yoyote inayoweza kutuanzishia game hii.” Walikubaliana kuingia mtaa huo jioni ya siku hiyo kujichanganya ili kupata lolote la kuanzia katika kesi hiyo iliyoonekana kuwatoa kijasho kidogo.’

    Walikubaliana kukutana baada ya muda kidogo wa mapumziko ambapo kila mmoja wao aliutumia kwa jinsi anavyojua yeye.



    ‘A Catholic priest murdered after returning from Rome’.



    Kilikuwa ni kichwa cha habari kilichosomeka juu kabisa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Daily Nation la siku hiyo, mwandishi wa gazeti hilo alieleza kwa kina habari hiyo aliyoifanyia uchunguzi wa kutosha na wa kuridhisha. Sajenti Maria alilishusha gazeti lile lililokuwa limeuficha uso wake na kulitua magotini pake na kuruhusu wazo moja lipite kidogo kisha akaendelea tena kuisoma habari ile iliyomsisimua sana kama riwaya tamu za Richard Mwambe, alipojiridhisha na habari hiyo aliandika vitu fulani katika kijitabu chake cha kumbukumbu kisha akalifunga na kuingia ofisini kwake ambako alimkuta koplo Otho’ amesinzia kitini, akamshtua na kumueleza juu ya gazeti lile kwa jinsi lilivyoandika kwa kina juu ya habari.

    “Sajenti, turudi kwa Fr Joe kwa mahojiano kidogo ili tujue kwa undani juu ya safari yake ya Roma na kama kulikuwa na uadui wowote na mtu,”

    “Positive, koplo” Maria alijibu na mara moja wakaelekea katika kanisa kuu la Familia takatifu kwa kazi hiyo.

    * * *



    “Marehemu Fr Gichuru hakuwa na mazoea ya kuhifadhi kumbukumbu sehemu? Ama kwa maandishi au njia yoyote ile?” lilikuwa ni swali kutoka kwa koplo Otho’

    “Yeah, alikuwa anaandika sana, daima alikuwa na diary yake” Fr Joe alijibu hukua akinyanyuka na kuingia kwenye chumba cha marehemu Fr Gichuru, kisha akarudi na diary ndogo mkononi mwake na kuiweka mezani, sajenti Maria aliichukua mikononi mwake

    “Fr, samahani kwa kukusumbua mara kwa mara lakini nafikiri ndani ya diary hii tunaweza kupata chochote kitakachotusaidia, kama unaturuhusu tuondoke nayo ili kuendelea na upelelezi”

    “Oh ninyi mpo kazini, usijali mama, nenda nayo ukimaliza kazi nayo uirejeshe kwa kumbukumbu hapa” Fr Joe aliwakabidhi ile diary na kuagana nao, akawasindikiza mpaka getini, walipokuwa wanaagana pale getini, mwanamke mmoja mnene lakini aliyeonekana ana mwili wa mazoezi akiwa kavalia sketi nyeusi, iliyobeba blauzi nyeupe na juu yake ikafunikwa na kijikoti cheusi, aliingia getini na kuwapita sajenti Maria na koplo Otho’ wakati wakiagana na Fr Joe. Jicho la sajenti Maria halikuondoka kwa yule dada aliyekuwa akitembea kwa mwendo wa wastani akielekea kanisani kulikokuwa kukiendelea na maombolezo. Baada ya maagano yale, sajenti Maria alirudi garini pamoja na koplo Otho’CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Koplo, umemuona yule dada aliyetupita pale?” Maria aliuliza

    “Nimemuona, halafu sura yake si ngeni kichwani mwangu” koplo Otho’ alijibu na kuongezea. Sajenti Maria alitulia kwa nukta kadhaa, akavuta kijidroo cha dashboard ya gari na kutoa kamera ndogo ambayo unaivaa kama saa mkononi, akateremka garini.

    “Nakuja koplo, Linda mkia wangu tafadhali” Maria alitamka hayo huku akiurudishia mlango wa gari ile na kurudi kule kanisani kwa kutumia njia ile aliyopita yule dada wakati huo akiivaa ile camera mkononi mwake. Ilikuwa ni hatua chache tu alimuona yule dada akiwa katikati ya watu akijipenyeza ili kupata eneo zuri la kumuezesha kujua kinachojir katika kanisa hilo ambalo lilijawa na waumini waliokuwa wakiomboleza kwa nyimbo na zaburi. Sajent Maria aliendelea kumuangalia kwa makini, alimuona akitoa simu yake na kuandika kitu kama ujumbe mfupi kisha kuirudisha kotini, na muda huohuo alijipenyeza tena kuelekea upande mwingine ndipo alipogongana kikumbo na sajenti Maria ambaye kwa uzoefu wake wa kazi ya kipolisi alikuwa tayari amekwisha mpekua kwa kumgusagusa.

    “Dada, we vipi? Mbona unagonga watu ovyo, huoni njia?” yule dada aliuliza

    “Samahani nilikuwa nasoma saa hata sikukuona, samahani sana” sajenti Maria aliomba radhi, kila mtu aliyekuwa pale aliawaangalia wanawake hawa. Sajenti Maria alikua amehisi kitu kigumu katika ubavu wa kushoto wa mwanadada yule na kwa uzoefu wake aligundua kuwa yule dada amehifadhi bastola katika ubavu wake, aliishusha saa yake machoni na kutazama kama picha aliyoipiga imetoka vizuri, akaridhika nayo kisha akajiondoa na kurudi garini.

    “Vipi?” koplo Otho’ aliuliza

    “Ah, clear, nina wasiwasi na yule dada, kwanza inaonekana ana bastola kiunoni mwake” Maria alijibu

    “Tumsubiri?”

    “Haina haja lumsubiri, huyo hapo anakuja, hakikisha hatumpotezi kwenye sight yetu.”

    Yule mwanadada alitoka getini na kupinda kushoto kwenye maegesho ya magari na kuingia kwenye moja ya magari yaliyopo hapo, na gari ile taratibu iliyaacha maegesho yale kuingia barabarani kuelekea upande wa Westland. Koplo Otho’ naye aliiondosha gari yao aina ya Peugeot 308, gari ya kisasa kutoka Uingereza, baada ya dakika kadhaa waikuwa kwenye foleni kubwa za Nairobi lakini macho yao yalikuwa makini kuitazama gari aliyopanda mwanadada yule isipotee. Kwa mwendo wa taratibu walikuwa katika barabara ya Mombasa kisha wakaiacha ile iendayo Nairobi central na wao kuifuata ile gari aliyokuwa sasa imekamata barabara ya Waiyaki kuelekea Westland, baada ya mwendo kidogo ile gari ilikunja kulia na kufuata barabara ya vumbi iliyoingia katikati ya nyumba zilizojengwa kwa mpangilio mahsusi kama quarter za shirika Fulani, Otho’ nae aliingia na gari yake kuifuata, sasa ailibaki gari mbili tu mbele aliyopanda yule dada na nyuma ya kina koplo Otho’ na sajenti Maria…



    Otho’ aliegesha gari yake mbele kidogo karibu na duka kubwa lililokuwa likiuza bidhaa muhimu kwa binadamu. Sajenti Maria alishuka kutoka katika gari na kutembea taratibu kuelekea kule aliko yule mwanadada, Otho’ alibaki kwenye gari akiangalia kwa mbali tukio hilo. Yule mwanadada aliongeza mwendo kidogo alipogundua kuwa anafuatwa, alitembea huku akitoa simu yake ya mkononi na kuongea na mtu Fulani, sajenti Maria aliona tayari kagundulika kama anamfuata huyo mwanadada, na yeye alitoa simu yake na kwasiliana na Otho’ ili amlinde katika hilo. Otho’ aliiacha gari pale dukani na kufuata ule mtaa kama mtu aliye na shughuli nyingine kabisa, kwa mbali alimuona sajenti Maria kasimama akitazamana na yule mwanadada, kati yao kulikuwa na nafasi kama ya mita mia moja hivi, Otho’ alimpita sajent Maria na kumsalimu kama hamjui huku akiendelea upande ule aliko yule mwanadada na alipomfikia alimsalimu vilevile na kuendelea na safari yake na kumpita yule mwanadada, baada ya mwendo kama wa mita hamsini alikunja kona na kusimama kuona nini kinaendelea.

    Sajenti Maria alibaki akitazamana na yule mwanadada kila mmoja akiwa na simu mkononi, mara nyuma ya Sajenti Maria ulisikika mlio wa pikipiki, Sajenti Maria alipogeuka nyuma kuipisha pikipiki ile alichelewa, dereva wa ile pikipiki alimgonga Maria na kumuangusha chini, sajenti Maria alijaribu kujiinua lakini kabla hajakamilisha zoezi hilo aligongwa tena eneo la mbavu na kuanguka chini, kisha yule muendesha pikipiki aliteremka na kuiegesha ile pikipiki huku ikiwa inanguruma na taratibu alimfuata sajenti Maria pale chini, alimtazama kwa dharau na kupandisha juu kile kioo cha kofia ngumu aliyoivaa.

    “Wewe ndiyo unajua kufatilia nyendo za watu siyo?” alimuuliza huku akimsogele karibu zaidi. Sajenti Maria alimwangalia kwa hasira mpaka uso wake ulipoteza kabisa ile haiba ya uanamke, yule jamaa alipomkaribia alichuchumaa ili kumsaili vizuri sajenti Maria, kwa kushtukiza sajenti Maria alirusha teke la nguvu lililotua katikati ya mapaja ya yule jamaa na kupiga sawasawa sehemu zake za siri, yule jamaa kabla hajajielewa teke lingine lilitua upande wa kulia wa shingo yake na kumpeleka chini, sajenti Maria alijiinua kwa haraka na kusimama kidete na kumuacha yule jamaa akiwa chini. Yule mwanadada alipoona mchezo ule wa kiufundi kutoka kwa sajenti Maria aligeuka ili apotee eneo lile, lakini hamad alijikuta akitazamana uso kwa uso na bastola ya Othorong’ong’o, alisimama ghafla na kujikuta hana la kufanya, Otho’ akatoa pingu zilizokuwa mifukoni mwake ili kumfunga yule mwanadada.

    “Weka mikono yako nyuma!” alimuamuru ili amfunge pingu hizo, yule mwanadada akaishikanisha mikono yake nyuma ya mgongo akiwa anatazamana na Otho.

    “Geuka” Otho alimuamuru, na yule mwanadada aligeuka na mkononi mwake tayari alikuwa na bastola amabayo aliificha upande wa nyuma kwenye sketi yake, aligeuka na kufyatua risasi iliyoenda na kupiga mguu wa Otho, yowe la maumivu lilimtoka Otho huku akiiachia bastola yake ikidondoka chini, sajenti Maria alichanganyikiwa afanye nini akiwa bado katika kuhamaki pikipiki nyingine ilitokea nyuma ya Otho na yule mwanadada akaidandia katika kiti cha nyuma, sajenti Maria alirusha risasi kwa bastola yake lakini hakuweza kupata shabaha nzuri kwani ile pikipiki ilikuwa imekwishakunja kona na kumuacha Otho akiwa chini mguu ukivuja damu, aligeuka kumwangalia yule mwenye pikipiki ya kwanza lakini hakumuona pale badala yake watu walianza kujaa eneo lile, sajenti Maria akavua shati lake alilovaa juu na kumfunga koplo Otho jeraha lake ili kuzifanya damu zisiendelee kumwagika kisha akajitahidi kumyanyua kutoka pale chini akisaidiwa na watu wachache walifanikiwa kumfikisha kwenye gari, sajenti Maria aliwasha gari na kuondoka eneo lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku mbili

    kabla ya mauaji ya Fr Gichuru

    Mtawa wa kike alikuwa amesimama katika kituo cha matatu akisubiri usafiri kuelekea mjini, kila mara alionekana akiiangalia simu yake, huku akiwa na kikapu mkononi alionekana kama anayekwenda sokoni. Mara gari moja Land Rover Defender ilikuwa ikitoka katika geti la kanisa hilo na kukunja kulia kuelekea mjini, ikasimama jirani kabisa na mtawa yule.

    “Sista, twende nikusaidie” ilikuwa ni sauti ya Fr Gichuru akimpa lifti yule mtawa, alipokwishakuketi sawia kitini waliondoka kuelekea upande wa mjini na Fr gichuru alianzisha maongezi.

    “Sista safari ya wapi saa hii?”

    “Nakwenda Kileleshwa estate, kusalimia jamaa kwani leo nina ruhusa kutoka kwa mama mkuu” yule mtawa alijibu.

    “Ooh, vizuri kuwatembelea ndugu siku mojamoja” Fr Gichuru alimueleza huku akiwa anakaribia katikati ya jiji la Nairobi

    “Ila kwanza nataka kwenda pale shule ya msingi Nairobi, ningeshukuru kama unganisaidia kufika pale maana usafiri wa kwenda kule ni mgumu” yule mtawa aliomba huku akimlegezea macho Fr Gichuru. Siku zote kumnyima mwanamke ombi lake siyo rahisi sana, Fr Gichuru aliiacha barabara kubwa na kuufuata barabara ndogo inayopita katika majumba ya watu kuelekea huko shule ya msingi, alipoyamaliza majumba na kuteremka kibonde kidogo kuliendea daraja ili kuvuka na kutokea upande wa pili, alikuta mtu aliyeanguka na pikipiki.

    “Oh God!” yule sista alihamaki, Fr Gichuru akasimamisha gari akataka kushuka kwenda kumsaidia yule jamaa aliyeanguka.

    “No usiende Fr ni hatari, huwezi jua nini kilichopo huko chini” Sista alimbembeleza Fr Gichuru, lakini haikuwa rahisi kwani moyo wa huruma wa kikasisi ulimsukuma kushuka.

    “Hapo hapo ulipo tulia” sauti ilitoka nyuma ya gari yake, alipogeuka alikutana na mtu aliyeshika bastola akimnyooshea yeye.

    “Nini tena jamani? Mbona sielewi kinachoendelea?” Fr Gichuru alilalamika

    “Tulikuwa tunakusubiri wewe na tunashukuru huyo sista wako amekuleta mahali pema peponi” yule jambazi alizungumza, “Haya haraka ingia katika gari iyohiyo siti ya nyuma” aliamuriwa, na bila kubisha alijipakia ndani yake na nyuma ya usukani yule mtawa aliyepewa lifti alikuwa tayari nyuma ya usukani kwa kuondoka.

    “Ha! Sista!” Fr Gichuru alipigwa na mshangao alipomkuta yule sista tayari ameketi kwenye usukani.

    “Aliyekwambia mi sista ni nani!?” alijibu yule mtawa huku akitoa kilemba chake kichwani na kuruhusu rasta zake ndefu kumwagika mabegani “Mimi nilikuwa nakutafuta wewe, naitwa kahaba Rose” alijitambulisha. Fr Gichuru alivalishwa soksi usoni ili asione anapopelekwa na safari ilianza. Mwendo wa muda kadhaa waliisimamisha ile gari na kumshusha Fr Gichuru kisha wakachukua gari nyingine na kuitelekeza ile ya mission palepale eneo la Madaraka estate pembeni mwa barabara ya Mbagathy, kisha wao wakaendelea na safari yao kuelekea barabara ya Mombasa na mpaka karibu na kiwanda cha saruji cha Bamburi na kupinda kushoto kuelekea kwenye eneo la viwanda, moja kwa moja waliingia kwenye godown kubwa na kumteremsha Fr Gichuru.



    Ndani ya chumba kidogo chenye vikorokoro vingi walimuhifadhi akiwa amefungwa kamba kwa nyuma.

    Yule mwanamke aliyejifanya mtawa alimvua ile soksi usoni na kumuacha huru akiweza kuona kwa mbali kutokana na giza lililotanda ndani humo.

    * * *

    “Kazi uliyonituma nimeimaliza, nipe changu” Rose alimwambia mtu mnene walipokutana tena katika chumba chao kilekile katika Plazza Hotel.

    “Usijali, mzigo wako upon a asante kwa kazi nzuri, lakini ole wako uitoe siri hii, nakuua” Bill mtu mnene alimpatia pesa nyingi kahaba Rose na kuagana nae.

    “Asante Bill” alishukuru huku akitoa machozi, machozi yenye pande mbili, furaha ya kukamata pesa nyingi ambazo hajawahi kuzishika maishani, na uchungu wa kumsaliti kasisi asiye na hatia. Alitoka na kubamiza mlango nyuma yake, moja kwa moja akaiendea lifti na kuteremka chini kabla ya kupotelea mitaani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bill akiwa na swahiba zake waliingia katika gari aina ya hammer na kuelekea kumuona mateka wao mioyoni mwao wakijua kazi imekwisha.

    Ukimya ulitawala katika lile godown isipokuwa kweny kijichumba kimoja kimoja tu ambako Fr Gichuru alikuwa akisali kwa kilatini kwa sauti tulivu ambayo kama ungekuwa karibu na dirisha lake ungeisikia vizuri tu.

    Mara mlango ulifunguliwa kwa ghafla na watu sita waliingia ndani ya kijichumba kile. Fr Gichuru aliendelea na sala yake kana kwamba hakuna mtu aliyeingia humo ndani.

    “Mmmh Sali sana tu mpaka milango ifunguke!” sauti hiyo ilimshtua Fr Gichuru na kuinua macho yake juu na kugongana na yale ya ya Bill mtu mnene

    “Bill!” aliita kwa mshangao

    “Unashangaa nini? Habari za Roma?” Bill alimuuliza Fr Gichuru

    “Nzuri tu, habari za ulikokwenda”

    “Salama tu Fr, leo tumeonana tena, sina mazungumzo mengi na wewe leo ila ninachohitaji ni ile Monstrance, tuambie ilipo tukaichukue usiku huu kisha tutakuachia huru, mimi sipendi kumwaga damu isiyo na hatia kama yako Reverent Father Frederick Gichuru” Bill aliongea kwa pozi huku akiruhusu pumzi zake kumtoka kwa shida. Fr Gichuru alimtazama mtu huyu mnene na kisha kuwatazama wale wengine watano, mara moja akamtambua Gichui, yule jambazi waliyekutana naye kanisani akipekuwa makabati.

    “Muulizeni huyu kama ameiona” alimueleza Bill huku akimtazama Gichui, “Ile ni mali ya kanisa ninyi mnaitakia nini?” akawauliza. Wote wakatazamana.

    “Gichuru, kama hutaki kutueleza utataulazimisha kufanya kitu tusichokitaka, haya mi natoka nawaacha vijana wangu utawaelekeza” Bill mtu mnene alizungumza na kutoka katika kile chumba akifuatiwa na wengine wawili, pale ndani wakabaki watatu. Cheetah na wenzake walimuadhibu vikali Fr Gichuru kwa mapigo makali sana kumlazimisha aseme, lakini Fr Gichuru hakufungua mdomo wake badala yake alikuwa akisali kwa kilatini ambacho wale jamaa hawakuelewa kitu. Mateke ya tumboni, mbavuni, mikanda ya kijeshi vyote vilikuwa ni masluub kwa Fr Gichuru.

    Lakini baada ya kumtesa kwa zaidi ya lisaa limoja Fr Gichuru alipoteza fahamu kabisa na kulala kama mfu.

    “Amekufa?” Mellina aliuliza

    “Hajafa huyu kazirai tu, lete maji baridi” Wambugu alimueleza Mellina, ndoo ya maji ikafika na kummwagia mwilini Fr Gichuru, akashtuka na kuhema kwa nguvu, akawatazama wale watesi wake mmoja baada ya mwingine.

    “Baba uwasamehe maana hawajui watendalo” baada ya kusema maneno hayo alianguka na kupoteza fahamu kwa mara nyingine…



    Kwa mbali alisikia mlango ukifunguliwa, ilikuwa ni ndoto tamu iliyomfariji moyo, alimuona Malaika akija pale alipolala na kumfungua zile kamba. Haikuwa ndoto kiuhalisia, mlinzi wa godown lile aliingia kwa kunyata ndani ya kile chumba kidogo alimfungua kamba na kumbeba mabegani mwake Fr Gichuru aliyekuwa hana fahamu na kujaribu kutoroka nae, alipita kandokando ya magari mabovu ili walinzi wenzake wasimuone kasha kwa kutumia kijimlango kidogo cha nyuma alitoka nje huku akiwa kambeba fr Gichuru kwa mtindo ule ule, baada ya mwendo mfupi alimuhifadhi katika nyumba ndogo jirani tu na eneo hilo, kasha yeye akaenda zake tena lindoni kwake, hakuna mtu aliyemgundu kwa hicho alichokifanya aliingia tena kimyakimya na kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

    Baada ya masaa machache Fr Gichuru alirudiwa na fahamu zake na kujikuta mahali tofauti na mwanzo, alijitazama na kujikuta hana zile kamba mikononi, yuko huru isipokuwa maumivu makali katika maeneo ya tumbo na mbavu yalikuwa yakimsumbua, hakujua ni jinsi gani amefika eneo lile, alijaribu kuinuka kutoka pale alipokuwa amelala, akaketi na kuegemea kabati kuukuu lililokuwa ndani ya kijichumba hicho na kushusha pumzi ndefu alipogundua kuwa hapo kwa vyovyote ni mahali salama. Akiwa katika tafakari hiyo alisikia nyayo za mtu zilizokuwa zikipitapita huku na huko upande wa nje, akajituliza kimya na kubaki kusubiri kuona ni nani huyo; mara kelele za mlango ambao bawaba zake zimekosa mafuta zilisikika na mlango ule uliacha kijinafasi cha kupenya mtu mwembamba, na punde tu mtu mmoja alijipenyeza na kuurudishia huo mlango nyuma yake.

    Kutoka ndani ya koti lake alitoa mfuko wa plastiki uliondikwa UCHUMI na kuuvirigua kisha akatoa kachombo ka plastiki na kufungua mfuniko wake.

    “Father, kula chakula, najua una njaa sana” yule mtu alimwambia Fr Gichuru. Ndani ya kichombo kile kulikuwa na chakula aina ya mokimo (mchanganyiko wa maharage, mahindi na viazi kisha husongwa kama ugali), Fr Gichuru alikula na kunywa maji yaliyokuwa jirani hapo bila kuangalia yana hali gani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kumaliza kile chakula, akajiweka vizuri na kumtazama yule mtu, sasa akagundua kuwa alikuwa ni mzee sana lakini bado likuwa na nguvu zake.

    “Wewe ni nani?” Fr Gichuru alimuuliza



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog