Search This Blog

Sunday 22 May 2022

HUJUMA - 4

 







    Simulizi : Hujuma

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    §§§§§

    “Usishtuke Kamanda, ni mimi,” yule mtu akamwambia, kisha akaanza kuvuta hatua za haraka haraka kuelekea moja ya majengo yaliyokuwa hapo mtaani, memgi yalionekana kama magofu tu kutokana na mapigano ya muda mrefu ya wenyewe kwa wenyewe, yaliachwa mahame. Aliingia ndani kufungua mlango mmoja uliochoka akampa ishara Kamanda aingie, naye akafanya hivyo. Kilikuwa ni chumba kidogo chenye kitanda na kiti kimoja, zaidi ya hapo hakukuwa na kitu chochote ndani yake.

    “Fasendy!” Kamanda aliita, alikuwa haamini kama mwanamke huuo kayaokoa maisha yake.

    “Ndiyo mimi Fasendy, lazima nilipe fadhila uliyonifanyia kule Uganda,” Fasendy alijibu huku akijiketisha kitandani, “Sikiliza Kamanda, fanya mambo yako yote lakini hakikisha unakuja kulala hapa na si vinginevyo, hapa ni sehemu salama sana kuliko kwingine kokote, mahoteli yote yamewekwa watu wanakusaka, kila kona unasakwa, kwa sababu shughuli uliyoionesha ndani ya haya masaa sabini na mbili imewashtua maharamia, wamejipanga upya,” Fasendy alimuasa.



    “Umejuaje yote hayo?” Kamanda akauliza.

    “Aaaah Kamanda, nafahamu mengi sana kuhusu hili swala unalolifuatilia ambayo wewe na serikali yako hamjui …” kabla hajamaliza sentensi yake, Amata akampiga swali, “Ina maana unajua Jamir alipo?” akauliza.

    “Kamanda, ndugu yako Jamir yupo hai lakini katika hali mbaya sana na hivi tunavyoongea kesho wamepanga kumuua ili na kutuma viungo vyake kwenu Tanzania,” Fasendy alijibu.

    “Wapi yupo nikamwokoe? Pamoja na wale ishirini na tano,” Kamanda akauliza kwa shauku kubwa, alipata nguvu za mapambano baada ya kujua kuwa Jamir bado yuko hai.

    Fasendy aliinama kichwa chini hakujua la kujibu, “Sikia Kamanda Amata, najua Jamir yuko hai, lakini huwezi kuamini kuwa sijui kafichwa wapi.”

    “Ok, lazima nijue alipo, kabla ya jogoo kuwika kesho alfajiri niwe naye mikononi mwangu na nijue wengine wako wapi, wacha wayachukue hayoi makombora lakini hawa binadamu ndiyo wa muhimu kwanza,” Kamanda aliongea kwa utulivu, “Asante kwa kuniokoa,” akanyanyuka.

    “Unaenda wapi?” Fasendy naye akanyanyuka na kusimama mbele yake.

    “Naenda Jazeera Palace, nataka kumjua aliyeweka mwili wa Hassna kwenye gari ile ni nani,” Kamnda alieleza.

    “Amata, unahatarisha maisha yako, nimeshakwambi kila hoteli hapa inatazamwa sasa wewe unataka kujitoa tena mzima mzima,” Fasendy alilalamika.

    “Hapana, muda hausubiri mtu, nina mengi ya kufanya, kama ni kufa wacha waniue sasa ama zao ama zangu,” Kamanda akamshika Fasendy mabegani, “Niache niende, tuonane hapa usiku wa saa 2 mi na wewe.” Akampita.

    “Kamanda!” Fasendy akaita, Kamanda Amata akageuka kumtazama mwanamke huyo, “Uwe mwangalifu sana hawa jamaa ni hatari,” akamsisisitizia.



    Kamanda Amata akatoka na kurudisha ule mlango akamwacha Fasendy ndani, akatokomea mitaani kwa hadhari kubwa ili asionekane ovyo. Kando ya barabara alikutana na kijana aliyekuwa akiuza vitu mbalimbla, Amata akanunua kofia aina ya cap na miwani ya jua, akaendelea na safri yake mpaka kituo cha tax.

    “Jazeera palace,” akamwambia yule kijana naye akaondoka na kwa kasi. Dakika tano tu alikuwa mbele ya hoteli hiyo, akateremka na kulipa ile tax, kisha kwa kuzunguka nyuma ya hoteli hiyo alifanikiwa kuingia kwenye korido za maofisi mbalimbali, alipishana na watu bila kujulikana mpaka kwenye ofisi ya usalama, akafungua mlango na kuingia ndani bastola mkononi.

    “Tulia, sitaki fujo,” kawapa amri vijana wawili waliomo ndani ya chumba, akawatoa vitini na kuwaweka chini kisha akaiendea mashine ya inayorekodi matukio ya kila siku, akarudisha nyuma mpaka saa 5:22 asubuhi ya siku hiyo. Akatazama kwa makini tukio lile.

    Vijana watatu walifika karibu kabisa na gari yake, wakafungua buti ya gari yao n a kutoa kitu kilicho katika mfuko mweusi, mwili wa mwanadamu, wakautia kwenye gari ya Amata. Kamanda Amata alijaribu kutazama sura za wale vijana, akaziweka akilini, kama kuna kipajai cha ajabu ambacho Amata alipewa ni kukariri vitu vingi tofauti kwa wakati mmoja, alihifadhi zile sura na baadae akajaribu kuinasa namba ya ile gari akaipata, akaamu kuingia msakoni. Wakati alipokuwa akitaka kutoka, alimkuta kijana mmoja kati ya wale akiwa anabofyabofya kitu kama simu ndogo, Amata akamwangalia yule kijana kwa jicho baya, akachomoa bastola na kumnyooshea.



     “Nakuua, niambie ulikuwa unawasiliana na nani?” akauliza Kamanda akiwa kakunja ndita usoni mwake, akakinyakua kile kidubwana na yule jamaa akataka kujifanya anajua, akamshika suruali Amata, konde zito la upande upande likatua shavuni mwake na kumtoa jino, akaendelea kujifanya mbishi, teke kali likapiga usoni mwake yule kijana akajigonga vibaya kisogo chake ukutani, akatua chini akiwa kimya. Kamanda Amata akatoka na kuufunga mlango kwa nje kisha akatokomea pasipojulikana.

    Alikuwa katikati ya mji, jua kali likiwaka, Kamanda Amata alitembea kwa haraka haraka, alipofika anapopahitaji, alatupa macho yake huku na kule akahakikisha usalama upo, akaingia kwenye mlango wa chuma wa nyumba hiyo akatulia tuli, ukimya ulitawala nyumba yote, nyumba ya Hassna, hakukuonekana dalili ya mtu, akiwa na bastola yake mkononi, alivuta hatua za taratibu huku akiangaza kwa umakini kuona kama kuna hatari yoyote, sebule ilikuwa nyeupe, hakuna mtu. Aliendelea mpaka chumbani, alisukuma mlango wa chumba cha kwanza, akatazama huku na kule, hakuna mtu, akakiacha chumba hicho na kukifikia kile cha Hassna, akasukuma mlango kwa nguvu kwa mguu wake, akatulia na ukimya ukamfuatia, akaingia kwa mnyato, akatupa macho yake kwa ufundi kabisa huku revolver yake ikiwa mkononi imeshikwa kwa umakini wa hali ya juu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chumbaq kilikuwa shaghala baghala, vitu vilikuwa vimetawanyika huku na huko, akajua kwa vyovyote kabla ya kifo cha Hassna lazima kuna purukushani kubwa ilifanyika, Kamanda Amata akasogelea kabati kubwa lililokuwa pembeni, kioo chake kilikuwa kimepasuka vibaya na kumwagika chini, damu zilionekana katika mbao ya kabati hilo, kwenye kijimeza kidogo kilichounganishwa na ile meza ya vipodozo kulikuwa na picha moja kwenye fremu, ilitulia ikiwa haijui nini kiliendelea, Kamanda Amata akaiendea na kuiiunua akaitazama sura ya Hassna iliyojaa katia fremu hiyo ndogo, akaibusu, kisha akatoka taratibu na kukiendea chumba alicholala usiku uliopita, mlango ulikuwa wazi. Akashusha pumzi, akaiweka bastola yake vizuri na kuingia kwa ghafla akajirusha mpaka kwenye kona ya chumba alipoinua jicho tu alikutana na mtu aliyetoka katika mlango wa bafuni kwa kasi akimwendea pale chini, pole sana , akampa pole ya kimoyomoyo, wakati tayari ile bastola mkononi mwake ilikuwa imebanja na kumfumua bega, yule mjinga akajibwaga chini damu ikitoka kama maji. Kamanda Amata akahakikisha hakuna mwingine mle ndani, akamwende na kumkanyaga kwa nguvu pale kwenye jeraha.



    “Kwa nini mmemuua huyu mwanamke?” akamwuliza.

    Yule bwana hakujibu, badala yake alikuwa katoa macho, “Sema!” Kamanda aling’aka na kuukandamiza mguu wake kwenye jeraha kwa nguvu zaidi, “Nani aliwatuma?” aliuliza tena.

    “Sh.. sh…sharon,” akajibu kwa taabu huku damu zikizidi kumwagika. Kamanda A,ata akachutama karibu yake, “Nitampata wapi?” akamwuliza.

    Kwa taabu sana yule mtu akasema, ““Jidka Dabaqayn, 512,” kinywa chake kilionekana kama kinataka kuongea kitu lakini kilishindwa, kikainamia upande mwingine, andipela.

    “Shiit !” Kamanda akajikuta akiropoka, akamwacha yule mtu na kusimama wima akimwangalia pale chini, Jidka Dabaqayn 512 akajisemea moyoni na kujiondoa taratibu kwenye ile nyumba. Akatokea mlango wa nyuma aliopitishwa asubuhi na Hassna, akatokea uwani, moja kwa moja akaelekea mahali palipowekwa turubai kubwa ambapo palikuwa pamefunikwa pikipiki kubwa sana aina ya Honda cc 350, akaliondoa lile turubai na kuitazama ile pikipiki kubwa, Hassna naomba nitumia chombo hiki ili nilipe kisasi kwa wakati kwa wabaya wako, akasema kimoyo moyo huku akiitazama ile mashine.

    Hakuwa na muda wa kupoteza aliitikisa na kuchungulia kwenye tenki, mafuta yalikuwepo, akaliwasha na kuliacha hapo kwa muda kadhaa kabla ya kuliondoa.



    §§§§§

    “Mi sielewi kabisa mnavyoniambia eti yule sheitwani amewatoroka,” Shalabah alikuwa akiongea kwa hasira, “Mtu mmeshamuwekea mtego na akakamatwa na polisi, ilikuwa ni kumfumua risasi ya kichwa tu.”

    “Shalabah, hapa mi naona kuna hujuma inayofanyika, humuhumu miongoni mwetu kuna msaliti ambaye anajua wazi yule jamaa alipo lakini anampa maelekezo  kutokla kwetu,” akajibu mtu mwingine.

    “Ndiyo, ndiyo, hata mimi nimeliona hilo,” mwingine akadakia.

    “Nani huyo niambieni sasa hivi ni lazima apate adhabu kali, tumeshapoteza watu wengi mpaka sasa, na alipofikia sasa atagundua siri nyingine nzito ambayo hatuko tayari yeye kuijua, nani anatuhujumu? Nani?” Shalabah alikuwa mkali.

    “Mwanamke uliyemkodi kwa ajili ya kumuua huyu shetani ndiye anayetuhujumu,” akajibu yule kijana. Shalabah akanyamaza kimya, hana la kusema, akakaumbuka tukio la Fasendy kuipiga risasi bahasha ya kamanda Amata mkononi badala ya kumuua na kusingizia alitingishwa.



    “Sasa mkaniletete Fasendy, namchinja mbele ya macho yenu, yuko wapi kwanza?” Shalabaha akahoji.

    “Tulikuwa naye Sierra 5 kabla ya kubadilishana lindo lakini hata hivyo kuna wakati aliondoka na hatukujua alienda wapi.

    “Fasendy,” Shalabah akasema kwa sauti ndogo huku akionekana wazi hasira kuutawala moyo wake, kifua chake kikipanda na kushuka kwa hasira, akapumua kwa nguvu, akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake ya mkononi akabofya namba Fulani nakuiweka simu sikioni.



    §§§§§

    Kwa mwendo wa taratibu, Kamanda Amata alipita nyumba moja baada ya nyingine akisoma vibao vilivyoning’inizwa milangoni kuonesha namba za viwanja, ilikuwa ni barabara kubwa inayopita katikati ya majumba ya kifahari yaliyotengwa huku na huku, bila shaka ulikuwa ni mtaa wa wazito, Jidka Dabaqayn. Moyo wake ulipiga kwa nguvu alipokutana na kibao chenye namba 512 ambazo chini yake kulikuwa na picha ya mapanga mawili yaliyowekwa mtindo wa X akajua amefika kwani alielewa nini maana ya alama hiyo. Akaegesha pikipiki lake nje na kuusukuma mlango, ulikuwa wazi akaingia kwa hatua za taratibu.

    SHARON aliinama kwenye sinki lililo pembezoni mwa meza yake ya chakula, alijitazama kwenye kioo kilichowekwa juu kidogo ya koki za bomba la maji lililofungwa katika snki hilo. Mshtuko mkubwa ulimpata, kwenye kioo hakuona taswira yake peke yake, alikuwa na mgeni aliyesimama nyuma yake. Akashusha pumzi kwa nguvu, akafikiri cha kufanya, aliwahiwa. Kamanda Amata aliyeonekana usoni kuwa na hasira alisimama bila kuzungumza akimtazama mtu huyo anayeitwa Sharon.



    Sharon aligeuka kwa ghafla ili amashtukize Kamanda, ndipo alipokutana ngumi nzito ya mbavu zake kutoka chini, akatoa mguno wa maumivu. Kabla hajatulia konde linguine lilitu kwenye korodani, Kamanda alikuwa bado kachutama chini wakati alikuwa akimkwepa Sharon. Sharon alilia kama mtoto huku mikono ikiwa imejishika sehemu nyeti. Kamanda Amata aliinuka kutoka pale na kujirusha mwa mtindo wa frying kick, na guu lake la kulia likapiga upande wa shavu la Sharon na kumpeleka chini akiangukia meza ya chakula na kusababisha ivunjike vibaya, Sharon alikurupuka na kunyanyuka haraka, kama mtu aliyezinduka usingizini, akainua kiti cha mbao na kumrushia Kamanda Amata, lakini kikapigwa kwa usatadi na mguu wa Amata kikatupwa pembeni. Kabla Sharon hajafanya lolote, makonde mazito mfululizo yalitua katika pande tofauti za mashavu yake, Sharon akavunjika taya.

    “Kwa nini mmemuua Hassna? Ana kosa gani kwenu?” akamuuliza

    “Alikuwa jeuri hataki kutuambia ulipo,” akajibu kwa ujeuri huku akivujwa na damu sehemu mbalimbali.



    “Mashetani wakubwa nyie, sasa mtanitambua mi nani,” kamanda alipokuwa akimaliza kusema hayo, Sharon alirusha teke lililopiga sehemu ya tumbo ya Kamanda, akapepesuka na kujipiga nyuma ya kochi, kabla hajajiweka sawa, Sharoni alikuwa tayari amejiweka sawa mkononi mwake akiwa na nusu kiti kilichovunjika, Kamtiga nacho Amata lakini kabla hakijamfikia Kamanda akageuka na kumpa mgongo, kile kiti kilitua mgongoni na kuvunjika tena, Kamanda Amata akageuka haraka na kumpa dhoruba ya ghafla, karate mbili za nguvu zilizotua shingoni mwake zilimlegeza, kabla akili haijamkaa sawa, alipigwa mapigo ya judo na kumfanya asijitambue, akajibwaga chini kama gunia.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sharon, udhalimu haulipwi,” Kamanda alimwambia huku akiichomoa bastola yake aina ya magnum 22, bila huruma alifyatua risasi na kuvunja goti la Sharon, kilio cha uchungu kilimtoka Sharon.

    “Maswali yangu ni matatu tu, yuko wapi Jamir na wale wengine ishirini na tano? Nani mnayemfanyia kazi? Nani anayewapa siri kutoka Tanzania?”

    Badala ya kujibu Sharon alibaki kujiangalia jeraha lake pale mguuni lilivyokuwa likitoa damu.

    “Nakuuliza wewe!” Kamanda aling’aka na kumkanyaga kwa mguu wake pale gotini.

    “Aaaaaaaiiiiggghhhrrrrr!!!!” Sharon alilia kwa uchungu, “Unaniumiza bwana,” akapiga kelele.

    “Kumbe wewe unaumia ila unawaumiza hawaumii, jibu maswali yangu haraka,” alimuamrisha huku akinyoshea bastola katika mguu mwingine.



    “Yaani we braza huna hata huruma wewe, binadamu gani wew…” kabla hajamaliza sentensi yake, teke moja kali la nguvu la mguu wa kulia lilitua katikati ya uso wa Sharoni na kumpeleka sakafuni.

    “Nasema, nasema,” akalalama.

    “Sema, haraka!” kamanda alipiga kelele, huku sura yake ikiwa imejikunja ndita, lakini bado  Sharon alikuwa mbishi, Kamanda Amata akarudisha bastola yake kiunoni na na kuchomoa kisu kidogo chembamba, akamchoma pajani.

    “Aaaaaiiiiiggghhhhhh! Basi basi nasema, aaaaaa weweeeee, nasema kila kitu, na- na- na- ssseeeemmmma” alipiga yowe la uchungu.

    Kamanda Amata alaitikisa kidogo kile kisu kikiwa bado ndani ya nyama, “Jamir yuko wapi?” akauliza.

    “Yupo yupo, yupo kule,” akajibu kwa taabu sana huku akiugulia maumivu.

    “Kule wapi?” Kamnda akauliza.

    “Bandani, bandani, yuko bandani, mzima hajafa,” Sharon akajibu.

    “Bandani ndo wapi? Nijibu,” kamanda akaendelea kuhoji, akakisukuma kidogo kile kisu.

    “Aaaaiighhhh, basi baaassssssssiiiii, niache nitasema,” akakohoa kidogo, “Kiwanda cha cha nguuuuoo,” akajibu kwa taabu huku mwili ukimtetemeka, macho yake yakianza kupoteza nguvu, damu ikimwishia mwilini.



    “Nani unayemfanyia kazi, nani bosi wako?”

    “Mr. Shalabah, Mr. Shal…” kabla hajamaliza, Kamanda Amata alimwachia ghafla na kujitupa pembeni, risasi iliyopigwa kutoka dirishani kwa minajiri ya kumuua Amata ilikosa shabaha nakupiga katikati ya paji la uso la Sharoni, akajibwaga na kutoa yowe la mwisho la kuagana na roho yake. Kamanda Amata kwa kasi ya ajabu alichomoa kisu na kuruka nacho huku akikirusha kwa ustadi sana kumuelekea huyo aliyefyatua risasi ile, alisikia mfurulizo wa risasi na kisha kimya kikatawala. Amata akasonya akiwa tayari na bastola mkononi, akainuka na kutazama dirishani, hakuna mtu, kakimbia? Alijiuliza, akatazma mezani akaona simu ya Sharoni ikiwakawaka akainyakuwa na kuitia katika mfuko wa shati kisha akaliendea dirisha, na kumkuta mtu akimalizia kukata roho, huku kile kisu kikiwa kimechoma katikati ya moyo wake na kuuzuia usifanye kazi.

    Akaitazama saa yake ilikuwa inakimbilia saa kumi alasiri, akatoka kwa mwendo wa haraka haraka na kukwea pikipiki yake, akaondoka eneo lile. Baada ya mwendo wa dakika kama tatu hivi akasimama na kuichomoa ile simu mfukoni, akaifyatua na kutazama simu zilizopigwa, simu ya mwisho kabisa ilikuwa imeandikwa Chief akaitazama namba ile na kuipiga kisha akaweka sikioni.

    “Hey Sharon, mbona hupokei simu kaka?” Shalabah alilalamika bila kusubiri hata salamu.

    “Jaribu kuwaheshimu marehemu Chief,” akajibu Kamanda Amata.



    §§§§§

    Wakati Sharon akipata kichapo kutoka kwa Kamanda Amata huku akibwabwaja siri, Shalabah au Chief alikuwa akiendelea na kikao cha dharula na wapiganaji wake, aliipokea simu akijuwa ni Sharon anayepiga, alishtuka kusikia sauti nzito asiyoijua.

    Shalabah aliitoa simu sikioni na kuitazama kwenye kioo, alijua labda kuna makosa katika kuitambua simu hiyo, la, ni yenyewe ya Sharon.

    “Unasemaje?” akauliza baada ya kuiweka tena sikioni.

    “Heshimu marehemu sio unaita ‘Sharon!’ ita marehemu Sharon,” Kamanda alijibu kwa nyodo na gadhabu.

    “Ina, inn-a maana Sh- shar- Sharon amekufa?” Shalabah alipata kigugumizi ghafla.

    “Bado wewe kabla jogoo hajawika, nitaitwaa roho yako,” Kamanda alizidi kumchanganya Shalabah.

    “Kwani we nani?”

    “Ninyi mnamtafuta nani? Mimi ni Amata Ric, Kamanda Amata, Tanzania Secret Agency namba moja,” alipojitambulisha akakata simu.

    Shalabah akabaki katoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango, simu ikimdondoka bila kujua, akajiachia na kutua kitini mikono akaibwaga mezani, akashusha pumzi ndefu, kisha akawaangalia waliokuwa mbele yake.

    “Namtala Fasendy hapa haraka, aletwe,” akatoa amri huku mwili ukimtetemeka, vijana waliokuwa hapo wakatoka na kufanya waliloagizwa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walipoondoka, aliufunga mlango kwa ndani na kuinua simu yake ya mezani, akaongea maneno machache na kuiweka chini katika kitako chake. Dakika mbili baadae, yule mwanaume mfupi, menene asiye na shingo aliingia ofisini hapo.

    “Vipi Shalabah,” alimuuliza.

    “Hussein,” akaita kwa sauti ya chini, Huseein akamsogelea na kusimama mbele yake, “Sharon ameuawa,” akamwambia.

    “Sharon, no! haiwezekani Sharon afe kijingajinga hivyo, Sharon ni mpiganaji kaka, afe kikondoo namna hiyo, mtu kaka Torabola miaka nenda miaka rudi, usiwe mjinga Shalabah, huyo nyau anataka kuwachanga kisaikolojia ili mjitokeze ovyo kumsaka awamalize, tuma mtu kwa Sharin sasa,” Hussein, my mnene alimwambia Shalabah.

    “Hivi inawezekana ee?” Shalabah akajibu kama mtu aliyekurupushwa usingizini. Tumaini jipya likachanua ndani ya moyo wake. Inawezekana, kamteka sasa anatucheza shere? Akanyanyuka kitini, “Naenda kwa Sharon, nyumbani,” akamwambia Hussein.



    Hussein akamuonesha ishara ya kidole ya kumkataza, “Usikurupuke, utauawa, lazima ujue kuwa unayepambana naye ni mtu wa vita, ana mbinu nyingi za kukunasa kama vile kinyonga anavyomnasa mdudu, vipi kama yupo hapo ndani kwa Sharon kakutegea ukifika akumalize? Shalabah, tuliza akili.”

    Shalabah akajiona jinsi alivyotaka kufanya ubwege, akarudi na kuketi na muda huo huo mlango uligongwa, akanyanyuka na kuufungua, Fasendy akasukumiwa ndani.

    “Mwanamke mshenzi sana wewe, unataka kutuzunguka sisi? Ama kweli, kikulacho ki nguoni mwako,” Shalabah akasema kwa hasira.

    “Vipi huyu, Shalabah?” Hussein akauliza.

    “Huyu ni hayawani, ametuuza kwa yule shetani mara kadhaa, anatusaliti,” Shalabah alijibu huku akiuma meno. Huseein akamwangalia Fasendy pale chini, akatikisa kichwa.

    “Mwanamke, umejihukumu mwenyewe, mpelekeni bandani, akatwe kichwa alfajiri ya kesho pamoja na yule Mtanzania,” Hussein akatoa amri na kisha wale vijana wakaondoka na Fasendy.

    “Tuma mtu kwa Sharon akamwangalie, usimwambie kuna nini,” Hussein akamwambia Shalabah, naye mara moja akafanya hivyo.



    8

    KAMANDA Amata aliegesha pikipiki yake kando ya ghorofa kubwa lililozungukwa na maduka mbalimbali yaliyokuwa yakiuza bidhaa anuai. Akaengesha pikipiki yake panapohusika, kisha akatulia pembeni akiitazama gari iliyosimama mita kama mia moja pembeni yake, aliijua fika kwani ndiyo aliyoiona kwenye picha za kamera za usalama pale hotelini, gari iliyohusika kwenye mauaji ya Hassna, leo mpaka kieleweke, alijisemea moyoni huku akiweka vizuri miwani yake.

    Alilolitarajia likatimia, watu wawili wakaja kwenye ile gari, mwanamke na mwanaume, kwa haraka alimtambua yule mwanamke, mhudumu wa mapokezi katika hoteli ya Jazeera Palace, na aliitambua sura ya yule mwanaume kwani naye alimuona katika wale watatu walioleta ule mwili pale hotelini,



    “Shiiit!!!” alijisemea kwa sauti ndogo, “mwanamke mseng* huyu,” akamtukana kwa sauti ileile ya kujisikia mwenyewe. Ile gari ikageuzwa pale maegeshoni na kuingia barabarani.

    Kamanada Amata akatikisa kichwa akajua mchezo aliochezewa pale hotelini, pindi alipokutana na yule mwanamke pale mapokezi, akachukuliwa kuzungushwa nyuma na kupewa ujumbe kuwa, polisi wanamtafuta kila mahali, ni wakati huo huo ambapo wale jamaa walikuja kuweka ile maiti kwenye gari yake, hakutaka nione kitendo hicho, huyu ni mmoja wao, alipowaza hilo ndipo alipokumbuka kuwa alipewa ujumbe kwenye kibahasha kidogo na alikwishasau kukisoma, akaingiza mkono mfukoni na kukitoa kile kibahasha, akakichana na ndani hakukuwa na ujumbe wowote zaidi ya kidubwasha kidogo kama heleni, alikigeuzaguza na kukielewa kidubwasha hicho, akakipachika sikioni na kukiminya katika kitufe chake kilichotengenezwa kwa jiwe la yaspi safi.



    …Kamanda Amata, karibu sana Mogadishu, nilijua kuwa utakuja na nilikuwa nakusubiri kwa hamu sana. Hii ni salamu yangu kwako mimi Fasendy. Nakumbuka sana yote uliyonitendea kule Ugandam hukupenda nife uliniacha hai, name nashukuru Mungu sikudhurika ijapokuwa nililala kitandani kwa miezi mingi hadi uti wa mgongo wangu ulipounga sawa. Nimetumwa kukuua, kukutoa roho yako, lakini siwezi fanya hivyo kwako Abadan. Najua uliko lakini hujui niliko. Hawa jamaa ni hatari sana na wamepania kukuua. Jana nilikuweka kwenye shabaha yangu lakini kwa kukusalimu niliipiga bahasha iliyokuwa mkononi mwako. Na sasa wamegundua kuwa nilifanya makusudi, wamenibaini kwani utendaji wa kazi yangu umekuwa mzito sana siku hizi, nakupenda Kamnda, nakupenda sana, lakini hili litanifanya niwe matatizoni na hawa watu, ninajua mengi. Ila najua wataniua, wataniua tu, lakini nitafanya niwezalo kukusaidia, usinitafute ila nitakutafuta mimi…



    Baada ya ule ujumbe kwisha kile kidubwasha kikatoa sauti ya bip, akakipachua pale sikioni na kukiweka mkononi, kiligeuka rangi na kuwa cheusi, kimeungua, akakitupa, alijua wazi hakijaungua kwa hitilafu bali ndivyo kilivyotengenezwa ili mtu akimaliza kusikiliza ujumbe wake basi huungua ili mwingine asije kupata siri hiyo. Akatoka pale aliposimama na kulikwea pikipiki lake tena akatazama kule ilikokwenda ile gari, akainua simu yake na kupiga namba alizokuta kwenye ile kadi aliyopewa na yule mwanamke wa hotelini.





    “Hello,” akaita

    “Yes Hello Jaffar,” yule mwanadada akaijibu.

    “Nahitaji kuonana na wewe sijui itawezekana?” Kamanda akauliza.

    “Yeah, bila shaka, labda uniambie ni wapi name nitakuja,” yule mwanamke akajibu.

    “Sawa nafikiri wewe ni mwenyeji zaidi, hivyo unajua mazingira mazuri yote yako wapi, nataka uje peke yako, umesikia, peke yako,” Amata alisisitiza lakini alijuwa wazi kuwa lazima wabaya wake watafika mahali hapo na hilo ndilo alilolitaka haswa.

    “Medinnah Club, saa 3:30 usiku, nitakuwa peke yangu,” yule mwanamke akajibu.

    “Ok, tukutane saa hiyo!”

    Uchovu ulikuwa wazi kwa Kamanda Amata, alitamani ajipumzishe lakini kila alipofikiria ni wapi kwa kujipumzisha ilimuia ngumu kupata jibu. aliliwasha pikipiki lake na kuifuata ile gari nyuma nyuma ingawaje tayari ilikuwa imekwishamuacha hatua kadhaa, alivuta mafuta ya pikipiki ile kubwa na haikumchukua muda kuiona ikiwa inakunja kona kushoto na kuiingia Jidka Afgooye, ikapunguza mwendo na kwenda taratibu mpaka katika nyumba nyingi zilizzojipanga kwa mstari ulionyooka katika eneo hilo. Akiwa umbali kama wa mita mia mbili kutoka iliposimama ile gari, Kamanda Amata alipunguza mwendo.



    Nataka nijue anapoishi huyu mwanamke, alipomuona akiingia kwenye ile nyumba yeye akaendelea kusubiri mpaka ile gari iondoke, dakika tano baadae yule mwananmke alitoka pale kwenye dirisha la gari nakuingia ndani ya nyumba hiyo, ile gari ikaanza kuondoka taratibu, Kamanda Amata naye akaanza kuifuata taratibu. Ile gari ilizunguka mtaa wa pili na watatu ikachanja mbuga kuelekea nje kidogo ya mji. Kamanda Amata yeye aliifuata bila kuipoteza akihakikisha kuwa lazima ampate mtu huyo anayeendesha gari hiyo.

    Ile gari ikaingia Jidka Waxaracadde na kuendelea na safari, akaiona ikiacha njia kuingia kushoto na kusimama getini, ikapiga honi kwa mtindo wake na geti lile likafunguliwa ile gari ikaingia na geti likafungwa nyuma yake.

    Mogadishu Textile, ni maneno makubwa juu ya paa la ghala hilo kubwa lililojengwa nje kidogo ya mji wa Mogadishu au Moqdishu kama wenyewe wanavyouita. Kamanda Amata akapita kwa mwendo wa kawaida na kuyasoma yale maandishi, kiwanda cha nguo, akajisemea mwenyewe huku akiendelea na safari yake isiyo na ukweli wowote. Alipojiridhisha kuwa hiyo gari imeingia katika jengo hilo akaamua kurudi kwenda kupumzika ili kulipisha giza lifike kwanza naye amalize kazi yake.

    Katika jengo lile lile, gofu alilooneshwa na Fasendy, aliingia taratibu kabisa na kujifungia huku pikipiki yake nayo akiifungia humo. Njaa ilimchonyota kwelikweli, lakini hakuwa na jinsi alihitaji kupumzika kwanza, na hamu yake kubwa ilikuwa ni kumsubiri Fasedny waliyepanga kukutana hapo jioni ya siku hiyo. Akajilaza usingizi juu ya kijitanda kidogo huku bastola yake ikiwa mkononi imeshikwa tayari kwa lolote.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§

    SHALABAH aliangusha machozi alipoukuta mwili wa Sharon ukiwa umelala bila uhai huku macho yakiwa yametoka pima kama mtu aliyekuwa akitafuta sindano gizani. Alimtikisa lakini hakujibu lolote. Akanyanyuka na kuwaangalia vijana aliokuwa nao kwa gadhabu.

    “Hifadhini mwili huu tutauzika kama desturi yetu, yatima huyu hakuwa na ndugu kama ninyi mlivyo,” aliwaambia vijana wake aliokuwa nao. Akanyanyuka na kutoka nje, moja kwa moja akaingia garini mwake na kuketi, akainua simu ya upepo na kuanza kuongea.

    “Sierra 4, Sierra 4,” akaita.

    “Sierra 1 unasikika,” sauti ikajibu.

    “Sharon ameuawa mchana wa leo, naomba sasa kuwa maini  na ulinzi kila kona ya Mogadishu lakini cha msingi pia ni kila mtu kujilinda mwenyewe, adui yetu amekuwa kama mbogo aliyejeruhiwa, atararua kila amwonaye, kwa kuwa sasa hajui nini anafanya, popote akioneka alipuliwe hapohapo,” akatoa maagizo na kukata simu. Kisha akawasha gari yake na kuondoka eneo hilo.



    §§§§§

    “ Nashindwa kukuelewa unachoniambia Shalabah,” Mr. Lonely alikuwa akiongea na kijana wake anayemwamini kabisa Shalabah kwa mtindo wake uleule wa kuoneka kwenye luninga, “Hivi inakuwaje kamtu kamoja kanawasumbua ninyi mko zaidi ya mia? Iaingia akilini kweli, yeye ana bastola nyie mna bunduki kubwa za kisasa, mnashindwa kumtengua kiuno, anawaua kama mtu anavyoua inzi.”

    “Mzee, tumetega kila aina ya mtego lakini yule jamaa kaikwepa,” Shalabah akajibu.

    “Ukiona anakwepa mitego yenu basi ujue kuwa ninyi si wategaji wazuri,” Lonely alidakia.

    “Sio hivyo Mr. Lonely,” Shalabah akalalamika.

    “Sasa nini? Na yule tuliyemkodi anafanya nini?” akauliza.

    “Hilo ndilo liakuja, yule mwanamke tumegundua kuwa ni msaliti anatusaliti kwa kumpa siri zetu adui,” Shalabah akaeleza. Mr. Lonely akashtuka kidogo, “Ati, anatusaliti?” akauliza kwa wahka mkubwa.

    “Ndiyo anatusaliti,”

    “Sasa umeamua nini kwa hilo?” akauliza kwa ukali.

    “Tumemuweka chini ya ulinzi na kesho asubuhi tunakata kichwa,” Shalabah akajibu.



    “Safi sana, mwanamke hana akili yule, mumkate kichwa na nyama yake mniletee niwape samaki wale,” kisha akamwangalia Shalabah aliyekuwa ameketi kwenye sofa kubwa akitazamana na luninga hiyo, “Sasa nataka ulinzi maridadi, kesho jioni inaingia meli kubeba makombora yote kumi yaliyobaki, najua hilo unafamu, sasa hakikisha hatutaki fujo kazini,” Mr Lonely aliongezea ombi hilo. Shalabah akaliacha jumba hilo na kuendelea na shughuli zake zingine.

    Jumba kubwa la Mr Lonely lilikuwa ni jumba pekee sana katika mji wa Mogadishu, kila aliyepita alipenda japo kupata picha ya jumba hilo lenye bustani ya kupendeza, matunda ya msimu na mambo mengi ya kuvutia. Ndani yake kulikuwa na mtu anayaeishi. Ukiacha jumba hilo, ndani yake kuna ghorofa iliyojengwa chini ya ardhi, ghorofa hiyo ndiyo ilikuwa akiishi mwenye Mr Lonely. Mr Lonely alikuwa akiishi peke yake katika jumba hilo, mfanya kazi wake wa upishi na msaidizi wake ndio watu pekee waliokuwa wakiishi ndani ya kasri hilo, lakini amini usiamini hata wao hawajawahi kumuona, wanapomaliza kupika chakula tu hukiweka mahala Fulani juu ya kitu kama meza hivi, na kile chakula uingia ndani na baadae kutoka. Alikuwa na pesa nyingi kuliko watu wanavyodikiria.     Alijipa jina la Mr. Lonely kwa sababu alikuwa akiishi peke yake hakuwa na mke wala hakuwa na mtoto, kwa ujumla alikuwa hana uwezo wa kuzaa, enzi za ujana wake alikuwa ni mwanajeshi katika jeshi la Sardenia, wakati wa vita ya pili ya dunia alikamatwa na askari wa Kijerumani na katika kumpa mateso ili kupata siri za kijasusi walimkata uume akabaki kibubutu. Alifanikiwa kutoroka kwa watesi wake hao lakini hakufanikiwa kupata uume wake. Lonely hakupenda kuonekana na watu, na wengi walijua kuwa mtu huyo amekwishakufa zamani kwani Mr. Lonely halikuwa jina lake halisi.



    DAR ES SALAAM  TANZANIA

    Saa 12 jioni.



    MADAM S alikuwa akifungafunga ofisi tayari kuelekea kwenye kikao cha baraza la usalama la Taifa ambacho kilikuwa kimepangwa kufanyika jioni hiyo katika ukumbi mdogo wa Kilimanjaro Square ulipo ndani ya jengo la Ikulu ya Dar es salaam. Kilikuwa kikao nyeti na wadau wote wa usalama walikuwa wakihitajika ili kutathimin hali halisi ya usalama kwa ujumla.

    Madam S aliegesha gari yake katika maegesho ya jengo hilo nyeti sana katika Taifa la Tanzania, jengo linalopitisha maamuzi magumu juu ya nchi hii. Kila aliyeshuka kwenye gari siku hiyo alionekana kuwa na mawazo mengi sana kuliko ilivyo kawaida. Mkuu wan chi aliwata haraka na mara moja bila kuchelewa.



    Ndani ya ofisi hiyo waliketi katika mtindo wa yai mbele yao kukiwa na meza kubwa kabisa ya mbao safi iliyokuwa na chupa za maji juu yake. Dakika chache baadae aliingia Rais wan chi kupiti mlango tofauti na ule waliopitia wale wajumbe. Wote walisimama kwa heshima na kutoa saluti kali kwa waliopaswa kufanya hivyo. Mkuu wan chi akawapa ishara ya kuketi nao wote wakafanya hivyo.

    “Nimekuiteni hapa ghafala lakini kama mnavyojua usalama wan chi yetu upo mikononi mwetu, hata kama nikikuita saa nane za usiku hauna budi kufika,” akakohoa kidogo kusafisha koo, “Sasa ndugu wajumbe nitawapa hii taarifa hapa ambayo ilifika leo asubuhi katika ofisi yangu, na haikuwa busara kama nisingewaambia, hivyo tumeitengeneza kwa vitini namna hiyo na kila mtu naomba apitie kwa harakaharaka aone kilichomo,” akawambia na katibu wake akagawa vitini hivyo kwa kila mjumbe. Kati ya wote ni Madam S tu aliyeonekana kutochanganyikiwa na taarifa hiyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeiwasilisha kwa Rais asubuhi hiyo. Hakuna aliyeongea wala kunongona, ila vijasho viliwatiririka kila mmoja kwa jinsi zake.



    Kishapo Rais akaendelea, “Natumaini mmesoma na mmeelewa sivyo?” wote wakajibu “Ndivyo!” kisha akaendelea, “Hivi hili Taifa tunalipeka wapi? Kama viongozi tunaopewa dhamana tunakuwa wa kwanza kutafuna mali ya umma na huu umma utaishije wazee wangu? Nadhani wenyewe mmeona hapo kilichofanyika kule Msanga Mkuu miaka zaidi ya kumi iliyopita, ukisoma ndipo sasa utagundua hujuma mbaya iliyofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali, leo hii tunapohangaika kuliokoa Taifa vijana wetu akina Gwamaka wanachinjwa, wanamwaga damu kwa ajili ya hawa watu. Wajumbe, taarifa hii imeletwa na Kamanda Amata aliyeko Somalia katika uwanja wa vita, yeye mwenyewe anasema ni uwanja wa vita, lakini ameweza kupa siri hii kubwa na mbaya kabisa, ni aibu!” Rais aliongea kwa wahka kubwa.

    Waziri wa mambo ya ndani akauliuza, “Mheshimiwa, yeye Kamanda hii siri ameipataje huko Somalia? maana nimeichunguza na nimeona huku mwisho imesainiwa na mtu ambaye tayari ni marehemu The Chammeleone ijapokuwa saini yenyewe imefutika futika, lakini nimeitambua,” baada ya kusema hilo kila mjumbe akafungua mwisho wa faili lake na kutazama. Kila mmoja alitikisa kichwa.



    “Mimi hilo silijui, mi nataka muone hiyo taarifa, na ninatoa amri, waziri wa Mambo ya ndani hawa watu wakamatwe mara moja, aliyekkuwa hai akamatwe aliyekufa mali zake zikamatwe, tutajua la kufanya,” Rais akasisitiza kwa uchungu, “Naomba hilo lifanyike leo maana tumepoteza wapiganaji ishirini na hatujui wako wapi, Gwamaka kijana wetu mahiri wa JW amechinjwa kama kuku, Sebeki komandoo wetu ameuawa kwa bomu, Jamir hatujui aliko Daudi nae alkadharika na meli yetu kubwa ya kisasa vyote hivi vinatughalimu naoma zoezi hili lifanyike usiku huu, na huyu Mr X kama ilivyoanishwa hapa najua nani nitampa kazi ya kumsaka.” Baada ya mazungumzo machache kikao kilivunjwa majira ya saa 2:30 usiku na kila mtu akatawanyika.

    Wakiwa nje Madam S alikuwa akibadilishana mawazo na viongozi wenzake wakiongea hili na lile.

    “Madam S!” akasikia akiitwa pembeni, akatazama huyo amwitae akamuona ni waziri wa ulinzi ambaye naye alikuwamo katika kikao hicho.

    “Madam S, kijana wako anafanya kazi nzuri sana, lakini hii siri kaipata vipi?” akauliza.

    “Ah hilo swala gumu mimi kujibu, yeye anajua mbinu zake jinsi ya kupata vitu kama hivi, na siyo hiyo tu amegundua siri nyingi sana juu ya hujuma hii, na wote wanaohusika, pale orodha uliyoiona na ndogo wapo na wengine wengi,” Madam akajibu. Waziri wa ulinzi alioneka uso wake kusawajika kwa mawazo ya dharula yaliyokuja bila kutegemewa.

    “Huyu ni kijana mahiri sana katika kazi yake,” waziri wa ulinzi akasifia.

    “Nami najivunia kuwa naye,” Madam S akamjibu. Katika moyo wa Waziri wa ulinzi kulikuwa na jambo lililojificha jambo hilo lisiloonekana kwa macho lilisomwa haraka sana na Madam S akaona lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo, akaingia katika gari yake na kujifungia mlango huku vyoo vyote vikiwa juu, akafyatua kidubwasha chake cha kuongelea na kukisogeza karibu na kinywa chake.

    “Hey Gina, uko wapi au umesinzia?” Madam S aaiuliza.

    “Nipo mama, nipo palepale Magogoni,” akajibu.

    “Ok, sogea hapa katika lango la Ikulu ila usiegeshe gari, ifuatilie gari namba STK 110A Toyota Landi Cruiser kisha nipe maelezo kila hatua.



    “Copy” Gina akajibu.

    Dakika tano baadaye, Gina alikuwa akisogea taratibu na gari yake binafsi aina ya Toyota Mark II akilifuata lile gari aliloelekezwa, akiwa peke yake ndani ya gari hiyo alikuwa akisikiliza muziki mwororo wa Whitney Huston uliokuwa ukipigwa kutoka katika chombo cha gari hiyo. Walipita barabara ya Kivukoni moaja kwa moja mpaka mtaa wa Magogoni na kukunja kushoto kuufuata mtaa huo walipofika barabara ya Luthuli wakakunja kulia. Gari aliyokuwa akiifuatilia Gina iliingia Sokoine Drive na kuambaa mpaka kwenye mzunguko mdogo unaoziunganisha Sokoina drive, barabara ya Chimara, ya Garden na ile ya Samora. Akaingia barabara ya Chimara na kutokea Ocean Roada akakunja kushoto.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda wote huo Gina alikuwa makini kuifuatilia gari hiyo mpaka ilipofika katika eneo la Sea View, Upanga, ikaingia katika moja ya majumba mazuri yaliyojipanga hapo.

    SOMALI HIGH COMMISION, lilikuwa bango la ukubwa wa wastani likining’inia katika lango kuu la nyumba hiyo ambapo ile gari ilikuwa ndani yake, Gina akainua mkono wake na kubofya kitufe Fulani katika saa yake na kuisogeza karibu na kinywa chake na kuongea.

    “Madam S, shabaha ni Somali High Commision,” alimpa ujumbe.

    “Chukua vithibitisho kama unaweza Gina,” Madam S akatoa amri.

    “Copy,” akajibu.







    §§§§

    Waziri wa Ulinzi alikaribishwa katika sebule kubwa ndani ya jumba hilo lililotandikwa zuria la gharama sana lenye manyoya ya samba, akakaribishwa kiti na kuketi, mhudumu wa ndani akamlete kinywaji baridi kwani alikuwa anajua kiongozi huyo upendelea kinywaji gani. Baada ya muda kidogo balozi wa Somalia aliungana naye pale sebuleni.



    “Ndiyo komredi, nipe habari maana uliponipigia simu nilishtuka kidogo,” yule Balozi akaanzisha mazungumzo.

    “Ni hivyo, tulikuwa tumeitwa Ikulu na swala lilikuwa hilihili swala letu la miaka mingi, juu ya ile plant kule Msanga Mkuu, kiukweli sisri hii sio siri tena kwani ipo ofisini kwa mkuu wan chi na amekwisha amuru baadhi ya vigogo wa serikali wakamatwe usiku huu, waliostahafu na hata waliokuwa kazini,” akapiga funda moja. Kabla hajaendelea kuongea balozi akaingiza kauli.

    “Lakini, akaunti yako imeshaitika? Mi yangu tayari, na nataka niende likizo nyumbani ili nikamalize na bwana Lonely maana alinambia ikikamilika kuna donge linguine, simtokusahau Komredi,” yule balozi alikuwa akiongea kwa furaha sana wakati mwenzake alikuwa kwenye mawazo mazito.

    “Swala sio pesa, je ukigongewa mlango usiku huu kuwa unatakiwa ukajieleze Ikulu itakuwaje?” akauliza yule Waziri.

    “Aaa Koredi, hapa ni nchi nyingine, hilo haliwezekani kwa maana unaweza kuharibi uhusiano wa kidiplomasia,” akajibu yule Balozi.



    “Ok, hali iko hivyo lakini swala si unajua liemeisha!” Waziri akasema.

    “Ndiyo najua na nimepata taarifa kuwa kesho ule mzigo utaondoka pale kuelekea Afghan, tumemaliza kazi wacha tunywe kaka,” aliongea kwa Kiswahili kilichochanganyika na kiarabu, vinywaji vikaletwa na wawili hao wakaburudika.



    §§§§§§

    “Vipi umepata lolote?” Madam S akamwuliza Gina.

    “Yap, mheshimiwa amekaa sana pale kwa balozi nafikiri walikuwa na kikao kizito najua,” Gina akaeleza akaonesha na vielelezo vya picha ya ile gari ikiwa inatoka katika lango la nyumba ya balozi.

    “Good Girl, unaanza kukomaa sasa Gina, endelea hivyohivyo ili wakati mwingine nikuweke mstari wa mbele,” Madam S alimtania huku akimpigapiga mgongoni, kisha akendelea “ Sikiliza Gina, siku zote unapotaka kufanya jambo la hatari inabidi uzingatie mambo matatu ya kiusalama, je ninapokwenda nitaajihakikishia vipi usalama wangu? Hilo ni swali muhimu sana najua unafahamu kuwa unatakiwa kuaangalia sana usalama wako, hivyo uwe mwangalifu.”

    “Mama usijali, katika swala la usalama niko vizuri tu labda itokee bahati mbaya, Kamnda kanifundisha mengi sana,” Gina akaeleza.

    “Najua, na anakupenda pia, anapenda uwe mke wake, lakini nasikitika kwamba haiwezekani,” Madam S alaimwambia.

    “Ah! Madam, Kamanda simuezi, kisimpitie mbele kabeba,” Gina alijibu.



    “Hapana hafanyi vile makusudi, wakati mwingine inabidi awe vile ni moja ya kazi, huwa anapenda kutumia wanawake kupata siri anazozihitaji ijapokuwa wakati mwingine ni kazi na dawa,” wote wakacheka na kugonganisha viganja vya mikono yao.



    Rejea MOGADISHU

    ILIKUWA imetimu saa mbili usiku Kamnda Amata alipokurupuka kutoka katika ndoto mbaya, sauti kali ya Fasendy ilimshtua kutoka katika ndoto hiyo. Akaketi juu ya kitanda kile kidogo akihema kwa nguvu, njaa ilikuwa kali sana alihisi hawezi kufanya lolote kwa jinsi alivyo, hakuwa na nguo za kubadilisha lakini hilo kwake halikuwa tatizo. Akainuka na kuiendea chupa yake ya maji, akapiga mafunda kama kumi ya nguvu kisha mengine akanawa, alihitaji kuoga lakini hakukuwa na bafu kati kijichumba hicho, inaonekana kilikuwa ni sehemu ya maficho ya Fasendy kwa jinsi kilivyo.

    Akatoka na kuangalia nje, mbala mwezi ilikuwa badoa haijaanza kung’aza mji huo, alijichomoza na kulitoa pikipiki lake akaufunga mlango na kulikwea, akaondoka eneo hilo. Safari hiyo iliishia kwenye mkahawa mmoja wapo uliopo mtaa wa tatu, hakujali lolote aliegesha pikipiki yake na kuingia mkahawani, akaagiza  chakula kinachofaa.



    MEDDINAH CLUB



    WAKATI Kamanda Amata akijipatia chanjo ya tumbo, kule klabu ya Meddina vijana watano walikuwa wameketi katika kona tofauti za ukumbi huo, wote wakiwa wameagizwa kuhakikisha wanammaliza Amata usiku huo. Walipewa taarifa na yule mwanamke mhudumu wa hoteli, yeye alifanywa kama chambo tu cha kumzubaisha Kamnda Amata usiku huo ili maharamia wale wamalize kazi yao.

    Walishajua ni wapi wataketi, hivyo kila mmoja alikuwa tayari na bastola iliyoshindiliwa risasi, hawakutakiwa kutoa taarifa yoyote zaidi ya kifo cha Amata, ndiyo iliyokuwa ikisubiriwa na Shalabah usiku huo, na aliamini hilo kwani alijuwa vijana aliowapeleka kule ni mahiri kati shabaha kuliko unavyofikiria.



    §§§§§

    Saa tatu kamili usiku huo, Kamanda Amata alifika nyumbani kwa yule mhudumu wa hoteli kwani machale yalikwishamcheza kuwa lazima hawezi kuja peke yake, hakuwa na haja ya kwenda Meddinah klabu, aliamua kumaliza mchezo huko uswahilini na kuwaacha wanaomsubiri kama wapo wabaki midomo wazi kupiga miayo. Aliegesha pikipiki yake nje na kuvuta hatua kuielekea nyumba hiyo.

    Alipoufikia mlango alitulia kidogo, akautazama vizuri ulikuwa haujafungwa, mlango ulikuwa wazi na uwazi mdogo ulikuwa ukionesha mpaka sebuleni, akachungulia ndani kwa jicho la kijnja hakukuwa na mtu sebuleni. Akasita kuingia,usije kuwa mtego, akajiwazia, baadae akaamua kugonga, hakujibiwa, akausukuma taratibu na kuingiza mwili wake ndani ya nyumba hiyo, utulivu ulikuwa umeijaza sebule yote, kwa mbali alikuwa akisikia miguno ya watu waliokuwa mapenzini, yaani katikati ya sherehe, akasogea karibu na korido inayoelekea huko vyumbani, alichokisikia kilikuwa sahihi. Yule mwanamke alikuwa kitandani na mwanaume wakifanya ngono. Akawatazama kupitia uwazi mdogo wa maungio ya mbao za mlango ambao haukushikamana vizuri, watu na starehe zao, akawaza.



    Taratibu akamtazama vizuri yule mwanaume, akamjua sura yake, akaikumbuka ni moja ya wale watatu waliomuua Hassna, hakuwa na papara, Kamanda akarudi sebuleni, bastola mkononi akaketi mahala tulivu na kusubiri wamalaize vyao. Muda si mrefu alianza kusikia vicheko vikali, akajua wameshamaliza dhambia zao, na kweli dakika hizo hizo alisikia hekaheka za kwenda bafuni kuoga mwanamke akisisitiza kuwa anawahi miadi. Viatu vya kiume vikasikika viukigonga sakafu kuja sebuleni, Amata akanyanyua bastola lake, revolver, akalitazamisha kule kwenye korido, yule mwanaume akasogea bila kumwona kwa maana alikuwa kama kivuli, yule bwana akaliendea jokofu na kujichaguli kinywaji alipogeuka kurudi kitini akakutana uso kwa uso na domo la bastola. Akatetemeka na kuangusha chupa na glass vilivyokuwa mkononi mwake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Keti chini taratibu sitaki vurugu,” alimwambia kwa sauti ya chini, yule jamaa akaketi bila tabu, mita moja ilikuwa katikati yao ili isitokee shida yoyote. Na mara ileile yule mwanamke naye akatokea, akakutana na dhahama hiyo.

    “Na wewe njoo, haya mpekue huyo kila alichonacho weka mezani, haraka,” yule mwanamke hakuamini akionacho akafanya hivyo akamaliza.

    “Haya we mwanamke, unanifanya mimi mjinga sivyo? Nina uhakika kabisa kuwa huyu bwana alishirikiana na Sharon na mtu mwingine kupakia ule mwili wa Hassna kwenye gari yangu pale hotelini, wewe hili unalijua, na ni dakika ileile uliponichukua na kunizungusha nyuma ukinambia kuwa polisi wananitafuta,” akatulia kidogo, “ sasa mimi si mjinga, nilikufuatilia yangu pale mjini supa maketi ukiwa na huyuhuyu mwanaume kwenye gari namba (akazitaja) na nikajua kuwa huwezi kuja kwenye miadi peke yako, na hilo nina uhakika, sasa miadi yetu ni hapa.”

    Hakuna aliyekuwa na la kuongea, wote walikuwa kimya, baada ya muda kidogo kama sekunde tatu hivi yule bwana akauliza, “Unataka nini kwetu sasa?” aliamua kujitutumua ilia aonekane mwanaume mbele ya huyo mwanamke wake.



     Risasi moja ya revolver ilifyatuka na kufumua pega la mwanaume huyo.

    “Huwa siulizwi maswali ya kitoto,” Amata alimwambia. Kilio cha maumivu kilitawala mle ndani yule mwanamke akipiga makelele kama kachanganyikiwa, akasimama kumuendea Amata, “Sitaki muuanie nyumbani kwangu, sita…” hakumaliza, kofi moja zito kutoka katika kono la Kamnda likamfikisha chini salama.

    “Nitawaacha hai mkiniambia tu bandani ndio wapi basi,” Kamanda akawaambia.

    “Bandani, bandani, bandani? We Jeinah mwambei atuache, jamani mwambie,” yule mwanamke akawa akimlazimisha mwanaume kusema.

    “Mogadishu Textile,” yule mwanaume akamasema maneno hayo mawili, alipomaliza tu, risasi nyingine ilifumua kichwa chake na kumuacha marehemu, Kamanda Amata akamchukua yule mwanamke akamkamata mkono na kutoka naye nje akimkokota mpaka kwenye pikipiki yake.

    “Panda!,” alimwamuru baada ya yeye kuwa tayari juu ya mashine hiyo. Yule mwanamke akapada.

    “Sasa unanipeleka wapi jamani?” akauliza yule mwanamke.

    “Utajua tukifika,” akajibu Amata na kuondoka kwa kasi eneo lile.



    §§§§§§

    Fasendy alitupiwa ndani ya chumba chenye giza, chumba ambacho hakikuwana kitu chochote wa mtu yeyote, alijiketisha karibu kabisa na kona ya chumba hicho, giza likiwa limemzunguka kila upande. Kila mara mwili wake ulimsisimka kana kwamba kuna jambo la hatani ndani ya chumba hicho, lakini hakuweza kuona kwa macho yake ya kawaida. Hata alipojaribu kutazama hapa na pale labda atapata sehemu ya kujiokolea, bado hali ilikuwa ni ndoto.

    Akatulia palepale alipofikia tangu mwanzo akisubiri hatima yake lakini bado hakukubali kufa kijinga namna hiyo. Haiwezekani alijiwazia mwenyewe na kujipa moyo wa kuendelea kukaa humo, lakini kichw achake kilionesha wazi kuwa ni ni mtu mwenye fikra nzito na ngumu. Fasendy alikuwa akijaribu kutazama njia ya kutorokea.



    Utulivu ulichukua nafasi katika masaa hayo ya usiku, aliamini kabisa kuwa Amata anaweza kuibuka kama mzimu na kuwaokoa, ijapokuwa alikuwa na uhakikia kuwa Amata hajui ni wapi alipo lakini alijipa moyo kuwa anawezaa kuongea naye kihisia kama ilivyo kwa majasusi wengi. Ukuta uliotenganisha vyumba vya jengo hilo ulikuwa ni ukuta mwembamba kama sita hivi. Kutoka mbali alisikia watu waliongea kuelekea upande alipofungwa yeye, lakini wale watu walipofika pale hawakufanya lolote juu yake bali walikwenda mpaka mlango wa pili na kuingia.

    “We mbwa koko, bado masaa machache tunakata kichwa chako, tuwapelekee zawadi mabosi wako kama tulivyofanya kwa yule mwenzio,” sauti hiyo iliyoongelewa kwa lugha ya kihabesh ilipenya katika ngoma za masikio ya Fasendy, akajua kwa sentensi hiyo kwa vyovyote atakuwa anaambiwa Jamir. Akasubiri viumbe wale waondoke pale na baada ya hapo alianza kufanya mawasiliano na mtu wa chumba cha pili kwa jinsi ya ajabu, na alielewa wazi kuwa kama ni Jamiri basi atajibu tu lugha hiyo. Fasendy alijipekua mifukoni kuona kama ana kitu chochote cha chuma lakini hakuwa nacho, alifikiri mara mbili na mwisho wake akakumbuka kuwa ana pete ya dhahabu kidoleni mwake, akaivua na kuishika kwa vidole barabara kabisa akaitumia ile pete kugonga gonga ukuta uliotenganisha vyumba hivyo. Jinsi alivyokuwa akigonga ilikuwa ni kwa mtindo maalumu, akagonga mara kadhaa na kusikiliza kama kuna jibu lolote kutoka upande wa pili, haikuwa hivyo.



    §§§§§

    Wakati Fasendy akifanya yite hayo, Jamir alikuwa amejilaza sakafuni, akiwa na uchovu na njaa ya siku kadhaa, mwili wake haukuwa na nguvu za kutosha kufanya lolote. Alihisi kuwa ni mwisho wake umekwishafika. Ingawaje yeye ni komandoo mzoefu aliyeshiriki vita ya ukombozi ya Comoro lakini njaa ilikuwa ni komandoo mkubwa zaidi. Jamir hakuona jua tangu afungiwe kwenye chumba hicho, alidhoofu kwa mengi, mawazo, aliiwaza sana familia yake aliona bora kama angeuawa lakini moyoni mwake bado alikuwa na mambo mengi aliyoyahifadhi ambayo angependa amwambie mtu yeyo te yule ili ayafikishe nyumbani Tanzania, kwani aliamini kuwa kwa mambo hayo basi hujuma hiyo ingepatiwa ufumbuzi.



    Alishtuka kutoka kwenye kausingizi ka mpito, akatulia kimya akisikiliza kijisauti hafifu cha kitu kinachogonga katika ukuta wa upande wa pili. Alisikiliza kwa makini, kwa kufunga milango. Kwanza alifikiri ni mdudu ambaye anafanya hivyo lakini aligundua kuwa si mdudu kwa sababu mpangilio wa sauti ile ya kugonga ulikuwa ni ule ule kila ukirudia na nafasi kati sauti moja na nyingine nin ileile kila inaporudia, alielewa nini maana ya ule ugongaji.



    …Jamir, Jamir… ilikuwa maana ya kule kugonga kulikofanywa kutoka upande wa pili, Jamir akainua kichwa chake kuutazama ule ukuta, hakuwa na nguvu ya kusimama ilimbidi kutambaa chini kuelekea eneo lile amalosikia ile sauti, akasota na kusota kwa kutumia tumbo mpaka akafuika eneo lile akatega sikio kusikiliza kutoka katika ukuta ule. Ukimya ulitawala, Jamir akakata tama akajua labda kweli ni mdudu, lakini mara kadhaa alijiuliza kama ni mdudu kwa nini agonge kwa jinsi ileile kila wakati? Hakupata jibu. akavua kiatu chake kwa taabu sana ambacho mbele kilikuwa na utepe wa chuma kwa ndani kidogo na ulitokeza nje kwa nusu milimita, haikuwa rahisi kugundua kama kuna chuma mbele ya kiatu hicho. Kwa kutumia nguvu hafifu za mkoni aliingiza ndani ya kiatu chake vidole vyake na kufyatua chuma kile, kikachomoza kwa mbele akakifungua kwa taabua nacho kikatoka, kama ni mdudu basi hatojibu, alijisemea.



    Alikumbuka alipokuwa Urusi katika mafunzo ya kikombandoo waliwahi kufundishwa jinsi mbalimbali ya kuwasiliana na mtu mwingine pasi na waliokuzunguka kujua, ikiwemo lugha ya macho, vidole, na hata hiyo ya kugonga kitu na kusikiliza idadi ya mapigo ya kitu hicho, mpangilio wake katika makundi na nfasi kati ya kundi moja na kundi linguine. Ilikuwa kila kundi la mapigo linatengeneza silabi Fulani na unapoziunganisha kitaalamu unapata neno kamili.



    Kwa jinsi Fasendy alivyogonga alikuwa akiita Jamir, Jamir. Kwa nguvu kidogo alizonazo nay eye akajibu ka kugonga vilevile kwa mtindo ulele akilirudia lile jina, Jamir. Mara upande wa pili akausiki ukigonga tena ukimpa ujumbe mwingine tofauti, mtu wa upande wa pili alijitambulisha kwa jina lake nay eye ni nani kwa mtindo uleule na akampa ujumbe Jamir kuwa ana uhakika usiku huo wataokolewa na Kamanda Amata kwani tayari yupo Mogadishu kwa siku tano.

    Jamir alijikuta anajivuta na kuketi sawasawa, kitendo ambacho alikuwa hawezi kukifanya hapo kabla, mara baada ya kusikia jina la mtu huyo, Kamanda Amata, alipata matumaini ya kuishi, aliamini sasa mkobozi kafika kama si yeye kukombolewa basi wale wengine wote, lakini mpaka muda huo ni yeye tu Jamir alikuwa anajua walipo kwani alisikia mara kadhaa maharamia hao wakiongea juu yao ama kwa redio au kwa ana kwa ana.

    Hakuwahi kukutana na Kamnada Amata tangu kuzaliwa kwake, lakini alizisikia sifa za kijana huyo machachari, mkorofi, jasusi la kimataifa ambalo linayanyima usingizi mashirika makubwa ya kijasusi kama CIA kwa jinsi anavyotumia akili katika kazi yake.



    §§§§§§

    Kamanda Amata alimbwaga yule mwanamke mhudumu wa hoteli katika chumba kile kidogo cha kwenye gofu.

    “Siwezi kutumia risasi yangu kuua mrembo kama wewe, utakaa hapa na adhabu yako utaiona nikirudi,” Kamanda Amata akamwambia yule mwanamke aliyekuwa akilia muda wote, akachukua kamba na kumfunga miguu yake yote kwa pamoja kisha akamfunga mikono kwa nyuma na kumtupia kitandani akihakikisha hana jinsi ya kujiokoa. Akamtazama usoni na kutikisa kichwa, akatoka na kufunga ule mlango kwa nje akakwe pikipiki lake na kupotelea mitaani.

    Ilitimu saa nne za usiku wakati Kamanda Amata alipokuwa amesimama pembezoni mwa jengo kubwa, godown la nguo, Mogadishu Textile, alikuwa akisubiri muda wake ufike ndipo aanze kazi aliyokuwa ameipanga, aliamini kwa vyovyote kadiri ya maelekezo ya wale wa kwanza kuwa hapo ndiyo bandani. Akalisogeza pikipiki lake kwa kulikokota mpaka karibu na jiwe moja kubwa lililofanya kitu kama pango akalipachika hapo, akajitazama alikuwa na bastola tatu, lakini ni moja tu iliyokuwa imejaa swwasawa nyingine zilitumika hapa na pale, nitapata nyingine hukohuko, alijisemea na kutoka kwenye lile jiwe, akautazama ukuta mkubwa uliozunguka jengo hilo, akajaribu na kutazama pande zingine akagundu ni urefu sawa kutoka kila upande. Juu ya ule ukuta kulikuwa na waya maalumu wa kuzuia wezi, daima waya huu huwa na umeme. Hakuwa na nmna ya kuupanda, alizunguka kuelekea lango kuu, kutoka mbali aliona walinzi wawili wakiwa pale mlangoni. Nitapitaje? Ni swali lililopita akilini mwake, alilisogelea lile lango huku akiwatama vizuri wale walinzi waliokuwa pale langoni, mmoja akiwa ameketi kibandani akimuliwa vizuri kabisa na taa ya umeme na mwingine alikuwa akitembea huku na huko. Akiwa katika kutafakari hilo mara akasikia honi za gari kutoka nyuma yake akalipisha na gari lile kubwa, gari la maji lilikuwa likiingia katika jengo hilo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



     Ilikuwa nafasi pekee kwake, kwa wepesi sana alidandia ngazi ya nyuma na kupanda haraka kisha akajibwaga katika keria ya juu kabisa ya tanki hilo akalala kimya. Ile gari ikasimama kwa ukaguzi na dakika mbili tatu ikaruhusiwa kuingia ndani, hivyo ikamsaidia Kamnda kufika ndani kabisa ya jengo lile lenye ua mkubwa katikati likiwa limezungukwa na maghala makubwa kama manne hivi. Akatulia kutoka kule juu ya gari akisikiliza kinachoendelea, yule dereva akaondoa lile lori kutoka hapo aliposimama akiongea na mtu mwingine, akapita kwenye magari mabovu ili kupata sehemu nzuri ya kuegesha, ni nukta hiyohiyo ya kuyapita yale magari mabovu Kamnada Amata aliporuka kwa ustadi na kutua chini kisha kwa haraka akaingia katika moja ya magari hayo yaliyochoka, akatulian akiangalia mienendo ya watu waliopo eneo hilo. Hakukuwa na watu wengi, nje katika uwa huo mkubwa palikuwa na vijana watatu, bila shaka walikuwa ni walinzi kutokana na silaha walizozibeba katika migongo yao, Kamanda Amata alijaribu kutazama huku na kule hakuona daliliya mtu mwingine, hivyo alikwishahesabu kuwa upande wan je kulikuwa na watu watano na wote wana silaha. Hakujua kuhusu ndani ya majengo hayo.

    Lengo lake lilikuwa ni kufanya uokozi usio na madhara, alimtaka Jamir tu aondoke naye, na alijua akimpata Jamir basi kazi itakuwa imekwisha kama sio kumalizika. Alihitaji kuingia ndani ya maghala yale lakini hakujua ni lipi hasa Jamir atakuwa amefungiwa, hakuyapa muda mawazo hayo, aliutazama mlango mkubwa ambao ulionekana umefungwa, na mwisho wa jengo lile refu kulikuwa na mlango mdogo ambao aliona yule dereva akiingia baada ya kuliacha lile lori lake maegeshoni. Kwa harakaharaka aliona ni kama mwendo wa mita mia mbili hamsini, na akikimbia ni kama robo dakika atakuwa ameufikia, lakini kulikuwa na taa zilizokuwa zikimulika eneo hilo, kazi ipo!



    Hakukuwa na jinsi, alitazama wale jama walivyoketi, kisha kama kishada alichomoka na kukimbia bila kufanya ukelele lakini hakufanikiwa kufika katika ule mlango, akiwa katikati mlinzi mmoja upande wa uani ambako yeye Kamnda hakumuona tangu mwanzo alimbaini.

    “Hey!!!” akaita.

    Mwito huo ulimshtua Amata akatumia akili ya haraka sana badala ya kunyoosha anakokwenda, akakunja kona ya ghafla na kumfuata yule mlinzi alipo kwa maana alijua kuwa akipiga zaidi kelele zake itakuwa ni hatari kwake, aliruka hewani na miguu yake ikatua katika shingo ya yule mlinzi aliyekuwa akiandaa bunduki yake kumlenga Amata. Alimnasa kwa miguu na kushuka nae mpaka chini kwa utulivu, akambana sawasawa mpaka roho ikamtoka. Samahani sikutaka kukuua lakini imebidi, alimwambia kwa mawazo huku akimvuta taratibu mpaka chini ya gari bovu, akaitazama ile bunduki, itanisaidia akawaza, akachukua na koti la yule marehemu akajivika akaiweka bunduki mgongoni, sasa haikuwa na haja ya kukimbia, alitembea akiambaa na ukuta kuufuata ule mlango.



    “Swaleh! Wapi unaenda?” mlinzi mwingine akauliza baada ya kumuona Amata akielekea kule mlangoni. Hakuoneasha wasiwasi wowote badala yake alichanganya miguu na kukimbia kwa mwendo wa taratibu huku akionesha ishara kuwa anaingia ndani atatoka muda si mrefu kwa kutumi mkono wake. Wale wenzake hawakuendelea kumfuatilia walimuacha aende. Kamanda Amata alipofika mlangoni na kuingia, kwenye korido nyembamba inayotokea ndani ya ghala hilo alikutana na yule dereva aliyekuwa akitoka wakati huo. Yule dereva akasimama akimwangalia mtu huyo.

    “We huku vipi? Si mmeshaambiwa msiingia ndani kwa kuwa huku tayari kuna wengine!” yule dereva alizungumza. Kwa kauli hiyo Kamanda Amata akajua kuwa ndani kuna walinzi wengine, akatumia viganja vya mikono yake kumpiga kwa nguvu mabegani, yule dereva na jinsi alivyokonda alikosa nguvu ya kustahimili pigo hilo, alirudi nyuma kwa nguvu na kujibamiza ukutani, kabla hajatua chini alijikuta akitazamana na domo la bastola iliyoshikwa kikakamavu na mwanaume aliyesimama mbele yake. Mwili ulimtetemeka, midomo ikamchezacheza, hakuamini anachokiona, akifikiria jinsi eneo hilo linavyowekwa ulinzi na wale maharamia ambao kila wanapoteka meli, mali zote huhifadhiwa kwenye maghala haya. Mkono wa kushoto wa kamanda amata ukainuka na kuweka kidole cha shahada katika midomo yake akiwa anamwambia yule dereva kimya! Yule bwana alisimama kama sanamu huku taratibu mkojo ukimtoka na kulowesha suruali yake. Kamanda Amata akatazama kushoto na kulia hakuna mtu. Akamsogelea yule jamaa palepale alipo, akamkaba koo kwa kono lake la kushoto.



    “Yuko wapi ndugu yangu mliyemteka?” akamwuliza, lakini yule jamaa hakuna alichojibu zaidi ya kuzidi kutetemeka, macho yake alikuwa akiyageuzia upande wa kushoto mara nyingi, Kamanda akaelewa kama huyo ndugu yake hayupo huko kushoto basi kuna hatari nyingine, kengele za hatari zikamuashiria hilo. Mara ghafla akajikuta akipigwa na kitu kutoka nyuma, kilitua kichwani kikafanikiwa kumchana ngozi ya kisogoni na kuruhusu damu kuvuja. Kwa kuwa aliyepiga hakuwa mzoefu hakuweza kutimiza alilokusudia. Kamanda Amata hakujali maumivu yake, aligeuka na kufyatua risasi na yule mtu akatupwa nyuma akaanguka chini kama mzigo akiwa hana uhai, alipogeuka tu alikutana uso kwa uso na mtu mwingine, alipotaka kufyatu risasi, ile bastola ilishikwa na kitu kama kamba au mnyororo ikamtoka na kuangukia chini. Hakupoteza muda, alimtemea mate yule jamaa, kwa ujinga wake akakwepa, konde moja zito likatua upande wa sikio, akayumba na kujishika sikio, Kamanda Amata akaruka na kujizungusha hewani, mguu wake ukatua sahavuni mwa yule bwana, akaanguka chini kama gunia la mashudu.



    Kabla Kamanda hajajiweka sawa, yule bwana alinyanyuka haraka na kusimama akimkabili Amata, yule bwana alipanga mikono yake na kuiweka miguu katika mtindo wa kupendeza, moja kwa moja kichwani mwa Amata ikaonekana anataka pambano la mikono, hewaa nitakuonesha, Amata akajisemea huku naye akijiweka tayari. Yule bwana akaanza makeke, akarukaruka na kurusha mguu wake wa kulia juu akauzungusha kwa kasi na kuuteremsha katika mtindo unaojulikana kama axe kick , labda hakujua anapambana na mtu wa namna gani, Kamanda Amata alijua pigo hilo litatua wapi katika mwili wake, kwa haraka akainua mikono yake na kuiweka katika mtindo wa X, mguu wa yule bwana ukatua katikati ya mikono ile na papo hapo Amata akaubana ule mguu na  kupiga teke moja kali lililotua kwenye korodani za yule jamaa, akalegea, Kamanda Amata akauzungusha ule mguu na kuushtua mifupa yake, yule bwana alishindwa kusimama na kujibwaga chini. Teke kali la usoni liliruhusu damu za yule bwana kutiririka na kumrudisha chini, Kamnda Amata alimuwahi na kumkanyaga kifuani, akachomoa bastola nyingine na kumuoneshea.



    “Kuwa mpole,” akamwambia yule bwana aliyekuwa anataka kujikukurusha bila sababu, akatulia mbele ya domo hilo la bastola.

    “Yuko wapi mtu wangu?” akauliza. Yule bwana akabaki kushangaa tu, hakuwa na la kujibu. Wakati huo huo aliskia michakacho ya miguu ya watu waliokuwa wakija ndani kutoka nje, akajiweka tayari, nukta hiyo hiyo, alimuona mmoja aliyeingia mlangoni na bunduki aina ya SMG, Kamanda Amata akajirusha upande wa pili na risasi zilizotoka kwenye bunduki hiyo zikachimba ukuta. Kamanda Amata alipotu akainua bastola yake iliyokuwa chini, sasa mikononi mwake zilikuwa bastola mbili, alijibiringisha chini na kutua kwa magoti, bila kuchelewa bastola yake ilikohoa na kumtumpa mbali yule askari aliyekuwa mlangoni, risasi ya pili ilipiga bega la yule aliyekuwa akipambana naye, naye akalala chini kimya. Kamanda Amata akamruka na kujibanza nyuma ya kitu kama kabati, akawasikia watu waliokuwa wakija wakikimbia.

    “Upande huu,” mmoja alimwambia mwenzie.

    “Hapana mimi nimesikia huku,” mwingine alijibu.

    Kamanda Amata akatulia palepale akawa anaangalia watu hao ni upande gani watatokea, alipoona wanakuja wote wawili kutoka mbele akarudisha bastola moja kwenye kikoba chake na kubaki na moja. Mtu wa kwanza akapita, wa pili alipofika lile eneo, akamdaka kwa mkono mmoa na kumvuti nyuma ya lile kabati, akampiga kabala ya maana na kumuwekea bastola katika sikio lake, alihakikisha yule kijana hawezi hata kupiga kelele.



    §§§§§

    FASENDY alishtuka alipusikia mlio wa bastola, akatulia kusikiliza kwa makini, akasikia wa pili kisha watu wakiongea ongea akajua kumekucha, akajua mzee wa kazi ameingia, akainuka na kuanza kupiga push up kujiweka tayari kwa mapambano, alichemsha mwili. Kisha akachukua ile pete yake na kugongagonga ukutani kuongea na Jamir upande wa pili, aligonga gonga kama dakika moja na nusu hivi kisha akatulia.

    Upande wa pili nao ukaanza kugongwagongwa, Fasendy akatega sikio na akili yake kusikiliza mlio huo hafifu kutokana na nguvu ndogo aliyokuwa akitumia Jamir kugonga.



    …Kamanda Amata bila shaka ameshafika…

    Ndivyo Fasendy alivyokuwa akimwambia Jamir kwa ule mtindo.



    …Nimesikia milio ya risasi, lakini sina uwezo hata wa kutembea…

    Akajibu Jamir, kisha kila mmoja akatulia kwenye selo yake akisubiri kuona kinachoendelea.



    Fasendy aliuendea mlango wa kijichumba hicho alichofungiwa, akajaribu kupapasa na kukipata kitasa, akajaribu kukitikisa lakini kilikuwa kimefungwa sawia, hakuweza hata kuutikisa ule mlango. Akahama kwenda upande mwingine, akajikwaa kwenye kitu kama chuma na kuanguka chini, “Shenzy” akatukana na kumalizia na tusi la nguoni, akakivuta kile chuma kumbe kilikuwa ni kipande tu, akainuka nacho na kusogea karibu na ukuta, afanye nini, akili ikamzunguka.



    …Jamir sogea mbali na huu ukuta…

    Alitumi lile chuma kugongagonga ukuta kumpa ujumbe ule Jamir, ikawa hivyo. Kwa pigo moja la nguvu, Fasendy aliupiga ukuta kwa lile chuma na ule ukuta ukaonesha udhaifu, ulikuwa ni ukuta wa inchi tano tu, pigo la pili liliangusha vitofali kama vine hivi, pigo la tatu likashusha vingine kama vitano, pigo la tatu likatengeneza tundu la yeye kupita, mara ule mlango wa kile chumba ukafunguliwa. Fasendy kwa kutumia hisia tu, akajua hapa nimekwisha, akaruka kwa ustadi wa hali ya juu na kupenya kwenye lile tundu akadondokea chumba cha Jamir, Mungu si Athumani na wala Athumani si Mungu, Fasendy alikuwa ameruka na lile chuma mkononi mwake, alipotu sakafuni akajibiringa vizuri na kulirusha kwa nguvu lile chuma kulenga lile tundu.

    Yule mlinzi alipoona Fasendy kapenya kwenye lile tundu aliamua kumfuata, alipomulika na tyochi yake na kujaribu kuchungungulia ndipo alipokutana nachuma hilo lenye tundu katikati, lilipiga usoni na kumsababishia maumivu makali. Yowe la uchungu lilimtoka na nukta hiyohiyo kama akili yao ilifanana, Fasendi alijirusha akatua kushoto mwa lile tundu akilipa mgongo na kuegemea ule ukuta kumbe na jinsi hiyohiyo Jamir alipata nguvu za ghafla na kujirusah akatua upande wa kulia wa tundu hilohilo akaketi vilevile kama Fasendy.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    §§§§§§

    Mlinzi mmoja alikuwa akihangaika kupiga simu ndani ya chumba kilichotumika kama ofisi, lakijni kila alipoweka sikioni kimya, kila aliporudia na kuweka sikio kimya, akaipiga chini ile simu alipogundua kuwa laini zote za simu zimekatwa, hakuna simu ya kutoka nje ya maghala hayo, alipogeuka tu alikutana na uso kwa uso na Kamanda Amata. Akajaribu kujichekesha, lakini akakuta uso wa Amata umedinda kwa hasira hakuna cheko wala tabasamu.

    “Twende ukafungue,” akamuamuru yule mtu. Naye kwa haraka akachukua funguo na kutangulia mbele huku Kamanda Amata akiwa nyuma yake.

    “Shamsiiiiii usifungueeee!!!” kelele ilitoka upande wa juu, Kamanda Amata akatazama kwa haraka na kujitupa mbele akampamia yule jamaa mwenye funguo wakaenda wote chini, akammnyang’anya funguo na kuzibana kwa meno, akachomoa kisu na kukirusha, kikampata yue jamaa kooni, akadondoka kutoka pale juu mpaka chini.

    “Ingieni ingieni, yupo huku!” kelele ilitoka kwa chini, kamanda Amata alitazama harakaharaka akaona watu kadhaa wenye silaha wakiingia ndani ya ghala hilo, kasheshe. Kamanda Amata alipokuwa akiondoka, yule bwana aliyekuwa na funguo akamdaka mguu, Teke la kisigino likatua kwenye pua yake, akaguna na kumuachia, Amata akageuka na kumzabua tekea kali la uso, lililomdondosha toka juu mpaka chini.



    “Yuko juu,” mmoja akasema.

    “Aaaaaa anawafunguliaaa,” mwingine akajibu kisha wote wakaanza kupanda ngazi kuelekea kwenye ile njia ya chuma iliyojengwa juu. Kamanda Amata alifika mlango wa kwanza na kujaribu kufungua lakini ulikuwa haufunguki. Alipotazama mbele kulikuwa na milango kama mine hivi. Mara akasikia mlango mmoja ukigongwa kwa ndani, akajua ni huohuo akaukimbilia na kutumbukiza funguo, mlango ukajibu.

    “Jamir, Jamir,” akaita.

    “Kamanda Amata,” sauti ya Fasendy.

    “Fasendy!,” naye akaita tena.

    “Asante Kamanda, lakini Jamir hawezi kutembea kwa jinsi alivyonieleza,” Fasendy akasema.

    “Yuko wapi Jamir?” akauliza.

    “Huyu hapa.” Kamanda Amata akavua bunduki aliyokuwa ameipachika mgongoni mwake na kumpa Fasendy, “Haya mama, un trabajo,” akampigapiga mgongoni, kisha akmuendea Jamir aliyekuwa bado ameketi kuuegemea ukuta. Akamtazama lakini hakuweza kufanya lolote kwa wakati huo, maharamia sasa walikuwa wakikimbia kwenye ile njia ya chuma kuelekea kule waliko Amata na watu wake.

    Fasendy akajitokeza mlangoni na kuiinua ile bunduki akaiweka sawa kwa kuiondoa usalama, akafyatua risasi mfululizo kuwaelekea wale jamaa, kelele za mayoe zikasikika wengine walijirusha chini bila kuambiwa wengine walianguka wakiwa hawana uhai, Fasendy alipoangalia chini, aliona bado kuna wengine, kazi ngumu.



    “Kamanda, tutoroke hapa hapafai,” alimwambia Kamanda Amata kwa lugha ya Kiswahili ambayo wale maharamia walikuwa hawajui chochote. Alipotaka kutoka pale alipo kuja ndani alikomuwacha kamanda na Jamir, alirudi tena nje na kumfuata askari aliyelala chini bila uhai, akachomo bunduki lake kubwa na kutoroka nalo. Akaingia kwenye kile chumba akihema akamkabidhi Amata lile jibunduki. Kamanda alipolipokea, akatukana tusi la nguoni, akalipachika begani mwake, lilikuwa ni RPG 7, akalitegua na kulifyatua, lile grenade lake likafyatuka na kupiga ukuta ulio mbele yao likaacha tundu kubwa la kupita Suzuki.

    “Fasendy twendeee!!!” Kamanda aliita kisha akamnyanyua Jamir na kutoka naye kwenye lile tundu, akajirusha mpaka chini, Fasendy naye akafanya vivyo hivyo. Kamanda Amata akachomoa bastola moja na kumpatia Jamir hata kama hakuwa na nguvu, ili mradi ajitetee kwa lolote.



    §§§§§§

    SIMU ya kitandani iliita kwa fujo, Shalabah akaamka na kutoa tusi baya, tusi lilikuwa likimlenga huyo anayepiga hiyo simu. Akainyanyua na kuiweka sikioni.

    “Hello, Hello, Chieeef, Chiefff,” ilikuwa sauti ya mtu anayehongea kwa kihoro.

    “Nini wewe ongea,” Shalabah akajibbu kwa ukali.

    “Tumevamiwa Chief, tut u tume vvvamiwa, bandani!” yule mtu akasema.

    Shalabah alijikuta anaishiwa nguvu, akasimama haraka akatoka kitandani na kuliendea kabati lake akafungua na kuto bastola mbili na shot gun moja akataka kutoka ndani.

    “Wewe!” ilikuwa sauti ya mkewe ikitoka pale kitandani,” Shalabah akageuka na kumwangalia, “Sasa mbona unaondoka bila nguo?” akauliza mkewe.

    Shalabah alipojiangalia, akajikuta kweli yuko uchi, kuchanganyikiwa! Akavaa nguo harakaharaka na kuchukua bunduki yake, unajua Somalia kila mtu anakaa na bunduki ndani, akatoka haraka na kuingia garini, akatoka kwa kasi kuelekea bandani. Njiani kote alikuwa akiuma meno kwa hasira, yaani huyu mshenzi kama ni embe nitamtafuna na maganda alijisemea huku akib akibadili gia na kuweka ile ya tano au mkoba kama mnavyoita vijana, akiwa katika barabara kubwa inayojulikana Alipishana na pikipiki kubwa iliyokuwa ikienda kwa kasi ya ajabu, akitazama harakaharaka na kuendelea na safari yake kwenda ghalani, kichwani mwake akiwa kagabhibika sana.



    §§§§§§

    DAR ES SALAAM ˜TANZANIA

    KATIKA chumba kimoja maalum cha mawasiliano, ndani ya jengo la makao makuu ya JW pale Upanga kulikuwa mo jopo la watu takribani sita wa vyeo vya juu kabisa vya Jeshi la Wananchi, kati yao akiwemo Mkuu wa Jeshi la Wananchi Jenerali Kamsumi pamoja na msaidizi wake Brigedia Kyambasa na wengine wane wanaowafuatia kwa vyeo vya kijeshi, walikuwa mo pia wanajeshi wa vyeo vidog lakini sio vya kawaida, pamoja nao, wote walikuwa macho yao katika luninga kubwa iliyofungwa ukutani, pale waliweza kufuatilian operesheni iliyokuwa ikifanywa na Kamanda Amata kule Mogadishu.

    TSA 2 alikuwa ndiye mtaalam wa kuunganisha mtambo huo na satellite ambayo iliweza kuwaonesha matukio yote kutokana na muunganiko kati ya ile satellite na ile chip aliyowekewa Amata mwilini mwake, waliweza kuona picha japo zilizofifia lakini bado waliweza kuona kinachoenndelea. Madam S alikuwa kimya kabia akifuatilia huku moyo wake ukiwa na kihoro ndani yake, aliona uzito wa kazi, akajua kweli Kijana wake ana kibarua.



    “Eeeeeeeee!!!!!!! Safi sana Kamanda Amata,” ilikuwa ni sauti ya Brigedia Kamsumi aliyesimama ghafla na kushangilia huku akipiga kofi moja kuonesha ishara ya furaha na wengine nao walionekana kumuunga mkono kwa kupiga makofi kwa kazi nzuri alioionesha Kamanda Amata kwa kumuokoa Jamir. Dakika hiyo hiyo, saa ya Madam S ikamfinya kumpa ishara kuwa kuna mesej inaingia, akairuhusu nay o ikaanza kutoa mkanda wenye maandishi.

    …Nimemuokoa Jamil lakini hali ni tete ninahitaji msaada…

    Madam S alimtazama mkuu wa majeshi na kumpa ishara ya kumsikiliza, akamuonesha uole ujumbe. Yule mkuu hata bila kufuata utaratibu alisimama na kuwageukia wasaidizi wake, wakuu wa vikosi mbalimbali.

    “Ndugu tunahitajina kutoa msaada wa haraka, Kamanda Anata ameomba, tunafanyje?” akauliza kwa kutupa swali kwa wasaidizi wake. Hakuchukua hata sekunde kumi, mwanajeshi mmoja mfupi aliyeshupaa alisimama akiwa amechafuka kwa vyeo mbalimbali vya kijeshi, alikuwa amevaa vazi la bluu bahari na kifuani mwake upande wa kushoto chini ya jina lake kulikuwa na picha kubwa ya chuma iliyoonesha alama ya bawa. Alikuwa ni mkuu wa kikosi cha wana anga cha JW.



    “Naomba nipeleke tai wawili sasa hivi, ni saa moja tu watakuwa pale, wakatoa msaada wa haraka,” akalieleza jopo huku akivaa kofia yake iliyokuwa mezani muda wote.

    “Sasa hiyo vita Kiongozi!” aliongea mwingine bila kujali utaratibu.

    “Ndugu wajumbe Jamir ni komandoo wetu na Kamanda Amata sote tunajua kazi yake, Komandoo mmoja ni sawa na batalioni moja , Kamanda Amata akisema jambo lazima lipewe kipaumbele huwezi kujua ni kitu gani anachokabiliana nacho kwa sasa, hatuna budi kutoa uamuzi, Kiongozi fanya uwezalo,” Mkuu wa Majeshi akaruhusu kutumwa ndegevita mbili kwenda Somalia kusaidia operesheni.



    §§§§§§

    Wakati kikao hicho kikiendelea hali ilikuwa si shwari kwa katika ubalozi wa Somalia, pamoja na kupokea pesa nyingi sana kutokana na biashara ile haramu, Balozi wa Somalia alijipanga kuondoka usiku huo huo, akijua kwamba akisubiri sana itakuwa ni jambo la aibu kuzuiliwa kuondoka nkatika nchi ya ugeni. Alipopewa habari na Waziri wa ulinzi juu ya sakata au opereshani inayoendelea, hakuona haja ya kupoteza muda, maadam alikuwa na uwezo wa kuondoka na usafiri wowote anaotaka, aliamua kuondoka usiku huo huo.

    Askari kanzu wa kitengo cha usalama wa Taifa walikuwa wametawanywa kuchunga baadhi ya watu wanaotuhumiwa kwa sakata hilo la hujuma, kila mmoja alitakiwa kuhakikisha mtu aliyepewa kumwangalia asimpotee hata nukta moja na taarifa kila baada ya dakika kumi azitoe katika ofisi ya Usalama wa Taifa. Ulikuwa ni usiku wa aina yake, wenyewe wakiwa wamelala na wake zao wakikenua kwa sababu pesa nyingi zimewafikia siku hiyo na kujaza vitabu vyao vya benki hawakujua kabisa mbilinge lililopo huko nje linalowasubiri pindi tu amri ikitolewa. Hawakuju kama wamepewa ulinzi huo usio rasmi, mwingine aliwaza kununua Vogue, mwingine kujenga hoteli, yule kule kuhamia USA na huyu huku kuongea wake wawili wanafunzi wa sekondari, kila mmoja aliwaza tu atatumiaje pesa hizo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Gina aliinua mkono wake na kusoma saa, ilimuonesha inakimbilia saa saba za usiku, aliendelea kutuli palepale katika barabara ya Sea View akihakikisha anaitazama nyumba ya Balozi wa Somalia, akihakikisha kuwa mtu huyo bado yuko ndani na asiondoke usiku huo, akiwa katika hali hiyo, akaona lango la mbele likifunguliwa na gari moja nyeusi, Marcedes Benz ilitokeza pua yake ikiwa imewasha taa, ikawasha indiketa za kulia na kuingia barabarani kuelekea mjini. Gina akaitazama kwa chati na kuona mtu aliyetuna katika kiti cha nyuma, mara simu yake ikaita, akaichomoa na kuiweka sikioni.

    “Ametoka na gari…” ilikuwa sauti iliyotoka kwenye ile simu na kuingia katika sikio la Gina, sauti ya mlinzi wa mlangoni katika nyumba ya balozi, mlinzi wa kampuni binafsi lakini ilhali ni mtu wa idara ya Usalama wa Taifa. Gina aliingia garini na kuondoka kuifuatilia ile gari taratibu, ilipita barabara ya Ocean Road na kuifuata mpaka Magogoni, ilipanda na barabara ya Kivukoni mpaka ikatokea katika kituo cha boti za kwenda Zanzibar, ile gari ikateremka chini kuifuata hiyo barabara na kusimama mbele ya mlango mkubwa. Yule Balozi akateremka, alikuwa peke yake, pale akapokelewa na mtu mwingine mwenye asili ya Kiarabu au Kizanzibari akaingia naye ndani.



    Gina alipiegesha gari yake mbele kidogo ya eneo hilo karibu kabisa na nji ya kuingilia ofisi za NASACO, akateremka na kuruka ukuta mfupi ulikuwa eneo hilo akapita kwa uangali bila kufanya kelele mpka eneo ambalo aliweza kuona japo kwa mbali kinachoendelea. Alimuona yule Balozi akteremka ngazi akiongozwa na yule bwana aliyempokea mpka kwenye boti moja ya kifahari iliyokuwa imeegeshwa hapo gatini, wakaagana na yule bwana kisha akaingia katika boti na dakika tatu zilizofuata ile boti ikaondoka kwa kasi. Gina aliitazama mpaka ilipopotelea katika giza la usiku katikati ya bahari, akatoka na kurudi katika gari yake, akaketi nyuma ya usukani, akavua miwani aliyokuwa ameivaa na kufyatua kioo kimoja cha miwani hiyo, akachomo memory card ndogo na kuipachika katika kishikio chake kisha akaingiza mahali Fulani kwenye dashboard, akabofya mahala Fulani na ikafyatuka luninga ndogo ya inchi saba akatazama picha alizokuwa akipiga kwa kutumia miwani hiyo, picha huyo Balozi akiwa pale bandari ndogo, aliitazama picha ya yule bwana aliyekuwa akiagana naye ambaye ndiye aliyempokea, akasoma maandishi ya nyuma ya boti ile yaliyochongwa kwa chuma nyuma yake ‘Sea Cruiser’ ya kiafuataiwa na namba ya usajili. Alipojiridhisha na kila kitu akaondoa gari uake huku akimpa taarifa Madam S kuwa Balozi ametoroka.



    MOGADISHU – SOMALIA

    FASENDY alimpa chupa ya maji Jamir, akayachukua na kuyanywa kwa fujo, kisha Kamanda Amata akatoa aina Fulani ya vidonge viwili akampa kula, akimwambia asivitafune ameze moja kwa moja. Dakika tano baadaye hali ya Jamir ilianza kurudi, nguvu ziliznza kumrudia, vile vidonnge vilivyokua na mchanganyiko wa vitamin zote na glucose kwa kiwango cha juu. Jamir alisimama japo hakikuwa kwa nguvu ileile lakini alifanikiwa.

    “Unajisikiaje?” Kamanda aliuliza.

    “Kidogo afadhali, hata naweza kusimama, maana wale jamaa sijui walitaka niweje japo najua walipanga kunikata kichwa asubuhi inayokuja,” Jamir akalekeza. Kamanda Amata akasonya, “Wakakate vichwa vya ndugu zao,” akamaliza kwa maneno hayo. Akamtambulisha kwa Fasendy harakaharaka. Kisha akawaeleza kwa kifupi juu ya yule mwanamke mateka aliyemfunga kamba ambaye alimhifadhi kwenye kile chumba kidogo.

    “Tusipoteze muda Kamanda, sasa tunafanya nini?” Jamir akauliza.





    “Sasa ni kuvamia ngome yao kuu, nataka tukawaokoe wale wengine ishirini na tano lakinisijui walipo wala huyu (akamuoneshea Fasendy) naye hajui walipo,” Kamanda akaeleza.

    “Kamanda, hawa jamaa wamehifadhiwa ndani ya chumba maalum katika bandari ya zamani ya Mogadishu, sasa shida tutaingiaje?” jamir alitoa jibu.

    “Mimi nilishawahi kuingia, lakini nilitumia njia ya bahari, nilipiga mbizi na kupitua kwenye bomba kubwa la kutoa na kuingiza maji katika eneo la chini la bandari hiyo,” kamanda alieleza.

    “Na hiyo ndo njia pekee salama ya kupita, kuna milango mikubwa mitatu, Kusini kuna mmoja ambao ukiingia unatokea gatini, Kaskazini nako upo mwingine ambao ukiingia unatokea eneo la kuegesha magari ambalo mbele yake kuna majengo yaliyokuwa ofisi na kupitia hapo unaweza kuteremka kwenda chini, njia zote zina ulinzi mkali sana, zinalindwa na watu wasiomjua Mungu ambao kuua kwao ni sherehe,” Fasendy akaeleza. Wote watatu wakatazamana.



    “Tungeweza kupita kwa njia hiyo ya kupiga mbizi, lakini vifaa sasa tutapataje,” Jamir akaonesha mashaka kwa hilo. Bado ilikuwa kitendawili, Kamanda Amata alitazama saa yake ilikuwa tayari inakimbilia saa saba za usiku.

    “Aaa Kamanda nimekumbuka, kule bandari mpya kuna kitengo cha wapiga mbizi unaonaje tukienda kuazima vifaa?” Fasendy akatoa wazo, Jamir akamwangalia mwanamke yule aliyeshupaa misuli utafikiri mwanaume mnnyanyua vyuma.

    “Tukaazime usiku huu?” Jamir akauliza.

    “No, yaani tukaazime, tuchukue hivyo vifaa kwa njia yoyote ile, tena naomba tuharakishe kabla ya alfajiri tumalize hii kazi,” Kamanda Amata akasema hayo na kuaharakisha kutoka mle ndani.

    “Watakuwa wanatusaka, hivyo tutumie miguu, sio mbali kutoka hapa, nitawaonesha njia ya siri,” Fasendy alieleza kisha akatangulia kutoka na Jamir akafuata na Kamanda Amata akawa nyuma na bastola yake mkononi kulinda usalama. Walizunguka nyuma ya gofu lile na kuteremkia bondeni, wakapita kwenye mikoko na kuambaa na uoto huo mpaka eneo lililokuwa na ukuta ambao uliwezekana kupandika kiurahisi, Fasendy akawaonesha ishara ya kukwea ukuta huo, yeye mwenyewe akawa kwanza kuukwea akifuatiwa na Jamir na baadae Kamanda Amata kisha wote wakatua ndani kwa utulivu, kwa kujificha ficha katika malori ya mafuta yaliyoegeshwa hapo, walipenya na kufanikiwa kufika eneo husika. Kulikuwa na walinzi watatu waliokuwa wakizunguka eneo hilo.



    Kamanda Amata akasogea mbele kabisa na kuwatazama wale walinzi jinsi walivyojipanga, akaonesha ishara ya vidole kumuonesha Faendy amtwae mmoja na Jamir amtwae wa pili yeye atamtwaa wa tatu, aliwapa maelekezo kwa mkono wasiue watu wasio na hatia bali wawalaze usingizi wa maana, alipoonesha ishara ya kuruhusu tu, kila mmoja allichomoka alipo na kupiga pigo moja kali kwa watu hao nao wote wakaanguka chini kila mmoja kwa sekunde yake. Kamanda Amata akautazama ule mlango, ulikuwa ni mlango wa chuma, uliofungwa madhubuti kabisa, akamwambia Fasendy na Jamir waangalie usalama huku na huko, pembeni kulikuwa na Fork Lift, mashine ya kuinulia mizigo mizito, akaingia na kuiwasha, nayo haikuwa na hiana hata kama operetta haimjui, akaisogeza taratibu mpaka kwenye ule mlango, akachomeka yale meno uvunguni na kuanza kunyanyua, sekunde thelethini tu ule mlango ulikuwa chini.

    Wakatulia kidogo, hakukua na lolote, wakaingia ndani ya chumba hicho, hakika Fasendy hakuwaongopea, walikuta vifaa vya kuogelea vingi vya kutosha, wakachagua na kujibebea kisha wakatoka na kutokomea kizani bila walinzi wan je kujua kinachoendelea ndani.



    §§§§§§

    Meli kubwa ya mizigo ilikuwa ikisogea taratibu katika bandari ya zamani ya Mogadishu, juu yake kwenye deki ya mbele kulikuwa na watu kama kumi wenye silaha kali wakiwa wamesimama kila mmoja alikuwa akiangalia upande wake. Walikuwa ni Maharamia wa Somalia wakiiongoza meli hiyo kuingia katika gati hilo huku wenzao wa pale bandarini wakifuarahia kwa kupiga risasi hewani kama watu waliorukwa na akili.

    Ile meli ilisogea taratibu sana huku ikisindikizwa na boti mbili ndogo, moja kila upande.

    “Iweke upande upande karibu na gati kuu,” ilikuwa sauti ya Hussein ikiongea kwenye simu ya upepo. Akatoka na kumwita kijana mmoja.

    “Sikia, sasa naomba uweke ulinzi wa kutosha hapa na ulinde kila kona maana sasa ndio tunafanya kazi,” Hussein akamwambia yule kijana, kabla hajamaliza simu yake iliita, akaichomoa na kuiweka sikioni.

    “Chief nipe habari, mbona unachelewa huku bandarini?” akaijibu simu na kumtupia swali.



    “Hussein, huku ni maafa, yule mshenzi kaondoka na mateka wetu na ametupotezea wapiganaji kama saba hivi,” Shalabah alimpa ujumbe huo Hussein. Simu ikawa nzito haikuweza kukaa sikioni tena, Hussein akahisi kuingiwa na ganzi ya miguu. Mh, safari hii tumepatikana akajiwazia hukua akiwa mpole ghafla.

    Ile meli kubwa iliyoandikwa maneno PARPADOS ubavuni mwake, ikasimama gatini kabisa na kufungua mlango wake wa nyuma. Wafanya kazi walikuwa wametingwa kuanza kupanga vitu ndani ya meli hiyo ambayo ilitakiwa ing’oe namnga usiku huohuo isionekane kama ilikuwa eneo hilo. Huseein akaingia kwenye lifti na kushuka mpaka chini ambako shughuli zilikuwa zikiendelea za kuyafungua yale makombora ili kuanza kuyapakia katika ile meli.



    §§§§§

    Kamanda Amata, Fasendy na Jamir walijitosa ndani ya maji na kupiga mbizi maridadi, kisha wakajivuta kuelekea lile eneo walilokusudia, Kamanda Amata, alikuwa mbele na wengine hao walikuwa wakimfuata, aliufikia ule ukuta uliojengwa ndani ya maji akapapasa na kuufuata kuelekea lile tundu alilopitia siku alipokuja huko chini. Alipofika pale hakuamini anachokiona, lile tundu lilikuwa limefungwa kabisa, akatikisa kichwa kisha akawaonesha ishara wenzake kuwa watafute njia nyingine kuweza kufika ndani ya jengo walitakalo. Kamanda Amata akazunguka mpaka kule kwenye lango kubwa alilojaribu kukata mnyororo na kufuili lake lakini nako alishangaa kuona kumefungwa upya na madhubuti zaidi, akaona kuwa siku hiyo hana ujanja mwingine wa kuingia kwenye ngome hiyo, waliendelea kutalii. Walipozunguka upande wa pili ndiko walikoona kile ambacho hawakukitarajia au hawakukijua, mkuku wa meli kubwa iliyosimama gatini, Fasendy akamuonesha ishara Kamanda Amata kuwa waifuate, kisha yeye akajigeuza ndani ya maji kwa jinzi ya kuoendeza.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dakika kadhaa waliifikia ile meli kubwa, Kamanda Amata akiwa ndani ya maji aliweza kuona mianga tu ya taa za huko nje na si zaidi, akawatazama wenzake akakuta nao wanamtazama yeye, akawapa ishara ya kuikwea ile meli pale ilipo, akatangulia yeye. Pembeni mwa meli ile kulikuwa na ngazi ya chuma inayopanda kwenda juu, akaikamata na kuikwea taratibu, kichwa chake kikajitokeza nje ya maji akatazama akaona kila mmoja alikuwa bize na shughuli yake, akakwea harakaharaka na kufika juu ambako alijitupia na kudondokea kwenye magunia yaliyopangwa eneo hilo la meli, akatulia kimya. Dakika moja baadae, Jamir alikuwa juu, Kamanda akampa ishara ya kuingia na akmuonesha mahali pa kujibana ili asionekane na watu hao. Fasendy naye akafika, akapewa ishara akaifuata. Wote watatu sasa walikuwa ndani ya deki la meli ile, wakiangalia kila kinachoendelea, wakagawana sehemu za kutega, kila mmoja akavua ile mitungi ya gesi na kubaki na nguo za kawaida. Kamanda Amata alikuwa akifikiri watateremka vipi kule chini ili kuweza kuingia ndani ya himaya ile, himaya ya Maharamia wasiosikia la muhazini wala mnadi sala.

    Kamanda Amata hakuona haja ya kupoteza muda, alinyata taratibu na kumuendea Fasendy, “Tunahitaji silaha,” akamnong’oneza, kisha akamwendea Jamir na kumpa ujumbe ule ule, wakajiweka tayari na kupanda juu, akawapa ishara na wote wakapanda kwa kasi ngazi za kwenda juu. Jamir alipoibuka mlangoni tu alikuta uso kwa uso na mtu mmoja aliyekuwa na nia ya kuteremka kule kwenye deki, alimkumba kwa nguvu na kumtupa nyuma, yule kijana aliposimama tu alichezea makonde manne ya maana akarudi ndani, Jamir akajirusha kwa uzuri sarakasi moja matata sana na alipotu mguu wake ukatua tumboni mwa yule mtu, akatoa mguno hafifu wa maumivu, akatulia kimya. Jamir aliivuta bunduki aina ya Sot Gun aliyokuwa nayo mkononi yule mtu, akajivuta mbele kidogo na kutazama huku na kule, hakuna mtu, kisha akatoka mpaka kwenye deki na kumpa ile bunduki Fasendy, yeye akabaki na bastola alipewa na Kamanda Amata.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog