Search This Blog

Sunday 22 May 2022

HUJUMA - 2

 







    Simulizi : Hujuma

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    4… nangumbu – Lindi Vijijini



    WATOTO wa shule ya msingi walisikika wakipiga kelele za woga, wakikimbilia madarasani na wengine porini. Waalimu wao walitoka nje kuangalia watoto hao wanakimbilia nini. Helkopta kubwa lilikuwa likitua katika uwanja wa shule hiyo.

    Nyumba kubwa iliyozungukwa na maua mengi ya kupendeza, ilikuwa mbele yao, gina aliielekea mpaka mlngoni na kugonga kengele. Kamanda Amata akaibuka mlangoni na kuwatazama wawili hao.

    “Karibuni sana,” akawakaribisha.

    “Kamanda sisi sio wa kukaa,” Scoba akamwambia.

    “Hata kama sio wa kukaa, lakini Gina hapa ni nyumbani kwake hawezi kuingia na kutoka,” Kamanda akawaambia huku akitoa miwani yake usoni, shati lake lilionesha wazi kuwa alikua ni mtu katoka shambani muda si mrefu.

    “Kamanda Amata, hali ya mama yako ni mbaya sana, unatakiwa kuja nyumbani kumsaidia,” Gina alimwambia Kamanda kama alivyoagizwa na Madam S.

    “Najua, na nanjua kuwa hali yake mbaya lakini kwa sasa mwacheni afe, sina msaada,” Kamanda Amata alijibu huku akiipachika tena miwani yake usoni.



    “Kamanda, hebu fikiri mara mbili juu ya hili, mpaka kukufuata na usafiri maana yake ni kuwa tuondoke sasa hivi,” Scoba alikazia.

    “Haitatokea, nimebanwa sana na shughuli za kilimo, mahindi yangu yananihitaji, mikorosho nayo ndiyo hiyo hapo, vyote hivyo vinanisubiri, mifugo yangu hata sina mtu wa kuniangalizia nikitoka,” Kamanda akawaambia. Mazungumzo yalikuwa magumu sana kati yao na Kamanda Amata, haikuwa rahisi kwa Kamanda kukubali wito huo.

    “Ninyi nani aliyewatuma, mpaka mnapoteza mafuta ya hilo chopa, kulileta huku porini kwetu?” Amata akauliza.

    “Tumetumwa na ofisi, bibi kachanganyikiwa anakuhitaji nyumbani,” Scoba akasisitiza. Gina wakati huo alikuwa ameingia ndani na kuwaacha wawili hao wakiwa bado na mvutano.

    “Sikiliza Scoba, nenda kamwambie Bibi, siwezi kuja hata kwa mkinivuta kwa bulldoza,” kamanda Amata akamaliza mazungumzo yake akanyanyuka na kuondoka zake. Akamtazama Scoba palepale alipomuacha yeye akapanda pawatila yake na kuingia kazini.



    §§§§



    Madam S, aliinama mezani, alionekana wazi kuchanganyikiwa kwa jibu alilolipata kutoka kwa Gina na Scoba.

    “Amekataa kabisa amesema hawezi kuja kwa lolote,” Gina akamaliza.

    “Hata wewe Gina umeshindwa kumbembeleza Kamanda aje, unaniangusha Gina, umeingia kitengo cha ujasusi lazima ujue sometime kutumia body language,” Madam S alimwambia Gina. Ukimya ukatawala kati yao, Madam S hakuwa na la kusema, akanyanyuka na kutoka nje ya ofisi, akachukua gari yake na kuondoka.

    Breki yake ya kwanza ilikuwa mbele ya ofisi ya wizara ya ulinzi, moja kwa moja akaingia katikia ofisi yam zee huyo anyependa kuitwa mheshimiwa pa si kuwajibika sawasawa kwa Watanzania.

    “Ndiyo Madam, najua umerudi na jibu zuri kinywani mwako,” mheshimiwa waziri akasema.



    “Hapana, hapa nimekuja kukwambia kuwa ofisi yangu haiwezi kiufanya kazi uliyonipa kwani uwezo tulionao ni mdogo sana kiutendaji mpaka tujipange nah ii itachukua miaka mingine sita,” Madam S akamwambia waziri wa ulinzi. Alipomtazama usoni waziri huyo alionekana kuvimba sura kwa hasira.

    “Madam S, wizara ikishakupa kazi imekupa, utajipanga vipi utajua wewe, sasa habari za kunambia kuwa hauko tayari mimi sizielewi, unajua kabisa kuwa hili tayari limeshaiweka ofisi yangu katika hali ya sintofahamu, Mheshimiwa Rais atanielewaje wakati nimemhakikishia kuwa kila kitu kitakuwa sawa?” Waziri wa ulinzi akaongea kwa ukali, huku akiwa amesimama, kauma meno yake na kupigapiga ngumi mezani kwake.



    Madam S naye alipoona hayo akawa amesimama akimtazama baba huyo aliyekuwa akipiga kelele bila mpangilio.

    “Sikia, mheshimiwa, ulimpomfukuza kazi Kamanda Amata ulitegemea nini?” Madam S akamwuliza waziri. Kimya kifupi kikatawala kati yao.

    “Kwa hiyo unasemaje?” waziri akamwuliza Madam S.

    “Nasema kazi haiwezekani, nenda kamwambie na mheshimiwa Rais hivyohivyo kuwa TSA haiwezo kufanya kazi hii mpaka miaka sita ijayo, watakapomtengeneza TSA 1 mwingine,” Madam S akamaliza na kugeuka kuondoka zake.

    “Madam,” waziri akaita, Madam S akasimama akageuka kumtazama, “Kibarua chako kipo mashakani,” akamwambia, huku akiwa ameuma meno kwa hasira. Madam S akatoka na kubamiza mlango nyumba yake.

    Hali ilikuwa tete kwa waziri wa ulinzi, aligundua kosa kubwa sana alilofanya miezi sita nyuma katika mkasa ambao uliandikwa kama riwaya na kupewa jina la Julai 7. Aliwaza na kuwazua hakuna jibu alilolipata juu ya hilo, alihisi uzee ukimjia kwa kasi, hasira zilimtawala, akatoka ofisini kwake mara moja na kuondoka zake.



    §§§§



    Kikao cha baraza la usalama la taifa kiliitishwa kwa dharula katika ofisi maalumu ndani ya Ikulu ya Dar es salaam, kikihudhuriwa na wadau wa juu kabisa wa usalama. Katika ofisi hiyo ndogo inyojulikana kama Mraba wa Kilimanjaro, hoja ilikuwa nzito juu ya hatima ya wapiganaji wa Tanzania waliokuwa huko Somalia, hakukuwa na habari kabisa juu ya wapi walipohifadhiwa, au kufichwa, wazima au wameuawa, hali ilikuwa tete katika ya wadau hao wa juu kabisa wa usalama ambao hatima ya usalama wa Watanzania ipo juu yao. Mwanamke pekee katika jopo hilo Madam S alikuwa akiwasikiliza kwa makini na akipinga kabisa swala la idara yake kuingizwa katika sakata hilo hali hana nguvu ya kutosha, mwanamke alitunisha misuli ndani ya ofisi hiyo mpaka kila mmoja akabaki kimya. Baada ya mazungumzo hayo lawama zote zikarudi kwa Waziri wa ulinzi kwa kuwa yeye ndiye aliyeng’ang’ania Kamanda Amata aachishwe kazi kwa kile kilichodaiwa utovu wa nidhamu.

    “Hatuwezi kufanya kazi hii bila ya Kamanda Amata,” akasema makamu wa Rais aliyekuwa akiongoza jopo hilo.



    “Hapo mheshimiwa nakuunga mkono, hatukufanya jambo la busara kabisa kumtoa kazini Kamanda Amata, na kwa sababu hiyo ndiyo maana hata sasa tunakutana hapa ambapo si kawaida yetu, kwa nini Kamanda Amata asirudishwe kazini?” Mkuu wa majeshi aliliambia jopo na kuungwa mkono na jopo zima. Waziri wa ulinzi alikuwa kimya, hakuongea kabisa alikuwa akiwasikiliza wajumbe hao.

    “Mimi nahitaji Kamanda arudi kazini, hapo ndiyo nitaifanya kazi hii kwa ufanisi wa hali ya juu,” Madam S akalieleza jopo. Uamuzi ukapitishwa wa kamanda Amata kurudishwa kazini, ikaandikwa barua na kusainiwa na jopo zima kama ilivyokuwa mwanzo, akakabidhiwa waziri wa ulinzi ahakikishe Kamanda Amata anarudi kazini.

    “Mheshimiwa waziri wa ulinzi, lazima tu ukubali kuwa umekata tawi ulilokalia,” Madam S alitamka maneno hayo na kumuudhi sana waziri wa ulinzi





    “Hapo mheshimiwa nakuunga mkono, hatukufanya jambo la busara kabisa kumtoa kazini Kamanda Amata, na kwa sababu hiyo ndiyo maana hata sasa tunakutana hapa ambapo si kawaida yetu, kwa nini Kamanda Amata asirudishwe kazini?” Mkuu wa majeshi aliliambia jopo na kuungwa mkono na jopo zima. Waziri wa ulinzi alikuwa kimya, hakuongea kabisa alikuwa akiwasikiliza wajumbe hao.

    “Mimi nahitaji Kamanda arudi kazini, hapo ndiyo nitaifanya kazi hii kwa ufanisi wa hali ya juu,” Madam S akalieleza jopo. Uamuzi ukapitishwa wa kamanda Amata kurudishwa kazini, ikaandikwa barua na kusainiwa na jopo zima kama ilivyokuwa mwanzo, akakabidhiwa waziri wa ulinzi ahakikishe Kamanda Amata anarudi kazini.

    “Mheshimiwa waziri wa ulinzi, lazima tu ukubali kuwa umekata tawi ulilokalia,” Madam S alitamka maneno hayo na kumuudhi sana waziri wa ulinzi.







    §§§§



    Ugeni mpya ulifika nyumbani kwa Kamanda Amata siku ya pili baada ya Gina na Scoba, waziri wa ulinzi akifuatana na ujumbe wa watu watatu. Kamanda Amata alikuwa akiendelea na shughuli zake za shamba.

    “Salama Kamanda?” sauti hiyo ikamshtua Amata kutoka katika kazi iliyoiteka akili yake, akaacha na kugeuka nyuma, akakutana uso kwa uso na waziri wa ulinzi aliyekuwa na bahasha mkononi mwake. Mheshimiwa waziri akavuta hatua mpaka aliposimama Kamanda Amata.

    “Samahani sana Kamanda kwa yaliyotokea, yaliyopita si ndwele tugange yajayo,” waziri wa ulinzi akamwambia Amata huku akiwa amekwishamfikia pale alipo, akamkabidhi ile bahasha. Kamanda akaipokea na kuifungua bila kusema chochote, akaisoma, barua ya kumtaka kurudi kazini. Alipokwishakumaliza kusoma, akainuan uso wake na kumtazama mzee huyo.

    “Asante, nitawajibu kwa maandishi,” kamanda akajibu na kuitia mfukoni ile karatasi kisha akapanda pawatila na kupotelea shambani. Waziri wa ulinzi na wapambe wake wakabaki wakitazamana, hakuna jipya, waliamua kuondoaka zao.



    “Taifa linautambua sana mchango wako katika mambo mbalimbali, umepigania haki, uliyaweka hatarini maisha yako kwa ajili ya Watanzania. Kumbuka ubinaadamu upo, hivyo serikali inakuomba kurudi kazini na kusaidia tena taifa lako ulipendalo, Watanzania wanahitaji akili, nguvu, umakini na utayari wako…”

    Ilikuwa sehemu ya barua aliyoandikiwa kutoka baraza la usalama la taifa, akaikunja tena ile karatasi na kuirudisha mfukoni. Akajaribu kufikiria mateso ya wapiganaji wa Tanzania ambao wapo huko Somalia kama wanayapata yatakuwa makali kiasi gani, moyo wake ukamuuma sana, akamfikiria madam S jinsi atakavyokuwa anahangaika katika hilo, Kamanda akaangusha chozi, akakata kauli na kurudi nyumbani kwake.

    “Nasafiri mara moja, naomba muangalie shamba na mambo mengine, nitarudi labda baada ya wiki moja au mbili,” Kamanda akawaambia watu anaoishi nao wakiwemo wafanyakazi wake wa mazingira, akamshika mkono binti yake Jenny.

    “Jenny, nitakuona nikirudi, sawa mrembo wangu?” Kamanda akaagana na binti yake. Jenny akaitikia kwa kutikisa kichwa.

    Baada ya kuweka sawa zana zake chache muhimu katika begi lake, Kamanda Amata akaingia ndani ya Land Rover Defender, gari ya kazi na kuelekea mjini.



    §§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ilikuwa ni siku nzito sana, Madam S alikuwa na uchovu wa ajabu, aliegesha gari yake katika maegesho ya nyumba yake huko Masaki na kuingia ndani kupumzika, kabla hajawasha taa akiwa anaelekeza mkono wake katika switch, taa ya sebuleni ikawaka yenyewe, akashtuka na kutazama huku na huko kwa hadhari kubwa.

    “We unafanya nini hapa?” akatamka baada ya kumuona Kamanda Amata akiwa ameketi kochini na mbele yake kwenye kijimeza kulikuwa na pombe kali aliyokuwa akiigida kwa madaha.

    “Nimekuja kwa mama yangu,” Kamanda akamjibu Madam S. madam S akamtazama kijana huyu, kisha akavuta hatua chache na kujitupa kwenye kiti. Hakushangaa kwa kamanda Amata kuwa ndani ya nyum,ba hiyo kwani anamju wazi utundu wake wa kucheza na vitasa vya kila aina na kuingia bila uharibifu.

    “Karibu konyagi,” Kamanda akamkaribisha Madam S, akamsogezea glass iliyojaa nusu.



    “Asante Kamanda,” Madam alijibu huku akiinyanyua glass na kupiga funda moja la nguvu.

    “Kamanda, hali ni tete hapa, mi nafurahi umekuja, na nilijua utakuja, ila umenyanyasa sana yule mzee. Kwa ujumla tumeshapoteza makomandoo wawili na wawili haijulikani walipo, ukiachana na wanajeshi wa maji ishirini wa Tanzania na watano wa Urusi pamoja na meli yetu kubwa ya kivita ililiyokuwa na makombora ya masafa marefu na uzito wa hali ya juu kumi na mbili, Mama amechanganyikiwa kupoteza mali zote hizo,” Madam S alimweleza Kamanda Amata.

    “Hujuma?” Kamanda akatupa swali.

    “Sijajua,” Madam S akajibu.

    “Hujuma, hiyo ni hujuma, ina maana hao maharamia na washirika wao wanajuaje serikali inapotaka kutuma watu kwenda kule? Mpaka wawaue kirahisi namna hiyo? Hujuma, Madam kubali kataa hiyo ni hujuma,” Kamanda alisisitiza juu ya hilo.

    “Kamanda, sikuwahi kufikiria hilo, sasa unaanza kunipa mwanga, ila mheshimiwa umemnyanyasa sana, au ni yeye?” Madam aliuliza.

    “Sijui labda ni wewe Madam, maana ukiwapa siri wale wanakupa pesa ya maana sana kuliko unavyofikiria,” Kamanda akajibu, akainua glass yake na kupiga funda moja.



    “Mi nimekuja kwa heshima yako, na kwa familia za wale wa liotekwa, lakini sio kwa sababu ya waziri wa ulinzi wala nani ni hayo mawili tu,” Kamanda akajibu, na kunyanyuka, “Mi naondoka tutaonana kesho,” akasema huku akivuta hatua kuuendea mlango.

    “Kamanda subiri TSA 5 atakuja kukuchukua, huwezi kwenda peke yak oleo,” Madam S akamwambia. Kamanda akageuka na kurudi kama hatua mbili akajishika kiuno na kumtazama Madam.

    “TSA 5?!” akauliza kwa mshangao.

    “Ndiyo, TSA 5, tuko namba tano sasa ila moja bado ilibaki wazi mpaka sasa, imeniwia ngumu sana kuteua namba hizo ukizingatia nilikuwa na Chiba tu,” Madam akamwambia.

    “Ok, 3 ni nani? 4 ni nani na 5 ni nani?” kauliza Amata.

    “Scoba TSA 03 idara ya usafirishaji na uokoaji, Dr Jasmin TSA 04 idara ya afya, Gina TSA 05 asiye na idara maalum,” akajibu Madam S, “nimewatawadha leo kwa mujibu wa sheria iliyowekwa ya kuunda na kuteua juu ya idara hii ya ujasusi,” akaongeza.

    Kamanda Amata akampongeza Madam kwa kumpa mkono, “Hata kama ungenishirikisha hao ndio ningekupendekezea kwa sasa, timu imetimia,” Akasema Kamanda.



    §§§§§



    Shalabah, alikuwa ametulia tuli juu ya kiti na kutazama kwa makini skrini iliyojitokeza mbele yake, Mr Lonely alikuwa akiongea na kijana huyo wa juu kabisa katika timu yake, akimpa hili na lile. Mr Lonely, alikuwa ni mtu asiyebishiwa, ila unaruhusuwa kumwuliza, na kauliu yake ni ya mwisho, akisema Fulani auawe basi auawe hakuna linguine. Yeye alikuwa akiishi ndani ya jumba lake la fahari sana lililojengwa baharini, chini, sio kila mtu alikuwa anaweza kuongea na huyo bwana, na hakun a aliyejua kama bwana huyo ana mke na watoto au hana kwani utaambia amesafiri lakini hukuwahi kumuona akitooka na gari ndani ya jumba hilo lakini amesafiri, kwa hiyo hakuna aliyeamini kama bwana huyo ni mtu wa kweli au wa kufikirika, lakini sauti yake ilisikika na picha yake ilionekana uingiapo sebuleni hapo kuzuingumza naye.

    “Hakikisha, yeyote anayekuja kufuatilia habari hii anauawa mara moja, mmefanya vizuri kuwauwa wale wawili, na hao wengine hakikisheni wanapata mateso mpaka wanakufa, pia watupatie na siri nyingine, kwani biashara ya safari hii ina tija sana na najua hawatakubali kuacha hivi hivi lakini we endelea kupanga vijana kwani mauzo ya bidhaa hii ni siku kumi zijazo na hao watu wao tutawazika wazimawazima,” maneno mazito ya Mr Lonely yalipenya katika ngoma za masikio ya Shalabah.

    “Sawa, Lonely,” akajibu Shalabah.



    “Hakikisha macho yote kuanzia uwanja wa ndege mpaka mahotelini yanafanya kazi sawasawa, jicho letu lililoko Tanzania linafanya vizuri, lazima tuitazame dunia kama tunavytokitazama kiganja cha mkono, kwa heri,” Lonely alamaliza kuongea, kabla Shalabah hajajibu chochote, ile skrini pale ukutani ikarudi taratibu chini mahali inapojihifadhi na kopo lenye maua ya kunukia likachukua nafasi yake.

    Shalabah alipoliacha jumba hilo, moja kwa moja alifika katika ofisi yao nyingine, ofisi ya siri ambapo alimkuta Sharoni na vijana wengine, akawapa maagizo yote yaliyotolewa na Mr Lonely na kumpa kazi Sharon ya kuimarisha ulinzi mpaka biashara ile itakapofanyika.

    “Kwani we una wasiwasi kuwa watatuma tena mtu? Hiyo sahau, tumeshaua wawili na tunao mkononi ishirini na saba, haji mtu hapa, serekali isiyo na akili itafanya hilo,” Sharon akamwambia Shalabah, wote wakacheka na kisha wakatoka eneo hilo kuelekea bandari ya zamani ambako kwa ujumla mambo yote yalikuwa hapo.



    5..Dar es salaam



    “Hebu nambieni kwanza juu ya hali ya usalama wa vijana wetu huko Somalia,” Mkuu wan chi ambaye dhamana ya taifa lote na watu wake lipo mkononi mwake alimuuliza waziri wa ulinzi aliyekuwa mbele yake, ukimya ukachukua nafasi, waziri hakujibu lolote, “Unajua kupoteza makomandoo wawili ni hasara sana kwa jeshi letu, wakati mnajua kuwa wapo na zipo idara nyeti za kuifanya kazi hiyo na siyo wanajeshi kwa kuwa wao wako kwa ajili ya kazi kubwa zaidi,” akaongeza. Waziri wa ulinzi alikuwa akiona muda hauendi kabisa kwa maswali aliyokuwa akibanwa na mkuu huyo.

    “Ah… eh…. Mh…. Unajua mheshimiwa, tulighafirika kidogo na kuwapeleka wale watu tukijua kuwa wataifanya kazi hiyo vizuri kutokana nja kwamba adui tuliyekuwa tukimkabili alikuwa kivita zaidi,” akajibu waziri.

    “Ni uzembe, lazima ukubali ni uzembe na hao mlioshirikiana juu ya hilo wote ni wazembe na mtawajibika kwa hili, naomba uende, sasa nitaamua mimi la kufanya juu ya hilo inaonekana wewe umeshindwa kama waziri,” akamaliza kuongea Mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu.



    §§§§



    “Kwa nini mpaka sasa, wapiganaji wetu wanapoteza maisha na we upo hapa unatazama?” swali kutoka kwa mkuu wan chi lilitua katika ngoma ya sikio ya Madam S.

    “Sikuwa na nguvu ya kutosha kukabiliana na swala hilo mkuu,” Madam S alijibu.

    “Sijakuelewa, hukuwa na nguvu kivipi na wakati mwingine ulikuwa na nguvu kivipi?” akaulizwa tena.

    “Mheshimiwa, wewe unajua kitengo chetu ndio kimeanza miaka mitano hii na mpaka sasa nilikuwa na watu wawili tu yaani TSA 1 na 2, kutokana na sakata la Julai 7 la kupambana na magaidi lilipokamilika TSA 1 aliachishwa kazi kwa ajili ya utovu wa nidhamu, nikabaki na TSA 2, ndio nikakuandikia barua ya kuomba kuongeza nguvu kikosini kwangu, ukanikubalia, nimeongeza juzi watu wa watatu, lakini bado sina TSA 1, nitafanyeje?” Madam S akajibu kinagaubaga na kumuona wazi mkuu wa nchui akikodoa macho kumshangaa.



    “Nani anayeweza kumuondoa kazini mtu wa kitengo cha ujasusi? Kile kitengo kiko chini yaofisi yangu ni mimi tu ninayeweza kumuondoa mtu au kumuingiza mtu na si mtu awaye yote, sasa popote alipo TSA 1 arudi kazini kwa amri yangu, na mara moja akabidhiwe hiyo kazi aende akaokoe jahazi,” Mkuu wan chi aliongea kwa hasira.

    “Sawa mkuu, TSA 1 amekwisharejea kazini,” Madam S akajibu.

    “Sawa, umefanya vyema, na nitafurahi zaidi ukinambia kuwa usiku wa leo atakuwa tayari ameondoka, kama hakuna ndege basi ya serikali itampeleka, asante, nasubiri jibu lako,” Mkuu wan chi akamaliza kuongea na kuagana na Madam S.

    Madam S akaiacha ofisi hiyo na kupita kwenye korido ndefu iliyomtolea kwenye sebule ya kupumzikia wageni, akapita mlango mkubwa na kuziteremka ngazi harakaharaka, akaingia kwenye gari yake na kuondoka katika viwanja vya Ikulu.



    §§§§§



    Gina alikuwa ameketi ndani ya ofisi aliyoizoea, macho yote yakiwa kwenye luninga akitazama habari za kimataifa kupitia channel ya Al-Jazeera. Akiwa hana hili wala lile, mlango wa ofisi ukafunguliwa bila hodi, mtu asiyemtegemea akaingia ndani.

    “Kamanda!” akajikuta akitamka.

    “Ndiyo mimi hakuna mwingine,” Kamanda Amata akajibu na kuvuta kiti chake, akaketi. Gina







    “Afadhali umekuja, maana bibi yako alikuwa amechanganyikiwa, na ofisi nzima pia,” Gina akajibu.

    “Najua, nimekuja kwa sababu ya Watanzania na si kitu kingine, naomba niaandalie safari ya kuelekea Somalia leo hii,” kamanda akaagiza.

    “Bila shaka, sasa nina furaha, kwa kuwa umekuja, unaonaje tukienda pamoja?” Gina akamwambia Amata.

    “Hapana, kwa sasa huwezi kutoka nje ya nchi au hata mkoa bila ruhusa ya bosi wako, Madam S, wewe umeshaingia katika kitengo nyeti cha kijasusi tayari jina lako litakuwa kati ya majina yanayosakwa na watu wabaya katika mitandao ya kimataifa, ikibidi utakuja lakini hatuwezi kuondoka wote ndivyo oda ilivyo,” kamanda Amata akamwelewesha Gina. Gina akabakio kasimama akimwangalia kijana huyu ambaye hakuwa naye kwa muda mrefu sasa kikazi.



    “Ok, nimeelewa,” Gina akajibu na kutoka kwenda katika kiti chake, akawasha kompyuta na kuanza kutembelea mashirika ya ndege ya ndani na nje kuangalia kama kuna lolote ambalo linapitia upande huo.

    Dubai airline, ilikuwa ni ndege inayoondoka kutoka uwanja wa Jomo Kenyatta, Nairobi usiku wa siku hiyo kuelekea Dubai kupitia Mogadishu. Kutoka Tanzania hakukuwa na kampuni yoyote ya ndege inayokwenda upande huo. Kamanda Amata alikubaliana na Gina kutumia uwanja wa Jomo Kenyatta kuingia Somalia, hiyo kwake aliona itakuwa mbinu nzuri ya kuwapoteza malengo kama kuna mtu anyevujisha taarifa. Kutoka Dar es salaam kwenda Nairobi alipata ndege ya shirika la Ethiopia.

    “Sasa fanya malipo yote, usimwambie mtu kama natumia Dubai airline, ila kila mtu ajue naingia Somalia kwa shirika la ndege la Ethiopia, hata madam S asijue,” kamanda Amata almwambia Gina wakati akimpa taarifa ya ndege hizo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kukamilisha itifaki zote, Gina na Kamanda Amata wakatoka kuelekea ofisi ya Madam S, pale waliwakuta wengine ambao wote walikuwa wakiwasubiri wawili hao. Moja kwa moja alikutana na Madam S aliyekuwa mbele ya meza yake kubwa ya ofisi.

    “Kamanda Amata, kwa mujibu wa sheria iliyoruhusu kuunda na kuteua idara ya Kijasusi ya TSA, nakurudishi cheo chako cha TSA 1 kuanzia sasa,” Madam S akamwambia maneno machache na wakati huo wote wengine walikuwa wima kwa heshima, akamrudishia beji yake pamoja na kitambulisho na kikasha chenye bastola kama kitendea kazi.

    Baada ya hayo wote wane wakampa salute Kamanda Amata wakati yeye akimpa salute Madam S.



    Madam S akampa Kamanda Amata bahasha ya khaki mikononi mwake huu yake ilikuwa imeandikwa kwa maandishi mazito, HUJUMA? Akaitazama na kuifungua ndani, maelezo yote akayakuta yakiwa yameandikwa kwa ufasaha kabisa, picha za Sebeki na Gwamaka, pia wapiganaji wote ishirini na tano picha zao zilikuwapo na majina na vyeo vyao, picha ya Daud na Jamil pia zilikuwapo na picha ya Manowari kubwa ya kijeshi.

    Kamanda Amata alishusha pumzi ndefu, akaitazama ile bahasha na kuiweka mezani kisha akachukua kalamu ya wino mzito na kuondoa alama ya kiulizo katika katika andishi HUJUMA? Likabaki kuwa HUJUMA.



    OFISI NYETI TSA (SHAMBA)



    “Ok, Kamanda, kaa tayari tunakuwekea GPS micro chip,” Chiba akamwambia Kamanda Amata wakati, Dr Jasmine akiwa tayari na sindano maalum ya kumchoma kwenye msuli wa mkono ili kupachika hiyo chip, akakunja shati lake na zoezi hilo likafanyika chini ya Chiba na Dr Jasmin.

    “Ok, Kamanda nakuona sasa kupitia satellite,” Chiba akamwambia Kamanda Amata ambaye wakati huo alikuwa akishikilia pamba iliyokuwa na dawa maalum ya kukausha damu na kuua bacteria.

    “Hii ni bastola mpya ya kisasa, inayoweza kupiga mpaka mita mia tano kwa nguvu ileile, bastola hii hawezi kutumia mtu yeyote mwingine ni wewe peke yako, ishike vizuri, niiunganishe,” Kamanda Amata akaikamata vyema na mkono wake ulioshika bastola ukapitishwa kwenye kifaa maalumu cha kielektroniki. Baada ya zoezi hiulo Chiba akaendelea, “ Hii bastola Kamanda ni teknolojia mpya kabisa iliyotengenezwa hapahapa nchini kwenye baada ya utafiti wa kina wa wataalamu wetu wa JW kule Mzinga, Morogoro.” Kamanda Amata akaigeuza geuza na kutikisa kichwa kuonesha ameikubali maana ilionekana ya kisasa hasa. Akakabidhiwa na vikorokoro vingine kwa ajili ya kazi zake zikiwemo silaha za siri za kijasusi, saa ya kisasa inayoweza kubeba risasi tatu zenye kipenyo cha milimita 3 na urefu wa sentimita moja.



    “Utatumia gari aina ya Kilimanjaro, hii ni gari mpya kabisa tuliyoiunda maalumu kwa kazi ngumu kama hizi, ina mwendo kasi wa kilomita 350 kwa saa, uwe mwangalifu sana kwani ni gari ya hatari katika kasi, kiti chake kina parachute na paa lake linafunguka kwa switch moja tu, ukibonyeza parachute na paa lake linafunguka wakati huohuo hivyo inaweza kukuokoa katika hatari yoyote, Kamanda Amata ni wewe mtu wa kwanza kutumia aina ya gari hii iliyotengenezwa hapa nchini, utaikuta pale uwanja wa ndege Mogadishu,” Chiba akamkabidhi funguo Kamanda Amata, na kumtakia heri na baraka kwa maana wote walijuwa uzito na ugumu wa kazi hiyo ndiyo maana wakamkabidhi vifaa vya kisasa kwa teknolojia mpya na ya kwanza kutoka Tanzania.

    “Kamanda vidonge hivi vitakufanya usisikie njaa, kwa masaa sabini na mbili, na hivi ni vya sumu na vingine vya kulevya kama utahitaji kuvitumia,” Dr Jasmin akampatia aina tatu ya vidonge.

    Madam S alikuwa akifuatilia kila jambo linalofanyika, akaridhika na mipangilio ya vijana wake.

    “Safi, Kamanda nakutakia kazi njema sana, sasa unatakiwa kufika katika kambi ya wanamaji pale Kigamboni uonane na mkuu wa kikosi, kanali Shemweta



    KAMBI YA JESHI LA WANAMAJI

    KIGAMBONI



    KAMANDA Amata alikuwa ndani ya chumba maalum, yeyeb pamoja na Madam S na maofisa wengine wa jeshi la wanamaji, pamoja nao waziri wa ulinzi alikuwapo.

    “Kamanda, unaona huu mchoro, meli yetu, imepotelea hapa, tulikuwa tukiifuatilia kila hatua kwa kutumia lada, lakini kufika hapa hatukuweza kuiopna tena, tuna uhakika kwa asilimia mia moja imetekwa na maharamia wa Somalia, kwa kuwa mele nyingi sana zinapotelea hapa,” alizungumza mwanajeshi mmoja aliyekuwa na nyota tatu mabegani mwake, akimuonesha Kamanda Amata ramani iliyopigwa kwa satellite kuonesha njia iliyokuwa ikipita meli hiyo kubwa ya kivita. Kamanda Amata akatazama kwa makini sana, daima alikuwa akitikisa kichwa kuonesha kuwa anaelewa anachoambiwa.



    “Kadiri ya taarifa za awali zilizotumwa na wapiganaji wetu ambao wamekwishatangulizwa mbele ya haki, meli hii haionekani kabisa majini hata pale Mogadishu, hivyo hawakuweza kujua kama ipo au imeondolewa,” Yule mwanajeshi akaendelea.

    “Lingine Kamanda, hawa jamaa ni hatari sana, uwe muangalifu tusije kukupoteza, Watanzania tunakupenda sana na tunaithamini kazi yako,” Waziri wa ulinzi aliendeleza hoja. Kamanda Amata akapiga saluti, akiwa ndani ya suti safi ya kijeshi. Kisha wote wakatoka, na Madam S akiwa na Kamanda Amata pamoja na waziri wa ulinzi wakaondoka na helkopta maalum kurudi mjini.







    JNIA – saa 2:00 usiku



    MADAM S alimpa mkono Kamanda Amata alipokuwa uwanja wa ndege wa kimataifa Dar es salaam tayari kwa safari.

    “Kila la kheri Kamanda, nakuaminia sana,” Madam alimwambia. Kamanda Amata akasaluti kisha akamuendea Gina na kumbusu.

    “Nahitaji urudi Kamanda, urudi na pua yako,” Gina alimwambia Kamanda.

    “Usijali, nitarudi na kila kitu changu,” Kamanda akaagana na wote pale uwanja wa ndege kisha akaingia katika chumba cha wasafiri tayari kwa safari.

    “Habari ya jioni,” mtu mmoja alimsalimu Kamanda Amata walipokuwa ndani ya chumba cha wasafiri.

    “Salama kabisa,” Kamanda akajibu na kuendelea kusoma gazeti lililo mkononi mwake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Unaelekea wapi?” yule mtu akamwuliza Kamanda Amata. Kamanda Amata akamtazama kuanzi kiatu alichovaa mpaka nywele, ndipo alipomgundua mtu huyo kwa mbali ana asili ya watu kama Wamburu.

    “Naenda Arusha, wewe je?” Kamanda akamwuliza.

    “Naenda Moqdishu,” yule mtu akajibu, akajikohoza na kuendelea, “Sasa unaenda Arusha kwa Ethiopia Airline!” akaongeza.

    “Hilo halikuhusu, nina uwezo wa kwenda Morogoro kwa British Airways,” kamanda alipomaliza kuongea hayo, tayari mlango ulikuwa wazi na abiria wakaanza kuingia ndegeni.



    §§§§§



    Yule mtu aliyekuwa akiongea na Amata pale uwanja wa ndege alikuwa mara kwa mara akienda maliwato ndani ya ndege hiyo. Kamanda Amata alikuwa ameketi siti za mbele ilihali yule bwana alikuwa siti za nyuma, kamanda Amata aliweza kumuona vizuri kwa kupitia miwani yake ambayo iliweza kumuonesha vinavyotokea nyuma yake.

    Baada ya kumtazama kama mara nne akienda maliwato, mara hii Kamanda Amata akainuka kutoka katika kiti chake na kuelekea upande wa nyuma wa ndege hiyo. Moja kwa moja akaenda mpaka katika mlango wa maliwato, akasimama kusikiliza kama mtu huyo anaongea chochote, akasikia lakini kwa sauti ya chini sana kutokana na mlango huo jinsi ulivyotengenezwa, kamanda Amata akachomoa kifaa kidogo chenye mfano wa koni akakiegesha hapo mlango na kusikiliza kila kinachoongelewa, alipoona kuwa mtu huyo anakaribia kumaliza mazungumzo Amata akashika kitasa cha mlango huo na kukifungua kwa nguvu kwa kukivunja, akausukuma mlango ndani na kuingia kisha akaufunga nyuma yake.



    Ndani ya choo hicho akakutana na yule bwana, Kamanda Amata akamtazama kwa jicho baya.

    “Nani ulikuwa unampa habari zangu?” akamwuliza.

    “Hapana, mimi nilikuwa naongea na ndugu zangu,” akajibu huku akitetemeka.

    “Ndugu zako ndio unawatajia jina langu?” Kamanda Amata akauliza, kisha akatazama kifaa alichokuwa anatumia kuwasiliana na jamaa hao, kilikuwa ni kifaa cha ajabu sana kidogo kwa mfano wa kiberiti, alikiunganisha kwa ufundi sana kupitia nyaya ndogo zinazosafirisha mawasiliano ndani ya ndege hiyo. Kamanda Amata akakitazama na kuzing’oa zile nyaya zake pale alipoziunganisha na zile zilizo kwenye mfumo wa ndege hiyo.

    Alipohakikisha anacho kile kidubwasha mkononi mwake, akamwamuru yule jamaa kutoka ndani ya choo kile.



    “Sasa utakwenda kukaa pale nilipokaa mimi na mimi nitakaa hapa ulipokaa wewe,” Kamanda alimwambia yule jamaa.

    “Ah, siwezi kukaa kule kwani mi sti yangu ni hii hii,” yule bwana alilalama. Kamanda Amata hakujibu, alimtandika kofi moja kali sana, mpaka yule bwana akakaa chini. Wahudumu wa ndege wakamfuata Kamanda kumwambia kuwa analolifanya haliruhusiwi ndani ya usafiri huo, wakamwomba akae kwenye siti yake. Kamanda Amata akawaonesha kitambulisho chake halisi. Hapo wakamwacha afanye atakalo, kwa kuwa huyo ni mtu wa kuaminika. Yule mtu akaketi kwenye siti ya Amata na Amata akakaa kwenye siti yake, sasa alikuwa akimwangalia kwa mbele.

    Baada ya kutua Nairobi, yule bwana aligeuka nyuma kwa woga kumtazama Amata, hakumwona.

    Kamanda Amata alishuka katika uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta bila yule bwana kujua. Baada ya kufanyiwa itifaki za kiusalama, hakuchukua muda mrefu alikwea ndege shirika la Dubai Airline na kuelekea Mogadishu, tayari kabisa kuanza kibarua alichotumwa.



    MOGADISHU – SOMALIA

    Uwanja wa ndege wa ADEN ADDE



    SHALABAH alikunja sura baada ya kupata taarifa kuwa Kamanda Amata hayupo katika ndege waliyoitarajia. Alionekana wazi kupumua kwa nguvu, akiwaza jambo.

    “Shalabah, vipi?” Sharon akamuuliza.

    “Huyo wanaemwita Kamanda Amata hayupo katika ndege tangu watoke Nairobi,” Shalabah akamwambia Sharon. Sharona naye akaonekana wazi kupigwa butwaa.

    “Atakuwa kaamua kukatisha safari?” Sharon akauliza.

    “Hapana, huyu anataka kutuchezea mchezo, nina uhakika yuko humohumo, kajificha sehemu, hebu ongea na watu wetu upande wa cargo kuwa wanaangalia vizuri, bado saa moja ndege itatua,” Shalabah akatoa maelekezo na Sharon akawapanga upya watu wake.



    “Vipi?” Fasendy akamwuliza Sharon, pindi alipotoka pembeni kuvuta sigara.

    Fasendy alikodiwa katika mpango huo ili kummaliza Kamnda Amata palepale uwanja wa ndege kwa kumdungua, alikuwa tayari kajipanga kwa hilo, alichoambiwa yeye ni kuwa atapewa maelekezo tu ya jinsi mtu huyo alivyo.



    §§§§



    NDEGE ya Dubai Airline ilikanyaga ardhi ya Mogadishu ikiitangulia ile ya Ethiopia ambayo maharamia hao walikuwa wakiisubiri kwani walishaambiwa kuwa Kamnda yuko humo, na walitahadharishwa kuhakikisha haingii mjini kwani ni mtu hatari sana. Mpaka dakika hiyo walikwishakubaliana na hilo kuwa mara hii wanapambana na mtu makini mwenye akili za ziada kwa mchezo tu aliowachezea kwenye ndege hiyo.

    Kamanda Amata alikiacha kiti chake, akaweka kijibegi chake mgongoni na taratibu kuziteremka ngazi za ndege hiyo na kwa mara ya kwanza aliweka unyanyo wake katika ardhi ya Mogadishu, uwanja wa ndege wa Aden Adde. Akiwa na miwani yake usoni aliweza kuona vyema kabisa katika mianga ya taa kali za umeme iliyokuwa ikimulika eneo hilo, akavuta hatua ndefundefu na kuelekea katika eneo la kukagulia mizigo. Kamanda Amata aliinyakua mizigo yake na kuibwaga mezani kwa mwanadada mrembo wa Kisomali, mwanadada yule alikagua vizuri kabisa mizigo ya kamanda lakini hakuona hata kitu kimoja cha hatari wakati ndani yake kulikuwa na silaha nyingi za kijasusi.



    Alipomaliza akatoka katika mlango mkubwa, huku akisindikizwa na kijana mmoja aliyekuwa akisukuma kile kitorori cha mizigo. Macho ya Kamanda Amata yalikuwa yakicheza huku na kule kuwaangalia wote waliopo katika uwanja huo ili aone kama adui yoyote. Kutokana na kazi zake za kijasusi aliweza kuitambua ni ya mtu kwa kumwangalia tu usoni mara moja. Akingiza mkono mfukoni na kutoa kidubwasa kidogo ukubwa wa kidole gumba akaminya sehemu ya katikati ambayo ilikuwa na kitufe chekundu. Gari moja iliyokuwa katikati ya nyingine ikawasha taa zake na kujiwasha injini, ikabaki inaunguruma.

    “Asante sana kijana nimekwishampata mwenyeji wangu,” alimshukuru yule kijana na kumpa dola za kimarekani hamsini. Yule kijana hakuamini, aliigeuza huku na huku ile noti hakuamini, akabaki kukenua huku akimwangalia kamanda Amata.

    “Unaitwa nani?” kamanda akamwuliza.

    “Naitwa Ahab,” yule kijana akajibu.

    “Una simu?” Kamanda akamwuliza.

    “Ndiyo, ndiyo ninayo,” akajibu na kuitoa simu ya kizamani kidogo iliyokuwa imeshikizwa kwa mipira.



    Akamnda Amata akatikisa kichwa na kumtazama kijana huyo aliyeonekana mjanja machoni na matendo yake pia. Kamanda Akachukua namba ya kijana huyo akamwahidi kumtafuta usiku wa siku inayofuata. Yule kijana akafurahi sana na kuondoka eneo hilo. Kamanda Amata akaisogelea ile gari ambayo hata hakujua ni nani aliyeiweka mahala hapo. Akafungua mlango na kuketi baada ya mizigo yake kuitupia kwenye buti ya gari hiyo. Akaketi kwenye kiti cha dereva na kujiweka sawa, ile gari ikamkumbusha kufunga mkanda.

    ‘Tanzania tumeendelea sana kiteknolojia,’ akajiwazia wakati gari hiyo ikimpa maelekezo mafupi juu ya matumizi, aliporidhika akaitoa mahali pale taratibu na kuiingiza katika barabara kubwa ya kutokea nje ya uwanja huo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    JAZEERA PALACE HOTEL



    KAMANDA Amata aliegesha gari katika maegesho ya hotel hiyo, akashuka na kutoa mizigo tayari kuelekea ndani.

    “Karibu sana Jazeera palace Hotel,” sauti tamu ya kike ikamkaribisha Kamanda alipokuwa pale mbele ya kaunta.

    “Asante sana, nimekaribia, natumaini kupata huduma safi na bora kuliko mahala popote nilipowahi kwenda,” kamanda akajibu karibisho hilo.

    “Usijali, kila huduma inapatikana,” yule msichana akamwambia.

    Baada ya kuandikisha na kumaliza kila kilichohitajiwa pale kaunta, Kamanda Amata akaingia kwenye lifti na kupanda ghorofa ya tatu.



    305, ilikuwa namba ya chumba iliyomtazama mbele yake, akaingia ndani na kuufunga mlango nyuma yake, kabla ya lolote, akachukua kifaa chake maalumu kwa kazi ya ukaguzi kama kuna kitu chochote cha hatari, alipohakikisha usalama upo aliweka vizuri mambo yake, akatazama simu yake ilikuwa saa saba za usiku, akajua bado dakika kumi na tano tu ile ndege ya Ethiopia itakuwa hapo Mogadishu, Kamanda Amata alitaka kuwa pale ili aone kinachoendelea; hasa kumuona yule mtu aliyemgundua akitoa maelezo fulani kwa ndugu zake, akabadili nguo na kuvaa mavazi ya kazi: suruari nyeusi, koti la suti jeusi lililotanguliwa na kabashingo nyeusi, shingoni akaninginiza mkufu mzito wa dhahabu, akaichukua bastola yake mpya kabisa aliyokabidhiwa na Chiba, akaiweka tayari na kuificha ndani ya koti hilo, akakusanya silaha zake za siri na kuzipachika katika sehemu mbalimbali za suruali yake, akajitazama kwenye kioo, akajiona kamili. Akaufunga mlango na kuteremka kwa ngazi mpaka chini, akatoka nje na kuingia kwenye gari yake aina ya Kilimanjaro, akaondoka kuelekea uwanja wa ndege. ‘Hakuna kulala…’







    Uwanja wa ndege wa ADEN ADDE saa 7.15 usiku.



    Kamanda Amata aliegesha gari yake na kuteremka kuelekea eneo ambalo wageni hufikia kusubiri mizigo yao. Usoni akiwa amevalia miwani yake yenye uwezo wa kupiga picha na kuona upande wa nyuma. Akavuta hatua chache na kusimama karibu na mti wa mtende ulio pembezoni tu mwa barabara inayotenganisha upande wa maegesho na upande wa jengo kuu la uwanja huo. Akijifanya kuwa hajui lolote au hana la maana mahala hapo, Kamanda Amata alitulia kwa kujiegemeza katika mti huo, akitazama wanaoingi na kutoka. Ilikuwa ni muda huohuo ndege ya Ethiopia ilitua katika uwanja huo.

    Punde si punde, lile alilolitarajia lilitukia; kutoka katika mlango mkubwa wa jengo lile alimuona yule bwana akitoka huku akisukuma kitoroli cha mizigo, mara kidogo akalakiwa na watu watatu, wanaume, akajaribu kuzinasa picha zao kwa kutumia miwani yake, akabahatika japo kwa shida kidogo. Baada ya tukio hilo aliwafuatilia kwa macho akitazama walikokuwa wakielekea, kutoka mbali aliwaona kana kwamba walikuwa wakilaumu jambo kutoka kwa huyo mwenzao waliyekuja kumpokea. Kamanda Amata kwa haraka kidogo akarudi katika gari yake na kuketi kitini, nyuma ya usukani, akiendelea kuwatazama huku miwani yake ikimuonesha kwa uzuri zaidi. Baada ya kusimama kidogo mahala fulani, ikaonekana wamekubaliana jambo, wakaingia garini wote wanne. Kamanda Amata akaitazama ile gari ilipokuwa ikitoka kwenye maegesho hayo na kuingia barabara kubwa, akaitazama namba zake za usajili na kuzikariri akilini mwake, kisha akaiacha kidogo itoke, na ye taratibu akawa anatoka kuelekea barabara kubwa, lakini kabla hajaingia barabarani gari nygine pick up, ilimpita mbele yake kwa kasi nay eye ikabidi asimame ghafla, baada ya hapo akaendelea kuifuata kwa mbali.



    §§§§§



    “Yaani wewe imekuwaje ukampoiteza yule wakati wote mpo ndege moja?” akauliza Sharon akiwa kageuza nusu ya mwili wake nyuma kwa yule mgeni.

    “Yaani Sharon, mi hata sielewi yule Bwana kanipotea vipi,” akajibu yule mgeni huku akibabaika. Kisha ukimya ukatawala kati yao.

    “Sasa mmeangalia vizuri kwenye mizigo?” Shalabah nae akauliza.

    “Ndiyo mkuu, tumetazama na hayupo, sasa sijui itakuwaje.”

    Baada ya mazungumzo marefu kati yao, ile gari iliegeshwa kwenye moja ya hoteli kubwa pale mjini, Jabir Hotel. Kamanda akamshuhudia yule bwana akishuka na kuwaacha wenyeji wake wakiendelea na safari nay eye akachukua uelekeo wa mlango mkubwa wa hotel hiyo huku akisaidiwa mizigo yake na mhudumu wa hapo, ile gari iliyomleta ikaondoka zake. Kamanda Amata akasukuti kwa nukta kadhaa, akaona kuwa hiyo ni nafasi pekee ya kuanzia kazi yake. Akaondoa gari yake na kuiacha ile hotel kuwaelekea wale jamaa wengine. Lakini haikuwa nia yake, alipofika mbele kidogo eneo lililokuwa na maghorofa mengi aliegesha gari yake katika supamaketi moja kisha yeye akashuka na kuingia ndani yake akiwa kama mteja, lakini lengo kubwa ilikuwa ni kuangalia kama kuna anayemfuata nyuma yake. Alipohakikisha kuwa hakuna, alitokea upande wa pili na kuchukua taxi.

    “Jabir Hotel tafadhali,” alimwambia dereva huku akiketi sawia katika kiti cha nyuma. Dakika kumi na tano hivi alikuwa tayari amekwishafika alipopakusudia, akamlipa dereva taxi na yeye kuuendea mlango wa hoteli hiyo. Jambo la kwanza alilofanya ni kuona kama anaweza kumpata yule kijana aliyemsaidi mizigo yule mgeni. Haikuwa tabu kumpata, alimwendea na kumwita kama mtu mwingine yeyote mwenye shida.



    “Samahani, kuna mgeni tumemleta hapa kama dakika thelethini zilizopita,” alijaribu kiumwuliza yule mhudumu naye kwa kuwa anapokea wageni wengi haikuwa rahisi kujua ni yupi, lakini baada ya kumuelekeza vizuri alimkumbuka japo hakuwa na uhakika.

    “Kama ni huyo yupo chumba namba 243,” akajibu yule mhudumu.

    Kamanda Amata akashukuru na kushika njia, akapanda ghorofa ya pili kwa kutumia ngazi na isha kutokea kwenye korido ndefu ambayo ilikuwa imetanganisha vyumba vingi upandee mmoja na mwingine. Akatazama milangoni huku na huku na kujikuta mbele ya chumba hicho, namba 243 ilisomeka mlangoni bila kificho, akatulia kusikiliza kama kuna lolote ndani humo. Ukimya ulikuwa sehemu kubwa ya chumba hicho, Kamanda Amata hakuwa na uhakika kama ni sahihi mtu huyo yuko humo ndani, alipotaka kukata tama alisikia kwa mbali maji yakimwagika, hapo akawa na uhakika kuwa mlengwa wake yupo. Akachukua funguo yake na kuitumbukiza tunduni, lakini akajikuta anakabiliwa na upinzani kwani ndani ya mlango huo kulikuiwa na funguo ambayo iliikwamisha ile yak wake kufanikisha zoezi hilo. Akaitazama ilivyokaa akaiona kuwa imekaa sawia, akaisukuma ikaangukia ndani kisha akaipachika ya kwake.

    Kitendo cha ile funguo kuanguka kilimshtua mtu wa ndani, Kamanda Amata alisikia nyayo za mtu aliyekuwa akitembea kuelekea mlangoni huku akipiga mruzi, akakinyonga kitasa wakati funguo yake tayari ilikwisharudi mfukoni, yule bwana alipokuwa akiipachika ile funguo kwa upande wa ndani, Kamanda Amata akaufungua mlango kwa ghafla na kumpiga usoni yule mtu.

    Sekunde tano tu, Kamanda Amata alikuwa kajaa ndani kuufunga mlango nyuma yake, huku bastola uyake ikiwa mkononi. Yule bwana alikuwa chini kwa kusukumwa na ule mlango.

    “We n… na….. nani? Aliuliza kwa kukatisha maneno.

    “Hunijui”?





    Yule bwana alionekana kuchanganyikiwa na kile kitendo, akawa anasota kwa makalio kurudi nyuma, akagota ukutani, hakuna njia.

    “Niambie ulikuwa unatoka Tanzania kwa nani?” Kamanda akamuuliza.







    “We mambo yangu unayatakia nini?” yule bwana akajibu kijeuri.

    “Sikiliza wewe bwege, sijaja kupoteza muda na mtu, nitakuuwa sasa hivi,” Kamanda alimtahadharisha yule bwana aliyeonekana kutokuogopa chochote. Akiwa katulia kamtumbulia macho Amata, kwa mara ya kwanza, Kamanda Amata aliiamuru bastola ile ndogo ifanye kazi yake, risasi moja ikavunja mguu wa yule bwana, akalia kwa uchungu, kisha Kamanda Amata akamwendea pale na kumkanyaga kwenye jeraha lake.

    “Aaaaaiiigggghhhh, unaniumiza!” alipiga yowe, akiongea kwa lugha ya Kiswahili, “Nitakwambia kaka, nitakwambia.”

    “Sema.”

    Kamanda Amata akalegeza mguu wake kutoka pale kwenye jeraha, akamtazama yule bwana pale chini, damu zikitiririka mguuni mwake. Mara ghafla yule bwana aliufyatua mkono wake uliokuwa na kisu mkononi kuulenga mguu wa Amata. Kamanda Amata aliuona mchezo huo kwa kuchelewa, akaruka nyuma lakini kile kisu kilipita kwenye suruali yake na kuchana kipande karibu na ugoko ila hakikufika kwenye ngozi. Kitendo kile kiliiamsha akili ya Kamanda Amata, kabla yul;e bwana hajafanya jambo linguine, teke kali lilitua mkononi mwake na kukiondoa kile kisu, teke la upande mwingine lilitua shavuni na kumrudisha chini. Yule bwana ijapokuwa alikuwa na jeraha mguuni mwake hakujali, alichomoa bastola kutoka kwenye kiuno chake lakini kabla hajafyatua tayari risasi ya Amata iliyotoka kimyakimya ilipenya kwenye paji la uso wake na kumlaza palepale chini; chali.



    Kamanda Amata akasonya kwa kukosa maelezo yoyote toka kwa huyo mtu. Akamwendea na kumpekua mifukoni, hakuwa na kitu chochote zaidi ya kiburungutu cha pesa za kisomali. Alipotazama kitandani aliona baadhi ya vikolokolo, akaviendea, na kuichukua hati ya kusafiria ya mtu huyo, baadhi ya kadi za kibiashara na kijitabu kidogo, akakiacha chumba hicho na kuondoka zake.

    Akiwa ndani ya gari yake, aliiangalia ile hati ya kusafiria na kuisoma hapa na pale, akamtambua kijana huyo kwa jina lake la Shaib, mwenye umri wa miaka thelathini na sita. Akaitupa pembeni na kupekuwa vitu vingine.



    …Dar es salaam Club, saa 6.30 mchana…



    Ilikuwa ni moja ya miadi aliyokuwa akitakiwa kufanya na mtu fulani hapo katika hiyo club. Kamanda Amata akawasha gari yake kuondoka kutoka katika eneo hilo, moja kwa moja akarudi hotelini kwake.



    SIKU ILIYOFUATA saa 2.00 asubuhi



    Kamanda Amata alikuwa akifuatilia habari katika televisheni ndogo iliyowekwa ndani ya chumba chake, kati ya habari zilizokuwa zikirushwa asubuhi hiyo ni pamoja na ile ya kukutwa marehemu ndani Jabir Hotel. Aliisikiliza kwa tabu kidogo kutokana na kuwa alikuwa haelewi lugha iliyokuwa ikitumika, alijaribu kuangali nyuso za watu waliokuwa eneo lile lakini hakuna aliyemhisi kwa lolote.

    Asubuhi hiyo aliiacha hoteli aliyofikia na kufunga safari kuelekea Ramada Plaza Hoteli, iliyopo pembezoni kabisa mwa bahari ya Hindi karibu na bandari ya Mogadishu, kwa maelezo aliyokuwa ameyasoma katika taarifa aliyopewa kuwa katika hoteli hiyo ndipo Gwamaka na Jamil walikuwa wamepanga. Kamanda Amata alikuwa na miadi feki aina mbili, mmoja katika hoteli hiyo na mwingine ni Dar es salaam Club.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamanda Amata aliegesha gari yake mbele ya hoteli hiyo kubwa, akashuka na kuufunga mlango wa gari hiyo ya kisasa, akasimama na kuangalia kwa makini lango kuu la hoteli hiyo, akavuta hatua mbili tatu mbele, akasimama na kuangalia vizuri, akajifanya anafunga kamba za viatu kisha akaendelea na safari yake mpaka mapokezi. Akakutana na mhudumu wa ofisi hiyo, msichana mrembo, mweupe wa haja, Kamanda Amata akamtazama kwa jicho la husuda.



    “Habari mrembo,” alimsalimu.

    “Nzuri, sijui nikusaidie nini?” yule mhudumu akajibu na kuuliza.

    “Ok, naitwa Jaffar kutoka Tanzania, nimekuja hapa nina shida kidogo, siku za nyuma kuna kaka zangu walikuja kikazi wakafikia hapa lakini mpaka sasa hatujapata habari za wapi, nimekuja kufuatilia habari zao,” kamanda alimueleza yule mhudumu.

    “Ok, naomba uingie ofisi namba tano kuna mtu atakuhudumia,” akajibiwa. Kamanda Amata bila hofu akaenda na kuingia katika ofisi hiyo, pale akamkuta bwana mmoja aliyevali nadhifu kabisa. akamsabahi na kumueleza shida yake.

    Yule bwana akamkazia macho Kamanda Amata.

    “Unasema unaitwa Jaffar?” akauliza.

    “Ndiyo,” akajibu Kamanda.

    Yule mtu akainua simu yake na kupiga namba Fulani, mara kijana mmoja akaingia na mabegi manne makubwa.

    “Hizi ni mali za kaka zako, ila taarifa nyingine ya kujua wapi walipo ndugu zako kiukweli hatujui, na hatuna msaada mwingine zaidi ya huu tuliokupa sasa,” yule bwana akajibu. Kamanda Amata akayatazama yale masanduku na kuwaamuru wale wahudumu wayafungue nao wakafanya hivyo; akatazama vitu vilivyomo katika masanduku hayo kwa harakaharaka aliporidhika akamshukuru yule bwana. Kwa kusaidiwa na wale wahudumu akatoka nay ale masanduku lakini muda huo tayari alikuwa amekwishayasoma mazingira ya hoteli hiyo.



    Saa 6.00 Mchana- Dar es salaam Club



    Akiwa ameketi kwenye moja ya viti vilivyojaa katika ukumbi wa club hiyo, Kamanda Amata alikuwa aking’aza macho huku na kule kumwangalia mgeni asiyemjua. Moyo wake ulijaa hasira sana na watu hao wanaojiita maharamia. Aliendelea kutulia pale huku akitazama wanaoingia na wanaotoka.

    Akiwa katika hali hiyo, mara waliingia watu watatu, wanaume walioongozwa na kijana mmoja aliyeonekana machachari. Walipita kona mbili tatu na kuelekea upande wa nyuma ambao ulikuwa na vyumba vya V.I.P, vyumba vilivyotumika kwa kazi au mazungumzo maalum. Akiwa katika kushangaa watu hao mara alihisi kitu kama bilauri ikitua juu ya meza yake, akageuka na kukutana macho na msichana aliyekuwa ameketi mbele yake bila kukaribishwa.

    “Usishtuke kaka Jaffar,” yule mwanadada akamwambia. Kamanda Amata akashtuka kusikia jina lake likitamkwa sawia na binti huyo, “Naitwa Farheen, nafanya kazi hoteli ya Ramada Plaza,” akajieleza. Kamanda akamtazama bila kummaliza.

    “Nikusaidie nini?” akamuuliza.

    “Sikia Jaffar, najua huko hapa kwa minajiri gani, lakini ninachokwambia usifanye hicho unachotaka kufanya, utajiweka hatarini, tukiachana hapa, hakikisha unauacha salama mji wa Mogadishu, tayari wanajua lile ulilolifanya leo pale Jabir Hotel, sina zaidi,” yule mwanadada akamaliza na kunywa kinywaji chake kisha akaondoka kutoka pale mezani na kuingia upande ule wenye vyumba vya V.I.P.



    Kamanda Amata alimtazama yule mwanamke na kisha akamfuata alikokwenda, alipouaona mlango alioingia naye akaelekea huko, hakuogopa, aliingia moja kwa moja ndani ya chumba hicho na akajikuta yeye na mwanadada yule tu wakitazamana.

    “Unanifuata?” akauliza, “Watakuua,” akaongeza huku akionesha ishara ya kukata shingo kwa mkono wake.

    “Bila shaka unajua mengi sana juu ya kaka zangu, nataka unieleze, nani aliyewaua?” kamanda akauliza.

    Yule mwanadada akatoa cheko la dharau, na alipotulia akamtazama kamanda huku akiweka vizuri gauni lake refu lililomfunika mpaka miguuni, “Wauaji, wamewaua kaka zako,” akatoa jibu tata. Kamanda Amata akageuka na kutoka ndani ya chumba kile akimuacaha yule mwanamke peke yake, kabla hajavuta hatua nne au tano akakutana na watu wengine wawili wakamzuia. Kamanda akasimama katikati ya watu hao na yule mwanamke, lakini yule mwanamke akatoa ishara ya kuwa wamuache aondoke, akaondoka zake.



    §§§§§§

    “Inaonekana sasa Tanzania wamemleta mtu makini, maana hata kuzifuata nyayo zake lazima hujipange, ama atakupotea au atakupoteza,” aliongea mmoja wa watu wale walioingia katika chumba cha V.I.P pale Dar es salaam Club.

    “Ndiyo, maana jinsi alivyoingia tu hapa Mogadishu imetosha kutuonesha kuwa ni mtu hatari, inabidi juu chini ashughulikiwe mara moja,” mwingine akadakia.

    “Aaaaa sio kazi kubwa kumtia mkononi yule mende, ni kumuotea tu chumbani kwake basi,” mtu wa tatu aliongeza.

    “Tutamuoteaje?” yule mjumbe wa kwanza akauliza kwa shauku huku akijivuta kwa mbele kusikiliza hoja hiyo.

    “Tunamtegea mtu chumbani kwake amsubiri, akiingia tu asimpe nafasi, ammalize,” wazo likatolewa, wote wakalipitisha. Baada ya hapo wakazungumza machache kati yao na kuagana wakiwa na mikakati kabambe ya kumnasa kamanda Amata.



    §§§§§§

    Kamanda Amata kwa hatua za taratibu alijivuta na kuingia ndani ya gari yake, akaketi kimya akitazama nyendo za hapa na pale, dakika arobaini na tano baadae aliwaona wale watu wakitoka ndani ya club ile na kuziendea gari zilizokuwa hapo, kila mmoja akaingia katika gari yake na kuondoka. Kamanda Amata akaichagua moja kati ya gari hizo tatu na kuifuatailia mpaka inapoishia.

    Kwa mwendo wa wastani alikuwa nyuma ya gari kama tatu hivi huku ile anayoifuata ikiwa mbele sana lakini alihakikisha kuwa haimpotei katika macho yake. Baada ya mwendo kama wa dakika ishirini na sita hivi, ile gari ikaingia katika jumba Fulani la kifahari ambalo lilizungukwa na ukuta mkubwa sana ulioziba eneo kubwa na kufanya jumba hilo lionekane kwa tabu. Kamanda akapita na kutupia jicho jumba hilo, mbele kidogo akaegesha gari yake na kutulia akisubiri ni wakati gani yule bwana atatoka. Akiwa ametulia ndani ya gari yake alijikuta akipitiwa na usingizi mtamu wenye ndoto mbalimbali, haloi hiyo ilikuwa ikimsumbua sana, wakati akigombana na hali hiyo aliiona ile gari ikitoka langoni na kurudi kwa barabara ileile iliyojia.



    Amata naye akaigeuza gari yake na kuifuata kwa mwendo wa wastani akihakikisha kuwa yule mtu asijue kabisa kama anafuatwa. Baada ya kupita mitaa kadhaa ile gari ilitokea upande wa baharini na kufuata barabara kandokando yake. Akiendelea kupishana na magari kadhaa makubwa kwa madogo, Kamanda Amata aliendelea kuifuata ile gari, sasa aliiona ikiongeza kasi kuliko mwanzo, akilini mwake akajua kwa vyovyote mtu huyo amejua kama anafuatiliwa. Amata naye akabadilisha gia na gari yake aina ya Kilimanjaro ikaanza kuinyanyasa barabara kwa mwendo kasi, akiwa katika kasi hiyo akiifukluza ile gari nyingine, alisikia sauti ya honi ya garimoshi, alipotazama vizuri kulikuwa na reli inakatisha eneo lile. Kizuizi cha barabar kilikuwa kikiteremka taratibu kuzuia magari yasivuke katika reli hiyo, lakini aliishuhudia ile gari anayoifuata ikivuka kwa kasi na kuvunja kile kizuizi ambacho tayari kilikuwa kimefika chini. Kamanda Amata alisonya kwa hasira kwani alielewa jambo alilofanya mtu yule, hakuwa na jinsi ilibisi kusubiri mpaka ile treni ilipomalizika, hakuweza tena kuiona ile gari, naye kwa kuonesha kuwa ni mwelevu akageuza gari na kurudi alikotoka hakuifuata ile njia.



    Breki ya kwanza ilikuwa ni katika hoteli ya Ramada Plazza, akaegesha gari yake na kuingia tena ndani ya hoteli hiyo. Mara hii alipita mapokezi na kuzunguka upande wa maofisi, akasimama katika mlango ulioandikwa ‘Security Room,’ akagonga, mlango ukafunguliwa, akaingia ndani na kukuta watu wawili.

    “Samahani hairuhusiwi mtu kuingia humu ndani,” mmoja wao akamwambia Kamanda Amata lakini kabla hajajibiwa alikuta akipewa kipigo cha dharula na kupoteza fahamu, vivyo hivyo kwa yule mwingine. Kamanda Amata akavuta droo na kupekua pekua huku akisoma tarehe za disc hizo ndogo zilizohifadhi kumbukumbu za matukio ya kila siku. Alipoona katika saraka hiyo hakuna anachokitaka akapekuwa saraka nyingine na kuiona ile aliyoihitaji, alipojiridhisha kuwa ndiyo hiyo akaipachika katika chombo maalum kwa kazi hiyo na kuanza kurudisha nyuma kuangali matukio ua siku hiyo.



    Aliirudisha nrudisha nyuma picha hiyo ya video iliyopigwa kwa kamera za usalama, ikionesha Jamil alivyokamatwa, akiamriwa kuweka mikono kichwani. Kamanda Amata alitazama kwa makini sana, akajaribu kuangalia sura za watu wale waliokuwa na silaha nzito za kivita, alitazama jinsi walivyompakia Jamil kwenye jeep na kuondoka nae. Kamanda Amata akaichukua disc hiyo na kuitia mfukoni kisha akatoka nje ya ofisi hiyo na kuondoka zake.

    Moja kwa moja akaenda kufuata taarifa za Sebeki baada ya kujua kuwa naye alikufa kwa mlipuko wa bomu mbele tu ya hoteli aliyofikia, nako alipata disc kama ile iliyohifadhi picha za video zikionesha mlipuko ule, Kamanda Amata alitazama kwa makini sana, mara hii aliona taswira ya mwanamke, alijaribu kurudisharudisha mara kwa mara kumwangalia mwanamke huyo lakini hakuweza kumtambua, aliichukua disc hiyo na kupotea zake.

    Dakika kumi na tano baadae alifika kwenye hoteli aliyofikia, hoteli ya Jazeera Palace, kabla hajashuka garini, alifungua kompyuta ndogo ndani ya gari yake, akapachika zile disc moja baada ya nyingine na kuzituma picha hizo katika idara ya usalama Tanzania ili zifanyiwe kazi. Alipohakikisha kazi imekamilika akateremka na kuvuta hatua kuingia ndani ya hoteli hiyo.







    “Ujumbe wowote!” akamwambia mhudumu wa mapokezi, yule mhuidumu akainama na kutoa bahasha moja ya kaki akampatia. Amata akainyakua na kuondoka zake kuelekea ghorofa ya juu. Alifika mlangoni mwa chumba chake, kabla hajashika kitasa alisimama kwa sekunde kadhaa, akagundua kuwa ndani ya chumba chake kuna mgeni, alitazama alama ndogo aliyoiacha kwenye kitaza cha mlango ambayo haikuwepo tena. Akachomoa bastola yake na kuiweka sawa, kisha akafungua mlango na kuuacha wazi bila yeye kuingia, ukimya ukatawala. Amata hakuingia ndani na wala aliyekuwa ndani hakutoka nje, waliwindana. kamanda Amata akaamua kuingia kwa kasi huku akijirusha kwa ustadi wa hali ya juu sana na kutua upande wa pili wa chumba, kwa haraka alimuona mtu aliyemtarajia nyuma ya mlango, yule jamaa alifyatua risasi iliyomkosa padogo Kamanda na kuchimba ukuta, Kamanda Amata akavingirika na kupita chini ya kitanda, risasi ya pili nayo ikamkosa padogo vilevile, wakati huo Kamnda Amata akawa tayari ametokea upande wa pili, kwa kasi ya ajabu alifyatua risasi iliyopiga sawia bega la mtu huyo.

    “Aaaaaaaaiiiihhhhgggghhhh!!!!” yowe la maumivu likamtoka yule mtu huku akiidondosha bastola yak echini. Ksbls hsjsfiks chini sakafuni risasi ya pili ilifumua kifua cha mtu huyo na kumbwaga chini. Kamanda Amata akawahi pale alipoanguka kabla hajakata roho.



    “Nani kakutuma?” akamwuliza, lakini yule mtu alikuwa akipumua na kuangusha mabonge ya damu kutoka kinywani mwake. Akamtazama Amata, lakini hakujua ajibu nini, “Wapi mmemweka Jamil?” akauliza tena.

    “Gha…la….ni…” akajibu kwa tabu.

    “Ghalani wapi?” Kamanda akauliza tena.

    “Ki…wa…nda… cha ngu…. Nguuuoo” baada ya kujibu hilo yule mtu akanyamaza kimya, roho ikauacha mwili.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amata akairudisha bastola yake katika mahali husika, akaugeuza mwili wa yule mtu na kupekuwa mifukoni, akatoa simu moja, zaidi ya hapo hakukuwa na kitu chochote kingine. Kamanda Amata aliitazama ile simu kwa makini sana, ilikuwa ni simu ya kisasa sana iliyofungwa mtambo wa GPS ambao unaweza kukuonesha mahali ulipo au mahali unapaotaka kwenda. Kamanda Amata akachana bahasha aliyopewa na ndani yake kukadondoka kijikadi kigumu kimoja, akakiokota na kukisoma.

    ‘Mujabba Club 2030’

    Akairudisha ndani ya bahasha ile na kuitia katika begi. Kisha akainua mkono wa simu na kubofya namba za chumba cha usalama cha hoteli hiyo.

    “Haraka sana mfike chumba namba 305 kuna shida,” akakata simu baada ya kutoa taarifa hiyo. Nukta chache tu mlango wa chumba chake ukagongwa, akawaruhusu kufungua. Vijana wawili waliokuwa na askari mmoja mwenye silaha waliingia na kulakiwa na dimbwi la damu, wakapigwa na butwaa.

    “Huyu ni nani na ameingiaje chumbani mwangu?” Kamanda akawauliza.

    “Hata sisi mzee hatujui, na ndo maana tunashangaa,” akajibu mmoja wa vijana wale.

    “Haya ondoeni mzoga wenu,” Kamanda akawaamuru, nao mara moja wakapiga simu na gari ya wagonjwa ikafika pamoja na polisi kadhaa. Kamanda Amata akatoa maelezo kwa maandishi, misatari miwili tu ilitosha na kuwarudisia faili lao. Yule askari aliposoma akamtazama kamanda usoni.

    “Ni hivi tu?” akauliza.

    “Ndiyo ni hivyohivyo tu,” akajibu Kamanda.



    §§§§§§

    Shalabah alionekana kuchanganyikiwa, alikuwa akizunguka huku na kule akiwa kama mtu aliyesahau kitu, viajana wake walikuwa wameketi kwa utulivu kabisa.

    “Sharon,” akaita, na Sharoni akainua uso kumtazama, “Tuna kazi kubwa.”

    “Huyu ni chui sijui au tumwiteje, maana hatabiriki,” Sharon alijibu.

    “Mpaka sasa amekwishatuondolea watu takriban watatu, tunamfanyeje mtu huyu?” Shalabah akauliza.

    “Leo ni kumfanyia uvamizi wa maana na kummaliza,” Sharon, ambaye ndiye kiongozi wa kikosi hicho hatari alitoa uamuzi.

    “Yule ni zaidi ya jeshi kaka, tutumie mbinu nyingine tu, lakini swala la kumvamia tusithubutu kulifanya,” Shalabah alitoa rai. Mara mlango wa chumba hicho ukafunguliwa, Fasendy akaingia kati ya wanaume hao.

    “Nimekuja,” Fasendy akasema.

    “Karibu sana, bila kuchelewa nataka uongoze kikosi hiki ukisaidiana na Sharon kumkabili mtu huyu, muilete roho ama ndani ya mfuko au mikononi mwenu, malipo makubwa umeahidiwa kutoka kwa Mr. Lonely,” Shalabah alimwambia Fasendy na kuitupa picha ndogo mezani, fasendy akaiokota na kuitazama.

    “Mbona umeshtuka?” Shalabah akauliza.

    Fasendy akatikisa kichwa juu chini, “Sasa Mogadishu imekuwa ndogo.”



    “Kwa nini unasema hivyo?” Sharon akauliza.

    “Huyu jamaa ni hatari sana, usije kujidanganya kumkabili ana kwa ana, huu ni ama mzimu au roboti ana akili ya ajabu ana mbinu za utatanishi,” Fasendy alieleza.

    Shalabah na Sharon wakatazamana, kisha wakarudisha macho yao kwa Fasendy.

    “Kwa hiyo unasemaje?” Shalabah akauliza.

    “Kufa atakufa tu lakini si kwa ngumi wala teke, huyu labda tumwekee sumu,” Fasendy akajibu.

    “Fasendy, mbona sikuelewi?” Sharon akauliza.

    “Utanielewa tu Sharon siku ukikutana naye, ninamaanisha huyu jamaa tujipange upya ili kumkabili,” Fasendy akaeleza.

    “Yuko Jazeera Palace chumba namba 305, fanya unaloweza, niletee majibu ya kuridhisha,” Shalabah alimpa maagizo Fasendy kisha yeye kuwaacha hapo na kuingia mlango mwingine.



    CLUB MUJABBA saa 2.30 usiku



    KATIKA kona moja ya ukumbi mdogo wa club hiyo, Kamanda Amata alitulia kimya akiwa na juisi baridi huku akisubiri huyo aliyemuachia ujumbe kule hotelini. Hakuwa na hofu kwa kuwa alikwishzoea kukutana na watu asiyowajua.

    Haikumchukua muda mrefu, mbele yake alimuona mzee wa makamo aliyeonekana kuishiwa nguvu tayari akiwa anatembea kwa msaada wa mkongojo, alitembea kwa taabu mpaka pale kwenye meza ya Kamanda Amata, akavuta kiti na kuketi kwa mtindo wa kutazamana. Kamanda Amata alimtazama shaibu huyo mwenye nywele nyeupe zilizojaa mvi, miwani ya macho, suti iliyomkaa vizuri na mkononi mwake alikuwa na saa kubwa ya gharama sana ikitanguliwa na pete ya dhahabu.

    “Kamanda Amata,” akaita kwa tabu huku akisindikiza maneno yake na kikohozi kikavu.

    “Yeah ndo mimi, wewe, wewe ni nani?” kamanda akauliza kwa uoga kidogo.

    “Haunijui, lakini utanijua mimi ni nani,” akasema yule mzee na kuanza kukohoa, akakohoa sana mpaka Kamanda akamwonea huruma.

    “Babu, nikupeleke hospitali,” kamanda akamwambia.

    Yule babu akamwangalia Kamanda usoni, “Ngoja kidogo,” akamwambia.

    Akakohoa tena mara mbili kwa nguvu, mkononi mwake kikadondoka kitu cheusi, akakipekuwa kwenye kohozi la njano, Kamanda Amata, alishikwa na kichefuchefu lakini alivumilia.



    “Kamanda Amata, kazi hii uliyopewa ni wewe tu unayeweza kuifanya kwa kuwa nakufahamu tangu ujana wako, nakufahamu tangu ukiwa C.C.P kabla hujatolewa kuja idara ya usalama,” yule mzsee akamwambia, akakohoa lakini sasa kikohozi kilikuwa cha kawaida, akaendelea, “Umeiona hiyo chip? (Kamanda akatikisa kichwa huku akiifuta kwa kitambaa) ndani yake kuna kila kitu juu ya sakata hili, Kamanda hii ni hujuma kubwa sana, mimi mwenyewe nimeijua wakati niko pale Msanga Mkuu, Mtwara, najua, najua sana,” akajishika mikono yake usoni na kuvua sura la bandia alilokuwa amelivaa usoni mwake, lililotoka na nywele zile nyeupe, akabaki na sura yake halisi.

    Mshtuko mkubwa ukampata Kamanda Amata, akabaki mdomo wazi, hakuamini anachokiona mbele yake, mzimu.

    “Usiogope, sio mzimu ni mimi,” Yule mzee akaongea kwa upole.

    “Mwalimu?” Kamanda akauliza.

    “Ndiyo ni mimi, sikufa kama unavyojua au niseme mnavyojua, ile ilikuwa ni mbinu yangu ya kutoroka na kwenda katika upeo wa macho na akili zenu, niko hai,” yule mzee alijieleza.

    “Ni ngumu kuamini, ni ngumu sana kuamini,” kamanda alisema huku akiwa kajishika kichwa chake.

    “Kamanda Amata, ninakuamini sana ndiyo maana nimejidhihirisha kwako, na ninajua kuwa hautamwambia mtu yeyote kuwa umekutana na mimi, lazima uchanganyikiwe, lazima Kamanda na ninajua kwa nini, lakini mimi kufa mbele ya macho yenu ilikuwa ni kuondoka kwa sababu nilishaijua hujuma inayokuja na ambayo ningehusishwa kwa namna moja au nyingine, sikuwa tayari kwa hilo, nikajiondoa kwa njia ile, sasa habari iko hivi,”



    Miaka kumi na nne iliyopita

    Wizara ya nishati na madini



    ILIKUWA ni ajenda ndefu iliyojadiliwa kwa siku kadhaa ndani ya ofisi hiyo nyeti katika serikali ya Tanzania.  Yote hiyo ilitokana na ugunduzi uliofanywa na  wanasayansi wa Tanzania wakisaidiwa na wale wa Urusi waliokaa katika pwani na bahari ya Hindi huko Mtwara. Madini ya Urani na mengineyo hatari kabisa kwa maisha ya binadamu na viumbe vingine yaligunduliwa kutoka katika kina kirefu cha bahari eneo la Msanaga Mkuu. Baada ya kugundulika na kuwa na uhakika kuwa ndiyo yenyewe serikali ya Urusi ilitaka kuingia mkaba na serikali ya Tanzania ili kuchimba na kurutubisha madini hayo hapahapa nchini. Baada ya kusainiwa kwa mikataba pale wizara ya madini; serikali hizo mbili zilikubaliana kugawana kwa asilimia, ile ya Tanzania 60% na ile ya Urusi 40%. Kwa mkataba huu ilikuwa Tanzania ifaidike sana. Kubaliano linguine lilikuwa ni lile la kuunganisha nguvu za kijeshi kwani nchi hizo mbili zilitaka kurutubisha madini hayo na kutengeneza silaha kali za na nzito za kivita.

    Katia ya watu waliokuwa wakifuatilia kila hatua ya mkataba na makubaliano hayo tangu kuanza kwa uchunguzi huo alikuwa ni mwanausalama mashuhuri sana katika idara ya usalama Tanzania ambaye mara kadhaa aliwahi kufanya kazi na mashirika makubwa kama NSA, CIA, MOSSAD na mengine mengi kwa kutoa ushauri au mafunzo fulani ya mbinu za kijasusi; hata alipostahafu bado serikali ya Tanzania ilimchukua kwa kazi maalum ikiwa ni pamoja na kuanzisha idara ya kijasusi, idara nyeti ya kushughulikia matatizo ya kimataifa katika Nyanja ya kiusalama. Mzee huyo waliyempa jina la ‘The Chamelleon’ lakini kwa jina lake halisi ni Mzee Mwambe, kachero aloyewahi kuwekwa kwenye jeneza mara kadhaa ikidhaniwa amekufa lakini alikuwa akifanya danganya toto. Mzee Mwambe alijichanganya katika kundi la watafiti wa Tanzania na kuangalia kila kinachofanyika, kwa kuwa serikali ilimuweka kwa malengo maalum alikuwa akipewa nafasi za juu makusudi ili akutane na watu mbalimbali na ajue nini kinazungumziwa katika mradi huo.



    ‘The Chamelleon’, aliushtukia mchezo mchafu unaotaka kufanywa na baadhi ya watu katika mradi huo. Tajiri mmoja mkubwa kutoka nchi za Magharibi, tajiri asiyeonekana kwa macho ya binadamu alikuwa akiyataka madini hayo ama yawe yamerutubishwa au yawe ghafi. Alitoa pesa nyingi sana kuhonga huku na kule na wale wenye uchu wakazipokea pesa hizo na kuzifanyia watakayo. Mmoja wa wanasayansi wakubwa wa Urusi alijiingiza kwenye sakata hilo na kuwa akitoa siri kwa tajiri huyo ya kuwa nini kinaendelea katika mradi huo. The Chamelleon aliyekuwa akiujua mchezo mzima huo, alikuwa akitoa taarifa zake katika idara ya usalama ya serikali ya Tanzania kuwa wakae macho na hujuma hiyo inayotaka kufanywa na baadhi ya wenye uchu wa pesa chafu. Kila aliyekuwa akihusika kwa namna moja au nyingine, serikali ya Tanzania ilikuwa makini kuwawajibisha na kuwatimua kazi wote wanaohusika, hakukuwa na mchezo hata kidogo.

    Baada ya miaka kadhaa ikajulikana kuwa ni nani anayetoa taarifa hizo serikalini, walijaribu kila mbinu ya kumshawishi The Chamelleon, kwa rushwa za aina mbalimbali lakini aliwakatalia katakata.

    Mkutano wake wa mwisho kabla ya kufa kwake aliufanya na Rais wa nchi pale katika Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma, kilikuwa kikao cha siri sana.







    CHAMWINO – DODOMA

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ULIKUWA ni mkutano wa siri lakini uliochukua muda mrefu wa kutosha ndani ya Ikulu hiyo ndogo pale Chamwino. Mzee Mwambe, kachero aliyekuwa kazini kwa shughuli maalum alikuwa akikutana na Rais, mkuu wan chi kujadiliana mambo kadhaa. Tayari aliiona hatari kubwa mbele yake, mpango kabambe wa kumuondoa duniani ili wapenda pesa wafanye kile watakacho.

    Alipogundua hilo alifanya haraka kumshawishi Rais kuanzisha kitengo hicho cha kijasusi katika Tanzania, TSA, wazo ambalo halikupingwa na mpango ulianza mara moja.

    “Sasa unajua kama ulivyosema kuwa ni muhimu kuwa na kitengo hicho, sawa, lakini unafikiri ni nani anaweza kukiongoza, muaminifu?” Mheshimiwa Rais alihoji.

    Mzee Mwambe alitoa maelekezo yote mpaka jinsi ya kukiweka kitengo hicho. Baada ya mazungumzo hayo ndipo alipompa taarifa mpya juu ya maendeleo ya kazi za ujenzi wa kituo cha kurutubisha Urani huko Mtwara, lakini alionesha wazi hofu yake ya kupangiwa njama ya kuuawa na wabaya wake ambao walikuwa wakifanya juu chini kuhujumu mkakati huo.



    “Nilifikiri kukukabidhi wewe kitengo hiki,” Mheshimiwa alimwambia Mzee huyo.

    “Hapana, mpe Madam S, yeye ni mtu wangu wa karibu na ni jasiri sana, msiri aliyebobea kwenye kazi hizi,” Mzee Mwambe akajibu kwa kutoa maelekezo.

    “Na upande wa vijana je?”

    “Nimemwandaa vyema Amata Ric, yeye atakuwa Kamanda wa kikosi, baadaye tutaona jinsi ya kuwapata vijana wengine wenye hari na uzalendo wa taifa lao, kama unavyojua nimempa kazi nyingi ngumu za kimataifa, amezifanya kwa ustadi wa hali ya juu sana, yeye amefuzu katika kila Nyanja ya mapambano, sasa yuko huko Sierra Leone, kuna kazi nyingine nimempa,” Mzee yule alieleza.

    Mheshimiwa Rais aliinamisha kichwa mezani, kisha akainua uso wake na kumtazama Mzee huyo.

    “Ok, mi nafikiri kazi uliyoifanya mpaka hapa imetosha, nikuondoa kwenye nafasi yako nisije kukupoteza kama walivyopanga wabaya hao,” Mheshimiwa Rais alionesha wasiwasi wake wa wazi wa kumpoteza Kachero wake wa juu kabisa ingawazje alikuwa amestahafu. Mzee Mwambe alikuwa kimya akimsikiliza, akakohoa kidogo na kusema, “Sawa, ni wazo zuri lakini huna budi kumchagua mtu makini kukaa pale”.

    Ilichukua masaa takribani matano kuhitimisha kikao hicho ambacho kilimuacha Rais na maswali mkubwa, shaka nzito na hofu ya kutosha, ‘wananisaliti?’ alijiuliza.



    §§§§§

    Ilikuwa ni baada ya kuagana na Rais pale Chamwino, Mzee Mwambe alikuwa akitoka na gari yake akiiacha barabara ya kuingilia Chamwino, sasa alikuwa alkiingia barabara kubwa ya Dodoma-Morogoro alipokutana na lori kubwa la mizigo lililoigonga gari yake kwa kishindo, ngao kubwa la chuma la lori lile liliifinya vibaya gari ya Mzee Mwambe na matairi makubwa kuibonda, kisha ile lori haikusimama, iliendelea na safari kama kilomita tano na dereva akaitelekeza na kuondoka.

    Hali ilikuwa tete, Mzee Mwambe alitolewa kwenye gari ile kwa shida na kukimbizwa hospitali ya Dodoma kwa matibabu, lakini wakiwa pale Dodoma ilionekana wazi kuwa hawezi kupata matibabu stahiki kwa jinsi alivyokuwa ameumia hasa kwa ndani, hivyo alipewa rufaa na usiku huohuo aliondoshwa na ndege ya serikali mpaka hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pale napo hali ilikuwa hivyohivyo, Mzee Mwambe aliondoshwa na kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, alikuwa huko kwa siku kadhaa ndipo taarifa mbaya ilipokuja Tanzania kuwa Mzee huyo, Kachero wa siku nyingi, The Chamelleon, amefariki dunia katika hospitali kubwa ya Appolo.

    Ilikuwa ni taarifa iliyotikisa idara nzima ya usalama katika serikalai ya Tanzania, wakati upande huu unasikitika basi upande mwingine ulikuwa unafurahia, tafrija kubwa iliangushwa katika hoteli ya Embassy pale Dar es salaam, tafrija ya kushangilia ushindi, ‘Tumekata mzizi wa fitna.’ilikuwa kama kauli mbiu.



    6…rejea, MOGADISHU

    CLUB ya MUJABBA



    “Kamanda Amata, mimi sikufa, ile ilikuwa ni mbinu niliyoipanga nikiwa hospitali mara tu baada ya kuipata nafuu na kuhakikishiwa uzima,” Mzee Mwambe alimwambia Kamanda Amata. Mshangao wa wazi ulionekana usoni mwa Kamanda Amata.

    “Usishangae Kamanda, inapobidi unafanya hivyo ili kujiondoa machoni mwa watu, na wapo wengi waliofanya hivyo hasa majasusi wan je kwa nini isiwe mimi.

    “Sasa unaishi wapi Mzee?” kamanda akauliza.

    “Naishi Tanzania, Lindi kwetu, mi nilirudi Tanzania mwaka mmoja baadae, na moja kwa moja nikaenda kuishi kwetu Lindi, lakini harakati zangu hazikukomea hapo, Kamanda, ukiwa mzalendo ni mzalendo tu na ukiwa fisadi ni fisadi mpaka vizazi vyako. Nilirudi na kuishi maisha duni sana hiyo ilikuwa ni mbinu yangu, nikapata kazi ya ulinzi palepale Msanga Mkuu kwenye duka moja kubwa la Prakesh, ambalo kutoka lilipo, kufika kwenye kile kinu hapakuwa mbali, hivyo niliendelea kufuatilia nyendo zote za ule mchezo bila wao kujua, nilikuwa nina uwezo wa kuingia mle ndani ya jengo lao kwa njia zangu mpaka nilipojua kilichopo, nilipotega vifaa vyangu vya kunasa sauti ndani ya ofisi ya mkurugenzi ambaye alikuwa na asili ya Uarabu ndipo nilipopata siri hii (akamwonesha ile memory card), nikajua kuwa ile meli lazima itekwe pale Somalia kwani huyu mkurugenzi alikuwa na mawasiliano na Maharamia, na ni mchezo uliochezwa, watu wanajua. Siku manowari ile ilipopakia yale makombora kwa ajili ya majaribio, nilikuwa naona kila kitu, kabla haijaondoka mimi niliondoka na kuja Somalia,” akakohoa kidogo kisha akaendelea na simulizi yake ambayo ilimuwacha Amata katika hali ya bumbuwazi,



    “Unasikia, Kamanda Amata, hawa jamaa wamejipanga, sasa kila unaporudi hotelini kwako hakikisha unapita kaunta utakuta ujumbe wako, ukiona siku hakuna ujumbe wowote ujue nimepatwa na hatari kubwa, naomba tuagane,” Mzee Mwambe akamaliza na kuiweka vizuri sura yake, kisha akainuka na kutoka ndani ya club ile. Kamanda Amata alikuwa akimwangalia mzee huyo mpaka alipopotea, moyoni mwake hakuwa anaamini wala hakuwa haamini, alifikicha macho mara kadhaa kuona kama yuko usingizini lakini sivyo.



                                                                         §§§§§

    Saa saba usiku, Kamanda Amata aliegesha gari yake kando kando ya hoteli moja iliyo pembezoni mwa bahari ya Hindi, hapo aliweza kuona mandhari nzuri ya usiku katika bandari ya zamani ya Mogadishu. Kutokana na maelekezo aliyoyapata katika ile memory card aliyopewa na yule mzee ‘The Chamelleon’ alihakikisha hakosei maelekezo hayo. Alijiweka sawa na kuteremka garini akiwa na nguo nyeusi tupu, mkononi akiwa na begi alilolishikilia. Kwa mwendo wa hadhari wa kukimbia na kutembea, aliambaa na ukuta mpaka kwenye kingo za gati la zamani kabisa la bandari hiyo, akatulia na kutazama huku na kule, aliona walinzi waliokuwa wakirandaranda, alipohakikisha hawajageukia upande wake, alivuka eneo hilo na kufikia kwenye miti mingi ya mikoko iliyoota sambamba na miisho ya ukuta huo, akatulia akisikiliza lolote lisilomhusu, alipoona hali ni shwari alifungua begi lake na kutoa vifaa kadhaa vya uogeleaji, akavaa tayari tayari kisha taratibu akaingia majini bila kumgutusha mtu yeyote.



    Kamanda alipiga mbizi na kujivuta mpaka kwenye kilindi cha bahari, Kamanda Amata akiwa anasaidiwa na mitungi ya hewa ya oksijeni mgongoni mwake kwa mbali aliona kitu kama ukuta uliojengwa ndani ya maji, aliuendea na kuufuata ulikokwenda, mbele kabisa alikutana na mlango mkubwa uliofungwa kwa mnyororo wenye kutu na kufuli lake lilikuwa kwa ndani, hakujali, alichomoa kijimtungi kidogo alichokipachika juu ya tumbo lake, akakimata mkononi, na kukibonyeza kwa juu kisha kikaanza kutoa moto wa gesi ambao haukuweza kuathiliwa na maji. Taratibu akakata ule mnyororo na kuugawanya huku na huku, akakirudisha kile kijimtungi mahala pake na kuutikisa ule mlango, bado ulikuwa ngangari, ukiszingatia ulikuwa umekandamizwa na msukumo mkubwa wa maji, akatoka na kutazama kama kumahala pengine penye mlango hakuona. Akiwa katika kurudi katika ule mlango, akaona kitu cha kustahajabisha kidogo. Kitu kama donge la hewa likipita mbele yake kutokea chini, likielekea juu. Hii kwa Kamnda ilikuwa na maana, akajibinua na kuelekea upande wa chini kule lilikotokea donge lile, akakutana na ukuta mwingine lakini hapa palikuwa na tundu kubwa ambalo angeweza kupeita bila shida, akachomoa tochi yake na kuingia taratibu huku akitazama huku na huko.

    Lilikuwa ni tundu refu sana, lakini alifanikiwa kufika mwisho wake, kote kulikuwa ni maji tupu. Alipofungua kijimlango kidogo kilichokuwa na chekeche la kuzuia takataka akafanikiwa kuingia ndani. Lilikuwa ni jengo kubwa, huku ardhini tungeliita ‘godown’, ndani yake Kamanda aliona mabaki na magofui mengi ya meli za zamani zilizotelekezwa. ‘Kwa nini jengo hili liwe huku?’ alijiuliza, kisha akaendelea kuogelea akipita huku na huko, akiwa anaelekea karibu kabisa na lile lango aliloshindwa kulifungua ndipo alipoiona meli kubwa iliyojikita chini na kufungwa na minyoronyoro mikubwa mikubwa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kerov Class-JWTZ 26-90, yalikuwa ni maandishi yaliyoandikwa katika upande mmoja wa meli hiyo juu kidogo ya tundu kubwa la kutolea nanga. Kamanda akatikisa kichwa kuashiri amegundua kitu, akaingia ndani ya meli hiyo na moja kwa moja akaingia chumba cha kuhifadhi makombora, alifika bila kupotea kutokana na ramani aliyoikuta katika memory card aliyopewa na yule mzee. Katika vishikio vya makombora hayo, ni vishikio viwili tu ambavyo havikuwa na makombora, ikiwa na maana mawili kati ya kumi na mbili yalikuwa yamekwishaondolewa, akayazunguka na kulifikia moja, akatulia pale, akalitazama mbele ya kichwa cha kombola hilo na kuona skurubu kadhaa zilizoshikilia sehemu hiyo ya mbele. Alikwishasoma muundo wa makombora hayo aina ya R-26 IBM, akatoa kifaa cha kufungulia skurubu hicho kinachotumia umeme wa betri ndogo ukubwa wa AAA, akafungua skurubu ya kwanza mpaka ya mwisho, kwa tahadhari kubwa akachomoa kichwa cha lile kombora, akakigeuzauza na kuona jinsi kiloivyotengenezwa kitaalamu, ni alama ya mlipuko ilichorwa kwa ndani, ikiwa na maana kuwa katika kichwa hicho ndipo penye mlipuko mbaya kabisa, yaani ndio bomu lenyewe, alipojiridhisha na hilo, akalegeza taratibu ile chemba yenye madini hatari ya Urani, akakichomoa kutoka kwenye kile kichwa kisha akakifunga vizuri katika jaketi lake.



    Alipomaliza kurudishia kile kifuniko kama kilivyokuwa mwanzo, akaitazama saa yake, ilikuwa inatimu saa nane usiku, akavuta mpira wenye hewa ya oksijeni na kutazama kipimo cha hewa aliyobakia nayo, ilikuwa haitoshi kustahimili zaidi ya dakika arobaini na tano. Akaamua kutoka eneo lile na kufikiri kurudi usiku unaofuata. Akapita njia ileile aliyoingia nayo na kutoka nje ya meli ile. Alipokuwa anatafuta lile tundu la kutokea ndipo alipohisi kitu kama mshale kikipenywa kati ya mgongo wake na mtungi wa gesi na kukata mikanda iliyoshikilia mtungi huo, ukafunguka. Kamanda akajua, tayari, ameonekana, akauacha mtungi ule ukidondoka taratibu, akachomoa bunduki yake aliyokuwa ameipachika mgongoni, bunduki kubwa yenye nguvu. Mbele yake aliwaona wapiga mbizi wawili wakija upande wakiwa na mihsale ya kuwindia Papa, Kamanda akaliweka vizuri bunduki lake na kufyatua, risari ya kwanza ilipiga kichwa cha mmoja wao. Wakati Kamanda anajiandaa kupachika risasi nyingine, mshale wa yule mwingine ukamchoma katika nyama ya mkono sehemu ya kati ya bega na kiwiko, maumivu makali yakampata Amata, kabla hajafanya lolote yule jamaa alimfikia, Kamanda akakabwa koo. Hakuna aliyeweza kuongea chochote. Kamanda alikukuruka lakini ilikuwa ni ngumu kutokana na maumivu makali ya ule mshale. Akanyosha mikono yake na kuifyatua mipira ya hewa kutoka katika mtungi wa yule mtu, akakosa hewa na kumuachia Kamanda. Amata akatumia nafasi hiyo, akajivuta mguu na kuchomoa kisu, akamchoma tumboni na kumuona yule mtyu akilegea taratibu.



    Akachomoa kitu kama tyubu ya dawa ya meno na kuifungua kicha akakipachika mdomoni, kidubwasha hicho kilihifadhi hewa ya oksijeni inayoweza kutumika ndani ya dakika kumi tu. Akajitahidi na kutoka nje ya ghala lile, Kamanda Amata akajivuta taratibu mpaka kwenye ile mikoko alipokuwa ameacha begi lake, hakulikuta, akajua kwa vyovyote wamemgundua, kengele za hatari kichwani mwake zikagonga, akajiweka kwenye hali ya tahadhari, akavua yale mavazi yake na kuyafunga pamoja kisha akaanza kutembea taratibu, mbele kidogo inapoishia ile mikoko na kuanza ule ukuta wan je kulikuwa na kijana mmoja mwenye bunduki kubwa akishika doria. Kamanda Amata akatazama pande zote hakumuona mtu zaidi ya huyo tu, akajitokeza na kumwita, yule bwana alipogeuka, Kamnda akamrushia kile kifurushi cha zile nguo, yule mlinzi akababaika nacho, sekunde hiyohiyo, Amata aliruka kiufundi na kutua kwa miguu kifuani mwa yule mlinzi na kumpeleka chini, akamkandamiza pale chini mpaka alipohakikisha amelegea kabisa, akamuachia na kuondoka taratibu akiambaa na ule ukuta mpaka kwenye gari yake, akiwa mbali kabla ya kuifikia akabonyeza swichi yake ya mkono na kuiwasha gari hiyo kisha akatulia kuangalia kama kuna mtu atakayeisogelea au la, kwa hatua za taratibu akaifikia na kufungu milango kisha akajiweka kwenye kiti cha dereva, akafungu droo ya chini ya dashboard, akatoa kikasha cha huduma ya kwanza na kujiganga jeraha lake la mkononi.

    Alipohakikisha yuko sawa, aliitoa gari yake taratibu na kuondoka eneo lile kurudi hotelini kwake.







    “Ujumbe wowote,” alimwambia mhudumu wa mapokezi, yule mwanadada akainama chini na kutoa bahasha, Kamanda akaipokea na kuifungua hatua chache kabla hajaondoka, akasoma ujumbe uliopo, ulikuwa ujumbe mfupi sana, akaondoka na kuzikwea ngazi taratibu kuelekea chumbani mwake.



    SEHEMU YA XIV



    Kamanda Amata hakutamani kukaa chini au kufanya starehe yoyote maana alijua wazi akipoteza dakika au sekunde basi maisha yake yako hatarini, alishaonywa uhatari wa hao watu hivyo kila nukta alikuwa katika kujilinda kwa nguvu zote.



    §§§§§§



    Ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Maharamia wa Mogadishu kumtega Kamanda Amata, kila walipojaribu waliambulia hasara tu. Mara kwa mara walikuwa wakiitana chemba na kujipanga upya mpaka upya ukaisha.

    Sasa hoja ya kumdhibiti Amata ikafika kwa mtu wa juu kabisa, Mr. Lonely.

    “Mi nashindwa kukuelewa Shalabah, huyo mtu ni mtu wa aina gani asiyewezekana kudhibitia, huyo ni Kunguni tu, nataka kichwa chake hapa ndani ya masaa sita tu” Mr. Lonely alitoa amri akiwa amewaka hasira.

    “Tumejaribu kila namna ya kumnasa lakini tumeshimdwa, zaidi watu wetu wanapungua kila kukicha mzee,” Shalabah aliongea na luninga iliyobeba taswira ya mtu huyo asiyeonekana, ila katika taswira hiyo alionekana jinsi alivyofura kwa hasira.

    “Mpaka mtu anaingia godown maana yake ameshajua kila kitu, hakuna mpelelezi yoyote ulimwengu huu amewahi kufika ‘kuzimu’ akarudi duniani, sasa huyu imekuwaje?” Mr. Lonely aling’aka kwa hasira zilizomfanya Shalabah kutulia kitini kwa upole, “Sasa nataka mfanye kazi niliyokupa mkiniaharibia biashara tu nakata shingo wote ninyi,” akamaliza na na ile luninga ikazama ardhini taratibu.

    Shalabah akaliacha jumba hilo na kuondoka na gari yake aina ya Jaguar kurudi katika kambi ya muda ili kuwapanga vijana wake.



    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Juu ya jengo moja refu lililokuwa mkabala na hoteli ya Jazeera Palace, bunduki kubwa aina ya M107.50 Calliber Long range lilikuwa limesimama kwa miguu yake miwili huku kwenye kitako kukiwa na mwanamke aliyevalia suruali aina ya cardet, akiwa kaweka jicho lake la kulia kwenye kiona mbali kilichofungwa juu ya bunduki hilo. Akiwa kalala chini kwa utulivu huku pembeni yake kukiwa na kijana mwingine aliyebeba bunduki ya AK 47, usoni mwake akiwa kapachika darubini ambayo ilimsaidia kutazama kule anakitazama mwanamke yule.

    “Umemuona?” yule kijana akamuliza Fasendy.

    “Nimemuona,” Fasendy akajibu, huku bado jicho lake likiwa kwenye kiona mbali na akimwangalia kijana huyu kwa makini akiwa na mawzo chungu mbovu kichwani mwake. ‘Kwa nini nimuue? Mbona yeye aliniachia uhai wangu kule Uganda?’ alijiuliza huku akitembeza mtutu wa bunduki yake taratibu akifuatilia mwendo wa Kamanda Amata aliyekuwa akitoka kuifuata gari yake.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog