Search This Blog

Sunday 22 May 2022

BONDE LA MAUTI - 2

 







    Simulizi : Bonde La Mauti

    Sehemu Ya Pili (2)





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nitakula nini mbona sioni jiko eneo hili lote? Nilimrudiashia swali badala ya kujibu swali lake. "Naona kijana bado ujanisoma maana unadhani chakula cha hapa kinapatikana kirahisi?. Tupigane nikupe chakula." Kwanini nipigane na wewe kwa sababu ndogo kama hii kama chakula kipo we nipe nile maana tangu niingie hapa sijaweka kitu chochote tumboni mwangu na hata ukinipiga haitakuwa haki kabisa maana mimi mwenyewe kwa sasa najihisi unyonge. Nilijitetea ili kuondoa farangati lililo mbele yangu. "Kumbuka sheria ya hapa inakupasa kufuata amri ukishidwa ni kifo na hilo sitanii kabisa maana na mimi nimetumwa kuwakilisha na ninatekeleza wajibu wangu wa kazi." Hakukuwa na wakati wa maongezi tena kwani mtesaji alinivaa kwa kasi ya ajabu akija katika mapigo makali kabisa ya tayga crow.Hii ni staili hatari mno maana kama usipo kuwa makini unatobolewa macho kabisa na ukipangua vibaya unachanwa ngozi kabisa.Nilijitahidi kumudu mashambulizi haya ya haraka maana niliona mtu huyu hatanii kabisa maana kila pigo alilokuwa analiachia halikukosea shabaha yake.Kadiri alivyo zidisha makonde ya kucha nami nilijidhatiti kwa kupangua kwa kasi zaidi maana nilikwisha ona mapungufu yake katika mabega maana kila pigo lilotoka lilionekana wazi katika mabega yake hivyo akunipa shida kumkabiri kwa uharaka zaidi. Tulidumu katika mpambano zaidi ya dakika kumi ila hakuna aliye fanikiwa kuingiza walau hata konzi kwa mwigine maana kila mbinu aliyo kuwa anahitaji kuitumia niliijua vilivyo na hii ikanipa uhakika kwamba kajifunza chuo kimoja na mimi.Yeye ni nani hasa na kwanini awe hapa kwa maadui wa nchi za Afrika.Nilibaki nikiwa na maswali yasiyo na majibu kichwani mwangu. "Nimekukubari kijana hakika wewe ni mwenzangu kweli maana nilifikilia ni mtego wa kuninasa katika mpango wangu." Aliacha kunishambulia baada ya kuona nimekuwa sawa naye katika mapigano ya mkono na hii ikanipa uhakika kwamba nimo kazini pamoja naye. "Niite Erick jina la pili ni kificho mimi ni Komandoo kama uonavyo alama hii kwenye ngumi yangu ya kulia nipo hapa kwa mpango maalum kama yako na mimi nitakuwa msaada mkubwa kuhakikisha unakamilisha kazi yako kwa wakati na nitakulinda hadi urudi nyumba salama maana hiyo ndiyo kazi iliyo nileta hapa na nilijua utafika tu.pole sana kwa ukaribisho wangu mbaya maana hiyo ndiyo kazi yangu ya hapa na inabidi niwe hivyo ili kulinda uhalisia wangu" Nashukuru kuweza kukufahamu maana nilikuwa na mashaka na wewe jinsi ulivyo na roho mbaya tena isiyo na utu kabisa. "Hata wewe utakuwa kama mimi maana ili uwe hapa kwa amani inakupasa uwe katili zaidi." ******************************** Kwingineko katika kambi hii viongozi walikuwa katika kikao chao siri wakijadiri juu ya ujio wa vijana wapya walio ingia katika Mpango wao kichwa kichwa maana wengi wao walionekana ni waandishi wa habari na wapelelezi. "Hakuna anayepaswa kutoka salama katika himaya yetu maana kosa moja litapelekea hasara kubwa kwetu na hatutajua cha kujibu kwa bwana Mkubwa maana tayari katoa pesa nyingi kwa ajiri ya watu hawa." Kiongozi wa kambi hii aliendelea kutoa hotuba yake kwa wajumbe wa chini yake akiwapatia maelekezo ya kutosha juu ya mateka wao wapya waliokamatwa baada ya kuwekewa mtego walipojaribu kufuatialia nyendo za kundi hili hatari Duniani lililokuwa likisifika kwa uuzaji wa madawa za kulevya na siraha za maangamizi hasa katika nchi za Kiafrika na Uarabuni.Maana kazi yao ilikuwa ni kuchonganisha pande mbili na kisha wanawapatia siraha na wapiganaji kundi linalokuwa na pesa ama madini .Mchezo wao ulikuwa umekuwa kero kwa Mataifa mengine kwani walitumia mwanvuli wa Nchi kubwa kufanya mabaya.Nchi iliyojaribu kupambana na kundi hili hiliishia pabaya zaidi maana watu hawa walikuwa wamenunua serikali nyingi hasa viongozi wa juu wa nchi na wa jeshi. "Kwa hiyo hawa vijana tunafanya nao kazi kama kawaida?" aliuliza mjumbe aliyekuwa amekaa mkono wa kulia wa mkuu wa kambi hiyo. "Mbona unaniulizia jibu uliza swali kamili na sahii maana wote watabadilishwa akili na tunawatuma katika nchi zao wenyewe wakawafunze adabu." Kikao hicho kilifungwa baada ya kujadili mambo yanayo wahusu na mhafaka ulipatikana wa nini cha kufanya. ************************************* "Kazi uliyo kuja kuifanya ni kubwa mno kijana itakubidi uwe makini katika kutumia mbinu zako za kijeshi maana hapa kuna watu wanafuatilia nyendo zako kwa ukaribu zaidi na siku si nyingi utaingia katika chumba C V C hapo utakwenda kufutwa kumbukumbu zako ili wakutumie watakavyo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nadhani unavyokula chakula hicho utakuwa unafikilia mbali zaidi maana pindi moja nilipokuwa kwenye misheni yangu ya kwanza yalinikuta kama haya yanayokwenda kukukuta ila yangu yalikikuwa ni mepesi maana nilikuwa kwa watu wasio na mbinu za kivita wala teknologia kama ya hapa."Nilimtazama huyu Erick nisimuelewe maana kama jambo liliwahi kumkuta mbona anachukulia kama kitu kidogo.Sikumwam ini kwa asilimia mia maana huo ni mwiko kwenye kazi zetu hupaswi kumwamini mtu yeyote hata kama ni baba yako.Aliendelea kunisimlia yaliyo mkuta. "Nilitumwa katika nchi ya Kongo kwenda kuchunguza mauaji yaliyo kuwa yakitokea kwenye machimbo ya dhahabu.Nilifanikiwa kuingia kwenye mgodi huo kwa kujifanya dokta.Nikawa mtu wa kuchunguza kila nyendo ya watu hawa.Nilikaa ndani ya kambi kwa miaka mitano lakini sikufanikiwa kupata majibu yangu yaliyonifanya niwe pale.Nilipata marafiki wengi zaidi katika mgodi huo hasa wachimbaji wa madini.Katika maisha yangu ya kazi sikuwa na mahusiano ya kimapenzi na yeyote maana nilijua hicho ndicho chanzo cha kufanya nishidwe misioni yangu. Mmoja kati ya rafiki yangu aliyekuwa ni mchimbaji alinifuata siku moja nikiwa nipo kwenye ofisi yangu akanipatia ujumbe ulio badilisha mtazamo wangu wa maisha nikajikuta nimekuwa mtu mwingine kabisa. Ujumbe huo ulikuwa katika bahasha ndogo yenye nakshi nakshi ya silver ukiwa na mchoro wa jumba kubwa la kifahali,nyuma ya bahasha kulikuwa na alama ya fuvu la kichwa lililo katika bonde. Niliifungua bahasha hiyo ili niweze kusoma kilicho ndani yake maana ilionekana ni ujumbe mzito kuliko zote nilizo wahi kuzisoma katika maisha yangu. Nilipo ifungua nilikutana na ujumbe wenye kutisha mno uliokuwa umeandikwa kwa rangi nyekundu tena kwa maandishi makubwa mno. BONDE LA MAUTI.(SIRI NZITO) Hakika tumependezwa na utendaji kazi wako Dr.Erick.tumekuchagua kati ya wengi uifanye kazi yetu nyepesi iliyo mkononi mwako kwa siri sana.Hakikisha unakuja na mzigo wetu ambao utapewa na huyo kijana aliyekupa barua hii.Kumbuka hii ni siri ya watu watatu tu walio kwenye kambi hii iliyo kufa na muda si mrefu itazikwa.Nenda chini ya mlimani utakuta mzigo mwingine nao ubebe kisha kesho saa saba na dakika kumi njoo kwenye uwanja wa ndege ulio ndani ya mgodi huu utakuta usafiri wako wa kukufikisha mahali tulipo. "Barua hiyo iliishia hapo na kuniacha na maswali lukuki maana mzigo wa kwanza nimeambiwa nimeushika na siuoni.Hakika niliwaza uko wapi mzigo huu na hawa ni nani hasa?sikupata jibu haraka ilinibidi nitumie ujuzi nilio kuwa nao kupata majibu yangu yote maana watu hawa inaonyesha wamenichunguza kwa muda mrefu hadi kufikia hatua ya kuniamini kiasi hiki. Napenda nikupe siri hii kijana katika kazi zetu hizi usipende kutuma wala kuandika ripoti kokote maana unaweza kujikuta mahali pengine kama kuna msaliti kwenye upeo wako.Hii njia ilinifanya nisijulikane kamwe. Nilizitazama mikono yangu kwa umakini zaidi sikuona chochote zaidi ya saa niliyopewa zawadi pindi moja na Daktari mwenzangu alikufa kipindi nimefika kwenye kambi hii na alinambia kwamba niitunze saa hiyo hadi siku akinidai.Kitu cha kushangaza alikufa jioni hiyo tu aliyo nipa saa na mwili wake ulikutwa umekatwa mikono.Jibu la kwanza nikawa nimejua chanzo cha yote ni saa na sasa wenye nayo wanaitaji mali yao.Je saa hii ina nini hasa mbona inaitajiwa mno na watu hawa kama ni dhahabu mbona zipo za kutosha? Nilijiuliza maswali yasiyo na majibu. Ilinibidi nitoke nje nikatafute mzigo wao mwingine walio kuwa wamenielekeza kwamba upo kwene bonde lililo nje ya mgodi huu.Nikalichukua begi langu la ngozi maana uwezi jua mzigo una ukubwa gani? Nilifanikiwa kufika katika bonde hili lakini sikuweza kuamini macho yangu yalicho kiona maana nilikuta kuna miili iliyo oza ya watu hakika mahali pale kulitisha mno.Sikuwahi kufikilia kama kuna mauaji makubwa kwenye eneo hili na nilikuwa nimechunguza muda mrefu lakini sikuwahi pata jibu langu.Leo nalipata jibu langu katikati ya bonde la kivuli hakika niliamini kwamba kazi hii si nyepesi na sasa imeanza rasimi na bado sijajua chochote.Hakika eneo hilo lilionekana ni la muda mrefu mno maana ilionekana kuna na mifupa kabisa kuonyesha pale ni sehemu ya kutupwa mizoga.Ajabu ni kwamba huwa watu wanao kufa kazini wanazikwa ama wanachukuliwa na jamaa zao ila hapa kunaonekana kuna miili mingi.Je miili hii inatoka wapi mbona sioni hata ndege wala mzoga? Nilijiuliza nisipate jibu. Nilipo piga hatua ili niondoke eneo hilo maana niliona kama nimepotea njia nilisikia sauti ya mlio wa simu ikiita kwenye mwili wa maiti iliyo karibu yangu.Hakika nilishtuka mno sikuwahi kufikilia kama maiti inamiliki simu na mbaya zaidi maiti hii naijua.Hakika nilijionea maajabu mengine kabisa maana mtu aliye toka kunipa ujumbe muda si mrefu tayari amekuwa mfu tena ndani ya muda mfupi.Na inavyo onekana amekufa muda si mrefu.nilibaki najiuliza maswli yasiyo kuwa na majibu maana jibu langu limeyeyuka gafla baada ya rafiki niliye mtegemea kwenda katika njia ya watu wote.Simu iliendelea kuita lakini nayo niliona kama ni mtego wa kuniangamiza maana inavyo onekana watu hawa hawana utani kwenye kazi yao.Niliamua wacha nipokee simu hiyo maana inaonekana ni kwa ajiri yangu maana mtu huyo ndiye aliyeniletea ujumbe na kuwa mahali pale ni kama sehemu ya ujumbe.Nilipokea simu na kusikia sauti nzito ya mzee wa makamo ikiniamrisha kusogea mbele kabisa ya maiti hizo nitakapo hiona maiti ninayo ijua nifuate maelekezo mengine.Hakika usiombe ukutane na dhahama kama lililo nkuta maana ni kazi kwelikweli kuitafuta maiti unayo ijua ili hali ni mifupa mitupu,ilinibidi kutii maana tayari nimeingia ndani ya bonde lenye uozo kwa kupenda kwangu,.....................

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Fuata maelekezo ninayokupatia na hakikisha hukosei" Sauti ya kizee iliendelea kukoroma kwenye simu ikinipatia maelekezo ya nini cha kufanya.Hakika jambo ambalo linanichanganya hadi leo hii sikuwahi kupata jibu watu hawa wote walikufa muda gani maana mimi ndiye nilikuwa daktari kwenye mgodi huu na nilihusika katika kutibu watu wengi lakini sikuwahi kuona watu wakifa wengi namna hii.Hapo ndipo nilipopata jibu langu la miaka mitano iliyo pita kwamba kwenye mgodi huu kuna mauaji ya kinyama.Kitu cha kushangaza naambiwa ni siri ya watu watatu tu na akiijua mtu wa nne inabidi afe. Baada ya kuwa nimeiruka miili isiyo kuwa na uhai na mingine ikiwa ni mifupa tu kwa muda usiozidi dakika tano simu iliyo kuwa mkononi mwagu ikaita tena.Niliinyanyua simu hiyo na kubofya kitufe cha kupokelea kisha nikaiweka kwenye sikio la mkono wa kulia. "Simama mahali hapo na ufuate maelekezo yafuatayo.Vua saa yako hiyo na ifungue kwenye mfuniko wa nyuma" Nikaivua saa hiyo ambayo nilipewa zawadi na dr wa kizungu ambaye alikuwa ni rafiki yangu wa karibu pindi ayajamkuta yaliyo mkuta.Amini usiamini duniani kuna siri tena siri nzito ambazo watu wanatembea nazo bila kujua kama ni hatari kuwa nazo.Sikuwahi kufikilia kama saa hii ina mitambo mikubwa namna hii.Hakika baada ya kukiondoa kifuniko cha nyuma cha saa ulitoka mwanga mkali mno wenye rangi ya kijani. "Vizuri sana na ongera kwa kutoka salama maana mwanga huo ni hatari kwa uhai wa kiumbe hai kama ukikumlika sehemu yeyote ya mwili huo unakuwa ndiyo mwisho wako.Mbele yako kuna kazi iliyo kufanya uwe hapo"Sauti ya kizee iliendelea kunipa maagizo ya kutisha na magumu kutekelezeka. "Utazame vizuri mwili ulio mbele yako kwa umakini kisha tumia mwanga huo kuuteketeza huo mwili.Kitakacho bakia kichukue na ukilete mahali nitakapo kuelekeza kukileta." Hakika macho yangu hayakuweza kuamini kitu nilicho kiona maana uwezi amini kabisa yaani mwili wa Dokta mwenzangu aliye kufa miaka mitano upo mbele yangu tena ukiwa bado ni mbichi kabisa kama vile amekufa muda si mrefu.Hakika nilihamini watu hawa ni hatari kabisa maana kama ni kuua hii ni hatari na sikuwahi kuifkilia kama ipo dunia hii. Siuwa na chaguo zaidi ya kufuata maelekezo niliyopewa na watu hawa.Nilichukua saa yangu hiyo na kuelekeza mwanga kwenye mwili wa Dokta.Nilishuhudia mwili wa dokta ukiyeyuka kama barafu iliyo kwenye jua yaani hakuna cha mfupa wala maini vyote viliyeyuka na kuisha kabisa.Kilicho baki pale ni jiwe lenye kun'gaa mno lenye rangi ya kijani pia kama mwanga unao toka kwenye saa yangu.Baada ya mwanga wa saa yangu kupiga kwenye jiwe hilo ulipotea nisijue kipi kimejiri.Nililibeba jiwe hilo lenye uzito kama wa kilogram moja na kuliweka ndani ya begi langu kisha nikaifunga saa mfuniko wake wa nyuma na nyenyewe nikaiweka kwenye begi. Safari ya kurudi kwenye mgodi ikaanza tena ila kwa muda huu nikiwa nina mawazo chungu nzima maana yaliyo nikuta kwa muda mfupi si mchezo.Nilifanikiwa kufika salama kwenye mgodi huo.Safari yangu moja kwa moja ilinipeleka katka nyumba yangu maana nilijua sina tena wakati wa kuwa katika kambi hii maana inavyo onyesha kwa maneno ya watu hawa ni lazima mahali hapa pateketezwe. Hakika sikupenda kutoka mikono mitupu eneo hili maana tayari nilikuwa nimeshajipatia mali ya kutosha kwenye eneo hasa madini mbali mbali hasa dhahabu na almasi na sikuwa tayari kutoka mikono mitupu.Baada ya kufika kwenye chumba changu nilipakia madini yangu kwenye begi langu dogo la kiunoni na kisha lile begi jingine lenye mali ya watu nisio wajua nikaliweka mgongoni nikasubiri maelekezo mengine. Nikama watu hawa walikuwa wakiniona maana muda huo simu niliyo kuwa nimeipata kwenye mwili wa maiti ikaita. "Kama umekuwa tayari njoo kwenye kiwanja cha helkopita haraka iwezekanavyo maana una dakika tano za kuwa maeneo haya". Hakika sikukawia kutoka maana nilijua muda si mrefu kitaumana maeneo haya muda si mrefu kama taarifa niliyo pewa. Nilifanikiwa kuingia salama kwenye helkopita na itaanza kuchochea moto na kunyanyuka taratibu. Hakika baada ya kunyanyuka nilishutuka mno baada ya kuona mgodi ukianza kulipuka tena ilionekana mabom yaliyo kuwa yametegwa kwenye mgodi huu yalikuwa ni makubwa mno maana hata ndege iliyumba yumba lakini ikawa sawa tena baada ya rubani kucheza nayo vizuri. Huo ndiyo ukawa ndiyo mwisho wa mgodi huo. Nikiwa katikati ya safari nilipewa kinywaji na mzee niliye mkuta kwenye helkopita hiyo.Baada ya kunywa kinywaji hicho sikujua kilicho tokea kabisa maana nilipoteza kumbukumbu kabisa.........

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    kama iliyo kwenye saa niliyopewa zawadi na dokta niliye mkuta kwenye bonde la mauti akiwa amekufa ambaye nilimyeyusha na saa yake nikakuta madini ndani ya mwili wake.Na sasa naiona nembo ileile ikiwa kwenye chumba hiki hakika nilijua sipo mahali salama maana picha yenyewe ilisadifu wao ni watu wa namna gani. Nikiwa bado natalii chumba hiki kwa tahadhari kubwa kwenye meza niliweza kuliona begi langu likiwa limetulia tuli.Ilinibidi ninyanyuke nikalikague maana nilikuwa nimeweka madini yangu ya thamani kabla ya kupoteza fahamu na nilitaka kujihakikishia kama yatakuwamo.Maana hayo ni kama mshahara wangu wote niliofanyia kazi katika mgodi. Hakika kila kitu nilikikuta ni salama kabisa. Baada ya muda ilinibidi kutoka katika chumba hicho maana niliona kama hakuna mtu wa kunijulia hali.hakika sikuamini macho yangu yalichokiona maana eneo hili lilionesha lina mitambo ya kila aina ni kama vile niko kwenye kiwanda cha vyuma hakika sikujua niko sehemu gani haswa ama ni chombo gani hicho. Ilinibidi nisogee mbele huko niliweza kusikia sauti za vuma vikigonganagong ana.Nikiwa ninatafuta wenyeji wangu katika sehemu hii isiyo eleweka mbele yangu nilimshudia kiumbe wa ajabu akija mbele yangu kwa kasi hakika hakika kwa ambaye ni mgeni kwenye maswala ya teknologia ungeshazimia zamani ila kwangu niliona ni jambo la kawaida.Mbele yangu alikuwapo Robort aina ya RKC2999992 huyu ndiye roboti asiye fikilia maana anafanya kazi ya kuua na si kushidwa hakika nilimtazama jinsi anavyopanga silaha zake kwa ajiri ya kunishambulia.Sikuwa na hofu yeyote maana najua jinsi gani ya kumdhibiti maana kwa jinsi alivyo tengenezwa kasi yake iko kwenye miguu lakini kwenye macho yake ama kamera hazina spid kali kwa haraka nilimrukia juu kwenye kichwa nikamchomoa nyaya zinazopeleka mawasiliano kwe copyuta yake na huo ndio ukawa ndiyo mwisho wa kiumbe huyo wa chuma. Nilishutuka baada ya kukuta kuna watu wanapiga makofi baada ya kuniona ninammaliza kiumbe huyo wa umeme hapo ndipo nilijua nilikuwa kwenye majaribio. "Karibu sana Dokta Erick kwenye kambi yetu kuu ya BONDE LA MAUTI kitengo cha Rc2222.hapa ndipo mashine bora duniani zinabuniwa na wewe umearikwa ili ujifunze mengi toka kwenye chama chetu hiki." Hakika sikujua kama tayari nipo mahali hapa hatari tena kwenye kitovu chao kikuu. Baada ya kupokelewa kwa mapokezi hayo mazito niliongozwa na mwenyeji wangu yule mzee aliye nipa kilevi kipindi napnda Elikopita.Hakika watu hawa walionyesha jinsi walivyo na nguvu za kijeshi maana niliweza kuzishuhudia ndege za kisasa zaidi zikiudwa na nyingi ni za kivita . "Dokta karibu tena katika eneo letu hili na labda kwanza nikutembeze kwenye mazingira yetu kabla ya kukuonyesha mahali pako pa kusaidia kazi. Kwanza jua mahali ulipo ni sehemu salama kabisa yaani upo kwenye Anga la juu katika chombo chetu kipya kilichobuniwa na Mtu mweusi na hatari kuweza kutokea na mtu huyo ndiye aliyekuteua uwe hapa.Chombo chetu kinaitwa E13C.Kina uwezo mkubwa wa kubeba tani milion mbili za uzito.Kinauwezo wa kusafiri anga za juu zaidi yaani kinaweza kusafiri hadi katika sayari nyingine kwa mwendo kasi kuliko rocket zenye uwezo mkubwa.Kwa sasa hakuna mashine yenye spidi kama hii.Sehemu hii ndipo mahali penye injini za kukiongoza chombo hiki ijapo kuwa kina injini nyingine za dharura ambazo sitokuonyesha kwa leo.Chombo hiki hakitumii mafuta bali kinatumia nguvu za jua kuweza kuendeleza kazi zake na hakiwezi kuonekana na satilait maana chenyewe ni kama satlait.Hakika hii ndiyo teknologia mpya kabisa kwa sasa."Tulisoge katika eneo jingine katika eneo hili nilishuhudia magari ya kisasa kabisa aina ya hama na magari madogo ya kifahali kabisa yakiudwa."Eneo hili ni kiwanda cha magari ya kisasa tofauti na yanayotumika kwenu haya ni mashine na si magari maana ni malobot na yanaweza kujiendesha yenyewe na kushambulia kama yameelekezwa. Kwa hiyo jiandae kutengeneza kitu bora kuliko hivi ulivyo viona na huu ndiyo mwisho wa maelekezo yangu labda mahali unapotaka kufanyia kazi jichagulie eneo lako maana tunakujua vizuri hasa kwenye mambo haya ya mashine." Hakika sasa niliona nimekumbushwa masomo ambayo niliyasahau ambayo tangu nijifunze sikuyafanyia kazi na sasa niliona nafasi ya kutengeneza mashine mpya umefika ila sikujua nitaunda mashine gani kuzidi hizi zote ambazo nimekwisha ziona na sikuwa na mchoro wowote akilini....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog