Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

MAUAJI YA KASISI - 3

 







    Simulizi : Mauaji Ya Kasisi

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kamanda, najua hauko sawa sana, lakini nakuombea urudi salama, mambo yakiwa magumu basi nipe taarifa nije kukusaidia kwa lolote,” Gina aliongea sikioni mwa Amata wakiwa bado wamekumbatiana, kisha wakaachana na Kamanda akaelekea katika chumba cha wasafiri, huko haikumchukua muda, akaondoka zake na ndege ya shirika la ndege la Kenya na kurudi katika jiji la Nairobi, sasa akiwa binafsi zaidi, hakuna aliyejua kama yupo huko zaidi ya Gina, katibu muhtasi wake.

    Masaa machache yalimchukua hewani na baadae kuikanyaga tena ardhi ya Kenya, moja kwa moja alirudi palepale katika hoteli ya Intercontinental maana alijua wazi kuwa si pengine pa kuanzia kazi zaidi ya hapo. Ni masaa ishirini na nne na kidogo alikuwa mahali hapa, aliingia chumbani kwake na kukagua harakaharaka kwa macho, akaona jinsi chumba kilivyopekuliwa kitaalamu lakini zile alama ndogondogo alizoziweka alikuta haziko vile kutokana na upekuzi huo, alijaribu kuangalia kama kuna kitu chochote chenye hatari kwake, lakini hakukuwako, alipojiridhisha akaweka vitu vyake sawa na kuketi kitini akiwa tayari na bastola yake mkononi, alijuwa wazi kwa vyovyote lazima wapo wanaojua juu ya ujio wake hivyo kuna uwezekano wa kuja usiku huo, alizima taa na kuketi macho kodo katika kiti kilichopo kwenye moja ya kona ya chumba hicho.



    Kamanda Amata hakukosea, katikati ya usiku alihisi mlango ukifunguliwa, akajiweka sawa tayari bastola yake iliyofungwa kiwambo cha sauti ikiwa mkononi mwake. Taratibuuuuu mlango ukasukumiwa ndani, na huyo mtu akajaribu kuwasha taa ya ndani lakini haikuwakam akachezesha mara kadhaaa ile switch lakini bado taa haikuwaka. Akavuta hatua chache ndani na kuingia kisha akarudisha mlango nyuma yake, kabla hajafanya lolote alijikuta akimulikwa na mwanga mdogo mwekundu katika kifua chake, akachangayikiwa hajui la kufanya, mara taa ya mezani ikawaka kwa mwanga hafifu.

    “Tulia hivyo hivyo,” sauti ya Kamanda Amata alitua katika masikio ya mtu Yule, kama alikuwa hajawahi kukutana na mtu huyu sasa ilikuwa zamu yake, miguu ilimchezacheza, alitamani kukimbia lakini haikuwa hivyo.

    “WE nani?” Yule mtu aliuliza.

    “Kwani we umekuja kumfuata nani?” Amata alijibu kwa swali. Risasi ya kwanza ikavunja mguu wa mtu Yule kabla hajajiweka vizuri pale chini alipokuwa akiugulia kwa maumivu tayari Kamanda Amata alikuwa amemfikia na kumkanyaga kwenye jeraha hilo lililokuwa likivuja damu mbichi.

    “Jibu maswali yangu, nikuache hai,” Kamanda alianza namna hiyo, “Nani amekutuma?” akaanza namna hiyo.

    “Mimetumwa na boss kaka,”

    “Sawa, nitajie jina lake,”

    “Mi simjui kaka, simjui kabisa,” alijibu huku akilia kwa maumivu.

    “Sikiliza wewe bwege, ukilia utasumbua watu kwenye vyumba vingine, jibu maswali kwa ufasaha, sawa?!” Kamanda aliuliza kwa ukali huku bado akikandamiza lile jeraha la Yule mtu.

    “Basi kaka nasema, nasema, usiniumize nasema,” akameza mate, kisha akaendelea, “Tumetumwa na mtu mmoja anaitwa Wambugu”

    “Kawatuma nini?” lilikuwa swali lingine kutoka kwa Amata.

    “Begi na nyaraka nyingine za muhimu kama zipo,”

    “Ok, nay eye yuko wapi?”

    “Kuna kazi nyingine anafanya huko mjini,” alipojibu hayo mara simu yake ya mkononi ikaita kutoka katika mfuko wa jeans, Amata akainyakuwa na kusoma jina lililopo hapo juu ‘Moriyo’, “Moriyo ndo nani?” Amata aliuliza tena.

    “Ni mwenzangu yuko hapo chini ananisubiri, tumeambiwa tupeleke haraka hilo begi,” Kamanda Amata hakupenda kupoteza muda, alimuwekea ile bastola katika sikio lake la kuume, “Usiniue kaka, nina watoto mimi watalelewa na nani?” alilia kwa uchungu.

    “Ungekuwa na watoto unaowajali, ungefanya kazi za kishetani kama hizi, sikuui lakini lazima uwe mlemavu ili siku zote za maisha yako umkumbuke Kamanda Amata,” alipotamka jina hilo, akamuona Yule jamaa akishituka na kuguna kama aliyekutana na jinamizi.

    “Umesema we nani?” aliliza hata akawa amesahau kama ana jeraha baya la risasi katika goti lake, “Amata, Kamanda Amata, na siyo mzimu ni mimi mwenyewe halisi, namtaka huyo Wambugu na mwenzake Bill,” Yule jamaa bado aliduwaa akimkodolea macho Amata, “WE umeshakufa kaka,” Yule jamaa aliongea kwa unyonge.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ni sawa, na sasa nimefufuka kutoa wafu kama nilivyosema,” kabla hajaendelea na lolote, Kamanda Amata alimshuhudia Yule jamaa akitapatapa akirusha miguu huku na kule, alipomtazama vizuri, aligundua tundu la risasi kifuani mwake, risasi imepigwa wakati gani, kitendawili. Alichosikia yeye ni mvumo hafifu wa kitu kama nyigu kumbe tayari chuma hicho kilishatumwa kutoa uhai wa mtu. Amata alitazama huku na kule bado ukimya ulitawala, mara akasikia nyayo za mtu zikitembea harakaharaka kwenye korido, akatoka haraka na kuufungua mlango , akashuhudia mtu akiishia kwenye lifti ya jingo hilo, haraka akakimbia na kuziwahi ngazi za kushukia chini na kuteremka nazo. Kamanda Amata alfika chini na kushsudia Yule mtu akiwahi kuingia katika gari Fulani, lakini kabla hajaisjia garini, tayari shabaha isiyo na chembe ya uongo kutoka katika mikono makini ya Kamanda Amata, Tanzania Secret Agency ilikuwa imeshafumua ubongo wa kiumbe huyo na kumfanya alalie kiti cha dereva bila uhai huku miguu ake bado ikiwa nje ya gari hiyo, kazi imeanza. Hakumjali marehemu wa ndani wala nje, aliichukua ile simu aliyokuwa ameichukua kwa Yule jamaa wa kule ndani na kuifungua, haikuwa na namba hata moja, akenda kwenye meseji pale mwili ulimsisimka hata nywele alihisi zina simama baada ya kukutana na ujumbe uliondikwa,

    ‘Hakikisha kahaba Rose anauawa kabla ya jua la asubuhi, kisha nitakupa kazi ingine,’

    ‘Kahaba Rose,’ Kamanda Amata alilirudia jina hilo akilini mwake mara kwa mara, akiwa amesimama kwenye kiambaza cha ukuta aliendelea kusukuti juu ya kahaba huyo kamanahusika na lolote katika sakata hili, lakini muunganiko wa matukio haukuwa sawa kwake, alimfikiria Yule mwanamke aliyepewa kumstarehesha kama ndiye lakini haikuwa hivyo, nwuisho alimua la kuamua, kumsaka kahaba ni kazi ndogo sana, aliweka bastola yake mfukoni na kuiendea simu iliyokuwa jirani, ‘simu ya jamii’ akukwanyua mkono kutoka katika kikalio chake na kubofya namba yenye tarakimu tatu na kusikiliza upande wa pili.

    “Yes hallo tukusaidie nini?” ilikuwa ni sauti ya polisi wa kikenya, ambayo ilitaka kumfanya Amata kucheka lakini hakufanya hivyo.

    “Intercontinental hotel, kuna mauaji yametokea na pia kwenye maegesho ya gari ya hoteli iyo hiyo pia kuna mauaji mengine yametokea,” kisha akakta simu, halafu akacheka kutokana nay eye kuiga lafudhi ile ya kikenya. Alitoka eneo lile na kubana sehemu nyingine, muda kidogo alishuhudia gari mbili za polisi waliofika eneo hilo na kuivamia hoteli hiyo, alipoona hilo kwake limewezekana, akabaki na kazi yingine ngumu ya kumpata kahaba Rose na vipi awe ahusiki na hili, lilikuwa swali linguine, akasonya na kuingia mtaani akiacha hekaheka za wale askari zikiendelea.



    ˜˜˜

    Jua change la Nairobi lilianza kuikwea anga tulivu la jiji hilo, watu huku na huko walikuwa wakiwahi makazini, wengien kwenye matatu na wengine kwa miuu yao wenyewe, ilimradi tu ilionekana asubuhi tulivu.

    Lakini hali haikuwa hivo katika kanisa kuu la Familia takatifu, wakiwa bado hawajaondokewa na majonzi ya kifo cha Fr Gichuru, asubuhi hii wanaamka na kupotelewa na monstrance ambayo ililetwa kutoka Vaticna, maalumu kwa ajili ya maadhimisho ya jubilee ya miaka mia moja ya ukristu nchini hapo. ‘Kwa nini wameichukua?’ lilikuwa ni swaligumu kidogo kwa maana hakuna aliyejua lolote juu yachombo hicho zaidi ya yeye anayekitafuta.

    “Tutaieleza nini Vatican?” sauti ya masikitiko ilimtoka mhashamu askofu Njue iliyotoka kwa tabu kidogo kutokana na uzee uliokuwa ukipiga hodi kwa kasi ya ajabu iliwafikia makasisi wachache waliokuwa wameketi pamoja nae katika meza yake kubwa anayoitumia kwa mikutano na wasaidizi wake hao, wakiwa katika hali ya ukimya hakuna aliyekuwa na jibu sahihi juu ya swali hilo lililoulizwa na baba Askofu.

    Habari ya kuibiwa kwa Monstrance hiyo ilitapakaa kama upepo wa pwani, kila mtu alisema lile ambalo kwake lilikuwa ni sahihi. Mapigano ya polisi na majambazi usiku uliotangulia lilikuwa gumzo linginem kukutwa kwa mwili wa Cheetah katika ghetto ilikuwa ndiyo habari ya kuvutia zaidi kwani jmbazi hilo sugu limetingisha sehemu mbalimbali lakini hakuna watu walioweza kumtia mbaroni, kila mtu hakuna aliyejua, jambazi huyo amekufaje, wengine walionekana kufurahia kifo hicho lakini wengine walisikitika ‘kwa nini hawakumkamata hai’ basi ilimradi ni mazungumzo mchanganyiko. Hakuna aliyezungumzia mauaji ya kasisi ambayo ni wiki moja tu imepita bali kila mtu alikuwa anavytiwa na vifo vya majambazi hao wawili na kuibiwa kile chombo kitakatifu. Magazeti hayakuwa mbali kupamba kurasa za mbele kwa picha na habari moto moto.

    Ni sergeant Maria tu aliyesimama katika uwanja wa kanisa hilo akiwa hana furaha sana, akiwa na askari wawili wenye furaha, walionekana wakizungumza jambo Fulani na paroko wa kanisa hilo Fr Joh Smith, wakipeana maelekezo ya hapa na pale, wakitazama hiki na kile, baada ya mazungumzo marefu waliagana na kuahidi kurudi tena kwa uchunguzi wa kina.

    “Afande,” mmoja wale askari aliita, Sargeant Maria akageuka kumtazama kwa jicho lake kali, “Inaonekana hauna furaha, nini tatizo zaidi?”

    “Furaha yangu ingekuwa kubwa kama Cheetah, angepatikana na roho yake, lakini haikuwa hivyo, kwa desturi ya majambazi lazima wamegeukana katika malipo,” Sargeant Mari alijibu huku akijiingiza kwenye gari ake.

    “Itakuwa Mellina kamgeuka Cheetah, hilo linawezekana? Maana aliyebaki hai ni yeye tu na hapa amekimbia,” Yule askari aliongeza maswali, Sargeant Maria Litulia kwa muda kisha akainua uso wake na kumwangalia kija huyu, “Umenipa wazo jipya, Mellina anaweza asiwe aliyemuua Cheetah, uko sawa, sasa nani? Wambugu au Bill!! Kazi bado ngumu, twendeni kituoni,” aliamuru huku akiwa anatoa kalamu na kijitabu chake akaandika mambo Fulani Fulani humo.



    Sergeant Maria akiwa tayari akili yaje imekaa vyema alimuru vijana wake waanze msako kumsaka Mellina popote atakapopatikana na aletwe akiwa hai ili aeleze kisha chote kabisa na sababu ya wao kufanya hayo yote. Jeshi la polisi likajipanga kuhakikisha ile monstrance inapatikana na Mellina anatiwa nguvuni wakati huohuo idara kubwa za usalamaa zimejipanga kumtia nguvu Bill Van Vetgand, wakiwa hata hawana habari ya ujambazi huo wakiuona kwao ni matukio ya kipolisi ya kila siku, wakiwa hawajui kuwa kuna muungano mkubwa katika hayo yote mawili, wao walikaza jicho lao kwa jasusi Bill pekee, wakiwa wamemtega kila upande kwa kila mtindo lakini walishangaa Bill hakuonekana mjini kote, ametoweka. Hali hii iliwafanya kuchanganyikiwa zaidi, atatowekeaje wakati njia zote za kutokea nje ya Nairobi zimefungwa na wanausalama? Hii iliwapa moyo FBI na vyombo vinine kuwa mtu huyu hatari bado yupo Nairobi, hivyo waliongeza msako tuli, msako usiyo na fujo.



    Siku hiyo asubuhi, kikao kifupi cha maafisa wa polisi kilikuwa kikiendelea katika ofisi ya mkuu wa polisi mkoa wa kati, Inspekta Saitoti.

    “Sargeant Maria, nahitaji hizo tafutishi haraka, Mellina kama nilivyokuagiza, namhitaji hapa, hiyo Monstrance lazima ipatikane kwa udi na uvumba, pia nahitaji uchunguzi wa kina juu ya mauaji pale hotelini ili tujue kama vina uhusiano au la,” Saitoti alizungumza kwa ukali huku akiirekebisha kofis yake kichwani mwake.

    “Sawa afande, opereshen inaendelea na kikosi kipo kazini, ripoti itakuja jioni afande,” Maria alijibu kiaskari.

    “Nakuaminia sana, piga kazi,” alimalizia Saitoti.

    Sargeant Maria alitoka ofisini akionekana kusawajika uso wake kwa mawazo lukuki, akapita kaunta na kuzunguka nyuma ya kituo hicho ambapo kuna mgahawa mdogo na kuketi ndani yake, kisha akaagiza sturungi (Sturungi ni chai ya rangi) ili imchangamshe kidogo. Akiwa katika meza hiyo pamoja na maafande wengine, mara kijana mmoja mchafu sana aliingia kwenye mgahawa huo na kuketi mbele ya sergeant Maria, wakatazamana macho, maria akakunja sura yake kuonesha hakuridhika kwa kijana huyo kuketi hapo.

    “Afande, nna njaa, ninunulie japo chai kisha nitakutatulia tatizo lako linalokuumiza kichwa,” yule kijana akajieleza, Maria alimwangalia tena na tena.

    “Niambie kwanza!” Maria alidai lakini yule kijana akawa kimya akimtazama afande huyo wa kike aliyeshupaa kwa misuli kama mwanaume…





    Sergeant Maria akamuagizia chai Yule kijana na kumpatia, naye akaanza kunywa kwa fujo bila kujali kama chai hiyo ni ya moto, alionekana hasa ana njaa kali asubuhi hiyo. Maria alitazama saa yake na kuona tayari asubuhi imepamba moto anahitaji kwenda katika majukumu mengine.

    “Naona una haraka ya kuondoka, subiri kwanza,” Yule kijana akamueleza Maria, naye akavuta subira, akatulia kitini na kuanza kusoma gazeti la Daily Nation. Yule kijana alipomaliza kunywa ile chai akamshukuru sana sergeant Maria aliyekuwa ameketi mbele yake.

    “Afande, usione mi nimevaa hivi labda ukafikiri ni kichaa au mvuta bangi, hapana, nina akili na ni mzima kabisa, hii ni moja tu ya miondoko ya mji mkubwa kama huu” akameza mate na kuendelea na hab ari yake ambayo sergeant Maria aliona kama anapotezewa muda, “Najua unaona kama nakupotezea muda, lakini kazi unayoenda kuifanya mimi ndio nitakupa msaada mkubwa sana, sikia, hiyo kesi unayoifuatilia ya Mauaji ya kasisi ni kesi pan asana kuliko wewe na wenzako mnavyoichukulia, ninyi mnatazama mauaji ya Fr Gichuru, na kumsaka muuaji na monstrance iliyopotea, lakini hali sivyo ilivyo, kwa uwezo wenu nyie lazima mtaishia katikati kwani katika kesi hiyo kuna mkono wa kimataifa, mkono nambao pambano lake lazima liwe la kimataifa vilevile,” kabla hajaendelea, sergeant Maria alimkatisha, “Unasemaje wewe?” Yule kijana akarudia kumwambia yale yote aliyokwisha sema, “Mimi nilishuhudia Fr Gichuru alivyotekwa, alivyofungwa na kupewa mateso makali, lakini usiku huo akatoweka pale alipofungwa, nilikuwa mlinzi katika godown moja ambalo huyo marehemu alifungwa, na tulipata shida sana baada ya kutoweka kwake, na wale waliomteka waliapa kumuua pindi tu watakapomuona, na ndivyo ilivyokuwa”

    Sasa sergeant Maria alionekana kuvutiwa na simulizi hii tamu ambayo iliifanya damu yake kuchemka kikazi, “Nambie kwa nini unasema ya kimataifa?” akamuuliza.

    “Nasema ya kimataifa kwa kuwa kati ya watu waliomleta kulikuwa na bosi wao ambaye kwa mazungumzo yao ya harakaharaka anatoka nje ya nchi na ndiye aliyewatuma hawa majambazi na aliwaahidi pesa nyingi sana,” Yule kijana akaeleza. Sergeant Maria akavuta kumbukumbu na kukumbuka kuwa walipoikuta maiti ya Cheetah kulikuwa na burungutu la hela, hela nyingi kuliko unavyofikiria zikiwa zimetupwa juu ya mwili huo, akatikisa kichwa juu chini kuonesha kuwa ameliafiki hilo. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ok, hebu nambie, hao waliomleta au kumteka hasahasa walikuwa wanataka nini kwake?” Maria alitupa swali linguine.

    “Walikuwa wanadai awaoneshe monstrance, lakini yeye alikataa kata kata ndiyo maana walimtesa sana hata kuzimia mara nyingi kwa kipigo,” Yule kijana alijibu.

    “Na alitoweka vipi?” Maria aliuliza, huku akindiki vitu Fulani katika kijitabu chake.

    “Hapo ndipo utata unapojitokeza, maana asubuhi mimi na mwenzangu tulipoenda kumtazama hatukumkuta, lakini miongoni mwetu mlinzi mmoja pia hakuonekana mpaka baada ya siku mbili tulipogundua mwili wake katika pipa la takataka ukiwa hauna uhai, tukateswa sana tuseme ni wapi ametorokea mateka wao lakini hatukujua, ndipo name nilipotoroka na kujificha huko Korogocho, najua kuwa sakata hili halijaisha ipo siku hata mi nitakuwa mikononi mwa wanaharamu wale, najua wataniua kwani ninalijua hili, nikaapa kumtafuta Yule atakayekuwa ameishika kesi hii ndipo nilipojua ni wewe nikakutafuta,” Yule kijana alimaliza maelezo yake.

    “Sasa wewe unanisaidiaje katika hili?” sergeant Maria aliuliza.

    “Sina msaada afande zaidi ni kukuambia tu, usiumize kichwa, ukilifuatilia hili hakika utakufa, waache wakubwa wafanye yao,” Yule kijana sasa aliongea kwa msisitizo kidogo. Sergeant Maria alikuwa akimuangalia kwa kugeuzageuza kichwa chake kana kwamba haelewi analoambiwa, akainama chini kufikiri kitu Fulani alipoiunua kichwa chake kumtazama Yule mtu, hakumuona pale alipokaa, badala yake kiti kile kilikuwa kimekaliwa na askari mwingine wa kike, wakasaliamiana lakini Mria alionekana kuchanganyikiwa kwa hilo, “Afande, aliyekaa hapa yuko wapi?” aliuliza. “Mbona hapa hapakuwa na mtu afande!” lile jibu likazidi kumdidimiza katia shimo la mawazo, akanyanyuka haraka na kutoka nje ya mgahawa huo, akatazama huku na huku asione mtu, akazunguka upande wa pili hali hiyo hiyo, akajishika kiuno na kufikiria mara mbili kama alikuwa amekaa na mzimu au binadamu wa kweli. Lakini katia yote hayo bado hali ilikuwa ileile kuwa Yule mtu hayupo pale.



    ˜˜˜

    “Baby, mbona hivyo? Unaniumiza mwenzio, umenitafuta usiku wenye baridi kali nije nikuliwaze lakini tuko kitandani, mwenzangu huoneshi ushirikiano, mmm sweet nambie shida nini?” Kahaba Rose alikuwa akinung’unika kitandani alipokuwa amelala na Kamanda Amata usiku huo, baada ya Amata kumtafuta kahaba huyo kati viunga vyote vya mji wa Nairobi, ndipo alipoambiwa na mmoja wa makahaba katika mtaa wa Koinange kuwa Rose alipata ‘Big Deal’ hivyo ni siku kadhaa hayupo barabarani, lakini kwa msaada walimuelekeza wapi anaishia naye kamanda akamfungia safari mpaka nyumbani kwake na kumkuta, akamchukua na kumueleza shida yake kuwa anataka huduma yake usiku huo, kwa kuwa Rose alikuwa hana kaziingine usiku huo alikubaliana naye na kutoka mpaka kwenye hoteli moja isiyo na jina katika mitaa ya Mathare na kuchukua chumba hapo. Kamanda Amata hakutaka penzi la kahaba huyo bali alikuwa na yake moyoni, alimtazama Yule kahaba na kutingisha kichwa, alikuwa mwanamke mzuri wa sura, mtamu wa umbo, mwenye miguu minene ya kuridhisha, hips zilizojaa, macho ambayo yakikutazama utaona jinsi mwili wako unavyolegea mbele yake, hakika alikuwa mrembo.

    “Sikia mrembo,” Amata alinguruma, “Yes Baby,” Rose alijibu huku akijisogeza na kujilaza juu ya kifua cha Amata, “nimekutafuta sana leo siku ya saba, ulikuwa wapi? Maana sifa za urembo wako zimenifikia nikiwa Kongo,” uongo ukaanza kuchukua nafasi, Rose akatabasamu na vibonyo viwili vikajitokeza katika mashavu yake.

    “Nilipata kazi ya wiki mbili kwa tajiri mmoja wa kizungu, ana pesa kama matundu ya neti, lakini hatujamaliza kazi yetu, simuoni tangu juzi na simu zake hazipatikani, kwangu si shida maadamu kanilipa parefu,” Rose alieleza kwa sauti yake tamu ya kumtoa nyoka pangoni.

    “Hongera motto mzuri, huyo tajiri ni nani anayeiacha starehe tamu kama yako na kutokomea?” Kamanda Amata alitupa swali. “Aaaa si unajua tena wenye pesa wanafanya lolote, muda wowote wanapoamua, anaitwa Mr Bill, lakini tusiongelee habari za mwanaume mwingine, tuongee yetu,” Rose alijibu.

    “Sawa, lakini mimi nataka nimuone Bill, amenidhulumu pesa yangu, kuna kazi alinipa nimemfanyia kwa ukamilifu lakini hajanilipa,” Amata aliendelea.

    “We Bill unamjua?” Rose akauliza kwa mshangao na kujitoa katika kifua cha Kamanda Amata. Amata akatoa picha ndogo na kumuonesha, “Huyu siyo?” akamuuliza na kumpa ile picha.

    “Ni yeye,” Rose alijibu huku akimrudishia ile picha, “Pole sana nafikiri itakuwa mmedhulumiana na si kakudhulumu, mbona ni mtu poa sana huyu!” aliendelea. “Lazima awe poa kwako lakini si kwangu, Bill alikupa deal gani mrembo?” alijibu hoja ya Rose na kumuunganishia na swali.

    “Aaa, starehe za ngono na kazi binafsi za kukutana na watu wake anaowataka,” Rose akaanza kumpapasa Amata maeneo ya kitovuni mara akaanza kukinyonya kitovu hicho huku mkono wake mmoja ukiwa safarini kuelekea ndani ya boxer ya Kamanda, hali ikawa tete kidogo kwani macho ya Kamanda yalipotua katika kiunno cha binti huyo alikuwa katika mtindo wa kifudifudi na kulifanya shuka llililomsiti kuangukia upande wa pili, alishuhudia kiuno kicho kutangulia na makalio yenye kuvutia, mkono wake ulitamani kuyaminyaminya lakini akajikataza kwani bado alikuwa hajakamilisha analotaka kwanza.

    “Baby, nipe cha asubuhi,” Rose alilalamika huku akijiinua na kupiga magoti huku akiiweka kati ya mapaja yake miguu ya Amata, mokono wake ukiwa tayari umeshachoropoa ndungula ya Kamanda na kuiweka nje.

    “Rose, najua na nitakupa subiri kidogo.” Akamtoa pale alipo na kuliendea dirisha kisha akamuita Rose pale dirishani, “Tazama,” akamuambia, “Nini?” Rose akauliza, Kamanda Amata akamgeukia Kahaba Rose na kumtazama usoni, “Leo hii usingeyaona haya yote kwa maana ulitakiwa kuuawa kabla ya mawio,” Rose alishtuka kwa kauli hiyo, Kamanda akaendelea, “Nilikuja kwako nikuokoe kwa hilo na siyo mapenzi, rafiki yako Bill alitaka kutekeleza mauaji hayo kwa kutumia vijana wake,” alipomaliza kumwambia hilo akaichukua ile simu ya Yule marehemu na kumuonesha ile meseji, Rose akajitupa kitandani na kulia kwa uchungu.



    ˜˜˜

    Wambugu alijikuta anashindwa kuchanganyikiwa baada kujua kuwa viajana wake wameuawa kule hotelini, na Kahaba Rose hayupo nyumbani kwake, alibaki kajifungia ndani akiogopa hata kutoka nje, macho yake yote yakiwa kwenye TV na simu yake. Hakuna akili nyingine iliyokuwa kichwani mwake zaidi ya kutoroka nje ya nchi, lakini kila alipomuwaza Bill alijikuta anaishiwa nguvu na kurejea kitini, maji yamezidi unga!

    ‘Nitagundulika,’ alijiwazia. Lakini bado maswali mengi yalikuja juu ya nani aliyetekeleza mauaji ya vijana wake pale hotelini, hakupata jibu. ‘Bill kaniachia msala, kanitoroka,’ alijiwazia mara kwa mara, lakini hakupata muda wa kujijibu, mara mlango wake ukagongwa, akashtuka nusu ya kuanguka ijapokuwa alikuwa ameketi kitini, taratiibu akaufuata mlango na kuufungua kwa woga, ‘Polisi?!’ alijiwazia, alipoufungua akakutana uso kwa uso na mwanamke kibonge alijitumbukiza kwenye baibui jeusi lililoruhusu macho tu kuonekana, kabla hajamkaribisha Yule mwanamke akapitiliza ndani na kuubamiza mlango nyuma yake.

    “Unatetemeka nini mwanaume?” Yule mwanamke akauliza, Wambugu akabaki ameduwaa kwa sauti hiyo aliyoitambua vyema, “Nyie ni washenzi, wewe na Yule nguruwe wako, Bill,” ilikuwa ni sauti kavu ya Mellina ikimueleza hayo Wambugu ambaye alionekana hana la kufanya, Mellina akaendelea, “Ujio wangu hapa unapopaona wewe mafichoni, ni kuchukua pesa yangu, nataka kusepa leo hii, mji ushachafuka, njagu kila kona, haya fanya fasta”

    “Mbona pesa zako tulimpa Cheetah,” Wambugu akajibu.

    “Cheetah!? Msinifanye mi mjinga, Bill kamuua Cheetah na nimeiona hiyo action kwa macho yangu kwa taarifa yako, sasa sema napata pesa sipati? Mi sina muda wa kupoteza,” Mellina alifoka.

    “Pesa nakupa Mellina, lakini naomba jambo moja,” Wambugu akatulia kidogo, kisha akendelea, “Mimi hapa nilikuwa nataka kutoroka na kiukweli Bill alishasema wewe uuawe, ila sioni umaana wa hilo, tufanye mpango tutoroke pamoja, unasemaje?” Mellina alitulia kimya kwa sekunde kadhaa, kisha akanyanyua uso wake kumtazama Wambugu, “Sikuamini hata kidogo,” Mellina alimwambia Wambugu, akatulia kidogo na kuendelea, “Nipe pesa kwanza mengine tutaongea.” Wambugu akavuta begi lake na kuingiza mkono ndani yake, alipoutoa akaibuka na donge nono la pesa, mellina akatabasamu alipokuwa anapokea pesa yake, akaitia ndani ya baibui lake na kugeuka kuondoka, “Kila mtu afe na dhambi zake,” alitamka maneno hayo akiwa ameshika kitasa tayari kutoka nje, mara nyuma yake akasikia mlio hafifu wa kilinda usalama cha bastola, kabla hajageuka, chuma baridi kikamgusa kisogoni, “Ha ha ha ha ha, huwezi kutoka hapa ukiwa hai, never” sauti ya Wambugu ilisikika nyuma yake …



    Mellina alisimama ghafla, akameza funda la mate lililokuwa kinywani mwake, hakugeuka haraka kwa kuwa hakujua adui yake sasa amejiandaa vipi.

    “Kwa hiyo ndio hila zako sio?” Mellina akamuuliza Wambugu huku bado akiwa anaangalia mbele.

    “Nilishapewa kazi na Bill nikumalize ili kuondoa ushahidi wowote usio na tija,” Wambugu alijibu kijeuri.

    “Kwa hiyo katika orodha uliyopewa, umeshaua wangapi?” Mellina aliuliza, alitumia mbinu ya kuongea ikiwa ni moja ya kumzubaisha Wambugu kabla hajapanga ni nini cha kufanya katika hali kama hiyo amabayo kwayo hakuna masikhara kwani maisha yako yapo kwa adui yako.



    “Bill alishamaliza kazi yake, na alishapata kile anachokitaka, hivyo basi ninyi mlioshiriki ambao mnaweza mkatoa siri hii lazima msiwepo katika uso wa dunia, Gichui amekwenda, Cheetah hayupo, umebaki wewe na Kahaba Rose ambaye muda si mrefu roho yake itakuwa mikononi mwangu,” Wambugu aliongea kwa pozi, wakati Mellina alikuwa akifikiri juu ya shambulizi linalofuata, shambulizi la ghafla ambalo akili yake ilikuwa ikiushawishi mwili nini cha kufanya ambacho madhara yake yatakuwa kwa adui.

    “Na katika hao wanaojua hiyo siri, wanaotakiwa kuuawa, unafikiri wewe haumo?” Mellina alimwambia Wambugu kauli ambayo ilimfanya kustuka kidogo, na kukumbuka kuwa kumbe hata yeye mwenyewe yupo kati ya wanaojua, akiwa katika kiutafakari hayo mara Mellina aligeuka kwa ghafla na mkono wake wa kulia ukakamata korodani za Wambugu.



    “Aaaaaaaaiiiiggghhhh!!!!!” yowe la uchungu likamtoka Wambugu na kuitoa ile bastola kichwani mwa Mellina. Sasa Mellina na Wambugu walikuwa wakitazamana, sura ya Mellina iliyogeuka kutoka katika uzuri wa kike na kuwa ya kikatili kama mnyama ilikuwa imekaza macho kwa Wambugu aliyekuwa akilia kwa maumivu.\

    “Sikia wewe mwanaume mjinga, Bill anataka kukuua na wewe vilevile, sasa kabla hajakuua yeye mimi naanza,” Mellina aliunguruma huku akizidi kuziminya korodani za Wambugu na kuzizungusha, maumivu makali yalikuwa yakimpata Wambugu kabla hajatulia, Mellina alimpiga kichwa kimoja cha nguvu na kumuachia Wambugu alipepesuka na kudondoke kwenye kijimeza kidogo kilichokuwa ndani ya chumba hicho hukun ile bastola ikiwa chini sakafuni, Mellina akaiokota, kulichukua lile koba lenye fedha na kuanza kuondoka.



    “Mellinaaaaaa!” Wambugu alipiga kelele hasa alipoona Mellina amenyanyua koba la fedha, Mellina aligeuka na ile bastola mkononi, “Kelele wewe kubwa jinga,” alimtuliza kwa mtindo huo huku akifyatua risasi kadhaa pembeni kabisa mwa pale alipoangukia Wambugu na kuchimba sakafu na ukuta kuacha mashimo, akatoa sonyo refu na kumuacha Wambugu hoi katota kwa mkojo.

    Mellina akaubamiza mlango nyuma yake na kukamata tax iliyokuwa ikipita hapo muda huo na kutokomea zake. Huku nyuma Wambugu alipopata akili alinyanyuka haraka na kukimbilia mlangoni hakuna alichoshuhudia zaidi ya vumbi jekundu lililobakisha hapo na ile gari, Wambugu alilikimbiza kwa miguu lakini hakufanikiwa alianguka chini na kuanza kulia akijigalagaza kama motto na mwili wote kuwa mwekundu kwa lile vumbi.



    “Bingo!” Mellina alijikuta akitamka neon hilo alipokuwa katika siti ya nyuma ya ile tax baada ya kupekuwa na kukuta maburungutu kadhaa ya pesa, “Wapi dada?” ilikuwa sauti ya dereva tax ikimuuliza Mellina, ndipo Mellina alipokumbuka kuwa yupo kwenye tax, “Nipeleke Nakuru,” Mellina alijibu. Yule dreva tax alikuwa kama kichaa vile, akakanyaga mafuta na kuchukua barabara ya kuelekea Nakuru,”



    §§§§§



    Madam S alikuwa amesimama karibu na dirisha la ofisi yake, dirisha kubwa lililokuwa likikupa mandhari nzuri ya bahari ya Hindi, alitazama upande huo wa bahari, alipotosheka akageuka na kurudi kitini kwake pale ambapo aliwaacha wageni wake wameketi.

    “Ndio Madam, unaonekana mtu mwenye mawazo sana,” mmoja wao alianzisha mazungumzo.



    “Yeah na ndilo swala hasa ambalo nimekuitieni hapa,” Madam S alijibu, akainua bilauri yake yenye maji na kunywa kisha akaitua mezani, “Kamanda Amata ametoweka hospitalini na haijulikani wapi alipo, mkiwa kama wanaintelijensia nataka mnipe maelezo ya kina labda nini mnakihisi kimetokea, maana leo ni karibu siku ya tatu, na hatuna maelezo yakutosha, hapa ninavyokuambieni mzee katuma fax na inabidi ifanyiwe kazi haraka. Nyote mnajua umuhimu wa Amata, kichwa chake kimejaa siri asilimia 99 za serikali, hivyo haiwezekani apotee tu namna hii,” Madam S alianza kuzungumza akionekana wazi kuwa swala hilo limemuumiza kichwa kuliko maelezo. Aliwatazama wale vijana wanne waliokuwa mbele yake waliotulia kama vinyago vya mmakonde maana hawakuwa wakitisika wala kupepesa macho.

    “Madam, Kamanda ni mtu wa kisasi sana asiyekubali kushindwa, je hatokuwa amerudi Nairobi kumsaka mbaya wake?” mmoja wao aliuliza. Madam S alionekana akiandika vitu Fulani kati kijidaftari chake cha kumbukumbu, kisha akainua uso na kumwangalia yule aliyeuliza, “Yote yanawezekana, tumetoa taarifa ofisi husika ya usalama pale Nairobi, nao wanajaribu kumwangalia kama yupo huko lakini bado hawajatupa jibu, ila sijui kwa maana hata yule msichana wake hakuna anachojua juu ya hili na hii si kawaida.” Alijibu Madam S.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ukicheki namba zake za siri kwenye mtandao vipi hazionekani?” mwingine aliuliza.

    “Namba zake nazo hazioneshi chochote, maana nimempa hiyo kazi Chiba lakini mpaka sasa anasema hamuoni kwa namba zake, akijaribu juelekeo wa simu anasema pia hazisomi kwa maana simu zake zote zilizimwa juzi pale airport na ndio signal ya mwisho inasoma hapo,” Madam S alishusha pumzi ndefu na kujiweka sawa kitini, “Dah, Kamanda!’ alijiwazia huku akifikicha jicho lake.

    “Kwa hiyo Madam unasemaje?” yule watatu aliuliza

    “Nataka mfanye kila njia mumtafute na hakikisheni mmempata kisha mniambie yuko wapi,” Madam S alimjibu, akawapa kazi ya kumsaka Amata kwa kuwa yeye hatakiwi kupotea mbele ya macho ya wakubwa wake kutokana na kazi na cheo alichonacho.



    Siku tatu nyuma…



    TAARIFA za kushushwa cheo kwa Kamanda Amata hazikumfurahisha hata kidogo, baada ya Madam S kutoka pale hospitali, Amata alitafakari sana na kuumia moyoni, alijikuta anamchukia kila mtu. Alipogundua kuwa wauguai wote wametoka na yuko peke yake katika kile chumba akatoka kitandani na kutorokea upande wa nyuma ambako alipitia katika dirisha kubwa la alluminium. Akachukua tax na moja kwa moja alielekea nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni.



    Akiwa nyumbani kwake alijua wazi kuwa lazima atatafutwa kwa mtindo wowote ule, alijaribu kuangalia kila kitu ambacho kingemfanya ajulikane alipo, simu, saa ya mkononi, headphone set na kila kitu, kitu kimoja alitaka kukisahau ‘micro chip’ ya kielektroniki ambayo alipandikizwa katika kwapa lake la kushoto ambayo inawasiliana na satellite moja kwa moja hivyo kutoka ofisi ya mawasiliano ya kitengo chao wanaweza kumuona muda wote kwa namba maalum ambazo zinamtambulisha. Kamanda Amata alijua wazi kuwa hiyo chip sasa ndiyo inayomweza kumuharibia, akaona isiwe tabu, alijaribu kuminyaminya katika kwapa lake na kugundua wapi ipo kutokana na umbo lake la mcheduara lenye ukubwa kama punje ya mchele, akavuta mtoto wa meza na kutoa kisu kidogo pamoja na forceps, akiwa anajiangalia katika kioo kikubwa kilicho mbele yake alinynyua mkono na kujichana pale alipohisi chip ile imewekwa, hakukosea, kwa kutumia ile forceps akakibana sawia na kukichomoa, damu zilimwagika lakini alidhibiti hali hiyo kwa shashi iliyokuwa hapo ndani kwake na kutia dawa kidogo aina ya Iodini au wengi tunaaita dawa ya joto, aliichukua ile chip na kuitia moto ikateketea kabisa, kisha akajipanga kwa safari. Gina alimfuata na kumpeleka uwanja wa ndege ambako alichukua ndege na kurudi Nairobi kwa kificho bila mtu kujua. Aliapa kumtia mkononi kila aliye jirani na Bill mpaka ampate Bill ili kazi yake aiache kwa heshima na si kwa dharau. Ndipo aliporudi Nairobi kwa hasira ya kumsaka Bill na vibaraka wake.



    Nairobi



    GARI aina ya Vogue iliegeshwa nje ya kanisa la Familia takatifu, kijana mmoja aliyevalia nadhifu, suti nyeusi iliyotanguliwa na kaba shingo la rangi ya cream aliteremka na kuufunga mlango wa gari hiyo kwa madaha, kisha akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa miwani myeusi akaipachika usoni mwake, naam, ushababi wake ulijitokeza waziwazi, akazunguka upande wa pili na kufungua mlango. Mwanamke mwenye umbo la wastani, lililojaa vizuri, anayevutia ukimwangali kuanzia kifuani mbala chini ya kiuno mashaalah taarabu ipo ya kuvutia, akiwa ndani ya suti ya kike ya kijivu, na uso wake ameuficha kwa miwani safi ya rangi ya udongo. Haikuwa rahisi kugundua kuwa huyu ni Kahaba Rose ambaye akiwa pale mtaa wa Koinange huvalia kijisketi kifupi kilichobana na chepesi ambacho huuacha mwili wake sehemu kubwa wazi. Alishikana mkono na kijana huyo kisha wakavuka geti mpaka kwenye kibanda cha mlinzi na kuomba kuonana na Paroko kama yupo, baada ya itifaki zote kufanyika ikiwa kutazamwa kama wana silaha yoyote kukamilika waliruhusiwa.



    Kati ya viti sita ni vitatu vilikaliwa, upande huu Kahaba Rose na Kamanda Amata na upande mwingine ni Fr Joe Smith, babu.

    “Karibuni sana, mumekuja kuandikisha ndoa?” alianza kuuliza yule kasisi.

    “Hapana, tumekuja kwa maswala ya kikazi, tunahitaji kuongea machache juu ya tukio zima la Fr Gichuru,” Amata alitonesha kidonda cha kasisi huyo mzee raia wa Marekani.

    “Mimi nimechoka na kuulizwa maswali kila wakati na wala sioni maendelea yake, mara Kenya Polisi, mara FBI, Mara MOSSAD, mara sijui nini, ah, nihurumieni jamani, kama kazi imeshindikana basi acheni mbona Gichuru amekwishakufa hawezi kufufuka hapa duniani tena, haya niambie na wewe unatoka wapi?” Fr Joe alilalama na mwisho kuomba utambulisho.



    “Naitwa Kamanda Amata, kutoka Tanzania.” Akampa na kitambulisho kidogo cha plastiki, yule kasisi mzee alionekana kama kupigwa na shock baada ya kusikia kuwa aliye mbele yake ni Kamnda Amata, mara nyingi alimsikia mtu huyu tu na kusoma baadhi ya visa vyake ambavyo vingine vimeandikwa kama riwaya, hakuawahi kufikiri kama bonadamu huyu yupo kweli au ni hadithi tu, sasa mbele ya macho yake anakutana na kiumbe huyu, alimkazia macho kana kwamba sijui kakutana na Malaika Gabrieli.



    “Wewe ni Kamanda Amata?” aliuliza huku akimnyoshea kidole na kumrudishia kile kitambulisho chake.

    “Ndiyo ni mimi,” Amata alijibu huku akikiweka kitambulisho chake katika mfuko wake maalumu ndani ya koti lake.

    “Kamanda Amata karibu sana,” alimkaribisha.

    “Asante sana nafurahi kukutana na wewe, sasa kilichonileta hapa ni juu ya mauaji ya kasisi, Fr Gichuru. Ningependa kujua juu yake kwa kifupi ili nijue wapi pa kuanzia,” Amata alianzisha mazungumzo ya kikazi. Fr Joe Smith, alimueleza Amata kila kitu kuanzi asafari yake ya Roma kwenda kuchukua ile monstrance mpaka aliporudi, na mazingira ambayo kifo chake kilitokea, akamueleza pia juu ya kupotea kwa Gichuru kwa takribani masaa 24 na yote yaliyotukia. Kamanda Amata alitulia kitini akisikiliza kwa makini huku akiandika vitu Fulani katika kijitabu chake kidogo.

    “Umesema majambazi hao wamechukua Monstrance, unafikiri kuna nini katika chombo hicho?” Amata aliuliza.

    “Kwa kweli sijui labda kwa sababu ya malighafi iliyotengenezewa, kwa maana ile monstrance imetengenezwa kwa dhahabu tupu na ni ya gharama sana pia ni ya kihistoria sana katika kanisa,” Fr Joe alieleza.



    “Baada ya mauaji ya Kasisi, umesema siku chache baadae mlivamiwa na majambazi ambao sasa ndio walikuja kuichukua hiyo Monstrance, siku ya tukio wewe ulikuwepo?”

    “Nilikuwepo, nilijificha huku juu ghorofani, niliangalia mapambano malali sana ya polisi na majambazi, lakini mwisho wa yote ile gari ya majambazi iligonga mti hapo nje na gari nyingine ikaja na kuchuku lile begi kisha wakaondoka, sasa hapo sijaelewa nini kimefanyika,” alijibu kwa ufasaha.

    “umesema siku ya mauaji mtawa wa kike Rose alishuhudia na pia umesema siku ya kuibwa hiyo monstrance mtawa huyohuyo alishuhudia, je huoni kuwa kuna uhusiano kati ya matuklio haya? Nikimaanisha kuwa Rose anahusika moja kwa moja, na yeye anaweza kutufungua masikio katika hili,” Amata alimshtua kidogo Fr Joe na kumuacha akiwa na bumbuwazi, aliporudiwa na fahamu alijibu.

    “Hapana, ni bahati tu labda niseme, mtawa Rose yeye anahudumu huko kanisani ndiyo maana haya yote yamemkuta huko, lakini kuhusika yeye sina uhakika na hilo,” Fr Joe alijibu kwa upole.



    “Naweza kumuona Sr Rose?” Kamanda Amata aliuliza, na bila kuchelewa alivuta simu yake na kupiga kwa masista, akongea maneno machache na kukata simu ile.

    “Kamanda Amata, tunahitaji kupata hii Monstrance, Vatican haitatuelewa kabisa, mimi naumia sana,” Fr Joe aliongea huku akitoa machozi.

    “Usijali father, itapatikana tu endapo mtanipa ushirikiano wa karibu,” Kamanda Amata alipokuwa akisema hayo mara mlango ukafunguliwa na mtawa Rose aliingia ndani ya ofisi ile na kuwakuwa watu hao wawili pamoja na Fr Joe, akakribishwa kiti na kuketi upande ule wa Fr Joe, akatulia na kutazamana na Amata.

    “Ahusiki tangu machoni pake,” Kamanda Amata alitamka hayo, kawa kuwa alitazamana macho na mtawa yule na kuyasoma kitaalamu na kugundua kuwa hana hatia, kwani mwenye hatia usomeka tangun machoni na katika pua zake.



    “Pole sana Sr Rose kwa mikasa iliyokukumba, tupo hapa katika kuona ni jinsi gani ambayo itatusaidia ili kupatikana kwa ile monstrance, nikuulize swali moja ulipopelekwa polisi kwa mahojiano ulihojiwa na askari gani, unaweza kumjua kwa jina?” Kamanda Amata aliuliza kitu ambacho hakuna kati yao aliwaza.

    “Anaitwa Sargean Maria,” Rose alijibu.

    “Ok, asante, nilitaka kujua hilo tu, sasa kuanzia sasa hutakiwi kumueleza mtu yoyote habari hii isipokuwa mimi tu kama nikihitaji,” Amata alisistiza, “Fr Joe, mimi nimekuja kufanya kazi hii kwa siri sana , hakuna anyejua uwepo wangu hapa Nairobi, naomba usimueleze mtu yoyote juu ya uwepo wangu hapa kwako na Nairobi kwa ujumla, mimi nitawasiliana na wewe kwa jinsi ninayoijua mimi tu, sawa father?”



    “Sawa, usijali Kamanda,” Fr Joe alijibu.

    “lakini kabla sijaondoka, naweza kutembelea chumba cha marehemu? Nahitaji kujua kama naweza kupata chochote cha kunisaidia katika kazi yangu,” Amata aliomba, Fr Joe akamchukua na kumpeleka katika chumba hicho kidogo chenye kitanda cha futi tatu na nusu, kilikuwa chumba cha kimasikini hasa, meza moja ya mbao ilibeba vitabu vichache na kitabu kimoja cha kumbukumbu, ukutani palikuwa na kanzu zilizoning’inizwa, bila shaka zilikuwa za marehemu, Kamanda Amata akavuta hatua fupi mpaka pale mezani na kunyanyua kile kijitabu cha kumbukumbu, akafungua kurasa moja baada ya nyingine, kijitabu hicho kikamvutia sana, akamtazama Fr Joe akaona yuko mbali kimawazo, akakitia katika mfuko wa ndani wa koti lake, kisha wakarudi mpaka pale ofisini na kauagana, akamchukua Kahaba Rose na kuondoka akiahidi kurudi tena muda wowote.



    Dakika chache baadae kahaba Rose na Kamanda Amata walikuwa tayari barabarani kuelekea mjini, mbele kidogo baada ya kuvuka eneo la St Paul kuelekea Westland hakuna aliyekuwa akiongea na mwenzake katika gari, Kamanda Amata alipinda kushoto na kuingiza gari katika maegesho ya supermarket ya Nakumatt.



    “Nawataka watu wawili kwanza,” alimueleza kahaba Rose

    “Nani na nani na wa nini?” Rose aliuliza

    “Mellina na Wambugu, hawa watanipa ramani nzuri ya wapi alipo Bill,”

    “Utawapata wapi? Kwa vyovyote kila mmoja yuko mafichoni mwake saa hii,” Rose alieleza

    “Mimi najua pa kuwapata na wewe unajua jinsi ya kuwapata,” Kamanda aliongea kwa kujiamini kama ilivyo kawaida yake, “Ok mpango utakuwa hivi, wewe utarudi nyumbani kwako, kwa kuwa wale jamaa wanakutafuta wakuue mimi nitakuwa pale ili niwashughulikie na wanipe ramani ya wapi Bill alipo.”

    Kahaba Rose hakuwa na la kupinga hoja hiyo alitikisa kichwa juu chini kuashiria kuwa ameelewa vyema mpango mkakati huo jinsi ulivyo. Rose aliinua mkono wake wenye saa na kuitazama.

    “Vipi, Saa ngapi?” Amata aliuliza.

    “Saa nane kasoro,” Rose alijibu huku akishusha mkono wake.

    “Ok, twende tupate chakula cha mchana kisha tuanze shughuli yetu,” kamanda alieleza huku akifungua mlango wa gari kushuka nje, naye Rose akafanya vivyo hivyo. Kati ya viti vingi vilivyo mbele yao wawili hawa walichagua viwili vilivyowafaa na kuketi kabla hawajaagiza juice wakati wakisubiri chakula cha mchana.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamanda Amata alijitahidi kutupa jicho huku na kule kuchunguza lolote ambalo linaweza kumsaidia katika sakata lake hilo lakini hakuna kitu, ila mara kadhaa alitabasamu kwa kumuona kijana mmoja teja jinsi alivyokuwa akirandaranda kwa mwendo wa madaha katika maeneo huyo bila kuchoka kuomba pesa ndogondogo kwa wateja wa eneo hilo, ilikuwa kero kwa kiasi Fulani kwa waliopo eneo hilo kila askari walipokuwa wakimtoa yeye alirudi kwa njia nyingine.

    “Vipi mbona unamshangaa huyo teja?” Rose aliuliza

    “Ah huwa napenda wanavyotembea,” Amata alijibu.

    “Kweli hauna kazi.” Rose alimkebehi Amata

    “Hata hii ya kumwangalia ni kazi pia,” Amata alijibu huku akitoa tabasamu lake la nadra mbele za watu. Wakiwa katika mazungumzo na Kahaba Rose mara Yule teja akaja mpaka pale katika meza waliyoketi Amata na Rose, huku udenda ukimtoka. Rose alijaribu kumfukuza na kuita askari wa ulinzi, lakini Kamanda Amata alizuia Yule kijana asiondolewe pale.



    “Muacheni, ni mgeni wangu huyu, mpeni juice tafadhali na biskuti kadhaa,” Kamanda Amata aliamuru na amri ikatekelezwa haraka. Kamanda Amata alitazamana uso kwa uso na kijana Yule ‘teja’ macho yao yaligongana na kuangaliana kwa kina, Yule kijana alikuwa akipepesa macho kwa mtindo wa ajabu sana, harakaharaka, akaifumba na kufumbua kwa mitindo tofauti, akigeuzageuza mboni zake kwa hali ya kupendeza, naye Amata alikuwa akimfanyia vivyo hivyo kwa kupeana muda, pembeni Rose alikuwa akifa kwa kucheke alipokuwa akiangalia wawili hao walipokuwa katika huo mchezo wa ajabu, mchezo wa macho. Baada ya kumaliza juice yake Yule kijana alinyanyuka akatoa ishara ya kuishukuru, Amata akampa shilingi mia ya Kenya na kumruhusu aende.

    “Mh, duniani kuna mambo” Rose alisema, Amata akageuka kumtazama Rose, “Kwa nini wasema hivo?” Amata aliuliza.

    “Si kama hivi, kijana Yule madawa yamemuharibu kabisa, ona sasa hata wazazi wake wamepata hasara ya kulea,” Rose alilalama.



    “Usiseme hivo, hawa ni watu wa kuwapenda tu, katika kupenda usibague maana leo kesho hujui ni katika mazingira gani utahitaji msaada wa nani.” Kamanda alimueleza Rose kwa upole.

    “Ok, sasa amekaa hapa anachekacheka tu na ndio mlikuwa mnafanya nini na macho?” Rose aliuliza.

    “Aaah hawa huwa hawapendi kuongea wao ni kuchekacheka tu kama ulivyoona na kuchezesha macho vile ni jambo wanalolipenda sana,” Amata alieleza. Alitupa jicho nje ya wigo wa supermarket ile na kumuona Yule teja akipotelea mitaani.



    §§§§§



    “Vipi afande mbona una mawazo mengi sana?” afande Otholong’ong’o alimtupia swali Sargeant Maria aliyekuwa amesawajika uso kwa mawazo na macho yake yakiwa yametopea kwa uchovu, aliinua uso na kumwangalia askari huyu kijana ambaye katika mapambano yao na majambazi aliumizwa mguu kwa risasi, sasa alikuwa amerudi nyumbani baada ya matibabu kukamilika. Alikuwa nyumbani kwake maeneo ya Kasarani kwa mapumziko akiuguza jeraha lake.



    “Nimepambana na kazi nyingi za upelelezi lakini hii inanitoa jasho afande,” Marina alieleza, “Kwa nini? Mbona kama imeisha maana wale wawili wamekufa bado huyo Mellina, na kumpata sio tabu, unafikiri atakuwa amekimbia?” Otho aliuliza.

    “Kukimbia sidhani., lakini hata hivyo pia anweza kuwa hayuko nchini, hali akijua kuwa swahiba zake wameuawa,” Marina alieleza.

    “Kazi ndogo afande, anzisha msako wa kwenye mabasi yote ya abiria, treni na hata ndege ili kumbaini kama bado yupo ao kakimbia, sambaza na picha zake kwenye maeneo husika,” Otho aliongea, huku akijaribu kuinuka pale kitini.



    “Otho! Ni point ambayo sikuwaza kichwani yangu, umenipa wazo, sasa lazima nimtie mkononi,” Maria alieleza lakini sauti kavu ya Otho ilimpa tena swali ambalo lilimrudisha Maria katika lindi la mawazo, “Na baada ya kumpata Mellina, nini kitafuata? Na hicho chombo kilichoibwa kanisani tutyakipataje?” lilikuwa swali gumu lililoulizwa na Otho. Maria alitulia kimya huku akichezea simu yake, akikosa jibu la moja kwa moja la kumpa Otho aliyeonekana akilisubiri kwa hamu sana, “Tumpate kwanza Mellina, yeye ndiye atatupatia picha nzima ya nini kilitokea na nani anahusika katika hilo, kishapo tutajua hicho chombo kipo wapi na jinsi ya kukipata, lakini Otho, kesi hii ina mambo ya ajabu mengi sana” Maria alimsimulia Otho juu ya Yule kichaa na maneno tata aliyomueleza na pia jinsi alivyomtoweka kimiujiza. Otho alimsikiliza bosi wake mpaka alipomalizia mkasa huo.



    “Ila majamazi sio watu aisee, kinachonichanganya wakati wa mapambano yetu, kuna gari nyingine ilikuja na kumchukua cheetah na hilo begi kisha wakaondoka zao, kwa akili ya haraka haraka inaonekana hapa kuna makundi mawili katika mchezo mmoja,” Maria aliongea kwa nhisia kali,

    “Kama ni hivyo bado shughuli ni pevu, apatikane Mellina kwanza kisha yeye atatupa mpango mzima kwa kibano cha nguvu,” Otho aliongezea.



    Mazungumzo kati yao yaliendelea yakilenga kazi na mambo mengi kwa ujumla. Walipokamilisha mazungumzo yao ndipo Maria aliporudi kazini na kutekeleza yale aliyoyaongea na Otho ya jinsi ya kumnasa Mellina, mchana uohuo shughuli hiyo mpya ilianza kwa kasi katika kila chombo cha usafiriu kinachotoka ndani ya Nairobi. Sergeant Maria alikuwa akisubiri kwa hamu aambiwe tu kuwa wapi Mellina kaonekana ili akamchukue na afunge kabrasha hilo la ‘Mauaji ya Kasisi’, lakini bado ilikuwa haijazaa matunda mpaka muda huo.





    Kamanda Amata aliegesha gari yake mbele ya nyumba ya kahaba Rose, na kukubaliana nae kuonana jioni ya siku hiyo ili kupeana raha kama kawaida yao, kazi na dawa. Rose alimwangalia sana Amata wakati alipokuwa tayari nje ya gari hiyo akainua mkono na kumpungia ishara ya kwa heri naye Amata alijibu kwa mtindo huohuo kisha akatia moto gari na kuondoka eneo hilo kurudi katika hoteli aliyofikia.



    Mara moja aliingia na kuoga harakaharaka kisha akabadilisha nguo lakini leo alitoka tofauti kidogo si kama tulivyomzoea, fulana moja nzuri ilitulia mwilini mwake iliyobeba maandishi madogomadogo katika upande wa kushoto wa kifua chake yaliyosomeka ‘lacoste’, na chini akiwa na jeans nyeusi ya bei mbaya na kiatu cha mtindo ule ule wa lacoste. Alipohakikisha kuwa sasa yuko tayari katika miondoko hiyo ya ujana, alijitokeza hadharani na kujichanganya mjini huku gari yake akiwa kaiacha palepale maegeshoni. Alipita mtaa wa kwanza na kuvuka ule wa pili, aliendelea kutembea kwa mguu mpaka mahali hasa alipopataka, kimvua cha rasharasha kilikuwa kikiendelea katika jiji la Nairobi, Kamanda Amata aliendelea kutembea kwa harakaharaka na kupita hapa na pale mpaka mahali hasa alipopatakam akachukua tax na kuondoka haraka, dakika kadhaa mbele alikuwa katika lango la kuingia sehemu ambayo waamini wa madhehebu ya Kikatoliki huja mara nyingi kufanya sala na tafakari eneo hilo, bustani ya ufufuko, ilijulikana kwa jina hilo.



    Akaingia langoni na kusimama kidogo kisha akafnya ishara ya msalaba na kuingia hatua tatu mbele akasimama tena, mara mtu mwingine akaungana naye palepale aliposimama, Kamanda Amata hakuonekana kumtilia maanani mtu huyo, aliyevalia suti nyeusi mwenye uso ulikunjanakunjana kama mtu aliyewahi kumwagikiwa na tindikali. Walisimama sambamba wote wakikaza macho kutazama mbele kila mmoja akiwa na rozali yake mkononi.



    “Kamanda Amata,” Yule mtu aliita kwa sauti ya kunong’ona bila kumwangalia Amata.

    “Unasomeka,” Amata alijibu

    “Umekuja kufanya nini huku ilhali maisha yako yapo hatarini?” Yule mtu akauliza

    “Hatari ndiyo chai ya asubuhi kwangu na kifo ni chakula cha jioni, achilia mbali mlo wa mchana ambao ni maumivu na mateso makali, nimezoea,” Amata alijibu.

    “Wewe ni jeuri, jibu swali langu, umekuja kufanya nini? Watakuua mara hii, wapo wengi pande tofauti,” Yule mtu alisema tena kwa mtindo uleule.

    “Mtu kama mimi siogopi kufa wala simuogopi muuaji, nipe ripoti kama inastahili,” Amata alijibu.



    “Usijali, mawingu ni mengi, yote yanakuzunguka, dhambi zako ni Mungu tu anayezijua na si mwingine awaye yote, unatakiwa kutubu kabla ya kifo chako leo hii,” Yule mtu akakohoa kidogo kisha akaendelea, “Usichelewe, dakika kumi zijazo hakikisha upo katika kitubio ndani ya kikanisa kile pale mbele yako,” Yule mtu alipomaliza kusema hayo akainamisha kichwa na kutoka nje. Kamanda Amata alisimama kwa sekunde kadhaa akitafakari yote, kisha akazunguka hapa na pale na kupotelea nje, alipofika upande wa pili wa bustani hiyo aliona kile kikanisa kikiwa wazi na watu wakiingia na kutoka, akatazama saa yake ilikuwa tayari dakika kumi zimefika. Akavuta hatua na kupanda ngazi mpaka ndani akageuka huku na huku na kukiona kile kisanduku maalumu cha kufanyia maungamo akakijongelea na kufungua pazia lake kisha akajitoma ndani na kupiga magoti akitazama katika kile kidirisha kikuukuu kinachomtengenisha muumini na kasisi, sauti kavu ikatokea upande wa pili, haikuwa sauti ngeni bali ni ileile aliyoisikia kule bustanini.



    “Nilijua utarudi Nairobi, na nimefurahi kukuona, ujio wako niliutambua mara moja tu kwa mauaji ya wale jamaa wawili pale Plazza Hotel katika chumba chako cha mwanzo,” ile sauti ilimwambia Amata, bumbuwazi lilichukua nafasi katika uso wa Kamanda Amata, alijiuliza ni vipi amekwishagundulika uwepo wake katika jiji hilo, alikaa kimya kidogo kisha akafungua kinywa chake, “ Wewe ni nani?” aliuliza.

    “Unataka kunijua mimi?” ileh sauti iliuliza

    “Ndiyo,” Amata alijibu.

    “Mimi ndiye niliyekuokoa katika mikono ya Bill pale Safari Park casino,” akajibiwa.

    ‘Safari Park casino,’ Amata alijiwazia sana juu ya sehemu hiyo, alijaribu kuvuta kumbukumbu ya siku ile lakini hakujua ni nani alimuokoa na kivipi, akili yake ilirandaranda huku na huko kuoanisha matukio lakini hajkupata jibu la uhakika katika hilo.

    “Hakuna kitu kama hicho, hakuna aliyeniokoa katika lile, jioneshe sura yako tafadhali,” Kamanda Amata alizungumza kwa kusita kisha akamuamuru mtu huyo kujionesha wazi na si kuendelea na ngonjera zake hizo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Utaniona tu. Amata ulikuwa umelala kwa sumu ulopewa na Bill, ulipochukuliwa na gari hukujitambua ndipo mimi nilipokufuatilia kwa nyuma mpaka eneo amb alo nilitumia kukuokoa, nikakuleta mpaka hospitalini kwa matibabu, Bill alitaka kukuua na hata sasa nafikiri anaamini hivo,” ile sauti iliendelea. Kamanda Amata kwa maneno yale alituliza moyo kidogo akajua kuwa kumbe anayeongea naye alikuwa ni mmoja kati ya wale walio upande wake, Amata hakujua kabisa nini kilitokea nyuma baada ya pale Safari Park, alitikisa kichwa kama mtu aliyeingiwa na sisimizi sikioni, “Sasa Bill yuko wapi?” Amata akauliza.

    “Hilo swali gumu sana, maana Bill si mtu wa kuonekana hovyo na sijui yuko wapi,” ile sauti iliendelea.



    “Nimekuja kwa kazi binafsi, nahitaji kichwa cha Bill nikakipambe nyumbani kwangu,” Amata aliongea kwa hasira sana.

    “Punguza hasira, mtumie yuleyule Malaya uliyekuwa naye pale atakuonesha Bill, Yule anajua kila kitu asikudanganye kwa lolote, Yule ni mwanamke wa Bill, na kitendo cha wewe kuiwa naye ujue Bill anakusoma kila hatua ufanyayo kupitia Yule mwanamke,” ile saiuti ilikuwa kama inayomgutusha Amata usingizini, akajiuliza mara kadhaa juu ya ujinga aliyoufanya kwa kuongea mengi na Rose kumbe alikuwa akipelelezwa, mwe, kweli muwinda huwindwa. Hasira zikakamata moyo wa Amata, “Unasema kweli?” aliiuliza ile sauti ya mtu asiyemjua.



    “Nikikudanganya itanisaidia nini mimi? Ujue kuwa muda wowote watakuua maana wameshakujua vilivyo kupitia Yule mwanamke Malaya. Sasa nenda kambane yuleyule, yeye ndiye atakupa kila kitu juu ya Bill mpaka alipojificha atakwambia,” Ile sauti ilizidi kusisitiza, Amata alibaki hajielewi kwa analolisikia, “Hakikisha saa tatu kamili usiku wa leo tunakutana pale KICC kwenye mgahawa wa juu kabisa Nairobi super café, kwa heri.” Ile sauti ikaaga. Amata akajinyanyua, na kutoka kwenye kile kiboksi ndipo alipogundua kuwa ni giza limeshaingia, harakaharaka akatpoka nje na kuelekea barabarani, tax ya kwanza aliidaka na kujitupia siti ya nyuma, akampa maelekezo dereva, tayari Kamanda Amata damu ilikuwa inachemka, anamuwahi Rose ili amchukue na huko atakakokwenda naye basi akambane vyema ili amueleze siri yote ya Bill.



    Dakika thelathini, ile tax ilikuwa imeegeshwa mbele ya nyumba ya Rose, lakini kabla hawajaifikia nyumba ile aliona gari ndogo ya kijivu ikitoka katika egesho la nyumba hiyo na kuondoka kwa kasi, Kamanda Amata aliitazama ile gari lakini hakuitilia maanani ijapokuwa wasiwasi ulimuingia. Alimlipa dereva tax na kumuacha aende zake, aliliendea geti la nyumba ya Rose na kulisukuma lilikuwa wazi, akapita moja kwa moja mpaka mlango wa kuingia katika sebule, aligonga kengele lakini hakukuwa na majibu, aligonga tena kwa tena lakini wapi, kengele za hatari zikalia kichwani mwake, akaichomoa bastola yake na kuiweka tayari kisha kwa mkono wake wa kushoto akanyonga kitaza kilichoiuachia mlango wazi.



    Kwa hatua za taratibu Kamanda Amata alisoge mpaka katika korido ya kuelekea vyumbani, aliitazama sebule ile iliyoonekana wazi kuwa kulikuwa na vurugu Fulani iliyotokea muda si mrefu, akaendelea kufungua mlango mmoja baada ya mwingine, akakifikia chumba cha Rose, kabla hata hajaingia ndani alikaribishwa na michirizi ya damu iliyokuwa imetoka chumbani humo na kuelekea mahali Fulani, aliitaza lakini hakujuwa wapi ilitoka na wapi ilielekea, moja kwa moja akaenda zake mpaka stoo ambako alikuta damu nyingi zimetapakaa, akajua kwa vyovyote kila kitu kipo chumbani, akawahi chumbani, alipofungua mlango tu aliakaribishwa na damu nyingi, damu bichi ambayo ndio kwanza bado ilikuwa ikizidi kumwagila kutoka katika kiwilikiwili kilicholazwa hapo kitandani, Kamanda amata aliirudisha bastola yake kiunoni na kukisogelea kile kiwilikiwili pale kitandani, akatema mate chini baada ya kujisikia kichefuchefu cha ghafla. Kitanda kilibeba mwili usio na kichwa, Amata akautazama ule mwili na kusikitika sana, akajikuta akitokwa na machozi, akavuta hatua kuondoka lakini akasimama mlangoni, ‘Je kama si mwili wa Rose!’ alijiuliza, akarudi kuukagua mwili huo, akaufunua taratibu nguo katika eneo la paja Rose alijichora tattoo ya nnge, kweli ni yeye, alijiridhisha na kuondoka eneo lile haraka kabla watu wa usalama hawajamkuta.



    Kamanda Amata aliingia hotelini mwake na kujifungia chumbani akitafakari, kichwa chake kilichanganywa kwa mawazo hakujua ni nini kinatokea, alimkumbuka Yule mtu kule kanisani aliyemwambia kuwa Rose anajua kila kitu juu ya Bill, kwa nini amwambie, na yeye anafika kwa Rose anakuta ameuawa, alijaribu kuunganisha picha lakini hakupata jibu, sasa aliona wazi kazi inakuwa ngumu, kama alijuwa kuwa kwa Rose ndiko atapata jibu basi haikuwa hivyo, utata, utata wenye utata.

    Dakika ishirini na tano zilimpita Amata akiwa kasimama mbele ya kioo kikubwa akijiangalia lakini hakujiona, akiwa amegubikwa na mawazo, hasira na chuki kwa mtu asiyemjua, aliona wazi kuwa mtu huyo amekwamisha harakati zake zote.



    KICC – NAIROBI



    MEZA MOJA iliyokuwa mbele ya kijana mtanashati, Melchior Ndege, ilibeba bia aina ya tusker na vitafunwa kadhaa. Kijana huyu aliyekuwa akinywa bia yake taratibu kana kwamba hana haraka katika hilo alionekana akipepesa macho yake huku na kule kuona kama Yule anayemsubiri amefika au la. Pembeni kukiwa na wateja wengine lakini yeye halikumfanya kujali hali hiyo, aliendelea taratibu kubarizi kwa macho akina dada warembo wanaojipitisha mbele yake, wakizani kuwa labda wangeitwa lakini wapi, hakukuwa na muito wala mruzi. Muda ulizidi kwenda, Ndege hakumuona mgeni wake, akili ikaanza kumzunguka, nini kimetokea maana muda wa ahadi yao ulishapita kwa dakika arobaini na tano na zaidi.



    §§§§§



    Mwanamke mmoja wa makamo kidogo aliteremka kwenye tax hatua chache kutoka katika jingo la mikutano la Kenyatta (KICC), alipokwishamlipa dereva tax alivuta hatua chache kulielekea jingo hilo, akaingia ndani na kutazama huku na kule, usalama ulikuwepo, akaiendea lifti na kubofya kitufe Fulani, dakika moja baadae mlango ule wa alluminium ulifunguka na Yule mwanamama kujitoma ndani, kidole chake cha kati kilichobeba pete kubwa ya haja, kikabonyeza namba 5 na 0 yaani 50, ile lifti ikamnyanyua na kumfikisha ghorofa ya juu kabisa, akashuka na kuiendea kaunta.

    “Tusker tafadhali,” aliitisha tusker ambayo ilikuja maramoja na kuanza kuimiminia tumboni mwake, huku akiangalia kwa makini Yule mwenyeji wake asiyemjua. Hapa na pale alianza kumuhisi kijana mmoja aliyeketi pembeni kabisa katika meza ya peke yake, akashuka na kuielekea ile meza huku akimuambia mhudumu amletee bia yake pale.



    “Naweza kujiunga nawe? Maana naona u mpweke sana,” Yule mwanamama alimueleza Ndege. Melchior alimtazama Yule mwanamama kwa makini, macho yake yalipanda na kushuka mpaka kifuani ambako hakuona matiti ya asili isipokuwa ya kuchonga, akacheka na kutikisa kichwa, “Kamanda Amata, salute kwako. Jinsin ulivyojiweka sikukutambua kabisa, hakika hakuna anyeweza kukutega kwa ubaya maana unajua jinsi ya kukwepana na kifo,” Ndege alimueleza Kamanda Amata ambaye alijitupia ndani ya vazi maridadi la kike na kuonekana wazi kuwa ni mwanamke, akiwa ameondoa ndevu zote kidevuni mwake, vipodozi na mekap alizojipaka zilimfanya aonekane mmoja kati ya wanamama mashangigi wa kutoka Mombasa.



    “Wewe ni nani?” Amata aliuliza sasa kwa sauti yake ya kawaida, huku mkono wake wa kulia ukiwa ndani ya pochi ambayo ililazwa mezani. Melchior Ndege alielewa ishara hiyo alijua wazi kuwa Kamanda Amata ndani ya pochi hilo amekamata bastola tayari kwa lolote, alimtazama macho yake na kuyaona hayana masihara hata kidogo.

    “Melchior Ndege, idara ya usalama wa taifa Kenya,” Ndege alijibu.

    “Umenifahamia wapi?” Amata aliuliza

    “Kamanda, tulikutana Arusha kwenye kozi ya kiintelijensia pamoja na watu wa Cuba na USA” Ndege alijieleza.

    “Sasa naanza kukumbuka, kijana wa Bwana Shikuku, siyo?”

    “Hapo umenena,”

    “Inaonekana umekuwa ukinifuatilia sana, kwa nini?” Amata aliuliza.

    “Hapana, sikufuatilii, ila nilikuona mara moja katika hali ambayo nilijua wazi upo katika hatari, tangu hapo nikaanza kukulinda kuhakikisha hushuriki na nilijua wazi kuwa umekuja kwa ajili ya Bill Van Getgand,” Ndege alipoeleza hayo, Amata alikunja sura kidogo kwa mshangao.



    “Wapi?” Amata akauliza.

    “Ujio wako kamnda ulijulikana tangu ukiwa JNIA pale Dar es salaam, watu wa Bill ambao walitapakaa kila kona iliyotia wasiwasi walikuona na kutoa taarifa huku kwa Bill, mpaka unatua JKIA hapa Nairobi walikuwa wamekuweka kwenye target yao, hawakupenda kukumaliza ila walitaka wajue hasa kuna nini ulichokifuata, watu wangu niliowatega pale uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta walinipa taarifa kuwa watu wa Bill wapo pale na inaonekana kuna mtu wanamsubiri, bahati mbaya hawakufahamu wewe. Hivyo nilifika na kuwafuata kwa nyuma, nilitazama ratiba ya ndege kujua ndege ile ilikuwa ikitoka wapi, nikaambiwa ni kutoka Dar es salaam, hisia zikaanza kunicheza juu yako. Ulipoingia hotelini pale Plazza wale jamaa walibaki nje wakisubiri labda kukuvamia au sijui kufanya nini, mimi niliondoka kwa kuwa niliitwa ofisini ambako nilipewa taarifa iliyonikosesha raha kabisa.” Ndege alitulia na kupiga funda moja la bia.



    “Taarifa gani?” kamanda aliuliza

    “Niliambiwa na Bwana Shikuku kuwa FBI wamesema sisi tuachane na Bill, wao ndio watakaofanya kazi ya kumnasa, nilihuzunika sana, nikaamua kuondoka zangu kwenda kutafuta sehemu ya kutuliza mawazo kwa muda, ndipo nilipopita pale Safari Park Hotel, na kukuona wewe pamoja na wale jamaa wane na mwanamke mmoja, kwa jinsi walivyojipanga tu nilielewa umetekwa, nikabadili mawazo nikaingia hotelini humo mpaka casino walipokupeleka na kufuatilia kila kitu. Pole sana Kamanda, Bill alidhamiria kukuua, hakukupa sumu kwenye pombe kwa maana nyote mlikunywa chupa moja, bali sumu ilikuwa kenye vipodozi vya Yule mwanamke aliyekupa akustareheshe, vuta kumbukumbu Kamanda, nilikuwa nafuatilia kila kitu, kila hatua na kila kipengele. ”

    Kamanda Amata alitulia kwa muda, akavuta kumbukumbu ya tukio hilo akakukumbuka kitu,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ilivyokuwa…



    Muziki laini ulikuwa ukipigwa katika casino ile, watu walikuwa wakiendelea kucheza kamali na michezo mbalimbali inayofanana na hiyo. Alipepesa macho na kushuhudia tu dhambi mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika jumba hilo. Kamanda Amata hakuwa na linguine alijivuta taratibu kuelekea kaunta, hakuweza kutoka nje wala kufanya nini, kwa maana Bill alimuwekea ulinzi wa nguvu, Amata alijuwa wazi kuwa yupo mtegoni. Mara Yule mwanamke aliyemfuata chumbani akaja kwake na kumkumbatia,

    “Mmm Sweetie, fanya haraka tukalale, Bill amesema nikakuburudishe usiku wa leo,” Yule mwanamke alimueleza Amata ambaye hakuonekana kuwa na hari ile iliyozoeleka, kichwa chake kilikuwa kimevurugika kikitafuta njia ya kujinasua. Alimkumbati Yule mwanamke kwa mkono mmoja na kumvutia mlango wa kutokea nje,

    “Tunywe kidogo hubby” Yule mwanamke aliendelea kumbembabemba Amata, akaingiza mfukoni mwake mkono na kutoka na pafyumu iliyoandikwa ‘Sunset’ kwenye kopo lake.



    “Nini hiyo?” Amata aliuliza.

    “Pafyumu, beibi, inanukia vizuri sana, check” baada ya Yule mwanamke kumueleza hayo aliifyatua ile pafyumu na kumpulizia usoni kiasi. Kisha akajipulizia kwapani huku nakule na kuirudisha pochini, akatoka na Amata na kuelekekea kwenye gari huku nyuma akifuatiwa na mtu mwingine. Wakaingia garini na kuondoka, Kamanda Amata alishangaa badala ya kuelekea hotelini ile gari ilikuwa ikichukua barabara ya kuelekea Embu, akawauliza wakamwambia kuna mzigo wanafuata kisha watarudi, mara akaona nguvu zinamuishia, mwili unachokia, macho yanakuwa mazito, kila alipojaribu kupambana na hali ile alishindwa kabisa, aliwaona wale jamaa kama madudu ya kutisha mbele yake, mpaka alipokutana na usingizi mzito wa kutokujitambua kabisa…



    Rejea KICC …



    “Niliwafuatilia kwa gari niliyoiba pale hotelini kwa mwendo mrefu mpaka nilipoona panafaa ndipo nikasababisha ajali ya makusudi na kukuokoa, lakini nilikukuta ukiwa na hali mbaya, povu zito likikutoka puani na mdomoni, nikakuwahisha klatika hospitali yetu pale Nairobi, kwa matibabu, ndipo bwana Shikuku akamtafuata boss wako Madam S na kumpa taarifa. Ofisi yako ilikodi ndege hapa Nairobi na kukuchukua mpaka Dar es salaam,” Ndge alitulia akimtazama Amata, kisha akafungua kinywa chake na kumwambia, “Ni mimi nilikutana nawe pale Nakumatt, Westland kama mbwia unga, ni mimi tulikutana pale kwenye bustani ya ufufuko ndani chumba cha kitubio, najua unamsaka Bill lakini Bill ametoweka, hayupo Nairobi na hajulikani alipo, ila Rose anajua kila kitu.”



    “Ndege, Rose ameuawa kikatili,” Amata alimwambia kwa kifupi. Ndege alishtuka sana kwa habari hiyo, “Unasema Rose ameuawa? Lini na wapi?” aliuliza.

    “Rose ameuawa nyumbani kwake, jioni hii, baada ya kukutana na wewe pale kwenye bustani ya ufufuko na kuniambia nikamuulize Rose kuwa anajua habari za Bill nikakuta kauawa kwa kukatwa kichwa ndani ya nyumba yake mwenyewe. Sikumkuta aliyemuua lakini nishuhudia gari iliyotoka hapo nje kwa kasi ilikuwa ya rangi ya kijivu, sikuweza kuisoma namba, lakini pia sikuona haja ya kuifuata,”



    “Dah! Rose, hivi nilikuwa nasubiri upate habari toka kwake kisha tuone tunafanya nini, bwana Shikuku amenambia nifanya kazi hii kwa siri sana.” Ndege aliongea kwa masikitiko.

    “Ok! Kuna watu wawili, Wambugu na Mellina, nawahitaji sana, kutoka kwao nitajua wapi pa kuanzia, lakini kifo cha Rose kimenikwamisha kwa mengi sana, watu wengi wanajua mi ni Malaya sana lakini svyo, kutoka kwa wanawake ndio mara nyingi tunapata habari za wahalifu tunaowafuata lakini pia tunaweza kuwakamata kwa urahisi wahalifu kwa kuwatumia wanawake hawa, Masikini Rose, lazima niilipe damu yake kwa damu.” Amata aliongea kwa masikitiko.

    “Usijali kaka, nilikujengea mazingira bila kujua, twende kwa Rose sasa hivi, mengine tutaongea mbele,” Ndege alimwambia Amata.

    “Ok, sawa, sikia Ndege, nimekuja hapa mimi binafsi, najua ofisi inanitafuta lakini usimwambie mtu kama niko hapa hata bosi wako usimwambie.” Amata alimsihi Ndege,

    “Dah! Samahani sana kaka, nilishamwambia Shikuku kama upo hapa,”

    Kamanda Amata alimtazama Ndege kwa jicho bay asana, “Tuyaache, hukuwa unajua, ila usimwambie mtu mwingine, na leo hii lazima tuonane na Shikuku tulidhibiti hilo haraka,” Kamanda Amata aliufungua mlango wa gari na kuketi upande wa kushoto, Ndge akaukalia usukani na kuondoka zao.



    “Imekuwaje ukavaa kama mwanamke leo?” Ndege aliuliza

    “Na we ilikuwaje ukajifanya teja au kasisi?” Amata nae aliuliza

    “Ah ah ah ah!!! Trust no one kaka,” Ndege alijibu.

    “Umeona ee? Muwinda huwindwa!”.



    Kwanza kabisa walifika hotelini mwa Kamanda Amata, kamanda akabadilisha nguo na kuingia ndani ya suti kama kawaida yake kisha wote wawili wakionekana vijana nadhifu wakarudi kwenye gari yao na Ndege akatulia nyuma ya usukani wakaendelea na safari.

    “Wewe unamtaka Bill? Lakini kuna kesi nyingine hapa inaungana nay a Bill. Kiasi kwamba lazima na hiyo uifanyie kazi ili upate picha kamili,” ndege alimwambia Kamanda.

    “Yeah, ya mauaji ya kasisi?” Kamanda aliuliza kupata uhakika.

    “Ndiyo hiyo, kwa sababu inaonekana Bill anahusika kwa namna moja au nyingine,”

    “Nimeshaanza kuifatilia ila nataka nimfahamu mtu anayeitwa sergeant Maria kwa kuwa yeye nasikia ndio kashika hiyo kesi,” Kamanda alimuelezea Ndege.



    “Usijali, kumpata Maria si kazi ngumu,” Ndege akajibu huku akiizungusha gari kwenye mzunguko wa Dagoreti corner, mtaa wa kwanza, wa pili, nyumba ya tano, Ndege alipita kama hataki kusimama mahali hapo na mbele alikunja kona na kuegesha gari karibu na duka noja kubwa la bidhaa mbalimbali, wakateremka, kwanza Ndege akaingia dukani na kununua jojo mbili wakagawana na kutembea taratibu wakiielekea nyumba ya Rose, walipofika mlangoni wakashangaa mlango uko wazi, Ndege akachomoa bastola yake na Kamanda akafanya vivyo hivyo, kisha kwa mwendo wa kunyata wakapita na kuingia ndani, chumba kwa chumba huyu upande huu na huyu upande ule, wakafika chumba cha maraehemu, kamanda alipotupa jicho kitandani hakuna ule mwili, akatazama huku na kule baadae kidogo Ndege akaungana nae, wote wakabaki hawana la kusema, mwili umeenda wapi hakuna jibu.



    “Ndege, nilinde tafadhali,” kamanda Amata alimwambia Ndege na kuirudisha bastola yake kiunoni mwake kisha akakijongea kitanda kile alichokuwa amelazwa marehemu, akatazama kwa makini ni mashuka yaleyale tu, alipokuwa anatoka, akaona kikaratasi kidogo chini karibu na kitanda, akakiokota, namba ya simu, akakitia mfukoni, mara wakasikia mlango ukifunguliwa na watu wakibishana, Kamanda na Ndege, wakajificha.

    “Mi nina uhakika ni humu humu maana pale si uliinama!” sauti moja ilimwambia mwingine

    “Hapa mi sina uhakika unajua,” ingine iliijibu ile ya kwanza

    “Tutakuwa tumecheza blanda kweli yaani, sasa tajiri tutampataje? Maana kasema yeye tumpate kwa simu na ye atatulipa kwa simu, hataki tuonane kwa sura.” Ile sauti ya kwanza ilisema.

    “Dah huu utata sasa, any way ngoja tuone, fasta basi wasije kutukuta,”



    Wale watu wakaingia ndani na kuelekea chumba kile kilichokuwa na ule mwili, wakapekua hapa na pale hawakuona kitu, kasha wakarudi mpaka chooni ambako walianzia kazia ile. Kamanda Amata aliyekuwa katika ficho lake akapata wazo haraka, akatoa peni yake na kijikaratasi kingine kasha akaandika namba yake ya simu anayotumia pale Kenya akachana katika mtindo uleule na kukitupa chini kwenye korido kasha akajificha tena.

    “Ah, we, hiki huku,” mmoja wa wale jamaa akakiona na kuikiokota kasha wote wakatoka nje na kuchukua gari yao wakatokome. Ndege na Kamanda wakatoka mafichoni mwao, “Dah, Kamanda kwa nini ulinizuia nisiwashambulie wale jamaa? Tungepata majibu ya maswali yetu,” Ndege alimlaumu Amata.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana, tunayemtaka sana ni Bill, na Bill mtu mwingine anayejua siri yake kama si Mellina basi ni Wambugu, unajua walikuwa wanatafuta nini?” Kamanda aliuliza

    “Sikuwaelewa,” Ndege alijibu. Kamanda Amata akatoa kijikaratasi na kumuonesha, namba ya simu.



    “Sasa mbona walisema wamekipata? Sielewi hapo!” Ndege alibaki njia panda.

    “Sikia ndege, ukisikia TSA namba 1, ndio mimi, nacheza na akli yako nakutangulia sekunde kadhaa mbele ndiyo maana ya Intelijensia, mi niliokota hii karatasi kabla yao, baadae nikaandika nyingine nikaweka namba zangu ndiyo ile walioiokota wao,” Kamanda Amata akamueleza Ndege.

    “Dah! We mkali kaka, sasa inakuwaje?” Ndege aliuliza

    “Tutafute sehemu tukae tusubiri watatupigia kasha tunawanasa na watatuambia tajiri wao yuko wapi,” Amata alijibu.

    “Lakini tufanye kitu Fulani, twende kwenye shirika la simu hii, tukaombe information zote za namba hii, miito iliyofanya kwa sauti na ujumbe ili tumtafute mtu huyu yuko wapi nan i nani,” Ndege alitoa ushauri, Amata akatikisa kichwa nan a kumpigapiga mgongoni kuashiria kuwa wazo zuri alilotoa.



    Wakatoka ndani ya nyumba ile na kuzunguka kule walikoacha gari yao, kwa haraka sana Kamanda Amata aliona ile gari yao haina upepo tairi moja, walipoikabia Kamanda Amata akamshika mkono Ndege na kupita naye wakaiacha ile gari yao pale na kuchukua tax kisha wakaondoka, wakamwambia dreva akawaache barabara ya Waiyaki maeneo ya Westland, wakamlipa nao wakaongoza kuelekea pale makao makuu ya kampuni ya simu ya Kenyatta Telecom, wakafika na kujitambulisha kasha wakapata kuonana na mhusika, mtu wa ICT, baada ya kujitambulisha na kusema shida yao, Yule kijana akafanya kazi hiyo kwa haraka na kuwakabidhi CD moja yenye kila kitu.

    “Hii ni MP3 ina audio, data na sms zote,” aliwaeleza. Kamanda Amata na Ndege walitazamana na kumshukuru wakimuachia shilingi za Kenya 5000 wakaondoka zao.



    Ndani ya ofisi ya Ndege pale katika jengo la KICC, kamanda Amata na Ndege walikuwa wawili tu ofisini humo wakiwa wameiweka CD ile katika chombo maalum na kuchambua simu zote zilizotoka na kuingia, meseji zote walisoma mpaka wakachoka, lakini hawakukata tamaa, simu a mapenzi ziliwafanya wacheke sana, meseji za nguoni zilizowaacha midomo wazi, wakiwa wamekata tama kabisa kuona kwamba katika namba ile hakuna wanachokiitaji, ndipo walipoona simu moja iliyowashtua, sauti ya mtu mwenye lafudhi ya kizungu, wakajua kwa vyovyote ataku Bill, walisikiliza ujumbe ule mpaka mwisho wakatazamana, haukua mbaya wala haukuwa mzuri, bali ulimtaka mwenye namba ile ajifiche na asionekane nje kwa usalama wake kwani kwa kufanya hivyo atahatarisha maisha yake. Waliinakili ile namba waliyoiona kwenye vitabu vya kumbukumbu vya kila mmoja kisha wakaamua kuondoka zao. Wakiwa njiani simu ya Amata ikaita na kawaida simu hiyo ilikuwa ikipigwa na Rose tu, akainyanyua akitabasamu, akabadilisha sauti na kuongea Kiswahili cha Kenya.



    “Sasa mkubwa, kazi imekamilika,” sauti ya upande wa pili ikasema.

    “Oh vizuri sana sana sana, sasa kwa kazi mliyofanya, nimeona pia tuonane niwapongeze kidogo, kama mpo radhi tuonane mahali pa utulivu,” Kamanda Amata alisema. Kimya kidogo kikatawala kati yao, “Sawa Boss, tukuone wapi?” ile sauti ikauliza.

    “Tuonane Dagoreti Corner the super pub saa mbili kamili usiku.”

    “Sawa boss,” ile sauti ilijibu. Ndegeakamtazama Kamanda Amata wakati akikata ile simu.

    “Bingo!” Ndege akatamka, akainua mkono na kutazama saa yake, saa kumi na mbili jioni.



    §§§§§



    Basi la Eldoreti, lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea kampala Uganda lilifika eneo la Kisumu, askari wa usalama barabarani katika kituo cha ukaguzi usiku huo wakalisimamisha. Mlango ukafunguliwa na mmoja wao akaingia na kuwatazama abiria, wengine walilala na wengine walikuwa wakiangalia filamu ya Kinigeria iliyokuwa ikiendelea ndani ya basi hilo.

    “Haya wote weka vipande yenu juu, tunataka kagua,” askari Yule aliyetangulia aliwaambia abiri, waliolala wakaamka na kila mmoja akatoa kitambulisho chake na kunyoosha juu, ukaguzi ukaanza.



    Karibu kabisa na mlango pale mbele alikuwapo mwanamke aliyevaa baibui jeusi na kuruhusu macho tu kuonekana. Askari aliyekuwa aikagua, akaichukua passport yake, Jamila Babiker, ilikuwa ni jina lililondikwa juu ya hati ile, Yule askari aliitazama kwa makini na kuigeuzageuza, akamtazama na Yule mwanamke kwa vizuri, kasha akashuka na ile hati mpaka kwenye ofisi yao ndogo iliyopo hapo, aikiwa na mwenzake waliendelea kuikagua na walipoona hawaridhiki katika hilo, wakamshusha Yule mwanamke na kumleta katika kile kiofisi.

    “Mamaa, hii hati yako mbona inatutia wasiwasi?” askari mmoja aliuliza

    “Kwa nini wasema hivo na kila siku natumia hiyo hiyo?” alijibu Yule mwanamke.

    “Ok, una uhakika na hilo? Sema ukweli kama ni feki tuelewane hapahapa tukuache uende,” askari mwingine alidakia.



    Wazo hilo likamfanya Yule mwanamke ababaike kujibu. “Hapana hiyo ni halali kabisa, ni hati yangu ninayotumia kila niendako. Yule askari akavuta simu yake na kupiga simu mahali Fulani, baada ya muda kidogo akatuka zile namba za ile hati ambayo alikuwa nayo pale mkononi mwake. Baada ya muda kidogo ile simu iliita tena na Yule askari akainyanyua, Yule mwanamke akajua sasa mambo yanaharibika maana anajua wazi alichokifanya katika ile hati. Baada ya Yule askari kumaliza kuongea na simu, akamtazama Yule mwanamke.



    “Unatufanya sisi wajinga sio?” Yule askari akamuuliza. Yule mwanamke akawa amejishika kiuno mkono wa kushoto na ule wa kulia ameuingiza kwenye mfuko wa lile baibui lake.

    “Wamesema ya nani kama si yangu?” aliuliza kwa jeuri.

    “Hii ni hati ya Elizabeth Wangari Joseph” Yule askari alijibu huku akiinuka na pingu mkononi, askari wa nyuma yake alikuwa akija kumkamata kwa nyuma, Yule mwanamke kwa wepesi wa ajabu, alipiga teke la nyuma ambalo lilitua sawia katika tumbo la Yule askari wa nyuma na kumsukuma mpaka kwenye lile basi akajibamiza mgongo na kuanguka chini, wakati huo Yule mwanamke akutoa mkono wake wa kulia ukiwa na bastola moja kwa moja akafyatua na kumpiga Yule askari wa mbele kifuani, akarushwa na kujibamiza kwenye ukuta wa ile ofisi, Yule mwanamke akageuka nyuma kwa kasi na bastola mkononi, risasi ya pili ilitua kichwani kwa Yule askari aliyeangukia kwenye basi.



    “Leo mtamjua Mellina, nyau nyinyi,” alitamka Yule mwanamke.

    “Mikono juu weka silaha chini!” askari mwingine aliyekuwa upande wa pili wa basi. Mellina alijiangusha chini na kuviringika kupita uvunguni mwa basi akatokea upande wa pili, aliposimama na kutazama nyuma alipaishwa juu kwa risasi ya askari aliyekuwa ndani ya gari, alilenga shabaha hiyo ya haraka kupitia dirisha la basi, Mellina alianguka chini na kutoa yowe la maumivu, aligalagala damu ikimmwagika kutoka katika bega lake la kulia, walea skari wakamfiki na kumtia pingu huku jeraha lake bado likivuja damu.

    “Mfunge kitambaa kwenye jeraha, asije akatufia njiani,” askari mmoja alipiga kelele, wakamfunga vyema, na kumchukua mzobemzobe wakisaidiwa na wananchi waliokuwa kwenye basi, wale wenye moyo mgumu, maana kelele zilitawala eneo hilo.

    Mellina hakuwa na ujanja, hakika, mbio za sakafuni huishia ukingoni.



    Taarifa hiyo ya kupendeza ilimfikia Sargeant Maria, tangu sakata hilo lianze, kwa mara ya kwanza Maria alitabasamu kwa bashasha, akainuka na kumfuata Inspekta Saitoti ofisini kwake.

    “Ndiyo afande,” Saitoti aliitikia hata kama hakuitwa, baada ya kupokea saluti ya utii. Maria akampa taarifa hiyo tamu ambayo ilimfanya ashibe hata kama hajala. Mara moja inspekta Saitoti akaamuru gari ya plisi kutoka kuelekea Kisumu kumleta huyo anayeitwa Mellina. Safari ikaanza, Sargeant maria akiwa katika cabin ya gari na askari kadhaa wakiwa nyuma, mwendo wa kasi wa gari hiyo ulifanya kila aliye barabarani kupisha.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine, jeshi la polisi mkoa wa Kisumu lilikuwa katika masikitiko makubwa kwa kupoteza askari wao wawili katika tukio hilo. Haikuwa kazi rahisi kukubali lililotokea lakini bado hali ilikuwa hivyo ilivyo.



    Baada ya masaa kadhaa gari ya polisi kutoka Nairobi iliingia katika uwanja wa Hospitali ya Avenue pale Kisumu. Sergeant Maria alikuwa wa kwanza kushuka na hakuuliza chochote moja kwa moja aliingia ndani ya hospitali hiyo na kuelekea katika wodi aliyoambiwa huku nyuma akifuatiwa na vijana wake waliovalia kishari kabisa na bunduki zao mgongoni. Mellina alikuwa hoi, drip ya maji ikiwa inaendelea kuingia mwilini mwake, Maria alisimama mbela ya kitanda hicho na kwa jicho la hasira huku akiuma meno alimtazama Mellina.

    “Ulifikiri utafika wapi wewe kiumbe?” Sergeant Maria alimuuliza Mellina. Mellina alimsonya Maria, na Maria aktabasamau na kuendelea kumwambia, “Huu ni mkono wa dola, haukimbiliki, haya nimekuja kukuchukua na dhambi zako utaenda kutubu Nairobi, ila lazima kitanzi kiitafune shingo yako, mwanaharamu wewe!” kisha Maria akaondoka na Mellina akabebwa katika kitanda maalum, akawekwa ndani ya gari la wagonjwa, kasha safari ikaanza kurudi Nairobi chini ya ulinzi mkali.



    §§§§§





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog