Simulizi : Nyuma Ya Pazia
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada ya kumuacha Dorice nyumbani kwao alielekea moja kwa moja nyumbani kwake. Alivua koti la suti na kujiwekea dawa tena kisha akajitupa kitandani huku mawazo mengi yakinjia kichwani. Aliinuka na kujiweka saw a na toti mbili za John Walker kisha akajitupa kuusukuma usingizi wa kizembe. Nao haukucheza mbali, ulimchukua yeye na uchovu wake.
Ghafla alikurupushwa na simu yake iliyokiwa ikiita na alipoitazama ilimuoneaha mpigaji ni Dorice hivyo haraka haraka aliipokea.
"Yes, nambie bibieh...." Aliongea Joachim.
"Vipi nije"
"Haaaa...halafu nilizani unanitania" Alionesha mshituko Joachim.
"Wewe mi namaanisha na tayari nishajiandaa"
"Okey isiwe tabu njoo"
"Sawa" Kwa furaha aliitikia Dorice na kukata simu.
Huku upande wa Joachim alianza kufikilia huu ya ugeni ule ila akaona haina shida. Alinunua vinywaji na kuviandaa ndani ya friji kwani alifahamu fika kuwa mgeni wake alikuwa mpenzi sana wa Serengeti via ya kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL). Hivyo alijipanga sawa sawa na ugeni ule kisha akampigia kujua yuko wapi.
"Nimekaribia kufika"
"Sawa"
Mara baada ya Dorice kuja walikaa wote pale sebureni huku wakilewa pamoja na maongezi ya hapa na pale kuhusu kazi na mambo mengine.
* * *
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada ya kukiona kifo cha kikikimbia mbio kutoka kwake Jack Loyce aliona ugumu wa kazi yake kwa mara ya kwanza. Kwani hadi wakati ule alielewa anacheza na mtu msenzi zaidi yake. Aliamua kuweka nguvu zake sote katika suala la kumtafuta Joachim ili aondoe roho ya Joachim. Aliendelea kujitibu mwenyewe huku akiendelea kujilaumu kwa makosa aliyoyatenda usiku wa kukia siku hiyo.
"Shit......sasa atanipenda"
Pembeni yak alikaa Mamruki hatari wa Kicanada aliyekuwa akimuangalia Jack Loyce vizuri na kumfatilia kwa kila jambo alilokuwa akilifanya na kuliongea wakati huo. Alifahamika kwa jina la Simon Jacob yeye alitua siku hiyo akiwa ametokea Jijini Ottawa nchini Canada huku akipitia mizigo yake ya dawa za kulevya nchini Mexico na kuingia Nchini asubuhi ya siku ile ambayo alimkuta rafikiye Jack Loyce akiwa na majanga yake. Huyu alikuwa ni hatari na mafia maradufu kwa Jack Loyce, huku akijizolea sifa kwa kutokushindwa na lolote analolitaka yeye huku akiacha matukio ya kuondoa roho za watu bila huruma wala mchezo tena kama mchezo wa kwenye Luninga. Huyo ndio Simon Jacob. Halo aliyoiona kwa Jack Loyce ilimshangaza kwani hakuwahi kuona mtu akimchezesha Jack kiasi kile.
"Nini tatizo Jack....?"Aliuliza Simon.
" Simon kesi zangu niachie mwenyewe na hili suala nalitatua mwenyewe hata kwa njia za aje kwa hiyo naomba iniachie suala langu mwenyewe." Aliongea huku akumuangalia kwa dharau Simon Jacob.
"Wewe ni mdogo kwangu Jack na Nina uwezo wa kuingilia masuala yako yote hats kama hutaki na hili swala limekuhelemea Avk hivyo lazima liishe na ndipo biashara zetu ziende vizuri na ili liishe nawekamo mikono yangu sasa.....Shenzi!!!" Aliongea Simon kwa hasira huku akiweka msisitizo kwa kuyasindikiza maneno yake kwa funda mbili za moshi wa sigara. Aliinuka katika kochi na kutoka nje ya chumba kile cha Hotel na kumuacha na vijana wengine watatu waliovalia suti zao nyeusi.
"Shit.." Aliongea kwa hasira na kuinuka katia kochi alilokuwa amekaa. Alielekea katika mabegi aliyokuja nayo Simon Jacob. Mara baada ya kufungua begi moja alikutana na silaha Kali nyingi zikiwemo kubwa na ndogo. Alitoa bastola moja aloyovutiwa nayo kisha akaijaza risasi na kutoa nje. Alianza kumfikilia vizuri Joachim Bartazar huku akitamani amtie tena mbaroni ili mradi tu asifanye makosa kama aliyoyafanya mwanzo . Alikuwa akiliangalia gari lake aina ya Range Rover Sport huku hasira za Joachim Bartazar zikizidi kimpanda. Ilikuwa mishale ya saa 1 na nusu jioni. Alikiwa akionekana sawa huku majeraha take aliyoyakanda vizuri yakionekana kwa mbali. Ghafla alishituliwa na mlio wa simu yake aina ya NOKIA ASHA 200 iliyokuwa ikiita kwa kuonesha namba ngeni. Alibonyeza kitufe cha kupokea na kuiweka sikioni kuongea chochote.
"Haloow....Naongea na Bob" Sauti ya upande wa pili iliongea na halo ndipo alipokumbuka uwepo wa dereva Taxi aliyemuagiza kazi ya kufuatilia makazi ya Joachim Bartazar Mara tu baada ya kusikia jina Bob Mara baada ya kujitambulisa hivyo kwa dereva yule.
"Naam ndio yeye nani mwenzangu?" Aliuliza ili apate uhakika je ni yeye?.
"Mie no yule dereva taxi uliyempatiia kazi ya ........."
"Subiri tusiongelee humu tukutane tuongee." Alidakia Jack Loyce huku akimkatisha asimalizie na kuingia katika gari ili aondoke.
"Mie nipo kinondoni wewe je?"
"Nipo Posta nakuja sasa hivi." Aliongea huku akigeuza gari na kuondoka katika maegesho ya New Africa Hotel pale Posta.
"Sawa usichelewe'
" Usijali" Alijbu huku akilitia moto gari kuelekea Kinondoni. Moyoni alifurahi kwani aliuona mwisho wa Joachim Bartazar anaeisumbua akili yake hadi wakati ule.
* * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huku ujio wa Dorice nyumbani kwake ilimfanya awe na furaha huku tabasamu lake likizisi kuchanua kadiri alivyomuangalia Dorice ambae alikuwa kavaa miwani yaani kalewa huku akiendelea kumchangamsha zaidi Joachim Bartazar. Alizidi kugundua vitu vingi ambavyo vilijificha katika uchechi wake huku akionekana mzuri Mara dufu hali iliyompelekea Joachim kuhisi labda nae kalewa hali ambayo haiwezi kumtokea hata any we pombe kali yoyote. Dorice alisimama alicheza , Dorice alimkumbatia Joachim na kufanya mambo mengi yaliyompa furaha Joachim tu. Akiwa katika halo ile ghafla simu ake iliita. Alipoanslia kioo cha simu kilionesha mpigaji ni Sauda na hapo ndipo alipokumbuka uwepo wa Sauda Mansoor. Aliipokea haraka haraka.
"Haloow..."
"Yani Joachim wewe ni wa kunitoroka Mimi tena bila kinipa hata taarifa.?" Alilaumu Sauda.
"Hapana sio hivo Sauda ila nitakuelezea kila kitu baada ya kikao kwani sasa hivi Niko na kikao nitakupigia." Alidanganya Joachim.
"Sawa." Aliitikia kishingo upande bila kuridhishwa na maelezo ya Joachim hivyo aliamua kutoka na kuelekea nyumbani kwa Joachim.
* * *
Mara baada ya kuonana na yule dereva Taxi Jack Loyce alielekezwa vizuri nyumbani kwa Joachim Bartazar maeneo ya Tegeta Boma huku nyumba yake ikiwa imejitenga. Alizamisha mikono mfukoni ili atoe ujira wa dereva yule ila alitoa bastola iliyofungwa kifaa maalum cha kuzuia sauti na kumchapa risasi tatu dereva yule kisha akarudi kwenye gari lake ili aende kwa Joachim Bartazar.
"Kwisha habari yako wewe mwanaharamu." Aliongea Jack Loyce huku akiingia barabara kuu kuelekea Tegeta.
"Kwisha habari yako wewe mwanaharamu." Aliongea Jack Loyce huku akiingia barabara kuu kuelekea Tegeta.Mwendo aliokuwa akitembea barabarani hapo uliwafanya Polisi waliokuwa doria usiku ule kuitilia mashaka kwani mara baada ya kuimulika tochi ya mwendo kasi waligundua gari ile ilikuwa na mwendo mkali hivyo haraka maafande wawili walilifungia mkia gari la Jack Loyce. Upande wake Jack Loyce hakuwa na taarifa ya kufuatwa nyuma na Polisi hivyo alikuwa kiendelea kulitia moto gari lake huku akifikilia jinsi ya kumchezesha Joachim Bartazar mchezo hatari.
* * *
Sauda Mansoor alikuwa akikata kona kuelekea mahala alipoishi mwanaume ambae yeye alitokea kumuona kama nyota kwake lakini ndio vile mwanaume mwenyewe hakuwa na muda nae bali akili yake ilitawaliwa na kazi tena kazi hatari kabisa nae ni Joachim Bartazar. Mara baada ya kuiona nyuma nzuri ya kijana huyo alisimamisha gari lake kisha akaanza kujifikiria ataingiaje. Ilipita kama nusu saa huku akiwa umbali wa mita mia mbili akiwaza na ndipo alipoona gari zuri aina ya Range rover sport ikisimama mbele yake umbali wa mita ishirini. Ilichukua dakika tano hivi hadi yule mtu kushuka na aliposhuka aliangalia ile gari ya Sauda kwa sekunde kadhaa na kuvuka barabara kuifuata barabara ndogo ielekeayo nyumbani kwa Joachim Bartazar. Hakutaka kupoteza muda alichukua simu yake na kutafuta namba ya Joachim na kuipiga. Simu iliita bila mafanikio na hapo alimuona yule mtu akiambaa na ukuta hadi alipopotelea katika kigiza fulani. Muda ule ule iliingia gari ya Polisi huku askari wawili wakishuka na kulifuata gari lililokuwa mbele yake yaani la yule mtu ambae hakumfahamu. Nae hakupoteza muda alishuka kwenye gari lake na kuwafuata wale askari ili kutambua nini kinachoendelea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Muulize huyo binti labda"Alisikia Askari mmoja akimwambia mwenzie na muda huo aliitwa kwa ukali.
"We binti hebu njoo hapa"
"Abee!"Alijisogeza karibu kwani alitarajia jambo hilo.
"Je,umemuona mwenye hili gari akielekea wapi?"Aliulizwa na hapo akatambua hatari iliyopo.
'Kwa nini afuatiliwe ma Polisi mtu yule ni nani?'
"Kaelekea usawa wa ile nyumba na kisha katembea na ukuta hadi kwenye kigiza hicho hapo nyuma"Alielekeza Sauda na hapo wale askari wakaangaliana. Kisha Sauda hakupoteza muda alirudi kwenye gari yake na kuchukua bastola yake kwani alihisi kitu kibaya kumkumba Joachim kisha alijaribu kupiga lakini haikupokelewa simu yake. Alishuka na kuwaona wale askari wakiwa bado wanashauriana cha kufanya kisha akavuka barabara na kuifuata nyumba ya Joachim. Alibonyeza kengere ili aje afunguliwe geti. Alikuwa akiwakata jicho la kuibia wale askari Polisi waliokuwa wakijishauri ambao wakati huo walikuwa wakimuangalia yeye nini anafanya. Ghafla geti lilifunguliwa na aliyefungua akiwa mtu mwingine tena aliyemfahamu huku akiwa na bastola mkono iliyokuwa ikimuangalia yeye Sauda.
"Shiiiih"ikuwa sauti ya Jack Loyce ikiashiria ukimya kwa Sauda huku kwa ishara akimvuta ndani haraka na kubana nae pembeni mwa gari ya Joachim mara baada ya kuskia sauti za mjongeo wa mtu akitoka ndani.
Alikuwa ni Joachim alikuwa na kaptula na tisheti huku akiwa makini kulikaribia geti lake na bastola yake mkono. Kitendo kile kilimfanya Sauda atoe mhemo mkubwa ili kumuweka sawa Joachim ambae papo hapo alichupa juu na kujitupa katika karo la maji lilokuwa pembeni yake huku risasi tatu zikimpita na kugonga geti na kuzalisha kelele zilizowatia shaka hadi askari waliokuwa nje. Sauda hakutaka kuwa mnyonge kwani nae mara baada ya kitendo kile aliusukuma kiwiko chake nyuma na kumpata vizuri Jack Loyce na kumpotezea uelekeo kisha yeye kuingia ndani spidi ambako alikutana na na mwanadada Dorice akihaha kwa kelele zile kwani pombe zote zilimtoka wakati ule.
Huku nje askari wale walikimbia kuelekea getini ili kujua kilichojiri eneo lile lakini ghafla walishtushwa tena na mlio wa risasi na kuanguka chini. Walikuwa wamechelewa kwani Jack alikuwa tayari ameshamchapa risasi mmoja wao mara tu alipowaona wakati akilinyatia karo alimojiruda adui yake kwa kitendn kile kimfanya apoteze ushupavu hivyo kumuachia nafasi Joachim ambae hakuifanyia makosa nafas4 yake bali alichomoka katika karo huku akiachia risasi kadhaa zilizo uvunja mkono wa Jack uliokuwa na bastola na kuchia yowe kali.
"Aaaargh"
Hapo Joachim hakuwa tayari kumuachia nafasi kwani nae Jack ingawa alivunjwa mkono ila alijitupa chini ili aikote bastola na kujibu shambulio lile akawa kachelewa kwani risasi mbili zilikuwa zimeingia katika kisogo chake na kuacha matundu mawili kichwani pake na kuwa mwisho wake Jack Loyce. Hakupoteza muda alielekea ndani haraka na kumkuta Sauda akiwa tayari kushambulia. Mara baada ya kuona ni Joachim walijikuta wakimkumbatia wote kwa pamoja lakini yeye aliwasukuma na kuelekea sehemu na kukubonyeza kitufe fulani na kuwataka waondoke haraka eneo hilo. Hawakupoteza muda walitoka huku Joachim akiwa wa mwisho na kukutana wale askari wawili mmoja akiwa chini alimzoa pale chini na kumuweka begani.
-
Hawakupoteza muda walitoka huku Joachim akiwa wa mwisho na kukutana wale askari wawili mmoja akiwa chini alimzoa pale chini na kumuweka begani.
"Tuondoke hapa haraka kabla ya dakika tano kuisha"Aliongea Joachim huku akiwaachia alama ya mshangao wengine. Haraka alimuweka yule askari katika gari yao na kumpa ishara yule mwingine aendeshe kisha yeye akaelekea katika gari ya Sauda na kulitia moto.
* * *
"BHOOOOMM!!"
Ilikuwa ni sauti iliyosikika mara baada ya dakika tano kupita tangu Joachim abonye kitufe ukutani pake. Sauti ile iliwashtua wakazi wa eneo lile huku wengine wakikimbia bila kuelewa nini tatizo.
* * *
Ni Dorice pekee ambae alikuwa haelewi nini kinaendelea katika wakati ule ila kwa mbali alisikia sauti yenye mlio mzito nae Joachim alivuta pumzi ndefu huku Sauda akiwa kimya hana la kuongea. Hakutaka kupoteza muda alimpeleka Dorice hadi kwao kisha akamwambia;
"Shiiih!usimwambie mtu yeyote yule kuhusu ulioyaona leo"
"Sawa"Aliitikia kwa uoga Dorice. Nae Joachim hakuchelewa alilitia moto gari la Sauda na kufutika machoni pa Dorice aliyekuwa kaduwaa tu. Ndani ya gari alibaki Joachim na Sauda pekee na huo ndio ukawa mwanzo wa maongezi yao ya kikazi.
"Mpigie opareta mpatie taarifa kwani hali ni mbaya kwa sasa."Aliongea Joachim huku akicheza na usukani wa gari lile.
"Sawa ila tukifika ndio lifanyike hilo swala"alijibu Sauda huku akimuangalia Joachim aliyukuwa bize kuangalia barabara mbele yake. Walifika nyumbani kwa Sauda kwa msaada wa Sauda kumuelekeza vizuri kwani hakupatilia maanani siku ya jana yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Karibu tena"lilikuwa neno lililomtoka Sauda mara baada ya kuingia ndani. Joachim alijitupa katika kochi kisha akawa akifikiria mambo yalivyokuwa yakienda na ndipo alipopata wazo la kuwasha luninga kubwa iliyokuwa pale sebuleni kwa Sauda na papo hapo anakumbana na taarifa maalum juu ya nyumba kulipuka huku akimuona yule askari akionekana akitoa maelezo juu tukio zima. Pia aliuona mwili wa Jack Loyce ukipitishwa na kupakizwa katika gari huku watu wakiwa wengi.
"Aaah!"alizima luninga ile na muda ule ule Sauda alitokea chumbani pake akiwa na taulo jeupe alilojifunga.
"Washa TV opareta kanambia kuna taarifa juu yetu na anaeongea ni Waziri wa ulinzi."aliongea Sauda. Haraka Joachim alibonyeza rimoti na papo hapo taarifa hiyo ikaonekana ikaonekana.
"......kwa hiyo watafutwe popote walipo na watawajibishwa kisheria kabisa na hili zoezi lianze mara moja. Kuanzia huyu Bwana Joachim Bartazar na hao mabinti wawili atawataja atakapopatikana." na ndipo alipomaliza Waziri huyo huku Joachim akitabasamu tu na kumuangalia Sauda.
"Huyo nae yumo katika orodha ya ubadhirifu hapa nchini na ndio maana ananitafuta na hii ni vita sasa."aliongea Joachim huku akiendelea kuangalia habari hiyo ambayo ilikuwa mwishoni.
"Sasa tunafanyaje?"lilikuwa swali la Sauda kwa Joachim.
"Naanza kwa kuiweka hadharani video ya huyu Waziri kisha nafuatia orodha nzima ya wahusika wa kumiliki makundi ya kiharifu na wala rushwa pia na hii itaanza kesho."aliongea Joachim huku akikunja nne miguu yake.
"Hapana,kesho ni Mazishi ya Mr. Maebo tuanze kesho kutwa"
"Mara baada ya mazishi mambo yatakuwa hadharani na lazima kinuke"alimalizia huku akiinuka na kukifuata chumba alichofikia jana akiwa hoi na kuoga.
* * *
Sasa mara baada ya kupambazuka hali ilikuwa mbaya huku makachero wakitanda Jiji zima kumtafuta muuaji na mlipuaji wa nyumba yake huku ikionekana alikuwa na mzigo wa madawa ya kulevya pia kisha kutokomea mjini. Hali ile ilichukua nusu saa kutanda nchi nzima huku picha za Joachim Bartazar zikisambaa Tanzania nzima. Waliomfahamu walishangaa kwani hakuwa na wasifu ule. Lakini upande wa pili kifo cha Jack Loyce kinawafikia kikosi cha Rising Mafias huku Papaa Paul akiwa ndie mhanga mkuu wa kifo kile kwani Jack Loyce alikuwa mtu pekee aliyemkubali kikosini hapo. Waziri wa Ulinzi na viongozi kadhaa waliokuwa na taarifa ya kuchunguzwa nao wanapatiwa taarifa kuwa marehemu wa tukio la usiku ni kijana wa Papaa hivyo wote vichwa vinawauma kwani walisikia kijana yule alikuwa akifahamu mengi juu yao na ndio maana Waziri alitoa oda ya kutafutwa popote alipo awe mzima au marehemu.
"Mheshimiwa yule auwawe kimya kimya bwana"aliongea Papaa Paul alipokuwa akiongea na Waziri.
"Mr. Paul acha akamatwe ndipo tutajua cha kufanya kama ni kuuwa au kufungwa maisha mimi ndiye ntakaye jua"aliongea kwa woga Waziri.
"Vijana wangu wako kazini wanamtafuta na nikimkamata kabla yako ni halali yangu huyo"aliongea Papaa na kukata simu kisha akamuangalia Simon Jacob aliyekuwa akisubiri Papaa amalize kuongea na simu.
"I want him (Namtaka!)"ilikuwa kauli ya Mzungu huyo kisha akaamka kutoka nje. Papaa hakuwa na jibu ila tu kutoa oda kwa kikosi chake kumsaka popote pale huyo mtu anaejiita Joachim Bartazar.
* * *
Saa 5:00 asubuhi.
Makaburi ya Kinondoni yalifulika watu huku wengi wao wakiwa katika mavazi meusi. Ulikuwa ni wakati wa kumua Mr.Harold Maebo kama ilivyokuwa kawaida huku nae Joachim akiwemo.
Saa 5:00 asubuhi.
Makaburi ya Kinondoni yalifulika watu huku wengi wao wakiwa katika mavazi meusi. Ulikuwa ni wakati wa kumuaga Mr.Harold Maebo kama ilivyokuwa kawaida huku nae Joachim akiwemo. Hakuna aliyetambua uwepo wako isipokuwa wachache kati yao akiwemo Injinia wao au opareta kama walivyozoea kumuita. Joachim alikuwa makini kuliko alivyokawaida huku akikutana na washirika wachache wa kijasusi wa kitengo chao cha siri na kutoleana ishara tu kwani hata wao walikuwa na taarifa ya kutafutwa kwake huku wakifahamu nini anachofanya. Wanasheria wote wa kampuni yake walikuwa eneo hilo huku vigogo na watu mashuhuli wakijazana kuuaga mwili wa mzee yule. Wakiwa katika hatua ya kushusha jeneza kaburini ghafla waliingia watu wengi eneo hilo huku wakiwa na bunduki mikononi na barakoa(mask) za soksi usoni tena wakiwa na mavazi meusi. Watu wote walishangaa huku wengine wakitaka kutimua mbio.
"Haruhusiwi mtu yoyote kusogea alipo tulieni hivyo hivyo"alitoa onyo mmoja wao kwa kutumia kipaza sauti alichokua nacho mkononi na kuwafanya watu wataharuki kisha watu wale wakaingia kukagua mtu mmoja baada ya mwingine kama vile wanausalama waliokuwa wakimtafuta mtu fulani. Walifanya zoezi hilo kwa takribani nusu saa. Hali ile ilimchanganya sana Joachim kwani alikuwa kaishaelewa kuwa wale ni akina nani na walikuwa wakimtafuta nani hivyo alikuwa akifikiria jinsi ya kuchomoka eneo hilo. Aliiweka sawa kofia yake kubwa aina ya Pama huku akiupeleka mkono wake katika koti lake lefu jeusi alilovaa na kuchomoa bastola kisha kupiga risasi kadhaa angani. Yalisika mayowe huku watu wakikimbia bila mpangilio na kulifanya zoezi la Joachim kufanikiwa. Kila mtu aliwazia roho yake huku wengine wakikanyaga juu ya makaburi. Hakupoteza muda ila alijichanganya huku akitoka nduki na kuelekea barabara na kuwaachia kesi walinzi wa mabosi waliokuwa pale kazi ya kupambana na Rising Mafias.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
* * *
Mara baada ya kuyaacha makaburi ya Kinondoni alipita vichochoro huku akiwaacha watu katika taharuki kwa jinsi alivyokuwa hali iliyomfanya nae ajishitukie. Hakupoteza muda alivua koti lake lefu na kofia huku akibaki katika shati la mikono mirefu na suruali nyeusi ya kitambaa. Alipotokea barabarani alipiga mkono taxi iliyokuwa ikija usawa wake na kumuelekeza anapoenda.
* * *
Taarifa za kupotea kwa Joachim Bartazar pale makaburini zilimuumiza kichwa Papaa Paul huku akizunguka tu ofisini kwake kwani taarifa za uwepo wa Joachim pale makaburini alizipata kutoka kwa moja kati ya mashushu wake wa siri. Alishika simu yake na kutafuta namba ya Waziri tena na kumpigia.
"Mr. Paul hukutakiwa kufanya ulichokifanya pale makaburini"aliongea Waziri.
"Huwezi kunifundisha kazi Waziri yule anatakiwa leo mikoni petu mapema hata kama atakuwa kanisani mimi nitamfuata hadi nimkamate au nimalizie mbali"alimalizia huku akikata simu na kutoka nje ya ofisi yake.
* * *
Dorice Kimaro au Manka wa kichaga kama alivyopenda kujiita. Alikuwa ni mtoto wa kipekee wa Bwana Daudi Kimaro,mchaga wa Marangu Mkoani Kilimanjaro na Bi Gloria Msuya mama wa kipare. Kutokana na kuzaliwa peke yake nyumbani kwao Dorice alikuwa akideka kwa mama yake na hata kwa baba yake ambae alikuwa mfanyabiashara Jijini hapa. Nini Dorice angetaka na Wazazi wake wasimpatie? Hivyo alifanikiwa kuchukua shahada yake ya kwanza ya uongozi wa biashara na masoko nchini Uganda katika Chuo Kikuu cha Kimataifa Cha Makelele na kuamua kurudi kufanya kazi nchini kwake. Haikuwa kazi kwake kupata kazi katika kampuni kubwa kama The HAMSHOT GROUP OF COMPANIES na yeye kupelekwa katika moja ya kampuni hizo nayo ni HAMSHOT ENTERPRENEURS LTD huku baba yake akichangia mwanaye kupata kazi katika kampuni hiyo. Alikuwa amekaa kwa muda wa miezi sita ndipo anapatikana mfanyakazi mpya mwenye tabia za kipekee na kuukosha moyo wake. Alikuwa mfanyakazi mcheshi aliyetambua kazi na wajibu wake kazini,ni huyo mfanyakazi aliyeweza hata kumfanya bosi wao aliyekuwa mkali kuwa mpole na muelewa si hivyo tu bali alitambua hali na tabia za kila mfanyakazi kwa muda mfupi tu nae ni Joachim Bartazar kijana aliyependwa na kila mfanyakazi. Huo ukawa mwanzo wa kumfahamu Joachim Bartazar na kutokea kumpenda sana ila kushindwa tu kumwambia yaliyo ndani ya moyo wake.
Mara baada ya lile tukio nyumbani kwa Joachim, Dorice hakutaka kuongea na mtu bali aliingia ndani na kuelekea chumbani. Alikuwa na wasiwasi juu ya Joachim.
"Joachim anamiliki bunduki?....na yule mwanamke sijui ni nani kwake halafu nae pia ana bunduki au ni mpelelezi nini?"yalikuwa maswali bila majibu yaliyopita kichwani mwake na ghafla alishtushwa na sauti ya mama ake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Dorice.....Dorice....njoo uone"haraka alikurupuka kutoka kitandani na kwenda sebuleni. Alichokiona kilikuwa ni cha kushangaza kwani ni nyumba ya Joachim ilikuwa ikizimwa moto uliolipuka na picha ndogo ya Joachim Bartazar ikinadiwa kwa maneno ya WANTED. Hakufurahishwa na kituko hicho hivyo alirudi chumbani kwake na kujitupa kitandani. Hakuchukua muda alipitiwa na usingizi.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment