IMEANDIKWA NA : NELSON NTIMBA
*********************************************************************************
Simulizi : Bonde La Mauti
Sehemu Ya Kwanza (1)
Kila kitu kilicho fichwa huwa kina madhara makubwa pindi kikifichuliwa kabla ya wakati wake.Hii ndiyo siri nzito iliyo fukiwa miaka 200 iliyo pita katika msitu wa Amazon .Eneo hatari kabisa kwa binadamu kukatisha ,Wengi walio jaribu kupita kona hiyo walikutana na bonde la mauti.Si wanyama wala mdudu lazima angekutana na dhahama hiyo isiyo poteza wakati .Wengi walitamani kujua siri hiyo nzito waliambulia patupu kwa maana kama ungelipata jibu basi upaswi kulivujisha nje ya msitu huu wa ajabu.Serikali mbalimbali zilizidi kumwaga watahalamu lukuki lakini jibu lililo kuwa lina rudi kwao ni Bonde la Mauti.Makomandoo waliteketea kila waingiapo katika Bonde hilo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nitakukata kiungo chako kimoja baada ya kingine hadi nivimalize vyote.uwezi kujaribu kufuata nyayo za mauti kipumbafu kama ulivyo ingia ingia .Kwenye bonde letu hakuna aliye wahi kutoka akiwa mzima maana wote waingia hao uishi siku chache za uchungu na wewe kuanzia leo utafurahia uchungu huo" Yalikuwa ni maneno ya mtesaji aliyekuwa amekamata dhana za kutosha za kufanyia mateso.Sikuwahi kufikilia kama siku moja nitafikia hatua mbaya kama hiyo katika kazi yangu ya uandishi wa habari.Na hii ndiyo siku mfumo wangu wa maisha ulibadilika nikajikuta nimekuwa kiumbe mwingine maana mateso yalikuwa ya kutosha na kama ungelishuhudia mateso yaliyomo kwenye gereza hilo ungezimia mwenyewe. Mtesaji alinisogelea akiwa na vifaa vyake vya mateso vilivyo kuwa ni vingi haswa vingine vilifanana na vya hospitali kabisa na vingine kama vya mafundi umeme ,ilikuwamo misumeno,mapanga,viwembe,na vifaa ambavyo sikuwahi kuvitia machoni. "Karibu katika kiwanda cha mateso mwandishi wetu .Siku nyingi nimetamani nikupate walau nikutie kiwembe ndani ya mwili wako ila upatikaniki.Asante sana kwa kijileta mwenyewe natumaini umeskia ombi langu" Yalikuwa ni maneno ya kejeri toka kwa mtesaji huyo aliyekuwa ni mweusi kama buti la jeshi alikuwa na sura iliyojaa makovu utafikili aliwahi kuogelea ndani ya asidi.Sura yake ilitosha kabisa kuonyesha alivyo rohoni . Kwa nini nipo hapa hilo ndilo swali unalopaswa kuniuliza maana kama ningelikuwa hai usingeliweza kusikia na kusoma historia yangu yenye matesao lukuki.na nitakusimlia mwanzo mwisho hadi unielewe .
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mtesaji alinisogelea akiwa ameliweka tabasamu lake bandia kama ilivyo kuwa kawaida yake.Sikuonyesha kuogopa kwa aina yeyote ila rohoni nilikuwa ninakaribia kuzimia kwani nilijua kitakacho kwenda kutokea muda si mrefu." Alinitizama kwa kitambo kidogo kisha akaniuliza swali dogo lakini lenye uzito mzito. "Wewe ni nani hasa hadi ujitoe kafara kwa ajili ya nchi yako?" Swali lake lilikuwa jepesi ila lilihitaji muda kuweza kujibiwa kwani liliulizwa kipindi cha hatari ambacho sikuwa tayari kuweka mambo yangu wazi.Kwa akili ya kawaida lingeonekana swali lake halina maana.Hila kwa ujuzi niliokuwa nao katika kazi yangu alionyesha ananijua tangu zamani ila hana uhakika maana aliuliza kwa kucheka na alinisogelea ili wenzake wasisikie kile alicho kiongea. "Utasema kwanini uliingia katika bonde hili maana unaonekana una kiburi sivyo?Leo tutaanza na mateso mepesi kijana haya yatakufungua kinywa ila ukijifanya nunda yatabadilishwa." Maneno yake yalikuwa ni ya mzaha kama vile kitu anachokwenda kukifanya ni cha kawaida sana.Shati langu lilichanwa na wakaniacha kifua wazi.Baada ya kuniondoa shati langu na kunitizama alionyesha mshutuko mtesaji huyo.Nilijua kuna kitu amekigundua katika mwili wangu ila bado sikujua ni kitu gani maana katika kifua changu mkono wa kulia kulikuwapo na mchoro wa ndenge aina ya tai hii ni nembo ya kikosi cha kikomandoo kinachofanya kazi kwa siri katika maeneo mbalimbali ya kijamii(tatuu)na kitu kingine nilikuwa nimejaa alama za mapanga na viwembe vya kutosha jambo hilo lilionyesha kwamba sio mgeni katika nyanja hiyo ya mateso maana kila kitu kilikuwa wazi.Alinisogelea tena kama mwanzo na kunionyesha ishara ya ngumi akainua mkono kama anayetaka kunipiga.Hapo niliweza kugundua kitu katika vidole vyake vya kati.Hakika naye alikuwa na alama kama yangu kabisa na hilo nikalitambua ndiyo maana aliniuliuliza mimi ni nani kwa siri.Ngumi yake ikatua kwenye uso wangu na ikafuata nyingine nzito iliyonitoa damu maana hii ilinichana mdomo kabisa. "Kijana hacha kiburi kabisa utaumia zaidi kama utaki kutoa ushirikiano na sisi." Haliomba apewe vifaa vyake vya kazi.Wakamsogezea kitoroli kile chenye vifaa hatari kabisa. "Karibu tena katika nyumba ya mateso kama nilivyo kuahidi ila usilaumu maana umekuwa mkimiya kama unaongea na mabubu wenzako." Mashine iliwashwa na akanisogelea akiwa na kifaa cha kurushia na umeme kifaa hiki kilikuwa kipya kabisa maana sikuwahi kukiona kabisa katika kazi kama hizi na sikukijua kabisa. Dhana hii ni mpya kabisa itakufanya useme walau kidogo tena kwa sauti.Maana inaonekana viwembe umevizoea sana hadi mwili wako hausisimki kabisa. Alichukua kibanio chenye waya mwekundu akakiweka katika mkono wangu wa kulia na kingine cha rangi nyeusi kwenye kifua karibu na titi la kushoto.Kisha akaninongoneza tena ."Jikaze mimi nipo kazini" mashine ile ikawashwa na kuanza kizipandisha voltage.Hakika nilitoa yowe la nguvu maana sikuwahi waza kama kuna mateso makali kiasi kama hiki na yenye kuumiza kupitiliza kiasi kile.Kufikia hapo nilijihisi kufa kufa maana bado walionyesha tabasamu tu wakifurahia kitu wanachokiona mbele zao. "Kwanini unatufuatilia,nani aliyekutuma na wewe ni nani hasa?" Niliulizwa swali na mmoja wa askari aliyekuwa yupo kimya muda wote aliyekuwa ameshika kisu chake mkononi. Niligundua kitu hapo hawa watu wana gawana majukumu maana mtesaji hausiki katika kuuliza maswali kabisa na wengine ni watazamaji na yupo anaye andika vitu fulani hasa vinavyo husiana na mateso hasa mambo ya maana zaidi. Mashine ikawashwa tena na hapa ikaongezwa voltage zaidi hakika uchungu ulizidi mara dufu ya mwanzoni lakini sikudhubutu kutoa ushirikiano kabisa. "Inaonekana unakiburi kweli kweli.Basi zoezi linabadilishwa kabisa maana hili umeliweza" Mashine ya umeme hiliondolewa vikaletwa visu vidogo kama vile vinavyotumika katika hospitali hasa katika upasuaji. "Nakuuliza mara ya mwisho tena kisha zoezi linaendelea kamautotoa ushirikiano" Nilijifikilia haraka katika maumivu haya yanayokwenda kunipata jibu lake nikalipata.....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilinibidi nitoe maelezo yanayo elekea kwenye ukweli hila si ukweli kabisa maana kosa moja lingepelekea kuhatarisha maisha yangu. Niwataza tena kwa tahathari maana wote walionekana wasio na utu.Katika watu hao walio kuwa wamenishikilia nilishampata mtu mmoja tu niliyekuwa nimemfahamu japo kwa uchache naye si mwingine bali ni huyo mtesaji ila sikutaka kumwamini maana nimemkuta akiwa na maadui kabisa japo alijitambulisha kwa siri.Ilinibidi nimwamini japo kwa muda huo maana kama asingelikuwa ni kunikonyeza kisiri ningelibaki kimya.Hivyo nikawa na ujasiri wa kutosha maana kama kuna baya litajitokeza atanisaidia kama alivyo nionyesha kupitia ishara za mwili. Jina langu naitwa Nelson Ntimba ni mwandishi wa habari wa kujitegemea pia mi ni mfanya biashara wa madini nimekuja hapa kama sehemu yangu ya kazi inavyonitaka maana popote pale penye harufu ya kazi lazima nipatafute.Ukweli nimevutiwa na utendaji wenu wa kazi hivyo ilinibidi niwatafute japo nipate maelezo ya kutosha maana uwezi kufanya kazi na watu usio wajua vizuri.Mnahitaji kitu gani kingine toka kwangu ? Nilimalizia kwa kuwauliza swali ili kuwatoa kwenye lengo. "Asante kijana kwa kutoa ushirikiano wako hafifu lakini mimi sijakubaliana na wewe kabisa maana unataka kutufanya kama matoi ya kuchezea.Tumekufuatilia tangu ulipo fika Marekani mfumo wako wa maisha tumeujua zaidi ya ujijuavyo tena unataka kutufanya wapuuzi.Sawa labda wenzangu wamekuelewa ila mmimi bado ujanishawishi kabisa maana pamija na hayo maelezo yako lazima ufe tu maana umejileta mwenyewe. Ila kabla ujafa utatufanyia kazi zetu kama tatu ndipo ufe kwa amani bila mateso makali." Alimaliza kwa kuwapa ishara waniamishe eneo hilo. Waliingia wanajeshi wawili wakanishika msobemsobe na kuanza kunitoa nje ya chumba hicho cha mateso. Hakika nilishangaa kitu maana pindi naingia ndani ya kambi hiyo sikuwaona askali walivyo kuwa wengi ila sasa niliweza kushuhudia wakiwa ni wengi tena wa mataifa tofauti kwani niliweza kuwaona wachina ,waharabu,wazungu,na waafrika pia.Nyuma yangu alikuwepo yule mtesaji akizungumza na wale wazungu walio kuwa wakinioji.Baada ya mwendo kama wa maili mbili nilifikishwa katika jumba lenye monekano mzuri japo si sana ila lilionekana ni bora kabisa.Ulinzi katika jumba hilo ulikuwa ni wa kutosha zaidi maana walinzi wa eneo hilo walikuwa wameshikilia mashine zao kwa ukakamavu kama vile wapo ikulu.Tulipo fika eneo hilo wale wanajeshi walio kuwa wamenishika walisimamamishwa na yule mtesaji.Akawaon gelesha lugha nisiyo ijua kama muda wa dakika mbili hivi.Jambo lililonishangaza ni kwamba walitii maelezo wakaniachia nikabaki na yule mtesaji. "Mbona unashangaa kijana uelewi lugha nini tayari upo jera japo hii ni ya uhuru kidogo si kama nyumbani?" Kumbe nafahamu kiswahili vizuri imekuwaje kuwaje uwe adui wa nchi yako?nilimuhuliza maswali mfulululizo. "Tulia usimwage mchele njoo hapa maana wewe ni mateka wangu kuanzia sasa mimi ndiye nitakuwekea ulinzi hadi pale kifo kikupate.Pole kama utakuwa unaumia maana hapa kifo ni kitu cha kawaida ukileta ujinga.Ilinibidi niwe mpole maana nilishaambiwa mapema ukatili wa ngome hii tangu hapo mwanzo kabla sijaingia kwenye misheni. Kuna kitu nimekiona kwenye kifua chako nambie ukweli maana hata mimi nilikuonyesha kitu hicho." Ukweli gani kama umeona mbona mimi sijakuuliza kuhusu niliyo yaona bora wewe umejua jina langu mimi sijakujua wala sijui kambi hii ni ya nini? Nilimrudishia maswali . "Wewe ni komandoo wa Tanzania bila shaka unatoka katika kikosi cha SNS.namba yako ya kazi ni SNS01.Kweli si kweli? Nilishangaa kuona anayajua mengi kunihusu hadi namba yangu ya kazi hakika niliona kutakuwa kuna jambo la ziada nyuma ya pazia. "Usishangae hata mimi ni kama wewe tu ila hapa nipo kwenye kazi kama wewe na taarifa yako ninayo mapema kwamba utanitembelea.Hila kabla sijakwambia majukumu yaliyo mbele yako nikwambie siri hii nzito kidogo.Nihaidi kama utaitunza maana ni hatari kama ikivuja." Nakuahidi siri hiyo itakuwa salama tu kwangu. "Vizuri sana kwa sasa haupo Marekani tena umeshaingia nchi nyingine kabisa tena upo ndani ya Msitu wa Amazoni." Nilishangaa kwa maelezo yake aliyo nipa maana pindi naingia katika kambi hii ilikuwa ipo Miami kwenye Jimbo la Frorida tena sasa hivi najikuta katika maeneo tofauti kabisa tena hapa Jeshi ni kubwa mno.Hakika niliona wazi hili ni BONDE LA MAUTI. "Usiwaze sana kijana nitakupatia maelezo ya kutosha muda ukifika hila hii siyo siri niliyo kusudia maana nilitaka upate picha jinsi walivyo jipanga usije ukafa kabla ya wakati."....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mtesaji huyo aliendelea kupiga domo ila mimi nilikuwa bize na upelelezi wa kambi hiyo ya kijeshi iliyo onekana ina vifaa vingi vya kisasa kabisa ambavyo sikuwahi kuvitia machoni hapo kabla.Askari hawa walionekana wana ufanisi mkubwa kabisa katika silaha za kisasa.maana niliweza pia kuziona ndege za kivita za aina mbalimbali zikiwemo helkopita pamoja na jet.hakika watu hawa niliwaona wa kawaida kumbe nimejiingiza kwenye bonde la kifo .Baada ya muda kama wa dakika kumi tayari tulikuwa mbele ya jumba kubwa la kijeshi lililo sheheni magari ya kivita jip pamoja na vifaru(tank) . "Karibu nyumbani kijana ,jisikie kama vile hapa ni kambi yako ya nyumbani.Ila leo naona umepata kisafisha macho maana umeshuhudia mwenyewe mzigo wa majaribio jinsi ulivyo.Na bado ujaona kabisa vitu borazaidi ya hapo.Kwanza nikwambie kitu kuna tekinorojia mpya ya ndege imebuniwa hapa yenye uwezo wa kuhisi kombora na kuhepa bila kuongozwa. Alinitolea maelezo yaliyo niacha kinywa wazi maana maishani mwangu nilifikilia kuendesha ndege bora kushinda zote sasa eti nasika wana teknojia iliyo nzuri na wamefanikiwa kuibuni ndege hiyo.Naweza kuku hulizia kitu ? Kabla ujauliza ingia ndani maana hapa kuna kanuni zake na itakubidi uzifuate kipindi chako chote cha kuwa hapa.Sheria ya kwanza inasema hivi (1)Kama wewe si mhusika wa sehemu za chemba huruhusiwi kuingia ikibainika umeingia kifo ni zawadi.(2)Ukitoa siri ya hapa kifo ni zawadi. Kama umenielewa usijari sana maana huu ni mwanzo na sheria utazisoma mwenyewe." mbona unanikwepa kwa kila swali ninalo kuuliza jina umenificha? " "kijana ujue eneo lote lina DSTV CAMERA na limepadwa mabomu ya kutosha" Niliingia katika chumba changu nilicho andaliwa maana tayari niliona sina mbinu ya kutoka katika mikono ya watu hawa kirahisi kama nulivyo ingia kirahisi maana ilinibidi nikubaliane na amri zao.Mtesaji huyo aliniacha katika chumba hicho nikiwa sina hili wala lile maana nilikwisha jua kazi yangu imeingia sehemu kubwa ambayo sikuitegemea kabisa kama nitakutana nayo.Ilipo timia saa tisa mchana simu iliyo kuwa katika chumba changu ili anza kuita.Nikaisogelea na kuipokea. "Njoo huku nje muda wa chakula soja umefika" ikakatwa sikupaata maelekezo ya kutosha ila ilini bidi kutii maana nilikwisha ambiwa kufuata amri katika kambi hii ni jambo la lazima hasa kwa mateka aliyepewa uhuru ndani ya kambi. Nilitoka nje kupitia mlango tofauti na ule wa mwanzo nilio tumia kuingia ndani ya jumba hili lenye vyumba vingi. Niliwakuta askari wengi wakuwa wamejipanga mstari kulingana na mavazi yao. Kuna kikosi niliona kimevaa sare za jeshi zenye rangi ya kijani kibichi.Hawa mara moja niliwatambua kwamba ni askari wa msituni . Nawengine walikuwa wamevaa kombati ya kawia iliyo kama overrol la watengeneza magari na katika kofia zao walikuwa na alama ya ndege.Nao nikajua hawa ni marubani.Nilipo endelea kuangalia niliweza kuwaona madakitari wakiwa katika mavazi yao ya kazi.Nikawa nimepata jibu langu la kwanza lililo nifanya niwafuatilie watu hawa tangu nikiwa somalia.. Nakumbuka mwezi mmoja nyuma nikiwa katika hoteli ya kifahali mjini Mogadishu katika disko la usiku waliingia Madaktari watatu na vijana watatu.Wakati wanaingia sikuwatilia mashaka maana niliona ni watu wa kawaida tu.waliingia katika eneo lililo jitenga wakaanza kubofya laptop zao ila vijana wao walikuwa wamesimama tuli kama walinzi wao. Baada ya muda kama wa nusu saa nili mshuhudia kijana mmoja kati ya wale akiinuka na kuanza kufanya vurugu kwa watu waliokuwa wakicheza mziki.Ilianza ikiwa ndogo ila baada ikawa babu kubwa maana watu hawakupenda kusumbuliwa na mtu mmoja .Ila kila aliyejipendekeza alihambulia vitasa vya kutosha maana huyu jamaa alikuwa ana spidi kama umeme.Ndani ya nusu saa ukumbi ukawa kimya maana kila aliyepata nafasi ya kutoroka alitoka nduki wala hakuna aliyekumbuaka kama ana bunduki wala amekuja na mtu kila aliyepata nafasi aliondoka nduki.Nikiwa nimekaa eneo langu la juu niliendelea kuchukua picha kwa siri maana nilikwisha pata habari ya kuuza asubuhi. Niliwashuhudia viongozi wazito wa waasi wa Somalia wakiwa kati ya washangilia walio salia katika ukumbi huo hakika hapo ndipo nilipo patwa na mashaka na watu hawa walio onekana ni Madaktari maana niliona wana ushirikiano na waasi wa Somalia alimaharufu kama A-lishababi kwa tafsiri ya kiswahili ni Vijana. Walionekana wakifanya biashara fulani ila kwa kuwa nilikuwa mbali ilinibidi nitulie nione mwisho wa mchezo.Sikuacha kupiga picha kila tukio muhimu lililo jitokeza.Baada ya mazungumzo wale Madaktari walitangulia kutoka wakawaacha wale vijana wao."Karibuni vijana hii ni Somalia kila raia ni mwanajeshi"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliwatolea maelekezo mmoja wa viongozi wa kikundi cha waasi cha AL-SHABBABI alionekana ni mtu wa mazoezi kwa mtazamo wake alikuwa amevaa mavazi yalio onesha ni mtu wa shari kabisa kwani alivalia kombati za jeshi kabisa zenye rangi ya kawia zikiwa na alama ya mwezi kwenye kola yake buti bora kabisa zilikuwa ndani ya miguu yake. "Naitwa Mahamudy Bin Salim ni jenero katika nchi hii na hawa ni wadogo zangu.Pleni sana vijana kwa kuingia katika majaribio ya kwanza katika nchi hii labda niseme tu ukweli nimewapenda jinsi mlivyo wachakaza vijana wangu.Maana wote mlio pigana nao ni wanajeshi bora ila nyinyi mmewazi ubora" Jenero Mahamud bin Salim alionekana ni muongeaji sana na muda wote alipokuwa akiongea kama mtu angelikuwa karibu naye basi angelowana maana aliongea kwa sauti kubwa na mate yalimtoka mdomoni kila aongeapo. Baada ya kuongea mambo mengi waliinuka kwenye viti vyao na kuanza kutoka nje ya ukumi huo.Safari yao iliishia katika magari ya kijeshi aina ya jeep yaliyokuwa yamepakiwa nje ya ukumbi huo.Sikuendelea kuwafuatilia maana ni hatari kwangu kuwafuatilia watu hawa kwani naweza kupoteza hata kile nilicho nacho. NDANI YA KAMBI YA ALISHABABI Magari ya mizigo yaliingia katika kambi ya Mashariki iliyo kuwa ikiongozwa na Salm bin Swalehe Mwarabu wa somalia mwenye nywele za timutimu. Salm bin Swalehe alijulikana Somalia nzima kwa ukatili wake na ubaguzi alio kuwa nao.Kama ungeliangukia katika mikono yake basi wewe ni chakula cha kisu ama risasi.Ukatili wake uliweza kuifanya kambi yake iwe miongoni mwa kambi bora za Al shababi kwa maana askari jeshi wake walikuwa watiifu.Uasi katika kambi hiyo ilikuwa ni ndoto. Magari hayo ya mizigo yaliingia moja kwa moja katika kambi hiyo hadi katika ghara lao la siraha. Salim aliwaagiza vijana wake wa vipimo kukagua mzigo huo baada ya kuona kwamba unalizisha kwa macho. "Mzigo ni ule ule mkuu ulio uagiza" Kijana wa Salim aliwasilisha majibu yake baada ya ukaguzi kukamilika. "Sawa wapatieni ruhusa waondoke nitawasiliana na mkubwa wao wa kazi" Kambi hii ya Salm kilikuwa ndicho kituo Muhimu kwa Kundi la Alshababi kwa maana dhana zao zote zilifikia hapo na kisha kusambazwa maeneo hatari yenye vurugu za vita. Na hiyo ndiyo kambi hatari zaidi niliyo weza kuishi nikiwa mpimaji wa siraha nisigundulike hadi siku umoja wa mataifa ulipo iangamiza kwa msaada wa ndege zisizo na rubani Dron.Mtoa siri nilikuwa mimi kwa kipindi hicho.(KISA HIKI UTAKIPATA KATIKA RIWAYA YA DHIKI KUU ) AMAZONI KAMBI YA BONDE LA MAUTI. "Kijana mbona umeganda hapo sogea mbele ujipange na wenzako hapo ujaja kushangaa kama ulizoea kupiga picha umekwisha" Ni sauti ya mwanajeshi aliye kuwa akiwasimamia wenzake katika shughuli hiyo ambayo sikujua maana yake maana tayari nilisha itwa kula ila sikuona dalilii ya chakula wala jiko eneo hilo.Nilisogea hadi nyuma ya madaktari hawa ambao bado ninawakumbuka vizuri kwani niliwahi kuwaona Somalia na leo hii ninakutana nao katika kambi hii ya BONDE LA MAUTI. Hakika hapa nilijua tayari nipo katika mikono ya watu wa aina gani hasa.Sikuvunjika moyo maana kati ya wakle madaktari niliweza kumuona yule mtesaji aliye kataa kuniambia jina lake lakini muda huu akiwa katika idara nyingine kabisa ya udaktari. "Karibuni vijana wapya katika kambi yetu ya kati inayojihusisha na kuanda mashine za kivita na hapo mlipo kila mtu anajua mwenyewe mahali alipo toka na sisi hilo si jukumu letu Kujua umetoka wapi.Napenda niwambie kitu kabla hamjaanza mazoezi ya ukaribisho kesho kutwa. Kambi hii imezungukwa na mabomu mazito pande zote yaani hakuna mtu kuingia wala kutoka pasipo ruhusa maaluum toka ngazi za juu kabisa.Wote waliomo katika kambi hii ni makomandoo bora kabisa kwa hiyo msifikilie kutoroka hata kwa dawa.Mbele yenu wapo walimu wenu walio katika nyanja mbalimbali maana wapo makomandoo upande wa siraha za nchi kavu na majini pia wapo marubani kama mnavyo waona hawa wote ni bora kabisa maana ni zao la kwanza la ngome hii nzito."Aliendelea kutoa maelezo ya msingi juu ya kambi hii hasa yakiwa ni kutuhasa tuondoe kichwani wazo la kutoka tukiwa hai katika kambi hiyo. Tayari niliona siko peke yangu aliye lazimishwa kutumikia kambi hiyo.Hawakujua mimi ni nani hasa ndilo kosa walilolifanya kubwa maana tayari kazi yangu ilikwisha anza tayari tena hata kabla ya muda wake kuwadia. "Natumaini kila mmoja ameshapata mwalimu wake na msimamizi atakaye mfunza kila kitu hadi pale atakapo kuwa tayari kufanya kazi iliyo mleta itimie."Baada ya maelekezo hayo kutoka kwa mwanajeshi huyo aliyekuwa amechafuka kwa nyota mabegani mwake akionyesha yeye ni Bligedia katika kambi hii alituruhusu tutawanyike.Sikuwa ninajua mahali tunapoelekea kwa muda huo zaidi nilibaki nimesimaa tuli nikitafakari kazi iliyo mbele yangu.Maana niliona ishakuwa ngumu maana sikujua wamenipangia mipango gani hapo mbeleni maana watu hawa walioneka dhahili ni watu wa shari.Nilishutuka baada ya kuisi mtu ananigusa katika bega langu la kulia nilipo geuka nilikutana na sura ya yule jamaa mtesaji akiwa tayari kabadilisha mavazi yake na wakati huu kavaa gwanda zake safi za kijani."Kijana mbona umeganda hapa uogopi kufumliwa kichwa namasnaipa?"Kuna masnaipa hapa ? "Mbona unauliza jibu kuwa makini maana wao wakikutilia shaka wanakuondoa maana wana roho ya mbwa watu hawa na hapa tulipo ni mahali pa kutolewa matangazo mtu asiye husika haruhusiwi kusimama wala kukaa ndani ya nusu saa maana kuna siri unaweza kuzisikia ambazo hazikuhusu." Maneno ya mtesaji yalinishutua mno ikanibidi nitoke eneo hilo kwa haraka maana inaonyesha nakaria nusu saa tangu nisimame hapo. "Mbona ujaenda kula ama huna njaa kabisa? Aliniuliza baada ya kuona ninaeleke kurudi ndani baada ya kukosa mwelekeo wa kambi hii. Nitakula nini mbona sioni jiko eneo hili lote ? Nilimrudishia swali baada ya kujibu swali lake. "Naona kijana bado ujanisoma maana unadhani chakula cha hapa kinapatikana kirahisi? Tupigane nikupe chakula."CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment