Search This Blog

Sunday 22 May 2022

RISASI NNE - 5

 







    Simulizi : Risasi Nne

    Sehemu Ya Tano (5)





    “Wesson and Smith, bastola ambayo baba yangu aliipata vitani mwaka 1944, baba yangu kapigana vita ya pili ya dunia, bastola hii na risasi nne, (akazitoa zile risasi na kuziweka mezani) hizi ndizo za kulipia kisasi, lazima zitafune kichwa cha Malyamungu,” Joru akamaliza kuongea na kuinua kikombe cha kahawa na kukiweka kinywani kabla ya kuvuta kwa hisia kahawa hiyo.

    “Joru, usifanye mchezo na kazi inayokukabili, kwa risasi hizi nne utamuua nani umwache nani?” Jack akauliza tena.

    “Jack, sihitaji kuua mtu zaidi ya Malyamungu na sasa wewe umeniongezea mwingine, kuua watu wawili kwa risasi nne kwangu mimi sio shida, nitatumia risasi mbili na mbili zitabaki,” Joru aliongea kwa kujiamini.

    “Inabidi uwe na shabaha ya kutosha,” Jack alimwambia Joru.

    “Sio shabaha ya kutosha tu, ila nina shabaha ya ajabu,” Joru aliongeza huku kikombe cha kahawa bado kikiwa mkononi mwake, bado hakijashuka chini. Jack alinyanyuka kutoka katika kiti chake akavuta hatua chache mpaka katika kabati kubwa akatoa bastola moja ya kisasa na kuja nayo mpaka mezani, akaiweka mbele ya Joru na kikasha cha risasi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nataka kuona shabaha yako ya ajabu,” Jack akamwambia Joru. Joru akaitazama ile bastola na kuinyanyua kwa mkono wake wa kulia mara tu baada ya kukiweka kikombe cha kahawa mezani, akavuta kile kikasha cha risasi akazipakua na kupakia risasi kumi ndani ya ile bastola, akavuta kiwambo cha sauti na kukifunga mbele ya mtutu wa bastola hiyo. Akainua macho na kutazama dirishani, dirisha la vioo, vioo ishirini na nane vilivyokuwa vimepangwa kwa ustadi, vilikuwa wazi vikiwa vimefunguliwa, kati ya kioo na kioo kulikuwa na uwazi wa sentimita zipatazo ishirini. Nje ya nyumba kulikuwa na mti mkubwa juu yake kulitua kungulu mmoja aliyekuwa akipiga kelele, Joru akaiweka vizuri ile bastola na kuinyanyua sekunde moja ilitosha kumlenga na kumfumua Yule kungulu.

    “Shiiiit, Impossible!!!” (haiwezekani!) Jack alishangaa kwa maana hakujua kama tayari Joru alikuwa akilenga kitu Fulani, hakuna kioo kilichovunjika lakini alishuhudia manyonya ya kungulu pale kwenye mti yakipukutika kwa fujo.

    “Naitwa Joseph Rutashobya, the point man,” Joru akajigamba. Jack alitikisa kichwa, akacheka kidogo na kugonganisha viganja vyake.

    “Basi sina shaka na wewe! Naamini unaweza kumlenga Malyamungu hata kutokea nje ya wigo wake, ijapokuwa tu umekiona kidole cha mguu wake,” Jack akasema na wawili hao wakacheka sana.



    §§§§§



    “Mtoto wa Mutebezi ndiye aliyemkaribisha kijana huyo,” mtu mmoja alikuwa akimwambia kibaraka wa Malyamungu, ambaye mara tu alipopata taarifa hiyo alipiga simu kwa Kalosi kule Jinja. Kalosi akatoa amri ya Jack Mutebezi kukamatwa ikiwezekana kuuawa pamoja na mgeni wake.

    Franko Besije, akatazama watu wake wapatao kumi aliofuatana nao kutoka Jinja kuja Masaka.

    “Inabidi twende Kampala, tukamuue Jack na mgeni wake, kazi inatakiwa ifanywe kwa ustadi wa hali ya juu sana, inasemekana Yule kijana ni hatari sana, kwa vyovyote Jack atakuwa kamkodi kwa ajili ya kisasi, bila kuchelewa, tayari kule kuna mtu anayewafuatilia nyendo zao na kila nukta ananipa taarifa, anasema bado wapo ndani ya nyumba mzee Mutebezi hawajatoka, sasa tusipoteze muda twendeni,” Franko aliwaambia wenzake, wote wakatoka na kuingia kwenye gari zao kisha kuondoka kwa kasi kutoka Masaka kuelekea Kampala.



    §§§§§



    Joru na Jack walitoka nje pamoja, wakaingia kwenye gari yao na kufunga milango, mbele yao kulikuwa na maduka mengi ya vitu mbalimbali. Jack alikuwa nyuma ya usukani, akatazama huku na huku na kisha taratibu akaitoa ile gari na kuiingiza barabarani. Safari ilikuwa ni kwenye nyumba ya Jack, nyumba iliyo mafichoni zaidi, kwani Jack alijenga mashambani. Ulikuwa ni mwendo mrefu kidogo barabara ya kuelekea Jinja. Jack kwa kuwa alikuwa mzoefu wa barabara hizo za Kampala alikuwa akipita vichochoroni.

    “Vipi, mbona unapita kwenye hizi njia mbovu, utaua gari yako,” Joru alimwambia Jack.

    “Kumbuka nilikwambia Malyamungu ana macho na masikio mengi, si ajabu hapa tunafuatailiwa,” Jack alisema.

    “Sio si ajabu, tazama kwenye kioo chako cha ndani, kuna gari nyeusi inakuja nyuma na nimeiona muda mrefu sana kila tunapokunja nayo inakunja papo hapo,” Joru akamwambia Jack. Jack akaendesha gari mpaka kwenye bar moja kubwa ya wazi, akaegesha hapo nje.



    “Chukua hii,” Jack akampa bastola Joru nay eye akachukua nyingine, “Tuketi hapa kama dakika kumi tumsome huyo mshenzi,” Jack alimwambia Joru na Joru akahafiki, wakateremka na kufunga milango bila kuweka lock wakaingia kwenye wigo wa bar hiyo na kuchagua viti vya pembeni, wakaketi. Wakaiona ile gari ikipunguza mwendo na kupita kidogo ile bar, Joru akaikazia macho kuona itasimama wapi, lakini hakufanikiwa. Ilipita dakika mbili, watu wawili waliovalia miwani nyeusi waliingia kwenye bar hiyo wakaketi karibu na mlango wa kuingilia. Jack na Joru wakawa wakiwatazama kwa chati wakijifanya hawana muda nao, wakiongea mambo yao. Mmoja wa watu wale alikuwa akaiandika ujumbe wa simu mara kwa mara.

    “Kaa mkao wa kula,” Jack alimwambia Joru.

    “Kwa nini?” Joru aliuliza.

    “Hawa maza faka nitawaanzishia msinambe sasa hivi,” Jack akamwambia Joru kwa kumnong’oneza.

    “Tufanye hivi, tuwaache kwa vyovyote watakuwa wanawapa taarifa wenzao, sasa unaonaje wakijikusanya ili tukiwaanzishia tunapukutisha wengi, unasemaje?” Joru alitoa pendekezo lingine. Jack alitulia kimya kwa sekunde kadhaa kisha akatikisa kichwa kuashiria kuwa amekubaliana na Joru. Wakaagiza vinywaji na vilaji wakawa wakinywa taratibu huku wakiendelea kuwatazama wale watu kwa makini, wakihakikisha hawawapotezi.



    §§§§§CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Franko na kundi lake walikuwa wakikaribia Kampala walipopata taarifa kuwa Jack na mgeni wake wapo katika The Great Nile Bar iliyopo katika viunga vya mji wa Kampala. Franko akawasisitizia kuhakikisha Jack na mgeni wake hawaondoki katika eneo hilo, na kama wakiondoka basi waendelee kufuatiliwa ili wanalizwe kabla hawajaleta madhara zaidi.

    Wale jamaa wakaendelea kunywa wakiwalinda Jack na Joru, wao kwa mawazo yao ni kwamba Jack na Joru hawajui lolote juu yao, kumbe hawakujua kama wanacheza na mwanajeshi wa Tanzania aliyekomaa katika medani za vita ijapokuwa hakuwahi kupigana vita ila hiyo ilitakiwa iwe ya kwanza, labda mwenyewe aliita ‘Kagera War II’.



    Saa kadhaa zikapita na ile bar bikazidi kuchangamka, watu walijaa na kujaa, madada wa kujiuza nao walikuwa wakiingia na vinguo vya ajabu ajabu, jua lilikuwa likituwa upande wa magaharibi na kufanya dhambi za Kampala kuchukua nafasi yake.

    “Joru, twende turudi, wewe ni sawa na kaka yangu au niseme ndugu yangu,” Jacj alianzisha mazungumzo.

    “Kwa nini Jack?” Joru akauliza.

    “Baba yangu mzee Mutebezi asili yake kabisa ni Kagera, Tanzania, alikuja huku miaka mingi sana wakati wa Obote, si unajua tena Wahaya na Waganda hatuna tofauti sana, na mwenyewe aliwahi kunambia kuwa kwao ni Mutukula” Jack alieleza.

    “Oh, Mutukula, home sweet home,” Joru alimalizia kwa kusema hayo, “Idd Amin alituma watu wake wakiongozwa na Malyamungu wakaua na kuchoma kijiji chetu chote hata sasa hakuna kijiji bali ni mapori na vichaka, Malyamungu alimuuwa mama yangu na baba yangu kwa bunduki aina ya Riffle, nakumbuka nilikuwa nimejificha kwenye vichaka na kisha hapo nilikimbia msituni,” akamalizia na machozi yakamtoka na kuyapamba mashavu yake, “Leo, jack Leo jua halitakuchwa bila kuishika roho ya Malyamungu mkononi mwangu,” akamaliza.



    “Joru, niliokota maiti ya baba yangu katika mto Kagera nikisaidiwa na wasamalia wema wachache, sikupenda kuitazama sana kwa sababu aliuawa kinyama sana, mkono wa Malyamungu ulifanya kazi hiyo akishirikiana na vibaraka wake, sote tunania mamoja, sote tuna kitu kimoja, sote tuna roho moja, sote tuna lugha moja,” Jack alimaliza kuongea na kugonga mikono yao.

    Joru aliziona gari mbili, land cruiser zikifika eneo lile, moja ilisimama upande wa kulia wa bar na nyingine ilipitiliza mpaka upande wa pili wa bar ile. Baada ya zote kusimama, watu kama kumi hivi waliteremka, kuna wale waliobaki nje na wengine wakaingia ndani na kuchukua nafasi sehemu mbalimbali na kuketi kisha wakaagiza vinywaji.

    “Kagera War II has to began,” (vita ya pili ya Kagera itaanza punde) alisema Jack huku akimtazama Joru.





    Joru akambania jicho moja kaushiria kuwa amemuelewa kwa lile alilosema. Dakika mbili zilikuwa nyingi sana, Joru na Jack wakagundua kuwa wamezingirwa pande zote na hao adui zao, Joru aliwatazama mmoja mmoja kisha akarudisha macho yake mezani.

    “Bila shaka kikosi chote cha Malyamungu ndiyo hichi!” Joru alisema.

    “Kwa ninavyoelewa mimi hawa wako kama kumi kuna wachache sana kule nyumbani,” Jack akamwambia Joru.

    “Safi, sasa hawa tunawafanyia hapa na kuwapunguza kadiri ya uwezo kisha tunaunganisha mpaka Jinja leo hii, lazima kazi imalizike na mi kesho nirudi Mutukula kabla hawajanikamata kwa maana nimevunja sheri ya kutoka nchini bila ruhusa ya mkuu wangu,” Joru.

    “Haina shaka mkuu,” Jack akaitikia na kunyanyuka kuelekea chooni, hiyo ilikuwa ni mbinu mojawapo ya kuanzisha mashambulizi katika eneo hilo, Joru alitazama vizuri na kujaribu kuona kama atalazimika kutumia silaha basi asiwazuru raia wengine, lakini alipenda atumie mikono yake zaidi.



    Baada ya Jack kutoka kwenda chooni, wawili wa wale jamaa nao walinyanyuka kuelekea upande ule, Joru alikuwa akiwaangalia jinsi wanavyojipanga na kunong’onezana hili na lile. Mmoja wao akaingia chooni na mwingine akasubiri mlangoni.

    Jack akiwa anajisaidia alihisi kushikwa bega, akageuka akakutana na mmoja wa wale vijana.

    “We vipi mbona? Mbona unakatisha watu starehe zao?” Jack akauliza.

    “Starehe?! Starehe we unaijua?” Yule kijana akauliza tena kwa kejeli. Jack akageuka ghafla na kiwiko cha mkono wake kikatua katika tumbo la Yule jamaa.

    “Aaaaaaaaiighhh!” akatoa yowe hafifu la uchungu huku akiwa kajishika tumbo na kujiinamia, Jack hakupoteza muda alimpiga kifuti kwa ule mguu wake mzima katika paji la uso na yule jamaa akahamisha mikono kutoka tumboni na kushika paji lake. Hakujibu shambulizi lolote, alikubali kufa kikondoo, aliposimama akakutana na uso mbaya wa Jack uliojikunja ndita za kutisha.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwa nini mnanifatafata sana hayawani nyie? Leo nakumaliza bila wenzako kujua fala mkubwa,” Jack alikoroma kwa sauti nzito huku jamaa akibaki kato macho, Yule jamaa aliingiza mkono nwenye kiuno cha suruali yake kwa haraka lakini Jack akamuahi, alimpiga kichwa kimoja maridadi, jamaa akayumba na kujibamiza ukutani, kabla hajajipanga na bastola yake mkononi, Jack aliruka na kuipiga teke ile bastola, ikamtoka mkononi na kuanguka pembeni. Yule jamaa kajirusha mzimamzima kuiwahi, lo, alikutana uso kwa uso na teke kali la mguu wa bandia likampasua katika paji la uso, kisha Jack akamkamata ukosi wa shati lake na kumnyanyua, hakuongea lolote, almtumbukiza kichwa katika singi la kunawia mikono na kulijaza maji. Yule jamaa alihangaika ili ajinasue lakini wapi. Akiwa katika purukushani hizo. Yule wanje alishangaa mwenzake anachelewa kurudi, tayari ilikuwa dakika tatu zimepita, akaamua kuingia chooni akipishana na watu wachache wanaoingia vyoo vingine bila kujua nini kinaendelea kwenye choio cha VIP, mlango ulibamizwa na Yule kijana wa pilia akaingia na kukuta jamaa yake tayari akiwa hana uwezo wa lolote. Akiwa katika kutahamaki tayari Jack alitoa bastola yake kwa haraka na kuifyatua moja kwa moja katika moyo wa kijana Yule, akapaishwa na kubamizwa ukutani kisha akatua chini kama gunia.



    “Wasalimie kuzimu,” Jack akajisemea kwa sauti ya chini, kisha akajiweka sawa na kutoka ndani ya choo kile.

    Joru alishangaa Jack anachelewa kutoka, akajua kwa vyovyote watakuwa wamembananisha, alitamani anyanyuke amfuate lakini mpango haukua hivyo. Lakini aliona hakuna jinsi ni bora anyanyuke akamsaidie mwenzake. Alipoinuka tu watu wawili waliokaa nyuma yake wakamdaka na kumshika kutoka nae nje. Bila fujo Joru alitulia na kukubali kuswagwa nje kama ng’ombe aendaye machinjioni.

    “Umekamatika leo!” Franko alimwambia Joru pindi alipofikishwa mbele yake, “Mpakieni kwenye gari tukamuue mbele,” akaongezea kisha yeye akageuka na kutangulia garini. Joru aliongozwa akiwa ameshikwa huku na huku kuelekea kwenye gari. Kama kuna kitu alikuwa anakisubiria basi ilikuwa ni hicho cha kulikaribia gari, akiwa ameshikwa na vijana wawili wakakamavu, nyuma tena kulikua na wengine wawili wenye silaha za moto ndani ya makoti yao wakati wengine bado walikuwa wakiendelea kuangalia hili na lile kama kuna shida yoyote itakayojitokeza.



    Joru kwa kutumia miguu yake miwili aliikanyaga bodi ya gari na kutembeza miguu yake kama mtu anayepanda juu kisha akaruka sarakasi kwa mtindo wa back wale waliomshika wakajikuta akiatoka mikononi, wakamuona akipita juu ya o na kutua nyuma kabisa ya wote wanne. Mmoja wa nyuma mwenye silaha aligeuka haraka lakini si matarajio yake alikutana na konde moja zito la kulia kutoka kwa Joru, bila kupinga akaenda chini mchangani, Yule mwingine alikuwa akijiandaa kutoa bunduki yake, ‘too late’ Joru alimsukuma kwa kanyagio la mguu wake tuymboni akarudi nyuma kama mita moja kisha teke kali lilimtoka Joru na kutua shavuni kwa Yule jamaa naye bila kipingamizi alitua chini.

    Sasa wale vijana walikuwa kama mbogo aliyejeruhiwa. Joru alijirusha juu na kuichanua miguu yake yote miwili, mateke hayo yaliwapata sawia waliokuja kusaidia, Joru akajidondosha chini na mara juu yake akaanguka mtu mfu aliyekuwa akivujwa damu kichwani, alipopepesa macho haraka alimuona Jack akiwa na bastola mkononi. Joru akabingirika na kupita uvungu wa gari, lakini alipoibuka upande wa pili, guu la Franko lilimkanyaga tumboni kwa nguvu.



    “Mende wewe unajifanya unajua kupigana sio? Haya pigana na mimi marehemu niliyeshindikana kuzimu mpaka shetani akanirudisha duniani,” Franko alimwambia Joru aliyekuwa kabana meno kwa maumivu.

    “Wapiganaji huwa hatuna maneno mengi,” Joru akamwambia Franko na muda huo huo, Joru akajizungusha kiufundi na kuchomoka katika mguu wa Franko, kisha akiwa bdo yuko chini hajajiinuwa alipiga teke moja kali lililotua kwenye visigino vya Franko, ilikuwa ni ngwala moja maridadi ambayo Joru tangu aanze mafunzo yake hakuwa kuitumia. Franko alinyanyuliwa mzimamzima kwa nguvu ya ngwala ile kabla hajafika chini Joru aliinuka haraka na kumdaka kisha akamshusha kwa nguvu katika goti lake na kuuvunja uti wa mgongo wa Franko. Bado jamaa waliobaki walikuwa wakimuandama Joru.



    Joru akatazama huku na huko kulikuwa na kijana mwingine aliyekuwa akija kwa kasi, kwa nguvu zake zote Joru aliinuka na Franko mikononi mwake na kumrusha kwa Yule jamaa lakini jamaa alikuwa makini sana akaukwepa mwili wa Franko kwa kuruka sama soti safi kwa maana alikuwa akijua mbinu ya Joru, lakini Joru alishangaa kumuona jamaa akitua chini akiwa mfu damu zikichurizika katika kisogo chake.

    “Brotherrrrrr!!!!!” ilikuwa sauti ya Jack ikimwita Joru, Joru alipogeuka aliona Jack akiwa kwenye wakati mgumu, sasa muda wa mikono haukuwa na nafasi, aliichomoa bastola aliyopewa na Jack, kwa kupitia uvungu wa gari, alifyatu risasi tatu zilizowatosha vijana haoa na kuwasambaratisha chini, Jack akachomoka akiwa anachechemea, watu walijaa eneo lile kuangalia mapambano hayo, ving’ora vya polisi vilisikika baada ya kupata taarifa ya uhalifu kutoka kwa meneja wa bar ile. Joru alimsaidia Jack na kumpakia kwenye gari la wale jamaa, kumbe dereva muda wote kajificha ndani hakutoka, Joru alipotaka kuingia kwenye usukani akamkuta dereva huyo kajikunyata kimya.



    “Endesha gari mpaka kwa Malyamungu,” Joru alimwamuru kisha akaingia upande wa pili, “Endesha haraka,” Joru aling’aka huku akimpa mbata moja kali iliyomfanya Yule dereva kujigonga katika usukani na gari ikapiga honi. Dreva akaiondoa ile cruiser kwa kasi kutoka eneo la ile bar kuingia barabara ya vumbi iliyowatolea Barbara kuu kisha wakaambaa zao na barabara ielekeayo Jinja.

    “Ongeza mwendo!!!!” Joru alimkaripia Yule kijana naye akaongeza mwendo kuelekea huko wanakotaka watekaji wake.

    “Pole Jack, nilijua wamekuweza wale, maana nilipoinuka tu wakanibana,” Jiru alimwambia Jack.

    “Hapana, niliwadhibiti wote wawili, wale mende tu, mtu niyemhofia ni Franko pekee kwani Yule jamaa mtata katika mapigano lakini nimeshangaa umemmaliza kama unavunja chawa,”

    “Nililijua hilo ndo maana nikatumia ujanja kummaliza,” Joru alijibu.



    §§§§§

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kalosi alikuwa katulia juu ya kiti chake cha magurudumu ndani ya ofisi nyeti ya baba yake, aliitazama saa ya ukutani ilimwambia inakaribia saa mbili kamili, akawasha televisheni UBC ili kupata habari za siku hiyo, lakini kabla hajaanza hata kuangali, simu ya mezani iliita, ilimtaka akajumuike na wenzake wa familia kwa chakula cha jioni.

    Dakika kumi baadae katika nyumba ya Malyamungu ambayo ilikuwa na ulinzi mkali na ilifungwa kamera za usalama zilizoweza kuona kila kitokacho na kuingia, Kalosi alikjiunga na wenzake, wakaketi mezani na mhudumu wa nyumba alikuwa akiwahudumia kwa vyakula na mapochopocho mbalimbali. Meza ilikuwa na watu wane, Malyamungu, mkewe na vijana wao wawili, Kalosi na Mark.

    Kalosi na Mark walikuwa najeshi tangu mwanzo, ila Kalosi aliamua kuacha baada ya baba yake kumdokeza lile analotaka kufanya, lakini Mark yeye alibaki jeshini akilitumikia taifa. Siku hiyo wote walikuwa nyumbani mezani wakisehereheke siku kumbukumbu ya siku ya ndoa ya baba na mama yao. Ilikuwa ni furaha kwa wane hao, vinywaji na nyama za kila aina zilikuwa zikiishia katika matumbo yao. Kupitia kamera za usalama waliona ile Cruiser ikiingia getini.

    “Mbona iko moja?” Mark aliuliza.



    “Ngoja tusubiri ripoti, kalosi alijibu na wote wakaendelea kuburudika,”

    Gari iliyowabeba Jack na Joru ilifika getini, Yule askari bila kuangalia akafungua geti na ile gari ikaingia ndani bila tabu, ikajivuta polepole kuelekea eneo la maegesho.

    “Simama hapa!” Joru aliamuru, ile gai ikasimama. Joru akatazama huku na kule. “Nyumba ya Malyamungu ipo wapi kati ya hizi?” Joru akauliza.

    “Inayowaka taa ndani,” akajibu Yule dereva. Joru akateremka na kumwamuru Jack aende na dereva Yule mpaka maegeshoni. Ikawa hivyo, Joru akapita kwa kuinama kufuata seng’enge iliyofunikwa vizuri kwa maua ya bugamvili akiwa kainama na bastola yake ileile ailiyopewa na Jack ikiwa mkononi.

    Mbwa wakaanza kubweka baada ya kupata harufu ngeni katika eneo lao. Joru hakupenda kelele za mbwa hao kwani alitaka kuingia kimya kimya katika nyumba hiyo, aliangalia kule sauti ya mbwa inakotokea na kuwaona mbwa wawili wakubwa wakija upande wake bila kuchelewa wala hakuwapa muda wa kumfikia risasi mbili kila mmoja ya kwake zilifanikisha kuwazima bila kelele, wakajibwaga katika nyasi na kupumzika kwa amani.

    Joru aliendelea kutembea taratibu kwa hadhari kubwa akitazama huku na kule.



    ‘…Damu ya Rutashobya haiwezi kupotea hivihivi…’



    Sauti ya baba yake ilianza kumrudia kichwani mwake nakumfanya Joru kushikwa na hasira zilizojaa gadhabu, akaongeza kasi ya miguu yake kuielekea nyumba ile akihakikisha kuwa hakuna anayemwona.



    ‘…Aaaaaaaaiiiiggghhhh, kimbia Joseph kimbia…





    JACK MUTEBEZI akiwa bado kamuwekea bastola Yule dereva alimuamuru kuegesha gari mahali pa kila siku anapoegesha. Hii ilikuwa ni kutaka kutowashtua wale walio ndani ya eneo hilo, kuanzia na walinzi mpaka malyamungu mwenyewe. Yule dereva akaegesha gari mahali pake na kutulia palepale kwenye usukani, Jack alizungusha macho yake huku na kule akatzama mazingira hayo yaliyokuwa yakimulikwa na taa zenye mwanga mithili ya mbalamwezi. Hakumuona Joru, lakini aliamini kijana huyo hawezi fanya makosa, Jack hakuweza kushuka na kufanya lolote kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia katika mguu wake ambao ameuunganisha na ule wa bandia kutokana na mikikimikiki aliyokumbana nayo siku hiyo. Alitulia katika siti ya nyuma akijaribu kufanya kitu ambacho ama kitakuwa msaada kwa Joru au kitasogeza mbele azma yao. Jack akageuka kwa dereva na kumkuta akiwa kakodoa macho yake mbele ya usukani.

    “Zaidi ya walinzi, kitu gani hapa kinasaidia ulinzi?” Jack akmuuliza Yule dereva.

    “Aaah mbwa na kamera za usalama,” akajibu kwa kitetemeshi.

    “Wapi ambapo kamera hizi zinongozwa?” akahoji.

    “Kuna sehemu mbili, moja ni nyumba kubwa na nyingine ni kibanda kile kule,” akajibu na kuoneshea mkono katika kibanda kilichopo umbali kama wa mita mia na hamsini hivi. Jack akaona hapo patakuwa pagumu kwa Joru kuifikia nyumba ile kama kamera hizo zitaendelea kufanya kazi. Akamwamuru Yule dereva ampeleke mpaka kwenye kile kibanda.

    “Kwa muda huu ni hatari kaka, watatuona tu halafu hawatatuacha hai,” Yule dereva akasema.



    “Kwa hiyo we unaogopa kufa?” Jack akamuuliza.

    “Ha! Kuna mtu asiyeogopa kufa?” Yule dereva akauliza. Jack akamuamuru kuteremka na kumtaka amuongoze mpaka kwenye kile kibanda, akimuoneshea bastola Yule dereva akateremka nje ya ile gari huku mikono yake ikiwa kichwani na kuongoza njia, Jack alikuwa nyuma yake akiwa na bastola yenye kiwambo cha sauti, walijaribu kupita kwa kujificha ili kamera isiweze kupata picha yao. Mahala Fulani hawakuwa na ujanja, kwani juu ya ule mlango wa kile kibanda kulikuwa na kamera inayaotazama mbele na hakukuwa na njia nyingine isipokuwa hiyo tu. Jack alipoinua macho akakutana uso kwa uso na kamera hiyo.

    “Shabash!” akajikuta akitamka neno hilo kwa hasira. Kwa kuwa alishajua kuwa ameonekana, akavuta hatua za haraka huku akimsukuma Yule dereva mpaka mlangoni, akatulia na kutazama huku na kule kama kuna alam yoyote endapo atagusa mlango huo.

    “We! Fungua mlango,” alimwamuru Yule dereva. Yule dereva akasita hakuufungua ule mlango, “Hutaki? Nakufumua kichwa chako sasa hivi,” Jack alimpa kitisho Yule dereva, lakini jamaa alionesha ununda wake. Jack akashikwa na hasira, akairudisha bastola kiunoni mwake, kitendo hicho kikamfanya Yule dereva kuanzisha shambulizi la ghafla, aligeuka na kumtandika ngumi moja kali Jack, Jack hakutegemea pigo hilo, hakuwa amejiandaa, kabla hajajiweka sawa, konde la pili na la tatu yakamuishia, akatema damu. Alipotaka kuchukua bastola yake ikamponyika na kuanguka chini, Yule dereva akaipiga teke ikaenda mbali kidogo, hakuna ujanja.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nalipiza kisasi cha rafiki zangu uliowaua kule The Great Nile Bar, na nakuhakikishi hamuwezi kufanikisha azma yenu kwani hivi sasa kamera zimekwishakuona wewe na mwenzio, zitazame hii, ile, na ile kule,” yule dereva alikuwa akimwambia Jack, ijapokuwa Jack aliambiwa atazame kamera hizo lakini aliujua ujanja huo, akajifanya anageuka ili atazame, Yule dereva aliachia konde zito, Jack aliliona akaepa na kuudaka ule mkono akageuka nao na kuuvunja kwa kuupinda begani mwake.

    “Utajutia uamuzi wako!” alimwambia Yule dereva, akambeba na kumbwaga chini kwa mbele, hakumchelewesha alimkanyaga kwenye koo lake, “Ulifikiri mi ni wa kuchezewa?” Jack aliuliza. Kabla hajakaa sawa kummaliza Yule jamaa alisikia michakacho ya miguu inayokuja upande huo. Mara risasi kama tatu zikasikika upande wake, kajirusha na kuinyakuwa bastola yake kisha kwa samasoti moja akatua nyuma ya maua marefu akatulia kimya.

    “Kadondokea wapi?” mmoja wa walinzi akauliza.

    “Simuoni, atakuwa kajificha,” mwingine akajibu huki akichomoa simu ya upepo na kutaka kuita malindo mengine. Jack akaona sasa mambo yataharibika, akaruka juu kama mzimu na kutua juu ya wote wawili na kwenda nao mpaka chini kisha akajinyanyua haraka na kutua pembeni, risasi moja ikafumua ile kamera ya mlangoni.



    Alipojaribu kupiga risasi nyingine, lo, bastola imeishiwa, hamna risasi katika chemba yake. Akaipachika kiunoni mwake na kumkabili mmoja wao aliyekuwa karibu kwa mikono. Makonde matatu ya nguvu yalivunja shingo ya askari Yule, wakati huo Yule wa pili alikuwa akija kasi, kwa umbali aliomfikia asingeweza kumshambulia na alishindwa kurudi nyuma ili atengeneze nafasi hiyo, akatumia mbinu ya kijinga, akamrukia na kuanguka nae chini kisha akajiviringa pembeni, lakini Yule mlinzi aliyeonekana hodari kwa michezo hiyo alijinyanyu kiufundi na kuwa wa kwanza kusimama. Jack kabla hajajiinua teke moja la mbavu lilimfanya agune kwa maumivu, akajitupa mbali na kujifanya kaelelemewa na maumivu, Yule mlinzi akaona tayari ushindi wake umeonekana akamjia taratibu kwa madaha. Jack akajifanya anajiinua kwa tabu na kujirudisha chini, kumbe alikuwa anasubiri akaribie.

    Jack alifuta mguu wake mzima kwa kasi na nguvu na kumpiga jamaa ngwala moja maridadi, Yule mlinzi bila kipingamizi alijibwaga chini na kukutana na bisu kali lililodidimia kifuani mwake, macho yakamtoka, roho ikatengana na mwili. Joru akaamka na kuchukua risasi akaijaza bastola yake, mara nyuma yake akasikia mlio wa bastola inayoondolewa usalama.



    “Tulia hapo ng’ombe wewe! Weka bastola chini na unitazame ili nikurarue vizuri,” alikuwa ni Yule dereva aliyevunjwa mkono akiwa ameshika shotgun ya mmoja wa wale walinzi ambao tayari walikuwa marehemu. Jack akaweka bastola yak echini, kisha akageuka kwa kasi na kurusha kisu kilichokuwa kimebanwa katika kizibao chake alichovaa juu, Yule dereva alijikuta koromeo lake likichanwa vibaya na kisu hicho, akarudi ardhini alikokuwa amelala tangu mwanzo na kuyaingia mauti. Jack akaokota bastola yake na kuwasachi wale jamaa mmoja kwa mwingine, hakuna cha maana isipokuwa alikuta kila mmoja akiwa na kidubwasha kidogo kilichokuwa kikiwaka taa nyekundu, alipokichunguza aligundua ni maalum kwa dharura na msaada, akagundua kuwa Yule dereva atakuwa alikibonyeza muda Fulani ndio maana wale walinzi wakaja kumsaidi. Jack akavikusanya vyote na kuvivunjavunja kisha akauendea mlango nwa kile kibanda na kuufungua kwa risasi moja, alikuwa amekwishachanganyikiwa, hakujua kama Joru mzima au la. Akaingia ndani ya kile kibanda na kukutana na mitambo ya usalama, luninga ndogondogo zilizokuwa zikionesha kila kona ya eneo lile, akatazama zote hakuna hata moja ambayo ilimuonesha Joru wala mtu yeyote. Hakuna linguine, aliifuata switch kubwa na kuizima, kamera zote zikazimika. Pembeni akaona kikabati cha chuma, kikabati kama cha kuwekea pesa benki ambacho komeo lake ni kama usukani wa boti, akakiendea, alipotaka kukigusa moyo wake ukasita, akafikiri mara mbili na kuamua kujipanga kwenda nyumba kubwa yeye mwenyewe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    §§§§§



    Tafrija ya familia iliyokuwa ikiendelea ndani ya nyumba ya Malyamungu, ilisita ghafla, Kalosi aliona kama kivuli kimepita katika moja ya vijiluninga vilivyopo katika sehemu maalumu ya sebule kubwa ya Malyamungu. Kila mtu akatulia, Kalosi akaziendea zile luninga kutazama ni kitu gani. Sheria ya eneo hilo ilikuwa ni kutotembea usiku hata kwa walinzi labda kwa ruhusa maalumu, hii ilikuwa ni kuruhusu wale wasio wahusika kuonekana kiurahisi na kamera hizo. Alipokaribia zile runinga mara ghafla zikazimika zote kumi na mbili.

    “Shiiitttt!” akang’aka.

    “Vipi?” mdogo wake akauliza, alipozitazama zile runinga zilikuwa giza, akachomoa bastola yake na kuiweka sawa.

    “Wazee, tulieni hapahapa, ulinzi dhidi yenu upo imara,” aliongea mdogo wa Kalosi ambaye ni mwanajeshi katika jeshi la Uganda, UPDF. Akajiweka tayari kwa lolote ili kuwalinda wazazi wake, bastola mkononi, akawa akichungulia nje kupitia dirisha moja baada ya jingine. Kalosi akatoa sonyo refu na kuuendea mlango mkubwa wa nyuma hiyo.



    “Mark, weka ulinzi nakuja, ngoja niende control room,” Kalosi akamwambia mdogo wake Mark aliyekuwa bado anaangalia angalia nje kupitia madirisha ya nyumba hiyo. Akamuonesha ishara ya dole gumba kaka yake akimaanisha ‘poa’.

    “Hapohapo ulipo tulia, hutoki kwenda popote, rudi ndani,” ilikuwa sauti kavu ya Joru ikimwamuru Kalosi. Kalosi alitazamana na domo pana la bastola aina ya Smith and Wesson, akatulia hana la kufanya. Joru akampa ishara ya kurudi alikotoka. Mkono wa kushoto Joru alikamata bastola nyingine iliyofungwa kiwambo cha sauti.

    “Rudi ndani,” akamwamuru tena Kalosi, “Usigeuke, rudi kinyumenyume mpaka nitakapokwambia,” Joru aliendeleza amri. Kalosi hakuwa na ujanja alianza kuvuta hatua kwa nyuma huku mikono yake ikiwa hewani.

    Mark aliposikia amri hiyo akajua tayari kumekucha, akajificha nyuma yan pazia kubwa ambalo lilikuwa kama mita tano kwa umbali tokea pale mlangoni, hivyo angeweza kumuona kwa uzuri Joru atakapoingia, aliiweka tayari bastola yake na kuikamata vyema kabisa, alianza kumuona Kalosi akiingia akiwa anarudi kinyumenyume. Akasubiri zamu ya Joru kuingia ili ammalize palepale, akaiinua bastola yake na kuielekeza kule mlangoni.



    §§§§§



    Jack aliendelea kutazama lile kabati la chuma, akapiga moyo konde na kuinua bastola yake, risasi mbili tu alikuwa amekwishafumua kitasa imara kabisa cha kabati hilo akaukamata mlango na kuuvuta, likabaki wazi, Jack hakuamini macho yake, mabunda ya noti yalikuwa yamepangwa kwa ustadi wa hali ya juu kabisa, akatazama huku na kule akachukua box la ukubwa wa wastani akayasunda ya manoti pamoja na kuliweka mezani. Chini kabisa ya zile noti alikutana na mabomu ya kurusha kwa mkono, guruneti, akatikisa kichwa.

    ‘Hivi hawa walikuwa wanajua siku moja kutakuwa na vita au vipi?’ akajiuliza Jack, ‘Sasa leo haya yatafanya kazi maalum hapahapa,’ akajijibu kisha akanyanyua lile boxi na kuiendea switch ya umeme, akazima taa zote za nje, giza likatawala. Jack akakenua kwa furaha ya kupata uficho huo. Akatoka na kutembea taratibu na lile box mikononi mwake mpaka kwenye ile gari, akatazama ndani hakuna funguo, akasonya, hakujua nini cha kufanya, akaamua kulitupia ndani lile box na kisha yeye mwenyewe kuamua kuikabili nyumba kubwa, akawa akitembea polepole mkono wa kulia akiwa na bastola yake na kushoto akiwa kakamatia bisu lenye hasira. Akazifikia ngazi na kuzikwea taratibu. Kitu cha kustusha kilimtokea, mbele yake alikutana na damu inayotiririka kwenye ngazi ikitokea ndani ya hiyo. ‘Joru!’ akajiwazia kwa mshtuko na kuongeza nguvu kuzipanda zile ngazi kuielekea ile nyumba.



    §§§§§



    Mark alijiweka tayari kwa shambulizi la ghafla lakini kabla hajafanya lolote, mfanyakazi wa ndani aliyekuwa akitokeas kwenye korido kuja sebuleni alikuta hali ile ya hatari, akapiga kelele za kushtukiza, kelele za woga, ambazo zilimvuruga kila mtu mle ndani. Mark alipoteza umakini kutokana na kelele hizo, akafyatua risasi lakini alipokuwa akiondoa usalama wa bastola ile Joru alikwishajua kuna hatari, tayari akajitupa chini huku bastola yake ngangari mkononi, ile risasi ikakosa shabaha na kuchimba ukuta. Yule binti akakimbia kutoka nje, hakuumaliza mlango kwani risasi nyingine ya Mark aliyomlenga Joru iliishia kwa Yule binti, akabwagwa chini chale damu zikitiririka kwa kasi. Joru muda huo huo akiwa chini hakupoteza nafasi, teke moja kali likamwangusha Kalosi kabla hajafanya lolote, kisha yeye akajiinua na haraka kugeuka kule ilikotokea ile risasi, nyuma ya pazia, bastola zote mbili mkononi, moja ikimtazama Kalosi aliyekua akijiinua na nyingine ikimtazama Mark pale dirishani alipokuwa kapigwa na butwaa baada ya kuona mwili wa msichana wa kazi ukimalizia tone la mwisho la uhai wake.

    Kwa kutumia bastola yake akamuonesha ishara Mark ya kuungana na mwenzake. Nukta hiyphiyo mlango ukasukumwa, Jack akajitoma ndani huku akijirusha sarakasi ili kupoteza shabaha ya yeyote aliyekusudia kumlenga, alipotua na kusimama tu, Mark alichomoa bastola nyingine na kuifyatua.

    “Aaaaaaaiiiiggghhhhh!!!!!” yowe la uchungu likamtoka Jack.





    Kitendo cha Jack kuanguka chini kilimuuma sana Joru, lakini hakuona haja kwanza ya kumsaidia wakati pembeni yake ana adui waliomzunguka. Aliuma meno na kuikamata sawia bastola yake aina Smith and Wesson, aliifyatua trigger na bastola ile ya kizamani ikato mbanjo wa aina yake, risasi yake ikmfikia Mark usawa wa moyo na kumpaisha mpaka kwenye kioo cha dirisha, alijipigiza na kutoka nacho nje, chali bila uhai. Joru akatikisa kichwa kwa kazi murua iliyoonesha na bastola hiyo ya kizamani. Kalosi alitaka atumie nafasi hiyo kumshambulia Joru, akachelewa, Joru alikuwa tayari amegeuka na kumzuia kwa teke moja kali lililotua tumboni na kumfanya Kalosi kujiinamia. Joru akamwamuru kuinuka.

    “Mfunge huyo kitambaa zuia damu” Joru akamwamuru Kalosi, amri hiyo ilimfanya Kalosi kujisikia vibaya sana akakaidi, kwa kumwangalia Joru kwa jicho la dharau.

    “Wewe ni nani?” sauti ya Malyamungu iliyafikia masikio ya Joru pale aliposimama.



    “Unataka kunijua? Subiri dakika moja tu,” Kisha akamtazama Kalosi na kumuamuru aelekee pale alipoketi baba yake. Kalosi akatii.

    “Kaka vipi?” Joru alimuuliza Jack.

    “Niko sawa, ni mkwaruzo tu begani,” Jack akajibu. Joru akiwa kamuweka kwenye shabaha Malyamungu na Kalosi alianza kunagusha machozi.

    Vilio vya uchungu vilimrudia masikioni mwake, alimkumbuka babaye na mamaye, jinsi walivyouawa kikatili na mtu huyo aliketi mbele yake.

    “Laiti ungejua kuwa siku hii inakuja basi ungeomba Mungu akuchukue mapema, wewe ni Malyamungu na mimi ni mali ya Mungu,” Joru aliongea kwa uchungu sana, “Sipendi kukuua lakini baba yangu uliyemuua pamoja na mama yangu na wanakijiji wengine, wamenituma, tangu mwaka ule wa 1977 leo hii nimekuja kutimiza azma hiyo, naitwa Joseph Rutashobya kutoka Tanzania, Mtukula ndani ya mkoa wa Kagera, Malyamungu huna haja ya kuishi kwa sasa, sina haja ya kukupa nafasi ya kusali kwa mara ya mwisho,” Joru aliongea kwa uchungu sana.

    “Joru, shoot them,” (Joru walipue hao!) ilikuwa sauti ya Jack kutoka pale chini. Joru aliisikia sauti ya Jack, akainua bastola yake na kulenga paji la uso wa Malyamungu, kisha akamwambia Joru.

    “Mimi nilishuhudia baba yako akimuua mama yangu na baba yangu, na wewe sasa ni dhamu yako kushuhudia hay ohayo,” Joru alimaliza na kuiweka tayari bastola yake ya kizamani iliyokuwa na risasi tatu tu baada ya ile moja kumuua Mark. Akaifyatua kwa hasira, na risasi moja ikatawanya kichwa cha Malyamungu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Noooooooooo!!!!!!” ilikuwa sauti kali ya kike, mama wa Kalosi aliibuka kutoka uvungu wa meza akiwa na shotgun mkononi mwake, akairusha kumrushia kalosi ili afanye yake. Kakutana na shabaha kali ya ajabu kutoka kwa Joru, ile shotgun ilipigwa risasi kwa kutumia bastola ya kisasa ambayo Joru aliikamatia mkono wake wa kushoto, na kudondoshea pembeni. Kisha mkono wake wa kulia ukafyatua tena bastola ile ya kizamani na mama wa Kalosi akatupwa chini akiwa hana uhai.

    Kalosi alishaindwa kuvumilia kushuhudia wazazi wake wakiuawa namna hiyo ilhali yeye yuko kando akitazama. Akamvamia Joru na kuanza kumshambulia, teke la kwanza lilitoa ile bastola mkononi mwa Joru, teke la pili likampata joru ubavuni, Joru akajipinda kutokana na maumivu aliyoyapata, akatema kipande cha damu. Kalosi akainua chupa ya pombe kali na kumrushia Joru, Joru akaruka hewani na kuipiga teke maridadi ikamrudia Kalosi na kumpiga usoni. Kalosi kabla hajajiweka sawa na bunduki nyingine mkononi, alijikuta akipaishwa na kujipigiza ukutani kisha akajibwaga chini bila uhai. Joru akageuka na kumuona Jack akiwa na bastola ile aliyoidondosha, bastola ya kale, Smith and Wesson.

    “Asta la vista Kalosi,” Jack alisema kisha akaanguka sakafuni mzima mzima.



    “Jack, Jack, Jaaaaaaccckkkk!!!!” Joru aliita kwa nguvu. Baada ya sekunde kadhaa, akaamua kumuinua, na kumuweka begani, akakusanya na bastola zao akatoka nje na kuikuta ile gari ikiwa palepale, akambwaga katika kiti cha nyuma na kuingia katika kiti cha dereva, akatazama gari haina ufunguo. Akabomoa mahali pa kuwekea ufunguo akaunganaisha viwayawaya mpaka gari ile ikawaka, akatia gia akaigeuza na kuondoka kwa kasi kuelekea geti kubwa la nyumba hiyo, hakujali kufunguliwa alipita na kugonga vyuma vya geti hilo kisha akakunja kona kali na kuingia barabara iliyokuwa ikienda kutokea barabara kuu.

    Mlipuko mkubwa ukatoke nyuma yake, bomu alilolitega Jack katika mtindo anaoujua yeye lililipuka na kufumua kibada chote kilichojaa mitambo ya mawasiano na usalama. Mara tena mlipuko mwingine ukatoakea katika nyumba ya Malyamungu. Joru akakanyaga mafuta na kuipata barabara kuu ya kuja Kampala. Akaendesha gari kama mwizi mpaka umbali wa kilomita hamsini, nje ya mji, akatafuta mahali kwenye kijiji ambapo kuna watu kidogo, akaegesha gari na kurudi kwa mguu mpaka sehemu iliyokuwa na vijana waliokuwa katika ulinzi wa sungusungu, akawauliza kama eneo lile kuna zahanati, wakamuonesha zahanati ya misheni, akaenda na kukuta iko wazi, akaomba vifaa vichache akapewa na kurudi ndani ya gari. Akampaka iodine katika jeraha lake na kumfunga kwa bandeji kisha akamchoma sindano ya Diclofenac na kuondoa gari kwa kasi.



    Saa kumi alfajiri ilimkuta Joru na majeruhi wake katika eneo la Masaka, katika bar ileile waliyokutana mwanzo. Joru, akazimamaisha gari katika maegesho ya bar hiyo, akaicha pale, akachukua mfuko na kuzisunda zile pesa zote, akambeba Jack mpaka kwenye moja malori yaliyokuwa hapo, akamsaka dereva akampata, akamwomba amfikishe mpakani, ikawa hivyo.

    Saa nne asubuhi Jack alipata fahamu, akainua kichwa lakini kilikuwa kizito sana, akakikuridisha kitandani.

    “Joru,” akaita. Joru alipatwa na furaha sana kuona swahiba wake amerudiwa na fahamu.

    “Jack, Jack, umeamka, asante Mungu,” Joru hakuamini kama mtu huyoi amekwisha amka.

    “Hapa ni wapi?” Jack akauliza.

    “ Tuko mpakani upande wa Tanzania, tuko salama,” Joru alimwambia Jack.

    “Oh, asante sana,” Jack alishukuru. Baada ya masaa mawili, Jack alikuwa akifanya mazoezi ya kutembea, ndipo alipojigundua kuwa ana jeraha katika ubavu wake. Jack alipigwa risasi mbili, moja begani lakini haikumwingia sawasawa na nyingine ilipiga ubavuni na kunasa ndani yake. Joru baada ya kumfikisha hospitali hiyo ya serikali alijitambulisha na kupatiwa msaada wa haraka.



    §§§§§



    Polisi walifika katika nyumba ya Malyamungu na kukuta maafa wasiyoyategemea, walikusanya miili isiyi na uhai kama nane hivi, wakati huo nyumba ya Malyamungu ilikuwa ikiteketea kwa moto.

    “The bastard has gone,” (Mwanaharamu amekwenda), kiongozi aliyekuwa akiongoza polisi hao katika operesheni ile alitamka maneno hayo wakati akitazama mwili wa Malyamungu ukifunikwa kwa mfuko maalumu wa plastiki. Akarejea katika gari yake kisha akaketi kimya akitafakari jambo, “Natamani kama ningemuua mimi vile lo,” Yule polisi akaendelea kujiseme kwa masikitiko, kisha wakaondoka na gari zao wakiwaacha kikosi cha zimamoto kikitimiza majukumu yake.

    Kama kuna habari ilifurahiwa na watu huko Uganda basi waliposikia kifo cha Malyamungu redioni. Walitamani kupiga vigelegele lakini haikuwa hivyo. Wengi wao waliachwa na makovu yasiyofutika, machozi ya kumbukumbu mbaya ya mtu huyo, ama aliwaua ndugu zao au alichoma moto nyumba zao.

    “Hakuna marefu yasiyo na ncha,” mwananchi mmoja alikuwa akiwaambia wenziwake pindi alipokuwa akiiacha luninga iliyokuwa ikionesha habari hiyo mapema asubuhi.



    §§§§§

    BAADA YA SIKU 2



    Joru na Jack walirudi katika hali zao za kawaida, wote walikuwa na furaha hasa baada ya kuitimiza azma hiyo iliyokuwa ikimtesa kila mmoja moyoni kwa jinsi zake. Jack alihesabu pesa zilizokuwa ndani ya fuko lile, si haba pesa ilikuwa ni nyingi ya kutosha. Akamwambia Joru jinsi alivyoipata pesa hiyo nyumbani kwa Malyamungu.

    “Safi sana Jack, pesa hii itajenga maisha yako, usirudi tena Uganda, tafuta ardhi na kujenga hapa kisha fanya miradi yako, mke na mtoto utawafuata au utawaita waje waungane nawe katika maisha mapya,” Jack alimtazama Joru kwa kumkazia macho. Akasimama na kumkumbatia rafikiye huyo ambaye urafiki wao ulikuwa ni wa siku sita tu mpaka hapo lakini tayari walikwishafanya mambo makubwa.

    Baada ya siku hiyo Joru alirudi nyumbani na kuungana tena na family ya Shibagenda, Kemi hakuamini kama mpenziwe huyo karudi salama. Siku hiyo alimkuta mzee Shibagenda mwenyewe nyumbani.

    “Joru, wewe ni mwanaume sasa, ulilolifanya nimelisikia, hongera sana, umekomaa,” Shibagenda akampongeza Joru.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haikupita muda mrefu, mipango ya ndoa na ya Joru na Kemi ikaanza ndani ya familia ya Shibagenda. Kabla ya ndoa hiyo Joru akiwa na Kemi pamoja na mtoto wao walikwenda kuzuru eneo ambalo kijiji chao kilikuwapo. Joru alisimama juu ya kilima kidogo akitazama vichaka vya migomba na mikahawa vilivyobadilisha taswira ya eneo hilo. Joru akaangukwa na machozi, akamtazama Kemi, akamtazama mwanawe.

    “Baba, uliniachia risasi 4, nimezitumia kama ulivyofikiri, nimekuja hapa kukwambia wewe, mama yangu pamoja na majirani wote ambao roho zao zilidhurumiwa na Malyamungu, Kazi mliyonituma nimeimaliza”.



    «««« MWISHO »»»»







0 comments:

Post a Comment

Blog