Search This Blog

Sunday 22 May 2022

JULAI SABA - 3

 







    Simulizi : Julai Saba

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Kamanda Amata alizunguka upande wa nyuma wa malori yale na kupita kati yake, uso kwa uso akiwa anatazamana na wale vijana walikuwa wakielekea kukutana kati ya malori yale. Hatua kama tano hivi walikutana katikati, Amata alisimama, na wale vijana walifanya vivyo hivyo, akakisukuma juu kioo kilichozuia macho yake cha lile kofia gumu la kuendeshea pikipiki, akawatazama wale vijana waliomshika Mwadawa, wakabaki wakitazamana na hakuna aliyeongea kati yao, Kamanda Amata akawaoneshea ishara kuwa wamuachie yule msichana, lakini amri hiyo hakuna aliyeitii badala yake wakageuka naye na kurudi walikotoka, mara nyuma yao wakasikia mlio wa bastola inayoondolewa usalama tayari kwa kazi, wakageuka na kutazamana na domo la bastola iliyofungwa kiwambo cha sauti ikiwa kwenye mikono imara ya Amata, bastola yenyewe, sura ya aliyeishika vyote viwili havikuonekana kuwa na masihara hata kidogo, hawakuwa na ujanja, walijikuta mikono yao ikilegea na kumuachia yule msichana, Mwadawa akatoka kwa hatua za haraka na kujificha nyuma yake, bado wakiwa katikati ya malori yale hakuna mtu yoyote eneo lile aliyejua kinachoendelea, Amata hakuona haja ya kuanzisha timbwili katika eneo lile kwa kuwa kungeweza kuleta madhara kwa Watanzania wengi ambao amani imewafanya wajinga hata kupenda kushangaa matukio ya hatari kama hayo kana kwamba wanaangalia sinema. Alimchukua Mwadawa, na bastola yake mkononi na kugeuka kuanza kuondoka huku akionesha kuwa hajali nyuma kuna nini, wale viajana walimtazama mpaka alipoishia katika yale malori akiwa na windo lao.



    Mwendo wa dakika kumi na tano, Kamanda Amata alimfikisha Mwadawa nyumbani kwake, na kumkuta Gina amekwishaandaa chakula, akawakaribisha na wote wakaketi vitini.

    “Asante Stephen,” ilikuwa ni sauti ya Mwadawa iliyoongea katika hali ya kutojiamini.

    “Karibu sana, hebu nambie hawa jamaa wamekufuata tangu lini?” Kamnda aliuliza, wakati huo alikuwa ameiwasha simu yake yenye uwezo wa kurekodi sauti.

    “Jana jioni niliwaona watu hawa karibu na nyumba ninayoishi, lakini sikuwafuatilia ijapokuwa walikuwa eneo lile karibu siku nzima, leo asubuhi nilikuwa nina shughuli zangu mjini ndipo nilipowaona kila ninapokwenda mpaka mchana huu nilipoona sasa hali inakuwa zaidi, walijaribu kunikamata mara mbili lakini nikawa nawakwepa kwa kujichanganya na makundi ya watu, mara ya mwisho hii nilijifanya nanunua matunda pale soko dogo nikawaona mmoja kushoto na mwingine kulia, nikaondoka nikakimbilia kule shimoni, nikaikumbuka kadi yako ulonipa ndo nikakupigia.” Mwadawa alieleza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kabla ya hapa uliwahi kuwaona hawa watu?” lilikuwa swali lingine zuri kutoka kwa Amata.



    “Kwa kweli hapana sijawahi kuwaona kabisa,” alijibu mwadawa.

    “Ok, hebu leo niambie ukweli bila kuficha, kampuni yenu ya ulinzi na matukio ya milipuko ya mabomu vina uhusiano wowote?”

    “Aah kwa kweli bwana Stephen, mi sina uhakika sana, ila tu siku ile ulipokuja ofisini nilisikia jambo moja likiongelewa ambalo lilinitia wasiwasi,” aliposema hayo Amata akajiweka vizuri, “Enhe, jambo gain hilo?” aliuliza.

    “Nilisikia wakiongelea sana lile jengo la JM MALL kwa sababu mimi nilikuwa nawapelekea chain a kahawa kule ofisini nilikuwa nasikia hilo pia walikuwa na ramani nahisi ni ya jengo hilo,” Mwadawa alieleza kwa kusitasita, Amata akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu nyingine aina ya Nokia Lumia na kufungua sehemu ya picha, “Huyu unamjua?” ilikuwa ni picha ya msichana aliyeonekana kama chotara wa kiarabu na kiswahili, Mwadawa aliichukua ile simu na kuangalia vizuri, akawa kama anajaribu kumgusa mwanadada huyo pichani, “Niambie unamjua?” swali la Amata lilimshtua Mwadawa, “Ndiyo namjua, nilimuona siku moja kabla yaw ewe kuja ofisini, alikuja pale ofisini kwetu akiongozana na kijana mmoja wa kiarabu lakini ni raia wa Kazakhistan,” alijibu kwa ufasaha.

    “Ok, unaweza kunambia ana uhusiano na boss wako bwana Scolleti?”



    “Bwana Scolleti, alinitambulisha hawa watu wote kuwa ni business partiners wake kutoka mbali, hivyo wana vikao vya kubadilishana mawazo juu ya biashara zao,” Mwadawa alieleza. Kamanda Amata akaichukua ile simu na kutafuta picha ingine akamuonesha Mwadawa, “Huyu unamjua?” lilikuwa swali lingine kwa Mwadawa.

    “Uuuuuuhhhhh!!!! Yeah, si ndiyo yule dada au?” alijibu kwa swali na kushusha pumzi ndefu. Amata akaizima ile simu na kuiweka mfukoni mwake, akajiweka vizuri pale alipoketi.

    “Ameokotwa amekufa jana, una habari na hilo?” Amata alimuuliza Mwadawa ambaye alijibu kwa kutikisa kichwa chake kushoto kulia kwamba hajui chochote, kisha akabaki ameduwaa, na mara machozi yakaanza kumdondoka.



    “Unalia nini?” Amata aliuliza

    “Dah, Stephan, huyu dada wakati anaondoka pale na wale vijana alinipa noti ya dollar mia moja ya Kimarekani akanambia, hatutaonana tena hela hii itakuwa kumbukumbu yako na msaada mkubwa kwa watakaohitaji, akanikabidhi na kuondoka,” Mwadawa aliangusha machozi ya haja kwa kilio. Kamanda Amata akainuka kutoka alikoketi kwenda kwenye kikabati kidogo na kutoka na kitu kama kitambaa laini akampatia Mwadawa kwa ajili ya kufuta machozi yake. Amata akatazamana na Gina aliyekuwa ameketi pembeni akijinywea coca cola yake huku akingali runinga kubwa iliyokuwa mbele yake. Baada ya kunyamaza kulia kule wote watatu walienda mezani na kupata chakula cha mchana, lakini Amata bado alikuwa kaidadisi huku na kule.



    “Boss wako Scolleti, ana biashara gain au kampuni ngapi?”

    “Kwa hapa Tanzania ana huu mradi wa zimamoto na pia ana kampuni kubwa ya kusambaza mafuta, ananunua mafuta Uarabuni na kuyaleta hapa, ana tanker zake zaidi ya mia mbili zinapeleka karibu nchi zote za SADC”

    “Du, amejiimarisha kweli, na yard yake ipo wapi?” Amata aliendelea kuchimbachimba

    “Yadi moja ipo pale External Mabibo karibu na hostel za chuo kikuu, lakini ile ni ndogo, kubwa kabisa ambayo pia ina matank makubwa ya mafuta ipo Bunju njia ya Bagamoyo, pale ndiyo kila kitu”



    “HARAKATI za ukombozi zinaendelea huko duniani na tunaamini ndani ya masaa sabini na mbili yajayo utakuwa huru ijapokuwa bado wamekaakimya hadi sasa” Mtu mmoja wa makamo alikuwa amesimama upande wa pili wa nondo za gereza akiongea na Jegan Grashan kwa lugha ambayo watu waliokuwa hapo hawakuelewa.

    “Itapendeza kuona taifa letu linakuwa huru dhidi ya utawala wa kibeberu wa Maghalibi, wao ni nani hata watake kuitawala dunia, ndugu piganeni kwa nguvu zote, na siku ya kiyama mtapata thawabu yenu, mimi nimepigana kadiri ya uwezo wangu na sasa niko hapa gerezani ila naamini wazi kuwa nitakuwa huru na nitaendelea na mapambano mpaka tulikomboe taifa nyonge ambalo Wamaghalibi hawataki kuliona duniani, Mungu mkubwa ndugu,” Jegan aliongea kwa hisia huku akiwa ameishika mikono ya ndugu yake huyo aliyeonekana kuwa ni mtu wa makamo kwa jinsi uso wake ulivyoonekana ukiwa na mikunjo michache na ngozi iliyoanza kuchoka kwa mbali.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usichoke kuomba, ndugu zako tutapigana mpaka mwisho,” alimalizia mazungumzo yake na kuziachia zile nondo, alipopiga hatua kadhaa alisimama na kugeuka nyuma kumwangali ndugu yake huyo Jegan Grashan ambaye pamoja na kukimbia katika mikono ya vyombo vya usalama nchi mbalimbali za dunia hatimaye alijikuta akinasa katika idara makini ya usalama ya Tanzania, idara isiyofanya mzaha kwenye kazi kama hiz, ikiongozwa na viongozi makini na ikifanya kazi na watu makini walio makini katika mambo yanayohitaji umakini. Ijapokuwa mara ya kwanza alijaribu kutoroka pale JNIA (Julius Nyerere International Airport) lakini mwisho wa yote alitiwa mkononi na vikosi mahiri vya usalama hapo Handeni Tanga akiwa mbioni kutoroka nchini shida ilikuwa ni jinsi gani ya kuvuka mpaka kwa maana kila uchochoro ulidhibitiwa kuhakikisha kiumbe huyu hatari asiye na chembe ya huruma hatoki nchini labda ageuke njiwa au upepo. Kila mtu alikuwa makini na kitengo chake mpaka pale walipopata fununu kutoka Mkoa wa Tanga kuwa inasadikiwa gaidi huyo amejichimbia huko.



    >>>>>Rudi Miaka Mitatu nyuma<<<<<

    >>>>>Handeni Tanga<<<<<<



    BAADA ya msako na uchunguzi mkali wa makachero wa serikali, takribani ya mwaka mmoja iliwachukua kupata fununu kuwa Jegran Grashan alikuwa huko Tanga katika eneo la Handeni, kwenye moja ya nyumba ambayo inasadikiwa huwa hakuna mtu anayeishi isipokuwa hutumiwa kama stoo ya kuhifadhia makorokoro kutoka katika kiwanda cha mkonge. Iliposadikiwa hilo mmoja wa makachero ambaye alipanga chumba eneo hilo la makazi ya watu ila ni mbali kidogo na lile shamba la mkonge ambako kunai le stoo tajwa. Baada ya kuishi eneo hilo na kuzoeleka na waenyeji alianza kufuatilia kwa umakini wote juu ya lile eneo na kuchukua kila kilichokuwa kikiongelewa kwenye vijiwe vya vijana au vilabu vya pombe, mara kadhaa amekuwa akienda kule shambani kwa ajili ya kujipatia kibarua cha siku moja au mbili, mara nyingine alipata na mara nyingine hakupata. Ndipo wakati Fulani zilipotangazwa nafasi za vibarua wenye ujuzi, naye alijitokeza akiwa na ujuzi wa kuendesha trekta, Mungu si Athumani akajipatia kazi ile na hapo ndipo alipoanza kwa umakini juu ya kazi yake iliyompeleka pale.

    Siku moja alipangwa kupeleka takataka huko katika ile stoo, kwake ilikuwa ni nafasi nzuri kwake. Kijana huyu ambaye daima aliizowesha jamii kuwa yeye ni mpenda miwani siku hiyo kama kawaida alikuwa na miwani yake nzuri, daima alipokuwa kazini miwani ile aliivua na kuiweka mahala ili aweze kufanya kazi zake, hata mabosi wake wale maburushi walimzoea kwa hilo. Ilikuwa ni mchana kama wa saa nane hivi alipoegesha treat lake karibu kabisa na mlango wa ile stoo, wale vibarua alokuwa nao wakafungua geti naye akaingiza lile trela la trekta kisha akashuka na kuingia mle ndani kwa minajiri ya kuwasidia wale wenzake kushusha zile takataka, akaivua miwani yake na kuiweka juu kwenye kidirisha Fulani ambacho kilitazamana na mlango mmoja ulioonekana katika jumba hilo. Baada ya kushusha takataka zote walionsoka na kurudi kazini. Muda ulipotimu wakafunga kazi na kuondoka, akiwa tayari keshaliacha lile eneo na wenzake akajifanya kukumbuka miwani yake, kwa kweli alionekana kuchanganyikiwa kwa namna moja au nyingine lakini walimpoza kuwa asijali siku ya pili ataiona miwani hiyo.

    Siku iliyofuata…



    KAMA kawaida vibarua waliingia kazini na jambo la kwanza yule kijana aliivua miwani nyingine aliyoivaa siku hiyo, hakuonesha kujali juu ya ile miwani aliyoiacha kule. Ilipotimu saa nane kama kawaida alikuwa juu ya trekta na wenzake wakienda kule stoo, walipofika jambo la kwanz ayule kijana akaiendea miwani yake nakuikuta kama ilivyo akaichukua na kuwaonesha wenzake kuwa ameikuta salama, kila mtu alifurahi. Baada ya kila kitu kumalizika walirudi kazini na kufunga ofisi kisha kutawanyika kila mmoja na anakoishi. Yule kijana aliketi chumbani kwake na akiwa kajifungia mlango, akaichukua ile miwani na kubetua kioo kimoja ambacho kilitoka katika ile fremu yake, akamisnya sehemu Fulani palepale alipotoa kioo kile na mara memori kadi ndogo ikatoka, akaichomoa na kuchukua dvcam yake kisha akaipachika ile kadi na kuwasha ile dvcam, sekunde kadhaa ikaonekana kwenye kile kioo kidogo picha ya watu watatu walioingia eneo lile jioni wakiwa na bunduki nzito zilizosheheni risasi, waliongea mambo mengi ambayo yote yalisikika vyema katika mashine ile, watu wale watatu aliwatambua vyema kwa kuwa mara nyingi aliwaona hata pale kiwandani, picha ikaendelea, mtu wa nne alionekana kuongezeka baada ya kama nusu saa ya ile picha kuendelea, huyu hakumjua, alimzoom mara kadhaa lakini sura yake haikuonekana vizuri kutokana na mwanga hafifu wa mbala mwezi, wasiwasi ulimjaa na kuamini maneno ya watu kuwa ndani ya stoo ile kuna watu wanaishi. Tafutishi yake ya pili ilimpa jibu sahihi la kuwa kuna mtu zaidi ya walinzi hujumuika usiku, lakini bado hakuwa na uhakika ni nani mtu huyo, taarifa hizo zenye kila dalili ya mafanikio zilifika makao makuu ya idara ya usalama wa Taifa, Kamanda Amata aliyekuwa akifuatilia na ndiye aliyemtuma kijana yule mbichi kabisa katika kazi hiyo alifurahi kuona majibu anayoyapata kuwa yalikuwa na uelekeo chanya.



    Jegan Grashan, mara baada ya kutoroka pale uwanja wa ndege mwaka mmoja uliopita, na kuwaacha Kamanda Amata, Madam S na Chiba hoi alipotelea mitaa ya Kujichanganya na wakazi wa eneo hilo waliokuwa kwenye pilikapilika nyingi, hakuna aliyemtilia shaka kwani utulivu wake ulikuwa na ngao tosha ya kujifunika, alikodi tax na ikampeleka moja kwa moja mpaka Posta kwenye bandari ndogo ya Zanziba na kuiwahi boti iliyokuwa inaondoka muda huo, wakati taarifa zinasambazwa kubana kila mahali tayari ile boti ilikuwa kilomita moja kutoka kwenye gati hiyo, Jegan Grashan aliiona Dar es salaam ikizidi kuwa ndogo na mara ikamezwa na maji ya bahari, baada ya dakika tisini ile boti ya Sea Express ilikuwa tayari ikiingia katika bandari ya Zanzibar, akiwa kama gaidi mzoefu alielewa wazi kuwa lazima pale langoni kutakuwa na ulinzi wa kumnasa, hivyo aliposhuka tu hakupita katika mlango mkuu bali alishuka na kuyaelekea madau yaliyoegeshwa mahali hapo na kukodi moja limpeleke Pemba, kutokana na pesa aliyolipa dau lile lilimpeleka mpaka Pemba usiku huo, masaa nane yaliisha wakiwa baharini kwenye mawimbi na dhoruba kali, Jegan Grasha alikaa Pemba kwa muda mfupi na kuondoka kwa dau lingine mpaka Tanga alipopokelewa na swahiba zake ambao walikuwa wkijua kila kinachoendelea na wakaja kumuhifadhi hapo wakimpatia kila kitu, walinzi waliokuwa wakiendelea kulinda stoo ile kubwa walielewa mchezo mzima, na daima walipoketi walikuwa wakijua kuwa mtu huyo anatafutwa hivyo walimshauri akae hapo kwa muda mpaka mambo yatakapotulia kumbe hawakujua kuwa kimya kingi kina mshindo mkuu.



    Katika idara ya utambuzi ya usalama wa Taifa, Picha zilizopigwa na ile camera ya kisasa iliyofungwa katika miwani aliyokuwa akiitumia yule kijana zilifanyiwa uchunguzi wa hali ya juu katika vifaa vya kisasa kabisa vilivyoweza kufananisha picha za mtu zaidi ya mia moja na baada ya kufanya utafiti huo uliochukua takribani siku nne jibu lililokuja lilikuwa lilelile kuwa mtu huyo si mwingine bali ni Jegan Grashan. Kazi ikawa ni jinsi gani ya kumtia mkononi mtu huyo hatari ambaye bila shaka yoyote lazima atakuwa na silaha za kujihami ambazo hazitojali kukuua iloimradi yeye aokoke, mkakati ukapangwa, wanajeshi watatu mahili wakaungana na Kamanda Amata kufanya kamato hilo usiku wa manane. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Chopa la kijeshi liliandaliwa na usiku huo liliruka kutoka uwanja wa ndege wa jeshi majumba sita ukonga na kuelekea Handeni Tanga, wakiongozwa na signal maalum iliyowekwa katika jengo lile katikati ya takataka na yule kijana alipoenda kumwaga taka siku ile.

    “Heyyyyyy!” zilikuwa kelele za rubani wa chopa ile akiwashtua wapiganaji wake, kisha akawaonesha ishara kuwa tayari wamekaribia. Kila mtu akajiandaa kwa kuvaa gas mask zao zilizowaficha sura zao, bunduki kubwa za kivita na silaha ndogondogo zilikuwa sambamba nao, rubani wa chopa ile aliishusha pembeni kidogo ya stoo ile, walinzi walipoona hayo wakahamainika na kuanza kutaka kuishambulia ile chopa, yule rubani akawasha taa kali sana iliyofungwa mbela ya chopa hiyo na kuwanya wale walinzi kushindwa shabaha na kuficha macho yao, Kamanda Amata na wale wapiganaji wa jeshi waliteremka kwa kuruka na kuvamia moja kwa moja jengo hilo, upinzani ulionekana dhahiri, kwani wale walinzi walionekana kumudu hasa mapigano ya silaha, walipoamuriwa kusalimu amri walibisha vikali na kushambuliwa kwa risasi ma kuuawa, moja kwa moja msako uliamia ndani ya jengo hilo huku askari wawili wakibaki nje kulinda usalama, Kamanda Amata na mmoja waliingi ndani, hawakutegemea kukuta jumba kubwa la kifahari lililojengwa chini ya ardhi, ndani ya chumba kimoja walimkuta Jegan Grashan akiwa ameketi bila wasiwasi wowote, hakuonesha upinzani wowote kama ilivyotegemewa, Kamnda Amata alitulia kwanza kuona mtu huyo katulia namna ile, akamwita Jegan asimame kutoka pale alipokaa na asogee, lol Jegan alikuwa amekalia bomu ambalo lilibaki muda mchache kulipuka, hakuna kulala.



    Yule mwanajeshi alimshika mkono Jegan na kumvuta kutoka naye nje, walipofika nje hawa kumaliza hata geti, ishara waliyoitoa kwa rubani ndiyo iliyosaidia rubani yule kuelewa na kuligeuza lili chopa haraka kuliondoa eneo lile, “Chiniiiiiiii !!!!!!” yule mwanajeshi alipiga kelele na wote wakalala chini pamoja na wale walioimarisha ulinzi walilala chini, mlipuko mkubwa ulitokea ile stoo yote ikateketea. Kamanda Amata alinyanyuka akiwa na maumivu makali mkononi mwake, kipande cha chuma kilimchoma na kumuumiza, walimkokota Jegan umbali kidogo na kuifikia ile chopa ambayo sasa ilikuwa imesimama kwenye mikonge wakampakia na kumfuga pingu na minyororo ya miguu, kisha wakaondoka zao.





    DUNIANI kuna mvutano mkubwa sana juu ya utwala na tawala zenyewe, huyu anasema hili juu ya mwenzake na huyu anatamka vile dhidi yake. Mvutano mkubwa unaonekana waziwazi kati ya taifa la Marekani na washirika zake wa Ulaya dhidi ya mataifa machache ya Mashariki ya kati, mataifa yanayosadikiwa kwa mbinu chafu za kigaidi za kuteketeza mamia ya wanadamu katika sehemu mbalimbali za ulimwengu kwa njia tofauti wanazozijua wao. Mataifa yanayojiita makubwa duniani yana ndoto za kufutilia mbali enzi na ujeuri wa mataifa haya machache ambayo yamejidhatiti na hayatetereki na vitisho kama hivyo, ambayo leo kesho yako tayari kuingia vitani dhidi ya mabeberu hawa wa maghalibi.

    Kitendo cha Marekani na washirika wake kuivamia ardhi ya Mashariki ya kati kwa minajiri ya kukomesha tawala za kidekteta zinazonyima watu haki zao kiliwachukiza watawala wa mataifa haya na ndipo walipoanza kujitutumua na kuendesha vita yao dhidi ya mataifa makubwa popote yalipo duniani, yalizalisha magaidi wakubwa, watu hatari ambao kwa namna moja au nyingine walijifunza mbinu zote za medani za kivita ndani ya mataifa yao na kufundishwa na wao wenyewe kisha wakageuka kuwa silaha mbaya zenye akili ya ajabu na kuitikisa dunia. Vichwa vinauma, mioyo inadunda, akili hazitulii, vikao vya mara kwa mara vinaitishwa vya kuangalia jinsi ya kukomesha hali hii, na muda huohuo vikao vingine vinaitishwa kuona jinsi gani ya kutengeneza shambulio lingine, la namna gani na wapi wakalitekeleze. Ni akili mbili zisizochangamana zilikuwa zikizungukana pande mbalimbali za sayari hii na kuwafanya watu kuishi pa si na amani. Wkati wao wanaanzisha kambi za jeshi kila kona ya dunia ndani ya ardhi za nchi za wengine hasa wanyonge kama Afrika, na wenzao waliimarisha makundi yao kila kona hasa Afrika.



    ˜˜˜



    Kikao kizito kilikuwa kikiendelea katika ofisi moja nyeti ya serikali, hoja ilikuwa ni ileile ya kuachiwa kwa Jegan Grashan au la, mara hii muda ulikuwa umekwisha sana hivyo kufanya kikao hicho kuwa na mvutano mwingine wa kipekee. Zilikuwa zimebaki siku tatu tu ili zile siku saba walizopewa kumuachia huru mtu huyo zitimie na endapo hatoachiwa basi shambulizi kubwa na lisilotegemewa lilikuwa limepangwa. Vikosi vya usalama havikulala, usiku kucha vilijipanga hapa na pale kuhakikisha wanansa kila aina ya milipuko inayosadikiwa kubebwa au kuwekwa mahali Fulani. Mitambo ya kisasa ilifungwa katika sehemu mbalimbali za mikusanyiko ya watu kama kwenye supermarket, vituo vya mabasi kama Ubungo, uwanja wa ndege na sehemu nyinginezo nyingi, askari kanzu walizagaa kila eneo kuhakikisha wananusa kila aina ya mazungumzo, usiku ndo usiseme, ilikuwa tabu sana kwa wale wapenda giza, vibaka, machangudoa, walevi, wazururaji na wote wanaofanana na hao. Idara ya uhamiaji nayo ilikuwa makini kuchunguza kila anayeingia nchini iwe kwa ndege, meli, gari au hata pikipiki kama sio baisikeli, vibali vya kusafiria vilipekuliwa kwa umakini wa hali ya juu kwa mitambo ya kisasa iliyoweza kugundua alama fichwa mbalimbali katika vijitabu hivyo, wapo waliokamatwa na hati feki lakini walipoonekana hawana dalili ya wale wanaowatafuta basi waliwaacha na adhabu kubwa kwao ilikuwa ni kuwarudisha kwao tu. Computer maalum iliyounganishwa na zile za usalama za mataifa ya maghalibi zilifanya kazi kubwa maana ziliweza kutambua mtu mpaka kijiji ulichozaliwa hata kama wewe ulikisahau kwa kuwa zilikuwa zimelishwa kumbukumbu nyingi.



    Muafaka ulikuwa mgumu sana katika kikao hicho lakini ukweli ni kwamba wengi walionekana kukubali bwana huyo kuachiwa ili kukomesha mauaji yanayofanyika na kupoteza maisha ya Watanzania wasio na hatia. Madam S bado alikuwa na ushawishi mkubwa wa kuwafanya wajumbe wa kikao hicho kubadili mawazo na kuytomuachia huru Jegan, kila alipokumbuka kauli na mifano ya kijana wake Amata au Kamanda kama ilivyozoeleka kuitwa alijikuta ana dei la kuzuia kuachiwa kwake, lakini wengine wote walitaka aachiwe. Waziri mwenye dhamana alijaribu kuwasihi jambo hilo lifanyike haraka maana ni masaa sabini na mawili yalikuwa yakijihesabu ili lile wasilolijua lifanyike. Walibaki kizani, kiza kinene kwa kuwa walipigana na adui wasiyemjua wala kumuona, ilikuwa ni kama kupiga ngumi gizani.

    Kikao kilifikia tamati, uamuzi wa kusubiri masaa ishirini na nne ulipitishwa na kila mjumbe alirudi katika majukumu yake wakati waziri mwenye dhamana alikwenda kuonana na mkuu wa nchi kujadili swala ilohilo.



    ˜˜˜



    >>>>>Upande wa pili nako kikao kiliendelea.



    “Hawataki kumuachia mpiganaji wetu,” yalikuwa maneno manne ya Shailan, aliyaongea huku akiwa akishikashika zile ndevu zake nyingi.

    “Kama hawatii tunachotaka basi tufanye yetu, hapa tuna masaa yasiyopungua sabini tu so hatuna budi kuanza kazi, nimeongea na Beishal, tayari amesema kuna watu wako njiani kuingia hapa wao watakuja kumaliza kazi kwa jinsi ambayo watabaki na hofu kuu maana hataitegemea kutokea.” Shakrum alizungumza kwa kujiamini sana huku taratibu akiwa anakunywa ile kahawa yake chungu kabisa ambayo upendwa kunywewa na watu wa Pwani.

    “Wasipotekeleza itakuwa ni kaburi lao sasa, kama wanakumbuka septemba 11 pale New York sasa wataona kwa macho yao kitachotokea hapa mbele ya macho yao,” Shailan aliijibu hoja ya Shakrum. Wakiwa katika kikao chao cha watu wachache mara simu ya mezani iliita na Shailan akampa ishara Shakrum aipokee naye akafanya hivyo. Baada ya dakika kadhaa alirudi kitini na kutazamana na Shailan, muda wote huo Scolleti alikuwa kimya bila hoja.

    “Vipi?”Shailan aliuliza

    “Mzigo tayari, Beishal kasema tusubiri, kutoka upande tusioujua jamaa watatokea na watakua hapa ndani ya masaa ishirini na nne,” Shakrum aakajibu.

    “Ok! Tuwasubiri tufanye kazi”

    Kimya cha ghafla kikapita kwa sekunde kadhaa, kisha wote wakacheka pamoja.

    “Shailan, kumbuka tuna yule Malaya wa jana, lazima ashughulikiwe,” Shakrum alikumbusha

    “Ooh gud, nenda ukamfanyie kama yule mwingine kisha nipe ripoti, na hakikisha Mwadawa anapatikana kuna mabo anayajua yule binti asije akayatapika,” Shailan akasisitiza.

    Shakrum akainuka kitini na kuvuta droo iliyokuwa kwenye kikabati kidogo na kuchukua bastola na kisu chenye urefu wa futi moja. Kisha akaondoka zake na kumuacha Shailan na Scolleti.



    ˜˜˜CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    >>>MALAWI

    >>>Uwanja wa ndege wa Karonga



    Karonga, mji mdogo ulio katika mkoa wa kaskazini katika nchi ya Malawi, maghalibi mwa ziwa Malawi au ziwa Nyasa kama linavyoitwa hapa kwetu.Ndege ndogo aina ya Sessna ilitua subuhi na mapema katika uwanja huo, ilipokwishaegeshwa mahali pake, mlango ukafunguliwa, watu wawili wanaume waliteremka na kuelekea eneo la mapokezi ambako watu wa uhamiaji walikuwa pale tayari kuwapa msaada wanaouhitaji. Haikuwa na shaka wala haikuwa na tabu, ndani ya dakika ishirini walikuwa nje ya uwanja huo tayari kuelekea kule wanakokutaka. Tax, ilikuwa ni usafiri pekee uliowapeleka moja kwa moja mpaka katika moja ya hotel za kawaida na kujipatia chakula huku wakipanga mikakati yao jinsi ya kuingia Tanzania, walishatahadaharishwa kuwa huko waendako kuna ulinzi wa hali ya juu hivyo watumie mbinu zote wawezazo kufanikisha adhma hiyo.

    Ndani ya lisaa limoja walikuwa kwenye Pwani ya Ziwa Malawi, pale walikuta shughuli nyingi za wavuvi zikiendelea, wakatazama huku na kule, wakaona boti moja iliyofungwa injini, wakaona ndiyo iwafaayo, wakaiendea na kumkuta kijana mmoja aliyekuwa akisuka nyavu zake tayari kujiandaa kwenda kuvua. Wakamwita na kuzungumza nae kuwa wanaomba awafikishe katika kijiji kingine mbele katika mwambao huo, alipotaka kuleta ubishi wakampatia pesa za kimarekani, akakubali, lakini akaomba wakubali aene na mwenzake, hawakupinga.

    Watu wanne walikuwa botini na safari ikaanza, boti ile ya mti ilikuwa ikikata maji kwa mwendo wa kasi kwani injini yake iliruhusu hilo. Walipofika mbali na pale walipotoka ndipo walipofanya lile walilopanga, waliwaua wale vijana na miili yao wakaitupa majini kisha wao wakamiliki ile boti, na kwa kuongozwa na dira waliyokuwa nayo, waliongoza chombo hicho kuelekea kaskazini maana kiliwapa uelekeo sahihi. Masaa manne hayakuwa haba wao kufika katika mapori Ludewa ambako walikitelekeza chombo hicho na wao kupotelea katika misitu hiyo mpaka Ludewa mjini, sasa wakagawana kila mtu kutumia usafiri wake na miadi ilikuwa ni kukutana Dar es salaam, mahala walipoelekezwa, kwa muda waliopanga.



    ˜˜˜



    Shakrum aliingia katika stoo kubwa waliyomfungia yule binti wa kihindi, akapigwa na butwaa kukuta mlango mdogo wa chumba cha siri walimomficha yule binti uko wazi, akasita, akasimama na kaungali kwa makini, kisha akanyata hadi kwenye ule mlango na kuangalia ndani yake, hakuna mtu, kamba waliyotumia kumfunga yule binti walizikuta pale chini, si kwamba zimekatwa bali zimefunguliwa na aliyefungwa ametoroka kwa amani. Shakrum hakuamini kilichotokea, akatazama huku na kule, juu na chini hakugundua kitu, ‘Ametokea wapi mwanaharamu huyu?’ alijiuliza lakini hakuna jibu alilopata, akiwa kashika kisu chake kwa mkono wa kulia na ule wa kushoto akiwa kama anajaribu kujua makali ya kisu kile kwa kugusagusa kwa vidole vyake, kijasho chembamba kilimtiririka na kurusu mvujo uliokuwa ukilowesha fulana yake aliyovaa, alipogutuka, alitoka nje haraka na kuwaendea walinzi kuwaliza kama wamemuona mtu yeyote kupita eneo hilo, lakini walidai hawakuona, Shakrum alisikitika sana lakini pia alijilaumu kwa kuwa hakuwaambia walinzi tangu kabla kama kuna mtu aliyefungiwa ndani ya jengo hilo. Hakuwa na la kufanya aliinua simu yake na kupiga kwa Shailan ambaye alishtushwa na habari hiyo pia. Wote walibaki midomo wazi hakuna aliyeamini kama binti yule angeweza kutoroka katikla mazingira kama yale, lakini ndiyo ilikuwa tayari imetokea.



    ˜˜˜

    ShaSha, alijificha nyuma ya kibanda kidogo ambacho hakikuwa mbali na geti la mlinzi, jirani kabisa na tenki kubwa la mafuta lililowekwa hapo, aliweza kuwaona Shakrum na wale walinzi walipokuwa wakiongea pale karibu na geti, alipoondoka na kuwaacha pale, ShsSha alinyata huku akiambaa na ukuta mpaka nyuma ya kibanda cha mlinzi na kutulia hapo, akawaangalia walivyokaa kizembe wakicheza draft hali silaha zao wameziweka chini, akakizunguka kile kibanda upande wa geti na kuona limefungwa akatazama huku na kule hakuna mtu akajitokeza, na kwa kasi ya ajabu akaruka teke lilitoa kisogoni mwa mmoja wao na kumsukuma mbele ambako aligongana kichwa na yule mwingine na wote kuanguka, kbla hawajakaa sawa, aliruka na kutua pale walipo, pigo moja la nguvu lilitua nyuma ya shingo ya mmoja wao na kumpotezea fahamu kisha yule mwingine alimpiga kwa kumkanyaga na kumrudisha chini sakafuni kwa kishindo, kwa jinsi alivyopiga kisogo pale chini alipoteza fahamu pia, ShaSha akawasachi na kutoa funguo kisha akajifungulia geti na kutoka nje, akachukua tax haraka na kumuamuru dereva amfikishe Ilala Hotel. Walipofika alimwambia amsubiri pale chini, kisha akaj na kumpatia pesa yake. ShaSha akaona wazi kuwa hapo sasa si mahala salama akafunga mabegi yake na kuondoka, akabadili hotel na kuhamia Kinondoni kwa Manyanya kwenye hotel ya kawaida ya Manyanya Hotel na kuweka kambi hapo.



    ShaSha, kama anavyojiita, msichana wa kihindi kwa umbo lake dogo lakini ni mtu mzima aliyestahili kitwa mwanamke, alikuwa nchini kwa kazi moja tu aliyotumwa na serikali yake kuja kumchunguza Scolleti na mambo yake maana katika nchi nyingi bwana huyu alimopita serikali nyingi zimelalamikia uwepo wake kwa kusaidia kutekeleza ama ujambazi au kuhatarisha hatari ya nchi hiyo kwa namna moja au nyingine. Mara hii serikali yake ya India iliamua kuingia kazini kumchunguza kila aendako ni nini anakifanya, sasa Tanzania, Scoletti anawasaidia freedom fighters kutekeleza lile taraja lao la kudai haki ya kufunguliwa ndugu yao, wakitekeleza milipuko mikubwa na mibaya na kuuwa mamia ya watu.

    ShaSha alikuwa pale White Sands hotel katika nyendo zake za kumfuatilia tajiri huyu, alipokutana na Amata na kumkaribisha juice, Amata alivutwa na uzuri wa sura ya binti huyu na macho yake yasiyo na pazia hayakuweza kuinyima raha roho yake iliyofungiwa ndani ya kifua chake kwa kuutalii mwili mdogo, shupavu wenye umbo la kuvutia. Angekosa kuwapo Gina katika eneo lile basi tayari labda mapenzi yangeamka, ama kweli, Inzi hufia kwenyew kidonda.



    ˜˜˜

    Kamanda Amata alikunja nne kwenye kiti chake cha kuzunguka, huku akimwangalia Gina aliyekuwa bize na kuchapa kazi mbalimbali alizopewa siku hiyo. Akiwa na mawazo mengi hakuna kingine alichofanya kwa siku hiyo zadi ya kushinda ofisini tu akitega skio huku na kule kuona kama atasikia lolote kat i ya yale anayoyahitaji, lakini mpaka muda huo haluna kilichojiri kabisa.

    Magazeti yote alikwishayapitia, hakuna jipya. Redio zote alshasikiliza lakini habari zilkuwa zilezile, hakuna kigeni. Alivuta kjitabu chake kidogo cha kumbukumbu na kutazama kurasa chache za kufanyia kazi, akajikohoza kdogo na kuendelea kusoma kumbukumbu zake.

    “Gina,” aliita, Gina akagutuka na kumwangalia Amata.

    “Niambie,” akatika kwa mtindo huo wa kipekee.

    “Nataka nikutume sehemu wewe kama katibu wangu muhtasi ukaniombee miadi ya kukutana na manager wa eneo hilo,” Amata alimueleza.



    “Bila shaka, ni wapi huko?” Gina akauliza.

    “Unakumbuka Mwadawa alitueleza juu ya ile kampuni ya Scolleti ya kusafirisha mafuta?”

    “Ndyo,”

    “Hapo sasa, uende, uombe miadi, nataka kukutana na manager ili tuongee maswala ya kibiashara,” akavuta mtoto wa meza na kutoa kadi ya kibiashara na kumpa Gina, “Hilo ndilo jina langu,” alongeza. Gina aliisoma kwa makini ile kadi huku akigeuzageuza kwa jinsi livyokuwa nzuri, yenye kuvutia kwa rangi rangi anuai, JOHN SIZIMBA, ilisomeka hivyo kwa maandishi ya rangi ya dhahabu.

    “Kijana una majina mengi ! hivi unayakumbuka yote?” Gna aliuliza huku akiiweka ile kadi katika mkoba wake.

    “Yote nayakumbuka,” akajibu. Baada ya kumaliza kazi yake, Gina alinyanyuka na kumuaga Amata kuwa anaenda huko alikomtuma, “Tunaenda wote. Mi nakuacha uingie utanikuta nje.”

    Baada ya kupambana na foleni za jiji la Dar hasa ile barabara ya Bagamoyo, iliwachukua lisaa limoja na nusu kufika Bunju, mbele kidogo ya Baobab Sekondari na moja kwa moja kwenye maegesho ya yadi kubwa lililoshehen malori kadhaa ya mafuta. Amata alegesha gari nje na kumtaka Gina kuwenda huku akiwa amemuunganisha na kinasa sauti katika sidiria yake. Gina alishuka na kuanza mwendo wake wa mikogo kulielekea get kuu, akagonga na kufunguliwa, akajitoma ndani.

    Kamanda Amata akajiweka sawa, na kukiwasha kiredio maalumu ambacho kingempatia mawasiliano yote yanayotoka humo ndani.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Karibu mrembo!” ilikuwa ni saut nene na nzto kutoka kwa pande la mtu alyekuwa ameketi nyuma ya meza kubwa iliyostahili kuwapo ndani ya ofisi hiyo nadhfu ilipambwa na kunukia udi.

    “Asante sana, nimekaribia,” Gina aliitikia, “Naitwa Gina Zingazinga, kutoka kampuni ya SCOTT,” alijtambulisha na kueleza kwa kifupi juu ya kazi wafanyayo. Yule bwana alionekana akifuatilia kila kitu kwa makin kabisa, Gina akamaliza utambulisho wake na kueleza kile kilchomleta.

    “Ok nimekuelewa, haina tatizo, tuna nafasi nzuri sana ijumaa baada ya swala ya mchana, tena utakutana na mkurugenzi mkuu atakuwepo, natumaini atafurahia ujio wenu,” Yule bwana alyejitambulisha kwa jina la Aidan,a alieleza kwa kirefu.

    “Asante sana,” Gina alishukuru na kuaga, akasindkizwa na Aidan mpaka katika uwanja ule ambao ni maegesho ya yale malori, wakaagana na kutoka. Akiwa anatoka katika geti lle kubwa alipishana na gari moja aina ya Prado nyeupe iliyokuwa ikiingia ndani ya yadi ile, aliitazama kwa jicho la wizi na kukumbuka vizuri gari ile.

    “Aidan!” Amata allitaja hilo jina mara tu Gina alipoketi kitin katka ile gari. Akageuza na kuondoka eneo lile na kurudi mjini. “Tutakuja ijumaa mchana,” Amata alirudia maneno yale yai le miadi.



    ˜˜˜



    “Karibuni sana Tanzania,” Shailan aliwakaribisha vijana wawili walioonekana kuchoka sana kwa safari. Vijana waliosafiri kutoka nchi ya mbali kuja kuungana na wenzi wao katika kile wanachokiita ‘kupigania uhuru’, hawakuja kufanya starehe bali walikuja kufanya kazi, kazi ya hatari ambayo kishindo chake kila mtu atashtuka na dunia itazizima kwa hofu kuu, walipania, walidhamiria, waliamua kufanya kile kinachoitwa mauaji ya kimbari, lakini wangeikumbusha vipi serikali kuwa wanamhitaji ndugu yao, kaka yao, aliyeko gerezani? Yote ilikuwa ni mipango inayosukwa chini kwa chini na watu hao hatari katika uso wa dunia.

    “Tumeshapata la kufanya, kabla ya lile tulilodhamiria, lazima tuwape tashwishwi kwanza kwa tukio dogo tu halafu watakapokuwa wameshtuka sasa tunawapa onyo kisha wasipojibu tunafunga kazi kabisa,” mmoja wa wale vijana alieleza.

    “Sasa tukiwashtua, huoni tutakuwa tumewapa mwanya wa kuongeza ulinzi?” Shailan aliuliza.



    “Hapana, lipi tumefikiria kufanya kama hitimisho kwa ndugu yetu hata wafanye vipi hawawezi kufikiria hilo, wataspigwa na mshangao tu, limetokeaje, watabaki midomo wazi wakishuhudia mamia ya wananchi wao yakiteketea kikemikali, hapo hawatakuwa na ujanja tena zaidi ya kutupatia kaka yetu na wao kubaki wakiomboleza, na hili litatokana na ugumu wa shingo zao,” aliongea kijana wa pili kwa sauti ya upole.

    “Ok, tumebaki na masaa 48 hivi, nina wasiwasi mmoja hivi, kuna spy wao mmoja hatari sana, huyu jamaa nashindwa kumuelewa ni intelijensi kiasi gani, tusipomwangalia atakuwa kikwazo katika mkakati wetu,” Shailan alieleza kwa masikitiko, akadakiwa na Scolleti, “Yeah ni kweli kabisa, anaitwa Kamanda Amata, mwanzoni wa mission yetu amewaua vijana wetu na sasa amekuwa ni kikwazo kikubwa sana.”

    “Nipe picha yake kama mnayo,” yule kijana aliomba. Shailan akachukua laptop yake ndogo na kufungua picha Fulani, kisha akamuonesha yule kijana.

    “Sasa, huyu tuachieni sisi, kabla ya tukio hili atakuwa tayari marehemu, na mipango yote itaenda kama ilivyopangwa, tutahahakisha kabla ya jua la jioni kesho mwili wake upo mikononi mwetu,” walijigamba.



    “Muwe waangalifu sana, Amata si mtu wa kuchezea hata kidogo, one mistake one goal, ameshakwamisha mambo mengi sana aisee,” Scolleti alizungumza.

    “Hamna shaka, Shakrum, endelea na ule mpango wetu kama tulivyoongea, hakikisha ile kemikali imesogea eneo la tukio hilo ndilo la maana, mimi na huyu swahiba tunamfungia kazi Amata ndani ya masaa kumi tu,” yule kijana aliongea kwa majigambo. ‘Unamjua Amata au unamsikia?’ alijiuliza Shakrum moyoni mwake. Kikao kikaendelea na mikakati mibaya ikapangwa dhidi ya Watanzania wasio na hatia, hali tete.



    ˜˜˜



    Mlango wa chumba cha Mwadawa uligongwa na watu wawili wakajikaribisha wenyewe mpaka ndani. Mwadawa alikuwa amejilaza kitandani akiangali habari kupitia runinga yake ya kisasa iliyofungwa sambamba na ukuta, alikurupuka kuwaona watu hao wawili waliojikaribisha baada ya kugonga mara moja tu, akaketi kitandani na kuwatazama, “Ninyi ni akina nani? Mbona mnaingia kwa mtu kibabe hivyo?” akawauliza.

    “Usijali utatujua tu, umejaribu kutukimbia lakini sasa tumekupata, sasa, sisi na wewe tuondoke mguu kwa mguu jioni hii,” mmoja wao alisisitiza

    “Mnipeleke wapi?” Mwadawa aliuliza kwa woga.

    “We utajua ukifika, fanya tunalotaka kabla hatujatumia nguvu,” walimuamuru. Mwadawa aliwatazama kwa zamu watu wale ambao hawakuwa hata na chembe ya tabasamu, mmoja wao alipoona msichana Yule anataka kuleta ubishi, akachomoa bastola na kumuoneshea, “Sasa unaondoka na sisi au tukubakishe ukae hapa ndani mpaka watu wasikie harufu ya uozo wako?” aliuliza mwingine huku akiifunga kiwambo cha sauti ile bastola. Mwadawa alijawa na woga, alitetemeka mwili mzima. “Tunayasitisha maisha yako kwa kuwa umejifanya kimbelembele na kumpatia siri usiyoijua Kamanda Amata, sasa hizi ni salamu kutoka kwa bosi wako Scolleti,” Yule mwenye bastola akailengesha kwenye paji la uso wa Mwadawa na kuifyatua mara kadhaa, Mwadawa alijibwaga kitandani akiwa chapachapa kwa damu, kisha wale vijana wakaondoka zao na kuufunga mlango kwa mtindo wa kuurudishia.



    Kamanda Amata aliitazama simu yake mara kwa mara hakuona ujumbe wowote kutoka kwa Mwadawa ambaye walikuwa wakichati muda si mrefu, alishangazwa na ukimya huo, akabofya ile namba na kupiga lakini wapi, haikupokelewa kabisa, akaishusha taratibu na kuitazama tena, akafungua meseji ya mwisho; ‘Magomeni Makuti, nyumba namba 434B, ukifika nishtue,’ ilikuwa ni moja kati ya meseji za miadi iliyokuwa ikipangwa kati ya wawili hao yaani Mwadawa na Kamanda Amata. Mwili wa Amata ulikuwa ukisisimka mara kwa mara, akhisi kuna jambo la hatari lakini hakuwa na uhakika ni jambo gani, alijinyanyua na kuifuata gari yake huku akiwa hajui ni wapi anakoelekea.

    Ilikuwa yapata saa mbili na nusu usiku alipoegesha gari yake mbele ya nyumba namba 434B, Magomeni Makuti, akashuka na kuzipanda ngazi chache zilizo kwenye kibaraza cha nyumba hiyo, alipoukaribia mlango mkubwa alikuta na mbibi mmoja akiwa anatoka ndani, akamsabahi na kumuuliza chumba cha Mwadawa, Yule bibi akamtazama Kamanda na kumtupia swali, “Na we nani tena? He huyu binti ana hatari huyu, hivi magonjwa yote haya haogopi?” Amata akacheka na kurudisha swali, “Bibi, kwa nini unasema hivyo, mimi ni bnamu yake bwana.”



    “Aaaaa binamu ndiyo hana maana kabisa, binamu nyama ya hamu wenyewe mwasema, haya bwana anaishi mlango huo wa tatu kulia, uwe mwangalifu kijana kuna madume mawili yameingia muda si mrefu,” Yule bibi alijibu huku akitoka nje na kumuacha Kamanda akiwa anaelekea ndani ya nyumba ile. Korido ndefu ilimkaribisha, akaipita na alipoukaribia ule mlango alihisi mwili ukisisimka na nywele kumsimama, akasita kidogo, akautazama na kugonga, haukufunguliwa, akainua simu yak e na kupiga, akaisikia ikiita ndani ya chumba hicho, akagonga tena na tena lakini hakupataa jibu, kengele za hatari zikamgonga kichwani, akatazama kupitia tundu la ufunguo, la haula, hakuamini akionacho, mwili wa Mwadawa ulijilaza kitandani, akagonga tena mlango lakini haukufunguliwa, wala Yule Mwadawa hakutikisika, akaufungua nao ukafunguka bila ubishi, hakuamini akionacho, sura wa Mwadawa aliyokuwa ikimwangalia ililowa damu na kisogoni mwake ndio kabisa, damu ilitapakaa na kuchafua shuka yote, Kamanda Amata alishikwa na ganzi, hakuamini kilichotokea na anachokiona, akavuta hatua zaidi na kuutazama mwili ule, alitikisa kichwa kuonesha masikitiko, hasira ikamtawala, alipotaka kugeuka, akagundua kitu, katika kiganja cha mkono wa Mwadawa, kipande cha karatasi, akakichomoa taratibu kana kwamba hataki kumuamsha huyo aliyelala, akakifungua na kukisoma kiliandikwa JULAI 7, hakuelewa maana ya ujumbe huo lakini pia hakuupuzia, akakiweka mfukoni na kutoka nje, akamuona tena Yule bibi.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mbona watoka kwa masikitiko, vipi, amekusaliti huyo, unaona!” Yule bibi aliendelea na swaga zake, Amata alipitiliza katika gari yake na kuondoka kwa kasi mpaka Yule bibi akabaki kushangaa. Alipotulia akapiga simu ya dharula kituo cha polisi na kuongea askari wa zamu pale Mgomeni, akawapa taarifa ya kutokea mauaji hayo na kuwaelekeza nyumba. Haukupita muda polisi wale walifika na gari yao mpaka katika ile nyumba, wakateremka na kuangalia hali halisi ya tukio lile, vipimo vya kitaalamu kama alama za vidole zilichukuliwa katika maeneo mbalimbali na walipomaliza, waliubeba mwili wa marehemu, huku nyuma wakiacha askari wakiendelea na mahojiano na wapangaji wengine. Kamanda Amata aliifuatili gari ya polisi kwa nyuma mpaka ilipofika Muhimbili na kuhifadhi mwili ule, walipoondoka, yeye akaingia na kukutana na Dr Jasmine ambaye alikuwa zamu siku hiyo, yeye kama daktari pia alibobea katika maswala ya uchunguzi wa maiti.

    Kamanda Amata aliutazama mwili wa msichana Mwadawa uliokuwa umelala katika kitanda cha mochwari pale Muhimbili, pembeni yake akiwepo Dr Jasmin, aliutazama tena na tena hakuamini kilichotokea lakini ukweli ulibaki kuwa uleule tu, Mwadawa ameuawa.

    “Vipi Kamanda?” Dr Jasmin aliuliza

    “Ah! Nilikuwa sijamaliza kazi na huyu msichana, alinisaidia katika sakata hili lakini najua wameshajua hilo ndo maana wamemmaliza,” Kamanda alimjibu Jasmin huku akijifuta kamasi jembamba lilioashiria uchungu wa ndani kwa ndani, akaufunika mwili ule na kuongoza nje ya chumba hicho kisichopendwa na watu akimuacha Dr Jasmin aendelee na uchunguzi wake wa kitabibu.





    >>>>Siku ilofuata



    Gina aliegesha gari katika maegesho ya kampuni ile ya uchukuzi na usambazaji mafuta, wakateremka wote wawili akitangulia Kamata Amata, JOHN SIZIMBA wa bandia. Wakakaribishwa na walinzi na kuongozwa hadi kwenye ofisi ya secretary, pale walimkuta mwanadada mrembo, mweupe, mwenye asili ya kiarabu aliyewakaribisha kwa heshima ya hali ya juu, “ Karibuni, bila shaka ni ugeni kutoka SCOTT,” Amata akatikisa kichwa kuashiria kuwa yuko sahihi, wakaongozwa mpaka kwa meneja mkuu, kutokana na Amata jinsi alivyojibadili ilikuwa vigumu kumgundua. Ndani ya ofisi ile ya meneja walikutana na mtu mnene mwenye tumbo kubwa aliyejaa vema katika kiti chake cha magurudumu kinachokuruhusu kuweza kuzunguka ufanyapo kazi ya hapa na pale. Mtu huyo ambaye nae alikuwa na asili isiyojulikana, mhindi si mhindi, mwarabu si mwarabu, tukimwita chotara tunakosea, tukimwita mwafrika tunajidhalilisha.



    Aliwapokea na kuwakaribisha viti, kisha yule sekretari akachukua kiti kingine na kuketi akiwa na makabrasha machache mkononi mwake.

    “Naitwa Mr John Sizimba, na huyu ni katibu wangu, kutoka kampuni ya Scott,” Amata alitoa utambulisho upande wake na baada ya hapo ukafuatia utambulisho wa upande wa pili, ndipo mazungumzo mengine yalipoendelea juu ya mambo ya kibiashara, baada ya hapo yule meneja aliwachukua Amata na Gina na kuwapeleka kwenye chumba maalum ambacho waliweza kuona uwekezaji huo jinsi ulivyojikita nchini na nje ya nchi, marafiki zao wa kibiashara sehemu mbalimbali za ulimwengu hasa katika bara Hindi. Kamanda Amata hakuwa akisikiliza kwa makini ila alikuwa akikichunguza chumba kile kila kona jinsi kilivyoweka nakshi na ile screen kubwa ambayo iliweza kuwaonesha mambo mengi sana, wakiwa katika chumba hicho, kijana mmoja aliingia ndani na kumnong’oneza kitu yule meneja.

    “Oooh Mr John, uniwie radhi, kuna dharula imejitokea sina budi kuagana nanyi, lakini karibuni wakati mwingine,” yule meneja aliagana na Kamanda Amata na Gina. Akili ya Kamanda Amata ikafanya kazi haraka sana, akagundua kwa vyovyote watakuwa wamemgundua, nae akaagana nae kisha yule sekretari akawaongoza nje, walipofika kwenye uwanja wa yadi ile, kulikuwa na wafanyakazi ambao kila mmoja alionekana kuwa na shughuli yake, wakapita mpaka geti kubwa pale wakakutana na kijana mmoja mwenye asili kama ya yule meneja, Amata akayasoma haraka macho ya yule mtu ambayo yalimpa majibu ya jambo alilolifikiria, hatari. Akatoka nje ya geti hilo na hapo pia akakutana na kijana mwingine mithiri ya yule wa kwanza, nywele za Amata zikasimama kuashiri kuna jambo si jema. Gina alilielekea gari lakini Kamanda Amata alimshika mkono na kumvutia upande wa pili kisha wakakodi tax mojawapo kati ya nyingi zilizopo nje ya eneo hilo na kuondoka zao. Hakuna aliyeongea katika tax hiyo mara kwa mara, Amata alikuwa akiangalia nyuma kuhakikisha kama kuna anayewafuata lakini hali ilikuwa shwari, hakukuwa na jipya.



    6





    SHAILA Shavrij ‘ShaSha’ aliendelea kutulia palepale njiapanda ya Ursino Road akisubiri kile alichokuwa akikisubiri, akiwa ndani ya gari ya kukodi kutoka kampuni Fulani ya jijini Dar, hakushusha hata kioo kimoja bali kiyoyozi kilifanya kazi yake ya kumrejeshea ubaridi, hali iliyo hadimu katika jiji la Dar es salaam. Akiwa gari yake kaitazamisha kule kwenye jingo la Kanisa la Kristo, macho yake hayakutaka kupoteza hata sekunde kuisubiri ile gari aliyoifuatilia ambayo ilikuwa imeingia pale kwenye ile barabara.

    Ama kweli, subira huvuta heri, dakika cache tu, ile gari ilitokea njia ileile na kuchukua barabara ya Bagamoyo kuelekea Mwenge. ShaSha naye akafanya hivyo hivyo, kati yake na lile gari aliruhusu magari mawili tu kumpita. Taa za barabarani zililipendezesha jiji hasa katika njia hii ielekeayo Bagamoyo.

    “Hakikisha hajui uwepo wako, maana malalamiko ya watu yamekuwa mengi, kwani Scoleeti ni nani au anafanya nini zaidi ya ufanya biashara aliyonayo?” ShaSha aliikumbuka sauti ya bosi wake siku alipokuwa akimpa majukumu ya kumfuatili tajiri huyu muuza mafuta.



    Scoletti Ramjo, mzaliwa wa Bombay, lakini alipitisha maisha yake ya ujana huko Mumbai, India, muumini wa dini ya Kiboora aliondokea kuwa mfanya biashara maarufu sana aliyewekeza katika nchi mbalimbali ndani na nje ya Asia, daima alikuwa ni mtu wa kubadilisha makazi kutoka haya kwenda yale, hakutulia mahali pamoja. Kila nchi aliyokaa mfanya biashara huyu, haikuchukua muda ama alifukuzwa au alisababisha matatizo ya kidiplomasia kati ya nchi hizo, alituhumiwa kushirirkiana na vikundi vya kigaidi, kutekeleza mipango michafu dhidi ya binadamu na ubinadamu wenyewe, kuhifadhi wahamiaji haramu ambao hata hawakujulikana kazi yao katika nchi enyeji. Baada ya kufukuzwa huku na huko, Bwana Scolleti aliingia Africa Mashariki miaka kadhaa, akaishi Nairobi na baadae kuhamia Dar es salaam ambako alianzisha kampuni mbili kubwa, moja ya kusafirisha mafuta kwenda nchi za SADC na nyingine ni ile ya zimamoto iliyopo Dar es salaama na kueneza matawi yake katika mikoa mikubwa mingine. Kama kawaida ya Tanzania, taifa la amani, huwa alimfuatilii mtu, linaamini kuwa kila mtu ni mwema, kumbe wapo chui katika ngozi ya kondoo.



    Alipokutana na waziri wa Viwanda na Biashara katika moja ya mikutano ya kimataifa ya kibiashara uliofanyika huko Tokyo, Japan, ndipo alipopitisha ombi lake la kuja kuwekeza katika nchi hii tulivu, wakati huo akiwa ametimuliwa kutoka Thailand baada ya kugundulika kuwa alikuwa akfadhili kikundi cha Tamir Tiger kwa kuwapa silaha kupigana na serikali huku yeye akifanya biashara zake haramu. Akakubaliwa, mipango ikawekwa mezani, mimi na wewe hatujui, labda kuna kiasi kilitolewa kama takrima kwa mabwanyenye, akaingia nchini, haikuchukua muda akaanzisha kampuni yake ya zimamoto na uokoaji yenye vifa vya kisasa kabisa, ilikuwa ni mapinduzi kwani tangu hapo huduma hiyo ilitolewa na kampuni ya jiji tu iliyobaki na gari noja lilichoka kila idara. Baada ya hapo akaanzisha ile ya uchukuzi na usafirishaji wa mafuta, akiwa mbioni kuiomba serikali wampe moja ya visiwa vya Mafia kunakosadikika kuna mafuta ili achimbe. Scolleti pamoja na washirika wake wakajikita katika mwamvuli huo na wakati wa mlipuko wa ubalozi wa USA hapa Dar na Nairobi, alishiriki kikamilifu katika kuwahifadhi na kuwapa kila wanalohitaji wataalamu hao mpaka wakafanikiwa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Tumechoka, kila nchi inatulaumu sisi juu ya huyu mtu,” aliongea bwana Premji, afisa usalama wa India, akimweleza ShaSha.

    “Uende Tanzania, maana tumeshajua kuwa yuko huko kwa muda sasa, hakikisha ukishajua anachofanya, haina haja ya kuwa hai, utajua utafanya nini, sisi tunataka ripoti tu.”



    ShaSha, mwanausalama mtukutu anayejulikana natika kazi, kwa kujiamini kwake na utendaji bora. Alikabidhiwa kabrasha la Scolleti ahakikishe anamtia mkononi kwa hali yoyote ile. shaSha baada ya kukabidhiwa jukumu lile alianza moja kwa moja kwanza kwa kutafuta ni mahali gani katika dunia hi alipojificha, haikuwa kazi ndogo, ilimbidi kusafiri sana kila nchi apitayo, mwisho akajikuta ndani ya Tanzania, akikabiliana na Scolleti, mtu ambaye hajawahi kumuona live isipokuwa kwenye picha tu. Katika chunguzi zake sasa anajikuta anagundua mambo mbalimbali yafanywayo na Scolleti, sasa akaanza kumfuatilia kila mahali akichukua picha mpaka za maswahiba zake, mara ya kwanza alimuona pale White sands Hotel alipokuwa na kikao na swahiba zake wenye ule mpango halifu, lakini Scoletti katika kujilinda ana macho mengi, alishajua uwepo wa SaSha eneo lile hivyo vijana wake wakaweza kumteka na kutoweka nao.



    SaSha aliitazama saa yake ya kwenye gari, ilimuonesha kuwa ni saa nne usiku na dakika kadha wa kadha, aliiacha ile gari ikiingia kwenye yadi kubwa pale Bunju na yeye akapiliza kama mtu yoyote asiye na shughuli na eneo lile, alipakumbuka sana kwa kuwa alishawahi kutekwa na kuhifadhiwa ndani ya yadi hiyo. Kwa mwendo wa taratibu akaegesha gari yake katika moja kilabu kikubwa cha pombe za kizungu mita kama mia nne kutoka ile yadi, akashuka na kujichanganya na wanywaji wengine, kila mtu alimuonea kijicho mtoto huyo wa Kihindi aliyeingia eneo kama hilo, wakware mate yaliwadondoka, wazinzi mioyo ilienda mbio na suruali kupata shida. SaSha, msichana mfupi, mwenye mwili wa wastani kadiri ya kilo 65 hivi, aliyevali fulana nyeusi iliyopambwa na maandishi ‘Mtoto wa Bongo’ ilifunika vijititi vidogo kama vya msichana ambaye hajavunja ungo, jeans nyeusi yenye kigozi ‘Lee’ ilisitiri eneo la chini la mwili wake likiyaficha makalio manene kidogo yaliyoning’inia kwenye kiuno chembamba kabla ya kubebwa na miguu iliyoonekana mikakamavu ingawaje ilikuwa ndani ya suruali.

    Hatua chache zilimfikisha katika kaunta ya bar hiyo na akaagiza kinywaji aina ya Savanna, kwa kuwa aliona jinsi alivyokuwa akitolewa macho na midume ile, akawaagizia pombe kila mmoja.



    Muda ulienda na masaa mawili yakakatika, binti yule akapita njia ya kwenda chooni na kuruka ukuta kutokea nje, upande wa pili wa bar hiyo, akapenyapenya mpaka akatoke barabara kubwa na kuiendea ile yadi. Mwanga mkali wa taa za pikipiki ulimmulika usoni, akajificha macho huku akiipa mgongo ilipompita alishangaa kuiona ikisimama eneo Fulani si mbali sana na pale, hakulifuatilia hilo, aliendelea na yake.







    SHAILAN na watu wake walikuwa katika meza ya duara ndani ya ukumbi mdogo wa mikutano katika yadi ndogo ya Mabibo, walikuwa wakihesabu masaa arobaini yaliyowabakia tangu kuishinikiza serikali imuachie huru ndugu yao mpigania uhuru, Jegan Grashan aliyefungwa na serikali ya Tanzania katika gereza kuu la Ukonga kwa miaka kadhaa. ?Unafikiri watamuachia?? mmoja wa wale vijana wageni aliyejulikana kama Tajan aliuliza. ?Tajan, unakata tama au vipi?? Shakrum alimtupia swali. ?Hapana kaka maana sioni jibu lolote kutoka kwao,? ?Wasipomuachia sisi kuanzia kesho ni kama tulivyoongea na tulivyopanga,? ?Na kuhusu Amata?? Tajana aliuliza tena, ?Maana tulitega bomu kwenye gari yake ila jamaa yule ana machale sana, akapanda tax, tukamkosa,? aliendelea. Shailan akawakatisha, ?Na hakikisheni Kamanda Amata anadhibitiwa vyema, hivi tunavyoongea ni kumzingira nyumbani kwake, haina haja kumkamata bali kumpoteza kabisa,? ?Ila Shailan, usikumbuke kupambana na Amata ukamsahau yule msichana wa Kihindi, hawa wawili wakiungana , maana sijui kama bado au tayari, tutakuwa na hali ngumu,? Shakrum akadakia. ?Usijali, kesho nchi hii itatetema kwa hofu na viongozi wao watapumua hewa ya mauti, dunia itazizima maana yale ya Nigeria, Somalia na Kenya ni cha motto, tutawaonesha patgazeti kisha picha lenyewe linakuja,? Shailan alijitamba huku akiipuliza kahawa yake ipoe kidogo, akainywa na kuagana na maswahiba zake, wakiwa tayari kila mmoja kachukua majukumu yake usiku huo. Tajan na kijana mwingine waliondoka na gari yao kueleka Kinondoni kwa Kamanda Amata, wakati Shakrum aliingia katika chumba kidogo cha mawasiliano. Giza lilikuwa limetawala, hakuna hata mbala mwezi iliyong?aa usiku huo isipokuwa nyota za mbinguni tu. Tajan aliegesha gari yake karibu na geti la nyumba ya Amata, akashuka pamoja na yule mwingine, wakaizunguka nyumba kila mtu upande wake, hakukuwa na njia nyingine zaidi ya ukuta mrefu ambao kuukwea ulitakiwa ujasiri wa hali ya juu, lakini hiyo haikuwa kazi kubwa kwa Tajan, alirudi nyuma hatua kadhaa na kuupanda kwa kasi kama ambavyo buibui apandavyo, na dakika moja tu alikuwa ndani ya wigo huo. Alitulia tuli, akisubiri kusikia kama kuna mchakacho wowote, alipoona kimya alitembea taratibu huku akiwa ameinama na bastola yake mkono ikiwa tayri kufuata amri itakayopewa na mshikaji, alilifikia dirisha kubwa la mbele, akajinyanyua kidogo kurusu paji la uso wake litangulie na macho yafuatie, hakukuonekana dalili ya mtu ndani mle. Akauendea mlango, akautazama kwa jicho lake kali, akachomoa funguo yenye uwezo wa kufungua loki kadhaa za ulimwengu huu, alipoitumbukiza tu, mlango ukajibu, akausukuma taratibu na kujitoma ndani. Hakuruhusu kelele yoyote isikike, akalivuta vazi lake na kufunika uso wote akabaki macho tu, mikono yake iliyovikwa gloves iliikamata bastola kwa ustadi, kwa mwendo wa kunyata, mwendo wa kininja, aliipita sebure na kukuta milango kadhaa, kati ya milango ile, mmoja ulikuwa unawaka taa hafifu na sauti ya muziki laini ilisikika kwa mbali. Tajan akajua sasa windo lake kalipata, akataka kuufungua mlango wa chumba kile, akasita, akabadili mawazo, akaiendea switch kuu ya umeme na kuiweka off, nyumba nzima ikawa giza, akatulia dakika kama mbili ili aone kama kuna mchakacho wowote baada ya giza hilo, hakuna. Akavuta hatua mpaka kwenye ule mlango, akanyonga kitasa, kikanyongeka, mlango ukajiachia kuruhusu nafasi ya mtu kupita, Tajan akaingia ndani na kutulia karibu na kabati paliponing?inizwa makoti na suruali kadhaa, alimuona mtu aliyelala kitandani na kujifunika mwili wote isipokuwa kichwa tu, alitulia palepale na kutoa kikopo kidogo chenye dawa kali ya usingizi, akanyunyiza, hewa ile ikajaa chumba kizima. Alipohakikisha zoezi hilo tayari, akakiedea kitanda na kumsukasuka aliyelala hapo, hakuwa Amata, bali Gina alikuwa kajipumzisha, hakuona haja ya kumuua, ?huyu nikimchukua, Amata atakuja mwenyewe? &#8776;&#8776;&#8776; Utulivu wa ndani ya jengo hilo usiku ule ulimfanya ShaSha afanye upekuzi wake taratibu sana, akichunguza kila droo na kila karatasi aone kama atapata vile avitakavyo, alivuta hili akavuta lile, alifunua hiki akafunua kile, lakini alihakikisha anarudisha katika mtindo ambao wewe au mimi si rahisi kugundua kuwa hapa pamepekuliwa. Taratibu akatoka ndani ya ofisi hiyo ambayo aliona wazi kuwa haina tija kwake, akavuta hatua chache za kunyata katika kigiza cha koridoni na kuufikia mlango mwingine, akautazama kwa makini hata jinsi ambavyo alikuwa anautazama ni kiintelijensia zaidi, akashika kitasa chake na kukinyonga, akashangaa kikiachia na mlango ule kufunguka taratibu. ShaSha akatulia kwanza, akavuta pumzi, akajua huu kwa vyovyote ni mtego, akavuta hatua fupi fupi za tahadhari huku akaingalia pande zote kwa makini mkubwa, akauachia mlango na kukamata bastola yake mkononi, kwa harakaharaka alikikagua chumba kile na kugundua kuwa pia ilikuwa ofisi nyingine kubwa ya kifahari, alihisi kuwa ile itakuwa ndiyo hasa anayoitafuta, alitulia kidogo, ukimya wa ndani ya ofisi hiyo ulimpa faraja ya kujua kuwa hakuna tatizo lolote kama sio shida, akairejesha bastola yake mahala pake nay eye kuiendea meza kubwa iliyopo hapo ambayo juu yake ilibeba kibao chenye maandishi mazuri ya kupendeza yaliyochorwa kwa nakshi safi ya rangi ya dhahabu ?Managing Director? na chini ya hiyo ?Mr Scolleti?, maandishi haya yalimvutia sana ShaSha. Moja kwa moja alianza na motto wa meza akavuta taratibu na kuangali makabrasha kadhaa yaliyopo hapo, akayachambua kwa harakaharaka, alipoona hayana tija akaamia upande mwingine na kufanya vilevile, lakini hapa alipata kitu tofauti, kabrasha moja inaonekana lilimfurahisha zaidi, aklichambua harakaharaka na katika baadhi ya kurasa zake alitumia kamera yake ndogo lakini yenye nguvu sana kupiga picha baadhi ya kurasa hasa mle anamomuhitaji. Alipojiridhisha akarudisha kama vilivyo, na kuweka kamera yake mahali husika kisha akatoka taratibu katika chumba hicho na kuurudishia mlango kama ulivyokuwa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamanda Amata alijua moja kwa moja anchokwenda kukifanya katika jengo hilo lililojengwa ndani ya yadi kiubwa ambayo mchan wake tu alikuwa hapo. Kwa kupitia nyuma ya ukuta wa yadi ile Amata aliweza kuruka na kuingia ndani kwa utulivu, akajibanza kando kidogo ya tenki bovu la mafuta lililotelekezwa hapo, akatulia akiangalia ustaarabu, alipotaka kutoka eneo lile alisikia mchakacho wa hatua zikija upande wake, akazisikiliza kwa makini ili agundue kama ni za mnyama au binadamu, lakini aligundua kuwa ni za miguu miwili, za binadamu, akatulia palepale bila kujitikisa, mara mtu aliyemkuwa akivuta hatua hizo akafika eneo lile, akasimama karibu kabisa na alipo Kamanda Amata lakini hakugundua kama kuna mtu. Yule mlinzi alitazama huku na huku, kimya, akaamua kuondoka, kabla hajavuta hatua ya pili, Kamanda Amata kama umeme aliibuka na kumpiga karate moja ya shingo iliyomfanya alegee na kuanguka, fahamu zikimtoka, Amata akamdaka na kumuweka chini taratibu asilete kokolo wala kelele. Akamruka na kuelekea upande wa pili, akajificha karibu kabisa na choo, akitazama walinzi jinsi walivyojipanga katika eneo lile. Ilikuwa ngumu kwake kuvuka kuelekea jengo lile lenye ofisi kwa sbabu kati yake na lile jengo palikuwa na uwazi mkubwa sana na taa zilizomulika kwa mwanga mkali, hivyo alitulia akipiga mahesabu jinsi ya kuvuka eneo hilo bila kuonekana na walinzi aliyoweza kuwahesabu na idadi yao kufikia kama sita hivi, wazo la haraka likamjia, akamkumbuka yule aliyemzima kwa karate kule nyuma, akageuza kurudi ili afanye lile alilolikusudia Tajan akajua sasa windo lake kalipata, akataka kuufungua mlango wa chumba kile, akasita, akabadili mawazo, akaiendea switch kuu ya umeme na kuiweka off, nyumba nzima ikawa giza, akatulia dakika kama mbili ili aone kama kuna mchakacho wowote baada ya giza hilo, hakuna. Akavuta hatua mpaka kwenye ule mlango, akanyonga kitasa, kikanyongeka, mlango ukajiachia kuruhusu nafasi ya mtu kupita, Tajan akaingia ndani na kutulia karibu na kabati paliponing?inizwa makoti na suruali kadhaa, alimuona mtu aliyelala kitandani na kujifunika mwili wote isipokuwa kichwa tu, alitulia palepale na kutoa kikopo kidogo chenye dawa kali ya usingizi, akanyunyiza, hewa ile ikajaa chumba kizima. Alipohakikisha zoezi hilo tayari, akakiedea kitanda na kumsukasuka aliyelala hapo, hakuwa Amata, bali Gina alikuwa kajipumzisha, hakuona haja ya kumuua, ?huyu nikimchukua, Amata atakuja mwenyewe?





    Kamanda Amata alijua moja kwa moja anchokwenda kukifanya katika jengo hilo lililojengwa ndani ya yadi kiubwa ambayo mchan wake tu alikuwa hapo. Kwa kupitia nyuma ya ukuta wa yadi ile Amata aliweza kuruka na kuingia ndani kwa utulivu, akajibanza kando kidogo ya tenki bovu la mafuta lililotelekezwa hapo, akatulia akiangalia ustaarabu, alipotaka kutoka eneo lile alisikia mchakacho wa hatua zikija upande wake, akazisikiliza kwa makini ili agundue kama ni za mnyama au binadamu, lakini aligundua kuwa ni za miguu miwili, za binadamu, akatulia palepale bila kujitikisa, mara mtu aliyemkuwa akivuta hatua hizo akafika eneo lile, akasimama karibu kabisa na alipo Kamanda Amata lakini hakugundua kama kuna mtu. Yule mlinzi alitazama huku na huku, kimya, akaamua kuondoka, kabla hajavuta hatua ya pili, Kamanda Amata kama umeme aliibuka na kumpiga karate moja ya shingo iliyomfanya alegee na kuanguka, fahamu zikimtoka, Amata akamdaka na kumuweka chini taratibu asilete kokolo wala kelele. Akamruka na kuelekea upande wa pili, akajificha karibu kabisa na choo, akitazama walinzi jinsi walivyojipanga katika eneo lile. Ilikuwa ngumu kwake kuvuka kuelekea jengo lile lenye ofisi kwa sababu kati yake na lile jengo palikuwa na uwazi mkubwa sana na taa za helogene zilimulika kwa mwanga mkali, hivyo alitulia akipiga mahesabu jinsi ya kuvuka eneo hilo bila kuonekana na walinzi aliyoweza kuwahesabu na idadi yao kufikia kama sita hivi, wazo la haraka likamjia, akamkumbuka yule aliyemzimishaa kwa karate kule nyuma, akageuza kurudi ili afanye lile alilolikusudia. Aliusukasuka ule mwili uliolala, akaona hakuna dalili ya mtu huyo kuamka muda huo, akatazama nguo zake, na kuona suruali inashahabiana na ile aliyovaa, akamvua koti na kulivaa kisha akachukua ile bunduki yake kubwa, gobole, akalipachika mgongoni, taratibu akatoka kwa kupitia upande ule alikotokea yule mlinzi, alipofika kwenye kona akasimama, kidogo, kama aliyekumbuka kitu, kweli alisahau kitu kimoja, sigara, yule mlinzi alikuwa anavuta sigara, akaenda na kuinyofoa kinywani mwake kisha akaipachika kati ya vidole vyake viwili cha kati na cha shahada, mkono mwingine ukiwa na tochi, akajitokeza. Mwendo wa kama mita mia akapishana na kundi la walinzi watatu, akajikausha na kujifanya mmoja wao, akapita katikati yao bila kuwaogopa. Baada ya kuyapita malori kadhaa, alilifikia jingo ambalo alilidhamiria, akauendea mlango mdogo ulio upannde wa nyuma nakufanya vitu vyake, sekunde chache alikuwa ndani ya jingo hilo, akatulia kutazama usalama kwa maana alijua wazi kuwa mle ndani kuna camera za usalama kwa kuwa aliziona mchana ule. Ndani ya kijichumba alimokuwamo hakukuwa na kitu kingine zaidi ya mandoo ya takataka, akasonya kwa hasira ya kuwa amekosea mlango, akageuka kutoka lakini akasita, aliporudisha macho ukutani kwa juu kidogo akakuta kuna kamera ndogo mfano wa taa iliyopachikwa kiufundi sana, akatikisa kichwa kuashiria kuwa chumba hicho si bure, kuna jambo, chumba cha takataka kiwekwe camera. Akatuliza akili na kuendea kwa upande wa pili ile camera ili isiweze kupata picha yake alipoifikia alifyatua kiwaya kidogo kilichokuwa kikipeleka mawasiliano kwenye chumba kingine. Akautazama ule ukuta kwa makini ulikuwa umepigwa chuping, akayasukuma sukuma magudulia ya uchafu, akagundua kuwa kumbe kilikuwa choo, choo cha kutumia maji, lakini hakuona kijitenki cha maji isipokuwa bomba dogo pembeni, haina mana. Kamanda Amata hakuelewa hata kwa nini chumba hicho ambacho kilikuwa choo, mara cha takataka kiliwekwa camera, akaachana nacho akaamua kutoka, alipotikisa mlango umefungwa, lo! Yeye hakuufunga, ?Nani kaufunga mlango?? alijiuliza, ?Au wameujua uwepo wangu?? hakupata jibu. Akiwa katika mawazo, alijiegemeza ukutani, mara akahisi kitu kama msumari kikimchoma, akageuka na kupapasa akakutana na kitu hicho, akakitazama kisha akageuka upande wa kulia na kugundua kuwa ile camera ilikuwa ikitazama pale, akatikisa kichwa, akajaribu kukibonyeza, mara ukuta wa mbele yake ukagawanyika taratibu na kuacha uwazi mkubwa, Kamanda Amata akatabasamu na kuvuka kwa tahadhari eneo lile mpaka upande wa pili. Sasa likiona kile chumba anachokitaka, akakijongea na kuufanyia kazi mlango wake kisha akaingia, na kuanza upekuzi wake, ofisi ya ?Managing Director?, akiwa amefanikiwa kupata kabrasha alitakalo ambalo lilikuwa kwenye sefu ya siri sana ambayo si rahisi kuigundua kwa mtu wa kawaida, aliamua kuitoa fotokopi yote katika mashine iliyopo hapohapo ofisini na kisha kuhifadhi vivuli vyake. Akiwa anajiandaa kutoka akaona mlango ukifunguliwa taratibu, akarudi nyuma na kujificha pembeni mwa kabati karibu kabisa na ua la plastick, hakuamini macho yake alipomuona mwandada yule wa Kihindi akiingia, naye akichakurachakura makabrasha lakini alishangaa kuona yeye kachukua kabrasha lingine, hakujua kwa nini.







    Barabara ya Mandela

    “Hakikisha unachomea vizuri, usiruhusu hewa hata kidogo kutoka,” Shakrum alikuwa akimwambia kijana mchomeaji aliyekuwa akifanya kazi ya kutengeneza kitu mfano wa tank la mafuta lakini likiwa na umbo la wastani. Ilikuwa usiku mnene kazi hiyo ilipokuwa ikifanyika, haikuwa kazi rahisi kwa jinsi ambavyo kijitanki hicho kilikuwa kikiendelea kusukwa.

    “Hapa vipi braza?” aliuliza Shakrum.

    “Hapa poa, sasa watatia akili, lazima taifa liteteme kwa hofu,” sauti ya Shailan ilikuwa ikijibu swali la Shakrum.

    Kazi iliendelea mpaka karibu na alfajiri, wakiwa mezani wanakunywa kahawa mara gari moja ndogo ikaingia

    Shakrum aliiacha meza na kuiendea hiyo gari, akafungua mlango na kukuta mwanamke aliyelazwa katika kiti cha nyuma, akamtazama na kutikisa kichwa.



    “Tajan, Amata yuko wapi?” akamuuliza.

    Tajan akafungua kitambaa kilichokuwa shingoni mwake akachukua sigara na kuiwasha, akaipachika kinywani na kupiga pafu kama nne za nguvu, kisha akamtazama Shakrum, “Amata hayupo nyumbani kwake, nimemchukua Malaya wake huyo, najua kwa vyovyote atamtafauta ndipo tutakapomkamata na yeye kiurahisi,” akajibu.

    “Ok, wazo zuri sana,” Shakrum alimpongea Tajan, akawaita walinzi na kuwaamuru wampeleke kwenye chumba maalum, wakafanya hivyo.



    ˜˜˜

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamanda Amata alitoka kwa upole wa hali ya juu katika ngome ile kwa kufuata ujia mrefu ambao hakujua hata ni wapi ulikoelekea, alijua wazi kuwa kurudia njia aliyoingilia ni hatari kubwa hivyo akaamua kutafuata njia nyingine kuweza kuwa huru nje ya jumba lile. Akiwa katika kupitapita ndipo alipokutana na kitu kama kivuli kikitua nyuma yake mita kadhaa kutoka yeye alipo, hisia zake zilimtuma hivyo akaamua kugeuka ili akubaliane na hisia hizo, kosa, alipogeuka tu kabla hajakaa sawa alijikuta akipata mateke mawili yaliyotua usoni mwake kwa mtindo wa round kick, Kamanda Amata alijitahidi kukwepa ijapokuwa lilikuwa ni shambulizi la ghafla lakini hakufanikiwa, aliyumba kidogo lakini mara akawa sawa na kuangalia uelekeo wa adui yake ambaye sasa alimuona akijiviringa chini kwa ufundi mkubwa, akajua kuwa adui yake si mtu wa mchezo hata kidogo, akajiweka sawa. Yule mtu akajiinua kwa kasi ya upepo lakini kabla hajakaa wima alijikuta akipata pigo takatifu lililotua kifuani mwake na kumpotezea uelekeo, Kamanda Amata baada ya kutoa shambulizi lile, kwa mguu wake wa kulia alikanyaga ukuta na kujizungusha hewani alipotua chini mikono yake mikakamavu ilitua na karate safi katika shingo ya adui yake na kumpeleka chini. Kamanda Amata alitulia wima akiwa kajipanga kwa shambulizi linguine lakini hakumuona adui yake pale mbele yake, kabla hajageuka kuangalia nyuma alihisi akipigwa ngwala kutokea upande wa nyuma, akaruka juu kwa sentimeta kadhaa, hakukosea kucheza na hisia zake katika kigiza kile kilichomfanya kila mmoja apambane na adui yake kwa tahadhari.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog