Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

MKANDA WA SIRI - 3

 







    Simulizi : Mkanda Wa Siri

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa 6:31 P.M

    Ilikuwa ni saa kadhaa zimepita baada ya Martin na Richard kuamka. Waliamka na maswali pasipo majibu. Martin alikuwa anamuuliza Richard, Richard alikuwa anamuuliza Martin. Hakuna aliyekuwa na majibu kwa maswali wakiyoulizana. Walilala muda mmoja, waliamka muda mmoja. Nani wa kumjibu mwenzake.

    Mara...simu ya Martin iliita. Alitoa kwa pupa mfukoni. Alikuwa Brown ndiye anapiga. Alijifikiria mara mbili, apokee ama asiipokee. Hakuwa na jibu la maana la kumpa Brown. Hakuipokea.

    Baada ya simu kukatika, ndipo aliona kulikuwa na 'missed call' thelathini katika kioo cha simu yake.

    Jamaa alipagawa!



    Saa 6:37 P.M

    Kule katika kasri ya Chifu hali ilikuwa mbaya sana. Bado Chifu alikuwa anaweweseka chumbani kwake kwa kupotea kwa mkanda wa siri. Binunu nae alikuwa akiutaja mara kwa mara pale sebuleni. Hali ikiyozidisha taharuki na wahka mkubwa katika nyumba ile. Mbaya zaidi hakuna aliyekuwa anajua mkanda umeelekea wapi?



    Upande wa Brown aliamua kuacha kumpigia simu Martin. Alikaa na kutafakari kwa kina kwanini Martin alikuwa hapokei simu yake..... Mawazo juu ya simu yake kutopokelewa na Martin yalikatishwa na mlio wa 'alarm' toka katika saa aliyoivaa katika mkono wake wa kushoto. Akiwa amekaa pale mgahawani ghafla saa hiyo ilitoa mlio mdogo huku ikiwaka taa nyekundu na kuzimika. Alarm!

    Sekunde ya kwanza alistuka sana, lakini sekunde iliyofuata alikuwa ameshapata uamuzi, alinyanyuka haraka kitini na kutoka nje ya Mgahawa. Kwa jinsi alivyotoka ndani ya Mgahawa, watu wote waligeuzia macho yao kwake. Yeye hakujali. Alitembea kwa kasi kuelekea hotelini huku saa yake ikiendelea kutoa mlio, sasa sauti ya 'alarm' ilizidi na taa nyekundu ikiwaka na kuzimika haraka haraka. Brown aliongeza kasi sasa akawa nusu anatembea, nusu anakimbia. Moyo wake ukimtekenya kwa kwa nguvu upande wake wa kushoto wa kifua chake, jasho likiwa linamtiririka, nywele zake alizokuwa amezifunga kwa nyuma sasa zilikuwa zinachezacheza kisogoni kwake, mara ziende kulia, mara ziende kushoto. Mkono wake wa kulia ukiwa ndani ya suruali yake, akiwa kaishika imara bastola yake. Mlio wa 'alarm' wa saa yake na ile taa nyekundu ikiyowaka na kuzimika vilikuwa vinamtaarifu kwamba kuna kitu!



    Yule Jamaa mwenye suti nyeusi alikuwa ameshafika mlangoni katika chumba cha Brown. Akijaribu kufungua mlango wa chumba kile kwa funguo wake maalum. Funguo wenye uwezo wa kufungua mlango wowote ule duniani bila kubisha. Na mlango wa chumba namba 208, chumba kikichomilikiwa na Brown kwa siku ile, ulisalimu amri. Bila shida wala ubishi mlango ulifunguka! Jamaa mwenye suti nyeusi akajitosa ndani mzimamzima, katika chumba kisichokuwa halali yake. Wakati huohuo Brown alikuwa ndani ya lifti akielekea katika ghorofa namba tatu kilipokuwepo chumba chake. Akiwa amewaachia mshangao mkubwa sana kina Irene pale mapokezi. Jamaa aliwapita kama hawaoni vile.....Akiwa kapoteza ule ucheshi na tabasamu lake la siku zote. Sasa sura ya Mr Na na na ilijaa tahayari. Kina Irene hawakuzisikia kabisa zile na na na ambazo walikuwa wameshazizoea. Hakika alijawa na mfadhaiko. Brown aliona kama lifti ilikuwa inamchelewesha vile alitamani kupandisha ghorofa kwa kupanda ngazi huku anakimbia ili afike haraka katika chumba chake. Lakini hakufanya hivyo. Alitulia ndani ya lifti, na ile saa yake ilizidi kutoa mlio lakini sasa taa nyekundu iliwaka moja kwa moja, haikuwa inazimazima tena.... Hatari! CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Brown alisimama ndani ya lifti. Akiwa na kihoro kikubwa sana, akili ikichemka, viungo vya mwili wake vikiwa vimechachamaa. Lifti ikafika katika ghorofa namba tatu. Ikasimama. Alishuka kwa haraka toka katika lifti, sasa alikuwa anakimbia kwa kasi kuelekea chumba chake, chumba namba 208.



    Brown alisimama ndani ya lifti. Akiwa na kihoro kikubwa sana, akili ikichemka, viungo vya mwili wake vikiwa vimechachamaa. Lifti ikafika katika ghorofa namba tatu. Ikasimama. Alishuka kwa haraka toka katika lifti, sasa alikuwa anakimbia kwa kasi kuelekea chumba chake, chumba namba 208.



    Kule Zanzibar, Martin na Richard sasa walirejea katika hali zao za kawaida. Walikuwa wanafikiria vizuri sana. Wakajua jinsi walivyokuwa karibu na hatari. Adui alikuwa anawatambua, lakini wao hawakuwa wanamjua adui yao. Ilikuwa sio hali nzuri kwao.



    "Rich hii ni mbaya sana kwetu, adui anatujua, na anafahamu nyendo zetu bila shaka, na anatulaza muda wowote autakao, na kutuamsha muda wowote autakao, hii ni mbaya sana kwetu mbaya mbaya mbaya sana... maana hata atakapotaka kutuua atatuua muda wowote autakao, sasa kabla hajaamua huo muda wakutuua sisi yatupasa tumuwahi yeye au wao.." Martin aliongea kwa sauti ya upole sana.



    "Ni kweli Martin, we should do something crucial ili tumtambue adui yetu ni nani, na kumwangamiza kabisa, ila kwa hali hii nimejifunza kwamba adui hana haja ya kutuua, labda kuna kitu anategemea kukipata toka kwetu ndipo atuue, maana kama kutuua angekuwa kashatumaliza zamani sana.." Richard nae aliongea huku akitoa maoni yake.



    "Yeah, na sababu ya kutotuua ni mkanda, endapo angeutia mikononi mwake mkanda tungekuwa marehemu zamani sana....shabaha yetu wote ni mkanda bila shaka, huu ndio unaotufanya tulazwe ovyoovyo, nd'o uliofanya tukampoteza Binunu katika mazingira ya kutatanisha, bila shaka adui yetu yupo huko mlikouchukua ule mkanda..."



    "Bara'bara Martin, yatupasa twende kwenye kasri, bila shaka hata Binunu watakuwa nae huko.."



    Majamaa wakapanga mipango yao vizuri kisha wakakubaliana jioni waende katika kasri ya Chifu Abdullah, kumuuwa adui yao, kumuokoa Binunu.

    Na waliamini watafanikiwa.



    Grand villa hoteli, Brown aliukaribia mlango wa chumba chake. Akatoa bastola yake. Akaishika imara kwa mkono wake wa kulia usawa wa kifua chake. Alikuwa ameacha kukimbia, sasa alikuwa ananyata taratibu akiwa kabana pumzi zilizokuwa zinalazimisha kuja kwa kasi kutokana na kukimbia.

    Ghafla...Taa ya saa yake ikiwa imebadili rangi, taa ya kijani sasa ilikuwa inawaka, huku ule mlio wa 'alarm' ukiwa umekata. Brown alishusha pumzi kwa pupa, pumzi zikatoa ukelele mdogo wa hewa. Mfyuuuuuu! Sasa aliusogelea mlango kwa pupa, akiwa hakubaliani kabisa na alichokiona kwenye saa yake.



    "Kwanini taa ya kijana na sio taa nyekundu? "



    Alifungua mlango taratibu akiwa amekata tamaa. Taa ya kijani ilimwambia kweli. Hakukuwa na mtu ndani!

    Alikuwa peke yake!

    Hakukuwa na kitu ambacho taa nyekundu ilimwambia awali. Brown alibabaika. Akasogelea kabati kubwa la nguo mle chumbani, akalifungua kwa tahadhari kubwa sana. Bastola akiwa kaitanguliza mbele. Taa ya kijani ilikuwa sahihi kwa mara nyingine tena. Hakukuwa na mtu ndani ya kabati! Akageuka taratibu na kuelekea bafuni......Akausogelea mlango wa bafuni, akausukuma kwa kutumia bastola yake. Mlango uliitika na kufunguka taratibu. Alitanguliza bastola yake mbele na kuingia bafuni. Kwa mara nyingine tena taa ya kijani ilikuwa sahihi. Bafuni nako hakukuwa na mtu! Alirudi tena chumbani, na bastola yake mkononi, moyo ukimuenda mbio vibaya sana. Mwili ukimtetemeka kama mwanafunzi muoga aliyekamatwa na mwalimu wa zamu tena mkali kwa kuchelewa namba, miguu ilimuisha nguvu, kichwa kilimzunguka, Jasho la kizungu lilimtiririka mwilini mithili ya maji ya bomba, moja ilikuwa haikai, mbili ilikuwa haisimami, tatu haitembei...



    "Inamaana hii saa imenidanganya leo, mmmh aaah nini kimenidanganya ni saa au macho yangu, si taa nyekundu nimeiona kwa macho yangu ilikuwa inawaka lakini? Brown alijiuliza mwenyewe akiwa amesimama katikati ya chumba chake.

    "Hapana, nilikuwa sahihi, mbona mlango wa chumba changu nimeukuta uko wazi wakati niliufunga na funguo niliondoka nayo, ni kitu gani sasa kimetokea? Aliendelea kujiuliza Brown lakini hakuwa na majibu ya maswali yake mwenyewe. Alijiongezea mkanganyiko tu. Saa ya kisasa ya kidijitali ya Brown ilitegwa pamoja na mlango wa chumba 208 kwa namna kwamba mtu akishika tu mlango wa chumba kile inatoa mlio wa 'alarm' na kuwaka na kuzimika taa nyekundu, na pindi mtu atakapokuwa ameingia chumbani kwake, taa nyekundu huwaka mfululizo bila kuzimika, na 'alarm' kuongeza sauti ya kulia. Sasa hayo yote yalitokea leo na kuonwa na kusikiwa na macho na masikio ya Brown lakini cha ajabu haikuwa hivyo kama ilivyomtaarifu, 'alarm' ililia na taa nyekundu iliwaka lakini chumba namba 208 hakukuwa na mtu.

    Lilikuwa ajabu la nane la dunia! CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Saa 12:02 A.M Zanzibar

    Martin na Richard walikuwa mita mia mbili nje ya kasri la Chifu. Walikuwa wanatafuta namna sahihi ya kuingia mle ndani. Nusu saa sasa lakini walikuwa hawajaipata namna sahihi ya kuingia ndani ya kasri. Mbinu waliyotumia awali wakina Binunu mpaka wakaupata mkanda waliiona si sahihi kuitumia tena leo. Wale watu ni makini lazima watakuwa wametafuta mbinu ya kuzuia mbinu yao ile. Walihisi hivyo. Jamaa walianza kusogea taratibu kuelekea kwenye kasri.

    Ndani ya kasri Malkia alikuwa ametulia tuli sebuleni. Akitabasamu. Mara kwa mara alikuwa anaiangalia simu yake ya mkononi. Ghafla, akaita.



    " Malolooooooo "



    "Naaaam Malkia" Malolo aliitika huku akielekea pale alipokaa Malkia.



    "Malolo...nje ya nyumba yetu kuna watu, kuwepo na watu nje ya nyumba yetu sio habari, habari ni kwamba kuna watu wabaya na wenye nia mbaya!" Malkia alisema bila kumwangalia Malolo usoni.



    "Umejuaje hayo yote Malkia?" Malolo aliuliza kwa mshangao mkubwa sana, huku akimwangalia Malkia usoni.



    ".......wapo usawa wa tank la maji ila nje ya ukuta sasa, nenda kawaambie walinzi, naamini wewe pamoja na walinzi mtafanikiwa kuwakamata, na muwalete hapa mbele yangu!"



    Malkia aliongea kwa ukali sasa. Malolo hakuuliza tena swali. Alitikisa kichwa juu-chini ishara ya kukubali, na alitoka nje uso ukiwa umetapakaa mshangao. Haraka haraka na kwa umakini mkubwa sana walinzi walipewa taarifa za kuvamiwa kwa kasri na Malolo. Nao hawakushangaa hata sekunde moja, wakajipanga vizuri na kuingia kazini. Wakati walinzi wanne walio na silaha wakienda kwa umakini mkubwa sana ule usawa wa 'tank' kwa ndani, wengine walitoka nje ya geti.



    Kule nje ya ukuta, usawa wa tank la maji, Martin Nguzu alihisi kitu. Kwa mara nyingine tena alidhihirisha kwanini aliitwa Martin Hisia. Alihisi! Martin alikuwa amezidiwa ujanja mara mbili na mtu ama watu asiowafahamu, Ilimuuma sana, lakini aliapa kimoyomoyo, hakuwa tayari kuzidiwa tena ujanja na mtu yeyote yule, hata awe jasusi kiasi gani, hakuwa tayari kurudia tena kosa. 'Kosa si kosa kurudia kosa.....'

    Kwa uwezo wake aliopewa na Mwenyezi Mungu tangu akiwa mtoto mdogo, uwezo wa juu kabisa wa kuhisi pale tu hatari inaposogelea mahali alipo. Kwa kutumia uwezo uleule, Martin Hisia alihisi kwamba kuna hatari ilikuwa inawasogelea kwa kasi kubwa sana pale walipokuwa yeye na Richard. Hisia zilimwambia hivyo na aliziamini....kwanini asiziamini hisia zilizowahi kumuokoa mara nyingi sana. Na hisia zake zilikuwa sahihi kama zilivyoanza kimaajabu kuwa sahihi siku ile alipowaambia wazazi wake wasilale katika nyumba yao kwakuwa kulikuwa na hatari njiani, wazazi wake walibisha sana, lakini Martin alilia kwa nguvu mpaka wazazi wake waliona kero na kukubali kuhama.. Siku ile familia nzima ilienda kulala kwa dada yake na mzee Nguzu, na usiku ule kilitokea kitu kilichomshangaza kila aliyesikia kwamba aliyewashauri wasilale katika nyumba yao ni mtoto Martin. Usiku wa manane nyumba yao iliungua moto, chanzo cha moto huo ni kitendawili mpaka leo. Tokea siku ile hisia za Martin ziliaminiwa na kila mtu pale kijijini kwao. Alishawaokoa marafiki zake mara kadhaa kushambuliwa na wanyama wakali walipoenda kuwinda mwituni. Alishawaokoa watu wa kijijini kwao mara kadhaa na hatari mbalimbali kwa kutumia hisia tu. Kumbuka mambo hayo alianza kuyafanya akiwa na umri wa miaka saba tu, na ndipo jina la Martin Hisia lilikuwa maarufu. Umaarufu wa Martin ulianzia huko kwao, katika visiwa vya Ukerewe na kusambaa kwa kasi katika mikoa yote ya kanda ya ziwa, na mwishowe Tanzania nzima. Kuenea kwa umaarufu wake wa kuwa na hisia za ajabu kulienda sambamba na kufutika jina la baba yake, na watu wote kumuita Martin Hisia badala ya Martin Nguzu!



    "Richard tuondoke hapa kuna hatari, hisia zangu zinasema....kwa jinsi tulipo kusonga mbele ni ushujaa lakini kurudi nyuma ni ushujaa zaidi" Martin alisema maneno hayo taratibu sana lakini yalipenya vizuri sana katika masikio yote mawili ya Richard. Na Richard hakubisha, unaanzaje kumbishia mwanaume yule mwenye hisia kuliko mwanaume yeyote yule duniani.

    Wanaume wakatokomea!



    Walinzi wote wa kasri ya Chifu Abdullah waliitwa usiku huohuo. Taarifa kama hakukuwepo na watu nyuma ya 'tank' hazikuingia kabisa katika ubongo wa Malkia. Alikuwa na uhakika wa asilimia mia tisa kwamba wale jamaa aliowalaza katika kiwanja cha Maisala walikuwa wameenda pale, tena walikuwa usawa wa 'tank' la maji. Ingawa hakutaka kusema alilitambua vipi hilo... Malkia alimalizia hasira zake kwa kuwakaripia tu walinzi.

    Wote walibaki wakimshangaa.





    Dar es salaam, Mwenge.



    JAMAA mwenye suti nyeusi alikuwa anatembea katika mitaa ya Mwenge. Alikuwa anatembea huku akiwaza jinsi alivyokiepuka kifo! Ilikuwa hivi....



    Jamaa alivyoingia tu ndani ya chumba cha Brown hakufanya chochote, akili yake ilimwambia moja kwa moja aende dirishani. Alipofika tu dirishani kwa kupitia dirisha alimuona yule mzungu akiwa katika jezi za timu ya taifa la Congo, nywele zilimsisimka, na kuzipongeza akili zake. Mzungu alikuwa anaenda katika mlango wa hoteli kwa kasi kubwa sana. Ndipo nae kwa ustadi mkubwa alipovunja dirisha la kioo la hoteli ile, bahati ilikuwa yake, alikutana na bomba nene la maji machafu likiwa linaelekea chini, jamaa alishuka chini kwa kutumia lile bomba la maji machafu, ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake, kwanza bomba lilikuwa linateleza sana, pili alikuwa anajianika endapo walinzi watakuwa makini kule chini, wangeweza kumuona.... lakini mwanaume alifanikiwa. Alipofika usawa wa ghorofa la na pili alikutana na dirisha lengine la kioo, sawa na lile alilolivunja awali chumba namba 208, akajua na kile ni chumba kile ..Kwa nguvu zake zote alipiga miguu yake yote miwili katika kioo cha dirisha! mikono yake ikiwa imelishika imara lile bomba la maji machafu. Vioo vilivyovunjika vilitangulia kuingia ndani ya chumba kisha ikafuatia miguu na kiwiliwili. Jamaa alivunja tena kioo cha chumba kingine na kuingia ndani. Mle ndani, alimkuta mzee wa makamo akiwa kalala na mwanamke kitandani, labda alikuwa mkewe..... Ukelele wa kioo uliwastua sana wale wageni walioenda kupumzika katika hoteli ya Grand villa. Walipigwa na butwaa!

    Huku wakiwa wamejifunika shuka jeupe lililoishia kifuani mwao. Walikuwa wamekalia mgongo kitandani, na walikuwa wanatazamana uso kwa uso na jamaa mwenye suti nyeusi, akiwa na bastola yake mkononi. Haraka kidole cha mkono wa kushoto cha shahada cha Jamaa kilisimama katikati ya mdomo wake, huku akiwa amewatolea macho, ishara kwamba wasiseme neno lolote, bwana na bibi waliishia kuguna tu, huku machozi yakiwatoka kimya kimya, yule msichana hakuweza kuidhibiti haja ndogo isimtoke, hakuwahi kuuona mdomo wa bastola. Jamaa wala hakujari, alisogea kinyumenyume hadi katika simu ya mezani ya mle chumbani, bastola ikiwa kaielekezea pale kitandani, akauvuta waya wa simu kwa mkono.

    Ukakatika! CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa mwendo wake wa taratibu na umakini mkubwa alisogea hadi katika mlango, aliikuta funguo ya mlango katika komeo, akafungua mlango na funguo akatoka nayo nje, kule nje akauingiza ule funguo, akawafungia kinje-nje. Pale kwenye korido aliisubiri lifti kwa sekunde kama kumi, akapanda, ikampeleka hadi ghorofa ya chini kabisa. Akatoka kwenye lifti akitembea taratibu. Pale mapokezi aliwapungia mkono wale wahudumu huku akitabasamu nao walitabasamu. Irene alimwita kwa ishara ya mkono huku akitabasamu. Sekunde ya kwanza jamaa alistuka, sekunde ya pili alielewa. Alienda pale mapokezi, alipofika akaweka funguo ya chumba cha wale wazee mezani. Irene na Paulina hawakuwa makini kuichunguza ile funguo. Jamaa akatokomea. Jamaa mwenye suti nyeusi alitembea hadi Mwenge. Akaingia katika choo cha stendi ya Mwenge. Akabadili zile nguo harakaharaka. Chooni aliingia jamaa mwenye suti safi nyeusi, jamaa aliyekuwa maridadi sana lakini alitoka mtu mchafu sana mwenye muenekano wa kiuendawazimu....ndio!..alikuwa mwendawazimu....ndio!..alikuwa Peter Kisali!



    Ndani ya kasri ya Chifu...Hali ya Binunu iliendelea kuwa mbaya. Kwa sasa familia ya Chifu ilikuwa imeajiri daktari mwengine, na siku aliyoajiriwa tu alikutana na kesi ya Binunu. Daktari alifanya kila alichowezakurudisha akili ya Binunu, lakini ilikuwa bado.



    Brown sasa alikuwa amehamia katika hoteli ya Double Tree. Baada ya tukio la kustaajabisha kule Grand villa, Brown aliona kuendelea kukaa katika hoteli ile ni kukisubiri kifo chake mwenyewe. Baada ya kukagua vitu vyake na kuvikuta vipo sawa, Brown alihama katika hoteli ile usiku uleule, bila kutambua huyo mvamizi alipitia wapi, aliona kuendelea kukaa katika chumba kile ni hatari zaidi.



    Jeshi la Polisi licha ya kulijua jina la mmiliki wa ile Range Rover VOGUE ambalo waliikuta maiti ya Mansour ndani yake, lakini ni wiki sasa walikuwa hawajamtia mikononi mmiliki wa Range Rover ile. Kifo cha Mansour kilibaki kuwa na utata. Licha ya tukio hilo ambalo liliandikwa sana katika vyombo vya habari mbalimbali nchini.

    Sasa katika meza ya Polisi walikuwa na faili la kesi nyingine yenye utata..... 'Kesi ya uvamizi na wizi wa madini katika hoteli ya Grand villa'.



    Wale majamaa mle chumbani walikaa ndani ya chumba wakiwa na hofu kubwa sana. Wakijua kwamba muda wowote yule mvamizi mwenye suti nyeusi angerejea na kwenda kumpora mali zake. Walikuwa hawana ujanja kwa kuwa walikuwa wamefungiwa mlango kwa nje. Yule mzee alikuwa ni mfanyabiashara wa madini toka Geita na alikwenda jijini Dar es salaam kwa minajili ya kuuza madini yake. Alifika uwanja wa ndege jioni ya siku ile, Muuza madini aliulizia hoteli yenye hadhi ya juu na ulinzi wa uhakika kwa dereva teksi, na dereva teksi alimwambia kwamba hoteli yenye sifa hizo ni Grand villa. Ndipo alipokodi teksi toka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere mpaka Kijitonyama katika hoteli ya Grand villa. Hiyo ilikuwa saa kumi na moja jioni.



    Muuza madini alifika hadi katika hoteli ya Grand villa na kukutana na kina Irene pale mapokezi na kukabidhiwa funguo ya chumba namba 103 katika ghorofa ya pili. Baada ya kuweka vitu vyake sawa chumbani kwake, alitoka kidogo.....



    Muuza madini alirejea baada ya nusu saa akiwa na mwanamke pembeni yake. Wakiwa wamelala kwa muda wa saa moja tu na huyo mwanamke, ndipo walipostukia dirisha lao likivunjwa kwa nguvu tokea nje na mtu kuingia ndani akiwa na bastola! Lakini cha ajabu huyo mtu hakuwafanya chochote zaidi ya kukata waya wa simu ya mezani na kisha kuwafungia mlango kwa nje. Bila shaka akitaka wasiwasiliane na mtu yeyote yule katika hoteli ile. Walikaa kimya wakiwa na hofu kubwa mioyoni mwao saa kadhaa, walikuwa wanahisi yule jamaa mwenye suti nyeusi angeweza rejea muda wowote ule. Na kilichokuwa kinapita katika kichwa cha yule mzee Muuza madini kuwa safari hii atakuja kuchukua almasi zake pamoja na kumuuwa!.



    Zilipita takribani saa tatu bila kutokea lolote. Jamaa mwenye suti nyeusi hakurejea. Waliamua kutafuta namna ili wapate msaada, simu ya mezani ambayo ingewawezesha kupiga mapokezi ili wapate msaada ilikuwa imekatwa waya! Muuza madini alienda mlangoni na kuanza kuupigapiga mlango kwa nguvu, sauti ya mlango ilisikiwa na walinzi waliokuwa wanatembeatembea katika korido ndefu ya hoteli ile kuimarisha ulinzi. Taarifa za mteja anayegonga mlango akiwa ndani zikapelekwa katika uongozi wa hoteli, harakaharaka chumba kilienda kufunguliwa kwa funguo ya akiba.



    Baada ya Muuza madini kuelezea kilichotokea kwa uongozi wa hoteli, haraka taarifa ile waliiripoti katika kituo cha Polisi Mabatini. Kosa alilolifanya Muuza madini hakuwa makini kabisa, yale mambo hakuyategemea, laiti angekuwa makini kidogo angetambua kwamba yule mwanamke ambaye alikutana nae tu pale Kona bar na kukubaliana kwenda kumstarehesha kwa malipo pale hotelini alikuwa ametoweka wakati wa hekaheka zile.



    Baada ya askari Polisi kuwasili na habari juu ya tukio lile kujulikana kwa wafanyakazi wote wa hoteli, ni Irene ndiye aliyedai kumtambua mvamizi.



    "Namjua aliyefanya hivyo!" Irene aliropoka katika kikao kati ya uongozi wa hoteli na Polisi. Watu wote walimwangalia yeye huku Koplo Baruani akiwa makini zaidi.



    "Ni nani aliyefanya hivyo?" koplo Baruani aliuliza kwa sauti yake ya upole.



    "Ni Mr Na na na....." Irene na Paulina walisema kwa pamoja.



    "Mr Na na na....?" Koplo Baruani alilirudia lile jina huku akiwaangalia kwa zamu wale wahudumu wawili.



    "Ndio afande...Mr Na na na ndiye itakuwa kafanya hayo" Irene alijibu.



    "Hebu elezea vizuri Mr Na na na nd'o nani?"



    "Ni mzungu...mzungu kwa ngozi lakini anaongea kiswahili, tena kiswahili fasaha.... ana...itwa Michael, Michael Zuuu nani sijui"



    "Uliandika maelezo yake katika kitabu wakati anawasili?"



    "Ndio"



    "Wewe kachukue kitabu cha wateja" Koplo Baruani alisema huku akimuonesha kidole Paulina.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Eeeeh umesema anaitwa Michael, kwanini mwanzo ulisema anaitwa Mr Na na na......"



    "Aaah mmmh anaongea kiswahili, tena kiswahili fasaha, lakini akifikia kwenye herufi na anairudia mara kadhaa"



    "Kwanini unahisi yeye ndo atakuwa mvamizi?"



    "Nilimuona alivyoingia kwa kasi baada tu ya huyu mteja kuingia hotelini na msichana...na pia alitoka kwa kasi bila kuaga, na hakurejea tena"



    "Inawezekana ukawa sahihi binti ama usiwe sahihi, umesema huyu mteja alikuja na msichana yuko wapi huyo msichana mwenyewe?"

    Swali la Koplo Baruani toka katika kituo cha Polisi cha Mabatini likazua kizaazaa kipya, kizaazaa cha kumtafuta msichana aliyekuja na yule mteja, lakini hawakumuona. Askari Polisi, Irene, pamoja na uongozi wa hoteli ya Grand villa walienda katika chumba alichopanga Brown, hawakukumkuta lakini dirisha lake ambalo lilikuwa limevunjwa liliwaaminisha yaliyosemwa na Irene. Walirudi kwenda katika chumba cha yule mteja kukagua, vitu vyote vilikuwa salama isipokuwa madini ya yule jamaa.

    Alikuwa ameibiwa!



    "Bila shaka huyo jamaa mwenye suti nyeusi atakuwa anashirikiana na huyo msichana... Huyo alikuja kukuchanganya tu ili huyo msichana apate nafasi ya kukuibia" Koplo Baruani alitoa mawazo yake.



    "Lakini mimi sijaelewa afande.... Mhudumu amesema huyo Mr na na na ni mzungu, lakini aliyekuja kuvamia katika chumba changu hakuwa mzungu, alikuwa mtu mweusi tena alikuwa amevaa suti nyeusi!" Muuza madini alisema huku machozi yakimdondoka.



    Hapo ndipo utata ulipoanzia!



    Saa 8:45 P.M Forodhani;



    Zanzibar Kama ilivyo desturi kwa wakazi wa visiwa vya Zanzibar ifikapo muda wa jioni... watu wengi hukusanyika katika eneo maarufu kama Forodhani. Katika eneo hilo watu lukuki hukusanyika kwa minajili ya kujipatia chakula cha jioni, na wengine huenda kama sehemu ya miadi na rafiki zao, lengo ni kukutana na jamaa zao na kubadirishana mawazo mbalimbali. Usiku wa siku hiyo watu walikuwa wamejaa wengi sana katika eneo hilo la Forodhani. Miongoni mwa watu hao walikuwemo Richard Philipo na Martin Nguzu. Nao walikuwa wakijipatia chakula cha jioni kama wafanyavyo wakazi wa wengi wa Unguja.



    Zanzibar: 08:48 P.M

    Ndani ya Kasri ya Chifu



    "Twende Forodhani sasahivi, adui yuko Forodhani Malolo!" Malkia alimwambia Malolo kwa sauti kubwa wakiwa sebuleni.



    "Adui yuko Forodhani?



    Kivipi? Umejuaje Malkia? Kwa namna gani? Mbona sikuelewi?" Malolo aliuliza maswali lukuki kwa sauti yenye mshangao mkubwa.



    " Twende Forodhani haraka brother! mambo mengine tutayajua hukohuko na maswali utauliza baada ya kurudi, ila jipange kwa vita...twenze'tu we don't have enough time for discussion here!" Malkia alisema huku akinyanyuka toka sofani.

    Na Malolo alinyanyuka.



    Malkia na Malolo walienda kwenye gari ndogo aina ya Toyota, Suzuki, gari hiyo ilikuwa miongoni mwa magari mengi yaliopo katika uwa mpana wa kasri ya Chifu. Walipanda na kuelekea Forodhani, huku Malolo akiwa na maswali kadhaa kichwani mwake juu ya uwezo wa ajabu wa Malkia aliokuwa anauonesha siku za hivi karibuni.



    Kule Forodhani kina Martin walikuwa wamekaa katika kibanda kimoja wakila chakula, bila kujua kuwa hatari ilikuwa njiani na ilikuwa inawafata kwa kasi kubwa sana! Wakiwa njiani Malkia alikuwa anaangalia simu yake mara kwa mara na kumuhimiza Malolo aongeze mwendokasi wa gari. Malolo alitia gia kweli. Nusu saa baadae walifika Forodhani. Waliukuta umati mkubwa wa watu. Huku makundi ya watu walikuwa katika meza zilizokuwa na samaki wa kukaanga, pweza na ngisi wakiwa wanakula huku wamesimama. Pamoja na umati mkubwa wa watu lakini waliwaona.

    Malkia ndiye aliyekuwa anatoa uelekeo juu ya sehemu alipo adui huku akiiangalia simu yake mara kwa mara. Ilikuwa kama simu yake ndio ilikuwa ikimuelekeza mahali alipo adui. Malolo alikuwa anashangaa huku akimfata Malkia kwa nyuma kimyakimya, akiwa tayari kwa lolote. Sasa kina Malkia walikuwa wamejificha katika kibanda kimoja cha muuza urojo huku wakiwashuhudia kina Martin wakila chakula. Walitulia tuli wakisubiri muda muafaka wa kuwavamia.



    Martin na Richard walikuwa wanakula. Mezani kwao ilikuwa...Martin anakula vibanzi kwa kuku na Richard alikuwa anakula vibanzi kwa mishkaki. Huku vyupa vikubwa vya maji ya baridi vikiwa pembeni mwao. Majamaa walikuwa wanakula huku kila mmoja kichwani mwake akitafakari kazi nzito iliyokuwa inawakabili.



    Ghafla! Vilitokea vitu viwili kwa mpigo.



    Kwanza hisia za ajabu, hisia zimpatazo Martin mara chache sana, hisia zinazowasilisha kitu kimoja tu siku zote, zilimjia. Hatari!

    Ilikuwa ni ishara kuwa walikuwa wanakaribiwa na hatari.



    Jambo la pili simu ya Martin iliita. Kuangalia jina katika kioo lilisomeka Brown. Safari hii Martin alipokea.



    "Hallo Martin Hisia" Brown aliita kwa kutoamini kwamba simu yake ilikuwa imepokelewa.



    "Nambie Mzungu"



    "Najua hali si ya kawaida, naomba unambie kwa percentage ngapi?" Bila kuleta malalamiko ya kutopokelewa simu yake, Brown alianza na swali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mbaya sana mzee, mbaya mbaya yaani, Its below 50%, hawa majamaa wamejipanga sana kumbe.." Martin alijibu kwa fadhaha.



    "Nipo Bongo now, nimekuja kuweka mambo sawa, hata mimi nimeona kuna vitu haviko sawa...ila hatuwezi kudhulumiwa na hao kenge!"



    "Vitu gani Brown?" Martin aliuliza huku zile hisia kwamba walikuwa karibu na hatari zikishamili mwilini mwake.



    "Kuna Mwendawazimu ananifatilia sana, ila nitamuonesha!"



    "Anaufatilia moto huyo!"



    "Utamuunguza haki ya Mungu nakwambia!"



    "Mko wapi sasa Martin, na vipi kuhusu Mkanda....?"



    "Tuko Zanzibar, kuhusu mkanda ni habari nzito sana, njoo utuongezee nguvu Bosi..wametuzidi ujanja bloody bastards!"



    "Naja huko kwa boti ya saa moja asubuhi..."



    "Welcome to the game!"

    Simu ikakatwa.

    Cha ajabu Brown aliongea bila kuweka zile na na na kama akivyoongea na kina Irene kule Grand Villa hoteli.....



    Martin alikuwa amelimaliza jambo moja , sasa lilibaki jambo moja, ni kuhusu hatari iliyokuwa inawakaribia ambayo alikuwa amejulishwa na hisia zake, hisia ambazo hazikuwahi kumdanganya hata mara moja tangu akiwa na umri wa miaka saba. Wakiwa wamejificha katika kile kibanda cha muuza urojo Malkia alimnong'oneza Malolo.



    "Malolo, kuna Mzungu atakuja kesho asubuhi, anaitwa Brown. Itabidi tumpokee sisi kabla ya wenyeji wake..." Malkia alisema kwa sauti ndogo lakini iliyosikiwa vizuri na masikio ya Malolo.



    "Mzungu tena! Anakuja kwenye misheni hii ama nyingine?" Malolo aliuliza kwa wahka mkubwa na kushangazwa sana na taarifa ile toka kwa Malkia.



    "Anakuja kwa hii mission Brother...Malolo bwana sasa unaogopa kwa kuwa umesikia Mzungu" Malkia alimuuliza huku akimwangalia na kutabasamu.



    "Usijari Malkia..tutamtaitisha huyo Mzungu, sijawahi kumuogopa mtu yeyote yule katika ulimwengu huu, na haitatokea, sina msamiati unaoitwa woga katika kamusi ya kichwa changu..."



    "Nakutania brother, sasa kuhusu hawa majamaa tuachane nao, huyo Mzungu i think ni muhimu zaidi kwa sasa, inaonesha anayajua mengi kuliko hawa" Malkia aliongea akiwa na uhakika tele.



    "Sawa, haina neno Malkia" Malkia na Malolo walirejea katika kasri ya Chifu Abdullah.



    Wakiwa njiani Malkia alimpigia simu Peter Kissali 'Mwendawazimu'.



    "Hallo Malkia mwenyewe, lete mpya.."



    "Mwendawazimu usimfuatilie huyo Mzungu"



    "Kwanini Malkia, kuna vitu anavijua yule, nahisi ni muhimu sana kwetu.."



    "Ni kweli ulisemalo, hata mimi nimeligundua hilo, na inawezekana ana uhusiano mkubwa na yule mzee wa kizungu aliyerekodi mkanda wa siri, lakini tatizo ameshagundua kama unamfatilia"



    "Sio kweli Malkia, sio kweli kabisa, namfatilia kiakili, hana ujanja huo wa kugundua, hana kabisa nakwambia.."



    "Kajua sasa Mwendawazimu, huyo mzungu inaonesha ni mtu hatari sana, nakupa oda mpya sasa...kesho asubuhi njoo Zanzibar, tuumalize huku huu mchezo"



    "Nimekusoma Malkia, wewe hesabu kuwa Game is over, si unajua kazi yetu nikikutana na Malolo..............." Peter alikuwa anaongea simuni peke yake, simu ilikuwa imekatwa zamani. Peter aliiangalia simu yake na kutabasamu.



    Njia nzima Malolo alibaki mdomo wazi. Akionesha mshangao wake waziwazi, alisikia kila kitu alichokuwa anaongea Malkia na Patna wake katika Operesheni mbalimbali, Peter, lakini alikuwa haelewi habari hizo nyeti Malkia alikuwa anazitoa wapi. Alitamani kamuuliza wakiwa mle ndani ya gari, lakini alinyamaza. "Nitajua tu.." Alijisemea kimoyomoyo.



    Saa 6:00 A.M Zanzibar

    Alfajiri ilikuja na jambo jipya lililozua taharuki kubwa sana!

    Gazeti linalomilikiwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, gazeti lenye wasomaji wengi zaidi Zanzibar, gazeti la Unguja Leo, habari katika kurasa yake ya mbele ilikuwa inamuhusu Martin Nguzu. Huku chini ya kichwa cha habari kukiwa na picha ya Martin. Gazeti lilikuwa na neno moja tu lililokolezwa kwa wino mweusi.. ANATAFUTWA!

    Habari ile ilikuwa inamhusisha moja kwa moja Martin Nguzu na mauaji ya Mansour. Alfajiri hiyo Martin na Richard kila mmoja alikuwa na nakala ya gazeti hilo mkononi. Martin alishairudia kuisoma habari hiyo mara saba lakini hakuielewa hata chembe.

    Kwanza ilimshangaza na kumpa taarifa mpya, hakuwa na habari kabisa kama Mansour alikuwa ameuwawa. Ajabu lengine ni kwamba.... muda ambao ulitajwa kuwa Mansour ameuwawa yeye alikuwa visiwani Zanzibar na Richard alikuwa shahidi wa hilo.

    Kwanza kwanini amuue Mansour..mshirika wake katika mambo kadhaa akiwa jijini Dar es salaam.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hii ngoma sasa imekuwa nzito sana, hivi Richard unamjua Mansour vizuri, si mtu wa kufa kama kondoo kama ilivyoandikwa hapa, jamaa alikuwa mkorofi sana, ni bingwa wa ngumi za mitaani, kama aliuwawa ndani ya gari, vurugu lake wasingekuta kiti hata kimoja haki ya Mungu nakwambia, kwanza waliwezaje kuingia ndani ya gari wakati funguo ninao mimi" Martin alisema huku akiuangalia funguo ya gari yake pale mezani, aliangalia juu huku akitafakari

    ".......kwa vyovyote vile aliyemuuwa Mansour atakuwa ni mtu hatari sana" Alishusha sura yake na kumwangalia Richard.

    "...... na inawezekana kifo chake kina uhusiano na hii misheni yetu ... " Alimalizia huku akimwangalia Richard.



    "Yaani mimi sielewi kabisa kitu gani kimetokea..." Richard aliongea wakiwa bado wanatazamana na Martin.



    ".....huu muda waliouandika hapa wewe ulikuwa Zanzibar, tena tulikuwa Maisala, kwanini utajwe wewe kama muuaji" Richard aliongea huku kidole chake kikiligusa gazeti pale mahali walipoandika muda aliofariki Mansour kwa mujibu wa madaktari walioufanyia vipimo vya uchunguzi mwili ule.

    "......hii ni mbaya sana kwetu best" Aliongea akiwa amekata tamaa.



    "Nahisi kuna msururu wa watu wengi sana katika hii ishu, tena watu makini wenye kujua wakifanyacho.... itakuwa Chifu ana watu Dar na Zenji, watu makini hivyo yatupasa tuwe makini sana" Martin alihitimisha.



    *****



    Ilitoka katika mdomo wa Msemaji wa jeshi la Polisi na kufika katika sikio la Mwandishi wa habari, baada ya kuridhika na uzito wa habari hiyo, alichukua kalamu yake na kuiandika vizuri sana katika karatasi nyeupe, kisha ile karatasi aliipeleka kwa Mhariri mkuu wa gazeti kama afanyavyo siku zote, habari ikapitishwa na Mhariri na ikakidhi sifa ya kuwekwa katika kurasa ya mbele ya gazeti la Unguja Leo. Gazeti likakamilika likiwa na habari ile, tena katika kurasa ya mbele kabisa! Gazeti likafika kwa wasambazaji wakubwa, kisha wadogo.....Gazeti likatembea mitaani likiwa na habari hiyo, pamoja na katika meza kadhaa za wauza magazeti, watu kadhaa wakanunua gazeti hilo, bara na visiwani..wakiwemo wakina Martin. Gazeti liliendelea kusambazwa mtaani na kufika katika kasri ya Chifu, ndani ya kasri hiyo likatua katika mikono ya mwanamke hatari wa kipemba! .........Malkia nae alianza kuisoma ile habari kwa utulivu mkubwa..



    Neno Anatafutwa lilikuwepo juu ya picha ya Martin katika kurasa ya mbele kabisa katika gazeti la Unguja Leo, lakini habari kamili ilikuwepo katika kurasa ya pili ya gazeti hilo. Malkia alifunua ukurasa mmoja na kuanza kuisoma.



    ANATAFUTWA

    Na Mwandishi wetu.



    'Mtu mmoja mkazi wa Mikocheni jijini Dar es salaam anatafutwa na jeshi la Polisi nchini kwa tuhuma za kufanya mauaji! Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 na ametambulika kwa jina la Martin Nguzu anatuhumiwa kwa mauaji ya kijana aitwaye Mansour. Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa jeshi la Polisi, kijana Mansour aliuuwawa kwa kuvunjwa shingo na maiti yake kutelekezwa ndani ya gari aina ya Range Rover Vogue yenye no za usajili T001 AFG. Kwa mujibu wa daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kijana huyo ameuwawa majira ya saa....'



    Malkia hakuendelea kusoma habari hiyo, alilitupa gazeti sofani na kusimama, akiwa amejishika mikono kiunoni, akapumua kwa nguvu, akatabasamu...Malkia alikuwa ameyapata mambo makuu mawili akiyoyahitaji sana, mwanzoni mbele ya kurasa ya gazeti alikuwa ameiona sura ya kijana aliyemlaza katika viwanja vya Maisala. Na sasa alikuwa amelitambua jina la kijana huyo. Bahati ilioje? Hivyo ndivyo vitu vikuu Malkia alivyokuwa anavitafuta sana.



    "This mission imekwisha...lakini.... lakini huyu jamaa bila shaka... ata...kuwa Ma...rtin, Martin Hisia" Malkia alihisi anasema taratibu kumbe sauti yake ilisikiwa na masikio ya Malolo.



    "Martin Hisia!" Malolo aling'aka kwa sauti kuu.



    "Ndiye, bila shaka atakuwa ndiye hiko kikaragosi wanachokikweza kwa sifa kemkem, eti...Martin Hisia!" Malkia alisisitiza kwa kejeri.



    "Kama ni kweli tuna kazi kubwa sana ya kufanya Malkia, Martin Hisia ni mtu hatari sana....."



    "Umeanza woga wako Mpumbavu wewe!, hamna cha Martin Hisia wala Martin nini sijui , kumbuka hawa mazuzu nilivyowafanya pale Maisala, na huyu Zuzu alikuwepo pia!, mbona hakuhisi kitu chochote, zile ni hadithi tu, sawa na hadithi za Abunuasi. Hadithi za kufikirika! Hadithi za Aliyeonja Pepo! Hadithi tu za kuwajengea watu uwoga. Wamuogope, wamtetemekee, eti Martin Hisia labda unambie ni Martin Mzembe anayependa kulala hovyo..achana na hadithi mwanaume, hadithi ni hadithi tu, let's go to the reality, Martin Hisia tuna......" Malkia alisema huku akikipitisha kiganja cha mkono wake wa kulia katikati ya shingo yake. Ishara kwamba Martin Hisia watamuua kwa kumchinja!



    "Mh, haya ila Martin Hisia ni..."



    "Shut up Malolo, tutagombana bure we khabithi mkubwa! uwoga na hofu hapa si mahala pake! Upo na mwanamke shupavu, mwanamke imara, mwanamke jasiri! Yakupasa nawe uwe mwanaume shupavu, imara na jasiri pia!" Malkia alisema kwa ukali.



    Malolo alinyamaza kimya.



    6:05 A.M Bandarini,

    Zanzibar



    Brown alikuwa amewasili katika bandari ya Zanzibar asubuhi ile kama alivyoahidi. Lengo ni kwenda kuungana na kina Martin Hisia katika harakati za kuusaka mkanda wa siri. Alikuwa abiria wa mwisho kushuka katika boti iliyokuwa inatoka jijini Dar es salaam. Aliteremka taratibu akiwa amevaa suruali ya jinzi ya bluu, na shati ya jinzi pia, huku akiwa amevaa raba kali chapa Nike, mgongoni alikuwa amelibeba begi dogo, huku nywele zake akiwa ameziachia shaghala bagala. Hakuzifunga.



    Alivyotoka tu getini alilakiwa na na sura isiyo na furaha ya Richard. Waliingia garini na kuelekea maskani kwao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mbona umekuja peke yako kaka, where is Martin Hisia?" Brown alivyoingia tu ndani ya gari aliuliza. Richard hakumjibu. Alichukua nakala ya gazeti la Unguja Leo lililokuwa pale mbele ya kioo na kumtupia Brown katikati ya mapaja yake. Brown nae hakuongea neno. Alielewa. Alilichukua lile gazeti na kuanza kulisoma. Ilimchukua takribani dakika zipatazo tano kwa Brown kuimaliza ile habari. Habari iliyomuacha na maswali lukuki kichwani mwake. Lakini hakupata shida sana, alikuwepo wa kumuuliza maswali yake, ni Richard.



    "Nimeielewa hii habari, lakini sijaielewa kabisa" Brown aliongea huku akimgeukia Richard aliyekuwa makini katika usukani.



    "Hiyo habari imetushangaza wote, hadi sasa hatuelewi sababu ya kuhusishwa kwa Martin katika hayo mauaji,....sasa mbaya zaidi picha yake imewekwa katika front page kabisa daah"



    "Lakini una hakika Martin hakumuua huyo jamaa?" "Nina uhakika asilimia miamoja. Muda ambao huyo jamaa ameuwawa, Martin nilikuwa nae huku, katika viwanja vya Maisala, tukiusaka Mkanda..."



    Brown alisugua pua yake huku akiangalia mbele. Ghafla akaropoka....

    "Itakuwa Mwendawazimu, bila shaka mwendawazimu anahusika, bloody bastard. Lazima nitamtoa uwendawazimu wake mimi, nitamponesha...atakuwa timamu naapa!" ".....daah sasa misheni imezidi kuwa ngumu kwetu, maana tutakuwa wawili, maana kwa jinsi hali ilivyo si vizuri Martin kutembea mitaani, he is most wanted..."

    Walikatisha mazungumzo yao, walikuwa tayari wamewasili nyumbani kwa Richard. Walishuka ndani ya gari na kuingia ndani ya nyumba. Kitu ambacho hawakuwa wanafahamu wao, walikuwa wanafuatwa kwa nyuma na gari ya kina Malkia toka bandarini....



    "Martin ni nini hiyo?" Kabla ya salamu....Brownaling'aka kwa nguvu pindi tu alipomuona Martin pale sebuleni.



    "Vipi Brown, mbona umeshangaa sana?" Martin aliuliza akiwa na mshangao mkubwa. Huku akimwangalia Brown ambaye alikuwa anamsogelea taratibu.



    "Una detector Martin, ni nani kakuwekea hiyo detector wewe?" Brown aliuliza swali huku akijua kabisa Martin hawezi kumjibu. Martin alibaki na mshangao wake, akiwa haelewi Brown alikuwa anaongelea nini.



    "Detector?" Kwake ulikuwa ni muendelezo wa habari za maajabu toka kuanza kwa operesheni hii hatari, OMS!



    Upande wa Richard, yeye alikuwa amesimama katikati ya mlango akiwa nae kahemewa huku kalishika mkononi lile begi dogo la mgongoni la Brown. Brown aliendelea kumsogelea Martin taratibu. Akamfikia. Martin alikuwa kasimama kizembe akisubiri kitakachotokea. Haki ya Mungu alikuwa Zoba! Martin alinyoosha mkono wake wa kulia, hadi katika kola ya shati la Martin, shati alilolivaa siku ile katika viwanja vya Maisala. Shati ambalo ndilo aliloenda nalo usiku, walipoenda kuvamia katika kasri ya Chifu na kunusurishwa na hisia za Martin, shati ambalo alilivaa jana tu alipoenda Forodhani kula chakula cha usiku, na leo aliamka nalo shati hilohilo, shati lenye rangi nyeusi, lenye nembo ya mamba wa kijani upande wa kushoto juu ya mfuko, nembo ikiyootambulisha kwamba ni shati toka kampuni ya mavazi ya Lacoste. Brown aliikunjua kola ya shati la Martin, akatoa kitu kilichokuwa kimenasa ama kimenasishwa chini ya kola hiyo. Alikishika mkononi, alitumia kama dakika moja kukibonyazabonyaza, kisha akakiweka juu ya meza, na ndipo saa yake ilipoacha kutoa mtetemo 'vibration'.



    "Hiki kidude mnachokiona hapa mezani kinaitwa DSL 'Detector of Sound and Location', kuna mtu kakuweka hii DSL.." Brown aliongea huku akiionesha kidole pale mezani. "......na huyo mjinga aliyekuweka awe mwanaume au mwanamke kinamuonesha kila mahali ulipo na unapoenda.." Brown aliacha kuongea na kuwaangalia wale majamaa wawili usoni. Aliridhika na umakini wao, akaendelea. "... bila shaka hivi sasa huyo mtu atakuwa sehemu fulani lakini anajua ulipo na amesikia neno la mwisho tuliloongea kabla sijaizima hii detector" Brown alieleza kwa kirefu.



    "Ni nani sasa atakuwa kaniweka hiko kidude?"



    "Hatuwezi kumjua kwa sasa. Ila cha muhimu kwa sasa tumetambua mapema uwepo wa detector katika shati lako. Bila hivyo tungekuwa tunatembea na adui kila tunapoenda, na kusikia mipango yetu yote, salama yako ilikuwa ni kutolivaa hili shati..." "Aisee, thanks Mzungu, umefanya kazi nzuri sana, ilikuwa hatari sana hii kwetu, hatari kwa Operesheni, hatari kwa hatma ya mkanda wa siri!"



    " Ni kweli, ila hii kwetu ni funzo, yatupasa tuwe makini, inaonesha kuwa adui nae ana mbinu kali sana, hii misheni siyo ya kutumia nguvu wazee, Hii ni ya kutumia mbinu, inatubidi tuache mbinu zipambane.......ni mbinu dhidi ya mbinu"



    "Daah kweli kabisa" Richard aliitikia kwa sauti iliyoonesha kuchoshwa na mambo yale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda huohuo, katika katika gari ndogo iliyopaki mita chache toka nyumba ya kina Martin ilikuwa taharuki. Malkia alikuwa kapagawa hasa, ugonjwa wa Chifu sasa ulihamia kwake. Mawasiliano aliyokuwa anayapata toka kwenye 'detector' iliyokuwepo kwa Martin yalikatika ghafla. Akahisi ile 'detector' aliyomuweka yule jamaa kwa usiri mkubwa sana ilikuwa imegundulika, akaamini bila shaka 'detector' ilikuwa imegunduliwa na yule mzungu aliyetoka Dar es salaam.



    "Pumbavu sana, yule mwehu itakuwa kaiona, mimi nilijua tu, ni heri tungeumaliza mchezo kwa kumshoot kulekule bandarini....akamalizia kwa tusi zito la nguoni" Malkia alisema kwa jazba, kwa hakika maji yalikuwa yamemfika katikati ya kichwa na mabega yake. Malolo alibaki kashangaa tu akiwa haelewi kitu. Ni yeye ndiye alimshauri Malkia wawapige risasi kulekule bandarini, lakini Malkia alipinga sana wazo la Malolo, akiwa na tamaa kusikiliza majadiliano ya wale jamaa. Lakini sasa subira yake ilikuwa imemponza. Saa ya mzungu iliharibu subira yake. Saa ya ajabu ya Brown iligundua uwepo wa 'detector' katika shati la Martin, na ndipo ilipoanza kutetemeka bila kuacha ili kumjulisha Bosi wake. Brown nae alielewa na macho yake yalifanya kazi kwa haraka, ndipo alipoiona katika kola ya shati la Martin.



    "Malolo hii ishu imekuwa kubwa sasa, naona hawa jamaa nao wako vizuri sana, nilikuwa nawachukulia poa kumbe sivyo kabisa.." Malkia aliongea huku akiwa mpole sana safari hii.



    "Nilisema zamani sana, lakini ulinipinga Malkia, tena ulinipinga kwa maneno makali sana, mi nilikwambia kwamba uwepo wa Martin Hisia katika misheni yoyote ile ni hatari zaidi ya neno hatari lenyewe...hajawahi kushindwa katika misheni yoyote yule jamaa, na siku zote ngao yake kubwa ni hisia alizojaaliwa na muumba, hisia ambazo wewe ulizibeza. Mimi na ujanja wangu wote lakini sijawahi kutamani kushindana katika misheni moja na Martin, jamaa ana nyota ya mbwa sijui yule.."



    "Malolo, inawezekana Martin ana hisia lakini Martin hana utaalamu wa kutisha, sasa huwezi kufananisha Hisia na Utaalamu, siku zote Utaalamu au taaluma ni bora zaidi ya hisia. Sasa huyu mtu aliyekuja sasa inaonekana ni mtaalamu bila shaka. Nimesema hawa jamaa wako vizuri kwa kuwa watatumia Hisia toka kwa Martin na Utaalamu toka kwa huyo mzungu, hapo ndipo ninapopata shida, kwakuwa watakuwa na vitu viwili ambayo ni muhimu sana katika misheni kama hizi, halafu nilikuwa sijakwambia kitu Malolo, siku ile katika viwanja vya Maisala, nilifanya mambo matatu kwa usiri mkubwa sana. Nilipulizia Rox katika gari ya kina Martin, nikampulizia Martin kisha kumpachika detector...."



    "E bwana weeee, Malkia we ni kiboko, naapa we ni mwanamke hatari zaidi kuwahi kufanya nae kazi, ulimudu vipi kufanya mambo yote hayo kwa muda mfupi kama ule, you're very brilliant yaani... SALUTE kwako" Malolo alisema huku mkono wake akiupeleka kwa kasi katika uso wake na kuurudisha mapajani, alitoa ishara ya saluti.



    "Malolo bwana, labda nilikuwa kiboko kabla huyu jamaa hajawasili Zanzibar, kuja kwake kumeharibu kila kitu, bora tungemshoot on the spot alivyoikanyaga tu ardhi ya Zanzibar, au ningemruhusu Peter ampoteze hukohuko Bongo, labda nisingekutana na huyu mzungu, ambaye ni kiboko yangu"



    "Kivipi Malkia, sijakuelewa hapo...Uko vizuri sana Malkia, unauwezo mkubwa wa kufikiri na unatenda kwa haraka pia..sasa nani anaweza kuwa kiboko yako? Maana kwa jinsi ulivyofanya hayo mambo matatu kwa muda mfupi kama ule kule katika viwanja vya Maisala, yaani kama Ronaldo vile, bao la kwanza umepiga kwa mguu wa kushoto, bao la pili umepiga kwa mguu wa kulia na bao la tatu umepiga kwa kichwa, umepiga bao tatu safi nyavuni.." Malolo alisema huku akimalizia kwa ishara ya kuruka juu na kupiga kichwa hewani.



    "Hahaha, Malolo bwana, you're comedian unajua wewe, halafu una akili sana, na mkweli, hunifichi kitu eti kwa kuogopa nitakasirika endapo utakisema, ndomana napenda sana kufanya misheni na wewe, ...mh mhhhh lakini kuna mtu kagundua uwepo wa detector yangu katika shati la Martin. Na sasa ameitoa..na hilo ndilo tatizo linaloniumiza kichwa"



    "Duuh! Ni nani huyo mtu?" Malolo aliuliza kwa nguvu, sasa mas'hala akiwa ameyaacha.



    "Ni yule mzungu niliyekwambia jana, ambaye leo wote tumemshuhudia akitua ndani ya ardhi ya Zanzibar, anaitwa Brown"



    "Brown!" Malolo aliropoka.



    Ingawa Malkia alilitaja jina hilo mara kadhaa, lakini sasa ndo lilitafsiriwa vizuri na ubongo wa Malolo.



    "Usinambie unamfahamu huyo mzungu Malolo?" "Brown Mrusi, nilijua tu, nilijua...yaani nilijua tu...." Malolo alitamka maneno hayo kwa sauti kubwa. Kisha aliwaza kimoyomoyo.



    "...sikuwa natamani kabisa siku hii ifike, sasa imefika, bila shaka huyu Brown atakuwa nd'o mtoto wa yule mzee aliyerekodi mkanda, bila shaka atakuwa nd'o yeye, ni mara kadhaa yule mzee alikuwa anamtaja mwanawe, Brown kafanya hivi....Brown kafanya vile.....Brown....Brown Van Dyke!, hii mbaya sana, siku nisiyopenda imewasili, lakini mbona kachelewa, au atakuwa siyo yeye lakini....lakini....." Maneno hayo yalikuwa yanapita katika ubongo wa Malolo, ndipo alipostuliwa toka mawazoni na Malkia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Come on Malolo! Mbona huongei sasa, ulijua nini? Unamfahamu huyo mzungu? Kivipi? Kwanini hukunambia tulivyomuona tu pale bandarini? Eeeeeh!" Malkia aliwaka sasa.



    "Ngoja" Malolo aligeukia siti ya nyuma ya gari. Akalivuta begi dogo lililokuwa katika juu ya siti ya kati. Akalipakata lile begi, akafungua zipu, alikuwa anatazamana na 'laptop' yake aina ya Toshiba, akaitoa nje. Akaifungua na kuiwasha. Alitulia tuli akisubiri 'laptop' iwake. Muda wote huo Malkia alikuwa anamwangalia tu Malolo, huku akiwa na donge la hasira moyoni mwake, kwanini Malolo amfiche? Akashindwa kuzihimili hasira zake. Akataka kuongea neno lakini akagairi, akaanza kuhesabu moja mpaka kumi kimoyomoyo....huu ndo mtindo anaoutumia mara zote pale ashikwapo na hasira. Alivyomaliza kuhesabu na hasira zikapungua kidogo, alifumba macho na kuangalia mbele....



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog