Search This Blog

Sunday 22 May 2022

NYUMA YA PAZIA - 4

 







    Simulizi : Nyuma Ya Pazia

    Sehemu Ya Nne (4)



    Hakufurahishwa na kituko hicho hivyo alirudi chumbani kwake na kujitupa kitandani. Hakuchukua muda alipitiwa na usingizi.



    * * *

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ni ndevu za bandia ndizo zilizoubadili muonekano wake huku akionekana kama kijana wa miaka therathini na tano hadi therathini na saba. Muonekano huo pia ulimfanya hata dereva wa taxi aliyekuwa na makamo ya miaka arobaini na ushehe hadi hamsini asifahamu kama yule ndiye yule Joachim Bartazar anayetangazwa kama muharifu mkubwa nchini huku akionekana kuripua nyumba yake iliyokuwa na madawa ya kulevya ndani yake. Akiwa bado anaangalia nje Joachim alishtushwa na habari juu ya uvamizi wa majambazi makaburini huku wakisadikika kumtafuta huyo Joachim Bartazar. Ilikuwa moja kati ya habari zinazozidi kumpatia raha na kumfanya azidi kutabasamu. Haikuwachukua muda mrefu waliwasiri sehemu ambayo Joachim aliagizwa kupelekwa na dereva tawi yule. Aliteremka na kumlipa ujira wake kisha yeye akageuka kulifuata Jengo moja lefu pale Posta. Hakutaka kumuachia nafasi mtu yeyote kumfatilia hivyo alitoa miwani yake mikubwa ya jua na kuiva huku ikichangia kupotea kwa Sura yake mbele ya watu ambao wangemfahamu kwa kumuona tu. Mara baada ya kuhakikisha gari aliyokuja nayo imetoweka kabisa alirudi nje na kukunja kushoto kwake huku akiifuata barabara kubwa na hapo alikunja kona na kukifuata moja kati ya vichororo vilivyokuwa vikiyatenga majengo pale Posta. Mara baada ya kufika mwisha alikunja kulia ambako mbele yake kulikuwa na mlango. Aliufungua na kuingia katika chumba kile kidogo. Alitoa kadi yake iliyofanana kidogo na ya benki kisha akaiweka katika tundo lililokuwa kama ufa mdogo na ghafla ukuta ule ulisogea na chumba kingine cha siri kilionekana. Aliingia humo na ukuta ule ukajirudisha. Chumba kile kilikuwa ni lifti iliyomsha hadi chini umbali wa mita kumi hivi. Mara baada ya lifti kufunguka Joachim alitembea moja kwa moja katika korido fupi iliyompeleka hadi kwenye ukumbi mkubwa ulikuwa na wafanyakazi wengi huku wakiwa bize na kazi zao. Sasa alikuwa Makao Makuu ya NDA (National Defence Agency) huku akipokelewa na wafanyakazi wenzie na wengine kumpatia moyo kwa kazi ile nzito aliyokuwa nayo. Muda uleule Sauda alikuja huku akiwa na faili kubwa huku akimtaka Joachim amfuate.

    Walielekea katika chumba cha kompyuta huku Sauda akimkabidhi Joachim faili lililokuwa na taarifa zote za Mambo aliyokuwa akifatilia.

    "Naomba uhack channel zote za TV nataka niwashangaze wananchi mara moja halafu weka hii disk"alimwambia Computerman aliyekuwa mle.

    "Sawa"alijibu kisha Joachim alirudi hadi kule ukumbini na kuwasha TV ili aone.



    * * *



    Ghafla!! Vipindi vyote katika televisheni vilikata huku kukifuatiwa na filamu ya kushangaza kabisa. Waziri wa Ulinzi alikuwa akitoa amri ya kuuwa kwa mgombea mwenzake katika moja ya hoteli huku mauaji hayo yakitekelezwa. Haikuishia hapo pia kulionyeshwa moja kati ya mikutano ya siri ikimuonyesha Waziri wa Ulinzi akiwa na Vigogo kadhaa wakiwaongelea maswala ya kupindua Nchi jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa mara baada ya kuwepo kwa mkutano wa Viongozi wa Afrika uliopangwa kufanyika Arusha. Mipango yao ilidai wakati kikao kikiendelea ungetokea uvamizi na kulipuliwa kwa Eneo lile. Habari hizi ziliishangaza nchi pia ubadhirifu wao pamoja uliokuwa ukifanywa na viongozi wakubwa. Pia orodha ya vikundi vyote vya kiharifu na wamiliki huku kundi la Rising Mafias likionekana kumilikiwa na kutumiwa na Viongozi wakubwa. Ilikuwa taharuki nchi nzima huku wananchi wakishangaa.



    * * *



    "Haloow!"ilikuwa sauti ya Waziri wa Ulinzi, Professa Alphonce Kaigimo mara baada ya kupokea simu yake na kuiweka sikioni.

    "Mheshimiwaaa pole sana"aliongea Papaa Paul.

    "Ya nini tena?"

    "Mambo hadharani kila mpango uko nje tena kila mtu anafahamu madudu yetu,Mheshimiwa Waziri!"aliongea Papaa Paul kwa kebehi.

    "Ah!sasa tunafanyaje Mr. Paul?"aliongea huku akijiweka sawa katika kiti cha gari.

    "Kila mtu anakufa na lake mie niko naenda uwanja wa ndege nimekodi ndege tayari kuondoka hapa Nchini."

    "Khaa!sasa ndio nini hicho fanya hata kunisubiri basi tuondoke wote"

    "Kila mtu afe kivyake Bwana"aliongea Papaa huku akikata simu.

    Akiwa bado katika taharuki ghafla simu yake ikaita tena huku namba mpya ikijionesha.

    "Halow!..Mheshimiwa Waziri mimi ni mhandishi wa.........!!"sauti ilisikika ikiongea harakaharaka mara baada ya Waziri kupokea na kuikata mara baada ya utambulisho wake.

    "SHIT!!"

    "Mwambie Kibu alete gari nyingine mambo yameharibika!"aliongea Waziri huku akiwa na wasiwasi usoni.

    "Kuna tatizo gani Boss?"aliuliza dereva wake ambaye alikuwa kama mlinzi wake ambaye alikuwa kama mamruki wake wa mauaji.

    "Mambo yote hadharani tuliyofanya na tuliyopanga na sijui nani kayatandaza?"

    "Mh!ngoja nimtaarifu sasa na huu msafara je?"

    "Ongeza spidi tuachane nao hapo mbele mataa"aliongea Waziri huku dereva yule akikanyaga spidi ya gari lile la kifahari.



    "Ongeza spidi tuachane nao hapo mbele mataa"aliongea Waziri huku dereva yule akikanyaga spidi ya gari lile la kifahari.



    * * * *



    Mara baada ya kuwaumbua wabaya wake taratibu alitoka pale makao makuu ya NDA na kuelekea nyumbani kwa Sauda ambapo ndipo alipoweka makazi yake kwa wakati huo. Mara baada ya kuingia ndani alielekea bafuni na kuzitoa ndevu zake za bandia na kujimwagia maji huku akitabasamu kwa kulisafisha jina lake upya na kuonekana shujaa. Alirudi hadi chumbani na kujitupa kitandani na kuruhusu usingizi kumchukua na kazi iliyobaki akiwaachia Jeshi la Polisi kuifanya kwani yeye kama mpelelezi aliishia pale.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    * * * *



    Mara baada ya kuwasili Airport Papaa hakutaka kupoteza muda kwani alijua kumenuka hivyo haraka haraka alielekea ndani ili akaguliwe na kuondoka nchini hata kabla hali ya hewa haijawa mbaya pale Airport.

    "Tulia hapo hapo na nyoosha mikono juu" Ilikuwa kauli iliyomshtua sana Papaa Paul ambae alikuwa akisubiria pasport yake ikaguliwe. Alitii amri kwani walifika Askari wengi wakiwa na silaha zao na kumuelekezea huku wakimuonya kwa mjongeo wowote ule atakaofanya. Alifungwa pingu huku msululu wa gari za Polisi ukiongezeka ili kuimarisha ulinzi maeneo ya Airport. Aliwekwa katika gari maalum na safari ya kumpeleka Oysterbay ilianza kwa ulinzi mkali. Mara tu taarifa za kukamatwa kwa Papaa Paul zilisambaa kwa muda mfupi huku Wananchi wakifurahia juhudi za Jeshi kwa kumfuatilia hadi hila zake za kutaka kutoroka Nchini. Pia taarifa zilifika hadi katika Kikosi chake cha Rising Mafias au Jeshi Jeusi ambao hawakukawia kuingia katika operesheni ya kumkomboa Kiongozi wao.

    "Vijana ni wakati wa kazi" aliongea Simon Jacob mamruki au marsenary hatari na tegemezi wa Papaa Paul.

    Msafara ulifika TAZARA na kuzuiwa na foleni iliyoonekana kubwa na kuzuia magari mengi. Polisi kadhaa walishuka na kuweka ulinzi katika gari aliyopakizwa Papaa Paul huku wengine wakienda kuongea na Askari wa barabarani aliyekuwa mbele akiongoza magari katika barabara hiyo. Waliomba waruhusiwe huku yeye akionekana kutowafuatilia na kuendelea kuruhusu magari ya upande mwingene jambo lililowashangaza askari wale waliokuwa na silaha zao mkononi.

    GHAFLA! Zilitokea gari nne aina ya Toyota Van nyeusi huku zikishusha watu wenye bunduki kwa mbele nakuanza kupiga risasi kuelekea kwa wale askari waliokuwa wakiongea na Trafiki kisha nae alichomoa bastola na kufanya shambulizi kwa askari wale. Ilikuwa kama mkanda wa sinema kwani kile kilikuwa Kikosi hatari cha Rising Mafias waliofanya mashambulizi haraka haraka bila kurudi nyuma wala kuogopa. Simon Jacob alikuwa akiongoza Kikosi hicho.Ndani ya dakika tano walifanikiwa kuwasambalatisha askari walikuwa eneo lile na wengine kukimbia kwani walienda na vifaa vya kazi. Simom Jacob ndiye aliyehakikisha anamuokoa Papaa paul kwani alielekea hadi katika gari alilowekwa na kutoka nae huku akihakikisha yuko safi na muda huo huo ilifika gari aina Range Rover sport na kumchukua Papaa na kutokomea. Hawakuchelewa nao waliingia katika gari zao na kuondoka kwa spidi huku wakiacha mauaji ya Polisi ishirini na wengine kujeruhiwa huku wengine wakijeruhiwa vibaya na wengine kutupa silaha na kukimbia.



    * * * *



    Mara tu baada ya kutoka kitandani alielekea chooni na kisha kwa mjongeo wa kivivu alielekea jikoni na kukutana na Sauda aliyekuwa akiangaika kupika mara baada ya kurudi jioni ile.

    "Oh!umerudi?" lilikuwa swali la Joachim kwa Sauda.

    "Bado!"alitania Sauda.

    "Hahahahahahah" (wote walicheka)

    "Kumbe umeelewa kuwa swali lako halina mushkeri eh"

    "Naam!" alijibu huku akichukua pakiti ya maziwa na kuanza kunywa.

    "Papaa Paul amekamatwa ila katoroshwa tena kwa shambulio kali kwa Polisi na wengi wamepoteza maisha" aliongea Sauda huku akikata moja ya nyanya iliyokuwa mkononi pake.

    "Unasema?"

    "Kakamatwa na ametoroka"

    "Saa ngapi ilikuwa?" aliuliza huku akiangalia saa yake.

    "Saa kumi uwanja wa ndege alikuwa anataka kuondoka nchini" alijibu Sauda huku akimuangalia Joachim usoni.

    "Saa hivi saa mbili! Kuna kitu kinafuatia hapa" aliongea huku akirudi haraka chumbani kuchukua shati lake.

    "Wapi sasa?" lilikuwa swali lenye mshangao ndani yake alilouliya Sauda.

    "Jiandae tuondoke hapa"

    "Kivipi Joachim?"

    "Leo sio pazuri hapa!"

    "Kwangu hapafahamiki bwana wasiwasi wako tu" alijibu Sauda.

    Wakati wakiendelea kubishana ghafla walisikia gari zikisimama nje. Haraka haraka Joachim alilisogelea moja ya dirisha na kuchungulia katika upenyo mdogo na kuwaona wazee wa kazi Jeshi Jeusi wakianza kuisogelea nyumba ya Sauda.

    "Wenyewe hao" ilikuwa kauli ya kunong'ona iliyopita masikioni mwa Sauda na kumfanya akikamate sawa sawa kisu chake cha kukatia nyanya. Joachim alichomoa bastola yake na kuiweka sawa kisha wakaongozana na Sauda hadi mlango wa mbele ili watoroke eneo lile.



    Taratibu Joachim aliambaa mpaka kwenye usawa wa korido na kuzima umeme katika menu swichi ilikuliruhusu giza litawale na iwe rahisi kwao kutoroka. Mara baada ya kumaliza alirudi na kumkamata mkono Sauda kisha wakaelekea katika mlango wa nyuma.

    "Fungua mlango" Aliongea Joachim huku akiwa nyuma ya Sauda aliyekuwa akiufungua mlango wakati huo. Alikuwa akiangalia nani ataingia kabla wao hawajatoka. Mara tu mlango ulipofunguka walitoka huku Joachim akitangulia na bastola yake mkononi.

    Walipokelewa na kiza totoro kilichofanikiwa kuumeza mwanga wa Mwezi uliokuwa ukijaribu kuangaza usiku ule. Taratibu waliambaa na ukuta wa nyumba ile huku kiza kikiwa moja ya kinga kwao.

    "Wengine wazunguke nyuma Alah" ilisikika sauti ikiamrisha na kuwafikia Joachim na Sauda.

    Kama walivyotarajia mbele kidogo alijitokeza jamaa akiwa na nguo nyeusi zilizofanana kabisa na gwanda katika mtindo wa ushonwaji na hata uvaaji kwani alivalia mavazi hayo na buti ndefu za kijeshi pamoja na kofia aina ya Bareti kichwani pake. Mkononi alikuwa na bunduki aina ya UZI aliyokuwa ameikamata barabara na kuonyesha yuko kazini.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Usimshuti ngoja nikuonyeshe" Yalikuwa maneno yaliyotoka kinywani mwa Sauda kwa mtindo wa kunongona lakini yalifanikiwa kupenya hadi katika masikio ya jamaa yule. Lakini kabla hajamaliza kugeuka kuangalia wapi sauti imetokea tayari kisu kilichokuwa mkononi mwa Sauda kimeshazama katika koo lake na kumfanya apige ukelele wa maumivu.

    "Aaaaaghh...."

    Hakutaka kumuachia nafasi haraka haraka aliruka na kuidaka tena shingo yake na kuivunja kisha akakichomoa kisu na kuifuta damu katika nguo za jamaa yule.

    "Tayari twende" Ndio kauli iliyomstua Joachim aliyekuwa akiushangaa wepesi wa bibie yule. Sauda iliikota bunduki ile ya Kiislaeli kumuonesha ishara Joachim ambaye alizidi kuduwaa kwa wepesi wa mrembo yule.

    Alimsogelea na kumkamata mkono kisha wakaelelea katika usawa wa ukuta na kumsaidia Sauda kuruka fensi ile. Mara baada ya Sauda kutua upande wa pili Joachim aliwaona watu watatu wakija usawa ule spidi na walifanana sana kimavazi na yule marehemu. Haraka alilala chini na kuanza kukroo (au kama ilivyozoeleka kutambaa) kufuata upande mwingine wa ukuta ili kupoteza uelekeo kuwa ametokea pale.

    "Mike... Mike... Mike..." Ilikuwa sauti iliyokuwa ikiita kuashilia wanamuamsha mwenzao. Sauti hiyo ilimfanya Joachim aongeze mwendo wa kutambaa.

    "Ameuawa!!! muda huu washeni tochi" Ilikuwa kauli ya kuamrisha na papo hapo mwanga wa tochi tatu ulionekana na kumfanya Joachim ajibane kwenye maua kuzuia asionekane.

    Akiwa hapo ghafla mwanga wa tochi moja ulimmulika na kumfanya aonekane kwa adui yake lakini kwa wepesi alichupa kwa kujiviringa na kupiga risasi za mfululizo kuelekea kwenye ule mwanga wa tochi.

    "Pah Pah Pah Pah...." kama alivyotarajia alifanikiwa kuusikia mguno wa yule jamaa kishindo cha kuanguka kufuatia pamoja na tochi ile. Mara baada ya hapo alijirusha haraka haraka ili kubadili eneo na kuwapoteza wale wengine huku akiachia risasi kufuata mwanga wa tochi. Shabaha zake hazikuwa za kubahatisha hivyo wote aliwashusha na hapo ndipo aliposhangaa mvua ya risasi zilizokuwa zikipigwa bila mpangilio kwa kumfuata yeye. Hakuchelewa alichupa haraka na kudaka ukuta kisha akajirusha nje kama mzigo.

    Mara tu baada ya kutua hakupoteza muda alirudi mpaka maeneo aliyomuacha Sauda na kutomkuta.

    "Shit!! huyu kaenda wapi?" lilikuwa swali alilojiuliza mwenyewe lakini kabla hajatulia alisikia sauti zikiamrisha tulia kwa mbali.

    "Sio Sauda huyo?" ndio lilikuwa swali lililopita kichwani mwake na kuafiki kuwa Sauda katekwa.

    Hakuchelewa aliamba na ukuta haraka haraka huku akikimbia ili kuepusha kutekwa kwa Sauda.

    Lakini kabla hajakaribia usawa wa kona ya kutokezea mbele katika geti alishituliwa na mlio mkubwa huku nae akitupwa umbali kidogo.

    "BOOOOM!!!!!"



    **********



    Kuwa mbali na Joachim kulimfanya amuwaze kila saa huku akiwa hang jibu sahihi la Joachim Bartazar anafanyia kazi gani bastola ile aliyomuona nayo siku ile? Pia yule mwanamke ni nani kwa Joachim?. Hayo ndio mambo yaliyomsumbua akili sana Dorice aliyekuwa akimpenda sana Joachim. Mara kadhaa amejaribu kumtafafuta lakini hapatikani katika simu yake jambo lilimfanya afadhaike sana.

    "Lini ntamuona tena?" ndio lilikuwa swali alilojiuliza wakati alipokuwa ofisini kwake.

    "Dorice..." Ilikuwa sauti ya bosi wake iliyomzindua katika mawazo ya Joachim.

    "Abeeh Boss"

    "Hebu fuatilia ile kazi tuliyoongea ujue imeishia wapi maana hawa watu siwaelewi. Sawa" Aliagiza Mzee yule wa makamo ya miaka Arobaini na tano hadi Hamsini (45-50).

    "Sawa bosi" Alijibu Dorice na kumfanya Mzee yule ageuke kuondoka mara baada ya kumaliza kutoa amri ile. Lakini alienda hatua kadhaa kisha akageuka na kumuangalia Dorice.

    "Dorice..."Aliita tena.

    "Abeeh! Bosi"

    "Kuna kitu nataka nikuulize kitu!" Ndio ilikuwa kauli ya Mzee yule.





    "Hivi Joachim yuko wapi siku hizi?" Ndio lilikuwa swali la Mzee yule lililomstua sana Dorice lakini akafanikiwa kuuficha machoni mwa Mzee yule.

    "Ah! hilo ni swali ambalo nakosa jibu lake sasa..... Maana hata mimi najiuliza sana." lilikuwa jibu la Dorice.

    "Nimekuuliza sababu simuelewi yaani halafu anatafutwa na Polisi kila mahari jambo linalonichanganya Joachim ni nani."

    "Yaani Bossi maswali unayojiuliza nami huwanajiuliza sana tu"

    "Oke... mi ngoja nitoke tukutane kesho na hiyo kazi" Alijibu huku akitoka nje ya Ofisi ya Dorice na kuondoka zake.

    Nae hakupoteza muda alitoka kwenda kufuatilia kazi aliyopewa na bossi wake huyo.



    *********************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Taratibu alijiinua pale chini alipokuwa huku akiwa na michubuko kutokana na kutupwa na mlipuko ule wa ajabu. Aliiangalia nyumba ya Sauda ambayo ilikuwa imesambaa na vipande vichache vya moto vikiendelea kushika hatamu. Lilikuwa tukio la kushangaza kwani haijawahi tokea nyumba kulipuliwa vile.

    "Hii ni RPG-4" Alinong'ona mwenyewe. Aliianza safari ya kurudi mjini huku akijikokota kwa maumivu. Kabla hajafika mbali alishtuliwa na sauti iliyokuwa ikimuamrisha.

    "Simama hapo hapo wewe mshenzi"

    Kwa ukimya alisimama na kugeuka nyuma ili amtambue nani anayemuamrisha vile. Kama alivyotarajia alikutana na njemba ikiwa na SMG mkononi huku ikiwa haina utani na roho yake.

    "Nilitaka ufanye hivo hivo. Sasa mikono juu na usijiguse." Liliamrisha tena lile njemba mara baada ya kujihakikishia aliyegeuka ni mtu sahihi anayemtafuta. Taratibu huku akiwa makini alimsogelea Joachim huku akimuonyeshea mtutu wa bunduki. Alipomfikia alianza kumkagua huku akiwa na tahadhari ya hali ya juu. Alipomaliza tu akatoa simu yake ili atoe taarifa juu ya kumkamata adui yao. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana kwani Joachim alirudi hatua moja nyuma huku akiruhusu kiwiko chake cha kushoto kufanya kazi kama alivyotaka. Alimpiga katika chembe na kumpatia maumivu makali yaliyomfanya ainame. Hakuchelewa aliachia teke la kulia na kumrusha yule njemba chini. Alifanya hivyo kwa spidi ya hali ya juu. Alimfuata yule jamaa ambae alikuwa akijizoa zoa pale chini kabla hajaikamata bunduki na kuiwahi upande wa Magazini. Aliichomoa haraka haraka na kumgonga nayo kichwani kisha akamuongezea ngumi iliyolivunja kabisa koromeo la njemba yule.

    "Pumbav!!" Alimsindikizia na tusi hilo wakati jamaa akigalagala pale chini na kupoteza uhai.

    Aliiokota ile bunduki na kuiweka ile Magazini kisha akaanza safari ya kurudi kwani alitambua uwepo wao. Kwa mbali alianza kuzisikia sauti za watu wale wakiambiana kumtafuta mwenzao ndio waondoke.

    "Asa! hawa watakoma kuringa" Aliongea mwenyewe Joachim huku akikoki bunduki ili kuruhusu risasi kuingia kwenye Chemba kisha akaiinua juu na kupiga risasi mbili.

    "Twendeni huko mlio unakotokea" ndio sauti aliyoisikia.

    "Njooni muone moto" Alinong'ona huku akipiga goti karibu na miti na kuitega vizuri bunduki ile inayofanya mashambulizi ya mfululizo na ya mojamoja. Alikaa mkao wa kulenga shabaha hivyo alikuwa akijiandaa na kundi lile linalokuja kwa spidi bila kuelewa mtego ule.

    "Pah" Ilikuwa sauti ya risasi aliyoiachia kwa ustadi mkubwa mara baada ya kumuweka kwenye tageti aliyekuwa mbele. Hakukosea kwani alimrusha juu na kumuangusha huku ikichukua uhai wake. Mara baada ya shambulio lile walijitupa chini na kuanza kumwaga risasi kuelekea upande aliokuwa Joachim. Lakini walikuwa wamechelewa kwani nae mara baada ya kuachia risasi alijirusha upande wa kulia kisha akatambaa hadi upande mwingine huku akiacha risasi zikimwagika alipokuwa. Hakuwa na haraka aliachia risasi nyingine mfululizo kuelekea kwa adui zake. Hakuwa na mkono wa kubahatisha hivyo katika risasi alizoachia alisikia milio tofauti. Wawili wakatangulia.

    Kama kawaida alihama eneo haraka haraka huku giza lile likimsaidia kutokuonekana huku uwepo wa ile miti mingi iliyozunguka maeneo yale kuwa kama uwanja wa vita. Mara baada ya mashambulio yale ya kushtukiza aligundua kuwa adui zake wameishiwa risasi kwani alizisikia bunduki zao zikifyata mara baada ya wao kuruhusu risasi kama kawaida. Haraka haraka alichupa na kuelekea usawa mwingine ili aweze kutambua kama walikuwa na silaha nyingine zaidi.

    Nao hawakuwa wazembe waliokota za wale wenzao na kujaribu tena mapigo lakini nazo ziligomea njiani. Mara baada ya kuona vile mmoja wao aliinuka na kuanza kukimbia. Hakufika mbali kwani mlio wa risasi ulisikika na kumfanya aruke mbele na kudondoka bila kutapatapa. Hali hiyo iliwatisha na kuwafanya wengine watulie pale chini walipokuwa bila kujigusa.

    "Haya amkeni hivyo hivyo" Aliamrisha Joachim nao wakafanya hivyo hivyo alivyotaka. Walikuwa watatu waliobaki katika wale saba waliokuja haraka haraka. Kisha nae alijitokeza katika kijimwanga kidogo ili waweze kumuona vilivyo.

    "Nyie ndio wababe sio" Aliuliza Joachim huku akiiweka sawa bunduki ile aliyoikwapua kwa mwenzao wa mwanzo. Alivuta triger ili kuruhusu risasi kwa ajili ya kumlenga mmoja wao na uwe kama mfano lakini nae risasi iligoma kutoka kuashiria hapakuwa na risasi katika silaha yake. Nao hawakutaka kuchelewa walirusha ngumi haraka haraka ili wamuwahi Joachim ambae alijua jambo hilo litatokea hivyo akawakingia kitako cha bunduki kama kinga na kuwafanya wapige ile bunduki. Aliitupa chini kisha akaanza kupangua mapigo tofauti tofauti kutoka kwa wale njemba wenye uchu na roho yake huku akitafuta jinsi ya kujipanga. Kwa wepesi aliruka juu na kuachia France kick iliyompata mmoja wao huku akimparamia aliyekuwa nyuma yake kisha akarusha ngumi kwa aliyekuwa kasimama. Alitaka kuwaonyesha ustadi wake katika fani ile aliyoibobea vizuri kabisa. Hakuwa mzito, aliruka mateke mawili mfululizo kumrudisha chini yule aliyekuwa akiamka mapema na kukaa kuwasubiri wainuke huku akiwa tayari kuwamudu wote.

    Mara tu baada ya kuja juu walijipanga huku mmoja wao akisukuma ngumi zisizokuwa na mpangilio ambazo hazikuzaa matunda kwani Joachim alikuwa akizikwepa kisha akamsukumia ngumi usawa wa kidevu na kumtengua taya.

    "Yalaah!!" alibweka yule jamaa na kusogea pembeni lakini hata kabla hajatulia alirushwa na teke safi lililompiga kifuani. Wengine walianza kurudi nyuma lakini Joachim hakutaka kitu kama kile kitokee kwani alisogea hatua kadhaa mbele na kuzunguka double kick na kuwatelemsha wote kwa ujumla.

    "Sasa naona mnaweza kunijibu maswali yangu" Aliongea Joachim mara baada ya kumkanyaga mmoja wao mgongoni.

    "Dah!! braza niue tu" Aliongea yule aliyekanyagwa kwa shida.

    "Huwa siui" Alijibu Joachim kwa dharau.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akijibu hivyo ghafla alimsikia mwingine akikoroma kama anaekata roho. Alipomuangalia aligundua kuwa ameshafariki kwani aliutafuna ulimi wake. Ghafla na yule mwingine aliyetenguka taya nae akafanya hivyo hivyo. Hapo ndipo akaelewa kuwa ule ulikuwa mtindo wao wa kujiua pale wanapozidiwa hivyo alimkamata yule mwingine na kumfinya shingoni katika mishipa ya damu na kumfanya apoteze fahamu.



    Baada ya hapo alimfungua kamba za viatu na kumfunga nazo kwa nyuma ya mti. Kisha akachua soksi zake na kumuwekea mdomoni ili atakapo rudiwa na fahamu asijiue kama wenzie. Aliangalia muda tena na kugundua ilikuwa saa tatu na nusu(09:30). Aliamua kurudi kwa kunyata kuelekea mbele ya geti la nyumba ya Sauda ambayo hadi wakati ule ilikuwa imebaki kama gofu tu. Mara baada ya kukaribia mbele aliiona gari moja ikiondoka spidi huku ikiwa na njemba mbili zenye silaha mkononi kuimarisha ulinzi wao.

    Aliposikiliza vizuri alisikia sauti ya kike aliyoifananisha na ya Sauda ambaye hadi wakati huo alikuwa hajamuona hadi wakati ule tangu walipotoka ndani. Hapo kwa wepesi alitambua kuwa tayari Sauda alikuwa katekwa na Mamafia hao.



    *******************************



    Wakati nchi ikiwa bado imeduwaa juu ya matukio ya Waziri wa Ulinzi na Usalama, Professa Alphonce kujihusisha na uhalifu na ugaidi yeye sasa aliamua kutorokea Nchi Kenya kupitia border ya Namanga ambayo ilipokea taarifa zake akiwa tayari ameruhusiwa kuingia Nchini humo.

    "Nahitaji kufanya kitu lazma tuipindue tu hii Serikali kama pesa ipo" Alimwambia dereva wake ambae ndiye kama mlinzi wake.

    "Hiyo ni kazi ndo sana yaani kama pesa ipo." Alijibu yule dereva.

    "Tena twende tutafute mamamruki(Masenaries) hatari huko Nairobi" Aliongezea.

    Ndio yalikuwa maneno yao ambayo wao walipanga kuyatekeleza kabla ya Msimu wa sikukuu.

    Waliingia Nairobi na kukodi chumba katika hoteli yenye hadi ya Nyota tatu The Sofitel Nairobi Hotel yenye kila anasa ndani yake.



    *******************************



    Haraka haraka alikimbia kuelekea kwenye gari lingine walilokuwa wamekuja nalo wale washenzi aina Land rover nyeusi. Alipoifikia alisikia mlio kama alam ukipiga na hapo ndipo alipoelewa nini kinafuatia kwani alijitupa chini haraka na muda huo huo ulifuatia mlipuko mwingine uliolirusha lile gari juu usawa wa mita 20 na kurudi chini likiwa halifai tena kwani liliwaka moto lote.

    "Mh! hii ni vita sasa" Alijisemea wakati anainuka pale chini na kuliangalia lile gari huku wale manunda wakipotelea gizani na mtoto wa kike Sauda.

    "Sasa watanikoma" alinong'ona mwenyewe huku akirudi kwa mateka wake aliyemuacha kwenye miti. Sauda alijenga nyumba ile kwa siri na ndio maana akaijenga mbali kidogo na makazi ya watu wengi ingawa alitumia gharama nyingi kupeleka umeme pale na Tank la maji. Hivyo hata valangati lile halikusikiwa na majirani ambao walikuwa mbali nae.

    "Amka!"Aliongea Joachim huku akimpiga makofi kadhaa jamaa yule aliyemfunga kama mateka wake.

    "Sikia sihitaji kukuua wala kukufanyia tendo lolote lile baya..... sasa basi nahitaji ushirikiano wako" Aliongea Joachim kwa upole na kwa msisitizo zaidi.

    "Najua unao uwezo wa kujiua ili kuficha siri nami ninao uwezo wa kukuwahi na kukufanya maisha uyaone machungu" Alikazia tena maneno yake kisha akamfungulia na kuanza kumkokota kwenda nae ndani ya geti kwani lenyewe lilibaki huku ukuta wa upande wa nyuma ulidondoka kutokana na mlipuko ule. Walipofika ndani ya fensi alimkalisha chini na kumtoa zile soksi mdomoni. Aliangalia saa yake tena na kugundua kuwa muda ulienda kwa dakika 35 yaani saa 4 na dakika 5. Alimgeukia yule jumaa pale chini aliyeonekana kuingiwa na mkwala wa Joachim Bartazar.

    "Ni wapi ilipo kambi yenu?" Ndio lilikuwa swali la kwanza lililomstua yule jamaa na kumfanya afikirie mara mbili jinsi ya kulijibu.

    "Swali langu limekuwa gumu eh!? lakini lina jibu"Aliuliza Joachim ambae alitamani sana sauti ya yule jamaa.

    "Mabibo!" Ndio jibu la haraka lililotoka kinywani mwa yule jamaa aliyeonekana kuwa na woga kwa mikwala ya Joachim.

    "Mabibo ipi?"

    "Tambua tu ni Mabibo bwana haihitaji kukuelekeza sana....." Alijibu kwa kujiamini huku akitikisa kiberiti lakini kabla hajamaliza kauli hiyo ya kishujaa alistukia kiganja kikavu kitua katika uso wake na kutoa sauti kali ya kibao.

    "Pwaah"

    "Ndio ulivyochagua"Aliongea Joachim.

    "Tuendelee na staili hiyo mana umeonekana kuitamani muda mrefu." Aliongezea tena huku akiangalia huku na huko kwa ajili ya usalama.

    "Mabibo ipi maana mie hata ukonda nafanya hivyo hunidanganyi mtaa wowote hapa nchini, sasa basi niambie ni wapi ilipo kambi yenu au alipo Mr. Paul!" Aliongea kwa mkazo zaidi safari hii na pale alipolitaja jina la Mr. Paul ambaye yeye anamfahamu kama Papaa Paul alishtuka.

    "Sikia nna uwezo wa kujiaua na usifanye chochote. Ila mke wangu ameenda kujifungua leo hivyo natamani nimuone mwanangu na hii ni ajira yangu." Aliamua kuongea kwa upole huku Joachim akimsikiliza kwa umakini sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nitakwambia kila kitu ila nahitaji usalama wangu na familia yangu..... nampenda mke wangu na nahitaji nimuone mwanangu." Aliongezea na kumfanya Joachim kuelewa maana ya yule mtu kujiacha hai hadi wakati ule.

    "Usalama wako ninao mimi na nikifahamu ninachohitaji utakuwa huru."

    "Lakini sio kwa RM Paul Addas" Aliongea vile yule jamaa na kumfanya Joachim kujiliza ni nani mtu huyo.

    "RM Paul Addas ndio nani?" Aliuliza Joachim.

    "Huyo ndio kiongozi na mmiliki halala kundi hili hatari la kigaidi la Rising Mafia..... Hili sio kundi kama mnavyodhani bali ni Jeshi tena kubwa kweli kweli na RM Paul Addas ndio kama kiongozi mkuu." Aliongea bila wasiwasi na kumfanya Joachim akae chini kusikiliza vizuri.

    "RM Paul Addas ndio huyo mnae muita Papaa Paul na huyo ni muasi wa nchini Ethiopia. Alikuja huku kwa kazi ya kufanya mapinduzi ya Uongozi wa juu wa nchi aliyoitiwa na Viongozi kadhaa wasiokuwa wazalendo na Nchi hii kama nilivyokuwa mimi baada ya kupewa maneno makali kuhusu nchi hii. Neno RM ni Rising Mafia ambalo ni kama utambulisho wetu mfano Mimi ni RM Davis Lenard." Aliendelea huku akimuangalia Joachim anayemsikiliza vizuri tena kwa umakini wa hali ya juu.

    "Hata siku moja hutokaa ujue wapi yalipo makao makuu ya watu hawa ili mie nilifanikiwa kunasa taarifa kuwa wapo nchini Ethiopia hata mimi na wenzangu wote mafunzo ya kijeshi tulienda kuyapatia huko kisha tukarudi huku kujiandaa na hiyo kazi huku tukifanya matukio madogo madogo kama mlivyokuwa mkiona. Sasa ukitaka kuuondoa mzizi wa RM Tanzania.... upo Kinyerezi na huko ndiko yaliko makao makuu kwani hata silaha nzito zilizofika ziko huko na hata mateka wetu hupelekwa huko." Alimalizia na kutulia.

    "Ni nani hao viongozi na wapo wangapi?" Ndilo swali alilotupia Joachim.

    "Nitakudanganya kama nikikuambia nawafahamu ila Waziri wa Ulinzi na Usalama ndie mstari wa mbele tena ameshafanikiwa kupandikiza Wanajeshi mia saba kutoka RM kwenda Jeshi la Ulinzi ili aweze kuitawala kwa urahisi nchi. Wapo wengi NYUMA YA PAZIA tena wanatoa misaada ya fedha nyingi kwa hili." Alimalizia na kumfanya Joachim auelewe zaidi mchezo ule mchafu huku dhamira za watu wale akizielewa zaidi.

    "Tena kabla ya msimu wa sikukuu Nchi itakuwa matatizoni kwa hili, wanaongezeka tena wenye uwezo zaidi na vyeo zaidi kwani wanatumia pesa na Mauaji ya kinyama zaidi. Na RM Paul ni hatari zaidi na ana hadi watu wa Nchi tofauti tofauti za Ughaibuni wameweka mikono yao na kuleta makomando wao." Alimalizia jamaa yule alijitambulisha kama RM Davis Lenard.

    "Umenipa ushirikiano mzuri sana na wakizalendo sana. Twende tukamuone mkeo hospitalini." Aliongea Joachim aliyekuwa kama na urafiki na mtu yule.

    "Sawa lakini nani jina lako?" Aliuliza RM Davis.

    "Jina kamili ni Luteni Kanali Frank Mapungo lakini nafahamika kama Joachim Bartazar na ndio jina langu la sasa katika kitengo cha National Defence Agency au NDA cha Kijasusi." Aliongea Joachim kwa ufasaha kabisa kutokana na kumuamini mtu yule. Lakini alipolitaja jina la Joachim Bartazar alisimama na kumuangalia sana na hata alipotaja NDA jambo lililomstua Joachim lakini akauficha mshtuko wake.

    "Joachim! kumbe ndio wewe?" Lilikuwa swali lililofuata baada ya kusimama kwake.

    "Naam, kwani vipi?" Nae akajibu huku akisimama.

    "Mtu hatari sana unayezungumziwa Kikosini kwa kutia doa mipango yao hatari hata kufanikiwa kuwatikisa. Nilikuwa sikufahamu ila leo nimeamini wewe ni Mwanajeshi tena kidume cha shoka." Aliongea Davis huku akipiga saluti ya kijeshi kwake na kumfanya Joachim atabasamu.

    "Pia umeongelea NDA yaani National Defence Agency ambayo ni kama taasisi ya kijasusi na kipelelezi ya siri sana ambayo hakuna mtu wala kiongozi anayeifahamu, Sio?" Aliongea Davis tena kwa umakini kama vile alikuwa ndani ya kitengo hicho.

    "Naam, mbona umekielezea vizuri hivyo unakifahamu?" Aliuliza Joachim.

    "Tena sana na hakina siri yoyote kwani kina Mamruki wawili wanaofanya kazi humo na ndio waliokuwa wakileta hizo taarifa zako na Mista au Marehemu Harold Maebo ili wakiteketeze kabisa ndipo waendelee na mipango mingine." Alimalizia Davis.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Uliijuaje mipango yote hii?" Aliuliza kwa mshangao Joachim.

    "Kabla ya kupewa mission hii nilikuwa Senior Secretary Servise kwenye kitengo cha RMG yaani Rising Mafia Goals na mie ndie niliyekuwa nikipanga vikosi vya uvamizi na hata taarifa za wapelelezi wote wanaotufatilia kisha kuuawa na ndipo alipokuja jamaa anaeyetambulika kama Luteni Albert Lao, Katibu Kiongozi wa Masuala ya Kigaidi ndani ya National Defence Agency na kuleta taarifa zenu wewe na Bwana Harold Maebo, Mkurugenzi wa National Defence Agency. RM Paul ndie aliyeagiza muuawe mapema na faili la taarifa zao liletwe ndipo akakabidhiwa hiyo kazi RM Jack Loyce kwa kazi hiyo ila ulinishangaza ulivyomuua kwani ulifanya nitamani kukuona ukoje au wa aina gani kwani RM Jack Loyce alikuwa tishio kambini na alipewa kazi za hatari tu." Alimaliza na kumduwaza Joachim kwa jina la Luteni Albert Lao.

    "Sasa nimegundua kuna mengi NYUMA YA PAZIA. Na kuna wengi NYUMA YA PAZIA la amani." Aliongea huku akitoka nje ya geti la boma la nyumba ya Sauda.

    Waliongoza huku wakifuata barabara kurudi barabara kuu. Walipofika barabarani ilikuwa imetimia saa 5 kamili usiku.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog