Simulizi : Mkono Wa Jasusi
Sehemu Ya Nne (4)
“Sitaki kukupoteza Debrah,” alimwambia mara tu ubishano kati yao ulipopamba moto pale ofisini.
Debrah alibaki kumwangalia tu boss wake, hakujua la kumjibu isipokuwa majibu yake yote yalikuwa moyoni mwake. Akakubaliana na boss wake na kuanza kuondoka.
“Debrah,” akamwita, “Mipango ya wenye nchi hiyo, achana nayo kama, rudi kwenye ofisi yako ya kawaida,” akamwambia. Lakini Debrah baada ya kumsikiloiza hakujibu neon aliamua kuondoka zake na kurudi nyumbani kwake. Roho ya ukaidi iliujaza moyo wake hata akaamua kufanya kazi hiyo kama yeye akiamini atakapoudhihirisha ukweli atakuwa shujaa katika mioyo ya watu lakini pia atakuwa ameteteza damu za wanyonge waliokufa migodini. Akiwa katika hilo ndipo anakutana na jinamizi la mauti linayoyachukua maisha yake katika ajali mbaya kabisa.
§§§§§
DUMISAN aliinama chini mezani kwake kwa nukta kadhaa na alipoinua uso wake akajikuta hayuko peke yake, akawaangalia watu wale waliokuwa mbele yake, wote aliwajua kwa majina na kazi zao katika idara ya usalama. Machozi yalionekana dhahiri shahiri katika macho ya kijana huyo aliyepewa dhamana kubwa ya uongozi katika idara nyeti ya usalama N.S.A.
“Debrah Mbongheni amekufa huko Durban usiku wa jana, natangaza hilo kiofisi kabisa ili utaratibu wa mziko ufanyike, tutamkumbuka kwa ujasiri, uchapakazi wake na kutokubali kushindwa kwake,” akamliza na kufuta machozi.
Wale vijana wakajipiga kwa ngumi vifuani mwao kisha wakaondoka pale ofisini bila kuongea neno. Ilisikitisha.
§§§§§
LERETI KHUMALO alifikishwa katika kliniki ya KwaZulu Natal alfajiri baada ya kukutwa amezirahi sakafuni. Mfanyakazi wake wa ndani ndiye aliyemgundua baada ya kuona muda wa kifungua kinywa mwanadada huyo haonekana sebuleni na si kawaida yake ndipo alipogonga mlango kwa nukta kadhaa na kukuta kimya, akawaita walinzi ambao walidiriki kuvunja mlango na kumkuta mwanadada huyo sakafuni akiwa kalala kimya, moja kwa moja wakamokota na kuita gari ya wagonjwa na kuwahi kumpeleka katika kliniki hiyo ambayo daima hutibiwa hapo na daktari wake maalumu.
“Hajafa, amezirai tu, ataamka,” Yule daktari mwanamke mwenye umri mkubwa aliwaambia wale vijana walioleta. Lereti alizimia alfajiri baada ya kusikia habari ya kifo cha Debrah, alijikuta akishindwa kuvumilia, mwili ukimuisha nguvu na kuanguka sakafuni kabla hajapiga kichwa chini kwa nguvu.
JOHANNESBURG – MONTECASSINO
DON ANGELO aliketi akiwa kazungukwa na mabinti kama ilivyo kawaida yake, makazi hoteli ya Michelangelo, starehe Montecassino hakuwa na lingine. Mabinti hao waliokuwa wakimminya hapa na pale katika mwili wake walisitisha zoezi hilo baada ya kijana mmoja mwenye umbo pana kuingia ndani ya chumba kile. Don Angelo akawapa ishara ya kuwa wawapishe kidogo, wakatoka na kuingia chumba kingine cha kando.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Zebel, nimekuita kwa kazi moja tu, Lereti Khumalo, ambaye sasa anaonekana kutafuta mbinu ya kuulinda mgodi wa baba yake ambao sisi na Robinson tunautaka, amelazwa katika kliniki ya KwaZulu Natal pale Durban, kwa mshtuko alioupata baada ya Debrah kuuawa jana,” akaweka mtemba wake kinywani na kuvuta kidogo kisha moshi wake kuupuliza kwa njia ya pua.
“Nimepata taarifa boss, tulikuwa tukisubiri amri yako,” Zebel akajibu.
“Ok, amri yangu ni hii, Lereti auawe palepale kliniki kwa njia zetu zilezile zisizotiliwa shaka na mtu yeyote, asante,” akamaliza na Zebel akaondoka ndani ya kile chumba na wale warembo wakarudi kuendelea kutoa huduma ile.
Zebel alipotoka tu katika jingo lile, akawasiliana na vijana wake wenye taaluma ya hali ya juu katika kuua, akawaagiza wafanye kazi hiyo kwa ustadi wa hali ya juu kabisa ndani ya saa nne wawe wameikamilisha.
§§§§
KAMANDA AMATA akajipekua mfukoni na kutoa kile kikaratasi, akakisoma kwa umakini sana kilikuwa kimeandikwa jina la mtu namahali anapoishi.
“Zebel Pinch, Springbok 320U,” akayarudia maneno hayo na kuyaweka akilini kisha akajiweka sawa kumtafuta huyo mtu aliyepata jina lake kwa hicho kikaratasi. Akiwa macho yake luningani ndipo akapata taarifa za huyo mwanamke Debrah aliyeku8fa ajalini huko Durban, akaisikiliza kwa makini sana taarifa hiyo ilipokamilika, akabadili ratiba. Akatoka na kuiacha hiyo hoteli, akaingia katika gari yake na kuelekea katika ofisi ndogo za N.S.A katika jiji hilo la Johanesburg. Alipoegesha gari yake nje akapokelewa na wahudumu waliomkaribisha kwa ukarimu wa Kiafrika. Moja kwa moja akafika mbele ya meza ya mkuu wa idara hiyo ndani ya jiji hilo.
Hakuwa na haja ya kuuliza jina kwa kuwa tayari alikwishaliona mezani ‘Mrs. Silolo Mbheki’.
“Naitwa Amata Ric au kamanda Amata,” akampa mkono, Yule mama akabaki katoa macho haamini kama ni sahihi anachokisikia au la.
“Unasema?” akauliza tena.
“Wewe ni Kamanda Amata, T.S.A?” Yule mama alihamanika, akampa mkono kwa mara ya pili naye akaupokea na kumsalimu namna hiyo.
“Mimi ndiye,” Kamanda akajibu.
“Karibu sana, yaani karibu sana, najua ujio wako una jambo, we mtu huwa nakusikia kwa mbali tu na kusoma habari zako vitabuni, watu wamekugeuza biashara kwa mikasa yako,” Yule mama akaongea huku akionekana kuwa na furaha ya ajabu.
“Poleni sana kwa kifo cha Debrah,” akatoa salamu ya rambirambi.
“Asante japo hatujapoa kwa maana alikuwa ni mtu muhimu sana kwetu, lakini basi,” Yule mama akajibu kwa kukata tamaa.
“Lakini amekufa akiwa kazini hana budi kupata nishani ya ushujaa,” Kamanda akaeleza kwa maoni yake.
“Hapana, hakuwa kazini,” akajibiwa. Jibu hilo lilipiga shoku Amata, akashusha pumzi kwa nguvu na kujiweka sawa.
“Hakuwa kazini?”
“Ndiyo hakuwa kazini. Ipo hivi Kamanda japo sitakiwi kusema, Debra alipewa jukumu la kufuatilia uchunguzi wa vifo vilivyotokea mgodini katika miezi hii mitatu, lakini kazi hiyo ilisitishwa baada ya siku nne tu tangu aianze, akarudi kituoni na kutakiwa kuendelea na kazi yake ya kawaida. Leo asubuhi ndiyo tunasikia juu ya kifo chake huko Durban, unaona, sasa hatujui nini hasa kilimrudisha huko,” Yule mama akaeleza wazi.
“Ok, inawezekana kuna mtu alimfuata huko au kuna kitu alikifuata huko,”
“Yeah inawezekana lakini mimi na wewe hatujui ni kitu gani,”
“Anaishi wapi?”
“Midrand nyumba yake ipo kitalu namba 3,”
“Ok, msiba upo huko au wapi?”
“yeah, msiba upo Midrand lakini nafikili mazishi yatakuwa Soweto nyumbani kwa wazazi wake,” Yule mama akaeleza.
“Asante sana, nikuache, niendelee na majukumu yaliyonileta nilipita tu kuwapa pole ya msiba,”
“Asante Kamanda Amata, salute kwako kijana, sifa zako zanatikisa mabeberu,” Yule mama akamwaga sifa huku akisimama na kumpa mkono wa kwaheri.
Ndani ya gari yake, Amata akarekebisha GPS yake na kuiongoza imwoneshe kitongoji cha Midrand, nayo ikanavigate sawia kabisa, akawasha gari na kufuata maeelekezo yaliyokuwa yakisikika ndani ya gari hiyo kuelekea Midrand.
Akiwa katikati ya safari yake, simu yake ikaita, akainyayua na kutazama kioo, zilikuwa namba za kawaida za nchi hiyo ‘Nani huyu?’ akajiuliza na kufytaua kisha akaiweka sikioni….
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hello! Mi’ Pa-me-la,” sauti ya mwanamke aliyekuwa akili ikatua katika ngoma ya sikio la Kamnda Amata.
“Pamela! Pamela yupi?”
“Nilikupa majuzi namba yangu pale Stesheni,” sasa alijibu kwa utulivu kidogo lakini bado alikuwa akivuta kamasi kurudi puani mara kwa mara.
“Oh, ok, niambie Pamela, uko wapi?”
“Nipo nyumbani nimefiwa na dada yangu,” akajibu.
“Pole sana mrembo, unaishi wapi japo nikutembelee kama hutojali?”
“Naishi Midrand,” akajibu. Jibu hilo likapasua moyo wa Amata, ‘Midrand?’ akawaza, kichwani alikuwa akijiuliza kama kuna uhusiano wowote kati ya misiba hiyo miwili yaani wa dada wa Pmela na ule wa Debrah. Baada ya dakika kama ishirini na tano hivi kwa mwendo wa kasi aliicha barabara kuu na kuchukua njia ya kawaida iliyotanguliwa na kibao kilichoandikwa Midrand Evenue, akaendesha polepole huku akitazama huku na kule kuona kama kuna nyumba yoyote yenye dalili za msiba. Alipokaribia kuimaliza ile barabara ndipo akaona nyumba moja iliyofungwa turubai za kisasa katika bustani kubwa na magari kadhaa yakiwa yameegeshwa. Akichukua simu yake na kupiga ile namba. Baada ya dakika kama tano alimwona Yule mwanadada akija taratibu nje ya nyumba hiyo akiwa ndani ya vazi jeusi likiashiria maombolezo.
Kamanda Amata akashuka garini na kumwita, Pamela akasogea hadi kwenye gari hiyo na moja kwa moja akaingia na kuketi katika kiti cha mbele.
“Pole kwa msiba,” akamsabahi.
“Asante, dada amekufa jana kwa ajali ya gari,” akaeleza huku chozi likianza kumdondoka.
“Ajali ya gari! Wapi?” Kamanda akauliza.
“Durban, alienda Durban kikazi,”
“Pole sana Pamela, nimekuja kukupa salamu zangu za rambi rambi,” Kamanda Amata akateremka pamoja na Pamela, akaifunga gari kwa swichi maalum kisha wakaongozana kuingia ndani ya nyumba hiyo. ‘Muuaji hupenda kushiriki misiba ya aliyowaua, si ajabu akawepo hapa,’ Amata akawaza akiwa anapanda taratibu ngazi kuingia ndani ya nyumba hiyo, kila alipopiga hatua alihisi nywele zikimsimama na mwili kusisimka. Kijana mmoja aliyekuwa ameketi mahala Fulani alikuwa akimtizama sana, kijana huyo alikuwa amevalia suti nyeusi na kofia ya pama nyeusi, macho yake alikuwa kayaficha kwa miwani ya rangi hiyohiyo.
Kamanda Amata akiwa kauzungusha mkono wake kiunoni mwa Pamela alikuwa akitembe taratibu huku wakiongea hili na lile mpaka ndani ya nyumba hiyo. Kwenye meza kubwa kulikuwa na picha kubwa ya Debrah iliyopambwa maua na mishuma miwili ilikuwa ikiwaka huku na huku, akaisogelea na kusimama kimya kwa nukta kadhaa kisha akasaini kitabu maalumu kilichokuwa hapo. Alipomaliza, akatoka tena na Pamela na kumhoji mawili matatu.
“Ina maana dada yako hakukwambia kaenda kufanya nini huko Durban?” akamwuliza.
“Hakunambia kwa kweli, mi nimerudi naye anaondoka,” Pamela akajibu.
“Ana rafiki au mna ndugu huko?”
“Vyote viwili hapana, nafikiri alikwenda tu kikazi maana kazi zake humfanya asitulie nyumbani, kabla ya hapo aliwahi kunambia ana business partiner wake huko Durban sasa labda alienda huko,” Pamela akaeleza kile anachokijua na Kamanda Amata akasikiliza kila kimoja huku akipembua mchele na chuya.
“Ok, pole sana, unamjua huyo rafiki yake? Kwa jina,”
“Hapana, ila nafikiri alikuwa na business card ngoja niitazame,” akajibu kisha akatoka pale waliposimama na kuingia ndani, dakika tatu zilitosha akaja na kadi hiyo mkononi, Kamanda akaipoke na kuisoma, moyo wake ukapiga kwa nguvu, ilikuwa ni kadi ya Lereti Khumalo.
‘Lereti atakuwa matatizoni kama hawa wawili walikuwa marafiki, lazima niende sasa,’ akawaza huku akifanya maamuzi kichwani mwake yeye mwenyewe.
“Ok, Pamela, mimi niende, nitakuja kesho tena,” akamuaga, wakakumbatiana kisha Amata akarudi kwenye gari yake. Alipokuwa ndani ya gari yake akachekecha akili kuona nini afanye, kulikuwa na mawili ya kufanya kwa nukta hiyo ama kumsaka mtu anayeitwa Zebel Pinch au amuwahi Leret Khumalo. Ilikuwa mtihani mgumu kuamua kwani kila moja lilikuwa na uzito wake na alipoangalia umbali ndipo akapambana na ugumu mwingine. Aliingia katika mtambo wake wa GPS uliofungwa ndani ya gari yake akatazama umbali kutoka Johanesburg hadi Durban, haukuwa mkubwa sana, ilikuwa ni Kilomita 567.6, kama angetumia gari ingemuweka barabarani kwa saa tano na dakika ishirini na tisa. Akaona kama ni kwenda huko ni bora kutumia usafiri wa ndege ambao ungemchukua si zaidi ya saa moja angani.
Akiwa katika kuwaza hilo ndipo aliposikia kioo cha gari yake kikigongwa na mtu kutoka nje, akawasha kijiluninga cha ndani kumtazama, hakumjua upesi kwani alikuwa katika mavazi meusi na aligeukia nyuma. Kamanda Amata akashusha kioo kile taratibu na mara huyo mtu akafungua mlango na kuketi kisha kabla hajafunga mlango ukajifunga wenyewe na kioo kikapanda juu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Twende,” akamwamuru Amata. Taratibu akaondoa gari na kuingiza barabarani.
“Leo umekamatika!” Yule mtu akamwambia Amata ambaye alikuwa haongei lolote mpka muda huo, aliongeza kasi ya gari alipoingia barabara kubwa na kuendesha kwa kasi ya kilomita themanini kwa saa.
“Tunaelekea wapi?” akauliza Amata.
“Swali zuri sana, twende hoteli ya Michelangelo, mkuu anakusubiri pale,” Yule mtu akaongea huku bastola yake ikiwa tayari kichwani mwa Amata.
“Mkuu wako nani? Don Angelo?” Amata akauliza kama hajui analoambiwa.
“Kumbe unamjua ee, basi leo hii anakuhitaji muonane ana kwa ana,”
“Mbona jana tulionana akanikimbia? Hata wewe kibaraka wake hutofika kumuona leo kabla hujawa marehemu. Yule bwana akamgonga Amata na domo la bastola.
“Ukileta ujeuri nitakuua mwenyewe,” akasema.
“Huna uwezo huo hata chembe,” Amata alijibu huku akibadili gia na wakati huohuo katika usukani wake akachezea vijibatani vidogo vilivyowekwa hapo.
“Angalia mbele!” Kamanda Amata alimwambia Yule bwana naye akageuka mbele kuona kuna nini, Amata akabonyeza moja ya batani hizo, kilichotokea kwenye dashboard upande wa abiria kilimuacha jamaa domo wazi. Kitu kama upanga wenye umbo la pembe tatu, ulichomoka kutoka mahali Fulani kwenye hiyo dashboard na kuchoma kwenye kifua cha Yule jamaa, akabaki domo wazi na macho yamemtoka pima, mikono yake iliachia bastola na kudaka lile bisu lakini haikuweza kulizuia.
“Asante Chiba kwa teknolojia yako,” akazungumza huku akirekebisha tai yake na gari ikizidi kuchanja mbuga, mbele kama kilomita nne hivi akachepuka na kuingiza gari katika uchochoro Fulani, akasimama, akapekua mifuko yake yote na kutoa kijitabu kidogo kilichoandikwa kwa karamu kwenye kurasa zake, akakipekua na kusoma lakini havikumsaidia, ila ukurasa wa mwisho ulimfurahisa zaidi.
‘Trip to Durban at 11:25 am, Johanesburg Airport’ ujumbe huo mfupi uliokuwa ukitaja saa ya safari ya Durban ulimpa mawazo Amata, akajua hawa jamaa wana safari ya huko saa hiyo tena kwa ndege, mwisho wa ule ujumbe kulikuwa na namba ya simu, akakiweka kile kijitabu katika trei maalum kisha akaichukua ile bastola na kumwekea kwenye koti lake, simu ya mkononi akapekua hapa na pale na kukuta jumbe zinazohusu sakata hilo lakini hazikumhusu yeye moja kwa moja, akachukua na kuiweka hapohapo kwenye hiyo trey kisha akamsukumia nje Yule jamaa.
“Tutaonana Durban!” akamwambia kisha akaondoa gari na kuigeuza kurudi mjini, akauchukua uelekeo wa kwenda uwanja wa ndege wa Johanesburg uliojulikana kama Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo. ‘Tutaonana huko huko mbuzi nyie, ama zenu ama zangu,’ akajisemea wakati akaiicha barabara ya Pretoria na kuingia barabara ya kawaida inayoelekea hapo Uwanja wa ndege, akaegesha gari yake mahala Fulani na kabla hajashuka, akachukua simu ya Yule jamaa na kuchezesha namba, hakuna aliyemjua. Akaichukua ile namba aliyoikuta pale kwenye kile kijitabu na kuiweka katika simu hiyo kisha akaipiga bila kujali ni nani ataipokea.
“Hello, Rajiv Khumar anaongea,” ikajibiwa kwa lugha ya kiingereza katika lafudhi ya Kihindi.
“Nilikuwa nauliza kuhusu safari yetu ya Durban ni muda uleule au kuna badiliko?” Kamanda akaongea kwa kuiga lafudhi za wazulu japo hakupatia sana, ukimya ukatawala, akaanza kupata wasiwasi. Mara ile simu ikakoroma, na Rajiv akarudi tena.
“Flight Schedule yenu haijabadilika, iko vilevile,” akamjibu.
“Ok, asante,” Kamanda akajibu kisha akairudisha ile simu na kuiweka mahala palepale, ndani ya hicho kijitrey alichoweka kile kijitabu na ile simu kulikuwa na mionzi ambayo ilikata aina yoyote ya mawasiliano inayoingia katika kitu kilichowekwa hapo, kama ni simu haiwezi kuita na mpigaji kutoka nje kila akipiga husikia tone ya kumjuza kuwa mtumiaji yuko nje ya eneo la mtandao. Kama mliweka kitu ambacho mnaweza kuifuatili basi pale haikuweza kuonekana.
Akateremka katika gari yake na kuelekea ndani ya jingo hilo la Uwanja wa ndege ambako kulikuwa na watu wengi wakiwa na pilikapilika za huku na kule. Akaiendea moja ya ofisi za ndege ya kukodi, akaulizia kama angeweza kupata usafiri akafanikiwa, akafanya malipo na kuulizwa muda ambao angependa kuondoka. Akazungusha akili harakaharaka, akakumbuka wale jamaa wataondoka saa tano na dakika ishirini na tano, basi yeye akaomba saa tano na kamili.
DURBAN – Saa 6:15 Mchana
NDEGE NDOGO iliyombeba Kamanda Amata ilitua katika Uwanja wa Ndege wa Luis Botha, Durban, Kamanda Amata alitazama kutoka dirishani na kuuona uwanja huo aliokunyaga miaka mitano iliyopita akiwa katika safari ya upelelezi juu ya kifo cha Khumalo. Na leo hii alikuwa tena hapo kwa kazi inayofanana na hiyo.
“Pole sana kwa safari, tumesfika,” Yule rubani akamshukuru Amata na kumpa mkono.
“Asante kwa safri nzuri,” Kamanda akashukuru na kuteremka taratibu kisha kuelekea nje ya uwanja huo baada ya kukamilisha taratibu zilizotakiwa. Hakuondoka, alipanda ghorofa ya juu kwenye mkahawa na kupata kinywaji huku akiangalia ndege zote zinazotua na kupaa kutoka katika uwanja huo.
Nusu saa baadae ilitua ndege ndogo na kuelekea katika maegesho palepale ambapo yeye alifikia, Kamanda Amata akachukua miwani yake na kuivaa kisha akzungusha vijinobu vidogo pembeni mwa miwani hiyo na kuweka picha ya mbele yake kuwa sawa katika muonekano.
Vijana wane walishuka katika ndege hiyo wakiwa wamevalia suti nyeusi, nywele zao ndefu hazikuwaficha Uzungu wao. Amata akatikisa kichwa kuashiria kuwa kwa vyovyote hao ndio anaowataka. Akateremka ngazi na kuteremka chini kabisa ya jingo hilo ili kuwaona kwa vizuri.
‘Sio watu wema hata kidogo,’ akajisemea wakati vijana hao wakiondoka kuelekea megesho ya uwanja huo. Akawatazama bila kuwaacha, wakachukua gari mbili tofauti na kuondoka zao, nyuma yao Kamanda Amata akachukua tax na kuwafuatilia kwa nyuma akimpa maelekezo dereva bila yeye dereva kujua kuwa kuna watu anaowafuatilia.
Wakiwa katika barabara ya Kentukcy bado Amata aliweza kuwaona vizuri mpaka walipoiacha barabara hiyo na kuingia katikati ya jiji hilo, baada ya kupita mitaa kadhaa, zile gari zilisimama katika moja ya majengo makubwa lenye shughuli mbalimbali za kibinaadamu.
“Egesha kwenye jingo hilo la mbele,” akamwambia dereva, naye akafanya hivyo. Amata akamlipa ujira wake na biashara yao ikaishia hapo. Akawatazama wale jamaa akawaona wakiingia katika hoteli moja iliyo ndani ya jingo hilo. Hakuwabugudhi, akatoka nje na kuchukua tax nyingine.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nipeleke Khumalo Tower,” akamwambia huyo kijana, wakaondoka mahala pale. Haukuwa mwendo mrefu walifika katika jingo hilo, akalipa na kushuka, moja kwa moja akaingia katika lifti mpaka ilipo ofisi ya Lereti, hakuna kilichobadilika zaidi ya rangi na maua yaliyopandwa katika vyungu, pia kipoza hewa kilichofungwa ndani ya jingo hilo kilifanya kazi yake bila upendeleo.
“Kaka kama nimeshawahi kukuona mahali,” sekretari wa Releti alimwambia Amata.
“Hapana, duniani wawiliwawili dada angu, nimekuja kumuona Lereti,” Kamanada akamwambia.
“Oh, Lereti hajafika kazini, anaumwa yupo kliniki ya KwaZulu Natal, samahani sana, njoo keshokutwa tafadhali,” Yule mwanadada akajibu. Kamanda Amata akashusha pumzi ndefu, kisha akasimama na kuaga akiahidi kurudi kesho kutwa yake.
KLINIKI YA KWAZULU NATAL
LERETI KHUMALO alikuwa kimya kitandani kalala, fahamu zake zilirudi sawia lakini hakuruhusiwa kuondoka muda huo kutokana na matibabu madogo madogo yaliyokuwa yakiendelea. Walinzi wake bado walikuwa makini nje ya kliniki hiyo na nje ya mlango wa chumba hicho alicholazwa. Haikuruhusiwa mtu hasiyejulikana kuingia bila kibali maalum.
Mchana huo walipokea watu kadhaa waliokuja kumtakia hali, kila mtu alipekuliwa ili kuona kama ana silaha yoyote inayoweza kumzuru bosi wao. Wakati huo ndani ya wodi hiyo ya V.I.P hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya yeye Lereti na mfanyakazi wake wa ndani ambaye ndiye alikuwa akimsaidia kwa hili au lile.
NJE YA KLINIKI HIYO
BMW nyeusi ilisimama katika maegesho ya kliniki hiyo ikifuatiwa na Subaru ya rangi hiyo. Kijana mmoja mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, akateremka na kuelekea mahali palipo na mgahawa mdoho kando tu ya kliniki hiyo. Kwenye gari nyingine hakuna aliyeshuka. Yule bwana akatembea kwa hatua ndogondogo akiwa na kijibegi chake mkononi, akaingia ndani ya mgahawa huo kisha akatokea mlango wa nyuma, akazunguka mpaka eneo la kutupa takataka, hakukuwa na mtu, akatembea harakaharaka na kufika usawa wa chumba cha kubadilishia nguo madaktari kutokana na vitu vilivyokuwa hapo ndani kwa jinsi alivyoviona kupitia dirishani, akalisogelea dirisha hilo la kioo na kulisukuma kwa juu kisha akajitoma ndani ya chumba hicho. Akaushika mlango na kuujaribu ulikuwa wazi, akapepesa macho huku na kule, akavuta moja ya koti lililoning’inizwa ndani ya kabati mojawapo, akalivaa, akachukua stethoscope akaipachika shingoni mwake, ndani ya kosti hilo alipopapasa kulikuwa na kitambulisho, akakichomoa na kukiangalia, akatabasamu alipogundua kuwa mwenye kitambulisho hicho ni daktari mzungu. Akafungua kikoba chake na kutoa kisu kikali, akakata leya nyembamba sana ya picha ile ya kitambulisho, akaibandua na kuibandika yak wake pale juu.
Ilichukua sekunde kama arobaini na tano kufanya tukio hilo, akakipachika kwenye mfuko wa koti lake. Kisha akachukua vitu Fulani kama peni ya chuma, akachukua na kingine kama kiberiti cha gesi akaviunganisha kwa jinsi ambayo mimi na wewe hatujui, sekunde kadhaa mkononi mwake alikuwa amekamata bastola ndogo kabisa yenye bomba nyembamba ukubwa wa peni, akaipachika mfukoni, ukiitazama kwa mbele pale mfukoni ni kalamu. Akachukua kijichupa chake kidogo kilicho ndani ya kile kikoba na bomba la sindano akafyonza kitu kama dawa kilicho ndani ya chupa hiyo, alipohakikisha iko sawa, akavesha kizibo chake ile sindano na kuitika katika kijiplastiki chake na kuiweka mfukoni. Akafungua mlango na kutoka kama mwenyeji wa mahali hapo.
§§§§§
KAMANDA AMATA alifika katika kliniki hiyo sekunde chache tu baada ya zile gari mbili kuwasili, alikuwa akizifuatilia tangu zilipoanzia safari katika lile jingo kubwa la kibiashara. Akashuka na kumlipa dereva tax kisha akajiweka koti lake vizuri na na kuipachika miwani yake usoni, alipotazama ndani ya zile gari aliwaona vijana kadhaa, gari ya nyuma watatu na yam mbele dereva peke yake, aliwaona moja kwa moja kupiti katika tinted za vioo vya zile gari ila kutokana na ubora wa miwani yake ya kijasusi tinted haikuwa na lolote, akavuta hatua na kuelekea kule kwenye ule mgahawa alikoelekea Yule mzungu kijana. Akapanda ngazi na kuingia ndani, hakumwona, kengele za hatari zikalia kichwani mwake, vinywelea vikamsimama, akatazama huku na kule akagundua kuna mlango unatokea nyuma, akaufuata na kupita mpaka nje.
Kulia kwake kulikuwa na ujia uliojengewa vijitofali akapita humo na kulipita lile teketeza taka, alipita madirisha ya wodi mbalimbali, mbele yake wakatokea watu wa usafi.
“Samahani kaka, huku huruhusiwi kuja ni hatari kwa afya yako,” Yule mwanadada aliongea kwa lafudhi ya Kizulu.
“Oh, nimepotea njia mimi ni mgeni hapa, lakini mmekutana na kijana mzungu huko mbele? Kavalia shati nyeusi na suruali kijivu,” akawauliza.
Wakatazamana kisha wakamtazama Amata.
“Hapana kaka!” wakajibu. Hakuna jinsi aligeuka kurudi ili kuwapisha wale wadada wafanye shughuli yao, walipoimaliza akaongoza tena njia ileile na alipofika kwenye lile dirisha akasita na kulitazama, liko wazi, akili ikafanya kazi, akajitoma ndani yake.
Juu ya meza ya chumba hicho, akakuta ile chupa bado iko pale, akaitazama kwa mbali bila kuigusa, akabaki kaduwaa, ilikuwa ni chupa yenye ya lethal yaani mchanganyiko wa barbitulate, paralytic na mchanganyiko wa potassium, ni sumu mbaya ambayo hutumiwa kwa watu wanaopewa vifo vya kuwapunguzia mateso ( euthanasia) katika nchi zilizoendelea ukimchoma binadamu kwa sindano haitamchukua hata dakika kumi tu kufa kwanza umlaza usingizi kisha umfanya ashindwe kupumua na Potassium chloride inakuja kusimamisha moyo na kumfanya mhanga afe kwa ugonjwa huo, labda apate huduma ya kwanza ndani ya muda huo mfupi.
Kamanda Amata alihamanika, akajua mambo yataharibika muda wowote. Akafungua mlango na kujikuta katia korido ndefu iliojawa na watu hapa na pale wakiwa wametingwa na shughulia zao, akapita haraka haraka katika hali ambayo kila mhudumu alishangaa na hiyo ikafanya kamera za usalama kumuona, wakatumwa askari wa usalama katika kliniki hiyo kumkata.
Mlangoni mwa wodi ile, wale walinzi walikuwa wamesimama bado wakilinda usalama, alipotaka kingie, wakamzuia.
“Kuna daktari huruhusiwi kuingia,” wakamwambia huku wakimtunishia vifua. Hakuwasikiliza, akawapiga kikumbo na kuingia ndani ya kile chumba, hakuna daktari, mtiririko wa damu ulikuwa chini ya kitanda cha Lereti. Wale walinzi wa Lereti wakaingia ndani kumfuata Amata wakiwa na bastola zao mkononi, wakashangaa kuona damu ikitambaa taratibu ndani ya chumba kile. Walipoangalia chini, mwili wa mfanyakazi wa ndani wa Lereti ulikuwa na majeraha matatu ya risasi. Lereti alikuwa bado kitandani, Kamanda Amata alitazama kwenye ile chupa ya drip akakuta bomba la sindano likining’inia.
“Shiiit!” akapiga kelele, na kumvamia Lereti, akachomoa kanula za kuingia maji mwilini na kuzitupa huko. Dakika hiyohiyo, wauguzi wakafika na kukuta hali hiyo, Amata akapiga kelele kuomba msaada, wale wauguzi wakamtoa Lereti haraka ka na kumpakia kwenye machela iliyokuwa hapo pembeni na kumkimbiza chumba kingine chenye mitambo tiba ya kisasa ambayo ingeweza kumuokoa dhidi ya kifo hicho cha jirani.
Ndani ya kliniki hiyo kuliibuka hali ya sintofahamu. Kamanda Amata akachungulia dirishani na kuona koti la daktari likiwa chini kwenye kinjia kilekile alichojia. Hakusubiri, alitoka kasi na kutokea mlango mkubwa, akawapita wale walinzi pale nje na kuziona zile gari zikiondoka kwa kasi, akachomoa bastola bastola yake huku akikimbia upande wa piali ambako lazima zile gari zizunguke kabla ya kutoka, alipofika usawa mzuri akajificha kwenye mtende na kulenga shabaha, maridhawa, iliyobomoa kioo cha mbele cha gari ya kwanza, risasi ya pili ilimpata dereva shingoni, akapoteza uelekeo, gari ya nyuma ikataka kuigonga ile ya mbele lakini Yule dreva alikuwa mahili, akapanda tuta huku kioo cha nyuma kikishuka na Kamanda akauona mtutu wa bunduki, akaruka na kutua eneo linguine akiziacha zile risasi zikiusulubu ule mnazi. Akiwa pale chini bastola yake ilibanja mara kadhaa na kushuhudia tairi za ile BMW zikifumuka na ile gari ikayumba na kuigonga nyingine ya mbele, milango ikafunguliwa, wakashuka vijana watatu wenye bunduki za maana na kutawanyika huku mmoja akimkabili Amata.
Nje ya kliniki hiyo ilikuwa ni patashika kati ya Kamanda Amata na wale jamaa, watu waliokuwa wakishangaa walipowaona wale jamaa wakawafahamu kiuraahisi na wengi wao wakaondoka eneo lile.
Kamanda Amata aljitupa chini na shabaha ya Yule jamaa ikamkosa, akaviringika chini na kupenya katika moja ya uvungu wa gari kabla hajatokea uoande mwingine, akaitazama miguu ya Yule jamaa ilikuwa ikija eneo lile, akaiweka sawa bastola yake na kufyatu risasi mbili zilizovunja ugoko wa yula jamaa na kujibwaga chini. Kamanda akajitokeza na kummaliza risasi ya kifua. Tayari bastola yake ilikuwa imekwisha, akaifutika nyuma ya suruali katika mkanda na kuinyakuwa bunduki ya Yule jamaa, alipotahamaki hakuwaona wali jamaa ila alishuhudia kelele za tairi za gari upande wa pili zikisugua barabara na kuondoka.
“Wewe ni nani?” sauti ilitokea nyuma yake, alipogeuka akautana na afisa wa polisi aliyekuja na timu ya vijana kama watano wenye silaha.
Kamanda hakujali akamwendea Yule jamaa na kumpekua.
“Acha! Usimpekue wewe si polisi,” Yule kiongozi wa polisi alitoa amri, lakini Amata hakujali, alipekua hapa na pale akatoa vifaa vya mawasiliano, akavigeuza geuza na kuvipachika sikioni kisha akatulia kwa nukat kadhaa.
“Mshafika mbali?” sauti moja ikauliza.
“Yeah hatupo mbali sana waweza kuja hata kwa mguu,” sauti nyingine ikajibu. Kamanda Amata akamwacha Yule jamaa pale chini akiwa marehemu, akajiinua na kusogea kando aking’aza macho huku na kule, akajua kwa vyovyote vile Yule aliyejifanya daktari hajaondoka eneo lile, wale wengine ilikuwa ni geresha tu. Aliamini mawazo yake kwa kuwa ni sekunde hizohizo alimwona kijana Yule akitoka mgahawani mara hii alikuwa na suruali nyeupe na shati la kijani, usoni naliweka miwani nyeusi. Kwanza Kamanda hakuwa na uhakika kama ni yeye au la, lakini kilichompa uhakika ni ile kalamu katika shati lake na kikoba chake ambacho kilisheheni zana za kijasusi za kuua bila shida.
Kamanda akavuka barabara na kumtazama uelekeo wake, mkono baso alikuwa na bunduki yenye nguvu, pistol aina ya AA 3, majasusi wengi hupenda kuitumia kwa kuwa imetengenezwa na kiwambo cha sauti ndani yake, hiyo hufanya kazi kimyakimya. Wale polisi walibaki wametulia kumtazama kijana huyo wasiyemjua anataka kufanya nini huku wakimfuata kwa mbali. Kamanda akavuka barabara na kujibana nyuma ya gari moja akitazama. ‘Mshakosea, sasa nawapa salamu za Don Angelo mumpelekee,’ akajisemea huku akiwa nyuma ya gari kubwa kidogo lililomficha na kumpa nafasi ya jicho tu kuona vya mbele.
Yule daktari akaikaribia gari Fulani nyeusi, akashika mlango aingia kuondoka, Kamanda Amata bila kosa alifyatua risasi mbili zilizoishia mgongoni mwa Yule daktari, akapiga yowe la uchngu na kujibwaga barabarani, muda huohuo ile gari aiaktolewa maegeshoni na kusimama barabarani, watu wawili wenye silaha wakashuka na kumimina risasi kuelekea aliko Amata lakini mwenzao alikuwa keshahama eneo lile muda mrefu, na kusogea karibu nao upande wa pili, kijana mmoja alimwokota byule dajtari aliyekuwa akihema kwa shida na kumpakia kwenye gari kisha wale wawili wakarudi na kuingia na ile gari ikaanza kuondoka. ‘Nilikuwa nawasubiri muingie nifanye yangu, washenzi ninyi,’ akiwa kajificha padogo sana kwenye moja ya gari lilioegeshwa hapo alilenga tanki la mafuta na kufyatua risasi tatu, ile gari ikalipuka na kupaishwa juu ikazunguka hewani kama mara tatu na kuanguka chini kwa kishindo.
Taratibu akajiondoka katika eneo lile na kutoweka…
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
POLISI WALIHAHA kumsaka Kamanda Amata wasimwone, kila uchochoro waliopita hakuwepo, walitawanyika kila mahali lakini hakuonekana, wengine wakajaribu kuwasiliana na watu walio kwenye mitambo ya usalama inayopiga picha sehemu mbalimbali za jiji hilo la Durban, lakini waliishia kumuona mtu huyo akijificha nyuma ya gari kisha akatoweka, baada ya mlipuko ule.
“Huyu si binadamu, lazima ni shetani!” alisikika mmoja wa viongozi wa jeshi la polisi akiwaambia wenzake.
“Atapoteaje hata kwenye kamera asionekane?” walijiuliza pa si na majibu. Wakajigawa wengine kumsaka Kamanda Amata na wengine kushughulikia upelelezi wa tatizo hilo ikiwamo kujua kulikoni kule kliniki hata kutokee kizaazaa hicho.
“Yaani kama sinema ya Schwazeneeger vile,” katoto ka kizungu kalimwambia mama yake wakiwa njini kutoka sokoni.
§§§§
Mara tu ule mlipuko ulipotokea na kile kizaazaa, Amata aliipiga risasi kamera iliyokuwa mbele yake na kuondoka eneo lile mpaka upande wa pili na kuikuta barabara nyingine, kabla hajasimamisha tax, akavua viatu vyake na kuviacha chini kisha akaingia kwenye tax na kuondoka eneo lile.
“Tunaelekea wapi tajiri?” Yule dereva akauliza. Akampa maelekezo naye bila shida alifika katika eneo husika.
Kamanda Amata akamlipa kisha akapiga hatua chache katika mtaa huo ulioonekana kuwa na Waafrika wengi kuliko Wazungu, akawaendea vijana Fulani wauza viatu, akanunua jozi moja ya viatu.
“Huu ndio mtaa wa Shilowane?” akawauliza.
“Nilijua tu we mgeni. Unatoka wapi?” kijana muuza viatu aliuliza.
Kamanda hakujificha akamweleza kuwa yeye ni Mtanzania.
“Aaaa wa nyumbaniiiiii!!!!” Yule kijana akashangilia kumbe na yeye alikuwa ni Mtanzania.
“Hongera kwa bishara, naona mbao imejaa,” kamanda akamweleza.
“Asante tunaganga njaa kwa watu huku, cha muhimu na kizuri ni kuwa watukubali sana hawa jamaa, tunaishi kwa amani,” Yule kijana akaongea kwa furaha sana.
“Ok, ni vizuri lakini usisahau nyumbani,” akamwambia huku akimpa mkono kumuaga.
Wakapiga picha ya pamoja kwa simu ya Yule kijana, wakaagana. Kamanda Amata akapita katika mtaa huo na kuitafuta nyumba anayoitaka. Alipoteremka mteremko mkali kidogo akakutana na barabara ya lami, akakunja kulia na kuielekea nyumba kubwa ya kisasa iliyozungukwa na miti mingi sana na bustani ya kupendeza, akavuta hatua mpaka getini, hakuona mtu yeyo tee neo hilo, akashika vyuma vya geti hilo na kuruka mpaka ndani, akatua taratibu bila kufanya ukulele wowote. Alipotua ndipo alipomwona mlinzi mmoja akiwa upande wa pili, moja kwa moja akamzunguka na kutumia dirisha la upande mwingine kujipenyeza ndani ya jumba hilo. Akapita taratibu na kuingia kwenye kijiofisi kidogo kilicho ndani ya jumba hilo. Ukutani alikaribishwa na picha kubwa ya Lereti Khumalo, akaibusu.
Akaanza kupekua hapa na pale mpaka alipokuta lile faili lenye mkataba wa kibiashara wa Mgodi wa Mzee Khumalo na Robinson, lakini pale alikuta mikataba miwili. Kamanda akapigwa na butwaa upi ni sahihi kati ya huu na huu mwingine, akavuta kiti akaketi, akaiperuzi harakaharaka yote miwili, ule wa pili nyuma yake uliandikwa kwa mkono maandishi yanayoonesha kuwa mkataba huo haukuwa sahihi, umerdurufishwa na kubadilishwa.
“Hii ni sababu?” akaongea kwa sauti ndogo, akaiweka pembeni ile mikataba, akavuta na faili linguine akakutana na ripoti ya vifo vya wale wachimbaji kule mgodini, nayo nakaipitia vyema ilieleza mambo mengi sana ikiwemo tatizo la mashine za hewa lililosababisha watu hao kukosa hewa safi na kufa. Akausoma kwa makini sana alipouelewa akaufunga na kuuweka pamoja na ile mikataba. Kamanda Amata alijua moja kwa moja kuwa ni mambo yale yanayohatarisha maisha ya mrembo huyu.
“Kwa nini watake kumuua?” akajiuliza.
“Lazima kuna linguine ambalo nitalijua tu,” akajijibu.
Akatazama huku na kule akaona kuna mkoba, akaunyayua na kutoa vilivyomo akaiweka ile mikataba na ile ripoti ya vifo, akauvaa mgongoni mwake, koti lake la suti akalipachika kwenye kiti cha ndani ya ofisi hiyo, akauvua mkanda wa kushikia bastola na kuutia ndani ya begi, bastola yake alkadhalika.
Akaandika memo ndogo na kuiacha mezani kisha akaondoka zake kwa njia ileile aliyoingilia na kumwona Yule mlinzi akiwa palepale, akatoka na kupotea.
Moja kwa moja alifika uwanja wa ndege na kuondoka kwa ndege ya kukodi kurudi Johanesburg.
HOTELI YA MICHELANGELO – JOHANESBURG
DON ANGELO alikuwa akizunguka zunguka ndani ya sebule yake akiwa hajui nini la kufanya, alipata pigo ambalo hakuwahi kulipata. Vijana wake waliokuwa hapo na viongozi wengine wa taasisi yake walikuwa kimya kabisa, wote wakiwa katika sare yao ya suti nyeusi na kofia za pama. Ni mchana huo tu walikuwa wamepoteza vijana watano kwa mpigo akiwemo muaaji mwenye taaluma hiyo aliyekuja kutoka Cape Town, aliaminiwa kwa kazi kama hizo lakini safari hii aligonga ukuta.
“Nani anayeitikisa ngome yangu, ngome ya chuma?” alipiga kelele, na wengine walibaki kimya.
“Nauliza serikalini, eti hawajui! Wanatufanya sisi vikaragosi? Katoka wapi huyu shetani mweusi anayetafuna nafsi yangu huku namwona?” aliendelea kupiga kelele na hakuna aliyejibu, kila mmoja alikuwa kwenye mawazo mazito.
“Na sasa ametoweka Durban, ni mjanja kiasi gani cha kutushinda sisi, sisi, sisi?” aliongea kwa msisitizo huku bado akitembea tembea, akainua mvinyo wake na kupiga funda moja kubwa la nguvu, akabeua.
“Kaenda wapi? Cape Town? Au kakimbilia Mozambique? Au wapi, eti ni Mtanzania, Tanzania ina ina mtu hatari nana hii? Lazima serikali iniambie ukweli imemkodi wapi mtu huyu anayetaka kuharibu mipango ya wanadamu,” akajitupa kochini.
“Zebel,” akaita, “Sikiliza, nina uchungu sana mpaka sasa vijana wangu kumi wamekufa kwa mkono wake, nahisi huu si mkono wa kawaida, ni mkono wa jasusi, jasusi linalojua kazi yake, na jasusi lazima apambane na jasusi. Zebel, namtaka huyo mtu hapa awe amekufa au maiti, nenda, tumi kila unachokitaka, na Yule mwanamke kama hajafa nataka amaliziwe,” akamaliza na Zebel akaondoka akiwaacha wale madigala wakibaki na boss wao mkuu Don Angelo kulijadili hilo.
§§§§§
KAMANDA AMATA alipofika Johanesburg, moja kwa moja aliiendea gari yake na kuingia ndani. Mara hii gari yake ilikuwa ya kijani. Kwa jinsi ilivyotengenezwa iliweza kujibadili rangi kila inapopigwa na jua kali. Akatoa yale makabrasha na kuyahifadhi kwenye box maalumu lenye madini yanayozuyia kilicho ndani kutoathirika kwa moto. Akakipachika chini ya siti ya dereva ambako ndiko kinakoishi daima. Akawasha simu yake ya ndani ya gari na kukuta missed call toka TSA makao makuu. Akaipiga tena kuiweka sikioni.
“Madam S” akaita.
“Yeah my son, nipe habari maana upo kimya sana,” akamwambia.
“Kazi inaendelea, na inakaribia ukingoni niko njiani kumbaini masterplan wa kila kitu, mpaka sasa nina majina mawili mkononi sasa nataka kuhakikisha nani ndiye hasa mkuu wa kitengo,” akajibu.
“All the best,” simu ikakasika. ‘Madam S, daima hupenda kujua kila kinachoendelea, mwanamke shupavu anayejali watu wa idara yake,’ akawaza na kutabasamu. Alipoitazama saa yake ilikuwa tayari saa kumi na mbili jioni. Akaiondoa gari yake taratibu na kuliacha eneo hilo.
Saa tatu usiku ilimkuta katika mgahawa wa kienyeji huko Soweto akipata chakula cha kawaida tu, aliepuka kubaki mjini kwa kuhofia kugundulika kurudi kwake kwa maana alikuwa na uhakika kuwa hakuna anayejua kama amerudi nayupo hapo Joh’burg.
Usiku ulipomtosha alijipanga kuingia kazini, sasa ni kuikabili nyumba ya Zebel na Zebel mwenyewe, alijua wazi kuwa kutoka kwake ataweza kujua A na B kwani ndilo aliloachiwa na marehemu Jesca katika kile kijikaratasi. Akawasha gari na kuondoka zake.
MTAA WA SPRINGBOCK
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
KAMANDA AMATA aliendesha gari yake taratibu akitafuta nyumba namba 320U kama alivyoelekezwa, haikuchukua muda kuiona, akaegesha gari mbali kidogo na kuteremka. Akatumia miguu kuja katika nyumba hiyo huku akihakikisha bastola yake ipo sawa, alipolifikia geti akakuta limefungwa, akatumia funguo zake za siri na kulifungua, akaingia ndani, moja kwa moja aliingia katika jumba hilo, hakukuta mtu, alipita hapa na pale akapekua huku na kule. Katika chumba cha kulala ndipo alipokuta kile anachokitaka, taarifa halisi ya vifo vile vya watu kumi na tano kule mgodini, iliyoandikwa na Dokta Nkosizulu, akaichukua na kutoka nayo mpaka mahali Fulani mlemle ndani ya lile jumba, akajua wazi kuwa kama mtu huyo atarudi, basi lazima apite hapo.
Akaketi kitini pembezoni tu mwa mlango, huku akitumia tochi yake ndogo kumulika alikuwa akiendelea kuisoma ile taarifa. Taarifa ile ya Dokta Nkosizulu ilieleza bila kificho kuwa watu wale wamekufa kwa kuvuta hewa ya sumu ya Carbon Monoxide, kisha ilieleza uchunguzi wote jinsi ulivyofanyika ikiwa ni pamoja na ubongo wa wahanga ambao ulionekana sehemu Fulani Fulani kuwa na rangi nyekundu, hili nalo ni tokeo mojawapo la mtu anayevuta hewa hiyo kwa wingi. Amata akatikisa kichwa na kujihisi chozi likitaka kumdondoka, alijawa na huruma sana kwa vifo vya hawa jamaa na vile alivyovichunguza vya watatu wengine, na lililomshangaza ni kuwa kwa nini wafe Waafrika.
‘Ushahidi wa mwisho nitaupata kwa Lereti, sasa bado hatua moja kisha utekelezaji wa kazi,’ akawaza na kucheka mwenyewe. ‘Yaani hapa kazi bado haijaanza, bado kabisaaaaaa,’ akiwa kazama kwenye mawazo hayo, akasikia mngurumo wa gari nje ikisimama, akainua bastola yake na kuiweka tayari mkononi mwake, lakini aliendelea kuketi palepale.
“Yaani huyu jamaa anatufanya sisi mabwege,” alisikika mwanaume akiongea kwa lugha ya kiingereza.
“Tutampata tu, atakufa kifo kibaya sana, naapa,” mwingine akadakia. Kwa kusikiliza michakacho ya viatu alijua watu hao wako watatu, ulikuwa mtihani kwani hakujua nani atakuwa ndiyo Zebel, lakini alitumia mbinu ya kiintelijensia kuwa watu wakiwa wengi atayefungua mlango na kuingi kwanza ndiye mwenye nyumba au mwenyeji kwa asilimia tisini. Hivyo akapanga na kupangua kichwani mwake akajua la kufanya, ‘Sina mda wa kupoteza’ akawaza.
“Lazima afe usiku huu!” sauti nzito ya mtu mwingine ilisikika, ‘Utakufa wewe kwanza, sekunde kumi zijazo,’ akajibu kwa kuwaza.
Mlango ukafunguliwa, na mtu wa kwanza akaingia akielekea kwenye ile sebule kubwa akifuatiwa na wawili nyuma yake….
KAMANDA AMATA kutoka pale alipoketi alimwangalia Zebel akiingia na kufuatiwa na wale vijana wawili, hakuwasemesha lolote. Aliwaona wale jamaa walivyojazia miili yao kimazoezi ijapokuwa hawakumfikia bado Zebel Pinch aliyeonekana kwenda heani na kujaa vizuri sana, kwa mtazamo wa kijasusi alioutumia Amata aligundua kuwa Zebel ni mtu hatari ndio maana hata Don Angelo aliamua kumuweka juu ya wengine. Alipoiendea swichi ya taa na kutaka kuiwasha; Kamanda Amata akawasha kupitia swichi iliyo nyuma ya mlango huo. Zebel alipoona taa inawaka ilhali yeye mwenyewe hajawasha, kabla hajaangalia upande ule wa mlango alijirusha kwa ustadi na kutua nyuma ya ukuta mfupi uliuotenganisha sebule na ile sehemu ya kulia chakula.
Wale vijana wawili walishindwa kumpotea Kamanda kwani walipotaka kuleta makeke tu, bastola ya Amata ilifanya kazi madhubuti kabisa na ikawatoa uhai kila mmoja wa sekunde yake, wakajibwaga chini na kuiacha meza nzuri ya kioo ikipasuka vipande vipande.
“Zebel Pinch! Inuka utazamane uso kwa uso na mkono uliomuua Tracy Tasha na wewe utaingia kwenye orodha ya mkono huo,” Kamanda alimwambia Zebel huku akiunguka kwa ufunsi kabisa ile sebule.
“Amata Ric, umejiingiza kwenye mchezo mzito usiouweza, kama uliingia kwenye nyumba hii kwa miguu yako utatoka kwa miguu yaw engine,” Zebel akajibu.
“Hujiulizi nimefikaje nyumbani kwako? Je unafikiri ningeshindwa kukuaa kwa bunduki yangu pindi tu ulipoingia? Sikutaka kufanya hivyo kwani nina mazungumzo na wewe kwanza kabla ya kifo chako,” Kamanda akatamba.
“Ha ha ha ha usinifanye mt0to kabisa, ujanja huo niliufanya zamani sana, kama una mazungumzo na mimi kwa nini hukunitafuta mchana kweupe?” Zebel akacheka na kuuliza.
“Mchana nilikuwa na kazi ya kuwafuta duniani wale vibaraka wako uliowatuma Durban wakamuue Lereti, wamemkosa na mkono wangu umewashukia wao,” kamanda akatonesha kidonda. Maneno hayo yalimuumiza sana Zebel, alitamani atoke pale alipojificha na kumchanachana vipande. Wakati yeye akili yake imetibuliwa na maneno hayo ya Amata, naye akatafuta mbinu ya kumvuruga akili ili amuwahi kimapigano; akachomoa simu yake na kupiga kisha akiweka loud spika.
“Yeah yupo hapa, fanyeni haraka mkichelewa mtakuta nimekwishamsambaratisha,” akaktya simu.
“Haya jiandae sasa leo tunakunywa damu yako,” Zebel akajibu, wakati huo Kamanda alikuwa kahamanika akajua akichelewesha mchezo ataumbuka kwani alishawajua hao jamaa kuwa kuua kwao ni moja ya misingi ya dini kisha wanakunywa damu yako. Alijirusha sawia kumfikia Zebel lakini kabla hajatua, alipigwa ngumi moja nzito katika uvungu wa paja, haikufika kwenye korodani lakini maumivu yake yalimfanya aiache bastola ikianguka chini paeke yake.
“Kumbe mtu mwenyewe laini namna hii, inaonekana unaua kwa kuvizia,” Zebel akazungumza huku akiinuka kutoka pale alipoketi na kumkimbilia Amata pale chini, kabvla hajafika Amata alijizungusha mtindo wa helkopta, mguu wake mmoja ulipita chini mtambaa panya na ule wa pili ulikuja kimo cha mbuzi huku mikono yake kaiweka chini kwenye sakafu kwa mtindo usiolezeka.
Zebel alililona lile pigo la Amata, pigo la ubunifu, akaruka kwa miguu yake hewani mguu wa Amata uliopita mtambaa panya ukamkosa lakini ule uliopita kimo cha mbuzi haukukosea hesabu, ulimpata na kumbwaga chini kama mzigo lakini Zebel alijitahidi asianguke kizembe namna hiyo, aliruka sarakasi na kushangaa Amata yuko hewani na kutandikwa teke moja kali lililompeleka chini na mguu mwingine ukatua sawia kwenye koo kwa uzito mkubwa. Kamanda Amata akajiviringa kama umbali wa mita moja na kuchomo kisu kisha akachoma katika nyama ya paja la Zebel, kikazama, akakitembeza kwa nguvu na kuchana nyama kama sentimita tatu kuja gotini. Zebel alipiga yowe kali la maumivu na kujipinda, akampiga kichwa kizito Amata kilichompepesua na kumtupa chini upande wa pili.
Zebel aliinuka na kukichomoa kile kisu, hakujali maumivu lakini kwa jinsi alivhokunja sura, utajua tu alikuwa na maumivu makali.
“Aaaaaaiiiiggghhhh!!! Bastard!” alipiga ukulele wa hasira na uchungu huku akimwendea Amata. Kamanda akatazama huku na kule akaivuta meza moja ndogo ya kioo kwa mguu yake na kuisukuma kumwelekea Zebel, akaruka ikampita chini, alipotua akajikuta anashindwa kusimama akaanguka chini, nukta hiyo hiyo Amata akaiwahi bastola yake na kumnyoshea.
“Tulia fala wewe! Haya nambie nani bosi wako zaidi ya Don Angelo?” akamwuliza huku domo la bastola likiwa limemtazama Zebel.
“Aaaaiiighhh! I will kile you bastard,” (nitakuua mwanaharamu), ZEbel aligugumia huku damu zikivuja pajani mwake.
“Kabla hujaniua, utakuwa ushakufa wewe, niambie nani boss wako zaidi ya Don?” kamanda aliongea kwa ukali.
“Nahesabu mpaka tano, nakuua, Moja…!”
“Never, I cannot tell you…” (Kamwe siwezi kukwambia)
“Ok, kumbe kuna mwingine zaidi ya Don Angelo, haya nitajie ni nani? Mbili…”
“Son of Bitch, I swear I will break your neck…” (Mtoto wa Malaya, naapa nitakuvunja shingo yako)
“Tatu! Kifo chako kimekaribia,” akamwambia huku akikanyaga kwa nguvu lile jeraha, maumivu makali yalimpenya Zebel.
“Ok, ok, ok pal, set me free, I will tell you everything,” (sawa, sawa, sawa rafiki, nitakueleza kila kitu)CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kamanda Amata akatikisa kichwa juu chini, akalegeza mguu kwenye lile jeraha, Zebel akatumia nguvu zake zote kujigeuza na kuipiga bastola ya Amata, ikamtoka mkononi, maumivu makali yalipenya kwe nye mifupa ya mkono wa Amata. Alipotahayari, alimwona Zebel akimjia kama mbogo aliyejeruhiwa. Kamanda akaruka hewani na kutawanya miguu yake, mateke mawili ya mfuatano yalimpeleka Zebel kwenye meza nayo ikafunjika vipande viwili. Zebel alinyanyuka na kuchukua mguu wa meza tayari kwa kumshambulia Kamanda Amata. Amata aliinua alikwepa na kumsindikiza kwa kipepsi maridadi cha uti mwa mgongo kisha akachomo kisu kiingine kidogo kwenye mkanda wa suruali yake na kumshindilia kichwani. Zebel alijibwaga chini kama mzigo na kutokwa na damu nzito.
Kamanda akainuka haraka na kumpekua pekua hapa na pale akakuta flash moja ndogo, sksichuyku ns kuitis mfukoni mwake, akachukua funguo na kuuendea mlango ulioonekana wa ofisi kwa jinsi ulivyo. Akacheza nao na kuufungua, hakupata tabu, juu tu ya meza aliliona faili analolihitaji. Akalinyakua bila kuuliza, akaiendea kompyuta kubwa ya mezani, akainua ile system unity, akafyatua loki zake na kung’oa hard disk. Alipohakikisha hivyo anavyo akaelekea jikoni na kufungua mtungi wa gesi kisha akaiacha imwagike kwa kasi. Wakati huo alisikia gari zikisimama huko nje, akajua wameshafika kusaidia wenzao. Hakupenda waingie, alichukua kiberiti cha gesi na kukiwasha kisha akakitupia humo na ile nyumba ikalipuka mlipuko mkubwa, akatoweka eneo lile.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment