Simulizi : Born To Die
Sehemu Ya Tatu (3)
“Hell no. Please Mbucha, don’t do that. (Hii Hapana. Tafadhali Mbucha, usifanye hivyo).” Mzee Muchakila, Baba wa Bonito alikuwa anaomboleza lakini tayari amri ilishatolewa.
Bila mchecheto, yule mwanajeshi alikoki SMG yake na kufyatua risasi ambazo hazikufahamika idadi yake kwa wakati ule. Zote ziliingia tumboni na kifuani kwa mama yule.
Bonito alitazama macho ya mama yake na aliyaona yakiwa yamemkodolea bila kutingishika. Hapo kama ni hasira, ndipo zilipomzidi kijana yule.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kitendo cha kuonadamu zikimtiiririka mama yake, kikamfanya apagawe kwa hasira lakini akishindwa cha kufanya zaidi ya kuendelea kusimama pale kwenye kidirisha kidogo ambacho kilikuwa kwa ajili ya kupitisha chakula kwenda sebule kubwa.
Baba yake alikuwa analia kama mtoto mdogo na kitendo bila kuchelewa, Mbucha aliamuru tena yule dada wa Bonito naye amaliziwe. Amri ikapita na kutimizwa.
“Haya sasa. Tumebaki mimi na wewe Muchakila. Kazi yako imeiponza familia yako. Tulikuonya muda mrefu uache uchochezi wa mgomo wa madktari, hukusikia hata kidogo. Look, now,” Mbucha aliongea huku akimuoneshea zile maiti za familia yake.
Mzee Muchakila alikuwa ni wakulia kwa maumivu sana yaliyokuwa yanazidi kila nukta ya sekunde.
“Niue na mimi tu.” Ndicho Muchakila alichokijibu.
“Ni lazima ufe Bro, lazima ufate uchafu wako huu.” Mbucha aliongea huku akiweka utani kidogo kwa kumsugua Mzee Muchakila kipara chake cha fedha.
“I mean, now. (Namaanisha sasa)” Mzee Muchakila aliongea safari hii bila kutoa zile sauti za kilio wala kwikwi ndani yake.
Mbucha akamwangalia Muchakila kwa macho makali na ya kuogofya kisha akamwita mwanajeshi mmoja ambaye alinong’ona naye kitu na yule mwanajeshi akatoka nje.
Aliporudi alikuwa kakamata ‘briefcase’ moja ya rangi nyeusi na kisha akamkabidhi Mbucha.
“You want to die, aah (Unataka kufa, aah)” Mbucha alimwambia Muchakila kama anataka kufa kutokana na ile kauli yake.
Wakati huo Bonito alikuwa anazidi kuangalia ile filamu bila kuonekana na wale wavamizi.
“I was born to die by the way. (Nimezaliwa kufa isitoshe)” Mzee Muchakila aliongea kwa jeuri na kumfanya Mbucha atoe tabasamu la kijinga na kufungua ule mkoba wake ambapo alitoa ‘groves’ na kuzivaa mikononi mwake.
Kisha akatoa kitu kama ‘praizi’, lakini chenyewe hutumika sana hospitalini kung’olea meno.
Akawapa ishara vibara wake kuwa wamkamate. Nao wakatii kwa kumkamata na kuanza kumlazimisha atanue mdomo lakini Mzee Muchakila alikuwa hafanyi hivyo hadi pale alipopigwa ngumi kadhaa za tumbo na nyingine shavuni, ndipo alipotulia kwa kuwa alinyong’onyezwa sana na mapigo yale.
Mbucha alisogea mbele yake huku wanajeshi wanne wakiwa wamemdhibiti vilivyo na kumtanua mdomo wake.
Hapo Mbucha aliingiza ile ‘praizi’ mdomoni mwa Muchakila na kuelekeza chuma kile kwenye gegu la Mzee Muchakila.
Akalibana jino lile kwa ile ‘praizi’ kisha akaanza kulazimisha kulinyofoa kwa kulizungusha zungusha kulia na kushoto kwa nguvu na sura yake ilionekana wazi kuwa alikuwa anatumia nguvu kufanya vile.
Mzee Muchakila alikuwa analia lakini sauti yake ilikuwa kama analia wakati kajazwa magodoro mdomoni.
Ni damu pekee ndizo zilikuwa zinatapakaa wakati tendo lile limemalizika. Mdomo wa Baba wa Bonito ulikuwa unamwagika damu kama maporoko fulani ya maji.
“Mtanueni tena.” Mbucha aliwaambia wale wanajeshi nao wakatii.
Kisha Mbucha alianza kuhangaika kutoa jino la pili kwa upande mwingine.
Ni wakati huo ndipo Mzee Muchakila alizidi kupagawa kwa maumivu hasa baada ya kutolewa lile jino la pili na yule mtu aliyeitwa Mbucha.
“It’s just a begining Doc. (Ni mwanzo tu Daktari)” Mbucha alimwambia hivyo Mzee Muchakila huku kaupeleka uso wake karibu kabisa na uso wa Mzee yule, daktari tegemezi katika nchi ya Kameruni.
Mzee Muchakila alitabasamu lakini badala litokee tabasamu lake la kawaida, likatokea tabasamu lililoambatana na damu nyingi mdomoni kwake.
“You can kill someone, but you can’t kill the truth. (Utamuua mtu fulani, lakini huwezi kuu-ua ukweli)” Mzee Muchakila aliongea na kutema mate ya damu pembeni.
“What a truth. Eee. (Ukweli gani. Eee)” Mbucha aliongea huku akiinyanyua shingo ya Mzee Muchakila akitaka aelezewe ni ukweli gani ambao Mzee Muchakila anausemea.
“Ukweli upi wewe mshenzi? Ukweli wa nyie kugomea kufanya kazi na kuacha wagonjwa wakiteseka vitandani kisa fedha? Fedha zitakupeleka wapi wewe mwanaume? Yale ni makaratasi tu, it’s just a paper. Lakini ni wangapi wanakufa pale kitandani kwa kukosa huduma zenu? Ni wangapi? Embu jiulize we mwenyewe Muchakila. Don’t you feel a shame? How damn are you?” Mbucha aliongea kwa hasira na kwa sauti ya juu kiasi kwamba hata wale wanajeshi walianza kupata mashaka hasa kutokana na mvua kule nje kuanza kupungua, hivyo sauti ingefika kwa majirani.
“Umeona hilo tu la kugoma. Humuoni chanzo cha sisi kugoma? Kule Bungeni mnachukua kiasi gani kwa kukaa na kusikiliza tu. Na mkipewa nafasi ya kuongea mnatukanana tu wenyewe. Hilo huoni? Mshahara wenu ni zaidi ya hawa vibaraka waliokuja na wewe. Wanafurahia kumbaka mke wangu na kuimaliza familia yangu kwa risasi zao. Nyie ni wajinga, na hamtoelewa kamwe kama hamuwezi kufi........”Mzee Muchakila hakumaliza kauli yake, mwanajeshi mmoja alimfata na kumpiga wkwa kitako cha bastola.
Mzee Muchakila alitabasamu tena, kisha akamgeukia Mbucha na kuendeleza kile alikianza kukiongea.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Marupurupu yenu ya siku moja, mnaona kama ni ya kunywea bia pekee. Lakini kuna walimu wanasubiria kiasi hicho kwa mwezi mzima, na ukitoka unaishia kwenye madeni. Huoni aibu? Waziri kama wewe, huoni aibu? Eti mnaita posho, na mnashangilia kabisa muongezewe.” Mzee Muchakila alimaliza kwa msonyo mrefu na baadae alimtemea mate ya damu Mbucha.
“Big mistake. (Kosa kubwa)” Mbucha aliongea huku akifuta mate ya damu usoni pake na kisha akauendea mkoba wake uliokuwa unavifaa sijui vya aina gani. Akaufungua na kutoa kifaa kingine na chenyewe kikiwa kama ‘praizi’ lakini kwa mbele kilikuwa kina makali.
Akawapa ishara wale wanajeshi wamkamate tena na kumtanua mdomo wake. Nao walifanya hivyo huku Bonito akiwa bado anashuhudia ile filamu ya kutisha pale kwenye kidirisha kidogo.
“Huu ndio unakupa kiburi cha kuongea utumbo wake. Ngoja sasa niuondoe.” Mbucha aliongea hayo huku akiupapasa ulimi wa Mzee Muchakila kwa ile ‘praizi cutter’. Na baada kumaliza kuongea, alikata kipisi cha mbele cha ulimi wa Mzee Muchakila na kumfanya mzee yule alie kwa sauti huku akiongea maneno ambayo hayaeleweki kutokana na kukatwa kipisi cha ulimi wake.
“Tamu ee. Ongea sasa.” Mbucha alisema kwa kejeli huku akikirudisha kile kifaa kwenye mkoba wake na kisha safari hii aliibuka na kisu kidogo ambacho mara nyingi hutumika hospitali kwa ajili ya kufanyia upasuaji, mkono mwingine alikuwa anachupa ya lita tatu iliyojaa ‘spirit’ ile nyeupe.
“Natumia vifaa vya hospitali kwa sababu wewe ulishindwa kuvitumia kuokoa maisha ya wananchi wetu. Ukakalia kugoma na kuandamana. Sasa nataka kuona mwisho wako Dokta.” Mbucha aliongea tena huku akijongea pale alikuwa amepigishwa magoti Mzee Muchakila.
“Mtoeni shati lake. Limelowa sana damu.” Mbucha aliwaamuru vibaraka wake, nao wakatii haraka kwa kutoa shati lile lililokuwa limelowa damu kutoka mdomoni mwa Muchakila.
Mbucha akampa chupa ya ‘spirit’ mwanajeshi mmoja, kisha akasogea karibu zaidi kwa Muchakila huku akiwa kama anapima makali ya kile kisu kidogo katika kidole gumba chake.
Muchakila alikuwa anatetemeka hasa kwa kuwa anajua makali ya kile kisu na maumivu yake pia. Ni zaidi ya wembe kwa jinsi kile kisu kinavyochana.
Mbucha akapitisha kwa nguvu kisu kile kwenye kifua cha Muchakila na kisha akakirudisha tena kwa kasi ile na kisu kile kikatengeneza alama kubwa ya ‘X’ kifuani kwa Muchakila. Na wakati Muchakila akiwa analia kwa maumivu, yule mwanajeshi mwingine alimpa chupa ya spirit bosi wake, naye Mbucha bila huruma wala uoga, alimwagia kiasi kikubwa cha spirit ile katika kidonda cha Muchakila.
Muchakila akawa mtu wa kulia huku akijaribu kutukana lakini asieleweke ni nini ambacho anakiongea kutokana na kipisi cha ulimi wake kukatwa.
Taratibu nguvu zilianza kumwishia Muchakila lakini kabla hajapoteza fahamu kabisa, Mbucha alirudi tena kwenye mkoba wake na kisha akaibua kitu kinginea anbacho mara nyingi huweza kubana kitu kwa nguvu bila kukiachia hata uvute vipi.
“Nyoosheni mkono wake.” Aliwaambia wale vibaraka nao kama kawaidia wakatii.
Mbucha akabana kucha ya Muchakila kwa kile kidude, na kwa nguvu nyingi akavuta kucha ile nayo ikang’oka kitu kilichofanya Mzee Muchakila kupoteza fahamu palepale.
Hata baada ya kupoteza fahamu, Bonito aliendelea kushuhudia mateso makali aliyokuwa anaendelea kuyapata baba yake. Aling’olewa kucha zote za mikono yake, na kisha zikafuata kucha za miguuni na kila tendo la kung’olewa kucha, lilienda sambamba na kumwagiwa Spirit.
Hatimaye zoezi liliisha na yule Mbucha kiongozi wao aliwaamuru wamuache Muchakila vilevile ila wao waondoke haraka kwani mvua ilikuwa imeanza kukatika hivyo kama Muchakila akipata fahamu muda ule, anaweza kupiga kelele zitakazowafikia majirani. Na si hivyo tu, kama majirani wanaowahi kuamka wakiona magari yao, basi itakuwa rahisi kwao kugundulika kuwa ndio waliofanya maovu yale.
Wakafanya hima kwa kukusanya chao na kuanza kuondoka huku wakiwa hawajui kama kuna mtoto ambaye ni Bonito alikuwa anatazama kile ambacho kimetokea toka mwanzo hadi mwisho.
Baada ya kuondoka wale wavamizi waliomvamia Mzee Muchakila, Bonito alipiga hatua za woga kwenda hadi pale ilipolala miili ya familia yake kipenzi. Alimwangalia baba yake kwa muda pale alipokuwa kalala, kisha akamwangalia mama yake ambaye alikuwa kalala juu ya damu zake na vidonda vya kutosha kwa sababu ya risasi.
Macho yakaenda hadi kwenye miili ya dada zake ambao walikuwa wamepigwa risasi za kichwa kila mmoja. Hakika yule mtoto mdogo alikuwa anashuhudia mambo ya kutisha na kuogofya. Hata mtu mzima hatoweza kuvumilia kuangalia ile picha iliyokuwa inatokea muda ule.
*****
“Peter. Miili ya wazazi pamoja ndugu zangu wakati naitazama, nilihisi kama natazama filamu. Lakini amini usiamini, ndiyo imenipa ujasiri leo hii naweza kupigana bila kuchoka na naweza kummaliza kila ambaye atakatiza mbele yangu kwa baya.
Sina chembe ya huruma katika nafsi na moyo wangu. Sina tofauti na simba dume mwenye njaa. Natafuna hata watoto pale njaa inaponikaba. Napigana kwa kuwa nina njaa ya haki, nina njaa ya kuona nchi yangu na bara zima la Afrika inaondokana na unyanyasaji na ubaguzi uliojikita baina yetu, nina njaa kubwa sana Peter.
Njaa ambayo kushiba kwake ni kuona wazazi wangu wanajivunia kuzaa mtoto kama mimi. Japo hawanioni lakini wanafurahia mimi kuwa hivi. Na naamini walifurahi zaidi pale nilipokiondoa kichwa cha yule mpumbavu aliyejivika madaraka na kuisukumia familia yangu kwenye mchanga.” Kamanda Bonito Muchakila alikuwa anamwambia Peter huku akiwa na hisia kali toka moyoni mwake.
“Peter. Najua utakuwa na maswali mengi sana kwa jinsi gani niliweza kuishi hadi hivi sasa naendelea kuvuta pumzi hii hapa Senegal na si Kameruni.” Kamanda Bonito aliongea kwa sauti ya upole baada ya yale maneno makali kumtoka kinywani mwake. Akaendelea,
“Nilipoona wazazi wangu wapo pale chini na damu zikiwa zimetapakaa nyumba nzima, ndipo nilipata akili mpya, akili ambayo ilikuwa kama imeshikwa kwa kile kitendo kilichotokea. Akili ambayo ilikuwa ni lazima ikae kimya wakati lile tendo baya likiwatokea familia yangu.
Nilipiga ukelele mkubwa na mkali ambao uliashiria hatari pale napoishi. Hata pale nilipoona hakuna jirani anayekuja, niliendelea kupiga kelele hizo huku nikiomba msaada kwa sauti yangu ya kitoto.” Bonito alikaa kimya na kuinuka pale kitini na kwenda kwenye dirisha la ofisini mle na kuanza kuangaza macho yake nje akimpa mgongo Peter aliyekuwa kimya akisikiliza ile hadithi ya kumsisimua mtu hata nywele.
“Majirani walipokuja kuangalia kuna nini hadi nipige kelele zote zile, hakuna hata mmoja aliyethubutu kuangalia maiti za wazazi wangu. Wote walipiga kelele na kukimbia kama wehu baada ya kuona damu zikiwa zimetanda sebuleni kwetu.
Hakuna aliyeweza kuangalia ile miili mara mbili na bila kusema chochote cha kusikitisha na hakuna aliyeweza kuangalia mara mbili bila kutoa machozi. Na zaidi, hakuna aliyeweza kuangalia zaidi ya mara mbili. Yaani ukiangalia mara moja na ya pili, ndio huangalii tena. Lakini mimi nilikuwa katikati ya maiili ile ambayo mingine ilikuwa ni maiti na nyingine ilikuwa imezimia lakini haitamaniki ukiiangalia.
Ni majasiri pekee, hasa wa kiume ndio waliweza kunitoa pale katikati ya ile miili na kunitoa nje lakini nao hawakuangalia ile miili zaidi ya mara mbili.
Polisi wakiongozana na msalaba mwekundu, walikuja mapema baada ya kupata taarifa zile na tendo lililofata ni kupima mapigo ya moyo ya mama yangu ambaya alicharazwa risasi zisizo na idadi kwenye tumbo lake. Huyo alishakuwa maiti tangu muda mrefu.
Baba yangu iligundulika kuwa mapigo yake ya moyo yanaendelea kuchukua nafasi taratibu katika mwili wake, ila naye alikufa baada ya siku mbili za kukaa chumba cha wagonjwa mahututi. Nikawa yatima rasmi.” Bonito aligeuka nyuma na bila kutegemea kutokana na ujasiri alionao Kamanda yule, alionekana akitoa machozi mbele ya Peter.
Bonito akafuta machozi yale na kisha akaikunja mikono yake kifuani na kuegemea ukuta wa ofisi ile. Akaendelea kumsimulia Peter.
“Taarifa zikatapakaa juu ya kifo cha familia yangu na mimi nikawekwa chini ya uangalizi wa Polisi huku nikiwa nahojiwa watu walifanya yale mauaji. Lakini sikuthubutu kuwataja wala kusema chochote na ndiyo iliyonisaidia kwani hata mle ndani ya Polisi kulikuwa na watu wanaofanya kazi ya Mbucha, yaani vibaraka wa Mbucha.
Waliniachia na mimi nikaenda kuishi kwa Baba yangu mdogo ambaye naye alikuwa kama chui aliyemuona swala baada ya mimi kwenda pale.
Manyanyaso yakawa manyanyaso kwangu. Kila kukicha ni kipigo cha mbwa mwizi. Kisa sikikufahamu mapema, lakini baadae nilikuja kugundua alifanya yale kwa kuwa alikuwa hawezi kuzalisha. Kisa cha kipumbavu kabisa.
Mipango ya MUNGU kuiingiza kwenye maisha yako ni kosa kubwa sana. Kosa hilo kwa hapa jeshini kwetu unapigwa risasi hadharani. Sasa yule baba yangu mdogo, akaweka kisa juu yangu kwa sababu ya mipango ya MUNGU. Nikaona isiwe tatizo, na umri wangu uleule, nikatoroka pale nyumbani kwa Baba Mdogo na kuingia mitaani.” Peter alitaka kuongea kitu lakini alishindwa cha kuongea na badala yake alibaki mdomo wazi baada ya kusikia mtoto mwenye umri wa miaka minne anaingia mtaani kusaka maisha yake binafsi na si kunyanyaswa.
“Its Crazy. Right?” Bonito alimuuliza Peter swali hilo kama kile lichofanya ni ukichaa.
“Real crazy. But made me greater. (Ukichaa kweli. Lakini imenifanya niwe imara)” Hakusubiri jibu la Peter, badala yake alijijibu mwenyewe.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akatoka pale ukutani alipoegamia na kuanza kuzunguka mle ofisini huku akizidi kumpa mkasa wake Peter.
“Huko mitaani nikawa ombaomba kama watoto wengine wa mitaani. Kuna muda ulifika nchi ikaingia katika machafuko ya kisiasa. Wakati huo ndio nilikuwa na miaka saba.
Iilikuwa ni hatari kupindukia. Unaweza ukajikuta upo katikati halafu hawa waliokuweka katikati wanarushiana risasi wao kwa wao. Vifo vilikuwa ni kila kukicha kwa pale nilipokuwa nimepafanya sehemu ya kujitafutia chakula na malazi.
Na uzuri niliingia mtaani nikiwa mdogo, hadi nafikisha umri ule, kulikuwa hakuna mtoto au hata mtu mzima aliyekuwa anaweza kunichezea. Nilikuwa katili kuliko katili mwenyewe.
Lakini sababu ya mimi kuwa hivyo, ilikuwa ni damu za wazazi wangu.
Damu zao zilikuwa zikichemka kichwani mwangu kila nilipochokozwa. Nilikuwa sioni shida kukuchana na wembe, au kukuchoma kisu au tendo lolote ambalo ni gumu kwa mtoto wa miaka saba na kushuka kulifanya.
Niliogopwa kama ukoma.” Bonito aliacha kuzunguka mle ndani na kurudi kwenye kiti chake na kukaa huku mikono yake ikiiweka mezani.
“Peter,” Alimuita Pater kwa sauti yake ngumu na nzito.
Peter akamwangalia usoni bila kusema neno.
“Mbucha aliyewaua wazazi wangu aliteuliwa na kuwa Waziri Mkuu wa Kameruni.” Hapo Bonito alirudisha mgongo wake nyuma na kuegemea kiti alichokuwa amekikalia.
“Wajua nilikuwaje baada ya kusikia taarifa hizo. Sidhani hata mamba anaweza kuwa vile pale ashikwapo na njaa. Na sidhani kama kuna mtu anaweza kuwa vile hasa kutokana na umri wangu. Niliapa kumtafuta na kummaliza yule mpumbavu na nilifanikiwa.”
“Zile vita za wenyewe kwa wenyewe pale nchini, zikawa zinasababisha silaha kuzagaa zagaa tu mtaani. Na mimi nikajipatia yangu kwa ajili ya kufanya nachojua. Nikawa jambazi mtoto. Napora mali kwa kutumia silaha. Na hali hiyo ikawa inanipa chakula kizuri kuliko mwanzo.
Hapo ndipo nikaamua kuanzisha kikundi changu cha uporaji ambacho kilikuwa kina watoto kama mimi na wengine walinizidi kidogo, lakini walitii nilichokuwa nawaagiza. Tukawa vijambazi vya hatari sana pale nchini.
Kuteka magari na unyang’anyi ikawa ndio jadi yetu. Wale wanajeshi kwenye mapambano, walikuwa wakifa sisi tunaokota silaha na kuzihiidfadhi kitu kilichosababisha tuwe na karakana kubwa ya kuweka silaha. Silaha ambazo baadae zilianza kutafutwa na watu kwa ajili ya kupigania.” Bonito alizidi kutiririka simulizi ya maisha aliyoyapitia katika dunia hii.
“Kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Japo kikundi chetu chenye watoto pekee kilikuwa kikubwa na kinajiamini kwa ulinzi, lakini siku moja serikali ya nchi ile ilivamia eneo letu ambalo tulikuwa tunaishi na kuanza kuliteketeza kwa risasi pamoja na mabomu.
Ilikuwa ni vita kubwa baina yetu na wanajeshi wa serikali. Rafiki zangu na udogo wao walikuwa wanadondoka chini kama matone ya mvua. Walikuwa wanakufa kama nyuki waliovukizwa moshi wenye sumu.
Nikiwa nimekata tamaa na nimejificha mimi na wenzangu kama watano hivi, mara tukaanza kusikia majibizano ya risasi yakitokea kwa mbali na mengine ya hawa waliotuvamia. Risasi hizo zilikuwa zinawajia hawa wanajeshi wa serikali.
Hapo na sisi ndipo tulipotoka pale tulipojificha na uzuri wale wanajeshi walikuwa wametupa migongo kwa sababu walikuwa wanapambana na wale wavamizi wapya. Hapo na sisi tukaanza kumwaga njugu zetu nyuma yao.
Dakika kadhaa, palikuwa kimya kabisa. Hakuna milio ya risasi bali magari tu. Na sisi tukajitokeza tukiwa na bunduki zetu kama wapiganaji imara.” Bonito alitoa tabasamu baada ya kunena kauli hiyo. Kisha tabasamu lake likapotea na kuendeleza simulizi ile mwanana iliyoteka kichwa cha Peter.
“Lilikuwa ni kundi la waasi wa pale Kameruni. Na baada ya sisi tuliobaki kujitokeza, alishuka kiongozi wao aliyejitambulisha kama General Zogwa Mzugwa. Huyu ni zaidi ya baba yangu, huyu ndiye alinifanya leo nimekaa hapa na kusimama napotaka.
General Zogwa alituona tu! Alitabasamu na kutufuata pale tulipo kisha akatutazama na kutuuliza maswali ambayo tuliyajibu kila mtu kwa mtazamo wake. Alitaka kutuchukua, lakini tulikataa kutokana na hali wanayoishi waasi pale nchini. Muda wowote wanavamiwa na kuteketezwa kama siafu. Heri tubaki pale lakini tuache mambo ya ujambazi. Hilo ndilo tuliona linafaa.
Lakini kuna kitu kilianza kunisukuma nitake kuongozana General Zogwa. Kisasi cha wazazi wangu na familia yangu pia. Ni vipi nitakilipa bila kumfuata yule General.
Hapo ndipo nilipomkamata General Zogwa na kumwambia nia yangu kuwa ni kutaka kumuua Waziri Mkuu wa nchi ile, Mbucha au Daniel Mbucha. General alishangaa lakini hakuwa na la kujibu kwa muda ule zaidi ya kunishika kichwa na kuniamuru nipande gari la jeshi alilokuja nalo. Na hata wale rafiki zangu walipoona kamanda wao naondoka, wakawa hawana budi zaidi ya kunifuata.”
******
Baada ya Bonito kuchukuliwa na General Zogwa, moja kwa moja alipelekwa zilipo kambi za Waasi wale wanaoenda kinyume na serikali yao kutokana na mambo yasiyowaridhisha nafsi au akili zao.
Huko Bonito akafundishwa zaidi njia za kujihami bila silaha pamoja na kufundishwa kutumia silaha mbalimbali zikiwemo bunduki kubwa na dhana za jadi.
Hadi anafikia umri wa miaka kumi na mitano, alikuwa kawiva na tayari kwa mapambano yoyote yatakayomkabiri na wakati huo wenzake alioondoka nao, wakiwa karibu naye, huku nao wakiwa mabingwa wa kutumia silaha mbalimbali kama ilivyo kwa Bonito.
Hatimaye ile siku ambayo alikuwa anaisubiri kwa hamu Bonito iliwadia. Siku ambayo alipewa ruhusa ya kwenda kummaliza Waziri Mkuu mstaafu wa nchi ile. Ni kisasi alichokuwa anakisubiri kwa miaka mingi sana. Muda ule ambao alikuwa anatimiza miaka kumi na mitano, ndipo General Zogwa akampa ruhusa ya kufanya kitu alichokuwa amekipanga kwa muda mrefu juu ya maisha ya Mbucha.
Akamvamia Mbucha akiwa na rafiki zake wa karibu, kisha akafanya kile alichokuwa kakipanga kukifanya. Hakuwa na huruma hata kidogo. Alichinja yeyote aliyekuwepo katika familia ile. Aliua hadi wajukuu wa Mbucha. Na baada ya kumaliza kazi hiyo, alikata kichwa cha Mbucha na kwenda nacho kwa General Zogwa kumuonesha mafanikio ya kazi yake. Hapo roho ikaridhika na ikawa kwatu, roho ikatakata.
*****
“Hata baada ya kumuondoa Mbucha, nilizidi kutumwa kwenda kumaliza viongozi wale waliokuwa madarakani kipindi kile. Na kiukweli niliwamaliza wengi sana wale niliokuwa naagizwa kufanya hivyo.” Bonito alizidi kukata mbuga kumuhadithia hadithi yake Peter.
“Lakini kilichokuwa na mwanzo, hakikosi kuwa na mwisho. Nilipotimiza miaka kumi na nane, kambi yetu ya waasi iligundulika na kuvamiwa na majeshi ya serikali. Huko karibu marafiki zangu wote waliteketea na kubaki mmoja ambaye naye alifariki wakati anajaribu kuniokoa mimi nisipigwe risasi.
General Zogwa kabla hajakata roho, alinielekeza pa kwenda na ndipo nilikuja hapa na kuanza maisha yangu mapya. Nilipofikisha miaka ishirini na nane, nikapewa ukamanda wa jeshi la kambi hii. Sasa nina miaka thelathini na minne, na bado nitaendelea kupigania haki za waafrika.” Alimaliza Kamanda Bonito na kumuangalia Peter aliyekuwa katulia kimya anasikiliza simulizi ile ya kusisimua na kuhuzunisha lakini iliyojaa ujasiri mwingi.
“Inasikitisha sana,“ Peter aliongea baada ya kimya kirefu. “ Lakini ushawahi kujiuliza nini chanzo cha haya yote na jinsi ya kumaliza?” Peter alimuuliza Kamanda Bonito.
“Chanzo ni serikali zetu kutoelewa mahitaji ya wananchi wake.” Bonito alijibu kiurahisi kabisa bila kitetemeshi na kukwama sauti yake. Peter alitabasamu na kutikisa kichwa chake kama mtu asikitikaye.
“Kwa nini unasikitika Peter.” Bonito alimuuliza baada ya hali ile.
“Nasikitika kwa kuwa umeangalia karibu sana. Umeangalia pekee ya ndani na si ya nje. Namaanisha umeangalia zaidi ya bara lako la Afrika na si nje ya Afrika. Kuna wachochezi wa mambo haya yanayoendelea ambao ni watu wa nje ya Afrika. Kazi yao ni kutengeneza silaha za maangamizi na kuja kuwapa nyie kwa ajili ya kupigania. Lakini lengo lao si kuwasaidia nyie mshinde vita au mpate uhuru, bali lengo lao wawatawale nyie. Embu fikiria kama utashinda vita na kuingia madarakani. Unadhani maamuzi yako ya kufanya mambo yatatoka wapi? Bila kubisha ni kwa hawa wanaowasaidia kuwapa silaha sasa hivi ambazo nyie mwaona ni kama mnasaidiwa.” Peter alimfumbua macho na ubongo Kamanda Bonito.
“Sitaruhusu madaraka yangu yaingiliwe na watu wengine.” Kamanda Bonito aliongea kwa kujiamini na kwa nguvu na hali.
“Then, hawa hawa wanaowapa silaha sasa hivi, watawapa silaha wengine ili wawapindue. Hivyo ndivyo ilivyo. Wanachochea mauaji, wanachochea mapinduzi ya damu na wanachochea kila kitu kibaya katika nchi zetu. Lakini sababu kubwa ya wao kufanya hivi ni nini? Ni maliasili zetu. Madini, wanyama na kila kitu, ndivyo wanavyovitolea macho kwa sasa.” Kamanda Bonito alikuwa kimya wakati kijana yule anatema maono yake. Peter hakuishia hapo na zaidi aliendelea.
“Siku ambayo utaingia madarakani, ni lazima watataka eneo ambalo ndio jicho ya serikali yako. Ukikataa kuwapa, wanakupiga kwa silaha zao. Na siku ambayo utasema unaenda kuongea kuhusu amani ili kumaliza mgogoro huu unaoendelea, ndio itakuwa siku yako ya mwisho. Watakupiga tu.” Alimaliza Peter.
“Nenda nje Peter.” Kamanda Bonito maneno yalimuingia na kujikuta akimtaka Peter aondoke mle ndani. Peter hakuwa na ajizi wala nini, akaondoka zake na kumuacha Kamanda yule akitafakari na kuyachambua maneno yale kwa kina huku akizidi kutanuka kwa kuangalia mbali zaidi ya yale aliyoambiwa na Peter.
**** CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Leo ndio siku niliyokuwa naisubiri kwa hamu,” Sauti ya kikakamavu ilimtoka Bonito ambaye alikuwa anatembea huku akiwa kama anakagua kikosi cha wanajeshi wake. Ilikuwa imepita wiki mbili tangu aongee na Peter. Na baada ya maongezi yale, alipata wasaha wa kukaa peke yake na kuchambua maneno ya Peter na baadae kupanga mkakati wa kuboresha kambi yake. Mkakati huo, ndio anaanza kuutimiza siku hiyo.
“Baada ya miezi sita, mtakuwa wanajeshi imara. Wanajeshi halisi wa kimapambano. Uoga na ujinga uliojijenga vichwani mwenu, vitakuwa vimetitia kwenye akili, ubongo na mbele yako. Wengine mtasema ni uonevu. Na wengine mtasema ni unyanyasaji. Na wengine mtadiriki kusema ni mateso. Lakini hayo si majibu. Bali jibu ni moja tu, haya ni mazoezi ya kujiweka imara.” Akiwa kavalia gwanda zake, na mawani nyeusi katika uso na macho yake, Kamanda Bonito alizidi kutema cheche kwa madaha na mikono yake ikiwa nyuma.
“Kuna njia moja ya kuishi hapa duniani. Nayo ni kwa kuamini kile unachokifanya. Kama ukiamini unachokifanya ni sahihi, amini kuwa hapa duniani wewe ni mshindi. Kama huna hata chembe ya kuamini ukifanyacho, ni bora uache kabisa maana utaumia na kupoteza nguvu zako bure. Kama huamini kuwa unaweza kuwa mwanajeshi shupavu kwa siku zijazo, ni bora ujiondoe mapema katika mazoezi haya. Hakuna ambaye atakugusa wala kukurudisha na kukulazimisha ufanye anachotaka yeye. “ Safari hii Bonito alisimama mbele ya jamaa mmoja mweupe na mwembamba sana, yawezekana ndiye mwambamba kuliko wote pale kwenye mstari. Akatoa mawani yake na kumsogezea yule jamaa uso wake mweusi na wenye mikunjo ya ndita kwenye paji lake.
“Do you read me boy? (Umenielewa kijana?)” Bonito alimuuliza yule jamaa kwa sauti ya kunguruma na kama ya kumtisha.
“Ye ye ye, yes sir. (Ndi, ndi, ndi, ndio mkuu)” Jamaa alijibu kwa utetemeshi na kwa sauti nyembamba akimanisha kuwa kamwelewa mkuu wake.
“Unaondoka au unabaki?” Kamanda Bonito alitupa swali lingine.
“Nabaki, sir.” Jamaa akajibu bado kwa utetemeshi vilevile. Kamanda Bonito akaanza kumuongelesha yule jamaa kwa sauti ya juu na ya kijeshi na kumfanya yule jamaa azidi kuogopa.
“Napokuuliza kama umenisoma au umenielewa yakupasa kujibu kiukakamavu kama mwanaume halisi, mwanajeshi bora na mwenye uwezo na nguvu na si kujibu kama unafanya mapenzi.” Bonito alifoka.
“Do you read me?( Umenielewa?)” Hapo sauti yake ilishuka kidogo na kuulekeza uso wake mbele ya uso wa yule jamaa.
“Yes Sir.” Jamaa akajibu kwa kikakamavu kidogo.
“Say. Yes Sir, yes.” Bonito alimuelekeza yule jamaa kwa sauti ya kikakamavu.
“Yes Sir, yes I read you.” Jamaa alionesha kuwa somo limemuingia.
“Good. (Vizuri)” Bonito alimaliza na kwenda hadi kwa Peter.
“Upo tayari kijana.” Aliulizwa Peter.
“Nipo tayari mku....” Peter alijibu lakini kabla hajamaliza akapewa zoezi hapo hapo.
“Twenty push up (Pushapu ishirini).” Peter bila kuuliza akaenda chini na kuanza kupiga ‘push up’ huku kakunja ngumi na akizihesabu mwenyewe. Alipofika ya kumi Kamanda Bonito akampa neno lingine.
“Kwa mkono mmoja.” Peter akaachia mkono mmoja na kuanza kulifanya zoezi lile la ‘push up’ kwa mkono mmoja huku anahesabu kwa nguvu hadi akamaliza zoezi lile. Akainuka na kusimama wima kama mwanajeshi imara.
“That’s how a soldier supposes to be. Do you understand me?(Hivyo ndivyo mwanajeshi anatakiwa kuwa. Mmenielewa?)”
“Yes Sir, yes.” Sauti za wanajeshi wale wapya zilijibu kwa kikakamavu. Kamanda Bonito akaanza kuongea kwa sauti ya kijeshi zaidi na zaidi kwani sasa aliamini wote wanataka kuwa wanajeshi imara, hivyo sasa akawa anawaonesha uimara hata kwenye kuongea.
“Kuanzia sasa, nyie ni wanajeshi mnaoingia kwenye mafunzo makali na magumu. Hakuna kufikiria mapenzi sasa hivi, hakuna kumfikiria mama yako. Sasa hivi unatakiwa ufikirie huko unapoenda. Kama hujamuaga mama au mpenzi wako hapo jana, hakuna nafasi hiyo tena kwa sasa. Sasa hivi ni muda wa wewe kujifunza kupigana na kujilinda.” Rai ilikuwa inatoka kwa sauti ya kikakamavu.
“Kamata begi lako. Na twende zetuuuu.” Kamanda Bonito alimaliza na kuanza kukimbia kutoka nje ya geti la kambi ile. Wale wanamafunzo wapya, nao wakashangilia kwa sauti ya juu huku wakiweka mabegi yao mgongoni na kuanza kumfata Kamanda Bonito kule alipoelekea.
Mama, watoto na wapenzi wa wanajeshi wale, walikuwa wanawaangalia watu wao wa muhimu jinsi wanavyokimbia kwa mstari na kwa hamasa. Wale waliobahatika kuwaona watu wao, waliwapungia mikono na wengine kuwapiga mabusu ya mbali.
******
Katika mazoezi yale, Peter na Vanessa nao walikuwepo kama kawaida. Walikuwa wameamua kujitoa nafsi na miili yao kwa ajili ya kuwa wanajeshi watakaopigania nchi yao na nchi wanayoishi.
Kule kambini walibaki wale wanajeshi wazoefu wakilinda kambi na kutafuta chakula pamoja na wanajeshi wapya.
Mchakamchaka ulikuwa unaendelea kwa kasi kubwa tangu walipotoka kule kambini. Hakuna aliyejua wanaenda wapi zaidi ya Bonito na baadhi ya viongozi wa kambi ile. Walikuwa wakikimbia mchakamchaka ule huku wakiimba nyimbo za kivita pamoja na za kuisifu nchi yao pendwa na bara zima la Afrika.
Ni vumbi pekee ndilo lilikuwa linachukua nafasi katika jua lile la saa saba, masaa sita tangu wanajeshi wale watoke kambini. Vumbi hilo lilitokana na kukimbia wale vijana na Kamanda wao. Vijana walikuwa katika hali ya ukakamavu na hakuna hata mmoja ambaye alikuwa akionekana kuwa analegalega licha ya kukimbia kwa mwendo mrefu.
****
Masaa mawili baadae, tayari walishafika mahala ambapo Bonito alikusudia kuwafikisha. Palikuwa ni pori tupu na penye njia nyingi huku moja pekee ndio ikionekana inapitisha magari. Haikueleweka pori hilo ni la wapi ila vijana wale walikuwa hawana muda nalo na zaidi walikaa kwenye vivuli vya miti na kupata maji pamoja na vyakula walivyokuwa wamebeba kwenye mifuko yao.
Baada ya nusu ya kumpuzika pale porini, mara walianza kusikia mingurumo ya magari kutoka kwenye il barabara ndogo lakini yenye uwezo wa kupitisha gari.
Hakuna aliyekuwa kabeba silaha kwa wale vijana wapya, hivyo wengi wao walijificha nyuma ya miti na vichaka na kuwaachia wale viongozi wao ndio wawe walinzi wao.
Gari zile zilifika pale walipokuwa wameweka makazi na kusimama. Zilikuwa ni gari za jeshi kubwa aina ya Jeep, mali iliyotengenezwa Marekani. Baada ya kusimama, alishuka mwanajeshi mmoja ambaye alionekana ndiye kiongozi wa msafara ule. Alikuwa ni mzungu, ambaye kwa kumwangalia, utamjua ni mtu wa Uingereza au Marekani. Akashuka toka kwenye Jeep ile kubwa ya kuweza kubeba wanajeshi hadi hamsini huku thelathini wakiwa wamekaa.
Mzungu yule alisimama a kuanza kuangaza huku na huko ili kuona kama yeyote. Alipoona kunaishara za kuwepo watu eneo lile, alianza kuonesha ishara fulani za mikono na hapo viongozi wa kambi ya Born To Die wakajitokeza nyuma ya miti iliyokuwa karibu na pale gari ziliposimamia.
Wakaenda kwa yule mzungu na kuongea naye kidogo, kisha Kamanda Bonito alitoa ishara ya kuwaonesha wale vijana wapya watoke kwenye sehemu walizokuwa wamejificha.
Vijana wakajitokeza na bila kuchelewa, wakapangwa mstari mmoja na yule Mzungu akaanza kuwapitia mmoja baada ya mwingine kama akaguaye gwaride. Walikuwa vijana karibu mia na hamsini hivyo ilichukua muda kiasi hadi kuwamaliza wote kuwapitia.
“Naitwa Dolph Moris, au The Taker kama huwezi kutaja Dolph.” Alijitambulisha yule Mzungu kwa lugha ya Kiingereza cha Kimarekani.
“Naitwa The Taker (Mchukuaji) kwa sababu ya kikosi nilichopo jeshini. Nipo peke yangu katika kambi niliyotoka huko Marekani. Mi’ ni Sniper (Mlengaji kwa kutumia bunduki na bastola au Mdunguaji kwa lugha rahisi) ambaye kwenye mafunzo yangu ya kwanza ya kulenga shabaha mita mia tano, nilikosa risasi mbili kati ya ishirini nilizopewa. Mara ya pili sikukosa hata moja kati ya risasi ishirini nilizokabidhiwa. Ilikuwa ni mita elfu moja. Naitwa The Taker kwa sababu nipo maalum kwa kuchukua tenda za kuua lundo la maadui. Risasi yangu moja, ikikosa kukuua, inakupa kilema cha maisha au inakufanya uwe mwehu. Nani anataka kuwa Mdunguaji.” The Taker alimaliza na kuuliza ambapo kwa haraka yule jamaa mwembamba kuliko wote alinyoosha kidole juu huku akijitaja.
“Mimi mkuu.” Alifanya hivyo kwa sauti ya kikakamavu.
“Vizuri. Na Utakuwa tu.” The Taker alimwambia yule jamaa ambaye alinyoosha kidole peke yake.
“Kabla hatujaanza safari, nataka kuwatambulisha watu watakao wasimamia kwenye mafunzo yenu.” Aliposema hayo, wakashuka wanajeshi wengine warefu na wenye miili mikubwa toka kwenye yale magari mawili yaliyokuja pale msituni. Walikuwa ni wanajeshi kumi na wote walijitambulisha kama makamanda wa mafunzo. Na baada ya kujitambulisha, The Taker alitoa simu yake ya mkonge na kuongea maneno fulani fulani na kuikata simu ile.
Dakika kadhaa, yalikuja mbasi mawili makubwa ya jeshi na wale vijana mia na hamsini, walianza kutenguliwa kwa makundi.Sabini wa kwanza walienda kupanda basi moja na sabini wengine walienda kwnye basi lingine huku wale waliobaki wakagawanywa kwa kwenda kupanda yale maroli ya Jeep. Viongozi wao, walipanda pamoja kwenye maroli na wengine kwenye mabasi. Safari ya kwenda mafunzoni ikawadia.
****
“Pity.” Vanessa alimuita Peter kwa sauti yake mwanana lakini yenye ujasiri ndani yake. Peter hakushughulika kuitika na badala yake alimuangalia usoni msichana yule mrembo na kutabasamu kuonesha kuwa kamsikia alivomuita.
“Ni siku nyingine tena ya kuyabadili maisha yetu kutoka kwenye dunia ya kuileta katika mapambano yaliyo hai. Mapambano kwa ajili ya damu iliyopotea. Sidhani kama kuna nafasi nyingine tutakaa na kuongea haya, lakini kama ikipatikana nitaongea haya haya.” Vanessa aliongea kwa taratibu huku akipapasa kifua cha Peter aliyekuwa kalala naye kitandani.
“Usijali Vanee. Hakuna kitakachotutengenisha katika maisha yetu kama MUNGU kaamua kutulinda. Cha msingi tuzidi kumuomba kila kukicha, sawa?” Peter aliongea huku anasugua midomo mizuri ya kimwana wake. Ilikuwa ni usiku wa saa tisa wakati wanaongea hayo na tayari walishafika kambini walipopaswa kufika. Usiku huo, nadhani ulikuwa ni usiku wa mwisho kwa viumbe hawa wanaopendana kuweza kuungana miili yao na kuwa mwili mmoja kwani siku mbili zilizokuja, zilikuwa ni siku za kuanza mafunzo magumu kutoka kwa wale wazungu.
“Tuzidi kumuomba yeye pekee, nadhani tutafika popote tunapotaka.” Vanessa aliunga mkono maneno ya Peter. Kimya kikachukua nafasi yake baada ya maneno hayo na ni mikono pekee ndio ilikuwa ikisikika inafanya kazi ya kupapasa hapa na pale hasa ile ya Vanessa ambayo ailikuwa inapenda sana kifua cha Peter.
“Aren’t you something to admire, cause your shine is something like a mirror. And I can’t help but notice, you reflect in this heart of mine. If you ever feel alone and glare makes me hard to find. Just know that I am always parrallell on the other side. (Wewe si kitu wa kutazama na kupendeza, kwa kuwa mng’aro wako ni kama kioo. Na sijiwezi bali kujua, unaakisi katika huu moyo wangu. Kama unajihisi u mpweke na mng’ao mkali unaniwia vigumu kukupata, basi tambua nipo sambamba na wewe kila wakati)” Ni wimbo wa Mirrorr uliyoimbwa naye Justin Timberlake ndiyo ulikuwa unatoka katika kinywa cha Vanessa kwa sauti nyembamba na nzuri akiwa anamwimbia mpenzi wake. Hakuishia hapo, akaendelea kutiririka mashairi ya wimbo ule.
“Cause with your hand in my hand and pocket full of soul. I can help you there’s not place we couldn’t go. Just put your hand on the past, I,m here trying to pull you though. You just gotta be strong. (Kwa sababu kwa mikono yako ndani ya mikono yangu na mfuko uliyojaa nafsi/matumaini. Nitakusaidia pale tutakapokosa pa kwenda. Wewe weka mkono wako katika ya nyuma, nipo hapa kukutoa huko. Unatakiwa kuwa imara). Maneno yalimtoka Vanessa kwa sauti ya msisitizo kwa akiimbacho. Akaendelea mbele zaidi ambapo kuna kiitikio cha wimbo huo. Safari hii Peter naye aliamua kuimba naye wimbo ule na kuzifanya sauti zao ziwe kama ala za muziki upigwao katika Kasri la Malikia wa Uingereza.
“Cause, I don’t wanna lose you now. I’m looking right at the other half of me. The vacancy that sat in my heart, is a space now you hold. Show me how to fight for now, and I’ll tell you, baby it was easy coming back into you once I figured it out. You were right here all along.
It’s like you’re my mirror. My mirror staring back at me
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
…………….. (Sababu sihitaji kukupoteza kwa sasa. Najiangalia moja kwa moja nusu ya mimi ( Yaani amwangaliapo mpenzi wake, anajiona nusu ya yeye). Nafasi tupu iliyo moyoni mwangu, ni nafasi uikamatayo wewe kwa sasa. Nioneshe jinsi ya kupigana, na nitakwambia, mpenzi ni rahisi kuja kwako pale nitakaporekebisha. Upo hapa siku zote. Ni kama kioo changu. Kioo kinaniangalia nikiangaliapo …………….”
Wapenzi wale wakaendelea kuimba wimbo ule kwa hisia hadi wakaumaliza ambapo waliumaliza kwa machozi ya furaha na upendo ndani yake. Hakika walikuwa mfano wa kuigwa kama wapenzi.
“Mbona hukuwahi kuniambia kama na wewe unajua kuimba?” Vanessa alimuuliza Peter kwa furaha.
“Mbona wewe hujawahi kuniambia? Au umeniona mimi tu.” Peter naye alijibu akiwa umeweka utani ndani yake ili asimkere mpenzi wake kwa yale majibu.
“Ha ha haa. Haya bwana. Basi wote tuna makosa. Ila unasauti nzuri sana My Pity.” Vanessa alimsifia mpenzi wake.
“Hata wewe mpenzi. Yaani pale unaposema ‘it’s like a mirror’. Ulikuwa unaniua balaa. Umebarikiwa Vanee.” Peter naye alimsifia Vanessa. Lakini yote hayo yalikuwa ni kujisahaulisha tu matatizo ya kidunia. Na walifanikiwa kurudisha furaha yao kwa muda ule mchache.
“Niambie. Umejifunza wapi sauti yako. Yaani kuongea, unaongea kwa sauti nene, lakini hapo ulivyokuwa unaimba, ni kama Justin Timberlake mwenyewe.” Vanessa alisaili huku akizidi kumwaga sifa nyingi.
“Mi ni msanii Vanee. Naweza kupiga kinanda na gitaa. Wakati nasoma sekondari, nilikuwa napiga vifaa hivi kanisani na pia kuongoza wanakwaya. Hapo ndipo nilijifunza pia na kuimba.” Peter alijibu swali Vanessa.
“Kwa hiyo unaweza kuimba zaidi ya hapa?” Vanessa aliuliza tena.
“Zaidi ya Justin mwenyewe.” Peter alijigamba huku akitabasamu.
“Embu niimbie wimbo mwingine nihahakikishe.” Vanessa alitoa ombi ambalo Peter hakuwa tayari kulifanya bali kumuahidi atatunga wimbo ambao utakuwa kwa ajili ya Vanessa.
“Nitafurahi sana nikiusikia wimbo huo My Pity.” Vanessa alionesha kuridhika na ahadi ya Peter. Akalala kwa deko juu ya kifua kipana kiasi cha kijana yule.
****
“Ukiwa hapa. Wewe si tena mwananchi. Wewe ni mwanajeshi. Na mwanajeshi kazi yake kulinda mali za taifa na taifa lenyewe. Kazi ya mwanajeshi ni kutetea maslahi ya nchi, kazi ya mwanajeshi ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake eidha kwa kumwaga damu yake, au kumwaga damu ya mtu mwingine. Hapa hakuna mapenzi, kuna kupambana. Hapa hamna mama wala baba, hapa kuna wanajeshi.” Ni sauti ya Kamanda Bonito ikiwa inapaa kwenda kwa wale wanajeshi wapya ambao walikuwa wamepanga mistari minne mirefu kwenda kushoto na kulia (Parallell).
Ni siku ya tatu tangu wafike pale walipopangiwa kufanyia mazoezi. Siku hii ilikuwa ni siku mahususi kabisa kwa vijana wale machachari kuanza kutumikia mafunzo ya jeshi la Waasi, nchini Senegal.
Kulikuwa kuna hali ya mawingu, hali ambayo ilionekana wazi kuwa mvua itanyesha siku hiyo. Baridi kali ya kuashiria mvua, ilikuwa inakita ndani ya miili michanga ya vijana wale ambao wengine walitoka vifua wazi baada ya kuchelewa kuamka na wale walimu wao wakitaka watoke haraka.
“Hapa hatujifunzi ushujaa. Tunajifunza ukakamavu na moyo wa kupambana. Kama unataka kuwa shujaa, nenda kakimbie mbio ndefu hadi ufe kama Marathon.” Akiwa ndani ya magwanda mazito na yaliyomkaa vema. Kamanda Bonito alikuwa anaongea huku akienda huku na huko. Miwani nyeusi aliyokuwa kaivaa wakati ule na ile kofia ya kikamanda, hakuna aliyekuwa anathubutu kutia neno au chochote kutoka kinywani kwake.
“Nani anamjua Marathon?” Kamanda Bonito aliuliza swali ambalo hakuna aliyelijibu.
“Marathon alikuwa ni kijana wa Kizungu. Anatoka huko Ulaya. Alipata ujumbe ambao alitakiwa kuufikisha kwa mfalme wake aliye mbali sana na huko ujumbe ulipotoka. Aliahidi kuwa ujumbe ule utafika salama na mfalme atausoma." Hadithi hiyo ya Bonito kuhusu Marathon wakati inatoka kinywa mwake, kundi zima la wanajeshi lilikuwa kimya likisikiliza.
"Akafumbata ujumbe ule ambao ulikuwa ni barua ndefu, kisha kwa kasi akaanza kukata upepo. Alikimbia muda mrefu bila kupumzika wala kufanya chochote njiani. Masaa yalikatika akiwa njiani anakimbia na mwisho wa safari hii ulikuwa ni kufikisha ujumbe ule kwa Mfalme wake," Bonito akaenda mbele ya kijana mmoja na kuusogeza uso wake katika uso wa kijana yule, wakawa wanaangaliana ana kwa ana kwa sentimita chache sana.
"Licha ya kuufikisha ujumbe ule, lakini hakuongea neno lolote bali alifia katika miguu ya mfalme wake aliyekuwa juu ya kiti kipana kama cha enzi. Alikufa huku anampa barua mfalme wake." Maneno yake yalitoka huku akipindapinda pua yake na saa nyingine kutoa mate ambayo yalimrukia yule bwana mdogo lakini jamaa wala hakuthubutu kusumbua.
"Huyo ni shujaa na ndio maana wamemuenzi kwa kuita zile mbio ndefu ni Marathon. Lakini hapa hatufundishwi ushujaa bali tunakuandaa uwe...." Kamanda Bonito aliuliza kwa sauti ya juu akimtaka yule bwana mdogo ajibu lile jibu.
"Ukakamavu na moyo wa kupambana.." Akajibu yule bwana kwa sauti ya juu zaidi.
"Safii. Wote sasa, tunajifunza nini hapa?" Kamanda Bonito aliuliza gwaride zima na wote wakajibu kwa sauti ileile.
"Nawaacha kwa hawa viongozi wengine. Hamna kuogopa, mmezaliwa kufa. Acha kazi ianze." Bonito alimaliza kuongea na wakati huohuo, Mzungu mmoja mrefu na mwenye mwili, alisogea mbele kwa mbwembwe nyingi na kusimama katikati ya mistari iliyopangwa pale uwanjani. Akaangalia juu kama mwenye kutazama jua lililokuwa linawia asubuhi ile yenye ubaridi wa kuifanya mifupa ikamatwe na ganzi. Mawani yake ya rangi ya kahawia, ikang'aa na bwana yule akatabasamu kidogo kabla hajaongea.
"Tuna siku ndefu sana leo. Kwanza kabisa ni lazima tuwatoe nyongo ya uzembe." Mzungu yule aliongea na kuzidi kutabasamu. "Wewe hapo, njoo mbele." Akaongea huku anamuoneshea kidole kijana mmoja mweusi na aliyebarikiwa kuwa na mwili mrefu kiasi.
Yule jamaa akasogea mbele hadi pale alipo yule mzungu anayefundisha. Akasimama mbele yake kwa ukakamavu lakini bila kujua alijikuta akipigwa kofi zito lililosababisha sauti ya hamaniko kwa vijana wengine.
Wakati yule jamaa anajaribu kusikilizia maumivu ya kofi lile, akajikuta anapokea kofi lingine la kisogoni na kumfanya apepesuke kama mlevi wa gongo.
Akiwa katika kupepesuka hukohuko, yule Mzungu alimkumba kwa bega la tumboni yule bwana na ghafla jamaa alitama mate makali yaliyoruka kama yametoka kinywani mwa swira.
Jamaa akaanza kugaa gaa chini huku akipumua kwa kasi.
"Naitwa Luteni Japhet Saigon. Niite Luten Gon." Yule mzungu aliyemkumba kijana wa watu alijitambulisha kwa mbwembwe kana kwamba alichokifanya kwa yule kijana ni sahihi.
"Hii ni moja ya njia ndogo sana ya kuutoa uzembe mwilini." Aliongea saa hii huku akimtazama yule jamaa aliyekuwa anagaa gaa pale chini.
"Mwanajeshi ananjia kadhaa tu za kuishi. Moja, kwa kujiamini, mbili kwa kujihami na tatu, ni kwa kujitambua afanyacho. Kuna sheria moja tu ambayo kila mwanajeshi huiamini duniani. Kama umeamua kung'oa jino moja lililoharibika, ni kheri ung'oe yote tu. Hii ndio imani yetu," Alizidi kujitapa Luteni Gon. "Kwa sasa mmeamua kuwa wanajeshi, na si wanajeshi tu! Bali wanamapinduzi, basi kuweni hivyo pekee. Mambo ya 'baby' na uchumba, ni baada ya kufanikiwa kupita hapa na kuwa huru kabisa. Na kwa mwanajeshi, hata siku moja hakuna siku ambayo atakuwa huru, labda siku ya kifo chake. Kwa maneno hayo, naweza kukwambia kuwa mwanajeshi hajui mapenzi yapo vipi na kama anayajua, basi tutamfanya ayasahau." Maneno mengi ya Luteni yalizidi kumwagika wakati ule kabla ya kuanza kazi moja tu, ya kutoa nyongo ya uzembe.
"Leo ndio tutaanza kazi iliyotuleta hapa," Aliongea tena baada ya kumaliza porojo nyingi. "Nipo na wenzangu kwa ajili ya kuwatoa nyongo tu. Naomba nipate makundi yenu yenye watu ishirini kila kundi." Aliongea Luteni na muda huohuo, vijana wakajikusanya na kukaa makundi aliyoyataka bwana yule. Makundi kumi na mbili yalitokea huku Vanessa na Peter wakiwa tofauti katika makundi hayo.
Kila kundi lenye watu ishirini lilipewa wanajeshi watano wakakamavu wakiwepo wazungu na waafrika ambao waliendesha vema zoezi lile la kutoa nyongo ya uzembe.
Bonito akiwa mbali kabisa na eneo lile, alikuwa yupo sehemu moja ambayo aliweka kitu kama chandarua chenye matobo makubwa na kamba zilizoshonewa zikiwa ngumu zaidi ya hivi vyandarua vyetu.
Chandarua kile kigumu kilifungwa kwenye miti mitatu na kuwa kama kitanda kilichoelea juu kwa juu. Bonito akawa juu ya kitanda hicho cha chandarua huku anasoma kitabu chenye wingi wa taharuki, kitabu kilichotungwa na gwiji wa Riwaya Tanzania, Bwana Hussein Issa Tuwa. Ni kitabu cha Riwaya Ya Mkimbizi.
Alikuwa hawafatilii kabisa wale vijana wapya katika mafunzo ya kuwaandaa katika uhasi wa nchi ya Senagal, akili yake aliilekeza kwenye Riwaya ya Mkimbizi.
Kila kundi lilipelekwa sehemu yake na katika sehemu hizo kulikuwa na vitu ambavyo viliogopesha kutazama hata havifikiriki kwa jinsi vilivyotisha.
"Hapa ni wewe na akili yako ndio utafanikiwa kuweza kuvuka. Kama unaakili ndogo, amini utafia hapa." Aliongea kiongozi ambaye alikuwa katika kundi alilopo Peter Madira.
"Sehemu hii kuna magogo yapatayo kumi na tano. Yanatoka kushoto na kulia, chini na juu. Cha msingi kuwa makini na uvukaji wako kuelekea kule mwisho." Alizidi kuelekeza yule kiongozi huku akiwaandaa baadhi ya wanajeshi wenzake kwa ajili kufanya kazi ya kufyatua yale magogo ambayo kiukweli yalikuwa makubwa na yalitisha katika macho ya wale vijana.
"Nataka vijana wawili waanze rasmi zoezi hili." Akaongea yule kiongozi lakini hakuna aliyejitokeza ndipo alipoamua kuchukua jukumu la kumuita Peter na jamaa mwingine mwenye mwili mkubwa kiasi na mrefu kwenda juu kuliko yule aliyekumbwa na Luteni Gon.
"Mmepaona pale," Yule kiongozi aliwauliza wakina Peter baada ya kusogea walipohitajika. Na wote macho yao yakaelekea kule walipooneshwa. "Kwenye ule mti," Akawaonesha mti ambao ulikuwa hatua zipatazo sabini toka pale waliposimama. Wote wakaonesha kuwa wamepaona. Yule bwana akaendelea kwa sauti.
"Umewaona hawa mabwana wa pembeni?" Akawauliza kuhusu wale wanajeshi wengine wanne waliokuwa wamesimama pembeni, wawili kushoto na wawili wengine kulia. Macho ya Peter na yule jamaa wakawatazama wale wanajeshi.
"Hawa ni maadui zenu. Tena maadui wenye silaha. Watakuwa wanaachia mitambo ambayo nyie mnatakiwa kuwa mnaikwepa kwa umakini mkubwa. Cha msingi ni akili yako kuwa inafanya kazi kwa kasi kubwa. Angalia upande wa kushoto, angalia na upande wa kulia. Hawa ndio maadui zako waliopo kila upande, hivyo cha msingi ni wewe kuwa unaangalia matendo yao ili ufanikiwe kuwakwepa mapigo yao.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ukilegea, unaweza kufa. Unaruhusiwa kujilinda pia kwa njia yoyote, lakini kubwa ni kukwepa kwa makini sana vitu utakavyokutana navyo." Alitoa maelekezo ya zoezi lile la kutoa uzembe. Aliongea mengi sana kuhusu zoezi lile na faida yake. Lakini kubwa zaidi ni kuwa mwepesi kufanya maamuzi pamoja akili yako kuwa haraka kugundua adui yako anataka kufanya nini. Hizo ndizo njia za jeshi, hakuna kitu kisichokuwa na faida.
"Nahesabu moja mpaka tatu, baada ya hapo mnatakiwa kuanza kuvuka sehemu hii. Unaruhusiwa kukimbia kwa kasi yoyote, lakini kumbuka, mapigo yanatoka juu, chini, pembeni na mbele unapoelekea. Kuwa makini na mbio zako na waangalie maadui zako wa pembeni matendo yao." Alimaliza yule bwana na akawaweka wakina Peter tayari kwa zoezi lile gumu kupata kutokea. Akahesabu moja mpaka tatu na hapo Peter na mwenzake wakaingia katikati ya wale waliowaita maadui zao ambao walikaa pembeni na katikati wakaacha.nafasi yenye ukubwa wa barabara iwezayo kupitisha magari katika njia nne. (Ukubwa wa Barabara ya Four Ways)
Peter ndiye alianza kuingia ndani ya zoezi lile gumu. Hatua tatu mbele aliona mwanajeshi wa upande wa kushoto akikata kamba kwa kisu kidogo na bila kutegemea gogo kubwa likachomoka toka kulia kama lililorushwa kwa mikono. Lilikuwa linamuelekea kifuani, kwa haraka Peter akalala chini na gogo lile likapita juu yake huku likiacha sentimita chache kumgusa.
Yule bwana mwingine alipoona hivyo akataka kughairi lakini alikutana na maneno mazito kutoka kwa yule msimamizi wa zoezi lile.
"Kama unakataa zoezi hili, basi utarudi mjini kwa miguu. Hapa tulipo, hupajui na wala kambini hupajui. Chukua hatua sahihi kabla hujafanya maamuzi." Aliongea kiongozi yule. Jamaa ikabidi aingie lakini kwa kujihami zaidi huku akitazama zaidi pembeni na kulia.
Akapiga hatua tano kwenda mbele wakati huo Peter naye alikuwa mbele yake kidogo tu, kama hatua nne. Mwanajeshi wa kushoto akakata kamba na kwa kasi nyingine, gogo likatoka mbele kwa mtindo uleule kama wa kurushwa likawa linakuja mbele yao. Lilikuwa refu ambalo lilienea ukubwa wa pale katikati walipokuwepo wakina Peter.
Peter akakimbia kwenda mbele kama analifata, alipofika usawa wa kukutana nalo, akalala chini kifudifudi na gogo lile likapita tena kwa juu.
Yule jamaa wa nyuma naye aliliona gogo lile, akafanya maamuzi ya haraka ya kulala chini na kwa bahati nzuri lilidondokea mbali na yeye hivyo akanusirika. Akasimama haraka ili aendelee na safari yake na wakati huo Peter naye alikuwa amesimama na alishuhudia wanajeshi wa upande wote wakikata kamba.
Yule jamaa wa nyuma alijikuta akisombwa na gogo lililotoka upande wa kushoto. Liligonga sehemu ya kulia ya bega lake na jamaa alitoa yowe la maumivu wakati gogo lile likimtupa pembeni ya uwanja ule.
Peter naye alikutana na msala kama huohuo.
Gogo moja liliibuka chini toka usawa aliposimama na bila kujua, alijikuta kalikwea na kupaa nalo juu kiasi cha mita kumi. Akiwa juu Peter huku gogo lile akiwa kalikalia kama baiskeli, akili yake akaifanya ifanye kazi haraka kabla gogo lile halijadondokea pale katikati alipotoka na kumuumiza vibaya katikati ya mapaja yake.
Alifanya kama kusimama juu ya gogo lile na wakati limebakiza sentimita kadhaa kudondoka chini, Peter alijirusha kwenda mbele na kutua chini kwa kulia tumbo na wakati huo mshindo wa gogo lile ulisikika nyuma yake hatua tano toka alipokuwa kalala.
Yule jamaa wa nyuma alishakiona cha moto hivyo alitolewa ulingoni na jamaa mwingine ambaye yeye alianza kwa kasi sana. Magogo mawili yaliyotumwa kwenda kwake, alikuwa anayakwepa kwa umahiri huku macho yale yakiwa yanaangaza kushoto na kulia kwa umakini mkubwa sana. **** Wakati Peter na kundi lake wakiwa katika kuhangaika huko kuyakwepa magogo yasiyo na fomula, hali ilikuwa tofauti kwa Vanessa ambaye hakuna aliyeamini kama msichana yule anaweza kuhimili mikiki mikiki ya zoezi lile gumu kabisa.
Katika msafara wa wale wanajeshi wapya, kulikuwa na wasichana watano pekee akiwepo na Vanessa ambaye alikuwa kama katiwa ndimu kwenye zoezi lile.
Gogo ambalo lilimkosa Peter kumkumba kifuani, yeye alicheza nalo kama Mchina katika uwanja wa mapigano ya fimbo na cheni.
Gogo lile lilikuwa linakuja mbele yake, aliliona vema sana. Kwa haraka akarudi nyuma ambapo alishakwepa gogo lingine lililoibuka toka chini. Baada ya kurudi nyuma, akaliacha gogo lile litue chini na lilipofanya hivyo kwa kasi akakimbia kulifuana na kisha akaruka juu na wakati huo gogo lile lilikuwa limedunda chini na kupaa tena juu ambapo Vanessa alikutana nalo kwa kulikanyaga baada ya kuruka kisha akiwa kulekule juu, Vanessa aliruka kiustadi kama mtu anayejitoma kwenye maji.
Vanessa akatua chini na kubingirika sarakasi ya chinichini na kisha akatulia kimya huku akiwa kapiga goti moja akitazama kushoto na kulia ambapo wale wanajeshi wawili wengine katika upande wa kushoto na kulia, walikuwa wanasogea haraka kwa ajili ya kuendelea kutegua magogo yalikuwa yanaendelea. Tayari washirika watatu wa Vanessa walikuwa wametolewa wakiwa na maumivu makubwa baada ya kukumbwa na magogo.
Vanessa akiwa kapiga hatua nyingi kwenda mbele, alinyanyuka haraka na kuanza kukimbia kwa kasi kwenda mbele. Hatua tano mbele, likachomoka gogo upande wa kushoto likiwa limelenga vema kumkumba usawa wa magoti yake. Vanessa kwa haraka akaruka sarakasi ya upande na gogo lile likapita huku likigusa nywele ndefu zilizopo kichwani kwake. Ziligusa nywele kwa sababu wakati linapita, Vanessa alikuwa karuka sarakasi ya upande lilipokuwa linatokea gogo lile na kumfanya awe kichwa chini na miguu juu lakini akiwa hewani na wakati huo gogo lilikuwa linapita chini yake.
Kamanda Bonito aliacha kusoma kitabu na kuangalia yale mambo anayofanya Vanessa kisha akatabasamu baada ya kumkumbuka Mzee Gomez, baba wa Vanessa. "Huyo binti ni hazina kubwa katika kuendesha kazi zangu. Ni zaidi yangu huyo. Sikutaka hata kidogo afe kama mama yake. Nataka siku akifa hasa katika mapigano ya hawa washenzi, basi afe huku akipambana na maadui zake. Anamafunzo yote ya kujihami na kikomando kidogo aliyapitia lakini mimi nilimkatisha asiendelee kwa sababu ya umri wake. Lakini mapigano mengine, ni mtu wa hatari sana huyo." Kamanda Bonito alikuwa anakumbuka maneno aliyowahi kuambiwa na Mzee Gomez.
Bonito alikaa sehemu ambayo anaweza kuona mafunzo yote yalivyokuwa yanaendelea. Alimtazama Vanessa na Peter kwa jinsi walivyokuwa wanaenda mbele japo Peter alitumia zaidi akili na ujanja kidogo huku Vanessa akitumia ujanja mwingi na akili kidogo. Nasema hivi kwa sababu gani?
Ni hivi.
Peter alitumia akili nyingi sana kwa sababu alikuwa anawatazama wale wateguaji na baada ya kuona matendo yao ya kukata kamba, basi akili yake inahamia kwenye wapi ambapo gogo litatokea. Pale linapotokea anatumia akili nyingine ya kuwaza afanye nini kulikwepa. Wakati wa kulikwepa ndipo anatumia ujanja mdogo ambao anao.
Lakini Vanessa yeye alikuwa anatumia ujanja na akili kidogo tu. Alikuwa hawatazami wale wateguaji bali kwenda mbele huku masikio yake yakiwa wazi kusikiliza adui yake anatokea wapi. Pale linapotokea gogo, basi yeye hutumia akili ndogo ya kulikwepa akisaidiana na ujanja wa mikunjo ya sarakasi zake. Wote walifanikiwa na walimfanya Bonito atabasamu na kuamini kuwa wale ni hazina kubwa sana katika jeshi lake akawa anasubiri aone kama watamaliza mbio zile.
Vanessa akiwa kabakiza hatua kama thelathini kufika mwisho, ndipo sasa akaanza kuona ugumu wa kufikia mwisho. Akiwa makini kabisa katika kuhisi na kusikiliza, ndipo magogo mawili yalitokea upande wa kushoto na kulia. Moja lilikuwa limelenga kichwa na lingine sehemu ya paja na yote yalikuwa yanakuja kwa pamoja na uzuri hisia za Vanessa zilienda sawa na kuyaona magogo yale.
Akili ikafanya kazi haraka na akajikuta anasimama kama anayasubiri magogo yale yavuke. Alipoona yanamkaribia akageuka upande wa kushoto linaotokea lile la kumlenga kichwa. (kumbuka yalikuwa yanakuja yamelala na kwa marefu hivyo inakuwa ngumu kurudi nyuma kwani yatakufikia kabla hujafika mbali).
Baada ya kuliona lile gogo la kichwani linakuja, akapiga hesabu za haraka katika kuyakwepa yote mawili. Kama akiliruka lile la juu basi hili la chini nalo litapita tu. Kwa hiyo alichofanya ni kama kulifata lile la kushoto na alipokaribia kulifikia, akajirusha tena kama anayeogelea na gogo lile la juu likapita kidogo juu ya kisogo chake na wakati huo gogo la chini nalo linapita na hivyo kuonekana kama magogo yale yamemuweka katikati. Yakapita kwa kasi na moja likadondokea kulia na lingine kushoto huku Vanessa akidondokea katikati na hali hiyo ikawafanya hata wale wateguaji kubaki katika taharuki ya ajabu na hilo likampa mwanya Vanessa ya kuongeza mbio za kufika mwisho. ***** Kwa upande wa Peter, akili nyingi ujanja kidogo, naye alijikuta katika sehemu ambayo Vanessa kafika. Magogo mawili yalikuwa yametokea lakini kwa upande wake yalikuwa yanakuja nyuma na mbele. Ilikuwa rahisi sana kuyakwepa lakini kwa bahati mbaya safari yake ikaishia pale alipofanikiwa kuyakwepa.
Akiwa anayaona vema magogo yale yanavyokuja huku moja la mbele limemlenga miguu na lingine limelenga mgongo, akakimbia kwa kasi kulifuata lile lililolenga miguu. Akaliruka na wakati huo akajigeuza na kulitazama lile la nyuma. Nalo akalikwepa kwa kujitupa kimgongo mgongo. Alipotua chini, gogo lile likapita juu yake. Akiwa bado hajaamka toka pale chini, wale wateguaji waliachia kamba nyingine na ghafla magogo mengine mawili yakajitokeza chini na kumnyanyua juu akiwa vilevile kalala kifudifudi. Ujanja ukamuisha katika kuutumia.
Magogo yale yakaenda juu mita kadhaa na kisha yakatua chini na kusababisha mgongo wa Peter kujipigiza na kuumia kiasi chake. Akawa anagaa gaa pale chini huku akionesha wazi kaumia.
Wanajeshi waliokuwa wanahusika na kutoa huduma ya kwanza, wakamfata Peter alipo na kuanza kumtoa ulingoni. Wakati anatolewa, yule kiongozi alitikisa kichwa kwa kukubali ile kazi aliyoifanya Peter. Vijana kumi tayari walikwishashindwa zoezi lile lakini Peter alibakiza hatua zipatazo ishirini ili amalize kwa bahati mbaya akakutana na kigingi kidogo kilichomtoa mchezoni.
****
Vanessa alikuwa anakwepa kwa kila njia zoezi lile lakini naye akiwa kabakiza hatua kumi, alikuta mtihani ambao ilibidi akubali kushindwa.
Akiwa katika kuzuia asikutane na magogo hayo, akaingia kwenye mtego mzito na wa hatari. Magogo matatu yaliachiwa pembeni, nyuma na mbele. Alifanikiwa kuyapita ya mbele kwa njia ileile ya sarakasi lakini lile la pembeni lilomgonga vibaya begani na kumrusha hadi nje ya dimba. Akawa anagara gara kwa maumivu makali. Wakaja watu wa huduma ya kwanza na kumtoa ulingoni huku Bonito akiwa mbali na kutikisa kichwa cha kukubali wale vijana walochokifanya.
Zoezi lile likaendelea hadi saa saba na wanajeshi wale walipoachwa, walijikuta wakitweta kwa njaa na maumivu ndipo chakula cha kutosha kililetwa na wapishi wa kambi ile ya mafunzo na vijana wale walianza kufakamia chakula kwa kasi.
****
"Tumefundisha majeshi mengi sana hapa Afrika. Na hakuna hata mwanajeshi mmoja aliyevuka hatua ishirini kwenye zoezi hili la kutoa uzembe," Luteni Gon au Japhet Saigon, aliongea mida ya saa kumi na mbili baada ya mazoezi makali yaliyokuwa yanajiri kila dakika. "Lakini kuna baadhi wameweza kuvunja rekodi hiyo. Vijana wanne wameweza kufika mbali na wa kwanza akiwa ni mwanamke. Yeye alibakiza hatua kumi na tatu amalize ndipo akakutana na pigo gumu.
Hongera binti," Alimpa hongera na wanajeshi wote walimtazama yule anayepewa hongera. Alikuwa ni Vanessa. Hata Peter hakuamini hilo. "Kesho kutwa tutaendelea na mazoezi mengine ya kuwajenga. Hili ndilo zoezi gumu kushinda yote. Hongereni mliofika mbali." Luteni Gon alimaliza na kuondoka na wenzake wakiwaacha wale vijana wapumzike kabla hawajaitwa kwa ajili ya kuoga na mambo mengine. **** "We' ni nani Vanessa," lilikuwa swali la Peter baada ya kukaa sehemu usiku wakiwa wanapiga soga za hapa na pale.
"Pity. Ni mimi Vanessa." Akajibu kwa sauti ya kubembeleza Vanessa.
"Hapana. Namaanisha we' ni nani katika maisha haya ya ki-asi? We' ni nani kiuhalisia. Umejifunza wapi mambo yote ambayo yanaongelewa hapa," Alitaka majibu ya kina zaidi Peter. Vanessa akatabasamu tabasamu la mchoko kisha akamtazama Peter kwa umakini.
"Maisha ni kucheza na nafasi Pity. Maisha ni kujua pa kupita kabla hujafika ulipokusudia kupita," Aliongea kwa utulivu Vanessa. "Baada ya mama kufariki na mimi kuwa kama tahira au mwenye tetenasi, baba alifanya jambo la kijasiri sana kwa kunipeleka kutibiwa China kwa dawa za kienyeji.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miaka mitano ya kukaa China, ilitosha kabisa kwa mimi kurudi katika hali yangu na baadae kuanza kujifunza mambo mengi yakiwemo mapigano. Sipo vizuri sana katika hilo lakini naamini nitaweza kufika Kongo na kumuondoa yule Mama na Familia yake nzima." Aliongea kwa hisia Vanessa. "Baada ya kucheza baadhi ya michezo ya kichina, baba alinichukua na kunipeleka kwa rafiki yake huko Cuba. Alikuwa ni komando yule bwana. Akanifunza mengi sana. Na leo hii, ndivyo vinavyonisaidia mimi katika kuniwezesha kuvuka vikwazo waviwekavyo hawa mabwana." Alimaliza Vanessa na Peter alijikuta akitabasamu bila kusema lolote. Akili ya Peter ikarudi nyuma kidogo na kukumbuka maneno ya baba yake ambayo siku zote aliyaona ndio maisha yake. Yaani aliishi kwa maneno ya baba yake.
"Peter," Baba yake siku moja alimuita kwa utaratibu wakiwa wanaelekea shambani kwa gari moja ndogo kwa ajili ya shamba. Peter akamtazama baba yake aliyekuwa nyuma ya usukani akiliongoza gari kwa makini. "Hata uje kupendwa vipi katika hii dunia, hakuna atakayekuja kukupa kila kitu kati ya hao waliokupenda. Mimi baba yako nakupenda sana tena sana. Na ninawapenda wote sawia kabisa.
Lakini msidhani nitawapa kila kitu. Kuna vingine mnatakiwa kujitafutia. Kitu cha muhimu ambacho naweza kukupa wewe, ni Elimu. Elimu ndio kipimo cha akupendaye. Kama mzazi hawezi kukupa elimu na uwezo anao, basi tambua huyo ana nia mbaya na wewe. Na wewe ukipewa elimu, rudisha kwa matokeo mazuri. Hii ni kwa sisi wazazi," Maneno hayo yakawa yanapita kichwani kwa Peter haraka sana. "Lakini kuna binadamu au watu, watakupenda wewe. Kamwe usidhani kuwa watakwambia kila kitu. Ni sawa na yeye kula ugali, kisha akakupigia simu na kukwambia mpenzi au rafiki yangu leo nimekula ugali. Hakuna akupendaye awezaye kukwambia hilo eidha kwa kuhofia ama kwa kuficha tu siri zake. Ugali ni mfano tu, ipo siku utaelewa kwa nini nakwambia haya. Utapendwa, na utapewa kila unachohitaji lakini hutapewa kile ambacho hujawahi kukifikiria kama kipo." Mzee Madira alimaliza na Peter hakujibu lolote wakati maneno yale yanamtoka baba yake.
"Pumzika kwa Amani baba." Peter alijikuta akitamka kwa sauti ya chini baada ya kumbukumbu zile.
"Unasemaje Pity." Vanessa alimuuliza mpenzi wake.
"Maisha ni njia ambayo huwezi kuamini kuwa utafika kule unapoenda. Utapenda, Utapendwa na Utatendwa, lakini utang'amua mengi ndani ya hayo. Sijajua kwa nini ulinificha, lakini nachojua ni unanipenda. Kuwa na amani Vanee. Nakupenda sana." Peter alimwambia Vanessa na kumchapa busu dogo la shavuni.
"Nakupenda pia Pity." Wakakumbatiana kumbatio dogo la upendo huku wenzao wakiwa wanafurahia usiku ule kwa pamoja. Siku ikaisha kwa namna hiyo.
"Kama unataka mwili uwe imara, basi ni lazima ukubali kuushurutisha na kushurutishwa. Hapa tunajifunza mambo mengi kuliko katika dunia yenu ya UKIMWI na Ushetani," Luteni Saigon aliongea huku kashika kipaza sauti kilichokuwa kama spika, akiwa mbele ya wanajeshi wengi waliokuwa wanachapa miguu katika fukwe za bahari iliyopita pembezoni mwa bara la Afrika. Haijulikani walikuwa wapi lakini baada ya kupumzika kwa siku tatu, walitolewa katika lile pori na kupelekwa katika bahari hiyo.
Wanajeshi wapatao ishirini walikuwa nyuma ya wale wanajeshi wapya katika kusimamia lile zoezi la siku hiyo. "Ukiwa hapa, amini wewe ni maji na si mavumbi. Utaoga ili tukutoe vumbi," Alibwata kwenye kipaza sauti Luteni Gon. Hakuishia hapo, akaenda kwa yule bwana mdogo aliyenyoosha kidole siku za nyuma akionesha kuwa anapenda kuwa mdunguaji. Akamuwekea kipaza sauti katika uso wake.
"Ukiwa hapa wewe ni nani?" Alimuuliza kwa sauti yule bwana hadi akahisi masikio yanaziba.
"Mimi ni maji." Jamaa akajibu kwa ukakamavu.
"Rudia tena," Safari hii Luteni aliuliza kwa sauti zaidi hadi yule jamaa akafumba macho.
"Mimi ni maji." Licha ya kuzibwa masikio kwa sauti kali, lakini jamaa alijibu kwa ukakamavu wa hali ya juu.
"Basi twendeni kupambana na maji," Luteni alitoa amri wakati wale vijana wapya wakiwa wamesimama eneo la ufukwe lisilo na maji. Baada ya kauli ile, vijana wote wakaanza kukimbia kuelekea kule kwenye kina cha maji huku nyuma wale wanajeshi wengine wakiwasindikiza.
"Anza kupiga 'push up' wote. Luteni aliongea baada ya wale vijana kufika kwenye kina fulani cha maji.
Wote wakaenda chini na kuanza kufanya walichoambiwa. Walikuwa wanafuata kile walichoambiwa.
"Juu........ Chini....." Luteni aliongea kwenye kipaza na pale alipowaambia chini, vichwa vyao vilizama kwenye maji lakini masikio yalikuwa nje. Aliposema juu wale vijana walipumua kwa kasi.
Vanessa nywele zake zilikuwa zinamsumbua, hivyo alianza kuhangaika kuzifunga kwa nyuma wakati zoezi linaendelea. Luteni Gon alimuona na mara moja alienda mbele yake kisha akamwambia aende chini, yaani apige "push up'.
Vanessa alipoenda, Gon alimkanyaga kisogoni kwa sekunde kadhaa. Alipomuachia, Vanessa aliinuka huku akipumua kwa kasi kutokana na kukosa pumzi.
"Nani kakwambia uinuke?" Aliuliza Gon na bila kujibu, Vanessa akarudi chini. Gon akaendelea na kipaza sauti chake.
"Unajua kuwa kila kitu kina umuhimu hapa duniani?" Vanessa aliulizwa.
"Ndio mkuu," Alijibu huku anapiga 'push up'.
"Niambie faida ya maumivu."
"Sijui mkuu," Hapo Luteni Gon alikamata fulana ya Vanessa na kumnyanyua juu akiwa kamkwida kwa nyuma. Akaongea huku mdomo wake ukiwa kwenye kipaza sauti kile.
"Faida ya kuu ya maumivu, inakufanya ujitambue kuwa umekufa au bado hujafa. Pumbavu wee." Alimjibu Vanessa na kumuacha adondokee kwenye maji.
Vanessa akaendelea kugaa gaa pale chini ya maji wakati huo Luteni Saigon alikuwa kaondoka eneo lile na kuendelea kuongea kwenye kipaza sauti alichokuwa kakikamata vema.
"Hapa ndio sehemu ya kujua kusema kwa heri uwananchi na karibu uwanajeshi. Hapa ndipo pa kukubadili kutoka kwenye uoga kwenda kwenye ujasiri." Wakati anaongea hayo, wale wanajeshi wapya walikuwa wanaendelea kupiga 'push up' kwa kwenda juu na kuzamisha tena miili yao majini. "Ukitoka hapa usidhani kuwa unaweza kuonewa na mpumbavu yeyote katika dunia hii. Labda ahera. Wewe si mbumbumbu tena, wewe ni zaidi ya muokozi. Jiamini katika maamuzi yako. Na ukisema hivi, basi hakikisha uliyoyasema yanatimia hata kama kwa kumwaga damu."Sauti ilizidi kupaa na wakati huo helikopta moja ilikuwa imekuja na kuelea angani bila kutua chini. Hali hiyo ilisababisha upepo mkali katika eneo lile na mawimbi ya bahari kusambaa.
Luteni Gon alipomaliza kuongea, alitupa kile kipaza sauti na kudandia helikopta ile. Akaondoka huku akiwaachia kazi wale wanajeshi wengine waendelee kutoa mazoezi yale ya ufukweni.
****
Baada ya kupiga 'push up' za kutosha, wakatolewa pale na kupelekwa sehemu moja ambayo haina maji. Wakaanza kukimbia mchakamchaka huku wakiimba nyimbo nyingi za ukombozi pamoja na nyimbo za taifa za mataifa mbalimbali ya barani Afrika.
Jua la utosi lilipokamata nafasi yake, mazoezi ndio yakaongezeka kule ufukweni. Waligawanywa katika makundi ya watu kumi-kumi kisha kila kundi likapewa dumu la lita mia tano. (Ni kama yale matanki makubwa meusi ya kujazia maji majumbani).
Matanki hayo waliamriwa waende nayo sehemu yenye kina kirefu cha.maji kisha wayajaze na kutoka nayo hadi ufukweni. Zoezi lilikuwa gumu kwa vijana wale. Nguvu kubwa ilihitajika kwa ajili ya kusukuma matanki hayo kutoka kwenye maji kwenda nchi kavu.
Maneno ya kulazimisha toka kwa wakufunzi wao, ndio yalikuwa chachu ya kufanya zoezi lile kwa nguvu zao zote.
Zoezi lilichukua takribani masaa mawili na hakuna hata kundi moja lililokuwa limefanikiwa kufikisha nje matanki yale.
"Kazi ilikuwa nzito sana leo. Lakini mmejitahidi. Leo tumeimaliza. Haya nendeni mkapate chakula kwanza." Kiongozi aliyeachiwa madaraka na Luteni Gon, aliongea na njaa kali iliyokuwa imewakaba vijana wale, walijikuta wakitimua mbio kwenda kule ambapo pamejengwa kambi ndogo na nje yake kuna wapishi wamesimama nyuma ya vyombo vyenye chakula.
Wale mabwana walipofika sehemu ile, hawakusubiri kupakuliwa. Wenye mikono ya haraka, waliingiza na kuibuka na vyakula walivyopikiwa. Yalikuwa mahindi ya kuchemsha, nyama ya kukaanga na pembeni kulikuwa na sahani zenye wali na maharagwe.
Wakazivamia hovyohovyo na kwenda pembeni kwa ajili ya kula chakula kile. Mida hiyo ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni.
Wakati wanakula, wengine walificha mahindi pamoja na nyama kwenye makoti yao. Wakabaki wakitafuna wali ambao mwingine uliingia na mchanga. Hilo ndilo jeshi, hutaki kula, basi utakufa na njaa.
Baada ya dakika tano, wakatokea wakufunzi wa kijeshi na kuanza kukimwaga chakula walichokuwa wanakula kwa kisingizio kuwa muda wa kula umeisha kwa hiyo ni muda wa mazoezi japo walisema yataendelea kesho.
"Nani kawaambia waokozi wa nchi wanakesho? Hakuna kesho wazee. Hapa ni kazi moja tu iliyokuleta. Siyo kula bali kujifunza. Nadhani mmejifunza pia kula kijeshi. Kesho hamtokula 'kitozi'" Alikuwa Luteni Gon akiongea huku yupo juu ya tairi kubwa la gari lililokuwa limenyanyuliwa juu na wanajeshi wapya kumi na tano.
Kila kundi la watu kumi na tano, walibebeshwa tairi kubwa la gari zaidi ya lile la trekta. Na wakati wanelinyanyua juu, walitakiwa kuwa kama wanakimbia yaani wanachapa miguu.
"Na mkinidindosha nyie wajinga, mnanilipa kwa mazoezi magumu kuliko haya. Hivyo usimtegee mwenzako hata kidogo." Alisisitiza Gon huku vijana wale wakijaribu kufanya kama walivyoambiwa.
Zoezi likadumu kwa nusu saa nyingine. Walipoachiwa, hakuna aliyekumbuka kuoga bali kukimbilia katika kambi wanazopumzika ikiwa tayari imetimu saa moja jioni. Huo ndio muda wao wa kusafi miili, lakini hakuna aliyefanya hivyo. Wakalala kwa sababu ya kuchoka.
Saa tatu usiku. Waliingia wanajeshi kwa kunyata huku wameshikilia mpira unaopitisha maji mengi kama ule wa kwenye magari ya kuzimia moto. Wakaruhusu maji kutoka na kuanza kuwamwagia wale wanajeshi ambao wote walikuwa wamelala fofofo.
"Inuka wote na toka nje jinsi ulivyo. Fanya haraka. Wa mwisho 'push up' mia moja kwa mkono mmoja." Luteni Gon aliongea kwa kipaza sauti chake baada ya wale jamaa kumwagiwa maji.
Wote wakakurupuka na uzuri walilala wakiwa na mavazi yao yaliyolowana wakati wa mazoezi ya kwenye maji.
Baada ya dakika mbili walikuwa tena ufukweni na upepo wa fukwe ukiwachapa vema mwilini mwao.
"Nani kawaambia kuna kulala hapa? Tena mnalala bika kuoga. Nani kawaruhusu?" Ndilo swali la kwanza kuwauliza wale vijana na wakati huo radi na ngurumo za mvua zilikuwa zinatoa ishara zake. Hakuna aliyejibu swali la Luteni. "Basi kama mnajua sana kulala bila kuoga, laleni hapa. Na nitakayemkuta kalala, ni halali yangu." Akaondoka Gon na wenzake huku akiwaacha wale vijana wamekaa pale ufukweni na baada ya dakika tano, manyunyu ya mvua yalianza kudondoka na kusababisha baadhi ya wanajeshi kuanza kulia kama watoto.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Peter na Vanessa kwa wakati ule walikuwa hawakumbukani tena. Yale ambayo yanawakumba, yalikuwa ni sababu tosha ya kutokumbukana.
Vanessa akiwa kajikunja kwenye baridi ile, aliingiza mkono wake kwenye koti na kisha akatoa muhindi mkubwa na kuanza kuutafuna. Kuna jamaa alikuwa pembeni yake, naye akatoa paja la nyama ya kuku akaanza kulitafuna huku wengine wakilia na baadae kuanza kuimba nyimbo za jeshi.
Kamanda Bonito ambaye muda wote alikuwa haonekani katika upeo wa macho ya wale vijana, alisikia sauti za wanajeshi wakiimba nyimbo mbalimbali. Akatikisa kichwa juu, chini kukubali wazo lake la kuwaleta wale vijana sehemu ile.
****
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment