Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

PASIPOTI YA GAIDI 'HUJUMA NA UZANDIKI' - 5

 







    Simulizi : Pasipoti Ya Gaidi 'Hujuma Na Uzandiki'

    Sehemu Ya Tano (5)





    CASINO LAS VEGAS

    DAR ES SALAAM

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Briston alipotoka pale New Africa moja kwa moja alielekea katika Casino kubwa ya Las Vegas kwenye makutano ya barabara ya Hali Hassan Mwinyi na ile inayoelekea Ocean Road. Ndani ya Casino ile jioni hiyo tayari watu walianza kumiminika kwa starehe mbalimbali. Miongoni mwa waliokuwa wakiingia, Briston Kalangila alikuwa mmoja wapo akiwa sasa ndani ya suruali ya jinzi ya bei mbaya na fulana ya pundamilia iliyomkaa sawasawa, tambo lake kubwa lilimfanya aonekane kama mnyanyua vitu vizito.



    Mkono mmoja mfukoni na mwingine ukining’inia alivuta hatua na kupishana na warembo kadhaa waliokuwa ndani humo wakiuza na kujiuza. Ndani ya casino hiyo muda huo wa saa kumi na moja ya nje kule tayri ulikuwa usiku kwani mataa ya rangi rangi yalikuwa yakipishana kuupendezesha, gizale lilikuwa dhahir shahir. Akajivuta mpaka kwenya meza moja ya duara iliyokuwa na viti vine na katikati ya meza hiyo kulikuwa na mchezo wa ‘gurudumi la bahati’, haukupita muda aliongezeaka mtu mwingine naye alionekana kujaa mwili, walishahabiana kwa nukta chache kana kwamba walikuwa mapacha, naye akaketi palepale, huyu alikuwa maji ya kunde ukiachana na ukubwa wa mwili wake alikuwa na sura ndefu kiasi yenye pua nyembamba.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kamanda Amata alikuwa mmoja kati ya wateja wa casino hiyo jioni hiyo, baada ya kuingia nyuma kidogo ya Briston, aliketi kaunta akipata kinywaji na kumtanabahi kila aingiaye na atokaye, kutokana na ile sehemu aliyoketi aliweza kuona hayo yote. Alimwona anyemtaka, Briston. Yule ni nani? Akajiuliza baada ya kumuona huyo aliyeongezeka, akapiga funda moja la kinywaji, kisha akashusha ile bilauri na kuendelea kuangalia upande ule kwa chati. Baadae zaidi akaja mtu mwingine kati yao, huyu alikuwa wa kawaida tu lakini alikuwa mrefu, mwembamba, aliketi kati yao, wakawa watatu. Katika meza hiyo kulionekana kuwa na mazungumzo mazito yaliyoleta shida ya muafaka.



    Yote hayo Amata alikuwa akiyatengeneza kadiri anavyoona hali ya waliyonayo watu hao. Alijitahidi kupata japo pizza za hao wengine lakini alishindwa kutokana na nyendo za watu ndani humo na pia. Akainua simu yake kubwa na kuandika ujumbe mfupi kwa Chiba akimtaka kuwapo nje ya casino hiyo haraka iwezekanavyo na kumwelekeza watu ambao anataka awajue ni akina nani.



    Baada ya dakika kama arobaini na tano hivi, wale jamaa walionekana kumaliza mazungumzo yao, akatoka Yule mwembamba na kwenda zake huku Briston na Yule mwingine wakibakia. ya casino ile na moja kwa moja akaegesha gari yake mahala salama na ambapo angeweza kumwona kila atokaye ndani ya jumba hilo, akateremka na kuchukua lap-lap akaanza kuifuta gari yake kana kwamba anamsubiri mtu fulani.



    Chiba aliwasili nje ya casino ile na moja kwa moja akaegesha gari yake mahala salama na ambapo angeweza kumwona kila atokaye ndani ya jumba hilo, akateremka na kuchukua lap-lap akaanza kuifuta gari yake kana kwamba anamsubiri mtu fulani.



    “…mrefu, mwembamba, kava kofia ya pama,” ujumbe uliingia kwenye kifaa cha Chiba kilichopachikwa sikioni kwa ufundi kabisa, akaendelea kufuta gari yake mara hii upande wa nyuma ili apate nafasi ya kumwona mtu huyo. Lengo lake lilifanikiwa, alimwona mtu huyo akitoka ndani ya jengo hilo, akasimama ngazini na kuwasha sigara yake. Wakati huo Chiba alikuwa nyuma ya gari yake, akafanikiwa kupata picha ya mtu huyo kwa simu yake kubwa nay a kisasa. Picha tofauti kama kumi hivi mpaka kijana huyo alipokuwa akipanda gari yake na kuondoka, kilichomwacha Chiba kinywa wazi ni gari iliyokuja kumchukua, ilikuwa na namba za kibalozi. Namba zile Chiba alizitambua mara moja kuwa ni namba za ubalozi wa nchi ya Nduruta. Akatikisa kichwa na kisha akaendelea na shughuli yake. Mara akapokea ujumbe mwingine uliyomtaka kummulika anayetoka.



    “…Ana tambo kubwa kava suti kijani juu mpaka chini,” ujumbe ulitoka ka Kamanda Amata. Mtu Yule alijitokeza nje, akapitiliza na kuteremka zile ngazi mpaka chini kabisa, na kuingia kwenye gari oja ya kisasa. Chiba alikamata picha zote alizozihitaji na kuzihifadhi kadiri alivyotaka, alipohakikisha zote amezipata, akaingia ndani ya gari yake na kujifungia kimya. akisubiri...



    ***



    Baada ya wale watu kuondoka, Briston alibaki peke yake pale mezani, Kamanda Amata akateremka taratibu na kumwendea palepale alipo, akavuta kiti na kuketi. Briston akamtazama kijana huyu mwenye macho maangavu yanayoonesha kila aina ya udadisi.



    “Mbona wajikaribisha mwenyewe, kijana huna adabu…”



    “Haina haja ya kukuzungusha, naitwa Amata Ric au wengi huniita Kamanda Amata bila shaka umelisikia jina hili na kama la basi ndiyo mimi mbele yako,” Amata akamwambia Briston. Briston akajiweka sawa kitini na kumwangalia tena kijana huyu.



    “Nikusaidie nini Kamanda sijui kidudu gani sijui, huna kinywaji?” akamwuliza kwa kejeli.



    “Sina haja ya kinywaji maana ni vingi nyumbani kwangu. Briston Kalangila TNS 301,” Amata alipotamka namba ya kazi ya huyo mtu, Bristoni alihisi akili kumpaa kwa sababu raia wa kawaida hawajui namba hizo.



    “U-u-mesema unaitwa nani?” akauliza tena, sasa kwa makini zaidi. Amata akaondoa miwani yake usoni, akabandua mustachi mzuzu wake bandia nay ale masharafa akabaki wa kawaida. Briston akashusha pumzi ndefu, “Umekuja kwa heri au kwa shari?” akauliza kwa hofu iliyoonekana wazi.



    “Sijaja kwa shari, ni kwa heri tu maana wakati mwingine huwa tunapenda kufanya kazi katika mazingira kama haya, wanausalama saba na zaidi wameuawa ndani ya jingo la Ikulu na mke wa Rais ametekwa na wewe ulikuwapo lakini hukufanya lolote hili ndilo limenileta kutaka kujua,” Amata akamchokoza bila kumyumbisha.



    “Hivi we una wazimu? Wale jamaa walivyovamia pale ulikuwepo, unajua waliingia na silaha gani au zenye uzito gani?”



    “Mzee, hukuwa mtu wa kushindwa kuzuia uvamizi ule kwa jinsi unavyojua kuorganize watu, kumbuka Rais aliyepita alikuweka kwenye kitengo cha runners kwa sababu ya weledi wako wa kupanga na kutengeneza mambo,” Amata akaendelea.



    “Narudia tena, unajua silaha walizokuwa nazo na uzito wake, ulitaka wote tufe halafu nini kitokee? Si ushukuru hao saba sijui wangapi waliokufa, kama huna la kuongea nitokee hapa!” akaongea huku jazba ikipanda.



    “Najua, walikuwa na Assault Shotgun, shambulizi lao walitumia risasi sabini na tisa tu lakini zilizopatikana ni themanini na moja...”



    “Kwa hiyo hizo mbili zimetoka wapi?” Bristona akadakiza swali.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ndiyo hicho nataka unijuze, risasi mbili ni za bastola ya Magnum 22 na katika katia ya wanausalama wanaomiliki silaha hiyo mmojawapo ni wewe, na ambaye upo pale Ikulu muda mwingi. Moja imeokotwa kwenye mlango wa chumba cha silaha pamoja na maiti ya mtunza stoo hiyo, na nyingine imeokotwa kwenye mlango wa kuingilia katika apartment ya Rais, ina maana katia ya watu wetu waliouawa, wewe kwa mkono wako umeuwa wawili, na ni hao nimekutajia…” Amata alieleza bila kusitasita na kumfanya Briston afure kwa hasira, macho yake yalibadilika.

    Briston alikumbuka matukio hayo yakamrudiarudia kwenye kumbukumbu zake wakati huo, alijaribu kupingana nayo lakini ilishindikana, “Hivi umetumwa?” akauliza.



    “Ndiyo,”



    “Na nani?” akauliza.



    “Na mama yako!” Amata akamjibu huku akirusharusha yale maganda ya risasi katika kiganja chake cha mkono, kisha akayatia mfukoni na kunyanyuka, “Kazi njema Briston kalangila,” akamuaga naye akatoka eneo lile.

    Briston Kalangila, alimtyazama kijana Yule akiondoka pale mezani kwake kwa mwendo wa mikogo, akajichanganya na wateja wengine mpaka alipoishia kaunta. Kwa hasira akapiga ngumi mezani na kisha akainua simu yake na kuongea machache alipomaliza akatulia tuli, mara hii kile kinywaji kilikuwa hakipiti shingoni, mishipa ya kichwa ilimdinda na kijasgho chembembe kilitiririka ijapokuwa mashine za nguvu za kupoza hewa zilikuwa zikiwajibika kufanya hivyo.



    “Yes boss!” sauti ya kike ikasikika mbele ya Kalangila, akainua uso wake na kumtazama binti huyo, mwembaba wa wastani mrefu mwenye shingo nyembamba, sura ndefu, meno yake meupe yalipangiliwa vyema na Malaika aliyesadifu kinywa hicho.



    “Sikia Lulu, fanya unaloweza, umtie mkononi huyu mtu naujua ubembe wako hawezi kuchomoka kwani hakuna mwanaume ngangari mbele ya mwanamke mrembo labda awe hanithi,” muda huohuo akamtumia picha ya Amata kwenye simu na kumwacha Yule binti aende zake. Briston akanyanyuka na kutoka kwenye ile casino kuelekea nje.





    Kamanda Amata alikuwa wa kwanza kuiacha casino hiyo na kutoka nje, moja kwa moja aliiendea gari aliokuja nayo Cjoba na kuingia siti ya mbele akaketi huku Chiba akiwa nyuma ya usukani. Kimya hakuna aliyeongea, wote macho yao yalikuwa yakiangalia kule kwenye lango la casino hiyo. Briston akatokezea na kuteremka ngazi taratibu akaelekea kwenye maegesho na kuingia ndani ya gari yake kisha akaiwasha tayari kuondoka.



    “Sasa?” Chiba akauliza.



    “Tunamfuatilia mguu kwa mguu, yaani usiku huu mpaka tujue nini anafanya na ikiwezekana nitakwenda kuikagua nyumba yake…”



    “Nyumba yake? Vipi kama mkewe na watoto wapo huko?” Chiba akamkatisha na kumuuliza.

    “Usijali, kila kitu kitajulikana papo hapo,” akiwa katika kusema hayo, ile gari ya Briston ikapita mbele yao na kupunguza mwendo, kioo cha upande ule waliokuwa akina Amata kikateremka taratibu kisha Briston akawaoneshea dole la kati na kile kioo kikapanda taratibu huku ile gari ikiselelereka barabarani kulifuata lango la kutokea. Chiba akaweka mkono katika katika funguo ya gari tayari kuwasha, Amata akamzuia huku akimwonesha ishara ya kidole kuangalia kule katika lango la kutoke casino. Chiba akainua macho na kumwona mrembo aliyesimama huku akichezea simu yake.



    “Kaka tupo kazini kaka, achana na hayo, kila siku bibi yako anakuonya…”



    “Aaaa bibi yako keshazeeka, ye mwenyewe enzi zake alikuwa hivihivi. Kazi na dawa; huyu lazima nimkamate leo hii, cheki mtoto Yule,” Amata akaongea.



    “Kwa hiyo tunamfuata Briston au?” Chiba akauliza.



    “Ameshatujua, tukisubutu tu tumeisha, Yule hafai kabisa. Sasa ipo hivi, kanifanyie utambuzi wa hizo picha za hao jamaa wawili, mi niache na huyu mrembo,” alimaliza kusema hayo akiwa tayari nje ya gari hiyo. Chiba akawasha na kuondoka eneo lile.



    ***

    Briston usiku ule moja kwa moja alielekea hoteli ya New Africa ambako daima hukutana na kijana wake Kubra Khaleb. Wawili hao walikutana kwa dharula haikuwa imepangwa kuwa hivyo.



    “Vipi comrade?” Kubra akauliza.



    “Mpango umestukiwa?” Briston akajibu huku akilisaidia feni kumpepea.



    “Unasema! Mpango upi?”



    “Mcehzo wote wa Ikulu umegundulika…”



    “Nani kagundua wakati kazi ile tumeifanya kwa umakini wa hali ya juu?” Kubra aliwasiwasika kwa hilo.



    “Sikiliza Kubra! Tulifanya kwa weledi wetu wote, lakini kuna watu wana vichwa vya ajabu, huyu jamaa tusipomdhibiti sasa tumeumia na anatufuatilia nyayo kwa nyayo,” Briston akaeleza.



    “Unafikiri atajua yote?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Kubrah! Kama kagundua kuwa silaha za waasi zilikuwa zinatoka Ujerumani na mpaka digala mwenye kamjua na kapambana naye, unafikiri hatojua kuwa mipango hii yote ina lengo moja? Sasa keshajua kilichotokea ndani ya Ikulu, keshanijua mimi, bila shaka keshakujua wewe. Na leo nimekutana na Kepteni Banzilahagi pamoja Kimosa Kabalege Yule afisa wa ubalozi katika idara ya usalama, sasa hapa sijui kama kawaona au vipi, maana baada tu ya kuondoka wale jamaa na ye akaja mezani kwangu…”



    “Ha! Yaani kaja mpaka mezani kwako umemwachia? Huku na silaha?” Kubrah akang’aka kuuliza.



    “Kubrah, nilikuwa nahitaji kujua nini anakijua juu ya hili, nimeona anajua lakini hasa ni swala la uvamizi zaidi ya hapo hakuna anachokijua,” akaeleza.



    “Good! Sasa inabidi tumdhibiti usiku huu,” Kubrah akaeleza mpango.

    “Ni sawa, kazi nimempa Lulu, nina uhakika atalifanikisha, akimpata atatupigia ili tukamalizie kazi,” akamwambia Kubrah.



    ***

    “Oooh una jina zuri sana Lulu, yaani kitu chenye thamani sana ambacho kwanza hakipatikani kirahisi,” Amata alimwambia mrembo huyo wakati akiwa naye ndani ya gari.



    “Mmmmmh maneno yenu tu hayo,” Lulu akajibu.



    “Napenda nikapitishe usiku huu na wewe,”



    “Waoh! Is it possible?” Lulu akatia shaka.



    “Hauamini?”



    “Siwezi kuamini moja kwa moja kwa sababu, umekaa pale ndani hata kumpapasa mwanamke yoyote hujajaribu…” Lulu akaeleza.



    “Uliniona?”



    “Aaaa sana, sisi huwa tuna macho mia…



    “Nyinyi na nani?” Amata akamkatisha.



    “Ah we! Tuko wengi tunafanya shughuli zetu hapa,” Lulu akaeleza huku macho yake akiyapeleka nje.



    “Nimekuchagua wewe, mrembo, unapenda tukamalizie usiku huu wapi? Nyumbani kwangu?” Amata akauliza huku mkono wake tayari ukipapasa paja la mrembo huyo, taratibu kutoka kwenye goti kuelakea pajani.



    “Nyumbani kwako namwogopa mkeo,”



    “Sina mke!”



    “Basi mpenzio,”



    “Ah… hapana sina mpenzi, nimekuchagua wewe leo…”

    “Napenda New Africa,” Lulu akachagua. Amata akaondoa mkono wake pajani mwa Lulu, akakamata gia ya gari huku mkono wa kulia ukitekenya ufunguo na gari hiyo ikawaka, akaweka gia namba moja na kuondoka taratibu.

    Iliwachukua takribani dakika kumi na sita tu kuwasili New Afrika, Kamanda Amata akangiza gari maegeshoni na kushuka na membo huyo akiwa mkono wake wa kuume kauzungusha kiunoni mwa mrembo huyo huku mabusu ya hapa na pale yakiendelea.



    “603,” mwanadada wa mapokezi alimtajia namba ya chumba huku akimkabidhi kadi maalumu ya kufungulia mlango wa chumba hicho.



    “Nahitaji whisky tafadhali…”



    “Mmmmh na Amarula!” Lulu akaongeza huku wakiondoka pale mapokezi na kumwacha Yule mwanadada akishughulikia hilo.

    Ndani ya chumba hicho Amata alimbwaga Lulu kitandani na kuanza kumpiga mabusu mazito ya kinywani huku Lulu naye akionesha ufundi wa hali ya juu katika kuumung’unya ulimi wa Amata. Kengele iliyogongwa mlangoni iliwaachanisha wawili hao na Amata akauendea mlango na kupokea vinywaji walivyoagiza. Lulu aliinuka na kpekua pochi lake, akatoa simu ndogo na kubofya haoa na pale na wakati huo Amata alikuwa amekwisha fika.



    “Achana na simu dear!” akamwambia.



    “Aaaa ndiyo nilikuwa nazima ili tule raha kwa raha, naomba nimalizie process basi,” Lulu akaongea kwa sauti ya kubana pua, Amata akamruhusu naye akabofya ‘send’ kisha akazima simu na kuitupa pembeni.



    ***

    Madam S alibaki akizunguka zunguka huku na huko, kichwa chake kilionekana kuchanganyikiwa wazi kabisa.



    “Chiba simaini unachoniambia kabisa, una uhakika na hilo jambo?” akauliza.



    “Bila shaka Madam, Amata aliniita kufika pale Las Vegas name nikafanya hivyo, na akanipa hizo ishara nikakamata picha za hao watu, nimezicheki hapa kwenye mtandao wetu na majibu ndiyo hayo,” Chiba akaeleza.



    “Banzilahagi, Kepteni wa Jeshi la Wananchi tena ana kitengo nyeti sana jeshini, kama atakuwa ndani ya mpango huu tumekwisha na katika hili lazima tuchukue hatua ya haraka sasa hivi, huyo Kimosa Kabalege naye pia!” Madam akazungumza huku akivuta kiti na kuketi, “Kamanda yuko wapi?” akauliza.



    “Aaaaa nimemwacha viungani ana misheni nyingine,” Chiba akajibu huku akibana kicheko kilichojionesha wazi mashavuni mwake.



    “Unacheka nini? Au unamfichia siri? Sema tu kama yuko na mwanamke, maana Yule sijui ana ugonjwa yaani sielewi…”



    “Aaaa hayo umesema wewe Madam mi husiniweke hatiani,” Chiba akamaliza kusema huku akiifunga kompyuta yake.

    Madam S akainua simu yake ya mkononi na kubofya namba Fulani kisha akaweka sikioni mwake kwa sekunde kadhaa,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapatikani…” akashusha simu hiyo na kupiga namba nyingine, akaweka tena sikioni.



    “Gina! Hello!” Madam alipoita jina hilo Chiba akafumba kinywa chake kwa hofu, anaharibu lo! Akawaza.



    “Uko wapi? (…) ok, sasa nataka uhakikishe unamchunga mtu anayeitwa Banzilahagi Yule kepteni wa jeshi, anaishi Makongo plot namba 703, nipe kila dondoo za nyendo zake,(…) ok vyema, fanya hivyo,” akamaliza na kukata ile simu. Chiba akashusha pumzi huku mikono sasa ikiwa kiunoni. Kisha akabofya namba ingine na kuweka sikioni.



    “Scoba! Unasomeka wapi? (…) ok! Nimekupata, sasa ipo hivi, nataka uweke jicho katika nyumba ya Afisa Baalozi Kimosa Kabalege na unipe dondoo zote za nyendo zake usiku huu na mpaka nitakapokupa amri nyingine,(…) ok, ok!” akakta simu na kuketi.



    “Naona mbananisho umeanza,” Chiba akamwambia Madam huku akiitazama saa yake.



    “Inabidi tufanye kazi kwa mtindo huo kwa kuwa mpaka sasa hawa tunawashuku,” akajibu Madam S.



    ***

    Lulu alimwonesha manjonjo ya kutosha Amata kitandani hapo, ilikuwa shughuli nzito ukizingatia walikuwa tayari wametanguliza kinywaji. Lakini ghafla, Amata alichomoka kutoka kitandani na kumwacha mwanamke Yule palepale, akaketi kiatandani.



    “Vipi jamani, unanikatisha utamu!” Lulun akalalamika. Amata akamwoneshea kiganja chake cha mkono kumuashiria anyamaze. Akaingiza mkono wake chini yam to na kutoa bastola, akavuta slider yake na kuiachia, risasi moja ikakaa sawa, kwa haraka akavaa bukta na kusimama pembezoni mwa kabati.



    “Kuna nini?” Lulu akauliza.



    “Shhhhhhh!!!!” akamwaonesha kwa kukiweka kidole juu ya midomo yake. Kisha akanyata na kuliendea dirisha na kujibana sawia pembeni yake. Dirisha lile likavutwa polepole kufunguliwa na mkono wenye bastola ukajitokeza kule pale kitandani, Amata akaiweka bastola yake pembeni na kwa kasi ya ajabu akakukamata mkono wa Yule mtu na kuukunja.



    “Aaaaaiiggghhh!” ule mkono ukateguka mifupa, akamvuta ndani kwa nguvu na yule jamaa akaingia na kioo cha dirisha, alipoingiza shingo akampa pigo moja kali la karate na yule jamaa akatua ndani kama mzigo na bastola ikimtoka mkononi na kuselereka mbali. Lulu akakurupuka kitandani na kupiga sarakasi moja maridadi akainyakua ile bastola. Amata hakutegemea kile kitendo alipogeuka tu, risasi moja ilipita karibu kabisa na uso wake na kufumua kioo cha dirisha. Akjitupa kwa nyuma na kukoswa na risasi nyingine kutoka kwa Lulu, Amata akainyakuwa bastola yake lakini kabla hajaishika vizuri, Lulu aliilenga kwa risasi na kuiondoa mahala pale, Amata akaikosa. Shabaha ya Lulu ilimshangaza Amata, akaona akizubaa na kudharau kwa kuwa mwanamke anaweza kuaibika. Aliinua taa ya mezani na kumrushia kwa nguvu, ikampiga usoni, Lulu akapoteza mwelekeo, wakati akijiandaa kufyatua risasi yake akajikuta akikutana na miguu mizito ya Amata iliyotua tumboni mwake na kumfanya ajibamize vibaya ukutani. Amata akajiinua lakini kabla hajawa wima, aliliona teke kali la mwanmke huyo likija usoni mwake, akaepa na mguu ule ukapita wakati huo na yeye akauzungusha wa kwake na kuupiga kwa chini wa yule mwanamke uliobaki wima sakafuni, akamchota ngwala maridadi na kumbwaga vibaya.



    “Mhhhh! Aaagh! Mpenzi unaniua?” Lulu akalalama huku akijaribu kujiinua. Amata akamwahi na kumkamata night dress yake akampiga kichwa kimoja maridadi na Lulu akalegea na kusihiwa nguvu, Amata akamsukuma na kupigiza ukutani, akaanguka kando akiwa hana fahamu na damu zikitiririka katika tundu za pua yake. Amata akamwacha pale chini na kuiendea suruali yake, akaivaa haraka na fulana yake ikafuta juu yake, bastola yake akaibana sawia kiunoni mwamke kisha akamwendea Yule jamaa aliyemwacha pale usawa wa dirisha baada ya kipigo kile akampekua na kumkuta na simu tu mfukoni mwake, akaichukua na kubofya kidubwasha cha kupigia kisha akaitoa loki yake na kupekuwa kwenye boksi la ujumbe mfupi.



    ‘…hakikisheni huyo Malkia anahifadhiwa vyema, safari inakaribia alfajiri ya kesho…’



    Baada ya ujumbe ule ukafuatiwa na mwingine ukisema…



    ‘…wapo chumba namba 603, muue mwanaume, mwanamke tuachie…’



    Amata akatabasamu kwa ujumbe ule na alipouchunguza akagundua kuwa ulitumwa na mtu mmoja kwa tofauti ya muda wa saa moja, akaujibu ule wa pili kwa kutumia simu ileile, akajua wazi wakiupokea ujumbe huo lazima hao walioutuma wachanganyikiwe.



    ‘…nimekufa mimi…’



    Kisha akautuma na kuitia ile simu mfukoni, akaunyakua mkoba wa Yule mwanamwali na kumwaga kila kilichopo, akakuta mashine ndogo ya kurekodi sauti, akaichukua zaidi ya hapo hakukuwa na kingine cha maana za ya kijitabu kidogo cha anwani za watu akakichukua na kutoka ndani ya chumba kile haraka, badala ya kutumia lifti kuteremka mara hii akatumia ngazi za kawaida tena isitoshe ngazi za dharula kwani alihofu kukutana na watu asiowatarajia, moja kwa moja akaiendea gari yake lakini kabla hajaifikia, alipojitokeza tu upande wa pili wa hoteli ile kutokea nyuma, alimwona kijana mmoja akiwa usawa wa tairi la mbele akifanya jambo Fulani kwenye gari hiyo. Amata akajificha na kuangalia kila kitu kwani alihofia hicho anachofanya kijana huyo. Baada kama ya dakika mbili hivi Yule kijana akatoka na kuliacha gari la Amata kisha akaingia kwenye gari kama ya tano hivi katika maegesho yale.



    Amata akafikiri moj na mbili, akapita kwa haraka nyuma ya gari zile, na kuiacha ile ya kwake, akiwa anakimbia huku kainama aliliifikia ile gari Toyota Mark II na kuchukua fungua yake yenye uwezo wa kufungua kila kitasa cha gari, akafungua buti na kujitia ndani kisha akafunga na kuacha nafasi ndogo ya kupata hewa, akatulia kimya.

    Ndani ya gari hiyo kulikuwapo vijana watatu, nao walikuwa kimya muda wote hakuna aliyeongea ila tu mitikisiko ya gari kila walipojigeuza. Baadae akasikia mmoja akijikohoza na kufuataiwa na kauli.



    “Asee huyu jamaa vipi hadi sasa!” mmoja akasema.



    “Dakika kumi sasa, sio kawaida maana tunachelewa,” mwingine akajibu kisha ukimya ukatawala tena.



    “Mpe taarifa Master juu ya hali hiii kisha yeye atatuambia la kufanya,” mtu wa tatu akatoa wazo na mara hiyo Amata akasikia mlio wa batani za simu akazisikiliza kwa makini sana ili aweze kugundua ni namba gani iliyopigwa, akatikisa kichwa baada ya kuona kasahau baadhi ya milio, hii anaweza Chiba, akajisemea moyoni. Lakini aktega sikio kusikiliza nini kitaongelewa.



    “Ee Master, jamaa hajarudi hadi sasa tuchukue hatua gani?” akauliza. Kisha ukimya ukafuata, Kamanda Amata akajua kwa vyovyote mtu wa upande wa pili atakua akiongea.



    “Sawa! Master,” kisha ukafuatwa mlio wa simu kukatwa. Amata akainua simu yake taratibu na kutuma ujumbe mfupi kwa kampani yake kuwajulisha kinachoendelea.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Huyu jamaa naye mbona haji? Au bado anakula raha, mh! Leo Lulu anal oleo,” mmoja wao katika gari ile akawaambia wenzake mara Amata akasikia mlio wa simu inayoita.



    “Yes! Ndio… he! Ok sawa!” Yule jamaa akaongea hayo katika simu kisha ile gari ikawashwa na kuondolewa mahala pale. Amata akaangalia kwenye uwazi mdogo wa buti hilo akaoana kuwa bado hawajaiacha hoteli ile na baadae wakaingia barabara ya Maktaba.



    ***

    Briston alitikisa kichwa akamwangalia Kubrah.



    “Ametuweza mshenzi huyu!” Bristona akasema.



    “Na mimi nimemuweza, subiri usikie,” Kubrah akajibu na kumfanya Briston kumtazama, “Mbona unaniangalia?” akamuuliza.



    “Umesema umemuweza?”



    “Ndiyo, we sikiliza tu ndani ya saa moja lijalo, nimemuwekea motto katika gari yake akiingia tu puuuuuu!” Kubrah akasema kisha wote wakaangua kicheko lakini Briston akanyamaza ghafla.



    “Vipi?” Kubrah akauliza.



    “Nasikitika kwa kifo cha huyu jamaa na Lulu, inabidi tuwe tayari, kesho asubuhi tukimuondoa Malkia na sisi tuondoke kisha plan B ichukue nafasi kwa kuwa kule Mpumbutu jamaa wameshaharibu na Mkuu wa wakuu amekasirika sana, anataka kuongea na huyu Rais wa hapa, sikia tutakuwa na kikao kizito pale Cape Town juu ya hili haraka iwezekanavyo,” Briston akamwambia Kubrah.



    “Tuondoke, tushughulike na huyu kimburu,” Kubrah akasema.



    “Hayuko peke yake, wako kama wane hivi, wote lazima washughulikiwe,” Briston akiajbu huku akifungua mlango kutoka. Nje ya hoteli hiyo kila mmoja alichukua gari yake na kuondoka. Lakini Kubrah aliitazama sana gari ya Amata na akaiona ikiwa palepale, ina maana huyu mshenzi bado yupo humu ndani? Akajiuliza. Na taratibu akaondosha gari yake pale hotelini huku akimwagiza mmoja wa vijana wake kuiangalia ile gari mpaka itakapoondoka.



    ***



    Ile gari aliyopanda Amata iliingia ndani ya majengo yasiyokwisha ambayo bado yalikuwa yakiendelea na ujenzi, ikaingia na kufika mahali ndani ya kitu kama chumba hivi. Ikasimama na milango ikafunguliwa huku wale jamaa wakiteremka hai hai.



    “Vipi huko?” mtu mmoja aliyeonekan kama mlinzi aliuliza.



    “Jamaa kauawa bwana na tunayemsaka inaonekana katoroka eneo lile,” akajibu mmoja wa walioshuka kwenye ile gari.



    “Kwa hiyo tunafanyaje?”



    “Mpango ni uleule, kesho asubuhi, tunaondoka na Malkia na kuelekea kisiwani kwani mpango mwingine unatakiwa kuchukua nafasi, weka kila kitu sawa kama mpango ulivyo,” akatoa maagizo ambayo Amata alikuwa akiyasikia vyema. Kwa kutumia simu yake akatuma ujumbe mfupi kumpa Madam S juu ya hayo anayoyasikia. Kisha akatulia palepale kusubiri watu hao watoke eneo hilo ili naye aweze kujitokeza na kufanya yake.



    IKULU

    USIKU UOHUO



    SIMU YA RAIS iliita kwa fujo, mheshimiwa bado alikuwa hajalala na wala hakuwa hata na lepe la usingizi, alipoitazama akajua ni ile simu nyeti ambayo huweza kukaa zaidi ya siku tatu bila kuita isipokuwa kwa jmabo muhimi na la kiusalama tu, akaitazama na kuona kwenye kioo TSA, akaiweka sikioni mara moja.



    “Taarifa kutoka TSA juu ya usalama wa taifa usiku huu, naomba kikao cha dharula kama inawezekana,” upande wa pili ukasubiri jibu. Bila kusita Mheshimiwa Rais akakubali kikao hicho usiku huo akakata simu na kutoa taarifa kwa wanausalama wachache juu ya ujio wa Selina ndani ya jingo hilo jeupe.



    Saa tisa usiku, mwanamama huyo aliwasili Ikulu na kupokelewa na mtu alioyeandaliwa na moja kwa moja alifikishwa kwenye ofisi ya Rais kwa mazungumzo.

    “Kwanza samahani kukukatisha usingizi,” akaanza kwa kusema hivyo.



    “Hapana Sellina, siwezi kupata usingizi kwa hali hii ambayo inanikabili, na najua ni wewe tu kwa sasa unaeweza kunipa jibu ambalo litanifariji, nipe maendeleo ya kazi niliyowapa,” Rais akamwambia kisha akatulia kitini.



    “TSA tupo kwenye uchunguzi wa hali ya juu sana katika swala la uvamizi wa Ikulu uliofanyika hapa na tumeshagundua mambo mengi sana kuliko unavyotarajia kusikia…”



    “Enhe…”



    “Kwanza kabisa, mkuu umezungukwa na maadfua kila kona ndani ya idara zako na nchi yako kwa ujumla. Uvamizi wa Ikulu ulipangwa na watu walio chini yako kwenye idara nyeti za uslama…” akamweleza kila kitu lakini hakutaja wahusika wa tukio hilo. Mheshimiwa Rais alikuwa katika hali ya hasira na uchungu alipokuwa akipokea taarifa hiyo fupi lakini iliyojaa utaalam wa kikachero wa hali ya juu, moyoni mwake alimshukuru aliyekuwa na wazo la kuanzisha idara hii ambayo sasa anaielewa umuhimu wake.



    “Sasa kuna watu ambao wapo chini ya jicho letu na tunahitaji kuwakamata mara moja ikiwezekana kwa amri yako usiku huu, hawa watatueleza vyema juu ya mpango mzima tangu mwanzo na nani anahusika,” Madam Sellina akaeleza na Rais akalipokea kwa kutikisa kichwa akiashiria kuwa amekubaliana naye. Lakini mpaka hapo hakuwa anajua ni nani na nani.



    “Nani na nani?” akauliza.



    “Wa kwanza ni Kepteni Benzilahagi…”



    “Kepteni? Wa jeshi au wa meli?” akauliza kwa hamaki.



    “Bora angekuwa wa meli, ni wa jeshi tena JW, tunamshuku kutokana na nyendo zake siku hizi, baadae nitakujulisha nyendo hizo lakini sio leo kwa sababu za kiusalama. Mbaya zaidi mtu huyu yupo kwenye kitengo nyeti sana ndani ya jeshi letu, nikiwa na maana kuwa anajua kila kitu, kila siri, kila mpango wa jeshi letu. Ni msaliti…”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Akamatwe na ahojiwe mara moja!” Rais akatoa amri na kupiga ngumi juu ya meza baada ya kutajiwa kitengo cha mtu huyo.



    “Na wa pili nani? Nataka kumjua!” akang’aka mheshimiwa.



    “Wa pili ni afisa ubalozi wa Nduruta anaitwa Kimosa Kabalege, sasa kwa huyu tulisita kwa sababu za kidiplomasia,” Madam S akaeleza.



    “Kamata, weka ndani ahojiwe. Sellina unataka kunambia hii ni njama kutoka Nduruta?” akauliza Mheshimiwa Rais huku akionekana wazi kuhamanika kwa mpango huo.



    “Ndiyo Mheshimiwa, kumbuka umeamuru vikosi vyako vya JW kuvaa kofia ya UN na kwenda kuendesha operesheni dhidi ya waasi wa X65, waasi hawa kwa uchunguzi wetu ni watu wa Rais Sebutunva wa Nduruta na washirika wake ambao siku hizi umeona wakikutenga katika mambo mengi ya ki-kanda. Tumegundua kwamba wafadhili wakubwa wa waasi hawa ni vyama vyenye mlengo wa kushoto huko Ughaibuni, kwa biashara ya mabadilishano wa vitu wao hupeleka Almasi na kupewa silaha nzito na za kisasa. Hivyo basi kama kisasi kutoka kwa jirani yao Sebutunva ndiye aliyefanya mipango yote ya kutekwa kwa First Lady akishirikiana na watu ambao ni mapandikizi ambao kila siku unakula na kunywa nao…”

    “Stop!!! Ishia hapohapo Sellina. Sasa nimeielewa TSA na kazi yake, mmefanya kazi kubwa sana na je habari zozote juu ya mke wangu?” akauliza kwa shauku.



    “Ninavyoongea na wewe hapa tupo kazini, na kwa kuwa tulikwambia ni saa sabini na mbili tutakuwa na jibu, nakuhakikishia tuko mbioni kumpata First Lady katika saa zizi hizi,” Madam S alimhakikishia Sellina hayo asemayo. Baada ya dakika chache zilizofuata waliagana huku...



    Oda ya kukamatwa Kepteni Benzilahagi ilifika makao makuu ya jeshi, Upanga. Usiku huohuo polisi wa jeshi, sita walikuwa ndani ya Nissan Patrol ya kijani wakielekea nyumbani kwa Kepteni huyo, walitumwa kazi moja tu, kumkamata Benzilahagi na kumpeleka walikoamriwa.

    Scoba alisthuliwa na simu iliyokuwa ikifanya fujo mfukoni mwake alipoikwapua alikutana na TSA 2.



    “Sema namba 2,” akaitikia.



    “Kuna jamaa wanakuja hapo, waache wafanye kazi, kutoka ulipo hakikisha tu operesheni imekwenda sawa wala usitie nguvu yoyote,” Chiba akamaliza.



    “Copy!”



    Alipoishusha simu hiyo aliona taa za gari zilizowashwa full zikicheza na kuyumbayumba akajua moja kwa moja kuwa hiyo gari iko kasi sana kupita maelezo.



    ***

    Kepteni Benzilahagi aliiweka vizuri bastola yake ikiwa full, akaipachika kiunoni mwake na kuvaa fulana yake pull neck pamija na jinzi yake nyeusi. Akaketi kitako akinywa pombe kali makusudi kusubiri kile anachokitarajia. Muungurumo wa gari ulimuondoa pale kitini, akasimama na kujiweka vizuri kitini huku simu yake iliyokuwa sikioni. Kengele ya mlango ikafuatia, akasimama na kuelekea mlangoni hapo, macho kwa macho akakutana na MP waliovalia kijeshi wakiwa kamili na barua yao mkononi ya kumkamata.



    “Mmetumwa kunikamata mimi?” akawauliza huku akiwarudishia ile karatasi.



    “Ndiyo, tunavyoongea hivi sasa unatakiwa kuondoka nasi,” wakamwambia.



    “Kwa kosa gani hasa?”



    “Kosa utalijua hukohuko ukifika,” wakamueleza.



    “Sawa hakuna tabu, nipeni dakika moja tu nimuage mama watoto kisha nakuja,” akawaambia, nao wakamruhusu na kumsubiri palepale. Benzilahagi akatembea kwa mikogo huku akipiga mluzi kuelekea chumbani.



    “Suzi! Suuuuzi! Mi naondoka Suzi naenda kazini…” akaongea huku akiingia chumbani na kuufunga mlango nyuma yake. Pumbavu sana, subirini hapohapo narudi, akasema kwa sauti ya kujisikia mwenyewe moyoni. Akavuta kabati kubwa na kulisukuma pembeni kisha akatoa funguo zake na na kufungua mlango uliokuwa nyuma ya kabati hilo, alipoingia ndani ya kijichumba hicho, akarudisha lile kabati palepale na kuufunga mlango kisha akateremka ngazi zinazokwenda chini kisha akapita kwenye kitu kama andaki na kutokea nje ya ukuta kulikokuwa na kitu kama chemba ya maji taka. Alipomaliza kuurudishia ule mfuniko wa chuma, akajipukuta vumbi na kutokomea katika majumba ya jirani.



    “Asee huyu jamaa anaaga kwa maneno au kapanda kitandani kabisa?” MP mmoja akauliza.



    “Ah kweli hebu tumfatilie hukohuko dakika kumi sasa,” mwingine aliyekuwa kiongozi wao akawaambia kisha akawaongoza kuingia ndani ya jumba lile, walipoufikia lango wa chumbani, wakagonga, kimya, hakuna jibu wakagonga tena na tena, kimya kilekile kikaendelea. Alipousukuma, ukafunguka, wakaingia chumbani, wakatanabahi hakuna mtu, kitanda tupu.



    “Unataka kusema kaondoka hapa hapa?” mmoja akauliza huku akitupa godoro upande wa pili, hakuna mtu. Mwingine alikuwa akipekuwa makabati bila mafanikio.



    “Jamaa katoroka, lakini kapitia wapi? Mbona hakuna mlango humu? Atakuwepo tu mumu humu. Dakika ishiririni ziliwachukua kupekua chumba hicho lakini hawakuona mtu wala nyau.



    “Ni aibu, tumewezwa!” Yule kiongozi wao akaongea huku mikono ikiwa kichwani na wakati huo akitoka nje ya chumba kile, “Hebu zunguka nyumba muifanyie ukaguzi huko nje,” akaamuru na vijana wake wakafanya hivyo.



    ***

    Scoba akiwa ndani ya gari yake ametulia tuli, aliona kitu kama kivuli kikipita nyuma ya ga ri hiyo, alipogeuka akamwona mtu, mwanaume anayeishia kizani. Machale yakamcheza, akainuka na kuufungua mlango taratibu kisha akafuata njia ile ambayo yule kijana aliingia. Kona ya kwanza nay a pili akasikia mlio wa injini ya gari iliyokuwa ikiwashwa na gari ile ikaondoka zake. Scoba akajikuta anashindwa la kufanya kwa wakati ule, akarudi haraka kwenye gari yake na alipoiwasha na kuigeuza akasimamishwa na wale MP.



    “Teremka chini ukiwa mikono kichwani,” akaamuriwa. Scoba akateremka na kusimama akiwa mikono kichwani. Wakampekua harakaharaka na kumwacha pembeni.



    “Unafanya nini hapa usiku huu?” mmoja akauliza.



    “Kuna mtu namsubiri,” akajibu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haujaona mtu kapita hapa sasa hivi?”



    “Nimemwona, alitokea upande huu!” akajibu.



    “Kaenda wapi?”



    “Kapita hapa hivi kaingia upande wa pili,” akawaelekeza na wale MP wakalekea upande ule, alipohakikisha wamepotelea kizani akawasha gri na kuondoka kwa kasi kuelekea upande ule ambao Benzilahagi amekwenda na gari, akajaribu kuifuata bila mafanikio, Kepteni Benzilahagi alikuwa ametoweka.



    ***

    Ukimya ukatawala, Amata akasukuma juu mfuniko wa buti lile, kwa uwazi mdogo akatazama nje hakuona kitu zaidi ya giza. Wameondoka, akawaza na kufungua lile buti kisha akatoka na kulifunga taratibu, akanyata na kujibanza kando ya pipa moja lililojaa zege ndani yake. Hakukuonekana kitu kingine zaidi ya giza lile na miale hafifu ya taa za nje iliyokuwa ikipenya kati ya uwazi na uwazi. Ijapokuwa kulikuwa na giza lakini Amata aliweza kuona kwa taabu mlango wa bati uliokuwa umerudishiwa tu, akavuta hatua mbili tatu na kuufikia alipotaka tu kuugusa akasikia michakacho ya hatua za binadamu kutoka upande wa pili wa mlango ule ambao ulikuwa haujafunga kabisa na kuruhusu nafasi kama ya milimita tano hivi kuwa wazi, akarudi na kujificha nyuma yake, akasubiri.



    “Tizo!” sauti ikaita kutoka ndani.



    “Sema we!” Tizo akaitikia. Amata akatikisa kichwa baada ya kujua kuwa jina la huyo kijana ni Tizo.



    “Usichelewe kaka, digala anatia timu sasa hivi ili tucheki mpango wa kesho,” ile sautin ikatoa maagizo.



    “Poa poa,” akajibu huku akiufungua ule mlango, akatoka na kuurudisha tena nyuma yake kisha akavuta hatua kuelekea kwenye lango kubwa la chumba kile.

    Kutoka alipojificha Kamanda Amata akapiga mruzi wa taratibu uliomfanya Tizo asimame pale alipo, kabla hajajua nini kinaendelea, alijikuta akipata pigo zito lililotua katikati ya paji lake la uso, kisha Amata akamdaka kabla hajafika chini. Tizo alikuwa hana fahamu, Amata akamburuza taratibu na kumpakia kwenye ile gari, ndani ya buti na kumfungia. Kisha moja kwa moja akauendea ule mlango na kuufuangua, kelele za ule mlango zilimfanya Amata kuganda kama kapigwa shoti ya umeme. Sekunde kadhaa mbele, akateremka ngazi zilizokuwa zikielekea chini ya jingo hilo na huko akakutana na mlango mwingine mzuri tena isitoshe ni wa kisasa. Akautazama kwa jicho lake la kikachero, kwa maana mlango huu haukuwa na kitasa.



    Chini yake kulikuwa na zuria zito, akalikanyaga na ule mlango ukafunguka, Amata alipitisha jicho harakaharaka na kuona ndani kile chumba kuna nini. Watu wawili walikuwa wamekati katik sebule safi, mmoja mwafrika na mwingine alikuwa na asili ya kichina si kichina, kifilipino si kilipino, alikuwepokuwepo tu. Akiwa katika kutafakari, akaona mtu wa tatu akiongezeka akiwa na vinywaji mkononi. TSA 1 akaitazama saa yake, saa zinayoyoma, karibu alfajiri itanikuta, akawaza kisha akapenyeza mkono katika mlango huo na kuupeleka upande wa kushoto kuitafuta swichi ya taa hiyo maana alijuwa kuwa kaatika sheria za mafundi umeme za kimataifa swichi ya taa huwekwa upande tofauti na ule ambao mlango hufungukia. Akaipata na kuibofya.



    “Ta!” mlio huo wa swichi ukafuatiwa na giza nene.



    “Aaaaa shittt! Tanesco! Hili shirika bora wabinafsishe tu, namna hii!” mmoj wa wale jama akapiga makelele. Amata kama umeme akajirusha ndani na bastola mkononi, akajibiringisha na kutua kwenye kona aliyoitaka. Risasi ya kwanza haikufanya kosa, ikavunja bega la mmoja wao, ile ya pili ikafumua kichwa cha mwingine. Taa zikawaka, Amata akageuza macho mlangoni na kuona domo la bastola likimtazama, akajikunja na kuruka back akiziacha risasi za bastola hiyo zichimbe ukuta wakati yeye keishatua upande mwingine.



    “Ah! Ah! Ah! Umejiingiza kwenye domo la mamba siyo?” Yule kijana aliyeonekana kujazia mwili wake akamwambia Amata,



    “Nilijua hutoweza kupafahamu hapa kumbe wewe mtundu sana kama nilivyopewa taarifa, sasa leo utaishia humu humu,” akaongeza huku bastola yake bado ikiwa mkononi.



    “Nini kimekuleta kama si kifo chako?” akauliza.



    “Nimemfuata First Lady,” Amata akajibu akiwa bado nyuma ya meza alikojificha baada ya ile sarakasi maridadi.



    “First Lady! Unajua sisi tulivyomchukua tulikuwa wangapi? Na unajua mbinu tuliyoitumia? Halafu wewe uje peke yako ukiamini kumpata. Kwa taarifa yako na alfajiri hii anaondoka anapelekwa hukooooo akale honeymoon!” Yule jamaa mawnye asili isiyo rasmi akasema. Amata kwa jicho lake la kikachero aligundua kuwa huyo jamaa aliyesimama kama mita tano hivi mbele yake alikuwa hatazami upande ule isipokuwa mwingine, akageuza jicho kwa chati na kumuona Yule aliympiga risasi ya bega akiwa anachomoa bastola yake taratibu, akasubiri mkono wake ukae sawa kiunoni na lilipotimia hilo, alijirusha na kumtandika teke la usoni, mguno wa uchungu ukasikika, kwa kasi ya ajabu Amata akaiweka sawa bastola yake na kuifumua taa, giza likarudi tena na milio ya risasi ikasikika huku na huko.



    “Umeniua bro!” sauti ilisikika kutoka pale chini, Amata akajua tayari washauana wenyewe kwa wenyewe.



    “Nikikutia mkononi wewe nyau utajua kilichomtoa kanga manyoya,” Yule jamaa akaunguruma kwa hasira.



    “Huwezi, na sasa nataka unieleze ni wapi alipo First Lady!”



    “Ha! Ha! Ha! Ha! Kweli huna akili nah ii ndiyo kwa heri yako,”

    baada ya ile sauti kumaliza maneno yale, Yule jamaa akaanza kupiga risasi ovyo ndani ya ile sebule huku akipiga na kelele za kutisha. Amata alijikunyata kimya kwenye moja ya kuta ambapo palikuwa na kabati kubwa la vitabu, risasi nyingine zilichimba kuta, nyingine zikapita karibu na kabati hilo, Amata alikuwa akiomba dua tu zisifike pale alipo. Risasi zile zilipotulia, harufu ya baruti ilitawala.



    “Aaaaaaaa hauna ujanja ushakufa wewe!” ile sauti ya Yule jamaa ikaendelea kutamba huku Amata akiskia hatua nzito zikivutwa kwa upole, akaendelea kutulia kuona kama mtu huyo atafika eneo lile. Punde tu mwanga wa kurunzi ukapiga pale alipo Amata, akaendelea kujibanza kiasi kwamba Yule jamaa hakuweza kumuona. Akasimama, akachukua simu yake na kuiweka sikioni.



    “Windo letu limejileta lenyewe, liko huku fikeni haraka tumalize kazi…” Yule jamaa aliongea kwa simu na mtu wa upande wa pili, kabla hajaishusha ile simu, Amata akajitokeza na bastola mkoni lakini kabla hajafyatua guu la Yule bwana likatua juu ya mkono wa Amata na kumpoka ile bastola, konde zito likatua shavuni, Amata akaenda chini.



    “Aaaaahhhh utanitambua leo,” lile jamaa lilikoroma huku likimfuata Amata na mikono yake likikunja ngumi. Likamdaka shingo, likamwinua.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aaaaaaiiihhhhh!” Amata alijaribu kupiga kelele na kujitikisa, wapi, alijikuta pumzi ikizidi kumwishia. Akajitahidi na kuinua mikono yake akaukamata uso wa Yule jamaa, vidole gumba vya kamanda vikatua machoni pa Yule bwana, akaanza kukandamiza. Jasho lilikuwa likimtoka Amata kwa mkabo ule lakini na yeye hakumwachia alikandamiza macho kwa nguvu na alikuwa akiongeza mkandamizo mpaka Yule bwana akaona isiwe tabu akamwacha na Kamanda akabwagika chini. Wakati jamaa anajipapasa macho yake kama yapo au la, alijikuta akipokea makonde mazito mazito ya siyo na hesabu ya liyompeleka chini.



    “Na sasa utanieleza vyema yuko wapi First Lady?” Amata akang’aka huku mishipa ya hasira ikimdinda kwenye paji la uso. Akamtandika teke moja lililotua shavuni na jamaa akajibwaga upande wa pili, akajaribu kujiinua na kutambaa kwa magoti huku Amata akimfuata kwa pembeni taratibu.



    “Niambie First Lady yuko wapi?” Amata akazidi kuuliza. Mara ghafla, Yule jamaa akaidaka miguu ya kamanda na kumnyayua hewani, Amata aliruka sarakasi na miguu yake ikapiga kwenye paa la juu, akahisi maumivu kwenye moja ya kisigino chake, lakini alivumilia. Yule jamaa aliokota kiti cha mbao na kumtandika mgongoni Amata akapepesuka, huku kile kiti kikitawanyika vipande vipande.



    ***

    Saa ya Chiba ikapiga ukulele, akaiinua na kuangalia kwenye kioo, kijitaa chekundu kilikuwa kikiwaka, haraka akaivuta kompyuta yake ndogo na kuifungua. Kamanda Amata, akawaza, punde tu ile saa ikamfinya, akaibofya kwa juu na kuruhusu ujumbe ule uingie, kijimkanda chembamba kikajitokeza.



    “Rescue First Lady…TSA 1”



    Chiba aliuelewa ujumbe ule, haraka akampigia Scoba na Gina wote walikuwa tayari katika kona tofauti za jiji, akawataka kuelekea Masaki haraka, nao ila kupinga waliitii amri ya TSA2 na kuelekea pande hizo.

    Chiba aliingia garii na kuondoka kwa kasi kuelekea eneo la tukio. Usiku huo hakukuwa na gari yoyote barabarani hivyo ilikuwa ni kupiga mwendo kadiri ya injini yako itakavyo.



    ***

    Briston Kalangila aliicha barabara ya Oysterbay na kuikamata ile inayoelekea Sea Cliff, mwendo wa gari yake ulikuwa wa kasi kiasi kwamba kila lilipokata kona tairi zilipiga kelele. Huku akiwa kauma meno moyoni mwake kulikuwa na jambo moja. Huyu jamaa anastahili akatwe vipande vipande, aliwaza huku akiendelea kuliweka guu lake zito kwenye pedeli ya mafuta na kuifanya gari hiyo kukimbia isivyo kawaida.

    Akili ya kikachero ya Briston alaifanya kazi, alipofika katika yale majengo, akapitiliza kwa kasi ileile na kwenda kusimama mbele kisha akateremka na kuziweka tayari bastola zake.

    Kazi moja tu, kwanza jamaa wameshaharibu mpango, iliyobaki ni kutoroka nchi, akajiongelea moyoni mwake huku akipachika sawia zile bastola na kuyafuata yale majengo kwa mlango wa nyuma ambao ni wachache waliujua.

    ***



    Scoba alikuwa wa kwanza kuwasili eneo lile akitokea upande wa Coco beach, mkononi akiwa na kitu kama simu alichokivaa kilikuwa kikimwonesha wapi mahala alipokuwa akitakiwa kufika, akaiinua na kuisogeza karibu na kinywa.

    “Nimetua salama uwanjani!” akasema na kushusha mkono huku nusu akikimbia na nusu akitembea.



    “Copy, nipo jirani,” Chiba akajibu na wote wakasikia kupitia vidubwasha vyao vidogo vilivyopachikwa sikioni.

    Dakika chache jumba lile lilizingirwa na watu watatu; Chiba, Scoba na Gina aliyeingia na kuegesha gari yake nyuma ya jingo lingine kabisa. Yeye ndiye aliyemwona Briston tangu aliposhuka kwenye gari yake na kuingia kupitia mlango mdogo wa nyuma ya majengo yale. Akatikisa kichwa kwa kuwa sasa alihakiki juu uhusika wa mtu huyo, anafata nini huku? Akajiuliza na kuinua mkono wake wenye saa akaizungusha pete ile ya pembeni mwa saa yake kisha akabonyeza kitufe cha pembeni na kuisogeza kinywani.



    “Briston Kalangila ameingia kwa mlango wa nyuma!” akapeleka ujumbe wa maneno ulioweza kuwafikia wote kwa wakati mmoja. Aliposhusha mkono wake na kuichomoa bastola tayari kwa lolote akauendea ule mlango aliyoingilia Briston, akasimama pindi tu alipoufikia, akatulia tuli! Akisikiliza nini kinaendelea ndani, kimya. Alipouweka mkono wake juu ya komeo ili kuufungua akasikia muungurumo wa gari nyingine, ilikuwa Land Cruiser ikasimama jirani kabisa na ile gari ya Kalangila, akashuka kijana mmoja mfupi aliyekomaa na kushupaa misuli. Gina akamkumbuka mtu huyo, alimwona kule New Afrika alipokuwa na Scoba, hakuwa mwingine, ni Kubrah Khaleb. Naye akauelekea ule mlango, Gina akajibanza nyumba ya pipa kubwa la takataka, akamtazama Yule kijana akiingia katika ule mlango kisha akaufunga nyuma yake. Gina akatuma taarifa nyingine kwa mtindo uleule na wote wakapata ujumbe huo. Kisha akachukua simu yake na kuingiza namba za siri akampa taarifa Madam S ya kuwa wapi wapo kwa wakati huo, alipoizima na kuipachika mahala pake, akauendea ule mlango na na kuusukuma taratibu nao ukasukumika, akajitoma ndani na kujificha nyuma ya simtank kubwa la maji.



    “He! He! He! We unafanya nini hapa! Na imeingilia wapi, le utachezea Masai,” sauti ya kimasai ilisikika nyuma ya Gina, hakutoa nafasi ya kusikiliza sentensi ya pili wala inayofuati, aligeuka na pigo moja la maana liliotua shingoni mwa Yule Masai na kumpelaka chini, kimya. Utaamka baadae! Akajisemea moyoni kisha akavuta hatua nyingine chache na kujificha kwenye kibaraza kilichokuwa na mlango wa kuingilia ndani. Kutoka ndani alisikia vipigo vya kimya kimya na miguno vikiendelea.

    ***

    Kutoka pale chini Amata alinyakua mguu wa kiti na kuurusha kwenda kwa Yule jamaa, akaudaka na kuuvunja kwa goei lake kisha akavitupa vile vipande huku na kule, akavua shati lake na kulitupa kando hukun akiuma meno kwa hasira. Aliiruka meza na kwa minajiri ya kutua pale alipo Amata, kosa! Amata akajizungusha na nyayo la guu lake likatua kwenye korodani, Yule jamaa alitoa yowe la uchungu, Amata akainuka na kuruka tik tak na miguu yake yote miwili ikapiga usoni na kumwinua wima kisha akajibwaga juu ya meza. Kwa haraka Yule jamaa akainuka na kukutana na Amata uso kwa uso, kwa mikono yake miwili akampiga Amata huku na huku kwenye masikio kisha konde moja zito likatua kwenye chembe, Amata akarudi nyuma na kugumia maumivu. Yule bwege akachomoa kisu kikali kutoka kwenye travota yake na kumjia Amata kwa kasi.



    “Aaaaaaaaggggghhhhhh! Im killliiinngggg yyyooooouuu!” pigo moja kisu kile lililikosa sikio la Amata, akaepa, pigo la pili likachana fulana aliyovaa kwa ubavuni na kuipapasa ngozi ya eneo hilo, damu zikaanza kuvuja. Pigo la tatu likatua kwenye nyama ya mkono kati ya kiganja na kiwiko. Akaitunisha misuli ya mkono, kile kisu kikatua na kuchoma sentimeta kama mbili ndani ya nyama ya mkono huo, Yule jamaa akakichomoa na kukiinua juu. Akakishusha kwa lengo la kupiga pembeni mwa shingo. Alipokishusha kwa nguvu, Amata aksogea kando na kupeleka pigo moja kali la karate likatua mbavuni na kuvunja ubavu mmoja.



    Mapigo ya kifo, akawaza akilini mwake huku akipeleka pigo la kung fu lililotanguliza vidole viwili vilivyoachama, pigo lila likatua tena mbavuni na vidole vile vikakamata mbavu, kwa hasira aliyokuwa nayo, Amata aligeuka mnyama, alivuta na kufyatua mbavu nyingine, akachomo mkono na kumtandika pigo kali la paji la uso, lililomzungusha Yule jamaa kisha bila kuchelewa Amata alaongeza pigo la mwisho lililotua katikati ya uti wa mgongo na kukamata vertebra, akafuta juu na kuzifyatua kisha kwa teke lake moja akamtandika mgongoni na kumwabwaga upande wa pili akiwa hana uhai, macho yamemtoka.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wasalimie kuzimu!” akamwambia huku akisimama wima baada ya pigo lile la nguvu. Taa za akiba zikawaka ndani ya chumba kile. Mbele ya Amata kulikulikuwako watu watatu; Briston, Khubrah na mtu mwingine.



    “Nilisikia habari zako kumbe unaweza ee?” Briston alimwambia Amata aliyekuwa kasimama imara tayari kwa lolote.



    “Naweza sana kuliko unavyofikiria, siamini kabisa kama wewe, Bristona Kalangila, namba 301 TNS unaweza kusaliti kazi yako. Lakini sio kosa lako, wewe ni pandikizi na dawa ya pandikizi kama wewe ni kung’olewa ili maoteo yasipate nafasi,” Amata alinguruma huku akisimama kawaida.

    Briston aliusukuma mwili wa Yule jamaa, akaitazama na ile mingine miwili, kisha akamwangalia Amata.



    “TSA 1 !” akatamka kwa sauti ndogo.



    “Niite Kamanda Amata, unstoppable! Kama ulikuwa hunijui ndio mimi,” Amata akainua kidole chake cha shahada na kumnyoshea mtu huyo mwenye tambo kubwa.



    “Umetudhalilisha, umeidhalilisha idara, nakwambia leo hii utaeleza kila siri iliyo moyoni mwako…”



    “Keleleeee!!!!” Briston akapiga ukulele na kufyatua risasi iliyopita milimita kadhaa kwa Amata.



    “Wewe unaweza kuniambia mimi maneno kama hayo, wewe ni motto mdogo sana kwangu, na leo nitakuchinja kama kuku. Mlete huyo!” Briston akaongea kwa hasira na mara kijana mmoja akatokea akiwa kamkamata nywele mke wa Rais na kusukuma kwa nguvu sakafuni.



    “Sasa atakatwa kichwa mbele ya macho yako!” Briston akamwambia Amata.



    “Kamwe hilo haliwezi kutokea, huyo atakayemkata kichwa atakata roho sekunde tano kabla hajatekeleza hilo,” Amata akajibu na kusimama huku kajishika kiuno na damu bado zikimvuja polepole kwenye jeraha lake la mkono. Yule kijana aliyemsukuma First Lady sakafuni akauvuta upanga mkali mwembamba mkononi mwake na taratibu akamwendea Yule mwanamke na kuuinua juu.



    “Na upanga huu ndiyo utakaokukata na wewe!” Briston akamwambia Amata.



    “Mchinje basi, mbona unaniangalia mimi?” Amata akamwambia Yule kijana, na alipoona anaanza kushusha ule mkono, Amata akapiga kisigino cha kiatu chake chini, kisu kisodo chembamba kikafyatuka mbele ya kiatu hicho na kikadidimia kwenye koromeo la Yule jamaa mwenye upanga. Akauacha upanga na kujichika koo huku akianguka chini na kukoroma vibaya. Kamanda Amata aliruka kutoka pale alipo na risasi za Briston zakachimba tiles za sakafu.

    Mara hiyo mlango ulifunguliwa kwa pigo moja la nguvu, Gina akabingirika ndani na miguu yake ikatua kifuani mwa Khaleb, kijana huyo akayumba lakini akasimama imara na kuikunja mikono yake kwa namna ya ajabu, pigo alililolipiga likapanguliwa na Gina kwa ustadi lakini mwanmke huyu alihisi maumivu kwenye mifupa yake kutokana na jinsi Khaleb alivyokomaa mwili. Pigo la pili lilimsukuma Gina na kujibamiza kwenye kabati.



    “Freeeza!” Scoba na Chiba wakaingia kwa mara moja ndani ya chumba hicho na mtupiano wa risasi haukuwa wa kawaida. Khaleb akaona wazi kuwa hapo mambo yameishaharibika, alitazama huku na huko na kufungua mlango wa kuingia ndani zaidi lakini kabla hajapotelea, Gina alikuwa tayari wima, aliruka sarakasi moja maridadi na kutua mgongoni mwa kijana huyo, akaenda chini na kuporomoka ngazini. Khaleb akainuka kwa haraka na kurudi juu, katikati ya ngazi hizo akakutana na Gina aliyefura kwa hasira. Gina akaruka hewani na kumchapa teke maridadi lililompotezea mwelekeo kijana huyo lakini haraka alijiweka sawa na kumdhibiti Gina kwa mapigo ya kimbunga, mwanamke huyo akajikuta anashindwa kuhimili kasi hiyo huku akivuta hatua kurudi alikotoka, Khaleb alimchapa teke moja matata la kifua lililomsukuma mpaka sebuleni ambako sasa mapigano ya risasi yalikuwa yametulia.

    Khaleb alipojitokeza tu akakutana uso kwa uso na Amata, pigo la kwanza lilitua mbavuni, Khaleb alipotaka kujishika kwa maumivu Amata akaruka teke kali na kumtwanga sikioni, majanga. Kijana huyo alipeleka mapigo kama kumi na tano ya karate kwa Amata lakini yote yalipanguliwa kwa ustadi, akajikuta anaishiwa.



    Khaleb akatumia hila, akajikunja na kujiweka tayari kwa mapigano, akamtisha Amata kama anampelekea pigo na Amata alipoepa, mwenzake akaruka sarakasi na kujipiga kwenye kioo kikubwa cha dirisha, kikapasuka naye akatoka nje, akainuka haraka na kukimbia. Chiba na Scoba bastola mkononi wakapita palepale dirishani na kuanza kumtoa mbio huku wakirusha risasi lakini Khaleb alikuwa mwepesi zaidi yao, alikwea ukuta kwa jinsi ya ajabu na kujitupa nje.

    ***



    Taa za gari za polisi zilipendezesha anga la nje ya majengo hayo, vijana walioongozwa na Inspekta Simbeye waliwasili dakika chache baada ya Madam S na Hosea Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa (TNS) kuwasili.

    Ndani ya sebule hiyo walikuta hali mbaya ya vifo na mapigano. Madam S alielewa kuwa ni dakika chache tu zilizopita mirindimo ya risasi ilisitishwa kutokana na harufu kali ya baruti. Bwana Hosea alipoingia tu alikutana macho kwa macho na Briston Kalangila, mtu wake katika idara namba 301 aliyemoa jukumu la kuongoza wana intelijensia ndani ya jengo la tukufu la Ikulu. Akatikisa kichwa na kumtazama kwa makini.



    “Huyu ni nani Briston?” akamtupia swali huku mkono wake ukimwoneshea mke wa Rais ambaye alikuwa ameketi na kuuegemea ukuta.



    “First Lady! Nimemkuta humu ndani,” akajibu huku akisimama.



    “Amekujaje?” swali la pili.



    “Ametekwa, na mimi kama mdau wa usama nilikuwa katika kumwokoa kutokana na kazi na cheo change nilipaswa kufanya hivyo nikiwa undercover,” Briston akaeleza, “Na hawa vijana nahisi majambazi ndiyo waliyokuwa wakinizuia mimi kufanya kazi yangu kama mwanausalama,” akaongeza.



    “Acha uongo Briston!” Madam S aling’aka, “Hivi unatufaya sisi hatuna akili siyo? Nani asiyejua uliyoyafanya? Na utaenda kueleza yote leo, tuliku suspect tangu siku za mwanzo, tutakuhiji zaidi na tutaujua ukweli,” Madam akang’aka.



    “Umeniuzi, umenisaliti, mchukueni!” Hosea akamwambia Madam S. inspekta Simbeye aliingia ndani ya sebule hiyo, na mara moja wakamtia pingu Briston na kutoka nae. Polisi wengine wakachukua miili ya marehemu na kuibeba machelani kuiondoa eneo lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pole sana mama!” Madam S alimpa pole First Lady huku akimwinua kutoka pale alipoketi, “Amata, pekua nyumba hii mwanzo mwisho. Simbeye majengo haya yaw echini ya ulinzi wa polisi mpaka amri nyingine itakapotolewa, ujenzi usimamishwe kwanza ili uchunguzi uchukue nafasi yake,” akamaliza na kuvua koti lake kubwa alilovaa na kumvika First Lady kwa kuwa nje kulikuwa na manyunyu mazito ya mvua.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog