Simulizi : Siri Ya Miaka 20
Sehemu Ya Tatu (3)
mke wa jimy alishuka kutoka ndani ya gari kisha akauliza bosi wako nimemkuta??? aliuliza hivyo hata bila salamu.... side alijibu hapana hajarudi kabisa siku ya leo... mke wa jimy aligundua kuwa side hakusema uwongo kwa sababu hata yeye alipotazama mule ndani ya geti hapakuwa na gari alilokuwa analitumia tom... kisha akaingia ndani ya gari lake na kuliwasha.... side alifungua geti mke wa jimy akaondokazake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
************
baada ya mke wa jimy kuondoka side alirudi ndani kwenye sehemu yake ya kupumzika lindoni... alikuta simu yake ikionesha mwanga... alipoiangalia aliona tom alikuwa amempigia muda mchache uliopita..... punde tom akapiga tena side alipopokea tom alianza kufoka... kwa nini unachelewa kupokea simu? ok hakuna mtu aliyekuja hapo nyumbani kunitafuta?? aliuza tom... side akamwambia kunamtu amekuja sasahivi kabla side ajamaliza kuelezea ghafla simu ya tom ikazimika chaji.
shit"" alisema hivyo tom kisha akaangalia saa yake ya mkononi ilikuwa ni saa 8 na dakika kumi... ni nani huyo aliyekuja nyumbani kwangu kunitafuta usiku wa manane kama huu.... tom alikuwa na shauku ya kujua mtu huyo ni mwanaume au mwanamke!!!!!bila shaka atakuwa ni bony""" alijisemea tom lakini hakuna namna kwa sababu kabla side hajatoa maelezo yaliyokamilika simu ya tom ilizimika chaji.... tom alizidi kuchanganyikiwa... aliamua asilale kwenye hotel hiyo.... aondoke huo huo...aliingia ndani ya gari lake na kulisha alichomeka simu yake chaji katika chaja ya kwenye gari kisha akaondoka kutafuta club inayokesha... alienda mpaka MAISHA CLUB Dodoma... alipofika aliagiza pombe kali aina ya vodka...alikunywa lakini aliona pombe haikamati kwenye kichwa chake... aliamua kuhama club.... alihamahama club mpaka pakakucha..... alifanya hivyo kuhamahama huenda kama kuna mtu anamfatilia basi asiweze kumnasa kwa urahisi..
*********
ule upande mwingine alionekana bony akiwa nyumbani kwake akifanya mazoezi ya viungo asubuhi.....ghafla alisikia simu yake ikiita alipoiangalia aliona ni tom ndiye alikuwa anapiga... alipoipokea tom alitoa maneno ya vitisho... alimwambia bony kuwa lazima itakughalimu maisha yako baada ya kuharibu na kuvuruga mipango yangu kisha tom akakata simu... kisha tom alielekea CRDB benki alitoa pesa zote akaacha shilingi elfu kumi pekee ili kulinda akaunti.......
tom alianza kufuga rasta kichani pia hakuwahi kunyoa ndevu tangu alipoingia Dodoma alibadilisha muonekano wa mavazi akaanza kuvaa jinsi na tisheti...
****BAADA YA MIAKA MIWILI(2) KUPITA****
Tom alibadilika kabisa alionekana ni mtu mwingine kabisa kutokana na ndevu kuwa nyingi pamoja na rasta kichwani hivyo ni ngumu kutambua kuwa huyu ni tom... siku moja alirudi Dar es salaam alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye nyumba yake cha kushangaza alikuta ukimya umetawala hapakuonesha dalili yoyote ya mtu kuwemo ndani... alichukua bastola yake akaiweka kwa upande wa nyuma ya jinsi kisha akaifunika kwa tishet ndefu aliyokuwa kaivaa... kisha akashuka kutoka ndani ya gari lake jipya aina ya RANGGER akafungua geti na kuingia ndani alistahajabu vile alivyoacha ndivyo alivyopatuka pakiwa vilevile mule ndani... kisha akazipiga hatua kuelekea kwenye mlango wa kile chumba alimochimba shimo na kumzika bosi jimy baada ya kumchinja shingo mpaka kufa... alichukua funguo alipofungua mara ghafla.
Tom alipofungua ule mlango mara ghafla alitaka kukimbia """ alikuta kunautofauti sivyo alivyoaacha vile mule ndani ya chumba aliona kile kitanda kilichokuwa juu ya lile shimo alilomzika bosi jimy kitanda kile hakikuwepo pale alipokiacha kilikuwa kando kabisa....lakini shimo halijafukuliwa.... ""Tom alifunga mlango na kuanza kutimua mbio kuelekea upande wa nje!!! alipofika nje alistahajabu hakuliona gari lake pale alipokuwa amelipaki.... haa!!! mbona maruerue alijisemea tom kisha alifikicha macho...aliamua kuondoka eneo hilo bila kupoteza muda......
kumbe gari hilo lilichukuliwa na bony alipachika funguo wa bandia kwenye mlango alifungua na kuliwasha gari hilo na kutokomea nalo ili apeleleze huenda kutakuwa na chochote cha kumuongoza ili amnase tom lakini hapakuwa na kitu chochote ambacho kingemuongoza yeye kumnasa tom.... hivyo aliamua kumfatilia mtu huyo amnase ili ampeleleze tom yuko wapi!!!! kutokana na rasta na ndecu nyingi bony hakuweza kumtambua kuwa huyo ndiye tom mwenyewe...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
tom alizidi kuchanganyikiwa aliamua kuelekea kwenye kituo cha Taxi alikodi taxi impeleke Dodoma.... dereva alimwambia mpaka dodoma utanipa elfu sitini tom hakutaka kupingana nae... alikubali.... kisha safari ikaanza......walikwenda umbali wa kilometa 40 hivi.... lakibi tom alihisi kama kaona kitu kwenye kioo cha upande wa kishoto.. alipoangalia vizuri alihisi kuna mtu anawafatili akageuka nyuma aliliona gari lake likiwa nyuma kama mita 50 lakini hakuweza kumtambua aliyekuwa akiliendesha...tom alistuka alihisi kuchanganyikiwa alimsihi dereva aongeze mwendo"" kwa sababu mteja ni mfalme dereva alifanya kile alichoambiwa na mteja wake..... tom alikuwa na wasiwasi mbaya zaidi alijitagidi kutazama kwa makini ni nani aliyekuwemo ndani ya gari lake!!!
**************
kule nyumbani kwa jimy""" sandra ambaye ni mke wa jimy alikuwa anampigia bony ili aulizie taarifa za tom... lakini bony hakupokea simu ya sandra....
tom alikuwa mjanja kupindukia alibuni mbinu.. alimwambia dereva asimamishe gari......dereva alisimamisha gari...bony alistahajabu kuona kitendo kile alihisi kunahatari kisha akamuona tom anashuka na kuitoa bastola yake huku akimwambia dereva usiogope.... dereva alitoa macho hakuamini alichokiona alihisi anatekwa kisha tom akamwambia dereva ampe simu yake pamoja na funguo wa gari .. tom alifanya hivyo ili kujihami yule dereva asije akawapigia simu mapolisi au akawasha gari na kukimbia..... kisha akafunga kifaa maalumu mbele ya bastola ili akifyatua risasi bastola isito mlio... alinyanyua mkono wake kisha akafyatua risasi kuelekea ule upande bony alipo... bony alijilaumu sana kwa kuacha zana zake za kazi... alipo ona mamba yamekuwa magumu aliamua kugeuza gari na kurudi dar.... tom alipo ona bony kakimbia na kutokomea alimteka dereva akamfunga kamba na kumziba mdomo kwa kitambaa kisha akamuweka ndani ya buti... baada ya tom kufanya hivyo aliingia ndani ya gari na kuliwasha aliliondo kwa kasi ya ajabu... mnamo majira ya saa kumi na mbili aliwasili Dodoma.... aliliongoza gari hilo kwa kuliendesha mpaka kwenye nyumba kubwa iliyokuwa na uzio mkubwa usionesha upande wa ndani.. mlinzi alitoka nje alipomuona tom alifungua geti haraka... kumbe nyumba hiyo ilikuwa ni ya tom...
walionekana walinzi wengi wakiwa wamevalia suti nyeusi na miwani nyeusi huku wakiwa na bastola zao kiunoni..... tom alishuka kutoka ndani ya gari na kuanza kuzipiga hatua kuelekea upande wa ndani huku alisindikizwa na walinzi wawili...
**********
Bony aliliendesha gari majira ya saa moja aliwasili dar... alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake... huyu mjinga angenitoa uhai lakini mbona hafanani na tom au atakuwa katumwa na tom alijisemea bony kisha akachukuwa simu yake na kumpigia sandra akamwambia leo nimemuona mtu kaingia kwenye nyumba ya tom mtu huyo ni mrefu anarasta na ndevu nyingi kidevuni. bila shaka atakuwa katumwa na tom...niachie kazi hiyo nitaifanya mimi nitakupa taarifa.
kumbe bony ni mpelelezi (police undercover) aliifanya kazi hiyo kwa miaka 15 alikuwa anapeleleza majasusi alijifanya yeye ni mtekaji nyara hivyo matajiri walimtumia kwenye shughuli zao za kijasusi bila kufahamu kuwa bony ni mpelelezi na anapokamilisha ushahidi huwakamata watu hao na kuwapeleka kwenye vyombo vya dola sheria ifuate mkondo wake... hata sikuile alipoingia ndani ya nyumba ya jimy hakufanya mauwaji... alizichukua nyaraka zile na kutokomea nazo ili afanye upelelezi wake kwa nini tom anataka nyaraka hizo na kugundua kuwa zilikuwa ni hati miliki za mali za marehemu jimy....
************
upande wa pili kule kwenye ngome ya tom wafanyakazi walionekana wakijiandaa kwenda kufanya tukio la ujambazi ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku...
tom alitoka nje kisha akaingia kwenye ile taxi akaiwasha na kuondoka zake alipofika nje kidogo ya mji alisimamisha gari na kufungua buti ili amtoe yule dereva amfungulie kamba aondoke zake....hakutaka kumdhuru.... mara ghafla..
mara ghafla tom alistahajabu kukuta dereva yule katulia tuli huku macho yake akiwa ameyafumba... tom alisikitika hakutaka kumdhuru dereva yule""
mara ghafla dereva alikurupuka... kumbe dereva yule alikuwa kapoteza fahamu... kwa m-banano wa hewa ndogo ndani ya buti ya gari... pia alikuwa humo kwa masaa mengi... tom alivunja laini ua simu ya dereva kisja akamrudishia simu yake na kumtishia kuwa endapo akitoa taarifa popote juu ya aliyoyaona basi atamtafuta na kumuuwa....namba za gari lako nimezikariri.... alisema tom kisha akamkabidhi funguo za gari...dereva yule hakuamini alijua ndio mwisho wa maisha yake... aliingia ndani ya gari huku akimtazama tom.... aliliwasha gari na kuliondoa kwa kasi kurudi dar es salaam"""tom alichukuwa simu yake kisha akampigia mmoja kati ya wafanyakazi wake amfate na gari alitoa maelekezo sehemu aliyopo.... baada ya nusu saa gari lilifika na kumchukua tom..
***********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wale wafanyakazi wa tom walifika sehemu ile walipokuwa wamepanga kufanya tukio la ujambazi... walivamia nyumba ya bilionea mmoja wakachinja walinzi na kuingia ndani walipora begi la pesa nyingi zaidi ya bilion moja pamoja na vitofali viwili vya dhahabu kisha wakatokomea kurudi kwenye ngome ya tom.....
Tom alifika nyumbani kwake huko kwenye ngome yake... punde wafanyakazi wake walifika walimkabidhi lile begi lilibosheheni vibunda ya noti.. pamoja na vile vitofali viwili vya dhahabu... tom alise yes well done"" kisha akawasha sigara na kuweka kunako mdomo..... kisha tom akaelekea upande wa chumbani kwake.... ndani ya jumba hilo kubwa la tom...kulikuwa na kamera (UCCTV( kila kona.. aliingia moja kwa moja chumbani kwake huku ulinzi mkali ukiwa nyuma yake.. alianza kupanga mipango ya kumnasa bony..
*******
kule nyumbani kwa bony pia wakati huohuo alikuwa aliandaa mikakati ya kumnasa tom..alichukuwa simu yake na kumpigia sandra mke wa marehemu jimy... alimwambia waonane siku ya kesho....
kisha bony alipanda kitandani na kuanza kuutafita usingizi......
asubuhi palipokucha tom aliwaagiza vijana wake wa kazi waende dar es salaam kwaajili ya kumnasa bony na safari ya kuelekea dar ikaanza..
tom alisisitiza namtaka bony akiwa hai au amekufa""" kisha akarudi zake ndani kwenye jumba hilo kubwa la kifahari... ilipofika majira ya saa tatu usiku vijana wa kazi waliwasili dar es salaam.....walivamia nyumba ya bony kwa ya simu maelekezo kutoka kwa tom..... bony aliona watu wameingia ndani ya uzio uliokuwa unaizunguka nyumba yake huku wamebeba siraha nzitonzito tena za kivita mmojawapo alikuwa amebeba (RPG) ni siraha inayowekwa bomu ndani yake maalumu kwa kutungulia ndege ikiwa angani"" mwingine alikuwa kabeba(SMG110) ikiwa na mkanda wake wa risasi" ni siraha inayoshambulia mfululizo bila kuondoa kidole kwenye kitufe cha kufyatulia risasi.... duh!!! kama wanakwenda kwenye vita..... bony aliweza kuwaona kupitia mitambo maalumu aliyokuwa ameitegesha ndani ya uzio wa nyumba yake... alifanya hivyo kwa miaka mingi.... kwa tahadhali kama mtu akiingia ndani ya uzio wake nyakati za usiku basi anapata taarifa kupitia simu yake ya mkononi aina ya iphone 6s. alikurupuka haraka akachukua bastola yake pamoja na kisu kisha akatokea mlango wa dharula uliopo jikoni... alipitia mlango huo mdogo akatokezea nje kabisa ya uzio wa nyumba yake.... kumbe nje kulikuwa na watu wengine wawili.. walibaki ili kulinda usalama kazi yao iende vyema..bony alikuwa na mbinu za kupambana endapo tukio hili litamtokea""" alifundishwa kwenye mafunzo ya ukomando walipopelekwa huko quba...mafunzo hayo walifuzu wawili tu yeye na mwingine mmoja kati ya watu 50....aliporudi kazini alipangiwa kitengo cha (upelelezi)....bony aliamua kutumia mbinu za kikomando ili kukabiliana na hao waliopo nje kimya kimya ili wale wa ndani wasisikie chochote kinachoendelea nje.....alinyata akamkaba moja kabali aina ya ngeta....kabali hii hupendwa kutumiwa na vibaka katika uporaji ...ukikabwa kabali hii hufurukuti wala hutoi sauti wala huvuti pumzi..... baada ya kumbana vyema kwa kabali hiyo mtu yule alishindwa kupumua akapoteza fahamu... kisha akanyata kumfata yule mwingine aliyekuwa aliyekuwa ndani ya gari huku kaacha mlango wazi ndiye dereva wao... alipomkaribia alimchomoa kwa kumvuta kutoka ndani ya gari kisha akampiga gumi kali sana kwenye shingo chini ya sikio... ngumi ile ilikwenda moja kwa moja kwenye mshipa wa fahamu chini ya sikio... yule mtu alipoteza fahamu pia.... kisha bony aliwateka na kuwafunga mikono na miguu kwa kutumia mikanda yao ya suluali na mashati yao. kisha akawavuruta akawaingiza ndani ya ule mlango wa siri wa kutokea nje ya uzio kisha akarudishia manyasi.
bony alinyata na kujificha upande wa pili mbali kabisa na nyumba yake... wale vijana wa kazi waliotumwa na tom... baada ya kuona bony hakuwemo ndani ya nyumba.. waliamua kutoka nje waondoke zao.... walistahajabu walipofika nje hawakuwakuta wale wenzao wawili...walipojaribu kuwapigia simu simu...kumbe bony alichukua simu zao na kuzima simu hizo......waliamua kusubiria huenda wakawaona... lakini hapakuonesha dalili yoyote ya wenzao kuwepo eneo lile... wale vijana watatu waliamua kuondokazao.... baada ya bony kuhakikisha kuwa wameondoka na kutokomea eneo lile..alitoka mafichoni na kurudi pale kwenye mlango wa dharula,,, aliwatoa watu wale na kubeba mmoja baada ya mwingine kuwaingiza kunako chumba kimoja alichokuwa akikitumia kufanya upelelezi pale anapowanasa waalifu. kisha akawafunga miguu na mikono kwenye viti alichukuwa dumu la maji na kuwamwagia kichwani... ghafla walipata fahamu.... akaanza kumuhoji mmoja.... lakini hakusema chochote kinachomuhusu tom alisema aliyewatuma sio tom... bony alikasirika sana kwa sababu mtu yule alimdanganya... alichukua msumari mrefu na nyundo... kisha akauliza tena. ni nani aliyewatuma?? yule mtu alikataa kusema tena wakati huu alikaa kimya bila kujibu chochote... bony alichukua gundi ya nailoni. kisha akamziba mdomo ili asipige kelele... kisha akauweka ile msumari mnene na mrefu kunako juu ya kiatu alichokuwa amekivaa yule mtu... bony alinyanyua nyundo.... na kugonga juu ya msumari ule uliingia moja kwa moja ndani ya kiatu na kutoboa mguu kisha akauwacha msumari huo hapohapo ... yule mtu alilia kwa maumivu mpaka haja ndogo ilimtoka.... hakuamini alichofanyiwa kwani mara ya kwanza alihisi bony anafanya mzaha... kisha bony aliindoka chumbani humo.. na baada ya dakika kadhaa alirudi na msumeno wa kukatia mbao... bony alizipiga hatua mpaka pale yule kijana mwingine alipokuwa amemfunga kwenye kiti..... akauliza ni nani kawatuma... kijana yule alisita kusema alikaa kimya.... bony alisimama kisha akauweka msumeno kunako paja la yule kijana... kisha akauliza tena ni nani kawatuma? yule kijana alikataa kusema bony alichukua gundi... yule kijana alipo ona hivyo aliamua kusema to... too...tom ndiye aliye tutuma tuje tukuangamize.....
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
************
kule kwenye ngome ya tom... alionekana tom akiwa na firaha huku akiwa amezungukwa na wanawake wanne juu ya kitanda ndani ya chumba chake... na upande wa nje ulinzi ulikuwa imara wa hali ya juu... walinzi wake wote walikuwa na siraha...ghafla simu ya tom ikaita.. alipoitazama aligundua ni ya kijana wake wa kazi anampigia... akaipokea.... punde tom alianza kufoka baada ya kupewa taarifa kuwa wamekwenda nyumbani kwa bony lakini hawakumkuta hawajafanikiwa kumnasa.. pia vijana wawili hawaonekani na simu zao hazipatikani.... Shit mbona mmefanya uzembe wa hali ya juu alifoka tom kisha akakata simu... tom alihisi kuchanganyikiwa bila shaka bony atakuwa kawateka vijana wangu wa kazi... na kama kawateka akiwabana watatoboa siri kuwa mimi napatikana wapi... shit hii itakuwa hatari kwangu. tom alijisemea moyoni kisha akamuita mlinzi wake wa karibu alimuamuru awatoe wamawake wale mule chumbani...baada ya wanawake wale kutolewa mule chumbani tom alisimama na kuchukua chupa ya pombe kali aina ya VODKA kabla hajaimimina pombe ile kwenye glasi... ghafla simu yake iliita alikwenda haraka kunako kitanda akaichukua simu ile alipoitazama alikuwa anapiga yule mmoja wa vijana wake waliotekwa alipoipokea alistahajabu si mwingine alikuwa ni bony akiongea kupitia simu ya kijana wake wa kazi......tom jasho lilimtoka hakutaka kuendelea kusikiliza simu ile... alikata simu kisha akanywa pombe ile mfululizo mpaka ikaisha ndani ya chupa.....
baada ya bony kupata muongozo wa maelekezo kutoka kwa wale vijana wa kazi wa tom.... kuwa ni wapi tom anapatikana aliamua kuwaacha huru... aliwatoa nje ya geti vijana wale hawakuamini kama wameweza kutoka salama
(((DAIMA UKWELI HUMUWEKA MTU HURU)))
vijana wale walitimua mbio na kutokomea kusikojulikana..
******BAADA YA MIAKA ISHIRINI KUPITA******
PRETORIA-SOUTH AFRICA... afrika ya kusini.. kwenye kiwanja cha ndege alionekana mtu moja kavalia siti nyeupe ni mrefu wa wastani... mtu hiyo alishuka kutoka ndani ya gari kisha akachukuwa mabegi yake mawili kuelekea ndani zaidi kunako sehemu ya kuingilia kwenye kiwanja cha ndege...
mtu huyo alionesha hati ya safari za kimataifa(INTERNATIONAL PASPORT).
pamoja na Viza(VISA ) alionesha vitu hivyo kwenye sehemu ya ukaguzi katika mlango wa kuingilia ndani ya kiwanja cha ndege yule mkaguzi aliziangalia na majina yalisomeka hivi
"""EDO JIMY MARTIN"""" kisha akaonesha tiketi yake ya ndege na kuruhusiwa kuingia ndani kabisa ya kiwanja cha ndege....
kumbe Edo ndiye yule mtoto pekee wa marehemu bosi Jimy aliyekuwa akisoma huko Afrika ya kusini tangu utoto wake... baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya juu aliamua kuridi nyumbani Tanzania pia kwenda kwenye kaburi la baba yake...mama yake Edo ambaye ni sandra alimpa mwanae taarifa ya kifo cha baba yake wakati huo Edo alikiwa bado mdogo alikuwa anasoma darasa la tatu... sandra alikuwa anawasiliana na mwanae mara kwa mara kupitia mitandao ya kijamii.. lakini hakuwahi kumwambia ni nani aliyesababisha kifo cha baba yake...
ilipofika majira ya saa mbili usiku EDO aliwasili Tanzania katika kiwanja cha ndege cha
MWL: JULIUS. K. NYERERE mama yake alikwenda kumpokea kisha wakaelekea nyumbani....
kwa kuwa sandra hakumuona mwanae kwa miaka mingi"""" kesho yake aliamua kumfanyia sherehe
taarifa hizo za ujio wa Mtoto wa jimy zilimfikia tom
Tom alizidi kuchanganyikiwa.... kisha akaandaa mpango wa kumteketeza Edo siku hiyo ya sherehe yake iliyofanyika MLIMANI CITY... tom na vijana wake wa kazi walianza safari ya kutoka Dodoma kuelekea Dar es salaam... mnamo majira ya saa moja tom aliwasili dar es salaam.
Tom na vijana wake wa kazi walielekea moja kwa moja mpaka MILLIZ HOTEL. akachukua chumba kimoja juu kabisa ghorofani... hotel hiyo haikuwa mbali sana na mliman city pia kutokana jengo lake kuwa refu tom aliweza kuliona vyema jengo la mlima city kwa kutumia binoculars (darubini) kisha akachukuwa begi la plasiki akalifungua akatoa vipande kama vitato vya chuma... kisha akaanza kuunganisha vipande hivyo kwa kuvipachika... aliunganisha kipande kipande kimoja baada ya kingine... aisee tom alikuwa moto wa kuotea mbali huwezi amini baada ya kukamilisha kuviunganisha vipande hivyo ilikuwa ni bunduki hatari sana"" bunduki hiyo aina ya SNIPER CONVO-7R bunduki hii ni maalumu kulenga mbali... pia bunduki hii inauwezo wa kulenga kilomita tano kutoka hapo ilipo....tom alifungua dirisha na kuiweka bunduki ile kuelekea kule ambapo sherehe inaendelea kisha akafunga kifaa maalumu mbele ya bunduki hiyo(silent) ili atakapofyatua risasi mlio usisikike...
kisha akaiseti vyema lenzi ya bunduki hiyo... ilionesha kuonesha mtu kwa ukaribu zaidi.. baada ya kumaliza aliwaamuru vijana wake wa kazi washuke upande wa chini kisha waelekee mlimani city
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***********
mule ndani ya ukumbi sherehe iliendelea watu walionekana mikono yao imeshikilia glasi ya mvinyo huku wakicheza muziki aina ya bluz (muziki wa miondoko ya taratibu)
alionekana binti mmoja akiingia ndani ya ukumbi... alikuwa kavalia gauni rufu lenye rangi ya pinki huku akiongozana na mwanamke mtu mzima.... walipoingia ndani Edo alionekana akizipiga hatua za harakaharaka. kuelekea ule upande aliokuwepo binti yule kisha akamkumbatia na kumbusu juu ya midomo yake(Lip kiss) kisha edo alishikana mikono na mwanamke yule mtu mzima akamsalimia.... punde walionekana watu wawili wakiingia ndani ya ukumbi..... watu hao walikuwa wamevalia suti za gharama.. mmoja alikiwa amevaa suti ya bluu yenye kupauka(ligh blue)
na mwingine alikuwa kavaa suti nyeusi... huku wamevalia miwani nyeusi... Edo alistahajabu kuwaona watu wale kwani zilikuwa ni sura ngeni machoni mwake.... kwa sababu watu waliokuwemo kwenye sherehe hiyo ni marafiki na watu wa karibu na familia yao tu..... edo alihisi huenda watu hao walikiwa ni marafiki wa marehemu baba yake hivyo hakuwajali...alimshika mkono yule binti aitwa Grace kisha akaonekana akimwambia kitu yule mama mtumzima"" mama yule alitabasamu ... punde Edo akaondoka na Grace kuelekea meza ya vinywaji.....wale vijana wa kazi wa tom walionekana kuzunguka zunguka mule ndani ya ukumbi... kumbe walikuwa wanaangalia kama kutakuwa na ulinzi(polisi) kwa sababu Edo ni mtoto wa bilionea marehemu jimy hivyo walihisi huenda kutakuwa na ulinzi wa hali ya juu...
Edo alionekana akimnong'oneza Grace kisha edo akanyanyuka pale walipokuwa wameketi na kuanza kuzipiga hatua kuelekea msalani(toilet)
wakati huo huo Bony alikuwa anaingia ndani ya ukumbi huo.... bony alifika hapo kwa kuchelewa kutokana na foleni ya mjini.....alikuja hapo kwa lengo la kumlinda Edo aliamini lazima kutakuwa na watu wabaya wanaotaka kumdhulu edo..... alipokuwa akiingia mlangoni alipigana kikumbo na mtu mmoja aliyekuwa amwvalia suti nyeusi mtu huyo alikuwa akiongozana na mtu aliye valia suti ya bluu..... bony aligeuka na kumuangalia mtu yule. lakini hakumjali.. aliingia ndani kunako ukumbi....
ghafla alijipapasa mifukoni"" aligundua kuwa amesahau simu yake ndani ya gari lake... alizipiga hatua kurudi nje akaelekea kule alipokuwa amepaki gari lake.... alipofika nje aliona mtu yule akiongea na simu.... bony aliifungua mlango wa gari lake lakini akili na masikio yake yalikuwa yakimsikiliza yule mtu alichokuwa akikiongea.... alisikika akisema "" hakuna ulinzi wowote hivyo itakuwa rahisi sana.. kisha akakata simu... bony aliingia ndani ya gari lakini hakuliwasha alikuwa akitazama nje kwa kupitia kioo cha mlango wa gari....aliona watu hao wameingia mdani ya gari walipoliwasha gari lao taa za nyuma ya gari zikawa bony alistuka kuona namba za gari... alilikumbuka gari hilo....ni gari ambalo liliwahi kuja nyumbani kwake lilibeba vijana wa kazi wa tom... baada ya gari hilo kuondoka bony aliliwasha gari lake na kuanza kuwafatilia watu wale ili abaini ni wapi wanaelekea huenda watu hao wanapoelekea ndipo tom yupo akamnase... aliwafuatilia lakini alianza kukata tamaa kwani watu hao walionekana tu wakizunguka barabara za kila mitaa bila kuwa na muuelekeo kwamba wanaenda wapi.... kumbe watu wale waliamua kufanya hivyo ili kama kunamtu anawafatilia asigindue ni wapi wanaelekea.... bony alikuwa akilifatilia gari hilo kwa nyuma kama umbali wa mita mia... ghafla aliona gari lile linakata kona na kuelekea barabara inayokwenda MILLIZ HOTEL... bony alilifatilia gari hilo ni kweli lilipofika.. milliz hotel watu wale walishuka na kuingia ndani ya hotel.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***********
ule upande wa pili kule ndani ya ukumbi.... edo alionekana akimuaga mama yake kwamba anatoka mara moja kisha atarejea kwani alikuwa na mazungumzo na grace hivyo wanatoka upande wa nje... kumbe grace alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Edo.....sandra alimruhusu mwanae aende.... edo alimchukua grace wakaanza kuzipiga hatua kutoka nje...
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment