IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TOM ni mchapakazi sana katika kampuni yetu..hivyo basi nimewaita kwenye kikao hiki kwa dhumuni la kuwataarifu kuwa kuanzia leo atakuwa....msimamizi mkuu katika sekta ya usafirishaji na safari za nje ya nchi...hivyo basi kuanzia leo kila kitu kitakuwa chini yake"",, kunayeyote mwenye swali??? hayo yaliku maneno ya mkurugenzi wa kampuni inayoitwa TNS...mwenye swali aulize!!! wafanyakazi wa kampuni ile walibaki kimya hakuna aliyeuliza swali...kisha wakasema kwa pamoja sawa bosi....
ok, mimi natarajia kusafiri kesho naenda Amerca kwa miaka mitano hivyo uwongozi wa kampuni namuachia TOM...alisema mkurugenzi JIMY..
wafanyakazi wote walipiga makofi na kikao kikafungwa....
************
Tom alionekana kuwa nafuraha sana....kisha akajisemea moyoni laiti kama huyu boya angejua mpango niliokuwa nimeupanga juu yake asingethubutu kuniachia kampuni"",, sasa amejikaanga mwenyewe kwenye kikaango cha moto....lazima usiku wa leo mpango wangu ukamilike....kisha akaingia ndani ya gari lake akaondoka....alielekea mpaka kwenye hoteli flani hivi kisha akaagiza mvinyo(wyne) akaanza
kunywa...ghafla simu yake ikaita" tom akaipokea na kuiweka sikioni kisja akasema ok Usichelewe hakikisha unamnasa kabla haijafika saa tatu usiku..kisha akakaya simu...aliendelea kunywa mvinyo taratibu....alikaa pale takribani masaa mawili kisha akapanda gari lake na kuondoka.....alielekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwake...alipofika nje ua geti alipiga honi...lakini hakuna aliyefungua geti aliamua kushuka mdani ya gari ili abonyeze kitufe cha kengele pale getini ghafla mlinzi alifungua geti....Tom alimfokea mlinzi kwa nini kachelewa kufungua geti...mlinzi alijibu kuwa alikuwa chooni anajisaidia..Tom alirudi ndani ya gari kisha akaliendesha kuliingiza ndani ya geti...wakati huo ilikiwa majira ya saa moja usiku"" Taa zilizokuwa juu ya uzio wa nyumba yake ziliwaka kwa mwanga mkali hivyo nyumba yake ilipendeza sana...ilionekana ni nyumba ya kifahari mtaani pale....Tom akalipaki gari lake kisha akafungua mlango lakini hakushuka kutoka ndani ya gari...alichukuwa simu yake kishs akampigia MKURIGENZI jimy ambaye ni mmiliki wa kampuni aliyokuwa anafanya kazi Tom...simu ya Jimy iliita lakini haikupokelewa...Tom aliendelea kupiga simu ile kama mara nne hivi bado simu haikupokelewa...
**********CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
upande mwingine alionekana mkurugenzi Jimy akiwa ndani ya gari akiliendesha....hakuweza kupokea simu ya Tom kwa sababu simu ya Jimy ilikuwa ndani ya droo ya kwenye gari pia kutokana na sauti kubwa ya mziki uliyokuwemo ndani ya gari hivyo haikuwa rahisi Bosi Jimy kusikia simu ile...
***********
Upande mwingine Tom alionekana kupaniki akajiuliza kwa nini Bosi Jimy hapokei simu?? aaah nisipokuwa makini sitoweza kufanikisha mpango wangu alijisemea moyoni Tom. kitenso kile cha bosi Jimy kutopokea sim kilimfanya Tom achanganyikiwe kwa sababu alijua kuwa bosi Jimy atasafiri Asubuhi sana hivyo asipomnasa usiku huo..mpango wake utakuwa umegonga ukuta...akaamua kupiga simu....simu ilipopokelewa Tom alisema BONY uko wapi?? sasa mpaka sasahivi haujagundia ni wapi Jimy alipo shit)"" alisema Tom......... ok fanya hivyo sasahivi isha Tom akakata simu..
alitoka mule ndani ya gari kisha akaelekea ndani....
mlimzi alishangaa kumuona bosi wake sivyo kama alivyomzoea mmh bosi kapatwa na nini?? au ameishavurugwa na MARY....daah yani bosi na pess zake anachanganywa na yule mwanamke mfupi kama mwala!!!! aah mapenzi bana...ngoja nifanye yangu yanayonihusu... kuchunguza chunguza huku kibarua kinaweza kuota nyasi nikakosa Ugali....alisema mlinzi yule katika nyumba ya Tom..
********
Tom alipoingia ndani kabla hajakaa vizuri simu yake iliita """aliyekuwa anapiga simu hiyo ni Bony Kumbe bony ni mtu anayetumiwa na matajiri mbalimbali kwenye uharifu na utekaji wakati mwingine matajiri hao humtumia kuuwa kabisa..
baada ya tom kupokea simu bonu alisikika akisema kazi yako tayari nipe changu....
Tom alicheka kwa cheko la dharau kisha akasema safi sana nitakuongezea asilimia hamsini ya pesa tulizokubaliana....kisha akakata simu...
Tom alitoka nje haraka akaingia ndani ya gari na kuliwasha kuelekea kule walipokubaliana na bony apelekwe bosi jimy baada ya kumteka...
********
mlinzi lifungua geti kisha tom aliliondoa gari kwa kasi utadhani amevamiwa...
milinzi alifumga geti huku anajiuliza maswali yasiyokuwa na majibu...Tom alifika lile eneo alilomwambia bony ampeleke bosi jimy..kisha akapaki gari lake ma kushuka..bosi jimy alikuwa amefungwa mikono kwa nyuma na alifunikwa kwa kitambaa cheusi machoni....aliposikia vishindo vya mtu mwingine kaongezeka bosi jimy alilia huku akisema msiniuwe jamani nitawapa kiasi chochote cha pesa mnachokitaka...Tom alicheka kicheko cha dharau kisha akamfanyia ishara bony ili amuingize jimy kwenye buti ya gari la Tom..
bony bila kuchelewa alifanya kama alivyoagizwa...
kisha Tom akatoa kitita cha pesa na kumkabidhi Bony walishikana mikono kisha bony akaingia kwenye gari lake na kuondoka zake...
pia Tom aliingia kwenye gari lake na kuliwasha kuelekea kwake...
alipofika..mlinzi alifungua geti kisha Tom akaingiza gari lile mpaka ndani akalipaki...alimuita mlinzi akampa noti ya shilingi elfu kumi akamuamuru akamnunulie vocha huko nje madukani...mlinzi alipotoka...Tom alijisemea moyoni sasa huu ndio muda muafaka wa kumtoa bosi jimy ndani ya buti na kumuingiza ndani...
*********
baada ua kufanikisha kumuingiza ndani.. Tom alimfunua kile kitambaa cheusi machoni wakati huo bosi Jimy akiwa kafungwa mdomo na gundi ya naironi ili aisipige kelele..alipofunuliwa kile kitambaa alstahajabu kumuona Tom.....CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jimy alijaribu kuongea lakini hakuweza kwa sababu alikuwa kafungwa mdomo...
kisha tom akachukua kisu na kuchinja shingo ya bosi wake...Jimy alirusharusha miguu mpaka akakata roho....ndipo jimi akatoka na kuingia stoo akachukua sururu kisha akarudi chumbani mule na kuanza kuchimba shimo ndani ya chumba hicho ili amzike bosi wake apoteze ushahidi...
gafla alisikia hodi...mlango ukigongwa..
Shit huyu mlinzi ataniharibia kila kitu..alijisemea kimoyoni Tom.......kisha akaongea kwa sauti ya juu nakuja kuna kazi namalizia kuifanya hiyo vocha iweke hapo sebuleni juu ya meza..
Mlinzi alifanya kama alivyoagizwa kisha akatoka nje kuelekea sehemu yake ya kazi upande wa getini.....alipoketi alijiuliza maswali inamaana bosi kahama chumba? kaamua kulala kwenye chumba kidogo cha wageni!!! mmh kulikoni?? alijisemea moyoni Mlinzi huyo anayeitwa side..
********
kule chumbani Tom hakuwa na amani hata chembe hajawahi kuuwa tangu azaliwe mbaya zaidi kauwa nyumbani kwake...dah!! nikiendelea kuchimba side atasikia kwa sababu ilikuwa ni usiku hivyo palitulia kulikuwa hakuna kelele kama inavyokuwa mchana...Tom alitoka chumbani akazipiga hatua kuelekea sebuleni akawasha redio kwa sauti mpaka mwisho""" kwa redio ile ya gharama ilikuwa na spika kubwa ambazo zilitoa sauti kubwa utadhani kunadisko mule ndani ya nyumba.... tom alifanya hivyo ili akiwa anachimba shimo mule chumbani mtu wa nje asisikie kama kunanini kinaendelea humo ndani....tom alianza kuchimba alipiga seruru za sawasawa...jasho lilikuwa linamtoka huku akipumua kwa pumzi za kutweta""" alipagawa sana alipokuwa akigeuka na kuitazama maiti ya bosi Jimy....alipiga sururu hatimae akamaliza kuchimba shimo lile...kisha akaivuruta maiti ya bosi jimy na kuitumbukiza ndani ya shimo lile Tiiiii"" kisha akaanza kufukia shimo lile..alifukia kama nusu saa hivi akawa kamaliza kisha akafuta zile damu zilizokuwa zimetapakaa chini ya sakafu...alipohakikisha hakuna hata tone la damu alifunga pazia vizuri la dirisha la chumba hicho kisha akafungua mlango wa chumba hicho na kutoka upande wa nje akiufunga mlango huo na ufunguo kisha akaondoka na ugunguo kuelekea chumbani kwake.....aliingia na kupitiliza moja kwa moja bafuni...akajisafisha mwili wake(kuoga) zile damu zilizoruka na kum-mwagikia mwilini wakati anamchinja bosi jimy....kisha zile nguo alizokuwa amezivaa wakati anauwa..akaziweka kwenye begi dogo (lasket) baada ya kumaliza Tom alitoka nje ya chumba chake na kuelekea sebuleni. kisha akafungua kabati dogo na kutoa chupa ndogo ya pombe kali aina ya VODKA" ,, kisha akamimina kwenye glasi na kupiga fundo moja alipo shusha glasi ilikuwa tupu!!! akamimina tena akapiga fundo moja akashusha glasi ikiwa tupu...alifanya hivyo mpaka ile chupa ndogo ya VODKA ikabaki tupu...alivyo mimina tena akagundua kuwa chupa ile ilikuwa tupu akafungua tena kabati ili aongeze chupa nyingine...ghafla akasita kisha akajisemea moyoni nikilewa sana nitakuwa mashakani hivyo naweza kukamatwa kizembe...endapo nitashtukiwa kuwa nimefanya tukio hili...kisha akacheka sana na kuanza kucheza ule muziki mkubwa uliokuwa unaimba kwenye redio yake....alipochoka kucheza aliamua kujitupa kwenye sofa na baada ya dakika kadhaa kupita Tom alipitiwa na usingizi akalala hapo hapo...
**********
kule nje mlinzi alishangaa sana...mmmh!!! mpaka sasahivi saa saba kasoro usiku mziki bado unalia tena kwa sauti kubwa...bosi kapatwa na nini..alijiuliza side bila kupata majibu....kisha akaendelea kuuchapa usingizi
alipostuka alisikia bado mziki unaimba kwa sauti kubwa alistuka akaamua kwenda kugonga mlango wa kuingilia ndani...aligonga bila mafanikio yoyote""" kutokana na mziki mkubwa alafu Tom alikuwa na ulevi kichwani mwake ukichanganya na usingizi mzito wa ulevi Tom hakuweza kusikia mlango ulipokuwa unagongwa...side aliamua kuchungulia kupitia dirishani...kwa sababu taa ilikuwa inawaka alifanikiwa kumuona Tom akiwa kajilaza kwenye sofa...kisha aliiona chupa ya vodka ikiwa tupu pale mezani...akagundua kuwa Tom atakuwa kanywa pombe hivyo amezidiwa na ulevi ndio maana kalala hapo selubeni kwenye sofa.......
Side alirudi kwenye sehemu yake ya kazi ule upande wa getini...
**********
Tom alistuka usingizini alipotazama dirishani aligundua pamesha kucha alistahajabu kujikuta yupo sebuleni huku mziki mkubwa ukiendelea kuimba kwenye redio..... alikurupuka haraka akazima redio kisha akazipiga hatua za harakaharaka kuelekea chumbani kwake...alioga kisha akavaa harakaharaka..akatoka nje kuelekea kwenye gari lake aliingia na kuliwasha gari...side alifungua geti Tom akaondoka zake...side akafunga geti huku akajiuliza maswali yasiyokuwa na majibu inamaana bosi kaanza kuchanganyikia au?? yani hata salamu tu...ananipita utadhani hajaona mtu hapa getini....wakati anajiuliza hivyo mara ghafla alisikia honi ya gari alipochungulia aliona gari la tom..akafungua geti..tom hakuliingiza gari ndani alishuka nakuelekea ndani alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake""" kumbe alisahau lile begi lililokuwa na ngo zake zenye damu...ni nguo zile alizokuwa amevaa kipindi anafanya tukio la mauwaji...alilichukua begi lile na kuelekea nje alipopaki gari.aliliweka begi lile kwenye buti kisha aliliwasha gari na kuondoka zake...
alipoingia kwenye barabara kuu matrafki walimsimamisha akaweka gari kushoto...kumbe siku hiyo ilikuwa ni wiki ya usalama barabarani..hivyo matrafki walikuwa wanakagua magari yote na kama gari lako linamakosa basi utatozwa faini...
Tom aliogopa sana mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda mbio alijisemea nani katoa taarifa juu ya mawaji niliyofanya...CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Trafki mmoja alilikaribia gari la Tom nakuanza kulikagua tom aliingiwa na wasiwasi..kisha trafki yule akamwambia fungua buti....tom alistuka wasiwasi ukaongezeka akajisemea moyoni nimekwisha""" wazo lilimjia kichwani sijui nishuke nikimbie??
Tom alibofya kitufe cha kufungulia buti ya nyuma na buti ikafunguka.. kisha yule trafki akazunguka mpaka nyuma ya gari ... wakati huo tom macho yalimtoka huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio sana...jasho lilimtoka ufululizo"" alimtazama yule trafki kwa kumkazia macho... ooh my god naomba asifungue hilo begi akifungua tu nimekwisha...alijisemea moyoni tom.
yule trafki aliangazaangaza macho mule ndani ya gari kisha akaligusa begi lile tom alipo ona hivyo akafungua mlango na kushuka kutoka ndani ya gari...alifanya hivyo ili trafki yule akifungua tu zipu ya begi lile"""",, Tom akimbie...trafki yule alibonyeza bonyeza begi lile""",, hakulijali.... akafunga buti kisha akamwambia tom waweza kwenda...
Tom hakuamini kama kaponea kwenye tundu la sindano.....hakutaka kuongea chochote aliingia ndani ya gari haraka na kuliwasha akaondoka zake...
Aliwaza hivi yule trafki angefungua begi lile sijui ingekuaje..?? duh!!! mungu mkubwa kaninusuru ingawa nimefanya kosa kubwa la kuondoa uhai wa binadam mwenzangu...
***********
Tom alizipanga gia hatimae akafika kazini kwake..ni ghorofa moja kubwa na refu sana kwa juu lilikuwepo bango kubwa lililo andikwa
TNS COMPANY LTD alipaki gari lake akashuka akaanza kuzipiga hatua kuelekea kunako ngazi ya kutumia umeme(lift) aliingia na akabonyeza kitufe kilichoandikwa B15...lift ilipofika B15 alitoka na kuzipiga hatua kuingia ofisini kwake....wakati anazipiga hatua moyoni alikuwa na furaha alijisemea sasa mimi ndiyo mmiliki halali wa kampuni hii kuanzia sasa....aliingia ndani ya ofisi yake mpya"" ofisi hiyo ni lie aliyokuwa ofisi ya mkurugenzi Jimy...
Tom iliketi kwenye kiti cha kuzunguka ndani ya ofisi hiyo kisha akatabasam...
************
upande mwigine wale wafanyakazi wa kampuni hiyo
walionesha kutokubaliana na mkurugenzi Jimy kumuachia kampuni Tom kwani tom alikuwa ni m-binfsi sana hakuwa na uhusiano mzuri na wafanyakazi wale kipindi alipokuwa meneja muajiri...
*********
kule ndani ya ofisi tom alipekuapekua kwenye mafail ili kutafuta nyaraka miliki za kampuni ili abadilishe jina na kampuni iwe mali yake...alitafuta bila mafanikio yoyote...aliamua kuiwasha kompyuta(komputer) aliyokuwa anaitumia bosi Jimy ndani ya ofisi hiyo...alipekuapekua mafaili yaliyo kuwemo ndani ya kompyuta (computer) ile lakini hakuona chochote kitakachomsaidia angalau apate nyaraka miliki za mali za Bosi jimy.....
"come on""......inamaana huyu boya alikuwa hatunzi kumbukumbu yoyote ya kuhusu mali zake?? alijisemea tom""" aliendelea kupekua fail moja baada ya jingine,,, mara ghafla aliona faili(file) moja limewekewa namba za siri(password) yes nahisi zitakuwa humu. kwa sababu tom alikuwa na ujuzi mkubwa kuhusu kompyuta(computer) alijaribu kutengua namba zile za siri zilizowekwa kenye fail hilo.....alifanya hivyo akashindwa. tom alikata tamaa...alikaa huku akitafakali nini cha kufanya ili aweze kuzitengua namba hizo za siri...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
upande mwingine alionekana bosi anayesimamia maswala ya kukodisha ndege binafsi....alistahajabu sana mteja aliyekodi ndege binafsi kisha akalipia gharama zote...hajafika mpaka mda huo....""" kumbe bosi Jimy alikuwa kakodi ndege binafsi kwa ajili ya safari yake ya kwenda Amerca....."""baada ya kuona hivyo yule bosi anayesimamia upande wa kukodisha ndege binafsi aliamua kupiga simu ya mteja wake ambaye ni marehemu bosi jimy...simu ya jimy haikupatikana alipiga simu hiyo mara kwa mara alipo ona bdo haipatikani alijiuliza huyu ni mteja wetu mzuri kwa miaka mingi hajawahi kuhailisha safari kwa kipindi chote ambacho alikodi ndege zetu......aliamua kumuamuru moja ya muwakilishi wa kampuni hiyo ya ndege aende kwenye kampuni ya TNS... ili akapate taarifa je bosi jimy kahailisha safari!! ili wampangie safari siku nyingine.
**********
ule upande mwingine TNS alionekana Tom akihangaika kutengua namba za siri zilizowekwa na bosi jimy ili kuficha yaliyomo ndani ya faili lile asione mtu yeyote zaidi yake...
YES!!!! wooow tom alisema hivyo baada ya kufanikisha kuzitengua namba zile za siri zilizofunga faili lile...alianza kutazama kwa makini huenda akaziona nyaraka miliki za mali na kampuni ya marehemu jimy...
**************
yule muwakilishi hatimae alifika kwenye kampuni hiyo ya TNS aliulizia kwa sekretari kama bosi jimy alimuachia taarifa yoyote ya kuhailisha safari yake....sekretari alishangaa akastahajabu sana....kisha akajibu hapana sijui kisha alimuongoza muwakilishi yule mpaka ofisini kwa Tom...mlango ulipogongwa tom alistuka sana alihofia huenda ni mapolisi....alisita kuitika kisha akatazama video record katika kompyuta kubwa iliyokuwepo ukutani....kompyuta ile ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuona mtu yeyete anayeingia ndani ya kampuni ile kuanzia nje kwa kupitia kamera zilizotegeshwa eneo lile lote.baada ya kuangalia aligundua kuwa ni mtu wa shirika la ndege..alimkumbuka kwa sababu tom ndiye aliyeagizwa na bosi jimy kufanya booking ya safari hiyo. alirusu aingie....
muwakilishi yule aliuliza kuwa kunataarifa zozote kuhusu bosi jimy kuhailisha safari? ili tumpangie safari siku nyingine atakapokuwa tayari. tom aliogopa sana alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akajibu kwa kudanganya ndiyo kahailisha kwa sababu ameugua ghafla.. tutawataarifu atakapopona....
ok nakutakia kazi njema...alisema yule muwakilishi wa shirika la ndege kisha akatoka nje na kuondoka zake...
Tom aliwaza kuwa abadilishe wafanyakazi wote wa kampuni ile kisha aweke wafanyakazi wapya....
nisipofanya hivyo basi nitastukiwa mapema...na nitakuwa matatani.
nyumbani kwa bosi jimy"" mkewe aliingiwa na wasiwasi kwa nini mumewe tangu jana hajarudi nyumbani wakati ilitakiwa asafiri leo...pia tangu jana napiga simu yake haipatikani!!!"" alijisemea moyoni mke wa bosi jimy"" kisha akaamua kuchukua simu yake na kupiga simu ya jimy pia ilikuwa haipatikani...jamani mume wangu sijui kapatwa na nini!!! alipata wazo kuwa ampigie Tom huenda akawa anafahamu ni wapi bosi jimy alipo.....
*********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kule TNS Tom liendelea kupekua mafail yaliyopo kwenye kompyuta alitabasam akafurahi sana baada ya kuona kile alichokuwa anakitafuta kisha akachukua FLASH DISC akaanza kuhamisha lile faili lililokuwa likionesha ni wapi nyaraka miliki za mali za bosi jimy alipozihifadhi.....kumbe huyu boya kahifadhi nyumbani kwake......shit huu utakuwa mtihani kwangu nitawezaje kuingia nyumbani kwa jimy .....wakati akitafakali juu ya mpango wa kuzipata nyaraka hizo....mara ghafla Tom kulistuka sana baada ya kuona simu ya mke wa jimy ikimpigia.....ooh my god huyu mwanamke anataka nini tena!!!!! au kastukia??? alijisemea moyoni Tom....alista kupokea simu ile kwa sekunde kadhaa kisha akaamua kuipokea....
mke wa jimy alipiga simu ile kuulizia kama Tom anataarifa zozote kuhisu jimy...
Tom alisema hajui chochote kisha akaongezea kusema kwamba mara ya mwisho kumuona bosi jimy ilikuwa jana mchana walipotoka kazini..hivyo hakuweza kufahamu bosi jimy alielekea wapi baada ya hapo.. je kunalingine?? aliuliza Tom swali hilo la mtego ili afahamu kama mke wake jimy kastukia chochote kuhusu unyama alioufanya....
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment