Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

SIRI YA MIAKA 20 - 5

 







    Simulizi : Siri Ya Miaka 20

    Sehemu Ya Tano (5)



    ************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kesho yake Edo alitafuta anuani ya nyumba ya Amida aliipata na alipokwenda nyumbani kwa amida alistaajabu kuambiwa Amida kauwawa usiku wa jana na mtu asiyejulikana hivyo maiti yake imesafirishwa kwenda Mwanza nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi Edo alizidi kuchanganyikiwa...alijiuliza hivi ni nani anayefanya mauwaji haya ya kikatili....kisha Edo akarudi nyumbani...sikumoja wakati amelala usingizi aliota kuwa baba yake kamtokea kama mzimu huku amelala chini akimuta Edo amwambie kitu... ado alikwenda mpaka hapo alipokuwa amelala baba yake... kisha baba yake akamwambia kuwa (BINADAMU SIO WOTE WEMA KUWA MAKINI NA DUNIA WAEPUKE MARAFIKI WABAYA KWANI ALIYETOA UHAI WANGU ALIKUWA RAFIKI YANGU WA KARIBU NI MTU NILIYEKUWA NAMUAMINI SANA...NA SI MAMA YAKO KAMA UNAVYOFIKIRIA) machozi yalimtoka Edo kwani sura ya baba yake ilikuwa inatisha...mwili wake ulionekana kuoza.. baba yake aliongea maneno hayo kwa uzuni huku kanyoosha mkono wake kumtaka edo amshike... edo alipopeleka mkono wake amshike baba yake... mzimu ule ulipotea..Edo alistuka usingizini...



    ****BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA***



    baada ya mwezi mmoja kupita Edo na Grace walipanga safari"" Edo aende kujitambulisha kwa baba yake Grace....siku iliwadia na safari ya kwenda Dodoma kwa baba yake grace ikaanza..



    Edo alizipa gia baraabara.... walipiga stori na grace huku grace akijitahidi kuongea maneno ambayo yalimfanya edo atabasamu muda wote.. edo aliliendesha gari hilo ambalo lilikuwa la marehemu baba yake... mnamo majira ya saa mbili usiku waliwasili dodoma.. edo aliona sio vyema kwenda ukweni usiku huo... hivyo waliamua kulipia chumba katika nyumba ya kulala wageni kwenye HOTEL iitwayo CALFONIA HOTEL... walipewa chumba wakaingia upande wa ndani ya chumba hicho... grace alijiandaa kuingia bafuni ili aoge kuondoa uchovu wa safari... kisha akaingia bafuni..

    wakati grace anaoga.... simu ya edo iliita.. alipoitazama aliona namba ya mama yake ikimpigia... alistahajabu sana... kumbukumbu ilimuijia kuwa simu hiyo ya mama yake aliisahau kule katika nyumba aliyopata nyaraka zile hati miliki ya mali za baba yake... edo alisita kuipokea simu ile.... simu ile iliita kisha ikakata... ghafla simu yake ikaita tena...ni namba ile ile ya mama yake aliamua kuipokea...

    "nitakata shingo yako na kichwa chako nitakipika supu... yaonekana ubongo wako ni mtamu sana... alisema mtu huyo aliyepiga simu kupitia simu ya marehemu mama yake Edo""kisha akakata simu..

    edo alipojaribu kupiga simu hiyo....haikupatikana hewani..

    Edo alionekana kuchanganyikiwa.. baada ya kusikia mameno yale yenye vitisho...

    kumbe aliyepiga simuhiyo alikuwa ni Tom.



    ********

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ule upande mwingine tom akiwa nyumbani kwake kwenye jumba kubwa na la kifahari..alikuwa anapanga mpango wa kumuangamiza Edo.. ili achukue nyaraka zile amiliki mabilioni pamoja na mali nyingine za marehemu jimy... aliamua kuwauwa watu wote wale ili asiwepo shahidi hata mmoja.... ili amiliki mali zile bila mtu yeyete kujua mali hizo alizitoa wapi....



    Asubuhi palipokucha Edo na grace walidamka na kujiandaa kwenda nyumbani kwa baba yake grace.. waliingia ndani ya gari na safari ikaanza.. grace alimuongoza edo kwa kumuelekeza njia... na hatimae walifika nyumbani kwa baba yake grace.... Grace alishuka mutoka ndani ya gari na kuanza kuzipiga hatua kuelekea kwenye geti ili abofye kengere wafunguliwe geti......baada ya kubofya alitoka mtu mmoja aliyevalia suti nyeusi na miwani... alipo ona ni grace aliruhusu waingie ndani ya geti.. Edo alistahajabu sana... kuona walinzi wengi wakiwa na siraha za moto.... alimuuliza grace humu ndimo anapoishi baba yako??? ndio karibu sana my love" alijibu grace"""

    edo alijiuliza inamaana baba yake grace anawadhifa gani mbona analindwa na walinzi wengi tena wakiwa na siraha za moto!!!! alijisemea moyonk edo".....

    edo hakujali sana.... alishuka kutoka ndani ya gari kisha grace akamuongoza kuelekea upande wa ndani...huku wakisindikizwa na ulinzi mkali nyuma yao..... walipoingia ndani grace hakumkuta baba yake... alipoulizia kwa mmoja wa walinzi waliokuwemo ndani aliambiwa kuwa baba yake katoka lakini atarejea muda si mrefu...



    *********



    Grace alitoka nje akamuacha edo upande wa ndani.. .. wakati huo huo ndio alikuwa anarejea baba yake grace"" alifurahi sana kumuona binti yake kwani,,, ni siku nyingi hajamuona...

    mama yako hajambo" aliuliza baba grace

    ndio mzima wa afya kabisa"alijibu grace""

    mbona hukunitaarifu kama unakuja!!?? aliuliza baba grace

    haa baba mwenda kwao haombi ruhusa"alijibu grace huku akicheka...baba grace alitabasamu huku sura yake ikionesha wazi kufurahia mwanae kaja kumtembelea.... kisha grace akasema baba nimepata mchumba nimemleta kumtambulisha kwako....

    ooh ni jambo jema binti yangu... hongera sana alisema baba grace....

    baba nyoa hizo rasta zako sizipendi...alisema grace kisha wakaanza kuzipiga hatua kuelekea upande wa nda i kule alipokuwa ameketi Edo""" huwezi amini kumbe baba yake grace ndiye yule Jasusi muuwaji TOM.....

    walizipiga hatua wakaingia ndani... wakati Edo hana hili wala lile huku akishangaa shangaa mandhari yya mule ndani .. mara ghafla Walikutana uso kwa uso na Tom... edo hakuonesha hali ya kushangaa kwa sababu alikuwa hamtambui kwa sura muuwaji aliye waangamiza wazazi wake.....lakini tom alimtambua vyema edo.... tom alistuka lakini alijizuia ili mwanae asistukie kinachoendelea Tom alikuwa anampenda binti yake hakuna mfano... kwa sababu alikuwa ni mtoto wake wa pekee.... Tom aliamini wazi kuwa edo hamfahamu kuwa yeye ndiye Tom muuwaji aliye waangamiza wazazi wake....edo alijitambulisha...Tom alitoka na kuelekea upande wa vyumbani... baada ya muda simu ya edo iliita akatoka nje kuipokea...

    alizunguka nyuma kisha akaanza kuongea na simu ile... kumbe pale alipokuwa amesimama edo.. ni kwenye dirisha la chumba alichoingia tom.... ghafla edo alistuka baada ya kusikia mtu akiongea na simu ndani ya chumba kile..... "kajileta mwenyewe kwenye mikono yangu nita mchinja kama nilivyo mchinja baba yake... edo alistuka sana haa!!! yani baba yake grace ndiyo muuwaji aliowaangamiza wazazi wangu!!!!! siamini... alijisemea moyoni edo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ************



    edo alirudi haraka upande wa ndani... akaketi ghafla tom alirudi kutoka chumbani mule... naye akaketi.. edo alimtazama tom kwa umakini mkubwa.. hakuamini alichokuwa akikisikia.. tom alihisi edo mamstukia kuwa ueye ndiyo aliyewauwa wazazi wake... kwa sababu edo alikuwa akimtizama usoni bila kukwepesha macho.. huku uso wa edo ukionekana kujawa ghadhabu.. wakati grace akiendelea kumpigisha stori baba yake.. edo aliona simu inayofanana na simu ile ya mama yake ikiwa juu ua meza iliyosheheni vito vya thamani vilivyonakshiwa madini mnalimbali...alicbukua simu yake kisha akapiga namba ya mama yake bila kuweka simu sikioni..ili ahakikishe kama ndiyo yenyewe... ghafla simu ile iliita mezani pale...ghafla walikutanisha macho... . tom alijua wazi kuwa tayari edo amestukia alitoa bastola haraka alipobofya kitufe cha kufyatulia risasi grace aliruka ule upande aliokuwa ameketi edo.. risasi ilikwenda moja kwa moja mpaka tumboni mwa grace.... tom akili zikamruka baada ya kuona kampiga risasi binti yake kipenzi yeye mwenyewe kwa mkono wake.... tom akiwa anashangaa kumtazama binti yake.... aisee kumbe Edo ni moto wa kuotea mbali....aliruka sarakasi akampiga Tom mtama aina ya YOKO HAMA mtama huu ni hatari endapo utapigwa ukiwa kwenye marumaru au kwenye sakafu yenye simenti...mtama ule ulimrusha tom kimo cha mbuzi kisha akadondoka chini.. bastola ilidondoka kando... kabla hajakaa sawa tom alimrukia tom na kuanza kumpiga mgumi za uso za kila rangi zisizokuwa na idadi... tom alimsukuma edo akaangukia kando...tom kunyanyuka na kuanza kutimua mbio.. alitokomea vyumbani....

    kule nje walinzi walisikia vurugu zile walikuja mbio... edo aliwapiga wote..wakawa hoi...taabani kisha akawanyang'anya siraha zao.. na kuwafungia ndani ya chumba kimoja... kisha akapiga simu polisi.. akaanza kumtafuta tom ndani ya jumba hilo la kifahari... kumbe kulikuwa na mlango wa siri kutokea upande wa nje.. tom alitoka nje akaingia ndani ya gari.. aliliondoa kwa kasi akaligonga geti likang'oka alipotoka nje ya geti alikua hakuna njia mapolisi walikiwa wameziba njia kwa magari yao huku wakiwa tayari kwa kumkabili Jasisi yuho ambaye ni tom. tom hakuwa na nanma alijisalimisha... alishuka kutoka ndani ya gari huku mikono yake ikiwa kichwani.. tom alikamata akapelekwa polisi ili sheria ifate mkondo wake..



    **********



    baada ya edo kuona tom kakamatwa alirudi haraka kumuangalia grace...alikuwa bado hajakata roho.... alimbeba haraka akamuingiza kwenye moja ya magari ya Tom na kumkimbiza hospitali..

    grace aliongezewa damu haraka kwa sababu damu nyingi zilimtoka baada ya kupigwa risasi.

    kisha akafanyiwa upasuaji ili waitoe risasi iliyokuwa tumboni mwake.....

    baada ya wiki moja grace alipona... akaruhusiwa kwenda nyumbani huku akiwa chini ya uangalizi wa madakri..



    tom alifikishwa mahakamani... akasomewa mashtaka alikili mashtaka pia akasema ukweli wa mambo yoye aliyoyafanya... pia alisema kile chumba alichomzika Jimy.. Hakimu wa mahakama kuu ya KISUTU aliamuru Tom atumikie kifungo cha maisha JELA.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Edo alikwenda kwenye nyumba aliyokuwa akiishi tom zamani.. alifukuwa lile shimo alilizikwa baba yake.. na kutoa mifupa kisha akafa mpango ikazikwa makaburini...

    baada ya mwaka kupita edo na grace walifunga ndoa... wakaishi kwa amani na furaha.



    **********MWISHO WA SIMULIZI HII**********



0 comments:

Post a Comment

Blog