Search This Blog

Sunday, 22 May 2022

BALAA - 5

 





    Simulizi : Balaa

    Sehemu Ya Tano (5)


    Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga mguu mwengine kule, alikuwa anayumba ndani ya chumba, alikuwa anakwenda mtindo wa zigzag, lakini Mwanasheria alifika alipopakusudia. Pale walipokuwa wale mahasimu wawili, Dokta Yusha na Dokta Kilumba. "Dokta Kilumba, daktari mkuu wa hospitali ya Kinyonga. Daktari msomi uliyekabidhiwa dhima kubwa katika wilaya hii. Dhima ya kuokoa uhai wa wagonjwa. Daktari makini sana, uliyepata mafunzo yako ya udaktari huko katika jiji la Mumbai, India. Daktari mzalendo, uliyekataa kufanya kazi mjini, na kuamua kuja huku wilayani, porini eti kuja kusaidia wananchi maskini wa huku kama ulivyodai mbele ya jopo la madaktari bingwa. Unakumbuka ulikataa kufanya kazi Muhimbili? Ulikataa kufanya kazi katika hospitali ya Taifa, hospitali iliyopo jijini Dar es salaam, unakumbuka Dokta? Ulikataa dokta, inamaana ulikuwa na mpango huu kabla ndomana uliamua kuja huku kujificha ili ufanye kwa amani ufarauni wako? Una roho mbaya sana Dokta Kilumba, Zaidi John Kilumba sindo jina lako, nakufahamu vizuri Dokta. Si ulisoma shule ya msingi Kigoma wewe? Au nikwambie mwaka uliomaliza? Jua nakufahamu vizuri sana kabla hujajifahamu. But to make story short, Dokta Kilumba maisha yako yapo mikononi mwangu, ni bahati mbaya sana kwako kwakuwa maisha yako yapo mikononi mwa mlevi, mlevi niliyekubuhu, mlevi niliyopitia mengi sana katika maisha yangu, kuishi na kifo kwangu ni sawa tu, kwa hiari yako na hii hasa kama bado unatamani kuishi naomba ujibu swali langu kwa ufasaha bila kunidanganya....." Mwanasheria mlevi kwa sauti ya kilevi aliweka nukta na kumeza mate, huku akimwangalia Dokta Kilumba kwa umakini mkubwa. Kiukweli Mwanasheria mlevi aliongea maneno yaliyowashangaza wote mle ndani. ***** Kule kambini porini Ngome, hali ya mpelelezi Daniel Mwaseba ilikuwa mbaya sana. Wale majamaa walikuwa walikuwa makatili kweli, walikuwa wamemchakaza Daniel Mwaseba vibaya sana. Walimwacha pale chini akiwa nyang'anyang'a, hatamaniki. Tano toka kundi lile la Six killers, jambazi sugu kabisa alisogea pale alipolala Daniel Mwaseba. Tano alimnyanyua Daniel kwa hasira toka pale chini na kumuweka begani, baada ya kumuweka begani toka akaona bega siyo sehemu sahihi, Tano akagairi, akamtoa begani Daniel na kumnyanyua juu, ilikuwa mithili ya mtu kalibeba pipa tupu. Daniel Mwaseba akiwa hoi bin taaban kule juu alifumbua macho yake, Daniel Mwaseba alifikiria harakaharaka, alitoa na kujumlisha akiwa hewani, baada ya kugawanya na kuzidisha akajua inampasa kufanya kitu kuokoa maisha yake. Tano, alimwachia Daniel taratibu, huku akiutega mguu wake ule mzima ili Daniel Mwaseba afikie katika goti la mguu ule, nia yake kuu ni kumvunja kiuno. Na kweli Daniel Mwaseba alikuwa anashuka kule juu kuelekea katika lile goti zima la Tano. Daniel Mwaseba aligari akiwa hewani. Aliruka sarakasi huku akiachia teke lililotua katika kidevu cha Tano. Ilikuwa Balaa! Lilikuwa pigo la ajabu lililomshangaza kila mmoja mle ndani. Hakuna aliyeamini uwezo ule wa ajabu aliouonesha Daniel Mwaseba. Pigo lile la ajabu liliondoka na meno mengine mawili ya Tano. Tano alikuwa amepoteza meno manne sasa. Huku Daniel Mwaseba akitua chini akiwa kasimama imara. Daniel Mwaseba alikunja ngumi huku aliwaangalia watu wale kwa zamu na umakini mkubwa sana. Sasa Daniel alikuwa tayari kwa lolote! Daniel mwaseba alizidisha umakini zaidi maana alijua yuko sehemu hatari sana, tena mbele ya watu hatari sana. Watu ambao kuuwa ni kitu kidogo sana kwao, hawajari, hawaogopi. Mbili wa Six killers naye kwa umakini mkubwa alisogea pale aliposimama Daniel Mwaseba. Mbili alikuwa makini, alikuwa ashazisikia habari kuhusu Daniel Mwaseba. Kwahiyo alikuwa makini kuzizima mbinu zote za Daniel Mwaseba. Mbili alimsogelea Daniel huku akijifanya kutabasamu. Wakati uleule Tano wa Six killers naye alikuwa anaamka pale chini, akiwa na ghadhabu pasi na mfano. Hasira za kufanywa namna ile tena mbele ya bosi wake, Don Genge. Tano naye alijizoazoa kwa taabu na kumsogelea Daniel Mwaseba. Ilikuwa kushoto Mbili kulia Tano, mbele ya mpelelezi makini, Daniel Mwaseba. Patamu hapo. Ghafla! Mbili wa Six killers alifanya kitu cha ajabu sana. Alidanda chini kwa nguvu. Mdando uliomfanya aruke juu na kuanza kujivingirisha mithili ya feni huku akiachia mapigo mawili kwa nguvu yaitwayo kificho. "Kificho ni pigo asili yake ni Thailand. Pigo ambalo mpigaji anapiga kwa siri hata ukiwa makini kiasi gani kumwangalia huwezi kujua katumia kiungo gani cha mwili kupiga, pigo la kificho likimgusa mpigwaji ni kifo moja kwa moja" Kwa bahati nzuri Daniel Mwaseba alikuwa anaujua vizuri sana mtindo ule wa kificho. Mwenyewe alishawahi kuutimia mara kadhaa mtindo ule wa kificho. Kumbuka katika simulizi iitwayo mpango wa siri. Siku zote, pigo la kificho huzuiwa kwa kificho. Daniel Mwaseba alifanya hivyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alizuia mapigo yale ya kificho kwa kificho. Kati ya watu waliokuwepo pale hakuna aliyeamini uwezo ule wa ajabu wa Daniel Mwaseba. Mara zote pigo la kificho huondoka na roho ya mpigwaji. Lakini cha kushangaza Daniel Mwaseba alikuwa bado anapumua baada ya pigo lile la kificho toka kwa Mbili wa Six killers. Bosi wa Six killers, Don Genge alikuwa anayaangalia yote hayo kwa umakini mkubwa sana, huku akitabasamu. Aliuhusudu sana uwezo uliokuwa unaoneshwa na vijana wake. Mbili alivyotua chini alijipanga imara, huku akimkuta Daniel Mwaseba akiwa imara zaidi yake. Wanaume wawili walikuwa tayari kwa kazi! Mmoja kutetea kazi haramu, mwengine kupinga kazi haramu. Mbili alirusha teke la nguvu kwa mguu wake wa kulia, teke lililokuwa linaenda katika sura ya Daniel Mwaseba, lakini Daniel aliliona. Alifanya mambo mawili kwa kasi ya haraka sana. Daniel alibonyea kwa chini kidogo huku akiufyatua ule mguu wa kushoto wa Mbili uliobaki chini. Kwa mara ya kwanza tangu waanze kupambana Daniel Mwaseba alikuwa amemuweza Mbili. Jamaa alidondoka chini vibaya sana. Ilikuwa mithili ya gunia la viazi limerushwa toka kwenye fuso. Daniel Mwaseba hakutaka kabisa kushangaa, aliruka juu kiasi na kutua kwa nguvu tena kwa miguu yake yote miwili katika tumbo la Mbili wa six killers. Mbili aliipatapata! Mkanyago ule ulimwingia barabara Mbili. Alitema majimaji mekundu mdomoni bila kupenda, Ilikuwa ni damu!. Daniel Mwaseba hakuzubaa, aliruka tena juu huku goti lake la mguu wa kulia likielekea shingoni kwa Mbili. Hili sasa lilikuwa pigo la kifo! Lakini cha ajabu goti lile la Daniel Mwaseba halikufika katika shingo ya Mbili. Ndio halikufika kabisa! Tano wa six killers aliingilia kati kumuokoa jamaa yake, maana bila hivyo, Daniel Mwaseba alikuwa ameshageuka mbogo! Tano aliruka juu nae na kumvaa Daniel Mwaseba hukohuko angani. Katika watu wote walikuwa mahali pale, Daniel Mwaseba hakuna mtu aliyekuwa hampendi kama Tano wa Six killers. Tano alikuwa sugu, Tano alikuwa jeuri, na kwa bahati mbaya kabisa ni Tano wa Six killers ndiye aliyemfata Daniel Mwaseba kule angani. Walipotua tu chini Tano hakujiuliza mara mbili, alimuwahi kwa kumbinya Daniel Mwaseba katika koromeo. Alimbinya hasa! Daniel alisikia maumivu makali sana, alitoa mkoromo usioeleweka, lakini yule jamaa aliendelea kumbinya. Akiongeza nguvu kila mshale wa saa wa sekunde ulivyokuwa unasogea kuelekea kulia. Balaa! Daniel Mwaseba alianza kuona watu wakiwa wamevaa mavazi meupe wakieleaelea hewani, kisha walitoweka ghafla. Mara likaja giza kubwa sana, kitu kimoja tu kikapita katika akili ya Daniel Mwaseba kwamba alikuwa nd'o anaelekea kufa. Baada ya kama dakika moja ya giza lile la ajabu, Daniel hakuelewa tena kilichokuwa kinaendelea duniani. Daniel Mwaseba nae alitoka duniani na kulifata lile giza la kutisha. Daniel Mwaseba aliwafata wale malaika weupe wakioelea hewani. Kule upande.... katika nyumba ya kulala wageni ya Mjaka hali ilikuwa ngumu sana kwa Dokta Kilumba. Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walikuwa wamembana vizuri sana daktari yule Mwanaharam. Pamoja na upole wake wote lakini cha ajabu Dokta Yusha sasa aligeuka mbogo. Jasho lilikuwa linamtoka huku akimnyanyasa daktari mwenzake. Tena alikuwa Bosi wake, kumbuka Dokta Kilumba alikuwa ndiye daktari mkuu wa wilaya ya Kilwa. Pamoja na hasira zake zote Dokta Yusha lakini mara kwa mara hakusita kuzishangaa mbinu za mateso akizotumia Mwanasheria mlevi. Mwanasheria alikuwa anatoa mateso ya hali ya juu kwa Dokta Kilumba, tena kwa mbinu zinazotumiwa na majasusi wa kimataifa. Dokta Kilumba alijitahidi sana kuvumilia mateso ya watu wale wawili.... Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi lengo lao kuu la kumtesa lilikuwa ni Dokta Kilumba awatajie mahali kambi ya watu wale hatari ilipo, na Dokta Kilumba alikuwa anaonesha utukutu. Hakutaka kabisa kuwatajia. Dokta Yusha akahisi yule jamaa labda amekula kiapo cha kutotoa siri. "Hata kama amekula kiapo atasema leo" Dokta Yusha alijisemea kimoyomoyo. Dokta Yusha alijisachi mfukoni na kutoa mashine ya kukatia kucha. Aliishusha suruali ya Dokta Kilumba mpaka magotini. Mwanasheria mlevi alikuwa makini akiangalia kitu alichotaka kufanya Dokta Yusha. Dokta Yusha aliichukua ile mashine ya kukatia kucha na kuanza kunyofoa vipande vidogovidogo kutoka katika paja la dokta Kilumba. Alikuwa ananyofoa na kuweka sakafuni vile vipande. Balaa! Maumivu makali aliyokuwa anayapata Dokta Kilumba yalimfanya alie kama mtoto mdogo, aliona paja na mwili wake wote kwa ujumla unawaka moto! Bila kupenda huku akipitia katika mateso makali Dokta Kilumba aliwatajia Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi mahali kambi ya Six killers ilipo. Baada ya kutajiwa hawakumuacha Dokta Kilumba pale. Walitoka nae kama rafiki. Mhudumu wa nyumba ile ya kulala wageni hakuelewa chochote kilichokuwa kinaendelea, hakujua kabisa kama mteja wake alikuwa ametekwa. Walitoka nae na kwenda nae hadi katika nyumba ya kulala wageni alikopanga Dokta Yusha na kumfungia kwa ndani katika chumba chake katika nyumba ile ya wageni aliyopanga. Usiku uleule safari ya kuelekea porini ngome ilianza, kambini kwa kundi hatari la Six killers. Pamoja na kupoteapotea sana kule porini lakini wazalendo hawa wawili wenye nia ya dhati ya kuokoa raia wema walifika katika eneo ambako kulikuwa na kambi ya kundi hatari la Six killers. Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walitumia saa zaidi ya mbili wakizitumia wakiwa nje wakitafuta namna ya kuingia mle katika kambi ile hatari. Lakini hawakupata namna yoyote ya kuingia kambini kwa kambi ile hatari. Hadi jua la asubuhi linachomoza Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walibaki wakiwa nje, bado wakihaha kutafuta njia ya kuwawezesha kujipenyeza mle kambini. Mle ndani ya kambi Daniel Mwaseba alikuwa katika hali ngumu sana. Ilikuwa ni hali mbaya zaidi kuwahi kukutana nayo mpelelezi huyu mahiri nchini Tanzania. Baada ya ule mbinyo wa nguvu shingoni, mbinyo aliopewa na jambazi katili, Tano wa Six killers Daniel Mwaseba alipoteza fahamu. Sasa mwili wake usio na pumzi ulikuwa katika chumba cha mateso cha watu wale makatili. Chumba kilekile alichowahi kuingizwa Dokta Yusha baada ya kutekwa kule hospitali Kivinje. Naam..... Chumba cha kifo kama walivyokuwa wanakiita wenyewe Six killers. Mwili wa mpelelezi Daniel Mwaseba ukiwa haujitambui ulilazwa katika sakafu ukisubiri muda wa kuja kutolewa uhai tu. Tangu saa tisa usiku mwili ule uliowekwa katika chumba kile cha kifo. Masaa matatu baadae Daniel Mwaseba alifumbua macho taratibu. Ni kudra za Mwenyezi Mungu tu zilimusha. Na kitu cha kwanza kukiona japo kwa shida katika chumba kile cha kifo kilikuwa ni kiti, kiti cha kifo! Kiti hatari sana kisichofaa kukaliwa na binadamu. Daniel Mwaseba alijinyanyua taratibu pale chini, akiwa bado yuko makini na kile kiti cha moto, kiti cha kifo! Daniel Mwaseba alikuwa anakiangalia kiti cha kifo huku akitabasamu. Kwa mwendo wa taratibu alianza kukisogelea kile kiti cha kifo! Daniel Mwaseba alikitambua kile kiti cha kifo. Naam...alikitambua! Daniel Mwaseba alikuwa anazijua vizuri sana habari za kile kiti cha kifo. Ni yeye ndiye aliyetumwa na waziri mkuu wa Jamhuri ya

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muungano wa Tanzania kukileta kile kiti nchini, toka katika Jamhuri ya watu wa China. Alikumbuka vizuri kuwa alimuuliza Waziri mkuu kuhusu matumizi ya kiti kile hatari, na alikumbuka kuwa jibu la Waziri mkuu lilikuwa fupi tu.. 'Ni kwa sababu za kiusalama' Daniel Mwaseba alienda China kwa shingo upande. Kwa kuwa hakuridhika kabisa na jibu alilopewa na Waziri mkuu wakati huo. Alikuwa anajua vizuri uwezo na maajabu wa kiti kile. Ni kiti hatari kuliko hatari yenyewe. Pamoja na kuwa na muonekano wa kiti kwa sasa lakini kilikuwa na uwezo wa kubadirishwa na kuwa silaha mbalimbali hatari. Kiti kilikuwa na uwezo wa kuwa Bomu kubwa hatari la maangamizi na kuleta athari kubwa sana sehemu litakaporushwa ama kutegwa. Kiti pia kilikuwa kinaweza kubadirika na kuwa bunduki kubwa za kivita. Uwezo hatari wa kiti kile nd'o sababu iliyomfanya Daniel Mwaseba aende China kukifata kiti kile kwa shingo upande. Sababu kuu ya mashaka ya Daniel ilikuwa.....Wakati huo nchi haikuwa na uhaba wa silaha katika maghala yake...na wala hakukuwa na tishio la usalama kwa nchi. Sasa kwanini nchi inunue gharama ghali na hatari namna ile? Pamoja na mashaka yake lakini Daniel Mwaseba alienda China, hakutaka kupinga kabisa agizo la Waziri mkuu. Alienda China salama na alirudi Tanzania salama. Na ni yeye mwenyewe ndiye aliyemkabidhi kiti kile Waziri mkuu tena nyumbani kwake. Utaratibu uliotumika kuleta kiti kile na kukabidhi uliendelea kuongeza mashaka kichwani mwa mpelelezi Daniel Mwaseba. 


    Na ni yeye mwenyewe ndiye aliyemkabidhi kiti kile Waziri mkuu tena nyumbani kwake. Utaratibu uliotumika kuleta kiti kile na kukabidhi uliendelea kuongeza mashaka kichwani mwa mpelelezi Daniel Mwaseba. Ashaenda kufata ama kuongoza msafara wa kwenda kuchukua silaha mara nyingi, na mara zote hukabidhi kwa Mkuu wa majeshi na wanajeshi wengine wenye vyeo vya juu huku wakishuhudiwa na Amiri jeshi mkuu. Kwa ujumla utaratibu uliotumika kuleta kiti kile ulimshangaza sana Daniel. Lakini mshangao na wasiwasi wa Daniel Mwaseba leo hii ulileta jibu, kiti kile hatari sana alikikuta ndani ya kambi hatari ya Six killers. Kimefikaje? Maswali mengi sana yalipita katika kichwa cha mpelelezi Daniel Mwaseba. Lakini maswali yote hakuwa na majibu yake kabisa, pamoja na kutopata majibu ya maswali yake lakini Daniel hakuacha kujiuliza maswali ingawa alijua hakukuwa na wa kumjibu . Lakini alijiuliza..... "Je kiti hiki kimekuja kwa bahati mbaya au makusudi katika kambi ya watu hawa hatari?" Daniel Mwaseba alijiuliza kimoyomoyo huku akikiangalia kile kiti. Bahati mbaya kwa maana kundi lile hatari labda walikiiba kiti kile toka mikononi kwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Justus Bitesigile, au Waziri mkuu alikuwa na dhamira tangu mwanzoni, dhamira ya kuwaletea kiti kile kundi hatari la Six Killers. Kwa dhamira hii wanayoifanya watu hawa. Daniel Mwaseba akajua umakini mkubwa zaidi unahitajika katika kutatua mkasa huu mzito! Mkasa wenye sura ya usaliti, mkasa wenye sura ya usiri mkubwa sana. Mkasa wenye nia mbaya kwa nchi ya Tanzania. Hisia kuwa kuna viongozi wakubwa toka serikalini pia wanahusika katika mkasa huu mzito zikatamalaki katika kichwa cha Daniel Mwaseba. Uwepo wa kiti kile mahali pale ulidhihirisha hilo. "Wakubwa, kwa dhamira ipi sasa? Iweje viongozi wa nchi wauwe wananchi wao?, kosa la wananchi ni lipi? Wananchi ndio waliowachagua hao viongozi, kwa hiyo moja kwa moja viongozi wana dhima ya kuwalinda wananchi, kuwahudumia wananchi, Kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za kijamii" Daniel Mwaseba aliendelea kujiuliza mwenyewe na kujielezea mwenyewe. Tena sasa sio kimoyomoyo tena, alikuwa anaongea kwa sauti ndogondogo...ya kunong'ona. "Sasa kwa mfano wananchi wote wakiuwawa na kundi hatari la Six Killers, tena kuuwawa kikatili na kwa makusudi watawaongoza kina nani hao viongozi waliopo katika mpango huu?" Mawazo pamoja na maswali yasiyokuwa na majibu ya Daniel Mwaseba yalikatishwa na makelele ya kitasa cha mlango, makelele ambayo ilikuwa ni ishara tosha kuwa kuna mtu alikuwa anafungua ule mlango kwa nje na kutaka kuingia ndani. Kwa kasi ya ajabu Daniel Mwaseba alijirusha na kurejea mahali palepale alipolazwa awali. Akalala kwa mtindo uleule kama waliomlaza awali. Daniel Mwaseba akazimia tena! Kelele zile za mlango zilienda sambamba na mlango kufunguka. Mle ndani ya chumba hatari cha mateso aliingia Komando Mbili wa Six Killers. Mbili akiwa kanuna kwa hasira. Bila kujulikana hata sababu ya Mbili kununa namna ile. Mbili alikuwa kapania kwenda kumuonesha Daniel Mwaseba kuwa yeye ni nani?. Na kwanini alipewa namba Mbili katika kundi lile hatari. Lakini kwa bahati mbaya kabisa alimkuta Daniel Mwaseba hajazinduka bado toka usingizini, usingizi wa kuzimia. Mbili wa Six Killers alimsogelea Daniel Mwaseba pale chini huku akitabasamu. Sasa Mbili aliacha kununa. Alipofika pale mahali ambapo alipolala Daniel Mwaseba, Mbili alijisachi mfukoni na kutoa sindano ndogo ya kushonea nguo. Nia yake kuu ni kutaka kuiingiza ile sindano katika mwili wa Daniel Mwaseba ili aone na kuthibitisha kama Daniel Mwaseba alikuwa amezimia kweli ama ulikuwa ni mchezo tu . Mbili wa Six killers alijisachi mfukoni, alitoa kisu kirefu na kikali mfukoni na kuchana suruali ya Daniel Mwaseba ile sehemu ya paja. Paja la Daniel Mwaseba sasa lilikuwa wazi, likiangaliwa na mtu hatari sana! Laiti lingejua paja lile kinachokuja kukutana nacho, bora lingebaki ndani hukohuko. Mbili alitoa sindano iliyokuwa imeviringishwa katika kipande cha gazeti. Ilikuwa sindano ndogo nyembamba ya kushonea nguo, lakini Mbili aliishika ile sindano kibabe na kuanza kuizamisha taratibu katika paja la Daniel Mwaseba. Balaa! Sindano ilianza kuingia taratibu katika nyama laini za paja za Daniel Mwaseba. Mwendo ule wa taratibu wa kuingia sindano ile ulienda sambamba na maumivu. Daniel Mwaseba alianza kupata maumivu taratibu....sindano ilipofika robo na maumivu sasa yakashamiri. Kumbuka Daniel Mwaseba alikuwa hajazimia kweli lakini ilimpasa kuvumilia maumivu yale makali, Daniel Mwaseba ilimpasa kutulia tuli kama maji ya mtungini. Mtikisiko wowote toka kwa Daniel Mwaseba ulikaribisha jambo baya sana..naam mtikisiko wowote ulikaribisha kifo! Ilikuwa ngumu sana kuvumilia maumivu yale makali ya sindano. kwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe maumivu yale yalikuwa hayavumiliki, tusingethubutu hata chembe. Lakini Daniel Mwaseba hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe. Mafunzo mbalimbali aliyoyapata Daniel Mwaseba yalimtoa katika ubinadamu kidogo na kuanza kumpeleka taratibu katika unyama! Amini usiamini Daniel Mwaseba aliyavumilia maumivu yale. Hakutikisika wala kuonesha ishara yoyote ile kwamba alikuwa hajazimia. Sindano ilipofika nusu, Mbili wa Six killer akaanza kuichezesha ile sindano ikiwa ndani ya paja. Balaa! Maumivu yakazidi maradufu. Kama kuna binadamu sugu duniani basi Daniel Mwaseba alikuwa ndio mwalimu wake. Pamoja na mtikisiko ule wa sindano, mtikisiko uliokuja na maumivu makali zaidi lakini Daniel Mwaseba alitulia, ilikuwa kama amefariki vile. Utulivu ule wa Daniel ukamfanya Mbili aamini kwamba Daniel Mwaseba alikuwa bado kazimia,

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaichomoa ile sindano kwa haraka sasa na kuamua kuondoka katika chumba kile cha mateso....chumba cha kifo!. Hilo ndio lilikuwa kosa la kiufundi ambalo Mbili wa Six killers atalijutia milele. Kosa la kiufundi na kwa bahati mbaya zaidi alilifanya mbele ya fundi. Kwa mkupuo mmoja Daniel Mwaseba alifungua macho yake yote mawili. Alivuta pumzi kwa haraka na kunyanyuka taratibu. Daniel alitembea kwa mwendo wa kimyakimya lakini wa haraka akimuwahi mbili pale mlangoni. Alimshika Mbili shingoni na kumrudisha Mbili ndani kwa nguvu. Sasa mkao ulibadirika....Daniel Mwaseba akakaa ule upande ulikokuwa mlango huku Mbili akiwa kwa ndani. Wote wakiwa wamejipanga tayari kwa mapambano. Mbili alikuwa na silaha ya kisu tu ambayo ilikuwa imetulia kiunoni, kisu alichotumia kukata suruali ya Daniel Mwaseba. Daniel alikiona kile kisu pale kiunoni. Lakini hakujari. Sasa Daniel alikuwa anautambua vizuri sana uwezo wa watu wale kimapambano. Sasa aliamua kupiga mapigo ya nguvu! Mapigo hatari wanayofunzwa watu maalum ili kuwapiga watu maalum. Mbili nae alisimama imara....tayari kwa lolote. Daniel nd'o alianza kushambulia, alirusha kareti ya nguvu iliyokuwa inaelekea moja kwa moja katika shingo ya Mbili, lakini mbili aliiona. Kwa kasi ya haraka aliinama kidogo huku akiachia ngumi ya kwa mkono wa kushoto, ngumi iliyokwenda katika tumbo la Daniel. Lakini Daniel nae alijiandaa kwa hilo, aliikwepa ile ngumi kiufundi mkubwa. Sasa mafahari hawa wawili wakawa wanatazama. Kila mmoja kasimama, tayari kwa lolote, tayari kwa chochote, muda wowote. Daniel ndiye alikuwa wa kwanza tena kuamua, alirusha ngumi nane za harakaharaka, nne kwa mkono wa kulia, nne kwa mkono wa kushoto lakini Mbili alizipangua zote, kirahisi sana. Zilikuwa ni ngumi mzito sana, ngumi moja ikitosha kabisa kumpeleka kuzimu mtu dhaifu kama wewe, lakini Mbili hakuwa mtu dhaifu, alikuwa mtu imara kabisa. Cha ajabu Mbili alikisahau kile kisu kiunoni....alikiacha kimetulia tu, labda alidhani atamuweza Daniel kwa mikono mitupu. Mbili nae alirusha ngumi usawa wa mwamba wa pua wa Daniel Mwaseba, lakini Daniel aliiona ngumi ile, aliikwepa huku akiachia ngumi ya nguvu sana kuelekea katika mbavu za Mbili. Mbili aliguna kwa maumivu, alishika mbavu zake kwa mkono wa kulia, lilikuwa kosa! Daniel Mwaseba alipeleka ngumi ya nguvu katikati ya sura ya Mbili. Mbili alipepesuka huku akiwa amechanganyikiwa, ashike mbavu ama sura. Kubabaika kwake kulitoa mwanya mwengine kwa Daniel, aliruka juu huku akipiga teke la kinyumenyume, teke lilomkumba kwa nguvu Mbili na kwenda kumgongesha ukutani vibaya sana! Mbili alikuwa amepatikana. Daniel hakutaka kumpa nafasi, alienda na kifuti pale ukutani na kulipata tumbo la Mbili barabara. Mbili alitapika damu! Daniel alimkaba kabali Mbili, akainyonga ile shingo kwa nguvu kuelekea upande wa kushoto! Roho mbaya ya Mbili ilisalimu amri, roho iliuacha ule mwili dhaifu na kuelekea kusikojulikana. Baada ya kufanikiwa kumuuwa Mbili wa Six Killers Daniel Mwaseba akauacha mwili wa Mbili pale chini na kuusogelea ule mlango wa kile chumba cha chumba cha mateso.....chumba cha kifo!


    Roho mbaya ya Mbili ilisalimu amri, roho iliuacha ule mwili dhaifu na kuelekea kusikojulikana. Baada ya kufanikiwa kumuuwa Mbili wa Six Killers Daniel Mwaseba akauacha mwili wa Mbili pale chini na kuusogelea ule mlango wa kile chumba cha chumba cha mateso.....chumba cha kifo! Alifungua mlango taratibu na kuchungulia kwa nje, kulikuwa shwari. Hakukuwa na lolote la kutilia shaka. Daniel Mwaseba akaiangalia ile nyumba ya bluu kwa hasira. Akijua kuwa watu wale makatili walikuwa mle ndani. Daniel Mwaseba akapiga hatua za haraka kuelekea kule kwenye nyumba ile ndogo ya bluu. Kule nje ya nyumba ile, walikokuwa Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi waliomaliza usiku ule wakiwa katika hali ya kusubiri. Hadi asubuhi inafika Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walikuwa bado wanasubiri, walikuwa hawajapata namna ya kuingia mle ndani ya kambi ya Six killers. Walibaki wamejibanza vilevile, sehemu ile nyuma ya mti mkubwa wakisubiri kudra tu za Mwenyezi Mungu ili waweze kuingia mle ndani. Na kwa bahati mbaya sana hadi sasa hizo kudra za Mwenyezi Mungu zilikuwa hazijawafikia bado..nao waliendekea kuzisubiri. Kule nje ya kambi Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi bado walikuwa wanasubiri, walikuwa wanasubiri nafasi yoyote ile ya kuwawezesha kuingia katika kambi hatari ya Six Killers. Hadi muda huo hawakuiona nafasi yoyote ya kuweza kuingia mle ndani. Na kwa kujificha tu pale nyuma ya mti sidhani kama wangeiona...... Hata wangekaa mwezi.... Baada ya kusubiri sana, Dokta Yusha alipata wazo na kumshirikisha Mwanasheria mlevi. Walikubaliana. Dokta Yusha alitoka pale nyuma ya mti walipokuwa wamejificha na Mwanasheria mlevi, kwa mwendo wa taratibu na umakini mkubwa alianza kuizunguka ukuta wa kambi ile hatari. Mwanasheria mlevi alibaki pale kwenye mti kwa dhumuni maalum. Yeye alikuwa anamlinda Dokta Yusha kwa macho na kutoa ishara endapo itatokea hatari yoyote. Hivyo ndivyo walivyokubaliana mashujaa wale. Dokta Yusha bila kujijua alikuwa anafanya mchezo wa hatari sana. Kuizunguka nyumba ile ilikuwa ni zaidi ya hatari, tena asubuhi namna ile. Mzunguko ule wa Dokta Yusha hatimaye ulimfikisha sehemu ulipokuwepo ule mti ulio karibu na ukuta wa kambi ile, mti uleule aliotumia Daniel Mwaseba kuingia mle kambini. Dokta Yusha nae alipata akili sawa na alizopata Daniel Mwaseba. Naam Dokta Yusha alipanda juu ya ule mti. Tofauti ilikuwa wakati Daniel Mwaseba alipanda mti ule na kuingia ndani ya kambi usiku wa manane... Yeye alipanda katika mti ule asubuhi na kutaka kuingia ndani ya kambi ya Six Killers asubuhi. Dokta Yusha alikuwa amefanya jambo hatari sana, kujianika mbele ya wauaji hatari wa Six Killers namna ile. Dokta Yusha alifika hadi pale kileleni, juu ya ukuta. Kutokea kule kwa juu alishuhudia vizuri mandhari ya kule ndani ya kambi, ambayo yeye alikuwa anayafahamu vizuri kabla. Kumbuka Dokta Yusha alipanda ule ukuta wa kambi ile hatari asubuhi jua likiwa limechomoza, na pia Dokta Yusha alikuwa kashawahi kuingia katika kambi ile, na kwa bahati nzuri zaidi alibahatika kutoka salama. Akiwa pale kwa juu alipeleka macho yake katika kibanda kilichokuwa pembeni kidogo mwa ile nyumba ya bluu. Dokta Yusha alikumbuka mengi sana wakati anakiangalia kibanda kile. Alimkumbuka yule askari aliyepoteza uhai wake katika kiti cha kifo ndani ya kibanda kile. Askari aliyekufa kwa kubadirika rangi na kuwa nyekundu sambamba na kiti kile na kupotea katika ulimwengu kwa kuyeyuka palepale katika kiti cha kifo. Dokta Yusha alimkumbuka yule jamaa aliyepambana nae katika kibanda kile, na kufanikiwa kumsukuma katika kiti cha kifo! Kilichopo ndani ya kibanda alichokuwa anakitazama. Nae aliyeyuka huku akibadirika rangi sambamba na kiti. Akiwa kule juu Dokta Yusha alijipa moyo, huku akijivika ujasiri kuwa lazima akapambane! Sasa dokta Yusha alifuta kabisa hali ya hofu katika moyo wake na kuona ni heri kufa kishujaa, kuliko kuishi ukiwa unashuhudia maovu yakiendelea kufanyika ulimwenguni. Kilikuwa ni kiapo alichoapa Dokta Yusha akiwa juu ya ukuta hatari....na alipania kukitekeleza kiapo chake. "Nitakufa nikipambana..." Dokta Yusha alihitimisha mawazo yake kwa kujisemea mwenyewe kimoyomoyo. Kwa taarifa tu, ule mti uliokaribu na ukuta wa kambi ya Six Killers uliachwa kwa makusudi na kundi la Six killers sehemu ile. Hawakutaka kuukata ingawa walikuwa na uwezo huo. Ni Moja wa six Killers ndiye aliyeshauri mti ule uachwe, kwa makusudi ili utumike kama mtego. Ndio...... Waliuacha mti ule wakijua adui yoyote akitaka kuingia katika ile nyumba lazima atautumia ule mti. Maana ndo sehemu pekee iliyokuwepo kwa mtu mjanja kuingia mle ndani ya kambi yao. Nao kule ndani hawakuzubaa hata chembe, wakiwa kule kwa ndani walikuwa wanaulinda kwa kuuangalia ule mti kila baada ya dakika tatu. Komando Moja wa Six killers akiwa kule kwa ndani alimshuhudia vizuri sana mtu akipanda katika mti wao. Mti wa mtego ulioachwa kwa sababu maalum. Na sasa sababu za kuachwa ule mti zilileta matokeo. Tena matokeo yenyewe yalitokea na kuonwa na Moja mtu ambaye ndiye alishauri mti ule uachwe kama mtego. Yeye ndio alikuwa zamu kuulinda mti ule. Na ilikuwa kazi rahisi sana kwake kumshudia mtu yule akiwa katika kilele cha ule mti wa mtego. Na alimshuhudia yule mtu hadi jinsi akivyoruka toka kule mtini mpaka pale katika ukuta wa kambi yao. Alivyofika juu ya ukuta alimshuhudia mtu yule akiangalia kibanda chao cha kufanyia mateso..kibanda chenye kiti cha siri, kiti cha kifo! Moja alimtambua mtu yule... "Dokta Yusuph Shaweji, daktari mfukunyuku umekifata kifo chako! Tena umekifata ukiwa unakikimbilia kwa kasi! Hahaha...umekutana na malaika mtoa roho hahaha" Moja aliongea peke yake huku akitoka nje taratibu kwa kicheko chake cha karaha. Wakati uleule ambao Moja wa Six Killers alikuwa anatoka nje ya nyumba ile ya bluu ili kwenda kumvia na kumuua kabisa Dokta Yusha kama alivyojiahidi mwenyewe akiwa ndani ndio wakati uleule ambao Daniel Mwaseba alikuwa anatoka kule kwenye kibanda cha mateso. Alikofanikiwa kumuua Mbili. E bwana wee! Komando namba moja wa kundi hatari la Six killers na Mpelelezi mahiri nchini Tanzania Daniel Mwaseba walikutana uso kwa uso.....Kumbuka Dokta Yusha bado yuko juu ya ukuta. Kwa upande wa jeshi la Polisi nalo halikulala kabisa, tangu siku ya kwanza kutokea kwa mkasa huu wa ajabu wa kupotea watu kimaajabu bila sababu kujulikana, jeshi la Polisi waliingia kazini. Jeshi la Polisi walianza

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kufanya msako wao kimyakimya. Lakini kimyakimya yao haikusaidia chochote. Walikuwa wanazunguka palepale bila kujua chanzo cha upotevu wa watu wale, wala kujua ni nani akiyewaficha watu wale. Unaweza sema bora Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walipiga hatua kubwa sana kuwakaribia wahalifu kuliko jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi hawakuwa wanajua lolote kuhusu uwepo wa kundi hatari la Six Killers ndani ya Kilwa. Mbinu ya kimyakimya ilivyoleta matokeo hasi hatimaye jeshi la Polisi waliamua kufanya msako wa hadharani. Makundi ya askari yalimwaga mitaani kujaribu kutafuta fununu yoyote juu ya kupotea kwa watu au mahali walikopelekwa na kwa lengo gani. Vijana wa Fresh Nigger walipata sana misukosuko ya kukamatwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano. Lakini hata hivyo hawakupata fununu yoyote ile, pamoja na kutumia hadi njia ya vitisho na mateso kwa wale waliokuwa wanawatilia shaka, kwa bahati mbaya kabisa hawakuwa wamepiga hatua yoyote ile. ***** Inspekta Jasmine Wahabu, alikuwa askari wa kike. Askari shupavu na jasiri aliyekuwa anategemewa sana na jeshi la polisi nchini Tanzania. Inspekta Jasmine alishafanikiwa mara kadhaa kuwatia wahalifu nguli mbaroni. Kufanikiwa huko kwa Inspekta Jasmine kulifanya azidi kutegemewa na nchi, kutegemewa na jeshi la Polisi. Inspekta Jasmine alitegemewa pia na raia wema. Baada ya wiki kadhaa za kuwatafuta wahalifu pamoja na watu na wanafunzi waliopotea katika mazingira ya kutatanisha kugonga mwamba. Inspekta Jasmine ndiye aliyepewa jukumu na Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania ili kwenda Kilwa kupeleleza juu ya upotevu wa watu hao. Inspekta Jasmine sasa alikuwa na siku ya pili ndani ya Kilwa lakini upelelezi wake ulikuwa haujamfikisha kabisa karibu na adui. Ilikuwa siku ya tatu sasa tangu inspekta Jasmine Wahabu awasili Kilwa ili kwenda kutatua utata juu ya kupotea kimaajabu kwa watu ndani ya Kilwa, tena katika hali isiyoeleweka hadi sasa. Siku hiyo ya tatu asubuhi na mapema Inspekta Jasmine ilimkuta akiwa amelala kitandani, katika nyumba ya kulala wageni aliyofikia. Ghafla alisikia sauti ya wimbo wa Daz P, simu yake ya mkononi ilikuwa inaita. Inspekta Jasmine alitupa shuka yake nyeupe pembeni na kuifata simu yake ambayo aliyokuwa anaichaji.


    Inspekta Jasmine alitupa shuka yake nyeupe pembeni na kuifata simu yake ambayo aliyokuwa anaichaji. 'Afande Dismas' inspekta Jasmine alisema kwa sauti ndogo. Inspekta Jasmine alikuwa amepigiwa simu na askari polisi aitwaye Dismas. Alibonyeza kitufe cha kijani cha kupokelea simu na kuiweka sikioni ili kusikiliza. Simu kutoka kwa Afande Dismas ilileta kwa inspekta Jasmine taarifa juu ya Dokta aliyekutwa amefungwa kamba katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi. Ilikuwa asubuhi, Mhudumu alimkuta Dokta Kilumba akiwa kafungwa mle chumbani alipokuwa anaenda kufanya usafi wa kile chumba. Mhudumu aliamua kumtaarifu Bosi wake kisha kupiga simu Polisi. Baada ya muda mfupi afande Dismas akiwa na askari wengine sita waliwasili pale. Na ndipo waliamua kumtaarifu inspekta Jasmine juu ya tukio lile. Tokea kule nyumba ya kulala wageni, Inspekta Jasmine alivaa nguo za kiraia haraka, alivaa suruali aina ya jeans na tshirt nyeusi na kuelekea eneo la tukio. Baada ya uchunguzi wa kiaskari mle chumbani walimchukua Dokta Kilumba na kumpeleka hospitali. Nia ni kuangalia athari aliyoipata Dokta Kilumba, huku askari Polisi wakiongozwa na inspekta Jasmine wakimsubiri kwa hamu apate nafuu kwa ajili ya mahojiano maalum ili awaeleze kitu kilichotokea mpaka ikatokea akafungwa namna ile. Baada ya kumuacha Dokta Kilumba pale hospitali na kuacha askari kadhaa kwa sababu za ulinzi na usalama. Inspekta Jasmine alitoka hospitali na kuelekea kituo cha Polisi. Mahali ilipokuwepo ofisi yake kwa kipindi chote atakachokuwa Kilwa kwa ajili ya operesheni hii. Alipoweka kitako tu katika kiti chake, simu yake ya mkononi iliita tena. Safari hii jina lililosomeka katika kioo cha simu yake lilikuwa Songelael.... "Hallo" upande uliopiga ile simu ndio ulioanza kuita. "Nambie Songe" inspekta Jasmine alijibu ile simu huku akiwa makini. "Sasa nimegundua kila kitu Inspekta kuhusu huu mkasa" Songelael aliongea kwa sauti ndogo simuni. Sauti iliyoonesha hakuwa sehemu ya kawaida. "Eeeh umegundua nini Songe" inspekta Jasmine aliuliza kwa shauku kubwa ya kutaka kujua hiko kitu alichokigundua Songelael. " Tusiongee sana Inspekta....njoo katika pori la Ngome sasahivi, ukiwa unakaribia kufika nipigie ili nikupe maelekezo, njoo na askari wengi inspekta " Songelael aliongea kwa kirefu simuni. Muda huohuo baada ya ile simu toka kwa Songelael gari tano za Polisi zikiwa na Polisi zaidi ya arobaini zilikuwa njiani kuelekea porini Ngome. Gari za polisi zilitembezwa kwa kasi sana huku zikiwa na Askari waliojipanga kivita, na silaha mzitomzito, walikuwa tayari kwa lolote, walikuwa na uhakika na wanachoenda kukifanya baada ya kuhakikishiwa na askari imara wa kike, inspekta Jasmine, kuwa wanakoenda ndio kwenye jibu la wahalifu wote wanaoisumbua Kilwa. Inspekta Jasmine mwenyewe alikuwa juu ya pikipiki kubwa aina ya Kawasaki, naye akielekea porini Ngome kwenda kuumaliza mchezo. Kule ndani ya kambi sasa, Mpelelezi Daniel Mwaseba walikuwa wanatazamana macho kwa macho na Moja wa toka kundi la Six killers. Kukutana ghafla na Mateka wao akiwa huru kulimfanya Moja asite kidogo, alibabaika kwakuwa hakujua Daniel katokaje katika chumba cha kifo, pia alibabaika kwa kuwa hakujua amfate yupi? amfate yule mtu aliyekuwa kule juu ya ukuta wa kambi yao ama aanze kupambana na huyu aliyepo mbele yake, Daniel Mwaseba. Kusitasita kwa Moja ilikuwa faida kubwa sana kwa Daniel Mwaseba. Baada moja alipata wazo la kutoa bastola yake iliyokuwa kotini, aliamua kuanza kummaliza Daniel Mwaseba kwa risasi, lakini alikuwa amechelewa sana........ Daniel aliruka sarakasi kwa kasi toka pale alipokuwa amesimama na kwenda kumvaa Moja kwa nguvu. Bastola ya Moja ilirudi tena ndani ya koti bila kupenda. Kule juu ya ukuta alikokuwa Dokta Yusha, alikuwa anashuhudia kila kitu. Sasa Dokta Yusha alikuwa anatafuta namna ya kudumbukia ndani kutokea kule juu ya ukuta. Baada ya kuvamiwa kwa nguvu na Daniel Mwaseba, Moja aliyumba kidogo kisha akasimama imara tayari kwa kupambana na Daniel Mwaseba. Ilhali sasa wote wakiwa mikono mitupu. Kabla hawajaanza hata kurushiana ngumi, Tatu wa Six Killers alitoka nje ya ile nyumba ya bluu, akiwa na bastola mkononi. Tayari kwa kuua! Balaa! Tatu wa Six Killers alivyotoka tu nje aliona mambo mawili kwa mpigo. Kwanza Komando Tatu alimwona Dokta Yusha akiwa anaelea hewani akiingia mle ndani ya kambi yao, Dokta Yusha aliamua kujirusha toka kule ukutani na wakati huohuo aliwaona Moja na Daniel Mwaseba wakiwa wanatazamana kwa chuki wakiwa tayari kwa kupambana. Bila kutegemea Tatu wa Six Killers nae akapatwa na mfadhaiko mkubwa, mfadhaiko kama alioupata Komando Moja wa Six Killers alivyokutana na hali hii. Daniel Mwaseba nae alimwona Tatu pale mlangoni. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka. Kwa muda ule aliona Tatu ni hatari zaidi ya Moja, kwa kuwa Tatu wa Six Killers alikuwa na silaha mkononi. Mpelelezi Daniel Mwaseba alitoka kwa kasi kubwa sana na kufanya kama anamvaa Moja lakini alipitiliza, moja kwa moja alienda kumvaa Tatu pale mlangoni kwa msukumo mkubwa. Msukumo ulioleta faida kubwa sana. Ughafla na nguvu ya msukumo ule uliomwacha Tatu wa Six Killers akiwa kalala chali ardhini bila bastola mkononi. Sasa Daniel Mwaseba ilimpasa kupambana na watu wawili hatari sana. Moja na Tatu wote toka kundi hatari la Six Killers. Moja wa Six Killers alikuwa amefura kwa hasira. Sasa alikuwa anamfata Daniel Mwaseba kwa ghadhabu, lakini kwa bahati mbaya kabisa hakumfikia Daniel, akiwa katikati katika safari yake ya kumfata Daniel Mwaseba alikutana na MTU! Alikutana na Dokta kijana, Dokta makini, Dokta shujaa, Dokta msomi, Dokta Shupavu, Dokta Mzalendo......Moja alikutana na Dokta Yusha! Tena Dokta Yusha akiwa imara kupambana na jambazi namba moja toka kundi hatari la Six Killers. Waligawana bila kutarajia, yaani ilitokea tu...sasa ilikuwa kila mtu na wake, Tatu wa Six killers na Daniel Mwaseba, Moja wa Six Killers na Dokta Yusha. Tatu wa Six Killers alivyotoka tu nje aliona mambo mawili kwa mpigo. Kwanza Komando Tatu alimwona Dokta Yusha akiwa anaelea hewani akiingia mle ndani ya kambi yao, Dokta Yusha aliamua kujirusha toka kule ukutani na wakati huohuo aliwaona Moja na Daniel Mwaseba wakiwa wanatazamana kwa chuki wakiwa tayari kwa kupambana. Bila kutegemea Tatu wa Six Killers nae akapatwa na mfadhaiko mkubwa, mfadhaiko kama alioupata Komando Moja wa Six Killers alivyokutana na hali hii. Daniel Mwaseba nae alimwona Tatu pale mlangoni. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka. Kwa muda ule aliona Tatu ni hatari zaidi ya Moja, kwa kuwa Tatu wa Six Killers alikuwa na silaha mkononi. Mpelelezi Daniel Mwaseba alitoka kwa kasi kubwa sana na kufanya kama anamvaa Moja lakini alipitiliza, moja kwa moja alienda kumvaa Tatu pale mlangoni kwa msukumo mkubwa. Msukumo ulioleta faida kubwa sana. Ughafla na nguvu ya msukumo ule uliomwacha Tatu wa Six Killers akiwa kalala chali ardhini bila bastola mkononi. Sasa Daniel Mwaseba ilimpasa kupambana na watu wawili hatari sana. Moja na Tatu wote toka kundi hatari la Six Killers. Moja wa Six Killers alikuwa amefura kwa hasira. Sasa alikuwa anamfata Daniel Mwaseba kwa ghadhabu, lakini kwa bahati mbaya kabisa hakumfikia Daniel, akiwa katikati katika safari yake ya kumfata Daniel Mwaseba alikutana na mtu! Alikutana na Dokta kijana, Dokta makini, Dokta shujaa, Dokta msomi, Dokta Shupavu, Dokta Mzalendo......Moja alikutana na Dokta Yusha! Tena Dokta Yusha akiwa imara kupambana na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    jambazi namba moja toka kundi hatari la Six Killers. Waligawana bila kutarajia, yaani ilitokea tu...sasa ilikuwa kila mtu na wake, Tatu wa Six killers na Daniel Mwaseba, Moja wa Six Killers na Dokta Yusha. Kule nje ya kambi ile hatari ya Six killers askari lukuki wa jeshi la Polisi walikuwa wameshakamilisha zoezi la kuizunguka ile kambi pande zote. Lilikuwa zoezi rahisi sana kwa askari Polisi tofauti kabisa na walivyotegemea, urahisi huo ulitokana na umakini wa Six Killers ulikuwa umepungua kutokana na upinzani wa watu wawili mle ndani, upinzani toka kwa Dokta Yusha na Mpelelezi Daniel Mwaseba. Askari Polisi walikuwa wanaongozwa na yule jamaa aliyempigia simu inspekta Jasmine, aliyejulikana kwa jina la Songelael Ntenga. Jamaa makini aliyewapigia simu askari Polisi na kuwaeleza uwepo wa watu hatari mahala pale. Kule ndani kabisa ya ile nyumba ya bluu. Walikuwa wamebaki watu wawili tu, komando Nne wa Six Killers na mkuu wa kundi hili hatari, Don Genge. Walikuwa wapo sebuleni wakiangalia runinga, bila kujua wala kuhisi kwamba walikuwa katika hatari kubwa sana. Walikuwa wamezungukwa na askari Polisi kwa nje, walikuwa wamevamiwa na Daniel Mwaseba na Dokta Yusha kwa ndani.


    Walikuwa wamezungukwa na askari Polisi kwa nje, walikuwa wamevamiwa na Daniel Mwaseba na Dokta Yusha kwa ndani. Wao walikuwa hawana wasiwasi wowote ule, wakijua kuwa hali ya usalama tayari imedhibitiwa vizuri, na vijana wao wawili, Moja na Tatu wa Six Killers, laiti wangejua. Pale nje mapambano yalianza......Tatu wa Six Killers alimfata kwa kasi Daniel Mwaseba huku akitanguliza kichwa chake mbele, lengo lake kuu ni kwenda kumzoa Daniel Mwaseba kwa kutumia kichwa chake kilichokomaa kwa shuruba na mazoezi. Daniel Mwaseba alikuwa aneshatambua tayari nia ya Tatu wa Six Killers, labda pengine kabla ya yeye kufikiria kufanya hivyo. Kumbuka siku zote Daniel Mwaseba alikuwa anaendeshwa na hisia, na mara zote hisia zake zilikuwa sahihi, hisia za Daniel Mwaseba hazikuwa kuwa hisia za uwongo. Ujio wa Tatu kwa kutumia kichwa Daniel Mwaseba aliutambua. Hakutaka kukwepa kile kichwa, Daniel alikomaza tumbo lake, kichwa cha Tatu wa Six Killers kilienda kukutana na tumbo imara la Daniel Mwaseba. Tumbo lililokuwa tayari kwa mkutano huo. Kama kichwa cha Tatu wa Six killers kilidhani kuwa kimekomaa basi kilikuwa kinajiongopea chenyewe, tumbo la Daniel Mwaseba lilikuwa zaidi yake. Tumbo lilikuwa limekomaa hasa! Au tunaweza sema limekomazwa na mmiliki wa tumbo lile, ambaye ni Daniel Mwaseba. Baada ya zuio la kichwa kile Daniel Mwaseba hakushangaa, alirusha teke la nguvu kwa kutumia mguu wake wa kushoto, teke ambalo lililokwepa na Tano wa killers kwa ufundi mkubwa sana. Upande wa pili wa mapambano, ule wa Dokta Yusha na Moja ilikuwa balaa. Dokta Yusha alipanga ngumi tayari kwa lolote huku Moja wa Six killers akimwangalia, najua unajua kwanini alipewa namba Moja huyu mtu. Moja wa Six Killers alikuwa mtu hatari zaidi ya watu wote katika kundi hili. Moja alikuwa makini na mtulivu sana katika mapambano, alikuwa anazijua mbinu zote za mapambano, hakuwa mtu wa papara kabisa. Kwa ujumla alikuwa anatumia akili na hesabu wakati wa mapambano. Dokta Yusha alirusha teke! Teke lililodakwa na mkono imara wa Moja wa Six Killers. Mguu wa Dokta Yusha ukiwa umeshikwa kwa juu, Moja alirusha ngumi Kali, ngumi iliyotua sawia katika korodani za Dokta Yusha. Dokta Yusha alitoa ukelele mkali huku akidondoka chini mithili ya gunia. Moja akimfata hadi pale chini. Alipiga kareti moja ya nguvu iliyompata Dokta Yusha kifuani. Dokta Yusha alikohoa bila kupenda, alikohoa damu! Moja hakutaka kumpa nafasi wala nafuu Dokta Yusha. Akiwa palepale chini, alimpiga kichwa cha nguvu Dokta Yusha katikati ya mwamba wa pua. Akiwa amelala ardhini sasa Dokta Yusha alianza kuchanganyikiwa. Aliiona dunia inazunguka, tena inazunguka kwa kasi kubwa sana, huku malaika mweusi mtoa roho akimsogelea palepale alipolala huku katanua mikono yake. Ilikuwa lazima Malaika mtoa roho aende maeneo yale. Moja hakuwa na huruma kabisa. Alikuwa anampiga Dokta Yusha mapigo mazito sana. Mapigo ambayo Dokta Yusha hakuweza kabisa kuyavumilia hata kidogo. Mara mlango wa ile nyumba ndogo ulifunguliwa. Walitoka watu wawili toka katika mlango ule...Don Genge mwenyewe akiwa na Nne wa Six killers walisimama katikati ya mlango. Wakishuhudia mapambano yale yasiyo rasmi. Kule nje Polisi wakiwa wana ongozwa na inspekta Jasmine walikuwa wamejipanga vizuri. Walikuwa wanasubiri amri tu ya bosi wao ili wavamie ile kambi. Hawakutaka kufanya makosa, kosa lolote lingeleta madhara makubwa sana, maana wale watu walikuwa wamewateka raia wema mle ndani. Ndani ya nyumba mapambano yaliendelea. Wakati Dokta Yusha kadhibitiwa barabara na Moja wa Six Killers, Daniel Mwaseba alikuwa bado anapambana na Tatu wa Six Killers. Daniel sasa alikuwa amemkaba roba kwa nyuma Tatu, huku Tatu jasho lilikuwa linamtoka. Ghafla katika uwanja wa mapambano akaongezeka mtu mwengine. Moja alimwacha Dokta Yusha pale chini na kumfata huyo mtu, huyo mtu alikuwa anaitwa Songelael Ntenga. Songelael Ntenga aliingia mle ndani wakati muafaka. Angechelewa dakika moja tungesema mengine juu ya maisha ya Dokta Yusha. Dokta Yusha akiwa pale chini alimshuhudia yule jamaa akiyepambana nae sasa akimfata Mwanasheria mlevi. Pamoja na kuchoka sana lakini Dokta Yusha alimuhurumia sana Mwanasheria mlevi, alijua hana uwezo wa kupambana na yule jamaa hatari, ambaye sasa aligeuka mbogo. Yeye mwenyewe alikuwa taabani lakini alijinyanyua juu kwa nguvu. Akitaka kumzuia Moja asiende kumdhuru Mwanasheria mlevi, kwake Mwanasheria mlevi alikuwa zaidi ya rafiki kwake, huku akiamini Mwanasheria mlevi hawezi kupambana kabisa. Alijidanganya.. Dokta Yusha hakutambua kabisa kama mtu tunayemtambua sisi kama Songelael Ntenga yeye alikuwa anamtambua kama Mwanasheria mlevi. Naam, Mwanasheria mlevi hakuwa mtu wa kawaida. Alikuwa ni afisa usalama wa Taifa wa ngazi za juu. Mtu makini anayeheshimiwa na Taifa hili, mzuri katika kupigana aina zote za mitindo ya kimapigano. Mwanasheria mlevi alikuwa ameenda Kilwa kwa kazi maalum. Kazi ambayo ipo ndio hii iliyopo mbele yake sasahivi. Mguu wa Moja ulivyokuwa unapiga hatua ya tatu haukufika chini mguu ule, Mwanasheria mlevi alimfata kwa kasi huku akiachia mapigo mawili hewani! E bwana eeee! Wote walioshuhudia alichokifanya Mwasheria mlevi walibaki midomo wazi! Moja alianguka chini kwa nguvu, mithili karushwa na shoti ya nguvu ya umeme. Akipigania roho yake. Don Genge aliyashuhua vizuri sana yale mapigo hatari ya Mwanasheria mlevi. Mapigo ambayo nashindwa hata kuyaelezea hapa. Sasa Don Genge akaona mambo mazito, maji yamezidi unga! Kwa kasi ya haraka akachomoa bastola yake na kumlenga Mwanasheria mlevi. Wakati huohuo Daniel Mwaseba alikuwa kamkaba Tatu wa Six Killers, nae alishuhudia kitendo kilichotaka kufanywa na don Genge. Kumbuka Daniel Mwaseba pia alishuhudia mapigo ya Mwanasheria mlevi, lakini hakushangazwa na mapigo yale. Alikuwa anamfaham Mwanasheria mlevi vizuri sana. Sasa Daniel Mwaseba alikuwa anapiga mahesabu nini cha kufanya. Dokta Yusha alibaki kahemewa tu, alihemewa na yale mapigo hatari toka kwa Mwanasheeia mlevi, alihemewa na ile bastola iliyo mikononi mwa Don Genge, ikiwa inamlenga rafiki yake mwenye maajabu, Mwanasheria mlevi. Dokta Yusha alikuwa haelewi kipi cha kufanya kipi cha kuacha. Don Genge huwa hatanii !!! Don Genge alivuta triga ya bastola tayari kwa kufyatua.. Paaaaaaa! Ulisikika mlio mkali wa bastola hewani. Kila mtu alipigwa na butwaa bila kujua nani kapigwa risasi ile, wote walijua

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kwamba Don Genge ndiye kafyatua risasi ile. Haikuwa hivyo! Ilikuwa ni bastola ya askari makini wa kike, inspekta Jasmine iliyopigwa hewani. Ndio iliyofanya kazi ile ya kuokoa uhai wa Mwanasheria mlevi. Kabla hata akili za watu pale hazijatulia, ghafla eneo lote lilizungukwa na askari Polisi. Ama hakika, kundi la Six killers walikuwa wamewezwa kisawasawa. Don Genge akiwa na bastola yake mkononi alitulia tuli, kidole chake cha shahada cha mkono wa kulia kikiwa bado kimeigusa triga ya bastola yake, ilikuwa afyatue ili afyatuliwe! Don Genge aliwaangalia askari wale lukuki kwa zamu. Akajua mwisho wake umefika, mwisho wa mchezo wao mchafu umefika. Sasa alitafuta namna ya kujiokoa. Hakuwa tayari kuingia katika mikono ya Polisi. Tokea palepale mlangoni aliposimama aliruka sarakasi za kinyumenyume kurudi ndani ya nyumba ya bluu! Askari wote walibaki mdomo wazi, hawakutegemea kabisa kutokea kitendo kile. Bila kujiuliza mpelelezi Daniel Mwaseba alitoka kasi kukimbilia mle ndani, huku akifuatwa kwa nyuma na Songelael Ntenga au Mwanasheria mlevi. Pale nje Moja, Tatu na Nne waliwekwa chini ya ulinzi imara wa askari Polisi, wakafungwa pingu. Wakawekwa chini ya ulinzi wa askari kumi kuwalinda, huku askari wengine wakiizunguka ile nyumba ya bluu aliyoingia Don Genge. Wakihakikisha Don Genge hana pakutokea. Askari walichanga karata zao vizuri sana. Kule ndani Daniel Mwaseba na Songelael Ntenga walifanya msako wa nguvu. Walitafuta kila chumba, walitafuta kila mahali, Daniel Mwaseba alipanda hadi darini lakini Don Genge hawakumuona! Ilikuwa kama hakuingia mle ndani. Daniel Mwaseba hakukubaliana na ukweli kuwa Don Genge alikuwa ameyeyuka! Atayeyuka vipi? Askari thelathini waliingia ndani ya nyumba ile, walipekua sana, lakini majibu yalikuwa yaleyale. Hakukuwa na Don Genge mle ndani. Walianza kuwatesa mateka wao ili wawaambie mahali atakapokuwa amejificha Don Genge. Hakuna aliyethubutu kusema. Wote walijibu kijeuri, wote walikuwa sugu! Hawakuwa na namna nyingine, wale kina Moja walipelekwa kituo cha polisi. Walionesha mahali walipowaficha watu waliowateka lakini hawakuonesha mahali alipo Bosi wao, Don Genge. Walikubali kuwataja wale madaktari wote waliohusika katika mpango huu wa BALAA lakini sio Don Genge, hawakumtaja kabisa. Manesi na madaktari wote walikamatwa kama vifaranga vya kuku. Ilikuwa rahisi sana. Hawakuwa na mbinu zozote za kuwazidi kina Daniel Mwaseba. 
    ***** 
    Baada ya mwezi mmoja wale wahalifu wa Six killers na madaktari wote walihukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama kuu kanda ya Kusini iliyopo huko Mtwara. Haikuwa kesi ngumu sana, wahalifu wote walikubali makosa yao. Ilimshangaza kila mtu. Suala la kupotea kwa Don Genge likabaki kitendawili kisicho na majibu. Wapo walioamini kuwa yule mtu katili kabisa alikuwa mchawi. Aliingia mle ndani na kuyeyuka! Lakini mawazo hayo hayakupata nafasi katika kichwa cha Daniel Mwaseba, hayakupata nafasi katika kichwa cha Songelael Ntenga, hayakupata nafasi katika kichwa cha Dokta Yusha, wote walikula yamini lazima wahakikishe wanamtia mikononi Don Genge, bila ya kujua watampata kwa namna ipi.


    UJUMBE MZITO KUTOKA KWA HALFANI SUDY:
    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog